12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1045 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Mwaka mpya 1434 Mhariri wa gazeti la AN- NUUR wa watendaji wake wanawatakia kheri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1434 Hijiria Mamlaka ya Zanzibar lazima Kiti chake Umoja wa Mataifa bado kipo Muungano uliopo umepitwa na wakati Karume aibuka shujaa Ukweli ni upi zaidi ya huu aliosema kule Dodoma? Tatizo si Farid wala Uamsho, ni madai ya wananchi Hata wa Serikali Tatu, Mkataba nao wasikilizwe pia Aliyekojolea Qur'an kizimbani Dar DKT. Amani Karume SHEIKH Farid Hadd Lipumba ahofia nchi ‘kutekwa’ na mafisadi Adai wanakimbilia pato la gesi Ashauri katiba mpya ilinde rasilmali za Taifa DAUDI Kapaya, mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Ukonga Majumba Sita, kitongoji cha Mogo Mkengeni, Aliyekojolea Qur’an afikishwa mahakamani Sheikh Ponda kulindiwa heshima yake Na Mwandishi Wetu jana alifikishwa katika mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kesi ya kukojolea Qur’an inayomkabili. Hata hivyo katika hali ya Inaendelea Uk. 4 DAUDI Kapaya (wa pili kutoka kushoto) akiwa mahakamani Kisutu jana.

Annuur Ijumaa

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Karume aibuka shujaa* Ukweli ni upi zaidi ya huu aliosema kule Dodoma?* Tatizo si Farid wala Uamsho, ni madai ya wananchi.* Hata wa Serikali Tatu, Mkataba nao wasikilizwe pia.Mamlaka ya Zanzibar lazima* Kiti chake Umoja wa Mataifa bado kipo.* Muungano uliopo umepitwa na wakatiLIpumba ahofia nchi “kutekwa” na mafisadi* Adai wanakimbilia pato la gesi.* Ashauri katiba mpya ilinde rasilimali za Taifa

Citation preview

Page 1: Annuur Ijumaa

ISSN 0856 - 3861 Na. 1045 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu Mwaka mpya 1434Mhariri wa gazeti la AN-

NUUR wa watendaji wake wanawatakia

kheri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1434 Hijiria

Mamlaka ya Zanzibar lazimaKiti chake Umoja wa Mataifa bado kipoMuungano uliopo umepitwa na wakati

Karume aibuka shujaaUkweli ni upi zaidi ya huu aliosema kule Dodoma?Tatizo si Farid wala Uamsho, ni madai ya wananchiHata wa Serikali Tatu, Mkataba nao wasikilizwe pia

Aliyekojolea Qur'an kizimbani Dar

DKT. Amani Karume SHEIKH Farid Hadd

Lipumba ahofia nchi ‘kutekwa’ na mafisadi

Adai wanakimbilia pato la gesiAshauri katiba mpya ilinde rasilmali za Taifa

D A U D I K a p a y a , mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Ukonga Majumba Sita, kitongoji cha Mogo Mkengeni,

Aliyekojolea Qur’an afikishwa mahakamani

Sheikh Ponda kulindiwa heshima yake Na Mwandishi Wetu jana alifikishwa katika

mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kesi ya k u k o j o l e a Q u r ’ a n inayomkabili.

Hata hivyo katika hali ya Inaendelea Uk. 4

DAUDI Kapaya (wa pili kutoka kushoto) akiwa mahakamani Kisutu jana.

Page 2: Annuur Ijumaa

2 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari

Mamlaka ya Zanzibar lazimaMAKAMO wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maaalim Seif Sharif Hamad amesema Muungano wa Tanzania uliyopo sasa tayari umepitwa na wakati na ufumbuzi pekee ni Muungano mpya, utakaotoa mamlaka kamili kwa Zanzibar.

Maal im Se i f ambaye amekuwa akipinga wazi wazi muundo wa Muungano huo tangu akiwa Waziri Kiongozi, mwishoni mwa miaka ya 1980, akiwa nje ya Serikali na sasa akiwa kiongozi wa pili Mkuu wa Serikali ya Zanzibar.

Akihutubia mkutano wa hadhara Mwanakwerekwe, Unguja hivi karibuni, Maalim Seif alisema Muungano wa Zanzibar na Tanganyika hauna ufumbuzi bali Zanzibar, inahitaji Muungano mpya:

“Muungano huu hauna ufumbuzi bal i tunataka muungano mpya kabisa wenye mamlaka kamili…Zanzibar iwe na mamlaka kamili na Tanganyika iwe na mamlaka kamili huo ndio muungano tuutakao,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema Zanzibar inadidimia kutokana na udhibiti wa Muungano kwa kukosa mawasiliano ya moja kwa moja na mataifa ya nje na mashirika ya kimtaifa.

“Kiti chetu tunacho Umoja wa Mataifa na mpaka leo hak i j aondo lewa , l ak in i kiliwekwa kando kidogo kwa hiyo barua iliyotoka Dar es Salaam, na sisi kwa bahati mbaya hatukuiuliza,” alisema na kufafanua zaidi kwamba:

“Sisi hatuna mamlaka ya kuzungumza na nchi yoyote wala shirika lolote la nje na halikuwa katika Katiba ya Muungano lililowekwa katika Muungano ni mambo ya nje…Mashirikiano ya Kimataifa katika ‘article of union’ hilo halimo,” alisema Maalim Seif.

A k i z u n g u m z a k w a kuj iamini Maal im Seif , alisema suala la Ushirikiano wa Kimataifa halikuwapo katika Mkataba wa Muungano, n a k u u n g i z w a k w a k e kulisababisha kuipotezea Zanzibar mawasialino na Mataifa ya nje.

“Serikali ya Muungano wenzetu walibadilisha wakaita

Na Mwandishi Wetu

‘Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa’ hilo ushirikiano wa kimataifa halimo katika ‘article of union’ wamelipenyeza,” alisema na kuendelea:

“Kwa hivyo wametukata miguu na unapeleka nyaraka za kusaidiwa zinaganda kwao, kwa hivyo Muungano huu hautufai Wazanzibari, hao wenye kusema Serikali hizi lazima tunawaambia lazima ni Mwenyezi Mungu tu, hilo unalisema wewe tu, nani kakutuma ukaseme hivyo,” alisema maalim Seif.

Maalim Seif , al isema Waziri Mkuu wa Tanzania mheshimiwa Mizengo Pinda, amekuwa akitoa vitisho dhidi ya watu wanaohitaji mabadiliko ya Muungano ili Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili:

“Mheshimiwa Pinda, anatoa vitisho anasema Muungano w e t u u m e s h a k o m a a …kukomaa kwa maana ya kupea sio kama ukoma…sasa anasema laa Mtanganyika awe Mtanganyika, Wazanzibari warudi kwao…kakwambia nani Pindaaaa, au ndiyo vitisho?,” alihoji Maalim Seif.

A l i s e m a k w a s a s a Mzanzibari hatishiki tena,

wakati wa vitisho umekwisha: “Mimi nawambia wananchi sababu za Muungano huu ni kuunganisha nchi za Afrika, hebu nambieni nani amekuja kujiunga?,” aliuliza na kuendelea:

“Kuna wakati baadhi ya viongozi wa Afrika walitaka kujiunga, wala haji. Maana kuna wakati Mzee Kaunda, alikuja akachungulia, lakini akasema aaaa sitaki,” alisema Maalim Seif.

Kuhusu wafanyakzi katika Balozi za Tanzania nchi za nje, alisema hakuna uwiano wa kuridhisha baina ya wafanyakazi katika ofisi hizo na wote wanatoka upande mmoja wa Muungano:

“Nilikuwa huko Ulaya kuna maofisa 23 Mzanzibari mmoja tu na Umoja wa Mataifa ndiyo kwanza kapelekwa juzi Muombwa, ukenda Uingereza kati ya 19 wote Mzanzibari mmoja, jee hiyo ni haki? Aliuliza na kuendela:

“Lakini watu wameshika Serikali mbili, yagujuuu!! tunasema tunadai na kudai haki sio vibaya na niwaambie kuna nchi ya Misri na Syria na Syria walipoona mambo hayendi vizuri wakajitoa wala hawakujitoa juzi nilishangaa mheshimiwa Pinda anatoa vitisho,” alisema Maalim Seif.

MAKAMO wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maaalim Seif Sharif Hamad.

LEO ni Muharam 1434, mwaka mpya wa Kiislamu. Huu ndio mwaka ambao k i l a M u i s l a m u anatakiwa aujali , auzingatie, authamini na kuuzoea. Kama ni kusherehekea mwaka mpya kwa Muislamu, basi sherehe yake ni leo.

T u m e l a z i m i k a kukumbusha juu ya umuhimu wa mwaka mpya wa Kiislamu kwa kuwa sehemu kubwa ya jamii ya Kiislamu nchini, na hata katika m a t a i f a m e n g i n e , imeshindwa kuutendea haki mwaka huu.

Wengi hawajui hata kalenda ya Kiislamu inakwenda vipi, wala hawajui matukio ya Kiislamu kwa mujibu wa kalenda ya Kiislamu yanapatikana vipi . Hii yote ni kasoro ya kushindwa kujenga mazoea ya kuzingatia kalenda yetu.

B a d a l a y a k e , Waislamu wamekuwa m s t a r i w a m b e l e kuandaa sherehe za mwaka mpya usiokuwa wa Kiislamu. Ikifika saa sita usiku Desemba 30 au 31, inakuwa vigumu kumtambua Muislamu kati ya wale w a n a o s h e r e h e k e a mwaka mpya huo.

K a r i b u w o t e w a n a s h a n g i l i a n a kushereheka mwaka mpya ambao hawajui historia yake wala

Tuuenzi mwaka mpya wa Kiislam

chanzo na sababu zake.

Tena utaona wengi wakisherehekea katika njia za uasi na ovu.

Tuseme tu kwamba ni Waislamu wachache s a n a w a n a o w e z a kuku ta j i a s iku ya Maulidi ya Mazazi ya Mtume (saw), kadhalika uchache huo utaukuta kwa wanaojua tarehe za Umra na hata Hija.

Pia hatuna shaka kusema kwamba, ni Waislamu wachache s a n a w a n a o p a n g a m i k a k a t i y a o y a kimaisha ya kila siku, katika kipindi chote cha mwaka kwa kuzingatia kalenda ya Kiislamu.

Kwa kuwa ni wajibu wetu kukumbushana, b a s i t u n a c h u k u a nafasi hii kuwajulisha Waislamu wote kwamba, mwaka wao unaanza leo, basi tuusherehekee kwa mijibu wa adabu zetu.

K w a k u j a r i b u kujizoesha, kuzingatia, kufuatilia na kuitumia kalenda ya Kiislamu katika shughuli zetu.

Tukifanikiwa hili, bila shaka tutakuwa t u m e i t e n d e a h a k i kalenda ya Kiislamu k w a k u i f u a t a n a kuifanyia kazi kwa vitendo, na hakika tutakua tumefaulu.

T u n a w a t a k i w a Waislamu wote mwaka mpya wa wenye heri tele.

Page 3: Annuur Ijumaa

3 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Habari

Karume aibuka shujaaC C M i n a k a b i l i w a n a kukwazwa na Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Usisikie wanasema iko hali nzuri GNU. Sio kweli. Kile ni kipingamizi kikubwa kwao na ndio Amani Karume akaanza kuwapiga DONGO kwa kuwaambia kuwa “Serikali ile ni makubaliano yetu wenyewe CCM”. Hii n i sawa na kuwambia mulitaka wembe wenyewe, umewakata, sasa kelele za nini?

CCM inakabiliwa na katalio la wananchi na jumuiya za kidini kwa sasa. Yote haya ni mambo makubwa yanayoikwaza CCM.

Amani Karume ni CCM muelewa anaefikiri kisasa zaidi. Na pamoja na kuwa hutuba yake imekuwa mwiba kwa wote wal iokuwepo mkutanoni pamoja na Marais wetu, hawakufurahika nae. Lakini kwa ujasiri mkubwa alionao Kamanda huyu wa vita asiekuwa na woga, amesema kila alichotaka kukisema hata kama kitamugharimu maisha yake yote baadae, basi historia ya alichokisema itabaki. Na ndio mara nyingi nikasema Karume ni tafauti, mkweli, hodari, na shujaa kwani hakuna kiongozi yoyote wa Zanzibar aliye na ujasiri wa kuweza kuwasema na kuwasema na kuwakosoa CCM ndani ya himaya yao kiasi kile kwa sasa na zamani kama si yeye Amani Karume.

K a r u m e , t a n g u a l i p o u n g a n i s h a w a t u kuwa katika GNU baadhi y a w a t u k a t i k a C C M wamekuwa wak imuona kama muasi katika chama chake mwenyewe ijapokuwa walikubaliana wenyewe lakini sasa wamemgeuka. Na ndio akasema aliyosema. Kuna mengi anayosemwa Karume kwayo kwa sasa likiwemo la Uamsho, na maoni ya katiba. Na bila woga na hili kawajibu kinaga ubaga. Kawajibu kwa hoja za msingi kwa utulivu na kituo bila kujali kuzomewa na kukimbilizwa amalizie hutuba yake haraka. Hakuyajali yote hayo, akakamilisha kusema yote kama alivyoyapanga.

Amani Karume kaondoka Kimwaga kama Mwenyekiti Mstaafu akiwa msafi kabisa kwa nchi yake Zanzibar na kwa Wazanzibari wenzake. Bwana Karume kajibu kwa uwazi kadhia ya vurugu za Zanzibar na kaweka bayana kuwa vurugu zile hazitokani ni vyama bali ni wanaharakati

Na Mwandishi Maalum ambao kwa nilivyofahamu mimi ni wananchi wa kawaida walioamuwa kujiunga kudai haki zao kikatiba. Huu ndio ukweli. Na kwa hili lazima CCM wachukie kwa sababu wao wanasambaza kasumba dunia nzima kuwa vurugu zile ni za makundi ya Kiislamu na CUF. Karume kawasuta!

Bwana Karume hakuishia hapo, kuhusu mchakato wa katiba ambao ndio hasa uliochochea vurugu zilioko Zanzibar sasa, ikiwa pamoja na kukamatwa na kutiwa rumande wanaharakati kama vile Sheikh Farid na wenzake. Mstaafu Karume alisema kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila vitisho. Akaongezea kuwa anayetaka Serikali tatu, mbili, na mkataba asikilizwe

na aheshimiwe wala asitishwe. Ukweli ni upi zaidi ya huu?

Hivi ni nani asiejuwa kuwa mchakato wa maoni ya katiba Zanzibar umegubikwa na vitisho kutoka kwa wana tume wenyewe, CCM, na hata viongozi wa Serikali zote mbili. Taasisi zote hizi zinahusika moja kwa moja na uvurujifu wa amani na haki kwa kuwatisha watu wasitoe maoni yao ambayo si matakwa ya chama na Serikali dhidi ya Muungano. Sasa ikiwa Farid kafungiwa ndani nani angelisemea hili mbele ya wenyewe? Ni Sheikh Amani Karume pekee, nani mwengine angeweza kumfunga paka Kengele, Kimwaga? Kila la her i Karume. Ujumbe umefika. RAIS mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

Inaendelea Uk. 4

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa mtandao wa kifisadi unajiandaa kuiteka CCM, baada ya kujua kwamba kuna mali ya asili ya kutosha nchini hasa baada ya kugunduliwa gesi nyingi nchini, hivyo unajipanga mapema kuchukua madaraka ili kuifisidi nchi.

Prof. Lipumba alisema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Bagamoyo hivi karibuni.

“Mtandao umejipanga watumie fedha kuhakikisha kwamba ndio utakaotoa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM 2015” alisema.

Alitahadharisha kuwa ikiwa wanatumia mamilioni ya fedha ili kumpata mgombea, maana yake ni kwamba wanaotoa fedha hizo za rushwa, wanawekeza ili baadae wapate faida kubwa. Hivyo aliwataka wakazi wa Bagamoyo kutokubali hali hiyo, vinginevyo watamalizwa kiuchumi.

Prof. Lipumba alisema kuwa kugundulika kwa gesi nyingi nchini, mafuta na uranium imekuwa kichocheo kikubwa cha watu kuamua kutumia kila njia kuhakikisha kwamba wanaingia madarakani. Lengo ni kwenda kufaidi mapato ya rasilmali hizo muhimu kwa maendeleo ya nchi, ambazo zinatarajiwa kuliingizia Taifa mabilioni ya fedha siku za usoni.

A l i s e m a T a n z a n i a imebarikiwa kuwa madini ya kila namna, dhahabu, almasi, huku katika maeneo ya Tunduru na Dodoma yakigunduliwa madini ya uranium, ambayo hutumika kwa ajili ya kufua umeme na kutengeneza silaha nzito. Alitoa mfano kwamba

Lipumba ahofia nchi ‘kutekwa’ na mafisadiNa Shaban Rajab robo tatu ya umeme nchi ya

Ufaransa unatokana na madini ya uranium.

Kumegunduliwa Nickel, makaa ya mawe makaa ya mawe ambayo ni mali ghafi ya kutengenezea chuma cha pua, vito kama rubi, tanzanite, imegunduliwa gesi asilia Kilwa, Mafia, Mkuranga na Mtwara. Mahali kwenye gesi kuna mafuta, iwapo kutakuwa na mikataba mizuri, watanzaia nao watakuwa watu wa daraja la kwanza”.

Hata hivyo alisema ana mashaka na matumizi ya mapato ya gesi na madini mengine pale yatakapoanza kuchimbwa, kwani hata baada ya kugunduliwa dhahabu mapema kidogo na kuanza kuchimbwa, bado dhahabu inayochimbwa serikali inashindwa hata kueleza ni kiasi gani cha mapato yanayopata kutoka sekta hiyo, kwa sababu fedha yote inachukuliwa na makampuni ya nje.

Prof. Lipumba amebainisha kwamba kuna kampuni moja ya Norway inayotafiti gesi katika eneo moja kusini mwa nchi, katika bahari ya Hindi linaloitwa Zafarani. Alisema kampuni hiyo ilipokwenda kutafuta gesi na mafuta, ilipochimba kisima cha kwanza wamekuta gesi nyingi yenye kipimo cha futi za ujazo trilioni tano.

Alisema kampuni iliwahi kufanya utafiti wa mafuta na gesi nchini Norway. Ilichimba visima 34 bila kugundua mafuta. Ilikata tamaa na kuhofia kufilisika hivyo kusitisha utafiyti wake. Alisema hata serikali ya Norway iliiomba kampuni hiyo ijaribu kuchimba kisima cha mwisho, na hapo ndipo walipogundua mafuta baada ya kuchimba kisima cha 35.

Alisema kampuni hiyo ilipotoa taarifa ya kugundua gesi nyingi katika pwani ya Tanzania, mara

moja bei za hisa zake ikapanda.Kufuatia kupatikana gesi

nyingi nchini , amewataka watanzania kuhakikisha kwamba wanakiingiza kipengele katika katiba mpya ijayo, kwamba rasilimali zote za asili Tanzania ni mali ya kila mtanzania. Kwamba zimnufaidishe kila mtanzania wa nchi hii.

Alisema kwa kuingia katika katiba kipengele hicho, ni rahisi kuibana serikali kuhakikisha kwamba watanzania hawaibiwi na hawadhulumiwi rasilimali zao, na kwamba hata mikataba yake itakuwa na maslahi kwa watanzania tofauti na ilivyo sasa.

Alisema chama cha CUF kimekuja na sera ya kutaka watanzania wanufaike na rasilmali zao, hasa baada ya kugunduliwa gesi na mafuta nchini.

K w a m b a k u t o k a n a n a kugunduliwa gesi nyingi na mafuta nchini, sehemu ya pato litakalotokana na rasilmali hizo ligawiwe kwa watanzania moja kwa moja.

“Maana yangu nini, ikiwa tuko watanzania milioni 45, kama mapato ya serikali yanayotokana na gesi ni dola bilioni nne na nusu, ukizigawa kwa watu milioni 45 maana yake ni kwamba, kila mmoja anastahili kuwa na dola 1,000”. Alibainisha Prof. Lipumba.

Alifafanua zaidi kwamba, dola 250 kutoka katika gawiwo la dola 1000 kwa kila mtanzania, zitaingizwa kwenye mfuko wa kutengeneza miundo mbinu hususan barabara, reli na katika mfumo wa umeme.

Dola nyingine 250 ziwekwe kwenye mfuko wa akiba, na dola 500 alipwe mtanzania moja kwa moja.

Alisema kuwa amelazimika kutoa ufafanuzi huo wa pato

litakalotokana na gesi kufuatia utafiti uliofanyika katika nchi za Mexico, Brazil na Indonesia. Alisema utafiti huo umebaini kuwa njia nyepesi ya kumsaidia mwananchi maskini aondokane na umaskini wake, ni kumkabidhi fedha taslim.

“Watu maskini wanapopata kipato hutumia vizuri fedha zao ili kuboresha maisha ya familio zao. Vile vile watu maskini wana vipaji vya ujasiria mali unaochochewa na hali zao. Lakini tatizo kwao hawana mitaji. Ikiwa watapata fedha taslim, watapata mitaji na wataweza kuanzisha shughuli zao za kibiashara na kujiajiri”. Alisema Prof. Lipumba.

Alifafanua zaidi kuwa njia ya kuwapatia watanzania fedha taslim zitakazotokana na pato la rasilmali za nchi yao ni rahisi. Alisema kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya vitambulisho vya uraia vinavyotumia alama za mwili, kila mtanzania anaweza kufikiwa na fedha hizo.

Alisema nchini India, kuna watu bilioni moja na milioni mia mbili, ambapo umewekwa utaratibu wa kutoa vitambulisho kwa raia kwa kutumia alama za mwili.

Kwamba mtu anapigwa picha katika mboni ya jicho na kuchukuliwa alama za vidole, viungo ambavyo alama zake hazifanani hivyo kuwa rahisi kuwatambua watu wanaostahili kupata mgawo huo wa serikali.

Aidha alisema teknolojia ya simu imekuwa njia rahisi zaidi kuwapatia watu fedha. Alisema iwapo serikali itaweka utaratibu wa akaunti ya benki kwa njia ya simu za mkononi kwa kila mtanzania, ni rahisi kumpatia raia huyo mgao wake kwa kumwekea kwenye akaunti yake na kwamba hilo linawezekana.

Hata hivyo aliendelea kuitupia

Page 4: Annuur Ijumaa

4 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Habari

MHESHIMIWA Amani k a r u m e a n a t a k a Wazinzibari wanaotaka serikali tatu nao wasikilizwe. M i m i n a k u b a l i a n a naye 100%. Hata hivyo inaonekana kuwa kuna watu imewakera sana, hasa CCM wahafidhina.

Karume alisema, kuhusu katiba mpya Watanzania wote na Wazanzibar pia wasikilizwe na watoe maoni yao hata yale tusiyoyapenda. Akaendelea kusema kwamba, kuhusu Muungano wapo wanaotaka serikali mbili – wasikilizwe, wapo wanaotaka muungano wa mkataba wa serikali mbili- wasikilizwe na wapo wanaotaka serikali tatu — wote wasikilizwe.

Aliposema muungano w a m k a t a b a k e l e l e zilianza, aliposema serikali tatu kelele ziliongezeka. Wapiga kelele hawakuwa na ujasiri wa kumzomea lakini walionekana kupiga kelele za kutokubaliana naye – kwa kuwa hawakufanya hivyo kwa wasemaji wengine ni dalili za wazi kwamba aliwakera wengi.

J a p o k u w a m a g a z e t i hayakuandika kwa upana habari hiyo, hotuba ile imefungua ukurasa mpya kuelekea serikali tatu ambayo ni Sera ya Chadema na CUF – muungano wa serikali mbili sasa ni njia panda.

Kabla ya kufikia hoja hiyo, Amani Karume aliwakubusha wajumbe kuhusu Chama cha ASP, akawaonesha wajumbe kadi yake ya uanachama wa ASP na kuwasomea malengo ya ASP yaliyoko

Hotuba ya Karume ndiyo yenye manufaa kwa CCM

Na Mwandishi Wetu

katika kadi ikiwepo kupigania mustakabali wa Wazanzibar. Indirectly, anataka Zanzibar yake.

Ukiunganisha nukta katika hotuba ya Mh Amani Karume utagundua kwamba anataka Wazanzibar wasikilizwe na kama wanataka serikali tatu nao wasikilizwe. Maana yake wakichagua serikali 3 waruhusiwe kama ilivyokuwa kwa serikali ya umoja wa Ki t a i f a wa l iyo ichagua wenyewe.

Ukiinganisha hotuba yake na kitendo chake kusimamia uundaji wa serikali ya umoja wa kitaitaifa akishirikiana n a M a a l i m S e i f i l i kuwaunganisha Wazanzibar – utagundua kuwa Karume anataka Zanzibar huru. Hiyo ni kwa maoni yangu.

Ukisikiliza vizuri utaona kuwa katika hotuba yake, alipika hii hali ya watu kutishana Zanzibar. Na kusema mtu akiwa na maoni tofauti anapewa jina lile… (Hakulitaja i la nadhani alimaanisha uamsho). Hii ina maana kwamba Amani Karume anawatetea kwa namna isiyo ya moja kwa moja viongozi wanaotaka muundo tofauti wa Muungano wa sasa (Waziri aliyetimuliwa na Rais Shein?). Na ukiunganisha nukta hapa anazunguzia kauli

kwamba wanaotaka muundo wa serikali ambao hauendani na sera ya CCM wajiondoe C C M - y e y e a n a t a k a Wazanzibar wasikilizwe siyo wana-CCM. Na hataki wana-CCM kufukuzwa hata kama ni kiongozi kwa kutoa maoni tofauti.

Na kwa maana hiyo, kwa kumsikiliza mantiki ya Amani Karume anawatetea pia wanaUAMSHO ambao nao wanataka muungano wa Mkataba, serikali tatu – nao wasikilizwe.

Ifahamike, Uamsho ni Wazanzibar i wasiotaka M u u n g a n o w a m f u m o uliopo. Rais Mstaafu Karume kaongea vizuri kabisa kwa niaba yao- kawatetea.

Kwa lugha nyingine, ni kana kwamba Uamsho nao walitoa hotuba yao ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM wakiwakiliwalishwa n a M w a n a c h a m a w a o – kimtazamo, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM– AMANI KARUME.

Nahitimisha kwa kusema, japokuwa Rais Mstaafu Karume alipinga vurugu na uvunjifu wa Amani Zanzibar na kusema kwamba wahalifu washitakiwe, ni wazi kwamba hakubaliani na Wazanzibar kulazimishiwa Muungano kwa staili ya sera ya CCM na kutaka Wazanzibar wapewe

uhuru wao wa kuchagua. Na wakichagua serikali tatu ambayo ni mhogo mchungu kwa CCM na iwe hivyo.

Na kwa mantiki hiyo, tusitarajie kwamba Uamsho

utaisha Zanzibar kirahisi na tusitarajie Muungano wa staili ya CCM utaendelea kulazimishwa Zanzibar – Hapana – nakataaa. Uamsho ni mtazamo kuhusu Mustakabali wa Zanzibar kwa macho ya baadhi ya Wazanzibar.

Kwa hiyo, hoja ya Uamsho ya kubadilisha muundo wa Muungano ingalipo na ndio kwanza inapata wanachama wenye hadhi kubwa.

Hapa tulipofika, njia ya CCM kukwepa Serikali tatu imefika mwisho.

Lipumba ahofia nchi ‘kutekwa’ na mafisadiInatoka Uk. 3lawama serikali ya CCM, kwamba imeshindwa kuwa na mipango ya kukuza uchumi na kuongeza ajira nchini.

Alisema Tanzania ina bahati ya kijiografia, inapakana na bahari, kuna ardhi inayokubali kila aina ya mazao, kila aina ya matunda, lakini leo Bagamoyo ambayo ni maarufu kwa zao la mananasi na maembe, miaka hamsini baada ya uhuru hakuna walau japo kiwanda cha kusindika matunda, zaidi ya kuozea mashambani.

“ B a g a m o y o m a t u n d a y a n a k u b a l i , m a n a n a s i yanakubali, maembe yanakubali, kwa nini miaka hamsini baada ya kujitawala bado juisi ya embe, nanasi, passion inatoka nje ya nchi. Tumeshindwa hata kuweka kiwanda cha kusindika matunda

kuinua wakulima, kuongeza ajira na pato la nchi, matunda yanaozeana mashambani”. Alihoji.

Alisema serikali imekuwa ikijisifu uchumi umekuwa. Alihoji uchumi gani unaokuwa ikiwa vijana hawapati ajira. Alisema uchumi unaokuwa unaongeza ajira kwa vijana.

Aidha aligusia rasilmali Bandari na bahari. Alisema nchi imezungukwa na nchi ambazo hazina bandari, lakini miaka hamsini baada ya uhuru serikali imeshindwa kutumia vizuri bandari zetu kuongeza pato na ajira kwa vijana.

Alisema nchi ni tajiri na ina ardhi inayokubali kila aina ya mazao, lakini bado kuna njaa, bei za vyakula zinazidi kupanda, bei ya mchele, sukari mafuta ya kupikia, zimekuwa bidhaa ambazo bei zake zinapaa kwasababu ya kukosekana sera bora, uongozi ulio makini na wenye dira.

A l i s e m a k u n a h i t a j i k a mabadiliko ya kisera ili kumudu kutumia vizuri rasilimali hizi za asili za nchi. Kwamba watanzania wana kila sababu ya kuwa katika neema iwapo kutakuwa na uongozi wenye dira na unaojali maslahi ya mtu wa kawaida.

Hata hivyo alidai uongozi huo hauwezi kupatikana ndani ya CCM kwani kimekuwa chama cha wala rushwa na mafisadi.

“Ushahidi upo na unatolewa na wana CCM wenyewe. Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu, aliwahi kusema kuwa kama mfanyabiashara anataka mambo yake yaende vizuri, basi apeperushe bendera ya CCM katika eneo lake la biashara. Ameenda kwanye uchaguzi kwenye wilaya yake kugombea ujumbe wa NEC, wamemshughulikia vilivyo. M p a k a y e y e m w e n y e w e anapiga kelele, anasema rushwa imekidhiri CCM. Wanatumia mamilioni ya fedha hata kwenye ujumbe wa NEC.” Alisema Prof. Lipumba.

Aliyekojolea Qur’an afikishwa mahakamaniInatoka Uk. 1

kutatanisha, kijana huyo alifikishwa mahakamani hapo pamoja na Haruna Ahadi, muuza duka ambaye ndiye Juzuu aliyokuwa akiisoma, aliporwa na kukojolea.

Habari zinaeleza kuwa kijana Ahadi, anashikiliwa kwa madai kuwa kwa kiasi fulani alichochea mwenzake kukojolewa Juzuu yake.

Kesi hiyo haikutajwa mahakamani hapo kwa kuwa hakimu aliyepangwa kuis iki l iza, Mh. Dudu, hakuwepo mahakamani akidaiwa kuwa amesafiri, hivyo mtuhumiwa kurudishwa rumande hadi Novemba 29 kesi yake itakapotajwa tena.

Siku ya Jumamosi mwezi uliopita, Daud Kapaya,

alikojolea kwa makusudi kitabu cha Qur’an (Juzuu Amma) huko Ukonga majira ya saa 4:38 usiku. Kesi yake ilifikishwa kituo cha Polisi Staki Shari Ukonga ambako yal ichukul iwa maelezo na kufungul iwa ja lada STKRB/19378/2012 la kosa la kukashfu dini dhidi ya mtuhumiwa.

Hii ni mara ya pili kijana huyo kufikishwa mahakamani hapo baada ya kudaiwa kuwa alikamatwa mkoani Tabora baada ya kutoweka jijini Dar mara baada ya kufanya tukio.

Katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda na wenzake, Wakili wa Sheikh Ponda na Mukadam Abdallah Saleh ,Juma Nassoro, al i taka kupewa maelezo ya awali ya mlalamikaji mahakamani

hapo, kutaka kujua mwenye kiwanja analalamikia nini.

Aidha wakili huyo aliiomba Mahakama kuzingatia haki za binadamu, akitaka mteja wake ambaye ni Sheikh Ponda, kuondolewa pingu awapo mahakamani hapo kwa kuwa yeye ni kiongozi wa kiroho na anafasi na heshima yake katika jamii.

Mahakama ilikubali madai ya wakili wa utetezi na kuamuru upande wa Jamhuri kumpatia wakili huyo maelezo ya mwenye kiwanja juu ya kile anachokilalamikia.

K a t i k a m a e l e z o y a m w e n d e s h a m a s h t a k a aliyetajwa kwa jina moja la Kweka, alisema washitakiwa walivamia hilo eneo la Markaz Chang’ombe kwa nia ya kujimilikisha kiwanja hicho. Pia alisema kuwa Bakwata ndio waliouza eneo hilo kwa

kampuni ya Agritanza Ltd, kupitia mkataba ulifanyika Juni 18, 2011.

Kufuatia maombi ya wakili wa watuhumiwa, Jamhuri kuahidi kuwa Sheikh Ponda hatokuwa na pingu pindi anapokuwa mahakamani hapo.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Bw. DPP Eliazer Feleshi, alileta pingamizi la dhamana kwa Mukadamu na Sheikh Ponda akidai kuwa usalama na maslahi ya Jamhuri yataadhiriwa ikiwa mtuhumiwa huyo atakuwa nje kwa dhamana.

Sheikh Ponda Issa Ponda na Bw. Mukadam Abdallah Saleh, walirejeshwa rumande baada ya dhamana zao kuendelea kufungwa hadi hapo kesi yao itakapotajwa Novemba 29 mwaka huu.

Page 5: Annuur Ijumaa

5 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Habari za Kimataifa

LOS ANGELESM A H A K A M A n c h i n i Marekani imemhukumu yule mtu aliyetengeneza filamu ya kuwatukana Wais lamu na Mtume Muhammad (saw) kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja amri ya mahakama ya kutofanya u h a l i f u k w a k i p i n d i cha miaka minne ikiwa ni sehemu ya hukumu kufuatia kutiwa hatiani kwa kufanya wizi katika benki siku za nyuma (breaching his probation’s terms).

Mark Basseley Youssef, mwenye umri wa miaka 55, ambaye alitengeneza na kuongoza filamu iliyozua vurugu kufuatia maudhui yake ambayo yanamtusi Mtume Muhammad (saw) na Waislamu kwa ujumla, atatumikia kifungo chake katika gerezani (US federal prison) baada ya kukiri makosa manne aliyotuhumiwa nayo ya kutumia vitambulisho feki.

Makosa hayo yanakiuka hukumu ya adhabu aliyopewa siku za nyuma ambapo alikutwa na hatia ya kuiba kitapeli katika benki mwaka 2010.

Youssef ni mhusika mkuu wa fi lamu inayokashfu U i s l a m u n a k u z u a maandamano makubwa sehemu mbalimbali duiniani, ambapo makumi ya watu walipoteza maisha katika wimbi hilo la maandamano. Filamu hiyo pia ilisababisha tuk io la shambul io la Sep temba 11 , ambapo

Aliyemtukana Muhammad (saw) aenda jela

Balozi mdogo wa Marekani nchini Libya Chris Stevens, aliuliwa Benghazi pamoja na wamarekani wengine watatu.

Mwezi Februari 2009, mahakama iliwatia hatiani Youssef na wenzake kwa kuiibia benki kwa njia za udanganyifu kwa kutumia utambulisho na namba za usalama za wateja katika matawi ya benki ya Wells Fargo California na kutoa kiasi cha dola 860 katika kaun t i za wa te j a hao . Alifungwa jela miezi 21 na kuamriwa kutotumia komputa au Internet kwa kipindi cha miaka mitano, vinginevyo ni mpaka apate kibali maalum. Pia alipigwa

PHINON PEINKamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay, ameitaka serikali ya Myanmar kuwapa haki za kiraia Waislamu nchini humo.

Bi. Navi Pillay, ambaye alikuwa akihutubia katika Mkutano wa Kimataifa wa Demokrasia huko Bali, Indonesia amesema serikali ya Myanmar inapaswa kuchukua hatua za kuwapa haki za kiraia Waislamu wa kabila la Rohingya na kuishi nao kwa uadilifu.

Aidha nchi hiyo kubadili sheria zake za sasa na kuwaruhusu Waislamu kuwa na haki ya uraia. Pillay amesema Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa kuhusu ukandamizaji na juhudi zinazofanywa nchini Myanmar kwa ajili ya kuangamiza jamii ya Waislamu wa Rohingya.

Shauri la Umoja wa Mataifa la kutaka kupewa uraia Waislamu wa Myanmar limetolewa siku moja tu baada ya wanaharakati wa haki za binadamu wa kimataifa kutoa wito wa kupelekwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar ili kukomesha ukandamizaji na mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu magharibi mwa nchi hiyo.

Katika hatua nyingine, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeituhumu serikali ya Ethiopia kuwa inafanya ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini humo.

Amnes ty In te rna t iona l imetoa tuhuma hizo kutokana na mwenendo wa serikali ya Addis Ababa wa kuwatia nguvuni Waislamu kwa kosa lililotajwa kuwa ni kushiriki kwenye maandamano ya amani ya kudai uhuru wa kidini.

marufuku kutumia majina ya kisanii wakati akitumikia adhabu yake ya kuwa chini ya uangalizi baada ya kumaliza kifungo cha jela.

Alikamatwa Septemba na kushtakiwa kwa kuvunja vipengele vinane ya adhabu ya uangalizi i l iyokuwa ikimkabili. Mwezi uliopita alikana tuhuma zote lakini wiki hii amekubali makosa manne huku mengine manne yakiondolewa.

Jaji wa Mahakama (District Judge), Christina A Snyder, a l isema kuwa Youssef , ambaye tayari ameshakaa rumande kwa wiki tano, atatumikia miezi 12 jela kufuatia kuvunja amri ya kuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka minne.

Misri yarejesha mabilioni ya dola ya mafisadi yaliyofichwa nje ya nchiCAIROWAKATI Ser ika l i ya Ta n z a n i a i k i e n d e l e a kupiga k imya kat ika kuwashughulikia mafisadi papa ambao wamebainika kuficha mabilioni ya dola za kimarekani katika m a b e n k i y a U s w i s i , Serikali ya Misri tayari imeshaanza kutaifisha na kurejesha mabilioni ya dola yaliyokuwa yamefichwa na viongozi wa enzi za utawala wa Hosni Mubarak.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali ya Misri amesema kuwa, nchi yake imefanikiwa kurejesha dola

bilioni moja na milioni mia nane za serikali ya nchi hiyo zilizokuwa zimeporwa na viongozi wa utawala uliong’olewa madarakani nchini humo.

Adel al Saeed, alibainisha kuwa vyombo vya sheria vya Misri bado vinaendelea na uchunguzi wake dhidi ya mafisadi na wale wote waliopora mali za Baitul Maal, wakati wa utawala wa Hosni Mubarak.

Aliongeza kuwa uchunguzi uliofanywa kuanza Februari 2011 hadi 31 Oktoba mwaka huu, umeweza kubaini na kukusanya dola bilioni moja na milioni mia nane zilizoporwa

na Hosni Mubarak, familia yake, na idadi kadhaa ya mawaziri na wafanyabiashara wakubwa nchini humo.

Amesema kuwa serikali ya Cairo inaendelea kuwasiliana na nchi nyingine kwa njia za kidiplomasia lengo likiwa ni kuzuia na hatimaye kurejeshwa mamilioni ya dola ambayo yalitoroshwa na viongozi wa zamani wa nchi hiyo. Utawala wa kiimla, ufisadi uliokithiri na ukandamizaji dhidi ya wananchi wa Misri ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha wananchi wa Misri kuanzisha harakati za kuiondoa mamlaka ya Hosni Mubarak. DOLA za Kimarekani

Mitambo ya nyuklia Iran kuanza kaziTEHRANMkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Fereydun Abbasi, amesema kuwa kat ika kipindi cha miezi michache ijayo, shughuli za awali za mitambo ya nyuklia iliyopo Bushehr, kusini mwa Iran zitafunguliwa rasmi.

Fereydun Abbas i , amesema mitambo hiyo ya nyuklia ya Bushehr itafunguliwa Januari au Februari mwakani na wataalamu wa Irani baada ya kufanyika majaribio kadhaa ya kitaalamu.

A m e o n g e z a k u w a kazi za wakandarasi wa Kirus i z inaf ik ia ukingoni na kilichobaki ni kukabidhiwa rasmi wa taa l amu wa I r an kuiendesha mitambo hiyo. Abbasi amesema hivi sasa mitambo ya Bushehr ina uwezo wa kuzalisha megawati 1000 za umeme, ambapo kiwango hicho kitaongezwa hadi kufikia megawati 4000 hadi 6000 na hatimaye kuingizwa kwenye gridi ya taifa.

UN yaitaka Myanmar kuwatambua Waislamu

Balozi mdogo wa Marekani nchini Libya Chris Stevens, aliuliwa Benghazi pamoja na wamarekani wengine watatu.

Page 6: Annuur Ijumaa

6 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Makala

“This is unfair. Very unfair. Kwa nini umfanyie mwanadamu mwenzako hivi? No. It is not fair. Why?”

Hivyo ndivyo alivyokuwa a k i s e m a n a k u k a r i r i mwenzetu mmoja mara kwa mara njia nzima toka tunatoka Ramallah mpaka tunaingia Nablus. Kwa nini? Ilikuwa ni baada ya kushuhudia moja ya vitendo vya kifashisti na kikaburu wanavyofanyiwa wananchi wa Palestina. Ilikuwa ni mwendo wa kiasi dakika mbili kutoka hotelini tulipokuwa tulikuta kizuizi cha askari. Hapo tukakuta askari wanne wa Israel wana silaha nzito nzito na vyombo vya mawasiliano. Barabara h i i n i miongoni mwa barabara nyingi ambazo Mpalestina haruhusiwi kupita na kama ni mgeni kama sisi tulivyokuwa, basi iwe ni kwa kibali maalum kutoka serikali ya Israil. Ni barabara kwa ‘Walowezi wa Israil tu.”

Tulikaa hapo dakika kadhaa wenye j i we tu wakiomba kwamba sisi ni ujumbe kutoka Tanzania na miongoni mwetu kuna watu wa kiserikali wenye hati za kusafiria za kidiplomasia. Baada ya majadi l iano marefu na askari hao kupiga simu kwa wakubwa zao ndio tukaruhusiwa kupita.

Baada ya kwenda kiasi mwendo wa dakika tatu hivi tunakukatana na barabara kuu ya kwenda Nablus. Kutoka hotelini tulipokuwa kufika barabara hiyo ni mwendo wa kiasi dakika tano, lakini kufika hapo Mpalestina itamchukua takribani dakika 20 au zaidi. Kwa nini hatakiwi apite njia hiyo ya mkato ambayo ni nzuri. Anatakiwa azunguke mbali ndio afike hapo.

Labda ni toe mfano. Jaaliya unatoka jijini Dar es Salaam kwenda Bagamoyo. Myahudi atapita Mwenge, Tegeta, Boko na kuingia Bagamoyo. Mpalestina atatakiwa kupita Kibaha, Mlandizi mpaka Chalinze, Msata ndio aingie Bagamoyo kupitia Msata. Safari ya nusu saa au saa moja wewe unatumia masaa manne.

Lakini hilo tuliache kwa siku nyingine. Muhimu kwa leo ni masikitiko yangu

Siku niliyokwama kuingia Masjid IbrahimNa Omar Msangi, Hebron

kushindwa kuingia Msikiti wa Kihistoria wa Nabii Ibrahim (a.s).

Ilikuwa kiasi saa kumi jioni Jumatatu, Novemba 12, 2012, tunaingia katika mji wa Hebron tukitokea Bethlehem. Tunapokewa

na wenyeji wetu ambao wanatupa maelezo mafupi juu ya mj i huo huku wakisisitiza kuwa tuna muda wa saa moja tu kwa hiyo hatutaweza kupita

maeneo yote muhimu ila watajitahidi kupita katika zile sehemu ambazo itakuwa rahisi kwa kila mmoja wetu kuona kiwango cha madhila, mateso, udhalilishaji na u v u n j a j i w a h a k i z a kibinadamu unaowasibu

wenyeji wa mji huo kutoka kwa Israil.

Mtaa wa kwanza tunaopita ni mwembamba kama ile mitaa ya Mji Mkongwe Unguja. Ni majumba ya

ghorofa kiasi tatu, nne na mengine ya kawaida. Pembeni mwa barabara kumetandazwa biashara za kila aina huku yaliyokuwa maduka yote yamefungwa. Juu baina ya majengo ya pande mbili za barabara/

njia, kumetandazwa waya ambazo zinaonekana kujaa takataka.

Sasa sikiliza maelezo: T u n a a m b i w a k u w a nyumba zote hizo pamoja

na fremu za maduka ni mali ya Wapalestina lakini wamepigwa marufuku na serikali ya Israil kufungua w a l a k u k a a . K i s a , baadhi ya majengo hayo yamechukuliwa na serikali na kupewa ‘walowezi’ wa Kiyahudi wanakaa juu ghorofani. Kwa hiyo Wapalestina wanaambiwa kwa sababu za kiusalama marufuku kufungua maduka hayo. Wanabaki wakipanga bidhaa zao chini.

Zi le waya baina ya nyumba na nyumba katika njia wanamopita watu, zinasaidia kuzuiya uchafu na mawe wanayorushiwa na Mayahudi wanaokaa juu ghorofani. Na kweli ukitizama unakuta taka na mawe yaliyojaa katika vizuizi hivyo. Tukitizama kwa juu tunaona ‘walowezi wa Kiyahudi’ wakitutizama kupitia madirishani.

“Nyie Waarabu sio watu, tokeni hapo”, tunasikia akisema kutokea juu ya ghorofa Muisrail mmoja huku akitupiga picha kwa kamera ya simu yake ya mkononi. (Alikuwa akisema Ki-Israel, tulipouliza nini anasema ndio tukapewa tafsiri hiyo na wenyeji wetu).

“Chukueni tahadhari wanaweza kuwarushia mawe”, anasema mwenyeji huyo.

Katika kona moja ya jengo kwa juu tunaona ‘kibanda’ cha askari amekaa askari na silaha nzito. Tunaambiwa hao ni wengi na wapo kwa ajili ya kiwalinda ‘walowezi hao wa Israil’.

“No photo”. Anasema askari yule baada ya kuona kamera z ik imuelekea . Lakini kama unavyojua waandishi wa habari. Picha kama hiyo kuikosa wanaona ni dhambi kubwa kwa hiyo kila mmoja anatafuta mahali pa kujificha na wengine kwa ukaidi ndio kwanza wanamsogelea askari yule ili wapate picha nzuri huku naye akiranda huku na huko kacharuka akitishia kwa mtutu wake.

“ Tw e n d e n i h a r a k a haraka kabla hali ya hewa haijachafuka”, anahimiza mwenyeji wetu. Tunapita mtaa wa kwanza wa pili tunakuta kizuizi cha polisi. Huo ni upenyo wa kuingia Masjid Ibrahim (Msikiti wa

Inaendelea Uk. 7

ASKARI wa Israeil wakiwazuia waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali kufika Masjid Ibrahim Hebron Jumatatu Novemba 12, 2012. Picha chini ni askari wa Israel.

Page 7: Annuur Ijumaa

7 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Makala

Inatoka Uk. 6

Siku niliyokwama kuingia Masjid IbrahimNabii Ibrahim) unaokisiwa kujengwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Tunaruhusiwa kupita ka t ika upenyo wenye m a s h i n e z a u s a l a m a (security) za ukaguzi na kutokezea kwenye uwazi ambapo kwa mbele kiasi meta 300 tunaona Msikiti wa Nabii Ibrahim. Lakini tunaposogea mbele tunakuta ukuta wa Polisi harakaharaka wanafunga njia ya kupita.

“ H u u n i M s i k i t i w a Wa i s l a m u , l a k i n i wanatuzuiya kuingia, unaona Waisrail wale wanaingia, wamegeuza Msikiti huu ni hekalu lao”, anaeleza mmoja katika wenyeji wetu. Kwa mbele tunaona Waisrail waliovaa vile vibandiko vya dini ya Kiyahudi wakipanda ngazi kuingia na kwa upande mwingine tunaona mabasi ya ‘Wayahudi’ yakirudi na watu ambao tayari washaingia msikitini humo sasa wanaondoka.

Tulisimama hapo kwa muda tukipewa maelezo juu ya Msikiti huo, lakini kubwa tukifahamishwa kuwa mpaka mwaka 1994 Msikiti huo ulikuwa chini ya mikono ya Waislamu. Wenyeji wakiswali hapo na watu kutoka nchi mbali mbali wakija kuutembelea. Lakini mwaka 1994 ilikuwa katika swala ya Subhi mwezi wa Ramadhani, Msikiti umefurika Waislamu wakifanya ibada, aliingia askari mmoja wa Kiyahudi na silaha akauwa Waislamu wengi na kujeruhi mamia. Kutoka siku hiyo, kwanza eneo lote linalozunguka msikiti likawekwa amri ya kutotembea na shule zikafungwa kwa miezi mitatu. Baadhi ya nyumba na shule jirani na hapo zikachukuliwa na kugeuzwa kuwa makazi na shule za Kiyahudi. Waislamu wakap igwa maru fuku kuingia katika Msikiti huo. Baadae serikali ya Israil ikadai kuwa Israil ndio yenye haki zaidi na Msikiti huo. Kwa hiyo wakatenga sehemu ambayo watakuwa wanaruhusiwa Waislamu kuingia na sehemu kubwa kuwa ni ya Waisrail. Lakini hata hiyo sehemu ambayo inaambiwa kuwa ni ya Waislamu nayo mtu hawezi

kuingia muda wowote atakao mpaka aruhusiwe. Vinginevyo marufuku kama sisi tulivyozuiwa.

B a a d a y a k u w a tumekwama kuingia Masjid Ibrahim, tukashika njia nyingine kuangalia nyumba za Wapalestina na shule zao ambazo zimetaifishwa na kupewa ‘Walowezi wa Kiyahudi’ na kwamba ni marufuku kwa Mpalestina kupita mtaa huo.

“ U n a o n a n y u m b a ile mimi nimezaliwa na kukulia pale, hivi sasa ni marufuku, siruhusiwi japo kukaribia nyumba yetu. Mimi nimesoma shule ile pale hivi sasa ni shule ya Kiyahudi tena inasomesha Wayahudi hawa wa siasa kali.”

Anasimulia mwenyeji w e t u m m o j a h u k u akituonyesha kwa kidole majengo hayo ambayo yapo kama mita 100 hivi kutoka pale tuliposimama.

“Msikimbie, msiogope, msiwaone wana bunduki nzito lakini wanatuogopa, sisi tunawaambia sisi sio magaidi, sisi hatuwachukii Wayahudi, hatuwachukii askari wa Israil, tunachotaka ni utu wetu, tuishi kama binadamu kama manavyoishi nyinyi askari, tunataka tubaki Wapalestina na ubinadamu wetu, sisi ni binadamu, oneni wenyewe i le ni nyumba yetu, ile ilikuwa ndio shule niliyosoma miaka ya 1980/90s, leo siruhusiwi kupita mtaa huu”, anasema kijana mmoja.

Anayasema hayo huku askari wa Israel , hata w a l i p o t o k e a h a t u j u i , wametuzingira mbele na nyuma, mbele hatuwezi kwenda maana wamesimama askari wasiopungua 20 na silaha nzito. Nyuma nako wapo wengi na silaha na magari mawili ya polisi. Barabara haipitiki tena.

Ilibidi turuke uzio wa barabara kuna kiuchochoro tukawa tunapita mpaka tukafika kwenye njia tuliyojia ya kupita Masjid Ibrahim kuelekea tulipotoka. Hata hivyo, katika wenyeji wetu wale, hakuna aliyekimbia. Ndio kwanza wakawa wanaimba kwa nguvu nyimbo za kuhamasishana kudai ardhi yao na haki zao. Ilikuwa ni kishindo cha sauti

ya hamasa na kuilani Israil hali iliyotufanya hata wale wageni ambao walikuwa washaingiwa na woga kupata mdadi.

Kwa wengi l i l ikuwa tukio la aina yake. Kwa hiyo waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali

kuwa kila aliyekuwepo wanamnasa na kumuingiaza katika kumbukumbu zao.

Walitusindikiza kwa nyuma na mitutu yao hadi tulipofika lango la kutokea huku wakituhimiza kufanya haraka. Wakati tunafika katika kituo cha ukaguzi

“ Wa m e n i k u m b u k a maana mimi muda mwingi nimekuwa katika jela za Israel na nadhani maisha yangu yote yatakuwa hivi, haya ndiyo majaaliwa yetu, lakini hatutakata tamaa muda wa kuwa tupo hai tutapigania

duniani ambao walikuwepo, ilikuwa hekaheka, sio ya kukimbia risasi, bali angalau kupata picha. Lakini wakati waandishi wanapigana vikumbo na kamera zao, askari wale nao baadhi yao walikuwa na kamera za video na wao wakihakikisha

kilichojaa polisi, mmoja akamwita mmoja wa wenyeji wetu ambaye nilikuwa nikiongea naye. Wakachukua muda kama dakika mbili tatu. Aliporudi namuuliza nini walikuitia akaniambia kuwa walimkumbuka ndio wakawa wanamhoji.

haki yetu ya kutambuliwa kama binadamu walio na haki ya kuishi kwa heshma na utu kama binadamu wengine.”

A l i e l e z a h u k u tukisukumwa kuharakisha kuondoka nje ya eneo la kuingilia Masjid Ibrahim.

WAANDISHI wa habari kutoka nchi mbalimbali wakiwa Palestina.

WAANDISHI wa habari kutoka nchi mbalimbali wakiwa Palestina.

Page 8: Annuur Ijumaa

8 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Makala

BINADAMU tunatakiwa kufahamu kusudi la Mwenyezi Mungu (Allah sw) kutuumba. Inatupasa kutambua lengo la maisha yetu hapa duniani na ahera tuendako.

M w e n y e z i M u n g u muumbaji kutulipa kile alichokusudia, inategemea zaidi tumefanya nini hapa ardhini (duniani).

Kama tumefanya uovu, tutalipwa kutokana na uovu. Malipo ya uovu bila

shaka ni adhabu kali. Kama tutafanya mema, basi mema hayo yatatusaidia kwenda peponi. INSHAALLAH.

Kutokana na picha hapo juu, naomba Waislamu tuandike Insha isiyozidi maneno (250) kwenda gazeti la Annuur, somo kuu likiwa linahusu ”Unaelewa nini kuhusu kaburi ukiwa kama Muislamu”.

NB:Uongozi wa Ann-uur

naomba mnisaidie kuitoa barua hii kama ombi la Insha kwa waumini kupitia gazeti letu.

Rashidi Idrisa Tindwa (BA Education first year 2012)

+ 2 5 5 7 5 3 0 7 1 1 8 5 , +255715416490

C H U O C H A W A I S L A M U MOROGORO.

UONGOZI WA SHULE UKISHIRIKIANA NA JUMUIYA YA WANATAALUMA WA KIISLAM TANZANIA (TAMPRO) WANAYOFURAHA KUWATANGAZIA WAZAZI NA WALEZI KUWAHI NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA.

AIDHA NAFASI ZIPO KWA WALE WOTE WANAOTAKA KUHAMIA KATIKA KIDATO CHA PILI, TATU, NNE, NA TANO.

TUNAO WALIMU WENYE SIFA NA MAKINI WATAKAOHAKIKISHA KUWA MWANAO ANAPATA ELIMU BORA NA MALEZI MEMA

USAILI WA KUJIUNGA NA SHULE UTAFANYIKA TAREHE 30/11/2012 KATIKA ENEO LA SHULE SAA TATU ASUBUHI.

DARASA LA QT NA PC LITAKUWEPO MASOMO YATAANZA MWEZI WA KUMI NA MBILI MWAKA 2012.

GHARAMA YA FOMU NI TSHS.10, 000KWA MAWASILIANO:

SIMU NO.0754 673327SIMU NO.0787 754244/0715 754244.WABILLAH TAWFIQ.

IMETOLEWA NA UONGOZI WA SHULE- TAMPRO.

SHULE YA SEKONDARI YA BONDENIS.L.P.2013, ARUSHA

NAFASI ZA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2013

Biamillaahi naanza, kwalo jinale JALILI, Kisha ninaandiliza, kwa swala yake RASULI, Ridhwani nafwatiza, kwa swahabaze RASULI, SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

MOJA NNE TATU TATU, hatunao ikhiwani, KUBWA sote sasa kwetu, ni kufanya TATHMINI, Tuchungue mambo yetu, pamwe na ya dini yetu,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

RISALA nawatumia, wa Bara na Visiwani, KAMBA tunoungania, ni MOJA ulimwenguni, Kamwe sitowabania, kwani nyote ikhiwani,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Iwafikie Unguja, kadhalika nako Pemba, Sisapoti Uunguja, bali hata na Upemba, DINI yetu ndio HOJA, sote inayotupamba,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Biamillaahi naanza, kwalo jinale JALILI,Kisha ninaandiliza, kwa swala yake RASULI,Ridhwani nafwatiza, kwa swahabaze RASULI,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

MOJA NNE TATU TATU, hatunao ikhiwani, KUBWA sote sasa kwetu, ni kufanya TATHMINI, Tuchungue mambo yetu, pamwe na ya dini yetu,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

RISALA nawatumia, wa Bara na Visiwani, KAMBA tunoungania, ni MOJA ulimwenguni, Kamwe sitowabania, kwani nyote ikhiwani,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Iwafikie Unguja, kadhalika nako Pemba, Sisapoti Uunguja, bali hata na Upemba, DINI yetu ndio HOJA, sote inayotupamba,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Sasa narejesha Bara, baada ya Visiwani, Nabtadi na Tabora, kisha Kigoma na Pwani, Kadhalika na Mtwara, Lindi na nyote kusini,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Kagera hadi Arusha, Dar na Kilimanjaro, Kote RISALA narusha, hadi kule Morogoro, Sitaki kuahirisha, au kuweka kiporo,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

RISALA kupeperusha, hino nayo ni IBADA, Dodoma napeperusha, Tanga, Manyara, Singida, Rukwa sitajiepusha, kutimiza hii ada,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Mara nakukumbukeni, kadhalika na Shinyanga, Nyote kwangu majirani, aula mkaniunga, Mwanza sikusahauni, na ndiko natia nanga,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Kadi tama nimefika, mwisho wa RISALA yangu, LENGONI sote kufika, ndo hasa shauku yangu, Na nilipoghafilika, nisamewe kosa langu,SOTE TUJITATHMINI, KWA YA MWAKA ULOPITA.

Abuu NyamkomogiMwanza

TATHMINI YA MWAKA (1433.H)

Page 9: Annuur Ijumaa

9 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Makala/Tangazo

Na Shekh Mustafa Rashad Rushdy

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu peke yake na rehema na amani zimfikie yule ambaye hakuna Mtume baada yake, na ninashuhudia k u w a h a k u n a M o l a apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika yetu tumekutuma uwe ni shahidi na mtoa biashara na muonyaji na ili mumuamini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni’ Surat Fath, aya ya 8 – 9. Heshima na utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, yeye ni mtukufu na yeye ndio mkubwa, yeye ndiye mwenye kibri na kuwaheshimu Mitume ni wajibu kwa sababu wao wamehifadhiwa na kufanya makosa, na kuwaheshimu wakubwa na kuwahurumia wadogo ni jambo la lazima na katika hadithi tukufu inaeleza kuwa (si mwenzetu kwa yule asiyewaheshimu wakubwa na asiyewahurumia wadogo na asiyehifadhi heshima ya wanachuoni wetu.

Bali Mtume (S.A.W) amembashir ia mwenye kumkirimu mkubwa kwa ukubwa wa umri pa le aliposema, (hamkirimu kijana, mtu mzima isipokuwa naye atampatia heshima na kuheshimu ni alama za wenye akili, na yule aliyepewa akili utamuona ni mwenye heshima katika maneno yake na mwendo wake na kukaa kwake na kazi zake.

Mtume (S.A.W) ana mifano bora ya heshima pale aliponyenyekea na pale alipokuwa mbora wa watu kwa unyenyekevu, yakawa maisha yake ni ya wastani na vyakula vyake vyepesi na godoro lake ni vitambaa, pamoja na hayo yo te alikuwa na utisho wake kwa watu. Hebu kumbuka pale alipoingia mwarabu mmoja kwa Mtume (S.A.W) ikaanza kutetemeka miguu yake na mwili wote kwa ujumla,

Heshima ni muongozo wa Kiislamu wenye nguvu na ulionyookandipo Mtume (S .A.W) akamwambia mwarabu yule kuwa, “Itulize nafsi yako kwa hakika mimi ni mtoto wa mwanamke ambaye alikuwa akila vyakula hata vile vya kawaida tu katika mji wa Makka tukufu”.

Alikuwa Mtume (S.A.W) katika vita vya badri pamoja na Abi Lubaba na Sayed na Ally Bin Twalib, wanapokezana ngamia mmoja.

Akasema Ally na Abi Lubaba hebu tushindane mwendo na mimi nitajiri sana wa kulipa wengi. Tujue kuwa heshima sio kiburi na kudharau watu na kujikweza na kuwabagua wengine. Bali heshima ni kumuheshimu wa mbali na wa karibu na unayemjua na usiyemjua, na kumpa kila mwenye haki haki yake na muongozo wa Uislamu ni kutokumdharau mwingine. Na Mitume yote ilikuwa midahalo yao ni kwa kutumia hoja na heshima na upendo na alikuwa kila Mtume akihojiana na watu wake kwa kusema, “Enyi watu wangu”, hii ni kwa utukufu na heshima.

N a m t u m w e n y e heshima ni yule mwenye kuheshimu wengine na kuwaweka watu sehemu zao, na inapopotea heshima na upendo pia hupotea. Na hapo ndipo mwenye nguvu humla mnyonge na tajiri humla masikini na (Rais) humla raia (kiongozi humla anayemuongoza.

Heshima haishii kwa kiongozi na anayeongozwa, huu ni uelewa finyu. Heshima ni muhimu hadi kat ika familia kama vile mume na mke pamoja na watoto wake. Hili ni daraja la wote kati ya viumbe wote. Na katika hadithi (yule ambaye asiyemshukuru Mwenyezi Mungu hawezi kuwashukuru watu, na kuvitukuza viumbe vya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa kutekeleza amri zake.

Amesema Mwenyez i M u n g u m t u k u f u , “Mmekuwaje hamuweki heshima ya Mwenyezi Mungu, na hali yeye amekuumbeni namna baada ya namna” Surat Nuuh aya ya 13 na 14.

Tunachukua fursa hii kuwatangazia Waislamu wanaume na wanawake nafasi za mafunzo ya Ualimu wa Maarifa ya Uislamu kwa shule za Msingi na Sekondari yatakayoanza Februari 2013.

SIFA NA MASHARTI YA KUJIUNGAMuombaji atimize sifa na masharti yafuatazo:-(i) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu Darasa la Watu wazima

kabla ya kujiunga.

(ii) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha Madrasa au Maarifa ya Uislamu katika kipindi cha dini shule za Msingi au Sekondari kwa muda usiopungua mwaka mmoja.

(iii) Awe anajua kusoma Qur’an kwa ufasaha.

FOMU ZINAPATIKANA CHUONI UBUNGO KWA GHARAMA YA SHILINGI ELFU TANO TU.

MUHIMU• Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11/2012.• Usaili utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 01/12/2012 saa 2 asubuhi.Wabillah Tawfiiq

MKUU WA CHUO

UBUNGO ISLAMIC TEACHERS’ COLLEGEP.O. Box 55105, Dar Es Salaam Tel: 2450069 Fax: 2450822, Mob:

0712557099, TANZANIA

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO UALIMU WA MAARIFA YA UISLAMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI - 2013

Page 10: Annuur Ijumaa

10 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Habari

Msikiti wa KIBUTA- Kitondwe “ B” Munga- Kisarawe Wanaomba Msaada wa Kuchimbwa KISIMA cha Maji.

Kwa Mawasiliano Piga No. 0656 092 436 au 0685 171 221

Msaada wa Kuchimbwa KISIMA

SERIKALI imetakiwa kuyapa uzito malalamiko ya Waislamu kuhusu mali za Waislamu zinazouzwa na Taasisi ya BAKWATA, kwa kuwa mali hizo ni Waqfu na hazipaswi kuuzwa.

Hayo yamesemwa na Maalim Ally Bassaleh, akiongea na Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa wiki iliyopita, katika Msikiti wa Idrisa, Kariakoo, Jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya Maalim Bassaleh imekuja baada ya kujiri matukio ya hivi karibuni yaliyosababisha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka baadhi ya Waislamu.

Alisema mali yoyote ya Waqfu iliyo chini ya Bakwata katika nchi hii, ni mali ya Waislamu na kwamba Bakwata au taasisi nyingine yoyote au kiongozi wa Kiislamu hana haki wala sheria ya kuuza mali za Waqfu kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

“Serikali inapaswa kuangalia kwa k ina mala lamiko ya Waislamu dhidi ya Bakwata, sio kuwasulubu wanaolalamika kwa nguvu za dola na kuwavumishia sifa mbaya. Inapaswa kuangalia chanzo cha malalamiko ya Waislamu na kutafuta ufumbuzi Ili kuepusha migongano na kuuzwa holela mali za Waislamu ambazo nyingi ni waqfu.” Alisema Maalim Bassaleh.

Alisema kuwa hata kama zitakuwepo sababu za kujaribu kuhalalisha uuzwaji wa mali hizo, bado zitakuwa hazina msingi wowote kwa kuwa mali hizo ambazo nyingi ni nyumba na viwanja, ni rasilmali ambazo Waislam na kila taasisi ya Kiislamu inahitaji kumiliki kwa maelendeleo ya jamii husika na si kuuza.

Alisema Bakwata ilimilikishwa mal i nyingi za Wais lamu zilizokuwa chini ya iliyokuwa Jumuiya ya Waislamu ya Eat Africa Muslim Welfare Society (EAMWS) il iyovunjwa na Mwalimu Julius Nyerere, hivyo Bakwata ilipaswa kuzisimamia kwa uadi l i fu na kusaid ia Waislamu na Uislamu kupiga hatua kimaendeleo, kuliko ilivyo sasa ambapo sehemu kubwa ya mali hizo zimeuzwa na nyingine kukodishwa kwa hasara.

Alisema licha ya kuuza mali za Waislamu, Bakwata badala ya kuwaunganisha Waislamu, limekuwa baraza linalotumika kinamna kuwagombanisha Waislamu wenyewe kwa wenyewe na kuwafanya Waislamu wasiwe na maelewano.

Akitoa mfano wa sakata l a k i w a n j a c h a M a r k a z i Chango’mbe, alisema waliouza ni taasisi ya Kiislamu (Bakwata) walionunua ni Waislamu, na wanaojaribu kukinusuru kuuzwa ni Waislamu.

Aliongeza kuwa kwa sababu ya kugonganishwa huko, hata walioshitakiwa hawakushtakiwa na Bakwata wala na anayedawa kununua kiwanja hicho, bali

Maalim Bassaleh ahoji uadilifu wa serikaliNa Bakari Mwakangwale aliyewashtaki anadai wameingia

katika eneo lisilo lao, wamepora ardhi isiyo yao, kuharibu mali na kufanya wizi wa mali zilizokuwa eneo hilo kwa ajili ya ujenzi.

Maalim Bassaleh, ambaye wakati Waislamu wanapata misukosuko hiyo aliyekuwa Makkah na kurejea mapema wiki iliyopita, aliwataka Waislamu kuwa makini kutokana na mwenendo ulivyo sasa dhidi ya Waislamu kutokana na Serikali na Maskofu.

Aliwataka wale ambao wamekumbwa na misukosuko hiyo, wamshukuru Mungu kwani alidai Muislamu wa kweli pamoja na kusema ameamini, ni lazima pia afikwe na misukosuko kama ilivyo wafika wale waliokuwa kabla yao.

“Na wale ambao wamepata machafuko kutokana na matatizo hayo wamshukuru Mwenyezi Mungu kama anavyosema katika Qur’an Tukufu, ‘hivyo watu wanahesabu kwamba wataachwa tu waseme kwamba sisi tumeamini bila ya kuletewa mitihani!’.

Pamoja na hayo, alisema Waislamu hususani wa Msikiti wa Idrisa wanapaswa kujiuluza kwa nini walitupiwa mabomu pamoja na kwamba walikuwa wametulia ndani ya msikiti wao.

Alisema taarifa alizozipata ni kuwa, waumini wa Msikiti huo hawakushiriki katika ghasia hizo kwa namna yeyote, na hata baada ya kuswali waliambiwa na viongozi wao warejee majumbani mwao. Lakini pamoja na hayo bado walijikuta wanapigwa mabomu na wengine kukamatwa.

Alisema hata baadhi ya vyombo vya habari viliripoti katika mtindo wa kulaumu kwamba, kwa kushuhudia waliona baadhi ya waandamanaji pale Kariakoo, wakitii amri ya kuacha maandamano na kukimbilia Msikitini, lakini askari wakawafuata humo humo na kuwakamata.

Aliongeza kuwa si hivyo tu, hata wale waliokamatwa huko nje ya Msikiti wengi wao walikuwa si Waislamu. Alinukuu gazeti moja lilivyoripoti kwa kuwataja kwa majina baadhi ya washtakiwa kuwa ni Ernest Silvesta, Josephat Aloyce, Edwin Sadoki, Stainl Mboja, na Ndiha Ndiganga.

A l i h o j i i w a p o w e n y e majina hayo waliokamatwa ni waumini wa msikiti wa Idirisa au ni waumini wa Msikiti upi hapo Kariakoo. Kwa ushahidi huo inadhihirisha kwamba waliofanya fujo walikuwa wengine kisha waliofuatwa na kupigwa mabomu ni waumini wa Msikiti wa Idrisa. Alihoji zaidi vijana hao waliokamatwa Msikiti wa Idrisa walifuata nini.

Hata hivyo Bassaleh alisema, si mara ya kwanza misikiti kupigwa mabomu. Kwamba limekuwa ni jambo la kawaida na hata askari kuingia na viatu na pengine na mbwa ndani ya

Misikiti na kunajisi. Hata hivyo alihoji, mbona hayasikiki hayo yakifanyika katika Makanisa yaliyowahi kuwa na vurugu?

Alisema kwa Waislamu msikiti ni pahali patakatifu, ni nyumba ya Mwenyezi Mungu, kitendo cha kupiga mabomu miskitini ni kuwatisha waumini wasi tamani kufika kat ika nyumba zao za Ibada kwa lengo la kuabudu.

Hivyo alivitaka vyombo vya dola kuchukua tahadhari kubwa kwani Waislamu wanaamini kwamba, hapana nyumba ya ibada iliyo takatifu kama msikiti, ndio sababu kwa mfano, hata viatu si ruhusa kuingia navyo ndani.

Akizungumzia kauli za viongozi wa makanisa juu ya kadhia hizo alisema, hali kwa jinsi ilivyo sasa ni tete. Aliitaka Serikali kukutana na viongozi wa dini kuangalia kilichowasibu. Pia alisema itakuwa nafasi nzuri ya kujua ni kwanini viongozi wa dini hii wakisema wanakamwatwa na wengine wakisema hawaguswi.

Alisema mambo mengi ambayo wanadaiwa kufanywa n a Wa i s l a m u y a m e k u w a yakizushwa na si ya kweli. Lakini serikali kila inapopata taarifa hizo za kizushi hukurupuka bila kufanya uchunguzi na kuanza kuwabughudhi Waislamu na Mashekh wao.

Kwamba ikichunguzwa kwa makini, ni dhahiri kwamba matukio yanayoendelea hivi sasa n i matukio ambayo yanatengenezwa ili kuwapaka matope Waislamu. Alitoa mfano wa mahakama ilivyotaja majina ya akina Josephat, Ernest, kukamatwa katika Msikiti wa Idrisa kuwa ni miongoni mwa walio kaidi amri ya Polisi.

Aidha alisikitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wa makanisa kupitia vyombo vya habari kuwa Waislamu wanachoma Makanisa. Alisema lengo la kauli hizo ni kuwachonganisha Waislamu na Serikali ili waonekane kwamba ni wabaya na kuanza kusakamwa na kuwazulia mambo.

Alitoa mfano kuwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na tabia ya kung’oa misalaba katika makaburi ya Wakristo ambapo walionyooshewa vidole ni Waislamu. Hata hivyo uchunguzi ulivyofanyika imebaini kuwa wanaofanya vitendo hivyo ni mateja (wavuta unga).

“Ile misalaba ni chuma, teja akiona kwake ni chanzo cha pesa, hung’oa na kwenda kuuza kama chuma chakavu, na si misalaba tu, wao (mateja) kila chuma huchukua kwani hata mifuniko ya makaro na mitaro barabarani huing’ao”. Alibainisha Bassaleh.

Akinukuu gazeti la Kikristo la Kiongozi, (la Ijumaa iliyopita), alisema Paroko mmoja wa Kanisa amenukuliwa na gazeti hilo akitoa tahadhari kwa wafuasi wake, akiwataka kujihadhari na wale wanaopitapita mahospitalini wakiwapa vyakula wagonjwa.

Alisema kauli ya Paroko huyo

imekuja baada ya kuwepo zoezi kwa vijana wa Kiislamu kila siku asubuhi hupita mahospitalini, hususani katika hospitali za Temeke, Kinondoni na Ilala, wakitoa misaada ya hali na chakula kwa wagonjwa bila kubagua dini zao.

Alisema hata yeye (Bassaleh) amekuwa akishiriki katika kutoa huduma hizo katika hospitali ya Ocean road, Jijini Dar es salaam. Mbali na huduma nyingine, lakini pia hufanywa usafi katika hospitali hizo kama sehemu ya huduma wanazozifanya Waislamu hao wafikapo katika hospitali hizo.

“Baadhi ya wagonjwa huamua kusilimu wenyewe kwa hiyari yao baada ya kufanyiwa wema na makundi hayo ya Kiislamu. Sasa hilo la kusilimu ndio limekuwa karaha kwa Maaskofu na sasa wanakuja na kauli za fitna. Taarifa zilizopo hivi sasa, wanakaria wagonjwa mia moja

walioamua kusilimu” Alisema Maalim Bassaleh.

Alisema hata katika kadhia ya hivi karibuni, Maaskofu walikwenda mbali zaidi kwa kuwataka Wakristo kuyalinda makanisa yao kwa mishale, mikuki, visu, mapanga na fimbo ili kupambane na Waislamu. Alisema kama kweli kauli hiyo imetoka kwa viongozi hao, huo ni uchochezi na ni kauli ya kuhatarisha amani miongoni mwa wananchi lakini hakuna aliyekamatwa.

Alihoji kama mameno hayo yangesemwa na Sheikh wa Kiislamu, akanadi Msikitini kwamba Waislamu wajiandae kwa visu, mapanga, mishale kulinda Miskiti yao… na wala asiwataje anaokusudia kupamba nao, sheikh asingefika siku ya pili bila kukamatwa.

lakini huyu anayesema wazi tujiandae kupambana na Waislamu, hashughulikiwi.

Maalim Ally Bassaleh.

Page 11: Annuur Ijumaa

11 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012Habari

Polisi wasababisha hasara ya milioni 30 Markaz Chang’ombe

Inatoka Uk. 12

Oktoba 20, 2012, kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi, wakiomba ripoti ya tukio la Markaz Chang’ombe.

“… kutokana na uharibifu ul iotokea chuoni hapo, likiwemo la uvunjwaji wa milango, madirisha, kuibiwa kwa Kompyuta tano, mashine za hospitali, amplifire ya Msikiti uliopo ndani ya Msikiti.

Kwa hiyo ni matarajio yetu kupatiwa ripoti hiyo.” ilisema sehemu ya barua hiyo na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Markaz.

Kuhusu Zahati iliyokuwa k a t i k a m c h a k a t o w a kuanzishwa chuoni hapo, alisema kufuatia uharibifu huo, Ubalozi wa Misri upo katika mchakato wa kutafuta vifaa vingine vipya ambavyo vingi vilitoweka baada ya Polisi kuvamia chuo hicho vingine kuharibiwa kwa mabomu.

Alisema pamoja na hasara waliyoipata, bado kuna juhudi zinafanyika kuhakikisha kituo hicho cha afya kinaanza kufuatia juhudi zilizofanywa na Balozi aliyemaliza muda wake na kwamba, balozi wa sasa pia anaendeleza juhudi hizo.

“Balozi wa sasa anafanya b i d i i z a i d i , a m e k u w a akikutana na Wizara ya Afya na maafisa mbalimbali wa afya ili kuhakikisha kituo hicho kinaanza kazi katika misingi ya sheria na taratibu za afya.” Alisema.

WAKATI BAKWATA, ikijihalalishia kuuza eneo la Waislamu la Markaz Chang’ombe, uongozi wa Chuo h icho umesema , u t a l a z i m i k a k u i o m b a Serikali ya Tanzania ardhi, ili kujenga Chuo Kikuu Cha Kiislamu endapo eneo lililobaki halitokidhi haja kama lilivyokusudiwa awali na serikali ya Misri.

Mkuu (Mudir) wa Chuo hicho, Dkt. Osama Mahmoud Ismail, akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Chuoni hapo, katikati ya wiki, alitoa ufafanuzi juu ya ndoto ya kujengwa Chuo Kikuu Cha Kiislamu nchini katika ardhi hiyo.

Dkt. Osama, aliyekuwa akiongea kwa niaba ya Balozi wa Misri nchi Tanzania, Bw.Hossam Moharam, alisema serikali ya Misri chini ya Rais wa zamani

wa Misri, Gamal Abdel Nasser, iliahidi kujenga Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini na kubainisha kuwa ahadi hiyo bado ipo kwa kuwa yalikuwa ni makubaliano ya kimaandishi kati ya serikali ya Tanzania na Misri.

Dkt Osama alisema, pamoja na kwamba ni miaka mingi imepita sasa, lakini kila kitu kinakwenda kwa mipango. Alisema mipango hiyo kwa sasa ipo katika mchakato kwa kuwa serikali ya Misri inakusudia kutekeleza ahadi ya kuleta Chuo Kikuu cha Kiislamu Afrika Mashariki.

“Kila kitu kina mipango yake, hivi sasa kuna mipango ya kuleta Chuo Kikuu cha Kiislamu watakachosoma Watanzania na watu wa Afrika Mashariki. Chuo kitafuata muongozo wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar Sharif cha Cairo, Misri.” Alisema Mkuu huyo wa Chuo.

Akifafanua kuhusu ufinyu wa ardhi kufuatia kumegwa na kuuzwa sehemu kubwa ya eneo lililotengwa hapo Chang’ombe, huku kukiwa na mchakato wa kuamsha fikra za kujenga Chuo Kikuu katika ardhi hiyo kama ilivyokusudiwa miaka 44 iliyopita, alisema ikiwa haitatosha watalazimika kuiomba Serikali ya Tanzania iwapa t i e eneo j i ng ine litakalokidhi haja.

Al isema Chuo hicho ki tagharamikiwa na na Serikali ya Misri kuanzia ujenzi na uendeshaji wake.

“Kama ardhi haitatosha basi tutakuwa tayari kuiomba Serikali ya Tanzania itupatie ardhi ili tuweze kujenga hicho Chuo Kikuu kama i l ivyokusudiwa awali .” A l i s e m a D k t . I s m a i l , akionyesha kusikitishwa na suala hilo.

Alisema lengo lao la kujenga uzio katika eneo hilo la Markaz, lilikuwa ni kuhifadhi ardhi hiyo ili kuweza kutekeleza lengo lililokusudiwa kama jiwe la msingi linavyoonyesha kuwa hicho ni Chuo Kikuu Cha Kiislamu.

Alisema kwa kuwa katika chuo hicho kwa sasa wanatoa elimu ya dini katika ngazi ya awali, Msingi na Sekondari, sasa walipenda Chuo Kikuu kianze au kiwe hapo hapo.

Kuhusu nani mwenye mamlaka ya eneo la Markaz, alisema hapo kuna maswala mawili, kwanza ni kuhusu jengo la chuo lililopo kwa

sasa, ambalo limejengwa na Misri na wao ndio wasimamizi na waendeshaji wa chuo hicho. Ama upande wa ardhi, alisema kuna wasimamizi wake na jukumu lao ni kutoa taarifa Polisi, na Ubalozi wa Misri kama kunatukio lolote.

Mwaka 1964, ujumbe wa iliyokuwa Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki (EAMWS), chini ya Sheikh Hassan bin Amir, pamoja na wazee wa TANU, ulifanya ziara katika nchi za Kiislamu

kutafuta msaada wa kujenga chuo Kikuu Cha Kiislamu na kuanzisha uhusiano na nchi za Kiislamu.

Gamal Abdel Nasser, akiwa Rais wa Misri wakati huo, alimuagiza Makamu wake Sharbasy, afanye makubaliano na mikataba na EAMWS kwa niaba yake.

Serikali ya Misri ilikubali kugharamia ujenzi wa chuo hicho. Hatimaye Mkataba wa makubaliano ukatiwa sahihi Mjini Cairo kati ya Tewa Said Tewa, kwa niaba ya EAMWS

na Makamu wa Rais wa Rai wa Misri (Sharbasy) kwa niaba ya Serikali yake.

Baada ya makubaliano hayo (1964), Serikali ya Misri iliahidi kujenga Chuo Kikuu cha Kiislamu ambacho ilikuwa kimilikiwe na kuendeshwa na EAMWS. Hata hivyo Jumuiya hiyo ilivunjwa na Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania (Julius Nyerere) baada ya ujumbe huo kurejea kutoka katika ziara za nchi za Kiislamu na badala yake Waislamu waliwaundiwa BAKWATA.

Mahafali Luqman Sekondari-SinzaInatoka Uk. 12

athari kubwa kuliko wengine.” Alisema Sheikh Yusuph.

Kwa upande wa walimu, Sheikh Yusuph alisema kuwa wao ndio warithi wa Mtume (saw) katika kazi hiyo. Mwalimu kwa mwanafunzi anatakiwa kuzungumza lugha inayofaa,

ikiwa atatumia lugha isiyo kubalika atakuwa ni mfano mbovu katika malezi na chanzo cha kumomonyoa maadili ya vijana.

A l i w a a s a w a h i t i m u kuhakikisha kuwa wanaporejea mitaani wasiwe chanzo cha matatizo, bali muda huo uwe ni wa kujipanga kwa ajili ya

kujiendeleza zaidi kwani ndio kwanza safari ndefu ya kusoma inaanza.

Jumla ya wahitimu 38 wa kidato cha nne wamehitimu mwaka huu na wale wa darasa la saba wakiwa ni watano. Kwa upande wa shule ya awali ni 23 na ambao wanatarajiwa kuanza darasa la mwakani kwanza (Grade I).

BAADHI ya viongozi wa Markaz Chang'ombe wakionesha sehemu zilizoharibiwa kufuatia uvamizi uliofanywa na jeshi la polisi Chuoni hapo hivi karibuni.

Ommary Abdallah Mketto, ambaye ni mlemavu wa ngozi (Albino) mkazi wa Mtoni Kijichi Dar es Salaam anaomba msaada kumwezesha kufungua biashara ya Stationary.

Licha ya kuwa na uwezo wa kufanya kazi, lakini kutokana na ulemavu wake wa ngozi na kutoona vizuri, Mketto amekuwa akikosa ajira kwasababu ya hali yake ya ulemavu.

Hivyo ameamua kujiajiri mwenye ili uepukana na maisha ya kuomba na tayari amefanikiwa kusajili biashara yake hiyo No 239430, Ragistration 12 Mach 2010- Kijichi Albinism Internet Café Agriculture katika Manispaa ya Temeke.

Msaada anaohitaji kijana huyu ni Mashine ya Photocopy, Printer, komputa na mtaji wa kufungua stationary.

Anapatikana Masjid Al Ihyau-Mtoni Kijichi na Masjid Mikocheni Islamic.Kwa mawasilianio zaidi: 0713-376426 au 0784-989860

Wabillah Tawfiq

Anahitaji msaada

Page 12: Annuur Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR12 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 16-22, 2012

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa na

Jumanne

JUMUIYA ya Waislamu Sinza, Jijini Dar es Salaam ipo katika mchakato wa kujenga kituo cha huduma za jamii zitakazozingatia maadili na misingi ya Uislamu.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Shule ya Sekondari ya Luqman, Ustadhi Amin Kinollo, katika mahafali ya tano ya kidato cha nne na darasa la saba katika shule ya Luqman Sekondari na Msingi, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ustadhi Amin Kinol lo alisema, Jumuiya hiyo kwa sasa inasimamia na kuendesha shule za Awali, Msingi na Sekondari zinazojulikana kwa jina la Luqman Islamic pamoja na Madrasatul- Ikhlas, zilizopo katika Msikiti wa Sinza Palestina, Jijini Dar es Salaam.

Alisema katika mipango ya baadaye ya Jumuiya hiyo, ni kujenga Hospitali ambayo

Mahafali Luqman Sekondari-SinzaNa Bakari Mwakangwale itazingatia maadili ya Kiislamu

katika kutoa huduma kwa jamii.

Ust. Kinollo aliongeza kuwa hivi sasa wapo katika mchakato wa kujenga jengo la ghorofa sita kwenye eneo lao (Plot) namba 936 Sinza Block ‘C’, ambalo litakuwa na ofisi za idara mbalimbali ikiwemo maktaba ya Kiislamu, ukumbi wa mikutano pamoja na kidato cha tano na sita.

“Kwa kutumia ipasavyo ardhi tulizozipata katika maeneo mbalimbali hapa nchini, Jumiya itajenga na kuanzisha Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya ujasiria mali kwa vijana na jamii kwa ujumla.” Alisema Ust. Kinollo.

Alisema pamoja na kuwepo mikakati hiyo, Waislamu na wadau mbalimbali kwa ujumla wanaombwa kutoa michango yao ya hali na mali ili kuweza kufikia malengo ya Jumuiya.

Aliongeza kuwamoja ya mafanikio yaliyopatikana tangu imeanzishwa Jumuiya hiyo, ni

CHUO Cha Kiislamu Cha Markazi Chang’ombe, Jij ini Dar es Salaam, kimepata hasara ya kiasi cha Shilingi 30,000,000, kufuatia uvamizi wa Polisi katika Chuo hicho hivi karibuni.

Kwa mijibu wa taarifa y a a w a l i y a J e s h i l a Polisi Wilaya ya Temeke, i l iyotumwa kwa Kituo cha Kiislamu cha Markaz Chang’ombe, imesema vitu vyote vilivyoharibiwa chuoni hapo thamani yake ni Tsh. 30,000,000.

Kwa mujibu wa barua h iyo ya Ja lada: CHA/IR/7902/2012, imesema liliripotiwa tukio la uharibifu

kuwaunganisha Waislamu kwa kutoa huduma za kiroho na elimu ya mazingira, kusaidia wajane na wazee wasiojiweza kiuchumi hususani katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Jumuiya imechukua jukumu la kusimamia na kutoa elimu ya Maarifa ya Uislamu katika shule zote za Msingi zilizopo katika Kata

ya Sinza.Akitoa mawaidha katika

mahafali hayo, Sheikh Yusuph Salum, alisema dhana ya elimu inakamilika kwa kukusanya sehemu tatu, yaani wazazi, walimu na wanafunzi.

Al isema wazazi wana as i l imia hamisn i ka t ika mafanikio ya mtoto kujifunza na asilimia thelathini inatoka

kwa mwalimu huku asilimia shirini ikitokana na juhudi za mwanafunzi mwenyewe.

“Wataalamu wanasema katika miaka mitano ya mwanzo ya mtoto anakuwa na uwezo wa kushika vitu kwa haraka. Hivyo mzazi akiwa na kauli zisizo na maadili, motto atshika hayo bila kujua athari zake. Ndio maana tunasema kuwa mzazi ana

Polisi wasababisha hasara ya milioni 30 Markaz Chang’ombe

Misri wasema ahadi ya kujengwa Chuo Kikuu ipo palepale

Na Azza Ally Ahmed uliotokea chuoni hapo kwa kuvunjwa milango, madirisha na kisha kuibiwa vitu mbalimabali.

Taarifa hiyo imeorodhesha vifaa vilivyoharibiwa kuwa ni mashine tatu za x-Ray, Kompyuta tano, Amplifire pamoja na Microphone moja. Taarifa hiyo imedai upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea na kwamba, hakuna mali iliyokamatwa wala watuhumiwa.

Maelezo hayo kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Chang’ombe k u p i t i a b a r u a y e n y e kumbukumbu namba CHA/CID/B.I/I /VOL.42/239, yamekuja kufuatia maombi yaliyotumwa kutoka katika kituo hicho kupitia barua ya

Inaendelea Uk. 11

Inaendelea Uk. 11

BAADHI ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Luqman, wakiwa katika mahafali ya tano ya kidato cha nne na darasa la saba katika shule ya Luqman Sekondari na Msingi, mwishoni mwa wiki iliyopita.