12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1020 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19-21, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= MOJA ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere, ni kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima. Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na Tanganyika, basi Tanganyika Fitna kuwagawa Zanzibar yakolea kutakuwa shuwari, lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya Wapemba na Waunguja. Waandishi kadhaa wa Bara wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu; na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa Wazanzibari. (Soma Uk. 10) Dkt. Shukuru Kawambwa. SERIKALI imetakiwa kutopuuza mapendekezo ya Waislamu ya kurejesha kipengele cha Dini katika zoezi la kuhesabu watu linalotarajiwa kuanza mwezi Agosti, ili kuweza kufikia malengo ya Sensa. Wito huo umetolewa na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Taifa, iliyohusu sensa ya watu na makazi 2012, iliyo fanyika Mjini Morogoro Crusade ya NECTA dhidi ya Waislamu: Waziri Kawamba kubeba Msalaba wa Ndalichako Matokeo mapya yazidi kufichua madudu Hayatokani na iliyodawa ‘factor’ ya 1. 5 Haijulikani Dr. Ndalichako ameyatoa wapi Profesa Mukandala naye awajibike Suala la Dini katika sensa bado laitesa serikali Na Bakari Mwakangwale, Morogoro Jumamosi ya wiki iliyopita. Wahariri hao walionyesha wasiwasi wao endapo suala hilo halitopatiwa ufumbuzi mapema na kusema huenda zoezi hilo linalohitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi wote na wadau mbalimbali likaingia dosari kubwa. Akichangia hoja hiyo iliyoteka semina kwa asilimia kubwa na kuwaweka wakufuzi kutoka Ofisi ya Takwimu katika wakati mgumu kwa kujibu hoja za wahariri hao, mmoja wa wahariri alisema, alitegemea Waziri Steven Wasira, kulipatia ufumbuzi katika semina yao iliyofanyika Inaendelea Uk. 12 MWENYEKITI wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Prof. Rwekaza Mukandala.

ANNUUR 120

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 120

ISSN 0856 - 3861 Na. 1020 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19-21, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

MOJA ya makosa makubwa al iyoyafanya Nyerere , ni kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima.

Miongoni mwa aliyowahi kuyasema Nyerere ni kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na Tanganyika, basi Tanganyika

Fitna kuwagawaZanzibar yakolea

kutakuwa shuwari, lakini Wa z a n z i b a r i w a t a a n z a kubaguana baina ya Wapemba na Waunguja.

Waandishi kadhaa wa Bara wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni maneno yenye ukweli usiopingika.

Hii ni fitna tu; na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa Wazanzibari. (Soma Uk. 10)

Dkt. Shukuru Kawambwa.

S E R I K A L I i m e t a k i w a kutopuuza mapendekezo ya Waislamu ya kurejesha kipengele cha Dini katika zoezi la kuhesabu watu linalotarajiwa kuanza mwezi Agosti, ili kuweza kufikia malengo ya Sensa.

Wito huo umetolewa na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kat ika semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Taifa, iliyohusu sensa ya watu na makazi 2012, iliyo fanyika Mjini Morogoro

Crusade ya NECTA dhidi ya Waislamu:

Waziri Kawamba kubeba Msalaba wa Ndalichako

Matokeo mapya yazidi kufichua maduduHayatokani na iliyodawa ‘factor’ ya 1. 5 Haijulikani Dr. Ndalichako ameyatoa wapiProfesa Mukandala naye awajibike

Suala la Dini katika sensabado laitesa serikaliNa Bakari Mwakangwale,

MorogoroJumamosi ya wiki iliyopita.

Wahariri hao walionyesha wasiwasi wao endapo suala hilo halitopatiwa ufumbuzi mapema na kusema huenda zoezi hilo linalohitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi wote na wadau mbalimbali likaingia dosari kubwa.

Akichangia hoja hiyo iliyoteka semina kwa asilimia kubwa na kuwaweka wakufuzi kutoka Ofisi ya Takwimu katika wakati mgumu kwa kujibu hoja za wahariri hao, mmoja wa wahariri alisema, alitegemea Waziri Steven Wasira, kulipatia ufumbuzi katika semina yao iliyofanyika

Inaendelea Uk. 12MWENYEKITI wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Prof. Rwekaza Mukandala.

Page 2: ANNUUR 120

2 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012 AN-NUUR TAHARIRI/HABARI

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro,

D'Salaam

Na Mwandishi WetuMAONI YETU

Waziri Kawamba kubeba Msalaba wa Ndalichako

KATIBU Mtendaji Dr. Joyce Ndalichako.

WAZIRI wa El imu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

M A T O K E O y a p i l i y a l i y o d a i w a kusahihishwa, sasa yamefumua madudu zaidi ndani ya NECTA.

I n a v y o o n e k a n a m a t o k e o h a y o yamebuniwa tu katika namna ya kuwadharau Wa i s l a m u k w a m b a hawatakuwa na akili ya kugundua uchakachuaji huo wa pili.

A k i t a n g a z a k w a kujiamini na kutamba, Katibu Mtendaji Dr. Joyce Ndalichako alisema kuwa, NECTA mwaka jana ilibadili utaratibu wa kufanya mitihani mitatu ya Maarifa ya Uislam na kuwa miwili, lakini mfumo wa kompyuta wa kujumlisha matokeo ukasahaulika.

Alisema, dosari katika matokeo ya somo hilo ilitokana na “kugawa X kwa 3” badala ya “kugawa X kwa 2”.

Akitumia maelezo hayo ya Dr. Ndalichako, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa aliwataka Waislamu kutofanya m a a n d a m a n o k w a sababu suala walilokuwa w a k i l a l a m i k i a limeshafanyiwa kazi na Wizara pamoja na Necta.

“Kwa kuwa sua la h i l i l i m e s h a p a t i w a ufumbuzi , nawasihi wananchi wajiepushe n a m a a n d a m a n o kwa sababu suala la msingi lililowafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo maandamano hayo hayatakuwa na t i j a , ” a l i s e m a D k . Kawambwa.

Dk. Kawambwa mbali na kumpongeza Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako kwa kushughulikia tatizo

hilo kwa wakati, alisema Wizara itaunda Tume ya kufuatilia suala hilo kwa undani ili lisijitokeze tena.

Hata hivyo, wakati Wa z i r i K a w a m b w a akitoa pongezi hizo, uchambuzi wa haraka haraka unaonyesha kuwa hakuna namna yoyote “factor” ya 1.5 inaweza kuzaa majibu ya pili kutokana na majibu ya kwanza.

H i i i n a o n y e s h a kuwa majibu ya awali yalichakachuliwa na haya ya pili yamechakachuliwa pia.

Yote hayatokani na alama halisi walizopata watahiniwa. Ni ya kubuni tu.

Baadhi ya walimu waliochambua matokeo hayo wanafahamisha kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA na Mweyekiti wa Baraza Profesa Rwekaza Mukandala wameonyesha dharau kubwa sana kwa Waislamu wa nchi hii.

W a k i f a f a n u a wamesema kuwa, kama Pro fesa Mukanda la

angekuwa japo na staha na kujali au kujuwa jukumu lake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani, hakuna namna ambayo wangepitisha matokeo ya awali.

“Kwa mtu anayejua kanuni za mit ihani , huwezi kupitisha matokeo ambayo wamefanya watu maelfu, halafu gredi ya mwanzo inaanzia D na hizo D zenyewe saba tu, lazima wangehoji kujua tatizo nini na katika kuhoji iliyodaiwa kuwa dosari na Ndalichako ingegundulika; lakini wao wamepitisha tu jambo linaloonyesha ama Baraza ni muhuri tu au hata huyo Profesa Mukandala mwenyewe naye n i sehemu ya mpango wa kuhujumu Waislamu.”

Amesema Mwalimu Idris Kassim akiongea na mwandishi.

“ H u y u P r o f e s a Mukanda la ambaye k w a h a k i k a m i m i namuhesh imu sana , inavyoonekana yeye ni

Inaendelea Uk. 3

WAKUU wa Shule za Kiislamu kupitia Baraza lao, wameandika tena barua Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupinga matokeo ya pili.

Matokeo hayo ni yale yaliyorekebishwa baada ya kupinga yale ya awali ambayo wanafunzi walifeli sana somo la Islamic Knowledge.

Awali taarifa ya Baraza la Mitihani ilieleza kuwa k i l i c h o t o k e a k a t i k a matokeo ya awali ni dosari na kosa la kibinadamu. Kwamba wakati awali kulikuwa na mitihani mitatu ya somo hilo, mwaka jana i l i fanya mabadiliko kukawa na mitihani miwili.

Hata hivyo, kat ika kutafuta wastani wa alama, likafanyika kosa badala ya kugawanya kwa mbili ikagawanywa kwa tatu. Kwa hiyo Baraza likasema kuwa limerekebisha dosari hiyo na kwamba limetoa matokeo sahihi.

Hata hivyo, Wakuu hao wa shule wanadai kuwa matokeo hayo ya pili ndio yamekuwa mabaya zaidi na kuonyesha kuwa kilichodaiwa kuwa ndio tatizo, siyo.

“Pamoja na kufanya marekebisho ya matokeo ya awali, bado matatizo m a k u b w a z a i d i yamej i tokeza ka t ika m a t o k e o h a y o . H i i inadhihirisha kuwa yapo matatizo makubwa zaidi na sababu nyingine zaidi ya kile kilichoelezwa na NECTA kwamba ndio kilisababisha makosa katika matokeo ya awali. Kilichowazi ni kuwa hakuna muunganiko wa kihesabu (mathematical combination) unaoweza kuzaa matokeo haya kwa kutumia ile “factor” ya 1.5 kama ilivyoelezwa na NECTA.”

Inasema sehemu ya

Waziri Kawamba aunde Tumebarua ya Wakuu wa Shule za Kiislamu kwa Wizara ambayo imenakiliwa kwa Mufti Sheikh Mkuu Issa Shaaban Simba, Islamic Educat ion Pannel na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu.

Katika maelezo yao wanasema kuwa kulingana na madaraja yaliyokuwa yametolewa awali, hakuna namna ambayo unaweza kufanya “mathematical combination” yoyote na ukatumia ile “factor” ya 1.5 ukapata matokeo ya pili.

Katika hali hiyo Wakuu hao wanasema kuwa kuna haja zile alama za awali za wanafunzi zilizokuwa zimetolewa na wasahihishaji ziwekwe hadharani, ndio ionekane hiyo gawanya kwa 3 ilivyotoa matokeo ya awali na namna gawanya kwa 2 ilivyotoa matokeo mapya.

U f u p i w a m a n e n o wanachosema Wakuu wa Shule za Kiislamu kama walivyosema Waislamu katika tamko lao kwa Waziri baada ya maandamano yao Ijumaa iliyopita, wanataka kuundwa Tume Huru ya uchunguzi.

K a t i k a d a i h i l o wanasisitiza kuwa tatizo halipo kwa somo moja tu, bali kwa masomo yote. Na zaidi wanasema kuwa bila ya Tume Huru, hakuna namna ambayo wananchi wanaweza kurejesha tena imani yao kwa Baraza la Mitihani.

Ni maoni yetu kuwa kama Wizara na Baraza la Mitihani hakuna kitu cha hujuma na kifisadi cha kuf icha , hakuna sababu yoyote inayoweza kumfanya Waziri asione mantiki ya kuunda Tume hiyo.

N i m a t a r a j i o y e t u basi kwamba Tume hiyo itaundwa na itakuwa na sifa stahiki ambazo zitafanya matokeo yake yakubalike.

Page 3: ANNUUR 120

3RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012AN-NUUR HABARI

Waziri Kawamba kubeba Msalaba wa NdalichakoInatoka Uk. 2muhuri tu wa kupitisha yale yanayopitishwa na kile kikundi cha Wakristo wakereketwa kinachojifungia miezi m i w i l i b a a d a y a mitihani kusahihishwa kikichakachua matokeo au naye pia ni katika kikundi hicho.” Amesema.

Akasisitiza akisema kuwa, inavyoonyesha Mwenyekiti wa Baraza l a Mi t i han i ana jua hujuma wanayofanyiwa Waislamu au amewapuuza sana na kuwaona hawana a k i l i , v i n g i n e v y o asingekubali matokeo ya mara ya pili yatoke bila kuyahakiki kwamba yapo sawa.

“Ilikuwa jambo jepesi kabisa, kuangalia tu iwapo ile “1.5 factor” iliyodaiwa kuwa ndiyo ilitoa matokeo yasiyo sawa, kama ikitumika inaweza kutoa matokeo ya pili, lakini hakujali kana kwamba walikubaliana na kuambiana kuwa hawa Waislamu hawana uwezo wala akili ya kugundua, buni tu majibu yoyote wape, hi i ni dharau kubwa kwa Waislamu na kujidhalilisha kwa Profesa na Baraza lake na kwa hakika na yeye i n a t a k i w a a j i u z u l u hatuwezi kuwa na imani naye tena”. Alisema Mwalimu huyo.

Wakati huo huo , taar i fa z i l izotuf ikia tukienda mitamboni zimefahamisha kuwa tayari Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu wameiandikia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuonyesha uchakachuaji kat ika matokeo ya mara ya pili.

“Pamoja na kufanya marekebisho ya matokeo ya awali, bado matatizo m a k u b w a z a i d i yameji tokeza katika ma tokeo hayo . H i i inadhihirisha kuwa yapo matatizo makubwa zaidi na sababu nyingine zaidi ya kile kilichoelezwa na

NECTA kwamba ndio kilisababisha makosa katika matokeo ya awali. Kilichowazi ni kuwa hakuna muunganiko wa kihesabu (mathematical combination) unaoweza kuzaa matokeo haya kwa kutumia ile “factor” ya 1.5 kama ilivyoelezwa na NECTA.”

Inasema sehemu ya barua ya Wakuu wa Shule za Kiislamu kwa Wizara ambayo imenakiliwa kwa Mufti Sheikh Mkuu Issa Shaaban Simba, Islamic Education Pannel na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu.

Mmoja wa Wakuu wa Shule hizo amesema kuwa matokeo ya mara ya pili ni mabaya zaidi kuliko ya kwanza na kwamba yamefichua ubovu mkubwa zaidi ndani ya NECTA jambo linalozidi kutilia nguvu ile kauli ya Waislamu kwamba hawana imani na Baraza hilo.

“ Ya l i y o j i t o k e z a katika matokeo ya pili, ni ushahidi tosha kuwa panahitaji uchunguzi huru na wa kina; matokeo ya kwanza na ya pili hayahusiani kabisa , inaonekana kuna mtu kakaa na kubuni tu.” Amesema Mkuu huyo.

“ Inavyoonesha n i kuwa baada ya mitihani kusahihishwa kuna watu wanaokaa wakajifungia mahali na kuamua shule gani na mwanafunzi gani wampe F au A bila kujali ana alama ngapi katika mtihani.” Amesema.

Akifafanua alihoji akisema kuwa katika ulimwengu huu wa IT, kuna haja gani mitihani baada ya kusahihishwa Baraza likae nayo kwa siri takriban miezi mwili mizima, inafanya nini?

“Ni katika kipindi hiki wale wanaodaiwa kuwa ni mawakala wa kanisa hukaa na kuchezea

matokeo watakavyo, mtu anapewa A huku ana alama 54 wakati mwenye alama 82 anapewa C au D au hata F.”

“Mi naamini kuwa wasahihishaji wanafanya kazi yao vizuri na kurekodi makisi sahihi, tatizo ni kile kikundi kinachokaa b a a d a e a m b a c h o hakijulikani kinaundwaje na kinatumia kanuni gani na ‘range gani’ katika kutoa gredi, hawa ndio wanaweza hata kumpa A mtu mwenye alama 40.”

Alisema akisisitiza kuwa katika barua yao kwa Wizara wamesema waz i kuwa b i l a ya kuundwa kwa Tume huru ya uchunguzi, tatizo katika NECTA haliwezi kupatiwa ufumbuzi.

A k a o n g e z a k u w a wanatoa muda maalum katika kuonyesha kuwa jambo hili ni nyeti na l inatakiwa kupatiwa

u f u m b u z i h a r a k a , vinginevyo watalazimika kuweka hadharani mambo mazito hadharani ambayo peng ine ya t a i f anya serikali kuona mantiki ya kuunda Tume.

Hata hivyo akasema kuwa kama itafikia hapo, itabidi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawamba awe wa mwanzo kuwajibika kwa kukingia k i fua NECTA.

Wa n a c h o s i s i t i z a Wakuu wa Shule hizo za Kiislamu ni kuwa tatizo halipo kwa somo moja tu bali kwa masomo yote na kwamba hata watoto wa Kikristo wapo wanaodhulumiwa makisi zao katika utaratibu ule wa watu wachache kukaa kutoa madaraja bila kuzingatia alama alizopata mwanafunzi katika usahihishaji.

WAISLAMU wakiwa katika maandamano ya kushinikiza Dkt. Ndalichako kujiuzulu.

Page 4: ANNUUR 120

4 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012 AN-NUUR HABARI

HAKUNA woga katika kulizungumzia suala la Muungano ikiwa katika kuuvunja au kuimarisha. Isiwe dhambi kwa wale wote wasiutaka Muungano huu.

Nimeshangazwa na kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) ambae pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega, alisema kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanz iba r. Askofu aliuliza wapi yalipotokea mawazo potofu ya baadhi ya Watanzania wanaotaka uvunjwe Muungano?

Anasema, “ tuwapige vita na wala tusiwaonee haya” “Muungano huu ni tunu tuliopewa na Mungu”. Ningalipenda Baba Askofu aelewe kwamba ni tatizo la Uongozi na Viongozi wa Tanzania Bara kutojiona kuwa ndio tatizo au wana tatizo katika suala zima la Muungano, watakapofikia na kujiona kuwa wao ndio tatizo basi, tatizo sugu baina ya Zanzibar na Tanganyika litaweza kuondoka mara moja. Wakikataa kujiona kama wao na vibaraka vyao walioko Zanzibar ndani ya Serikali na Chama ndio tatizo sugu, basi Muungano ambao Wazanzibari hawautaki utavunjika na utawaangukia w e n y e k u u l i n d a k w a mabavu.

Mhashamu Askofu Norbert Mtega, unakumbusha kwa kuidurusu sura ya (Rum 1:18-23) “ Ghadhabu ya Mungu imedhihir ishwa kutoka mbinguni dhidi ya waasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijuulikane”.

Uamsho wanataka ukweli w a m k a t a b a w a N c h i yao utolewe ili wahusika (wananchi) wapate kujua u k w e l i . S e r i k a l i y a Muungano inauficha. Ilikuwa ni wajibu wenu Maaskofu kusaidia jambo hili lisifichwe

Askofu Mtega hana heri kwa Zanzibar

Na Ibrahim Mohammed Hussein

ili ukweli upate kubainika. Ukiisoma Lawi 25:43 utaona wanakumbushwa Watawala wasitawale kwa nguvu ila wamche Mwenyezi Mungu. Natumai lengo la aya hiyo kwa Watawala ni kuwaonya watawala waepukane na matendo ya watawala wa Misri.

“ Wa k a w a t u m i k i s h a wana wa Israel wakaugua kwa sababu zile dhulma walizotendewa, wakalia, kilio chao akakisikia Mwenyezi Mungu na kawakomboa kutokana na utumwa na kuyafanya maisha yao kuwa uchungu”.

Hali kadhalika, wananchi wa Zanzibar ni watu wa Mungu. Ni Nchi na taifa aliloliumba yeye mwenyewe. Kilio chao cha kudhulumiwa chamfika Mungu, hakimu mwenye haki, kwa hiyo tangu mapema Roho wa Mungu awakumbusha wote wenye mamlaka.

“Enyi wakuu, watendeeni raia wenu kwa uadilifu na haki, mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye Bwana mbinguni”

Mhashamu Norbert Mtega haya ndio yanayopaswa k u h i m i z w a w a t a w a l a kuacha kuf icha ukwel i na kuwadhulumu raia na kuwaonea hasa vitendo vilivyofanywa na Serikali ya Muungano kwa Wananchi wa Zanzibar. Watu wengi wameuwawa na kunajisiwa, k u i b i w a n a k u f u n g w a magerezani na kila aina ya manyanyaso. Askofu Mtega, haya ndio ilikuwa wajibu wako na wenzako kuyakemea na sio kutoa rai ya kutaka kuwapiga vita bila ya kuwaonea haya wale wenye mawazo ya kuukataa Muungano. Sio daraja yako kupiga vita watu, bali kusaidia ukweli upate kudhihirishwa katika kadhia ya Muungano. Watu wanamkataa Mungu na hujatoa rai ya kuwapiga vita seuze wanaoukataa Muungano.

Nae Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amesema, katika siku za hivi karibuni kumezuka vikundi vya baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa dini ya Kiislamu kufanya vurugu kwa visingizio vya kudai maslahi ya waumini wa madhehebu ya dini ya Kiislamu.

Mwinyi anasema, vikundi hivyo ni vya shari vyenye kujihusisha na vitendo viovu kama vile kuchoma nyumba, makanisa na kupiga watu kwa

madai kwamba wanapigania Uislamu. Mwinyi hakuishia h a p o a k i w a f a n a n i s h a Muamsho na Al-shabab, Boko haram na Al-kaida. Sh. Ali Hassan Mwinyi alikuwa wapi wakati wa vikundi vya shari vilipokua vikipiga watu hapa Zanzibar na kuiba ndani ya majumba huku wakiingiliwa watoto wa watu mbele ya macho ya wazazi wao? Mwinyi atueleze ipo rekodi ya kauli yake alioitoa kukemea na kulaani vitendo vya kinyama vilivyokua vikifanywa na Janjawiri. Mwinyi sema kweli kinachokuuma ni Muamsho k u s e m a “ M u u n g a n o hatuutaki”.

Je? unashirikiana na Askofu pale aliposema tuwapige vita na wala tusiwaonee haya wale wanaotaka Muungano uvunjike. Tunaelewa kwamba ndani ya Muungano huu ndio umepata neema za dunia ambazo ni za kupita tu tena na watoto zako takriban wote wamefunikwa kwa neema za Muungano huu. Sasa lazima wawe maadui kwako wale wote wasioutaka Muungano kwa vile Muungano mbele yako ndio kila kitu chako. Hapana shaka inakuuma k u w a o n a Wa z a n z i b a r i wamekuwa kitu kimoja.

Baada ya kauli ya Askofu ya kutaka kuwapiga vita wale

wote wanaukataa Muungano na kauli ya Mwinyi juu ya Viongozi wa Muamsho kutokana na msimamo wao juu ya Muungano, Sasa kuna kundi linalojiita wenyeji wa Unguja wa asili ya Wasegeju kutoka Bara. Hawa wametoa vipeperushi na kusema wao wanautaka Muungano na wakilaumu marekebisho ya katiba ya Zanzibar na kuitisha kura ya maoni iliyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Wanasema wanahitaji katiba mpya ya Zanzibar i l i “KUFUTA MFUMO HUO” Wasegeju hao kama walivyojiita wenyewe katika vipeperushi walivyo vimwaga nchi nzima ambavyo gazeti la Mwananchi la tarehe 4-6-2012 wamekitia na limeweza kusomwa kwa ufasaha. Katika kutilia mkazo dai lao Wasegeju hao wanasema: Kuwapo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar isiyokuwa na Umoja wa Kitaifa.

Ni dhahiri ukikusanya maneno ya Askofu Mtega ambayo yametiwa ndani ya gazeti la Nipashe la tarehe 11-6-2012 pamoja na maneno ya Rais mstaafu Mwinyi ndani ya gazeti hilo hilo la Nipashe, utagundua kwamba kundi hilo la Wasegeju wa Zanzibar liliungwa mkono

na baadhi ya Viongozi wa ki-hafidhina waliokuwemo ndani ya Serikali na Chama.

Kundi hili halitaki Serikali ya Umoja wa Kitaifa na viongozi wa Ki-hafidhina wakataka viongozi wa CUF ndani ya Serikali wafukuzwe huku zikichochewa fitna za Wapemba na wa Unguja yenye malengo ya kuwagawa wananchi ili Muungano uzidi kukitisha mizizi yake hapa Visiwani Zanzibar. Hili ndio kundi hatari kundi hili kwa muda mrefu walikua wakijiita ni Waafrika bila ya kutaja kabila.

B a a d a y a k u s e m w a kwa kuambiwa kwamba ni wababaishaji, kwa vile Nyerere alikua Muafrika vile vile lakini akiijua kabila yake na akisema kwamba yeye ni Mzanaki, basi iweje hawa Waafrika wa Zanzibar wasizijue kabila zao?

Sasa hivi ndio kwa mara ya kwanza wanajiita ni Wasegeju kwa hivyo ndio wanautaka Muungano lakini hawaitaki Serikali ya Kitaifa. Hapa kuna wimbo mkongwe wa wazazi wetu waliokuwa wakituimbia nao ni huu:

Msegezu ana ng’ombee Nami nina ng’ombe zangu

Namwambia tuchanganye Hataki kwa heri nakwenda zangu.

Ni kweli Muungano kwa Wazanzibar i unadosar i kubwa kutokana na historia ya ukandamizaji na mabavu yaliofanywa kwanza na utawala wa Tanganyika na baadae Tanzania Bara, juu ya Zanzibar. Ipo haja ya Zanzibar na Tanganyika kurudi kama zilivyokuwa kabla ya tarehe 26 April, 1964. Nini maana yake? Hapo ndipo penye dhana ya nchi mbili na Serikali mbili zilizoungana, Moja nchi ya Zanzibar, ya pili Tanganyika.

Huko jamani sio kuvunja M u u n g a n o . H u k o n i kuzirejesha Nchi mbili katika hali ya usawa ili ziweze kuheshimiana.

Muungano huu wa miaka 48 iliopita ni dalili tosha kuwa haufai kwa sababu moja tu utawala wa Tanganyika na Watazania Bara kwa kiasi cha nusu karne (karne moja ni miaka mia moja) iliyopita, wametumia nguvu zao za kidola, kukimbilia umoja, kwa kutumia ujanja, uwongo, unafiki, uonevu, unyanyasaji, ubaguzi, fitina, dhidi ya Zanzibar na baina ya Wazanzibari.

Wazanzibari wanayo haki na uhuru wa kuongea na kuandika kwa kuzitetea haki za nchi yao kitu ambacho akina Wasegeju wa Unguja hawakipendi wakiungwa mkono na baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo. Zanzibar ha i towaja l i wa le wote wasioitakia mema nchi ndio maana imeweka msimamo wake hadharani na bila ya woga wala kiwewe.

MZEE Ali Hassan Mwinyi.

Page 5: ANNUUR 120

5RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012AN-NUUR Makala

KAMA tunavyokumbuka, nchi yetu imeingia katika kipindi muhimu, cha kuandika Katiba mpya, kupitia kile k i n a c h o j u l i k a n a k a m a “mchakato wa mabadiliko ya Katiba”. Katika kipindi hichi matukio mengi yamejitokeza ambayo, kwa njia moja ama nyengine, yanaweza kuwa yana uhusiano na suala hilo.

Hata hivyo, yapo matukio ambayo hayana uhusiano wowote na suala hilo, lakini, kwa baha t i mbaya sana , wasioipendelea mema nchi yetu wamekuwa wakiutumia mwanya huo, kama fursa ya kueneza chuki baina ya makundi mbali mbali; kuhamasisha vitendo vya kibaguzi, matusi, kashfa, dharau na vitisho.

Kwanza kabisa, hatuna budi tujikumbushe kuwa chama cha wananchi, CUF, ni chama cha mwanzo kabisa kilichodai mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katka kipindi kigumu, na kwa muda mrefu, huko nyuma wakati chama tawala, kwa kutumia nguvu zake zote, kimekuwa kikilipinga shauri hilo. Na vyama vyengine vikiwa kimya kabisa.

Chama cha CUF kilifanya hivyo kikiamini ndio muarubaini pekee wa kuzipatia dawa ya k u d u m u k e r o n y i n g i z a muungano wetu zinazoongezeka siku hadi siku. Kwa bahati mbaya sana, na kwa kuonesha nia mbaya kabisa juu ya suala hilo, vyombo vya dola katika tarehe 26 na 27 mwezi wa Januari, mwaka 2001, vilitumia nguvu zisizo za kawaida, kuyazima maandamano ya CUF yaliyokuwa yana lengo jema la kudai mabadiliko ya katiba na hatimae kusababisha mauwaji ya wanachama na wapenzi wa chama chetu wasiopungua 45; wengine kutiwa ulemavu wa maisha; wengine kuharibiwa mali zao; wengine kuwekwa magerezani; wanawake kubakwa, watoto kuwachwa mayatima na Tanzania kuzalisha wakimbizi kwa mara ya kwanza. Yote hayo yaliwafika wana-CUF, wakiwa na nia njema ya kuitafutia nchi yao mustakbali mwema. Hivyo basi ni chama cha CUF kwa kupitia kupotezwa kwa roho, heshma na utu wa wanachama wake, ndio kilichotoa njia hadi pale wanaharakati wengine walipojiunga kulipigia debe dai hilo la katiba mpya.

Hatuna budi kumshukuru na kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, kwa uwamuzi wake wa kuitikia kilio cha Watanzania n a k u r u h u s u m c h a k a t o wa mabadiliko ya katiba, tena kwa kupitia mchakato utakaowahusisha wananchi moja kwa moja. Tunamshukuru Mhe Rais Kikwete, kwani tunafahamu fika viongozi wenzake wote waliotangulia walishindwa kufanya hivyo. Mara moja bunge lilipoamua kwa kauli moja kupitisha azimio la kutaka kufufua serikali ya Tanganyika katika kipindi cha Awamu ya Pili cha Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mwalimu Nyerere kwa kutumia nguvu yake ya ubaba wake wa Taifa alilipinga Bunge zima, na kusema yeye haruhusu

UVCCM wamepotokaWazanzibari tusikubali kugawanywa

Na Ahmed Omar Khamis

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika.

Kupitia mchakato huo, vyama vya siasa na jumuiya mbali mbali vya kiraia na taasisi za kidini zimekuwa zikiendesha harakati mbali mbali na kuweka wazi misimamo yao kuhusiana na suala hilo. Chama cha siasa kilichopevuka kidemokrasia, lazima kiheshimu misingi ya demokrasia ya kweli, na katu hakioni haja ya kumuingilia mtu, ama kikundi chochote, katika kuonesha kile anachoamini, juu ya suala fulani, alimradi tu kila mmoja anafanya hivyo kwa kumuheshimu mwengine, na kwa kujali umuhimu wa amani ya nchi yetu. Nikiwa ni Mzanzibar, naamini kuwa pamoja na kuwepo kwa mchakato huo, suala la kuendelezwa kwa umoja, udugu na mshikamano wa Wazanzibari ni jambo la msingi. Siamini hata kidogo kuwa mchakato wa mabadi l iko ya kat iba unatoa fursa kwa watu kukejeli misingi ya umoja wa kitaifa wa Wazanzibari iliyofikiwa kwa gharama kubwa, kuwakejeli na kuwabagua Wazanzibari kwa kuzingatia visiwa wanavyotoka au asili za makabila yao.

Wakati vikundi mbali mbali hapa Zanzibar vikiendelea na harakati zao za kuweka hadharani yale wanayoamini kuhusiana na mchakato huu wa katiba, Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM, bila shaka kwa kuruhusiwa, na bila ya kukemewa na uongozi wa chama chao, walifunga vibwebwe kuanzisha matusi, kashfa, malumbano na vitisho kwa chama cha CUF, viongozi wake na wananchi wenye asili ya kisiwa cha Pemba, kwa kisingizio cha kupambana na jumuiya ya UAMSHO. UVCCM iliitumia fursa hiyo kutoa yale ambayo mimi naamini ndio yaliyomo ndani ya nyoyo na nafsi zao kwani kipindi chote kilichopita tokea kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa

hapa Zanzibar waliikosa fursa hiyo. Hii ni kutokana na kuwa viongozi wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar waliapa kuwa hawatamvumilia yeyote ambaye atathubutu kutaka kuvunja umoja wa Wazanzibari uliopo.

Kwa vitendo hivi, imenifanya niamini bi la ya wasiwasi wowote kwamba UVCCM hawakuridhishwa na kufikiwa kwa maridhiano na Umoja wa kitaifa wa Wazanzibari. Chuki dhidi ya Umoja wa Wazanzibari na Serilikali yao umejitokeza wazi kufuatia kauli ya Baraza Kuu la UVCCM lililokutana hivi karibuni. Baraza Kuu la UVCCM lilikutana hivi karibuni, na kutoa kauli nzito kupitia Katibu Mkuu wao, Matrin Shigella, kwa kusema Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzizibar, inayoongozwa na Mhe. Dr Ali Shein, inahusika na Vurugu hizo. Dr. Ali Mohamed Shein alitoa taarifa Rasmi kuhusiana na vurugu hizo, na kuzipinga kauli kama hizo za uchochezi, zilizowahi kutolewa hapo kabla na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Bwana Vuai Ali Vuai aliyedai kuwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Serkali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar anahusika na vurugu hizo. Kupitia taarifa yake Dr Shein aliupinga hadharani uzushi huo. Ni jambo la kushangaza kuona UVCCM wanarejea tena kauli hiyo ya shutuma dhidi ya Serikali, na kupingana na Rais. Mimi naweza kuita huo ni utovu wa adabu na maadili. UVCCM, kwa kutumia mwanya wa UAMSHO, inaendesha programu ya kiufundi, kukabiliana na Seririkali ya Umoja wa Kitaifa, kwa kufanya vitendo viovu vya kuhatarisha amani ya nchi na umoja wa Wazanzibari. Miongoni mwa vitendo hivyo ni hivi vifuatayo:-

1. Kukihusisha moja kwa moja chama cha CUF, na

taasisi za kidini, na yale yote yanayofanywa na taasisi hizo. Hili limekuwa likifanyika kwa kupitia majukwaa yao ya kisiasa na magazeti wanayoyadhibiti. Kwa mfano katika mikutano ya UVCCM, iliyofanyika maeneo mbali mbali ya Unguja, kama vile Jang’ombe, Masumbani- Z iwa tuwe na Magogon i , ijulikanayo kama “mikutano ya Borafia na Baraka Shamte”, pamekuwa pakitamkwa wazi wazi kuwa CUF ina uhusiano na taasisi za kidini. Maskani ya CCM ya Kachochora imekua ikiandika wazi wazi, na inaendelea kuandika hadi sasa, katika ubao wake wa Uchochezi, na kwa maandishi makubwa, kuwa taasisi hizo na vikundi hivyo ni chama cha CUF. Kuwatukana viongozi wa CUF na wale wa serikali ya Zanzibar wanaotokana na chama cha CUF. Kwa mfano katika mikutano ya “Borafia na Baraka Shamte” matusi ya wazi yalikuwa yanatolewa, kwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

2. Kuwahusisha viongozi wa CUF, na wale wa serikali ya Zanzibar, watokanao na chama cha CUF na taasisi na vikundi hivyo. Kwa kutumia mikutano yao hiyo maneno ya wazi ya kumtaja Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif, kuhusika na taasisi za kidini, yamekuwa yakitolewa. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, ametamka wazi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Zanzibar, Mhe Abuubakar Khamis Bakary, ana uhusiano na taasisi za kidini. Halkadhalika, kwa kupitia gazeti la NIPE HABARI, ambalo linaandikwa na timu kabambe ya UVCCM, wamekuwa wakimuandika wazi wazi Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Waziri wa

Katiba na Sheria, kuwa wao ndio wanaoratibu vikao vya taasisi za kidini bila ya kuonyesha ushahidi wowote.

3. Kufanya kampeni za kuwabaguwa Wazanzibari wenye asili ya kisiwa cha Pemba na kuhubiri chuki dhidi yao, bila hata kujali kuwa Rais na Makamo wake ni miongoni mwao. Kwa mfano Tauhida Carlos Nyimbo, Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Mjini Maghribi, ametamka wazi wazi katika majukwaa ya mikutano yao kuwa wao (UVCCM) wanataka muungano wenye muundo wa serikali nne (4), ya Tanganyika, ya Unguja, ya Pemba na ya Muungano, muundo ambao utavibagua visiwa vya Pemba na Unguja, na kila kimoja kuwa na serikali yake, jambo ambalo bila shaka ni kinyume na sera ya CCM ya serikali mbili (2) kuelekea moja (1).

Maskani maarufu ya CCM ijulikanayo kama Kachochora w a m e k u w a b i l a k i f i c h o wakichapisha maneno ya wazi ya kuwabagua Wapemba: kama vile Muungano ni kati ya Tanganyika na Unguja, sio nyinyi Wapemba. Kama hamuutaki, rudini kwenu. Vitendo vya kibaguzi pia vimekuwa vikifanywa kwa kuandikwa vijarida vyenye ujumbe wa kuwataka Wazanzibari wenye asili ya kisiwa cha Pemba wahame Unguja na warudi kwao. Katika Vijarida hivyo amekuwa akitukanwa matusi ya nguoni Rais Mstaafu wa Zanzibar na Muasisi wa Maridhiano, kipenzi cha Wazanzibari Mhe Amani Abeid Amani Karume.

4. Kutoa vitisho kwa wananchi. Kwa mfano katika mikutano yao wamekua wakisisitiza kwamba watarejesha tena upya vipigo vya zamani, kwani silaha zao, za nondo na visu, bado wanazo.

Tu k i w a Wa z a n z i b a r i , tunaoipenda nchi yetu, lazima tulaani, kwa nguvu zote, vitendo hivyo, vinavyosimamiwa na UVCCM, vyenye ishara ya k u w a c h o n g a n i s h a u p y a Wazanzibari, kuwatia chuki baina yao na kuwagawa. Tusiwe tayari kuona Zanzibar inarudishwa katika hali mbaya iliyokuwepo huko nyuma na watu wachache wasioionea uchungu nchi hii.

Tunatoa wito kwa Wazanzibari na Watanzania wote, kuheshimu sheria za nchi na kutumia busara na hekima, katika kufikisha ujumbe wa kile ambacho kila mmoja wetu anaamini kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya katiba, bila ya kuathiri, umoja, amani na utulivu wa nchi yetu. Mchakato huu bila shaka ni zalio la suluhisho la kudumu la Muungano wetu. Tunategemea k u p i t i a m c h a k a t o h u u , Muungano mpya wa Tanzania usio na kero utazaliwa, nao ni ule utakaozipatia Zanzibar na Tanganyika mamlaka yao kamili kama dola mbili.

Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania.

(Imeandikwa na Ahmed O m a r K h a m i s , K a i m u Mkurugenzi na Afisa wa Habari na Uenezi Jumuiya ya Vijana – JUVICUF Taifa.)

Page 6: ANNUUR 120

6 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012 AN-NUUR MAKALA

KWA Watanzania wengi wasio na taarifa sahihi, Mwalimu Nyerere alikuwa ni mlinzi imara wa Usekula ndani ya chama tawala na Serikali. Lakini mikutano yake ya siri na viongozi wa Kanisa, inathibitisha wazi kwamba Mwalimu alikuwa tofauti kabisa na vile alivyodhaniwa na wengi. Dhulma wanayofanyiwa Waislamu nchini katika Elimu, kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kama ilivyobainika hivi juzi ni matokeo ya Mfumo-Kristo aliouasisi.

Waislamu wanajua, Wakristo waadilifu wanajua, Maaskofu wanajua, Wasomi waadilifu wanajua, vyombo vya habari vinajua, kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa adui mkubwa wa Uislamu katika eneo zima la Afrika Mashariki, ingawa baadhi ya hao niliowataja, wanaficha ukweli huu kwa kutumia propaganda za ulaghai na kuhamisha ajenda.

Katika mazungumzo yake ya siri, August 2 mwaka 1970 na Rev. Robert Rweyemamu, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) wakati ule, Nyerere amenukuliwa katika Kitabu ‘Development and Religion in Tanzania’, kilichoandikwa na J.P Van Bergen akisema ameanzisha Idara ya Elimu ya Siasa katika TANU, na kwa makusudi amemteua Mkristo kuiongoza, si kwa sababu ni mwanasiasa mahiri, isipokuwa kwa sababu ya imani yake thabiti ya Kikatoliki.

K i t a b u h i k i a m b a c h o kimechapishwa na Kanisa Katoliki, kimebainisha wazi kwamba hiyo ndiyo sababu Padri Mushendwa, Mkatoliki Mkereketwa, akafanywa kuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Siasa ya TANU. Kwa kifupi, Nyerere aliendeleza tu ule ubaguzi dhidi ya Waislamu katika elimu ulioachwa na Waingereza. Alikuwa anafahamu hasira za Waislamu katika eneo la elimu. Aliandika katika kitabu chake ‘Freedom and Unity’ kwamba upogo (disparity) katika viwango vya elimu, unaweza kutumiwa kama jambo la kisiasa:

“The enmity which could be stirred by the evil minded between Muslims and Christians as we all know, the colonial government did not concern itself very much with education and therefore the majority of those who managed to acquire did so in the mission schools, and are therefore mostly Christians. Here again, then we have a division by its very existence constitutes a political threat to unity” (p. 179).

Tafsiri: “Uadui unaoweza kuchochewa na fikra mbaya kati ya Waislamu na Wakristo kama wote tunavyofahamu, Serikali ya Kikoloni haikujihusisha zaidi na Elimu, kwa hiyo wengi waliobahatika kupata elimu walipata katika Shule za Kanisa, wengi wao ni Wakristo. Kwa hiyo hapa tuna mgawanyiko ambao kuwepo kwake unaleta

‘Crusade’ ya Nyarere katika elimuNa Said Rajab

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

tishio la kisiasa kwa umoja” `(P.179)

Waislamu wa Tanganyika ambao walioongoza harakati za mapambano ya kudai Uhuru kutokana na ukandamizaji wa Wakoloni bado hawajavuna matunda ya kazi yao tangu Uhuru upatikane mwaka 1961. Waislamu wengi wa sasa wanajiuliza kuhusu hatima ya fumbo hili kubwa. Upogo wa Kielimu kati ya Waislamu na Wakristo hapa nchini unaendelea kama kawaida.

Waislamu wamebaguliwa na kuhujumiwa kielimu ndani ya nchi yao wenyewe, kabla na baada ya Uhuru. Uzoefu waliopata kutokana na hujuma walizofanyiwa na Nyerere, umewafunza kwamba n i makosa kumtarajia Mkristo, hata akionekana muadilifu kiasi gani mbele ya umma, kulinda maslahi ya Waislamu. Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake:

“ E n y i M l i o a m i n i ! Msiwafanye wasiri wenu watu wasiokuwa katika ninyi, hao hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yale yanayokudhuruni. Bughudha (yao juu yenu) inadhihirika katika midomo yao. Na yanayofichwa na vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekubainishieni dalili (zote) ikiwa ninyi ni watu wa kufahamu” (Qur 3:118).

Nyerere alihakikisha kwamba pengo la kielimu kati ya Wakristo na Waislamu, Tanzania Bara na Visiwani, kamwe halipungui na

badala yake linaongezeka zaidi, ingawa katika kitabu chake, au majukwaa ya siasa anajifanya kulipunguza. Hizo ndiyo hila zao. Maneno na vitendo vyao haviendi pamoja. Dk. Joyce Ndal ichako anadanganya kwamba hujuma iliyofanyika dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu ni makosa ya kibinadamu, wakati anajua wazi kwamba Baraza lote la Mitihani ni miliki ya Wakristo. NECTA imekuwa kama Kigango au Parokia ya Wakristo! Hawataacha kuwafanyia ubaya Waislamu katika mazingira kama hayo!

Utafiti uliofanywa na G. A. Malekela, Profesa Mkristo katika Kitivo cha Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umefichua kwamba katika Sekondari za Serikali Tanzania Bara mwaka 1983, Wakristo walikuwa asilimia 78 na wasio Wakristo asilimia 22. Bila ubishi Wakristo wamezidi mno, licha ya ukweli kwamba Waislamu wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania wote.

U t a f i t i m w i n g i n e p i a uliofanywa na ‘Udhamini wa Waislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ‘(DUMT) na kuchapishwa na Jarida la ‘Al - Haqq International’ umeonyesha kwamba idadi ya wanafunzi Waislamu imekuwa ikipungua katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vya umma hapa nchini.

Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam peke yake, utafiti

umeripoti kwamba idadi ya wanafunzi waliodahiliwa katika kipindi cha mwaka 1986-1990 ilikuwa 4,191. Katika idadi hii, wanafunzi Waislamu walikuwa 586 tu au asilimia 13, wakati Wakristo walikuwa 3,609 au asilimia 87.

Kwa hiyo kutokana na ushahidi kama huu wa kiutafiti, si bahati mbaya katika kipindi chake chote cha miaka 24 bila kuingiliwa, kama Rais wa Tanzania (1961 -1995), Nyerere akiwa Mkatoliki, mara zote amemteua Mkristo kuongoza Wizara ya Elimu. Mara zote Waislamu wamekuwa wakilalamika kwamba upendeleo huu wa Wakristo katika shule za sekondari na Elimu ya Juu, umewafanya wadhibiti nafasi zote muhimu katika utawala na taasisi za umma.

H a l i h i i i m e w a f a n y a Waislamu nchini wabaki na fursa chache mno na wafanye kazi za kawaida kabisa zisizohitaji elimu au taaluma yoyote kama udereva na uhudumu wa ofisi. Waislamu wanadai mgao wa haki katika keki ya taifa.Tangu tupate uhuru, idadi ya wanafunzi Waislamu katika vyuo vikuu vya umma inazidi kushuka. Hali hii si matokeo ya makosa ya kibinadamu, bali ni mkakati maalumu wa mawakala wa kanisa Serikalini.

Marehemu Prof. Kighoma Mal ima, Muis lamu wa kwanza kuongoza Wizara ya Elimu na Utamaduni mwaka 1987, aligundua dhulma hii kubwa wanayofanyiwa wanafunzi Waislamu, ambayo Dk. Joyce Ndalichako anaiita ni makosa ya kibinadamu. Makosa ya Kibinadamu kwa Waislamu tu!

Prof. Malima alichukua hatua ya kubadili utaratibu huo mbovu na kuanzisha utaratibu wa kuchagua wanafunzi kwa kutumia namba badala ya majina, ili wanafunzi wote wawe na haki sawa. Utaratibu huu mpya ulipotekelezwa kwa mwaka mmoja, idadi ya wanafunzi Waislamu waliofaulu na kujiunga na sekondari za umma iliongezeka kwa asilimia 40.

Lakini kama kawaida yao, mawakala wa Kanisa ndani ya Serikali na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) wakaanza kumuandama Prof. Kighoma Malima na kumchafua kwa propaganda zenye sumu. Mfumo-Kristo ukahakikisha Prof. Malima anaoondoka Wizara ya Elimu na Utamaduni, na ule utaratibu wa kuchagua wanafunzi kwa kutumia namba ukaondolewa pia.

Kadinali Pengo alitangaza kupitia vyombo vya habari

kwamba “Malima ni mtu Hatari” na vyombo vya habari vikaendesha kampeni maalumu ya kumuandama P r o f . M a l i m a k i l a alipokwenda, na hata baada ya kujiondoa Serikalini na CCM. Hatimaye Malima akafa ghafla jijini London Uingereza katika mazingira ya utatanishi. Kosa lake kubwa Prof. Malima lilikuwa ni kuhoji Mfumo-Kristo unaohujumu Waislamu.

Kama ilivyo Tanzania Bara, Waislamu wa Zanzibar pia wamebaguliwa kielimu na nafasi zao za kusoma nje zimehujumiwa kwa sababu ya Muungano wa kulazimisha kati ya Tanganyika na Zanzibar ambao umeunda Tanzania. Mohammed Mwinyi Mzale, aliyepata kuwa Waziri wa Elimu Zanzibar aliwahi kutamka kwamba wajumbe 12 wa Kamati ya pamoja ya kuchagua wanafunzi kwa ajili ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya juu ndani na nje ya Tanzania ‘Joint Selection Committee’ (JOSECO), hakuna hata mmoja aliyetoka Z a n z i b a r. A l i b a i n i s h a wazi kwamba Wanafunzi waliopata ‘Scholarships’ za Zanzibar, wanapokwenda kwenye balozi za Tanzania nchi za ng’ambo walikuwa wakifukuzwa kwa kisingizio kwamba hawamo kwenye ‘Scholarships’ za Jamhuri ya Muungano, licha ya ukweli kwamba Zanzibar ilikuwa ik ichangia kias i chake kwenye bajeti ya Elimu ya Juu ya Muungano.

B w a n a M o h a m e d Mwinyi Mzale alibainisha waz i kwamba vyombo vinavyosimamia Elimu ya juu Tanzania ni vya ‘Muungano’ kwa maneno tu, lakini kwa vitendo na miundo yake ni vya Tanganyika. Bunge la Jamhuri ya Muungano linatunga sheria kwa maslahi ya Tanganyika, ambayo ni pacha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Nimalizie kwa kumuomba Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako aache kutoa majibu mepesi kwa masuala magumu kama haya. Madai ya Waislamu kuhusu kuhujumiwa kielimu ni sahihi na ya muda mrefu mno. Hayajapatiwa ufumbuzi mpaka leo kwa sababu ya kutanguliza propaganda za kijinga, badala ya kuleta m a j a w a b u h a l i s i k w a tat izo. Imefikia mahali sasa Waislamu wameamua kupigania haki zao wao wenyewe kwa kuwa taasisi za umma zilizowekwa kufanya kazi hiyo zimewasaliti. Na Insha-Allah haki hizo zitapatikana siku moja!

Page 7: ANNUUR 120

7RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012AN-NUUR MAKALAHIVI karibuni Mahakama moja nchini Marekani ilimuhukumu Tarek Mehan (Muislamu) kifungo cha miaka 17. Alishitakiwa kwa tuhuma za ugaidi baada ya kusilimu na kuonesha k u p i n g a u v a m i z i w a Marekani katika nchi za Waislamu.

Ifuatayo ni tafsiri ya kauli ya Tarek Mehan mbele ya Hakimu kabla ya kwenda kutumikia kifungo hicho.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwengi wa Fadhila, Mwengi wa Rehema

Miaka mine iliyopita mwezi kama huu nilikuwa namalizia zamu yangu ya kazi katika hospitali moja ya umma. Wakati naelekea kwenye gari langu, watu wata tu wakanisogelea . Wakaniambia nichague ama kuyafanya mambo yawe mepesi au kuyafanya yawe mazito. Wakanambia njia nyepesi ni kukubali niwe mpelelezi (shushushu) wa serikali, na wakaniahidi ya kuwa kama ningekubali h i v y o , n i s i n g e w e z a kufikishwa mahakamani wala kwenda kizimbani. Na hii ndiyo njia nzito.

FBI pamoja na wapelelezi h a w a w a l i f a n y a k a z i kubwa na serikali kukubali kupoteza mamilioni ya dola kuniweka ndani, kunitesa na mwisho kabisa leo hii wamenisimamisha hapa mbele yenu nihukumiwe kwa mara nyengine tena niwekwe ndani.

Wiki chache zilizopita, watu wengi wamejaribu kunipa rai mbalimbali juu ya kile ambacho nigepaswa kukisema mbele yenu. Wapo walionishauri nikiri au kukubal i kosa kwa kutarajia kuwa na matumaini ya kupunguziwa adhabu. Wengine walishauri niongee ukweli tu vyovyote vile iwavyo. Lakini ninachotaka kuk i fanya n i kuongea kuhusiana na maisha yangu walau kwa dakika chache.

Wa k a t i n i l i p o k a t a a kuwa mpelelezi serikalini nilishitakiwa kwa kosa la jinai la kuwaunga mkono M u j a h i d i n a a u k a m a wanavyopenda kuwaita; ‘Magaidi’, kupigana kwa ajili ya kuzitwaa dola za Kiislamu duniani kote. Mimi, hata hivyo, sikuzaliwa katika nchi ya Kiislamu. Nimezaliwa na kukulia hapa hapa Marekani na hichi ndicho kinachowakasirisha w e n g i . N i t a k u w a j e Mmarekani baadae niamini haya ninayoyaamini? Na pia kuwa na nafasi hii niliyonayo? Kwa kila jambo ambalo mtu anakabiliana nalo kwenye mazingira anamoishi ,linakuwa ni jambo ambalo linaonesha mtazamo wake

Kauli ya Tarek Mehanmbele ya Mahakama

na mimi sina tofauti na hali hiyo. Hivyo, kutokana na sababu mbalimbali naweza kusema ni kwa sababu ya Marekani ndio maana niko hivi nilivyo.

N i k i w a n a u m r i w a miaka wa sita, nilijaribu kukusanya magazeti yenye habar i za kuchekesha . B a t m a n a l i p a n d i k i z a wazo fulani ndani ya akili yangu. Alini tambulisha P A R A D A I M U j i n s i dun ia i l i vyo : kwamba kuna wakandamizaji na wakandamizwaji na kwamba kuna wale wanaosimama kuwalinda au kuwatetea wanaokandamizwa. Hii ilivuma sana kipindi mimi ni mtoto. Nilivutiwa na kitabu chochote ambacho kilionesha hali hii.

Baadae nikaanza elimu yangu ya sekondari na n i k a c h u k u w a s o m o l a historia. Nilijifunza ni kiasi gani mtazamo ule ulivyo

duniani. Nilisoma kuhusu Wamarekani wazawa na kile kilichowaingiza kwenye mikono ya walowezi wa Kizungu. Nil isoma pia kuhusu jinsi madhuria wa walowezi hao wa Kizungu na wao walivyokandamizwa chini ya udhalimu wa mfalme George wa tatu.

Nilisoma kuhusu Paul Revere, Tom Paine, na jinsi Wamarekani walivyoanzisha uasi wa kijeshi dhidi ya wanajeshi wa Waingereza u a s i a m b a o h i v i s a s a tunashrehekea kama vita ya kimapinduzi ya Marekani. Nikiwa kama kijana niliweza pia kuendelea na safari mbalimbali masafa machache kutoka pale tunapoishi. Nil isoma kuhusiana na Herriet Tabaman, Nat Turner, John Brown na mapambano dhidi ya utumwa ndani ya nchi. Nilisoma pia kuhusu Emma Goldman, Engene Debs na mapambano kuhusu

umoja wa wafanyakazi, na masikini.

Nilisoma kuhusiana na Anne Frank, akina Hittler na j insi walivyowatesa wachache na kuwaweka ndani wapinzani. Nilisoma kuhusu Rosa Parks , Malcolm X na Martin Luther King kuhusu mapambano dhidi ya haki za raia. Nilisoma kuhusu Ho Chi Minh na jinsi Wavietnam walivyopigana miongo kadhaa ili kujikomboa kutokana na mvamizi mmoja dhidi ya mwengine. Nilisoma kuhusu Nelson Mandela na mapambano dhidi ya ubagzi wa rangi huko Afrika ya Kusini. Kila nilichosoma miaka hiyo kilithibitisha kile ambacho niianza kujifunza kipindi nikiwa na umri wa miaka sita: kwamba kupitia historia, kulikuwa na mapambano yasiyoisha kati ya wanaokandamizwa na wakandamizaji. Kwenye kila moja ya pande hizo mbili, nilijikuta nikiegemea k w a w a l e w i l i o k u w a wanakandamizwa na mara zote niliwaheshimu wale wal ioj i to lea kuwal inda bila kujali tofauti zao za kiutaifa wala za kidini. Na wala sikuwahi kupoteza m i h u t a h a s a r i y a n g u niliyosoma darasani. Leo hii naongea hapa, bado mihutasari hiyo ipo katika hali nzuri chumbani kwangu.

W a t u w o t e h a o niliowasoma historia zao kila mmoja anamzidi mwenzake. Nilivutiwa na mambo mengi kuhumuhusu Malcolm X. Lakini zaidi ya yote nilivutiwa zaidi na wazo la mageuzi ailolitoa. Sijui kama mmeona muvi (filamu) ya Malcolm X ya Spike Lee. Ni muvi zaidi ya masaa matatu na nusu. Malcolm anaeonekana mwanzoni mwa muvi hiyo ni tofauti na yule Malcolm anaeonekana mwisho wa muvi. Alianza akiwa kama mahabusu ambaye hana elimu, lakini anamalizia akiwa kama mume, baba na kiongozi anayelindwa na mwenye ushawishi mkubwa kwa watu wake. Pia ni Muislamu wa kweli anaeenda kuhiji Makka na mwisho anakufa kama shahidi. Maisha ya Malcolm yal inifundisha kwamba Uislamu si jambo au kitu cha kurithi; sio utamaduni au jambo la kikabila. Ni njia ya maisha, jambo la kiakili kila mmoja anaweza kuchaguwa

bila kujali anatOka wapi au amekulia wapi.

Hili ndilo lilinipelekea mimi kuangalia kiundani Uislamu na nilivutika sana. Nilikuwa bado kijana, lakini Uislamu ulijibu swali ambalo hata wanasayansi wakubwa wakubwa hawakuweza kul i j ibu; swal i ambalo lilipelekea matajiri na watu mbali mbali maarufu kwenye mfadhaiko na kujinyonga kwa kushindwa kulijibu: nini lengo la maisha? Kwa nini tumeumbwa? Kwa nini tumeletwa duniani? Pia Uislamu uliweza kujibu swali la kwa nini tunaishi.

Nilienda moja kwa moja kwenye kitabu kitakatifu cha Qur’an na pia kuangalia mafundisho ya Mtume M u h a m m a d ( s . a w ) i l i kuianza safari ya kuelewa. Hii yote ilikuwa inahusu nini. Maana ya Uislamu kwangu kama mwanadamu, kwa watu wanaonizunguka, kwa dunia nzima na zaidi ya kadiri nilivyosoma ndivyo nilivyoweza kuuthamini Uislamu kama vile kipande cha dhahabu. Hii ilikuwa kipindi ambacho niko kijana lakini hata leo hii, pamoja na shinikizo za miaka michache iliyopita, nasimama mbele yenu, mbele ya kila mtu ndani ya mahakama hii kama Muislamu ninaejidai au kujivunia nafasi hiyo.

Pamoja na hayo, fikira zangu nazielekeza kwa m a m b o y a l i y o k u w a y a k i w a k u t a Wa i s l a m u wengine sehemu mbalimbali d u n i a n i . K i l a s e h e m u nilipoangalia, niliweza kuona nguvu zilizotumika ambazo zilijaribu kuvunja au kuharibu kile nilichokipenda sana. Nilisoma jinsi Wasovieti walivyowafanyia Waislamu wa Afghanistani. Nilisoma kile Waserbia walichokuwa wakiwatendea Waislamu wa Bosnia. Nilisoma kile Warashia wal ichokuwa wakiwafanyaia Waislamu wa Chechnia. Nilisoma Israil ilichofanya huko Lebanon na pia inachoendelea kukifanya kule Palestine – wakipata msaada mkubwa kutoka Marekani.

Pia nilisoma kile Marekani y e n y e w e i l i c h o k u w a ikiwatendea Waislamu. Nilisoma kuhusu vita ya Ghuba na mabomu ya Urenium ambayo yaliuwa maelfu kwa maelfu na kusababisha janga la kansa kwa watu wa Iraq.

Nilisoma kuhusu vikwazo vilivyowekwa na Marekani kuzuia chakula, madawa na vifaa vya matibabu visiingie Iraq, na hali hii, kutokana na takwimu za Jumuia ya

Inaendelea Uk. 8

Malcolm X

Page 8: ANNUUR 120

8 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012 AN-NUUR MAKALA

Kauli ya Tarek Mehan mbele ya Mahakama

Madola, zaidi ya watoto laki tano walipoteza maisha.

N a k u m b u k a u s a i l i uliochukuwa takriban saa nzima aliyofanyiwa Madeline Albright (Waziri wa zamani wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani) pale alipoeleza mawazo yake kwamba watoto hawa walipoteza maisha ‘ilikuwa bei stahili’. Niliangali tukio la tarehe 11 Septemba pale kundi la watu walipojikuta wakichukuliwa kwenye ndege za kuteka nyara na kuzirusha kwenye majengo yao kulekea kule walikouwawa watoto hawa. Nikaangalia Marekani pale walipoivamia Iraq. Niliona athari za mashambulio na hofu zilizokuwepo siu ile ya mwanzo ya uvamizi. Watoto waliokuwakwenye wodi hospitalini na majeraha ya marisau ya makombora kutoka Marekani. Hakuna hata moja kati ya haya yote ambalo l i l ioneshwa au kuripotiwa na Televisheni ya CNN.

Nilisoma kuhusu mji wa Haditha ambako Waislamu 24 akiwemo mzee wa miaka 76 ndani ya kiti chake cha magurudumu, wanawake pamoja na watoto wadogo walipigwa risasi na askari wa Kimarekani. Pia nilisoma kuhusu Abeer al – Tanabi, msichana wa miaka 14 wa Iraq aliyebakwa na askari watano wa Kimarekani ambao baadae walimuuwa na familia yake kwa kuwapiga risasi za kichwa na miili yao kuichoma moto. Nataka niwaoneshe tu kuwa mnayoweza kujionea, kuwa wanawake wa Kiislamu hawaruhusiwi kuonekana hata nywele zao na watu wanoweza k u w a o w a ( w a s i o k u w a maharimu zao). Hebu leo jaribu kufikiria huyu binti kutoka kijijini, anaejiheshimu, nguo zake kuchanwachanwa na kunajisiwa na askari wa Kimarekani na wala sio mmoja, wawili, watatu wala wane bali watano. Hata leo hii ninapokaa humu jela, nasoma kuhusu milipuko isiyoisha ambayo inaendelea kuuwa Waislamu kila kona ya dunia. Hivi karibuni, mwezi uliopita, tulisikia kuhusu Waislamu 17 wa Afghanistan wengi wao wakiwa wanawake na watoto waliouliwa kwa kupigwa risasi na askari wa Kimarekani ambae baadae aliteketeza kwa moto miili yao.

Hizi ni simulizi ambazo zinaonekana kwenye vichwa vya habari, lakini moja miongoni mwa mambo ya msingi ni nililojifunza ndani ya Uislamu ni la uaminifu na undugu – kwamba kila Muislamu wa kike ni dada yangu na kila Muislamu wa kiume ni kaka yangu. Na kwamba so te , kwa pamoja ni sawa na mwili mmoja ambapo tunapaswa kumlinda kila mmoja wetu. Kwa maneno mengine ni

Inatoka Uk. 7

Paul Revere

kwamba, nisingeweza kuona mambo haya wanafanyiwa kaka na dada zangu – wakiwemo wale Waamerika wachache – halafu nikabaki kimya. Huruma yangu kwa wanaokandamizwa iliendelea lakini sasa hivi imekuwa kama jambo la mtu binafsi zaidi, kama ilivyokuwa heshima yangu kwa wale waliowalinda watu hao.

Nilimtaja Paul Revere – alipokuwa ametoka usiku, ilikuwa ni kwa lengo la kuwaonya au kuwahadharisha watu kwamba Waingereza walikuwa wanaenda huko Lexington kwa aji l i ya kuwakamata Sam Adams na John Hancock baadae kufikia mapatano ya kubinafsisha silaha zilizohifadhiwa huko na mwanamgambo mmoja. Wal ipof ik ia mapatano, walimuona mwanagambo yule akiwasubiri akiwa na silaha mkononi. Kutokana na vita hivyo, yakaja mapinduzi ya Amerika. Kuna neon la Kiarabu lenye kuelezea maana juu ya vile wanamgambo walivyofanya siku ile. Neno hilo ni JIHAD, na hii ndio inayohusiana na kesi yangu.

Picha zote hizo za video pamoja na tafsiri zake na mabishano ya kitoto juu ya, ‘Oh, alitafsiri aya hii na, Oh, aliisahihisha ile sentensi na

ule ushahidi wote ukabadilika kuwa ni kitu kimoja. Waislamu ambao walikuwa wakijilinda au kujihami kutokana na waliokuwa wakitendewa na askari wa Kimarekani ndivyo Waingereza walivyofanya huko Marekani. Hii ilikuwa wazi kwa kupewa kesi kwa kosa ambalo sijawahi kufanya. Mashahidi wa serikali ya Marekani wenyewe wanatofautiana dai hili na tulileta wataalamu mmoja baada ya mwengine juu ya suala hilo ambao walitumia masaa kadhaa kuchambua kila neno nililoliandika ambayo yalionesha msimamo na imani yangu.

Baadae nilipoachiwa huru, serikali ikapeleka majasusi kujaribu kuniingiza kwenye orodha ya hao wanaowaita magaidi i la sikuonesha u s h i r i k i a n o . K i t u c h a kushangaza, hata hivyo, baraza la wazee wa mahakama kusikia jambo hili. Kwa hivyo, hii sio kesi kuhusu nafasi yangu kwa Waislamu kuwauwa Wamarekani, ikiwa na maana kwamba Waislamu lazima wazilinde nchi zao kutokana na wavamizi – Wasovieti, Wamarekani au Wakina Martin. Hichi ndicho ninachoamini. Ndicho siku zote nilichokuwa nakiamini na ndicho nitakachoendelea

kukiamini siku zote. Huu sio ugaidi wala sio siasa kali. Hizi ni alama ambazo usoni mwenu ambazo zinaashiria: ulinzi wa nchi yako au ardhi yako.

Kwa hivyo sikubaliani n a w a n a s h e r i a w a n g u w a n a p o s e m a k w a m b a nisikubaliane na imani yangu – hapana, nakataa. Kila mwenye akili timamu na ubinadamu wa kweli hana hiari ila ni kukubaliana nami. Endapo mtu atavunja nyumba yako na kukuibia na kuihujumu fami l i a yako , man t ik i hapa inatuonesha kwamba utafanya iwezekanavyo kumtoa huyo mvamiz i nyumbani kwako. Lakini leo hii inaonekana kwamba kama sehemu iliyovamiwa ni ardhi ya Kiislamu na kama huyo mvamizi ni Mmaekani, hivyo kutokana na sababu mbali mbali hali ghafla hubadilika. Kwa akili ya kawaida eti huu huitwa ugaidi na watu ambao hujihami au kujilinda kutokana watu wanao wauwa, eti huuitwa “magaidi’’ ambao wanawauwa Wamarekani. L a k i n i w a z o k w a m b a Wamarekani walivamiwa na Waingereza karne mbili na nusu zilizopita, kama vile ambavyo hivi sasa Waislamu wanavyofanyiwa na askari wa Kimarakani ndani ya mitaa yao, kwa Waingereza ilikuwa ni ukoloni tu na sio ugaidi.

Wakati Sagenti Bales alipowauwa Waafghanistan mwezi uliopita, uzito mkubwa wa vyombo vya habari ulielekezwa kwake kususu usalama wa maisha yake, PTSD yake na ulinzi nyumbani kwake kana kwamba yeye ndiye muathirika. Uzito mdogo ulielekezwa kwa wale aliowauwa, kama vile sio binadamu. Bila shaka hili linapuuzwa na kila mmoja katika jamii, iwe walilitambua hilo au hawakulitambua. Hata wanasheria wangu il iwachukuwa takribani miaka miwili ya mjadala, maelezo ya kuweka wazi suala hili kabla hawajafikia hatma ya kulifikiria zaidi walao wakakubaliana na ukweli wa kile nilichokuwa nikikisema.

M i a k a m i w i l i s a s a ! Ingechukuwa muda mrefu kama huo kwa watu wenye akili ambao kazi yao ni kunilinda, baadae kunileta mbele ya jopo la mahakimu kwa kigezo kwamba wao ni wenzangu leo hii sikujaribu mbele yao kwa sababu ya malalamiko ya Wamarekani. Sina watu ninaoshirikiana nao – kwa kuonesha ukweli

huu, serikali ikaamuwa kunishitaki, si kwa sababu walitaka kufanya hivyo ila kwa kwa sababu tu walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Nilisoma kitu kimoja darasani: Marekani inaweza kuunga mkono sera ambazo si za haki dhidi ya watu wachache – matendo ambayo hata sheria iliyalinda. Hapa kitu cha msingi ni kurudi nyuma na kujiuliza; tulikuwa tunafikiria nini? Utumwa, Jim Crow, mfungwa wa Wajapani kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia, kila mmoja aliungwa mkono na jamii ya Wamarekani, na wote wali l indwa na Mahakama Kuu. Lakini muda kadiri ulivyoenda na Marekani kubadilika, watu na mahakama zake walirudi nyuma kuuliza: tulikuwa tunafikiria nini??

N e l s o n M a n d e l a alionekana kama gaidi na serikali ya Afrika ya Kusini na akahukumiwa kifungo cha maisha jela. Lakini muda ulipita na dunia ikabadilika wakatambua kwamba sera zao zilikuwa ni za ukandamizaji na kwamba Mandela hakuwa gaidi, hivyo, walimwachia huru. Baadae tena Mandela akawa raisi wa Afrika ya Kusini. Hivyo, kila jambo lina sababu – hata suala zima la “ugaidi’’ na “magaidi’’ lina sababu pia. Hii yote inategemeana na muda na mahala na nani atakuwa mwenye nguvu muda huo.

Ndani ya macho yenu mimi ni gaidi, na ni kweli kabisa kama nimesimama hapa nikiwa na suti hii ya rangi ya chungwa. Siku moja Marekani itabadilika na watu wataikumbuka siku hii. Wataangalia ni kwa vipi mamia kwa maelfu ya Waislamu waliuwawa na wengine kutiwa vilema na wanajeshi wa Kimarekani ndani ya nchi za kigeni. Kwa hali hii mimi ni mmoja wapo ninaeenda jela kwa kula njama kuwauwa na kuwatia vilema watu ndani ya nchi hizo kwa sababu nawaunga m k o n o m u j a h i d i n a n a kuwalinda. Watarudi nyuma kuona ni jinsa gani serikali ilivyotumia mamilioni ya dola ili kuniweka ndani nikiwa kama gaidi. Lakini kama tungeweza kumrudisha Abeer al-Janabi duniani leo hii ambaye alibakwa na askari wenu tukamuweka kama shahidi na kumuuliza nani magaidi hasa, kwa kweli asingeninyooshea kidole mimi.

Serikali inasema kwamba n i l i sh ik i l iwa ku tokana na ghasia na mauwaji ya Wamarekani. Lakini nasema, kama Muislamu ninaeishi zama hizi, naweza kufikiri kuwa hakuna uongo, kejeli na kebehi kama hii.

Page 9: ANNUUR 120

9RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012AN-NUUR MAKALA

Uhalisia na tatizo:

AINISHO la Mazingira, au mazingira asilia, ni neno ambalo linakusanya viumbe vyote hai na visivyo hai ambavyo vimetokea kwa asili duniani.

K w a k i p i n d i k i r e f u , tumeshuhudia mashambulizi mfululizo dhidi ya mazingira, wakati madola ya magharibi na makampuni yao, moja kwa moja au kwa mlango wa nyuma, wakiharibu misitu, mito na hali ya hewa katika kiwango ambacho kinahatarisha maisha ya baadhi ya wanyama. Imefikia mahali tumeshuhudia vyama na taasisi za kupigania haki na ustawi wa wanyama, vikikusanya saini za watu, kwa lengo la kupinga uchafuzi na uharibifu wa mazingira, unaohatarisha maisha ya wanyama.

Siku hizi, mamilioni ya tani za mabaki ya taka za viwandani kutoka kwenye viwanda vya nchi za magharibi, zinaletwa kwenye nchi zinazojulikana kama dunia ya tatu; na hiyo imekuwa ni biashara nono sasa. Matokeo yake, maeneo ya ardhi na mito katika nchi hizo, imechafuliwa kwa kuwa sehemu kubwa ya taka hizo ni sumu. Mfano ‘batteries’ na madini ya ‘Lead’, vina athari ya moja kwa moka kwenye mfumo wa ufahamu wa binadamu(human nervous system).

Hii imeleta madhara makubwa kwa wafanyakazi na maelfu ya watu wengine ikiwemo vifo. Lakini mdahalo wa mazingira na tabianchi unaoendelea kwenye vyombo vya habari na miongoni mwa wanasiasa wa Magharibi, umeleta sintofahamu kubwa ambayo imesababisha kupuuzwa kwa kiini hasa cha tatizo la mazingira.

Mwelekeo ambao mdahalo wa tabianchi umechukua, unaondoa mazingatio kutoka kwenye tatizo halisi la kimazingira linaloukabili ulimwengu hivi sasa! Mdahalo huu haupaswi kuishia kwenye mabadiliko ya tabianchi na kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa (carbon emission) . Sambamba na mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa binadamu, mdahalo pia lazima uzingatie ubadhirifu wa mataifa ya magharibi na makampuni yao.

Kupunguza tu uzalishaji wa gesi ukaa, wakati ukiendelea kuchafua ulimwengu kwa namna nyingine, haitaweza kuondoa majanga ya kimazingira kwa nchi za dunia ya tatu, ambazo zinaathirika vibaya kwa uwiano usio sawa!

JUNI 5, kila mwaka ni siku ya mazingira duniani. Maadhimisho ya siku hii kimataifa mwaka huu, yamefanyika jijini Rio de Janeiro, Brazil na kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro. Pamoja na juhudi zote za kimataifa, lakini suala la mazingira duniani imekuwa ni changamoto ya kudumu. Fuatana na Mwandishi SAID RAJAB, ambaye anachambua chanzo cha tatizo la mazingira na ufumbuzi wake.

Tatizo la mazingira, chanzo na ufumbuzi wake!

Mijadala na midahalo ya kisayansi inayoendelea kwenye ulimwengu wa magharibi, kuhusu tabia za watu wa kawaida, zinazochafua mazingira katika dunia ya tatu, wakati mwingine inapotosha uhalisia wa mambo. Sikusudii kujadili ukweli wa kisayansi hapa, lakini ni vyema kuzingatia ukweli kwamba taasisi za kisayansi zinategemea misaada ya kifedha kutoka kwenye makampuni makubwa ya magharibi, ili kuendesha tafiti zao.

H a l i h i i i n a s a b a b i s h a matokeo ya tafiti hizo yatiliwe shaka, hususan pale tafiti h izo z inapogusa maslahi ya makampuni makubwa yanayochafua mazingira kwa kiwango kikubwa. Masuala yanayopaswa kujadiliwa katika mijadala ya mazingira na tabianchi ni kama haya:

Vipi dunia itaweza kuepuka vitisho vyote vya majanga ya kimazingira? Nini kinasababisha majanga ya kimazingira, ambayo dunia inashuhudia leo? Nani anayehusika na hilo? Je? ni lazima maendeleo ya kiuchumi duniani, yafanyike kwa gharama ya mazingira?

Majawabu ya mataifa ya magharibi kwa maswali haya, yamelenga zaidi kuhakikisha kwamba uchafuzi wa mazingira na tabianchi, haviwi kikwazo kwa faida kubwa wanazopata, kutoka kwenye makampuni yao, ambayo kiukweli ndiyo hasa yanayoleta majanga ya kimazingira duniani.

Kwa kuzingatia falsafa yao ya ‘free market forces’,ufumbuzi wao kwa majanga ya kimazingira, unayafanya mazingira yenyewe, yawe majeruhi wa uchu wa wale wanaosababisha majanga hayo duniani! Majanga ya kimazingira duniani, ni dalili nyingine ya kufeli kwa mfumo wa kibeberu, ambao umekuwa ukisababisha migogoro ya kila aina duniani!

Migogoro ya chakula na uchumi duniani, iliyoshuhudiwa siku chache zilizopita, siyo ya mwisho katika mfumo wa kibeberu. Bado mingine inakuja! Migogoro hii imeacha mamilioni ya watu duniani wakiwa taabani, waka t i wachache kab i sa wakineemeka; kwa gharama ya walio wengi.

Sababu zinazofanya mfumo wa kibeberu ushindwe kabisa kutoa masuluhisho sahihi kwa matatizo ya binadamu duniani ni kutokana na Itikadi yake. Itikadi hii, ambayo imejengwa juu ya fikra ya ‘compromise’, imezifanya fikra dhaifu za

WATOTO wengi nchini Somalia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula.

binadamu kuwa msingi wa kutunga sheria.

Wazo la kutenganisha dini kutoka kwenye uendeshaji wa maisha ya kila siku (siasa), umemfanya binadamu awe chini ya udhibiti wa wabunge wa kibeberu, ambao wanaamini kwamba lengo la maisha ni kutumbua maraha; na kupata faida ndiyo kigezo cha kufanya mambo, bila ya kuzingatia masuala mengine.

Mapungufu mengine ya mfumo wa kibeberu, katika kutoa masuluhisho sahihi, ni mtazamo wake kwamba matatizo ya kiuchumi ni upungufu wa rasilimali, ukilinganisha na matumizi yanayoongezeka (theory of scarcity). Hali hii imefanya mazingatio ya uchumi wa kibeberu yaishie kwenye uzalishaji, tena kwa gharama ya mgawanyo mzuri na kukidhi mahitaji ya msingi ya binadamu.

Kwa mfano Marekani, ambayo ndiyo ngome ya mfumo wa kibeberu, mwaka 2003 uzalishaji uliongezeka, wakati kiwango vya umasikini pia kiliongezeka na kufikia watu millioni 1.3. Isitoshe hakuna nafasi ya uadilifu katika shughuli za uchumi wa kibeberu, kwa sababu ni aina ya uchumi unaolenga zaidi kupata ‘material values’. Unachukulia kuongezeka utajiri kwa mtu binafsi ni mafanikio, bila ya kuzingatia matokeo yake kwa jamii na mazingira.

Muasis i wa mfumo wa uchumi wa Kibepari, Adam Smith alizungumzia hali hii wakati alipotamka kwamba “uchu ni maadili ya mtu binafsi, na maadili haya yanadhibiti uchumi.” Falsafa kama hizi zina madhara makubwa kwa binadamu na mazingira, na tumeshuhudia uharibifu na uchafuzi wa mito, misitu, hali ya hewa, na mashamba, kama matokeo ya shughuli za makampuni ya Magharibi

duniani kote.Iwe Indonesia au Amerika ya

Kusini, shughuli za makampuni haya ya Magharibi zinafyeka kwa kiasi kikubwa misitu ya dunia. Misitu hii, ambayo inachangia moja kwa moja kupunguza gesi ukaa hewani, inatishiwa ku toweka . Mbaya za id i , makampuni hayo hayo, ndiyo vinara wa kutoa hotuba nzuri zinazovutia, kuhusu kulinda na kuhifadhi mazingira!

Watu barani Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na hata Ulaya, wameshuhudia uchafuzi wa ardhi waliyokuwa wakiishi. Hii imefikia hatua hata baadhi ya watoto wao kuzaliwa na ulemavu na watu wengine kupata magonjwa ya ajabu, kutokana na taka za sumu, ambazo hutupwa baharini, mitoni na mabwawani.

Wakati hotuba nzuri kuhusu kupunguza ‘carbon emission’, ili kunusuru tabianchi zikitolewa kwenye majukwaa, taka za sumu zinaendelea kupelekwa katika nchi za dunia ya tatu, ambako zinamaliza watu, zinachafua ardhi inayofaa kwa kilimo, ikiwa ni pamoja na kuharibu maisha ya viumbe hai wa majini.

Kuna gharama kubwa sana katika kulinda mazingira, iwapo kupata faida kubwa na kupunguza gharama, ndiyo lengo kuu la shughuli za kampuni husika.Kwa mujibu wa mantiki ya kibeberu,kipaumbele cha kupata faida kubwa, kinazidi hoja ya kulinda mazingira na heshima ya binadamu.

Kwa kuwa utekelezaji wa mfumo wa kibeberu, ndiyo sababu kuu ya binadamu na mazingira kuangamia, watu wenye kutafakari wangejiuliza, mabeberu wana n ia gani kujifanya wanaguswa sana na uhai wa binadamu kwa siku zijazo, kwa kulinda na kuhifadhi mazingira?

Mtazamo wa kiislamu kuhusu maisha umejengwa juu ya msingi

thabiti wa imani kwamba, binadamu, uhai, maisha na ulimwengu, vyote vimeumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Uislamu ni ujumbe ulioletwa na Mwenyezi Mungu kwa binadamu, ili umtoe binadamu huyu gizani na kumuingiza kwenye nuru.

Na binadamu atakapokubali kwa dhati Itikadi hii, ataifanya kuwa msingi wa fikra na mawazo yake, ikiwa ni pamoja na kuifanya kigezo kwa vitendo vyake vyote. Muislamu anaamini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameshusha ujumbe wa mwisho kwa binadamu, ambao unadhihirisha, mema na maovu, ukweli na uongo.

Katika masuala yote ya maisha na kuhusu ufumbuzi wa matatizo yote, Muislamu anarejea kwenye Itikadi ya Kiislamu (Aqeedah), ambayo kutokana na hiyo, mfumo kamili wa maisha unatoka.

Mfumo huu unaratibu vyema mahitaji yote ya binadamu, kwa wakati wote, mahali popote na wala hauathiriwi na mazingira wala maslahi binafsi ya watu. Mfumo wa kiislamu unatatua matatizo ya binadamu kwa kuzingatia mahitaji yote, ya kiroho, ya kibinadamu, ya kimaadili na ya vitu. Itikadi ya Kiislamu inaratibu maslahi haya katika namna madhubuti ambayo inatambua maslahi yote.

Kwa hiyo maslahi binafsi au ya kupata vitu (material benefits) hayapewi kipaumbele kwa gharama ya maslahi mengine. Maslahi yote ya kijamii yanaangaliwa kwa uzito wake na maamuzi sahihi yanafanywa kwa msingi wa uratibu sahihi wa maslahi yote. Kupata maslahi ya vitu kwa gharama ya maisha ya binadamu au mazingira, hakiwezi kuwa kigezo sahihi kwa jamii iliyo sawa. Na mizania ya maslahi yote hayo haiwezi kukaa vizuri iwapo binadamu ataachiwa kutunga sheria.

Itaendelea toleo la Ijumaa

Page 10: ANNUUR 120

10 RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012 AN-NUUR MAKALA

ALIPOFARIKI dunia Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 14 mwaka 1999, gazeti la Guardian la Uingereza liliniomba niandike makala maalumu ya kuyatathmini maisha yake. Nilipokuwa naanza kuiandika tathmini hiyo iliyochapishwa siku ya pili yake, niliyakumbuka a l i y o w a h i k u y a s e m a M w e n y e k i t i M a o w a C h i n a k u m h u s u J o s e f Stalin, mtawala wa pili wa Muungano wa Sovieti baada ya Vladimir Lenin.

Nami nikayatumia maneno hayo hayo kuanzia makala yangu kwa kuandika: Julius Nyerere was “a great leader who made great mistakes,” as one ruler once famously said of another. (“Julius Nyerere alikuwa “kiongozi mkubwa (adhimu) aliyefanya makosa makubwa,” chambilecho mtawala mmoja aliyewahi kumuelezea hivyo mtawala mwenzake.)

Nyerere alifanya makosa ya kinadharia, ya kifikra na ya kiutendaji katika utekelezaji wa sera zake. Sikulidhukuru jina la Stalin kwa sababu sikutaka wasomaji wangu wafanye kosa la kudhania namfananisha Nyerere na Stalin. Siamini kama Nyerere alikuwa na uovu wa Stalin. Na kama ilivyokuwa kwa Stalin si yote ya Nyerere yaliyokuwa maovu. Alitenda mema yanayostahiki sifa.

Watu wa kale wasema: “Kheri ya mja ni ulimi wake na shari ya mja ni huo huo.” Kwa ulimi wake Nyerere aliwahi kutamka maneno ya maana na mengine ya kibahaluli. Baadhi ya maneno yake yalikuwa kama lulu na baadhi yalikuwa kama utumbo kama pale, kwa mfano, aliposema kuwa hakuna watu waitwao Waswahili. Nilimsikia akiyasema hayo alipotoa hotuba katika ukumbi wa London School of Economics alipokuwa ziarani London kabla ya kuuacha urais.

Yote hayo yaonyesha kwamba Nyerere alikuwa mja, mtu kama watu wengine. Hakuwa Mungu, hakuwa malaika. Wala hakuwa mtume na hata hakuwa mpigaji ramli. Na si kila alichokitamka kilikuwa sahihi. Lakini binadamu yule alikuwa na ulimi uliowalaza wengi na kuwafanya waache kufikiri kwani alikuwa na kipaji cha kuwafanya waamini kwamba kila ali lolisema lilikuwa la kweli kabisa na hivyo hapakuwa na haja ya kumfanya mtu mwengine alifikirie. Ilikuwa nadra kumpata mtu aliyethubutu kumpinga au kumkosoa, hasa kadamnasi. Walikuwapo waliochelea kukiona cha mtema kuni na wengine waliridhia

Nyerere na fitna ya Upemba na UungujaNa Ahmed Rajab

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

kuwa vibarakalla vya kuitika tu ‘hewala bwana.’

Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima.

Miongoni mwa aliyowahi k u y a s e m a N y e r e r e n i kuwa ati iwapo Zanzibar itaachana na Tanganyika, basi Tanganyika kutakuwa shuwari lakini Wazanzibari wataanza kubaguana baina ya Wapemba na Waunguja na halafu wataendelea kutafutana asili zao.

Tangu w ik i i l i yop i t a waandishi kadhaa wa Bara wamekuwa wakiyanukuu haya kana kwamba ni maneno yenye ukweli usiopingika. Hii ni fitna tu; na inatumiwa kuwatisha na kuwagawa Wazanzibari.

Wakoloni walipowaona wanaowatawala wanaungana kuwapinga, basi walitumia m b i n u y a k u w a g a w a wazidhoofishe nguvu zao ili waendelee kuwatawala.

Mbinu kama hiyo inatumiwa siku hizi na baadhi ya viongozi wa CCM wa Bara pamoja na baadhi ya waandishi wa huko huko Bara ‘walioshtushwa’ na mwamko wa k is iasa uliowafanya Wazanzibari wawe na ujasiri wa kuujadili kwa mapana na marefu Muungano wa Tanzania.

Ujasiri huo umewafanya wengi wao waseme kwamba ama wanaupinga muundo

wa sasa wa Muungano au hawautaki kabisa na wanataka Zanzibar iwe dola huru yenye mamlaka yake kamili.

Huo si mwamko wa leo au wa jana; tumekuwa tukiugusia miaka nenda miaka rudi lakini tukionekana kuwa ni wazushi na wazandiki. Sasa mambo yanajidhihiri yenyewe. Matokeo yake ni kwamba waliokuwa wakijidanganya sasa wamegutuka na hawajui jinsi ya kulizuia hilo wimbi la uzalendo Wakizanzibari minghairi ya kutumia hoja finyu za kikabila na udini.

Mmoja amefika hadi ya kuandika kuhusu ‘Waarabu’ na ‘watu Weusi’ kana kwamba hao wanaonasibishwa na Uarabu ni wa rangi aina ya pekee iliyo tofauti kabisa na ya Wazanzibari wasio na asili ya Kiarabu. Mwandishi huyo huyo alitishwa na sura rahimu ya Sheikh Farid Hadi Ahmed, mmoja wa viongozi wakuu wa Uamsho.

Aliandika kwamba baada ya kuiona picha ya Sheikh Farid yalimjia mawazo kwamba Uamsho si jumuiya ya kidini na wala si ya Wazanzibari na kwamba Sheikh Farid ametumwa (hakusema na nani) kuwafitinisha Wazanzibari. Alichotaka kusema mwandishi huyo ni kwamba kwa vile Sheikh Farid ana asili ya Kiarabu basi Uamsho inataka kuurejesha usultani.

Ni uchambuzi uchwara, tena wenye kutumia lugha ya kibri. Unashtua kwa vile ni ‘uchambuzi’ wa hatari

unaofanana na simulizi za Wahutu wa Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Hizi fitna za ‘Upemba’ na ‘Uunguja’, za ‘ubwana’ na ‘utwana’ na za ‘ugaidi’ wa Uamsho ni fitna zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya uongozi au ya uandishi.

Hila wanazotumia ni kwanza, kuwafitinisha Wazanzibari kwa kutia fitna za kikabila na za kidini. Kwa mfano, wanawatisha wahafidhina wa CCM/Zanzibar, wale wenye kusherehekea kaulimbiu ya ‘Mapinduzi Daima’, kwa kuwaonya ya kuwa Uamsho ina “msukumo wa Kiarabu” na kwamba kusudio lake ni hatimaye kuyapinga Mapinduzi na kuirejesha Zanzibar katika ‘utumwa’. Maneno ya kijinga kabisa.

H i l a y a o y a p i l i n i kuwagonganisha vichwa Waungu ja na Wapemba kwa kutumia hoja zisizo na mshiko wowote wa kimantiki. Wanasema wamewapata Wapemba wengi wenye kutaka Muungano uendelee kama ulivyo. Wamewahoji na matamshi yao kusambazwa na magazeti fulani nchini. Huu ni mfano mzuri wa propaganda ya kitoto.

Hila yao ya tatu ni kutumia lugha kuparaganya mambo. Ingawa Uamsho ni jumuiya kamili, wao, badala yake, wanasema kuwa hiki ni kikundi. Sio kundi bali ‘kikundi.’ Na wanaishtumu jumuiya hiyo kuwa ‘inawatumia’ baadhi ya vijana kufanya vitendo vya kihuni vya kuchoma moto makanisa. Hakuna ushahidi wa hili.

Nne, wanajaribu kuwatisha Watanzania na hasa wakuu wa dunia hii kwa kuifananisha Jumuiya ya Uamsho na mitandao ya kigaidi ya Al-Qa’eda, Boko Haram na Al-Shabab. Bila ya shaka wenye kueneza fitna hii hawajui walisemalo na wanajikashifu, si mbele ya Watanzania wenzao tu: bali hata machoni mwa balozi za nchi za Magharibi.

Sijui kama wanaelewa ya kuwa maofisa wa baadhi ya balozi za Maghar ib i wameshakutana na viongozi wa Uamsho katika juhudi zao za kuitathmini Jumuiya hiyo na wanayaelewa makusudio halisi ya Uamsho.

Kwa hakika, kinyume na wanavyoandika baadhi ya waandishi wa Bara, Jumuiya ya Uamsho haikuzuka juzi. Imekuwako kwa muda wa takriban miaka 10 sasa. Jumuiya hii ni kama mwavuli

ambao chini yake kuna jumuiya mbalimbali za Kiislamu, pamoja na ile ya Maimamu.

U a m s h o i m e k u w a ikiendesha harakati zake kwa msaada wa taasisi za nchi za Magharibi. Ilikuwa miongoni mwa waangalizi rasmi wa Uchaguzi Mkuu uliopita na ripoti yake kuhusu uchaguzi huo ni ya kupigiwa mfano kwa maelezo yake ya kina.

Kat i ya wafadhi l i wa Jumuiya hiyo katika harakati hizo za kuangalia uchaguzi lilikuwa shirika la USAID la Marekani. Hata vizibao wanavovaa baadhi ya viongozi wa Uamsho na vikuza sauti vyao walipewa na Wamarekani wakati huo wa uchaguzi uliopita.

Wenye kujuwa mambo watakwambia kwamba kuna tofauti kubwa kama ya mbingu na ardhi kati ya jumuiya ya Uamsho na mtandao wa Al-Qa’eda au kundi la al-Shabab. Huwezi kabisa kuzifananisha falsafa zao au makusidio yao. Hata Boko Haram nayo licha ya mbinu inazozitumia inatofautiana sana na al-Qa’eda.

Huko Zanzibar mafatani h a w a w a n a w a s h i r i k a wanaojulikana. Nao ni wale wanaochomwa na kuwapo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Ndiyo maana wakaruka harakaharaka kuwatupia lawama za machafuko ya hivi karibuni viongozi wa C U F w a l i o m o k w e n y e SUK na kutaka watimuliwe kutoka serikalini. Na ni wao waliohusika na vipeperushi vilivyotolewa wiki iliyopita kuwafitinisha Wapemba na Waunguja.

Na n i haohao wenye kujaribu kuwachimba waasisi wakuu wa Maridhiano yaani Rais mstaafu Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.

Inasikitisha kuwaona baadhi ya Wabara wenye kujigamba kuwa ni wasomi wakitaka mijadala ya kisiasa ipigwe marufuku katika majukwaa ya kidini. Hawaelewi kwamba ni dhima ya dini za Ukristo na Uislamu kuzungumzia na kuyatafutia ufumbuzi mambo yanayoyagusa maisha ya kila siku ya waumini wa dini hizo. Na mambo hayo yawe yepi kama si ya kisiasa?

La kutisha ni kuwa ‘wasomi’ hao wanamtaka Rais Jakaya Kikwete awachukulie hatua za kimabavu wakuu wenzake walio serikalini kwa kisingizio kuwa ati wanaunga mkono harakati za Uamsho.

Ulimwengu haukufunga macho wala haukuziba masikio. Unawaona na kuwasikia. La ajabu ni kwamba wanasiasa na

Inaendelea Uk. 11

Page 11: ANNUUR 120

11RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19 - 21, 2012AN-NUUR SHAIRI/MASHAIRI/MAKALA

[1]Amani na iwe kwenu,Enyi ndugu isilamu,Hii ni bora kaumu,Mungu kasisitizia.

[2] Twamshukuru manani,Juu aliye mbinguni,Kwa kutupa ihsani,Leo hii kufikia.

[3] Pwani nimezoeleka,Nipeni kijimkeka,Chini niweze jiweka,Utenzi kuwaletea.

[4] Leo nawaomba eti,Mkae juu ya viti,Ili msikie hati,Hii hapa ya wosia.

[5] Hati hii si haba,Minawapa kama huba,Wekeni kama akiba,Hakika itawafaa.

[6] Alipobanwa Mtume,Ili na yeye asome,Ni lazima tujitume,Njia yake kufatia.

[7] Popote mtapolala,Mkaidumishe sala,Ni nguzo iliyo bora,Mungu ameihusia.

[9] Mking’ang’ania shuka,Shetani atawashika,Fajiri mtairuka,Masijidi kukimbia.

[lO] Adhuhuri muishike,Alasiri msichoke,Magharibi mkumbuke,Insha ikija ingia.

Enyi ndugu Islam[ll] Iacheni isirafu,Tena msiwe wachafu,Na muwe ni watiifu,Nyumbani mnapokaa.

[12] Naanza kwenu mabinti,Kwa makini namketi,Muisikilize hati,Kitu gani yawambia.

[13] Pindi mpatapo nyumbaHakikisha waipamba,Vizuri kwa kuiremba,Wasije wakabomoa.

[14] Muonao wanacheka,Moyoni wanakeleka,Leo kesho wanataka,Kuona mnalegea.

[15] Na mkigombana ndani,Na mumeo wa ubani,Usitoe hadharani,Aibu mtajitia.

[16] Kupatana ni thawabu,Mume usimpe tabu,Tena usimwite babu,Mtume amehusia.

[17] Hijabu msizitupe,Kwenye giza na kweupe,Msije mjiziuke,Heshima tajishushia.

[18] Sasa kwenu kina kaka,Tuheni nageuka,Msikize kwa hakika,Nini hati yawambia.

[19] Msiitumie pombe,Kuweni bora viumbe,Msifiwe kila pembe,Uwe baba ulo bora.

[20] Matusi na yaacheni,Yanawashusha thamani,Mtakuwa vichwa gani,Kilichokosa sitara.

[21] Na wote mushikamane,Mume mke mjitume,Kwa pamoja na mlime,Chakula kujipatia.

[22] Mke atalokwambia,Vizuri kulisikia,Na kazi kulifanyia,Utaona manufaa.

[23] Mke usimwite mama,Usije pata shutuma,Ikaja kuwa laana,Mungu kisha iamua.

[24] Msirukwe na mioyo,Ndiyo mkasema siyo,Siyo mkasema ndiyoHati hilo yakataa.

[25] Hakika dhambi ni tamu,Kwenye yoyote sehemu,Hivyo inatulazimu,Hilo kuliepukia.

[26] Ukijifanya mbishi,Kwa mikiki utaishi,Tena kwa muda mfupi,Hati yakupasulia.

[27] Enyi mlo lukuki,Tena ndugu marafiki,Wabillah tawfiq,Kwa herini nawambia.

Mwalimu Swalehe Ndimbe Mkuu Shule ya SekondariMkuu Rombo - Kilimanjaro-

Nyerere na fitna ya Upemba na UungujaInatoka Uk. 10

waandishi wenye kuchochea hisia kama hizo wamesahau ni nyakati gani tulizo nazo na ni ulimwengu gani tulio nao. Katika ulimwengu wao wa leo Wazanzibari wanasema hawakubali tena kugawanywa kwa propaganda za kikabila au za kidini.

Inatisha kwamba kuna wanasiasa na waandishi waliosahau kwamba siku hizi kuna Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) na mahakama nyingine mahsusi za kimataifa, mithili ya ile Mahakama Maalumu ya Sierra Leone. Mahakama kama ile ya Sierra Leone inaweza kuundwa mara moja na Umoja wa Mataifa kuwatia adabu wenye kupalilia fitna zinazoweza kuzusha mauaji ya kimbari.

Ni hiyo Mahakama Maalumu ya Sierra Leone iliyomhukumu Charles Taylor, rais wa zamani wa Liberia, kifungo cha miaka

80 baada ya kupatikana na hatia ya kuishushia nakama Sierra Leone.

Dhana waliyonayo baadhi ya wasomi na waandishi wa Bara ni kwamba viongozi wa Uamsho ni mijitu isiyosoma. Kuna mmoja aliyepandwa na jeuri na kuandika kwamba mbali na kujua kusoma Qur’an viongozi hao ni watu wasiojuwa kuandika wala kusoma.

Ukweli ni kwamba viongozi wa Uamsho n i wasomi waliohitimu masomo ya chuo kikuu na wana shahada za juu za uzamili katika fani mbalimbali kama vile za uhandisi, sayansi na jiografia. Ni wasomi wa nyanja zote — za dini na dunia.

Mfano mzuri ni Sheikh Msellem ambaye mbali na kuwa gwiji wa tafsiri ya Qur’an pia alisomea taaluma ya hali ya hewa.

Baadhi yao walisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako walivutiwa na hotuba za kidini za Professor Malik,

mtaalamu wa fani ya hesabati, ambazo ziliwashajiisha na kuwafanya wawe na mwamko wa Kiis lamu. Wengine walisoma kwenye vyuo vikuu vya nje vikiwemo vile vya Sudan, Saudi Arabia na Qatar.

N i w a z i k u t o k a n a na r ipot i na taar ifa zao kwamba baadhi ya wasomi na waandishi wetu wa Bara wanawadharau Wazanzibari. Nadhani hizo dharau zao ndizo zinazowafumba macho wasiweze kuona nani hasa aliyechochea fukuto hili la upinzani dhidi ya makandamizo ya walioshika hatamu za utawala wa Muungano.

Maandishi yao yamebainisha wazi kwamba hawaamini ya kuwa Unguja na Pemba si majimbo wala koloni za Bara. Inakirihisha kuona namna wengi wao wanavyozitapika hadharani chuki zao (na udini uliowapamba) bila ya hata staha na uvumilivu wa kimaadili. (Makala hii imechapishwa kwa hisani ya Ahmed Rajab)

Salamu ninaitoa, itokayo kwa Manani Msomaji itikia, pia uipe thamaniKama utapuuzia, utakuwa hatianiTofauti tuziache, hebu tusome nyakati.

Waislamu nchini, haki zetu twabaniwaKwa nini hatuungani, ili kuzipiganiaWengi watoka kundini, tena kwa hoja za bandiaTofauti tuiziache, sasa tujenge ya mbele

Dhulma ikifanyika, hailengi kundi mojaKwa nini unaponyoka, hutaki kuwa pamojaHaki haiwezi fika, kwa nguvu za mmojaTofauti tuziache, tufate Aqida moja.

Sisi ni Watanzania, twaishi bila thamaniKama tutajiengua, tutapataje amaniJaribu kufikiria,jambo hili akiliniTofauti tuziache, tuondoe uhaini

Baraza la Mitihani, limedhuru huu ummaTukaingia barabarani, kupinga hii dhulmaCha ajabu na huzuni, wengi wa karudi nyumaTofauti tuziache, sasa tujenge yajayo

Siku zote penye haki, dhulma huenda kandoWatake ima hawataki, tutavumisha mdundoHatutaweza kubaki, hata watupe kipondo.Malumbano tuyaache, hebu tuilete haki

Muda sasa mewadia, kuacha mitafarukuWote tuiweke nia, Dhulma ni marufuku Haki tutapigania, mchana ima usikuTofauti tuziache, sasa tujenge yajayo

Mchakato wa Katiba, shime tusibaki nyumaDada, kaka, mama, baba, sote twingie wazimaTukaondoe misalaba, inayoturudisha nyumaMuda sasa mewadia, tuvunje wetu ukimya.

Sensa ya watu makazi, na yenyewe yatujiaHapa tuwe watambuzi, si, tu, kuikimbiliaKama haitakuwa wazi, takwimu hatutatoaTofauti tuziache, sasa tuimarishe nguvu

Jihad ni njia yetu, kwa nini tuna kimbiaUma uite haki yetu, kwa dini hii kuifiaUoga katu si kitu, kwa dini hii kupiganiaTofauti tuziache, haki tuitawalishe

Tuunganishe mikono, umoja wetu kujengaTuyang’ate yetu meno, na kanga vizuri kufungaUislamu wa maneno, sasa mwisho kuujengaTofauti tuziache, sasa tuipiganie haki

Wale wenye mitazamo, tofauti ya kidiniHebu ifike kikomo, sasa tuihami diniUkishindwa funga domo, sikusaliti wauminiMuda sasa mewadia, unafiki kuuacha

Taasisi za kidini, marumbano ya nini?Hebu tukae chini, tufikiri kwa makiniMtatamka kitu gani, kesho mbele ya Manani?Tofauti tuziache, sasa tujenge Umoja.

Dini yetu ya haki, usawa na uadilifuKatu haitaki chuki, wala mambo ya uchafu Dhulma haiitaki, kwa viumbe wa RaufuTofauti tuziache, sasa tujenge umoja.

Kumi na tano beti, nimefika kileleniMuungwana haliteti, jambo baya maishaniKama hatajenga chuki, huyo mashakaniWepesi wa maamuzi, ni kina cha kufikiri.

Mwl. Mohammed MakimuUbungo Islamic Teachers College (UITC),DAR ES SALAAM [email protected] - 0715 465158

TOFAUTI TUZIACHE, SASA TUJENGE YA MBELE

Page 12: ANNUUR 120

RAJAB 1433, JUMANNE JUNI 19-21, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagaration Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR Soma AN-NUUR

kila Ijumaana Jumanne

Suala la Dini katika sensa bado laitesa serikaliInatoka Uk. 1Dodoma, na kuwakutanisha viongozi wa dini hivi karibuni, lakini inavyoonyesha ni kama Waziri huyo alizidi kuvurunda.

“Mkuu wa nchi hii yupo (Rais Jakaya Kikwete) kupitia nyinyi hebu lifikisheni, tena msimame kidete wakae na hawa watu (Waislamu) chondechonde suala hili lifanyiwe kazi.” Alisema Mhariri kutoka gazeti la Msemakweli.

Akifafanua alisema kwamba, wakati akitoka kwake siku ya Ijumaa (iliyopita) akianza safari kuelekea katika semina hiyo Mjini Morogoro, alishuhudia Misikiti kadhaa alimokuwa akip i ta mada i l ikuwa ni hiyo kuwa endapo serikali haitorejesha kipengele cha dini hawatohesabiwa.

Wanahabari hao walihoji sababu za kuondolewa kwa kipengele cha dini, na kikwazo ni kipi katika kukirejesha, ambapo leo kinaleta mvutano husasani ukizingatia sasa kunaibuka takwimu nyingi za idadi ya wananchi na dini zao ambazo zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na kukosekana kujua ukweli halisi ni upi.

Walihoji, ikiwa Serikali imepanga bajeti ya kuwanunulia nyama wananchi wa jamii ya Wahazabe, walioweka sharti la kupewa nyama ya Pundamilia, ili waweze kuhesabiwa, vipi ipuuze suala muhimu la Serikali kujua idadi ya wananchi wake kwa upande wa dini zao.

“Kuna watu wal i sema hawatohesabiwa ikiwa vitu hivi (nyama) havitapatikana, kwa mujibu wa maelezo yenu hili limefanyiwa kazi kuwa watapelekewa nyama. Vipi hawa wengine (Waislamu). Hawa watu wana ushawishi mkubwa kwa watu wao katika vikundi vya dini, kwa nini lisifanyiwe kazi mapema. Walishatoa mapendekezo yao wakipuuzwa hamdhani kuwa itavuruga utaratibu mzima wa zoezi la sense”? Alisema na kuhoji mmoja wa wanahabari hao.

Wahariri hao waliendelea kuwabana Maafisa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wakisema wao ndio wahusika wa kila takwimu humu nchini, kwamba wananchi wanatarajia kujua kupitia ofisi hizo kuwa Taifa l ina walemavu wangapi , wazee wangapi, wanaume na wanawake wangapi, wakahoji vipi hawataki kujua au kuwa na takwimu za dini.

Walihoji uhalali wa takwimu za idadi ya dini kuwa zinatoka wapi na kwamba kitengo cha Serikali cha Takwimu,

kutokuwa na kipengele hicho ndio leo kumekuwa na taasisi nyingi zinazojitolea takwimu hizo.

Wa l i s e m a , w a o k a m a wanahabari wanaelewa hali hali ilivyo mitaani na joto lake kwa wanaodai suala hilo kurejeshwa na ndio sababu kila mmoja amekuwa akihoji na kuwasihi kulitafutia ufumbuzi wa haraka utakao leta tija kwa ujumla.

Akijibu hoja na maswali ya wahariri hao kwa ujumla, msimamizi wa semina hiyo, kitengo cha uhamasishaji, i l iyolenga kutoa mafuzo kwa vyombo vya habar i namna ambavyo zoezi hilo litakavyoendeshwa, Bw. Said Amir, alisema wao hawana majibu juu ya suala hilo, na kuwataka kutochukua muda mrefu kujadili suala hilo.

Kuhusua takwimu zilizopo kuhusu idadi ya Dini, Bw. Ameir, alikiri kuibuka kwa asasi za Serikali na zile za watu binafsi na kusema kuwa hizo takwimu sio sahihi na kila mmoja anatoa kwa malengo yake.

“Ni kweli z ipo taasis i zinazotoa hizo takwimu na zingine ni za Serikali na zinatofautiana lakini hazina ukweli kwa kuwa sio sahihi, na kila mmoja anatoa kwa malengo yake.” Alisema Bw. Ameir.

Alisema, haelewi ni kwa nini kipengele hicho kiliondolewa huku akiwataka wanahabari hao kufika katika Ofisi za Taifa za Takwimu, Jijini Dar es Salaam, kupekua kumbukumbu huenda wakaona sababu za kukiondoa kipengele hicho.

“Nisingependa kuzungumzia hilo kwa mapana, ama kwa nini liliondolewa njoo pale Takwimu upekue unaweza kupata sababu za msingi za kuondolewa. Hilo lipo nje ya uwezo wetu na tumeliacha kwa mamlaka husika sisi kwetu ni gumu, inawezekana wanaodai hilo ni wengi kweli.” Alisema.

Akifafanua kuhusu suala la Wahazabe, alisema tayari wameshughulikia suala hilo katika sehemu husika, na kwamba mikoa yao itatoa bajeti na watapelekewa nyama ili waweze kushiriki katika zoezi hilo.

Awali akifungua semina hiyo, i l iyofanyika katika ukumbi wa Edema, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Joel Bendera, alisema vyonbo vya habari ni viungo muhimu katika kufanikisha zoezi hili kwa kuwaeleza wananchi lengo la Sensa, kuwa ni kupanga maendeleo yao na si vinginevyo.

Alisema bila kuwa na idadi ya wananchi huwezi kupanga maendeleo yao kwa ufanisi, kwani watu ndio rasilimali kuu ya nchi, hivyo alidai njia muhimu ni kujua idadi sahihi ya watu katika maeneo ya umri, jinsia, hali ya ajira na uwezo wao kiuchumi kwa ujumla.

“Takwimu za namana hii zitaiwezesha Serikali kutunga

na kutengeneza sera. Sensa ya mwaka huu ni muhimu na ya pekee kwa kuwa itatoa dira ya mwaka 2020, katika mkakati wa kupunguza umasikini nchini.” Alisema Bw. Bendera.

Alisema, mafanikio ya sensa yanategemea namna watu watakavyo elimishwa na kwamba zoezi zima litakuwa

halina maana kama litakuwa halijaeleweka, kwani alidai mafanikio yake itategemea n i n a m n a g a n i w a d a u watakavyolipokea.

Alisema, hili si zoezi la Serikali pekee bali bali ni la mashirika ya umma, binafsi, dini pamoja na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.

BAADHI ya mihadhara inayoendelea Zanzibar kuhoji Muungano.