17
ISSN 0856 - 3861 Na. 1138 SHAWWAL, IJUMAA , AGOSTI 15-21, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz ‘Hujuma’ Mtambani? Kama siafu, Waislam wanusuru msikiti Viongozi kuzungumza leo na Waislam Mansour , kafara ya kupata mamlaka kamili Z’bar-Seif Hakuna katiba mpya bila Serikali tatu Wengi Zanzibar wasikilizwe - Riyami Ushauri kutoka Nigeria: Dar wamalizeni Boko haram wenu Vinginevyo mtalia na kusaga meno… WALIFIKA ‘Salafi’ Kigoma kutoka Yemen kutoa Da’wah. Waka waa mbia Waislamu wasipeleke watoto wao shule kwa sababu fizikia, kemia na jiografia, ni elimu za kikari. Mtu mmoja akawauliza, kutoka Yemen mpaka Tanzania, wametumia kipando gani. Wakasema, ndege. Bila shaka unaweza kukisia  j i n s i s wa l i na j aw a b u hili lilivyobadili sura ya mazungumzo. Swali la m singi tunalotakiwa kujiuliza hapa ni hili: Huu ujinga wa kiwango hiki umetoka wapi? Soma Uk. 8 Masahaba waliwahijia wazee wao waliokwisha kuzeeka ilipofaradhishwa Hijja na waliokufa bila kuhijji. Hivi sasa waislamu wengi wanakufa bila kuhijj na kuacha mali zaidi ya malipo ya Hijja. Uislamu hauwatambui wazee hao mpaka wahijiwe! Umeshawaokoa wazazi wako na kuwarudisha katika Uislamu? Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora. Gharama zote ni Dola 4,500. Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 0777468018/0685366141/ 0657606708. (14) WASITIRI WAZAZI WAKO! WAISLAMU wakiwa katika jitihada za kuzima moto Masjid Mtambani Dar juzi.  MAALIM Seif.  MANSOUR Yusuf Himid.

ANNUUR 1138

Embed Size (px)

Citation preview

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1138 SHAWWAL, IJUMAA , AGOSTI 15-21, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

    Hujuma Mtambani?Kama siafu, Waislam wanusuru msikitiViongozi kuzungumza leo na Waislam

    Mansour, kafara ya kupatamamlaka kamili Zbar-Seif

    Hakuna katiba mpya bila Serikali tatuWengi Zanzibar wasikilizwe - Riyami

    Ushauri kutoka Nigeria:Dar wamalizeni Boko haram wenu

    Vinginevyo mtalia na kusaga menoWA L I F I K A S a l a f i Kigoma kutoka Yemen kutoa Dawah.

    W a k a w a a m b i a Waislamu wasipeleke watoto wao shule kwa sababu fizikia, kemia na jiografia, ni elimu za kikafiri.

    Mtu mmoja akawauliza, kutoka Yemen mpaka Tanzania, wametumia

    kipando gani. Wakasema, ndege. Bila

    shaka unaweza kukisia j insi swali na jawabu hili lilivyobadili sura ya mazungumzo.

    S w a l i l a m s i n g i tunalotakiwa kujiuliza hapa ni hili: Huu ujinga wa kiwango hiki umetoka wapi? Soma Uk. 8

    Masahaba waliwahijia wazee wao waliokwisha kuzeeka ilipofaradhishwa Hijja na waliokufa bila kuhijji. Hivi sasa waislamu wengi wanakufa bila kuhijj na kuacha mali zaidi ya malipo ya Hijja. Uislamu hauwatambui wazee hao mpaka wahijiwe! Umeshawaokoa wazazi wako na kuwarudisha katika Uislamu? Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora. Gharama zote ni Dola 4,500. Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 0777468018/0685366141/0657606708.

    (14) WASITIRI WAZAZI WAKO!

    WAISLAMU wakiwa katika jitihada za kuzima moto Masjid Mtambani Dar juzi.

    MAALIM Seif. MANSOUR Yusuf Himid.

  • 2 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Makala

    Inaendelea Uk. 11

    Usiparamie behewa usilojua litokako wala Mambo hupangwa hayajitokezei tuNdio maana kusoma ni amri namba 1

    Na Omar Msangi

    ZIPO baadhi ya hoja hushangaza sana, na kwa hakika inadhihirisha msiba ulio katika jamii ya Waislamu. Sote, iwe ni Tanzania, Kenya, Uganda, Marekani, nchi za Ulaya na Asia, tumefahamu uwepo wa mujahidina wa ISIS, Al-Nusra na a k i n a A b u b a k a r a l -Baghdadi kupitia vyombo vya habari-BBC, CNN, Sky News, Aljazeera, mitandao ya internet na vingine kama hivyo. Katika kutufikia habari hizo, wapo walioamini kuwa hao ni mujahidina na wanachosema kuwa wanapigania kusimama kwa Khilafah ni kweli. Lakini wapo pia walioona kuwa huo ni mchezo wa kuigiza. Ni katika zilezile covert operations na clandestine .

    K wa v i l e m a s u a l a haya yanagusa maisha n a m u s t a k b a l i w a walimwengu wote kwa ujumla, wasomi na watafiti, huwa yanapoibuka mambo kama haya yanayogusa m a s l a h i ya k i d u n i a , hujitahidi kuzama na kutizama ukweli wa jambo lenyewe ukoje kinyume na inavyotangazwa na hata kutizama madhara yake na malengo ya washiriki katika jambo hilo. Ni katika kufanya hivyo, leo tunaambiwa kuwa hawa ISIS, ni mujahidina bandia. Ni mawakala wa mabeberu, na hilo wanalodai kuwa ni kupigania kusimama kwa Khilafah, ni mradi wa mabeberu. Kiroja hapa ni kuwa yule yule Muislamu wa Tanzania aliyewajua ISIS kupitia BBC na CNN, ukimjia na taarifa za kitafiti kuwa hivyo anavyofikiri, sivyo, huja na hoja kuwa taarifa za maprofesa, taasisi fulani, na wasomi wamesema, sio hoja za kutengua Mujahidina, kwa sababu hoja zinazokubalika katika Uislamu kama msingi wa kutoa fatwa ni Quran na Sunnah!!! Sasa hapa unajiuliza, mtu kama huyu unamsaidiaje?

    A l i y e w a h i k u w a M w a n a s h e r i a M k u u wa Marekani , ( former U.S. Attorney General), Ramsey Clark, ameandika

    uchambuzi alioupa jina: 1958-1991, Iraq: A Classic Case of Divide and Conquer.

    K a t i k a m a k a l a n a uchambuzi huo anasema k u wa I r a q i m e k u wa shamba la bibi na uwanja wa harakati chafu na angamizi za Marekani (U.S. covert actions ) toka mwaka 1958 pale wanaharakati wa Iraq wakiongozwa n a A b d e l K a s s e m walipofanya mapinduzi kuondoa utawala wa kifalme uliowekwa na Uingereza mwaka 1921 ambao ulikuwa ukiwaacha mabeberu kuchota mafuta wanavyotaka. Mara baada ya kungoa utawala huo wa kifalme mwaka 1960, serikali mpya ya Iraq ilisaidia kuanzishwa kwa Umoja wa Wauza Mafuta ya Petrol- Organization of Petroleum Exporting Countr i es (OPEC) , i l i kukabiliana na unyonyaji wa nchi za Ulaya kwenye nishati hiyo. Nini kilifuatia?

    The CIA plotted Kassem's assassinat ion and U.S. generals in Turkey devised a mil i tary plan, ca l led "Canonbone," to invade northern Iraq and seize its oil fields (2). In 1963, Kassem and thousands of supporters were massacred in a CIA-backed coup.

    H i v y o n d i v y o a n a v y o s e m a Wi l l i a m Ramsey Clark, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani mwaka 1967 hadi 1969, wakati wa Rais Lyndon B. Johnson., kwamba i l i kurejesha masilahi yake ya kibeberu, M a r e k a n i i l i a s i s i n a kutekeleza mapinduzi yaliyosababisha mauwaji ya malefu ya wananchi wa Iraq.

    Mwaka 1968 chama cha Baathi (Baathist Party) kilishika madaraka na mwaka 1972 kikatangaza kutaifisha makampuni yote ya mafuta yaliyokuwa yakimilikiwa na Marekani na Uingereza na kwamba sasa yatakuwa mali ya Iraqi Petroleum Company chini ya kibwagizo- (slogan) "Arab Oil for the Arabs." Yaani, mafuta ya Waarabu kwa manufaa ya Waarabu.

    Kufuatia hatua hiyo, baada ya kikao cha Rais Nixon, Henry Kissinger (National Security Advisor) na Shah wa Iran, CIA waliwachochea Wakurdi watangaze kujitenga na Iraq na kwamba watapewa k i la a ina ya msaada z i k i w e m o s i l a h a n a mafunzo ya kijeshi. Katika ripoti iliyoitwa Pike Report

    William Ramsey Clark, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani mwaka 1967 hadi 1969.

    GHOROFA ya kwanza ya Msikiti wa Mtambani u l i o p o K i n o n d o n i jijini Dar es Salaam, imeteketea kwa moto Jumatano jioni wiki hii, wakati wa swala ya Magharibi.

    Moto huo umeteketeza sehemu yote ya ghorofa hiyo, ambako ndiko yalipo madarasa ya shule ya sekondari Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary), ofisi za walimu, maktaba ya shule na bweni la wanafunzi.

    Wa m e s h u h u d i wa Waislamu kwa umoja wa o , wa k i j i t o k e z a k w a w i n g i k u t o a mchango wao katika jitihada za kunusuru Msikiti huo. Wengi walifurika Msikitini hapo wakichota maji kutoka katika kulatain na kuyapandisha juu ghorofani katika juhudi za kuzima moto huo.

    Aidha, tunatambua jitihada za watu wa zima moto ambao walifika na magari yao kusaidia kuz ima moto huo , kiasi kwamba ilifika mahal i yaka ish iwa maji hali iliyowalazimu Wais lamu wengine kuchota maji katika kulatain na kujaza katika moja ya magari hayo ili kuendelea kusaidia kuzima moto huo.

    Moto huo umeteketeza vifaa vya wanafunzi, magodoro, of is i za walimu na vifaa vyake, ofisi ya Mkuu wa Shule, maktaba ya vitabu, stationary pamoja na ukumbi wa kufanyia mitihani.

    H a t a h i v y o , t u n a m s h u k u r u M w e n y e z i M u n g u k w a m b a h a k u n a mtu a l iye far ik i au kujeruhiwa kufuatia m o t o h u o . We n g i walikuwa wameelekea k a t i k a s w a l a y a Magharibi na kubakia wanafunzi wa kike ambao walinusurika.

    Hata hivyo, kuna hasara kubwa ya vifaa n a j e n g o a m b a y o i m e p a t i k a n a . K wa

    Mtambani wasaidiwekifupi tunaweza kusema Shule imeathirika sana. Wanafunzi wamekosa madarasa ya kusomea, vifaa vyao vya mafunzo vimeungua, maktaba imeungua, pa kulala pameungua, ofisi za walimu nazo zimeungua.

    Kwa kuzingatia athari hii kubwa kielimu kwa vijana wetu wanaosoma shule ya sekondari ya Kiislamu Mivumoni pamoja na walimu wao, tunachukua nafasi hii kuwaomba Waislamu kusaidia kwa hali na mali kurejesha mandhari ya kuendelea masomo katika shule hiyo.

    Kama walivyojitokeza na kusaidiana bega kwa bega kuuzima moto uliotokea, basi litakuwa jambo jema na la msingi t u k a j i t o k e z a v i v y o hivyo kuwawezesha wanafunzi hao, ambao walikuwa wanajiandaa k wa m i t i h a n i ya o , kurejea katika masomo yao ili kupunguza athari inayoweza kuwapata kitaaluma shuleni hapo kutoka ana janga hili la moto lililowakumba.

    S o t e t u n a kumbukumbu kwamba M i v u m o n i I s l a m i c seminary pamoja na uchanga wao, mwaka wa kwanza wa kidato cha nne waliweza kufaulu kwa alama za juu na kuwa miongoni mwa shule bora kabisa hapa nchini.

    Itakumbukwa kuwa shule hii iliyopo Masjid Mtambani, iliweza kutoa mwanafunzi ka t ika wanafunzi kumi bora waliofaulu vizuri zaidi katika mtihani wa kidato cha nne nchini mwaka jana.

    Kwa pamoja , k i la jambo linawezekana. Tu t o e s a d a k a z e t u k u s a i d i a k u r e j e s h a sehemu ya jengo la Mivumoni/Mtambani na miundo mbinu yake i l iyoteketezwa kwa moto.

  • 3 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Habari

    Hujuma Mtambani?KAMA siafu, Waislamu walipishana kat ika ngazi na ndoo zao za m a j i k u z i m a m o t o Mtambani.

    H a wa k u j a l i k u wa h u k o k a t i k a n g a z i wanakoelekea ndiko kulikokuwa na moto ukiunguruma kwa ukali kutokana na upepo.

    Kutokana na moto huo ulioteketeza sehemu ya ghorofa ya pili ya Msikiti wa Mtambani, uongozi wa Msikiti huo umesema kwa sasa hawajui kama ni ajali ya kawaida au hujuma.

    Kauli hiyo ya awali ya uongozi wa Msikiti, inakuja baada ya kutokea moto juzi Jumatano wakati wa adhana ya swala ya Magharibi, na kuteketeza kwa kiasi kikubwa madarasa ya Shule ya Sekondari (Mivumoni Islamic), Ofisi za Walimu na ukumbi wa mikutano.

    K a t i k a k u n u s u r u Msikiti huo, maelfu ya Waislamu waliofurika M s i k i t i n i h a p o walionekana kuchota ma j i k u t o k a k a t i k a kulateni, na kupanda nayo juu ghorofani wa k i p i s h a n a k a m a siafu, bila kujali huko walikokuwa wakipanda moto ulikuwa ni mkali.

    W a i s l a m u h a o wali lazimika ki j i toa muhanga, baada ya g a r i z a z i m a m o t o (fire) kuishiwa maji na kulazimika wengine kuchota maji katika kulateni na kujaza katika moja ya magari hayo moja wapo likiwa la kampuni ya Altmet (T377AWG) na kuyarusha juu kutumia m i p i r a ya k e , h u k u wengine wakipanda na ndoo hizo moja kwa moja ghorofani.

    Hata hivyo, gari la Fire, lenye namba za usajili STK 6852, lililazimika kuondoka katika eneo la tukio kufuata maji, na kurudi baada ya muda, ambapo pia baadae lilifika gari (Tenka) la kitengo cha moto (Fire) kutoka Badarini (SU 37054), ambalo, lilifika na maji.

    Na Bakari Mwakangwale Akiongea na An nuur, katika tukio hilo Katibu wa Msikiti huo, Sheikh Abdallah Ally, alisema kufuat ia tukio hi lo hawawezi kusema moto huo umesababishwa na shot i ya umeme au ni hujuma, bali ni jambo ambalo linahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kubaini hayo.

    Hatujui kama ni ajali ya kawaida au hujuma, jambo hili tunatakiwa kuanzia sasa kuanza kulichunguza na kubaini ukweli wenyewe upo namna gani.

    Mpaka sasa hatuwezi tukasema ni shoti ya u m e m e m o j a k w a moja au ni hujuma na vinginevyo, lakini ni vitu ambavyo inabidi tuvifanyie uchunguzi wa kina. Alisema Sheikh Abdallah.

    An nuur, ilishuhudia chumba, kama bweni, ambacho wal ikuwa wanatumia wanafunzi k ikiwa kimeteketea chote na magodoro yake, ofisi ya walimu na vifaa vyake, Ofisi ya Mkuu wa Shule , maktaba ya vitabu, pamoja na ukumbi wa kufanyia mitihani.

    Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto Masjid Mtambani.

    Viongozi wa msikiti huo, walitoa shukrani k w a Wa i s l a m u n a kampuni za zima moto zilizotoa msaada wao katika kuzima moto huo.

    Kwa upande wake Sajenti Laurent Upunda, wa kitengo cha uokoaji Kanda ya Ilala, alisema moto ulikuwa mkubwa na ulitumia maji mengi na muda mrefu mpaka kufanikiwa kuuzima.

    Alisema, moto huo umeathiri katika ghorofa ya juu ambapo paa lote limeteketea kwa moto, hata hivyo alibainisha kwamba hukuwa na taarifa au kushuhudia kifo na majeruhi katika uokoaji na uzimaji wa moto huo kwa ujumla.

    Alisema, walipata taarifa za moto huo majira ya saa 12:41, jioni, ambapo walifika

    katika eneo la tukio na kwa kushirikiana na wananchi, waliweza kuudhibiti kwa kiasi kikubwa na kuepusha maafa za id i ka t ika maghorofa mengine ya Msikiti huo na majengo ya jirani.

    A l i s e m a , c h a n z o cha moto huo bado hakijajulikana kwani mpaka hapo watakapo kutana na wahusika wa Msikiti na kufanya mahojiano nao.

    Hivi karibuni msikiti huo umekumbwa na misukosuko ambapo b a a d h i y a w a t u wamekuwa wakidai kuwa huo ni msikiti wao na wakabidhiwe.

    Hata hivyo, watu hao wakiwemo wanaojiita wadhamini na wale wa n a o d a i wa k u d a i kuwa kiwanja ulipo msikiti huo ni ardhi yao iliyotolewa na wazee w a o w a l i o k w i s h a kutangulia mbele ya haki, kila wakiambiwa wa j e wa k a b i d h i w e msikiti huo mbele ya waumini, hawajitokezi.

    Ajali hii ya moto, imekuja huku kukiwa na kesi mahakamani ambapo viongozi wa msikiti wameshitakiwa na wanaodai kuwa wadhamini.

    Mansour, kafara ya kupatamamlaka kamili Zbar-SeifK U K A M A T W A n a kuwekwa rumande Bwana Mansour, aliyewahi kuwa kada wa CCM, imetajwa kuwa hiyo ni kama kafara na ishara nzuri ya kupata Zanzibar huru yenye mamlaka kamili.

    Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, akiongea katika mkutano wa hadhara hivi karibuni.

    Kwa upande mwingine, sarakasi za kisiasa katika safari ya kusaka katiba mpya zinaendelea ndani na nje ya Bunge Maalum la Katiba.

    Wa l i o n j e k u t o k a Zanzibar, sasa wanasema kuwa hakuna katiba mpya itakayopatikana kama matakwa ya Wazanzibari walio wengi hayatasikilizwa na kupatikana maridhiano.

    Hayo yamesemwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi, CUF, na wale wa Kamati ya Maridhiano, wakisema kuwa msimamo wa wengi Zanzibar, ni mfumo wa muungano wa serikali t a t u , n a h i v y o C C M wasi j idanganye kuwa w a n a w e z a k u p u u z a maoni na msimamo wa Wa z a n z i b a r i , h a l a f u mambo yakawa shwari.

    Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa

    Na Mwandishi Wetu alisema kuwa msimamo wa Wazanzibari ni serikali tatu kama ilivyoainishwa katika rasimu ya katiba.

    A k a s i s i t i z a k u w a uandikwaji wa katiba mpya kwa Wazanzibari, ni safari ya kufikia mamlaka kamili.

    Na hivyo, hawatakubali k u o n a w a k i w e k e w a vikwazo njiani kama hili la CCM kutaka msimamo wa serikali mbili uendelee.

    Kwa upande mwingine Jussa akasema kuwa, i l i t ak iwa bunge h i lo k u s i t i s h w a h a d i maridhiano yapatikane na wajumbe kujadili rasimu iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba.

    Hata hivyo, akasema k u w a u m e e n d e l e a kufanyika alioita usanii na maigizo, ukisimamiwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta anayetajwa kuwa na ndoto za kuwania urais mwaka 2015.

    N a y e M j u m b e w a Kamati ya Maridhiano ya Umoja Kitaifa, Eddi Riyami ametaka Bunge hilo lisitishwe, kwani Wazanzibari hawako tayari kuona likiendelea.

    Aliwataka mawaziri, Stephen Wasira (Ofisi y a R a i s - M a h u s i a n o na Uratibu) na William Lukuvi (Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Uratibu na Bunge) kuondokana na dhana kwamba katiba mpya inaweza kupatikana,

    Inaendelea Uk. 4

    MSIKITI wa Mtambani ukiungua moto juzi jioni.

  • 4 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Habari

    WAISLAMU wametakiwa kupiga mbio katika kila jambo, na hasa katika elimu ili kurejesha hadhi na nafasi ya Uislamu katika dunia hii wakiwa ni Makhalifah wa Allah.

    Aidha, wamekumbushwa watizame zile zama za akina Ibn Sinna na wengine ambao walikuwa ndio chimbuko la elimu katika fani mbalimbali zinazounufaisha ulimwengu hivi leo.

    Katika nasaha zake akifungua semina juu ya Epistemolojia ya Kiislamu na ukuzaji mitaala iliyofanyika katika Chuo Kikuu c h a Wa i s l a m u , M o r o g o r o , Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, amehimiza usomaji katika fani mbalimbali na kutizama nyuma, ni wapi Waislamu walifanya makosa na kujikuta wakitupwa nyuma wakati ni wao walikuwa chimbuko la elimu lililoitoa dunia katika giza.

    Katika hali hiyo, suala la epistemolojia akalipa uzito na kwamba Waislamu katika vyuo vikuu vya Kiislamu na katika taasisi mbalimbali za elimu za Waislamu, wanatakiwa kulipa suala la elimu kipaumbele.

    Katika kutilia mkazo suala la elimu, nasaha zikatolewa pia kuwa pamoja na kwenda kwa kasi, lakini Waislamu wakatakiwa kufanya kila kitu katika ubora wa hali ya juu kwani hayo ndiyo maelekezo ya Uislamu.

    Mambo yasifanywe ovyo ovyo na katika viwango vya chini, bali iwe katika viwango vya juu kabisa.

    Kwa hiyo, kuanzia ngazi ya elimu ya msingi, sekondari na vyuo v ikuu, Wais lamu wahakikishe kuwa wanatoa elimu bora itakayotoa wahitimu ambao watasaidia jamii kuondokana na matatizo mbalimbali yaliyopo.

    Aki toa nasaha h izo , Dr . Ahmad Totonji amesema kuwa, Muislamu asikubali jambo lisilo na ubora, wala asifanye jambo, ila ahakikishe kuwa analifanya kwa ubora kabisa.

    Na katika mtizamo huo, Dr. Totonji akasema kuwa kwa wahadhiri katika vyuo vikuu, kama mtu atakaa kwa kipindi kama cha miaka mitatu hajafanya utafiti wala kuchapisha kazi yoyote, basi ajihesabu kuwa yupo mahali asipostahiki kuwepo. Atafute mahali pengine pa kwenda.

    Na hiyo ni kumaanisha kuwa wasomi katika taasisi za elimu za Kiislamu, wanahimizwa kufanya utafiti na kuchapisha kazi ambazo zitasaidia katika kusukuma mbele maendeleo ya Waislamu na ulimwengu kwa ujumla.

    Katika kutilia mkazo jambo hilo, Profesa Omar Hassan Kasule kutoka IIIT, akasema kuwa ili kufikia ubora unaostahiki, ni lazima Waislamu kufanya haraka kuondoa tatizo la mifumo miwili ya elimu ambayo inaonekana kana

    Waislamu watakiwa kupigambio kurejea katika uongozi

    Bilal akumbusha zama za Ibn SinnaDr. Totonji ahimiza ubora kwa kila kituProf. Kasule ataoa somo la epistemolojia

    Na Mwandishi Wetu

    kwamba inagongana (madrasa/shule).

    Amesema, kumekuwa na mtindo wa kugawa elimu katika matapo mawili, elimu ya dunia na elimu ya akhera, jambo ambalo halipo katika epistemolojia ya elimu katika Uislamu.

    Prof. Kassule amesema kuwa kama Waislamu hawatafanya juhudi za haraka kuleta elimu zote

    hizi pamoja kama ilivyokuja katika Iqra, wataendelea kuzalisha wahitimu waliochanganyikiwa wasio na mchango wa maana katika dunia yao wala katika kufanikisha akhera yao.

    Ni kutoka na hilo, akahimiza vyuo vikuu na taasisi za elimu za Kiislamu, kuandika upya vitabu vya kiada na rejea vya taaluma mbalimbali ambavyo vitakuwa

    vimekusanya kwa mfano fizikia au elimu ya biashara na yale mafunzo ya msingi katika Mwongozo wa Kiislamu (Quran na Sunnah) ili kutoa msomi ambaye atakuwa Muislamu bora na wakati huo huo bingwa katika fani yake iwe ni udakitari, uhandisi n.k

    Wakati huo huo, Waislamu wametakiwa kuhakikisha kuwa wanaondokana na hisia na dhana hasi dhidi yao, bali wapiganie kujenga umoja na kushikamana pamoja.

    A k i z u n g u m z i a m a d a h i y o , D r . A h m a d T o t o n j i amehimiza kuvumiliana na kwamba watu watizame yale y a n a y o w a u n g a n i s h a n a wanavyoweza kusaidiana katika kuondoa madhaifu ya kila mmoja wao.

    Almuhimu amesisitiza kuwa watu wasijengeane uadui, bali kila mmoja avumiliwe kutokana na udhaifu wake.

    Semina ya Epistemeolojia ya Kiislamu, ilifunguliwa Jumamosi iliyopita na kufungwa Jumatatu wiki h i i , ik ihudhuriwa na wajumbe takriban 400 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

    Katika washiriki wa ndani ya MUM wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Hajat Mwantumu Malale, walikuwepo pia Waziri wa Elimu Dr. Shukuru Kawambwa ( a l i y e s h i r i k i u f u n g u z i ) , Abdurahman Omar Kinana, ambaye ni Makamo wa MDF, taasisi inayomiliki MUM, Dr. Ramadhani Dau, Katibu Mkuu wa MDF, Masheikh mbalimbali na wakuu wa taasisi za elimu za Kiislamu.

    Walikuwepo pia washiriki kutoka Saudi Arabia, Indonesia na Saudi Arabia.

    Semina nyingine kama hii itafanyika mwakani Kano, Nigeria ikifuatiwa na Msumbiji mwaka 2016.

    Mansour, kafara ya kupata mamlaka kamili Zbar-SeifInatoka Uk. 3

    huku Wazanzibar wakitengwa.Hoja ya Riyami kuwa Zanzibar

    inatengwa anaijenga katika msingi ule ule kuwa msimamo wa Wazanzibari ni kuwa na serikali kamili yenye mamlaka na yenye meno na siyo iliyopo sasa.

    Ni kwa mtizamo huo, kujadili rasimu inayotaka ubakie mfumo wa sasa wa serikal i mbil i , unaonekana kama kutaka kuzima matakwa ya Wazanzibari kubaki katika mfumo wa muungano wanauona kuwa unawahujumu na kuwadunisha.

    K wa u p a n d e m w i n g i n e , Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui ametetea msimamo wa UKAWA kususia bunge.

    A k a s i s i t i z a k u w a C U F hawatarejea kwa sababu zile sababu zilizowatoa Ukawa ndani ya Bunge bado zipo palepale.

    Huu ni usaniiNi kama mtu kujitekenya mwenyewe kisha akacheka mwenyewe na CCM ndiyo wanavyofanya hivyo, alisema Mazrui.

    V i o n g o z i w o t e h a o , wa m e ya s e m a h a y o k a t i k a mkutano wa CUF uliofanyika katika viwanja vya Kibandamaiti hivi karibuni.

    Wakat i huo huo, Kat ibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Wazanzibari wanahitaji amani na siyo fujo, ili kuishi kwa upendo bila ya kubaguana.

    Na kuuhusu mchakato wa katiba mpya, alisema, Samweli Sitta anacheza na kanuni ambazo zilitungwa na wajumbe wa Bunge hilo, ili kuharibu mchakato huo.

    A l i s e m a S i t t a a m e k u wa akisimamia mijadala bungeni inayolenga kuwajadili watu na kutoa matusi badala ya kujadili rasimu iliyopo mbele yao.

    Alisisitiza kwamba hakuna m j u m b e k u t o k a U k a w a

    atakayeshiriki na kupitisha katiba ambayo haina uhalali kisheria.

    Akizungumzia suala la Mansour Yussuf Himid, aliyekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria, alisema ni ishara nzuri kwake.

    Mansour amepata mtihani wamemkamata na sasa hivi yuko ndanikwenda jela ni ishara nzuri hata mitume walikwenda jela Nabii Yussuf si alikwenda jela yaliyomkuta Mansour ni ishara nzuri ya kupata mamlaka kamili ya Zanzibar, alisema Maalim Seif.

    M a a l i m S e i f a m b a ye n i Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema: Njia zile zile walizonipitisha mimi ndizo wanazompitisha Mansour,.

    A l i o n g e z a : K w a n z a walinifukuza kwenye Chamak i s h a w a k a n i t i a n d a n i walipochoka wakanambia toka na Mansour wamemfukuza CCM na sasa yuko ndani.

    Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal akiwa na baadhi ya washiriki wa semina ya MUM.

  • 5 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Habari za Kimataifa

    R A I S wa m p i t o wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bi. Catherine Samba Panza, amemteua Bi. Mahamat Kamoun, kuwa Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.

    Rais Samba Panza amemteua Kamoun kuwa Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito, zikiwa zimepita wiki mbili tangu yafikiwe makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya wanamgambo wa Muungano wa Seleka na kundi la Kikisto la Anti Balaka huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

    Bi. Mahamat Kamoun, anakuwa Muislamu wa kwanza kushika wadhifa wa uwaziri mkuu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru kutoka kwa mkoloni Mfaransa mwaka 1960.

    Uteuzi huo umeelezwa kuwa umefanyika zikiwa ni jitihada za kujaribu kuwa na serikali yenye kushirikisha makundi yote ya kisiasa na ya kidini itakayokubalika na wananchi wote.

    Kabla ya kuteuliwa k u wa Wa z i r i M k u u , Bi. Mahamat Kamoun ambaye ni Muislamu alikuwa mshauri wa Rais Samba Panza siku za nyuma. Pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Hazina kuanzia mwaka 2003 hadi 2013 katika kipindi cha uongozi wa Rais aliyepinduliwa, Francois Bozize, aliyeondolewa madarakani mwezi machi mwaka jana.

    I m e e l e z w a k u w a , m i o n g o n i m w a c h a n g a m o t o k u b w a zitakazoikabili serikali ya Bangui ni j insi ya kuyashirikisha makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha kwenye serikali mpya nchini humo.

    Uteuzi wa Bi. Kamoun, umefanyika ndani ya wiki mbi l i baada ya kusainiwa makubaliano ya usitishwaji vita kati ya makundi hasimu ya waasi ya Anti Balaka na Seleka huko Brazzaville, mji mkuu wa Kongo.

    Hata hivyo kuteuliwa mwanasiasa Muislamu kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumeibua hisia mseto kutoka kwa watu na makundi mbalimbali ya

    Waziri Mkuu wa kwanza Muislamu ateuliwa A.Katinchi hiyo.

    Mapema wiki hii kundi la Muungano wa SELEKA katika Jamhuri hiyo ya Kati umepinga uteuzi wa Bi. Kamoun, kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo na kukataa kushiriki katika serikali ijayo.

    I n a v y o o n e k a n a h a l i h a i j a w a k a m a i l ivyotaraj iwa, kwani muda mfupi tu, baada ya kutangazwa uteuzi wake, Muungano wa Seleka ulitoa taarifa inayosisitiza kususia kushiriki katika serikali ijayo.

    S a b a b u ya S e l e k a kususia serikali hiyo i m e t a j w a k u w a n i kupuuzwa kwao na Rais wa nchi hiyo. Taarifa ya Seleka imesisitiza kwamba, walipaswa kushauriwa kuhusiana na uteuzi wa Waziri Mkuu.

    Aidha taarifa ya Seleka imesema bayana kwamba, uteuzi wa Bi. Mahamat K a m o u n , h a u w e z i kusa id ia kupat ikana amani na maridhiano ya kitaifa nchini humo.

    Kamoun al i teul iwa kuwa Waziri Mkuu baada ya kujiuzulu Bw. Andre Nzapayeke, aliyekuwa akishikilia wadhifa huo. Nzapayeke na serikali yake, wamejiuzulu ili kupisha utekelezwaji wa hati ya makubaliano ya k u s u k u m a m b e l e gurudumu la serikali ya mpito; makubaliano ambayo yalitiwa saini hivi karibuni huko Congo Brazzaville.

    Makundi hasimu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, mwishoni mwa mwezi ul iopita yal i t ia saini hati ya makubaliano ya amani. Pamoja na hayo, mapungufu yal iyoko katika hati ya makubaliano hayo kwa upande mmoja na kutofungamana na Hivi sasa hitilafu kati ya pande mbili katika nchi hiyo zimeshika kasi zaidi. Inaonekana kutiwa saini makubaliano ya makundi y a n a y o h a s i m i a n a kumeongeza hitilafu za miongoni mwa makundi hasimu.

    Ijumaa iliyopita mirengo mbalimbali ndani ya kundi la Kikristo la Anti-Balaka i l igeukana na kuanza kupigana. Mapigano hayo yamesababisha raia wengi kujeruhiwa na maelfu ya wengine kuyakimbia makazi yao.

    Baadhi ya viongozi wa Seleka wametangaza wazi kwamba, wanapinga makubaliano yaliyofikiwa h i v i k a r i b u n i h u k o Brazzaville. Mgawanyiko ndani ya kundi la Seleka umekuwa mkubwa kiasi kwamba, baadhi ya weledi wa mambo wanaona halitakuwa jambo geni kuona likiibuka kundi jingine na kujitenga.

    Aidha mapigano baina ya wapiganaji wa Seleka na Anti-Balaka yameendelea kushuhudiwa licha ya pande mbili kutia saini hatia ya makubaliano ya amani.

    Wanajeshi wa Ufaransa n a o w a m e e n d e l e a

    k u w a u n g a m k o n o w a n a m g a m b o w a Kikristo wa Anti-Balaka, hali ambayo imeifanya Jamhuri ya Afrika ya Kati iendelee kuwa uwanja wa mapigano na machafuko huku Waislamu wakiwa ndio waathirika wakuu wa machafuko hayo.

    Mwezi Machi mwaka 2013 Michel Djotodia, kiongozi wa kundi la Seleka, alijitangaza kuwa Rais baada ya kumpindua Francois Bozize.

    Kuingia madarakani Bw. Djotodia ambaye ni Muislamu, kulitumiwa vibaya na baadhi ya wapinzani wake ambao walianzisha fitina za kidini

    na kusababisha nchi hiyo kutumbukia kwenye vita vya ndani vya kidini kati ya serikali ya Djotodia na wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka.

    M a p i g a n o h a y o yamesababisha maelfu ya Waislamu kuuawa huku mamia ya maelfu ya wengine wakilazimika kuikimbia nchi kutokana na ghasia hizo.

    Kufuat ia sh in ik izo za nchi za Magharibi n a b a a d h i y a n c h i jirani, Michel Djotodia alilazimika kuachia ngazi mwezi Januari mwaka h u u k w e n y e k i k a o maalum cha viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Katikat i mwa Afr ika (ECCAS), uliofanyika mjini N'Djamena, Chad.

    Baada ya hapo aliingia madarakani Rais wa mpito wa Kikristo, Catherine Samba Panza, ambapo kul i tara j iwa kwamba kungepunguza migogoro ya ndani na kurudisha udhibiti wa kisiasa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Hata hivyo mambo yalizidi kwenda kombo chini ya uongozi wake na dunia ikashuhudia machafuko na mgogoro wa kihistoria ambapo Wa k r i s t o w a A n t i -Balaka walishika silaha na kuanzisha mauaj i ya kinyama dhidi ya Waislamu katika kile ki l ichotajwa kuwa ni kulipiza kisasi dhidi ya kilichoitwa jinai za Seleka walipokuwa madarakani.

    Mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yaliushtua ulimwengu kiasi kwamba taasisi za kimataifa za kutetea haki za binadamu zilipiga kelele na kulaani mauaji hayo, sambamba na kutaka watenda jinai hizo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria. (irib.iri).

    SERIKALI ya Kenya imekwama katika mpango wake wa kutaka iruhusiwe kufanya upelelezi wa raia katika mawasiliano binafsi pasipo idhini y a m a h a k a m a . Serikali imelazimika k u o n d o a j a r i b i o l a k u r u h u s u S h i r i k a la Upelelezi la Taifa (NIS) kusikiliza kwa siri maongezi ya simu na mawasiliano binafsi

    Kenya wakataa ujasusi wa kimarekani ya raia, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti wiki iliyopita.

    Spika wa Bunge la Kenya, Justin Muturi alitangaza kuondolewa kwa marekebisho hayo katika Bunge la Taifa.

    A wa l i s e r i k a l i ya K e n ya i l i p e n d e k e z a kurekebishwa sher ia iliyopo sasa ili kuruhusu pasipo hati ya mahakama, k u f a n ya u c h u n g u z i , ufuatiliaji na uingiliaji

    wa mawasiliano binafsi ya watu wanaoshukiwa kufanya makosa.

    Kama sheria ilivyo sasa, NIS inaweza kufuatilia au kusimamisha mawasiliano binafsi ya washukiwa wa uhalifu, iwapo tu itakuwa na hati ya kisheria.

    Wakosoaji umelaumu v i k a l i m a r e k e b i s h o y a l i y o p e n d e k e z w a kwamba ni kinyume cha katiba.

    Bi. Mahamat Kamoun.

  • 6 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Makala

    WAZIRI wa Mambo ya Nje wa serikali ya awamu ya kwanza ya Rais Barack Obama wa Marekani, Hillary Clinton, amesema kuwa Rais huyo ndiye aliyehusika na kuundwa kwa kundi la kigaidi la Daesh.

    Hil la ry C l in ton ambaye inaonekana kuwa anajitayarisha kwa ajili ya kugombea kiti cha Rais katika uchaguzi ujao mwaka 2016, amesema utendaji na mitazamo ya Rais Obama imesababisha kujitokeza kundi la DAESH ambalo amedai kuwa limeteka baadhi ya maneo nchini Syria na Iraq.

    Clinton alisema kuwa makosa ya Rais Barack Obama katika mgogoro wa Syria na uzembe wake katika kukabiliana na serikali ya nchi hiyo, ndiyo sababu kuu ya kujitokeza kundi hilo.

    Pamoja na kuwepo hisisa za kisiasa juu ya wagombea wa uchaguzi ujao wa urais nchini Marekani, matamshi hayo ya Hillary Clinton yanaonesha kuwa wanasiasa wa nchi hiyo hawaridhishwi na utendaji wa serikali ya Washington katika kukabiliana na ugaidi.

    Hali hiyo imeleta tafsir i kwamba, anapoonekana mtu aliyekuwa karibu na Rais wa Marekani, akimtaja Obama kuwa alihusika katika kuunda kundi pinzani la Daesh nchini Iraq, basi hicho ni kielelezo kwamba kuna malalamiko ndani ya Marekani juu ya utendaji wa serikali katika uwanja huo yamevuka mipaka ya watu wa Republican na kuenea katika jamii nzima ya Marekani.

    Wakosoaji wa serikali za Obama akiwemo Hillary Clinton, wanaamini kuwa, serikali ya Marekani i l iyaunga mkono makundi yote ya upinzani ya Syria bila kujali mielekeo na itikadi zao kwa ajili ya kufikia malengo yake nchini humo, yaani kuingoa madarakani serikali ya Rais Bashar Assad na kuunda serikali yenye mielekeo ya Kimagharibi nchini Syria.

    Kwamba katika miezi ya mwanzoni mwa machafuko nchini Syria, utendaji na muelekeo ya makundi ambayo baadaye yalikuja kujulikana kama Jabhatun Nusra na Daesh haukuwa wazi, lakini tangu hapo awali ilijulikana waziwazi kwamba kuna makundi ya kiitikadi za Kiislamu katika safu za wapinzani wa serikali ya Rais Bashar Assad. Kwa muda mrefu makundi hayo yalikuwa yakipewa himaya na misaada ya kifedha na kisilaha kutoka muungano wa nchi za Magharibi na za Kiarabu na y a l i w e z a k u t e k a b a a d h i ya maeneo ya ardhi ya Syria kwa kutumia misaada hiyo. Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zilikuwa zikiamini

    Clinton adai Rais Obama anahusika kuundwa Daesh

    Hillary Clinton.

    kwamba, muungano wa makundi yanayompinga Bashar Assad, yakiwemo yale yanayoitwa yenye misimamo mikali, yanaweza kudhibitiwa na kwamba katika mchakato wa kuunda serikali

    Sheikh Naeem Qassim.

    mpya baada ya Assad, makundi yenye mielekeo ya Kimagharibi na kisekulari yatapata ushindi. Hata hivyo hali inaonyesha kwamba vita ndani ya Syria, vilivyoanzishwa na Wamagharibi

    vimekuwa sababu ya kujitokeza makundi yaliyopo hivi sasa, ambayo yanawania kuangusha serikali ya Rais Assad.

    Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wanaharakati wa Kundi la Hizbullah nchini Lebanon Sheikh Naeem Qassim, amesema kuwa Marekani kwa kushirikiana na nchi nyingine za eneo la Mashariki ya Kati ndizo zilizounda kundi la Daesh na kulipeleka nchini Syria.

    Sheikh Naeem Qassim amesema kuwa, njama za Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na kundi la Daesh za kutaka kuiangusha serikali ya Rais Bashar Assad wa Syria zimegonga mwamba.

    Ameongeza kuwa, uhusiano wa Hizbullah na Hamas bado ni imara na kusisitiza kwamba harakat i hizo mbil i daima zimekuwa zikielekeza nguvu zao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

    Sheikh Qassim amepuuza matamshi yanayotolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu kwamba, mapambano ya Wapalestina dhidi ya Wazayuni yamesambaratika.

    Sheikh Qassim alisema kuwa, vita vya Gaza vimetoa funzo na somo zuri kwa adui Mzayuni na kusisitiza kwamba, kwa mara ya kwanza kabisa Netanyahu amekiri wazi juu ya kuwepo utulivu na usitishaji vita.

    SWAHIBA wangu mmoja siku zote hupenda kusisitiza kwamba, katika ulimwengu wa leo asiye na elimu au weledi na ufahamu wa mambo ya dunia yake basi ataishi kwa taabu na atakuwa mfano wa bendera ambayo hufuata upepo. Tukiachana na ya sahiba wangu hayo, waswahili wana msemo wao mashuhuri usemao: Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hivi ndivyo hali ilivyo hii leo katika ulimwengu tunaoishi. Vyombo vya habari vya Magharibi vimehodhi kila kitu; lakini kwani ukweli unaweza kuuficha siku zote? Ghiliba na hadaa za Wamagharibi zimefahamika sasa. Kwa hakika njama za Wamagharibi dhidi ya Uislamu hazikuanza leo wala jana; lakini bila shaka katika siku za hivi karibuni zimeshadidi mno. Kuibuka makundi yenye misimamo ya kupindukia ambayo yanajiita kuwa makundi ya Kiislamu kama al-Shabab huko Somalia, Boko Haram nchini Nigeria, Jabhat al-Nusra

    Kundi la Daesh; Mujahidina au Magaidi? Na Salum Bendera kule Syria na sasa Daesh huko

    Iraq ni mifano ya wazi kabisa ya njama za maadui wa Uislamu nyuma ya pazia la makundi hayo.

    T u k i t u p i a j i c h o y a l e yanayofanywa na makundi haya itafahamika wazi malengo hasa ya makundi hayo. Kwa mfano, mambo yanayofanywa na Boko Haram Nigeria kama mauaji kuwateka nyara wasichana wa shule na mengine mfano wa hayo, ni matukio ambayo humfanya mtu kwa uchache kutilia shaka kama kweli kundi hilo linapigania Uislamu na haki za Waislamu. Sasa limeibuka kundi Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi DAESH. Imekuwa ni jambo la kawaida kusoma au kusikia katika vyombo vya habari juu ya jinai na mauaji ya kutisha yanayofanywa na kundi hili. Kwa hakika kundi hili la kigaidi ambalo licha ya kudai kuwa linafuata mienendo ya jihadi ya kisalafi, lakini kwa hakika ni mfuasi wa fikra potofu za Kiwahabi ambazo ni fikra mgando na zilizopitwa na wakati. Kwa maana kwamba, mitazamo na fikra kama hizi hazina nafasi

    kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu.

    K u n d i l a D a e s h hutumia ukati l i , utesaj i na mauaji ya kutisha ambapo mfano wa jinai hizo ni mauaji ya umati ya raia wasio na hatia nchini Syria, mauaji ambayo hutekelezwa hadharani na kuwajumuisha watoto wadogo, wanawake na vizee. La kusikitisha zaidi ni kwamba, kundi hili la kigaidi linafanya mauaji haya kwa jina la Uislamu na utawasikia wakisoma dua ndefu na kumsabihi Mwenyezi Mungu kabla ya kumchinja mtu au kumpiga risasi.

    Uislamu upi na Mungu yupi anayeruhusu kuuawa nafsi isiyo na hatia yoyote? Je hii ni jihadi ya kutaka kuasisi dola la Kiislamu au ni ugaidi na jinai dhidi ya binadamu? Harakati za kundi la Daesh kwa hakika ni fitna kubwa ya karne. Msiba mkubwa zaidi ni kuwepo watu wanaoshabikia mauaji ya kundi hilo na kuwamiminia sifa lukuki wapiganaji hao wakiwaita kuwa ni mujahidina. Historia ya kundi

    Inaendelea Uk. 7

  • 7 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Habari

    hilo inarejea nyuma mwaka 2004, yaani wakati Abu Musab Zarqawi alipoasisi mtandao uliokuja kujulikana kwa jina la Jamaat Tawhid wa Jihad huku akiwa kiongozi wake. Baada ya Zarqawi kutangaza utiifu wake kwa Osama bin Laden, mkuu wa zamani wa mtandao wa al-Qaida, kundi hilo liligeuzwa na kuwa tawi la taasisi ya al-Qaida nchini Iraq. Baada ya Marekani kuivamia Iraq, kundi hilo taratibu lilijionyesha kuwa lililokuwa likiendesha jihadi dhidi ya vikosi vya Marekani nchini humo. Ni kutokana na hali hiyo ndio maana vijana wengi waliokuwa wakitaka kupambana na vikosi hivyo vamizi, wakajiunga nalo ambapo haraka likageuka na kuwa kundi lenye nguvu la wanamgambo nchini Iraq.

    Mwaka 2006 Zarqawi aliuawa na uongozi wa kundi hi lo ukachukuliwa na Abi Hamzah al-Muhajir ambaye alikuwa kiongozi wa mtandao wa al-Qaida nchini humo na mrithi wa Zarqawi mwenyewe. Mwishoni mwa mwaka 2006 kuliundwa kundi la wanamgambo kupitia makundi kadhaa ya Iraq ambalo lilikuja kujulikana kwa jina la Daulatul-Islam fil-Iraq huku kiongozi wake mkuu akiwa ni Abu

    BAADA ya kupita mwezi mmoja tangu utawala wa Kizayuni wa Israel uanzishe mashambulio ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Gaza, hatimaye Umoja wa Mataifa imeunda kamati ya wataalamu itakayochunguza jinai za kivita zilizofanywa na utawala huo hasibu huko Gaza.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, kamati hiyo itakayokuwa na wataalamu watatu, itachunguza kwa kina vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na jinai za kivita huko Gaza.

    Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kamati hiyo inapaswa kutoa matokeo ya uchunguzi wake mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ifikapo mwezi machi mwakani.

    J u l a i 3 1 m wa k a h u u , Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, alitangaza wazi kwamba, utawala wa Israel kwa makusudi kabisa, umekiuka sheria za kimataifa na kutenda jinai za kivita katika eneo la Gaza.

    Tayar i wapigania haki mashuhuri wa kisiasa kutoka nchi za Amerika ya Kusini wamesaini taarifa ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuikalia kwa mabavu ardhi za Palestina na mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza.

    Taarifa hiyo imesainiwa na Rais Evo Morales wa Bolivia, Fidel Castro Rais wa zamani wa Cuba na Manuel Zelaya, Rais wa zamani wa Honduras. Wanasiasa hao wa Bolivia, Cuba na Honduras wameishutumu Marekani na nchi za Ulaya kwa kuiunga mkono Israel na kutaka kuungwa mkono kampeni ya kuususia na kuuwekea vikwazo utawala wa Israel.

    Wapalestina wasiopungua 1,940 wakiwemo watoto 470 wameuawa shahidi na wengine karibu ya 10,000 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza yaliyoanza Julai 8.

    Wakati usitishaji vita kati ya Waharakati wa Mapambano wa Palestina-Hamas na utawala wa Kizayuni ukiingia katika siku ya nne, maafisa wa Palestina na Israel Jumanne wiki hii waliendelea na mazungumzo

    UN kuchunguza udhalimu wa Israel Gaza

    yao yasiyo ya moja kwa moja huko Cairo mji mkuu wa Misri huku raia wa Kipalestina walio katika mzingiro huko G a z a w a k i k a b i l i w a n a uhaba mkubwa wa dawa. Wanaharakati wa Hamas

    wa n a t a k a k u h i t i m i s h wa mzingiro wa kiuchumi katika Ukanda wa Gaza uliodumu kwa miaka saba sasa, lakini Tel Aviv inasema kuwa itatekeleza suala hilo iwapo Hamas itapokonywa silaha, sharti ambalo limepingwa

    n a W a n a h a r a k a t i h a o . Waziri wa Vita wa Israel, Moshe Yaalon ametahadharisha kuwa utawala wa Israel utaanzisha tena mashambulizi baadaye iwapo pande mbili hizo zitashindwa kufikia makubaliano.

    Kundi la Daesh; Mujahidina au Magaidi? Inatoka Uk. 6 Omar al-Baghdadi. Mwezi April

    mwaka 2010 vikosi vya Marekani vilimuua Abu Omar al-Baghdadi na Abu Hamzah al-Muhajir katika operesheni ya kijeshi. Ni baada ya hapo ndipo Abu Bakar al-Baghdadi alichukua uongozi wa kundi hilo akimrithi Abu Omar al-Baghdadi. Mwanzoni mwa mwaka 2011 sambamba na kuanza kwa mgogoro na vita nchini Syria, kundi linalojulikana kwa jina la Jabhatu Nusra kwa ajili ya Watu wa Sham ambalo ni tawi la Dola la Kiislamu la Iraq liliundwa nchini humo humo na haraka likageuka kuwa moja ya makundi yanayoendesha vita dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad. Hatimaye mwaka 2013 Abubakar al-Baghdadi alitangaza kuyaunganisha pamoja makundi ya, Jabhatu Nusra na Dola la Kiislamu la Iraq na kuzaliwa kundi la Daulatul-Islam fil-Iraq wa Sham kwa kifupi Daesh (ISIS). Hata hivyo upinzani wa al-Qaeda dhidi ya hatua ya kuyaunganisha pamoja makundi hayo na uungaji mkono kwa Jabhatu Nusra, uliibua vita kati ya Daesh na kundi la Jabhatu Nusra nchini Syria, vita ambavyo hadi sasa vimeshapelekea zaidi ya wanamgambo 1000 wa makundi hayo kuuawa.

    Mbali na jinai na mauaji ya kinyama ya DAESH, kundi hili

    limekuja na mambo ya ajabu ajabu kama Jihad Nikah. Wachambuzi wa mambo wanasema huu ni uzinzi na ukandamizaji kwa jina la jihadi ya ndoa. Magaidi hao wa Kitakfiri hivi karibuni waliamua kufungua ofisi za ndoa kwa shabaha ya kuwarubuni wanawake ili waelekee Syria n a I r a q k wa s h a b a h a ya kuwahudumia wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la Daesh wanaopigana na serikali za Syria na Iraq. Shirika kutetea haki za binadamu la Human Right Watch (HRW) lilitangaza kuwa, magaidi wa kitakfiri wamefungua ofisi hizo katika mji wa al Bab ulioko katika jimbo la Halab nchini Syria. Wanamgambo wa Daesh wamekuwa wakiwashawishi na kuwarubuni wanawake na wajane kuorodhesha majina na anwani za makazi yao kwa lengo la kwenda kutoa huduma ya ngono kwa wanamgambo wa Daesh. Sasa hawa wanaweza kuitwa mujahidina au ni magaidi wanaotenda jinai kwa jina la Uislamu? Hivi kweli kundi hi l i l imeufahamu Uis lamu unavyoapaswa?

    Waislamu tuwe macho na njama za makundi kama haya ambayo si ya Kiislamu, au yameufahamu vibaya Uislamu au pengine yanatumiwa na maadui wa Uislamu kuharibu sura nzuri ya dini hii tukufu.

    Rais Evo Morales wa Bolivia.Fidel Castro Rais wa zamani wa Cuba.

    Kiongozi wa Hamas, Khaleed Mashaal.

  • 8 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Makala

    YAPO maelezo ya watu waliofika Kigoma miezi ya hivi karibuni wakitokea Yemen kama wana-Dawah wakitaka kukutana na kuf ikisha ujumbe kwa Waislamu. Mada yao kuu ilikuwa kuwataka Waislamu wasipoteze muda wao kupeleka watoto wao shule kwa sababu elimu z i n a z o s o m e s h wa h u k o ni za kikafir i . Maelezo ya n a y o t o l e wa n i k u wa mtu mmoja alisimama na kuwauliza kuwa kutoka Yemen mpaka wamefika Tanzania, wametumia kipando gani. Wakasema, ndege. Bila shaka unaweza kukisia jinsi swali na jawabu hili lilivyobadili sura ya mazungumzo.

    Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza hapa ni hili: Huu ujinga wa kiwango hiki umetoka wapi? Huku kupumbaa kwa kiwango hiki kumeingiaje katika jamii ya Waislamu? Mtu anashawishi mabinti wa Kiislamu wasisomee udakitari kwa sababu hiyo ni elimu ya kikafiri, lakini mkewe akipata tatizo anampeleka hospitali na kuhudumiwa na John au hata Anna dakitari bingwa wa magonjwa ya kike!

    M t u a n a t o k a Ye m e n , anapanda Boeing 777 hadi Dar es Salaam, hapandi ngamia, anafika anakwambia usipeleke mtoto shule; unaona umefikiwa na Sheikh mkubwa kabisa na kakuambia kitu cha maana unamsikiliza unamkubalia! Mtu anatoka Dar es Salaam anapanda FastJet hadi Mwanza au Mbeya, anakwambia mtoe mtoto wako Nyasaka asisome fizikia kwa sababu ni ukafiri, unamsikiliza unakubali! Mtu anatoka Tanga au Arusha, kapanda basi hadi Kondoa au Masasi, hakupanda punda au kutembea kwa miguu, anakwambia mtoe mtoto wako shule maana huko hakufundishwi ila ukafiri, unakubali. Unamtoa mtoto wako shule unampa aende naye!!!

    Hapa ndio ninapojiuliza, huu ujinga na kupumbaa huku kumetoka wapi na kumeingiaje katika jamii ya Waislamu?

    Kiasi mwezi mmoja uliopita, yupo bwana mmoja alipata ajali. Akiwa mahututi hajitambui, a k a p e l e k wa M u h i m b i l i . Taarifa zilipowafikia baadhi ya jamaa zake, wakaja juu. Kwa nini mlimpeleka hospitali? Mngemuacha hivyo hivyo na majeraha yake na viungo vyake vilivyovunjika. Yeye si ametoa watoto wake shule

    Ushauri kutoka Nigeria:Dar wamalizeni Boko haram wenu

    Vinginevyo mtalia na kusaga meno

    Na Omar Msangi

    kuwa kusoma ni ukafiri, sasa atatibiwa vipi na elimu ya kikafiri!

    Jumatatu wiki hii ilifungwa semina juu ya epistemolojia ya K i i s l a m u , i l i y o k u wa ikifanyika katika Chuo Kikuu cha Waislamu, Morogoro. Semina hii ilihudhuriwa na washiriki takribani 400 kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Arabuni. Nigeria, ndiyo iliyokuwa na washiriki wengi zaidi, kiasi cha 35 na wengi wao wakiwa ni maprofesa na wahadhiri kutoka vyuo vikuu. Nilijitahidi sana kukutana na

    wengi katika washiriki hao, katika mazungumzo binafsi, ili kupata picha kamili ya tatizo la Boko Haram, lilivyo. Labda niseme kuwa wote, japo niliongea nao mmoja mmoja , na pengine b i la kujua kuwa nilishaongea na mwingine na aliniambia nini, maelezo yao yanalingana na wanasema, huo ndio uoni na msimamo wa Waislamu wote wa Nigeria na hata Wakristo (ukiacha wale hamnazo na wanaotumiwa au wenye chuki binafsi zilizowapofua). Lakini pia wote wal i toa

    nasaha zinazofanana, kwamba Waislamu na Watanzania, wasifanye kosa walilofanya wao, kwa sababu tutajuta. Wanasema, wao walifanya kosa ambalo hawakujua kuwa lingewagharimu kiasi hiki. Kwamba, walipoibuka watu wanaosema kupeleka watoto shule ni haramu, waliwaona kama wapuuzi tu na kwamba hakuna Muislamu Mnigeria mjinga atakaye wasikiliza. Lakini wanasema, pengine kwa kuwepo kundi kubwa la vijana wasio na kazi, kila uchao Boko Haram wakawa wanapata vijana wa kuwashabikia na kuwakubali. Hiyo ikawa hatua ya kwanza.

    Katika hatua ya pili wanasema kuwa ni pale, serikali ilipotaka sasa kuwadhibiti, lakini ilikuwa tayari imechelewa (au serikali yenyewe nayo ilikuwa katika mkakati huo. Hii ni dhana yangu tu, sio yao.). Hatua ya kukamata viongozi wa Boko Haram, ikaleta fujo kubwa. Vijana wakawa wanavamia na kulipua vituo vya polisi, wala haikujulikana silaha walipata wapi.

    K a t i k a h a t u a ya t a t u , wanasema kuwa, takribani wale vijana wote waliokuwa wakijulikana kuwa ni Boko Haram, waliuliwa. Nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, wal ikuwa wakisakwa na vyombo vya dola.

    Katika hatua ya nne, ni kuja hiki kikosi kazi kipya ambacho hakijulikali, ila kiongozi wake tu anayejitokea katika vyombo vya habari kutoa kauli na madai mbalimbali. Hii ni hatua pia ambayo iliambatana na Boko Haram, ghafla kuwa na silaha nzito za kijeshi zikiwemo machine guns, makombora, rocket launchers, mabomu, magari ya kivita mengi yasio na idadi mpaka helkopta.

    Kaskazini mwa Nigeria, hasa kule ambako panaonekana kuwa kitovu cha mashambulizi ya Boko Haram, pako chini ya hali ya hatari, na hivyo sheria na kanuni za kijeshi ndio zinadhibiti eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuwepo vizuizi vya barabarani vyenye polisi na jeshi, kila baada ya masafa kadhaa. Lakini hata hivyo wanasema, watapita Boko Haram na msururu wa magari yao ya kijeshi watavamia mtaa au kijiji na kufanya mauwaji na kuondoka na hawakamatwi.

    Katika lile tukio mashuhuri l a k u t e k w a w a s i c h a n a w a s h u l e , w a n a s e m a , mfano wake chukulia pale Morogoro, Msamvu, ndipo

    Inaendelea Uk. 9

  • 9 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Makala

    Dar wamalizeni Boko Haram wenuInatoka Uk. 8ilipo shule, watoto wanatekwa na wanachukuliwa kuelekea Chalinze, halafu hapo katikati, wa n a i n g i a p o r i n i . M a g a r i hayaonekani yalipotelekezwa, wala watu wakijitolea kuwa wapo tayari kuingia katika pori hilo, serikali haitaki. Hakuna anayeruhusiwa kuingia. Na wanasisitiza kuwa sio msitu mnene kama ilivyo misitu ya huku Afrika Mashariki na Kati. Ni vichaka kwa sababu, Kaskazini mwa Nigeria, ni eneo la kueleka jangwani.

    Almuhimu wanachosema ni kuwa ilipofikia Boko Haram, huna namna ya kusema kuwa wanaofanya hayo ni kile kukundi cha vijana wa Kiislamu wa Kinigeria walioanza kusema kuwa kwenda shule ni haramu. Inavyoonekana ule ulikuwa mkakati wa kutafuta kianzio ambao kwanza unawachanganya Wa i s l a m u n a k u p a r u r a n a wenyewe kwa wenyewe. Pili, u k i f a n i k i wa j a p o k i d o g o , unawazamisha Waislamu katika ujinga. Tatu, kama wanavyofanya ISIS kule Iraq na Syria, kutangaza Uislamu kuwa ni dini ya mauwaji, ukatili na ushenzi na ndio maana wanakatazana kusoma. Na nne, kutumika katika kiwango cha kuleta machafuko katika nchi. Hapa wanaangamia Waislamu na Wakristo. Ndio maana katika nasaha zao, wasomi hawa kutoka Nigeria, wakasema kuwa Wakristo wasije wakajidanganya kuwa hili ni tatizo la Waislamu, shauri lao Waislamu!!!

    Kama jamii ya Waislamu, nadhani kuna haja ya kuchukua hatua za haraka, vinginevyo, itakuwa majuto ni mjukuu. Suala la elimu lipo wazi, wala si katika yale mambo mutashabihati. Kwa nini Masheikh zetu wanakaa kimya na kuwatizama watu wakipita mitaani kuwapumbaza na kuwapotosha na kuwatia ujinga Waislamu juu ya suala la elimu? Kwa nini hatuwasikii wakisimama na kutoa maelekezo kwa Waislamu na kusimama kuchukua hatua juu ya watu hawa ambao mimi nasema ni kama wale akina Abu Baghdadi wanaotumiwa kuungamiza Uislamu (ama kwa kujijua au kwa mzigo wa ujinga walio nao).

    Nchi hii ina sheria ambapo, hata mzazi anaweza kushitakiwa kama atamnyima mtoto wake haki ya kusoma. Kwa nini taasisi za Kiislamu hazichukui hatua dhidi ya watu wanaowatoa watoto wa Kiislamu shuleni na vyuoni?

    Katika hotuba yake ya ufunguzi wa semina hii ya epistemolojia ya Kiislamu, Makamu wa Rais, Mheshimiwa Gharib Bilal, pamoja na kuwahimiza Waislamu kutoa elimu bora kabisa kwa vijana

    wao kwa manufaa ya taifa na wao wenyewe, alirejea zile zama bora kabisa katika historia ya Kiislamu ambapo wanazuoni wa Kiislamu ndio walikuwa wakiongoza katika fani mbalimbali za elimu zilizoleta mapinduzi makubwa katika sayansi na tekinolojia hivi

    leo katika Ulaya na ulimwengu kwa ujumla. Wakati huo, Ulaya ilikuwa kizani kabisa.

    Inavyoonekana, wanachotaka kufanya hawa wanaowatia ujinga Waislamu wasipeleke watoto wao shule, wanataka kufuta ile historia ya Waislamu kuwa ndio mabwana wa elimu walio wastaarabisha Ulaya na ulimwengu kwa ujumla. Wanataka kuleta blanketi la ujinga lifunike umma wa Kiislamu kwa hiyo kufuta hata ile historia ambayo wenyewe wa Ulaya wanakiri kuwa Uislamu na elimu kutoka ulimwengu wa Kiislamu ndiyo iliyowastaarabisha na kuwaibua katika ushenzi na kuwa

    taifa la sayansi na tekinolojia. Wanataka kufuta hii kasi na harakati za Waislamu kurejea katika kiti chao cha kuongoza dunia katika elimu na nyanja zote.

    Ukitizama kwa makini, vita ya makafiri dhidi ya Waislamu hivi sasa inakuja katika njia na namna

    mbili. Moja, ni hii ya kuwafuta katika rekodi za kihistoria kuwa nao walitoa mchango wowote katika elimu. Kuwatia ujinga na wakionekana wajinga fulani tu, hata ukisema kuwa huko zamani walikuwa hivi, hakuna atakaye kusikiliza. Pili, ni hili linalofanywa na ISIS, na wanajihadi bandia wote. Kwamba, pamoja na kutimiza masilahi ya sasa hivi na ya baadae ya mabeberu, lakini pia wanatumika kufunika ile rekodi mbaya ya askari wa Kikristo katika Crusade na wakati huo huo kufuta rekodi safi ya askari wa Kiislamu waliopigana na kushinda vita kadhaa katika

    h i y o C r u s a d e . Wa k a t i wa Crusade, Wakristo walikuwa wakikimbilia kuishi katika miji ya Waislamu kutokana na jinsi jeshi la Waislamu lilivyokuwa likiwatendea wema raia wa Kikristo kila walipo baada ya miji yao kutekwa. Kinyume chake, Crusaders, walikuwa wakiuwa Waislamu kila walipowakuta. Wawe ni watoto, akina mama, wazee n.k. Hili ndilo wanalofanya ISIS hivi sasa.

    Na kwa maana hiyo, wote hao, wanao watoa watoto shule na vyuoni, wale wanaopita mitaani wakisema kuwa kusoma kemia, biolojia na uhandisi ni haramu, pamoja na wale wa jihad bandia na akina Abu Fulani, wetu, wote hao ni mawakala wa mpango mkakati wa kuungamzia Uislamu. Wanaweza wakawa wanajua au wasijue wakiwa wanaendeshwa kwa remote control.

    Hebu tufanye utafiti kidogo tujue, wapi walipata mafunzo yao (training) na kuibuka na hoja hizi za shule haramu. Hebu tufanye utafiti kidogo tujue hawa Abu Fulani, walipata training wapi na nani wapo nyuma yao.

    Hata hivyo, muhimu na la haraka zaidi kwa sasa, Masheikh zetu na viongozi wa taasisi za Kiislamu, watafute namna ya kukabiliana na watu hawa wanaowatia Waislamu ujinga. Kama wanavyosema Waislamu wenzetu wa Nigeria, tukifanya ajizi, tutalia na kusaga meno.

    DKT. Bilal akisalimiana na Mkuu wa Chuo MUM Hajat Mwatum Malale alipowasili kufungua semina Jumamosi iliyopita.

    ROCKET Launcher

  • 10 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014

    Inaendelea Uk. 13

    Makala

    KUANZIA mwishoni mwa wiki iliyopita, Marekani imeanza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State. Katika tangazo lake, Rais wa Marekani Barack Obama alisema kuwa ametoa amri IS washambuliwe k w a m a l e n g o m a w i l i : Kwanza ni kuwadhibiti IS wasiwahilikishe watu wa Yazid waliozingirwa katika milima wa Sinjar. Hatua hii ya Marekani, ilitanguliwa na taarifa za takriban wiki nzima, ikielezwa jinsi IS wanavyouwa watu wa Yazid huku picha zikisambazwa katika vyombo vya habari zikionyesha maiti zilizozagaa, akina mama na watoto waliokimbia makazi ya o wa l i o k o m i l i m a n i wa m e z i n g i r wa h a wa n a mahali pa kwenda. Inadaiwa kuwa IS waliapa kuwamaliza watu wa Sinjar kwa madai kuwa wanafuata dini ya kale inayohusiana na Zorostiani (Zorostianism).

    Jambo jingine linalotajwa na Marekani kuwa ni sababu ya kuwapiga IS kutoka angani, ni kulinda wafanyakazi wa Marekani waliosambaa katika maeneo mbalimbali ya Iraq kwa ajili ya maslahi ya nchi hiyo. Obama alisema kuwa mashambulizi hayo yanaweza kuchukua muda mrefu kwa sababu hawataruhu IS kuingia Baghdad ambapo kuna maofisa wa Marekani wanaotizama masilahi ya nchi hiyo. Kwa upande mwingine amesema k u wa k a m we M a r e k a n i haitaruhusu IS kuteka na kukamata mji mkuu wa Jimbo la Wakurdi (Kurdish region).

    Erbil, ambapo hivi sasa ISIS wanapigwa na Marekani ili wasiingie katika eneo hilo, ni kitovu cha visima vya mafuta katika mkoa/jimbo la Kurdistan. Hata kabla Bush hajavamia Iraq 2003, makampuni makubwa ya mafuta ya Kimarekani, ExxonMobil na Chevron yalishaingia katika eneo hilo na kufanya uwekezaji mkubwa wa kuvuna petroli. Sasa ni wazi kuwa Washington, haiwezi kuruhusu IS waingie na kuvuruga uvunaji huo wa mafuta. Na kwa upande m w i n g i n e , h i l i n i e n e o ambalo litakuwa kama nchi inayojitegemea na hadi sasa kumejaa Wamarekani wengi, ukiacha hao waliopo katika ExxonMobil na Chevron, upo pia ubalozi mdogo na makampuni mbalimbali.

    Mwandishi Steve Coll , akizungumzia mada hii katika

    Obama hapingi Khilafah ya Abu Baghdad. Ni yake

    Anawalinda ExxonMobil , ChevronAnatekeleza mkakati wa CNS 2004Mambo hupangwa hayajitokezei tu

    Na Omar Msangi

    makala yake, Oil and Erbil alimnukuu Rais Barack Obama akieleza ni kwa nini aliamuru IS wapigwe. Katika moja ya kauli zake, Obama alisema maneno yafuatayo:

    The Kurd i sh r eg i on i s functional in the way we would like to see. So we do think it is important to make sure that that space is protected.

    Kwamba, mkoa wa Kurdish unaendesha mambo yake kama Marekani inavyotaka, na kwa hiyo ni lazima ulindwe. Pigia mstari maneno-Kama M a r e k a n i i n a v y o t a k a . Obama aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Thomas Friedman.

    Steve Coll anasema Obama aliyasema hayo baada ya kupitia taarifa aliyopewa n a w a t a a l a m u w a k e wakimwambia kuwa maelfu ya Wamarekani wanaishi Erbil, wengi wao wakiwa ni wale wenye makampuni ya mafuta na gesi katika mji huo na hivyo, isiruhusiwe ISIS kuwavurugia mambo yao. Lakini pia izingatiwe kuwa Rais wa Marekani hawezi kusimama na kutangaza kuwa

    anawapiga ISIS kwa lengo la kuyalinda makampuni ya mafuta ya Kimarekani pamoja na wafanyakazi wao. Lazima litafutwe neno ambalo litaonekana kuwa Marekani ni msamaria mwema anayeingia Iraq kuwalinda Yazid na Wakristo wanaouliwa na ISIS. (Soma Oil and Erbil by Steve Coll.)

    Msomaji wangu mmoja aliniambia kuwa taarifa za kunukuu vyombo vya habari, wasomi na watafiti, sio vigezo v i n a v y o k u b a l i k a k a t i k a Uislamu. Lakini nimwambie k u wa h u y u S t e ve C o l l , anayetamka hapa kuwa hilo ndio lengo la kuwapiga ISIS; ni msomi na Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Columbia (Graduate School of Journalism at Columbia University). Ni mwandishi mtaalamu katika masuala ya inteligensia na usalama ndani na nje ya Marekani (issues of intelligence and national security in the United States and abroad.)

    Nimetangulia kuyasema haya kwa sababu mara tu Marekani ilipotangaza kuwa inaanza kuwashambulia ISIS,

    watu kadhaa walinipigia simu na kunitumia ujumbe kama kuniambia kuwa hatua hiyo ya Marekani ni kwa vile haitaki kusimama kwa Dola ya Kiislamu na kwamba katika redio moja ya Kiislamu, watu wanapiga simu na kutuma ujumbe kuzungumzia suala hilo. Nadhani tunakuwa wepesi sana wa kusahau. Mwaka 2004, Marekani na Uingereza zil ivamia Iraq zikidai kuwa zinafanya vile kwa misingi ya kibinadamu, kuwanusuru wananchi wa Iraq, lakini pia zikitumia hoja

    ya kuwa Saddam Hussein ana silaha za maangamzi-Weapon of Mass Distruction (WMD). Mwisho wa yote hakuna silaha ya maangamizi iliyopatikana wala nusura iliyopatikana kwa wananchi wa Iraq kama ilivyo kwa Walibya hivi leo. Walichofanya ni kupandikiza mbegu ya fitna, machafuko na mauwaji yasiyo na sababu wala kuonekana mwisho wake.

    Miaka 10 baadae, Marekani hiyo hiyo, inawawezesha ISIS kuingia Iraq na kufanya unyama wote waliofanya, kisha sasa inasema inakuja kuwaokoa Yazid na Wakurdi. Suala hapa sio Marekani kuwapiga ISIS kwa vile haitaki ukhalifah usimame kama ambavyo ha ikuwa suala n i WMD ulioifanya kuvamia Iraq. ISIS na Mradi wa Ukhalifah ni watoto wa makafiri/mabeberu, na watoto hawa kazi waliyopewa, kwa kujua au kwa ujinga wa kutumiwa bila kujua, ni kutengeneza mazingira mapya ambayo yatamuwezesha bosi wao kuwashambulia katika kutekeleza mradi wake wa kistratejia kiuchumi, kijiografia

    BAADHI ya wapiganajiwa ISIS wakiranda katika miji walioteka.

  • 11 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014Makala

    iliyowasilishwa katika Kamati ya Usalama ya Bunge la Marekani (The House Select Committee on Intelligence), mradi huo uliitwa "cynical enterprise, hata katika muktadha wa c l andes t ine operations", kwa sababu ya ubaya wake kwa Wakurdi waliotumiwa bila kujijua. Taarifa ya Pike inasema kuwa si Kissinger, Shah wala Rais Nixon, aliyekuwa akitaka Wakurdi washinde. Ila tu, walikuwa wakitumiwa kwa kiwango fulani kwamba wakileta vurugu itatosha kuirejesha serikali ya Iraq katika mstari unaotakiwa. Ripoti inasema:

    Neither the Shah "nor the President and Kissinger desired victory for [the Kurds]. They hoped the insurgents would [maintain] a level of hostilities to sap the resources of [Iraq]."

    Wakati Wakurdi wanaamni kuwa wanasadiwa wajitenge, wajitangazie nchi huru kutoka Iraq, kumbe wanatumiwa kuleta fujo, wauwawe ili mabeberu wapate mradi wao. Na ndio maana, baadae tena baada ya Saddam Hussein kushika madaraka na kuwa kibaraka mtiifu wa Marekani, Wakurdi walitelekezwa na Saddam Hussein akaachiwa kuwachinja kama kuku mpaka kuwapiga kwa silaha za sumu.

    Z o e z i s a s a l i m e g e u k a . Mkakati wa miaka ya 1990s hasa baada ya kuporomoka kwa Urusi na kuonekana kuwa kitisho kilichobakia ni Uislamu, kinachotakiwa sasa ni Iraq, kugawanywa. Wakurdi tena wakiwa na agenda yao ile ile ya kujitenga, sasa wanatumiwa tena. Wanaotumiwa pamoja nao ni ISIS. Ila hapa, wa kuja kuangamizwa ni ISIS. Mahesabu ya sasa yanaashiria kwa Wakurdi kupewa nchi yao, ila wabakie kuwa vibaraka na nchi dhaifu isiyo na uwezo wa kuleta kitisho chochote kwa Israel.

    Na katika mradi huo, Iran chini ya Shah, ilikuwa ikitumika kupitisha pesa na silaha kwenda kwa Wakurdi, kama ambavyo leo Saudi Arabia na Qatar zinavyotumika katika suala la ISIS na mradi wa Khilafah. (Tazama: Gerard Chaliand and Ismet Seriff Vanly, People Without A Country, 1980, 184. (2) Will Safire, New York Times, Feb.12, 1976. (3) Chaliand and Vanly.

    Kama nilivyogusia, katika hali ya kusikitisha, mwaka 1975, baada ya Iraq kukubali kushirikiana na Iran katika matumizi ya ule mlango wa bahari wa Shatt-al-Arab, Marekani iliwatelekeza Wakurdi. Hapo ndio mkono wa chuma wa Saddam ukawaangukia Wakurdi. Wakauliwa sana. Baadhi ya watu na taasisi za kimataifa zilipopaza sauti kuilaumu Marekani kwa kuwatelekeza Wakurdi, jibu la

    Usiparamie behewa usilojua litokako wala

    Kissinger lilikuwa jepesi kabisa, alisema:

    "Covert operations should not be confused with missionary work." (Chaliand and Vanly).

    Kwamba, kazi ya kupigania masilahi ya kibeberu kupitia njia chafu, hadaa na ulaghai wa kila namna, zisidhaniwe kuwa ni kama kazi za wamishionari.

    Ni j ambo la kus ik i t i sha kuwa wakati katika Hadithi mashuhuri ambayo Masheikh zetu wanainukuu mara kwa mara inawataka Wais lamu wawe makini, wawe waangalifu, wachukue tahadhari, isitokee kwa Muislamu kuwa mjinga na mzembe kiasi cha kuumwa na nyoka mara mbili katika shimo moja, leo Waislamu (Wakurdi) hao hao, na Waislamu sisi, tunaumwa katika shimo lile lile. Ila sasa huenda ni koboko (black mamba), yule wa mwanzo alikuwa kifutu!

    Itakumbukwa kuwa mwaka 1979, Shah alipinduliwa, akaja Ayatollah Khomein na serikali ya Kiislamu ya Iran. Hali ikachafuka tena. Zbigniew Brzezinski , aliyekuwa Mshauri wa Usalama wa Marekani (National Security Advisor ) akamtaka Saddam Hussein kuishambuilia Iran ateke Shatt-al-Arab waterway. Mwaka 1980 Marekani ikaisaidia Iraq kwa taarifa za kiintelijensia na silaha kupambana na Iran. Nchi za Kiislamu, ikiwemo Saudi Arabia, Misri, Kuwait, zikatakiwa kuimsaidia Saddam. Zikatoa

    Inatoka Uk. 2

    mamilioni ya dola, fedha na silaha.Hata hivyo, wakati Saddam

    Hussein yeye akiona kuwa anapendwa na Marekani kwa msaada anaopewa, wanaotoa m s a a d a k wa u p a n d e wa o walikuwa na haya ya kusema:

    "We wanted to avoid victory by both sides." Alinukuliwa mmoja wa maofisa wa serikali ya Reagan akisema kama alivyonukuliwa na gazeti la New York Times. Naye Henry Kissinger akanukuliwa akisema kwa ufedhuli:

    "I hope they kill each other" and "too bad they both can't lose."

    Kwamba, anataraji Iraq na Iran wataendelea kuuwana na hakuna atakayeshinda.

    (Tazama: Dilip Hiro, The Longest War, 1991. (2) S. Hersh, New York Times, Jan.26, 1992.)

    M c h e z o n d i o h u o h u o unaofanyika leo Syria, Iraq, Somalia na pengine popote ambapo Waislamu wanapiganishwa proxy war.

    Baada ya kutoka vitani inaelezwa kuwa Iraq iliingia katika mradi mkubwa wa kujenga nchi yake. Haraka haraka ikaimarika kwa kila eneo. Hilo nalo halikutakiwa. Mabeberu wakatafuta sababu ya kuipiga Iraq wairejeshe nyuma zama za kiza. Katika kitabu chake, Hidden Agenda Behind the Gulf War, Pierre Salinger anaeleza jinsi Kuwait ilivyotumika kumchokoza Saddam, ikiwa ni pamoja na kuiba mafuta ya Iraq, mpaka Iraq ikaivamia nchi hiyo. Ikawa sababu

    ya Iraq kupigwa mwaka 1991/93. Clean BreakUpo mpango mkakati wa Israel

    unaitwa, A Clean Break: A New Strategy for Securing the Realm.

    Huu ni mpango makakati ambao kwa kifupi unajulikana kama, "Clean Break" report, ambao uliandaliwa mwaka 1996 ikiwa kama mwongozo wa sera ya Israel ya kumsaidia Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Kufuatia mwongozo huo (policy blueprint) kwa Netanyahu, Marekani nayo ikitumia taasisi yake ya Institute for Advanced Strategic and Political Studies ililazimika kuja na kitu ilichokiita, "Study Group on a New Israeli Strategy Toward 2000", wahusika wakuu wa Study Group hiyo wakiwa ni Richard Perle, James Colbert, Charles Fairbanks, Jr., Douglas Feith, Robert Loewenberg, David Wurmser, na Meyrav Wurmser.

    Ndani ya mwelekeo huo wa sera ya Netanyahu na ufafanuzi wa timu hii ya akina Richard Perle, ndio ndani yake unakuta maelekezo ya kumwondoa Saddam Hussein, na ndipo ikalazimika kusingiziwa kuwa ana silaha za maangamzi. Lakini pia mkakati huo, unagusia Pxoxy war inayoendelea hivi sasa Syria na mambo ya ISIS kuwa ni katika mipango ya kuwatumia wapiganaji wa Kiislamu kuleta machafuko Syria na Iraq na kuzidhoofisha kabisa nchi hizo ili Israel ibakie salama. Kwa mara ya kwanza mpango huo unadaiwa kubuniwa na mzayuni (Zionist strategist) Oded Yinon, mwaka 1982.

    Ambalo tunatakiwa kufahamu hapa ni kwamba, kabla hata ya Marekani kuvamia Iraq kumwondoa Saddam Hussein kwa kisingizio cha kuwa na silaha za maangamizi, mipango na mikakati ya kuigawa Iraq ilishaandaliwa na kuwekewa muda wa utekelezaji (time table) na nani watatumiwa (mujahidina bandia).

    Tazama-U.S. Considers Dividing Iraq Into Three Separate States After Saddam Is Gone-FORECASTS & TRENDS, Oct 1, 2002 na U.S. 2002 Pre-invasion Plan to Divide Iraq Into Three Separate States After Saddam by Gary D. Halbert)

    Kuna mambo mawili makubwa yalitizamwa katika mkakati huo. Mosi ni ule mkakati wa Israel kutaka pasiwe na nchi ya Kiarabu madhubut i ya kupimana nayo ubavu. Pili, akishaondolewa Saddam ambaye alifanikiwa kuwaweka Sunni

    Inaendelea Uk. 12

    MMOJA wa watoto waliojeruhiwa katika inayoendeshwa na ISIS Iraqi.

  • 12 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 201412 MAKALA/Mashairi

    Usiparamie behewa usilojua litokako wala Inatoka Uk. 11na Shia kama taifa moja, hakuna kiongozi yoyote kibaraka ambaye ataweza kuwaleta tena pamoja Shia na Sunni kuwa na serikali imara. Unatajwa mfano wa Afghanistan, a m b a p o h a d i s a s a Rais Hamid Karzai anatawala tu mji mkuu Kabul, unaolindwa na Marekani.

    L a k i n i y a w e z a p i a , w a k i a c h w a wakaweza kujiweka wenyewe wakarudi k a t i k a z i l e z a m a ambapo Iraq ilikuwa kitovu cha ustaarabu k a t i k a u l i m we n g u wa K i i s l a m u , k wa hiyo i futwe kabisa na jina Iraq lisiwepo tena. Kwa hiyo, hata katika kuigawa katika sehemu tatu, ramani i n a y o c h o r w a h i v i sasa inaweka sehemu yenye utajiri mkubwa wa mafuta kuwa kwa Wakurdi ambapo ni rahisi kwa Marekani kuweka kambi zake za kijeshi na kuvuna m a f u t a k u p i t i s h i a Uturuki.

    M a h e s a b u y a Marekani na Israel ni kuwa hata wale ambao w a t a b a k i a k u w a kama Sunni Arabs na Shia Arabs (nchi za Wasuni na Washia), w a t a k u w a d h a i f u n a wa l i o d h i b i t i wa k i a s i k w a m b a hawatafurukuta na mafuta yao, itafaidi zaidi Israel.

    C h a n g a m o t o i l i y o t a j w a k a t i k a kutekeleza jambo hili ni kuwa haitakuwa rahisi kuwashawishi watu wa Iraq wala nchi za Kiarabu na jumuiya ya kimataifa kuifuta Iraq. Kwa hiyo? Lazima kujenga mazingira y a k u w a f i k i s h a Wairaq, Waarabu na walimwengu kuona kuwa hakuna namna ya kunusuru hali, ila kwa kila watu kuwa na nchi yao. Vipi? Vita (proxy war) na mauwaji ya kikatili ya ISIS.

    Ndani ya kutekeleza m k a k a t i h u u w a kuwapata Waislamu

    hamnazo kupigana n a k u u w a w a t u ovyo, ikata jwa pia changamoto nyingine, kuwa ukatili na mauwaji y a t a k a y o f a n y i k a , yatakuwa ya kutisha mno. Ndio hayo unaona w a t u k w a m a m i a wanauliwa na kukatwa vichwa vinatundikwa katika vyuma na miti au hayo ya kutaka kuangamiza Wakristo na Yazid!

    H a t a h i v y o , k a m a a l i v y o w a h i kusema a l iyekuwa Wazi r i wa Mambo ya Nje wa Marekani Madeleine Albright aliposhutumiwa juu ya vifo vya watoto zaidi ya milioni wa Iraq katika miaka ya mwanzo ya 1990s akasema hiyo ni gharama stahiki kwa masilahi ya Marekani; m a u w a j i h a y a y a kikatili ya ISIS nayo ya n a y o o n e k a n a n i gharama stahiki!!!

    Ukisoma uchambuzi w a P e p e E s c o b a r ( U . S . I R A Q E X I T STRATEGY: CIVIL WAR), utaona kuwa ule mkakati wa Marekani wa kulivunja kabisa jeshi la Iraq na kufuta kabisa taasisi za kisiasa, kikiwemo chama cha Baath na kisha kuondoa jeshi lake mwaka 2008

    iki iacha Iraq ikiwa haina jeshi madhubuti, yote ilikuwa katika mkakati wa kufungua mlango wa machafuko, vita ya wenyewe kwa wenyewe na kisha haya ya ISIS, kama hatua ya kutekeleza ule mpango mkakati ulioelezwa katika 1996 "Clean Break"

    Pengine nimalizie kwa kusema kuwa k a m a a l i v y o s e m a R a i s wa M a r e k a n i Barack Obama, kwa hivi sasa Marekani haikusudii kuwapiga n a k u wa a n g a m z i a k a b i s a I S I S , b a l i kuwadhibiti tu kuingia wasipotakiwa. Hiyo inafanyika kwa sababu ISIS hawajakamilisha k a z i w a l i y o p e w a . Wanatakiwa kuuwa watu-Washia, Wakurdi, m p a k a h a s i r a z a Washia nazo zipande sana, wauwane kiasi cha kutosha ndio sasa a je msuluhishi wa kuwasuluhisha Sunni, Shia na Wakurdi. Lakini wakati huo huo, wale ISIS waliokusanywa kutoka nchi mbalimbali, watafutiwe tanuri la kuangamizwa. Wapo watakaouliwa kupitia carpet bombing na wapo watakaolundikwa k a t i k a k a m b i n a magereza ya mateso kama yale ya AbuGhraib, Afghanistan.

    WAKIMBIZI wa Yazid wanaotishiwa kuangamizwa na ISIS.

    Waislamu Dar walaani mauaji Palestina Inatoka Uk. 16Wapalestina huduma za msingi za kibinadamu n a v i t e n d o v y a kinyama vya ukataji na uharibifu wa hifadhi ya maji ya kunywa na kupigwa marufuku bidhaa kwenda nje na kuingizwa ndani ya Gaza, ni mambo ambayo hayakubaliki na wanalaani hatua hiyo.

    W a i s l a m u h a o k u p i t i a m a a z i m i o y a o w a m e s e m a , wa n a l a a n i u k a t i l i endelevu na uvamizi ambao uliwafukuza Wapalestina wanaume, Wanawake na watoto kupitia mauaji ya halaiki na kuharibu mamia ya miji ya Wapalestina.

    Tunalaani unyimaji endelevu wa haki za binadamu wa kurejea k wa m a m i l i o n i ya wakimbizi wa Palestina k we n ye a r d h i ya o ambamo walifukuzwa kikati l i na ambayo ilitaifishwa kwa ajili ya matumizi ya Wazayuni wa Ki - I s ra i l i tu . Imesema taarifa hiyo.

    Taarifa hiyo yenye maazimio yapatayo k u m i , i m e s e m a

    k u w a W a i s l a m u c h i n i y a k a m a t i h i z o wa n a on ye sh a m s h i k a m a n o w a o kwa wapenda uhuru wote, watafuta haki na waungaji mkono wa haki za binadamu wa dunia nzima

    Taarifa hiyo imesema, inalaani mashambulizi ya nguvu ya kijeshi yanayofanywa Gaza, yakijumuisha sehemu za ibada, mahospitalini, mashuleni pamoja na ulengaji wa kikatili wa raia hususan wanawake na watoto.

    Aidha wameeleza kuwa mbali ya kulaani, lakini pia wanatukuza upinzani wa kijasiri wa watu wa Palestina wanaokandamizwa, h u k u wa k i wa o n e a huruma kwa maswahibu yanayowapata.

    Tunawahurumia kwa masaibu yenye k u v u n j a m o y o n a tuna j i funga kat ika kunyanyua sauti zetu na kupinga, lakini t u k i u n g a m k o n o kat ika k i la baraza inayostahiki kusaidia kupatikana kwa haki yao isiyotenganishika. Walieleza Waislamu hao.

    Maalim Seif aomba msaada Ujerumani Inatoka Uk. 16wa pande hizo.

    Balozi huyo aliongeza kuwa anaelewa Zanzibar inazo fursa nyingi za kiuchumi na biashara, i k i w e m o k i l i m o cha viungo na utalii ambazo wawekezaji wa Ujerumani wanaweza k u z i t u m i a k a t i k a kufungua miradi yao.

    Katika mazungumzo yake, Balozi huyo wa Ujerumani ameipongeza Zanzibar kwa juhudi kubwa ilizozichukua kufanikisha maridhiano ya kisiasa na kufikia maamuzi ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

    Akizungumzia suala la utafutaji wa Katiba mpya hapa nchini , B a l o z i K o c h a n k e , alisema wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya mchakato huo na wa n a s u b i r i k u o n a hatua zitakazoweza kuchukuliwa baada ya ku j i tokeza kwa mkwamo katika hatua hii ya Bunge la Katiba.

    Awali Maalim Seif alimueleza Balozi huyo kwa urefu mchakato huo ulipofikia, ikiwemo kasoro zilizojitokeza tangu mchakato huo ulipoanza hadi kufikia sasa.

  • 13 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014

    Inaendelea Uk. 14

    MAKALA

    Obama hapingi Khilafah ya Abu Baghdad. Ni yake

    Inatoka Uk. 10na kidini pia. (Tazama: The Engineered Destruction and Political Fragmentation of Iraq, Global Research, July 01, 2014 )

    Propaganda ya ugaidiP e n g i n e t u a n z e k w a

    k u j i k u m b u s h a m a m b o yafuatayo. Moja ni kuwa uwepo kitisho cha aduni wa nje, (outside enermy), imekuwa ni kisingizio na propaganda ambayo imekuwa ikiendelezwa kupitia vyombo vya habari ikilenga kukuza na kuhuisha kitisho hiki kibaki katika akili za watu na kuwaaminisha kuwa kipo na ni cha kweli. Pili, ni ukwei ambao umethibiti kuwa vita dhidi ya ugaidi na kitisho cha ugaidi wa Al Qaeda, ni kama matofali ya kujenga kile kinachoitwa US-NATO military doctrine, ambayo inakuwa kisingizio cha kuanzisha harakati za k u p a m b a n a n a u g a i d i (counter-terrorism operations Worldwide) na kuingilia kati kama msamaria mwema. Inajulikana pia kuwa, Al Qaeda, na makundi yanayodaiwa kuwa na uhusiano na al-Qaida, yamekuwa yakitumiwa na US-NATO katika migogoro na machafuko mbalimbali, hasa katika nchi za Waislamu kama intelligence assets toka vita ya Afghanistan dhidi ya Urusi. Hivi sasa katika machafuko Syria, Al Nusrah na ISIS, wanatumiwa kama foot-soldiers wa US-NATO. Ni wao Al Nusra na ISIS, wanaofanya kazi ya kutafuta wapiganaji wapya kutoka nchi mbalimbali na kutoa mafunzo. Hali hii imewafikisha watafiti na wachambuzi wa siasa za Marekani kuhitimisha kuwa wakati katika kauli za wazi Marekani inalani ugaidi na kutangaza vita na nchi yoyote wanayodaiwa kuwa inawahifadhi magaidi (harboring terrorists), lakini k a t i k a h a l i h a l i s i , h a o wanaodaiwa kuwa magaidi wanazalishwa na kupewa uhai na nchi hiyo hiyo. Kwa hiyo, katika ujumla wa yote haya, unachoweza kusema ni kuwa kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi ikiongozwa na Marekani (GWOT), inaweka jiwe la msingi kwa Marekani kujipa ruhusa kuwasaka inaodai ni magaidi (Islamic terrorists) popote walipo na kwa maana hiyo, kutoa sababu na uhalali kwa Marekani na washirika wake kuingia na kuingilia nchi yoyote na wakati wowote bila ya kusubiri mijadala katika Baraza la Usalama la Umoja

    wa Mataifa.Hii inatupeleka katika kitu

    kinaitwa: The Caliphate Project and The US National Intelligence Council Report. Juni 29, 2014 kiongozi wa Islamic State in Iraq and Al Sham (Syria)-ISIS, Abu Bakr al-Baghdadi alitangaza kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu baada ya kuteka miji kadhaa ya Iraq. Kufuatia tangazo hilo, wafuasi wa Abu Bakr al-Baghdadi, ambaye anajulikana pia kwa jina la Ibrahim ibn Awwad, hivi sasa wanamwita Khalifah Ibrahim ibn Awwad. Ambacho pengine ni muhimu kueleza hapa ni kuwa agenda hii ya kutangaza Dola ya Kiislamu, ni mpango uliobuniwa toka mwaka 2004 ambapo tunaambiwa kuwa katika kipindi hicho cha utawala wa George Walker Bush, Baraza la Usalama- National Intelligence Council (NIC), la nchi hiyo, lilikuja na mpango ambao ungechochea haya yanayofanyika hivi leo kwa malengo yaliyokuwa yakitaraj iwa. I l i kujenga

    hoja kwa wanasiasa na kada nyingine, ukatengezwa mpango kuonyesha kuwa ikifika mwaka 2020 kutakuwa na wapiganaji wa Kiislamu watakaokuwa wakitaka kusimamisha Dola ya Kiislamu kuanzia Asia, Uarabuni , Ulaya, Afr ika na Marekani. Na kwamba ikifika hapo, huo utakuwa ndio mwisho wa Ukristo na utamaduni wote wa Magharibi kwa sababu wanajihadi hao watakuwa wakiuwa kila asiye Muislamu na kila atakaye wakataa hata miongoni mwa Waislamu. NIC ikatayarisha taarifa ya kurasa 123 kuelezea jambo hilo na namna ya kukabiliana na kitisho hicho ikipewa jina la Mapping the Global Future. Kuibuka kwa ISIS na Abu Bakr al-Baghdadi, na jinsi walivyotangazwa kama watu wanaotaka Dola ya Kiislamu (kwa maana ya PR waliyofanyiwa mpaka kuteka akili za Waislamu kwa sehemu kubwa) na kwa upande mwingine kuwa kila wanapopigana, ama hufanya

    kweli mauwaji ya kutisha au hupigwa propaganda kuwa wa n a f a n ya v i t e n d o v ya kishenzi vya kuuwa watu ovyo, kunaendana kabisa na kile kilichoelezwa kuja kutokea na kwamba ikitokea, hatua gani zichukuliwe.

    Rejea jinsi ISIS wanavyouwa watu walivyongia Mosul na miji mingine ya Iraq. Katika baadhi ya matukio, zinaonyeshwa maiti zikiwa hazina vichwa, vichwa vikiwa vimekatwa na kuchomekwa katika miti. Tizama vile visa vya kuuwa na kuwatimua Wakristo katika miji wanayoteka kisha unganisha na hili la hivi karibuni la kutaka kuwaangamiza watu wa dhehebu la Yazid. Hadi wiki hii, wazee, watoto na akina mama wa Yazid, wanaonyeshwa wa k i wa wa m e j i k u n ya t a milimani bila ya chakula wala maji na mahali pa kujisiri kutokana na jua, mvua na usiku. Kilichofuatia ni kilio na wito kutoka kona zote duniani kuwa jumuiya ya kimataifa iingilie kati kuwanusuru watu hao wasiangamizwe na ISIS. Na ndio hapo Obama akatangaza kuanzisha mashambulizi. (Vuta fikra kwa tukio hili pekee la kutaka kuwaangamiza kabisa watu wa Yazid, Uislamu unatizamwaje hivi sasa na wasio Waislamu!!! Wapi katika historia anaonekana Mtume (s.a.w) au maswahaba kufanya haya.)

    Ukilitizama jambo hili kwa mtizamo wa propaganda, utaona kuwa NIC walibuni jambo hili ili kwanza kuutia doa Uislamu na kuupa sura ya nunda ambalo ni hatari na kwamba ulimwengu mzima unatakiwa kuungana kuliangamiza. Na hili ndilo analosema Prof Michel Chossudovsky pale alipoandika akisema:

    From a propaganda standpoint, the objective underlying the Caliphate project as described by the NIC is to demonize Muslims with a view to justifying a military crusade.

    Ukitoka katika ngazi hiyo ya propaganda ya kuupaka matope Uislamu, hapana shaka sasa unafungua mlango wa hatua ya pili ya kuingia kijeshi kutekeleza kile kilichoelezwa katika ukurasa wa 83 wa mkakati huo wa NIC- Mapping the Global Future. Inaelezwa kuwa ripoti hii ya mpango mkakati wa NIC, pamoja na kuwakilishwa katika Ikulu ya Marekani, Congress na the Pentagon, ilipelekwa pia kwa washirika wa Marekani, Ulaya na hivyo kujenga msimamo

    WAKIMBIZI wa Yazid wanaotishiwa kuangamizwa na ISIS.

  • 14 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014

    Obama hapingi Khilafah ya Abu Baghdad. Ni yake

    MAKALA

    mmoja na wa pamoja kuwa Uislamu na Waislamu ni hatari kwa ustaarabu wa Magharibi/Ukristo.

    Threat emanat ing f rom the Muslim World , kama ilivyodaiwa katika ripoti ya NIC, inaelezwa kuanzishwa mradi wa Khilafah (caliphate project) ambao ndio utakuwa inawapa kisingizio US-NATO kuingia popote kijeshi kupambana na Waislamu, bila kupigiwa kelele na walimwengu kwa sababu ule unyama na ukatili, kama huu unaoonyeshwa na ISIS, tayari utakuwa ushawakinaisha watu. Na kwa upande wa makamanda wa ngazi za juu za majeshi top officials, kila wakati waendelee kuamini kuwa magaidi wa Kiislamu (Islamic terrorists), wanatishia mustakbali wa ulimwengu wa Ulaya/Amerika.

    I k i t i z a m wa k wa j i c h o la ki j iografia, kisiasa na kiuchumi, ni kama alivyosema Dick Chenney wakati akitoa ufafanuzi juu ya ripoti ya NIC mwaka 2004 aliposema kuwa hawa mujahidina wa kusimamisha khilafah watataka kusimamisha dola ya Kiislamu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma Uislamu ulivyotawala kutoka Arabuni, Indonesia, Afrika hadi Ulaya wakidhibiti kila kitu. Ili kukoleza fitna inaelezwa kuwa kuibuka kwa wanaharakati hao wa dola ya Kiislamu kutaibua wimbi jipya la magaidi duniani kote. Kama alivyonukuu Prof Michel Chossudovsky kutoka katika ripoti hiyo ya NIC, kuibuka kwa wapigania Khilafah kutaleta mauwaji ya kishenzi na wimbi la ugaidi kutokea nchi za Kiislamu kwa sababu kila ambaye atakuwa anapinga m p a n g o , h u o a t a k u w a akiuliwa. Ukitizama mauwaji yaliyokuwa yakitangazwa kufanywa, na yanayoendelea kufanywa na ISIS, utaona kuwa yanaendana kabisa na kinachoelezwa katika repoti hii ya NIC ya mwaka 2004. Na kwa hiyo, kuingia Marekani kuanza kuwashambulia ISIS, sio kwa sababu hawa ISIS ni Mujahidina na Marekani haitaki kusimama Khilafah. Sababu ni kuwa hicho ndio kilikuwa kinatafutwa na kilichopangwa toka awali miaka kumi iliyopita kuwa watafutwe watu (mawakala-agents na mamluki-mercenaries) wa kuanzisha varangati la jihadi bandia wauwe watu ovyo, ili yapatikane manufaa ya namna tatu kwa makafiri. Moja kuupaka matope Uislamu. Pili, kujenga uhalali kwa nguvu

    Inatoka Uk. 13

    Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani, Dick Chenney.

    zote za kimataifa kuungana kuupiga vita Uislamu. Tatu, kuwapa makafiri kisingizio cha kuingia mahali popote k u wa p i g a Wa i s l a m u n a kufanya chochote katika nchi husika kwa kisingizio cha kuleta amani na kuondoa ugaidi. Nne, na katika kufanya hivyo, yanapatikana manufaa ya kibeberu- kudhibiti na kupora rasilimali za Waislamu.

    Mradi wa Khilafah (Caliphate Project)

    K a m a i l i v y o t a n g u l i a kuelezwa, uchambuzi wa ripoti ya NIC unaonyesha kuwa kuanzisha harakati za kusimamisha Khilafah kwa njia ya silaha na kuuwa watu kwa kisingizio kuwa wanampinga Khalifah, kutazalisha wimbi la ugaidi ambalo litakuwa ndiyo sababu ya kuhalalisha na kuendeleza Americas Global War on Terrorism (GWOT). La kuzingatia hapa kama walivyoeleza watafit i na wachambuzi mbalimbali ni kuwa, mradi wa kusimamisha Khilafah, kama ulivyo leo mikononi mwa ISIS, al-Nusra

    na wengine, umetengenezwa na CIA kwa ushirikiano na MI6 na Mossad. (Tazama: The Islamic State, the Caliphate Project and the Global War on Terrorism, na Who is Abu Musab Al-Zarqawi? From Al-Zarqawi to Al-Bagdahdi: The Islamic State is a CIA-Mossad-MI6 Intelligence Asset)

    Magazet i ya Austra l ia mwanzoni mwa wiki hii , yalichapisha picha ambazo ilidaiwa kuwa zilichukuliwa kutoka katika mtandao wa mmoja wa mujahidina wa IS, Khaled Sharrouf. Picha hizo zinaonyesha maiti za askari wa Syria waliokatwa vichwa, miili kando na vichwa kando. Kilichowagusa watu wengi, ni pale anapoonyeshwa mtoto wa miaka chini ya kumi akijaribu kunyanyua kichwa cha mmoja wa watu hao waliouliwa na mujahidina wa IS. Gazeti moja likiripoti habari hiyo likasema:

    A shocking image of what is believed to be the young son of an Australian man holding a decapitated head in Syria showed how barbaric the Islamic State (IS) "terrorist army" is.

    Gazeti hilo l i l imnukuu

    Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott akisema mapema Jumatatu, baada ya kuona picha hiyo iliyopigwa kutoka katika mji wa Raqa, Syria na kutumwa katika Twitter ya Khaled Sharrouf.

    Katika picha hiyo ya kutisha, mtoto wa Sharrouf akidaiwa kuwa na umri wa miaka 7 tu, anaonekana akijitahidi kunyanyua kichwa hicho kilichopondwapondwa baada ya kukatwa kutenganishwa na kiwiliwili halafu chini ya picha hiyo kuna maneno ya Khaled Sharrouf, akisema, That is my boy.

    Ik iwa na maana kuwa anafurahiya ujasiri na moyo baridi usioogopa wa mtoto wake huyo wa miaka 7!!!.

    Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott, akiongea na kunukuliwa na redio- ABC radio (Australian Broadcasting Corp. radio), akiwa Uholanzi, amesema kuwa picha hizo zinaonyesha na kuthibitisha "just how barbaric the Islamic State is.

    Akimaanisha ni jinsi gani dola ya Kiislamu ilivyo ya kigaidi yenye ukati l i wa kishenzi.

    "What we've got to appreciate is that Islamic State -- as they're now calling themselves -- is not just a terrorist group, it's a terrorist army and they're seeking not just a terrorist enclave but effectively a terrorist state, a terrorist nation."

    Abbott akaongeza akisema k u w a h a w a I S , k a m a wanavyojiita, sio tu kwamba ni kikundi cha kigaidi, lakini ni jeshi la magaidi ambao wanataka kusimamisha taifa la kigaidi.

    Na kisha akasema: "This does pose extraordinary problems... not just for the people of the Middle East but for the wider world. And we see more and more evidence of just how barbaric this particular entity is."

    Kwamba hawa IS, si tatizo tu kwa Mashariki ya Kati wanakotaka kusimamisha Khilafah yao, bali hatari kwa dunia nzima. Na kwa hiyo akasema kuwa Austral ia i taungana na Marekani , kwanza katika kutoa misaada ya kibinadamu kwa wale wa n a o c h i n j wa n a I S n a kisha katika kuwadhibiti IS. Anachosema Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott, ndicho kilichozungumzwa katika ile ripoti ya NIC mwaka 2004.

    Katika taarifa nyingine kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, babu wa mtoto huyo anaelezwa kububujikwa na

    Inaendelea Uk. 15

  • 15 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 15-21, 2014

    Obama hapingi Khilafah ya Abu Baghdad. Ni yake

    Inatoka Uk. 14

    MAKALA

    machozi baada ya kumwona mjukuu wake akichezea vichwa vya watu waliouliwa na mujahidina.

    Australian grandfather in tears at severed head photo, kinaeleza kichwa cha habari na kusema kuwa mzee Peter Nettleton, ambaye binti yake akiitwa Tara, ni mke wa mujahidina Khalid Sharrouf aliye katika IS, anaitaka serikali ya Australia i fanye ki la l iwezekanalo kumrejesha mjukuu wake huyo.

    Inaelezwa kuwa Khaled S h a r r o u f n i m m o j a wa mamia kwa maelfu ya vijana wa Kiislamu wanaoendelea kupumbazwa na bangi la j ihad bandia na kuingia S y r i a w a k i j i a m i n i s h a kuwa wanapigana jihad ya kusimamisha khilafah Syria ambayo itasambaa duniani kote.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Julie Bishop amenukuliwa akisema kuwa kitendo cha Khalid kumwacha mtoto mdogo wake kuchezea vichwa vya watu waliouliwa, kinaonyesha ni kwa kiasi gani hawa:

    jihadists whose "barbaric ideology" threatened Australia's way of life, na akasema kuwa ni kwa sababu hiyo suala hilo litakuwa agenda kuu katika kikao chake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ambaye alitarajiwa kuwa Sydney Jumanne ya wiki hii.

    Na katika mkutano wa mwaka ujulikanao kwa jina la Australia-US Ministerial Consultations (AUSMIN), Kerry alisema kuwa dunia hivi sasa inakabiliwa na kitisho cha ushenzi na wehu wa mujahidina na hivyo ni lazima ulimwengu wa wapenda amani na watu wastaarabu waungane kukabiliana na mujahidina h a wa a m b a o wa n a t o k a katika nchi mbalimbali na wa k i s h a i n g i a k wa I S I S , wakirejea makwao wanazua balaa.

    Kwa k az i i l iy o fany wa kwa muda mfupi sana na hawa ISIS, ambao baadhi ya Waislamu wamewashabikia kuwa ni Mujahidina, sasa lebo wanayopewa Waislamu na dola ya Kiislamu ni ile ya wehu, ushenzi, ukatili, mauwaji na kila uovu. Ukisoma historia ya Vita ya Msalaba (Crusade),

    h a ya n d i y o ya l i y o k u wa yakifanywa na wapiganaji wa Kikristo kutoka Ulaya. Lakini kila Waislamu waliposhinda, W a k r i s t o w e n y e w e wameandika na kusifu jinsi Wakristo na wote wasio kuwa Waislamu walivyofanyiwa wema na jeshi la Kiislamu. Ilivyo sasa ni kama mkakati wa NIC 2004, unafunika historia na uovu wa Crusade kwa haya yanayofanywa na ISIS. Na hapa izingatiwe kuwa ilichofanya NIC mwaka 2004 ni kubuni scenario, kuwa jaaliya ikiwa hivi, tunafanyaje. Kwa vile kulikuwa na mpango mkakati wa namna ya kuidhibi t i Mashariki ya Kati na nchi za Kiislamu, ikaweka mikakati ya kuunda mazingira halisi ya hilo kutokea katika namna ambayo itasemwa kuwa imetokea kama ilivyotabiriwa au kama wataalamu walivyokisia.

    Kwa hiyo kuibuka kwa ISIS na kisha IS na mauwaji waliyofanya hadi Barack Obama na akina Abbott kufikia mahali pa kusema kuwa hawa IS ni magaidi washenzi wanaohatarisha amani ya dunia, ni jambo lililokwishapangwa. Ni mujahidina bandia na wajinga (fooled foot soldiers) pekee tu na washabiki wao walio katika nchi mbalimbali wanaodhani kuwa haya mambo yanajitokea tu. Na Waislamu kwa hakika hawatakiwi kuwa katika ujinga wa kiwango hicho, kwani matokeo yake ni kujiingiza katika mambo ya kuwaangamiza badala ya kusonga mbele katika kuuhuisha Uislamu na kuleta maendeleo kwa ummah wa Kiislamu na kuonyesha kuwa kweli Uislamu ni rehma kwa walimwengu.

    HitimishoUnaweza kuja na hoja ya

    msingi kabisa kwamba yote haya kwamba IS wanauwa watu kikatili , ni uwongo mtupu. Ni propaganda kama i l ivyokuwa i le ya WMD. Lakini ukisema hivyo, inabidi ukubali pia kuwa Mradi wa Kusimamisha Khalifah chini ya ISIS, unatumiwa na maadui wa Uislamu kuupaka matope Uislamu na kuonekana kuwa Dola ya Kiislamu ni hatari kuruhusiwa kuwepo duniani. Katika Iraq na kisa cha WMD, ni maofisa katika serikali ya Iraq na katika wananchi wa Iraq waliotoa uliodaiwa kuwa

    ushahidi kuwa Saddam Hussein ana silaha za maangamizi, ushahidi ambao Collin Powel aliutumia katika kulishawishi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa idhini kwa Marekani kuipiga Iraq. Ni katika hali kama hiyo, akina al-Baghdadi wanatumiwa hii leo kuwapa kauli akina Abbott kuja na madai kuwa Dola ya Kiislamu ni ushenzi na kitu hatari kwa dunia nzima.

    Lakini pia inabidi urejee nyuma pia utizame ukweli wote. Moja ni yale yanayotajwa katika nyaraka mbalimbali kwamba yalikwishapangwa kama mkakati wa makafiri kupambana na Uislamu na kwa ajili ya masilahi yao ya kibeberu. Utizame