20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1194 DHULQAAD 1436, IJUMAA , SEPTEMBA 11-17, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] Tanganyika si Guantanamo ya kutesa Masheikh Mansour awaliza Waislam MAALIM Seif Sharif Hamad (kushoto) na Mhe Edward Lowassa. MAELFU ya wakazi wa Zanzibar waliohudhuria mkutanao wa uzinduzi wa kampeni za Urais, Ubunge na Uwakilishi wa UKAWA ulifanyika juzi Jumatano katika Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar. Maalim kumrejesha Sheikh Msellem Apokewa kwa Tala' al Badru 'Alayna, Pemba Msiwape kura wasiotaka maelewano - Moyo

ANNUUR 1194.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 1194.pdf

ISSN 0856 - 3861 Na. 1194 DHULQAAD 1436, IJUMAA , SEPTEMBA 11-17, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

Tanganyika si Guantanamoya kutesa Masheikh

Mansour awaliza Waislam

MAALIM Seif Sharif Hamad (kushoto) na Mhe Edward Lowassa.

MAELFU ya wakazi wa Zanzibar waliohudhuria mkutanao wa uzinduzi wa kampeni za Urais, Ubunge na Uwakilishi wa UKAWA ulifanyika juzi Jumatano katika Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar.

Maalim kumrejesha Sheikh Msellem Apokewa kwa Tala' al Badru 'Alayna, PembaMsiwape kura wasiotaka maelewano - Moyo

Page 2: ANNUUR 1194.pdf

2 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Makala

Fethullah-Gulen

“N A p o p o t e u t a k a p o k w e n d a uelekeze uso wako

upande wa Msikiti mtukufu na popote mtakapokuwa e lekezeni nyuso zenu upande wake tumefanya hivyo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale ambao wamefanya dhulma miongoni mwao kwa hiyo msiwaogope na niogopeni mimi, na ili niitimize neema yangu juu yenu na ili mpate kuongoka”. [Al-Baqarah 150].

Baada ya kufika Mtume (s.a.w.) Madina na kuitukuza alipitisha muda wa miezi 16 au 17 na hali ya kuwa anaelekea katika swala zake upande wa Msikiti wa mbali. Ilikuwa Al-Kaaba wakati huo imejazwa masanamu (kama kawaida ya washirikina). Alipokuwa Mtume (s.a.w.) amepelekwa kwa dini ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutoonyesha umuhimu wowote upande

Mafundisho ya Qur’an-Baqara: 150wa masanamu, kwa sababu hiyo alizuiliwa kwa kipindi maalum kuelekea katika wala zake upande wa Al-Kaaba ili aonyeshe msimamo wake wa thabiti na mkazo upande wa masanamu.

K w a u h a k i k a k u n a uhusiano imara kati ya hakika ya Ahmad na kati ya hakika ya Al-Kaaba, na alikuwa Mtume (s .a .w.) anahisi kufuatana na maumbile yake ambayo amemuumba juu yake Mwenyezi Mungu tokea tangu – jambo hilo na anapenda kuelekea upande wa Al-Kaaba na ana shauku kubwa ya jambo hilo, na kuelekea huko na kufanya shauku kumewekwa wazi na Qur’an tukufu:

“Kwa hakika tunaona kugeukageuka kwa uso wako kuelekea mbinguni”. [Al-Baqarah 144]

Ama lengo la Mtume ( s . a . w . ) k u t o k a n a n a kugeuzageuza uso wake kuelekea mbinguni, ni kutaka kwake aweke, Mwenyezi Mungu mtukufu hukumu mpya katika maudhui ya kukibadilisha Qibla. Ndiyo alikuwa anangojea khabari kutoka mbinguni. Kwa sababu hiyo tunaona aya baada ya hapo na mwisho wake inamfikishia habari njema kwa kusema: “Tutakuelekeza Qibla unachokiridhia”. [Al-Baqarah 144].

Jambo la wazi ni kwamba ni vigumu kuifahamu hakika hii na haifahamu isipokuwa mtu kama Mtume (s.a.w.) ambaye alikuwa anauelewa uhusiano huu ulio imara kati yake na kati ya Al-Kaaba.

Ukweli kwa kuelewa kwa maumbile yake.

Ndiyo, ilikuwa hakika ya Al-Kaaba na uhusiano na Mtume, isipokuwa ni kwamba masuala ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu ambayo ndiyo sababu ya kupelekwa kwake, yalikuwa na umuhimu mkubwa sana katika utukufu wa Al-Kaaba na kule kuwa kwake ni Qibla cha swala, kwa sababu hiyo alielekea Mtume (s.a.w.) wakati yuko Makkah katika swala zake upande wa Msikiti wa mbali na akaendelea juu ya utaratibu huo muda mwingine huko Madina vile vile.

Ama, Mayahudi kwa hakika wao, walianza kudai kutokana na kuwa Qibla cha Waislamu ni upande wa Msikiti wa mbali – kwamba wao ndiyo asili na kwamba Waislamu wanawafuata wao, ili wafanye kupitia maudhui hayo hoja kwa dini yao. Na lau angetaka Mtume (s.a.w.) angekigeuza Qibla akakielekeza kwenye Al-Kaaba wakati wa kufika kwake tu Madina.

Isipokuwa yeye hakuwa a k i f a n y a m a m b o k w a matakwa yake na raghba yake, bali alikuwa wakati wote amefungamana na Mwenyezi Mungu mwenye kufanya ikhlasi kwake katika kila jambo. Katika mambo yake anangoja maamrisho kutoka kwake, hali ya kuyapa nguvu maamrisho hayo juu ya matakwa ya moyo wake kwani alikuwa ni mtu wa kilele anayetazamia vipeo vya mbali vya kibinadamu. Isipokuwa yeye hakusahau

kuwa kwake ni mja; Mjumbe anayetekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Kama ambavyo Mtume (s.a.w.) kutokana na kuelekea kwake katika swala yake upande wa msikiti katika swala aliwasha nuru ya uongofu katika nyoyo za watu wengi katika Mayahudi, mifano ya Abdillah Bin Salam, na inawezekana kwamba sifa ya Mtume huyu ilikuwa imetajwa katika vitabu vyao. Kwa hali yoyote ile kwa hakika walikuwepo baadhi ya Mayahudi ambao waliongoka kwenye Uislamu na baada ya miezi 16 au 17 katika kuelekea huko upande wa Msikiti wa mbali makusudiwa yalitimia na haukubakia mikononi mwa watu hawa ushahidi wowote ambao wanaweza kuutumia dhidi ya Waislamu. Maana hakukuwa ni jambo lililo katika uwezo wa Mushirikina kusema:

“ N y i n y i m n a e l e k e a upande wa Al-Kaaba ambayo imejazwa kwa masanamu yetu ikiwa ni hivyo basi dini yetu ndiyo asili”.

Na hakukuwezekana kwa Mayahudi kusema: “Nyinyi mnaelekea kwenye Qibla chetu ikiwa ni hivyo, basi dini yetu ndiyo asili”.

Katika mfano wa mazingira kama haya, il ikuja amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuelekea upande wa Msikiti mtukufu akauthibit isha muungano kati ya dhati ya Mtume (s.a.w.) na dhati ya Al-Kaaba yenye kutukuzwa.

Kuna ishara nyingi katika Agano la Kale katika mambo yanayofungamana na Nabii

I s a ya ( A S ) z i n a a s h i r i a kwamba matukio yatapita k a m a ya l i v y o p i t a k wa sababu baadhi ya Mayahudi walikuwa wanasema kwa kujengea juu ya ishara hizo “Hakika Qibla cha Mtume anayekuja kitakuwa Makkah Ama Muhammad ataacha kuwa anaelekea katika swala zake upande wa Baytul-Almu Qaddasi” Na maneno haya yanatoa mwangaza juu ya baadhi ya pande za maudhui haya.

“Na ili niitimize neema yangu juu yenu”. [Al-Baqarah 150]

M a a n a : k w a h a k i k a kuelekea kwenu katika swala upande wa Msikiti wa mbali kulikuwa ni neema isipokuwa neema ya asili iliyokuwa kubwa sana ilikuwa katika kukutana wapenzi. Maana kukutana kwa Mtume (s.a.w.) – mwakilishi wa umma wa Kiislamu – na Al-Kaaba, na kutoka hapo kupanda baada ya hapo kuelekea Sidrat Al-Mutaha ili afuzu kwa kuipata neema ya Mwenyezi Mungu uso kwa uso na hili linawezekana tu kwa kuelekea upande wa Al-Kaaba. Na cheo ni kama hivyo, atakuwa Mwenyezi Mungu mtukufu ametimiza neema yake na huo ni utukufu, ameuchagua Mwenyez i Mungu kwa utukufu huo umma huu ambao ameeneza juu yake neema zake.

(Imenukuliwa kutoka Kitabu: Miyangaza ya Qur’an katika mbingu ya hisia, cha Muhammad Fethullah Gullen kilichotafsiriwa kwa Kiswahili na Sheikh Suleiman Amran Kilemile)

Tanganyika si Guantanamo ya kutesa Masheikh TANGANYIKA sio

G u a n t a n a m o ya kutesea Masheikh na

watuhumiwa wa ugaidi.A m e s e m a h a y o

mgombea urais kupitia CUF, Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad.

Na kwa maana hiyo, a t a h a k i k i s h a k u w a kanuni za Utawala Bora zinatumika kukomesha ‘Guantanamo’ hizo za kidhalimu.

Maalim Seif Shariff Hamad amesisitiza jambo hilo, ambalo limekuwa likisemwa na kukaririwa na mgombea urais kupitia C H A D E M A , E d wa r d Lowassa.

Akasema kuwa, viongozi wa sasa wa serikali ya CCM wameiuza Zanzibar kwa Bara hali inayopelekea hata kudharauliwa kwa M a h a k a m a K u u y a Zanzibar.

M g o m b e a h u y o wa U r a i s , Z a n z i b a r ,

Na Mwandishi Wetu ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za kugombea urais Zanzibar kupitia chama cha CUF.

Mkutanao huo ulifanyika juzi Jumatano kat ika Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar.

Akitumia msemo ule u l e wa M h e s h i m i wa Lowassa, Maalim Seif amesema, serikali ya CCM imeifanya Tanganyika ni Guantanamo ya kutesea Masheikh na akaahidi kuwa katika mambo ya mwanzo kufanya akiingia madarakani, ni kukomesha mtindo huo wa kunyakua Masheikh na Wazanzibari kwenda kuwatesa Bara.

H i y o n i m a r a y a kwanza kwa Maal im Seif kugusia suala la Masheikh wa Zanzibar toka walipokamatwa na kupelekwa rumande katika magereza za Bara zaidi ya miaka miwili sasa.

A l i s e m a , h i l o n i suala jepesi, linalohitaji tu uzalendo na uelewa

wa mambo kwani hata kwa Katiba na Sheria za sasa, Mahakama Kuu ya Zanzibar ina hadhi sawa na ile ya Tanganyika.

Akashangaa inakuwaje ser ikal i ya Zanzibar , inayoj inadi kuwa ina Rais, kufikia mahali pa kuidharau hata Mahakama Kuu yake kiasi cha kaucha watu wake kunyakuliwa kwenda kuhukumiwa na Mahakama za Tanganyika.

A k a s i s i t i z a k u w a Masheikh waliowekwa r u m a n d e B a r a watarudishwa na kama wana tuhuma za kujibu, basi watafikishwa katika mahakama za Zanzibar.

Akasisitiza kuwa, ili kuweka mambo sawa ya kimuungano na kuondoa mkanganyiko ulioko hivi sasa, kama wataingia madarakani, watarejesha Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ambayo ndiyo yenye maoni ya wananchi.

Na kwamba watapigania kurejea kwa Tanganyika

yenye mamlaka kamili na Zanzibar yenye mamlaka kamili, zikiunganishwa na serikali ya muungano.

“Kama mtanichagua kitu cha kwanza, nawaahidi wananchi wa Zanzibar ni kupata serikal i ya muungano yenye serikali tatu… Zanzibar kuwa n a m a m l a k a k a m i l i na kurejesha rasimu ya Jaji Warioba’’ amesema Maalim.

Katika jumla ya mambo aliyosisitiza Maalim Seif ni pamoja na lile la utawala bora ambapo alisema kuwa mtindo wa janjaweed, watu wanaovaa soksi usoni kuficha nyuso zao wakapiga watu, mwisho wao ni Oktiba 25.

A k a s e m a , a n a t a k a kuijenga Zanzibar yenye amani ambapo mwananchi atakuwa akitembea kifua mbele bila ya hofu.

“Mambo ya watu kuvaa soksi usoni wanapiga watu mwisho Oktoba 25, siwezi kukubali Wazanzibari

wanadhalilishwa ndani ya nchi yao.” Alisema.

Kwa upande wake Mzee Hassan Nassor Moyo amewataka Wazanzibar wasifanye kosa kuwapa kura watu wasiotaka maelewano.

“ N a w a o m b a Wazanzibari mnaopenda amani , kura mt i l ieni Maalim Seif.”

“Viongozi wote Zanzibar wasiotaka maelewano msiwape kura zenu.”

Alisema na kusisitiza M z e e M o y o h u k u akishangiliwa kwa nguvu.

Akiwa Kada mkongwe wa CCM, Mzee Moyo a m e k u wa a k i s i s i t i z a kuwa huu ni wakati kwa Wazanzibari kusahau yaliyopita, wafute siasa za chuki , bal i walete maelewano ili kujenga Zanzibar yenye mamlaka kamili na maendeleo ya kweli.

Kwa mt izamo huo, a l i f a n ya k a z i k u b wa

Inaendelea Uk. 3

Page 3: ANNUUR 1194.pdf

3 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Habari

KAMA ni mabadiliko, wanayahitajia zaidi Waislamu.

Na muda wenyewe wa kuyaleta ni huu katika uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa na Masheikh waliopo katika Gereza la Segerea, Jijini Dar es Salaam, wakiwataka Wais lamu kuzingat ia mustakabali wao kisiasa wakati huu wakielekea katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Masheikh na Waislamu hao wanaotuhumiwa kwa ugaidi, wametuma salamu hizo kupitia mpasha habari wa gazeti hili wakisisitiza kuwa, japo hiv i sasa kuna kibwagizo kuwa Watanzania wanahitaji m a b a d i l i k o , l a k i n i Waislamu wanayahitajia zaidi.

Bali na kama alivyosema M w a l i m u N y e r e r e , haielekei kuwa mabadiliko hayo watayapata ndani ya CCM.

Kwa hiyo, ni wakati kwa Waislamu kupima na kuona kama mabadiliko hayana dalili kuja kupitia chama hicho kikongwe, wayatafute nje ya CCM.

Na mabadiliko yenyewe n i k u o n a k u wa n c h i inaongozwa kwa misingi ya haki na uadilifu ambapo dhulma na uonevu dhidi ya Waislamu unakomeshwa.

M a s h e i k h h a o wamesema, kwa kuzingatia h a l i h i y o Wa i s l a m u wanatakiwa kuwa makini z a i d i k wa k u a n g a l i a C h a m a n a v i o n g o z i watakaowachagua na kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu, mbele yao hakuna chaguo zaidi ya C C M n a U K AWA kwa ngazi zote kuanzia Udiwani, Ubunge pamoja na Uraisi.

Wakizielezea pande hizo mbili (CCM na UKAWA) wamesema, kwa upande wa Chama Tawala (CCM) hakuna Muislamu asiyejua madhila ya Chama hicho kwao, kwani utawala wa sheria umekuwa kipofu na kiziwi usio sikia wala kuona hujuma na dhulma wanayofanyiwa Waislamu.

“Nyinyi mnajua zaidi yaliyotufika chini ya CCM, Waislamu tumedhalilishwa vya kutosha na kunyimwa haki zetu za msingi katika awamu zote za utawala wa chama hicho.”

“ L a k i n i p i a tumejidhulumu nafsi zetu wenyewe kwa kukiuka maagizo ya Mtume (s.a.w) kuwa Muislamu wa kweli haumwi na nyoka mara mbili katika shimo moja.”

Waislamu wanahitaji mabadilikoNa Bakari Mwakangwale “Sisi tumekuwa kila

mwaka wa uchaguzi , CCM inakuwa na uhakika kuwa ina mtaji wa kura za Waislamu.”

Umesema ujumbe toka Segerea ukiwahimiza Waislamu kwamba angalau katika kura zao waonyeshe kuwa hawapo na CCM hata kama wakiingia kwa ‘mabao yao ya mkono’ lakini wawe na uhakika kwamba Waislamu hawapo nao.

W a m e s e m a watuhumiwa hao wa ‘Ugaidi’ walio rumande kwa mwaka wa pili sasa.

W a m e s e m a , h i v i sasa nchi inapita katika kipindi cha mabadiliko

na hiyo haipingiki kwani ni lazima yatokee na kwamba tayari Waislamu wamejitokeza kwa wingi katika kujiandisha hivyo k i l i c h o b a k i n i wa p i waelekeze kura zao kwa lengo la kuweka viongozi watakao watendea haki kwa mujibu wa sheria na Katiba.

Wa k i u l e z e a u m o j a wa vyama vya upinzani U K AWA , wa m e s e m a kuwa, wapo wanaoona k u w a u m o j a h u o umemsimamisha Mh. Edward Lowasa, ambaye alikuwa ndani ya CCM hiyo hiyo.

Lakini wakasema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa

‘Mfumo’ wa Serikali ya CCM, uliopo madarakani n d i o u n a o e n d e l e z a d h u l m a n a u b a g u z i dhidi ya Waislamu kama ulivyowanyima OIC na Mahakama ya Kadhi.

“ H a k u n a k i o n g o z i mwenye ubavu wa kuzuia linalotakiwa na mfumo uliopo ndani ya Serikali ya CCM, suluhisho sahihi ni kuondoa mfumo na kuleta mfumo mbadala utakaotenda haki sawa kwa makundi ya wapiga kura wote, bila kujali itikadi zao kama ilivyo sasa.

“Tusiposhiriki kuleta mabadiliko, tutaendelea kubaki kuwa ni raia wa daraja la pili na idhilali

haitokoma.” K i m e s e m a c h a n z o

hicho, kikinukuu salam za Masheikh kwa Waislamu.

Masheikh hao kupitia chanzo hicho, kikawataka M a s h e i k h M u s s a Kundecha, Mohammed Issa pamoja na Ramadhani S a n z e , k u s i m a ma n a kuunganisha nguvu za Waislamu katika kuelekea katika uchaguzi Mkuu pamoja na kulingania zaidi suala la umoja na amani.

“Tuna waomba sana nyie viongozi, unganisheni nguvu za Waislamu, si sahihi kuwaacha nj ia panda katika kipindi hiki.” Kimesema chanzo hicho kikifikisha salamu hizo kupitia An nuur.

Tanganyika si Guantanamo ya kutesa Masheikh Inatoka Uk. 2k u p i t i a K a m a t i y a Maridhiano kufanikisha kuwakutanisha Maalim Seif na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, hali iliyowezesha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzbar

Hata hivyo, amekuwa a k i p i g w a v i t a n a w a h a f i d h i n a n d a n i ya chama h icho ha l i iliyopelekea kuvuliwa uanachama wake.

Maelfu ya wafuasi na wapenzi wa CUF, na UKAWA wal i j i tokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za urais kupitia CUF, uliofanyika Kibanda M a i t i Z a n z i b a r , j u z i Jumatano.

Katika uzinduzi huo, pamoja na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, viongozi mbalimbali, pia tukio hilo limehudhuriwa na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupi t ia C H A D E M A c h i n i ya mwamvuli wa UKAWA, E d wa r d L o wa s s a n a mgombea mwenza Juma Duni Haji.

Katika salamu zake, L o w a s s a a l i w a t a k a Watanzania, wapenzi wa UKAWA kuondokana na hofu ya kuibiwa kura, ba l i wa j iamin i kuwa watashinda.

“Wakati umefika tukatae dhana ya kuibiwa (kura), wananchi wameamua mabadiliko na lazima tuachane na dhana eti wapinzani wakichukua nchi kutatokea vurugu, hayo ni maneno yasiyokuwa na msingi wowote.” Alisema Lowassa.

Wakati huo huo, Maalim S e i f S h a r i f f H a m a d

jana alipata mapokezi makubwa Pemba, ambayo ya n a s e m e k a n a k u wa hayajawahi kutokea katika historia ya kisiwa hicho.

Umati wa watu kutoka kona mbalimbali za Pemba, u l imiminika kumlaki toka uwanja wa ndege na kumsindikiza kwa miguu hadi uwanja wa Tibirizi, Chake Chake.

Katika waliotia fora katika mapokezi hayo, ni wapiga dufu wakiimba kasida ya Tala' al Badru 'Alayna, ambayo aliimbiwa Mtume Muhammad (s.a.w) alipoingia Madina akihama kutoka Makkah.

Kwa upande mwingine, palikuwa na kundi kubwa la wazee na watu wa makamo wakivalia kanzu safi na

makoti wakimzunguka Maalim huku Masheikh wakitangulia kuomba Dua.

K a t i k a D u a h i y o ya kuomba ushindi na kuiombea Zanzibar baraka na ustawi, waliombewa pia wale wahafidhina waliodaiwa kutoitakia mema Zanzibar kwamba Mungu awazindue waione haki na waweze kuifuata.

WA T U w a l i p i g a kimyaa, wengine wakibubujikwa na

machozi.

Mansour awaliza WaislamNi jinsi Masheikh walivyodalilishwa…Huku viongozi wa CCM, wakishangilia

Na Alghaithiyya, Zanzibar Hiyo i l ikuwa wakat i Mansour Himid akielezea u o v u n a u d h a l i l i s h a j i waliofanyiwa Masheikh huku baadhi ya viongozi wa CCM na SMZ wakishangilia.

A k a s e m a , k u i r e j e s h a CCM madarakani, ni sawa na Wazanzibari kukubali kuendelea kudhalilishwa na kufanyiwa vitendo vya utovu wa adabu.

A k i z u n g u m z a k a t i k a mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CUF, Mansoor Yussuf Himid ambaye ni Mshauri wa Katibu Mkuu wa

Inaendelea Uk. 5

Bi. Aisha Sururu (Katikati) akiongea na wanawake katika semina ya kinamama wa Kiislamu iliyofanyika Markazi Chang’ombe jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Page 4: ANNUUR 1194.pdf

4 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Tahariri/Tangazo

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Program hii itaendeshwa hapa UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL kwa wanafunzi wa Kiislamu wanaojiandaa kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2016 Masomo yafuatayo yatafundishwa na kutahiniwa:1. Elimu ya Dini ya Kiislamu2. Mathematics.3. Arabic language 4. English language5. Introduction to ComputerADA: Tshs 100,000/= kwa program yote (Italipwa yote kabla ya kuanza masomo.)Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni BURE baada ya kulipa ada.Muda wa masomo:Jumatatu - Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi—8:30 mchana.Jumamosi kuanzia saa 2:00 Asubuhi—8:30 mchana Masomo yataanza rasmi tarehe 21/09/2015Jiandikishe kuanzia 11/09/2015 ofisi ya Mkuu wa Shule Ubungo Islamic High School kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:00 mchana .

Wahi mapema nafasi hii adhimu Wabillah tawfiiq

MKUU WA SHULE

P.O.BOX 55105 , TEL: NO 2450069, Mob: No 0687 820895 & 0716 960456 Dar Es Salaam.

Bismillahir Rahmanir Rahiim

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

PRE-FORM ONE PROGRAMITAANZA TAREHE 21/09/2015 - 27/11/2015

YUPO bwana mmoja katutumia ujumbe a k i s e m a k u w a

itakuwa ni jambo la hatari Waislamu kuweka rehani haki zao kwa kina Lowassa na Magufuli. Katika kujenga hoja yake akasema kuwa uraia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una haki z a k e z i l i z o a i n i s h wa kikatiba. Kwamba kila raia wa kundi lolote katika jamii ana haki zote zinazofungamana na uraia wake. Kinga ya haki za kiraia na kijamii, ni Katiba ya nchi. Kiongozi anaweza kuwa na nafasi yake katika dhamana ya utawala. Lakini yeye hawezi kuwa hakikisho la haki za raia.

Akisherehesha zaidi akasema kuwa hivi sasa nchi imeingia kat ika kampeni za kumchagua Rais wa tano wa nchi hii. Katika kipindi hichi, wagombea kupitia vyama vyao watanadi Ilani zao ambazo zi ta jumuisha ahadi mbalimbali pamoja n a s e r a . Wa g o m b e a watakuwa na ahadi nyingi, lakini lazima izingatiwe k u w a h a w a t a w e z a kutekeleza jambo kinyume na Katiba halikadhalika sheria za nchi. Kwa maana hiyo, mgombea yoyote asiaminike iwapo atatoa ahadi ya kufanya jambo ambalo lipo nje ya Katiba na kinyume na sheria zilizopo.

Kwa upande mwingine, h a k i z o t e z a k i r a i a zilizoainishwa kikatiba, zisinadiwe wala kuwekewa ahadi na mgombea kwa sharti la kumpigia kura. H a k i h i z o h a z i h i t a j i kuwekewa ahadi, bali kutekelezwa na yeyote atakayeingia madarakani kwa sababu zilishatolewa na katiba.

Kwa maneno mengine, Rais yeyote, kutoka chama chochote, anakuwa na wajibu wa moja kwa moja kutekeleza haki za kiraia na kijamii. Na kwa maana hiyo basi, Waislamu kama jamii, hawana sababu ya kufungamanisha haki zao kikatiba na kisheria na ahadi za mgombea urais. Kufanya hivyo ni kuziweka rehani haki zao kwani hakuna uhakika wa moja kwa moja kuwa mgombea huyo atashinda.

T u s e m e k u w a t u n a k u b a l i a n a n a y e mia kwa mia. Na labda t u o n g e z e k u w a l a

Waislamu kuambulia patupu UKAWAmuhimu kwa Waislamu ni kuzitambua haki zao na kama uongozi uliotangulia ulikuwa hauwatekelezei, wa j i u l i z e , k o s a l i p o wapi? Kama kosa au mazingira yaliyopelekea w a d h u l u m i w e n a kuhujumiwa yatakuwa n i y a l e y a l e , h a t a kama utakuja utawala mwingine, kwa maana ya kuingia madarakani chama kingine, bado hali ya Waislamu haitabadilika. Na hili ndilo tungependa kulijadili hapa na kutoa maoni yetu.

Kosa liko wapi? Katika kujiuliza swali hilo, lipo jambo moja la kuzingatia. K a m a w a l i v y o s e m a Wa s wa h i l i , u n a we z a kumuongoza ng’ombe mpaka mtoni , lak in i kunywa maji ni hiyari yake. Na hapa tunadhani ndipo lilipo kosa la msingi. Nchi imeweka katiba na sher ia z inazotambua haki za k i la ra ia na inayotamka wazi kuwa ni marufuku kuwabagua watu, iwe kwa dini zao, rangi zao, makabila yao au mahali wanapotoka n.k. Katiba pia imeweka wazi na kutambua haki ya kuwa ama Muislamu, Mkristo na kufanya yote yanayohitajika ndani ya dini uliyochagua. Sasa n c h i / s e r i k a l i i f a n y e n i n i z a i d i ya h a p o ? Kuwalazimisha Waislamu wakatae kubaguliwa na kudhulumiwa? Kama Wa i s l a m u w e n y e w e ndio wanapenda na ndio starehe yao, CCM na Serikali wao wafanye nini! Kwa nini wengine wao hawalalamiki kuhujumiwa haki zao? Kama Waislamu walikuwa wakidhulumiwa na CCM na serikali yake hata katika yale mambo ambayo n i hak i yao kisheria na kikatiba, basi ni Waislamu wenyewe wamependa. Nchi/Serikali imewafikisha kisimani kwa Katiba na Sheria nzuri , lakini haiwezi kuwalazimisha kunywa maji.

Mtadhulumiwa vipi halafu mkubali. Si dini yenu inasema, msidhulumu w a l a m s i k u b a l i kudhulumiwa? Si dini yenu inasema, mumsaidie mwenye kudhulumiwa na pia mumsaidie dhalimu? Wa i s l a m u wa j i u l i z e , wamemsaidia vipi huyu CCM na serikali yake wa n a ye d a i k u wa n i dhalimu toka kadhia za

kunyimwa elimu, MoU, mauwaji ya Mwembechai, mabucha ya nguruwe, OIC, Mahakama ya Kadhi na hili la kukamatwa na kuteswa Masheikh? Mbona hawathubutu kuwafanyia h a y o w a c h u n g a j i , mapadiri na maaskofu. Kwa upande huo ni kama alivyojisemea Alhaji Alli Hassan Mwinyi, Mbunge Muislamu katuhumiwa, kakamatwa na pembe za ndovu akamfunga, lakini akamuonea haya Padiri mwenye kosa hilo hilo, akamuachia huru! Kwa nini Muislamu huyu afungwe na Padiri asamehewe? H i v i M z e e ‘ R u h s a ’ angefanya kinyume chake, a k a m f u n g a M b u n g e Mkristo akamuachia huru ‘Sheikh’ mwenye kosa sawa na la Mbunge huyo Mkristo, angethubutu ku ja kuyasema hayo hadharani? Redio na Televisheni zikirusha ‘live’ kama alivyofanya la Aburabi? Na kama angethubutu, unadhani angemaliza muda wake salama?

Waislamu wamefanya n i n i k u i f a n ya C C M i t a m b u e k w a m b a inavyofanya sio vizuri. Si ni ndio Masheikh hawa hawa wanaitwa katika chai na majukwaa ya kisiasa na kuisifia CCM na viongozi wake? CCM wathubutu k u w a f a n y i a h a y o maaskofu waone? Lakini wanajua, watawafanyia h a y o Wa i s l a m u n a hata mabaya zaidi ya hayo , hakuna lo lo te litakalotokea. Wataendelea kukalia viti vyao kwa raha mustarehe!

Sasa kosa hapa la nani? La CCM au la Waislamu? Na kama hali ndio hii, h a t a a k i j a L o wa s s a , si itakuwa mambo ni yale yale? Mathalani Wa i s l a m u wa k i s e m a k u wa wa t a m c h a g u a Edward Ngoyay Lowassa kwa sababu ameahidi kwamba akiingia Ikulu atatumia Katiba na Sheria za Nchi kuhakikisha kuwa Masheikh walio ndani wanapata haki zao, kama akishindwa kutekeleza na akawabamiza zaidi Waislamu, watafanya nini? Kama ndio hawa hawa ambao wanadai kutendewa isivyo na Serikali ya CCM na wakajikuta hawana la kufanya?

Toka amesimulia yule Ustadh Jamal yaliyomkuta ‘Shimoni’ huku wenzake waliojitaja kuwa ni Sabato na Pentekoste wakiendelea na shughuli zao mitaani h u r i a , M a s h e i k h n a Waislamu kwa ujumla wamefanya nini? Masheikh k i m y a a ! ! ! Wa n a o n a muhimu kwanza wampate Mufti wao! Ili afanye nini? Labda akamalizie biashara i l iyoachwa na Muft i

aliyetangulia ya kuuza eneo la Wakfu, Kinondoni Muslim!

Tujiulize, hivi ingekuwa ni ki jana wa Kikristo a m e s i m u l i a k u w a amekutana na Pol is i akawaachia wenzake wawili waliojitambulisha kuwa ni wa Madh’habi ya Shafii na mwingine, Ibadh, ila yeye kwa vile kavaa Msalaba shingoni, a k a r u s w a k i c h u r a kuingizwa katika ‘difenda’ kuelekea ‘Guantanamo’ Via ‘Shimoni’, Maaskofu wangekuwa kimya mpaka leo? Wabunge Wakristo, vyama vya siasa, taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) na vyombo vya habari, wote hawa, wangekuwa k i m ya m p a k a s a s a ? Kampeni hizi za akina Lowassa na Magufuli zingekuwa zikiendelea tu na hali ikiwa shwari kabla serikali haijasema kuwa imemfanya nini askari yule?

Kuna yule mwanamke Muislamu aliyekamatwa kwa kuwa mtuhumiwa wa ujambazi alijificha upenuni mwa nyumba yake, akiwakwepa polisi. Akateswa kikat i l i na katika namna mbaya ya kumdhalilisha. Kuachwa akiwa katika hali zake bila ya maji wala cha kujihifadhi, mpaka siku zake zikaisha! Tuseme Tanzania Media Women's Association (TAMWA), T a n z a n i a G e n d e r Networking Programme Mtandao(TGNP Mtandao), Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA), Legal and Human Rights

Centre (LHRC) na wengine kama hao hawajasema. Inaweza kueleweka. Na akina mama wa Kiislamu je? Kuna Baraza la akina m a m a wa K i i s l a m u , kuna vitengo vya akina mama katika BAKWATA, Baraza Kuu, na wasomi, wataalamu Waislamu-T a n z a n i a M u s l i m Professionals Association (TAMPRO) wakiwemo wanasheria wanawake n d a n i y a k e ! K i p i kinawashinda kulichukua suala hili, kulijengea hoja na kulishughulikia!

Ukijiuliza maswali haya ndio utajua ukweli kwamba aje Lowassa au Magufuli, Waislamu hawana chao maana wenyewe ndio wamejiweka kihivyo. Kila atakayekuja atabamiza apendavyo, wakibaki kushangilia na kupiga kofi.

K a m a L o w a s s a n i m a b a d i l i k o , n a mabadiliko ni Lowassa, basi mabadiliko haya hayatakuwa na maana yoyote kwa Waislamu muda wa kuwa Waislamu wenyewe hawajabadilika kwanza. Tutawalaumu bure akina Magufuli na Lowassa kumbe tatizo ni sisi wenyewe.

Na hii ndiyo kanuni ya Qur’an. Mabadiliko ya Lowassa au muendelezo wa sera za CCM chini ya Magufuli, yatatunufaisha vipi wakati nyoyo zetu na hali zetu ni zile zile tukiwa chini ya makucha ya CCM ya Nyerere , Mwinyi , Mkapa na Kikwete?

Page 5: ANNUUR 1194.pdf

5 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

GHARAMA za kifedha z i t a k a z o t u m i k a kuwahudumia watu

wanaotafuta hifadhi nchini U j e r u m a n i , z i n a we z a kufikia Euro zisizopungua b i l i o n i k u m i i f i k a p o mwishoni mwa mwaka huu, kiwango ambacho ni mara nne ya kile kilichotumiwa na serikali ya Berlin mwaka jana kwa ajili ya wakimbizi.

Ofisi ya takwimu ya Ujerumani imeripoti kuwa Euro bilioni 2.4 zimetumika kuwahudumia wakimbizi wapya 203,000 waliongia nchini humo mwaka jana.

M k u t a n o k u h u s u Wakimbizi ul iofanyika m w e z i J u l a i k w a kusimamiwa na Bunge la Ujerumani ulikadiria bajeti ya Euro bilioni 5.6 kwa ajili ya kuwapokea wakimbizi 450,000, huku wimbi la hivi karibuni la wakimbizi kutoka eneo la Mashariki ya Kati na Afrika likipita makadirio ya awali.

Wakimbizi wasiopungua laki nane wanatazamiwa kuwasili Ujerumani hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Katika siku za hivi karibuni maelfu ya wakimbizi kutoka Syria wamefanikiwa kuondoka Hungary baada ya kukwama nchini humo kwa siku kadhaa na sasa wanaelekea Austria na Ujerumani nchi ambazo zimetangaza kuwa tayari kuwapokea.

Wakati hali ikiwa hivyo, Shir ika la Kuhudumia W a k i m b i z i D u n i a n i UNHCR, limezitaka nchi za Ulaya zichukue wakimbizi laki mbili.

“Nchi za Umoja wa Ulaya lazima zikubali kuwapa hifadhi wakimbizi laki mbili kama sehemu ya ‘Mkakati wa pamoja’ wa kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi duniani”.

Hiyo ni kauli ya Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Antonia Guterres, ambaye amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kutumia nguvu zao zote kutatua mgogoro uliopo.

Hayo yamejiri wakati ambapo mwishoni mwa wiki maelfu ya wakimbizi kutoka Hungary wameingia nchi jirani ya Austria.

S e h e m u k u b w a y a wakimbizi hao ambao ni kutoka Syria, wanatazamiwa k u e l e k e a U j e r u m a n i . Austria imesema wakimbizi 6,000 wameingia nchini humo na wengine wengi

Ujerumani kutumia Euro bilioni 10 kwa wakimbizi

wanatarajiwa kuwasili katika kile kinachotajwa kuwa na mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu vita vya Yugoslavia katika muongo wa 1990.

U l a y a i n a k a b i l i w a na wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambapo watu 300,000 wakiwa wameyaweka maisha yao hatarini kuvuka Bahari ya Mediterenia na kueleka katika nchi za bara hilo mwaka huu pekee. Wakimbizi hao ni kutoka nchi za Afrika na Mashariki ya Kati.

Za id i ya watu 2 ,600 wamefariki dunia wakijaribu kuvuka bahari hiyo, akiwemo mtoto wa Syria aliyeitwa Aylan Kurdi, aliyekuwa na umri wa miaka mitatu, ambaye picha ya maiti yake iliyoonekana akiwa amelala pwani nchini Uturuki baada ya kusombwa na maj i , imeibua huzuni kubwa katika nyoyo za watu kote duniani.

Rais Vladimir Putin wa Urusu amesema mgogoro huo wa wakimbizi umesbabishwa na sera mbovu za Umoja wa Ulaya, kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Rais Vladmir Putin alisema I jumaa i l iyopita kuwa, mgogoro wa wahamiaji unaolikabili bara Ulaya kwa

Rais Vladmir Putin

sasa umetokana na sera mbovu za kigeni za nchi za bara hilo, hususan zile ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU).

Kiongozi huyo alisisitiza k u w a , u i n g i l i a j i w a Wamagharibi katika mambo ya ndani nchi za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika ni moja ya sababu za kuibuka mgogoro wa wahajiri katika nchi za EU.

Rais Putin alisema viongozi wa Ulaya wameingia kwenye mtego wa Marekani kwa kukubali kufuata kibubusa sera zake, hususan katika ulimwengu wa Kiislamu na

kwa mantiki hiyo migogoro ya kisiasa katika nchi za Syria, Libya, Somalia, Yemen na kwingineko imewafanya raia wa nchi hizo kukimbilia usalama wao barani Ulaya.

"Wanawatwisha watu sera zao kwa lazima bila ya kujali itikadi zao za kidini, utamaduni wao na muundo wa jamii. Hilo lazima litaleta matatizo makubwa", alisema Putin.

Ra is huyo wa Urus i ametahadharisha kuwa, EU na Marekani zisipobadili sera zao za kigeni, mgogoro huo utakuwa mpana zaidi katika siku za usoni. Irib.

Mwanzilishi wa tovuti ya whistleblower J u l i a n P a u l

Assange, ametoa siri ya makubaliano yaliyofanywa na nchi za Qatar, Uturuki na Saudi Arabia ya kuiangusha serikali ya Syria.

Assange alifichua siri hiyo katika televishen ya Urusi akisema kuwa, makubaliano h a y o ya l i p i t i s h wa n a kusainiwa kwa siri mwaka 2012 na nchi hizo tatu, huku nchi za Magharibi kama vile Ufaransa, Uingereza na Marekani wakiunga mkuno makubaliano hayo.

Aidha alisema washirika wa Marekani katika nchi za Mashariki ya Kati walisaini makubaliano hayo kwa ajili ya kukuza uhasama dhidi ya serikali ya Syria, kiasi kwamba serikali ya Saudi Arabia ili kuonyesha uhasama wake, i l i f ikia hatua ya kukiuka hata mapendekezo ya waanzilishi wa fikra hiyo ambao ni serikali ya Marekani katika suala hilo.

Uthibitisho wa kuwepo m a k u b a l i a n o h a y o n i miungoni mwa nyaraka nyingi za siri , ambazo zimeonyesha uovu wa baadhi ya mata i fa na serikali za Mashariki ya Kati zinazotafuta nguvu kibabe ikiwemo msimamizi wao mkuu (utawala Saudi Arabia).

Qatar, Saudia zilikubaliana kuibomoa Syri- Assange

Habari za Kimataifa

Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad a l iwataka Wazanzibar i k u t o k u b a l i k u e n d e l e a kuwaunga mkono watu ambao wanahus ika na udhalilishaji wa Masheikh.

M a n s o o r a l i s e m a n i j a m b o l a k u s i k i t i s h a kuona wapo baadhi ya v i o n g o z i w a n a p a n d a majukwaani na kufurahia kile kinachotendeka dhidi ya Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho ambao kesi yao imekuwa ikipigwa kalenda kila siku badala ya kusikilizwa na kupewa hukumu kwa mujibu wa makosa yao.

“ N d u g u z a n g u Wazanzibari, msije kukubali hata siku moja kuwarejesha madarakani viongozi wote wanaochangia au kufurahia udhalilishaji wanaofanyiwa Masheikh zetu, leo hi i a n a s i m a m a k i o n g o z i jukwaani na kufurahia

Mansour awaliza WaislamInatoka Uk. 3 k i l e w a l i c h o f a n y i w a

Masheikh wetu hivi nani hajui kama Masheikh wetu wamedhalilishwa na ku…” amesema huku akionesha uchungu.

W a k a t i M a n s o o r akiyasema hayo, uwanja u l i k u w a k i m y a w a t u wametulia wakimsikiliza kwa makini namna anavyojenga hoja na kuonesha kwamba alichokuwa akikizungumza kikiingia akilini mwao.

M a n s o o r a m e h o j i w a t u w e n y e k u j i i t a wana Mapinduzi, lakini wakashindwa kuyatekeleza malengo ya Mapinduzi ambayo yameasisiwa na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambapo alitaka wananchi wote kuishi bila ya ubaguzi.

“Ni jambo la kushangaza ndugu zangu, vikosi vya ulinzi na usalama ambao wa m e p o t e z a r o h o z a o kwa ajili ya Mapinduzi na

kutaka kujitawala, leo hii wao ndio wanahusika katika kuwadhalilisha Wazanzibari, w a o n d i o w a m e k u w a w a k i w a d h a l i l i s h a , w a k i w a k a s h i f u n a wakiwanajisi Wazanzibari, inasikitisha kuona vikosi h i v y o h i v y o l e o h i i wakiwatesa Wazanzibari, wakiwapiga wakiwavua nguo ndugu zetu wa kike na kuwakadhifu hadharani, inasikitisha sana na baadhi ya viongozi wanapanda majukwaani wakifurahia na kucheka, tunaelekea wapi ndugu zangu?” Alihoji Mansoor.

Mansoor alisema viongozi wa aina hiyo hawafai kupewa n a f a s i t e n a ya k u r u d i madarakani kwa sababu wakirejeshwa wanaweza k u ya f u r a h i a t e n a ya l e matendo mabaya waliokuwa wakifanyiwa Wazanzibari ya

kudhalilishwa utu wao.Alisema kwa sasa haoni

kama kuna kiongozi wa C C M a m b a ye a t a we z a kurejesha heshima na hadhi ya Zanzibar.

H i v y o a m e w a t a k a Wazanzibari kumuunga m k o n o M a a l i m S e i f wampitishe kwa kumpa k u r a n y i n g i i l i a we z e kuirejesha hadhi na heshima ya Wazanzibari ambayo imepotea kutokana na mfumo mbovu uliopo unaoongozwa na chama cha mapinduzi.

Mansoor alisema jambo la msingi kwa wote na Watanzania ni kurejeshwa kwa mamlaka kamili ya Zanzibar na mamlaka ya Tanganyika ambapo alisema viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ndio watakaoweza kutetea Muungano wa usawa na haki.

Page 6: ANNUUR 1194.pdf

6 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015Makala

NI A N Z E k w a k u m s h u k u r u Allah (S.W.) kwa

kukumbuka kuanzishwa kwa shule ya awali katika Msikiti Mkuu wa zamani wa Same mjini. Uanzishwaji wa shule hii ulitokana na Ijitimai ya kitaifa iliyofanywa Mkoa wa Kilimanjaro Wilayani Mwanga chini ya uongozi wa Tablighi ya kituo cha Gongolamboto jijini Dar es salaam. Niliteuliwa n a A m i r i wa M k o a wa Kilimanjaro Bw. Atumani, kuhamasisha Waislamu wa Wilaya ya Same, na kusambaza kadi za mualiko.

Tulifanikiwa katika Msikiti wa Same kukodisha basi lililojulikana kwa jina ‘Sirori’ la Bw. Habibu Mndeme (marehemu). Tulijaza gari tukiwa na viongozi wa Bakwata wa Wilaya, akina mama, kina baba na vijana. Ijitimai hiyo ilifanyiwa katika eneo ambalo ni kiwanja cha ekari arobaini 40, ambalo lilikuwa ni la kujenga Kituo cha Tablighi , Shule na Chuo cha dini ya Kiislamu. Mahudhur io ya l ikuwa makubwa kiasi kwamba Station Master aliombwa na akakubali kuwa treni iliyobeba Waislamu kutoka Mombasa isimame chini ya eneo hili liliopo karibu na barabara ya kwenda Lang’ata, na ikasimama Waislamu wakashuka.

Walihudhuria Waislamu wa n c h i m b a l i m b a l i waliwemo wa Zambia n.k. Kul ikuwa kumejengwa sehemu ya kuwekwa jiwe la msingi, na mgeni wa heshima wa kuweka jiwe hilo alikuwa mi Mufti Hemedi bin Juma (Al-marhum). Nilipiga picha za shughuli zote zilizofanyika kwa muda wa siku tatu. Lakini sasa maktaba yangu inanisuta na kuwasuta Waislamu.

Kundi la Matabl ighi la kima mama walifanya kazi kubwa sana tena sana Allah S.W. Awalipe ujira wao Insha’allah. Wakina mama wa Msikiti wa Same chini ya kiongozi wao Fatuma Kasagho tuliporudi Same, nilikuwa Katibu wa Msikiti huo, aliniambia kuwa niwaelekeze j insi ya kuanzisha Shule ya chekechea hapo Msikitini, maana waliyoyasikia katika Ijitimai yanatosha, kwani kumbe kuwapeleka watoto wa Kiislamu katika chekechea za Kanisa ni kuwaritadisha. Palitokea msuguano na uongozi wa Msikiti kwa upande mmoja na Mtaa na Wilaya kwa upande mwingine, B a k wa t a , wa k i s e m a k u w a w a o h a w a k o tayari kendesha shule. Hawana pesa, hawana u w e z o . H a t a h i v y o kina mama wakasema kuwa wata j i tegemea wao kama kina mama katika kuendesha shule hiyo, kama kina baba

Viongozi Bakwata Mwanga mtajibu nini kwa Mola wenu

watawasaidia ni hiyari yao.

I l i p o f i k a m w a k a wa 1991 Mama huyo kiongozi, aliwahamasisha kina mama wakawatoa watoto wote waliokuwa wakisoma katika Kanisa na tukaanzisha Shule hiyo ambayo imesimamiwa na kina mama mpaka leo ina robo karine. Nasema Alhamdul i l lah k isha Alhamdulillah. Maktaba yangu inanisuta! Kwa sababu ninazo kumbu k u m b u z a p i c h a z a Wahadhiri mbalimbali waliohadhiri wakati huo; na ya aliyekuwa Mufti wakati huo Sheikh Hemedi bin Juma, wakati akiweka jiwe la msingi la kituo hicho; na kanda za kasseti nilizorekodi zinanisuta, kuwa kwa robo karine, eneo lile ambalo Matablighi

walijenga majengo zaidi ya matatu yakafikia hatua ya kupauliwa, lakini viongozi wa Bakwata Mwanga wakasema eneo lile ni la kwao ukazuka mvutano wa kesi kiasi kwamba Tablighi waliacha eneo lile baada ya kesi ya miaka mingi, wakaenda kuomba eneo jingine.

B a a d a y a m i a k a k a d h a a , n i l i k u w a na hamu ya kwenda kuona kilichoendelea. Nilikuta pori na zile kuta za yale majengo waliyojenga Matablighi z i k i w a z i m e a n z a kuyeyushwa na mvua. Bakwata waliopigania eneo hilo kuwa ni lao hakuna walichofanya. Nilizichukua picha hizo hapo. Baada ya robo karine nilienda tarehe 27/08/2015 kushuhudia maendeleo

yaliyofanywa na Viongozi wa Bakwata Mwanga. Innalillahi wa innailaihir rajiuun. Hakuna kitu. Nikajiuliza, kwa nini waliwapora eneo l i le Tabligh mpaka kupeleka kesi mahakamani?

K a t i k a e n e o l i l e , nilikuta kimebaki kile kisehemu kilichojengwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, kwa kuwa kijengwa kwa matofali ya sementi, nacho kimechoka hata lile jiwe la msingi limeanza kubomoka kama linavyoonena katika picha na mandhari yake. Na yale majengo yaliyokuwa yamejengwa kwa matofali ya kuchoma na Matablighi, ya m e b o m o l e wa y o t e k i a s i k w a m b a h a t a misingi yake haionekani, a m b a p o M a t a b l i g h i walishapeleka mbao za

kupaulia, na baadhi ya majengo walishaweka fremu na kuezeka kama inavyoonekana kwenye picha.

Na eneo limekuwa ni makorongo, na sehemu ya eneo na jiwe la msingi ni uwanja wanachezea mpira watoto wa shule. Nilipouliza kwa robo karine sasa, Bakwata wana mpango gani na eneo lile walilowanyang’anya Tabligh, sikupata jibu. Labda tu niwakumbushe viongozi wa Bakwata wa Wilaya ya Mwanga kuwa, kila kitu tulichofanya n a w a n a c h o f a n y a kinarekodiwa, na mwenye sifa ya kujua kila kitu-Allah Subhana wa Taaallah. Na siku ya Qiyama sio picha nilizopiga katika ile Jitimai wala hizi nilizopiga kwa mara ya pili na ya tatu zitakazoonyesha kama ushahidi wa kilichotendeka na kinachotendeka mahali pale; bali ni kila aliye kwamisha mradi ule wa kituo cha Tablighi atajibu. Kama ni kwa Qibri chake, ukubwa wa cheo chake, ukubwa wa elimu yake, umaarufu wake kwenye d o l a n a u w e z o w a kuwachangisha Waislamu p e s a z a k u e n d e s h e a k e s i z i l i z o k wa m i s h a maendeleo yao kama haya ya robo karine, yote hayo yatawekwa wazi siku ya hukumu.

Nimalizie kwa kusema k u w a , 1 9 9 2 i l i a n z a k u t a f u t wa A r d h i ya kujenga Kituo cha Kiislamu Same Kirinjiko, 1994, eneo likapatikana. Kazi ya kufeka eneo ilianza, na ujenzi ikaanza 1996 na Shule ikaanza 2000. Sasa ni kituo kikubwa cha Kiislamu kikiwa na shule ya msingi, sekondari na chuo cha ualimu. Vijana wa Kiislamu wanahitimu kila mwaka katika ngazi mbalimbali.

M a k t a b a y a n g u inanisuta! Kuwa, katika Wilaya ya Mwanga juhudi z i le z imekwamishwa na Bakwata. Wasiwasi w a n g u m k u b w a n i pale niliposhiriki futari Mwanga mwaka jana na kiongozi aliyetualika futari hiyo akatoa ahadi kuwa itafutwe Ardhi yenye wasaa ya kujengwa s h u l e n a c h u o c h a Kiislamu, ataleta marafiki zake wasaidie kujenga chuo hicho lakini hadi sasa sijasikia chochote. Sijui kuwa katika futari ya mwaka huu kulikuwa na mrejesho gani. Allah S.W. atuzindue katika kiza hiki totoro cha kiuongozi w i l a y a n i M w a n g a Insha’allah.

(Khatibu Juma Mziray. 0757 01 33 44. 31/08/2015)

JIWE LA MSINGI LILOWEKWA NA MUFT HEMED LILIVYO KWA SASA

MAJENGO YA SHULE YALIYOJENGWA WAKATI WA HARAKATI ZA MARKAZ MWANGA.

Page 7: ANNUUR 1194.pdf

7 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015MAKALA

NIANZE tu kwa k u s e m a I n n a a Lillah Wa-Innaa

Ilayh Raji’un. Hivi ndivyo alivyotufundisha Allah (swt) katika Suratul – Baqara [02:156] aliposema, “Wale ambao ukiwasibu msiba husema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea”. Aya hii imewalenga wale wenye kusubiri pindi wanapopatwa na msiba. Kumradhi kwa msemo nilioanza nao.

Waislamu tumeingia katika mtihani mzito wa kulazimishwa kupenda j a m b o m o j a k u b w a ambalo Allah Mtukufu ametuwekea kama njia ya kuingia katika maisha ya milele. Nasema hivi kwa sababu jambo lenyewe lipo lakini tunaliogopa mno, nalo ni kifo. Hali inatisha, inasikitisha, inaumiza, inachosha, inamaliza upeo wote wa kufikiri!!? Kifo ni njia pekee ambayo Allah (swt) ameiweka ili iwe njia pekee ya kukutana naye na kumuona ikiwa t u t a f a n i k i wa k u p a t a mwisho mwema. Siyo wote watakaofanikiwa kumuona Allah (swt).

A l l a h M t u k u f u anasema, “AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.” (Qur-An 67:01-02).

Ndugu zanguni, kwa hali iliyopo, hatuna sababu ya kuipenda dunia. Mimi sikusuii kupenda dunia lakini nikuulize swali moja wewe unayetamani kuishi sana. Ukane imani yako uishi, au udhihirishe imani yako uuwawe? Kumbe mavazi, ndevu, na majina yetu sasa ni tiketi ya kifo, kuteswa, kudhalilishwa!!? Kupigwa, k u t e s wa , k u d u n g wa sindano tunaona ni jambo dogo siyo? Hizo sindano wanazodungwa ndugu zetu hatujiulizi zina nini? Tusubiri nasi yatukute.

Vyombo vyetu leo vinavyojiita vya usalama havina haja tena ya kufanya

Tusilazimishe ndoa kama hatupendwi!Na Juma Jumanne upelelezi, bali wanaishia

tu kuangalia mwonekano wa n j e . U k i o n e k a n a umebeba jembe, basi moja kwa moja wanasema huyu ni mkulima? Mtu unajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu kwa sababu hali inatisha. Mambo yanayofanyika ni mazito na ukijaribu kunasibisha hali hii na namna tunavyochakarika mtaani, ni vitu viwili tofauti.

L a k i n i t u t a m b u e k u w a , k w a h a k i k a hakuna mwanadamu a t a k a y e e p u k a n a n a kifo. Hawa madhaalimu wanaowatesa ndugu zetu watambue kuwa yupo Mfalme wa haki! Yupo Jabaar. Yupo Qahaar!! Watutese , watufanye wa n a v y o t a k a l a k i n i w a t a m b u e k w a m b a watawaua Waislamu lakini Uislamu utabaki kwa kuwa aliyeuleta hana sifa ya kufa! Hana sifa ya kusinzia wala kula. Wasubiri punde tu watakutana na adhabu za Allah aliye juu.

A l l a h M t u k u f u anasema, “Kabla yenu zimepita nyendo nyingi; basi tembeeni kat ika ulimwengu muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanao kanusha” [Qur-an: 03:137].

Misri siyo mbali, wafike washuhudie aliyejifanya mungu anavyodhalilika. W a m u o n e F i r ’ a u n aliyejiita mungu. Fir’aun aliyewatesa wana wa Israili kwa kuwapa kazi ngumu, kuwaulia watoto wao na kila aina ya madhila. Yeye na jeshi lake wote waliangamizwa.

P a m o j a n a h a l i kama hii, lakini bado Waislamu wanaipenda CCM. Wanawapenda w a n a - C C M ! J a p o hujidai tunawachukia, cha ajabu tukikutana kwenye siasa tunagonga ‘cheers’! Tunawasaidia kufanikisha azma yao ya k u e n d e l e a k u k a a Ikulu. Kinachotufanya tujipendekeze kwa hawa madhaalim ni kipi haswa!? Anayetoa riziki yupo, au hayupo!!? Ipi tofauti yetu na mwanamke anayejidai hampendi mumewe ilhali wat o t o wanaende lea kupatikana!!? Anajidai kumsema vibaya mumewe, lakini mimba zinaingia na watoto wanapatikana.

N i n y i W a i s l a m u mnaoipenda CCM hii, ni kwa sababu ya elfu

tano mnazopewa kipindi cha kampeni au mna ajenda nyingine. Hivi ni kweli tamaa zetu ndio zimetufikisha hapo!!!?

Siku moja nipo maeneo ya stendi, nasubiri mzigo k u t o k a M b e ya , k wa pembeni yangu alikuwepo dereva bodaboda akasema yeye yupo tayari kupigia kura jiwe kuliko kuipigia CCM. Kwa msis i t izo akasema:

“ K w a n a m n a nilivyoichoka CCM, hata k i k i k o s e k a n a c h a m a p i n z a n i i k a wa j i w e limesimamishwa dhidi ya CCM, mimi nalipa jiwe kura yangu”.

S i k u t a k a k u d a d i s i sana kwa kuwa, hakuna jipya alilosema zaidi ya kuongeza nguvu katika k i le n inachokiamini . Maslahi binafsi, ulafi, unafiki na mengineyo ndiyo yanayotufanya tuendelee kuipenda CCM. Tusilazimishe ‘ndoa’ kama hatupendwi, hatupendwi tu. Ya nini tujipendekeze.

Leo nakubali kupiga kampeni, siyo kumpigia Lowassa bali kampeni ya kutoipigia kura CCM. Aliyosema Ustadh Jamal Yasin itoshe kuwa kampeni ya kuifuta CCM.

K a t i k a g a z e t i l a Mzalendo toleo nambari 2308 la Jumapili Agosti 30 – Septemba 5, 2015, kwenye ukurasa wa mbele kabisa wanasema; ‘Rekodi ya Dk. Magufuli Dar yamshinda Lowassa’. Akaendelea kusema kwamba, Lowassa a t u m i a d a k i k a n a n e kuzungumza, ilani ya ukawa yakosekana, lakini kama haitoshi wakasema

eti ashindwa kuzungumza atakavyotatua changamoto za wananchi.

H i v i n d i v y o waandishi wa gazeti hili walivyoandika. Lakini mimi niseme tu kuwa, suala la kutumia muda mchache s i y o t a t i z o k wa n g u , kwa sababu kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti kabisa. Hata kama Lowassa angesimama na kusalimia tu, kisha akakaa kitako bado nampa b ig up . Kwani CCM wameanza lini kusimama na kuzungumza, mpaka wametuundia TOT ya mipasho kutupumbaza kwa maneno yao, lakini hakuna kitu!? Mara ngapi CCM wanasimama na ilani yao na wanayofanya ni vingine kabisa? Lakini suala la kutozungumzia namna atakavyotatua changamoto pia halina nafasi kwenye kampeni hii. Sisi tunachotaka ni utatuzi wa changamoto na siyo kujua namna z i t a k a v y o t a t u l i w a . Hata kama akisimama kutangaza tu kwamba, msiipigie kura CCM, b i n a f s i n a m u e l e w a kwa kuwa mimi siyo mhamiaji bali raia wa nchi hii . Waliyofanya CCM na wanayoendelea kutufanyia Waislamu h a ya h i t a j i i k a m p e n i jamani!!

Kusema kwamba Dk. M a g u f u l i a m e t u m i a muda mrefu (dakika 58), ndio tayari ameshatatua changamoto hizo? Mambo aliyokuja nayo mgombea wa CCM yana upya gani? Tumechoshwa na maneno, tunataka kuona utendaji.

Hata kama angetumia siku nzima kuzungumza pale uwanjani, kwetu sisi wenye kujua hali iliyopo, tungeona hana jipya tu.

Lakini pia, kusema kwamba kauli za viongozi w a d i n i z i l i o n e s h a kununuliwa, sina haja ya kujua wamenunuliwa kwa bei gani. Kwenye nukta hii niwakumbushe tu waandishi hawa kwamba, hawakusikia kauli za Benjamini William Mkapa? K u w a i t a w a p i n z a n i wapumbavu na malofa ndiyo sawa siyo?

S e r i k a l i y e t u y a CCM ina ugomvi na Waislamu. Kwa namna wanavyowashughulikia W a i s l a m u , l a i t i wangeelekeza nguvu hizo kwa vibaka, wezi, majambazi, makahaba na mfano wa hayo, hali ingekuwa shwari kabisa.

Chama Cha Mapinduzi, C C M h a t a k a m a wakiandika ilani ndefu, urefu wa barabara zote za lami ilizojenga, bado sitawaelewa. Nafasi yao kwenye kampeni hizi ni kutangaza mafanikio ya ilani zao zilizopita na sababu za kushindwa kutatua yale waliyoahidi, n a s i y o k u wa n a n g a wapinzani. Wapinzani wanayo haki ya kuponda chama tawala. Hatukatai kama wamefanya, lakini siyo kama ilivyotakiwa kufanywa. Wamefanya chini ya kiwango kwa m u d a m r e f u s a s a . Watupishe!

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (katikati) siku alipowakabidhi Ilani ya Uchaguzi wa chama hicho kwa mgombea wake wa Urais, Dk. John Magufuli.

Page 8: ANNUUR 1194.pdf

8 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015Makala

MWENYEZI Mungu hawaadhibu watu mpaka awaletee

mjumbe. Hivyo ndivyo Qur’an inavyotwambia. Kwa upande mwingine, katika mazingira ya dharura, jambo lililo haram, laweza kuruhusiwa, lakini kwa kiwango cha kuondoa dharura ila isiwe ni jambo la kufurahiwa na kuachwa liwe la kawaida na kuzoeleka.

Kwa kipindi kirefu hapa nchini , Waislamu, hasa wafanyabiashara, walikuwa katika kilio cha kuendesha biashara zao kupitia benki ambazo ni za mfumo wa riba. Hata hivyo, jitihada zilizofanywa na baadhi ya Waislamu, kwa rehema za Allah (SWT), imepatikana Benki ya Amana ambayo imeondoa dharura hiyo.

Hivi sasa mfanyabiashara Muislamu akifanya biashara zake kupitia benki za mifumo ya riba, itakuwa ni kwa kutaka mwenyewe na hivyo ajiandae kumjibu Mola wake juu ya dhambi hiyo.

Ili kujua ni kwa namna gani Benki za Kiislamu zinafanya k a z i , n a z i n a wa s a i d i a v i p i n a k u wa w e z e s h a wafanyabiashara, fuatilia m a h o j i a n o h a y a n a M k u r u g e n z i M t e n d a j i wa Amana Benki upate kuelimika.

Asalaam aleikum Dr. Muhsin; ni mara yetu ya k w a n z a k u k u t a n a n a ningependa nichukuwe nafasi kukupongeza kwa kuteuliwa na bodi ya Amana Benki katika uongozi na usimamizi wa Benki hii ya Kiislam Tanzania. Tunashukuru kwa kutupa muda wako kwa ajili ya kuongea nasi. Lengo letu ni kutaka kuwasaidia watanzania walio wengi waelewe nini Amana Benki na uendeshaji wake katika kuzingatia Sharia za Kiislamu na mchango wake katika mfumo wote wa kibenki nchini.

Jibu: Waleikumsalaam, Ahsante sana, na karibu sana Amana Benki.

Kwanza kabisa napenda nianze kwa kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru kwa dhati kabisa wadau wetu wote kwa muitikio wao ambao wamechangia katika ukuaji wa Amana Bank tokea kuanzishwa kwake mwezi November 2011 mpaka hivi sasa tunapokaribia miaka mi nne.

Natoa shukrani za dhati kwa wateja wetu ambao wametupa muitikio mzuri kwa kutumia huduma zetu. Pia nawashukuru wanahisa wetu kwa uwekezaji wao na uvumilivu wao katika kipindi cha mwanzo wa Benki

ambacho kwa kawaida huwa ni kigumu kwa wawekezaji. N a t a m b u a m c h a n g o mkubwa wa wakurugunzi wa A m a n a B e n k i k wa mawazo yao na muongozo wa o . Wa f a n ya k a z i wa Amana Benki nawapongeza s a n a k wa we l e d i wa o ambao umeiwezesha Benki kuweza kufikia hatua hii na pia nawataka waongeze juhudi na ubora wa utendaji katika uwanja huu ambao una ushindani mkubwa wa kibiashara. Naishukuru sana Benki Kuu ya Tanzania na serikali kwa ujumla kwa kuwezesha uanzishaji wa taasisi ya kifedha inayofuata misingi ya Kiislamu na naviomba vyombo vyetu hivi vitusaidie kutengeneza mazingira mazuri zaidi ya kutuwezesha kufanya shughuli zetu kwa ufanisi mkubwa.

Swali: Je ni kitu kipi kinakupa muongozo katika uendeshaji wa shughuli za Amana Benki?

Jibu: Ni Dira yetu. Dira yetu inatuelekeza tujizatiti kuwa ni chaguo la kwanza n a k u o n g o z a k a t i k a utoaji huduma za kibenki zinazofuata Sharia za Kiislam katika masoko yetu. Dira hii inafuatiwa na dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa na za kipekee zinazofuata Sharia za kibenki za Kiislamu kikamilifu kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyo wazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Pamoja na kuzingatia dira na dhamira hizi, Benki

yetu pia inazingatia misingi m i t a n o m i k u u k a t i k a kuendesha shughuli zake ambayo ni Uadilifu, Taaluma, Uwazi, Uaminifu na Usikivu. Tumejikita pia katika sifa kuu nne katika utendaji wetu wa kila siku ambazo ni uzingatiaji wa ubora wa hali ya juu wa kiutendaji na utoaji wa huduma kwa kuzingatia wito uliotukuka. Sisi wafanyakazi wa Amana Benki tunazingatia sifa hizi katika utendaji wetu na mahusiano yetu na kwa wadau wetu wote.

Kwa kuzingatia Dira, Dhamira na misingi mikuu, tumejikita katika kuijenga Amana Benki katika maadili ya hali juu na kuipanua huduma hii kwa kuanzia na maeneo yote ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuzingatia mkakati wa muda wa miaka mitano ambao unafanyiwa marekebisho kila baada ya mwaka mmoja. Tunajenga Benki ambayo inazingatia matakwa ya Jamii na uboreshaji wa mazingira.

Swali: Tueleze kwa ufupi kuhusiana na mfumo huu wa fedha wa Kiislamu.

Jibu: Mfumo wa fedha wa K i i s l a m n i m f u m o unaofuata misingi ya Sharia (Fiqh al muamalat) ambao una jumuisha benk i za Kiislam, bima za Kiislamu (Takaful) na masoko ya dhamana (sukuk). Mfumo huu umeendelea kuenea kwa kasi sana katika miaka ya karibuni sio tu katika nchi za Kiislamu, lakini

umeenea duniani kote. Hali hii imepelekea mfumo huu kuingia katika mjumuisho wa kifedha (financial inclusion) katika uchumi wa mataifa m b a l i m b a l i l i k i we m o Tanzania. Kinyume kabisa na mfumo wa kisekula ambao uti wake wa mgongo ni misingi ya riba, mfumo wa Kiislamu pamoja na mambo mengine kama ilivyo katika Sharia, umeharamisha misingi ya riba katika utendaji wake:

“Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa”. Quran 3:130

Hadi sasa, nchi nyingi katika maeneo ya Asia, Afrika, Mashariki ya Kati, Bara la Ulaya, na Amerika, zimeamua kuutumia mfumo huu kufuatia umadhubuti wake juu ya mfumo wa k isekula na kupelekea kukubalika katika jamii mbali mbali zilizo na zisizo za Kiislamu. Kwa mujibu wa mkutano wa kumi wa uchumi wa Kiislamu – WIEF (World Islamic Economic Forum) uliofanyika Octoba, 2014 Dubai UAE, thamani ya mfumo wa fedha wa Kiislamu umefikia dola trilioni nane ($8 Trillion) ambayo ni sawa na 11% ya uchumi wa dunia ikiwa na ongezeko la 6.3% kwa mwaka wakati mfumo wa kisekula ukiwa na ongezeko la 5.3% kwa mwaka.

Swali: Nini hasa tofauti kati ya mifumo wa fedha wa Kiislamu na ule wa kisekula?

Jibu: Katika jamii yetu kuna hali ya mkanganyiko miongoni mwa watu wengi juu ya mfumo wa fedha wa Kiislamu ambapo wapo wanaoona kwamba mfumo huu hauna chochote cha zaidi isipokuwa ni kubadilisha na kuupachika jina la ‘Mfumo wa Kiislamu’, na riba na kuiita faida. Hii ni hoja ambayo inaharibu mawazo, fikra na mitazamo ya baadhi ya watu. Tofauti iliyopo katika mifumo hii ni pamoja na:-

Benki za Kiislamu hazitoi mikopo ya fedha taslim kama ni sehemu ya uwekezaji wake, bali inajikita katika ununuaji wa bidhaa na utoaji wa huduma kwa kutoa nafasi kwa wateja wake kulipa kidogo kidogo. Wakati benki zisizo za Kiislamu hutoa mikopo ya fedha taslim kwa

njia ya riba, kitu ambacho kinawapelekea baadhi ya wakopaji kuzitumia fedha walizokopa kinyume na malengo ya mkopo ule. Hali hii ndio inayopelekea wakopaji wengi kushindwa kulipa madeni yao na kuingia katika matatizo na kuziingiza benki katika matatizo pia.

B e n k i z a K i i s l a m u zinajikita na uuzaji wa bidhaa tu ambazo zimethibitika kutokuwa na madhara kwa jamii wakati benki zisizo za Kiislamu hujishughulisha na kuwezesha shughuli mbali mbali bila kuzingatia athari itakayoipata jamii kupitia shughuli zile, mfano wa shughuli hizi ni pamoja na utoaji mikopo kwa kampuni zinazouza na kusambaza aina mbali mbali za ulevi na sigara pamoja na mikopo kwa kampuni zinazoendesha michezo ya kamari.

Swali: Je mfumo huu wa fedha wa Kiisalamu, ni kwa ajili ya Waislamu pekee?

Jibu: Pamoja na kwamba ni matarajio ya Waislamu wengi kuwa na mfumo wa kifedha unaokidhi mahitaji yao ya kila siku; lakini kwa sababu mfumo huu umekua ni wenye kukidhi kwa ufanisi mkubwa mahitaji ya k ib iashara , na kwa sababu biashara ni shughuli zinazofanywa na jamii zote, hivyo basi, benki za Kiislamu zipo kwa ajili ya watu wote, sio Waislamu pekee.

Swali: Je, kuna mahusiano gani baina ya benki na mteja katika kupokea fedha?

Jibu: Benki za Kiislamu hupokea fedha kwa mikataba miwili; mkataba wa kuweka a k i b a n a m k a t a b a wa uwekezaji. Katika mkataba wa uwekezaji, mteja wa benki anakuwa ni mshirika katika uwekezaji ule. Hushirikiana na benki katika biashara, na hupata faida na hasara k u l i n g a n a n a u k u b wa wa ushiriki wake na kwa kuzingat ia matokeo ya biashara inayofanywa. Ikiwa matokeo ni mazuri na faida huwa nzuri na ikiwa matokeo ya biashara sio mazuri, mteja nae hupata gawio dogo. Pia ieleweke kuwa wateja wanapata gawio kwa kuzingatia faida ya uwekezaji kabla ya kutoa gharama za uendeshaji wa benki.

Swali: Ni utaratibu gani Amana Bank inatumia katika kuwekeza fedha za wateja wake?

Jibu: Katika Benki za Kiislamu, asilimia tisini (90%) ya uwekezaji wake u n a h u s i s h a k u u z a n a kununua mali au kutoa huduma kufuatia maombi husika ya mteja wake. Kwa

Inaendelea Uk. 9

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Kiislamu Amana, Dr. Muhsin Masoud.

Biashara ya riba sasa basiAmana Benki yatoa ufumbuzi

Page 9: ANNUUR 1194.pdf

9 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015Makala

mfano mteja anapokwenda benki na mahijati ya mkopo kwa ajili ya ununuzi wa malori kwa ajili ya biashara zake, benki za Kiislamu hazitampatia fedha taslim, bali zitanunua yale magari na kumuuzia mteja yule kwa faida pamoja na kumpa fursa ya kufanya malipo kidogo kidogo.

S wa l i : A m a n a B a n k i n a i t h i b i t i s h i a j e j a m i i kwamba inafuata misingi ya Sharia za Kiislamu kikamilifu katika shughuli zake?

Jibu: Benki za Kiislamu zina mfumo wa usimamizi wa mambo ya Sharia ambao upo katika ngazi mbili, ngazi ya juu na ngazi ya chini. Katika ngazi ya juu, kuna bodi maalum ya usimamizi wa Sharia inayoundwa na wataalam waliobobea na wenye weledi wa Sharia katika miamala (Fiqh al muamalat). Bodi hii ndiyo inayotoa miongozo juu ya utayarishaji wa huduma na mikataba, kuthibitisha taratibu za uendeshaji, bidhaa na huduma zinazotolewa, mikataba na maadili ya kushughulika na mteja. Lakini bodi hii pia huendesha mapitio na ukaguzi wa Sharia (Sharia Compliance Reviews) na kutoa maamuzi kufuatia ukaguzi huo. Katika ngazi ya chini na ya ndani ya benki, kunakuwa na kitengo maalum kinachohusika na usimamizi wa Sharia katika shughuli za kila siku ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa miamala yote na kuwasilisha ripoti kwa bodi ya Sharia kwa maamuzi.

Swali: Ni yapi mafanikio na changamoto zinazozikabili benki za kiislam Tanzania?

Mkurugenzi mtendaji Jibu:

Mafanikio yaliyopo ni pamoja na;-

Kwanza kabisa ni Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kutoa leseni ya uendeshaji wa benki za Kiislamu Tanzania. Baada ya kuona umuhimu wa kuwepo benki za Kiislamu hapa nchini, Benki Kuu ya Tanzania haikusita kutoa ruhusa licha ya kutokuwepo kwa Sheria wala kanuni mahsusi zinazotoa miongozo ya uendeshaji wa benki za Kiislamu hapa nchini.

P i l i , M c h a k a t o w a utayarishaj i wa kanuni m a h s u s i ( r e g u l a t o r y framework) za uendeshaji wa benki za Kiislamu Tanzania unaendelea. Benki Kuu tayari imechukua hatua za matayarisho ya kanuni hizo mahsusi katika kunyanyua mfumo huu na kurahisisha u e n d e s h a j i wa k e k wa manufaa ya watumiaji na taifa kwa jumla. Mchakato huu

Inatoka Uk. 8

unajumuisha pia utayarishaji wa Bodi Kuu ya Usimamizi wa Sharia (Central Sharia Supervisory Board) kwa benki za Kiislamu.

Tatu, kuwepo kwa semina mbali mbali zinazohusu mfumo mzima wa fedha wa Kiislamu zinazolenga kutoa mafunzo ya mfumo huu kwa wadau mbal i mbali ambapo kwa kiasi kikubwa zimeisaidia jamii kupata mwamko na kuona uzuri wa mfumo huu huku benki zenyewe za Kiislamu zikifaidika kwa kuongeza ujuzi unaosaidia kuboresha utendaji wao.

Nne, Kuanzishwa kwa bima ya Kiislamu (Takaful) ni sehemu kubwa ya mafanikio ya mfumo mzima wa fedha wa Kiislamu; bima ya Kiislamu itasaidia jamii kwa kiasi kikubwa kufikia malengo hasa ya ukamilifu wa mfumo huu kwa kuwa

hata benki za Kiislamu z i t a k u a z i m e f a n i k i wa kuendesha shughuli zake kwa kushirikiana kwa karibu sana na kampuni za bima ya Kiislamu.

Tano, kuanzishwa kwa p r o g r a m u z a m a s o m o ya mfumo wa fedha wa Kiislamu (Islamic Finance Courses) katika ngazi za cheti, diploma, shahada ya kwanza na shahada ya pili katika vyuo vikuu vilivyopo hapa nchini, mfano wa vyuo hivyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Zanzibar (Zanzibar University) na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (Musl im Univers i ty o f M o r o g o r o ) . H a t u a h i i itawezesha kupatikana kwa wataalam wengi wenye ujuzi wa utendaji na uenezi wa mfumo huu.

Na mwisho , n i j ins i jamii ilivyoupokea mfumo huu kwa mikono miwili jambo ambalo limepelekea

ukuaji wa kasi hata zaidi ya matarajio ya wengi katika wadau wa fedha nchini.

M f a n o , s i s i A m a n a Benki ikiwa ndio benki ya kwanza ya Kiislamu Tanzania, tumeweza kukua na kufungua matawi sita yaliyopo katika miji ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza na ipo mbioni kufungua tawi la saba kabla ya mwisho wa mwaka 2015 katika eneo la Mbagala Zakhiem Dar es Salaam. Amana Benki katika kipindi hiki kifupi imeweza kukuza amana za wateja kutoka TZS 30.3 billion mwaka 2012 hadi kufikia TZS 152.2 billion mpaka mwezi Juni 2015 na kukuza portfolio ya mikopo kutoka TZS 16.8 bilioni 2012 mpaka kufikia 101.8 bilioni 2015. Vile vile tumefanikiwa kutengeneza ajira kwa kuwa na wafanyakazi wafikao 122.

Kwa upande wa pili, benki za Kiislamu zinakabiliwa na changamoto kama zifuatazo:-

Kwanza, mchakato wa kutunga sheria na kanuni za kuendesha benki za Kiislamu nchini unakwenda pole pole sana. Hili linafanya benki za Kiislamu zisiwe na uwezo wa kupata msaada stahili kutoka kwa Benki Kuu ya Tanzania pale unapohotajika.

Pili, kutokuwepo kwa bima ya Kiislamu ambayo ni sehemu ya mfumo mzima wa Kiislamu na ni msaada mkubwa katika utimilifu wa uendeshwaji wa mfumo huu nchini. Kwa mfano, benki za Kiislamu ambazo kwa asilimia kubwa zinajikita katika uuzaji wa bidhaa, bidhaa hizi huhitaji kukatiwa bima kupitia kampuni za bima za Kiislamu; kutokuwepo kwake kunapelekea bidhaa hizi kukatiwa bima isiyo ya Kiislamu chini ya dharura na kupelekea baadhi ya jamii kutilia mashaka juu ya uhalali wa baadhi ya miamala inayofanywa na benki za Kiislamu hapa nchini.

Ta t u , k u w e p o k w a baadhi ya wanajamii ambao hawana uelewa wa kutosha k u h u s i a n a n a m f u m o huu, lakini wanajaribu kuuzungumzia vibaya kwa kusema mfumo huu na ule usio wa Kiislamu ni sawa

sawa bali umebadilishwa jina tu. Hali hii imepelekea w a n a j a m i i w e n g i n e kuukwepa kabisa mfumo huu. Hili wanalolifanya watu wa namna hii ni kosa kubwa ambalo linapelekea kuwazuia watu wasiende katika kheri. Qurani 36: 17 inakataza binadamu kusema na kutenda asiyo na ujuzi nayo kwani hakika siku ya Kiyama atakua na jukumu kwa aliyoyatenda na aliyoyasema.

S wa l i : N i k i t u g a n i ungependa kuwashauri wasomaji wetu juu ya Amana Bank.

Jibu: Napenda nimalizie mazungumzo haya mafupi kwa kuwaahidi wadau wetu wote na hususan wateja wetu kuwa kila siku Amana Benki tunajikita zaidi katika uboreshaj i wa huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Nawaomba sana wadau wetu wote wasisite kabisa kutukosoa pale ambapo hawataridhika na huduma zetu; kwa hakika, sisi ni benki sikivu na tupo tayari kusikiliza maoni kwa ajili ya kuboresha.

Nawahakikishia wadau wetu kuwa tunaliendesha jahazi hili katika maadili yaliyotukuka na yanayofuata uwazi, weledi na usikivu wa hali ya juu kutoka kwa wadau wetu wote; wateja, wanahisa, wakurugenzi, serikali na jamii yote kwa ujumla. Benki yetu inatumia teknolojia ya kisasa ambayo inatuwezesha kufanya miamala yetu kwa uharaka na umakini wa hali ya juu. Vilevile ningependa ieleweke kuwa benki hii inafuata misingi ya Sharia za Kiislamu lakini haibagui katika uwekezaji, ajira na kutoa huduma kwa wateja. Amana Benki inatoa huduma zake kwa watu wote.

Ningependa vile vile niwashauri wasomaji wetu wajitahidi sana waweze kufika katika matawi yetu mbali mbali yaliyopo jijini Dar es Salaam, (Tandamti na Lumumba yaliyoko Kariakoo, Golden Jubilee Tower lililoko katikati ya jiji, Nyerere Road lililoko Jengo la DRTC, Barabara ya Nyerere), Tawi la Mwanza lililopo katika barabara ya Kenyatta na Tawi la Arusha li l ilopo Hugo House ili waweze kupata maelezo zaidi kuhusu Amana Bank na namna itakavyoweza kuwaendeleza kiuchumi.

Karibuni sana Amana Benki mufaidike na huduma za kisasa zinazozingatia maadili mema na zisizo husisha riba.

Amana Bank – Idara ya Usanifu bidhaa na Usimamizi wa Sharia (2015)

Page 10: ANNUUR 1194.pdf

10 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

Makala

WI K I i l i y o p i t a kulifanyika Dua y a k u i o m b e a

Z a n z i b a r a m a n i n a utulivu katika kipindi cha uchaguzi. Waislamu mbali mbali wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, walikusanyika k a t i k a v i wa n j a v ya Maisara mjini Zanzibar kwa ajili ya kuomba dua ya kuiombea Zanzibar amani na utulivu, hasa katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh Abdallah Talib, alisema mara nyingi amani ya Zanzibar hutoweka kutokana na sababu za kisiasa hasa inapofika wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa katika kuendeleza amani ya nchi wakati wote. Akasisitiza kuwa suala la kudumisha amani na utulivu ni mchakato unaopaswa kuendelezwa, ili kuinusuru nchi kuingia k a t i k a m a c h a f u k o yasiyokuwa ya lazima, na kwamba kila mwananchi ana jukumu la kuhakikisha kuwa amani ya nchi haichezewi.

Naye Amir wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar Sheikh Ali Abdallah akasema d u a h i y o ya k i t a i f a imefanyika nchi nzima katika viwanja mbali mbali Unguja na Pemba. Dua hiyo iliyotanguliwa na sala ya Alasiri viwanjani hapo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini ya Kiislamu, serikali na vyama vya siasa wakiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha ADC Mhe. Hamad Rashid Mohammed.

Kuomba dua ni jambo jema sana na kwa hakika ni ibada. Na kila mja anavyoomba Dua kwa Mola wake, ndivyo Allah anavyomridhia. Kinyume na mwanadamu ambaye, h a t a k a m a a t a k u wa mkarimu vipi , lakini ombaomba ikizidi, hata kama anayemuomba ana shida kweli, hufika mahali

Zanzibar ilete tobaSio kuomba amani, baraka, neemaMufti Ka’bi awasaidie viongozi SMZ

Na Omar Msangi

akakereka.Hata hivyo pamoja

na ukweli huo, lazima tuwe wa wazi na tuseme ukwel i kwamba dua h i i ya Z a n z i b a r i n a walakini, tena mkubwa. Nitafafanua. Kwanza hii imeitwa kuwa ni dua ya kuiombea Zanzibar amani na utulivu katika uchaguzi mkuu ujao. Pili, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh Abdallah Talib, amesema “amani ya Zanzibar hutoweka kutokana na sababu za kisiasa inapofika wakati wa uchaguzi mkuu.”

Sasa turudi nyuma toka zimeanza siasa za vyama vyingi, tujiulize, nani walikuwa wakiwavamia w a t u n a k u w a p i g a o v y o k u a n z i a z o e z i la kuandikisha wapiga kura, wakati wa kupiga kura na hata baada. Nani walikuwa wakivamia akina mama majumbani mwao kuwaibia v i to vyao vya dhahabu na kuwabaka? Nani walikuwa wakiwatuma watu hawa na kuwalinda wasifikishwe katika vyombo vya sheria?

K wa b a h a t i n z u r i Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff Hamad na Hamad R a s h i d wa l i k u we p o . Wote hawa walipokuwa pamoja katika upinzani, wanajua na wakisema hadharani habar i ya vikosi na ‘ janjaweed’ waliokuwa wakitumiwa na SMZ (CCM) kufanya

uharamia huo wa kupiga watu na kuvuruga amani ya Zanzibar. Sasa hili la kuomba dua kumtaka Mungu alete amani au la kuambiana ukweli wanasiasa kuwa waache uharamia huo? Mahali pengine Sheikh Talib anasema kuwa suala la ulinzi wa amani ni la kila Mzanzibar. Sawa kabisa. Lakini katika mazingira haya ya ‘Janjaweed’ na vikosi, mwananchi wa kawaida afanye nini? Kwa nini hamuwaambii ukweli wanasiasa?

Turudi nyuma mauwaji ya 2 0 0 1 . Wa t u wa l e waliouliwa kosa lao nini? Ile kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia kuonyesha kutokuridhika k w a o n a u c h a g u z i ulivyoendeshwa, ndio hukumu yao kupigwa risasi na kufanyiwa kila aina ya udhalimu?

Pamoja na kuwepo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bado juzi hapa wakati wa uandikishaji wapiga kura, ya ‘Janjaweed’ yalijitokeza tena ambapo watu walipigwa sana katika baadhi ya maeneo na ushahidi ukitolewa kuwa watu waliofanya uovu huo ni katika wale wale ‘vikosi’. Unaposema v i k o s i m a a n a y a k e unasema serikali. Sasa kama huku sikumfanyia stizai na kumcheza shere Allah Subhana Wataallah nini! Kwamba serikali i toe vikosi vihujumu wananchi, hali ambao

hapana shaka inahatarisha amani na utulivu, halafu viongozi hao hao wa serikali wanakusanyika Maisara kumwomba Allah (SWT) alete Amani katika nchi!

Ambacho tungetaka kusikia, ni Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar kuja na kauli thabiti kwamba yaliyopita yamepita, hakutakuwa tena na visa vya vikosi kupiga watu au kuja na njama za ‘magoli ’ ya mkono katika uchaguzi huu, mambo ambayo ndiyo huvuruga amani. Serikali ikisha hakikisha hayo, ndio sasa iwatake wananchi, kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha kwamba amani inadumu. Na Dua, Itqaaf zifanyike.

Wakati Masheikh wale akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu wa Muft i She ikh Fadhi l Soraga, wananyanyua mikono na Maalim Seif kuomba Allah (SWT) aimiminie neema, amani, utulifu na Baraka Zanzibar, Masheikh wenzao wapo gerezani Bara kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Masheikh wale wamesema m e n g i ya l i we m o ya kudhalilishwa na hata kunajisiwa.

Sheria ya Kiislamu a m b a y o M u f t i w a Zanzibar anaijua vyema, inasema kuwa lau watu wangesikilizwa tu kwa madai yao, kuna watu wangedai damu na mali za

watu. Bali ni juu ya mwenye kuleta madai , kuleta ushahidi kuthibitisha madai yake. Ni mwaka wa pil i sasa, serikali h a i j a we z a k u f i k i s h a ushahidi mahakamani kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya Sheikh Msellem Alli na wenzake. Ambayo t a f s i r i ya k e ya we z a kuwa Masheikh wale wamekuwa wakiteswa n a k u a d h i b i wa k wa dhulma. Wala hawafikirii taabu wanayopata wake na watoto wa Masheikh hawa kwa kukosa huduma muhimu za maisha. Kisa wakuu wa kaya wapo ndani kwa tuhuma ambazo kwa miaka miwili, Mahakama haijaweza kuzithibitisha! Katika dhulma kama hii, unanyanyua mikono kumwomba Al lah i l i akupe nini?

Tu l i t a r a j i a k a t i k a mkusanyiko ule, badala ya Mufti kuongoza Dua, angemuuliza Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff Hamad, kwa kosa gani Sheikh Msellem yupo ndani mpaka sasa? Kuwa Mufti maana yake kutoa fat’wa, na maadhali hiki ni cheo na wadhifa unaotambuliwa katika mfumo wa uongozi wa Serikali ya Zanzibar, tulitarajia Mufti Sheikh Saleh Omar Kabi atoe fat’wa juu ya suala la S h e i k h M s e l l e m n a wenzake na awashauri viongozi wa serikali juu ya kadhia hii.

Kunyanyua mikono k u o m b a D u a k w a Allah yaweza kutuletea balaa zaidi . Afadhali tungejikalia kimya na dhulma zetu mpaka hapo tutakapoamua kuzibadili nyoyo zetu. Na Qu’ran inasema wazi , Al lah habadili yaliyo kwa waja mpaka wenyewe wabadili yaliyo katika nafsi zao. Kama ndani ya nafisi zetu imeondoka huruma, huku dhulma na kuonea watu kukitamalaki, hiyo amani na utulivu, ije ili akae wapi.

A n g a l a u E d w a r d Lowassa amekuwa japo na ujasiri wa kutamka kwamba k a m a a k i c h a g u l i w a atalishughulikia suala la Masheikh wale kwa kutumia sheria zilizopo. Sisi ambao ndio wenyewe, wenye watu wetu, wenye Masheikh wetu, tunaona ni nuksi hata kuwataja tu! Halafu tunakusanyika k u m w o m b a M u n g u a t u m i m i n i e B a r a k a tele, tunawiri ili tuzidi kuwadhulumu zaidi waja wake!

MAKAMU wa Kwanza Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na Katibu wa Muft, Sheikh Soraga wakitoka katika dua iliyofanyikia katika viwanja vya Maisara Zanzibar hivi karibuni.

Page 11: ANNUUR 1194.pdf

11 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 201511 AN-NUURMakala

TU N A E N D E L E A kushuhudia mengi katika kampeni hizi

za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Ni vioja, ni uwongo, ‘unafiki’, na mfano wa hayo kwa namna ya ajabu kabisa ambayo haijawahi kutokea. Kinachofanyika sasa, pengine tukiite mipasho kama ile ya wasanii wa taarabu. Kuna watu wanaonekana kuwa na vipaji hivyo vya uimbaji wa taarabu, lakini wamejikuta wapo kwenye siasa labda kwa ajili tu ya kupata ‘unga’.

B i l a s h a k a k w a wafuatiliaji wazuri wa vyombo vya habar i , watakuwa wamemsikia vema kabisa, ‘kiungo mpya wa yanga aliyesajiliwa kupitia dirisha dogo’. ‘Mchezaji huyu ambaye alifanyiwa rasmi majaribio kwenye mechi ya kirafiki iliyorushwa moja kwa moja kupitia vituo vitatu vya matangazo, TBC 1, Star Tv na Azam Tv’, anaonekana hana kiwango licha ya kusajiliwa kwa gharama kubwa kuziba pengo la mchezaji aliyehamia i l iyokuwa t imu yake ya zamani’. Hakuweza k u o n e s h a k i w a n g o kilichotarajiwa na wengi wanaomfahamu, hususan wafadhili jambo ambalo l inaweza kuwavunja moyo mashabiki wa timu hii ambayo imekuwa kinara kwa takriban miaka hamsini sasa’.

Akiwa katika t imu yake ya zamani, mchezaji huyu ndiye a l ikuwa ‘ t e a m c a p t a i n ’ n a aliongoza vizuri kabisa japo hawakufanikiwa kuchukua kombe hata moja. Alikuwa mchezaji mzuri, mwenye nguvu na stamina barabara ikizingatiwa kwamba ni ‘Padri’, hivyo yeye na wanawake ni kama “mashariki na magharibi”. Siyo kama wachezaji wengine ambao mara nyingi hujichanganya na wanawake na kupoteza viwango vyao.

Kwa watu weledi wa mambo ya propaganda, wa n a t a m b u a v ye m a kwamba, ‘aliyecheza pale siyo ‘Willy’, bali katumika kama mdoli tu’. Ni kama mtu anapopandwa na mashetani husema vitu vya ajabu, vya kuchanganya na mara nyingine anaweza kuj ipigiza, kukimbia ovyo na mfano wa hayo. Hayo yote, anafanya yule aliyejificha ndani ya mwili

CCM yavunja rekodi usajili dirisha dogoNa Juma Jumanne

wa huyo mtu. Imefika mahali watu

w a n a a n z a k u r u d i nyuma, hususan wale wal iomwamini huyu anayeitwa Dokta. Wanaona labda yupo sahihi na a m e o n g e a m a m b o ambayo kweli yametokea. B inafs i s ip ingani na baadhi ya kauli zake ila ninachokataa hapa ni kwamba, hajasema yeye. Kwa wale waliomsikiliza kwa makini watakubaliana n a m i k wa m b a , ya l e maneno yaliyokuwa na yanayoendelea kumtoka yana ‘rangi ya kijani’ i l iyoiva kabisaaa….! ! Jiulize mwenyewe, majani kijani kibichi yanatoka wapi maj ira haya ya kiangazi!?

L a k i n i k u n a wa p o waliofika mbali kabisa wakasema kwamba, isije ikawa kuondoka kwa Slaa na ‘kutamkishwa’ m a n e n o k a m a h a ya kunatokana na ugonjwa kama ule unaowasumbua Waislamu? Nilipotaka kujua ni ugonjwa gani huo, nikakutana na swali badala ya jibu! Nikaulizwa ina maana hujui ugonjwa u n a o wa t a f u n a n i n y i Waislamu? Nikapata hamu ya kujua gonjwa hilo, ndipo nilipoambiwa kwamba, huo utaasisi wenu na u-manhaj umeusahau!? Lakini kubwa zaidi ni kwamba, ‘mchezaji huyu alikuwa na matarajio ya kuwa team captain kwa mara nyingine’. ‘Suala la kumpa u-kepteni mchezaji mpya ambaye hajazoea, hajajua fomesheni ndilo h a s w a a m s i n g i w a

usajili feki uliofanywa bila kuangalia uwezo wa mchezaji ambaye tangu hapo ni veterani’.

Wa k a z i d i k u s e m a k w a m b a , k w a h i y o k inachoende lea s iyo Richmond tu, kuna mambo kama yenu Waislamu yameingilia katikati! Kwa hali hiyo, usishangae yanayoendelea kwa kuwa mgombea anayetokea chama chenye rangi kama ya maneno uliyoyaona kutoka kwa ‘Dokta’ Slaa ni baba mmoja, mama mmoja. Hapo nilichoka mwenyewe…..!!

Lakini amini usiamini, k w e n y e m f u m o w a kinachoitwa demokrasia h a k u n a m wa n a s i a s a msafi. Wanatofautiana tu viwango vya kuiba. Waangalie wanaomtetea M a g u f u l i w a k o j e , wamefanya nini, hali zao kimaisha na mengineyo. Ikiwa kwenye sakata la akaunti ya Escrow wa m e h u s i k a m p a k a viongozi wa dini, sembuse hawa wasiomjua mungu! Wananchi msiyumbishwe na watu wanaote tea matumbo yao.

Ndugu zanguni ikiwa maneno haya yana ukweli au uzushi, tubaki kwenye agenda yetu. Wenyewe ndio wanasema! Na mimi siyo mzungumzaji sana, hivyo huwa napata fursa ya kusikia na kujifunza mengi. Ushauri wangu ni kwamba, tusikubali kuburuzwa kila wakati jamani. Hawa watu ni waongo mno. Leo Slaa ndio anapata u jas i r i wa kugusia mambo ya

Waislamu? Haongei yeye. Ukiangalia kwa jicho pevu, ndio utaweza kumuona ‘shetani aliyempanda kichwani’.

Wa t u k a m a h a w a wapo kila kona ya dunia. Mathalani, aliyekuwa waziri wa zamani wa ser ikal i , Bw. Nalai la Kiula ametamka maneno ambayo ni wazi kabisa huyu mtu ‘ameishiwa au amefilisika kifikra’! Sisi tunafahamu kwamba, hizi ni tuhuma ambazo bado hazijathibitishwa. Kumbe yeye na ‘uoni wake mdogo’ ameshajua kwamba hawa masheikh wa Uamsho ni magaidi!? Hata maana yenyewe ya ugaidi haijui, anafuata tu mkumbo. Hawa ndio watu ambao ‘maombi yao na dua zao huzielekeza CCM pindi wanapopatwa na matatizo’. Wanaipenda CCM kuliko hata ‘Mungu’ wao wanayemwamini.

N a y e m w e n y e k i t i wa Chama cha Kijamii (CCK), Bi. Constantine A k i t a n d a , a m e d i r i k i kusema kwamba, kwa kauli ya kutaka kuwaachia watuhumiwa wa Uamsho wanaodaiwa kusababisha uvunjifu mkubwa wa amani Zanzibar, Lowassa amedhih i r i sha kuwa aki ingia madarakani atasababisha mfarakano mkubwa zaidi katika jamii.

Akaendelea kusema kuwa, hal i ya amani i m e r e j e a Z a n z i b a r n a s a s a w a n a n c h i wanafanya shughuli zao

za maendeleo bila hofu ya vitendo vya kigaidi kama ilivyokuwa awali. “Hivyo, mtu anapokuja na kutoa ahadi ya kuwaachia watuhumiwa waliokuwa wanazusha hofu kubwa v i s i wa n i , n i l a z i m a atazamwe kwa shaka”. Hawa ndio watu wetu, japo unaweza kujiuliza kwamba, huyu ni raia wa Tanzania au mhamiaji!

A m a n i i p i anayoizungumzia iliyopo Z a n z i b a r ? K u b a k wa mwanamke, tena mchana wa Ramadhani kwenye zoezi la vitambulisho vya wapiga kura ndiyo amani hiyo!? Angetuweka wazi kwenye nukta hii ili twende sawa, tujue ni akina nani anaowakusudia kwamba wanaishi kwa amani sasa! Ni vitendo vipi hivyo anavyodai kwamba, ni vya kigaidi? Sisi tumekaa kusubiri hukumu kwa masheikh zetu, kumbe wenzetu t a y a r i w a n a f a h a m u kinachoendelea!!

Naye Maria Sarungi, mmoja katika Watanzania maarufu katika mtandao wa twi t ter , anasema kwamba, “Kama vyombo vya habari vya Tanzania vingekuwa kama vya Marekani, kichwa cha habari kutoka mkutano wa Jangwani kingesema; “Mgombea Urais atangaza kuwasamehe wabakaji na magaidi”. Mwanamama huyu ndio kachelewa pengine kuliko wote. Bila shaka akipewa wadhifa wa u r a i s i , j a m b o l a mwanzo kufanya litakuwa kuruhusu ‘Maria na Janeti’ kuoana kanisani kwa kigezo cha limesemwa na linafanyika Marekani!

Wosia wangu kwa mara nyingine ni kwamba, kila mtu ana haki ya kusema lakini siyo kila kisemwacho ni sahihi. Tutumie vema neema ya akili ili itusaidie sisi na jamii kwa ujumla. Kampeni yetu ni kuitoa CCM madarakani kwa sababu haitutendei haki. Kama Lowassa hafai, basi waliomuweka kwenye wadhifa wa Uwaziri Mkuu ndio hawafai zaidi. Hata kama Lowassa akiwa bubu, hata asiposema chochote, hata akisema atatuua sote, sisi lengo letu CCM itoke tu, kwa kuwa tumeshajifunza kwamba maneno na matendo yenu wanasiasa wa CCM hayawafikiani na uhalisia.

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Harun Lipumba.

Page 12: ANNUUR 1194.pdf

12 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 201512 MAKALA

Inaendelea Uk. 16

Inaendelea Uk. 16

MTUME Paulo anasema mahali fulani kuwa inabidi watu waombe kulingana na mapenzi ya Mungu, kitu ambacho kinaleta utata wa mantiki katika hatua mbili, ya kwanza ni kama mtu anaweza kujua mapenzi ya Mungu ni yapi katika jambo fulani ili aelekeze maombi yake hapo. Jibu katika hatua hiyo ni hapana, kwani njia rahisi zaidi ya kujua kama kitu hiki au kile kinaendana na mapenzi ya Mungu ni kuangalia sheria, na mara nyingi tatizo linakuwa siyo hilo. Suala ni mwelekeo wa baraka; nini Mungu anachobariki wakati huo.

Tatizo la pili ni kuwa m a o m b i h a y a w e z i kutenganishwa na hisia za kile ambacho kila mmoja we t u k a m a b i n a d a m u anakitaka, na ndani ya kila mmoja kuna hisia ya faida na hasara, kwa kuangalia jambo fulani kwa upande wowote ule. Ndiyo maana maombi kwa mfano ya kushinda mchezo wa soka ni aina ya kichekesho, lakini kwa upande fulani ni sahihi, kwani huwezi kuwa na dhana kuwa Mungu haipendi timu pinzani, lakini ni wazi anaweza kutoa baraka kwa

Mabadiliko: Nafasi ya Lowassa katika siasa za TanzaniaNa Anil Kija timu yenu kwa siku hiyo.

Inategemea mtiririko wa baraka zake.

Inapokuja katika suala la uchaguzi mkuu nchini hapo Oktoba 25, kuna suala gumu la kuelewa mtiririko wa baraka uko upande gani, kati ya wahafidhina ambao hawawezi kutazamiwa kule ta mabadi l iko , na wanaoyataka. Tofauti moja ya kina ni kuwa licha ya migawanyiko yao, makundi yao na fitina zisizoisha, wahafidhina wana uzoefu wa dola, na kiwango kikubwa cha utii, ndiyo maana watu wengi wanawaamini kulinda amani na utulivu. Lakini historia, na hata maandiko, hayaonyeshi kuwa utulivu ndiyo lengu kuu daima.

Hivyo uwezekano wa mabadiliko upo, lakini m a b a d i l i k o ya n a a i n a mbi l i kwa mant ik i ya mfundishaji wa Uyunani ya Kale, Aristotle (aina sita za serikali, tatu njema na tatu mbaya). Aina ya kwanza ya mabadiliko, ambayo kila mtu anataka, ni mabadiliko chanya ambayo ndiyo mema, nchi kwenda mbele kwa mwelekeo bora zaidi, na aina ya pili ni mabadiliko hasi, ambayo kwa lugha ya maandiliko ni hukumu. Nchi ipewe kiongozi wa kuifikisha gizani, iangamie.

K w a m a a n a h i y o ,

swali halisi kwa mtiririko wa maandiko ni kama kilichopo hapa nchini hivi sasa ni mabadiliko (chanya) ambayo ni baraka, au ni hukumu ambayo ina maana ya mabadiliko hasi, nchi iparaganyike, ianze au ipanue mitafaruku kwa

nj ia is iyo ya kawaida. Mabadiliko hasi ya moja kwa moja yanaanza na uasi, kwa mfano ule uasi wa Katiba Mpya ulioongozwa na Kanisa Katoliki kuelekea mwisho wa 2010, baada ya mgombea wao, kasisi muasi Dk. Wilibrod Slaa

kushindwa katika kura ya urais. Tungeparaganyika.

M a b a d i l i k o a m b a y o yanatafutwa sasa yana asili yake katika uasi huo, lakini yamebadilika sura na kurudi katika hali ya kawaida, kuwa dhamira yake siyo

MO J A y a s i f a za kizazi cha I b r a h i m u

hadi wakati wanatoka Kanaani na kuingia Misri, ni utajiri mkubwa hasa wa mifugo, ishara ambao inaonekana pia kwa baadhi ya watu wenye sifa ya kuwa karibu kabisa na Mungu,

Lowassa na Yakobo: Baraka za utajiri kwa vipindi tofauti vya kazi ya Mungu

kwa mfano Ayubu, na ukiacha Mfalme Daudi, mwanawe, Sulemani. Ni suala lisilopingika kuwa utajiri ni baraka za Mungu kwa mtu fulani, ila kutokana na hisia moja au nyingine ya Injili, mara nyingine huonekana vinginevyo. Ziko fikra zilizopanuka

duniani, kuwa utajiri ni wizi, ufisadi, uharamia tu.

Hata hivyo, ukiangalia k w a m a k i n i k a t i k a maandiko unakuta kuwa hata pale uharamia, wizi au 'ufisadi' unapokuwepo, bado utajiri ni baraka kwa sababu mhusika anaishi maisha ya raha. Suala ni kuwa baraka hizo zinaanzia wapi, kama Mungu anamkirimu mtu ambaye ni mwizi au haramia, au anabarikiwa licha ya kuwa mwizi au haramia. Fikra ya kikuhani ingependelea kuwa mtu anapofikia hatua ya kuwa mwizi au haramia baraka iondolewe, hukumu yake ishuke, lakini maandiko hayaonyeshi hivyo.

Ukifuatilia maandiko, unakuta kuwa Mungu anatumia baraka ya utajiri

katika maeneo mawili: kwanza kuwastawisha walio karibu naye ili k u j e n g a v i z a z i v ya wanaoamini, wasiingiliane n a w a s i o a m i n i wakaharibikiwa. Hii ni azma ya familia tajiri kuoana wao kwa wao, na kama imani yao inatosha, hulka ya wazazi inaendelea miongoni mwa wana wao, na siyo kuharibikiwa kwa kuchanganyika na wasioamini , wasiot i i amri muhimu za maisha. Ndiyo maana Ibrahimu akamtuma mkuu wa watumisi wake kutwaa binti kule Irak.

I b r a h i m u a l i k u wa hataki mwanae Isaka a o e m i o n g o n i m wa w a - K a n a a n i , a k i w a na uhakika kuwa hali hiyo itateteresha imani ya Mungu (wa kweli)

katika nyumba ya Isaka. Mtumishi akafika Padan Aramu kwa ndugu yake Ibrahim aitwaye Nahori, akapokelewa na binti mwenye adabu na heshima kisimani kabla hajafikia nyumbani, kumbe ndiye mteule wa kurudi naye. Rebeka alikuwa ndugu wa Isaka kama j ins i Sara alivyokuwa kwa Ibrahimu.

Yakobo alifaulu kuinua nyumba yenye itikadi njema kwa njia ambayo baba zake hawakufaulu, yaani Ibrahimu na Isaka. Nyumbani kwa Ibrahimu ilibidi Hajira aondoke na mwanae Ishmaeli k wa n i wa s i n g e we z a kukaa nyumba moja na Sara (na Isaka), na katika nyumba ya Isaka ambayo mke alikuwa mmoja,

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CHADEMA-UKAWA, Mhe. Edward Lowassa.

Mhe. Edward Lowassa.

Page 13: ANNUUR 1194.pdf

13 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

Mchezo wa kuwapatia watu kula kila baada ya miaka 5

“M a h a k a m a K u u inaelekea kuhalalisha u o n g o k a t i k a

kampeni za kisiasa”. Hivyo ndiyo lilivyonadi gazet i la mtandaoni kutoka Marekani la “The Huffington Post” la tarehe 16/06/2014. Nalo gazeti la Kiengereza la “the Guardian” la April 2014 likaandika; “ Mahakama kuu kuamua ikiwa kampeni za uongo ni halali”.

Hii i l ikuwa ni kesi i l i y o z u a m j a d a l a mkubwa na kuteka watu wengi mno, mahakama kuu nchini Marekani (Supreme Court) ndio waliokuwa wanasikiliza kesi hii, kubwa zaidi ni kuwa mahakama hiyo iamue ik iwa kusema uongo kuruhusiwe kaika kampeni.

Kwani sheria ya Ohio “An Ohio law” inakataza wagombea kusema uongo wakati wa kampeni, lakini shirika la SBA-List (The Susan B. Anthony List) linalojishughulisha na kampeni za kupinga utoaji mimba nchini Marekani na linawaunga mkono wanasiasa wanaounga mkono kampeni hiyo, mwaka 2010 lilipeleka kesi mahakama kuu kupinga sheria hiyo ya Ohio.

Nianze kwa kunukuu maneno ya mchangiaji mmoja wa mada hii katika mtandao kuwa ; “Marekani i n a e n da mb a l i z a i d i kwani baada ya uhuru wa kuzungumza, sasa wanaelekea kuruhusu na uhuru wa kusema uongo”. Nami niseme kwamba hii ni hasara ya uhuru uliopindukia. Naamini u h u r u u k i p i n d u k i a mipaka, basi unaleta balaa.

Hata Rais Barack Obama aliwahi kusema kuwa; “Hatuwezi kuwa na uhuru wa asilimia mia moja kisha tukajihakikishia usalama wa asilimia mia moja”.Hata mimi nasema kuwa uhuru kwangu una mipaka.

Tu ya a c h e h a y o ya Marekani turudi nyumbani k isha tuyal inganishe hayo na haya ya kwetu sisi , hasa ukizingatia kuwa tayari kampeni za uchaguzi wa October 25, zimeanza. Wasikiliza kampeni yatupasa tuwe makini kwani kuna watu ni wachanganyaji wazuri wa nzima na mbovu bi la ya kugundulika. Wanachanganya ukweli na uongo na wanachanganya

Na Rashid Abdallah

akili za wasikilizaji pia. Propaganda ni kitu kibaya zaidi kuliko uwongo. Siku zote uongo ni uongo na hauna chembe ya ukweli. Lakini propaganda ni jambo ambalo linakuwa na chembe ya ukweli na uwongo pia kwa maslahi ya k i s i a s a , n i k a m a kuchanganya tui kidogo (juisi ya nazi) na maziwa k i d o g o , u s i p o k u w a mtaalaumu utashindwa kung’amua kuwa haya si maziwa safi.

W a n a s i a s a

wanaochanganya tui na maziwa, mbovu na nzima, ukweli na uwongo kwa wakat i mmoja , wapo hata hapa kwetu. Kama kampeni wangekuwa wanazifanya kwa uongo mtupu, ingekuwa rahisi s a n a k wa wa n a n c h i kugundua na mwisho kuachana nao. Lakini mara nyingi wananchi tunadanganywa kwa s a b a b u k a m p e n i z i n a e n d e s h w a k w a p r o p a g a n d a , y a a n i uwongo hapo hapo na

ukweli hapo hapo. Kwa hiyo inakuwa ngumu sana kwa mwananchi wa kawaida kugundua lipi lilikuwa na ukweli na lipi ni la uwongo. Watakuja wabunge, wawakilishi na wagombea wengine m a j i m b o n i m w e n u , w a t a k u j a n a m e n g i mazuri katika masikio yenu lakini hayotokuwa yote n i ya kwel i i la mengine yatakuwa ya uongo ili kufanikisha kile wakitakacho. Wapo watakaokuwa wanatoa

hongo pesa, vitenge na mambo mengine ilimradi tu wazisuuze roho zenu mupate kuwachagua. Ili kuwa na uhakika na unaekwenda kumchagua, ni bora kuacha kupokea rushwa, kwani sayansi inatuambia kuwa moyo w a b i n a a d a m u u n a kawaida ya kuathirika ya yule anayeutendea wema. Hivyo ukichukua pesa ya mtu mwisho wa siku moyo unaweza kuwa mzito kutomtilia kura japo hafai kwa sababu tayari umeshaathirika na wema ulionfanyiwa.

Dunia ni mchanganyiko wa mambo yote machafu na mazuri , ni kama u n g o u l i o b e b a k i l a kitu, kwani wakati sisi tukitahadharisha juu ya uongo wa baadhi ya wanasiasa kwa wananchi na tukiwaeleza kuwa wawe makini na watu hao, kuna watu wao wanaanzisha kabisa kampeni ili uongo uruhusiwe katika siasa. Ndivyo dunia ilivyo.

Naamini kampeni hii ya kupinga sheria ya Ohio kwa kule Marekani kama ingekuja Tanzania basi wapo wanasiasa a m b a o w a n g e i v a l i a njuga na kuitetea kwa sauti pana huku mizizi ya shingo ikiwatoka na jasho likiwakatika, kama vile ambavyo Marekani haikukosa wa kuitetea, afadhali kuwa hadi sasa SBA-List hawajashinda kesi ile na hapa kwetu tusingekosa SBA-List wa Kitanzania.

Utendaji wa wagombea ni moja ya kipimo kizuri cha wananchi kumpima mgombea wao, ushiriki wake katika masuala ya kijamii na wala si ule ushiriki wa kinafiki wa siku za karibu na uchaguzi. Ya w a p a s a m u t a l i i vizuri tangu mwanzo aliwaongozaje hadi leo hii anataka tena ridhaa yenu ili awaongoze tena.

Wapo pia wagombea w a n a o e n d e s h w a n a misimamo ya vyama vyao, misimamo ambayo ni kinyume na matakwa yenu, mukimrudisha mtu kama huyu bungeni au katika baraza la wawakilishi kisha akaendelea kufanya vile vile, hatutokuwa na wa kumlaumu isipokuwa ni sisi wenyewe ambao t u m e m r u d i s h a t e n a uongozini. Mwanasiasa bora ni yule anayejali matakwa ya watu wake na sio misimamo ya chama chake ambayo inakwenda

Inaendelea Uk.14

Page 14: ANNUUR 1194.pdf

14 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

Mchezo wa kuwapatia watu kula kila baada ya miaka 5

Inatoka Uk. 13kinyume na matakwa yao. Mwanasiasa huyo ni yupi? Wewe unamjua zaidi. Ukiwa mpiga kura utakuwa unamjua ni yupi anayekujali na yupi anayejali tu kinachosemwa kutoka makao makuu yake.

Kila jimbo linajua kuwa mbunge wetu alikuwa ni mtu wa kuishi Dar es Salaam tu au alikuwa na ushirikiano na sisi. Wale wa kuishi Dar halafu akichomoza sura yake wakati wa uteuzi na chama chake kikampitsha sasa anataka apitishwe na wananchi, hukumu ya mtu kama huyu munaijua nyinyi hata akaja na maneno ya namna gani yatakuwa tu ni sehemu ya propaganda za kisiasa la wala si ukweli.

Wale wanaosema siasa ni mchezo mchafu wanazo sababu. Moja ni kuwa wanasiasa wana tabia ya kuchanganya ukweli n a u o n g o . A n a we z a kuwaahidi mambo mengi yaliyompita kichwa au asiyoweza kuyatekeleza ilimradi tu achaguliwe kisha ndio imepita hiyo.

Kampeni z imeanza

BAADHI ya wajumbe waliopo katika timu ya kampeni ya mgombea Urais kwa tiketi ya CCM wakiwa katika picha ya pamoja. Kulia ni Dk. Harrison Mwakyembe na katikati ni Makongoro Nyerere siku ya uzinduzi wa kampeni wa hicho hivi karibuni.lakini nyinyi ni mashahidi kuwa viongozi waonataka r i d h a a ya k u o n g o z a

wa n a t o a a h a d i k i l a wapitapo kila wanapo simama na kuzungumza

na watu wao wanaahidi, ahadi kumi hadi ishirini. Hivi ni kweli wanaweza

k u z i t e k e l e z a ? Au n i s e h e m u y a m c h e z o wao mchafu ili kuingia madarakani? Yatupasa tufikiri na tutulize akili zetu ili kumpata kiongozi bora.

N i m a l i z i e k w a kuwatakia kampeni za amani vyama vyote . Jeshi la polisi l iwepo kulinda watu na wala si kuendeshwa na vyama. Amani ni jambo muhimu katika nchi yetu, nchi kama hii na ilivyo na watu wengi mambo yakiharibika basi yanaharibika kweli kweli.

H i v y o k i l a c h a m a k i h e s h i m u c h a m a chengine, matusi yasiwepo n a w a l a k u s i w e p o na kampeni za uongo, waeleze wanachi ambalo utaweza kulitekeleza na wala usitie chumvi kwa ambalo una uhakika liko nje ya uwezo wako.

Wananchi tuzidi kuwa makini na wagombea w a o n g o w a n a o j a z i a yasiyowezekana, wasio na akili na uwezo wa k u o n g o z a . U m a k i n i unahi ta j ika kumpata kiongozi bora, vinginevyo, kupiga kura i tabakia mchezo wa kuwapa watu kula kila baada ya miaka mitano.

SH U K U R A N I z o t e anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola mlezi

wa ulimwengu na rehema na amani zimfikie mbora wa Manabii na Mitume Muhamad (saw) na jamaa zake na shahaba zake wote.

Ama baada ya utangulizi huu mfupi kwa yakini Mwenyezi Mungu mtukufu amemuumba mwanamke akiwa ni binadamu mwenye haki zote kuanzia utukufu, uhuru na kumiliki na pia kufikiri, kufanya kazi na mengineyo.

A m e s e m a M we n ye z i

Usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika ibada na majukumu

Na Dk. Akili Mohamed Akili

Mungu mtukufu, “Kwa h a k i k a Tu m e m t u k u z a binadamu (mtu), aya ya 70 Israi. Na wala Mwenyezi Mungu hakubagua kuwa utukufu ni kwa wanaume peke yao na akasema juu ya uhuru kwa wote kwa mambo yasiyodhuru wengine kwa wanamume na wanawake. “Hapana kulazimisha katika dini” (Albakarat 256).

Kwamba kuna uhuru kamili katika imani au kukosa imani, lakini atakayeamini atapata maisha bora hapa duniani na akhera na lililo bora ni uhuru wa kila jambo la kimaisha ya akhera na aya tukufu haikutenga uhuru kwa wanamume tu. Na amesema Mwenyezi Mungu juu ya kusaidiana watu wote wanamume na wanawake, walio Waislamu na wasio Waislam. “Na saidianeni kwa wema na kumcha Mungu, na wala msaidiane kwa madhambi na uadui” Surat Almaaida aya ya 2.

B a s i wa n a m u m e n a wanawake katika asili ni sawawasa kwa wastani wa mambo yote aliyoyalazimisha Mwenyezi mMungu kwa watu, ili tu wapate maisha bora hapa duniani, basi na wajenge nchi na waingie

peponi kwa wale wanaoitikia wito wa ibada sawasawa akiwa ni mwanamke au mwanamume. Na wataingia motoni kwa wale wenye kumuasi Mungu na wala pepo haikuandaliwa kwa ajili ya wanamume tu peke yao na yametiwa nguvu juu ya hayo pale aliposema Mwenyezi Mungu mtukufu, “Yeyote mwenye kufanya mema awe mwanamume au mwanamke, naye akiwa ni muumini basi tutampa uhai mzuri na tutawalipa ujira wao kwa uzuri zaidi kwa yale waliyoyatenda” Annahli 97.

N a n e n o l a k e , “ N a akawajibia Mola wao mlezi, kuwa mimi sipotezi matendo ya mtendaji miongoni mwenu awe ni mwanamume au mwanamke” al Imrani 195.

Na amesema Mtume (saw), “Kwa hakika wanawake ni ndugu wa wanaume” Ameitoa Abuu Daudi kwa mapokezi sahihi.

Umekuja Uislamu na kumuweka mwanamke katika sehemu yake ya kawaida na kumrudishia haki zake na utu wake pamoja na daraja lake ambalo alinyang’anywa chini ya kiza cha dhulma na uharibifu kwa desturi mbaya.

Ukati nguvu Uislamu juu ya mmoja na makuzi yao kati ya wanamume na wamawake. “Na kumuumbia mwanamume kuwa na mkewe na kusambaza kutokana na wao, wanaume wengi na wanawake na muogopeni Mwenyezi Mungu ambaye a t u w a u l i z e n u j u u y a kuunga udugu, kwa yakini hakuacha kuwa Mwenyezi Mungu kwenu ni mwenye kuwasubiri” Surat Nisai aya ya 1.

Na umekataa Uislamu msimamo wa washirikina na kung’ang’ania alama zao na kutofahamu nafasi ya mwanamke katika maisha n a k u wa s h i n a k a t i k a nidhamu ya maisha sawa na mwanamume. Bali yeye ni chanzo kikuu cha kuendelea familia na kwa hivyo basi, U i s l a m u u m e m t a z a m a kama ni zawadi toka kwa Mwenyezi Mungu na Qur’ani ikamtanguliza katika kumtaja k u l i k o m w a n a m u m e . A m e s e m a M w e n y e z i Mungu, ”Humpa amtakae m wa n a m k e n a h u m p a a m t a k a e m wa n a m u m e a u h u m c h a n g a n y i a mwanamume na mwanamke, n a h u m f a n ya a m t a k a e ngumba” (49-50) Shura.

Kwa hakika katika jamvi la heshima na utukufu n a m a p e n z i k wa v i l e anavyoiandaa jamii kinafsi ili kuipokea kila mtoto kwa utulivu na nafsi iliyoridhia na kuaminia misaada ya Mwenyezi Mungu amesema mwenyezi mungu mtukufu” (na wala msiwaue watoto wenu kwa kuogopa umasiki, sisi tunawaruzuku wao na nyinyi” Israi 31.

K a m a U i s l a m ulivyomtukuza mwanamke tangu akiwa bado kijana na kumpa mambo yake muhimu na matakwa yake maalum katika maisha yake, nayo ni kuitengeneza nyumba yake na kumchagua mume akasema (saw) “Asiozeshwe mwanamke mkubwa ha ashauriwe na mwanamke mdogo hadi atoe idhini mwenyewe” Wakasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni ipi idhini yake? Akasema “Ni kule kunyamaza”. Ameipokea Imam Muslim.

Na Uislamu umemuwekea mwanamke kila kitu chake cha lazima na kumpa haki zake nyingi kama vile, uhuru wa kumiliki kwa njia ya usawa na mwanamume.

Inaendelea Uk. 15

Page 15: ANNUUR 1194.pdf

15 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

KUNA hatar i i l iyo jitokeza na ambayo inaonekana kukua

katika karne yetu hii ya baadhi ya watu kujinadi kwamba wao ni wapenzi wa Sunna lakini hatimaye wanaipinga Sunna hiyo hiyo wanayo dai kuipenda na kuitetea. Funga ya siku tisa za mwanzo katika mwezi wa Dhul-Hijjah {Mfunguo tatu}, ni Sunna maarufu mbele ya Wanazuoni wetu walio bobea katika somo la Sunna na Fiq-hi miongoni mwa wanazuoni walio tangulia na walio ishi au wanao ishi katika karne yetu hii. Kwani Sunna hii imethibiti kwa Hadithi ya Bwana Mtume {Swalla Allahu Alaihi wa sallama} iliyo sahihishwa na Wanazuoni wajuzi na weledi wa somo la Hadithi. Na miongoni mwao ni Almarhuum Sheikh Muhammad Nasirid diin Al-Albaaniy.

Katika wakati huu kuna wajasiri walio ondoa khofu nyoyoni mwao na haya nyusoni mwao, wakashamiri kutaka kuikataa Hadithi ya Bwana Mtume kwa lengo la kutaka kuifuta Sunna hii ya kufunga katika siku tisa za mwanzo za Dhul-Hijjah.

Funga hii ni maarufu vile vile katika madhehebu ya Fiq-hi, katika madhehebu ya Imamu Shafiy, Hambali na kadhalika sio taabu sana kuujua umuhimu wa Sunna hii kwa sababu imo katika vitabu vingi maarufu vile vya

Ni nani anayekataa funga ya siku tisa za Dhul-Hijjah?Na Abdallah A. Bawazir

zamani na hivi vya sasa.A l - m a r h u u m S h e i k h

A b d u l - A z i z B i n B a a z i aliulizwa kuhusu mtu anaye ikataa Sunna hii, akajibu kama ifuatavyo:

“Huyo ni mtu mjinga (hajui Sunna) inatakikana afundishwe”.

Kwa sababu hilo liko wazi katika Hadithi nambari 2437 katika Sunan Abi Dawood kwamba Bwana Mtume {Swalla Allahu Alaihi wa sallama} alikuwa akifunga siku tisa za Dhul-Hijjah.

L a k i n i k wa u p a n d e mwingine, huenda ikawa kuna baadhi ya wasomi walio tatizika katika Sunna kwa sababu ya Hadithi

nyengine sahihi inayo ashiria kugongana na Hadithi hii. Yaani ile Hadithi yenye kauli ya Bi. Aysha {Radhiya Allahu An-haa} isemayo:

“ S i k u p a t a k u m u o n a Bwana Mtume {Swalla Allahu Alaihi wa sallama} kamwe katika hali ya kufunga katika siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah”.

W a n a z u o n i w e t u wameuzungumzia sana mgongano wa Hadithi mbili hizi katika vitabu vinavyo sherehesha Hadithi hii . Lakini kwa mwenye kufikiri kidogo tu, atagundua kuwa hapa hakuna mgongano wa kumfanya mpenda Sunna asifunge siku hizo kwa

sababu ifuatayo:Hadithi yenye kauli ya

Bi. Aysha inakanusha na Hadithi tunayo itegemea sisi hapa inathibitisha na katika kaida {kanuni za fani ya Hadithi} zetu sisi ni kwamba katika mgongano wa aina hii , Hadithi inayopewa umuhimu wa kwanza na kufanyiwa kazi ni ile Hadithi inayothibitisha na wala siyo ile inayo kanusha.

Sasa inaonekana kuwa ni kawaida hapa nchini kwetu kila unapo karibia mwezi wa Dhul-Hi j jah k a m a h i v i , M a s h e i k h wetu wakubwa kubishana kuhusu funga ya Arafa. Wengine wanasema siku ya

kufunga Arafa ni ile siku ya kisimamo katika uwanja wa Arafa huko Makka. Na wengine wanasema kwamba funga hiyo inategemea mwezi mwandamo hapa kwetu hata kama siku hiyo itatofautiana na siku ya kisimamo cha huko Makka. Wakati mwengine mjadala huu unakuwa mkubwa kiasi cha kuwapelekea baadhi yao kuandaa muhadhara ili kutetea siku moja hiyo tu katika mwaka. Si hivyo tu bali baadhi yao wanatenga khutba maalumu siku ya I jumaa juu ya Mimbari ili kutetea siku moja hiyo katika mwaka. Mjadala huu upo mpaka leo hii, inabidi tuwaulize Masheikh wetu hawa wanao vutana maswali yafuatayo:

Mosi, ni upi msimamo wa o j u u ya f u n g a ya siku tisa za Dhul-Hijjah? Wanakubali kwamba hiyo ni Sunna au hawaikubali? Kama hawaikubali, basi itabidi wayakubali maneno ya Al-Marhuum Sheikh Bin Baazi kwamba wanahitaji kuelimishwa. Lakini kama wanakubal i pia i tabidi tuwaulize sababu i l iyo wafanya wao washabikie sana funga ya siku moja tu ya Arafa na kuzipuuza siku nane za kabla ya siku ya Arafa?

Pili, Vitabu vya Fiq-hi na vitabu vya Hadithi karibu vyote au vil ivyo vingi, vinaeleza kwamba tofauti iliyopo baina ya funga mbili hizi; funga ya siku nane kabla ya Arafa na funga yenyewe ya Arafa, ni kwamba funga ya siku nane ni Mustahabu { S u n n a } n a f u n g a y a Arafa yenyewe ni Sunna Muakkada {iliyo kokotezwa} tu. Lakini zote ni Sunna na zote zimethibiti kutoka kwa Bwana Mtume {Swalla Allahu Alaihi wa sallama}. Kwa maana hiyo basi, hii tofauti ya ziada Masheikh zetu hao wameipata wapi? Kwani kuna kauli inayosema kwamba kat ika mwezi wa Dhul-Hijjah funga ya Sunna ni ya Arafa peke yake? Yaani, Bwana Mtume alikuwa akifunga siku moja tu ambayo ndio Arafa?

K wa n i n i M a s h e i k h zetu badala ya kuzozana katika mihadhara yao na Mimbari zao kwa ajili ya kuitetea siku moja tu ya Arafa, hawakubaliani na sisi kuwahimiza watu katika mwezi wa Dhul-Hi j jah kufunga siku tisa zote za mwanzo na Arafa ikawa humo humo? Hawaoni kwamba kwa utaratibu huu mizozo na mabishano baina yetu yatakuwa yamefikia mwisho na kuisha?

(Kwa mawasiliano 0773 215 898)

Usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika ibada na majukumuInatoka Uk. 14

A m e s e m a M we n ye z i M u n g u m t u k u f u , “Mwanamume ana fungu lake katika mali ya wazazi na ndugu wa karibu na mwanamke ana fungu lake katika mali za wazazi na ndugu wa karibu, ikiwa mali ni kidogo au nyingi, ni fungu maalum” Nisai 7.

N a U i s l a m u ameheshimu umi l ik i huu na kuutukuza kwa kumpa uhuru mwanamke wa kutumia. Amesema M w e n y e z i M u n g u “ w a p e n i w a n a w a k e mahari zao za wajibu na wakitamani wenyewe kwa nafsi zao, basi kuleni kwa vizuri kabisa” Nisai 4. Na Qur’ani imemuweka s a wa m wa n a m k e n a mwanamume mbele ya

sheria haki na wajibu, kama vile haki ya kufungu mkataba na masharti yake na haki ya kushitakiwa, kutetea haki zake mbele ya mahakama.

Amesema Mwenyezi Mungu “Na wao wana haki sawa na mfano wa wanamume kwa wema” Albakarat 228.

Na imekuja kat ika hadithi tukufu kwamba Mtume (saw) amesema, “Kwa hakika wanawake ni ndugu wa wanamume”. Ameipokea Imamu Abuu Daudi na Tirmidhi.

H i v y o b a s i , m w a n a m u m e n a mwanamke ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na huenda mwanamke mcha Mungu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko m wa n a m u m e . “ K wa

hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye kumuogopa sana Mwenyezi Mungu” Hujurat 13. Hivyo pepo haikuandaliwa kwa ajili ya wanamume tu pasi na wanawake.

Kwa yakini Qur’ani tukufu imekuwa mfano bora kwa wanawake pale a l iposema Mwenyezi Mungu mtukufu, “Na amepiga mfano Mwenyezi Mungu kwa walioamini, pale mke wa Firauni aliposema Mola nijengee mimi kwako nyumba peponi na uniokoe mimi d h i d i ya F i r a u n i n a matendo yake na uniokoe mimi dhidi ya watu wenye dhuluma, na Mariam bint Amrani, ambaye amehifadhi tupu yake na

tukampulizia sisi kutokana na Jibril na akathibitisha maneno ya Mola wake mlezi na vitabu vyake na kuwa miongoni mwa watu wema”. Atahrimi 11-12.

Kwa yakini umekuja U i s l a m n a t a b i a nzuri, na vyanzo vya kumyanyua mwanamke, na kumuhifadhi yeye na heshima zake, na kumrudishia haki zake zilizotekwa tangu muda mrefu, na kumpa haki zake zote kwa ukamilifu mbele ya watu wote, ili watu wote wajue utukufu na ukuu wa dini ya Kiislam na uadilifu wake kati ya viumbe. Mwenyezi Mungu ndiye ambaye anayeongoa katika haki na njia iliyonyooka.

Page 16: ANNUUR 1194.pdf

16 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

Inatoka Uk. 12

Mabadiliko: Nafasi ya Lowassa katika siasa za Tanzaniakuvunja nchi, bali kuondoa umaskini uliokithiri. Ila dhamira hiyo bado ipo katika lindi la ukungu wa fitna, kwani inasulubiwa kuhusu kukubalika (yaani, miongoni mwa makuhani) kwa kiongozi wake Edward Lowassa kuwa hakidhi viwango vya usafi vilivyowekwa na mtiririko wa fitna katika CCM. Aliwahi kuhusika na mkataba wa kuzalisha umeme binafsi, tunaambiwa ulileta taabu.

Kumbe taabu yenyewe ilisababishwa na wabaya w a k e , w a l i o k a t a a kuidhinisha mkopo mdogo tu kukamilisha mradi wa kutwaa mtambo, ukachelewa takriban miezi sita. Licha ya kuwa fitna inalenga tukio hilo (kwa uwongo kuwa ulikuwa mpango mbaya, wa mtambo wa megawati 100 ambako serikali inalipa kwa miaka miwili, wakisahau ulikuwepo tayari mtambo wa megawati 100 ambako serikali inalipa kwa miaka 20), suala halisi ni utajiri wa Lowassa, Ndiyo nanga ya mabadiliko nchini; chanya au mbaya?

Ndiyo hapa linakuja suala la utajiri wa Lowassa, kuwa unatokana na ufisadi kama wahafidhina wanavyosema, au ni baraka za Mungu hasa kutokana na uhitaji wa mabadiliko katika wakati unaokuja. Kuna vielelezo viwili vya suala hilo, au tuseme baada ya kupangua hoja ya msingi, kuwa kama utajiri wa Lowassa unatokana na ufisadi, kwanini waliokaa

madarakani miaka yote h a w a n a u t a j i r i k a m a wa kwake, na hajawahi kutuhumiwa kwa wizi halisi? Ujanja wa hapa na pale (ten percent), kungemfikisha alipo, au ujasiriamali?

Ukiangalia kwa karibu unaona kuwa utajiri wa Lowassa ni sehemu ya agenda ya kimaandiko kuhusu mabadiliko, kwani Mungu anainua mali binafsi akiwa na Ibrahimu, na Lowassa ni kielelezo cha hilo na kupitia kwake mfumo wote ubadilike. Dhana ya Misri, ya Farao, ni kuitegemea dola, watu wote wawe watiifu. Wawe mali ya serikali , wa t u m wa wa s e r i k a l i , wakulima wabaki katika ardhi ya serikali hawana chao.

Wahafidhina hudai miiko ya uongozi inawafanya v iongozi wawe kar ibu na watu; dhana potofu. Hali halisi ni kuwa miiko hiyo inahamisha hisia ya ujasiriamali kutoka katika azma ya kufanya kazi fulani yenye faida, kuipeleka azma hiyo katika kituo cha kazi, mtu akusanye kwa siri ajenge nyumba (labda hata ya kifahari), na ya kupangisha, na hata kwa mwandani wake mmoja au wawili. Anabaki "kiongozi msafi," ila akifanya ujasiriamali halisi na kufaulu, wakipata mwanya wowote wanasema ni mwizi. Mwalimu alidai kuwa utajiri wa Lowassa ulitokana na kuwa mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano pale Arusha; majuzi mfitini

mmoja alidai unatokana na uwaziri mkuu.

Huyu mfitini, anayejiamini sana kuwa ni mwadilifu, aliwahi kutibiwa katika hospitali ya mkwewe (kwa mujibu wa taarifa za wakati huo) kwa maradhi ya mguu kwa takriban wiki moja. Bili iliyofikishwa serikalini na malipo yakaidhinishwa ni shilingi milioni 100 - huo siyo ufisadi! Ni ujanja ujanja tu wa kila siku, na unakubalika kwa sababu mtu wa aina hiyo anajitwalia kidogo tu na haweki mfumo hatarini. Lowassa na Rostam Aziz, kwa vile ni wafanyabiashara halisi, wanaweka mfumo hatarini, waubadilishe.

M g o m b e a w a C C M a n a p a n i a k u o n d o a watu wachache wabovu,

aulinde mfumo, wakati umasikini unatokana na mfumo wa Misri, wa dola hodhi, iliyoshika kila kitu, kuneemesha watawala . Baada ya kukwama miiko ya uongozi, wahafidhina wa n a j i t a m b u l i s h a k wa kutokuwa na uhusiano wa kibiashara na makampuni binafsi, hasa ya nje. Ndiyo yanayoyasumbua mashirika ya u m m a n a wa t e t e z i wake bungeni, wasiotaka ya k a g u s wa . Ya k i i n g i a mikononi mwa watu binafsi yatalipa kodi, tusipoteze s h i l i n g i t r i l i o n i m b i l i kulipa madeni TANESCO, ya ubadhirifu na kulinda uwekezaji.

K u i n g i z a m t a m b o kutakuwa ujasiriamali, bila ulinzi maalum wa uwezo

wa kuzalisha kama sasa. Hivyo hisia ya kina ya kutaka mabadiliko ambayo ni aina ya maombi, huleta uwezekano wa mabadiliko kufikiwa katika njia isiyo ya mparaganyiko wa moja kwa moja. Kuna hatari ya mikasa kwani dhambi za Watanzania na hasa katika kuua siyo Albino tu, ila watu wa aina tofauti ili mtu afikie utajiri, ni nzito. Huwezi kuhakikisha kuwa hakuna hukumu i la maombi ya mabadiliko chanya na kumtumia Lowassa aliyefaulu kutetemesha mfumo, aondoe mwiko wa kutobinafsisha, atue mizigo. Uhakika haupo ni uwezekano.

Lowassa na Yakobo: Baraka za utajiri kwa vipindi tofauti vya kazi ya Mungu

Inatoka Uk. 12bado wazazi, au Rebeka, aliwatofautisha wanae, na wakatofautiana kabisa. Yakobo alioa wake wawili ambao n i ndugu wa tumbo moja, wakafuatana na wajakazi wao, Yakobo akiwa amepata utajiri mkubwa wa mifugo. Wajakazi nao wakazaa na Yakobo kwa kuruhusiwa na wake zake, wakafikia wana 12.

Bi la uta j i r i Yakobo asingeweza kuinua kizazi cha wana nao (mabinti zake hutajwa kwa nadra) na hapakuwa na tofauti kati yao kuhusu nani mwana wa mke mkubwa au mdogo, mwana wa mke au mjakazi. Ila kwa vile 'Shetani anaishi milele,' tofauti zao zilianzia kwa

baba yao kumpenda sana Yusufu, kama mwana mwenye heshima, adabu, msikivu na hata haiba ya kupendeza. Kijicho hicho kikawa nyenzo ya utukufu wa Mungu, wakataka kumuua i l a ika i sh ia kumuuza kwa msafara wa wa-Ishmaeli, akanunuliwa Misri, akastawi.

Kielelezo kuhusu ubaya wa ndugu zake Yusufu na jinsi Mungu alivyokuwa na nia na ubaya huo, ili

Yusufu aondolewe katikati yao na kuandaa ujio wa ukoo wa Yakobo nchini Misri. Ni hapo historia yote ya unabii na sheria pale Musa anapoinuliwa m i a k a 8 0 0 b a a d a y e (kuanzia 2300 BC hadi 1500 BC) inaposimama.

Kuinua na kuteketeza himaya au kibri katika maisha ya watu, siyo mzunguko hasi wa mema na mabaya, wa vicheko na vilio, ila mtiririko wa kuvunja nguvu za

Ibilisi, ambaye baada ya Gharika Kuu anachukua sura ya Mungu Jua wa Babeli aliyeabudiwa pia Misri (na kwingineko duniani). Ndiye mjenzi wa ule mnara wa Babeli, akatukuzwa, na ndiye hasa anayehitaji sadaka ya binadamu amuongezee mtu nguvu, atawale . Ndiyo hapo inakuja ibada ya sananu (huruhusu sanamu zifanywe kwa mfano wake), na historia ya wokovu. Katika kila

mfumo wa jamii kuna msuguano na mtiririko wa matukio ya kupambana kwa jema na baya, jema likiwa ni kutenda mema peke yake bila fidia kutoka kwa Mungu; baya ni kutenda utakalo, kutoa sadaka upate nguvu.

Kuna uhusiano wa karibu kati ya utajiri wa Lowassa na hawa wakuu wa zamani, kuwa utajiri w a o u l i w a w e z e s h a kuwa huru, kutoogopa kutofautiana na mfalme, Farao wakati Ibrahimu akiwa Misri, na Abimeleki wakati akiwa Kanaani. Katika mazingira yetu, m f a l m e a l i k u w a n i M w a l i m u N y e r e r e wakati akiwa hai, na fikra ya Mwalimu akiwa

Inaendelea Uk. 17

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CHADEMA-UKAWA, Mhe. Edward Lowassa (katikati)

Page 17: ANNUUR 1194.pdf

17 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

Lowassa na Yakobo: Baraka za utajiri Inatoka Uk. 16amekufa, au uongozi wa chama tawala kama walinzi wa fikra hiyo. Lowassa amekuwa kiongozi huru mjasiriamali, m f a n y a b i a s h a r a aliyefaulu; wengine hudunduliza kidogo wakichota serikalini.

Kuna uwezekano mkubwa wa Mungu kukamilisha kazi ya kupangua kabisa dhana potofu za Azimio la Arusha za kuitenga Tanzania na mitaji duniani, na kuwabana viongozi wategemee ajira ili wawe watiifu kwa chama na serikali, yaani Nyerere na warithi wake. Ndiyo msingi wa ubadhirifu, wizi uliokithiri na huku viongozi wote w a n a j i a m i n i n i wasafi, kwani wizi wa kudokoa hatma yake ni maisha bora katika ngazi ya famil ia . Akili za walioenda shule kwa jumla zinajielekeza katika u d u n d u l i z a j i n a kupinga uwezekaji, ubinafsishaji.

Endapo hali hiyo itafikiwa, utakuwa muujiza wa Mungu k u m w i n u a m t u mmoja awe na nguvu, a l e t e m a f u r i k o ya wafuasi akiwa CCM apangue hila za mwenyekiti wa chama kuhusu nani awe mgombea, aweke aliyefaa zaidi, na yeye aende kugombea upinzani. Ni aina ya mnara wa Babeli kisiasa, na chanzo chake ni u-Yakobo wa Lowassa, kama ile hadithi ya Uyunani ya mtu akigusa kitu huwa dhabahu. Ni kuanza na ng'ombe u u z e w a c h a c h e uweke hizo fedha benki, ukope nyingine uunde kampuni ianze kujilipa, kila wakati.

Kuna uwezekano p i a w a k u u n d a kampuni za madini hasa kutokana na hali ya kutapakaa kwa madini mkoani Arusha na Manyara, nje ya ushiriki katika maeneo mengine ya biashara, kama kununua mashamba

na kukata viwanja vya bei mbaya baada ya miaka kumi, n.k. Au kununua viwanja sehemu za mijini na kujenga maghorofa baadaye, iwe ni mtu binafsi au kwa ubia na wengine, n.k. Ni vitu ambavyo ukivifikiria vinawezekana, lakini baraka za Mungu ni kumwezesha mtu mmoja afanye hivyo, ili aipangue milki ya CCM.

Mungu aliitingisha Misri akitumia silaha n d o g o , y a S a r a mke wa Ibrahimu ambaye Ibrahimu alimwambia kokote watakapokwenda a s e m e n i n d u g u yake Ibrahimu, ili watoe posa kwake, na s iyo kumwua n a k u m c h u k u a Sara. Ila alijua kwa u f i c h o M u n g u angejitambulishwa k w a o h i m a , wamrudishe Sara.

Uta j i r i wa mtu m m o j a u n a m p a nguvu, mradi kuna kitu kama utawala wa sheria na siyo udhalimu wa moja kwa mo ja , kuwa huru na utawala, na kwa kushiriki kwake k i s i a s a , k u w e z a kuweka tofauti kati ya itikadi iliyopo, n a i n a y o t a k i wa . Lowassa anaogopwa na watu wa CCM k u w a a n a w e z a k u r u d i a s e r a z a awamu ya pili za Rais Ali Hassan Mwinyi ambazo Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum anajizuia tu kuzitamka waziwazi, kuondoa mizigo ya mashirika ya umma begani mwa serikali. Nje ya baraka ya utaj ir i , kazi hiyo i s i n g e f a n y i k a , n a k w a m a a n a h i y o u p o k a b i s a uwezekano kuwa inaweza kufikisha mabadiliko, au iwe ni mchango muhimu w a m a b a d i l i k o makubwa kwa idadi ya wabunge, kupooza utukufu wa CCM.

Kibri cha CCM ni kukataa watu wengine kuwa huru k u k a a k we t u n a kununua mali, pamoja na kushirikiana na wageni kununua mali kutoka kwa wenyeji, wampe mwenyej i

mtaji wa kufanya b i a s h a r a , k i l i m o bora, s iyo kuishi kat ika umaskini , n a wa o wa f a n ye biashara wastawi. Ndiyo huu mfumo jadi wa ardhi kuwa mali ya serikali ili watumwa wa serilali, wakulima, wabaki katika ardhi hiyo wasiwe na uwezo wa kumwuzia mgeni kwa bei ya soko, na akinunua ana haki tu ya kutumia, huweza k u n y a n g ' a n y w a na kina Magufuli w a k a t i w o w o t e kama alivyotangaza m a j u z i . M u n g u anachokitaka hapa nchini ni unyeyekevu wa kukubali kuwa wengine wana haki wa k i t a k a k u i s h i hapa nchini, ambayo inategemea mfumo wa mali binafsi ili wanunue bila hatari ya kunyang'anywa na warithi wa Farao na Abimeleki. Mungu akiwa mmoja, hiyo i n a w e z e k a n a . Ubaguzi wa kina unatokana na ibada ya sanamu, ya kila taifa na mzimu wake.

S u a l a n i k a m a Mungu atafanikisha

m a b a d i l i k o y a mfumo kwa kuingia mali binafsi, na siyo tu mabaliko ya Baraza la Mawaziri waingie U K AWA , h a l a f u waendeleze f i tna ile ile, wakatae mali binafsi, waendeleze u m a s k i n i . K w a u p a n d e f u l a n i baraka ya Mungu k w a L o w a s s a kufikia madarakani inategemea dhamira hiyo. Kama ana nia ya mabadiliko ya kweli, kupangua mfumo huu wa jadi, na kuacha kibri cha kufukuza makampuni ya nje, wawe na haki sawa hapa nchini kama raia wengine. Endapo atabania dhamira yake atake kufuata mfumo uliopo licha ya baraka za Mungu kwake, kuwa mtu huru kuupangua m f u m o k w a n i haitegemei CCM, kuna hatari ya utabiri mbaya kwake ambao u l i t a j w a m w e z i Januari na mtabiri Hassan Yahya pamoja na Sheikh Sharrif Mwitongo kutimia. N i k u a m b i w a 'kahubiri Ninawi.' wewe useme 'sitaki....'

1.Bismillahi nakaa, ndugu zangu sogeeniNinayo ya kutongoa, si mengi kukuchosheniMachache ya manufaa, naomba yasikizeniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha2.Kuchapo twaona ndoa, zafungwa misikitiniSherehe zimeenea, kila kona mitaaniKwa wingi twahudhuria , mashahidi si utaniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha3.Mtume katuusia, enyi ndugu ikhwaniWake wema kuchagua, tuwapendao nyoyoniTuishi nao kwa nia , ya kudumu maishaniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha4.Mashekhe Makadhi pia, wajibu wamebainiKhutuba watusomea, waadhi, nasaha ndaniTwapaswa kuzingatia, tukaishi furahaniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha5.Kuozwa mke sheria, kutoka kwa RahmaniKaka usije zembea, kujifanya hayawaniKaa na mwenza tulia, si kwema vichochoroniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha6.Bi Harusi nawe poa, mpende wako mwandaniSasa umeshaolewa, ukome vibarazaniHakuna ila umbeya, na matusi ya nguoniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha7.Ndoa inahitajia, subira iwe usoniMmoja akikosea, muombane samahaniVisasi kutobakia, na kumlani shetwaniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha8.Kila siku kumbukia, hili liwe akiliniNdoa ni kama mauwa, yalopandwa upenuniUsipo yamwagilia, yatachanua kwa niniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha9.Harusi twaziombea, kwa wetu Mola MananiZisiingie madoa, tukaishi kwa huzuniZihifadhi Ya Jalia, na ibilisi fattaniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha10.Namalizia kwa dua, mikono tunyanyuweniAmina kuitikia, ni wetu utamaduniAllah tutakabalia, waja wako tuauniTusizichezee ndoa, ni kifungo cha maisha

SULUHU A. HAMZAC/O ZAINAB H. MTIMA (0777 357 031)ZANZIBAR 0776 720 588

NDOA

1.Dua tumuombe Mola, Muumba asiye shakaHana sifa ya kulala, wala bado hajachokaKafika kila mahala, dunia kaizungukaDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada2.Tuombe kwa zetu shida, Mola atatuauniTwahitajia msaada, sisi kwake masikiniTufanye ni kawaida, asubuhi na jioniDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada3.Hata tukiwa rahani, kuomba tusisahauInazidisha Imani, ya Mola kutodharauHili liwe akilini, na wakati ndio huuDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada4.Mtume katuhimiza kila jambo ni kwa duaHilo tusijepuuza, ovyo tukajiendeaChochote unachoanza, Mola kumuelekeaDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada5.Unapotoka nyumbani, dua iwe ya awaliKujikinga na shetani, wasije kukukabiliMengi majanga njiani, Mungu ayapishe mbaliDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada6.Unapokwenda kazini, kutafuta cha halaliAu la msikitini, swala tano kuziswaliNa iwe hata sokoni, dua kuacha muhaliDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada7.Popote unapokwenda, dua ndio ngao yakoMuumba atakulinda, uepuke masumbukoDua ikisha kushinda, mwenzangu huna mashikoDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada8.Ukiingia chooni, dua usijeiachaUepukane na jinni, huko yeye hujifichaHuo ni utamaduni, uwe nao kutwa kuchaDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada9.Enyi ndugu Islamu, lengo ni kukumbushanaDua kuomba muhimu, uwe nacho au hunaSote tushike hatamu, haya kwetu ni bayanaDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada10.Hapa nimehitimisha, sinalo la kuongezaMachache nilofikisha, anza leo kujifunzaMikono nimeiosha , ni kwenu kutekelezaDua tuombeni sana, ni ubongo wa ibada

SULUHU A. HAMZAC/O ZAINAB H. MTIMA (0777 357 031)P. O. BOX 1898ZANZIBAR0776 720 588

KUOMBA DUA

TAASISI YA ELIMU YA WEC Inawatangazia nafasi za masomo ya Kidato cha kwanza na masomo ya awali PRE-Form One Course itaanza 01/10/2015 hadi 1/12/2015. Tarehe ya kuripoti ni 27/9/2015. Katika shule zake zilizopo Kibaha Pwani.

Masomo yatakayofundishwa (Pre form One):•Hisabati•Kiingereza•Kompyuta•Sayansi•Biashara Shule zina mandhari nzuri ya

kusomeshea na Maabara za kisasa. ADA (Pre-form one course ) Bweni

shs.150,000/= Kutwa shs 80,000/= Madaftari na kalamu zitatolewa

bure shuleni. Kwa mawasiliano: 0754-395186,

0656-313889, 0659-573004, 0786-959522, 0789-887799, 0784-489476, 0765-198360, 0719-904904, 0768-904904.

MASOMO KIDATO CHA KWANZA 2016 (PRE FORM ONE COURSE) 2015

Page 18: ANNUUR 1194.pdf

18 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

KILA ninapomuangalia Samia Suluhu Hassan, n i n a p a t a s h i d a

kufikiria ni kwa namna gani atafanikiwa kushawishi umma wa Wazanzibari kumpigia kura Daktari John Pombe Magufuli itakapofika tarehe 25 mwezi ujao wa Oktoba. Siku hiyo ndiyo siku ya upigaji kura katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kutakuwa na kura ya kumchagua Rais wa Jamhuri, Mbunge wa kuingia Bunge la Jamhuri na Diwani wa kufanya maamuzi kwenye Baraza la Madiwani katika Halmashauri mbalimbali.

Lakini katika siku hiyo, pia Watanzania wa upande wa Zanzibar, ambao unapokuja uchaguzi mkuu wa Jamhuri huwa wanakuwa na kura mbili – Rais na Mbunge – watapata haki ya kupiga kura nyingine tatu za uchaguzi mkuu wa Zanzibar. Kura hizo ni ya kumchagua Rais wa Zanzibar, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, ambalo ndilo Bunge kwa wao kwa ajili ya kuyaamua masuala yanayoihusu Zanzibar peke yake, pamoja na kura ya Diwani, ambaye huingia katika mabaraza ya madiwani yakiwa nje ya mfumo wa Muungano.

Sasa wakati Samia, mwenye asili ya Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, anazunguka mikoa ya Tanganyika kumuombea kura Dk. Magufuli, atawajibika k u r u d i k wa o Z a n z i b a r kufanya kazi hiyo hiyo. Samia ambaye elimu yake ni ya kiwango cha Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) aliyoipatia nchini Marekani, katika masuala ya uongozi wa fedha, baada ya kuanza kusomea takwimu kiwango cha cheti, ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea mwenza.

K wa k u wa m g o m b e a mwenza, jukumu lake ni kusimama sambamba na Dk. Magufuli anayegombea urais. Magufuli akichaguliwa, moja kwa moja atakuwa amteua Samia kuwa ndiye makamu wake wa Rais . Kuf ik ia hatua hiyo, Samia atakuwa na wajibu wa kujipa muda kuzunguka kwenye majimbo ya Zanzibar kumpigia chapuo Dk. Magufuli ambaye sio tu ni mgeni machoni pa Wazanzibari, bali kwa hakika hafahamiki kisiasa.

K w e l i a n a s i k i l i k a n a akisema hili na lile akiwa katika majukumu yake ya kikazi kwa wadhifa wa uwaziri, tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza naibu waziri wa ujenzi baada ya kuingia serikali ya awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa na baadaye kupandishwa kuwa waziri kamili, lakini hakujisumbua kuwa karibu na Wazanzibari.

Inawezekana kwa kujua mazingira ya Zanzibar na ugeni wa Dk. Magufuli, ndipo CCM wakamteua Samia kushika ugombea mwenza wakitarajia kwa uanajike wake, atamudu kuuvuta umma umkubali daktari huyo na kushuhudisha mapenzi yao kwake kwenye sanduku la kura. Ni utabiri uliokwenda

Samia ana kazi ngumu kumnadi Magufuli Z’bar

Mwenyewe ashajipalia mkaa...Baada ya yale ya Katiba Dodoma

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli (kulia) akiwa na mgombea mwenza Bi Samia Suluhu Hassan.

Na Mwadini Ali

mrama. Ninavyoyaona mambo, na kwa kuwa Samia ni mwanamke kama wanawake wengine, lakini pia kwa jinsi ninavyoijua siasa ya Zanzibar, uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi u t a w a r u d i a w e n y e w e wajumbe wa Mkutano Mkuu au viongozi wakuu wa chama hicho.

Hakuna historia hata nduchu ya mwanamke wa Kizanzibari kupata umbele katika mwenendo wa siasa za Zanzibar. Hao waliotajwa na kutajika, basi si katika kupanda majukwaani wao wenyewe na kuhutubia u m m a . H a t a k i d o g o . Wanawake hao ambao naona ni wachache wa kuhesabu vidoleni, walipata umaarufu kupitia migongo ya waume zao walipokuwa katika kilele cha mafanikio kwenye nyadhifa za kisiasa Zanzibar.

Wanasiasa waliosifika Zanzibar, walijenga taswira nzuri katika jamii kwa kuwa walikuwa wakifuatana na wake zao kwenye shughuli za kisiasa, hasa zilizowafikisha k u p a n d a m a j u k w a a n i kuhutubia. Kwa hivyo wake zao walitambulika tu kwa sababu ndio mbeleko za waume zao. Hilo moja.

L a k i n i j i n g i n e litakalomletea shida Samia katika kumtafutia kura Dk. Magufuli, ni ukweli kwamba yeye mwenyewe amejiangusha, kiasi cha kufikia hatua kwa sasa kuonekana amepotea njia katika kupigania haki za wanawake wenzake, bali kwa zaidi ya hapo, mustakbali wa nchi yake.

Samia alikuwa mwanamke m a k i n i n a s h u p a v u alipokuwa akifanya kazi za harakati wakati akiwa kwenye mashirika ya hiyari ambako alijikurubisha mno

na wanawake kuyatambua matat izo ya ki jamii na kushiriki kupanga mikakati ya namna ya kuyashughulikia.

Kwa wakati wote, alikuwa bega kwa bega na wanawake. Hichi kilikuwa ni kipindi cha miaka ya 1990 wakati hajagusa ulingo wa siasa kabisa. Ingawa alikuwa serikalini, lakini kazi zake akiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) zilimuweka karibu zaidi na jamii. Alipata bahati ya kuwa Meneja Msimamizi wa mradi katika shirika hilo kati ya mwaka 1985 na 1987. Akarudi serikalini na kuwa Ofisa Mipango katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Baadaye akachupa na kushiriki kwa kasi safari hii shughuli za kijamii. Ni hapa al ipewa dhamana ya kuongoza Mtandao wa Mashirika ya Hiyari (NGOs) alikofanya kazi kwa miaka kadhaa kama Mkurugenzi Mtendaji (1988/1999).

Wanaomjua wanasema leo kuwa Samia alipokuwa kule chini, alikuwa mwanamke s h u p a v u k wa h o j a n a mipango. Akijishirikisha na alikuwa mwenye huruma na maono ya mbali katika kupigania haki za wanawake na mafukara. Ni mtizamo huo uliwachochea wanawake wen zak e k u msh awish i kuingia kwenye siasa wakati miaka hiyo ya 1990 inafikia ukingoni. Taarifa zinasema alianza kujisogeza kwa wanasiasa wa kiutawala na Alhamdulillah, alionekana wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2000.

M w a n a m k e m m o j a ambaye yungali kwenye asasi

za kiraia akisaidia kuwajenga wanawake na watu wa hali za chini moyo wa kutambua matatizo yao na kujitahidi kujikwamua, ameniambia alikuwa mmoja wa wanawake wa l i o k u wa m s t a r i wa mbele kumshawishi Samia kupigania nafasi za kuingia Baraza la Wawakilishi kupitia Viti Maalum.

Ni vipi jina lake liliingia akilini mwa Amani Abeid Karume, aliyeshika urais mwaka 2000, sijapata kujua. Lakini hapo ndipo alipoingia Baraza la Mapinduzi baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Jinsia na Watoto.

Ikumbukwe ni wakati CCM iliposhutumiwa kuidhibiti Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ikatumia mwanya kuvuruga uchaguzi na kujitangazia ushindi kwa kila ilichokitaka. Kunapotokea janga kama hilo na ukasikia mtu amepenya na kuteuliwa nafasi kubwa kama uwaziri, ujuwe kuna mengi yalikuwa yanaendelea kabla. Au labda ni ukweli pia kwamba katika mazingira hayo hayo, hata asiyefikiriwa hupenya na kupata nafasi kubwa ya kisiasa au ya utendaji kwenye asasi ya serikali.

Samia aliingia uchaguzi wa 2005 akitafuta jimbo sasa. Alipofanikiwa akarudishwa Baraza la Mapinduzi, safari hii akiteuliwa kuongoza Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji chini ya Rais Karume. Sifa zake ni nyingi kiutendaji mote alimopita.

Pengine shida kwake ilianzia alipoingia siasa za kibunge uchaguzi wa 2010. Aligombea ubunge jimbo la kwao Makunduchi, akashinda. Akateuliwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, chini ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Ukafika muda wa taifa kuingia katika utafutiaji wa katiba mpya ya jamhuri, ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Rais kuipatia jamhuri Katiba itakayodumu kwa miaka 50 mingine ijayo. Bunge la Jamhuri likatunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 ambayo imeelekeza kuwepo Bunge Maalum la Katiba litakalojadili Rasimu ya Katiba i takayokuwa imeandikwa na Tume ya Mabadi l iko ya Kat iba . Bunge hil i l i l ipokutana mjini Dodoma, baada ya kuandaa Kanuni, lilifanya uchaguzi wa viongozi . Akapatikana Samuel Sitta kuongoza bunge, na Samia

akawa naibu wake. Hapo ndipo Samia alipoingizwa mjini. Bunge lile lilifanya kazi ambayo haikuwafurahisha w e n g i , w a l a k u k i d h i viwango na matarajio ya wananchi ya kupata Katiba kwa kuwa CCM ilidhibiti kila kitu na kufanikiwa kuivuruga Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba, na kupandikiza mapendekezo yake.

Kwa sehemu kubwa, Katiba iliyotoka kutokana na bunge lile, inazidi kuikandamiza Zanzibar. Kwanza imeondoa p e n d e k e z o l a k u we p o Muungano wa mfumo wa serikali tatu, na kadhalika imerudisha utamaduni uleule wa kuzuia mabadiliko ya mifumo ya uongozi ukiwemo wa kuiwezesha Zanzibar kutumia fursa zaidi za kujenga uchumi kwa manufaa ya watu wake. Matokeo haya yamechangiwa sana na Samia, kama kiongozi msaidizi wa Bunge Maalum lile, ambaye al isimamia mkakati wa chama chao akishirikiana na wajumbe wenzake wa CCM waliopuuza matumaini ya Wazanzibari kupata katiba inayotambua haki yao ya kujiongoza.

Mwisho wa bunge lile ukawa mwanzo wa wakati mgumu kwao kujitokeza kwa umma kwa ku jua walichokifanya na CCM wenzao wa Tanganyika, ni kinyume cha matarajio ya Wazanzibari na mustakabali wa nchi yao.

Suala la Katiba mpya l i m e h a n i k i z a a k i l i n i mwa Wazanzibari wengi. L i n a c h u k u l i w a k a m a ukandamiza j i wa hak i za Zanzibar. Hapohapo inaaminika suala hilo ndilo lililochochea utawala wa CCM kuwakamata masheikh walio chini ya Jumuiya ya Uamsho na kuwasweka gerezani miaka mitatu sasa bila ya mashitaka yao kutolewa ushahidi.

H a k u n a n a m n a walioshiriki kujenga katiba i n a y o o n e k a n a k u z i d i kuikandamiza nchi huku ikidhoofisha na kuhilikisha v i o n g o z i wa K i i s l a m u kwa kuwanyima haki zao za kifamilia na faragha, wataungwa mkono leo wanapotaka r idhaa ya wananchi.

Samia hajafanikiwa kufuta mtizamo huo. Hisia za chuki dhidi ya CCM zinaongezeka nguvu. Samia alipofika Zanzibar kumtambulisha Dk. Magufuli baada ya kuteuliwa Dodoma, aliona mapokezi ya l i v y o k u wa . H a k u n a kilichobadilika.

H a t a l e o h a l i n d i y o imekuwa ngumu zaidi . Kwa hivyo basi, ninaamini haitakuwa rahisi kwake k u p e n ye z a c h e m b e ya imani kwenye nyoyo za Wazanzibari, kuwashawishi wavoti kwa ajili ya Dk. Magufuli na CCM

Page 19: ANNUUR 1194.pdf

19 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

MAKALA

El i m u n i m a a r i f a anayopata mtu ambayo kwayo, humuwezesha

kuvitazama na kuvijua vitu kwa uhalisia wake. Elimu ndiyo imekuwa nyenzo pekee ambayo athari yake inaonekana katika nyanja zote za kimaisha; kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiteknolojia n a n y i n g i n e n y i n g i . Maendeleo yanayotajwa na kuonekanwa leo, msingi wake mkuu ni elimu. Ndiyo maana Allah (swt), kitu cha mwanzo kabisa kumpa Adam (as) ni elimu. [Qur-an: 02:31]. Vile vile, mtume Muhammad (saw) wakati anapewa wahyi, aliambiwa soma. [Qur-an: 96:01].

Kwa mujibu wa ayah hizo mbili, tunapata picha kwamba e l imu ni k i tu muhimu kuliko vitu vingine vyote. Elimu humtofautisha kati ya mwenye nayo na asiyekuwa nayo. Wawili hawa, kamwe hawawezi kufanana. Allah Mtukufu ameuliza swali ndani ya Qur-an, kwamba; “Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua?” [Qur-an: 39:09].

U h a l i s i a u n a k a t a a k wa m b a , a n a ye j u a n a asiyejua watakuwa sawa. Ndiyo maana hata Malaika walipoulizwa majina ya vitu walisemaje?, “Wakasema: S u b h a n a k a , W e w e umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima” [ Qur-an 02:32]. Lakini Adam (as), kwa kuwa alishapewa elimu ya vile vitu, kwake jawabu lilikuwa jepesi pale alipotakiwa kutaja majina ya hivyo vitu.

Wanadamu kwa utashi wao wamezigawa elimu katika makundi mawili makuu, ambayo ni elimu ya dini na elimu ya mazingira/m u o n g o z o . N a d i r i k i kusema hivyo kwa sababu, Mtume Muhammad (saw) alipoamrishwa kusoma, hakuambiwa asome dini au elimu ya mazingira, bali aliambiwa soma kwa jina la Mola wako. Haya makundi mawili tuliyoyatengeneza sisi , ni kitu kimoja. Ni kama wale wanaosema tusichanganye siasa na dini!

Kwa kutambua hilo, nami nimeipa makala hii anuani, Elimu Zetu Zinatusaidiaje, k wa m a a n a ya e l i m u zote mbili. Kwa kiwango kikubwa kabisa elimu hizi mbili kama tulivyozigawa s i s i , “ z i n a i s h i m a i s h a ya kutegemeana”. Lakini pamoja na kutegemeana huko, moja ina umuhimu zaidi kuliko nyingine, nayo ni elimu ya muongozo. Elimu ya kumjua Allah Mtukufu ni ya muhimu zaidi kwa kuwa ndiyo inayoweka nidhamu ya namna mwenye elimu inayoitwa ya mazingira, aweze kuishi kwa maelekezo

Elimu zetu zinatusaidiaje?Na Mwandishi Wetu

yake Allah (swt).Elimu hii ya muongozo

ni kama tumbo/fuko la uzaz i (womb) , ambalo h u m t e n g e n e z e a m t o t o m a z i n g i r a s a d i f u k wa kuruhusu maingiliano ya kimfumo ambayo hayana athari kwa mtoto. Vile vile, tumbo hili la uzazi hufanya kazi ya kuzuia muingiliano ambao una madhara kwa kiumbe (mtoto). Kwa sura hii, unaweza kuona ni jinsi gani elimu ya muongozo i l i v y o k u wa n a n g u v u , ukilinganisha na elimu ya mazingira.

Kwa upande mwingine, elimu ya mazingira nayo ina mchango mkubwa sana endapo itatumiwa vema, ikiwa chini ya ulinzi wa elimu ya dini. Masuala yote yahusuyo teknolojia na mengine mengi, ni zao la elimu hii inayoitwa ya mazingira . Lakini p ia , i f a h a m i k e k w a m b a , ugunduzi wa hizi teknolojia tunazojivunia leo, ni matokeo ya tafiti mbali mbali za k isayansi z i l izofanywa kwa kutumia vitabu vya elimu ya dini, hususan Q u r - a n . Wa l i c h o f a n ya watafiti ni kuoanisha yale yaliyoandikwa kwenye Qur-an na kuyaingiza kwenye utendaji kwa majina yao. Tutaona kwa kina kwenye makala zingine inshaallah, mi fano ha i ya mambo ambayo tunayaita elimu ya mazingira, kumbe yapo ndani ya Qur-an.

Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba hawafanani wanaojua na wasiojua, wenye elimu na wasio na elimu kuna nukta ya msingi hapa ningependa tuiangalie kwa makini sana. Mwenye kujua anayekusudiwa hapa, ni yule ambaye amelijua jambo na akafuatisha kwa vitendo kwa kukatazika na kuamrika (kutekeleza maamrisho). Elimu haishii kujua tu, bali utendaji ndio utakaotoa tafsiri sahihi kwamba wewe

Baadhi ya wanafunzi Waislamu wa shule za msingi Wilaya ya Temeke waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, wakiwa katika dua maalumu iliyoandaliwa na Baraza la Wazee wa Buza, iliyoongozwa na kusimamiwa na Mzee Mikidadi Khalfan na kufanyika Masjid Lillah jijini Dar es Salaam mwisho wa wiki iliyopita.

una elimu na ujuzi kadhaa wa kadhaa. Matumizi ya elimu ya mtu ndiyo yanayoweza kumtofautisha na mwingine asiyekuwa na elimu.

Hebu tuangal ie kwa uchache umuhimu wa elimu katika jamii na madhara ya kutokuwa/kutoitumia vema elimu. Kama tulivyosema hapo awali kwamba, elimu ni ile ambayo humuwezesha mtu kuvijua/kuvitizama vitu kwa uhalisia wake. Ikiwa ukweli ndio huo, basi mwenye elimu husika ataweza kufanya/kutenda jambo kwa uadilifu kwa kutoa tafsiri sahihi kutokana na weledi aliokuwa nao kwenye taaluma aliyonayo. Kinyume chake, ni ufisadi, uwongo, ubadhirifu, dhulma, k u r u b u n i w a , r u s h w a , upotoshaj i na mengine yenye kufanana na hayo. Faida ya elimu inapatikana katika maeneo mbali mbali, lakini kwa uchache tuangalie zifuatazo:

Nyenzo Kuu ya Kufikia Lengo:

Kama Waislamu, bila shaka tunatambua vema lengo la kuumbwa kwetu, nalo ni kumuabudu Allah (swt). Kama tulivyoona hapo awali kwamba, kitu cha mwanzo kupewa Adam (as) na Mtume wetu Muhammad (saw) ni elimu. Lengo lao na letu ni moja tu, kumuabudu Allah Mtukufu. Hivyo basi, namna pekee na rahisi kabisa ya kufikia ndoto tulizonazo, lengo la kuumbwa kwetu na malengo mengine, ni kwa kupitia ELIMU. Elimu zote mbili zina nafasi kubwa mno katika kujua halali na haramu na kuweza kuviepuka. Elimu ya mazingira kwa mfano, inasaidia kujua aina mbali mbali za vijenzi vilivyotumika kutengeneza vyakula tofauti – tofauti. Hii huwapa fursa Maulamaa wetu kuweza kutolea fataawa mbali mbali kwa hoja na dalili kadha wa kadha.

Uadilifu: Aghalabu, watu

wenye elimu hususan ya muongozo hufanya mambo kwa uadilifu tofauti na wale wasiokuwa na elimu. Watu wasiokuwa na elimu wanayo nafasi kubwa mno ya kuleta tafsiri za kupotosha. Mathalani, usawa na uadilifu vinaweza kutumiwa kwa moja kuchukua nafasi ya kingine. Si lazima ki la mwenye kufanya jambo kwa usawa anakuwa amefanya uadilifu, lakini mwenye kufanya uadilifu anakuwa amefanya vyote viwili kwa wakati mmoja, kwa maana ya usawa na uadilifu. Kufanya uadilifu, kunategemea na uelewa (elimu) katika hilo unalofanya.

Umakini Katika Kufanya Maamuzi: Weledi wa mtu huweza kupimwa kwa namna anavyopokea mambo na kuyatolea maamuzi. Mtu mweledi, mwenye kuitendea vema el imu yake hana kawaida ya kukurupuka. Kwa hali hiyo, maamuzi yake yatakuwa yana asilimia kubwa ya ufanisi na usahihi. Mtu wa namna hii haoni haya kusema sijui kwa jambo ambalo halijui, tofauti na mjinga ambaye hujitutumua kujibu kitu asichokijua.

Elimu ni Maisha: Nyenzo kuu ambayo inatumiwa leo hii katika kufikia malengo mbali mbali ni elimu. Mipango mizuri, utendaji mzuri yote yanatokana na matumizi sahihi ya elimu. Ndio kama a l ivyosema mwandishi mmoja kwamba, e l imu siyo maandalizi ya maisha, bali ndiyo maisha haswaa’. [ John Dewey, 1859-1952, philosopher, psychologist, education reformer].

Elimu humjengea mtu uwezo wa kufikiri zaidi na hivyo kuweza kugundua mambo mengi ambayo humpatia wepesi katika shughuli zake mbali mbali za kila siku. Maendeleo yote tunayoyaona leo hii, ni matokeo ya elimu mbali mbali walizosoma wanadamu. Miundo mbinu mizuri ya

barabara, vyombo vya usafiri, mawasiliano na mengine mengi tunayofurahia, hii yote ni elimu.

K u wa n a M s i m a m o : Watu wenye elimu, ndio a m b a o w a n a k u w a n a misimamo kwenye imani zao, kwenye mambo mbali mbali ya kijamii. Ni kwa sababu wanatambua vema wanachokisimamia, hivyo hawatetereki kwa lolote kwa kule kutambua pande zote za shilingi. Wanafahamu madhara ya kufanya na kutofanya jambo kadhaa. Wenye e l imu hawaishi kwa dhana, bali wanatafiti kwanza hakika ya jambo kama lina tija au vinginevyo.

Huepusha Migogoro Isiyokuwa na Sababu za Msingi: Migogoro mingi husababishwa na kutokuwa na elimu. Namna nzuri ya kusuluhisha, pia ni jambo ambalo linahitaji elimu. Ndio maana kuna vituo maalum vya mambo ya ushauri nasaha kwa kujua nafasi ya elimu.

Kushinda Ushirikina: Watu wengi ambao hujihusisha na mambo ya ushirikina ni wale wasio na elimu. Angalia, kwa mfano mauaji ya albino, mauaji ya vikongwe hususan wenye macho mekundu n.k. Wanafanya haya kwa kutumiwa au wenyewe, wakiamini wanaweza kupata wanachokitaka kama vile mali na mengineyo. Elimu hususan ya muongozo ndiyo yenye nafasi kubwa ya kumuepusha mtu na mambo machafu kama haya ya ushirikina. Allah Mtukufu ameahidi kusamehe dhambi zingine zote zisizokuwa ushirikina kwa amtakaye.

El imu Humuwezesha Mtu Kwenda na Wakati. Mabadiliko ya kiteknolojia ya n a k we n d a k wa k a s i ya a jabu. Wenye el imu ndiyo wanaonufaika na mabadiliko haya, na ndio w a n a o y a c h a n g a m k i a kutokana na kuwepesisha baadhi ya kazi. Matumizi ya internet kwa mfano, yanawanufaisha wenye elimu peke yao. Namna rahisi na nafuu kabisa ya kusoma siku hizi ni kupitia mitandao.

Page 20: ANNUUR 1194.pdf

20 AN-NUURDHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 201520 MAKALA AN-NUUR

20

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

DHULQAAD 1436, IJUMAA SEPTEMBA 11-17, 2015

baada ya Julai 7, 2015, M a h a k a m a y a M j i n i Morogoro, kuamuru pande mbili, upande wa Jamhuri na upande wa ute tez i kuwasilisha hoja zao ndani ya siku 21, yaani hoja za utetezi na hoja za upande wa Jamuhuri (Serikali).

Kwa mujibu wa Wakili wa Sheikh Ponda, Bw. Juma Nassoro, ameeleza kuwa siku hiyo ya Ijumaa (Septemba, 4, 2015) kesi hiyo inayomuweka mahabusu mteja wake kwa mwaka wa pili sasa, ilikuwa ipangiwe tarehe ya hukumu, jambo ambalo limekwamishwa na upande wa Jamhuri.

A l i s e m a , h a l i h i y o imesababishwa na upande wa mashitaka (Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kushindwa kuwasilisha hoja zao kwa maandishi kama ambavyo Mahakama inayosikiliza k e s i h i y o M o r o g o r o , ilivyoziamuru pande mbili.

Akifafanua zaidi Wakili Nassoro, alisema Julai 7, 2015 baada ya wao (upande wa utetezi) kukamilisha kutoa ushahidi, Mahakama iliamuru kuwa pande zote mbili wapeleka hoja za majumuisho ya kesi ndani ya siku 21, kuanzia siku hiyo, ambazo zilikoma Agosti 28, 2015.

Alisema, baada ya hapo hatua iliyokuwa inafuatia ni kesi kupangiwa Tarehe ya hukumu, kwa matarajio k wa m b a , k i l a u p a n d e utakuwa umejumuisha hoja zao (Final submissions) kama Mahakama ilivyoamuru Julai, 7.

“ S i s i t u l i w a s i l i s h a majumuisho yetu ndani ya siku 21, kabla ya Agosti 28, 2015, kama Mahakama i l i v y o a m u r u J u l a i 7 , tukitegemea pia upande wa J a m h u r i ( S e r i k a l i ) nao wangewasilisha kwa muda huo au kabla, lakini upande wa Jamhuri wao hawakufanya hivyo, badala yake leo (Ijumaa iliyopita) wameomba waongezewe muda zaidi’ . Amesema Wakili Nassoro.

K u f u a t i a h a l i h i y o , upande wa utetezi uliiambia Mahakama kuwa baada ya Ser ikal i kushindwa kuwasilisha hoja zao kwa maandishi kwa muda wote

Bado Serikali ina hamu kuwa na Pondahuo wa wiki tatu, hawana nafasi tena ya kupeleka maelezo yao.

Wakili Nassoro, alisema hawana nafasi hiyo kwa sababu utaratibu haukuwa wao (upande wa utetezi) wapeleke hoja kisha wao (Serikali) wajibu hoja bali amri ilikuwa ni pande zote wapeleke hoja zao kwa maandishi kwa wakati mmoja na hapakutakiwa majibu yoyote.

“Kwa manaa hiyo kama wataruhusiwa, maana yake ni kwamba wao (Serikali) watakuwa wanajibu hoja zetu za upande wa utetezi, k wa m a a n a h i y o s i s i hatutokuwa na nafasi ya kujibu tena.

Mahakama, baada ya malumbano ya kisheria kwa pande hizo mbili (Serikali na utetezi) iliamua kuahirisha kesi kwa mara nyingine mpaka Septemba 18, 2015, ili iweze kutoa uamuzi iwapo upande wa mashitaka (Serikali) wafaili maelezo yao au Mahakama itoe hukumu.

W a k i l i N a s s o r o , alilalamikia mwenendo huo wa Serikali na kusema kwamba, inaonekana wazi kuwa upande wa mashitaka wanakusudia kuchelewesha hukumu hiyo kwa maslahi yao kwani akadai inaonyesha hawataki kuona hukumu ya kesi hiyo ikisomwa kwa sababu wanazozijua wao.

“Hawakuwa na sababu y o y o t e ya m s i n g i ya kutokuwasilisha hoja zao ndani ya muda uliowekwa na Mahakama na badala yake wameamu kuchagua kutokuwasilisha ili waweze kuongezewa muda jambo ambalo linafanya hukumu ya kesi kuchelewa ili hali Sheikh Ponda, yupo mahabusu kwa miaka miwili sasa bila sababu za msingi”. Alisema Wakili Nassoro.

Hiv i sasa kes i h iyo ipo katika mchakato wa kusubiri hukumu, baada ya Mahakama kusikiliza mashahidi wa pande zote mbi l i ambapo upande wa Jamuhuri (Serikali) ulisimamisha mashahidi tisa, wakati upande wa utetezi ulipeleka mashahidi wawili tu.

Kadhia ya Shkh Ponda, imekuwa na mlolongo mrefu wa kisheria, ambapo pamoja na kwamba hadi sasa hajahukumiwa, lakini yupo ndani kwa miaka miwili sasa, kutokana na dhamana yake kuzuiliwa na DPP.

Na Bakari Mwakangwale

SERIKALI inaonekana kuelemewa na hoja za upande wa utetezi katika kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda, baada ya kukwama

kuwasilisha hoja zake, katika kesi inayoendelea M j i n i M o r o g o r o , i l i kutolewa hukumu.

SERIKALI inaonekana kubanwa ‘mbavu’ katika kesi inayomkabili Sheikh

Ponda Issa Ponda, baada ya kushindwa kuwasilisha hoja zake katika Mahakama ya Mjini Morogoro, kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Hali hiyo imejidhihirisha Ijumaa ya wiki iliyopita,

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiteta jambo na Wakili wake Juma Nassoro/

W A P A L E S T I N A wa m e wa s i l i s h a r a s m i mapendekezo yao kwa Umoja wa Mataifa (UN) wakitaka bendera yao ipeperushwe katika makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Vatican pia wamewasilisha pendekezo kama hilo.

Vat ican na Palest ina z i n a t a m b u l i w a k a m a wanachama watazamaji wa UN, lakini Palestina inapigania kutambuliwa rasmi kama nchi huru yenye mamlaka kamili ya kujitawala.

Pendekezo la Palestina la kutaka bendera yake ipepee katika makao makuu ya UN limeungwa mkono na nchi 21 zikiwemo nchi kadhaa za Kiarabu na Kiafrika.

Wapalestina wataka bendera yao ipeperushwe UNVi o n g o z i wa d u n i a

wanatarajiwa kukutana katika kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuanzia mwezi ujao na iwapo pendekezo la Palestina l ikapigiwa

kura kabla ya mkutano huo na likipitishwa, bendera ya Palestina itakuwa kati ya nyingine 193 za nchi wanachama wa UN kufikia mwishoni mwa Septemba mwaka huu. (irib).

BENDERA ya Taifa la Palestina

Kwa muislamu Hijja ni wajib mara moja katika umri wake isipokuwa aliyepewa afya njema na mali. Huyu ananyimwa Rehma za Allah akipitisha miaka mitano bila kurudia Hijja. Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

(25) MWENYE UWEZO AHIJI KILA MIAKA MITANO