Click here to load reader

ANNUUR 1037

  • View
    10.057

  • Download
    2

Embed Size (px)

Text of ANNUUR 1037

Sauti ya Waislamu

Tapeli ajizolea fedha kutoka kwa WaislamUk. 7

Rungu la NECTA lawaponda tena WaislamuSafari hii ni kwa Walimu wa Stashahada Ni mchezo wa kuondoa Dini baada ya Qubah (?) Zanzibar nayo kubanwa au wawe na NECZA yao

ISSN 0856 - 3861 Na. 1037 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uk. 3 Washenga wa maadui wa Sensa ilikuwa Baraka Zanzibar watolewe serikalini Kumbe ilisilimisha Mkristo mmoja Aanze kuondoka Mwinyihaji Makame Au aseme Bububu adui alikuwa nani? Uk. 4 Wanadhani tna, farka itawapa Urais 2015 Waislamu watakiwa kutembelea wafungwaNa Bakari Mwakangwale WITO umetolewa kwa Waisamu Jijini Dar es Salaam, kujitoa na kwenda Magerezani kuwatembelea Waislamu, kwa ajili ya kuwasaidia kwani wengi walioko huko wanahitaji Inaendelea Uk. 3

MWENYEKITI wa CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Julius Mtatiro katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Levolosi, Jijini Arusha, mwishoni mwa wiki iliyopita. Habari kamili Uk. 16.

Ubaya Ubaya sasa kuleta balaa UngujaUamsho watakiwa kuanzia Jihad Jangombe Waje kwa Baraza la Mji Zanzibar ingare

DKT. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania.

2S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected] Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/TangazoAN-NUURKhuzaimah, na Al-Hakim). Wako miongoni mwetu Waislamu wanaojizuilia kwenda Hijja kwa dhana ya kuwa wanachohitaji kutoa ni kingi na hakirudi. Hii ni dhana potofu haiendani na mafundisho ya Dini. Ni potofu kwa sababu lengo la Uislamu ni kupata radhi za Mola, kuepukana na moto, na kupata pepo. Hijja inamhakikishia Muislamu haya yote kwa mpigo. Lakini pia dhana hiyo ni potofu kwa sababu anachokitoa mtu kwa kufunga safari ya Hijja au Umra hakipotei; kinarudishwa na kuzidishwa. Katika Hadithi iliyopokelewa na Anas bin Malik (RA), Mtume(SAW) amesema: Mwenye kufanya Hijja na mwenye kufanya Umra ni wageni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hupewa wanachoomba, na (Allah) anajibu dua zao, na hurudishiwa walivyotoa, dirham (au shilingi) moja kwa dirham (au shilingi) milioni moja. (Al-Baihaqy). Nguzo ya kwanza katika nguzo za Hijja ni kuhirimia. Wanaume wote kubadili nguo na kuvaa nguo za aina moja. Mashuka mawili meupe, moja juu mabegani na la pili kufunga kiunoni. Hapa tunajifunza kitu kimoja muhimu. Nacho ni usawa kwa binadamu. Hakuna nafasi ya kuwepo alama alama zinazowatofautisha watu kwa mataifa yao, utajiri wao, vyeo vyao, n.k. na zinazowafanya wajinasibishe na cheo, kabila, mali, utaifa au kundi fulani. Hali hii inatoa nafasi ya mtu kujijua zaidi. Kiburi, majivuno, kujiona, chuki, miongoni mwa maasi yaliyo ndani ya moyo wa mtu yanakuwa havana nafasi. Mtu anapata nafasi ya kupata hisia ya utu wake, na hali itakavyokuwa siku ya kufufuliwa. Hivyo Hijja ni fursa kubwa sana inayomsaidia mtu katika kukumbuka mwisho wake, kujenga Uislamu wake, na kumkumbuka sana Mola wake. Kisimamo cha Arafa kinatoa wasaa zaidi watu milioni tatu hukutana katika uwanja mmoja. Huo ni mfano wa siku ya Qiyama ambapo Allah atatukusanya wanadamu wote walioumbwa na kuishi katika uso wa ardhi pamoja katika uwanja mmoja. Wenye akili wanatakiwa wanufaike na mkusanyiko huo kwa kuikumbuka siku hiyo ya kiyama. Watu wote wanaokwenda Hijja kwa ajili ya Allah (SW) ni vyema wakaweka mapatano baina ya watu waliokuwa wamekhasimiana. Haji mtarajiwa anatakiwa

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA OKTOBA 5 - 11, 2012asuluhishane na kila Mwislamu aliyekuwa amekhasimiana naye. Kwa maneno mengine, anatakiwa akamilishe imani yake kwa kuondoa chuki, hasama, kuondosheana kinyongo, kusuluhishana na kupeana radhi na Waislamu wenzake ambao ndio ndugu zake wa kiroho. Ibada ya Hijja inaanzia mtu anapokuwa nyumbani kwake na katika nchi yake. Muislamu anatakiwa aondoke kwa safari ya Hijja akiwa amelipa madeni yake yote anayodaiwa, na amewaridhisha watu wake wa nyumbani kwa kuwaachia mahitaji yao ya maisha kwa muda wote anaotarajiwa kuweko safarini. Hivi ndivyo Muislamu anatakiwa anapoondoka kuelekea Makka kuitikia wito wa Mola wake, anatakiwa aondoke huku ndani ya moyo wake ukiwa umejaza mapenzi kwa Mola wake (SW), Mtume wake Muhammad (SAW), na ndugu zake Waislamu wote. Ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu (SW) ametuwekea Hijja ili tujenge umoja wa Kiislamu kimataifa. Swali la kujiuliza ni je, sisi tunaotoka nchi moja tunajuana? Je, tunashirikiana? Je, tuna mshikamano? Ni vyema safari hii mahujaji wakajenga umoja na kufahamiana kabla ya kuondoka kwenda Hijja ili kujenga umoja unaofahamika katika nchi yetu kwanza. Ni ajabu taasisi za kusafirisha na kuhudumia mahujaji nchini kusafirisha Mahujaji na kutekeleza ibada zote huko Makka na kurejea nyumbani bila ya Mahujaji wa taasisi moja kujuana na wa taasisi nyingine hali ya kuwa wanatoka Taifa moja. Si kisimamo cha Arafa wala Minna, kote huko kupishana tu. Hutokezea wachache miongoni mwao wakajuana kwa bahati. Lakini bado hakuna juhudi inayochukuliwa kujenga mtandao angalau wa wale waliobahatika kwenda Hijja wakafahamiana vizuri. Katika hali hii kweli lile lengo kuu la Hijja linapatikana? Vipi kuhusu falsafa ya Hijja tunaifahamu? Kuna haja ya waandaaji wa Hija kulishughulikia tatizo hili. Mahujaji wafahamiane na kushikamana tangu nyumbani. Tumalizie kwa kusema, kama ambavyo Mwenyezi Mungu amewajaalia afya njema, masurufu na wasaa kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija, tunamuomba awajaalie pia Hija njema na iliyokamilika. Hija maq buul.

AN-NUUR

Kila la kheri mahujaii wetuHIVI sasa Waislamu, wake kwa waume kutoka nchi mbalimbali duniani wanaelekea nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya Uislamu, ambayo ni ibada ya Hija. Hapa kwetu Tanzania kadhalika, ndugu zetu wa Kiislamu ambao wamejaaliwa kupata masurufu ya kutekeleza ibada hiyo, nao wamekuwa katika hatua za mwisho kuelekea Saudia kwa lengo hilo hilo. Uislamu umejengwa katika nguzo tano. Kushuhudia kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na Bwana Mtume Muhammad (SAW) ni mjumbe wake, kusimamisha sala tano, kutoa zaka, kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwenda Hijja. (Bukhari na Muslim). Kwa bahati mbaya Waislamu wengi tunazisoma na kuzikariri nguzo hizi bila ya kuzingatia uzito na umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku. Uislamu haumkubali mtu yoyote ambaye hakutimiza nguzo za Dini, inapokuwa mtu huyo amepewa na Mwenyezi Mungu uwezo wa kuzitimiza. Mwenyezi Mungu (SW) anaamuru ifuatavyo: Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Al-Baqara, 2:196) Hapa Mwenyezi Mungu (SW) anataka Waislamu waitekeleze ibada na nguzo ya Hijja. Na kwa wale wanaokwenda Hijja, anawataka waitimize ibada hiyo kwa ukamilifu. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo kwa yule awezaye kwenda huko. Na atakayekufuru (atakayekanusha) basi

MAONI YETU

Mwenyezi Mungu si mhitaji kuwahitaji walimwengu. (Al Imran, 3:97) Kwa maneno mengine, ni wajibu kwa kila mwenye uwezo kwenda Hijja kwa ajili ya Mola wake. Mwenyezi Mungu (SW) anaichukulia Hijja kuwa ni haki yake kutoka kwa viumbe vyake waliomuamini na ambao amewapa uwezo. Na kwa kuwa anayetoa uwezo ni yeye Mwenyewe (SW), basi anamjua kila aliyempa uwezo na asiyempa. Hivyo, kwa ambaye amepewa uwezo na kwa sababu yoyote ile, hakwenda kuhiji Makka, basi ajue kuwa Mola wake hamuhitajii kwa lolote. Tuna hakika kwamba Waislamu wengi wanajua faida za Hijja. Hivyo Muislamu hana budi kutanguliza kwenda Hijja kwanza kuliko kwa mfano, kufanya harusi inayogharimu thamani ya Hijja zaidi ya moja. Katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira (RA), Mtume (SAW) amesema: Mwenye kufanya Hijja bila ya kusema maneno machafu na bila ya kufanya vitendo vichafu, atasamehewa madhambi yeke atakaporudi kama siku aliyozaliwa na mama yake. (Bukhari, Muslim). Kwa mapenzi yake subhanahu Wataala, Rehema za Allah hazisimami kwa yule anayekwenda kuhiji peke yake. Bali wapenzi wote wa Mahujaji wananufaika kwa uhakika kutokana na dua watakazoombewa na Hajji. Hoja hii imebainishwa na Mjumbe wa Mwenyezi M u n g u ( S AW ) k a t i k a Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira (RA) kama ifuatavyo: Husamehewa madhambi yake mwenye kuhiji pamoja na wale watakao-ombewa na mwenye kuhiji. (AlBazzari, At-tabraany, Ibn

UBUNGO55105, Tel: 2450069, 0754 260241 ISLAMIC HIGH SCHOOL P.O. BoxFax: 2450822 Dar es Salaam E-mail: [email protected]

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu. Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana. Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni: 1. Elimu ya Dini ya Kiislamu 2. English Language 3. Arabic Language 4. Mathematics 6. Introduction to Computer Ni programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012) Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu. Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107 MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU Wabillah Tawfiiq MKUU WA SHULE

Maandalizi ya Kidato cha Kwanza 2013

Rungu la NECTA lawaponda tena Waislamuhakutaka kutajwa jina lake gazetini. Mwalimu huyo anasema M G O G O R O k a t i y a kuwa kisingizio cha NECTA Waislamu na Baraza la k u w a k u n a Wa r a k a w a Mitihani Tanzania unazidi Wizara usiotambua Islamic kupanuka baada ya Baraza knowledge hayana mashiko h i l o k u z u i y a m a t o k e o kwa sababu yapo pia masomo ya baadhi ya wanachuo mengine ambayo hivi sasa kwa madai kuwa NECTA yanatambuliwa na Baraza haitambui somo la Maarifa la Mitihani Tanzania kuwa ya Uislamu. yanafanya miunganiko Baadhi ya wanafunzi