60
25 JUNI, 2013 1 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Sita - Tarehe 25 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Ifuatazo Iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:- Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA (CCC) kwa Mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and Audited Accounts of TCRA Consumer Consultative Council (TCRA – CCC) for the Year Ended 30 th June, 2012). MASWALI NA MAJIBU Na. 457 Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kuwa Wabunge MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA aliuliza:- Moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na pia Ibara ya 67(2)(g) ya Katiba ya Jamhuri

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

  • Upload
    others

  • View
    5

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

1

BUNGE LA TANZANIA________________

MAJADILIANO YA BUNGE___________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Hamsini na Sita - Tarehe 25 Juni, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Ifuatazo Iliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NATEKNOLOJIA:-

Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRAConsumer Consultative Council (TCRA (CCC) kwa Mwakaulioshia tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and AuditedAccounts of TCRA Consumer Consultative Council (TCRA –CCC) for the Year Ended 30th June, 2012).

MASWALI NA MAJIBU

Na. 457

Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kuwa Wabunge

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA aliuliza:-

Moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia nakuishauri Serikali na pia Ibara ya 67(2)(g) ya Katiba ya Jamhuri

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

2

ya Muungano wa Tanzania inaeleza kukoma kwa mtu kuwaMbunge endapo mtu huyo amepewa madaraka ya AfisaMwandamizi katika Utumishi wa Umma.

(a) Je, ni kwa maana gani Wabunge ambao niWakuu wa Mikoa au Wakuu wa Wilaya wanatimizamajukumu yao ya Kibunge?

(b) Je, ni kwa namna gani viongozi haowanakiuka Ibara ya 67(2)(g)ya Katiba pamoja na kuwawanateuliwa na Rais?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa ChristowajaGerson Mtinda, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a)na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge ambaoni Wakuu wa Mikoa au Wilaya wanatimiza majukumu yao yaKibunge kwa kuzingatia Ibara 63(3)(a) – (e) ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, WaheshimiwaWabunge ambao ni Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawakiukiIbara ya 67(2)(g) ya Katiba kama il ivyonukuliwa naMheshimiwa Mbunge. Ibara hiyo inafafanua kuwa mtuanaweza poteza sifa za kuwa Mbunge iwapo ameshikamadaraka ya Afisa Mwandamizi katika Utumishi wa Serikaliya Jamhuri ya Muungano isipokuwa madaraka ambayo Raisanaweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibuwa Katiba au Sheria iliyotungwa na Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, Katiba iliyopo inampaMheshimiwa Rais mamlaka ya kuteua Watanzania wenyesifa kuwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wakiwemoWaheshimiwa Wabunge. Hata hivyo hoja ya kutenganishamajukumu ya mihimili yetu ya dola imejitokeza pia katika

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

3

mapendekezo yaliyowasilishwa na wadau kwenye Tume yaMabadiliko ya Katiba. Hivyo basi ni matumaini ya Serikalikwamba uamuzi kuhusu suala hili utapatiwa ufumbuzi kupitiamchakato wa mabadiliko ya Katiba yanayotarajiwakufanyika kabla ya kupatikana kwa Katiba mpya ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa NaibuSpika, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwakuwa swali langu lilikuwa linahusu ni kwa namna ganiWabunge ambao ni Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanatimizamajukumu yao ya Kibunge na jibu lililotolewa ni kwambawanatimiza kutokana na Ibara ya 63(3)(a) – (e).

Swali langu; kwa kuwa Ibara hiyo inasema kwambaWabunge kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimamia Serikalina iliwahi kutokea hapa Bungeni Wakuu wa Wilaya kadhaawaliwahi kuuliza maswali yao Bungeni na aliyekuwa kwenyekiti wakati huo aliwaambia wao ni sehemu ya Serikali kwahiyo hawawezi kuuliza Serikali kwa sababu wao ni sehemuya Serikali.

Je, katika Ibara hiyo ni kwa namna gani Wabungehawa wametimiza majukumu yao ya kuishauri na kuisimamiaSerikali?

Swali la pili; kwa kuwa jibu limesema kwamba huumwingiliano wa hii mihimili ya dola uko katika mchakatounaendelea wa Katiba Mpya. Sasa hivi bado tunaendeleakutumia Katiba ambayo ipo na Wabunge hao ambao wamohumu ndani bado wanaendelea na majukumu yao ya kuwaWakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa na wote ni Wabungewa Viti maalum. Nia ya kuanzishwa Viti Maalum ni kumfanyaMbunge wa Viti Maalum aweze kupata uzoefu ili baadayeagombee Jimbo. Kwa namna hiyo Wabunge hawa wa vitimaalum ambao wanapangwa katika Wilaya au Mikoaambao hawajatoka kupitia Wabunge wa Viti Maalum; ni kwanamna gani watapata uzoefu katika maeneo yao iliwasimame kugombea Majimbo kama ambavyo tunatakiwasasa hivi? Ahsante sana. (Makofi)

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

4

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Christowaja ukagombeeJimbo la nani? Mheshimiwa Waziri wa Nchi majibu. (Kicheko)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE: Atagombea Jimbo la Singida Kusini sijui Kaskazini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kumkumbushaMheshimiwa Mtinda kwamba Wakuu wa Wilaya na Wakuuwa Mikoa kama nilivyosema sio Maafisa Waandamizi waSerikali, hawa ni political leaders na ndiyo maana Sheriainayotumika kwao ndiyo inatumika kwetu hata kwenyemafao.

Kwa hiyo, unatakiwa ujue tu kwamba hawa ni politicalleaders hivyo bado nasisitiza kwamba hakuna lolote ambalolimekiukwa katika Sheria hii. Lakini pia kufanya kazi kule badowanatimizia majukumu yao ya kusimamia Serikali wakiwahapa na bado wanasaidia Serikali katika kutekeleza yalemaamuzi ambayo yamepitishwa na Bunge. Kwa hiyo,hakuna mgongano wowote.

Ni kama mimi hapa, mimi ni Mbunge lakini pia ni Wazirinatumia Sheria ileile. Nafanya kazi ya Serikali lakini badonatekeleza majukumu yangu ya Kibunge na wananchiwangu hawalalamiki na wanapata raha kama vileunavyowakilisha wewe. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mtindanataka nikuhakikishie kwamba hakuna mgongano wowote.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka ieleweke kwambania ya Serikali pia ni kuwafanya hawa Wabunge hawa waViti Maalum vijana walioteuliwa kuwapa uzoefu namna yakuendesha Serikali, namna ya kutawala. Si suala la kusimamiaSerikali lakini pia namna ya kuongoza. Ni namna nzuri ambayotumejiwekea kuandaa viongozi wa baadaye na ndiyomaana utakuta kada ya Wabunge walioteuliwa humu ndanini vijana ambao ndiyo wanarithishwa madaraka yabaadaye.

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

5

Kwa hiyo, nataka nikwambie kwamba hakuna hitilafuyoyote lakini pia hakuna anayewakataza kuuliza maswalihapa. Hakuna, tumewasikia wakichangia hapa unless mimipeke yangu ndiyo nimesikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakuu wa Wilaya wengiwamechangia hapa, wameishauri na wameisimamia Serikalikwa kauli na maneno yao na kama mnabisha hilonitakwenda kuchukua Hansard ili niwaonyeshe. Hakuna hatamtu mmoja wala Kanuni zetu hazimzuii Mkuu wa Wilaya auMkuu wa Mkoa kusema ndani ya Bunge hili hapana.

Sisi Mawaziri ndiyo tunaweza tukachangia hojaambayo imewasilishwa na Waziri mwingine au hoja ambazozimeletwa na Wizara husika. Lakini Wakuu wa Mikao na Wilayawanaweza kuchangia hoja yoyote ya Serikali wakiwa ndaniya Bunge hili. (Makofi)

Na. 458

CDA Kuwezesha Makao Makuu ya SerikaliKuhamia Dodoma

MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:-

Serikali iliunda Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA) kwa lengo la kustawisha Mji wa Dodoma nakuiwezesha Serikali kuhamishia Makao Makuu yake Dodoma.

(a) Je, ni kwa kiasi gani Mamlaka ya UstawishajiMakao Makuu (CDA) imefanikiwa kuiwezesha Serikalikuhamia Dodoma?

(b) Kwa kuwa Wananchi wa Dodoma wanahitajiardhi kwa ajili ya kujenga na kuendeleza Mji wa Dodoma naCDA haijagawa viwanja kwa wananchi tangu mwaka 2004na wananchi wa Dodoma wanahitaji ardhi kwa ajili yakujenga na kuendeleza Mji.

Je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Dodoma?

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

6

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa FelisterAloyce Bura, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Dodoma,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, wakati nilipokuwanajibu swali namba 778 la Mheshimiwa David Mchiwa Malole,Mbunge wa Dodoma Mjini, swali Namba 147 la MheshimiwaAnne Kilango Malecela, Mbunge wa Same, Mashariki, hapaBungeni yaliyohusu Serikali kuhamia Dodoma nililieza Bungelako Tukufu kuwa:-

Serikali itahamia Dodoma baada ya kufikia hatuanzuri ya ujenzi wa miundombonu na huduma mbalimbalizinazohitajika kwa ajili ya kuweka watu wa ziada Dodomana kuendesha shughuli za Serikali.

I l i kuiwezesha Serikali kuhamia Dodoma naimekamilisha uandaaji wa Mipango Kabambe ya Mji waDodoma, Upimaji na ugawaji wa viwanja 63,954 vya makazina biashara, ujenzi wa barabara na mirefeji ya maji ya mvua,utandazaji wa mabomba ya mfumo wa majisafi na majitakakatika maeneo yaliyopimwa, ujenzi wa nyumba za Serikali300 na nyumba nyingine 480 zinazomilikiwa na CDA nakupangishwa kwa watu mbalimbali.

Aidha CDA imetoa viwanja kwa ajili ya kujenga ofisikwa baadhi ya Wizara na Taasisi; kutenga eneo la kujengakiwanja cha ndege cha kimataifa na kutenga na kupimaeneo la kituo cha kisasa cha mabasi. Vilevile, Serikaliimepandisha hadhi Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuwaHospitali ya Rufaa na imeanza mchakato wa maandalizi yaSheria ya Mji Mkuu wa Dodoma. Lakini pia hivi sasa inajengaKituo Kikubwa cha Upimaji wa Magonjwa ya BinadamuTanzania pale UDOM, Dodoma.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

7

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, siyo kweli kuwa CDAhaijagawa viwanja kwa wananchi tangu mwaka 2004.Kumbukumbu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2004 hadi2008 jumla ya viwanja 10,289 vilipimwa na kumilikishwa kwawananchi wa viwanja 9,479 vilifanyiwa maboresho.

Aidha kuanzia mwaka 2008 hadi sasa Mmalakaimekamilisha upimaji wa viwanja zaidi ya 9,000 katika maeneombalimbali. Baadhi ya viwanja hivi vimeshaanza kugawiwakwa wananchi ambao wanatakiwa kulipia gharama zausanifu, upimaji, fidia na ufunguaji wa barabara katikamaeneo hayo. (Makofi)

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili yanyongeza. Pamoja na majibu hayo ya Serikali. Kwa kuwakatika Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2025, Mpangowa Serikali wa kuhamia Dodoma haukuonyeshwa. Pamojana hayo suala la kuhamia Dodoma haupo kwenye Mpangohuo wa Serikali.

Je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Dodoma?

Swali la pili, kwa kuwa tunashuhuduia majengomakubwa ya Wizara mbalimbali za Serikali zikiendeleakujengwa katika Jiji la Dar es Salaam na kwa kuwa CDAambayo ilipewa jukumu la kuendeleza Mji wa Dodomainapewa shilingi milioni 500/- kama fedha za maendeleo nahata kwa mwaka wa fedha uliopita fedha za maendeleohazikufika kama ilivyopangwa katika Bajeti ya Serikali.

Je, Serikali ina nia kweli ya kuhamia Dodoma?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, anasema suala lakuhamia Dodoma halipo katika mpango wa maendeleo waVision 2025. Lakini nataka kumhakikishia mpango wa kuhamiaDodoma uko kwenye nyaraka muhimu zaidi kuliko hii kwasababu uko katika sera ya Chama cha Mapinduzi ambayondiyo inaongoza Dira ya Maendeleo ya 2025.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

8

Kwa hiyo nataka Mheshimiwa Felister Bura ajuekwamba kwa madaraka, kwa uongozi na uendeshaji wa nchisera ya Chama cha Mapinduzi ni kubwa na ni nyaraka kubwazaidi kuliko Dira 2025. Kwa sababu Dira 2025 inatokana nasera na miongozo ya CCM. Kwa hiyo, hilo ni jambo kubwana limeainishwa katika sera ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kwamba CDA haipatifedha za maendeleo na imepata milioni 500/-, hapana. CDAimepata fedha za maendeleo nyingi zaidi kuliko Halmashaurinyingi. Serikali imetoa fedha kupitia mkopo uliochukuliwa naSerikali World Bank zaidi ya shilingi bilioni 32/- ambazozinatekeleza mradi mkubwa wa miundombinu katikaDodoma na nyie wote Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi.

Barabara nyingi sana zinajengwa, mifereji ya majitakainajengwa hapa mjini zote hizi ni fedha za maendeleo. Fedhaza maendeleo kwa tafsiri sio fedha zile tu za madafuzinazokusanywa kwa kodi za Watanzania. Fedha zamaendeleo ni zote zinazotengwa na Serikali hata zile ambazofedha zinazotoka nje ya nchi. Ndiyo maana Dodomaimependelewa kupewa fedha hizi nyingi zaidi kulikoHalmashauri zote zinazotekeleza mradi huu. Dodomaimepewa mara mbili ya kiwango ambacho Halmashaurinyingine zimepewa. Kwa hiyo fedha za maendeleo zipo nakazi kubwa inaendelea na hii ni awamu ya kwanza.Tunaendelea na uboreshaji wa miundombinu Dodomampaka tutakapomaliza miundombinu yote ambayoinakusudiwa kwa Makao Makuu, Dodoma.

MHE. ENG. MUHAMMED HABIB JUMA MNYAA:Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa yakuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa dhamira ya Serikalikuhamia Dodoma ni ya muda mrefu na kuna nchi zilihamishaMakao Makuu yao na zikaja Tanzania kufuata au kuiga nakutizama mipango ya Tanzania kama vile Lilongwe na Abujamiaka mingi iliyopita.

Wao wamejenga Makao Makuu yao na wamehamiamiji hiyo na kwa kuwa jibu hili la kujenga miundombinu,

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

9

kiwanja cha ndege, nyumba 350 ni majibu hayo hayoyanayotolewa na Serikali. Kwa kuwa hivi sasa pia kunampango wa kuendeleza Mji wa Kigamboni ambao tunaonanguvu kubwa ya Serikali inaelekezwa huko kuliko Dodoma.

Je, ni mipango gani hiyo unayosema ni zaidi ya vision2025 ni sera ya CCM kwamba jambo moja halijakamilika kwamuda wa zaidi ya miaka 25 sasa kunaelekezwa nguvukwenye mji mwingine? Tupe sababu na hiyo mipango kwaninihaijafanyika?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA,URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, ni kweli nchi nyingikama alivyosema Nigeria wamejifunza. Lakini sio hizo tuTanzania ni mwalimu wa mambo mengi sana. Tanzaniakutokana na busara ya viongozi wetu na sera nzuri za vyamavyetu TANU, ASP na CCM hatuwezi kuacha hilo, wala sio lakuhamia Dodoma tu, hata ukombozi. Base ya ukombozi niTanzania katika nchi zote za Kusini mwa Afrika. Kwa hiyo, sualala kujifunza Tanzania usilione tu hilo la kujenga Mji MkuuDodoma, mambo mengi sisi tumewafundisha natunawakaribisha wataendelea kujifunza.

Lakini pia sisi tunajenga Mji wa Dodoma kwa utaratibuwetu. Haiwezekani Abuja wamejenga kwa miaka miwili kamaunavyosema kwa muda mfupi na sisi tukaiga hapana. Sisitunayo Master Plan yetu na tunakwenda kulingana na MasterPlan tuliyoipanga na utaratibu wetu. Hii ni Serikali huru nalazima iendeshwe kwa mipango yake ya ndani. Hatuwezikuiga Abuja walivyofanya.

Lakini iko tofauti kubwa kati ya Mji wa Kigamboni naDodoma. Mji wa Kigamboni ule umewekwa maalum kwa ajiliya wawekezaji binafsi, sio mji wa Serikali. Dodoma ni MakaoMakuu ya nchi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mnyaa umetoa mifanomiwili tofauti. Unguja ni Mji vilevile Dodoma tunajenga MakaoMakuu lakini huwezi kusema Pemba ni sawa na Dodomahapana, ingawa Pemba ni Mji. Dodoma ni Mji lakini ni MakaoMakuu. Unaona hiyo inayoongezeka. Makao Makuu. Kwahiyo, hiyo ndiyo tofauti kati ya Kigamboni na Dodoma.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

10

MHE. HEZEKIA H. N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa NaibuSpika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogola nyongeza, wananchi wa Dodoma wangependa wapatenia thabiti kabisa ya Serikali kuhamia Dodoma kwa sababutumeshuhudia hivi karibuni baadhi ya Taasisi za Serikali zilikuwaziko hapa Dodoma zimepewa ruhusa kuhamia Dar es salaam.Lakini vilevile ninazo taarifa kuwa kuna tetesi za Idara zaSerikali zilizokuwa hapa nazo zinajipanga kuhamia Dar essalaam. Nia thabiti ya Serikali kuhamia Dodoma iko vipikatika msimamo huo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi nia thabitimajibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA,URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibuswali la nyongeza la Mjomba wangu Mheshimiwa ChibulunjeMbunge wa Chilonwa kama ifuatavyo pamoja na weweMheshimiwa Naibu Spika, Mjomba wangu ninakujibu.

Nia ya kuhamia Dodoma, nia ya Serikali ya kuufanyaMji wa Dodoma kuwa Mji Mkuu ipo pale pale. Kwa hiyo kamahii inatosha basi ichukuliwe kama ndiyo kauli thabiti ya Serikali,kuwa nia ya Serikali ya kuwa na Makao Makuu Dodoma ikopale pale na Serikali itaendeleza mipango yote inakusudiana inayotaka kuitekeleza ili kuifanya Dodoma iwe MakaoMakuu ya nchi yetu.

Hizo fununu anazosema kuwa Wizara za Serikalizinahamia Dar es Salaam, hapana tunayo Wizara yaTAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ninazungumza kwa niaba yaWaziri Mkuu yuko hapa, Waziri wake na Wizara hii iko Dodoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haijatangazampango wowote wa kuhamisha Makao Makuu ya Ofisi hiikubwa kabisa ya TAMISEMI hapa Dodoma hakuna. Kwahiyo, Mheshimiwa Chibulunje na Waheshimiwa wenginewananchi wa Dodoma hizo habari za uvumi ninafikiri siyo zauhakika uhakika ni huu ninaousema mimi hapa kwa sababumimi niko Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI iko Waziri Mkuu.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

11

Kwa hiyo, hizi ni habari za uhakika kuwa TAMISEMI ikoDodoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, LAPF ni Shirika lina wenyewe,wafanyakazi wamewekeza katika Shirika la LAPF Mifuko yoteMakao Makuu yake wamefanya ni Dar es salaam. Kwa hiyo,ili kuleta ushindani na kutoa huduma bora zaidi kwawanachama wake ambao ndiyo wenye mfuko ni kweli kuwasasa Makao Makuu yanke sehemu kubwa siyo kwambawanavunja hii inagawa mkiangalia pale Dodoma badowamewekeza Kitega Uchumi kikubwa sana nawameendelea kuwekeza na UDOM lakini kwa kiasi kikubwawatahamia Dar es salaam, kwa sababu mifuko mingine yoteiko Dar es salaam na sehemu kubwa ya Wanachama wakeni rahisi zaidi kupafikia Dar es salaam na wengi zaidi wakoDar es salaam na LAPF kwa kiwango fulani na yenyeweinafanya biashara.

Ili mtandao wake wa biashara uweze kukamilikaimeonekana ni vizuri wakiwa Dar es salaam ili wawezekutekeleza mipango yao vizuri, lakini hiyo haimaanishi na walahaina mahusiano ya kuondoa Makao Makuu Dodoma.

NAIBU SPIKA: Tunakushukuru sana Waziri na pole sanakwa maswali hayo. Waheshimiwa Wabunge mmekaa hapamiezi karibia miezi miwili, mitatu kama kweli mmepata nafasiya kutembelea Mji wa Dodoma mtaona mabadiliko nimakubwa sana ya maandalizi ya ujenzi wa Dodoma.Tunaipongeza sana Serikali kwa hilo, ni Swali la MheshimiwaJeremiah Meshack Opulukwa.

Na. 459

Matatizo Makubwa ya Walimu Meatu

MHE. MESHACK J.OPULUKWA aliuliza:-

Liko tatizo kubwa la walimu wa Meatukucheleweshwa kupandishwa cheo na pia palewanapopandishwa daraja hawalipwi stahili zao:-

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

12

Je, ni lini Serikali itashughulikia na kuyaondoa kabisahaya matatizo yanayowakabili walimu wa Meatu?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI (ELIMU): Mheshimiwa Naibu Spika, kwaniaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ninaomba kujibu swali laMheshimiwa Meshack Jeremiah Opulukwa, Mbunge waMeatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imedhamiriakuondoa tatizo la walimu kuchelewa kupandishwa madarajana kulipwa stahili kama ifuatavyo:-

• Kuimarisha na kuboresha mfumo wa taarifaza Utumishi na Mishahara Serikalini LAWSON kwa kuwekeataratibu za kiutumishi za kushughulikia malimbikizo yamishahara, kuhamisha, ukomo wa utumishi na marekebishoya taarifa za mtumishi.

• Katika mwaka wa fedha 2013/2014, Serikaliitaboresha idara ya Utumishi wa walimu (TSD)kifedha narasil imali watu il i iweze kumudu majukumu ikiwemoupandishwaji madaraja walimu.

• Aidha Serikali imeunda Kamati ya kuchambuana kutoa mwongozo kwa ajili ya kushughulikia changamotoya upandishwa madaraja walimu. Mwezi Januari, 2013,mapendekezo ya Kamati yaliwasilishwa katika Baraza lamajadiliano ya pamoja katika ya sekta Elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetoa maelekezokwa Wakurugenzi wa Halmashauri wote nchini kutosababishamadeni na kuhakikisha kuwa wanatenga fedha zakuwapandisha madaraja watumishi wakiwamo walimu nakuhakikisha marekebisho ya mishahara yanalipwa kwawakati. Mwaka wa fedha 2013/2014, Serikali imetenga nafasiza kuwapandisha vyeo walimu 39,602 walio katika Mamlakaya Serikali za Mitaa na shilingi milioni 64 zimetengwa kwa ajiliya kuwapandisha madaraja walimu 330 wa Halmashauri yaWilaya ya Meatu.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

13

Serikali itaendelea kuwajengea uwezo watendaji iliwaweze kutumia mfumo wa HCMIS kikamilifu na kutatuachangamoto zilizopo. (Makofi)

MHE. MESHACK J. OPULUKWA: Mheshimiwa NaibuSpika, kwa kuwa kuna walimu zaidi ya 100 kwenyeHalmashauri ya Meatu ambao walipandishwa daraja mwakajana mwezi wa nne, lakini baadaye mwezi huohuo wakatiwalikuwa wamepewa barua za kupandishwa madarajawalinyang’anynywa zile barua kuwa zilikosewa na kurudishwaTSD, sasa ni lini walimu hawa ambao wameshapanda darajatoka mwaka jana mwezi wa nne watapata stahili zao kamaambavyo barua zil ivyokuwa zikielekeza kabla yakunyang’anywa?

Swali la pili. Kuna walimu ambao waliomba likizowakaruhusiwa kwenda likizo kwa mujibu na taratibu zauombaji wa likizo, lakini kati ya walioomba likizo ni baadhiyao tu ndio ambao walilipwa fedha ya kwenda likizo.

Je, ninapenda kuuliza ni taratibu zipi zilizotumikakuwabagua walimu hawa baadhi wakalipwa lakini walewengine hawakuweza kulipwa fedha zao za likizo? Ahsantesana.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI (ELIMU): Mheshimiwa Naibu Spika, kwaniaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ninaomba kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Meshack Opulukwa, Mbunge waMeatu, kama ifuatavyo:-

Upo ukweli kuwa Tume ya Utumishi Ofisi ya Rais ilitoamaelekezo ya mfumo wa upandishaji wa madaraja ambayomwezi Januari walisitisha kufanya hivyo kwa Watumishi wotenchini wakiwemo walimu na kibali hicho kimetolewa tenamwezi Aprili ili kuendelea na mchakato wa upandishaji wamadaraja baada ya kuondoa kasoro amabzo zilikuwazimejitokeza na kwa hiyo walimu wale ambaowalinyang’anywa barua zao sasa watarudishiwa naHalmashauri kupitia TSD pale Meatu ili mchakato ule

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

14

uendelee pamoja na uratibu wa fedha za kuwalipa walimuhawa kwenye malimbikizo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini fedha hizi zamalimbikizo mara nyingi zinalipwa na Hazina. Kwa hiyo,Halmashauri zote nchini kupitia TSD wanachofanya sasa nikuratibu na kuorodhesha walimu wote ambaowamepandishwa na kubadilisha ngazi za mishahara ili rekodizile ziende Utumishi, Utumishi watoe kibali Hazina na Hazinaianze kulipa na ulipaji wake unapitia katika account zawalimu wenyewe moja kwa moja. Kwa hivyo, utaratibuutaendelea kupitia maelekezo haya.

Lakini swali la pili la likizo ni kweli kuwa nchi nzimatunao walimu katika kila Halmashauri wanapaswa kwendalikizo ikiwa ni haki yao ya msingi na kila Mtumishi anatakiwakwenda likizo mara moja ile ambayo anatakiwa kulipwafedha zake.

Kwa hiyo, inawezekana pia kuwa hela ambazoTAMISEMI tunazituma katika Halmashauri hazitoshi au hazikidhimahitaji ya walimu wote wa Halmashauri na kwa hiyo MaafisaElimu ambacho tumewashauri ni kuandaa orodha ya walimuwanaopaswa kwenda likizo ikiwezekana miezi kabla ya waleambao watalipwa kulingana na fedha ambazo sisitumepeleka ili waweze kulipwa na tumewasihi Maafisa Elimukuimarisha mawasiliano kati yao na walimu wetu ili kuondoatofauti ambazo zinaendelea kuwafanya walimu kuwa nauhakika wa lipi baada ya mawasiliano hayo ili kuondoakasoro hizo za kutokuwa na taarifa ambazo MheshimiwaMbunge ulikuwa unahitaji.

Kwa taarifa hii kupitia Bajeti zetu za mwaka huu wa2012/2013 tumeongeza viwango hivi vya fedha ambavyotunatuma kwenye Halmashauri kwa ajili ya kulipa likizo ilizisaidie kuongeza idadi ya walimu wanaokwenda likizo kamahaki yao ya msingi ili walimu hawa waweze kulipwa fedhazao zote. Kwa hiyo, huo ndiyo utaratibu tunaotumia katikaHalmashauri zetu.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

15

NAIBU SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Dkt. MaryMwanjelwa, swali moja la nyongeza.

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: Mheshimiwa NaibuSpika, ninakushukuru sana kwa kuniona kwa kuwa tatizo lawalimu wa Meatu linafanana sana na Walimu wa Jiji laMbeya licha ya kwamba walimu wa Jij i la Mbeya,wamecheleweshwa sana kupandishwa madaraja, lakini piawanashushwa madaraja na walimu hawa wa Jiji la Mbeyaunakuta wamejiendeleza mpaka Vyuo Vikuu, lakini ajabu nikwamba wanaambiwa kwamba kupandishwa kwaomadaraja kulikosewa hawajalipwa stahili zao.

Kwa hiyo, nilikuwa ninataka Mheshimiwa Waziriatueleze sintofahamu hii ya walimu wa Jiji la Mbeya ni ninitatizo na lini watapewa haki zao?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI (ELIMU): Mheshimiwa Naibu Spika, jambohili kama nilivyoeleza kwenye jibu la nyongeza la MheshimiwaOpulukwa linaikabili karibu kila Halmashauri nchini. Tatizo laManispaa ya Mbeya ninalifahamu, hatuna Katibu wa TSDMbeya, suala hili la Katibu wa TSD ni la Ofisi ya Rais Utumishiambalo linapaswa kuwapeleka Makatibu wa TSD na Mkoamzima wa Mbeya. Tuna Makatibu wasiozidi watano katikaHalmashauri zote saba. Kwa hiyo, bado tuna upungufu waMakatibu TSD ambao watafanya kazi ya kuwapandishawalimu hawa. Usitishaji wa kutopandisha madaraja kwaWatumishi wote uliofanywa na Utumishi ulitoa nafasi yakufanya uratibu kwenye maeneo haya lakini kwa Manispaaya Mbeya tumetoa maelekezo ya kuhamisha Katibu TSDkutoka Rungwe mmoja aende Manispaa ili kuokoa tataizohili ambalo linawakabili sana walimu wa Manispaa ya Mbeya.

Hii sasa akishakuwa pale ataweza kutatua matatizoya msingi ingawa atakuwa na kazi kubwa ya kuweza kupitiaucheleweshaji ambao umejitokeza katika Manispaa ile ilikuwafanya walimu hawa. Hii itakuwa ni pamoja na malipoyao kama ambavyo nimeeleza kwenye jibu la nyongeza laMheshimiwa Opulukwa.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

16

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ninawaonalakini muda hauko upande wetu. Swali la Mheshimiwa Dkt.Augustine Lyatonga Mrema, kwa niaba yake MheshimiwaJames Mbatia.

Na. 460

Kesi Inayozuia Mji wa Himo Usipimwe Viwanja

MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y. MHE. DKT. AUGUSTINELYATONGA MREMA) aliuliza:-

Inasemekana kuwa kesi bandia tangu 2002-2013inayozuia Mji wa Himo usipimwe viwanja na kujengwa.

(a) Je, inakuwaje kesi inakaa Mahakamani kwa miakazaidi ya kumi (10) bila kumalizika?

(b) Je, Serikali inakusudia kumaliza vipi mgogoro waviwanja Himo?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu na kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Augustine Lyatonga Mrema, Mbunge wa Jimbo la Vunjo,naomba kutoa maelezo ya utangulizi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa ipo kesi Na.1/2003 iliyofunguliwa na Ndugu Augustino Temu na Paul Lyimokwa niaba ya wananchi wengine 345 dhidi ya Halmashauriya Wilaya ya Moshi Vijijini, wakipinga upimaji wa viwanjakatika eneo la Mji wa Himo kwa madai kwamba eneolinalotakiwa kupimwa ni eneo la asili hivyo hawakubaliani naupimaji huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayomafupi sasa ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Augustine Lyatonga Mrema, lenye sehemu (a) na (b) kamaifuatavyo:-

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

17

(a)Mheshimiwa Naibu Spika, kesi hii imechukua mudamrefu kwa sababu kumekuwa na maombi mengi kutoka kwawalalamikaji wa kesi hii. Mfano maombi ya hayo ni maombiNa.1/2008, yaliyowasilishwa Mahakamani na walalamikajikuitaka Halmashauri kuthibitisha kama upimaji wa viwanjauliokwishafanyika ulifuata taratibu za upimaji na maombi Na.14/2012 ambayo walalamikaji wameomba Mahakamakuzuia upimaji wa viwanja katika eneo hili mpaka kesiitakapomalizika.

Ninapenda kuliarifu Bunge lako kwamba maombihaya mawili tayari yamekwisha sikilizwa na hivi sasatunachokisubiri ni Mheshimiwa Jaji aliyekuwa akisikiliza kesihii aweze kwenda kuimalizia kusikiliza na tunaamini kuanziamwezi julai mpaka August mwaka huu 2013 kesi hii itakuwaimemalizika.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kesi hii badoiko Mahakamani, Serikali haiwezi kuingilia maamuzi yaMahakama na kwamba inasubiri maamuzi yatolewe ndiposhughuli za upimaji wa viwanja ziweze kuendelea katika eneolenye mgogoro. Hivyo, kumalizika kwa mgogoro huukutategemea maamuzi yatakayotolewa na Mahakamakufuatia kesi inayoendelea. (Makofi)

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwakuwa mradi huu wa kupima Mji wa Himo na Miji mingineunahitaji sana Future Master Plan ya Miji yetu yote ikiwemoDodoma, Dar es salaam na kwingineko Serikali haionikwamba kabla ya kuanzisha mradi wowote ule kuna ideaconcept physibility study for project realization na ProjectManagement na inategemea sana time, cost and qualitysasa kesi hii imekuwa Mahakamani kwa zaidi ya miaka kumina moja sasa.

Ni nini communication strategy ya Serikali kwa sababuya integration ya time kwa wakati huu ili kuweza kuondoamuda umekuwa mrefu ili project hii ya Himo na Future Plansza Miji mingine yote tuwe na maabara ya kufikiri badala ya

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

18

kuingiza Taifa kwenye migogoro kama hii inayoendelea Himosasa hivi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa letu?

Haki inayocheleweshwa ni haki inayonyimwa,Mheshimiwa Naibu Waziri kwa nini kusiwepo na meza yamazungumzo nje ya Mahakama. You better have a badsettlement outside the court rather than Judgment in theCourt ili kuweza kumaliza mgogoro huu tuweze kuokoa mudana Miji yetu iweze kupanuka nchi nzima?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaNaibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuuninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya MheshimiwaJames Mbatia, Mbunge wa kuteuliwa, kama ifuatavyo:-

Swali la kwanza, Serikali ina communication strategygani ya kuhakikisha kuwa kesi hii inamalizika ninadhani katikajibu langu la msingi nilishaeleza kuwa tunatarajia ndani yamwezi Julai mpaka mwezi August kesi hii itakuwa imekwishamalizika, na ninapenda tu kulieleza Bunge lako Tukufu kuwakesi hii imeshikiliwa na Majaji watatu Jaji Mziray aliyeko sasahivi ni Jaji wa tatu na suala hili limekuwa likichelewa kutokanana walalamikaji wenyewe wa kesi hii na kama ambavyoMheshimiwa Mrema mwenyewe ameuliza kesi hii imekuwaikionekana ni kesi ya bandia kwa sababu hata haowalalamikaji wengine 345 hawajawahi kuthibitisha kamakweli ni walalamikaji katika kesi hii.

Lakini pia suala kubwa katika kesi hii imekuwa nimgogoro wa namna bora ya kufikia kiwango cha fidiawamekuwa wakikaa na kama ambavyo mwenyeweumekwishakueleza katika swali lako namba mbili, kuwa ni kwanini badala kutumia usuluhishaji wa Mahakama kwa ninihatutumii mbinu zingine kusuluhisha mgogoro huu kamaambavyo nimeshaeleza katika maombi ya pamoja yamwaka 2008 na maombi namba 14 ya mwaka 2012.

Mheshimiwa Jaji Mziray alielekeza kesi hii iende katikahatua ya usuluhishi na imekuwa ikifanyika lakini meza ya

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

19

mazungumzo wao wenyewe walalamikaji wamekuwawakishindwa kufikia muafaka na ndiyo maana imeondokakatika hatua hiyo tumeshamaliza maombi yale sasa hivimwezi wa saba na mwezi wa nane Mheshimiwa Jaji Mzirayakienda ni kuimaliza kabisa. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Swali fupi sana la nyongeza MheshimiwaJoseph Selasini, nilikuona.

MHE. JOSEPH R. SELASIN: Mheshimiwa Naibu Spika, kesibandia zinazofanana na kesi hii zipo nyingi katika Mahakamazetu hapa nchini. Je, ni lini Serikali itafanya utafiti wa kesikama hizi na kutumia njia za usuluhishi i l i ziondokeMahakamani kwa ajili ya kujenga dhana ya kuwapatiawananchi haki ambayo wanaitafuta kwa muda mrefu?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaNaibu Spika, Mheshimiwa Selasini ametaka kujua ni lini Serikaliitafanya utafiti wa kufahamu kesi zilizorundikana katikaMahakama zetu ambazo zinaonekana labda ni za bandiakama hii ya Mji wa Himo.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kwamba Serikali kupitia Mahakama ipo katikampango wa kufanya uchambuzi kesi zote zil izokoMahakamani, kuzipitia kwa kina, kuangalia zimewasilishwamahakamani hapo mwaka gani, lakini si hilo tu, tuna mpangokuanzia mwezi huu julai mwaka 2013 kuanza na Mji wa Arusha,Mji wa Mwanza pamoja na Jiji la Dar es Salaam, tunaanzishaKamati inayoitwa Bench Bar Judiciary Committee.

Katika Kamati hii tutakaa Uongozi wa Mahakamapamoja na Uongozi wa Mawakili ili kupitia kesi zote nakuwapa taarifa kwa wale Mawakili ambao wanajulikana kwakuweka pingamizi Mahakamani watataarifiwa mbele yaMawakili wenzao ili waone kama kweli ni sahihi kesi hizikupigwa danadana kwa muda mrefu kama ambavyoumeelezwa.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

20

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini si hiyo tu, ukiangaliakatika Mahakama Kuu kitengo cha ardhi, jana tarehe 24tumeshaanza vikao vya Mahakama katika Mkoa wa Mtwara,Tanga na katika Mkoa wa Mwanza. Tunaandaa programupia nchi nzima na tutaweka kalenda hiyo wazi kabisa ilituweze kumaliza kesi zote zenye mlundikano. KatikaMahakama ya ardhi tayari sasa hivi tumeanza na kesi zotezza mwaka 2009 na tutakuja za mwaka 2010, 2011 mpakahivi sasa. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Tuendelee na ofisi ya Makamu wa RaisMazingira, swali l inaulizwa na Mheshimiwa MhandisiAthumani Mfutakamba.

Na. 461

Uhifadhi wa Mazingira

MHE. ENG. ATHUMANI R. MFUTAKAMBA aliuliza:-

Baada ya Mkutano wa kwanza wa uhifadhi wamazingira duniani kumalizika mwaka 1992 huko Rio DeJanerio, sasa ni miaka ishirini na moja (21) imepita:-

(a) Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kulindaathari za mabadiliko ya tabianchi na kupeleka elimu vijijiniambako kunatokea mafuriko na ukame?

(b) Je, baada ya mazungumzo ya Doha naCancum, Tanzania imejipangaje kuzuia hasara na upotevuwa mali unaotokana na Nchi za Ulaya, Marekani, China naIndia ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa kuingizahewa ya ukaa (CO2) kupitia viwanda vyao duniani?

(c) Je, Serikali itawasaidiaje wananchi wa Igalulana maeneo mengine nchini yaliyokumbwa na ukameuliosababisha mazao na mifugo kufa miaka mitatu mfululizokutoka na athari ya tabianchi?

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

21

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Eng. Athuman Rashid Mfutakamba, Mbungewa Igalula, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Serikali imeweka utaratibu wa kuendeshavipindi vya redio na runinga na maadhimisho mbalimbali yamazingira kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi nanamna ya kukabiliana nayo.

Aidha Serikali ina washirikisha Watendaji katika ngaziza Halmashauri na wanavijiji katika utekelezaji wa miradiinayohusu mabadiliko ya tabia nchi. Kwa mfano tangumwaka 2011/2012 Serikali inatekeleza miradi ya vijiji vyamfano eco-villages katika vijiji vya Chololo Mkoani Dodoma,Luguru Morogoro na Zanzibar chini ya ufadhili wa Jumuiyaya Ulaya.

Vilevile utekelezaji wa mradi wa kuhimili mabadilikoya tabianchi unaofanyika ili kuwezesha upatikanaji wa majikatika Wilaya za Igunga, Mbinga, Misenyi kwa upande waTanzania Bara na Chakechake kwa upande wa Zanzibar.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya mikutanoya Cancun na Doha, na Durban - South Africa, Tanzaniaimekamilisha kuandaa mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchiambao unatoa mwongozo wa hatua zinazotakiwakuchukuliwa na sekta mbalimbali katika kukabiliana namabadiliko ya tabianchi.

Ili kutekeleza mkakati huo baadhi ya sekta zimeanzakuandaa mipango ya utekelezaji. Kwa mfano Wizara yaKilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Maji zimeshaanzamaandalizi ya kuandaa mipango ya aina hiyo. Aidha Serikaliimeandaa mpangokazi wa kuandaa mpango wa muda wakati na muda mrefu wa kukabili mabadiliko ya tabianchikatika sekta mbalimbali.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

22

Vilevile Serikali inaendelea kutekeleza miradi miwilimikubwa ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi inayofadhiliwana mfuko wa nchi maskini duniani na mfuko wa dunia wakuhimili mabadiliko ya tabianchi (Adaptation Fund –AF) katikaukanda wa Pwani.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inawashauriwananchi wa Igalula na maeneo mengine nchini kuzingatiaushauri unaotolewa na watalaam wa Kilimo na Mifugo katikamaeneo hayo kuhusu aina ya mazao yanayoweza kustawina ufugaji wenye tija.

Aidha, wananchi na wkaulima wanashauriwakuzingatia ushauri unaotolewa na Mamlaka ya hali ya hewanchini kuhusu mwenendo wa hali ya hewa.

MHE. ENG. ATHUMAN R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru kwa majibu mazuri ya Waziri, ninamaswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, biashara ya hewa ukaa katika misituinayomilikiwa na green resources kule Mufindi pamoja naMuheza na Manyara wanafaidika kwa biashara hiyo, Wazirianaweza kuniambia utaratibu huo unaweza kusaidiwa kwavijiji vya Igoweko, Mienze, Luoya na Lutende pamoja na Turaambao wanahifadhi misitu ya vijiji kwa kutumia mpango waPFM (Participatory Forest Management) ili nao wawezekufaidika kwa fedha za kutoka Ulaya na Marekani?

Swali la Pili, kwenye agenda ya 21 kulikuwa na sualamtambuka la Nishati Mbadala Vijijini.

Je, Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingiraikishirikiana na Wizara ya Nishati na Madini wanawezakusaidiaje wananchi wa Igalula ili wasiendelee kukata mitikwa ajili ya mkaa na kuni na kupata nishati mbadala ya solapamoja na biogas kama wanavyofanya Thailand?Nashukuru sana.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

23

NAIBU SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziriwa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Terezya PiusLuoga Huvisa Gama (Kicheko/Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napendakutoa shukrani kwa kunitambua kwa majina yangu yote.Ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu biashara ya hewaukaa ambayo inaendeshwa na kampuni ya green resource,ninachoweza kusema ni kwamba ni kweli green resourcekutoka Serikali ya Norway ndiyo wamekuwa Taifa la kwanzakuendesha hii biashara, lakini biashara hii ya Kimataifa inataratibu zake na ninapenda kuwaelimisha wananchi wotekupitia Bunge lako Tukufu kwamba Biashara hii inatakiwamwekezaji pamoja na mwananchi wapewe gawio. Gawioni lazima liwe nusu kwa nusu. Wanachofanya green resourcewanatoa gawio la ten percent tu ambapo ni ukiukwajimkubwa wa taratibu za kimataifa. Kwa hiyo, mpaka sasa hiviOfisi ya Makamu wa Rais haijatoa kibali cha kuwaruhusukuendelea na biashara hiyo mpaka watakaporekebishataratibu hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu hizo zikikamilika,Taifa zima na sehemu zote zinazohifadhi misitu basi watawezakufaidika na biashara hii ya hewa ukaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili linalohusuagenda ya 21 kuhusu nishati mbadala. Ni kweli kabisakutokana na mabadiliko ya tabianchi tunahitaji kuwa nanishati mbadala na suala hili tumeshaliongelea mara nyingisana hasa kwenye mikutano yetu ya kimataifa kwambawakati wote nchi ambazo zinaendelea zilikuwa zinanyonyahewa ukaa bila kujua, lakini sasa hivi tumeshajua na ndiyomaana mazungumzo yanaendelea katika mikutano yakimataifa ili nchi zinazoendelea ziweze kupata fidia yakufanya hiyo kazi ya kunyonya hewa ukaa. Tunapopata hizopesa, hizo pesa zitatusaidia sana kuwaelimisha wananchi nakutumia kwenye nishati mbadala.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

24

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla hatujapata hizo pesa,nitoe wito kwamba Wabunge tuendelee kuwaelimishawananchi pamoja na kwamba tunatumia kuni na mkaa, basitutumie majiko banifu ili tuweze kutumia kuni kidogo na mkaamdogo. Lakini vilevile tuendelee kupanda miti kwenyemashamba yetu, tutumie kilimo mseto ili tusivune miti hiyokwenye misitu badala yake tuvune kwenye mashamba yetu.

NAIBU SPIKA: Swali fupi sana la nyongeza, naombaMwenyekiti wa Kamati ya Wabunge marafiki wa MazingiraMheshimiwa Hilda Ngoye.

MHE. HILDA C. NGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa nafasi hii na kwa kunitambua vile vile.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa suala lamazingira ni suala la mtambuka na wote tunafahamu hivyo,na kwa kuwa huko vijijini kumeanzishwa taasisi mbalimbalizisizo na kiserikali NGO’s ambazo zinafanyakazi nzuri sana yakuelimisha na wameanzisha miradi midogomidogo yakusaidia wananchi ili kudhibiti matatizo ya uharibifu wamazingira.

Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuzitambua hizi taasisizisizo za kiserikali, ambazo zinafanyakazi nzuri sana kwawananchi wetu. Serikali inawasaidiaje wananchi hawaambao wapo kwenye vyama hivi ili waweze kuendeleakufanyakazi nzuri ya kuhifadhi mazingira?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongezeWabunge wote ambao wapo kwenye asasi hiyo, kwa sababusisi Wabunge ndiyo tunaotakiwa kuwa viongozi wa kuhifadhimazingira. Kwa hiyo, nitoe wito hata kwa Wabunge wenginewaingie kwenye chama hicho cha rafiki wa mazingira ilituweze kuonesha mfano na kuelimisha wananchi kwa ujumla.(Makofi)

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

25

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali linalohusuNGO’s pia nizipongeze NGO’s zote ambazo zinasaidia kwahali na mali kuhifadhi mazingira ya nchi yetu, ili maisha yetuyawe endelevu. Ninajua kabisa kuna NGO’s nyingi ambazoni rafiki wa mazingira, wanatoa elimu, wanafanyakazimbalimbali, tunazitambua na kwa kutambua hukotumeanzisha mashindano ambapo Rais anatoa tuzo yamazingira kwa wale wote ambao wamefanya vizuri na tuzohii inafanyika kila baada ya miaka miwili. Tulitoa mwaka janatutatoa tena mwaka kesho.

Kwa hiyo, ninaomba NGO’s zote ziwasiliane naMkurugenzi wa Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais ili wawezekuingia kwenye tuzo hii. Lakini wanapowasiliana basi wapitiekwenye Halmashauri zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna miradimidogomidogo ya UNDP ambapo Ofisi ya Rais ni mdhibiti,na kila mradi wanapata milioni hamsini. Kwa hiyo tunaombaWabunge NGO’s zilizoko kwenye majimbo yenu muwashauriwaandike miradi hii ili waweze kupata milioni hamsinikuendeleza shughuli mbalimbali zinazofanyika na NGO’s.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuendelee naswali linalofuata kwa sababu ya muda, nawaona kabisa lakinimuda hauko upande wangu. Swali la Wizara ya Nishati naMadini, Mheshimiwa Shaffin Ahmedali Sumar.

Na. 462

Wilaya ya Uyui Kupatiwa Umeme

MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza:-

Wilaya ya Uyui haina Hospitali ya Wilaya na pia kunakituo kimoja cha Afya ambacho hakina huduma ya umeme.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka umemeambao umepita umbali wa kilomita tisa(9) tu kutoka kwenyeKituo cha Afya?

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

26

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini napenda kujibu swali la Mheshimiwa ShaffinAhmedali Sumar kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia wakala wanishati vijijini REA inatekeleza mradi wa kuepeleka umemeWilaya ya Uyui katika maeneo ya kituo cha Afya cha Upuge,Ndono, Ufulama, Mbutu, Mogwa, Ntubugo, Nyangabe,Muhulidede Magiri/Mayombo, Kigwa A na B, Goweko, PolisiImalakaseko, Igalula na Inala - Tabora Mjini. Mradi huoutatekelezwa chini ya mpango kabambe wa umeme vijijiniawamu ya pili.

Mheshimiwa Naibu Spika, zabuni ya kuwapataWakandarasi wa kazi hizi ilitangazwa mwezi Desemba, 2012na kufunguliwa mwezi Machi, 2013. Kazi za mradi huuzitahusisha:-

(i) Ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa KV33 umbali wa kilomita 8;

(ii) Ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa Kv0.4 umbali wa Km2;

(iii) Kufunga transfoma tatu zenye uwezo wa KvA50; na

(iv) Kuunganisha wateja wa awali wapatao 70.

Gharama ya kazi hizi inakadiriwa kuwa shilingi milioni451.21. Kazi hizi zinatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka2013.

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri,naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

27

Kwa kuwa, jirani na Kata ya Upuge kuna Kata yaIkongolo ambapo kuna vijiji vya Kanyenye, Majengo naIkongolo ambavyo havikutajwa kwenye jibu la msingi nabadala yake kuna vijiji vingi vimetajwa ambavyo havimoJimbo la Tabora Kaskazini.

Je, nini mpango wa Serikali wa kuvipatia umeme vijijihivi vya Kanyenye, Majengo na Ikongolo?

Swali la pili, kwa kuwa, kuna maeneo mengi nchiniambayo yamepitiwa na nyaya za umeme lakini huduma hiiya umeme haijasambazwa katika maeneo mengi yanayotoahuduma za jamii. Ni nini tamko la Serikali kuhusiana nakupeleka umeme na kwa muda gani?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Naibu Spika, kamaambavyo aliuliza kwenye swali la msingi, hasa alichotakakujua ni kama kuna mpango wowote wa kupeleka umemekatika kituo cha afya cha Upuge na hii nimehakikisha kabisakwamba tunapeleka umeme Upuge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Kata yaIkongolo na Vijiji vya Kanyenye na Majengo sasa hivitunaandaa phase ya tatu ya mpango wa kupeleka umemevijijini. Tutajaribu katika mpango huo basi tuweze kuviwekavijiji hivi ili tuweze kutekeleza miradi hii kwenye mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili amesema juuya maeneo ambayo yamepitiwa na nyaya zinazosafirishaumeme. Tunayo program ya underline transformer, kwenyemaeneo yote yale ambayo umeme umepita tuweze kuwekatransformer na tuweze kuwasambazia wananchi umeme, nahii tutaifanya kadiri ambavyo tutakuwa tunafanikiwa kupatafedha kwa sababu kazi yake si kubwa maana umeme uponi kuweka transformer na kuwasambazia wananchi.Tutajitahidi kufanya hivyo kadiri tutakavyoweza kupata fedha.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

28

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkitazamamuda wetu ni almost umeisha na nina maswali manne hapa.Kwa hiyo, ninawaomba radhi. Mheshimiwa Faith Mitambo,Mbunge wa Liwale, swali kutoka Makunjiganga.

Na. 463

Upungufu kwenye Sheria ya Madini

MHE. FAITH M. MITAMBO aliuliza:-

Sheria za Madini zilizopo sasa zinawanyima fursa nahaki wamiliki wa maeneo husika kumiliki na kuchimba madiniyanapogundulika kwenye maeneo yao wanayomilikikisheria:-

(a) Je, kwa nini Serikali hairekebishi sheria hizo iliwamiliki wa maeneo husika yanayogundulika kuwa narasilimali za Madini wawe na haki ya kumiliki au kuwa nashares na mtu mwingine atakayeruhusiwa kuchimba madinikweneye eneo hilo?

(b) Inapotokea mahali paligundulika kuwa namadini tayari pana miradi ya kudumu kama hospitali, shulena miradi mingine mikubwa ya uchimbaji inatakiwakuchimba madini kwenye maeneo hayo Je, Serikali inasemanini juu ya fidia kwa wamiliki wenye taasisi hizo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini naomba kujibu swali la Mheshimiwa FaithMohamed Mitambo, lenye sehemu (a) na (b) kamaifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Madini yaMwaka 2010 imetoa fursa kwa wazawa na wageni kumilikileseni za aina mbalimbali, zikiwemo za utafiti (PL), uchimbaji

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

29

wa kati, (ML), uchimbaji wa mkubwa (SML) na uchimbajimdogo (PML) kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na njekufanya shughuli za madini bila ubaguzi. Hata hivyo, umilikiwa leseni hizi haumpi mtu au kampuni kumiliki ardhi mpakaakidhi masharti ya kifungu Na. 95 cha Sheria ya Madini yaMwaka 2010 na Sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilirekebisha sera yamadini 1997 na sheria ya madini ya mwaka 1998 na kupatasera ya madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya Mwaka2010. Mabadiliko haya yanatokana na dhamira ya dhati yaMheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ya kuainishana kuondoa na kuboresha mapungufu yaliyokuwepo katikasera na sheria ya awali ikiwemo suala la mikataba na kuundaTume ya Jaji Mark Bomani ya mwaka 2008. Serikali itaendeleakufanya marekebisho kadiri itakavyohitajika kwa kushirikianana wadau.

Aidha, kifungu cha 95 cha Sheria ya Madini yaMwaka 2010 kinamzuia mmiliki wa leseni ya madini kuanzakuchimba bila kupata ridhaa ya mmiliki wa ardhi.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 95 chaSheria ya Madini ya Mwaka 2010 kinatoa mwongozo kwammiliki yeyote wa leseni za madini kuomba na kupata ridhaaya mmiliki halali wa ardhi kabla ya kuanza shughuli za utafutajiuchimbaji madini.

Kwa mujibu wa kifungu hicho na kwa mujibu wa Sheriaya Ardhi, Na. 4 ya mwaka 1999 kama il ivyofanyiwamarekebisho kwa nyakati mbalimbali, mmiliki halali wa ardhianastahili fidia ili kupisha shughuli za uchimbaji paleitakapoonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Baadhi ya sehemu zil izopata fidia baada yakufanyiwa tathmini kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (1999) nipamoja na Tarime (maeneo ya Nyamongo na Nyabigena),Buzwagi (maeneo ya Mwime na Mwendakulima) na Geita(maeneo ya Katoma na Nyakabare). (Makofi)

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

30

MHE. FAITH M. MITAMBO: Ahsante sana MheshimiwaNaibu Spika. Mheshimiwa Naibu Waziri, kumekuwa namkanganyiko wa kati ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010na Sheria za Ardhi. Hivyo kufanya viongozi wa ngazi za Serikaliza Vijiji kutoa vibali na kuwaruhusu wachimbaji kuchimba nakufanya shughuli za machimbo bila kufuata taratibu. Je,Serikali ipo tayari kufafanua mkanganyiko huu wa Sheria yaMadini inayogongana na Sheria ya Ardhi?

Swali la pili, je ni taratibu kuwaruhusu wachimbajiwadogo wadogo na wakubwa kufanya shughuli zao zauchimbaji katika maeneo ambayo tayari yana leseni ya PML,ML, SML na PL? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. STEPHENJ. MASELE): Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna mkanganyikowowote katika Sheria ya Ardhi kama nilivyoieleza Sheria Na.4 ya Mwaka 1999 na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama katika Sheria yaArdhi, Sura 113 hasa kipengele Na. 2 ambacho kinazungumziatafsiri ya ardhi. Inasema wazi ardhi ni sura ya nchi sehemuambayo ni sura ya dunia na inaeleza kabisa kwamba ardhini pamoja na vitu vilivyopo chini ya ardhi. Lakini isipokuwamadini na mafuta. Sasa ukiangalia Mheshimiwa Mbungeanachooeleza hapa ni mkanganyiko wa nani anamiliki kulechini ya ardhi. Lakini Kifungu Na. 4 cha Sheria hiyo hiyo yaArdhi inaeleza kabisa kwamba Rais ndiyo trustee ama superiorland lord ambaye ndiye anayesimamia ardhi kwa niaba yaWatanzania wote na sisi Watanzania ikiwemo WaheshimiwaWabunge humu ni wapangaji tu na tunapanga hivyo kupitiaTitle Deed zetu ambazo tunalipia kwa miaka 33 na miaka 99na kila mwaka tunalipa hiyo land rent.

Kwa misingi hiyo sasa Sheria ya Madini hasa KifunguNa. 35 ambacho kinampa haki mmiliki yoyote wa leseni hasaleseni ya utafiti kufanya shughuli zake za leseni za utafiti. Lakinihakimmilikishi ardhi ile kama nilivyoeleza hapa kwenye Surahii na tafsiri ya Sheria ya Ardhi.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

31

Kwa hiyo, Mheshimiwa Naibu Spika, hakunamkanganyiko bali Sheria hizi zote zinafanya kazi kwa pamojana Sheria hizi ni lazima zizingatie Sheria nyingine. Kwa hiyo,Sheria ya Ardhi izingatie Sheria ya Madini na Sheria ya Madiniizingatie Sheria ya Ardhi.

Na. 464

Kampuni Ndogo Kutumia Soko la Mitaji

MHE. DIANA M. CHILOLO K.n.y. (MHE. DEVOTA M.LIKOKOLA) aliuliza:-

(a) Je, Serikali itakuwa tayari kuhamasisha wananchiwenye kampuni ndogo kutumia soko la mitaji ili kuondokanana tatizo la mitaji?

(b) Je, ni kwa jinsi gani Serikali itatekeleza jambo hilo?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA M. SALUM)alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Devota Likokola, Mbunge wa Viti Maalum, lenyesehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mamlaka yaMasoko ya Mitaji na Dhamana (Capital Markets Structure andSecurities Authority (CMSA), ilifanya utafiti mwaka 2006 ilikubaini mapungufu na kupata mapendekezo ya namna yakuzishirikisha kampuni ndogo na za kati kushiriki kwenye sokola mitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mapendekezo yautafiti huo ilikuwa ni kuanzishwa kwa safu nyingine mbadalakwenye soko la Hisa la Dar es Salaam itakayohusika nauorodheshwaji wa kampuni ndogo na za kati zisizo na historiaya utendaji na ambazo haziwezi kukidhi vigezo na mashartiya safu kuu ya soko la hisa yaani (Main Investment MarketSegment).

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

32

Kwa kuzingatia mapendekezo haya, Serikaliimechukua hatua ya kulegeza masharti na vigezo vyakuorodheshwa kwenye soko la Hisa. Madhumuni ya hatuahii ni kukuza ujasiriamali na kuziwezesha kampuni changa,ndogo na za kati kushiriki kwenye soko la Mitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali pia imefanyamarekebisho ya kanuni za kusimamia soko la Mitaji ili ziwezekutumiwa na kampuni ndogo na za kati. Taratibu za Soko laHisa la Dar es Salaam nazo pia zilibadilishwa ili kuruhusukuorodheshwa, kuuzwa na kununuliwa kwa hisa za kampunindogo na za kati. Aidha, zoezi hili lilijumuisha kutengenezakanuni maalum za usajili wa wataalam kwa ajilii ya kuzileana kuzishauri kampuni zinazotarajia kuorodheshwa kwenyesoko la kukuzia ujasiriamali.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maandalizikukamilika, CMSA ilitoa matangazo kwenye vyombo vyahabari ili kuzishawishi kampuni za kutoa ushauri elekezi kutumamaombi ya usajili kwa Mamlaka, yaani CMSA. Hadi kufikiasasa, ni kampuni nne za wataalam washauri zimejitokeza nakusajiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana naCMSA itaendelea kutoa elimu ya kuhamasisha wananchiwenye kampuni ndogo na kati kutumia fursa za soko la mitajiili kujipatia mitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli zao zakiuchumi.

Vile vile, CMSA kwa kushirikiana na Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi wanaangalia namna ambavyo elimukuhusu masoko ya mitaji inaweza kuingizwa kwenye Mitaalaya Vyuo na Shule za Sekondari ili kupanua wigo wa elimu yamasoko ya mitaji na dhamana hapa nchini. (Makofi)

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri,napenda kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

33

La kwanza, ili uweze kunufaika na soko la hisa nikununua hisa na kuuza hisa pale zitakapopanda bei. Kwakuwa hisa zinapopanda bei wateja huwa siyo rahisi kupatataarifa wakiwemo Waheshimiwa Wabunge wengiwamenunua hisa.

Je, Serikali itakuwa tayari sasa kutoa taarifa kwawateja kwa maandishi ili zinapopanda bei wateja wawezekuuza hisa kwa lengo la kunufaika na soko hili la hisa?

Swali la pili. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziriamekiri kwamba sasa masharti ya soko la mitajiyamelegezwa. Na kwa kuwa kampuni ndogo na za kati sasaziko nyingi mikoani na Ofisi hii iko Dar es Salaam tu.

Je, Serikali itakuwa tayari kufungua Ofisi hata Ofisi zaKanda ili kampuni ndogo na za kati ziweze kunufaika kukopakwenye soko hili la mitaji? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA M. SALUM):Mheshimiwa Naibu Spika, kikawaida CMSA na Dar es SalaamStock Exchange inakuwa inatoa taarifa zake hususan katikavyombo vya habari kawaida wanatazama kampuni zenyewezinakuwa zinatangaza ule mwenendo wa shares, shareprices.

Sasa tukiangalia kwa wale ambao watakuwa naelimu hasa ya finance pamoja na Capital Market Structurewatakuwa wanafuatilia ule mwenendo hasa hususan kwenyetaarifa za habari walikuwa wakati wa ile statement yabiashara na uchumi wanakuwa wanatoa hizi taarifa ofcourse kwa mtu wa kawaida ambaye atakuwa hana elimuatakuwa hajui the work of DSE hatafahamu.

Lakini hata hivyo tumeshazungumza na Dar es SalaamStock Exchange kuanza sasa kutoa elimu kwa njia rahisi kwalugha nyepesi kabisa ili mwananchi tu wa kawaida ambayeana fedha zake lakini hajui wapi pa kwenda kuzipeleka awenaye anafahamu kwamba kuna hili soko la hisa ambako

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

34

anaweza kwenda kuuza, anaweza kwenda kununua sharesna yeye akawa mmiliki wa hizi kampuni. Kwa hivyo hilotunaangalia mikakati ili ya kuweza kuhamasisha zaidi kwakutoa elimu.

Lakini kuhusu kufungua hizi Taasisi hizi za masoko katikamikoa mingine. Kwa kuanzia tumeanza na Dar es Salaamkweli kwa sababu ni mji ambao ni mkubwa unakuwa sanakibiashara. Lakini kuna intention ya kwenda katika Mikoamingine. Kwa sababu ku-manage Stock Exchange ni kaziambayo inahitaji weledi na inahitaji taaluma kubwa sanana inahitaji vile vile teknolojia kubwa sana na teknolojiainakuwa inabadilika badilika.

Kwa hivyo kwa sasa tuko Dar es Salaam lakini intentionyetu hasa ni kwenda katika Mikoa mingine ili wananchiambao wapo katika hiyo mikoa mingine wapate fursa nawao kuwekeza na kuwa wamiliki katika makampuni hayo.Ahsante sana. (Makofi)

Na. 465

Biashara ya Kubadilisha Fedha Nchini

MHE. MARGARETH A. MKANGA aliuliza:-

Je, Serikali inadhibiti vipi mwenendo wa biasharakatika maduka ya kubadilisha fedha yaliyoko nchini kwasasa?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET ZEBEDAYOMBENE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Margareth Agnes Mkanga, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, maduka yote yakubadilishia fedha za kigeni yanaendeshwa kwa mujibu wakanuni za maduka ya kubadiilshia fedha za kigeni ya mwaka

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

35

2008, yaani The foreign Exchange Bureau De Change,Regulations 2008. Kanuni hizo ziliwekwa kwa mujibu wa ibaraya 5(a) na 7(1) ya Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992inayompa mamlaka Gavana wa Benki Kuu ya kusimamiamaduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, chini ya vifungu vya kanunihizi, maduka yote ya kubadilisha fedha za kigeni lazimayaanzishwe kama kampuni; yamilikiwe na kuendeshwa naWatanzania, yaanze na mtaji usiopungua shilingi 40,000,000/=; hayaruhusiwi kusafirisha fedha nje ya nchi, yanatakiwakuweka kumbukumbu ya mauzo na manunuzi kwenye nukushiyaani (computer) na kutoa stakabadhi inayochapishwakutoka kwenye nukushi inayoonesha muda wa mauzo aumanunuzi ya fedha; yanatakiwa kuwasilisha taarifa za bei zakuuza na kununua fedha za kigeni kila siku na kila mwezi; namwisho, yanatakiwa kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa kilamwisho wa mwaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukabiliana na matatizombalimbali yanayojitokeza, Benki Kuu inafanya yafuatayo:-

Kwa maombi mapya ya leseni, waombajiwanatakiwa kuleta maelezo yao binafsi (CV), Vyanzo vyamitaji yao, pamoja na rekodi ya malipo ya kodi kwa kipindicha miaka mitatu. Hutoa mafunzo ya kanuni za uendeshajiwa maduka ya uuzaji na ununuzi wa fedha za kigeni nakuwafanyia usaili Wakurugenzi na Waendeshaji waandamizikabla ya kutoa leseni mpya; huongeza muda wa lesenibaada ya kujiridhisha kuwa duka husika limetimiza kanuni zauendeshaji. Pia, Benki Kuu hutoa elimu kwa umma kuhusuumuhimu wa kudai stakabadhi za ununuzi na uuzaji wa fedhaza kigeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakaguzi wa mabenkihupitia maduka yote kuangalia na kusimamia utekelezaji wakanuni za kuendesha maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

36

Aidha, wanaokiuka kanuni hupewa adhabuzifuatazo:- hupewa onyo kali; hulipa faini isiyopungua shilingi2,500,000/=; hufungiwa biashara kwa muda wa miezi 3 hadi6; na mwisho, hunyang’anywa leseni kwa mujibu wa Sheria.

MHE. MARGARETH A. MKANGA: NashukuruMheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa nafasi. Kwa vile tatizola kupewa stakabadhi unaponunua au unapouziwa imekuwani kubwa hapa nchini.

Je, Serikali ina uhakika gani wa komputa za kutoastakabadhi hizi hasa kwa zile Taasisi au Kampuni zakubadilisha fedha zilizoanza mwanzoni kabla ya utaratibuhuu?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE):Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina uhakika wa hizocomputer ambazo zimewekwa kwenye Bureau kwa sababuzinakaguliwa mara kwa mara. Kuna Kitengo Maalum chaBenki Kuu ambacho kinafanya kazi ya kukagua mabenkipamoja na taasisi zote zinazojihusisha na masuala ya kifedha.Kwa hiyo, nina uhakika wa hizi computer upo. Suala lakudai risit i kwa kweli ni suala la wananchi husikawanapokwenda kwenye maduka ya kubadilisha fedhakwenye maduka kununua bidhaa mbalimbali, huduma mbalimbali ni wajibu wetu sisi sote kudai hizi risiti. Lakini vile vile nasisi tunapokwenda kwenye Bureau De Change twende navitambulisho vyetu kama Passport na nyaraka zinazohitajikaili waweze kuziingiza katika kompyuta hizi kwa ajili ya kuwekakumbukumbu sahihi. (Makofi)

Na. 466

Lugha za Matusi kwa Watumiaji wa Simu

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA K.n.y. (MHE. MCH. DKT.GETRUDE P. RWAKATARE) aliuliza:-

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ilifanya zoezila kusajili na kuorodhesha namba za watumiaji wa simu za

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

37

mikononi kwa madhumuni ya kudhibiti matumizi sahihi nausalama kwa watumiaji wa simu lakini bado kuna baadhi yawatu hutumia simu hizo kusambaza ujumbe mfupi (SMS) namaneno ya kuzusha:-

Je, Serikali inasema nini juu ya tatizo hilo?

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NATEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Getrude Rwakatare, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa Wizara kupitiaMamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA ilifanya zoezi la kusajilinamba za watumiaji wa simu za mikononi ambapo hadi sasanamba za simu milioni ishirini na nne mia nne na tatu elfu miasita tisini na tisa zimesajiliwa. Usajili huu wa namba pamojana mambo mengine, ulikuwa na lengo la kupunguzamatumizi mabaya ya simu za mikononi.

Mheshimiwa Naibu Spika, usajili wa namba za simuulikuwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikalikuzuia matumizi mabaya ya simu hizo. Hata hivyo,changamoto kadhaa zilijitokeza na kuendelea kuwepo kwamatumizi mabaya ya simu. Changamoto hizo ni kamaifuatavyo:-

(i) Muda uliokuwa ukitolewa wa siku 30 wa kusajilisimu, hivyo watu kupata mwanya wa kuzitumia simu hizovibaya katika kipindi hicho ambacho siku 30 ambazo tulizitoakama siku za msamaha.

(ii) Vile vile baadhi ya Mawakala wa kusajili simuwalisajili simu hizo bila vitambulisho au kwa majina halisi yawatumiaji.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

38

(iii) Vile vile kutokuwepo kwa vitambulisho vyataifa ambavyo vingeweza kuhakiki majina halisi ya mtumiajiilikuwa ni changamoto nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika kukabilianana matumizi mabaya ya simu, imefanya mambo yafuatayo:-

(i) Tumekamilisha Kanuni za Sheria yaMawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) zitakazodhibitimatumizi mabaya ya simu.

(ii) Vile vile tumeondoa siku 30 kipindi ambachomtu alikua akiweza kutumia simu bila kujisajili kipindi hichosasa hakitakuwepo.

(iii) Vile vile tumeamua kuzima simu zote ambazohazijasaliwa ifikapo tarehe 10 Julai, 2013.

(iv) Vile vile kama Serikali tumeendeleakukamilisha zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifakama njia muhimu ya kuhakiki watumiaji halisi wa simu hizi.

(v) Vile vile tutashirikiana na jeshi la polisi katikakuwasaka na kuwakamata wale wote wanaotumia simuvibaya.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Nakushukuru sanaMheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa nafasi ya kuuliza swalila nyongeza. Kwanza nishukuru kwa majibu ya Serikali. Lakinipamoja na majibu hayo Serikali imekiri kabisa kwamba tatizobado lipo. Bado matumizi mabaya ya simu yapo.Changamoto ambazo Serikali imezitaja ni pamoja naMawakala kutokutumia vitambulisho wakati wa kusajili hizisimu card. Vile vile kutokuwepo kwa vitambulisho vya kitaifa.Sasa ningependa kujua swali la kwanza:-

Serikali inatoa kauli gani kwa Mawakala ambaowanasajili simu card bila ya kutumia vitambulisho?

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

39

Swali la pili. Kwa kuwa vitambulisho vya kitaifa nimuhimu sana. Ningependa kujua sasa ni lini Serikali itatoavitambulisho hivi kwa Watanzania wote? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Sijui kama hili la mwisho ataliweza?Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa yale ambayo una ubavu nayo,majibu?

NAIBU WAZIRI WA SAYANSI, MAWASILIANO NATEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziriwa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swalimoja la nyongeza la Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, Mbungewa Busanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya kusajili watumiajiilikuwa ni kazi ya makampuni ya simu, uamuzi ulikuwa ni waSerikali, lakini tuliwapa shughuli hiyo wenzetu makampuni yasimu kwamba, kwa wale wanaoenda kupata sim card mpyana wale waliokuwa na sim card za zamani, basi wenzetuwataweka utaratibu wa kuwasajili.

Lakini bahati mbaya, kama nilivyosema awalikumejitokeza tatizo la kutokuwepo na uaminifu kwa walewaliopewa kazi ya kusajili kwamba, inawezekana kabisaukaenda pale kwenye meza ya kusajili ukasema umesahaukitambulisho, lakini mimi naitwa Juma Athumani na ukasajiliwahivyo. Tulichogundua ni kwamba, kumekuwa na majina fakekwamba, simu imesajiliwa kabisa lakini jina lililoandikwa nifake na watu wengi wanatumia simu hizo kufanya uhalifu,kueneza message za uchochezi pamoja na matusi nakadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ambacho tumefanyani kwanza, tumeimarisha Kanuni za Sheria hii ili kutoa adhabuzaidi inapobainika kwamba, hakukuwa na uamini fu katikausajili. Lakini pili, kama nilivyosema, ni hili suala la vitambulishovya taifa kwamba, itakapofika sasa kila mtu amepatakitambulisho cha Taifa tutafanya uhakiki upya wa zoezi hili, ilikila aliye na sim card basi, simu ile iwe imesajiliwa kwenyejina lake halisi.

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

40

Mheshimiwa Naibu Spika, jingine la kuongeza tu nikwamba, Mwanasheria Mkuu hapa atakubali kwamba,Sheria ni jambo moja, lakini Sheria zinafanya kazi katikautamaduni wa kwenye jamii. Tunafahamu kwamba, naulitokea mfano Mheshimiwa Naibu Spika na wewe ulikuwani victim kwamba, wapo wenzetu walienda kwenye jukwaawakatangaza namba za Viongozi ili watu wawatumiemessage. Na ile haikatazwi Kisheria, kinachokatazwa Kisheriani yule anayetuma message sasa kutumia vibaya ile simu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mategemeo yetuni kwamba, sisi pamoja na kwamba, haikatazwi Kisheria mtuku-share namba ya mtu mwingine, wenzetu wangekuwa naustaarabu wa kutofanya hivyo. Kwamba, pamoja nakwamba, huvunji Sheria, lakini kuna misingi ya ustaarabukwenye jamii. Kwa hiyo, baadhi ya vitu vina-reflect zaidiustaarabu wa watu kuliko uimara wa Sheria zetu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawashukurunisana kwa ushirikiano wenu katika kipindi hiki cha Maswali.Maswali yamekamilika, ninayo Matangazo machache,naomba masikio yenu, tuanze na Wageni.

Kwanza nimkaribishe sana Mheshimiwa MosesMachali, Mbunge mwenzetu, ambaye sasa amewezakuwasili humu Bungeni, tuko na yeye humu ndani baada yakupata matatizo yale aliyoyapata. Tunaishukuru sana Serikali,kwa ushirikiano ambao mmempa, mkubwa sana. Natunakupa pole Wabunge wote kwa yale yote yaliyokupata;tunaamini kabisa mguu wako utazidi kupata nafuu. Karibusana Mheshimiwa Machali. (Makofi)

Lakini pia niwakaribishe Bungeni Wabunge ambaohawakuwepo; nimkaribishe Mheshimiwa Joyce Mukya, nimuda mrefu sana hakuwepo. Karibu sana Bungeni. Tunatakakumwona mjomba wetu, karibu sana Joyce. (Makofi)

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

41

Wageni wengine walioko Bungeni, ni pamoja nawanafunzi waliokuja kujifunza kutoka shule ya Viganga –Kongwa. Pale mlipo, wale Walimu na wanafunzi wa Viganga– Kongwa? Karibuni sana, pale kwenye kona, karibuni sanasana Walimu wangu na wanangu. (Makofi)

Wanafunzi 50 na Walimu wao kutoka Shule ya Msingiya Sokoine Dodoma? Karibuni sana Wanafunzi na Walimuwa Sokoine Dodoma, karibuni sana. (Makofi)

Wanafunzi 60 na Walimu wao kutoka PCEA SaintColumbia Nursery and Primary Schools za Dar-es-Salaam.Karibuni sana, watoto wazuri jamani. Karibuni sana Walimuna Wanafunzi. (Makofi)

Wanafunzi na Walimu wao na Mwenyekiti wa Bodikutoka Shule ya Sekondari Kimagai – Mpwapwa, ambao niWageni wa Mheshimiwa Gregory Teu. Ahsanteni sanaWanafunzi wa kutoka Kimagai; kwa Kigogo inabidi iitwe“Chimagai,” karibuni sana. (Makofi)

Wageni 16 ambao ni Makatibu wa kutoka Jimbo laTabora Kaskazini, wageni wa Mheshimiwa Shaffin Abdallah.Karibuni sana Wanyamwezi wote kutoka Tabora Kaskazini.Muwe makini tu, Dodoma magari ni mengi kuliko Taborahasa, mnapokatiza barabara. (Makofi)

Wageni 28 ambao ni Madiwani kutoka Baraza laMadiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo – Iringa, ambaoni wageni wa Mheshimiwa Profesa Peter Msolla. Ahsantenisana Waheshimiwa Madiwani na kwa hatua hii niwapongezesana Mabaraza ya Madiwani ambayo yametutembeleahapa Bungeni katika kipindi chote cha Bajeti na nitoe witokwa Waheshimiwa Madiwani wengine wa Halmashaurinyingine, wanapopata nafasi kutembelea Bunge na kujifunzana kuona namna ambavyo Bunge linafanya kazi kwasababu, kazi zao kwa sehemu kubwa zinaendana na namnaBunge linafanya kazi. (Makofi)

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

42

Kwa hiyo, kwa Madiwani walio wengi nchi nzimaBunge, ni mahali pa kujifunza mambo mengi yanayohusu kazizao. Tunawakaribisha sana. (Makofi)

Kuna wageni wa Mheshimiwa Naibu WaziriMakongoro Mahanga wageni 112 kutoka Sherehe ArtsAssociation, pale Mlipo? Karibuni sana, wengi wa hawaWaheshimiwa Wabunge, ni “Washehereshaji,” Ma-MC nawatu wa namna hiyo. Karibu sana na miongoni mwao wakowageni wa Mheshimiwa Sitta, Bwana Joshua Malembeka,Nesta na Doris, tunawakaribisha sana, karibuni sana. (Makofi)

Matangazo ya Kazi; Mwenyekiti wa Kamati ya Bungeya Kilimo, Mifugo na Maji, Mheshimiwa Prof. Peter Msolla,Profesa Msolla, anawaomba Wajumbe wa Kamati hiyo,tutakapomaliza shughuli zetu asubuhi hii basi wakutaneUkumbi Namba 227. Muda si mrefu tutamaliza shughuli zetu,tutakapomaliza Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji mkutaneUkumbi 227, Jengo la Utawala.

Mheshimiwa Jenista Mhagama, Mwenyekiti waKamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, anawaombaWajumbe wa Kamati yake ya Maendeleo ya Jamii, mkutanetutakapomaliza mambo yetu hapa, Msekwa C.

Mheshimiwa Victor Mwambalaswa, Mwenyekiti waKamati ya Bunge ya Nishati na Madini, anawaombaWajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini Mkutanetutakapomaliza mambo yetu haya katika Ukumbi waMsekwa, kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Pindi Chana, Mwenyekiti wa Kamati yaBunge ya Katiba, Sheria na Utawala, anawaomba Wajumbewa Kamati hiyo, mara baada ya shughuli zinazoendelea hivisasa zikimalizika, basi wakutane Ukumbi wa Basement. Kamatiya Mheshimiwa Pindi Chana, ya Katiba, Sheria na Utawalatutakapomaliza tu basi wakutane Basement.

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

43

Mwisho kuna wale wazee wetu 30 kutoka Butiama,sijui wamekaa upande gani? Karibuni sana, karibuni sana;mtupelekee salaam zetu kwa Mama Maria huko Butiama.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nawaomba mwendelee nauvumilivu kidogo. Kuna Kauli fupi mbili (2) zinafuata naombatuzisikilize, baada ya mambo hayo tutakuwa tumefika mahalipazuri, nitawapa maelekezo fulani, lakini tutamaliza mapemasana, nawaahidi leo. (Makofi)

Katibu tuendelee?

KAULI ZA MAWAZIRI

Ajali Zinazotokana na Matumizi ya Pikipiki

NAIBU SPIKA: Kauli za Mawaziri. Mheshimiwa Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilishaTaarifa kuhusu ajali za barabarani zinazotokana na matumiziya pikipiki nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, matatizo ya ajira kwa vijana,usafiri na usafirishaji nchini ulifanya Serikali, ikubali kuidhinishapikipiki za matairi 2 na matairi 3, maarufu kama Bajaji,kutumika katika biashara ya usafiri na usafirishaji wa abirianchini. Uamuzi huu ulifanywa ili kuongeza wigo wa ajira kwavijana, ili kuwapa uwezo wa kupata kipato kwa kazi halali.

Mheshimiwa Naibu Spika, sote ni mashahidi wanamna uamuzi huu ulivyosaidia kwa kiasi kikubwa kuwapatiavijana wengi nchini shughuli ya kuwapatia kipato halali nakuwaepusha na uwezekano wa kushawishika kujiingiza katikashughuli haramu, ikiwemo uhalifu.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

44

Pamoja na kutoa ajira kwa vijana, uamuzi huu waSerikali, pia umesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo lausafiri katika maeneo mengi nchini, hasa katika maeneoambayo usafiri wa magari wa uhakika haupo.

Maeneo mengi ambayo magari ya abiria hayawezikufika sasa, yanafikika kirahisi kwa pikiki. Wananchi wa kipatocha chini wanaweza kutoka eneo moja kwenda jingine kwagharama nafuu, tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya uamuzihuo wa Serikali.

Aidha, katika miji mingi yenye msongamano mkubwawa magari barabarani, hususan Jiji la Dar-es-Salaam, pikipikizinasaidia sana wananchi kuepuka msongamano na kuwahikatika shughuli zao za kujipatia kipato na kurejea majumbanikwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo mambomengi mema siku zote hayakosi changamoto, matumizi yapikipiki katika usafirishaji wa abiria yanakabiliwa nachangamoto mbalimbali, ambapo kubwa kuliko zote ni ajalinyingi za barabarani zinazohusisha pikipiki.

Matumizi ya pikipiki nchini yamesababisha ongezekokubwa sana la ajaili za barabarani ambazo zimegharimumaisha ya watanzania wenzetu wengi sana. Pamoja naupotevu wa maisha, ajali hizi zimesababisha ulemavu wakudumu kwa watu wengi na kupoteza viungo vyao nakuwafanya wawe tegemezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa takwimu zaJeshi la Polisi Nchini, katika kipindi cha kuanzia Januari 2012hadi kufikia mwezi Mei, 2013 idadi ya pikipiki zilizosajiliwa nchinzima ilikuwa 10,036. Mikoa inayoongoza kwa wingi wa pikipikikwa mujibu wa takwimu hizi ni Jiji la Dar-es-Salaam lenye jumlaya pikipiki 2,024; katika idadi hiyo ya pikipiki Kinondoni inajumla ya pikipiki 1,735 Temeke 1,363 Ilala 1,334. Mikoainayofuatia kwa idadi kubwa ya pikipiki ni Morogoro, Arushana Kilimanjaro.

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

45

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha Janurihadi Disemba 2012 kulitokea jumla ya ajali 5,763 ambazozimegharimu maisha ya Watanzania 930, naomba kurudia;katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2013, Januari hadiDisemba 2013 kulitokea jumla ya ajali 5,763 ambazozimegharimu maisha ya Watanzania 930 na kuwajeruhiwengine 5,532. Mkoa wa Dar-es-Salaam, uliongoza kwa kuwana ajali 2,479 ambapo Wilaya ya Kinondoni ilikuwa na ajli1,007 Temeke 769, Ilala 703.

Ajali hizi zimesababisha vifo 164 na majeruhi 2,765 idadihii ni kubwa sana. Mikoa inayofuatia kwa ajali ni Arusha,iliyokuwa na ajali 569 zilizosababisha vifo 65 na majeruhi 420.Mkoa wa Morogoro ulikuwa na ajali 431 zilizosababisha vifo54 na majeruhi 328 na Kilimanjaro ilikuwa na ajali 294zilizosababisha vifo 52 na majeru 266.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha Januarihadi Mei, 2013, takwimu zinaonesha kuwa kumetokea ajaliza pikipiki 2,415 nchi nzima. Ajali hizo zimesababisha watu352 kupoteza maisha yao na wengine 2,368 kujeruhiwa.

Mkoa wa Dar-es-Salaam umeongeza kwa matukio yaajali 2,161 zilizosababisha vifo 56 na majeruhi 1,211 kwamchanganuo ufuatao; Wilaya ya Kinondoni ajali 515, vifo 22,majeruhi 549. Temeke ajali 269, vifo 19 na majeruhi 354 naIlala ajali 357, vifo 15, majeruhi 307. Takwimu za Mikoa mingineinayoongoza kwa ajali ni Mkoa wa Morogoro uliokuwa naajali 186 zilizosababisha vifo 15 na majeruhi 117. Arusha ajali118, vifo 16 na majeruhi 102; Kilimanjaro ajali 130, vifo 36,majeruhi 120. Mkoa wa Pwani, ajali 114 zilizosababisha vifo23 na majeruhi 167.

Mheshimiwa Naibu Spika, matukio ya ajali za pikipikini mengi na kwa mujibu wa takwimu nilizozitaja hapo juu,idadi ya vifo na majeruhi ni kubwa kwa kiasi cha kusababishaHospitali nyingi nchini kuanzisha Wodi maalum za majeruhiwa pikipiki.

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

46

Tusipochukua hatua za makusudi, Taifa letulitaendelea kuathirika na ajali hizo ambazo zinachukuamaisha ya watu wetu na kuongeza idadi ya yatima,walemavu na watu wasiojiweza na kuwafanya wawetegemezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vyanzo vikuu vya ajali zabarabarani zinazohusisha pikipiki ni pamoja na kutokujuaSheria, Kanuni na Taratibu za matumizi ya barabara, ambapomadereva wengi wa pikipiki hawana leseni za udereva.Uendeshaji wa hatari wa pikipiki barabarani kwa mwendokasi na kupita magari mengine bila sababu, kupita katikataa za kuongozea magari (Traffic Lights) bila kuruhusiwa,kudharau Askari wa Usalama Barabarani wanaoongozamagari katika makutano ya barabara, kupakiza abiria watatuau zaidi katika pikipiki moja, maarufu kama mshikaki, namatumizi ya ulevi kwa waendeshaji wa pikipiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu nyingine nimiundombinu ya barabara ambapo baadhi ya barabarazinakosa alama au zinakuwa na alama zilizofifia ambazo siorahisi kuonekana. Barabara kutumika na makundi yote yawatumiaji (Traffic Mix), ambapo magari, baiskeli, pikipiki,mikokoteni na watembea kwa miguu pamoja na ubovu wabarabara, wote hutumia njia moja. Madereva wa magarikutoheshimu wapanda pikipiki ni sababu nyingineinayosababisha ajali za pikipiki nchini.

Madereva wa magari mara nyingi wamekuwahawatoi ushirikiano mzuri kwa madareva wa pikipiki,wanapokuwa barabarani. Tabia hii ya madereva wa magariinatokana na mtazamo hasi kuhusu waendesha pikipiki,ambapo watu wengi wanaamini kuwa waendesha pikipikihawana nidhamu ya barabarani.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati mbalimbaliinafanywa na Jesho la Polisi katika kukabiliana na wimbikubwa la ajali za pikipiki, ili kunusuru hali hii. Mikakati hiyo nipamoja na usimamizi na udhibiti wa watoaji na watumiajiwa usafiri huo; usimamizi huu unafanywa kwa kutumia Kanuni

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

47

za SUMATRA za mwaka 2010 zinzohusu usafirishaji wa abiriakwa kutumia pikipiki. Waendesha pikipiki kutoa taarifa zauhalifu na makosa ya wanapoona wenzao wanakiukataratibu.

Kuandaa operations mbalimbali kwa lengo lakuhakikisha kuwa waendeshaji wa pikipiki wanafuata Sheriakatika uendeshaji, ni pamoja na kuwa leseni halali, upakiajisalama wa abiria, matumizi ya kofia ngumu (Helmet) nauendeshaji wa kujihami.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati mingine ni pamojana kutoa utoaji wa elimu kwa kutumia vyombo vya habarikama Redio, Television na Magazeti. Kuandaa vipeperushivya elimu kwa waendesha pikipiki, kutoa mafunzo katika vituombalimbali vya waendesha pikipiki.

Mafunzo haya yanafanywa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Wadau mbalimbali kama asasi zisizo zaKiserikali na Vyuo vya Udereva Nchini, hususan VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, njia nyingine ya utoaji waelimu ni kushirikisha waendesha pikipiki katika michezo. Katikamaeneo mbalimbali nchini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana nawadau na wadhamini wa michezo huandaa michezombalimbali inayowahusisha waendesha pikipiki na makundimbalimbali ya watumiaji wa barabara. Wakuu wa Polisi waUsalama Barabarani wa Mikoa, huandaa michezo hii nakutumia fursa hiyo, kutoa elimu ya usalama barabarani kwawaendesha pikipiki. Mfano wa michezo hiyo ni kombe laMpinga (Mpinga Cup) lililofanyika katika Mkoa wa Kipolisi waKinondoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeanza kukuelezeauamuzi wa Serikali, kuhusu pikipiki kutumika katika usafirishajiwa abiria, faida zinazopatikana na changamoto kubwazilizojitokeza kutokana na matumizi ya pikipiki katikausafirishaji. Idadi ya pikipiki nchini ni kubwa na inazidikuongezeka kila siku.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

48

Idadi ya ajali, vifo na majeruhi, nayo inazidikuongezeka siku hadi siku kadiri pikipiki zinazvyoongezeka.Ukitazama takwimu nilizotoa awali utagundua kuwa upouhusiano mkubwa kati ya idadi ya pikipiki na ajali zinazotokea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa takwimu hizi ni wazitunalo tatizo kubwa sana katika sekta ya usafirishaji wa abiriakwa kutumia pikipiki. Naomba nitumie fursa hii kwa kutumiaBunge lako Tukufu, kuwaomba Waheshimiwa Wabunge,wasaidie katika kuwahamasisha vijana, hasa madereva waboda-boda kuhakikisha kuwa wanapata mafunzo yaudereva, kujifunza Sheria za usalama barabarani nakuziheshimu.

Kuepuka kuzidisha abiria, kuepuka kuvuka taa zakuongozea magari iwapo taa hazijawaruhusu kufanya hivyo,kuzingatia maelekezo ya Askari wa Usalama Barabaraniwanaoongoza magari katika makutano ya barabara.Kutumia kofia ngumu zilizo na viwango kwa usalama wao naabiria wanaowasafirisha, badala ya kuvaa tu ili mradiwasibughudhiwe na Polisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa wito kwa wananchiwote wanaotumia usafiri wa pikipiki, kutokubali kupandapikipiki bila kuvaa kofia ngumu (Helmet). Kuwasisitiza marakwa mara madereva waliowabeba kuendesha pikipiki kwamwendo wa wastani. Kuwa makini na kufuata kikamilifuSheria za Usalama Barabarani kwa usalama wao. Aidha,ninawaagiza Polisi wa Usalama Barabarani kuwadhibiti kwamujibu wa Sheria na Kanuni zilizopo waendesha-pikipikiwakorofi wasiopenda kufuata Sheria za Usalama Barabaranibila kushurutishwa.

Kujiepusha na upendeleo, kujiepusha na rushwakatika kutekeleza wajibu wao na kusimamia kikamilifu mkakatiwa Polisi Jamii katika eneo hili, ili kupunguza changamotozinazoikabili sekta hii ya usafiri na usafirishaji wa abiria kwakutumia pikipiki.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

49

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la kupambana nachangamoto hizi ni letu sote ni vema wadau wotewashirikiane kwa pamoja kwa manufaa ya wananchi badalaya wengine kukaa pembeni na kutoa lawama kwa Serikali.

Iwapo tunakubaliana kuwa jambo hili lina maslahikwetu na kwa wananchi wetu basi ni vema tuweke nguvuzetu pamoja ili kukabiliana na changamoto hizi.

Napenda kutahadharisha kuwa jeshi la polisi litakuwamakini na madhubuti katika kusimamia Sheria hivyo ni vyemakila muhusika afuate Sheria.

Kwa kufuata Sheria tutajiepusha na bugudha zisizona maana, tutaepuka migogoro na polisi, tutapata fursa yakushiriki kikamilifu katika kukuza kipato chetu na kuepukautegemezi kiuchumi lakini muhimu zaidi tutaokoa maisha yawasafirishaji na abiria wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasihi waendesha pikipikiambao wengi ni vijana kutambua kuwa maisha yao nimuhimu sana kwa Taifa letu. Nawaomba viongozi wa ngazizote kuanzia Mitaa, Kata, Wilaya mpaka Taifa kuchukuahatua kupunguza vifo na walemavu wanaotokana na ajaliza pikipiki katika maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwakunipa fursa hii naomba kuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana nakushukuru sanaMheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Kauli yapili Mheshimiwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya nchi.

Waheshimiwa Wabunge tuendelee kuvumilia kidogokwa muda mfupi sana ujao.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

50

Mauaji Yanayofanywa na Askari Polisi

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) yaKanuni za kudumu za Bunge toleo la Aprili, 2013 naombakuwasilisha ufanunuzi kuhusu kauli niliyoitoa nikijibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah lililotokana naswali la msingi namba 290 tarehe 28 Mei, 2013 kwa kusemakuwa mauaji ambayo yanafanywa na askari polisi ni mauajiya kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 28 Mei, 2013 wakatiwa kipindi cha maswali na majibu wakati nilipokuwa nikijibuswali la nyongeza la Mheshimiwa Rashid Ali Abdallahlililotokana na swali la msingi Namba 290 la MheshimiwaKhalifa Suleiman Khalifa, Mbunge wa Gando, kuhusu raiakuuwawa mikononi mwa Polisi, nilitumia maneno yafuatayo:-

“ Mauaji ambayo yanafanywa na askari ni mauaji yaKisheria”.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa wa Kanuniya 46 fasili ya kwanza ya kanuni za kudumu za Bunge toleo laAprili, 2013 napenda kutoa ufafanuzi wa Kauli hiyo kufuatiamuongozo wa Spika ulioombwa na Mheshimiwa HamadRashid Mohamed, Mbunge wa Wawi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 18 (a) chaSheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwamapitio mwaka 2002 kinampa haki mtu yoyote akiwemoaskari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yakeau mali ya mtu mwingine ikiwemo mali ya Serikali na taasisizake ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza jukumuhilo kifungu cha 18 (b) na (c) cha Sheria hiyo kinatoa uwezokisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi chakusababisha madhara au kifo katika mazingirayanayoainishwa kisheria ambayo ni pamoja na hayayafuatayo:-

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

51

(a) Kuokoa uhai wake au uhai wa mtu mwingine;

(b) Kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokeekwake au kwa mtu mwingine;

(c) Kumzuia mtu anayetenda tendo ovu lakubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume namaumbile; na

(d) Kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku auunyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba motoau kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtuau mali.

Mheshimiwa Naibu Spika, chini ya Sheria hiyo yaKanuni ya Adhabu kifungu cha 77 na 78 kinabainisha kwambaaskari Polisi, Hakimu au Afisa yoyote wa jeshi ambayeamekasimiwa mamlaka ya kuzuia au kutawanyamaandamano yasiyo halali anaweza kutumia nguvukutekeleza jukumu hilo na hata wajibishwa kisheria kwa kosala jinai au madai kwa madhara yoyote yatakayotokea katikakutekeleza kihalali jukumu hilo.

Mheshimiwa Spika, aidha kifungu cha 21 cha Sheriaya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura Namba 20 kamailivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 kinampa mamlaka nakuweka mipaka ya matumizi ya nguvu katika kufanikishaukamataji salama pasipo kusababisha madhara makubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutafsiri Sheria, kanunina taratibu mbalimbali nilizozitaja hapo juu Mahakama katikanyakati tofauti imetoa msimamo wa Kisheria juu ya suala hili.Mathalani kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuriya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa kutoka Tanzania LawReport ukurasa 122 ambapo Mshtakiwa alimjeruhi kwa

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

52

panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake nakuanza kumshambulia mahakama ya Rufaa pamoja nakuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatianikwa kutumia nguvu kupita kiasi ilibainisha kuwa mshtakiwahakustahili adhabu kubwa kwani alitenda kosa lile wakatiakijihami (self defence) dhidi ya mashambulizi kutoka kwamlalamikaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikumbwe pia kuwa kifungucha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi sura ya322 pamoja na kanuni za kudumu za utendaji wa jeshi la polisiPolice General Orders Namba 274 vinampa haki ya kisheriaaskari polisi kubeba na kutumia silaha za moto zikiwemobunduki na mabomu anapokuwa katika utekelezaji wamajukumu yake ya kila siku. Sheria na Kanuni hizo zimewekamasharti na utaratibu wa matumizi ya silaha hizo ambapokila askari anayekabidhiwa silaha hizo anawajibika kwamatumizi yasiyo sahihi ya silaha alizokabidhiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa msingi huo tarehe28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali 290 nilitumia maneno mauajiyanayofanywa kisheria nikimaanisha mauji yanayotokeakatika mazingira niliyoyaeleza hapo juu. Si nia ya Serikalikuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyovinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu kama ambavyoilitafsiriwa na Mheshimiwa Mbunge. Serikali itaendeleakuhakikisha kuwa kila mmoja atatimiza wajibu wake kwamujibu wa Sheria na yoyote atakayekiuka ajue Sheria nimsumeno.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuwahakikishiaWaheshimiwa Wabunge kuwa jeshi la Polisi litaendeleakutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria zilizotungwana Bunge lako Tukufu pamoja na kanuni na taratibu zilizopokwa weledi wa kutosha. Aidha kwa kuzingatia maelezo hayojeshi la polisi limekuwa na litaendelea kuwachukulia hatuaza kisheria na za kunidhamu askari wake wote watakaokiukamatumizi sahihi ya silaha wanazokabidhiwa.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

53

Mheshimiwa Naibu Spika, jeshi la polisi litaendeleakuheshimu haki za raia na kujitahidi kutumia busara katikakutatua migogoro. Hata hivyo natoa tahadhari kuwa paleinapotokea kuwa migogoro inaelekea kuhatarisha usalamawa raia, amani na utulivu wa nchi. Jeshi la polisi halitakuwana kigugumizi hata kidogo kutumia nguvu kurejesha usalama,utulivu na amani na hatimaye kuwafikisha wahusikamahakamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Global Peace Index nikipimo kinachotumiwa ulimwenguni kiasi cha amani katikataifa. Katika mwaka wake wa saba sasa inapima nakuyapanga mataifa 162 kwa kuangalia viashiria chanya nahasi vya amani hususani uwepo wa vurugu au hofu ya vurugukatika nchi hizi. Kila nchi inapimwa kupewa alama kwakutumia viashiria 22 vya amani ya ndani nchi ikiwemo kiasicha uhalifu, idadi ya polisi kwa watu laki moja na kiasi chaOrganized Crimes.

Mheshimiwa Naibu Spika, Global Peace Indexilianzishwa na Institute for Economics and Peace kwawaandalizi wa jukwaa la kujitegemea la wataalam kwakutumia takwimu zilizokusanywa na kutolewa na taasisi yaEconomic Intelligence Unit.

Taarifa na takwimu zinazotumika zinapatikana katikavyanzo vinavyoheshimika na kuaminika duniani kamaInternational Institute of Strategic Studies, banki ya dunia,Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na taasisi zake,taasisi za amani na Economic Intelligence Unit.

Mhesheshimiwa Naibu Spika, kipimo hiki kinafanyikakwa kuangalia viashiria mbalimbali ikiwemo vigezo vyauwepo wa amani kama demokrasia, uwazi, elimu na ustawiwa taifa. Global Peace Index imekusudia kuchangia kwa kiasikikubwa katika majadiliano kuhusu amani duniani nainaaminiwa na kutumiwa na mashirika mengi ya kimataifa,Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ikiwemo Benki ya Duniana umoja wa mataifa. (Makofi)

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

54

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa yahali ya amani duniani iliyotolewa na Global Peace Indexmwaka huu amani duniani imepungua kwa asilimia tanokatika kipindi cha miaka sita tangu 2008. Uhasama baina yanchi umeendelea kupungua na kumekuwa na ongezekokubwa la migogoro ya ndani ya nchi.

Nchi kumi zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka uliopitani Iceland, Denmark, New Zealeand, Austria, Switzerland,Japan, Finland, Canada, Sweden na Ubelgiji. Wakati nchizil izofanywa vibaya zaidi kwa ukosefu wa amanizimeongozwa na Afghastan iliyoshika namba 162 ikifuatiwana Somalia, Syria, Iraq, Sudan, Pakistan, DRC, Urusi, Korea yaKaskazini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu imeendeleakushika nafasi ya 55 kama ilivyokuwa mwaka 2012 kwakupata alama 1.89 takwimu hizi zinaonyesha kwambaTanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi za AfrikaMashariki na nchi inayotukaribia ni Uganda ambayo iponafasi ya 106. Watanzania tunao wajibu wa kulinda nafasiyetu katika jukwaa la Kimataifa kwa manufaa ya Taifa letukiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ripoti hii nchi yetuimeendelea kuwekwa juu katika jukwaa la kimataifa kwasuala la amani. Bado nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa chaamani pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na watuwasioitakia mema nchi hii kwa kusababisha vurugu kwasababu mbalimbali zisizo na mashiko.

Watu hawa na mkakati wao wa kuichafua nchi yetukimataifa hautafanikiwa kwa kuwa Serikali ipo makini naitaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarishausalama nchini na kuwalazimisha wote wasiopenda kufuataSheria na kuzitii kwa lazima demokrasia isiyo na mipaka nivurugu, uhuru pia usio na mipaka ni vurugu pia. Utamaduniwa kutoheshimu Sheria na taratibu unaendelea kujengekanchini kwa kisingizio cha Demokrasia na kudai haki.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

55

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nitumie fursahii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwaujumla kuheshimu na kufuata Sheria za nchi bila shuruti.Kuepuka kuweka mashindano ya kutotii Sheria na kulifanyajeshi la polisi ndiyo liwalazimishe kutii. Sote tukifuata sheria zanchi matukio ya vurugu na migogoro yatapungua sana nchinimwetu, hili linawezekana tukitimiza wajibu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi nakushukuru sana. Mwongozonilimwona Mheshimiwa Rajab. Miongozo miwili eeh, haya!Mwongozo pia, mitatu hiyo.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru, kwa kutumia Kanuni zetu za BungeIbara ya 68 (7). Wakati wa kipindi cha maswali na majibuhapa Bungeni leo wakati linajibiwa Swali Namba 458lililoulizwa na Mheshimiwa Felister A. Bura, katika swali lake lanyongeza Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Mheshimiwa Lukuvikatika majibu yake alisema kwamba Dodoma inapata fedhanyingi kuliko Halmashauri zozote hapa nchini na fedhazenyewe siyo zile fedha za madafu ni fedha za World Bank.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uelewa wa wengiunaposema fedha za madafu maana yake ni fedha ambazohazina thamani. Sasa kwa kuwa kauli hii na lugha hii imetokakwa Waziri mzito, Waziri mwenye dhamana kubwa ina maanani kauli ya Serikali. Tunaomba mwongozo wako fedha hizi zamadafu nchini kwetu kulinganisha na Fedha za World Bankni fedha za aina gani?

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMSI: MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru nasimama mbele ya Bunge lakoTukufu kwa kanuni namba 68 (7) nakurejea na kanuni namba63 (1) ambayo napenda ninukuu kanuni namba 63 (1)inasema:-

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

56

“Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katibayanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadilianokatika Bunge ni marufuku kabisa kusema uongo Bungeni nakwa sababu hiyo Mbunge yoyote anapokuwa akisemaBungeni anawajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa Kauli aumaelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyeweanaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au lakubahatisha tu”.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa iliyotolewa naMheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi sitaki kusemakama Mheshimiwa Waziri kasema uongo siwezi mimi kusemamaneno haya kutokana na malezi niliyolelewa lakinininachotaka kusema kwamba maelezo aliyoyatoa hayanaukweli na ni ya kubahatisha.

NAIBU SPIKA: Ziko mbili

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMSI: Ya Waziri waMambo ya Ndani.

NAIBU SPIKA: Kuhusu ajali za pikipiki?

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMSI: Sawa sawa naam.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika takwimualizozionyesha katika kauli yake ukurasa wa pili anasemakwamba Mikoa inayoongoza kwa uwingi wa pikipiki kwamujibu wa takwimu hizi ni jiji la Dar es Salaam yenye jumla yapikipiki 2400. Akaendelea kusema kwamba katika idadi hiyoWilaya ya Kinondoni ina jumla ya pikipiki 1735, Temeke inapikipiki 1363 na Ilala ina pikipiki 1334.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukizijumlisha hizi unapata4,432. Kwa hiyo, hoja yangu ni hapo nataka kupataMwongozo wako juu ya ukweli wa takwimu hizi.

NAIBU SPIKA: Nakushukuru kwa umakini wako.

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

57

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru na mimi nataka kutumia kanuni ya 68 (8)utaniwia radhi kidogo kwa sababu la kwangu nilitaka kutoataarifa lakini nisingeweza kumsimamisha Mheshimiwa NaibuWaziri wakati anajibu swali kwa hiyo nilisubiri mpaka nipatewakati muafaka.

Mheshimiwa Naibu Waziri Majaliwa Kassim Majaliwaalipokuwa anajibu Swali 459 lakini kufuatia swali la nyongezala Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa alirudia kauli yakwamba Mbeya ni Manispaa karibu mara tatu, mara nnehivi, sasa hii inaweza ikawaaminisha Watanzania kwambaMbeya ni Manispaa lakini wana Mbeya wenyewe watakuwawanashangaa hivi tulishakuwa jiji miaka mingi iliyopita leotumerudishwa kuwa manispaa. Kwa hiyo, nil itakaMheshimiwa Naibu Waziri nimpe taarifa na Watanzaniawengine wanaosikia kwamba Mbeya siyo Manispaa ni Jijitena la siku nyingi sana. Hilo ndilo la kwangu.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana tunashukuru kwa hilo lamwisho umelimaliza wewe mwenyewe Mbeya ni Jiji kwa hiyohalihitaji maelezo mengine yoyote ya ziada. Tuanze na la pilikutoka mwisho Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, kama una la kusema kwa kifupi sana atafuataMheshimiwa William Lukuvi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza nikiri nilishtuka sana MheshimiwaMbunge aliposema taarifa imejaa uwongo wa hali ya juuwakati ni wazi mtu yoyote makini anatambua kwa kweli hilini kosa tu la uchapaji. Kwa hiyo kwanza kwa niaba ya Wizarayangu naomba radhi kwa kosa hili la uchapaji hii idadi yapikipiki ni kama alivyonisaidia kuzijumlisha jumla yake ni 4,432.

Kwa hiyo, tutawaomba tu Waheshimiwa Wabungewakati mwingine makosa ya namna hii jamani msitupige kwalugha kali sana mnatushtua halafu tunadhani ni jambo kubwakweli. Ahsante sana. (Makofi)

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

58

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBUNA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu hojaya Mheshimiwa Rajab, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nilipokuwa najibu swali laMheshimiwa Bura yeye alisema kwamba CDA pamoja naumuhimu wake imetengewa shilingi milioni 500 tu kwa ajili yamaendeleo. Mimi nikasema hapana siyo Shilingi milioni miatano (500) tu imetengewa zaidi ya shilingi bilioni 32 hii ni tafsiriya fedha za kigeni yaani imetengewa dola zenye thamaniya shilingi bilioni 32 na nikasema zaidi kwamba hizi fedhazimetokana na mkopo ambao Serikali imeingia kwa ajili yakujenga miundombinu ya Dodoma.

Sasa kwa vyovyote vile kukopa World Bank ni foreignmoney ndiyo tafsiri yangu. Lakini niliposema shilingi 500 kwatafsiri yake alisema shilingi milioni 500 ni lugha ya kawaidasijui kama mimi ni mtu wa kwanza kusikia pesa za madafu(Tshs).

Mheshimiwa Naibu Spika, tafsiri yangu ya lugha yamadafu nilikuwa narahisisha kumuambia kwamba hizi shilingimilioni 500 ni fedha za ndani, shilingi za Tanzania kamaalivyosema yeye siyo hela ya madafu.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Hata Nyerere alitumia.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (SERA,URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Naibu Spika, hela yamadafu ni lugha ambayo si rasmi sana lakini ni hela ya ndanihuwa tunatumia lugha hiyo sana.

Kwa hiyo haina tafsiri tofauti na shilingi za Tanzaniakwa hiyo nilichotaka kumthibitishia Mheshimiwa Bura nikwamba milioni 500 zilizotengwa maendeleo ni fedha zandani zinazotokana na kodi ya Watanzania lakini zile shilingibilioni 32 ni thamani ya fedha za kigeni ambazo zimeletwaDodoma kwa ajili ya kujenga miundombinu. Kwa hiyo 32bilioni ni fedha za kigeni tafsiri yake lakini 500 ni shilingi zaTanzania.

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

59

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri.Mambo haya ni sawa sawa tu na Mheshimiwa Chombohalipokuwa anafafanua hapa na kutofautisha tofauti ya rahana starehe Kiswahili kigumu kidogo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge niwashukuru sana bahatimbaya nilishasimama Mheshimiwa Kesy, bahati mbaya sana.Ungeniwahi ningekupa nafasi, tunakaribia mwisho wamkutano wetu wa 11 ambao ulikuwa ni Bunge la Bajeti.Bado shughuli kubwa mbili tu, ambayo ni Muswada waFinance Bil l na Muswada wa Appropriation. Hiyoitashughulikiwa kadiri ambavyo mipango itakavyopangwa.Ndiyo maana mnaona kamati ya Bajeti wameshaondokahapa wakifika mahali pazuri tunaweza tukashughulikia keshoau kesho kutwa kutegemeana na mrejesho tutakaopatakutoka kwa Kamati ya Bajeti, baada ya kuweka mamboyote sawasawa.

Naomba katika kumalizia shughuli hizi mbiliWaheshimiwa Wabunge tuendelee kupeana ushirikianoambao tumepeana tangu mwanzo ili kazi yetu iwezekukamilika. Kwa vile mkutano huu umekuwa ni mrefu sanana mimi baada ya hapa sitarudi tena kwenye kiti hiki,nichukue nafasi hii kuwashukuru sana WaheshimiwaWabunge wote kwa ushirikiano mkubwa sana ambaommetupatia uongozi wa Bunge katika kipindi chote chaBunge hili la Bajeti, naomba niseme asanteni sana.

Tulipoanza tulikuwa kama tunapanda mlima lakinitumefika mahali mwisho vizuri tumeelewana, tumewafanyiaWatanzania kazi njema sana. Kwa hiyo, nasema ahsantenisana. (Makofi)

Lakini vile vile niseme ahsante sana kwa Wananchiwa Kongwa kwangu binafsi kwa kuniamini, kuendeleakuniamini na niwahakikishie kwamba baada tu ya Bunge hilinitarudi huko, nitapita kila mahali kuwachambulia jinsi Bajeti

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462351463-HS...Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA

25 JUNI, 2013

60

hii ilivyo na maana kwao namna gani inatafsiriwa kwa maanaya maji, umeme, barabara, mishahara ya wafanyakazi namambo yote safi kule Kongwa.

Kwa hiyo hilo wakae mkao wa kunisubiri niendenikawachambulie na naomba Wabunge na nyinyi muendekwenye majimbo yenu mkawaeleze Bajeti hii ina maana ganikwa wananchi msiendekeze huu upotoshwaji unaoendeleakatika nchi wakati mambo mnayapanga nyinyi wenyewehalafu tena mnanyamazia. (Makofi)

Kwa hiyo, ni kazi ya kila Mbunge tukishatoka hapakwenda kueleza kwa wananchi wake namna ganiamefanikiwa kuwapenyezea maendeleo wananchi wake.Kama hakufanikiwa shauri yake. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge baada ya maneno hayonimshukuru sana Mheshimiwa Spika, kiongozi wangu AnneSemamba Makinda, kwa uongozi wake imara na mahiri.Tunaendelea kumwombea. Kwa kweli amefanya kazi kubwana ni matumaini yetu sote tunakubali kwamba kaziiliyofanyika ni kubwa sana na nzuri. (Makofi)

Baada ya maneno hayo kwa vile Order Paper ya leoimekamilika niwaombe Wajumbe ambao Kamati zenumnaenda kukaa vikao hivi sasa, basi mkitoka hapa mwendemoja kwa moja kwenye vikao vyenu. Kwa jinsi hiyo, basinaomba niahirishe shughuli za Bunge mpaka kesho saa tatukamili asubuhi. (Makofi)

(Saa 5.00 Asubuhi Bunge liliahirishwa Mpaka Siku ya Jumatano, tarehe 26 Juni, 2013)