86
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Tisa – Tarehe 14 Septemba, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu NDG. STEPHEN KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na maswali yetu Ofisi ya Waziri Mkuu. Mheshimiwa Zubeda Hassan Sakuru, Mbunge wa Viti maalum sasa aulize swali lake. Kwa niaba yake Mheshimiwa Sophia Mwakagenda. Na.109 Serikali Kufuta Sherehe za Mwenge MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA (K.n.y. MHE. ZUBEDA H. SAKURU) aliuliza:- Sherehe za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kutumia fedha nyingi za walipa kodi huku Watanzania wengi wakiwa na maisha duni. Je, Serikali haioni umuhimu wa kurudisha Mwenge wa Uhuru katika Makumbusho ya Taifa na kuzifuta sherehe hizo?

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE

___________

MKUTANO WA KUMI NA MBILI

Kikao cha Tisa – Tarehe 14 Septemba, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu

NDG. STEPHEN KAGAIGAI-KATIBU WA BUNGE:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza namaswali yetu Ofisi ya Waziri Mkuu. Mheshimiwa Zubeda HassanSakuru, Mbunge wa Viti maalum sasa aulize swali lake. Kwaniaba yake Mheshimiwa Sophia Mwakagenda.

Na.109

Serikali Kufuta Sherehe za Mwenge

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA (K.n.y. MHE. ZUBEDAH. SAKURU) aliuliza:-

Sherehe za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kutumiafedha nyingi za walipa kodi huku Watanzania wengi wakiwana maisha duni. Je, Serikali haioni umuhimu wa kurudishaMwenge wa Uhuru katika Makumbusho ya Taifa na kuzifutasherehe hizo?

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI,AJIRA NA VIJANA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa ZubedaHassan Sakuru, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenge wa Uhuru nichombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu JuliusKambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara yakuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Dhana na falsafa yaMwenge wa uhuru inatokana na maono ya mbali kupitiakwenye maneno yaliyosemwa tarehe 9 Desemba, 1961nanukuu:-

“Sisi tumekwisha uwasha Mwenge wa Uhuru nakuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro umulike ndani na nje yamipaka yetu, ulete matumaini pale ambapo hakunamatumaini, ulete upendo mahali penye chuki na heshimamahali palipojaa dharau”

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haioni umuhimu wakuweka Mwenge wa Uhuru katika makumbusho ya Taifa nakuzifuta sherehe zake kwa sababu zifuatazo:-

(i) Mbio za Mwenge wa Uhuru huwakumbushaWatanzania falsafa nzito ya Mwenge wa Uhuru inayotoataswira ya Taifa ambalo Waasisi wetu walitaka kulijenga Taifalenye amani, linalojitegemea na lenye kuheshimu misingi yautu na usawa wa binadamu. (Makofi)

(ii) Mwenge wa Uhuru kupitia mbio zakeumekuwa ni chombo cha kuchochea maendeleo yawananchi, kwa mfano, kwa kipindi cha miaka mitanoiliyopita, miradi ya maendeleo 6,921 yenye thamani ya shilingitrilioni 2.5 ilizinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi. (Makofi)

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

(iii) Kila mwaka, Mbio za Mwenge huambatanana ujumbe maalum unaohamasisha masuala muhimu yaKitaifa kwa wananchi nchi nzima. Kwa mfano, kwa mwakajana 2017 ujumbe ulikuwa “Shiriki kukuza uchumi wa viwandakwa maendeleo ya nchi yetu”. Mwaka huu wa 2018 ujumbeni “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwamaendeleo ya Taifa letu”. Aidha, kila mwaka wananchihukumbushwa kuendelea na mapambano dhidi ya UKIMWI,malaria, rushwa na dawa za kulevya. (Makofi)

(iv) Mwenge wa Uhuru unaimarisha Muunganowetu, Mwenge wa Uhuru huzunguka nchi nzima TanzaniaBara na Zanzibar. Wanaokimbiza Mwenge wa Uhuruwanatoka sehemu mbili za Muungano. Kwa kufanya hivyo,Mwenge wa Uhuru unazidi kutuunganisha kama watanzania.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwamba Mwengewa Uhuru unatumia fedha nyingi za walipa kodi. Kwa mfano,kwa mwaka 2017, Serikali i l itenga shilingi milioni 463kugharamia shughuli za Mwenge wa Uhuru ukilinganisha nakiasi cha miradi 1,582 iliyozinduliwa yenye thamani ya shilingitrilioni 1.1 ni dhahiri kuwa hoja ya gharama kuwa kubwasiyo ya msingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri.Majibu ya swali yamejitosheleza hatuwezi kuchukua tunu yaTaifa tukaipeleka kwenye makumbusho. Tunaendelea naswali lingine, Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, bado sijauliza maswali ya nyongeza.

WABUNGE FULANI: Hajauliza maswali ya nyongeza.

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa WabungeWaliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Majibu ya swali yamejitoshelezaMheshimiwa Sophia.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

WABUNGE FULANI: Aaaaaaa.

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge Waliongea bila mpangilio)

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Haiwezekani, hichokitu hakipo.

MWENYEKITI: Tuendelee na Mheshimiwa Haji Dau.

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge Waliongea bila mpangilio)

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, hiyo ni kinyume na Kanuni.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dau.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Swali la nyongezasijauliza.

MBUNGE FULANI: Limejitosheleza nini, Kanuni ganimnayofuata?

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge Waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombamtulie.

WABUNGE FULANI: Hatukubali, haijawahi kutokea.

MWENYEKITI: Nasema hivi majibu yamejitosheleza.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Why?

MWENYEKITI: Hii ni tunu ya Taifa.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Why? Sijauliza swalila nyongeza, why?

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

(Hapa baadhi ya WaheshimiwaWabunge Waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombatuendelee. Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji swali lingine.

Na.110

Ucheleweshwaji wa Mishahara kwa Watumishi wa Umma

MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza:-

Kumekuwa na ucheleweshaji wa mishahara kwawatumishi wa umma:-

Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo hilo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waFedha na Mipango, napenda kujibu swali la MheshimiwaMwantumu Dau Haji, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Waraka waHazina Na.12 wa mwaka 2004, watumishi wa ummawanatakiwa kulipwa mishahara yao kabla ya tarehe 25 yakila mwezi. Kumbukumbu za malipo ya mishahara kwawatumishi wa umma zinaonyesha kuwa, kuanzia Julai, 2017hadi Agosti, 2018 watumishi walilipwa mishahara yao kati yatarehe 20 na 24 ya kila mwezi. Hivyo basi, napenda kuliarifuBunge lako Tukufu na umma kwa ujumla kuwa hakunaucheleweshaji wa malipo ya mishahara kwa watumishi waumma.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mantumu swali lanyongeza.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Namshukuru Naibu Waziri kwa majibu yakemazuri aliyoyatoa hivi sasa. Kwa kuwa hakunaucheleweshwaji wa mishahara, napenda kuuliza maswaliyangu mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Serikaliinasema nini kuhusu uongezaji wa mishahara kwa watumishihao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali inasemanini kuhusu upandishaji wa madaraja mbalimbali kwawatumishi wa umma?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya MheshimiwaMwantumu Dau Haji, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaameuliza Serikali inasema nini kuhusu uwekezaji wamishahara ya wafanyakazi. Napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kwamba mshahara ni mali halali ya mfanyakazimwenyewe hivyo kuhusu uwekezaji ni mfanyakazi mwenyeweanaamua mshahara wake nini aufanyie, akitaka kuuwekezawote yuko huru kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusuupandishwaji wa madaraja, Serikali yetu siku zote imekuwaikiwatendea haki wafanyakazi wetu kwenye upandishaji wamadaraja na kila mwaka wafanyakazi hupandishwamadaraja.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia, Mheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa VitiMaalum, Mheshimiwa Asha Abdallah Juma kwa niaba.

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Na.111

VETA Kuingizwa Katika Sera ya Elimu ya Msingi

MHE. ASHA ABDALLAH JUMA (K.n.y. MHE. KHADIJANASSIR ALI) aliuliza:-

Sera yetu ya Elimu inatueleza kuwa elimu ya msingi nihadi kidato cha nne:-

Je, ni lini Serikali itaboresha kiwango hiki cha elimuya msingi hadi kufika ngazi ya Ufundi Stadi yaani VETA?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa elimu waTanzania unasimamiwa na Sheria ya Elimu Na.25 ya mwaka1978. Sheria hii inabainisha wazi kuwa elimu ya msingi ni miakasaba kuanzia Darasa la Kwanza hadi Darasa la Saba. Hivyo,napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa, elimu yamsingi inatolewa kwa muda wa miaka saba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutoaelimu ya msingi kwa miaka saba bila kuunganisha namafunzo ya ufundi stadi. Sababu kubwa ya kufanya hivyo nikwamba maudhui yaliyopo kwenye mtaala wa elimu yamsingi bado yanakidhi mahitaji ya sasa ya wahitimu wa ngazihiyo ya elimu ya msingi lakini pia muda ambao wanafunziwa elimu ya msingi wanakaa shuleni hauwezi kutoshakuunganisha na mafunzo ya ufundi stadi. Hivyo, mafunzo yaufundi stadi yataendelea kutolewa na Mamlaka ya UfundiStadi.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kulifahamishaBunge lako Tukufu kuwa Serikali inaendelea na jitihada zakuongeza nafasi za udahili katika Vyuo vya Mafunzo ya UfundiStadi. Juhudi hizi ni pamoja na kujenga Vyuo vipya vya UfundiStadi na vilevile kufanya ukarabati wa Vyuo vya Maendeleoya Wananchi ili viwe na mazingira fanisi ya kujifunzia naviweze kutoa mafunzo katika fani mablimbali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Asha Abdallah Juma.

MHE. ASHA ABDALLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, bado vijanawengi wanaomaliza darasa la saba wanakuwa hawajapatanafasi kwenye vyuo vya ufundi au kuendelea na masomo yasekondari. Ni lini Serikali itaboresha elimu ya msingi kuhusishamafunzo ya ufundi ndani yake il i kuwaasaidia walewanaobaki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mtaala wa VETAni mmoja nchi nzima wakati mahitaji yanatofautiana sehemuna sehemu. Kwa mfano, mikoa yenye gesi wangefundishwamambo yanayotokana na gesi, mikoa ya uvuviwangefundishwa taaluma za uvuvi na mikoa ya madini vivyohivyo. Sasa Serikali ina utaratibu gani kuhusu kuingizacomponent hiyo katika mitaala yake?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu ya maswalihayo ya nyongeza.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali yanyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuhusu suala lawanafunzi ambao wanamaliza darasa la saba lakinihawapati nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari,kama ambavyo nimesema kwenye majibu yangu ya msingi,Serikali inafanya kazi kubwa ya kuongeza nafasi za udahili

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

kwenye vyuo vya ufundi kwa kujenga vyuo vipya vya ufundipamoja na kuboresha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niseme kwambakatika mtaala wa elimu ya msingi kuna somo la stadi za kaziambalo limewekwa mahsusi kwa ajili ya kuwapatia vijanawetu angalau ujuzi ili hata yule anayemaliza elimu yake yamsingi awe tayari ana uwezo wa kufanya jambo katikamazingira yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusumtaala wa VETA kwamba unafanana, kimsingi masuala yaufundi yanatakiwa yaangalie mazingira halisi ya mahaliufundi unapofanyika. Kwa hiyo, suala la kuangalia masualaya gesi au masuala ya uvuvi ndiyo jambo ambalo limekuwalikifanyika. Kwa hiyo, niendelee kutoa wito kwa wotewanaotoa mafunzo ya ufundi stadi wahakikishe kwambamitaala yao inazingatia mazingira halisi ya pale ambapowanatoa mafunzo ili kuwawezesha wananchi wa eneohusika kuongeza tija katika shughuli wanazozifanya.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwalongo nimekuona naMheshimiwa Toufiq.

MHE. EDWARD F. MWALONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa sasa wakutumia VETA na vyuo vya FDC kutoa mafunzo ya ufundi stadiumekuwa ni wa polepole sana na idadi kubwa ya vijanawanamaliza shule za sekondari hawana ujuzi kabisa. Je,Serikali inaonaje sasa ikaanza kubadilisha baadhi ya shule zasekondari ambazo tumezijenga katika Halmashauri zetukuwa shule za ufundi ili kusudi zisaidie vijana hawa kupataelimu ya ufundi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Mwalongo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niseme kwambaSerikali tayari imeshaona hiyo changamoto na ndiyo maanazile shule za ufundi ambazo awali zilikuwa zimebadilishwamafunzo ya ufundi yaliondolewa tayari Serikali imeshachukuajukumu la kuzikarabati zile shule saba za ufundi za Kitaifa nakuziimarishia vifaa vya kufundishia na karakana zake zotezimeimarishwa. Nitoe wito kama alivyosema MheshimiwaMwalongo, Serikali itafurahi sana kama kuna Halmashauriambayo ina shule na wanaona kwamba inakidhi vile vigezovya kutoa mafunzo ya ufundi tuko tayari watuambie ilitwende kuikagua na tutapenda tu kuongezea idadi yawanaofanya mafunzo ya ufundi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Toufiq.

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa baadhi ya shuleza msingi zina vituo vya ufundi stadi, mfano, katika Wilayaya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi MvumiMission na Shule ya Msingi Chamwino lakini hakuna vifaawala walimu wa kutosha. Je, Serikali ina mkakati gani wakuvifufua vituo hivyo siyo kwa Wilaya ya Chamwino tu lakinikatika shule zote za msingi ambazo ziko Tanzania hii?Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLIJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la dada yanguMheshimiwa Fatma Toufiq, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru kwaswali lake zuri kwa sababu ni kweli zile shule zipo lakini kwakweli hali yake haijakaa vizuri, niliona nilipozitembelea. Kwa

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

hiyo, tayari Serikali imeliona na kwa kupitia Mradi wa KukuzaUjuzi hapa Nchini (ESPJ) ambao Wizara yangu inautekelezakwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, tutafanya tathminiya shule hizo na kwa awamu tutaanza kuzifanyia maboreshokwa kuzipelekea vifaa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Salma Kikwete.

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Tunaamini na tunajua kwamba elimu ndiyo msingiwa kila kitu katika maisha ya mwanadamu na mafanikio yaelimu ni pamoja na kuwa na zana za kufundishia pamojana kujifunzia. Kwa kuwa, vitabu vyetu vya kiadahuchapishwa nje ya nchi yetu na tukiamini kwamba elimu nijambo tete katika ustawi wa Taifa letu, je, ni lini vitabu hivivya kiada vitachapishwa hapa nchini ukizingatia Serikali yetuni ya viwanda? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la MheshimiwaMama Salma Kikwete, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimshukurusana kwa kuleta swali hili hapa Bungeni na nitumie nafasi hiikuonyesha masikitiko yangu makubwa sana kwa makampuniya Kitanzania ambayo yanafanya kazi ya uchapishaji. HayaMakampuni yametuangusha kweli kweli, tumelazimikakwenda kuchapa vitabu nje kwa sababu unapoyapamakampuni ya Kitanzania kwanza kuna mengine ambayoyamekuwa yanachapa vitabu, kitabu kimekaa kamasambusa yaani wanakata hovyo hovyo lakini pia wanatumiamuda mrefu kuvichapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuhusu swali lakekwamba Serikali ina mpango gani, kutokana nachangamoto hiyo, Serikali imeamua kununua mashine yauchapaji na hapa tunapoongea tayari tumekwishaiagiza.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Kwa hiyo, tunategemea hilo suala sasa tutakuwa tunalifanyawenyewe.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri waElimu. Tunaendelea na Wizara ya Madini, MheshimiwaAugustino Manyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe aulizeswali lake.

Na.112

Kufungua Mgodi wa Nyakafuru

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:-

Je, ni l ini mgodi utafunguliwa katika eneo laNyakafuru Wilayani Mbogwe baada ya utafiti kuchukuamuda mrefu kwenye eneo hilo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Madini,majibu ya swali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. DOTO M. BITEKO)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMadini napenda kujibu swali la Mheshimiwa AugustinoManyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Nyakafuru lenyeleseni ya ukubwa wa kilomita za mraba 17.53 linamilikiwana Kampuni ya Mabangu Limited Resources, kampuniambayo Kampuni tanzu ya Resolute Tanzania Limited kupitialeseni ya kutafuta madini PL Na.5374 ya mwaka 2008. Lesenihiyo ambayo ilihuishwa mara mbili na baadaye kuongezewamuda wa kipindi cha miaka miwili yaani extension kuanziatarehe 24 Oktoba, 2016 ili kukamilisha kazi ya upembuziyakinifu na itamaliza muda wake tarehe 23 Oktoba, 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, marekebisho yaSheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika mwaka 2017

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

yaani The Written Laws Miscellaneous Amendment Act 2017yaliondoa uhitaji wa leseni ya utafutaji wa madinikuongezewa muda wa kufanya utafiti baada ya muda waleseni kuhuishwa kwa mara ya pili kumalizika. Kwa sasasehemu ya eneo hilo la leseni hiyo imevamiwa na wachimbajiwadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa mashapoyanayofikia takribani tani 3.36 yenye dhahabu ya wakia203,000 yamegunduliwa na jumla ya Dola za Kimarekanimilioni 1.83 zimetumika kufanya utafiti katika eneo la mradi.Aidha, Tathmini ya Athari ya Mazingira ilishafanyika na kupewacheti cha tarehe 16/10/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, isitoshe, Kampuni yaMabangu Mining Limited kupitia Kampuni mama ya Resolute(Tanzania) Limited inadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzaniakiasi cha jumla Sh.143,077,421,804 ikiwa ni deni la kodi ambalowanatakiwa kuli l ipa. Mgodi wa Nyakafuru unawezakuendelezwa baada ya deni hilo kuwa limelipwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masele.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, naomba kuuliza maswali mawili madogo yanyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwaeneo hili la Nyakafuru limekuwa chini ya utafiti kwa mudamrefu na tayari wachimbaji wadogo wameshalivamia. Je,Serikali iko tayari sasa kuwamilikisha wachimbaji haowadogo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, eneo pia laNakanegere Mlimani nalo limekuwa chini ya utafiti kwa mudamrefu. Serikali inasemaje juu ya uwezekano wa kuwapatiawananchi kuchimba kwa leseni za wachimbaji wadogowadogo?

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. DOTO M. BITEKO):Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili yaMheshimiwa Augustino Manyanda Masele, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuwamilikishawananchi kwenye eneo hilo, nieleze tu kwamba MheshimiwaMbunge anafahamu wananchi wa Nyakafuru ndiyo waowako pale wanaendelea na shughuli. Kwa kuwawanaendelea na shughuli pale na kwa maelekezo tuliyopewakazi yetu ni kuwasaidia wachimbaji wadogo, wale ambaohawako rasmi tuwarasimishe ili waweze kupata vibali halisiwaweze kuchimba kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la Nakanegere,eneo hili lote linamilikiwa na kampuni moja na lenyeweutaratibu wake utakuwa kama ule wa Nyakafuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Martha Umbulla, swali lanyongeza.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kuniona. Kama lilivyo suala la madini katikaJimbo la Mbogwe, Mkoa wetu wa Manyara maeneo mengiyana madini kulingana na utafiti uliofanyika. Hivi sasauchimbaji huo unafanywa kiholela na sina hakika kamaSerikali ina mkakati wowote ama ina taarifa na suala hilo.Je, Serikali sasa iko tayari kutupa takwimu ama hali halisi yamadini yaliyoko katika Mkoa wetu, Wilaya za Mbulu, Simanjirona Kiteto?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. DOTO M. BITEKO):Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la MheshimiwaFelister Bura, kama ifuatavyo:-

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Buraatakumbuka kwamba wakati tunawasilisha bajeti yetupamoja mambo mengine tulitoa machapisho na majaridambalimbali ambayo ndani yake yalikuwa yanatoa takwimukwa ujumla kwenye sekta ya madini kwa kila Mkoa, Wilayana maeneo mbalimbali. Naamini Mheshimiwa Bura akiendakukapitia kale kakijitabu atapata taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hili jambo lingineambalo ameeleza juu ya wananchi kuchimba kwenyemaeneo mbalimbali kwenye Mkoa Manyara. Nisemekwamba Serikali inazo taarifa za wachimbaji wadogokuvumbua. Mara ugunduzi unapotokea, kazi yetu ya kwanzani kupeleka usimamizi ili kudhibiti usalama lakini vilevilekudhibiti mapato ya Serikali. Nataka nimhakikishieMheshimiwa Bura ugunduzi wowote unaotokea katika Mkoawa Manyara tunafahamu na tayari kuna usimamizi ambaounafanywa na Ofisi zetu za Madini kwenye Kanda pamojana Mikoa.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuweka taarifa sahihi, mimi naitwa Martha Umbullana siyo Bura.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Martha Umbulla.Tunaendelea na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mheshimiwa Muhammed Amour Muhammed, Mbunge waBumbwini sasa aulize swali lake.

Na. 133

Vifo vya Askari wa Jeshi la Ulinzila Wananchi (JWTZ) Nje ya Nchi

MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED aliuliza:-

Kwa kipindi cha kirefu sasa nchi yetu imekuwaikipeleka Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) nje ya nchiambako kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe nakusababisha misiba mikubwa sana kwa Askari wetu:-

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Je, Serikali inasema nini kuhusiana na kadhia hiyo?

MWENYEKITI: Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,majibu ya swali hilo Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Muhammed Amour Muhammed, Mbunge waBumbwini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania kamaMwanachama wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika,Jumuiya za Kikanda kama East Africa Community na SADCna Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu inao wajibu wa kushirikikatika Ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali. Madhumuniya kupeleka askari wetu huko ni kwenda kulinda amani nasio kushiriki kwenye mapigano. Kwa bahati mbaya sana, yapomatukio ya kushambuliwa kwa askari wetu yaliyofanywa navikundi vya waasi yaliyopelekea kupoteza maisha ya baadhiya askari wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Wananchi waTanzania limechukua hatua ya kutoa mafunzo ya kutoshakwa vikosi vyetu vinavyopewa jukumu hili, pamoja nakuwaongezea vifaa vya kisasa ili waweze kujilinda dhidi yamashambulio ya vikundi vya waasi. Hivyo, mtazamo waSerikali ni kuendelea kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amanikatika nchi mbalimbali ili kutimiza wajibu wetu Kimataifa nahuku tukichukua kila tahadhari kuepusha maafa yaliyowahikutokea.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Muhammed swali lanyongeza halafu Mheshimiwa Masoud.

MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Majibu ya Serikali hayatoshelezi, niafadhali tu kidogo. Pamoja na majibu hayo, nina maswalimengine mawili ya nyongeza.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kuna kaulimitaani zinasemwa na Watanzania kwamba Tanzaniainashiriki hasa hasa kwa maslahi binafsi ya kukomba mali zaDRC kwa mfano. Je, Serikali ina matamshi gani kwa lengola kuwaosha Watanzania kutokana na tuhuma hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Jeshi letulinapopigwa kwenye vita hasa pale DRC kuna kauli pia kwaWatanzania wanaamini kwamba Jeshi la Uganda linashirikikatika kulipiga Jeshi la Tanzania kwa kuwa wakati fulanikihistoria Waganda na Watanzania walipapurana kivita. Je,ni ipi kauli ya Serikali kuhusiana na kadhia hii? Ahsante.

MWENYEKITI: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Muhammed Amour, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa bahati mbaya sanamaneno kama haya yanatolewa na Watanzania ambaokwa kweli wanatakiwa wao wawe wazalendo na kuwezakupongeza juhudi za Serikali za kuwasaidia wenzetu ambaowako katika hali ambayo haina amani katika nchi yao.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna suala la kukombamali za DRC kwa maslahi binafsi, halipo. Tanzaniahaishughuliki na kuchukua chochote sehemu yoyotewanayolinda amani. Majeshi yetu yako kule kusaidia kurudishahali ya amani, kuwalinda wananchi dhidi ya waasi ambaowanapigana katika maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kwamba Jeshi laUganda linashiriki katika kuwapiga Watanzania pia halinaukweli wa aina yoyote. Matukio yote yaliyotokea tunaushahidi wa kutosha kwamba ni vikundi vya waasi. Mwanzoniwalikuwa M.23 na sasa hivi kuna vikundi vingine ambavyo

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

vinatokea katika nchi mbalimbali za jirani pale lakini hakunaukweli kwamba Majeshi ya Uganda yanashiriki katikakuwapiga askari wa Tanzania. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALUM: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru, nina swali moja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kuna vikundi vyawaasi ambavyo vinapelekea kufanya hujuma kwa Vikosivyetu vya Kulinda Amani DRC - Kongo na maeneo menginena pale inapotokea maafa kwa hawa askari wetu kupotezamaisha huwa kuna malipo maalum kutoka Umoja waMataifa lakini hata Serikali yetu nayo huwa kuna kiwangocha fedha ambacho wanatoa. Je, Serikali hasa ina mkakatigani wa ziada kuleta Muswada hapa Bungeni kuongezamuda wa kulipa wajane au wagane pale ambapo wanajeshiwanapoteza maisha katika kulinda amani DRC Kongo naSudan Kusini na maeneo mengine? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongezaya Mheshimiwa Masoud, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Umoja waMataifa na Serikali ya Tanzania imekuwa ikilipa mafaoyanayohusiana na ushiriki wa askari wetu katika Ulinzi waAmani sehemu mbalimbali. Vinapotokea vifo basi kunafedha maalum na kuna viwango maalum vilivyopangwaambavyo hutolewa na Umoja wa Mataifa na Tanzania sisitunatoa kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi na Kanuni za Majeshizilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuongeza fedha kwawajane, ni suala ambalo tunalitafakari kwa madhumuni yakuweza kuboresha maslahi yote kwa ujumla siyo moja moja.Kwa sababu kuna maslahi mengi ambayo wanajeshi hawa

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

wanatakiwa wayapate. Sasa hivi Sheria ya Ulinzi wa Taifainapitiwa pamoja na Kanuni zake ili kuangalia ni viwangogani vya maslahi gani ambavyo vimepitwa na wakati iliviweze kuboreshwa kwa pamoja.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri.Tunaendelea na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, MheshimiwaLucia Michael Mlowe Mbuge wa Viti Maalum sasa aulize swalilake.

Na. 114

Mfumo Chakavu wa Mabomba ya Maji Nchini

MHE. LUCIA M. MLOWE aliuliza:-

Mfumo wa mabomba ya maji kwenye maeneo menginchini ni chakavu hivyo kusababisha upotevu mkubwa wamaji:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kubadilishamabomba yote chakavu katika nchi i l i kuokoa majiyanayopotea kutokana na uchakavu huo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali laMheshimiwa Lucia Mlowe, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli sekta ya majiimekuwa inakabiliwa na changamoto ya upotevu wa majikutokana na uchakavu wa miundombinu iliyojengwa miakamingi iliyopita. Katika kukabiliana na changamoto hizo,Serikali imeendelea na jitihada za uwekezaji katika ukarabatiwa miundombinu chakavu maeneo mbalimbali ya mijiniikiwemo Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza,Morogoro, Singida pamoja na ukarabati wa miradi ya kitaifa

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

ya Makonde, Wanging’ombe, Maswa, HTM, MugangoKiabakari na Chalinze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Miradi yaMaji Vijijini, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleoimeendelea kuimarisha Programu ya Uendelevu wa Hudumaya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kwa kutumia Mfumo waMalipo ya kwa Matokeo (Payment for Results -PforR naPayment by Results – PbR) ambapo kwa pamoja zinalengakuhakikisha kasi ya uendeshaji, matengenezo na ukarabatiwa miundombinu ya miradi ya maji vijijini inakuwa endelevuna wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jitihada hizo kwa pamojazitasaidia kupunguza hali ya upotevu wa maji katika miradiya maji mijini na vijijini.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlowe, swali la nyongeza.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswaliya nyongeza, nina maswali mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Waziriamekiri kwamba kuna tatizo la upotevu wa maji kutokanana miundombinu mibovu. Hivi navyoongea bado kuna tatizokubwa sana la uvujaji wa maji, mfano, Kisasa kunamabomba hivi sasa yanaendelea kutiririsha maji lakini sionijuhudi inayoendelea hadi sasa hivi. Je, wana mkakati ganikuhakikisha tatizo hili linatatuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Jimbo laNjombe Kusini, Kata ya Ihungilo kuna mradi wa Utengule –Ngalanga ambao vifaa vilivyonunuliwa vilinunuliwa chini yakiwango na hadi sasa hivi vifaa hivi, mabomba na viungiovyake vinaendelea kutitirisha maji na wananchi wanakosahuduma ya maji. Je, Waziri yuko tayari kwenda kutatua tatizohili katika Kata hii ya Ihungilo?

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya maswalihayo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza yaMheshimiwa Mlowe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, upotevuwa maji ni changamoto kubwa kwa sababu lina sehemumbili, kwanza ni miundombinu yenyewe na pili ni wafanyakazitunasema non commercial revenue water losses ambalolinatokana na baadhi ya wafanyakazi kushirikiana nawananchi katika kuiba maji. Tunapamba na mambo yotehaya mawili na kuhakikisha kwamba tatizo la upotevu wamaji linamalizika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mheshimiwa Mbungealivyosema sasa hivi kuna changamoto hizo lazima mtuakiona changamoto hiyo tuwasiliane na Mamlaka za Maji,tuwape taarifa ili waweze kwenda kumaliza tatizo hilo. Kilakwenye Mamlaka ya Maji tumeweka toll free number ambayoni namba ya simu ambapo unaweza kupiga simu bure kuelezawapi kuna tatizo la upotevu wa maji na mara mojautakapofanya hivyo sisi tutachukua hatua za kuwezakupambana na upotevu huo wa maji. Hili la Kisasa kamaalivyosema Mheshimiwa naamini wataalam wanguwamesikia na watakwenda kulishughulikia mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kuhusu vifaavilivyo chini ya kiwango. Ni kweli kabisa katika miradi mingisana iliyojengwa vijijini, vifaa vingi vilivyopelekwa nawakandarasi viko chini ya kiwango na tumechukua hatuambalimbali za kisheria na tutaendelea kuchukua. Naombatu nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwendapamoja tuhakikishe kwamba tatizo hili tunaliondoa iliwananchi wale waweze kupata maji safi na salama.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Willy Qambalo.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Miradi ya maji katika Viji j i vya Getamok,Endonyawed, Kansai, Matala na Fusmai katika Wilaya yaKaratu ambayo ni zaidi ya asilimia 50 ya ile miradi kumi katikakila Wilaya haifanyi kazi kwa sababu ya kujengwa chini yakiwango. Tatizo kubwa ni kama ilivyoelezwa katika swali lamsingi mabomba yanavuja. Mheshimiwa Waziri yuko tayarisasa kuja Karatu ili ajionee mwenyewe jinsi wananchi naSerikali walivyohujumiwa lakini pia akae na Halmashauri ilikuona ni namna gani miradi hiyo inafufuliwa? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mbunge,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kamanilivyosema maeneo mengi hasa ya vijijini miradi mingiiliyotekelezwa ilitekelezwa chini ya viwango. Wamewekamabomba ambayo yako chini ya viwango, wamewekavalve ambazo ziko chini ya viwango. Sisi tunahakikishakwamba sasa tatizo hili linamalizika na pale ambapomkandarasi ameweka vifaa ambavyo viko chini ya viwangoanatakiwa aviondoe na afanye kazi hiyo na aweke vifaaambavyo vina viwango vinavyokubalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekubaliana naMheshimiwa Mbunge tutakwenda tutaona tatizo hilo natutalitatua kwani nia ya Serikali naendelea kusema tena nikuhakikisha kwamba tunawapelekea wananchi maji safi nasalama.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Deo Ngalawa.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Wananchi wa Jimbo la Ludewa huwawana kawaida ya kujiongeza. Miradi mingi ambayoinafanyika kwenye Jimbo la Ludewa wananchi wanakuwawameianza kabla ya Serikali. (Makofi)

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania ni shahidi alipofikamaeneo ya Mlangali alishakuta watu wameshajichangishashilingi milioni 90 na wakawa wanaiomba Serikali shilingimilioni 50 kwa ajili ya kumalizia. Niishukuru Serikali ilitupa ilehela. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna miradimbalimbali inaendelea kwenye Kata ya Mavanga na LudewaMjini. Je, Serikali ipo tayari kutusaidia na kuhakikisha mfanomiradi ile ya Ludewa Mjini, Iwela na Lifua inakamilika katikakipindi kifupi iwezekanavyo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge waLudewa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kawaida nia yaSerikali ni kuhakikisha kwamba Watanzania wanapatahuduma ya maji safi na salama na kwa muda mfupi. Kwahivyo, nitahakikisha kwamba miradi ya Ludewa Mjini namaeneo mengine aliyoyataja Mheshimiwa Mbungetutatekeleza kwa muda mfupi ili Watanzania wa maeneoyale na maeneo mengine yote Tanzania waweze kupata majisafi na salama. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ruth.

MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni miaka zaidi ya 50 yaUhuru lakini maeneo mengi ya wafugaji bado wanakunywamaji kwenye mabwawa pamoja na wanyama, binadamuwanachota maji, wanyama pia wanakunywa hapo.Nimeona hili Mkuranga Kijiji cha Beta, nimeona hili juzi Mondulikatika Kata ya Nararami. Kwa nini hii shilingi milioni 50iliyotolewa kwa kila kijiji isitumike kwenda kuchimba visima

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

virefu katika yale maeneo ambayo hakuna maji nabinadamu wanakunywa maji kwenye mabwawa nawanyama? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaRuth, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaelewa kwambamaeneo mengi ya nchi yetu yana changamoto kubwa yamaji, mijini na vijijini. Serikali tumejipanga vizuri, kwa mfanotu, juzi tumepata mkopo wa bei nafuu kutoka Benki ya Duniaambapo tumepata takribani shilingi za Kitanzania bilioni 800na pesa nyingi kati ya hizo zitapelekwa vijijini kutatuachangamoto ya maji kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema.Siyo hivyo tu, kwenye bajeti yetu hii ya mwaka huu tunatakribani shilingi bilioni 630 kwa ajili ya kupeleka maji vijijini.Nataka niwahakikishie Watanzania kwamba Serikalitumejipanga na kila kijiji tutawapelekea maji safi na salama.

MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la MheshimiwaHasna Sudi Katunda Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kusini.

Na. 115

Miradi ya Maji Jimbo la Kigoma Kusini

MHE. HASNA S. K. MWILIMA aliuliza:-

(a) Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu miradi yamaji ya Kali, Rukoma, Ilagala, Kandego, Uvinza na Ngurukaambayo wakandarasi wamesimama kwa ukosefu wa fedha?

(b) Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili yakukamilisha miradi hiyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hasna SudiKatunda, Mbunge wa Kigoma Kusini, lenye sehemu (a) na(b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Programu yaMaendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Kwanza chini yaMpango wa Vijiji 10 kwa kila halmashauri, Miradi ya Maji yaRukoma na Kandaga ilitekelezwa katika Halmashauri yaKigoma na miradi ya maji katika vijiji vya Kalya, Ilagala, Uvinzana Nguruka ilitekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wakandarasi wamiradi hiyo walikuwa wamesimama kutokana nachangamoto ya kifedha. Katika bajeti ya mwaka 2017/2018,Serikali tulitumia kiasi cha shil ingi bil ioni 1.01 katikaHalmashauri ya Uvinza kwa ajili ya kuendelea kukamilishamiradi ya maji ambayo haijakamilika ikiwemo miradi ya Kayla,Ilagala, Uvinza na Nguruka. Aidha, Halmashauri ya Kigomailitumia jumla ya shilingi bilioni 581.2 kuendelea kukamilishamiradi ya maji vijijini ikiwemo Rukoma na Kandaga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2018/2019, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.8 nashilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya Halmashauri za Wilaya ya Uvinzana Kigoma mtawalia ili kuendelea na utekelezaji wa miradiya maji. Aidha, halmashauri zote nchini zimeshauriwakuwasilisha kwa wakati hati za madai ya wakandarasiwanaojenga miradi i l i ziweze kulipwa mapemaiwezekanavyo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hasna.

MHE. HASNA S.K. MWILIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri lakini tumekuwana tatizo kubwa la wakandarasi hawa, kwa mfano, Mradiwa Nguruka Mheshimiwa Rais alifanya ziara tarehe 23 Julai,2017 akatoa tamko hadi Desemba. 2017 Mradi wa Ngurukauwe umekamilika.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Mheshimiwa Mwenyekiti, pesa zinaletwa na Serikaliwakandarasi hawa hawakamilishi miradi hii na mradi waNguruka wananchi wanaona pesa zinaingia lakini hawapatimaji. Mradi wa Uvinza pesa zinaletwa lakini wakandarasihawakamilishi ili wananchi wapate maji. Mradi wa KandagaMheshimiwa Waziri wewe ni shahidi tarehe 17 Julai, 2018tulifanya ziara pale ukampa mkandarasi wiki mbili lakini hadileo hii hakuna maji yanayotoka pale. Swali langu la kwanza,je, Serikali ina kauli gani kwa hawa wakandarasi ambaowanalipwa pesa lakini hawakamilishi miradi kwa wakati?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, tarehe 29Julai, 2018, Mheshimiwa Waziri Mkuu alifanya ziara kwenyeKijiji cha Mwakizega na wananchi wakamlilia kwambatunahitaji maji na tamko tukaambiwa tuandae taarifa yamradi wa maji i l i tuweze kuwasil isha Wizarani. Hivinavyoongea Injinia wa Maji Halmashauri ya Uvinza yuko hapaDodoma ameshawasilisha andiko hilo la mradi ambalolinagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.9. Je, ni lini sasa Wizaraitatuletea pesa ili tuanze kutekeleza huu mradi mpya waMwakizega? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya maswalihayo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hasna,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza kwamba Serikaliinachukua hatua gani kwa wakandarasi ambaowanashindwa kukamilisha kazi kwa wakati. Kuna taratibumbalimbali Serikali inachukua kama mkandarasi anashindwakukamilisha kazi kwa wakati. Hatua ya kwanza, kamamkandarasi anachelewesha kazi tunampiga faini kutokanana ucheleweshaji na kila siku mkandarasi huyo analipa fainiinategemeana na mradi wenyewe na kiasi cha gharama zamradi. Hatua ya pili ambayo kama mkandarasi atashindwakutelekeza kazi kwa wakati tunaweza kumfutia usajili na

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

mwisho wake hatoweza kufanya kazi yoyote ya ukandarasikwenye sekta zote za ujenzi pamoja maji na sekta zote hapanchini. Tutawasimamia wakandarasi wote tuhakikishekwamba wanafanya kazi kwa wakati na wanazimaliza kwawakati ili Watanzania ambao wamesubiri maji kwa mudamrefu waweze kupata maji na salama kwa mudaunaostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili MheshimiwaMbunge amezungumzia kuhusu andiko, andiko tumelipokeana kama kawaida andiko lolote lazima lipitie michakatombalimbali. Mara litakapokamilika tutaweza kutoa fedha ilimradi huo uweze kutekelezwa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwakajoka na MheshimiwaKitandula.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swalila nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uko mradi ambao unatakakutekelezwa kwenye Mji wa Tunduma na SADC naMheshimiwa Waziri katika Bunge lililopita alisema kwambaameshampeleka consultant pale. Wananchi wa Tundumawanataka kujua mpaka sasa mradi umefikia kiwango ganikatika maandalizi ya utekelezaji?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge waTunduma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli consultant ameendakwa aji l i ya mradi huo lakini taratibu za utekelezajizinakwenda hatua kwa hatua. Kwanza consultantanakwenda kufanya study analeta hiyo study tutaipitiabaadaye kama pesa ipo utafuata mchakato wa kutafutamkandarasi ili aweze kufanya kazi hiyo.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kitandula.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka huutumetenga fedha kwa ajili ya kufanya usanifu wa Mradi waKupeleka Maji Makao Makuu ya Wilaya ya Mkinga kutokaMto Zigi kuelekea Horohoro lakini mpaka sasa hakuna daliliyoyote ya jambo hili kufanyika. Ni lini usanifu huu utaanza?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaMbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu MheshimiwaMbunge kwamba usanifu huo utaanza mara moja,tunajipanga kuhakikisha kwamba tunatafuta wataalam iliwakafanye kazi hiyo.

MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la MheshimiwaEdwin Mgante Sannda, Mbunge wa Kondoa Mjini, swali lakelitaulizwa na Mheshimiwa Felister Bura.

Na. 116

Miundombinu ya Chanzo Kikuucha Maji cha Chemchem Kondoa

MHE. FELISTER A. BURA (K.n.y. MHE. EDWARD M.SANNDA) aliuliza:-

Mtandao wa miundombinu ya usambazaji wa majitoka chanzo kikuu cha maji ya chemchem katika Jimbo laKondoa Mjini ni ya zamani na chakavu. Katika ziara yakemwaka jana, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi kutupatiafedha za ukarabati wa miundombinu hiyo:-

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hiyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Maji naUmwagiliaji, majibu ya swali hilo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali laMheshimiwa Edwin Sannda, Mbunge wa Jimbo la KondoaMjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambuauchakavu wa miundombinu ya usambazaji maji katikachanzo kikuu cha maji ya chemchem katika Jimbo la KondoaMjini. Serikali imekwishafanya tathmini ya awali ya ukarabatiwa chanzo hicho unaokadiriwa kugharimu kiasi cha shilingibilioni 4.1. Ukarabati wa chanzo hicho unatarajiwa kufanyikakatika mwaka wa fedha 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelezakuboresha huduma ya maji kwa wananchi wa Jimbo laKondoa Mjini, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikalikupitia Halmashauri ya Mji wa Kondoa ilikamilisha uchimbajiwa visima vinne vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni2.6 kwa siku. Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa majikutoka kwenye visima hivyo unaendelea. Kazizinazotekelezwa ni pamoja na ulazaji wa bomba kuu lenyeurefu wa kilomita 9.912, ulazaji wa mabomba ya usambazajimaji yenye urefu wa kilomita 30.172 na ujenzi wa vituo vyakuchotea maji 33. Kukamilika kwa mradi huo kutawanufaishawakazi wapatao 13,191 wa maeneo ya mitaa yaKwapakacha, Bicha, Kilimani, Kichangani na Tura.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Felister.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, kwanzatunaishukuru Serikali kwamba tumechimbiwa visima vinnekupitia Halmashauri ya Mji wa Kondoa. Pamoja na visimahivyo ambavyo vimechimbwa bila ukarabati wa

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

miundombinu ya maji, uchimbaji wa visima hivihavitawasaidia sana wananchi wa Kondoa Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo katikabajeti iliyopita tuliomba fedha kwa ajili ya ukarabati wamiundombinu hiyo. Naomba kujua Serikali imetenga fedhakiasi gani kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya zamaniukizingatia kwamba maeneo kama Kwapakacha, Kilimanina Bicha katika uchimbaji wa visima hivyo kuna maeneowatatumia miundombinu ya zamani? Je, Serikali iko tayarikujenga baadhi ya miundombinu ili wananchi wa KondoaMjini wapate maji? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa ahadiya ukarabati wa miundombinu ya maji katika Mji wa Kondoani ya ahadi ya viongozi wa Kitaifa na hasa waliotembeleaKondoa Mjini mwaka jana akiwemo Mheshimiwa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, ahadi hizozitatekelezwa lini? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, swali la takwimulitakuwa la tatu unaweza kuliacha maana ameuliza maswalimatatu Mheshimiwa.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ninavyosema maranyingi, nia ya Serikali ni kuhakikisha kila eneo tunapeleka majisafi na salama. Kwa upande wa Kondoa Mjini sasa hivi tunamradi ambao utahakikisha kwamba tunapeleka maji kilaeneo la Kondoa Mjini ambapo kama nilivyosema kwenyeswali la msingi kwamba sasa hivi tunajenga miundombinuya kilomita 9.12, tunajenga miundombinu ya kusambazamaji kilomita 30.172 kwa sababu kuchimba visima ni jambolingine na kuweka miundombinu ni jambo linguine. Kwakuli jua hilo, Serikali tunaendelea sasa hivi kujengamiundombinu hiyo tuhakikishe mwananchi kila eneo anapata

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

maji safi na salama. Tunategemea mradi huu utamalizikahivi karibuni na wananchi watapata maji hayo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nsanzungwanko naMheshimiwa Komu.

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Mji wa Kasulu ni kati ya miji ambayoinasubiri kwa hamu sana fedha za mkopo wa India katikaile miji 17. Hii ni kwa sababu Mji wa Kasulu unakabiliwa natatizo la maji na hata machache yaliyopo ni machafu, kwahiyo, kutibu tatizo hilo ni fedha za Mfuko wa India. Sasaniapenda kujua miradi hiyo 17 inaanza lini ikiwa ni pamojana Mji wa Kasulu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilola nyongeza.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge waKasulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tuna mradi mkubwawa India ambapo siyo miji 17 sasa itakuwa miji 25 na mradihuo utagharimu shilingi za Kitanzania trilioni 1.2. Tenda yakwanza ilitangazwa tarehe 17 Agosti, kwa ajili ya pre-qualification na consultancy na itafunguliwa tarehe 17Septemba. Kwa Mheshimiwa Mbunge yeyote anayehitajikujua information za mradi huu anaweza kupata kwenyewebsite ya Benki ya Exim ya India. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Komu.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali mojadogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Moshi Vijijinihali iko kama Kondoa, miundombinu mingi imejengwa sikunyingi na imechakaa. Kwa kutambua hilo, Mamlaka ya Maji

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

(MUWSA) imefanya kazi kubwa ya kukarabati miundombinuhiyo katika Kata mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana kulikuwepo namradi mmoja katika Kata ya Mabogini ambao ilikuwainahusu vijiji vinne na Wizara ilipokuja kuzindua kwa kuonakazi kubwa iliyofanywa na MUWSA katika Kata zingine iliahidikutoa shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kuendelea kusambazamaji kwenye vijiji vingine vitano vya Mvulei, Muungano naMsarikia. Nataka kujua ni lini fedha hizo zitapelekwa MUWSAili waweze kutekeleza ahadi hiyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu ya swali hilokwa ufupi.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Komu, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakubaliana nayeye kwamba MUWSA inafanya kazi nzuri na tunawapongezasana na tumewapa miradi mingi kwa ajili ya Moshi Vijijini nawanafanya kazi kubwa. Serikali tuko tayari wakati wowotewakituletea, kwa sababu tumeshawapa kibali cha kupelekamkandarasi kuanza kufanya kazi hiyo na wakati wowotewatakapoleta certificate kwa ajili ya malipo ya mkandarasisisi tumejipanga vizuri na tutaweza kuwalipa ili kazi hiyoiendelee. Mheshimiwa Mbunge naomba uwasiliane naMUWSA kujua wamefikia wapi lakini sisi tuko tayari fedhatunayo wakati wowote tutaweza kuwalipa waendelee nakufanya kazi hiyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Swali la mwisho, MheshimiwaMftaha kwa ufupi kabisa.

MHE. MAFTAH A. NACHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Mtwara Mjini kuna Mradi wa Maji ambaounatekelezwa na Serikali kutoa maji Kijiji cha Lwelu kuelekeaKata za Ufukoni, Magomeni na maeneo mengine ya MtwaraMjini lakini mkandarasi yule anasuasua sana na tayari kasha-

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

rise certificate Wizara bado haijamlipa na mradi umesimama.Je, Serikali inatoa kauli gani ili kuhakikisha mkandarasi yuleanalipwa na mradi ule unaendelea haraka ili wananchi waMtwara Mjini wapate maji? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kauli tu ya Serikali.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge waMtwara Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna miradi mingihapa nchini inaendelea na huu mradi wa Mtwaratunaufahamu vizuri na kila mwezi sisi tunaendelea kulipa,hata leo tunafanya malipo kwa wakandarasi. Tutahakikishakwamba na mkandarasi huyo tunamlipa ili aweze kuendeleakumaliza kazi hiyo ili wananchi wa Mtwara Mjini wawezekupata maji safi na salama. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Waziri wa Maji naUmwagiliaji kwa majibu mafupi na mazuri. Tunaendelea naWizara ya Nishati, Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola,Mbunge wa Mufindi Kusini, sasa aulize swali lake.

Na. 117

Kupeleka Umeme katika Kata za Jimbo la Mufindi Kusini

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:-

Serikali imekuwa na mpango kabambe wa kupelekaumeme vijijini:-

Je, ni lini Serikali itawapelekea umeme wananchi waKata Itandula, Nyololo Shuleni, Maduma, Udumka, Kilolo,Kiyowole na Idete?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati,majibu ya swali hilo.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Nishati, napenda kujibu swali la MheshimiwaMendrad Lutengano Kigola, Mbunge wa Mufindi Kusini, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatekeleza Mradi waKusambaza Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA), Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza kuanzia Julai,2017 hadi Juni 2019. Katika Wilaya ya Mufindi jumla ya vijiji 53vitapatiwa umeme kupitia mradi huu unaotekelezwa namkandarasi Kampuni ya Sengerema Engineering GroupLimited aliyepewa kazi za mradi huo kwa Mkoa wa Iringa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la MufindiKusini, mradi utapeleka umeme katika Kata za Makungu,Igowole, Mninga, Nyololo, Isalavanu, Mbalamaziwa naKasanga ambapo Vijiji vya Lugolofu, Mukungu, Lugema,Ibatu, Kisasa, Makalala, Ikwega, Itulituli, Lwing’ulo, Njojo,Nyololo Shuleni, Mjimwema, Idetero, Kimandwete, Ukemele,Udumuka, Lyang’a, Kilolo, Ihomasa pamoja na Maduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi za mradi katika Wilayaya Mufindi zinahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongowa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 139.63, njia ya umemewa msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 170,ufungaji wa transfoma 85 za kVA 50 na 100, pamoja nakuwaunganishia umeme wateja wa awali 2,596. Gharamaya mradi ni shilingi bilioni 11.92. Kwa sasa mkandarasiameshasimika nguzo za umeme wa line kubwa za HT kwaasilimia 90 na nguzo za umeme wa line ndogo LV kwa asilimia95 kwa jimbo la Mufindi Kusini. Kazi ya ufungaji transfoma nakuunganisha wateja itaanza mwishoni mwa Septemba, 2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vingine vya Kata yaItandula, Kiyowole na Idete vitapatiwa umeme katikamzunguko wa pili wa mradi wa REA III unaotarajia kuanzaJulai, 2019 na kukamilika Juni, 2021. Ahsante.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

MWENYEKIT: Mheshimiwa Kigola.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na nitoepongezi kwa mkandarasi ambaye amepangwa kwenyeJimbo langu la Mufindi Kusini kwa kazi nzuri anayoifanya.Tulikuwa tuna tatizo la transfoma pale Ihowanza baada yakumpa taarifa nimepata taarifa kwamba ameshaipeleka napale Mbalamaziwa tulikuwa tuna tatizo la transfomaameshaipeleka na sasa hivi mkandarasi yupo site. Kwa kazihiyo nzuri, naipongeza sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezinaomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali langu lakwanza kuna vitongoji vingi sana kwenye Jimbo langu laMufindi Kusini ambavyo havikufanyiwa survey na tulikuwatumeandika hata majina tukapeleka pale TANESCO, je, vilevitongoji ambavyo vilikuwa vimerukwa mara ya kwanza navyenyewe vitapewa umeme?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ningemuombaWaziri kama atapata nafasi kwa sababu kwenye Jimbolangu la Mufindi Kusini hawajaja, je, atakuja sasa kufanyamkutano akielezea vizuri matumizi haya ya umeme?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yamaswali hayo ya nyongeza.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya MheshimiwaMendrad Lutengano Kigola, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tumepokea pongeziza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo miradi ya REAIII inavyoendelea katika Wilaya ya Mufindi hususani katikajimbo lake. Namshukuru kwa kulithibitishia Bunge lako kamamkandarasi yupo anaendelea vizuri na kweli mkandarasiSengerema ni miongoni wa wakandarasi ambao wanafanyakazi zao vizuri. (Makofi)

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nimpongeze yeyemwenyewe Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia masuala yanishati katika jimbo lake, anafanya kazi vizuri. Ndiyo maanakatika maswali yake ya nyongeza amekiri kwamba kulikuwana tatizo la transfoma kwenye kata alizozitaja na kutokanana maelekezo ya Mheshimiwa Waziri transfoma hizozimeshafika katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake moja ameuliza nilini vitongoji ambavyo havijafikiwa na umeme vitapata?Nataka nilitaarifu Bunge lako Tukufu na Mheshimiwa Mbungekwamba Serikali inaendelea kufanya upembuzi yakinifukwenye Mradi wa densification II baada ya kufanikiwa kwadensification I, ambayo itahusisha mikoa 17 pamoja na Mkoawa Iringa na katika vitongoji ambavyo vitasalia vitapatiwaumeme katika mradi wa ujazilizi awamu ya pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusukutembelea katika Jimbo lake la Mufindi Kusini na hususanWilaya ya Mufindi, nataka nimuahidi Mheshimiwa Mbungekwamba baada ya Bunge hili kwa kweli tutatembelea Mkoawa Iringa kwa sababu mpaka sasa hivi tuna vijiji takribani 20vinatakiwa kuwashwa umeme lakini pia kuna mradi ambaounaendelea wa BTIP ambao kwa kweli umefanya vizuri. Hivyo,nataka nilitaarifu Bunge ipo kazi ya kufanya katika huo Mkoawa Iringa na Jimbo lake la Mufindi Kusini, kwa hiyo, tutakuja.Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwamoto na MheshimiwaJuma Nkamia.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naomba nichukue nafasi hii nimpongezeNaibu Waziri pamoja na Waziri husika kwa kazi nzuri ambayomnafanya ya kuhakikisha wananchi wanapata umeme.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri aliwahikufika baadhi ya vijiji kikiwemo Kijiji cha Kihesa Mgagao naumeme tayari umeshafika. Naomba awaondoe wasiwasi

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

wananchi wa sehemu umeme umefika hasa vitongojikwamba umeme watapata au hawatapata?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Kata za Ukwega,Kising’a, Nyanzwa, Udekwa na Winome hawajapata umemehaujapimwa kabisa. Naomba niulize ni lini wataendakupimiwa ili nao wawe na uhakika wa kuingia kwenye nchimpya ya viwanda?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Nishati, majibu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanaomba nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwamajibu mazuri ya Serikali. Kwa kweli mradi wa REA IIIunaendelea vizuri na umeshaanza katika mikoa yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la nyongeza laMheshimiwa Mwamoto, napenda kwanza nimpongezeMheshimiwa Mwamoto anavyofuatilia masuala ya umemekatika Jimbo lake la Kilolo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nilifika katika Jimbola Mheshimiwa Mwamoto na kijiji cha Nghuruwe pamoja naKihesa Mgagao kulikuwa na changamoto kubwa sana. Kijijicha Nghuruwe kilishapata umeme na sasa wanaendeleakupeleka umeme katika Kijiji cha Kihesa Mgagao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaMwamoto kabla ya mwezi huu kuisha vitongoji vyote vyaKijiji cha Kihesa Mgagao vitakuwa vimeshawashwa umeme.Kadhalika bado vitongoji vyake saba katika maeneo yakaribu na Kihesa Mgagao, navyo tutavitembelea wiki ijayonamhakikishia kwamba na vyenyewe vitapata umeme kablaya mwisho wa mwezi ujao. Nampongeza sana MheshimiwaMbunge. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Juma Nkamia.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru na mimi kunipa nafasi hii niweze kuuliza swalimoja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Chembakwenye Kata za Kidoka, Jangalo na Msaada pamoja namaeneo ya vijiji vyake, kumekuwa na nyaya za umeme kwamuda mrefu lakini tatizo lililopo sasa ni kuwasha tu. Je, Serikaliinanipa majibu gani ya uhakika kwamba ni lini maeneo hayayatapelekewa transfoma ili kuwasha umeme katika maeneohayo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru sana Mheshimiwa Nkamia anavyofuatiliamasuala ya umeme katika Jimbo lake la Chemba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpe taarifaMheshimiwa Nkamia, nivyoongea hivi sasa transfoma tatuzinakwenda katika Kijiji cha Kidoka kwa ajili ya kuwashaumeme, lakini kesho pia wataendelea kupeleka nguzopamoja na transfoma na nyaya katika Kijiji cha Msaada.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kij i j i cha Jangalo,namwomba Mheshimiwa Mbunge tushirikiane baada ya vijijihivi kuwashwa tutaendelea na Kijiji hicho. Wakati kazi hizozinavyoendelea kule Kwa Mtoro nimhakikishie MheshimwaMbunge yapo magenge sita yanafanya kazi hivi sasa ili nayenyewe kabla ya mwisho wa mwezi wa kumi iwezekuwashiwa umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sanaMheshimiwa Nkamia anavyoshirikiana na Serikali. Ahsante.

MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la MheshimiwaShaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto.

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Na. 118

Kata ambazo Hazikupata Umeme wa REA III – Lushoto

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:-

Kata za Gare, Kwai, Kwemashai, Makanya, Kilole,Ngwelo na Ubiri hazikufikiwa na REA III mpaka sasa:-

Je, ni lini sasa Serikali itafikisha umeme kwenye katahizo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Nishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa AlhajiShaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatekeleza Miradi yaKupeleka Miradi ya Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati(REA). Mradi wa REA III mzunguko wa kwanza ulianza Julai,2017. Vijiji vitakavyopelekewa umeme kwenye Jimbo laLushoto ni pamoja na Magamba, Kwegole, Kwehungulu,Kwebarabara, Maboi, Milemeleni, Kungului, Shume A,Makunguru, Shume B, Ngazi, Mhezi, Kwezindo, Kweboi, Nkelei,Viti, Langoni B, Vuli A na Kwemakulo, Mradi huu unatarajiwakukamilika Juni, 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya mradi huuzinahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovoti33 yenye urefu wa kilomita 5.67, njia ya umeme wa msongowa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 46, ufungaji watransfoma 23 za 50 kVA pamoja na kuwaunganishia umemewateja wa awali 520. Gharama za mradi ni shilingi bilioni1.9.

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vijiji vya Kata ya Gare, Kwai,Kwemashai, Makanya, Kilole, Ngwelo na Ubiri vitapatiwaumeme katika mzunguko wa pili wa mradi wa REA IIIutakaoanza Julai, 2019 na kukamilika Juni, 2021. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Shekilindi.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa nimpongeze Naibu Waziri kwamajibu pia niendelee kumpongeza Waziri Kalemani na Naibupamoja na timu yake kwa kutuma wataalam kuja ku-surveykatika Kata za Kwekanga, Mbwei, Migambo, Nguli, Lushoto,Magamba na Mlola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, je, pamojana ku-survey kata zote hizo pamoja na alilozitaja, ni lini sasawananchi wangu watakuja kupimiwa hawa ili wawezekupata umeme kwani umeme ni huduma ambayo walikuwawanaisubiri kwa muda mrefu sasa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mkandarasialiyepewa kazi ya kujenga umeme katika Halmashauri yaWilaya ya Lushoto tokea mwaka jana mpaka leo hiiamejenga kitongoji kimoja tu ambacho ni cha MagambaMabughai. Hii inaonyesha uchelewaji mkubwa sana, je,Serikali haioni sasa kuwa kuna haja ya kubadilisha mkandarasihuyu kuweka mkandarasi mwingine ambaye anaendana nakasi ya hapa kazi tu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Nishati majibu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanapenda kumpongeza sana Mheshimiwa Shekil indianavyofuatilia masuala ya umeme katika Jimbo lake laLushoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tunakubali kupokeapongezi kwa kazi nzuri zinazofanywa na sehemu nyingine yamkandarasi lakini zipo changamoto kweli kwa mkandarasina nimeongea na Mheshimiwa Mbunge. Kwanza nilikuwa

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

nimempa vijiji vinne tu kati ya vijiji kumi na mbili, nimpe taarifaMheshimiwa Mbunge kwa niaba ya wananchi wa Lushototumemuongezea vijiji vingine vinane vipya ambavyovimeshafanyiwa survey na mkandarasi anaanza kuvifanyiakazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu lini vitapelekewaumeme, tunapoongea hapa mkandarasi ameshawekamagenge mawili, anaendelea na usambazaji wa nguzopamoja na kufunga nyaya katika Kijiji cha Magamba pamojana Mabughai. Kwa hiyo, ni matarajio yetu kwamba ndaniya mwezi huu wataviwasha vijiji hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la pilli la uwezowa mkandarasi, ni kweli mkandarasi huyu alianza kwakususasua lakini tumeshakaa naye na ameshawekamagenge kumi na mawili kwenye Jimbo la MheshimiwaMbunge ni matarajio yetu mbali ya kumbadilishatutamsimamia, tutamshinikiza, tutahakikisha kwambaanafanya kazi na anakamilisha ndani ya wakati.

MWENYEKITI: Umeme upo vizuri Waheshimiwa,maswali naomba yawe kwa ufupi, Mheshimiwa Shangazi,Mheshimiwa Almas na Mheshimiwa Ndassa.

MHE. RASHID R. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Mimi naona wivu wenzanguwanapotoa pongezi kwamba maeneo yao umemeumeshapatikana, sasa mimi nina masikitiko makubwakwamba bado katika Jimbo la Mlalo, Halmashauri hiyohiyoya Lushoto, kata nne bado umeme haujawaka katika Kataza Mbalamo, Shagayu, Mbalu na Hemtoe. Barua ya kutokaREA kwenda kwa mkandarasi imetoka tangu mwaka jana.Nataka Mheshimiwa Waziri anipe commitment ni lini katikakata hizi na zenyewe umeme utawaka katika Jimbo la Mlalo,Halmashauri ya Lushoto?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mheshimiwa Shangazi kwa maswali yake mazurina kweli naungana na yeye kwamba kati ya maeneoambayo mkandarasi alikuwa hajaanza kazi rasmi ni pamojana Jimbo la Mheshimiwa Shangazi. Tunapoongea hapa naleo asubuhi tumeongea na Mheshimiwa Shangazi namkandarasi ameshapeleka makundi manne, ni matarajioyetu atafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimuahidi MheshimiwaShangazi kwa niaba ya wananchi wake, mimi baada yaBunge hili kuisha Mheshimiwa Shangazi tutafuatana mimi nanaye tutakwenda kusimamia mguu kwa mguu mpaka vijijivyake vyote ambavyo havijapatiwa umeme sasa vitapatiwaumeme. Awape uhakika wananchi wake kwamba Serikalihii haina mchezo kwenye suala la umeme vijijini.

MWENYEKITI: Safi kabisa Mheshimiwa Waziri,Mheshimiwa Maige.

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushuru sana kuniruhusu niulize hili la nyongeza, lakinikwanza nianze na shukurani kubwa sana, Mheshimiwa Waziriwa Nishati alikuja jimboni kwangu kuzindua REA III. Naombanimuulize Mheshimiwa Waziri kwa nini mkandarasi hajaanzakazi kwenye barabara ile ya kuja nyumbani kwangu, kijiji chakwetu Kasenga, Majengo, Ikongolo, Kanyenye na Nzubuka?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru sana Mheshimiwa Maige kwa swali lake lanyongeza. Kwanza nikubaliane na Mheshimiwa Maige,ameshafanya vijiji kumi na viwili kwenye jimbo lake lakini vijijivya barabara ndiyo anaendelea navyo. Kwa hiyo, ni shaukuya Mheshimiwa Maige na wananchi kwamba vijiji vyotevingepatiwa umeme kwa siku moja. NimhakikishieMheshimiwa Maige kwamba hivi sasa anaendelea na Kijijicha Lipogolo na kuna Kitongoji kinaitwa Kwa Muni ndipoanakosimika nguzo. Kwa hiyo, niungane na Mheshimiwa

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mbunge kwamba ameshamaliza vijiji vya ndani sasaameanza kufanya kazi katika vijiji vya kandokando mwabarabara. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Maige vijijivyake kumi na moja vilivyobaki, vyote vitapelekewa umemekatika round hii ya kwanza.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndassa.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Tarehe 11 Julai, 2017, narudia tarehe 13 Julai,2017 Mheshimiwa Waziri alikuja Nyamatala kuzindua umemeKimkoa na uzinduzi ulifanyika katika Kijiji cha Nyamatala hadileo ni kijiji kimoja tu ambacho kimeshawashwa umeme lakinikisingizio wanasema hakuna nyaya, nguzo na transfoma.Naomba majibu ya Serikali, hivi vijiji ambavyo vilikuwavimepangwa kuwashwa umeme vitawashwa lini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mheshimiwa Ndassa na kwa kweli niseme tukatika Mkoa mzima wa Mwanza nitoe marekebisho kidogoya hoja ya Mheshimiwa Ndasa, ni vij i j i 21 tayarivimeshawashwa umeme siyo kijiji kimoja. Ni kweli kabisakatika jimbo lake Kijiji cha Nyamatala ambapo tulifanyauzinduzi tayari kimeshawashwa umeme na sasa wanaendeleana kijiji kinachofanya kwenda Sangabuye. Nikubaliane naMheshimiwa Ndassa kwamba speed ya mkandarasi haikuwanzuri, lakini tangu wiki iliyopita ameshaleta nguzo 500 katikajimbo lake ni matarajio yetu kwamba sasa speeditaongezeka. Nimwombe Mheshimiwa Ndassa tushikirianeatuletee maeneo yenye changamoto il i kazi i ianzekutekelezwa haraka iwezekanavyo.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, najua wengimna maswali ya umeme lakini muda wetu hauruhusu,tumwamini Mheshimiwa Waziri na Naibu wake wako vizuri,naamini tukija Bunge lijalo maswali yatapungua. (Makofi)

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea Wizara yaMaliasili na Utalii, Mheshimiwa Yahya Omary Massare, Mbungewa Manyoni, sasa aulize swali lake.

Na. 119

Asilimia 70 Inayochukuliwa Mtu Anapokata Mti

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:-

Mjasiliamali au mtu yeyote anapokata mti anatakiwaachukue 70% ya kile anachokilipia:-

(a) Je, ni lini recovery rate ya 30% ya mbaoilifanyiwa utafiti?

(b) Je, ni taasisi gani ilifanya utafiti huo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, napenda kujibu swali la Mheshimiwa YahayaOmary Massare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, lenyesehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mauzo ya miti ya Serikali kwaajili ya kuvuna hufanyika baada ya kufanya tathmini ya ujazowa miti kwa kupima unene na urefu wa miti inayotarajiwakuuzwa. Ujazo huu hauhusishi ujazo wa matawi, majani namizizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zilizowahi kufanywa nawataalam wetu wa misitu kati ya mwaka 1996 hadi 1999wakati wa kutekeleza Mradi wa FRMP (Forest ResourceManagement Programme), zilibainisha kuwa mteja anawezakupata mbao kati ya asilimia 60 – 70 ya ujazo wa mtiuliopimwa kama atachakata magogo hayo kwa kutumia

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

mashine zenye ufanisi wa kiwango cha juu ambazo ni framesaw au band saw. Mashine hizi hupatikana kwenye viwandavikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika viwanda vidogovidogo na vya kati ambavyo hutumia mashine zenye uborawa chini kiwango cha uzalishaji ni kati ya asilimia 20 - 43ambapo wastani ni asilimia 30 ya ujazo wa mti. Utafiti huuulifanywa kati ya mwaka 2005 na 2007 na wataalam kutokaChuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo chaViwanda vya Misitu cha Moshi (FITI). Teknolojia duni, uelewamdogo na usimamizi hafifu ndiyo chanzo cha kuwa na ufanisihuo mdogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia utafiti huona ufanisi wa teknolojia iliyopo sasa ya msumeno wa mkonona msumeno wa duara (circular saw) hauwezi kuzalishambao zenye ujazo wa zaidi ya asilimia 30 ya ujazo wa mtiuliopimwa. Kiwango cha asilimia 30 kitaalam tunakiitarecovery rate.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Massare na MheshimiwaGekul.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo mawiliya nyongeza pamoja na majibu mazuri sana ya MheshimiwaNaibu Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, tofauti yamajibu haya kwamba kuna asilimia 60 na 70 na kuna asilimia30, wadau hawa wanapita katika njia moja na wanachukuavibali sehemu moja na wakaguzi wa vizuia, wanakagua bilakujua huyu katoka kwenye mashine ya kisasa au mashine yakizamani. Kwa mpango huo, inamaanisha kwamba kunamwanya mkubwa sana wa rushwa, kuna mtu atatoka naasilimia 60 na mwingine asilimia 30. Je, sasa Serikali inakujana mkakati gani uliobora kabisa kuepusha watumishi ambaosio waaminifu kufanya kazi ambayo imenyooka kwa dhamira

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

iliyopo sasa ya Awamu hii ya Tano kwamba tunatakawananchi watendewe haki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni lini sasa Serikaliitaona njia bora zaidi ya kusaidia wadau hawa wajasiriamali,wale ambao wana mashine za kizamani wawezekuwezeshwa na kupata mashine hizi za kisasa ili kuondoamkanganyiko huu ambao unasababisha mwanya mkubwawa rushwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi kwa maswali hayo mawili ya nyongeza.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Omary Massare, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hiikumpongeza kwa sababu yeye ni mdau mkubwa sana wamazao yatokanayo na misitu na kwa kweli amekuwaakifanya kazi nzuri sana na amekuwa mshauri mzuri sanakatika masuaa mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mkakati ambaoWizara imeweka, Serikali kwa kweli imeweka mkakatimkubwa wa kuhakikisha tunawahamasisha wananchi wotewahakikishe wanapata teknolojia za kisasa, mashineambazo ni bora kwa sababu hizi mashine zingine kwa kwelizinafanya upotevu mkubwa sana na hasara ni kubwa. Katikasuala hilo ndiyo maana tumeweka mkazo kwamba walewote ambao wanakuwa na zile mashine ambazozinapoteza sana kwa kweli hawaruhusiwi. Pale ambapoitabainika kwamba baadhi ya watumishi wetu katikamaeneo kadhaa wanaruhusu hizo mashine zitumike kwarushwa basi tunaomba mtusaidie kututajia majina ili hatuakali ziweze kuchukuliwa kwa watumishi wa aina hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu namna yakuwasaidia Watanzania hawa, kwa kweli ziko njia nyingi zakuwasaidia Watanzania lakini nitumie nafasi hii

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

kuwahamasisha kwamba wajaribu kutafuta mikopo ya ainambalimbali. Kuna aina nyingi za mikopo sasa hivi, kuna ilemikopo inayotolewa na Halmashauri, kuna mifuko mingiinatoa mikopo basi wachukue mikopo ili waweze kupatamashine ambazo ni bora ambazo zitawafanya wapatemazao mengi zaidi kuliko mashine ambazo ziko hivi sasa.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Gekul, swali fupi lanyongeza.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kumekuwa na kauli ya Serikali kwamba kilaHalmashauri wapande miti 1,500,000 kwa ajili ya kuhifadhimazingira yetu. Nafahamu Wizara hii, Wizara ya TAMISEMIpamoja na Mazingira wanahusika na hawa wana mbeguza miti mbalimbali. Kwa nini msione umuhimu wa kutoa mitikatika Halmashauri zetu hiyo 1,500,000 ili tuipande na kuhifadhimazingira kwa sababu mkitegemea Halmashauri watoefedha, wanunue hiyo miti Halmashauri zetu hazina fedha,kwa nini msitupe hiyo miti 1,500,000 tupande?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo kwa ufupi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaPauline Gekul, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa ni sera yaSerikali kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchinizinapanda miti angalau kila Halmashauri 1,500,000 lakinikumekuwa na upungufu wa miche ya kupanda. Hivi sasakama Serikali tumechukua hatua kwa kutumia Wakala wetuwa Misitu kuhakikisha kwamba wanashirikiana naHalmashauri kwanza kwa kuwapatia mengi lakini katikamaeneo mengi kuwapa miche ile ambayo tayaritumeshaiotesha ili kusudi zile Halmashauri ziende kufanya kaziile ya kupanda katika maeneo mbalimbali. Siyo tu suala lakupanda lakini baada ya kupanda pia Halmashauri

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

zihakikishe kwamba zinailinda ile miti na kuhakikisha kwambakweli inakua sio tu inapandwa halafu inaachwa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa muda wetu unaendeleakwisha. Tunaendelea na Mheshimiwa Mbaraka Kitwana Dau,Mbunge wa Mafia sasa aulize swali lake.

Na. 120

Papa Aina ya Potwe

MHE. MBARAKA K. DAU aliuliza:-

Papa aina ya potwe (whale shark) ni samaki ambayeduniani kote anapatikana Australia na Tanzania katika Kisiwacha Mafia tu:-

Je, ni lini Serikali itakuja na mpango mkakati wakumtangaza samaki huyo pamoja na vivutio vingine vyautalii kama vile scuba diving na sport fishing duniani ili kuvutiawatalii nchini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yaswali hilo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, napenda kujibu swali la MheshimiwaMbaraka Kitwana Dau, Mbunge wa Mafia, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, papa aina ya potwe (whaleshark) anapatikana katika maeneo mbalimbali dunianihususan nchi zilizoko katika maeneo ya tropiki kama Australia,Taiwan, Pakistan, India, Ufilipino, Indonesia, Afrika Kusini,Kenya, Msumbiji na kwa Tanzania anapatikana katika Visiwavya Mafia (Kilindoni), Pemba na Zanzibar. Samaki huyu nimmoja kati ya samaki wakubwa sana duniani na uzito wakeunaweza kufikia mpaka tani zaidi ya 20 na urefu kufikia zaidiya mita nane na hivyo kuwa kivutio kikubwa cha watalii.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Bodi ya UtaliiTanzania inaendelea kutangaza vivutio vya utalii ndani nanje ya nchi vikiwemo vivutio vya Wilaya ya Mafia ikijumuishapapa aina ya potwe kwa kutumia mikakati mbalimbali yautangazaji kama vile vipeperushi; majarida mfano (AfrikaAsilia, Selling Tanzania, Tan Travel, Tanzania Explore Magazinena Tanzania Map; tovuti yenye anuaniwww.tanzaniatourism.com; mitandao mbalimbali ya kijamiimfano youtube, instagram, twitter, facebook; Tanzania TourismApp inayopatikana kwenye Google Play Store kwenye simuza mkononi aina ya smart phone. Vilevile, utangazajihufanyika kwa kutumia maonesho mbalimbali ndani na njeya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana namikoa na wilaya inaendelea kubaini maeneo ya fukwe katikamwambao wa bahari ya Hindi kwa ajili ya uendelezaji washughuli za utalii kama vile kuzamia (scuba diving), kuogelea(swimming), michezo ya kuvua samaki (sport fishing), kupigambizi (snorkeling) na sunbathing. Aidha, Serikali inaendeleakutoa elimu kwa wananchi hususan wavuvi ili kuwatunzasamaki aina ya papa potwe. Hivi karibuni, Serikali itazinduastudio ya utalii, channel ya utalii itakayokuwa chini ya Shirikala Utangazaji Tanzania (TBC) na utambulisho wa Tanzania(Destination Branding). Hatua hii itaongeza ufanisi katikakutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dau, swali la nyongeza.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninamaswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, moja yamatishio ya samaki aina hii ni anapoingia katika mitego yawavuvi huwa anajeruhiwa kwa sababu wao wanakuwahawamli lakini anapata majeraha katika kumnasua kwenyezile nyavu. Matokeo yake kwa kuwa ngozi yake iko verydelicate, akipata michubuko anakufa. Sasa kwa kuwasamaki huyu ni wa season anapatikana kuanzia miezi ya

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

mwanzo ya Septemba mpaka Machi, je, Serikali haioni sasaipo haja ya kutengeneza quota system ambapo msimu wapotwe maeneo ya Kilindoni anapopatikana papigwemarufuku ya kuvua samaki wengine ili kumnusuru samaki huyukwa sababu huenda akaondoka Mafia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, utalii katikaKisiwa cha Mafia una gharama kubwa sana. Kila mtaliianayeingia eneo la hifadhi ya bahari analazimika kulipa dola24 kwa siku moja. Kutokana na ughali huu, inalazimishabaadhi ya watalii kuanza kushindwa kuja Mafia. Je, Serikalisasa ina mpango gani kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugona Uvuvi kupunguza kiwango hiki cha entrance fees za kuingiamaeneo ya marine park ili kuweza kuvutia watalii wengi kujaKisiwani Mafia? Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Uvuvi majibu.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza yakaka yangu Mheshimiwa Mbaraka Kitwana Dau kamaifuatavyo;

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongezaMheshimiwa Naibu Waziri wa Utalii Mheshimiwa Hasunga kwamajibu mazuri ya msingi hasa pale aliposema anaitaka jamiiiweze kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa samaki hawa aupapa huyu anayeitwa papa potwe ama pia ninachukuapongezi nyingi sana kwa kaka yangu Dau kwa kuwa mshirikamzuri wa kulinda rasilimali zetu za Taifa ambazo zimekuwani kivutio kikubwa cha watalii katika visiwa vyetu hivi vyaMafia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala alilolisema lakuweka utaratibu maalum Wizara yetu tunalichukua ili kusudisasa tuwe na wakati wa uvuvi katika eneo la Kilindoni nakuna wakati ambapo tutazuia ili kuwapisha papa potwewaweze kustawi. Bila ya kufanya hivyo, papa potwewatahama Mafia na tutasababisha utalii wa papa potweuweze kutoweka katika eneo hili la Mafia. (Makofi)

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili juu ya tozombalimbali ambzo zinachukuliwa na Wizara yetu kupitiakitengo chetu cha MPRU kwa maana ya hifadhi ya baharina zile zinazokwenda Wizara ya Utalii, mimi naombanimhakikishie kwamba sisi Wizara yetu ya Mifugo na Uvuvina Wizara ya Maliasili na Utalii tutakaa kwa pamoja nakufanya review ya hizi tozo na kodi hizi zinazohusika katiakutalii huu ili kusudi tuweze kuhakikisha kwamba wataliiwaweze kuvutika kwa wengi zaidi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Yussuf swali fupi lanyongeza.

MHE. YUSSUF HUSSEIN SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, kidogo nimeguswa hapa. Huyu papa ni papammoja na hadhuru mwanadamu na mara nyingi kwa kulekwetu sisi huwa mwezi Desemba wanatoka Somaliawanakuja zao mpaka wanakuja kupiga kambi Minai –Zanzibar wanakuwa kwa wingi sana na huyu papa huwaanawafuata wale dolphins. Mara nyingi huwa anawafuatawale dolphins, swali langu kwa Mheshimiwa Waziri, kipindicha Desemba mpaka Februari wanakuja na kurudi ni kipindiambacho tunaweza tukafanya utalii mkubwa sana katikaeneo letu la kuanzia mpakani na Kenya Duga mpakaZanzibar. Je, Wizara yako imejipangaje sasa kutumia fursa hiiambayo wale dolphins na huyu papa wanatangaza nchiyetu wenyewe, sisi tutumie tu hiyo fursa. Lini tutatumia hiyofursa ya kujenga hoteli katika ukanda huo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba katika kipindi hiki hawapotwe wanakuwa wengi sana katika maeneo haya auwanakuja katika maeneo haya. Pia kuna vivutio vingi sanaambavyo vipo katika ukanda wa bahari yetu hasa katikafukwe zetu hizi za bahari ambazo tunaweza tukafanya nandiyo maana Serikali sasa hivi iko mbioni katika kuhakikishakwamba tunaanzisha mamlaka ya kusimamia fukwe zoteza bahari kusudi tuweze kufaidika na huu utalii wa baharini

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

ambao tulikuwa hatujautumia kwa muda mrefu sana. Kwahiyo, naamini katika hizi jitihada, pale ambapo zitakuwazimekamilika na sheria itakapokuwa imeletwa hapa Bungenibasi hizi jitihada zitakuwa zimekwenda sambamba na hilowazo la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziriwa Maliasili. Tunaendelea na Wizara ya Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, Mbunge wa Msalala sasaaulize swali lake.

Na. 121

Kuanzisha Mkoa Mpya wa Kipolisi Kahama

MHE. EZEKIEL M. MAIGE aliuliza:-

Jeshi la Polisi kupitia IGP Ernest Mangu ambaye alifanyaziara Wilayani Kahama mapema mwezi Agosti, 2016alitangaza kuanzisha Mkoa mpya wa Kipolisi wa Kahamana Wilaya za Kipolisi za Msalala, Ushetu na Kahama; na wilayahizo mpya za kipolisi zinakabiliwa na uhaba mkubwa waaskari na vitendea kazi vyao hasa vyombo vya usafiri:-

(a) Je, ni watumishi wangapi wamepangwaWilaya mpya ya Kipolisi ya Msalala?

(b) Je, Serikali iko tayari kusaidia vyombo vyausafiri hasa magari na pikipiki Wilaya ya Kipolisi ya Msalala?

(c) Je, Serikali imejipangaje kujenga ofisi za polisiwilaya na nyumba za makazi kwa askari katika Wilaya zaMsalala, Ushetu na Kahama Mjini?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, Mbunge wa Msalala,lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua uhitaji wahuduma ya kipolisi katika maeneo ya Ushetu, Msalala naKahama. Aidha, maombi ya Msalala kuwa Wilaya ya Kipolisiyameshakamilika na maombi ya Kahama kuwa Mkoa waKipolisi yanaendelea kuzingatiwa. Kwa sasa Wilaya ya Msalalaina jumla ya maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali57.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nia ya Serikali kuona kuwavitendea kazi kwa Jeshi la Polisi vinapatikana ili kurahisishautoaji wa huduma za polisi kwa wananchi. Wilaya mpya yaMsalala imepatiwa mgao wa gari moja jipya na taratibu zausajili zitakavyokamilika gari hilo litapelekwa Msalala kwaajili ya kuhudumia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Msalala, Ushetu nakahama Mjini ni miongoni mwa wilaya 65 nchini ambazohazina majengo ya vituo vya polisi vyenye hadhi ya wilaya.Hata hivyo, halmashauri ya wilaya imeshatenga eneo kwaajili ya ujenzi wa kituo na makazi ya askari na ujenzi utaanzamara pale fedha zitakapokuwa zimepatikana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Maige, swali la nyongeza.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibuyake mazuri na hasa hili la kukubali ombi la kutuletea angalaugari moja kwa ajili ya kusaidia shughuli za polisi. Pamoja nahayo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwakutambua kwamba Jeshi la Polisi lina idadi ndogo sana yaaskari, wananchi wa Msalala pamoja na kanda nzima yaziwa walishaanzisha utaratibu wa ulinzi wa jadi (Sungusungu)ambao ni askari wa kujitolea na husaidia sana shughuli zapolisi kukabili matukio pale ambapo polisi wanakuwahawajafika. Kwa bahati mbaya sana Wizara ya Mambo ya

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Ndani na Jeshi la Polisi limekuwa likitoa ushirikiano mdogosana kwa watu hawa ambao wanafanya kazi kwa kujitoleana mara nyingi wamekuwa wakiwa-harass pale tukiolinapotokea badala ya kuwatafuta wahalifu wanakwendakukamata wale viongozi wa Sungusungu na kuwalazimishaau kuwataka kwamba wasaidie kutaja au kutoa taarifaambazo zingeweza kusaidia Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua Serikali auWizara inachukua au ina mkakati gani wa kushirikiana naJeshi la Sungusungu ili kusaidia jitihada ambazo tayari zipokwa sababu pia askari wenyewe wa polisi si wengi kamaambavyo jibu limejitokeza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kumekuwepona matukio mengi ya askari polisi kubambikizia wananchikesi mbalimbali jambo ambalo limekuwa likiwavunja moyosana wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi, jambo hililimekuwa likijitokeza kwenye vituo mbalimbali hasa vilivyokoKata ya Isaka , Kata ya Bulige na hata Kata ya Bulyanhulu.Je, ni lini Mheshimiwa Naibu Waziri atakuja kukutana nawananchi wa maeneo hayo ili kuweza kusikia kero hii nakuweza kukemea askari hao wenye tabia mbaya? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwaufupi ya maswali hayo mawili ya nyongeza.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaMwenyekiti, kuhusiana na swali lake la kwanza natakanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba siku zotetumekuwa tukihamasisha na tunaona umuhimu wa ushirikiwa wananchi katika kushirikiana na vyombo vya dolakukabiliana na uhalifu nchini na ndiyo maana kupitiaKamisheni yetu ya Polisi Jamii ambayo tunayo, tumekuwatukiandaa utaratibu mzuri, ili utaratibu huo ambao umekuwaukitumika wa kushirikisha wananchi, ikiwemo Polisi Jamii,ikiwemo Sungusungu, uweze kufuata misingi ya kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kupitia Kamisheni yetuhii ya Polisi Jamii tumekuwa tukitoa miongozo mbalimbali,

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

ili wananchi waweze kutekeleza majukumu yao bilakukinzana na sheria za nchi yetu. Kama kutakuwa kunamambo yametokea ambayo yanaweza kuwayamesababishwa aidha na kutokana na uelewa mdogo waufahamu wa sheria wa jinsi ya hawa ambao wanaisaidiaPolisi kutekeleza hizi shughuli za Polisi Jamii ama itakuwamengine yametokea labda kwa makosa mengine, labdaMheshimiwa Mbunge labda atuwasil ishie tuwezekuyashughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali lake la pilikuhusiana na ubambikaji kesi, binafsi nilifanya ziara katikaMkoa wa Shinyanga na moja katika mambo ambayoniliyakemea baada ya kutembelea baadhi ya vituo namagereza katika maeneo ya Mikoa ile ya Kanda ya Ziwa nakupata malalamiko ya baadhi ya wananchi ambaowalikuwa wamesema wamebambikiwa kesi, moja ni jambohili ambalo tulilichukulia kwa uzito unaostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba, ombi lake la kutaka nifanye ziara katikajimbo lak mahususi, kwa ajili ya kufanya kazi hii ambayotumeshaifanya katika maeneo mengine ya Mkoa waShinyanga na mikoa mingine nchini ambayo imesaidia sanakupunguza malalamiko haya kwa wananchi tutaifanyabaada ya Bunge hili kumalizika tutaandaa hiyo ziara yakwenda jimboni kwake kwa ajili ya kushughulikia jambo hilimahususi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ungando, swali fupi lanyongeza.

MHE. ALI S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Swali langu la nyongeza. Sasa hivi Kibiti imekuwaKibiti salama, je, Serikali ina mpango gani wa kuboreshamaslahi ya Polisi?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuhakikishakwamba, inaboresha maslahi na mazingira ya utendaji kazi

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

wa vyombo vyetu vya Polisi hatua kwa hatua na kadiri yauchumi wa nchi utakavyokuwa unaimarika.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa MaulidSaid Mtulia, Mbunge wa Kinondoni, swali lake litaulizwa naMheshimiwa Zainab Vullu.

Na. 122

Serikali Kuzuia Biashara ya Ukahaba

MHE. ZAYNAB M. VULLU (K.n.y. MHE. MAULID S. MTULIA)aliuliza:-

Serikali inafanya juhudi kubwa ya kuzuia biashara yaukahaba kwa kuwakamata wauzaji na wanunuzi nakuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. Pamoja na jitihadahizo bado biashara hiyo haramu inaendelea kwa kasi ileile:-

Je, Serikali ina mpango gani mbadala wa kuzuiabiashara hii haramu?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuwa kwa mudamrefu Serikali imekuwa ikipambana na watu wanaojihusishana vitendo vya ukahaba nchini. Jeshi la Polisi limekuwalikifanya misako kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwakubaini na kukamata watu ambao wanajihusisha na vitendohivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ukahaba ni sualamtambuka ambapo kulikabili kunahitaji ushirikiano wawadau wengi. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitiaJeshi la Polisi, imeandaa mkakati wa kushirikisha taasisi

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

nyingine za Serikali kama vile TAMISEMI, Wizara ya Katiba naSheria, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii na kupunguzahatimaye kumaliza vitendo hivi ambavyo vinautia doautamaduni wa nchi yetu. Aidha, mkakati huu unahusishaujenzi, kutoa elimu ya madhara ya ukahaba, faida zaujasiriamali na kuwashirikisha viongozi wa dini katikakufundisha maadili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zaynab Vullu.

MHE. ZAYNAB M. VULLU: Mheshimiwa Mwenyekiti,asante sana. Kwa kuwa, biashara mara nyingi ni muuzaji namnunuaji; na kwa kuwa, biashara ya ukahaba mara nyingiinaita machangudoa; na kwa kuwa, katika bahari kunachangudoa, kuna changuchole, kuna changufatundu. Je,Serikali haioni kuna haja sasa ya hawa machangu wenginewakakamatwa na wakapewa elimu ya kutosha, waachanena vitendo vya ukahaba kwa sababu, wao kamahawakwenda sokoni, hii biashara haitakuwepo. Je, Serikaliina mpango gani sasa wa kuhakikisha wasichana wotewanawawezesha kwa mikopo na elimu ya ujasiriamali,pamoja na juhudi alizozisema Mheshimiwa Naibu Waziri?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, pamoja najuhudi za Serikali, Taasisi Zisizo za Kiserikali, na baadhi ya raiakumekuwa na mkusanyiko mkubwa wa biashara hii maeneombalimbali, ikiwemo eneo maarufu kwa Uwanja wa Fisi,Mburahati, Dar-es-Salaam na biashara hii inafanyika katikatiya maeneo wanayoishi wananchi. Je, Serikali haioni sasa kunahaja ya kwenda katika maeneo hayo kwa kushirikiana nawadau mbalimbali kuvunja hayo maeneo, kujengamiundombinu ambayo itawawezesha wasichanawaliojiingiza katika biashara hizo kwa kutokutarajia kutokanana hali ngumu ya maisha na pia wataepukana na maradhiya UKIMWI; Serikali ikiweza kujenga hiyo miundombinu nakuwapa mikopo hawa wasichana haioni kwamba, tutakuwatumekwamua Taifa ambalo tunalitegemea? (Makofi)

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, manenomazito hayo.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza swali lake na concernyake Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na janga hil i.Naungana mkono na yeye kabisa kuhusiana na umuhimuwa kushughulika sio tu na wauzaji, lakini wanunuzi, lakini situ na wanunuzi, mpaka na mazingira ambayo walewanayaweka. Maana kuna wengine sio wanaouza, kwamfano wenye madanguro, ni watu ambao sio wauzaji nasio wanunuzi, lakini wanahamasisha hivi vitendo. Kwa hiyo,yote hayo na wote ambao wanashiriki kwa namna mojaama nyingine katika hii biashara kuna haja ya kuhakikishakwamba, tunachukua hatua na ndivyo ambavyo Serikaliinafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kumekuwa nachangamoto mbalimbali ambazo nadhani Bunge hili niwakati muafaka wa kuzitafakari. Moja ni changamoto yasheria; labda nitoe mfano wa sheria ambazo penginezinakwaza mapambano dhidi ya vita ya makahaba.Ukiangalia kwenye Kanuni ya Adhabu Namba 176(a), Suraya 16, adhabu ambayo inatakiwa itolewe kwa watu ambaowanafanya biashara ya madanguro wanasema ni fine isiyozidi500/= ama iwapo ni kosa la mara ya pili na kuendeleaatatozwa fine isiyozidi 1,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mtaona kwamba,adhabu kama hii inaweza kuwa inahamasisha utendaji wahuu uhalifu. Kwa hiyo, kuna haja ya Mheshimiwa Mbunge naBunge lako Tukufu kuangalia na kutafakari juu ya sheria hiziambazo zimepitwa na wakati ili hatimaye kazi kubwaambayo inafanywa ya kuwakamata hawa makahaba kilasiku, pamoja na wahamasishi wanaoshiriki na wanunuziiweze kuwa na tija kwani mara nyingi wanapokamatwawanarudia tena makosa kwa sababu, ya wepesi wa sheriazilizopo. Kwa hiyo, kimsingi hilo ni jibu la swali lake la kwanza.

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusiana na elimu;nimhakikishie kwamba, tunaendelea kutoa elimu, lakinivilevile na mamlaka nyingine kama ambavyo nimezungumzakatika swali la msingi kwamba, kwa sababu, suala hili nimtambuka tumekuwa tunashirikiana kama Serikali namamlaka nyingine na taasisi mbalimbali, ili kuweza kutoaelimu kwa jamii juu ya madhara haya, ikiwemo kuwashirikishavilevile viongozi wa dini ambapo nilizungumza kwamba,viongozi wa dini ni sehemu muhimu sana katika kutoa elimuya maadili juu ya wananchi.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, muda sio rafiki.Tunamalizia swali letu la mwisho, Mheshimiwa Saed AhmedKubenea, Mbunge wa Ubungo, sasa aulize swali lake.

Na. 123

Kukithiri kwa Vitendo vya Uhalifu

MHE. SAED A. KUBENEA aliuliza:-

Kumekuwepo na vitendo vingi vya uhalifu hapa nchinikwa watu kuvamiwa, kupigwa, kujeruhiwa na kuporwa malizao na hata kuuawa:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kukomeshavitendo hivyo vya uhalifu ambavyo vinatishia usalama waraia na mali zao?

(b) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongezajuhudi za ulinzi wa raia na mali zao ili kudumisha amani nautulivu nchini?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Saed Ahmed Kubenea, Mbunge wa Ubungo,lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Jeshila Polisi ina mipango mbalimbali ya kukomesha vitendo vyauhalifu kwa kuimarisha doria za miguu, pikipiki na magari,pia kufanya misako dhidi ya uhalifu na wahalifu. kutoa elimukwa jamii kuhusu mbinu za kukabiliana na uhalifu, kufanyaoperation za mara kwa mara na kushirikisha jamii kwenyeulinzi wa maeneo yao kupitia dhana ya Polisi Jamii.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendeleakufanya juhudi za kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao kwakuendelea kuajiri askari na kuongeza vitendea kazi pia, kwakutumia falsafa ya kugatua madaraka. Serikali imeshapelekawakaguzi katika tarafa, jimbo, kata, shehiya ili kushirikikikamilifu kwa kuyabaini maeneo tete ambayo huwa nivyanzo vya uhalifu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kubenea.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Pamoja na majibu ya Naibu Waziri, swali langumsingi wake ni kwamba, wananchi ambao wameumizwa,wametekwa, wamepotea, sio suala la kuimarisha Vituo vyaPolisi kwenye ulinzi shirikishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwasasa Serikali inalinda viongozi wake wakuu ardhini na angani;na kwa kuwa, sasa baadhi ya wananchi, hasa wale ambaowamekuwa na misimamo mikali ya kuikosoa Serikali, kamawaandishi wa habari, wanaharakati na hasa viongozi auwanasiasa wa upinzani. [Maneno haya sio sehemu ya TaarifaRasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu je, Serikali inampango gani wa kushikika wa kulinda raia hawa ambaowamekuwa wakijitolea kutetea nchi yao kwa maslahi yaWatanzania wote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni lini Serikaliitakamilisha uchunguzi na kuleta ripoti Bungeni ya matukioya kihalifu yanayofanana na ugaidi ambayo wamefanyiwa

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

watu mbalimbali, akiwemo Mheshimiwa Tundu Lissu,Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, AbisalomKibanda na Dokta Stephen Ulimboka na wengineo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu yamaswali hayo ya nyongeza.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nataka nichukuefursa hii kumpinga na kumkosoa vikali kabisa MheshimiwaSaed Kubenea, kutokana na utangulizi wa swali lake ambaloameuliza; na kimsingi Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania, kupitia Jeshi la Polisi, imekuwa ikihakikisha inalindausalama wa raia wote na mali zao. Hakuna matabaka katikakusimamia ulinzi wa raia na mali zao, hiyo ndio kazi ya Jeshila Polisi ya kila siku kwa hiyo, kusema kwamba kuna watuwanakosoa Serikali, sijui kuna watu wana nini, hizo ni kaulipotofu na si sahihi na nadhani kwa mamlaka yakoungeelekeza hata zifutwe katika Hansard. Kwa sababu, niupotoshwaji mkubwa kwa jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika hilo suala lakulinda usalama wa raia na mali zao jitihada kubwazimekuwa zikifanyika. Imani yangu ni kuwa kwa kadriambavyo tunakwenda mbele tumekuwa tukifanya hivyo kwakutumia mbinu mbalimbali za kitaalam, kukusanya taarifaza kiintelijensia, kufanya doria, kuangalia maeneo tete,kuangalia takwimu, kumbukumbu za uhalifu nchini na ndiomaana mpaka leo nchi yetu imeendelea kuwa salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoelekea katika Serikaliya Uchumi wa Viwanda, Serikali ya Uchumi wa Kati, tunaaminikabisa kutakuwa kuna mabadiliko makubwa sana yakiteknolojia katika utekelezaji wa majukumu yake kwenyevyombo vyetu vya dola. Kwa hiyo, tutakapoimarisha nakuwekeza katika maeneo ya teknolojia tunaamini kabisa kazihii itafanywa katika mazingira mepesi zaidi.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu uchunguzi. Kaziya uchunguzi imekuwa ikiendelea kufanyika, ingawa kazi yauchunguzi kama alivyozungumzia yeye katika eneo mahususila ugaidi, lina changamoto nyingi kwa sababu, tuhuma zaugaidi zinahusisha taarifa nyingine ambazo zinatoka katikamamlaka za nchi nyingine, lakini na taasisi nyingine nje yaJeshi la Polisi. Kwa hiyo, katika kufanya uchunguzi ambaounahitaji taarifa kupata katika nchi nyingine, kupata katikamamlaka nyingine, si jambo ambalo linaweza likawalimefanyika kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, mpaka sasakutokana na matukio mengi yaliyojitokeza kuna hatua kubwaimeshafikiwa katika uchunguzi wa kesi mbalimbali, zikoambazo zimeshafika mwisho, ziko ambazo zinaendeleakuchunguzwa. Pale ambapo uchunguzi utakamilika hatuazitachukuliwa kwa wahusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe wito kwa watu woteambao wanahusika kutoa ushirikiano kwa mamlaka katikakutekeleza majukumu yake. Mfano huu ambaoameuzungumzia wa kesi ya Mheshimiwa Tundu Lissu,tumekuwa mara nyingi tukitaka ushirikiano kutoka katikachama hiki ambacho Mheshimiwa Kubenea anatoka, ilituweze kupata watu ambao wanaweza kutusaidia kutupataarifa, ikiwemo dereva yule ambaye alikuwa na MheshimiwaTundu Lissu, lakini wenyewe wamekuwa wakifanya jitihadaza kufifisha kupatikana kwa dereva huyo. Kwa hiyo,ushirikiano kwa wananchi ikiwemo na wewe mwenyeweMheshimiwa Mbunge na chama chake ni muhimu katikakukabiliana na kuharakisha uchunguzi wa kesi yetu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri kwamajibu sahihi na naagiza maneno yote ya upotoshajialiyoyatoa katika maswali yake ya nyongeza yafutwe kwenyeHansard.

Waheshimiwa Wabunge, tumemaliza wakati wetuwa maswali na sasa ni wakati wa Matangazo. Tutaanza na

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Matangazo ya Wageni waliopo Bungeni asubuhi hii, tunaanzana wageni walioko Jukwaa la Mheshimiwa Spika:-

Tuna mgeni wa Mheshimiwa Spika, Mbunge ambayeni SACP Gils Muroto, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.Karibu sana Kamanda wetu wa Mkoa wa Dodoma katikaBunge letu. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Watapata tabu sana.

MWENYEKITI: Ahsante sana Waheshimiwa Wabungekwa makofi hayo kwa Kamanda wetu.

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge ni wageniwatano wa Mheshimiwa Joseph Kakunda, Naibu Waziri Ofisiya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kutoka Jimbola Sikonge, wakiongozwa na Ndugu Thomas Juma Mayunga,ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya MsingiElimu Maalum Sikonge, mwenye ulemavu wa ngozi nabingwa wa mbio za mita 100 Kitaifa mwaka 2017/2018kwenye mashindano maalum ya UMISHUMITA. Karibu sanamwanafunzi wetu katika Bunge letu na hongera sana kwakazi nzuri. (Makofi)

Wageni sita ni wa Mheshimiwa Elias Kwandikwa,Naibu Waziri wa Ujenzi, ambao ni viongozi wa Chama chaWastaafu kutoka Kahama na Ushetu na wapiga kura wakewakiongozwa na Ndugu Wanga Mathew. Karibuni sanawageni wetu. (Makofi)

Wageni 17 wa Mheshimiwa Anthony Mavunde, NaibuWaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na Ajira, ambao niWanakwaya wa New Testament ya Kanisa la Mlimwa C,wakiongozwa na Ndugu Stanford Mirambwe. Karibuni sanawanakwaya wetu. (Makofi)

Wageni watano wa Mheshimiwa Sonia JumaMagogo, ambao ni ndugu zake kutoka Ilala, Jijini Dar-es-Salaam. Karibuni ndugu zetu. (Makofi)

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Wageni watano wa Mheshimiwa VenanceMwamoto, kutoka Chama Cha Wasioona Tanzania,wakiongozwa na Ndugu Clement Ndahani. Sijawaona(Makofi)

Wageni watano wa Mheshimiwa Zaynab Bakar,ambao ni familia yake kutoka Pemba. Wale pale, karibunisana wanafamilia wetu. (Makofi)

Mgeni mwingine ni wa Mheshimiwa Stanslaus Mabula,ambaye ni ndugu Stephen Kabindile, mdogo wake, kutokaJijini Mwanza. Karibu sana mdogo wetu. (Makofi)

Wageni wanne wa Mheshimiwa Aeshi Hillary, ambaoni jamaa zake kutoka Mkoa wa Tanga, wakiongozwa naMzee Jakubu Othman. Karibuni wazee wetu katika Bungeletu. (Makofi)

Mgeni mwingine ni mgeni wa Mheshimiwa WillyQambalo, ambaye ni ndugu yake kutoka Jijini Dar-es-Salaam,ndugu Jaferson Makere. Karibu, yuko pale juu. (Makofi)

Mwingine ni mgeni wa Mheshimiwa Amina Makilagi,ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwigobero, Musoma,Mkoani Mara, Ndugu Mfungo Bunini. (Makofi)

Wageni wengine ni waliotembelea Bunge kwa ajiliya mafunzo. Wajumbe 30 wa Baraza la Wazazi la ChamaCha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kimara, Jijini Dar-es-Salaam.Karibuni Wajumbe wetu wa Baraza la Wazazi. (Makofi)

Pia kuna wanafunzi 100 na Walimu nane kutoka shuleya Jumapili ya kanisa la Moravian, Jimbo la KaskaziniDodoma. Karibuni sana wanafunzi wetu. (Makofi)

Vile vile wapo wanafunzi 84 na Walimu 10 kutokaShule ya Green View English Medium Primary School ya JijiniMwanza wakiongozwa na Mwalimu Mkuu wao, MwalimuKennedy Joshua. Karibuni sana wanafunzi wetu kwa ajili yamafunzo katika Bunge letu. (Makofi)

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Wapo pia wageni sita kutoka Kisasa, Jijini Dodoma,ambao wamekuja kujifunza namna Bunge linavyoendeshwa,wakiongozwa na ndugu Glory Shayo. Karibuni sana kwa ajiliya mafunzo yenu. (Makofi)

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye niSpika wa Bunge la Wanachuo cha Ardhi, ndugu KamaraMuberwa. Karibu sana Spika la Bunge la Wanachuo. (Makofi)

Wengine ni Wakazi tisa (9) wa Mkoa wa Arushaambao wamekuja kujifunza namna Bunge linavyoendeshashughuli zake. Wakazi tisa wako pale, karibuni sana kwa ajiliya mafunzo. (Makofi)

Wanafunzi wawili (2) kutoka Chuo Kikuu cha Dar esSalaam wanaosomea Sheria mwaka wa nne (4). Karibunisana wanafunzi wetu. (Makofi)

Tangazo lingine ni tangazo la WaheshimiwaWabunge, mnatangaziwa kwamba Wizara ya Maliasili naUtalii imeandaa Tamasha la Urithi ili kuenzi utamaduni naurithi wa Mtanzania. Tamasha hili linaitwa Urithi Festivalcerebrating our Heritage na litakuwa linafanyika mweziSeptemba kwa kila mwaka kuanzia mwaka huu 2018.Dhumuni la Tamasha ni kuenzi na kunadi kiutalii hazina kubwaya utamaduni mila na desturi za makabila yote nchini,ambayo ni zaidi ya 128. Tamasha litasherehekewa mwezimzima wa Septemba.

Uzinduzi rasmi utakuwa kesho tarehe 15 Septemba,2018 katika uwanja wa Jamhuri ambapo Mgeni Rasmianatarajiwa kuwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hivyo, Mheshimiwa Spika anawatangazia Wajumbe waKamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii kushiriki katika uzinduzi huo.Aidha, Waheshimiwa Wabunge na Mawaziri wotewatakaokuwepo kesho wanaombwa kujumuika na MgeniRasmi saa 3.00 asubuhi katika kuadhimisha siku hii muhimukwa Taifa letu. Pia wote mnahamasishwa kuvaa nguo za

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

asili na utamaduni katika siku hiyo ya uzinduzi ili kutoahamasha kwa wananchi kuthamini mavazi ya asili. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kukamilishamatangazo hayo, sasa namkaribisha Mheshimiwa Spikaaweze kuendelea na shughuli zilizobaki. (Makofi)

Hapa Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti

SPIKA: Katibu.

KATIBU WA BUNGE:

TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mwongozo waSpika.

SPIKA: Katibu.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mwongozo waSpika.

KATIBU WA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa mujibuwa Kanuni ya 29(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo laJanuari 2016, naomba kutoa taarifa kwamba shughuli zotezilizowekwa kwenye Orodha ya Shughuli za Mkutano wa 12wa Bunge sasa zimemalizika.

SPIKA: Katibu.

KATIBU WA BUNGE:

HOJA YA KUAHIRISHA BUNGE

SPIKA: Hoja ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa WaziriMkuu karibu. (Makofi)

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, leo hii tunafikiatamati ya Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge lako Tukufuambao ulianza kikao chake cha kwanza tarehe 4 Septemba,2018. Hivyo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungumwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuhitimisha shughulizote zilizopangwa kwenye Mkutano huu tukiwa na afyanjema.

Mheshimiwa Spika, vile vile nashukuru sana nanikushukuru wewe binafsi kwa umahiri wako mkubwa wakuliongoza Bunge hili Tukufu, ukisaidiwa na Mheshimiwa NaibuSpika na Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge. Aidha,nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamichango mizuri mliyoitoa kwa kusema na kwa maandishiwakati wa mijadala ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa naSerikali kwenye Mkutano huu. Napenda niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge wenzangu kuwa Serikali imepokeamichango yenu ambayo inaamini itasaidia sana kuboreshautekelezaji wa mipango ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, niungane na WaheshimiwaWabunge wenzangu kukupa pole kufuatia taarifa zakuhuzunisha za kifo cha Mheshimiwa Stephen Hillary Ngonyani,aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini kilichotokea tarehe 2Julai, 2018. Aidha, natoa pole kwa familia ya marehemu nawananchi wote wa Korogwe Vij i j ini kwa kumpotezamwakilishi wao. Vile vile katika kipindi hiki wapo baadhi yaWabunge wenzetu ambao wamepoteza wapendwa wao.Kipekee natoa salaam za pole kwa Mheshimiwa JosephLeonard Haule maarufu Profesa J., Mbunge wa Mikumi naMheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi maarufu Mr. Sugu,Mbunge wa Mbeya Mjini kwa kuondokewa na wazazi wao.Kadhalika niungane na Bunge zima kumpa pole MheshimiwaRais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, kwa kufiwa na dada yake Bi. Monica JosephMagufuli. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pemapeponi. Amina.

Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwapa poleWatanzania wenzangu waliopoteza ndugu, jamaa na

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

marafiki na wengine kupata ulemavu katika matukiombalimbali ya ajali za barabarani; wakiwemo watalii wane(4) kutoka nchi za Hispania na Italia waliofariki dunia baadaya gari lao la utalii kugongana na lori Wilayani Monduli.Tunamwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemumahali pema peponi na awape nafuu majeruhi wotewapone haraka.

Mheshimiwa Spika, naomba niungane naWaheshimiwa wenzangu kumpongeza MheshimiwaChristopher Kajoro Chiza, Mbunge wa Jimbo la Buyungu kwakuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kufuatia uchaguzimdogo uliofanyika hivi karibuni. Ushindi huu ni ishara ya imanikubwa walionayo wananchi wa Jimbo la Buyungu kwaSerikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati wa mkutano huuWaheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswaliya msingi yapatayo 123 na maswali ya nyongeza 380 ambayoyalijibiwa na Serikali. Vile vile Serikali ilitoa kauli kuhusu haliya sukari nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingineWaheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili Miswadamitano (5) iliyowasilishwa na Serikali katika Mkutano huu.Aidha, Bunge lako Tukufu lilipokea na kupitisha Taarifa yaKudumu ya Bunge ya Sheria ndogo kuhusu uchambuzi waSheria Ndogo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Miswada ya sheria iliyojadiliwa nakupitiwa na Bunge lako Tukufu katika mkutano huu ni kamaifuatavyo:-

(1) Muswada wa Sheria kulitangaza Jij i laDodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018 (TheDodoma Capital City (Declaration) Bill, 2018);

(2) Muswada wa Sheria wa Bodi ya Kitaalam yaWalimu Tanzania wa mwaka 2018 (The Teachers ProfessionalBoard Bill, 2018);

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

(3) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheriambalimbali Na.2 wa mwaka 2018 (The Written Law(Miscellaneous Amendments) No.2 Bill, 2018);

(4) Muswada wa Sheria za Marekebisho ya SheriaMbalimbali Na.3 wa mwaka 2018 (The Written Laws(Miscellaneous Amendments) No.3 Bill, 2018); na

(5) Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubiakati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ya Mwaka 2018 (ThePublic Private Partnership (Amendments) Bill 2018).

Mheshimiwa Spika, napenda kurejea tenakuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango yaomizuri iliyotolewa wakati wa kujadili Miswada hiyo muhimuyenye manufaa mingi kwa nchi yetu. Serikali itafanyia kazimaoni na ushauri uliotolewa kwa lengo la kuhakikishakwamba utekelezaji wake unawanufaisha wananchi nchinikwetu.

Mheshimiwa Spika, niwapongeze na kuwashukuruWaheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri kwa kazi nzuri yakuwasilisha Miswada iliyojadiliwa katika Mkutano huu pamojana kutoa ufafanuzi mbalimbali wakati wa kujibu hoja zaWaheshimiwa Wabunge. Aidha, nimpongeze MwanasheriaMkuu wa Serikali pamoja na Wataalam wake kwa kazi nzuriya kuandaa Miswada iliyowasilishwa katika Mkutano huu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nipitie maeneo yamsisitizo kisekta. Kabla ya kuhitimisha Mkutano huu naombanieleze masuala yafuatayo ili kuweka msisitizo kwa viongozi,watendaji na wananchi kwa ujumla katika kutekelezamajukumu yao ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inasimamia ipasavyoutekelezaji wa bajeti sambamba na kuongeza uwajibikajina nidhamu ya matumizi ya fedha zilizoelekezwa katikavipaumbele mbalimbali kama ilivyoidhinishwa na Bunge lakoTukufu. Hali kadhalika Serikali inaendelea kuimarisha ukaguzi

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

katika ngazi zote na ufuatiliaji wa karibu wa miradi yamaendeleo na kufanya tathimini ya mara kwa mara ilikuhakikisha kwamba miradi na kazi vina uwiano na thamaniya fedha za umma zinazotolewa kwa Serikali kwa lughanyingine value for money.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango naBajeti ya mwaka 2018/2019, Serikali inashirikiana na sektabinafsi, wadau wa maendeleo na wananchi wote ili kufikiamalengo yaliyokusudiwa. Aidha, Serikali iliwasilisha BungeniMuswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Kati yaSekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018 (The PublicPrivate Partnership (Amendment) Bill, 2018). Marekebisho hayoya Sheria yanalenga kuimarisha mfumo wa kitaasisi nakisheria katika kusimamia miradi ya ubia. Vilevile, kutatuachangamoto zilizopo katika miradi ya PPP ili kurahisishauibuaji, uidhinishaji na utekelezaji wake sambamba nakuchochea haraka maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Dhamira ya Serikali ya Awamu yaTano; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, ameweka dhamiraya dhati ya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kutimizandoto na matarajio ya Watanzania ya kujenga nchi yenyeuchumi imara. Katika kipindi hiki, tumeshuhudia mambomakubwa aliyoyafanya yakiwemo kujenga ari ya uzalendokwa kuilinda na kuisemea nchi yetu bila woga; kudumishaamani, utulivu na mshikamano; kuimarisha ulinzi na usalama;kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhilaiwapo sitotaja japo kwa uchache hatua mbalimbali tenaza makusudi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tanochini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais katika kuwaleteamaendeleo Watanzania na kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, wenzetu Wachina wanao msemousemao “Empty Talk, Harm the Country” ambao kwa tafsiriisiyo rasmi ya Kiswahili unamaanisha “Porojo, hudhuru Nchi”.Msemo huo uliotumika sana kipindi Uchina inaingia katika

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

maboresho ya kiuchumi miaka ya 70 na 80 chini ya Kiongoziwa kipindi hicho mwana mageuzi Deng Xiaoping, ulilengakuhamasisha uchapa kazi kama ilivyo sasa falsafa ya Serikaliya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kipindi kinachokaribiamiaka mitatu sasa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amedhihirisha situ kwa uzalendo wake kwa Taifa lakini pia katika kusimamiamipango ya maendeleo lakini pia kulinda rasilimali za Taifakwa lengo la kuwanufaisha Watanzania wa kizazi kilichopona kijacho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua mchango waMheshimiwa Rais, naomba nitaje baadhi ya maeneo ambayoyanaakisi moja kwa moja juhudi zake hizo:-

(1) Kujenga ari ya kufanya kazi;

(2) Kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikajindani ya utumishi wa umma na kukemea uzembe;

(3) Kuendesha vita dhidi ya rushwa na ufisadikwenye taasisi za umma sambamba na kuanzishaMahakama ya Mafisadi;

(4) Kuimarisha ulinzi wa rasilimali za nchi ikiwemomadini na maliasili;

(5) Kufufua Shirika la Ndege la Tanzania il ikuimarisha usafiri wa anga na kukuza sekta mtambukazikiwemo utalii, afya na kilimo;

(6) Kujenga reli ya kisasa kwa kiwango chakimataifa (SGR);

(7) Kuendeleza ujenzi wa barabara zikiwemobarabara za juu (flyovers);

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

(8) Kununua meli (Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyikana Ziwa Victoria) na kuweka vivuko vipya (Lindi-Kitunda,Kigongo Ferry, Ukerewe na kadhalika);

(9) Kujenga vyanzo vipya vya umeme kama vilemradi wa kuzalisha umeme wa maji megawati 2,100 katikabonde la Mto Rufiji;

(10) Kusambaza umeme hadi vijijini sanjari nakuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya awamu ya tatuya mpango wa REA ili kufikia lengo lililokusudiwa;

(11) Kutekeleza mradi wa bomba la mafutakutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga hapa kwetuTanzania;

(12) Kuimarisha huduma za afya hususanupatikanaji wa dawa, vifaa na vifaatiba katika vituo vyotevya kutolea huduma za afya pamoja na ujenzi wa Vituo vyaAfya na Hospitali za Wilaya;

(13) Kutoa Elimumsingi Bila Malipo kwa watoto waKitanzania;

(14) Kuhakikisha miradi yote ya majiinayotekelezwa inakuwa bora, yenye uwiano na thamanihalisi ya fedha pamoja na kukamilishwa kwa wakati; na

(15) Kuimarisha kilimo, ushirika na bei za mazaoya biashara.

Mheshimiwa Spika, juhudi zote hizo zinafanywa kwalengo la kuiwezesha nchi yetu kufikia malengo ya dira yaTaifa ya kuwa na uchumi wa kati unaoongozwa na viwandaifikapo mwaka 2025. Niwaombe Watanzania wenzangutuendelee kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katikakuleta maendeleo. Kadhalika, nitoe wito kwa wawekezajikutumia fursa ya uwepo wa mazingira mazuri nchini yauwekezaji, biashara na upatikanaji wa malighafi wa kujenga

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

viwanda mbalimbali hususan vya kuchakata mazao yakilimo.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Kilimo; Hali ya ChakulaNchini; hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula na upatikanajiwake hapa nchini imeendelea kuimarika. Tathmini iliyofanyikamwezi Juni, 2018 inaonesha kwamba uzalishaji wa mazaoya chakula katika msimu wa 2017/2018, ni tani milioni 16.9.Kati ya hizo tani milioni 9.5 ni mazao ya nafaka na tani milioni7.4 ni mazao yasiyo ya nafaka. Kutokana na uzalishaji huona kwa kuzingatia mahitaji ya chakula nchini ambayo ni tanimilioni 13.6, kutakuwa na ziada ya tani milioni 3.3. Hivyo,nchi itajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 124.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Serikali inaendeleakuwasihi wananchi kutumia akiba hiyo ya chakula kwauangalifu kwani zipo nchi jirani ambazo zina uhaba mkubwawa chakula. Vilevile, naziagiza taasisi zote zinazosimamiaelimu ya lishe na afya kuongeza nguvu zaidi ili kupunguzakiwango cha udumavu na utapiamlo hususan kwa watotowadogo kwenye maeneo mengi nchini.

Mheshimiwa Spika, Upatikanaji wa Pembejeo zaKilimo; Serikali inaendelea kuhakikisha upatikanaji wauhakika wa pembejeo muhimu za kilimo kwa wakati. Katikamsimu wa kilimo 2018/2019 hadi kufikia mwishoni mwa mweziAgosti, 2018, upatikanaji wa mbolea aina zote umefikia kiasicha tani 215,207 na matarajio kwa msimu huu wa 2018/2019ni kutumia tani 485,000. Vilevile, Serikali imeweka mikakatithabiti ya upatikanaji wa mbegu bora kwa mazao yakipaumbele. Wakala wa Mbegu wa Serikali (ASA) umepangakuzalisha na kusambaza tani 40,000 na sekta binafsi nainatarajia pia kuingiza tani 20,645 za mbegu bora.

Mheshimiwa Spika, nitoe shukrani sana kwa Taasisi yaBill and Melinda Gates Foundation kwa kukubali kushirikianana Serikali kuboresha mfumo wa Taifa wa upatikanaji wambegu bora nchini. Mfumo huo utahusisha uboreshaji wauzalishaji wa mbegu mama katika vituo vya utafiti;kuimarisha na kuboresha miundombinu ya mashamba ya

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Wakala wa Mbegu wa Serikali (ASA); na kujenga uwezo waTaasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI); na kuboreshamfumo wa menejimenti ya upatikanaji, usambazaji namatumizi ya mbegu bora nchini.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo msimu wa kilimounaanza miezi michache ijayo, Serikali itahakikishaupatikanaji na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa mazaombalimbali. Mathalan, Serikali itawezesha upatikanaji namatumizi ya ekapaki milioni saba za viuatilifu vya zao lapamba kwa mwaka 2018/2019. Aidha, Serikali imetengajumla ya shilingi bilioni 10 katika msimu wa mwaka 2018/2019, kwa ajili ya kupambana na wanyama na waduduwaharibifu kama vile quelea quelea, viwavijeshi na panyapamoja na visumbufu vingine vya mazao.

Mheshimiwa Spika, Serikali iliamua kurejesha ununuziwa mazao hayo makuu ya biashara kupitia vyama vyaushirika kwa lengo la kuwanufaisha wakulima. Katikakufanikisha azma hiyo, Serikali inasimamia matumizi yamifumo mbalimbali ya masoko ikiwemo Stakabadhi zaGhala na Soko la Bidhaa (Commodity Exchange). Matumiziya mifumo hiyo yamechangia kuboresha ununuzi wa mazaohayo. Kwa mfano, biashara ya mazao hayo ambayoimekuwa ikifanywa kwa njia za mnada na kusimamiwa naVyama vya Ushirika imeleta chachu ya ushindani na hivyokumpatia tija mkulima.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa zao la pambahadi kufikia Agosti 2018, kilo milioni 226 za pyenye thamaniya Shilingi bilioni 248.6 zilikusanywa. Aidha, Vyama vya Ushirikavimeendelea kusimamia ubora wa pamba katika msimu wa2018/2019 ambao umeongezeka maradufu ikilinganishwa namsimu wa 2017/2018. Kwa mfano, msimu wa 2018/2019,pamba ya daraja la kwanza il ikuwa asil imia 44.2ikilinganishwa na asilimia 22.7ya msimu wa 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, katika zao la korosho, mfumo waununuzi kupitia Vyama vya Ushirika unapata mwitikio mzurikutoka kwa wakulima na wanunuzi. Hali hiyo, imesaidia

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

wakulima kupata bei za ushindani ambapo kwa msimu 2017/2018, ilifikia Sh.4,100 kwa kilo ikilinganishwa na Sh.2,700 yamsimu wa 2016/2017. Aidha, uzalishaji umeongezekaambapo jumla ya tani 296,281 za korosho ghafi zenye thamaniya shilingi takribani trilioni 1.12 zilikusanywa na kuuzwa kupitiaVyama vya Ushirika ikilinganishwa na tani 265,000 kwa msimuuliopita.

Mheshimiwa Spika, zao la kahawa, kwa msimu huuwa 2018 uzalishaji wake unakadiriwa kuwa tani 65,000ikilinganishwa na tani 42,513 za msimu wa 2017/2018. Hadisasa, tani 14,664 zimeshauzwa kupitia Vyama vya Ushirika 643na kuingiza Dola za Marekani elfu 24.4 Serikali inaendeleakusimamia mwenendo wa masoko ya kahawa hadi sasa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu zao la tumbaku hadi kufikiaAgosti 2018, wakulima wamekusanya na kuuza tumbaku kiasicha kilo milioni 33.1 zenye thamani ya shilingi bilioni 119.5kupitia Vyama vya Ushirika. Hadi sasa tunaendeleakukabiliana na changamoto zinazokabili zao hili la tumbakuikiwemo na masoko.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa zao la chai, hadikufikia Agosti 2018, kiasi cha tani 31,814 za majani mabichiya chai yenye thamani ya shilingi bilioni 9.9 kimekusanywana kuuzwa kupitia Vyama vya Ushirika katika Mikoa yaNjombe, Iringa, Tanga na Mbeya. Serikali inaendeleakuimarisha ununuzi wa majani mabichi ya chai maeneo yotekwenye mikoa inayozalisha.

Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa mbegu za mafutaya kula; sambamba na azma ya Serikali ya kuweka mkazokatika kusimamia uzalishaji na masoko ya mazao makuumatano ya biashara ambayo ni pamba, kahawa, korosho,chai na tumbaku, Serikali pia, imedhamiria kupanua wigokwenye mazao mengine muhimu ikiwemo zao la chikichi,alizeti na ufuta ili kukidhi uzalishaji wa mbegu za mafuta hapanchini. Katika kutekeleza azma ya Serikali kuhusu kuongezauzalishaji wa mafuta ya kula nchini, tarehe 28 Agosti, 2018nikiwa Mkoani Kigoma nilizindua kampeni maalum ya

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

kuendeleza zao la chikichi ambalo kwa sasa linatambulikakama zao kuu la sita la kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, malengo ya kampeni hiyo nikuhakikisha kuwa Mkoa wa Kigoma na maeneo mengineyenye fursa ya kulima zao la chikichi yanaimarisha kilimohicho. Hatua hiyo, inakusudia kuiwezesha Tanzania kuachanana uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje baada ya mudamfupi. Hivi sasa, nchi yetu inatumia takribani Dola zaMarekani milioni 294 kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafutahayo. Kampeni hiyo inaendelea katika hatua mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwambatunajitosheleza kwa mahitaji ya mafuta ya kula, Serikaliimeweka mikakati ya kuendeleza zao la chikichi kamaifuatavyo:-

(1) Tumeanzisha Kituo cha Utafiti wa zao lachikichi mkoani Kigoma kwenye eneo la Kihinga;

(2) Kuandaa Mpango Mkakati wa uzalishaji wamiche bora ya chikichi milioni 20 ifikapo mwaka 2021. Kwakuanzia, Mwaka wa Fedha 2018/2019, Serikali inakusudiakuzalisha miche bora ya chikichi milioni 10 na kusambazwakwa wananchi wenye nia ya kulima chikichi;

(3) Kuandaa Mpango Mkakati wa miaka mitanowa utafiti wa mbegu bora ili kuongeza tija kutoka tani 1.6hadi kufikia tani nne(4) za matunda ya chikichi kwa hekakwa mwaka;

(4) Kuweka mazingira mazuri ya kuvutiawawekezaji na matumizi ya teknolojia ya kisasa kwa ajili yauchakataji wa zao la chikichi; na

(5) Kusimamia vituo vikuu vya uzalishaji vyaGereza la Kwitanga na Ilagala na JKT Bulombora yaliyokoMkoani Kigoma na tumetenga ardhi kwa ajili ya uwekezajikwa wawekezaji wa ndani na nje wanaohitaji kuwekezakwenye zao la chikikichi.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Spika, nitoe wito kwa wananchikuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la chikichi ili tuwezekujitosheleza kwa mafuta ya kula na ziada kuweza kuuzanje. Vilevile, nitoe rai kwa wawekezaji kuanzisha viwandavya kuchakata chikichi na mazao yake.

Mheshimiwa Spika, Upimaji wa hiari wa VVU;itakumbukwa kuwa tarehe 19 Juni, 2018, Jijini Dodoma,nilizindua kampeni ya Kitaifa ya kupima kwa hiari VVU pamojana kuanza mapema matumizi ya dawa za kufubaza (ARV)kwa wale watakaogundulika kuwa na maambukizo.Kampeni hiyo, ijulikanayo kama “FURAHA YANGU, PIMA,JITAMBUE, ISHI” iliwalenga Watanzania wote kujitokezakupima na kutambua afya zao hususan wanaume ambaohawajitokezi kwa wingi kupima na kutambua afya zao.Wanaume wengi tumekuwa tukitumia wenza wetu katikakutambua kama tumeathirika au la. Tunakaa majumbanitunasubiri tu, ukimwona mwenza wako anarejea kutokakliniki na furaha na wewe unajipa matumaini kuwaumesalimika. Sasa wanaume wenzangu tubadilike, tuanzekuchukua hatua za kupima na kutambua afya zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikiwa kinara wa kampeni hiyo,napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi kufikia mweziSeptemba, 2018 tayari mikoa 14 imeanza kutekeleza Kampenihiyo. Mikoa hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa,Kigoma, Manyara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe,Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga. Niwapongeze Wakuuwa Mikoa hiyo kwa kutekeleza jukumu lao na niwatakewaendelee kuhimiza wananchi waliopo kwenye maeneo yaohususan wanaume kutambua afya zao kuhusu maambukizoya VVU kupitia kampeni hii.

Mheshimiwa Spika, niwatake Wakuu wa Mikoaambayo bado haijaanza kutekeleza Kampeni hiyo kuanzamara moja. Kwa kutambua umuhimu wa Kampeni hii,if ikapo Desemba Mosi, 2018 wakati wa kilele chaMaadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani tutafanya tathminiya utekelezaji kwa mikoa yote nchini. Kwa msingi huo, nisisitize

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

wadau wote wenye mapenzi mema na nchi hii wasaidiekutekelezaji kampeni hiyo.

Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Serikaliinafanya juhudi za kufikisha kampeni hii katika Ligi kuu yaMpira wa Miguu Tanzania Bara kwa kushirikiana na Shirikishola Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Tunafanya hivyo kwakutambua kuwa Mpira wa Miguu ni mchezo unaoongozakwa kupendwa duniani na Tanzania. Aidha, kufuatia hatuaya Kituo cha matangazo ya Televisheni cha Azam kuamuakuonesha ligi yetu, watu wengi wamepata mwamko wakutazama na kufuatilia michezo ya Ligi kuu Tanzania. Hivyo,tuna uhakika wa kuwafikia wananchi wengi nakuwahamasisha kuchukua hatua za kupima VVU na walewatakaogundulika kuwa na maambukizi kuanza mapemamatumizi ya ARV.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia kukupongezawewe mwenyewe binafsi kwa kuonesha mfano, pia kwakupima na kuwahamasisha Waheshimiwa Wabunge waBunge lako Tukufu kupima na kutambua afya zao. Kwa hiyo,tunaamini kampeni hii pia itabebwa na WaheshimiwaWabunge wote ili iweze kuenezwa nchini kote.

Mheshimiwa Spika, Uagizaji wa Mafuta ya Kula naSukari; katika Mkutano huu ulijitokeza mjadala kuhusu sualala usimamizi na uangalizi wa mafuta ya kula na sukari. Serikalikwa upande wake inaimarisha taratibu za uingizaji wa sukarina mafuta ya kula kwa kuweka madaraja na usimamizimakini. Aidha, naagiza Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kukamilishajukumu hilo kwa wakati. Pia, nategemea vyombo vya Dolakuongeza ushirikiano na mamlaka husika (TRA, TFDA, Bodi yaSukari na TBS) kudhibiti uingizaji holela wa sukari na mafutaya kula ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya magendo.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Michezo; katika nyanjaya michezo naomba nitoe pongezi za dhati kwa Timu yaTaifa ya Wanawake (Kilimanjaro Queens) kwa kutwaa kombela Afrika Mashariki. Vilevile, nawapongeza vijana wetu wa

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kuwa washindiwa tatu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenyemashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Pianimpongeze Mwanamasumbwi wa Kitanzania HassanMwakinyo kwa kumchapa Bondia Mwingereza SamEggington kwenye raundi ya pili ya pambano lao lamasumbwi li l i lofanyika huko Birmingham, Uingereza.Hongereni sana wanamichezo wetu na endelezeni moyo huowa kizalendo mliouonesha katika kulitangaza Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019 Tanzaniaitakuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa miguu kwavijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON-Under 17)yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika. Hii nifursa nyingine ya kipekee ya kulitangaza Taifa letu katikanyanja za Kimataifa. Serikali kwa kushirikiana na wadaumbalimbali inaendelea na maandalizi stahiki ambayoyatahusisha ukarabati wa viwanja vitakavyotumika katikamashindano hayo.

Mheshimiwa Spika, natoa wito kwa wananchiwatumie vizuri uwepo wa mashindano hayo kujijengeakipato hususan kupitia biashara ya bidhaa na huduma kwawageni. Vilevile, natoa wito kwa Watanzania wote kuwawazalendo kwa kuunga mkono timu zetu zinazoshirikimashindano ya kimataifa ili zipate mafanikio.

Mheshimiwa Spika, wakati nikielekea kuhitimishahotuba yangu hii kuna masuala ambayo ningependakuyasisitiza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Kudumisha Amani; ni vematukatambua kwamba vita ya kiuchumi aliyoitangazaMheshimiwa Rais, mafanikio yake yatategemea kwa kiasikikubwa uwepo wa amani, umoja na mshikamano waKitaifa. Tarehe 22 Oktoba 1987, Baba wa Taifa, Hayati MwalimuJulius Nyerere akiwa Mjini Dodoma aliwahi kusema nanaomba nimnukuu:

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

“Tuna haki ya kujivunia umoja huu na amani hii,maana ndivyo vilivyotuwezesha kupambana na matatizomakubwa ya vita ya uchumi, na hata ya kisiasa”. Mwisho wakunukuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimenukuu maelezo hayo yaMheshimiwa Rais wa Kwanza wa Tanzania ili kuwakumbushaWatanzania wenzangu kwamba amani tuliyonayo ni muhimukatika kufikia malengo yetu ya kiuchumi. Hivyo, tuidumishe,tuithamini na tuilinde amani tuliyonayo.

Mheshimiwa Spika, Maandalizi ya msimu wa kilimo;kuanzia mwezi Septemba, 2018 maeneo mbalimbali ya nchiyetu yameanza kupata mvua za vuli ambazo huashiriakuanza kwa msimu mpya wa kilimo. Serikali inahakikishaupatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu bora,mbolea na viuatilifu kwa ajili ya msimu huu mpya wa kilimounawezeshwa. Hivyo, nitumie fursa hii kuwahimiza mawakalana wafanyabiashara waliopewa jukumu la kusambazapembejeo kuhakikisha kuwa zinawafikia wakulima kwawakati. Aidha, niwasihi wakulima kuandaa mashamba yaomapema ili waweze kutumia vizuri mvua za vuli ambazozinaanza kunyesha katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Kuimarisha na kusimamia Ushirika;katika kipindi kifupi Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwakurejesha imani ya wananchi kuhusu ushirika. Aidha, katikakipindi hicho wananchi wameendelea kuona na kunufaikana hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katikakusimamia sekta ya ushirika.

Mheshimiwa Spika, napenda kulihakikishia Bunge lakoTukufu kuwa Serikali inaendelea kujenga ushirika imara sanjarina kuhakikisha kwamba wakulima wananufaika nausimamizi mzuri wa vyama vya Ushirika. Hivyo, naendeleakuwasisitiza viongozi wenye dhamana katika kusimamiaushirika nchini kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwamujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo dhidi yawatakaothubutu kuhujumu ushirika.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Mheshimiwa Spika, nihitimishe hotuba yangu kwakumshukuru Katibu wa Bunge na watendaji wa Ofisi ya Bungekwa kazi kubwa ya kuratibu vikao vya Mkutano huu. Aidha,niwashukuru watendaji wa Serikali kwa kufanikisha shughulizilizopangwa na Bunge lako Tukufu kwa weledi na ufanisimkubwa. Kipekee, niwashukuru wanahabari wote kwakufikisha habari kuhusu Mkutano huu kwa wananchi.Nivishukuru pia vyombo vya ulinzi na usalama kwa hudumawanazozitoa kwa washiriki wa Bunge hili bila kuwasahaumadereva waliotuhudumia wakati wote tukiwa hapaBungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwatakia safarinjema Waheshimiwa Wabunge, niwaombe wanaporejeamajimboni kwao kuwaeleza wananchi mambo yaliyojiri hapaBungeni. Wapeni taarifa wananchi juu ya matarajio yetukwao na kuwasihi waendelee kutuunga mkono kwenyejitihada zetu katika kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe14 Novemba, 2018 siku ya Jumanne, saa tatu kamili asubuhilitakapokutana tena katika ukumbi huu Jijini Dodoma.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Spika, naafiki.

SPIKA: Hoja imetolewa na imeungwa mkono kwelikweli. Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwahotuba yako nzuri, ahsante sana. Sasa Mheshimiwa WaziriMkuu ametoa hoja ya kuahirisha Bunge Wajibu wangu nikuwahoji. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

SPIKA: Basi Waheshimiwa Wabunge, namshukuru sanaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa kweli kwa mara nyingine kwahotuba yake, pamoja na mambo mengine aliyoyazungumziaamemtaja Bondia Hassan Mwakinyo ambaye amefanyajambo kubwa sana la kutuletea heshima kubwa katika nchiyetu.

Sasa Waheshimiwa Wabunge kwa heshima kubwanaomba nimlete kwenu bondia Hassan Mwakinyo, pale uliponaomba usimame. (Makofi/Vigelegele)

Hapo, hapo tu. Ahsante sana WaheshimiwaWabunge, ndugu yetu Hassan Mwakinyo tunakupongezasana, tuna fahari kubwa sana kwamba wewe ni mwenzetuna umeliletea taifa letu heshima kubwa sana na ni matarajioyetu kwamba bado utasonga mbele na kupata matajimakubwa zaidi kuliko hata hapo. (Makofi)

Tutakapomaliza kuahirisha kila kitu hapa nitaombaWasaidizi mtamchukua Hassan Mwakinyo aende ampemkono Mheshimiwa Waziri Mkuu atakapokuwepo popotepale. (Makofi)

Ahsante sana, naomba ukae, karibu sana.

Tunawapongeza Wabunge wa Tanga. Mimi sikujuakama Tanga inaweza ikatoa Bondia. Nilijua bondia anawezakutoka Usukumani hivi, kwa Wanyamwezi hivi wabebamizigo mizito, lakini kumbe ndiyo hamna chochote huko.(Makofi/Vicheko)

Ndiyo Mheshimiwa Aeshi.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. KHALFAN H. AESHI: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii nataka kuomba mwongozowako, tumekuwa tukiwachangia sana Ma-Miss humu ndanileo hii tunaomba Mheshimiwa Mwongozo wako sisi Wabungeat least tuweze kumchangia hata Sh.20,000/= kila mmoja

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

kwa sababu tumekuwa tukichanga sana. Mheshimiwanaomba mwongozo wako. (Makofi)

SPIKA: Kwa makofi haya limeafikiwa si ndio eeeh?

WABUNGE: Ndiyooo.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, Sh.20,000/= nindogo.

SPIKA: Tumeshahoji ni Sh.20,000/=. Ahsante sana.

(Bunge liliridhia kila Mbunge kukatwa Sh.20,000ikiwa ni pongezi kwa Bondia Hassan Mwakinyo)

SPIKA: Pia naomba niwatambulishe Wabunge wawili(2) ambao safari hii walienda kwenye Ibada ya Hija nawamerudi salama na sasa Wabunge hawa ni Maalhaj.Kwanza ni Mheshimiwa Mussa Shekilindi, Mbunge wa Lushoto.Sasa yeye rasmi ni Mheshimiwa Alhaj Mussa Shekilindi; na wapili ni Mbunge wa Bagamoyo Mheshimiwa ShukuruKawambwa, sasa ni Alhaj Shukuru Kawambwa. (Makofi)

Ahsante sana.

WABUNGE FULANI: Umemsahau Masauni.

SPIKA: Alienda pia? Oooh!

WABUNGE FULANI: Eeeh. (Makofi/Vicheko)

SPIKA: Samahani Waheshimiwa naambiwa piaEngineer Masauni ameenda Hija safari hii. Kwa hiyo tunayeAlhaj mwingine Mheshimiwa Masauni. (Makofi/Vicheko)

WABUNGE FULANI: Sheikh Nassir.

SPIKA: Na Sheikh Nassir eeeh? Jamani ameongezekana mwingine Sheikh Nassir. (Makofi)

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

Ahsante sana. Sasa tumewataja jamani pamoja namambo mengine, wale wenzangu mimi wenye vijicho pembeaaah sasa hawa Maalhaj jamani. (Makofi/Vicheko)

Waheshimiwa Wabunge jana niliwaambia kwambanitafanya zoezi kidogo la takwimu ya kuona Bunge letu likojekiusomi. Sasa nimefanya kidogo homework yangu lakininitataja takwimu chache tu. Takwimu zangu zinaniambiakwanza upande wa umri Mbunge kijana kuliko wote niMheshimiwa Halima Bulembo ana miaka 27 na Mbungemwenye umri mkubwa kuliko wote ana miaka 75, kwa leohayupo hapa. (Makofi/Kicheko)

Kwa ujumla ilikuwa baadhi ya watu wanapendakuliita Bunge hili ni Bunge la vijana, lakini niwaambie baadaya takwimu zangu hizi, Wabunge wenye umri wa miaka 40na kwenda mbele ni asilimia 80 ya Wabunge wote. Kwahiyo, haya maneno ya kusema Bunge la Vijana siyo kweli.Unajua ujana wakati mwingine ni attitudinal, mtu anafikiribado kumbe umri umeshakwenda. (Makofi/Kicheko)

Sasa upande wa elimu nianze na kundi maalum laViti Maalum. Kwanza kwenye elimu huku nimeangalia elimuya sekondari na kwenda mbele, hawa wa elimu ya msingisikuweza kuwaangalia vizuri, kwa hiyo takwimu hiyonitaiacha mpaka siku nyingine.

Elimu ya sekondari kwa Viti Maalum wote wenye elimuya sekondari ni 24. Katika hao 24 CUF watano (5), CHADEMAwatano (5) na CCM 14. Wenye Certificate na Diploma CUFwane (4), CHADEMA nane (8) na CCM 16. Wenye Bachelorna kuendelea CUF mmoja (1), CHADEMA 23 na CCM 32.Katika Viti Maalum upande wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ni11 kwa ujumla wake; 10 CCM na CHADEMA mmoja (1). Hizitakwimu zinasaidia kuonesha wale wanopendaga kusemaooh ooh, kumbe siyo kweli bwana, bado CCM inatamba.(Makofi)

Basi na uchambuzi mwingine bado unaendelea. Kwakweli, Maprofesa tunao saba (7) na wote saba (7) ni wa CCM.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

PhD kwa nyumba nzima hii ziko 29; mmoja (1) CUF, mmoja(1) CHADEMA na 27 CCM. Maana yake watu kwenyemitandao wanasema ooh CCM imejaza vihiyo, sasa takwimuhizo. Kwa ujumla wake wapo baadhi huwa wanasemaBunge hili ndiyo Bunge ambalo tangu historia haijawahikutokea Bunge la namna hii. Kwa aina hii ya elimu niliyoielezahili ni Bunge la Kumi na Moja toka tupate uhuru, hakuna Bungelimewahi kuwa na wasomi wengi kuzidi hili Bunge la Kumina Moja. Huo ndiyo ukweli wenyewe na ndiyo hali halisi.(Makofi)

Nilikuwa naangalia kule Buyungu kwa MheshimiwaChiza walipogombea wale wa CCM walikuwa kama 22(around that number). Wale wagombea waliogombea kwaCCM peke yake wote 22 ni ma-graduate, Buyungu. Yaanihiyo inakupa picha ya mabadiliko ya nchi sasa nainapoelekea, yaani kama Buyungu hali ni hiyo basi kwavyovyote vile na kwingine nako kutakuwa kumechangamkakwa namna hiyo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya matangazo hayoniliyoyatoa, sasa naomba tusimame ili tusikilize Wimbo waTaifa, Brass Band mnaweza mkaendelea sasa.

(Hapa Wimbo wa Taifa Uliimbwa)

SPIKA: Ahsante sana, mnaweza mkakaa. Kwenyetakwimu zangu takwimu moja muhimu sikuisema ni kwambawale wenye 1st Degree na Masters ujumla wake humu ndanini 161, ni nyingi sana hizi. Katika hizo CUF wanazo 14,CHADEMA wana 31 na CCM wanazo 114. (Makofi)

Sasa Waheshimiwa Wabunge wakati MheshimiwaWaziri Mkuu anaahirisha alipokuwa anataja tarehe yakukutana tena kwa mara nyingine ilitajwa tarehe 14Novemba, lakini nimepata rekebisho hapa kwamba itakuwamapema zaidi kidogo, tarehe 6 Novemba, ni sawa Katibu?Ni tarehe 6 Novemba, tunaomba radhi au twende 14?

WABUNGE FULANI: Hapana.

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1537263288-14...ya Chamwino, vituo hivyo viko katika Shule ya Msingi Mvumi Mission na Shule ya Msingi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

SPIKA: Turudi 6 eeh?

WABUNGE FULANI: Ndiyo.

SPIKA: Kwa nini mnataka tuharakishe? Kwa hiyoWaheshimiwa Wabunge ni tarehe 6 Novemba, tuwekeratiba/diary zetu vizuri.

Basi baada ya hayo naomba sasa tusimame, kwamaana hiyo, sasa naomba niahirishe shughuli za Bunge haditarehe 6 Novemba, 2018, kama Mheshimiwa Waziri Mkuualivyosema.

(Saa 5.50 Asubuhi Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Jumanne,Tarehe 6 Septemba, 2018, Saa Tatu Asubuhi)