12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1047 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOV. 30 - DES. 6, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Tume ya Warioba hoi Zanzibar Yatakiwa itoe kwanza Tanganyika iliko Ndio ije na mambo ya Katiba, Muungano Askari kutoka Bara wadaiwa kutesa watu Msiba: Wazungu wavamia Kondoa Ni baada ya kusikia ni Makao Makuu ya Tabligh Waritadisha mamia kila mwaka Pahi wakati… Wana-Bakwata, Ansaar Sunna wakiparurana NECTA haitendi haki Zanzibar-Shamhuna Wizara ya Kawambwa yapuuza WEMA Mamia kuzuiwa kufanya mtihani Z’bar Na Ibn Charo Ali Amesema kweli Borafya… Asumini sasa hazinukii tena Kikwajuni, Unguja Zitanukia vipi kwa matusi haya hadharani? Ngoma kapewa kiziwi, haachi mpaka ipasuke Aliyosema Dr. Amani Karume Dodoma SIKU moja Mtume (s.a.w) akiwa na maswahaba zake Msikitini aliingia kafiri mmoja akaenda katika kipembe kimoja ndani ya msikiti akawa anakojoa. Maswahaba walitaharuki Inaendelea Uk. 2 Na Mwandishi Wetu “TANGANYIKA haionekani, iko wapi? Itoeni kwanza Tanganyika ndipo tuzungumze masuala ya Katiba na masuala ya Muungano.” Hayo ni maoni ya baadhi ya wananchi yakionyesha jinsi wananchi na wakazi wa Zanzibar walivogeuza maoni ya mabadiliko ya Katiba kuwa jukwaa la kujadili mambo ya Muungano na kero zake. Inaendelea Uk. 3 MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikaguzwa ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Sekondari Mpendae, alipotembelea ujenzi huo. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamuhuna. Borafia Silima Juma. Innalillahi Waina illahi Rajiuun Mzee Kiangi afariki. Anazikwa leo Mriti, Ugweno Habari zaidi wiki ijayo

ANNUUR 1047.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: ANNUUR 1047.pdf

ISSN 0856 - 3861 Na. 1047 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOV. 30 - DES. 6, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Tume ya Warioba hoi ZanzibarYatakiwa itoe kwanza Tanganyika ilikoNdio ije na mambo ya Katiba, MuunganoAskari kutoka Bara wadaiwa kutesa watu

Msiba: Wazungu wavamia Kondoa

Ni baada ya kusikia ni Makao Makuu ya TablighWaritadisha mamia kila mwaka Pahi wakati…Wana-Bakwata, Ansaar Sunna wakiparurana

NECTA haitendi haki Zanzibar-Shamhuna

Wizara ya Kawambwa yapuuza WEMAMamia kuzuiwa kufanya mtihani Z’bar

Na Ibn Charo Ali

Amesema kweli Borafya…

Asumini sasa hazinukii tena Kikwajuni, Unguja

Zitanukia vipi kwa matusi haya hadharani?Ngoma kapewa kiziwi, haachi mpaka ipasukeAliyosema Dr. Amani Karume Dodoma

SIKU moja Mtume (s.a.w) akiwa na maswahaba zake Msikitini aliingia kafiri mmoja akaenda katika kipembe kimoja ndani ya msikiti akawa anakojoa. Maswahaba walitaharuki

Inaendelea Uk. 2

Na Mwandishi Wetu

“ T A N G A N Y I K A haionekani, iko wapi? Itoeni kwanza Tanganyika n d i p o t u z u n g u m z e masuala ya Katiba na masuala ya Muungano.”

Hayo ni maoni ya baadhi

ya wananchi yakionyesha jinsi wananchi na wakazi wa Zanzibar walivogeuza maoni ya mabadi l iko ya Katiba kuwa jukwaa la kujadil i mambo ya Muungano na kero zake.

Inaendelea Uk. 3

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikaguzwa ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Sekondari Mpendae, alipotembelea ujenzi huo. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamuhuna.

Borafia Silima Juma.

Innalillahi Waina illahi Rajiuun

Mzee Kiangi afariki. Anazikwa leo Mriti, Ugweno

Habari zaidi wiki ijayo

Page 2: ANNUUR 1047.pdf

2 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Makala

w a k a t a k a k u m v a m i a kumtia adabu. Lakini Mtume Muhammad (s.a.w) akawazuiya. Akawaambiwa wamwache amalize mkojo wake. Alipomaliza, Mtume akamwita na kuongea naye kwa upole na kumweleza kuwa alichofanya si katika utu na ubinadamu na akamweleza pia nini heshma ya msikiti. Baadhi ya taarifa zinasema kuwa mtu yule alisilimu. Na kilichomvuta za id i n i u le upole na ubinadamu aliofanyiwa japo yeye alikuwa amefanya ufedhuli kama namna tu ya kuwakera, kuwaudhi n a k u w a f a n y i a j e u r i Waislamu.

Yapo maelezo mengi juu ya hekma ya hatua hii aliyochukua Mtume (s.a.w) ya kutaka mtu yule aachwe amalize mkojo wake. Moja ni kuwa laiti maswahaba wangemkurupusha wakati bado anakojoa, bila shaka ingekuwa patashika na najisi ingesambaa eneo kubwa. Kwa hiyo hata wakati wa kutoharisha ingekuwa kazi ngumu. Lakini kwa kumuacha kumaliza, ni kwamba mkojo ulikuwa sehemu moja na ilikuwa rahisi kusafisha.

Nimekumbuka kisa hiki baada ya kutizama DVD y a m k u t a n o w a C C M uliofanyika uwanya wa Mabata tarehe 4 Novemba,

2012. Baada ya kuwasikiliza wazungumzaji wote ikiwa ni pamoja na Kiongozi mmoja mwandamizi wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, Zanzibar na Mwenyejkiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafia Silima Juma, nimejiuliza maswali matatu: Moja, lau waliotukanwa nao wanaandaa mkutano kujibu matusi yale, hali itakuwaje? Pili, hapa wanaotukanwa ni Waislamu/Uislamu au Wazanzibari? Tatu, nchi ikishakuwa na viongozi kama hawa, inakoelekea ni wapi?

Ukisikiliza yaliyosemwa katika mkutano ule, ni wazi ulikuwa umeandaliwa kwa minajili ya kuwatukana watu fulani binafsi na wanachama wa CUF na chama chao kwa ujumla. Kwa hiyo pengine ambalo ningetaka kujua mimi ni nini ilikuwa majibu ya waliotukanwa. Hata hivyo, nimeamua kuandika makala haya kuchambua mkutano huo kwa sababu kubwa moja. Umetajwa Uislamu. Imetajwa dini ya Kiislamu. Walioporomosha matusi ni Waislamu. Na Muislamu akifanya jambo la ovyo, anawatukanisha Waislamu wote na dini yenyewe. Kama vi le ambavyo aki fanya jambo zuri kwa kujinasibu na Uis lamu, Wais lamu kwa ujumla na Uislamu unanasibishwa na wema huo.

U k i a c h a s a l a m u y a Assalaam alaikum ambayo

yawezekana kuchukuliwa k a m a a d a t u a m b a y o hata baadhi ya Wakristo w a m e z o e y a k u i t u m i a , mzungumzaji wa mwanzo katika mkutano huo alianza kwa kunukuu Qur’an pale Mwenyezi Mungu aliposema kuwa hakuwaumba majini na wanadamu (kwa sababu nyingine yoyote) ila wapate kumwabudu. Hii ni aya ya Adh-dhaariyati ya sura ya 51 aya ya 56 ambayo inasema: “Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu.”

Wazungumzaji waliofuatia kila mkoja kwa namna yake, nao wakagus ia mambo makubwa mawili. Uislamu, silka na akhlaq za Wazanzibari. Katika moja ya maneno yake Mzee Borafya Silima Juma akafikia kukumbuka zamani ambapo akisema watu Unguja wakitayarisha kanzu zao za Aljumaa siku ya Akhamisi na wakienda Ijumaa wananukia uturi. Lakini siku hizi dini inaharibiwa na watu aliodai kuwa hawakusoma Ukutani. Akasema watu hao hata Babu Majaa hawakusoma, lakini wanajifanya masheikh.

“ S i e d i n i t u n a i j u a , msituharibie dini bwana…Aljumaa unaingia pale na uturi (lakini) ile ladha ya Unguja imekwisha. Hata ukipita Kikwajuni asumini hazinukii.”

Alisema Mzee Sil ima Inaendelea Uk. 4

YAPO mafunzo mengi katika Qur’an kwamba katika kupigania haki, ikhlas inakuwa na nafasi k u b w a s a n a k a t i k a kupata ushindi na wala sio maguvu.

Na ndio pale Qur ’an inaposema , “Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wafanyao subra.” (2: 249)

Fundisho hili na kanuni hii ilitolewa pale Banii Israil wakiongozwa na Talut walipotakiwa kupambana na Jaluti na majeshi yake waliyemuona mbabe sana.

Lakini tunaambiwa pia kuwa ilivyo katika maumbile, iwapo mtu atakataa kuonewa, kubaguliwa na kudhalilishwa, dhalimu hata awe na maguvu kiasi gani atashindwa. Hii maana yake ni kuwa ukiona mtu anadhalilishwa, basi kakubali.

Katika miaka ya 1990s aliyekuwa Waziri wa Elimu Profesa Kighoma Ali Malima alisema kuwa alipoingia Wizarani hapo aligundua mfumo ambao ulikuwa unawezesha na kurahisisha kubaguliwa watoto wa Kiislamu katika kupata elimu ya juu. Akabadili m f u m o u l i o k u w e p o . Ghafla idadi ya watoto wa Kiislamu waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza ikaongezeka kwa asilimia 40.

Hata hivyo haikupita muda Waziri huyo aliondolewa katika Wizara hiyo na mfumo wa zamani ukarejeshwa na ile idadi ya watoto wa Kiislamu ikaporomoka tena na kuendelea hivyo mpaka leo.

K w a n i n i M a l i m a aling’olewa Wizara ya Elimu? Kwa nini mfumo uliosiriba mwanya wa upendeleo na ubaguzi uling’olewa pamoja na Malima?

Je, Waislamu wamejiuliza maswali haya na wamechukua hatua gani. Inawezekana wanasema, wananung’unika. Lakini wamechukua hatua gani?

Yapo matukio mengi yaliyosemwa na kuwekwa

‘Jaluti’ NECTA!katika maandishi na taarifa r a s m i k w a m b a w a p o vijana wengi wa Kiislamu walifaulu kwenda kidato cha kwanza miaka ya 1960s mpaka 1990s, lakini taarifa za kufaulu kwao zikafichwa na nafasi zao wakapewa watoto wa Kikristo. Mtoto Mkristo lakini anasoma kwa jina la mtoto wa Kiislamu.

Wapo pia watumishi wa serikali, mfano Mzee Abdurahmani Mwalongo na Bori Lilla ambao nao waliwahi kueleza waliyo yaona j insi watoto wa Kiislamu wanavyominywa wasipate fursa ya kupata elimu ya juu.

Ukiacha yo te hayo , yapo haya yaliyoibuka h iv i majuz i baada ya kutokea tatizo la watoto wa Kiislamu kufelishwa katika somo la Maarifa ya Uislamu. Katika jumla ya mambo yaliyosemwa na yanayoendelea kusemwa juu ya sakata hilo ni kuwa kuna utaratibu wa siri wa kutunuku baada ya mitihani kusahihishwa ambapo ndipo wanapochinjwa watoto wa Kiislamu.

I n a d a i w a k u w a Kamati hiyo ya kutunuku imedhibitiwa na Wakristo w a t u p u n a n d i y o huwahujumu Waislamu na kuzifanya shule za Kanisa kutesa kila mwaka bila kujali kuwa katika kufanya hivyo wanasababisha watoto wengine kuteseka.

Kinachodaiwa ni kuwa hakuna kanuni wala utaratibu unaojulikana rasmi wa kutunuku jambo linalofanya kamati hiyo kufanya mambo yake inavyotaka.

Kwa mfano inadaiwa kuwa wakati inajulikana A inapatikana kwa kupata alama kuanzia 81 mpaka 100, wanaweza wakashusha ikawa chini ya hapo kwa wale wanaotaka kuwafanya watese na kuwapandishia wale inaotaka wateseke.

M a d a i y a l i y o p o n i kuwa wakati watahiniwa w a s o m o l a B I B L E KNOWLEDGE wakipata A kuanzia 80, watahiniwa wa somo la ELIMU YA D I N I YA K I I S L A M U wanaweza wakipata 80

wakapewa B. Kwa maana kuwa ili watahiniwa wa somo la ELIMU YA DINI YA KIISLAMU wapate A lazima waanze na alama 81.

Ni kwa utaratibu huo huo kwa mfano ukipata kuanzia 65, 66, 67, 68, 69 kwenye BIBLE unaweza kupewa B, lakini kwa ELIMU YA DINI YA KIISLAMU hizo zote (65-69) zikafanywa C. Kwa maana kuwa B katika Islamic imewekwa kuanzia 70.

Kwa upande mwingine inaweza kufanywa kuwa alama 50, 51, 52, 53, 54, 55, 56, 57, 58, 59 kwa BIBLE zikawa C, lakini wa ELIMU YA DINI YA KIISLAMU zote hizo zikafanywa ni D.

Kwamba mtoto aliyepata alama 65 katika Divinity (Bible) anapata B lakini kwa yule wa Elimu ya Kiislamu akipata 69 anapewa C.

Kwa utaratibu huo huo,

aliyepata 50 katika Divinity atapata C wakati Muislamu kwa 50 hiyo hiyo anapewa D kwa sababu kwa Maarifa ya Uislamu inaweza kuwekwa kuwa D ni 35 mpaka 59.

Kama tulivyotangulia kusema haya yote ni madai. Ni tuhuma zilizoibuka baada ya lile sakata la ‘kuchakachuliwa’ kwa matokeo ya mtihani wa Somo la Dini ya Kiislamu na inadaiwa kuwa hii ndio njia mojawapo na mkakati mmoja wapo wa kuzifanya seminari za Kikristo zitese kila mwaka. Yapo na mengine mengi yanadaiwa katika kufanikisha mkakati huu.

Ambalo kidogo linakuwa gumu kufahamika ni kuwa i n a k u w a j e Wa i s l a m u wanaendelea kukubali mfumo huu kuendelea pamoja na madai yote haya? Je, ndio tuamini kuwa wamekubaliana na hali hii?

Ukirejea yale ya Prof. Malima, yale yaliyosemwa na Bor i L i la na Mzee Abdurahmani Mwalongo na haya madai ya sasa juu ya Kamati ya Kutunuku, wachukulie Wakristo walivyo hapa nchini, hivi wangekubali watoto wao wasome na kufanya mitihani ya kitaifa katika mfumo huu?

S w a l i n i j e , kinachoshindikana kubadili mfumo huu nini?

W a n a c h o s h i n d w a Waislamu kutaka ufanyike uchunguzi wa kina na huru kujua ukweli nini?

K a m a h a k u n a k i t u k i n a c h o f i c h w a , k a m a hakuna mizengwe, mantiki ingeelekeza kuwa kutokana na tuhuma nzito kama hizi, basi ufanyike uchunguzi huru na wa kina ili kubaini ukweli.

Asumini sasa hazinukii tena Kikwajuni, UngujaInatoka Uk. 1

Page 3: ANNUUR 1047.pdf

3 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Habari

Tume ya Warioba hoi ZanzibarM a o n i m e n g i

yanayotolewa yanahusu muundo wa Muungano kuliko masuala mengine yaliyomo katika Katiba, kama haki na wajibu wa raia, haki na wajibu wa serikali, ulinzi na usalama, madaraka ya umma, madaraka ya Rais, madaraka ya Bunge na Mahakama.

Kinachozungumzwa na walio wengi ni muundo wa Muungano, kwamba wanataka Ser ikal i ya Tanganyika ijipambanue na iwe na mamlaka yake kamili, kisha Zanzibar nayo iwe na mamlaka kamili na baadaye ndiyo nchi mbili ziketi kuamua kuunda muungano kwa baadhi ya mambo.

Aki toa maoni yake Suleiman Juma Suleiman, mkazi wa Kianga, alihoji ilipo Tanganyika na kwa nini Watanganyika wenyewe hawaidai nchi yao.

“Tanganyika haionekani, iko wapi? Itoeni kwanza T a n g a n y i k a n d i p o t uzungumze masua l a ya Katiba na masuala ya Muungano,” alisema Suleiman.

Naye Ramadhan Faki mkazi wa Kianga, alisema hivi sasa Wazanzibari wengi wanataka serikali yao iliyo huru na yenye uamuzi wa mambo yote ya ndani na ya nje, hasa kwa sababu wanaona kama viongozi wao hawawezi kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano.

N u k t a h i y o h i y o ikazungumzwa na Hassan M o h a m e d A b d a l l a h al iyesema kuwa yeye a n a t a k a S e r i k a l i y a Tanganyika irudi, ndipo masuala ya kuimarisha muungano yajadiliwe.

K w a w a l e wal iozungumzia haki za binadamu wengi wao wanaelezea unyanyasaji unaofanywa na polisi.

“Tumechoka vipigo, jambo si jambo bakora zinatembea, sasa kwani hawa askari kutoka Bara w a m e l e t w a Z a n z i b a r ku l inda wananchi au kutukomesha?” Alihoji Haji Ali Haji.

H a j i a l i s e m a y e y e anaamini wananchi wanayo haki ya kutoa mawazo yao kuhusu serikali yao au jambo lolote linalohusu maslahi yao.

“Sisi (wananchi) tunao

uhuru wa kutoa mawazo, sasa kwa nini tunaposema kile tunachokitaka, tunapigwa na kunyanyaswa?” Alihoji Haji.

Tathmini kwa ujumla inaonyesha kuwa watu wengi wanataka Zanzibar

iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika.

Baadhi ya Wazanzibari wanadai kuwa mfumo wa muungano u l iopo

unamdhalilisha Rais wao kwani hata ki tarat ibu inampasa Rais wa Zanzibar kupata kibali cha Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa anaposafiri nchi za nje.

“Zanzibar haitambuliki kimataifa kuwa ni nchi na

dola kwa maana kuwa ili Rais Shein akisafiri nchi za nje apokelewe anahitaji kibali cha Waziri Benard Membe; Rais wa nchi gani anayehitaji kibali cha Waziri ili apokelewe kama Rais?” Amehoji mwananchi mmoja.

Msiba: Wazungu wavamia KondoaWANAFIKRA ya Dini na Jaula-Fiisabilillah Tabligh, wanadaiwa kuwaponza wananchi wa Kondoa na hasa Pahi kwa kusababisha wilaya hiyo kuvamiwa na Wachungaji ambao hivi sasa wanaritadisha mamia ya Waislamu kila mwaka.

Taarifa zinasema kuwa mipango na mikakati mikubwa ya makanisa ya Ulaya na Marekani iliwekwa katika kuivamia Kondoa baada ya taarifa kufika huko kwamba ni Makao Makuu ya Tabligh kwa Tanzania na Afrika nzima.

Katika mipango hiyo, inaelezwa kwamba mnamo miaka ya 1998-2000, walifika Wazungu watatu wakiwemo Wa m a r e k a n i w a w i l i (wanawake) na Mjerumani mmoja.

Walifika wakidai kutaka kujifunza lugha na mila za kabila la Warangi.

Mpasha haba r i we tu anaarifu kuwa wageni hao walipokelewa na ndugu mmoja aitwaye Halifa Nchasi (ambaye sasa ni Katibu wa Pahi Islamic Center) na ndugu huyu akawafundisha hawa Wazungu lugha ya Kirangi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wale wanawake walifikia kuishi maisha ya mwanamke wa kawaida wa Kirangi wakishiriki shughuli zote zifanywazo na mwanamke wa kabila hilo kuanzia kuteka maji, kukata kuni hadi kubeba mtoto mgongoni na wakapewa majina ya Kirangi-mmoja akiitwa Mwasu na mwingine Sware.

I l ikuwa n i baada ya kukubalika kama ni sehemu y a j a m i i y a Wa r a n g i , walianzisha mradi uitwao “COMPASSION” ambao ulilenga kuwasaidi Waislamau masikini hususan katika huduma ya afya.

Chin i ya mradi huo , wakaanza kumimina misaada kutoka Ulaya wakianzia na kuweka magari matatu katika vijiji vitatu- moja Pahi

Na Mwandishi Wetu kwenyewe, jingine Kinyasi na jingine Salare.

Magari hayo yalikuwa ni kwa aj i l i ya kubeba wagonjwa kwa kila mwenye mgonjwa kwa kuchangia fedha ya mafuta tu Sh 10,000 kupelekewa mgonjwa wake hospitali ya Wilaya Kondoa mjini kwani tarafa nzima ya Pahi haina hospitali.

Kilichofuatia ni Wazungu hao kuomba kupataiwa ekari 7 ili wajenge zahanati hapo Pahi.

Kwa jinsi walivyokuwa wamejijenga haikuwa tabu kwa uongozi wa serikali ya kijiji kutoa ardhi hiyo baada ya kuwataka ushauri wanakijiji ambao 99% ni Waislamu.

Wa k r i s t o w a k a j e n g a zahanati yao na ikawa pia ndiyo kituo cha kuwakusanya wale Waislamu masikini kwa ajili ya mafunzo maalum kila Jumamosi ambapo wakitoka huko hupatiwa mche wa sabuni, madaftari n.k.

Habari zinasemam kuwa baada ya muda waliomba tena ekari 7 kwa ajili ya kujenga shule ya wasichana.

Hivi sasa wanaendesha shule ya wasichana (bweni na kutwa- boarding na day) yenye kuchukua wasichana 600 na kila mwaka.

K u p i t i a s h u l e h i y o inakadiriwa kuwa takriban wasichana Waislamu 10 huritadi kila mwaka.

Hi i n i mbal i na z i le famil ia z inazor i tadi na watoto wao kupitia mradi wa Compassion.

Kwa sasa COMPASSION imeanzisha mtindo wa “Family Friends” ambapo familia moja masikini ya Kiislamu huunganishwa na familia ya Kikristo huko Ulaya na Marekani na hiyo familia ya nje huisaidia familia ya ndani kwa hali na mali.

Hili nalo limezidisha hatari ya Waislamu kuritadishwa na tayari familia kadhaa zimesharitadi familia nzima.

Hata hivyo pamoja na hatari hiyo, kwa upande wa Waislamu wenyeji wa hapo Pahi wamebaki katika hali

ya kugawanyika wakipigana vita.

A n s w a r S u n n a h wamegawika makaundi mawili yenye kupingana na hawa wanaosema wao ni Bakwata pia ni faraka tupu.

Kwa ujumla hali ya Pahi na vijiji vingi vya Kondoa ni mbaya huku Kondoa sasa ni ikiwa Jimbo la Kanisa Katoliki lenye Askofu wake kamili.

Ambalo linapasa kusisitizwa hapa ni kuwa mikakati hii ya kuir i tadisha Kondoa iliwekwa baada ya Wazungu hawa kusoma kwamba Pahi ni Markaz Kuu ya Fisabiylillahi Tabligh Barani Afrika.

N a n i k w e l i P a h i kulifunguliwa Markazi Kuu ya Fiysabiilillahi Tabligh Afrika mwaka 1981.

Lakini hadi sasa kuna ekari 110 zimekaa tu pasina kutumika mbali na Msikiti uliowekwa jiwe la msingi na aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee Aboud Jumbe.

Pia kuna taasisi nyingine iitwayo IDA inazo ekari

16 nazo zimelala pasi na kufanyika chochote hapo kwa miaka sasa.

Allah anatuambia katika Qur ’an “Na hawatoacha kukupigeni v i ta mpaka wakuri tadisheni kutoka kwenye dini yenu wakiweza..” (Al Baqarah 2:217)

(Habari hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na Sheikh Mohammed Issa ambaye siku ya Jumamosi terehe 24 Novemba, 2012 aliingia Kondoa akiwa amealikwa kuhudhuria sherehe za ufungaji wa shule ya Kiislamu Iqra English Medium School inayoendeshwa na Pahi Is lamic Center, yenye Makao Makuu kijiji cha Pahi, Tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa yenye Waislamu takriban 95%. Kondoa kuna vijiji huwezi kukuta Mkristo hata mmoja lakini hivi sasa kuna kasi kubwa ya kuritadi. Hii ni kutokana na juhudi za Wazungu hawa katika mradi wao unaoitwa “Evangelizing Muslims”)

Sheikh Mohammed Issa (wa pili kutoka kulia)

Inatoka Uk. 1

Page 4: ANNUUR 1047.pdf

4 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala

Asumini sasa hazinukii tena Kikwajuni, Unguja

Inatoka Uk. 2

huku akishangiliwa ambapo akifafanua juu ya watu wanaoharibu dini Unguja alisema kuwa ni wale wa Uamsho ambao hawana heshma hata kwa bendera yao yenye maneno ya Mwenyezi Mungu.

“…Kwa Sheikh Mjanasiri (katika dhikri) bendera inachukuliwa kwa udhu, inawekwa chini kwa udhu…lakini Uamsho anatoka yeye na mwenzie washalawitiana… (wanaikamata)”

Akiwachambua watu aliodai kuwa wanaharibu d in i Ungu ja akasema: “Wanaovunja dini Unguja wanatoka Kisiwa cha Pili (Pemba)”. Kisha akawageukia akawauliza Masheikh wa Pemba: “Nyie mmesoma nini nyie hata Msikiti Baraza hamkujui, Ukutani mnakujua nyinyi, Babu Majaa mesoma nyie, mnatuharibia dini kwa umaa....i wenu basi.”

“Dini tunaijua sie, dini Imani....wao wanachojua kibaya ulevi tu, lakini..”

Na mara kadhaa Mzee Silima akitumia maneno, “Wal l ah i l Adh i im” na “ M t u m e M u h a m m a d ” , huku akiigiza kina mama wanavyoweka vidole na sauti katika mipasho.

Almuhimu ukiwasikiliza w o t e w a l i o o n g e a , wanawakilisha Waislamu na kwa baadhi ya maneno y a o w a n a w a s e m e a Waislamu na kuusemea Uislamu. Na haya walifanya katika muktadha kwamba waliokuwa wakiwatukana ndio wanaoharibu Zanzibar na silka za Wazanzibari.

Sasa sikiliza yaliyosemwa na hao walioanza na aya tukufu ya Qur’an na kuwashutumu wengine kwamba wanaharibu Uislamu Zanzibar. Nilitamani sana kama ingewezekana maneno yao yawekwe kama yal ivyokuwa neno kwa neno, lakini haiwezekani. Itakuwa ni kukariri matusi jambo ambalo siwezi na kwa maadili ya gazeti au chombo chochote cha habari hakiwezi kufanya jambo hilo. Kwa hiyo nitakachofanya hapa ni kutaja tu baadhi ya maneno nitakayoweza na mengine kuyataja kwa lugha za ishara na kiungwana katika namna ambayo msomaji atafahamu.

Katika jumla ya maneno yaliyotamkwa katika mkutano huo wa CCM wa Uwanja wa Mabata, ni kuwaita watu kwa majina kwamba ni “maluuni”,

“wendawazimu”, “mbwa”, “mashoga” n.k. Sasa labda tuulize, haya ndiyo maadili ya Uislamu? Ni kweli Allah hakuumba watu na majini ila wapate kumwabudu. Je,

kuwatukana watu katika majukwaa ndio kumwabudu Allah?

“Dini tunaijua bwana..Dini Imani,..”, ametwambia Mzee Borafya. Je, “Dini Imani”

yenyewe ndio hii ya kuwataja watu kwa majina na kuwaita mbwa mbele ya hadhara?

Lakini mambo mazito zaidi yametajwa. Watu wametajwa kwa majina na kutukanwa

kuwa wanafanyiana mambo yaliyokuwa yakifanywa na mabaradhuli wa Kaumu Lut-Sodoma na Gomora. Bara nako kuna vyama vya upinzani, tena vyenye upinzani mkali dhidi ya CCM. Lakini nililo na uhakika nalo ni kuwa, haijatokea n a h u e n d a h a i t a w a h i kutokea, mtu wa CCM Bara akasimama katika mkutano wa hadhara akamtukania mtu wa Chadema mkewe au kumtaja kwa jina na kumtukana kuwa “anafanyiwa mambo ya Kaumu Lut”. Akimtukana sana atamwita fisadi, sio matusi ya nguoni ya mahusiano ya mke na mume au ya mabaradhuli wanaume kwa wanaume.

Hayo yamefanywa katika mkutano wa CCM Uwanja wa Mabata na haikutajwa lugha ya ishara. Imesemwa wazi fulani “anak....” Na la kusikitisha zaidi, wazee na akina mama watu wazima ukiwatizama wameacha w a j u k u u n y u m b a n i , wanashangilia, wanacheka huku wengine wamepiga hijabu safi kabisa!

Ndio hapa najiuliza, hizi ndio silka za Mzanzibari k u p o r o m o s h a m a t u s i hadharani? Hii ndiyo silka ya Wazanzibari kuwatukania watu wake zao mbele ya hadhara? Huu ndio utamaduni wa wazee na kina bibi wa Kizanzibari wa kuchekelea n a k u b u r u d i k a v i j a n a wakiporomosha matusi ya kwenye madanguro hadharani? Sasa kama hawa ndio walioshika hatamu za uongozi, ndio wanaodhibiti serikali na vyombo vya dola, tunatarajia nchi iende wapi zaidi ya kuangamia kila uchao? Je, wanaotukanwa h a p a n i W a i s l a m u , Wazanzibari au wote kwa pamoja? Kila atakayeangalia DVD ile na kusikia matusi yale atakaloishia kusema ni “hao ndio Waislamu, hao ndio Wazanzibari!”

Mzee Borafia kasema neno la kweli kwamba Asumini siku hizi hazinukii Zanzibar. Labda turudi katika historia ambayo si ya zamani sana. Huo wakati ambao tunaambiwa kuwa Zanzibar zilikuwa zikinukia asumini, mitaa ilikuwa imejaa vijana wavuta bangi, walevi, mateja wa ‘unga’ na wazee ambao vinywani mwao yanatoka matusi huku wazee wenzao wakiona kama burudani tu, wakicheka na kushangilia?

SEHEMU ya hotuba ya M a k a m u M w e n y e k i t i Mstaafu wa CCM Zanzibar kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

“Yapo mambo madogo madogo yanafanywa na wanaharakati sio wanasisa, lakini Serikali yetu imara na Serikali zetu zote mbili imara.

Uvunjifu wa amani hauwezi kuachwa bila kushughulikiwa. Nazipongeza Serikali zote mbili kwa hatua ambazo wamechukua, lakini pia nakubalina mia kwa mia juu ya Azimio la Mkutano Mkuu wa kuiunga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwa nini nasema hivyo, ndugu Mwenyekiti Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ni mwana wetu wenyewe. Tulishirikiana sote wana-CCM pamoja na chama kikubwa cha upinzani kule ambacho ni CUF, vikao vingi vimefanywa, mi sikuwepo, vikiwa vikiongozwa na Makatibu Wakuu wetu.

Wa m e t u p a t a a r i f a mbalimbali mpaka tukafikia mahala tukakubaliana tuiunde Serikal i hiyo. Maelezo a l iyo toa Rais Kikwete (Jakaya) ni sahihi kabisa, mie naunga mkono kwa sababu ndiyo ya kwetu wala sitafuni maneno. Sina sababu ya kufanya hivyo.

Sasa iweje leo baadhi ya wenzetu wawe na wasiwasi na kitu ambacho tumekiunda w e n y w e ? N i s i k i l i z e n i vizuri, kabla hatujaiunda hiyo Serikali yenyewe ya Umoja wa Kitaifa, sisi CCM tulichukua dhamana, tulisema tulipenda iwe hivyo.

Lakini dhamana ya mwisho juu ya mustakabal i wa Zanzibar, ipo katika mikono ya Wazanziabar wenyewe, w a o n d i o w a m e a m u a hamkuamua nyie si mpo hapa, tulikwenda kwenye

Mkutano Mkuu wa Nane wa Taita CCM, Kizota Dodomakura ya maoni matokeo ya kura ya maoni si mmeona?

Kwa hivyo Serikali hii i m e u n g w a m k o n o n a Wazanzibar wenyewe, kilicho salia sasa hivi kuiunga mkono Serikali hiyo, vyenginevyo tutampa tabu mwezetu Dk. Shein (Rais wa Zanzibar), na hususani maneno maneo yakianza kwetu.

Lingine ambalo nataka nilizungumze kidogo ni la mchakato wa Katiba. Watanzania wote, Bara na Zanzibar, wanatoa mawazo yao.

Sasa katika kutoa mawazo lazima tuvumiliane. Kwamba wapo watu wa aina nyingi. Kuna wengine wanataka Muungano, ndiyo wana haki ya kuutaka sana tena. Wengine wanataka Muungano wa Serikali mbili, wengine wanata Serikali mbili za Mkataba, muwastahamilie wote hao, wengine mie B u n g e n i n i m e w a s i k i a wanataka Serikali tatu.

Muwavumilie. Uvumilivu unakushindeni sasa hivi na ndio tupo hapa katika Mkutano Mkuu wa Chama Chama Cha Mapinduzi. Jifundisheni uvumilivu, mnaweza vizuri tu, mnajitia tu hapa.

N y i e h a m j u i u s e m i unaosema kwamba mvumilivu hula mbivu. Basi jifundisheni kuvumilia. Wavumilieni wote wanaotoa mawazo, kwani mawazo hayo mnakusanya nyie, si kuna chombo maalum kimewekwa! Watafanya kazi yao halafu watatoka na moja wapo, CCM Oyee.

Na kwa nini iwe nongwa? Lakini jambo linalonishangaza mimi ni kwamba wakitokea watu wakitoa mawazo tofauti, haoo wanaitwa majina ya ajabu ajabu. Achene bwana kuitana majina ya ajabu ajabu. Sio haki wala sio utu. Nimetanguliza kusoma haki, halafu manajiita wana ASP! Ni ASP ipi hiyo?

Lakini jengine ndugu Mwenyekit i , watu kule Z a n z i b a r w a n a t i s h a n a t i shana , wanawaambia wenzao eeeh, hao wanatoa mawazo haya, wanasema hawa wanataka kumleta Sulutani Baraghashi.

Baraghashi mwenyewe atoke wapi? Hivi kweli m n a a m i n i B a r a g h a s h i atarudi, kwanza ashakufa, CCM Oyeee.

Lakin i l a p i l i h ivyo nyinyi Katiba ya Zanzibar hamuisomi. Ni Katiba ya Kisultani ile? Ile ni katiba ya Jamhuri. Hebu amkeni. Halafu katiba yenyewe m m e i p i t i s h a w e n y e w e mmeiandika wenyewe.

Pandu Amiri Kificho, huyo hapo. Ni mtu wa Sultan huyu? Ndio mkubwa wa Baraza letu na katiba anaipitisha yeye, mtu wa Baraza letu. Msiwatishe watu si vizuri.

Ndugu Mwenyekiti, juzi hapa uliwaalika kina James Mbatia na Shibuda (John) tena wote hao wanatoka vyama vya upinzani. Nyinyi ni vijana wadogo, nimekusomeeni mie, hamjui hekma ya viongozi wenu wa CCM.

Mwenyekiti kawaalika makusudi wale, wamekuja kusema maneno yasiyo ya kipinzani, wamesema maneno ya msingi mazito tena ya kutukumbusha sisi CCM, kwamba nyinyi bwana ndiyo Chama tawala hebu basi jiwekeni vizuri zaidi ili muendelee kutawala.

L a k i n i M w e n y e k i t i , maneno yale yangesemwa na mmoja wetu, tena haswa kule kwetu, angeitwa jina lilelile. Jifunzeni kutoka kwa viongozi wenu waliowatangulia ili muimarishe chama chenu, matumaini ya Chama hiki yamo mikononi mwenu vijana.” Inaendelea Uk. 5

Page 5: ANNUUR 1047.pdf

5 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Habari mchanganyiko

Mwandishi Wetu NECTA haitendi haki Zanzibar-Shamhuna

BARAZA la Mit ihani Tanzania halitendi haki katika kusimamia mambo yake jambo linalosababisha kufeli kwa wanafunzi wengi Zanzibar.

Madai hayo yametolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA) kwa Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seifa Shariff Hamad.

K a t i k a m a d a i h a y o WEMA imesema kuwa Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Baraza la Mitihani, imekuwa ikifanya mabadiliko katika mitaala na kanuni za mitihani bila ya kuishirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, jambo ambalo limekuwa likileta athari kubwa kwa wanafunzi Zanzibar.

Malalamiko hayo yamekuja kufuatia kutolewa habari kuwa mamia ya wanafunzi wa kidato cha sita wamezuiwa kufanya mitihani ya kidato cha sita wakidaiwa kuwa hawana sifa.

Wakati awali ikijulikana kuwa mwanafunzi akiwa na ‘pasi’ tatu anaruhusiwa kufanya mtihani huo, mwaka huu NECTA imesema kuwa ni lazima sasa kuwa na pasi tano.

Madai ya WEMA ni kuwa mabadiliko hayo hayakufikishwa kwa mamlaka husika Zanzibar

na hivyo kushindwa kuifanyia kazi hali ambayo sasa inakuwa ya kuwashutukiza wanafunzi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamuhuna ametoa malalamiko hayo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko Makao Makuu ya Wizara hiyo Mazizini, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika sekta ya elimu.

M h e . S h a m u h u n a amefahamisha kuwa Wizara ya Elimu Tanzania kupitia Baraza la Mitihani la Taifa, mara nyingi imekuwa ikafanya maamuzi bila ya kuishirikisha Wizara ya Elimu Zanzibar, jambo ambalo linawapa ugumu wa kutekeleza mipango yao ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi kuweza kuyafahamu mabadiliko yanayofanywa na Baraza la Mitihani.

Ametoa mfano wa maamuzi yaliyofanywa hivi karibuni na Baraza la Mitihani ya kuwazuia baadhi ya wanafunzi kutofanya mitihani yao ya kidato cha sita hapo Februari mwakani kwa madai ya kutotimiza mashariti

ya kufanya mtihani huo, kwamba Wizara yake haikuarifiwa mapema juu ya masharti mapya ya sifa za kufanya mtihani wa kidato cha sita.

Amesema, Wizara hiyo imekuwa ikikwepa kuiarifu Wizara yake juu ya mabadiliko yanayofanywa na Baraza la Mitihani la Taifa, na badala yake imekuwa ikiziarifu Skuli binafsi, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Amesema, hali hiyo imekuwa ikichangia kutoa matokeo mabaya kwa wanafunzi wa Zanzibar kutokana na kutoarifiwa mapema juu ya mabadiliko yanayofanywa ikiwa ni pamoja na kubadilika kwa ratiba za mitihani pamoja na muongozo wa kufundishia “Syllabus” kwa baadhi ya masomo.

Akizungumzia suala hilo Makamu wa Kwanza wa Rais amezishauri Wizara hizo kukaa pamoja na kujadiliana juu ya hatua bora za kuchukuliwa katika kuondosha tofauti hizo, na kuelezea haja ya kuwepo kwa mashirikiano ya karibu baina ya Wizara hizo mbili.

Baada ya kupokea taarifa ya Wizara hiyo iliyowasilishwa na

Naibu Katibu Mkuu Bw. Abdalla Mzee, Maalim Seif alihoji juu ya uhaba wa madarasa ya kusomea pamoja na vikalio katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba.

Pia ameelezea haja ya kurejeshwa kwa huduma za dakhalia ili kuwaondoshea usumbufu wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali, hoja ambayo imeungwa mkono na uongozi wa Wizara hiyo kwamba wamel i f ik i r ia kwa muda mrefu suala hilo lakini bado wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mwanaidi Saleh amesema Wizara hiyo ina dhamira ya kurejesha huduma hiyo kwa wanafunzi wakati wowote hali ya bajeti itakaporuhusu.

Katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idrisa Ahmada Rai, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais juu ya mipango ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kukifanya kuwa kituo bora zaidi cha elimu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

P r o f e s a R a i a m e s e m a miongoni mwa dhamira kuu za chuo hicho ni kutoa wahitimu wa ngazi mbali mbali ambao wataweza kukabil iana na changamoto za karne ya 21 ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameupongeza uongozi wa Chuo kicho kutokana na mafanikio m a k u b w a y a l i y o f i k i w a

pamoja na mipango imara ya kukiendeleza.

Hata hivyo ameutaka uongozi wa SUZA kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa malengo yake ili kuweza kukamilisha malengo hayo kwa wakati muafaka.

Katika ziara hiyo Maalim Seif pia alitembelea ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Sekondari Mpendae pamoja na ujenzi wa skuli ya sekondari Tunguu, ambapo amewataka wakandarasi wa ujenzi huo kukamilisha kazi zao kwa wakati.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais amefanya mazungumzo na ujumbe wa serikali ya Uturuki ukiongozwa na Waziri wa Chakula, Kilimo na Mifugo wa nchi hiyo Bwana Mehmet Mehdi Eker.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea haja ya kukuza mashirikiano katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi zikiwemo biashara na utalii.

Bwana Aker amesema Uturuki imepata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita baada ya kufanya mabadiliko ya sera yake ya kilimo, jambo ambalo limeongeza uzalishaji hasa katika kilimo cha mpunga.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ameiomba Uturuki kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Zanzibar katika kilimo cha umwagiliaji ikizingatiwa kuwa nchi hizo zina uhusiano wa muda mrefua.

(habari kwa hisani ya Hassan Hamad (OMKR)).

Asumini sasa hazinukii tena Kikwajuni, UngujaInatoka Uk. 4

Moja ya mambo ambayo yamekuwa yakisemwa ni kuwa watu kutoka Bara wanaharibu maadil i ya Zanzibar ambayo kwa kiasi kikubwa ni yale ya Kiislamu. Sasa labda niulize, na haya ya kutukana watu katika majukwaa yametoka Bara? Nani katika wale waliokuwa wakitukana na kushangilia matusi yale anatoka Newala, Sumbawanga au Muleba?

Kwa hakika baada ya kusikiliza yaliyosemwa katika mkutano ule, niliona kuwa pengine namna ya kuisaidia Zanzibar ni kuwa na mfumo wa serikali moja. Zanzibar iwe kama Arusha, Mbeya, Lindi au hata Wilaya kama ilivyo Bagamoyo. Nilifikiri hivi kwa kuona kuwa pamoja na ufisadi unaotajwa katika CCM na viongozi wa serikali, kitaifa na serikali za mitaa; lakini kwa Bara hakuna haya ya kutukanana na kushabikia matusi. Watu wanakamiana katika majukwaa lakini kwa

kutaka maendeleo.Kwa hiyo Zanzibar ikiwa

mkoa au Wilaya, imani yangu ni kuwa nidhamu itakuwa moja na mfumo mmoja pia. Aibu hii ya kutukanana na siasa hizi za chuki na uhasama zitakuwa zimeondoka. Ila tu linaweza kuzuka tatizo kama lile lililoikumba Kigoma, Tabora, Tanga, Pwani, Mikoa ya Kusini na mikoa yote yenye Waislamu wengi. Kwa maana kuwa mfumokristo unaweza kuidumaza Zanzibar zaidi, lakini angalu siasa za matusi, chuki, vitisho na uhasama zitakuwa zimekoma.

H a t a h i v y o , w a k a t i nikitafakari hayo, nilibahatika kupata kanda ya mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi, CUF. Huo ulikuwa mkutano wa hadhara wa kwanza baada ya viongozi wa chama hicho kutukanwa sana. Kwa hiyo mtu ungetarajia kuwa huenda mkutano huo ungekuwa wa kujibu mapigo. Na kweli ulikuwa wa kujibu mapigo, lakini kwa staili nyingine.

Zilielezwa jitihada za kuimarisha chama ikiwa ni

pamoja na kupata wanachama wapya ambapo baadhi yao walipewa kadi siku hiyo. Zikatajwa barabara ambazo mpaka sasa hazipitiki kwa ubovu hasa wakati wa mvua na wakahimizwa Wabunge na Wawakilishi wa maeneo hayo kutekeleza wajibu wao. Wakahimizwa pia wananchi kujitokeza kutoa maoni yao kwa Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba na kwamba wawe huru kutoa maoni yao kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kisheria.

N a j i n g i n e k u b w a lililozungumzwa ni kuinasihi serikali na vyombo vyake, kutekeleza mambo yake kwa mujibu wa sheria. Ijali haki za binadamu na kanuni zote za utawala bora. Serikali ijali na kuwatendea haki raia.

Kama walivyosema baadhi ya wazungumzaji katika mkutano huo, kuongeza wanachama na kushughulikia matataizo ya wananchi na kuwatetea, ndio namna yao ya kujibu matusi.

N a k w a m b a h i y o ndiyo itakuwa nguvu yao watakapokutana na CCM

Oktoba 2015.Kama nilivyotangulia

kusema kuwa nimeandika makala haya kwa sababu moja muhimu: Uislamu umehusishwa. Na mimi naona Uislamu na Waislamu h a w a k u t e n d e w a h a k i katika mkutano ule. Kama zimetajwa Aya za Qur’an, kama yametajwa maadili ya Uislamu, maana yake ni kuwa wazungumzaji waliwakilisha Waislamu na waliyozungumza yalitokana na maadili ya Uislamu. Na Uislamu umesisitiza kuwa Damu na Heshma za watu ni vitu vitakatifu, visiharibiwe.

Ka t ika mku tano u l e wa CCM, wametajwa pia walioitwa watu “Weusi” wakionekana kuwa watu bora huku walioitwa “Waarabu”, wakipuuzwa. Wakatukanwa pia “Watu wa Kisiwa cha Pili” huku hata wale “Wapemba” waliokuwa katika mkutano u le wak ike je l iwa kwa kuambiwa kuwa wao wana akili-“wengine mpo hapa lakini mna akili.”

Haya si katika mafundisho ya Uislamu na ingekuwa vyema kama wanasiasa

wangeshikamana na sera na mambo yao ya k i -CCM badala ya kuingiza masuala ya Uislamu huku wanayoongea yanapingana na Dini yenyewe.

Wa k i s h i k a m a n a n a mambo yao ya ki-CCM na wapayuke watakavyoweza. Kama alivyojisemea Borafia kuwa ngoma kapewa kiziwi, itapigwa mpaka itoboke. Yashakuwa kama yale ya “Sumun bukmun ‘umyun fahum laa yarjiun.”

Lakini swali la msingi ni je, kwa mtindo huu wa kipiga ngoma ya matusi mpaka itoboke, Zanzibar inakwenda wapi?

Kwa mtindo huu wa kupiga ngoma ya chuki, uhasama na ubaguzi wa Weusi na Weupe, Wapemba na Waunguja, tatizo litakuwa muungano wa serikali mbili au nafsi za Wazanzibari wenyewe.

Qur’an ina msemo wake inasema: “Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao. (13:11)

Page 6: ANNUUR 1047.pdf

6 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala

MACHOZI yanatiririka kwa furaha baada ya kupita kizuizi cha mwisho cha askari wa Israil sasa naitizama Qubat Sakhrah kwa chini yake ukionekana Masjid Aqsa-Baitil Muqadas (Misikiti wa Aqsa).

Kaswida ya Twalaal Badiru…aliyoimbiwa Mtume Muhammad (s.a.w) inasikika kutoka vipaza sauti vya Msikiti. Wamefurika kina mama Qubat Zakhrah na wanaume wakiharakisha k u c h u k u a u d h u k u i n g i a Msikitini.

Kasida ya Twalaa l Badru… inaendelea natafakari kwa nini inaimbwa, nakumbuka kwamba ilikuwa Sikukuu ya mwezi mosi Muharram na watu walifurika Msikini hapo kwa sherehe za Muharram.

Baada ya Kasida Imam akasoma aya na kutoa maelezo juu ya tabu aliyopata Mtume na Maswahaba katika kupigania Din i ha l i ambayo nd iyo iliyopelekea kuhama Makkah kwenda Madina na siku hiyo kufanywa ndio mwanzo wa mwaka wa Kiislamu (Hijriya) ambapo wakati huku kwetu tunasherehekea mwaka wa Kikristo, nchi zote za Kiislamu Alhamisi iliyopita ilikuwa siku kuu ya mwaka mpya.

Baada ya kuchukua udhu huku machozi yakizidi kutiririka kana kwamba siamini kama nipo pale panapotajwa katika Qur’an ikisema, “Suhaana ladhiy asraa bi’abdihi lailan minal masjidil haram ilalmasjidil Aqswaa ladhiy baaraknaa haulahuu…”, mahali ambapo walipita Mitume wengi.

Machozi ya furaha na huzuniMasjid Aqswaa imedhibitiwa na Israil

Na Omar Msangi, Yerusalem

Mahali ambapo ndio ilikuwa kituo ambapo Mtume (s.a.w) alipanda kwenda mbinguni na kurejea na swala tano.

Qur’an inasema: “Utukufu ni wake Yeye Ambaye alimpeleka mja wake usiku (mmoja tu)

kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makkah) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baitil Muqaddas-Falastini) ambao (tumeubariki na) tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake. (17:1)

S iamin i kwamba n ipo

Baitil Muqaddas kwanza kwa sababu ya umbali, kutoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka hapo. Lakini pili na ambalo ndio kubwa zaidi, ni kutokana na ardhi hiyo hivi sasa kukaliwa na Israil (toka mwaka 1967). Kwamba pamoja na kupata Viza

ya kuingia West Bank, bado utakumbana na vikwazo vingi sana mpaka kuweza kupenya na kufika katika Msikiti huo.

Na pengine ili upate picha ya ugumu huo, Mpalestina anayeishi Ramallah haruhusiwi kukanyaga Yerusalem. Ni kama hivi unakaa Magomeni, Mapipa, lakini huruhusiwi kufika Kariakoo. Kwa hiyo hata kama unakwenda Kigamboni au Mbagala itabidi uende Ubungo upite mpaka Buguruni, Temeke na kupita barabara ya Kilwa. Kwa Wapalestina wazaliwa wa Yerusalem wamepewa vibali maalum na magari yao yana namba (plate number) za njano ambazo ndio pekee huruhusiwa kuingia Yerusalem. Kwa hiyo ilibidi mwenyeji wetu ambaye ni Mpalestina mwenyeji wa Nablus, atupeleke mpaka kizuizi cha Kalandia (Kalandia Check Point) akarudi na kutuacha sisi wageni kukabiliana na askari wa Israil mpaka kufika. Yeye haruhusiwi kabisa kukanyaga sio Baitil Muqas pekee tu, lakini Yerusalem yote wakati mji huo ni wa Wapalestina. Hivi sasa Israil ina mpango wa kuutwaa mji huo kuwa Mji Mkuu wao badala ya Tel Aviv kwa hiyo kuna kila namna ya kuwatimua hata Wapalestina wanaoishi ndani ya Yerusalem wahame. Na hii wanafanya kwa kuyafanya maisha yao yawe magumu sana ikiwa ni pamoja na kuwakatia maji mara kwa mara, kughasiwa na polisi, kuwekewa vizuizi kutembea na kwenda katika shughuli za kutafuta rizki n.k. mpaka waone bora kuondoka.

Panakimiwa tunasimama kwa Inaendelea Uk. 7

Moja ya Misikiti iliyopo Bethlehem, Palestina.

Yule Afisa wa Baraza la Mit ihani Tanzania aliyekuwa amesimamishwa, amerejeshwa kazini.

Huyo ni Joseph Elias Mbowe ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Takwimu na Matumizi ya komputa.

K u s i m a m i s h w a k a z i kwa Mbowe kulitokana na sababu kuwa yeye ndiye alikuwa na dhamana katika kutoa matokeo ya ‘Islamic Knowledge’ yasiyo sahihi hali iliyozua mtafaruku.

Kwa nafasi yake hiyo, ilionekana kuwa yeye pamoja na Kamati ya Kutunuku, hakuwa mak in i ka t ika kutekeleza wajibu wake.

Kwamba kulikuwa na uzembe kwa vile alishindwa kugundua kuwa matokeo ya somo la ‘Islamic Knowledge’ 2012 yalikuwa na dosari.

An nuur ilipowasiliana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani jana Dr. Joyce Ndalichako alikiri kurejeshwa

Aliyezua balaa NECTA sasa arejeshwa kazini Na Mwandishi Wetu kazini Mbowe akisema kuwa

Kamati iliyoundwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi imegundua kuwa haikuwa kosa la makusudi kutoa matokeo ya Islamic Knowledge ambayo sio sahihi.

Hata hivyo, kutokana na madai ya Waislamu, hilo halikuwa jambo la bahati mbaya bali ni kutokana na utaratibu wa kuhujumu Wa i s l a m u u n a o d a i w a kuwepo kwani kama si hivyo, vilikuwepo vigezo vyote vya tathmini ambavyo vingewezesha kugundua hata kama kulikuwa na kosa la kibinadamu kama NECTA yenyewe ilivyodai.

Awali Baraza pamoja na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza kuwa tayari ishachukau hatua kwa mtumishi aliyesababisha kutolewa matokeo yasiyo sahihi ambapo baada ya Waislamu kulalamika, Baraza lililazimika kubadili matokeo na kutoa matokeo mapya.

Kulingana na uzito na unye t i wa sua l a h i l o , kilichokuwa kimetarajiwa ni kuwa hatua makini zingekuwa zimechukuliwa kuhakikisha kuwa makosa kama hayo hayatokei tena.

Pamoja na mtafaruku ul io tokea kat ika kutoa matokeo ya uwongo katika somo la ‘Islamic Knowledge’, yapo madai kuwa kuna matatizo makubwa katika taratibu za utunuku ambapo jambo hilo limekuwa siri na lisilo kuwa na kanuni maalum za kueleweka na zilizo wazi.

K w a s a b a b u h i y o inadaiwa kuwa kumekuwa na mkanganyiko na ukiukaji wa kanuni za kitaalamu za kuweka “Cut Off Score”, “Pass Mark” na “Grade Range”.

Baada ya kutolewa matokeo ya mara ya pili, yalileta mkanganyiko mkubwa zaidi baada ya kuonekana kuwa watahin iwa wal iokuwa

DKT. Joyce NdalichakoInaendelea Uk. 7

Page 7: ANNUUR 1047.pdf

7 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala

Machozi ya furaha na huzuniInatoka Uk. 6ajili ya swala ya dhuhri. Baada ya swala Imam anatoa maelezo juu ya mauwaji yanayoendelea kufanywa na Israil, maelezo ambayo yanamtoa machozi kila mwenye kuelewa kinachosemwa hata kama hajui Kiarabu.

M u d a h a k u n a m a a n a mwenyeji wetu alituonya kuwa kufuatana na mashambulizi yaliyoanza Gaza hali inaweza ikawa ngumu katika vizuizi au hata kuzuiliwa watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa hiyo haraka haraka tunazunguka Msikiti na kupiga picha baada ya kuleta Dua na nyiradi mbalimbali. Nje ya ukuta wa Msikiti na kwa hakika mji mzima wa inayoitwa Yerusalem ya zamani, wote umezungukwa na ukuta toka kale wenye milango saba ya kuingilia. Na mara kadhaa Israil hufunga milango, hakuna anayeingia wala kutoka.

Nje ya ukuta wa Msikiti tunakumbana na askari wa Israil wanaolinda moja ya milango ya kuingilia. Tunawapita na kuanza safari ya kiasi cha dakika 20 kutoka nje ya eneo la ‘Old Yerusalem’ kupitia mitaa membamba iliyojaa maduka mithili ya mitaa ya Mji Mkongwe Zanzibar tofauti ikiwa moja tu, lakini kubwa sana na muhimu. Pamoja na tabu yote waliyo nayo ambapo wakati mwingine hukatiwa hata maji na kupewa kwa masaa tu kwa siku, mitaa hii ya biashara kama Darajani ni misafi. Huoni taka hata kidogo. Iwe ni duka la nguo, viatu, matunda au mgahawa, ndani na nje ni kusafi.

Pamoja na kuwa kuna utaratibu wa jumla (wa mamlaka ya mji) kufanya usafi, lakini kila

mwenye mlango wa biashara ya aina yoyote, anajali pia usafi wa eneo lake. Ukinunua kitu kama ni nguo ukitoa katika boksi lake, halitupwi ovyo. Yupo mtu wa kuzoa taka hizo na kuzipeleka mahali pa taka kabla hata ya watu wa mamlaka ya mji kupita.

Kabla ya kutoka nje kabisa, tunafika Masjid Omar Bin Khatab ambao unatizamana na Kanisa kubwa maarufu, Kanisa la Watu wa Mwisho (The Church of the Holy Sepulture) ambapo

Wakristo wanaamini kuwa hapo ndio alisulubiwa Yesu na mwili wake kuoshwa kabla ya kwenda kuzikwa mahali jirani na hapo kiasi kama robo kilometa, maarufu ‘The Garden Tomb’. Hii ni bustani ambayo inadhaniwa kuwa asili yake ni ile bustani ya Joseph of Arimathea.

H a b a r i h i i i n a e l e z w a katika Biblia kwamba mahali aliposulubiwa Yesu palikuwa na bustani na katika bustani hiyo palikuwa na kaburi jipya ambapo hapakuwahi kuzikwa

mtu kabla (John 19:41).Bustani hii ndiyo inayodaiwa

kuwa ya Joseph wa Arimathea aliyekuwa tajiri mkubwa na kwamba bustani hiyo ndiyo imeendelezwa mpaka leo.

Tuliingia hapo tukaoneshwa mahali inaposadikiwa kuwa ndio alisulubiwa Yesu na mwili wake kulazwa. Ila haraka haraka nikatoka na kuingia Masjid Omar na kuchukua udhu na kuswali rakaa mbili. Huo ni msikiti ambao ulijengwa na Khalifah Omar Ibn Khattab ambaye alipofika Yerusalem alikuta Kanisa hilo akatakiwa kuswali hapo lakini akasema lau kama ataingia hapo ataacha historia mbaya ambapo Waislamu wa zama zijazo nao wataona kuwa kitendo cha kuingia Kanisani ni sunna. Kwa hiyo akaamuru na kusimamia kujengwa Msikiti ambapo aliswali. Huo ndio Msikiti wa Omar ambao mpaka leo upo.

Jirani kabisa na mahali hapo ndio penye bustani inapoaminika kwamba alizikwa Yesu kabla ya kufufuka kama wanavyoamini Wakristo. Tuliingia hapo na kuingia katika pango na kuona sehemu inayodaiwa kulazwa mwili wa Yesu (Nabii Issa).

Jambo moja muhimu la kugusia hapa ni kuwa tofauti na ilivyo kwa miji ya Makkah na Madinah ambapo ni miji ya Waislamu, hakuna Wakristo; huwezi kusema kuwa Bethlehem alipozaliwa Yesu (Nabii Issa), ni mji wa Wakristo. Kwa hakika ikifika wakati wa swala huwezi kujua kuwa huo ndio mji alikozaliwa ‘Mwokozi wa Wakristo’ kwa sababu adhana inasikika kila kona kutoka Misikiti mbalimbali. Na siku ya Jumapili, kama ilivyokuwa siku hiyo tulipoingia Bethlehem na kuingia katika Kanisa lililojengwa mahali inaposadikiwa kuwa ndipo alipozaliwa Yesu (Church of Nativity), hapakuwa na harakati zozote za wananchi na wakazi wa

eneo hilo kwenda kanisani kama inavyokuwa katika miji yenye Wakristo japo wachache. Kwa hakika Kanisa hilo limekuwa muhimu kwa watalii tu, lakini sio kwa ibada kama ilivyo Msikiti wa Makkah na Madinah.

Safari haikuwa ngumu sana ya kurejea Ramallah kwa sababu kwa vile tulikuwa tunatoka Yerusalem, hapakuwa na kukaguliwa na askari. Hata hivyo tunapoingia mjini, tunakumbana na ha l i ya huzuni . Watu wamejinamia, watoto katika baadhi ya mitaa na barabara wamekusanyika wakiwa na bendera za Palestina wameweka mishumaa chini kwa huzuni wanaiwasha. Nauliza hii ina maana gani ambapo ninaambiwa hawa watoto wanawakumbuka na kuwalilia watoto wenzao ambao waliuawa jana kutokana na mashambulizi ya Israil. Wakati huo huo tukapata habari kuwa Waziri Mkuu wa Israil ametangaza kukusanya jeshi na wanajeshi wengi wa Israil tayari wapo mpakani mwa Gaza.

Mji ambao kwa wiki nzima ulikuwa katika sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa 24 wa kutangazwa taifa la Palestina, ghafla nyimbo na hotuba za sherehe zimesimama. Watu wapo katika majonzi, wakiomba dua na kuungana na wenzao wa Gaza ambao wanashambuliwa toka angani kwa ndege za kivita.

Ni katika hali hii, wenyeji wetu wanatuomba tukatize muda wetu wa kukaa, badala ya kuondoka Jumamosi tuondoke Ijumaa maana huenda hali ikawa mbaya na mipaka ikafungwa. Tunawasihi tubaki hiyo siku moja tumalizie ratiba yetu. Kama kuna baya litakalotokea litakuwa limepangwa. Na zaidi tunaona vibaya, vipi wenyeji wetu wakarimu tuliokaa nao kwa wema na udugu wa kweli, tuonyeshe haraka ya kuwakimbia katika tabu? Japo wenyewe wanatuambia “nyinyi nendeni, sisi tumezoeya, sisi haya ndiyo maisha yetu, ndiyo majaaliwa yetu, ila haturidhii ndio maana tunapambana, na wala hatutakata tamaa, msaada mkubwa tunaotarajia kutoka kwenu, ni kuelewa hali hii kinyume na propaganda inayopigwa mkaungana nasi japo kwa dua.”

Muda ulipofika, kwa hakika tuliondoka kwa huzuni huku tukitizama nyuma kuwaangalia watu wakarimu wa Palestina ambao hatujui mabomu ya Israil yataendelea kuwauwa mpaka lini.

Mashambulizi haya ambayo ni kama yanatuaga au kutuhimiza kuharakisha kuondoka Palestina, yananikumbusha ile familia ya Sha’bi kule Nablus ambayo iliangamizwa kwa kombora la Israil. Aliuliwa babu, bibi, baba, mama na watoto wote baada nyumba kupigwa kombora mwaka 2002. Nyumba ya familia hiyo iliangamizwa ili jeshi la Israil lipate mahali pa kupaki vifaru vyake.

Tulipotembelea nyumba hiyo siku ya Jumanne 13 Novemba, 2012, tulikuta nyumba za jirani na nyumba hiyo zikiwa zimebandikwa picha za watu wa familia hiyo na kuandikwa kuwa hao ni Mashahidi na kielelezo cha uharamia na ukatili wa wavamizi Israil.

KANISA lililojengwa alipozaliwa Yesu (Church of Nativity),

Aliyezua balaa NECTA Inatoka Uk. 6

wamepata “F” na “S”, wote wamepewa “D”.

Ziko namna mbili tu za kueleza jambo hili ambazo ni ama matokeo ya pili nayo ni ya kuchakachua kwa maana kuwa hayatokani na alama halisi katika karatasi za mitihani au kuna tatizo la kuweka ‘Class Interval’ kubwa sana isiyozingatia kanuni za kitaalamu.

Na kwa utaratibu huu usio wa kitaalamu, ndipo unaweza kuona mtoto a l iyepata alama 51 anapewa D wakati mwingine kwa alama hizo anapata C.

Ikiwa hili la kutofuata kanuni za kitaaluma na ki taa lamu ndio sahihi , hiyo inaweza kujibu swali ni kwa nini Kamati ya Kutunuku ilitoa matokeo “yaliyochakachuliwa” ya Islamic Knowledge, bila ya

kuwa na wasiwasi.Madai ni kuwa kama

kungekuwa na uwazi na kama kusingekuwa na ‘mizengwe’, Kamati hiyo isingethubutu kutoa matokeo potofu.

Kwanza, kwa kupitia kanuni husika za kitaaluma n a k i t a a l a m u , m f a n o ‘Statistical Data’, Kamati hiyo ingegundua kuwa kuna kosa.

Lakini kama kungekuwa na utaratibu wa kupitia kazi za Kamati kuona kama ni sahihi, kwa maana kuwa isingekuwa siri, Kamati isingethubutu kufanya kosa hilo.

Ni kutokana na yote hayo, maombi ya Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu lilikuwa kuwa uchunguzi ufanyike kwa masomo yote na sio kwa mwaka jana tu, bali angalau kwa miaka mitano iliyopita.

H a t a h i v y o , h i l o ha l iku fany ika na sa sa kwa kurudishwa kazini

aliyetuhumiwa kusababisha kosa ambalo lilisababisha NECTA kuingia katika wakati mgumu wa kutoa matokeo mapya na kuiondolea sifa ya kuaminika; haitarajiwi t ena kama kuna ha tua zozote zitakazochukuliwa kurekebisha mfumo uliopo.

Taarifa tul izozipata t u k i e n d a m i t a m b o n i zinafahamisha kwamba, Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu limeandaa mkutano wa viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za Kiislamu nchini kujadili yatokanayo na taarifa ya Kamati i l iyoundwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Mkutano huo utafanyika Desemba 9, 2012 jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi ikiwa ni pamoja na mahali utakapofanyika mkutano huo zitatolewa baadaye.

(Soma Tahariri uk. 2)

Page 8: ANNUUR 1047.pdf

8 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala

MWAKA 1964, ujumbe wa iliyokuwa Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki (EAMWS) ulikutana na Rais wa M i s r i w a k a t i h u o , Gamal Abdel Nasser, na kuingia mkataba wa kujengewa Chuo Kikuu Cha Kiislamu, nchini Tanzania.

Katika jiwe la Msingi lili lopo Chuoni hapo, l i n a o n y e s h a k u w a limewekwa mwaka 1968, na kuanisha kujengwa Chuo Kikuu Cha Kiislamu, katika maeneo ya Chang’ombe, Jijini Dar ea Salaam.

Ni miaka minne toka ujumbe wa EAMWS, ukutane na Rais Nasser, na kupata ofa hiyo ndiyo jiwe la msingi liliwekwa kat ika ardhi h iyo ya Chang’ombe, hizo ni juhudi na malengo ya viongozi hao wa Jumuiya hiyo ya Waislamu iliyokuwa na malengo madhubuti na ya dhati ya kuuendeleza Uislamu na Waislamu nchini Tanzania.

Lakini hadi leo baada ya Jumuiya hiyo kuvunjwa na kisha kuwaundia Waislamu BAKWATA, na kurithisha mali zote zi l izokuwa chini ya Jumuiya hiyo, imeshindwa kutimiza ndoto na malengo ya EAMWS na kwa kiasi fulani ustawi wa Uislamu unaweza kusema kuwa umedumaa chini ya BAKWATA nchini.

Kufuatia hali hiyo, Chuo hicho kimebakia na jukumu la kutoa elimu ya Awali, Msingi na Sekondari (Thanawiy) pamoja na mafunzo ya Kompyuta na kuwa maarufu nchini kwa jina la Chuo Cha Markazi Chang’ombe, huku ahadi ya kuwa au kuanza kwa Chuo Kikuu ikiwa bado ipo hewani!

Tokea kuanza kwake ku toa e l imu ya d in i katika ngazi hizo, Chuo kimetoa wanafunzi wengi na kwa asilimia kubwa ya Waislamu, Masheikh, Maustadhi na wanaharakati

Kazi zinazofanywa na Markaz Chang`ombeNa Mwandishi Wetu

mbalimbali wenye hadhi kubwa kubwa hivi sasa ndani na nje ya nchi, wamepitia katika Chuo hicho.

Chuo hicho, ambacho k i n a s i m a m i w a n a kuendeshwa na Wamisri, kutoka katika Chuo Cha Al-Azhar Sharif kilichoko nchini Misr, kimekuwa kimbilio la Waislamu, kuanzia vijana wake kwa waume, wazee na hata watoto wenye uwezo wa kujiweza kusoma.

M u d i r ( M k u u ) w a Chuo hicho kwa sasa a n a y e f a h a m i k a k w a majina ya Dkt. Osama Mahmoud Ismail, anasema majukumu ya Markazi Chang’ombe, kwa kuwa ni Taasisi ya kidini imelenga kufundisha usahihi wa Dini ya Kiislamu kwa vijana wa Kiislamu na Waislamu wote kwa ujumla.

M a f u n d i s h o h a y o yamelenga na kuzingatia zaidi uadilifu, kusamehana na si kulipa kisasi, umoja

na mshikamano miongoni mwa wanajamii pamoja na kuhesh imu d in i zingine kama Qur an inavyofundisha.

Markazi Chang’ombe, mbali ya kutoa elimu hiyo ya dini, lakini pia inajukumu la kuendesha darsa katika Misikiti mbalimbali Jijini Dar es Salaam, pamoja na kuandaa na kutoa hotba za ibada ya swala ya Ijumaa katika baadhi ya Miskiti ya Jijini. Miongoni mwa Miskiti hiyo inayopata huduma hizo ni Masjid Swalihina Keko, Lindi Kariakoo pamoja Masjid Makonde Kariakoo.

Mbali na hayo uongozi wa Markazi chini ya Mudir, Osama, hufanya harakati za kuandaa kozi za Maimamu na Walimu wa Madrasa pamoja na kuendesha mafunzo ya dini kwa kina mama katika Wilaya zote nchini kwa utaratibu maalum.

Chuo Cha Markazi Chang’ombe kat ika kutoa huduma ya kiroho (Daa’wa) kwa Waislamu hushiriki kikamirifu katika ibada za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kuandaa na kusimamia mashindano ya usomaji wa Qur an na kutoa majaji wa kusimamia mashindano mbali mbali na ha ta Kuendesha Darsa za Qur an, kutoa mafundisho ya Hadithi za Mtume Muhammad, sambamba na kujibu maswali ya masuala y a h u s u y o U i s l a m u kutoka kwa Waislamu.

M u d i r , O s a m a a n a s e m a , M a r k a z i Chang’ombe, kwa hapa nchini ina matawi mawili moja likiwa Jijini Arusha na lingine Mkoani Iringa, ambapo matawi yote hayo uratibu wa shughuli zake hufanywa Chuoni hapo (Chang’ombe) ambapo ndiyo makao Makuu. Kwa ujumla Mudir, Osama anabainisha kwamba

Markazi Chang’ombe, h a i f u n g a m a n i n a Taasisi yoyote bali wao ni wawakil ishai wa Chuo Cha Al-Azhar Sharif, na lengo kubwa n i k u w a u n g a n i s h a Waislamu duniani kote.

Kwa maana hiyo, masomo yafundishwayo h a p o y a n a f u a t a muongozo wa Chuo cha Al-Azhari Sharif, k w a n i h a t a v i t a b u vinavyotumika Az-har, ndivyo vinavyotumika Markazi Chang’ombe, halikadhalika walimu kutoka Az-har ndiyo walimu wa Chuoni hapo pia, ambao huja kwa awamu na kukaa kwa muda maalum.

Katika kukuza taaluma ya kimasomo, katika ngazi ya juu Chuo cha Al-Azhar Sharif, hutoa nafasi maalum kila mwaka kwa wanafunzi wa Markazi Chang’ombe, kwenda kusoma Misri, katika ngazi ya chuo kikuu, (Al-Azhar Sharif),

MKURUGENZI wa Kituo cha Kiislamu cha Markaz Chang'ombe, Dkt. Osama Mahmoud Ismail (wa pili kulia waliosimama) Wa kwanza kulia ni Mwalimu wa Chuo hicho, Sheikh Yahya Mkali akiwa na baadhi waalimu na wanafunzi chuoni hapo.

Page 9: ANNUUR 1047.pdf

9 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala/Habari

HALI ya kisiasa Zanzibar bado ni tete chini ya SMZ-GNU. Polisi wanaendelea k u w a c h a r a z a b a k o r a raia wasiokuwa na hatia, kukamatwa na kuvamiwa ndani ya nyumba zao. Kwa maneno ya Mussa Ali Mussa, Kamishna wa Polisi Zanzibar, anasema ‘polisi Zanzibar wanafanya kazi kitaalamu na kisayansi’ zaidi kuliko wananchi wengi wanavyofikiri. Naam, sadakta – wanafanya kazi zao vizuri na kwa ‘sayansi na teknolojia zaidi’.

L a k i n i n i n a c h o t a k a kukisema leo ni kitu kimoja muhimu, wasomaji mjue kuwa tuko wapi kwa sasa, na tunaelekea wapi kama Zanzibar kama nchi. Kada wa CCM, Mzee Borafya Silima Juma, alipokuwa anataka Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini — ndani ya ukumbi wa mkutano wa CCM wakati anapojieleza dhidi ya mpinzani Maalim Mussa, Borafya alisema mambo yafuatayo kama ndio MAADUI WAKUBWA WA ZANZIBAR: GNU, CUF na UAMSHO — hawa ndio maadui watatu kwa Zanzibar.

Borafya aliomba kura kupitia ‘maadui’ hawa. Kwa maana kuwa anawatambua na atapambana nao na alipata Uenyekiti kwa kura nyingi sana. CCM kilibariki kwa hali yoyote mawazo haya. Na CCM taifa kadhalika, na ushahidi upo kuwa CCM walikubaliana na Borafya kwa sababu majina baadaye yalipekwa kunakohusika, na huyo mhusika mkuu baada ya kuona majina yao (Borafya na Maalim Mussa) na baada ya kuangalia video, alicheka sana na kusema kuwa ‘mkateni Maalim Mussa’ na Borafya atatufaa ‘with smiling face’.

Hiyo ndio hali halisi ya Zanzibar na muelekeo wa

Mbele kiza ZanzibarNa Mwandishi Maalum

GNU. kweli GNU itadumu? Itabaki hai kwa mazingira haya?

Katika mkutano wa juzi Amani kwa Mabata, makada wa CCM walikri kuwa wana silaha na watazitumia kwa ajili ya kukihami chama chao, kuihami Zanzibar na uvamizi wa aina yeyote ile. Hii ndio hali tete inayoikabili Zanzibar sasa. Kada wa Chama tawala ana t angaza kuwa wao wanamiliki silaha na mtu huyu ameachwa na vyombo vya dola. Hatujui Polisi, Jeshi na Vikosi watakuwa kazi yao nini!

N a k u m b u k a k a t i k a ufungaji wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu, CCM walitakiwa ‘wawashughulikie wapinzani kwa mikono yao kwanza, then, ndio kama watawapeleka polisi ni hiari yao, lakini kwanza wameshawapa kisago cha nguvu’. Kauli hii iliungwa mkono pale pale (on the spot) na mfungaji mkuu wa kampeni hiyo, Balozi Seif Ali Iddi (Makamo wa Pili wa Rais) alipoacha kulisemea bali ikaonekana kana kwamba analihimiza.

Kuna mengi yametokezea tokea uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu — imekuwa kama v i le kuna v isas i vilivyokuwa vimejificha katika nafsi na mioyo ya watu.

Sasa hali ya Zanzibar inatia shaka sana: kumeongezwa m a k a c h e r o z a i d i , kumeongezwa wanajeshi zaidi Unguja na Pemba. Nasikia hata Polisi kutoka Bara wameongezwa sana- wale akina Juma, Ame, Mafunda, Pandu n.k (hawaamiki sana). Wanaoweza kufanya kazi vizuri ni akina John, Grace, Macha, Nkrumazina etc.

Leo Maalim Seif anasema eti ‘hashirikishwi kikamilifu ndani ya GNU’. Mbona mimi nilikuwa najua toka ile siku namba moja. Na nilisema si yeye, si mawaziri wake — wote wanaonekana si chochote si lolote.

CCM hawawezi kukubali hata siku moja kuwapa CUF ndani ya serikali nafasi kubwa na muhimu. Jamaa zetu wanaendelea kukamatwa ki- siri siri. Na inafanywa kisayansi kama alivyosema Mussa Ali Mussa, Kamishna wa Polisi Zanzibar.

H a l i h i i i n a j e n g a mustakbali mwema kwa Zanzibar au ndio tunaweka mazingira ya kuichafua na kuisambaratisha?

RUPIA (fedha) iliyokuwa inatumiwa na dola ya Zanzibar.

GARIMOSHI lililokuwa likifanya safari zake katika miji ya kisiwa cha Unguja wakati wa uhai wa dola ya Zanzibar.

MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amechangia kiasi cha 3 Milioni, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa kuisaidia Shule ya Daarul Arqam, ya Jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif aliungana na Waislamu na kutoa kiasi hicho na kufanya jumla ya fedha yote iliyochangwa kufikia 7,010,000 milioni, kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme linaloikabili Shule hiyo ya Kiislamu iliyopo Amani Gomvu, Kigamboni

Maalim Seif achangia Daarul Arqam DarNa Bakari Mwakangwale nje kidigo ya Jiji.

Maalim Seif aliyekuwa Mgeni rasmi katika Mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la Saba na Awali, aliongoza harambee hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya shule hiyo.

Harambee hiyo imefuatia hitajio la kiasi cha Shilingi Milioni Tisini, ili kuweza kufikisha Umeme wa gridi ya Taifa, Shuleni hapo, ambapo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo, Mh. Said Ali Mbarouk, kwa upande wake alichangia 1.2 Milioni.

Akiongea kwa niaba ya Mgeni rasmi, katika mahafali

hayo, Mh. Mbarouk, alisema nishati ya umeme ni kitu muhimu katika ulimwengu wa sasa kwani ufundishaji wa kisasa unahitaji mambo ya Kompyuta na mitandao kwa ujumla.

Alisema, haipendezi kijana wa Kiislamu amalize kidato cha nne kisha asijue kutumia Kompyuta kwa ufasaha, kwani katika Ulimwengu wa sasa matumizi ya Kompyuta ni lazima katika maisha ya kilimwengu ya leo.

Alisema, ili kutatua tatizo hilo, Makamo wa kwanza wa Rais, wa Zanzibar, Maalim Seifu, atachangia kiasi

cha Shilingi Milioni Tatu, huku akiahidi kuonana na wadau mbalimbali waweze kuchangia zaidi ili kuondoka tatizo hilo Shuleni hapo kwa muda mfupi.

“ N a m i m i a m b a y e nimemwakil isha kat ika shughuli hii, katika suala la umeme nitachangia kiasi cha Shilingi Milioni moja, kwa kuwa nimeguswa na maendeleo ya kituo hiki hivyo ni lazima niunge mkono” Alisema Mh. Mabaruok, akiunga mkono harambee hiyo.

Akijibu risala kwa ujumla

Inaendelea Uk. 11

Page 10: ANNUUR 1047.pdf

10 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala

Na Khalid S Mtwangi

VIWANJA VILIVYOPIMWAKONGOWE- MJI WA KIBAHA

VINAUZWA(SURVEYED PLOTS AT KONGOWE-

KIBAHA TOWNSHIP) Plan Na E`373/109 Reg. No. 70995

Plots No. Eneo / Sqm Bei5 2,259 13,554,000 6 1,566 9,396,0008 1,984 11,904,0009 3,564 21,384,00010 2,842 17,052,00011 3,732 22,392,00015 2,292 13,752,00016 2,367 14,202,00017 2,423 14,538,000

NB: Kila Sqm ni shilingi Elfu 6000/tu.Kilo Mita Moja kutoka Barabara ya Morogoro,

Kuna Umeme, Maji na Barabara.Kwa mawasiliano zaidi piga simu zifuatazo.

0755 090754 au 0715 090 754

P E N G I N E s i o k w a mwandishi huyu tu bali bila shaka kumekuwa na wasomaji wengine walioona maajabu baada ya kuyasoma na kuyatafakari mawazo na maoni ya Bwana Evarist Chaha l i a l iyoko huko milimani Caledonia. Si dhani kama imefikia kiasi cha yeye kuvaa kilt, sijui ya nasab gani lakini bila shaka kuna machache ya huko ambayo yamenasa. Maoni yake yanaelekeza huko. Inasemekana kuwa sheria za Scotland (ama Uskochi kama Mhariri anavyokuita) zinatoa haki kwa kiasi kikubwa sana kuliko nchi nyingine nyingi Ulaya. Mtuhumiwa kwa mfano haki zake zinalindwa kwa kiwango kikubwa z a i d i k u l i k o E n g l a n d ambako naambiwa ndiko chimbuko la “Common Law” zinazotumika hata petu Tanzania. Samahani kama nimekosea mimi si mtaalam wa sheria kabisa. Nilikokuwa nikifanya kazi nilikuwa nikichekwa ati sikuwahi hata kuona zile kuta nne za darasa!

Sasa inawezekana kabisa kuwa baada ya kuishi huko Caledonia kwa muda mrefu na kuwa mlaji wa “HAGGIS” na “HIGHLAND CREAM” iliyoiva hasa (Whisky), Bw Evarist Chahali ametekwa akili kwa kiwango kikubwa tu kiasi cha kuwa na moyo wa kutaka kupatikana kwa haki hata kwa yule anayetuhumiwa kuwa mhalifu. Katika makala zake zote anaonyesha upevu kabisa wa mawazo hata kama mwandishi huyu hakubaliani na mengine ya mawazo yake. Lakini kwa mazowea tuliyonayo hapa Tanzania, tunaposoma makala kama yake ikiwa ni yale yaliyoandikwa na waandishi wa magazeti na wale waandishi wa makala tu kama yeye na mimi, huwa hakuna busara ama juhudi ya kutafuta haki kama anayoionyesha huyu Bw Evarist Chahali. Ikiwa kama bwana huyu ni Mkristu, basi kweli yeye anafuata mafundisho ya dini yake kwa karibu kuliko wengine wengi nchini humu. Mungu (Allah, SWT) akubariki.

B w a n a C h a h a l i n a

Kilichotokea Mbagala, matatizo yetu ni Uislam na Ukristowasomaji wengine, ile yule mtoto kukojolea Mas-haf ama Qur’an si jambo la ajabu. Labda Mhariri na wasomaji w e n g i n e h a w a t a p e n d a kusoma hivyo lakini ukweli unajulikana miongoni mwa idadi kubwa ya Waislamu kuwa jamii kubwa miongoni mwa Wakristo, wanadharau sana Uislamu na Waislamu. Haya ni kufuatana na mahubiri ya viongozi wao hasa hawa wa madh-hebi yaliyozuka kama uyoga wakati wa masika. Inafahamika kuwa ni agenda ya wanaojiita “Walokole” kufuta kabisa Uislamu duniani (hata Ukatoliki). Pia matamshi mengi ya Papa wa sasa Benedict XVI yanaashiria kabisa chuki dhidi ya Uislamu. Ushahidi upo. Yeyote anayefuata taarifa za habari za dunia na msomaji wa magazeti atafahamu ukweli huo. Hata yale matamshi ya baadhi ya viongozi wa Ukristo hapa Tanzania hakika yanashiria kuwa labda wangefurahi kama ingetokea “Inquisition” mara tena hata kama ni humu Tanzania tu. Nakubali pengine ukweli huu haupendezi, lakini umefika wakati hata wahariri wa magazeti wakubali kuwa ni vizuri ukweli utoke ili ipatikane nafasi ya kuondoa yale yaliyo mabaya yasiyopendeza. Huu si uchochezi, kinachotafutwa ni kuwepo uhusiano mzuri miongoni mwa wananchi wote Tanzania bila kuelewa ile kasumba ya kuwa bora kuliko mwingine ambayo inaonekana miongoni mwa baadhi (sehemu kubwa tu) ya ndugu Wakristo.

Nimekueleza kuwa haya n i maon i ya Wa i s l amu wengi nchini. Baada ya mkasa wa kukojolea Qur’an waliomkamata yule kijana Emmanuel hawakumdhuru kwa aina yeyote pamoja na hasira zao wale Waislamu. Ila hawakupata ushirikiano mzuri kutoka kwa mama yake yule kijana hivyo walimpeleka kituo cha Polisi kutafuta haki. Jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna gazeti hata moja nchini humu lililoandika taarifa hii iliyokweli tupu. Hicho kilikuwa ni kitendo cha kutafuta haki ambacho kabisa wale waliotekeleza h a w a w e z i k u l a u m i w a .Waliongozwa na wazee walio na heshima zao wa sehemu ile. Mmoja wao alikuwa ndiye kiongozi wa dini wa sehemu hiyo, Sheikh Kingo. Ni huyu ndiye alikuwa akishirikiana na Polisi katika tafrani ile. Haiwezekani kuwa waandishi wa habari hawakuweza kupata

taarifa kama hiyo iliyo sahihi; hakika ama hawakutaka kutafuta ukweli ama basi tu kwa vile hapa pana Waislamu wakorofi, basi hapawezi kuwa na usalama. Ukweli ulikuwa ni kwamba ilikuwa takriban siku tatu baada ya yule kijana kupelekwa Polisi ndio Waislamu waliona kuwa wanaonewa kwa sababu hakuna hatua zilizokuchukuliwa kumpeleka Emmanue l mahakamani kitafuta haki.

Bwana Evarist Chahali ni kawaida kabisa kuwa malalamiko kutoka kwa Wai s l amu nch in i humu hayatiwi maanani na hubezwa tu. Tukio hili ni mfano mmoja na ukweli haukuanikwa wazi na magazeti wala Polisi wenyewe. Wakati Kamada wa Polisi akitokea kwenye vyombo vya habari akitoa maelezo hafifu na vitisho, yeye alikuwa anajua ukweli uko wapi. Sina hakika kama ni kosa la jinai ama la kiutawala kukosa kutoa ukweli wote katika tukio kama hilo. Lilikuwa ni kosa kubwa, na adhabu yake pia ilikuwa kubwa, katika shirika nililokuwa nikilifanyia kazi nilipokuwa kijana.

U l i v y o a n d i k a t a r e h e Novemba 14, 2012 kuwa M ATAT I Z O Y E T U S I UISLAM AU UKRISTU……si kweli tupu Bwana Chahali. Mwandishi wa habari wa siku nyingi Bwana Salva Rweyemamu aliwahi kuulizwa akihojiwa katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC) anaonaje hali ya usalama Tanzania huko mbele. Haya yalitokea baada ya maswali juu ya umasikini uliozagaa nchini wakati kuna wengine wanatanua tu. Bw Rweyemamu bila kujiuma ulimi alisema kuwa yeye anadhani kunaweza kutokea fujo za kidini humu Tanzania. Ni takriban miaka saba au minane imepita tangu atabiri hivyo. Nilipokutana naye baada ya kumsikia kwenye radio hiyo ya BBC mimi nilimuunga mkono kabisa.

Si kazi ngumu kufahamu sababu za kuweko mfarakano kiasi hicho, labda tu msomaji azibe masikio na afumbe macho. Kwanza viongozi wa siasa na wale wa dini kila siku wamekuwa wanakosoa tofauti kubwa iliyopo ya walicho nacho na wasio nacho. Hakika hilo ni “time bomb”. Lakini pia lipo lile bonde la ufa kubwa lililopo kati ya Waislamu na Wakristo katika yanja nyingi muhimu nchini humu. Huko

nyuma kwa sababu ya uzalendo wao Waislamu hawakujali sana kama wakuu wa wilaya wote ni Wakristo ama Waislamu. Lakini hivi sasa wametambua kuwa wamekuwa wakidanganywa kwa muda mrefu sana. Ingawa labda halisemeki, lakini ukweli ni kwamba Waislamu wengi wanamlaumu Mwalimu Julius Nyerere kuwa aliwahadaa na kuwatumia. Haya ni baada ya kuona yaliyoandikwa katika vitabu ambavyo vimehaririwa na Kanisa Katoliki humu nchini na nje ya nchi pia. Usiseme hakuna ushahidi. Haya Bwana Evarist Chahali wewe na mimi tunawezaje kupoza hasira hiyo ili uhusiano miongoni mwa Wananchi wetu uwe mzuri sana wa kidugu?

Baada ya kusoma haya utaona kuwa lawama za mfumo wa kibaguzi sio “debe tupu”;. Kwanza ukubali kabisa kuwa malalamiko yao yanabezwa tu. Kila siku walio juu wanasema malalamiko hayana ushahidi ilihali kila siku ushahidi hutolewa na ul io kat ika maandishi. Juzi tu katika kipindi cha HAMZA KASSONGO HOUR kinachorushwa na Channel Ten, Sheikh Khamis Mataka alitamka wazi wazi kuwa Serekali huwa haijali malalamiko ya Waislamu. Wanapoandika barua hata ile “acknowledgement” ambayo ni tendo la kiheshima la kiofisi wao huwa hawapati. Huu ni ukweli Bw Chahali. Halafu umeandika kuwa ni muhimu

kwa Waislamu kuwekeza katika elimu. Huo ni ukweli kabisa; lakini kuna mawili hapa ambayo utafakari. Moja ni kuwa huko juu wizara ya elimu imekaliwa na wengi wasio Waislamu. Ukweli ni kwamba hujuma ni kubwa sana.

Katika kitabu chake ambacho kimepigwa marufuku hapa Tanzania na ambacho unaweza kukisoma kupitia internet ama kwa vile wewe uko Ulaya unaweza kukisoma bila wasi wasi wa kukamatwa, Prof. Hamza Njozi katoa mifano miwili ya hujuma za wazi kabisa. Waliovumbua hujuma hizo mmoja kesha fariki ambaye alikuwa mwalimu wa siku nyingi, Mzee Bori Lila. Wa pili naye ni mwalimu wa siku nyingi Mwalimu Abdurahmani Mwalongo. Bila shaka utakumbuka kuwa Marehemu Kighoma Malima alizongwa sana alipokuwa Wazir i wa El imu. Moja alilolifanya na hivyo kuwaudhi wengi, hasa jamaa wa Kikristo, ni kuhakikisha kuwa mitihani inasahihishwa bila kuweko majina ya watahiniwa kwenye karatasi za majibu yao. Namba tu ndizo zilizotumika. Matokeo yake ni kwamba idadi ya Waislamu waliofaulu mitihani ilipanda kiasi cha 80%!! Jaribu kuchunguza mwenyewe. Hivi sasa kuna malalamiko makubwa dhidi ya utendaji unaotiliwa mashaka mkubwa wa National Examinat ion Counci l of Tanzania. Kuna mkurugenzi mmoja amesimamishwa kazi kutokana na malalamiko hayo ambayo kwa mara ya kwanza serekali ilisikiliza na kuchukua

Inaendelea Uk. 11

Page 11: ANNUUR 1047.pdf

11 AN-NUURMUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012Makala

Matatizo yetu ni Uislam na UkristoInatoka Uk. 10

hatua. Lakini hayo ni baada ya kutishia maandamano makubwa.

Hilo la kuwekeza katika elimu Bw Chahali ni sahihi kabisa. Tangu zamani Waislamu walitambua umuhimu wa kusoma shule. Baba yangu Al Marhum Mzee Shabani Mtoka Mtwangi, alikimbia shule ya msingi ya Ujiji mnamo 1928 kwa sababu ya shinikizo la kubatizwa. Jambo hilo lilikuwa la kawaida liliwafanya vijana wengi wa hapo Ujiji ambao ni mji wa Waislamu, kukimbia shule. Uonevu huo unaendelea mpaka leo kwani watoto wa Kiislamu wanaosoma shule za makanisa wanalazimishwa kuhudhuria misa. Wale watoto wa Kikristo wanaosoma shule za Kiislamu katu hawalazimishwi kuingia misikitini. Kwanza sijui ni lini mara ya mwisho ulikuwa huku nyumbani, lakini hata ukiuliza utaambiwa kuwa hivi sasa Waislamu wamecharuka katika jitihada ya kujenga na kuendesha shule zao hasa za sekondari ingawa kweli standard zao ni za chini. Hivi si kweli kuwa serekali inawapa mapesa mengi sana makanisa kuendesha shule zao na hospitali zao? Waislamu wameona ile Memorandum of Understanding kati ya Serekali na Makanisa. Waislamu hawana bahati hiyo. Kwa ufahamisho hivi karibuni mwandishi huyu alistaajabu kukutana na kijana ambaye kamaliza chuo kikuu baada ya kusoma sekondari moja ya Waswahili pale Ujiji!! Hata hivyo Bw Chahali vigingi bado ni vingi. Unazungumzia

“affirmative action” Bw Chahali. Hilo linawezekana tu Ulaya na Marekani.

N i l i w a h i k u m s i k i a aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw Tony Blair (naye Mscot) akipendekeza kitu kama hicho ili kuwasaidia vijana wenye asili ya Kiafrika ambao walikuwa hawafanyi vizuri katika mitihani yao. Kama ulivyoelekeza Marekani nako walipitisha sheria ya upendeleo kujaribu kuwainua Wamarekani Weusi ambao hali yao kielimu na ajira ilikuwa kama ilivyo leo hapa Tanzania kwa Waislamu. Suala hapa ni kama hilo linawezekana Tanzania? Jibu kutoka kwangu ni kwamba halitawezekana kwa sababu viongozi wa Kikristo wana sauti kubwa

sana. Huweza hata kutoa amri kwa Serekali na ikafuatwa na wao hujigamba hivyo. Kama ni msomaji wa magazeti ya nchi hii utakumbuka kuwa hata Rais kawahi kukemewa hadharani na kuambiwa azungumze vizuri na viongozi hao wa dini kama anataka kura za waumini wao. Yuko yule aliyethubutu kumpa Rais saa arobaini na nane atoe jibu kwa suala alilolitoa kiongozi huyo wa dini. Tafadhali soma kijitabu kilichotolewa na Kanisa Katoliki kiitwacho “ M A F U N D I S H O YA KANISA KUHUSU JAMII” kilichoandikwa na Padre Vic Missien na kutafsiriwa na Mariam (?) Kessy (Mrs). Wameandika hivi: Waislamu wataendelea kudai haki zao wakati wao wanaunda kundi dogo, na pia wataendelea kukiuka haki hizo kwa Wakristu kwa kuwa Wakristu ni wengi na ndio WANAOSHIKILIA AMA WANAOONGOZA SEREKALI”. (Mkazo wa mwandishi huyu).

Haitoshi ni sera ya Makanisa kujaribu kukandamiza Uislamu na Waislamu kama anavyoeleza Padri Dr John Sivalon katika k i t a b u c h a k e K A N I S A KATOLIKI NA SIASA ZA TANZANIA BARA 1953 HADI 1985; mwaka Mwalimu Nyerere alipong’atuka. Ndugu yangu Bw Chahali “affirmative action” haiwezi kuja kwa hiari

nchini humu!Nimalize kwa kukupa

hongera Bw Evarist Chahali kwa kuwa muwazi kiasi hicho ukitoa maoni yako ambayo naamini kuwa wewe unayaamini kuwa ni njia moja ya kuwapatanisha Waislamu na Wakristo nchini humu, Tanzania yetu hii tunayoisifu kisiwa cha amani. Amani ambayo hata hivyo ni “brittle” (bahati mbaya sijui Kiswahili chake). Naomba nikujulishe kwamba mimi ni mtu mzima; wajukuu wangi hupenda kuniita mzee ingawa kila siku nawakataza wasiniite MZEE. Nimefanya kazi hapa Tanzania katika shirika la umma kwa muda wa miaka thelethini na nne hivi; nikianzia karani wa chini kabisa. Kwa hiyo mpaka nilipostaafu nimekutana na watu wengi wa kila aina, Wa k r i s t o n a Wa i s l a m u wenzangu. Nimeona mengi na nimesikia mengi kwa hiyo haya niliyoandika yanatokana na uzoefu huo wa siku nyingi.

Siku moja nilikuwa nimepata bahati ya kuzungumza na msomi mmoja ambaye alikuwa “dDan” wa Kitivo kimoja pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika mazungumzo yetu hayo nilipata nafasi ya kudokeza kuwa kwani yeye hafahamu kama Wakristo wengi, hasa wasomi , wanawadharau sana Waislamu, hata kama Muislamu akiwa msomi?

Huyu bwana alikuwa ni mtu bara bara na mkweli kwani alikubaliana na mimi kuwa rai yangu ilikuwa sahihi. Bwana Chahali kwa kusoma magazeti tu ukachambua yale wanayoyandika wahariri na waandishi wao utayatambua kuwa haya n inayosema ni kweli na hayatokani na chuki yoyote ile. Waandishi wa magazeti wa Kenya wao huwa ni wakweli panapkuwa na jambo ambalo wanaona makanisa wamekosea. Bila shaka unatambua kwamba hao waandishi wa Kenya nao wengi ni Wakristo. Waandishi wa Tanzania hawana ujasiri huo ama hakika wamepikika w a k a i v a k a t i k a y a l e wanayofundishwa na viongozi wao wa Kikristo. Lakini Baba Askofu Mkuu Mstaafu Elinaza Sandoro wa KKKT amehubiri mara nyingi kuwa hapawezi kuwa na amani ambapo hakuna haki

Kwa ufahamisho tu ni kwamba ninao ndugu na jamaa wasio Waislamu ambao uhusiano wetu ni mzuri sana kama udugu unavyostahili; lakini haya ni maoni yangu yanayoshindikizwa na hoja na ushahidi kamili. Bado nikupe hongera Bwana Evarist Chahali kwa mawazo yako yanayoleta faraja kwa mtu anayetafuta ukweli. Endelea kutuelimisha. Endelea kufaidi haggis!

Maalim Seif achangia Daarul Arqam DarInatoka Uk. 9

ya Meneja wa Shule za Daarul Arqam, Ustadhi Shawwal AbdulAziz Msami, i l i yo l a l amik ia dhu lma inayofanywa na Baraza la Mitihani dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu.

Mh. Mbaruok, alisema anakubaliana na madai ya Waislamu kwani al idai hata Zanzibar, katika Shule mbalimbali zimewalalamikia, kwamba kuna tatizo ndani ya Baraza la Mitihani.

Alisema, wao kama Mawaziri, wamemtuma Wazir i wa El imu wa Zanzibar, azungumze na Waziri wa Elimu wa Tanzania Bara, kuhusiana na kutatua kero hiyo ambayo inazikumba sio tu Shule za Kiislamu bali hata Waislamu wengine wanaosoma katika Shule za kawaida.

“Ombi hili tumelichukua, tumeanza kulifanyia kazi, lakini p ia kupi t ia kwa Makamo wa Kwanza wa

Rais, naamini atalifanyia kazi suala hili kwa kadri atakavyojaaliwa.” Alisema Mh. Mbarouk.

Katika hatua nyingine, Mh. Mbaruok, a l isema Uislamu leo una maadui wengi, akawataka Waislamu kuelewa hivyo kwani alidai kwamba kiongozi mmoja wa nchi kubwa duniani alidai Uislamu ni moja ya maadui wake.

“Vita hivi havihitaji ubavu, havihitaji fedha vinahitaji bongo (akili), vinahitaji taaluma ya hali ya juu. Kwa hivyo viongozi wa Shule hii pamoja na walimu mmefanya kazi kubwa sana kuwaandaa vijana kupambana na vita iliyopo.” Alisema Mh. Saidi Ali Mbarouk.

Waziri Mbaruok, alisema katika taaluma inayotolewa kwa vijana hao Shuleni hapo ni lazima iwe ya vitendo ili wawe tayari kukabiliana na hali ya kiulimwengu hivi sasa.

Akisherehesha aya ya Qur

an, alisema Mwenyezi Mungu amesema, hawatokuwa radhi Manaswara na Mayahudi, mpaka wafuate mila zao, kwa maana hiyo akasema vituo hivyo vikikosa kutoa taalamu inayoendana na mila na desturi ya Kiislamu kwa vijana wa Kiislamu, zitapoteza pesa nyingi lakini na vijana wataishia kufuata mila na desturi nje ya Uislamu.

Awali Meneja wa Shule h iyo Ustadhi Shawwal Msami, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, alisema ipo haja kwa Baraza la Mitihani la taifa kufanyiwa mabadiliko ili liweze kutoa haki sawa kwa watahiniwa wa dini zote.

Alisema, wao kama Shule wamestushwa na taarifa za hivi karibuni kutoka kwa wasemaji rasmi wa Serikali kuwa iliwezekana alama za ufaulu kwa watahiniwa wa somo la Maarifa ya Uislamu, k u k o s e w a n a k u w a p a madaraja ya chini tofauti na uhalisia.

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

WAISLAMU wa Masjid Swabirina-Kitunda Mzinga wanatoa shukrani za dhati kwa Waislamu waliotoa misaada yao ya hali na mali katika kufanikisha ujenzi wa Masjid Swabirina. Kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa hatuna budi kuwashukuru na Mwenyezi Mungu awazidishie kila heri inshaallah.

Hivi sasa kunahitajiwa kuendelea na hatua inayofuata ya ujenzi ambayo ni kumimina zege kwa ajili ya kuendeleza ghorofa ya pili. Aidha inakusudiwa kuanza ujenzi wa nyumba ya Imam na vyumba vya madarasa kwa ajili ya kusomeshea watoto wetu. Hivyo kwa mara nyingine tena, tunawaomba msaada wenu wa hali na mali ili kufikia malengo hayo.

Vifaa ninavyohitajika kukamilisha zoezi hili ni nondo, saruji, mchanga na kokoto.

Mtume (saw) aliwahi kusema, “Ukijenga Msikiti Allah (sw) atakujengea nyumba peponi”.

Shime Waislamu tusaidiane katika heri.Kwa mwenye kuitikia wito wetu, mchango wake

anaweza kuuwasilisha katika akaunti ya Msikiti – KCB Bank, Masjid Aswabirina A/C Na 3300386233, Pia Tigo Pesa 0714 565 619

Wabillah TawfiqUst. Khatib Yunus Juma

Amir Jumuia ya Waislamu Kata ya Kiwalani.

Msaada wa ujenzi wa Masjid Aswabirina-Kitunda

Page 12: ANNUUR 1047.pdf

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR12 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 30 - DESEMBA 6, 2012

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila

Ijumaa

MHADHIRI maarufu wa Mihadhara ya Dini ya Kiislamu, Ustadhi Imani Petro, amefariki Dunia. Inalillahi Wainna Illayhir Rajiuuna.

I m a n i P e t r o ( 4 4 ) , ametangulia mbele ya haki Novemba 26, 2012, siku ya Jumatatu wiki hii, majira ya jioni (Magharib), akiwa nyumbani kwake Tabata, Jijini Dar es salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mamia ya Waumin i wa Dini ya Kiislamu na wasio Waislamu walifurika nyumbani kwa marehem, kwa ajili ya kuhudhuria mazishi yake, ambayo yalifanyika mara baada ya swala ya Adhuhuri maeneo ya Tabata Magengeni, Jijini Dar es Salaam.

M a r e h e m u P e t r o , atakumbukwa kama mmoja wa wahadh i r i hoda r i , waliojaaliwa kuichambua Biblia katika Mihadhara ya Dini kati ya Waislamu na Wakristo, ndani ya nchi na nchi jirani.

Na katika harakati hizo enzi za uhai wake ameweza kuingiza mamia ya Wakristo katika Uislamu.

Imani Petro afarikiNa Bakari Mwakangwale

Awal i , Imani Pe t ro , kabla ya kuwa Mhadhiri katika mihadhara ya kidini alikuwa Mkristo wa dhehebu la Pentekoste na mwaka 1986, alikuwa Mchungaji katika Kanisa la Pentekoste Mzambarauni (Mburahati), na alisilimu mwaka 1991.

Marehemu, aliwahi kuwa kiongozi wa kikundi cha Mihadhara cha Nyuki , kilichojumisha wahadhiri mbalimbali wa Jijini Dar es Salaam, alikuwa ni mmoja wa hadhiri wachache ambao walipenda zaidi kufika vijijini na kuitangaza na kuulingania Uislamu, akitumia zaidi Biblia.

Aidha , Imani Pet ro , a l iwahi kukamatwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kisha kupelekwa N g e r e n g e r e , M k o a n i Morogoro akisadikiwa kuwa ni kwao, chini ya ulinzi mkali, kama ilivyo kawaida ya Serikali zetu zinavyoshughulikia masusla ya Waislamu, hususani unapoyagusa Makanisa.

Marehemu, alikubwa na mkasa huo akiwa katika

harakati zake za kuuchambua Ukristo.

Marehemu Iman Petro, alizaliwa mwaka 1968, Jijini Dar es Salaam, akiwa ni mwenyeji wa Mkoa wa Morogoro, katika Kijiji cha Mkulazi.

I m e e l e z w a k u w a Marehem, Petro, alianza kuungua mwanzoni mwa mwaka huu, akiwa Mbinga, Mkoani Ruvuma, katika shughuli zake za Da’awa.

Pamoja na jitihada za famil ia yake kumpatia msaada wa kimatibabu, lakini hali ilizidi kudhoofu siku hadi siku mpaka pale alipofikwa na umauti kwani ahadi yake ilikuwa imetimia na maradhi hayo kuwa ni sababu tu ya kifo chake.

M w e n y e z i M u n g u anasema, “Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuichelewesha.” Qur an 15:5.

Marehemu ameacha mke mmoja (mjane) na watoto wanne.

Mwenyezi Mungu amlipe amali njema kulingana na juhudi zake katika Uislamu, na amsamehe pale alipokosea. Amin.

ALMARHUUM Imani Petro enzi za uhai wake

BENKI inayotoa huduma za kibenki kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu nchini, Amana Bank, wiki iliyopita iliadhimisha mwaka mmoja tangu ilipofungua milango ya huduma kwa wateja mwishoni mwa Novemba mwaka 2011.

M a a d h i m i s h o h a y o yaliambatana na wiki ya H u d u m a k w a Wa t e j a , ambapo Benki hiyo ilitoa nafasi kwa wananchi na wateja kujifunza zaidi juu ya huduma zake.

A k i z u n g u m z a n a waand i sh i wa haba r i , Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Idris Rashidi , al isema kuwa wameamua kusherekea mwaka mmoja wa Amana Bank kwa kuanza na wiki ya huduma kwa wateja.

Alisema wiki hiyo ya huduma kwa wateja ilianza Novemba 19 hadi Novemba 23, 2012.

Amana Bank yaadhimisha mwaka wa hudumaNa Shaban Rajab Alisema lengo la kuweka

wiki hiyo ni kuwapa wateja na jamii kwa ujumla fursa ya kupata elimu kuhusu huduma za kibenki zinazofuata Shariah kikamilifu.

Aliongeza kuwa Amana Bank inajivunia kuwa benki ya kwanza Tanzania inayofuata Shariah kikamilifu, ikiwa na lengo la kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee zinazozingatia maadili ya Kiislamu.

Dkt. Rashid, ambaye katika kilele cha sherehe hizo alikuwa miongoni mwa watendaji waliokuwa wakitoa huduma kwa wateja katika tawi la Tandamti Kariakoo, alisema benki hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa njia iliyo wazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wadau wote.

Katika kipindi ha mwaka m m o j a , A m a n a B a n k imefanik iwa kufungua matawi matatu ambayo ni Tawi la Tandamti, lililoko mkabala na soko kuu la Kariakoo, tawi la Barabara ya

Nyerere na Main Branch. Pamoja na kuanza na

mtandao huo wa matawi, Amana Bank pia imeongeza huduma ambazo zinalenga kumrahishia mteja kupata huduma za kibenki popote alipo.

Hivi karibuni benki hiyo ilizindua huduma ya Amana Mobile Banking.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo, ilieleza kuwa huduma hiyo inamuwezesha mteja kupata huduma kupitia simu yake ya mkononi.

Kwamba kwa kupitia huduma hiyo, mteja anaweza kujua salio la akaunti yake, kununua muda wa maongezi, kuomba kitabu cha hundi n.k.

A m a n a I n t e r n e t Banking imetajwa kuwa ni huduma nyingine ambayo imezinduliwa na Amana Bank.

H u d u m a h i y o inamuwezesha mteja kupata huduma za kibenki kupitia mtandao wa intaneti. Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Idris Rashidi.