56
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA IDARA YA UTAFITI NA UDHIBITI UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: UTAFITI KIFANI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO (A CASE STUDY OF IODATED SALTS) 2013

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

  • Upload
    others

  • View
    13

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAT A A S I S I YA K U Z U I A N A K U P A M B A N A N A R U S H W A

I D A R A YA U TA F I T I N A U D H I B I T I Udhibiti Wa bidhaa bandia: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto

(A CASE STUDY OF IODATED SALTS)

2 0 1 3

Page 2: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE
Page 3: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

iii

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIATA A S I S I YA K U Z U I A N A K U PA M B A N A N A R U S H WA

IDARA YA UTAFITI NA UDHIBITI Udhibiti Wa bidhaa bandia: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto

(A CASE STUDY OF IODATED SALTS)

2 0 1 3

Page 4: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

iv

MUHTASARI (EXECUTIVE SUMMARY)

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya utafiti huu kwa lengo la kutoa ushauri wa namna bora ya kuimarisha mfumo wa usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto kwa mamlaka zinazohusika katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi kwa matumizi ya binadamu na wanyama. Aidha, madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: (i) kutathmini hali ya upatikanaji na matumizi ya chumvi yenye madini joto, (ii) kupima uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, (iii) kutathmini utaratibu wa mawasiliano ya wadau katika mpango na (iii) kuangalia utekelezaji wa sheria na hatua zinazochukuliwa dhidi ya wakiukaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto.

Utafiti huu ulifanyika katika mikoa ya Dar Es Salaam, Kigoma, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mwanza, Mtwara, Rukwa, Singida na Tanga. Taarifa za msingi zilikusanywa kwa kutumia dodoso, “checklists”, miongozo ya majadiliano (interview guides/schedules), majadiliano kwa njia ya vikundi (Focus Group Discussions - FGDs), ziara za watafiti katika maeneo ya uzalishaji wa chumvi na unyambulisho (analysis) wa kimaabara wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi zinazoagizwa kutoka nje na kuuzwa katika ‘supermarkets’. Viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi kutoka katika kaya, maduka, masoko na minada vilipimwa kwa kutumia “Rapid Salt Test Kits”. Taarifa za upili zilipatikana kwa kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo sera, sheria, taratibu na kanuni zinazohusiana na udhibiti wa bidhaa bandia na chumvi yenye madini joto (Iodated salt); na taarifa za kazi zilizofanywa na wadhibiti na watafiti wengine.

Matokeo ya utafiti huu yanaainisha upatikanaji na matumizi ya chumvi yenye madini joto; uwazi katika habari, elimu na mawasiliano; utoaji wa taarifa za uwajibikaji; ushirikishwaji wa wadau na kukubalika kwa mpango, uratibu wa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi; usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto; ufanisi na kufaa kwa mpango; changamoto zinazoukabili mpango; na maoni ya wadau juu namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo.

Upatikanaji na matumizi ya chumvi yenye madini joto: Matokeo yanaonesha kuwa asilimia 78 ya kaya zinatumia chumvi yenye madini joto kwa kiwango pungufu na toshelevu. Asilimia 62 ya kaya zinatumia chumvi yenye madini joto kwa kiwango toshelevu (>15 ppm) na asilimia 16 ya kaya zinatumia chumvi yenye madini joto kwa kiwango pungufu (<15 ppm). Kulingana na Shirika la Afya duniani (World Health Organization), matumizi ya chumvi yenye madini joto (kiwango toshelevu - >15 ppm) katika ngazi ya kaya yanapaswa kuwa zaidi ya asilimia 90 ili kuwezesha kuondokana na madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto. Asilimia 65 ya sampuli ya chumvi ya mawe kutoka katika maduka ya reja reja, sokoni na kwenye minada zimebainika kutokuwa na madini joto. Aidha, asilimia 25 ya sampuli za chumvi zilizofungashwa katika pakiti zilizokusanywa kutoka katika maduka ya rejareja hazikuwa na madini joto. Kuhusiana na sampuli za chumvi kutoka ‘supermarkets’, mchanganuo wa kimaabara unaonesha kuwa asilimia 54.6 ya chumvi hizo hazikuwa na madini joto.

Page 5: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

v

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Aidha, asilimia 27.3 ya sampuli za chumvi hizo zilikuwa na madini joto kwa kiwango pungufu (<25 ppm) na zimechanganywa na madini joto kwa kutumia ‘potassium iodide’ ambayo hairuhusiwi kisheria kutumika hapa nchini. Ni asilimia 18.2 tu ya sampuli hizo zilikuwa na madini joto kwa kiwango toshelevu yaani > 25 ppm. Kiwango toshelevu cha madini joto kinachotakiwa kwa sampuli zilizonyambulishwa katika maabara ni 25 – 75 ppm katika ngazi ya uuzaji (retail level).

Uwazi katika Habari, Elimu na Mawasiliano: Matokeo yanaonesha kuwa asilimia 48.6 ya wahojiwa hawakubaliani na dhana kuwa chumvi yote inayouzwa katika maduka ina madini joto. Aidha, asilimia 40.9 ya wahojiwa hawakubaliani na dhana kuwa jamii imeelimishwa na kuwezeshwa kuitambua chumvi yenye madini joto. Kuhusu upatikanaji na kueleweka kwa habari za mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, wahojiwa wanaeleza kutopatikana (37.3%) na kutokueleweka (29.7%) kwa habari za mpango huo. Hii inaashiria kuwepo kwa udhaifu katika mikakati ya utoaji habari, elimu na mawasiliano.

Utoaji wa taarifa za uwajibikaji: Matokeo yanabainisha kuwa asilimia 24.7 ya wahojiwa wanakubaliana na dhana kuwa wazalishaji na waagizaji wa chumvi wanatoa taarifa za uwajibikaji kwa Serikali, asilimia 37.3 hawakubaliani na waliobaki (38%) hawana uhakika na kutolewa kwa taarifa hizo. Hii inaashiria kuwepo kwa uwajibikaji mdogo miongoni mwa wazalishaji na waagizaji wa chumvi.

Ushirikishwaji wa wadau na kukubalika kwa mpango: Matokeo yanaonesha kuwa asilimia 38.1 ya wahojiwa wanakiri kukubalika kwa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi na 48.2% hawana uhakika na kukubalika kwa mpango husika.

Uratibu: Matokeo yanabainisha kuwa asilimia 32.6 ya wahojiwa wamekubali kuwa mpango husika unaratibiwa vyema na kwamba Serikali inatoa mrejesho (feedback) kwa wadau. Aidha, ni asilimia 16.3 tu ya wahojiwa wanakubali kuwa kuna miundombinu inayojitosheleza ya kupokelea na kushughulikia malalamiko ya wadau wa mpango wa kuondoa tatizo la upungufu wa madini joto.

Usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria na kanuni: Matokeo yanaonesha kuwa asilimia 55.5 ya wahojiwa wanaeleza kuwepo na kufanya kazi kwa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto na asilimia 85 wanafahamu kuwa kuchanganya madini joto katika chumvi ni sharti la lazima. Aidha, asilimia 40.1 wanakubali kuwa vyombo vinavyosimamia na kutekeleza sheria na kanuni vinafanya kazi ipasavyo. Asilimia 40 wanaeleza kuchukuliwa ipasavyo kwa hatua dhidi ya wakiukaji wa sheria na kanuni. Hata hivyo, baadhi ya maafisa afya (18.8%) walieleza kutochukua hatua yoyote dhidi ya wakiukaji.

Ufanisi na kufaa kwa mpango: Imebainika kuwa asilimia 66.3 ya wahojiwa wanaeleza kuwa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi unafaa na unatoa matumaini ya kupungua kwa madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto mwilini ikiwemo uvimbe wa tezi la shingo (goiter). Kwa upande mwingine, asilimia 33.2 ya wahojiwa wanakubali kuwa mpango una ufanisi na jitihada za Serikali zinawiana na mafanikio yaliyopatikana.

Page 6: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

vi

Changamoto: Utafiti umebaini changamoto zinazoukabili mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, changamoto hizo ni pamoja na uelewa mdogo wa madhara ya upungufu wa madini joto kwa wadau na baadhi ya viongozi wa serikali wenye dhamana ya kutoa maamuzi, upatikanaji endelevu wa fedha na vitendea kazi (rapid salt test kits na vyombo vya usafiri) kwa ajili ya ukaguzi na ufuatiliaji, ukaguzi na uchukuaji wa sampuli za chumvi wa mara kwa mara hasa ukaguzi madhubuti kwa wazalishaji kabla ya chumvi kusambazwa, udhaifu katika utekelezaji wa sheria na kanuni, kukubalika kwa dhana ya matumizi ya chumvi yenye madini joto na uwepo wa wazalishaji wadogo wa chumvi wanaoingiza sokoni (kwa walaji) chumvi isiyo na madini joto

Maoni ya wadau ya kukabiliana na changamoto: Utafiti umebaini changamoto zinazoukabili mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, changamoto hizo ni pamoja na uelewa mdogo wa madhara ya upungufu wa madini joto kwa wadau na baadhi ya viongozi wa serikali wenye dhamana ya kutoa maamuzi, upatikanaji endelevu wa fedha na vitendea kazi (rapid salt test kits na vyombo vya usafiri) kwa ajili ya ukaguzi na ufuatiliaji, ukaguzi na uchukuaji wa sampuli za chumvi wa mara kwa mara hasa ukaguzi madhubuti kwa wazalishaji kabla ya chumvi kusambazwa, udhaifu katika utekelezaji wa sheria na kanuni, kukubalika kwa dhana ya matumizi ya chumvi yenye madini joto na uwepo wa wazalishaji wadogo wa chumvi wanaoingiza sokoni (kwa walaji) chumvi isiyo na madini joto.

SHUKRANI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa shukrani zake za dhati kwa wale wote walioshiriki katika kufanikisha utafiti huu. Kwa kuwa si rahisi kuwataja wote walifanikisha utafiti huu, shukrani za pekee ziwaendee wadau wote walioshiriki katika utafiti huu ambao ni wananchi; wazalishaji, waagizaji, na wauzaji wa chumvi; Maafisa Afya na Maafisa wa Taasisi ya Chakula na Lishe na Mamlaka ya Chakula na Dawa.

Page 7: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

vii

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

ORODHA YA VIFUPISHO

NCCIDD National Council for Control of Iodine Deficiency Disorders

NGOs Non Governmental Organizations

TFDA Tanzania Food and Drugs Authority

UNICEF United Nations Children’s Emergency Fund

WHO World Health Organization

TASPA Tanzania Salt Producers Association

TDHS Tanzania Demographic and Health Survey

SPSS Statistical Package for Social Science

TFNC Tanzania Food and Nutrition Centre

KAPB Knowledge, Attitudes, Practices and Beliefs

FGDs Focus Group Discussions

TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa

URT United Republic of Tanzania

IOCs Iodized Oil Capsules

IDD Iodine Deficiency Disorder

ppm parts per million

TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Page 8: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

viii

YALIYOMO

MUHTASARI (EXECUTIVE SUMMARY).........................................................................................................iv

SHUKRANI ................................................................................................................................................... vi

ORODHA YA VIFUPISHO ............................................................................................................................. vii

YALIYOMO ................................................................................................................................................. viii

ORODHA YA MAJEDWALI........................................................................................................................... ix

SURA YA KWANZA ........................................................................................................................................ 1

1.0 UTANGULIZI ................................................................................................... 1

SURA YA PILI ................................................................................................................................................. 4

2.0 MBINU ZA UTAFITI ................................................................................................................... 4

2.1 CONCEPTUAL FRAMEWORK ................................................................................................ 4

2.2 Maeneo ya Utafiti ...................................................................................................................... 5

2.3 Ukusanyaji wa Taarifa ............................................................................................................ 5

2.4 Upatikanaji wa Sampuli Wakilishi ....................................................................................... 5

2.5 Ukubwa wa Sampuli ................................................................................................................ 6

2.6 Uchambuzi na Uchanganuzi ................................................................................................. 6

SURA YA TATU .............................................................................................................................................. 8

3.0 MATOKEO YA UTAFITI ............................................................................................................ 8

3.1 WASIFU WA WAHOJIWA.......................................................................................................... 8

3.2 UPATIKANAJI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO ........................................................8

3.3 UTAWALA (GOVERNANCE) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO ........................................................................................................................................... 15

3.4 URATIBU (COORDINATION) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO ........................................................................................................................................... 20

3.5 USIMAMIZI (ENFORCEMENT) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO ........................................................................................................................................... 21

3.6 UTENDAJI (PERFORMANCE) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO ........................................................................................................................................... 24

3.7 CHANGAMOTO KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO ...............26

3.8 MAONI YA WADAU KUHUSU UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO .....26

SURA YA NNE ............................................................................................................................................. 28

4.0 MJADALA .......................................................................................................28

SURA YA TANO....................................................................................................................................35

5.0 MAPENDEKEZO NA HITIMISHO .....................................................................35

5.1 MAPENDEKEZO .............................................................................................35

5.2 HITIMISHO .....................................................................................................38

MAREJEO .................................................................................................................................................... 39

Page 9: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

ix

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

ORODHA YA MAJEDWALI

Jedwali 1: Mchanganuo wa wasifu wa wahojiwa kiumri na kielimu

Jedwali 2: Mchanganuo wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi zilizokusanywa kutoka katika kaya

Jedwali 3: Mchanganuo wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi ya mawe zilizokusanywa kutoka katika maduka ya reja reja, sokoni na kwenye minada.

Jedwali 4: Mchanganuo wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi za pakiti zilizokusanywa kutoka ‘katika maduka ya reja reja.

Jedwali 5: Mchanganuo wa kimaabara wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi zilizokusanywa kutoka ‘supermarkets’

Jedwali 6: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu utunzaji wa chumvi katika vifungashio na vyombo maalum vinavyotakiwa katika ngazi ya uzalishaji na kaya ili kuzuia kupotea kwa madini joto

Jedwali 7: Mwitikio wa wadau kuhusu athari za chumvi isiyo na madini joto

Jedwali 8: Mwitikio wa wadau kuhusu uwepo wa chumvi yenye madini joto katika maduka yote

Jedwali 9: Mwitikio wa wadau kuhusu kuelimishwa na kuwezeshwa kwa jamii kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto

Jedwali 10: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu upatikanaji na kueleweka kwa habari za mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

Jedwali 11: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu wazalishaji na waagiza wa chumvi kutoa taarifa za uwajibikaji kwa serikali

Jedwali 12: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kukubalika na wadau wote kwa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

Jedwali 13: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu Serikali kutoa mrejesho (feedback) kwa wadau wa hatua na mikakati ya usimamizi wa mpango wa madini joto katika chumvi

Jedwali 14: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kujitosheleza kwa miundombinu ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya wadau

Jedwali 15: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu uwepo, kufanya kazi kwa sheria, kanuni na taratibu; na ulazima wa kuchanganya madini joto katika chumvi

Jedwali 16: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu vyombo vya usimamizi wa sheria kutekeleza wajibu wao ipasavyo

Page 10: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

x

Jedwali 17: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kuchukuliwa kwa hatua stahili dhidi ya wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu

Jedwali 18: Mwitikio wa maafisa afya kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya wazalishaji na wauzaji wanaouza chumvi isiyo na madini joto kwa kipindi cha 2009 hadi 2012

Jedwali 19: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu usimamizi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto ili kutoa matumaini ya kupunguza idadi ya wagonjwa wa uvimbe wa tezi la shingo (goiter)

Jedwali 20: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kuwiana kwa jitihada za serikali na mafanikio ya mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

Jedwali 21: Mchanganuo wa changamoto zinazoukabili mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

Jedwali 22: Mchanganuo wa maoni ya wadau (wahojiwa) kuhusu udhibiti wa viwango vya madini joto katika chumvi

Page 11: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

1

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

SURA YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI

Biashara ya bidhaa bandia ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili nchi mbalimbali duniani hivi sasa. Kimsingi, bidhaa bandia ni bidhaa zinazotengenezwa kwa lengo la kumlaghai mtumiaji kwa kuwekewa nembo, alama na maelezo ya bidhaa yanayofanana na bidhaa halisi inayotambulika. Katika biashara hii, mtumiaji anaweza kununua bidhaa bandia akiamini kuwa ni bidhaa halisi (bila kujua) au kwa hiari yake (akiwa anajua) kutokana na hali ya uchumi wake (bei nafuu). Soko la bidhaa hapa nchini limevamiwa na bidhaa bandia na baadhi ya watumiaji wanaziona kuwa ni muhimu na pengine ndiyo njia pekee iliyo rahisi ya kufurahia manufaa yatokanayo na uwepo wa soko huria na hata wengine wakishindwa kuzitofautisha na bidhaa halisi. Uelewa mdogo kuhusu bidhaa bandia na athari zake na umaskini wa kipato miongoni mwa wananchi ni kati ya sababu za msingi zinazochangia kukua kwa biashara ya bidhaa bandia hapa nchini.

Miongoni mwa bidhaa zinazotumiwa na watu wote ni pamoja na chumvi, ambayo iwapo itakuwa bandia1 inaweza kuleta madhara makubwa kiafya. Kwa mujibu wa kifungu cha 4 na 5 vya kanuni za chumvi yenye madini joto za 2010 za sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 (The Tanzania Food, Drugs and Cosmetic Act No. 1 of 2003), hairuhusiwi kutengeneza, kuagiza, kuuza au kusambaza chumvi isiyo na madini joto kwa matumizi ya binadamu na wanyama (URT, 2003). Sheria na kanuni zinaagiza chumvi ya matumizi ya binadamu na wanyama ichanganywe na madini joto kwa kuwa matumizi ya chumvi bandia (chumvi isiyo na madini joto) yanaweza kusababisha magonjwa au madhara yatokanayo na upungufu wa madini hayo.

Madini joto ni sehemu muhimu ya virutubisho vidogo (micronutrients) yanayohusika na ukuaji wa kimwili na kiakili wa binadamu. Madini haya ni sehemu muhimu ya homoni za kikoromeo (thyroid hormones) ambazo ni ‘thyroxin’ na ‘triiodothyroxine’ na upungufu wa viwango vya madini joto katika damu husababisha uzalishaji duni wa homoni hizi. Upungufu wa homoni hizi huathiri ukuaji na ufanyaji kazi wa ubongo, misuli, ini, na figo na hivyo kusababisha upungufu wa madini joto (Iodine Deficiency Disorders –IDDs).

Athari ya ‘IDD’ inayoonekana wazi ni uvimbe wa tezi la shingo (goiter) lakini yapo madhara mengine hatari zaidi (yasiyo wazi) ikiwemo kuharibika kwa ubongo, vifo vya watoto wachanga, akina mama wajawazito kujifungua watoto walemavu, mimba kuharibika au watoto kuzaliwa kabla ya wakati (watoto njiti). Aidha, watoto wanaozaliwa na akinamama wenye upungufu wa madini joto huweza kupata mtindio wa ubongo ambao ni ulemavu wa kudumu. Hapa nchini, madhara ya upungufu wa madini joto ulitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1963 (Latham, 1965) na kati ya 1980 na 1990.

1 Chumvi bandia katika utafiti huu ni chumvi isiyo na madini joto au yenye kiwango cha madini joto pungufu iliyofungashwa katika vifungashio vyenye nembo na maandishi ya kuonesha ina madini joto kwa kiwango toshelevu

Page 12: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

2

Hivyo, uwepo wa chumvi bandia unadhoofisha juhudi za serikali zilizokwisha chukuliwa dhidi ya madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto tangu miaka ya 1980. Juhudi hizo ni pamoja na kugawiwa kwa vidonge vyenye madini joto (Iodised Oil Capsules-IOCs) na kuridhiwa kwa mkakati wa kudumu wa kuchanganya madini joto katika chumvi tangu mwaka 1996. Mkakati huu ulikuwa na lengo la kuondoa na kutokomeza kabisa athari zitokanazo na upungufu wa madini joto ifikapo mwaka 2000 (Kavishe na Mushi, 1993).

Tathmini za mkakati huu zilifanywa kupitia tafiti (surveys) mbalimbali na kuonesha mafanikio makubwa katika kupunguza madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto ikiwemo uvimbe wa tezi la shingo (goiter). Mafanikio hayo ni pamoja na kupungua kwa tatizo la ugonjwa wa ‘goiter’ kutoka asilimia 25 mwaka 1980 hadi asilimia 7 mwaka 2004 na takribani asilimia 95 ya watoto wa umri wa miaka 6 - 12 walikuwa wamekingwa na madhara ya upungufu wa madini joto. Tafiti hizi zinaonesha mafanikio makubwa ya kuwakinga mamilioni ya watoto kutokana na athari za upungufu wa madini joto, hasa vifo na uharibifu wa ubongo.

Hata hivyo, hatua za makusudi zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa ili kufuatilia uwekaji madini joto kwenye chumvi, usambazaji, utunzaji na kuimarisha utekelezaji sheria na kanuni zinazosimamia uzalishaji, uagizaji, usambazaji na uuzaji wa chumvi Tanzania Bara na Zanzibar na kuhakikisha kuwa chumvi yote kwa matumizi ya binadamu na wanyama inachanganywa na 75 -100 ppm za madini joto kwa ngazi ya kiwanda na isiyopungua 37.5 ppm katika sehemu za mauzo kama ilivyoelekezwa na sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto (URT, 1978; URT, 1979; URT, 1992; URT, 1993).

Pamoja na mafanikio yaliyofikiwa baada ya mkakati wa kuchanganya madini joto katika chumvi hapa nchini kuridhiwa na kutekelezwa, utafiti umebaini kuwepo kwa chumvi bandia (chumvi isiyo na madini joto), uelewa mdogo wa wadau na walaji, udhaifu na vitendo vya rushwa katika usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto. Haya, yanaweza kulirudisha nyuma Taifa la Tanzania katika kutokomeza athari za upungufu wa madini joto. Uzoefu unaonesha kuwa upungufu wa madini joto hujirudia pale viwango vya madini joto vinapokuwa chini ya viwango vinavyotakiwa au pale chumvi isiyo na madini joto inapotumiwa. Hivyo, ni muhimu kufanya usimamizi na utekelezaji endelevu wa sheria na kanuni ili kuhakikisha upungufu wa madini haya haujirudii na kuleta madhara ya kiafya kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kutokana na kushamiri kwa biashara ya bidhaa bandia ikiwemo chumvi, umuhimu wa madini joto mwilini na malalamiko ya wananchi juu ya uwepo wa chumvi bandia katika masoko ya walaji, ndizo zilizokuwa sababu za msingi zilizoisukuma TAKUKURU kufanya utafiti katika eneo hili.

Page 13: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

3

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kutoa ushauri wa namna bora ya kuimarisha mfumo wa usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto kwa mamlaka zinazohusika katika usimamizi mpango wa kuongeza madini joto katika chumvi kwa matumizi ya binadamu na wanyama. Aidha, madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kama ifuatavyo:

(i) Kutathmini hali ya upatikanaji na matumizi ya chumvi yenye madini joto,

(ii) Kupima uwazi, uwajibikaji, na ushirikishwaji katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi,

(iii) Kutathmini utaratibu wa mawasiliano ya wadau katika mpango,

(iv) Kuangalia utekelezaji wa sheria na hatua zinazochukuliwa dhidi ya wakiukaji.

Page 14: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

4

SURA YA PILI

2.0 MBINU ZA UTAFITI

2.1 CONCEPTUAL FRAMEWORK

Kufikia malengo (effectiveness) na ufanisi (efficiency) wa udhibiti wa chumvi yenye madini joto kunategemea moja kwa moja utawala (governance) katika mchakato mzima; yaani kusimamia sheria, kanuni na taratibu (enforcement), uratibu (coordination), na udhibiti (control) hususan pale panapozingatiwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishaji. Msingi wa utafiti huu ni dhana ya kuwa: Udhibiti wa chumvi yenye madini joto hauna ufanisi na hauleti matokeo yanayotakiwa na kwamba ufanisi wa udhibiti una mahusiano ya moja kwa moja na utawala (governance). Aidha, watafiti katika kazi hii walipima usimamizi wa sheria (enforcement) kwa kuangalia uwekaji na utekelezaji wa miongozo/kanuni (rules) na adhabu (sanctions). Kwa upande wake, uratibu ulipimwa kwa kuangalia mfumo wa mawasiliano (communication system) na majibu ya utekelezaji wa maazimio (feedback). Kuhusu udhibiti (control), utafiti ulipima usimamizi (monitoring) na tathmini (evaluation) ya udhibiti.

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: UTAFITI KIFANI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO (CASE STUDY OF IODATED SALT)    

4    

SURA YA PILI

2.0 MBINU ZA UTAFITI

2.1 CONCEPTUAL FRAMEWORK Kufikia malengo (effectiveness) na ufanisi (efficiency) wa udhibiti wa chumvi yenye madini joto kunategemea moja kwa moja utawala (governance) katika mchakato mzima; yaani kusimamia sheria, kanuni na taratibu (enforcement), uratibu (coordination), na udhibiti (control) hususan pale panapozingatiwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishaji. Msingi wa utafiti huu ni dhana ya kuwa: Udhibiti wa chumvi yenye madini joto hauna ufanisi na hauleti matokeo yanayotakiwa na kwamba ufanisi wa udhibiti una mahusiano ya moja kwa moja na utawala (governance). Aidha, watafiti katika kazi hii walipima usimamizi wa sheria (enforcement) kwa kuangalia uwekaji na utekelezaji wa miongozo/kanuni (rules) na adhabu (sanctions). Kwa upande wake, uratibu ulipimwa kwa kuangalia mfumo wa mawasiliano (communication system) na majibu ya utekelezaji wa maazimio (feedback). Kuhusu udhibiti (control), utafiti ulipima usimamizi (monitoring) na tathmini (evaluation) ya udhibiti.

Chanzo: Utafiti

 

 

 

 

           

SABABU  ZA  KIUTAWALA  (GOVERNANCE  FACTORS):  Uwazi,  uwajibikaji  na ushirikishaji  

Utendaji Kufaa/ufanisi  

SABABU  ZA  KIUCHUMI  NA  KIJAMII  (SOCIO-­‐ECONOMIC  FACTORS): Kipato, elimu, dhana  

USIMAMIZI  WA  UTEKELEZAJI  WA  SHERIA,  KANUNI  NA  

TARATIBU

 

Uzalishaji/uingiza

ji    

Uchakataji  

 Ulaji  

 

Uuzaji  

 

Chanzo: Utafiti

Page 15: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

5

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

2.2 Maeneo ya Utafiti

Utafiti huu ulifanyika katika mikoa ya Dar Es Salaam, Kigoma,Lindi,Manyara, Mara, Mbeya, Mwanza Mtwara, Rukwa, Singida naTanga. Mikoa hii ilichaguliwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo: uzalishaji wa chumvi katika mikoa husika, viwango vya matumizi ya chumvi yenye madini joto kimikoa (viwango vya chini, kati na juu) kama ilivyoainishwa katika “Tanzania Demographic and Health Survey” ya mwaka 2010 (TDHS 2010) na mikoa kuwa mipakani.

2.3 Ukusanyaji wa Taarifa

2.3.1 Taarifa za Msingi

Taarifa za msingi zilikusanywa kwa kutumia dodoso, checklists, miongozo ya mahojiano (interview schedules and guides), majadiliano kwa vikundi (FGDs) na ziara za watafiti katika maeneo ya uzalishaji wa chumvi.

2.3.2 Taarifa za Upili

Taarifa za upili zilipatikana kwa kupitia nyaraka mbalimbali kama zilivyoainishwa hapa chini:

Sera, sheria, taratibu na kanuni zinazohusiana na udhibiti wa chumvi yenye madini joto (Iodated salt),

Taarifa za kazi zilizofanywa na wadhibiti, na watafiti wengine zikiwemo taarifa za uzalishaji na uchanganyaji wa madini joto (iodation), “KAPB (Knowledge, Attitudes, Practices and Beliefs) surveys, Iodine Deficiency Disorder elimination reports and workshop proceedings, Tanzania Food and Nutrition Centre presentations and reports on iodine deficiency”.

2.4 Upatikanaji wa Sampuli Wakilishi

Maeneo ya utafiti (mikoa) yalipatikana au kuchaguliwa kwa vigezo vifuatazo: (i) viwango vya upatikanaji wa chumvi yenye madini joto hapa nchini kama ilivyoanishwa katika TDHS (2010); mikoa ya Tanzania bara iligawanywa katika makundi matatu ambayo ni mikoa yenye upatikanaji wa chumvi kwa kiwango cha chini (poor access – Lindi na Mtwara), upatikanaji kwa kiwango kisichoridhisha (unsatisfactory access – Rukwa na Kigoma) na upatikanaji wa kutosha (adequate access – Mara na Dar Es Salaam). Vigezo vingine vilikuwa ni kuchagua mikoa inyozalisha chumvi (Dar Es Salaam, Lindi, Mtwara, Manyara, Kigoma na Tanga), kuchagua mikoa iliyoko mipakani (Mbeya, Mwanza na Mara).

Aidha, sampuli ya wahojiwa na aina ya chumvi vilipatikana kwa kutumia mbinu za kupata sampuli kwa utaratibu maalum (non random sampling) na bila kufuata utaratibu (simple random sampling) kama ilivyoainishwa hapa chini:

Page 16: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

6

· Bila utaratibu: Njia hii ilitumika katika kupata sampuli ya wahojiwa walio katika makundi ya watu wengi. Wahojiwa waliopatikana kwa njia hii ni watumiaji (walaji) wa chumvi, wauzaji wa chumvi na wazalishaji na waagizaji wa chumvi. Sampuli za aina za chumvi (salt brands) kutoka masoko, minada na maduka ya reja reja zilipatikana kwa njia hii pia.

· Kwa utaratibu maalum: Utaratibu huu ulitumika kuwapata wadau waliohojiwa kwa nafasi za kazi zao. Wadau hao ni pamoja na wadhibiti wa bidhaa bandia na chumvi yenye madini joto ambao ni maafisa kutoka Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Tanzania Food and Drug Authority (TFDA), na maafisa afya wa halmashauri za majiji, manispaa, wilaya na miji. Sampuli za aina za chumvi (salt brands) kutoka katika “supermarkets” zilipatikana kwa njia hii.

2.5 Ukubwa wa Sampuli

Jumla ya wadau 600 walihojiwa kwa kutumia zana mbalimbali kama zilivyoanishwa katika kipengele cha 2.3.1 hapo juu. Aidha, sampuli 119 za chumvi za aina tofauti (different brands) zilizofungashwa katika pakiti zilikusanywa kutoka katika maduka ya reja reja, sampuli 95 zilizotokana na aina (brands) 11 za chumvi kutoka ‘supermarkets’ na sampuli za chumvi za mawe 220 zilikusanywa kutoka katika masoko, minada na maduka ya jumla na reja reja. Aidha, sampuli zingine 3023 za chumvi zilikusanywa kutoka kwa watumiaji (katika ngazi ya kaya). Sampuli hizi zilikusanywa kwa msaada wa wanafunzi wa shule za msingi ambapo walimu wakuu waliombwa kuwaagiza wanafunzi kuleta kiasi kidogo cha chumvi inayotumika majumbani mwao. Kila mwanafunzi aliwakilisha kaya moja na alitakiwa kuleta chumvi ya ujazo wa kijiko kimoja cha chai. Sampuli hiyo ya chumvi iliwekwa katika mfuko wa nailoni ambao kila mwanafunzi alielekezwa kuufunga mara baada ya kuweka chumvi husika. Lengo la kuwaagiza wanafunzi kufunga mifuko lilikuwa ni kuzuia upotevu wa madini joto.

2.6 Uchambuzi na Unyambulisho

Taarifa zilizokusanywa kwa kutumia dodoso, checklists, interview schedules, majadiliano kwa vikundi (Focus Group discussions - FGDs) na ziara za watafiti katika maeneo ya uzalishaji wa chumvi zilisafishwa (cleaning), kuchambuliwa, kuhaririwa (editing), kuwekewa alama (coding) na kuingizwa katika kompyuta na kunyambuliwa kwa kutumia programu mahsusi ijulikanayo kama Statistical Package for Social Science (SPSS).

Page 17: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

7

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Ili kubaini uwepo wa madini joto (test for iodine), sampuli za chumvi zilizokusanywa kutoka katika kaya, maduka, minada na masoko zilipimwa kwa kutumia “Rapid Salt Test Kits (MBI Kits)”. Kwa kufuata maelekezo ya Kits hizo, kiasi kidogo cha chumvi kiliwekwa kwenye kisosi (saucer) na kuwekewa tone la chemikali, uwepo wa madini joto (iodine) ulioneshwa na mabadiliko ya ghafla ya rangi ambapo chumvi ilibadilika na kuwa ya rangi ya kibuluu (light blue to dark colour). Chati za rangi (colour charts) zilizokuwa kwenye kits zinazofanana na kukubaliana na kiasi cha madini joto cha 0 ppm (hakuna madini joto), <15 ppm (kiwango pungufu), na >15 ppm (kiwango toshelevu) zilitumika kukadiria viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi. Aidha, unyambulisho wa viwango vya madini joto katika sampuli zilizokusanywa kutoka katika ‘supermarkets’ ulifanywa katika maabara za Taasisi ya Chakula na Lishe (Tanzania Food and Nutrition Centre – TFNC).

Page 18: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

8

SURA YA TATU

3.0 MATOKEO YA UTAFITI

Sura hii inatoa matokeo ya utafiti, juu ya wasifu wa wahojiwa; upatikanaji na matumizi ya chumvi yenye madini joto; utawala (governance), uratibu (coordination), usimamizi (enforcement), utendaji (performance) na changamoto katika udhibiti wa chumvi yenye madini joto; na hatimaye maoni ya wadau kuhusu udhibiti wa chumvi yenye madini joto.

3.1 WASIFU WA WAHOJIWA

Sehemu hii inaonesha wasifu wa wahojiwa katika utafiti huu. Wasifu unajumuisha mgawanyiko wao kwa kigezo cha umri na kiwango cha elimu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa wahojiwa wengi (67%) walikuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 40, na kwamba zaidi ya asilimia 70 kiwango chao cha elimu ni kuanzia sekondari hadi chuo kikuu (jedwali 1).

Jedwali 1: Mchanganuo wa wasifu wa wahojiwa kiumri na kielimu

Umri Asilimia Kiwango cha Elimu Asilimia

Miaka 18 -30 35.2 Elimu ya msingi 23.4

Miaka 31 -40 32.2 Elimu ya sekondari 60.3

Miaka 41 -50 18.1 Astashahada 3.3

Miaka 51 -60 11.1 Stashahada 8.3

Zaidi ya miaka 60 1.4 Shahada 4.5

Jumla 100.0 Jumla 100.0

3.2 UPATIKANAJI NA MATUMIZI YA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

Katika kufanya tathmini ya upatikanaji na matumizi ya chumvi yenye madini joto, utafiti ulikusanya sampuli za chumvi kutoka maeneo manne tofauti: kwanza ni chumvi iliyokuwa imeshanunuliwa na wanakaya na ipo nyumbani tayari kwa kuliwa au kutumiwa. Pili, ni chumvi ya mawe ambayo ilikuwepo kwenye maduka ya rejareja, sokoni na kwenye minada kusubiri wateja au walaji ambao aghalabu huwa ni watu wa kipato cha chini. Tatu, ni chumvi inayouzwa kwenye maduka makubwa yajulikanayo kama ‘supermarkets’ ambayo walaji wa kipato cha kati na juu ndiko wanakonunua bidhaa mbalimbali ikiwemo chumvi na nne chumvi ya pakiti iliyokuwa inauzwa katika maduka ya rejareja.

3.2.1 VIWANGO VYA MADINI JOTO KATIKA NGAZI YA KAYA

Kuhusiana na sampuli zilizopatikana kutoka kwenye kaya, matokeo yanaonesha kuwa asilimia 78 ya sampuli za chumvi zilikuwa na madini joto ambapo takribani asilimia 62 ya chumvi hizo zilikuwa na madini joto kwa kiwango toshelevu (>15 ppm) na asilimia 16 zilikuwa na madini joto kwa kiwango pungufu (<15 ppm) (Jedwali 2). Aidha, asilimia 22 ya sampuli za chumvi hizo hazikuwa na madini joto (0 ppm).

Page 19: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

9

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Mikoa ya Mara, Dar es Salaam na Mwanza inaonesha kuwa na viwango vikubwa vya matumizi ya chumvi yenye madini joto (kwa viwango toshelevu) yaani 81.6%, 81.4%, na 76.1%, mtawalia. Mkoa wa Lindi ulikuwa na kiwango cha chini zaidi cha matumizi ya chumvi yenye madini joto toshelevu (16.0%). Hata hivyo, viwango vya matumizi ya chumvi yenye madini joto toshelevu katika mikoa hiyo havijafikia kiwango cha zaidi ya asilimia 90 kilichopendekezwa na shirika la Afya Duniani. Hivyo, juhudi za makusudi za kuinua kiwango cha matumizi ya chumvi yenye madini joto zinapaswa kuchukuliwa, mikoa ya Lindi na Mtwara ikipewa kipaumbele zaidi.

Jedwali 2: Mchanganuo wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi zilizokusanywa kutoka katika kaya

Mkoa Upatikanaji wa chumvi yenye madini joto

Viwango vya madini joto (%)

Idadi ya sampuli

Sampuli zenye ma-dini joto (%)

0 ppm <15 ppm >15 ppm

Dar Es Salaam 324 95.0 5.0 13.6 81.4

Kigoma 201 97.5 2.5 83.6 13.9

Lindi 250 28.4 71.6 12.4 16.0

Manyara 319 62.9 40.1 18.4 44.5

Mara 213 96.7 3.3 15.1 81.6

Mbeya 299 100.0 0.0 34.1 65.9

Mwanza 258 85.7 14.3 9.6 76.1

Mtwara 211 68.3 31.7 24.2 44.1

Rukwa 356 73.0 27.2 19.1 53.9

Singida 273 75.5 24.5 15.8 59.7

Tanga 319 80.0 20.0 11.6 68.4

Jumla 3023 77.9 22.1 16.3 61.6

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (World Health organization – WHO), matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa kiwango toshelevu (>15 ppm) katika ngazi ya kaya yanatakiwa kuwa ni zaidi ya asilimia 90. Kiwango hiki ndicho kinachokubalika katika kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto (ICCIDD, UNICEF and WHO, 2001). Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya bado yako chini ya kiwango kilichopendekezwa.

Aidha, matokeo yanaonesha kupungua kwa matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa asilimia 6 na 4 ikilinganishwa na TFNC (2004) na TDHS (2010), mtawalia. Hivyo, kiwango cha matumizi ya chumvi yenye madini joto kinaonesha kushuka ikilinganishwa na utafiti uliofanyaika hivi karibuni (yaani TDHS 2010).

Page 20: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

10

3.2.2 VIWANGO VYA MADINI JOTO KATIKA NGAZI YA MADUKA YA REJA REJA, MINADA NA MASOKO

Matokeo yanaonesha takribani wastani wa asilimia 65 ya sampuli za chumvi za mawe zilizokusanywa kutoka katika maduka ya reja reja, minada na masoko hazina madini joto. Ni asilimia 35 tu ya sampuli hizo zina madini joto ambapo asilimia 22 ina madini joto kwa kiwango pungufu (< 15 ppm) na asilimia 13 ina madini joto kwa kiwango toshelevu (> 15 ppm). Sampuli zote za chumvi ya mawe zilizokusanywa katika mikoa ya Dar Es Salaam na Manyara hazikuwa na madini joto na sampuli zote zilizokusanywa kutoka mkoa wa Mbeya zilikuwa na madini joto kwa viwango pungufu na toshelevu (Jedwali 3).

Jedwali 3: Mchanganuo wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi ya mawe zilizokusanywa kutoka katika maduka ya reja reja, sokoni na minadani

Mkoa Viwango vya madini joto (%) Jumla

0 ppm <15 ppm >15 ppm

Dar Es Salaam 100.0 0.0 0.0 100.0

Kigoma 13.3 73.4 13.3 100.0

Lindi 64.3 21.1 14.3 100.0

Manyara 100.0 0.0 0.0 100.0

Mara 50.0 50.0 0.0 100.0

Mbeya 0.0 30.0 70.0 100.0

Mwanza 81.8 4.5 13.7 100.0

Mtwara 74.9 25.1 0.0 100.0

Rukwa 54.3 13.1 32.6 100.0

Singida 80.0 20.0 0.0 100.0

Tanga 94.7 5.3 0.0 100.0

Wastani 65.0 22.0 13.0 100.0

Matokeo ya majadiliano kwa vikundi vya maafisa afya yanaonesha kuwa chumvi ya mawe isiyo na madini joto huingia katika soko la walaji kutoka kwa wazalisha wadogo wa chumvi ambao ama hawana uelewa juu ya umuhimu wa madini joto katika chumvi au hawana mtaji wa kuwawezesha kuzalisha chumvi nyingi na hivyo kutokuwa na motisha ya kununua madini joto ya kuchanganya katika chumvi wanayozalisha. Aidha, maafisa hawa wanaeleza udhaifu katika mfumo wa udhibiti wa chumvi unachangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa chumvi ya mawe isiyo na madini joto katika soko la walaji. Kwa mantiki hii, uchanganyaji wa madini joto katika chumvi inayozalishwa na kundi hili ni changamoto kubwa katika mpango wa kuondoa upungufu wa madini joto hapa nchini.

Pia, imebainika kuwa chumvi nyingine ya aina hii huingia sokoni kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu ambao hununua chumvi isiyochanganywa na madini joto kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kusindika samaki na ngozi na kisha kuifungasha katika mifuko yenye nembo ya madini joto na kuiuza kwa walaji hasa waishio vijijini.

Pamoja na ukweli kwamba, wazalishaji wadogo huchangia kiasi kidogo cha chumvi katika matumizi ya taifa, wanao ushawishi katika soko kwani chumvi

Page 21: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

11

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

yao (isiyo na madini joto) huleta ushindani na kuchochea ukiukwaji wa sheria na kanuni zinazozuia uzalishaji na uuzaji wa chumvi isiyo na madini joto. Aidha, chumvi zao huingizwa katika maeneo ya vijijini ambako wengi wa walaji wana uelewa mdogo na wana vipato vidogo na hivyo hupendelea kununua chumvi hiyo kwani inapatikana kwa bei nafuu na kwamba bei yake ni ya chini ikilinganishwa na bei ya chumvi yenye madini joto. Kuendelea kutumika kwa chumvi hii kunawaweka wananchi wengi wa maeneo haya katika hatari ya kukumbwa na magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto. Ili kufikia malego ya mpango wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto ni muhimu sana kushughulikia uwekaji wa madini joto katika chumvi inayozalishwa na kundi hili ikiwemo kuwatambua na kuwawezesha.

Hivyo, uwepo wa kiasi kikubwa cha chumvi zisizo na madini joto (65%) ni ishara ya udhaifu katika usimamizi wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 na kanuni za chumvi yenye madini joto. Udhaifu huu umeruhusu chumvi isiyo na madini joto kuingia katika soko la walaji. Pia, matokeo haya yanaashiria kutokuwepo uelewa wa kutosha miongoni mwa wadau kuhusu umuhimu wa matumizi ya chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya.

Kuhusiana na sampuli za chumvi zilizofungashwa katika pakiti zilizokusanywa kutoka katika maduka ya reja reja, matokeo yanaonesha kwa wastani kuwa takribani asilimia 25.0 ya sampuli za chumvi hizo hazikuwa na madini joto. Asilimia 6.0 ya sampuli za chumvi hizi zilikuwa na madini joto kwa kiwango pungufu yaani chini ya 15 ppm (jedwali 4).

Jedwali 4: Mchanganuo wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi za pakiti zilizokusanywa kutoka ‘katika maduka ya reja reja

Nchi na aina/chapa (brand name) ya chum-vi

Idadi ya sampuli

Viwango vya madini joto (%)

0 ppm <15 ppm >15 ppm

Kenya (Kay Salt, Ken Salt, Malindi Salt, Mzuri Salt, Silver Salt, na Sun Salt, Salt)

51 0.0 0.0 100.0

Tanzania (Sawa Salt, Mchinga Salt, Buffalo Salt, Sungura Salt, Jiko Salt, Mnete, Sun-shine Salt*, na Sun star Salt*)

70 30.4 8.7 60.9

Zambia (Best Salt) 8 100.0 0.0 0.0

Jumla/wastani (weighted mean) 119 25.0 6.0 69.0

* Baadhi ya pakiti za chumvi aina ya Sunshine na Sunstar inayopakiwa mjini Sumbawanga hususan inayosafirishwa na kuuzwa katika wilaya ya Nkasi haina madini joto.

Page 22: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

12

3.2.3 MCHANGANUO WA KIMAABARA WA VIWANGO VYA MADINI JOTO KATIKA CHUMVI ZINAZOAGIZWA KUTOKA NJE YA NCHI NA KUUZWA KATIKA “SUPERMARKETS”

Kutokana na jamii ya kipato cha kati na kile cha juu kupenda kutumia chumvi inayouzwa katika “Supermarkets”, utafiti ulikusanya sampuli za chumvi (zilizofungashwa katika chupa au makopo ya plastiki) kutoka katika “Supermarkets” hizi na kuzifanyia uchunguzi/unyambulisho wa kimaabara katika maabara za Taasisi ya Chakula na Lishe (Tanzania Food and Nutrition Centre - TFNC) kama ilivyoainishwa katika kiambatanisho 1. Sampuli hizi zilipelekwa katika maabara baada ya madini joto katika chumvi nyingi kutotambuliwa na ‘test kits’ zinazotumika katika mfumo wa udhibiti na usimamizi (monitoring) hapa nchini na hivyo kulazimu kupata mbinu mbadala (alternative methods) katika maabara za TFNC.

Sheria hapa nchini zinaelekeza kuagiza na kuuza chumvi iliyochanganywa na madini joto kwa kutumia “Potassium Iodate”. Matokeo yanaonesha kuwa ni asilimia 18.2 tu ya sampuli za chumvi zilizofanyiwa uchunguzi wa kimaabara zilichanganywa na madini joto kwa kutumia “Potassium Iodate” kama inavyotakiwa na sheria. Asilimia 27.2 ya sampuli hizo zilichanganywa na madini joto kwa kutumia “Potassium Iodide” na asilimia 54.6 ya sampuli hizo hazikuwa na madini joto (jedwali 5 na picha 1). Potassium Iodide hairuhusiwi kutumika hapa Tanzania kwa kuwa si thabiti na imara (unstable) na haiwezi kustahimili hali ya joto na mkandamizi wa juu wa hali ya hewa (high humidity) katika ukanda wa kitropiki na hivyo madini joto katika chumvi hupotea kadiri muda unavyopita. Pia, mfumo wa udhibiti na usimamizi hapa nchini kwa kutumia ‘test kits’ hauwezi kutambua madini joto katika chumvi iliyochanganywa na “Potasium Iodide” ikilinganishwa na Potassium Iodate ambayo inatambuliwa na inastahimili hali ya joto na mkandamizo wa hali ya hewa ya nchi za kitropiki. Hivyo, kuendelea kuagiza chumvi ya aina hii (iodised salts) ni kuongeza gharama katika mfumo wa udhibiti na ufuatiliaji wa madini joto katika chumvi.

Page 23: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

13

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Jedwali 5: Mchanganuo wa kimaabara wa viwango vya madini joto katika sampuli za chumvi zilizokusanywa kutoka ‘supermarkets’

Nchi na aina/chapa (brand name) ya chumvi

Idadi ya sampuli

Viwango vya ma-dini joto (ppm)

malighafi ya madini joto iliyotumika

Marekani (American Garden) 11 18.0 Potassium Iodide

Uingereza (Saxa Table Salt) 05 0.0

Uingereza (Heritage Table Salt,) 06 0.0

Uingereza (LO Salt) 04 0.0

Uingereza (Saxa Coarse Sea Salt) 06 0.0

India (Tata Topp Super Refined salt)

12 0.0

Uholanzi (Nezo Fine Table Salt) 10 17.6 Potassium Iodide

Dubai-UAE (Daily Fresh Double Refined Iodised Salt)

13 27.5 Potassium Iodate

Afrika Kusini (Cerebros Iodated Table Salt)

09 37.0 Potassium Iodate

Kenya (Cost Refined Iodised Table Salt)

13 5.6 Potassium Iodide

Nchi haijulikani (Salt 143454) 06 0.0

Jumla 95 - -

Picha 1: Baadhi ya sampuli za chumvi kutoka ‘supermarkets’ ambazo hazina madini joto (0 ppm)

Aidha, matokeo yanaonesha kuwa asilimia 60 ya sampuli za chumvi zilizothibitika kuwa na madini joto, zina viwango chini ya 25 -75 ppm inayotakiwa katika ngazi ya uuzaji (retail level). Chumvi hizi ni zile zilizochanganywa na madini joto kwa kutumia “Potassium Iodide” ambayo si thabiti, hii inaonesha huenda madini joto yaliendelea kupotea zilipofikishwa hapa nchni zikiwa katika “supermarkets” husika (jedwali 5 na picha 2).

Page 24: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

14

Picha 2: Baadhi ya sampuli za chumvi zenye viwango chini ya 25 ppm na zimechanganywa na madini joto kwa kutumia ‘Potassium Iodide’ ambayo haistahimili hali ya kitropiki

Picha 3: Baadhi ya sampuli za chumvi zilizobainika kuwa na viwango toshelevu vya madini joto zikiwa zimechanganywa na madini hayo kwa kutumia ‘Potassium Iodate’

Page 25: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

15

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Uwepo wa chumvi zisizo na madini joto au zenye viwango pungufu kutoka nje ya nchi ni ishara ya udhaifu katika mfumo wa udhibiti na usimamizi. Udhaifu huu umewezesha chumvi hizo kupenya katika soko la walaji bila kutambuliwa na mamlaka zinazohusika.

Kwa matokeo haya, chumvi nyingi inayogizwa kutoka nje ya nchi haina madini joto au ina madini joto kwa viwango pungufu kwa kuwa haichanganywi na madini joto au huchanganywa kwa kutumia ‘Potassium Iodide’ isiyohimili hali ya kitropiki na chumvi husika kuendelea kupoteza madini joto inapokuwa hapa nchini. Chumvi hii ipo sokoni na kwa walaji na kwa mantiki hii, mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua za makusudi na za haraka za kudhibiti chumvi kutoka nje ya nchi ili kulinda afya ya watanzania.

3.3 UTAWALA (GOVERNANCE) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

3.3.1 UWAZI

Uwazi umejengwa katika mtiririko huru wa habari na machapisho ya kutosha ya maamuzi, utekelezaji, maelekezo, kanuni na sheria kwa wadau wote. Habari na machapisho husika sharti vipatikane na kueleweka kwa urahisi. Utafiti huu ulitaka kujua iwapo habari kuhusu utunzaji wa chumvi, athari za matumizi ya chumvi isiyo na madini joto, uwepo wa chumvi yenye madini joto katika maduka na kuwezeshwa kwa jamii kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto zinapatikana na kueleweka kwa urahisi.

Kuhusu wahojiwa kufahamu kuwa chumvi yenye madini joto inapaswa kutunzwa katika vifungashio maalum ikiwemo mifuko ya nailoni au magunia yenye nailoni ndani, matokeo yanaonesha kuwa takribani wastani wa asilimia 77 na 72 ya wahojiwa wanakubali kuwa wanafahamu kuwa chumvi inapaswa kutunzwa katika vifungashio maalum katika ngazi ya uzalishaji na kaya, mtawalia. Aidha, baadhi ya wahojiwa hawana uhakika juu ya chumvi kutunzwa katika vifungashio maalum katika ngazi ya uzalishaji (13.1%) na kaya (15.7%).

Kwa upande mwingine, takribani asilimia 10 na 12 ya wahojiwa hawakubaliani na dhana kuwa chumvi inapaswa kutunzwa katika vifungashio na vyombo maalum katika ngazi ya uzalishaji na kaya, mtawalia. Kundi la wahojiwa la maafisa afya linaongoza kwa kukubaliana na dhana ya chumvi kutunzwa katika vifungashio maalum katika ngazi ya uzalishaji (84.6%) na kaya (89.6%) huku kundi la walaji na wauzaji likiongoza katika kutokubaliana na dhana hii katika ngazi ya uzalishaji (14.1%) na kaya (23.9%) ikilinganishwa na makundi mengine (jedwali 6). Tofauti katika viwango vya kukubaliana na kutokubaliana na dhana ya utunzaji wa chumvi katika vifungashio maalum yaweza kutokana na viwango tofauti vya uelewa kuhusu mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi baina ya makundi ya wahojiwa na kutopatikana kwa habari (elimu) juu ya utunzaji wa chumvi.

Page 26: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

16

Jedwali 6: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu utunzaji wa chumvi katika vifungashio na vyombo maalum vinavyotakiwa katika ngazi ya uzalishaji na kaya ili kuzuia kupotea kwa madini joto

MWITIKIO Utunzaji katika ngazi ya uzalishaji (%)

Utunzaji katika ngazi ya kaya (%)

Walaji na wau-

zaji

Maafi-sa afya

Waza-lishaji

na waa-gizaji

Wastani Walaji na wau-

zaji

Maafisa afya

Wastani

Nakubaliana sana

33.3 57.7 34.6 41.9 23.6 58.6 41.1

Nakubaliana 40.5 26.9 37.5 34.9 31.4 31.0 31.2

Sina uhakika (undecided)

12.1 3.8 23.3 13.1 21.1 10.4 15.7

Sikubaliani 9.2 11.6 2.3 7.7 18.4 0.0 9.2

Sikubaliani sana

4.9 0.0 2.3 2.4 5.5 0.0 2.8

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0

Kuhusiana na dhana kuwa matumizi ya chumvi isiyo na madini joto yana madhara kwa afya ya jamii na kuwa chumvi zote zinazouzwa madukani zina madini joto, utafiti umebaini kuwa wahojiwa wengi (wastani wa 84.1%) wanakiri kuwa matumizi ya chumvi isiyo na madini joto yana madhara kwa afya ya jamii (jedwali 7).

Jedwali 7: Mwitikio wa wadau kuhusu athari za chumvi isiyo na madini

MWITIKIO Chumvi isiyo na madini joto ina madhara kwa afya (%)

Walaji na wau-zaji

Maafisa afya Wazalishaji na waa-gizaji

Wastani

Nakubaliana sana 48.7 76.9 51.2 58.9

Nakubaliana 28.5 19.2 27.9 25.2

Sina uhakika (un-decided)

8.4 0.0 11.6 6.7

Sikubaliani 8.4 0.0 4.7 4.4

Sikubaliani sana 6.0 3.9 4.6 4.8

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

Kuhusiana na uwepo wa chumvi yenye madini joto katika maduka yote, wastani wa asilimia 36.9 ya wahojiwa wanakubaliana na dhana kuwa chumvi yote inayouzwa madukani ina madini joto. Wengi wa wahojiwa (48.6%) hawakubaliani na dhana hii wakiongozwa na kundi la walaji na wauzaji (43.5%). Wahojiwa wachache hawakuwa na uhakika iwapo matumizi ya chumvi isiyo na madini joto yana madhara kwa afya (6.7%) na kama chumvi zote zinazouzwa madukani zina madini joto (15.7%)(rejea jedwali 8). Wahojiwa wengi (48.6%) kutokubaliana na dhana kuwa chumvi zote zinazouzwa madukani zina madini joto inaashiria udhaifu katika mfumo wa udhibiti (ukaguzi) wa chumvi unaosababisha kujipenyeza kwa chumvi isiyo na madini joto katika soko la walaji.

Page 27: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

17

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Jedwali 8: Mwitikio wa wadau kuhusu uwepo wa chumvi yenye madini joto katika maduka yote

MWITIKIO Chumvi zote zinazouzwa madukani zina madini joto (%)

Walaji na wauzaji

Wazalishaji na waa-gizaji

Wastani

Nakubaliana sana 12.9 20.6 16.7

Nakubaliana 15.1 25.3 20.2

Sina uhakika (unde-cided)

12.9 16.0 14.5

Sikubaliani 43.5 35.1 39.3

Sikubaliani sana 15.6 3.0 9.3

100.0 100.0 100.0

Kwa upande wa elimu na kuwezeshwa kwa jamii, utafiti huu ulitaka kujua iwapo jamii imeelimishwa na kuwezeshwa kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto. Matokeo yanaonesha kuwa wastani wa asilimia 35.1 ya wahojiwa wanaeleza kuwa jamii imeelimishwa na kuwezeshwa kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto na wastani wa asilimia 40.9 wanaeleza kuwa jamii haijaelimishwa na kuwezeshwa kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto. Asilimia kubwa ya walaji na wauzaji (68.8%) hawakubaliani na dhana kuwa jamii imeelimishwa na kuwezeshwa kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto (jedwali 9).

Hata hivyo, wastani wa asilimia 23.8 ya wahojiwa hawakuwa na uhakika kama jamii imeelimishwa na kuwezeshwa kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto. Kundi la maafisa afya lenye dhamana ya kuielimisha na kuiwezesha jamii kutambua na kutumia chumvi yenye madini joto linaongoza makundi yote ya wahojiwa kwa kutokuwa na uhakika kama jamii imeelimishwa na kuwezeshwa (42.3%). Hii inaashiria kuwa mamlaka zinazohusika na usimamizi na udhibiti wa chumvi zinapaswa kuelekeza nguvu nyingi katika uelimishaji wa jamii ili kuiwezesha kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto na hivyo kuikinga jamii dhidi ya magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto mwilini.

Jedwali 9: Mwitikio wa wadau kuhusu kuelimishwa na kuwezeshwa kwa jamii kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto

MWITIKIO Kuelimishwa na kuwezeshwa kutambua na kutumia chumvi yenye madini joto (%)

Walaji na wauzaji Maafi-sa afya

Wazal-ishaji na waagizaji

Wastani

Nakubaliana sana 5.3 7.7 18.6 10.5

Nakubaliana 10.7 42.3 20.9 24.6

Sina uhakika (unde-cided)

15.2 42.3 14.0 23.8

Sikubaliani 44.4 7.7 25.6 25.9

Sikubaliani sana 24.4 0.0 20.9 15.0

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

Page 28: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

18

Aidha, kupatikana na kueleweka kwa urahisi kwa habari katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, matokeo yanabainisha yafuatayo: kwa wastani asilimia 30.6 ya wahojiwa wanakubaliana kuwa habari za mpango zinapatikana, asilimia 31.1 hawana uhakika na asilimia 38.3 hawakubaliani na dhana kuwa habari za mpango zinapatikana kwa urahisi kwa wadau wote.

Maafisa afya wanaongoza kwa kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wa habari (43.3%) na kundi la walaji na wauzaji linaoongoza kwa kutokubaliana na dhana ya upatikanaji wa habari (45.6%). Aidha, kuhusiana na kueleweka kwa habari, wastani wa asilimia 35.0 ya wahojiwa wanakubaliani na kueleweka kwa habari husika, asilimia 35.1 hawana uhakika na kueleweka kwa habari na asilimia 29.7 hawakubaliani na dhana ya kueleweka kwa habari za mpango. Kama ilivyo katika upatikanaji wa habari, kundi la maafisa afya linaongoza kwa kutokuwa na uhakika wa kueleweka kwa habari (50%) na kundi la walaji na wauzaji linaongoza kwa kutokubaliana na uelewekaji wa habari (46.6%). Rejea jedwali 10 kwa mchanganuo na udondoti (details) zaidi. Hii inashiria kutokuwepo kwa mikakati madhubuti ya kufikisha elimu, taarifa na mawasiliano mengine kuhusu matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa wadau.

Jedwali 10: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu upatikanaji na kueleweka kwa habari za mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

MWI-TIKIO

Upatikanaji wa habari (%)

Kueleweka kwa habari (%)

Walaji na wauzaji

Maafisa afya

Wazal-ishaji na waagizaji

Wastani Walaji na wauzaji

Maafisa afya

Wazal-ishaji na waagizaji

Wastani

Nakubali-ana sana

4.8 11.5 14.0 10.1 4.5 7.7 16.4 9.5

Nakubali-ana

9.0 26.9 25.5 20.5 8.6 42.3 25.6 25.5

Sina uhakika (unde-cided)

20.7 42.3 30.2 31.1 22.6 50.0 32.6 35.1

Si-kubaliani

45.6 19.3 16.2 27.0 46.6 0.0 11.6 19.4

Si-kubaliani sana

19.9 0.0 14.0 11.3 17.7 0.0 14.0 10.3

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0

3.3.2 UWAJIBIKAJI

Kutokana na kwamba Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na.1 ya mwaka 2003, kanuni za chumvi na maelekezo mengine vinaelekeza kuwa wazalishaji wa chumvi wanapaswa kuchanganya madini joto, utafiti ulitaka kujua iwapo wazalishaji na waagizaji wa chumvi wanatoa taarifa za uwajibikaji kwa serikali kuhusiana na uchanganyaji wa madini joto katika chumvi.

Page 29: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

19

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Matokeo yanaonesha kwa wastani kuwa wahojiwa wengi (47.3%) hawakubaliani na dhana kuwa wazalishaji na waagizaji wa chumvi hutoa taarifa za uwajibikaji kwa serikali, asilimia 24.7 wanakubaliana na dhana hii, na asilimia 28.0 hawana uhakika kama taarifa za uwajibikaji hutolewa kwa serikali.

Walaji na wauzaji (63.0%) kwa upande mmoja hawakubaliani na dhana hii na maafisa afya (42.3%) kwa upande mwingine hawana uhakika na kutolewa kwa taarifa za uwajibikaji kwa serikali (jedwali 11). Matokeo ya majadiliano ya vikundi yamebainisha kuwa taarifa za uwajibikaji kutoka kwa wazalishaji wa chumvi hutolewa katika vikao vya baraza la Taifa la kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto (National Council for Control of Iodine Deficiency Disorders - NCCIDD) kupitia chama cha wazalishaji (Tanzania Salt Producers Association - TASPA). Matokeo haya yanaashiria kuwa uwajibikaji wa wazalishaji na waagizaji wa chumvi katika mpango wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto bado ni mdogo.

Jedwali 11: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu wazalishaji na waagiza wa chumvi kutoa taarifa za uwajibikaji kwa serikali

MWITIKIO Utoaji wa taarifa za uwajibikaji kwa serikali (%)

Walaji na wau-zaji

Maafisa afya Wazalishaji na waa-gizaji

Wastani

Nakubaliana sana 4.4 3.8 16.3 8.2

Nakubaliana 11.7 7.7 30.2 16.5

Sina uhakika (un-decided)

20.9 42.3 20.9 28.0

Sikubaliani 47.2 42.4 18.6 36.1

Sikubaliani sana 15.8 3.8 14.0 11.2

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

3.3.3 USHIRIKISHAJI

Mafanikio ya mpango wowote ule yanategemea mpango husika kukubalika kwa wadau wake wote. Utafiti huu ulitaka kubaini iwapo mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi unakubalika kwa wadau wote na matokeo ya hilo yalikuwa ni kama ifuatavyo: kwa wastani, asilimia 68.1 ya wahojiwa wanakubaliana kuwa mpango huu unakubalika kwa wadau, asilimia 28.0 hawana uhakika na asilimia 13.9 hawakubaliani na dhana ya kukubalika kwa mpango huu.

Takriban asilimia 30 ya walaji na wauzaji hawakubaliani na dhana hii na asilimia 46.2 ya maafisa afya hawana uhakika kama mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi unakubalika kwa wadau wote (jedwali 12). Uwepo wa wahojiwa wengi hususani maafisa afya (46.2%) kutokuwa na uhakika kuwa mpango unakubalika au la ni ishara ya ushirikishwaji mdogo miongoni mwa wadau.

Page 30: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

20

Jedwali 12: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kukubalika na wadau wote kwa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

MWITIKIO Kukubalika kwa mpango (%) Walaji na wau-

zajiMaafisa afya Wazalishaji na

waagizajiWastani

Nakubaliana sana 19.9 15.3 30.2 21.8

Nakubaliana 32.9 38.5 37.2 36.3

Sina uhakika (undecided) 16.8 46.2 20.9 28.0

Sikubaliani 21.4 0.0 9.3 10.2

Sikubaliani sana 8.8 0.0 2.3 3.7

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

3.4 URATIBU (COORDINATION) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

3.4.1 MAWASILIANO

Mrejesho kuhusu shughuli za mpango ni nyenzo muhimu katika kuleta tija na ufanisi wa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi. Utafiti huu ulitaka kufahamu kama Serikali inatoa mrejesho (feedback) kwa wadau juu ya hatua na mikakati ya usimamizi wa mpango husika. Matokeo yanadhirisha kwa wastani kuwa asilimia 32.6 ya wahojiwa wanakubaliana kuwa Serikali hutoa mrejesho, asilimia 18.0 hawana uhakika kama serikali hutoa mrejesho na asilimia 49.4 hawakubaliani na dhana ya serikali kutoa mrejesho kwa wadau (jedwali 13).

Jedwali 13: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu Serikali kutoa mrejesho (feedback) kwa wadau wa hatua na mikakati ya usimamizi wa mpango wa madini joto katika chumvi

MWITIKIO Serikali kutoa mrejesho kwa wadau (%)

Walaji na wauzaji

Wazalishaji na waagizaji

Wastani

Nakubaliana sana 4.5 9.4 6.9

Nakubaliana 16.6 34.9 25.7

Sina uhakika (undecided) 22.0 14.0 18.0

Sikubaliani 42.7 23.3 33.0

Sikubaliani sana 14.2 18.6 16.4

Jumla 100.0 100.0 100.0

Walaji na wauzaji wa chumvi wengi (56.9%) hawakubaliani na dhana ya utoaji wa mrejesho kwa wadau, wakilinganishwa na kundi la wazalishaji na waagizaji wa chumvi. Wahojiwa wengi (49.4%) kudai kuwa hakuna mrejesho (feedback) inayotolewa katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi ni ishara ya udhaifu katika mfumo wa mawasiliano miongoni mwa wadau wa mpango huu. Hii inaathiri upatikanaji wa habari juu ya hatua zilizofikiwa, utambuzi wa maeneo yenye matatizo, kujua fursa na changamoto zinazojitokeza na kiwango cha matumizi ya chumvi yenye madini joto kinachokubalika (>90%) kutofikiwa.

Page 31: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

21

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

3.4.2 USHUGHULIKIAJI WA MALALAMIKO

Mpango wenye mafanikio unapaswa kuambatana na miundombinu imara ya kupokelea na kushughulikia malalamiko ya wadau. Utafiti huu uliwataka wahojiwa kueleza iwapo mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi una miundombinu inayojitosheleza ya kupokea na kushughulikia malalalmiko ya wadau. Matokeo yanaonesha kuwa kwa wastani wa wahojiwa wengi (51.4%) wakiongozwa na kundi la walaji na wauzaji (70.4%), wanaeleza kuwa hakuna miundo mbinu inayojitosheleza kupokea na kushughulikia malalamiko ya wadau.

Jedwali 14: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kujitosheleza kwa miundo mbinu ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya wadau

MWITIKIO Kujitosheleza kwa miundo mbinu ya kupokea na kushughu-

likia malalamiko (%)Walaji na

wauzajiWazalishaji na

waagizajiWastani

Nakubaliana sana 1.5 4.7 3.1

Nakubaliana 7.8 18.5 13.2

Sina uhakika (undecided) 20.3 44.2 32.3

Sikubaliani 49.7 14.0 31.8

Sikubaliani sana 20.7 18.6 19.6

Jumla 100.0 100.0 100.0

Asilimia 32.3% ya wahojiwa wakiongozwa na kundi la wazalishaji na waagizaji (44.2%), hawana uhakika wa kuwepo kwa miundo mbinu na wahojiwa wachache (16.3%) wanakubaliana na dhana ya kuwepo kwa miundombinu toshelevu (jedwali 14). Matokeo haya yanahimiza kufanywa juhudi za makusudi za kuanzisha na kuimarisha miundombinu ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya wadau.

3.5 USIMAMIZI (ENFORCEMENT) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

3.5.1 USIMAMIZI NA UFUATILIAJI (MONITORING)

Kusimamia na kufuatilia mchakato wa uwekaji wa madini joto katika chumvi na matokeo yake kwa jamii ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mchakato huu una leta ufanisi na tija. Utafiti ulitaka kufahamu iwapo wadau wanajua kuwepo na kufanya kazi kwa sheria, kanuni na taratibu zinazodhibiti uchanganyaji huo wa madini joto katika chumvi na iwapo wahojiwa wanajua kuwa uchanganyaji wa madini joto ni sharti la lazima kisheria. Matokeo yanaonesha kuwa kwa wastani wa asilimia 65.5 ya wahojiwa wanakubaliana na kuwepo na kufanya kazi kwa sheria, kanuni na taratibu, asilimia 29.7 hawana uhakika na asilimia 14.8 hawakubaliani na dhana ya kuwepo na kufanya kazi kwa sheria, kanuni na taratibu.

Page 32: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

22

Jedwali 15: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu uwepo, kufanya kazi kwa sheria, kanuni na taratibu; na ulazima wa kuchanganya madini joto katika chumvi

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: UTAFITI KIFANI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO (CASE STUDY OF IODATED SALT)    

23    

Jedwali 15: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu uwepo, kufanya kazi kwa sheria, kanuni na taratibu; na ulazima wa kuchanganya madini joto katika chumvi

MWITIKIO Kuwepo na kufanya kazi kwa sheria, kanuni na

taratibu (%)

Kuchanganya madini joto katika chumvi ni

lazima (%)

Walaji na

wauzaji

Maafisa afya

Wazalishaji na

waagizaji

Wastani Walaji na

wauzaji

Maafisa afya

Wazalishaji na

waagizaji

Wastani

Nakubaliana sana 10.1 26.9 20.8 19.3 40.4 57.7 58.1 52.1 Nakubaliana 24.4 42.3 41.9 36.2 36.8 38.5 23.3 32.9 Sina uhakika (undecided)

32.6 30.8 25.6 29.7 9.4 3.8 16.3 9.8

Sikubaliani 22.6 0.0 4.7 9.1 10.1 0.0 2.3 4.1 Sikubaliani sana 10.3 0.0 7.0 5.7 3.3 0.0 0.0 1.1

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0 100.0  Kuhusiana na kuchanganya madini joto katika chumvi kuwa ni sharti la lazima kisheria, matokeo yamebainisha kwa wastani kuwa wahojiwa wengi wanakubaliana kuwa sharti hilo ni la lazima kisheria (85.0%). Rejea jedwali 15 kwa mchanganuo na udondoti (details) zaidi. Matokeo haya yanaashiria kuwa wahojiwa wengi wana uelewa mkubwa juu ya kuwepo na kufanya kazi kwa sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia uwekaji wa madini joto katika chumvi. Pia, wana uelewa mkubwa kuhusu ulazima wa kuchanganya madini joto katika chumvi kama sheria na kanuni zinavyoelekeza.  Mafanikio ya mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi yanatokana na usimamizi madhubuti wa sheria kwa vyombo vinavyohusika kutimiza wajibu ipasavyo. Utafiti huu ulitaka kufahamu iwapo vyombo vilivyopewa mamlaka ya kusimamia sheria katika mpango wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi vinatekeleza wajibu ipasavyo. Imebainika kuwa wastani wa asilimia 40.7 ya wahojiwa wanakubali kuwa vyombo vinavyosimamia sheria vinatimiza wajibu ipasavyo, asilimia 27.9 hawana uhakika, na asilimia 31.4 hawakubaliani na dhana kuwa vyombo vinavyosimamia sheria vinatimiza wajibu ipasavyo (jedwali16). Walaji na wauzaji wengi (64.9%) hawakubaliani na dhana kuwa vyombo vya kusimamia sheria zinatekeleza wajibu ipasavyo na sehemu ya maafisa afya (38.5%) ambao ndiyo wenye dhamana ya kusimamia na kutekeleza sheria na kanuni husika hawakuwa na hakika kama vyombo hivyo vinatekeleza wajibu ipasavyo. Hii inaashiria kuwa maafisa afya ama hawafahamu vizuri kuwa kusimamia na kutekeleza sheria na kanuni za chumvi ni jukumu lao au hawajashirikishwa vya kutosha na kuwezeshwa kutekeleza jukumu husika.

Kuhusiana na kuchanganya madini joto katika chumvi kuwa ni sharti la lazima kisheria, matokeo yamebainisha kuwa kwa wastani wa wahojiwa wengi wanakubaliana kuwa sharti hilo ni la lazima kisheria (85.0%). Rejea jedwali 15 kwa mchanganuo na udondoti (details) zaidi. Matokeo haya yanaashiria kuwa wahojiwa wengi wana uelewa mkubwa juu ya kuwepo na kufanya kazi kwa sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia uwekaji wa madini joto katika chumvi. Pia, wana uelewa mkubwa kuhusu ulazima wa kuchanganya madini joto katika chumvi kama sheria na kanuni zinavyoelekeza.

Kimsingi, mafanikio ya mpango huo wa kuchanganya madini joto katika chumvi yatatokana na usimamizi madhubuti wa sheria kwa vyombo vinavyohusika kutimiza wajibu wake ipasavyo. Utafiti huu ulitaka kufahamu iwapo vyombo vilivyopewa mamlaka ya kusimamia sheria katika mpango wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi vinatekeleza wajibu wake ipasavyo. Imebainika kuwa kwa wastani wa asilimia 40.7 ya wahojiwa wanakubali kuwa vyombo vinavyosimamia sheria vinatimiza wajibu wake ipasavyo, asilimia 27.9 hawana uhakika, ambapo asilimia 31.4 hawakubaliani na dhana kuwa vyombo vinavyosimamia sheria vinatimiza wajibu wake ipasavyo (jedwali16).

Walaji na wauzaji wengi (64.9%) hawakubaliani na dhana kuwa vyombo vya kusimamia sheria zinatekeleza wajibu wake ipasavyo na sehemu ya maafisa afya (38.5%) ambao ndiyo wenye dhamana ya kusimamia na kutekeleza sheria na kanuni husika hawakuwa na hakika kama vyombo hivyo vinatekeleza wajibu wake ipasavyo. Hii inaashiria kuwa maafisa afya ama hawafahamu vizuri kuwa kusimamia na kutekeleza sheria na kanuni za chumvi ni jukumu lao au hawajashirikishwa vya kutosha na kuwezeshwa katika utekelezaji wa jukumu hilo la msingi.

Page 33: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

23

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Jedwali 16: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu vyombo vya usimamizi wa sheria kutekeleza wajibu wao ipasavyo

MWITIKIO Vyombo kutekeleza wajibu ipasavyo (%)

Walaji na wau-zaji

Maafisa afya Wazalishaji na waagizaji

Wastani

Nakubaliana sana 2.9 3.8 14.0 6.9

Nakubaliana 8.0 53.8 39.5 33.8

Sina uhakika (undecided) 24.2 38.5 20.9 27.9

Sikubaliani 45.4 3.9 16.3 21.8

Sikubaliani sana 19.5 0.0 9.3 9.6

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

Aidha, matokeo ya mahojiano kwa vikundi yanaonesha kuwa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 na kanuni za chumvi yenye madini joto za mwaka 2010 vipo, vinafanya kazi na vimetoa wigo mpana wa adhabu dhidi ya wakiukaji. Wahojiwa wameeleza kuwa tatizo ni usimamizi na utekelezaji dhaifu wa sheria na kanuni hizo unachangiwa na sababu zifuatazo:- (i) uwezo mdogo wa wakaguzi (upungufu wa vifaa hususani -“rapid salt test kits”, mafunzo kuhusu ukaguzi wa chumvi kwa maafisa afya na rasilimali watu na fedha), (ii) vitendo vya rushwa katika ukaguzi na uendeshaji wa kesi mahakamani (iii) uelewa na ushiriki mdogo wa jamii katika udhibiti wa chumvi isiyo na madini joto, (iv) udhaifu katika uratibu wa kazi za udhibiti wa chumvi (kutokueleweka vizuri kwa majukumu ya maafisa afya) kati ya wizara ya afya (TFDA) na TAMISEMI na (v) uingiliaji wa kisiasa katika utendaji wa kazi za ukaguzi.

Hivyo, juhudi za makusudi zinapaswa kufanywa ili kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni na kuufanya mpango huu uwe na ufanisi, tija na wenye kusimamiwa kwa urahisi bila kuongeza gharama.

3.5.2 HATUA ZINAZOCHUKULIWA DHIDI YA WAKIUKAJI

Utafiti ulitaka kujua kama hatua stahili zinachukuliwa dhidi ya wakiukaji wa sheria, kanuni na taratibu. Matokeo yanaonesha kuwa wastani ya wahojiwa asilimia 40.0 wameeleza kuwa hatua stahili zinachukuliwa dhidi ya wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu, asilimia 31.2 ya wahojiwa wameeleza kutochukuliwa kwa hatua stahili dhidi ya wakiukaji ambapo asilimia 28.8 ya wahojiwa walieleza kuwa hawana uhakika juu ya uchukuliwaji wa hatua hizo (jedwali 17). Walaji na wauzaji wa chumvi wengi (65.6%) hawakubaliani na dhana kuwa hatua zinazostahili endapo huchukuliwa dhidi ya wakiukaji.

Page 34: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

24

Jedwali 17: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kuchukuliwa kwa hatua stahili dhidi ya wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu

MWITIKIO Kuchukuliwa kwa hatua sitahili (%) Walaji na wau-

zajiMaafisa afya Wazalishaji na

waagizajiWastani

Nakubaliana sana 5.7 7.6 14.0 9.1

Nakubaliana 11.9 46.2 34.7 30.9

Sina uhakika (undecided) 16.8 46.2 23.3 28.8

Sikubaliani 48.5 0.0 14.0 20.8

Sikubaliani sana 17.1 0.0 14.0 10.4

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

Kuhusiana na aina za hatua zinazochukuliwa dhidi ya wakiukaji, matokeo yanaonesha kuwa takribani asilimia 34.0 ya maafisa afya waliohojiwa walieleza kuwa kuelimisha na kuonya wakiukaji ni miongoni mwa hatua wanazochukua dhidi ya wakiukaji ikifuatiwa na kuharibu chumvi isiyo na madini joto inapokamatwa (28.0%), hatua zingine zinazochukuliwa ni kama ilivyoainishwa katika jedwali 18 hapo chini. Takribani asilimia 19 ya maafisa afya waliohojiwa walieleza kutochukua hatua yoyote dhidi ya wakiukaji licha ya kukiri kuwahi kukamata wakiukaji wa sheria na kanuni. Hivyo, sehemu ya wahojiwa (31.2%) wakiongozwa na kundi la walaji na wauzaji (65.6%) kudai kuwa hatua hazichukuliwi ipasavyo na kitendo cha baadhi ya maafisa afya kukiri kutochukua hatua, kinaashiria kuwepo kwa udhaifu mkubwa katika usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi.

Jedwali 18: Mwitikio wa maafisa afya kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya wazalishaji na wauzaji wanaouza chumvi isiyo na madini joto kwa kipindi cha 2009 hadi 2012

Hatua zilizochukuliwa Asilimia (%)

Kuelimisha juu ya umuhimu wa matumizi ya chumvi yenye madini joto na kuwaonya wakiukaji wasiendelee kuuza chumvi isiyo na madini joto

34.4

Kuharibu bidhaa (chumvi) 28.0

Kufikishwa mahakamani 18.8

Hakuna hatua zilizochukuliwa 18.8

Jumla 100.0

3.6 UTENDAJI (PERFORMANCE) KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

3.6.1 KUFAA (EFFECTIVENESS) KWA MPANGO WA KUCHANGANYA MADINI JOTO KATIKA CHUMVI

Kufaa kwa mpango wowote kunaweza kupimwa kwa matokeo yake kwa jamii na wadau husika. Utafiti huu ulitaka kujua iwapo usimamizi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto unatoa matokeo yanayoridhisha na hivyo kutoa matumaini ya kupungua kwa magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto.

Page 35: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

25

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Matokeo yanaonesha kuwa kwa wastani asilimia 66.3 ya wahojiwa wanaeleza kuwa usimamizi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto unatoa matumaini ya kupungua kwa magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto wakiongozwa na kundi la maafisa afya (92.3%). Aidha, asilimia 18.4 hawana uhakika na kupungua kwa magonjwa hayo ambapo asilimia 15.3 hawakubaliani na dhana ya kuwepo matumaini ya kupungua kwa magonjwa (jedwali 19). Hata hivyo, asilimia 36.5 ya walaji na wauzaji wanaeleza kutokuwepo kwa matumaini ya kupungua kwa ugonjwa wa tezi la shingo.

Jedwali 19: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu usimamizi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto ili kutoa matumaini ya kupunguza idadi ya wagonjwa wa uvimbe wa tezi la shingo (goiter)

MWITIKIO Matumaini ya kupungua kwa wagonjwa wa ‘goiter’ (%)

Walaji na wau-zaji

Maafisa afya Wazalishaji na waagizaji

Wastani

Nakubaliana sana 15.6 50.0 32.6 32.8

Nakubaliana 30.4 42.3 27.9 33.5

Sina uhakika (undecided) 17.5 7.7 30.1 18.4

Sikubaliani 26.0 0.0 4.7 10.2

Sikubaliani sana 10.5 0.0 4.7 5.1

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

3.6.2 UFANISI (EFFICIENCY) WA MPANGO WA KUCHANGANYA MADINI JOTO KATIKA CHUMVI

Ufanisi wa mpango wa kuchanganya madini joto kwenye chumvi unaweza kupimwa kwa kulinganisha jitihada za serikali na mafanikio yaliyokwishapatikana. Kwa kuzingatia hilo, utafiti huu ulilenga kujua iwapo jitihada za Serikali zinakuwa na matokeo tarajiwa. Matokeo yanabainisha kwa wastani kuwa asilimia 33.2 ya wahojiwa wanaeleza kuwa jitihada za serikali zinawiana na mafanikio ya mpango, asilimia 40.6 wakiongozwa na kundi la maafisa afya (50.0%), hawana uhakika kama jitihada na mafanikio vinawiana na asilimia 26.1 wakiongozwa na kundi la walaji na wauzaji (42.4%), wanaeleza kuwa jitihada na mafanikio haviwiani (jedwali 20).

Jedwali 20: Mwitikio wa wahojiwa kuhusu kuwiana kwa jitihada za serikali na mafanikio ya mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

MWITIKIO Jitihada na mafanikio vianawiana (%) Walaji na wau-

zajiMaafisa afya Wazalishaji na

waagizajiWastani

Nakubaliana sana 5.5 7.7 11.6 8.3

Nakubaliana 12.3 34.6 27.9 24.9

Sina uhakika (undecided) 29.8 50.0 41.9 40.6

Sikubaliani 40.2 7.7 7.0 18.3

Sikubaliani sana 12.2 0.0 11.6 7.9

Jumla 100.0 100.0 100.0 100.0

Page 36: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

26

3.7 CHANGAMOTO KATIKA UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

Ili kubaini iwapo kuna changamoto zozote zinazokwaza mafanikio ya mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, utafiti uliwataka wahojiwa kueleza kama kuna changamoto zinazoukabili mpango huu. Matokeo yanaonesha kuwa mpango huu unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uelewa mdogo wa madhara ya upungufu wa madini joto kwa wadau na baadhi ya viongozi wa serikali wenye dhamana ya kutoa maamuzi (19.2%), ikifuatiwa na upatikanaji endelevu wa fedha na vitendea kazi (rapid salt test kits, vyombo vya usafiri) kwa ajili ya ukaguzi na ufuatiliaji (17.0%). Changamoto zingine ni kama zilivyoainishwa katika jedwali 21 hapo chini.

Jedwali 21: Mchanganuo wa changamoto zinazoukabili mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi

Na. Changamoto Asilimia

1. Uelewa mdogo wa madhara ya upungufu wa madini joto kwa wadau na baa-dhi ya viongozi wa serikali wenye dhamana ya kutoa maamuzi

19.2

2. Upatikanaji endelevu wa fedha na vitendea kazi (rapid salt test kits, vyombo vya usafiri) kwa ajili ya ukaguzi na ufuatiliaji

17.0

3. Ukaguzi na uchukuaji wa sampuli za chumvi wa mara kwa mara hasa ukaguzi madhubuti kwa wazalishaji kabla ya chumvi kusambazwa

11.1

4. Udhaifu katika utekelezaji wa sheria na kanuni 10.2

5. Kukubalika kwa dhana ya matumizi ya chumvi yenye madini joto 7.8

6. Kuwawezesha walaji kuwa na utashi wa kiwango cha juu cha kutumia chum-vi yenye madini joto

7.2

7. Idadi toshelevu na mafunzo kwa maafisa afya (wakaguzi) 7.0

8. Ushirikiano wa dhati miongoni mwa wadau katika udhibiti wa viwango vya madini joto kwenye chumvi

6.2

9. Uwepo wa wazalishaji wadogo wa chumvi wanaoingiza sokoni (kwa walaji) chumvi isiyo na madini joto

5.1

10. Uaminifu wa wazalishaji na wauzaji 4.1

11. Bei kubwa na upatikanaji endelevu wa madini joto (Potassium Iodate) 3.0

12. Upatikanaji wa mitaji kwa wazalishaji wadogo (umaskini miongoni mwa wa-zalishaji wadogo) na bei ndogo ya chumvi wanayozalisha ikilinganishwa na gharama za uzalishaji

2.1

Jumla 100.0

3.8 MAONI YA WADAU KUHUSU UDHIBITI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO

Kuhusu kukabiliana na changamoto katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi, utafiti uliwataka wahojiwa kutoa maoni yao yatakayowezesha mpango huu kuwa na ufanisi na tija. Matokeo yanaonesha kuwa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia chumvi yenye madini joto (37.2%) na kuimarishwa kwa ukaguzi (26.7%) ni miongoni mwa maoni yaliyopendekezwa na wahojiwa wengi kwa ajili ya kuboresha mpango huu. Maoni mengine yaliyotolewa yameainishwa katika jedwali 22 hapo chini.

Page 37: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

27

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Jedwali 22: Mchanganuo wa maoni ya wadau (wahojiwa) kuhusu kuboresha udhibiti wa viwango vya madini joto katika chumvi

Na. MAONI ASILIMIA1 Elimu juu ya mpango wa kuchanganya madini joto katika chum-

vi, umuhimu wa kutumia, kutunza na kutambua chumvi yenye madini joto itolewe kwa wadau wote

37.2

2 Ukaguzi uimarishwe kuanzia kwa wazalishaji hadi kwa wauzaji ili kuhakikisha kuwa chumvi yote kwa ajili ya matumizi ya bin-adamu na wanyama inachanganywa na madini joto kwa viwango takiwa kabla haijawafikia walaji

26.7

3 Hatua kali zichukuliwe dhidi ya wazalishaji, waagizaji, wakaguzi na wauzaji wanaohusika katika mchakato wa uuzaji wa chumvi isiyo na madini joto

13.2

5 Vitendo vya rushwa vidhibitiwe wakati wa ukaguzi ili kuondoa tatizo la uuzaji wa chumvi isiyo na madini joto

9.3

6 Chumvi isiyo na madini joto kutoka kwa wazalishaji wadogo izuiliwe na kudhibitiwa ili isiingizwe sokoni

5.4

7 Umuhimu na madhara ya upungufu wa madini joto viingizwe ka-tika mitalaa kuanzia shule za msingi hadi vyuo ili kukuza uelewa wa jamii

2.4

8 Mafunzo ya uzalishaji bora na uchanganyaji wa madini joto katika chumvi yaendelee kutolewa ikiwemo ziara za ndani na nje ya nchi ili kujifunza uzalishaji wa chumvi yenye ubora unaotakiwa

1.7

9 Wizara itoe vifaa vya kutosha (rapid salt test kits) kwa ajili kufani-kisha kazi ya ukaguzi

1.6

10 Madini joto yauzwe kwa bei yenye ruzuku kupitia Taasisi ya chakula na lishe – TFNC

1.3

11 Wazalishaji wa chumvi wawezeshwe kwa kupatiwa mikopo na ru-zuku na watafutiwe masoko

1.2

Jumla 100.0

Page 38: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

28

SURA YA NNE

4.0 MJADALA

Sura hii inajadili tatizo la chumvi bandia (isiyo na madini joto) na namna ya

kukabiliana nalo kwa lengo la kuuboresha na kuufanya mpango wa kuzuia na

kudhibiti madhara au magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto kuwa

endelevu na wenye ufanisi na tija hapa chini. Aidha, mjadala huu unajikita zaidi

katika maeneo yafuatayo:

· Matumizi ya chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya

· Habari (information), Elimu na Mawasiliano

· Vitendo vya rushwa katika usimamizi na utekelezaji wa sheria

o Matumizi ya chumvi kutoka kwa wazalishaji wadogo

o Matumizi ya chumvi ya kuagiza (kutoka) nje ya nchi

o Usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria (law enforcement)

4.1 Matumizi ya Chumvi yenye Madini Joto katika ngazi ya kaya

Matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa kiwango toshelevu katika ngazi ya kaya ndiyo msingi wa mafanikio ya mpango wa kuondoa madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto mwilini. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti, matumizi ya chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya ni takribani asilimia 78 ambapo matumizi ya kiwango toshelevu (>15 ppm) ni asilimia 62 na pungufu (<15 ppm) ni 16%.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (World Health organization – WHO), matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa kiwango toshelevu (>15 ppm) katika ngazi ya kaya yanatakiwa kuwa zaidi ya asilimia 90. Kiwango hiki ndicho kinachokubalika katika kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto (ICCIDD, UNICEF and WHO, 2001).

Kwa mantiki hii, kiwango cha matumizi ya chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya bado hakijafikia lengo husika. Hii ni dhahiri kuwa sehemu ya wananchi wa Tanzania wanatumia chumvi yenye kiwango pungufu (16%) na isiyo na madini joto kabisa (22%) na hivyo kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto. Hivyo, uhakika kuwa chumvi yote imechanganywa na madini joto kwa kiwango toshelevu inapaswa kuwa hatua ya kwanza katika mchakato wa kuondoa madhara au magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto mwilini hapa nchini.

Kulingana na matokeo haya, kutofikiwa kwa lengo la matumizi ya chumvi yenye madini joto (>90%) katika ngazi ya kaya huenda kumesababishwa na mambo yafuatayo:- (i) udhaifu katika usimamizi wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi katika ngazi ya uzalishaji/uchanganyaji wa madini joto, (ii) uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimu wa kutumia chumvi yenye madini joto, (iii) uwepo wa

Page 39: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

29

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

madini joto bandia (yaliyochakachuliwa) katika soko ambayo yakichanganywa kwenye chumvi yanatoa kiwango cha chini cha madini joto katika chumvi, (iv) bei kubwa ya madini joto (potassium Iodate) kwa wazalishaji wadogo, (v) utunzaji mbaya wa chumvi katika vyombo vinavyoruhusu unyevunyevu, joto na mwanga kupenya na kisha madini joto kupotea kama gesi au kimiminika – kutokana na uelewa mdogo wa walaji, (vi) uuzwaji wa chumvi isiyo na madini joto inayooagizwa kutoka nje ya nchi kupitia ‘supermarkrkets’ (vii) Uwepo wa wazalishaji wadogo waliotapakaa katika maeneo mbalimbali wanaouza chumvi isiyo na madini joto kwa bei ya chini na (vii) uvumi na upotoshaji kuwa chumvi yenye madini joto ni mbaya kwa afya na inaathiri mfumo wa uzazi. Mambo haya kwa pamoja yanaakisiwa na viwango visivyofikia lengo la matumizi ya chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya.

Ili kuongeza matumizi ya chumvi yenye madini joto na kufikia lengo lililowekwa, yafuatayo hayana budi kutekelezwa: (i) kuimarisha uzalishaji na masoko ya chumvi yenye kiwango toshelevu cha madini joto na kuhakikisha kuwa kaya zote zinapata na kutumia chumvi hiyo, (ii) kuelimisha wadau juu ya madhara ya upungufu wa madini joto na hivyo kuongeza utashi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa jamii, (iii) kuanzisha, kuimarisha na kuendeleza vyama vya wazalishaji wadogo na kuviwezesha ili wazalisha wadogo wauze chumvi yenye madini joto, (iv) kuanzisha, kuimarisha na kusimamia mfuko (revolving fund) wa kununulia madini joto (Potassium Iodate) na pembejeo zingine ili kuboresha teknolojia ya chumvi na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chumvi yenye madini joto, na (v) kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto vinatekelezwa ipasavyo na hatua stahili kuchukuliwa dhidi ya wakiukaji.

4.2 Habari (information), Elimu na Mawasiliano

Habari, elimu na mawasiliano ni zana muhimu katika kufanikisha mpango wa kuondoa madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto, huongeza uelewa na utashi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa viwango vidogo vya upashanaji habari, uelewa wa wadau na mawasiliano katika mpango wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto. Hali hii inapunguza ufanisi wa mpango huu na hivyo kutofikiwa kwa malengo yanayotakiwa katika kuondoa madhara na magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto hapa nchini.

Katika kufikia malengo yaliyowekwa, ujumbe wa kimawasiliano na kielimu lazima ueleze kwa ufasaha uwajibikaji thabiti na kulenga hadhira mbalimbali katika ngazi zote za jamii. Ni muhimu hadhira lengwa ijumuishe: viongozi wa kitaifa ili kuleta ushindi wa kisiasa; wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na wauzaji ili kuwa na matokeo mazuri katika utekelezaji wa sheria na kanuni; wataalam kutoka Serikalini, sekta ya afya, wasomi na taasisi za elimu na utafiti ili kupata michango (kimawazo na kiweledi), msaada na uungwaji mkono; na jamii kwa ujumla ili kukuza uelewa, kukubaliwa kwa mpango na kutambuliwa kwa thamani ya ziada (added value) ya matumizi ya chumvi yenye madini joto.

Aidha, mawasiliano yawe sehemu muhimu ya usimamizi, utekelezaji na usambazaji wa chumvi yenye madini joto katika kuhakikisha kukubalika na kutumika kwa chumvi yenye madini joto kupitia kampeni na hamasa mbalimbali. Mawasiliano yasaidie kutafuta ufumbuzi wa uvumi na upotoshaji katika usimamizi na utekelezaji wa mpango wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi.

Page 40: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

30

Ili kuongeza matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa jamii, mikakati thabiti ya mawasiliano, utoaji taarifa na elimu inapaswa kuanzishwa, kusimamiwa na kuendelezwa kwa lengo la kupanua na kuendeleza uelewa na utashi wa wananchi katika kutumia chumvi yenye madini joto. Mikakati husika sharti ifungamanishwe na mifumo iliyopo katika sekta za afya, elimu, viwanda, madini na TAMISEMI kwa njia shirikishi na fanisi zaidi.

Mikakati ya mawasiliano ilenge kutoa taarifa na elimu ya kiafya, kiuchumi na thamani ya kijamii ya madini joto katika milo ya kila siku kupitia mitalaa ya shule na vyuo, vyombo vya habari na njia zingine za mawasiliano. Mikakati hii pia ilenge kubadili tabia, desturi na mazoea ya wadau kuelekea matumizi ya chumvi yenye madini joto.

Pia, elimu iendelee kutolewa ili kuongeza na kuendeleza utashi wa matumizi ya chumvi yenye madini joto, nembo ya Taifa ya madini joto izinduliwe na kutangazwa kitaifa na itumike kurahisisha utambuzi wa chumvi yenye madini joto na iwe hamasa kwa jamii kutumia chumvi hiyo. Uvumbuzi wa njia bora za kuimarisha uelewa miongoni mwa wadau kupitia kwa viongozi wa dini, vyama vya kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali na viongozi wa serikali za mitaa (ngazi ya kitongoji na mtaa (grass root levels) vinaweza kutumiwa ili kuleta tija na ufanisi zaidi katika kuondoa na kuzuia madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto.

Kupitia mikakati madhubuti ya mawasiliano, taarifa na elimu, uelewa mbaya na upotoshaji kuhusu umuhimu wa kutumia chumvi yenye madini joto vitabainishwa na kushughulikiwa kabla ya kuleta madhara kwa jamii.

4.3 Vitendo vya rushwa katika usimamizi na utekelezaji wa sheria

Vitendo vya rushwa katika usimamizi na utekelezaji wa sheria huathiri mafanikio, ufanisi na uendelevu wa mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna vitendo vya rushwa katika shughuli za kila siku za usimamizi (ukaguzi) wa chumvi na uendeshaji wa kesi za watuhumiwa waliokamatwa na chumvi zisizo na madini joto. Vitendo hivi vimechangia kutofikiwa kwa lengo la zaidi ya 90% ya matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa kuwa, vinadhoofisha usimamizi na kuruhusu uwepo wa chumvi isiyo na madini joto katika masoko ya walaji.

Juhudi za makusudi zinapaswa kufanywa ili kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa katika usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi na hivyo kuufanya mpango wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi kuwa wenye ufanisi na endelevu. Miongoni mwa hatua zinzopaswa kuchukuliwa ni:- (i) kuelimisha wadau juu ya miundombinu ya maadili na madhara ya rushwa katika usimamizi wa chumvi yenye madini joto, (ii) kuhamisha watumishi waliokaa katika vituo vya kazi kwa muda mrefu ili kuvunja mtandao wa mazoea yaliyojengeka, (iii) kutoa motisha na zawadi kwa watumishi wanatekeleza majukumu yao ipasavyo (barua za pongezi, mafunzo, kupandisha vyeo), na (iv) kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi wanaothibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Uwepo wa vitendo vya rushwa katika usimamizi na utekelezaji wa sheria unaashiriwa na ongezeko la matumizi ya chumvi isiyo na madini joto kutoka

Page 41: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

31

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

kwa wazalishaji (hususani wazalishaji wadogo) na wafanyabiashara (waagizaji wa chumvi) kama ilivyoainishwa katika 4.3.1 na 4.3.2 hapo chini.

4.3.1 Matumizi ya chumvi kutoka kwa wazalishaji wadogo

Miongoni mwa wazalishaji wa chumvi hapa nchini ni wazalishaji wadogo wa chumvi waliotapakaa katika maeneo mengi hapa nchini hususan katika mikoa ya Dar Es Salaam, Kigoma, Lindi, Manyara, Mtwara, Singida, na Tanga. Matokeo ya majadiliano kwa vikundi vya maafisa afya yanaonesha kuwa chumvi ya mawe isiyo na madini joto huingia katika soko la walaji kutoka kwa wazalisha wadogo wa chumvi ambao ama hawana uelewa juu ya umuhimu wa madini joto katika chumvi au hawana mtaji wa kuwawezesha kuzalisha chumvi nyingi na hivyo kutokuwa na motisha ya kununua madini joto ya kuchanganya katika chumvi wanayozalisha. Kwa mantiki hii, uchanganyaji wa madini joto katika chumvi inayozalishwa na kundi hili ni changamoto kubwa katika mpango wa kuondoa tatizo la upungufu wa madini joto hapa nchini.

Pamoja na ukweli kwamba, wazalishaji wadogo huchangia kiasi kidogo cha chumvi katika matumizi ya taifa, wanao ushawishi katika soko kwani chumvi yao (isiyo na madini joto) huleta ushindani na kuchochea ukiukwaji wa sheria na kanuni zinazozuia uzalishaji na uuzaji wa chumvi isiyo na madini joto. Aidha, chumvi zao huingizwa katika maeneo ya vijijini ambako chumvi yenye madini joto haipatikani kwa urahisi na wengi wa walaji wana uelewa mdogo na vipato vidogo na hupendelea kununua chumvi hiyo kwa kuwa bei yake ni ya chini ikilinganishwa na chumvi yenye madini joto. Aidha, kuna upotoshaji (misconception) kuwa chumvi yenye madini joto si nzuri kiafya, inaleta magonjwa na sehemu zingine walaji wanaamini kuwa inaathiri mfumo wa uzazi (punguza nguvu za kiume). Hivyo, kuendelea kutumika kwa chumvi hii kunawaweka wananchi wengi wa maeneo haya katika hatari ya kukumbwa na magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto.

Ili kufikia malego ya mpango wa kuondoa madhara yanayotokana na upungufu wa madini joto, ni muhimu sana kushughulikia uwekaji wa madini joto katika chumvi inayozalishwa na kundi hili ikiwemo kuwatambua na kuwawezesha. Hata hivyo, uangalifu unahitajika wakati wa kushughulika na kundi hili kwa vile usimamizi na utekelezaji wa sheria waweza kuwa mgumu kutokana na ukweli kwamba (i) wazalishaji wadogo hawana mtaji au utaalam wa kuchanganya madini joto, (ii) wazalishaji wadogo wengi hawako katika biashara rasmi (hawajasajiliwa), (iii) uingiliaji wa wanaharakati na wanasiasa wakati wa kuchukua hatua dhidi ya kundi hili (kutetewa kama wapiga kura) na (iv) ugumu wa kuwafikia na kuwaelimisha baadhi ya walaji wanaopata chumvi kutoka kundi hili.

Hali hii inaamuru utekelezaji wa mikakati maalum itakayowawezesha wazalishaji wadogo kuweza kuwa sehemu ya mpango wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi na hatimaye kuikoa jamii kuondokana na matatizo yanayotokana na upungufu wa madini joto mwilini. Pamoja na mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa iliyotolewa katika 4.3 hapo juu, mikakati mingine ni pamoja na kuwatambua na kuwasajili wazalishaji wadogo, kuanzisha/kuendeleza na kuwezesha (kifedha, kiutalaam na uelewa) vyama vya ushirika vya wazalishaji wadogo wa chumvi, kutafuta soko au mnunuzi wa chumvi ya wazalishaji wadogo atakayenunua chumvi yao na kisha kuiwekea madini joto na kuifungasha, na kufanya usimamizi (ukaguzi) maalum na endelevu.

Page 42: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

32

4.3.2 Matumizi ya chumvi ya kuagiza (kutoka) nje ya nchi

Utandawazi na soko huria vina matokeo muhimu katika uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa chumvi na hivyo kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni ni jambo muhimu na la msingi sana katika udhibiti wa chumvi isiyo na madini joto. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa chumvi nyingi inayotumika hapa nchini inaingizwa kutoka nchi za Kenya, Afrika Kusini, Marekeni, Uingereza, India, Uholanzi, Zambia na Falme za Kiarabu (Dubai). Chumvi nyingi inayoagizwa na kuuzwa katika ‘supermarkets’ (54.6%) imebainika kutokuwa na madini joto na asilimia 60 ya chumvi iliyothibitika kimaabara kuwa na madini joto ina viwango pungufu ya <25 ppm inayotakiwa katika ngazi ya uuzaji (retail level).

Katika kuhakikisha kuwa chumvi zote zinazoagizwa hapa nchini zinakidhi viwango vilivyowekwa kisheria, usimamizi katika sehemu za kuingilia zikiwemo bandari, stesheni za magari moshi, vituo vya magari unaimarishwa. Sambamba na mikakati ya kuzuia na kupambana na rushwa iliyotolewa katika 4.3 hapo juu, taasisi zinazohusika na udhibiti wa biashara ya chumvi katika maeneo ya kuingilia hazina budi kuwa na watumishi wa kutosha, waaminifu, waliowezeshwa (kimafunzo, vitendea kazi) na wanaotambua na kuelewa majukumu yao ya kufanya kazi ya ukaguzi, uchunguzi na tathmini ya mpango wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto kupitia matumizi ya chumvi yenye madiji joto.

4.4 Usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria (law enforcement)

Shughuli za kila siku za usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi ni wajibu wa Taasisi ya Chakula, Dawa na Vipodozi (Tanzania Food, Drugs and Cosmetics – TFDA) kwa kushirikiana na mamlaka za Serikali za Mitaa. Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 inaipa mamlaka TFDA kusimamia na kutekeleza kanuni za chumvi yenye madini joto. Aidha, sheria hiyo (kifungu cha 105) inawatambua maafisa afya wa halmashauri za Miji, Wilaya, Manispa na Majiji kama wakaguzi na kifungu cha 106 kinawapa maafisa hao mamlaka ya kufanya ukaguzi. Vifungu 115 na 123 vya sheria hiyo vinatamka adhabu zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya wakiukaji waliotiwa hatiani. Hivyo, usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto katika ngazi ya halmashauri umekasimiwa kwa maafisa afya wa halmashauri husika.

Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwepo kwa udhaifu katika usimamizi wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto katika ngazi ya halmashauri hapa nchini. Pamoja na mambo mengine, udhaifu huo unachangiwa na uwepo wa vitendo vya rushwa wakati wa ukaguzi na uendeshaji wa kesi mahakamani; upungufu wa watumishi, vitendea kazi, mafunzo na fedha; uelewa na ushiriki mdogo wa jamii katika udhibiti wa chumvi yenye madini joto; uingiliaji wa kisiasa katika utendaji wa kazi za ukaguzi na uchukuaji hatua dhidi ya wakiukaji wa kanuni; na uelewa mdogo wa maafisa afya juu ya wajibu na majukumu yao katika usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto.

Page 43: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

33

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huu, sheria na kanuni za kudhibiti chumvi zilizotungwa zimeelezwa kuwa zinatoa mfumo wa kisheria wenye wigo mpana wa adhabu za kuchukuwa dhidi ya wakiukaji. Ili kutoa matokeo yanayotarajiwa, taasisi husika zinahitaji kujengewa uwezo katika rasilimali watu na fedha, taaluma (mafunzo endelevu) na vitendea kazi. Hivyo, juhudi za makusudi za kujenga na kuimarisha uwezo wa taasisi zinazohusika na usimamizi na utekelezaji wa mpango huu zinapaswa kuchukuliwa hususani katika maeneo yaliyolezwa kuwa na upungufu (rasilimali watu, vitendea kazi, fedha na mafunzo). Hii itaziwezesha taasisi hizi kusimamia na kutekeleza sheria na kanuni kwa ufanisi kuanzia ngazi ya uzalishaji na/au uagizaji wa chumvi hadi ngazi ya walaji.

Aidha, baada ya taasisi hizi kujengewa uwezo, usimamizi na utekelezaji wa kanuni za chumvi unapaswa kuimarishwa na kufanywa kuwa endelevu ili uweze kufanya kazi zake ipasavyo ikiwemo: (i) kusimamia mchakato wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi na matokeo yake juu ya hali ya madini joto katika jamii na kuhakikisha ufanisi na matokeo tarajiwa ya mpango wa uchanganyaji wa madini joto; (ii) kuwahamasisha na kuwamotisha wazalishaji, waagizaji na wauzaji kutii sheria na kuzalisha, kuagiza na kuuza chumvi yenye madini joto pekee; (iii) kukusanya na kufanya mapitio endelevu ya taarifa za utekelezaji wa mpango wa kuchangaya madini joto katika chumvi kwa lengo la kubaini matatizo kama vile ukiukwaji wa sheria na kanuni na kisha kuchukua hatua stahili ili kufikia malengo yaliyowekwa; (iv) kufanya upimaji wa mara kwa mara wa viwango vya madini joto katika chumvi kwa wazalishaji na wa vipindi maalum katika mfumo wa usambazaji, wauzaji wa reja reja, na ngazi ya kaya ili kubaini uwepo na utofauti wa viwango vya madini joto katika chumvi na hivyo taarifa kutolewa, kupitiwa na hatua stahili kuchukuliwa mapema iwezekanavyo.

Aidha, usimamizi (monitoring) wa madini joto katika chumvi uhusishe wadau wengine kama Asasi zisizo za Serikali (NGO), Asasi za kujitolea, viongozi wa dini na serikali za mitaa (ngazi ya kitongoji na mtaa) kwa kuhusisha njia zenye gharama kidogo kwa mfano kutumia “field test kits”. Hii itasaidia katika kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii au jumuiya.

Ili kuwa na uhakika wa usalama na viwango sahihi vya madini joto katika chumvi inayomfikia mlaji, usimamizi wa viwango vya madini joto katika chumvi katika ngazi ya uzalishaji na uagizaji toka nje ya nchi lazima vifanywe kabla chumvi haijaingia sokoni. Maabara za taasisi zinazosimamia mpango huo zinapaswa kupima na kuthibitisha viwango vya madini katika chumvi inayozalishwa hapa nchini na inayoagizwa kutoka nje ya nchi kama vinakidhi viwango vilivyowekwa na hivyo kusaidia kasi ya kuchukua hatua dhidi ya chumvi isiyokidhi viwango.

Ili kufikia lengo la zaidi ya asilimia 90 ya matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa kiwango toshelevu, Tanzania inapaswa kuendelea kushirikisha wadau wa sekta zote zinazohusika katika uzalishaji, uagizaji, usambazaji, usimamizi, na utekelezaji wa mpango wa kuchanya madini joto katika chumvi. Ushirikishi wa wadau muhimu katika mpango huo wa uchanganyaji wa madini joto katika chumvi hapa nchini utasaidia malengo yafuatayo kufikiwa kwa haraka na kwa ufanisi:

Page 44: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

34

(i) chumvi isiyo na madini joto kutoka kwa wazalishaji au waagizaji haingii katika soko la walaji,

(ii) viwango vya madini joto kutoka kwa wazalishaji hadi walaji ni vile vinavyotakiwa,

(iii) juhudi na mafanikio yaliyofikiwa vinaungwa mkono na kuendelezwa kwa kuratibu mikakati inayohusisha wadau na sekta muhimu

(iv) upatikanaji wa madini joto (potassium iodate) unakuwa endelevu na

(v) utetezi (advocacy) na uhamasishaji wa kisiasa na utashi wa kutumia chumvi yenye madini joto vinaimarishwa.

Page 45: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

35

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

SURA YA TANO

5.0 MAPENDEKEZO NA HITIMISHO

5.1 MAPENDEKEZO

MWANYA WA RUSHWA

UDHAIFU/TATIZO MAPENDEKEZO

Upatikanaji, matu-mizi na utunzaji wa chumvi yenye ma-dini usiyokidhi ki-wango katika ngazi ya kaya

Udhaifu katika uratibu, ufuatiliaji (ukaguzi), Usi-mamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni

· Kuhakikisha kuwa wakaguzi wana vifaa (test kits) na fursa ya muda muafaka ya kupima sampuli katika maabara kwa ajili ushahidi mahakamani

· Kuelimisha wakaguzi juu ya umuhimu wa kuchanganya madini joto ili waweze kuweka kipaumbele katika ukaguzi wa chumvi miongoni mwa majukumu yao ya ukaguzi wa ubora wa vyakula.

· Kuimarisha utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi katika ngazi zote (ku-toka ngazi ya uzalishaji/uagizaji hadi walaji)

Uwepo wa wazalishaji wadogo waliotapakaa ka-tika maeneo mbalimbali wanaouza chumvi isiyo na madini joto kwa bei ya chini

· Kuanzisha, kuimarisha na kuendele-za vyama vya ushirika vya wazalishaji wadogo wa chumvi

· Kuwaelimisha juu ya umuhimu wa ma-dini joto na kuwawezesha kitekinolojia na kimitaji.

· Kutoa ruzuku ya madini joto kwa kuz-ingatia umuhimu wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto katika jamii na taifa kwa ujumla. Lengo ni kurahisi-sha upatikanaji wa madini joto na kwa bei wanayoimudu wazalishaji wadogo

· Kutafuta soko au kampuni ya kununua chumvi ya wazalishaji wadogo kabla ya kuwekewa madini joto na kisha kui-wekea madini hayo

Utunzaji mbovu wa chum-vi unasababisha kupotea kwa madini joto

· Kuelimisha wauzaji na walaji kuhusu umuhimu wa chumvi yenye madini joto na namna bora ya kutunza chumvi husika

Uuzaji wa chumvi isiyo na madini joto inayonunuli-wa kwa matumizi men-gine (kusindika samaki na ngozi) na kupenyezwa sokoni

· Kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto vinatekelezwa na kutumika kwa chumvi zote ikiwemo ya kusindikia samaki, ngozi na matu-mizi mengine

Page 46: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

36

MWANYA WA RUSHWA

UDHAIFU/TATIZO MAPENDEKEZO

Kuongezeka kwa bei ya madini joto (Potassium Iodate – KIO3) na uwepo wa madini joto bandia (yaliyochakachuli-wa) sokoni

· Kudhibiti uuzaji holela wa madini joto

· Kuchukua hatua dhidi ya wachakachuaji wa madini joto

· Kuona uwezekano wa kutoa ruzuku ya ma-dini joto

Uagizaji na uuzaji wa chumvi isiyo na madini joto na/au chumvi iliyo-changanywa na madini joto kwa kutumia ‘potas-sium iodide’ kutoka nje ya nchi

· Kuimarisha ukaguzi katika maeneo ya kuingizia chumvi ili kudhibiti na kupiga marufuku chumvi isiyo na madini joto au iliyochanganywa na ‘potassium io-dide’ (iodised salts) kuingizwa nchini

· Kuchukua hatua dhidi ya waagizaji wa-naokiuka sheria, kanuni na taratibu husika

Uwazi mdogo Uelewa mdogo kuhusu umuhimu wa matumizi ya chumvi yenye madini joto na madhara ya upungufu wa madini joto mwilini miongoni mwa wadau (wa-zalishaji, watunga sera, wataalam wa afya na wa-nanchi)

· Kuelimisha wadau kuhusu umuhimu wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto mwilini kwa jamii na taifa kwa ujumla

· Kuelimisha wazalishaji, waagizaji, wau-zaji na walaji juu ya umuhimu wa ku-tumia na kutunza chumvi yenye madini joto

· Kuwaelimisha na kuwajengea uwezo walaji na wauzaji wa reja reja wa kudai na kutaka kuuziwa chumvi yenye ma-dini joto.

· Kuingizwa katika mitalaa somo juu ya madhara ya upungufu wa madini joto kuanzia shule za msingi hadi Vyuo.

Utashi mdogo wa kutumia chumvi yenye madini joto na upendeleo wa kutumia chumvi ya mawe inayouz-wa kwa bei nafuu

· Kutambua na kuondoa uelewa mbaya na upotoshaji (misconceptions), imani na kasumba kuwa chumvi ya mawe isiyo na madini joto ndiyo nzuri ili ku-ondoa vikwazo katika kukubalika kwa chumvi yenye madini joto.

· Kutangaza na kuhamasisha faida ya ma-tumizi ya chumvi yenye madini joto ka-tika kampeni zinazohusisha kuonesha nembo rasmi za chumvi yenye madini joto ili kuwawezesha walaji kuitambua na kuitumia chumvi yenye madini joto.

Udhaifu na ufinyu wa ba-jeti katika mfumo na mika-kati ya upashanaji habari, utoaji elimu mawasiliano na utetezi (advocacy)

· Kuimarisha na kuwezesha mfumo na mikakati ya upashanaji habari, ueli-mishaji na utetezi (advocacy) ili kuon-geza uelewa kuhusu umuhimu wa ku-ondoa madhara ya upungufu wa madini joto na kuongeza utashi na tabia ya ku-tumia chumvi yenye madini joto

Page 47: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

37

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

MWANYA WA RUSHWA

UDHAIFU/TATIZO MAPENDEKEZO

Uwajibikaji mdogo Udhaifu katika utoaji wa taarifa za uwajibikaji ku-toka kwa wazalishaji

· Kuwahimiza na kuwaelekeza wazalishaji na waagizaji kutoa taarifa za uwajibikaji katika uchanganyaji wa madini joto ka-tika chumvi

Ushirikishwaji mdogo

Ushirikishwaji dhaifu wa wadau katika udhibiti wa chumvi

· Kuimarisha uratibu na kuwashiriki-sha wadau ipasavyo katika udhibiti wa chumvi yenye madini joto.

Mawasiliano dhaifu Udhaifu katika utoaji wa mrejesho (feedback) kwa wadau

· Kuimarisha mfumo wa utoaji wa mreje-sho (feedback) kuhusu taarifa za shu-ghuli, mafanikio, changamoto na fursa za mpango wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto

Miundombinu dhaifu ya kupokea na kushu-ghulikia malalamiko ya wadau

· Kuanzisha, kuimarisha na kuitumia mi-undombinu ya kupokea na kushughu-likia malalamiko ya wadau

Udhibiti na usimam-izi dhaifu

Udhaifu katika mfumo wa ufuatiliaji, usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni kutoka ngazi ya wazalishaji hadi kwa wa-laji

· Kuhakikisha kuwa wakaguzi wana vifaa (test kits) na fursa ya muda muafaka ya kupima sampuli katika maabara kwa ajili ya ushahidi mahakamani.

· Kuwaelimisha wakaguzi juu ya umuhimu wa kuchanganya madini joto ili waweze kuweka kipaumbele katika ukaguzi wa chumvi miongoni mwa ma-jukumu yao ya msingi ukaguzi wa ubora wa vyakula.

· Kuimarisha utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi katika ngazi zote (ku-toka ngazi ya uzalishaji hadi walaji).

Udhaifu, upendeleo na vi-tendo vya rushwa katika kuchukua hatua dhidi ya wakiukaji wa sheria na kanuni

· Kuelimisha wakaguzi na wadau wengine juu ya madhara ya rushwa na upende-leo katika uchukuaji wa hatua dhidi ya wakiukaji na hivyo kuwawezesha ku-chukua hatua kama sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto zinavyoele-keza

· Kuchukua hatua dhidi ya wanaojihusi-sha na upendeleo na rushwa

Upungufu wa watumishi, vifaa, fedha na mafunzo

· Kuimarisha taasisi zinazohusika na usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi (kuongeza bajeti, vi-faa, watumishi na mafunzo) ili kuleta ufanisi na tija katika shughuli za mpan-go wa kuondoa madhara ya upungufu wa madini joto

Kuingizwa kwa chumvi isi-yo na madini joto kutoka nje ya nchi

· Kuimarisha ukaguzi katika bandari na mipakani kwa kuwawezesha maafisa fo-rodha/wakaguzi kutumia ‘test kits’, ku-pata taarifa na takwimu za uagizaji kabla ya chumvi kufika na kuwapa mamlaka ya kuchukua hatua pale inapobidi

· Kuwaelimisha waagizaji juu ya umuhimu madini joto katika chumvi na kuwataka kuagiza chumvi yenye madini joto

Page 48: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

38

MWANYA WA RUSHWA

UDHAIFU/TATIZO MAPENDEKEZO

Upungufu katika ufanisi na matokeo ya mpango

Uwezekano wa kuongeze-ka kwa matukio ya ugon-jwa wa uvimbe wa tezi la shingo na kupungua kwa mafanikio yaliyofikiwa na mpango

· Kuimarisha ukaguzi (udhibiti na uhaki-ki wa ubora)

· Kufanya utafiti (surveys and survailance) kwa lengo la kutathmini kuongezeka au kupungua kwa matumizi ya chumvi ye-nye madini joto na magonjwa yatokan-ayo na upungufu wa madini joto

5.2 HITIMISHO

Lengo la kuzuia na kuondoa madhara na magonjwa yatokanayo na upungufu wa madini joto kupitia uchanganyaji wa madini joto katika chumvi linaweza kufikiwa katika mikoa yote hapa nchini. Hata hivyo, uzoefu wa utafiti huu unaonesha kuwa ili kufikia lengo la kuondoa madhara hayo ya upungufu wa madini joto nchini, kunahitajika usimamizi fanisi wa viwango vya madini joto nchini kutoka ngazi ya uzalishaji hadi kufikia ngazi ya kaya na kufuatiwa na utekelezaji madhubuti wa sheria na kanuni zilizopo. Ni muhimu usimamizi huo kuwa endelevu kwa kuwa madhara ya upungufu wa madini joto hujirudia pale uchanganyaji wa madini joto unapokatizwa au kuvurugwa.

Page 49: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

39

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

MAREJEO

Children’s Fund (UNICEF)/World Health Organization (WHO). 2001. Assessment of iodine deficiency disorders and monitoring their elimination: A guide for programme managers. Second edition. Geneva, Switzerland: ICCIDD/UNICEF/WHO.

Field E, Robles O, Torero M. (2007). Can Public Policy Affect Malnutrition? The role of Geography: Iodine deficiency and schooling attainment in Tanzania SITE conference. Harvard and the University of Michigan Mimeo, Harvard University.

International Council for the Control of Iodine Deficiency Disorders (ICCIDD)/United Nations

Kavishe F and Mushi S. (1993) Nutrition-relevant Actions in Tanzania. A Case Study for the XV Congress of the International Union of Nutrition Sciences. Adelaide: United Nations Administrative Committee on Coordination, Sub-committee on Nutrition.

Latham MC. (1965). A goitre survey in Ukinga, Tanzania (formerly Tanganyika). Transactions of the Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene; 59(3): 342–8.

Msuya J.( 1999). Nutrition Improvement Projects in Tanzania: Appropriate choice of institutions matters. ZEF Discussion Papers on Development Policy. Born: Center for Development Research, Universitat Bonn:1-13.

Section 16(1) and (2), Dar Es Salaam.

Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC). 2004. Prevention and control of iodine deficiency disorders in Tanzania. Second National IDD Survey. TFNC Report No. 2002. Dar Es Salaam, Tanzania: TFNC.

TDHS (2005).Tanzania Demographic and Health Survey, National Bureau of Statistics, Dar Es Salaam.

TDHS (2010).Tanzania Demographic and Health Survey, National Bureau of Statistics, Dar Es Salaam.

United Republic of Tanzania (1994). Iodation Regulations, Dar Es salaam.

United Republic of Tanzania (2010). The Tanzania Food, Drugs and Cosmetics (Iodated Salt) Regulations, Dar Es Salaam.

United Republic of Tanzania(1978). The Food (Control of Quality) Act, Dar Es Salaam.

United Republic of Tanzania(1979). The Mining Act, Regulations made under

United Republic of Tanzania(1992). The Food (Iodated Salt) Regulation,; The Mining (Salt Production

WHO (1994). Iodine and health: Eliminating iodine deficiency disorders safely through salt iodization. Geneva: World Health Organisation.

Page 50: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

40

VIAMBATISHO (APPENDICES)

Kiamb. 1: Laboratory report from Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC)

Page 51: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

41

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

Page 52: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

42

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: UTAFITI KIFANI WA CHUMVI YENYE MADINI JOTO (CASE STUDY OF IODATED SALT)    

44    

 

 

Page 53: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

43

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

noteS

Page 54: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt)

44

noteS

Page 55: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE
Page 56: TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA · 2019-06-13 · UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa ChUmvi YenYe madini Joto (Case Study of iodated Salt) iv MUHTASARI (EXECUTIVE

UDHIBITI WA BIDHAA BANDIA: Utafiti Kifani Wa Chumvi Yenye Madini Joto

(Case Study of Iodated Salt)