15
i Hussein Issa Tuwa WiMBO wa GaIDI ToLEO la KiDIJITALI DAR ES SALAAM UWARIDI APP

Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

  • Upload
    others

  • View
    31

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

i

Hussein Issa Tuwa

WiMBO wa GaIDI ToLEO la KiDIJITALI

DARESSALAAM

UWARIDIAPP

Page 2: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

ii

WIMBO WA GAIDI Kitabu cha TuwaKadabra Productions

UHARIRI

Kimehaririwa na rafiki yangu, mdogo wangu, na swahiba wangu muadilifu, Kalunga Mrisho Matovolwa.

USANIFU

Mpangilio wa kurasa na usanifu wa jalada vimefanywa na mshirika wangu mbunifu, el maestro Twaha Hamisi Ubwa.

TAHADHARI

Hii ni kazi ya kubuni. Majina, wahusika, mahala na matukio yote yaliyotajwa katika kitabu hiki ni aidha matokeo ya ubunifu wa mtunzi tu au yametumika

kibunifu tu. Kufanana/Kutajwa kwa aina yoyote na mtu yeyote wa kweli, aliye hai au aliyekufa, matukio au maeneo yoyote ya kweli ni kwa bahati tu na/au ni kwa

lengo la kuleta uhalisia katika kisa cha riwaya hii.

ONYO Haki zote zimehifadhiwa. Kamwe hairuhusiwi kuchapisha kazi hii, au kuidurufu, kuiuza kwa mara ya pili, kuikopesha au kuiazimisha, kwa njia ya kibiashara au

vinginevyo, au kuisambaza popote pale bila ya kwanza kupata idhini halali kutoka kwa Hussein Issa Tuwa, au vinginevyo kuisambaza kwa mafungamano ya aina

yoyote ile bila kumhusisha Hussein Issa Tuwa, na bila ya sharti kama hili kushinikizwa kwa mnunuzi husika.

Riwaya hii imeidhinishwa kuwekwa kwenye mfumo wa kidijitali wa Uwaridi App na Hussein Tuwa, Mwenyewe.

Hakimiliki © 2015 Hussein Issa Tuwa ISBN 978-9987-9710-6-0

Page 3: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

iii

“Nimeagiza nguvu zote za vyombo vyetu vya dola na vya kijasusi kuwasaka waliohusika na shambulizi hili la kigaidi na kuwafikisha mbele ya sheria. Hatutatofautisha baina ya magaidi waliofanya shambulizi hili, na wale wanaowahifadhi.”

-George W. Bush, Ikulu ya Marekani, mara baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001

Ni nani angedhania kuwa miaka kadhaa baadaye, maneno, “…nguvu zote za vyombo vyetu vya dola na vya kijasusi kuwasaka waliohusika…”, ya rais wa Marekani yaliyotolewa mwaka ule wa 2001, yangekuja kutekelezwa kwa namna iliyokuja kubadili kabisa maisha ya kijana mmoja asiyetarajiwa kabisa wa kitanzania?

Hakuna.

Page 4: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

1

UTANGULIZI

i miaka mitatu tangu kuuawa kwa Osama bin Laden nchini Pakistani. Wanamgambo wa Al-Qaida walikuwa wamesambaratika. Wengi miongoni mwao wakiwa wameuawa, ilhali wengine wakikamatwa na majeshi ya Marekani nchini Pakistani… na kikundi cha wachache wengine kikiwa kimefanikiwa kutoroka na kukimbilia eneo la Waziristani lililo kaskazini mwa Pakistani, kwenye kitongoji cha Miramshah kilichokuwa kinadhibitiwa na washirika wao wakuu, wapiganaji wa Taleban. Huko wakapata hifadhi baada ya kifo kile kichungu cha kiongozi wao.

Na tangu wakati huo, hali ya wakaazi wa kijiji kilichokuwa kiasi cha kilomita saba kutoka kwenye ile ngome ya watalebani iliyowahifadhi wale wanamgambo wachache wa Al-Qaida, imekuwa ni ya mashaka makubwa. Njaa ilikuwa imetawala, mahitaji yote muhimu yakatoweka, maradhi hayakuwa na wa kuyatibu, magonjwa ya mlipuko na yatokanayo na lishe duni yakishamiri… na roho za wanakijiji kile zikiwa sio

Page 5: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

2

mikononi mwao tena, bali mikononi mwa wapiganaji wa Talebani waliokidhibiti kijiji chao.

Kwa nini? Kwa kuwa Osama Bin Laden alikuwa ameuawa na

wamarekani… na taarifa ziliwafikia watalebani kuwa tabibu aliyefika mahala ambapo Osama alikuwa amejificha kwa ajili ya kumtibu binti wa mpiganaji yule mwenye msimamo mkali ndiye aliyetoa siri ya mahala Osama alipokuwa, kwani wamarekani walivamia eneo lile siku mbili tu baada ya tabibu yule aliyeaminika kuwa alikuwa akiiunga mkono Al-Qaida kufika eneo lile. Kwa kuwa Al-Qaida ilisambaratika kwa muda baada ya kifo cha Osama, Taleban wakachukua jukumu la kulipiza kisasi kwa kifo cha mshirika wao mkubwa kwa niaba ya Al-Qaida.

Hivyo basi, pale binti wa Osama aliyekuwa akishikiliwa na wanajeshi wa Pakistani kabla ya kukabidhiwa kwa wamarekani, alipofanikiwa kupenyeza taarifa kwa watalebani kupitia kwa mmoja wa watendaji wa jeshi la Pakistani aliyekuwa akiiunga mkono Al-Qaida kuwa tabibu huyo alikuwa akiongea kwa lugha ya kipashtuni yenye lafudhi ya watu watokao kwenye kijiji kile, ilitosha sana kuwajulisha watalebani kuwa daktari aliyemchomea utambi Osama kwa wamarekani hadi akauawa, alikuwa

Page 6: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

3

ametokea kwenye kijiji kile kilichokuwa kiasi cha kilomita saba tu kutoka pale kwenye ngome yao.

Kilichofuatia kilikuwa ni kizazaa kikubwa pale kijijini. Mauaji, mateso, na utekaji nyara viliwaandama

wanakijiji, ikitafutwa familia ya tabibu aliyemchoma Osama kwa wamarekani. Msako wa nyumba hadi nyumba ulioendeshwa ukazaa matunda pale familia ya tabibu aliyehusika kumchomea utambi Osama ilipowekwa kizuizini kwa wiki nzima na kuwekwa kwenye wakati wa mateso na vitisho visivyosemekana. Wanafamilia walibakwa, wakapigwa mijeledi na baadhi yao wakauawa huku wengine wakishuhudia. Siri ikabidi itolewe. Tabibu wa Osama akatajwa na wanafamilia wake mwenyewe, wakati huo yeye akiwa jijini Islamabad akiendelea na shughuli zake kama kwamba hakuhusika na kifo cha Osama.

Watalebani wakamfuata huko huko kwa lengo la kumuua. Lakini sio kabla ya kumtesa na kumhoji kikatili. Tabibu akakiri kuwa hakuwa peke yake… alikuwa ana mwenzake ambaye alikuwa amebaki kule kule ambako watalebani walikuwa wametokea.

Hah! Watelebani wakahamanika.

Ni nani huyo?

Page 7: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

4

Tabibu akagoma kusema. Na anaposema yuko kule kule walipotoka wao…

anamaanisha nini, ndani ya ngome yao? Tabibu akapiga kimya. Au yuko kule kule kwenye kile kijiji cha wasaliti alichozaliwa yeye? Tabibu akazidi kugoma kutoa ushirikiano. Na watalebani wakazidisha mateso. Na tabibu akaamua kufa na siri yake. Akajitutumua kumpora silaha mmoja wa watesaji wake

ili awateketeze, nao wakamuwahi na kummiminia risasi. Kifo cha Osama kikalipizwa… miezi mitatu tu baada ya kifo chake. Lakini sasa watalebani wakabakiwa na kitendawili kikubwa. Je, msaliti mwingine wa Osama alikuwa ni miongoni mwa wale maswahiba wao wa Al-Qaida waliowahifadhi ndani ya ngome yao? Au alikuwa kwenye kile kijiji alichotokea yule tabibu, walichokibatiza jina la ‘Kijiji cha Wasaliti’, kilichokuwa jirani na ile ngome yao?

Sasa huyu ndiye alikuwa anasakwa, na kijiji kile kikawekwa chini ya karantini kabambe na watalebani. Hakuna atakayetoka wala kuingia kwenye kijiji kile. Mpaka msaliti huyo na wengine kama yeye watakapobainishwa na kuuawa.

Page 8: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

5

Kijiji kikawa kimetengwa na dunia. Jitihada za majeshi ya Pakistani kukiokoa kijiji kile

hazikufua dafu asilani, kwani Waziristani ilikuwa ni ngome kuu ya watalebani, na hakukuwa na namna ya kuiangusha isipokuwa kwa kuipenya kijasusi kama jinsi alivyopenyezwa yule tabibu mzaliwa wa kijiji kile ndani ya kundi la Al-Qaida.

Na hilo lilikuwa haliwezekani tena sasa. Watalebani walikuwa wakimshuku kila aliyewaendea na

kila waliyemuona kuwa si miongoni mwao. Hali ikafikia pabaya. Wapiganaji wote wa Al-Qaida waliokuwa

wamehifadhiwa kwenye nyumba salama ya uongozi wa watalebani wakawa chini ya uangalizi na uchunguzi mkali. Miongoni mwao alikuwamo msaliti, na watalebani walidhamiria kumtia mikononi na kumuangamiza. Ilikuwa ni mahojiano ya mara kwa mara, mitihani ya hapa na pale kwa wale Al-Qaida waliokimbilia mikononi mwa washirika wao wa kitalebani. Hakukuwa na muamana tena baina yao.

Amani ikapotea. Ndani na nje ya ngome ile kubwa ya watalebani. Jumuiya ya kimataifa ilifanya bidii za kila namna kuwaokoa wakaazi wa kijiji kile bila mafanikio yoyote. Serikali ya Pakistani pamoja na kulaani kwake

Page 9: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

6

kuuawa kwa Osama ndani ya nchi yake bila ya wao wenyewe kushirikishwa, haikufua dafu, kwani Taleban siku zote wamekuwa wakiamini kuwa serikali ya Pakistani ilikuwa ni kibaraka wa wamarekani.

Marekani ikatoa tamko. Talebani iwaachie huru wanakijiji wale waondoke

kijijini pale na kwenda kwenye kambi za wakimbizi nje ya kitongoji kile cha Waziristani, na iwasalimishe wapiganaji wote wa Al-Qaida iliowahifadhi, ama si hivyo ndege za maangamizi zinazoruka bila ya rubani, yaani drones, zitatumwa kuisambaratisha ngome yao.

Talebani wakagoma. Si hivyo tu, na wao wakatoa tamko. Wamarekani wakituma hizo ndege wajue pia wataua raia

wa kijiji wasio na hatia… na watalebani watakuwa wanaua kila mmarekani watakayemuona, popote pale duniani.

Ngoma ikazidi kuwa nzito…

Page 10: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

7

Kijiji cha Dargah Mandi, kilomita saba magharibi mwa kitongoji cha Miramshah, Waziristani ya Kaskazini, nchini Pakistani.

i saa saba za usiku. Baridi kali ilikuwa ikipambana na mashuka mazito yaliyokuwa yakijaribu kuihifadhi miili ya wanakijiji waliorundikana upande mmoja wa eneo pana la tambarare lililokuwa mpakani kabisa mwa kijiji kile kilichojaa madhila makubwa na mashaka mazito. Ni kijiji cha Dargah Mandi kilichokuwa ndani ya kitongoji cha Waziristani ya Kaskazini, nchini Pakistani.

Wanakijiji walikuwa wamejikunyata wakisubiri msaada waliokuwa wameutarajia kwa muda mrefu bila matumaini ya kuupata. Wapiganaji wa Taleban wenye silaha walikuwa wamewazingira wanakijiji wale kutoka pande zote za eneo lile, nao wakiusubiri msaada ule ambao kwa hakika na wao walikuwa wakiuhitaji, maana hali kijijini Dargah Mandi ilikuwa tete kila upande.

Mbele yao, kiasi cha kama mita mia tatu hivi kutoka pale ambapo wale wanakijiji walikuwa wamejikunyata huku wakiwa wamewekewa mitutu ya bunduki za wapiganaji wale wenye roho zisizosita kutekeleza mauaji, kulikuwa kuna uwanja mpana wa wazi wenye majani

Page 11: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

8

mafupi, na kwenye maeneo sita tofauti ya uwanja ule, kulikuwa kuna mioto iliyokuwa ikiwaka kutokana na marundo ya kuni zilizowashwa kwa kusudio maalum, ikitupa miale yake hewani na kuleta mwanga kiasi eneo lile na wakati huo huo ikiacha baadhi ya maeneo ya uwanja ule kuwa na kiza kizito.

Dakika zilisonga na baada ya muda ulioonekana kuwa ni mrefu kuliko uhalisia wa muda wenyewe, miungurumo ya ndege ilisikika ikitokea angani upande wa mwisho kabisa wa eneo lile la wazi lililowekewa mioto, eneo ambalo liliiishia kwenye korongo refu sana lililoanguka umbali wa mita zipatazo mia saba kwenda chini, ambako kulikuwa kuna mto mkubwa sana uliokuwa ukipeleka maji kwa ghadhabu isiyosemekana hadi kwenye bahari ya Arabia (Arabian Sea), kilomita nyingi kusini mwa Pakistani.

Dargah Mandi haikuweza kabisa kuingilika kutokea upande ule hatari, ambapo hakuna binadamu ambaye angeweza kukiingia kijiji kile kwa kulikwea korongo lile kutokea kule chini kwenye mto ule mkali.

Na ni kutokana na uhatari wa eneo lile ndipo watalebani waliojaa hila na shuku zisizo ukomo, walipoelekeza kuwa ndege zile za misaada ziangushie marobota makubwa ya chakula na madawa kwenye eneo lile, kisha ndege zitakazoangusha misaada ile zigeuzie huko huko angani na

Page 12: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

9

kwenda zake. Hakukuwa na ruhusa kabisa kutua pale kijijini wala sehemu yoyote ya eneo walilolidhibiti vilivyo la Waziristani ya Kaskazini.

Ndege ya kwanza ikatokeza kutokea nyuma ya milima mingi iliyolizunguka eneo lile, na minong’ono ya viherehere ikazagaa miongoni mwa wanakijiji.

Ndege ikazidi kukurubia huku ikizidi kushuka. Watalebani wakazidi kujizatiti kwa silaha makini wakiwa miongoni mwa wanakijiji ambao sasa waliwakusanya kuwafanya kama ngao zao dhidi ya shambulizi lolote kutoka kwenye ndege ile. Na hata pale walipoanza kujizatiti namna ile, ndege nyingine tatu zilionekana kutokeza juu ya vilele vya milima iliyolizunguka eneo lile, na dakika kumi baadaye marobota makubwa yalionekana kuanguka kutoka angani. Mayowe yalizagaa, wanakijiji wakazidi kujirudisha nyuma ili kuwa mbali na eneo lile la wazi lililokuwa likimulikwa kwa ile mioto kutoka pembe sita tofauti. Lakini muda si muda, parachuti zikafunuka kutoka kwenye marobota yale makubwa, nayo yakaanza kushuka taratibu huku yakinesanesa hewani kwenye anga ile ya usiku.

Wanakijiji na watalebani walijitahidi kwa kadiri walivyoweza kufuatilia ushukaji wake kwenye kiza cha usiku ule wenye mbalamwezi hafifu, lakini haikuwa rahisi.

Page 13: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

10

Marobota yalizidi kushuka, kila moja kwa uelekeo wake… kila moja likiwa na shehena muhimu kwa wanakijiji wa Dargah Mandi ndani yake… lakini pia juu ya kila mgongo wa marobota yale, kulikuwa kuna siri kubwa…

Page 14: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

11

1

AKOMANDOO WANNE walishuka kwa parachuti wakiwa wamelala juu ya migongo ya marobota makubwa ya chakula cha msaada yaliyokuwa yakiangushwa na ndege za msalaba mwekundu kwenye kile kijiji cha Dargah Mandi. Wote wanne walikuwa wamevaa nguo maalum za kupigia mbizi majini bila ya kulowa.

Lengo lao lilikuwa ni moja tu. Kumchomoa mtuhumiwa muhimu wa ugaidi

aliyehifadhiwa kwenye ngome kuu ya watalebani ndani ya kijiji kile, akiwa ni mmoja wa wapiganaji wa Al-Qaida aliyetajwa kuwa mshirika mkuu wa hayati Osama bin Laden aliyeratibu shambulizi la kutisha kwenye majengo ya World Trade Center, maarufu kama Twin Towers jijini New York huko Marekani mnamo mwaka 2001. Sasa ngome iliyosalia ya Talebani iliyokuwa inawahifadhi baadhi ya wapiganaji wa Al-Qaida waliobakia, yeye akiwemo, ilikuwa imezingirwa na majeshi ya ushirika wa Marekani na Pakistani. Shambulizi kubwa la anga lilikuwa limeandaliwa na wamarekani. Upinzani wa Talebani

Page 15: Hussein Issa Tuwa W iMBO wa G aIDI

Hussein Tuwa Wimbo wa Gaidi

12

ulikuwa unaelekea kushindwa, na wamarekani wakiingia ndani ya ngome ile hakutakuwa na garantii ya mtuhumiwa yule kunusurika.

Isipokuwa kama atatolewa mle ngomeni kabla majeshi ya washirika hayajavamia.

Lakini kivipi? Ndipo nafasi ilipojitokeza pale Talebani walipokubali

wanakijiji wapelekewe vyakula vya msaada kwa njia ile. Marobota yalitua kwa vishindo ardhini na kuviringika

shaghalabaghala, kila moja upande wake. Makomandoo waligaragazwa vibaya na yale marobota makubwa, lakini kwa kuwa walikuwa mahiri kwenye kazi zao na walishalifanyia mazoezi mara kadhaa tukio lile kabla ya siku ile, kila mmoja alifanikiwa kujirusha pembeni na kubaki akiwa amejilaza kimya kwenye majani mafupi ya eneo lile, macho yao yakitafuta uelekeo ambao kila mmoja aliamini kuwa ni kusini ya pale walipoangukia, wakiyaacha yale marobota makubwa kabisa yakiendelea kubingirika huku yakijizonga na zile parachuti zilizoyashusha.

Kule kwa wanakijiji wenye njaa, watalebani walikuwa wakiyafuatilia yale marobota kwa umakini kwa kadiri walivyoweza. Kwa namna fulani ambayo sio bahati mbaya, marubani waliokuwa wakiyadondosha yale