8
HALI YA UHISANI TANZANIA 2018 UTAFITI WA KITAIFA KUHUSU UHISANI NA UTAMADUNI WA KUJITOLEA

HALI YA UHISANI - FCSthefoundation.or.tz/wp-content/uploads/2018/08/Utafiti...02 Hali ya Uhisani Tanzania 2018 Utangulizi Huu ni muhtasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo ya Utafiti

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

HALI YA

UHISANI TANZANIA 2018 UTAFITI WA KITAIFA KUHUSU UHISANI

NA UTAMADUNI WA KUJITOLEA

02

Hali ya Uhisani Tanzania 2018

Utangulizi

Huu ni muhtasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo ya Utafiti wa Kitaifa kuhusu Hali ya Uhisani na Utamaduni wa Kujitolea nchini Tanzania. Utafiti huu umefanywa na wataalamu wa Strategic Connections ya Kenya kwa kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi Aprili mwaka 2018. Umefadhiliwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Tanzania Philanthropy Forum (TPF).

Madhumuni ya utafiti

Utafiti huu umelenga kupata taarifa muhimu kuhusu hali ya uhisani au utamaduni wa kujitolea

kwa jamii nchini Tanzania. FCS na TPF wanahimiza wadau kutumia matokeo ya utafiti huu kama njia ya kubadilishana uzoefu katika tasnia nzima ya uhisani na kujitolea kwa jamii, kuhamasisha umuhimu wa uhisani miongoni mwa jamii ya watoaji na pia kuweka mwongozo wa kuendeleza uhisani Tanzania.

Inafaa muhtasari huu kusomwa kwa pamoja na taarifa kamili na ya kina ya utafiti kuhusu uhisani na utoaji. Muhtasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo ni kama yafuatavyo.

MUHTASARI: MAMBO MUHIMU, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO YA UTAFITI

Maelezo ya Jumla ya Utafiti: Muktadha wa mambo muhimu

1. Tafsiri ya Uhisani na Utoaji kwa Jamii

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupata tafsiri ya falsafa ya uhisani kwa maoni na mantiki ya Watanzania. Utafiti huu umeibua tafsiri zifuatazo:-

a. Uhisani : Ni hali ya kutoa au kujitolea kwa hali au mali (fedha, utaalam au vitu)kwa manufaa au kwa lengo la kusaidia wengine kwenye jamii, hasa kusaidia ustawi wao.

b. Wahisani: Hawa wanaweza kuwa mtu mmoja mmoja au shirika ambao wanatenga kiasi cha rasilimali zao (zilizo rasmi na zisizo rasmi kwa utaratibu maalum au bila mpangilio) ili kusaidia wenye uhitaji, wasiojiweza na kuimarisha ustawi wa watu na jamii.

c. Wanaharakati wa Uhisani: Hawa ni pamoja na watu binafsi au taasisi zinazojishughulisha na kuratibu shughuli za uhisani/utoaji kwenye jamii. Mara nyingi hutafuta rasilimali na kuzitumia kufanya uratibu huu ili kuhamasisha uhisani na utamaduni wa utoaji kwa lengo la kusaidia watu na kuimarisha ustawi wa jamii.

Pia, Utafiti huu umebaini kuwa Uhisani/Utoaji na Wanaharakati wake hutokea tu pale mambo yafuatayo yatakidhi:-

a. Sababu za hisani: Motisha kubwa inayosukuma utoaji lazima iwe ni kuchangia katika kuinua

maisha ya watu wengine kwenye jamii.

b. Wapokeaji/wanaofaidika: Mchango unaotolewa na wahisani hauna budi kumfikia moja kwa moja mhitaji au wahitaji katika jamii au kulenga jambo muhimu linalogusa watu kama kuhifadhi mazingira nk.

c. Aina ya uhisani/utoaji: Hisani inaweza kuwa katika hali mbalimbali kama vile fedha, muda, mali au vifaa, utaalamu nk.

d. Moyo wa kujitolea: Kwa kawaida ni lazima kuwepo moyo na utashi wa kutoa kwa ajili ya watu wengine, yaani rasilimali inayotolewa haina budi iwe ya mhisani/mtoaji mwenyewe na atoe kwa wengine bila kulazimishwa.

2. Wajihi wa asasi za Uhisani/Utoaji zilizoshiriki katika utafiti huu:

Idadi kubwa ya wahisani hapa Tanzania ni asasi za kiraia (AZAKI), ambazo nyingi zimesajiliwa kama asasi zisozojiendesha kibiashara (hazilengi kutengeneza faida kwenye kazi zao). Wadau wakubwa wa uhisani wamesambaa katika sehemu kubwa ya nchi lakini mikoa ya Kanda ya Magharibi, ya Kusini pamoja na mkoa wa Dar es Salaam kwa pamoja wanachangia zaidi ya nusu (55%) ya wahisani wote nchini.

Pia utafiti umeonyesha kuwa zaidi ya nusu ya waliohojiwa (56%) katika utafiti huu

Hali ya Uhisani Tanzania 2018

03

wamethibitisha kuwa walikuwapo kwenye mtandao au ushirika wa utoaji wakati asilimia 44 hawakua wanachama wa kikundi au ushirika wowote wa uhisani. Hali hii inatoa fursa kwa TPF kuliorodhesha kundi hili la mwisho kama wanaharakati wa uhisani/utoaji.

3. Hadhi ya kisheria ya taasisi zilizohojiwa

Kuhusu hadhi ya kisheria ya taasisi zilizoshiriki, utafiti unaonyesha kuwa, saba kati ya kumi (au 72%) ni asasi zisizoendeshwa kibiashara na kutengeneza faida; zikifuatiwa na vikundi vya ushirika (7.8%) na makampuni yenye ukomo katika hisa (6.5%). Taasisi nyingine ni Wadhamini (3.9%), taasisi za dini (3%) na taasisi za kimataifa zisizo za kiserikali na Wakfu au mifuko (1%).

4. Vyanzo vikuu vya rasilimali-fedha kwa shughuli za maendeleo Tanzania

Utafiti umebaini kuwepo kwa aina nne za vyanzo vya fedha kwa taasisi zilizohojiwa:

1. Ufadhili kutoka asasi za kimataifa zisizo za kiserikali (28.75%)

2. Wahisani binafsi (17.3%) 3. Fungu kutoka mapato ya mwaka (13%) 4. Wadau wa maendeleo (8.7%) 5. Makampuni (1.1%), na 6. Serikali (2.2%).

Utafiti unaonyesha hali ya usawa kati ya vyanzo vya uhisani kutoka ndani na vile vya kutoka nje

ya nchi. Chanzo kikubwa cha uhisani kwa jamii katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kilikuwa ni Wadhamini na Mifuko au Taasisi waliotoa karibia nusu ya fedha zote za uhisani (45.1%), wakifuatiwa na taasisi/mashirika ya kimataifa ya maendeleo (41.2%) na mwisho ni vyanzo vya ndani vya asasi zenyewe (31.3%).

5. Mizania ya ufadhili kutoka vyanzo mbalimbali

Taasisi na asasi zilizohojiwa zimeonyesha kuwa kwa pamoja zilipata kiasi cha dola za Kimarekani zaidi ya milioni 500 katika kipindi cha miaka mitano kilichoishia mwaka 2017. Hii ni sawa na wastani wa dola za Kimarekani 100 milioni kila mwaka. Vyanzo vikuu vitatu vilivyotoa fedha nyingi zaidi katika kipindi hicho ni:

1. Mashirika na asasi za kimataifa (71.7%). 2. Wadhamini na mifuko maalum (12%). 3. Wadau wa maendeleo wa kimataifa

(4.5%). Iligundulika pia kuwa wakati ambapo wahisani wanapata rasilimali zao kutoka kwa watu binafsi na familia, makampuni, serikalini na vyanzo binafsi katika taasisi zao, rasilimali hizo ni chache sana na zinaunda jumla ya asilimia 10 tu katika sekta ya Uhisani hapa Tanzania. Zaidi ya nusu ya waliohojiwa (57%) na utafiti huu walibainisha kuwa wanapata ruzuku na rasilimali zao kutoka nje wakati asilimia 43 walisema wanapata kutoka vyanzo vyote viwili, yaani ndani na nje ya nchi.

Vyanzo vya kutafuta Maendeleo

Matokeo ya mashirika yaliyoshiriki katika tafiti

Hapana, 44%

Ndiyo, 56%

ASASI ZA KIMATAIFA ZISIZO ZA KISERIKALI

29%

WAHISANI BINAFSI

17%

MAPATO YA MWAKA

13%

WADAU WA MAENDELEO

9%

Hali ya Uhisani Tanzania 2018

04

6. Maeneo makuu ya Uhisani

Maeneo ambayo Uhisani ulijikita zaidi yalikuwa yafuatayo: kujikimu kimaisha (54.4%), elimu (53.7%), afya (45%) na utawala (43%). Nyingine ni pamoja na mazingira (32.9%), kilimo (23%), msaada wa dharura (15%), michezo na utamaduni (14%) pamoja na maji, usafi wa mazingira na afya (19%).

7. Uhisani na Utamaduni wa Kutoa nchini Tanzania

Utafiti umebaini kuwepo kwa utamaduni wa kutoa na kusaidiana miongoni mwa jamii ya Watanzania. Utoaji huu unajikita katika kuziwezesha jamii hasa zile zinazohitaji msaada wa hali na mali kwa ajili ya ustawi wao. Pia kuna utamaduni wa wanufaika na hisani mbalimbali kutoa shukrani kwa kile kinachotolewa na wahisani kwa ajili ya ustawi wao.

Uhisani katika Mikoa

KANDA YA ZIWA

21%

MIKOA YA KASKAZINI

19%

MIKOA YA MAGHARIBI

17%

PWANI

14%

KUSINI

11%

ZANZIBAR

10%

UKANDA WA KATI

9%

Sehemu Muhimu za kuwekeza

KUJIKIMU KIMAISHA

54%

ELIMU

54%

AFYA

45%

UTAWALA

43%

MAZINGIRA

32%

KILIMO

23%

USAFI WA MAZINGIRA NA

AFYA

19%

MSAADA WA DHARURA

15%

MICHEZO NA UTAMADUNI

14%

8. Mgawanyo wa Uhisani Tanzania

Mtazamo wa hali ya mgawanyo wa fedha katika mikoa 7 ya Tanzania unaonesha kuwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiongoza kwa kuwa na watoaji wengi (20.5%), ikifuatiwa na mikoa ya Kaskazini (18.6%) na mikoa ya Magharibi (16.7%). Mikoa mingine ni Pwani (14.1%), Kusini (10.9%) na mikoa ya Ukanda wa Kati (9%).

9. Changamoto zinazokabili Uhisani na wahisani Tanzania

Utafiti umebaini changamoto kubwa zinazoikabili sekta hii kuwa ni pamoja na: a. Mifumo isiyo rafiki au isiyofaa ya

udhibiti ya mamlaka za serikali,b. Kutokuwa na uwezo wa kubadilisha

vyanzo mbadala vya rasilimali,c. Ukomo katika kujifunza na

kushirikiana,d. Mapungufu katika uwajibikaji

miongoni mwa wadau wa uhisani, na

e. Kukosekana kwa njia salama na rafiki za utoaji.

Hali ya Uhisani Tanzania 2018

05

10. Mwenendo wa Uhisani katika Mashirika ya Biashara

Utafiti umeainisha kuwepo kwa ongezeko la shughuli za uhisani miongoni mwa mashirika hapa nchini Tanzania. Uhisani huu kutoka kwa mashirika haufuati mpangilio wowote, yaani unafanywa na taasisi zenye usajili na wakati mwingine hakuna kumbukumbu inayowekwa au kuainisha kuwa ulifanyika. Taarifa na takwimu kuhusu utoaji kutoka kwa mashirika bado ni chache sana hapa nchini. Utoaji unaofanywa moja kwa moja na mtu binafsi ndio umekuwa njia muhimu sana ya watu wenye ukwasi kuhisani jamii lakini taasisi na utoaji wenye weledi hivi sasa unaanza kuonekana. Ongezeko hili la moyo wa uhisani linatokana na muda ambao wana harakati wa hisani wanautoa kwa ajili ya kuhamasisha utoaji kwenye mitandao ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali licha ya kwamba moyo wa utoaji siku hizi umeongezeka miongoni mwa wananchi. Hivi sasa mashirika yanafurahia uhusiano na uwiano uliopo kati ya utoaji na biashara zao.

Hisani za mashirika huchukua njia mbalimbali. Utafiti umeonesha kuwa fedha ndiyo njia kuu iliyofumika kuhisani wahitaji, lakini pia wapo waliotoa muda wao, wengine ujuzi wao ili kusaidia utekelezaji wa jambo fulani katika jamii. Uhisani wa nyenzo za kazi, uwekezaji katika jamii na kutoa nafasi kwa mitandao ya asasi na vikundi ni njia mojawapo zinazotumika katika kuhisani japo sio maarufu sana. Utafiti umegundua kuwa sekta za elimu na afya ndizo zilizovutia uhisani zaidi. Sekta hizi zinachukuliwa kama sekta zinazohitaji uhisani zaidi kutokana na umuhimu wake katika maendeleo ya wananchi wa Afrika. Utafiti

umebaini pia kuwa wahisani wengi hawapendelei sana kuhisani shughuli za sekta hizi na badala yake wanapenda kuwezesha miundo mbinu yake inayosababisha upatikanaji wa huduma duni hata kama wahisani wanakubali kuwa elimu na fya ni maeneo muhimu yanayohitaji kuhisaniwa zaidi.

Uhisani na utoaji kwa ajili ya majanga (kama vifo) na sherehe (kama harusi) zilionesha kupewa umuhimu mkubwa na wahisani ikilinganishwa na shughuli nyingine za maendeleo za muda mrefu kama afya, elimu na kadhalika.

Utafiti umeonesha ongezeko la vijana wanaojihusisha zaidi katika vikundi vya utoaji vinavyohusishwa na vijana wenye ushawishi katika jamii wanaoshiriki katika utoaji. Mwamko huu wa utoaji miongoni mwa vijana umeongeza hamasa na kufanya suala la utoaji uwe fasheni miongoni mwa vijana ambao ndio idadi kubwa ya wananchi katika nchi hii.

Kuongezeka kwa mashindano ya kuwania rasilimali miongoni mwa asasi za kiraia nchini na kati ya asasi za ndani na zile za kimataifa kunaongeza sababu ya kutafuta rasilimali zaidi. Ni dhahiri kuwa, kuna haja ya kuja na mbinu mpya ili kuongeza ari na moyo wa utoaji miongoni mwa wananchi. Utoaji na uhisani katika jamii utatokana na uwajibikaji na uwepo wa taarifa miongoni mwa AZAKI na kati ya asasi za hapa nchini na zile za kimataifa kujenga hoja kuhusu umuhimu wa kuongeza upatikanaji wa rasilimali. Uhisani wa ndani unahitaji nidhamu ya uwajibikaji na kubadilishana taarifa miongoni mwa AZAKI ili kujenga uaminifu na nia ya dhati miongoni mwa wahisani wa ndani.

Hali ya Uhisani Tanzania 2018

06

HITIMISHO Utafiti ulihitimisha mambo yafuatayo kutokana na matokeo yaliyojiri:

1. Kwamba kuna utamaduni wa utoaji uliojengeka miongoni mwa watanzania unaochochewa na dhamira ya kuimarisha ustawi na maendeleo ya wananchi licha ya wajibu walio nao wale wenye nacho kwa wengine. Ukiachilia mbali watetezi wa suala la uhisani, uhisani mara nyingi hauko kwenye mpangilio mahsusi. Hali hii inafaya upatikanaji wa taarifa na takwimu kuhusu uhisani, wigo wa uhisani, uwajibikaji muundo na mpangilio wa uhisani kuwa vigumu kueleweka.

2. Licha ya ukweli kwamba idadi ya Watanzania wanaotoa hisani kuongezeka, kiasi halisi cha fedha kilichotolewa kwa wananchi wahitaji wakiwamo watu binafsi ni cha chini kuliko kile kinachotolewa na watetezi na wanaharakati wa uhisani. Vile vile, kiasi cha rasilimali zilizopatikana kutoka nje ya taasisi kinazidi sana kile kilichopatikana ndani ya taasisi hiyo. Hali hii inafanya utoaji unaofanywa nchini kuonekana bado mdogo na kutofikiwa inavyotarajiwa. Changamoto zilizopo ni pamoja na uchache wa taarifa sahihi, uaminifu, ukosefu wa motisha na kukosekana kwa uungwaji mkono.

3. Uratibu unaoongoza tasnia ya uhisani umemegeka na hauko wazi kwa wadau. Hii inadhihirishwa na utitiri wa sheria

ngumu na zisizotekelezeka kwa urahisi na wadau wa uhisani. Pia hakuna motisha ya kutosha kwa taasisi zinazojihusisha na uhisani licha ya ukweli pia kuwa suala zima la uhisani kuwa bado gumu kueleweka na kukubaliwa ipasavyo na wadau.

4. Mifumo na uwezo wa uongozi wa pamoja katika kuratibu, kuhusisha, chukua hatua za pamoja kwa kushirikishana taarifa kuhusu uhisani bado haujaendelezwa katika tasnia hii. Imebainika kuwa karibu asilimia 50 ya taasisi zinazojihusisha na uhisani zilizoshiriki katika utafiti huu hazikuwa wanachama wa mtandao wowote ule wa uhisani.

5. Kupungua kwa nafasi ya AZAKI na ushindani baina yao katika kuwania rasilimali zinazozidi kupungua kumeongeza hamasa, ari na hamu miongoni mwa taasisi zinazojipambanua na uhisani kama njia ya kuimarisha utoaji. Hata hivyo, jitihada hizi zinarudishwa nyuma na ukosefu wa uwezo, sheria madhubuti na kanuni zisizojenga moyo wa uhisani na kukosa uaminifu miongoni mwa taasisi. Kuna haja ya kuendelea kuzijengea uwezo taasisi ili kuziwezesha zithamini uhisani wao na kutumia rasilimali chache walizo nazo.

Hali ya Uhisani Tanzania 2018

07

MAPENDEKEZO Kwa matokeo ya utafiti huu, mapendekezo yafuatayo yalitolewa yakizilenga Foundation for Civil Society, Tanzania Philanthropy Forum na wadau wa uhisani kufanya kila wawezalo ili kuendeleza sekta hii ya uhisani:

1. Kufanya utetezi ili kutoa kipaumbele katika kuzifanyia mabadiliko sheria, sera na muundo wa taasisi zinazosimamia na kuratibu shughuli zinazofanywa na asasi za uhisani hapa nchini. Jambo hili linalenga katika kuunganisha tafsiri mbalimbali na uelewa kuhusu uhisani na wahisani katika muktadha wa Tanzania.

2. Kuishirikisha serikali ili iwezeshe uwepo wa kipengele cha sheria ya kodi kinachotoa nafuu katika kuomba msamaha wa kodi au punguzo kuwalinda watu binafsi, makampuni na biashara zenye mipango na nia ya kutekeleza mipango mkakati ya muda mrefu ya uhisani.

3. Kuwekeza katika kuzijengea uwezo AZAKI ili ziweze kushiriki kikamilifu na kuanzisha mahusiano ya muda mrefu

baina yake na sekta binafsi na serikali kwa nia ya kugawanya rasilimali na kuchangia shughuli za pamoja.

4. Kutoa mwongozo na kuinua kiwango cha ufahamu miongoni mwa wananchi kuhusu dhana na shughuli zinazohusu uhisani zinazofanyika hapa nchini. Uwekaji wa kumbukumbu za matukio na taarifa za mafanikio kuhusu uhisani una mchango mkubwa katika kujenga na kuongeza hamasa na majadiliano kuhusu uhisani.

5. Kuwatambua vinara katika kuikuza tasnia ya uhisani na kushirikiana na vyombo vya habari ili kuikuza na kuiweka dhana ya uhisani kama njia mbadala ya kukabiliana na upungufu wa rasilimali fedha kutoka kwa wafadhili wa kimataifa katika siku za usoni.

P.O Box 7192, 7 Madai Crescent,

Ada Estate, Plot No. 154

T: +255 22 2926084 - 9 • F: +255 22 2760062

W: www.thefoundation.or.tz