333
15 MEI, 2013 1 BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Sita - Tarehe 15 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Randama za Makadirio ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. JOSEPHINE J. NGENZABUKE (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

  • Upload
    others

  • View
    11

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

1

BUNGE LA TANZANIA_____________

MAJADILIANO YA BUNGE_______________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Ishirini na Sita - Tarehe 15 Mei, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI:

Randama za Makadirio ya Wizara ya Uchukuzi kwaMwaka wa Fedha 2013/2014.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biasharakwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

MHE. JOSEPHINE J. NGENZABUKE (K.n.y MWENYEKITIWA KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA):

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwandana Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara yaViwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

2

MHE. JOSHUA S. NASSARI – MSEMAJI MKUU WA KAMBIYA UPINZANI WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA:

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwaWizara ya Viwanda na Biashara Kuhusu Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Swali letu la kwanza leo ni Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi wa Umma, litaulizwa na MheshimiwaPhilipa Mturano.

Na. 209

Taasisi za NIDA na RITA Kuunganishwa

MHE. PHILIPA G. MTURANO aliuliza:-

Kuna ushabihiano mkubwa kati ya kazi zinazofanywana Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakalawa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

Je, kwa nini Serikali isiziunganishe Taasisi hizi ili mojaiwe Idara chini ya nyingine ili kupunguza gharama kubwa zauendeshaji?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Ummana kwa ridhaa yako naomba kujibu swali la MheshimiwaPhilipa G. Mturano, Mbunge wa Viti Maalum, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka ya Vitambulishovya Taifa NIDA ni Taasisi ya Muungano iliyoanzishwa kwamujibu wa Ibara ya 36(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganoya Tanzania kupitia amri ya Rais iliyotolewa katika tangazo

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

3

la Serikali Namba 112 la tarehe 30 Julai, 2008. NIDAimeanzishwa kwa lengo la kuweka mfumo na kuwezeshautoaji wa vitambulisho vya Taifa katika Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa usajili, Ufilisi naUdhamini yaani RITA ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria yaWakala wa Serikali Sura ya 245 kwa lengo la kushughulikiamasuala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini kwa upande waTanzania Bara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Upande wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar masuala ya Usajili, Ufilisi na Udhaminiyanashughulikiwa na vyombo viwili kwa mujibu wa Sheria zaZanzibar. Kuna Ofisi ya Mrajisi wa Vizazi na Vifo ambayoinashughulikia usajili wa vizazi na vifo na Ofisi ya Mrajisi Mkuuambayo inashughulikia masuala ya Ufilisi na Udhamini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa vyombo hivivimeundwa kwa malengo tofauti haiwezekani kuviunganishakutokana na Sheria ilizovianzisha. Hata hivyo Serikaliimeupokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na itaufanyiakazi ili kuona namna bora ya kuviwezesha vyombo hivikutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

MHE. PHILIPA G. MTURANO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina swalimoja tu la nyongeza.

Kwa kuwa moja ya sifa ya kupata vitambulisho vyaTaifa ni kuwa na cheti cha kuzaliwa na kwa kuwa wananchiwengi hasa vijijini hawana vyeti vya kuzaliwa. Je, Serikaliinampango gani wa kuhakikisha kwamba wananchi hawawanapata vyeti vya kuzaliwa?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaPhilipa Mturano kama ifuatavyo.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

4

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kamaambavyo tulieleza katika hotuba yetu ya Bajeti ya tarehe 3,May mwaka huu RITA imeshaanza kampeni ya usajili kupitiampango wa Usajili wa Watoto chini ya miaka 5 lakini piatunayo kampeni ya usajili wa watoto wenye miaka 6 mpaka18 katika shule mbalimbali.

Lakini pia tunajitahidi kufanya kampeni zingine kwawatu wazima ambao hawana vyeti vya kuzaliwa lakini si hiitu tunataka tubadilishe sheria yetu ya usajili wa vizazi na vifoili ikiwezekana tuweke masharti maalum mtu asipate ajirakabla hajaonyesha cheti za kuzaliwa, mtu asipate leseni yabiashara kabla hajaonyesha cheti cha kuzaliwa pamoja naleseni nyingine mbalimbali na tunaamini kwa kufanya hiviitatusaidia kuongeza viwango vya usajili, ahsante sana.

MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti,asante. Kwa kuwa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifaimekuwa ikienda pole pole sana na hadi sasa tunavyoongeaWatanzania wengi hasa walioko Mikoani hawajaanza kupatakabisa vitambulisho. Nini mpango wa Serikali kuhakikisha nawale walioko Mikoani wanaanza kupata harakaiwezekanavyo?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Utumishinapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Njwayokama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, NIDA ni chombo kipya nawote tunafahamu masuala haya ya utambuzi siyo masualaya kuyafanyia haraka mimi nimwombe tu MheshimiwaMbunge awe na subira. Tumeanza sasa hivi kutoavitambulisho kwa Watumishi wa Taasisi za Serikali pamoja navyombo vingine na tayari usajili ulikwisha anza katika watuwengine mbalimbali katika Mikoa mbalimbali.

Suala hil i si dogo inabidi pia NIDA wajitahidikuwasiliana na mifumo mingine ya usajili wa vizazi lakini piaya vifo. Kuna wengine wanaweza wakawa wamefariki lakini

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

5

ukajikuta umetoa kitambulisho cha Taifa kwa hiyo ni masualaambayo lazima kuwa waangalifu lakini tunajitahidi natutaongeza kasi. (Makofi)

Na. 210

Suala la Watoto Wanaozagaa Mitaani/Mijini Wakiombaomba

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE aliuliza:-

Idadi ya watoto wanaozagaa mitaani na mijiniwakiombaomba imezidi kuongezeka.

(a) Je, Serikali imefanya utafiti wowote kujua idadiya watoto wanaoishi katika mazingira hayo?

(b) Je, kuna mpango gani mahsusi uliokusudiwana Serikali wa kuwasaidia watoto hao ili waondokane nashughuli hiyo ya kuombaomba?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afyana Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la MheshimiwaMchungaji Luckson N. Mwanjale, Mbeya vijijini, lenye sehemu(a) na (b) kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kwakushirikiana na Shirika la kuhudumia watoto Duniani yaaniUNICEF na wadau wa masuala ya watoto ilifanya utafiti katikajiji la Dar es Salaam mwezi Juni 2012 ili kubaini kuwa ukubwawa tatizo la watoto wanaoishi mitaani. Utafiti huu ulilengaDar es Salaam zaidi kutokana na ukweli kwamba wengi wawatoto hawa wanaishi katika jiji hili ukilinganisha na Mikoamingine. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa jumla yawatoto 5580 wanaishi na kufanya kazi mitaani. Wavulanawalikuwa 4520 ambao ni sawa na 81% na wasichanawalikuwa 1060 sawa na 19% ya watoto wote.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

6

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha utafiti huu ulibainikwamba watoto hao wanatoka katika Mikoa karibu yotenchini na hata nje ya nchi. Vile vile ilibainika kwamba zikosababu mbalimbali zinazochangia watoto hawa kukimbiafamilia zao na kuingia mitaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika zoezi la utafiti huojumla ya watoto 185 waliweza kurudishwa na kuunganishwana familia zao toka Dar es salaam kwenda Mikoa mbalimbali.Kati ya idadi hiyo watoto 128 ni wavulana na 57 ni wasichana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha ulinzi nausalama wa watoto wote wanaoishi katika mazingira hatarishinchini Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, alizinduaMpango Kazi wa Taifa awamu ya pili yaani 2013/2017 wahuduma na matunzo kwa watoto mwezi Frebuari, 2013.Mpango kazi huu wa taifa umeainisha hatua mbalimbalizitakazochukuliwa na jamii, wadau na Serikali kwa upandemmoja ili kukabiliana na changamoto zinazohusu watotowalio katika mazingira hatarishi.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Waziri au yaSerikali. Lakini kwa kuwa karibu nchi zote duniani zinakuwana ombaomba, ukienda Marekani, ukienda Ulaya hapo,ukienda Asia, ombaomba wako wengi kila mahali.

Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watuwazima lakini kitu kinachonishangaza ni hawa watoto vijanahawa wanakuwa omba omba mitaani na je, haki yao yakupata elimu hawa watoto iko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili. Je, Wizaraitakuwa tayari kutenga pesa za kutosha au Bajeti kubwa kwaajili ya kuhakikisha kwamba Ustawi wa Jamii unashughulikiawatoto hawa ambao wanazagaa mitaani?

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

7

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii naomba kujibu maswali mawili yaMheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haki ya kupata elimu kwawatoto wote ni haki ya msingi na ni jukumu la kwetu sisi woteyaani wazazi, jamii, halmashauri na serikali kuu kwa pamoja.

Ni matumaini yangu kwamba Wizara kwa upandemmoja inaainisha miongozo, inatoa taratibu inawezeshawataalam wetu kufahamu na kuweza kutekeleza kazi zaoza kuweza kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingirahatarishi na kuweza kuwapatia huduma kwa misingi nataratibu zilizoainishwa. Lakini vile vile Halmashauri zina jukumukubwa baada ya kufanya zoezi la kuwatambua watotowanaoishi katika mazingira hatarishi zoezi ambalo limefanyikatoka mwaka 2005 hadi 2012 ambalo watoto zaidi ya 850,000wameweza kutambuliwa katika mazingira hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuzichambuaasasi zinazoshiriki katika kuwasaidia watoto bado jukumu lakuelimisha watoto na kupata haki zao za msingi limo katikakila Halmashauri ambazo sisi ni wajumbe katika mabarazahayo ya Halmashauri. Ni wajibu wetu katika kila Halmashaurikuhakikisha kwamba inawatambua watoto hao na inaandaataratibu za kimsingi kuweza kupata haki zao za msingi hasaelimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Wizara kutengaBajeti, Bajeti zimetengwa na nawashukuru WaheshimiwaWabunge kwa kupitisha Bajeti yetu ya Wizara ya Afya naUstawi wa Jamii na naamini katika ustawi huo wa jamii kunamaeneo kadhaa ambayo Wizara imetenga fedha katikamatumizi yakeikiwemo kutoa uwezeshaji wa kufundishawataalam ambao wakifika kwenye Halmashauri zetuwataweza kutoa jukumu la kuweza kuhakikisha watoto hawawanapata huduma za msingi lakini vile vile kuzitambua asasizinazotoa huduma hizo kwa watoto na kushirikiana nazokatika kutoa hizo huduma lakini vile vile kuwezesha

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

8

Halmashauri zetu kuhakikisha kwamba wanatoa hudumastahili kwa watoto. (Makofi)

MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya msingi ya MheshimiwaWaziri amesema watoto waliopo mitaani wengine wanatokanje ya nchi. Je hawa waliotoka nje ya nchi wameingiajenchini na kuweza kuwa ombaomba katika nchi yetu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri jibu kwa kifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo.

Watoto wanaweza kutoka nje ya nchi haina maanakwamba ametoka nje ya nchi akaingia hiyo ni upandemmoja lakini upande wa pili tukubali kwamba tuna kambiza Wakimbizi na tuna watu kutoka nje ambao wako nchinina watoto wanaweza kutoroka katika maeneo hayowakaingia katika miji yetu. Kwa hiyo, utaratibu wa mtotokuingia ambaye ametoka nje ya nchi anaweza kuingia kwanjia mbalimbali ambazo zinamruhusu mtoto kuingia.

MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuwa suala la watoto hawa ombaomba asilimiakubwa hasa Dar es Salaam utakuta wazazi wao wakopembeni. Kwa hiyo, wao ndiyo wanaosababisha watotowao wanasakizia kuja kuomba kule barabarani. Je, Serikaliina mpango gani kuchukulia hatua hawa wazazi kabla yahawa watoto ili kuepusha watoto hawa kuomba?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii, naomba kujibu swali la MheshimiwaMbunge, kama ifuatavyo.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

9

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoainisha katikajibu la msingi kwamba katika maeneo ya kushughulikiawatoto wa mitaani na watoto ambao wanashiriki katika zoezila kufanya ombaomba na hasa wale wazazi ambaowanakuwepo na watoto wao pembeni ni suala ambaloHalmashauri zetu zinatakiwa kulishughulikia na tuna toa agizokwa Halmashauri kuweza kuwashughulikia wale wazaziambao wanajimudu lakini wanatumia watoto kama sehemuya mtaji wa kuweza kujinufaisha.

MWENYEKITI: Tunaendelea tunaingia sasa Wizara hiyohiyo, Mheshimiwa Anne Kilango.

Na. 211

Afya Bora kwa Mtoto wa Tanzania

MHE. ANNE K. MALLECELA aliuliza:-

Jukumu la kuhakikisha afya bora ya mtoto ni la wazazi,lakini Serikali nayo inao wajibu wa kuweka mazingira mazuriya kuweza kupata watoto wenye afya bora na hivyo kupataTaifa bora lenye nguvu.

Je, Serikali inajihusisha vipi kikamilifu kufanyamaandalizi ya mazingira bora ya kuhakikisha kwamba Taifalinapata watoto wenye afya bora na hivyo kupata Taifa lakizazi kizuri zaidi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Niaba ya Waziri wa Afyana Ustawi wa Jamii naomba kujibu swali la Mheshimiwa AnneK. Malecela, kutoka Same Mashariki, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kuu la Sera ya afya nikuboresha afya na Ustawi wa Jamii kwa Watanzania wotekwa kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuwa na jamii ya watu

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

10

wenye afya bora wanaoweza kujipatia maendeleo yaowenyewe na Taifa kwa ujumla. Sera hii pia imeweka msisitizona kipaumbele kwa makundi maalum ya jamii wakiwemowanawake na watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha kwambaTaifa linakuwa na watoto wenye Afya bora Serikaliinatekeleza mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkakatiwa tatu wa Sekta ya Afya yaani Health Sector Strategic PlanIII na mkakati wa Taifa wa lishe. Mikakati hii inalenga katikakuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma za kinga, tiba,lishe zenye ubora, gharama nafuu, endelevu na zenyekuzingatia usawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inahakikisha kuwa,watoto wanapatiwa chanjo ya kudhibiti magonjwayanayozuilika kwa chanjo kama kifua kikuu, polio, tetanus,nimonia, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo na kuharisha.Aidha watoto wamekuwa wakipatiwa vyandarua il ikuwakinga na mbu wanaoeneza malaria na pia kuwapatiadawa za minyoo na vitamin A kila baada ya miezi sita.

Vile vile, mtoto anapozaliwa anapatiwa joto, dawaya macho, anaanzishiwa kunyonya ya mama ambayo nimuhimu sana katika ukuaji na afya ya mtoto kimwili, kiakili nakisaikolijia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Wizara imewekamazingira mazuri ya kutoa huduma ya ufuatiliaji na ukuaji wamaendeleo ya mtoto katika kliniki zote za afya ya uzazi namtoto nchini. Aidha Taasisi ya chakula na lishe yaani TFNCinatoa ushauri wa lishe kwa kuzingatia utumiaji wa maziwaya mama pekee hadi umri wa miezi sita na baadae kuanzavyakula vya nyongeza, matumizi ya madini joto na nyongezaya matone ya vitamin A. Watoa huduma za afya nchiniwameendelea kujengewa uwezo ili kuboresha huduma zaafya kwa watoto. Dawa muhimu hotolewa bure kwa watotochini ya umri wa miaka mitano aidha elimu ya afya kwa jamiina mazingira zimeendelea kutolewa kwa kutumia njiambalimbali, ili kuwa na watoto wenye afya bora.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

11

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata majibu ya Serikali lakini nina maswali mawiliya nyongeza. Tanzania tuna watoto wengi sana ambaohawapati malezi ya uhakika na mtoto ni mali ya Jamhuri.

Kwa kuwa wakati mtoto yule anakuwa, ubongo wakeunakuwa na maswali mengi sana, ambayo maswali hayayasipopata majibu ya uhakika wakati anapokuwa. Mtotohuyo anaweza akaishia kuwa binadamu asiye na maadili auakaishia hata kuwa jambazi kwa sababu ya kutokupatamalezi mazuri aliyopata majibu wakati ubongo wake unatakamajibu.

Je, Serikali inasaidiaje hawa watoto wadogo ambaohawapati malezi ya uhakika na mwisho tunaishia kupata Taifaambalo lina watoto wengi ambao hawana maadili na wengiwanaishia kuwa majambazi.

Pili, kwa kuwa takwimu za uhakika zinaonyeshakwamba, takribani asilimia arobaini na mbili (42%) ya Watotowa Tanzania wanapata utapiamlo na utapiamlounawaathiri katika kukua kimwili na kiakili pia.

Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wakinadharia wa kurejesha wa akina mama Afya ambao miminiliwaona miaka ya 60 nilipokuwa ninakuwa na nikaonamichango yao ambayo ilinisaidia hata mimi kufika hapanilipofika? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA AFYA Na USTAWI WA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii, naomba kujibu kama ifuatavyo:-

Ni kweli kwamba malezi ya mtoto katika umri mdogoyanachangia kwa kiwango kikubwa sana namna mtoto huyoatakavyokuwa na atakavyoweza kumudu maisha yake hapobaadaye. Suala la malezi kama Serikali tumeainisha katikasehemu mbili kubwa.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

12

Kwanza, baada ya mama kujifungua na kupatahuduma zote stahili zinazotolewa, lakini pia mama huyoanapata ruhusa ya uzazi, likizo siku 84 na baada ya likizo yasiku 84, anapata muda saa mbili karibu kila siku ili aweze kutoafursa ya kuweza kunyonyesha na kuhudumia mtoto wake.Baada ya pale, tumeanza na sera ya kuanzisha elimu ya awalikwa watoto kwenye shule zetu.

Katika tafsiri hiyo maana yake, mtoto anakuwaanaingia katika mazingira ya shule na kupata mafundishona baadhi majibu ya maswali ambayo anakuwa anajiulizamtoto huyu, anapokuwa maeneo ya shule na majibu hayoanapatiwa na walimu ambao wanawasaidia watoto katikamakuzi.

Vilevile, ni kweli utapiamlo ni moja katika changamotozinazowakabili watoto wetu. Hata hivyo, umuhimu wakuwepo akina mama lishe kama Wizara ya Afya na Ustawiwa Jamii tumeanza kuweza kuona namna ambavyo vituovyetu vya Afya vinatoa huduma na wataalam waliopokatika kliniki wanatoa huduma kwa mama juu ya lishe yakena mtoto. Pia, anapata Vitamins na Chanjo.

Hata hivyo, tuna mpango tunaoungalia hivi sasakama tafiti juu ya uwepo wa watoa huduma vijijini ambaowatakuwa na uwezo huo. Hivi sasa mpango huo umeanzamaeneo ya Ifakara na vijana wenye kiwango cha elimu yakidato cha nne, wanapata mafundisho ya miezi tisa nabaada ya mafunzo wanarudi katika maeneo ya Kaya zaona kuanza kuwahudumia wananchi. Moja katika mamboambayo wanaweza kuhudumia ni pamoja na kutoa elimuya lishe.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa kuwa, takwimu za Mheshimiwa Anne K.Malecela, za asilimia arobaini na mbili (42%) za watotowalioko kwenye tatizo la utapiamulo ni za mwishoni mwamiaka ya sabini, (1970) na Ubongo wa mtoto unakuwa kwaasilimia themanini (80%)akiwa na mwaka 0-8. Mentalstagnation ya miaka 1970 imesababisha sana wataalam

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

13

wetu wa sasa kukalili zaidi, ndiyo maana tunapata madaktariambao baada ya kufanya operation ya mguu, wanafanyaya kichwa, wahandisi wanafanya maamuzi magumuambayo yanasababisha magorofa yanaanguka na mamboya namna hiyo.

Je, takwimu za sasa za mental stagnation ya kizazi yacha sasa ukilinganisha cha miaka ya sabini ikoje?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu waziri unajibu vizurina kuwa makini lakini jaribu kujibu kwa ufupi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya naUstawi wa Jamii, naomba kujibu swali kama ifuatavyo:-

Sina hakika juu ya tafsiri ya mental stagnationsambayo anaielezea na hasa akihusisha juu ya mambokadhaa ambayo yanatokea na moja wapo likiwa ni jangala ghorofa kuanguka. Nachoweza kusema ni kwamba,ukuwaji wa mtoto na Afya njema unachangia sana katikakumwezesha kuwa na akili na uwezo mkubwa wa kutambuamazingira yake na kuweza kumudu maisha yake.

Vilevile kuwa na uwezo wa kusoma na kuwa nauwezo wa kuweza kutumia yale aliyosoma vizuri kwamaendeleo ya maisha yake. Hicho ndicho ambacho nawezakusema kwa sasa, lakini juu ya takwimu ya kwamba sasamental stagnation imepungua kwa kiasi gani auimeongezeka kwa kiasi gani nafikiri hii inahitaji utafiti zaidi.

MHE. EUGIN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza.

Kwa kuwa, wajibu wa kwanza wa kulinda nakuhakikisha kwamba mtoto anakuwa na afya njema ni wajibuwa mzazi au wazazi wote wawili. Kwa kuwa wakowanawake wenye afya nzuri lakini kutwa hutembea nawatoto wachanga barabarani wakuwa wanaomba omba

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

14

na kwa kuwa jambo hili linaathiri sana afya za watoto hao.Je, Serikali inawaambia nini wakina mama hawa ambaowana afya nzuri, waaache kutembea na watoto kama ombaomba?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu kama ifuatavyo:-

Nilishaeleza kwamba, katika kuhudumia watotomaeneo yamegawanyika na kila mmoja anapata eneo lakela kuweza kushughulikia. Nimeelezea kwamba, Halmashaurindiyo Serikali iliyopo kwenye maeneo ambayo watu tunaishina sisi wenyewe kama viongozi kwenye kila Halmashauri,tunatakiwa kutambua watoto wanaoishi katika mazingirahatarishi, wakiwemo wakina mama ambao wanatembea nawatoto mtaani wakiwa wanaomba.

Hata hivyo, kila Halmashauri inabidi itafute namnaabavyo inaweza kuwasaidia akina mama ambao hawananamna ya kujiwezesha kiuchumi waweze kujihudumia waona watoto na hivyo kuachana na tabia ya kuombaomba.

Na. 212

Kuboresha Huduma za TBC Nchini

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR aliuliza:-

TBC Taifa ni chombo chenye ubora katika kutoahabari hapa nchini.

(a) Je, ni Mikoa mingapi inakosa matangazo ya TBC hadisasa?

(b) Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha kuwa TBCinasikika nchi nzima?

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

15

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo napenda kujibu swalila Mheshimiwa Amina Abdullah Amour, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Mikoa ambayo haipatihuduma ya radio ni mikoa tisa (9) ambayo ni kaskazini Unguja,Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Kaskazini Pemba, KusiniPemba, Mtwara, Geita, Njombe na Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mikoa ambayo haipatihuduma ya Televesheni ni kumi na mbili (12) ambayo niKaskazini Pemba, Kusini Pemba, Geita, Iringa, Katavi,Manyara, Mtwara, Njombe, Ruvuma, Shinyanga na Simiyu.Upatikanaji wa huduma ya Televisheni katika mikoa hiyo ukokwenye mpango wa utekelezaji wa huduma ya Televishenikupitia mradi wa Dijitali.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua tatizo lausikuvu wa Radio na uonekanaji wa Televisheni kwa baadhiya maeneo ya nchi. Mpango wa Serikali ni kuhakikishamatangazo ya TBC yanamfikia kila Mtanzania popote aliponchini. Katika kutekeleza mpango huo, Serikali inaendeleana mpango wake wa kufunga mitambo ya FM Radio katikamiji mikuu na Mikoa yote nchini kwa kadri fedhazinavyopatikana na baada ya hapo katika miji yote yaWilaya. Hadi sasa TBC imefunga mitambo ya Radio ambayomatangazo yake yanasikika katika mikoa ishirini na moja (21)na matangazo ya Televisheni ya TBC yanapatikana katikamikoa kumi na nane (18). (Makofi)

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri yenye kuleta matumaini. Nitakuwana maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, Bajeti yako nindogo. Je, mipango hii itatekeleza?

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

16

Pili, Kwa kuwa TBC inaendeshwa kibiashara, kwa ninihizo pesa zinazopatikana zisitekeleze mipango hii?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali lanyongeza kama ifuatavyo:-

Ni kweli kwamba, Bajeti yetu ya Wizara ya Habaribado ni ndogo na tunaendelea kufanya mazungumzo nakamati ya Bajeti kuona kwamba tunaweza kuongeza fedha.Hata hivyo, bado kazi hiyo mnayo ninyi wenyewe tarehe 20,siku ambayo tutawasilisha Bajeti hii na kuipitisha hapa ilimipango yetu hiyo iweze kutekelezeka.

Pili, TBC tayari inayo mpango mkakati, managementna Bodi inaendelea kujipanga na kuona kwamba fedhazinazopatikana zinaelekezwa katika kutekeleza miradimbalimbali katika shirika hili la TBC.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwa kuwa, usikivu wa Shirika la Utangazaji TBC nihafifu sana katika Wilaya ya Ngorongoro, hivyo wananchiwa Ngorongoro kulazimika kusikiliza shirika la utangazaji laKBC Kenya. Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwambaeneo hilo la Tanzania usikivu wa Shirika lake la Utangazajiunakuwa murua?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali lanyongeza kama ifuatavyo:-

Ni kweli tunatambua kwamba, maeneo mengi hataWabunge wengi hapa watasimama kuona kwamba lipotatizo la usikivu wa radio katika maeneo mbalimbali. Lengola Serikali ni kuhakikisha matangazo haya yanafika mahalipopote. Naomba sana tarehe 20 mtupitishie Bajeti yetu, ilituje na mikakati ambayo tunaweza tukatekeleza na kuondoatatizo hili katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

17

MHE. MCH. PETER MSINGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwa kuwa, Shirika la TBC wakati Mkurugenziwake alikuwa ni Tido Muhando lilikuwa ni kama ndegeinayopaa na lilikuwa linatangaza matangazo yake kwaufasaha bila lawama. Na kwa kuwa sasa hivi ni kama Ndegeambayo iko grounded na limekuwa likifanya shughuli zakekwa upendeleo hasa kukibeba Chama cha Mapinduzi. Nilini sasa Shirika hili litafanya kazi vizuri ili Watanzania warudisheimani kama enzi za Tido Muhando?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali lanyongeza kama ifuatavyo:-

Nataka niseme tu kwamba sisi kama Serikalitungependa kuona Shirika la TBC linafanya kazi vizuri katikaviwango vizuri na tayari tumewataka management na bodiya TBC kuja na mpango mkakati ili shirika hili liweze kufanyakazi kwa ufanisi. Nikuhakikishie tu kwamba, Serikali itaendeleakusimamia shirika hili na kuona kwamba linafanya kazi vizuri.Hata hivyo, shirika hili linafanya kazi bila upendeleo wowotewa chama chochote cha siasa.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Bali na changamoto za TBC kushindwakutanua wigo na changamoto zinazowakabili za vifaa, lakinipia kumekuwa na tatizo kubwa la wafanyakazi wa TBCkupata maslahi duni. Hata hawa ambao unawaona Dodomawanashindwa kuongea tu, lakini maslahi yao ni duni sana,na hiyo inatokana na Serikali kutotenga fedha za kutosha nawanafanya kazi kwa sababu ni wazalendo wa Taifa lao. Je,ni lini Serikali mtaboresha mishahara ya wafanyakazi wa TBC?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu kamaifuatavyo:- TBC inawafanyakazi ambao ni sawasawa nawafanyakazi wengine katika Serikali. Kwa hiyo, suala lamaslahi madogo ni la watanzania wote ambao wanafanyakazi Serikalini. Tutaliangalia kadri ambavyo maslahiyanaboreshwa kwa wafanyakazi wengine, hili tunalipokea

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

18

na mimi naamini kabisa itakapofika wakati wa kusoma bajetiya mishahara, tutakuwa tunaelewa kwamba TBC mishaharayao imeongezeka kwa kiasi gani. (Makofi)

Na. 213

Kujenga Barabara za Mkoa kwa Lami

MHE. MTUTURA A. MTUTURA aliuliza:-

Je, Serikali itaanza lini kujenga barabara za mikoazitokazo Tunduru – Wenje, Nalasi – Njenga na Azimio –Makande kupitia Lukumbule kwa lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa MtuturaA. Mtutura Mbunge wa Tunduru Kusini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara zilizotajwa naMheshimiwa Mbunge yaani; Tunduru – Wenje (Chamba)yenye urefu wa kilometa 85.57; Azimio – Lukumbule hadiMakande yenye urefu wa kilometa 65.69 na Nalasi – Njengayenye urefu wa kilometa 20; zote ni barabara za mkoa nazinahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara(TANROADS).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa kipaumbele chaSerikali ni kukamilisha ujenzi wa barabara kuu kwa kiwangocha lami na kuendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajiliya matengenezo ya barabara tajwa ili ziendelee kupitikamajira yote ya mwaka katika kiwango cha changarawe.

MHE. MTUTURA A. MTUTURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili yanyongeza. Barabara ambazo zimetajwa za Tunduru – Wenjena Azimio –Makande, licha ya kwamba ni barabara za Mkoavilevile ni barabara za kuisalama kwani zinaunganishwa nanchi jirani ya Msumbiji. Hivi punde tumeona barabara kadhaa

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

19

ambazo zinaunganisha nchi yetu na nchi nyingine zimekuwazikiwekewa lami. Je, Serikali haioni umuhimu kwamba,barabara hizi zina sifa sawasawa na zile nyingine ambazozinawekewa lami nazo ziwekwe lami?

Pili, katika Jibu la msingi, Mheshimiwa Naibu Waziriamesema kwamba sasa hivi kipaumbele ni barabara kuukwa maana ya trunk road, ndizo zinazowekewa lami. Je,Naibu Waziri utasema nini juu ya barabara za vijiji na zaHalmashauri ambazo zinawekewa lami katika baadhi yaMikoa? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri swali fupi nawewe jibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa MtuturaA. Mtutura, kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa, ni kweli barabara anazozisemazinaweza zikawa za kiusalama, hata hivyo kutokana nampango ambao tumeuweka, barabara ziko nyingi zaidi yakilometa 86,000 kwa nchi nzima na barabara za Halmashauriziko kilomita 52,000. Sasa tunasema kwamba ngoja tumalizekwanza hizi barabara kuu, pamoja na umuhimu wakekwamba zingine ni za usalama, zingine zinaunganisha Mikoa,tutakapomaliza hiyo network ya barabara kuu, tutaanzakuangalia barabara za Mikoa na vilevile tutazi-rank kulinganana umuhimu wa barabara husika, ndiyo tutaanza kuzijengakwa kiwango cha lami.

Kuhusu barabara za vijiji, au za vijijini ambazo unasemakwamba zingine zimewekewa lami, ni kweli inawezekanakuna baadhi ya barabara ambazo zinahudumiwa naHalmashauri. Kwa mfano tumesema kwenye Miji, MakaoMakuu ya Wilaya, ziko barabara angalau waanze kujengakilomita mbili mbili kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara.Kwa hiyo, kuna baadhi ya barabara kwa mazingira fulani,tumeanza kuzishughulikia kwa utaratibu wa namna hiyo.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

20

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kuniona. Kwa kuwa tatizo la Tunduru Kusinilinalingana kabisa na la Korogwe Vijijini, haswa kwenyebarabara ya kutoka Old Korogwe, Kwashemshi, Bumbuli nakutokea Soni, ambayo ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Raisya mwaka 2010. Je, barabara hii itawekwa lini lami?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, lami, wewemwambie tu Bajeti ikipita imeshapita, utamwekea?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ngonyanikama ifuatavyo:-

Kama tulivyoelezea jana kwamba, ahadi zile za Raisza Uchaguzi za mwaka 2010, tutazishughulikia, namna jinsitutakavyokuwa tunapata fedha. Kwa hiyo, miradi yote ile,malengo yetu tujitahidi tuweze kufika, kwenye 2015 tuwetumetekeleza ahadi hizo. (Makofi)

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kunipa nafasi hii. Kwa kuwa barabara yaSumbawanga-Kanazi kilomita 75 na Kanazi-Kizi-Kistalikekilomita 76, Kizi-Kistalike-Mpanda, kilomita 95 na Mpanda-Mishamu, kilomita 100, zimetengewa shilingi bilioni 28, nimiujiza ipi itakayotumika kuzijenga barabara hizi zenyekilomita 346 kwa bilioni 28? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kachomekea lakiniwewe jibu tu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakosokama ifuatavyo:-

Naomba nilieleze Bunge hili kwamba, barabara hizianazozungumza, kasoro hii inayotoka Mpanda kwendaMishamu, hiyo ni barabara ambayo tutatangaza tendermwaka huu wa fedha 2013/2014, kwa hiyo, hiyo haijaanza.

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

21

Kwa hiyo, suala la idadi ya fedha zilizotengwa,tunakwenda kwa ujenzi, tunajenga kwa awamu, kwa hiyo,Makandarasi hawa ambao wako kule kwenye hizo sites,wanapoleta zile certificates ndiyo tutawalipa, kwa hiyo,fedha hiz kwa mipango yetu ni kwamba zinatosha angalauwao waendelee na kazi, wakizalisha zaidi, Serikali itatafutafedha za ziada kuweza kuwalipa.

MWENYEKITI: Tunaendelea, Wizara ya Katiba naSheria.

Na. 214

Kujenga Mahakama za Mwanzo Chunya

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA aliuliza :-

Wilaya ya Chunya inakabiliwa na upungufu waMahakama za Mwanzo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakamaza Mwanzo katika Kata zote za Wilaya hiyo?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Katiba na Sheria na kwa ridhaa yako naomba kujibuswali la Mheshimiwa Victor K. Mwambalaswa (Mbunge waRukwa) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Wilaya ya Chunyainakabiliwa na upungufu mkubwa wa Mahakama zaMwanzo.

Baadhi ya Mahakama zimesitisha kufanya kazikutokana na ubovu wa majengo, lakini ili haki iwafikiewananchi ipasavyo ingefaa kila Kata iwe na Mahakama yaMwanzo na hiyo siyo kwa Chunya tu ila ni kwa nchi nzima.

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

22

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni uwezo wa Serikaliwa kujenga Mahakama zote hizo. Kwa sasa upo upungufuwa Mahakama za Mwanzo 751, za Wilaya 62 na za HakimuMkazi 13 nchi nzima. Mahakama ikishirikiana na Ofisi ya WaziriMkuu TAMISEMI imeandaa mpango kabambe wa kujengaMahakama hizi. (Makofi)

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kunipa nafasi ili niulize maswalimawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kumchelewesheahaki mwananchi ni sawasawa na kumnyima haki na kwakuwa wananchi wengi wenye makosa hayo ambayohayajahakikiwa hukaa sana Rumande kwa sababu tu yakutokuwa na Mahakama ya Mwanzo, pia kutokuwa naWatumishi, huu mpango ambao Mheshimiwa Waziri anasemawameandaa mpango, ni mpango gani, maana yake Wizaraya Elimu na Wizara ya Afya zina mipango ambayoinaonekana ya kujenga vyumba na kuandaa Watumishi, sasaWizara ya Katiba na Sheria ina mpango gani?

La pili, kwa kuwa kwa Wilaya ya Chunya, achaMahakama ya mwanzo, hata Mahakama ya Wilaya,wamepata chumba kwenye jengo la Mkuu wa Wilaya ndiyowanajibanza huko.

Je, Serikali inasemaje kuhusu kuijengea ChunyaMahakama ya Wilaya? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, specific.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Victor K. Mwambalaswa, kama ifuatavyo:-

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

23

Swali la kwanza kuhusiana na Mahakama inampangogani wa kujenga Mahakama hizi za Mwanzo ili wananchiwaweze kupata haki. Sisi pia tunalitambua hili na sisi piatunatambua na tunaumia, lakini ndiyo kama ambavyonimeeleza Takwimu.

Mahakama za Mwanzo ni 751, za Wilaya napendakurudia tena ni 62 tunazihitaji na za Hakimu Mkazi 13, lakinikwa kushirikiana na TAMISEMI, lakini pia kwa kushirikiana naninyi Wabunge, kupitia wananchi wenu na sehemu nyingiwamejitahidi kufanya, ukiangalia katika Mahakama yaWilaya ya Mkuranga, tayari hivi sasa tumekwenda paletumehamasisha wameshajenga jengo la Mahakama yaWilaya wamefikia sehemu ya l inter, lakini pia katikaMahakama ya Mwanzo Karatu tayari na wenyewe wamefikasehemu nzuri tu hivi sasa wanakwamishwa na mvua.

Kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabungewashirikiane na TAMISEMI lakini pia washirikiane na wananchikuhamasisha na pale ambapo ninyi mtaishia, sisi kamaMahakama tutajitahidi kuwaunga mkono ili Mahakama hizituweze kuzijenga kwa wingi zaidi.

Sisi kama Mahakama pia hatujakaa bure, katikampango wetu wa Mahakama kwa mwaka huu kwa Bajetiambayo mmetupitishia, tumeahidi kujenga Mahakama zaMwanzo10, lakini kwa kuwa Bajeti yenyewe ni ndogohatuwezi kusema tutajenga zote kwa pamoja.

Katika swali la pili, ametaka kujua ni lini tutajengaMahakama ya Wilaya ya Chunya, kwa kweli nimpongezesana Mheshimiwa Mwambalaswa, toka mwaka 2008, wakatiMheshimiwa Chikawe akiwa Waziri wa Katiba na Sheria,tarehe 14, Februari, aliulizia Mahakama hizi za Mwanzo naMahakama ya Wilaya ya Chunya. Napenda kumwahidikwamba kwa mwaka 2014/2015 tutajenga Mahakama yaWilaya ya Chunya.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

24

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Mkoa wetu wa Iringa una uhabamkubwa sana wa Mahakama za Mwanzo na hivyokusababisha Mahakama za Mwanzo kama Iramba,Mahenge, Mlolo, kutembelewa na Mahakimu wengine waMahakama za Mwanzo, hii inasababisha wananchiwanapokwenda kwenye Mahakama, wanakosa Mahakimuna kusababisha kesi nyingi sana kuchelewa.

Naomba Mheshimiwa Waziri, ni lini sasa tatizo hililitakwisha ili Mahakimu waweze kuenea kwenye Mahakamazote za Mwanzo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri jibu kwa kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Kabati,kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa napenda tu kutoa utangulizi kwamba,tuna upungufu wa Mahakimu 1600, lakini kama Serikalihatujakaa kimya, tunajitahidi kila mwaka basi kuajiri walauMahakimu 300 na tumeanza mpango huu kuanzia mwaka2011/2012 tumeshaajiri Mahakimu 300 na katika mwaka 2012/2013 kipindi kinachoishia Juni, 2013 tutaajiri tena Mahakimuwa Mahakama za Mwanzo 300, mpaka hapo tatizo hililitakapokwisha.

Napenda tu kumhakikishia Mheshimiwa Ritta Kabati,kuhusiana na Mahakama ya Mwanzo ya Mahenge na Mlolokutembelewa, tutajitahidi pindi watakapoajiriwa tupelekeMahakimu katika Mahakama hizo ili wananchi wawezekupata haki.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru, na mimi niulize swali moja dogo la nyongeza.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

25

Tatizo ambalo liko Chunya, kama jinsi ambavyo swalila msingi lilikuwa, ni sawasawa kabisa na tatizo ambalo likoArumeru, kwenye Halmashauri yangu ya Meru na mwakajana nilimwuliza Waziri na nikajibiwa na Naibu Waziri ambayeametoka kujibu swali hapa, kwamba wangekuja Arumeru,na kwa sababu hapa watu wanaulizia ujenzi wa Mahakamampya, lakini kule kwangu Arumeru yako majengo yaMahakama ambayo yalikuwa yanatumika ambayoyalishajengwa siku nyingi. Lakini leo hii hayatumiki kabisa.Mfano mzuri, ni Mahakama iliyokuwa King’ori, ambayo jengolipo tu leo hii ni mazalia ya Popo, jengo la pale Nkwangua,jengo la Mahakama pale Pori Barazani ambalo lina kila kitu,kuna umeme, maji, chumba cha Mahakama, cha Mahabusu,lakini majengo yote haya hayatumiki.

Sasa kwa sababu sisi hatuombi kwenda kutujengeamajengo mapya ya Mahakama…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nassari, swali, swali.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nitaomba Mheshimiwa Naibu Waziri atuambie tu kwamba nilini au Wizara ina mpango gani basi kuhakikisha kwambaMahakama zinaanza kufanya kazi ili wananchi wawezekupata haki zao? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi,muda wetu ni mdogo sana.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nassarikama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa kama Mahakama haipendi kuachajengo lifikie hatua hiyo na mpaka limefikia hatua hiyo itakuwani masuala ya uchakavu na kwa kuwa ina ufinyu wa Bajetindiyo maana imeshindwa kutekeleza adhima hiyo iliMahakama iweze kufanya kazi. Lakini napenda tukukuhakikishia kwamba kwa Bajeti ya mwaka huu ya mfukowa Mahakama tutajitahidi kuzipa kipaumbele Mahakama

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

26

hizo ili wananchi wa Arumeru, hususan King’ori na PoriBarazani, waweze kupata haki yao. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea, Wizara ya Fedha.

Na. 215

Hatima ya Wanahisa wa National InvestimentCompany Limited (NICOL)

MHE. PHILEMON K. NDESAMBURO aliuliza:-

Kampuni ya National Investiment Company Limited(NICOL) iliyoasisiwa na Watanzania na kuhamasishwa naViongozi Wakuu wa Serikali na Siasa kwa kuwatakawananchi wajiunge na kununua Hisa, haisikiki tena kwa zaidiya miaka mitano sasa na inasemekana kuwa Kampuni hiyoimefilisika:-

(a) Je, ni nini hatima ya wanahisa wa Kampuni hiyo?

(b) Je, Serikali inachukua hatua gani kwa uongozi waNICOL kwa kuwatapeli wananchi?

(c) Je, Serikali inasema nini juu ya utapeli wa aina hiyo nipamoja na ule wa DECI, UPATU, DOLA JETI?

WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali laMheshimiwa Philemon Ndensamburo, Mbunge wa MoshiMjini, lenye vipengele (a) (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, hatima ya wanahisawa Kampuni ya NICOL itaamuliwa na wanahisa wenyewekwa kuzingatia sheria iliyoanzisha Kampuni hii. NICOLilianzishwa na kusajiliwa chini ya Sheria ya Kampuni, Sura ya212 ya Sheria za Tanzania. Sheria hii inazo Kanuni na taratibuzinazoelekeza namna ya kuendesha Kampuni na kulindamaslahi ya wanahisa wenyewe.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

27

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari wanahisawenyewe wamechukua hatua dhidi ya uongozi wa Kampuniyao wakati wa mkutano wa mwaka wa wanahisa uliofanyikaJanuari, 2013. Ikumbukwe kwamba, uongozi huo wa Kampunihaukuwekwa na Serikali bali na wanahisa wenyewe kupitiaBodi ya Wakurugenzi na pindi wanahisa wanapoona kunaumuhimu wa kuchukua hatua dhidi ya uongozi, wanafuataKatiba na Sheria zilizopo.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna utapeliwowote kuhusiana na uanzishwaji na uendeshaji wa shughuliza NICOL. Serikali kupitia Bunge lako Tukufu ilipitishamarekebisho ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania) ili kuruhusu uanzishwaji waMipango ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective InvestmebtSchemes), ambapo, kupitia utaratibu huu Kampuni ya NICOL,Unit Trust of Tanzania (UTT) na TTCIA zinaendesha shughuli zake.Hivyo Kampuni ya NICOL ipo kisheria na haifananishwi naDECI, UPATU na DOLA JET.

Kilichotokea katika Kampuni ya NICOL siyo utapelihasa, bali kutokuwa na weledi wa kutosha katika menejimentiya fedha, kwani NICOL ilichukua mikopo mikubwa nawakaiwekeza katika vitega uchumi ambavyo baadhi yakevimefilisika na hivyo kuiletea NICOL hasara, hiyo hasaraimepunguza thamani ya Kampuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapinga nahaitambui uendeshaji wa shughuli za kifedha kwa mifumoya udanganyifu. Serikali kupitia Bunge lako Tukufu ilifanyamarekebisho ya Sheria Na. 8 ya mwaka 2006 kwa kuongezamafungu ya 171(b) na (c) kwenye Sheria ya Kanuni zaAdhabu, Sura ya 16 kuharamisha mifumo isiyo rasmi ambayondiyo hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge Ndesamburo.

Kwa mujibu wa vifungu hivyo vya sheria, ni kosa lajinai kwa mtu yeyote kuendesha au kushiriki katika mifumoya fedha ambayo siyo rasmi. Mfumo usiyo rasmi ulioendeshwana DECI uliweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria hiyo nawahusika waliweza kufikishwa Mahakamani.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

28

MHE. PHILEMON K. NDESAMBURO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante, sasa ninayo maswali mawili madogoambayo ningependa kupata majibu kwa niaba ya wanahisawa NICOL.

Viongozi wa NICOL ni wanahisa tena wakubwa waNICOL na ndiyo wanaoiendesha NICOL, inaeleweka wazikwamba, katika dunia ya sasa, si rahisi kuwekeza kwenyeKampuni au kwenye kitega uchumi ambacho kitaleta hasara,wanahisa wanaamini, ni ujanja ujanja ulitumika kununuaViwanda vilivyokuwa vimeharibika, havina faida yoyote, ilawale waliohusika walifaidika kwa fedha zile.

Je, Serikali haioni kuna haja ya kuchunguza nakuchukua hatua kwa wale walihusika? (Makofi)

La pili, DECI ilipostopishwa, Serikali ilichukua zile fedhana kuziweka wanakojua, lakini wale watu waliokuwawamewekeza, mpaka sasa hawajapata faida yoyote nafedha zao hawajapata, ni lini Serikali itawapa zile fedhaambazo zilikuwa zimechukuliwa kutoka Benki? (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakujibu maswali mawili ya nyongeza ya MheshimiwaNdesamburo kama ifutavyo:-

La kwanza, ni kweli, ilibainika kwamba, viongozi yaaniBodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya NICOL, walikuwa ndiyosehemu ya ushauri, wanahisa walipogudua kwambautaratibu ule ulikuwa haufai, ndiyo maana walichukua hatua.

La pili, kwa nini Kampuni kuwekeza katika vyombovinavyoleta hasara. Ni kweli inatakiwa kuwekeza katikavyombo ambavyo vinaleta faida, na ndiyo maana Mamlaka(CMSA) yenye mamlaka ya kuratibu iliwashauri wawekezekatika Makampuni mengine yanayoleta faida, na hatua hiyoilikuwa haijakamilika baada ya kuwa Bodi ya Wakurugenziilikuwa imesimamishwa, lakini suala hili liko Mahakamani, kwamgogoro wa wanahisa kutaka haki yao.

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

29

La pili, kwa nini na kwa sababu gani mpaka sasa hiviNICOL, wanahisa wake hawajapata faida zao. Suala hililinashughulikiwa na baadaye Waheshimiwa Wabunge nawananchi watapata matokeo yake.

MWENYEKITI: Tunaendelea, Wizara ya Nishati naMadini. Mheshimiwa Riziki S. Lulida. Waheshimiwa Wabunge,muda wetu wa maswali kwa kweli ni mdogo sana.

Na. 216

Kupeleka Umeme Vijijini

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU (K.n.y. MHE. RIZIKI S.LULIDA) aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka umeme vijiji vya Ngongo-Mikole, Mchinga-Kitomanga na Mchinga - Kijiweni?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE GEORGEB. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa RizikiS. Lulida, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa kuwafikishiaumeme wananchi wa vijiji vya Ngongo-Mikole, Mchinga-kitomanga na Mchinga- Kijiweni, umejumuishwa katikaMpango Kabambe wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili chini yauwezeshaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Zabuni yakuwapata wakandarasi wa kazi hizi ilitangazwa mweziDesemba, mwaka 2012 na kufunguliwa mwezi Machi, mwaka2013 na kazi za ujenzi zinatarajiwa kuanza wakati wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi za mradi huuzitajumuisha ujenzi wa njia za umeme za misongo mbalimbali,ufungaji wa transfoma na kuwaunganishia wateja wa awali1,237. Gharama za Mradi zinakadiriwa kuwa shilingi bilioni 4.64.(Makodi)

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

30

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu ya MheshimwaWaziri, ningependa nimwulize maswali yafuatayo:-

Kwanza, ahadi za utekelezaji wa miradi katikamaeneo yaliyotamkwa na Mheshimwa Waziri, pamoja namaeneo mengine kama vile Matandu, Somanga, pamojana Miteja, imekuwa inachukua muda mrefu sana na majibuya Wizara kwamba, muda wowote itakekeleza.

Sasa ningependa kujua time frame, kwamba ni mudagani ambapo hii miradi itakuwa imekamilika na wananchihawa wakanufaika na miradi hiyo ya umeme?

Swali la pili, kipindi ambacho Mheshimiwa Waziriulifanya ziara katika Mikoa ya Kusini, ulitoa punguzo kwawananchi kuweza kulipia rate maalum kwa ajili ya Mikoa hiyoya Lindi na Mtwara kwa maana ya maeneo ambayoinapatikana gesi, punguzo li le l i l ikwisha muda naukaongezea tena muda, lakini bado muda ule unakaribiakwisha, wananchi bado hawajahamasika kwenda kulipiaumeme.

Je, pale ambapo umeme utakuwa umeshashushwakatika maeneo yale punguzo hili litaendelea kuwepo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibumaswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Murtaza A.Mangungu, kama hivi ifuatavyo.

Ni kweli katika awamu ya pili REA tunavyo vijiji vingisana zaidi ya 1,200 katika nchi nzima, ambavyo tunatarajiakuvitekeleza katika mwaka 2013/2014. Lakini kubwa hapa niwakati wa Bajeti yetu, niwaombe sana WaheshimiwaWabunge pamoja na fedha kwamba bado tunaendeleakujiweka sawa, lakini katika hizo zilizopo basi mtusaidie tuwezekupitisha Bajeti yetu ili tutekeleze miradi hii.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

31

Mheshimwia Mwenyekiti, ni kwamba nilipofanya ziara,ni kweli katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, tuliamuakuwahamasisha wananchi kwa kupunguza bei ya kuwekaumeme kwenye majumba yao. Tulipunguza na kuweka kiasicha shilingi 99,000/=. Offer hii inakaribia kwisha. Kwa hivyotutajaribu kuangalia hali ya mazingira yatakavyokuwa napengine tutakuja na makubaliano mengine mapya kwawakati huo.

MHE. ZAYNABU M. VULLU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Ninalo swali moja la nyongeza. Kwakuwa Serikali kupitia mradi wa REA, imeishanza kusambazonguzo za umeme, kwenye Wilaya ya Kisarawe, kutokeaMlandizi, Mzenga, Kuruwi. Kutokea Kisarawe mjini kuelekeaMwanarumango – Msanga.

Kwa kuwa waya hizo zimewekwa hazijawekwatransformer wala kufikishwa umeme kuna hatari ya watukuiba hizo nyaya za umeme na serikali kupata hasara. Kwakuwa kuna viwanda vimeanza kujengwa kule vinategemeakupata umeme ili viweze kufanya kazi ya kuzalisha na halikadhalika kupata ajira kwa vijana na wananchi wanaoishimaeneo ya Wilaya hiyo ya Kisarawe.

Je, Serikali inasema nini, kuhusu kupeleka umeme huona kuanza kufanyakazi ili kuwapa matumaini wananchi waWilaya hiyo ya Kisarawe?

NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibuswali la nyongeza la Mheshimiwa Vullu, kama hivi ifuatavyo.

Ni kweli tuna mpango na Mradi unatekelezwa wakusamba umeme katika maeneo ya Kisarawe,Mwanarumango hadi Msanga. Utekelezaji wake uko katikahatua hiyo aliyoisema Mheshimiwa Mbunge, ambayoinaashiria ukamilifu wake, kilichobakia pale ni kuwasha nakufanya majaribio. Nimwondoe wasi wasi MheshimiwaMbunge, kwamba wakati wowote mradi huuutakapowashwa wananchi watafurahia tu.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

32

Kwa kweli shughuli iliyokwishafanywa na Mkandarasini kubwa na inafikia ukingoni. Tuvute subira muda wowotemwezi na ujao unaweza umeme ule ukawashwa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleaswali linalofuata la Mheshimiwa Vicky Paschal Kamata.Litaulizwa kwa niaba yake na Mheshimiwa Maria I. Hewa.

Na. 217

Hitaji la Umeme Kama Nishati Mbadala ya Kupikia

MHE. MARIA I. HEWA (K.n.y. MHE. VICKY P. KAMATA)aliuliza:-

Umeme ni nishati mbadala ya kupikia inayowezakuwasaidia wanawake wa vijijini ambao hutumia mudamwingi na kutembea muda mrefu kutafuta kuni hasa katikamikoa inayozunguka Ziwa Victoria:-

(a) Je, ni vijiji vingapi vimepatiwa umeme katikawilaya za Geita, Nyang’wale na Chato ambazo ndizozinaunda Mkoa wa Geita?

(b) Je, asilimia ngapi ya wanawake waishio vijijiniwaliounganishiwa umeme katika wilaya nili zozitaja?

(c) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikishakwamba inafikia lengo la kufikia 30% ya wananchi waishiovijijini katika Mkoa wa Geita kama Ilani ya Uchaguzi wa CCMya 2010 inavyoelekeza?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE) Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kujibuswali la Mheshimiwa Vicky P. Kamata, lenye sehemu (a) (b)na (c) kama itufavyo:-

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

33

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti maeneo ya Wilaya ya Geitaambayo tayari yanapata umeme wa gridi ya taifa ni pamojana vijiji vya Kaswama, Kanyara, Mwatulole, Kalangalala,Mseto na Mji wa Geita. Kwa Wilaya ya Chato vijiji vyaMganza, Nyisanzi, Nyamilembe na kazunguti vinapataumeme kutoka Wilaya ya Biharamulo, unaozalishwa kwamitambo inayotumia mafuta ya dizeli.

Aidha Wilaya za Mkoa wa Geita ni miongoni mwaWilaya zinakazonufaika na mradi wa umeme unaofadhiliwana Serikali ya Marekani yaani Millenium ChallengeCorporation (MCC). Baada ya mradi kukamilika, jumla yavijiji 14 vitanufaika. Vijiji hivyo kwa Wilaya ya Geia ni:- (i)Bukondo, Saragulwa, Nyamigota, Katoro, Nyarugusu,Rwamugasa, Ikina, Bukoli, Chigunga na Chikobe. Lakini kwawilaya ya Chato ni Buselesele na kwa Wilaya ya Nyang’waleni Nyarubele, Nyangwale na Msalala. Jumla ya watejawaliounganishiwa umeme kwa wilaya ya Geita kwa sasa ni6,121.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti,ili kuhakikisha kuwa lengo laSerikali la kufikia 30% ya wananchi wanafikiwa na hudumaya umeme, Serikali imejipanga kusambaza umeme kwaawamu kadiri ya upatikanaji wa fedha chini ya Wakala waNishati Vijijini (REA). Vijiji na maeneo yatakayopatiwa umemekaika awamu ya pili ya REA mkoa wa Geita inayotarajiwakutekelezwa kuanzia mwaka huu ni vijiji 68. Aidha mradiutawaunganisha na wateja wa awali 6,902 na Gharamazinakadiriwa kuwa shilingi bilioni 16.6. Orodha ya ijiji husikavipo kwenye jibu la msingi ambalo nimekwisha mpatiaMheshimwia Mbunge.

MHE. MARIA I. HEWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, niulize maswali mafupi mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishawahi kukaa mudamfupi Biharamulo na nikawa nimelala pale. Umeme wa paleni hafifu kabisa. Ambapo ndiyo unategemewa kutumiwakatika maeneo mbali mbali.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

34

Umeme huo, kama ndiyo huo ninouzungumza. Je,utatosheleza kuusambaza tena, kama ndiyo Biharamuloyenyewe, umeme ni hafifu? (Makofi)

La pili, umetoa orodha ya vijiji na sekondari nyingi tuza mkoa wa Geita, ambazo zitapatiwa umeme kwa kutumaREA II, unaniruhusu nimpe orodha hii Mheshimiwa VickyKamata, kwa maana ya kuzungumza sasa ni lini, hivi vijiji nasekondari karibu zote za Geita zitapatiwa umeme, wakatiatakapoanza ziara zake katika mkoa wa Geita, ni lini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, unaombwa ujibukwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimwia Mwenyekiti, napenda kujibumaswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maria I. Hewa,kama hivi ifuatavyo:-

Kwamba umeme ule unaotoka Biharamulo kamandiyo unaotarajiwa kusambazwa ni hafifu. Tatizo hilitumelishughulikia na linaenda sambaba na ufungaji wamashine mpya katika wilaya za Biharamulo, Ngara naMpanda.

Ni hiyo jana tarehe 14 Mei, 2013 nil ikuwaninazungumza na Mpanda pale wanajaribu hawana cranekubwa ya kushushia generator ile lakini imeishafika. Napendakusema ya kwamba kama Ngara wanahangaika kushukagenerator, inawezekana zija-check, lakini inawezekana hataBiharamulo napo wanajaribu kushusha generator na hataMpanda wanajaribu kushusha generator yao.

Napenda nimhakikishie ya kwamba mradi huu namashime zile generator zitaboreshwa na Biharamulokutakuwa kuna umeme ambao utakuwa wa uhakika sana.Lakini REA II ni linini?

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

35

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba dhamira ya Serikali ya Chama chaMapinduzi, ni kuhakikisha kwamba tunasambazo umeme kwavijiji vya REA II, kama tulivyo ahidi na kama tulivyoviorodhesha.Kwa hiyo, nimhakikishe kwamba hiyo orodha niliyompatiaampatie Mheshimiwa Mbunge, aende akatambe nayo nakwamba CCM, itahakikisha inatekeleza miradi ya umeme.

MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,maeneo mengi katika nchi hii leo kumekuwa kuna utaratibuwa wananchi kulilipia umeme. Gharama za kuunganishiaumeme TANESCO, ikiwemo kulipia na nguzo na badala yakewanachukua muda mrefu sana kabla hawajapelekewaumeme.

Kwa mfano, Maeneo ya Kata ya Buongwa Jiji laMwanza na Kata ya Mkolani, wananchi wamelipia gharamaza kuunganisha umeme toka mwaka 2012, mwezi Desemba,mpaka sasa hawajapewa umeme. Sasa ninaiuliza Serikalihuu mfumo wa TANESCO, kukopa fedha kwa wananchi nakufanya nazo biashara na wanakaa nazo muda mrefu, halafuwanapeleka umeme pale ambapo wataamua wao. Huumfumo umeanza lini na Serikali itaukomesha lini? Ili wananchiwanapolipia umeme waunganishiwe haraka kwa kadiriinavyowezekana?

NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI (MHE. GERGE B.SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibuswali la nyongeza la Mheshimiwa Wenje, kama hivi ifuatavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninasikitika kwambakama kweli Mwanza hali ndiyo hiyo na taarifa hizi mimininazipata kila mara. Ucheleweshaji siyo wa kiasi hicho.Niseme tu kama wako mahali popote iwe wilayani au mkoani,wanakochelewa kuwafungia wateja wao wakishakuwawamelipia, hili ni kosa kubwa na wanapaswa kwa hakikakuchukuliwa hatua kwa sababu kwenye takwimu zetuhaionekani hiyo.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

36

Ucheleweshaji unakuwepo kidogo kwa muda wa wikimoja, wiki mbili au wiki tatu, lakini siyo wa kiasi hicho.Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge tuonane baada yahapa tuelezane ukweli huo na tushughulikie.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Swali la Wizara ya Maji linatakaloulizwa na MheshimwaJerome D. Bwanausi.

Na. 218

Mradi wa Maji – Chiwambo

MHE. JEROME D. BWANAUSI aliuliza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. NinaombaKabla ya swali langu halijabiwa, lisomeke kama hivi ifuatayo.

Serikali iliahidi kutoa Sh.580,000,000/= kwenye mabanoimeandikwa (Milioni mia tano themanini elfu tu). Iwe Serikaliiliahidi kutoa Sh.580,000,000/= (Milioni mia tano themanini)kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya majiya mradi wa Chiwambo katika Jimbo la Lulindi kupitia ahadiya Mheshimiwa Rais:-

Je, ni l ini fedha zitakamilishwa il i mradi huouwanufaishe wananchi wanaokabiliwa na tatizo kubwa lamaji?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jerome D. Bwanausi,Mbunge wa Jimbo la Lulindi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuwa Serikali iliahidikutoa Shilingi millioni 580 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wamaji wa Chiwambo katika wilaya ya Masasi. Maradi huounahudumia wakazi wapatao 45,994 katika vijiji 23 vya Katasita (6) za Namalenga, Chiungutwa, Lulindi, Sindano, Mchauruna Mbuyuni. Serikali imeanza kutekeleza ahadi yake yaMheshimiwa Rais kwa mradi huo wa Chiwambo ambapo

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

37

hadi sasa shilingi milioni 130 zimetolewa kwa ajili ya ukarabatiwa mradi huo. Fedha hizo zimetumika kununua na kulazamabomba mapya ya nchi 6 yenye urefu wa kilomita 5.4 katiya kilometa 11 za bomba kuu la kutoa maji kwenye chanzocha chemche ya Lulindi hadi kwenye tanki la kuhifadhia majilililopo katika kijiji cha Nagaga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa2013/2014, kiasi cha shilingi milioni 530 kimetengwa katikaBajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa ajili yaukarabati wa mradi huo.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibumazuri. Lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, amekirikwamba mradi huu ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, aliyoitoaalipotembelea kwenye jimbo la Lulindi.

Je, anawadhibitishiaje wananchi wa Kata hizi (6),kwamba mradi huo ambao unatekelezwa na Serikali na siyoHalmashauri, utakuwa umepata fedha katika kipindi hiki chaBajeti ya 2013/2014?

Kwa kuwa katika jibu la msingi la Mheshimiwa Waziri.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaombautulivu kidogo. Samahani.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Kwa kuwa kwenye swalilake la msingi Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba upelekajiwa fedha hizi umekuwa wa kusuasua. Je, yuko tayari sasaWizara ya Maji kutangaza tenda ili kumpata Mkandarasimakini atakayemaliza mradi huu kwa pamoja?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Mbunge ametaka tuwahakikishie wananchikwamba ule mradi sasa utatekelezwa.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

38

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ni muhimu sana.Ni mradi ambao ulijengwa mwaka 1955 na umekarabatiwatu kidogo mwaka 1990. Kama ilivyo kwenye jibu la msingi,mradi huu unahudumia vijiji 23. Kwa hiyo, umuhimu wakuukarabati haraka ni mkubwa sana, kwa sababu impactyake itakua kubwa kwa wanananchi.

Kwa hiyo jibu langu la msingi ni kwamba tumejipanga,na ndiyo maana Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya imetengamilioni 530 hizi siyo hela ndogo ni hela nyingi. NiwapongezeHalmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kuliona hili na kutoakipaumbele kwa Miradi ya Maji, na wilaya nyingine ziigemfano huo. (Makofi)

Sasa kwamba tunaahidi vipi Wizara ya Maji kupelekafedha. Ninataka nimhakikishie tutafuatilia na mimi nitapangaziara kwenye kuukagua Mradi huu vizuri ili tuone kwambaunatekelezwa kwa wakati na wananchi wa wilaya ya Masasikatika sehemu ya Jimbola Lulindi wanapata maji.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswaliyamekwisha, na ni vigumu kumpa kila mtu nafasi kwenyeswali la nyongeza, kutokana na muda uliokuwepo.

Matangazo. Wageni waliopo jukwaa la Spika. Nimgeni wa Mheshimiwa Dr. Harrison G. Mwakyembe, Mbungena Waziri wa Uchukuzi, ambaye ni Enginer DeogratiusRumiruzu (Mbunge na Waziri wa Uchukuzi wa Burundi). Karibusana Mheshimiwa Waziri kutoka Burundi. Welcome to TheParliament of Tanzania. (Makofi)

Wageni waliofika Bungeni kwa ajili ya mafunzo.Wageni wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaaam, ambaoni wenyeviti wa Serikali za Mitaa 60 kutoka Dar es Salaam,karibuni. Pamoja na hao wameambatana na Danyl Kapwanina Dominic Malindi kwenye mafunzo hapa Bungeni. Karibunisana Bungeni. (Makofi)

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

39

Mheshimiwa John Joel, anawatangaziaWaheshimiwa Wabunge wote wanaotoka Mkoa wa Mtwara,Lindi na Pwani, kuwa wanaombwa kuhudhuria mkutano wamashauriano wa kujadili changamoto, zilizojitokeza katikatasnia ya Korosho msimu wa 2012/2013. Mkutano huoutafanyika siku ya Alhamisi tarehe 16 Mei, 2013 kuanzia saa8.00 mchana katika ukumbi wa Royal Village, hapa Dodoma.Wabunge wote wa mikoa hiyo wanaombwa kuhudhuria.

Mheshimiwa Margareth S. Sitta, - Mwenyekiti waKamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, anawatangaziaWaheshimiwa Wabuge wote kuwa leo Jumatano tarehe 15Mei, 2013 saa 8.00 mchana kutakuwa na shughuli ya utoajivyeti vya kuwatambua wadau waliochangia maendeleo yaChuo Kikuu HUria. Shughuli hiyo itafanyika katika ukumbi waPius Msekwa.

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo atakuwa Waziri waElimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawamba,Mbunge, akiambatana na Mkuu wa Chuo Mheshimiwa Dkt.Asha-Rose Migiro. Aidha Waheshimiwa Mawaziri naWabunge ambao mtapokea vyeti hivyo mnaombwakuzingatia muda.

Mheshimiwa Victor Mwambalaswa, Mwenyekiti waKamati ya Bunge ya Nishati na Madini, anawatangaziaWajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, kuwa leo tarehe15 Mei, saa 7.00 mchana kutakuwa na kikao cha Kamati.Kikao hicho kitafanyika katika ukumbi Namba 231 ghorofaya pili jengo la utawala.

Nachukua nafasi hii Waheshimiwa Wabunge kwanzakuipongeza Klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuchukuaubingwa wa nchi hii katika soka na ninatoa pongezi hizi kwaklabu hiyo na Mwenyekiti wake Yssuf Manji na mimi nikiwakama Mbunge wa Klabu hiyo inatoka katika Jimbo langu.(Kicheko/Makofi)

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

40

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014Wizara ya Viwanda na Biashara

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kutoa hoja kwamba. Kutokana nataarifa ilyowasiizhwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda naBiashara, pamoja na Taasisi zake ambayo ilichambua Bajetiya Wizara ya Viwanda na Biashara na Tasisi zake zilizochiniyake tarehe 4 Aprili, 2013. Sasa Bunge lako Tukufu, likubalikupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya fedha ya Wiwara ya Viwanda na Biashara, naTaasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, WahEshimwia Wabugne,wakirejea hotuba niliyoisoma Bungeni mwaka 2012/2013.Wataona kuwa tuliazimia kwanza kuendeleza Viwandavikubwa na vya kati. Pili kuendeleza viwanda vidogo nabiashara ndogo, tatu kuendeleza biashara ya ndani ya a nje.Nne kuendeleza masoko ya ndani na ya nje na tano kutoahuduma bora kwa wadau wa Sekta za viwanda na Biashara.

Aidha nilisisitiza kuwa katika kukuza uchumi waviwanda mtazamo wetu usjielekeze kwenye ujenzi wakiwanda kimoja kimoja, bali ujielekeze kwenye mchakatompana wa ujenzi wa viwanda na kutengeneza ajira zakutosha kwa Watanzania. Kwa maana ya Industrializatization.Fikra zetu na mtazaomo wetu tuvielekeze huko na ndikotunakokwenda hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeamua sasa masuala yaViwanda Biashara na Maksoko yatafanywa na Wantanzaiawote na ninatoa wito kuwa wakati umefika na wakati ni huu.Kama msimamizi wa Wizara hii tutahakisha kuwa Wantanziawote bila mlolongo au urasimu kwa waliokwishanza nawanaotaka kuanza kuendeleza viwanda biashara namasoko, tutendelea kuwawezesha.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

41

Mhehimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kumshukuruMwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwabuheri wa afya na hivyo kutekeleza majukumu yetu yakustawisha maisha ya jamii ya Watanzania. Kipekee sana,namshukuru Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwana imani nami pamoja na Naibu Waziri Mheshimiwa GregoryGeorge Teu, Mbunge wa Mpwapwa, kwa kuendelea kutupadhamana ya kuongoza na kusimami majukumu ya Wizaraya Viwanda na Biashara. Napenda kumhakikishiaMheshimiwa Rais kuwa tunaendelea kwa ari na nguvu zaidikuyatekeleza majukumu hayo kwa kutoa ushirikianounaotakiwa kwa Baraza la Mawaziri, Waheshimiwa Wabungena Watanzania wote kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naishukuru kwa dhati Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Uchumi , Viwanda na Bishara chiniya uongozi wa Mwenyekiti wake Mheshimiwa MahmoudHassan Mgimwa, Mbunge wa Jimbo la Mufumdi Kaskazini(CCM) na Makamu wake Mheshimiwa Dunstun LukaKitandula, Mbunge wa Mkinga (CCM) kwa kuiongoza kamatihiyo. Ni matumaini yetu kuwa Kamati hiyo itaoa msukumompya katika kushughulikIa masuala ya sheria, sera na mikakatiya kisekta.

Vile vile, napenda kuwapongeza wanakamati wotekwa umakini wao katika kujadili Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara yangu. Napenda KuwathibitIshia kuwa,maoni yao yamezingatiwa na ndiyo yalikuwa msingi mkuukatika kuboresha Hotuba ninayoiwasilisha leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Niruhusu pia niishukuruKamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biasharaambayo imemaliza muda wake chini ya aliyekwuaMwenyekiti wake Mheshimiwa Mahmoud Hassan MgimwaMbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini (CCM) na Makamuwake Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo, Mbungewa Mbinga Mashariki (CCM). Nikiri kuwa tulinufaika sana naumahiri wao na ushirikiano makini katika kuchambua kushaurina kusimamia maendeleo ya sekta yetu.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

42

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hiikukushukuru wewe mwenyewe, Naibu Spika, Wenyeviti waKamati za Kudumu za Bunge, Katibu wa Bunge na Watendajiwote wa Ofisi ya Bunge pamoja na Bunge lako Tukufu, kwaushirikiano tunaoupata kutoka kwenu katika kuwasilishamasuala mbalimbali ya Wizara yangu, ikiwemo Miswada yaSheria na mapendekezo ya Bajeti ya Wizara hii. Napendakuwahakikishia kwamba, Wizara yangu itaendelea kutoaushirikiano unaohitajika ili kuleta matokeo yanayokusudiwakatika sekta yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hiikumpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mbungewa Jimbo la Katavi (CCM) kwa Hotuba yake inayobainishamafanikio na mwelekeo wa utendaji wa Serikali ya Awamuya Nne. Vilevile, nawapongeza Mawaziri walionitanguliakuwasilisha hoja zao hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwashukuruwananchi wa Jimbo langu la Handeni kwa ushirikiano waounaoniwezesha kuendelea kutekeleza ipasavyo majukumuyangu kama Waziri na yale ya kuwawakilisha katika Bungelako Tukufu. Pia, kwa namna ya kipekee naishukuru familiayangu hususan mke wangu, watoto, ndugu na marafikizangu wote kwa ushirikiano, upendo na dua zao ambazozimekuwa nguzo muhimu katika ufanisi wa kutekelezamajukumu hayo ya kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazishukuru pia Wizara,Taasisi za Serikali na wadau wote, hususan Asasi za SektaBinafsi zikiwemo Chama cha Wadau wa Ngozi Tanzania -LAT; Baraza la Kilimo Tanzania - ACT; Baraza la Taifa la Biashara- TNBC; Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania - CTI; Chamacha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania -TCCIA; Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania - TPSF; Chama chaWafanyabiashara Wanawake - TWCC na Vikundi vya BiasharaNdogo (VIBINDO) kwa michango yao katika kuendeleza Sektaya Viwanda, Biashara, Masoko na Viwanda Vidogo naBiashara Ndogo ambazo Wizara yangu inaisimamia. Aidha,

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

43

nawashukuru wananchi wote na vyombo vya habari kwaushirikiano wao hususan kwa maoni yenye kujenga nakuelimisha umma kuhusiana na utendaji wa Wizara na sektakwa ujumla. Ari hiyo ambayo ni chachu muhimu katikamaendeleo ya sekta na uchumi wetu kwa ujumla naombaiendelezwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenawashukuru Naibu Waziri, Mheshimiwa Gregory George Teu;Katibu Mkuu - Bi. Joyce K. G. Mapunjo, Naibu Katibu Mkuu -Dkt. Shaaban R. Mwinjaka; na Wakuu wa Idara, Vitengo naTaasisi zilizo chini ya Wizara, kwa mshikamano na ueledi waokatika kuongoza na kusimamia utekelezaji wa majukumu yakisekta. Nawapongeza na kuwashukuru pia wataalam nawatumishi wote wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwakujituma na kutuandalia ushauri wa kitaalamuunaotuwezesha kufanya maamuzi mbalimbali yenye lengola kuendeleza Sekta ya Viwanda, Biashara, Masoko naViwanda Vidogo na Biashara Ndogo. Vilevile, napendakuwashukuru wale wote ambao kwa njia moja amanyingine, tulishirikiana nao katika maandalizi ya hotuba hiininayoiwasilisha leo. Namshukuru pia Mpiga Chapa Mkuu waSerikali na wachapishaji wengine kwa kuchapishamachapisho ya Wizara yangu kwa ubora na kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuungana naWaheshimiwa Mawaziri na Wabunge wenzangu kuwapapole ndugu na jamaa kwa kuondokewa na mpendwa wetu,Mheshimiwa Salim Hemed Khamis - Mbunge waChambani(CCM), Mwenyezi Mungu mwingi wa rehemaamrehemu na ampumzishe kwa amani mahali pema Peponi.Amina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapitio ya utekelezaji wabajeti kwa mwaka 2012/2013. Katika Hotuba ya Bajeti yamwaka 2012/2013, Wizara iliazimia kutekeleza yafuatayo:-

· Kuendeleza viwanda vikubwa;

· Kuendeleza viwanda vidogo na biashara ndogo;

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

44

· Kuendeleza biashara ya ndani na nje;

· Kuendeleza masoko; na

· Kutoa huduma bora kwa wadau wa Sekta yaViwanda na Biashara.

Katika eneo la kukuza uchumi wetu kupitia viwanda,mwelekeo wetu ulikuwa kwenye mchakato mzima wa ujenziwa viwanda (industrialization) badala ya mtazamo wa ujenziwa kiwanda kimoja kimoja (Industries). Fikra zetu (mindset)na mtazamo wetu (attitude) ni vyema tukauelekeza huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu imedhamiriakuendeleza Sekta za Viwanda, Biashara, Masoko na ViwandaVidogo na Biashara Ndogo licha ya changamototunazokutana nazo hasa uhaba wa rasilimali fedha. Nia yetuni kushirikiana na sekta zinazozalisha mali moja kwa moja ilituelekee kwenye uchumi wa viwanda tunapoelekea mwaka2025. Lengo hilo linawezekana, kwani hata taarifa za uchumizinaonesha dhahiri kuwa hivi sasa uzalishaji viwandanipamoja na Sekta za Huduma, Ujenzi, Utalii na Miundombinuhasa ya barabara, reli na bandari inachangia kwa kiasikikubwa katika Pato la Taifa. Huo ni mwelekeo mzuri hasatukizingatia kuwa duniani kote, ushahidi, uzoefu na historiaya uchumi vinaonesha hakuna uchumi ulioendelea, hatakwa nchi zinazoendelea hivi sasa (emerging economies) kwakutegemea kilimo pekee. Hivyo, napenda kutumia fursa hiikulieleza Bunge lako Tukufu utekelezaji uliofanyika katikakipindi cha 2012/2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya sekta ya viwanda,biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo;Wizara imekuwa ikisimamia na kutekeleza sera na mikakatiya sekta kupitia Mpango mkakati wa Wizara wenyekubainisha dira, dhima na malengo ya Wizara kwa kipindicha miaka mitano. Katika kutekeleza mipango ya kisekta,Wizara imekuwa ikizingatia malengo ya Dira ya Taifa yaMaendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010;Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

45

(MKUKUTA II), Kilimo Kwanza, Mpango wa Maendeleo waMiaka Mitano (2011/2012 - 2015/2016) na Mpango Elekezi waMwaka 2011 – 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda. Katikakipindi cha mwaka 2012, Sekta ya Viwanda ilikua kwa asilimia8.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.8 mwaka 2011.Kiwango hicho kimetokana na kuongezeka kwa shughuli zauzalishaji viwandani hususan usindikaji wa vyakula,utayarishaji wa vyakula vya wanyama, mafuta ya alizeti,uzalishaji wa vinywaji, saruji na bidhaa za chuma. Pamojana ukuaji wa sekta kuongezeka, bado ongezeko hilo liko chiniya lengo la asilimia 15 lililoainishwa katika Dira ya Taifa yaMaendeleo (Vision 2025). Mchango wa Sekta ya Viwandakatika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 9.7 mwaka2011 na kufikia asilimia 9.85 mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012,uzalishaji katika baadhi ya viwanda kama vile vya chuma,vinywaji na sigara uliongezeka. Ongezeko hilo lilitokana nakuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hizo katika soko la ndani.Uzalishaji wa chuma uliongezeka kwa asilimia 16.9 kutokatani 39,955 mwaka 2011 hadi kufikia tani 46,690 mwaka 2012.Uzalishaji wa bati uliongezeka kwa asilimia 5.9 kutoka tani76,912 mwaka 2011 hadi tani 81,427 mwaka 2012. Uzalishajiwa saruji uliongezeka kwa asilimia 7.2 kutoka tani milioni 2.4mwaka 2011 hadi tani milioni 2.6 mwaka 2012. Uzalishaji wanyavu za uvuvi uliongezeka kwa asilimia 79.9 kutoka tani164 mwaka 2011 hadi tani 295 mwaka 2012. Vilevile, uzalishajiwa bia uliongezeka kwa asilimia 4.7 kutoka lita milioni 323.4mwaka 2011 hadi kufikia lita milioni 338.7 kwa mwaka 2012na uzalishaji wa sigara uliongezeka kutoka sigara milioni 6,630mwaka 2011 hadi kufikia sigara milioni 7,558 mwaka 2012,sawa na ongezeko la asilimia 14.0, na uzalishaji wa konyagiuliongezeka kwa asilimia 8.7 kutoka lita milioni 15.4 mwaka2011 hadi lita milioni 16.8 mwaka 2012.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012, Sektaya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo imechangia asilimia27.9 katika Pato la Taifa. Sekta hiyo imeajiri Watanzania

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

46

milioni 5.2 wanaofanya kazi katika jasiriamali (enterprises)zipatazo milioni tatu. Kati ya hizo, jasiriamali 1,675,385 zikovijijini, jasiriamali 466,049 zipo Dar es Salaam na zilizobaki935,256 zipo katika maeneo mengine ya mijini. Asilimia 54.3ya jasiriamali hizo zinamilikiwa na wanawake na asilimia 45.7zinamilikiwa na wanaume. Shughuli za uzalishaji na kuongezathamani zinachukua asilimia 13.6 ya jasiriamali hizo. Hiiinaashiria kwamba msukumo mkubwa zaidi unahitajikakatika kukuza sekta ya uzalishaji na uongezaji thamani ili iwezekutoa mchango zaidi katika ajira na pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Biashara kwaujumla ilikua kwa asilimia 7.7 kwa mwaka 2012 ikilinganishwana ukuaji wa asilimia 8.1 mwaka 2011, ikiwa ni pungufu kwaasilimia 0.4. Hii ni kutokana na kushuka kwa bei ya baadhi yamazao katika soko la kimataifa kama vile pamba (asilimia18.3), korosho (asilimia 1.9), karafuu (asilimia 14.9), kahawa(asilimia 6.9) na madini (asilimia 4.2). Aidha, mchango wasekta katika pato la Taifa ulikuwa asilimia 12.3 mwaka 2012ikilinganishwa na asilimia 12.2 mwaka 2011.

Mheshimiwa Mwenyekiti, thamani ya mauzo njeiliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 5,097.3 mwaka2011 hadi Dola za Marekani milioni 5,912.3 mwaka 2012, sawana ongezeko la asilimia 16. Ongezeko hilo lilitokana nakuongezeka kwa wingi wa bidhaa zilizouzwa nje. Kwamfano, mauzo ya pamba yaliongezeka kutoka tani 40,300mwaka 2011 hadi tani 132,000 mwaka 2012, ikiwa ni ongezekola asilimia 227.4.

Vilevile, mauzo ya pamba yaliongezeka kutoka Dolaza Marekani milioni 61.1 mwaka 2011 hadi Dola za Marekani164.9 mwaka 2012, sawa na ongezeko la asilimia 167.6.Thamani ya mauzo ya bidhaa za viwandani iliongezekakufikia Dola za Marekani milioni 1,047.3 mwaka 2012ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 861.5 mwaka 2011,sawa na ongezeko la asilimia 21.6. Takwimu hizo na za miakaya nyuma zinadhihirisha kuwa bei ya bidhaa za viwandanizimekuwa haziyumbi ikilinganishwa na mazao ghafi. Serikaliinaendelea kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

47

kuongeza thamani mazao ili kupunguza uuzaji wa bidhaana mazao ghafi nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nije kwenye Sekta yaMasoko. Bei ya mazao makuu ya chakula ya mahindi,mchele, maharage, ngano, ulezi, na mtama zimeongezekakatika kipindi cha mwaka 2012/2013. Kwa mfano, wastaniwa bei ya jumla kwa gunia la mahindi la kilo 100 ilipandakutoka Sh. 43,309/= mwaka 2011/2012 na kufikia Sh. 65,028.3mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 50.2; na beiya gunia la maharage la kilo 100 il ipanda kutokaSh. 123,606/= hadi Sh. 131,336.90 sawa na ongezeko la asilimia6.89. Kupanda kwa bei ya mazao makuu ya chakula pamojana sababu nyingine ni kutokana na kupanda kwa bei yamafuta ya petroli kulikosababisha ongezeko la gharama zauzalishaji na usafirishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei ya baadhi ya mazao yabiashara kama vile chai, kahawa aina ya robusta na mkongeziliongezeka katika kipindi cha mwaka 2012/2013, kutokanana ongezeko la bei za mazao katika soko la nje. Kwa mfano,bei ya zao la chai ilikuwa wastani wa Sh. 206/= kwa kiloikilinganishwa na wastani wa Sh. 196/= mwaka 2011/2012,sawa na ongezeko la asilimia 5.1. Vilevile, bei ya mkongeilipanda hadi Sh. 1,249.80 kwa kilo ikilinganishwa naSh. 1,114/= mwaka 2011/2012, sawa na ongezeko la asilimia12.2. Bei ya mbegu ya pamba ilipanda kutoka wastani waSh. 1,000/= mwaka 2011/2012 mpaka Sh. 1,200/= kwa kilomwaka 2012/2013, sawa na ongezeko la asilimia 20.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,kumekuwa na ongezeko la bei ya mifugo kwa ng’ombe,mbuzi na kondoo. Kupanda kwa bei hizo kumechangiwana ongezeko la ubora wa mifugo na ongezeko la mahitaji.Wastani wa bei ya jumla ya ng’ombe daraja la pili iliongezekahadi Sh. 480,467/= ikilinganishwa na Sh. 427,438/= mwaka 2011/2012, sawa na ongezeko la asilimia 12.41. Bei ya ng’ombedaraja la tatu il ipanda hadi Sh. 367,393/= kutokaSh. 328,151/= mwaka 2011/2012, sawa na ongezeko la asilimia11.96. Bei ya mbuzi ilipanda hadi Sh. 46,576/= kutoka

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

48

Sh. 42,323/= mwaka 2011/2012, sawa na ongezeko la asilimia10.05, wakati bei ya kondoo ilipanda hadi Sh. 38,482/= kutokaSh. 37,078/= katika kipindi hicho hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa maelekezoya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Wizara kwakushirikiana na Taasisi 18 zilizo chini Wizara yangu, imeendeleakutekeleza malengo ya Sekta za Viwanda, Biashara, Masokona Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo kamayalivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitanowa Wizara (Strategic Plan 2011/2012 – 2016/2017) ambaoumezingatia utekelezaji wa maelekezo ya Ilani ya Uchaguziya CCM. Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka2010, umewezesha kupatikana kwa mafanikio mbalimbaliya kisekta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha ushiriki waSekta Binafsi katika uwekezaji na biashara katika soko laushindani, Wizara imechukua hatua kuimarisha ushiriki waSekta Binafsi katika uwekezaji na biashara ili kushiriki vyemakatika soko la ushindani. Hatua zilizochukuliwa ni pamojana kuipa nguvu ya kisheria Mamlaka ya Maeneo Huru yaUzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA) kusimamia uwekezaji katikaMaeneo Maalum ya Uwekezaji (Special Economic Zones – SEZ).

Katika maeneo hayo, wawekezaji wa sektambalimbali wataweza kuzalisha na kuuza bidhaa katikamasoko ya ndani na nje ya nchi. Wizara kupitia EPZA kwakushirikiana na Serikali za Mitaa, imeendelea na jitihada zakutenga maeneo maalum ya uwekezaji katika Mikoailiyobaki ya Simiyu, Katavi, Geita na Njombe. Vilevile, EPZAimelipa fidia katika maeneo ya SEZ ya Mbegani - Bagamoyona Ujiji - Kigoma. Jitihada za kutafuta fedha kwa ajili yamaeneo ya Bandari - Mtwara, Bunda - Mara, Mererani –Manyara na mengineyo zinaendelea. Pia, NDC imetengamaeneo kwa ajili ya kuvutia uwekezaji: TAMCO - Kibaha,Kange - Tanga na KMTC - Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kujenga naKuimarisha Ujuzi Katika Biashara na Kuweka Msukumo Zaidi

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

49

Katika Kutumia Fursa za Masokol; katika mwaka 2012/2013,Wizara kupitia Chuo cha Elimu ya Biashara (College of BusinessEducation – CBE) imeendesha mafunzo ya ujasiriamali yamuda mfupi ambapo jumla ya washiriki 53 walipata mafunzohayo. Mafunzo yalihusu mbinu za kubuni biashara, namnaya kupata mtaji, ujuzi wa kusimamia na kuendeleza biashara,utafutaji masoko na stadi za kuimarisha ubora wa bidhaa.Vilevile, SIDO iliendesha mafunzo kwa wajasiriamali 4,766katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na kutoa elimu yaujasiriamali, uongozi wa biashara, stadi za kazi, usindikaji wavyakula, ujuzi wa kiufundi katika uzalishaji wa mafuta ya kula,ngozi, ubanguaji korosho na uhifadhi wa vyakula vya ainambalimbali.

Chini ya Mradi wa EDF10, jumla ya Wajasiriamali 125na Maafisa Biashara 16 kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Kanda ya Kusini na Kanda ya Ziwa walipata mafunzo chiniya uwezeshaji wa wataalam kutoka SIDO, BRELA, GS1 na TBS.Mafunzo yalihusu utumiaji wa nembo za ubora, kuwekamipango ya biashara vizuri na kuitekeleza, kudhibiti uborawa bidhaa, utengenezaji na utunzaji wa mitambo naujasiriamali. Aidha, mafunzo hayo yamewezesha wajasiriamalikuanza na kuweza kuuza bidhaa zao kwenye ‘Supermarkets”.Vilevile, Wizara kupitia SIDO iliweza kutoa huduma za uganikwa wajasiriamali 9,660 nchini kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakuimarisha na kuwezesha Kituo cha Mafunzo na Uzalishajiwa Bidhaa za Ngozi Dodoma, DIT kampasi ya Mwanza hapoawali ikiitwa Tanzania Institute of Leather Technology (TILT)na Vituo vya Chama cha Wadau wa Ngozi Tanzania (LeatherAssociation of Tanzania - LAT) vya Dar es Salaam na Morogoro.Vituo hivyo vilitoa mafunzo ya usindikaji wa ngozi nautengenezaji wa bidhaa za ngozi kwa washiriki 351 katikaMikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Iringa, Mbeya, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga, Dodoma naTabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ina sera, mikakati,sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza Sekta za Viwanda,

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

50

Biashara, Masoko na Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo,ambazo ndiyo msingi wa kuimarisha uendelezaji na ukuzajiwa mauzo nje.

Katika kuendeleza na kukuza mauzo nje, Wizaraimetayarisha na kusimamia utekelezaji wa Mkakati waKukuza Mauzo Nje unaojumuisha Mfumo wa KuendelezaUzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZ), Maeneo Maalum yaKiuchumi (SEZ), Masoko ya Mipakani (Border Markets), Kamatiya Kitaifa na za Kikanda (EAC na SADC) za Kuondoa VikwazoVisivyo vya Kiushuru (Non Tariff Barriers-NTBs), Vituo vya Pamojavya Mipakani (One Stop Border Posts - OSBPs), Alama yaUtambuzi wa Bidhaa (GS1), Kamati za Pamoja Mipakani (JointBorder Committees - JBCs) na Mfumo wa Stakabadhi zaMazao Ghalani.

Vilevile, kwa kutambua umuhimu wa biashara katikamazingira ya utandawazi, Wizara inaandaa Mfumo wa Sokola Bidhaa (Commodity Exchange) na kutumia mfumo wauhamasishaji biashara na masoko kupitia maonesho ya kitaifana kimataifa (Trade Fairs, Exhibitions, Expos and TradeMissions).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuimarisha kifedhaBenki ya Maendeleo TIB ili Kiwe chombo madhubuti chakuchochea mapinduzi ya viwanda nchini kwa kutoa mikopoya muda mrefu na riba nafuu kwa wawekezaji wakubwa,wa kati na wadogo nchini kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imelenga kuiongezeaBenki ya Maendeleo TIB mtaji wa Shilingi bilioni 500 katikakipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2010, ili kuimarishauwezo wa utoaji mikopo ya muda mrefu kwa wawekezajihususan kwenye kilimo na viwanda. Mwaka 2010/2011, Serikaliilitoa jumla ya Shilingi bilioni 50 na mwaka 2012/2013, Shilingibilioni 50. Hadi sasa, Serikali imekwishatoa Shilingi bilioni 100kwa Benki hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee kuhusukuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe ya mchuchuma,

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

51

chuma cha liganga na viwanda vya kemikali na mboleakatika kanda za maendeleo kikiwemo kiwanda cha mboleaaina ya urea Mkoani Mtwara na kuwezesha Kiwanda chaMinjingu kuzalisha mbolea bora ya NPK na MPR ili kufikia lengolililowekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia kusainiwa kwamkataba wa ubia kati ya NDC na Kampuni ya SichuanHongda Group, tarehe 21 Septemba, 2011, Kampuni ya ubiaiitwayo Tanzania China International Mineral ResourcesLimited (TCIMRL) ilianzishwa kwa ajili ya kutekeleza Miradi yaMakaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Ligangakwa mfumo unganishi.

Mradi wa Makaa ya Mawe unatarajiwa kuzalishaumeme wa megawati 600 ambao utatumika katikauchenjuaji na uyeyushaji wa madini ya chuma na ziadakuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Tayari uchorongaji wamakaa ya mawe ili kubainisha wingi na ubora umekamilikaambapo makaa yaliyohakikiwa yanatosheleza kuzalishaumeme wa megawati 600 kwa kipindi cha miaka 80.Kampuni ya TCIMRL inatarajia kufua umeme kwa kuanzia naMegawati 300 mwaka 2015/2016.

Kazi ya uchorongaji kwa upande wa chuma chaLinganga inaendelea na inatarajiwa kukamilika Desemba,2013. Ujenzi wa mgodi unatarajiwa kuanza Januari, 2014, iliuzalishaji wa chuma uanze mwaka 2015/2016. Awaliilipangwa kuzalisha tani 500,000 za chuma kwa mwaka, lakinibaada ya tafiti za mahitaji ya soko, kiwandakitakachojengwa kinatarajiwa kuzalisha tani milioni moja zachuma kwa mwaka.

Hata hivyo, utekelezaji wa mradi unakabiliwa nachangamoto ya ubovu wa barabara hususan eneo la Itoni –Mchuchuma – Liganga ambapo Serikali ilikubali kutoa Shilingibilioni 1.7 mwaka 2012/2013 kukarabati eneo hilo. Wizarainashirikiana na Hazina kuharakisha upatikanaji wa fedha hizoili kuimarisha barabara katika eneo hilo na kurahisishausafirishaji wa mitambo mikubwa.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

52

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika juhudi za kuanzishaviwanda vya kemikali na mbolea kwa kutumia gesi asili yaMtwara, makampuni matatu kati ya 10 yaliyojitokezayalichaguliwa katika awamu ya kwanza ili baadaye yachujwekupata mwekezaji mahiri. Makampuni hayo ni DeepakFertilizer and Petrochemical Ltd ya India; TATA Chemicals Ltdya India na Polyserve Group Ltd ya Misri.

Hata hivyo, hatua ya kushindanisha makampunimatatu haikufikiwa kufuatia makubaliano kati ya Kampuniya Wentworth Resources Limited (WRL) na Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC) ya kuanzisha kiwanda cha mboleakwa kutumia gesi asili. Tayari upembuzi yakinifu na uchimbajiwa visima zaidi vya gesi ili kupata malighafi ya kutosha yakuzalisha mbolea aina ya Urea na kemikali ya Methanol kwamatumizi ya viwanda umefanyika. Kutokana na tatizo kubwala umeme nchini, kipaumbele cha kutumia gesi asili ya MnaziBay kimeelekezwa kwenye uzalishaji wa umeme na hivyokuleta changamoto ya uanzishaji wa viwanda vya Urea nakemikali ya Methanol.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kampuni ya Minjingu Minesand Fertilizer Ltd (MMFL) inayozalisha mbolea aina ya MinjinguRock Phosphate (MRP), ilifanya upanuzi wa kiwanda na sasakina uwezo wa kuzalisha tani 100,000 za MRP kwa mwakaikilinganishwa na tani 75,000 za awali. Kufuatia kuboreshwakwa mbolea ya MRP kwa kuongezwa virutubisho vya sulphurna micro nutrients za zinc (Zn), boron (B), magnesium (Mg) nakuongeza wingi wa nitrogen (N) hadi kufikia asilimia 10 naSerikali kutoa ruzuku kwa mbolea ya Minjingu - Mazao,mahitaji yameongezeka. Mbolea ya MRP iliyoboreshwa(Minjingu - Mazao) ina ubora sawa na NPK.

Hivyo, MMFL wana mpango wa kupanua uwezo wauzalishaji hadi tani 600,000 kwa mwaka. Kwa upandemwingine, Kampuni ya Paradeep Phosphate Ltd kutoka Indiaimekwishaleta maombi ya kuwekeza katika utengenezaji wambolea katika Kanda ya Kusini. Kiwanda hicho kinatarajiakuzalisha tani 750,000 za mbolea kwa mwaka na kitagharimuDola za Marekani Shilingi bilioni 1.5 na kuajiri watu 3,000.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

53

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vilivyobinafsishwachini ya Sekta ya Viwanda na Biashara ni 74 na kati yake niviwanda 17 tu ndivyo havifanyi kazi. Juhudi za kufufuaviwanda hivyo zinafanyika chini ya Consolidated HoldingCorporation (CHC) iliyoko chini ya Wizara ya Fedha, kwakuzingatia utaratibu wa urekebishaji wa mashirika ya umma.Hivi sasa, majadiliano yanaendelea kwa kushirikiana nawadau mbalimbali na wamiliki wa viwanda hivyo il ikukubaliana jinsi ya kuvifufua. Ni matarajio ya Wizara kuwazoezi linaloendelea litakamilika haraka iwezekanavyo iliufufuaji wa viwanda hivyo uanze. Kama inavyoonekana, niviwanda vichache (17) havifanyi kazi lakini wakati huo huomiradi mipya iliyopata leseni ya kuanzisha viwanda nitakribani 542 katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine linahusu kuboreshavivutio kwa aji l i ya uwekezaji kwenye viwandavitakavyotumia malighafi mbalimbali zi l izopo nchinivikiwemo viwanda vya nguo, ngozi, usindikaji matunda,mbogamboga na usanifu wa madini ya vito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika jitihada za kukuzauwekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani katikamazao, madini ya vito na Ngozi, Wizara imeendeleakushirikiana kwa karibu na Wizara ya Fedha ili kutoa vivutiombalimbali kwa wawekezaji. Vivutio hivyo ni pamoja namisamaha ya kodi kwa wawekezaji wanaozalisha bidhaana kuuza nje kupitia mfumo wa EPZ, kuandaa maeneo nakuyawekea miundombinu ya msingi kama maji, umeme nabarabara kama ilivyofanyika katika eneo la uwekezaji laMheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa na kuboresha mazingiraya uwekezaji kwa kupunguza muda wa kusajili makampuniyanayowekeza katika maeneo ya EPZ, muda wa kutoa lesenina muda wa kufungua na kufunga biashara katika maeneohayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Mamlaka yaEPZ imeendelea kubainisha maeneo ya uwekezaji ya EPZ naSEZ na kuhamasisha uwekezaji ndani ya maeneo hayo. Kwamwaka 2012/2013, makampuni 29 yamepewa leseni za

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

54

kujenga viwanda chini ya EPZA na tayari makampuni matanoyamekwishaanza uzalishaji. Makampuni hayo yatawekezamtaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 113 na kuajiriwatu 9,254. Idadi hiyo itafanya jumla ya makampuniyanayozalisha chini ya EPZ kufikia 70, jumla ya mtajiuliowekezwa kufikia Dola za Marekani bilioni moja na jumlaya ajira za moja kwa moja kufikia 23,000.

Vilevile, ujenzi wa miundombinu ya maji machafukatika Eneo Maalum la Uwekezaji la Benjamin William MkapaSpecial Economic Zones (BWM-SEZ) umekamilika ambapoviwanja 18 katika eneo hilo vimetolewa kwa wawekezaji.Maeneo mapya ya SEZ na EPZ yanayoendelea kujengwa nasekta binafsi kwa mwaka 2012/2013 ni Rusumo Falls SEZ(Kagera) na Kamal EPZ Industrial Park, Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendeleakuimarisha Sekta ya Ngozi kwa kutekeleza Mkakati wa Kufufuana Kuendeleza Sekta na Viwanda vya Ngozi Nchini. Kutokanana jitihada hizo, Sekta Ndogo ya Usindikaji wa Ngoziimeongeza viwanda kutoka vitatu vya awali hadi viwandanane mwaka 2012/2013 vyenye uwezo uliosimikwa (installedcapacity) wa kusindika vipande vya ngozi milioni 12.4 kwamwaka kufikia hatua ya awali (Wetblue). Kati ya hivyo,vipande vya ngozi za ng’ombe ni milioni 1.7 na vya mbuzina kondoo ni milioni 10.7.

Hata hivyo, matumizi halisi ya uwezo (capacityutilisation) kwa mwaka 2012 ni wastani wa vipande milioni6.6 vya ngozi vikijumuisha vipande 936,000 vya ngozi zang’ombe na milioni 5.7 vya ngozi ya mbuzi na kondoo.Usindikaji umewezesha ongezeko la thamani ya ngozizilizouzwa nje ya nchi kutoka Shilingi bilioni 10.6 mwaka 2011hadi Shilingi bilioni 62.3 mwaka 2012. Vilevile, sekta hiyoimewezesha kuongezeka kwa ajira kutoka watu 1,500 mwaka2011 hadi 2,000 mwaka 2012. Wizara kwa kushirikiana na LATimewawezesha wadau wapatao 38 kushiriki Maonesho yaSaba Saba (Dar es Salaam International Trade Fair) na wadau18 kushiriki Maonesho ya Nane Nane.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

55

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012/2013, Serikaliiliongeza ushuru kwa ngozi ghafi zinazouzwa nje kutokaasilimia 40 hadi asilimia 90 au Sh. 400/= hadi Sh. 900/= kwakilo kulingana na ni ipi kubwa. Matokeo ya hatua hiyo niongezeko la usindikaji wa ngozi ghafi ndani ya nchi kutokavipande vya ngozi za ng’ombe 166,773 kati ya Januari naJuni, 2012 hadi vipande 343,860 kwa kipindi cha Julai hadiDesemba, 2012. Usindikaji wa ngozi za mbuzi na kondoo naouliongezeka kutoka vipande 778,023 hadi vipande 1,173,875kwa vipindi hivyo. Hilo ni ongezeko la vipande 177,087 vyang’ombe, sawa na asilimia 106.18 na vipande 395,852 vyambuzi na kondoo sawa na asilimia 50.88. Thamani ya mauzonje ya ngozi zilizosindikwa yalifikia jumla ya Shilingi bilioni 50.85(ngozi za ng’ombe Shilingi bilioni 32.25 na ngozi za mbuzi nakondoo Shilingi bilioni 18.6) katika kipindi cha Julai, 2012 hadiFebruari, 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi mipya ya viwandavya ngozi inayoendelea kujengwa ni pamoja na MERUTANNERY LIMITED yenye uwezo wa kusindika ngozi zang’ombe vipande 156,000 kwa mwaka na vipande vya ngoziza mbuzi 468,000 kwa mwaka. Kwa sasa ujenzi wa majengoumekamilika, usimikaji wa drums zipatazo 10 unaendelea nauzalishaji unatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2013. Kiwandakitaajiri wafanyakazi 30 kwa kuanzia.

Mradi mwingine ni Kiwanda cha Xinghua InvestmentCo. Ltd, kinachojengwa Mkoani Shinyanga. Kiwanda hichoni kikubwa chenye uwezo wa kusindika ngozi za ng’ombevipande 936,000 kwa mwaka na ngozi za mbuzi na kondoovipande milioni 2.2 kwa mwaka. Kiwanda hicho kinaendeleana ujenzi wa majengo na usimikaji wa drums kubwa zipatazo38. Ujenzi unatarajiwa kukamilika na kuanza usindikaji mweziAgosti, 2013. Usindikaji wa ngozi utafanyika hadi hatua yamwisho (finished leather) na kitaajiri wafanyakazi 500.Viwanda hivyo vikikamilika na kuanza uzalishaji kuna uhakikawa kusindika ngozi zote zinazozalishwa hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

56

na Uvuvi na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu, Dodoma(Capital Development Authority-CDA) imetenga eneo lenyeukubwa wa ekari takriban 110 kwa lengo la kuanzisha nakuendeleza Vijiji vya Viwanda (Industrial Villages). Maeneohayo ni maalum kwa ajil i ya kuchochea na kuvutiawawekezaji katika viwanda vya bidhaa za ngozi nchini. Tayarikazi za kupima, kuweka mipaka na kuandaa michoro/ramani ya eneo husika imefanyika na hati miliki imepatikana.Manispaa ya Singida nayo imetenga eneo lenye ukubwa waekari 120 katika Kata ya Ng’aida kwa ajili ya kuanzisha nakuendeleza Kijiji cha Viwanda vya kusindika ngozi nakutengeneza bidhaa za ngozi. Upimaji wa eneo na uidhinishajiwa mchoro wa eneo husika unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana nawadau kikiwepo Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na Mamlakaya EPZ imeendelea kuandaa taarifa mbalimbali ikiwa nipamoja na machapisho, majarida na business profiles pamojana matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu fursa zauwekezaji katika miradi ya viwanda kwa lengo lakuhamasisha na kuvutia uwekezaji nchini. Kutokana najuhudi hizo, kwa kipindi cha Julai, 2012 hadi Machi, 2013, Kituocha Uwekezaji nchini kilisajili jumla ya miradi ya viwanda 157na Mamlaka ya EPZ ilisajili jumla ya miradi 29 na kufanya jumlaya miradi iliyosajiliwa katika Sekta ya Viwanda kuwa 186.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sekta yaViwanda Vidogo na Biashara Ndogo na kuendelezaProgramu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini kwa KutoaUshauri, Mafunzo, Mitaji na Huduma za Kiufundi kwaWajasiriamali, Wizara imeendelea kusimamia na kuratibuutekelezaji wa Programu ya Muunganisho wa UjasiriamaliVijijini (MUVI) inayotekelezwa kwa kuzingatia mlolongo wathamani kwa mazao ya alizeti, mihogo, mifugo, matundana nyanya ili kuongeza vipato vya wakulima na kupunguzaumasikini. Programu hiyo inatekelezwa katika Mikoa sitaikijumuisha Wilaya 19 ambazo ni Iringa Vijijini na Kilolo, Mkoawa Iringa; Simanjiro, Hanang na Babati, Mkoa wa Manyara;Bagamoyo, Rufiji na Mkuranga, Mkoa wa Pwani; SongeaViji j ini, Namtumbo na Mbinga, Mkoa wa Ruvuma;

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

57

Sengerema, Kwimba na Ukerewe, Mkoa wa Mwanza;Muheza, Korogwe, Kilindi na Handeni, Mkoa wa Tanga; naWilaya ya Njombe ambayo kwa sasa iko Mkoa mpya waNjombe.

Katika mwaka 2012/2013, vyama na vikundi vyawazalishaji na wakulima 54 vimewezeshwa kuanzisha vikundimama vya ujasiriamali. Pia, programu imewezeshaupatikanaji wa pembejeo hasa mbegu za alizeti (tani 4900)na vipande milioni 2.2 vya mbegu za muhogo. Vilevile,programu imeanzisha mashamba darasa; vitalu vya micheya maembe, michungwa na milimao yenye jumla ya miche220,000. Shamba la majaribio ya malisho ya mifugo ekari sitalimeanzishwa, wafugaji 48 wamewezeshwa kufanya safariya mafunzo ya mbinu za kisasa za kufuga, kuchinja nakutunza malisho na mazingira. Majukwaa ya kuratibu shughuliza sekta za mazao matano yaliyochaguliwa katika ngazi yaMkoa na Wilaya yaliendelea kukutana na kujadili mambombalimbali ya kuendeleza mazao husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa MUVIumewaongezea tija walengwa hususan katika uzalishaji wambegu bora za alizeti aina ya RECOD iliyobuniwa na ChuoKikuu cha Kilimo cha Sokoine. Mbegu hiyo imewawezeshawasindikaji kukamua lita 20 za mafuta ya alizeti kutoka katikakila kilo 50 za mbegu bora ukilinganisha na kilo 80 mpaka 90za mbegu za zamani. Wakulima wa Hanang‘ wamebunimradi wa kutengeneza mkaa wa kupikia kutokana namakapi ya mbegu za alizeti. Katika Mkoa wa Iringa tijaimeongezeka kwa wakulima wa nyanya na sasa wamewezakupata kwa wastani Shilingi milioni 15 kwa ekari ya mbegubora ya nyanya ikilinganishwa na chini ya Shilingi milioni 10hapo awali. Vilevile, tija imeongezeka kwa wakulima wambegu mpya ya muhogo kutoka Mkoa wa Mwanza na sasashina moja linatoa hadi kilo 10 za muhogo ikilinganishwa nambegu asilia inayotoa hadi kilo nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuongeza mchangowa Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (SMEs) katika Patola Taifa kutoka asilimia 33 ya GDP hivi sasa kufikia asilimia 40

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

58

mwaka 2015; Kama nilivyoeleza katika hotuba yangu yamwaka 2012/2013, ilibainika kuwa mchango halisi wa sektakatika Pato la Taifa ni asilimia 27.9 badala ya makadirio yaawali ya asil imia 33. Wizara imeendelea kusimamiamaendeleo ya Sekta hiyo na kuhakikisha uchangiaji wakeunaongezeka kwa kuhamasisha uanzishaji wa ViwandaVidogo na Biashara Ndogo na kuimarisha ukuaji wa viwandavidogo vilivyopo kupitia mikakati na programu mbalimbaliikiwemo ODOP na MUVI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya teknolojia mpya 159zimepatikana kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili yamatumizi ya miradi ya uzalishaji katika kipindi cha mwaka2012/2013. SIDO kupitia vituo vyake vya uendelezaji wateknolojia vilivyopo Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Lindi, Kigomana Shinyanga iliwezesha utengenezaji na usambazaji kwawatumiaji mashine mpya 462 za kuongeza thamani mazaona bidhaa pamoja na vipuri 2,631.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutoa elimu nakuwajengea uwezo wakulima wa kusindika mazao kablaya kuyauza kama vile usindikaji wa asali, utengenezaji wamvinyo, utengenezaji wa juisi pamoja na ufungashaji wabidhaa kwa kutumia teknolojia ya TBS ; Wizara kwakushirikiana na SIDO imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwaWajasiriamali i l i kuwaimarisha katika kuendesha nakuendeleza shughuli za biashara na miradi ya uzalishaji.Mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na usindikaji wa nafaka namatunda kwa wajasiriamali 857 na usindikaji wa ngozi nabidhaa zake kwa wajasiriamali 1,431. Mafunzo ya ujuzimaalum pia yalitolewa kuhusu usindikaji wa mafuta ya alizeti,utengenezaji sabuni, mishumaa, chaki, utengenezaji wamizinga ya kisasa ya usindikaji wa asali.

Vilevile, jumla ya wajasiriamali 8,382 kupitia kozi 408wamepata mafunzo ya maarifa na stadi za kuimarishashughuli zao za uzalishaji mali. Wizara imeendelea kuongezamtaji wa Mfuko wa Wafanyabiashara Wananchi (NEDF) ilikuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata mikopo yakuwawezesha kuwekeza katika miradi ya kuongeza thamani.

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

59

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia SIDO,imewaunganisha wazalishaji wadogo na makampunimakubwa na ya kati kwa nia ya kuwawezesha kupatateknolojia, ujuzi na masoko. Wajasiriamali 134wameunganishwa na makampuni mbalimbali kwa ajili yakuwauzia bidhaa na huduma zao.

Baadhi ya viwanda hivyo ni vya kusindika mafuta yakupikia, bidhaa za plastiki, kuchambua pamba, saruji, biana soda na wameunganishwa na supermarkets katika Mikoaya Mbeya, Iringa, Tanga, Arusha, Dar es Salaam, Morogoro,Mwanza, Shinyanga, Singida na Manyara. Hatua hiyoimewasaidia wajasiriamali wadogo kuzalisha bidhaa zenyeubora na kukuza biashara na vipato vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakuijengea uwezo kwa kuwaongezea bajeti na kuwawezeshawatumishi wake kupata mafunzo mbalimbali. Katika mwaka2012/2013, SIDO ilitengewa Shilingi bilioni 7.664 ikilinganishwana Shilingi bilioni 6.420 zilizotengwa mwaka 2011/2012.

Wizara pia imeiwezesha SIDO kupeleka watumishi 157katika mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Jitihadanyingine ni kuendelea kuongezea mtaji Mfuko waWafanyabiashara Wananchi (National EntrepreneurshipDevelopment Fund - NEDF) na kushawishi wadau wamaendeleo kutekeleza programu zao kupitia SIDO, kwamfano, programu ya MUVI na Usindikaji wa Mazaoinayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA).

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya wajasiriamali 3,567nchini kote walipewa mikopo ya thamani ya Shilingi bilioni3.47 kupitia Mfuko wa NEDF kwa ajili ya kuendeshea miradiya uzalishaji na biashara. Kati ya mikopo hiyo, asilimia 33ilitolewa kwa miradi ya vijijini na asilimia 51 ilitolewa kwawanawake. Mfuko huo umetoa ajira kwa watu 7,192 wengiwao wakiwa ni wanawake sawa na asil imia 52 naumechochea ongezeko na ukuaji wa jasiriamali ndogoambazo zimechangia kupanua wigo wa kukusanya kodi namapato ya Serikali.

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

60

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2012/2013, Wizara kwa kupitia SIDO imehamasisha wananchikushiriki katika ujenzi wa kongano (industrial clusters) nailitenga Shilingi milioni 500 katika bajeti yake ili kuanza ujenziwa kongano katika Mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Manyara,Morogoro na Singida.

Hadi mwisho wa mwezi Desemba, 2012, Shilingi milioni80 zil ikuwa zimetolewa kwa aji l i ya ujenzi huo nazimewezesha kuanza ujenzi kwa hatua za awali katika Mikoaya Dodoma na Singida. Wizara inaendelea kushirikiana nawadau wengine wakiwemo Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa na Sekta Binafsi katika kutenga na kuendeleza maeneokwa ajili ya viwanda vidogo na biashara ndogo. Jumla yamaeneo 142 yametengwa na Halmashauri za Wilayambalimbali hadi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuhamasishamatumizi ya fursa za masoko ya ndani, kikanda na kimataifazikiwemo fursa za Masoko ya AGOA, EBA, China, Japan,Canada na India ili kukuza biashara ya nje kwa kiwangokikubwa; katika kipindi cha mwaka 2012/2013, Wizarailihamasisha jumuiya ya wafanyabiashara kuhusu fursa zamasoko ya bidhaa na huduma zilizopatikana kupitiamajadiliano ya kibiashara baina ya nchi na nchi, kikanda nakimataifa kwa kutoa taarifa hizo kwa wafanyabiasharakupitia taasisi zao. Taarifa za fursa hizo zimekuwa zikitolewakwa njia ya mikutano ya ana kwa ana, redio, magazeti,vipeperushi, maonesho ya biashara, semina na warsha zakikanda. Matokeo yake, mauzo ya bidhaa kwenye masokohayo ya upendeleo yamekuwa yakiongezeka kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mauzo ya bidhaa katikaSoko la Ulaya yalishuka kutoka Dola za Marekani milioni 1,382.0mwaka 2011, na kufikia Dola za Marekani milioni 744.2mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa kwenye Jumuiyaya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika yalikuwa Dola zaMarekani milioni 1,430.1 kwa mwaka 2012 ikilinganishwa naDola za Marekani 1,158.9 mwaka 2011, hivyo kuwa na urarichanya wa Dola za Marekani 327.7.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

61

Mheshimiwa Mwenyekiti, thamani ya mauzo yabidhaa za Tanzania katika soko la nchi za Jumuiya ya AfrikaMashariki yalikuwa Dola za Marekani milioni 613.3 kwa mwaka2012, ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 352.4 mwaka2011, ambapo manunuzi ya bidhaa ni Dola za Marekanimilioni 678.6 na kusababisha urari hasi wa biashara wa Dolaza Marekani milioni 65.3. Kushuka kwa mauzo yetu kwenyeSoko la EAC kulichangiwa na baadhi ya changamotoikiwemo tatizo la ushindani usio wa haki ambapo baadhi yanchi wanachama huingiza malighafi bila ushuru (Uganda list).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu imetoamafunzo ya mbinu mbalimbali za kuwajengea uwezowajasiriamali ili waweze kuyafikia masoko ya nje kwa njia yawarsha na semina. Mafunzo kuhusu utayari wa biashara namauzo ya nje (Training for Trade and Export Readiness)yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Maendeleo ya BiasharaTanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na SIDO na TBS yalitolewakwa wajasiriamali 55 katika Mikoa ya Arusha na Dar esSalaam. Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wajasiriamalikujua masharti na mahitaji ya soko hususan viwango vyaubora wa kimataifa ili kuziwezesha bidhaa kuhimili ushindani.Mafunzo mengine yalihusu namna ya kutoa taarifa kwaShirika la Biashara la Dunia (WTO) juu ya mabadiliko ya sheriaau hatua mbalimbali zinazochukuliwa na nchi wanachamakuhusu Sheria na Kanuni za WTO ili kuleta uwazi (transparency)katika biashara. Wadau 50 kutoka Wizara na Taasisi za Serikaliwalishiriki mafunzo hayo huko Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia majadiliano yaMkataba wa Ubia wa Uchumi kati ya Jumuiya ya AfrikaMashariki na Jumuiya ya Ulaya, nchi wanachama wa EACikiwemo Tanzania zimeendelea kunufaika na Soko la EU kwakuuza bidhaa zake bila kutozwa ushuru wala kuwekewaukomo. Vilevile, EU imekubali jedwali la miradi ya maendeleo(EAC Development Matrix) liwe sehemu ya Mkataba wa EPAna kuonesha nia ya kuifadhili miradi husika kwa kushirikianana nchi wanachama wa EAC. Majadiliano hayo badoyanaendelea katika maeneo ya Sura ya Uasili wa Bidhaa (Rulesof Origin), Muundo wa Kitaasisi na Utatuzi wa Migogoro,

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

62

Ruzuku katika Kilimo, Kodi kwa Mauzo ya Nje (Export Taxes)na suala la kutoa Upendeleo kwa Mataifa (Most FavouredNations – MFN).

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusainiwa Itifakiya Soko la Pamoja mwezi Novemba, 2009 na kuzinduliwamwezi Julai, 2010, nchi wanachama zimeendelea kurazinishasera zao ili kwenda sambamba na matakwa ya Itifaki yaSoko la Pamoja. Hatua ya Soko la Pamoja inategemewakuongeza zaidi fursa za masoko ya biashara ya huduma, sokola mitaji, uhuru wa watu kuingia nchi wanachama nakuanzisha shughuli za kiuchumi na uhuru wa kufanya kazipopote katika nchi wanachama. Kwa kutambua fursazitokanazo na Soko la Pamoja, Wizara kwa kushirikiana naTCCIA, CTI, TPSF, VIBINDO na TAFOPA imeendeleakuwahamasisha wafanyabiashara kuzichangamkia fursa hizokwa lengo la kuongeza kipato na hatimaye kuchangia katikaukuaji wa uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakutekeleza Itifaki ya Biashara ya Jumuiya ya Maendeleo yaNchi za Kusini mwa Afrika ikiwa ni pamoja na kuendelea namajadiliano kwa lengo la kuondoa vikwazo vya kibiasharavisivyokuwa vya kiushuru na ujenzi wa Vituo vya PamojaMipakani (OSBP) ili kurahisisha biashara kati ya nchi na nchi.Mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kufikiwakwa punguzo la ushuru wa bidhaa mwezi Desemba, 2012ambapo sasa bidhaa zote ziingiazo miongoni mwa nchiwanachama hazitozwi ushuru. Vilevile, nchi wanachamazimefanikiwa kukamilisha Itifaki ya Biashara ya Hudumaambayo inatoa mwanga kwa nchi wanachama kuanzakulegezeana masharti katika biashara ya huduma baada yakukamilika kwa uondoaji ushuru wa bidhaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2012/2013, Wizara imefanya utafiti juu ya gharama za kufanyabiashara nchini uliobainisha kuwepo vikwazo vya biasharavisivyo vya kiushuru kati ya Tanzania na nchi za Jumuiya yaAfrika Mashariki na kupendekeza njia za kuviondoa. Katikakushughulikia vikwazo hivyo, Wizara imeendelea kushiriki

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

63

vikao vya Kamati ya Kitaifa na ile ya Kikanda vyenye lengola kupokea taarifa, kufuatilia na kuondoa vikwazo hivyo.Wizara yangu ilifanikiwa kusaini Mkataba wa Ushirikiano naRwanda mwezi Oktoba, 2012 wenye lengo la kuondoleanavikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru na kukuzabiashara kupitia mipakani (Cross Border Trade). Kupitiamajadiliano hayo, wafanyabiashara wa Tanzania wameanzakufaidika kwa kuuza bidhaa zao Rwanda baada yakuondolewa kwa vikwazo hivyo. Vilevile, kupitia majadilianohayo Tanzania na Kenya mwezi Machi, 2013 zilisaini Hati yaMakubaliano (Memorundum of Understanding) yaliyowezeshaKenya kuondoa kikwazo kilichokuwa kinazuia bidhaa zamaua kutoka Tanzania kuingia Kenya wakati wa kusafirishwakwenda Ulaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia TanTrade inampango wa kuanzisha vituo vya biashara vya kanda katikaMikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza. TanTrade tayariimefanikiwa kupata jengo la kupanga NSSF, Mwanza kwaajili ya kituo cha biashara Kanda ya Ziwa na taratibuzinafanyika ili kupata fedha za kulipia kodi ya pango nakupata kibali cha kuajiri watumishi kwa ajili ya Ofisi hiyo mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jit ihada zakuhamasisha ushiriki wa wajasiriamali katika maonesho yabiashara kimataifa ndani na nje ya nchi, Wizara kupitiaTanTrade iliendelea kuwawezesha wajasiriamali kushirikikatika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) kwa kuwatengea maeneo; kuwapa mafunzo yaujasiriamali, mbinu za kibiashara, ufungashaji, mawasiliano;na mbinu za kupenya na kuyafikia masoko ya kimataifa.Wizara imekuwa ikiwawezesha kwa kuwatengea nakugharimia maeneo ya maonesho wajasiriamali wa Sektaya Ngozi na Bidhaa za Ngozi kushiriki katika Maonesho yaDITF.

Kufuatia juhudi hizo, katika Maonesho ya DITF ya 36ya mwaka 2012, washiriki wa ndani walikuwa 1,341 sawa naongezeko la asilimia 4.41 ikilinganishwa na washiriki 900 wamwaka 2011. Vilevile, Wizara kupitia TanTrade imeratibu ushiriki

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

64

wa wajasiriamali katika Maonesho ya Kimataifa ya Rwanda(Rwanda International Trade Fair - RITF) 2012 na ya Kimataifaya Nairobi (Nairobi International Trade Fair - NITF) 2012 ambapojumla ya wajasiriamali nane walishiriki Maonesho ya RITF na23 ya NITF.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendelea na utafitiwa masoko kwa kufuatilia mienendo ya bei ya mazao makuuya chakula na biashara, na bidhaa za viwandani kwa lengola kupanua wigo wa mahitaji na kuwapatia wazalishaji beinzuri zaidi. Bei ya mkulima kwa mazao makuu ya biasharayakiwemo kahawa aina ya arabica, chai, pamba, mkongena korosho iliongezeka kwa viwango tofauti. Bei ya mlajikwa mazao makuu ya chakula hususan mahindi, mchele,ngano, ulezi, mtama, maharage, uwele na sukari ziliongezekakatika msimu wa 2012/2013 ikilinganishwa na bei za msimuwa 2011/2012.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imefanya utafitikuwezesha kupata soko la tumbaku ya Tanzania nchini Chinana Uturuki. Wafanyabiashara kutoka China wameonesha niaya kununua tumbaku hiyo. Wizara inafanya pia juhudi zakuwezesha tumbaku ya Tanzania kuingizwa katika orodhaya bidhaa zinazoruhusiwa kuuzwa nchini China bila ushuruna ukomo (duty free quota free) kupitia Mkataba Maalumwa Upendeleo (Special Preferential Tariff Agreement).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naShirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO)na Sekta Binafsi kwa kuhusisha kikamilifu vyama vya wenyeviwanda na wafanyabiashara wa Tanzania Bara na Visiwanikama vile TPSF, CTI, TCCIA, ZNCCA, TAHA, TWCC, TeaAssociation of Tanzania na Cashewnuts Processors Associationimewezesha kuendeleza matumizi ya mfumo wa utambulishowa kitaifa kwa bidhaa kwa kutumia Nembo za Mistari (barcodes), kupitia kampuni ya GS1 (Tz) National iliyoanza kazirasmi Agosti, 2011. Matumizi ya mfumo huo umewezeshabidhaa za Tanzania kupenya kwa urahisi zaidi katika soko landani na Kimataifa. Hadi kufikia Machi, 2013, jumla ya

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

65

wazalishaji 370 wamesajiliwa na kutumia huduma hiyo nabidhaa 6,200 zimepata alama ya GS1. Baadhi ya viwandavinavyotumia mfumo huo ni Kampuni ya Chai ya Kagera(Kagera Tea Company), TBL, Konyagi Tz Ltd na SBC CompanyLtd.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naWizara za Sekta ya Kilimo, Sekta Binafsi, Washirika waMaendeleo, Asasi zisizo za Kiserikali na Taasisi za Elimu ya Juuimekamilisha Mkakati wa Masoko ya Mazao na Bidhaa zaKilimo ili kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Masoko ya Mazaona Bidhaa za Kilimo. Waraka wa Baraza la Mawaziri kutoataarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Masoko yaMazao na Bidhaa za Kilimo umeandaliwa na taratibu zakuridhiwa na Baraza la Mawaziri zinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelezamiundombinu ya masoko ya Mikoa na kuanzisha masokokatika vituo vya mipakani ili kukuza biashara ya ndani nakikanda, Wizara kwa kupitia Mradi wa District AgriculturalSector Investment Project (DASIP) inaendelea na maandaliziya kujenga masoko saba ya mipakani katika maeneo yaMtukula - Missenyi, Kabanga – Ngara; Nkwenda na Murongo– Karagwe; Mnanila – Buhigwe/Kasulu; Remagwe –Tarime naBusoka - Kahama. DASIP imeingia mikataba na WashauriWaelekezi wa kuandaa michoro na kusimamia ujenzi kwamasoko hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Mkakatiwa Kukuza Mauzo Nje na Mpango Unganishi wa Biashara;Programu ya Kuendeleza Sekta ya Biashara (Trade SectorDevelopment Programme - TSDP) iliandaliwa na kuwasilishwakwa Washirika wa Maendeleo (Development Partners - DPs)ili kupata fedha za kuitekeleza. Majadiliano na nchi yaSweden kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (SIDA)ambao wameonesha nia ya kugharimia eneo la kurazinishasheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa viwango vyamazao ya chakula na mifugo (Sanitary and Phytosanitary-SPS-standards) yanaendelea.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

66

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuendeleza biasharaya ndani ikiwa ni pamoja na kujenga dhana ya kutumiabidhaa zilizozalishwa Tanzania (Nunua Bidhaa za Tanzania);kutokana na Serikali kutambua umuhimu wa kukuza,kuendeleza na kulinda viwanda vya ndani, kuanziaSeptemba, 2012, Serikali ilifanya maamuzi kupitia Waraka waUtumishi Na. 1 wa Mwaka 2012 kuwa Ofisi za Serikali na Taasisizake zitanunua samani zilizotengenezwa na viwanda vyandani kwa kutumia malighafi za hapa nchini.

Sambamba na hilo, Wizara imeendelea kuhamasishawananchi kupitia majukwaa mbalimbali kupenda nakununua bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya ndanikwa kutumia kaulimbiu ya ‘Nunua Bidhaa za Tanzania JengaTanzania’. Kaulimbiu hiyo inakwenda sambamba nauboreshaji na ufungashaji wa bidhaa zinazozalishwa nawajasiriamali hapa nchini ambapo Wizara kupitia TBS imetoamafunzo ya ubora wa bidhaa na ufungashaji kwawajasiriamali wadogo 292 katika Mikoa ya Manyara, Mtwara,Singida na Tanga. Vilevile, sampuli za bidhaa 359 za Tanzaniazilipimwa katika maabara za TBS.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada za kuendeleakupanua wigo wa biashara mtandao, Wizara imefanikishamfumo wa utoaji wa taarifa zinazohusu masuala ya viwandana biashara kwa wadau kwa wakati, katika ngazi za Wilaya,Mkoa na Taifa. Vilevile, Wizara inazingatia matumizi yaTEKNOHAMA katika kupokea, kutunza na kusambaza taarifambalimbali zinazohusu Sekta. Wizara inatumia mtandao waintaneti na teknolojia ya simu za viganjani kusambaza taarifaza bei ya mazao ya kilimo na mifugo. Kwa upande wamifugo, taarifa za bei hupatikana pia kupitia tovuti:www.lmistz.net.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2012/2013,Wizara imeboresha Tovuti yake (www.mit.go.tz) ili kuongezaufanisi katika mawasiliano na utoaji taarifa kwa njia yamtandao. Wizara pia inaratibu uanzishwaji wa Tovuti yaBiashara ya Kitaifa - National Business Portal kwa kushirikianana Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma (PO -

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

67

PSM) na Wakala ya Serikali Mtandao (e-Goverment Agency -EGA). Zoezi la kufanya upembuzi yakinifu limeanza kwakumtumia Mtaalam Mwelekezi ambaye ameanza kazi mweziFebruari, 2013 na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo mwishonimwa mwezi Mei, 2013. Kazi ya uundaji wa National BusinessPortal itaanza baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara itashughulika nasuala la kupanua matumizi ya simu za viganjani katika kutoataarifa za bei ya mazao na masoko kwa wakati; aidha,kuangalia uwezekano wa kuanzisha mbao za matangazokatika ngazi ya Wilaya na Mkoa ili kutoa taarifa mbalimbaliikiwemo bei na masoko kwa wakati muafaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara katika kipindi chamwaka 2012/2013, imekamilisha Mkakati na Mfumo Mpanana Unganishi wa Taarifa za Masoko nchini (IMIS) kwakuwatumia wataalam waelekezi kutoka kampuni ya DataWorks Associates. Mfumo huo unalenga kuimarisha mifumoiliyopo ya ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za masoko.Hatua inayofuata ni kuufanyia majaribio mfumo huo nakuandaa Mwongozo wa Mtumiaji na Mwendeshaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarishausambazaji wa taarifa za masoko nchini hasa maeneo yavijijini, Wizara kwa kushirikiana na SIDO kupitia MUVI iliendeshamafunzo kwa wakusanya taarifa za masoko kutoka Mikoayote pamoja na Wilaya 19 zinazotekeleza Mradi wa MUVI.Wanahabari kutoka katika vituo vya redio za kijamii(Community Radios) nane walishiriki. Aidha, Wizara kupitiakampuni ya Nuru Infocom, ilitoa mafunzo juu ya utumiaji wasimu za viganjani katika ukusanyaji wa taarifa za masokokwa washiriki 80 yaliyofanyika mwezi Septemba, 2012.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyotamka katikahotuba yangu ya mwaka 2012/2013, Mamlaka ya Maendeleoya Biashara Tanzania (TanTrade) imeanzishwa na ilizinduliwarasmi tarehe 1 Julai, 2011. Mamlaka hiyo inaendelea nautekelezaji wa majukumu yake ambayo ni pamoja nakuendeleza biashara ya ndani na ya nje. Mamlaka pia,

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

68

imefungua Ofisi yake huko Zanzibar na inategemea kufunguamatawi huko Arusha, Mbeya na Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Bodi ya Stakabadhi ya Mazao Ghalani imetoa leseni zabiashara kwa maghala 44 na waendesha maghala 21.Makampuni mawili ya ukaguzi wa maghala yamepewa lesenikwa ajili ya ukaguzi wa maghala yanayohifadhi mazao.Mfumo wa Stakabadhi za Maghala umeendelea kupanukana unatekelezwa katika Mikoa ya Dodoma (mahindi);Kilimanjaro (mahindi, mpunga na kahawa); Lindi (korosho);Manyara (mahindi, mbaazi na pamba); Mbeya (mpunga);Morogoro (mpunga na mahindi); Mtwara (korosho); Pwani(korosho); Ruvuma (korosho); na Tanga (mahindi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi imeendelea kutoaelimu ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa wadau kwakutumia semina, matangazo katika redio na luninga,vipeperushi na Mikutano ya ana kwa ana. Mafunzo maalumyametolewa kwa Watendaji Wakuu wa Maghalayanayosajiliwa katika mazao ya korosho, mahindi nakahawa.

Vilevile, kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilayaza Kwimba, Magu na Misungwi na Taasisi za Fedha, Bodiimepanga kuendesha mafunzo kwa wakulima ili wawezekuuza mpunga kwa kutumia mfumo wa stakabadhi katikamsimu wa 2013/2014. Bodi itahamasisha matumizi ya mfumowa stakabadhi katika Mikoa ya Katavi na Sumbawanga kwamazao ya mahindi, mpunga, alizeti na ufuta. Tathmini yaawali ya ukaguzi wa maghala na kuangalia utayari wawakulima imekwishafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi kwa kupitia Mradi waAfrican Green Revolution Alliance (AGRA) imeandaa mfumowa kusajili, kutoa taarifa na udhibiti wa kumbukumbu zakiutendaji zinazohitajika kwa kila mwendesha ghala. Pamojana hilo, Bodi inaratibu uanzishwaji wa Electronic WarehouseReceipt System ambao utawezesha kukusanya taarifa ikiwani pamoja na kuandaa daftari la kumbukumbu za wadau.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

69

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuendeleza Miundombinuya Masoko ya Mikoa na Kuanzisha Masoko Mpakani kamavile Karagwe, Kigoma, Holil i, Horohoro, Namanga,Sumbawanga, Taveta na Tarakea. Uendelezaji wamiundombinu ya masoko ya Mikoa na kuanzisha masoko yamipakani ni kama nilivyoeleza kwa kina katika aya ya 65.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naSekta Binafsi ilianzisha Jukwaa la Wadau wa Masoko ya Mazaoya Kilimo (National Marketing Development Forum-NMDF)kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa masoko ya mazaoya kilimo. Katika mwaka huu wa fedha, Wadau walifanyamkutano wa nne wa jukwaa kujadili masuala ya maendeleoya masoko, uendeshaji, uratibu na ugharamiaji wa jukwaahilo. Taasisi ambazo Wizara inashirikiana nazo katikakuendeleza jukwaa ni pamoja na Mtandao wa Vikundi vyaWakulima Tanzania (MVIWATA), Rural Livelihood DevelopmentCompany (RLDC), Tanzania Horticulture Association (TAHA),Horticultural Development Council of Tanzania (HODECT),Agricultural Council of Tanzania (ACT), Tanzania AgriculturalMarket Development Trust (TAGMARK), Bodi za Mazao naVyama vya Ushirika.

Mafanikio ya ushirikiano huo ni pamoja naushirikishwaji wa wadau katika kuandaliwa kwa Mkakati waKuendeleza Mazao ya Bustani (Horticulture DevelopmentStrategy), maandalizi ya Mkakati wa Masoko ya Mazao,maandalizi ya Mkakati wa Mfumo Mpana na Unganishi waTaarifa za Masoko na mapitio ya utekelezaji wa Programuya Kuendeleza Sekta ya Kilimo kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha udhibitiwa bidhaa duni (substandard goods) kutoka nje ya nchi,Wizara kupitia Shirika la Viwango Tanzania imeendeleakuimarisha ukaguzi wa ubora wa bidhaa zinazoingiaTanzania kupitia mipaka yake. Shirika limefungua Ofisi tanokatika vituo vya mipakani vya Horohoro, Sirari, Holili,Namanga na Bandari ya Tanga. Kwa sasa, tathmini inafanyikakwa ajili ya kufungua Ofisi katika vituo vya Mtambaswala,Mtukula, Rusumo na Tunduma.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

70

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mapitio ya utekelezajiwa mpango wa mwaka 2012/2013, Sekta ya Viwandailiendelea na Utekelezaji wa Mkakati Unganishi wa UendelezajiViwanda Nchini kwa kuendeleza Uhamasishaji wa Uwekezajina kutoa Kipaumbele kwa Viwanda Vinavyoongeza thamaniya Mazao ya Kilimo. Wizara imeendelea kutekeleza MkakatiUnganishi wa Kuendeleza Viwanda Nchini (IIDS) ikilengamaeneo ya kipaumbele ya usindikaji wa mazao ya kilimokama vile matunda, mbegu za mafuta, bidhaa za ngozi,madini, mbolea, kemikali, mashine na mitambo ya viwanda.

Wizara na Taasisi zake imeendelea kutoa msukumomkubwa kwa kutekeleza miradi ya chuma cha Liganga naMaganga Matitu au Kasi Mpya; kuzalisha umeme kwakutumia makaa ya mawe ya Mchuchuma na Ngaka Kusini;kuzalisha umeme kwa kutumia upepo wa Singida; kuzalishaviuadudu wa kuua viluwiluwi vya mbu waenezao malaria;uwekezaji katika miradi mikubwa ya Maeneo ya Uzalishajikwa Mauzo Nje (EPZ) na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ);miradi ya ushirikiano na UNIDO na JICA na utekelezaji waMikakati ya Kuendeleza Sekta Ndogo za Ngozi na Viwandavya Ngozi, Nguo na Mavazi. Kufuatia juhudi hizo, jumla yamiradi ya viwanda 186 ilisajiliwa kwa kipindi cha mwaka2012/2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara il iendeleakuhamasisha uanzishaji wa viwanda katika maeneombalimbali nchini hususan Kanda ya Kusini kwa sababu yakuwa na gesi asili inayohitajika kwa matumizi ya viwanda.Viwanda hivyo ni pamoja na cha saruji cha Dangote CementCo. Ltd kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani milionitatu kwa mwaka na kuajiri jumla ya wafanyakazi 5,000.

Kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la MtwaraMikindani. Tayari vifaa vya awali vya ujenzi wa kiwanda hichovimewasili Mtwara. Kiwanda kingine cha saruji katika Kandaya Kusini ni cha Lee Construction Materials Company Limited(tani 300,000), Kilwa Masoko – Lindi ambacho tayari ujenziumekamilika na MEIS Cement Company, Lindi ambachoujenzi umekamilika na mitambo kusimikwa.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

71

Miradi mingine ya viwanda vya saruji ambayo ikokatika hatua mbalimbali za ujenzi ni pamoja na Dar es SalaamCement Company (DCC), Mbagala - Dar es Salaam; LakeCement Company (LCC) tani 500,000, Kimbiji - KigamboniDar es Salaam; Fortune Cement Company, Vikindu –Mkuranga - Pwani; Athi River Cement Company, (tani1,500,000) Tanga; Rhino Cement Company, Mkuranga - Pwanichenye uwezo wa uzalishaji wa (tani 750,000) kwa mwakana Kisarawe Cement Company, Kisarawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kufuatilia Miradi yaTANCOAL, kasi mpya na umeme wa upepo (Mkoani Singida)inayoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia NDC na SektaBinafsi, kazi ya uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wamashapo ya chuma cha Maganga Matitu na makaa yamawe ya Katewaka imekamilika. Taarifa ya awali inaoneshakuwepo kwa tani milioni 49.22 za chuma na tani milioni 34za makaa ya mawe. Mradi una lengo la kuzalisha tani 330,000za chuma ghafi (sponge iron) kuanzia mwishoni mwa mwaka2014 na utazalisha tani 250,000 za chuma cha pua (steel) kwamwaka. Madini ya chuma yaliyohakikiwa yanatoshakuzalisha chuma ghafi kwa muda wa miaka 78. Pia, mradihuo utazalisha umeme kiasi cha megawati 25 utakaotokanana teknolojia itakayotumika ya Direct Reduction of Iron Ore(DRI).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekamilishauandaaji wa Mpango Kabambe (Master Plan) wa KutekelezaMkakati Unganishi wa Kuendeleza Viwanda (IntegratedIndustrial Developement Strategy - IIDS). Mpango huoumebainisha miradi takriban 50 ya kutekeleza. Wizaraitachapisha mpango huo na kuusambaza kwa wadau kwautekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kutekeleza vema mkakatiwa Kuendeleza Sekta Ndogo ya Nguo na Mavazi kwaKushirikiana na Sekta Binafsi, Wizara imeanzisha Kitengo chaKuendeleza Sekta ya Nguo na Mavazi (Textile DevelopmentUnit –TDU), chenye lengo la kutatua changamoto mbalimbalizinazokabili viwanda vya nguo zikiwemo huduma za umeme,

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

72

bandari na ushuru. Kitengo hicho kimetembelea viwandavyote vya nguo nchini na kufanya mikutano na wadau ilikutambua changamoto zinazoikabili sekta hiyo. Baadhi yamafanikio yaliyoanza kuonekana ni kama yafuatayo:-

(a) Uhusiano kati ya wenye viwanda vikubwa navidogo vya sekta ndogo ya nguo na mavazi nchiniumeboreshwa. Hivi sasa wafumaji nguo wadogowanaotumia hand looms wanaweza kupata malighafi(nyuzi) kirahisi kupitia makubaliano ambayo yamefanyika katiyao na viwanda vya 21st Century, Afritex na Mwatex haliambayo haikuwa rahisi hapo awali;

(b) Kuboresha utendaji wa viwanda kwakushughulikia ujuzi wa kiufundi wa wafanyakazi nawasimamizi. Kiwanda cha Mwatex kimekubali kutumikakama kituo cha kutolea mafunzo ya ujuzi wa ufumaji(weaving). Utaratibu wa kuleta wataalam wakufunzi 30kutoka nje ya nchi kuja kufundisha waendesha mitambounaendelea;

(c) Kushauri na kuhamasisha wamiliki wa viwandavya nguo nchini kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaambalimbali (product diversification) na kuondokana nauzalishaji wa khanga na kitenge pekee. Tayari viwanda vyaMwatex na Karibu Textile Mill vimeonesha nia ya kuwekezakatika kupanua wigo wa bidhaa za nguo wanazozalisha;na

(d) Kitengo kimeunganisha viwanda ambapo kwasasa wakuu wa viwanda wanakutana kila baada ya miezimitatu na wameweza kuwaunganisha na vyombo vya fedhaili kuweza kupata mitaji mfano Hero Textiles ya Dar es Salaamna Mbeya Knitwear Ltd. Viwanda vya nguo nchini vimewezakuongea kwa sauti moja matatizo yao hususan ya uingizajinguo kutoka nje na masuala ya ukwepaji kodi. Vilevile,Kitengo kwa kushirikiana na VETA kinaandaa mpango wamafunzo ya kuongeza ujuzi kwenye sekta ya nguo hasaupande wa mavazi il i kuondoa tatizo linalowafanya

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

73

wawekezaji wasite kuwekeza katika viwanda vya mavazinchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelea nauhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vipya hasa katikaSekta Ndogo za Nguo na Mavazi, Ngozi na Viwanda vyaKusindika Mazao ya Kilimo. Wizara kwa kushirikiana na wadauikiwemo Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), BRELA na Mamlakaya EPZ, imesajili miradi mipya 186 na imeendelea kuhamasishana kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Viwanda na Biashara.Katika kipindi cha mwaka 2012/2013, Kituo cha UwekezajiNchini kilisajili jumla ya miradi ya viwanda 157, kati yake miradimiwili ni ya kuzalisha nguo na minne ya kusindika ngozi.Aidha, Mamlaka ya EPZ ilisajili miradi mbalimbali 29, kati yakemiradi minne ni ya kuzalisha nguo na mavazi na saba yakusindika mazao ya kilimo na mifugo. Hii inafanya jumla yamiradi ya nguo na ngozi kuwa 17, ya kuzalisha nguo ikiwasita na usindikaji ngozi/bidhaa za ngozi 11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naShirika la Kimataifa la Kuendeleza Viwanda (UNIDO)inaendelea kutekeleza mradi wa kujenga uwezo wawafanyakazi wake na wadau wakuu wa kuandaa nakuchambua sera ya viwanda na zinazohusiana ambapomafunzo yamekuwa yanatolewa.

Kufuatia mafunzo hayo, Ripoti ya Hali ya Ushindaniwa Sekta ya Viwanda nchini (Tanzania Industrial CompetitiveReport) 2012 iliandaliwa na kuzinduliwa tarehe 20 Novemba,2012 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Viwanda Afrika(Africa Industrialization Day - AID). Ripoti hiyo inatoamapendekezo ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Viwanda nchiniinachukua nafasi yake ya kuendeleza uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naUNIDO iliendelea kutekeleza Mradi wa African Agribusinessand Agro-processing Development Initiative (3ADI). Mradi huounalenga uongezaji thamani katika mlolongo wa thamanikwa mazao ya korosho, nyama na ngozi. Kwa upande wazao la korosho, mradi unahusisha vikundi vinane vya

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

74

wajasiriamali wadogo (SMEs), wengi wao wakiwa vijana nawanawake na viwanda vikubwa viwili. Mambo yaliyofanyikana kukamilika ni pamoja na kuandaa kabrasha la mafunzo(cashewnut technical training manuals); kufanya mafunzo,kuboresha mashine za kubangua korosho zinazotengenezwanchini; kuhamasisha matumizi ya maeneo ya Kongano(clusters) ambapo vikundi vitatu kati ya vinane vyawajasiriamali wadogo vimehamia katika Kongano la SIDOMtwara; na kununua mashine za kubangua korosho kwaKikundi cha Kitama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa zao lanyama, kazi zilizofanyika ni pamoja na ripoti ya mlolongowa thamani; usanifu wa nyumba za machinjio (slaughterhouses) kwa miji ya Mbeya na Iringa; usanifu na ununuzi wavifaa vya ujenzi wa mahali/meza za kuchinjia (slaughter slabs)kwa Mbeya na Iringa Vijij ini; ununuzi wa vifaa kamakompyuta kwa Bodi ya Nyama pamoja na uandaaji wa ripotiya fursa za malisho na mahusiano na wachinjaji. Vilevile,kwa upande wa ngozi, kazi zilizofanyika ni pamoja na ripotiya mlolongo wa thamani wa zao la ngozi; uendeshaji wamafunzo ya ubora; uandaaji wa patterns na kozi yakutengeneza patterns; na ushauri wa uboreshaji wa Chuocha Taaluma ya Ngozi cha Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naUNIDO iliendelea kutekeleza Mradi wa Industrial Upgradingand Modernisation. Mafunzo kwa wakufunzi Watanzania iliwaweze kutoa mafunzo kwa wanaviwanda na uchambuzi(diagnostic analysis) wa kubainisha matatizo ya Sekta yaUsindikaji Maziwa umekamilika kwa viwanda vitano nauchambuzi kuhusu usindikaji wa mafuta ya alizeti kwaviwanda vitano umeanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naSerikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA)inatekeleza Mradi wa Kaizen kwa ajili ya kutoa mafunzoyenye lengo la kuongeza tija, ufanisi, usimamizi wa shughuliza viwanda na kuongeza ubora wa bidhaa. Awamu yamajaribio i l ikwishafanyika kwa kutoa mafunzo kwa

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

75

wajasiriamali 113 wenye viwanda vya nguo na mavaziwaliopo Mkoa wa Dar es Salaam. Makubaliano kati yaWizara na JICA ya kutekeleza mradi wa Kaizen yalisainiwamwezi Oktoba, 2012 na mradi umeanza kutekelezwa mweziAprili, 2013. Sekta zitakazofaidika na mradi huo ni pamojana viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo katika Mikoa yaDar es Salaam, Morogoro na Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelea kushirikikatika Kuandaa Mpango Kazi wa Sera ya Viwanda yaJumuiya ya Afrika Mashariki na mapitio ya sera ya viwandakatika SADC na kufanya maboresho kulingana na mahitajiya nchi yetu; Wizara imeshiriki ipasavyo katika kukamilishaMpango Kazi wa Kutekeleza Sera ya Uendelezaji Viwandakwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Uhamasishaji (sensitisation)wa Mpango Kazi husika unaendelea sambamba nauhamasishaji Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya Jumuiya yaAfrika Mashariki ili wadau waweze kuelewa na kuwa tayarikutekeleza.

Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda kwa nchiwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusinimwa Afrika (SADC) imekamilika na kupitishwa na Baraza laMawaziri wa Biashara wa SADC (CMT) mwezi Novemba, 2012.Rasimu hiyo itawasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa NchiWanachama wa SADC unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti,2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inaendelea kufuatiliauboreshaji wa utendaji wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki(FTC)na malimbikizo makubwa ya madeni. Hata hivyo, haliya sasa ya uzalishaji imeimarika kutokana na juhudizinazofanywa na uongozi wa kiwanda ambapo uzalishajiumeongezeka kutoka mita milioni 2.05 mwaka 2011 hadimita milioni sita mwezi Aprili, 2013. Ajira imeongezeka kutokawafanyakazi 656 mwaka 2011 hadi 800 mwezi Aprili, 2013.kutokana na kiwanda kuwa na mitambo ya kizamani (1960s).Juhudi za pamoja zinafanywa ili kiwanda kiweze kupatamitambo ya kisasa.

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

76

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekamilisha uandaajiwa Rasimu ya Sheria ya Biashara ya Chuma Chakavu baadaya kujadiliwa katika ngazi ya Makatibu Wakuu (IMTC).Muswada wa kutunga sheria hiyo unafanyiwa maboresho ilikuwasilishwa Baraza la Mawaziri kwa maamuzi na hatimayeKamati ya Sheria na Katiba ili kuwasilishwa rasmi Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sekta ya ViwandaVidogo na Biashara Ndogo kuhusu kupitia na kutathiminiutekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo naBiashara Ndogo na kutoa mapendekezo kwa madhumuniya kuhuisha; katika kipindi cha mwaka 2012/2013, Wizarailifanya tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo yaViwanda Vidogo na Biashara Ndogo katika eneo la watoahuduma kwa Sekta il i kubainisha aina za hudumazinazotolewa na Wizara na Taasisi za Umma, Washirika waMaendeleo na Sekta Binafsi. Zoezi hilo limekwishafanyikakatika Mikoa ya Dar-es-Salaam, Iringa, Morogoro, Ruvuma,Tanga, Mtwara, Mwanza, Arusha, Dodoma na Mbeya nakufikia jumla ya Taasisi 150. Matokeo ya awali yanaoneshakuwa wengi wa wajasiriamali wadogo wamenufaika nahuduma hizo kote mijini na vijijini ingawa watoa huduma zateknolojia bado ni wachache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara kwa kushirikiana na UNWOMEN ilifanya tathmini yaushiriki wa wanawake wajasiriamali waishio mipakani katikasoko la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na changamotozinazowakabili.

Tathmini hiyo ilibaini kuwa ushiriki wa wajasiriamalihusika ni hafifu na changamoto kuu ni pamoja na uelewamdogo kuhusu masuala ya Itifaki ya Jumuiya ya AfrikaMashariki, Uasili wa Bidhaa (Rules Of Origin), biashara zaokutokuwa rasmi na kuwa na uelewa mdogo wa sheria nataratibu za forodha. Wadau hao wamekubaliana kuanzishamitandao ya wanawake wajasiriamali wa mipakani ili kuwana sauti moja kuhusu masuala yanayohusu biashara zao.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

77

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naTanTrade imeunda vikundi vya akina mama na kuanzishamadawati ya jinsia katika vituo vya mipakani vya Mutukula,Kabanga, Namanga, Rusumo na Sirari. Wizara kupitiaTanzania Women Chambers of Commerce -TWCCimewezesha uandaaji na ushiriki wa Mtandao waWafanyabiashara Wanawake wa Afrika Mashariki katikaMkutano uliofanyika Dar es Salaam, mwezi Novemba, 2012uliolenga kupanua wigo wa masoko ya bidhaa na hudumazinazozalishwa na wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kujenga uwezo wakutoa huduma za ugani katika maeneo waliokowajasiriamali hasa vijij ini, Wizara kwa kushirikiana nawataalam kutoka SIDO, BRELA, TCCIA, GS1 na TBS, imeendeshamafunzo yaliyolenga kuboresha bidhaa zinazozalishwa nawajasiriamali ili ziweze kushindana katika soko la ndani nanje hasa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC. Mafunzohayo yalijumuisha Wajasiriamali kutoka Mikoa ya Mbeya,Ruvuma, Lindi, Shinyanga, Mara, Kagera, Geita, Simiyu,Kigoma, Iringa, Rukwa, Mtwara na Mwanza. Warsha hizozil iwezesha kuandaa mipango ya biashara vizuri nakuitekeleza, kutengeneza bidhaa bora, utengenezaji nautunzaji wa mitambo na ujasiriamali. Jumla ya Wajasiriamali125 na Maafisa Biashara 16 walifaidika. Warsha hizozimewezesha wajasiriamali kuanza kutumia nembo za uborana kuweza kuuza bidhaa zao kwenye ‘Supermarkets’. Wizarakupitia SIDO i l iweza kutoa huduma za ugani kwawajasiriamali 9,660 nchini kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakuhamasisha Manispaa na Halmashauri za Wilaya na Mijikutenga maeneo na sekta binafsi kushiriki kujengamiundombinu hasa majengo ya uzalishaji kwa ajili yauongezaji thamani mazao ya kilimo ndani ya maeneoyaliyotengwa. Wizara imehamasisha Watendaji waHalmashauri za Manispaa, Kata na Vijiji umuhimu wa utengajiwa maeneo ya kufanyia kazi wajasiriamali wadogo katikaeneo la Bahi, Korogwe, Kongwa, Dodoma Mjini, Muheza,Mpwapwa, Tanga Mjini na Handeni. Kutokana na jitahada

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

78

hizo, Halmashauri ya Mpwapwa imetenga eneo la konganola karanga na Kongwa imetenga kongano la zabibu. Vilevile,Mkoa wa Tanga umetenga eneo la Mwahoka barabara yaPangani eneo ambalo linatarajiwa kutumika nawajasiriamali kati ya 800 na 2000, eneo la Majani Mapanakwa ajili ya maduka 41 ya kuuza unga na mashine 8 zakusindika na eneo la Manundu limetenga hekta 50 kwa ajiliya uwekezaji wa Sekta ya Viwanda Vidogo na BiasharaNdogo. Jitihada hizo zitaendelezwa katika mikoa minginenchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuwawezeshaWajasiriamali kushiriki katika maonesho ya ndani na nje yanchi, Wizara imeendelea kuratibu ushiriki katika maoneshoya bidhaa za wajasiriamali yaliyoandaliwa na SIDO.Maonesho hayo yalifanyika katika Kanda ya Kusini (Lindi),Kanda ya Ziwa (Mwanza) na Kanda ya Pwani (Morogoro).Wajasiriamali 252 walipata fursa ya kutangaza bidhaa zaokama vile vyakula vilivyosindikwa, sabuni, bidhaa za uhunzi,ngozi, nguo, chumvi, mashine na zana za kazi. Pamoja nakutangaza bidhaa, washiriki wameweza kuboresha bidhaazao kutokana na mafunzo waliyoyapata na maonimbalimbali ya wateja na wageni wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeratibu maoneshoya Mwezi wa Mwanamke Mjasiriamali (Month of WomanEnterprenuer-MOWE) yaliyofanyika katika viwanja vya MnaziMmoja mwezi Novemba, 2012. Maonesho hayo yalishirikishawanawake wapatao 200 kutoka Mikoa yote ya Tanzania.Wizara ilitumia fursa hiyo kutoa mafunzo kwa washiriki kuhusukuboresha biashara wanazozifanya kwa kutumia taasisi zaSIDO, FCC, BRELA, TBS, TCCIA na GS1. Mafunzo hayo piayaliwezesha washiriki kusajili biashara zao, kuanza michakatoya kupata viwango vya ubora na kupata nembo zautambuzi wa bidhaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kujenga uwezo wauzalishaji wa zana za kilimo, Wizara kupitia SIDO imeimarishaVituo vya Kuendeleza Teknolojia (Technology DevelopmentCenters – TDCs) vilivyopo Arusha, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro,

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

79

Lindi, Mbeya na Shinyanga ili viweze kuzalisha zana za kilimo.Mashine za kusindika mazao ya kilimo kwa ajili ya kuwasaidiawakulima kuongeza thamani ya mazao ya muhogo na alizetizilizalishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada za kupanuawigo wa masoko ya upendeleo kwa bidhaa zetu, mwaka2012/2013, Wizara imeendelea kufanya majadiliano yakibiashara na nchi za China, Japan, Malaysia, Indonesia, KoreaKusini, Uturuki, India, Czechoslovakia, Urusi, Falme za Kiarabu,Marekani, Mexico, Costarica, Ujerumani, Umoja wa Ulaya,Pakistani, Finland, Nigeria, Sudan, Sudani ya Kusini na Oman.Pia Wizara imeendelea kushiriki majadiliano ya kibiashara yaKikanda na Kimataifa na hasa yale ya EAC, SADC, AU,COMESA-EAC-SADC, Ubia wa Uchumi na kati ya Jumuiya yaAfrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya (EAC EU- EPA) na yaleya Shirika la Biashara la Dunia (WTO) kupitia Duru la Doha(Doha Round).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio yaliyopatikanakutokana na majadiliano hayo ni pamoja na Tanzania kusainimakubaliano ya ushirikiano wa biashara na uchumi na Uturukiyenye lengo la kukuza biashara na uwekezaji. Kupitiamakubaliano hayo, tayari mwezi Desemba, 2012, Uturukiilizindua safari za ndege kupitia Uwanja wa Ndege waKilimajaro, hatua ambayo imesaidia kurahisisha biasharakwa wauzaji wa maua na mboga mboga nje na hivyokupunguza adha na gharama ya kusafirisha mizigo yaokupitia uwanja wa ndege wa Nairobi kabla ya kusafirishakwenda nje. Makubaliano hayo pia yamesaidia kukuza Sektaya Utalii na kuanzishwa kwa Kituo cha Wafanyabiashara katiya Uturuki na Tanzania kiitwacho ABITAT , ambachokilizinduliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Aprili, 2013. Vilevile,China imeweza kuongeza fursa za masoko ya bidhaa zaTanzania kuingia soko la China kutoka asilimia 60 hadi 95bila kutozwa ushuru kwa bidhaa za kilimo, uvuvi, mifugo,madini na bidhaa za viwandani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwezi Februari, 2013,Tanzania ilisaini Mkataba wa ushirikiano wa Biashara na

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

80

Uchumi na Oman. Makubaliano hayo yanalenga kukuzaushirikiano katika Sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, na Usafiriwa Anga. Zaidi ya makampuni 30 yameonesha nia ya kujakuwekeza Tanzania. Majadiliano kati ya taasisi za Oman naTanzania kuhusu namna ya kuanzisha ushirikiano kupitia sektahusika yanaendelea. Pia, majadiliano ya biashara baina yanchi na nchi yamewezesha Korea Kusini kufungua Kituo chaBiashara jijini Dar es Salaam ili kusaidia uratibu na kupatikanataarifa za biashara na uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imefanyia mapitioSheria ya Anti Dumping na Counterveiling Measures Act, 2004kwa nia ya kuihuisha ili kuendana na mfumo wa WTO kuhusumasuala ya dumping kwa kujumuisha wadau wote muhimuTanzania Bara na Visiwani. Rasimu ya Mapitio ya Sheria ikotayari na Rasimu ya Waraka wa BLM kuhusu mapendekezoya Marekebisho ya Sheria ya Anti Dumping na CounterveilingMeasures Act, 2004 imeandaliwa tayari kupelekwa CabinetSecretariat.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi Septemba, 2012,Tanzania imeongezewa muda wa Mpango wa AGOA hadimwaka 2015, ili kuzisaidia nchi za Afrika zilizoko Kusini mwaJangwa la Sahara ikiwemo Tanzania kuendelea kufaidika nafursa za Soko la Marekani kwa bidhaa za nguo na mavazibila kulipa ushuru na bila kuwepo kwa ukomo (Duty FreeQuota Free Market Access). Tanzania na nchi wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaendelea na majadilianona Serikali ya Marekani yenye lengo la kuanzisha mkatabawa Ushirikiano wa Biashara na Uwekezaji (Partnership for Tradeand Investment Agreement-PATIA) ili kukaribisha wawekezajikutoka Marekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2012/2013, vituovya Biashara vya Tanzania vya London na Dubai vimeendeleakuvutia wawekezaji wa nje ili kuwekeza Tanzania. Vilevile,Vituo vimetafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za Tanzaniakatika masoko ya Ulaya na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).Kituo cha Dubai kimewezesha wajasiriamali watano kushirikikwenye maonesho ya Global Village ambapo jumla ya Shilingi

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

81

milioni 150 zilipatikana kutokana na mauzo ya bidhaa zasanaa za mikono, majani ya chai na kahawa. Kituo hichovilevile kimewezesha Kampuni za Tanzania kuuza mbao ainaya mitiki (Teak), dhahabu, Tanzanite, mashudu, karafuu nanyama ya mbuzi katika soko la UAE vyenye thamani ya zaidiya Shilingi bilioni 100. Pia, Kituo kilisambaza jumla yamachapisho 5,000 kutoka vituo vya utalii kama TANAPA,Ngorongoro, TTB, na Kamisheni ya Utalii Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia mafanikioyaliyopatikana kutokana na Vituo vya London na Dubai,Wizara imeanza maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja nakutenga fedha za kuanzisha vituo vingine katika bajeti yakeya mwaka 2013/2014. Vituo hivyo vinategemewa kuanzishwaChina, Ubelgiji, Afrika Kusini na Marekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naWTO iliendesha mafunzo kuhusu uandaaji wa kutoa taarifa(notifications) kwa Maafisa 22 kutoka Wizara na Taasisimbalimbali za Serikali. Warsha hiyo ilifanyika mweziNovemba, 2012 huko Bagamoyo, Pwani. Lengo la warshahiyo lilikuwa ni kujenga uwezo na uelewa wa jinsi ya kuandaanotifications kwa Wizara na Taasisi ambazo zinawajibikakutoa taarifa hizo (enquiry points).

Mheshimiwa Mwenyekiti, majadiliano ya kuanzishwakwa Eneo Huru la Biashara la Utatu (Tripartite Free Trade Area- FTA) linalojumuisha Kanda za COMESA, EAC na SADC lenyenchi zipatazo 26 na soko lenye wakazi wanaokadiriwa kufikiamilioni 750 yalianza rasmi Septemba, 2012. Majadiliano hayoyamejikita katika maeneo ya Mtangamano wa Biashara(Market Integration); Maendeleo ya Miundombinu(Infrastructure Development) na Maendeleo ya Viwanda(Industrial Development).

Makubaliano yamefikiwa katika tafsiri ya Kanuni nataratibu za kuendesha mikutano ya majadiliano, mpangokazi, ratiba ya mikutano na majadiliano ya kibiashara.Vikundi Kazi vimeundwa katika maeneo ya Vigezo vya Uasiliwa Bidhaa (Rules of Origin); Ushirikiano wa Forodha (Customs

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

82

Cooperation, Documentation, Procedures and Transit relatedissues); Vikwazo vya Kiufundi vya Biashara (Technical Barriersto Trade), Usalama wa Afya ya Binadamu, Mimea naWanyama (Sanitary and Phytosanitary Measures-SPS); VikwazoVisivyokuwa vya Kiushuru (Non Tariff Barriers); na Ulegezaji waViwango vya Ushuru (Tariff Liberalization).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeshiriki kwenyemajadiliano ya uanzishwaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedhawa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Monetary Union). Hadisasa jumla ya vifungu sabini na saba (77) vimejadiliwa.Maeneo ambayo hayajafikiwa muafaka na yenye mvutanoni pamoja na Macro economic Convergence Frameworkna Legal and Institutional Framework ambayo yanahitajimwongozo kutoka Baraza la Kisekta la Mawaziriwanaosimamia majadiliano ya Itifaki ya Uanzishwaji waUmoja wa Fedha. Majadiliano kuhusu Mpango Kazi (RoadMap) juu ya mchakato wa Uanzishwaji wa Itifaki ya Umojawa Fedha yamekamilika. Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja waFedha utaanza rasmi mara baada ya miaka kumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeratibu vikao vyaKamati ya Kitaifa inayoshughulikia masuala ya Vikwazo vyaBiashara Visivyo vya Ushuru kwa kuendelea kufuatilia, utoajitaarifa na mikakati ya kuondoa vikwazo vya biasharavisivyokuwa vya kiushuru, (NTBs). Kamati ya Kitaifa yaKusimamia Masuala ya Afya za Binadamu, Wanyama naMimea (National SPS Commitee) ilikutana tarehe 4 Desemba,2012 na kukubaliana kuwa na mkakati wa kuimarishauzalishaji wa nyama ya kuku usimamiwe na Wizara yaMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi ili sekta hiyo iweze kuhimiliushindani. Kamati za kikanda zimekuwa zikikutana nakupeana taarifa juu ya hali ya vikwazo visivyokuwa vyakiushuru na kupendekeza hatua za kuviondoa.

Baadhi ya vikwazo hivyo ambavyo vil ikuwavinalalamikiwa na wafanyabiashara ni pamoja na tozo yaDola za Marekani 200 kwa kila gari la biashara lililokuwalinaingia Tanzania, kuongeza masaa ya kazi kuwa 24 katikavituo vya bandarini na Namanga, kuwa na Kituo Kimoja cha

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

83

Kukagua Mizigo (One Stop Centre) katika Bandari ya Dar esSalaam na hivyo kupunguza gharama za kufanya biasharana msongamano bandarini baada ya kujenga vituo vyabandari ya nchi kavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuendelea na Majadilianoya Kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha wa SADC na KulegezaMasharti katika Sekta ya Biashara ya Huduma. Wizara imeshirikikatika majadiliano ya uanzishwaji wa Umoja wa Forodhawa Nchi za SADC.

Majadiliano hayo yanafanyika kulingana namapendekezo ya tafiti mbalimbali zilizofanyika kuhusumuundo bora unaofaa wa Umoja wa Forodha wa SADC.Tafiti hizo zilifanyika katika maeneo manne. Maeneo hayo niwigo wa pamoja wa kukusanya ushuru (Common ExternalTariff-CET); Ukusanyaji wa mapato; namna ya kugawanamapato na mfuko wa fidia (Revenue Collection, Distribution,Sharing and Compensatory Fund). Sheria na muundoutakaotumika katika utekelezaji wa Umoja wa Forodhaunaotarajiwa (Legal Administration and InstitutionalFramework); na Urazinishaji wa Sera za Biashara(Harmonization of Trade Policies).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara vilevile imeshirikikatika majadiliano ya kulegeza masharti ya Biashara yaHuduma katika sekta ndogo sita za kipaumbele ambazo niFedha, Uchukuzi, Utalii, Mawasiliano, Ujenzi na Nishati. Ilikutekeleza kazi hiyo, Wizara imeunda kikosi kazi cha kitaifakuratibu majadiliano ya masuala ya biashara ya huduma.Kikosi kazi hicho kinaundwa na wataalam kutoka Wizarasaba, Idara za Serikali kumi na Asasi Binafsi nne na kufanyajumla ya wajumbe wa kikosi kazi kuwa ishirini na moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Taifa ya Biashara yamwaka 2003 inafanyiwa mapitio ili kuendana na mabadilikombalimbali yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka tisa tanguilipotungwa. Maoni ya wadau kupitia warsha za kikanda kwanchi nzima ikiwemo Zanzibar yamekusanywa. Mkakati waKisera (Trade Strategy Development Paper - TSDP)

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

84

unaandaliwa ili kuwezesha kutayarisha andiko la kisekta(Sectoral Papers) na hivyo kuandaa rasimu ya Sera ya Taifaya Biashara ambayo itazingatia maoni ya wadau likiwemosuala la jinsia katika utekelezaji wa Sera hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendelea kuratibuna kukamilisha marejeo ya Sera ya Taifa ya Biashara kwa NchiWanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemoTanzania. Zoezi hilo lilifanyika chini ya Shirika la Biashara laDunia (WTO) mwezi Novemba, 2012 huko Geneva Uswisi.Lengo la marejeo hayo ni pamoja na kutoa taarifa kwawanachama wa WTO na wadau wa ndani na nje wakiwemowawekezaji kuhusu Sera za Biashara na Mazingira ya Uchumikwa ujumla katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemoTanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naWizara za Sekta ya Kilimo imeandaa mwongozo na kutoaelimu katika Halmashauri zote nchini kuhusu dhana yamnyororo wa thamani, ambapo masuala ya miundombinuya masoko yamezingatiwa kama kigezo muhimu katikakuendeleza mfumo wa masoko ya mazao wenye ufanisi. Kwakuzingatia mwongozo huo, Halmashauri za Wilaya kupitiaMipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) huibuamahitaji ya miundombinu ya masoko husika kama vilemasoko, maghala, minada ya mifugo, miundombinu yausindikaji kama mashine, barabara za vijijini na cold rooms,na kuandaa mipango ya utekelezaji kupitia DADPs.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara, imeanza zoezi laUfuatiliaji na Tathmini (M & E) wa miundombinu ya masokokatika Wilaya zote ili kubaini hali halisi ya miundombinu nakutathmini mahitaji ya miundombinu hiyo kwa kila Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kushirikiana naHalmashauri za Kasulu, Nanyumbu na Songea KuendelezaMasoko katika Mipaka ya Kilelema, Mtambaswala, Darajala Mkenda mtawalia; ujenzi wa masoko katika vituo vyamipakani vya Mtambaswala Wilayani Nanyumbu, MkendaBridge Wilayani Songea Vijijini na Nyamgali Wilaya ya Kasulu/

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

85

Buhigwe unaendelea chini ya usimamizi wa Halmashauri zaWilaya hizo. Ujenzi wa masoko hayo chini ya ufadhili wa Mradiwa TASP unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni 2013. KwaWilaya ya Kasulu, awali soko lilitarajiwa kujengwa katika eneola Kilelema lakini Halmashauri husika ilibadilisha eneo la mradikwa kuwa soko la Kilelema litajengwa kupitia utaratibumwingine unaoihusisha Benki ya Maendeleo ya TIB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza nia yaSerikali ya kufanikisha ujenzi wa Masoko ya Segera naMakambako, Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa Mikoaya Tanga na Njombe na Halmashauri za Wilaya za Handenina Njombe imekamilisha maandalizi ya awali ambayo nipamoja na upembuzi yakinifu, maandalizi ya MpangoKabambe (Master Plan), utengaji wa maeneo ya kutosha,tathmini ya athari za kimazingira (Environment ImpactAssessment) kupitia Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) nautoaji wa elimu kwa umma. Wizara imewakutanishawahusika wa Mikoa ya Tanga na Njombe na Benki yaMaendeleo ya TIB ili kufanikisha ujenzi wa masoko hayo. Benkiimetembelea maeneo husika na kufanya majadiliano naUongozi wa Mikoa hiyo. Taratibu za kupata hati miliki zamaeneo yaliyotengwa zinaendelea. Hii ni pamoja naHalmashauri kulipa fidia kwa wale waliopisha ujenzi wamasoko hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda naBiashara inaendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta katikauanzishwaji wa Vituo vya Pamoja vya Mipakani (OSBP). Vituovya Pamoja vinajengwa katika mipaka ifuatayo; Tanzaniana Kenya (Holili/Taveta), Tanzania na Uganda (Mutukula), naTanzania na Burundi (Kabanga/Kobero). Hadi sasa ujenzi wakituo cha Kobero umekamilika wakati ujenzi wa OSBP kwaupande wa Kabanga bado haujaanza, hivyo maofisa waTanzania watahamia upande wa Kobero nchini Burundimpaka pale ujenzi wa kituo kwa upande wa Tanzaniautakapokamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa OSBP ya mpakawa Mutukula kwa upande wa Tanzania umekamilika kwa

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

86

asilimia 85. Ujenzi wa OSBP ya Holili/Taveta kwa upande waTanzania umefikia asilimia 95 wakati kwa upande wa Kenyawapo katika hatua za awali za ujenzi wa OSBP ya Taveta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada za kupunguzagharama za biashara na kuboresha mazingira ya biasharana uwekezaji nchini, Wizara kwa kushirikiana na wadau wasekta ya umma na binafsi imeanzisha Kamati za PamojaMipakani (Joint Border Committees – JBCs katika vituo sabavya mipakani: Mtukula, Namanga, Kabanga, Rusumo, Sirari,Kasumulo, na Tunduma. Kamati za Pamoja Mpakani (JBC) niKamati zilizoanzishwa kwa lengo la kuziwezesha Taasisi zaUdhibiti mipakani kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo lakupunguza gharama za kufanya biashara kwa kurahisishaupatikanaji wa huduma zinazotolewa na Taasisi hizo.Wajumbe wa Kamati hizo hutoka sekta ya umma na binafsina hukutana kila robo mwaka. Ili kufanikisha uendeshaji waKamati hizo, Wizara kwa kushirikiana na wadau imeandaamwongozo wa kuingiza na kutoa mizigo na bidhaa mipakanikwa lengo la kupunguza muda na gharama zinazotumikana wafanyabiashara na wasafirishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kupitia Sheria Sita ilikuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa masoko yamazao na mifugo, Wizara kwa kushirikiana na wadauimefanya mapitio ya sheria za The Agricultural Products(Control of Movement) Act na The Export Control Act nakuwasilisha mapendekezo kwa Mwanasheria Mkuu waSerikali kwa ajili ya kufuta Sheria ya The Agricultural Products(Control of Movement) Act na kuifanyia marekebisho Sheriaya The Export Control Act kulingana na mapendekezo yawadau. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadaumbalimbali imeandaa rasimu ya kanuni za kutekeleza Sherianne za biashara ambazo zinatokana na marekebisho ya sheriambalimbali za biashara za mwaka 2012. Sheria hizo nipamoja na Sheria ya Alama za Bidhaa (Merchandise MarksAct, Cap 85). Sheria ya Makampuni (Companies Act, Cap212), Sheria ya Majina ya Biashara (Business Names Act, Cap213) na Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(Tanzania Trade Development Authority Act, Cap 155). Rasimu

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

87

za Kanuni hizo ziko kwa Mwasheria Mkuu wa Serikali kwa ajiliya uhakiki kabla ya kusainiwa na Waziri wa Viwanda naBiashara ili kuanza kutumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kushirikiana na Bodiya Stakabadhi za Maghala, Uongozi wa Mkoa wa Kagerana Vyama vya Ushirika ili kuanzisha matumizi ya Mfumo waStakabadhi kwa zao la kahawa kwa msimu wa ununuzi wa2013/2014, katika kuendeleza Mfumo wa Stakabadhi zaMazao Ghalani katika Mazao ya Kahawa, na Mazao MengineMahindi, Mpunga na Alizeti; Wizara kupitia Bodi ya Leseni zaMaghala imetoa mafunzo kuwezesha kuanzishwa kwaMfumo wa Stakabadhi kwa zao la kahawa Mkoani Kagera.Uhakiki wa maghala yanayofaa kwa kazi hiyo umefanyikana kwa kuanzia utekelezaji wa mfumo wa maghalautafanyika kwa majaribio katika Wilaya ya Ngara. Wizaraimekubaliana na Mkoa wa Kagera kufanya ziara ya mafunzokwa vitendo kwa kuwachukua wadau wa zao la kahawakutembelea maeneo ya mfumo wa maghala (Lindi, Mtwarana Tunduru – Songea) ili kubadilishana uzoefu na kujioneajinsi mfumo unavyofanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekamilisha Rasimuya Sera na Mkakati wa Kitaifa wa Miliki Bunifu (NationalIntellectual Property Policy and Strategy) na kazi ya kukusanyamaoni ya wadau imekamilika. Mkutano wa kwanza wawadau umefanyika Februari 2012 Mkoani Dar es Salaam kwaKanda ya Mashariki na Mkutano wa Wadau kwa Kanda yaNyanda za Juu Kusini, Mkoani Mbeya umefanyika Februari,2013, na Kanda ya Ziwa umefanyika Aprili, 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana nawadau imekamilisha maandalizi ya kuanzisha Soko la Bidhaa(Commodity Exchange). Rasimu ya Waraka wa Baraza laMawaziri kuhusu uanzishwaji wa Soko hilo umeandaliwa nakujadiliwa katika ngazi ya Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.Kikosi Kazi chenye Wajumbe kutoka Sekta ya Umma na Sektabinafsi kimeundwa ili kuratibu uanzishaji wa soko hilokikisimamiwa na Kamati ya Usimamizi (Steering Committe)iliyoko chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

88

Wizara yangu inaendelea na maandalizi ya kuanzisha Sokola Bidhaa hususan kufanikisha ujenzi wa maghala chini yautaratibu wa PPP, kuweka mfumo wa taarifa unaounganishamasoko na maghala, kurekebisha sheria ya WRS na kutoaelimu kwa wadau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2012/2013, Taasisi za Uwekezaji, Utafiti, Maendeleo yaTeknolojia na Mafunzo zilizo chini ya Wizara (TIRDO, TEMDOCAMARTEC, NDC, EPZA na CBE) zimetekeleza yafuatayo:Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la TIRDO limeendeleakutoa mafunzo na kuhamasisha utumiaji wa mfumo waufuatiliaji kwa wazalishaji viwandani na wajasiriamali ilibidhaa zao ziweze kuingia kwenye masoko kwa ushindani.Wazalishaji katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na pia Mikoaya Kusini (Mtwara) walipatiwa mafunzo ya utekelezaji wamfumo wa ufuatiliaji. Uhaba wa rasilimali fedha umefanyamfumo huo wa ufuatiliaji kushindwa kuwekwa kwenyemfumo wa kikompyuta (computerised traceability system) nakuweza kuuboresha zaidi mfumo huo wa kujaza karatasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelea KusaidiaUtendaji wa Kampuni ya GS1 kama Mshauri wa Kiufundi Chiniya Uendeshaji wa Sekta Binafsi. Shirika la TIRDO limeendeleakutoa ushauri wa kitaalam wa jinsi ya matumizi ya nemboza mistari (bar-codes). Shirika kwa kushirikiana na taasisinyingine limeweza kuwapatia GS1 (Tz) National Limited Ofisina Kampuni imeanza kazi ya kutoa nembo ya mstari (BarCodes) kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi. Hadi sasamakampuni 151 yamekuwa wanachama wa GS1 hapa nchinina bidhaa 2,500 zimepata nembo za mstari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la TIRDO limeendeleakutoa ushauri wa kitaalam (technical evaluation) kupitia Benkiya Maendeleo (TIB) kuhusu uanzishwaji wa viwanda kwakutumia mikopo ya TIB. Wawekezaji wanne (4) katika mikoaya Pwani (Kiwanda cha kutengeneza filter za magari), Dares Salaam (Kiwanda cha nyama/soseji) na Arusha (Kiwanda

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

89

cha kuzalisha juisi na cha kuzalisha maji) walipata ushauriwa kitaalam uliowawezesha kupata mikopo ya TIB. Aidha,Shirika la TIRDO limeendelea kutoa ushauri wa kitaalam kwawazalishaji viwandani kuhusu uzalishaji wa bidhaa bora bilakuchafua mazingira. Viwanda vya ALAF, TCC, Tanga Cementna, Coca Cola (Bara na Visiwani) vilipata ushauri huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Shirika la Uhandisi naUsanifu wa Mitambo (TEMDO) katika kuendeleza UtoajiHuduma za Kihandisi Viwandani kwa Lengo la KuongezaUzalishaji, Ubora wa Bidhaa, Kuhifadhi Mazingira na MatumiziBora ya Nishati; Utoaji wa huduma za kihandisi na mafunzozilitolewa na TEMDO kwenye viwanda vya sukari (KilomberoSugar Company na TPC Limited), viwanda vya vinywaji(Tanzania Breweries Limited na Banana Investments) naTANALEC. Huduma kubwa iliyotolewa katika kipindi hicho nimafunzo ya Afya Kazini, Usalama na Mazingira (OccupationalSafety, Health and Environment – OSH&E). Jumla yawafanyakazi 56 walipata mafunzo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TEMDO imebuni nakuuendeleza teknolojia ya machinjio za kisasa na zakuongeza thamani ya bidhaa zitokanazo na mabaki yamifugo mbalimbali. Kazi ya uboreshaji wa mashine na vifaavya machinjio ya kuku umekamilika vikiwemo kifaa chakuchinjia, kupasha joto na cha kunyonyoa kuku. Vilevile, shirikalimetengeneza mashine na vifaa ambavyo hutumikakutayarisha mifupa kwa ajili ya kuondoa madini ya fluoridekwenye maji na zimefungwa katika kituo cha maji wilayaniMeru. Kwa sasa ubunifu wa teknolojia ya kutengeneza gundikutokana na mabaki ya mifugo unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuendelea namaboresho pamoja na uhawilishaji wa teknolojia mbalimbaliikiwa ni pamoja na teknolojia ya kuteketeza taka za hospitali(bio-medical waste incineration), TEMDO imeendeleakuboresha kiteketezi cha kuchomea taka za hospitali na takangumu (bio-medical/solid waste incinerator). Uboreshajiuliofanyika umehusisha utengenezaji wa kiteketezi kisichotoamoshi mwingi na kisichotumia maji (smokeless hospital solid

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

90

waste incinerator). Kiteketezi hicho kimebuniwa ili kupunguzagharama za uendeshaji hasa katika matumizi ya maji.Kiteketezi cha aina hiyo kimefungwa katika hospitali zaLugalo, Bagamoyo na Babati Manyara. Kiteketezi kilicho borazaidi kimefungwa katika hospitali ya St. Elizabeth, Arusha kwamajaribio. Vilevile, ubunifu na utengenezaji wa mtambo wakusaga karanga ili kutengeneza siagi ya karanga (peanutbutter machine) umefanyika na mashine hizo zinatumiwa nawajasiriamali wasindikaji. Mashine hizo ni za kupukuchua nakukaanga karanga na kutoa siagi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Kituo cha Zana zaKilimo na Ufundi Vijijini (CAMARTEC) kufanya Utafiti naUendelezaji wa Teknolojia za Kilimo na Ufundi Vijijini; Kituokimeunda na kukamilisha majaribio ya mashine ya kuvunampunga inayoendeshwa na Power tiller ikiwa ni moja yautafiti unaotokana na kusikiliza mahitaji halisi ya wakulima.Mashine hiyo imefanyiwa majaribio Mkoani Kilimanjaro. Kituokimefanikiwa kutengeneza jumla ya matrekta 14, tela nnena plau nane zitakazotumiwa na trekta hilo. Awali, plau hizozilikuwa zikiagizwa nje ya nchi.

Halikadhalika, Kituo kimezalisha mashine mbili zakusaga. Pia Kituo kimefanikiwa kuuza trekta moja kwamkulima mkoani Katavi na kinaendelea kukamilishaviunganisho vyake kwa ajili ya kuuza pamoja na matrektamatano kwa Serikali ya mitaa Mkoni Katavi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kimefanikiwa kujengamitambo ya biolatrini katika shule moja ya sekondari MkoaniDar es Salaam, moja Mkoa wa Mara na moja Mkoa waArusha. CAMARTEC kwa kutumia mafundi waliopatamafunzo yanayotolewa kwa kupitia mradi wake wa ujenzina usambaji wa mitambo midogo imejenga mitambo 201ya biogesi na kuisambaza katika ngazi ya Kaya katika mikoaya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya na Kagera.Kiasi hicho ni sawa na asilimia 80.4 ikilinganishwa na lengola mitambo 250. Aidha, teknolojia hiyo inasaidia kuhifadhimazingira na kuongeza matumizi ya mbolea bora katikakilimo.

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

91

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kimetengeneza nakueneza majiko 2,042 yanayobana matumizi ya mkaa kwamatumizi ya kaya. Teknolojia hiyo inapunguza matumizi yakuni na hivyo kuhifadhi mazingira. Kituo kimetengenezamitambo nane ya kuchemshia maji kwa kutumia mionzi yajua na kuzisambaza sita katika hospitali ya AICC ya mkoaniArusha na mbili kwa wakulima mkoani Arusha kwa matumizimbalimbali. Kituo pia kimetengeneza na kusambaza mashinetatu za kukamulia mbegu za nyanya, mbili Mkoani Kilimanjarona moja mkoani Arusha, pia kimetengeneza na kusambazamashine mbili za kukatia malisho ya wanyama mkoani Dares Salaam na Arusha. Kituo kimetengeneza mashine sita zakufyatua tofali za udongo-saruji na zimekamilishwa kwaasilimia 80. Mashine hizo zitasambazwa kwa watumiajimikoani Arusha na Manyara. Vilevile, Kituo kimefanikiwakuboresha miundombinu katika karakana na eneo laCAMARTEC Tawi la Nzega.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza miradi yaMchuchuma na Liganga, tafiti za kuhakiki wingi na uborawa madini yaliyopo, kukamilisha uhakiki (Due Diligence) waMradi wa Kasi Mpya wa kuzalisha chuma ghafi (Sponge Iron)na kuendelea kulinda na kusimamia rasilimali zilizopo katikamashapu ya Mchuchuma na Liganga zinaendelea. Shirika laMaendeleo la Taifa (NDC) kwa kushirikiana na mbia (SichuanHongda) kupitia kampuni tanzu ya Tanzania ChinaInternational Mineral Resource Limited (TCIMRL) inaendeleana kukamilisha ujenzi wa kambi ya makazi ya watafiti katikamaeneo ya Mchuchuma na Liganga. Kazi ya uchorongaji wauhakiki (Confirmatory Drilling) imekamilika katika eneo laMchuchuma wakati Geophysical Prospecting imekamilikakatika eneo la Liganga. Jumla ya mashimo 40 yenye kinacha zaidi ya mita 8,800 yamekwishachimbwa katika eneo laMchuchuma. Taarifa kamili ya uchorongaji pamoja na usanifuwa mgodi (Mine Design) na upembuzi yakinifu kwa Mradiwa Mchuchuma unategemea kukamilika hivi karibuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukamilisha ujenzi waKiwanda cha Kuzalisha Viuadudu (biolarvicides) kwa ajili yaKuua Viluwiluwi kwenye mazalia ya mbu wa malaria (TAMCO,

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

92

Kibaha), Wizara kupitia NDC inatekeleza Mradi wa KuzalishaViuadudu (Biolarvicides) vya kuulia Viluwiluwi wa MbuWanaoeneza malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Cuba.Ujenzi wa majengo ya kiwanda ulianza Januari 2012 naunategemewa kukamilika mwezi Oktoba 2013. Ununuzi wamitambo ya kiwanda unaendelea na baadhi ya mitambotayari imekwishafikishwa katika eneo la mradi. NDCinaendelea na ujenzi wa miundombinu ya maji taka. Majisafi yamekwishafikishwa katika eneo la kiwanda na kazi yakuunganisha umeme inaendelea. NDC inafanyamazungumzo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili pindiuzalishaji wa viuadudu utakapoanza mwezi Novemba 2013,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iwe mnunuzi na mratibuwa usambazaji na utumiaji wa viuadudu hivyo. Nia nikuhakikisha kuwa viuadudu vitakavyozalishwa vinatumiwanchini badala ya kulenga soko la nje pekee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendelea kufuatiliautekelezaji wa Mradi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka Kusini,Songea unaotekelezwa na Tancoal Energy Ltd ambayo nikampuni ya ubia kati ya NDC na Intra Energy Corporation(IEC). Mradi huo unaendelea vizuri na hadi kufikia Januari,2013, tani 166,775 zilikwishachimbwa, tani 71,862 zikiwazimechimbwa kwa kipindi cha Januari, 2012 hadi Desemba,2012. Makaa hayo huuzwa kwa viwanda vya Saruji vya Tangana Mbeya na vya Jasi na sehemu iliuzwa nchi za Malawi,Mauritius, Kenya na Uganda. Kwa sasa, soko la makaa yamawe bado ni dogo kwa vile uzalishaji wa umeme ambaoungetumia makaa ya mawe kwa wingi haujaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua za kujenga kituo chakuzalisha umeme zinaendelea. Majadiliano kati ya TANCOALna TANESCO kuhusu Mkataba wa Kuzalisha Umeme (PowerProduction Agreement-PPA) yanaendelea na yakihitimishwauzalishaji wa umeme utaanza. TANCOAL imepanga kuzalishaumeme wa MW 120 - 200 kuanzia mwaka 2015 na kuongezahadi MW 400 ifikapo 2016. Hata hivyo, kuanza kwa uzalishajiwa umeme kunategemea kasi ya ujenzi wa njia ya umemewa msongo mkubwa wa Kilovoti 220 kutoka Songea hadiMakambako unaojengwa na Serikali kupitia TANESCO kwa

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

93

msaada wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida). TANCOALitajenga msongo wa umeme wa Kilovoti 220 kutoka Ngakahadi Songea na kukamilika 2015/2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa kuzalisha umemekwa kutumia upepo Singida unategemewa kuanza uzalishajiwa Megawati 50 mwaka 2014 na kuongezeka kwa Megawati50 kila mwaka hadi kufikia Megawati 300 mwaka 2019.Umeme huo utaunganishwa katika Gridi ya Umeme ya Taifakupitia kituo kikuu cha umeme (High Voltage Substation)kilichoko Singida. Gharama za kutekeleza mradi huo awamuya kwanza ya MW 50 zinakadiriwa kuwa Dola za Marekanimilioni 136. Wizara kupitia NDC na kwa kushirikiana na Wizaraya Fedha inatafuta mkopo wa masharti nafuu kutoka Benkiya EXIM ya Serikali ya Watu wa China. Tayari ridhaa ya Serikali(Letter of Support) imewasilishwa EXIM Bank na Wizara yaFedha kwa hatua zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inaendelea kufuatiliaufufuaji wa Kiwanda cha General Tyre (EA) Ltd (GTEA) naKuanza Uzalishaji wa Matairi ambapo Shirika la Maendeleola Taifa (NDC) linaendelea na jitihada za kutekeleza azmaya Serikali ya kufufua kiwanda hicho kwa kushirikiana na SektaBinafsi. Aidha, Wizara kupitia NDC imekamilisha ukarabatiwa baadhi ya majengo ya Kiwanda pamoja na kuandaaMpango wa Biashara (Business Plan).

Mhandisi Mshauri wa Viwanda (Consulting IndustrialEngineer) amekamilisha uhakiki/ukaguzi wa mitambo iliyopo(plant and equipment evaluation/audit) katika kiwandahicho. Vilevile, Mshauri huyo amekamilisha uchambuzi wakina wa mahitaji na gharama ya kufufua mitambo yakiwanda hicho ili kuvutia wawekezaji ambao watafanyaupanuzi wa Kiwanda pamoja na miundombinu yake. NDCitaendelea kutafuta wabia wenye uwezo na uzoefu wauzalishaji wa matairi ya magari kwa lengo la kufufua nakupanua. Wawekezaji mbalimbali kutoka Afrika ya Kusini,Jamhuri ya China, India, Taiwan, na kadhalika. wameoneshania ya kushirikiana na NDC katika kufufua na kupanuakiwanda hicho. Vilevile, utaratibu wa kuhakikisha upatikanaji

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

94

wa fedha na ufumbuzi wa madeni ya kiasi cha shillingi bilioni38 kufikia Machi, 2011, unaendelea kufuatiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukamilisha Tafiti naKuanzisha Kiwanda cha Kuzalisha Magadi Soda (Ziwa Natronna Engaruka, Arusha), hivi sasa, NDC imekamilisha upembuziyakinifu kuhusu Hydrolojia, kemia, ecology, na ResourceAssessment ya Ziwa Natron ili kubaini athari katika mazingirana kuandaa hatua stahiki zitakazochukuliwa kulindamazingira hayo. Taarifa ya upembuzi huo ambayoimetayarishwa na Mshauri Mwelekezi wa Chuo Kikuu cha Dares Salaam, imekwishakabidhiwa NDC. Pia, NDC inakamilishautafiti kuhusu athari kwenye Ziwa Natron, mazalia na uhamajiwa ndege aina ya Korongo unaoweza kusababishwa namradi.

Sambamba na utafiti uliofanyika na unaoendeleakufanyika eneo la Ziwa Natron; tafiti nyingine zinafanyikakatika eneo la Engaruka lililoko umbali wa kilomita 58 kutokaZiwa Natron katika Wilaya ya Monduli kubaini upatikanajiwa magadi katika eneo hilo ili kupata chanzo kingine chamagadi mbali na kile cha Ziwa Natron. Utafiti katika eneohilo umefikia hatua ya uchorongaji wa kina (detailed drilling)ili kuhakiki mashapo (reserve) ya malighafi hiyo na ubora wakekatika viwango vya kimataifa na hatimaye kuvutiawawekezaji wa ndani na nje katika kuendeleza mradi huo.Matokeo ya uchorongaji wa awali yalionesha kuwepo kwamagadi mengi yenye makadirio ya lita za ujazo milioni 4.7.NDC inaendelea na utafiti wa kina kwa kuchoronga mashimo12 ili kuweza kubaini wingi wa magadi yaliyopo katika eneohilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuanzisha Viwandavya Kusindika Nyama, Mpira na Mazao mengine ya Kilimo,NDC inakusudia kuanzisha mashamba makubwa ya kilimona ufugaji kwa ajili ya viwanda vya nyama (Meat ProcessingPlants) ikiwa ni pamoja na usindikaji wa mazao yake. NDCinaendelea na uboreshaji wa mashamba ya mpira ya Kihuhwina Kalunga Wilayani Muheza na Kilombero kwa kuandaa

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

95

mpango wa muda mrefu wa kuendeleza viwanda vyamazao ya mpira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kujenga Maeneo yaViwanda (Industrial Parks) Sehemu za TAMCO, KMTC, Kange,na kadhalika, katika eneo la Viwanda la TAMCO Kibaha;NDC imekamilisha michoro (layout design) ya eneo la wazilenye ukubwa wa hekta 88 kwa ajili ya ujenzi wa viwandavipya (Industrial Estates) katika eneo la TAMCO – Kibaha. Zoezila upimaji wa viwanja na maeneo ya miundombinu(cadastral survey) limekamilika na kuidhinishwa na Wizara yaArdhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Vilevile, NDC imekodisha kiwanda cha kuunganishamagari cha TAMCO kwa mwekezaji atakayeunganishamagari ya mizigo na mashine nyinginezo. Detailed Design yamiundombinu ya barabara, maji safi na maji takaumekamilika. Ujenzi wa miundombinu hiyo pamoja nausanifu wa kituo cha umeme (Power Sub Station) unasubiriupatikanaji wa fedha. Vilevile, uhamishaji miliki wa eneo laTAMCO kwenda NDC umekamilika. NDC imeingia mikatabana wawekezaji watatu ambao wamejitokeza kutaka kupataviwanja katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juhudi za kuhamisha umilikiwa eneo na Kiwanda cha Kilimanjaro Machine ToolsCompany (KMTC) kwenda NDC zinaendelea ikiwa ni pamojana ulinzi na utunzaji mazingira na mali katika eneo lakiwanda. Mfumo wa maji umefanyiwa matengenezo na sasaunafanya kazi vizuri. Pia, Shirika linafanya ukaguzi wa kina(Health Check) katika Kiwanda cha KMTC kwa lengo lakuboresha uendeshaji wake. Ili kuvutia wawekezaji kwa eneola wazi, NDC imeandaa hadidu za rejea kwa ajili ya kufanyacadastral survey na baada ya hapo ujenzi wa miundombinuya msingi utaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, michoro ya eneo la viwandakatika eneo la Kange Tanga imekamilika na kuidhinishwana Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiwani pamoja na kutolewa kwa hati miliki kwa viwanja husika.

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

96

Shirika pia l imewasil iana na TANESCO kwa lengo lakuunganisha umeme katika eneo hilo. Pia, Shirikalimekamilisha utaratibu wa kupata mkandarasi atakayejengauzio na barabara za ndani katika eneo la Kange. Kazi yakuvutia wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza katika eneo laKange inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Mamlaka yaEPZ i l iendelea kuhamasisha uwekezaji wa kujengamiundombinu na kuzalisha katika Maeneo Maalum yaUwekezaji (EPZ/SEZ). Kwa mwaka 2012/2013; jumla yamakampuni 29 yamepewa leseni za kujenga viwanda chiniya EPZA na tayari Makampuni 5 yamekwishaanza uzalishaji.

Makampuni hayo yatawekeza mtaji wa jumla ya Dolaza Marekani 113 milioni na kuajiri watu 9,254. Idadi hiyoitafanya jumla ya makampuni yanayozalisha chini ya EPZkufikia 70, mtaji uliowekezwa kufikia Dola za Marekani bilionimoja na jumla ya ajira za moja kwa moja (directemployment) kufikia 23,000. Pia katika mwaka huu wa fedhaMamlaka ya EPZ ilikamilisha uandaaji wa kanuni za mfumowa SEZ ambao ulianza kutumika rasmi mwezi Oktoba, 2012.Mfumo huo wa SEZ ambao huruhusu pia wawekezajiwanaouza soko la ndani, utaleta ongezeko kubwa lawawekezaji kupitia Maeneo Maalum ya Uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Bagamoyo SEZ linaukubwa wa hekta 9,000 (ekari 23,000) na litaendelezwa katikamfumo wa mji wa kisasa wa viwanda na biashara. Eneolitahusisha miundombinu ya bandari mpya katika eneo laMbegani, ujenzi wa uwanja wa ndege, eneo la viwandavikubwa na vidogo, eneo la biashara, utalii, teknohama,maghala, makazi na kadhalika. Katika kipindi cha mwaka2012/2013, Wizara kupitia Mamlaka ya EPZ imekamilishaupembuzi yakinifu na kwa kusaidiana na Benki ya Dunia (WorldBank) wamekamilisha uandaaji wa Mpango Kabambe(Master Plan). Zoezi la ulipaji wa fidia limefanyika kwa asilimia25 ambapo hekta 1,500 kati 6,000 zilizofanyiwa uthamini tayariwamelipwa fidia.

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

97

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Mtwara SEZlimekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutokana na tafitiza gesi na mafuta zinazoendelea katika pwani na ndani yabahari ya Hindi. Makampuni ya British Gas, Ophir, Start Oil naPetrobras yanaendelea na tafiti katika eneo hilo. Kutokanana umuhimu wa eneo hilo, katika mwaka 2012/2013,Mamlaka ya EPZ kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandariwametangaza eneo la hekta 110 kuwa eneo huru la Bandari(Mtwara Freeport Zone) ambapo tayari makampuni 18 yandani na nje yameonesha nia ya kuwekeza ndani ya eneohilo. Aidha, Kampuni ya Solvochem (T) Ltd kutoka Lebanoninaendelea na ujenzi wa kiwanda cha vifaa vya plastic katikaeneo la bandari kupitia EPZA. Kiwanda hicho kitakamilikamwishoni mwa mwaka huo na kitaajiri watu 250. Mamlakaya EPZ kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari wanaendeleana taratibu za kuanzisha Mtwara SEZ kwenye eneo la hekta2,600.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Kigoma SEZ nimashuhuri kwa biashara kati ya nchi za Burundi, DRC naZambia. Eneo la hekta 3,000 limetengwa kwa ajili ya EPZ/SEZambapo awamu ya kwanza ni uendelezaji wa hekta 690.Katika mwaka 2012/2013, Mamlaka ya EPZ kwa kushirikianana uongozi wa Mkoa wa Kigoma wamekamilisha upembuziyakinifu, uandaaji wa Master Plan na ulipaji wa fidia kwanusu ya wadai ambapo Shilingi bilioni 1.5 zimelipwa. Tayarimakampuni ya City Energy, Rutale na Macis yameonesha niaya kujenga viwanda katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya eneo lililofidiwaBagamoyo hadi sasa ni hekta 1,468. Aidha, Wizara kupitiaMamlaka ya EPZ imepeleka kiasi cha Sh. milioni 550 kwaMthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanya uthamini katikaeneo la China Tanzania Logistic Centre. Mradi wa Tanzania -China Logistic Centre utatekelezwa kwa ubia baina ya Chinakupitia Kampuni ya YIWU - Pan African InternationalInvestment Corporation na Tanzania kupitia Mamlaka ya EPZ.Mradi utahusisha ujenzi wa eneo la biashara na viwanda vyakuunganisha vifaa (light assembly) na vya kuongeza thamanikatika mazao kwenye eneo la ekari 60 Kurasini, Dar es Salaam.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

98

Maandalizi ya Mkataba wa Makubaliano ya Ubia baina yanchi mbili pia unaendelea. Kutokana na kutopatikana kwafedha yote iliyopitishwa kwenye bajeti ya 2012/2013, fidia yaeneo lililobaki Bagamoyo, pia maeneo ya Tanga, Songea,Kigoma na Kurasini haikuweza kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Mamlaka ya EPZ ilikamilisha utengaji wa maeneo ya EPZ/SEZkatika mikoa 20 ya Tanzania Bara. EPZA kwa kushirikiana naSerikali za Mikoa mipya ya Simiyu, Geita, Njombe na Kataviwanaendelea na juhudi za kupata maeneo ya EPZ na SEZkatika Mikoa hiyo kupitia Sekretariati za mikoa naHalmashauri za Wilaya husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bunge lakotukufu kwamba Chuo cha CBE kimepata Mkuu wa Chuo(Rector). Katika mwaka 2012/2013, Chuo kimepitia mitaalayake katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahadaili kuimarisha mafunzo kwa vitendo yanayolenga mahitajiya soko la ajira. Mitaala hiyo iliwasilishwa NACTE nakuidhinishwa ili iweze kutumika. Chuo kwa kushirikiana naTaasisi ya Uendelezaji Utalii Zanzibar (ZIToD) na NACTEkinatekeleza mradi uitwao “Improving the Labour MarketResponsiveness of Technical Education in Tanzania” wenyelengo la kuimarisha ubora wa utendaji wa wahitimu katikasoko la ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia tarehe 17 hadi 24Machi, 2013, Chuo cha Elimu ya Biashara kikishirikiana nawataalam kutoka Chuo Kikuu cha Maastricht cha Uholanzina Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini,kiliendesha mafunzo kwa wakufunzi wake juu ya utekelezajiwa mafunzo yenye mwelekeo wa kiutendaji. Vilevile, mitaalamipya ya shahada ya kwanza katika ujasiriamali, menejimentiya rasilimali watu na elimu ya biashara itaandaliwa katikarobo ya tatu na nne ya mwaka wa fedha. Baada ya Chuokupitia mpango kazi na bajeti ya mwaka 2012/2013 upya,zoezi la kuandaa mitaala mipya ya shahada ya uzamililimeahirishwa hadi mwaka mpya 2013/2014.

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

99

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo kimeendeshamafunzo ya muda mfupi mara mbili ambapo jumla yawajasiriamali wadogo 53 walishiriki. Mafunzo yaliyotolewayalijumuisha mbinu za kubuni biashara, namna ya kupatamtaji wa biashara na mbinu bora na endelevu za kusimamiana kuendeleza biashara; utafutaji masoko na stadi zakuimarishsa ubora wa bidhaa. Chuo kimeandaa andiko lakuandaa mpango kabambe (Master Plan) katika Kampasizake tatu. Andiko hilo litatangazwa kwa kuzingatia taratibuza zabuni (tendering process) i l i kumpatia mtaalamatakayeandaa Mpango Kabambe (Master Plan) wa Chuo.Chuo kimefanya ukarabati mdogo katika majengo yakekatika Kampasi zake zote tatu. Maeneo yaliyofanyiwaukarabati ni pamoja na mifumo ya umeme, maji safi na majitaka, na uboreshaji wa vyoo. Katika mwaka 2012/2013, Chuokimewapa ruhusa ya kwenda masomoni na kulipia gharamaza masomo kwa wakufunzi wanne. Kati ya hao, wakufunziwatatu wanasoma katika ngazi ya uzamivu (PhD) namkufunzi mmoja anasoma katika ngazi ya uzamili (MasterDegree).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,malengo ya Wizara katika masuala ya ushindani na udhibitiwa bidhaa na huduma kupitia TBS, TANTRADE, COSOTA , BODIYA MAGHALA, FCC, FCT na SIDO yalikuwa ni kuratibuushindani, sera, kanuni za biashara na kusimamia ubora wabidhaa na huduma; kuthibitisha umahiri wa baadhi yamaabara, mafunzo, utafiti na maendeleo ya teknolojia nakuwezesha maabara zake kuthibitishwa umahiri wa utendajikazi zake. Utekelezaji wa malengo ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia mwezi Machi2013, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kupitia kwa mawakalawake wa ukaguzi wa magari limefanikiwa kukagua magari22,338. Vilevile, Shirika liliendelea kutekeleza mkakati wakudhibiti bidhaa duni kutoka Nje ya Nchi. Hadi kufikia mweziMachi 2013, Shirika lilikuwa limetoa jumla ya leseni 16,276 zaubora wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje. Ongezeko hilola leseni limetokana na kuanzishwa kwa utaratibu wa kuhakiki

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

100

ubora wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja Tanzania(Preshipment Verification of Conformity to Standards - PVoC).Ili kurahisisha utekelezaji wa mfumo wa PVoC, mnamo tarehe02 Julai, 2012, Shirika lilianzisha kitengo maalum karibu naBandari ya Dar es Salaam na Ofisi ya Forodha cha kusimamiaPVoC kwa lengo la kuwahudumia wateja wa bidhaazinazoingizwa nchini kwa ukaribu zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika lina maabara sabazenye vifaa vya kisasa na wataalam. Maabara hizo ni zaKemia, Uhandisi Umeme, Uhandisi Mitambo, Uhandisi Ujenzi,Chakula, Ugezi (Metrology) na Nguo/Ngozi/Kondomu. Katiya maabara hizo, maabara za Ugezi, Chakula, Kemia naNguo/Ngozi/Kondomu zina vyeti vya umahiri (AccreditedLaboratories). Vilevile, Shirika limeendelea kutoa mafunzokuhusu Mifumo ya Uhakiki wa Ubora (ISO 9001:2008 and ISO17025) katika taasisi mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia Machi, 2013,Shirika limepima sampuli za bidhaa mbalimbali zinazofikia6,077 katika maabara zake za Chakula, Kemia, Uhandisi,Nguo/Kondomu pamoja na Ugezi (Metrology). Kati yasampuli hizo, 82 ni za Wajasiriamali Wadogo na wa Kati(SMEs).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia Machi, 2013,jumla ya wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) 219 kutokakatika Mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro Iringa na Mbeyawalipata mafunzo ya ufungashaji bora wa bidhaa zao. Idadiya wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs) waliopata vyetimpaka kufikia robo ya tatu ya mwaka 2012/2013, ambavyovitawapa uwezo wa kutumia nembo ya ubora ya TBSwalikuwa 14 tu.

Vilevile, viwanda 60 vya wajasiriamali wadogo nawakati (SMEs) katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Kilimanjaro,Tabora, Dodoma, Rukwa, Morogoro, Kigoma, Pwani,Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam, na Singida vilifanyiwaukaguzi kwa lengo la kuvisaidia na kuvielekeza ili viwezekuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa.

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

101

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Shirika laViwango Tanzania (TBS) wamefikia makubaliano juu yakuoanisha (harmonise) viwango kwa baadhi ya bidhaamuhimu ili kuwezesha wafanyabishara wa nchi wanachamawa SADC kufanya biashara bila vikwazo. Hadi sasa, nchiwanachama zimekubaliana kupeleka majina ya bidhaa tanoambazo zinauzwa nje zaidi (5 most traded goods) katikasekretariet ya SADC ili kuweza kuoanisha viwango kwabidhaa hizo na kurahisisha upatikanaji wa masoko yake.Chombo kinachosimamia uoanishaji huo kimeundwaambacho ni SADCSTAN.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka ya Maendeleo yaBiashara Tanzania (TanTrade) huendesha mafunzo kwaJumuiya ya Wafanyabiashara wa Tanzania hususanWajasiriamali Wadogo na wa Kati (SMEs) ili kuwapa uwezokupitia mafunzo na ushauri. Kwa mwaka 2012/2013, katikavipindi viwili tofauti, TanTrade kwa kushirikiana na Shirika laKijerumani GIZ iliendesha mafunzo kwa wajasiriamali kwaawamu mbili katika Mikoa ya Dar es Salaam na Arusha.Vilevile, TanTrade kwa kushirikiana na GIZ ilifadhili na kuratibusafari ya mafunzo kwa Watanzania kumi na tano (15)kutembelea maonesho ya matunda na mbogamboga (FruitsLogistica) Berlin na maonesho ya bidhaa zinazozalishwa kiasili(Biofach), Nuremberg nchini Ujerumani kuanzia tarehe 4 hadi17 Februari, 2013.

Mashirika hayo ni wazalishaji na wamiliki wa kampunibinafsi tisa na maofisa watano (5) kutoka Taasisizinasosimamia masuala ya biashara. Safari hiyo ililengakujifunza kwa kutembelea maonesho ili kuweza kuona uborawa bidhaa zinazouzwa katika Soko la Ulaya na kujua mahitajina vigezo vinavyohitajika katika soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,TanTrade kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara,Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Uboreshaji Mazingira yaBiashara na kwa msaada wa Kituo cha Biashara chaKimataifa (ITC), ilifanikiwa; kuwezesha kuanzishwa kwa vikundivitano vya wafanyabiashara wanawake, katika mipaka ya

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

102

Kabanga, Rusumo, Mutukula, Sirari na Namanga; Kutoamafunzo katika mpaka wa Kabanga, ambapo jumla yawajasiriamali 43 walipata mafunzo na kati yao 38 wakiwa niwanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza nia yaSerikali ya kukuza na kutafuta masoko ya bidhaa zakitanzania, TanTrade kwa kushirikiana na Wizara pamoja nawadau wengine iliandaa Maonesho ya 36 ya Biashara yaKimataifa ya Dar es Salaam yaliyofanyika kuanzia tarehe 28Juni, - 8 Julai, 2012 katika uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K. Nyerere.

Katika maonesho hayo ya kimataifa maarufu kamaSabaSaba, jumla ya makampuni 1,341 ya ndani na 435 kutokanje ya nchi walifanikiwa kuonesha bidhaa zao. Kwa upandewa biashara, ahadi za mauzo ya nje (Export Enquiries)zipatazo Dola za Marekani milioni 93.8 zilipatikana, vilevilemauzo ya papo kwa papo yalikuwa Dola za Marekani milioni19.7. Ahadi za manunuzi toka nje zilikuwa ni Dola za Marekanimilioni 115.3. Bidhaa zilizopata maulizo kwa wingi ni pamojana asali, viungo (spices) kama iliki na tangawizi pamoja nabidhaa za mikono. Halikadhalika, bidhaa za viwandani ikiwani pamoja na nguo, samani za ndani na vifaa vya jikonivilipata maulizo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuona umuhimu waasali na bidhaa zitokanazo na nyuki kuwa ni bidhaazinazopatikana kwa wingi Tanzania, Wizara kwa kuzishirikishaTanTrade, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utaliipamoja na wadau wengine kwenye sekta hiyo waliandaamaonesho ya Asali (1 - 7 Oktoba, 2012) ambayo yaliratibiwana TanTrade. Katika maonesho hayo, Halmashauri 73 kutokawilaya mbalimbali za Tanzania, taasisi za umma saba pamojana washiriki binafsi 14 walishiriki. Pia, katika maonesho hayo,kulikuwa na jumla ya waoneshaji bidhaa na huduma 159kutoka vikundi na mtu mmoja mmoja wa Halmashauri zaWilaya, makampuni, taasisi, na mashirika ya umma. Kwaupande wa biashara mauzo yaliyofanyika wakati wamaonesho hayo yanakadiriwa kuwa Shillingi milioni 89.

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

103

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kutafuta masoko yanje kwa kuratibu Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya nchiza nje; katika kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinapata fursaza masoko ndani ya nchi, kikanda na kimataifa, TanTradekupitia Kitengo cha Taarifa za Biashara inaendelea na jukumula kupokea/kukusanya, kuchambua, kuhifadhi nakusambaza taarifa za biashara, takwimu na machapishombalimbali kutoka vyanzo mbalimbali vya nje na ndani yanchi. Wafanyabiashara ndani na nje ya nchi wapatao 78walipata taarifa za biashara wakiwamo wafanyabiasharabinafsi, asasi mbalimbali, wakulima, watafiti, walimu wa vyuovikuu na wanafunzi. Taarifa hizo zilisambazwa kupitiamaonesho ya 36 ya DITF na wengine kutembelea Kitengocha Biashara, kutumia barua pepe, kupiga simu na kutumanukushi (fax).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ilishiriki maoneshomakubwa ya dunia yajulikanayo kama EXPO 2012yaliyofanyika katika mji wa Yeosu, Korea ya Kusini kwa lengola kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini. Makampuni 10kutoka Tanzania yalishiriki katika EXPO 2012. Makampuni hayoyaliteuliwa na Kamati ya Maandalizi ya Kitaifa chini ya uratibuwa Wizara ya Viwanda na Biashara na TanTrade yaliuzabidhaa mbalibali kama vile kahawa, korosho, bidhaa zaviungo, bidhaa za ngozi, bidhaa za nguo, bidhaa za mikono,bia, konyagi, mvinyo, chai, Zanzibar Dhow na Zanzibar Door(Miniature).

Mheshimiwa Mwenyekiti, bidhaa hizo zilikuwa kivutiokikubwa kwa watu wengi na kuwezesha kupatikana kwamiradi mitano (5) ikiwemo ya ununuzi wa korosho kutokanchi ya Armenia, Ununuzi wa korosho na iliki kutoka Dubai,Ununuzi wa viungo kutoka Tajakistan na India na Ununuziwa kahawa kutoka Korea ambapo hawa wotewaliunganishwa na wauzaji wa Tanzania moja kwa moja.Katika maonesho hayo, miradi mbalimbali iliwasilishwakwenye EXPO 2012 na kutafutiwa wabia. Miradi hiyo ni ZanzibarIntergrated Community Maniculture Development Project-ZNZwenye lengo la kuhifadhi mazingira ya bahari na ufukwe ilikupunguza uvuvi holela pamoja na shughuli mbadala za

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

104

kuongeza kipato cha wananchi; Pemba SustainableAquaculture Development Project-PSTZ unaolenga kuhifadhimazingira pamoja na ufugaji wa samaki aina ya kaa nakilimo cha mwani; na Community Capacity Enhacement toalternative Enviromental Conservation Project – MECAunaolenga kuhifadhi ufukwe kwa upandaji wa mikoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ya Leseni za Maghala(TWLB) imetoa leseni za biashara kwa maghala 44 nawaendesha maghala 21 katika msimu wa 2012/2013.Halikadhalika, jumla ya kampuni mbili za wakaguzizimepewa leseni kwa ajili ya ukaguzi katika maghalayanayohifadhi mazao na wastani wa vitabu 160 vyastakabadhi vimethibitishwa na kutolewa katika msimu wa2012/2013. Vilevile, Bodi il iendelea kusimamia lesenizinazotolewa na imeanza mchakato wa kuwapelekaMahakamani waendesha maghala waliopoteza mazao yawakulima katika maghala. Upotevu huo ni ule unaozidikiwango cha unyaufu kilichokubaliwa. Aidha, Wizara kwakushirikiana na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirikatunaangalia jinsi ya kupunguza kero kwa wakulima kwakufanya mapitio ya sheria na kanuni za Mfumo wa Stakabadhiza Maghala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ilisimamia utekelezajiwa mfumo wa stakabadhi kwa msimu wa mwaka 2012/2013.Pia, bodi ilitembelea mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ajili yakuangalia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mfumohususan ununuzi na uuzaji wa korosho. Gineri ya KNCU naChama cha Ushirika cha Oridoy (Babati) kilitembelewakutathmini matumizi ya mfumo kwenye zao la Pamba.Vilevile, Bodi kwa ushirikiano wa Wizara ya Kilimo, Chakulana Ushirika, na Viwanda na Biashara, imeanza kuanishamaeneo yanayohitaji marekebisho katika Sheria Na. 10 yamwaka 2005 na kanuni zake za mwaka 2006.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi inaandaa MpangoMkakati wa Bodi wa miaka mitano na kutekeleza mpangowa kujengea uwezo wadau ikiwemo wakulima vijijini kuhusumfumo wa Stakabadhi na kuhamasisha matumizi ya mfumo

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

105

na faida zake. Bodi imeendelea kutoa elimu kwa wadauwengine kwa nyakati tofauti kwa kutumia matangazo katikaredio na luninga, vipeperushi na mikutano ya ana kwa ana.Mafunzo maalum yametolewa kwa Watendaji Wakuu waMaghala yanayosajiliwa katika mazao ya korosho, mahindina kahawa.

Vilevile, kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilayaza Kwimba, Magu na Misungwi na Taasisi za Fedha, Bodiitaendesha mafunzo kwa wakulima ili waweze kuuzampunga kwa kutumia mfumo wa stakabadhi katika msimuwa 2012/2013. Ukaguzi wa Maghala husikaumekwishafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi imejipanga kufanyauhamasishaji wa kina katika mikoa ya Katavi naSumbawanga ili kuanzisha matumizi ya mfumo kwa zao lamahindi, mpunga, alizeti na ufuta. Tathmini ya awali yaukaguzi wa maghala na kuangalia utayari wa wakulimaimeshafanyika. Katika maeneo mengine ambako mfumounatumika kwa muda mrefu sasa wameendelea pia kupataelimu ya mfumo ili kuongeza tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chama cha HakimilikiTanzania (COSOTA) kimeimarisha ofisi zake za kanda za Ofisiza Dar es Salaam na Mbeya, kwa kuajiri Afisa Leseni atakaesimamia ukusanyaji wa mirabaha. Hadi kufikia Februari 2013,COSOTA imekusanya mirabaha ya jumla ya Shilingi milioni98.8. Kati ya hizo, Shilingi millioni 88.0 ziligawiwa mwezi waMachi 2013 zikiwa ni makusanyo ya Julai- Desemba, 2012 nazilizobaki zitaingia katika mgao wa Julai, 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada dhidi yauharamia wa kazi za sanaa, COSOTA imeendelea na zoezila ukaguzi, ukamataji wa kanda na CD bandia nakuwafungulia kesi za jinai watuhumiwa mbalimbali. Hadikufikia Januari 2013, COSOTA imepokea na kusikiliza kesi nakusimamia mashitaka yanayohusiana na ulipaji wamirabaha. Jumla ya mashitaka yaliyopokelewa ni 26 dhidi

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

106

ya kazi za hakimiliki na kushughulikia migogoro 23 ya wasaniimbalimbali na migogoro 14 imepatiwa ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, COSOTA imefanya kampeniya uhamasishaji wa masuala ya hakimiliki kupitia vyombovya habari, mikutano, na kutoa mafunzo kwa maafisa uganina maafisa leseni na kutoa elimu kwa watafiti mbalimbalikuhusu hakimiliki na hakishiriki. COSOTA imesajili wasanii wamuziki 403 na kazi zao 9,839; wasanii wa filamu 22 na kazizao 737 pamoja na wasanii wa kazi za maandishi 51 na kazizao 1,437. Hadi kufikia Februari, 2013, COSOTA imekusanyajumla ya Shilingi milioni 9.32 kama ada ya usajili wawanachama na ada za mwaka za wanachama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala waVipimo (WMA), imekuwa ikifanya ukaguzi wa vipimombalimbali vitumikavyo katika biashara ikiwemo mizaniitumikayo katika ununuzi wa mazao ya wakulima. Kwamwaka 2012/2013, jumla ya vipimo 576,744 vilikaguliwaikilinganishwa na Vipimo 545,506 vilivyokaguliwa mwaka2011/2012. Wamiliki 5,627 walitozwa faini kwa makosambalimbali waliyofanya kuhusiana na vipimo ikilinganishwana wamiliki 5,503 waliotozwa faini kwa mwaka 2011/2012,na wafanyabiashara 10 walifikishwa mahakamani kwamakosa mbalimbali yanayohusu vipimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Wakala waVipimo, imeendelea kuwapa mafunzo watumishi wake. Kwamwaka 2012/2013, watumishi 193 walipata mafunzo ya ainambalimbali ili kuwaongezea weledi katika kazi. Vilevile,wakala ilipanga kununua magari 20 kwa mwaka 2012/2013na hadi kufikia Machi 2013, magari 11 yalikwisha nunuliwana kusambazwa mikoani. Magari tisa yaliyobakiyatanunuliwa katika robo ya nne ya mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kaguzi na uhakikiwa vipimo, Wakala imeendelea kutoa elimu kwa ummakupitia vyombo vya habari (Magazeti, Redio na Televisheni)pia kuzitumia vyema fursa kama vile za maonesho ilikuelimisha umma. Wakala imeshiriki katika maonesho sita

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

107

(6) ya biashara (DITF), MOWE, NaneNane, SIDO, Maonesho yaNyanda za Juu Kusini ya SMEs na Maonesho ya Ufunguzi waMkoa Mpya wa Katavi. Vipindi vitano (5) vya redio na vipindivitatu (3) vya luninga vilitayarishwa na kurushwa hewani.Makala zaidi ya 30 zilitayarishwa na kuchapishwa kwenyemagazeti. Machapisho ya vipeperushi mbalimbali yapatayo9,000 yalifanyika na kusambazwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Wakala waVipimo, inalo jukumu la kusimamia matumizi sahihi ya vipimokatika Sekta ya Mafuta na Gesi ili kuepuka udanganyifu namatumizi yasiyo sahihi ya vipimo. Vipimo vilivyo sahihihuwezesha Serikali kupata mapato yake sahihi na watumiajiwa mafuta na gesi kupata bidhaa hiyo kwa thamani yafedha yao. Katika kuimarisha kitengo hicho, Wakalaimeendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wake wa bandarina kwa mwaka 2012/2013 mtumishi mmoja amekwishapatamafunzo maalum ya usimamiaji wa usahihi wa vipimobandarini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Vipimo katikakudhibiti usahihi wa vipimo vitumikavyo katika gesi asilia naile itokanayo na mafuta ya petroli; kwa kushirikiana na wadauwake inaandaa rasimu ya kanuni za gesi aina ya LPG (LiquefiedPetroleum Gas) ili kusimamia kiasi cha gesi inayojazwa kwenyemitungi na kwa hali hiyo, kumlinda mlaji na vipimo visivyosahihi. Vilevile, Wakala imeendelea kufanya utafiti nauchambuzi wa mfumo wa vipimo vinavyotumika katikausambazaji wa gesi asili (Natural Gas-NG) nchini ili kuwezakupata taarifa sahihi ya vipimo hivyo vinavyotumika kwenyemfumo huo. Kwa kufanya hivyo, itasaidia mchakato wakuandaa rasimu ya kanuni ya gesi asili itakayokidhi usimamiziwa matumizi sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukamilishaji wa sheria mpyaya vipimo unaendelea na kwamba tarehe 28/11/2012mapendekezo ya sheria hiyo kupitia Waraka wa Baraza laMawaziri ilijadiliwa na IMTC na kutoa ushauri wa kuboreshawaraka huo. Kwa sasa Wizara kwa kushirikiana na Wakala

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

108

wa Vipimo, inafanya maboresho ili uweze kuwasilishwaBaraza la Mawaziri kwa hatua zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Wakala wa Usajili waBiashara na Leseni (BRELA), katika kuboresha utoaji wa hudumaza Wakala, hadidu za rejea za kumpata mshauri mwelekeziwa kuandaa mifumo ya kiteknolojia ya kuwezeshaupatikanaji wa taarifa na huduma kupitia mtandao wakompyuta (online registration system) zimeandaliwa. Wakalainakamilisha taratibu za kuwezesha wateja kulipia ada zahuduma za usajili kupitia Benki za NMB na CRDB. Ili kufanikishauanzishaji wa online registration, Sheria ya Ushahidi (theEvidence Act), inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuruhusunyaraka za mitandao kutumika kwenye ushahidi. Pia wakalainapaswa kuwa na jengo linalofaa kufunga mitambo yakiteknologia na ukamilishwaji wa mifumo ya ICT ili masijalazote ziweze kuwasiliana kwa njia ya kielektroniki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uboreshwaji (digitisation) waMasijala ya Taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara,Hataza (patent) na Leseni za Viwanda umekamilika. Wakalainaendelea na maboresho ya masijala ya Alama za Biasharana Huduma (Trade and Service Marks) ili kuanzisha mfumowa masijala ujulikanao kama Intellectual PropertyAutomation System- IPAS.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na marekebishoya Sheria za Makampuni na Majina ya Biashara kupitishwana Bunge Mwezi Aprili, 2012, Wizara kwa kushirikiana na BRELA,na wadau wengine imeandaa Kanuni za kutekeleza Sheriahiyo na kuwasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikalikwa uhakiki kabla ya kupitishwa na Waziri wa Viwanda naBiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala imeendelea kutoaelimu kwa njia ya semina, na maonesho mbalimbaliyanayofanyika nchini. Katika maonesho yote na semina,Wakala hutoa huduma ya usajili papo kwa hapo. Wakalaimewaelimisha watendaji wa TCCIA Tanzania nzima ili

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

109

waweze kutoa huduma ambazo sio za kisheria kwawananchi ikiwa ni pamoja na elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala imenunua kiwanjaNo. 24 eneo la Ada Estate, Kinondoni, na taratibu za kumpatamtaalam wa usanifu majengo na kusimamia ujenzi zimefikiahatua za mwisho za tathimini. Inategemewa ifikapo mweziMei mwishoni 2013, mtaalam atakayechora na kusimamiajengo hilo atakuwa amepatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Ushindani (FCC)ilikamata na kuadhibu waagizaji bidhaa bandia themaninina mbili (82) kwa kukiuka Sheria ya Alama za Bidhaa. Katikakaguzi hizo, Tume ya Ushindani pia ilifanikiwa kukamatabidhaa mbalimbali kama vifaa vya kompyuta (computeraccessories), mipira ya ndani ya pikipiki (vee-rubber), taulo zausafi za wanawake (always), simu za mkononi (Samsung),maandishi ya luninga (Eurostar), miswaki, na vifaa mbalimbalivya umeme na ujenzi ambazo zimehifadhiwa katikamaghala ya Serikali zikisubiri utaratibu wa kuharibiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Julaimpaka Desemba 2012 , Tume imefanya uchunguzi wa awalikatika makampuni mbalimbali na mgogoro wa bidhaa zamafuta ya petroli. Tume imefanya uchunguzi katikamuungano wa makampuni na taarifa itatolewautakapokamilika. Vilevile, Tume iliangalia muungano wamakampuni (mergers) mbalimbali ili kuona yanaleta tija naufanisi katika soko. Jumla ya maombi nane yaliwasilishwakwa Tume na kufanyiwa kazi, kati ya hayo makampunimatano, maombi yao yalikubaliwa na kupitishwa bilamasharti na mengine matatu yaliyobakia yako katika hatuaya uthibitisho na uchunguzi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la KuhudumiaViwanda Vidogo (SIDO) limetafuta, kuzifanyia marekebishona kutoa teknolojia mbalimbali kwa wajasiriamali kutokandani na nje ya nchi. Shirika linasimamia vituo vya maendeleoya teknolojia ndani ya mitaa ya viwanda vidogovilivyoanzishwa ili viweze kubuni, kutengeneza na hatimaye

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

110

kuuza bidhaa na mashine mbalimbali kwa wananchi, nakuwaelekeza namna nzuri ya kuzitumia kuanzisha miradi.Vituo hivyo pamoja na teknolojia zinazozalishwa ni:- Arusha(mashine za kukamua miwa na zana za kilimo), Iringa(mashine za mbao na usindikaji wa mtama), Kigoma(mashine za kusindika mawese na mazao ya mchikichi),Kilimanjaro (mashine za kutengeneza chaki na bidhaa zaujenzi), Lindi (mashine za kusindika korosho na mihogo),Mbeya (mashine za usindikaji wa maziwa na zanazinazolenga kupunguza uharibifu wa mazingira) na Shinyanga(mashine za kusindika ngozi na kutengenezea bidhaa zangozi). Huduma zilizotolewa zimewezesha uzalishaji nahatimaye upatikanaji wa bidhaa mbalimbali za viwandavidogo mijini na vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia SIDOinatekeleza Mkakati wa Zao Moja kwa Wilaya Moja (ODOP),imewezesha wajasiriamali nchini kote kuzalisha bidhaakutokana na malighafi zinazopatikana katika sehemu husikana kuchangia maendeleo ya viwanda vidogo vijijini. Mkakatihuo umewezesha kutengenezwa na kusambaza mashinempya za aina mbalimbali 462 kupitia vituo vya kuendelezateknolojia vilivyopo mikoa ya Arusha, Iringa, Kigoma,Kilimanjaro, Lindi, Mbeya na Shinyanga. Kati ya teknolojiampya zilizosambazwa ni pamoja na za usindikaji mkonge,muhogo, viungo, asali ukamuaji mafuta ya kula na usindikajingozi. Huduma zilizotolewa zimewezesha uanzishwaji waviwanda vidogo 80 vilivyozalisha nafasi za kazi 582.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maandalizi ya kujengamiundombinu ya kongano za alizeti yanaendeleakukamilishwa katika mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara.Uhamasishaji wa sekta binafsi kushiriki kujenga miundombinuhasa majengo ya uzalishaji ndani ya maeneo yaliyotengwana Halmashauri za Wilaya na Miji unaendelea. Taratibu zakutayarisha michoro, kutafuta vibali vya ujenzi, kujengamiundombinu kwenye maeneo, kuweka maji, umeme nakukamilisha taratibu za manunuzi ya huduma kwa kuwapatawakandarasi watakaoshiriki katika ujenzi wa majengo yamfano zinaendelea.

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

111

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ya viatamiziinakusudia kuwawezesha wajasiriamali wenye mawazo yaubunifu kuyatumia kutengeneza bidhaa au mfumo wauzalishaji wenye tija. Bidhaa au mifumo hiyo mipya baadayehuwa msingi wa kuanzisha viwanda vidogo na kuongezauzalishaji, biashara, kuongeza kipato, kuleta ajira na kujengauchumi. Programu hiyo iliendelea kutekelezwa katika mikoaya Dar-es-Salaam, Mbeya, Mwanza, Rukwa na Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la kuandaa mafunzoya aina mbalimbali ni kuwawezesha wajasirimali kupataufahamu na stadi zinazowawezesha kuanzisha na kuendeshamiradi yao vyema. Mafunzo yaliyotolewa yaliendeshwa katikaMikoa yote na wajasiriamali 4,766 walinufaika. Mafunzo hayoyalilenga kutoa uelewa na ujuzi wa kiufundi katika uzalishajimali kama usindikaji wa mafuta ya kupikia, ngozi, ubanguajikorosho, kuhifadhi na kusindika vyakula vya aina mbalimbali.

Mafunzo hayo pia yalielekezwa katika kujenga nakuimarisha mbinu za kibiashara na uendeshaji wa miradi yakiuchumi kwa walengwa hasa uongozi, masoko, ubora wabidhaa, mbinu za uzalishaji mali, utunzaji wa vitabu,uendeshaji na utunzaji mashine na uongozi wa vikundi navyama. Kwa ujumla, mafunzo yamewawezesha wajasiriamalikupata maarifa na stadi za kuimarisha shughuli zao zauzalishaji mali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Ofisi ya SIDO Mkoawa Manyara umekamilika na jengo limekwisha anzakutumika rasmi. Vyuo vya mafunzo na uzalishaji vilianzishwakatika mikoa mbalimbali ili kuwa chimbuko la kutoa stadiza kazi kwa mazao na bidhaa maalum kwa maeneo hayo.Tafiti hufanywa il i kubaini fursa za maarifa na ujuzivinavyohitajika ambavyo hufuatiwa na kuandaliwa mafunzomaalum kuziba mianya hiyo. Katika kipindi hicho cha mwaka,mafunzo ya ujuzi maalum yalitolewa na vyuo vya Njombe(usindikaji wa vyakula), Dar es Salaam (uzalishaji wa bidhaazitokanazo na kamba za asili) na Tanga (bidhaa zitokanazona makumbi ya nazi). Jumla ya wajasiriamali 220 walishirikikatika mafunzo hayo.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

112

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,maonesho matatu ya bidhaa zilizozalishwa na wajasiriamalinchini ya vyakula vilivyosindikwa, sabuni, bidhaa za wahunzi,bidhaa za ngozi, nguo, chumvi, mashine na zana za kaziyalifanyika katika Kanda ya Kusini (Lindi) na kuwashirikishawajasiriamali 197 ambapo mauzo ya bidhaa zao yenyethamani ya Shilingi milioni 45 yalifanyika. Maonesho ya Kandaya Ziwa (Mwanza) na kuwashirikisha wajasiriamali 264ambapo mauzo ya bidhaa zao yenye thamani ya Shilingimilioni 182 yalifanyika. Pamoja na kufanya mauzo ya bidhaazao, walibadilishana mawazo, kujifunza kutoka kwa wenzaona kujenga msingi wa masoko mapya. Maonesho ya tatuyalihusisha Kanda ya Pwani (Morogoro) na kuwashirikishawajasiriamali 200 ambapo mauzo ya bidhaa zao yenyethamani ya Shilingi milioni 60 yalifanyika. Pamoja na kufanyamauzo ya bidhaa zao, walibadilishana mawazo, kujifunzakutoka kwa wenzao na kujenga msingi wa masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utoaji wa huduma kwenyevituo 20 vya habari unaendelea vizuri na kwa kipindi chamwaka 2012/2013, jumla ya wajasiriamali 3,620 wametumiahuduma za vituo hivyo kufanikisha miradi na biashara zao.Vituo hivyo hutoa taarifa mbalimbali kuhusu uendelezaji waujasiriamali yakiwemo masoko. Ofisi zote za mikoa isipokuwaya Mkoa wa Pwani zina vituo vya habari ambapowajasiriamali hupata habari zote zinazohusiana na uanzishajina uendelezaji wa miradi ya uzalishaji na biashara ikiwa nipamoja na teknolojia, mafunzo na masoko. Vituo hivyovinapaswa kuwa na sehemu ambako wajasiriamaliwanaweza kuweka sampuli za bidhaa zao ili wananchiwaweze kuona. Hadi sasa mikoa ya Dodoma na Rukwa ndiyoiliyo na sehemu za wajasiriamali za kuoneshea bidhaa zao(display facility) ambazo zimejidhihirisha vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Julaimpaka Desemba, 2012, jumla ya kesi nne zilisikilizwa nakutolewa maamuzi na kesi tano zinaendelea na mchakatowa kusikilizwa. Pia, Baraza la Ushindani (FCT) l i l iwezakukamilisha Mpango Mkakati mpya wa kipindi cha 2012/2013– 2015/2016. Rasimu ya Mpango Mkakati huo ilijadiliwa

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

113

kwenye kikao cha wadau wote muhimu wa Baraza tarehe28/09/2012. Uidhinishaji rasmi wa Mpango Mkakati huounatarajiwa kufanyika mwaka 2013. Baraza limefanyamafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wake ili kuwajengeauwezo zaidi katika maeneo yao ya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza limefanya mapitio yaSheria ya Ushindani na kubainisha upungufu kadhaaunaohitaji kufanyiwa marekebisho. Upungufu huo ni pamojana kukosekana kwa Makamu wa Mwenyekiti na muda waWajumbe kukoma kwa pamoja. Baraza kwa kushirikiana naTume ya Ushindani limefikisha mapendekezo ya marekebishoya sheria Wizarani ili mchakato wa kuyafikisha Bungeni uanze.Mapendekezo hayo yameandikiwa Waraka wa Baraza laMawaziri ambao kwa sasa uko katika hatua ya kujadiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza la Taifa la Utetezi waMlaji (NCAC) linasimamia maslahi ya mlaji kwa kupelekamaoni yake kwenye Tume ya Ushindani, Mamlaka za Udhibitina Serikali kwa ujumla. Katika mwaka 2012/2013, Barazalimeendelea kupokea na kusambaza taarifa na maoni yenyemaslahi kwa mlaji; Kuanzisha Kamati za Mlaji za Mikoa naSekta na kushauriana na Kamati hizo; wenye viwanda, Serikalina jumuiya nyingine za walaji katika mambo yenye maslahikwa mlaji. Ili kumlinda mlaji, elimu kwa mlaji imetolewa kwakuanzia katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar esSalaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vituo vya Biashara Nje yaNchi. Kituo cha Biashara cha Tanzania Dubai (TTC-Dubai) Kwamwaka 2012/2013, Kituo kimeendelea kuvutia wawekezajiwa nje ili kuwekeza Tanzania na kutafuta masoko kwa ajiliya bidhaa za Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu(United Arab Emirates – UAE). Juhudi zilizofanyika kwa mwakahuo ni kama zifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutafuta masoko yabidhaa za Tanzania, Kituo kimeratibu na kuwezesha ushirikiwa wajasiriamali watano wa Tanzania kwenye maoneshoya Global Village yaliyofanyika Dubai kwa miezi sita. Kituo

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

114

kimewezesha kampuni za Tanzania kuuza mbao aina yaTeak, dhahabu, Tanzanite, karafuu, mashudu na nyama yambuzi katika soko la Umoja wa Falme za Kiarabu, ambapomauzo ya zaidi ya Shilingi bilioni 100 yamefanyika.

Vilevile, Kituo kimewezesha Kampuni ya Ms Faisal Oilskuwekeza katika usambazaji wa vilainishi (lubricants) nchinikwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biasharahiyo kwa nchi zote za Afrika Mashariki na Kusini. Mauzo yaokwa sasa wamefikia zaidi ya Shilingi billioni 10. Baadaye,wanakusudia kujenga kiwanda cha kutengeneza vilainishihivyo nchini. Aidha, Kampuni ya ISSG Group ya Dubai,imewekeza katika uchimbaji wa dhahabu eneo la Morogoro.Uzalishaji wa majaribio tayari umekwishaanza na jumla yaShilingi bilioni 2 zinatarajia kuwekezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kimendelea kuwakitovu cha habari za utalii na kuwasilisha machapisho yautalii kwa mawakala wa utalii na wanajumuiya wa UAE.Jumla ya machapisho 5,000 kutoka TANAPA, Ngorongoro,Tanzania Tourist Board-TTB, Kamisheni ya Utalii Zanzaibar nakampuni binafsi ya Bobby Tours ya Arusha yamesambazwa.Pia, Kituo kiliratibu ushiriki wa Tanzania kwenye World RouteDevelopment Forum ambapo washiriki kutoka viwanja vyandege vya JNIA, Mwanza, mashirika ya TCAA, TAA, KADCOna TTB walishiriki na kuweza kuvitangaza viwanja vyetu navivutio vyetu vya utalii. Shirika la Ndege la Uturuki lilisainimakubaliano na KADCO ya kutumia Uwanja wa KIA kwandege zake za abiria. Aidha, Tovuti za mawakala wa utaliiwa Tanzania, Kampuni ya Bobby Tours ya Arusha na Shirika laViwango Tanzania (TBS) waliunganishwa na Tovuti ya Kituocha Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukuza biashara,Kituo cha Biashara cha Tanzania Londoni (TTC-London)kimefanya utafiti wa bidhaa zenye sifa ya kupata masokonje katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar esSalaam na Nanenane (Dodoma) ambapo utafiti wamakampuni yenye bidhaa zenye sifa ya kupata masoko njeulifanyika na sampuli za bidhaa 12 kukusanywa.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

115

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maonesho ya Bidhaa zaChakula yalifanyika London na makampuni sita ya MarketResearch and Export Agent ya Dar es Salaam, Amir Hamza(T) Ltd ya Bukoba, KYM’S Enterprises ya Kibaha, Kagera TeaBlenders Ltd ya Kagera, Nature Ripe Kilimanjaro Ltd ya Dar esSalaam, na TanTrade (Zanzibar) yalishiriki. Kongamano lakiuchumi kati ya Afrika na Ireland lilifanyika tarehe 22 Oktoba,2012 mjini Dublin ambapo fursa za kibiashara na uwekezajizilizopo kati ya Afrika na Ireland zilijadiliwa na mikakati yakuimarisha mahusiano hayo iliwekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kiliendelea kuvutiauwekezaji kama vile usafiri wa reli ambapo Kituo kiliwezeshaKampuni ya SMH RAIL ya Malaysia kufanya mawasiliano nakampuni ya TAZARA na walifanikisha kusaini mkataba waushirikiano mwezi Oktoba 2012. Kituo kilishiriki katika mkutanowa masuala ya gesi na mafuta uliohusu nchi za AfrikaMashariki ambapo wadau 150 wakiwa ni wawekezaji,waandishi na maafisa balozi na Serikali za Ethiopia, Somalia,Kenya, Msumbiji, Uganda na Tanzania walishiriki. Kutokanana mkutano huo, wawekezaji kutoka Kampuni ya ChicagoBridge and Iron Company (CBI) walitembelea Kituo kwaushauri wa mipango ya ziara nchini Tanzania ambayoyalifanyika tarehe 16 Oktoba 2012 ili kudadisi fursa za uwekezajikatika Sekta ya Nishati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utangazaji wa fursa zauwekezaji kupitia chapisho la International Investor ulifanyikaambapo sera, mikakati na fursa za biashara na uwekezajiTanzania vilitangazwa.

Aidha, vivutio vilivyoko nchini Tanzania vilitangazwakupitia semina ya Utalii - Redditch, maonesho ya Utalii ya(WTM) London yaliyofanyika mwezi Novemba 2012, ambapoMakampuni 60 ya Tanzania yalishiriki. Vilevile, Kituokiliendeleza mahusiano ya Kimataifa kwa kushiriki MkutanoMkuu wa mwaka wa Britain Tanzania Society katika mkutanowa shirika la mkonge, Mkutano wa Shirika la Sukari, Mkutanowa Shirika la wataalamu wa kilimo (CABI) ambao Wajumbewake ni wanachama wote wa Jumuiya ya Madola

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

116

(Commonwealth Agricultural Bureau International) naMkutano wa Shirika la Nafaka (International Grain Council).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maendeleo yaRasil imali Watu. Wizara ina Watumishi 232 wa kadambalimbali. Kwa mwaka 2012/2013, imejaza nafasi 32zilizowazi na imepandisha vyeo watumishi 28. Kwa upandewa kuwajengea uwezo watumishi, Wizara imewezeshakuwapeleka jumla ya watumishi 48 katika mafunzo ya mudamfupi na mrefu ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Awamuya Pili ya Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma yamiaka mitano kuanzia mwaka 2008 hadi 2012, ambayoinalenga kuimarisha utendaji unaojali matokeo na kuimarishauwajibikaji katika Utumishi wa umma, katika mwaka 2012/2013, watumishi wote wamesaini Mikataba ya Kazi kwaMfumo wa Wazi wa Mapitio ya Tathmini ya Utendaji Kazi –MWAMTUKA, (OPRAS).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeunda Kamati ambayo ni Dawati la KushughulikiaMalalamiko na Kero za wadau wa ndani na nje. Kamati hiyoimejumuisha Wajumbe kutoka kila Idara na Vitengo. Kamatiimeweka utaratibu wa kupokea, kukusanya, kufuatilia nakutafuta ufumbuzi wa malalamiko na kero na kuwasilishataarifa kwenye Menejimenti ya Wizara. Umewekwa mudamaalum wa wiki moja kushughulikia malalamiko na kero nakutoa mrejesho kwa wadau ndani ya muda maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masuala mtambuka,kwa upande wa kupambana na Rushwa, Wizara imeendeleana jitihada za kupambana na kudhibiti rushwa kwawatumishi wake kwa kutoa mafunzo ya Sheria mbalimbaliza kazi, zikiwemo Sheria Na. 8 ya mwaka 2002 ya Utumishiwa Umma, na Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria ya Fedhaili kuwawezesha kufanya kazi na kutoa maamuzi kwakuzingatia matakwa ya sheria tajwa. Ili kuweza kutoahuduma bora zinazokidhi viwango vilivyoainishwa katikaMkataba wa Huduma kwa Mteja, Wizara imetoa mafunzo

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

117

ya elimu ya huduma kwa mteja kwa watumishi wa Wizara ilikuwapatia mbinu mbalimbali za kuhudumia wateja. Wizarapia, ilitoa mafunzo kuhusu maadili ya utendaji katika Utumishiwa Umma na kuwakabidhi vijitabu hivyo kwa mujibu waKanuni Na. 66 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka2003.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mazingira,Wizara kwa kushirikiana na NEMC na wadau mbalimbaliimeendelea kutekeleza mikakati inayohusu utunzaji wamazingira pamoja na programu ya utekelezaji wa Sheria yaUsimamizi na Utunzaji wa Mazingira. Wizara imehamasishamiradi mipya itakayoanzishwa kutimiza masharti ya uzalishajisalama viwandani na kuhimiza miradi ya zamani ambayohaikuwa na mifumo salama kwa mazingira ijenge mifumohiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kupambana naUKIMWI/VVU, Wizara imeendelea kutoa mafunzo ya kujikingana maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na kuhamasishaupimaji wa afya za wafanyakazi kwa hiari.

Pia, Wizara imeendelea na jitihada za kuwawezeshawatumishi waliojitokeza na watakaojitokeza wanaoishi navirusi vya UKIMWI kupata huduma ya virutubisho, lishe nausafiri. Waelimishaji rika walipewa mafunzo upya yakuwawezesha kupata mbinu mpya ambazo zimewezeshakuwaelimisha watumishi wenzao na familia zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kujumuisha Masualaya Jinsia katika Sera, Mikakati, Programu na Bajeti ya Wizarana Kutoa Mafunzo kwa Wataalam katika Masuala ya Jinsia,Mwongozo wa Taifa wa kuratibu masuala ya Jinsia katikaUtumishi wa Umma unaelekeza uanzishwaji wa programuya masuala ya jinsia ya kisekta, Dawati na Kamati ya KuratibuMaendeleo ya Jinsia katika sekta. Wizara imetoa mafunzokwa maafisa 50 kutoka Idara na Taasisi chini ya Wizarakuhusiana na uchambuzi wa masuala ya jinsia katika Sektaya Viwanda na Biashara.

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

118

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa hudumaza Sheria, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheriawa Serikali, inaendelea kupitia sheria, mikataba na mashaurimbalimbali ya Wizara na Taasisi kwa lengo la kuboreshautekelezaji wake na kulinda maslahi ya nchi. Pia, Wizarainazingatia matumizi ya njia za amani katika kutatuamigogoro inayohusu sekta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya jukumu la Wizarani kutoa taarifa zinazohusu masuala ya Viwanda na Biasharakwa wadau na kwa wakati. Wizara inazingatia matumizi yaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA katikakupokea, kutunza na kusambaza taarifa mbalimbalizinazohusu Sekta. Kwa mwaka 2012/2013, Wizara imeboreshaTovuti yake (www.mit.go.tz) ili kuongeza ufanisi katikautekelezaji wa majukumu yake. Wizara kwa kushirikiana naOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (POPSM) naWakala ya Serikali Mtandao (eGA) inaratibu uanzishwaji waTovuti ya Biashara ya Kitaifa (National Business Portal).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha usimamiziwa Mapato na Matumizi ya Serikali kwa kuhakikisha kwambaSheria/ Kanuni na taratibu za fedha,zinazingatiwa. Kwamwaka 2012/2013, Wizara imefanya ukaguzi wa kawaida nakutoa taarifa za kila robo mwaka katika Kamati ya Ukaguziya Wizara. Ukaguzi maalum ulikuwa ukifanyika pale ambapokuna hitaji la kufanya hivyo.

Pia, Wizara imekuwa ikitekeleza ushauri unaotolewakatika taarifa za ukaguzi ili kuhakikisha kwamba mapungufuyaliyobainishwa yanarekebishwa; imeratibu na kusimamiavikao vya Kamati ya Ukaguzi na Kamati ya Kusimamia naKudhibiti Mapato na Matumizi ya Serikali na kuwasilisha taarifangazi husika kwa wakati. Wizara imesimamia na kujibu Hojaza Ukaguzi wa nje na kushiriki katika vikao vya Kamati yaBunge ya Hesabu za Serikali (PAC); imeandaa na kuwasilishataarifa za mwaka za mapato na matumizi kwa kufuatamfumo wa IPSAs na imeratibu na kuandaa taarifa za mapatona matumizi na kuziwasilisha kwa wakati.

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

119

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza Sheria yaUnunuzi wa Umma Na. 21 ya Mwaka 2004 na Kanuni zake zamwaka 2005, Wizara imeandaa Mpango wa Manunuzi waMwaka 2012/2013 kulingana na Sheria hiyo na kusimamiautekelezaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wamalengo ya kisekta, Wizara na Taasisi zilizo chini yakezilikabiliwa na changamoto mbalimbali. Moja kati yachangamoto hizo ni uhaba wa rasilimali fedha ambaoumepunguza kasi ya Wizara katika kuendeleza viwanda,biashara, masoko na viwanda vidogo na biashara ndogonchini. Kwa mfano, Wizara bado haijapata fedha za kutoshahususan za kulipia fidia katika maeneo huru ya Bagamoyo,Tanzania-China Logistic Centre (Kurasini) pamoja na ulipajifidia kwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya EPZ katika mikoaya Tanga, Ruvuma na Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda piaimekabiliwa na mlolongo mkubwa wa kodi, ushuru na tozowanazotozwa wenye viwanda. Hivi sasa viwanda vinatozwakodi na tozo mbalimbali zipatazo 25. Vilevile, kumekuwa nachangamoto ya gharama kubwa za kufanya biashara (costof doing bussiness) na uwekezaji kutokana na kuongezekakwa bei ya umeme na maji; kukatika mara kwa mara kwaumeme kunakosababisha uharibifu wa mitambo pamoja nabidhaa zilizoko kwenye mtiririko wa uzalishaji; Kushuka kwathamani ya Shilingi; Mitambo chakavu na teknolojia duni zauzalishaji na Upungufu wa wataalam wenye umahiri katikafani mbalimbali viwandani (specialised industrial skills, e.g.leather and textiles technologists etc.).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushindani usio wa hakikutokana na bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi kutolipiwaushuru stahiki kwa kukwepa kodi au kutaja thamani ndogoya bidhaa husika (under invoincing and under declaration)umeendelea kuwa changamoto kubwa. Changamotonyingine ni ukosefu wa maeneo ya uwekezaji wa viwandapamoja na ukosefu wa mitaji ya kuanzisha viwanda vyakuendeleza biashara. Aidha, uendelezaji wa usindikaji wa zao

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

120

la korosho na pamba kwa ukamilifu wake katika uchumiwetu bado ni changamoto kubwa kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kukabiliana nachangamoto na kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara,Wizara na Taasisi zake zimechukua hatua zifuatazo:Kutayarisha maandiko mbalimbali yatakayosaidia sekta hiyokunufaika na mikopo ya kibenki pamoja na Mpango wa Ubiakati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi - Public PrivatePartnership (PPP). Pia tuliendelea kushirikiana na Taasisinyingine zinazohusika na maendeleo ya teknolojia kama vileCOSTECH katika kuwawezesha na kuendeleza ubunifu wataasisi za TIRDO, CAMARTEC na TEMDO ambazo zimefaidikana fedha za Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Vilevile, tumeshirikiana na sekta nyingine katikakuboresha mazingira ya biashara na kusaidia kupunguzagharama za kufanya biashara. Jitihada hizo zinajumuishakurahisisha taratibu za usajili wa Makampuni kupitia BRELAkwa kuweka fomu zote za maombi ya usajili mbalimbalikwenye tovuti yake na kufupisha muda wa kusajili kutokasiku tano hadi kufikia siku tatu. Pia SIDO inahamasishaujasiriamali na kuelimisha umma kuhusu kufanya shughulirasmi na katika vikundi ili kuondokana na mtizamo hasi katikakufanya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi.

Aidha, Wizara kupitia taasisi zake za FCC, CBE,COSOTA, SIDO, TBS, WMA, TWLB na TANTRADE zinashirikiana ilikumsaidia mwananchi katika kupata elimu ya biashara,mbinu za kufanya biashara kiushindani, kumlinda mlaji dhidiya bidhaa bandia pamoja na manyanyaso ya soko na piakusimamia matumizi sahihi ya vipimo na viwango katikabiashara.

Vilevile, wananchi wanafahamishwa kuhusu fursambalimbali za masoko na matumizi yake yakiwemo yaJumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Uchumi Kusinimwa Afrika (SADC), masoko ya upendeleo na masokomaalum kama AGOA, India na China. Kuendelea kutekelezamiradi muhimu ya maendeleo kupitia NDC, EPZA, SIDO,

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

121

CAMARTEC, TEMDO, TIRDO na kuendeleza majadiliano nawashirika wa Maendeleo (Sector Dialogue) ambaowanasaidia sekta hii hususan nchi rafiki na taasisi za kimataifaili kushirikiana na kupata teknolojia inayohitajika kuendelezasekta hii ya kipaumbele cha Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bajeti ya mwaka 2013/2014,imelenga kutatua changamoto zilizotajwa, kuongezaubunifu katika utendaji wetu, kuongeza ushirikiano na sektabinafsi kwa kupitia mfumo wa PPP, kutafuta fedha zaidi nahivyo kuendeleza sekta hiyo, ili itoe mchango wake kamainavyotegemewa katika mpango wa miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka 2013/2014,Sekta ya Viwanda ina malengo yafuatayo:-

(i) Kuendelea na utekelezaji wa MkakatiUnganishi wa Uendelezaji Viwanda nchini kwa kuendelezauhamasishaji wa uwekezaji na kutoa kipaumbele kwaviwanda vinavyoongeza thamani ya mazao ya kilimo;

(ii) Kufuatilia miradi ya TANCOAL, Kasi mpyaMchuchuma na Liganga na Umeme wa Upepo (MkoaniSingida) inayoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia NDCna Sekta Binafsi. Mradi wa kiwanda cha kuzalisha viuaduduvya mazalia ya mbu waenezao malaria TAMKO, Kibaha;

(iii) Kusimamia utekelezaji wa Mpango Kabambewa Kuendeleza Viwanda (Master Plan);

(iv) Kufuatil ia utekelezaji wa miradi yaMchuchuma na Liganga unaoendeshwa kwa ubia kati yaSerikali ya Tanzania na Kampuni ya Sichuang Hongda ya nchiniChina;

(v) Kuendelea kutoa mafunzo ya kuongeza tija,ufanisi pamoja na ubora wa bidhaa kwa wenye viwandakupitia program ya Kaizen kwa kushirikiana na Shirika laMisaada la Japan (JICA) pamoja na UNIDO;

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

122

(vi) Kuendelea kushiriki katika uhamasishaji wautekelezaji wa Mpango Kazi wa Sera ya Viwanda ya Jumuiyaya Afrika Mashariki na ukamilishaji wa Sera ya Viwanda kwanchi za SADC na kufanya maboresho kulingana na mahitajiya nchi yetu;

(vii) Kufuatil ia ufufuaji wa viwandavilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi, ufufuaji waGeneral Tyre na Urafiki;

(viii) Kukamilisha sheria na kuandaa Kanuni zabiashara ya chuma chakavu;

(ix) Kuendeleza utekelezaji wa Mkakati waKuendeleza Viwanda vya Ngozi na Bidhaa za Ngozi; naMkakati wa Viwanda vya nguo na mavazi;.

(x) Kuendelea kuhamasisha, kuhifadhi na kulindamazingira katika shughuli zote za uzalishaji viwandani;

(xi) Kufuatilia uendelezaji na uwekezaji katikamaeneo ya EPZ na SEZ ikiwemo ulipaji wa fidia kwa maeneohusika; na

(xii) Kufanya tathmini ya maendeleo ya Viwandaili kubaini changamoto zinazokabili sekta na kuzitafutiaUfumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka 2013/2014,Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ina malengoyafuatayo:-

(a) Kupitia na kutathimini utekelezaji wa Sera yaMaendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo na kutoamapendekezo kwa madhumuni ya kuhuisha;

(b) Kujenga uwezo wa kutoa huduma za uganikatika maeneo walioko wajasiriamali hasa vijijini;

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

123

(c) Kuhakikisha teknolojia zinazofaa zinatafutiwautaratibu wa kuzalishwa kwa wingi na kusambazwa kwawatumiaji;

(d) Kujenga misingi ya kusaidia uzalishaji wabidhaa mpya kutokana na ubunifu wa wajasiriamali;

(e) Kuhamasisha Halmashauri na kuandaamwongozo utakaosaidia Halmashauri kutenga maeneoyanayohamasisha sekta kupanuka;

(f) Kuratibu utoaji wa mikopo kupitia Mfuko waNEDF;

(g) Kuwawezesha wajasiriamali kushiriki katikamaonesho ya ndani na nje ya nchi; na

(h) Kuwezesha uzalishaji wa zana za kuongezathamani mazao ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka 2013/2014,Sekta ya Biashara ina malengo yafuatayo:-

(i) Kuendeleza majadiliano kati ya nchi na nchi,Kikanda na Kimataifa kwa lengo la kupanua wigo wa fursaza masoko yenye masharti nafuu na kuvutia wawekezaji;

(ii) Kuendeleza majadiliano ya Mkataba wa Ubiawa Uchumi kati ya Jumuiya Afrika Mashariki na Jumuiya yaUlaya (EAC - EU - EPA Negotiations) kwa lengo la kupatamisaada ya kifedha na kiufundi ambazo zitasaidia kupunguzachangamoto za uzalishaji duni;

(iii) Kuendeleza majadiliano ya kuanzishwa kwaEneo Huru la Biashara la Utatu (Tripartite Free Trade Area -FTA) linalojumuisha Kanda za COMESA - EAC na SADC ilikupanua wigo zaidi wa fursa za masoko ya bidhaa zetu;

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

124

(iv) Kuendelea na majadiliano ya kuanzishaUmoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACMonetary Union) kwa lengo la kurahisisha biashara;

(v) Kuendelea kuimarisha Kamati ya Kitaifainayoshughulikia ufuatiliaji, utoaji taarifa na utekelezaji wamikakati ya kuondoa Vikwazo Visivyo vya Kiushuru (NTBs) kwalengo la kurahisisha biashara;

(vi) Kuendelea na majadiliano ya kuanzishwa kwaUmoja wa Forodha wa SADC (SADC-Customs Union) nakulegezeana masharti katika sekta ya Biashara ya Huduma(Trade in Services Liberalization) ili kupanua wigo wa Biasharaya bidhaa na huduma;

(vii) Kuimarisha vituo vya biashara vilivyopoLondon na Dubai ili kuendelea kutangaza masoko ya bidhaaza Tanzania na fursa mbalimbali na kuvutia wawekezaji nawatalii nchini;

(viii) Kuanzisha vituo vipya vya biashara kwakuanzia nchini China na Afrika Kusini na pia kupelekaWaambata wa Biashara nchini Marekani na Ubelgiji kwalengo la kuitangaza Tanzania na kuunganishawafanyabiashara wa Tanzania na masoko ya nje;

(ix) Kutekeleza Mkakati wa Kukuza Mauzo Njeambao umelenga mazao, bidhaa za huduma za kipaumbelezenye fursa na uwezekano wa kuendelezwa kwa haraka nakutoa matokeo ya haraka –(Quick Wins) na Mpango Unganishiwa Biashara ya Tanzania.(Tanzania Trade Integration Strategy-TTIS);

(x) Kuendelea kushiriki majadiliano ya Duru laDoha kwa lengo la kutetea maslahi ya Tanzania katikamajadiliano yanayoendelea;

(xi) Kuhamasisha Jumuiya za Wafanyabiashara nawananchi kwa ujumla juu ya fursa mbalimbali za masoko yabidhaa na huduma zitokanazo na majadiliano mbalimbali;

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

125

(xii) Kukamilisha zoezi la Mapitio ya Sera ya Taifaya Biashara ya mwaka 2003; na

(xiii) Kushiriki kikamilifu katika majadiliano kati yaJumuiya ya Afrika Mashariki na Marekani (EAC-US Trade andInvestment Partnership) yenye lengo la kukuza biashara nauwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka 2013/2014,malengo ya Sekta ya Masoko ni yafuatayo:-

(i) Kuendelea kushirikiana na wadau kuendelezamiundombinu ya masoko nchini;

(ii) Kuendelea kushirikiana na wadau katikakuendeleza Vituo vya Ukaguzi wa Pamoja Mipakani (One StopBorder Post - OSBP) ;

(iii) Kuimarisha Kamati za Kufanya Kazi PamojaMipakani (Joint Border Committees – JBCs) ili kuboreshamazingira ya kufanya biashara mipakani;

(iv) Kukamilisha marekebisho ya sheriazinazokinzana na uboreshaji wa mazingira ya biashara;

(v) Kuandaa Sera ya Walaji (consumer policy);

(vi) Kushirikiana na wadau kukamilisha maandaliziya kuanzisha Soko la Mazao na Bidhaa (CommodityExchange);

(vii) Kuendeleza mfumo wa stakabadhi za mazaoghalani ili uweze kutumika katika uanzishaji wa Soko laMazao na Bidhaa;

(viii) Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi nakusambaza taarifa za masoko kwa wadau kwa wakati;

(ix) Kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko yamipakani, kikanda na kimataifa; na

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

126

(x) Kutangaza bidhaa za Tanzania katika masokoya ndani na nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya EPZA kwamwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kukamilisha ulipaji wa fidia katika eneo EPZBagamoyo;

(ii) Kuanza uendelezaji wa miundombinu yamsingi (barabara, umeme, maji safi na maji taka) pia ujenziwa Bandari mpya katika eneo la Mbegani kwa kushirikianana sekta binafsi;

(iii) Kukamilisha mikataba ya ubia na kuanzauendelezaji wa mradi wa Tanzania China Logistic Centre;

(iv) Kupima na kufanya tathmini katika maeneoya EPZ Mikoani Arusha na Mwanza na kuandaa Master Planskwa maeneo ya EPZ/SEZ ya Mtwara, Mara, Tanga, Songeana Manyara;

(v) Kukamilisha ulipaji fidia katika maeneo yaRuvuma, Tanga na Kigoma;

(vi) Kuanzisha viwanda vipya vya uzalishaji 35katika maeneo ya EPZ na SEZ; na

(vii) Kuanzisha mradi wa uwezeshaji wajasiriamali(EPZ Incubator) kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kuwekezakupitia mifumo ya EPZ na SEZ.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya Shirika laMaendeleo la Taifa (NDC) katika mwaka 2013/2014 ni kamaifuatavyo:-

(i) Kuendeleza utekelezaji wa miradi ya makaaya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga;

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

127

(ii) Kukamilisha ujenzi wa Kiwanda cha KuzalishaViuadudu (biolarvicides) vya kuua viluwiluwi wa mbuwaenezao malaria katika eneo la TAMCO, Kibaha;

(iii) Kuzalisha umeme kwa kutumia makaa yamawe ya Ngaka Kusini, Songea;

(iv) Kukamilisha upatikanaji wa mkopo wa mradiwa kuzalisha umeme kwa kutumia upepo Singida na kuanzaujenzi;

(v) Kukarabati Kiwanda cha General Tyre, Arushaili kukifufua na kuanza uzalishaji wa matairi;

(vi) Kukamilisha tafiti na kuanzisha kiwanda chakuzalisha magadi soda eneo la Ziwa Natron na Engaruka,Arusha;

(vii) Kuanzisha viwanda vya kusindika nyama,mpira na mazao mengine ya Kilimo;

(viii) Kuendeleza utekelezaji wa mradi wa KasiMpya wa kuzalisha chuma ghafi;

(ix) Kujenga maeneo ya viwanda (Industrial parks)sehemu za TAMCO, KMTC na Kange;

(x) Kujengea uwezo wananchi wa maeneo husikakufaidi miradi inayotekelezwa na NDC; na

(xi) Kuratibu uendelezaji wa kanda za maendeleoza Mtwara, Tanga, Kati na Uhuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya CAMARTEC kwamwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kuunda zana za kilimo hifadhi zitakazotumikakwenye trekta lililoundwa CAMARTEC;

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

128

(ii) Kukamilisha uundaji wa mashine ya kuvuna,kupura na kupepeta mpunga na kuifanyia majaribio kwenyemikoa ya Kilimanjaro na Mororgoro;

(iii) Kuunda mashine ya kufunga majani kwa ajiliya kuboresha matumizi ya malisho kwa kuongeza muda wakukaa rafuni;

(iv) Kuendelea kujenga mitambo mikubwa yabiogesi kwa ajili ya kufua umeme kwenye shule na taasisinchini kwa kuanzia na mikoa ya Manyara, Mara, Kagera naMwanza;

(v) Kuendeleza uundaji wa mashine kukatakatamalisho ya wanyama zinazoendeshwa kwa injini;

(vi) Kueneza vifaa vya matumizi ya nishati yabiogesi (biogas appliances) katika maeneo kulikojengwamitambo ya biogesi ili kuifanya teknolojia hiyo kuwaendelevu;

(vii) Kutoa mafunzo kwa wajasiriamali juu ya ujenziwa nyumba za gharama nafuu na usanifu wa mitambo yabiogesi; na

(viii) Kutoa mafunzo kwa watumiaji wa zana zakilimo ili kuongeza tija katika kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya TEMDO kwamwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kutoa huduma ya ushauri wa kihandisipamoja na mafunzo katika viwanda kumi vya kati navikubwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji, ubora wa bidhaa,faida, kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya nishati;

(ii) Kuboresha miundombinu ya kiatamizi nakutoa huduma kwa wajasiriamali watengenezaji wamashine na vifaa kwa matumizi ya viwanda vya kati(machinery and equipment for light industries). Lengo ni

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

129

kuwezesha wajasiriamali wawili kufikia uwezo wa kuendeshaviwanda vya kati;

(iii) Kubuni, kuendeleza na kuhamasishautengenezaji wa mtambo mdogo wa kuzalisha umemekutokana na nguvu ya maji (Mini Hydro Power Plant) kwamatumizi ya uzalishaji wa umeme vijijini pamoja na mtambomdogo wa kurejesha maji (Small Scale Water Recycling Plant)mijini;

(iv) Kuendeleza na kuboresha chasili (prototypedevelopment) cha mtambo wa kurejesha taka za plastiki namtambo wa kuzalisha umeme kutokana na mabaki yamimea (generation of electricity from biomass and municipalsolid wastes); na

(v) Kuendelea na maboresho pamoja nauhawilishaji wa teknolojia mbalimbali ikiwa ni pamoja nateknolojia ya kuteketeza taka za hospitali (bio-medical wasteincineration), teknolojia ya machinjio na kuongeza thamanikatika mabaki ya mazao ya mifugo na teknolojia ya vifaavya hospitali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya TIRDO kwamwaka 2013/2014 ni ifuatavyo:-

(i) Kufanya tafiti zenye lengo la kupata teknolojiaza kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo (Valueaddition on Agro products);

(ii) Kutoa huduma za kitaalam viwandani zenye lengola kuongeza uzalishaji wa bidhaa bora bila kuchafuamazingira pia zinazolenga matumizi bora ya nishati;

(iii) Kuendelea kutekeleza mkakati wa kuimarishasekta ya ngozi na viwanda vya ngozi ili kupunguza uharibifuwa mazingira kwa kurejesha taka za ngozi ili kutengenezabidhaa kama Leather Boards;

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

130

(iv) Kukamilisha mchakato wa kuhakiki(Accreditation) na kuboresha maabara ya mazingira na yavifaa vya kihandisi ili ziweze kufikia viwango vya kimataifana kuweza kutoa huduma bora kwa wazalishaji viwandani;

(v) Kutekeleza mfumo wa ufuatiliaji wa mazao(traceability) kwa kutumia teknohama na pia kusaidiautendaji wa kampuni ya GS1 (Tz) National Ltd. kama mshauriwa kiufundi;

(vi) Kutoa huduma za kitaalam kwa wawekezajiwanaotaka kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo katikasekta ya uzalishaji bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo(agro-processing, industries) kupitia benki ya rasilimali (TIB);

(vii) Kujenga tovuti ili kusaidia wazalishaji wadogona kati kutangaza bidhaa zao waweze kupata masoko yandani na nje ya nchi;

(viii) Kuendelea kukusanya maoni ya wadau kuhusukurejea Sheria ya Bunge Na. 5 ya mwaka 1979 iliyoanzishaTIRDO ili Shirika liweze kufanya utafiti kuendana na mabadilikoyanayoendelea duniani; na

(ix) Kukamilisha mchakato wa mpango wamatumizi bora ya ardhi ya TIRDO (land use Plan) ili kuzuiauvamizi na kuainisha matumizi yanayolenga kuleta tija kwashirika na viwanda kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya Shirika laViwango kwa mwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kuendeleza utekelezaji wa utaratibu wakupima ubora wa bidhaa zote mahali zinapotoka kabla yakuingia nchini (Preshipment Verification of Conformity toStandards – PVoC);

(ii) Kuendelea kuimarisha utaratibu wa kukaguaubora wa bidhaa zilizo sokoni ukiwemo ukaguzi wa magarikabla ya kuingia nchini;

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

131

(iii) Kuendeleza juhudi za kutoa elimu nakuhakikisha kwamba maabara zote za Shirika zinapata vyetivya umahiri (laboratory accreditation) i l i kuwezeshakukubalika kwa bidhaa nyingi zaidi za Tanzania katika sokola ndani na nje;

(iv) Kushirikiana kwa karibu na vyombo vinginevya Serikali kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), MkemiaMkuu wa Serikali, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishatina Maji (EWURA), Tume ya Ushindani Halali (FCC), Mamlakaya Udhibiti wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingia nchini nizenye ubora unaokubalika;

(v) Kuongeza idadi ya leseni kutoka leseni 120 kwamwaka kufikia leseni 150 katika mwaka 2012/2013;

(vi) Kuongezeka idadi ya upimaji sampuli kutoka9,300 kwa mwaka hadi kufikia 10,900 katika mwaka 2012/2013;

(vii) Kutayarisha viwango vya taifa vinavyofikia 150vikiwemo viwango vya sekta ya huduma katika mwaka 2012/2013; na

(viii) Kuendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamalinchini kote kuhusu viwango vya udhibiti wa ubora wa bidhaana kuongeza vyeti vya ubora wa bidhaa zinazoagizwakutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2013/2014, Baraza la Ushindani litatekeleza malengoyafuatayo:-

(i) Kusikil iza kesi za rufaa zinazotokana namchakato wa Udhibiti na ushindani wa Biashara kwenye soko;

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

132

(ii) Kujenga uwezo zaidi wa Baraza katika kushugulikiakesi hizo kwa kuimarisha rasilimali watu na Wajumbe waBaraza;

(iii) Kutoa elimu kwa umma juu ya kazi za Baraza naumuhimu wake katika uchumi; na

(iv) Kuanza taratibu za kununua kiwanja kwa ajili yaujenzi wa Jengo la Ofisi ya Baraza kwa kuwa kwa sasa Barazalipo kwenye jengo la kupanga (Ubungo Plaza).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Usajili waBiashara na Leseni (BRELA). Malengo ya Wakala wa Usajili waBiashara na Leseni kwa mwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kuendelea na maandalizi ya utaratibu wa kuwekamifumo ya kiteknolojia itakayowawezesha wadau kupatataarifa na huduma kwenye mifumo ya kompyuta (On lineregistration systems) kwa wakati;

(ii) Kuboresha usajili wa makampuni na majina yabiashara kwa kutumia mfumo na mashine za kisasa ‘specialmachine readable certificates’;

(iii) Kufanya marejeo ya sheria zinazosimamiwa naWakala ili ziweze kwenda na wakati;

(iv) Kuboresha mifumo ya uwekaji na utunzaji waMasijala tano za kisheria zinazosimamiwa na Wakala ilikuweza kushabihiana na mifumo ya kitekinolojia na hatimayekurahisisha utoaji huduma;

(v) Kuendelea kuelimisha umma kuhusu shughuli zaWakala na umuhimu wa kusajili biashara;

(vi) Kuendeleza watumishi na kuwawekea mazingiramazuri ya utendaji kazi ili kuongeza tija na uwajibikaji;

(vii) Kuendeleza mahusiano na mashirika ya kimataifaambayo Tanzania ni Mwanachama;

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

133

(viii) Kuanza kwa ujenzi wa Jengo la BRELA kwaajili ya Ofisi na Masijala;

(ix) Kutoa huduma za usajili kwa wateja wa BRELAkwa mtindo wa papo kwa papo katika maoneshombalimbali kama Sabasaba, Nanenane, Wiki ya Utumishiwa Umma, makongamano na katika warsha zinazoandaliwana Wakala au Wadau wengine kama SIDO, MKURABITA nawengineo fursa zinapotokea; na

(x) Kuendeleza na kuimarisha mahusiano mazurina ushirikiano na taasisi mbalimbali za ndani ya nchi katikakufanikisha shughuli za Wakala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka wa 2013/2014,Tume ya Ushindani (FCC) imepanga kutekeleza yafuatayo:-

(i) Kudhibiti na kupambana na uingizaji nauzalishaji wa bidhaa bandia;

(ii) Uchunguzi na usikilizaji wa kesi za ushindani;

(iii) Utafiti wa masoko ili kubaini matatizo yaushindani usio wa haki wa masoko husika na hatua zakurekebisha; na

(iv) Kumlinda na kumwelimisha mlaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika kipindi cha mwaka2013/2014, Baraza la Taifa la Utetezi wa Mlaji litatekelezayafuatayo:-

(i) Kusimamia maslahi ya mlaji kwa kupelekamaoni yake kwenye Tume ya Ushindani, Mamlaka za Udhibitina Serikali kwa ujumla;

(ii) Kuendelea kupokea na kusambaza taarifa namaoni yenye maslahi kwa mlaji; na

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

134

(iii) Kuanzisha Kamati za Mlaji za Mikoa na Sektana kushauriana na Kamati hizo; wenye viwanda, Serikali najumuiya nyingine za walaji katika mambo yenye maslahi kwamlaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka 2013/2014,Bodi ya Leseni ya Maghala (TWLB) itatekeleza yafuatayo:-

(i) Kusimamia utekelezaji wa Mfumo waStakabadhi za Maghala katika maeneo yote yanayotekelezamfumo huo hapa nchini;

(ii) Kutoa elimu ya Mfumo kwa wadau hususaniwakulima waishio vijijini;

(iii) Kujenga uwezo kwa wakulima na wadauwengine wa mfumo kwa kuwapa mafunzo ya mfumo waStakabadhi za mazao ghalani;

(iv) Kuratibu shughuli za wadau wa Mfumo waStakabadhi za maghala;

(v) Kuwaunganisha wakulima na taasisi za fedhakupitia Vikundi na Vyama vya Ushirika ili waweze kujipatiamikopo; na

(vi) Kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano namakongamano ya kitaifa na kimataifa yanayojadili maswalayanayohusiana na mfumo wa stakabadhi za maghala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la KuhudumiaViwanda Vidogo. Malengo ya SIDO kwa mwaka 2013/2014ni yafuatayo:-

(i) Kuimarisha uwezo wa kuzalisha nakusambaza mashine ndogo ndogo za kusindika mazao;

(ii) Kuwezesha usambazaji wa teknolojia vijijinikwa kupitia programu ya Wilaya Moja bidhaa Moja (ODOP);

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

135

(iii) Kusaidia uanzishwaji wa kongano za viwandavidogo vya kusindika alizeti;

(iv) Kusaidia shughuli za ubunifu na utengenezajiwa bidhaa mpya kupitia programu ya kiatamizi;

(v) Kujenga chumba cha kufundishia cha Kituocha mafunzo ya ngozi cha Dodoma;

(vi) Kuanzisha vituo vidogo vya kuuzia bidhaa zawajasiriamali hasa mazao ya shamba katika barabara kuu;

(vii) Kuhakikisha upatikanaji wa vifungashio kwabidhaa za wajasiriamali wadogo;

(viii) Kuhawilisha teknolojia zi l izobuniwa nakujaribiwa ili ziweze kupatikana kwa wingi na kutumikakuzalishia mali;

(ix) Kutoa elimu ya ujasiriamali, uongozi wabiashara, usindikaji wa vyakula na kuzingatia ubora wabidhaa;

(x) Kujenga Ofisi ya SIDO ya Mkoa wa Pwani;

(xi) Kuwezesha vyuo vya mafunzo na uzalishaji vyaSIDO kufanya kazi;

(xii) Kuchangia kukamilisha ujenzi wa vituo vyamafunzo na uzalishaji wa vyakula vya Morogoro na Dar esSalaam;

(xiii) Kuwezesha wazalishaji wadogo kupatamasoko ya bidhaa na huduma zao, kwa kutengenezamiundombinu ya kupokea na kusambazia habari zakibiashara, kutengeneza sehemu ya kuonyeshea bidhaa zawazalishaji wadogo; na

(xiv) Kutoa huduma za kifedha ikiwa ni pamoja naushauri na mikopo pale itakapojidhihirisha kuhitajika.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

136

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chama cha HakimilikiTanzania (COSOTA); malengo ya COSOTA kwa mwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kufungua Ofisi ya Kanda ya Hakimiliki mjiniArusha kwa ajili ya Kanda ya Kaskazini na mjini Dodoma kwaajili ya Kanda ya Kati na Magharibi;

(ii) Kukamilisha marejeo ya Sheria ya Hakimiliki naHakishiriki ya mwaka 1999;

(iii) Kuanza utaratibu wa kusambaza stika(Hakigram) wasambaziji wote wa kazi za muziki na filamu;

(iv) Kuhamasisha wanunuzi wa CD, kanda zamiziki na filamu kununua kanda na CD zenye Hakigram; na

(v) Kuingia mkataba na makampuni binafsi kwalengo la kukusanya mirabaha na kufanya operesheni dhidiya kazi bandia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa 2013/2014,Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinalenga kutekelezayafuatayo:-

(i) Kuimarisha mafunzo yenye mwelekeo wakiutendaji katika nyanja za biashara yaani: Menejimenti yaUnunuzi na Ugavi, Utawala na Uongozi wa Biashara, Uhasibu,Menejimenti ya Masoko, Taaluma ya Mizani na Vipimo,Taaluma ya Habari na Mawasiliano na Taaluma nyinginezinazohusiana na hizo katika ngazi za astashahada,stashahada, shahada na stashahada ya uzamili;

(ii) Kuandaa mitaala mipya ya shahada yakwanza katika Ujasiriamali, Menejimenti ya Rasilimali Watuna Elimu ya Biashara. Vile vile Chuo kitaandaa mitaala yashahada ya uzamili;

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

137

(iii) Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwawajasiriamali wadogo wadogo na wakati ili kuwasadiawafanye biashara zao kwa ustawi mkubwa zaidi;

(iv) Kufanya utafiti na kutoa machapisho;

(v) Kuandaa mpango kabambe wa Chuo(Master Plan) katika Kampasi zake tatu yaani: Dar esSalaam,Dodoma na Mwanza;

(vi) Kununua ardhi ekari 500 kwa ajili ya upanuziwa shughuli za kampasi ya Dar es Salaam; na

(vii) Kukarabati majengo ya Chuo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo ya Mamlaka yaMaendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa mwaka2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kuwajengea uwezo wajasiriamali ili wawezekuzijua fursa na changamoto za masoko ya ndani na nje najinsi ya kuzimudu;

(ii) Kuwawezesha wanawake wafanyabiashrakwenye sekta isiyo rasmi katika mipaka ya Jumuiya ya Afrikaya Mashariki, ambayo ni mipaka ya Kabanga, Mutukula, Sirarina Namanga;

(iii) Kukuza Biashara na Kutafuta Masoko ya Ndanikwa kuratibu Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF,2013);

(iv) Kutafuta masoko ya nje kwa kuratibumaonesho ya Biashara ya Kimataifa ya nchi za nje;

(v) Kuwaunganisha wafanyabiashara na wadauwengine na fursa mbalimbali zikiwemo masoko ya ndani nanje ya nchi, kuwapa uelewa wa mwenendo wa bei za bidhaakitaifa na kimataifa;

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

138

(vi) Kuendeleza soko la ndani kwa Kusisimuamaendeleo ya biashara katika Sekta muhimu za kiuchumi;

(vii) Kutoa huduma ya taarifa za kibiashara;

(viii) Kushiriki katika kuboresha mfumo na sera zabiashara; na

(ix) Kuimarisha Ofisi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya Wakala waVipimo (WMA) kwa mwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kuendelea kuimarisha usimamizi wa matumiziya vipimo vilivyo sahihi nchini kupitia uimarishwaji wa uhakikina ukaguzi wa vipimo hivyo kwa lengo kuu la kumlinda mlaji;

(ii) Kuendelea kuongeza mbinu za utoaji waelimu ya matumizi ya vipimo hivyo kwa umma ili kuongezauelewa wa matumizi yake na ufungashaji wa bidhaa kwakiasi sahihi ili mnunuzi aweze kupata bidhaa hiyo kulinganana thamani ya fedha yake;

(iii) Kuendelea kuimarisha Kitengo cha VipimoBandarini (WMA Ports Unit) chenye jukumu la kusimamia,kuhakiki na kukagua usahihi wa vipimo vitumikavyo kupimiakiasi cha mafuta yaingiayo hapa nchini ili kiweze kutoahuduma hiyo kwa ufanisi;

(iv) Kukamilisha kazi ya utafiti na uchambuzi wamfumo wa vipimo vitumikavyo katika usambazaji wa gesiasilia (Natural Gas) ilikuweza kukamilisha zoezi la utengenezajiwa kanuni za gesi hiyo itakayokidhi usimamizi wa matumizisahihi ya vipimo hivyo;

(v) Kuendelea na zoezi la kuandaa kanuni mpyaya ufungashaji wa gesi kwenye mitungi itokanayo na mafutaya petroli (LPG) kwa kuwashirikisha zaidi wadau ili kuwezeshausimamizi wa usahihi wa kiasi cha gesi inayowekwa kwenyemitungi hiyo;

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

139

(vi) Kuendelea na kazi ya ujenzi wa kituo chakupimia magari yanayosafirisha mafuta katika eneo laMisugusugu, pwani, kituo cha Mwanza na Iringa;

(vii) Kuendelea na taratibu za kukamilisha utungajiwa Sheria mpya ya Vipimo (Legal Metrology Act) ili kukidhimatakwa ya sasa ya biashara na pia kuzingatia maridhianoyaliyofikiwa na nchi kikanda na kimataifa kuhusu masualaya vipimo; na

(viii) Kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwakuongeza vitendea kazi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaavya kitaalam na vyombo vya usafiri imara na vya kutoshakwa ofisi zote ili kuhakikisha huduma za Wakala zinazowafikiawalaji/wadau wengi zaidi, kwa haraka na ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya Kituo chaBiashara cha Tanzania Dubai-(TTC-Dubai) Kwa mwaka 2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kuongeza msukumo kwenye kuongeza mauzoya nyama ya mbuzi na kondoo hususan baada ya kukamilikakwa ujenzi wa machinjio ya Ruvu na ya mwekezaji binafsimkoani Kagera na bidhaa za majini (sea food), kwa kusaidiaMakampuni ya sekta hiyo kushiriki katika maonesho maalumyatakayofanyika Dubai mwezi Novemba, 2013;

(ii) Kuandaa kongamano la uwekezaji kwenyeSekta ya Ngozi nchini India kwa nia ya kupata wawekezajitoka India kuwekeza kwenye usindikaji na kuongeza thamanimazao ya sekta ya ngozi;

(iii) Kutoa msukumo wa kutangaza fursa zauwekezaji kwenye sekta ya Real Estate Development hususankatika mji mpya wa Kigamboni; na Maeneo ya SpecialEconomic Zone – SEZ ya Bagamoyo; na.

(iv) Kufuatilia mapendekezo yaliyotolewa na kituokuhusu juhudi zinazohitajika kuwekwa ili kuongeza mauzoya bidhaa za Tanzania kwenye soko la Dubai hususan kwa

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

140

mazao kama mananasi, kakao, viungo, korosho namaparachichi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Malengo ya Kituo chaBiashara cha Tanzania London - (TTC-London) kwa mwaka2013/2014 ni yafuatayo:-

(i) Kukuza biashara kwa kushiriki katikamaadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Kimataifa la kahawa(ICO) yatakayofanyika nchini Brazil mwezi wa Septemba,2013;

(ii) Kuandaa Mkutano kwa kushirikiana naUbalozi na wadau wengine kuhusu Kuvutia uwekezaji katikasekta mbalimbali hasa katika kilimo, miundombinu nahuduma;

(iii) Kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzaniakupitia maonyesho mbalimbali ya utalii yatakayofanyikakatika miji mikubwa ya Uingereza; na

(iv) Kukuza Diplomasia ya Uchumi kwa kushirikikatika shughuli za mashirika ya Kimataifa ili kubaini fursa zakibiashara na kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na maendeleo yarasilimali watu, kwa mwaka 2013/2014, Wizara inatarajiakuajiri watumishi wapya 72, kupandisha vyeo watumishi 61,kuthibitisha kazini watumishi 11 na kuwapeleka mafunzo yamuda mfupi na mrefu watumishi 70. Aidha, Wizara itaendeleakutoa huduma kwa watumishi wanaoishi na UKIMWI/VVUwaliojitokeza kwa mujibu wa Waraka Namba Moja wamwaka 2004, kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishiwa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masuala mtambuka;Wizara itaendelea na jitihada za kupambana na kudhibitirushwa kwa watumishi wake kwa kutoa mafunzo ya Sheriambalimbali za kazi zikiwemo Sheria Na. 8 ya mwaka 2002Utumishi wa Umma, Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria ya

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

141

Fedha ili kuwawezesha kufanya kazi na kutoa maamuzi kwakuzingatia matakwa ya sheria husika. Ili kuweza kutoahuduma bora zinazokidhi viwango vilivyoainishwa katikaMkataba wa Huduma kwa Mteja, Wizara itaendeshamafunzo ya elimu ya huduma kwa mteja kwa watumishi 50ili kuwapatia mbinu mbalimbali za kuhudumia wateja.

Vilevile, Wizara inatarajia kuimarisha dawati lakushughulikia malalamiko ya Sekta ya Viwanda na Biasharaili kuweza kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea na jitihada za kuwawezesha watumishiwaliojitokeza na watakaojitokeza wanaoishi na virusi vyaUKIMWI kupata huduma ya virutubisho, lishe na usafiri. Pia,Wizara itaendelea kutoa mafunzo ya kujikinga namaambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na kuhamasishaupimaji wa afya za wafanyakazi kwa hiari.

Aidha, waelimishaji rika watapewa mafunzo ilikuwawezesha kupata mbinu mpya ambazo zitawawezeshakuwaelimisha watumishi wenzao na familia zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara pia, inatarajiakuendelea na kutoa huduma kwa Watumishi na wanaoishina virusi vya UKIMWI waliojitokeza ili kuweza kutoa mchangowao kwa Wizara na Taifa kwa ujumla; kuajiri watumishiwapya 72; kupandisha vyeo watumishi 61; kuthibitisha kaziniwatumishi 11 na kuwapeleka mafunzo ya muda mfupi namrefu watumishi 70.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naNEMC na wadau mbalimbali itaendelea kutekeleza mikakatiinayohusu utunzaji wa mazingira pamoja na programu yautekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.Wizara itahamasisha miradi mipya itakayoanzishwa kutimizamasharti ya uzalishaji salama Viwandani na kuhimiza miradiya zamani ambayo haikuwa na mifumo salama kwamazingira ijenge mifumo hiyo.

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

142

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara itaendeleakuzingatia masuala ya jinsia katika kupanga na kutekelezasera, mikakati na mipango mbalimbali ya kisekta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shukrani. Naomba uniruhusukuwashukuru kwa dhati nchi rafiki na Mashirika ya Kimataifaambayo yamekuwa yakitoa na yanaendelea kutoa misaadambalimbali kusaidia Sekta ya Viwanda na Biashara. Misaadana michango hiyo imekuwa chachu na nyenzo muhimu kwaWizara yangu kuweza kutekeleza majukumu yake. Nchi rafikini pamoja na Austria, Canada, China, Denmark, Finland,India, Ireland, Japan, Korea ya Kusini, Marekani, Norway,Sweden, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani na Uswisi. Mashirikaya Kimataifa ni pamoja na: Benki ya Dunia, DANIDA, CFC,ARIPO, DFID, EU, FAO, IFAD, JICA, Jumuiya ya Madola, KOICA,Sida, UNCTAD, UNDP, UNIDO, USAID, WTO na WIPO.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maombi ya Fedha KatikaMwaka 2013/2014. Katika mwaka 2013/2014, Wizara inatarajiakukusanya Shilingi 40,330,000 kutokana na uuzaji wa nyarakaza tenda, faini kwa kukiuka sheria ya leseni, pamoja namakusanyo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka wa 2013/2014,Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini yakeinaomba kutengewa jumla ya Sh. 78,502,631,820/= kwa ajiliya kutekeleza majukumu ya kuiendeleza Sekta ya Viwanda,Biashara, Masoko na Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo.Kati ya fedha hizo, Sh. 29,665,989,000/= ni kwa ajili ya matumiziya kawaida na kiasi cha Sh. 48,836,642,820/= zimeombwakwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Matumizi ya Kawaida. Katikafedha za matumizi ya kawaida ya Sh. 29,665,989,000/=, Sh.22,225,249,000/= zimetengwa kwa ajili ya mishahara (PE) naSh. 7,440,740,000/= zimetengwa kwa ajili ya Matumizi Mengine(OC). Aidha, kati ya Fedha za mishahara (PE),Sh. 2,296,161,000/= zimetengwa kwa ajili ya mishahara yaWizara na Sh.19,929,088,000/= zimetengwa kwa ajili yamishahara ya Taasisi.

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

143

Vilevile, katika Sh. 7,440,740,000 zilizotengwa kwa ajiliya matumizi mengineyo, Sh. 5,976,859,000/= zimetengwa kwaajili ya matumizi ya Wizara na kiasi cha Sh. 1,463,881,000/=zimetengwa kwa ajili ya Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sh. 48,836,642,820/=zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, Sh.42,100,000,000/= ni fedha za ndani na Sh. 6,736,642,820/= nifedha za nje zitakazotokana na Washirika wa Maendeleo.Aidha, katika fedha za ndani zi l izotengwa,Sh. 40,900,000,000/= ni mahsusi kwa maeneo ya kimkakatiinayohusu maendeleo ya miradi chini ya EPZA (SEZ Bagamoyona Tanzania – China Logistic Centre); NDC (Liganga,Mchuchuma, Mradi wa kuzalisha viuadudu vya kuuaviluwiluwi wa mbu waenezao malaria - Kibaha, General Tyre(EA) Ltd, Mradi wa Magadi Soda wa Ziwa Natron/Engaruka,Mradi wa Kufua Umeme kwa Upepo - Singida) na SIDO (SMESIndustrial Infrastructure Expansion & Capacity Building). PiaSh. 1,200,000,000/= ni kugharamia miradi na mipango minginemuhimu ya maendeleo kwa Wizara na Taasisi nyingine 15 zilizochini ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sh. 6,736,642,820/=fedha za nje za maendeleo zitakazotokana na Washirika waMaendeleo, Sh. 3,024,594,076/= ni za mradi wa MUVIutakaogharimia kuboresha mlolongo wa thamani kwamazao yaliyochaguliwa na Mkoa husika, upatikanaji wambegu bora na masoko. Sh. 547,581,904/= ni za mradi waASDP zitagharimia kuimarisha Mfumo wa Taarifa za Masoko,kuboresha na kukamilisha Mkakati wa kukuza mfumo waStakabadhi za Mazao Ghalani, kuanzisha Soko la Mazao naBidhaa nchini (Commodity Exchange); Kuratibu, kufuatilia nakutathmini uendelezaji wa miundombinu ya usindikaji ilikuongeza thamani mazao ya kilimo - Tanzania Bara naKuendelea kushirikiana na wadau kuendeleza miundombinuya masoko nchini.

Aidha Sh. 1,583,000,000/= za mradi wa Support forTrade Mainstreaming zitatumika kujenga uwezo wa Taasisi

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

144

mbalimbali zinazochangia kuendeleza biashara kwa kutoamafunzo kwa wataalam wa Taasisi.

Pia mradi wa Support for Gender Mainstreaming inTrade Sector na Micro and Small Enterprise DevelopmentStrategy wenye Sh. 337,179,000/= zitatumika kufanyauchambuzi wa sera za Sekta ya Viwanda, Biashara, Masokona Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo kwa lengo lakuhusisha masuala ya jinsia katika sera na mikakati ya Wizara.Sh. 816,100,000/= za mradi wa Integrated IndustrialDevelopment Programme ni za kutekeleza Programu zaUNIDO zinazojumuisha Mradi wa Accelerated Agribusinessand Agro-processing Development Initiative (3ADI) unaolengauongezaji thamani mazao ya kilimo na Industrial Upgradingand Modernisation ambao unalenga kuboresha ufanisi waviwanda hasa viwanda vidogo na vya kati ambavyovinahitaji msaada kidogo ili kuzalisha bidhaa zenye uborana zinazoweza kuingia katika masoko ya nje.Sh. 428,187,840/= ni za mradi wa Strenthening TWLB Capacityfor efficiency in Warehouse Receipt System (WRS) serviceprovision in Tanzania zitagharimia kuimarisha uwezo wa TWLBi l i kuleta ufanisi kwa kutoa mafunzo, kununua vifaa,kuimarisha ukaguzi, na kuandaa database ya mazaoyanayohifadhiwa ghalani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napendakukushukuru tena wewe na Waheshimiwa Wabunge wotekwa kunisikiliza. Hotuba hii inapatikana pia kwenye tovutiya Wizara www.mit.go.tz. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Wazirikwa kusoma kwa umakini sana. Sasa namwita Mwenyekitiwa Kamati Mheshimiwa Mgimwa.

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

145

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA – MWENYEKITI KAMATIYA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): MheshimiwaMwenyekiti, kwa mujibu wa kanuni ya 99(7) ya Kanuni zaBunge, Toleo la 2007, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamatiya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara kuhusu utekelezajiwa majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara (Fungu 44)kwa Mwaka 2012/2013 na Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilipata fursa yakupitia majukumu, mafanikio na changamoto za utekelezajiwa shughuli za Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja nakupokea Taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli zaUendelezaji wa Sekta Viwanda, Sekta ya Viwanda vidogona Biashara ndogo, Sekta ya Masoko na Sekta ya Biashara.Kamati ilijadili taarifa hizo kwa kina ikiwemo ile ya Makadirioya Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2013/2014 na hatimayekuishauri Wizara hiyo ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwepochangamoto mbalimbali, Kamati inaridhishwa na mafanikioyanayopatikana katika sekta hizi kwa kutumia rasilimalindogo za Serikali na kupanga vipaumbele ndani yavipaumbele ili kuleta matokeo ya haraka yanayokusudiwaya kisekta. Aidha, mafanikio yaliyopatikana yanatokana nakuzingatia na kutekeleza maagizo ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda imewezakuongeza uzalishaji wa bidhaa viwandani ambaoumechangia ukuaji wa Sekta ya Viwanda kufikia asilimia 9.9mwaka 2008, kutoka asilimia 8.5 mwaka 2006 na katikamwaka 2011 sekta hii imechangia asilimia 7.8. Katika mwaka2012 uzalishaji viwandani umeendelea kuimarika na hivyokuchangia ukuaji wa asilimia 8.2. Aidha, mchango wa sektaya viwanda katika Pato la Taifa nao umeendeleakuongezeka kutoka asilimia 8.9 mwaka 2005 na kufikiaasilimia 9.4 mwaka 2008 na mwaka 2011 ulikuwa asilimia 9.74.Mwaka 2012 sekta hii imechangia asilimia 9.85 kwenye Patola Taifa, bado ongezeko hil i l ipo chini ya malengo

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

146

tuliyojiwekea la asilimia 15 lililoainishwa katika Dira ya Taifaya Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Sekta yaViwanda Vidogo na Biashara Ndogo zimetoa mchangomkubwa katika ajira takribani 5,000,000 sawa na asilimia 23.4.Sekta hii imechangia asiliamia 27.9 kwenye pato la Taifa.Aidha, mchango katika Sekta ya Biashara ulikua kwa asilimia8.1 mwaka 2011 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 8.2 kwamwaka 2010. Katika kipindi cha mwaka 2012 sekta hii imekuakwa asilimia 7.7. Kwa upande wa Pato la Taifa sekta hiiilichangia asilimia 12.2 mwaka 2011 ikilinganishwa na asilimia12.1 mwaka 2010. Kwa mwaka 2012 imechangia asilimia12.3. Ongezeko la ukuaji na uchangiaji huu umetokana nakuongezeka kwa fursa mbalimbali za masoko kwa bidhaana uboreshaji wa mazingira ya kibiashara katika masoko yandani na nje ya nchi, yaani EAC, SADC, EU, Asia, Marekani namashariki ya mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Sekta yaMasoko, kumekuwa na ongezeko la bei ya mazao makuuya chakula hali inayopelekea kuwepo na mfumuko wa beimara kwa mara. Hata hivyo, Serikali imeendelea na jitihadaya kukabiliana na tatizo hili pamoja na kujenga masokoyanayokidhi viwango vya kimataifa katika maeneombalimbali nchini. Pia uanzishwaji wa mfumo wa stakabadhiza mazao ghalani kumesaidia wakulima kuwa na uhakikawa bei za mazao wanayoyalima. Hata hivyo, utekelezaji wamfumo huu unahitaji usimamizi wa karibu kuhakikishawakulima wote wanafaidika na mfumo huu, hivyo Kamatiinaiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikianana Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuhakikisha inafanyiamarekebisho Sheria ya Stakabadhi Ghalani na kuileta Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji waMpango wa Maendeleo wa Taifa katika Sekta ya Viwandana Biashara kwa Mwaka 2012/2013, takwimu zinaonyeshakuwa, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 52.0 kwa ajili yaMradi wa Mchuchuma na Liganga lengo ikiwa ni kuimarishabarabara za Itoni – Mkiu - Mchuchuma na Mkiu - Liganga

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

147

pamoja na kuongeza ujuzi wa wataalam. Hata hivyo,utekelezaji wake upo kwenye ngazi ya upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mradi waKiwanda cha Viuadudu - Kibaha, Pwani, Serikali ilitenga kiasicha Shilingi bilioni 3.26 kwa ajili ya malipo ya Mhandisi Mshauri,kutoa mafunzo kwa wataalam, ujenzi wa mfumo wa majisafi na majitaka na usanifu wa kituo cha umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa eneo laTAMCO – Kibaha limekusudiwa kuwa eneo la viwandavidogo na kati. Serikali imeweza kukamilisha michoro yaeneo, upimaji wa viwanja na usanifu wa miundombinu yabarabara, maji safi na taka. Hata hivyo, mpaka sasa badomiundombinu hususan barabara za uhakika kwa ajili yawawekezaji hazijakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huukwa upande wa majengo ya kiwanda na usanifu wamitambo umekamilika. Kwa upande wa mradi wa MagadiSoda- Bonde la Engaruka, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingimilioni 700 kwa ajili ya upembuzi akinifu na kuchimbavisima12. Hata hivyo, mpaka sasa utafiti wa uwingi wamagadi umekamilika na bado inaendelea kutafuta taarifaza uwekezaji kwenye mradi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha kuwaSerikali ilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 50.2 kwa ajili yakukamilisha ulipaji wa fidia katika maeneo maalum yauwekezaji- Export Processing Zones (EPZ) kwa Bagamoyo naKigoma ingawa tathmini ya fidia inaonyesha kuwa eneo laBagamoyo thamani yake ni Shilingi bilioni 58.8 na eneo laKigoma thamani yake ni Shilingi bilioni 2.8. Kwa upande wautekelezaji kiasi cha Shilingi bilioni 16.9 zimelipwa kwa eneola Bagamoyo, yaani hekta 1,600 kati ya hekta 5,700. Kwaupande wa eneo la Kigoma kwa mwaka huu wa fedhahakuna malipo yoyote yaliyofanyika hadi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Serikali kuwamstari wa mbele katika kuandaa na kusimamia miradi ya

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

148

Maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa kila mwaka, Kamati inashangazwana utekelezaji wa kusuasua wa miradi hii ya kimkakatiambayo ni kipaumbele cha Serikali katika kukuza uchumi wanchi. Kiasi cha fedha kilichopokelewa kwenye miradi hiimpaka sasa ni kidogo mno na hivyo hakitoi taswira halisi yauwajibikaji wa Serikali kama kweli ni Mipango ya Maendeleoya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji waMalengo ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kipindi chamwaka 2012/2013, Kamati ilielezwa kuwa kwa upande wamafanikio, Wizara imeweza kutekeleza mambo ya msingiyafuatayo:-

(i) Wizara imeweza kusimamia na kuratibu Sektaya Viwanda na hivyo kuendelea kuongeza uzalishaji wabidhaa viwandani na kukua kwa asilimia 8.2. Mfano,usindikaji wa ngozi umeongezeka kutoka futi za mraba6,038,00 mwaka 2005 hadi futi za mraba 37,305,215 mwaka2009 kwa kiwango cha wet-blue; kuna viwanda vya nguo22 hadi sasa ikilinganishwa na viwanda 17 vilivyokuwepomwaka 2006; viwanda vya bidhaa na ujenzi vimeongezekavikiwemo vile vya chuma, cement, vinywaji na chakula,maziwa na viwanda vya madawa ya binadamu;

(ii) Imeendelea kufufua na kuendeleza viwandavilivyobinafsishwa, kuanzisha viwanda vipya pamoja nauendelezaji wa viwanda katika maeneo maalum ya EPZ;

(iii) Wizara kupitia Mamlaka ya Maeneo Maalumya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Shirika la Maendeleola Taifa (NDC) imeendelea kutenga maeneo maalum yauwekezaji katika Mikoa yote nchini;

(iv) Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogoimeendelea kukua na kuchangia kiasi cha asilimia 27.9 katikapato la Taifa na kuajiri kiasi cha Watanzania milioni 5.2ikihusisha wajasiamali milioni tatu;

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

149

(v) Thamani ya mauzo ya bidhaa za njeiliongezeka hadi Dola za Kimarekani milioni 5,098.8 mwaka2011 ikilinganishwa na Dola milioni 4,323.1 mwaka 2010;

(vi) Wizara imeendelea kuboresha Mfumo waStakabadhi ya Mazao Ghalani na hivyo kuongeza ushindaniwa manunuzi ya mazao na hatimaye kuongeza bei ya mazaoya mkulima;

(vii) Wizara imeendelea kushirikiana na Wizara zaKisekta kufanikisha ujenzi wa masoko na miundombinuikiwemo yale masoko ya mipakani;

(viii) Wizara kwa kushirikiana na TIRDO, imewezeshasekta binafsi kutumia mfumo wa utambuzi wa bidhaa kwakutumia nembo za mistari (Bar Code); na

(ix) Imeendelea kuboresha mazingira ya kufanyabiashara ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilielezwa kuwapamoja na baadhi ya mafanikio haya, bado Wizarainakabiliwa na changamoto zifuatazo katika utekelezaji wamajukumu yake:-

(i) Upungufu wa Bajeti kwa ajili ya utekelezaji wamajukumu ya Wizara, na fedha kutofika kwa wakatiuliopangwa;

(ii) Uhaba wa umeme na maji kwa ajil i yashughuli za uzalishaji viwandani;

(iv) Ushindani usio wa haki katika masuala yabiashara na ukosefu wa masoko ya uhakika kwa bidhaazinazozalishwa hapa nchini;

(iv) Miundombinu hafifu na isiyo na tija inayoathirisekta shindani ya Viwanda;

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

150

(v) Ukosefu wa wataalamu na teknolojia duni; na

(vi) Uingizaji wa bidhaa dhaifu katika soko landani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana nachangamoto za kisekta, Wizara imejitahidi kuchukua hatuambalimbali zikiwemo kuzingatia ushauri wa Kamati ya Bungeya Uchumi, Viwanda na Biashara ambayo imekua ikitoamichango, ushauri na maelekezo mbalimbali ambayoyamelenga kuimarisha sera na mifumo mizuri ya ukuzaji wasekta ya viwanda na uzalishaji viwandani, kufanya biasharapamoja na kutafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje yanchi. Aidha, Kamati imeendelea kutoa msisitizo wakuboresha mazingira wezeshi ya kufanya biashara ndani nanje ya nchi na hivyo kuvutia wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni na ushauri wa Kamatikwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda naBiashara imeendelea kuchangia uchumi hasa katika shughuliza uzalishaji, usindikaji usambazaji na masoko. Sekta hizi badozina nafasi kubwa ya kuliwezesha Taifa kuondokana naumasikini na kulifikisha katika kiwango cha uchumi wa katiwa Viwanda. Haya yote yanawezekana ikiwa Serikali itawezakusimamia ipasavyo na kuratibu shughuli zote za msingizinazohusu sekta hizi na kukabiliana na changamotozifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2012/2013 Wizara ilitengewa na kuidhinishiwa na Bunge kiasicha Sh. 170,199,842,000/=; kati ya fedha hizoSh. 38,819,055,000/= zilikuwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaidana Sh. 131,380,787,000/= zilikuwa kwa ajili ya Matumizi yaMaendeleo. Maombi haya ya fedha yaliidhinishwa na Bungebaada ya kuridhika na mchanganuo wa shughuli zilizohitajikakutekelezwa na Wizara hii kwa kipindi hicho. Hata hivyo,mchanganuo unaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi Februari,2013 Wizara ilikuwa imepokea asilimia 23 tu ya fedha

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

151

iliyopitishwa na Bunge, na hadi kufikia mwezi huu wa Mei,Serikali haijatekeleza ahadi yake ya kumalizia fedha zilizobaki.Kwa mwenendo huu wa ufinyu wa bajeti kwa Wizara nafedha kuchelewa kufika kwa wakati, ni dhahiri:-

(i) Serikali haitaweza kufikia malengo yakeiliyojiwekea ya kuleta mabadiliko ya uchumi kutoka kiwangocha uchumi wa chini unaotegemea kilimo kufikia kiwangocha uchumi wa kati unaotegemea viwanda;

(ii) Wizara imeshindwa kutekeleza majukumuyake ya msingi hivyo matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchiyetu kama vile ukosefu wa ajira, umaskini wa kipato, ufinyuwa wigo wa kodi, na thamani hafifu kwenye mazao yakilimo na maliasili yataendelea kuwepo;

(iii) Kuendelea kuwepo usimamizi hafifu wakuboresha upatikanji wa huduma za kuendeleza Sekta zaViwanda, Biashara, Masoko na Viwanda Vidogo; na

(iv) Fedha kwa ajili ya matumizi mengine (OC)imeendelea kupungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inajiuliza kuwa,kama Bunge limeidhinisha fedha kwenda kwenye Wizarahusika, ni nani mwenye mamlaka ya kupinga maamuzi yaBunge? Kwa staili kama hii: Je, tutaweza kweli kutimizamalengo yetu tuliyojiwekea kwenye utekelezaji wa Mpangowa Maendeleo wa Taifa?

Kamati inaliomba Bunge lako Tukufu lihakikishe fedhazote zilizoidhinishwa kutolewa kwa Wizara hii zipatikane iliiweze kukamilisha majukumu yake ya msingi iliyojiwekea hasakwa upande wa miradi ya maendeleo. (Makofi)

Jedwali. Na 1. Bajeti ya mwaka 2012/2013 iliyopitishwakwa Wizara ya Viwanda na Biashara ikiwianishwa na fedhailiyokwisha tolewa hadi mwezi Februari 2013.

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

152

Maelezo Bajeti Fedha % ya Bajeti iliyopitishwa iliyokwishatolewa iliyopitishwa 2012/2013 hadi mwezi Feb.2013 2012/13 vs

Fedha iliyo- kwishatolewa hadi Februari

2013

Matumizi Mishahara 31,378,315,000 15,814,856,107 50%yakawaida Matumizi 7,440,740,000 3,729,029,500 50%

mengine

Jumla 38,819,055,000 19,543,885,607 50%

Bajeti Fedha 123,713,139,000 16,807,814,775 14%ya zaMaendeleo Ndani

Fedha 7,667,648,000 2,673,307,987 35% za Nje

Jumla 131,380,787,000 19,481,122,762 15%

Jumla 170,199,842,000 39,025,008,369 23% Kuu

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia ExportingProcessing Zones (EPZ) imeendelea kuhamasisha uwekezajipamoja na ujenzi wa baadhi ya miundombinu katikamaeneo ya EPZ/SEZ. Pia imeendelea kutoa fidia katikamaeneo maalum ya uwekezaji, mfano eneo la Kurasini ilikutekeleza mradi wa Tanzania - China Logistics Centre naeneo la mradi wa EPZ – Bagamoyo. Maeneo haya ni yakimkakati yaliyopewa kipaumbele kwenye utekelezaji waMpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2012/2013ambayo yanategemewa kuongeza ajira, soko la malighafinchini pamoja na kuvutia uwekezaji na biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa zoezi hili laulipaji wa fidia umekuwa wa kusuasua na hivyo kuondoa iledhana kuwa ni kweli Miradi ya Kimkakati. Mfano, katika Bajeti

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

153

ya mwaka 2012/2013 Wizara iliomba na kuidhinishiwa naBunge kiasi cha Shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kulipa fidia yaeneo la Kurasini na wadau wetu wa maendeleo (China)wangetoa Shilingi bilioni 600 hii ikiwa na maana ya uchangiajiulikuwa wa uwiano wa 1:10 ili kutekeleza mradi huu ambaounatoa ajira takribani 25,000. Hata hivyo, mpaka sasa Serikaliimekwishatoa kiasi cha Shilingi milioni 550 tu kati ya Shilingibilioni 60 na kwa upande wa mradi wa EPZ - Bagamoyo(Tanzania Mini Tiger Plan), Serikali imekwishatoa kiasi chaShilingi bilioni 10.9 tu, kati ya Shilingi bilioni 50.2. Maombi hayaya fedha yalikuwa Maalum na yalitakiwa yatoke kwamkupuo mmoja yaani ringfenced.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaona kuwa kwamwenendo kama huu wa utoaji hafifu wa fedha kwenyemiradi tuliyoipa kipaumbele kwenye Mpango wa Maendeleoya Taifa kamwe hatutaweza kuimaliza kama tulivyopanga.Pia kuna hatari kubwa ya kupoteza wahisani/wadau wamaendeleo kwenye miradi mikubwa kama hii ambayotuliwahihikishia kushirikiana nao ipasavyo.

Serikali inabidi ielewe kuwa Dunia ya sasa ni yakiushindani na kibiashara na muda haupo upande wetu, kilanchi inapenda kupata fursa za kuingia ubia kama hizi zakwetu na zinajitahidi kuweka mazingira wezeshi ya kupatawawekezaji. Sisi fursa kama hizi tunazichezea tu nahapaonekani mahali ambapo tumekuwa serious kwenyemiradi kama hii na kuona matokeo (impact) bora. Kwa kuwamaombi ya fedha hizi yalikuwa ringfenced na Serikaliilikwishayatolea uamuzi, Kamati inaiagiza Serikali kuhakikishainatoa fedha zote zilizobaki kabla ya mwaka mpya wa fedhahaujaanza, ili miradi hii itekelezeke mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzoefu unatuonyesha kuwanchi nyingi duniani zinalinda viwanda vyao vya ndanipamoja ya kuwa kuna ushindani. Lazima tuhakikisheviwanda vyetu vinazalisha na kutosheleza soko la ndani nala nje kwa kutumia malighafi tunayozalisha nchini. Kwakuzingatia haya, Kamati inatoa ushauri ufuatao:-

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

154

(i) Serikali iongeze jitihada za kufufua Kiwandacha General Tyre (EA) Ltd ikiwemo upatikanaji wa fedha kwaajili ya kulipa madeni yote. Hii itasaidia kuongeza ajira, wigowa ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi na pia kusaidiakukuza uchumi;

(ii) Miradi yote inayotekelezwa kupitia Shirika laMaendeleo la Taifa (NDC), yaani mradi wa makaa ya mawewa Mchuchuma na wa Chuma cha Liganga, mradi wakuzalisha umeme wa Ngaka, mradi wa kuzalisha umeme waupepo na mradi wa kutengeneza Viuadudu (Biolarvicides)vya kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria na ule wa uchimbajiwa magadi (Soda Ash) –Ziwa Natron; isimamiwe nakuratibiwa vizuri il i ikamilike kwa wakati uliopangwa.Kukamilika kwa miradi hii sambamba na kujenga uwezo waWizara wa kuandaa Sera ya Maendeleo ya Viwanda naKuboresha Utendaji wa Viwanda kutasaidia kupatikana kwaumeme wa uhakika, ajira na kuongeza mapato na hivyokusaidia kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.

(iii) Kamati inaipongeza Wizara kwa kuwezakusimamia ipasavyo ujenzi wa Viwanda vipya vya Saruji nahivyo kuongeza uwezo wa uzalishaji na upatikanaji wa ajirampya. Mfano, Tanzania Portland Cement Co. Ltd kimeongezauwezo wa uzalishaji kutoka tani 700,000 mwaka 2008 hadi1,400,000 mwaka 2011; Tanga Cement kutoka tani 500,000hadi tani 1,200,000; na Mbeya Cement kutoka tani 250,000hadi 350,000 katika kipindi hicho.

Hivyo kutoka mwaka 2006 hadi 2011 uwezo wauzalishaji wa saruji kwa viwanda vyote vitatu uliongezekakwa wastani wa asilimia 95.4 (kutoka tani 1,514,073 hadi tani2,959,164). Kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vipya vya saruji,yaani Athi River Cement Co. – Tanga, Mbagala Cement Co.- Dar es Salaam na Arusha Cement Co. - Arusha kutasaidiaupatikanaji zaidi wa saruji na hivyo kuachana na tabia yakuagiza saruji toka nje inayouzwa kwa bei ya chini kutokanana ruzuku inayotolewa kwa viwanda vyao na hivyokupelekea viwanda vyetu kujiendesha katika ushindani usiowa haki. Kamati inashauri Serikali kuchukua hatua za kutoza

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

155

kodi au ushuru kwenye saruji inayoagizwa toka nje ili kulindauzalishaji wa ndani. (Makofi)

(iv) Viwanda vya sukari vilivyopo nchini pamojana vile vidogo kwa ujumla vinazalisha takribani tani 304,000na mahitaji yetu ni tani 400,000. Jitihada za makusudizinahitajika kuongeza uzalishaji ili kuweza kukidhi mahitajiya ndani. Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha inaongezaujenzi wa viwanda vipya vya sukari sambamba na kongezakilimo cha miwa ili kutosheleza mahitaji na kulinda bei zawalaji na hivyo kuondokana na utaratibu wa kuagiza sukaritoka nchi za nje.

(v) Serikali inahitaji kufanya jitihada zaidi katikakuhamasisha kilimo cha mazao yanayozalisha mafuta ya kulakama vile alizeti, karanga na mawese. Takwimu zinaonyeshakuwa bado hatujajitosheleza katika uzalishaji wa mbeguzinazotoa mafuta. Tunazalisha tani 320,000 za mbeguzinazotoa tani 90,000 tu za mafuta wakati mahitaji yetu nitani 350 hadi 450,000 za mafuta ya kula na hivyo kutoshelezaasilimia 40 ya mahitaji yetu. Jitihada hizi ziendane na udhibitiwa viwanda vinavyoagiza mafuta toka nje viagize mafutayasiyosafishwa (crude oil) ili yasafishwe hapa nchini. Pia Serikaliifuatilie malalamiko yanayotolewa na wananchi kuhusuuwepo wa Bandari bubu zinazotumika kupitisha bidhaambalimbali ikiwemo ya mafuta ya kula, na watakaobainikakuhusika na tuhuma hizo wachukuliwe hatua kali kwani niwahujumu wa uchumi na wanaikosesha Serikali mapato.(Makofi)

(vi) Kwa upande wa viwanda vya korosho badovimeshindwa kuhimili ushindani wa soko na vinginevimeshindwa kufanya kazi. Hii imetokana na viwangovikubwa vya kodi zinazotozwa kwenye vipuri na vifungashio,bei kubwa ya korosho ghafi kwa wabanguaji wa ndanikupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ukilinganisha nawanunuzi kutoka nje ambao hupewa ruzuku ya asilimia 30na nchi zao na pia ukosefu wa umeme wa uhakika na mitajiya kuendeshea viwanda. Kamati inaitaka Serikali kutafuta

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

156

suluhisho la matatizo haya ili kusaidia wakulima wa koroshona wamiliki wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Viwango la Taifa(TBS) limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha linadhibitiuingizaji wa bidhaa zisizo bora na hivyo kukuza matumizi yaviwango na hivyo kulinda afya ya walaji, usalama wa walajina kulinda mazingira ya nchi yetu. Hata hivyo, Kamatiimebaini kuwa pamoja na juhudi hizi, Shirika linakabiliwa naupungufu wa wafanyakazi. Idadi ya sasa ni wafanyakazi 197tu ambao wanatakiwa kufanya kazi na kuzunguka Tanzanianzima kuhakikisha kuwa bidhaa zenye ubora unaokubalikatu ndio zinatengenezwa au kuingizwa nchini na zinakidhiviwango vya kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika (TBS) hili limekuwalikilalamikiwa mara kwa mara kwamba halifanyi kazi yakeipasavyo. Ukweli ni kwamba shughuli za kiuchumizimeongezeka na hivyo shughuli za Shirika zimeongezeka nahaziendi sanjari na idadi ya wafanyakazi waliopo hivyolinashindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na upungufuwa wafanyakazi. Mfano, mwaka 2010/2011 Shirika liliombakibali cha kuajiri wafanyakazi 35 lakini Serikali ilitoa kibali chakuajiri wafanyakazi 18 tu. Hata hivyo, kibali hichohakikutekelezwa kwa sababu Serikali ilisitisha ajira. Mwakauliofuata wa 2011/2012 Shirika lil iomba nyongeza yawafanyakazi 15 tu. Ombi hili halikufikiriwa.

Mwaka 2012/2013, Shirika liliomba tena wafanyakazi62 lakini Serikali ilitoa kibali cha kuajiri wafanyakazi 32 tu. Hatahivyo, ajira zilisitishwa tena mwezi Februari mwaka 2013. Kwatakwimu hizi ni dhahiri Shirika (TBS) haliwezi kufikia malengoyake iliyojiwekea; mfano, Shirika la Viwango la Kenya (KEBS)lina wafanyakazi zaidi ya 1000 na lina ofisi za kanda zikiwemoMombasa, Kisumu, Garisa, Nyeri, Nakuru na katika entry pointsmbalimbali za mipakani. Kamati inaishauri Serikali kuhakikishainatoa kibali cha ajira ya watu 62 iliyoomba mwaka 2012/2013 ili Shirika hili liweze kutekeleza majukumu yake ikiwemokufungua ofisi za kanda na vituo vya mipakani na hivyokusogeza huduma zake karibu zaidi kwa wananchi.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

157

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta Viwanda Vidogo naBiashara Ndogo inahusisha sekta zote za uchumi ambazozimejikita katika jasiriamali za kuzalisha (asilimia 13.6),kununua na kuuza (asilimia 55), huduma (asilimia 30) nanyinginezo (asilimia 1). Sekta hii imeajiri Watanzania takribanimilioni 5.2 na mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa kwasasa umefikia asilimia 27.9. Kwa kuzingatia umuhimu wasekta hii inayohusisha wajasiriamali wa viwango na kadambalimbali za mtaji na elimu, Kamati inashauri kamaifuatavyo:-

(i) Serikali ikamilishe ahadi yake iliyoitoa kwenyebajeti ya Mwaka 2012/2013 ya kuwapa SIDO kiasi cha Shilingibilioni tatu kwa ajili ya kuratibu na kuendeleza programumbalimbali za Wajasiriamali. Wizara mpaka sasa haijapokeafedha hizo licha ya kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu alisisitizaSIDO wapewe hizo fedha;

(ii) Kwa kuwa shughuli nyingi za sekta hii zikokatika sekta isiyo rasmi, basi Serikali haina budi kufanyamchakato wa kurasimisha sekta hizi ili iweze kupata mapatoyake yatokanayo na kodi;

(iv) Serikali iongeze juhudi ya kutoa elimu ya uendeshajiwa miradi ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja naukuaji wa biashara;

(iv) Serikali iboreshe fursa ya kupatikana mikopoyenye riba nafuu kwa wajasiriamali pamoja na kuendelezaprogramu mbalimbali zinazosimamia na kuboresha shughuliza wajasiriamali; na

(v) Serikali iendelee kuweka vivutio vyakuhamasisha na kuwezesha sekta hii ya wajasiriamalikuchangia uchumi wa nchi yetu kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chini ya mfumo wa ‘PPP’,Serikali lazima iongeze jitihada za kukuza uwekezaji waviwanda kupitia Sekta Binafsi pamoja na kuimarisha nakuboresha mazingira mazuri ya kuendesha viwanda. Jukumu

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

158

hili lazima liambatane na kuweka mazingira wezeshi kwaSekta Binafsi kufanya biashara na hivyo kuwa mhimili mkuuwa ukuaji wa uchumi. Hatua hizi zitatusaidia kufikia malengoyetu ya kujenga uchumi imara kupitia viwanda utakaohimiliushindani wa ndani na nje ya nchi na hivyo kufikia lengo lakuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kamainavyoelekezwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa yaMwaka 2025, Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa MiakaMitano 2011/2012 - 2015/2016 na Awamu ya Pili ya Mkakatiwa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taarifainayoandaliwa na Benki ya Dunia, ‘Doing Business 2013’; katiya nchi 185 duniani, Tanzania ni nchi ya 134 katika kurahisishamazingira wezeshi ya ufanyaji biashara (Ease of doingbusiness). Kamati bado inaitaka Serikali kuhakikisha inapitiana kufanya marekebisho ya Sheria, Kanuni na Taratibumbalimbali zinazokinzana na kuleta urasimu mkubwa katikakufanya shughuli za biashara, kufanyia tathmini Mpango waKuboresha Mazingira ya Uwekezaji nchini pamoja nakuondoa tatizo la ucheleweshaji au kutokutoa maamuzi kwawakati. Ni dhahiri kuwa hatutaweza kuendelea bila ya kuwana msukumo wa hali ya juu wa kuboresha mazingira yakufanya biashara na kuwekeza ili kuongeza kasi ya kuwavutiawawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Marekebisho haya yatatoa fursa ya kushiriki kikamilifukatika mahusiano ya kibiashara baina ya nchi na nchi(Bilateral Trade); Makubaliano ya Kibiashara ya Kikanda(Regional Trading Agreements – RTAs); Mpango waMtangamano wa Utatu (COMESA – EAC - SADC TripartiteFree Trade Area Arrangements); na Soko la Pamoja la Jumuiyaya Afrika Mashariki (EAC) juu ya Uhuru wa Biashara ya Bidhaa(Free Movements of Goods), Uhuru wa Biashara ya Huduma(Free Movement of Services) na Uhuru wa Kuhamisha Mitaji(Free Movement of Capital).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda nimojawapo ya sekta iliyopewa kipaumbele chini ya Sheria yaUwekezaji ya Mwaka 1997 (TIC Act, 1997). Pamoja na kuwa

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

159

kodi ni muhimu katika kugharamia shughuli za Serikali, nafuukatika kodi ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza mazingiramazuri kwa ukuaji wa uchumi na hivyo kuwa na wigo imarawa kodi kwa siku za usoni. Unafuu wa kodi unaotolewakwenye sekta hii ambao hutegemeana na aina ya mradi nipamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango chasifuri, misamaha ya kodi chini ya maeneo ya maalum yauzalishaji kwa ajili ya kuuza nje (EPZ) kama vile misamahakwenye kodi ya mapato kwa miaka 10 (Tax Holiday) nanyingine.

Kamati inatoa wito kwa wenye viwanda kujiandikishakwenye kituo cha uwekezaji na maeneo ya EPZ ili kutumiafursa hizi kupata unafuu katika uzalishaji na kuongezaushindani. Matatizo ya wenye viwanda hayatokani sana namfumo wa kodi bali yanatokana na matatizo ya upatikanajiwa umeme wa uhakika, miundombinu hafifu, teknolojia duni,ujuzi wa kusimamia biashara katika mazingira ya kisasa yaushindani. Hali hii inasababisha hasara kubwa kwa wenyeviwanda kutokana na gharama kubwa za uzalishaji na piakupunguza fursa za ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaipongeza Serikalikwa kusimamia mchakato wa kuendeleza Sekta ya Viwandana Biashara ili kuwezesha nchi kufikia uchumi wa kati waviwanda ifikapo mwaka 2025. Pamoja na malengo mazuriya Serikali, Kamati inatoa angalizo lifuatalo ili malengo hayoyatimie:-

(i) Sekta ya viwanda na biashara mafanikio yakeyanategemea sana uwepo wa miundombinu bora yabandari, reli na barabara ili kuwezesha usafirishaji wamalighafi na bidhaa ndani na nje ya nchi. Kuna hatari kubwaviwanda vyetu kufungwa kutokana na kutokuwezakusafirisha bidhaa walizozalisha kwa kutumia barabara kwasababu inaharibiwa na magari yaliyobeba mizigo mizitokuliko ustahimilivu wa barabara.

Hivyo, Serikali itilie mkazo ufufuaji wa reli kwa ajili yausafirishaji wa bidhaa na mizigo.

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

160

(ii) Bado kuna urasimu mkubwa katikakusimamia kuingiza na kusafirisha mizigo kupitia Bandari yaDar es Salaam, pia Serikali haijatoa kipaumbele katikaupanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Tanga au Mtwara,hivyo kuna hatari mizigo mingi kupitia bandari za nchi yaKenya (Mombasa, Lamu), Msumbiji, Angola au Namibiaambazo zote zipo kwenye programu za upanuzi nazinaunganishwa na miundombinu bora ya barabara na reli.

(iii) Serikali iendelee kuhamasisha uwekezaji katikaviwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo,uvuvi na misitu kupitia uimarishaji wa viwanda vilivyopo nauanzishwaji wa viwanda vipya vya usindikaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo maalum yauwekezaji ‘Export Processing Zones’ (EPZ) na ‘SpecialEconomic Zones’ (SEZ) ni maeneo muhimu ya kukuzaviwanda, kuongeza ajira, kukuza teknolojia, kukuza mauzoya nje na kuhamasisha uongezaji wa thamani. Mifumo kamahii imesaidia kukuza uchumi kupitia viwanda kwa nchi zaIreland, China, Vietnam, Jordan, Afrika ya Kusini na kadhalika,il i kuzalisha ajira kwa wingi kupitia viwanda, Serikaliilikwishatoa agizo kuwa kila Mkoa utenge maeneo maalumya uwekezaji. Kamati imeona kuwa agizo hili ni zuri kwa ajiliya maendeleo ya nchi yetu. Hata hivyo inatoa angalizokuwa:-

(i) Serikali ijiandae kulipa fidia kwa Mikoa 20ambayo imekwishatenga maeneo hayo, ucheleweshaji wamalipo haya kwa wakati unakuwa mzigo mkubwa wamalipo kwa Serikali kwa sababu thamani ya ardhi inakuwaimepanda;

(ii) Maeneo yaliyotengwa yaendelezwe kwahatua kutokana na vipaumbele vilivyopo na misaadatunayopata; na

(iii) Maeneo yaliyotengwa yatengenezeweMpango Mpana (Master Plan).

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

161

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Tawi la Yangahapa Bungeni, napenda kuipongeza Young Africans kwaubingwa waliotwaa. Tawi la Yanga Bungeni linamwagizaRais wa Yanga ndugu Yusuf Manji kwamba ubingwa ulehautanoga kama tarehe 18 hawatawapa kipigo wapinzaniwao wa jadi Simba na hii itasaidia kuboresha safari ya mtaniwetu Mwenyekiti Mheshimiwa Aden Rage. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inapendakumshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara - MheshimiwaDkt. Abdallah O. Kigoda, Naibu Waziri - Mhe Gregory Teu,Katibu Mkuu, pamoja na Wataalamu wa Wizara na Taasisizilizochini ya Wizara kwa kuwa tayari kutoa ufafanuzi nakupokea maoni na ushauri wa Wajumbe wa Kamati wakatiwote wa mjadala wa makadirio haya. Ni matarajio yaKamati kuwa ushirikiano huu utaendelea katika mwaka ujaowa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeekabisa, napenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamatiya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara ambaowameweza kutoa maoni na michango ya mawazo yaombalimbali katika kuboresha makadirio haya ili hatimayeyaletwe mbele ya Bunge hili Tukufu. Naomba nitumie nafasihii kuwatambua Wajumbe wote kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa - Mwenyekiti,Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula - Makamu Mwenyekitina Wajumbe ni Mheshimiwa Margareth Agness Mkanga,Mheshimiwa Haji Khatib Kai, Mheshimiwa Ester Lukago MinzaMidimu, Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, MheshimiwaAhmed Juma Ngwali, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina,Mheshimiwa Dkt. Titus Mlengeya Kamani, Mheshimiwa JoyceJohn Mukya, Mheshimiwa David Zakaria Kafulila, MheshimiwaShawana Bukhet Hassan, Mheshimiwa Said Mussa Zubeir,Mheshimiwa Vicky Pascal Kamata, Mheshimiwa Naomi AmiMwakyoma Kaihula, Mheshimiwa Khatibu Said Haji,Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe, Mheshimiwa AminaMohamed Mwidau, Mheshimiwa Josephine Jonson

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

162

Genzabuke, Mheshimiwa Eng. Habib Juma Mnyaa naMheshimiwa Mohamed Hamis Misanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru sanawewe mwenyewe binafsi na Mheshimiwa Naibu Spika kwakutupatia maelekezo mbalimbali kwa Kamati yetu ambayowakati wote yamefanikisha kazi za Kamati. Aidha, napendapia kumshukuru na kumpongeza Katibu wa Bunge - Dkt.Thomas D. Kashililah, Katibu wa Kamati ya Uchumi, Viwandana Biashara Ndugu Michael Kadebe kwa kuratibu shughuliza Kamati hadi taarifa hii kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, sasanaliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirioya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara(Fungu 44), kama alivyowasilisha mtoa hoja muda mfupiuliopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Sasa nimwite Msemaji waKambi ya Upinzani Wizara ya Viwanda na Biashara.

MHE. HIGHNESS S. KIWIA - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kusoma hotuba ya KambiRasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusumapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2012/2013 namapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kwamujibu wa Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Bunge toleo la mwaka2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ninaposoma hotuba hiini takribani miaka 15 tangu tuingie rasmi kwenye Sera yaUbinafsishaji na ambayo kiuhalisia imefeli na Wizara hii yaViwanda na Biashara inatoa tathimini nzuri zaidi kuonyeshajinsi ambavyo sera hiyo imeshindwa katika utekelezaji wake,ni bahati kuwa leo waziri aliyesimamia jukumu la kubinafsishaviwanda vyetu ambavyo leo kila mmoja analia kuwa

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

163

vimekufa, mashine na mitambo yake zinauzwa kama chumachakavu ndio huyo huyo aliyepewa jukumu la kuvisimamiana au kuvifufua viwanda vilivyouawa na sera hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaamini kuwa utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji imeshindwana sasa ni wakati muafaka wa kufanya tathimini kama Taifana tujipange upya kwa maslahi ya nchi yetu sasa na vizazivijavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda ilipanukakatika karne ya 19 hadi katikati ya karne ya 20 katika nchizilizoendelea karibu nusu ya wafanyakazi wote walijikitakatika sekta hiyo. Nusu ya pili ya karne ya 20, sekta ya tatu naya nne, yaani biashara na huduma zilianza kuwa nawafanyakazi wengi zaidi. Tanzania iliwahi kuwa na viwandavingi vya uzalishaji mali, kwa sababu viwanda vinawezakuinua uchumi wa Taifa na kuondoka katika daraja la kuwanchi maskini duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwasisi wa nchi yetu tayarialikwishatufikisha katika hatua ambayo tayari tulikuwatunakaribia kutoka gizani na kuanza kuona nuru (First, it isimportant to be persistent. It will always be dark before wecan see good days) kwani viwanda alivyoviasisi kwa nianjema ya kuimarisha uchumi wa nchi hii, lakini madaktari namaprofesa wa uchumi waliona Mwalimu alikosea nawakaviuza viwanda vyetu badala ya kuvitafutia tiba yakuvifanya viwe na tija zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kupiga hatua zakimaendeleo, Serikali na sekta binafsi inaanzisha mpangokabambe wa kufufua baadhi ya viwanda vilivyouawa nabaadhi ya viongozi. Hakuna asiyefahamu kama Tanzania inamalighafi za kutosha ambazo zinaweza kutumikakutengeneza bidhaa viwandani na kuuzwa ndani na nje yanchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malighafi hizo zinazopoteakutokana na viongozi kutoweka mikakati ya kuwasaidia

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

164

wananchi kwa kuwapa elimu na namna ya kuanzishaviwanda vidogo na vikubwa vya kutosha vya kusindika nakutengeneza bidhaa mbalimbali ili kuinua uchumi. Ukweli nikwamba kuna viwanda vingi ambavyo havifanyi kazikutokana na ukosefu wa mitambo imara na hivyokusababisha uzalishaji wa bidhaa kuwa chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utekelezji wa bajetiya mwaka 2012/2013 na mipango ya mwaka 2013/2014; hadikufikia Februari, 2013 Wizara hii ilikuwa imepokea kiasi chaasilimia 23 tu ya fedha yote ya bajeti iliyokuwa imeidhinishwana Bunge, kwa upande wa fedha za maendeleo ni kiasi chaShilingi bilioni 16.807 ya fedha za ndani sawa na asilimia 14ndiyo kilikuwa kimetolewa na Hazina, wakati fedha zamaendeleo kutoka nje zilipokelewa asilimia 35. Kambi Rasmiya Upinzani, inaona kuwa Serikali haina nia wala mpangowa kukuza viwanda vyetu na ndiyo maana haitoi fedhaambazo zimepitishwa na kuidhinishwa na Bunge hili kwa ajiliya sekta hii muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa letu.Tunataka majibu, nini kilipelekea mgawanyo huu wa bajetikuwa kiasi kidogo hivyo? Je, tuna uhakika gani kuwa bajetiya mwaka huu itatekelezwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedhauliopita kilitengwa kiasi cha Shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kulipiafidia eneo la Kurasini ili kupisha ujenzi wa kituo cha Biasharakati ya Tanzania na China (Tanzania – China Logistic Centre),jambo la kushangaza ni kuwa kwa mwaka huu wa fedhazimetengwa Shilingi bilioni moja tu kwa ajili ya EPZ. Pamojana marekebisho yaliyowasilishwa na Waziri wa Fedha,ambayo nimeyaona yamewasilishwa Mezani, Kambi Rasmiya Upinzani inataka kujua ni kwanini mwaka huu wa fedhazimetengwa fedha kidogo kiasi hicho, wakati tunatumiaShilingi bilioni 60 kulipa fidia? Mbona hatutengi fedha kwaajili ya kuendeleza mradi kama lengo ni kuondoa utegemeziwa EPZ kwa Serikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2012/2013 Serikali iliendelea na ahadi yake kuwa itakifufuaKiwanda cha Matairi cha General Tyre cha Arusha, na mpaka

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

165

mwezi Machi, 2011 kiwanda hiki kilikuwa kinadaiwa jumlaya Shilingi bilioni 38.

Aidha, mpaka sasa Serikali haijaweza kumpata mbiamwingine kwa ajili ya kuendeleza kiwanda hicho kutokanana ukweli kuwa bado Serikali haijakamilisha utaratibu wakuachana na mwanahisa mwenza, Kampuni ya ContinentalAG.

Kambi Rasmi ya Upinzani, inataka kupata majibu nitaratibu gani zinazokwamisha Serikali katika kuachana nambia mweza ili uzalishaji uweze kuanza kwa kumtafuta mbiampya?

Aidha, ni kwanini Serikali isitenge fedha za kutoshakulipa hayo madeni inayodaiwa ili kiwanda hiki kiweze kuanzauzalishaji? Ni kiasi gani cha mtaji kinachohitajika kwa ajili yakufufua kiwanda hicho, ikiwa tayari mhandisi mshauri waviwanda ameshakamilisha taarifa yake kuhusiana nauchambuzi wa kina wa mahitaji ya gharama ya kufufuakiwanda hicho? Je, kiasi cha Shilingi bilioni 6.3 kilichotengwamwaka huu wa fedha 2013/2014 kinatosha katika kufufuakiwanda hicho?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilitoa waraka waUtumishi Na.1 wa mwaka 2012 ambao ulitoa mwongozokuhusu utaratibu wa kununua samani za ofisi za Serikalikutoka kwa wazalishaji wa ndani na malighafi za samanihizo ziwe zimezalishwa humu nchini, na utekelezaji wawaraka huo ulianza tarehe 01 Oktoba, 2012.

Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kupata majibu yakina juu ya utekelezaji wa waraka huo na ni hatua ganizitachukuliwa dhidi ya Afisa maduhuli ambaye atakiukawaraka huo na kununua samani za ofisi kutoka nje ya nchi?Aidha, tangu kuanza kutekelezwa kwa waraka huo, ni Idarangapi za Serikali zimetii na kuutekeleza kikamilifu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) limepata ridhaa ya Serikali kuratibu utekelezaji wa

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

166

miradi mbalimbali kama vile uzalishaji wa umeme nausafirishaji wake, mawasiliano, madini, kilimo, misitu na uvuvina miundombinu ya barabara inayotekelezwa chini yakinachoitwa Mtwara Development Corridor. Upembuziyakinifu kwa baadhi ya miradi hiyo tayari umekwishakamilika.Aidha, utekelezaji wake unafanyika chini ya mpango mpanawa SADC.

Aidha, kuanzisha na kuendeleza maeneo huru yauzalishaji na uanzishaji wa bandari huru. Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali kulieleza Bunge katika miradi hiyohadi sasa ni miradi gani ambayo imekwishakamilika nauendeshaji wake ukoje?

(a) Ushirika kati ya NDC na Intra Energy Ltd:

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Shirika laMaendeleo la Taifa inamiliki asilimia 30 katika kampuni yaTanCoal. Kampuni hiyo inayojishughulisha na uchimbaji wamakaa ya mawe kwa sasa inatarajia kuanza kuzalishaumeme wa 400MW, na kati ya hizo 200MW zinatarajiwakuzalishwa mwaka 2014 hadi kufikia mwaka 2017 uzalishajiwa 400MW nyingine utakuwa umekamilika.

Aidha, hazina ya makaa ya mawe ya tani 38,039ilikuwa imehifadhiwa mpaka mwezi Januari 2013, hiiinatokana na ukweli kuwa uzalishaji mkubwa wa umemekutokana na makaa ya mawe bado haujaanza kutekelezwakikamilifu na hii inatokana na majadiliano ya muda mrefukati ya TANCOAL na TANESCO kwa ajili ya mkataba wakuzalisha umeme – PPA.

Kambi Rasmi ya Upinzani, inataka kujua ni linimajadiliano hayo yataweza kufikia ukomo ili tuanze kuzalishaumeme kwa kutumia makaa ya mawe na hatimaye tuwezekuondokana na umeme ghali wa kutumia nishati ya mafutahapa nchini?

(b) Mradi wa kuzalisha umeme wa upepo –Singida:

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

167

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ambaounashirikisha Shirika la Maendeleo la Taifa na Kampuni binafsiinayoitwa Power Pool East Africa Ltd kwenye mradi wa nishatiumeme kwa nguvu za upepo, ambao upo takriban kilometa12 mashariki mwa Halmashauri ya Singida.

Mradi unatarajiwa kuzalisha jumla ya Megawati 300,lakini mradi huo unatarajia kuanza kuzalisha Megawati 50,kwa mujibu wa Power System Master Plan (PSMP) mradiulitarajiwa kuanza rasmi mwaka 2012/2013.

Aidha, kwa mujibu wa randama ya Wizara ukurasawa 55 inasema kuwa nanukuu: “Wizara inaendeleakushughulikia upatikanaji wa fedha Dola za Marekani milioni136 kutoka EXIM Bank ya China ambayo imekubali kutoamkopo wenye masharti nafuu na tayari ridhaa ya Serikali(Letter of Support) imewasilishwa EXIM Bank na Wizara yaFedha.”

Kambi Rasmi ya Upinzani, inataka kujua Kampuni yaPower Pool EA iliwezaje kupata ubia huu na NDC na ni kwanini NDC kwa kushirikiana na Serikali ndiyo imekwendakutafuta fedha za mradi huu kwa kutumia guarantee yaSerikali? Waziri aweke wazi wamiliki wa Power Pool EAmaana habari za kuaminika zinaonyesha kuwa wamiliki wamradi huu ni ndugu na jamaa wa Wabunge na Mawaziri waCCM ambao ni Maswa Kagoswe, Isaac Joseph Mwamanga,Emmanuel Kasyanju, Prosper Tesha, Lennard Tennende naAthuman Ngwilizi, na hivyo wametumia ushawishi waoSerikalini kupata ubia huu ili kufaidika kifedha. (Makofi)

Aidha, tunataka kujua kama Serikali ilifanya uchunguziwa kina (vetting) juu ya wamiliki, uwezo na uhalali wakampuni hii ya Power Pool EA katika kuzalisha umeme kablaya kutoa ridhaa ya Serikali juu ya mkopo huo mkubwa ili

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

168

isijekuwa hii nayo ni “Richmond” nyingine, na kama iliwahikufanya mradi mwingine popote wa kuzalisha umeme kwanjia ya upepo.

(c)Mradi wa uyeyushaji chuma ghafi uliopo Ludewa:

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika hili la NDC liko kwenyeubia na kampuni ya MM Steel Resources Public LimitedCompany (MMSR PLC), ambapo kampuni ya ubia inayoitwa“Maganga Matitu Resource Development Limited (MMRDL)”iliyopo Wilaya ya Ludewa kwa ajili ya matumizi ya chumaghafi kutoka eneo la maganga matitu ambalo ni sehemuya machimbo ya Liganga na Katewaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka2012/2013 ilitengewa Shilingi bilioni 7.9 kwa ajili ya miradi yote,na mradi wa mchuchuma Sh. 1,779,763,501/=.

Kwa mwaka wa fedha 2013/2014, NDC imetengewaShilingi bilioni mbili kwa ajili ya mradi wa Mchuchuma wakufua umeme kwa kutumia makaa ya mawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi ya Upinzani inatakakujua uwezo wa kiutawala (Managerial and TechnicalAspect) kwa Shirika hili kuweza kushiriki mchakato mzima wautendaji kwa Makampuni haya yote ambayo Shirika linamikataba kwa kufungua Kampuni za ubia, kutokana naukweli kwamba Serikali ndiyo inayowekeza fedha za walipakodi kwa mujibu wa vitabu vya Randama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba Serikaliimekuwa ikipoteza fedha nyingi kutokana na kutokuwemokwenye utawala na uendeshaji kwa kampuni tulizo na hisa,kutokana na kukosekana kwa usimamizi dhabiti wa hisa zetu.

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

169

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la KuhudumiaViwanda Vidogovidogo (SIDO). SIDO imekuwa ni taasisi yenyemsaada mkubwa kwa wajasiriamali wadogo na wa katihapa nchini, inafanya nini katika kuingia ubia na wananchikatika kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazaoya kilimo, (ushirikiano na wakulima kama vile miwa,Morogoro, Manyara, Mbinga, Tanga na kadhalika), alizeti,matunda na kadhalika badala ya SIDO kutafuta fedha auSerikali kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2013/2014, SIDO imeweka malengo mengi baadhi yake niyafuatayo: kuimarisha uwezo wa kuzalisha na kusambazamashine ndogondogo za kusindika mazao, kuwezeshausambazaji wa teknolojia vijijini kwa kupitia program yaWilaya moja kwa moja, kuwezesha wazalishaji wadogokupata masoko ya bidhaa na huduma zao, kwa ktengenezamiundombinu ya kupokea na kusambazia habari zakibiashara na kutengeneza sehemu za kuonyeshea bidhaaza wazalishaji wadogo, kutoa huduma za kifedha ikiwa nipamoja na ushauri na mikopo pale itakapojidhihirishakuhitajika, kutoa elimu ya ujasiriamali, uongozi wa biashara,usindikaji wa vyakula na kuzingatia ubora wa bidhaa nakadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa malengohaya muhimu sio jambo jepesi kama kweli tunahitaji tijaipatikane kwa Watanzania. Hivyo basi kwa bajeti yamaendeleo ambayo imetengwa ya jumla ya kiasi cha shilingi6,224,594,000/=, kati ya fedha hizo za ndani ni shilingi3,000,000,000/-, huu ni mzaha kwa nchi inayojipanga upyakuanzisha viwanda vya msingi katika uongezaji thamani kwamazao ya kilimo. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikuliangalia upya suala la mgawo wa fedha za ndani kwaSIDO.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa taasisi hii mbaliya kutoa huduma kwa wajasiriamali wadogo bali pia nitaasisi inayofanya biashara, hivyo basi, Kambi ya Upinzaniinaitaka Serikali kutumia uzoefu wa SIDO badala ya kuwa

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

170

Mshauri Mwelekezi katika uanzishwaji wa viwanda vidogobali kuingia ubia na vikundi na wajasiriamali mbalimbalikuwekeza katika viwanda vidogovidogo. Tunaamini kabisakwa njia hii kuwa ushauri wanaoutoa utakuwa ni endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Viwango la Taifa –TBS. Shirika hili ndilo lenye jukumu la msingi la kuhakikishabidhaa zote zinazozalishwa nchini au kuingizwa nchini tokanje zinakuwa na ubora unaoridhisha kabla havijaingizwakwenye soko letu la ndani. Kwa bahati mbaya ni kwambakumetokea malalamiko makubwa toka kwa watumiaji wabidhaa kuwa baadhi ya bidhaa zinakuwa hazina uboraunaohitajika, miongoni mwa bidhaa hizo ni zile zinazohusupembejeo za kilimo ambapo watumiaji wake wamepatahasara kutokana na kutumia pembejeo hizo, “Serikaliimezinyang’anya leseni ya uagizaji na usambazaji wa mboleanchini kampuni ya Mohamed Enterprises Ltd na Stacokutokana na kusambaza mbolea feki. Aidha, alibainisha kuwakutokana na uchunguzi uliofanywa asilimia 80 ya mboleailiyosambazwa katika Mkoa wa Ruvuma ni feki.” Kauli yaMheshimiwa Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Chakula naUshirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbolea kwa wakulima nimaisha, hivyo uzembe wowote wa wahusika kutokutimizawajibu wao maana yake ni hujuma kwa wakulima. Kwa kauliya Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa 80% ya mboleailiyosambazwa Mkoani Ruvuma ilikuwa ni feki, maana yakeni kwamba TBS hawakufanyakazi yao ya msingi na hivyo kwavyovyote wanatakiwa wawajibike kwa hasara waliyoipatawakulima na pili suala la kunyang’anywa leseni kwa Kampunizilizokuwa zinaingiza na kusambaza mbolea haitoshi, baliwanatakiwa wafunguliwe mashtaka ya kuhujumu uchumina kulipa fidia kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma.Uswahiba wa wafanyabiashara na CCM, rushwa na ufisadi,ndio vinavyoiua nchi hii. Kambi Rasmi ya Upinzani inatakaSerikali ieleze hatua zilizokwishachukuliwa kwa sakata hilola mbolea feki kwa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu gazeti la

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

171

Mtanzania la Jumanne, Machi 05, 2013 “Dkt. Kigoda alitoaagizo hilo Dar es Salaam jana, alipokuwa akizindua bodimpya ya Shirika hilo, baada ya kuvunja bodi ya zamani kwakutokuridhishwa na utendaji wake. Dkt. Kigoda alikiri kuwahivi sasa bidhaa bandia zimezagaa kwa kiasi kikubwa sokoni,hivyo akataka bodi hiyo mpya kuhakikisha bidhaa zote zenyeubora hafifu zinatokomezwa”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kauli hiyoya Waziri ni dhahiri walaji wamekwishapata madharamakubwa sana kutokana na kununua bidhaa zisizo na uboraunaokubalika. Hoja ni kwa vipi wale ambao madharayamekuwa ni makubwa mno watakavyofidiwa na TBS?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa randama nikwamba TBS imeweka malengo ambayo ni pamoja nakuendeleza utekelezaji wa utaratibu wa kupima ubora wabidhaa zote mahali zinapotoka kabla ya kuingia nchini,kuimarisha utaratibu wa kukagua ubora wa bidhaa ukiwemoukaguzi wa magari kabla ya kuingia nchini, kutayarishaviwango vya Taifa vinavyofikia 150 vikiwemo viwango vyasekta ya huduma katika mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiasi cha shil ingi1,865,148,000/- kilichoombwa na TBS kwa mwaka wa fedhawa 2013/2014 kwa kazi zinazohitajika kutekeleza malengoyake, inawezekana zikawa ni chache kutokana na hali halisiilivyo kama alivyodokeza Mheshimiwa Waziri kuwa bidhaazenye ubora hafifu zimejaa sokoni na hivyo ni jukumu la TBSkuhakikisha vinaondolewa sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBS na ukaguzi wa magarinje ya nchi. Shirika la Viwango Tanzania limekuwa nautaratibu wa kukagua bidhaa mbalimbali ndani na nje yanchi ili kuweza kubaini ubora wake na kutoa hati maalumza ubora kabla ya bidhaa hizo kuruhusiwa kuingia kwenyesoko la nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na uwepo wakitengo maalum kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo, Shirika hili

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

172

limeonyesha udhaifu mkubwa sana katika kufanya ukaguziwa magari unaofanywa na kampuni mbalimbali nje ya nchikwani waliopewa kazi hiyo ni makampuni ambayo hayanauwezo wala sifa ya kuweza kuifanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinataka kupata majibu ni kiasi gani cha fedha ambachomnunuzi wa gari anatakiwa kutoa kama ada ya ukaguziwa gari pindi anaponunua, kwani kwa mujibu wa taarifa yaSerikali ni kuwa ni dola za Marekani 150 kwa gari, ila uhalisiani kuwa ukiagiza gari unatakiwa kulipia kati ya dola zaMarekani 300 hadi 450 kama ada ya ukaguzi wa gari. Ninikauli ya Serikali kuhusiana na viwango hivi vya ada yaukaguzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taarifazilizotolewa na Serikali ni kuwa tangu mwaka 2002 ni kuwakiasi cha dola 18 milioni kiliweza kutumika kama ada yaukaguzi wa magari na fedha zilizoingia nchini ni kiasi chadola 2.2 milioni tu. Kambi ya Upinzani, inataka kujua ni kwanini Serikali ilipata kiasi kidogo namna hiyo cha fedha nakuna utaratibu gani wa kuhakikisha kuwa tunawezakukusanya mapato zaidi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo makampuni ambayoyalifungiwa na TBS kufanya kazi ya ukaguzi kutokana namakampuni hayo kutokufikisha fedha Serikalini, makampunihayo ni pamoja na Jaffer Al Garage (Dubai), PlanetAutomotive (Singapore), Quality Gerage (Hong Kong) na WTMya (Uingereza). Kambi ya Upinzani, inataka kupata majibu nihatua gani zaidi zimechukuliwa dhidi ya makampuni hayona fedha kiasi gani zimerejeshwa? Vilevile ni kiasi gani chafedha kilichokusanywa kutokana na faini wanazopigwawamiliki wa magari ambao wanaingiza magari yao bilakukaguliwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, TRA na uuzaji wa magari.Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa watu nawafanyabiashara wanaoagiza magari toka nje kwa kutozwaushuru ambao ni tofauti kulingana na bei halisi ya kununulia

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

173

magari yao kama inavyooneshwa na nyaraka za “bill oflading”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malalamiko hayoyanatokana na kile kinachosemekana kuwa TRA wanakuwana orodha za bei za kununulia magari ya aina mbalimbalikutoka nchi mbalimbali ofisini kwao. Hivyo kufanya beiinayoonyeshwa na nyaraka za ununuzi kukataliwa na Maofisawake na kutoza ushuru kwa kuangalia bei walizonazo ofisinikwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kuwaeleza Watanzania ni lini TRA imeanzakujihusisha na biashara ya kuuza magari badala ya kukusanyaushuru? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Ushindani waKibiashara - Fair Competition Commission. Kama ilivyokuwakwa TBS, Tume hii nayo inahusika moja kwa moja katikakuliokoa Taifa letu kuwa jalala la kutupia bidhaa zisizo naubora na viwango jambo linalosababisha bidhaazinazozalishwa hapa nchini kuonekana zina bei kubwakulinganishwa na bidhaa zinazotoka nje. Bidhaa nyinginezinazalishwa hapahapa nchini na kuwekwa nembo kuwazinatoka nje ya nchi na kuingizwa kwenye soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madhara ni makubwa kwaviwanda vya ndani na uharamia huu sio kama haujulikanina vyombo na mamlaka husika, kwa mfano mdogo ni kamanilivyoeleza hapo juu, Waheshimiwa Wabunge walipopatanafasi kutembelea viwanda vilivyojificha kwenye maeneoambayo hayakutengwa rasmi kuwa ya viwanda na bidhaazake kuingizwa sokoni kinyemela. Kambi Rasmi ya Upinzaniinauliza Tume hii iko wapi wakati hayo yakifanyika nakuonekana kuwa bidhaa za ndani sio shindani kwa mlaji wamwisho wakati bidhaa feki ndizo zinanunuliwa kutokana nabei kuwa ya chini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi za Utafiti, Mafunzo naMaendeleo ya Teknololoji. Taasisi hizo kwa kiwango kikubwa

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

174

ni kwa ajili ya kutoa usaidizi wa kuibadilisha sekta nzima yaviwanda ili iweze kuleta tija kwa Watanzania kwa kuwakichocheo kikuu katika ukuzwaji wa uchumi kwenye sektanyingine za uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na umuhimu wataasisi hizi za utafiti, bado Serikali hii ya CCM haioni haja yakuwekeza fedha za kutosha kwa ajili ya kuzifanya ziwezekutimiza majukumu yake kikamilifu pamoja na badhi yataasisi kama CAMARTEC kuweza kuzalisha trekta ililobuniyenyewe kwa kutumia teknolojia ya ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kwa mwakahuu wa fedha taasisi ya TIRDO imetengewa kiasi cha shilingi130,000,000 tu kwa ajili ya kufanya utafiti na kusambazateknolojia zilizohakikiwa, kutekeleza mfumo wa ufuatiliajimazao kwa kutumia teknolojia na kuhakiki maabara yamazingira na vifaa vya kihandisi. Aidha, taasisi ya CAMARTECimetengewa kiasi cha shilingi 200,000,000 kwa ajili ya kujengaukuta kuzungukia eneo lake, kuendeleza uzalishaji wa trektalililobuniwa na CAMARTEC, kununua na kufunga jenereta ladharura ili kukabiliana na kukatika kwa umeme, kuendelezautafiti na uendelezaji wa teknolojia mbalimbali za zana zakilimo. Kambi Rasmi ya Upinzani, haikubaliani na mgawanyohuu wa rasilimali katika Fungu la Maendeleo na hasa kwenyemaeneo ya utafiti kutokutengewa fedha za kutosha ni dhahirikuwa hatuna nia ya dhati ya kuimarisha sekta hii ya viwandahapa nchini. Tunataka maelezo ya kina ni kwa nini Wizara hiihaioni umuhimu wa kuwekeza kwenye utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chama cha HakimilikiTanzania – COSOTA. Kwa mujibu wa Sheria ya Hakimiliki,Namba 7 ya mwaka 1999 (Copyright Act No.7 ya 1999)inasema kuwa kazi za cha pamoja na zingine Kifungu cha47(a) kinasema kuwa “to promote and protect the interestsof authors, performers, translators, producers of soundrecordings, broadcasters, publishers, and, in particular, tocollect and distribute any royalties or other remunerationaccorded to them in respect of their rights provided for in thisAct”

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

175

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, Chama chaHakimiliki Tanzania (COSOTA), ndio chombo chenye mamlakaya kusimamia, kuendeleza na kulinda haki za wasanii. Mojaya haki ya msanii ni mapato halali kutokana na kazi yake yakisanii. Hivi sasa wasanii wengi nchini na hasa wasanii vijanawa muziki wananyonywa na makampuni makubwa yenyenguvu kwa sababu COSOTA haina dhamira kutetea nakulinda kazi za wasanii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inapendekeza kuwa COSOTA itoe kanuni kudhibitibiashara ya nyimbo za wasanii kama miito (ring tones). NchiniMarekani miito ya simu ni kazi za kisanaa na wasanii (contentcreators) hulipwa si chini ya asilimia kumi (10%) ya mapatokutoka kwenye mitandao ya simu (network providers).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa nchini hakuna kanuniza kuongoza biashara hii ambayo imetokana na maendeleoya teknolojia. Wasanii wetu wamekuwa wananyonywa kwasababu ya kukosekana kwa kanuni hizi na hivyo biashara hiikuwa na usiri mkubwa jambo linalopelekea haki kukosekana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inataka uwepo uwazi katika biashara ya Ringtonesna tunataka vijana wetu wapate malipo halali. Haisadiikuendelea kuwatumia wasanii kuimba kwenye majukwaaya kisiasa na kuwatosa badala ya kuwasaidia kupata hakizao. Tunataka uwazi na haki katika biashara hii na ring tonesna ijulikane kiasi gani cha Kodi kinapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Taarifa Rasmiza Bunge, ni kwamba Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwaikitoa mapendekezo kadhaa kuhusiana na kuimarishaCOSOTA, kama vile “Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmiya Upinzani inapendekeza kuwa Sheria ya Hakimiliki naHakishiriki Na.7 ya mwaka 1999 ifanyiwe marekebisho kwalengo la kuipa meno zaidi ya kulinda haki na kuhakikishawasanii wananufaika na kazi zao. Moja ya mapendekezo nikuifanya COSOTA kuwa chombo chenye nguvu zaidi katika

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

176

kulinda kazi za Wasanii kuliko ilivyo hivi sasa. MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo katika sehemu ya marekebishotunayopendekeza, Kambi Rasmi ya Upinzani tunataka SuraNa. 218 ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, ifanyiwemarekebisho ili kuunda Mamlaka ya Hakimiliki Tanzania(Copyright Regulatory Authority of Tanzania (CORATA) badalaya kuiacha COSOTA kama ilivyo hivi sasa”. Hansard ya tarehe11.8.2011.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri huu ulitokana naukweli kwamba COSOTA ipo kisheria lakini haina nguvukisheria au meno kupambana na uharamia ulipo katika tasniaya hakimiliki jambo linaloinyima nchi na wasanii haki zaostahiki kutokana na kazi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Hansard 18 Juni,2012inaonyesha kuwa “Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wakumbukumbu zilizopo, Serikali mwaka 2006 kupitia Gazeti laSerikali Na. 18 la tarehe 10 mwezi wa Februari, ilianzishautaratibu wa HAKIGRAM kama stiker maalumu za kazi halaliza wasanii zinazotolewa na COSOTA. Kambi ya Upinzanitunapendekeza utaratibu huo uendelee na Mamlaka yaMapato (TRA), ihusike kukusanya mapato kwa ajili ya kazihiyo na COSOTA wataratibu utoaji wa HAKIGRAM. Hii itaendasambasamba na kuzuia uchakachuaji wa HAKIGRAM hizo ilikutopoteza lengo la kuweka mfumo huo. Stiker zisitolewe naTRA bali zitolewe na COSOTA na TRA isimamie eneo la mapatotu. Hii itasaidia kwani stiker hizi hazitatumika kupata mapatopekee bali pia kuweka kumbukumbu muhimu za kazi zawasanii”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kwamba juhudihizo zote zimeshindwa kuwanufaisha wasanii na Serikali,kwani bado kuna wajanja wachache wanaochukua “lionshare” katika biashara nzima ya sanaa na kuacha wasaniikatika mlolongo mzima wa kazi za sanaa kukosawanachostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinataka kupata taarifa kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Uhuru

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

177

wa bidhaa iliyopitishwa na Bunge kwa shinikizo la Wabungewa Upinzani. Sheria ile inataka kila kazi ya sanaa inayouzwanchini kama CD, DVD na kadhalika iwe na stamp za TRA.Tunapenda kujua kuwa atakayepewa stamp hizo ni nani?Msanii au Msambazaji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, uelewa wa mnyororo wathamani (value chain) wa biashara hii ni muhimu sana.Wasanii wetu huuza haki zao kwa wasambazaji kwa sababuya umaskini, ni vizuri kuhakikisha kuwa hakimiliki inabakiakwa msanii na msambazaji azuiwe kikanuni (Fair CompetitionRegulation) kuwa mzalishaji (producer). Hii itasaidia sana“authors” na “producers” kubakia na hakimiliki namsambazaji auziwe na producers/authors haki ya kusambazatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, ni muhimu sanastamp zitolewe kwa msanii na mzalishaji tu (producers) nasio distributors. Hii itatoa nguvu kwa wasanii na itakataunyonyaji wa wasambazaji kwa wasanii wetu ambao hivisasa wamegeuzwa waajiriwa wa makampuni ya usambazajiwa kazi za sanaa. COSOTA na FCC wasikwepe wajibu waowa kusimamia tasnia na kudhibiti ushindani ili wasanii waTanzania wafaidi jasho lao ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya viwanda. Ukuaji wasekta ya viwanda kwa mwaka 2011/2012 ulikua kwa asilimia7.8 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.9 mwaka wa fedha2010/2011 na mchango wake katika Pato la Taifa uliongezekakutoka asilimia 9.6 mwaka 2010/2011 na kufikia asilimia 9.7mwaka 2011/2012. Ongezeko dogo la mchango wa sektahii haukuweza kumnufaisha mwananchi moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2008, idadi yaviwanda vilivyokuwa vinafanyakazi kwa upande waTanzania Bara ni 729. Kati ya idadi hiyo ya viwanda,vilivyokuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ni (383), Arusha(51), Mwanza (39), Singida (27), Tanga (27), Kagera (26) na

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

178

Kilimanjaro (24). Kati ya viwanda hivyo vilivyokuwepo mwaka2008, viwanda 643 vinamilikiwa na watu binafsi na viwanda72 vinamilikiwa na Serikali na vilivyobaki 14 vinamilikiwa kwapamoja kati ya Serikali na sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha kuwaviwanda 549 vinamilikiwa kwa asilimia mia moja na wazawana viwanda 121 vinamilikiwa na wageni toka nje ya nchi navilivyobaki takriban viwanda 59 vinamilikiwa kwa ubia katiya Serikali na watu binafsi au wageni na wazawa. Aidha,kati ya viwanda 729 vilivyokuwepo mwaka 2008, asilimia 93au viwanda 680 ni viwanda vya uzalishaji bidhaa, kati yahivyo asilimia 93, viwanda 240 vinajihusisha na uzalishajibidhaa za chakula, vinywaji na tumbaku na mashine zakusaga nafaka 61.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu walioajiriwa katikaviwanda hivyo walikuwa ni watu 117,622 na kati ya hao107,388 wako katika viwanda vya uzalishaji, viwanda vilivyoDar es Salaam vimetoa ajira kwa wafanyakazi 34,554 auasilimia 29. Viwanda binafsi 643 vimeajiri jumla ya watu103,237 ikilinganishwa na jumla ya watu 12,394 waliokuwawanafanyakazi kwenye viwanda 72 vinavyomilikiwa naSerikali. Viwanda vilivyokuwa vinamilikiwa na wazawa viliajirijumla ya watu 53,950 kwa kulinganisha na watu 42,192walioajiriwa na viwanda vinavyomilikiwa na wageni. Aidha,walioajiriwa na viwanda vinavyomilikiwa kwa pamoja katiya Serikali, watu binafsi (wageni, wazawa na nchi za nje) ni21,515, hii ni kwa mujibu wa Annual Survey of IndustrialProduction, 2008.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa mpango wamaendeleo wa miaka mitano, mwaka huu wa fedhavipaumbele kwa Wizara hii ya Viwanda na Biashara nikuwezesha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji, hasakatika maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ/SEZs), kuendeleana utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Biashara na UwekezajiKurasini (Kurasini Logistical Trade Hub), utekelezaji wa miradiya makaa ya Mawe Mchuchuma na Liganga pamoja na

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

179

magadi katika Bonde la Engaruka. Aidha, ni uendelezaji waviwanda vinavyotumia rasilimali zinazopatikana hapa nchinikama vile usindikaji wa bidhaa za kilimo, nguo, makaa yamawe, gesi asilia na chuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchunguzi uliofanywa nagazeti la Raia Mwema ulibaini kampuni kadhaa kubwa namaarufu nchini zinazojihusisha na biashara ya chumachakavu katika mfumo unaoikosesha nchi mapato kupitiakodi. Moja ya kampuni hiyo ni ile iliyopata kuuziwa na Serikalibaadhi ya viwanda vya nguo, pamoja na mashamba yamkonge na chai, ambayo badala ya kuwekeza imekuwaikiuza mitambo waliyokuta katika viwanda hivyo kamachuma chakavu, bila kuzingatia utaratibu na mikataba yamauziano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nyakati tofauti nyarakaza mauzo zinaonyesha kuwa wamekwishauza mitambombalimbali kwa jumla ya Sh. 438,184,000. Mitambo iliyouzwani ile ya viwanda walivyouziwa na Serikali katika Mikoa yaMorogoro, Dar es Salaam na Mara, Mjini Musoma. Mauzo kwamitambo ya viwanda walivyonunua vilivyopo Dar es Salaamkwa awamu ya kwanza yalifanyika Februari 15, mwaka 2010(Sh. Milioni 8.6), mauzo ya awali ya pili ni Agosti 12, mwaka2010 (Sh. 108,625,000). Uuzaji mwingine wa mitambo ya mojaya viwanda vilivyonunuliwa na kampuni hiyo MkoaniMorogoro ulifanyika Februari 22, 2010, kwa mauzo yaSh.72,500,000. Mkoani Musoma mauzo ya mitambo kamachuma chakavu yalifanyika Aprili 24, mwaka jana, kwathamani ya Sh.248,359,000. Mmiliki wa viwanda hivyoanajulikana na mwanaye ni Mbunge katika Bunge letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali, kuwaeleza Watanzania ni kwa vipi viwandavitafufuliwa wakati waliobinafsishiwa viwanda hivyowanang’oa mitambo na kuuza kama chuma chakavu naviwanda vinabaki kuwa maghala kwa maana kwambamashine zilizong’olewa zilikuwa zinafanyakazi kwa asilimiamia na kufanya kiwanda kuhimili kiasi kikubwa cha pamba

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

180

il iyozalishwa hapa nchini, lakini mashine zil izoletwazinafanyakazi kwa asilimia kumi tu? Tutawezaje kukuza ajirakama viwanda vyetu vinauwawa makusudi, mitamboinang’olewa na kuuzwa kama chuma chakavu na Serikaliipo, inaona na haichukui hatua yoyote? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi imekuwaikisema mara zote kuwa mambo haya yanatokea kutokanana ukweli kwamba waliobinafsishiwa viwanda ni washirikawa Karibu na CCM. Jambo hilo limepelekea kutokuchukuliwakwa hatua zozote kwa watu hao ambao wanakiukamikataba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkazo wa uendelezaji waviwanda hasa vinavyotumia malighafi za kilimo utapelekeakubadilika kwa mfumo ambao umezoeleka wa kilimo kuwandio sekta inayotoa ajira zaidi na sekta ya viwanda kuwandio mhimili mkuu katika utoaji wa ajira. Ili kufikia hapoushirikiano kati Serikali na sekta binafsi ni muhimu sana ilikufufua sekta ya viwanda upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ndogo ya nguo. Ukuajiwa uchumi usiozalisha ajira ndiyo moja ya sifa za uchumi waTanzania katika kipindi cha muongo mmoja (2001 – 2011).Taarifa ya hali ya umasikini nchini (PHDR 2011) kwa kukatatamaa kabisa, imesema licha ya kasi ya ukuaji wa uchumiwa Tanzania kuwa kubwa na ya kuridhisha, uzalishaji wa kazi(ajira) umekuwa ni wa kukatisha tamaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha katikakila Watanzania 650,000 wanaoingia katika soko la ajira kilamwaka 610,000 wanakosa ajira. Uchumi unashindwakuzalisha ajira za kutosheleza vijana wanaoingia kwenye sokola ajira. Hata vijana wasomi waliosoma kwa fedha za walipakodi nao wanahangaika mitaani bila kazi kwa kipindi kirefumara baada ya kuhitimu masomo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekamilishauandaaji wa Mkakati wa Kuendeleza Sekta ndogo ya Nguona Mavazi. Mkakati huo umeandaliwa kwa ushirikiano na

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

181

Gatsby Charitable Foundation (GCF) ya Uingereza na TanzaniaGatsby Trust (TGT). Madhumuni ya Mkakati huu ni kufufua nakundeleza sekta ndogo ya nguo na mavazi ambapo itaanzana uanzishaji wa Kitengo cha Kusimamia mradi husika (TextileDevelopment Unit –TDU).

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vyetu vya nguovinaweza kuwa na ushindani kutokana na gharama ndogoza wafanyakazi (Tanzania US$ 0.4 kwa saa), ikilinganishwana India (0.75), China (0.9) Turkey (4 USD), Misri (0.9), Italy (24USD) na umeme. Changamoto inayokabili sekta hii ni ukosefuwa umeme wa uhakika; gharama kubwa za upatikanajimitaji – riba: Tanzania (16-17 %), USA (4%), China (6%), Italy(4%); mashine nyingi za zamani ambapo (90%) ya mashinezina zaidi ya miaka kumi na 50% zina zaidi ya miaka 20 nakumekuwa na uwekezaji mdogo. Viwanda vya mavazivimeshindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa zakodi ya pango, umeme usio wa uhakika, viwanda kujikitakatika utengenezaji wa khanga na vitenge tu, viwangovidogo vya kuingiza mbinu za uhandisi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti waChama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda(TCCIA) katika Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Edgar Nkunda,katika ushuhuda wake kuhusu uongezaji thamani bidhaaza pamba, kwani alipata kuwa ni mmiliki wa kiwanda changuo kwenye hatua fulani ya mchakato wa kutengenezanguo. Alikuwa akinunua nyuzi (yarn) kutoka kwenye viwandavikubwa na kutengeneza vitambaa (fabrik) baada yamchakato wa usokotaji (weaving) kama ilivyo kwenyemnyororo wa kuongeza thamani wa sekta ya nguo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, “Kiwanda chake kidogokilitoa ajira kwa watu 40. Mwaka 2007 na 2008 tatizo lamgawo wa umeme likayumbisha biashara yake”. Mwaka 2008na 2009 mdororo wa uchumi duniani ulitikisa sio wateja waketu bali sekta nzima ya pamba. Haya mambo mawili, mgawowa umeme na kukosa soko la bidhaa zake, yalimfanya afungebiashara, akang’oa mashine za kiwanda chake na kuuza

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

182

kama chuma chakavu. Vijana wenzake 40 wakakosa kazina yeye akaingia katika biashara ya kutengeneza batikianayofanya hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, duniani kote sekta ya nguondio hutumika kutoa ajira nyingi sana kwa wananchi na hasawanawake. Sekta ya nguo ni sekta mkakati ya kukuza ajiranchini, sekta ya nguo pekee inaweza kutengeneza ajira100,000 hapa nchini kwa kiwango cha sasa cha uzalishajiwa pamba. Uzalishaji wa pamba nchini ukiongezekamaradufu na kufikia angalau marobota milioni 1.5, sekta yanguo itaweza kuzalisha ajira mpaka 250,000 kupitia kwenyeuchambuzi (ginneries), nyuzi (spinning), vitambaa (weaving)na nguo (garments). Hii ni kwa mujibu wa Raia Mwema, Toleola 271, tarehe 5 Desemba, 2012, Tunahitaji uamuzi mgumukisiasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, misingi hii ya ajira siokwamba haikuwapo. Waasisi wa taifa waliona umuhimu huuna ndio maana wakati mwaka 1967 hapakuwa na chembeya pamba ya Tanzania iliyokuwa ikifanyiwa mchakato ilikupata nguo (kwa maana ya kuongeza thamani hapa hapanchini), mwaka 1975 kulikuwa na viwanda vinane vya nguo.Utafiti unaonyesha kuwa mahitaji ya matumizi ya nguo hapanchini ni sawa na marobota milioni mbili kwa mwaka. Kwahiyo, pamba tunayoiuza nje kama ‘yarn’ hurudi nchini kamavitambaa au nguo zilizokamili. Hivyo kazi nyingi sanazinakuwa zimepelekwa nje kwa kuuza pamba ghafi nje yanchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka tunaanza mchakatowa ubinafsishaji kulikuwa na viwanda takribani 12 vya nguo,ikiwa ni pamoja na kiwanda kikubwa cha nyuzi Tabora.Watanzania kwa maelfu waliajiriwa kwenye viwanda vyanguo. Hivi sasa ni viwanda vichache kati ya vilivyouzwa kwawawekezaji binafsi vinafanya kazi. Vingi ukiondoa kiwandacha 21st Century cha Morogoro na A to Z cha Arusha,vinatumia malighafi kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suluhisho la kujinasua na

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

183

balaa hili kwa sasa ni sekta ya viwanda vidogovidogokupata msaada mkubwa toka ndani na nje kama kweliSerikali ina dhamira ya kweli kuwasaidia wadau katika sektahii kuwekeza katika eneo la weaving na garments.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyaraka za Wizara zinasemakuwa, “… kati ya viwanda vya zamani vilivyokarabatiwana kufanyiwa upanuzi ni pamoja na Kiwanda cha Zana zaKilimo (UFI) ambacho sasa kinaitwa Tanzania Steel Pipes (TSP),Dar es Salaam”. Nini hatma ya uzalishwaji wa zana za kilimokwani kiwanda cha UFI kimebadilishwa na kuwa kiwandacha kuzalisha mabomba na kiwanda cha ZZK Mbeyalimekuwa ni ghala la kiwanda cha bia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mwekezaji aliyenunuaUFI alikuwa na mtaji wa kutosha ni kwa nini asiendeleekuzalisha zana za kilimo na uzalishaji wa mabomba uwepo?Uagizaji wa zana za kilimo toka nje ya nchi ni mkubwa sanakwa sasa kutokana na msukumo wa Serikali kwenye kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Waziri waViwanda, Biashara na Masoko, Mheshimiwa Nazir MustafaKaramagi (Mb), akiwasilisha Bungeni makadirio ya matumiziya fedha kwa mwaka 2006/2007, alisema nanukuu: “Kwaujumla uwekezaji katika viwanda unaendelea kuongezekana kutoa nafasi za ajira. Kati ya viwanda vipya vilivyoanzishwani pamoja na China Paper Corporation cha Kilimanjaro (ajira60), Kahama Ginnery and Oil Mill Ltd cha Shinyanga (ajira120) na Merchandise Products Group cha Kibaha (ajira 20)na viwanda vingine vya kusindika samaki katika Mikoa yaKanda ya Ziwa. Aidha, kati ya viwanda vya zamanivilivyokarabatiwa na kufanyiwa upanuzi ni pamoja naKiwanda cha Zana za Kilimo (UFI) ambacho sasa kinaitwaTanzania Steel Pipes (TSP), Dar es Salaam; Kiwanda cha NyuziTabora (TABOTEX); Tanzania Dairy Ltd, cha Tanga; TanganyikaInstant Coffee (TANICA), Kagera na Tanzania PharmaceuticalIndustries Ltd (TPI), Arusha”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango waMbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Tabora Kaskazini hapo

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

184

tarehe 26 July 2012 alisema kwamba “MheshimiwaMwenyekiti, pia tuna Kiwanda cha Nyuzi New TABOTEX,imedhihirika kuwa kiwanda hiki hakitumiki ipasavyo, tayariwakulima wamelima pamba jinsi ilivyoahidiwa na uongoziwa kiwanda hicho, lakini mpaka sasa haijanunuliwa nakiwanda hicho, jambo ambalo limeleta usumbufu mkubwakwa wakulima wa pamba”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kauli hizo mbili, KambiRasmi ya Upinzani inaona kuna tatizo juu ya utendaji waKiwanda cha Nyuzi-Tabora, kwani Serikali ilitoa kauli hiyomwaka 2006 na ushuhuda wa Mbunge ulitolewa mwaka2012. Inawezekana kabisa Kiwanda cha Nyuzi cha Taborabaada ya kuuzwa kinafanya kazi ambayo ni tofauti auhailingani na iliyokuwepo kama ilivyo kwa kiwanda cha Uficha Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni, inataka kupata majibu ya kina kuhusumafao ya kustaafu kwa waliokuwa wafanyakazi 834 wakiwanda cha nguo cha Mutex, kwani Serikali iliwapelekeamafao yao kiwango cha kiasi cha shilingi elfu themanini natatu (83,000) tu kila mmoja, kwa watu ambao walifanya kazikwa zaidi ya miaka 20 sio tu kwamba ni dharau, bali nidhihaka kubwa kwa wastaafu hawa na ndio maanawalikataa kupokea kiasi hicho cha fedha ambacho hakitoshihata nauli ya kumsafirisha mtu mmoja kwenda nyumbanikwake achilia mbali kusafirisha familia. Tunaitaka Serikalikama imeshindwa kulipa haki zao ama iwaachie nyumbaza kiwanda walizokuwa wanaishi ama wauze nyumba hizokwa wafanyakazi hao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vidogo vidogo navya kati- (SMEs). Kwa mwaka wa fedha 2011/2012, sekta yaviwanda na biashara ndogondogo ilichangia takribanasilimia 28 katika pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kwamba katikanchi nyingi zinazoendelea kuna sehemu kubwa ya biashara

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

185

ambayo kwa njia moja au nyingi haikidhi vigezo vya kuifanyakuwa rasmi na hivyo kuingia kwenye mfumo rasmi wauchumi. Kuna kila dalili kuwa hazijafanyika juhudi za kutoshaza kuhamasisha na kutoa mafunzo ya kutosha kwa wahusikaili kuingia kwenye mfumo wa rasmi wa uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na tafitizilizofanywa na “The Tanzania Private Sector Foundation,FinScope na Esaurp” kwa kutumia vigezo tofauti lakiniwalifikia mwafaka kuwa hapa Tanzania kuna kati yaviwanda milioni 2.5 na 3 ambavyo havijarasimishwa(backyard production), lakini vinafanya kazi. Aidha,inakadiriwa kwamba asilimia 48 ya uchumi wa Tanzania upokwenye sekta isiyo rasmi. Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha“Transforming the Informal sector, how to overcome thechallenge” kilichotolewa na taasisi ya ESAURP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa safari zaKamati ya kudumu ya Bunge yenye jukumu la kusimamia sektaya viwanda ilijionea ni jinsi gani viwanda vingi vya raia wakigeni vinavyozalisha bidhaa mbalimbali katika mazingiraambayo sio mwafaka kwa uzalishaji na bidhaa zaozinaingizwa kwenye soko kwa nembo ya made in China auIndia wakati zinazalishwa Tanzania. Kambi Rasmi ya Upinzaniinaamini kabisa hadi Waheshimiwa Wabunge wanapelekwakutembelea maeneo hayo, ni dhahiri Serikali na vyombovyake vya dola inafahamu, hoja ni kwa nini hatuahazichukuliwi ili kuhakikisha Serikali inapata inachostahili namazingira stahili kwa wafanyakazi katika viwanda hivyoyanaboreshwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kitabu hichocha ESAURP kilichonukuu taarifa ya Intergrated Labour ForceSurvey (ILFS) ya mwaka 2006, ulinganisho wa sekta isiyo rasmikati ya mwaka 2001 na mwaka 2006 inaonyesha kuwa watuwalio kwenye sekta isiyo rasmi ilizidi kuongezeka kutoka watu2,013,832 na kufikia watu 3,312,774, ambalo ni ongezeko latakriban asilimia 65 kwa kipindi cha miaka mitano. Watuwengi wanaojihusisha na sekta ndogo ya biashara ya

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

186

wachuuzi ndio wanaoongezeka, sawa na asilimia 57 ya sektanzima isiyorasmi. Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kuelezani kwa nini sekta hii isiyo rasmi inazidi kuwa kubwa wakatibajeti kwa taasisi husika za kuhakikisha urasimishaji washughuli za kiuchumi zinatolewa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi za Fedha naUwezeshaji wa Viwanda. Sekta ya viwanda vidogo nabiashara ndogo kwa mujibu wa taarifa rasmi za Serikali kwaWaheshimiwa Wabunge (Randama ya Wizara), ilichangiatakribani asilimia 28 katika pato la Taifa kwa mwaka wafedha 2012 na kutoa ajira kwa Watanzania milioni 5.2 hukuikihusisha wajasiriamali milioni tatu. Kitabu cha Mpango waMaendeleo ya miaka mitano, uk. 71, unaonyesha kuwa sektaya viwanda kwa mwaka 2011 ilikuwa imeajiri watu 120,000na ilitarajiwa kuajiri jumla ya watu 221,000 ifikapo mwakawa fedha 2015/2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinapenda kupata taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Wazirialieleze Bunge, takwimu za hao Watanzania walioajiriwa nasekta ndogo ya viwanda na biashara zina ukweli kwa kiasigani, kulinganisha na takwimu zilizopo katika Mpango waMaendeleo kama nilivyozinukuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba yaMheshimiwa Waziri kwa mwaka wa fedha 2012/2013 alitoaahadi kuwa Serikali itaanza kulifanyia kazi eneo hili na kutoamapendekezo ya kuboresha mchakato wa ujenzi waviwanda katika uchumi wetu. Nchi zote zilizofikia hadhi yanchi za kipato cha kati zimekuwa zikitekeleza na kuzingatiamikakati ya jinsi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ahadi hiyo yaMheshimiwa Waziri inaonyesha dhahiri kuwa Serikali hainampango wa kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa ambapowahusika walishindwa kutimiza/walivunja masharti aumatakwa ya mkataba au kufufua viwanda visivyofanya kazi.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza Bunge hadi

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

187

sasa viwanda vilivyobinafsishwa kama vile vinavyojihusishana uchakataji wa mazao ya kilimo hasa korosho, pamba namatunda ikoje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwekezaji katika viwandavipya hapa kwetu, hasa kwa Watanzania ni kazi ngumu sanakutokana na ukweli kwamba, sekta ya benki bado haijakuakiasi cha kufanya uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu.Hivyo ingekuwa ni bora zaidi kwa viwanda vilivyokuwepokuvifanyia ukarabati wa kuondoa mashine ambazozimepitwa na wakati kiteknolojia na kuweka mashine/mitambo mipya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitendo chochote chauanzishaji wa viwanda ambacho hakitahusisha umiliki wawananchi, ni dhahiri kuwa kosa lililofanyika wakati wauanzishwaji wa Mashirika ya Umma ambayo hatimaye ilikujasera ya ubinafsishwaji litakuja kujirudia na hapo ndipo uhalaliwa uwepo wa Serikali ileile utaanza kuhojiwa, “kutenda kosasi kosa bali kosa ni kurudia kosa”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Randamaya Wizara kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ilieleza kwambaSerikali ililenga kuongeza mtaji wa shilingi bilioni 500 kwa TIBkatika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2010 na hadi mwakawa fedha 2012/2013, Serikali ilikuwa imeweka shilingi bilioni60. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza Bungena wananchi, je, hizo shilingi bilioni 500 ni kwa ajili yauanzishwaji wa viwanda tu au ndio fedha hizo kwa ajili yauwekezaji katika sekta mbalimbali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa MkakatiUnganishi na Mpango Kabambe wa Sekta ya Viwanda(Integrated Industrial Development Strategy and Master Plan)unalenga Mwambao wa Pwani kuwa Kitovu cha KuendelezaViwanda na Kukuza Mauzo Nje (Water Front Industrial andExport Frontiers). Mkakati huo unalenga kufanya usindikaji wamwanzo (primary processing) Mikoani, usindikaji wa kati nausindikaji kwa ajili ya mauzo nje kufanyika katika maeneo ya

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

188

Mwambao wa Pwani ambao utakuwa kitovu chakuendeleza viwanda na kukuza mauzo nje. Kambi Rasmi yaUpinzani inaona dhana hii inaweza kuwa na mapungufukutokana na ukweli kwamba viwanda vya usindikaji wamwanzo vinatakiwa viwekwe maeneo ya uzalishaji na kilakona ya Tanzania kuna uzalishaji wa zao moja muhimuambalo ni tofauti na eneo lingine, hivyo kuweka viwandahivyo katika ukanda wa Mwambao wa Pwani ni kosa lakiufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masoko. Ukubwa au udogowa soko una mahusiano ya moja kwa moja na tija katikauzalishaji viwandani. Kwa mahusiano haya ya soko nauanzishwaji wa viwanda na ukuaji wa uchumi yana athariza moja kwa moja katika uwekezaji katika sekta ya viwanda.Kwa nchi inayohitaji kujikamua katika lindi la umaskinikuanzisha viwanda bila ya kuwepo kwa mkakati makini wakuhakikisha kuwa bidhaa zitakazozalishwa zinapata sokoinaweza kuwa ni msingi wa kuua viwanda hivyo kutokanana ushindani wa bidhaa ambazo tayari ziko sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vingi nchiniTanzania vinazalisha kwa ajili ya soko la ndani na wastaniwa asilimia 22.6 ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetundizo zinazouzwa katika masoko ya nje ya nchi na mauzoya bidhaa nje ya nchi yanajumuisha tumbaku, bidhaa zakaratasi, nguo na vyakula vilivyosindikwa. Bado viwandavingi vya Tanzania havijatoa msukumo wa kutosha katikakutangaza bidhaa zake na kutumia vizuri fursa za masokoya kikanda. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulielezaBunge ni mkakati gani wa makusudi imeuweka ili bidhaa zaviwanda vyetu hasa vile vidogo na vya kati viweze kupatamasoko nje ya nchi? Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuweka hadharani aina ya bidhaa zitakazozalishwana masoko yake ili tathmini ya uanzishwaji huo ifanyikevyema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.(Makofi)

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

189

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Kiwia.Sasa Waheshimiwa Wabunge tuna wachangiaji sita natunaanza na Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina naMheshimiwa Said Mussa Zubeir ajiandae.

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaMwenyekiti, ninashukuru kwa kuniona. Nianze kwa kuungamkono hoja na kwa kweli hotuba ya Waziri imeletamatumaini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati ninachangia hotubaya Waziri wa Viwanda na Biashara mwaka juzi, nilizungumzakwa masikitiko makubwa sana nikieleza jinsi viwanda vyetuvilivyouwawa kutokana na Sera ya wakubwa wawili ambaowote sasa hivi ni marehemu. Marehemu Ronald Reaganaliyekuwa Rais wa Marekani pamoja na Magreth Thatcherakiyekuwa Waziri Mkuu. Wao walikuja na Sera ya sekta binafsikuwa mhimili wa uchumi na wakasema kuwa sekta ya Ummahaifai. Kwa hiyo, baada ya hapo tukaanza kuuza viwandavyetu kwa bei powa na kwa wawekezajia ambao wenginewalikuwa ni matapeli na hawakuweza kuendeleza viwandahivyo na wakageuza hata matumizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niliwahi kusimamiaviwanda vyote na Mashirika yote kwa miaka sita kuanzia1986-1991, nimekuwa nikisononeka sana na hata ilipokujaDira yetu ya Maendeleo (Vision 2025) kwamba ifikapo mwaka2025 tutakuwa ni nchi yenye uchumi wa kati na yenyeviwanda vingi, mimi niliendelea kuwa pessimistic, nilionakuwa haiwezekani kwa sababu viwanda vingi vimeuwawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikiri kwamba baadaya kufanya utafiti na kuzungumza na watu wa NDC na kujuakazi nzuri inayofanywa na NDC na imeelezwa hata katikahotuba ya Mheshimiwa Waziri, nimeanza kuwa na matumainikuwa ifikapo mwaka 2025, tunaweza kuwa na viwanda vingi.NDC tumeambiwa ifikapo mwaka 2016 itakuwaimeshaanzisha kiwanda cha Soda Ash, Chuma cha Liganga

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

190

pamoja na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma wameshapatamwekezaji, Makaa ya Mawe ya Ngaka wanaendelea vizurina wanaweza ku-export. Nimefurahi kuwa NDCwamekabidhiwa General Tyre na watazalisha sasa matairiyenye uhakika, pia NDC wamekabidhiwa wafufue ileKilimanjaro Machine Tools, wamekabidhiwa mambo mengina wanafanya kazi nzuri, nimezungumza nao nawanasimamia ile Wind Power ya Singida lakini nimesikitikakuwa hawawezi kufufua kiwanda cha Mangula MechanicalMachine Tools kwa sababu mitambo yake ilishauzwa na mtummoja anakabidhiwa aanzishe shule, hiyo imenisikitisha sanaingawa nimemsikia Waziri anasema watafufua Kiwanda chaMungula nitashukuru sana kama itakuwa hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru MheshimiwaRais kwa kuihimiza NDC ifufue viwanda vya nguo.Wameagizwa na Rais wafufue viwanda vya nguo nawatasaidia pia kuanzisha viwanda vya Agri-business au Agro-industries ili kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali,naomba sana UFI, Ubungo Farm Impliments iliuzwa kwa mtuambaye aligeuza matumizi, anazalisha mambomba lakinihatuwezi kuendelea bila kuwa na kiwanda kinachozalishazana za kilimo. Naomba tuanzishe kiwanda cha aina yaUbungo Farm Impliments na tufufue kiwanda cha Mangula.Naiomba Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara yaMaji, waharakishe miundombinu ya umeme na maji ilikusaidia viwanda hivi ambavyo vinaanzishwa kwa harakaili tuweze kuwa nchi yenye viwanda vingi ifikapo 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye SIDO, SIDO ndiyotegemeo la wananchi wa kawaida. Naiomba Serikali isaidieSIDO waeneze viwanda vidogo, Ngara, Kibondo, Panganina kila mahali. Tutaweza kufaidika na viwanda vya SIDOiwapo tutapata umeme wa gridi huko vijijini. Kwa hiyo, Serikalini moja wafanye kazi hiyo. (Makofi)

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

191

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie TBS. TBS haifanyikazi yake vizuri. Tumeona majengo yanavyoporomokakutokana na uhafifu wa vifaa vya ujenzi lakini mnavyoonamajengo yanaporomoka hivyohivyo ndivyo watu wavyokufakutokana na vyakula vya ajabu vinavyokuwa imported. Sikuhizi hata watoto wadogo wanapata kisukari, wanakuwahigh pertensive, shauri ya hivyo vyakula kutoka nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye suala la sera yauzawa. Mimi kama senior citizen ni lazima nisisitize sera yauzawa. Tumejifunza kutoka Malaysia mbinu ya kusimamiautekelezaji wa miradi muhimu, inaitwa Big Results Now au ilePresidential Delivery Bureau. Tumejifunza, hicho ni kitu kizurilakini ngoja niwakumbushe kwamba kama tumejifunza hivyotujue kwamba Malyasia ilivyo sasa ni kutokana na sera yaoya uzawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye miaka ya themanini,Waziri Mkuu aliyekuwepo Mahadhir Muhammad aliwaelezaWachina waliokuwa wanamiliki uchumi wa Malaysia,akawaambia kwamba tusipowashirikisha wazawa waMalyasia, indigenous Malays, watawachinja. Baada ya hapo,wakaanzisha sera za upendeleo na sasa hivi wazawa waMalaysia wanashindana kibiashara pamoja na Wachinaambao sasa hivi wazawa wameinuliwa sana kiuchumi. HiliBaraza la Uwezeshaji ni kitu kidogo sana, wanasaidia VICOBA,wanasaidia SACCOS, sisi tunataka tuwe na akina Mengiwengi, tuweze kumiliki uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati najifunza mambo yaMarxism-Leninism, nilipenda sana dhana ya superstructureversus economic base. Sisi Watanzania wazawa tupo kwenyesiasa tu, we are not in control ya economic base. Kwa hiyo,ni lazima tufikie huo wakati ambao tunakuwa kwenyeeconomic base. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka sana kablasijaishiwa na muda, kabla sijaenda Ngara, namkumbukaaliyekuwa Waziri wa Viwanda, Iddi Simba. Mheshimiwa Iddi

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

192

Simba alifanya kazi nzuri sana ya uzawa. Aliorodheshabiashara ndogondogo ambazo zinatakiwa zifanywe nawazawa lakini sasa hivi zinafanywa na Wachina na Wakoreakule Kariakoo. Ni lazima sasa tuwafikirie wazawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nchi kama Ethiopia,mimi nimekaa Ethiopia miaka kumi nikiwa consultantkwenye African Union, yale majengo yote na viwanda vyoteni vya Wahabeshi. Kenya pia…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa!

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: Ooh myGoodness!

MWENYEKITI: Muda wako umekwisha.

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: Sijazungumziasuala la Ngara.

MWENYEKITI: Sasa ni zamu ya Mheshimiwa Said MussaZubeir.

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nami nimshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi warehema na mwenye kurehemu, kwa kunipa nafasi hii leoasubuhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kwakumpongeza Waziri i la nasikitika kwamba Wizara hiihaikutendewa haki, Wizara hii ni kubwa tofauti na mudailiyopewa. Mimi ninasema imepewa nusu siku, maana yakehata siku haijatimia, sasa hivi saa sita, ikifika saa sabatunakwenda lunch tukirudi Waziri anakuja ku-wind up. HiiWizara ni kubwa, tunapozungumzia viwanda na kamatunahitaji maendeleo ya nchi hii yapo kwenye viwanda.

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

193

Kama watazungumza watu wanne na nina hakika Wabungewengi wanataka kuongea, sidhani kama tutafikia mahali.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee haraka harakakuhusu suala la fedha za maendeleo za bajeti iliyopita. Leotunazungumzia bajeti ya mwaka 2013/2014, mimi nirudimwaka 2012/13. Fedha za ndani za maendeleo, hapapanashangaza sana na inabidi mtu ufike mahali ujiulizemaswali mengi. Hivi are we serious? Ni lazima tujiulize kwelisisi tuna uhakika wa tunachokizungumza kwambatutakifanya na kitakuwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za ndani ziliidhinishwana nilifurahi sana kwa sababu zilikuwa zinatosheleza, karibushilingi bilioni 123 kwa ajili ya maendeleo kwenye Wizara hii.Ukiziangalia fedha zenyewe zilikuwa zinaelekea kwenyemaeneo mawili muhimu au matatu lakini moja unawezaukasema kwamba linaweza likasubiri. Ukiangalia katikamaeneo hayo mawili muhimu yaliyokusudiwa hizi fedhaziende, mpaka leo tunazungumza kwamba hiyo bajetiambayo ndiyo tunaipa mgongo, kulikuwa na minitigerambayo ilikuwa imetengewa shilingi bilioni 50.2 katika hizoshilingi bilioni 123. Kulikuwa na Logistic Center Tanzania andChina, wao vilevile walikuwa wanahitaji shilingi bilioni sitini.Cha kushangaza au jambo la kutia aibu ni kwamba mpakahivi leo, hawa wengine wamepewa shilingi bilioni 10.9, hawawengine unaweza ukasema wamepewa shilingi milioni miatano hamsini na tano Watanzania wakasikia wamepatakasoro labda shilingi bilioni tano kumbe siyo shilingi bilioni nishilingi milioni mia tano yaani nusu bilioni. Leo tunamalizamwaka hakuna chochote kilichotendeka, hivi kweli tunahitajimabadiliko ya nchi hii? Hili ni swali tunatakiwa tukae tujiulize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni afadhali tuwe na jambomoja la kufanya kuliko ku-disperse pesa ambapo baadayekunakuwa hakuna kitu chochote kilichofanyika, kama viletuna mark time. Hili halitusaidii kugeuza Bunge hili kama labdanyumba ya Ibada, kwa sababu nyumba ya Ibada ndiyo watu

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

194

hukaa wakagawana sadaka. Sadaka ile inaweza isimsaidiemtu kushiba wala kumwondoshea hamu, ndivyo tunavyofanya lakini ni afadhali tukatenga fedha kidogo lakinitukahakikisha kwamba hizi fedha zimefikia mahali…

TAARIFA

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa!

MWENYEKITI: Nimekuona Mheshimiwa Ester Bulaya.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nilikuwa nataka nimpe taarifa mchangiaji kwamba nyumbaya Ibada huwa hawagawani sadaka. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa endelea.

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesikia, inawezekana ya kwake yeye, ya kwetu sisitunagawana sadaka na aghalabu hupata waumini wotena pengine isisaidie chochote ikawa mtu kapata tu sadaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata leo memokwamba kuna uwezekano wa kupelekwa shilingi bilioni 25.Namshukuru Waziri wa Fedha kwa kufanya utaratibu huuharaka lakini bado ninasema tumechelewa. Katika shilingibilioni 25 hizi ningeomba basi zielekezwe upande mmojaangalau zipelekwe kwenye Logistic Center ambapo badozitakuwa hazijafanya kazi, tunahitaji zingine karibuni shilingibil ioni 35, sasa Waziri atakapokuja ku-wind up hi l iatatuelezaje? Tufanye kitu kimoja kikamilike kulikokuzitawanya na hizi shilingi bilioni 25 ambazo tunasikia leoimefanyika transaction na zitakuwa zimeingia Wizarani.Naipongeza Serikali kwa hili lakini nauliza, je, shilingi bilioni35 zitakwenda kwa muda gain?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati hapa mbeleyangu, nimepokea marekebisho kuna fedha ambazozinategemewa kwenda na zitakuja kwenye Appropriation

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

195

Bill mwezi wa Saba. Ni sahihi, zikiongezwa hizi, bado piatutakuwa hatujafikia mahali maana yake 25 na zile 550ukiongeza na hizi 31 ambayo moja ndiyo tulikuwa tunakujanayo kwenye bajeti hii, ndiyo kwanza hizo sitini hazijatimia,tupo kwenye 56, hatujafikia hata sitini. Yote tisa, kumi hatahizo sitini sasa hivi siyo sitini tena sasa hivi zipo 94. Sijuiatakapokuja Waziri atatuthibishiaje kwamba tusije tukawatuna dump na hizi sasa halafu tukakaa miaka miwili kujakutafuta hizo 34 zitakazokuwa zimebaki au karibuni 40hazitakuwa tena 34 zitakuwa tena ni mia moja. Sisi kazi yetuitakuwa ni ku-mark time tu. Ninaomba sana kama kwelitunataka kuwasaidia vijana karibu elfu ishirini na tano kuwezakupata ajira kwenye Logistic Centre hili suala lifanyike harakasana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi si ajira za watu 25,000 niajira karibu za watu laki moja mpaka laki mbili. Kivipi? Ajiraya moja kwa moja ni watu 25,000 lakini hili jengo kwanzawale Wachina pale wao watawekeza karibuni shilingi bilioni600, ni fedha nyingi sana. Wakiwekeza pale chochotekitakachotokea kile kitega uchumi kitakuwa bado kipoTanzania kitatusaidia tu. Hii ni faida ya kwanza. Faida ya pilitutatoa ajira nyingine zitakazokuja ambazo zitakuwa niindirect ni nyingi tu. Kuna hotel ambazo zitapata watu wengisana kwa sababu watu watakuja, kwa sababu hii itakuwani kitovu katika Afrika, hii itakuwa ni sehemu kubwa sanakatika Tanzania yetu na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili tunalozungumza ni sahihikuna ajira ambazo sisi hatujaziona, hizi za indirect ni nyingisana zitakazojitokeza, kuanzia mahoteli, magari hatauwanja wa ndege kwa sababu watakuwa wanamiminika,hawa watakoleta hizi bidhaa na watakaokuja kufuata hizibidhaa pamoja na Tanzania yenyewe kunufaika. Tanzaniaitanufaika vipi? Ni lazima tutakapokuwa na ukubwa wainvestment kama hii, viwanda vitapanuka automatic kwasababu kuna bidhaa ambazo zitakuwa zinahitajika, kwa hiyokuna viwanda ambavyo havipo sasa hivi vitakuwepo.

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

196

Tutakuwa tuna uhakika wa soko kwamba tunalo hapahapa.Hata malalamiko ya watu wa korosho, watu wa pambahaya yote yataondoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeomba Serikaliijitahidi sana na hili suala…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Said Mussa,sasa namwita Mheshimiwa Msigwa ajiandae MheshimiwaEustace Katagira.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba nisiwe mbalina mchangiaji aliyepita kuhusiana na muda mfupi ambaotumepewa kama Wabunge kuijadili Wizara hii ambayokimsingi ni Wizara nyeti, ni Wizara muhimu kwa ukuaji wauchumi wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna idadi kubwa sana yawatu ambao hawajaajiriwa, watu ambao hawana kazi,watu ambao hawawezi kujikimu. Kwa hiyo, naomba sijui niWaziri au Bunge, kwa kweli next time tusingefurahi sanakupewa muda mfupi wa watu wachache wachachekuchangia, ninaamini Wabunge wana mawazo mengi sana,hata wale watu wa Kamati wana mawazo mazuri sanaambayo yangesaidia kuiboresha Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema Taifa letu linawatu wengi sana ambao hawajaajiriwa na sera mbovuzimetufikisha hapa tulipofika. Ukiangalia mikataba ambayoSerikali ilikuwa imesaini au ilikuwa imejiandaa katika MKUKUTAI, ni kwa kukubaliana na masharti ya wafadhili wa nje ambaowlaiitaka Serikali isifanye production, ifanye service tu. Kwa

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

197

hiyo, matokeo yake viwanda vingi vikawa vimekufa, watuwaliopewa umiliki wa viwanda hivyo wamejikutawanageuza yanakuwa magodauni na idadi kubwa yawananchi hasa vijana wamekosa ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamheshimu sanaMheshimiwa Waziri na nina uhakika kabisa na weledi wako.Naamini kwamba Wizara hii unaweza ukai-transform. Kunamsemo mmoja wanasema if the only tool you have in yourhands is a hummer you tend to treat every problem as a nail.Kama kifaa pekee ulichonacho mkononi mwako ni nyundo,utafikiri matatizo yote ni msumari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivi?Napenda nijikite kwenye eneo la Wamachinga ambao wapowengi katika Taifa letu hususani hata katika Manispaa yanguya Iringa Mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wamachinga wamekuwawanapuuzwa, Wamachinga wamekuwa wakidharauliwa nakwenye hotuba yako kidogo umezungumzia kuhusu biasharandogo. Ni idadi kubwa sana ya wananchi wa Tanzania hawawatu ambao ni voiceless, hawa watu ambao ni maskini,ambayo ni unprivileged, lakini kila mahali wanafukuzwakama digidigi kwenye nchi yao wenyewe. Nchi ambayo tunawatu ambao wana weledi wanaweza wakakaa, wakafikirinamna gani ya kutatua tatizo la Wamachinga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jamii yetuWamachinga wameonekana ni watu ambao wanaletakero, hasa kwa viongozi wanasiasa na wafanyabisharawakubwa. Wanaonekana wanatutinga katika maisha yetu,wanatuvuruga, hatujakaa chini kama Taifa kuona ni namnagani tutatue tatizo la Wamachinga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Polisi wamekuwawakitumika kuwapiga Wamachinga. Kwa bahati mbayaSerikali iliyoko madarakani inadhani kutatua matatizotunayokabiliana nayo ni kupiga watu virungu. Likitokea tatizo

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

198

la Wamachinga wanapigwa, maandamano wanapigwa,as if tool tuliyonayo ni nyundo tu. Fundi mzuri ana vifaambalimbali, kuna sehemu unahitaji sellotape, sehemunyingine unahitaji bisibisi, sehemu nyingine unahitaji waya,lakini solution ya kuwapiga tu hawa watu, tunawaonea.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hili kwa uchungumkubwa sana na ninataka ni-site eneo la Iringa ambakotumekuwa na matatizo ya Wamachinga na Tanzania nzima,kwa nini hatuna model ambayo itatusaidia wananchi woteTanzania tuepukane na tatizo hili, tukakaa chini kutatua tatizohili badala ya kuona ni kero. Suala la Wamachinga halikoTanzania tu, tumeona Wamachinga wanatengewa maeneoUlaya, ukienda Marekani, ukienda South Afrika kule nimekaaDurban miaka mitano, Johannesburg, Cape Town, kunamitaa inafungwa Wamachinga wanafanyakazi zao vizuri nawanapata chakula. Hawa ni watu maskini kabisa wa chini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wanasiasa wote tuwewakweli katika maisha yetu, tunawatumia sana vijana hawawakati wa kura, we just using them kama stepping stone.Nitoe mfano mmoja, mimi nilikuwa sina hela wakati wakampeni, akina mama wanaouza ndizi walikuwa na imanina mimi, vijana ambao ni Machinga wanauza soksi kunamwingine mpaka alinipa zawadi ya soksi, mama alinipa ndiziakasema Msigwa nina imani na wewe, naomba ukatuteteetunanyanyasika. Huyu mama alikuwa mjamzito kwenyeJimbo langu, akasema mtoto huyu nikijifungua kwa sababunaamini utashinda nitampa jina la Peter Msigwa au jina lamke wako Victoria. Alipojifungua yule mama amempa jinayule mtoto anaitwa Peter Junior lakini yule mamaanakimbizwa kama swala kwenye nchi yake mwenyewe.Mtaa mmoja unaweza ukafunguwa kwa siku moja yaJumapili watu wakafanya biashara zao, wakafanya usafi nauchumi wetu ukakua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri kwamba ni kipindi kimefika sasa, Leaders are problems

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

199

solvers, ni solution gani tunayo-offer? Naomba katika majibuyako nijue solution gani tunayo-offer kwa ajili ya kutatua tatizohil i la Wamachinga ambalo ni kubwa. Ni kwa niniWamachinga wa Mwanza wanaweza wakakaa na Mkuuwa Mkoa Mwanza Hotel, wakala naye chakula halafuwamachinga wa Iringa wakakimbizwa na Polisi. Kwa niniPolisi watumike kuwapiga Wamachinga wakati siyo kazi yao,mpaka nao wa-riot ndiyo Mkuu wa Mkoa anawaita.Nasikitika kitendo cha juzi Iringa, Mkuu wa Mkoa, Mkuu waWilaya, Meya wamekusanyika wamewa-deploy Polisi kutokaMafinga wamejazana wanawapiga vijana ambao hawanahatia, siyo majambazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Waziri, suala hilihalipo Mkoa wa Iringa tu, kwa nini tusichukue mifano yaMwanza, tusichukue mifano ya Mbeya, tuchukue mifano yaMoshi tukahakikisha tunairasimisha sekta hii, hawa watuwaishi vizuri katika nchi yao, tuwatafutie utaratibu mzuri wakuondokana kero hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema tusipokuwamakini, haya matatizo ya kuzalisha watu ambao hawanaajira ni kutokana na mipango mibovu ya MKUKUTA I ambayoimefeli. Sasa hivi tumekuja na neno lingine tena tunasemaBig Results Now, lakini tusipokuwa waangalifu, yatakuwa nimaneno maana tuna Mpango wa Miaka Mitano, tuna BigResult Now, tuna Kilimo Kwanza, tuna MKUKUTA vyotevinashindikana, tunakuja na maneno. Ninaomba tujipangevizuri, tutafute solution, leaders are problem solvers.Changamoto zitakuja tu kama Taifa, lakini badala yakujipanga vizuri, kutumia Polisi kila wakati Police brutality,tunawafanya vijana hawa wachukie Serikali yao.Tunatengeneza Taifa lenye chuki, tunatengeneza watuwazoeane na mabomu ya Polisi bila sababu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba MheshimiwaWaziri, nina imani na wewe, ni mtu mwenye busara, ni mtuambaye ni hazina katika Taifa letu, wewe kama wewe lakinisiyo Chama chako. Una hazina kubwa, ninaamini hili suala

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

200

likikaa kwako, utalijadili vizuri, tukae pamoja mezanitujadiliane tuliondoe tatizo la Wamachinga. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa quotation yaJim Rohn anasema; Don’t wish it were easier; wish you werebetter. Kama Viongozi tutapata changamoto kubwa lakinihebu tukae katika position nzuri. Anamalizia kwa kusema,don’t wish for less problems; wish for more skills. NaiombaWizara yako itafute skills nyingi tofauti ambazo hata upandewa pili huku ziko, tukae pamoja, tutoe mawazo yetu, tutatuetatizo hili la Wamachinga ambalo kimsingi linaua Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri katika majumuisho yake aelezee suala hil i laWamachanga. Mimi sitaunga mkono hoja hii mpaka kwanzaWaziri aniambie suala la Wamachinga litatatuliwa namnagani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Nashukuru. Sasa namwita MheshimiwaEustace Katagira na Mheshimiwa Nimrod Mkono ajiandae.

MHE. EUSTACE O. KATAGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kuniruhusu na mimi nichangie katika hojahii ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitangulie kusema kwambaWaziri ambaye ni hazina katika nchi, anatokana na Chamaambacho ni hazina katika nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la usafirishajiwa mazao ya kilimo nje ya nchi. Nitangulie kwa kusemakwamba mimi ni mdau katika usafirishaji wa mazao ya kilimonje ya nchi hususani kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii katika nchi zoteambazo zinahitaji maendeleo, mtu au shirika ambalolinasafirisha mazao nje yaani exporter, huwa wanaangaliwa

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

201

kwa jicho zuri kabisa. Huwa wanaonekana kwamba ni watuau ni jamii au kampuni ambayo inaleta na kujenga uchumiwa nchi. Inaingiza pesa za kigeni katika nchi na inasaidiakatika kuendeleza nchi kwelikweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nidiriki kusema kwamba leohii kama utajaribu kusafirisha kahawa nje ya nchi, umetafutasoko, unataka kwenda kuuza nje ya nchi, zao ni la wakulima,hutaweza kusafirisha kahawa hiyo mpaka umelipa ushuruambao unaitwa export permit fee. Ninachotaka kuelezahapa, hii export permit fee siyo kusema kwamba ni leseni yakawaida, unakuwa umeshakata leseni ya kawaida yakusafirisha zao la mwananchi, zao la mkulima, lakini kwakilo ambayo unataka kuisafirisha kuipeleka nje kuiuza kwaniaba ya mkulima, itabidi kila kilo uilipie kitu kinaitwa exportpermit fee na kama kweli hujalipa hiyo export permit fee,kahawa yako haitatoka bandarini kwenda kwa mnunuzi nchiza nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninapendekezakwamba hii charge kwa mkulima isiwepo, iondolewe.Nasema hivyo kwa sababu mnaweza mkafikiria kwamba hiini pesa ndogo, hii siyo ndogo. Katika mwaka huu kwa mfano,wakulima wa Wilaya mbili za Kyerwa na Karagwe wamelipasi chini ya shilingi milioni 200 kama export permit fee yakupeleka zao kwenda kuuzwa katika masoko ya nje. Mkulimawa kahawa anakuwa ameshapata makato makubwamengine, ameshalipa levy, ameshalipa ushuru wa utafiti namakato mengine. Kwa hiyo, mimi nadhani hii pesaingemrudia akaweza kumaliza mahitaji yake ya kawaida,kama kusomesha watoto, kama kuchangia maendeleokatika Wilaya yake na katika Kijiji chake. Naomba waunganeMheshimiwa Waziri wa Biashara na Viwanda na MheshimiwaWaziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wahakikishe kwambahii kitu ya export permit fee mkulima anaondolewa naanaweza kubaki nayo imsaidie katika shughuli zake zakuendesha maisha na kuchangia maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sina shida naninatambua kazi nzuri inayofanywa na Bodi za Mazao kama

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

202

Bodi ya Kahawa lakini ni muhimu mkulima aangaliwe vizurilakini pia aweze kupata pesa inayomfaa ambayo inakuwafaraja kwake, ambayo itamfanya aweze kuendelea kupatamapato mazuri tusije tukaingia katika matatizo waliyonayoZone ya Korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siongelei Wilaya ya Kyerwana Wilaya ya Karagwe peke yake, naongelea Kagera nzima,naongelea Kigoma, naongelea Mara naongelea wakulimawote wa zao la kahawa ambalo linauzwa nchi za nje.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda. MheshimiwaWaziri amekuja na maneno mazuri leo akiongelea viwandaambavyo vitaanzishwa, viwanda vya saruji, viwanda vyakusindika mafuta lakini nazidi kusisitiza kwamba ni muhimutuangalie jinsi mwananchi atakavyo-participate katikamtiririko huu wa uanzishwaji viwanda. Isije wakaja wagenipeke yao wakaanzisha viwanda, kama ilivyokwishaelezwa,lakini na wananchi waweze ku-participate, mwisho wa sikuna wananchi waweze kusema tuko katika nchi yetu na sisitumo katika mtiririko wa maendeleo yanayojitokeza katikasekta ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziriameongelea habari ya financing ambayo itapatikana. Hiiipatikane kwa ajili ya wananchi na wenyewe kuwa wabiana ku-participate katika sekta ya viwanda. Zipatikane softloans lakini pia zenye riba pungufu, nikimaanisha kwambahiyo 5% ambayo itakuwa inasaidia katika kulainisha gharamaya financing kwa wananchi wanao-participate katikaviwanda, haitatosha. Kwa sababu bado kutakuwa kunariba kubwa ya kubeba katika uendelezaji wa viwanda.Ningependekeza kwamba hiyo riba ipungue zaidi yamsamaha wa five percent peke yake. Pia, hizi soft loans ziwena grace period ambayo ni nzuri ya kusaidia wananchiwaweze ku-participate wenyewe mwisho wa siku wasemekwamba tumo katika nchi yetu. Tunakwenda pamoja namabadiliko yanayotekea na tunaweza mwisho wa sikutukasema kwamba na sisi tumefaidika. (Makofi)

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

203

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuasa MheshimiwaWaziri, ahakikishe kwamba pesa hizo kwenye dirisha maalum,zisije zikawa ni maneno na maandishi peke yake lakinizikachomolewa zikaenda katika maeneo mengine. Zikaendakujenga maghorofa ya kupangisha, zikaenda kwenyemaeneo mengine ambayo siyo intended kwa shughuli hiyo.Nawaasa wenzangu hata Wakaguzi wa Mfuko huo, wawewanahakikisha mwisho wa siku kwamba pamoja na mengineyote ambayo wanayakagua na kuyaangalia na kuyatoleataarifa, waseme pia wamekagua hizo funds, hizo financingsna kwamba zimetumika jinsi zi l ivyopangwa na jinsiilivyotarajiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara na nchi jirani. Yakomasoko yanapangwa kujengwa katika maeneo ya mpakanihususan kule kwangu katika eneo la Murongo na katika eneola Nkwenda. Tunaomba na ninapendekeza na ninashaurimasoko haya yajengwe haraka, yasibaki kwenye michoro,yasibaki kwenye karatasi yasibaki kwenye maneno iliwananchi waweze kuyatumia na waweze kuweka ushindanina nchi jirani ambao tunafanya biashara nao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazidi kupendekezakwamba hapo kwenye masoko haya ya mpakani na ambayosasa hivi yako, Serikali ihakikishe kwamba zile sera za ushuru,zile sera za malipo pale mpakani ziwekwe wazi kabisa.Nachotaka kumaanisha...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa nashukuru, ni kengele yakoya pili.

MHE. EUSTACE O. KATAGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa namwita Mheshimiwa NimrodMkono na Mheshimiwa Asaa Hamad ajiandae.

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

204

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii Wizara ina matatizomakubwa mno. Wizara ya Viwanda na Biashara. Naanzakwa kusema kwa nini kuna matatizo ndani ya Wizara hii.Nini maana ya biashara? Utakuwa na kiwanda lakinikiwanda chako ni lazima kizalishe mali ambayo inauzika.Anayepima kwamba mali inauzika ni kwamba unasajili,unapata cheti cha kuonyesha kwamba hizi bidhaa zakozinaweza kuuzika na zinafaa. Ndani ya Wizara hii kuna Kitengomaalum kinaitwa BRELA. BRELA ilianzishwa mwaka 1999 nasababu ya kuanzishwa kwake ilikuwa ni kuhakikisha kwambakazi inakwenda haraka iwezekanavyo. Ofisi yao iko paleLumumba lakini hata kiti cha kukaa hakuna. Mafailiyamepangwa mpaka kwenye choo kuna faili pale. Hiyo ndiyoBRELA iliyoko pale. Wanafanya nini? Wanasajili Hatimiliki zaalama za biashara yaani trade mark and service mark. BRELAinasajili alama za patents au mnaita hataza, yaani siku hiziKiswahili patents inaitwa hataza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni member waAfrica Region Industrial Property Office ambayo iko Harare.Nadhani nchi za Afrika zinafanya muungano kwambawashirikiane katika kusajili hizi Hatimiliki ama patent and trademark services, wana common registration. Sheria hii, ingawasisi ni members mpaka sasa hatushiriki, hiyo ni Wizara yaViwanda na Biashara. Sasa mwekezaji anakuja kuwekezahapa, azalishe mali, aziuze hapa na pia azipeleke nje ya nchi.Kama bidhaa hizi hazifai ama ni inferior ama ni feki, hawezikupata ushindani maalum au ushindani bora. Maanamwekezaji atakuwa anaogopa nikiwekeza Tanzania, kulehawalindi mali ama hawalindi bidhaa hizi na kuna nyingiambazo ni feki zinauzwa mitaani, je, anaweza kuwekezanchini ama la? Mimi nasema haiwezekani mpaka kuwe kunalevel plain field. Wenzetu Kenya wana registry nzuri ambayoinafanya kazi, wenzetu Burundi wanayo, Tanzania hapana,ofisi imeoza. Ushauri wangu ni nini? Nasema tufumue BRELA,fumua upya kabisa, leta wataalamm waunde chomboambacho kinafanya kazi kuweza kusaidia hapa Tanzania

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

205

tupate uwekezaji unaofaa vinginevyo hatuwezi kuingiakwenye ushindani unaofanya kazi. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kwamba kamaumepata production, ni muda gani inakuchukua wewekufanya registration ya patent kwa mfano, ama servicemark? Nchi jirani zinachukua miezi mitatu, hapa inachukuamiaka miwili ama miaka mitatu kusajili patent moja. Hiiregistry inafanya kazi ama ni usanii uko pale? Nataka nipatemajibu, vinginevyo sitaunga mkono hoja hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, kama kuna ushindanilabda trade mark yako iko-infringed, unapeleka maombiyako kwamba upate usuluhishi ama uende Mahakamani,inakuchukua muda gani kufanya hivyo. Utakuta ndani yaWizara ya Viwanda na Biashara, Kitengo hiki kiko very weak,hakifanyi kazi. Vijana wanaofanya kazi pale, wako chini yahamsini, ni wachache sana lakini alama zinazokujakuandikishwa pale ni maelfu na maelfu ya alama, kwa hiyo,inachukua mwaka mzima ama miaka mitatu kusajili, tutafikawapi katika ushindani wa leo? Ushauri wangu, vunja Kitengocha BRELA kiundwe upya ili kitoe huduma ambacho kilitakiwakifanye vinginevyo haina maana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mengi ya kusemamaana mambo mengi nimeyasema kwa maandishi.Naomba usome kwa karibu kabisa uone ni jinsi gani yakujinasua na tatizo tulilonalo katika Wizara ya Viwanda naBiashara. Ahsante sana. Siungi mkono mpaka nipate jibu lamsingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Mkono.Sasa namwita Mheshimiwa Asaa Othman Hamad naajiandaye Mheshimiwa Dkt. Augustine Mrema.

MHE. ASAA OTHMAN HAMAD: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Baada ya kumshukuru MwenyeziMungu, nianze kwa kusema kwamba uwezo wa MwenyeziMungu ni mkubwa na tumwombe Mwenyezi Mungu asijeakamrejesha Baba wa Taifa leo akaja akatuona hivi tulivyo.(Makofi)

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

206

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baba wa Taifa katuachiarasilimali ya viwanda ndani ya Tanzania na alifanya hivyokwa kuamini kwamba Mtanzania ataweza kukombokakiuchumi kwa kupitia rasilimali hii ya viwanda. Sekta yaviwanda miaka ya 1970, 1978, 1979, Tanzania ilikuwa kwenyechati ya dunia kwa nchi zinazoendelea. Leo tukiitazamaBUKOP, TANICA Kagera, Tanga, Dar es Salaam, Mwanza,Morogoro na kwingineko, Watanzania wako hoi bin taabani.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wengi waowalikuwa wanamudu chakula cha siku moja na hii ilikuwainatokana na ajira ya viwanda. Tumeviua viwanda vyotekwa Sera ya Ubinafsishaji. Ubinafsishaji huu hatukufanyaupembuzi yakinifu kama tulivyozoea. Hatukusema kwambasasa tunahitaji utafiti wa kina. Walipokuja waliokuja tukaitawawekezaji, tukawauzia kwa bei poa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inaliza leo kama siyokusikitisha, Morogoro na kwingineko, unakwenda pale ma-godown badala ya kuzalisha bidhaa ya ngozi, wanaita nima-godown ya kuweka tumbaku. Cha kusikitisha zaidiwawekezaji hawa ambao mimi nawaita wababaishaji,wengine tumewapa viwanda na fedha tumewapa kutokakwenye taasisi zetu za fedha humu ndani. Hivi tujiulize kwanini ikawa hivi? Kama tulikuwa na fedha za kuwakopeshawawekezaji kutoka nje, tulishindwaje leo kuiendeleza SIDO?SIDO i l ikuwa ndiyo mkombozi pia kwa viwandavidogovidogo. Biashara ambazo akina mama vijijini naowangemudu kuziendesha lakini tunawapapatikia watu,hatuwajui miguu, hatujui kichwa, tunakamata tumbo,tunawaita wawekezaji, tumewajaza mapesa hatima yaviwanda vya Tanzania leo ni hapa tulipofikia. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu yangu Dkt. Kigoda,nitakuomba sana katika huo mchakato, leo hebu usemeneno kwa ndugu zetu wa Kusini ya Tanzania, viwanda vyaovya korosho. Mwenzako mmoja aliwaambia viwanda hivi ni

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

207

mufilisi, vimeshauzwa kabisa. Sasa leo wape neno wapatematumaini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitakusaidia kwenyeuwanja mmoja, kwenye kilimo na bidhaa zake. Kitabu chaWaziri kimezungumzia viwanda vya saruji na kadhalika lakiniAgricultural Industrial Relation ndicho kitakachoweza kuwamkombozi kwa nchi hii ya Tanzania. Agriculture hii ya pamba,korosho, katani, tumbaku bila kusahau matunda na mazaomengine mfano mbogamboga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, akina mama wetu hizishughuli wanazimudu, hebu Serikali ielekeze nguvu huko. Leoviwanda tumeshaviua, wazee wale waliokuwawanategemea waume zao na watoto wao kwenye ajiraile, ndiyo wale leo wanahangaika na mabeseni yambogamboga na Mgambo virungu juu. Sasa hali hiitutawatendeaje haki watu hawa ikiwa bughudha ndani yanchi yao waliozaliwa ni hii? (Makofi)

Mwisho Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya viwandana biashara ni pamoja na ndugu yangu kataja Wamachinga.Hawa nao hawana raha, maneno ya kwetu hawana buraha,Mheshimiwa Kigoda ameelewa. Hebu tuwapeni nafasi. Nchini yao, nchi hii ni yetu sote na wao wana haki kama vilealivyo nayo Mtanzania mwingine. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa EPZ na miminiuguse, kuna dhuluma kubwa inayotendeka hivi sasa naunaelewa wazi kwamba dhuluma haidumu na ikidumu ninakama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi hawawamezuiliwa maeneo yao. Serikali hadi sasa haijawafanyiachochote, mradi umekwama, maeneo hayaendelezwi,hatma yao hawaijui, wanaumia ilhali chao wanacho.Kuwafanyia hivi, ni kuwadhulumu na dhuluma, nasema tenaMwenyezi Mungu hatakubaliana nayo, tutakuja kutafutamchawi lakini ni sisi wenyewe. (Makofi)

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

208

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira imepotea kwenyeviwanda ambapo ni mamilioni ya Watanzania leowangekuwa wako huko. Hebu Mheshimiwa Dkt. Kigoda,utakapokuja hapa kufanya summary, waeleze kidogoWatanzania wapate matumaini, juu ya Mradi wa KurasiniLogistic Centre. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi ambao kama Serikali,maana tunajishauri kwa mambo ambayo tayari MwenyeziMungu keshayaweka mikononi mwetu, hebu fanyeni hikitunashauriana. Tunashauriana kwa haya yaliyokuwa ni ya heritayari yameshapatiwa ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la Kurasini, ajirazilizokuwa zimeelekezwa kwa kuanzia ni 25,000. Kwa Dar-es-Salaam leo, tusingekuwa na sababu ya kufukuzana naWamachinga wale. Hatima yake tumesema kwamba kunamradi wa Boda-Boda. Viongozi wa Serikali wanakwendakufungua mradi wa Boda-Boda, hebu Serikali na ikae sasakwa harakaharaka ione ni gharama kiasi gani inaingia yatiba kwa wale wanaopata maumivu, ni wangapi wanaokufakwa mwezi, lakini ni wangapi wanaoibiwa kupitia Boda-Boda hizi? Mradi wa Boda-Boda si suluhisho. Suluhisho laTanzania ni kurudisha viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, Ndugu yanguWaziri Kigoda, Mheshimiwa Rais katamka ufufuaji waviwanda na kuvijenga vipya; nitakuomba utueleze nimikakati gani ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefukabisa, sekta ya viwanda Tanzania utairejesha kama vileMwalimu mwenyewe alivyokusudia kabla ya kuondokakwake Duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naheshimu muda wako,nakutakia kila la kheri Waziri Kiogoda, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Hamad,sasa namwita Mheshimiwa Dkt. Mrema.

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

209

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba na mimi nimpongeze sana Waziri waBiashara na Viwanda, Mheshimiwa Dkt. Kigoda na Msaidiziwake kwa kazi nzuri. Kazi wanayoifanya kule kwenye Jimbola Vunjo, kazi wanayoifanya kule Himo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua ni nia ya Serikalikwamba wanataka kuujenga ule Mji wa Himo, licha tukwamba baadaye tutaomba uwe Makao Makuu ya Wilayaya Moshi Vijijini badala ya kuwa kule Manispaa ya Moshi, lakinikazi wanayoifanya pale ni nzuri sana. Kwanza, ni suala lakujenga masoko ya kimataifa, biashara za kitaifa naviwanda. Maswali kwamba mbogamboga, mambo ya ndizi,vitunguu, nyanya, vitapata masoko ya kimataifa. Biasharaya utalii sasa itafanyika Himo badala ya kufanyika Moshi naArusha peke yake. Kwa hiyo, ninachosema ni kwamba,ninaomba Serikali haya mawazo mazuri ya kupendeza, yakufanya Mji wa Himo uwe Kituo Kikubwa cha Utalii muendeleenayo, namshukuru sana Waziri wa Viwanda na Biashara naMsaidizi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nitakuwa mwizi wafadhila kama sitamshukuru sana Mheshimiwa Rais JakayaKikwete kwa sababu alifika pale na ndiye aliyetoa ushaurikwamba tuwe na masoko mawili, soko la ndizi na soko lanafaka. Pia nimshukuru sana Waziri Mkuu, uliniahidi, ile ahadini deni kwamba, utakuja kukagua ile kazi; nakukumbusha,nashukuru umeniambia utakuja. Kwa hiyo, ni matumainiyangu Waziri Mkuu utazunguka nchi nzima kuona namna ganimtaujenga Mji wa Himo uwe ni Kituo Kikubwa cha Viawanda,utalii na biashara za Kimataifa watu wa Kenya, Uganda,Ethiopia, Somalia, waweze kuja kununua bidhaa pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wetuMheshimiwa Waziri wa Viwanda ni kwamba, Mkoa waKilimanjaro, Mkuu wa Mkoa wetu, tena nilikuwa namwombaWaziri Mkuu, yule Mkuu wa MKoa usimwondoe mapemampaka amalize kazi hii mliyompa pamoja na Sekretarieti yake.Kazi ya kujenga ule Mji wa Himo, yale masoko mawili yaKimataifa, soko la ndizi na mbogamboga Njia Panda na Soko

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

210

la Nafaka kule Lokolova inaendelea. Tumeshapima yalemasoko na Hati tunayo. Pill i, tumeshaandika andikolinaloonesha ni kazi gani zinatakiwa zifanyike pale na lile sokola ndizi tumeshapeleka barabara pamoja na kujenga vyoona kadhalika. Namshukuru sana Waziri Mkuu kwa kuwa karibuna mimi. Kila nikikutana na wewe lazima nikukumbushehabari ya Soko la Lokolova pamoja na la ndizi pale NjiaPanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Kil imanjarotumeshapiga hatua. Tumeshaandika Memorandum ofUnderstanding, Mkuu wa Mkoa wetu na Sekretarieti ya Mkoa,Benki ya TIB wamekubali kwamba watawekeza. Mwaka janamwezi Oktoba walishafanya makubaliano kwamba wakotayari kutoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya hayo masoko mawili.Nawashukuru sana kwa sababu hiyo inawezekana kwasababu Serikali, mmekubali kutoa Bank Guarantee la sivyowasingekubali hivihivi. Halafu pia watu wa TIB mwaka huumwezi wa Aprili, wameshafika pale na kuangalia Master Planna michoro kuona yale masoko yataendelea namna gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilichokuwanataka ni kuishukuru sana Serikali, kwa sababu nitakuwamwizi wa fadhila, nyie mnanitendea mema, halafu miminikose shukrani; hiyo sitafanya. Nitaendelea kuwaungamkono so long as na mimi mnanisaidia, you scratch my backI scratch yours, kama mnavyofanya. Kwa hiyo, hongera sanaWaziri Mkuu, hongera sana Rais wangu, hongera sana Wazirina juzi ulimtuma Naibu Waziri wako kule kukagua ile kazi.Hizo ndio kazi zinatakiwa zifanyike. Kwa hiyo, hilo la kwanza,nilitaka niwashukuru sana, mkinikamilishia kazi ile na mimikazi yangu ya Ubunge itakuwa imeeleweka vizuri. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusu ujenzi waviwanda katika makazi ya watu. Pale nina mgogoromkubwa sana na ninamshukuru sana Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Iko barua yake hapa nzurisana CE.91/329/01/E87 ya terehe 27 Januari mwaka huu.Anamwandikia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

211

Wilaya ya Moshi. Ni kuhusu malalmiko ya ujenzi wa kiwandakatika makazi ya watu, Kiwanja Namba 16, Kitalu F, Himo.Naomba Waziri wa Biashara na Viwanda, nikusomee ili msijemkaji-contradict, Serikali ni moja Wizara hii inakuwa namsimamo halafu Wizara nyingine inatofautiana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Mipango Mijiamepokea barua ya malalamiko yenye kumbukumbu nambahiyo, ilikuwa ni barua yangu ya tarehe 9/1/2013, kutoka kwaMbunge wa Jimbo la Vunjo, aliyomwandikia MheshimiwaWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayohususomo hilo hapo. Ninakushukuru Waziri, unavyopokea baruayangu, unanijibu sawia. Anasema Wananchi wa Kijiji cha NjiaPanda, Himo, wanalalmika kuwa kuna mtu anajengakiwanda cha maji, biskuti na vinywaji ndani ya eneo lamakazi. Maelezo na vielelezo viambatanishwa kwenye baruahiyo, vinaonesha kuwa kiwanda hicho kinajengwa kwenyeKiwanja Namba 16, Kitalu F, Himo, ndani ya eneo la makazi.Pili, maeneo ya jirani yaliyotengwa kwa ajili ya huduma yakuabudia na matumizi ya umma, yameongezewa kwenyekiwanja hicho na kubadilisha matumizi bila idhini yaMkurugenzi wa Mipango Miji, kama ilivyoainishwa kwenyeKifungu Namba 6(1)(k) na 30(1) yakisomwa kwa pamoja naSheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007. Waziri anasemakwamba ni kweli katika upangaji wa miji, maeneo yaviwanda hutengwa mbali na makazi ya watu kwa sababuni matumizi yanayokinzana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barua kutoka Wizara yaArdhi inasema kwa kuzingatia malalamiko hayo yawananchi, Wizara inakutaka yaani Mkurugenzi Mtendajianaambiwa, kufuatilia malalamiko hayo kwa undani nakuhakikisha kuwa kiwanda hicho hakijengwi na kamakimeanza kujengwa uagize kusimamishwa ujenzi huo. Maramoja peleka Mthamini wa kupata thamani ya maendeleoyaliyokwishakufanyika na umtake mwendelezaji kulipa fainikama ilivyoainishwa kwenye Kifungu cha Sheria 34(1) chaSheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 na kwa kiwangokilichoidhinishwa kwenye Kanuni za Adhabu za Sheria ya Ardhiya Mwaka 1999 zilizopo kwenye Tangazo la Serikali Namba

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

212

84 la mwaka 2001 kwa kosa la kujenga bila kibali cha kubadilimatumizi kutoka kwa Mkurugenzi Mipango Miji. Kasaini LinusShayo, Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimeamua kuileta hiibarua hapa kwa sababu kule kuna mgogoro mkubwa. Watuwanatumia ubabe, wanatumia madaraka, unakwendakujenga kiwanda kwenye makazi ya watu. Nashukuru Wizaraya Ardhi kwa kuwa na msimamo ulionyooka. Nimeangalia,ni wewe peke yako, Wizara ya Ardhi mmethubutu kuchukuamsimamo huo. Sasa naomba na Wizara ya Biashara naViwanda, tusaidiane kwa sababu ule Mji wa Himoumeshaharibika. Nitamngoja Waziri wa Ardhi wakati wakekwa sababu ule Mji wa Himo ukienda kuuliza eneo la viwandaliko wapi? Hawakutenga, wamejenga kila mahali. Yalemaeneo ya wazi yote yamejengwa. Kwa hiyo na sisi tunasemaMji wa Himo utakuwa Mji Mkuu wa Wilaya ya Moshi Vijijini.Sasa ni Mji gani huo hauna maeneo, hakuna viwanja vyamichezo, hakuna makaburi, hakuna maeneo ya viwanda.Kwa hiyo, mimi ninachotaka kuomba hapa, nitakuombaWaziri Mkuu unisaidie kwa sababu kama mnafanya kazitakatifu, kazi nzuri hiyo ya kuwekeza kwenye Mji ule wa Himo,kupanua utalii na haya masoko ya Kimataifa, halafu ule Mjiunajengwa kienyeji bila kuzingatia masharti ya Mipango Miji,tutakuwa tumefanya makosa makubwa sana.

Mheshimiwa mwenyekiti, namalizia kwa kusemakwamba, kwanza naishukuru tena Serikali. Namshukuru Raiswangu, namshukuru Waziri Mkuu, namshukuru Waziri waViwanda na Naibu wake kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pili,namshukuru Mkuu wa Mkoa na Sekretarieti yake kwa kazinzuri wanayofanya kule Himo, kujenga ule Mji uwe wa kisasa.Hizo dosari ndogondogo nitaongea na Waziri wa Ardhi,aweze kunisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wamejenga nyumba,halafu eti Mipango Miji ya Wilaya ya Moshi wanasematuwaache waendelee; nyie Dar-es-Salaam mnabomoanyumba ambazo zimejengwa katika maeneo yasiyostahili,kule kwangu hakuna mtu anayenisaidia yabomolewe yale

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

213

majengo ambayo yataharibu mandhari ya ule Mji wa Himo.Kwa hiyo, ninachosema Waziri wa Ardhi, unisaidie. Nitakujakwako tujenge kamji kadogo kazuri kakisasa pale Himo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja mia kwa mia. (Makofi)

MWENYEKITI: Mchangiaji wetu wa mwisho, niMheshimiwa Kayombo.

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya Mheshimiwa Wazirikusoma hotuba yake, nilikuwa nimeamua kutounga mkono,lakini nilipoyaona haya ambayo ameyaongea nakiri kusemakwamba nimeridhika, namtakia kila baraka za MwenyeziMungu aweze kufanikiwa katika kazi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana naWaheshimiwa Wabunge waliokwishazungumza juu ya ufinyuwa bajeti katika Wizara hii. Hii haioneshi dhamira ya kweli yaSerikali ya kuinua viwanda lakini mahsusi ningependa kuonaSIDO wanasaidiwa zaidi na kile kituo chetu cha China LogisticCentre kinaweza kupewa fedha zaidi na TBS inawezeshwakwa kupewa wafanyakazi zaidi ili waweze kuangalia afyazetu kupitia vipimo wanavyopima katika bidhaa mbalimbalizinaingia nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ninalotaka kujikitazaidi ni mradi wa Ngaka. Waheshimiwa Wabunge yapomatatizo ya umeme nchini na hapa tulipitisha umeme wadharura miaka miwili iliyopita lakini hakuna mafanikio,suluhisho liko hapa kwenye makaa ya mawe. Sasa Serikali,mimi sioni ina kigugumizi gani kwa nini huu mradi haiuwekeikipaumbele. Kwa nini kwenye miradi mingine Serikali inawekafedha; kwenye mradi wa makaa ya mawe Ngaka, Mbinga,Kijiji cha Ntunduwaro, Serikali inalala usingizi, haiweki fedhana haitaki kuweka fedha? (Makofi)

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

214

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Spika aliundaKamati Ndogo ya kuangalia mradi wa makaa ya mawe naMheshimiwa Mgimwa, ambaye sasa ni Waziri wa Fedha,alikuwa kwenye Kamati hiyo; yapo mapendekezo lakinibado hayo mapendekezo hayatiliwi mkazo na walahayatiliwi maanani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umeme ambao unatumikasasa TANESCO inaununua kwa senti za Dola ya Marekani 42.Umeme wa makaa ya mawe ni senti 12 tu. Kkwa ninimnawatesa wananchi wa Tanzania kwa kuwapa umemeghali wakati wanaweza kupata umeme ulio nafuu zaidi?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunaacha haowawekezaji wenyewe tu waweze kujenga mtabo huu, kwanini tusiweze kutafuta fedha za ndani za kujenga mtambowa kufua umeme wa makaa ya mawe? Kwa nini TANESCOisishiriki katika ujenzi huu wa makaa ya mawe kwa ajili yausalama wa nchi yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo tatizo la mazingira. Yalemakaa ya mawe yanasafirishwa kwa malori. Mimi naaminikwamba kabla ya kuanza huu mradi, tathmni ya mazingirailifanyika. Sasa kwa nini Serikali, iruhusu huu mradi kuanza nakusafirisha kwa malori ambayo yanasababisha vumbi nawananchi wote wa kutoka kule Ntunduwaro, Rwanda,Paradiso, Amani Makoro, wote wanakohoa sasa hivi.Namwomba Mheshimiwa Waziri afanye analoweza kwakushirikiana na wawekezaji na Serikali yetu kuona kwambabarabara ya kutoka Kitai kwenda Rwanda mpaka Lituiinajengwa kwa kiwango cha lami ili kuwapunguzia adhaya vumbi hawa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko tatizo la fidia na hili nitatizo kubwa. Hivi juzijuzi mlituona kwenye TV tuko palekwenye eneo la mgodi na wananchi walikuwa wakali sana.Baadhi ya viongozi wa NDC, wanasema Mbunge alikuwaanashirikiana na wananchi kuwashawishi wagome. Mimi sikohapa kuiwakilisha Serikali, mimi kazi yangu ni kuwawakilisha

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

215

wananchi na nitaendelea kuwawakilisha wale wananchivizuri wa Kata na Vijiji vyote katika Jimbo la Mbinga Mashariki,Serikali timizeni wajibu wenu. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Yes!

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: Kwanza kwa niniMheshimiwa Waziri mradi huu ulianza kabla ya kumaliza keroza fidia kwa wananchi? Hili ni kosa la msingi. Kwa nini mpakasasa wenzetu wa Shirika la NDC hawaoni hali hii na walahawahangaiki. Hata pale ambapo Mheshimiwa Mkuu waMkoa alituita Viongozi kwenye mkutano wa daharura ilikuangalia baada ya mgodi kufungwa, NDC hawakutumamwakilishi. Mheshimiwa Waziri hii ilikuwa dharau nafikiri kwaMheshimiwa Mkuu wa Mkoa. Mimi naomba wenzetu wa NDCwajifunze kushirikiana na Serikali ya Mkoa na Serikali yaWilaya. Kila linalotokea pale Wilayani, Mheshimiwa Mkuu waWilaya, Mheshimiwa DED, Mheshimiwa Mwenyekiti waHalmashauri, Mbunge na Diwani ndio wanahangaika kilasiku kwenda Ntunduwaro. Kwa nini mnaacha hii kazi kwaLocal Government peke yake wakati nyie ndio wenye mradina sisi hatupati chochote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa ninaomba Shirikala NDC, kwa mradi huu pia lifikirie kutoa share angalau kwakiwango fulani kwa Kijiji cha Ntunduwaro, ili na wao wawezekuona mafanikio ya mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, Serikali imeji-committ kulipa fidia kwa wananchi wale ifikapo tarehe 15Juni, mwaka huu. Naiomba Serikali itimize ahadi hii.Nimeshamwandikia Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 24mwezi uliopita juu ya jambo hili. Hatutaki kuona tena vuruguzinatokea katika Kijiji kile wala mimi sipendi kuona ule mgodiunasimamishwa kwa sababu tu ya tatizo la fidia wakatiambapo tuna muda mrefu wa kutatua tatizo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kuwasilisha. Naunga mkono hoja. (Makofi)

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

216

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kupata taarifa ya Serikali juu ya hatma ya Kiwandacha Tanganyika Packers kilichopo katika Jimbo la Kawe Dares Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufilisi wa Kiwanda hikiulifanyika tarehe 19 Aprili, 2002. Mali za Kiwanda husikazilikabidhiwa/uzwa kwa Kampuni ya Al-Ghurair InvestimentL.L.C ya Falme za Kiarabu ili wazitumie katika kujenga vitegauchumi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwekezaji husikahaukufanyika kama ilivyotarajiwa, hali iliyopelekea Serikalikuanza mchakato wa kukirudisha ndani ya miliki yake. Kauliya mwisho ya Serikali hapa Bungeni ilibainisha kwamba wakokwenye majadiliano na mwekezaji husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama inavyoeleweka katikaeneo husika kuna shughuli mbalimbali za kibinadamuzinazoendelea. Kuchelewa kwa Serikali kufanya maamuzikunaweza kupelekea kuibuka kwa mgogoro mwingine katiya watumiaji na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupata majibu juuya hatma ya eneo hili. Kama majadiliano baina ya pandembili, Serikali na mwekezaji yalifanyika, walikubaliana nini?Je, mchakato wa utekelezaji wa makubaliano hayo unaanzalini?

MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuchangia kuhusu mradi wa China Logistic Centre.Katika bajeti ya mwaka 2012/2013, Bunge lako Tukufuliliidhinisha jumla ya shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kulipa fidiawananchi maeneo ambapo mradi utafanyika. Jambo lakusikitisha, hadi mwaka unamalizika ni shilingi milioni 550 tundizo zilizotolewa. Je, Serikali inatuambia nini kuhusiana namradi huo?

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

217

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ni muhimu sanakwa nchi yetu. Mradi huu ungeinufaisha nchi yetu kiuchumikwani nchi nyingi za Afrika Mashariki na SADC zingetengemeauzalishaji wa bidhaa katika maeneo haya lakini pia mradihuu unategemewa kutoa ajira kwa Watanzania 25,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukumbuke kuwa mradi huupia unatakiwa na nchi nyingi za Afrika na sisi tunauchezeana kupoteza fursa za kiuchumi na kijamii (ajira). Hayayanaweza kuja kuwa majuto na wazee walisema majuto nimjukuu. Hivyo, Serikali inashindwa nini kutoa kiasi hicho chafedha kwa ajili ya watu wake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali iliangaliesuala hili kwa makini sana vinginevyo hatutakuwa pamoja.Kwa hiyo, Serikali iangalie uwezekano wa kumalizia pesazilizobakia kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

MHE. DKT. BINILITH S. MAHENGE: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Wazirina timu yake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vya zao la pareto.Hadi sasa Tanzania kuna kiwanda kimoja tu cha zao la paretokilichopo Mafinga cha PCT kinachoshirikiana na Kampuni yaMarekani ijulikanayo kama MGL. Kampuni hii inatumia fursahii kuwapunja wananchi kwa kununua pareto kwa bei yachini sana. Tunaomba Serikali itafute wawekezaji wenginewakubwa ili kuleta ushindani katika sekta hii ya zao la pareto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kuna wanunuziwadogo wadogo wananunua pareto na uwepo waoumeongeza tija sana kwa wananchi kwani bei ya paretoimeogezeka kutoka shilingi 1700 kwa kilo moja hadi shilingi2400 kwa kilo moja. Huyu mwekezaji mkubwa wa Marekanianawapiga vita hawa wawekezaji wadogo ili abaki pekeyake. Tunaomba Serikali iwasaidie wawekezaji wazalendo

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

218

kwa kuwapa ruzuku ili waanzishe kiwanda cha paretokitakachotoa ushindani kwa kiwanda hiki cha PCT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,sekta ya viwanda ni muhimu sana kwa ustawi wa Taifa hapanchini. Hakuna Taifa ambalo litakuwa na maendeleo yoyoteyale bila viwanda. Ni vyema Serikali ije na mpango kabambewa kufufua viwanda ambavyo havifanyi kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uanzishwaji waviwanda vipya hasa vya kusindika mazao ambayoyanazalishwa hapa nchini. Tukifanya hivyo, tutakuza uchumikatika nchi hii na ukizingatia unapokuwa umeongezathamani ya mazao umewasaidia wananchi walio wengi hasawa vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri sana Serikali ijengekiwanda cha kusindika tumbaku katika Mkoa wa Tabora.Kiwanda hiki kama kitajengwa katika Mkoa huo kitasaidiasana kupandisha thamani ya zao hilo kwa Mikoa ya Tabora,Shinyanga, Mbeya, Kigoma na Katavi. Mikoa hii ni jirani nayote inazalisha zao la tumbaku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda vyakukoboa korosho; ni vyema Serikali ikajenga viwanda vipyana vile vya zamani ambavyo havifanyi kazi vifufuliwe iliviweze kufanya kazi. Tukisaidia kuimarisha viwanda ambavyovina mahusiano ya moja kwa moja na mazao ya wakulima,tutaimarisha uchumi kwa kiwango kikubwa na kukuzauchumi kwa matabaka ya wananchi wanaoishi Mijiji naVijijini. Naomba Serikali ije na tamko litakalosaidia sanakutatua tatizo la ukosefu wa viwanda vinavyohusiana namazao ya wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda vyambolea; ili tuweze kuwa na uzalishaji wa chakula cha kutoshanchini na mazao ya biashara, ni lazima Serikali ijenge kiwandacha mbolea. Kiwanda hiki kikijengwa kitapunguza gharama

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

219

kubwa zinazotumiwa na Serikali kwa ajili ya kuagiza mboleakutoka nje na kuifanya Serikali kutumia fedha nyingi kwa ajiliya kununulia pembejeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masoko; Serikaliifanye jitihada za kuandaa mipango ya kutafuta masokoyatakayowasaidia Watanzania kuuza mali zao ambazozitakuwa sio malighafi. Kama tunataka kuiandalia nchi yetumfano mzuri lazima Wizara ijikite kwa dhati kuwatafutiamasoko wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuendelee lazima Serikaliiwekeze katika miundombinu ya umeme wa uhakika hasavijijini. Umeme vijijini ni muhimu sana kwa ajili ya kuondoaumaskini hasa wa wananchi waishio vijijini. Naomba Wizaraihakikishe imewekeza kwenye makaa ya mawe ili tupateumeme wa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania kwa sasaimesheheni bidhaa feki, TBS wanatakiwa kujiimarisha kwakuwa na watu wengi wa kufuatilia kazi za kila siku. Leo kilaMtanzania anapata hasara kwa kuuziwa bidhaa feki. Ni aibukwa Taifa letu. Pia majengo yanaugua na hata kuporomokakutokana na matumizi ya bidhaa feki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado kuna Mikoa na Wilayaambapo maeneo ya EPZ hayajatengwa. Je, Wizara inakusudiakuwachukulia hatua gani viongozi kama hawa kwa kuwawanachelewesha mpango wa Serikali na maendeleo yawananchi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelezo ya Waziri katikabajeti yanatia matumaini. Kama uwekezaji ukifanyika, je,Serikali imejipanga vipi kuhakikisha vijana wetu wanapata

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

220

ajira kwani uzoefu umeonyesha kuwa siku hizi hapa Tanzaniakazi za Wamachinga zinanyonywa na wageni hasa Wachinahuko Kariakoo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali iandaekijitabu ambacho kitaonyesha kila Mkoa na maeneo ya EPZna fursa zilizopo katika eneo husika kwa maana ya kwambakama mwekezaji anataka kuanzisha kiwanda cha matundabasi apate taarifa ya kutosha kuhusu Mikoa iliyo na fursa yakuwekeza.

MHE. RACHEL M. ROBERT: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia mambo kadhaa katika hotuba yaWizara hii nyeti katika kuinua uchumi wa kipato chaMtanzania mmoja mmoja au kikundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya viwanda. Pamojana sekta hii kukua kwa asilimia 8.2 mwaka huu 2012/2013bado kuna changamoto nyingi sana. Ni Sekta ambayoinaendelea kuliongeza pato la Taifa kila mwaka. Ni vemaSerikali ione sasa umuhimu wa kuongeza viwanda vingivikiwemo vya nguo hata katika Mikoa inayolima sana zaohili ukiwemo Mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukosekana kwa viwandahivi katika maeneo haya kunawafanya wakulima wa zao lapamba kukata tama. Mbali na kukosa soko la uhakika, beiya pamba bado hairidhishi na kuendelea kushuka kila mara.Serikali inatambua kuwa zao la pamba ni muhimu sana nalinaongoza kulipatia Taifa pato kubwa sasa. Kwa nini Serikaliisijenge viwanda vya nguo na mafuta kuliko kutegemeaviwanda vya watu binafsi ambavyo baadhi ya viwanda nakama si vyote vina tabia ya kulalia wakulima. Serikali ioneumuhimu wa kujenga kiwanda cha kusindika mafuta,kuchambua pamba na nguo hata kimoja katika Kandaambako kuna wakulima wengi wa pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uzalishaji wa nyavuza uvuvi ni zuri sana kwani kuna ongezeko kubwa la uzalishajiwa nyavu kutoka tani 165 mwaka 2011 hadi tani 295 mwaka

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

221

2012. Serikali inadhibiti vipi ubora wa nyavu hizi? Tumekuwatukijionea jinsi wavuvi wetu wanavyonyang’anywa nyavu hivilakini wazalishaji wa nyavu hizo wakiendelea kutengenezanyavu hizo zisizo na viwango. Naomba Serikali iangalie upyana kwa umakini viwango vya nyavu za uvuvi katika viwandavinavyozalisha ili wavuvi wasipate hasara wanapozinunuana kwenda kuzitumia thereafter wanakamatwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ongezeko la beiya mifungo mfano ng’ombe, mbuzi na kondoo, badowafugaji hawanufaiki kwani kumekuwa na tabia yawafanyabiashara kwenda vijijini na hasa wakati wa njaa nakuwapangia bei wafugaji ambapo mwisho wa sikumfanyabiashara ndio anapata faida. Naomba Serikali ije nabei rasmi ya mifugo hiyo il i kumnusuru mfugaji huyoanayetegemea mifugo yake ili ainue uchumi wa maisha yakena jamii inayomzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwakuanza kujenga kiwanda cha ngozi cha Xinghua InvestmentCo. Ltd Mkoani Shinyanga. Naomba sasa Serikali isimamiekwa karibu kiwanda hiki kiishe kwa wakati ili wananchiwapate ajira na wafanyabiashara wa ngozi waweze kupatasoko lakini pia Serikali iangalie kwa umakini zaidi maslahi yawafanyakazi watakaoajiriwa katika kiwanda hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa Kiwanda chaTRIPLE S cha kusindika nyama kilichopo Shinyanga, Serikaliihakikishe kinakamilika na kuanza kazi mara moja. Uwepowa viwanda hivyo Mkoani Shinyanga/Simiyu kutaleta hamasakwa wafugaji wengi kufuga kitaalamu na kisasa zaidi iliwaweze kupata soko katika viwanda hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya masoko, katikakitabu cha Hotuba ya Waziri nimeona kuna mkakati wa seraya masoko ya mazao na bidhaa za kilimo. Ni vyema sasasera hii iharakishwe ili iweze kuwakomboa wakulima hasawa mazao ya pamba na korosho ambapo bei zakezimekuwa hazitabiriki.

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

222

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kuwasilisha.

MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: MheshimiwaMwenyekiti, naipongeza Serikali kwa kuwa na mpangokabambe wa kufufua viwanda pamoja na kujenga viwandavipya lakini huu ujengaji wa viwanda uende sambamba namiundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 80 ya wananchiwako vijijini na wengi wamejielekeza kwenye kilimo, wenyekulima matunda, alizeti, korosho na kadhalika na wako tayarikuongeza kilimo kwenye mazao hayo. Tatizo kubwa hukovijijini hakuna kiwanda cha kubangua korosho, kutengenezamafuta, kutengeneza juice kutokana na matunda, pamojana jitihada waliyokuwa nayo, wakulima hawa hawawezikuondokana na umaskini kutokana na kuwa mapatowanayopata ni madogo, kutokana na kuwa hawanaviwanda vya kutosha huko vijijini. Zao la korosho limeshamirihuko vijijini lakini wakulima wanauza bei ndogo kutokanana kwamba hazijakobolewa, inabidi zisafirishwe nje kwendakukobolewa halafu zinarudi hapahapa Tanzania kwa beikubwa, zao tunalima hapa nchini lakini wanaonufaika ni nchiza nje. Kwa kuwa Serikali imejipanga kujenga hivi viwanda,naomba itekelezwe azma yao kwa vitendo na kwa namnahiyo Serikali itaweza kuongeza mapato nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali kwa yalemaeneo ambayo wanataka kujenga viwanda na ikiwawananchi ambao wamevunjiwa maeneo yao, walipwe kwaharaka ili kuepukana na migogoro inayojitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uingizaji wa bidhaa fekibado unaendelea nchini licha ya jitihada ya Serikali kuwekasheria. Naiomba Serikali iangalie upya sheria hii ili iwezekwenda na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kisungurakidogo, naiomba Serikali itoe pesa zote ambazo zimekuwabudgeted kwenye Wizara hii ili miradi hii iweze kutekelezwa.

Page 223: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

223

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei ya vifaa vya ujenzi. NajuaSerikali haijihusishi na biashara au uendeshaji wa viwanda.Hata hivyo, najua kwamba ni jukumu la Serikali kusimamiaau kuweka misingi ya sera za bei. Inashangaza kuona bei yasaruji inayotengenezwa/ inayozalishwa Mbeya ina bei kubwaMkoani Mbeya kuliko bei ya saruji hiyohiyo katika Mikoa yaMorogoro, Dar es Salaam na kadhalika. Hali hii haikubalikina tunaomba Serikali kupitia Wizara iingilie kati jambo hili.Wote tunajua malighafi nyingi inayotumika kwa ajili yauzalishaji saruji inapatikana katika Mkoa wa Mbeya; sasaiweje wananchi wasifaidike na kiwanda hicho? Nini faidaya kuwa na kiwanda katika Mkoa huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei za bati na nondo piazipo juu sana, zinakatisha tamaa! Hali hii inapunguza kasi yawananchi kujijengea nyumba bora. Naomba Serikali piaiingilie kati ili kuhakikisha kwamba bei ya vifaa hivyoinadhibitiwa ili kuwapa wananchi nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, napenda pia kujua nilini kiwanda cha nyama cha Mbeya (Tanganyika Packers)kitaanza uzalishaji wa nyama baada ya kusimama kwamuda mrefu sana. Nashauri Serikali ilitolee jambo hili maelezoya kina kwa sababu kukiacha kiwanda hicho katika hali yasasa ni sawa na kufukia mamilioni ya hela ardhini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza, naomba kuunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nampongezaMheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda naBiashara pamoja na timu yake kwa juhudi zao za kulifanyaTaifa hili kuwa la viwanda.

Page 224: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

224

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa tulilokuwanalo hapa Tanzania, ni ubora wa bidhaa zetu, lazimauangaliwe kwa makini ili tuweze kushindana na nchi zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ubora piana vifungashio ni tatizo kubwa (Packing). Ili kuepuka matatizohayo ni vizuri TBS iongeze nguvu kuongeza watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu kwa ajili ya kuuzabidhaa ambayo ni bora kwa matumizi ya hapa hapa nchinikwetu ni muhimu na hata nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda cha nguo chaMbeya Textile kimefungwa na hakifanyi kazi na mitamboinazidi kuondolewa na wananchi walifanya maandamanomakubwa ya kupinga ung’oaji wa mitambo. Je, Serikaliinatoa tamko gani juu ya Kiwanda hicho?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwambanaunga mkono hoja hii lakini naomba jibu hasa la Kiwandahiki cha nguo.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, pongezi kwa Waziri, Naibu Waziri na Wataalamwote wa Wizara kwa kuandaa hotuba hii na kuileta hapaBungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ndogo inayopangwakwenye Wizara hii na fedha kidogo sana inayotolewa kwaWizara hii ni kikwazo kikubwa kuwezesha Wizara hiikutekeleza malengo yake na kazi zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawezaje kutoa Taifa hilikutoka kwenye uchumi wa biashara ndogo ndogo nakwenda kwenye uchumi wa kutegemea viwanda wakatiSerikali haiwekezi kwenye maendeleo na viwanda?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Viwanda VidogoVidogo (SIDO) lina wataalam wazuri wenye uwezo mzuri. SIDOina uwezo wa kuajiri vijana wengi sana wanaotoka Vyuo

Page 225: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

225

vya VETA. SIDO inaweza kuinua kilimo chetu kutoka kwenyekilimo cha mkono kwa kutengeneza Power tillers na tractorndogo ndogo. SIDO wanaweza kabisa kuwezesha uwepowa viwanda vidogo/mashine za kuchakata mazao mfano,kukamua mafuta ya karanga, ufuta, alizeti, matunda nakadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO iwezeshwe kupatafedha za kutosha kuinua kipato cha Taifa na Watanzaniawenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tumekuwa soko labidhaa mbalimbali kutoka nchi jirani kama vile, Kenya, SouthAfrica, Zambia, Zimbabwe na kadhalika. Hata kwa bidhaaambazo zinaweza kutengenezwa hapa nchini. Ni kwa ninitumefungua milango wazi kuruhusu kila kitu kuletwa hapabila kuweka viwango ili kuviwezesha viwanda vyetu kupatasoko kwa bidhaa za ndani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao vijana wengi mitaanihawana kazi, hivi kweli tunaingiza (import) hata toothpick,cotton buds, viberiti, hii ni aibu kwa Taifa hili. Tuna mbaotuna cotton tumeshindwa nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilieleze Bunge ni kwanini hakuna viwango (standards) vya Taifa vya uboraunaotakiwa kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi. Tanzaniaimekuwa sehemu ya kuleta chochote hata kama hakifai.Bidhaa za Kichina zipo dunia nzima, lakini bidhaa ya Kichinazinazoletwa hapa nchini ni zile dhaifu zisizokuwa na viwangona Serikali imeruhusu haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bidhaa feki ni tatizo kubwahapa nchini na wananchi wamepata hasara kubwa kwakununua bidhaa feki.

(i) Vifaa vya umeme vingi madukani ni feki nawanaouza wanajua na Serikali inajua.

(ii) Vyakula vinavyoingia kutoka nje vingi ni feki,watu wanakula vitu feki, wanaathirika kiafya.

Page 226: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

226

(iii) Madawa feki yanaingizwa madukani, watuwanatumia badala ya kutibu maradhi, tunapata magonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwa TBSManagement imebadilishwa bado hatujaona mabadilikokuhusiana na utendaji kudhibiti bidhaa feki. Vinaingiaje hadivinauzwa madukani wakati tunayo taasisi inayoshughulikiaviwango?

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vyotevil ivyobinafsishwa na wawekezaji wameshindwakuviendeleza au wamebadilisha matumizi nini hatma yake?

(i) Nini hatma ya Kiwanda cha Nyuzi Taboraambacho kinaozea pale na baadhi ya mashine zimeanzakung’olewa kwa wizi kinyemela huku Serikali iko kimya?

(ii) Kiwanda cha Urafiki – Ubungo tumeingia ubiana Mchina, nini kinaendelea pale. Tulikuwa tunazalisha kangana vitenge vya ubora mkubwa from Urafiki, leo hakuna,Serikali inatuambia nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyakazi wa Kiwandacha Karatasi, Mgololo (SPM) wamekuwa wanalalamika kwamiaka mingi kuhusu mwekezaji wa kiwanda hicho na Serikaliimeshindwa kuwasaidia.

(i) Mwekezaji wa kiwanda hicho aliponunuakiwanda hicho 2005 mkataba wake ulikuwa kuwalipawafanyakazi waliokuwepo kwanza kabla ya kuwapa ajirampya.

(ii) Mpaka leo hakulipa chochote kwawafanyakazi wale na wengine wamedai mpaka wamekufa,amegoma kulipa. Ni lini wafanyakazi hao watalipwa madaiyao? Wanaodai mpaka leo ni 750 na wengine wamekufabila kulipwa.

(iii) Mwekezaji analipa mshahara kwawafanyakazi baada ya siku 60 (miezi miwili) anatumia sheriagani?

Page 227: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

227

(iv) Mwekezaji anakata makato mengi kwenyemshahara wa wafanyakazi wanabakiwa na fedha kidogosana kwa nini?

MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongezaviongozi wa Wizara hii; Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu naWatendaji wengine. Pamoja na pongezi hizi napenda kutoamchango wangu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ubunifu ni muhimusana katika kuendesha sekta ya viwanda hapa nchini. Kwamfano, ili Kilimo Kwanza kifanikiwe katika nchi yetu lazimasekta ya viwanda ipewe kipaumbele kwa kubuni viwandavya kila aina kulingana na mazao yanayozalishwa katikaeneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE); napenda kuchukua nafasi hii kutoa ushauri kwa Wizarakuwa ipitie upya mtaala wanaoutumia kutolea elimu katikaVyuo vya Elimu ya Biashara (CBE) kwani ni wa zamani naumepitwa na wakati na hivyo ni ngumu kuhimili ushindanikwa wahitimu wa vyuo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mtaala unaotumika kwasasa kwa vyuo vingi hasa vinavyotoa Shahada ni mfumowa Umilisi yaani Competency syllabus. Ni mfumo unaoruhusuujifunzaji Shirikishi na unaofikirisha zaidi. Pia nashauri co-subjectkwa wanafunzi wote toka Stashahada/Cheti hadi Digrii(Shahada) liwe la Ujasiriamali ili kuwafanya wanafunzi wetuwanaohitimu katika vyuo hivi wawe wajasiriamali badalaya kutangatanga barabarani kwa kutafuta ajira za maofisini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la EPZ limekuwa nikama wimbo ambao hauna wasikilizaji. Naomba kuulizamaswali yafuatayo kuhusu EPZ.

(i) Tangu mpango huu ubuniwe, umeletamafanikio yapi hapa nchini?

Page 228: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

228

(ii) Wananchi waliotwaliwa maeneo yao hasawale wa Bagamoyo, Songea, Tanga, Kigoma, Bundawamelipwa fidia halali?

(iii) Kwa nini EPZ isiwe kwa kila Wilaya?

(iv) Hasara na faida za EPZ ni zipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna baadhi ya viwandavilibinafsishwa kwa wawekezaji uchwara, lakini hadi sasahakuna mafanikio yoyote au vimebadilishwa matumizi. Je,Serikali inatoa kauli gani kuhusu viwanda vya aina hiyo?Kwani Serikali haiwezi kuvifufua viwanda hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Viwanda vya Nguo;napenda kuishauri Wizara kufanya yafuatayo ili kuwezakujenga na kuimarisha Viwanda vya Nguo hapa nchini:-

(i) Angalau kila Mkoa/Kanda iwe na kiwandakimoja cha nguo.

(ii) Pamba ya hapa nchini itumike kuzalisha nguokatika viwanda hivyo.

(iii) Serikali na taasisi zake kama vile Jeshi, Polisi,wanafunzi na wafanyakazi wengine walazimishwe kushonanguo katika viwanda hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unyanyasaji na ubaguzi wawafanyakazi; kuna madai kuwa baadhi ya viwanda hasavile vinavyomilikiwa na Wahindi na Waarabu hapa nchinihuwabagua kimishahara, posho na marupurupu mengineyona pia kuwadhalilisha na kuwadharau wafanyakazi weusi(wazawa).

(i) Je, Wizara inalifahamu tatizo hilo?

(ii) Ni hatua zipi zinachukuliwa na Wizara kulindamaslahi ya wafanyakazi katika viwanda hivyo?

Page 229: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

229

(iii) Serikali ina mpango gani wa kuwawezeshawazawa kuanzisha viwanda vyao hapa nchini?

(iv) Viwanda vya kuchapa/uchapishaji hapanchini Tanzania vinakabiliwa na matatizo gani. Je, Serikaliimejiandaaje kutatua matatizo hayo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali mengineyanayohitaji utatuzi; Wizara inasaidiaje wafanyabiasharawadogo wanaokwenda katika nchi za China, Dubai, Turkey,Thailand, India, South Africa kwa kuwaongezea mitaji isiyona riba? Je, Serikali inafahamu kuwa wafanyabiashara haohunyanyasika sana kwa kudhulumiwa katika nchi hizo? Hatakama ni soko huria, kwa nini hatuna Tume ya Bei hapa nchini?Ni lini Tume hii itaanzishwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupanga ni kuchagua; nisababu zipi za msingi zilizopelekea TBS kuweka utaratibu wakukagua magari yaliyotumika toka nje ya nchi katika nchi zaDubai, Japan na Hong Kong? Je, nchi zingine zenye hudumahiyo ni zipi? Kwa nini kama kupanga ni kuchagua, tusikaguemagari hayo hapa nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuisemea Tarime; Serikali inampango gani mahsusi wa kuufanya ukanda wa Sirari,Wilayani Tarime kuwa ukanda maalum wa kibiashara?

(i) Je, Wizara imejipanga vipi kujenga masokoya kisasa na yenye hadhi katika mipaka ya nchi hususani eneola Sirari, Wilayani Tarime.

(ii) Je, wizara imejipanga vipi kuanzisha viwandavya kusindika mazao ya aina mbalimbali Wilayani Tarime?

(iii) Ni lini wataalam wa Wizara hii ya Viwandana Biashara watafika Wilayani Tarime kutoa elimu yaUjasiriamali kwa wananchi wa Tarime?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali ya fikra na utafiti;malighafi, nguvu ya umeme, rasilimali watu, mtaji, masoko

Page 230: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

230

ya uhakika, sera za Serikali, historia ya nchi na uimara waSerikali, ni baadhi ya mambo yanayoweza kushawishi ustawiwa viwanda hapa nchini. Je, Wizara imefanya utafiti wowotekuhusu suala hili na kama bado kwa nini haijafanya? Kamaimefanya inatoa au inakuja na nadharia gani kuhusu sektaya viwanda hapa nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Viwanda vya Nguo hapaTanzania vinakabiliwa na matatizo haya: uzalishaji ni ghalisana, ukosefu wa masoko ya uhakika, ubunifu mdogo, ufundiduni, miundombinu mibovu, rushwa na kukosekana kwa hakina mtaji duni, tatizo la umeme. Je, Serikali kupitia Wizara hiiinawashauri nini wamiliki wa Viwanda vya Nguo hapa nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ya Viwanda naBiashara inaishauri nini Serikali kuhusu uanzishwaji wa viwandavya kusafisha malighafi ya madini kama vile dhahabu hapanchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Viwanda vya Samaki hapanchini hasa Kanda ya Ziwa vinasaidiaje kukuza uchumi wanchi hapa nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mbao nyingizinazozalishwa kienyeji hapa nchini. Je, Serikali ina mpangogani wa kuanzisha Heavy Duty Timber Industries kwa kila mkoahapa nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Wizara hii imejipanga vipikuzalisha vitu/vifaa vinavyopendwa sana na watalii hapanchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda ni muhimusana ili kuinua pato la Taifa na la mtu mmoja mmoja. Sayansina Teknolojia ni muhimu ili kufanikisha suala la ukuaji waviwanda hapa nchini. Je, mpango wa maendeleo katikanchi yetu, umehusishaje sekta ya viwanda/ Science andTechnology ili kuinua pato la Mtanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, naungamkono hoja.

Page 231: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

231

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuCOSOTA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni za utekelezaji washeria ya COSOTA zinasema waziwazi kwamba, vituo vyatelevisheni na redio wanapaswa kulipa mirabaha kwawasanii kupitia COSOTA. Tatizo lililopo ni kwamba TCRAhawatoi ushirikiano kwa COSOTA katika kutoa taarifa.

Suala hili Waziri alipeleke Wizara ya Mawasiliano iliTCRA waagizwe kutoa taarifa za mapato ghafi kwa vituovya redio na televisheni kwa COSOTA. TCRA kugoma kutoataarifa ni uhalifu na kutenda kosa. COSOTA mara mojawatangaze zabuni kupata kampuni ya kufanya monitoringya airtime. Kuanzia tarehe 1 Julai, 2013 mirabaha ya televishenina redio ianze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, agizo la Waziri la kufanyamabadiliko ya kanuni za COSOTA Act litekelezwe mara mojaili kuhakikisha kuwa biashara ya miito ya simu (RBT)inaendeshwa kwa haki na mikataba ya wasanii isimamiwena COSOTA na mapato halali yapatikane kwa wasanii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sticker za TRA zitolewe kwaWasanii na Producers na sio kwa distributors. FCC izuieukiritimba dhidi ya wasanii unaofanywa na distributors.Distributors kamwe asiwe Producer. Tuangalie sheria zetuvizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile mapatoyakusanywayo na TRA kutoka kwenye stickers asilimia 50%ielekezwe COSOTA ili kuisaidia COSOTA kusimamia masualaya Hakimiliki. Hakuna haja ya sticker mbili i.e Hakigram naTRA ones. TRA waelezwe lengo la sticker sio mapato tu balikupambana na uharamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ya COSOTA iundweharaka sana ili kuweza kusimamia vema masuala yacopyright. Wajumbe wa Bodi wawe watu makini sana wenyenia ya dhati ya kuisaidia tasnia ya hakimiliki.

Page 232: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

232

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Kigoma.

(i) Soko la mpaka wa Kapunga (Tanzania/Burundi).

(ii) Kigoma SEZ nayo sijaona kipaumbele chake.

(iii) Focus: Viwanda vidogo vya usindikaji.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianzekwa kumpongeza Waziri na timu yake yote kwa uwasilishajiwa bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sekta ya Viwanda;ukisoma ukurasa wa nane wa kitabu cha hotubaunazungumzia kuhusu hali ya viwanda vyetu nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali halisi ya viwanda vyetunchini inasikitisha sana kwa kuwa pamoja na Serikali kuoneshakuwa imekua, lakini katika uhalisia wake ni mbaya. Kwa niniSerikali imebinafsisha viwanda, lakini haifuatilii kama kweliwawekezaji wanafanya biashara waliyokubaliana nayo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya wawekezaji wetukwenye sekta hii ya viwanda either ni matapeli au madalalikwa sababu kuna baadhi ya viwanda vyetu tokavimechukuliwa na wawekezaji ama vimefungwa kwa mudamrefu bila kufanyika chochote au mitambo imefunguliwawawekezaji wanabadilisha kabisa matumizi na viwandavingine vimegeuzwa maghala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa nijue kamaSerikali inatambua na kama ilishawahi kuchukua hatuayoyote kwa wawekezaji wa aina hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mpango ganiumewekwa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyakazi wanaouzabia ma-barmaids ambao wamekuwa hawana mikataba,wanapata matatizo makubwa katika kazi zao wakati waoni kama maajenti wa kuuza bia, kinywaji ambacho

Page 233: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

233

kimekuwa kikichangisha mapato makubwa sana katika nchiyetu, tumeshuhudia wenyewe waajiri wao wakiwanyanyasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maeneo ya EPZA; Serikaliilijitahidi kuhamisha na kutenga maeneo maalum kwa ajiliya uwekezaji, lakini maeneo hayo mengi yalikuwayanamilikiwa na watu binafsi yanahitaji fidia ili yawezekutumika kama ilivyokusudiwa. Kwa mfano, eneo lililotengwakatika Mkoa wetu wa Iringa lililopo katika Wilaya ya Kilololimetengwa muda mrefu sana. Eneo hili mpaka leolinawanyima fursa wananchi wa Iringa, eneo hilo kuwekezana kutengeneza ajira kwa wananchi wanaozunguka eneohilo. Nilipoleta swali Bungeni kuhusiana na jambo hiloniliambiwa tatizo ni eneo hilo linahitaji fidia. Je, lini sasamaeneo hayo wananchi watapewa fidia ili yaweze kutumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunao wawekezajimbalimbali ambao wamekuwa wakiwekeza wanafanyabiashara katika sekta mbalimbali. Serikali ina mpango ganiwa kuweka sheria ili watoe asilimia fulani ziweze kusaidiajamii?

MHE. STEPHEN M. WASIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mkoani Mara kuna EPZ ambayo ardhi imelipiwa fidia ambayoimegharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili. Baada ya kulipa fidiapale Bunda, hakuna hatua yoyote inayoendelea. Bilakuchukua hatua za kuendeleza ardhi, watu wanaozungukaeneo hilo wataanza kurejea kwa kuvamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO inahitajika sanakufanya kazi kama zamani. Tunao vijana wengi hawana kazi.Viwanda vidogo vinaweza kuwa suluhu. Tunaomba hudumaya SIDO katika Wilaya ya Bunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tufanye jitihada kufufuaviwanda ambavyo vilibinafsishwa lakini vikaachwa. Mfanowa viwanda hivyo ni Viwanda vya Korosho, Ngozi, Nguo,Nyuzi na kadhalika. Hata vinavyofanya kazi chini ya uwezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha na pia naungamkono hoja.

Page 234: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

234

MHE. NAOMI A.M. KAIHULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kwanza nioneshe masikitiko yangu makubwa kwawahusika wa ratiba kuipangia Wizara nyeti kama hii siku yakujadiliana kuipa siku moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kweli hawa watungajiwa hii ratiba wanaitakia nchi hii heri, maana sekta hii inagusamasuala ya wananchi mfano:-

(1) Ajira nyingi sana zinazalishwa kwenyebiashara.

(2) Masuala ya uchumi kama viwanda vikubwana vidogo viko huko.

(3) SIDO inayowasaidia wanyonge hasawanawake.

(4) Viwanda ni chanzo cha uzalishaji wa vifaavya kilimo kwanza.

(5) Fedha za kigeni na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi hili suala limetendeka,sasa iwe mwisho safari ijayo ni zaidi ya siku moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalolingezungumzwa kama muda ungekuwepo ni hili la ukosefuwa maono ya Serikali yetu hii. Badala ya kuweka Wizara hiikipaumbele cha kwanza ili i-generate (izalishe ajira, vifaa vyamkulima, umeme, maji, mavazi na kadhalika) sisi hapatunakubaliana na bajeti finyu inayopewa, hiki nini? Tunakuwakama vile ni Mataahira. Tafadhali sana ongezeni uchokozihuko mnakokwenda kudai maana watu hawaelewiwanafikiri huenda nyie watu wa Wizara ndiyo hamjuikupanga mipango na kutengeneza (projects michanganuo).

Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kusahau mamboyanayopaswa kufuatilia ambayo hayahitaji fedha baliusimamizi imara na msukumo wa dola ni hili la Chuo cha

Page 235: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

235

Biashara, Campus ya Dar es Salaam mpaka sasa ahueniimepatikana. Shukrani lakini jambo muhimu sana kwa ajiliya lengo la kupata elimu ili yasijetokea yale yaliyotokeakwenye Baraza la Mitihani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachohitajika ni majengona facilities zinazoendana na level, hadhi ya chuo hicho nahili litawezekana pale ambapo mipaka ya chuo itarejeshwatoka mikono ya mafisadi ambao ndiyo wanashikilia maeneoya chuo hicho. Mmoja anaendesha kiwanda ndani yamaeneo ya chuo. Mwingine anaendesha bar na kadhalikandani ya mazingira ya chuo. Inashindikana kwa ajili yawahusika wengine waliotoa na kupokea rushwa. Jambo hililishughulikiwe mara moja. Uongozi uliopo sasa naaminiunaweza kazi hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitangulize hayamachache kwanza.

MHE. MARIA I. HEWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awaliya yote naunga mkono hoja.

(i) Kuanzisha Kiwanda cha Kusokota Nyuzi zaPamba. Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania itaendeleakuwatesa wakulima wa pamba nchini kama haitawekamkakati wa kuwajengea kiwanda tajwa hapo juu hasaKanda ya Ziwa. Ni nini kikwazo? Ushauri wangu kwa Serikalini kujenga kiwanda hicho ili tujitegemee na hapo hapopamba ya Tanzania kupata thamani.

(ii) Kiwanda cha Saruji, Kanda ya Ziwa. Sipingimahali viwanda vya saruji, hapa nchini vilipojengwa hivi sasa,lakini ni lini ukanda wa ziwa utapata pia Kiwanda cha Saruji?Kiwanda cha Tanga kiko mbali cha Dar es Salaam na piaMbeya ni mbali sana. Ushauri wangu ni baada ya Mtwaraiwe Mwanza.

(iii) MWATEX, swali nauliza, je, Kiwanda tajwahapo juu kimeuzwa kwa mwekezaji? Je, kama kiliuzwa,wafanyakazi walioachishwa kazi nyakati hizi stahili zao

Page 236: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

236

zililipwa zote? Ushauri wangu kwa Serikali ni Serikali kuwamakini sana kuvibinafsisha viwanda nchini kwa sababuwawekezaji wengine hawana uwezo wa kuviendeshakiendelevu.

(iv) Mheshimiwa Mwenyekiti, kundi hili liitwaloMachinga ni kubwa kwa wingi wao kila mmoja wetutunawajua. Je, kama jamii tu inawafahamu, je Serikaliinasema nini juu ya kukosa kwao ajira au kujiajiri? Ushauriwangu ni Serikali kujipanga vizuri, ni jinsi gani uamuzi uliofikiwawa kuwajengea Machinga Complex ili waweze kuyatumiamaeneo hayo vizuri kwa mpangilio wa kitija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nawasilisha nanaunga mkono hoja.

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMANZINA: MheshimiwaMwenyekiti, nianze kwa kuunga mkono hoja na kumpongezaWaziri kwa hoja yenye matumaini. Wizara ya Viwanda naBiashara ni Wizara ambayo tunaitegemea sana kutufikishakwenye nchi ya ahadi, nchi yenye uchumi wa kati A semiindustrialized Economy.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Wizara itoesupport kubwa kwa NDC ambayo naiona iko serious katikakuanzisha na kufufua viwanda vilivyokufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuma cha Liganga naMakaa ya Mawe ya Mchuchuma ni rasilimali muhimu sana.Ni ukombozi mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba usimamie vizuri TBS,lazima TBS ifanye kazi yake kwa uadilifu na uzalendo. Nchiyetu haiwezi kuendelea kuwa a dumping place ya bidhaahafifu na hasa vyakula. Tunapukutika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO kama nilivyosemakwenye mchango wangu wa kauli ndiyo tegemeo lawananchi wa kawaida. Tusambaze viwanda vidogo hukovijijini huko Ngara na kwingineko. Nishaiomba SIDO kuja

Page 237: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

237

Ngara kutoa elimu ya ujasiriamali na ikiwezekana itusaidiemizinga ya kisasa tuweze kufuga nyuki kisasa. Hii ni katikaule utaratibu wa zao moja kwenye kila Wilaya. Ngara inazao la Kahawa lakini eneo ninalotoka la Rulenge, sisi hatulimikahawa, lakini tunaweza kufuga nyuki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kwakuanzisha mchakato wa Soko la Kimataifa la Kabanga hukoNgara. Najua soko hili linajengwa na Mradi wa DASIP kwaufadhili wa ADB, lakini najua Wizara ya Viwanda na Biasharainahusika na mchakato huu pia. Naiomba Wizara isaidiekuanzisha masoko ya mpakani ya Murusagamba na RusumoWilayani Ngara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Ngara inayopakana nanchi za Rwanda na Burundi na haiko mbali na nchi ya Kongo– Kinshasa, inafaa sana kama mahali pa kuanzisha utaratibuwa EPZ au Special Economic Zone. Naomba mtaalam ajeNgara kuona hali ilivyo. Ni muhimu pia kuiwezesha Ngarakufanya biashara na Rwanda na Burundi.

(i) Naiomba Wizara ianzishe Kiwanda chaKuzalisha Zana za Kilimo aina ya UFI au kumnyang’anyaKiwanda cha UFI Mwekezaji aliyebadilisha matumizi kwakuzalisha mabomba.

(ii) Kiwanda cha Mangula kilikuwa kinazalishaspare parts kwa ajili ya Viwanda vya Sukari pamoja naLandrovers. Kwa nini tusinunue mitambo tena na kukifufuabadala ya kumwachia mtu majengo kuanzisha shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, Hotuba yakoinaleta matumaini isiwe ni intentions tu. Tutumie mbinu yaBig Results Now. Tutekeleze huo mpango wako wa kuanzishaviwanda. Watumishi ambao hawawezi kubadilisha mindsetwawe fired. Muwekeane (performance contracts), mikatabaya utendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu la kuwawezeshawazawa kumiliki viwanda ni muhimu sana. Wazawa

Page 238: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

238

(Watanzania weusi) hawawezi kuendelea kuwa Manambakwenye nchi yao. Lazima wawe na BIG Stake kwenye uchumiwao siyo kuishia kupiga siasa (Superstructure) bila kumilikiEconomic Base. Viwanda vyetu ndivyo vitakavyotoa ajiraya uhakika kwa vijana wetu.

MHE. AMINA M. MWIDAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze mchango wangu kwa masikitiko makubwa sana nakubwa linalonihuzunisha ni kwa nini Wizara nyeti na muhimukama hii ambayo lengo lake kuu ni kukuza uchumi nakuongeza pato la Taifa na kuondosha umaskini wa kipatokwa wananchi, inapewa siku moja ya kuijadili bajeti yake.Kwa kweli hii si haki hata kidogo kwani inatunyima haki yamsingi ya kuijadili Wizara hii na kutoa maoni yatakayopelekeakuisaidia Wizara, kwa njia moja au nyingine. Kwa siku mojahii ni kama vile funika kombe mwanaharamu apite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine kubwa niupungufu wa bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yaWizara na hata hizo chache zinazotengwa pia hazifiki kwawakati, ukiangalia mpaka Februari, 2013 Wizara imepokeaasilimia 23 tu ya fedha zilizotengwa, hii ni aibu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwendo huu wakusuasua na ufinyu wa bajeti kwa Wizara na fedha kuchelewakufika kwa wakati. Hii inaonesha wazi kabisa kuwa Serikalihaina nia ya dhati ya mabadiliko wanayoyaongea ya kutokakatika uchumi wa chini wa kutegemea kilimo na kwendakwenye uchumi wa kati wa viwanda na biashara. Kusemaukweli kwa mwendo huu wa bajeti, hii itakuwa ni ndoto zaalinacha hazitakamilika abadani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tuna miradi yakimkakati mikubwa kabisa ya Tanzania China Logistic Centrena Bagamoyo EPZ, pesa zinazotakiwa kwa fidia tangumwaka 2010 ni bilioni 60 na bilioni 50, mpaka leo Serikali badoimelala. Nampa pole sana Mheshimiwa Waziri kwani hatauwe na degree sita za uchumi kama huna fedha kwenyeWizara yako hutaweza kufanya chochote. Ni lazima Serikaliitoe pesa hizi kama ilivyokwishaahidi kwani hatuko tayari

Page 239: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

239

kuwapoteza hawa wadau, kuna nchi kibao zinaukodoleamacho huu mradi wa logistic centre ni kama vile tunachezeashilingi chooni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo yaliyotengwakwenye baadhi ya mikoa kwa ajili ya uwekezaji EPZ/SEZ kamaTanga – neema, Mtwara, Kigoma na mikoa mingine.Tathmini ya maeneo hayo imefanyika tangu 2008/2009 kwaTanga ilikuwa ni bilioni 42.3, pesa ya fidia kwa kipindi hichompaka leo lazima itakuwa imeongezeka. Lakini wasiwasimkubwa ni lini hasa watalipwa hawa watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri suala hililinatugusa sana kwani wananchi waliohamishwa maeneohayo wameathirika kisaikolojia na wamerudi nyumakimaendeleo. Niiombe Serikali isiwahamishe watu tena kamahawajajipanga kwani ni hasara kubwa kwa Serikali nawananchi kwa ujumla. Najua kwenye Wizara yako kunawataalam wazuri kabisa, lakini tatizo kubwa ni fedha, hivyoSerikali lazima kutekeleza wajibu wake ili kuweza kufikiamalengo yaliyowekwa kwenye Wizara.

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nchiyoyote duniani hutegemea kukuza uchumi wake kwenyesekta ya viwanda, lakini pia nchi yoyote duniani hupanuaajira kwa wananchi wake kwenye sekta hiyo hiyo ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nchi yetu ikiwa navijana wengi ambao hawana ajira, Bajeti ya mwaka 2012/2013, iliidhinisha Shilingi Bilioni 60 kwa ajili ya kulipia fidia yamakazi ya wananchi kwenye eneo la Kurasini, eneo ambalolinatarajiwa kujengwa mji wa viwanda China – LogisticCenter.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko hadi mwakawa fedha umekwisha, Serikali iliipatia Wizara kiasi cha ShilingiMilioni 550 tu katika bajeti hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwekezaji akifuatiliakwa Serikali au Wizarani kujua kwamba tayari wamekamilisha

Page 240: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

240

kulipa fidia eneo hilo la mradi, tukumbuke kwamba zipo nchiambazo zinaunyemelea mradi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iwapo Serikali itashindwakutoa fedha hizo kwa wakati, mwisho mwekezaji huyo bilashaka mradi huo ataupeleka kwa wenginewanaounyemelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, endapo mradi huu ambaounatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 25,000 kwa Watanzania, basidunia itatucheka, lakini pia Watanzania watafahamukwamba Serikali yao imekuwa ikiwafurahisha kwa manenomazuri, lakini haina nia ya dhati kuwasaidia na kuwakomboakiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa Serikali hadi sasaimeshindwa kukamilishwa kulipa fidia ya Bilioni 60 na kwakuwa fidia hiyo hadi sasa imeongezeka na imefikia Bilioni 94.Je, Serikali kweli itaweza kulipa nyongeza hiyo ya thamaniiliyoongezeka na je! Serikali iko serious na mradi huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012 TBS ilipatashutuma na lawama nchi nzima hadi kupelekea aliyekuwaMkurugenzi wake Charles Ekerege kusimamishwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shutuma hizo na lawamakwa upande mmoja sawa lakini kwa upande mwingineshutuma hizo na lawama zinafaa zielekezwe moja kwa mojakwa Serikali iliyoko madarakani, kwa sababu haiingii akilinina wala haifanani nchi kama Tanzania yenye watu zaidi yaMilioni 40 badala yake TBS iwe na wafanyakazi 197 na iwezekudhibiti bidhaa zenye ubora nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na upungufu wawafanyakazi mwaka 2010/2011, Shirika liliomba kibali chakuajiri wafanyakazi 35, lakini Serikali ilitoa kibali cha kuajiriwafanyakazi 18 tu. Hata hivyo, kibali hicho hakikutekelezwa,Serikali ilisitisha ajira, mwaka uliofuata shirika liliombanyongeza ya wafanyakazi 15. Ombi hilo halikufikiriwa kabisana mwaka wa bajeti 2012/2013, Shirika liliomba tena kibali

Page 241: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

241

cha kuajiri wafanyakazi 32 tu. Hata hivyo, kibali hichohakikutekelezwa kwa sababu Serikali ilisitisha ajira mweziFebruari mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitamwomba MheshimiwaWaziri atakapokuja kufanya majumuisho atuambie ni lini sasaShirika la TBS l itapatiwa wafanyakazi wa kutosha il iwasilalamike kila wakati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukiona jinsiShirika linavyofanya kazi, lakini hata hivyo linashindwa kufanyakazi kwa ufanisi zaidi kutokana na upungufu huo. Ni muhimusasa Serikali kuipatia TBS rasilimali watu ya kutosha ili wafanyekazi yao kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majirani zetu Kenyawamefanikiwa sana kwenye Shirika lao la Viwango KEBS, kwanini wamefanikiwa, Serikali ya Kenya imeliwezesha Shirika lakekwa kulipatia wafanyakazi zaidi ya 1,000. Vile vile Kenyaimefanikiwa sana na mfumo wa sheria ya PVOC. MheshimiwaMwenyekiti, nini maana ya PVOC? PVOC ni mpango waudhibiti ubora ambao hutumika kuthibitisha kuwa bidhaazinazoingizwa nchini kutoka nchi mbalimbali zinakidhimatakwa ya viwango kabla ya kusafirishwa kwenda nchihusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri na niseme kuigajambo jema si dhambi. Kwa hiyo, tuangalie ikiwa Kenyautaratibu wanaotumia wa kukagua bidhaa zinapofika nchiniunawasaidia, tofauti na sisi bidhaa zinazokaguliwa nje yanchi, basi tuige, kuiga jambo jema si dhambi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimetoa ushaurihuo, nimetoa ushauri huo kwa kuzingatia kauli ya MheshimiwaNaibu Waziri wa Viwanda na Biashara hapa Bungenialipokuwa akij ibu swali aliposema Mawakala wetuwanaokagua bidhaa nje ya nchi sio waaminifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangiakuhusiana na maendeleo ya viwanda. Mheshimiwa Waziri

Page 242: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

242

Mkuu hivi karibuni alizungumza kwamba, nchi yetu iko kwenyemapinduzi ya viwanda. Viwanda vyetu vidogo vidogovimekuwa vikiathiriwa sana katika uzalishaji wake na tatizola umeme, umeme limekuwa ni tatizo kwa sababu umemeumekuwa ukikatikakatika kila baada ya masaa kadhaa,kutokana na tatizo hilo, viwanda vimekuwa vikisimamishautendaji wake wa kazi kwa muda unaotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mapendekezo yangu kwaWizara kushirikiana na Wizara ya Nishati kutatua tatizo laumeme ili kuweza kuvikomboa viwanda vyetu vidogovidogo. Vile vile Serikali ilitamka wazi kuwa imeandaamkakati wa kuendeleza sekta ya nguo na mavazi il ikuboresha teknolojia ya viwanda vya nguo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili mradi huo uweze kufikiamalengo yake ni lazima Serikali ifanye juhudi za makusudi zamiradi ya makaa ya mawe, lakini kwa umeme huu huu wakukatikakatika kila wakati malengo haya hayatafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango na mikakati hiiambayo utekelezaji wake unahitaji mambo mengi kufanyikakwa kutegemea eneo lingine basi mashirikiano katikakufanikisha hili uwekewe mkazo zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuishukuru Serikalina Wizara hii husika kwa kufanikisha ununuzi wa mashine zauchimbaji makaa ya mawe. Hii inaweza kutusaidia napengine kuelekea mahali ambako Watanzania wangependatuwe. Nashukuru.

MHE. HAMOUD A. JUMAA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuanza kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi warehema kwa kupata nafasi hii ya kuchangia Hotuba ya Bajetiya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii piakumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa Hotuba yake ya Bajetinzuri na yenye kutekelezeka. Hakika kwa mipango hii Serikali

Page 243: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

243

itatatua matatizo yaliyopo katika sekta hizi muhimu naikumbukwe sekta hii ina mchango mkubwa katika kukuzauchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kuchangiahoja hii iliyokuwa mbele yetu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais alituahidikujenga soko la kisasa Mlandizi na Kiwanda cha KusindikaNyanya, lakini mpaka leo hakuna utekelezaji wa aina yoyote.Tunaomba maelezo kutoka kwa Mheshimiwa Waziri waViwanda, Biashara na masoko atuambie hizi ahadi zaMheshimiwa Rais zitatekelezeka lini, kwani ni muda mrefusasa na wananchi wa Kibaha Vijijini bado wanaendeleakupata hasara kwa kukosa mahali pa kusindikia mazao yaokipindi chote hiki. Pamoja na uhitaji wa soko hilo, kwaniikumbukwe kwamba tunapochelewesha miradi hiitunapoteza mapato ambayo yangetokana na ushuruambao ungetozwa kutokana na miradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Serikali yetukufanya juhudi kubwa katika sekta hii lakini bado inakabiliwana changamoto nyingi, changamoto zote hizo zinafanyabidhaa zetu kuwa na bei kubwa hivyo kumuumiza sanamwananchi wa kawaida. Pia kuporomoka kwa sarafu yetukatika soko la dunia limekuwa kikwazo kikubwa, piaifahamike kwamba matumizi ya fedha za kigeni yanaathirisana uchumi wetu na watu wetu pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itilie mkazona kusimamia hilo na kukataza biashara ndani ya nchizifanyike kwa fedha za kigeni na badala yake shilingi yetundio itumike katika matumizi yote. Kufanya hivyo kutaletaheshima ya sarafu yetu na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile gharama kubwa yamalighafi na vipuri toka nje, kupanda kwa bei za mafutayaani bidhaa za petrol, hapa kuna changamoto nyingi sanakwani kwa nchi yetu imekuwa kawaida kwa mwaka mmoja,bei hizi za mafuta kubadilika kila mara bila kuwa na sababu

Page 244: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

244

za msingi, ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani ambazohawana bandari na wanakuja kuchukua mzigo wa mafutahapa kwetu, lakini wamekuwa wakisimamia bei moja yanishati hii ya mafuta kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni changamoto kubwana napenda kuishauri Serikali iweke mikakati madhubuti,kwanza ya kuzuia hii milipuko ya bei na zaidi kushirikishawadau wote kutafuta mbinu za kuwezesha kutatua matatizohaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi ambazo ziko juukiuchumi zilifanya juhudi kubwa kuwa na sera nzuri yaviwanda, kuwekeza katika viwanda na kuboresha sekta hiyo,siku zote viwanda huleta faida nyingi ukiachilia mbali kukuzaajira kwa watu wake, lakini kikubwa ni ukuaji wa uchumiwa nchi, viwanda vyetu vingi vimekufa yamebakia magofutu, lakini tuna uwezo wa kutafuta wawekezaji kuja nchinikuwekeza katika viwanda. Ifike mahali kama Taifa tuwe namkakati maalum wa kukuza viwanda nchini na utiliwemkazo mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuikumbushaSerikali kutokuwasahau wenye viwanda vidogo vidogo tenakuwawezesha ili wainuke. Miaka ya hivi karibuni kumetokeawabunifu wengi ambao ubunifu wao unahusu zaidi viwanda,lakini tumeishia tu kuwasifu na kuwaacha kama walivyo.Naishauri Serikali kuwajali na ikiwezekana katika Bajeti yaViwanda, Biashara na Masoko watengewe bajeti yao ilitupate wataalam wetu wenyewe katika fani ya kugunduavitu na kutengeneza. Hii itailetea sifa nchi yetu na kuzidikututangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kibaha Vijijini tunaupungufu wa viwanda, viko vichache, tunaiomba Serikalikuangalia hilo, pale panapotokea mwekezaji kuja kuwekezakwenye sekta ya viwanda, basi Serikali iwaelekeze Kibahakwani tuna maeneo makubwa na ya kutosha kujengwaviwanda vikubwa na itasaidia upatikanaji wa ajira ambaondio kilio cha vijana nchini.

Page 245: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

245

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunaiomba Serikalikutujengea Chuo cha Ufundi katika Kata ya Kwala auMagindu ili kuweka mazingira yatakayowezesha vijanakupata mafunzo na kuanzisha viwanda vidogo vidogovitakavyotumia rasilimali zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualala mazingira, hapa nagusia zaidi viwanda vyetu nchiniambavyo havifuati Sheria ya Mazingira nchini. Kufanya hivyoni kutotii mamlaka na Sheria zilizopo, naomba Serikali kutiliamkazo kwenye hilo kwani Sheria zipo na wasimamizi wamazingira wapo pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, wafanyakaziwanaofanya kazi katika sekta ya viwanda wamekuwawakilalamikia suala la kufanya kazi bila vitendea kazimaalum ambapo baadaye hupata maradhi ama kuathirikana kuishia kutelekezwa na waajiri wao pasipo msaadawowote huku hao wamiliki wa viwanda hivyo wakijua kabisakutokumpatia mfanyakazi vifaa maalum (safety equipments)ni kosa. Naishauri Serikali kufanya ukaguzi wa kila marakwenye viwanda hivi na adhabu kali kutolewa kwa wotewatakaobainika kutenda makosa kama hayo ili kuwalindawatu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumaliziakuikumbusha Serikali kuwa katika Bunge li l i lopitanilizungumzia kuhusu Serikali kutenga eneo maalum lakuegeshea magari yote yanayoingia nchini hata yale ya transitsehemu moja ili kuwezesha Serikali kuingiza mapato kupitiamradi huo. Nilipendekeza mradi huo ujengwe Kibaha kwanisisi tuna maeneo ya kutosha na pia itasaidia kupunguzamsongamano wa sehemu za kuuzia magari mjini, kwani hivisasa imekuwa kero, kila baada ya kilomita mbili utakutanana yard ya magari zilizozagaa mjini na kusababisha mandharimabaya ya miji yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza pia aina hiyoya uuzaji magari mitaani uwekwe katika mfumo huu wakuyatengea sehemu moja kama wafanyavyo nchi nyingine,

Page 246: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

246

hii itasaidia pia kuliingizia pato Taifa kwani kupitia mradi huoambao utakuwa chini ya Serikali wadau watakuwa wakilipiagharama na hivyo kupata fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda naBiashara. Maendeleo ya kiuchumi yoyote dunianiyanategemea kwa kiwango kikubwa uwekezaji katika sektaya viwanda sambamba na uwekezaji wa hali ya juu katikauzalishaji wa nishati ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sana nchiyetu kwa kipindi kirefu imekuwa haitilii maanani katikauwekezaji wa viwanda nchini baada ya viwanda vingivilivyoanzishwa baada ya nchi yetu kupata uhuru kuwavimekufa na kubinafsishwa, viwanda vil ivyokuwavinamilikiwa na umma wa Watanzania. Baada ya nchi yetukuruhusu na hatimaye kufungua milango tayari kwakuondokana na mfumo wa uchumi hodhi na kuingia katikamfumo wa soko huria hapa nchini, mambo yamebadilikakabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi hikitumeshuhudia changamoto mbalimbali ikiwemo ujio wawawekezaji kutoka nje ya nchi wenye shahada za kuwekezakatika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo sekta yaviwanda, madini, kilimo na sekta za ujenzi. Sekta ya viwandana biashara inategemea sana maendeleo katika sektazingine kama vile maendeleo ya sekta za usafirishaji za reli,bandari, barabara, mabenki, huduma za bima, maendeleoya rasilimali watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza kwa dhatiWizara ya Viwanda na Biashara kwa kuchukua hatua nakuanza utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa makaa yamawe na hatimaye kuanza kwa shughuli za uzalishaji wachuma huko Mchuchuma na Liganga.

Page 247: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

247

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushirikiano baina ya Shirikala Maendeleo la Taifa la NDC na wawekezaji wa Kampuniya Kichina, hatua hii ni hatua sahihi na ya kupigiwa mfano,kwani Mwenyezi Mungu katujaalia madini haya muhimu yamakaa ya mawe na madini ya chuma. Makaa ya mawejumlisha madini ya chuma sawasawa na chuma cha pua naumeme. Kwa lugha nyepesi ni kwamba, uchenjuaji wamadini ya chuma unategemea sana uwepo wa makaa yamawe ambapo tunapata vyote katika eneo moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupatikana kwa chumakutasaidia sana mapinduzi katika sekta ya viwanda nakusaidia ujenzi wa miundombinu ya reli na madaraja nabandari, pia majengo na vipuri vya mitambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: MheshimiwaMwenyekiti, kuhusu TBS na TFDA; TBS iko chini ya Wizara yaViwanda na Biashara wakati TFDA iko Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBS kazi yake ni kuhakikishaubora wa vifaa na bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula hasapacked food za ndani na nje ya nchi ili kulinda afya ya walajina usalama wa walaji na kulinda mazingira ya nchi yetu.TFDA inafanya kazi ya kusimamia na kudhibiti usalama naubora wa dawa na chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maoni yangu vyombohivi vilivyo chini ya Wizara tofauti vifanye kazi pamoja, hivyoWizara hii ya viwanda na biashara wakae na Wizara ya Afyaili TFDA iwe Idara mojawapo katika Wizara ya Viwanda ikiwachini ya TBS iwe chini yake kwa sababu kazi zake ni mojazinafanana. Hiyo itasaidia ufanisi wa kazi kwani vyombo hivivitakuwa pamoja kudhibiti ubora na usalama wa bidhaaza nchini na zitokazo nje ya nchi, kwani yapo pia malalamikokuwa TBS haifanyi kazi yake ipasavyo kwani sababu niupungufu wa wafanyakazi na Serikali ilikuwa imesitisha zoezila utoaji vibali vya ajira 2010/2011.

Page 248: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

248

Mheshimiwa Mwenyekiti, shirika liliomba kibali chakuajiri wafanyakazi 18 hawakutekelezwa, 2011/2012 shirikaliliomba wafanyakazi 15, ombi halikutekelezwa na 2012/2013,shirika liliomba tena wafanyakazi 62 walipata kibali cha kuajiri32 tu. Hivyo basi, TBS na TFDA wakifanya kazi pamojawatashirikiana wafanyakazi walionao ili mradi tu wafanyiwemafunzo ili waweze kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu elimu ya ujasiriamalikatika kuendeleza biashara; nashauri elimu hii itolewe hasakwa wale akinamama waliojiunga pamoja kufanya shughulizao za biashara na waliopo katika viwanda vidogo vidogo(SIDO) ili kuwasaidia wawe na ufanisi katika shughuli zao.Hali hii itapunguza umaskini kwani watapata faida ya kaziyao wakiwa na ujuzi wa elimu ya ujasiriamali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu EPZ na SEZ; Serikaliituambie eneo la EPZ/SEZ lililotengwa wananchi watalipwalini fidia na maeneo hayo kuanza kutumika kamailivyokusudiwa? Kwani wananchi wanashindwa kuendelezashughuli zao katika maeneo yale kwani inajulikana Serikaliimeshayachukua kwa ajili hiyo. Lini miundombinu yakiuwekezaji itajengwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri maeneo hayoyatumike kama ilivyopangwa ili kuongeza uchumi nakuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo husika. Vile vilemaeneo yakikaa muda mrefu bila kutumika yanawezakuvamiwa tena na wananchi kwani wataona hakunakinachoendelea.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naipongeza Wizara kwa Hotuba nzuri inayooneshania ya kuinua sekta muhimu ya Viwanda na Biashara. HakunaTaifa lolote duniani linaloweza kupiga hatua ya maendeleobila kuimarisha sekta ya Viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya kilimo ambayoinaajiri asilimia themanini (80%) ya Watanzania, haiwezikupiga hatua kama hakuna viwanda, kwa sababu viwanda

Page 249: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

249

ndiyo vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao ya kilimoili tuweze kupata bei nzuri ya mazao yaliyoongezewathamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa viwanda ukokatika kutatua tatizo la ajira linalokabili vijana wetu wengiwa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokuwa hatunaviwanda, maana yake ni kwamba, tunapeleka ajira hukuambako tutauza mazao yetu yakiwa ghafi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni kwa zao lapamba, asilimia kubwa ya zao la pamba tunalolima hapanchini, tunauza nchi za nje zikiwa katika hali ghafi na kwakufanya hivyo, maana yake kwanza tunapata bei ndogo yapamba na pili tunapeleka ajira nje ya nchi kwa maanapamba ikifika huko nje ya nchi ndiyo kuna viwanda vya nyuzina nguo na bidhaa nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli tunatakakusonga mbele kimaendeleo na kiuchumi hatuna namna, nilazima tuwe na mkakati wa makusudi wa kuwa na viwandavya kati na viwanda vikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kumshukuru Mungu sana kwa kunipa fursa hii yakuchangia, kutoa kero na kuwasilisha mapendekezo namaoni yangu kuhusiana na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bidhaa bandia;mbali na juhudi zinazooneshwa na Serikali kwa kupambanana bidhaa bandia bado hali siyo nzuri na hali inatokana naukubwa wa kazi ikilinganishwa na uchache wa watumishi,vifaa na fedha za kuifanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli tunayo niathabiti ya kuzuia bidhaa bandia hapa nchini, basi ipo haja

Page 250: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

250

ya kuongeza nguvu na pia sheria zetu kuhusu bidhaa bandiana adhabu ziangaliwe upya, huku kikosi kamili cha ufuatiliajiwa kazi za udhibiti kuundwa upya na kipewe uwezo kamiliwa kuzuia, kukamata na kushtaki huku maabara zikijengwakatika kila Entry Point na bandari, mipaka na viwanja vyandege ili kazi hiyo iweze kuwa na tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda; nipende tukuleta masikitiko yangu kuhusu viwanda vya umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vilijengwa siyo tukupunguza umaskini kwa kutengeneza faida, bali kutoa ajiraambalo ndio lilikuwa lengo kuu la Serikali ya awamu yakwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima kama Taifa tuangalieupya jinsi gani ya kuanzisha tena viwanda vingine vya ummakwa ajili tu ya kutoa ajira kwa wananchi ambapo faida yakehaipo Direct kwa Serikali ila kwa wananchi na hii itapunguzasana, uhalifu na itapunguza lawama kwa wananchiwanaolaumu Serikali kwa ukosefu wa ajira. Pia badoinawezekana kujenga na kuvikopesha Vyama vya Ushirikana kuweka taratibu maalum ambazo kimsingi zitazuia nakuepuka ubadhirifu. Bado tunayo nafasi ya kujenga viwandavichache kwa majaribio kabla ya kulifanya zoezi hilo nchinzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalosikitikanalo ni kuhusu biashara za maua ya plastic na pikipiki nabaadhi ya bidhaa zinauzwa na wachuuzi wa Kichina hapanchini. Lazima kuwe na tofauti ya wanaozalisha nawafanyabiashara. Serikali ihamasishe wawekezaji wa Kichinawaje hapa nchini kujenga kiwanda kuliko kuleta bidhaa nawao kuja kuziuza hapa nchini. Ikiwezekana basi itungweSheria itakayoweza kabla ya bidhaa kuingizwa na mwekezaji,basi kwanza uwezekano wa kuweka viwanda hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukaguzi wa magari(TBS); bado napenda kushauri sana ukaguzi wa magariufanyike nje na ndani ya nchi ili kuwe na ushirikiano na

Page 251: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

251

tuangalie jinsi ya kuokoa fedha za Watanzania zinazokwendanje ya nchi kwani taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali (CAG) ulionesha katika USD 8m ni 2.2mpeke yake ndio fedha iliyokuja hapa Tanzania, hiyo inaoneshabado fedha nyingi sana za kigeni huenda au hubaki nje yanchi na hii siyo nzuri kwa uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu waliokuwawafanyakazi wa MUTEX; waliokuwa wafanyakazi wa MUTEXwaliahidiwa humu Bungeni kuwa wangepewa nyongeza kwafedha ambayo walishindwa kuipokea kwa kuwa ilikuwa nikidogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu 834 ukiwagawanyashilingi milioni 70, kila mtu atapata shilingi 83,933/= ambapohaitoshi hata nauli ya mtu mmoja nauli ya kurudi walipotokahuko makwao kuja Musoma (MUTEX) kwa kulitumikia Taifakama watumishi wa kiwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua juhudi ya Wizaraya kufuatilia fedha za malipo ya waliokuwa watumishi wakiwanda hiki. Napenda sana kuiomba Serikali ikae nakuuthamini mchango wa waliokuwa wafanyakazi wa MUTEXili walipwe na waondokane na adha hiyo ya kuilaumu Serikali,kwani sasa wamejenga chuki kubwa sana dhidi ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mategemeo yangu katikamajibu ya Mheshimiwa Waziri au Naibu Waziri ataeleza ni linifedha ile itaongezwa ili kupunguza hasira ya waliokuwawatumishi wa MUTEX.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kuongelea Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Tanzania. Vipo vyuo vingi vya binafsi katika nchi, lakiniSerikali inacho chuo kimoja ambacho kipo Dar es Salaamna kina Matawi Mwanza na Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo hiki kipo katika hali

Page 252: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

252

mbaya ukilinganisha na chuo hiki na Chuo cha Homboloambacho kinamilikiwa na TAMISEMI. Ukifika katika Chuo chaBiashara, Dar es Salaam huwezi kuamini kama kinamilikiwana Serikali. Chuo hiki kipo katikati ya Jiji, lakini kinatia aibu,madarasa ni ya hovyo. Cha kushangaza sehemu ya eneolake limeporwa na Wahindi na wamefanya kiwanda karibuna madarasa na Walimu na wanafunzi hupata kadhia kubwawanapofundisha. Ni kwa nini Serikali imeruhusu ardhi ya chuohiki kuchukuliwa na kuminya nafasi ya kujipanua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ikitazama chuo hikikiwe na hadhi kulingana na elimu inayotolewa pale, kamaTAMISEMI wameweza Serikali Kuu inashindwa nini? CBEukusanyaji ada zaidi ya bilioni 12, lakini wanashindwakujenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee viwanda fekivilivyozagaa nchini. Vipo viwanda vya kutengeneza bidhaambalimbali kama mabati, gypsum board, na kadhalika.Viwanda hivi viko chini ya viwango na katika mazingiramabovu vingine viko katika nyumba za watu (makazi)viwanda hivi ni vya Wachina. Cha kushangaza zaidi viwandahivi wamiliki wamepewa vibali vyote kama TBS, Leseni, TICna kadhalika, Serikali inasema nini juu ya viwanda hivi.Pamoja na kuwa chini ya viwango, lakini pia wafanyakazikatika viwanda hivi ambao ni Watanzania wanafanya kazikwa malipo duni na katika mazingira yasiyofaa.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nachukua fursa hii kushauri au kuchangia kwa maandishikatika Wizara hii ya Viwanda na Biashara, ushauri wangukimsingi umelenga katika maeneo muhimu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa la viwanda nabiashara Tanzania linasababishwa na mambo mengikutokuendelea, lakini suala la gharama za umeme na ukosefuwa umeme bora na wa kutosha ni sababu tosha za kuzorotakwa ukuaji wa uchumi katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokuwepo na umeme wa

Page 253: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

253

uhakika na bora na gharama kubwa za nishati hiyo zimefanyaviwanda vyetu vichache vilivyopo vishindwe kujiendeshavizuri na hivyo vingine kufa na vingine kuzalisha bidhaaambazo baada ya uzalishwaji bidhaa hizo zinauzwa kwabei kubwa na kupunguza uzalishwaji kwani watu wengiwenye kipato cha chini na cha kawaida wanashindwakununua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, ili kuwepo naufanisi katika viwanda na biashara zetu, ni lazima sana ufanisiwa kutosha katika sekta ya nishati uzingatiwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu mwinginekatika viwanda na biashara ni Serikali kutambua kuwa, ribaza mabenki yetu ya kibiashara ni kubwa sana, hivyo kukatishatamaa wafanyabiashara wa ndani ambao wana malengoya kuanzisha biashara zenye sura ya kimiradi; kama viwandana biashara kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu sana Serikalikuangalia uwezekano wa kusaidia suala la riba hasa kwaWatanzania wanaotaka kuanzisha viwanda na biasharakubwa kubwa katika Taifa letu, riba katika mikopo imekuwani kikwazo kikubwa sana kwa uanzishwaji wa viwanda.Kwani ilivyo sasa kiwango cha riba kinachotozwa ni kikubwasana na hivyo kuvunja moyo watu wenye nia na malengoya kuanzisha viwanda vidogo vya kati na vikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashaka yangu makubwasana yako pia kwenye mradi wa Kurasini Logistic Hub ambapomtazamo wangu unaona mradi huu hautaweza sanakusaidia kuendeleza nchi yetu hasa katika sekta ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kurasini Logistic Hubukitazama malengo yake kwa ndani utaona ni kwa namnagani mradi huu utakavyosaidia kuua hata viwanda vichacheambavyo vitakuwepo, kwani kuwa na kituo kikubwa chausambazaji wa bidhaa kutoka China tena bidhaa ambazozimekwishatengenezwa ni hatari kubwa kwa uchumi waviwanda vyetu.

Page 254: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

254

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha General Tyreutaratibu wa kukifufua umeanza na kimsingi napongezajuhudi hizi lakini cha kusikitisha ni kwamba, wakati kiwandahiki kinafungwa kuna wafanyakazi wengi walisitishwa kazi,lakini mpaka leo wengi wao hawajalipwa mafao yao. Hivyo,naitaka Serikali iwe na utu kidogo na kufanya juhudi za kulipawatu hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwakuomba Serikali kuwatazama wafanyabiashara wadogo(Machinga) kwa umakini na kuwatambua pia kamawazalishaji katika Taifa lao.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kuwasilisha kwako mchango wangukatika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda naBiashara kuhusu makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi yakekwa mwaka 2013/2014 kama ilivyowasilishwa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naanza kwakumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa uwasilishaji wake mzurina wenye weledi uliotukuka. Pia nampongeza Naibu Wazirikwa uwezo mkubwa alioonesha katika utekelezaji wamajukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya viwanda nchiniimekuwa ngumu sana hasa vile ambavyo vilibinafsishwa kwataasisi na wafanyabiashara. Vingi kati ya viwanda hivivimebadilishwa matumizi havijaendelezwa kamailivyokusudiwa na Serikali. Naishauri Serikali iangalie upya seraya kutowekeza kwenye viwanda. Ni wakati mzuri sasakuwekeza katika Viwanda vya Ubanguaji wa Korosho,Nyama na Nyuzi. Ikiwezekana wale ambao wameshindwakuendeleza wanyang’anywe ili Serikali iwekeze mtaji wakuviendesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na viwandavikubwa kuhitaji mtaji mkubwa katika uwekezaji, naishauriSerikali iweke mkazo katika viwanda vidogo vidogo. Hivyo,SIDO wapewe mtaji wa kutosha ili kuwekeza na kuinua sektaya viwanda nchini.

Page 255: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

255

Mheshimiwa Mwenyekiti, juhudi za makusudi zifanyikekuhakikisha kuwepo na udhibiti wa bei za bidhaa ili kuondoahali ya mfumuko wa bei usio na maelezo. Sheria ya mapatoIncome Tax Act, Cap 332 kifungu 33 kinazuia wafanyabiasharakupata Super Profit. Hivyo ili kumlinda mtumiaji ni lazimaSerikali iweke udhibiti wa bei za bidhaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali isimamie ipasavyowafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuvamia na kushirikikatika biashara ndogo ndogo, kama maduka ya bidhaaambapo Watanzania wana uwezo mkubwa wa kuzifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Mizani apewemtaji wa kutosha ili aweze kushiriki ipasavyo katika uwekezajimpya katika sekta ya gesi. Hii itasaidia sana Serikali katikaudhibiti wa mapato na bidhaa zitokanazo na gesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono jitihada zakuanzisha kiwanda cha kuua mazalio ya mbu kwa ushirikianowa NDC na Serikali ya Cuba, jitihada ziongezwe ili ujenzi wakeukamilike kwa haraka ili vita dhidi ya malaria iwe rahisi nakuwapunguzia wananchi mzigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri waViwanda na Biashara kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya viwandainategemewa sana kukabiliana na tatizo kubwa la ajiranchini. Hata Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa anafunguaBunge hili 2010 alionesha nia ya kukuza sekta hii ili kuwezakukabiliana na tatizo hilo na kupata fedha za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipo viwandavilivyochukuliwa na wafanyabiashara/wazalishaji kwamakusudi ya kuendeleza uzalishaji. Cha kusikitisha bado vipoviwanda ambavyo havifanyi uzalishaji kufuatana namapatano na Serikali. Namwomba Mheshimiwa Waziri

Page 256: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

256

anisaidie wakati anahitimisha ni viwanda vingapi havijaanzauzalishaji kufuatana na makubaliano na ni kwa nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera ya Serikali ni kuinuaviwanda vya nchini kwa kununua vitu vinavyozalishwa hapanchini ili kuvijengea uwezo wa kifedha. Kinyume na hili,nataka Mheshimiwa Waziri atoe kauli leo, ni kwa nini Serikalina taasisi zake hupendelea kununua vifaa vinavyotoka njeya nchi mfano, samaki, magunia, na kadhalika angali vituvyote hivi vinapatikana hapa nchini. Ni kwa nini hifadhi yachakula inanunua magunia toka nje ya nchi wakati wapowazalishaji wa magunia nchini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya bidhaa zaviwanda kama vile mabati, misumari, nondo, samakivinapanda bei mara kwa mara, jambo linalowatesa sanawananchi katika ujenzi wa nyumba. Hata hivyo, hali hiihufanya kodi za nyumba kuwa juu na kuwaumiza sanawapangaji walio wengi. Namshauri Mheshimiwa Waziri naSerikali kuunda Tume ya Bei itakayomlinda mlaji i l ikuondokana na tatizo la kupanda bei za vifaavinavyozalishwa viwandani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusupongezi kwa Mheshimiwa Waziri/Serikali; napendakumpongeza Mheshimiwa Waziri na watendaji wake waWizara kwa kazi nzuri wanayofanya katika Wizara hii muhimukwa maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu soko la KimataifaMakambako; soko la Kimataifa la Makambako liliahidiwakuanza mapema sana, lakini hadi leo hakunakinachoendelea. Aidha, wananchi ambao wapo kwenyeeneo hili wanadai fidia, cha kushangaza hadi leo hakunafidia yoyote iliyotolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri

Page 257: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

257

atoe maelezo ni lini soko hili litaanza kujengwa na kufanyana lini wananchi hawa watalipwa fidia zao. Soko hili nimuhimu sana katika uchumi wa nchi na nyanda za juu Kusini.Makambako ni mpitio wa mikoa yote ya Kusini.

MHE. MAGALLE JOHN SHIBUDA: MheshimiwaMwenyekiti, Hotuba ya Wizara hii ni maelezo mema yakutambulisha azma njema kwa ustawi wa maendeleo yauongozi wa utawala bora wa maslahi jamii ya mchakatowa uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itambulishena iwaarifu Watanzania inatekeleza juhudi zipi za kuipatiasoko pamba mbegu ambayo inagusa maslahi ya wananchiwasiopungua milioni kumi (10) vivyo hivyo naomba ushuhudawa dhati ambao ni ufafanuzi makini wa vitendovinavyotekelezwa kuhusu pamba kuwa MKUKUTA kwawakulima wa pamba kupitia Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la NDC linasimamiamaslahi mapana ya viwanda vya kugusa ustawi wa jamiina Taifa. Naomba maelezo ya kwa nini Serikali ina ukimyakuhusu NDC kuibua kiwanda cha uwezo mzito wa Kiwandacha Kusindika Nyama kilicho sambamba na utajiri wa mifugoambayo ipo katika jamii ya wananchi milioni 20.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maswa tuna eneo lakuwezesha Viwanda vya Ngozi na Nyama. Je, Serikali inatoafursa zipi zitekelezwe na Halmashauri ya Maswa tupateviwanda hivi vya kuhudumia wigo mpana wa maeneo yawafugaji wa Kanda ya Ziwa. Naomba maelekezo yakutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na kazi njema.

MHE. SUSAN A.J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,viwanda ni eneo/muhimu la kuweza kukuza uchumi wa nchiyoyote ile na ndio maana nchi za Ulaya kupitia Industrializationau Industrial Revolution zilianza kuendelea kwa kasi kubwa.Ni jambo la kusikitisha kuwa, Tanzania iliyokuwa na Viwanda

Page 258: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

258

vingi, sasa Viwanda hivyo vimebinafsishwa na kibaya zaidihavifanyi kazi zetu za asili. Matokeo vingine vimekuwa ma-godown na vingine kubakia magofu. Mfano, mzuri nikiwanda cha UFI (Ubungo Farm Implements) ambachokiliweza kutengeneza nyenzo za kilimo kama majembe, rato,sururu, mapanga na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kwa kuwa asilimia 80ya Watanzania wakulima tena maskini, hivyo ilikuwa busarasana kuwa na kiwanda cha aina hii ili kuwafanya wakulimakupata bidhaa hizi kwa urahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kilimanjaro Machine Toolsnayo hivyo hivyo, lakini kubwa zaidi ni kile cha Arusha GeneralTyre ambacho kilitengeneza magurudumu mazuri na yenyekudumu sana. Sasa hivi tunashuhudia tyres nyingi kutokanje hususan Mashariki ya Mbali good year, Dunlop, Michelinna kadhalika. Tyres ambazo hazina ubora kama zilivyokuwakwa General Tyre. Swali la kujiuliza ni je, Serikali haioni Seraya ubinafsishaji ni janga kwa nchi yetu? Pia je, ni kwa niniSerikali inabinafsisha hata vile viwanda muhimu kwa nchiyetu? Ni vyema Serikali ikapitia Sera hii ya ubinafsishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Viwanda VidogoSIDO, Shirika hili limefanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwawananchi na imesaidia sana vijana kujiajiri wenyewe. Nivyema basi, Wizara isaidie Shirika hili ili liweze kusaidia vijanawetu hasa ikizingatiwa kwamba, ni vigumu sana vijanakuajiriwa na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBS ni chombo cha viwangoTanzania, lakini cha ajabu chombo hiki kimekuwa hakifanyikazi yake vizuri na ndio sababu kila siku malalamiko hayaishi,bidhaa bandia zimejaa madukani. Je, tatizo ni upungufuwa rasilimali watu au vifaa kwa ajili ya ukaguzi au ni rushwa?Unakwenda dukani unauliza bidhaa unaulizwa unatakagenuine au fake kwa maana ya low quality, je, ni kweli TBShawayaoni haya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la kusikitisha kuona

Page 259: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

259

raia wa nje wakifanya biashara ambazo kimsingizingefanywa na Watanzania. Nimeishi nje ya nchi na sikuwahikuona wageni wakifanya biashara ndogondogo kama ilivyoTanzania. Unapoona wenzetu Wachina wanauza vituvodogovidogo vya kutembeza ni hatari na inaweza ikavunjaamani kama ilivyofanyika Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita.

MHE. KOMBO KHAMISI KOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, katika kukuza uchumi wa nchi kinahitajikakuwepo kwa kiasi kikubwa cha afya ya wananchi waliomokatika Taifa. Taifa ambalo lina watu wenye afya boralinasaidia kuongezeka kwa uzalishaji na nguvu kazi katikaTaifa na vile vile husaidia kuongezeka kwa uchumi na patola Taifa. Ni lazima na wajibu wa Serikali kukubali kuwekezakisasa katika suala zima la matibabu, dawa na vitendea kazipamoja na watendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukuza uchumi wa nchi nilazima Serikali ikubali kuvifufua Viwanda ambavyo kwa njiamoja au nyingine vimechangia kuanguka kwa pato la Taifa:-

(1) Kuwepo kwa uhai wa Viwanda kutasaidiakuwepo kwa ongezeko la ajira, lakini kutakuwepo piauchangiaji wa kukuza pato la Taifa.

(2) Kuanguka kwa Viwanda vya KubanguliaKorosho, Nguo na kuviweka nyuma Viwanda vya Tanga nakufikia hatua ya kufa kumehujumu uchumi wa nchi.

(3) Uingizaji wa bidhaa feki ndani ya nchi hususanmadawa ya wanadamu.

TBS kuangalia Sheria zinazowaongoza zaidi kuongezaadhabu ili kudhibiti uingizaji wa bidhaa mbovu. Mawakalani wachache sana hasa kwa China na India ambaowanakagua bidhaa kabla hazijapakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema Serikali ikalielezaBunge hili, ni kwa nini Tanzania packers imekufa? Viwandavya minofu ya samaki je, ni lini Serikali itavirejesha na

Page 260: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

260

kuviimarisha Viwanda hivi. Serikali ina mkakati gani katikahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufa kwa ViwandaVidogovidogo (SIDO) ambavyo vilikuwa vikitengeneza vipurikumeua uchumi wa Taifa na pia kuangusha biasharakunahitaji kufufuliwa kwa SIDO ili tukuze uchumi wa Taifa.Tufufuwe Viwanda vya mbolea. Ni wakati muafaka waSerikali kuweka mkazo katika uwekezaji wa Viwanda vyakimkakati na virutubisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chuma cha Ligunga, Gas naUranium Indicator ya kukuza uchumi ni kukuza Viwandavidogovidogo, mfano, SIDO. UFI ambacho Kiwanda hikiuzalishaji wake mkubwa ni zana za kilimo, lakini kwa sasaviko chini kabisa kiuzalishaji.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ufufuaji wa Viwanda Vidogovidogo hapa nchini ni muhimusana katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwavijana hapa nchini. Nashauri Wizara na Serikali kwa ujumlakutazama upya suala la ufufuaji wa Viwanda hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, BRELA, taasisi hii imekuwaikisajili nembo na majina ya biashara mbalimbali hapa nchini,lakini taasisi hii imekuwa ikihusishwa kwa kiwango kikubwana vitendo vya rushwa katika kuhudumia wateja wanaofikapale. Je, ni kwa nini Serikali haioni umuhimu wa kutumiataasisi hii na kuunda kwa upya, lakini pia kufungua ofisiMikoani ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Ni watumishiwangapi wameshakamatwa na tuhuma hizi za rushwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Viwanda Vidogo Vidogo(SIDO); Viwanda hivi vimekuwa ndio tegemeo la wananchihapa nchini. Hata hivyo, Viwanda hivi haviendelezwi nahavina vifaa vya kisasa ili kutoa huduma kwa wingi na kwaubora unaotakiwa. Je, Wizara ina mkakati gani wakuendeleza Viwanda hivi Vidogo hapa nchini? Je, kwakiwango gani SIDO katika Mikoa yetu inatengewa mafunguya kutosha ili kutoa huduma kwa ufanisi kwa wajasiriamali?

Page 261: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

261

MHE. LUCY P. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO); Shirika hili ndilopekee litakaloweza kuwafikia wakulima vijijini na kuwezakusambaza machine ndogo ndogo za kusindika mazaomfano, kutengeneza jam, tomatopaste, juice, peanut butterna kadhalika. SIDO ina mkakati mzuri kupitia vijijini, kilaWilaya kuzalisha bidhaa moja. Je, program hii imefikia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo ya SIDO hayawezikukamilika bila Serikali kuwapa SIDO fedha za kutosha. Fedhawanazopewa kila mwaka ni pungufu ya walizoomba.Tukumbuke siyo tu kusambaza Viwanda, inabidi watoemafunzo ya kutumia mashine hizo, masomo ya ujasiriamali,wawezeshe wakulima jinsi ya kuweza kupata vifungashio iliwaweze kuuza nje na kushindana na soko la Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Viwango (TBS);Shirika hili ni kuhakikisha bidhaa zote zinatoza nje aukuzalishwa nchini zinakuwa na ubora na zisizokuwa namadhara kwa mtumiaji. Cha kusikitisha mpaka sasa hivi,bado kuna bidhaa nyingi madukani, mfano, vifaa vyaumeme, magari, bado mteja anaweza kwenda dukanianaulizwa anataka Original au fake, hii ni hatari. Je, vifaahivi vinaingiaje ndani ya nchi? Ndio maana kumetokeamatukio ya nyumba kuwaka moto utokanao na short zaumeme. Siyo hilo tu Serikali kupitia Bunge lako Tukufu iliwahikutoa tamko ni marufuku kuuzwa kwa mitumba (nguozilizovaliwa) nguo za ndani (brazia, chupi), lakini bila kuogopavijana wanapita mitaani na nguo hizo wakiziuza mchanakweupe na taasisi hii ya TBS ikiwafumbia macho. Je, TBSimepuuza maagizo ya Bunge na Serikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Viwanda nchi zotezilizoendelea mfano China, Korea, Malasyia zote hizizilihakikisha zinawekeza katika viwanda, lakini hapa kwetuviwanda vilibinafsishiwa kwa watu binafsi. Matokeo yakeviwanda vingi havikuendelezwa na vingi kugeuzwamatumizi ya awali. Je, nini hatua ya Kiwanda cha TanganyikaParkers cha Kusindika Nyama pale Kawe, Dar es Salaam.

Page 262: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

262

Kiwanda hiki ki l ikuwa na mitambo yote tenainafanya kazi. Je, mitambo ile kwa sasa hivi ipo wapi? Hiini sawa na kiwanda mama cha Machine Tools kilichopoKilimanjaro. Hiki kilikuwa Kiwanda cha Kuzalisha ViwandaVidogovidogo ni zaidi ya miaka sita, nimekuwa nikiuliziaKiwanda hiki, lakini Serikali imekuwa ikitafuta mwekezaji, je,mpaka leo bado inatafuta Mwekezaji? Je, mwekezajiasipopatikana Serikali ina mkakati gani na Kiwanda hiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha General Tyrehiki ni Kiwanda kilichokuwa kinazalisha matairi yenye uborakatika Afrika ya Mashariki na ya kati. Ni jambo la aibu, Serikalikutoliweka maanani suala hili na kuruhusu Kampuni ya Kenyaya Dunlop ndio wana-supply matairi hapa nchini nakutupumbaza na kusahau kabisa kuhusu kufufua Kiwandachetu. Serikali itupe majibu ya uhakika na time frame ni liniKiwanda cha General Tyre kitaanza kazi?

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, suala la Viwanda katika nchi yetu badohalijaweza kusaidia katika pato la Taifa na ukuaji wa nchisambamba na upatikanaji wa ajira hususan kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanguka na kufa kwaViwanda vingi hapa nchini kumechangia kwa kiasi kikubwakuzorota kukua kwa uchumi wetu. Moja ya vielelezo vyaukuaji wa uchumi wa nchi ni kuwepo kwa ViwandaVidogovidogo. Malengo ya MKUKUTA ni kukuza Sekta yaViwanda kwa asilimia 15 ili kuongeza thamani ya mazao yetuya kilimo. Je, Serikali imewezaje kuwashawishi wenyeViwanda kuhamia vijijini badala ya kubaki na kuwekeza Dares Salaam, je, ni namna gani Wizara itarejesha Viwandaambavyo kwa sasa vimegeuzwa magodauni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ninukuu kauli yaMheshimiwa Asha Rose Migiro alipokuwa anazungumza naviongozi katika Mkutano wa 15 wa All Summit ambapoalisema:- Afya ya mama na mtoto ndiyo chachu amakielelezo cha Afya ya Taifa na Serikali inapowekeza katikaAfya ya Mama na Mtoto ndiyo moja ya ishara za uchumi

Page 263: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

263

kinara wa nchi. Aliendelea kusema afya na maendeleo nimambo pacha. Tunahitaji kuwa na nguvu ya fedha, utashiwa Kisiasa na Service delivery commitment ili kukuza afya yamama na mtoto.

MHE. NAMELOK E.M. SOKOINE: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na changamoto nyingi zilizopo katikaWizara hii bado kuna mafanikio mengi na ifikapo 2025Viwanda vingi vitakuwa vimefufuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara ifanyieharaka ufufuaji wa Viwanda vya General Tyre, ArushaKiwanda hiki kilikuwa moja ya Kiwanda chenye kuzalishamatairi bora Afrika Mashariki. Kiwanda cha Philips Arusha,Tanganyika Parkers mjini Arusha na ukichukulia Mkoa waArusha kuna wafugaji wengi, hivyo wananchi wangepataajira na kuweza kusindika nyama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iliuza Viwanda vyaNMC, lakini cha Mjini Arusha kilikodishwa kwa Kampuni yaMonabai na Mzawa (Mtanzania). Jambo la kushangaza,Wizara haijampa Mkataba wa muda mrefu walahawajamuuzia, wakati Mtanzania huyo amekopa pesa nyingibenki. Je, Serikali ina mpango gani wa kumuuzia aukumkodisha kwa mkataba wa muda mrefu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukaguzi wa magari nje yanchi, kufanya ukaguzi wa magari nje ya nchi tunatozwa 450$,lakini fedha halali ni 150$, je, Serikali inasemaje juu ya hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO inafanya kazi nzuri sanakuwafundisha wajasiriamali wadogowadogo. Wizaraiwezeshe SIDO fedha za kutosha wafungue matawi zaidi nakupanua wigo wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, Hotuba ya Waziri inatia moyo sana, nawaombeamafanikio katika utekelezaji wa mipango yao hii, lakini ninayoyafuatayo:-

Page 264: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

264

Je, Serikali inayo dhamira ya kweli ya kuinua viwandana biashara? Kama ndiyo, kwa nini fedha kidogozilizoidhinishwa hazijatoka ni 30% tu? Naomba fedha zaLogistic Centre zitolewe ili tupate manufaa yaliyotarajiwa.Fedha za SIDO na hasa NEDF ziongezwe ili wajasiriamaliwaweze kupata mikopo, lakini pia ni wakati sasa SIDO iweWilayani waliko watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Ngaka; kwa ninimradi huu ulianza bila kutatua kero za fidia kwa wananchi?Sasa hivi Serikali imeahidi ilipe fidia hii sasa mpaka ifikapo15/6/2013. Naomba ahadi itekelezwe kuepuka vurugu kwamradi na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika taarifa yake (pressrelease ya Tancoal ya kwanza kabisa waliahidi kujenga Chuocha Ufundi cha Ngaka. Mpango huu baada ya kubadilishauongozi Intraenergy hauonekani ni lini kitajengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi kwaWaziri kwa kuunda Tume ya pamoja ya kushughulikia powerstation, je, mazungumzo haya yatamalizika lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kwaumahiri huo huo unaweza kuwakutanisha REA, Tancoal, NDCna TANESCO, kuona uwezekano wa kujenga mtambomdogo wa MW 5-10 ili kufufua umeme kwa ajili ya wananchiwa Ntunduraro, Ruanda, Vijiji vya kati ya Litumba Ndyosi,Kinduila Juu na Chini mpaka Matiri. Mpango huu ni waharaka zaidi na una matokeo ya haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kwaumahiri huo huo hatuwezi kutafuta fedha za ndani kujengahuo mtambo wa umeme (220MW) ili kupunguza gharamana kuihusisha TANESCO zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mazingira; magariya Tancoal yamesababisha vumbi kwa wananchi. Hivyo,barabara ya Kitai-Ruanda-Lituhi iwekwe lami kwa kushirikianana wawekezaji, inawezekana la sivyo, mradi huu unawezakufungwa kwa sababu ya mazingira.

Page 265: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

265

MHE. ALI KHAMISI SEIF: Mheshimiwa Mwenyekiti, nchinyingi zinazohesabiwa kupata maendeleo ya viwandazimeanza kwa kuwa na Viwanda vidogovidogo. Nchi yaIndia pamoja na kuwa na Viwanda vikubwa pia maendeleoyao yanategemea Viwanda vidogovidogo. Hapa nchini kazihiyo ya kuvisaidia huvilea Viwanda vidogovidogo inafanywana SIDO.

Leo uwezo wa SIDO, kifedha ni mdogo mnoukilinganisha na majukumu yake. Katika hali hiyo ni dhahiriSerikali bado haijakuwa makini kuwawezesha SIDO ili na waoSIDO waweze kuwasaidia wajasiriamali kuwa na Viwandavidogo ili waweze kuongeza thamani bidhaa zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanaotegemeazao la korosho kama zao la uchumi, mapato yao hayalinganisana na kazi inayotokana na kilimo hicho. Hii inasababishwana bei isiyoaminika ya korosho na kukosa Viwandavilivyokuwa vikitumika Kubangua Korosho hasa huko Kusinimwa nchi yetu, Viwanda hivyo vilibinafsishwa na mpaka leohavifanyi kazi. Serikali ina mpango gani wa kuwataka haowenye Viwanda hivyo wanavifanyia matengenezo ili vifanyekazi iliyokusudiwa, kama si hivyo Serikali inahamasisha vipi iliViwanda vipya vijengwe vya kuongeza thamani zao lakorosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya ongezeko laViwanda na uzalishaji wa bidhaa katika Viwanda hivyo, badobidhaa zetu ni ghali ukilinganisha na bidhaa kama hizozinazotoka nje, mfano, saruji ya hapa nchini ni ghali zaidiukilinganisha na saruji kutoka nje. Hii hali itaendelea mpakalini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili pamba yetu ipate bei nzuriinabidi pamba hiyo iongezee thamani hapa nchini, lakini piapamba hii ilitumika hapa nchini kwa kiwango kikubwa kwakutengenezea nguo, lile suala la kutegemea pamba yetukuuzwa nchi za nje utapungua. Sasa Serikali imejipangavipi kuwashawishi wawekezaji wa Viwanda vya nguo hapa

Page 266: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

266

nchini ili baada ya kuagiza nguo iwe sisi tunasafirisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote nampongeza sana Dkt. Kigoda na Naibu Waziriwake pia watendaji wote wa Wizara kwa kukabiliana nachangamoto mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, napenda kupatamaelezo ya Wizara kupitia bodi ya leseni ya maghala kwenyempango wa stakabadhi ghalani kuwa inawasaidiaje Vyamavya Msingi vya Tandahimba na Newala ambavyo vimeibiwakorosho zao karibu au zaidi ya bilioni mbili na wenye Viwandavya Newala I – Agrofocus, lakini Bodi ya Leseni za maghalaiko kimya licha ya kufikishiwa kadhia hii.

MHE. ABASI ZUBERI MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nachukua nafasi hii kuwapongeza, Mheshimiwa Waziri, NaibuWaziri na Katibu Mkuu na Wafanyakazi wote wa Wizara, kwakazi nzuri. Nina swali moja tu; ni lini Wananchi wa Shimo laUdongo katika Kata ya Kurasini, Mradi wa EPZ Tanzania ChinaLogistic Centre wataanza kulipwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha

MHE. ENG ATHUMAN R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini mkakati wa Wizarakufufua Kiwanda cha Nyuzi Tabora – TABORATEX kwanihakifanyi kazi tangu kubinafsishwa takribani miaka kumi sasa?Vijana Igalula wako tayari kuajiriwa katika Kiwanda hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazungumzo na mwekezajimwingine kutoka Dubai na Pakistani yuko tayari kujiunga namwekezaji huyu kama Wizara itahamasisha wote wawilikuendeleza mazungumzo. Mbunge atatoa ushirikiano kwanitayari huyu mwekezaji mwenza amekwisha kukikagua hichoKiwanda japokuwa baadhi ya mashine zimeng’olewa nakuhamishwa!

Page 267: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

267

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tabora na hasa Igalula,tunafuga nyuki na asali ya ubora wa juu. Wizarainawasaidiaje wafugaji hawa wa nyuki kupata vifaa nakiwanda cha kuchuja asali na nta na kuuza soko la nje nandani kwa bei ya ushindani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki Kuu ina jukumu lakuimarisha thamani ya fedha yetu, kudhibiti mfumko wa beina pia kukuza uchumi mpana (Macro-economics). Amerika,Japani, Korea ya Kusini na Benki Kuu zao zimesaidia sanaviwanda kukua. Je, BoT imesaidiaje Wizara hii kukuza viwandaTanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, dola 480 milion kila mwakazinatokana na Tumbaku Mkoa wa Tabora. Je, Wizaraimehamasisha wawekezaji wangapi mpaka sasa kujengaKiwanda cha Tumbaku Tabora ili ajira na thamani ya zaokuongezeka Tabora?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maembe ya kisasayanastawi Tabora, Wizara ihamasishe tupate Kiwanda chaMatunda Tabora na hususan Igalula.

MHE. MARYAM S. MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nchi za wenzetu zilizoendelea; kwa mfano, Korea, Japanina kadhalika, zinategemea viwanda. Cha kushangaza,Tanzania viwanda vingi vimekufa na viwandavilivyobinafsishwa havifanyi kazi wala havitoi ajira. Vilevileviwanda hivi vilivyobinafsishwa vingekuwa vinafanya kazi,tungepunguza tatizo la ajira ambalo ni tatizo sugu kwa vijanawetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mpango ganiwa kuvikagua Viwanda vyote vilivyobinafsishwa kwawawekezaji? Kama wawekezaji hawa wameshindwakuviendeleza viwanda hivi wanyang’anywe na Serikaliiwakabidhi wawekezaji wengine ambao wana uhakika wakuviendeleza.

Je, hawa wawekezaji waliopewa viwanda hivi

Page 268: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

268

wakashindwa kuviendeleza na wakafanya uharibifu katikaviwanda hivi (kuvitelekeza); na Wananchi ambao siyowaadilifu wakang’oa vyuma hivyo na kuamua kwenda kuuzavyuma chakavu; Serikali inawachukulia hatua gani za kisheriawawekezaji hawa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya wakulima wamatunda wamekuwa hawana soko la uhakika, vilevilemsimu wa matunda, matunda haya yamekuwa yakiharibikamashambani. Je, ni lini Serikali itashirikiana na ShirikalaViwanda Vidogo Vidogo (SIDO) na kuwezesha SIDO kujengaviwanda vidogo vidogo vya usindikaji wa matunda katikaMikoa ambayo inazalisha matunda kwa wingi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wajasiriamali wadogowadogo (viwanda vidogo vidogo), wamekuwawakihangaika sana kutafuta soko la bidhaa ambazowanazalisha (soko la nje na soko la ndani).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na Wachinawengi ambao wanauza bidhaa ndogo ndogo Kariakoo; kwamfano, maua na kadhalika na kusababisha hawawajasiriamali wetu wadogo wadogo kukosa soko na hataukiangalia hizo bidhaa zao wanazouza siyo madhubuti (feki).Je, Mheshimiwa Waziri haoni sasa kuna umuhimu wa kudhibitihizi bidhaa ndogo ndogo ambazo zinaingizwa na Wachinaambazo siyo madhubuti ili wajasiriamali wa viwanda vidogovidogo wapate soko?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia Wamachingawamekuwa wakipata tabu, kwani hawapo Dar es Salaampeke yake hata nchi za wenzetu pia wapo. Askari wa Jijiwanawapiga Wamachinga hawa, kuwanyang’anya vituvyao, kuwazidishia umaskini na wanakosa raha na amani.Je, Serikali ina mpango gani wa kuwatafutia soko la uhakikaWamachinga hawa ili waepuke adha hii wanayoipata?

MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,Wizara ya Viwanda na Biashara, ilipaswa iwe na mjadalawa siku mbili na siyo siku moja. Hii ni Wizara muhimu, yenyekubeba uchumi wa nchi hii kupitia viwanda.

Page 269: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

269

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama yaliyotamkwa naMheshimiwa Waziri yatatekelezeka, hakika tutapanua nakuongeza Pato la Taifa na la Mtanzania. Nashauri Serikaliianzishe viwanda vya lime ili iuzwe katika migodi yote nchinibadala ya kuacha migodi iagize limestone nje ya nchi. Ipolimestone nyingi Makanya, Same, Singida na maeneo mengiya Tabora. Serikali iungane na Sekta Binafsi (PPP) ili maeneohayo yaanzishe viwanda vya limestone.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wawekezaji walionunuaviwanda vya zamani na hawajaviendeleza, wanyang’anywewapewe wanaoweza kuviendesha. Tanzania tunahitaji ajira.Uchumi wa nchi utaendelezwa na Sekta Binafsi. Waliouzamashine wadaiwe walipe. Mfano, Kiwanda cha MaguniaMkoani Kilimanjaro, leo hii ni go-down. Wizara ya Viwandaifanye makubaliano na Consolidated Holdings i l iyo-coordinate uuzwaji wa viwanda. Serikali ifute hati za viwandavilivyouzwa ambavyo haviendelezwi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo haja kubwa sanawapelekwe Waambata na Wakurugenzi wa Vituo vyaBiashara katika Nchi kama China, Japani na kadhalika.Kamati ya Mambo ya Nje imelisema hili kwa miaka zaidi yamiwili. Diplomasia ya uchumi itafanikiwa waambata haowakiwepo katika Balozi zetu muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SIDO ni ya msaada sana kwaviwanda vyetu vidogo vidogo, hakuna haja kuagiza mashinenje ya nchi. SIDO wana utaalamu wa kutosha, wawezesheviwanda vya kuongeza thamani katika mazao katika Kandazetu Nchini; mfano, Rukwa - mahindi, Rukwa - mahindi,Ruvuma - mahindi, Kigoma - mahindi, Tanga - matunda,Kilimanjaro - tangawizi na ndizi, watengeneze wao mashine.Ajira zitapatikana, Pato la Taifa litapatikana na pato laMwananchi litapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Soko la Afrika Masharikilinahitaji bidhaa hizi zilizosindikwa mfano unga, mafuta yakula, wine, tomato source, juice na kadhalika. Serikali isaidieviwanda hivi vianzishwe na Sekta Binafsi katika maeneo yotenchini.

Page 270: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

270

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ipange na Wizara yaFedha, Serikali ilinde bidhaa za ndani na hivyo kuletamaendeleo kwa viwanda vilivyoko na vitakavyoanzishwa.Mali na bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vyetu, bidhaakama hizo zisiagizwe kutoka nje unless kama uzalishajihautoshi. Mfano, Kiwanda cha Kibo Match Moshi, Serikaliinakiacha kife kwa sababu ya madeni. Kiwanda chakutengeneza na kusindika Kahawa Moshi, nacho kinaelekeakufilisika kwa sababu ya deni la TRA/NSSF, wakati Serikaliinashuhudia mitambo chakavu ya miaka kabla ya Uhuruikiwa ndiyo inatumika. Serikali inafanya nini kukinusurukiwanda hiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha Ngozi MkoaniKilimanjaro (Himo), kinafanya semi-processing Tanzania nafinal processing Nairobi. Ajira zinakosekana kwa upungufukama huu. Serikali isaidie kiwanda hiki ili kilete ajira kwaWatanzania na Pato la Taifa kutohaha na ngozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBS inaweza kufanya vizuriinatakiwa iungwe mkono. Kubadilisha Wakurugenzi kila leo,tena bila uwazi wa kutosha, unaleta hisia ya rushwa auundugunization. Wakurugenzi waajiriwe kutokana naqualification, experience na uwezo wao wa kufanya kazi.Aajiriwe Mkurugenzi aliye qualified katika fani ya TBS (qualityet cetera).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakaguzi wa bidhaa nje yanchi, Kampuni zipewe tender kwa uwazi. Maslahi binafsikipindi hiki yataua Taifa hili, we have had enough; ni wakatiUtaifa ututawale zaidi. Yameandikwa mengi katika magazetikuhusu Uongozi wa Wizara kutokutaka uwazi kuhusu tenderza nje na ajira za ngazi ya juu katika TBS.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika Awamu ya Kwanza ya Uongozi wa Hayati Baba waTaifa, Mwalimu J. K. Nyerere hapa Tanzania, kulikuwepo na

Page 271: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

271

kiwanda cha magari maarufu kama “Nyumbu”. Uzalishajiwa magari hayo aina ya Nyumbu ungekuwa badounaendelea, Wananchi wengi waishio vijijini na hasawakulima wakubwa wa pamba, tumbaku, mahindi, nganona kadhalika, wangepata unafuu kwa kuuziwa magari hayokwa bei nafuu na hivyo kupata urahisi wa kusafirisha mazaoyao hadi kwenye soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tupo katika era ya sayansina teknolojia, nashauri Kiwanda kile kifufuliwe ili kuharakishaMaendeleo ya Nchi yetu kwa kuwa na magariyanayotengenezwa hapa hapa nchini. Yanayowezakuwarahisishia wakulima wetu katika maeneo mengi yenyekilimo kikubwa hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. JOHN PAUL LWANJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja na kuipongeza Serikali kwakuhamasisha ujenzi wa viwanda vingi vya saruji hivi karibuni.

Viwanda hivi vinaonekana kujengwa zaidi Ukandawa Pwani kuanzia Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga na hivyokuyaachia maeneo mengine hususan Kanda ya Kati naMagharibi bila Kiwanda cha kutegemea na hivyo bei ya sarujikuendelea kuwa juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kwa miaka mingi sasanimekuwa nikiisihi Serikali ione uwezekano wa kuwashawishiwawekezaji wajenge Kiwanda cha Saruji eneo la Itigi,Manyoni, Mkoa wa Singida, kutokana na malighafi nyingi yagypsum au jas, lakini ahadi zimechukua muda mrefu bilamafanikio. Naiomba Serikali irejee ombi hili kwa kuwashawishiwawekezaji kuwekeza eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kama haiwezekanikujenga Kiwanda cha Saruji, basi walau Kiwanda chakuzalisha Plastor of Pain (PoP) kutokana na malighafi hiyo yagypsum.

Page 272: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

272

MHE. ENG. GERSON H. LWENGE: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote, naunga mkono hoja hii nakuwapongeza Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wote, kwaHotuba nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ilitenga eneo paleMakambako la kujenga Soko la Kimaitafa to 1997, hadi leoimefika miaka 16 hawajalipwa fidia pamoja na ahadi yakufanya hivyo. Je, hilo eneo la ekari 300 utafanyika uthaminiupya? Ni lini basi Wananchi wale watalipwa; na ni lini sokohilo litajengwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Njombewanalima viazi mviringo, lakini soko lake ni tete na hasawanunuzi kulazimisha Wananchi wajaze lumbesa. Je, Serikaliina mkakati gani wa kuzuia tabia hii ya kutofuata sheria yaujazo wa kilogramu 100 kwa gunia?

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuishauri Serikali kupitia Wizara hii ya UchumiViwanda na Biashara katika mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na malalamikomakubwa na ya muda mrefu ya wananchi katika Mikoa mingiya nchi yetu kuhusu maeneo yaliyochukuliwa na Serikalikupisha mpango wa EPZA. Madai ya wananchi ni kushindwakulipwa fedha za maeneo yao huku wakiendelea kuzuiliwakuyatumia maeneo yao katika shughuli zao za kimaisha yakila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali kuona haliya fedha ya kuwalipa wananchi hawa. Naishauri Serikaliiwaruhusu wananchi hawa kuyatumia maeneo haya mpakahapo Serikali iwaruhusu wananchi hawa kuyatumia maeneohayo mpaka hapo Serikali itakapokuwa tayari kuwalipa kwatathmini mpya itakayofanyika muda huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujua hatuazinazochukuliwa juu ya ufufuaji wa Kiwanda cha Urafiki kwanikwa muda mrefu imekuwa uzalishaji wa Kiwanda hiki

Page 273: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

273

haueleweki. Je, ni hatua zipi zinachukuliwa kukiendelezaKiwanda hiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka pia kujua ni hatuagani zinaendelea kuchukuliwa katika kukifufua Kiwanda chaGeneral Tyre Arusha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali itupatiemajibu kuhusiana na mradi mkubwa wa Kurasini LogisticCentre. Ni kwanini umekwama kuanza hadi sasa wakatibajeti iliopita ziliidhinishwa 60 bilioni kwa ajili ya mradi huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na faida nyingizinazotarajiwa kupitia mradi huo utakapokamilika, lakinifaida ya ajira za kuanzia 25,000, ambazo zinategemewakuongezeka kadri muda utakavyokwenda: Je, Serikali haionikuchelewa kuanza kwa mradi huu, kuna hatari ya kupotezafursa hii adimu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna taarifa kwamba mradihuu unamezewa mate na nchi nyingi za kiafrika. Hivyo,naiomba Serikali kwa umakini kabisa itueleze hatua za harakailiyopanga kuzichukua kukamilisha uanzishaji wa mradi huumuhimu kwa manufaa ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itueleze, nimafanikio gani makubwa yaliyopatikana toka kuanza kwautaratibu mpya wa ukaguzi wa mizigo nje ya nchi (PVOC):Je, malengo tuliyokusudia ya kupunguza uingizaji bidhaahafifu umefanikiwa?

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Mwenyekiti,bila kupoteza muda, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ilinami niweze kuchangia na kutoa maoni yangu kufuatiahotuba ya Bajeti ya Wizara hii kama ilivyowasilishwa kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, nianze kwakusema kuwa sote tunajua kuwa hivi sasa Serikali yetu yaChama cha Mapinduzi iko katika harakati kubwa za kukuza

Page 274: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

274

uchumi wa Taifa letu ili kuupiga vita umaskini. Hili ndiyo lengokuu lililoko kwenye Ilani ya Chama chetu. Kati ya juhudizinazofanyika katika kutekeleza ilani hiyo ya kukuza uchumini pamoja na kuvutia wawekezaji wa nje na wa ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa minajili hiyo ya kuvutiawawekezaji, Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko inayokazi kubwa sana ya kufanikisha lengo hili kuu. Kama Wizarahii ikilala, basi maana yake ni kuwa uwekezaji utadorora.Viwanda vitadorora na kufa. Matokeo yake kudorora hukoni Watanzania kupoteza ajira kwa kukosa kazi. Wakulimana wafanyabiashara kukosa masoko ya kuuzia bidhaa zao,wawekezaji kukimbia na mbaya zaidi Serikali kukosa mapatokupitia kodi na matokeo yake uchumi kuanguka na kufakabisa. Haya yakitokea, wananchi watashindwa kupiga vitaumasikini na kazi yote tunayofanya itakuwa kazi bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, Wizarahii ya viwanda biashara na masoko ina kazi kubwa na nafasiya kipekee ya kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wetukutokana na majukumu ya Wizara. Hakuna mwekezajiambaye atakuja kuwekeza sehemu ambayo mathalananajua kuwa uwekezaji wake hautalindwa au hakunaushindani halali wa kibiashara. Mwekezaji hawezi kujakuwekeza kwenye soko ambalo limejaa bidhaa feki, sokolililojaa bidhaa bandia na hafifu kama soko letu lilivyo kwasasa. Kwa mantiki hiyo basi, mchango wangu wa leo utajikitazaidi katika changamoto na matatizo sugu yanayoiandamaOfisi ya Wakala wa Usajili na Leseni za Biashara (BRELA) nahasa Kitengo cha Msajili wa Hataza ‘patents’ na alama zabiashara (trade and service marks) Ofisi ya BRELA iko chini yaWizara hii na kitengo ninachozungumzia leo kinajulikana zaidikwa Kiingereza kama the Office of the Registrar of Patents,Trade and Services Marks.

Mheshimiwa Mwenyekiti, BRELA ilianzishwa tarehe 28Oktoba, 1999 chini ya Sheria ya Executive agencies Act, no 30ya mwaka 1997. Ofisi ilianzishwa kufuatia Tangazo la SerikaliGN 8 October, 1999, lengo la kuanzisha ofisi hii ilikuwa nikupunguza urasimu usiokuwa na maana wa kiserikali. Kitengo

Page 275: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

275

hiki cha masijili wa alama za Biashara na Hataza (Patents)kiko chini ya BRELA, lakini naamini ndiyo chenye matatizomakubwa sana kuliko kitengo kingine chochote. Matatizoyanayosababishwa na kitengo hiki, yanachangia kwa kiasikikubwa sana kukatisha tamaa wawekezaji kuja kuwekezana kufanya biashara hapa nchini. Yamkini ili mtu afanyebiashara, anatakiwa awe au abuni alama ya biasharaitakayomsaidia kutofautisha bidhaa zake na bidhaa zawafanyabiashara wengine. Alama za biashara ni kamachombo cha habari ambacho muuzaji au mzalishajianakitumia kuwasiliana na wateja sokoni. Kutangaza nakuuzia bidhaa au huduma yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi huo, basi alamaza biashara ni kitu muhimu na chenye thamani kubwa sanasokoni. Kwa mfano, AZAM PEPSI au COCA-COLA ni alamaza biashara zenye thamani kubwa ya mabilioni ya Shilingi navinatumika kwa ajili ya vinywaji baridi na bidhaa nyingine.Alama hizi za biashara zinasajiliwa na kulindwa na sheria ya(Trade and Service Marks Act 1986 CAP 326 REF 2002). Sababukubwa ya kusajili na kulinda alama hizi ni kuwa kama kilamtu angeruhusiwa kwa mfano kutengeneza pombe yake yakienyeji mfano ulanzi halafu akaiita PEPSI au COCA-COLAmaana yake ni kuwa biashara ya Makampuni haya makubwaingekuwa imeshaharibika kabisa siku nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya kazi zinazofanywa naOfisi ya BRELA ni kusajili hati za hataza na alama za biashara.Tatizo sugu linayoikabili ofisi hii ni kuwa shughuli hii ya usajiliwa alama za biashara inachukua muda mrefu mno! Kaziambayo nchi za wenzetu inachukua chini ya miezi mitatuhapa kwetu inachukua mwaka zaidi ya mmoja na wakatimwingine hata miaka zaidi ya mitano! Ni kitu cha kawaidakabisa kukuta ombi la kusajili alama za biashara lililopelekwamwaka mmoja hadi mitatu iliyopita halijafanyiwa kazi yoyotena ofisi hii kabisa! Yaani lipo lipo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine hataukifuatilia unaambiwa faili halionekani, yaani mtu amepelekaombi la kusajili alama yake ya biashara amelipa ada

Page 276: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

276

ambayo ni Sh. 50,000/= lakini kwa zaidi ya mwaka mmojahadi mitatu hajajibiwa kama ombi lake limekubaliwa au la!Haiwezekani mtu akae ofisini akalie ombi la mtu kwa zaidiya mwaka mmoja bila majibu na hapo hapo tusemetunavutia wawekezaji? Tunavutia wawekezaji gani? Kwakupiga ramli! Ushahidi wa ucheleweshaji huu uliopita kipimoupo na kama Waziri akitaka nitampatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo tisa, kumi ni paleambapo unakuta ombi hilo l imeshakubaliwa nalimeshatangazwa katika gazeti kwa mujibu wa sheria, adaya usajili ambayo ni Sh. 60,000/= imeshalipwa, lakini ofisi hiiinashindwa kutoa cheti cha usajili kwa zaidi ya miaka hatamiwili hadi zaidi. Kama taratibu za usajili zimekamilika,kikawaida kutoa cheti, haiwezi kuchukua zaidi ya siku mbiliau tatu, lakini katika ofisi hii inachukua miaka miwili hadimitatu na wakati mwingine zaidi ya miaka mitano. Narudiatena, ushahidi wa ucheleweshwaji huu wa kipuuzi upomwingi na kama Waziri anataka nitampatia!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ucheleweshwaji wa namnahii ni uzembe na matumizi mabaya ya Ofisi, haukubaliki hatakidogo, hata mtu atoe visingizio gani! Huu ni uzembe wahali ya juu na hili halikubaliki hata kidogo! Nachelea kusemakuwa ucheleweshaji wa namna hii siyo kuvutia wawekezajiila ni kufukuza wawekezaji! Mwekezaji hawezi kuja kufanyabiashara na ofisi kama hizi. Bila alama yake ya biasharakusajiliwa kwa wakati, hawezi kuwa na uhakika kama sheriaitamlinda huko sokoni!

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi, ofisi hii hainakawaida ya kujibu hata barua za wateja wanaofuatiliamaombi yao ambayo yamekwama katika ofisi hii miakanenda miaka rudi. Ukiwa na bahati, sana sana utapewa jibula mdomo kuwa faili halionekani. Faili litaachaje kuonekana!Kama ofisi hii inapoteza mafaili kiasi hiki, inasajili nini? Hiihaikubaliki hata kidogo! Wengine hawawezi wakawawanajenga uchumi kwa kuvutia wawekezaji huku wenginewanaubomoa uchumi huo kwa kukatisha tamaawawekezaji.

Page 277: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

277

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utafiti wangu usiorasmi, nimegundua sababu kubwa zinazosababishaucheleweshaji huu katika ofisi hii kuwa ni hizi zifuatazo:-

Uongozi mbovu na usiokuwa na maono. Kwakiongozi yoyote mchapa kazi, BRELA ni kisima chakutengeneza hela na kuingizia Serikali mapato. Kamamaombi yote yanayopelekwa BRELA kusajiliwa yangekuwayanafanyiwa kazi, kwa kila hatua na kwa wakati, mapatoyake yangeongezeka sana. Vile vile kama Makampuni yotemfu yangefutwa au yanayoshindwa ku-fi le returnsyangefuatiliwa na kupigwa faini kama sheria inavyoelekeza,BRELA ingetengeneza mabilioni!

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalan niongelee kero yaucheleweshaji wa utoaji matangazo wa maombi ya usajiliwa alama za biashara. Hili nalo ni tatizo lingine sugu tena lakujitakia kwa mujibu wa sheria. Msajili wa Hataza na alamaza biashara anatakiwa achapishe jarida ambamo atakuwaakitangaza maombi ya usajili yaliyoletwa kwake kwa usajili.Lengo la kutangaza ni kutoa fursa kwa watu wenginekupinga au kutoa maoni yao kuhusu ombi lililotangazwa.Jarida linalochapishwa na ofisi hii linajulikana kama “ThePatents Trade and Service Marks Journal” na linatakiwa liwelinachapishwa mara moja kwa mwezi. Kila tangazo mojalinalotolewa humu, mwombaji lazima alipie Sh. 15,000/= lakinicha ajabu ni kuwa kuna ucheleweshaji mkubwa wa kutoahata kijarija hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya mwaka 2,000maombi yote yalikuwa yanatolewa kwenye gazeti la Serikali.I l i kuharakisha utoaji wa matangazo, Msaji l i alianzakuchapisha jarida hili baada ya kutungwa kwa sheria ndogoza alama za biashara za mwaka 2000 (The Trade And ServiceMarks Regulations 2008 GN 40 of 2008) kijarida chenyewe nirahisi mno kukiandaa, unahitaji tu komputa moja na printermoja basi. Pamoja na urahisi wa kutengeneza kijarida hiki,cha ajabu ni kuwa hata utoaji wa kijarida hiki nako kunaucheleweshaji uliopindukia.

Page 278: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

278

Mheshimiwa Mwenyekiti, utashikwa na mshangaoukiambiwa kuwa kuna maombi mengi ya usaji l ihayajatangazwa kwa miaka zaidi ya miwili hadi mitatuwakati kazi kama hii ingefanyika kirahisi kama kungekuwana uongozi makini na uwajibikaji. Japo huu ni mwezi watano naambiwa kijarida hiki mwaka huu kimetoka marambili tu badala ya kutolewa japo mara moja kila mwezi.Kuna nini hasa kinachozuia uchapishaji wa maombi yoteyaliyo tayari kwenye hili jarida? Kwa nini wasichapishe volumehata tano kwa kila mwezi ili kumaliza msongamano wa hayamaombi? Kwa nini wasiajiri mtu mmoja au wawili ambaokazi yao itakuwa ni hii ya kuanda a hiki kijarida tu? Kunatatizo gani? Naomba Mheshimiwa Waziri afuatilie uzembehuu na atupe majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani hata kazi rahisiya kuchapisha jarida lao la matangazo ambalo kilaanayetangaza kule analipia Sh. 15,000/= na linauzwa shilingi5,000/= lishindwe kutoka kila mwezi kama inavyotakiwa.Yamkini wakati BRELA kuna application zaidi ya 3000 zinasubirimatangazo tangu mwaka 2012. Jarida hili lilitoka mwaka2012 mwezi Novemba. Mwezi Desemba wa mwaka 2012halikutoka! Januari mwaka huu halikutoka! Februari likatokana maombi yaliyotangazwa ni machache ukilinganisha nayanayosubiri kutangazwa! Mwezi wa Machi halikutoka!Nasikia la mwezi Aprili ndiyo limetoka wiki iliyopita na kwaminajili hiyo la mwezi Mei halijatoka na halitatoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama siyo uzembe ni nini?Kwani kuna ugumu gani na gharama gani kutoa hichokijarida kila mwezi? Kwanza kiko in black and white nahakifanyiwi binding yoyote. Ni ku-print tu. Lakini utashangaainamchukua mtu zaidi ya miezi minne kukitoa, wakatikinatakiwa kutoka kila mwezi. Mimi nafikir i dawa nikubinafsisha tu BRELA ili apatikane mtu anayejua maana yakufanya na kusajili biashara na alama za biashara. Mbonawenzetu Kenya wameweza? Ukiingia kwenye mtandao waounakuta majarida yao ya kila mwezi na kila mwaka kuanziaJanuari mpaka Desemba, yapo mtandaoni katika tovuti yaoya http;//wwe.kipi.go.ke/index.php/past-ip-journals.

Page 279: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

279

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wenzetu Wakenya,jarida lao linatolewa kila mwezi na linaingizwa mtandaonikila mwanzo wa mwezi ukitembelea matandao wa BRELAkwenye tovuti yao ya http;//www.brelaz.org/?section=publication &page=journals, unachokutana nacho ni aibuna kituko! Wame-post vijarida 10 tena vya zamani vyamwaka 2010 basi! Hii ni aibu na ni uzembe uliopindukia!Mheshimiwa Waziri tupia macho BRELA na peleka vijanawenye bongo zinazochemka na wachapa kazi na siowazembe na wapiga kelele kwenye vyombo vya habariwakati ni madudu tu yanafanyika pale!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchache wawatumishi ofisi hii ya Msajili wa Hataza na Alama za Biasharaina upungufu mkubwa sana wa wasaidizi wa msajili (assistantregistrars) Ofisa Masijala, Wachunguzi (examination officers)makarani, Makatibu Mahsusi na Watumishi wenginembalimbali ukilinganisha na maombi yanayopelekwa katikaofisi hii kila mwaka. Mimi nafikiri watumishi wote pale na hasawanaotakiwa washughulikie maombi ya usajili hawazidikumi. Ni vigumu kwa idadi hii ndogo ya watumishikushughulikia maombi yote yanayotolewa kwenye ofisi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Wakala wa Usajilina utoaji leseni za biashara ni ofisi inayojitegemea, nashauriwaajiri wafanyakazi wa kutosha mara moja. Kwani fedhazote wanazokusanya kama ada na tozo mbalimbaliwanapeleka wapi? Gharama ya kupeleka ombi la kusajilialama moja ya biashara ni Sh. 50,000/=, na tangazo lake nielfu Sh.15,000/= na ya cheti ni Sh. 60,000/=, jumla ni Sh. 125,000/= achilia mbali tozo nyingine ndogo ndogo za ziada! Kwafedha zote hizi, kwanini hawaajiri watumishi wa kutosha nakumaliza kero hii ya ucheleweshaji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namshauri Waziriafuatilie hili na ahakikishe kuna wafanyakazi wa kutosha palewenye elimu na ari ya kuchapa kazi na wenye kusimamiwabarabara kufanya kazi siyo kugeuza ofisi ya Serikali kijiwe iliTaifa letu lisonge mbele.

Page 280: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

280

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mishahara midogona ukosefu wa motisha kwa wafanyakazi ukifika katika ofisihii utaona mara moja kuwa wafanyakazi walioko palewamekata tama. Hawana motisha wala ari ya kufanya kazi.Sababu kubwa ni kuwa mishahara na marupurupu yao nimidogo mno! Kwa kuwa Wakala wa Usajili na utoaji leseniza biashara ni ofisi inayojitegemea. Nawashauri waangaliejinsi ya kuwahamasisha wafanyakazi wao. Kwaniniwasiwaige wenzao wa TRA wakalipa mishahara inayovutia?Kwani mishahara ya hawa watumishi inalipwa na nani?Fedha zote wanazokusanya wanapeleka wapi kamahawawezi kuzitumia ili kuleta tija?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukosefu wa vitendeakazi na uwekaji wa kumbukumbu mbovu, hili nalo ni tatizolingine sugu. Ofisi hii ina upungufu mkubwa sana wa vitendeakazi na hasa komputa, uwekaji wa kumbukumbu katika ofisihii bado unategemea makaratasi na mafail i yakeyanahifadhiwa vibaya. Mbaya zaidi sehemu mafaili hayayanakohifadhiwa siyo salama na mara nyingi nyarakamuhimu zinapotea. Ni kitu cha kawaida kabisa katika ofisihii kukuta nyaraka mbalimbali ulizopeleka kusajili maombiyako hazipo na ukiuliza unaambiwa hazionekani, letanyingine!

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nchi za wenzetuzinahifadhi kumbukumbu zao vizuri na hasa kwenye mtandaowa komputa ofisi hii kwao kutumia komputa kuhifadhikumbukumbu bado ni ndoto. Katika ofisi hii ukitaka kupatataarifa za alama fulani ya biashara iliyosajiliwa pale ni lazimausubiri utafutiwe faili uletewe. Bado haijawezekana kufanyasearch au kutafuta habari za faili fulani kwa kutumiacomputer. Mara nyingi ukitaka taarifa za alama fulani yabiashara unaambiwa faili halionekani! Hii inatokea maranyingi tu na siyo mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeambiwa na mmoja wawapiga kura wangu kuwa mwaka 2008 ofisi hii ilijaribu kuanza

Page 281: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

281

utaratibu wa kutumia computer kuhifadhi kumbukumbu nakushughulikia maombi ya usajili wa alama za biashara.Naambiwa pia kuwa walijitahidi sana kwani ukipeleka ombilako, linaingizwa kwenye computer na unapatiwa nambaya ombi lako.

Naambiwa pia kuwa hii ilifanikiwa kwa msaada waWorld Intellectual Property Organisation (WIPO) lakini sasanaambiwa kuwa shughuli hii yote imetumbukia nyongo.Maombi mengi ya usajili yaliyopokelewa tangu mwaka 2008hayajafanyiwa kazi yoyote kwa sababu eti ule mfumo waowa computer waliouanzisha uime-crash, zimegoma,zimesinzia, zimeharibika, sijui zimetafunwa na kirusi gani!

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yaani sisi badala yakutumia computer kuturahisishia kazi, sasa zinafanya kazizisiende kabisa. Namwomba Mheshimiwa Waziri afuatilie hilina alishughulikie mara moja. Hatuwezi kuvutia wawekezajikwa kuwaambia kuwa oh, samahani mzee, maombi yenuya kusajili alama za biashara mliyoleta tangu mwaka 2012hayawezi shughulikiwa kwa sababu computer zetu zimeuguakifafa! Huku ni kufanya mchezo na kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ukosefu wa mafunzoya mara kwa mara kwa wafanyakazi na usimamizi wakutosha wa kazi, pia nadhani kazi haziendi kwenye ofisi ilekwa sababu hakuna utaratibu wa kuhakikisha watumishipale wanapewa mafunzo ya mara kwa mara ili kwenda nawakati. Pili, nadhani usimamizi wa kazi pale uko legelege.Kwa nini tusiwe tunapeleka watumishi hawa waende kwawenzetu wakajifunze wao wanafanyaje kazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naambiwa kuwa wenzetupale Kenya wamepiga hatua nzuri sana katika ofisi yao yausajili wa Hataza na Alama za Biashara. Kila mtumishi paleanajua anachotakiwa kufanya na siyo kuhudhuria ofisini ili

Page 282: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

282

mradi siku iende. Wenzetu mtumishi akifika ofisinianakabidhiwa idadi ya mafaili ya kushughulikia kwa siku hiyona kama hatayamaliza, basi itamlazimu afanye kazi kwamuda wa ziada na hata siku za wikiendi i l i amalizeassignment yake. Namshauri Mheshimiwa Waziri aliangaliepia hili alifuatilie kwa umakini ili ofisi hii ibadilike. Lazima nasitubadilikie jamani! Muda wa kufanya kazi kwa mazoeaulishapitwa na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, mimi naaminikabisa tutaweza kuvutia wawekezaji kama tukimalizamatatizo haya madogo madogo ambayo ni kero kubwasana. Mara nyingi hivi vitu vidogo vidogo ndivyovinayokatisha tamaa. Haya mambo ya njoo kesho aukeshokutwa hayatatufikisha popote. Huu ni muda wakubadilika na ningeshauri Waziri afuatilie kitengo hiki.Mwekezaji anachotaka ni vitendo na siyo ahadi au maneno.Anataka kujua muda na ratiba ambao ombi lakelitashughulikiwa na kukamilika na kifanyike kwa vitendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashindwa kuelewa,kwa nini BRELA wanasuasua katika huduma zao? Chakushangaza, badala ya kuboresha kwanza huduma zao iliwatu wapate value for money, wanakuja na hekaya zaabunuasi za kuongeza ada za usajili, tena wanataka baadhizilipwe kwa dola za Marekani badala ya fedha za kitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi ni kuwa, uzembewa BRELA umepitiliza na unakifu. Mfano tarehe 4 Novemba,mwaka 2009 walizindua kitu wanaita Mkataba wa Hudumakwa Wateja, yaani Client Service Charter na ukiangaliaukurasa wa tisa wanaonyesha muda utakaotumika,mathalan kushughulikia ombi la kusajili alama za biashara.Walidai kuwa watakuwa wanajibu ndani ya wiki mbili naitatangazwa na kusajiliwa ndani ya siku 90. Huu wote ulikuwani uongo na sanaa ya hali ya juu, maana hawafuatiwalichoahidi na hata ukiandika barua ya malalamiko kwaMtendaji Mkuu wa BRELA kuhusu ucheleweshaji unaofanywahupati jibu!

Page 283: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

283

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi utadaije kuwa utasajiliwa alama ya biashara ndani ya siku 90 wakati hata kijaridachako unachotakiwa utoe kila mwezi kinakushinda nainachukua zaidi ya miezi minne kutoa nakala moja? Miminashauri Mheshimiwa Waziri aifuatilie na aifumue BRELA, atoemwongozo na kama nilivyosema, kama anahitaji ushahidiwa haya niliyosea nitampatia mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu kule Uingerezamaombi kama haya ya kusajili alama ya biashara lazimayashughulikiwe ndani ya kipindi cha wiki mbili. Ndani ya wikimbili lazima ujue kama ombi lako limekubaliwa au hapana.Ndani ya mwezi mmoja lazima liwe limetangazwa kamamleta maombi amemaliza taratibu zote za ndani ya siku tisini(90 days) lazima liwe limesajiliwa na cheti kutolewa. Kwawenzetu kama ombi lako halijashughulikiwa katika kipindikilichoonyeshwa kwenye mwongozo, basi ni lazima utapewamaelekezo tena kwa maandishi, ni sababu ipi inacheleweshaombi lako na unatakiwa ufanye nini ili ombi lako lisongembele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kwani ni ninikinamshinda huyu msajili wetu? Au hata kazi kama hiitunasubiri management kutoka nje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayonaunga mkono hoja.

MHE.SALUM KHALFAN BARWANY: MheshimiwaMwenyekiti, kutokana na kugundulika kwa gesi asilia nchinikuwa na changamoto kadha zimekuwa zikij itokezakuhusiana na manufaa yatokanayo na rasilimali hii. Kunamigogoro kadhaa imejitokeza kwa wananchi kwamba kwasasa hawaoni faida yoyote kuhusiana na rasilimali hii. Serikalikupitia Mawaziri wake akiwemo Waziri Mkuu wameshawahikuonyesha dhamira ya kutaka wananchi ambao maeneoyao rasilimali hii inatoka wananufaika kupitia viwandavitakavyojengwa huko.

Page 284: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

15 MEI, 2013

284

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata katika hotuba yaMheshimiwa Rais aliyoitoa kupitia vyombo vya habarializungumzia umuhimu wa kuwepo viwandavitakavyozalisha malighafi zitokanazo na gesi kama mboleaplastic na nilu. Naomba Mheshimiwa Waziri katikamajumuisho yake alieleze Bunge na wananchi wa Lindi naMtwara ni lini ujenzi wa viwanda hivi utaanza na ni maeneogani yametengwa kwa shughuli za ujenzi wa viwanda hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya Waziriimegusa maeneo kadhaa kuhusiana na ukanda wauwekezaji (EPZ) kama Bagamoyo Mkuranga na kadhalika,lakini sijasikia kabisa Mkoa wa Lindi ukiingizwa katika zonehiyo. Sababu ni nini? Hakuna maeneo au kuna ukiritimbagani unaosababisha kutotengwa kwa maeneo hayo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la korosho,limekuwa likileta kero na manung’uniko kila mara hukuwananchi wakilalamikia bei ndogo ya zao hilo. Aidha, kwaupande wa viwanda vyake, vimebinafsishwa na kwa sasavimegeuzwa maghala ya kuhifadhia mazao na vitu vingine.

Naomba Mheshimiwa Waziri katika majumuisho yakeaeleze kuna mpango mkakati gani wa kuhakikisha zao lakorosho lina pata soko la moja kwa moja kutokana na kuuzakorosho ghafi na/au zile zilizokuwa Processed badala yakusubiri wanunuzi wa sasa ambao tayari wanaonekana nitatizo kwa maendeleo ya wakulima wetu?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, orodha yetuimekwisha na jioni hii ya leo Mheshimiwa Mtoa Hojaatakamilisha hoja yake. Kwa hiyo, nasitisha shughuli za Bungempaka saa 11.00 jioni ya leo.

(Saa 6.57 mchana Bunge liliahirishwa hadi saa 11.00 Jioni)

Page 285: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

285

15 MEI, 2013

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, naombakumshukuru Mungu, kwa kunipa afya hii leo na naombaniwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge, ambaowameonesha kwamba, wanampenda sana Waziri wangu,lakini hawakipendi Chama cha Mapinduzi. Napendakukushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia na kujibubaadhi ya hoja zilizojitokeza katika Hotuba ya Waziri waViwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, naungamkono hoja iliyo mbele yetu kama ilivyowasilishwa naMheshimiwa Dokta Abdallah A. Kigoda, Waziri wa Viwandana Biashara, kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru sana Serikali yaCCM kupitia Wizara ya Fedha, kwa kuwa sikivu na kufanyamarekebisho ya Bajeti ya Maendeleo, Fungu 44 - Wizara yaViwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.Kwa kuzingatia ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti,pamoja na Kamati ya Kudumu ya Sekta ya Uchumi, Viwandana Biashara kuhusu mahitaji mapya ya Fungu 44 la Wizara yaViwanda na Biashara na Masoko, Serikali imeongeza shilingibilioni 30 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa EPZ DevelopmentProject, Code Number 4933, Kurasini Logistics Hub, ambaoupo chini ya Kifungu cha Namba 1003 - Policy and Planning,kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014. Hivyo, Mradi huuutakuwa na jumla ya shilingi bilioni 31 ikijumuisha shilingi bilionimoja ambazo tayari zimetengwa kwenye Mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kwa mwaka 2012/2013, Serikali imekuwa sikivu vilevile, imetoa jana shilingi bilioni25 kwa ajili ya kukamilisha fidia ya Mradi huu wa EPZ hukoKurasini. Hii inajumuisha na fedha ambazo zimetengwa kwamwaka unaokuja, yaani shilingi bilioni 30 pamoja na ile moja,bilioni 31, ukiunganisha na bilioni 25 za mwaka huu ambaounaishia Juni, jumla inakuwa shilingi bilioni 55, ambazozinatosha kwa awamu hii ya kwanza ya Mradi huu katika

Page 286: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

286

15 MEI, 2013

eneo hilo la Shimo la Udongo, lenye hekari 38.12. Kwa hiyo,tunaipongeza sana Serikali na hasa kama nilivyosemakwamba, tunaipongeza sana Kamati ya Bajeti pamoja naKamati ya Kisekta ya Uchumi, Viwanda na Biashara, kwa kazinzuri hii ambayo wanafanya kusaidia pale ambapo inabidiisaidiwe. Kipaumbele ambacho kilikuwa mbele yetu hiki chaEPZ kusema kweli kama tusingefanya bidii hii kupitia Kamatihizi, ingekuwa ni pengo kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndiyo maananatanguliza kabisa shukurani zangu kwa Kamati hizi mbiliambazo zimefanya kazi nzuri sana kwa Wizara hii ya Viwandana Biashara kwa wakati kama huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii, kuwaombaWaheshimiwa Wabunge wote, mtuunge mkono kwa kupitishabajeti hii ili itupe nafasi ya kutekeleza wajibu na majukumuyetu kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 kamailivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi binafsi, Waziri wangu,Menejimenti ya Wizara, pamoja na Taasisi zote zilizo chini yaWizara hii na Watumishi wote, tumedhamiria na tunakusudiakufanya kazi hii muhimu ambayo ipo mbele yetu. Wajibu wetumkubwa tulionao kwa hivi sasa ni kuibadilisha nchi hii kiuchumiili tufikie nchi yenye kipato cha kati (Middle Income Country),ifikapo mwaka 2025 na hii ndiyo dhamira na hii ndiyo kauliambayo sisi tunafanya nayo kazi kama Wizara, kamaWatumishi wote wa Wizara pamoja na Taasisi zake zotekwamba, angalau nchi hii ifikie kwenye hatua ya kuwa nchiya kipato cha kati ifikapo 2025. Ni kazi kubwa ambayo ipombele yetu, nawasihi sana Wabunge wote ambao mkohapa, tushirikiane sisi wote kwa pamoja kutekeleza azma hiiambayo ipo mbele yetu chini ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeamua sasa kuongezana kuendeleza viwanda vidogo, tunaendeleza viwanda vyakati na vile vikubwa. Hii ni pamoja na kukuza na kuendelezabiashara kubwa na ndogo kwa kupanua wigo wa masokoya ndani pamoja na yale ya nje kwa bidhaa zilizoongezwa

Page 287: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

287

15 MEI, 2013

thamani. Sisi sote tunaelewa kuwa, hakuna nchi iliyoendeleabila viwanda. Sekta ya Viwanda ndiyo Sekta pekee ambayoinaweza kupunguza kama si kuondoa kabisa umaskini ulioponchini kwa kuongeza ajira kwa vijana wetu na kuongezakipato chetu. Tutekeleze sasa kwa mafanikio makubwa, yaanibig results, now kwa kushirikiana pamoja na wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kuanza kujibu hojambalimbali za Waheshimiwa Wabunge, nakushukuru wewebinafsi tena kwa kunipa nafasi hii. Kutokana na muda,naomba kusema kwamba, hoja zote za WaheshimiwaWabunge zitajibiwa kwa maandishi na kusambazwa kwaWaheshimiwa Wabunge wote muda siyo mrefu wakati tupohapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huu wajumla, sasa napenda kufanya majumuisho kwa kutoamaelezo mafupi, yenye ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zaWaheshimiwa Wabunge, zilizotolewa wakati wakichangiaHotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, alipokuwa akiwasilishaHotuba ya Makadirio ya Mapato ya Wizara yake, pamojana Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alipokuwaakiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara yake, pamoja na Hotuba ambazo zilishatanguliaza baadhi ya Mawaziri ambao Wabunge wamechangia nahoja hizo zinahusiana moja kwa moja na Wizara ya Viwandana Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kwa ruhusayako nijikite kwenye hoja ambazo zipo very specific, ambazozimechangiwa na Waheshimiwa Wabunge katika kuungamkono hoja hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa GaudenceKayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki, alitaka kujua kwavile CAMARTEC imeonesha uwezo wa kutengeneza trekta,sasa ni wakati mwafaka kwa Serikali kuiwezesha iwezekuzalisha matrekta mengi zaidi. Nasi tunasema kwamba, hiini mojawapo ya Taasisi za Utafiti chini ya Wizara hii yaViwanda na Biashara. CAMARTEC inatoa changamoto nyingi

Page 288: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

288

15 MEI, 2013

kubwa katika kuendeleza viwanda kupitia utafiti pamoja nakutoa huduma kwa wadau wa Sekta hii. CAMARTECwanabuni trekta dogo la matumizi mengi ambalo linasaidiasana kwa wakulima wadogo na wale wakulima wa kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara yaViwanda na Biashara, imekuwa ikisaidia CAMARTEC kupitiafedha za maendeleo ambazo ndizo zilizotumika kutengenezatrekta hilo linalojulikana kama fast tractor. CAMARTEC inahitajijumla ya shilingi bilioni nne kwa kufungua kiwanda chakutengeneza matrekta. Vilevile Wizara kupitia Shirika laMaendeleo la Taifa (NDC), tayari imefanya mpango wakuipatia CAMARTEC eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda husikapale Kilimanjaro Machine Tools.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na ufinyu wabajeti, CAMARTEC imeanza mazungumzo na Benki yaRasilimali Tanzania, yaani Tanzania Investment Bank (TIB), ilikuweza kupata mkopo wa shilingi bilioni nne kuiwezeshakushiriki kuanza kuzalisha matrekta. Makubaliano haya yaawali kati ya CAMARTEC na TIB tayari yamekwishakamilikana upembuzi yakinifu, yaani feasibility study imeanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa MahmoudMgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, anapenda kujuaKiwanda cha MPM Mgololo pamoja na kwamba kinazalishakaratasi, lakini hakina kiwanda cha kutengeneza mifuko.Mifuko mingi inatengenezwa Kenya. Sasa alitaka kujua kwanini kiwanda hiki cha MPM Mgololo hakina uwezo wakutengeneza mifuko. Kiwanda cha MPM Mgololo kisheriahakiruhusiwi kutengeneza mifuko, kwa kuwa watakuwawanakiuka Shera za nchi. MPM Mgololo ndiyo wazalishajipekee Tanzania wa bidhaa ya karatasi toka malighafi ya mitina hivyo kama wataanza kujikita kwenye biashara yakutengeneza vifungisho ni dhahiri kwamba, watamiliki sokona kukosekana ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, nchi nzima inaviwanda sasa hivi vipatavyo vinane vikubwa vya kufungashiaau vya kifunganishi vya karatasi, ambazo wangeweza

Page 289: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

289

15 MEI, 2013

kutengeneza MPM Mgololo ambao hawaruhusiwi kisheria.Kwa hiyo, viwanda hivi vinane naona vitakidhi hii shughuli auhii kazi ya kutengeneza mifuko badala yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ezekiel Maige,Mbunge wa Msalala, pamoja na Wabunge wengine;Mheshimiwa Munde Tambwe - Mbunge wa Viti MaalumTabora, Mheshimiwa Said Juma Nkumba - Mbunge waSikonge na Mheshimiwa Murtaza Mangungu - Mbunge waKilwa Kaskazini, wao wanapenda Serikali ije na mkakati wauhakika wa kufufua viwanda vya kuchakata pamba nambolea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi nasema, takwimuzilizopo zinaonesha kuwa, vipo viwanda 60 vya kuchakatapamba hapa nchini. Viwanda hivi vipo katika Mikoainayolima pamba kwa wingi, ambapo Mkoa wa Mwanzakuna viwanda 21, Mkoa wa Shinyanga una viwanda hivi vyapamba 29, Mkoa wa Mara una viwanda vinne, vilevile Kagerakuna viwanda vya pamba, Morogoro, Kilimanjaro, Pwani naManyara. Mikoa hii ya Kagera, Morogoro, Kilimanjaro, Pwanina Manyara, wana kiwanda kimoja kimoja cha pamba.Viwanda hivi vina uwezo wa kuchakata marobota yapatayo327,074 ya pamba kwa mwaka wakati uzalishaji ni takribanimarobota 228,051 kwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda hivi vinamilikiwa naVyama vya Ushirika chini ya usimamizi wa Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika na kampuni binafsi. Wizara ya Kilimokupitia Bodi ya Pamba, yaani TCB, imeandaa mkakati wakuendeleza Zao la Pamba, ambapo kilimo cha mkataba katiya wakulima na wanunuzi wa pamba kinatekelezwa. Kwaupande mwingine, mkakati wa kuendeleza sekta ya nguona mavazi umeandaliwa na unaendelea kutekelezwa naWizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Kiwanda chaMbolea, kama nilivyosema, Wabunge hawa wanataka kujuakuhusu Kiwanda cha Mbolea; mkakati uliopo ni kujenga.Wizara kupitia NDC, imeendelea na juhudi za kuanzisha

Page 290: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

290

15 MEI, 2013

viwanda vya kemikali na mbolea kwa kutumia gesi asilia hukoMtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Said Amour Arfi,Mbunge wa Mpanda Mjini, anapenda kujua kiwanda chakusindika tumbaku kitajengwa lini Tabora? Wizara inatekelezamkakati unganishi wa kuendeleza Sekta ya Viwanda, ambaomoja ya vipaumbele ni katika kuongeza thamani mazao yakilimo, ikiwemo zao hili la tumbaku. Kwa hiyo, azma yakujenga kiwanda Tabora ipo pale pale na sehemu kubwaya viwanda hivi ambavyo naviongelea tayariimeshaongelewa na Mheshimiwa Waziri wakati anahitimishaBajeti yake hii ya Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Omari Nundu,Mbunge wa Tanga Mjini, anataka kujua kwa nini wakulimawameacha kulima katika maeneo yao ambayoyametengwa kwa ajili ya EPZ. Suala hili liangaliwe tena upyaili liweze kutoa nafasi kwa maeneo ambayo yametengwalakini hakuna kinachoendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi waliopo katikamaeneo haya yaliyotengwa kwa ajili ya EPZ, ambayo taratibuza utoaji ardhi hazijakamilika, Serikali imewaruhusu kuendeleana shughuli za kimaendeleo ambazo siyo za kudumu ilikutowakwamisha katika shughuli zao za kila siku za uzalishajimali. Kwa hiyo, hivi ninaposema, mamlaka hii ya EPZ inatengamaeneo mbalimbali katika nchi nzima, Mikoa yote Tanzanianzima, kule ambako utaratibu huu haujakamilika, hainamaana kwamba wale ambao maeneo yao yametwaliwayakae bure tu. Kwa hiyo, ruhusa inatolewa kwamba,wanaweza kuendelea na shughuli za kilimo mpaka hapoambapo taratibu zitakamilika za kutwaa maeneo hayo chiniya EPZ pamoja SEZ.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa HezekiahChibulunje, Mbunge wa Chilonwa, anataka kujua kiwandacha kusindika zabibu katika eneo lake kitapatikana lini, kwasababu Chilonwa kuna zabibu za kutosha. NimjulisheMheshimiwa Mbunge kwamba, utaratibu wa kujenga

Page 291: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

291

15 MEI, 2013

kiwanda cha kusindika zabibu katika eneo hilo upo.Nampongeza Mheshimiwa kwa juhudi anazozifanya katikaJimbo lake na maeneo mengine ya Mkoa wa Dodomakutokana na kujishughulisha na kilimo hiki cha zabibu. Mkoawa Dodoma na Wilaya zake pamoja na maeneo ya Mvumina Kongwa ni maarufu sana katika kilimo hiki cha zabibu nakweli haja ipo ya kujenga kiwanda cha kusindika zabibu iliMkoa wa Dodoma uendelee kuzalisha mvinyo. Kiwandahiki ambacho kitajengwa eneo la Chilonwa kitasaidiawakulima wa eneo la Kongwa, Mvumi na Chilonwa yenyewe,kwani watapata kiwanda cha kusindika zabibu na hivyokupata mvinyo kwa wingi. Zabibu zinazalishwa nchinizinaongezwa thamani kwa kubadilisha bidhaa kama mvinyona hivyo kukuza ajira na kuongeza kipato kwa Wananchi.

Mheshimiwa Albert Ntabaliba, Mbunge wa Manyovu,yeye anataka kujua Soko la Mnanila Kasulu litajengwa lini?Maandalizi ya ujenzi wa soko katika eneo la Mnanila kupitiaMradi wa District Agriculture Sector Investment Project(DASIP), yamefikia hatua za mwisho. Soko hili ni moja yamasoko saba ya mipakani ambayo yatajengwa kupitia Mradihuu. Maeneo mengine ambayo yanahusika ni Mtukula kuleMisenyi, Kabanga kule Ngara, Kwenda kule Karagwe,Mrongo, Remagwe kule Tarime na Busoke kule Kahama.Zabuni za ujenzi wa masoko haya zimetangazwa mwezi Aprilimwaka huu na ujenzi wa masoko hayo unatarajiwa kuanzamwezi Juni, 2013 na kukamilika katika kipindi kisichozidi miezisita.

Mheshimiwa Dkt. Agustino Mrema, Mbunge wa Vunjo,ameomba kuharakisha ujenzi wa soko la matunda nambogamboga la Himo na Soko la Nafaka Lokolova. Natakanilieleze Bunge hili Tukufu kwamba, Tarehe 17 Mei, 2013,keshokutwa, kuna swali hili litajibiwa ndani ya Bunge hili Tukufu,nafikiri sitakuwa natenda haki kujibu sasa hivi. Kwa ufupi nikwamba, Mkoa wa Kilimanjaro umeingia makubaliano naBenki ya TIB kujenga soko la mbogamboga la Himo na sokola nafaka kule Lokolova. Majibu mengine kamili atayapatatarehe 17 Mei, 2013 kipindi ambacho nitakuwa najibu swalila msingi kwa swali lake hili.

Page 292: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

292

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mohamed Missanga, Mbunge waSingida Magharibi, alisema Wilaya ya Ikungi inazalisha sanamiwa na inafaa kwa uzalishaji wa sukari. Wizara iangalieuwezekano wa kupata mashine kwa ajili ya kuanzishaviwanda vidogo vya kuzalisha sukari. Kwa muda mrefu, Shirikala SIDO limekuwa na suala la kubuni na kutengenezamitambo midogo ya kusindika miwa, lakini mpaka sasahalijafanikiwa kutengeneza mashine hizo. SIDO itajitahidikutafuta teknolojia hiyo nje ya nchi ili kuwaunganishaWananchi wote wakiwemo wale wa Ikungi wanaozalishamiwa waweze kuzalisha kwa teknolojia hiyo na kuwezakuanzisha viwanda vidogo vya kusindika miwa. Hivyo, ni sualala subira, Mheshimiwa Missanga kipindi ambapo teknolijia hiimpya itakuwa imekamilika, jambo hili litawezekana. Tuvutesubira ili jambo hili nalo liweze kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja ya Mradi waTanzania – China Logistic Centre uliidhinishiwa shilingi bilioni60 kwa mwaka 2012/13, ambazo zilikuwa ni fungu maalum.Wakati napongeza Kamati zile mbili; Kamati ya Uchumi,Viwanda na Biashara na Kamati ya Bajeti, kwa kutenga kiasicha shilingi bilioni 30 mwaka huu ambao tunaombea bajeti.Niseme tu kwamba, mwaka 2012/2013, Serikali imekuwa sikivuimetoa shilingi 25 bilioni katakana na kiasi cha shilingi bilioni60 kilichokuwa kimeombwa. Fedha hizi zitalipa fidia kwaWananchi wa Kurasini ambao wataathirika na Mradi waTanzania – China Logistic Centre. Kwa suala hili, naomba nitoemajibu kwamba, Wizara inaendelea kufuatilia uwekezaji waujenzi wa miundombinu katika maeneo ya EPZ na ulipwajiwa fidia kama nilivyosema awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kwamba, Serikaliihimize uzalishaji wa mbegu za mafuta ya kula nchini na piaiongeze udhibiti wa viwanda vinavyoagiza mafuta nje yanchi, kusudi badala yake yatumike yanayosafishwa hapanchini. Wizara ya Viwanda na Biashara, inatambua umuhimuwa kuzalisha mbegu bora ili kuongeza uzalishaji wa mafutaya kula ndani ya nchi na kupunguza uingizaji wa mafutakutoka nje. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula naUshirika, inaendelea na utafiti wa mbegu bora za kukamua

Page 293: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

293

15 MEI, 2013

mafuta. Mafuta yanayoagizwa kutoka nje yanatozwa kodikulingana na degree of processing, ambapo mafutayanayosafishwa hutozwa asilimia 25 na semi-refined asilimiakumi, kwa ajili ya kudhibiti uagizaji wa mafuta kutoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nihitimishe kwakuwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge na kuwaombakuunga mkono hoja hii iliyo mbele yetu na kuipitisha. Lengolikiwa ni kuhakikisha kuwa, matarajio ya Watanzania kwaSekta hii yanapatikana kwa kupata baraka za Bunge ilikuwezesha utekelezaji wa malengo yanayotekelezeka,ambayo yamesheheni katika bajeti hii. Kuunga kwenu mkonohoja hii ni muhimu sana ili kutoa fursa ya kuelekeza uchumiwetu unaozingatia mahitaji ya nyakati tulizonazo sasa nanyakati zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziriwa Viwanda na Biashara. Sasa namwita mtoa hoja.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, nianze kwa kukushukuru wewe. Pili, nawashukuruWaheshimiwa Wabunge wote, kwa michango yao, ambayowameitoa hapa Bungeni leo katika kujadili hoja yetu yaWizara ya Viwanda na Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge waliochangia ni61, kumi wamechangia hapa Bungeni kwa kuzungumza naWabunge 51 wamechangia kwa maandishi. Napendakuwahakikishia kwamba, kwa sababu ya muda, tutaandaamajibu haya vizuri na tutayawasilisha kwa WaheshimiwaWabunge.

Namshukuru sana Naibu Waziri, kwa utangulizialioutoa na kwa kweli amegusia mambo mengi ya kimsingi,ambayo ni maeneo yaliyoguswa sana na michango yaWaheshimiwa Wabunge katika kujadili bajeti yetu.

Page 294: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

294

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongezasana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara,Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa na Kamati yake yote, kwamsaada mkubwa waliotupa katika kuifanya bajeti yetu kufikiakiwango hiki hapa leo. Tunakiri kwamba, Kamati hii kwetu sisikama Wizara ndiyo think tank yetu. Kwa hiyo, ushauriwanaoutoa na kwa sababu tunafanya kazi kwa karibu, niushauri ambao tunaupokea moja kwa moja. Vilevile,namshukuru Mheshimiwa Highness Kiwia, Waziri Kivuli waWizara hii, kwa hoja mbalimbali ambazo amezitoa. Ninahakika kwamba, utoaji wa hoja hizo ni katika kuboreshashughuli nzima zitakazofanywa na Wizara yetu na wala sikutokutilia maanani lugha inayotumika katika kutoa hoja hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wizara ya Viwanda naBiashara, tunachokiangalia hivi sasa ni kuona ni jinsi gani nchiyetu itafufua utaratibu mzima na mchakato mzima wakujenga viwanda ili kuhudumia Sekta mbalimbali za Uchumikatika Taifa letu. Ndiyo maana tunasema sasa hivi hailetimantiki kuzungumzia kiwanda kimoja kimoja, lazima wotetuangalie process of industrialization. Tukifika hapo, tutajikutalile lengo letu la kuelekea 2025 na kuwa semi-industrializedcountry tunaweza tukalifikia kwa jitihada zetu wote. Sasa hivitunafuatilia mkakati unganishi wa ujenzi wa viwanda ambaotunauita Integrated Industrial Development Strategy, ambaowengi wa Wabunge hapa mnaufahamu. Mkakati uleukiusoma kwa makini, umegawa Sekta ya Viwanda katikamaeneo matatu.

Kwanza, lazima nchi yetu ihangaikie na ishughulikieujenzi wa viwanda mama na ndiyo maana tunaweka msisitizomkubwa sasa kwenye miradi ya chuma, makaa ya mawena hivi sasa tumepata gas. Tunaelewa kwamba, hivi ndiyovitakuwa viwanda vyetu basic na viwanda hivi vitatupahatua ya kuelekea kwenye ujenzi wa viwanda nchini. Vilevilekatika mkakati huu, tunaangalia viwanda vya kati, sekta yanguo, viwanda vya kemikali, lakini pamoja na hayo,tunaangalia viwanda vya usindikaji wa mazao yetu ya kilimoili kuongeza thamani ya mazao yetu na bidhaa zetutunazouza katika masoko. Hatimaye kama maelezo mengi

Page 295: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

295

15 MEI, 2013

yalivyotoka kwa Waheshimiwa Wabunge, tunaangalia sualazima la uendelezaji wa viwanda vidogo vidogo kupitia Taasisimbalimbali hususan SIDO.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tunafahamu, sasa hivitukiangalia mfumo wa ujenzi wa viwanda katika uchumiwowote na katika nchi yoyote, hata nchi za mashariki yambali na nchi zinazoendelea; tunaona moja kwa mojakwamba, uzalishaji mkubwa unafanywa na small andmedium scale enterprises, ndiyo wanaozalisha kwa wingiukilinganisha na vile viwanda vikubwa. Sasa ndiyo maanatunasema, katika mkakati huu wa Integrated IndustrialDevelopment Strategy, hapo ndiyo tunapopaangalia.Tukishafika hapo, masuala ya biashara na masokoyanafuatilia na hatimaye sekta hii sasa kufanya kazi begakwa bega na Sekta ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Hotuba ya WaziriKivuli na Waheshimiwa Wabunge mbalimbali,wamezungumzia suala zima la ubinafsishaji. Suala laubinafsishaji kama nilivyosema mwanzo, ni vyema sotetukalielewa vizuri, kwa sababu tunapozungumzia ubinafsishajini lazima tuelewe maana yake ni nini. Maana yake kubwani kuondoa umiliki wa umma katika viwanda vyetu nakupeleka kwenye sekta binafsi. Njia zinazofanyika ni pamojana kuuza kiwanda moja kwa moja au kiwanda kile kupewawafanyakazi na management au kununua share (Hisa) aukuingia ubia au kukodisha baadhi ya viwanda hivyo.

Kimsingi, baada ya kuleta taratibu za TanzaniaInvestment Centre na taratibu nyingine, maana yake mojakwa moja ni utaratibu wa kukubali kwamba, sasa katikauendeshaji wa viwanda, moja kwa moja tutategemea sektabinafsi na katika ile miradi ambayo ni mikubwa, ndipotutaingia katika utaratibu wa Public Private Partnership. Sisihili tukilielewa, linatueleza moja kwa moja kwamba, sasa hivitukizungumzia Sera ya Ubinafsishaji is outdated,tunachoangalia ni yale matokeo yake yaliyojitokeza.Inaweza ikatokea hoja kwamba, ubinafsishaji viwanda vingivimekufa, lakini ni vizuri tukapima kwamba kuanzia miaka hiyo

Page 296: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

296

15 MEI, 2013

ya 90 mpaka sasa, tuna viwanda vingapi vipya na vya ainagani? Viwanda vingapi vimeanzishwa kupitia Sekta Binafsiau ushiriki kati ya Serikali na Sekta Binafsi na kadhalika.

Leo nilipozungumzia hotuba yangu, nilielezeakwamba, kwa muda wa miaka sita, EPZ na SEZ tayari mpakasasa ina viwanda zaidi ya sabini vipya vinavyofanya kazi.Vilevile kuna viwanda vingine sasa hivi tayari tunataka ku-employ katika maeneo haya. Vyote hivi ni viwanda katikanchi hii.

Mheshimiwa Naibu Waziri, amezungumza hapakwamba, viwanda vinavyochakata pamba hapa Tanzaniani vingi sana. Tunachotaka kusema ni kwamba, tuna haja yakuangalia ni maeneo gani tuyape umuhimu mkubwa ilikuinua sekta yetu ya viwanda.

Suala la shareholding ya Mradi wa Umeme wa Upepokule Singida, kuna masuala yamejitokeza hapa, lakini nafurahikwamba, Mheshimiwa Waziri Kivuli amesoma na waleshareholders. Nimefuatilia na BRELA, sikuona katika Wajumbewale kwamba, kuna Mbunge au ndugu yake Mbunge auyeyote yule. Sasa kama kuna taarifa nyingine zinawezakupatikana kutoka BRELA, nadhani zitaweza kuthibitisha hilo,lakini mimi kama Waziri, sikuliona katika maelezo haya.

Kiwanda cha General Tire tunakipa umuhimumkubwa, ambacho amekizungumzia Mheshimiwa Kiwia. Hiyotumekwishasema, kimezungumzwa pia na MheshimiwaNtukamazina. Vilevile, hata katika Bajeti ya mwaka ujao,tumekitengea kiwanda hiki karibu shilingi bilioni sita, tunatakakifufuke kwa sababu kinazalisha zao muhimu sana hasa katikasekta ya usafiri.

Mheshimiwa Ntukamazina, ametoa hoja mbalimbali;Wizara ianzishe Viwanda vya Zana za Kilimo na taratibu zakufufua viwanda vingine kama Mang’ula Complex; hilitunaendelea nalo sasa hivi na ndiyo maana katika hotubayangu nimesema, tayari CHC imeshaanza kuitisha wamilikiwote wale wenye viwanda ambavyo havifanyi kazi na kati

Page 297: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

297

15 MEI, 2013

ya hao, wako Mang’ula Complex wameshafika kule,wamepeleka Business Plan zao na nina hakika kwa kuendeleahivi, tunaweza tukafikia mahali pazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mheshimiwa Dkt.Augustine Mrema, aliuliza katika mchango wake kwamba,hatukutaja masoko yake mawili yale ya Himo. Sisi tulifikiriayale ni ya Kimataifa siyo ya mipakani. Pale tulikuwatunazungumzia masoko ya mipakani, lile tumeshali-categoriseni soko la kimataifa, kwa hiyo, ndiyo maana hatukulitaja. Kilekiwanda kinachojengwa Himo mjini, tunajua kwamba kunautaratibu ambao kiwanda kikijengwa, Wizara kwa kushirikianana NEMC lazima itoe kibali; tutafuatilia hili na kuona uhalisiwa kiwanda hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Gaudence Kayombo, amezungumziasuala la Ngaka, ambalo ni muhimu kwa sababu ule ni mojaya Mradi himili katika ujenzi wa uchumi wetu hasa tukizingatiakwamba, kile ni mojawapo ya kiwanda mama. Kamanilivyosema kwenye maelezo yangu asubuhi, tutalifuatiliasuala hilo vizuri na tayari kwa bahati nzuri, NDCimeshashirikisha Uongozi wa Wilaya, wa Mkoa na hataMheshimiwa Mbunge, ameonesha moyo mkubwa sanakushiriki katika suala hili.

Tunachotaka ni kwamba, Mradi ule uendeleeusiathirike na Wananchi waelewe kwamba ule Mradi ni waona wao wau-support badala ya kuleta matatizo ambayohayatasumbua eneo la Ngaka peke yake, bali yatasumbuauchumi wetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Hamoud Abuu Jumaa, Mbunge waKibaha, amezungumzia sana masuala ya SIDO. Umuhimu wakutenga fedha za kutosha katika Taasisi hii ili kusaidiawajasiriamali wadogo na wafanyabiashara ndogo ndogo nawale wenye viwanda vidogo. Hili vilevile limezungumziwatena na Mheshimiwa Deogratias Ntukamazima, MheshimiwaNamelok E. M. Sokoine, Mheshimiwa Susan Lyimo,Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mheshimiwa StephenWassira, Mheshimiwa Kombo Hamis Kombo, Mheshimiwa Lucy

Page 298: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

298

15 MEI, 2013

Owenya na Mheshimiwa Murtaza Mangungu. Hili tunalielewavizuri na ndiyo maana tumekuwa tunajitahidi sana, pamojana fedha za ndani tunazozipeleka SIDO, tuna utaratibumaalum wa Programu ya Movie, ambayo inapata fedhakutoka nje ambazo zinasaidia ku-supplement fedha ambazowanapewa SIDO katika kuendeleza sekta hiyo ya viwandavidogo vidogo na biashara ndogo ndogo.

Mheshimiwa Peter Msigwa, ameniuliza Serikali inawekamikakati gani kuondoa matatizo ya Machinga. Hoja niliyoitoaasubuhi, ni hoja ambayo mimi kama Waziri niliyepewadhamana ya kuendesha biashara, biashara ndogo,wajasiriamali, ninaitoa kwa uzoefu kwamba, hawatunaowaita Wamachinga, wengine wanaitwa wale wanao-offer door to door services, hawapo Tanzania peke yake.Wapo katika nchi nyingi tu Duniani, wote WaheshimiwaWabunge hapa ni mashahidi, ukienda Morocco utawakuta,South Africa utawakuta, London unawakuta, lakini ni watuambao tuko nao katika maeneo yetu. Sasa bugudha hiziwanazozileta Wamachinga kwa Serikali au kwa Halmashaurina bugudha wanazopata Wamachinga kutoka Halmashaurini lazima sasa tukae tuziweke sawasawa. (Makofi)

Zipo By Laws ambazo zinaweza zikafanyiwa kazi, hawawana Taasisi zao, kama nilivyozitaja mchana, kuna VIBINDO,ASBO, TAMDA, zipo kama sita hivi. Tunaweza tukazungumzatu, tukakuta Wamachinga wanafanya kazi zao, wanaingizariziki zao na tatizo kubwa katika nchi hii ni ajira na wanaohusikani vijana. Kwa hiyo, ndiyo maana nasema kwamba, hili nisuala ambalo tunatakiwa tushirikiane kati ya Serikali,Halmashauri za Mji na wao wenyewe Wamachinga ilikuliweka sawa; hiyo ndiyo ilikuwa maana yangu kubwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la MheshimiwaShibuda Magalle, aliulizia kwa nini tusiweke kiwanda kikubwacha nyama kule Shinyanga. (Makofi)

Napenda kukuhakikishia Mheshimiwa Shibudakwamba, tayari NDC imeshafanya tafiti na sasa hivi

Page 299: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

299

15 MEI, 2013

inaendelea kutafuta wabia na tutaangalia utafitiwalioufanya, kama umepitwa na wakati tutawaagizawarudie tena feasibility study hiyo, ili tuweze kuanzishaviwanda hivyo muhimu katika maeneo yale. Tuna mifugomingi nchini, viwanda kama hivi vitasaidia sana katika sualazima la kuongeza mlolongo wa thamani ya fedha.

Mheshimiwa Asaa Othman Hamad, amezungumziaumuhimu wa Kurasini Logistic Centre, kwa kweli ile ni muhimusana. Nami nasema kwamba, kama alivyoeleza MheshimwaWaziri, sasa hivi tumekwisha kupata bilioni 25 na tunachotakakufanya mara moja ni kuzitoa fedha hizi pale KidongoChekundu, ili tuchukue zile eka 38, kazi ya kuanzisha hii LogisticCenter ianze. (Makofi)

Tunajua kwamba, pale tutaweza kupata ajira,biashara itakua, lakini pana multiplier effect kubwa sanakatika miradi kama hii na ndiyo maana tunasema,tukishamaliza kukamilisha kulipa fedha zile, tayari mara mojaWachina wanaingia na bilioni 600, tunapata ajira ya watuelfu 25, tutakuwa tumejenga utaratibu mzuri katika uchumiwetu. (Makofi)

Kwa hiyo, hilo tunalifuatilia kwa karibu sana, hili pialimezungumziwa na Mheshimiwa Mbarouk Salim Ali, Mbungewa Wete, Mheshimiwa Khatib Said Haji, Mbunge wa Konde,Mheshimiwa Gaudence Kayombo, Mbunge wa MbingaMashariki na Mheshimiwa Haji Khatib Kai, Mbunge waMicheweni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalolimezungumzwa kwa kina sana ni lile ambalo amelizungumziaMheshimiwa Nimrod Mkono, Mbunge wa Musoma Vijijini. Miminataka nikuhakikishie Mzee Mkono kwamba, hoja zoteulizozitoa tumezikubali na mimi kama Waziri, nitazifanyia kazi.Kitu kikubwa nilichoanza kukifanyia kazi pale FCC, palikuwana uongozi wa kukaimu na sasa tumeshafanya mpango wakupata CO ambaye siyo tena wa kukaimu. Najua kunaprogramu mbalimbali zinazokwenda pale kushirikiana na

Page 300: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

300

15 MEI, 2013

World Intellectual Property Organisation ku-automate sehemuya pale.

Naelewa kwamba, BRELA tuna utaratibu wa kujengaofisi na kiwanja tumekwisha kupata. Sasa napendakukuhakikishia kwamba, ushauri ulioutoa na hasa tukizingatiakwamba tija imepungua pale, tutahakikisha kwamba, eneolile linafanya kazi kwa ufanisi. Nimeshtuka uliposematunachukua siku 120 kutoa documentation, lakini wenzetuKenya wanachukua siku chache. Ushauri wako tumeuchukuana ninakuhakikishia kwamba, tutaufanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalolimechangiwa ni suala zima la mpango mkakati wakuhakikisha Zao la Korosho ghafi na zilizobanguliwa zinapatasoko la moja kwa moja, badala ya mfumo wa sasa wa kusubiriwanunuzi na kuonekana kuwa ni tatizo kubwa kwa wakulima.Hili amelizungumzia Mheshimiwa Salum Barwany, lakini vilevileamelizungumzia Mheshimiwa Asaa Hamad, aliposemaviwanda vya Korosho tunafanyaje; hicho ndiyo kilio.

Kwanza, tukiangalia suala la viwanda vya korosho,sasa hivi kumeshatokea utaratibu mzuri sana; NSSF ,wamesema wao wapo tayari kutoa asilimia 60 za uwekezajina wawekezaji wale kutoa asilimia 40 ili kukarabati viwandahivi. Mimi nafikiri hiyo ni fursa ambayo tunatakiwa tuichukueharaka sana na kwa taarifa yako, sasa hivi tayari kunaviwanda vitatu; Kiwanda cha Mtama, Newala na kinginekimojawapo tayari vimeshaingia katika utaratibu huu. Vingivya viwanda hivi matatizo yake makubwa ni ukosefu wamitaji. Kwa hiyo, hilo ni eneo ambalo tutawezakuhamasishana na Wizara ya Kilimo, wanaosimamia sektainayosimamia viwanda hivi ili kuvifanyia kazi. (Makofi)

Vilevile, Mheshimiwa Barwany ni nia ya Serikali sasahivi na tuko katika maandalizi ya kuanzisha soko la bidhaaza mazao (Tanzania Commodity Exchange). Tunadhanimfumo wa soko huu kwa zao kubwa kama korosho, utaletaushindani wa bei na kwa kuwa utawashirikisha wanunuzi

Page 301: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

301

15 MEI, 2013

wengi wa ndani na nje ya nchi, tunaweza kupata soko lauhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, limejitokeza tena suala lahaki miliki, nimeshalizungumza katika hotuba yangu na tayarinimeshatoa agizo kwa COSOTA waanze mchakato wa kuonakwamba wanaweka Kanuni. Ingewezekana kabisatukasema tungoje marekebisho ya sheria, yakachukua mudamrefu, lakini nadhani mabadiliko ya Kanuni yanawezakuweka sawasawa hali hii na kuhakikisha kwamba, wasaniiambao nao ni vijana wengi tu wanaotafuta kazi katika nchiyetu, wakaanza kupata mapato yao na kupunguza tatizohili la ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda unavyoonekana,unatutupa mkono, lakini kama nilivyosema mwanzoni, hojazilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni nyingi sana,tutajaribu kuzijibu zote, tutawakabidhi watazisoma na ushauriwaliotupa katika ufuatiliaji tutafuatilia.

Kabla sijamaliza, kulikuwa na tatizo linalohusu,nadhani ni Tandahimba kama sitakosea kwa MheshimwaNjwayo; kulikuwa na wakulima wa Korosho ambao waliwekakorosho zao katika kiwanda fulani na baadaye wakaambiwakorosho zile zimepotea. Taarifa tulizozipata ni kwamba, huyoaliyesema kwamba korosho zile zimepotea, ameona niafadhali suala lile liende mahakamani. Kwa hiyo, suala hilolitakwenda mahakamani, nadhani litafuatiliwa kwa utaratibuhuo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,narudia tena kukushukuru sana na kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote. Naishukuru Kamati ya Fedhana Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Bajeti.(Makofi)

Waheshimwa Wabunge, tunataka kwenda kwenyeMkakati wa Integrated Industrial Development Strategy.Tunaomba mtupe fedha hizi tuanze, kumi inaanza na moja

Page 302: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

302

15 MEI, 2013

na sasa hivi tuko kwenye tatu, hakika Mungu akijaalia,tutakuwa na viwanda katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 44 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Kif. 1001- Administration and HRManagement … .... .... .... ..... ...... Tshs. 7,101,168,000

MWENYEKITI: Utaratibu wetu mnaufahamu,watakaobahatika ndiyo hao hao.

MHE. MUHAMMAD IBRAHIM SANYA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Kwanza, kwa furaha kabisa,nashukuru kupata hii nafasi kwa sababu niliomba kuchangiana bahati mbaya sikufanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo ningelisisitizakwenye suala zima la EPZ, nchi nyingi hasa za Mashariki yaMbali kama vile Malaysia, Thailand, Indonesia, hata Chinayenyewe, walipata mafanikio makubwa kutokana namaamuzi yaliyokuwa na vitendo ndani yake. Maamuzi yakwenye vitabu hayamfikishi mtu katika maendeleo halisi.(Makofi)

Leo, kwa mara ya kwanza kabisa nasimama katikaBunge hili na kusema kwamba, Kamati ya Biashara naViwanda, ninaipongeza na ninaipongeza kwa umahiri wakewa kuleta haya marekebisho. Kama ingelikuwa hayahayakuletwa ya kuongeza bilioni 30 katika Kurasini Hub, basileo pengelitoka maji hapa. Kwa nini nikasema hivyo?(Makofi)

Page 303: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

303

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Kurasini Projectau Hub au Logistics Hub ni pahala ambapo patatoa ajiraisiyopungua 25,000. Siku zote tunalia vijana hawana kazi; nihapa pa kuanzia, ingawa hizi fedha zilizotengwa badohazijafikia kiwango kinachotakiwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sanya, omba ufafanuzi.

MHE. MUHAMMAD IBRAHIM SANYA: Naam!

MWENYEKITI: Omba ufafanuzi wa kifungu hicho, kwasasa unachangia. Unatakiwa uombe ufafanuzi. Unazodakika tano za kuomba ufafanuzi.

MHE. MUHAMMAD IBRAHIM SANYA: Sasaninachoomba hapa ni kutaka kujua; tumepewa bilioni 30 nahuu mpango ni bilioni 60. Bilioni 30 zitatolewa tena mwaka2014 au tutasuasua kwa milioni moja au milioni moja na lakitano kama tulivyokuwa tumeanzia mwaka jana ili tumalizehili suala kwa vile suala hili linagombaniwa sana na baadhiya nchi za Kiafrika kutaka kuchukua hii nafasi ambayo sisi leotumeikwamua kwa asilimia 50? (Makofi)

Je, mwaka 2014 tutamaliziwa hizi bilioni 30 ili hii Projectimalizike tutoe ajira na nchi ipate faida na viwanda viwepo?Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Godfrey Zambi.

Waheshimiwa Wabunge, tuliposema dakika tano,ilikuwa kwa watu watano tu. Upo upungufu wa muda,tunatoa fursa kwa wengine na wao waweze kutoa mchangowao. Kwa hiyo, tukiweza kuchangia kwa muda mfupi,mkitaka dakika tano tano, ninayo orodha ya watu watanohapa. (Makofi)

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana. Ninataka nipate ufafanuzi kutoka kwaMheshimiwa Waziri au maelezo.

Page 304: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

304

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida ya kujenga viwandanchini ni pamoja na kuhakikisha kwamba, Wananchi wetuwanafaidika na bei ya mazao au bidhaa zinazotengenezwakatika viwanda hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachotokea kule Mbeya,nitoe mfano tu; kuna Kiwanda cha Saruji. Bei ya Sarujiinayozalishwa Mbeya, inauzwa kati ya Sh.16,000, Sh.17,000mpaka Sh.18,000. Saruji hiyo hiyo inayozalishwa katikaKiwanda cha Saruji pale Mbeya, ukienda Mikoa ya Morogorona Dar es Salaam, inauzwa hadi Sh.14,000 mpaka Sh.15,000.Sasa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya kile kiwanda kilipowamekuwa wanajiuliza; kwa nini bei ya saruji Mbeya ambakoinazalishwa ni kubwa zaidi kuliko maeneo mengine ambakowanaipeleka na kwa gharama za usafiri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na malalamikomakubwa sana kutoka kwa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya;inawezekana kuna bidhaa nyingine na maeneo mengine yanamna hiyo. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri atueleze.Tunajua Serikali haihusiki na uzalishaji, lakini masuala ya beina udhibiti wake, haya hayawezi kuachiwa watu wauzewanavyotaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunamwombaMheshimiwa Waziri, awaeleze Wanambeya na Watanzaniawengine ambako inawezekana kuna viwanda, lakiniwanashindwa kufaidika na viwanda hivyo kwa sababu tu yabei kuwa kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

Kwanza kabisa na mimi napenda kumpongezaMheshimiwa Waziri, kwa kupeleka fedha kwenye Halmashauriya Wilaya ya Bunda, kwa ajili ya malipo ya EPZ. Niliongeleasuala hili mwaka 2012 na akaahidi na fedha zimepelekwa,lakini sasa kuna utata; nilipomwuliza Mheshimiwa Waziri

Page 305: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

305

15 MEI, 2013

aliniambia zimeenda bilioni 2.5, lakini Wananchi kulewanasema wametangaziwa bilioni 1.2. Kinachowashangazazaidi, tayari EPZ walishaenda kufanya tathmini. Sasa hiviHalmashauri imeenda inafanya tathmini upya na mbaya zaiditathmini hiyo inapunguza ekari, inapunguza ukubwa wa eneoambao tayari EPZ walishaifanya. Tunajua Serikali ina dhamiranjema ya kuhakikisha wale Wananchi wanalipwa na wengini wazee.

Sasa wanataka kujua; Mheshimiwa Waziri atamkezimeenda kiasi gani, kwa sababu sasa hivi kuna wenginewanasusia, haiwezekani mtu ana ekari tano alipwe fidiashilingi 1,000,000, mwingine shilingi 500,000 na wale ni wazeewa muda mrefu kule, siyo vijana kama mimi labdawangelisema wanachakachua au wanafanya ujanja ujanja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamwomba MheshimiwaWaziri awaeleze Wananchi wa Tairo, ni kiasi gani ambachokimepelekwa; hizo bilioni 2.5 ambazo uliniambia au bilioni 1.2ambazo Wataalam wa Halmashauri wanaenda kuwaambiakule? Ahsante. (Makofi)

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: MheshimiwaMwenyekiti, nilitaka kujua suala la Kisera; ni vyema kuwa naviwanda vidogo vidogo na kueneza teknolojia rahisi ili kuletamaendeleo kwa watu wetu.

Je, Serikali ina mpango gani madhubuti wa Kitaifakatika kuimarisha SIDO na hasa ukitilia maanani hata Ofisi zaSIDO Mikoani na Wilayani hazifanyi kazi vizuri?

MWENYEKITI: Ninakushukuru Mheshimiwa Innocent,specific ameuliza suala la sera na ndiyo hasa kifungu hiki.Sasa kila mtu akianza kuuliza suala la kiwanda chake kwenyeJimbo lake itakuwa tatizo. Mheshimiwa Zitto!

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, mudamfupi uliopita nimepokea message inasema hivi; sikilizanyimbo hifadhi katika simu yako au tuma dedication yanyimbo kali na mpya kwa kupiga 15600, shilingi 19 kwa dakika

Page 306: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

306

15 MEI, 2013

moja na usajili wa shilingi 30 kwa siku tu. Hii ni baadhi yamifano ya promotion ambazo Makampuni ya Simuyanafanya kwa kutumia kazi za sanaa.

Agizo ambalo Mheshimiwa Waziri amelitoa leo, kwavyovyote vile Wasanii wetu na hasa Vijana wa Bongo Flevawatakuwa wamelipokea kwa furaha kubwa sana. Kwasababu sasa wataondoka kwenye unyonge wa kunyonywakutokana na kazi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yni kwamba,tulivyoanza hizi kelele za kutaka Makampuni ya Simu nawachuuzi (Content Providers), waanze kuwalipa Wasanii hakizao stahili. Baadhi ya Makampuni, yameanza kuwajazamamilioni Wasanii wetu mbalimbali. Leo hii msanii MwanaFA, ametoa taarifa yake kwenye vyombo vya habari,inaonesha kwamba, amelipwa Sh.18,000,000 katika kipindicha miezi mitatu, wakati siku chache zilizopita alikuwaanalipwa Sh. 1,000,000, Sh. 2,000,000, Sh.600,000.

Kwa hiyo, hizi juhudi zinaonesha kabisa kwamba,zinaweza zikazaa matunda na agizo lako kwa COSOTA,kuweka hizi kanuni kuhakikisha biashara hii sasa inakuwaregulated vizuri, itaweza kuwasaidia sana vijana wetu nakuweza kutengeneza ajira. Kilio ambacho wasanii wa mudamrefu kama akina Sugu, akina Kitime na kadhalika, sasakitakuwa kimepata jibu lake mwafaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo moja ambalonilikuwa ninaomba litolewe ufafanuzi na Mheshimiwa Waziri.Kwa mujibu wa Kanuni Na. 3 ya Sheria ya COSOTA ya mwaka1999 inasema kwamba; Vituo vya Televisheni na Rediovinapaswa kwanza kupata leseni kutoka COSOTA, kwa ajiliya kuendesha kazi ya kupiga miziki na kadhalika.

Pili, kulipa mirabaha kwa Wasanii ambao nyimbo zaozinatumika. Kanuni hii ipo kwa mujibu wa Sheria ya Hatimiliki,lakini haitekelezwi. Hata Televisheni ya Taifa au Redio ya Taifakama TBC na TBC1 hawalipi mirabaha hiyo lakini ipo kwenyeSheria.

Page 307: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

307

15 MEI, 2013

Tatizo lililopo ni kwamba, tunaambiwa TCRA, hawatoitaarifa hizo kwa COSOTA ili kuweza kupata lile pato ghafi nawaweze kuwagawia wasanii. Ninaomba sasa utoe agizo lakuhakikisha kwamba, Sheria hii inatekelezwa ili wasanii wetuwaweze kupata haki zao jinsi inavyostahili na tuwezekumalizana na jambo hili kuanzia tarehe 1 Julai, 2013.Ninaomba maelezo yako Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nchiyetu imebahatika kuwa na rasil imali nyingi sana natumebahatika pia kupata wawekezaji katika sektambalimbali. Je, ni lini Serikali itakuja na sheria mahususi yakuweza kuwabana hawa wawekezaji ili waweze kuchangiaasilimia fulani ya pato lao kwa jamii; yaani Corporate SocialResponsibility badala ya sasa hivi tumeona wawekezaji wengiwanachangia tu kile wanachoguswa? (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru. Mheshimiwa SuzanLyimo.

MHE SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Wote tunatambua kwamba, wanawake hapaTanzania ni zaidi ya asilimia 51. Wanawake hawa kutokanana mfumo dume, walishindwa kuingia kwenye vyombo vyamaamuzi, lakini majority wamejiingiza zaidi kwenye masualaya kiuchumi na wengi wao ni wajasiriamali.

Ninaomba kauli kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, wanamkakati gani kuhakikisha wanawasaidia akina mama hawakatika kupata masoko? Ninaelewa kwamba, kuna NGOmbalimbali kama EOTF, ambayo imekua ikiwasaidia akinamama; lakini Serikali ina mikakati gani kuwasaidia akinamama hawa ambao wanajitahidi sana katika suala zima lakiuchumi hapa nchini?

Ninakushukuru. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. ABBAS Z. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti,suala la Kisera la EPZ.

Page 308: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

308

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulifanya ziara Viongozi waWizara ya Viwanda, Viongozi wa Ardhi na wenyewe wa EPZ,tukaongea na Wananchi wa Kurasini, nikiwa mimi Mbunge,Mkuu wa Wilaya na Diwani, wakatuelewa, hakukuwa namgogoro. Tuliwaahidi Wananchi wale mwezi huu wa Mei,ndiyo tutaanza kuwalipa na hao wakubwa walisema tayariwanazo shilingi bilioni 60 mkononi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo ninamwombaMheshimiwa Waziri, aniambie ili nikawaambie Wananchiwangu ni lini tutaanza kuwalipa kwa sababu tayari tuliwaahiditutaanza kuwalipa mwezi Mei, 2013? Pale Shimo la Udongopembeni ndiyo kuna Mtaa wa Kurasini, ambao leo una miakakaribu saba, Wananchi wale hawajalipwa fidia. SasaMheshimiwa Waziri ungeliniambia ni lini tunakwenda kuwalipaili nikawaambie na zile bilioni 60 sasa hazipo zipo shilingi bilioni30? (Makofi)

MHE. AMINA MOHAMED MWIDAU: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Ninataka kupata ufafanuzi kuhususuala la EPZ Neema Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili la EPZ ni kuhusu fidiana niliuliza mwishoni mwa mwezi huu kwenye kipindi chamaswali. Mheshimiwa Naibu Waziri alinijibu kuwa, watalipwakabla ya mwaka wa fedha kwisha na zikipatikana fedhakutoka Hazina. Leo alipokuwa anatoa ufafanuzi kwenye hojaza Wabunge, alimjibu Mheshimiwa Omar Nundu, kwenyemaeneo ambayo utaratibu haujakamilika, taratibu hizonadhani ni za kulipa fidia, wanaweza wakaruhusiwawakaendelea na shughuli zao za kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti hapo nimepata mashakasana, ninamwomba Mheshimiwa Waziri atoe ufafanuzi, kwasababu atakuwa anawachanganya Wananchi. Kwanza,mashaka yangu makubwa ni kuwa pesa hizi sasa hazipo nahawajui watalipwa lini. Kwa hiyo, inawachanganya sanakisaikolojia. Vilevile kuna wengine ambao walikuwawamejenga nyumba za kudumu tu, siyo wale ambaowalikuwa wakilima.

Page 309: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

309

15 MEI, 2013

Sasa wakiambiwa wafanye shughuli za kiuchumiambazo siyo za kudumu, labda ni kil imo ambachokutokupanda miti ya kudumu na nyinginezo. Sasa na waleambao wamepata matatizo kama hayo watawafidia vipi?Ninaomba Serikali isifanye siasa, inyooshe maneno iliWananchi wasichanganyikiwe. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru. Mheshimiwa Lwanji.

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Hotuba yaMheshimiwa Waziri asubuhi ya leo hii, ameainisha mafanikiomengi tu upande wa uwekezaji hasa kwenye viwanda vyasaruji. Nimeangalia ninavyoona Sera hii kidogo naona kamakuna tatizo, kwa sababu viwanda vingi hivi vimewekwaupande mmoja wa nchi na kuacha maeneo mengine bilaviwanda hivi vya saruji, ambavyo tunavihitaji sana na hasaKanda hii ya Magharibi. Ukiangalia upande wa Mkoa waSingida, kuna malighafi nyingi tu ya gypsum pale, ambayomagari huja kuchukua kila siku kupeleka katika viwandavingine mbali na mahali hapo.

Ningelipenda nipate ufafanuzi juu ya sera hii kwambani lini maeneo haya ambayo hayana viwanda muhimu vyaSaruji yatakumbukwa?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, mkitakaufafanuzi kwa maswali machache wengi tutapata nafasi.Mheshimiwa Maryam.

MHE. MARYAM S. MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa na swali lakisera. Viwanda vingi viko mikononi mwa wawekezaji nahavifanyi kazi na havitoi ajira. Viwanda hivi vimekuwa sasavinachukuliwa vyuma chakavu, vinauzwa na kubomolewa.Je, Serikali ina tamko gani kuhusu viwanda hivi na hao

Page 310: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

310

15 MEI, 2013

wawekezaji kama havifanyi kazi virejeshwe mikononi mwaSerikali au viwanda hivi vibinafsishwe tena?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba majibu.

MHE. JOHN S. MAGALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami ninashukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati ninachangia kwamaandishi, niliomba kauli ya Serikali kuhusu masuala yaProgramu ya Viwanda na Masoko kwa Mazao ya Mifugopamoja na Pamba. Ikitambulika kwamba, Zao la Pamba,linategemewa na Watanzania wasiopungua milioni 14 naMazao ya Mifugo Wananchi wasiopungua bilioni 25.

Je, Mheshimiwa Waziri sasa atatoa kauli gani elekezi,ambayo itatekelezwa kuhakikisha ya kwamba, wanaongezathamani ya mazao ya pamba kwa kuwa na CommercialAttachees, kwa sababu Balozi zetu hazina madalali wa kuuzapamba; hivyo, hivi sasa hatuna mashindano ya bei yapamba, bei ya pamba ni dhulumati. Ninaomba ukomboziwa Serikali na vivyo hivyo ninakukaribisha Maswa tujetujadiliane. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru. Mheshimiwa Mkono.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii.

Mimi langu ni la kisera tu. Nimeshukuru sana Waziriameeleza vizuri kwamba, hiyo hoja ni nzuri na ataifanyia kazi.Suala kubwa ni time; tunaposema kazi ya BRELA mojawapokubwa ni kusajili Hati Hataza na Alama za Biashara na time isof the essence. Hiki Kitengo kimeshindwa kufanya kazi.Tulijaribu mwaka 1999 kuki-reform na kufanya kwambasomething unique itokee.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkono, tunakuombauongeze sauti kidogo.

Page 311: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

311

15 MEI, 2013

MHE. NIMROD E. MKONO: Naam!

MWENYEKITI: Sogelea mic, ongeza sauti kidogo auhamia mic nyingine.

Waheshimiwa Wabunge, tunaomba utulivu kidogo.

MHE. NIMROD E. MKONO: Ilikuwa ni kwamba, lazimawabadilishe, mwaka 1999 walisema urasimu ukome tunaundaBRELA. Mpaka sasa, BRELA badala ya kuundwa upyaimekuwa inasuasua, haifanyi kazi na watu incompetentwamo mle ndani. Katika mambo ya alama za biashara, timeis of the essence; swali langu ni hili; je, mta-reorganize upyaama ni kubadilisha watu tu lakini system inabaki vilevile? Hilindilo lilikuwa swali langu la msingi. Ahsante sana.

MWENYEKTI: Haya ninakushukuru. MheshimiwaMwaiposa!

MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,mimi swali langu pia ni la kisera. Nilipokuwa ninachangiakwa maandishi nilimwomba Mheshimiwa Waziri wakati wahitimisho anieleze ni kwa nini Serikali pamoja na Tasisi zake,zinanunua bidhaa zinazozalishwa viwanda vya nchi za nje,zikiwepo samani za kutumia maofisini, pamoja na maguniayanayotumika kuhifadhi nafaka?

Nikamwomba pia kwamba, kwa sababu Sera yaSerikali i l ikuwa ni kuchochea viwanda vyetu kwakuwahamasisha Wananchi wanunue bidhaa zinazozalishwakatika viwanda vyetu vya ndani; sasa anieleze kwa nini Serikaliyenyewe haiwi mfano mzuri wa Sera hiyo?

MHE. MTUTURA A. MTUTURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana.

Sera Kuu ya Serikali yetu Tukufu ya Chama chaMapinduzi ni kuondoa kero za Wananchi; hiyo ndiyo Sera Kuu.

Page 312: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

312

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua kutoka kwaMheshimiwa Waziri, kutokana na maelezo yake juu ya namnaya kulinusuru zao la korosho, ameeleza kwamba, kutakuwana mpango wa kuanzisha viwanda. Mpango huu kwanamna yoyote ile ni mpango wa muda mrefu na msimu huuunaokuja wananchi wa Tunduru na maeneo menginewanategemea kuuza korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, misimu miwili mfululizokutokana na sheria hii ya Stakabadhi Ghalani, Serikali pamojana Vyama vya Ushirika vimeshindwa kusimamia sheria hiimpaka wananchi wakaweza kupata tija.

Je, Serikali kupitia Wizara hii ambayo ndiyo iliyotungasheria ile ya Stakabadhi Ghalani, haioni kwamba, sasa hivi niwakati muafaka sheria hii wakaisimamisha mpaka paleaidha, viwanda hivyo vitakapokuwa tayari au watakapoletamarekebisho sahihi kwa ajili ya Sheria hii?

MHE. ENG. ATHUMANI R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Swali langu la kisera linahusu zao lamisitu, zao la asali. Wizara ina mpango gani katika kuwasaidiawafugaji wa nyuki ili asali wanayovuna iongezewe thamanina pia sera ya kutafuta masoko ya nje ili wapate bei nzuri yaasali pamoja na nta?

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa dakika moja ama mbili.

Mwaka jana wakati tukijadili Wizara hii, nilizungumzana Mheshimiwa Waziri Kigoda kuhusu madai ya waliokuwawafanyakazi wa Kiwanda cha Matairi cha General Tyreambacho leo tumekiona kwenye bajeti na tuna-appreciatekazi nzuri ambayo inafanywa na NDC ili kukifufua. Lakini sasaWaziri anasema pesa ndiyo zimetumwa kuwalipa waliokuwawafanyakazi na wapo wanaokiri kwamba kweli wamelipwa,lakini wapo ambao wanalalamika kwamba, hawajalipwakabisa na ndiyo swali ambalo nililiuliza mwaka jana.

Page 313: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

313

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wasiwasi wangu isijeikawa kwamba pesa zimetoka Wizarani, lakini kule chini kunawatu wamezipiga dafrau. Naomba Mheshimiwa Waziriatuambie tu kwamba, ana uhakika kama watu wote kweliwamelipwa? Kama pengine taarifa si sahihi, basi nimpebaadhi ya watu na namba zao za simu ili awasiliane nao nawalikuwa wafanyakazi ili wampe madai yao na wamwambieni kwa jinsi gani ambavyo hawajalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napenda kupataufafanuzi kutoka kwa Mheshimiwa Waziri kuhusu wafanyakaziwa General Tyre. Nashukuru.

MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwanda vingi nchi hiiambavyo vilifungwa ghafla, vingine vilifungwa taratibu vikiwakwenye mikono ya Serikali. Matokeo yake ni kwamba, kunawananchi ama wafanyakazi wengi sana waliokuwawanafanya kazi kwenye viwanda hivyo ambao hawakulipwaterminal benefits zao, kwa mfano, Kiwanda cha Mwatexkilichopo Jijini Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninachohitaji kutokakwa Waziri ni kwamba, je, Waziri yuko tayari kufanya stocktaking kujua kwamba viwanda vilivyofungwa vikiwa chini yaSerikali, ni wafanyakazi wangapi ambao hawakulipwa theirterminal benefits na wengine walikwenda wakafungua kesikwenye Mahakama mbalimbali katika maeneo mengi nchihii ili wafanye stock taking kutumia reference kesi ya MWATEXMwanza ili wafanyakazi waweze kulipwa haki zao. Napendakupata ufafanuzi.

MHE. SUZAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kitabu cha Waziri,ukurasa wa nane amezungumzia suala la MKUKUTA na KilimoKwanza ili kuondoa umaskini.

Page 314: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

314

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanaolimampunga, maana miaka yote wanasema wananchi wakorosho na pamba, lakini sasa hivi kilio kikubwa ndani ya nchiyetu hususani Wilaya ya Kilombero KPL wakulima wapatao3,000 walihamasishwa na wakalima mpunga wakapata sanamwaka jana na mwaka huu wamepata sana, lakini chakushangaza Serikali ikaingiza sokoni mchele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba majibu yaSerikali, wananchi hawa wakulima wa mpunga hususankuanzia Kilombero na Tanzania nzima, je, Serikali ina mpangogani wa kuwaongezea thamani mchele wao ili wapatekuuza?

MHE. VICENT J. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa ubinafsishaji waviwanda, Kiwanda cha MUTEX pia kilibinafsishwa kwa bei yakutupwa na waliokuwa wafanyakazi wa MUTEX 834 waligomakuchukua shilingi milioni 70 walizokuwa wametengewa kwasababu zilikuwa hazitoshi, wakigawana kila mtu anapata sh.83,000/=. Mheshimiwa Waziri akijibu swali langu alisema,Serikali itawaongeza fedha hizo, lakini mpaka sasahawajapewa fedha. Wamenituma niulize na wameombanisimung’unye maneno, je, Serikali ya CCM imewadhulumu?Wanaomba ufafanuzi.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru.

Mheshimiwa Waziri amezungumzia suala la Serikalikuwatambua Wamachinga kwa namna ambayo sijawahikumsikia kiongozi wa juu wa Serikali akizungumzia kwa maanahonestly na dhamira.

Sasa basi, wakati Serikali imeshaonesha dhamira naiko tayari kukaa chini kupitia Vyama vyao ambavyoMheshimiwa Waziri amevitaja, amesema vipo kama sita,wakati tunaelekea kwenye hilo, kwa nini Serikali sasa isitoe

Page 315: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

315

15 MEI, 2013

tamko kwamba, Wamachinga popote wanapofanyashughuli zao katika mipaka ya Tanzania wasibughudhiwempaka pale Serikali itakapokaa na kujadiliana nao wayforward kwamba, tunakwenda kufanya nini huko mbelekatika mazingira ya amani na utulivu kwa sababu Serikaliimeshawatambua na kuwakubali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nitajidhulumu nafsi kamanisipokushukuru na kukusifu Mheshimiwa Dkt. Kigoda kwanamna ulivyo-present leo na kujibu hoja za Wabunge kamaDokta na kama Waziri wa Serikali bila kuonesha kamaMwenezi wa Chama kama alivyofanya Mheshimiwa Magufulijana. (Makofi)

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi kwenyehili suala la Kurasini Logistic Hub. Nina mashaka kidogo nakwamba jambo hili linaweza likaenda likaua kabisa viwandavya Tanzania, kwa sababu kinachoonekana hapa nikwamba, ni Wachina wanakwenda kuwa na megawholesale katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna yoyote ileikitokea hivyo, maana yake ni kwamba, hata vile viwandavidogo ambavyo Serikali imeanza kuvisaidia vitakwenda kufa,kwa sababu Wachina watakuja na products zao zikiwazimeshatengenezwa kabisa. Maana yake ni kwamba, watuwatakuwa wananunua bidhaa hapo Kurasini na viwandavidogovidogo ambavyo vimeanza kuchipukia na ambavyoSerikali imeanza kutilia mkazo vinaweza vikafa kabisa kwasababu Tanzania itakuwa ni kama mega wholesale yabidhaa za China ambazo tayari zipo ready made.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi juu yajambo hili.

MHE. HIGHNESS S. KIWIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kwanza nianze na kumpongeza Mheshimiwa

Page 316: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

316

15 MEI, 2013

Waziri Kigoda kwa namna ambavyo leo hii amewezakuyapokea maoni ya Kambi ya Upinzani tofauti na ambavyoMawaziri wengine wamekuwa wakifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijielekeze kwenye suala lakisera linalohusiana na kero kubwa inayotokana na mfumowa ushuru ambao TRA sasa wanautumia kwa upande wabidhaa zinazotoka nje ya nchi, hususani magari. Kwa sasaTRA hawa hawazingatii tena taarifa ya ununuzi wa magarihaya, wao sasa wamekuwa kama ni wauzaji wa magarimaana wana bei zao, unanunua gari lako nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapokwenda kwenyehatua ya import duty, wao wanakwambia wewe umenunuakwa shilingi milioni tano, wanakwambia gari hili thamani yakeni shilingi milioni kumi. Sasa huu ni ukandamizaji, lakini pia nikuingilia mfumo wa negotiation baina ya muuzaji na mnunuzi.

Sasa napenda nipate kauli ya Waziri juu ya mfumohuu ambao ni kandamizi na unanyanyasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

MHE. MARIA I. HEWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kuna kaulimbiu inasema, maisha bora kwa kilaMtanzania, mgawo wa Viwanda vya Saruji uko Tanga, Dares Salaam, Mbeya na sasa hivi mnapeleka Mtwara. Maishabora kwa Kanda ya Ziwa angalau Kikanda tukaweka Singidaau Kigoma au Tabora angalau Mwanza. Je, MheshimiwaWaziri anasema nini baada ya Mtwara, anaifikiriaje Kandaya Ziwa?

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Kisera mradi wowote unapoanza uwewa Serikali au wa wawekezaji wa nje, lazima wananchiwanaohusika katika eneo kama watalazimika kuondokawalipwe fidia. Jambo hili limekuwa tofauti pale Mtunduwalokatika mradi wa Ngaka. Naomba ufafanuzi.

Page 317: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

317

15 MEI, 2013

MHE. DEOGRATIUS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Katika mchango wangu wamaandishi nilieleza jinsi Ngara inavyopakana na Rwanda naBurundi na hatuko mbali na Congo na nikaishukuru Serikalikwa soko la Kimataifa la Kabanga, lakini nikaiomba Wizaraiangalie soko la mpakani la Mrusagamba ambako kunabiashara nyingi sana kati ya Burundi na Tanzania. Ahsante.

MWENYEKITI: Nakushukuru. Wachangiaji wotewalioomba wamepata nafasi na tumetimiza wachangiaji 27.Samahani, Mheshimiwa Sakaya!

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana. Napenda tu kupata ufafanuzikutoka kwa Serikali kuhusiana na hoja yangu ambayonimeitoa wakati nachangia kwa maandishi. Niliomba sualakuhusiana na mwekezaji Mhindi wa Kiwanda cha Karatasi,Mgogolo, huko Mufindi ambaye amekiuka mkataba wake.Wakati anachukua ule mkataba mwaka 2005 alikubalianakwamba, awalipe watumishi wote haki zao kabla hajaingiamkataba mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yake hakuwalipampaka leo, watumishi 750 hawajapata kulipwa maslahi yaompaka leo. Lakini pia mwekezaji huyu amekuwa anawalipamshahara baada ya siku 60, lakini sheria inasema ni mwezimmoja, mtu alipwe, lakini yeye analipa mishahara miezi miwili.Naomba kujua Serikali inasema nini kuhusiana na mwekezajihuyu wa Kiwanda cha Karatasi Mufindi.

MWENYEKITI: Nakushukuru sana, wachangiaji 28 nawote mmepata nafasi within 30 minutes, which is very good.

Mheshimiwa Waziri majibu, mtajigawa kutokana namaswali mbalimbali.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali ni mengi, lakinitumegawana kidogo hapa na naomba nianze kujibu swalila Mheshimiwa Sanya kama ifuatavyo:-

Page 318: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

318

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Sanya anataka kujua kama ile albakibaada ya kupokea shilingi bilioni 30 kutoka Serikalini...

MWENYEKITI: Weka Microphone vizuri!

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kujibu maswali yaWaheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Sanya ametaka kujua kwambakutokana na deni lile la shilingi bilioni 60 ambalo lilikuwa ni lamradi wa EPZ, sasa Serikali imetoa shilingi bilioni 30, je, hii albakiitalipwa lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema wazi kwamba,Serikali sikivu ya CCM sasa hivi imetenga fedha katika bajetihii ya mwaka 2013/2014 kiasi cha shilingi bilioni 30 ambazozitalipwa mwaka huu wa bajeti ambayo tunaiomba 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema vile vile kwamba iposhilingi bilioni 25 ambayo tumepokea jana kuhusu mradi huu.Kwa hiyo, jumla hapa itapatikana shilingi bilioni 55 na kwenyebajeti ya mwaka 2013/20134 kulikuwa na shilingi bilioni mojaambayo ilitengwa kabla ya nyongeza ya shilingi bilioni 30,kwa hiyo, kuna jumla ni shilingi bilioni 56 ambazo Serikali sikivuitalipa kuhusu mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunasema kwambatukipokea hizi fedha za jana shilingi bilioni 25 za bajeti hiiambayo inaishia Juni pamoja na zile bilioni 31 ambazozinakuja kwenye bajeti inayofuata ya mwaka 2013/2014 natumesema kwamba, fedha hizi kwa awamu ya kwanza kwaeneo ambalo lipo Shimo la Udongo ambalo lina ekari 38.12,hili tutaanza nalo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu Serikali sikivu imesemakwamba, hili deni lingine ambalo linabaki ili kutimiza azmaya deni lote ambalo ni bilioni 60 maana yake sasa limepandampaka 94, litalipwa mwaka 2014/2015.

Page 319: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

319

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la MheshimiwaMtemvu ambalo nalo kidogo linahusiana na hili linatokanana kwamba ahadi ambayo Serikali iliitoa kuhusu malipo ya...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri usirudie swali,jibu tu!

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa!

Suala la Mheshimiwa Mtemvu tunatoa ahadi kwambaahadi ilikuwa ni Mei, lakini pesa tumepokea jana. Kwa hiyo,utaratibu utafanywa wa malipo ya fidia, kwa hiyo, wananchiwa Shimo la Udongo wataanza kulipwa.

Mheshimiwa Mwidau alizungumzia kuhusu Tanga,bahati mbaya kwenye swali lake hatuwezi kujibu hili, lakinikwa sasa hivi nasema kwamba Tanga kuna mradi ambaoulikuwa unahusu maeneo makuu matatu ambayo ni Tanga,Bagamoyo na Songea, Ruvuma. Sasa huu ni mradi wa MiniTiger Tanga – Bagamoyo ambayo jumla ilikuwa ni shilingi bilioni50.2...

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaombautulivu!

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Bilioni 50.2na tayari tulishapokea bilioni 10.9 kuhusu miradi hiyo Tangaikiwemo. Sasa baada ya kupokea bilioni 10.9, albaki ambayoimebaki Serikali imeahidi kwamba inaliangalia na tutawezatukawasiliana nao kabla ya mwaka huu kwisha tuangaliemradi huu wa min tiger ambao unahusu maeneo haya yaTanga, Bagamoyo na Ruvuma ili iweze kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Mwaiposaanasema kwamba, samani na magunia yananunuliwa nje,badala ya hapa ndani. Naungana naye mkono kwamba,tulinde bidhaa za ndani, kauli yetu sisi kama Wizara tunasemakwamba, nunua bidhaa Tanzania, jenga Tanzania. Bunge

Page 320: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

320

15 MEI, 2013

limeonesha mfano, kwani Ofisi za Waheshimiwa Wabungesamani zote zitatengenezwa na Magereza. Kwa hiyo, tuungemkono hilo kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni laMheshimiwa Lema ambalo ni kuhusu Kurasini Logistic Centreambapo anasema kwamba, baada ya kuingiza Wachina,kwa hiyo Wachina wata-dominate kiasi kwamba viwandavidogo vidogo vitakufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema si kweli hata kidogo,kwa sababu nia yetu kubwa ya kuleta wawekezaji wenyeuwezo mkubwa sana, wanakuja na shilingi bilioni 600 naimpact yake ni kwamba, wataajiri wafanyakazi 25,000 na sisitumesema wazi kwamba, sasa hivi ni Big Results Now na hukondiko tunakokwenda, kwa hiyo, hiyo ni changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba nimwachie Mheshimiwa Waziri ili aweze kuendeleana maswali mengine. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri!

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA(K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA): MheshimiwaMwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biasharakatika hoja hii ya mshahara wa Waziri kuna masuala matatuambayo yamejitokeza, nayo ni masuala yanayoingilianamoja kwa moja na masuala ya Wizara ya Kilimo, Chakula naUshirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ni suala laMheshimiwa Shibuda ambalo ni suala la pamba na mkakatiuliokuwepo; ni kweli kwamba, kwenye zao la pamba kunazaidi ya Watanzania 40% wanashiriki kwenye zao la pamba,lakini kwa sasa hivi tatizo tulilokuwa nalo ni tatizo la ubora wapamba na uzalishaji mdogo tuliokuwa nao, tija yetu bado nindogo sana.

Page 321: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

321

15 MEI, 2013

Kwa hiyo, sisi kwenye upande wetu wa kilimo, jamboambalo tumejikita kufanya sasa hivi ni kutengeneza mkakatiambao tutazunguka kwenye pande zote za uzalishaji wapamba ili tutengeneze mazingira ya kuondoka kwenyeuzalishaji ambao unazingatia kilo 400 kwa ekari twende tufikekwenye kilo 1,000 au 1,200 kama wanavyofanya wakulimawengine kwa daraja la wastani, lakini na pamba yenyewelazima iongeze ubora ili iweze kuongeza ushindani kwenyemasoko ya dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni laMheshimiwa Mtutura ambaye ameuliza kama tatizo lakorosho kwa misimu miwili, tatizo lililotokea ni tatizo la mfumowa Stakabadhi Ghalani. Nadhani Mheshimiwa Mtuturaanafahamu na kwenye hoja ya Wizara ya Kilimo tulisema,tatizo siyo mfumo wa Stakabadhi Ghalani kusema ukweli, balini usimamizi uliotokea kwenye mfumo huo na uharibifumwingine wa makusudi uliotokea kwenye mfumo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wake watatizo la Tunduru, nimelisema wakati tunamaliza hoja yaKilimo, tatizo la Tunduru linafanana na tatizo la Mkuranga nabaadhi ya Wilaya za Mkoa wa Lindi na Mtwara. Viongozi wetuwa Ushirika wengine kusema kweli wametuhujumu katikasuala hili na bado tupo kwenye kuwafanyia uchunguzi nauchunguzi umekamilika kwenye baadhi ya maeneo namatatizo ya viongozi wa ushirika hata kwake Tunduru yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tusiuangalie tumfumo tukasema mfumo wa Stakabadhi Ghalani unamatatizo, ulipofanya vizuri wakulima wamenufaika, lakinibaada ya watu kuingia, ni matumizi mabaya ya Governmentguarantee na monopoly pia ya soko na ndiyo maanatunasema kwamba, tukiuondoa mfumo wa StakabadhiGhalani sasa hivi mbadala wake ni nini? Tukiondoa mfumowa Stakabadhali Ghalani maana yake turudi kule tulikokuwana kule tulikokuwa hakukuwa kuzuri sana kwa mkulima vilevile.

Page 322: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

322

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sisi kama Serikalitumejipanga, mfumo wa stakabadhi ghalani utaendelea,lakini tutabaki na usimamizi mkali zaidi. Kusema kweli kamatulivyosema, katika hali hii, ni vizuri tufahamishane kwamba,hatutaoneana haya katika hili, anayedhulumu wakulimaataumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ni la MheshimiwaSusan Kiwanga ambaye amezungumzia suala la mchele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tuwe wakweli.Mpunga unavunwa mwezi wa Tano, Sita na Saba na mweziwa Nane unakamilika kuvunwa. Hatua iliyochukuliwa naSerikali ya kuingiza mchele, imeamuliwa kwenye Baraza laMawaziri mwezi wa Kumi na Mbili mwishoni ambapo bei yamchele sokoni ilikuwa ni shilingi 2,700/= kwa kilo. Mpungauliokuwa unavunwa mwezi wa Tano, Sita na Saba ni katikamaeneo ya huko Bahi, Kyela, Idodi, Mpanda na kwingineko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yako na Bungehili mpunga uliovunwa bei ya juu kwa wakulima ilikuwa nishilingi 35,000/=. Sasa wachuuzi walikuwa wanakwenda, mtuananunua magunia 500 au 1000, anahifadhi ndani ilibaadaye mwezi wa kumi na moja mpunga ule alionunuakwa shilingi 25,000 au 30,000 auuze kwa shilingi 100,000/= hichondicho kilichokuwa kinatokea. Huwezi kuniambia kwamba,mkulima alikuwa amebaki na gunia zake 100, amekaa nazomiezi sita, siyo kweli! Nimetoka Bahi nimekwenda Mpanda,Idodi, maeneo yote niliyojaribu kuuliza nimekuta waliokuwana mpunga kweli wapo lakini ni wachuuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulichosema na mwaka huutumekisema tena kwamba, jamani sasa hivi tumekwendaBahi tumekuta mpunga unavunwa, watu wananunua kwash. 30,000/= lakini watauhifadhi ili baadaye wauuze kwa sh.100,000/=. Sisi kama Serikali jukumu letu ni kumlinda mkulimakwa maana ya kwamba, hiyo bei ya sh. 30,000/= anayopewaleo ni ndogo sana. Jukumu letu pia ni kumlinda mlaji.Tukiruhusu mchele uuzwe shilingi 2,800/= kwa kilo mfumukowa bei utapanda na utafikia hatua ya juu sana.

Page 323: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

323

15 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nisemewazi kwamba, hatua hii imechukuliwa na sasa hivi tunaonamchele kwa wastani umesimama kwenye bei ya kati ya sh.1,700/= na 1,800/= kwa kilo ambalo ndilo lilikuwa lengo laSerikali. Lengo la Serikali siyo kumuumiza mkulima. Hata hiihatua iliyochukuliwa na Serikali, haikumuumiza mkulima,imewaumiza walanguzi waliokwenda wakanunua magunia,wengine wana magunia mpaka 10,000/= ndani mwaowameyafungia, wanasubiri nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa NaibuWaziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Haya Mheshimiwa Dkt.Kigoda!

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Zambi kwenye misingi ya biashara kunatofauti za bei, price differential, lakini vilevile tofauti hizizinaweza kuleta hoja ya kuhodhi bei. NamshukuruMheshimiwa Mbunge kwa kunipa taarifa hii. Namhakikishianitaifuatilia nipate majibu yake ni kwa nini sementi inauzwabei ghali pale inapozalishwa kuliko kule inakopelekwa?

Mheshimiwa Ester Bulaya, bila wasiwasi wowote EPZimepeleka shilingi bilioni 2.5. (Makofi)

Mheshimiwa Innocent Kalogeris, tutaimarishaje SIDO?Kwanza tunajitahidi sana kuhakikisha tunatenga bajeti kubwakatika Wizara yetu. Pamoja na kuzipangia bajeti kubwa,tunaziingiza katika utaratibu wa kupata mpaka fedha zakigeni na ndiyo maana mnaona programs mbalimbali kamamovies, ambazo zinaangaliwa na SIDO. Kwa hiyo, tunaaminitukiziimarisha kifedha zitaweza kusaidia wajasiriliamali wengi.

Mheshimiwa Zitto Kabwe wazo lake tumelichukua. Vilevile nasema hapa itabidi tushirikiane na Wizara yaMawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kwa sasa hivi nina taarifa

Page 324: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

324

15 MEI, 2013

kwamba COSOTA wameingia ubia kwa utaratibu wa PPPkuangalia ni jinsi gani sasa wasanii wanaweza kupata malipoyao kutoka TV na redio. Tuliangalia hilo, tunalifuatilia natutawapeni feedback.

Mheshimiwa Ritta Kabati, ameongelea juu yawawekezaji kutoa, wanaita social corporate responsibility?

MWENYEKITI: Hivyo hivyo.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa kweli si lazima, lakini mwekezaji yeyoteambaye ni makini na mahiri ni lazima alifikirie hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuwawezeshawanawake, tunafanya maonesho ya Saba Saba ambapotunawakaribisha wanawake wengi. Vile vile ukiangalia kupitiaSIDO, orodha ya wajasiriamali kwa tafiti tulizofanyawanawake ni karibu asilimia 54.7 ukilinganisha na wanaumeambao ni asilimia inayobakia, lakini wanawake ni wengi zaidi.Kuna taasisi inayoendeshwa na Mama Anna Mkapa, EqualOpportunity Trust Fund ambayo inaendelea na akinamama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi na Balozi wa Marekanitulianzisha AWEP - Africans Women Entrepreneurship Program,ambayo inaendeshwa na Wamarekani na Serikali yetu yaTanzania ambapo wanawake sasa watapata fursa yakupeleka bidhaa zao katika soko la AGOA, Marekani. Kwahiyo, kuna taratibu nyingi zinafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwidau, suala la, ahaa, tayariameshajibiwa.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaLwanji, amesema Viwanda vya Saruji vimewekwa upandemmoja wa nchi. Inawezekana ni kweli kutokana na malighafiinayopatikana huko, lakini sasa hivi kama mnavyofahamututakuwa na Kiwanda cha Kusindika Mafuta kikubwa sanakatika Afrika Mashariki cha Mount Meru Millers, Singida

Page 325: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

325

15 MEI, 2013

ambacho kitahusisha karibu wakulima 100,000. Tayaritumeshakipa kibali na taratibu za kuanzisha uzalishajizinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lilizungumzwa suala lakwamba viwanda vingi havifanyi kazi, mashine zinauzwakama chuma chakavu, Serikali inafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza kwenyehotuba yangu...

MWENYEKITI: Samahani Mheshimiwa Waziri,ungemtaja na Mheshimiwa aliyezungumzia suala hilo.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, samahani sana, ni Mheshimiwa MariamMsabaha. Kama nilivyosema katika hotuba yangu, CHCimeanza kuwaita wale wote ambao viwanda vyao havifanyikazi na vinasuasua. Ndiyo maana tuliishaanza na viwandavinne au vitano. Tutahakikisha kwamba wale ambao tutaonahawataweza tena itabidi tuvichukue viwanda vile ili viuzweau vichukuliwe na Serikali ili kufanyiwa shughuli nyingine.

Mheshimiwa Nimrod Mkono, aliongelea suala laurasimu na incompetency. Nakubaliana na MheshimiwaMbunge, lakini hapa Bungeni siwezi kumwambia kwamba,sasa hivi nita-reorganize, ni lazima nikaangalie. Lakini ni sualaambalo kama nilivyosema kwenye maelezo yangu ya awali,tutalifanyia kazi kuona FCC inafanya kazi na inakuwa niefficient entity ya kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mfutakambaamezungumzia zao la asali. Kama Mheshimiwa Mbungeatakavyoona, Wizara ya Viwanda na Biashara kwa makusudikabisa, sasa inafanya Maonesho ya Kitaifa ya Zao la Asali.Lengo lake ni kuhamasisha uongezaji wa thamani ya zao hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kwa sababumaonesho haya ni ya Kitaifa, yanasaidia kuleta watuwengine ambao wanahitaji asali yetu na hivyo kuwa ni soko.

Page 326: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

326

15 MEI, 2013

Hivi karibuni tunaanza mradi mzuri tu wa asali, sehemu zaSingida ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu, alikwendakufungua maonesho yale kuhusiana na zao hili hili la asali.Kwa hiyo, jitihada zinafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambieMheshimiwa Nassari bila kusita kwamba, tumepeleka shilingimilioni 83. Kwa hiyo, akaulizie huko, labda matatizo wakatimwingine yanatokea huko, lakini nimethibitisha kabisakwamba tumepeleka shilingi milioni 83.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie MheshimiwaWenje kwamba, tuko tayari kufanya stock taking, walahatuna matatizo. Lakini nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbungekwamba, tukishapata hiyo stock taking na figures hizo kamatulivyopata za MUTEX na MWATEX tutazipeleka CHC,wakaziangalie ili waweze kuona Hazina inaweza kutoa kiasigani cha hizo fedha kama kweli zipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa VincentNyerere, ameongelea suala la wafanyakazi 584. NimwelezeMheshimiwa Mbunge kwamba, nalifahamu sana na leo tenanimeongea na CHC, kwa sababu sasa liko mikononi mwaCHC. Nadhani hili linahitaji tulizungumzie kwa ukaribu zaidikuliko kutoa majibu ya haraka haraka ili hasa kupata uhakikani kwa nini Halmashauri kule haitaki kuchukua hizi fedha? Walewanasema fedha zipo. Sasa hilo tatizo liko katikati, lakini nisuala ambalo tunaweza tukalifuatilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie MheshimiwaSugu kwamba, kutoa tamko sasa hivi kwanza ni lazimatuangalie ule utaratibu wa vile VIBINDO wanafanya nini,wanasema nini, na hizo Halmashauri. Tukifikia hatua tukakaakatika mkao mzuri, tutatoa tamko mara moja, lakini we areserious kwamba, hawa ni wajasiriamali, wanatafuta riziki zao,hivyo ni lazima watafute na ajira ni tatizo katika nchi yetu.Kwa hiyo, hilo hatuwezi kuliacha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie MheshimiwaHighness Kiwia kwamba, kero ya ushuru wa TRA tumeipokea,

Page 327: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

327

15 MEI, 2013

tutalipeleka kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha au TRA ilikuona wanaweza kulitolea kauli gani maana ni suala la TRAkabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Maria Hewa,amesema Singida tunapeleka viwanda na hata hicho chaMount Meru, sasa sijui ulisema cha saruji au cha nini! Mwanzatutaangalia uwezekano huo, lakini moja ya eneotunalolisemea sasa hivi ni maeneo yote haya. Kigomainaondoka kwa sababu imeshatenga eneo la EPZ, nadhanina Tabora na Mwanza pia, haya ni maeneo ambayo tukipatawawekezaji tutawaita waje huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya MheshimiwaKayombo ni kwamba, Serikali haiwezi kuingia mahali mpakaiongee na wadau. Nadhani suala hili tumeshalifikisha mahaliambapo sasa Serikali na wadau tunazungumza. Ni kwamba,hatujafikia mahali ambapo tunakubaliana kuhusu huu ulipajiwa fidia. Hata hivyo, nina hakika, tumalizeni hili ili kiwandachetu kule kifanye kazi kwa faida ya watu wa Ngaka,Mtunduwalo na uchumi wa nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hoja ya MheshimiwaNtukamazina. Nakubaliana na hoja yake, tutaangaliautaratibu wa kujenga soko la mpakani Mrusagamba, lakininaomba pia Mheshimiwa Mbunge ahamasishe Halmashauriyake ili na sisi kama Wizara ya Viwanda na Biashara kupitiaMfuko wa ASDP tuone tunasaidiana vipi kuanza masoko hayakwa sababu ni muhimu kwa uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa MagdalenaSakaya, amezungumzia kuhusu Kiwanda cha Mgololo. Kwakweli nimekifuatilia sana, hawalipwi baada ya siku 60.Walikuwa wanachelewa kulipwa, lakini sasa almost wanalipaon time, lakini siku 60 hapana!

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale watumishi wengine 750kama Mheshimiwa Sakaya atakumbuka vizuri, hili sualawalilipeleka Mahakamani. Kwa hiyo, sasa hivi mimi nawenzangu na Ofisi ya Waziri, Uwezeshaji, tunataka kujaribu

Page 328: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

328

15 MEI, 2013

kulidadavua litoke nje ya Mahakama ili tuone tunafanyajekatika kulitatua nje ya Mahakama na kuwapa haki zao walewafanyakazi. Maana yake likiwa Mahakamani litachukuamuda mrefu na inawezekana hata mwekezaji akashinda, younever know. Sasa ni afadhali tulitoe nje tuone namna yakulishughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kujibu hayo…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri bado una laMheshimiwa Susan Lyimo na Mheshimiwa Amina.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, l i le la Mheshimiwa Lyimo kuhusiana nauwezeshaji, nilimjibu lile la African Women Entrepreneurprogram AWEP.

MWENYEKITI: Okay, uliunganisha na la MheshimiwaKabati, sawasawa. Haya la Mheshimiwa Amina.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, la Mheshimiwa Amina pia nimeshalijibu.

MWENYEKITI: Okay.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1002 - Finance and Accounts... ... ... ... Sh. 422,884,000/=Kif. 1003 - Policy and Planning... ... ... ... ...Sh. 2,780,334,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1004 - Government Communication Unit... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...Sh.161,520,000/=

MWENYEKITI: Endelea Mheshimiwa.

Page 329: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

329

15 MEI, 2013

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naitwa Rebecca Michael Mngodo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Hii subvote 1004,kasma ya 220600, Clothing, Bedding, Footwear, and Services.Popote ninapoiona hii kasma inanitia maswali mengi sanakwa sababu labda siku za nyuma ilikuwa inahitajika, lakinisidhani kwa wakati kama huu ambapo tuna watoto wengiambao wamefiwa na wazazi kwa UKIMWI, tunahitajikununulia watu bedding, footwear, and services ambazohatuzielewi ni zipi. Hii kasma inaonekana hata katikaAdministration and Human Resources Management .Ningeshauri kwamba kasma hii iondolewe na fedha yoyoteambayo iko katika kasma hii ielekezwe katika ku-strengthenmambo yanayohusu watoto na wanawake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, item 220600 subvote1004 kuna shilingi 6,000,000/=, ukurasa wa 243.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, hii item 220600 ya clothing, bedding,footwear and services ni kwa ajili ya kugharamia sare zawatumishi katika maonesho ya sekta za viwanda na biashara.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1005 - Internal Audit Unit... ... ... ... ... ...Sh. 174, 200, 000/=Kif. 1006 - Legal Services Unit... ... ... ... ... Sh. 86,114,000/=Kif. 1007 - Management Information

System... ... ... ... ... ... ... ... ... ... Sh. 207,197,000/=Kif. 1008 - Procurement Management

Unit... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ....Sh.196,537,000/=Kif. 2001 - Industry... ... ... ... ... ... ... ... ...Sh. 4,170,485,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 330: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

330

15 MEI, 2013

Kif. 2002 - Small and Medium Enterprises Division... ... ... ... ... ... ... ... Sh. 5,441,588,000/=

MHE. HASNAIN M. MURJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,subvote 2002 kifungu kidogo 270800, Current Grant to Non –Financial Public Units – (General)

MWENYEKITI: Okay!

MHE. HASNAIN M. MURJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Current Grant to Non – Financial Public Units – (General). SisiMtwara pale tuna vikundi vya akinamama, huwawanabangua korosho na vile vikundi korosho zao ni nzuri kwasababu wanabangua kwa mikono. Hata hivyo, wanapatatatizo kubwa sana katika packing.

Sasa je, hizi shilingi bilioni 4.7, zitawasaidiaje ili kuwezakupata packing machine pamoja na vifungashio ili na waopia waweze kuuza mazao yao katika soko la AGOA kamaalivyosema Mheshimiwa Waziri? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni kwa ajili ya taasisi za viwandana biashara na siyo taasisi za akinamama.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 3001 - Commerce... ... ... ... ... ... ... ...Sh. 1,932,608,000/=Kif. 4002 - Commodity Market

Development... ... ... ... ... ... ..Sh. 6,981,354,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO WA MAENDELEO

Fungu 44 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko

Kif. 1003 - Policy and Planning... ... ... ... Sh. 56,080,179,000/=

Page 331: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

331

15 MEI, 2013

Kif. 2001 - Industry... ... ... ... ... ... ... ... ...Sh. 15,616,100,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamatiya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2002 - Small and Medium Enterprises Division... ... ... ... ... ... ... ... ... Sh. 6,224,594,000/=

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ningependa kupata ufafanuzi katika kasma ya 4486,Agriculture Sector Development Programme. Kwenye fedhaza ndani hakujatengwa chochote. Kama unavyojuatumetoka kupitisha mpango maalum wa kukuza ajira kwavijana wanaojihusisha kwenye sekta ya kilimo na hapainahusu viwanda vidogo vidogo. Kuna vijana wengi ambaoni graduates, wamemaliza vyuo na baada ya kukosa ajirawameamua kuanzisha viwanda vidogo vidogo kupitiakwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepitisha bajeti ya Wizaraya Kilimo, hakuna fedha yoyote ambayo imetengwa kwaajili ya kuhakikisha inasaidia vijana. Trend hii pia inaendeleakatika Wizara hii, hakuna fedha zozote ambazo zimetengwakwa ajili ya utekelezaji wa kuhakikisha vijana ambao wana-invest kwenye kilimo wanaweza kujikomboa na tatizo kubwala ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kupataufafanuzi kutoka kwa Waziri, ni kwa nini hawajatenga fedhazozote za ndani katika kifungu hiki na badala yakewanategemea fedha za nje ambazo ni ndogo na hatunaguarantee nazo?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:Mheshimiwa Mwenyekiti, fungu hil i ni ASDP na nimapendekezo ya wafadhili. Wafadhili huwawanapendekeza kwamba, watafadhili katika eneo hili.Fedha hizi ni za kuimarisha mfumo wa taarifa za masoko nakuendeleza ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa taarifahizo ambazo zinatumika katika mradi huo.

Page 332: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

332

15 MEI, 2013

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 4002 - Commodity Market Development... ... ... ... ... ... ...Sh. 965,770,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

TAARIFA

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kutoa taarifa kuwa, Kamati ya Matumiziimepitia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yaViwanda na Biashara kwa Mwaka 2013/2014, kifungu kwakifungu na kuyapitisha bila mabadiliko yoyote. Naomba sasaBunge lako Tukufu liyakubali makadirio haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na kuafikiwa)

(Makadirio ya Matumizi ya Wizara yaViwanda na Biashara kwa Mwaka 2013/2014

yalipitishwa na Bunge)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri nakushukuru sana.

Mheshimiwa Waziri hili suala la Wamachinga nabodaboda, ambalo juzi Mheshimiwa Waziri Mkuu alilitoleamaelezo vizuri sana. Suala la Mama Lishe, hawa wanamahitaji kama sisi. Naomba Wizara yako pamoja na

Page 333: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1461930868-HS... · 2016-04-29 · Lakini aina ya ombaomba walioko mitaani ni watu wazima

333

15 MEI, 2013

Halmashauri ziweke utaratibu wa kuhakikisha na hawawanajiona ni sehemu ya Taifa hili na wao wapatiwe heshima.(Makofi)

Tumeweka suala la MKURABITA, lakini watu wengihawaelewi MKURABITA. MKURABITA ni Mkakati wa KurasimishaBiashara za Wanyonge, na hii ni sera ya Chama chaMapinduzi. Sasa sisi chama ndiyo tuwe wa mbele kusimamiasuala hili. (Makofi/Kicheko)

Baada ya maneno haya, nakushukuru weweMheshimiwa Waziri na Waheshimiwa Wabunge kwa kazi nzurimliyoifanya leo.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Sasa naahirisha Bunge mpaka kesho saatatu asubuhi. (Kicheko)

(Saa 1.04 jioni Bunge liliahirishwa mpaka siku ya Alhamisi,Tarehe 16 Mei, 2013 Saa Tatu Asubuhi)