Upload
others
View
3
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
UTANGULIZI
Shirika la TUSONGE ni shirika la Kijamii linalofanya kazi
katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa
Maeneo ya mradi huo ni Wilaya ya Siha katika kata mbili
ambazo ni Ivaeny na Biriri. Katika Manispaa ya Moshi
shirika la TUSONGE linafanya utekelezaji katika kata za
Msaranga na Majengo. Pia Wilaya ya Moshi vijijini kata ya
Njia panda shirika la TUSONGE limeweza kupata mradi
mpya wa ulinzi na usalama wa watoto.
Miradi ya ambayo shirika la TUSONGE linajishughulisha
nayo kwa sasa ni MRADI WA KIUCHUMI,
BINADAMU PAMOJA NA ULINZI NA USALAMA
WA WATOTO.
Katika kipindi cha miezi mitatu mwezi (April -
TUSONGE imeweza kutekeleza shughuli mbali mbali
ndani ya jamii ya Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha
SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
Katika kipindi cha miezi mitatu TUSONGE imeweza
kutekeleza shughuli zifuatazo:
(i) Mafunzo ya Waendesha Baiskeli maarufu kwa jina
la bodaboda: Shirika la TUSONGE liliweza kuanza rasmi
utekelezaji wa wa kutoa elimu kwa njia ya sekta ambapo
elimu kuhusu usafiri wa bodaboda. Mafunzo yalitolewa kwa
vijana 40, wanawake (6) na wanaume (34). Elimu
iliibua hisia miongoni mwa wanajamii. TUSONGE
ilishirikiana na Afisa wa polisi wa Manispaa ya Moshi
katika kutoa elimu hii kwa vijana kwa muda wa wiki 8.
Baada ya Mafunzo hayo TUSONGE iliweza kufanya
uzinduzi rasmi wa sekta hiyo ya usafirishaji na k
kwa wahitimu wa mafunzo hayo. TUSONGE na jamii kwa
ujumla inaamini kwa kupitia elimu hiyo ajali na vifo
vinavyotokana na boda boda vitapungua kwa kiasi
kikubwa.Aidha Kuwawezesha wasichana kuweza kufanya
biashara ambayo mfumo na mitizamo iliona
wanaume zaidi.
TUSONGE - CDO
� Shughuli zilizofanyika kwa kipindi cha miezi
mitatu
� Mradi wa uelimishaji haki za binadamu
� Shuhuda kutoka kwa wanufaika wa mradi wa
TUSONGE
� Kuvunja mzunguko kwa vikundi
� Mchango wa viongozi wa vicoba kata ya msaranga
� Elimu kuhusu kuimarisha kazi za shirika
� Mpango wa baadae shirika la TUSONGE
Shirika la TUSONGE ni shirika la Kijamii linalofanya kazi
katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Maeneo ya mradi huo ni Wilaya ya Siha katika kata mbili
ambazo ni Ivaeny na Biriri. Katika Manispaa ya Moshi
ya utekelezaji katika kata za
Msaranga na Majengo. Pia Wilaya ya Moshi vijijini kata ya
imeweza kupata mradi
linajishughulisha
, HAKI ZA
ULINZI NA USALAMA
July, 2016),
TUSONGE imeweza kutekeleza shughuli mbali mbali
ya Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.
TUSONGE imeweza
Waendesha Baiskeli maarufu kwa jina
hirika la TUSONGE liliweza kuanza rasmi
utekelezaji wa wa kutoa elimu kwa njia ya sekta ambapo
Mafunzo yalitolewa kwa
vijana 40, wanawake (6) na wanaume (34). Elimu hii
iliibua hisia miongoni mwa wanajamii. TUSONGE
ilishirikiana na Afisa wa polisi wa Manispaa ya Moshi
katika kutoa elimu hii kwa vijana kwa muda wa wiki 8.
Baada ya Mafunzo hayo TUSONGE iliweza kufanya
uzinduzi rasmi wa sekta hiyo ya usafirishaji na kutoa vyeti
kwa wahitimu wa mafunzo hayo. TUSONGE na jamii kwa
ujumla inaamini kwa kupitia elimu hiyo ajali na vifo
vinavyotokana na boda boda vitapungua kwa kiasi
Aidha Kuwawezesha wasichana kuweza kufanya
biashara ambayo mfumo na mitizamo iliona kama ya
(ii)Elimu kuhusu haki za wanawake kata ya
Msaranga: TUSONGE imeweza kuwa na wanufaika
ambao wameonyesha mwitiko wa kufanyia kazi mafunzo
waliyoyapata kuanzia mwaka 2014
wameona kuwa elimu ya ujasiriamali na ushawishi na
utetezi iliyotolewa katika Kipindi cha
kuwaongezea ujasiri wa kuwa na uthubutu wa kuomba
mafunzo ya ziada kutoka TUSONGE ili kuweza kutatua
changamoto zinazowakabili wanawake
TUSONGE ilitoa mafunzo hayo kwa muda wa wiki tatu.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wanawake waweze
kusimama katika nafasi zao na kutetea haki zao za msingi
kuanzia ngazi ya familia kama sheria ya wanawake
CEDAW 1979 inavyoainisha. Mafunzo haya yameweza
kusaidia baadhi ya wanaume pia kutambua haki ambazo
wanawake wanatakiwa kuzipata. Sambamba na hilo
TUSONGE iliweza kujenga uelewa kuhusu haki za
wanaume pamoja na watoto kama ilivyoainisha kwenye
umoja wa mataifa na sheria ya mtoto ya mwaka 2009.
Mafunzo hayo yameweza kuongeza ujasiri kwa wanawake
kuhusu kudai haki na kuwajibika kama wanawake ndani ya
familia hadi jamii. Baada ya elimu
TUSONGE iliweza kufanya tathimini ili kupima uelewa
uliotokana na mafunzo hayo. Tathimini hiyo ilionyesha
asilimia 100% ya waliofundishwa kukiri kuwa wameona
mwanga kwani kabla ya mafunzo hawakujua nini maana
ya haki ya mwanamke kisheria.
(iii) Elimu kuhusu ulinzi na usalama wa watoto
TUSONGE imeweza kutengeneza sera ya ulinzi na usalama
wa watoto katika, imeweza kutoa elimu ya haki za watoto
katika shule ya msingi Himo Pofo na Rongoma, kuunda
kamati ya ulinzi na usalama wa watoto kati
���� Toleo la 7
Mkurugenzi wa Shirika la TUSONGE Aginatha Rutazaa akitoa
mafunzo kuhusu haki za wanawake kata ya Msaranga.
kwa kipindi cha miezi
Mradi wa uelimishaji haki za binadamu
Shuhuda kutoka kwa wanufaika wa mradi wa
Mchango wa viongozi wa vicoba kata ya msaranga
Elimu kuhusu kuimarisha kazi za shirika
Mpango wa baadae shirika la TUSONGE
Elimu kuhusu haki za wanawake kata ya
TUSONGE imeweza kuwa na wanufaika
ambao wameonyesha mwitiko wa kufanyia kazi mafunzo
waliyoyapata kuanzia mwaka 2014-2016. Wanawake hawa
wameona kuwa elimu ya ujasiriamali na ushawishi na
Kipindi cha 2014-2016 iliweza
a ujasiri wa kuwa na uthubutu wa kuomba
mafunzo ya ziada kutoka TUSONGE ili kuweza kutatua
changamoto zinazowakabili wanawake katika jamii.
toa mafunzo hayo kwa muda wa wiki tatu.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wanawake waweze
ma katika nafasi zao na kutetea haki zao za msingi
kuanzia ngazi ya familia kama sheria ya wanawake
inavyoainisha. Mafunzo haya yameweza
kusaidia baadhi ya wanaume pia kutambua haki ambazo
wanawake wanatakiwa kuzipata. Sambamba na hilo
E iliweza kujenga uelewa kuhusu haki za
wanaume pamoja na watoto kama ilivyoainisha kwenye
mtoto ya mwaka 2009.
Mafunzo hayo yameweza kuongeza ujasiri kwa wanawake
kuhusu kudai haki na kuwajibika kama wanawake ndani ya
familia hadi jamii. Baada ya elimu hiyo kutolewa
TUSONGE iliweza kufanya tathimini ili kupima uelewa
uliotokana na mafunzo hayo. Tathimini hiyo ilionyesha
asilimia 100% ya waliofundishwa kukiri kuwa wameona
mwanga kwani kabla ya mafunzo hawakujua nini maana
Elimu kuhusu ulinzi na usalama wa watoto
TUSONGE imeweza kutengeneza sera ya ulinzi na usalama
wa watoto katika, imeweza kutoa elimu ya haki za watoto
katika shule ya msingi Himo Pofo na Rongoma, kuunda
kamati ya ulinzi na usalama wa watoto katika Kata ya
7 ���� April –June 2016
Mkurugenzi wa Shirika la TUSONGE Aginatha Rutazaa akitoa
mafunzo kuhusu haki za wanawake kata ya Msaranga.
Kilema Kusini, kuunda klabu ya haki za watoto shule ya
msingi Himo Pofo na Rongoma. TUSONGE imeweza
kugundua matukio ya ukatili wanayofanyiwa watoto na
kufikisha sehemu husika kwa msaada zaidi pamoja na
kufuatilia kesi na matukio yanayohusu ukatili dhidi ya
watoto.Aidha viongozi wa serikali za mitaa na waalimu
wamekuwa mstari wa mbele kuunga jitihada hizi mkono
kwani ni jukumu letu sote kulinda watoto wetu.
Mafanikio yaliyojitokeza
Kupitia miradi hiyo shirika la TUSONGE limeweza kuona
mafanikio mbali mbali yaliyojitokeza kwa wanufaika wa
miradi:
� Ongezeko la uelewa kuhusu haki za watoto
� Kuibua matukio ya ukatili waliyokuwa wanafanyiwa
watoto. Jumla ya matuki 7 yako katika hatua kubwa ya
ufuatiliaji
� Watoto wameongeza ujasiri wa kutoa taarifa pale
wanapofanyiwa ukatili.
� Mahusiano baina ya wazazi, walimu, viongozi wa
serikali, viongozi wa dini, pamoja na polisi
yameimarishwa.
MRADI WA UELIMISHAJI HAKI ZA BINADAMU
Mradi umeendelea katika kutekeleza azma ya kujenga
mazingira yenye usawa na usalama ili wanawake, vijana
na watoto waweze kushikiri na haki zao kulindwa. Mradi
ulianza na utekelezaji wa miradi ya jamii na sasa umeweza
kuwashirikisha mashirika mbinu shirikishi na tuliyojifunza
katika utekelezaji wa miradi ya haki za binadamu kwenye
jamii kwa kutumia kitabu cha Mwongozo. Ushiriki Nguvu
Yetu ni kitabu cha mwongozo cha kutolea Elimu ya Haki
za Binadamu na nyenzo kwa asasi za kiraia, viongozi,
vijana na makundi yanayofanya kazi za haki na ushiriki wa
wanawake,watoto na/ au vijana.Jumla ya mashirik 19 toka
Arusha na Kilimanjaro yaliweza kushiriki na kutendea kazi
ndani ya asasi zao na pia jamii kwa ujumla.
Lengo kuu la kitabu cha mwongozo
Lengo la msingi la Kitabu hiki cha Mwongozo ni kuwezesha
asasi za kiraia zinazofanya kazi na wanawake, watoto
kushirikisha na kuhamasisha jamii juu ya haki za binadamu
kupitia utekelezaji wa miradi ya kijamii ya haki za
binadamu. Mnamo mwezi wa tano TUSONGE kwa
kushirikiana na EQUITAS waliweza kutoa elimu ya kitabu
hiki kwa mashirika 19 yatokayo Moshi, Arusha na SIHA.
Mbinu ya utoaji elimu
Mbinu shirikishi ni mbinu ya utoaji elimu ambayo
ilitumika katika uandaaji wa mwongozo huu. Hivyo, kazi, na
miradi inakusudia kutoa zaidi uelewa na ujuzi na italenga
zaidi kutoa ufahamu wa haki za binadamu na kuhamasisha
kuchukua hatua kupitia vikundi vinavyoshiriki kutafakari
kwa kina juu ya uzoefu wa maisha yao na kutambua
mabadiliko wanayoyataka katika jamii zao.
Mashirika haya yameweza kuunda timu nne, mbili zikitoka
Arusha na nyingine Moshi ambazo kwa kushirikiana na
jamii za Boma ya Mbuzi, Mabogini kwa Moshi na Sokoni
One na Majengo kwa Arusha zimeunda miradi ya
utekelezaji Kitabu cha Mwongozo kwa kuangalia maswala
ya haki za binadamu yaliyomo kwenye jamii hizo. Lengo la
miradi hii ni kuwapa uelewa wanajamii kuhusu Kitabu cha
Mwongozo na pia mashirika kupata fursa ya kuongeza
uelewa wa Kitabu na mbinu zake ili waweze kutumia katika
miradi yao.
Jamii imeonyesha mwamko mkubwa wa kupokea Kitabu
cha Ushiriki Nguvu Yetu pamoja na utayari wa kutumia
hatua tano za utekelezaji miradi ya haki za binadamu
kwenye jamii zao. Hatua hizo ni Kuchunguza hamasa,
Kuchunguza muktadha, Kulenga badiliko, Kuchukua hatua
na mwisho ni ufuatiliaji na tathmini.
SHUHUDA KUTOKA KWA WANUFAIKA WA
MRADI WA TUSONGE
Raheli Dismas, nina umri wa miaka 25, nimejiunga na
TUSONGE mwaka 2014, kabla ya hapo nilikuwa nina mtaji
wa MPESA kiasi cha shilingi 50,000/= tu, ambapo wateja
walikuwa wakirudi kutokana na kukosa fedha ya kutosha
kuwapatia. Baada ya kujiunga na mradi wa TUSONGE na
kupata mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa
kumbukumbu za biashara, mtaji umeongezeka hadi kufikia
500,000/=. Pia nimeweza kushirikiana na mume wangu
kuongeza bidhaa za duka baada ya mtaji wa duka
kuongezeka kutoka 200,000/= hadi 400,000/=. Hivyo
basi, hali ya utegemezi kwangu imepungua kwa kuwa
ninaweza kukidhi mahitaji ya familia bila kumtegemea
mume wangu.
TUSONGE - CDO
Watoto wakitumia mbinu shirikishi ya kuainisha wadau
mbalimbali ambao wanalinda haki zao
Uk. 2
Watoto wakitumia mbinu shirikishi ya kuainisha wadau
mbalimbali ambao wanalinda haki zao
Lucy Mroso, 41 ninaishi kata ya Msaranga, nimejiunga
na mradi wa TUSONGE mwaka 2014, nilifanikiwa kupata
mafunzo mazuri ya ujasiriamali na haki za binadamu.
Mafunzo haya yaliniwezesha kuwa mbunifu wa biashara.
Niliweza kubuni biashara ya kuuza cement kata ya
Msaranga kwa sababu katika eneo la Msaranga watu
wengi wananunua viwanja kwa ajili ya kujenga, hii
imenisaidia kupenda biashara yangu kwa kuwa ninapata
faida. Mtaji wa biashara hiyo kupitia vikundi vya
TUSONGE ni shilingi 4,000,000/=. Kwa kweli
namshukuru sana Mungu na pia nashukuru sana
TUSONGE kwa jitihada ya kutuinua wanawake kiuchumi.
TUSONGE Oyeee
Frida Mboya, nina umri wa miaka 35, ninaishi kata ya
Biriri, biashara yangu ni duka la rejareja. Nilijiunga na
TUSONGE mwaka 2014, kabla ya kujinga na TUSONGE
nilikuwa nikiendesha biashara ya vitu vidogo vidogo
nyumbani kwangu. Niliweza kupata ushauri kutoka
vikundi vya TUSONGE na nikahamasika kujiunga na
kupata mafunzo ya ujasiriamali. Baada ya mafunzo
niliweza kupata wazo la kuboresha biashara yangu,
nimefanikiwa kuongeza mtaji wa biashara yangu kutoka
200,000/= hadi 1,500,000/= kwa kipindi cha miaka
miwili. Mtaji huu umeniwezesha kuhamisha biashara
yangu kutoka nyumbani na kukodisha chumba cha duka
Biriri Makiwaru. Nimeweza kuongeza bidhaa za duka.
kwa kweli nafurahia kujiunga na TUSONGE kwani
sikuwahi kuwaza kushika mkononi kiasi cha shilingi
milioni moja. Mungu ibariki TUSONGE.
Mnufaika Frida akiwa katika biashara yake ya mboga
mboga pamoja na duka la bidhaa za rejareja
KUVUNJA MZUNGUKO KWA VIKUNDI
Katika kipindi hiki cha miezi mitatu shirika la TUSONGE
limeweza kupata mialiko kutoka kwa wanufaika baada ya
kumaliza miaka mitatu ndani ya mradi. Kikundi cha
VICOBA cha vijana kata ya Msaranga kinachojulikana kwa
jina la Alfa chenye jumla ya wanachama 18 kiliweza
kumaliza mzunguko wake hivi karibuni. Mmoja wa viongozi
wa kikundi hicho siku ya kusherehekea sikukuu hiyo,
aliweza kusema kuwa ni changamoto kubwa kusimamia
vijana katika kuwawezesha kuheshimu maadili ya kikundi
lakini kupitia mafunzo ya TUSONGE ya uongozi, viongozi
wameweza kuwa wavumilivu na kusimamia kikundi hicho
hadi kusherehekea miaka mitatu ambapo wameweza
kukusanya hisa za shilingi 8,400,000/=.
Mgeni rasmi alipongeza kikundi cha vijana kwa kuweza
kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni
pamoja na mahudhurio hafifu. Aliwapongeza kwa kuweza
kuzitatua wenyewe na kuzimaliza pasipo hata ofisi ya
TUSONGE kufahamu kwa kufuata katiba ya kikundi.
Sambamba na hilo, alisema kuwa viongozi wa vikundi vya
vijana wanapaswa kuwa makini hususani kwa suala la
mikopo, hivyo basi kabla ya kutoa mkopo kwa
mwanachama ni vema mtu huyo ajadiliwe kwa kina,
ajulikane anapoishi na uwezo wake wa kuweza kurejesha
deni hilo kwa wakati.
MCHANGO WA VIONGOZI WA VICOBA KATA
YA MSARANGA
Shirika la TUSONGE limeona mabadiliko chanya ya mradi
hususani kata ya Msaranga. Vikundi hivi vimeweza kusonga
TUSONGE - CDO
Raheli akiwa ndani ya biashara yake ya duka kata ya Biriri
eneo la Makiwaru
Mkurugenzi wa TUSONGE Aginatha Rutazaa akikabidhi faida
kwa mnufaika wa kikundi cha vijana
Uk. 3
ujasiriamali uliopo. Vikundi vimeweza kufuatiliwa kwa
ukaribu sana na kuweza kutatua changamoto zao
wenyewe chini ya uongozi wa VICOBA KATA. Uongozi
huo umekuwa na vikao vya mara kwa mara vyenye
lengo la kujadili maendeleo ya vikundi vyote ikiwa ni
pamoja na changamoto zinazokabili vikundi hivyo.
TUSONGE imewasisitiza viongozi kuwa wamoja na
kuepuka masuala ya siasa na kuwa wakweli na wawazi
katika mambo yanayoendelea kwenye jamii.
ELIMU KUHUSU KUIMARISHA KAZI ZA SHIRIKA
Shirika la TUSONGE ni shirika ambalo linapenda
kujifunza kila siku na kushirikisha uzoefu na mashirika
mengine. Katika kipindi cha miezi mitatu shirika la
TUSONGE limeweza kupata fursa ya kushiriki katika
mafunzo mbalimbali likishirikiana na wadau wengine.
lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na
kujifunza ili kuboresha kazi za shirika zinazoendelea.
Madhara ya kiini tete ya kilimo bora yaliyotolewa
na MVIWATA: TUSONGE iliweza kushiriki katika
mafunzo hayo ili kuongeza uelewa kuhusu kilimo.
Kutokana na mpango mkakati wa shirika wa miaka
mitano unaoonyesha mpango wa shirika kuwawezesha
wanufaika wa mradi kufanya biashara kwa njia ya sekta
ikiwa ni pamoja na kilimo, TUSONGE ilitumia fursa hizi
kupata uzoefu kuhusu kilimo. Elimu hii itasaidia
kuandaa mikakati ya kufikisha elimu ya kilimo kwa jamii.
MPANGO WA BAADAE SHIRIKA LA TUSONGE
1. TUSONGE ina mpango wa uendeshaji wa pikipiki
(bodaboda) kwa vijana wa kike. Hii ni kutokana na
ombi ambalo vijana hao waliomba rasmi kwa kutaka
kujua kuendesha boda boda ili waweze kuongeza
kipato.
2. Mpango wa kuainisha majina walengwa kwenye sekta
zinazofanana ambazo ni duka, nguo, chakula,
kilimo na usafirishaji na kuziweka kwa pamoja ili
kuanza maandalizi ya elimu kwa njia ya sekta ya
nayotarajiwa kuanza rasmi mwaka ujao.
3. Kunukuu kwa ufanisi zaidi visa, matukio na mabadiliko
chanya yaliyojitokeza katika miradi ya TUSONGE.
4. Kuongeza vikundi vya ujasiriamali katika maeneo ya
vijijini ili kusaidia makundi ya pembezoni wakiwemo
walemavu ili kujikwamua kiuchumi.
5. Kufanya kazi kwa kushirikiana na wataalamu mbali
mbali ikiwemo maafisa kilimo ili kuweza kutoa elimu
kwa pamoja kuhusu biashara kwa njia ya sekta.
6. Kuwajengea uwezo wanufaika wa mradi wa kuwa na
ujasiri wa kutoa elimu waliyoipata kutoka TUSONGE
na kuelimisha wanajamii wengine hata bila kuwepo
TUSONGE. hii itasaidia mwendelezo na umiliki
shirikishi wa mradi wa TUSONGE.
7. Kuweka mikakati ya uendelevu wa Elimu ya Ulinzi na
usala wa watoto, Klabu za haki za watoto Mashuleni na
Kamati ya ulinzi na usalama ivilivyoanzishawa huko
Kilema Kusini.
8. Kuandaa na kuendesha tathimini ya matumizi ya
Kijarida cha Mwongozo na matokeo yake ndani ya
jamii za Arusha na Kilimanjaro.
JARIDA HILI LIMETOLEWA KWA UFADHILI
WA:
Mkate wa Dunia - Ujerumani
Kituo cha Haki za binadamu - Canada
Na Ulinzi na usalama wa watoto - UK
MAONI, USHAURI TUMA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
TUSONGE CDO
P.O. Box 1326 – MOSHI
Simu: 0272754158
0769-475577
TUSONGE - CDO
Viongozi wa VICOBA kata wakiwa katika mazungumzo ya
pamoja kuhusu maendeleo ya vikundi kata ya Msaranga
Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo TUSONGE wakiwa
Uk. 4