Upload
others
View
147
Download
35
Embed Size (px)
Citation preview
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 1
KITABU: NGUZO MAMA
MWANDISHI: PENINA MUHANDO
WACHAPISHAJI: DUP
MWAKA: 1982
UTANGULIZI
Tamthiliya ya Nguzo
Mama iliyoandikwa na Penina Muhando inayasawiri na kuyaelezea matatizo
mbalimbali yanayowakabili na kuwaelemea wanawake wengi wa Tanzania na
Afrika
kwa ujumla. Wanawake wengi wamekuwa wakinyanyasika kwa kunyanyaswa na
kuteswa
na waume zao. Penina Muhando anathibitisha hayo kwa kutueleza maisha
waliyokuwa
wakiishi wanawake wa Patata.
MAUDHUI
DHAMIRA KUU: UKOMBOZI WA
MWANAMKE
Penina Muhando ndani ya kitabu hiki cha Nguzo Mama anaelezea na kuonesha
juhudi
mbali mbali zifanywazo na wanawake katika kujikomboa kutoka minyororo ya
utumwa
wa mwanaume na manyanyaso mazito anayoyapata kutoka kwa mwanaume na
jamii nzima
inayomzunguka. Mwandishi, baada ya kusawiri maisha halisi ya mwanamke wa
Kiafrika na manyanyaso anayoyapata kama vile kupigwa, kufanyishwa kazi kuliko
uwezo wake, mfano :- kulima peke yake, kufua, kuosha vyombo, kukusanya kuni
n.k., anaamua kutumia
kipaji chake kuelezea jinsi gani mwanamke anaweza kujikomboa. Katika kitabu
cha
Nguzo
Mama, mwandishi anawaonesha wanawake wa Patata wahangaikavyo katika
kujikomboa. Ukombozi huo umegusa nyanja zote za maisha yaani kisiasa,
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 2
kiuchumi
na kijamii.
Kiuchumi katika kujikomboa, wanawake wa Patata wanaamua
kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itawawezesha kujipatia fedha kwa ajili ya
maendeleo. Miradi ikashamiri sehemu zote za Patata.
‘’……….Miradi tutatilia
mikazo, miradi ya kila aina vilabu vya pombe, maduka ya khanga, ushirika wa
kushona, kupika, hoteli na mengi……..’’(uk 52).
Bila Pili yeye akaamua kuanzisha kilabu cha pombe ili
aweze kujikomboa kwenye maisha magumu yanayomkabili.
„’Kaamua Bi
Pili, Pombe kujipikia, na kilabuni kuiuza
Pesa akipata, Pesa msema
kweli
Na nguzo mama itasimama’’ (uk 14).
Mwandishi anaonesha umuhimu wa pesa katika kujikomboa
kwa wanawake, kwani pesa ndio hasa iletayo maendeleo stahiki. Hali kadhalika Bi
Moja na wenzake nao wakajiunga na kuanzisha viwanda vyao vya kufuma
mapambo ya
nyumbani.
„‟Kutokea Bi
Moja, Na lake jipya kiwa nda kuanzisha
Mapambo ya nyumbani kufuma
Mapambo akiyauza na pesa
kujipatia
Itakuwaje nguzo mama
isisimame’’ (uk 17).
Kijamii, wanawake wa Patata wamehamasika kwa kuanzisha
vikundi vya akina mama, ambavyo vitasimama imara kutetea maslahi yao na
kusaidiana wao kwa wao katika kujikomboa. Mfano mzuri ni kikundi lcha kina Bi
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 3
Nne, yeye alikuwa kiongozi wa umoja huo akiwahamasisha wanawake wenzake ili
waweze kuinua „‟nguzo Mama‟‟
„’Bi Nne anapiga
makofi nao
Anasimama na kutoa hotuba
Nguzo mama hoyee’’ (uk 11).
Bi Nne naye hakuwa nyuma katika kazi yake ya ualimu.
Akaanzisha Umoja wa Walimu, nia ikiwa kuwasaidia kutatua matatizo yao
mbalimbali yanayowakabili katika ufundishaji, Bi Nne anawashauri walimu
wenzake
kuanzisha umoja huo ili kwanza waanze na matatizo yao yanayowakabili katika
hatua ya kujikomboa kama wanawake.
„’Kutokea Bi
Nne, wenzake wengi
Makubwa hawakujitakia,
vizuri walishauri
Tuanze na yetu matatizo,
Ndani yah ii yetu kazi
Kazi yetu ya kufunza vyema
kuichapa
Vigingi vikitokomea, vyema vijana watafunzika
Wakifunzika wote Patata
‘’Nguzo Mama itasimama’’ (uk 20).
Hapa Penina Muhando anaonesha elimu kama njia moja
wapo itakayoweza kuwakomboa wanawake pale aliposema;
„’Vigingi
vikitokomea, vyema vijana watafunzika, wakifunzika wote Patata nguzo mama
itasimama’’
Mwandishi pia anaonesha ushirikianao wa jamii nzima,
wanawake kwa wanaume kutasaidia sana katika kuleta ukombozi wa mwanamke
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 4
na
mwanamke peke yake, abadani hatoweza kusimamisha „’Nguzo Mama’’
‘’Bi Nane ‘’Tushirikishe
wanaume pia. Nguzo mama ina faida kwa wote
Tuite na watoto wote faida
kwa wote – wao taifa la kesho’’
Kwa hiyo, mwandishi licha ya kuonesha utakiwaji wa
jamii nzima katika ukombozi wa mwanamke, pia anaonesha faida za ukombozi
huo
hazitamlenga mwanamke tu bali na jamii nzima inayomzunguka mwanamke.
Pia umoja nao unachorwa na kuoneshwa kama njia
itakayowezesha wanawake waweze kujikomboa.
„’Bora tufanye
mikutano
Labda na maandamano
Maazimio tuyatangaze
Tukupambeje maua’’ (uk 7).
Mikutano kama ilivyo kawaida yake ingewezesha
kuwapasha watu wengi zaidi juu ya ukombozi wa mwanamke na manyanyaso
wapatayo.
Hivyo watu wengi wangehabalishwa katika uwanja wa siasa. Nafasi za uongozi
kwa
wanawake ni moja kati ya njia ambazo zingemwezesha mwanamke kujikomboa.
Katika tamthiliya hii, mwandishi anaonesha juhudi
mbalimbali zifanywazo na wanawake wa Patata katika kuchukua uongozi wa
Serikali.
„‟………Akina
mama watapewa vyeo, orodha tumeshapanga. Tutapata mawaziri, mameneja,
mabalozi
na kadhalika. Wengine tayari wameshapata kama mnavyofahamu’’ (uk 52).
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 5
Baadhi ya wanawake ambao walipata uongozi ni Bi Nne
ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya vyeo.
„‟He! Kweli nimekumbuka looo!
Nimechelewa mkutano wa kamati ya vyeo
Na mimi ndiye mwenyekiti, si
mnajua tunavyokazana kuwaombea mabibi vyeo maana wanasahauliwa. Lazima
tufanye
huo mkutano’’ (uk 42).
Bi Tatu yeye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya malezi
bora
„’My God !
Mmeona! Tena Shangazi mwenyewe ndiye mwenyekiti wa malezi bora’’ (uk 50).
Ukombozi wa fikra pia umeoneshwa kama tatizo linalowasumbua
wanawake wa Patata. Mfano anamuonesha Bi Nane dhidi ya madai aliyoambiwa.
Bi
Nane hasa alipokubaliana na kila kitu alichoelezwa na Bi Nne.
DHAMIRA NDOGONDOGO
1.
UONGOZI MBAYA
Uongozi mbaya ni kati ya dhamira zilizooneshwa kwenye
tamthiliya ya Nguzo Mama. Mwandishi wa tamthiliya hii, Penina Muhando
anaanza
kwa kuonesha umuhimu wa kiongozi katika jamii yoyote ile. Pia anaonesha
kiongozi kama mtu aliyeshikilia jamii anayeweza kuipeleka jamii anayeweza
kuipeleka jamii yake kwenye neema au mdomo wa samba kutegemeana na
uongozi wake
atakavyokuwa anaupeleka.
„‟……..Tena
kwetu sie kiongozi huongoza njia
Aweza kuwapeleka kwenye
neema
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 6
Au mdomoni kwa samba……..‟‟ (uk 22).
Lakini viongozi hao, wengi wao wamekuwa wakizipeleka
jamii zao kwenye mdomo wa samba, kwani viongozi hao hutumia uongozi kama
dhama
ya kuonesha wao ni watu watukufu na walio kwenye daraja la juu katika jamii.
Wakiamuawatakavyo bila kufuata miongozo iliyopo katika uongozi huo.
„‟ Bi Nane
akawaza
Kumbe kazi hii ya uongozi au
uwenyekiti
Inampa mtu uwezo wa kufanya
Mambo kinyume cha
kawaida……‟‟ (uk 24).
Penina Muhando anaonesha uongozi mbovu kama ndio
chanzo cha matatizo yanayoikabili jamii ya Wanapatata. Viongozi kama akina Bi
Nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashauri, wanaoneshwa kama viongozi
wabovu
wanaosababisha kuwa na matatizo katika jamii ya Patata.
„‟ Lahaula!
Kumbe ndio maanawatu wengi wanaulilia uwenyekiti, kwani ni rahisi kazi yake,
kiholela mambo kujifanyia masikini Patata si ajabu kumbe vurugu kutapakaa’’
(uk 25).
Mwandishi anaonesha vurugu zinazoisonga Patata kuwa
zimechangiwa na uongozi mbovu. Udikteta pia unaoneshwa kuwa ni zao la
uongozi
mbovu uliopo kwenye jamii ya wana Patata. Viongozi kama mwenyekiti wa
kamati ya
mashauri wamechorwa kama madikteta, wanaotumia uongozi wao watakavyo,
wajisikiavyo kutoka mioyoni mwao au vile waambiwavyo na watu wao wa karibu
bila
kufuata misingi na miongozo waliyowekewa
na katiba ya jamii zao. Mwenyekiti wa kamati ya mashauri anatumia vitisho
kumlazimisha Bi Nane kusemaasichokijua ili mradi tu yeye ni kiongozi. Pia
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 7
mwenyekiti anaonesha udikteta wake pale alipotaka kuamua kesi aliyosikiliza
upande mmoja tu wa mashtaka, tena maelezo hayo kapewa wakati mshtakiwa
hayupo.
„‟……..Vipi
mtu atakubali kutoa ushauri kutumia vitisho!
Kufuatilia maelezo ya
mshtaki peke yake
Tena yaliyoelezwa wakati
mshtakiwa hakuwepo
Vipi mtu atamshauri
mshtakiwa
Bila kujua mawazo yake’’ (uk 24).
Pia mwandishi anaonesha udikteta uliokithiri
unavyoitawala jamii ya Patata, yaani mtu mmoja anaweza kuamua maamuzi
yanayotakiwa
kufanywa na kamati nzima. Tena ajifanyiaye mambo bila kushirikisha kamati hiyo.
Mfano ni pale mwenyekiti wa kamati ya mashauri walipokaa na kuunda kamati ya
watu wawiliili wamshitaki Bi Nane.
„‟ ….Vipi watu hawa, wawili, moja, mbili kujifanya wao
kikao.
Katiba gani inasema
mwenyekiti peke yake
Awe na kikaocha kuamua
mashauri
Au asaidiane na mtu si
mwanakamati
Mwenyekiti na mshtaki kuwa kikao?!
Sijapata kusikia, hiki ni
kikao cha hila.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 8
Kusema sitajisumbua, kimya
akijikalia’’ (uk 24).
Mwandishi anaendelea kutuonesha maajabu ya uongozi
mbaya ya wana Patata ulivyokithiri, kwani wale viongozi walikuwa
wanategemewa
ndio haohao wanaofanya mambo ya ajabu.
„’Na ajabu
kupita yote
Vipi mwenyekiti bila kamati
Akatoa ushauri katika
mashtaka?’’ (uk 25).
Hapa msimulizi alikuwa anaendelea kutuonesha jinsi
mambo yalivyo mabaya hapo Patata.
Kwa wema na huruma
‘’Mwanangu mie sijui labda
kamuulize Bi Nne’’
(uk 54).
Chizi anamshangaa Bi Saba, kwani licha ya kuwa
kiongozi hajui hata ninimaana ya Nguzo Mama. Chizi anaendelea kusema;
‘’Lakini juzi kachaguliwa
katibu
Sijui wa kamati gani ile.
Nimesahau’’ (uk 55).
2.
DHULUMA
Penina Muhando anaitumia vyema kazi yake ya usanii
kueleza tatizo la dhuluma lilivyoigubika jamii yetu ya leo. Katika tamthiliya
yake ya Nguzo Mama anajaribu kutuonesha jinsi jamii ya Patata, kama zilivyo
jamii nyingine, ilivyooza kwa dhuluma, hasa kwa wanawake wajane pindi tu
wanapofiwa na waume zao.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 9
Katika tamthiliya ya Nguzo Mama, mwandishi anatumia
mhusika wake Bi Saba kuonesha jinsi ganiwanawake wengi wa Kiafrika
wanavyodhulumiwa mali na ndugu za waume zao pindi tu wanapofariki. Bi Saba
baada ya tu ya kufiwa, shemeji walikuja na kugawana vitu vya Bi Saba pasipo
kumuachia hata kitu. Watoto nao walichukuliwa, wakimwacha Bi Saba masikini
akihangaika huku na kule bila mafanikio.
‘’ Haa! Shemeji mmerudi
kuchukua hata kitanda!
Hata sufuria! Nitalala wapi
na nitapika wapi jamani?’’
(uk 43).
Mwandishi anaendelea kueleza uozo wa dhuluma ndani ya
Patata ilivyoletamatatizo na huzuni kwa wanaodhulumiwa huku wakikosekana
watu
wa kuwasaidia, hakuna mtu wa kumsaidia mwenzak, dhuluma imetapakaa kila
mahali
Patata.
„’Akalia Bi Saba
tena akalia, hana wa kumsaidia
Mumewe kafa nduguze wamekuja
juu,
Pesa wamechukua senti tano
haikubaki
Vyombo na nguo zote wakagawana
Roho ikampasuka Bi Saba
kuwaona hao ndugu
Walivyogombania mali wasiyochuma
„’Kiti hiki
changu’’ Mie lile jembe’’
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 10
‘’Mie suruali hizi’’ ili
mradi ilikuwa zogo’’
(uk 43-44).
Mwandishi pia anaelezea juu ya dhuluma, kwa kitu au
mali uliyoichuma kwa jasho lako mwenyewe, ukahangaika huku na kule kutafuta
mali hiyo lakini mwisho wanakuja wachache kukudhuluma mali hiyo. Mfano Bi
Saba.
Uongozi mbaya pia umesababisha kuondoka kwa demokrasia
kwa watu wa Patata, kwani wachache wenye
madaraka ndio wanaoonekana kupewa kipaumbele kuzidi wenzao,
wanaowaongoza.
Mfano ni pale Chizi alipokuwa anamuuliza Bi Nne akimwonesha kuwa yeye ni
mtu
mkubwa na anapewa kipaumbele zaidi. Ansema;
‘’…….Lakini bibi yangu
aliniambia
Binadamu wote sawa, lakini
wengine ni sawa zaidi.
Na huyu ni mmoja wa hao’’ (uk 58).
Pia mwenyekiti wa kamati ya mashauri hafuati demokrasia inayotakiwa kwa
kumlazimisha na
kumpa masharti yaliyo kinyume kabisa na katiba,yenye kuonesha udikteta
uliokithiri usiofuata na unaoepuka kibisa demokrasia .
„’ Jambo la pili
nakueleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kufanya mkutano bila kibali
cha
ofisi hii. Na ofisi hii lazima iletwe kumbukumbu za mikutano yote iliyofanyika
hapa Patata. Sheria hii ipo na inajulikana kwa hiyo urudi ufuate mashauri
yangu’’ (uk 25).
Viongozi wa Patata wanaoneshwa pia viongozi wasiopenda kuwajibika katika
kufanya kazi za
kuliletea taifa lao maendeleo yao, wawapo tu! Kazi kuongea maneno
yasiyotekelezwa. Mfano ni Bi Tatu, yeye ni kiongozi wa malezi bora lakini
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 11
ameshindwa hata kulea watoto wa kaka yake anayehangaika mtaani (chizi). Pia
anashindwa hata kujishughulisha kufanya vijibiashara.
„’My God!
Mmeona! Tena Shangazi mwenyewe ndiye mwenyekiti wa kamati ya malezi bora
yeye
mwenyewe hafanyikazi…..‟‟(uk 50).
Licha ya kuwa kiongozi wa Patata hawapendi kuwajibika,
lakini pia wanaoneshwa kama wasiokuwa na elimu, na wasiojua nini kinaendelea
hata kwenye uongozi wao. Viongozi kama hawawezi kubadilisha kama jamii
yoyote ile kama ilivyo kwa jamii
ya Patata. Chizi anasema;
„‟…..Siku moja nikamwendea, labda niwe kweli chizi
‘’Shikamoo’’ ‘’Marhaba’’ Bi
Saba nieleze.
Nini kitu Nguzo Mama, naona hapa Patata mambo
yamevurugika, kila ninakogeuka nasikia nguzo mama, Nguzo Mama kitu gani?
Vizuri, alijibu.
Yeye alihangaika huku na kule ili ajiletee maendeleo
yake nay a watoto wake, lakini bado mumewe alipofariki nduguze wakaja na
kumdhulumu jasho halali.
„’Atawaambiaje
watu hawa,
Kuwa vyote walivyochukua
Zaidi ni jasho lake
Watoto wake wapenzi mwenyewe
aliwalea
Wakati wao baba mnatindi
akiyachapa
Na pesa kwa pombe kuangamiza
Pesa ya ndugu yao iliishia
chooni’’ (Uk 44).
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 12
3.
ELIMU
Katika tamthiliya hii ya „‟Nguzo Mama‟‟, dhamira ya
elimu inaoneshwa kama jambo la muhimu sana kwenye maendeleo ya jamii yoyote
ile. Mwandishiameonesha kuwa kila nyumba ya mafanikio au maendeleo yoyote
yale
kuna elimu. Bi Nne anakubaliana na ukweli huu pale alipokuwa anasisitiza somo
la ushonaji liingizwe kwenye mitaala ya wanafunzi mashuleni ili waweze
kujifunza kushona vitu mbalimbali kama mapambo na nguo. Kisha wauze wapate
maendeleo.
„’……….Pia somo
la ushonaji litatiliwa mkazo mashuleni. Kila shule italifundisha ili watoto
wetu wajue kushona, wavae vizuri na kupamba nyumba zao vizuri’’ (uk 18).
Bi Nane naye anaonesha na kuthibitisha ukweli juu ya
umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii ya Patata. Yeye anaonesha kuwa
kama
watu hawatopata elimu, basi hata maendeleo hawatayasimamisha yakasimama.
„‟…….Tuvitoe
vigingi vile vituzuiavyo
Kazi yetu ya kufunza vyema
kuichapa vigingi vikitokomea, vyema vijana watafunzika
Wakifunzika wote Patata.
Nguzo Mama itasimama’’ (uk 20).
Ukosefu wa elimu nao unaoneshwa kama tatizo kubwa kwa
jamii ya Patata linalosababisha kukosekana kwa maendeleo na kuwakomboa
wanawake.
Viongozi wanaoneshwa kama watu wasiokuwa na elimu, wasiojua hata
kinachoendelea
kwenye uongozi wao. Mfano ni pale Chizi alipomuuliza Bi Saba ambaye ni
kiongozi
kuhusu maana ya Nguzo Mama. Lakini Bi Saba anaonekana hajui chochote kuhusu
Nguzo Mama. Baada ya Chizi kumuuliza Bi Saba anajibu;
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 13
„’Mwanangu mie
sijui labda kamuulize Bi Nne’’.
Yaani Bi Saba anaonekana mtu asiye na elimu kabisa,
kwani hajui hata jambo alifanyalo, Chizi anaendelea kutuhabarisha kuhusu Bi
Saba,
„’Lakini sijui
kachaguliwa katibu sijui wa kamati gani ile. Nimesahau’’ (uk 55)
Elimu pia inaoneshwa ilivyopana na katika hayo mapana
yake ya kila sehemu ina umuhimu wake. Elimu ya malezi, kama zilivyo elimu
nyingine, inaonekana kuwa na umuhimu mkubwa sana katika jamii hasa
ikizingatia
kwenye kipindi hiki ambacho magonjwa ya ajabu yanayoizunguka jamii kama vile
Kisonono, Kaswende na Ukimwi. Hivyo mwandishi anasisitiza kuwepo na elimu
ya
malezi itakayowasaidia vijana na wanawake hasa wale wanaotupa watoto kwenye
mapipa na vyooni. Sharti wapate elimu ya malezi waache tabia hiyo….
‘’……….Pia wasichana kutupa
watoto kwenye mapipa, kuna semina wiki ijayo kuzungumzia swala hili, ni aibu
kubwa sana kwetu’’
(uk 52).
4.
USALITI
Usaliti kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni tendo la kuchonganisha watu
kwa
kuchukua maneno ya huku na kuyapeleka huku ili wapate kugombana . Kama
tafsiri
ya usaliti ilivyo, Penina Muhando amefanikiwa kuonesha dhamira hiyo kwa ustadi
mkubwa, pale alipowachora wahusika wake kama wasaliti, mfano ni pale walimu
walipomsaliti mwenzao Bi Nane kwa kutoa siri za vikao wanavyovifanya na
kumpelekea Bi Nne, ambaye anaonekana kama adui wa Bi Nane.
„‟……..Tena
Mwenyekiti mimi nilikwambia hao walimu wengine hawampendi huyu Bi Nane,
yeye tu
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 14
ndiye anayejiweka kimbelembele kama wanampenda mbona walimu hao hao
wanatoka
wanakuja kunieleza mipango yao? Sema basi tukusikie’’ (uk 22-23).
Matokeo ya usaliti huu yalimuweka pabaya Bi Nane,
kwani alisongwasongwa na kuhangaishwa na uongozi wakimtuhumu kama msaliti
na
mvuruga Amani anayetaka kusimamisha maendeleo ya Patata.
„’Lahaula!
Sawa hawajakaa makubwa
yakawakuta!
Barazani wakaitwa mashtaka
kuyajibu’’ (uk 20).
Mwandishi anaendelea kutuonesha usaliti
ulivyosababisha Bi Nane kuingia kwenyematatizo pale mwenyekiti alipokuwa
anamuhoji.
„’Kwa kifupi ni
kwamba, tumepata habari kwamba wewe umeanzisha kikundi cha kupinga juhudi
za
wenzetu hapa Patata za kusimamisha Nguzo Mama. Tena kikundi hicho cha
walimu
watupu kinabagua wasio walimu. Tena kikundi hicho kimekuwa kikifanya
mikutano
kupanga njama za kuchafua juhudi za wenzenu’’ (uk 21).
Mwandishi Penina Muhando pia ameonesha dhamira yenye
kufanana na usaliti japokuwa kitafsiri sio usaliti. Dhamira hiyo ni watu
kuukataa ukweli ambao kimsingi upo kwa kifupi twaweza kuita „‟kana‟‟ au
„‟kukana‟‟
yaani tamka kuwa si kweli au kuwa haipo hali ya kuwa yawezekana ipo. Mfano
mzuri ni jamii ya Patata, kama zilivyo jamii nyingine, watu kuwakana na
kuwakataa ndugu zao kwasababu tu ya matatizo waliyonayo. Katika Nguzo
Mama Chizi ameonekana kulalamika
baada ya baba yake kumkana na kumkataa, na alipokwenda kwa shangazi yake
naye
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 15
pia alimkana tena huku akimdhihaki kwa kumtukana na kutaka kumuitia mbwa
wamng‟ate.
„’Niende wapi?
Kaka yako alinikana na wewe unanifukuza’’ (uk 50).
Dhamira hii inatuonesha jinsi mambo yalivyobadilika
kweny jamii zetu, wazazi kama tegemeo la watoto wao wenye matatizo na hivyo
wengi wao wamekuwa wakiwaacha na kuwaua kwa madai kuwa ni mikosi/nuksi .
Bi Tatu anaoneshwa kama ndugu wa kambo wa Chizi
anayepaswa kumsaidia lakini mambo yakawa
tofauti Chizi alipokwenda kwake,
‘’Chizi umefuata nini huku
nyumbani kwangu. Hebu toka hapa tuna shughuli za wageni’’ (uk 50).
Bi Tatu anaendelea kufoka na
kumtukana waziwazi Chizi pale alipomwambia, CHIZI ‘’Shangazisina nguo’’
Bi TATU ‘’Usiniite Shangazi
. Toa balaa lako hapa, ukirudi nitakuitia mbwa akuume’’ (uk 50).
5.
UMASIKINI NA MAGONJWA
Umasikini ni hali ya kukosa mali, yaani mtu kutoweza
kukidhi haja ya mahitaji yake ya kila siku. Kuishi chini ya kiwango
kinachotakiwa. Umasikini, kama tatizo kubwa linalozisumbua nchi za dunia ya
tatu, limejadiliwa kwa kina na Penina Muhando. Patata ni moja ya jamii za watu
masikini wasioweza kujimudu kimaisha wahangaikao huku na kule kusaka riziki
bila mafanikio. Jamii ya Patata inaonekana ikisumbuliwa na shida chungu nzima.
Bi Tano shida zimemwandama, watoto wake wanapata tabu, hata hela ya
kuwanunulia
nguo hana sembuse chakula. Watoto wake siku nyingine wanashinda na njaa
wakiangalia siku inavyopita, jua likitokea mashariki kuelekea magharibi.
‘’Taabu, taabu! Taabu!
Watoto wangu hawana chakula
Hawana nguo, hawana chakula
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 16
Watoto wanashinda na njaa.
Wanalala na njaa’’ (uk 40).
Hali kadhalika Chizi naye anaonesha hali hii ya
umasikini pale anapolalamika kuumwa na njaa, na njaa yenyewe inaonekana si ya
siku moja tu bali ni muda mrefu, bkwani anaelezea kuwa njaa hiyo huwa
haijimuisha.
„’Labda tuite
njaa
Kama hii inayomuuma
Njaa kamwe haimuishi’’ (uk 31).
Mwandishi pia anaelezea umasikini ulivyotawala Patata
kiasi ambacho watu wanashindwa hata kubadili nguo, yaani wao wamekuwa na
nguo
za „‟kauka nikuvae‟‟.
„’Bi Pili :
Nimeifua mchana huu, asubuhi si nilidamkia shambani…..’’(uk 36).
Mumewe bwana Sudi anajibu,
‘’Kelele! Sasa mimi nitavaa
nini
Utaikausha kwa moto hiyo
nakwambia
Mimi nataka kurudi, nilikotoka
nimeacha pombe kafiri unATAKA WENZANGU WAIMALIZE!
Kausha hiyo nguo haraka
kabla sijakupiga’’
(uk 36).
Mwandishi Penina Muhando haishii hapo katika kuonesha
umasikini ulivyoibuka Patata, bali anazichunguza na kuzifichua sababu
zinazoleta umasikini huo. Moja kati ya sababu hizo ni uvivu na kutojituma
katika kufanya kazi. Wananchi wa Patata ni wavivu na hawajitumi. Wanawake
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 17
wapo
tu wanapiga soga huku miguu waitandaza kwenye mikeka. Mfano Bi Moja yeye
asilani yumo ndani tu anashinda utadhani mwali anayefundwa. Kutwa domo
akilipiga tena huku miguu kainyosha , na kamwe hutamwona jasho likimtoka
akifanya kazi.
‘’Mwenzenu miye nashangazwa
na maneno ya Bi Moja
Hiyo dhahabu na fedha, na
huu wake uturi
Wapi atavipata, kumbe ndani
anashinda
Miguu kainyosha na domo
kujipigia
Kamwe sijamuona, akilitoa
jasho kazi kujifanyia
Wapi niambie inapatikana
fedha na dhahabu
Bila kazi kufanyia, niende
na mie Chizi
Nyingi nikajitolee’’ (uk 47-48).
Kama ilivyo kwa wanawake wa Patata, wanaume ikiwa ni
mara mbili yao kutwa nzima kiguu na njia, wanaume hawajui hata jembe lashikwa
vipi. Wao ni pombe tu pombe na wao, kutwa nzima wanashinda vilabuni,
wakinywa
na kupiga zogo tu mara hiki mara kile. Uvivu umewajaa hawataki kabisa
kujishughulisha. Kazi zote wamewaachia wake zao hata zile za kuihudumia
familia. Hata kile kidogo kinachozalishwa na wake zao basi huwapokonya.
‘’Huyu Bi Pili rohoni
anasikitisha, Atakufa masikini hohehahe kama mie, Lakini ninashangaa kala nini
bibi huyu, Walahi sijaonamwingine hodoni kumpita lakini yule wake mume, nini
kamlisha kazi zote afanya yeye bi Pili, matunda yote ale Bwana Sudi.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 18
Jasho lake Bi Pili laishia
kilabuni, huyu wake bwana Sudi Matindi anayatandika usiku na mchana siku moja
nitamuuliza Bwana Sudi, Dawa gani aliyompa Bi Pili na mie nikabahatika mke
kujipatia awe kama Bi Pili ambye taabu yote atakubali, watoto anizalie na pia
anilelee, chakula anilimie na pia anipikie. Nguo anifulie na pombe anipatie.
Nikipata yote haya!
Mie my God!‟‟ (uk 48-49).
Kama ilivyo shilingi yenye pande mbili, ndivyo kila
mwenye umasikini maradhi nayo hayaeshi. Jamii ya Patata inaoneshwa kama jamii
yenye kusumbuliwa na maradhi mbalimbali hasa ya mlipuko kama vile
kipindupindu.
„‟……Nimeishi
siku nyingi, Na mengi nimeyaona, ugonjwa wa kaputula na ule wa magunia
Pia kipindupindu vile vita
vya mdachi.
Na yule Nduli Amini Lkini ya
Patata.
Sijui niite vita au
ugonjwa’’ (uk 31).
ZINGATIA
Umasikini pia umeoneshwa wakati Bi Moja alipokuwa
anamdai mume wake fedha za kununulia khanga (Shabani).
„’Nimekwambia
mie hela sina sasa unataka nikaibe?’’ (uk 35).
6.
UVIVU NA UZEMBE
Uwajibikaji ni hali ya kufanya jambo pasipo hiari,
yaani unalazimika kulifanya. Tofauti na ilivyo kawaida kwa watu wa jamii ya
Patata wenyewe wamekuwa si wawajibikaji, yaani hawawajibiki ipasavyo katika
kufanya kazi. Wananchi wa Patata wanaoneshwa kama watu wavivu wasiopenda
kujituma katika kufanya kazi. Dhamira hii, Penina Muhando anaonesha kama
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 19
chanzo
kilichosababisha kufifia na kushindwa kuinua Nguzo Mama. Mfano mzuri ni pale
wanawake wa Patata waliposhindwa kuinua „‟Nguzo Mama‟‟. Mfano Bi Moja
yeye
anaacha kuinua kuvuta Kamba na kuanza kuongea na Bi Tano kuhusu khanga.
Kwa
muktadha waliokuwepo wasingepaswa kuzungumzia mambo hayo. Bi Tano
anamuelekeza
kuwa ni kwa Mwarabu na pia anamtahadharisha kuwa anapaswa kuziwahi la sivyo
zitakwisha. Mara Bi Moja anaondoka na hapo Bi Nane anashituka na kuuliza,
„‟ Sasa jamani
Bi Moja anakwenda wapi tena!!
Bi Moja akiwa mbali anajibu,
‘’Aaa jamani nitarudi lakini
khanga hizi sizikosi’’ (uk
34).
Bi Sita naye anaoneshwa kama mwanamke asiye
muwajibikaji na asiyejali umuhimu wa kazi za maendeleo, kwani naye baadaye
anaacha kuvuta kamba na kumfuata mwanaume eti kwasababu alimkonyeza ili
amfuate
licha ya umuhimu uliopo kwenye kuinua „’Nguzo
Mama’’.
Bi Sita aliiacha na kuamua kumfuata Maganga . Bi Tano
naye kuona mumewe Maganga anamuita Bi Sita anaamua kumfuata Maganga na
Bi Sita.
„‟……Mara
anatokea Maganga, Bi Sita anamfuata wanachekeana. Maganga anamfanyia
ishara
amfuate’’
Bi Tano anaona yanayofanyika
upesi anaacha kamba na kuwafuata’’ (uk 38).
Bi Tatu naye kwake Nguzo Mama si mali kitu Zaidi ya
mume na sherehe, hivyo anawasusia wewnzake kamba kutimkia kwenye Volvo
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 20
lililomfuata na kuelekea kwenye pati ambayo kwake yeye ni muhimu Zaidi
kuliko Nguzo Mama.
‘’Jamani mie naondoka
mnaiona Volvo hiyo imenifuata mie’’. Anaendelea kusisitiza ‘’Siyo utani ndugu
nyangu, Tunakwenda kwenye pati na mume wangu leo saa moja lazima nipalilie
unga
kwa baba watoto wangu ati. Nitakula nini’’ (uk 41).
Hata viongozi nao wanaonekana wababaishaji waliojaa
maneno matamu mdomoni lakini pasipo uwajibikaji kwa vitendo. Bi Nne kama
kiongozi naye anaondoka kwenye kazi muhimu, kazi ya vitendo itakayowezesha
maendeleo ya mwanamke kupatikana na kwenda kwenye vikao, kazi ya kupiga
soga
bila utekelezaji.
„’Hee! Kweli
nimekumbuka. Loo!
Nimechelewa mkutano wa
kamati ya vyeo na mimi ndiye mwenyekiti……‟‟ (uk 42).
Kwa kutowajibika huko wanawake hao wa Patata
wakasababisha kushindikana kuinua kwa „’Nguzo
Mama‟‟, nguzo ambayo ni egemeo lao la
maendeleo. Na ndiyo ufunguo ambao ungeweza kuwaondoa kwenye minyororo ya
utumwa
na ukandamizwaji wa siku nyingi. Lakini kutowajibika kukawakosesha. Penina
Muhando pia anaonesha ugumu wa maisha wa watu wa Patata unavyotokana na
kutowajibika kwao. Bi Moja anaonekana kama mwanamke asiyejishughulisha na
kazi
yoyote ile kutwa yumo ndani tu katulia, kwa hali kama hii ya kutowajibika ndiyo
hasa chanzo cha umasikini.
‘’Mwenzenu mie nashangazwa
na maneno ya Bi Moja
Hivyo dhahabu na fedha na
huo wote uturi
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 21
Wapi ataupata, kumbe ndani
anashinda
Miguu kuinyosha na domo
kujipigia.
Kamwe sijamuona akilitoa
jasho kazi kujifanyia…….‟‟
(uk 42).
7.
MAPENZI NA NDOA
Penina Muhando katika „‟Nguzo Mama‟‟ anaelezea mapenzi
yasivyokuwa ya kweli, yanayojali pesa na usaliti kati ya wanandoa. Mfano ni
Maganga (mume wa Bi Tano) na mkewe Bi Tano, Maganga anaonekana kutokuwa
na
mapenzi ya kweli kwa kumsaliti na kumchukua Bi Sita.
„’Wee Bi Sita
mshenzi, unanichukulia mume wangu hivihivi kimachomacho’’ (uk 39).
Usaliti huu wa mapenzi unaleta sononeko la moyo kwa Bi
Tano. Pia unaleta hali ngumu kwa familia ya Bi Tano, kwani watoto wanalala njaa
kwa kukosa chakula na mahitaji muhimu kwa kuwa Maganga (baba yao)
anamaliza
pesa zote kwa wanawake.
Mwandishi pia anaonesha mapenzi yanayoendeshwa na pesa
kuliko utashi wa mtu na mgtu, mFano ni pale Bi Tatu alipowaambia wenzake
alipofuatwa na mumewe.
„’Sio utani
ndugu yangu, Tunakwenda kwenye pati na mume wangu leo saa moja usiku,
lazima
nipalilie unga kwa baba watoto wangu ati, nitakula nini’’ (uk 44).
Pia anaonesha swala la mwanaume kuwa na mke zaidi ya
mmoja lisivyokubaliwa na wanawake na jinsi gani wanavyohangaika kulibadilisha
swala hili.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 22
8.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII
Katika tamthiliya ya Nguzo Mama mwanamke amechorwa kama
sehemu tofauti. Kwanza amechorwa kama chombo cha starehe kilichopo kwa ajili
ya
kustarehesha wanaume. Mwanamke hapa anatumia mwili wake kama bidhaa
iuzwayo
sokoni na kumpatia faida. Mfano ni Bi Sita ambaye ni changuidoa.
“Mwenzio nautafuta huo muda
siupati.
Laiti ningeupata wengi zaidi
kunasa.
Kwani mmoja,
wawili wanafaa kitu gani?” (uk 29).
Mwanamke pia amechorwa kama jasiri anayejitoa mhanga kuusema ukweli. Hapa
tunamuona Bi Nne anayeamua kumwambia ukweli mwenyekiti juu ya
kutokubaliana
kwake na maamuzi aliyoyatoa.
“Sikubali Mwenyekiti kama
nashtakiwa haki ninayo ya kutoa maelezo vile ninavyotaka.
Nitaeleza kwa maandishi
nakala wanaohusika wote nitawapa. Kesho nitakuletea ahadi ninaweka,
ukishasoma
maelezo yangu ukae ukihukumu. Lakini kabla ya hapo sipokei hukumu wala
ushauri” (uk 29).
Mwanamke pia ameoneshwa kama kiumbe duni kisicho na
thamani wala uwezo wakugfanya jambo lolote katika jamii. Katika kijiji cha
Patata wanaume waliwadharau na kuwabeza wanawake wakiwaona kama watu
wasiokuwa
wakamilifu (uk 46).
Uvumilivu nao umeoneshwa kama sifa ya mwanamke kwenye
tamthiliya hii. Mwanamke anaonekana kutokata tama katika juhudi zake za
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 23
kuingua Nguzo Mama licha ya ugumu
unaowakabili (uk 11).
Mwanamke amechorwa kama mtu anayekandamizwa na
asiyepewa haki zake za msingi. Mfano ni Bi Saba alipodhulumiwa vitu vyake na
nduguze mumewe na kuambiwa hana haki ya kurithi vitu vya marehemu mumewe
(uk
43).
Pia katika utandawazi huu, mwanamke anaonekana kupata
misukosuko hata pale aliposimamia kwenye haki yake ya msingi. Mfano Shaba
alipompiga mkewe eti kwasababu alikwenda kwenye kikao(uk 57).
Mwanamke ameonekana kama mtumwa wa mumewe. Hii
inaonekana pale Bwana Sudi alipokuwa anamtumikisha mkewe Bi Pili kufanya
shughuli zote za nyumbani na shambani yeye akiwa anakunywa pombe tu (uk 49).
Mwanamke anachorwa kama kiongozi wa familia ndiye
aikuzaye jamii, kama hapatokuwepo na mwanamke katika jamii, hakuna jamii
itakayoweza kuwepo. (uk 44-45)
UJUMBE
*Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
*Kwa kila jambo la maendeleo jamii nzima (yaani
wanaawake, wanaume,wazee,vijana na watoto) lazima washirikiane.
*Ulevi ni adui wa maendeleo.
*Uongozi bora ni muhimu katika kufikiamalengo.
*Malezi bora ni muhimu katika familia
*Wanawake wanafanikiwa kujikomboa siku watakayoamua
kuungana na kushirikiana
*Wanawake nao wapewe nafasi za uon gozi.
MIGOGORO
1. Bi Pili na mumewe (Bwana Sudi)
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 24
Chanzo cha mgogoro wao ni pesa. Bwana Sudi anataka
kuchukua pesa za mkewe alizouzia pombe. Suluhisho ni Sudi kumpiga mkewe
baada
ya kukataa kumpatia pesa hizo.
2. Bwana Sudi, Shaba na Totolo.
Chanzo ni baada ya Shaba na Totolo kumtetea Bi Pili
mke wa Sudi asipigwe na mumewe. Suluhisho ni Shaba na Totolo kumwacha
Bwana
Sudi aendelee na matusi juu yao, kwani waligundua kuwa alikuwa amelewa.
3. Bi Tano na Wanakikundi
Chanzo ni kutonunuliwa kwa vitambaa. Suluhisho ni
kugawana vitambaa hivyo kwa kila mwanakikundi akauze kivyake.
MSIMAMO
Msanii ana msimamo wa kimapinduzi kwa kuyatolea macho
matatizo yanayowakabili wanawake katika kujikomboa na vipi wafanye ili waweze
kujikomboa.
FALSAFA
Msanii anaamini kwamba ili wanawake wajikomboe lazima wawe na msimamo,
maelewano, pamoja na
umoja na ushirikiano pasipo wivu wala kubaguana.
FANI
MUUNDO
Msanii ametumia muundo wa moja kwa moja. Tamthiliya
hii imeanza kuonesha jinsi nguzo mama ilivyolala na harakati za kina mama
kastika kunyanyua nguzo mama. Mchezo umegawanyika katika sehemu nne.
MTINDO
Msanii ametumia mtindo wa dayolojia na masimulizi.
Vilevile ametumia lugha ya kishairi ili kuleta mvuto katika mchezo wake. Pia
msanii ametumia nyimbo na mianzo ya hadithi za fasihi simulizi. (uk 3).
MATUMIZI YA LUGHA
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 25
MISEMO/ NAHAU
a)
Utakiona
cha mtema kuni (uk 42).
b)
Watoto
ni taifa kesho (uk 55).
c)
Utakufa
kibudu (uk 22).
d)
Akachanganya
ulimi {uk 57).
e)
Dume
Malaya si dume roho yako kusumbua (uk 40).
METHALI
i)
La
mgambo likilia lina jambo (uk 45).
ii)
Aso
mwana aeleke jiwe (uk 45).
iii)
Umoja
ni nguvu utengano ni udhaifu (uk 33).
TAMATHALI ZA SEMI
TASHIBIHA
*Anatembea kama kapigwa bumbuazi (uk 9).
* Sikilizeni na sauti kama ndege nyikani (uk 30).
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 26
*Wanaswagwa kama mbuzi (uk 44).
*Amevaa kama mkulima wa bara (uk 24).
TASHIHISI
-Hasira zikampanda Bi Nane (uk 8).
SITIARI
-Mbwa mume wako
anayefuata wanawakeovyo.
MBINU NYINGINE ZA KISANAA
TAKRIRI
-Wakajaribu , wakajaribu (uk 5).
-Mwachie! Mwachie! Mwachie! (uk 8).
-Toka! Toka! Toka usirudi tena (uk 8).
-Akaenda, akaenda, akaenda (uk 40).
MDOKEZO
*Wakavuta…….wakavuta……….(uk 35).
*Siku moja ………ngojeni niwaoneshe (uk 49).
*Ee ndiyo malezi ya watoto wetu………(uk 52).
*Hebu tutazame kwanza kwanini hawasogei….(uk 58).
TANAKALI SAUTI
*Lu lu lu lu lu lu lu lu lu! (uk 2 na 18).
*Ai ai ai ai ai ai ai ai ai ai! (uk 2).
MATUMIZI YA KIINGEREZA
-My God (uk 32,
49, 50).
LUGHA ZA MATUSI
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 27
-Shika adabu yako
(uk 39).
-Malaya mkubwa wewe (uk 39).
-Mbwa wee! (uk 39).
-Mbwa mume wako anayefuata wanawake ovyo (uk 39).
WAHUSIKA
1. Bi Moja
*Mke wa Shabani
*Hakuwa na msimamo katika kusimamisha Nguzo Mama.
*Alikuwa na tama.
*Hafai kuigwa na jamii.
2. Bi Pili
*Mke wa Sudi
*Alinyanyaswa na mume wake.
*Ni mvumilivu katika matatizo.
*Ni mlezi bora wa familia.
*Anafaa kuigwa na jamii.
3. Bi Tatu
*Ni mpenda starehe.
*Hapendi kazi ambazo hazina mshahara.
*Anambembeleza mume wake kwa kuogopa kuachwa.
*Hafai kuigwa na jamii.
4. Bi Nne
*Ni mtu asiyependa maendeleo ya wenzake.
*Ana wivu, mbinafsi, mfitini na ana chuki binafsi.
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 28
*Hafai kuigwa na jamii.
5. Bi Tano
*Ni mke wa Maganga.
*Ana hasoira sana.
*Hakumpenda Bi Sita.
6. Bi Sita
*Alikuwa kahaba na alikuwa anatembea na waume za watu.
*Ni mkorofi na hakupenda ushirikiano.
*Hafai kuigwa.
7. Bi Saba
*Alifiwa na mume wake.
*Ni mlezi swa watoto.
*Ni kiumbe duni kwani shemeji zake walimnyang‟anya
mali zake zote na hata watoto baada ya mume wake kufa.
8. Bi Nane
*Alipenda ushirikiano na swenzake.
*Alikuwa na elimuya kutosha.
*Alipenda kuelimisha wenzakekatika shughuli za
maendeleo.
*Hakuwa na chuki na mtu.
*Anafaa kuigwa.
9. Chizi
*Nmpenda demokrasia.
*Alipiga vita uoga.
*Ni mfichua maovu yaliyoko katika jamii
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 29
*Anaonesha wazi matatizo yanayosababisha
wanawakekushindwa kujikomboa.
*Anafaa kuigwa na jamii.
10. Mwenyekiti
*Ni mtu mwenye uongozi mbaya
*Anapenda kusiliza majungu na fitina.
*Anawachukia wanawake wasomi.
*Hafai kuigwa na jamii.
MANDHARI
Mandhari ya tamthiliya hii ni ya kubuni. Yanasawiri
maisha ya vijijini na kiasi maisha ya mjini, kwani tunaona mwandishi ameonesha
mandhari ya vilabuni, uwanjani na nyumbani. Mandhari yaliyooneshwa yanaoana
sana nan chi za Kiafrikaa vile Tanzania, kwani unyanyasaji na ugandamizwaji wa
wanawake wa Kitanzania ni sawa kabisa na wale wa Patata.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu Nguzo Mama linasadifu yale yaliyomo
ndani ya kitabu hiki. Kitaswira “Nguzo Mama” ni umoja wa wanawake Tanzania
(U.W.T) ambao uliundwa kwa lengo la kuwatetea, kuwalinda na kuwapa haki na
maendeleo wanawake sawa na wanaume. Tamthiliya hii inaonesha harakati za
wanawake wa Patata wakiwemo wakulima, wasomi, waalimu, makahaba na
wanaungana
kuimarisha umoja na maendeleo yao. Wanafungua miradi mbalimbali kama vile
kushona, kupika pombe, pamoja na tofauti zilizopo kati yao kama vile uzembe,
majungu, fitina na kutoelewana.
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA
MWANDISHI
KUFAULU
Kimaudhui mwandishi Penina Muhando amefaulu kwa kiwango cha juu
katika maudhui yaliyomo ndani ya mchezo huu, kwani amefaulu kutueleza
www.mwalimuwakiswahili.co.tz 0717104507 Uk 30
matatizo
yaliyowapata wanawake wengi wa Kiafrika hususani Tanzania.
Kifani, mwandishi ametumia lugha rahisi inayoeleweka, lugha
ya kishairi inayofurahisha pia na nyimbo zinazoburudisha. Hivyo kufanya mchezo
usichoshe.
KUTOFAULU
Kimaudhui, Penina Muhando ameshindwa kutueleza hatma ya wanawake
wa Patata na jamii nzima baada ya kushindwa kuinua nguzo mama.
Kifani, matumizi ya lugha ya matusi ni udhaifu wa mwandishi,
kwani matusi ni lugha isiyotakiwa katika jamii.