Upload
others
View
10
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
1
TAASISI YA UTAFITI NA UTETEZI WA MASUALA YA
ARDHI
(HAKIARDHI)
KONGAMANO LA MIAKA 10 YA SHERIA ZA ARDHI TANZANIA
27-29 MEI 2009
2
YALIYOMO
1.0 UTANGULIZI ................................................................................................................................. 4
1.1 IGIZO KWA NJIA YA USHAIRI KUTOKA PARAPANDA THEATRE GROUP. ................................................ 4 1.2 MGENI RASMI - NAIBU WAZIRI WA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – NDUGU AGGREY
MWANRI ............................................................................................................................................... 4 1.3 MADA: I - CHANGAMOTO ZA URASIMISHAJI ARDHI KATIKA MFUMO WA SASA WA MILKI– NA ENG. L.
M. SALEMA, (MKURABITA)................................................................................................................ 6 1.3.1 Washiriki walichangia mada kama ifuatavyo: .......................................................................... 7 1.3.2 Maoni ya Mkurabita ............................................................................................................... 8 1.3.3. Maoni kutoka kwa Mgeni Rasmi - Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa....... 8
2.0 MADA II – TATHMINI YA SERIKALI JUU YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA ARDHI,
UZOEFU, MAFUNZO NA CHANGAMOTO - MWASILISHAJI JANE KAPONGO, WIZARA YA
ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI ............................................................................................ 9
2.1 MADHUMUNI YA WIZARA ................................................................................................................ 9 2.3 MAONI NA MCHANGO WA WASHIRIKI ................................................................................................ 9 2.4 MAONI YA WIZARA ....................................................................................................................... 10 2.5 MASWALI NA USHAURI................................................................................................................. 10 2.6 MWONGOZO KUTOKA WIZARA YA ARDHI ....................................................................................... 11
3.0 MADA: MTAZAMO WA ASASI ZA KIRAIA JUU YA UMADHUBUTI, UDHAIFU NA
CHANGAMOTO ZA MFUMO WA MILKI YA ARDHI TANZANIA – MWASILISHAJI –
OXFAM/HAKIARDHI ........................................................................................................................ 11
3.1 MAMBO YALIYOJITOKEZA ............................................................................................................. 12 3.2 MATOKEO ..................................................................................................................................... 12 3.3 MASWALI NA MAONI .................................................................................................................... 12 3.4 MAELEZO KUTOKA KWA MWASILISHI ............................................................................................ 13
4.0 MADA - UZOEFU NA CHANGAMOTO ZA MFUMO WA UTATUZI WA MIGOGORO YA
ARDHI – NA BAHATI MLOLE, MSAJILI WA MABARAZA YA ARDHI – WIZARA YA ARDHI. .... 13
4.1 MAONI NA MASWALI KUTOKA KWA WASHIRIKI ............................................................................... 14 4.2 MWONGOZO KUTOKA WIZARA YA ARDHI ...................................................................................... 15
5.0 MADA – UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MATUMIZI BORA YA ARDHI, UZOEFU,
CHANGAMOTO NA MAFUNZO - NA GERALD MANGO – MKURUGENZI MKUU, TUME YA
TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI ............................................................................. 15
5.1 MCHANGO WA MAWAZO KUTOKA KWA WASHIRIKI ......................................................................... 16 5.2 MCHANGO KUTOKA KWA MWASILISHI WA MADA KUTOKA WIZARA YA ARDHI ................................ 16
6.0 MADA YA CRT - ELIKARIBU GAYEMI, UJAMAA CRT RESOURCE TRUST .................... 17
6.1 CHANGAMOTO ............................................................................................................................... 17 6.2 MAWAZO YA WASHIRIKI ................................................................................................................ 18
6.3 NAFASI YA MWANAMKE KATIKA UMILIKI WA ARDHI............................................... 18
MASWALI NA MAONI YA WASHIRIKI .......................................................................................... 19
6.4 MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI – HAKIARDHI, DKT. NG’WANZA
KAMATA ............................................................................................................................................. 19
7.1 UZOEFU KUTOKA KENYA KWENYE MASUALA YA ARDHI - MWASILISHI: ODENDA LUMUMBA ........... 20 7.2 HITIMISHO ........................................................................................................................... 23 7.3 MASWALI KWA UPANDE WA KENYA ......................................................................................... 23
7.4 MAJIBU .................................................................................................................................... 23
3
8.0 UZOEFU WA UGANDA KWENYE MASUALA YA ARDHI - MWASILISHI: ESTHER
OBAIKOL ............................................................................................................................................ 24
8.1 CHANGAMOTO KWA TAASISI BINAFSI ........................................................................................ 24 8.2 HITIMISHO ........................................................................................................................... 25
9.0 UZOEFU WA RWANDA KWENYE MASUALA YA ARDHI - MWASILISHI: JOHN
MUYENZI ............................................................................................................................................. 25
9.1 UZOEFU KATIKA KUTENGENEZA NA KUTEKELEZA SERA NA SHERIA ZA ARDHI ............................. 25 9.2 CHANGAMOTO ZINAOIKUMBA SEKTA YA ARDHI NCHINI RWANDA .............................................. 26
10.0 MJADALA WA MCHANA ...................................................................................................... 27
11.0 MAAZIMIO YA KONGAMANO ............................................................................................ 28
11.1 USHIRIKI WA WANANCHI NA WANAVIJIJI KATIKA MAAMUZI YANAYOHUSIANA NA ARDHI HUSUSANI
KWENYE NGAZI YA VIJIJI. NINI KIFANYIKE? .......................................................................................... 28 11.2 UWEKEZAJI KATIKA ARDHI YA VIJIJI UNAENDANA SANA NA MAMBO HAYA MAWILI:- ...................... 29 11.3 KWANINI MIGORORO KWENYE SEKTA YA ARDHI IPO KWA KIWANGO CHA JUU WAKATI SHERIA ZA
UTATUZI ZIPO? .................................................................................................................................... 30 11.4 NINI KIFANYIKE ILI WANAWAKE WAFAIDIKE NA SHERIA ZA ARDHI NAMBA 4 NA 5 ZA MWAKA 1999?
........................................................................................................................................................... 31 11.5 FIDIA ZA ARDHI NA KUPATIWA ENEO MBADALA. JE, LINAKIDHI MAHITAJI YA WAFIDIWA? NINI
KIFANYIKE? ........................................................................................................................................ 31 11.6 HUDUMA ZA ARDHI ( UPIMAJI, UTOAJI WA HATI) HAZIENDANI NA HALI HALISI. NINI KIFANYIKE? ... 31 11.7 UKOMO WA KIASI CHA ARDHI ANACHOWEZA KUPATA MTU MMOJA NA KUMILKI KIHALALI. ............. 32 11.8 KILIMO CHA MASHAMBA MAKUBWA NA UHAKIKA WA CHAKULA KWA WANANCHI NA TAIFA KWA
UJUMLA. ............................................................................................................................................. 32 11.9 MFUMO WA UMILIKI WA WAFUGAJI- UTAMBUZI ........................................................................... 32
12.0 KUFUNGA KONGAMANO ........................................................................................................ 33
4
TAASISI YA UTAFITI NA UTATUZI WA HAKI ZA ARDHI
Kongamano la Miaka 10 ya Sheria za Ardhi Tanzania 27-29 Mei 2009
1.0 Utangulizi
Mkurugenzi Mtendaji wa HAKIARDHI - Ndugu Yefred Myenzi aliwakaribisha
washiriki wa Kongamano saa 3.58 asubuhi na kuwafahamisha lengo la Taasisi la
kukutanisha wadau mbalimbali kujadiliana na kushirikishana uzoefu wao kuhusu
masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka 10 tangu sheria za ardhi
namba 4 na sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 zilipotungwa na Bunge.
Kongamano hili litawahusisha waalikwa kutoka nchi jirani za Afrika Mashariki ili
kushirikisha maendeleo katika mifumo yao ya milki ya ardhi na utekelezaji wa sheria zao
kwa lengo la kujifunza uzoefu wao na kujenga mahusiano na ushirikiano katika masuala
ya ardhi.
Mkurugenzi Mtendaji alisema mada mbalimbali zitajadiliwa kuhusu masuala ya ardhi
kutoka asasi za kiraia na sekta binafsi. Mada hizo zitajikita katika tathmini, mafunzo na
changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa sheria za ardhi kwa vipengele
mbalimbali tangu 1999 hadi 2009. Aliwaomba washiriki kuchangia mawazo, kujadili na
kupendekeza nini kifanyike ili kuboresha upatikanaji wa haki ya ardhi kwa kila
Mtanzania.
Baada ya Utambulisho, Mgeni rasmi - Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa – Ndugu Aggrey Mwanri alifika na kukaribishwa na washiriki wote.
1.1 Igizo kwa njia ya ushairi kutoka Parapanda Theatre Group.
Igizo maalum juu ya matatizo ya ardhi – ujumbe wa barua pepe ambayo ilivuta hisia za
washiriki wote na kutoa changamoto kwa washiriki kwamba watumie nafasi hii
“KUZUNGUMZA”.
1.2 Mgeni Rasmi - Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Ndugu Aggrey Mwanri
Naibu Waziri aliomba radhi kwa kuchelewa na kusema amekuja kwa niaba ya Waziri
Celina Kombani ambaye bahati mbaya ilibidi aende kwenye majukumu mengine ya
Kitaifa. Waziri aliwakaribisha nchini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania washiriki
kutoka nchi jirani za Mozambique, Kenya, Uganda na Rwanda na kuwashukuru
waandaaji wa Kongamano hili muhimu kumwalika na kuahidi kushiriki kwa jinsi muda
utakavyomruhusu. Mh. Waziri alielezea umuhimu wa kuwepo mifumo imara ya
usimamizi na matumizi ya ardhi vinginevyo migogoro itakuwa haiishi. Alitoa wito kwa
Asasi za Kiraia n.k. kutumia nafasi zao na rasilimali walizonazo kuunga mkono juhudi za
serikali kuwa na mtandao wa asasi zote za masuala ya ardhi kwa kutoa elimu juu ya
sheria za ardhi na elimu ya uraia kuwawezesha wananchi kujua haki zao. Aliwaomba
5
wadau waungainshe nguvu ili kuwe na mfumo mmoja wa utoaji elimu kwa wananchi
ambao hatimaye unawezesha ufuatiliaji na kupima mafanikio kwa nchi kuliko mashirika
haya yakifanya kazi katika maeneo ambayo tayari serikali imeshatekeleza
yanayofundishwa.
Mh. Waziri alisema kuna changamoto nyingi katika kuhakikisha sheria zinatekelezwa:
Tanzania imebarikiwa na kuonekana kuwa kimbilio la wawekezaji wanaotafuta
nishati mbadala inayotokana na mimea. Ni vyema kutahadharisha matumizi ya
ardhi inayofaa kwa uzalishaji wa chakula isitumiwe kuwa maeneo ya kilimo cha
nishati uoto. Alitoa rai kwa serikali za vijiji kuwa makini katika kuidhinisha
maeneo kwa ajili ya uwekezaji wahakikishe wananchi wanajikimu kwa chakula.
Matumizi ya ardhi ya vijiji yafuate taratibu kama ilivyo katika sheria za ardhi na
serikali za mitaa. Hii inapunguza malalamiko yasiyo ya lazima. Kumekuwa na
malalamiko ya mara kwa mara kuwa vyombo vya utekelezaji vinafanya maamuzi
bika kuwashirikisha. Hii huleta migogoro.
Kuna wananchi wakorofi ambao wamekuwa wanakalia maeneo makubwa bila
kuyaendeleza. Pale inapobainika wananchi wanahodhi ardhi kubwa bila
kuifanyia maendeleo serikali ya kijiji iwajibike kuwashauri kupitia mkutano
mkuu wa kijiji ili kuwe na matumizi bora ya ardhi husika.
Aligusia pia migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imejitokeza mara kwa
mara. Mh. Alishauri mabaraza na mahakama za ardhi viachiwe kufanya kazi bila
kungiliwa na kila kundi liheshimu maamuzi ya vyombo hivyo. Halmashauri za
Wilaya na vijiji vitenge maeneo ya shughuli mbalimbali na kuweka mipaka ili
kila mtumiaji wa ardhi asimwingilie mwingine katika eneo lake.
Umuhimu wa umilikishwaji ardhi kisheria bila kutumia rushwa.
Aliwaomba wananchi kuepukana na matumizi ya maeneo yaliyohifadhiwa ili
kuepusha bomoa bomoa zisizo za lazima. Mh.Waziri alisema anaamini washiriki
watatumia nafasi hii ya Kongamano kuibua na kujadili masuala muhimu kwa
maendeleo ya taifa ili kusaidia serikali kufikia hatua ya juu kabisa katika
kumletea maendeleo Mtanzania. Aliwashukuru waandaaji wa Kongamano
kuwaalika washiriki kutoka Halmashauri za Wilaya na kusema kwa nafasi zao
hao ndio watendaji kila siku wa masuala ya ardhi na watabadilishana uzoefu na
kujifunza mbinu ambazo zinaweza kutumika kukabiliana na changamoto
zinazotokana na kazi zao.
Mheshimiwa Waziri alitambua uwepo wa washiriki kutoka Kenya, Rwanda na
Uganda na kuelezea kwamba swala la ardhi limeibua mjadala mkubwa sana
kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu namna inavyopaswa kuwa na
mfumo unaozingatia maslahi ya kila mwanajumuiya na kwamba mkusanyiko huu
utakuwa na mjadala wenye mwelekeo wa kupata suluhu ya kudumu kwa matatizo
6
yenye sura ya Afrika Mashariki. Alimaliza kwa kuwaomba washiriki watumie
mwanya wa ushiriki mpana wa Kongamano hili kutoa maazimio
yanayotekelezeka kwa kila mdau aliyeshiriki ili kutoa mwongozo wa namna ya
kukamilisha sehemu kidogo zilizobakia katika utekelezaji wa sheria za ardhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa HAKIARDHI alimshukuru mgeni rasmi kwa Hotuba nzuri
ambayo kwa kuifikiria haraharaka ni kama imetoa tathmini, changamoto za uwekezaji na
uhakika wa chakula. Pia ameshukuru kwamba Serikali inatambua mchango wa Asasi za
Kiraia katika swala zima la masuala ya ardhi. Pia alimshukuru Waziri kwa kukubali
kuwa mshiriki.
Mkurugenzi Mtendaji alipitia ratiba na kuwafahamisha washiriki mada zitakazojadiliwa:
SIKU YA KWANZA – 27/5/2009
1.3 Mada: I - Changamoto za Urasimishaji Ardhi katika mfumo wa sasa wa Milki– Na Eng. L. M. Salema, (MKURABITA)
Eng. Salema kutoka MKURABITA alitoa mada kuhusu Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali ambapo alieleza kuwa umiliki salama na endelevu wa ardhi ni nyenzo
muhimu ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Alisema kama unamiliki ardhi
na unatumia nje ya sheria zilizopo wewe ni mnyonge. Kama una shamba au ranchi na
huna kitambulisho kwamba hilo shamba ni lako – (hati) huwezi kuaminika hata benki
hata kama kwenye shamba hilo kuna nyumba kubwa.
Eng. Salema aliwafahamisha washiriki sababu za serikali kuanzisha mpango huu kuwa ni
baada ya kufanya tathmini na kugundua kwamba shughuli za biashara sekta isiyo rasmi
ina wananchi wengi zaidi kwa hiyo juhudi za dhati ni lazima zifanywe ili kurasimisha.
Kwa mfano utafiti uliofanywa (2004-2006) ulibainisha kuwa 88% ni sekta isiyo rasmi.
Miji mikubwa 70% ya wananchi wanaishi makazi ambayo hayajapimwa.
Wananchi wanatakiwa kuhakikisha ardhi waliyonayo inatambuliwa kisheria na ili uweze
kutumia ardhi hiyo ni lazima uisajili kisheria ili yeyote anayeweza kupata taarifa aweze
kupata. Utafiti uliofanyika nchi kadhaa kuhusu mpango huu umedhihirisha kwamba:
Wamiliki wanahamasika kuwekeza kwenye ardhi yao
Migogoro ya mipaka na hata matumizi unapungua kwenye ardhi iliyorasimishwa.
Thamani ya ardhi inaongezeka
Wananchi wanapata mikopo katika mabenki kwa kutumia ardhi kama dhamana.
Pamoja na hayo, serikali inatambua kuna umuhimu wa maboresho katika sheria za ardhi,
yametolewa mapendekezo kwamba usajili ufanyike ngazi ya Wilaya bila matatizo.
Sheria inasema ardhi ni mali ya umma na Rais ndiye mwenye dhamana. Je ni kweli
wananchi wanakubali ardhi ni mali ya umma?. Je Tuendelee kusema au tutengeneze
kanuni rasmi au tukubali ardhi inaweza kumilikiwa na mtu binafsi. Tumetizama sera.
7
nyingi zinagusa sheria ya ardhi. (Zingine zote zinazoitambua sera ya ardhi kama ardhi
mama. Majukumu chini ya Wizara ya Ardhi/TAMISEMI. Katika kubadili mfumo –
Kuwe na tume ambayo wadau wakijadiliana wana mamlaka ya kuamua mambo
muhimu.
Vijana waweze kupima mashamba ya vijiji vyao
Tumependekeza – ndani ya Wizara ya Ardhi kuwe na agency ya kupanga/kupima
na kupokea kodi za ardhi/real estate agency. Mijini na baadae vijijini.
Umiliki wa ardhi uwe mikononi mwa Watanzania. Tusiwape watu wa nje ardhi
yetu kwa sababu migogoro mingi inatokana na hiyo.
Ili ardhi ilete tija lazima kuwe na namna kwa mfano usipoiendeleza (plot e.g.)
kwa muda fulani unaweza kunyang‟anywa. Badala ya mtu kunyang‟anywa –
atozwe kodi.
MKURABITA inathibitisha kwamba ardhi ikirasimishwa inalipa. Na imependekeza
wizara ya Ardhi ifanye kazi ya kupanga matumizi muhimu ya ardhi. Pamoja na kwamba
hatujatamka kwamba nchi yetu ni ya kibepari, tuzungumze kwamba ili kilimo kishamiri
tuwe na kilimo cha kisasa ambacho tunaweza kuwa na kada ya wakulima wazuri.
Pamoja na kurekebisha sheria – kujenga uwezo ili urasimishaji ufanyike mamlaka
ya chini.
Katika hali yetu ya maendeleo tunategenea sekta isiyo rasmi na ukimwambia mtu
akopee hati yake na jirani yake ameuziwa nyumba juzi kwa ajili ya kutolipa
inatisha. Kuwe na mpango maalum wa kumwezesha huyu asipoteze chake.
Tupeni mawazo yenu ili kuboresha hapa.
1.3.1 Washiriki walichangia mada kama ifuatavyo:
i. Wakulima wadogo wadogo watanufaika vipi na mpango huu?
ii. Inakuwaje tuukumbatie mfumo wa ubepari wakati tunajua hata siku moja
haujaleta manufaa kwa mwananchi wa kawaida?
iii. Je elimu ya mpango huu imetolewa ya kutosha? Juu ya umiliki, matumizi au
kuuza kwa ajili ya faida yao? Je watalindwa? Bila kuuza kwa watu wa nje?
iv. Umilikaji wa ardhi – kama ardhi ni ya kwangu na familia na eneo ni langu je
nitakuwa na ukomo? kwa mfano umiliki wa miaka 33 au 99. Je baada ya hapo
nitakuwa sio Mtanzania?
8
1.3.2 Maoni ya Mkurabita
Watu wengi wanafikiri kwamba MKURABITA ilianzishwa kwa msukumo wa
De Sotto. Hii si kweli. Kabla ya hapo, chama cha CCM kilifanya maamuzi
wananchi wamilikishwe ardhi. Baadae Dr. De Sotto na Mkapa walikaa.
Mawazo yao yalifanana kwamba kuna watu wengi wanamiliki mali isiyo
rasmi. Kukafanyika Kongamano mwaka 2003 ambalo lilihudhuriwa na watu
mbalimbali. Alichosema De Sotto ni kwamba kama wananchi watabaki bila
kurasimishiwa wataendelea kuwa duni vinginevyo kule Peru walifanikiwa.
Kuna maboresho na mapendekezo yaliyotolewa ila hatuwezi kukataa kwamba
ni ukweli sekta isiyo rasmi haifai.
Watu wanafikiri kurasimisha ardhi ni ubepari. Ule ni wa Carl Max. Ubepari
wa sasa ni tofauti, unatambua mchango wa mtu. Wanataka kuwe na amani.
Wala hauendeshwi na serikali ni shirikishi (corporate world) ndio inafanya
kazi. Ni swala la utaalam.
Kuhusu kwamba elimu haitoshi – Kuna mpango wa elimu wa miaka 10. Hii
ni pamoja na namna ya kulinda haki za wamiliki. Kwa sasa watu wengi
wametambua thamani ya ardhi na wanauza sana. Wakiwa na hati watapata
pesa zaidi. Tena zipatikane katika ngazi ya kijiji. Halmashauri za kijiji hata
sasa zinashughulikia mikataba mingi kuliko Commissioner wa Ardhi.
Kuhusu kama ni mpango wa serikali kunyang‟anya ardhi – Eng. Salema
alisema, kwanza milki ya kimila haina ukomo. Ukomo uko kwenye ardhi ya
mijini. Na haiwezi kunyang‟anywa bila kutumia sheria. Hamna sababu ya
kuwa na woga.
1.3.3. Maoni kutoka kwa Mgeni Rasmi - Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mazingira ya kwetu hakuna ubepari kwamba njia za uchumi zimejengwa kwa kutowajali
wengine na kuwatupa nje. Hapa tunazungumzia mahusiano ya uzalishaji mali.
MKURABITA ukisema unalima pamba – unatumia harvester. Moja ya namna ya
kuwasaidia wananchi wanyonge ni kuwaunganisha kwenye ushirika. Kama unataka
kuwasaidia utapitia pale. Vinginevyo utawafanya wawe vibarua. Mashirika kama benki
– hawatawajua. Serikali imeingiza “msuli” intervention. Tunapigania ushirika ndio
unaoweza kusaida. Je ni kweli ukisharasimisha wananchi watatoka? Kuna soko huria na
limekubalika, kazi yake ni nini? Hii iko katika „sheria ya utashi na urari‟. Law of demand
and supply.
Watu wazugumze „planned market economy.‟ Unaweza kusema tuweke sheria.
Tunachopigania hapa ni faida nyingi – „super profit‟. Wenzetu nchi za Ulaya wanaweka
ruzuku katika kilimo, mifugo ili kusaidia mipango katika kipindi cha mpito.
Baada ya maswali na majibu Mratibu wa Kongamano William Ole Nasha
alimshukuru Naibu Waziri na washiriki wote waliochangia na kuahidi kuendelea
kujadili.
9
2.0 MADA II – TATHMINI YA SERIKALI JUU YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA ARDHI, UZOEFU, MAFUNZO NA CHANGAMOTO - Mwasilishaji Jane Kapongo, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi
Mada hii ilitolewa na Dada Jane Kapongo ambaye alielezea majukumu ya Wizara ya
Ardhi Mijini na Vijijini. Dira hasa ni kuwa mlezi wa umiliki na ulinzi wa ardhi nchini.
Na dhima yake ni kuwa na mazingira wezeshi. Alisema Wizara ya ardhi imefanya juhudi
kubwa ya kuwaelimisha wananchi kuhusu sheria za ardhi na yeye binafsi amehusika
kwenye kuendesha mafunzo hayo.
2.1 Madhumuni ya Wizara
Kuimarisha usalama wa milki za ardhi
Kuboresha mtandao wa kijiographia nchini
Kuweka mpango endelevu wa watu/nyumba zinazokidhi mahitaji
Kuendeleza utafiti wa vifaa vya ujenzi wa nyumba bora kwa bei nafuu
Ushirikiano/mawasiliano na uratibu wa masuala ya kitaifa/kimataifa na kikanda.
Mtoa mada aliwafahamisha washiriki wa Kongamano umuhimu wa wizara ya Ardhi
kushirikiana na Asasi za Kiraia katika kutekeleza sheria za ardhi kwa sababu mlengwa
wa wote ni mwananchi. Bahati mbaya sana hata katika kupanga bajeti ya serikali sekta
zinazopewa umuhimu zaidi ni Afya/Kilimo/Elimu, n.k. na sio ardhi.
Alisisitiza umuhimu wa kuwa na wataalam/wateule wa masuala ya sheria za ardhi ili
utekelezaji uwe rahisi.
2.3 Maoni na mchango wa washiriki
Mshiriki mmoja alisita kukubaliana na swala zima la elimu juu ya sheria.
Alisema watu wengi haijawafikia. Kuna umuhimu sana kwa wananchi kutoa
elimu hii. Bila hizi ASASI kazi ya Wilaya inaweza kuwa ngumu. Aliunga
mkono ushirikiano na kutoa mfano kwamba sehemu anayotoka (Arusha) hamna
sehemu ya utatuzi wa migogoro na hata kama milki ingetolewa bila elimu bado
migogoro itakuwepo.
Mtafiti wa Nishati Uoto vijijini- alisema Sheria za ardhi ni tatizo. Tatizo la fidia
kwa wawekezaji wanaochukua mashamba ya wananchi ni kubwa mno. Fidia ni
ndogo sana. Wananchi hawana ujuzi wa hesabu hata za ekari. Utawaelekezaje
kama hawaelewi sheria na hawaijui.
Uendelezaji wa ardhi ni changamoto vijijini kuliko mijini. Kama Wizarani kuna
mikopo ya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi – Je Wizara inawasaidiaje
waliopata viwanja kupata mikopo hii?
10
2.4 Maoni ya Wizara
2.4.1 Mafunzo - Idara ya utawala na usimamizi wa ardhi - ndani kuna kitengo
ambacho Sheria ya Ardhi Na. 4 na 5 zinapatikana. Hapa kitengo hiki hushirikiana na
wadau wote katika utekelezaji wa sheria za ardhi. Inaratibiwa na WB/EU.
2.4.2 Fidia – Ndani ya sheria imeelezwa namna ya kudai fidia. Iwapo mtu wa nje
anataka kuchukua sehemu. Kuna utaratibu maalum kuhusu fidia.
Watu hawaelewi sheria. Pamoja na elimu inayotolewa – „public awareness‟ ngazi
ya mkoa. Inatakiwa ngazi ya juu zaidi. Mtoa mada alikubaliana na washiriki
kwamba kuna sehemu Wizara haijafika ndio maana inatambua kazi za NGOs.
Utoaji wa vifaa – Kuna miongozo ya kutoa sheria za ardhi na migogoro ya ardhi.
Kuna kamati maalum ya watu 9 inayosimamia miongozo hii.
2.4.3 Utatuzi wa Migogoro
Kama Wizara kuna mabaraza hasa sehemu zenye migogoro mingi. Kutathmini kama
wajumbe wamechaguliwa vizuri bila „conflict of interest‟.
2.4.4 Mikopo ya Nyumba
Mikopo ya nyumba ni kwa watumishi wa serikali tu. Utaratibu wa kupata ni kwamba
ukipata kiwanja unatakiwa upate hati/mchoro/mchanganuo wa ujenzi na unapewa
mkopo ambao unakatwa kwenye mshahara wako.
2.5 Maswali na Ushauri
2.5.1. Swala la mikopo ya nyumba kama ni kwa wafanyakazi wa serikali tu ifutwe.
2.5.2 Je mikopo kwa ajili ya kupima viwanja. Wananchi wanaweza kupewa fidia
kwa kupata ardhi mbadala au fedha. Fidia hiyo ili iweze kuwafikia wananchi ina
thamanishwa kiasi gani. Tunataka kujua eneo kiasi gani ni bei gani?
2.5.3 Vyeti vya kimila – Katika vijiji vingine hamna hata fomu na kupata cheti
cha kijiji ni vigumu. Je wananchi wafanyeje.
2.5.4 Mikopo kwa ajili ya wafanyakazi – Watekelezaji wenyewe wanajigawia
mikopo na viwanja – kuna dhana ya upendeleo, wananchi watapata kweli?
2.5.5 Ukuaji wa miji na vijiji – Wote tunajua kuwa ili mtu aendelee tunahitaji
ardhi/watu na siasa safi. Vijiji havijapata vyeti kwa hiyo ardhi haijapatikana.
2.5.6 Utekelezaji wa vijiji na mpango bora. Kuna matatizo mengi ya mipaka
vijijini. Kama hayatatatuliwa, tunawekeza kwenye matatizo ya baadae. Kama
juhudi zisipofanyika, kuna watu watakaopimiwa sehemu zenye matatizo ambazo
zinaweza kuwa hata haziko kijijini kwao. Mfano mzuri ni Rufiji. Matatizo
mengine ni ya Wizara ya Ardhi – wananchi kuna mambo tunayofahamu ya
kughushi taarifa ambazo sio sahihi. Tunapandikiza matatizo.
11
Mwongozo:
Mshiriki mmoja alishauri kwa sababu hili ni kongamano – sio busara kuelekeza
maswali kwa mtoa mada – washiriki wachangie na kutafuta utatuzi. Alisema fidia
kweli ni tatizo kubwa – sheria Na. 4 ilisema utaanzishwa mfuko unaosaidia na kanuni
imeshatungwa.
2.6 Mwongozo kutoka Wizara ya Ardhi
Kuhusu kufuta mikopo, watu wengine hawana pa kukopea. Serikali inaweza
kutumia ardhi kama rasilimali mtu anaposhindwa kulipa. Mtumishi anakatwa
kutokana na mshahara wake.
Mpimaji wa viwanja ni Halmashauri ambazo ziko chini ya serikali za mitaa.
Sheria No. 5 ni mpya, kama sio mtaalam wa maswala ya ardhi. Pale ambapo
tunatekeleza inatakiwa tuungane na Halmashauri husika
Utatuzi wa Migogoro ya mipaka – Kwa mujibu wa sheria Halmashauri za kijiji
husika ndio zinashughulikia. Vijiji haviwezi kupata cheti kama kuna migogoro ya
mpaka wa kijiji.
Sehemu iliyopimwa viwanja – watu wanalipwa fidia. Viwanja vinatangazwa na
mwananchi yeyote yuko huru kununua. Sasa hivi wananchi wameamka na
wanathamini maeneo yaliyopimwa. Na ni vyema kuchukua yanapotangazwa.
Wilaya ya Rufiji – Wizara imeamua kuanzisha idara zinazoshughulika na
matatizo ya ardhi. Kwa kuwa watu wa Rufiji wameeleza matatizo yaliyopo, mtoa
mada aliahidi kuyapeleka ofisini kwa utatuzi.
SIKU YA PILI - 28/05/09
3.0 MADA: MTAZAMO WA ASASI ZA KIRAIA JUU YA UMADHUBUTI, UDHAIFU NA CHANGAMOTO ZA MFUMO WA MILKI YA ARDHI TANZANIA – Mwasilishaji – Oxfam/HAKIARDHI
Malengo ya Sheria ya Ardhi 1999 ambayo ndio kiini cha tathmini hii yalielezewa.
Matokeo – baada ya sheria za ardhi kutungwa.
Je haki zilizokuwepo zinafuatwa? Mchambuzi alielezea jinsi hali ilivyo – Sheria
inaeleza wazi kwamba mtu akiondolewa kwenye eneo lake atapata fidia lakini
watu hawapati.
Pia tumeona kuwa sheria ya kimila ina matatizo.
Sehemu za Ihefu, Kilosa,Mabwegere, Nkasi, Mpanda, Mvomero, Mwanga, Same,
Mikumi n.k. watu wameondolewa bila sheria kufuatwa. Japo sheria zipo wazi.
Watendaji wapo mstari wa mbele kuumiza watu kwa maamuzi mabaya bila kuwa
na madaraka hayo kisheria. Maamuzi ya viongozi wa hali ya juu – yanatishia
watu.
Wawekezaji walioacha maeneo miaka mingi wanaondoa wafugaji katika maeneo
hayo
Kuondolewa wafugaji maeneo mbalimbali
12
Hata ripoti ya „Control & Auditor General‟ imeonesha jinsi ambavyo fidia
haiwafikii wananchi.
Kesi ya NAFCO – tumeona zilianza muda mrefu – ranchi zinagawanywa kwa
watu wachache.
Kuna swala la viongozi kujitwalia ardhi na kuwakosesha wananchi haki yao
Lengo ni kuhakikisha hamna mtu anamiliki ardhi kubwa kuliko mwingine
Sheria haikulinda maslahi ya wananchi
Lengo la sheria ya ardhi ni kuhakikisha ardhi inagawanya kulingana na vigezo
vya matumizi
Watu wamehodhi ardhi kubwa huku wananchi wakigombania ardhi ndogo
Kiasi cha fedha kilitengwa kwa walioondolewa Ruaha National park –lakini fedha
hazijulikani zilipo.
Kuwe na taratibu na sheria zanazomsaidia mwananchi
Kuna tatizo katika mkakati wa utekelezaji wa sheria ya ardhi. Hata kwenye
mabaraza bado kuna migogoro mikubwa. Wale wanaotunga sheria hawazifuati.
3.1 Mambo yaliyojitokeza
Rushwa, Migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Migogoro kati ya wakulima
wadogowadogo na wawekezaji, Matatizo ya fidia, Mgongano wa maslahi,
Sheria/matamshi ya siasa, Wafugaji kuhamishwa, n.k.
3.2 Matokeo
Umaskini, watoto hawaendi shule, huduma za elimu duni, kutumia nguvu bila sababu,
rushwa, watoto hawapati ada ya kwenda shule kutokana na wazazi wao kukosa mahali pa
kulima, mifugo ilikufa mingi, vurugu kwa mfano. Kilosa/Mpanda. Risasi zilitumika.
Uchomaji wa nyumba za wananchi – Kilosa, kutozwa faini na kuchukuliwa mali za
wananchi, zilioneshwa shuhuda na risiti ambazo wananchi wamelipishwa kwa kuweko
kwenye maeneo ambayo wana haki kuwepo. Uvunjaji wa heshima na haki za binaadam.
“Ukiuliza wafugaji waende wapi, nami nitakuuliza walitoka wapi”
3.3 Maswali na Maoni
Kama ilivyoelezwa, Ihefu – wananchi hawalipwi fidia. Je ni kiasi gani ambacho
hakijalipwa? Nini kimefanyika kuhakikisha wananchi wanapata haki yao?
Fact Finding – kama kweli wafugaji wanaonewa – serikali ina mpango
gain unaofanyika ili wafugaji wapate haki zao. Bado kuna maeneo watu
wanatakiwa wapate elimu. Tuangalie pande zote.
Pale Chuo cha Ardhi kuna „master plan na land use plan‟ vijijini.
Matatizo mengi yangeweza kuepukika kama hizi zingetumika vizuri.
Siasa inatawala kwa wataalam kwa sababu kama wataalam watafanya kazi
zao bila kuingiliwa na wanasiasa, tutaepuka migogoro mingi.
13
Utekelezaji wa Sheria – Hatua gani imechukuliwa kuhakikisha kwamba
serikali inasaidia kutekeleza sheria? Nini kifanyike ili kuhakikisha elimu
inatolewa. Kama elimu haitolewi, miaka kumi ijayo kutakuwaje?
Serikali inachangia ukiukwaji wa sheria. Jamii inaamini serikali lakini
wananchi hawapatiwi haki zao (fidia).
Mshiriki mmoja alisema Mada imelenga kwenye mapungufu tu – Je huu
ndio mtazamo wa Asasi za Kiraia? Watekelezaji wa sheria ni
serikali.halmashauri/CSOs au wote pamoja? Ardhi ya umma haiko chini
ya wana vijiji. Na anaamini yako mazuri pia ambayo inabidi kukiri.
Kuhusu swala la fidia, mwananchi alipwe kutokana na bei halisi ya soko.
Awepo mtoaji na mpokeaji. Thamani ya ardhi pia izingatiwe. Aidha
mhusika apewe fidia na kupewa eneo jingine sio kumlipa fidia bila kujali
atakwenda wapi.
Athari za kuhamishwa ziangaliwe. Chanzo ni nini. Je tathmini
imefanyika na ninapohamishiwa kuna fidia. Na je huduma ambazo
mwananchi alikuwa anapata alipokuwa atazipata aendapo?
Sheria kama ilivyo inasema fidia ifanywe kwa haki na usawa na kwa
wakati unaostahili. Sheria ya ardhi ya 2004 – thamani ya mazao
inatambuliwa. Hata kama kuna maendelezo. Kuna malipo ya usumbufu.
Usafiri wa Tani 7 kwa kilomita kama 20. Interest rate wa muda wa
malipo.Je madhara ya kuhamishwa ni yapi na faida ni ipi.
3.4 Maelezo kutoka kwa Mwasilishi
Fidia imezungumziwa kwa kina karibu na watoa mada wote na pia washiriki
wamechangia. Inawezekana ni hisia lakini wananchi wanalalamika ndio maana
tunazungumza. Labda ni hisia zangu lakini sio binafsi. Haya ndio yaliyojitokeza.
Je sheria imeshindikana. Kutekelezeka? Kulikuwa na matatizo ndio maana
sheria ikatungwa. Mengi yamewekwa lakini utekelezaji wake haupo.
Kwa kuongea tunatatua. Kwa mfano wananchi waende wapi? Nikijibu walitoka
wapi? Jinsi matamshi ya viongozi wa serikali yanavyokatisha tamaa – je
itawasaidia?
4.0 MADA - Uzoefu na Changamoto za mfumo wa Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi – Na Bahati Mlole, Msajili wa Mabaraza ya Ardhi – Wizara ya Ardhi.
Mtoa mada (B. Mlole) aliwafahamisha washiriki wa Kongamano kwamba mfumo wa
utatuzi wa migogoro uliundwa baada ya Tume ya Rais ikiongozwa na Prof. Shivji
kubaini kuwa kuna migogoro mingi ya ardhi. Ilipendekezwa kwamba chombo hiki
kianzie kijiji mpaka ngazi ya kitaifa. Aliainisha vyombo vya utatuzi wa migogoro kuwa
ni:
14
Baraza la Ardhi la Kijiji
Baraza la Kata
Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
Mahakama Kuu – Kitengo cha Ardhi
Mahakama ya Rufaa.
Iliundwa (Land Disputes Courts Act) Sheria ya Utatuzi wa Migogoro No. 2, 2002
ambayo ilianza kutumika 1.10.2003. Haikuwezekana kuanza mapema kwa sababu
ilianza kanuni. Kwa hiyo tunapofanya tathmini, kipimo kiwe miaka 41/2 iliyopita.na sio
miaka 10 kama ilivyo sheria za ardhi. Migogoro mingi ya ardhi hasa kwa mijini
inatokana na kugawa sehemu moja kwa watu zaidi ya mmoja ama kwa kukosa
kumbukumbu au kwa makusudi. Aidha Maafisa Ardhi wa Wilaya hawana mamlaka ya
kufuta milki yeyote. Kwa upande mwingine wananchi pia ni chanzo cha migogoro.
Katika kuunda mabaraza Wizara inatoa kipaumbele kwa Wilaya zenye migogoro mingi
na ambazo zipo mbali na mabaraza ambayo tayari yanafanya kazi. Matatizo mengi na
migogoro yalianza kusikilizwa Novemba 2004.
Kwa.mfano migogoro ya upangishaji nyumba, wanandoa wanapogombea mali, kuweka
nyumba rehani n.k. Kwa miaka 41/2 kulikuwa na mashauri 38,023. Mashauri 20,374
yamepatiwa ufumbuzi na mengine yanaendelea kufanyiwa kazi.
Sheria inasema vyombo vya utekelezaji viimarishwe kuanzia ngazi ya vijiji mpaka Taifa.
Lakini chombo hiki kiko chini ya Wizara tatu, i.e. TAMISEMI, Wizara ya Ardhi na
Wizara ya Sheria na Katiba. Na wakati mwingine utekelezaji unachukua muda mrefu
japo kuna mwongozo wa mabaraza migogoro mingi hususan ile isiyosimamiwa na
mawakili inachukua wastani wa mwezi 1 hadi miezi 6. Kwa sababu hiyo wananchi
wengi wamefikia hatua ya kuongeza au kupunguza thamani za mali zao ili waweze
kufungua kesi katika Mabaraza ya ardhi na nyumba ya Wilaya badala ya kwenda katika
mabaraza ya kata au mahakama kuu – kitengo cha ardhi. Hii inadhihirisha kwamba
wananchi wanaelewa thamani ya ardhi. Pia mabaraza ya Kata/Vijiji hayafuati sheria na
mara nyingi ni kwa sababu hayajaundwa kama inavyotakiwa.
Maafisa ardhi wazingatie sheria kwa kufuata waraka wa TAMISEMI. Wananchi pia
washirikishwe kuchangia hoja.
Wakurugenzi waelekeze sheria
Swala la Elimu – vijiji ambavyo havina vitabu vya sheria waende kuchukua.
Changamoto kwa waliopo vituo vya sheria – kuwasaidia wananchi wanaokosa haki zao
kwa kutoelewa sheria.
4.1 Maoni na maswali kutoka kwa washiriki
Ardhi nchini kwetu haikuwa mali ya Taifa – imekuwa hivyo baada ya serikali
kuchukua hatua. Kuna wakati Kampuni fulani ya Belgium walikuwa na eneo
likaitwa lao na linaitwa Belgium bandarini. Mwl. Nyerere akataifisha.
15
Maana ya kusema tuna ardhi ya kutosha - si kweli. (Takwimu za Tz. Bara na
Visiwani) Inabidi tuishi na kufikiria watoto wetu wataishi vipi. Unapompa mtu
ardhi kwa miaka 99 kweli unajali vizazi vijavyo?
Mfano – uwekezaji 1966 Korogwe. Tatizo la kutoa ardhi bila kutizama kesho
ndio matatizo anayopata Rais Mugabe Zimbabwe.
Wafugaji – ukisema nataka ranch unapata – ukisema nataka sehemu ya malisho ni
tatizo. Tukitaka nchi yetu iwe na amani tutenge maeneo ya kutosha ya ufugaji na
kilimo.
Kupima vijiji na kugawa ardhi kwa wanavijiji ni muhimu.
Parapanda arts walisema tuzungumze. Rais Kikwete alisema ataunda serikali
inayosikiliza nasi tunasema serikali itusikilize.
Jambo la kusikitisha kusikia kwamba Rais anachukua ardhi ya wananchi.
Viongozi wa nchi ambao tumewapa madaraka wanachukua ardhi – wanawapa
watoto wao. Sheria inasemaje kuhusu hilo. Je wakubwa wako nje ya sheria?
Inavyotokea kwa mfano – Waziri Mkuu akijibu swali la John Cheyo
alivyomuuliza wafugaji wanapofukuzwa waende wapi na kujibu kwani wametoka
wapi. Ina maana hao – sheria zibadilishwe ili kila mtu aweze kurudi alikotoka?
Baraza la ardhi la Kata linashughulikia pia makosa ya jinai pamoja na migogoro
ya ardhi. Kesi inapowafikia ya ardhi inajinaishwa.
Fidia sio kweli fidia zinalipwa na serikali kuu. Wakati mwingine ni Halmashauri
husika.
Watendaji wanavunja Katiba na sio utekelezaji wa sheiria ya ardhi. Kama ofisi ya
ardhi haipo – au kijiji hakina masjala na Halmashauri za kijiji haziweki
kumbukumbu inakuwa vigumu.
Wawekezaji kuna kitu vijiji havijui. Wanataka mwekezaji apewe hati ya mila.
Vinginevyo akipewa hati ya kawaida ardhi inakuwa sio ya kijiji tena.
Wahariri/waandishi wa habari/watoa mada wasiogope mabosi. Unaposema someni
sheria? Wewe sheria hukusoma inayosema huyo mwananchi umlipe? Watu wa serikali
mnajipendelea. Tunapokuja tungeondoka tumeridhika lakini huduma haziridhishi. Haya
ni mawazo ya wananchi tunataka baraza la Taifa la Ardhi bila kubadilisha katiba – sheria
zitabadilishwaji?
4.2 Mwongozo kutoka Wizara ya Ardhi
Swala la Baraza la Kitaifa haliko katika mfumo wa mabaraza yaliyoongelewa
5.0 MADA – Utekelezaji wa Mipango ya matumizi Bora ya Ardhi, Uzoefu, Changamoto na mafunzo - Na Gerald Mango –
Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
16
Misingi na malengo ya sheria ya mipango ya matumizi ya ardhi namba 6, 2007 ni
kuwezesha usimamizi na ufanisi wa matumizi ya ardhi yote nchini, kuwezesha wamiliki
na watumiaji wa ardhi kuwa na matumizi endelevu na uzalishaji bora katika ardhi, baada
ya kugundua kuwa vijijini hamna mwendelezo mzuri na wala uhakika wa milki. Pia
mpango huu unahakikisha maendeleo endelevu. Kuna jitihada ya kupambana na
uharibifu wa mazingira ya ardhi na vyanzo vya maji ambao unahusisha malengo ya
milenia, MKUKUTA na Dira ya Taifa. Pia kuboresha kilimo ili kuchangia pato la taifa.
Kuhakikisha hakuna uharibifu wa vyanzo vya maji kama ilivyotokea Bonde la Usangu.
Kuhakikisha upatikanaji maji ya umwagiliaji na nishati ya umeme.
Sera mbambuka za mipango ya matumizi ya ardhi
Mipango mbalimbali ilianzishwa kuhakikisha matumizi bora ya ardhi kama National
Environment Action Plans (NEAP), Sera ya Taifa ya ardhi 1995 – iliyolenga kuhakikisha
miliki za ardhi na kurahisisha umilikaji wa rasilimali ardhi kwa wananchi, Sera ya
Mazingira ya 1997, Kamati ya Mazingira ya Bunge, Sera ya Maafa, Sera muhimu za
rasilimali ardhi zilizoundwa k.m. madini, kilimo na mifugo, wanyamapori, uvuvi, misitu,
maji, nishati, makazi na miundombinu.
5.1 Mchango wa mawazo kutoka kwa washiriki
Vijiji vichache sana ndivyo vilivyofikiwa na mpango huu. Je kuna uhalali gani kuwa
mpango wa Taifa kama haujafikia sehemu kubwa?
Wanavijiji wamepewa majukumu makubwa na uwezo wao ni mdogo. Hawana hiyo
Land use plan. Tunachokosa hapa ni cost benefit analysis. Mwananchi wa chini
anaendelea kukandamizwa.
Sheria yetu ya ardhi inatoa kibali kiasi gani na ana masharti gani? Kwa mfano Malaysia
lazima kuwe na mzawa kama unataka kuwekeza. Sheria ya uwekezaji inashirikisha vipi
wazawa?
Wilaya zilizoko ndani ya mpango huu kwa mfano wafugaji wa Ihefu walipelekwa vijiji
kadhaa. Walipofika walishindwa kuendeleza ufugaji. Kwa sababu aina ya majani
haikufaa mifugo yao. Mnada haujawahi kuuza hata ngombe mmoja. Sehemu kama
Kisarawe kuna josho moja tu – Maeneo kwa ujumla hayafai yana mbung‟o wengi.
Namna gani wadau wanahusishwa? Je kuna utafiti uliofanywa kujua sababu kwa nini
hawaendi sehemu husika walikohamishiwa? .
5.2 Mchango kutoka kwa Mwasilishi wa Mada kutoka Wizara ya Ardhi
Ndugu Mango alikiri kuwa hiyo ni changamoto. Mkakati gani wa kutekeleza? Mafunzo
hayajafanyika.
17
Aliomba mashirika yasiyo ya kiserikali washirikiane na Wizara na Serikali kwa ujumla
kubadilishana mawazo kuona jinsi ya kutatua tatizo hili.
Mpango wa Taifa unatafsiri sera – sio utekelezaji. Tume inajenga uwezo wa
Halmashauri za Wilaya.
Wawekezaji – hatuamini uwekezaji toka nje. Tunasema Wizara ya Kilimo isitegee
wawekezaji wa nje. Hakuna atakayetekeleza haya. Watauza na kupeleka nje.
Mwekezaji ni mwananchi mwenyewe. Vijana wawezeshwe waendeleze Kilimo
wapatiwe pembejeo na vifaa vya kisasa vya kilimo kama tractor na ardhi ya kutosha. Hao
ndio wawekezaji tunaoongea.
6.0 MADA YA CRT - Elikaribu Gayemi, Ujamaa CRT Resource Trust
Hii inajumuisha wafugaji/waokotaji matunda.
Kuboresha maisha ya watu – kufundisha haki zao, kujenga uwezo wa watu, maisha yao
kwa kutumia maisha.
CRT iko Ngorongoro, Mbulu, Hanang, Simanjiro, Kiteto na Karatu.
Kazi kubwa ya CRT ni kutoa mafunzo ya sheria za ardhi ambazo hutoa mwongozi wa
kuendesha mikutano mikuu ya kijiji, matumizi bora ya ardhi, mabaraza ya vijiji, namna
ya kusimamia maliasili na utawala bora.
Pia uundaji wa sheria ndondogo ili kusimamia rasilimali. Kuchora ramani eneo la
mifuko, kilimo na makazi na kuwaelezea wananchi jinsi ya kupata vyeti vya kumiliki
ardhi.
6.1 Changamoto
Wananchi wanalazimika kugawa ardhi kufuata ramani za vijiji
Kuna mkanganyiko wa sheria ya ardhi ya vijiji na Sheria ya wanyamapori
Serikali mara nyingi hutumia nguvu iliyo nayo kuingilia mamlaka halali za vijiji
Upimaji wa vijiji ni gharama sana
Mara nyingine siasa hutumika badala ya sheria
Mara nyingi ardhi iliyotengwa kwa ajili ya wafugaji haiheshimiwi na ubinafsi
unatawala na inashangaza miaka kumi ya sheria za ardhi bado ardhi ya wafugaji
inatambuliwa kama ardhi isiyo na shughuli yeyote.(iliyo wazi) mfano Sukenya,
NAFCO, etc.
Wafugaji bado hawatambuliwi kama wachangiaji wa uchumi wa taifa
18
Bado utumiaji wa ardhi kwa wafugaji unaangaliwa kama sio mzuri na matokeo
yake wafugaji wanahamishwa mara nyingi bila kujali sehemu wanazokwenda.
Mfano mzuri ni wa Kilosa
Wakati umefika kwa Serikali kutambua kwamba wafugaji ni muhimu kwa uchumi wa
Taifa na kuelewa kuwa kubinafsisha ardhi ya wafugaji ni kukataa kwamba ardhi ya vijiji
hivyo sio ya wananchi wa sehemu hiyo ambao ni wafugaji. Kuna haja ya kufanya utafiti
wa kujua wafugaji wanaishije na kutafuta njia ya kuwaingiza katika mpango mkakati wa
mipango ya kuendeleza taifa.
6.2 Mawazo ya washiriki
1. Tanzania tuna tatizo kukubali ufugaji asilia ni ufugaji endelevu. Shinikizo serikali
iwepo sera kutambua ufugaji asilia kama ni mfumo wa maisha.
Usalama wa maeneo ya ufugaji ngazi ya vijiji ni mdogo au haupo
Kufanya utaratibu wa vijiji vinavyopakana vyenye matumizi ya pamoja wapange
mipango yao pamoja
Benki ya ardhi tumeambiwa ipo, nani anaweza kujua kuna nini ndani ya benki
hiyo isije ikawa watu wanahangaika kumbe ardhi wanayohaingaikia iko kwenye
benki tayari
2. Matatizo ya wafugaji – watendaji wamekubali wamekosa. Kuna sheria gani na
fidia gani imetolewa kwa mfano mfugaji mmoja aliuziwa ngombe wake badala ya
shs. Laki tatu kwa ngombe waliuzwa 8,000/= Hii ni upotevu wa mali na ni
uhalifu pia.
3. Wanakijiji wanawapa wawekezaji ardhi na baadae hao wawekezaji wanapata hati.
Ardhi mwanzoni ilikuwa ya kimila na baadae inabadilishwa kuwa ya hati. Na
anakuja kiongozi na kusikia haya anakaa kimya.
4. Ufugaji – kuna upungufu wa malisho, Ni matatizo makubwa. Zamani kulikuwa
na utaratibu wa sheria – kupunguza wanyama ambao hawana afya sijui siku hizi
vipi Na je, ili kuweza kuepuka migogoro ni vigezo gani vitatumika?
5. Wanaopanga ni watu husika. Wanakubaliana. Wanatakiwa wawepo wakulima.
Eneo endelevu – Kigezo ni mazingira. Timu ni kukusanya takwimu ya matumizi
ya baadae. Wakati mwingine wafugaji hawafiki kwenye mikutano matokeo yake
mipango inapangwa na watu wengine.
Mwekezaji kupata ardhi
Mfano Kituo cha uwekezaji (TIC) ili apate ardhi lazima kuwe na raia - asilimia 51%.
Kuna wageni wajanja akishaoa anakuwa amehalalishwa. Na kwa kijijini lazima
kuwe na muhtasari wa Halmashauri kwanza. Lazima kijiji kiwe na Land Plan.
Sasa hivi maombi mengi yamekwama kwa sababu hiyo. Ili Rais ahamishe milki
lazima mwekezaji aende kijiji husika aelezee manufaa ya umma yatakayopatikana
na uwekezaji wake – Maelezo yanaenda kwa Commissioner wa Ardhi naye baada
ya kuridhika yanapelekwa kwa Rais.
6.3 Nafasi ya Mwanamke katika umiliki wa ardhi
19
Sheria za ardhi na sera zimetoa fursa kwa wanawake. Tumepiga hatua. Kiwango
cha haki hamna mafanikio sana – kuna mila ambazo zimeshindwa kumkwamua
mwanamke.
Wajane na waume wapya – analazimishwa kuolewa ili arithi mali za mume wake.
Hii ni tabia hatarishi hasa maambukizi ya magonjwa n.k.
Maswali na maoni ya washiriki
Ni kweli wanawake wananyanyasika. Mfano toka Kilombero.
Wanawake wa Datooga-Iraqw pia mila zinawaumiza. Wanafanya kazi nyingi shambani
na kufuga lakini hawarusiwi hata kushiriki katika mipango ya fedha zinatopatikana
kutokana na jasho lao.
Uzoefu - tulipotoa elimu ya miliki bado desturi zinashida. Katika sehemu nyingine
kumetolewa elimu ya umilikaji wa ardhi kwa wanawake. Katika vijiji vingine upimaji
wa mashamba kwa ajili ya wote – wanawake na wanaume umefanyika ili kuwapa
wanawake fursa ya kumiliki ardhi.
Uwakilishi kwenye mabaraza – wakina mama hawajajengewa uwezo. Kama uwakilishi
hauleti maslahi kwa wenzao.
Ukweli ni kwamba makabila mengi nchini bado yana mila potofu. Makabila mengine
ukoo ni kwa mama kwa hiyo hao ni rahisi wanawake kumiliki ardhi.
Kuna mambo mengi yanakwamisha hili, mahari ni tatizo kubwa tu. Kwa mfano
wasukuma. Kama tumeweza kubadilisha maneno – kwamba wanawake huolewa na sio
kwamba watu huoana. Mwanamke anatumikia mahari aliyolipiwa. Unyanyapaa
umezidi. Wanawake wakiwezeshwa kama wanavyopewa viti maalum wawekewe mfuko
maalum. Ni bora wananchi wenyewe wakasimamia matumizi ya ardhi. Jukumu
alilopewa Rais ni kubwa mno. Watendaji wake wanamchezea. Uhawilishaji – tulisema
kuhawilisha ardhi inaweza kuleta matatizo. Kila inapotokea matatizo ya ardhi wanavijiji
ndio wanaoumia na sehemu kubwa ya waTanzania wanaishi vijijini (80%).
Vipande vitakavyotolewa havina maana. Ardhi ya watu ikitakiwa inachukuliwa. Hakuna
mwananchi wa Tanzania anayekalia nje ya utaratibu wa sheria.
Tuna benki – ziada ya pesa ipo – wanaitoa wapi. Sehemu kubwa ni ya wananchi.
Wananunua dhamana za serikali (government bonds). Hiyo hiyo ya umma inanunua –
pesa inamlipa mlaji – ambazo ni zetu. Kuna viini macho vinafanyika.
6.4 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi – HAKIARDHI, Dkt. Ng’wanza Kamata
20
Akichangia mada alisema uundwaji wa sheria 1999 – sheria 2001 ilianza kutumika.
Mabenki yamesema sheria haijakaa vizuri kuwawezesha kukopesha. Mh. Mkapa
akasema nimeshinikizwa sana. Msukumo ulitoka wapi – haukutoka kwa wananchi.
7.0 SIKU YA TATU 29/05/2009
Kongamano lilianza kwa Washiriki wote kujiandikisha saa 3.00 asubuhi.
Hii ndio ilikuwa siku rasmi ya kufunga kongamano hili lililoishi kwa jumla ya siku tatu.
Katika siku hii mada mbali mbali pia zilijadiliwa kwa mapana na marefu lakini kubwa
zaidi kwa siku hii ilikuwa ni kupata uzoefu kwenye masuala ya ardhi uliotolewa na
wawakilishi wa asasi zinazoshughulika na masuala ya ardhi kutoka nchi za Kenya,
Uganda na Rwanda.
7.1 Uzoefu kutoka Kenya kwenye Masuala ya Ardhi - Mwasilishi: Odenda Lumumba
Katika kuwasilisha uzoefu huu, mwasilishi aligusia mambo mengi sana kuanzia kwenye
ngazi ya mwanakijiji, mwananchi wa kawaida, taasisi za kiraia na za kibinafsi na serikali
kuu na zile za mitaa kwenye suala zima la kuhakikisha kuwa watu wote wa nchi husika
wanafaidika na rasilimali hii muhimu ya ardhi. Mwasilishi pia aligusia udhaifu uliopo
kwenye mifumo ya kusimamia ardhi ndani ya nchi za Afrika ya Mashariki. Pia hakusita
kuzungumzia uimara wa mifumo hii pale tu itakapoweza kutumika vyema na kuwa
chachu ya kuwaletea maendeleo endelevu Wananchi na sio wageni wanaokuja ndani ya
nchi zetu kutengeneza Faida kubwa ya ziada wakati wananchi wakiwa hawana hata hiyo
akiba ya kuanzia.
Mwasilishi aliendelea kwa kusema yafuatayo:
Suala la ardhi kamwe haliwezi kubadilika ikiwa wale wasomi wachache
wanaotuongoza kwenye nchi zetu hawatobadilika. Viongozi wetu ndio
waliotufikisha hapa tulipo leo, ambapo Wananchi wengi hawana ardhi ya kutosha
kwaajili ya makazi na kilimo. Mfano mzuri ni nchini Kenya ambapo inaaminika
kuwa Wananchi wa tabaka la juu walioko kwenye serikali, mashirika ya umma na
wamiliki wa makampuni makubwa ndio wanaomiliki maeneo makubwa ya ardhi
wakati Wananchi wa kawaida wakiwa wamejikusanya kwenye maeneo
yaliyofurika watu na nyumba zisizo na mpangilio sahihi (squatters) wakiwa na
vijipande vya maeneo ya kukaa.
Taasisi kubwa za kigeni mfano Shirika la fedha duniani (IMF) pamoja na Benki ya dunia
(WB) ndio zimekuwa na sauti kubwa sana kwenye maamuzi ya nchi zetu za kiafrika.
Sauti hii imepelekea viongozi na wataalamu wetu kusubiri hadi sera na sheria zetu
ziidhinishwe na mashirika haya ndio zianze kutumika. Na kwa kiwango kikubwa
mashirika haya yamekuwa yanazilazimisha serikali zetu kufuata yale ambayo
yatawanufaisha wawekezaji kutoka nje ya nchi. Mfano mzuri ni sera ya ardhi ya nchi ya
Kenya ambayo imekaa sasa takribani miaka saba (7) pasipo kupitishwa kutokana na
shinikizo la mashirika haya. Pia kuna mifano kama ya nchini Zimbabwe ambapo baada
21
ya serikali kupitisha mfumo ambao hungewasaidia wazawa kumiliki ardhi kupitishwa,
nchi hiyo imewekewa vikwazo vya kiuchumi na nchi nyingi za Ulaya na Amerika.
Kuhusiana na suala la Shirikisho la Afrika ya Mashariki na suala zima la umiliki
wa ardhi kwa pamoja. Hapa jambo kubwa linalotakiwa kufanywa na serikali zetu
ni kuwajengea imani ya kutosha wanachi wa nchi zote kuwa hakuna yeyote
atakayepoteza haki yake kwenye ardhi aliyokuwa anamiliki. Pia serikali za nchi
zote inabidi kuwaeleza wananchi kuwa hakuna ardhi ya nchi moja itakayovamiwa
na wanchi wa nchi nyingine kwa kisingizio cha kuwa kuna ardhi nyingi na ya
kutosha. Mfano mzuri ni wasiwasi walionao Wananchi wa nchi ya Tanzania kuwa
kuifanya ardhi iwe ya pamoja kutapelekea wao kupoteza ardhi yao ambayo
wameitunza kwa miaka mingi sasa. Wananchi wa pande zote za Shirikisho la
Afrika Mashariki watakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi yatakayo
kuwa na manufaa kwa pande zote.
Nchi za Afrika ya Mashariki sio masikini kwa maana ya rasilimali, ni matajiri
sana lakini ufukara wetu upo ndani ya viongozi wetu tuliowachagua na kuwateua
kuongoza sekta muhimu mfano za ardhi, madini, wanyamapori, misitu, maji na
nyinginezo nyingi. Viongozi hawa wamekuwa wakiwajali sana wageni
wanaokuja kwa majina ya wawekezaji na kusahau kuwawezesha Wananchi
wazawa ili waendeleze uchumi wa nchi yao.
Wageni kutoka ng‟ambo wamekuwa wakipewa hakimiliki za ardhi na serikali
zetu wakati huo huo wenyeji wakibaguliwa waziwazi. Wenyeji hawaonekani
kama wana uwezo wa kuwekeza kama hawa wageni kutoka Ulaya, Amerika,
Uarabuni na Asia.
Sheria nyingi hasa kwenye maeneo ya ardhi, madini na wanyamapori
zinaonekana kama vile zimewekwa kwa lengo moja tu la kumnyanyasa mwenyeji
dhidi ya matajiri na wageni. Ukiangalia hata kwa nchi kama Tanzania
wanaolalamika kudhulumiwa ardhi zao na viongozi wakubwa ni wananchi na
wakulima wadogo wadogo walioko vijijini. Lakini wakati huo huo kuna sheria
namba tano (5)ya ardhi ya mwaka 1999, Sheria ya Ardhi ya Vijiji. Sasa inakuwa
ngumu kuelewa kwanini bado huyu mwanakijiji anaendelea kudhulumiwa haki
yake wakati kuna sheria zilizotungwa kumlinda.
Serikali za Afrika ya Mashariki zimekuwa na kisingizio kuhusiana na kinachoitwa
soko huria. Viongozi wetu wanasema kuwa kinachoharibu uchumi na umiliki
wetu wa ardhi ni soko huria. Lakini ukweli ni kuwa soko haliwezi kujiendesha
pasipo sisi wenyewe kutaka nini kifanyike. Soko siku zote huelekezwa na sio
lenyewe kutuelekeza sisi. Soko hili ndio lililopekea watu wachache kujilimbikizia
ardhi na rasilimali nyingine nyingi kutokana na wao kumiliki uchumi wa nchi.
Tatizo la ukabila pia bado ni kubwa sana kwenye nchi zetu za Afrika ya
Mashariki. Kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara kwenye baadhi ya
makabila yakigombania ardhi kwenye mipaka yao. Mfano mzuri ni nchini Kenya
22
ambapo mara kwa mara kumekuwa kunaibuka mapigano yanayohusianisha
makabila mbali mbali. Lakini hata nchini Tanzania kumekuwepo na mapigano
haya kwa miaka ya karibuni tofauti na kipindi cha utawala wa Rais wa kwanza
Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Mapigano haya yamekuwa yanapelekea
uharibifu wa mali ndani ya ardhi pamoja na Wananchi kuyakimbia maeneo yao.
Swali la kujiuliza hapa ni kwamba ikiwa nchi za Afrika Mashariki zinafanana
sana kwenye maeneo mengi ya mifumo ya kumilki ardhi, iweje leo shirikisho la
Afrika Mashariki lishindwe kuundwa kutokana na suala la ardhi?. Kuna mambo
mengi sana yanayofanana kuliko yale yanayotofautiana. Mfano kwenye kumilki
kimila ni Uganda pekee ambayo haina umiliki huu lakini nchi nyingine zote zina
mfumo huo. Suala la dola kumiliki rasilimali linafanana kwa nchi zote. Tofauti
kubwa ni kwenye milki ya hatima (radical titles) kwani kwa Tanzania mamlaka
hiyo iko chini ya Rais wakati kwa Kenya na Uganda ipo chini ya Wananchi.
7.1.1 Mwasilishi wa mada pia alifafanua mambo ya muhimu na ya kuzingatia kwa
nchi za Afrika ya Mashariki katika kulinda rasilimali za nchi zao husika. Mambo
haya ni kama yafuatayo:-
1. Taasisi zetu za kiraia ndizo zenye jukumu la kulinda rasilimali za nchi zetu.
Taasisi hizi zina jukumu la kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kuzilinda
rasilimali hizi kwa kuzishinikiza serikali zetu kuweka sera na sheria
madhubuti za kulinda rasilimali hizi. Pia kuna kila sababu ya taasisi hizi
kuwaonyesha Wananchi kuwa wanazo sababu za kuomba ushirikishwaji
kwenye maamuzi yanayohusiana na rasilimali zao mfano ardhi na madini.
2. Suala la mipaka linapelekea kukosekana kwa ujirani mwema baina ya nchi za
Afrika Mashariki. Kumekuwa na migogoro mingi baina ya nchi hizi na
mifano mizuri ni baina ya Uganda na Kenya ambapo kwa sasa kuna
kukosekana kwa amani kwenye mpaka baina ya nchi hizi kwenye eneo la
Migingo. Pia hapo kwenye miaka ya 1970 hali hii ilishatokea baina ya
Tanzania na Uganda; pia miaka ya karibuni kumekuwa na mgogoro kwenye
mpaka wa Rwanda na Uganda. Migogoro ya aina hii ni ya kushughulikia kwa
umakini wa hali ya juu ili isiathiri kuundwa kwa shirikisho la Afrika ya
Mashariki.
3. Kuwepo na mabadiliko ya dhati kwenye taasisi na idara za kiserikali kama
nchi za Afrika Mashariki zinataka mabadiliko ya dhati kwenye kuleta ulinzi
wa rasilimali za nchi hususani ardhi na madini. Ni kweli kabisa kuwa idara za
serikali zinachangia sana kwenye kubinafsisha rasilimali za nchi kwa wageni
ambao wanakuja kwa majina ya wawekezaji. Ndio maana kuna kila sababu ya
kufanya mabadiliko ya kitaasisi pamoja na ya watendaji ndani ya taasisi hizi.
23
7.2 HITIMISHO
Ardhi ndio suala lililo mbele ya uundwaji wa shirikisho la Afrika Mashariki. Ni suala la
kuzungumza na kufikia muafaka ili liondoe ugomvi na vita hapo baadae baina ya nchi
husika.
Ni suala la wazi na la msingi sana kwa kila mtu, taasisi, serikali na kila kikundi pasipo
kujali itikadi za kisiasa, kidini au kikabila. Wananchi wajipange kwa sababu eneo la
Afrika Mashariki linahitaji ukombozi. Hili vuguvugu la ukombozi inabidi lianzie
Tanzania na kwenda nchi nyingine. Tuangalie isije kuwa muongo huu mmoja sio kwaajili
ya Faida ya watu wote ila Faida kwa watu wachache wenye elimu na ujanja wa kutumika
mamlaka za serikali watakavyo wao.
7.3 Maswali kwa upande wa Kenya
1. Tueleze uzoefu wa MKURABITA kwa nchi ya Kenya?
2. Ni jambo zuri kuwa na ardhi ya pamoja Afrika Mashariki lakini wananchi wa
Tanzania tunasita kwasababu tupo wengi na nchi hizo nyingine hazina ardhi ya
kutosha kwa sehemu kubwa kutokana na mifumo yao ambayo ina utofauti Fulani
na Tanzania. Halafu pia kuna tatizo la uwekezaji kwenye ardhi ya Tanzania
jambo linalotupa wasiwasi wa kuendelea kupoteza ardhi yetu?
3. Wakati Tanzania tuna ardhi ya jumla kwenye maeneo ya mijini na vijijini. Lakini
kwa Uganda, Kenya na Rwanda hawana ardhi ya aina hii. Je, huoni kuwa
litakuwa tatizo kwa upande wa Tanzania?
4. Pia kiuchumi Tanzania iko nyuma ukilinganisha na Kenya. Je, huoni suala la
kuacha ardhi iwe wazi itapelekea kudidimiza zaidi uchumi wetu?
7.4 Majibu
Mwasilishi alijibu maswali haya kwa kifupi na kwa ujumla kama ifuatavyo.
Tuache suala la kuwatenga Wakenya kwenye ardhi. Kwa sababu lazima tujue
kuwa ni nani hasa tunayemtenga. Mbona tayari familia za matajiri tayari zina
maeneo makubwa ya ardhi hapa nchini Tanzania maeneo ya mkoa wa Arusha.
Kwahiyo kukataa kwenu Watanzania kuwa na ardhi ya shirikisho ni kuwazuia
wanyonge wengi kutoka Kenya na sio wale matajiri wakubwa ambao tayari wana
maeneo makubwa tayari nchini Tanzania.
24
8.0 Uzoefu wa Uganda kwenye masuala ya ardhi - Mwasilishi: Esther Obaikol
Mwasilishi ni Mkurugenzi wa Taasisi ya masuala ya ardhi ya nchini Uganda yaani,
Uganda Land Alliance (ULA). Mwasilishi katika uwasilishi wake alizungumzia masuala
mengi yanayohusiana na ardhi nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. Baadhi
ya mambo muhimu aliyoyagusia ni pamoja na yale mambo yanayoendelea
kushughulikiwa kwenye sera na sheria za ardhi nchini Uganda. Baadhi ya mambo ya
muhimu sana yaliyopo kwenye mchakato huo ni pamoja na:-
Kuandikisha maeneo ambayo yameachwa na wakoloni lakini bado hayamilikiwi
na wananchi wa kawaida. Hii itasaidia kila mtu kumiliki ardhi.
Kuangalia makundi madogo na wafugaji ili wapate ardhi ya kutosha. Kwa sasa
makundi haya yanapata tabu kwenye kupata ardhi ya matumizi.
Utatuzi wa migogoro kwenye jamii zinazohama hama kutoka eneo moja kwenda
eneo jingine. Mfano jamii za Kimaasai na Karamajong”.
Kuimarisha mila kwenye utatuzi wa mogogoro ya ardhi kwa kuimarisha vyombo
vya kimila kwenye maeneo husika. Hili ni suala muhimu sana kwani litasaidia
kwenye kumaliza migogoro mingi inayoibuka katika maeneo ya vijijini.
Utambuzi wa haki za wanawake kama wazalishaji wakubwa kwenye ardhi na
kuanzia ngazi ya familia, ukoo na taifa kwa ujumla. Kutambua umilki wa ardhi
kwa wanawake kutapelekea wao kuwa na nguvu kubwa kwenye ardhi na kuipatia
jamii maendeleo makubwa.
Kuingiza suala la jinsia kwenye utawala na usimamizi wa ardhi kwa njia ya
kimila. Hii itasaidia kuepuka unyanyaswaji na uonevu wa kundi moja dhidi ya
kundi jingine. Na inaaminika kuwa kuwepo kwa usawa baina ya makundi ya
kijinsia kutapelekea uzalishaji kuongezeka kwa hali ya kuridhisha zaidi.
8.1 Changamoto kwa taasisi binafsi
Mwasilishi kwa kuuchukua uzoefu wake wa nchini Uganda pia alielezea kwa undani
changamoto nyingi zinazozikabili taasisi za kibinafsi kwenye maeneo yao ya kazi.
Changamoto hizo ni kama zifuatavyo
Kuna siasa nyingi sana kwenye masuala ya ardhi nchini Uganda jambo
linalopelekea kukosekana kwa muafaka kwenye usuluhishi wa kesi za ardhi. Hii
imechangiwa sana na Viongozi wa serikali kuingilia masuala yanayohusiana na
ardhi kwa masilahi yao binafsi na familia zao.
25
Kukosekana kwa sera na sheria za mazingira kitu kinachopelekea kuwepo na
ugumu katika kuwabana wale wanaoharibu mazingira ambao wengi wao ni
wamiliki wa makampuni makubwa na viwanda vikubwa.
Wananchi wengi wana uelewa mdogo wa masuala ya muhimu ya kijamii
yanayowaathiri wao na maisha yao hali inayopelekea kudhulumiwa haki zao
za kimsingi. Uelewa huu mdogo unasababishwa na juhudi ndogo za serikali
katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na sera na sheria mbalimbali.
Kukosekana kwa habari za kutosha na za uhakika kuhusiana na masuala ya
ardhi kwa wananchi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.
Mfumo mfu wa haki za ardhi nchini Uganda kutokana na waongozaji wabovu
kutoka serikalini.
Mwamko mdogo kwenye masuala ya ardhi kwa wananchi wa Uganda.
8.2 HITIMISHO
Kimsingi changamoto na matatizo kwenye masuala ya ardhi ni mengi sana kwenye nchi
za eneo la Afrika Mashariki na hayatofautiani kwa kiasi kikubwa sana kutoka nchi moja
hadi nyingine. Kwahiyo kuna kila sababu ya wananchi wa pande zote mbili kukaa na
kuyaangalia kwa makini masuala haya na kuweka mustakabali wa kudumu kwenye
kulinda ardhi na rasilimali nyingine kwenye ukanda huu.
9.0 Uzoefu wa Rwanda kwenye masuala ya ardhi - Mwasilishi: John Muyenzi
Mwasilishi alizungumzia mambo mengi sana yanayohusiana na ardhi ya nchi ya Rwanda
na mgawanyo wake kwa wananchi wa nchi yake. Pamoja na hayo alizungumzia pia
matatizo yanayoikumba sekta ya ardhi nchini Rwanda akihusianisha na eneo zima la
Afrika Mashariki. Rwanda ina jumla ya 26, 338 skwea (square) kilomita na ina jumla ya
watu 10, 473,282
9.1 Uzoefu katika kutengeneza na kutekeleza sera na sheria za ardhi
Mwaka 1999 kulikuwepo na kongamano la kimataifa lililoenda kwa jina la Land and
Villagelization, taasisi ya RISID ndio walioandaa kongamano hilo. Ni kutoka katika
mapendekezo ya kongamano hili ndipo serikali ilipoyachukua na kuyaingiza kwenye sera
ya sheria ya ardhi. Katika mapendekezo haya mambo ya kimsingi yaliyochukuliwa na
kuingizwa kwenye sera hii ni kama vile:-
Wanawake walipata uwezo wa kupata na kumiliki ardhi sawa na wanaume
kwenye familia zao au/na pale anapofariki mume.
26
Watoto wote wakawa na uwezo sawa wa kupata na kumiliki ardhi toka kwa
wazazi wao kwa njia ya kurithi au kupewa kama zawadi au sehemu ya mali
stahiki kama sehemu ya familia.
Mwaka 2004 ndio sera ya ardhi ilipotungwa na kupitishwa na mwaka 2005 sheria ya
ardhi ilipitishwa. Sheria iliyoitwa Organic Land Law ambayo pamoja na mambo mengine
inalinda ardhi zote za kimila na hati. Hakuna unyanyasaji wa kijinsia katika kumiliki
ardhi. Mume na mke wana haki sawa katika kumiliki ardhi. Mtoto wa kike na kiume
wana haki sawa ya kupata na kumiliki ardhi.
Kazi za sasa zinazofanywa na serikali ya Rwanda kwenye sekta ya ardhi
Mgawanyo wa ardhi kwenye eneo la Jimbo la Mashariki ya Rwanda, kwenye
mikoa ya Nyagatare, Gatsibo, Kirehe, na Kayonza.
Mpango bora wa matumizi ya ardhi kwenye maeneo ambayo hayajafanyiwa
mpango huu ili kuilinda ardhi kukaa bure pasipo na matumizi yanayoeleweka.
9.2 Changamoto zinaoikumba sekta ya ardhi nchini Rwanda
Watu wengi wanategemea ardhi kidogo kwaajili ya makazi na kilimo. Hii ni
kutokana na kuwa ardhi ya Rwanda ni kidogo ukilinganisha na idadi ya watu
waliopo Rwanda.
Ndoa za mitala bado ni eneo linaloleta utata katika umiliki wa ardhi nchini
Rwanda pamoja na kwamba kuna sera na sheria ya ardhi. Wanaume wa Rwanda
wamekuwa wakiongoza kwa kuoa wanawake wengi wakati ardhi waliyonayo ni
kidogo jambo linalosababisha matatizo makubwa linapokuja suala la urithi.
9.3 Maswali
1. Rwanda ina mpango gani kwenye kasi ya ongezeko la ongezeko la watu
ukitegemea kuwa eneo la ardhi waliyonayo ni dogo sana ukilinganisha na idadi ya
watu?
2. Kuna mpango wowote wa serikali ya Rwanda kutambua watu wanaomiliki ardhi
kwa majina tofauti tofauti?
9.4 Mwasilishi wa mada alijibu Maswali haya kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Kimsingi siwezi kusema kuwa Rwanda tuna sera ya uzazi wa mpango. Ila serikali
iliyopo madarakani kwa sasa inasema kuwa nchi ya Rwanda haina rasilimali
kama vile madini n.k kwahiyo watu wake ndio rasilimali yake muhimu zaidi
katika kujiletea maendeleo.
Pia ni kweli kabisa kuwa asilimia tisini (90%) ya Wanyarwanda wote
wanategemea kilimo. Kwahiyo serikali inajaribu kuwaambia watu wajiondoe
kwenye kilimo na kutegemea sekta nyingine ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi
nzuri kwa njia ya utegemezi wa kisekta kama vile viwanda n.k.
27
Lakini pia mfumo wa Rwanda hauruhusu wageni kupewa ardhi kwa kiwango
kikubwa kwa sababu moja kubwa ambayo ni uhaba wa ardhi hiyo ambayo hata
wananchi wake wenyewe haiwatoshelezi kwa kiwango kinachotakiwa.
10.0 Mjadala wa mchana
Baada ya chakula cha mchana na kabla ya kufunga kongamano Washiriki walikaa kwa
Majadiliano ya jumla. Lengo la Majadiliano hayo likiwa ni kupata uelewa wa jumla wa
nini Washiriki walichojifunza kwa muda wa siku zote tatu. Washiriki katika mjadala huu
waliangalia katika mada zote zilizowasilishwa kwenye kongamano. Katika mjadala huu
masuala yafuatayo yalijadiliwa:-
1. Suala la ardhi ni suala ambalo linahitaji kuzungumzwa kwa umakini mkubwa
sana hasa suala la kuwepo na ardhi ya Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Watanzania ni lazima kwanza wajitosheleze wenyewe na kuridhika kuwa wana
ardhi ya kutosha ndipo wenzetu wa nchi za jirani waanze kufikiriwa ni maeneo
gani watapata.
2. Inawezekanaje Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kukopesha pesa
wafanyakazi wa umma? Je wao ni benki ya mikopo?. Serikali lazima ingalie
uwezekano wa kila raia wa Tanzania kujipatia mkopo huu wa kuwawezesha
kujijengea makazi yao ya kudumu pasipo kuwepo na ubaguzi wa raia huyu
anafanya kazi katika sekta ya umma au ya binafsi.
3. Kwa jinsi upimaji huu wa viwanja unavyofanywa hasa kwenye maeneo ya jiji la
Dar es Salaam, inaonekana wazi kabisa kuwa unafanywa kwa manufaa ya watu
wachache ambao wana pesa zao kuliko kufanywa kwa manufaa ya wananchi wote
wa Tanzania bila kujali uwezo wao wa kipesa au kivyeo.
4. Zilipotungwa sera na sheria za ardhi za mwaka 1995 na 1999 kwa mfuatano huo
wananchi wengi wa Tanzania walijua sasa wamepona na uonevu waliokuwa
wakifanyiwa na watu waliokuwa na uwezo wa kipesa na kielimu. Lakini leo
tunaadhimisha miaka kumi ya sheria za ardhi namba nne (4) na namba tano (5) za
1999 bado wananchi wanaendelea kuteseka kwa kiwango kikubwa zaidi. Kwanza
kwa mtazamo wa kina zaidi utagundua kuwa matatizo kwenye sekta ya ardhi ndio
yameongezeka zaidi hasa baada ya kuanza kuingia hawa wanaoitwa wawekezaji
kwenye ardhi ya kijiji na kukingiwa kifua na serikali kuu na serikali za mitaa
wakati wananchi wa kawaida wakibaki bila ya kuwa na usaidizi wa aina yoyote
ile.
28
11.0 MAAZIMIO YA KONGAMANO
Siku ya mwisho ya kongamano wawasilishi pamoja na Washiriki walikaa kwa pamoja na
kujadiliana kwa kina yale yote waliyoweza kukaa na kuyapata ndani ya siku zote tatu za
kongamano hili la maadhimisho ya miaka kumi (10) ya sheria za ardhi za mwaka 1999
nchini Tanzania. Maazimio haya yalifikiwa kwa lengo moja tu nalo ni kuyatekeleza yale
yote ambayo wataazimia hapo na kuwa ndani ya waandaaji, yaani taasisi za
(HAKIARDHI na PINGOS FORUM), serikali ya Tanzania pamoja na Washiriki wote
kila mmoja kwa nafasi yake. Maazimio hayo yaliyofikiwa ilikuwa kama ifuatavyo:-
11.1 Ushiriki wa wananchi na wanavijiji katika maamuzi yanayohusiana na ardhi hususani kwenye ngazi ya vijiji. Nini kifanyike?
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
Tupange ni kwa jinsi gani wanavijiji wanaweza kufahamu masuala muhimu na ya
Kimsingi yanayohusiana na ardhi kwenye vijiji vyao kwa mujibu wa sheria
zilizopo.
Suala sio kutoeleweka kwa mfumo wa sheria za ardhi. Ila tatizo kubwa ni
kwamba mifumo hii ilianzia juu kwenda chini ndio maana wananchi wengi
hawayaelewi kwa undani masuala haya yanayohusiana na sera na sheria za ardhi.
Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na maamuzi halali ya wananchi
kunakofanywa na baadhi ya Viongozi wasio waadilifu na walio mafisadi wa
rasilimali za nchi yetu ya Tanzania hasa hasa kwenye sekta ya kilimo.
Kumekuwa hakuna utatuzi wa dhati wa migogoro ya ardhi nchini hasa kwenye
maeneo ya vijijini toka mwaka 1995. Hali hii imetokana na kutoshirikishwa kwa
wananchi kwa kiwango kinachoridhisha kutoka ngazi ya wilaya hadi ya kijiji.
Viongozi wamekuwa wakifanya maamuzi ya kibabe pasipo kujali masilahi ya
wananchi walio wengi.
Wanavijiji wapelekewe mafunzo ya katiba na sheria mbalimbali ili kufahamu haki
zao za Kimsingi. Mafunzo haya yaanze kutolewa kuanzia ngazi ya shule ya
msingi na kuendelea.
Ikumbukwe pia kuwa taasisi za kiraia na taasisi za kidini zina jukumu kubwa sana
la kutoa elimu ya kiraia kwa wananchi hasa wa mikoani na vijijini ambao
inaonekana kama wamesahauliwa na serikali. Ingawa serikali inatakiwa ijue kuwa
ni jukumu lake kutoa elimu kwa wananchi wake.
Wanawake hasa wa vijijini wanatakiwa kuelimishwa kuhusiana na haki zao za
Kimsingi ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye mfumo mzima wa kutoa
maamuzi yanayowagusa kuanzia ngazi ya familia hadi ya kijiji ili waweze
kufaidika na sheria mbalimbali Mfano wa sheria za ardhi za mwaka 1999, namba
29
4 na 5. Hii imetokana na sheria kutoa fursa kwa wanawake lakini bado hawana
ushiriki mkubwa na unaotakikana.
Wanakijiji inabidi waelimishwe umuhimu wa kutafuta taarifa sahihi kabla ya
kufanya maamuzi yoyote mazito yanayohusiana na rasilimali zilizoko kwenye
maeneo yao kama vile ardhi.
Serikali iache kuingilia maamuzi ya wananchi, Mfano mzuri ni maamuzi
yanayofikiwa kwenye vikao halali ya mikutano mikuu ya vijiji ambayo
inaingiliwa na Halmashauri za Wilaya. Viongozi wa Halmashauri za Wilaya
wamekuwa wakipuuzia maamuzi ya wanavijiji na kufanya kinyume na
walichoamua hasa hasa kwenye sekta ya ardhi.
11.2 Uwekezaji katika ardhi ya vijiji unaendana sana na mambo haya mawili:-
(i) Ukiukwaji wa taratibu husika.
(ii) Kukosekana kwa uwezo wa kujadiliana baina ya wanavijiji na wawekezaji.
Nini kifanyike?
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
Serikali iache kukumbatia wawekezaji kwa kusikiliza taarifa zao pekee pasipo na
kuziona za muhimu pasipo kuwasikiliza wananchi wa kawaida wanaojua mambo
mabaya ya kinyanyasaji wanayofanyiwa na wawekezaji hawa kwenye maeneo yao
wanayoishi.
Bunge lihusishwe kwenye mchakato mzima wa uwekezaji na wawekezaji kwa
sababu ndio wawakilishi wakubwa wa wananchi. Na wabunge wengi wanajua
matatizo ya wananchi kuliko wanavyojua mawaziri na watendaji wengine wa
serikali ambao ndio wanaosaini mikataba na wawekezaji hawa ambayo mwisho wa
siku yanakuwa na madhara kwa wananchi wa maeneo husika. Mfano mzuri ni huko
mkoani Shinyanga, wilaya ya Kahama ambako kuna uharibifu mkubwa wa
mazingira kwenye maeneo ya machimbo ya madini.
Lengo la sheria za ardhi za mwaka 1999 kwanza litimizwe ambalo ni kuwasaidia
wanavijiji wa Tanzania halafu ndio wawekezaji waletwe kwenye maeneo
yanayobaki baada ya wanakijiji kujitosheleza kwa kiwango cha kutosha.
Serikali iache wanavijiji wenyewe ndio waingie mikataba na wawekezaji hawa. Hii
itasaidia kuondoa kiburi cha hawa wawekezaji ambao baada ya kuchukua ardhi
huanza kufanya yale wanayojisikia ikiwa ni pamoja na kuwanyanyasa wananchi
pasipo na sababu za Kimsingi.
Wawekezaji wapewe maelekezo ya Kimsingi kuwa ili kupata ardhi ya kijiji ni
lazima wapiti kwenye mikutano mikuu ya vijiji na waache tabia ya kuwahonga
baadhi ya wananchi kama walivyofanya wazungu enzi za ukoloni. Hii imetokea
30
maeneo ya wilaya za Rufji na Kisarawe mkoani Pwani ambako wawekezaji
waliwahonga
11.3 Kwanini migororo kwenye sekta ya ardhi ipo kwa kiwango cha juu wakati sheria za utatuzi zipo?
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
Elimu ni tatizo kubwa sana, Mfano kwenye mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata
hayana elimu ya kutosha kuhusiana na nini wanachotakiwa wafanye. Kwa hiyo
kinachotakiwa Kimsingi ni kuongeza elimu kwa wahusika ili kupunguza
migogoro hii.
Migogoro ni sehemu ya maisha kinachotakiwa ni serikali na taasisi za kibinafsi ni
kutoa elimu ili vyombo vinavyohusika ili kuviwezesha kutoa maamuzi sahihi. Hii
itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kiwango kikubwa hasa kwenye
maeneo ya vijijini.
Tatizo ni utekelezaji mbovu wa sheria hizi kwa baadhi ya watendaji wa serikali
kuanzia ngazi ya kijiji hadi ya taifa. Maafisa ardhi wa wilaya wamekuwa chanzo
kikubwa cha kusababisha migogoro iongezeke kwa kutoa maamuzi ambayo
yanawakanganya wananchi. Kuwepo na ushirikiano wa dhati baina ya
watekelezaji wa sheria na wananchi wa maeneo husika.
Mpango bora wa matumizi ya ardhi ndio mtatuzi mkubwa wa migogoro ya ardhi.
Hii ni kwasababu utapelekea migogoro baina ya makundi mbalimbali kupungua,
Mfano baina ya wakulima na wafugaji, vijiji na vijiji na baina ya taasisi za
serikali na wanavijiji.
Wawekezaji ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya vijijini. Hali
hii imetokana na wao kuingia kwa kutofuata taratibu zinazotakiwa kisheria jambo
linalopelekea kuibuka migogoro baina yao na wanavijiji. Kinachotakiwa ni kwa
wawekezaji hawa kufuata sheria zilizowekwa pamoja na kuheshimu taratibu za
maisha za eneo wanalofanya uwekezaji.
Muingiliano wa sheria moja kwa nyingine pia ni chanzo cha kuongezeka kwa
migogoro ya ardhi kwenye maeneo mengi ya nchi. Mfano pale ambapo sheria ya
ardhi inaziba mianya sheria nyingine kama za Wanyamapori na Madini zinatoa
mianya kwa maeneo hayo kuvamiwa na kuchukuliwa na wageni. Cha kufanya ni
kuhakikisha kuwa kunakuwepo na muhoanisho baina ya sheria mbalimbali ili
kukwepa mikanganyo isiyo ya lazima.
31
11.4 Nini kifanyike ili wanawake wafaidike na sheria za ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999?
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
Kuwepo na mfuko maalum wa kuwasaidia wanawake wanyonge kupata ardhi ya
makazi na kilimo ili kuwepo na usawa kwenye uchumi baina ya wanaume na
wanawake.
Wanawake wapewe elimu maalum ili kuwawezesha kuzijua haki zao za Kimsingi
kwenye ardhi na kwenye familia zao hasa pale inapotokea wanataka
kudhulumiwa haki zao na waume zao au ndugu za waume zao kwenye mirathi.
Taasisi za kiraia kama vile Mtandao wa Kijinsia Nchini Tanzania (TGNP) watoe
elimu za haki za wanawake kwenye maeneo ya vijijini na kuacha kukaa na
kufanya maeneo ya mjini. Hii ni kutokana na kuwepo matatizo mengi ya
unyanyasaji wa wanawake maeneo ya vijijini yanayopelekea wao kupoteza haki
zao.
11.5 Fidia za ardhi na kupatiwa eneo mbadala. Je, linakidhi mahitaji ya wafidiwa? Nini kifanyike?
Kimsingi fidia hii haitoshi pekee kwa sababu mara nyingi inakuwa hailingani na
eneo halilotoka huyu mfidiwa. Wananchi wamekuwa wakipewa maeneo madogo
kulinganisha na kule waliko ondolewa.
Wananchi wanaofidiwa maeneo huwa wanalalamika kupelekwa mbali na huduma
za kijamii. Maeneo wanayopewa mara nyingi yanakuwa na uhaba wa huduma za
kijamii kama vile maji, shule, hospitali na dispensary, umeme pamoja na barabara
nzuri. Hali hii inapelekea wananchi kupoteza nguvu kubwa kwenye kutafuta
huduma hizi.
Wananchi wapewe somo la fidia ili waweze kuelewa aina ya fidia wanazotakiwa
kupatiwa kutokana na kuhamishwa kwenye eneo Fulani na serikali kupisha ujenzi
au maendelezo yoyote yale yenye Faida kwenye uchumi wa taifa.
Mara nyingi wafidiwa wamekuwa hawapewi fedha za kujengea
wanapohamishiwa maeneo mapya. Kutokupewa fedha za ujenzi kumepelekea
wengi wao kushindwa kujenga tena maishani mwao na kuziacha familia zao
zikiwa hazina nyumba za kujisetiri.
11.6 Huduma za ardhi ( Upimaji, Utoaji wa hati) haziendani na hali halisi. Nini kifanyike?
32
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
Maafisa ardhi wa Halmashauri za Wilaya wawe wanatoa elimu kwa wanavijiji
kabla ya kuanza kufanya kazi za upimaji na utoaji wa hati za umilki wa ardhi ili
kuepukana uibukaji wa migogoro ya mara kwa mara.
Sheria zifuatwe ili wananchi wote bila kujali cheo chake ili kuwepo na huduma
sawa za upimaji na utoaji wa hatimiliki za ardhi.
Serikali ishirikiane na taasisi za kiraia katika kutoa elimu ya matumizi bora ya
ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi baina ya vijiji ili kuruhusu upimaji wa ardhi
ya vijiji na kuweza kutoa hatimiliki za ardhi kwa mujibu wa sheria.
Maafisa upimaji wa ardhi wa mijini na vijijini waache kuomba rushwa kutoka
kwa wananchi wanaohitaji kupimiwa maeneo yao ili kupata hatimiliki za ardhi.
11.7 Ukomo wa kiasi cha ardhi anachoweza kupata mtu mmoja na kumilki kihalali.
Sheria ya ardhi namba 4 na 5 za 1999 zinaweka wazi kwenye vifungu vyake kiasi
ambacho mtu mmoja anaweza kupata na kumiliki kwa wakati mmoja. Kwa
Mfano kifungu cha 76 kinaweka kiwango cha mtu mmoja mmoja kumiliki ardhi.
11.8 Kilimo cha mashamba makubwa na uhakika wa chakula kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
Serikali kama iko makini na kupunguza njaa miongoni mwa wananchi wake basi
iache kuwaruhusu wawekezaji kuingia kwenye maeneo ambayo yapo tayari kwa
kilimo cha mazao ya chakula. Mfano mzuri ni kule wilaya ya Mbarali ambako
mashamba ya Kapunga yaliyokuwa maarufu kwa kilimo cha mpunga yamepewa
kwa wawekezaji wanaolima mazao ya nishati mbadala (jatropha).
Serikali pia isiruhusu mashamba makubwa yauzwe kwa matajiri wakubwa
ambayo huyageuza matumizi kwa kujenga hoteli kubwa na kufanya wananchi
waliokuwa wanategemea chakula kutoka kwenye mashamba hayo kubaki na njaa
isiyokuwa na kikomo.
11.9 Mfumo wa umiliki wa Wafugaji- utambuzi
Washiriki walichangia kama ifuatavyo:-
33
Serikali itenge maeneo ya Wafugaji na yaachwe kuingiliwa na wakulima na
watumiaji wengine. Pia maeneo haya yaheshimiwe na jamii nzima pasipo
kusumbuliwa na mamlaka nyingine yoyote ile. Kufanya hivi kutasababisha
kupungua kwa migogoro na mapigano baina ya wakulima na Wafugaji.
Nyanda za malisho kitaifa zianzishwe kwenye maeneo yenye rutuba nzuri kwa
ufugaji. Kuanzishwa kwa nyanda hizi kutapekea hata Wafugaji kujifunza mbinu
bora za ufugaji wa mifugo pasipo kuingilia mashamba ya wakulima na pasipo
kuharibu vyanzo vya maji na mazingira.
12.0 KUFUNGA KONGAMANO
Kongamano lilifungwa jioni ya tarehe 29/05/09 na mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi ya taasisi ya HAKIARDHI Dk. Ngw‟anza Kamata. Ambaye pamoja na
mambo mengine aliwaomba Washiriki wote kutoka ndani ya jiji la Dar es Salaam na
wale wa mikoani pamoja Washiriki wote kutoka kwenye taasisi nyingine za kiraia
hata wale wa serikali kuu na serikali za mitaa kutumia yale yote yaliyojadiliwa kwa
siku zote tatu katika kuhakikisha kuwa kila mtu anapata haki yake kwenye sekta nyeti
ya ardhi.
Mwenyekiti aliwakumbusha Washiriki kuwa ardhi ni rasilimali muhimu sana kwenye
maisha ya kila siku ya Watanzania wote hasa wale wenye kipato cha chini. Lakini
wananchi hawa wamekuwa wakidhulumiwa ardhi yao na watu wachache walioko
ndani ya dola na nje ya dola lakini kwa kushirikiana na baadhi ya watu wa kwenye
dola.
Na katika soko hili la ardhi hasa ya vijiji hakuna fursa inayotolewa kwa wanunuzi na
wauzaji kukaa na kujadili bei ya ardhi hiyo inayouzwa pasipo wao kushirikishwa.
Tiba ya matatizo haya ya ardhi ni kwa tabaka hili la chini kufahamu haki zake na
kuzidai pasipo uoga wa aina yoyote ile. Cha msingi hapa ni kwa tabaka onewa
kuanzisha vuguvugu. Vuguvugu la kulinda maslahi ya wengi litasaidia pale mtu
mmoja wa Rufiji atakapoguswa basi watu wa Kilombero, Ngorongoro, Hanang na
kwingineko wajue wameguswa wote kwa kuwa wapo kwenye tabaka moja.