51
ISBN 9976 906 92 7 ISBN 978-3-928936-99-6

SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

  • Upload
    others

  • View
    107

  • Download
    9

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

ISBN 9976 906 92 7 ISBN 978-3-928936-99-6

Page 2: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Monte Wilson

Sheria Muhimu Zaidi katika Kuishi

Page 3: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

RVB International

1 Thomas Schirrmacher: GOD Wants You to Learn Labor and Love

2 Thomas Schirrmacher: Legends About the Galileo-Affair

3 Thomas Schirrmacher: World Mission – Heart of Christianity

4 Thomas Schirrmacher: Law or Spirit – an alternative View of Galatians

5 Thomas Schirrmacher: Human Rights Threatened in Europe

6 Thomas Schirrmacher: Be keen to get going – William Carey’s Theology

7 Thomas Schirrmacher: Love is the Fulfillment of the Law

8 Thomas Schirrmacher: Studies in Church Leadership

9 Monte Wilson: The Most Important Rule for Living

10 Monte Wilson: Principles of Success in Business

11 Th. Schirrmacher (Ed.): A Life of Transformation – From Politician to Good Samaritan – A Festschrift for Colonel Doner

12 Thomas Schirrmacher DIOS Quiere Que tu Aprendas, Trabajes y Ames

13 Christine Schirrmacher La Vision Islamica de Importantes Enseñanzas Cristianas

14 Thomas Schirrmacher Sheria au Roho

15 Thomas Schirrmacher Upendo ni Utimilifu wa Sheria

16 Thomas Schirrmacher Mateso ya Wakristo Yanatuhusu Sisi Sote

17 Monte Wilson Sheria Muhimu Zaidi katika Kuishi

Page 4: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Monte Wilson

Sheria Muhimu Zaidi katika Kuishi Masomo juu ya Amri Kumi

Kimetafsiriwa na Emmanuel E. Buganga

RVB International

Page 5: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Die Deutsche Bibliothek – CIP

Bibliografische Information Der Deutschen Bibliothek Die Deutsche Bibliothek verzeichnet diese Publikation in der Deutschen Nationalbibliografie; detaillierte bibliografische Daten sind im Internet über http://dnb.ddb.de abrufbar. Bibliographic information published by Die Deutsche Bibliothek Die Deutsche Bibliothek lists this publication in the Deutsche Nationalbibliografie; detailed bibliographic data are available in the Internet at http://dnb.ddb.de

ISBN 978-3-928936-99-6 © Copyright 2001, 2007 by

Reformatorischer Verlag Beese www.rvbeese.de / [email protected]

Printed in Germany

ISBN 9976 906 92 7 © Kwa Toleo la Kiswahili, 2007

2nd edition 2009 Trans-Africa Swahili Christian Ministries

P.O. Box 772, Mwanza, Tanzania Toleo la Kwanza, 2007 Nakala 5,000

Kimetolewa na Inland Publishers, S.L.P. 125, Mwanza, Tanzania E-mail: [email protected]

Maandiko Matakatifu:

The Holy Bible in Kiswahili Union Version, 1994

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupiga chapa, kurudufu au kutoa kitabu hiki kwa njia yoyote ile bila idhini ya

Trans-Africa Swahili Christian Ministries, Idara ya Maandiko. __________________________________________________________

Kimepigwa Chapa na: Inland Press, P.O. Box 125, Mwanza, Tanzania (East Africa) TEL. +255 28 2560175 [email protected]

Page 6: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Gebende Hände (Mikono Itoayo) nchiniUjerumani ni shirika lisilo la kibiasharalikisaidia maskini na wahitaji katika nchi30 duniani kote. Nia yetu ni kuwasaidia

watu wajisaidie wenyewe.

Jamii ya Kikristo hushiriki jukumu kubwahapa, hivyo kitabu hiki kimekusudiwa katika kuwachochea Wakristokujisaidia wao wenyewe na kusaidia mataifa yao. Mungu akutaka WEWEujifunze, utumike na upende!

Mch. Horst-Jürgen Kreie, Meneja

Dk. Thomas Schirrmacher, Rais

Ikiwa unataka kuagiza nakala zaidi kwa usambazaji miongoni mwaviongozi wa Kikristo au ikiwa unahitaji maandiko zaidi au ushauri, tafadhaliwasiliana nasi kwa anuani ifuatayo:

Gebende Hände

www.gebende-haende.dewww.giving-hands.de

Kitabu hiki kimetolewa kwako na:

(Muhuri wa taasisi-sambazaji)

Page 7: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

YALIYOMOSura ya Kwanza

Sheria Muhimu Zaidi katika Kuishi…………………………………………9

Sura ya Pili

Usijifanyie Miungu………………………………………………................13

Sura ya Tatu

Mungu si Kiambishi-Awali………………………………………...............17

Sura ya Nne

Kusherehekea Imani Yako…………………………………………………21

Sura ya Tano

Kuheshimu Wazazi………………………………………………………….25

Sura ya Sita

Kuheshimu Uhai……………………………………………....…………….29

Sura ya Saba

Masharti kwa Tendo Kuu la Ndoa…………………………………………33

Sura ya Nane

Kujipatia Mali………………………………………………………………...37

Sura ya Tisa

Sema Ukweli……………………………………...…………………………41

Sura ya Kumi

Tosheka……………………………………………………………………...45

Maelezo ya Maneno…………………………………………………...……48

Anuani…………………………………………………………………….…..50

6

Page 8: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

DIBAJI

Dk. Monte Wilson ni Mchungaji mwenye mafanikio, mzoefu katikaulimwengu wa biashara, mwanzisha-miradi ya mashirika ya kibiashara yaKikristo katika Ulimwengu wa Tatu, na mshirika katika asasi za maendeleo zinazoongoza duniani pote. Akiwa ni Rais wa Taasisi ya WaamerikaWeusi Kujisaidia Wenyewe (African American Self-Help Foundation),anawapenda watu wote duniani, weusi kwa weupe, maskini kwa matajiri,wale wanaomfunza na watu wanaotafuta ushauri wake.

Ukiachilia hayo, yeye ni rafiki yangu mwema! Hii ndiyo sababu nawezakukueleza kutoka moyoni: Uko katika mikono mizuri unapofuata ushauriwake ndani ya kitabu hiki!

Ingawa sote tunashiriki kutoa Huduma ya Kwanza katika Ulimwengu waTatu, tukiwalisha wenye njaa na kuwasaidia walioachwa wahanga wa vitavya wenyewe kwa wenyewe; sote tunaamini kwamba katika siku za usonitutaweza kusaidia Kanisa na jamii katika nchi maskini za Afrika, Amerikaya Kusini na Asia (na mahali pengine pote), ikiwa watu wengi kadriinavyowezekana, hususani wakristo wengi iwezekanavyo watajifunzakusimama kwa miguu yao wenyewe kulingana na kanuni za Biblia. Hivyowatakuwa huru kuwa viongozi katika makanisa yao na kuongea mbele yajamii zao.

Hii ndio sababu tunachapa vitabu vinavyosaidia watu wajisaidie wenyewewakifuata mashauri ya Mwumba katika Biblia.

Mbali na kitabu cha Dk. Monte Wilson ‘Sheria Muhimu Zaidi katika Kuishi’,tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wamaisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara”; pia kitabuchangu “Mungu Akutaka Ujifunze, Utumike na Upende”, na kitabu chaMke wangu juu ya Uislamu “Mtazamo wa Uislamu juu ya MafundishoMakuu ya Ukristo” ili vigawiwe bure kwa watenda kazi pamoja nasi.

Mungu akubariki na kukupatia upako wakati usomapo kitabu hiki naKITABU CHAKE, Biblia.

Thomas Schirrmacher

7

Page 9: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;
Page 10: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Kwanza

Sheria Muhimu Zaidi katika Kuishi

Amri Kumi za Mungu zimepata kuenezwa vibaya mara nyingi. Baadhi yasababu hizo ni kwamba wapo wanaozungumza juu ya Amri hukuwakifanya yachukizayo. Baadhi ya uenezaji huu mbaya unatokana nawatumishi wanaowahukumu baadhi yetu wanaojitahidi kutii na kishakudhihirishwa kama watu wabaya kabisa miongoni mwa wakosefu. Aidhakuna tatizo la kutalakisha (kutenganisha) Sheria kutoka kwa Mtoa Sheria:yaani Mungu. Ikiwa unafikiri Sheria hizi ni za kinasibu* tu zilizokusanywana kuwekwa pamoja na baadhi ya Wayahudi kututesa, badala yakuzitazama kama udhihirisho wa Mungu apendaye, basi sheria hizizitakusukuma mbali katika uelewa.

Vipi iwapo unasoma Amri Kumi katika jicho la mtu anayeamini kuwaMungu ni mnyonge au halingani na desturi zetu - mawazo yanayotawalasana siku hizi – ni jinsi gani sheria hizi zingeonekana kwako? Kwa upandemwingine, ni vipi iwapo ulianza na wazo kwamba Mungu wa Amri Kumi niMungu wa upendo na kwamba Yeye ni mwema na kila kitu anachoamuruni kwa ajili ya mema yetu? Je, unafikiri hili lingeweza kubadili mwitikiowako kwa Amri Kumi

Sheria za Mchezo

Kama Mwumba wetu, Mungu ajua ni njia ipi iliyo bora na yenye siha* katika kuishi maisha yetu. Ajua kipi kifanyacho kazi (sio kwa muda mfupi bali kwamuda mrefu) na kipi kisichoweza. Ajua kipi kitakachotusababishiamadhara makubwa na kipi kitatuletea furaha ya kudumu. Ajua kipikitatutunza katika njia ya kuelekea kwenye afya ya kiroho na furaha yamilele na kipi kiwezacho kutupeleka tukizungushwazungushwa kuelekeashimoni.

Napenda kucheza mpira wa miguu. Sikuuvumbua mchezo huo.Sikuvumbua utengenezaji wa kifaa chenyewe. Sikuziunda sheria. Kamanataka kucheza na wengine, kama nataka kushindana katika mchezo huu, kama nataka kuruhusiwa kuwa uwanjani, ni lazima basi kukubali na

9

Page 11: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

kuzitunza sheria. Maisha yamekuja kwetu kwa njia ile ile. Tunza sheriaama sivyo utatolewa nje ya uwanja.

Huku si kusema kwamba utunzaji sheria utakupatia tiketi ya bure kuingiambinguni. Kinyume chake, sote twajua kuwa hakuna hata mmoja awezaye kuzishika sheria hizi kikamilifu. Kama Wakristo tunaelewa kwamba, ni kwa imani yetu katika Kristo na kile alichokifanya kwa ajili yetu kwa kufa katikanafasi yetu-katika nafasi ya wavunja sheria. Lakini pia kama Wakristo,twajua kuwa katika kumpendeza Mungu, kuendelea katika hali yakuponywa na kufanywa kamili, amri hizi ni muhimu.

Nani ni Mwangalizi?

Amri ya kwanza inatueleza kwamba ni lazima tusiwe na mungu wa ziadakwa Mungu aliyejifunua kwetu katika uumbaji, katika Yesu Kristo na katikaBiblia. Mungu haruhusu ushindani. Yeye ni Mungu na wewe si Mungu.Yeye ni Mungu, wote wanaojidai kuwa ni miungu ni waigizaji. Yeye niMungu na anataka kukubaliwa kama Mungu pekee wa kweli.

Mungu anahitaji uaminifu kamili na utii kamili. Hatuwezi kuwatumikiamabwana wawili au mabwana zaidi. Oh, tunajaribu kuwa na mabwanawengine. Tunajaribu kumtumikia Mungu na kumfanya Yeye kipaumbelenamba moja na wakati uleule kumtumikia mungu wa tamaa au anasa aukutaka kujulikana. Lakini hilo haliwezi kufanya kazi kamwe. Utiifu wetumkamilifu waweza kwenda kwa mtu mmoja au kitu kingine tu. Munguasema utii ni kwake tu.

Je, umeshawahi kufanya uamuzi wa kwenda kusoma shule fulani aukuchagua kazi fulani au mtu wa kuoa? Je, wakumbuka ni jinsi gani, marauchaguzi huu ulipofanywa, hukuhitaji kufikiri tena juu ya machaguo yakomengine au mbadala zaidi? Je, wakumbuka jinsi ulivyokuwa umelenga naulivyokuwa umetulia? Mara umfanyapo Mungu kuwa Mungu wako mmojana pekee, mambo hutulia kabisa. Huyu ndiye Mungu nitakayemtumikia;hizi ni Sheria alizoziweka. Mwisho wa mjadala.

Kumfanya Mungu kuwa Mungu wako wa pekee humaanisha kuwavipaumbele vyote, maamuzi yote, shauku zote na ndoto zote au maonovinawekwa chini yake. Je, ametoa miongozo, kanuni au sheria katikaBiblia ambazo zitakuwa na matumizi katika mambo hayatunayoyazungumzia? Ni kitu gani hicho anachohitaji?

Kumfanya Mungu kuwa Mungu wako pekee humaanisha kuwa utachezamchezo kwa sheria zake. Hatuwezi kusema twampenda Mungu natukipuuza sheria yake. Yote mawili kwa kawaida huenda pamoja kwa

10

Page 12: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

sababu sheria za Mungu ni udhihirisho wa asili yake. Kukataa kimojawaponi kukataa na kingine.

Kumfuata Mungu

Watu wamfuatao Mungu peke yake ni majasiri. Moyo na akili vilivyotulizwakatika utii vyaweza kutenda kwa malengo na kwa haraka. Hakuna haja yakusimama na kuanza kufikiria ni sheria zipi utakazotafuta kuzifuata.Hakuna mashaka juu ya heshima ya Nani ni muhimu zaidi kwako.

Kumfuata Mungu peke yake pia huleta ongezeko la uelewa wa fikra. Kunamkanganyiko mkubwa wa ndani wakati tuwapo hatuna hakika juu ya yulealiye juu ya maisha yetu au yule atakayetutawala. Pindi uaminifu wetuunapotulizwa, akili zetu hujifunza haraka kufikiri mawazo ya Mungu,kutathmini kama Mungu atathminivyo, kuona kama Mungu aonavyo.

Wakati unapochagua kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, akili naroho, maisha huchukua umuhimu wa kina. Matendo yako yote, maamuziyako yote, kila kitu ufanyacho sasa kina lengo moja: wataka kuishi kwa ajiliya Mungu na kumpendeza yeye kwa vile unavyokuwa na kwa yoteuyatendayo. Unalitendaje hili? Tazama Sheria zilizobaki!

Kumbukumbu la Torati 6:4-7Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja.Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, nakwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno hayaninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; naweuwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katikanyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

Kutoka 32:15,16Basi, Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbiliza mawe mikononi mwake; mbao zilizoandikwa pande zote mbili,upande huu na upande huu ziliandikwa. Na zile mbao zilikuwakazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu,yaliyochorwa katika zile mbao.

11

Page 13: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Kutoka 20:3(Amri ya Kwanza) Usiwe na miungu mingine ila mimi.

1 Timotheo 2:5Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu nawanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.

12

Page 14: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Pili

Usijifanyie Miungu

Umekwishaamua kumfuata Mungu. Katika ari* yako mpya uliyoipata,unatamani kudhihirisha upendo na heshima yako kwake kwa uhuru nakwa moyo kadri uwezavyo. Unataka kumwabudu Yeye kwa namna alivyona kwa kile alichokitenda kwako. Hii ni haki pekee na alama ya yule ambaye kweli amekwishaamua kwamba yeye si Mungu au Mwokozi wakemwenyewe. Hata hivyo ni kwa jinsi gani twamwabudu Mungu kwa usahihi? Je, kuna njia isiyostahili ya kuabudu? Je, twaweza kuendelea kutafutakumpenda Mungu kwa kufuata njia ambazo kwa kweli zinamchukizayeye? Amri ya pili yasema, ndiyo, kuna vipimo vya kumwabudu Mungu.

Baadhi ya watu wanajaribiwa kuikimbilia amri hii kwa sababuhawamiliki vijumba vya sanamu au madhabahu za sadaka. Kupiga magotimbele ya ndama wa dhahabu sio kitu ambacho wameshakichunguza kwamakini. Vilevile, wengine tunafikiri amri hii hailingani na mazingira yetu.Lakini zingatia kile hasa kinachozuiliwa hapa. Kile anachosema Mungu nikwamba tusihamishie kwa mwingine (kwa mfano, mwenzi, mtumishi waMungu au mwanasiasa) au kwa kingine (kwa mfano, kazi, fedha ausanamu) kile kilicho chake peke yake. Sasa jiulize mwenyewe kama HILIlaweza kuwa jambo linalolingana na mazingira yetu.

Kuna habari katika Biblia inayotokea wakati Musa akiwa juu yamlima akipokea Amri Kumi. Watu walio chini bondeni wanaamua kuwaMusa harudi, hivyo wanamwomba Haruni, mtu wa cheo cha pili kutokakwa Musa, kuwaongoza. Pia wanaamua kwamba lingekuwa wazo zurikuchonga ndama wa dhahabu wakitumia vito vyao vyote vya thamani nakuitumia katika ibada siku itakayofuata.

Katika kuisoma habari hii utaona kuwa Haruni anaitaja huduma hii yaibada kama sikukuu kwa BWANA (Kutoka 32). Hafikiri kuwa anaabudumungu mwingine. Yawezekana ng’ombe huyu anakwenda kuwakilishauweza na nguvu za Mungu! Kipi chaweza kuwa kosa katika hili? Wawezakusema, Hata hivyo hawajageukia Mungu wa uongo kwa hiyohawajavunja amri ya kwanza. Lipi laweza kuwa kosa la vielelezo-vioneshi* (zana-oneshi) katika kuabudu?

13

Page 15: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Lililo kosa ni kwamba vielelezo-vioneshi haviwezi kumchora Mungu jinsialivyo. Kwa asili yake vitaweza, kwa mafanikio makubwa, kuashiria sifambalimbali za Mungu lakini kwa kufanya hivyo vinamwakilisha kimakosakwa kutofunua kikamilifu jinsi alivyo.

Viwakilishi hivyo pia hufanya hatari ya kutuongoza kumhusisha Mungu nakitu tulichotengeneza katika hali ambayo viwili huwa kimoja: ndamahawezi kumwakilisha Mungu, inakuwa ni mnyumbuliko* wa Mungu. Kwamaneno mengine, wakati mioyo yetu inaweza kuwa ikitafuta kumpendaMungu kwa uaminifu, tunaweka kiumbe mahali pa Mwumba. Kujiepushiambali na kosa hili hatari na la kipumbavu, amri hii yatuambia tujitenge navielelezo-vioneshi ambavyo ni vya kumwakilisha Mungu.

Lakini hapa kuna zaidi ya onyo la kutoweka ndama wa dhahabu nyumbanimwako. Acha turejee nyuma kwenye ukweli kwamba kile tunachoendeleakuambiwa ni kutohamishia kwa kitu au mtu mwingine kile kilicho chaMungu peke yake. Kipi kilicho cha Mungu pekee? Vipi kuhusu kumtumainiMungu pekee katika wokovu wetu? Je, wokovu, msamaha wa dhambi zetu ni kitu anachoweza kukitoa Mungu pekee? Ndiyo. Sasa ni vipi iwapotwaanza kumtazama mwingine au kitu kingine nje na kile alichokifanyaMungu kwa ajili yetu katika Kristo Yesu?

Viongozi wa Kiroho Wamejazwa na Ndama?

“Sawa sawa Monte, kwa hakika sitaanza kuweka matumaini yangu kwakiongozi wa uzushi au mtumishi kwa ajili ya wokovu wangu”. Lakini je,kuna watu ambao idhini yao ni yenye hatari kwetu kiasi kwamba tutafanyalolote bora ili kuwapendeza? Kukataa au kutofurahishwa kwao ni jambolenye maumivu makubwa kiasi kwamba twahisi kama tumemkoseaMungu? Je, kuna watu wanaojaribiwa kuwaruhusu wengine kuwa na ainaya ushawishi au hata mamlaka juu yao yaliyo kama ya mungu-mtu?

Kuna watu wanajihisi kuwa ni wadhaifu sana, wanajitazama wao wenyewe kama wajinga au wasiotaka tu kuchukua wajibu kwa machaguo yao; hivyohuwatwika wengine maisha yao. Sizungumzi juu ya watoto au wazeeambao ufahamu wao unapungua: Ninawazungumzia watu ambao wanauwezo kamili wa kufanya uchaguzi na kuwajibika kwa machaguo hayo,lakini bado wanaruhusu mtu mwingine kuendesha maisha yao. Kwangu nijambo moja kujifunza kutoka kwa mwingine, na ni jambo jingine kwangukuigeuzia akili yangu juu ya wengine.

Kuna nyakati ambapo inashawishi kufanya biashara na mungutunayemwona kuliko Mungu tusiyemwona. Washauri, viongozi wa kiroho,wahudumu na wengineo; wote ni vipawa vya ajabu wanapojishughulishanasi. Lakini hakuna hata mmoja wao anayeruhusiwa kuchukua nafasi ya

14

Page 16: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Mungu. Maisha yetu, vipawa na talanta zetu, na safari yetu ya kiroho nivyetu peke yetu. Mungu hatawauliza wengine juu ya yale uliyoyafanyakatika maisha yako; Yeye atakuuliza wewe. Na kwa kuwa unawajibikakwake kwa machaguo yako, lazima uwe mwenye kufanya uchaguzi.Hakika kuna nyakati unapohitaji walimu na viongozi lakini mwishoniutakuwa ni wewe unayetoa hesabu kwa yale uliyoyafanya auhukuyafanya.

Kutoka 20:4-6(Amri ya Pili) Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kituchochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, walakilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwakuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Kumbukumbu la Torati 11:16Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageukana kutumikia miungu mingine na kuiabudu.

Isaya 42:8Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampamwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.

Warumi 1:22, 23Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika, wakaubadiliutukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura yabinadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na yavitambaavyo.

Matendo 12:21-23Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme,akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao. Watuwakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti yamwanadamu. Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababuhakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.

15

Page 17: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;
Page 18: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Tatu

Mungu si Kiambishi-Awali*

Maneno yana nguvu. Wengi wetu huwakumbuka wale marafiki, walimu auwana-familia ambao walituambia kwamba sisi tu wajinga, wabaya(hatupendezi) au wanene. Tunawakumbuka pia wale waliotuamini,waliotusaidia, waliotuambia kuwa tulikuwa maalum au tulijaliwa vipawa.Hakika, nguvu ya maelezo - iwe ni chanya au hasi (iwe ni yenye kujengaama kubomoa) – kwa kiasi kikubwa ilizingatia uthamani au umuhimu wamtu aliye nyuma ya maneno. Hata hivyo, maneno yenyewe yametuadhibukwa miaka yote hii.

Kwa upande mwingine, wengi wetu pia wamekuwa na uzoefu wenyekuumiza wa kutafuta kusema kitu chema au chenye kusaidia na kishatunatambua kuwa; mtu tuliyekuwa tunazungumza naye alifasili manenoyetu kuwa ni yenye kumwumiza. Nyakati hizo ni za kutuchanganya kwasababu wakati maneno yetu yalikuwa wazi kwetu (kama ilivyokuwa niayetu kusema tuliyotenda), yalikuwa yanaeleweka vema kwetu, kwaupande wa mwathirika alituelewa kinyume (kusema vile ambavyohatukusema). Kwa kweli kuna hizo nyakati ambapo maumivuhusababishwa na ishara zetu za mawasiliano zenye kugongana: Kinywakinasema jambo ambalo maisha yetu au tabia zetu zinapingana nalo.

Fikiri juu ya hili: Ni wengi wetu wangapi wameshatupilia mbali misaadakutoka kwa watu fulani? Wakati mwingine twafanya hili kutokana naunyenyekevu wa kiongo, nyakati nyingine tunafanya hili kwa sababutunadhani kuwa jamaa ana nia iliyofichika kwa kuwa mwema. Lakini piakuna wale watu ambao maneno yao hubeba uzito kidogo kwa sababudaima husema mambo mazuri kwa kila mmoja bila kujali ni hali gani, bilakujali ni mtu gani au kipi walichotenda. Iwe sawa au isiwe, twaaminikwamba inapotokea maneno kutumiwa sana bila heshima yanayostahili,maneno hukosa thamani.

Maneno ni vyombo vinavyotafuta kubeba maana au taarifa kutoka mtummoja kwenda kwa mwingine. Maana zilizokubalika kwa neno husikahutusaidia kuweka mipaka kulizunguka ili maana yake isivuje, ikiliachaneno likiwa dhaifu na maana yake kutoeleweka. Tuwapo waangalifu namakini zaidi katika uchaguzi wetu wa maneno, ndivyo uwezekano wa

17

Page 19: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

mawasiliano mazuri huwa mkubwa. Tunapogundua kwa usahihi zaidi kilekinachosikiwa, kikilinganishwa na kile kinachosemwa- matumaini zaidi nikwa mawasiliano yenye mafanikio.

Biblia imejaa maelekezo kuhusu matumizi sahihi au yenye busara yamaneno. Kitabu cha Mithali hutueleza kwamba maneno mengi sanayanaweza kutusababishia matatizo makubwa, kwamba manenoyanaweza kupenya kama upanga au kuweka mafuta ya uponyaji kwenyeroho iliyojeruhika. Katika barua yake kwa Wakolosai, Mtume Pauloalisema kwamba tunahitaji kuyakoleza maneno yetu kwa kuyatia munyu*,kujifunza jinsi ya kuongea vema zaidi kwa kila mtu. Katika siku hizo,chumvi ilikuwa alama ya uaminifu na unyofu (chembechembe za chumvihushikamana, tofauti na chembechembe za mchanga au hata sukari).Chumvi ilikuwa pia mali yenye thamani hivyo basi mtu mwema alikuwa“mwenye kustahili heshima kwa chumvi yake”.

Kuheshimu Jina la Mungu

Hapa, katika amri hii ya tatu tunapewa sheria maalumu kabisa kuhusumatumizi ya jina la Mungu. Ni lazima litumiwe ifaavyo na kwa heshima.Halipaswi kutumika katika njia yoyote ambayo italitukanisha jina lake.

Fikiria kwa muda juu ya mtu umpendaye sana. Yawezekana mpendwahuyu ni babu, shangazi au mjomba, au mwenzi wa ndoa. Mtu huyu ni yuleunayemheshimu, ungependa wengine kumwona kama unavyomwona,ukiamini kuwa kama watamfanyia jambo watajisikia kama ambavyoungejisikia juu ya mtu huyu. Sasa, ni vipi ikiwa jina la mtu huyu linakuwajina la laana, yaani herufi chache kujaza nafasi iliyoachwa wazi wakati akili haiwezi kutafuta neno lifaalo? Ni jinsi gani utaitikia jambo hili?

Moja kati ya chunguzi zenye kunishangaza nilipokuwa nikisoma maisha ya Yesu ni kwamba, kamwe hakujilinda. Ungeweza kumwita majina yoyote,kumtemea mate, chochote n.k. Lakini kama ungempuuza Baba yakeulikuwa na hakika ya kukabiliana na hasira yake.

Kutumia jina la Mungu kinyume sio tu kulitumia kama kiambishi-awali(kipachikwa au kiongezwa) kwenye neno la laana. Pia tunalitumia kinyume jina lake pindi tulitumiapo bila kufikiri-herufi tano (M-U-N-G-U) pasipo kituchochote kilichowekwa ndani yake. Fikiria kutumia jina la Mwumba wetuna Mwokozi kama sauti isiyo na maana ili kujaza ukimya usiotakiwa!

Wakati tutumiapo vibaya jina la Mungu, tunapolipa tafsiri nyingine nakulitumia kama neno la kuelezea hasira au karaha au chuki au kama sautiya kujaza ukimya; tunadunisha umuhimu wa Yeye alivyo kwetu na kwa

18

Page 20: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

wale wanaosikiliza. Katika kulitumia kinyume jina la Mungu, katika halihalisi tunashusha heshima yake.

Je, ni jinsi gani twaweza kulitumia jina la Mungu kwa ubatili au kwa njiaisiyofaa na kisha kugeuka na kutafuta kudhihirisha upendo au tumaini auheshima kwake? Wakati sipendekezi kulishika jina la Mungu kama aina yaneno hatari lenye usihiri*, naamini kuwa wakati tunapodunisha jina lakekatika mazingira fulani, tunadunisha matumizi yake katika mazingira yote.Hatuwezi kujipatia nguvu kutoka katika jina lake kwa kulitumia kama laanasiku ya Jumamosi usiku na kisha kutegemea jina hilo hilo kuwa na nguvutunapoabudu Jumapili asubuhi.

Nafsi Iliyo Nyuma ya Neno

Tunapojadili uwezo wa maneno ni lazima tukumbuke kuwa, si tu uchaguziufaao wa maneno ndio unaozingatiwa, lakini pia nafsi (mtu) iliyo nyuma yamaneno. Je, mtu husimama nyuma ya maneno yake? Je, mtu huyuhupewa heshima kwa kusema anachomaanisha na kumaanishaanachokisema? Kwa maneno ya Yesu, je, ‘ndiyo’ yao ni ndiyo na ‘hapana’yao ni hapana?

Katika mazingira ya kulitumia jina la Mungu, je, ninaishi katika hali ambayowakati nizungumzapo juu yake watu hutaka kusikiliza? Je, maisha yangu,jinsi ninavyoishi, humwongezea heshima ninayotarajia awe nayo kwa haowanaonizunguka? Au maisha yangu yako katika hali ambayo kila tamko laMungu husikika kama kufuru?

Je, yawezekana kutolitukanisha kabisa jina la Mungu kwa vinywa vyetu,kutolitumia kabisa katika njia isiyofaa; na huku twaishi katika hali ambayowakati tusemapo sisi tu wamtafutao au wamwaminio Mungu, watuhumfikiria Mungu katika uduni? Je, huu si uvunjaji wa Amri ya Tatu?

Wakati amri inapotuambia tusifanye hili na lile, ninapendekeza kwamba,pia inatuambia kuwa tunapaswa kufanya jambo jingine, jambo chanya(linalokubalika), kama unataka. Kwa mujibu wa amri hii, kama tunapaswakutolitukanisha jina la Mungu, tunapaswa kufanya kila kitu kwa uwezowetu kuongeza heshima ya jina lake kwa watu. Kwa maneno mengine,tunapaswa kuishi katika hali ambayo itawasaidia wengine kumwonaMungu kama Mungu mwenye uweza, ukweli, wema, usafi, uzuri, upendona rehema. Kwa maneno mengine kazi yetu ni kuwasaidia wenginewamwone Mungu kikamilifu kama alivyo.

19

Page 21: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Kutoka 20:7(Amri ya Tatu) Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako,maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajayejina lake bure.

Mathayo 12:22-28,31Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu;akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wotewakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? LakiniMafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwaBeelzebuli mkuu wa pepo. Basi Yesu akijua mawazo yao,akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyikaukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake,haitasimama. Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu yanafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? Na mimi nikitoapepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwasababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. Lakini mimi nikitoapepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwishakuwajilia…Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kilaneno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuruRoho hawatasamehewa.

Wakolosai 4:5,6Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu,mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Yakobo 1: 26Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwahatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyohaifai.

Yakobo 3:10-13Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu,haifai mambo hayo kuwa hivyo. Je! Chemchemi katika jichomoja hutoa maji matamu na maji machungu? Ndugu zangu, Je!Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalikachemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazizake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

20

Page 22: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Nne

Kusherehekea Imani Yako

Daima hunishangaza kusikia watu wakisema juu ya Ukristo kama dinimbaya ambayo iko kinyume na watu kuwa na furaha. Umekwisha tazamakatika Agano la Kale na kuona sikukuu na karamu watu hawawalizofanya? Wakati mmoja Mungu anawaambia watu wake kuuzaasilimia kumi (10%) ya mifugo yao na kununua vinywaji ambavyo kwavyowangesherehekea. Je, wakumbuka habari ya Yesu arusini? (Yoh.2).Sherehe inaendelea barabara hadi mhudumu wa mvinyo anapotangazakuwa yuko karibu kuishiwa mvinyo. Mariamu anamwendea Yesumwanawe kumwuliza kama analo la kufanya juu ya jambo hili. Kisha Yesuanakwenda kuyageuza maji kuwa mvinyo bora zaidi. Je, anatumia nafasihii kuelezea Uungu wake? Hapana. Je, anatenda mwujiza ili kila mtuaweze kuuona uweza wake? Hapana. Kwa urahisi na amanianatengeneza mvinyo ili kuongeza furaha ya sherehe.

Wakristo wanapaswa kufurahia maisha, kuonesha vipawa vyao katikakuwahudumia wengine, kufurahia vipawa vya uumbaji wa Mungu nadaima kuzoelea maisha tele waliyoahidiwa na Yesu (Yoh.10:10). Je, hililaonekana kama maisha yenye kuchosha? Je, hili laonesha kama Munguanataka tuwe watu wasio na furaha? Kwangu laonekana kuwa Munguanataka tuzoelee kwa kina furaha, zaidi ya tuwezavyo kufikiri.

Mazoezi

Ninapendekeza kuwa moja ya sababu ambazo wengi wetu hushindwakuzoelea aina ya furaha Mungu anayoitaka kwetu inaweza kurejewakatika amri hii. Waziwazi, Mungu anatutarajia kufanya kazi kwa nguvusana (“siku sita fanya kazi”), vilevile kupumzika na kuabudu. Kwa manenomengine, maisha yetu yawe na ulinganifu kati ya kazi na mapumziko,kuwahudumia wengine na kumwabudu Mungu.

Wale wote wanaoshindwa kuhusisha au kulinganisha vema kati ya kazi naibada, kwa ujumla watashindwa kuzoelea maisha kama Mungualivyokusudia. Ikiwa najitoa nafsi yangu kufanya kazi ngumu lakininashindwa kujizuia (kuacha kufanya kazi au kupumzika) na kuabudu;kujizuia na kujifurahia nafsi yangu, kujizuia na kukumbuka ni Nani

21

Page 23: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

aliyenipa muda huo, nguvu, nafasi, na mahitaji kwa ajili ya familia yangu na kuwatumikia wengine; nitajithibitisha mwenyewe kuwa ni mwenye ubinafsi na nisiye na shukrani. Kama nitatumia muda wangu wote kuabudu nakwenda kwenye mikutano ya kidini, basi nashindwa kuvitumia vipawa natalanta Mungu alizonipa kumtumikia yeye hapa duniani nilipowekwa naninashindwa kuwatumikia wengine kama nilivyopaswa.

Kukumbuka kumwabudu Mungu kila wiki hutuzoeza kujua Mungu ni nani,na sisi tulivyo kwake kama wana wa kiume na wa kike. Kukumbukakumwabudu Mungu kila wiki huzifikisha shughuli kwenye ukomo ili tuwezekukumbuka kwamba, pasipo Mungu, hakuna baraka, hakuna mafanikio ya kweli na hakuna maisha tele.

Watu washindwao kutii amri hii kwa kawaida huangukia katika tanzi yakujifasili* wenyewe kwa kulingana na kazi zao badala ya kujifasili kwakulingana na uhusiano wao na Mungu. Vibaya zaidi, kama kila kitukinakwenda mrama kazini, kama nashindwa kila kitu kazini kwangu,ninajifasili mimi mwenyewe kuwa mshindwa. Badala ya kusema“nimekosea hapa” inakuwa “mimi ndiye kosa lenyewe”. Hata hivyo, ikiwaninakumbuka kitu cha kwanza na kilicho kikubwa kwangu ni kuwa, mimi nimtoto wa Mungu na ninajifasili binafsi kwa mahusiano yangu naye, basimtazamo wangu ni wa ki-milele zaidi, kiafya na wa kuheshimika kwaMungu.

Jambo lenye UtaratibuIbada inayotakiwa hapa ni jambo lenye utaratibu. Rudi nyuma na usomeAgano la Kale na Jipya. Watu wa Mungu daima wamekuwa wakija pamojakwa ushirika unaodhihirisha ibada. Mara moja kwa wiki, watu wakewalikusanyika kuuambia ulimwengu uliowazunguka, “Huyu ndiye Mungutunayemwabudu” na walifanya hivyo kwa msaada wa mifumo na miundombalimbali.

Kanisa la Kikristo daima limekuwa likikusanyika Jumapili kumwabuduMungu. Sio kwamba sherehe na maadhimisho ya kidini yenye utaratibu nimuhimu tu, bali pia ni yenye msaada sana. Mimi na wewe si malaika bali tunyama na damu. Twahitaji muda na mahali na miundo kusaidia shughulizetu za kiroho.

Fikiria juu ya hili. Wakati Yesu alipotuambia kumkumbuka yeye wakatitulapo Chakula cha Bwana alitupatia mkate na divai halisi. Hakutuachia tumawazo au fumbo tata bali tulipewa vielelezo halisi kutusaidia sisikumkumbuka yeye katika hali maalumu kabisa. Hakika, twawezakukamatwa na maadhimisho na taratibu kiasi kwamba tunasahau kwamba yanatuelekeza kwa Nani. Lakini nashangaa kwa kuwa siku hizi jaribu si

22

Page 24: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

kupotelea kwenye taratibu bali kushindwa kwelikweli kulifikia lengo laibada kwa sababu tulikataa msaada wa taratibu hizo.

Pia ninapendekeza kuwa si tu nyakati na mahali zinazotusaidiakumwabudu Yeye, bali pia kuendelea kufanya ushuhuda-shirika* katikautamaduni unaotuzunguka. Wakati Israeli ilipochukuliwa utumwani nakulazimishwa kuishi katika utamaduni wa kigeni unaomchukia Mungu,daima waliendelea kutafuta kumwabudu Mungu pamoja (ki-ushirika) kama familia ya kiroho, wakitoa ushuhuda wa Mungu wanayemtumikia. Swali lakuvutia lipaswalo kuuliza hapa ni, Je, Israeli wangeendelea kuwepo kamawangeshindwa kukutana pamoja kama watu wamoja katika kumwabuduMungu na kutiana moyo kila mmoja?

Wakati mtu afanyapo mapendekezo kama hayo, haraka atasikia watuwasemavyo jinsi ambavyo kanisa hili lilivyo baya au jinsi mtumishi yulealivyo mwovu; na jinsi gani “Ninaweza kumwabudu Mungu peke yangusebuleni kwangu vizuri zaidi kuliko katika kanisa zee lililokufa”. Hata hivyo,amri hii si kwa ajili ya maonjo (matakwa) binafsi ya kiroho bali ni juu ya ainaya ushuhuda niutoao kwa ulimwengu unaonizunguka. Na swali ni hili,Naweza au nitaweza kuendelea kumwabudu Mungu kama nipaswavyo nakutoa ushuhuda nipaswao ikiwa sitasimama kama kitu kimoja na waaminiwenzangu? Je, ushuhuda wa Kikristo utaendelea kuwepo pasipo umojautokanao na ibada zenye utaratibu.

Kutoka 20:8-11(Amri ya Nne) Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanyakazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato yaBWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, walamjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliyendani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanyambingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Marko 6:31Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahalipasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababuwalikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasiya kula.

23

Page 25: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Waebrania 10:24,25Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo nakazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyodesturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwakadri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

24

Page 26: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Tano

Kuheshimu Wazazi

Nilipokuwa mtoto mdogo, moja kati ya mashujaa wangu alikuwa ni babuyangu. Nilipenda kuwa karibu naye alipokuwa akiendesha gari yake,nikisikiliza masimulizi ya habari za watoto wake watano ambao babayangu alikuwa mkubwa wao. Katika tukio moja nakumbuka nilipomwambia tatizo lililokuwa linanikumba shuleni na jinsi mwalimu fulani “mjinga”alivyokuwa chanzo cha huzuni zangu zote. Haraka alinikaripia nakuniambia kwamba, “Wilson usifanye namna hiyo”. Babu yangu hakuamini juu ya mtu anayejiweka pembeni akiwa na maumivu ya kimyakimya, akiliajinsi alivyotendewa vibaya: aliamini juu ya tendo la kuwajibika. Pasipomashaka yoyote katika akili yangu nilichukua tahadhari ya kutozungumzanamna ile tena. Kwa kweli ilikuwa rahisi sana: Wilson usifanye kwa jinsihiyo.

Kwa kawaida watu hujishughulisha sana ili kuishi kwa kiwango chamatarajio na hadhi ya vikundi ambavyo wao ni sehemu yavyo. Jambo hili ni kweli katika familia. Jitihada zozote tulizonazo juu ya imani na maadilimema ya baba na mama zetu, ukweli utabaki kuwa inatuuma sana kuipitamipaka ambayo ni muhimu sana kwao. Twataka wafurahishwe nasi nahivyo twatafuta tuwe wenye kuwapendeza. Sio tu kwamba huu ni mwitikiowa kawaida, kwa kawaida ni wenye kuleta siha njema.

Kuwaheshimu mama na baba zetu ni kuheshimu urithi wetu. Kutoka kwawazazi wetu tumepata uhai, matunzo, lishe, hekima na utaratibu wamsaada wakati tulipokuwa tukijifunza kutembea kwa miguu yetu miwili nabaraka nyingine nyingi za kushangaza. Pia tumekuja katika ulimwenguuliojaa barabara, magari na baraka nyingine nyingi tulizopewa na “wazazi”wetu waliotutangulia. Hatukuitengeneza dunia tulimozaliwa: ilikuwa nizawadi.

Ni mama na baba zetu waliotupatia shule yetu ya awali, mahusiano yetu ya awali na serikali (“usifanye hiki…fanya hiki…au kingine”), masomo yetu yaawali kuhusu kazi, uzalishaji na jinsi ya kujipatia maisha, na uzoefu wamafunzo mengine muhimu. Hakika baadhi ya wazazi wanafanya kazi nzuri zaidi ya wengine lakini hata hao wazazi wasiojali au wanaotelekezamajukumu yao, wamewafundisha watoto wao jinsi wasivyopaswa kuishi.

25

Page 27: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Upatano

Wazazi wa mtoto ni vielelezo vya awali vya jinsi ya kuishi maisha. Ikiwawazazi husema kile wanachomaanisha na kumaanisha kile wasemacho,yawezekana mtoto akafanya vilevile. Ikiwa wazazi wanaishi katika maadiliwanayoyakiri waziwazi, mtoto atafanya vilevile. Ikiwa wazazi wanaishikatika umoja wa kanuni adilifu nyumbani, maadili mengine kanisani namengine tena kazini, mtoto ataliona hilo na kutenda vilevile.

Sisi sote tuna wajibu mbalimbali katika maisha. Tu watoto wa kiume au wakike, waume au wake, mama au baba. Tunawajibu kazini, wajibumwingine katika kanisa, na mwingine kwa marafiki. Haya ndiyo maisha.Changamoto kwetu ni kutunza imani na amali* za kimsingi na kutunzamambo yaleyale mema tunayoyathamini bila kujali wajibu tuufanyao. Hivindivyo ninamaanisha “upatano”.

Ni kweli kuna mienendo inayofaa katika mazingira fulani na isiyofaa katikamazingira mengine. Jinsi unavyofanya nyumbani pamoja na familia yakoitakuwa tofauti zaidi na unavyokuwa kazini kwako mbele ya mkuu wako.Hata hivyo, ni mara ngapi tumekuwa mfano wa kinyonga tukichukua imanina maadili ya kundi tulilomo na kubadilika pindi tu tubadilishapo mazingiraharaka? Je, hiki ni kitendo cha mwenye hekima, mtu mwenye afya kiroho?Hivi ndivyo tutakavyo watoto wetu waenende wakati wakuapo?

Moja kati ya vyanzo vikubwa na muhimu zaidi vya maisha yenye nguvu niupatano. Wakati kila upande wa imani zetu, viwango vya maadili na hisiavinapouwiana na matendo yetu katika kila eneo la maisha yetu, tunaupatano. Na wakati tuna upatano tutakuwa na nguvu za kiroho ambazohazipatikani kwa watu ambao ni “Wakristo” tu nyumbani au kanisani.

Kupenda

Ni baraka kubwa kulelewa na mama na baba wa ajabu ambao daimawalikuwepo kwa ajili yangu. Waliniamini, walinitia moyo, walinifahamishajuu ya umuhimu wa imani katika Mungu na waliniadabisha kwa kulinganana sheria sawia za kifamilia. Kulikuwa hakuna uongo, hakuna dharau kwamzazi yeyote, hakuna kuiba. Kutii Amri Kumi ilikuwa lazima. Tulipaswakufanya kazi ngumu kuzunguka nyumba yetu, kutunza makubaliano yetuna kuhudhuria kanisani kwa uaminifu. Utatu wa kimaadili ulikuwa kazi, utiina heshima. Na ikiwa tulishindwa kuyatunza haya au sheria nyingine,tungekutana na matokeo ya adhabu kali kutoka kwa mama na baba-kwakawaida baba. Kwa kifupi, wazazi wangu waliwapenda watoto wao wanne.

Nawezaje kusema nawapenda watoto wangu ikiwa naruhusu au kutiamoyo kwa kuwa mfano wa kutenda tabia ambayo haimpendezi Mungu?

26

Page 28: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Nawezaje kusema nawapenda watoto wangu ikiwa sitafuti kuwaandaliakuishi maisha kwa njia ambayo itawapatia nafasi kubwa ya mafanikio?Kama nawajali watoto wangu nitawapatia aina ya maagizo na mazingirayatakayorutubisha imani na tabia ambazo zitampendeza Mungu nakufanya maisha yenye siha wakati wakuapo na watakapoishi peke yao.

Kuwapenda watoto si kuwa na hisia za joto na wema kwao, lakini nikuenenda mbele zao katika njia ambayo itawapatia mlengo bora kuelekeakuwa watu wenye afya, wanaowajibika na wenye mafanikio. Nawafahamuwazazi ambao hawakuwaruhusu watoto wao kujihatarisha kwa hofu yakuwa wangeumizwa, ambao wamezilinda sana hisia za watoto wao, hivyowatoto hao hawajakabiliana na aina ya changamoto ambazozingewaandaa kupambana na dunia watakayokutana nayo wakatiwanaondoka nyumbani. Wazazi hawa daima hufikiri kuwa, kuwa wakalikwa watoto wao lingekuwa ni kosa kwani wakati wangesoma Biblia zaowangeona kwamba Mungu wao wa upendo aliyeko mbinguni ni mkalikama wazazi wao. Kwa kweli, Mungu anasema kwamba moja kati ya njiaambazo twaweza kujua kuwa tu watoto wake ni kwa kupitia nidhamu yake.Kwa maneno mengine, mahali pasipo na nidhamu hakuna upendo(Ebr.12:5-8).

Stadi za Maisha

Je, watu wafuatao wana kitu gani shirika (wana sifa gani zinazofanana)?

• Makatibu wasioweza kueleweka wakati waongeapo

• Watu waliokwenda shule kwa miaka 12 lakini hawawezi kuandikasentensi nzuri yenye kueleweka

• Watu wenye miaka 21 wasiojua kutunza fedha zao

• Watu wenye miaka 25 wasio na marafiki waliowafahamu kwazaidi ya miaka 5

• Watu wenye miaka 30 wanaodhani kwamba masaa 40 ni wikindefu ya kazi

Moja kati ya vitu ambavyo wana shirika ni mzazi ambaye hakuwafundishastadi za kimsingi za kuishi kwa mafanikio. Je, hii inamaanisha kwambawazazi wao hawakuwapenda? La, hasha! Je, inamaanisha kwambawatoto wao watapata ugumu kushindana katika soko na kuzoelea kileambacho maisha hutoa? Ndio.

27

Page 29: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Stadi kuu za mawasiliano, busara katika mahusiano, tabia bora zakazi, mienendo ifaayo na mbinu zifanyazo kazi katika kufanya maamuzi nivitu stahiki* ambavyo wazazi watapenda kuwapatia watoto wao. Hiihaimaanishi kwamba watapaswa kuwafundisha kila kitu, ila tu watafanyakila kitu kuona kuwa mafundisho yanapatikana.

Kutoka 20:12(Amri ya Tano) Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Munguwako.

Mithali 22:6Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hataatakapokuwa mzee.

Mathayo 15:4(Yesu) Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako namama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa naafe.

Waefeso 6:1Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyohaki.

Waebrania 12:5-8Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimiemoyo wako ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwanaampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Nikwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kamawana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hakuna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipommekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.

28

Page 30: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Sita

Kuheshimu Uhai

Biblia hufundisha kuwa sisi wanadamu tuliumbwa kwa mfano wa Mungu.Kwa kushikilia imani hii inayojithibitisha yenyewe pasipo shaka, Jamii yaKimagharibi imejiambatisha* kwenye thamani ya asili na utu wa binadamu, na imeimarisha sheria za kulinda thamani na utu huo. Kwa kuzikubali AmriKumi kama kipima-maadili cha sheria za kijamii, baba na mama zetu wakwanza wa Ustaarabu wa Kimagharibi walishikilia kwamba kuua ilikuwamoja kati ya vitendo vikuu vilivyopaswa kukemewa kwa sababu kiliharibumfano (taswira) halisi wa Mungu.

Bayana ni kuwa, si kuua kulikokuwa kinyume na sheria bali uuaji wakidhalimu au wa kukusudia. Mungu yuleyule aliyetuamuru sisi tusiuealiwaruhusu Waisraeli kushiriki vitani kupambana kinyume na maadui zao. Mungu aliyetuamuru tusiue, aliwaamuru Waisraeli wapigane vita namaadui zake. Mungu aliyetuamuru tusiue, aliwaagiza Waisraeli kuwauawatu ambao walifanya vitendo vibaya vya mauaji.

Ni wazi kabisa, kujiepusha na uuaji wa mtu mwingine si jambolililokusudiwa hapa. Fikiri juu ya mpendwa mmoja ambaye yuko karibukabisa kuuawa na mwizi. Je, tabia yetu inaheshimika iwapo hatufanyijambo lolote kuzuia kitendo hicho? Vipi kuhusu mtu kama Hitler ambayealikusudia kuwaangamiza binadamu wote wale ambao hakuwathaminikwa lolote lile? Je, kutotenda lolote kwa mtu huyo haitokuwa sawa na kuizawadia tabia yake? Na vipi juu ya mtu mwenye hasira sana kwamajirani zake, je, wasingemwua kama wangepata njia ya kuondokana nahilo? Je, wamejiepusha na kuivunja sheria hii? Kwa mujibu wa Kristo jibu ni hapana, hawajajiepusha. Ni kwamba hasira ya moyo ya kutaka kuua nidhambi sawa na kutaka kuchukua silaha na kumwua mtu kidhalimu.

Kwa uwazi kabisa Mungu huuthamini uhai na anatutaka sisi tufanye vivyohivyo. Kwa upande mmoja, hii inamaanisha kuwa tujiepushe na uuaji;lakini kwa upande mwingine tufanye chochote kilicho muhimu kulinda aukutunza uhai hata kama hii inamaanisha kuondoa uhai wa mwingine. Kwamaneno mengine, amri hii si rahisi kujishughulisha nayo kamainavyoonekana! Labda njia bora ya kusema hili ni kusema kwamba, wakati uhai ni kitu kitukuka, uhai wenyewe si thamani kuu ya mwisho. Thamani

29

Page 31: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

kuu ya mwisho ni ipi? Ni mapenzi ya Mungu kama ayatazamavyo kwamakini matendo ya binadamu (yaani, matendo yetu huzingatia mapenziyake?).

Ikiwa maisha yangelikuwa thamani kuu ya mwisho basi ingelikuwa ni kosa kwa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki. Ikiwa maisha yangelikuwathamani kuu ya mwisho basi ingelikuwa ni kosa mtu kutoa uhai wake ilikusaidia tendo la kiungwana. Ikiwa maisha yangelikuwa thamani kuu yamwisho basi ningelikuwa nimefanya makosa kuuondoa uhai wa jamaaambaye waziwazi alikuwa akitafuta kumwua mtu asiye na hatia. Ikiwamaisha yangelikuwa thamani kuu ya mwisho basi Mungu asingeliruhusuYesu kuuawa kwa niaba ya wenye dhambi.

Thamani ya kuwa Mwanadamu

Baada ya hayo yote kusemwa, napenda kurudi kwenye wazo la thamaniya ubinadamu. Sisi wanadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Watuwote. Mfagia barabara ninayempita na kumfanya kama kitukisichoonekana ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Mtoto anayeingilia kati unapoongea kwenye simu muhimu ameumbwa kwa mfano wa Mungu.Wenye matatizo ya akili wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Mfanyakaziambaye tabia zake hutusumbua ameumbwa kwa mfano wa Mungu.

Tunawatendeaje watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu walio nathamani kamilifu? Kwa kiwango cha chini kabisa naamini ni lazima tutunzeAmri Kumi za Mungu kwa watu hawa. Tusiwaue, tusiwaibie, tusizigeukefamilia zao, tusiwadanganye na tusitamani kile kilicho chao.Napendekeza, hii humaanisha pia kwamba wakati inapowezekana nainapofaa tutafute kuongeza uhai kwa wengine; kuongeza thamani ya malizao, kuongeza heshima ya familia zao, kuongea vizuri juu ya wengine nakufurahi wakati wale wanaotuzunguka wanapofanikiwa. Kwa manenomengine, wakati Amri zinapozuia tabia fulani zinatupendekezea tabiafulani nyingine.

Katika kujiepusha na uuaji wa kidhalimu ni lazima pia tutafute kuwatendeawengine kwa heshima, kwa kurejea nyuma katika thamani yao kamabinadamu. Fikiri, ikiwa watu wote unaowaona leo wangekuzoelea wewekama wewe ulivyowaona kuwa ni wenye thamani sana; unaowaona kuwasi kama meno kwenye furuweli*, watu wa kusukumwa huko na huko, watuwa kutendewa hila au kuvumiliwa bali kama watu walioumbwa kwa mfanowa Mungu. Fikiri, ni kipi kingetokea kwenye mahusiano yako na watuwengine ikiwa wangejua kwamba unawathamini sana kwa jinsi walivyokama watu walioumbwa na Mungu, na kwa kile ambacho wangetendakwako? Fikiri, kipi kingetokea kama mawazo yako daima yangekuwa, “ Ni

30

Page 32: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

kwa jinsi gani namheshimu mtu huyu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu?”Fikiri jinsi ambavyo ungejisikia kama wengine wangekutendea vivyo hivyo.

Kutoka 20:13(Amri ya Sita) Usiue.

Mathayo 5:21, 22Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua,itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneayendugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea nduguyake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Mathayo 7:12Basi yo yote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyohivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Mathayo 22:39Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kamanafsi yako.

31

Page 33: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;
Page 34: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Saba

Masharti kwa Tendo Kuu la Ndoa

Tunapokuja kwenye suala la mapenzi, Ukristo umepata kutangazwavibaya sana. Ungedhani kuwa Shetani ndiye aliyeumba uwezo wa kufanya mapenzi, na kila mtu aliyefurahia mapenzi, alikuwa dhambini! Hata hivyobado Biblia iko wazi hapa. Mungu alitupatia uwezo wa kufurahia mapenzi.

Soma Wimbo Ulio Bora. Tazama hamu, mahangaiko ya kimapenzi, jinsiwapendanao waelezavyo miili ya wanaowapenda: kiko pale kwa kilammoja kukisoma. Hata hivyo, baadhi ya wengine wanajaribu kusambazawanayoyasoma kuwa sawa na ponografia (picha na maelezo ya mapenzi)yenye kusheheni* misemo ya mafumbo na upendo wa Kristo kwa Kanisalake, Bibi harusi wake. Hata hivyo, bado naamini kuwa tunapotezaufahamu ambao Mungu aliukusudia kwetu kuuhusisha kwa wapendwawetu wakati tunapozidi kurohosha* kitabu hiki.

Mungu hayuko kinyume na raha. Kipekee zaidi, Mungu hayuko kinyumena mahaba au raha za kimapenzi. Zaidi, si kwamba hayuko kinyume tu,bali pia yuko kwa ajili ya hilo! “Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yakeyakutoshe siku zote; Na kwa upande wake ushangilie daima” (Mithali 5:18, 19). Je, hii inaonesha kuwa Mungu yuko kinyume na raha za kimapenzi?Je, hii inaonesha kuwa Mungu ni mwenye kujichanganya juu ya mahaba?Au inaonesha kuwa Mungu alikusudia kwa ajili yetu kuwafurahia wenziwetu?

Wazo kwamba miili yetu na ulimwengu huu wa maada* ni vitu viovu ni kosa la kale sana ambalo Kanisa limekuwa likipambana kinyume nalo. Mungualituumba sisi wanadamu, akatazama kazi yake na kuiona kuwa ni njema(Mwanzo 1:31). Na katika kifungu hiki, anatangaza kuwa moja kati ya miitoyetu kama wanadamu, ni kuijaza dunia. Ni wazi kuwa hili litahitajimahusiano ya kimapenzi ambayo yanajumuishwa kwenye kile alichokiona na kusema kilikuwa “chema” juu ya uumbaji wake wa mwanadamu.

Inakubalika, matamanio ya kimapenzi ya wanadamu yanawezakupotoshwa na kisha wanaume na wanawake kuangukia katika mitegoyote ya dhambi na huzuni. Lakini, je, matendo yetu sisi wenye dhambihubatilisha kile Mungu alichokisema bayana juu ya mahusiano ya

33

Page 35: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

kimapenzi? Matamanio ya chakula yanaweza kupotoshwa: je, hili lawezakutuongoza kusema kinyume juu ya kula kama kitu hatari sana au kibayaikiwa kitafurahiwa? Mamlaka yanaweza kutumiwa vibaya: je, kwa hiyotunakataa mamlaka katika mifumo yetu yote?

Kinachozuiliwa katika amri hii sio kuwa kinyume na mapenzi balikinahusika na nani unayeweza kufanya naye mapenzi.

Uaminifu

Kwa tendo la ndoa kukubalika na kufurahiwa, kuwa kama Mungualivyokusudia, ni lazima liwe katika mipaka ya mtu mme na mtu mkeambao wameoana…kila mmoja kwa mwenzake! Tukirudi nyuma kwenyekifungu katika kitabu cha Mithali nilichokinukuu hapo juu, kinafuatwa naonyo lifuatalo, “Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatiakifua cha mgeni?” (mst. 20)

Ongezeko la furaha ya mapenzi huhitaji ongezeko la viwango vya hatari(kutokuwa salama) na ukaribu. Kutokuwa salama kunahitaji imani. Wakati watu wawili waendapo kitandani kila mmoja kwa mwenzake, si tu miili yaoiliyo uchi bali pia na roho zao. Wakati unapoitoa nafsi yako kwa mwenziwako hutoi mwili tu, pia unatoa mwili wako na roho yako. Hii humpatiamwenzi wako nguvu ya ajabu juu yako ambayo kwayo aweza kukutendeajema au baya. Kutunza hali ya kuendelea kujitoa kwa mwenzi wako katikahali bora na kujenga mahusiano yenye siha lazima kuweko nakuaminiana. Na pasipo kuaminiana hakuna uaminifu.

Uaminifu unahitaji kupewa nafasi ikiwa tunahitaji kuwa na maisha yenyesiha ya mapenzi. Lakini uaminifu unaohitajiwa si ule wa kuwa fundimkubwa katika tendo la ndoa. Mapenzi yenye siha yanahitaji uhusianowenye siha. Ndoa uhusisha zaidi ya tendo la ndoa: inahusisha jamii,familia na urafiki. Hakuna kati ya uzoefu huu unaowezekana pasipouaminifu. Wakati mwanamume au mwanamke wanapovigeuka viapo vyao wanasema kwamba matamanio na hisia zao ni muhimu sana kulikofamilia, kuliko viapo vyao, na kuliko matakwa ya Sheria ya Mungu.Mtazamo huo utaharibu familia, ambayo katika mpango wa Mungu, ni kiinicha afya ya Kanisa na jamii.

Kila mmoja kutunza ahadi zake - katika lugha ya Biblia, kila mmojakutunza agano lake - ni muhimu kwa afya, ni maisha yanayomheshimuMungu. Watu wasiotunza ahadi zao mara chache sana ni wenyekufanikiwa. Na ikiwa watazoelea kiwango fulani cha mafanikio, hakidumumuda mrefu. Yawezekanaje? Mafanikio uhitaji imani toka kwa wengine, na nani atakayemwamini mtu anayeshindwa kutunza ahadi zake?

34

Page 36: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Kutoka 20:14(Amri ya Saba) Usizini.

Mithali 5:18-21Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshesiku zote; Na kwa upande wake ushangilie daima. Mwanangu!Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni?Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA,Na mienendo yake yote huitafakari.

Mathayo 5:27, 28Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia,Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwishakuzini naye moyoni mwake.

Waefeso 5:25, 28Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo nayealivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake…Vivyo hivyoimewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yaowenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

35

Page 37: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;
Page 38: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Nane

Kujipatia Mali

Ukristo ni dini ya hapa duniani kabisa. Kwa hili namaanisha kuwa Ukristo si maombi, kusifu wala si dini ya mambo ya mbinguni pekee balihushughulika na maisha ya kila siku yanayotuhusu wanadamu. Moja katiya mahitaji hayo ni mali na vile tunavyomiliki. Je, tunayo haki ya kumilikimali? Je, kuna viwango au mipaka ya jinsi tunavyopaswa kujipatia mali auvitu tunavyomiliki? Kwa jinsi ya kuvutia, sheria iliyo kinyume na kuibainakwenda sambamba na kutupatia mawazo ya Mungu juu ya mali.

• Wakati Sheria inapozuia wizi, inalinda mali binafsi.

• Wakati Sheria inapozuia kuchukua kitu kisicho mali yako,inatangaza kuwa iko njia sahihi ya kujipatia mali.

• Wakati sheria inapotuamuru kuwa tusiwaibie wengine, inatuambia kwamba hatuna haki juu ya mali za wengine: kwamba wachagueau wasichague kutupatia mali au kushirikiana nasi katika vituwanavyomiliki, hilo lote ni suala baina ya mtu na Mungu.

• Leo watu wengi hudhani kwamba ikiwa watajiepusha kuibakutoka katika duka la nguo au kuiba fedha kutoka katika kituo cha mafuta, basi wameishika Sheria. Lakini Biblia yatuambia kuwakuna njia mbalimbali za kuiba.

Mizani ya Uongo

Mithali 30:23 inakataza matumizi ya hila wakati mtu atakapo kufahamuthamani ya kitu. Kama ulikuwa unauza wakia* ya dhahabu, itakuwa ni wizikuacha mchanganyiko wa madini mengine kwenye dhahabu na kuiuzakama dhahabu safi kabisa. Itakuwa pia ni wizi kurekebisha mizani ili itoeuzito wa uongo.

Ni wakati gani tufanyapo haya? Wakati fundi makanika anapoondoa vifaavizima vya injini na kuweka vilivyotumika akimwambia mwenye garikwamba vilikuwa vimenoki (haribika), anaiba. Wakati unapodanganya juuya hali ya paa ya nyumba yako ili kufanya thamani ya mauzo yakekupanda, unaiba. Wakati wowote tunapowasilisha kitu kisicho

37

Page 39: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

halisi-mfano tunapopitisha saa feki ya Rolex badala ya ile halisi,tumemwibia yule aliyenunua.

Ukweli, hata kwa mtu anayejihudumia mwenyewe (mfano hotelini,akijihudumia isivyopaswa), ni wazi kwamba tabia hiyo inaonwa kwa ukaribu sana. Je, twataka kuendelea kufanya biashara na nani? Na mtuambaye tabia yake inakueleza wazi kuwa waweza kumwamini. Wakatifundi makanika ajapo kwangu na kuniambia, Bwana Wilson gari yakohaihitaji marekebisho yoyote, nitakuwa na hakika ya kuendelea kutumiahuduma zake na pia kuwaambia marafiki zangu juu yake.

Udanganyifu

Kushindwa kuwapatia watu mishahara yao ya haki pia ni kuwaibia (Rum.13:7-8). Kila wakati tunapokataa kumpa mtu fedha anazostahili tunafanyaudanganyifu. Wakati wowote ninapozuia fedha imstahiliyo mtu,tunawadanganya. Ikiwa nina kitu ambacho kwa haki ni mali yako lakinininakataa kukupatia kitu hicho, mimi ni mwizi.

Ikiwa nakopa fedha kutoka kwako na sikurudishii tena, na sifanyi jitihadayoyote ya kuwasiliana tena nawe juu ya mkopo, lakini kirahisi kabisanaamua kutokukulipa, ninakuibia. Ikiwa kwa bahati mbaya gari yanguinaacha njia na kuigonga gari yako na kuiharibu na sifanyi chochote iliuelewe kile nilichokufanyia, nimekuibia.

Ikiwa ninaahidi kukulipa mshahara fulani na kisha nashindwa kutunzaahadi yangu, nimekuibia. Nawafahamu waajiri ambao kwa kawaidahuwatia hamasa wauzaji wao kwa kuwaahidi bakshishi* fulani. Hata hivyo,wakati mmoja wao anapofikia lengo lililowekwa ili kujipatia zawadi,wanaambiwa kwamba kihalisia hawakufanya hivyo. Aidha walishindwakuuza kitu fulani au hawakuona maandishi madogo (ambayo awalihayakuwepo) yaliyoweka masharti kwamba, walihitaji kuwasiliana na ofisiyao wiki mbili kabla ili kuwafahamisha waajiri kuwa walikuwa karibu kufikiakiwango. Kwa maneno mengine, mwajiri aliwadanganya wafanyakaziwake.

Twaweza pia kumdanganya Mungu kwa kushindwa kumpatia yeyesehemu ya mapato yetu. Malaki 3 yatuambia kwamba kiwango kidogoMungu atakacho ni asilimia-kumi ya mapato yetu. Hutupatia sisi talanta,raslimali, vitu, uwezo, nafasi na baraka za vitu na hutuomba tumpatiesehemu tu ya mapato yetu. Akiwa ni Mungu wa haki hachukui zaidi kutokakwa maskini zaidi ya afanyavyo kwa tajiri, na wala hachukui zaidi kwa tajirizaidi ya afanyavyo kwa maskini. Kila mmoja hutoa asilimia-kumi. Kamaunapenda kutoa zaidi ni vizuri kwako lakini chote kinachohitajika niasilimia-kumi.

38

Page 40: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Wizi Unaofadhiliwa na Serikali

Siku moja Mfalme Ahabu aliamua kwamba anataka sehemu fulani ya kitukilichomilikiwa na mtu aitwaye Nabothi (1 Wafalme 21). Alitoa ofa ilianunue kitu hicho lakini alishindwa. Nabothi hakuwa tayari kukiuza.Mfalme alikasirishwa sana juu ya jambo hilo, lililomsumbua mkeweYezebeli. Kisha walifanya shauri kumnasa Nabothi atende kosa la jinaihivyo basi angeuawa na kisha wangeingilia kati ili waitaifishe mali yake.

Mfalme na mkewe walikuwa wamefanya baadhi ya vitu vya hila vyenyekuchukiza sana lakini hili lilikuwa baya sana kiasi kwamba Munguakamtuma mtumishi wake Eliya, ili awafahamishe kuwa Mungu ameonawalichokitenda na angewahukumu kwa ajili ya hilo. Kama ambavyo watu binafsi hawapaswi kuiba, vivyo hivyo kwa serikali pia. Kupitisha sheria zakuchukua vile vinavyomilikiwa na raia binafsi hakulifanyi tendo lile kuwa nihalali.

Swali: Wakati siendi mlango unaofuata na kuiba fedha kutoka kwa jiraniyangu; je! yawezekana kumwibia, kwa kuipigia kura sheria ambayo bilahaki itataifisha fedha zake alizozipata kwa taabu kwa ajili ya mustakabali*wangu (au faida yangu)?

Njia ya kibiblia ya kujipatia utajiri sio kwa kuchukua vile vinavyomilikiwa na wengine bali kupitia kazi, kujitoa dhabihu, imani na ukarimu. Ndiyo, kunanyakati ambapo watu huachwa bila njia ya kujihudumia wenyewe. Watuhawa wanahitaji hisani yetu ili waweze kutembea kwa miguu yao. LakiniBiblia aiioni hisani kama chanzo cha kudumu cha mapato bali kama hatuaza muda tu.

Kumilikiwa na Mali Tunazomiliki

Kila kitu tulichonacho chaweza kurejeshwa nyuma kwenye wema waMungu. Ni yeye anatufanya tayari kuzalisha na kumiliki vyote tulivyonavyo. Ni muhimu kwa afya zetu za kiroho kukumbuka hili. Kama tukishindwahapa, basi tuko katika hatari mbaya ya kumilikiwa na mali zetu.Tunashikilia baraka hizi kama zawadi zinazopaswa kuangaliwa kwa ajili ya Mungu na chini ya Mungu. Kadri turuhusupo kwa haraka vitu kututawala,vitu hivyo huacha kuwa baraka na kuwa vijisanamu vya miunguvinavyotawala roho zetu.

Ukarimu huzuia kwa kiasi kikubwa tabia hiyo yenye hatari. Kutunza familiazetu kubwa, kutoa kwa mashirika ya wema (yenye kuwasaidia maskini,wasiojiweza au wahanga) na Makanisa, kuwahudumia wengine wakatiwawapo kwenye mahitaji; ni njia za kutukumbusha sisi kwambatumebarikiwa kuwa baraka kwa wengine, na sio kujilimbikizia wenyewe.

39

Page 41: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Watu wakumbukao kwamba vyote wanavyomiliki vimetoka kwa Munguhawagubikwi na huzuni pindi wanapoondokewa na mali zao au kwa njiafulani wanaposumbuka na kushuka kwa mapato. Wanajua kwamba kamaMungu alivyowabariki wao wakati uliopita, anaweza na atafanya hivyo kwa siku zijazo. Yeye ni asili kamilifu ya jinsi walivyo na ya vyote walivyonavyo.Kwa watu wa imani, hakuna haja ya kuiba kutoka kwa mwingine kwasababu wanajua kwamba Mungu hubariki kazi zilizojaa imani.

Kutoka 20:15(Amri ya Nane) Usiibe.

Mwanzo 1:27-28Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungualimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Munguakawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke,mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, nandege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu yanchi.

Mithali 6:6-11Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapatehekima. Kwa maana yeye hana akida, wala msimamizi, walamkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu,utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Badokulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upateusingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Nauhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Waefeso 4:28Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kaziiliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu chakumgawia mhitaji.

2 Wathesalonike 3:10Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

40

Page 42: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Tisa

Sema Ukweli

Yesu alisema, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima…” (Yohana 14:6).Mungu aliye Kweli, kila kitu kinyume na ukweli kiko kinyume naye. Hiiinatusaidia kutambua kwa nini Sulemani alisema kuwa Mungu huchukiandimi za uongo na mashahidi wa uongo (Mithali 6:16-19). Mwenendo huokwa ujumla huwasilisha kimakosa Mungu alivyo, pia tunavyopaswa sisikuwa kama watoto wake wa kike na wa kiume; ndio maana maandikodaima yanaweka tabia hiyo katika hali mbaya kadri inavyowezekana.

Wakati Paulo anatuambia kwamba daima tunapaswa kusema ukwelikatika upendo (Waefeso 4:25), wengi wetu yawezekana hutumia mudamwingi kusema nusu-ukweli (uongo)…na si “katika upendo”! Wakatimwenye madaraka anatuuliza kwa nini ripoti haikuwa tayari, tunampahabari ya kuhuzunisha juu ya watoto wagonjwa ambao kwa kwelihawakuwa wagonjwa, tumedanganya. Wakati askari polisianapotukamata kwa kuendesha kwa kasi, tunamwambia kwamba tunaharaka kwenda kumwona baba yetu kabla hajafa (sawa, siku mojaatakufa, kwani hatakufa?), tunadanganya. Wakati tuwaambiapo marafikizetu kwamba tunajipatia fedha nyingi kumbe sivyo, basi tunadanganya.Na habari mbaya juu ya haya yote ni kwamba Mungu hafikiri hili kama nijambo lenye kupendeza, analichukia.

Leo kudanganya ni jambo lenye kutakiwa sana. Wana-matangazohutuambia majaribio yao kuwa yamethibitisha ubora wa vitu vyao zaidi yavile wanavyoshindana navyo na kumbe daima wanadanganya.Wanasiasa hutupatia ahadi ambazo hawana nia ya kuzitimiza wakatiwagombeapo nafasi. Watumishi huwaambia wenzao juu ya maelfuwanaofikiwa na makanisa yao, kumbe wanashindwa kuona kwambawanajumuisha katika kiwango hicho wale ambao huvutwa tu na jengo lakanisa. Kwa makusudi, wajenzi hutudanganya juu ya gharama za ujenziwa nyumba zetu. Tunadanganya juu ya umri wetu, uzito wetu na maksi zawatoto wetu. Na tena, Mungu huchukia tabia hiyo.

Kudanganya hupunguza uwezo wa wengine kutuamini. Wakati manenoyetu yachukuliwapo kwa wepesi, matarajio ya mafanikio katika biasharaau katika mahusiano huwa madogo, tena kwa muda mrefu. Kwa upande

41

Page 43: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

mwingine, wale watunzao ukweli, maelezo ya kweli yenye kukubalika, nauwasilishaji sahihi wa nani-nini-wapi-lini, hawa ni watu tunaotaka kuwanao, na kushirikiana nao maisha yetu.

Aina moja maalum ya uongo ambayo inaweza kuharibu taifa ni kiapo chauongo; kudanganya kwa kuapa (Kumbukumbu 19:16-21).

Mfumo mzima wa haki utavunjikavunjika katika vipande kama hatuwezikuamini ushahidi wa kimahakama. Kihistoria, hii ndio sababu adhabu kwamakosa yenye mtindo huu wa uongo huwa ni kali sana. Katika Israeli yaAgano la Kale adhabu ya kiapo cha uongo ilikuwa ni adhabu ambayoingeweza kumwondosha kabisa yule aliyeapa kwa uongo kama alikuwaamekwishaaminika. Kwa maneno mengine, ikiwa nilidanganya kwa kuapa kuhusu kumshuhudia mwuza duka aliyekabwa, ningepaswa kulipa maliposawa ya adhabu ambayo mtuhumiwa (ambaye kwa kweli hakumkabamwuza duka) angelipa baada ya ushuhuda wangu kuaminiwa.

Aina nyingine ya kudanganya ni usengenyaji. Hii hutokea wakati mtuhutafuta kuharibu heshima ya mwingine. Usengenyaji hutokea wakatinidanganyapo juu ya mambo ya mshindani wangu katika biashara.Usengenyaji hutokea wakati mtu aongeapo jinsi ambavyo mkewe daimahusahau kuweka urari katika kitabu cha hundi* ya fedha wakati ukweli nikwamba alisahau mara moja tu! Ni usengenyaji kwa mke kuwaambiawasichana majirani zake jinsi mume wake anavyomtendea kamamtumwa, kutomruhusu kamwe kutumia hata kiwango kidogo cha fedhabila ruhusa yake, wakati ukweli ni kinyume chake. Ni usengenyeji wakatitunapobuni habari ya kumdhalilisha mpinzani wa mgombeatunayempenda katika siasa.

Hata hivyo, kuna matukio machache wakati kusema ukweli -kuhusishamaelezo yote - sio mbinu sahihi. Wakati Rahabu alipodanganya ilikuwalinda wapelelezi kutoka Israeli alisifiwa na Mungu kwa kufanya hivyo(kumbuka kwamba jina lake liko katika “Ukumbi wa Imani wa Heshima”katika Waebrania 11). Katika nyakati za vita, kitendo cha kuficha sehemuya ukweli ni muhimu. Hakika kuna matukio wakati mtu binafsi au taasisi haina haki juu ya habari iliyoombwa: kwa mfano, kuwaficha Wayahudinchini Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Watu watakao kumpendeza Mungu, watamanio maisha yaliyojaamafanikio katika kila eneo na katika kila jaribio, watakuwa ni watuwaliojitoa kwa ajili ya kweli. Iwe ni mahusiano ya muda mrefu au biasharaya muda mrefu, wale walio na heshima ya kuwa wakweli daimawataongoza katika mchezo.

42

Page 44: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Kutoka 20:16(Amri ya Tisa) Usimshuhudie jirani yako uongo.

Kumbukumbu 17:6Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili,au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja.

Kumbukumbu 19:18-19Nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu yanduguye; ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyianduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Mithali 19:5Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongohataokoka.

Waefeso 4:25Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwamaana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.

43

Page 45: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;
Page 46: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Sura ya Kumi

Tosheka

Rafiki yako mpendwa alipandishwa kazi yenye mshahara mkubwa, jiraniyako alijinunulia gari zuri wakati wewe bado unaendesha lile la zamaniambalo limeunganishwa kwa nyaya na misumari. Haya yote yanakuathirikwa namna gani?

Wengi wetu kwa kweli hatujishughulishi na uuaji au kuabudu mbele yasanamu lakini amri hii ya kujiepusha kutamani kile kinachomilikiwa namwingine ni kweli inahusiana na wengi wetu. Iwe ni kwa kusikika sanakwenye luninga au radio, mawakala wa matangazo wanatutaka tuwetusiotosheka na vile tulivyonavyo. Wakati mwingine inaonekana kwambautamaduni wetu kwa jumla unachochewa na matakwa yasiyozimika yakuhitaji vitu zaidi na zaidi na umepigwa na tauni* ya hisia za kutotosheka.

Sasa, amri hii haihukumu matakwa. Hakuna chochote kibaya katikakutaka vitu au kutafuta kupata mafanikio makubwa. Swali hapa lingekuwakwa nini unahitaji vitu hivi? Ni kwa sababu unataka uonekane mwema aubora kuliko jirani yako? Ni kwa urahisi tu wa kutaka heshima? Ni kwasababu umiliki wa vitu vingi zaidi na zaidi vitakusaidia kuamini kuwaMungu anakupenda? Ikiwa hivi ndivyo vinavyochochea matakwa yako,basi kuna tatizo.

Kuwa na nia ya kutunza familia zetu, kuacha urithi kwa wajukuu zetu,kuwajali wengine au kuwa kadri tuwezavyo kuwa ni matakwa yenyekuheshimiwa. Lakini ikiwa matakwa yetu yaliyojificha ni kutamani utukufuau heshima basi tutakuwa na matatizo. Katika kujihusisha kwangu na kaziza wema na uwakala wa kusaidia zaidi ya miongo* mitatu (miaka 30)naweza kukuambia kuwa asilimia kubwa ya watu wanachochewa natamaa. Wanakuwa wanahusika na jitihada hizo ili kutamani sifa kutokakwa wengine, waonekane kama “watu wazuri”, na kujipatia heshimamaalumu kutoka kwa marafiki zao.

Kutamani kunaweza kukua kama saratani* katika moyo wa kazi zetu namahusiano. Kimyakimya inakula kwenye kiini hadi ganda la mwonekanowetu wa nje linapovunjikavunjika vipande, ikidhihirisha utupu wa madaiyetu ya tabia njema na heshima. Tofauti na kuua, kuiba au kudanganya,amri hii ya kipekee haielekezi kuzuia kitendo bali kuzuia tabia.

45

Page 47: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Biblia hufundisha kwamba tamaa huleta matatizo makubwa katika familiazetu (Mithali 15:27). Yawezekanaje isishindwe kufanya hivyo? Watuwenye tamaa wamejazwa na hofu ya vitu; nguvu zao kwa ujumlazimeelekezwa kwenye umiliki wa mali. Lakini si kwamba tamaa huletamatatizo katika familia zetu tu lakini pia katika Kanisa, mahali petu pa kazina katika jamii kwa ujumla.

• Kutamani sifa, mamlaka na heshima ya kiroho kutaharibu mfumowa mahusiano yenye siha ndani ya jumuia ya Kanisa.

• Kutamani utajiri na mafanikio ya washindani wetukutatusababisha tutake mali zao kwa nguvu na hivyo kuuhesabiahaki uongo wetu juu ya mali au huduma zao.

• Kutamani ukuu juu ya raia wenzetu wapendwa kwa ajili yamustakabali wetu wenye ubinafsi hutupeleka kwenye daraja lachuki, ukanaji wa wajibu binafsi na kujihesabia haki kwa kupuuzahaki za wengine juu ya mali na vitu vyao wanavyomiliki.

• Kumtamani mke wa jirani yetu, nyumba, biashara au akaunti yake ya benki ni kusema kuwa hatuna shukrani kwa jinsi au vile Mungu alivyotuzawadia sisi. Hii ndio sababu watu wenye tamaa huzamakwenye rindi* la madeni. Hawawezi kufanya kazi kwa uvumilivukwa kile wanachokitaka, wakati huohuo wakitumaini katikaMungu; lakini hutaka matakwa yao yenye tamaa kutimizwa kwaharaka. Lakini tamaa haiwezi kamwe kutimizwa.

Kutamani huambatana na imani kwamba majirani zetu hawastahili kuwana vile walivyonavyo au wasiwe na vingi kama sisi tulivyonavyo. Kutamanihutiwa nguvu na kiburi. Watu wenye tamaa hawawezi kusaidia bali waowenyewe hujiweka katika hali ya kuwa bora kuliko wengine walivyo. Au,katika hali nyingine, wanawaweka majirani zao katika nafasi ya kuonekana wasiofaa kuwa na vitu wanavyovimiliki.

Kutamani hutufanya kuwa wabaya, uharibu mfano (taswira) wa Mungundani yetu. Wakati roho ya Ukristo huchochewa na nia ya kutumikiawengine, yaani kuwa “kwa ajili” ya afya zao na hali zao: kutamanihutuweka katika nafasi ya kuwa kinyume na wengine. Zaidi ya kutakakuyatoa maisha yetu kwa wengine, tunaangalia njia ya kuyatoa maisha yajirani yetu kwa ajili yetu.

Kutaka kujipatia zaidi katika maisha si dhambi. Kutaka kile kilicho chamwingine ndio dhambi. Kufanya kazi ili upate zaidi si vibaya. Hata hivyo,kuzifungia nafsi zetu kwenye vile tunavyomiliki ni upumbavu. Zaidi ya yote, ni “vitu” kiasi gani vitatufanya tujisikie wenye thamani au kutoshelezwa?Kwa mtu mwenye tamaa, kutamani zaidi ni shimo lenye giza.

46

Page 48: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Watu wenye tamaa wanatafuta kujaza utupu ndani ya roho zao kileambacho Mungu pekee aweza kukijaza. Ukitoshelezwa na Mungu pekeena kuona kila kitu kingine kama vikolezo juu ya keki, yote yatakuwa shwari. Tosheka kwamba Mungu amekukubali kupitia imani yako katika YesuKristo na kile alichokifanya kwa ajili yako miaka 2,000 iliyopita msalabani,kisha ona kila kitu na kitu kingine chochote kuwa vinakuja kama ziada, nahutatamani kamwe.

Kutoka 20:17Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako;wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake,wala punda wake, wala chochote alichonacho jirani yako.

Luka 12:15Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtuhaumo katika wingi wa vitu vyake alivyonavyo.

Mathayo 6:24-34Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maanaatamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana nahuyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mlenini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidiya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, walahawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbingunihuwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenuambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkonommoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua yamashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti,nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yakeyote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Munguhuyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwakalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? AuTuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwasababu Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yotemtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa keshoitajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

47

Page 49: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

MAELEZO YA MANENO

Amali: Mambo yote mema yenye kuthaminiwa na jamii husika.

Ambatisha: Unganisha

Ari: Nguvu yenye msukumo moyoni.

Bakshishi: Zawadi, nyongeza au ziada mtu apewayo kuliko kiwango cha kawaida.

Fasili: Fafanua au pambanua, eleza maana.

Furuweli: Chombo chenye meno kishikacho mnyororo wa baiskeli kwenye tairi ya nyuma.

Hundi: Cheki au kitabu maalumu cha kuchukulia fedha benki.Kiambishi: Kipande au sehemu ya neno inayowekwa kwenye mzizi

wa neno, nayo hubeba maana ya kisarufi ili kukamilisha maana ya mzizi iliyokusudiwa. Mfano, A-na-tembe-a: A-, -na-, ni viambishi awali ambavyo hutokea kabla ya mzizi ambao ni –tembe-; na –a ni kiambishi tamati kinachokamilisha maana ya neno. Kiambishi A- hudokeza nafsi ya tatu umoja, -na- hudokeza wakati uliopo. (Katika kitabu hiki neno kiambishi-awali limetumika kama neno la nyongeza litumiwalo bila sababu za msingi)

Kurohosha: Kufanya au kulipa jambo tafsiri ya kiroho na si katika uhalisia wake.

Luninga: Televisheni au Kiona mbali.

Maada: Kitu chochote chenye uzito na kiwezacho kuchukua nafasi.

Mwongo: Kipindi cha miaka kumi.

Munyu: Chumvi; -aina ya madini iwekwayo kwenye chakula ili kukoleza ladha.

Mustakabali: Hatima, mwisho.

Nasibu: Kwa bahati, bila kupangwa au bila kuwapo kwa makubaliano fulani.

Rindi: -enye kiwango kikubwa au kingi; kina kirefu.

Sheheni: -enye kujaa, jaza.

Siha: Afya.

48

Page 50: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;

Stahiki: -enye sifa au –enye kukubalika.

Tauni: Ugonjwa usambaao na kuua kwa haraka jamii kubwa ya watu.

Urari: Mlinganyo, ulinganifu wa vitu viwili au zaidi, usawa n.k.

Ushuhuda-shirika: Ushuhuda unaojumuisha kundi la watu k.v. Kanisa, na si mtu mmoja mmoja.

Usihiri: Hali ya kuwa na nguvu za kimiujiza zenye kuweza kutenda jambo (sihiri- nguvu zenyewe).

Vielelezo-vioneshi/Zana-oneshi: Vitu vitumikavyo katika kusaidia kuongeza ufahamu juu ya kitu fulani k.v. sanamu, picha n.k.

Wakia: Kipimo cha gramu 353; sehemu moja ya kumi na sita ya ratili (kipimo kitumikacho sana katika uuzaji wa dhahabu).

49

Page 51: SHERIA MUHIMU ZAIDI KATIKA KUISHI - bucer.de · tunakupatia kitabu chake juu ya Uchumi wa kibiblia kama mwongozo wa maisha yenye mafanikio “Kanuni za Mafanikio katika Biashara ”;