1
6 - - 7 MTANZANIA IJUMAA OKTOBA 25, 2019 MTANZANIA IJUMAA OKTOBA 25, 2019 TOLEO MAALUM MAFANIKIO YA TAFORI TOLEO MAALUM MAFANIKIO YA TAFORI UTANGULIZI Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) ilianzishwa kwa Sheria Na. 5 iliyopitishwa mwaka 1980 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kupitia Sheria hiyo Taasisi ilipewa jukumu la kufanya, kusimamia, na kuratibu tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi ya teknolojia bora na uendelezaji wa misitu nchini. Katika huu muda wa miaka minne, TAFORI imetekeleza majukumu yake kwa kufuata Mpango wa II wa Utafiti wa Misitu wa Taifa (National Forestry Research Master Plan (NAFORM II: 2011 - 2020). Kupitia Mpango huo vipaumbele vifuatavyo vya utafiti vimeainishwa: Usimamizi na uendelezaji wa Misitu ya Asili; Misitu ya Jamii na Misitu Shamba; Misitu ya kupandwa na Uborehaji wa Miti; Ukadiriaji wa Mazao ya Misitu: Uchumi-Jamii: Sera na Ugani; na Kazi Misitu na Matumizi ya yake. Pia Taasisi imepewa jukumu la kulea utafiti wa ufugaji nyuki hapa nchini kuanzia mwaka huu (2019). Pamoja na Makao Makuu ya Taasisi kuwa Morogoro, kuna vituo saba vya utafiti vilivyopo Dodoma, Kibaha, Malya, Moshi, Mufindi, Tabora, na Lushoto. Dira ya TAFORI ni kuwa kitovu cha mafanikio katika tafiti za misitu, ukuzaji wa teknolojia bora na usambazaji wa taarifa za kisayansi zinazohusu misitu Tanzania. Dhamira ya TAFORI ni kufanya, kusimamia na kuratibu tafiti za misitu, kusambaza taarifa za kisayansi na kukuza teknolojia zinazofaa katika maendeleo ya misitu na maliasili Tanzania. M A F A N I K I O YALIYOPATIKANA KATIKA KIPINDI HUSIKA Katika kipindi cha miaka minne hadi sasa, Taasisi imeendelea kufanya shughuli zake za kitafiti na maendeleo. Katika kipindi cha miaka minne, Taasisi imeweza kufanya tafiti mbalimbali. Yafuatayo ni maelezo ya baadhi ya tafiti ambazo zimefanyika: Kubaini Chanzo cha Kufa/ kukauka kwa Miti katika Mashamba ya Miti ya Serikali na Sekta Binafsi Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa miti ya Misindano na Cypress iliyopandwa katika Shamba la Miti la Meru-Usa ilinyauka na kukauka kutokana na usimamizi hafifu wa kilimo cha mfumo wa “Taungya”. Hii ilisababishwa na baadhi ya wananchi wanaolima mazao yao ya chakula ndani ya Shamba la Miti kukata baadhi ya mizizi na kupogolea miti zaidi ya kiwango kinachotakiwa na kusababisha baadhi ya miti kukauka. Miti ya Misindano na Cypress iliyopandwa katika Shamba la Miti la Sao Hill ilionekana kukauka kutokana na wadudu waharibifu aina ya “Pine needle aphids” (Eulachnus rileyi) na “Cypress aphid” (Cinara cupressivora). Wakati huo huo miti ya Misindano na Grevilea iliyopandwa Shamba la Miti Kilimanjaro Magharibi ilikauka kutokana na ugonjwa wa kuoza kwa mizizi (root rot disease) unaosababishwa na “fangasi” jamii ya Armillaria. Vilevile, utafiti ulibaini kuwa miti ya Misindano iliyopandwa Shamba la miti Kawetire na Mbizi ilikauka kutokana na upungufu wa madini aina ya “Boroni” kwenye udongo. Miti aina ya Misindano katika Mashamba ya Miti yanayosimamiwa na “Programu ya Panda Miti Kibiashara” yaliyoko katika Mikoa ya Njombe, Iringa, Morogoro (Kilombero) na Ruvuma, iliyopandwa mwanzoni mwa mwaka 2018, ilikauka kutokana na ugonjwa aina ya “Pitch cánker” unaosababishwa na “fangasi” aina ya Fusarium circinatum. Katika kipindi hicho, kumejitokeza mdudu aitwaye Paranaleptes reticulata (Girdling beetle) anayeshambulia miti aina tofauti kwa kuikata na hatimaye miti hiyo kukauka na kuanguka. Taasisi ilipendekeza namna mbalimbali za kudhibiti kufa/kukauka kwa miti ili kupunguza hasara ambayo Taifa linaipata kutokana kufa kwa miti. Matokeo ya utafiti huu yataisaidia Serikali na wadau kukabiliana na majanga ya wadudu waharibifu wa misitu. Kutokea kwa wadudu waharibifu na magonjwa kwenye misitu kwa sasa inatokana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo mabadiliko hayo yameongeza wigo wa usitahimilivu wa wadudu JAMHURI YA MUUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA MAFANIKIO YA TAASISI KUANZIA 2015 HADI 2019 ULIZI S kt Bi f i Dr. Revocatus Mushumbusi Kaimu Mkurugenzi Mkuu - TAFORI Vyanzo Maji Wilayani Mwanga Kwa muda mrefu kumekuwepo na kupungua kwa maji katika vyanzo vinne ya maji katika Wilaya ya Mwanga. Maeneo haya ni Kindoroko, Minja, Kamwala na Mramba. Upunguaji wa maji hayo umekuwa ukihusishwa na uwepo wa miti ya kigeni aina ya Acrocarpus na aina mbali mbali za Mikaratusi. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti hayakuwa na miti ya kigeni mipya au michanga zaidi ya ile iliyopandwa miaka ya 1900 ambayo utumiaji wake wa maji ni mdogo kutokana na kuwa na umri mkubwa. Hata hivyo ilionekana kuwepo na miti michache ya umri mdogo aina ya Acrocarpus lakini ilikuwa mbali sana na vyanzo vya maji. Iligundulika kuwa chanzo cha kupungua kwa maji ni shughuli za kibinadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vya maji na kandokando ya mito. Sababu nyingine ni kuharibika kwa misitu ya hifadhi na umwagiliaji unaofanyika bila utaratibu wa aina yoyote. Matokeo ya utafiti huu yanatoa ujumbe kuwa, upungufu wa maji katika maeneo kadhaa nchini unatokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika katika maeneno husika, na sio kusingizia miti. Kikubwa Muhimu ni Mamlaka mahalia kuelimisha wananchi wanatakiwa waelimishwe naili kujua kutambua athari za uharibifu wa mazingira zitokanazo na kukata miti au ufyekaji misitu hovyo. Kusambaza Taarifa za Moto wa Misituni Taasisi imekusanya na kusambaza taarifa kuhusu moto wa misituni kwa kutumia takwimu za “satellite”. Taarifa inaonesha kuwa moto wa misituni bado ni kubwa na limeathiri eneo la misitu lenye kilometa za mraba 100,903 (ambalo ni sawa na asilimia 11.14 ya eneo lote na Tanzania Bara). Maeneo yaliyoathirika ni mikoa ya Lindi, Katavi, Mbeya, Tabora na Ruvuma. Wizara kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kuelimisha umma kuhusu kuchukua tahadhari na kuzuia moto wa misitu. Matokeo ya utafiti huu, yatasaidia Serikali na Wadau wengine kujiweka tayari na pia kuchukua tahadhari na majanga ya moto kwenye maeneo yenye misitu. Uanzishwaji wa Majaribio ya Kiutafiti ya Upandaji Miti Taasisi ilifanikiwa kuanzisha majaribio 30 ya kiutafiti ya upandaji sahihi wa miti kwenye eneo la takribani hektari 100. kwa kufadhiliwa na Mfuko wa Misitu nchini. Majaribio haya yako kanda ya Ziwa, Kati, Mashariki, Kaskazini na Nyanda za juu Kusini. Aina ya miti iliyopandwa kwenye majaribio hayo ni pamoja na Misindano (Pine) tofauti, Mikaratusi tofauti, Msanduku (Cypress), Mvule (Milicia excelsa), Mkangazi (Khaya anthotheca), Mfudufudu (Gmelina arbórea), Mkenge (Albizia lebec), Mkwaju (Tamarindus indica), Migunga (Acacia spp), Mwerezi (Cedrella odorata).. Kutokana na matokeo ya majaribio haya itakuwa rahisi kubaini ukuaji wa miti mbalimbali wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakiathiri mwenendo wa ukuaji wa miti maeneo kadhaa nchini. Utafiti juu ya Ufuatiliaji wa Uoto unaojitokeza baada ya Mianzi kufa katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Msitu wa Udzungwa Scarp, Wilaya ya Kilolo Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa chanzo cha kufa kwa mianzi hiyo ni umri kwa maana kuwa mianzi inapofikisha umri wa miaka 60 hadi 70 hutoa maua na baadae kufa kizazi chote. Kwenye maeneo ambayo mianzi ilikufa, uoto wa asili wa miti unaibukia. Spishi aina ya Polyscias fulva (Mdeke); Macaranga spp (Mpalala) na Dombeya burgessiae (Mtowo) ndio zinatawala katika uotaji kwenye maeneo hayo. Vilevile, utafiti uligundua kuwa mbegu za mianzi zilizodondoka zenyewe katika udongo zilikuwa zinaota. Hali hii inaashiria kuwa hakuna wasiwasi tena juu ya uharibifu wa ardhi kwenye maeneo yaliyokuwa yameachwa wazi baada ya mianzi kufa. Matokeo ya utafiti huu yatawasaidia Maafisa Ugani kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya mbinu bora ya kuhifadhi misitu ya asili kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Uanzishwaji wa Mashamba ya Mbegu Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini, Tanzania Mashamba ya mbegu za miti aina ya Misindano na Mikaratusi yenye ukubwa wa hekta 10 yalianzishwa wilayani Mufindi na Lushoto. Mbegu za kuanzisha mashamba hayo zilikusanywa kutoka kwenye miti yenye ubora wa kutoa mbegu iliyoko Njombe, Mufindi na Lushoto. Mashamba haya yana umri wa mwaka mmoja na yanaendelea vizuri. Mashamba haya yanaendelea kutunzwa na Mbegu husika zitatumika katika waharibifu na magonjwa yanayoathiri miti/misitu. Utafiti juu ya Umri wa Uvunaji wa Miti ya Misindano na Misaji Utafiti huu ulifanyika ili kubaini umri sahii wa miti aina ya misindano (Pines) na misaji (Teak). Vigezo vilivyotumika kubaini umri sahihi ni pamoja na takwimu za ukuaji wa miti msituni (ongezeko la ujazo), uchumi na ubora wa mbao. Utafiti umeonesha kuwa umri wa kuvuna miti aina ya misindao kwa ajili ya matumizi ya mbao kwa kutumia vigezo vilivyotajwa hapo juu unaweza kushushwa toka miaka 25 hadi 18. Miti ya Misindano pia inaweza kuvunwa ikifikisha umri wa kuanzia miaka 11 kwa ajili ya uzalishaji wa karatasi. Kwa miti ya misaji umri unaweza kushushwa toka miaka 40 hadi 20 kwa ajili ya matumizi ya mbao. Matokeo haya yanaonesha kuwa miti hii inakua haraka kwa sasa kuliko miaka iliyopita na haya yanaweza kuwa matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. Hii itasaidia serikali na watu binafsi kupata mapato mapema badala ya kusubiri miaka mingi zaidi kama ilivyozoeleka bila kuathiri ubora wa mazao. Pia kumekuwa na mwitikio wa wananchi kupanda miti baada ya umri wa kuvuna kupungua. Matokeo haya yatachangia maendeleo ya uchumi wa viwanda nchini kwa kuongeza malighafi za kutumika katika viwanda vya misitu na kupatikana kwa muda mfupi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Utambuzi na Uhifadhi wa Miti iliyopo kwenye Bonde la Mto Rufiji Kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali, TAFORI ilifanya utafiti ili kutambua miti yote iliyopo kwenye eneo la mradi wa mto Rufiji ambako Serikali inajenga Bwawa kubwa la maji kuzalisha umeme katika Pori la Akiba la Selous. Iligundulika kuwa zipo aina 159 za miti katika pori hilo (ikiwa ni ndani na nje ya eneo la mradi wa kufua umeme). Katika eneo la mradi iligundulika kuwepo na aina 72 za miti ambapyo kati ya hiyo, aina nne tu za miti zinahitaji uangalizi maalum kwa mujibu wa IUCN. Miti hiyo ni Croton jatrophoides Dialium holtzii (Mpepete), Millettia micans (Pangapanga) na Dalbergia nitidula. Sampuli za miti yote iliyokutwa kwenye eneo la mradi pamoja na ile miti iliyoorodheshwa na IUCN ilikusanywa na kuhifadhiwa kwenye Herbarium ya Taifa iliyopo Arusha, TAFORI katika Kituo cha Lushoto na katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya rejea. Matokeo ya utafiti huu yatasaidia Serikali na Wadau mbalimbali kujua rasilimali zilizopo katika Pori la Akiba la Selous na kutengeneza mikakati ya kutunza aina ya miti inayohitaji uangalizi maalum. Kubaini Sababu za Kukauka kwa Sababu nyingine ni kuharibika kwa misitu ya hifadhi na umwagiliaji unaofanyika bila utaratibu wa aina yoyote. Matokeo ya utafiti huu yanatoa ujumbe kuwa, upungufu wa maji katika maeneo kadhaa nchini unatokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika katika maeneno husika, na sio kusingizia miti. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa chanzo cha kufa kwa mianzi ni umri kwa maana kuwa mianzi inapofikisha umri wa miaka 60 hadi 70 hutoa maua na baadae kufa kizazi chote. Kwenye maeneo ambayo mianzi ilikufa, uoto wa asili wa miti unaibukia. Uoto wa miazi kwenye Hifadhi Asilia ya Misitu ya Uzungwa Scarp Mdudu aina ya Paranaleptesi reticulata (Girdling beetle) akishambulia Mikaratusi katika Shamba la miti la Korogwe Maandalizi ya Sampuli kwa ajili ya Utafiti wa ubora wa Mbao Utafiti juu ya uzalishaji wa baadhi ya Miti ya asili kwa kutumia njia ya Vikonyo kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali kupitia juhudi za Serikali na Wadau wengine. Udhibiti wa Miti vamizi katika maeneo ya malisho na mashamba Taasisi kwa kushirikiana na Taasisi za Elimu na Utafiti katika nchi za Uswisi, Kenya, Afrika kusini na Ethiopia inatekeleza mradi wa kudhibiti miti vamizi katika eneo la Usambara Mashariki na Kahe Moshi. Mradi huu wa miaka sita (2015 - 2021) una lengo la kulinda bioanuai, huduma zitolewazo na mazingira na uchumi wa jamii kwa kupunguza gharama na athari zinazotokana na miti vamizi katika mashamba na malisho ya mifugo. Mafaniko ya mradi huu ni pamoja na kuishirikisha jamii kwa kuipatia mafunzo ya vitendo juu ya namna ya kupambana na miti/magugu mashambani na kwenye malisho ambayo ni rafiki kwa mazingira na uchumi. Pia mradi huu unasomesha watanzania sita katika Shahada za Uzamivu (mmoja) na Uzamili (watano) katika vyuo mbali mbali hapa nchini ili waweze kulisaidia Taifa kudhibiti miti/mimea vamizi na athari zake katika rasilimali za asilia. Kushirikiana na Wadau mbalimbali kupanda miti kwa ajili ya nishati ya kuni Katika jitihada za Taasisi za kuboresha utunzanji wa misitu ya asili hapa nchini Taasisi imeshirikiana na taasisi mbalimbali kimeratibu upandaji miti kwa mfano katika eneo la Magereza Wilayani Lushoto lenye ukubwa zaidi ya Hekta 40, ambapo miti zaidi ya 50,000 aina ya Mikaratusi imepandwa, ambao hadi sasa ina umri wa miaka mitatu. Maeneo mengine ambapo miti imepandwa kwa ushirikiano na wananchi ni wilayani Handeni, Mkuranga, Morogoro na Moshi. Lengo la mradi huu wa upandaji miti ni kupunguza utegemeze wa miti kutoka kwenye misitu ya asili kwa ajili ya mahitaji ya nishati ya kuni. Upembuzi Yakinifu katika Shamba tarajiwa la Miti la Mpepo, Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma Taasisi ilifanya utafiti wa awali wa kubainisha hali ya hewa (mvua, joto, upepo, unyevunyevu), aina ya udongo na uoto wa asili uliopo katika maeneo ya shamba tarajiwa la miti ili kubaini ni aina gani ya miti inaweza kupandwa. Kulingana na hali ya hewa, udongo na uoto wa asili na vijishamba vidogo vya miti vilivyopo pembezoni mwa eneo la Mpepo, ilishauriwa kuwa miti aina ya Misindano (Pinus patula, Pinus tecunumanii, Pinus maximinoi), Mikaratusi (Eucalyptus saligna, Eucalyptus grandis, Eucalyptus maidenii) na Migrevilia (Grevillea robusta) ipandwe katika eneo husika. Matokeo ya upembuzi huu yamepelekea kuanzishwa Shamba jipya la Miti la Mpepo, Mkoani Ruvuma. TAFORI yathibitishwa kusimamia mamlaka ya kisayansi ya mimea kwenye mkataba wa CITES Mkataba wa kimataifa unaoshughulikia biashara ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka ujulikanao kama “Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Fauna and Flora – (CITES)” umeitambua TAFORI kuwa mamlaka ya kisayansi ya mimea Tanzania. Mkataba huu wa kimataifa umetokana na makubaliano baina ya nchi mbalimbali. Lengo ni kuhakikisha biashara ya kimataifa ya wanyama na mimea haiathiri au kupunguza uwepo wake. Kusambaa kwa taaarifa mbalimbali za hali hatarishi kwa mimea na wanyama kuliweka sababu kubwa wa uanzishwaji wa mkataba huu. Biashara ya kimataifa ya viumbe hai inakadiriwa kuwa na thamani ya mabilioni ya pesa. Biashara hii inatofautiana kati ya wanyama na mimea pia uhusisha mazao yatokanayo na wanyama na mimea kama vyakula, ngozi, magamba, mizizi, mbao na madawa. Kwakuwa biashara hii inavuka mipaka ya nchi, juhudi za kimataifa katika kusimamia matumizi sahihi ya bidhaa hii zinahitajika. Hivyo basi Taasisi itaendelea kutoa ushauri katika masuala yote ya kiutafiti yanayohusu rasilimali Misitu ili kuwa na biashara endelevu ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka. Uandaaji wa Mwongozo wa Kupanda Kloni za Mikaratusi Tanzania Mwongozo huu umeandaliwa kufuatia uhitaji mkubwa wa wadau mbalimbali wa upandaji wa kloni za Mikaratusi katika maeneo makubwa. Mwongozo huu unatoa maelezo ya kloni bora katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi ya Tanzania kwa kuzingatia taarifa za tafiti. Mwongozo unafafanua juu ya utunzaji bora wa kloni ili kupata mazao bora na kwa wingi. Maeneo yanayofaa na yasiyofaa kupanda kloni yamefafanuliwa bayana. Wadau wote wanaojihusisha na shughuli za upandaji miti wanaalikwa kusoma na kufuata mwongozo huo kwa ajili ya kupata mazao ya miti yaliyo bora na kuzuia matatizo ya uharibifu wa mazingira. Mwongozo huu unasambazwa kwa wadau ili usaidia kutoa elimu ili kuepukana na majawabu yanayokinzana ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa upandaji wa mikaratusi. HITIMISHO Katika kipindi cha miaka minne (2015 hadi 2019) Taasisi imeendelea vema kutekeleza majukumu yake. Tafiti ambazo zimefanyika zimechangia kwenye uhifadhi endelevu wa misitu yetu. Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na wadau wa maendeleo kwa kufanikisha tafiti hizi. Imeandaliwa na: Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania

MAFANIKIO YA TAASISI KUANZIA 2015 HADI 2019 YA TAASISI 2015...6 - MTANZANIA - 7 IJUMAA OKTOBA 25, 2019 MTANZANIA TOLEO MAALUM MAFANIKIO YA TAFORI TOLEO MAALUM MAFANIKIO YA TAFORI IJUMAA

  • Upload
    others

  • View
    14

  • Download
    1

Embed Size (px)

Citation preview

  • 6 - - 7MTANZANIA IJUMAA OKTOBA 25, 2019MTANZANIA

    IJUMAA OKTOBA 25, 2019TOLEO MAALUM MAFANIKIO YA TAFORI TOLEO MAALUM MAFANIKIO YA TAFORI

    UTANGULIZITaasisi ya Utafi ti wa Misitu Tanzania (TAFORI) ilianzishwa kwa Sheria Na. 5 iliyopitishwa mwaka 1980 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kupitia Sheria hiyo Taasisi ilipewa jukumu la kufanya, kusimamia, na kuratibu tafi ti na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi ya teknolojia bora na uendelezaji wa misitu nchini. Katika huu muda wa miaka minne, TAFORI imetekeleza majukumu yake kwa kufuata Mpango wa II wa Utafi ti wa Misitu wa Taifa (National Forestry Research Master Plan (NAFORM II: 2011 - 2020). Kupitia Mpango huo vipaumbele vifuatavyo vya utafi ti vimeainishwa: Usimamizi na uendelezaji wa Misitu ya Asili; Misitu ya Jamii na Misitu Shamba; Misitu ya kupandwa na Uborehaji wa Miti; Ukadiriaji wa Mazao ya Misitu: Uchumi-Jamii: Sera na Ugani; na Kazi Misitu na Matumizi ya yake. Pia Taasisi imepewa jukumu la kulea utafi ti wa ufugaji nyuki hapa nchini kuanzia mwaka huu (2019). Pamoja na Makao Makuu ya Taasisi kuwa Morogoro, kuna vituo saba vya utafi ti vilivyopo Dodoma, Kibaha, Malya, Moshi, Mufi ndi, Tabora, na Lushoto.

    Dira ya TAFORI ni kuwa kitovu cha mafanikio katika tafi ti za misitu, ukuzaji wa teknolojia bora na usambazaji wa taarifa za kisayansi zinazohusu misitu Tanzania.

    Dhamira ya TAFORI ni kufanya, kusimamia na kuratibu tafi ti za misitu, kusambaza taarifa za kisayansi na kukuza teknolojia zinazofaa katika maendeleo ya misitu na maliasili Tanzania.

    M A F A N I K I O YALIYOPATIKANA KATIKA KIPINDI HUSIKA

    Katika kipindi cha miaka minne hadi sasa, Taasisi imeendelea kufanya shughuli zake za kitafi ti na maendeleo. Katika kipindi cha miaka minne, Taasisi imeweza kufanya tafi ti mbalimbali. Yafuatayo ni maelezo ya baadhi ya tafi ti ambazo zimefanyika:

    Kubaini Chanzo cha Kufa/kukauka kwa Miti katika Mashamba ya Miti ya Serikali na

    Sekta Binafsi Matokeo ya utafi ti huo

    yanaonesha kuwa miti ya Misindano na Cypress iliyopandwa katika Shamba la Miti la Meru-Usa ilinyauka na kukauka kutokana na usimamizi hafi fu wa kilimo cha mfumo wa “Taungya”. Hii ilisababishwa na baadhi ya wananchi wanaolima mazao yao ya chakula ndani ya Shamba la Miti kukata baadhi ya mizizi na kupogolea miti zaidi ya kiwango kinachotakiwa na kusababisha baadhi ya miti kukauka. Miti ya Misindano na Cypress iliyopandwa katika Shamba la Miti la Sao Hill ilionekana kukauka kutokana na wadudu waharibifu aina ya “Pine needle aphids” (Eulachnus rileyi) na “Cypress aphid” (Cinara cupressivora). Wakati huo huo miti ya Misindano na Grevilea iliyopandwa Shamba la Miti Kilimanjaro Magharibi ilikauka kutokana na ugonjwa wa kuoza kwa mizizi (root rot disease) unaosababishwa na “fangasi” jamii ya Armillaria. Vilevile, utafi ti ulibaini kuwa miti ya Misindano iliyopandwa Shamba la miti Kawetire na Mbizi ilikauka kutokana na upungufu wa madini aina ya “Boroni” kwenye udongo. Miti aina ya Misindano katika Mashamba ya Miti yanayosimamiwa na “Programu ya Panda Miti Kibiashara” yaliyoko katika Mikoa ya Njombe, Iringa, Morogoro (Kilombero) na Ruvuma, iliyopandwa mwanzoni mwa mwaka 2018, ilikauka kutokana na ugonjwa aina ya “Pitch cánker” unaosababishwa na “fangasi” aina ya Fusarium circinatum. Katika kipindi hicho, kumejitokeza mdudu aitwaye Paranaleptes reticulata (Girdling beetle) anayeshambulia miti aina tofauti kwa kuikata na hatimaye miti hiyo kukauka na kuanguka. Taasisi ilipendekeza namna mbalimbali za kudhibiti kufa/kukauka kwa miti ili kupunguza hasara ambayo Taifa linaipata kutokana kufa kwa miti. Matokeo ya utafi ti huu yataisaidia Serikali na wadau kukabiliana na majanga ya wadudu waharibifu wa misitu. Kutokea kwa wadudu waharibifu na magonjwa kwenye misitu kwa sasa inatokana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo mabadiliko hayo yameongeza wigo wa usitahimilivu wa wadudu

    JAMHURI YA MUUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MALIASILI NA UTALII

    TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA

    MAFANIKIO YA TAASISI KUANZIA 2015 HADI 2019

    ULIZI S kt Bi f i

    Dr. Revocatus MushumbusiKaimu Mkurugenzi Mkuu - TAFORI

    Vyanzo Maji Wilayani MwangaKwa muda mrefu kumekuwepo

    na kupungua kwa maji katika vyanzo vinne ya maji katika Wilaya ya Mwanga. Maeneo haya ni Kindoroko, Minja, Kamwala na Mramba. Upunguaji wa maji hayo umekuwa ukihusishwa na uwepo wa miti ya kigeni aina ya Acrocarpus na aina mbali mbali za Mikaratusi. Matokeo ya utafi ti yamebaini kuwa katika maeneo yaliyofanyiwa utafi ti hayakuwa na miti ya kigeni mipya au michanga zaidi ya ile iliyopandwa miaka ya 1900 ambayo utumiaji wake wa maji ni mdogo kutokana na kuwa na umri mkubwa. Hata hivyo ilionekana kuwepo na miti michache ya umri mdogo aina ya Acrocarpus lakini ilikuwa mbali sana na vyanzo vya maji. Iligundulika kuwa chanzo cha kupungua kwa maji ni shughuli za kibinadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vya maji na kandokando ya mito. Sababu nyingine ni kuharibika kwa misitu ya hifadhi na umwagiliaji unaofanyika bila utaratibu wa aina yoyote. Matokeo ya utafi ti huu yanatoa ujumbe kuwa, upungufu wa maji katika maeneo kadhaa nchini unatokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika katika maeneno husika, na sio kusingizia miti. Kikubwa Muhimu ni Mamlaka mahalia kuelimisha wananchi wanatakiwa waelimishwe naili kujua kutambua athari za uharibifu wa mazingira zitokanazo na kukata miti au ufyekaji misitu hovyo.

    Kusambaza Taarifa za Moto wa Misituni

    Taasisi imekusanya na kusambaza taarifa kuhusu moto wa misituni kwa kutumia takwimu za “satellite”. Taarifa inaonesha kuwa moto wa misituni bado ni kubwa na limeathiri eneo la misitu lenye kilometa za mraba 100,903 (ambalo ni sawa na asilimia 11.14 ya eneo lote na Tanzania Bara). Maeneo yaliyoathirika ni mikoa ya Lindi, Katavi, Mbeya, Tabora na Ruvuma. Wizara kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kuelimisha umma kuhusu kuchukua tahadhari na kuzuia moto wa misitu. Matokeo ya utafi ti huu, yatasaidia Serikali na Wadau wengine kujiweka tayari na pia kuchukua tahadhari na majanga ya moto kwenye maeneo yenye misitu.

    Uanzishwaji wa Majaribio ya Kiutafi ti ya Upandaji Miti

    Taasisi ilifanikiwa kuanzisha majaribio 30 ya kiutafi ti ya upandaji sahihi wa miti kwenye

    eneo la takribani hektari 100. kwa kufadhiliwa na Mfuko wa Misitu nchini. Majaribio haya yako kanda ya Ziwa, Kati, Mashariki, Kaskazini na Nyanda za juu Kusini. Aina ya miti iliyopandwa kwenye majaribio hayo ni pamoja na Misindano (Pine) tofauti, Mikaratusi tofauti, Msanduku (Cypress), Mvule (Milicia excelsa), Mkangazi (Khaya anthotheca), Mfudufudu (Gmelina arbórea), Mkenge (Albizia lebec), Mkwaju (Tamarindus indica), Migunga (Acacia spp), Mwerezi (Cedrella odorata).. Kutokana na matokeo ya majaribio haya itakuwa rahisi kubaini ukuaji wa miti mbalimbali wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakiathiri mwenendo wa ukuaji wa miti maeneo kadhaa nchini.

    Utafi ti juu ya Ufuatiliaji wa Uoto unaojitokeza baada ya Mianzi kufa katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Msitu wa Udzungwa Scarp, Wilaya ya Kilolo

    Matokeo ya utafi ti yameonesha kuwa chanzo cha kufa kwa mianzi hiyo ni umri kwa maana kuwa mianzi inapofi kisha umri wa miaka 60 hadi 70 hutoa maua na baadae kufa kizazi chote. Kwenye maeneo ambayo mianzi ilikufa, uoto wa asili wa miti unaibukia. Spishi aina ya Polyscias fulva (Mdeke); Macaranga spp (Mpalala) na Dombeya burgessiae (Mtowo) ndio zinatawala katika uotaji kwenye maeneo hayo. Vilevile, utafi ti uligundua kuwa mbegu za mianzi zilizodondoka zenyewe katika udongo zilikuwa zinaota. Hali hii inaashiria kuwa hakuna wasiwasi tena juu ya uharibifu wa ardhi kwenye maeneo yaliyokuwa yameachwa wazi baada ya mianzi kufa. Matokeo ya utafi ti huu yatawasaidia Maafi sa Ugani kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya mbinu bora ya kuhifadhi misitu ya asili kwa faida yetu na vizazi vijavyo.

    Uanzishwaji wa Mashamba ya Mbegu Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini, Tanzania

    Mashamba ya mbegu za miti aina ya Misindano na Mikaratusi yenye ukubwa wa hekta 10 yalianzishwa wilayani Mufi ndi na Lushoto. Mbegu za kuanzisha mashamba hayo zilikusanywa kutoka kwenye miti yenye ubora wa kutoa mbegu iliyoko Njombe, Mufi ndi na Lushoto. Mashamba haya yana umri wa mwaka mmoja na yanaendelea vizuri. Mashamba haya yanaendelea kutunzwa na Mbegu husika zitatumika katika

    waharibifu na magonjwa yanayoathiri miti/misitu.

    Utafi ti juu ya Umri wa Uvunaji wa Miti ya Misindano na Misaji

    Utafi ti huu ulifanyika ili kubaini umri sahii wa miti aina ya misindano (Pines) na misaji (Teak). Vigezo vilivyotumika kubaini umri sahihi ni pamoja na takwimu za ukuaji wa miti msituni (ongezeko la ujazo), uchumi na ubora wa mbao. Utafi ti umeonesha kuwa umri wa kuvuna miti aina ya misindao kwa ajili ya matumizi ya mbao kwa kutumia vigezo vilivyotajwa hapo juu unaweza kushushwa toka miaka 25 hadi 18. Miti ya Misindano pia inaweza kuvunwa ikifi kisha umri wa kuanzia miaka 11 kwa ajili ya uzalishaji wa karatasi. Kwa miti ya misaji umri unaweza kushushwa toka miaka 40 hadi 20 kwa ajili ya matumizi ya mbao. Matokeo haya yanaonesha kuwa miti hii inakua haraka kwa sasa kuliko miaka iliyopita na haya yanaweza kuwa matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. Hii itasaidia serikali na watu binafsi kupata mapato mapema badala ya kusubiri miaka mingi zaidi kama ilivyozoeleka bila kuathiri ubora wa mazao. Pia kumekuwa na mwitikio wa wananchi kupanda miti baada ya umri wa kuvuna kupungua. Matokeo haya yatachangia maendeleo ya uchumi wa viwanda nchini kwa kuongeza malighafi za kutumika katika viwanda vya misitu na kupatikana kwa muda mfupi zaidi

    kuliko ilivyokuwa hapo awali.

    Utambuzi na Uhifadhi wa Miti iliyopo kwenye Bonde la Mto Rufi ji

    Kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali, TAFORI ilifanya utafi ti ili kutambua miti yote iliyopo kwenye eneo la mradi wa mto Rufi ji ambako Serikali inajenga Bwawa kubwa la maji kuzalisha umeme katika Pori la Akiba la Selous. Iligundulika kuwa zipo aina 159 za miti katika pori hilo (ikiwa ni ndani na nje ya eneo la mradi wa kufua umeme). Katika eneo la mradi iligundulika kuwepo na aina 72 za miti ambapyo kati ya hiyo, aina nne tu za miti zinahitaji uangalizi maalum kwa mujibu wa IUCN. Miti hiyo ni Croton jatrophoides Dialium holtzii (Mpepete), Millettia micans (Pangapanga) na Dalbergia nitidula. Sampuli za miti yote iliyokutwa kwenye eneo la mradi pamoja na ile miti iliyoorodheshwa na IUCN ilikusanywa na kuhifadhiwa kwenye Herbarium ya Taifa iliyopo Arusha, TAFORI katika Kituo cha Lushoto na katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya rejea. Matokeo ya utafi ti huu yatasaidia Serikali na Wadau mbalimbali kujua rasilimali zilizopo katika Pori la Akiba la Selous na kutengeneza mikakati ya kutunza aina ya miti inayohitaji uangalizi maalum.

    Kubaini Sababu za Kukauka kwa

    Sababu nyingine ni kuharibika kwa misitu ya hifadhi na umwagiliaji unaofanyika bila utaratibu wa aina yoyote. Matokeo ya utafi ti huu yanatoa ujumbe kuwa, upungufu wa maji katika maeneo kadhaa nchini unatokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanyika katika maeneno husika, na sio kusingizia miti.

    Matokeo ya utafi ti yameonesha kuwa chanzo cha kufa kwa mianzi ni umri kwa maana kuwa mianzi inapofi kisha umri wa miaka 60 hadi

    70 hutoa maua na baadae kufa kizazi chote. Kwenye maeneo ambayo mianzi ilikufa, uoto wa asili wa miti unaibukia.

    Uoto wa miazi kwenye Hifadhi Asilia ya Misitu ya Uzungwa ScarpMdudu aina ya Paranaleptesi reticulata (Girdling beetle) akishambulia Mikaratusi katika Shamba la miti la Korogwe

    Maandalizi ya Sampuli kwa ajili ya Utafi ti wa ubora wa MbaoUtafi ti juu ya uzalishaji wa baadhi ya Miti ya asili kwa kutumia njia ya Vikonyo

    kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali kupitia juhudi za Serikali na Wadau wengine.

    Udhibiti wa Miti vamizi katika maeneo ya malisho na mashamba

    Taasisi kwa kushirikiana na Taasisi za Elimu na Utafi ti katika nchi za Uswisi, Kenya, Afrika kusini na Ethiopia inatekeleza mradi wa kudhibiti miti vamizi katika eneo la Usambara Mashariki na Kahe Moshi. Mradi huu wa miaka sita (2015 - 2021) una lengo la kulinda bioanuai, huduma zitolewazo na mazingira na uchumi wa jamii kwa kupunguza gharama na athari zinazotokana na miti vamizi katika mashamba na malisho ya mifugo. Mafaniko ya mradi huu ni pamoja na kuishirikisha jamii kwa kuipatia mafunzo ya vitendo juu ya namna ya kupambana na miti/magugu mashambani na kwenye malisho ambayo ni rafi ki kwa mazingira na uchumi. Pia mradi huu unasomesha watanzania sita katika Shahada za Uzamivu (mmoja) na Uzamili (watano) katika vyuo mbali mbali hapa nchini ili waweze kulisaidia Taifa kudhibiti miti/mimea vamizi na athari zake katika rasilimali za asilia.

    Kushirikiana na Wadau mbalimbali kupanda miti kwa ajili ya nishati ya kuniKatika jitihada za Taasisi za kuboresha utunzanji wa misitu ya asili hapa nchini Taasisi imeshirikiana na taasisi mbalimbali kimeratibu upandaji miti kwa mfano katika eneo la Magereza Wilayani Lushoto lenye ukubwa zaidi ya Hekta 40, ambapo miti zaidi ya 50,000 aina ya Mikaratusi imepandwa, ambao hadi sasa ina umri wa miaka mitatu. Maeneo mengine ambapo miti imepandwa kwa ushirikiano na wananchi ni

    wilayani Handeni, Mkuranga, Morogoro na Moshi. Lengo la mradi huu wa upandaji miti ni kupunguza utegemeze wa miti kutoka kwenye misitu ya asili kwa ajili ya mahitaji ya nishati ya kuni.

    Upembuzi Yakinifu katika Shamba tarajiwa la Miti la Mpepo, Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma

    Taasisi ilifanya utafi ti wa awali wa kubainisha hali ya hewa (mvua, joto, upepo, unyevunyevu), aina ya udongo na uoto wa asili uliopo katika maeneo ya shamba tarajiwa la miti ili kubaini ni aina gani ya miti inaweza kupandwa. Kulingana na hali ya hewa, udongo na uoto wa asili na vijishamba vidogo vya miti vilivyopo pembezoni mwa eneo la Mpepo, ilishauriwa kuwa miti aina ya Misindano (Pinus patula, Pinus tecunumanii, Pinus maximinoi), Mikaratusi (Eucalyptus saligna, Eucalyptus grandis, Eucalyptus maidenii) na Migrevilia (Grevillea robusta) ipandwe katika eneo husika. Matokeo ya upembuzi huu yamepelekea kuanzishwa Shamba jipya la Miti la Mpepo, Mkoani Ruvuma.

    TAFORI yathibitishwa kusimamia mamlaka ya kisayansi ya mimea kwenye mkataba wa CITES

    Mkataba wa kimataifa unaoshughulikia biashara ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka ujulikanao kama “Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Fauna and Flora – (CITES)” umeitambua TAFORI kuwa mamlaka ya kisayansi ya mimea Tanzania. Mkataba huu wa kimataifa umetokana na makubaliano baina ya nchi mbalimbali. Lengo ni kuhakikisha biashara ya kimataifa

    ya wanyama na mimea haiathiri au kupunguza uwepo wake. Kusambaa kwa taaarifa mbalimbali za hali hatarishi kwa mimea na wanyama kuliweka sababu kubwa wa uanzishwaji wa mkataba huu. Biashara ya kimataifa ya viumbe hai inakadiriwa kuwa na thamani ya mabilioni ya pesa. Biashara hii inatofautiana kati ya wanyama na mimea pia uhusisha mazao yatokanayo na wanyama na mimea kama vyakula, ngozi, magamba, mizizi, mbao na madawa. Kwakuwa biashara hii inavuka mipaka ya nchi, juhudi za kimataifa katika kusimamia matumizi sahihi ya bidhaa hii zinahitajika. Hivyo basi Taasisi itaendelea kutoa ushauri katika masuala yote ya kiutafi ti yanayohusu rasilimali Misitu ili kuwa na biashara endelevu ya wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka.

    Uandaaji wa Mwongozo wa Kupanda Kloni za Mikaratusi Tanzania

    Mwongozo huu umeandaliwa kufuatia uhitaji mkubwa wa wadau mbalimbali wa upandaji wa kloni za Mikaratusi katika maeneo makubwa. Mwongozo huu unatoa maelezo ya kloni bora katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi ya Tanzania kwa kuzingatia taarifa za tafi ti. Mwongozo unafafanua juu ya utunzaji bora wa kloni ili kupata mazao bora na kwa wingi. Maeneo yanayofaa na yasiyofaa kupanda kloni yamefafanuliwa bayana. Wadau wote wanaojihusisha na shughuli za upandaji miti wanaalikwa kusoma na kufuata mwongozo huo kwa ajili ya kupata mazao ya miti yaliyo bora na kuzuia matatizo ya uharibifu wa mazingira. Mwongozo huu unasambazwa kwa wadau ili usaidia kutoa elimu ili kuepukana na majawabu yanayokinzana ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa upandaji wa mikaratusi.

    HITIMISHOKatika kipindi cha miaka

    minne (2015 hadi 2019) Taasisi imeendelea vema kutekeleza majukumu yake. Tafi ti ambazo zimefanyika zimechangia kwenye uhifadhi endelevu wa misitu yetu.

    Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na wadau wa maendeleo kwa kufanikisha tafi ti hizi.

    Imeandaliwa na:Kaimu Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Utafi ti wa Misitu

    Tanzania

    /ColorImageDict > /JPEG2000ColorACSImageDict > /JPEG2000ColorImageDict > /AntiAliasGrayImages false /CropGrayImages false /GrayImageMinResolution 300 /GrayImageMinResolutionPolicy /OK /DownsampleGrayImages true /GrayImageDownsampleType /Bicubic /GrayImageResolution 300 /GrayImageDepth -1 /GrayImageMinDownsampleDepth 2 /GrayImageDownsampleThreshold 1.50000 /EncodeGrayImages true /GrayImageFilter /DCTEncode /AutoFilterGrayImages true /GrayImageAutoFilterStrategy /JPEG /GrayACSImageDict > /GrayImageDict > /JPEG2000GrayACSImageDict > /JPEG2000GrayImageDict > /AntiAliasMonoImages false /CropMonoImages false /MonoImageMinResolution 1200 /MonoImageMinResolutionPolicy /OK /DownsampleMonoImages true /MonoImageDownsampleType /Bicubic /MonoImageResolution 1200 /MonoImageDepth -1 /MonoImageDownsampleThreshold 1.50000 /EncodeMonoImages true /MonoImageFilter /CCITTFaxEncode /MonoImageDict > /AllowPSXObjects false /CheckCompliance [ /None ] /PDFX1aCheck false /PDFX3Check false /PDFXCompliantPDFOnly false /PDFXNoTrimBoxError true /PDFXTrimBoxToMediaBoxOffset [ 0.00000 0.00000 0.00000 0.00000 ] /PDFXSetBleedBoxToMediaBox true /PDFXBleedBoxToTrimBoxOffset [ 0.00000 0.00000 0.00000 0.00000 ] /PDFXOutputIntentProfile () /PDFXOutputConditionIdentifier () /PDFXOutputCondition () /PDFXRegistryName () /PDFXTrapped /False

    /CreateJDFFile false /Description > /Namespace [ (Adobe) (Common) (1.0) ] /OtherNamespaces [ > /FormElements false /GenerateStructure true /IncludeBookmarks false /IncludeHyperlinks true /IncludeInteractive false /IncludeLayers false /IncludeProfiles false /MarksOffset 6 /MarksWeight 0.250000 /MultimediaHandling /UseObjectSettings /Namespace [ (Adobe) (CreativeSuite) (2.0) ] /PDFXOutputIntentProfileSelector /NA /PageMarksFile /RomanDefault /PreserveEditing true /UntaggedCMYKHandling /LeaveUntagged /UntaggedRGBHandling /UseDocumentProfile /UseDocumentBleed false >> > ]>> setdistillerparams> setpagedevice