Upload
others
View
21
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR
OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA
HESABU ZA SERIKALI ZANZIBAR
RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA
HESABU ZA SERIKALI
KWA MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI
YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016
ii
YALIYOMO
SURA YA KWANZA…………………………………………………………………………………..……1
1.0 UTANGULIZI ...................................................................................................... 1
2.0 MAJUKUMU YA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI . 1
3.0 UPEO NA MADHUMUNI YA RIPOTI YA UKAGUZI ................................................... 2
4.0 NJIA ZILIZOTUMIKA KATIKA UKAGUZI ................................................................. 3
5.0 MAJUKUMU YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI ............... 5
6.0 UMUHIMU WA KUFANYA UKAGUZI ....................................................................... 5
7.0 SHUKURANI ....................................................................................................... 6
SURA YA PILI……………………………………………………..………………………………………..7
8.0 MATOKEO YA UKAGUZI KWA MWAKA 2015/2016 .................................................. 7
9.0 UTEKELEZAJI WA HOJA ZA UKAGUZI ULIOPITA WA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 7
10.0 UWASILISHAJI WA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016 KWA AJILI YA UKAGUZI ...................................................................................................................... 7
11.0 AINA YA HATI ZA UKAGUZI ............................................................................... 10
SURA YA TATU………………………………………………………………………………………….…13
12.0 MAMBO YALIYOBAINIKA KATIKA UKAGUZI WA MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ........................................................................ 13
13.0 UKAGUZI WA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016 ................................. 13
14.0 SHIRIKA LA MAGAZETI ..................................................................................... 13
15.0 SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR (ZBC) ......................................................... 20
16.0 CHUO CHA KILIMO –KIZIMBANI ........................................................................ 25
17.0 MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR (ZAWA) ............................................................... 29
18.0 MAMLAKA YA VITEGA UCHUMI ZANZIBAR (ZIPA) ................................................ 37
19.0 CHUO CHA UTAWALA WA UMMA -IPA ................................................................ 42
20.0 CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR (ZITOD) ...................................... 47
21.0 CHUO CHA UANDISHI WA HABARI. .................................................................... 52
22.0 CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR ............................................................ 57
23.0 CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) ....................................................... 61
iii
24.0 SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA ......................................................................... 65
25.0 MAMLAKA YA UVUVI WA BAHARI KUU ............................................................... 70
26.0 SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR ....................................................................... 74
1
RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA
SERIKALI KWA MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR - KWA MWAKA WA FEDHA
2015/2016
SURA YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anawajibika kukagua mahesabu
yote ya Serikali, Mashirika ya Umma ,Taasisi za umma pamoja na Miradi mbali mbali
ya maendeleo na baadae kutoa taarifa za ukaguzi huo kila mwaka. Taarifa hiyo
itaeleza udhibiti na uhifadhi wa fedha na mali za Umma.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu 112(5) Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu anawajibika kuwasilisha kila taarifa ya ukaguzi wa
mahesabu atakayoitoa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 112(3) cha Katiba.
Kutokana na mabadiliko ya kazi za ukaguzi kumekuwa na mafanikio makubwa
katika utendaji na uwajibikaji katika sekta za umma kwenye matumizi ya rasilimali
za umma. Aidha, kuimarika kwa mfumo wa fedha pamoja na utekelezaji wa sheria
za fedha na manunuzi za umma kumechangia kwa kuimarika kwa uwazi na
uwajibikaji katika taasisi za Serikali pamoja na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya
maendeleo na kuleta tija kwa wananchi.
2.0 MAJUKUMU YA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU
ZA SERIKALI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anawajibika kikatiba kukagua
mahesabu ya Taasisi za Serikali na baadae kutoa taarifa zake za ukaguzi huo kila
mwaka. Taarifa hizo zitaelezea hali halisi za mapato na matumizi ya fedha kutoka
Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na utekelezaji
wa sheria mbali mbali zikiwemo sheria za fedha, sheria za manunuzi na sheria
nyenginezo.
Kwa mujibu wa kifungu 112 (3) cha Katiba ya Zanzibar 1984,Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu anawajibika kufanya yafuatayo:-
2
“a) Kuhakikisha kwamba fedha zote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu
wa Hazina ya Serikali ya Zanzibar, matumizi yake yameidhinishwa na iwapo
nitatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo basi nitaidhinisha fedha
hizo zitolewe
b) Kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa
yanatokana na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Mapinduzi
au fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi, na ambazo zimetumika kwa ajili ya shughuli zilizohusika na matumizi ya
fedha hizo na kwamba matumizi yamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusu
matumizi hayo; na
c) Angalau mara moja kwa mwaka kufanya ukaguzi na kutoa taarifa juu ya ukaguzi
wa hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hesabu zinazosimamiwa na
watumishi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hesabu za Mahkama zote za
Zanzibar, hesabu za Tume au vyombo vyengine vinavyohusika na Baraza la
Wawakilishi ”.
Ukaguzi wa mahesabu umefanywa kwa kuzingatia miongozo na vigezo mbali mbali
vya ukaguzi ili kukidhi matarajio ya wadau wetu na wananchi kwa ujumla. Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaendelea kufanya uchambuzi wa
njia bora zaidi kwa kufanya ukaguzi utakaoleta tija na kuongeza wigo na maeneo
yanayokaguliwa kwa lengo la kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika sekta za
umma.
3.0 UPEO NA MADHUMUNI YA RIPOTI YA UKAGUZI
Ripoti hii imekusanya taarifa za ukaguzi wa mahesabu ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar yakiwemo Mashirika ya Umma na Taasisi mbali mbali za Serikali kwa
kuzingatia taarifa za mapato na matumizi ambazo zimeelezwa kwenye taarifa za
ukaguzi zilizotumwa kwa Taasisi husika.
Ukaguzi ulifanyika kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya taasisi kuu za ukaguzi
(ISSAIs) ili kutoa uhakika kama taarifa za fedha zinaonyesha sura halisi. Taratibu za
ukaguzi zinajumuisha uchambuzi na kumbukumbu za taarifa mbali mbali, mifumo ya
udhibiti wa ndani, mifumo ya taarifa za kisheria zinazosimamia uendeshaji wa taasisi
zilizokaguliwa.
3
Taarifa hizo zinaonesha kwa muhtasari matokeo ya ukaguzi uliofanyika kwa misingi
ya sampuli, kwa hivyo matokeo ya ukaguzi kwa kiasi kikubwa yalitegemea
kumbukumbu za taarifa na nyaraka tulizoziomba na kuwasilishwa kwa ajili ya
kufanya ukaguzi.
Taarifa hizo zilijumuisha mahesabu ya mwisho wa mwaka ambapo ziliandaliwa kwa
mujibu wa viwango vya kitaifa na kimataifa vya uhasibu kwa sekta ya umma.
Taarifa hizo ni kama zifuatazo: -
I. Mizani ya Hesabu
II. Taarifa ya Mapato na Matumizi
III. Taarifa kuhusu mabadiliko ya mtaji
IV. Taarifa ya mtiririko wa fedha
V. Taarifa ya uwiano wa bajeti na kiasi halisi cha matumizi
VI. Sera za uhasibu na maelezo ya taarifa za fedha
4.0 NJIA ZILIZOTUMIKA KATIKA UKAGUZI
Katika kufanya ukaguzi wa Hesabu kwa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali
tulizingatia taratibu za ukaguzi zifuatazo: -
i. Kutoa barua za kushiriki ukaguzi kwa taasisi inayokaguliwa kabla ya kuanza kazi
za ukaguzi inayoeleza madhumuni na upeo wa ukaguzi, maeneo yanayotarajiwa
kufanya ukaguzi na kuelezea majukumu ya ukaguzi kwa mkaguzi (Engagement
Letter).
ii. Kuandaa mkakati na ujumla wa ukaguzi unaonesha muelekeo mzima wa ukaguzi,
vigezo vitakavyotumika katika hatua za mwanzo za kutathmini Mashirika ya
Umma na Taasisi za Serikali zinazokaguliwa.
iii. Kufanya kikao cha kuanza kazi za ukaguzi (Entrance Meeting) ambapo katika
kikao hicho uongozi wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali zinazokaguliwa
kwa lengo la kupata uelewa kabla ya kuanza kazi za ukaguzi.
iv. Kujadiliana na uongozi wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali kuhusu
utekelezaji na utendaji kwa kipindi cha mwaka husika.
v. Kupitia na kuhakiki nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kupata uelewa wa shughuli za
Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali.
4
vi. Kutumia njia na mbinu nyingine za ukaguzi kama ilivyoainishwa kwenye
muongozo wa ukaguzi (Regularity Audit Manual).
vii. Kutoa ripoti ya ukaguzi mawazo kwa uongozi ambayo itakuwa inaonyesha
kilichobainika wakati wa ukaguzi na kutoa nafasi kwa uongozi kutoa maelezo
kuhusu ripoti hiyo.
viii. Kutoa rasimu ya ripoti ya ukaguzi kwa uongozi inayoeleza hoja za ukaguzi
zilizobainishwa na kutoa muda kwa uongozi kuweza kujibu hoja hizo.
ix. Kufanya kikao cha mwisho (Exit Meeting) na mkaguliwa baada ya kumaliza
ukaguzi ambapo katika kikao hicho hupitia kwa pamoja hoja zilizojitokeza wakati
wa ukaguzi.
x. Kutoa ripoti ya mwisho kwa uongozi wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali
inayoonesha matokeo ya ukaguzi ikiwemo hoja za ukaguzi na kutoa nafasi kwa
uongozi na mkaguliwa kuweza kujibu hoja hizo.
xi. Kutoa ripoti ya ukaguzi kwa uongozi inayoonesha hati ya ukaguzi aliyopata
mkaguliwa kuhusiana na taarifa za fedha.
Aidha mbinu za kuangalia viashiria vya maeneo hatarishi katika Mashirika ya Umma
na Taasisi za Serikali zilizokaguliwa zilitumika katika ukaguzi ambapo mbinu hizi za
ukaguzi zinasisitiza haja ya kuelewa kwa kina mazingira ya taasisi inayokaguliwa
ikiwemo mfumo wa udhibiti wa ndani, kutathmini vihatarishi na kubaini viashiria
vitakavyoathiri udhibiti wa ndani.
Mbinu za ukaguzi zinatekelezwa kwa kutumia muongozo na utaratibu wa ukaguzi, ili
kuhakikisha kwamba mbinu za ukaguzi zinaenda na wakati ambapo Ofisi inafanya
mapitio ya muongozo wa utaratibu na ukaguzi kila mwaka kwa kuimarisha ukaguzi
na kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote muhimu yanajitokeza katika fani ya
ukaguzi na uhasibu pamoja na mabadiliko ya mifumo ya sheria yanazingatiwa
ipasavyo.
Aidha utendaji wa mashirika ya umma na taasisi za Serikali zilizokaguliwa
umeangaliwa na kuonesha viwango vya kiutendaji kifedha na kiuendeshaji. Utendaji
wa kifedha umepimwa kwa kuangalia faida au hasara iliyopatikana kwa kipindi cha
mwaka husika. Utendaji wa kiuendeshaji umepimwa kwa kuangalia ni kwa kiasi gani
taasisi imeweza kufikia malengo yake ya msingi.
5
5.0 MAJUKUMU YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA
SERIKALI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anawajibika kikatiba kukagua
mahesabu ya Mashirika ya Serikali pamoja na Taasisi za Serikali kama ilivyoainishwa
katika Katiba ya Zanzibar,1984 na sheria nyenginezo na baadae kutoa taarifa zake
za ukaguzi huo kila mwaka. Taarifa hizo zitaelezea hali halisi za mapato na
matumizi ya fedha pamoja na utekelezaji wa sheria mbali mbali zikiwemo sheria za
fedha, sheria za manunuzi na sheria nyenginezo.
Baada ya kumaliza ukaguzi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
anawajibika kutoa maoni juu ya mahesabu hayo na kuonesha hali halisi ya taarifa za
hesabu iwapo zinatoa sura sahihi na halisi kwa kipindi kilichokaguliwa. Maoni hayo
yatahusiana na mambo yafuatayo: -
i. Kutoa ushauri juu ya mambo yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kuhusiana
na shughuli za Taasisi zinazokaguliwa.
ii. Kuzuia na kupunguza matumizi ya Fedha za umma yasiyokua na tija
iii. Kuongeza makusanyo na kuzuia upotevu wa fedha na rasilimali za umma.
iv. Kuzuia hasara au kutoa tahadhari juu ya hasara inayoweza kutokea kwa
uzembe, upotevu,kukosa uaminifu,udanganyifu au rushwa kuhusiana na
fedha au rasilimali za umma.
v. Kuongeza uchumi, tija na ufanisi katika kutumia fedha za umma.
6.0 UMUHIMU WA KUFANYA UKAGUZI
Lengo kuu la kufanya ukaguzi ni kumuwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali kutoa maoni ya ukaguzi huru kuhusiana na hesabu za Taasisi
zilizokaguliwa ikiwemo Wizara, Idara, Wakala na Serikali pamoja na Mamlaka mbali
mbali za Serikali. Vile vile kubaini kwamba hesabu hizo kama zinatayarishwa kwa
kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya Uhasibu katika sekta ya umma au
kwa viwango vya kimatifa vya taarifa za fedha. Ufanisi wa ukaguzi unategemea
mawasiliano mazuri na uongozi wa taasisi inayokaguliwa.
Aidha tunahakikisha kwamba ukaguzi tunaofanya unalenga kutoa kipaumbele katika
maeneo muhimu ili kuchangia maendeleo katika sekta za umma na hatimae
kuimarisha maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
6
Ni imani yangu kwamba kuimarika kwa kazi za ukaguzi kutaongeza na kuimarisha
uwazi na uwajibikaji katika mapato na matumizi ya fedha na rasilimali za umma na
tunategemea ufanisi na tija vinapatikana kwa kila rasilimali itakayotumika kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla.
7.0 SHUKURANI
Napenda kutoa shukurani kwa wote waliochangia kwa namna moja au nyengine
kuanzia kazi za ukaguzi, ufuatiliaji maeneo mbali mbali yaliyokaguliwa hadi
kukamilika kwa ripoti hii ya ukaguzi ya mwaka 2015/2016.
Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
jitihada mbali mbali zinazochukuliwa katika kuimarisha Ofisi hii kiutendaji na
watendaji kwa ujumla. Vile vile napenda kuwapongeza na kuwashukuru
wafanyakazi wote wa Ofisi hii kwa juhudi zao wanazochukuwa hadi kufanikisha
kukamilika kwa ripoti hii kwa wakati.
Hali kadhalika, ninawashukuru viongozi na watendaji wakuu wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na watendaji wa taasisi mbali mbali za Serikali kwa
mashirikiano mazuri wanayotupa wakati wa kutekeleza kazi zetu za ukaguzi.
Mwisho, ninapenda kuishukuru Kamati ya Kuchunguza Hesabu za Serikali (PAC) na
Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa za Baraza la Wawakilishi
na wengineo kwa ujumla wao wamechangia maendeleo makubwa yaliyopatikana
katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
………………………………...
FATMA MOHAMED SAID
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI
ZANZIBAR
7
SURA YA PILI
8.0 MATOKEO YA UKAGUZI KWA MWAKA 2015/2016
Katika ukaguzi wa mahesabu ya mwaka 2015/2016 imebainika kwamba uwekaji wa
kumbukumbu na taarifa mbali mbali za mahesabu ikiwemo fedha na rasilimali za umma
pamoja na udhibiti wa ndani umeimarika.
9.0 UTEKELEZAJI WA HOJA ZA UKAGUZI ULIOPITA WA MWAKA WA FEDHA
2014/2015
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu imekuwa ikitoa ripoti zenye ushauri na
mapendekezo mbalimbali katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali za umma kwa
lengo la kuwa na utawala bora unaoheshimu sheria za fedha na manunuzi na sheria
nyenginezo.
Kufuatia tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa tumebaini kwamba
mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti za ukaguzi za mwaka uliopita 2014/2015
yamefanyiwa kazi na kuonesha matumaini ya kuimarika kwa nidhamu ya matumizi ya
fedha na rasilimali za umma.
Tunapongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha na rasilimali za umma na kupelekea
kuimarika kwa utendaji na uwajibikaji katika Mashirika na Taasisi za umma.
Hata hivyo kumejitokeza dosari za usimamizi wa fedha na ukiukwaji wa sheria za fedha
na manunuzi ya umma kwa baadhi ya Mashirika na Taasisi na kupelekea mapungufu
katika hesabu za mwisho wa mwaka.
10.0 UWASILISHAJI WA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016 KWA
AJILI YA UKAGUZI
Kwa mujibu wa kifungu namba 24(2) cha sheria ya fedha No. 12, 2005, inazitaka
Taasisi zote za Serikali zitayarishe na kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali, hesabu za mwaka, zinazojumuisha Mapato na matumizi ya Taasisi
husika. Aidha kifungu No.8 cha sheria hiyo, kinawataka wasimamizi wa fedha katika
Taasisi za Serikali kuwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
hesabu zao za mwisho wa mwaka ndani ya miezi mitatu baada ya kukamilika kipindi cha
mwaka.
8
Tunatoa pongezi kwa Mashirika na Taasisi mbali mbali za Serikali kwa jitihada
walizochukuwa za kuwasilisha hesabu za mwisho wa mwaka kwa mujibu wa sheria.
Uwasilishwaji wa hesabu za mwisho wa mwaka kwa ajili ya ukaguzi kutoka kwa
Mashirika na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kama ifuatavyo: -
Nam Fungu Shirika/Taasisi Tarehe iliyowasilishwa kwa
ukaguzi
2014/2015 2015/2016
1. Ruzuku Shirika la Magazeti 01/10/2015 30/09/2016
2. Ruzuku Shirika la Utangazaji
Zanzibar
29/09/2015 26/07/2016
3. Ruzuku Chuo cha Kilimo
Kizimbani
28/09/2015 27/09/2016
4. Ruzuku Mamlaka ya Maji (ZAWA) 29/09/2015 29/09/2016
5. Ruzuku Mamlaka ya Vitega
Uchumi Zanzibar(ZIPA)
10/09/2015 30/09/2016
6. Ruzuku Chuo cha Utawala wa
Umma
29/09/2015 30/09/2016
7. Ruzuku Chuo cha Maendeleo ya
Utalii
30/09/2015 30/09/2016
8. Ruzuku Chuo cha Uandishi wa
Habari
30/09/2015 30/09/2016
9. Ruzuku Chuo cha Sayansi za Afya
Zanzibar
23/10/2015 09/11/2016
10. Ruzuku Chuo Kikuu cha Taifa
(SUZA)
23/09/2015 27/09/2016
11. Ruzuku Mamlaka ya Uvuvi wa
Bahari Kuu
29/09/2015 29/09/2016
9
12. Linajitegemea Shirika la Bandari 28/09/2015 09/09/2016
13. Ruzuku Shirika la Meli na
Uwakala
23/09/2015 27/09/2016
14. Linajitegemea Shirika la Biashara la
Taifa (ZSTC)
Haikuwasilishwa
kwa wakati
Haikuwasilishwa
kwa wakati
10
11.0 AINA YA HATI ZA UKAGUZI
Hati za ukaguzi zinatolewa kutokana na matokeo ya ukaguzi ambapo hati hizo huonesha
aina ya hati inayotolewa kulingana na taarifa za mahesabu yaliyokaguliwa yenye
kuonyesha hali halisi ya mahesabu hayo.
Aina tofauti ya hati za ukaguzi zinatolewa kwa mazingira tofauti kulingana na usahihi wa
hesabu zilizokaguliwa. Hati zenyewe ni kama zifuatazo:-
Hati inayoridhisha, Hati isiyoridhisha, Hati yenye mashaka na Hati mbaya.
11.1 Hati inayoridhisha
Hati ya aina hii inatolewa pale ambapo ukaguzi umejiridhisha kutokana na kukidhi
viwango vilivyotumika katika uaandaji wa mahesabu, usahihi wa taarifa pamoja na
ushahidi uliopatikana wakati wa ukaguzi, na kupelekea kutoa sura sahihi na halisi ya
mahesabu hayo.
11.2 Hati isiyoridhisha
Hati ya aina hii inatolewa pale ambapo ukaguzi umejiridhisha kwamba taarifa za
mahesabu zilizoandaliwa imebainika kuwa zina dosari kubwa na za umuhimu, dosari
ambazo zinaweza kusababisha taarifa za hesabu kupoteza uhalisia wake na hivyo
kutoaminiwa na kupelekea kutokuonyesha sura sahihi na halisi ya mahesabu hayo.
11.3 Hati yenye shaka
Hati ya aina hii hutolewa baada ya Ukaguzi kujiridhisha kuwa, kulingana na ushahidi wa
kiukaguzi mambo yafuatayo yamejitokeza.
Taarifa za fedha zilizoandaliwa zina dosari kubwa ambazo zinaweza kuathiri
mahesabu endapo zikichukuliwa aidha moja baada ya moja au kwa ujumla wake
kwenye taarifa hizo haitoweza kuleta sura sahihi na halisi za mahesabu hayo.
Pale ambapo Ukaguzi umeshindwa kupata taarifa, nyaraka na vielelezo vya kutosha
vitakavyosaidia kufanya ukaguzi na kuweza kutoa maoni ya ukaguzi kwa mahesabu
hayo.
Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha mapato na matumizi yasiyokua na nyaraka muhimu
na kufanya matumizi bila ya kuwa na kibali halali au matumizi ya mapato ambayo
hayakuidhinishwa kutumika.
11
Kutozingatiwa kwa Sheria na kanuni mbalimbali ambapo kunapelekea madhara
makubwa ambayo yanaweza kusababisha kutokutoa sura sahihi na halisi ya
mahesabu hayo kwa mfano, kuwa na vitu ambavyo vilitakiwa kuripotiwa kwenye
taarifa za mahesabu lakini havikuripotiwa na manunuzi ya vifaa hayakufuata Sheria
na kanuni za manunuzi.
Kufanya matumizi ambayo hayakuleta tija kwa Taasisi husika.
Kutofanyika kwa usuluhisho wa benki hali inayopelekea kushindwa kupata usahihi
wa salio la fedha mwishoni mwa mwaka wa fedha.
11.4 Hati mbaya
Hati hii hutolewa pale ambapo ukaguzi umeshindwa kupata nyaraka na vielelezo vya
kutosha wakati wa ukaguzi ili kuweza kutoa maoni ya ukaguzi kutokana na mapungufu
yaliyojitokeza na kushindwa kugundua mambo ambayo yanaweza kusababisha madhara
makubwa katika Mashirika na Taasisi.
Hati zilizotolewa ni kama ifuatavyo: -
Nam Fungu Shirika/Taasisi Aina ya Hati
iliyotolewa
2015/2016
1. Ruzuku Shirika la Magazeti Hati inayoridhisha
2. Ruzuku Shirika la Utangazaji Zanzibar Hati inayoridhisha
3. Ruzuku Chuo cha Kilimo Kizimbani Hati inayoridhisha
4. Ruzuku Mamlaka ya Maji (ZAWA) Hati inayoridhisha
5. Ruzuku Mamlaka ya Vitega Uchumi
Zanzibar(ZIPA)
Hati inayoridhisha
6. Ruzuku Chuo cha Utawala wa Umma Hati inayoridhisha
7. Ruzuku Chuo cha Maendeleo ya Utalii Hati inayoridhisha
8. Ruzuku Chuo cha Uandishi wa Habari Hati inayoridhisha
12
9. Ruzuku Chuo cha Sayansi za Afya
Zanzibar
Hati inayoridhisha
10. Ruzuku Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Hati inayoridhisha
11. Ruzuku Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu Hati inayoridhisha
12. Linajitegemea Shirika la Bandari Hati inayoridhisha
13. Ruzuku Shirika la Meli na Uwakala Hati inayoridhisha
13
SURA YA TATU
12.0 MAMBO YALIYOBAINIKA KATIKA UKAGUZI WA MASHIRIKA NA
TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Ukaguzi uliofanyika katika Mashirika na Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imebainika kujitokeza kwa kasoro za kiutendaji kwa baadhi ya Mashirika na
Taasisi hizo ambapo hoja mbali mbali za ukaguzi ziliainishwa katika ripoti za ukaguzi
zilizotolewa kwa Mashirika na Taasisi hizo na baadhi ya hoja hizo zilipatiwa maelezo na
vielelezo vilivyokosekana wakati wa ukaguzi.
13.0 UKAGUZI WA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
Ukaguzi wa hesabu za mwisho wa mwaka 2015/2016 umebaini kwamba kumekuwa na
mabadiliko makubwa katika uwekaji wa kumbukumbu za mahesabu pamoja na udhibiti
mzuri wa rasilimali za umma na kupelekea mafanikio katika ufungaji wa hesabu za
mwisho wa mwaka kwa Mashirika na Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Matokeo ya ukaguzi wa hesabu hizo kwa Mashirika na Taasisi za Serikali pamoja na
maoni ya ukaguzi wa hesabu hizo ni kama ifuatavyo: -
14.0 SHIRIKA LA MAGAZETI
14.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/2016
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Shirika la Magazeti yameonekana kupanda kutoka shilingi 1,233,854,256 kwa
mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 1,369,924,774 kwa mwaka 2015/2016 kukiwa na
ongezeko la shilingi 136,070,518 sawa na asilimia 11 ya ongezeko.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Shirika la Magazeti yameonekana kupungua kutoka shilingi 684,011,998
kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 616,889,381 kwa mwaka 2015/2016 kukiwa
na upungufu wa shilingi 67,122,617 sawa na asilimia 10 ya mapungufu.
14
14.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016.
THE CORPORATION OF GOVERNMENT NEWSPAPER (CGN)
AS AT 30TH JUNE 2016
STATEMENT OF FINANCIAL POSITION
Assets Notes 2015/16 2014/15
15
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
Uchambuzi wa hapo juu unaonesha uwiano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito. Hata hivyo uwezo wa Shirika wa kulipa dhima zake za mpito
umepungua ukilinganisha na mwaka 2014/2015. Katika mwaka wa fedha 2015/2016
uwezo wa Shirika la Magazeti kuweza kulipa dhima zake za mpito ni mdogo
ukilinganisha na vigezo vya kiuhasibu juu ya uwiano wa mali za mpito na dhima za
mpito ambapo kwa mwaka huu Shirika lingeweza kulipa dhima za mpito na kubakisha
kiwango kidogo cha mali za mpito hivyo kuashiria kuwepo kwa hali isioridhisha ya
mwenendo wa Shirika hilo.
2015/2016 2014/2015
Mali za mpito (current assets) 600,362,509 843,630,958
Dhima za mpito (current liabilities) 362,473,034 629,404,553
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities
1.6:1 1.3:1
16
THE CORPORATION OF GOVERNMENT NEWSPAPER (CGN)
AS AT 30TH JUNE 2016
STATEMENT OF COMPREHENSIVE INCOME
17
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Hesabu za hapo juu zinaonyesha kwamba Shirika la Magazeti limepata faida ya shilingi
3,810,751.00 kwa mwaka 2015/2016. Ambapo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Shirika
lilipata hasara ya shilingi 215,198,816.00. Ukaguzi umebaini kwamba faida hiyo inaweza
kuongezeka iwapo hatua za kuongeza mauzo na kupunguza gharama za uendeshaji
zitachukuliwa.
14.3 MATOKEO YA UKAGUZI
UCHAMBUZI WA KIFEDHA KATIKA UTENDAJI WA SHIRIKA
14.3.1 Uwezo wa Shirika katika upatikanaji wa mapato
Own source revenue to total revenue = Own source /Total Revenue
30 /06/2016 30/06/2015
Owne source
revenue to total
revenue
Mapato ya ndani /
Mapato kwa jumla
883,221,624 720,388,256
1,369,924,774 1,233,854,256
64.5 58.4
Uchambuzi wa kifedha hapo juu unaonyesha kuwa hali ya Shirika kujitegemea kupitia
vyanzo vyake vya ndani vya mapato inaonekana kuimarika na kufikia asilimia 64.5 kwa
mwaka wa fedha 2016 ukilinganisha na asilimia 58.4 kwa mwaka wa fedha 2015.
18
14.3.2 Uwezo wa Shirika kujiendesha kiufanisi pasipo kutegemea Ruzuku
kutoka Serikali kuu
Operating Self- Sufficiency = Business Revenue / Total Expenses
30 /06/2016 30/06/2015
Mapato ya ndani
Jumla ya gharama
za uendeshaji
883,221,624 720,388,256
1,366,114,230 1,449,053,072
0.65 0.50
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha kwamba uwezo wa Shirika kukidhi gharama za
uendeshaji kupitia vyanzo vyake vya ndani unaonekana kuimarika na kufikia asilimia
0.65 kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 ukilinganisha na asilimia 0.50 kwa mwaka wa
fedha wa 2014/2015. Hata hivyo bado uwezo wa Shirika kukidhi gharama za uendeshaji
kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato ni mdogo.
14.3.3 Hali ya Ukwasi katika Shirika
Uwezo wa Shirika kuweza kumudu kulipa dhima za Mpito
Current Ratio = Current Assts / Current Liability
Uwiano wa mali za
mpito na dhima za
mpito
30 /06/2016 30/06/2015
Mali za mpito 600,362,509 843,630,958
Dhima za Mpito 362,473,036 629,404,553
Uwezo wa kulipa
dhima za mpito
1.66:1 1.34:1
Uchambuzi wa hesabu hapo juu unaonyesha kuwa uwezo wa Shirika kuweza kumudu
kulipa dhima za mpito ni mkubwa hali inayoonesha kuimarika kwa Shirika na kufikia
uwiano wa 1.66:1 kwa mwaka wa fedha 2016 ukilinganisha na uwiano wa 1.34:1 kwa
mwaka wa fedha 2015.
19
3.4.4 Uwezo wa Shirika kujiendesha kwa Faida
Gharama za Uendeshaji ukilinganisha na Mapato.
30 /06/2016 30/06/2015
Mapato 1,369,924,774 1,233,854,256
Matumizi 1,366,114,023 1,449,053,072
3,810,751 (215,198,816)
Uchambuzi wa hesabu hapo juu unaonyesha kuwa Shirika la Magazeti limeendelea
kuimarika kwa kujiendesha kwa faida na kufikia Shilingi 3,810,751 kwa mwaka 2016
ukilinganisha na hasara ya Shilingi 215,198,816 iliyopatikana katika kipindi cha mwaka
2015. Kuimarika huko kutokana na kuongezeka kwa kasi ya ukusanyaji mapato pamoja
na kupungua kwa gharama za uendeshaji.
Maoni ya Ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Shirika la Magazeti kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na vigezo
vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Shirika la Magazeti limepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa fedha
unaoishia 30 Juni, 2016.
20
15.0 SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR (ZBC)
15.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/2016
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Shirika la Utangazaji Zanzibar yameonekana kuongezeka kutoka shilingi
1,975,771,397 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 2,262,200,453 kwa mwaka
2015/2016 kutokana na ongezeko la shilingi 286,429,056 sawa na ongezeko la asilimia
14.5.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Shirika la Utangazaji yameonekana kuongezeka kutoka shilingi 652,636,529
kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 655,058,367 kwa mwaka 2015/2016 kukiwa
na ongezeko la shilingi 2,421,838 sawa na asilimia 0.4.
21
15.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
22
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 543,642,228 336,736,829
Dhima za mpito (current liabilities) 990,265,055 780,256,306
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities 0.5:1 0.43:1
Uchambuzi wa hapo juu unaonesha uwiano wa Mali za mpito ni mdogo ukilinganisha na
dhima za mpito, hata hivyo uwezo wa shirika kumudu kulipa dhima za mpito bado upo
chini mbali ya kuongezeka kwa mwaka 2015/2016 ukilinganisha na mwaka 2014/2015.
Shirika la Utangazaji halina uwezo wa kuweza kulipa dhima zake zote za mpito kutokana
na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dhima hizo.
23
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka
24
Uwiano wa Mapato yanayokusanywa na Shirika (Own Revenue) na Mapato yote (Total
Income) kwa mujibu wa hesabu za mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mapato yanayokusanywa na Shirika (Own
Revenue) 552,545,818 533,671,743
Mapato yote (Total Income) 2,262,200,453 1,888,935,963
Asilimia ya mapato yanayokusanywa
na shirika kwa mapato yote 24.42% 28.25%
Uchambuzi wa mapato ya Shirika unaonyesha kuwa Shirika linategemea sana ruzuku
kutoka Serikalini ambayo ni sawa na asilimia 75.57 ya mapato yake yote kwa mwaka wa
fedha 2015/2016. Hivyo Shirika bado halijaweza kuendesha shughuli zake kwa
kutegemea mapato yake wenyewe bila ya kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.
Aidha, uchambuzi unaonesha kwamba Shirika limepata hasara ya shilingi 270,179,901
kwa mwaka 2015/2016 ukilinganisha na hasara ya shilingi 151,841,502 iliyopatikana
kwa mwaka 2014/2015. Ikiwa ni ongezeko la shilingi 118,338,399 ambapo ni sawa na
asilimia 0.78 ya hasara ya mwaka uliopita.
Mwenendo wa hesabu za shirika unaonesha kuna uwezekano wa kupungua kwa hasara
iwapo juhudi zaidi zitachukuliwa katika ukusanyaji wa mapato sambamba na kupunguza
gharama za uwendeshaji.
Maoni ya Ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Shirika la Utangazaji Zanzibar kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura halisi na sahihi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Shirika la Utangazaji Zanzibar limepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
25
16.0 CHUO CHA KILIMO –KIZIMBANI
16.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/2016
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Chuo cha Kilimo yameonekana kupanda kutoka shilingi 681,015,093 kwa
mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 965,613,430 kwa mwaka 2015/2016 kukiwa na
ongezeko la shilingi 284,598,337 sawa na asilimia 29.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Chuo cha Kilimo yameonekana kuongezeka kutoka shilingi 879,336,974
Kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 1,030,647,506 kwa mwaka 2015/2016
kukiwa na ongezeko la shilingi 151,310,532 sawa na asilimia 17.
26
16.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
KIZIMBANI AGRICULTURAL TRAINING INSTITUTE
27
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uchambuzi wa hesabu za Chuo zinaonesha kwamba, Chuo hakina dhima za mpito
kutokana na kukosekana kwa madeni.
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 182,751,612 195,976,580
Dhima za mpito (current liabilities) NIL NIL
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities
NIL NIL
28
29
Ukaguzi umebaini kwamba Chuo cha Kilimo Kizimbani kinaendelea kupata hasara
ambapo kwa mwaka 2015/2016 Chuo kimepata hasara ya shilingi 111,138,282
ukilinganisha na mwaka wa fedha 2014/2015 ambapo chuo kilipata hasara ya shilingi
199,321,881.
Maoni ya Ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Chuo cha Kilimo Kizimbani kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Chuo cha Kilimo Kizimbani kimepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
17.0 MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR (ZAWA)
17.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/2016
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Mamlaka ya Maji yameonekana kuongezeka kutoka shilingi
14,634,315,587.52 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 15,707,554,021 kwa
mwaka 2015/2016 kukiwa na ongezeko la shilingi 1,073,238,423 sawa na asilimia 7 ya
ongezeko.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Mamlaka ya Maji yameonekana kupungua kutoka shilingi
15,482,116,196.87 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 10,092,122,038 kwa
mwaka 2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 5,389,994,159 sawa na asilimia 35
ya upungufu.
30
17.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
31
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 9,130,415,580.46 8,374,551,891.33
Dhima za mpito (current liabilities) 2,275,908,879 2,037,884,357.00
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities
4:1 4:1
Uchambuzi wa hapo juu unaonesha kwamba uwiano wa mali za mpito na dhima za
mpito wa Mamlaka ya Maji kwa mwaka wa fedha 2015/2016 unaonesha mali za mpito
ni kubwa ukilinganisha na dhima za mpito. Hali hii imechangiwa na kuongezeka kwa
mali za mpito ikiwemo kiwango kikubwa cha wadaiwa kwa mwaka 2015/2016.
Aidha imebainika udhaifu katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato na kupelekea
wadaiwa wengi kushindwa kulipa madeni yao kwa wakati na hatimae kufutwa kwa
madeni ya wadaiwa hao. Mamlaka inashauriwa kuchukua jitihada za makusudi katika
ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato kutoka kwa wadaiwa.
32
33
Uchambuzi unaonyesha kwamba Mamlaka inaendelea kupata hasara ambapo kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 ilipata hasara ya shilingi 524, 845, 759.89 na mwaka wa
2014/2015 ilipata hasara ya shilingi 847,800,609. Hasara hiyo inaonekana imepungua
kwa shilingi 322,954,849.46 . Hata hivyo bado jitihada za makusudi zinahitajika
kuchukuliwa na Mamlaka kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na gharama
kubwa za uchakavu zinazotokana na uchakavu wa visima, mahodhi ya kuhifadhia maji
na mashine.
Aidha, mwenendo wa hesabu za Mamlaka unaonesha kuwepo na uwezekano wa
kupunguza hasara hiyo iwapo juhudi zaidi zitachukuliwa katika ukusanyaji wa mapato
sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji.
UWIANO WA MAPATO YA MAMLAKA
Uwiano wa mapato yanayokusanywa na Mamlaka (Own Revenue) na mapato yote
(Total Income) kwa mujibu wa hesabu za mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Makusanyo ya Mamlaka (Own
Revenue) 6,025,274,270.66 5,806,519,774.34
Mapato mengineyo 9,682,279,750.17 8,827,795,813.18
Mapato yote (Total Income) 15,707,554,020.83 14,634,315,587.52
Asilimia ya mapato
yanayokusanywa na Mamlaka
kwa mapato yote 38.4 39.7
Asilimia ya mapato mengineo 61.6 60.3
Uchambuzi wa mapato ya Mamlaka unaonyesha kuwa Mamlaka inategemea sana
ruzuku kutoka Serikalini na Washirika wa maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 61.6
ya mapato yake yote kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Hivyo Mamlaka inashauriwa
kuongeza jitihada katika ukusanyaji wa mapato yake yenyewe ili kupunguza utegemezi
kutoka Serikalini na Washirika wa maendeleo.
34
Mapato ya Mamlaka yanatokana na vianzio mbalimbali ni kama ifuatavyo: -
Mapato yanayokusanywa na Mamlaka: -
35
17.3 MATOKEO YA UKAGUZI
17.3.1 Visima vilivyochimbwa na mradi wa Ras - Al- Khaimah
Ukaguzi umebaini kwamba kuna visima vimechimbwa kupitia mradi wa Ras al Khaimah
kwa ajili ya kuendeleza upatikanaji wa maji mijini na vijijini. Ujenzi huo ulifanyika kwa
awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa visima 50, awamu ya pili 50 na awamu
ya tatu 50. Ujenzi ambao ulianza tangu mwaka 2013 hadi kufikia 2016.Hadi ukaguzi
unamalizika visima vilivyokamilika na kutumika ni 22, Pemba 12 na Unguja 10 idadi
ambayo ndogo ukilinganisha na hali ya mahitaji ya huduma hio.
17.3.2 Kutokupata taarifa za ukodishwaji wa vibanda vya kuuzia maji
Katika kupanua wigo wa ukusanyaji mapato, Mamlaka ya Maji Zanzibar imeingia katika
mikataba ya uuzaji maji na watu mbali mbali katika vituo vyake vikuu vikiwemo Kiosk
cha Msikiti Mabuluu, Kiosk cha Kijito Upele na Kiosk cha Chaani kwa kipindi cha mwaka
mmoja kuanzia tarehe 8/12/2014 hadi tarehe 7/12/2015, lakini ukaguzi umeshindwa
kupata taarifa sahihi kutoka kwa wahusika wa uuzaji wa maji hayo ikiwemo:
Idadi ya maji ya nayouzwa kila siku
Idadi ya fedha zinazokusanywa kila siku
Ripoti ya kila mwezi ya uuzaji wa maji
Ripoti ya mwaka na tathmini halisi ya maji na mauzo husika.
Aidha ukaguzi umebaini kwamba mikataba hiyo ya ukodishwaji imeshamaliza muda
wake hadi ukaguzi unakamilika Mamlaka imeshindwa kuwapa mikataba mipya wahusika
na wanaendelea na uuzaji wa maji hadi tunakamilisha ukaguzi huu pasipo kuwa na
mikataba mipya.
MAMLAKA YA MAJI PEMBA
17.3.3 Malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu) shilingi 9,150,000
Ukaguzi umebaini kuwa jumla ya shilingi 9,150,000 zimekosa vielelezo husika kinyume
na kanuni ya 94 (4) ya kanuni ya fedha ya Zanzibar ya mwaka 2005. Kwa hali hiyo,
uhalali wa malipo hayo haukuweza kuthibitishwa.
36
Baadhi ya malipo hayo ni kama ifuatavyo:-
Hati namba Hundi
namba
Fedha
zilizolipwa
Aliyelipwa Maelezo
5/7
14/7/2015
000610 5,120,000 Moharash
Restaurent
Malipo ya fedha
kwa ajili ya
kugharamia
futari kwa
wafanyakazi wa
mamlaka
Pemba kwa ajili
ya mwezi
mtukufu wa
ramadhani.
22/8
17/8/2015
2,520,000 Alhabna
Restaurent
Malipo ya fedha
kwa ajili ya
kugharamia
chakula cha
wageni wa ADB
na viongozi wa
mamlaka ya
maji.
38/6
27/6/2016
001019 1,510,000 Mamlaka ya
maji
Malipo ya fedha
za tende
wanazolipwa
wafanyakazi wa
mamlaka ya
maji Pemba kwa
ajili ya mwezi
mtukufu wa
ramadhani.
37
17.3.4 Deni la fidia shilingi 387,895,000
Ukaguzi umebaini kuwa jumla ya shilingi 387,895,000 zinadaiwa na wananchi mbali
mbali kwa ajili ya kukatwa kwa vipando vyao ili kupisha upitishaji umeme na ulazaji wa
bomba za maji safi. Deni hili ni la mda mrefu.
Deni la fidia kwa upitishaji umeme.
Namba Wilaya inayohusika Kiwango
1 Chake Chake 58,589,000
2 Wete 96,852,000
3 Mkoani 60,842,000
4 Mkoani 171,612,000
Jumla 387,895,000
Maoni ya Ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Mamlaka ya Maji Zanzibar, kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura halisi na sahihi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Mamlaka ya Maji imepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa fedha
unaoishia 30 Juni, 2016.
18.0 MAMLAKA YA VITEGA UCHUMI ZANZIBAR (ZIPA)
18.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Mamlaka ya Vitega Uchumi yanaonyesha kupungua kutoka shilingi
2,020,717,904 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 1,992,907,960 kwa mwaka
2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 21,955,973 sawa na asilimia 1.1 ya
upungufu.
38
Matumizi
Matumizi ya Mamlaka ya Vitega Uchumi yameonekana kupungua kutoka shilingi
2,290,497,499 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 1,708,343,740 kwa mwaka
2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 582,153,759 sawa na asilimia 25 ya
upungufu.
39
40
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 1,840,099,869.12 1,620,845,442.99
Dhima za mpito (current liabilities) 389,004,614.00 297,006,214.00
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities
4.7:1 5.5:1
Uchambuzi wa hapo juu unaonesha uwiano wa Mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito, hata hivyo uwezo wa Mamlaka ya Vitega Uchumi kumudu kulipa
dhima za mpito umepungua kwa mwaka 2015/2016 ukilinganisha na mwaka
2014/2015. Mamlaka ya Vitega Uchumi ina uwezo wa kukidhi dhima zake zote za mpito
kutokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dhima hizo.
41
42
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uchambuzi wa hesabu unaonyesha kwamba Mamlaka ya Vitega Uchumi inaendelea
kupata hasara ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 imepata hasara ya shilingi
201,080,568.68 na mwaka wa 2014/2015 imepata hasara ya shilingi 248,923,686.81.
Hasara hiyo inaonekana imepungua kwa shilingi ni 47,843,118.13 sawa na asilimia 23.8
ya upungufu. Hata hivyo bado jitihada za makusudi zinahitajika kuchukuliwa na
Mamlaka ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Aidha, mwenendo wa hesabu za Mamlaka unaonesha kuwepo na uwezekano wa
kupunguza hasara hiyo iwapo juhudi zaidi zitachukuliwa katika ukusanyaji wa mapato
sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji.
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Mamlaka ya Vitega Uchumi kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura halisi na sahihi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Mamlaka ya Vitega Uchumi imepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
19.0 CHUO CHA UTAWALA WA UMMA -IPA
19.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Chuo cha Utawala wa Umma yanaonyesha kupungua kutoka shilingi
2,656,374,870 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 2,273,296,195 kwa mwaka
2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 383,078,675 ambapo ni sawa na asilimia
0.14 ya upungufu.
Matumizi
Matumizi ya chuo cha Utawala wa Umma yameonekana kupungua kutoka shilingi
2,386,042,878 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 2,078,772,856 kwa mwaka
2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 68,053,248 ambapo ni sawa na asilimia
0.03 ya upungufu.
43
HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
44
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 674,772,056 1,212,838,077.48
Dhima za mpito (current liabilities) 475,696,457 50,000
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities 1.4 : 1 24256 : 1
Uchambuzi wa hapo juu unaonesha uwiano wa Mali za mpito ni mdogo ukilinganisha na
dhima za mpito, hata hivyo uwezo wa chuo kumudu kulipa dhima za mpito bado upo
chini mbali ya kuongezeka kwa mwaka 2015/2016 ukilinganisha na mwaka 2014/2015.
Chuo cha Utawala wa Umma hakina uwezo wa kuweza kulipa dhima zake zote za mpito
kutokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dhima hizo.
45
46
Takwimu zinaonyesha kwamba Chuo cha Utawala wa Umma kimepata faida ya shilingi
51,121,918.65 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambapo kwa mwaka wa fedha
2014/2015 faida ya chuo ilikuwa ni shilingi 312,353,563.20 ikiwa ni upungufu wa shilingi
261,231,644.55 sawa na asilimia 83.6 ya upungufu. Kupungua kwa faida kumetokana
na ongezeko la gharama za uendeshaji.
19.2 MATOKEO YA UKAGUZI
19.2.1 Kasoro katika ukusanyaji wa mapato
Ukaguzi umebaini kwamba kuna kasoro zenye jumla ya shilingi 5,777,000 katika
ukusanyaji wa Ada za malipo kwa wanafunzi mbali mbali, baada ya kufanya mahojiano
na wanafunzi imebainika kuwa wanafunzi hao walikua wakipewa stakabadhi za malipo
ambazo zinasemekana kuwa sio sahihi ukilinganisha na stakabadhi za malipo
zinazotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Fedha hizo zililipwa kwa stakabadhi zifuatazo:
S/N Jina la mwanafunzi Kozi Stakabadhi
namba
Tarehe Shs.
1 NOURDIN ALI MMANGA DPA IV 496421 25/8/2015 490,000
2 SABRINA KEIS MWINYI DRM IV 496423 25/8/2015 490,000
3 WARDA MOHD RASHID DRM IV 496424 25/8/2015 490,000
4 SALUM ALI NASSOR CHRM II 496485 26/8/2015 490,000
5 ALLY MBARUKU FENESI DBIT II 496429 26/8/2015 515,000
6 SALHA YUSSUF MBARUK DRM IV 496442 26/8/2015 490,000
7 TABIA KHAMIS MJUMBE DRM IV 496443 26/8/2015 490,000
8 MOHD ALI JUMA CHRM II 496486 26/8/2015 490,000
47
9 BADRU HAJI SETI DIR III 496928 26/8/2015 220,000
10 BILAL AMOUR AMEIR DIR III 496453 27/8/2015 490,000
11 SAID MOHD KHAMIS DRM IV 496422 27/8/2015 490,000
12 SAIRA HAFIDH KHAMIS CRM II 496444 27/9/2015 490,000
13 NASSRA HASSAN IDDI CPR II 496484 28/8/2015
142,500
Jumla 5,777,500
Maoni ya Ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Chuo Cha Utawala wa Umma kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura halisi na sahihi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Chuo Cha Utawala wa Umma kimepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
20.0 CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR (ZITOD)
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar yanaonekana kupungua kutoka
shilingi 849,902,817 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 654,848,400 kwa
mwaka 2015/2016kukiwa na upungufu wa shilingi 195,054,417 ambapo ni sawa na
asilimia 23 ya upungufu.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Chuo cha Maendeleo ya utalii Zanzibar yameonekana kupungua kutoka
Shilingi 896,579,628 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia Shilingi 749,543,835 kwa
mwaka 2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 147,035,793 ambapo ni sawa na
asilimia 15.62 ya upungufu.
48
20.1 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
49
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 206,472,788 348,157,874
Dhima za mpito (current liabilities) 40,622,738 32,548,098
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities
5.08:1 10.7:1
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwiano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito. Hali hii inaonesha Chuo cha Maendeleo ya Utalii kina uwezo wa
kuhimili na kukidhi madeni yake.
50
51
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uchambuzi unaonyesha kwamba Chuo cha Maendeleo ya Utalii kinaendelea kupata
hasara ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ilipata hasara ya shilingi 62,062,832
na mwaka wa 2014/2015 ilipata hasara ya shilingi 44,120,951 Hasara hiyo inaonekana
imeongezeka kwa shilingi 18,431,122 sawa na asilimia 42.24.
Jitihada za makusudi zinahitajika kuchukuliwa na Chuo cha Maendeleo ya Utalii
kupunguza gharama za uendeshaji
Aidha,mwenendo wa hesabu za Chuo cha Maendeleo ya Utalii unaonesha kuwepo na
uwezekano wa kuongezeka kwa hasara hiyo iwapo juhudi zaidi hazitochukuliwa katika
ukusanyaji wa mapato sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji.
UCHAMBUZI WA KIFEDHA (FINANCIAL ANALYSIS)
Katika ukaguzi na uchambuzi wa kifedha uliofanyika kwenye taarifa za fedha za mwaka
2015/2016 za Chuo cha Uandishi wa Habari yafuatayo yalibainika:-
Uwezo wa Chuo katika ukusanyaji wa mapato
Owne source revenue to total revenue = Own source /Total Revenue
30/06/2016 30/06/2015
Owne source
revenue to total
revenue
Mapato ya ndani /
Mapato kwa jumla
349,718,280 466,718,616
780,882,180 852,947,917
44.8 54.7
Uchambuzi wa kifedha hapo juu unaonyesha kuwa bado Chuo kinategemea Ruzuku
kutoka Serikali kuu kwa kiwango kikubwa ikiwa ni chanzo kikuu cha mapato kutokana
na kwamba uwezo wa kukusanya mapato kupitia vyanzo nyake vya ndani ni
mdogo.Uwezo wa Chuo katika ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani
umepungua na kufikia asilimia 44.8 kwa mwaka wa fedha wa unaoishia Juni 2016
ukilinganisha na uwiano wa asilimia 54.7 katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia
Juni 2015. Kutokana na uchambuzi uliofanyika bado uwezo wa katika ukusanyaji wa
mapato kupitia vyanzo vyake wenyewe ni mdogo.
52
Uwezo wa Chuo kujiendesha kiufanisi pasipo kutegemea Ruzuku kutoka
Serikali kuu
Operating Self- sufficiency = Business Revenue / Total Expenses
30 /06/2016 30/06/2015
Mapato ya ndani
Jumla ya gharama
za uendeshaji
349,718,280 466,718,616
842,945,012 896,579,628
0.41 0.52
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha kwamba uwezo wa Chuo kukidhi gharama za
uendeshaji kupitia vyanzo vyake vya ndani umepungua na kufikia asilimia 0.41 kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 ukilinganisha na asilimia 0.52 kwa mwaka wa fedha
2014/2015. Hata hivyo bado uwezo wa chuo kukidhi gharama za uendeshaji kupitia
vyanzo vyake vya ndani vya mapato ni mdogo.
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Chuo cha Maendeleo ya Utalii
Zanzibar kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura halisi na sahihi
kufuatana na vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar kimepata hati inayoridhisha kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
21.0 CHUO CHA UANDISHI WA HABARI.
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Chuo cha Uandishi wa Habari yameonekana kuongezeka kutoka shilingi
430,521,925 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 491,586,700 kwa mwaka
2015/2016 kukiwa na ongezeko la shilingi 61,064,775 sawa na asilimia 14 ya ongezeko.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Chuo Cha Uandishi wa Habari yameonekana kuongezeka kutoka shilingi
438,207,002 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 445,440,319.40 kwa mwaka
2015/2016 kukiwa na ongezeko la shilingi 9,266,683 sawa na asilimia 21 ya ongezeko.
53
HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
54
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 41,711,083.10 12,511,072.50
Dhima za mpito (current liabilities) 18,883,890 23,221,600.00
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio) = current
assets/current liabilities
2.2:1 0.54:1
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwiano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito. Hali hii inaonesha Chuo cha Uandishi wa Habari kina uwezo wa
kukidhi dhima za mpito.
55
56
Uchambuzi unaonyesha kwamba Chuo cha Uandishi wa Habari kimepata faida ya
shillingi 19,955,768.35 kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Faida hiyo inaweza
kuongezeka iwapo jitihada za makusudi zitachukuliwa ikiwemo kupunguza gharama za
uendeshaji, pamoja na udhibiti mzuri wa ukusanyaji wa mapato.
UCHAMBUZI WA KIFEDHA (FINANCIAL ANALYSIS)
Katika ukaguzi na uchambuzi wa kifedha uliofanyika kwenye taarifa za fedha za mwaka
2015/2016 za Chuo cha Uandishi wa Habari yafuatayo yalibainika:-
Uwezo wa Chuo katika ukusanyaji wa mapato
Own source revenue to total revenue = Own source /Total Revenue.
30 /06/2016 30/06/2015
Own source
revenue to total
revenue
Mapato ya ndani /
Mapato kwa jumla
173,339,500 137,014,800
491,586,700 430,521,925
35.3 31.8
Uchambuzi wa kifedha hapo juu unaonyesha kuwa bado Chuo kinategemea Ruzuku
kutoka Serikali kuu kwa kiwango kikubwa ikiwa ni chanzo kikuu cha mapato kutokana
na kwamba uwezo wa kukusanya mapato kupitia vyanzo nyake vya ndani ni mdogo.
Uwezo wa Chuo umeongezeka na kufikia asilimia 35.3 kwa mwaka wa fedha unaoishia
Juni 2016 ukilinganisha na uwiano wa asilimia 31.8 katika kipindi cha mwaka wa fedha
ulioishia Juni 2015. Pamoja na ongezeko hilo bado uwezo wa ukusanyaji wa mapato
kupitia vyanzo vyake wenyewe ni mdogo.
57
Uwezo wa Chuo kujiendesha kiufanisi pasipo kutegemea Ruzuku kutoka
Serikali kuu Operating Self- sufficiency = Business Revenue / Total Expenses
30 /06/ 2016 30/ 06/ 2015
Mapato ya ndani
Jumla ya gharama
za uendeshaji
173,339,500 137,014,800
471,630,931.65 450,621,312.5
0.37 0.30
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha kwamba uwezo wa Chuo kukidhi gharama za
uendeshaji kupitia vyanzo vyake vya ndani umeongezeka na kufikia asilimia 0.37 kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 ukilinganisha na asilimia 0.30 kwa mwaka wa fedha
2014/2015. Hata hivyo bado uwezo wa Chuo kukidhi gharama za uendeshaji kupitia
vyanzo vyake vya ndani vya mapato ni mdogo.
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Chuo Cha Uandishi wa Habari kwa
mwaka wa fedha unaoishia Juni 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Chuo cha Uandishi wa Habari kimepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
22.0 CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR
Taarifa ya Mapato
Chuo cha Sayansi za Afya kwa mwaka wa fedha 2015/2016 kimekadiria kukusanya
jumla ya shilingi 1,470,505,000 ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2016 jumla ya
shilingi 1,179,863,350 zimekusanywa sawa na asilimia 80.2 ya makadirio.
Taarifa ya Matumizi
Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Chuo cha Sayansi za Afya kimekadiria kutumia jumla
ya shilingi 1,470,505,000 ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2016 jumla ya shilingi
1,118,962,741 zimetumika sawa na asilimia 76.1 ya makadirio.
58
59
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesabu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 98,949,975 25,953,365
Dhima za mpito (current liabilities) 32,464,240 72,875,379
Uwiano wa mali za mpito na
dhima za mpito (current ratio)
= current assets/current
liabilities
3:1
0.4:1
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwiano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito. Hali hii inaonesha Chuo cha Sayansi za Afya kina uwezo mzuri wa
kukidhi dhima za mpito.
60
61
Uchambuzi wa hapo juu unaonesha kwamba Chuo cha Sayansi za Afya kimepata ziada
ya shilingi 79,623,975 kwa mwaka 2015/2016.
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Chuo cha Sayansi za Afya kwa
mwaka wa fedha unaoishia Juni 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Chuo cha Sayansi za Afya kimepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha 2015/2016.
23.0 CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA)
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yameonekana kupungua kutoka
shilingi 12,566,712,308 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 10,955,608,931 kwa
mwaka 2015/2016 kukiwa na upungufu wa shilingi 1,611,103,377 sawa na asilimia
12.82 ya upungufu.
Taarifa ya Matumizi
Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimekadiria
kutumia jumla ya shilingi 14,756,438,319 ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2016
jumla ya shilingi 11,102,420,135 zimetumika sawa na asilimia 75.23 ya makadirio.
62
HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
63
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesbu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwiano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito kwa mwaka 2015/2016 umeongezeka ukilinganisha na mwaka
2014/2015. Hali hii inaonesha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kina uwezo wa kuhimili na
kukidhi dhima za mpito.
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 3,279,746,078 3,241,466,096
Dhima za mpito (current liabilities) 218,321,692 243,943,395
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities 15.02 : 1 13.3:1
64
65
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha kwamba mapato ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar
kwa mwaka wa fedha 2015/2016 yamepungua kufikia shilingi 10,955,608,931
ukilinganisha na shilingi 12,566,712,308 kwa mwaka 2014/2015. Aidha, ukaguzi
umebaini kwamba matumizi ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar yameongezeka kufikia
shilingi 11,102,420,135 ukilinganisha na shilingi 10,056,040,950 kwa mwaka
2014/2015.
Ukaguzi umebaini kwamba upungufu wa mapato hayo umechangiwa zaidi na kupungua
kwa misaada ya fedha kutoka kwa wahisani wa maendeleo kutoka shilingi
3,187,770,101 kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi kufikia shilingi 1,054,736,308 kwa
mwaka wa fedha 2015/2016. Aidha upungufu huo umechangiwa na mapato mengineyo
kutoka shilingi 192,994,549 kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi kufikia shilingi
133,385,782 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Maoni ya Ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kimepata hati inayoridhisha kwa mwaka
wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
24.0 SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA
Taarifa ya Mapato
Mapato ya Shirika la Meli Zanzibar yameonekana kuongezeka kutoka shilingi
7,540,478,026.71 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 8,721,602,539.62 kwa
mwaka 2015/2016 ikiwa ni ongezeko la shilingi 1,181,124,514 sawa na asilimia 15.5.
Taarifa ya Matumizi
Matumizi ya Shirika la Meli Zanzibar yameonekana kuongezeka kutoka shilingi
6,342,649,518.15 kwa mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi 10,959,437,155.20 kwa
mwaka 2015/2016 kukiwa na ongezeko la shilingi 4,626,787,637.10 sawa na asilimia 73
ya ongezeko.
66
67
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesbu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwiano wa mali za mpito ni mdogo ukilinganisha
na dhima za mpito kwa mwaka 2015/2016. Hali hii inaonesha shirika la meli na uwakala
halina uwezo wa kuhimili na kukidhi dhima za mpito.
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 513,957,790.27 863,739,670.31
Dhima za mpito (current liabilities) 2,154,703,649.31 2,053,778,383
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities 0.2:1 0.4:1
68
69
Uchambuzi unaonyesha kwamba Shirika la Meli na Uwakala limepata hasara ya shilingi
552,967,502.85 kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Hasara hiyo inaweza kupungua
iwapo jitihada za makusudi zitachukuliwa ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji,
pamoja na udhibiti mzuri wa ukusanyaji wa mapato.
MATOKEO YA UKAGUZI
Kukosekana kwa mikataba ya utoaji wa huduma za uwakala
Shirika la Meli na Uwakala hutoa huduma mbalimbali za uwakala kwa meli mbali mbali
za kigeni ambazo hazina usajili hapa Zanzibar.
Ukaguzi umebaini kwamba hakuna mikataba ya makubaliano baina ya Shirika la Meli na
wamiliki wa meli. Kufanya hivyo ni kwenda kinyume na Sheria ya Fedha ya Zanzibar
namba 12 ya mwaka 2005 pamoja na kanuni zake.
Wamiliki wenyewe wa meli (Shipping Liners) ni kama hawa wafuatao:-
CMA CGM
EMIRATE (WILHELMSEN)
PIL
UAFL
MSK
MSC
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Shirika la Meli na Uwakala kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Shirika la Meli na Uwakala limepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
70
25.0 MAMLAKA YA UVUVI WA BAHARI KUU
Taarifa ya Mapato
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu kwa mwaka wa fedha 2015/2016 imekusanya jumla
ya shilingi 2,913,640,961.51 ambapo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 imekusanya
jumla ya shilingi 1,917,891,250 kukiwa na ongezeko la shilingi 1,095,749,711.51 sawa
na asilimia 60.28
Taarifa ya Matumizi
Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu imetumia jumla ya
shilingi 1,758,591,435.12 ambapo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 imetumia jumla ya
shilingi 1,755,598,234.16 kukiwa na ongezeko la shilingi 2,993,200.96 sawa na asilimia
0.17 ya ongezeko.
71
HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
DEEP SEA FISHING AUTHORITY
BALANCE SHEET AS AT 30TH JUNE 2016
Assets Notes 2015/16 2014/15
72
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesbu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
Uchambuzi wa hesabu za Mali za Mpito za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu
zinaonekana kuongezeka kutoka shilingi 3,603,205,347.87 kwa mwaka wa fedha
2014/2015 hadi kufikia shilingi 4,401,230,258.05 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Aidha dhima za mpito zinaonekana kupungua kutoka shilingi 369,905,014 kwa mwaka
wa fedha 2014/2015 hadi kufikia shilingi 8,984,500 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 4,401,230,258.05 3,603,205,347.87
Dhima za mpito (current liabilities) 8,984,500 369,905,014
73
Uchambuzi unaonyesha kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu imepata ongezeko la
shilingi 1,155,049,526.40 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ukilinganisha na shilingi
62,293,015.85 kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Ziada hiyo inaweza kuongezeka zaidi iwapo jitihada za makusudi zitachukuliwa ikiwemo
kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na udhibiti mzuri wa ukusanyaji wa mapato.
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu
kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi
kufuatana na vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu limepata hati inayoridhisha kwa mwaka
wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
74
26.0 SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR
Taarifa ya Mapato
Shirika la Bandari Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2015/2016 imekusanya jumla ya
shilingi 29,916,824,568.20 ambapo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 imekusanya jumla
ya shilingi 25,543,319,987.20 kukiwa na ongezeko la shilingi 4,373,504,581 sawa na
asilimia 17
Taarifa ya Matumizi
Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Shirika la Bandari Zanzibar limetumia jumla ya shilingi
23,886,625,020.50 ambapo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 imetumia jumla ya shilingi
21,858,491,535.80 kukiwa na ongezeko la shilingi 2,028,133,484.70 sawa na asilimia
9.3 ya ongezeko.
75
HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
76
Uchambuzi wa hesabu za mwisho wa mwaka.
Uwiano wa mali za Mpito Ukilinganisha na Dhima za Mpito kwa mujibu wa hesbu za
mwisho wa mwaka ni kama ifuatavyo: -
Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwiano wa mali za mpito ni mkubwa ukilinganisha
na dhima za mpito kwa mwaka 2015/2016. Hali hii inaonesha Shirika la Bandari
Zanzibar lina uwezo wa kuhimili na kukidhi dhima za mpito.
2015/2016 2014/2015
Mali za Mpito (current assets) 18,045,555,484.92 19,840,101,259.35
Dhima za mpito (current liabilities) 4,949,873,792.70 6,434,625,586.66
Uwiano wa mali za mpito na dhima
za mpito (current ratio)
= current assets/current liabilities
3.6:1 3.08:1
77
78
Uchambuzi unaonyesha kwamba Shirika la Bandari Zanzibar limepata faida ya shilingi
4,620,772,945.52 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ukilinganisha na shilingi
4,166,260,540.68 kwa mwaka wa fedha 2014/2015. Faida hiyo inaweza kuongezeka
zaidi iwapo jitihada za makusudi zitachukuliwa ikiwemo kupunguza gharama za
uendeshaji pamoja na udhibiti mzuri wa ukusanyaji wa mapato.
Maoni ya ukaguzi
Kutokana na ukaguzi uliofanyika kupitia vitabu na kumbukumbu za mahesabu kwa
mujibu wa sheria na kanuni za ukaguzi, hesabu za Shirika la Bandari Zanzibar kwa
mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2016 zinaonesha sura sahihi na halisi kufuatana na
vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo Shirika la Bandari Zanzibar limepata hati inayoridhisha kwa mwaka wa
fedha unaoishia 30 Juni, 2016.
1.0 UTANGULIZI2.0 MAJUKUMU YA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI3.0 UPEO NA MADHUMUNI YA RIPOTI YA UKAGUZI4.0 NJIA ZILIZOTUMIKA KATIKA UKAGUZI5.0 MAJUKUMU YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI6.0 UMUHIMU WA KUFANYA UKAGUZI7.0 SHUKURANI8.0 MATOKEO YA UKAGUZI KWA MWAKA 2015/20169.0 UTEKELEZAJI WA HOJA ZA UKAGUZI ULIOPITA WA MWAKA WA FEDHA 2014/201510.0 UWASILISHAJI WA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016 KWA AJILI YA UKAGUZI11.0 AINA YA HATI ZA UKAGUZI11.1 Hati inayoridhisha11.2 Hati isiyoridhisha11.3 Hati yenye shaka11.4 Hati mbaya
12.0 MAMBO YALIYOBAINIKA KATIKA UKAGUZI WA MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR13.0 UKAGUZI WA HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/201614.0 SHIRIKA LA MAGAZETI14.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/201614.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016.14.3 MATOKEO YA UKAGUZI14.3.1 Uwezo wa Shirika katika upatikanaji wa mapato14.3.2 Uwezo wa Shirika kujiendesha kiufanisi pasipo kutegemea Ruzuku kutoka Serikali kuu14.3.3 Hali ya Ukwasi katika Shirika
15.0 SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR (ZBC)15.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/201615.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
16.0 CHUO CHA KILIMO –KIZIMBANI16.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/201616.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
17.0 MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR (ZAWA)17.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2015/201617.2 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/201617.3 MATOKEO YA UKAGUZI17.3.1 Visima vilivyochimbwa na mradi wa Ras - Al- Khaimah17.3.2 Kutokupata taarifa za ukodishwaji wa vibanda vya kuuzia maji17.3.3 Malipo yasiyokuwa na vielelezo (nyaraka pungufu) shilingi 9,150,00017.3.4 Deni la fidia shilingi 387,895,000
18.0 MAMLAKA YA VITEGA UCHUMI ZANZIBAR (ZIPA)18.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI
19.0 CHUO CHA UTAWALA WA UMMA -IPA19.1 TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI19.2 MATOKEO YA UKAGUZI19.2.1 Kasoro katika ukusanyaji wa mapato
20.0 CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR (ZITOD)20.1 HESABU ZA MWISHO WA MWAKA 2015/2016
21.0 CHUO CHA UANDISHI WA HABARI.UCHAMBUZI WA KIFEDHA (FINANCIAL ANALYSIS)
22.0 CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR23.0 CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA)24.0 SHIRIKA LA MELI NA UWAKALA25.0 MAMLAKA YA UVUVI WA BAHARI KUU26.0 SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR