44
Kimehaririwa na Gideon Byamugisha na Glen Williams Sauti Zenye Matumaini Viongozi wa dini wanaoishi au walioathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI

Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

  • Upload
    others

  • View
    35

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

Kitini cha TUMEITWA KUHUDUMIA kinajumuisha matendo, vijitabu vyenye kuhusisha matendo na miongozo midogo kuhusu mambo yanayohusu VVU na UKIMWI, vilivyoandaliwa kwa matumizi ya viongozi wa kanisa, hasa kwa nchi zilizo Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Madhumuni ya mambo yaliyomo ni kuwawezesha wachungaji, mapadre, watawa wa kike na wa kiume, walei viongozi wa kanisa na waumini wao pamoja na jamii ili waweze:

qKutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ya janga la VVU na wito wa Kikristo wa kuitikia kwa huruma.

qKushinda unyanyapaa, ukimya, ubaguzi, kukataa, woga na kukataa kubadilika, hali ambazo zinazuia kanisa na jamii katika kukabiliana na mambo yanayohusu VVU na UKIMWI kwa ukamilifu zaidi.

qKuwaongoza waumini wao na jamii katika mchakato wa kujifunza na kubadilika kutakakopelekea kwenye matendo na mienendo ya kikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ili kupunguza kuenea kwa VVU na kupunguza athari za janga la VVU.

TUMEITWA KUHUDUMIA ni wazo la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini, ambao wanatayarisha na kutoa vitabu na video vinavyohamasisha mbinu madhubuti na michakato ya kijamii ya kuhudumia, kusaidia na kuzuia VVU na UKIMWI katika nchi zinazoendelea duniani, hasa zilizoko Afrika chini ya Jangwa la Sahara.

TUMEITWA KUHUDUMIA inatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, shirikisho la muungano wa makanisa, na taasisi nyingine za kidini, miundo ya kimataifa ya makanisa, wachapishaji, wasambazaji na washika dau wengine.

WAHARIRI

Kasisi Kiongozi Gideon Byamugisha ni mchungaji aliyebarikiwa katika Kanisa la Uganda na mtunzi wa vitabu vingi vinavyohusu masuala ya VVU na UKIMWI na kanisa. Pia yeye ni Mwenyekiti mwanzilishi wa ANERELA+.

Glen Williams ni mwandishi kuhusu afya na maendeleo kimataifa, na ni mhariri wa Mtiririko wa Maandiko ya Mikakati ya Kuleta Matumaini.

ISBN 978 1 905746 10 1

Kimehaririwa na Gideon Byamugisha na Glen Williams

Sauti Zenye MatumainiViongozi wa dini wanaoishi

au walioathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI

Page 2: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa
Page 3: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

Sauti Zenye MatumainiViongozi wa dini wanaoishi au

walioathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI

Kimehaririwa na Gideon Byamugishana Glen Williams

Page 4: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa
Page 5: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

Shukrani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .4

Vifupisho na maana za maneno . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .4

Utangulizi mfupi: Kitini cha Tumeitwa Kuhudumia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .5

Maneno ya Utangulizi ya Kasisi Kiongozi Gideon Byamugisha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .8

Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .9

Ushuhuda wa 1: Mch Ayano Chule, Nigeria . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .11

Ushuhuda wa 2: Elsa Ayugi Ouko, Kenya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .13

Ushuhuda wa 3: Alhaji Mamman Musa Pumta, Nigeria . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .15

Ushuhuda wa 4: Mch David Balubenze, Uganda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .17

Ushuhuda wa 5: Anisia Karanja, Kenya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .19

Ushuhuda wa 6: Sheikh Ali Banda, Zambia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .21

Ushuhuda wa 7: Mch Paul Muwanguzi Sentamu, Uganda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .23

Ushuhuda wa 8: Mch Ephraim Disi, Malawi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .25

Ushuhuda wa 9: Sister Leonora Torach, Uganda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .27

Ushuhuda wa 10: Mch Christo Greyling, Afrika ya Kusini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .29

Ushuhuda wa 11: Jacinta Mulatya, Kenya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .31

Ushuhuda wa 12: Dr Pat Matemilola, Nigeria . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .33

Ushuhuda wa 13: ‘Mark’, Kameruni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .35

Ushuhuda wa 14: Mch Philippe Ndembe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . . . . . . . . . . . . .37

Kiambatanisho: Maana za misamiati . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .39

Yaliyomo

Sauti Zenye Matumaini

Page 6: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org4

SAUTI ZENYE MATUMAINI

Tunapenda kuwashukuru kwa dhati watu na mashirika yote yaliyochangia katika kukamilisha SautiZenye Matumaini.

Umoja wa Jamii ya Kueneza Injili na World Vision International ambao wamegharamia upembuzi,kuendeleza wazo na mpango kazi uliopelekea kwenye kuanzisha Tumeitwa Kuhudumia.Tunawashukuru mno kwa uaminifu wao, kwa kututia moyo na kwa uvumilivu wao. Tunapenda piakuwashukuru Baraza la Makanisa ya Diakonia,World Vision ya Afrika ya Kusini, Mch Dr Anne Bayley,Mch Christo Greyling, Sr Alison Munro, Logy Murray, Dr Welly den Hollander, Dr Lennart Karlsson,Tracey Semple, Mch Gary Thompson na Phumzile Zondi kwa msaada wao wa warsha za upembuzina mikutano ya mipango.

Aidha tunawashukuru sana CAFOD, ICCO na Meal-a-Day, ambao wamegharamia utayarishaji,uchapishaji na usambazaji wa kitabu hiki.

Kwa hakika tunawiwa mno na watu wafuatao ambao wamesoma na kuchangia katika hatua zamwanzo za uandishi wa kitabu hiki: Mheshimiwa Dr Justice O. Akrofi, Dr Sylvia J. Anie, Mch Brianna Mch Lynnel Bergen, Ken Casey, Dr Jenny Coley, Dr Rena Downing, Jean na Mch Sid Garland,Mch Sammy Gumbe, Mch Jape Heath, Anisia Karanja, Paulina Kumah, Roger Lees, Jo Maher, MchZebedee Masereka, Dr Pat Matemilola, Mch Fatusi Olayemi na Lucy Y. Steinitz.

Hendrix Dzama na Sheikh Ali Banda kwa ukarimu walitoa ushauri kwa kunukuu kutoka kwenyeBiblia na Koran.

Zaidi ya yote tunapenda kwa mioyo yetu yote kuwashukuru viongozi 14 wa dini ambao kwa mioyomyeupe wameturuhusu kuchapisha ushuhuda wao ndani ya kitabu hiki. Kwa kutushirikisha wana-vyojisikia, uzoefu wao na mtazamo wao juu ya VVU na UKIMWI, wanasaidia kubomoa kiambazacha ukimya, unyanyapaa na kujikana ambavyo bado vinazingira janga la VVU.

SShhuukkrraannii

Kanoni Gideon ByamugishaMwenyekiti, ANERELA+

Glen WilliamsMhariri wa Maandiko, Mikakati ya Kuleta Matumaini

VViiffuuppiisshhoo nnaa MMaaaannaa zzaa MMaanneennooUKIMWI ni Upungufu wa Kinga Mwilini

ANERELA+ ni Mtandao wa Afrika wa Viongozi wa Dini Wanaoishi au WalioathiriwaBinafsi na VVU na UKIMWI

ARV ni ufupisho wa maneno kwa lugha ya Kiingereza yanayomaanisha dawa yavirusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha

VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI

ICASA ni Kongamano la Kimataifa la Afrika kuhusu UKIMWI na Magonjwa yaNgono

KENERELA+ ni Mtandao wa Kenya wa Viongozi wa Dini Wanaoishi au WalioathiriwaBinafsi na VVU na UKIMWI

MVIU ni Mtu Anayeishi na VVU na UKIMWI

UNERELA+ ni Mtandao wa Uganda wa Viongozi wa Dini Wanaoishi au WalioathiriwaBinafsi na VVU na UKIMWI

VCT ni Ushauri-Nasaha na Kupima VVU kwa Hiari

Page 7: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

5www.stratshope.org

Utangulizi MfupiKuhusu kitini cha Tumeitwa Kuhudumia

Katikati ya maumivu na mahangaiko yoteyanayosababishwa na VVU na UKIMWI, watuwengi wamekuta ni vigumu kuuona uso waMungu wa Upendo. Bado kuna utamaduniimara wa Kikristo ambao tunapata kumjuaMungu kweli, si kwa jitihada ya akili, bali kwakuwaonyesha wengine upendo.

Waraka wa kwanza ya Yohana unasema:“Wapenzi, na tupendane; kwa kuwa pendolatoka kwa Mungu. Na kila apendaye ame-zaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.” (1 Yohana 4:7). Barua ya Yohana inaendeleakusema: “Kama mtu akisema, NampendaMungu naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yakeambaye amemwona, hawezi kumpenda Munguambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa nayeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu,ampende na ndugu yake”. (1 Yohana 4:20-21)

Hata hivyo, kuiweka kanuni hii kwenye matendo, sio rahisi wala vyepesi. Kinyumechake, inaweza kuwa vigumu sana kuwa-onyesha upendo watu ambao imani zao, tabiazao na viwango vyao vya maisha ni tofauti sanana vyetu. Bado tofauti hizi haziwafanyi kuwa pungufu katika familia ya binadamu, iliyo-umbwa kwa mfano wa Mungu. Na kamatukithubutu kuonyesha upendo wetu kwawengine, maarifa yetu juu ya upendo waMungu yanakua.

Yesu alisema: ‘Mpende jirani yako kama nafsiyako’. Katika nchi nyingi duniani makanisa naWakristo binafsi wanaitikia wito wa Kristo kwakufanya shughuli zinazohusu changamoto nyingi za VVU na UKIMWI ndani ya jamii zao.Afrika chini ya Jangwa la Sahara, mara nyingimakanisa yamekuwa mstari wa mbele katikajitihada za kuzuia madhara ya VVU na UKIMWI.Wanaonyesha kwa vitendo kwamba wamejisikiakuitwa kuhudumu kwa wale walioambukizwaau kuathiriwa na janga la VVU. Kwa mfanowamefanikiwa kubuni njia za kufanyaupatikanaji wa huduma muhimu za afya kwawatu wanaoishi na VVU, na kuwapa elimu,

msaada wa kijamii na huduma za afya watotoyatima waliotokana na UKIMWI.

Hata hivyo, kwa ujumla Makanisa yamekuwahayafanyi vizuri sana katika kushughulikiamatatizo kama kujikinga na UKIMWI, unyanya-paa unaotokana na UKIMWI, aibu, ubaguzi,tamaduni na mambo ya kijinsia yanayohusutabia hatarishi za kujamiiana. Kukataa ukweliwa VVU na UKIMWI ndani ya jamii za kanisaupo kwa kiasi kikubwa. Pamoja na kuwakujamiiana ndio njia kuu ya kuenea kwa VVUmiongoni mwa nchi nyingi, ni mara chachesana inazungumziwa ndani ya kanisa kwa uwazina katika hali isiyo ya kuhukumu.

Hivi hili ni la kushangaza kuliko? Wengi wetutunaona vigumu kuzungumzia mambo yanayo-husiana na kujamiiana, jinsia na vifo. Wakatiambapo hofu zetu zinatuzuia kueleza au hatakutaja hizi ajenda zinazosisimua, jamii zetuzimelemewa na mizigo ya matatizo yenye mizizi katika mambo yahusianayo na kujamii-ana afya na utofauti wa kijinsia: maambukiziyatokanayo na kujamiiana, mimba zisizota-kiwa, ugumba, magombano nyumbani,unyanyasaji wa kijinsia, na VVU na UKIMWI.Tunahitaji kwa haraka ‘kuvunja ukimya’ sio tukuhusu VVU na UKIMWI bali pia kuhusu kuja-miiana, tabia za kujamiiana na uhusiano usiosawia kati ya wanawake na wanaume. Hililinahusika zaidi kwa makanisa na jamiinyingine za kiimani ambazo mara nyingi pasipokukusudia wanachochea unyanyapaa, kukata-liwa na kubaguliwa kunako tokana na VVU naUKIMWI.

Kwa kweli makanisa hasa yaliyoko Afrika chiniya Jangwa la Sahara wana uwezo mkubwa wakuwaimarisha watu binafsi na jamii kuhusuufahamu, mtazamo, ujuzi na mikakati wanayo-hitaji katika kushughulikia masuala yanayohusukujamiiana, jinsia na VVU na UKIMWI. Muundowa taasisi zao - kutokea ngazi ya kijiji hadiKitaifa - zimepanuka zaidi ya idara yeyote yakiserikali. Wana majengo ambayo watuwanaweza kukutania, uongozi na wafanyakazi

Page 8: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org6

SAUTI ZENYE MATUMAINI

wenye ujuzi; wana mahusiano na jamii, viongozi wa kisiasa, maafisa wa serikali,wafanyabiashara, asasi zisizo za kiserikali(NGOs) na makundi mengine ya kiimani. Wanamagazeti yao na vipindi katika radio naruninga. Wanaendesha hosipitali, kliniki, shulena taasisi nyingine za elimu na mafunzoambazo hutoa taarifa na huduma kwa mami-lioni ya watu. Wana wachungaji, mapadre,watawa wa kike na wa kiume na watumishiwengine wanaotoa huduma za kichungaji, msaada wa kijamii na habari kwa familia najamii.

Pia makanisa yana mila imara za muda mrefukwa mfano; kuzaliwa,kuoa, kifo na ugonjwaambazo zinaweza kutumiwa kama mlango wakuingizia elimu na ujuzi mpya. Wanachamawake wamejiunga katika mitandao ya vyamana vikundi vyenye miundo ya namna yake, sheria na taratibu zao, wanamiliki ofisi nashughuli kwa ajili ya makundi fulani ya watukama watoto, vijana, wanafunzi, wanawake nawanaume. Zaidi ya yote, vitu vyote hivi vyakijamii na vifaa tayari vipo na ni endelevu.Kwa ujumla makanisa yanajumuisha rasilimalikubwa ya kijamii - japo kwa kiasi kikubwa haitumiki ipasavyo - katika kukabiliana nachangamoto ya janga la VVU.

Katika miaka ya karibuni, viongozi wengi wakanisa wametambua uhitaj wa juhudi za kuka-biliana na mambo yanayosababishwa na jangala VVU kwa nguvu na kwa uwazi katika upanawake. Ili kusaidia juhudi hizi, Wadhamini waMikakati ya Kuleta Matumaini wanatayarishavitini vya Tumeitwa Kuhudumia. Hii itaju-muisha jumla ya vijitabu vya miongozo ina-yoelekeza kutenda mambo yanayohusiana naVVU na UKIMWI kwa viongozi wa kanisa (walio-barikiwa na wasiobarikiwa) hasa walioko Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Mamboyatakayokuwa katika vitini vya TumeitwaKuhudumia yatatayarishwa ili kuwawezeshawachungaji, mapadre, watawa wa kike na wakiume, walei viongozi wa kanisa na wauminiwao na jamii ili waweze:

Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia,kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendomadhara ya janga la VVU na wito waKikristo wa kuitikia kwa huruma.

Kuushinda unyanyapaa, ukimwya, ubaguzikukataa, woga na kukataa kubadilika, haliambazo zinazuia kanisa na jamii katika kukabiliana na mambo yanayohusu VVU naUKIMWI kwa ukamilifu zaidi.

Kuwaongoza waumini wao na jamii katikamchakato wa kujifunza na kubadilikakupelekea kwenye matendo na mienendo yakikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familiana jamii ili kupunguza kuenea kwa VVU nakupunguza athari za janga la VVU.

Yaliyomo kwenye kitini cha TumeitwaKuhudumia yatakuwa ni machapisho 10 yenyemitazamo na ukubwa mbalimbali, kwa matu-mizi ya makundi ya kanisa na jamii katikangazi tofauti tofauti za uelewa na uzoefu juuya janga la VVU.

Mpango wa Tumeitwa Kuhudumiaunatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa,uwakilishi wa shirikisho la muungano wakanisa, taasisi nyingine za kidini, jumuia zakanisa za kimataifa, na mitandao, wachapaji,wasamba-zaji na washika dau wengine.Tunakukaribisha ushiriki katika TumeitwaKuhudumia, sio tu kwa kutumia yaliyomokwenye kitabu hiki kwa waumini wako au jamiiyako, bali pia kwa kutuandikia kuhusu uzoefuwako, ambao tungependa kuuweka kwenyetovuti ya Mikakati ya Kuleta Matumaini: www.stratshope.org.

Wenu katika imani na ushirika,

Glen WilliamsMhariri wa MaandikoWadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini

Page 9: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

7www.stratshope.org

Kuhusu ANERELA+Mtandao wa Afrika wa Viongoziwa Dini Wanaoishi au KuathiriwaBinafsi na VVU na UKIMWI(ANERELA+) ni mtandao wabara la Afrika wa viongozi wadini wa Kiafrika kutoka imanimbalimbali. ANERELA+ ilizindu-liwa mnamo mwezi wa Oktobamwaka 2003 mjini Kampala,Uganda, wakati wa mkutano wa11 wa Kongamano la Kimataifala Mtandao wa Dunia wa WatuWanaoishi na VVU na UKIMWI.Wajumbe wa ANERELA+ wame-dhamiria kufanya kazi bilakujali utofauti wa imani.

Ushiriki wa ANERELA+ katikatoleo hili - unaonyeshwa nashuhuda za Wakristo 12 naWaislamu wawili katika haliambayo haibadilishi kwa namnayeyote mtazamo huo. Badalayake, ukweli unaonyesha kwamba kwa sasa wengi waondani ya ANERELA+ ni Wakristo.Na kwa jinsi hiyo habari nyingizilizoelezwa humu zitakuwazinahusiana na makanisa, lakinizinaweza kuhusishwa na kutu-miwa katika mazingira ya imaninyingine.

Kuhusu Mwanzo wa Matumaini kuhusu VVUna UKIMWI wa World Vision International

Mwanzo wa Matumaini nimwitikio wa World Visionkuhusu janga la VVU na UKIMWIduniani. Ulizinduliwa mwaka2001, Mwanzo wa Matumainiunakusudia kupunguza athari zajanga la VVU na UKIMWI kupitianjia tatu ambazo ni kuzuia,kuhudumia na kushawishi.Mwanzo wa Matumaini unata-mbua taasisi za kiimani kamawadau wakuu katika kukabilianana mambo yote yanayohusianana janga la VVU na UKIMWI.Kwa hiyo mkakati wa msingi waMwanzo wa Matumaini ni

kuanzisha uhusiano mahususina makanisa na taasisi nyingineza kiimani. Viongozi wa diniwanaoishi au kuathiriwa binafsina janga la VVU na UKIMWIwanao uwezo wa kufanyamajukukmu muhimu ya uongozikatika kukabiliana na janga laVVU na UKIMWI ndani ya jamiizao za kiimani. Kwa kutambuauwezo huo, Mwanzo waMatumaini wana furaha ya kuwawadau washiriki wa ANERELA+na Wadhamini wa Mikakati yaKuleta Matumaini katika toleohili muhimu.

Page 10: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org8

SAUTI ZENYE MATUMAINI

Maneno ya Utangulizina Mchungaji Kasisi Kiongozi Gideon Byamugisha

Mamilioni ya watu duniani kote wanaendelea kuambukizwa VVU na kufa kwa UKIMWI. Baadhi ya maeneo ya dunia yameathirika zaidi kuliko mengine. Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado ndikoambako maumbukizi mapya ya VVU yako juu zaidi, vifo vitokanavyo na UKIMWI na watoto wanaoachwayatima kutokana na UKIMWI. Hata hivyo, maambukizi mapya ya VVU yanaongezeka katika bara la Asiana Mashariki ya Ulaya, hata nchi za Marekani ya Kati na Karebiani nazo hazijasitirika.

Habari njema ni kwamba ongezeko la kasi la maambukizi ya VVU na vifo vya UKIMWI vinazuilika. Aidhamaambukizi mapya ya VVU yanaweza kuzuilika na VVU na UKIMWI vinaweza kuhudumiwa, hivyo watuwanaoishi na virusi sio tu wanaweza kuishi muda mrefu bali wanaweza pia kufurahia maisha yenyehadhi nzuri. Hili kwa hakika linawezekana, ili mradi tunaweza kuushinda unyanyapaa, aibu, kukataliwa,na kubaguliwa ambavyo bado vinazuia hatua mahususi za kukabiliana kikamilifu na janga la VVU naUKIMWI.

Hata hivyo, kwa sasa athari za VVU zinazidishwa zaidi na unyanyapaa, aibu, kukataliwa na kubaguliwamambo ambayo yanazidi kumhatarisha mtu mmoja mmoja na kwa ujumla wao na pia kuzidisha athariza maambukizi ya VVU. Hofu ya kugundulika kuwa mtu ameambukizwa pia inawazuia watu hata kupimaVVU, ukiachilia mbali kujitambulisha kwamba wameambukizwa baada ya kupima. Inazuia juhudi zakuvunja mnyororo wa maambukizi ya VVU, na inawavunja moyo watu kutafuta na kutumia hudumazote zilizopo za kujikinga na VVU na UKIMWI, matibabu, huduma na misaada.

Pamoja na hayo, maumivu ya hisia ya mtu binafsi, familia, jamii na taifa ya wanaoishi na VVUyanaongezwa na kuzidishwa na hofu ya - na uhalisi wa - kukataliwa, kulaumiwa, aibu, kudhoofika navifo vinavyosababishwa na VVU na UKIMWI. Hali hii inawasababisha watu binafsi na kwa ujumla waokulikataa janga hili, kuwa na sera zisizofaa au zisizokidhi haja, kutokuwa na mipango na shughuli zina-zolenga kuzuia VVU na UKIMWI, huduma, matibabu na misaada katika ngazi zote. Hatimaye, unyanyapaa, aibu na lawama vinapunguza nafasi ya maisha ya mtu binafsi, familia, jamii, mataifa namabara kwa sababu ya mitazamo mibaya, hukumu za kimaadili zisizo sahihi na sera za ubaguzi.

Lakini waumini wa imani wakiwaona viongozi wao wanazungumzia hali zao wenyewe kuwa wana maambukizi ya VVU, itawakomboa wao. Hao wanaoishi na VVU wataacha kujisikia kunyanyapaliwa nakiambaza cha ukimya ndani ya jamii zetu kitavunjika kwa haraka. Kuushinda unyanyapaa ni mwanzo tuwa mipango mikubwa ya kufunguka kwa uwezo wa makanisa na jamii za imani nyingine ndani ya Afrikakatika kukabiliana na UKIMWI ana kwa ana.

Kila shuhuda ndani ya kijitabu hiki zinaonyesha waziwazi ushujaa, tumaini na ujasiri unaohitajika katika kukabiliana kwa mafanikio kushinda ‘kujinyanyapaa’ na ‘unyanyapaa wa kijamii’. Baadhi yashuhuda hizi zitakufanya ulie. Zingine zitakukasirisha. Zingine zinaweza kukufanya utikise kichwa kwakuonyesha kutokuamini. Kama shuhuda hizi zitasaidia kuvunja ukimya unaohusiana na VVU na UKIMWIkatika sehemu zako za ibada, makazi, kazini au mashuleni; kama zitakusidia kuzungumzia kwa uwazina ukweli bila kificho kuhusu imani potofu na kutokukubaliana na mambo ambayo bado yanazuia waumini wako, jamii au taifa kufanya yanayopasa kwa uhakika; kama zitasaidia kujadili zaidi nakufanya vizuri kama vikundi, kusanyiko au jamii; ndipo juhudi za watu hawa, waliopata ujasiri wakuzungumza kwa uwazi, hazitakuwa za bure.

Mchungaji Kasisi Kiongozi Gideon Byamugisha Kampala, Uganda

Page 11: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

9www.stratshope.org

UtanguliziSehemu hii inawakilisha habari kuhusu:

Kitabu hiki kinahusu NINI.

Kitabu hiki ni kwa ajili ya NANI.

KWA NINI kitabu hiki kimeandikwa.

JINSI GANI kitabu hiki kinaweza kutumika.

NINI?Kitabu hiki kinaleta pamoja uzoefu wa viongoziwa dini 14 wa Afrika - Wakristo 12 na Waislamwawili ambao aidha wanaishi na VVU auwameathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI.Inahusisha viongozi waliobarikiwa na watuwengine wasiobarikiwa ambao wana majukumuya kiuongozi katika jamii zao za kiimani. Wotehawa walishiriki mkutano wa kimataifa wakujenga uwezo kwa viongozi wa dini wanaoishiau kuathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI, uliofanyika Mukono, Uganda mnamo mweziNovemba 2004.1 Huu ulikuwa ni mkutano waimani mbalimbali, ulioandaliwa na ANERELA+na World Vision International.

Watu 11 miongoni mwao walioeleza shuhudazao katika kitabu hiki wameambukizwa VVU.Wengine watatu wamepima na kukutwahawana maambukizi, lakini maisha yaoyameathiriwa kwa kiasi kikubwa kwakuwahudumia ndugu wa karibu, marafiki auwafanyakazi wenzao ambao wamekufa namagonjwa shirikishi yanayosababishwa naUKIMWI.

Katika shuhuda hizi wanaeleza jinsi ambavyoVVU vimeathiri maisha yao kwa kiasi kikubwa,lakini pia imani zao zimewawezesha kukabili-ana na changamoto zenye kukatisha tamaazinazosababishwa na janga la VVU maishanimwao. Kati ya changamoto hizi, nyingi zinamizizi katika unyanyapaa, kukataliwa, kubaguliwa na kutokupata habari sahihi kuhusuVVU na UKIMWI mambo ambayo yamo ndani yajamii zenyewe za kiimani.

NANI?Mwanzoni kijitabu hiki kiliandikwa kwa upanamahususi kwa viongozi wa kanisa, ikiwa nipamoja na mapadre na wachungaji; watawawa kike na wa kiume; viongozi walei wakanisa, wafanyakazi na wanafunzi wa shule zaBiblia, vyuo vya theolojia na taasisi nyingineza mafunzo za kanisa; wafanyakazi wa hospi-tali za kanisa na vituo vya afya; viongozi waakina mama makanisani, ushirika wawanaume na makundi ya vijana; asasi za dinizisizo za kiserikali (NGOs); na mitandao nataasisi za kanisa za kitaifa, kikanda nakimataifa.

Yanaweza pia kunakiliwa na kutumiwa na jamiizingine za kidini na taasisi zisizo za dini kamavyama vya kupambana na UKIMWI mashuleni,vyuoni na katika vyuo vikuu, vyuo vya ualimuna asasi zisizo za kiserikali (NGOs) na makundiya kijamii yanayojishughulisha na kuhudumia,kusaidia, kushawishi na kujikinga na VVU naUKIMWI.

Kijitabu hiki kimetayarishwa ili kiweze kutu-mika pasipo mwezeshaji kupitia mafunzo yoyote maalumu.

Japokuwa viongozi wote wa dini wanaoelezashuhuda zao katika kijitabu hiki ni Waafrika,uzoefu wao unafanana kila mahali pasipokujali mipaka ya kijiografia.

KWA NINI?Kijitabu hiki kina madhumuni makuu matatu:

Kwanza, kuwezesha vikundi vya kanisa na jamiikujadili VVU na UKIMWI, afya, tabia za kuja-miiana na mambo yanayohusiana na dini natamaduni kwa uhuru na uwazi zaidi kulikoinavyokuwa kawaida.

Pili, kuonyesha kwamba kuwa na uambukizowa VVU sio sababu ya kuwa na aibu, kuvunjika

1 Kongamano la ufuatiliaji wa Kongamano lililofanyika Bangkok la Viongozi wa Dini Wanaoishi au Kuathiriwa Binafsi na VVU na UKIMWI, liliofanyikaMukono, Uganda, tarehe 1 - 7 Novemba, 2004, liliandaliwa na ANERELA+ na World Vision International. Kupata taarifa za mkutano huo, tafadhaliwasiliana na ANERELA+, 25 St Emins Street, Hurst Hill, Johannesburg, South Africa 2092.

Page 12: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org10

SAUTI ZENYE MATUMAINI

moyo, kukosa tumaini na kukatishwa tamaa aukubaguliwa.

Tatu, kusaidia kupunguza unyanyapaa unao-tokana na VVU ndani ya jamii za kidini kwakuonyesha kuwa viongozi wa dini pia wana-ambukizwa VVU, lakini kwamba wanawezakuishi kwa matumaini na kwa uwazi na virusi,wakimtumikia Mungu kwa kumaanisha na vizurizaidi kuliko awali.

JINSI GANI?Yaliyomo ndani ya kijitabu hiki ni utajiri wauzoefu ambao msomaji anaweza kuutumia kwakupata habari mwenyewe, au kunukuu wakatiwa kuwasilisha mada, kuandika nyaraka,mahubiri, mahojiano au warsha.

Hata hivyo, tunapendekeza kuwa kijitabu hikikinaweza kutumiwa na vikundi vya watu 10hadi 20 katika njia zifuatazo:

1. Mpangilio: Kila kipindi kidumu kwa dakika60 hadi 90 na kiongozwe na mwezeshajimmoja.

2. Maandalizi: Mwezeshaji achague ushuhudawa kujadili. Ikiwezekana atoe nakala ya kivulicha ushuhuda ili kila mtu kwenye kikundi awena nakala.

3. Kuanza: Anza kipindi kwa maombi, ombauongozi wa Mungu wakati wa majadiliano, naneema ya kuheshimu maoni na michangotofauti tofauti ya washiriki.

4. Misamiati: Tumia bango kitita, ubao au kadikubwa, andika maneno yafuatayo:

UnyanyapaaAibuKukataliwaKubaguliwaKutokufanyiwa kituKutendewa vibaya.

Uliza kikundi waeleze wanavyolielewa kilaneno la hapo juu kuhusiana na VVU na UKIMWI,andika maelezo yao mahali ambapo kilammoja wao anaona; kwa mfano kwenye bangokitita, ubaoni au kwenye kadi kubwa. Angaliakama tafsiri hizo zinalingana na tafsiri zilizo

kwenye kiambatanisho cha kijitabu hiki. Ulizani maneno gani wenyeji wanayoyatumia yenyemaana ya misamiati hiyo na uyaandike mahaliambapo kila mmoja wao ataona.

5. Ushuhuda: Wapatie washiriki nakala yaushuhuda. Waombe watu watatu au wannekusoma kwa sauti ushuhuda huo. Kamawashiriki hawana nakala za ushuhda, waruhusuwaandike wakati ushuhuda unasomwa. Fafanuakitu kisichoeleweka.

6. Tafakari ya Maandiko: Soma vifungu ndaniya Biblia (au Korani) vilivyowekwa chini yaushuhuda. Kifungu hiki kinatufundisha ninikuhusiana na mambo yaliyojitokeza katikaushuhuda?

7. Majadiliano: Uliza kikundi maswali yafu-atayo, halafu andika majibu katika bango kitita au ubaoni:

(a) Ushuhuda huu unaonyesha nini kuhusuunyanyapaa, aibu, kukataliwa, kubaguliwa,kutokufanyiwa kitu na kutendewa vibayakunakohusishwa na VVU na UKIMWI?

(b) Ni maumivu gani, hofu, masumbufu namashaka yaliyojitokeza kwenye ushuhuda huu?

(c) Ni kitu gani kingine kinakugusa wewe kilicho muhimu kwenye ushuhuda huu?

(d) Jinsi gani kikundi chako au washarika wakowanaweza kuchukua hatua juu ya baadhi yamambo yaliyojitokeza kwenye ushuhuda?

8. Hitimisho: Jumuisha majibu ya maswali ya7 (a) - (d) hapo juu na uliza ni nani kwenyekikundi angetaka aidha:

kuhusika kwenye shughuli yeyote ambayowalikubaliana baada ya kujadili swali la 7(d) au

kukutana tena ili kujadili ushuhudamwingine wa kwenye kijitabu. Kwenyekipindi kingine rudia kwa ufupi Hatua ya 4(Misamiati) kabla ya kuendelea na kipindi.

9. Maombi ya Kufunga: Funga kipindi kwamaombi ya kumshukuru Mungu kwa uongoziwake.

Page 13: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

11www.stratshope.org

Ushuhuda wa 1:

“Nilizaliwa katika mji wa Konso kusinimwa Ethiopia. Nikasoma huko AddisAbaba na baadaye nikasomea ufundi

umeme. Nikafanya kazi hiyo kwa miaka kadhaampaka nilipokutana na Askofu wa kanisa laKilutheri la Kristo la Nigeria, ambayealinikaribisha nchini kwake nikajifunze theolo-jia. Hivyo kati ya mwaka 1994 na 1998nikachukua shahada ya theolojia nchini Nigeria.

Mnamo mwaka 1998 nikaoa mwanamke waKinigeria na tukarudi Ethiopia, ambako nilifundisha shule ya Biblia ya Konso mpakaDesemba mwaka 2000, ambapo mke wangualizaa mtoto wa kiume. Alipofikisha umri wamiezi sita akapata majipu ambayo yalikuwahayaponi.

Daktari akapendekeza nipate kitabu kiitwacho“Pasipo na Daktari” ambapo nilijifunza kuwamajipu yasiyopona ni dalili ya uambukizo waVVU. Mwanangu alipimwa VVU na kugunduliwakuwa ameambukizwa. Nilipimwa na kugundu-liwa kuwa nimeambukizwa VVU pia ilasikumwambia mke wangu. Nilipendekeza turudi Nigeria ambapo tulirudi mwaka 2001, nanikapata kazi katika Dayosisi ya Kianglikana yaJos. Nikawa nasomea Shahada ya Udhamili yamasomo ya Biblia wakati nikiendeleakufundisha theolojia hapo.

Mke wangu akaanza kuumwa mwezi wa Oktoba2002. Akapimwa na kugunduliwa kuwa ame-

ambukizwa VVU. Afya yake ikazidi kudhoofukwa haraka na akalazwa hospitalini. Nilimtiamoyo aamini kuwa kufa sio kitu cha kuogopa.Ina maana ya kwenda kuwa na Kristo tu.Nakumbuka wakati alipokuwa anakufa,akinipungia kwaheri, kwani alikuwa dhaifusana hata hawezi kusema. Kabla ya kufarikialisema hajawahi kuona mtu aliyemhudumiakama nilivyofanya.

Baada ya mke wangu kufariki mwanangu alihitaji matibabu ya hospitali pia, lakini akafariki mnamo tarehe 26 Septemba 2004.Nilihangaikia gharama za matibabu ya mkewangu na mwanangu pia. Kwa neema ya Munguna kwa upendo na msaada wa kanisa laAnglikana Dayosisi ya Jos na marafiki wenginenchini Nigeria, gharama zote hizo zimelipwa.

Kabla mwanangu hajafariki, nilikaribishwakukutana na Kasisi Kiongozi Gideon Byamugishakwenye kongamano la wachungaji huko Jos.Waandaaji walinikaribisha kwa kuwa walikuwawanajua hali yangu kuwa nilikuwa nimeambu-kizwa VVU. Niliwapa changamoto wajumbewalioshiriki ili kusema ni wangapi wameambu-kizwa VVU, lakini hakukuwa na yeyoteambaye angalau hata amepima, hivyohawakuwa wanajijua hali zao kuhusiana naVVU. Baadaye nilifahamu kuwa wachungaji 25walikuwa wamepima VVU. Baada ya mkutanoGideon alinitembelea nyumbani kwangu nakunikaribisha Uganda, ambako nilikaa miezi

Ayano ChuleMchungaji Ayano Chule, kutokaEthiopia, alifundishwa kama Mchungajiwa Kilutheri na akabarikiwa na Kanisa laKianglikana la huko Nigeria. Kwa sasaanaishi Abuja Nigeria, ambako anafanyakazi kama Mratibu wa Kanda ANERELA+Afrika Magharibi.

Page 14: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org12

SAUTI ZENYE MATUMAINI

sita nikishirikiana na taasisi mbalimbali zina-zohusika na shughuli za VVU na UKIMWI,nikipata ujuzi na uzoefu kwa kazi yangu yasasa na ANERELA+ katika Afrika Magharibi.

Kama viongozi wa dini wanaweza kutafsiri tatizo la VVU kuwa njia za kuwasaidia watu nakumpendeza Mungu, hiyo itakuwa ibada yakweli kwa kila dini, kwa sababu dini zote zina-sisitiza huruma kwa binadamu wengine. Ni lazima tubadilishe VVU kuwa nafasi ya mawazoendelevu na njia ya kuushinda ujinga. Lakinikwanza ni budi tuukubali ujinga wetu nakutengeneza nafasi ya kuhudumia, kupenda nakusaidia watu wanaoishi na VVU.

Nimejifunza kwamba kuwa na uambukizo waVVU kumenipa nafasi bora zaidi ya kumtumikiaMungu. Theolojia ambayo ni eneo nililosomeana ninalolipenda, linahusika tu na jinsi yakushughulika na yale yanayotokea dunianikuhusiana na Mungu. Dunia haiko yenyewe tuila ina mwenyewe, ambaye ni Mungu. Dunia

ina makundi mbalimbali ya dini, yote yapo kwaajili ya Mungu. Maisha ya mwanadamu ndichokitu cha thamani zaidi kwa Mungu.

Umuhimu wa kitheolojia kuhusu VVU hainamaana kuwa ni ishara ya kukataliwa na Mungu.Na wala sio jambo la hofu ya kutisha, au laanaya kuepukwa. Mungu anatoa ufumbuzi kwakila tatizo la binadamu. Ni juu yetu, kamaviongozi wa dini kung’amua ufumbuzi waKimungu kuhusu VVU. Kama hatuwezi ni kosaletu wenyewe. Tunatakiwa kutafsiri VVU katikanjia bora ya kufikia makusudi ya Mungu kwajamii za watu.

Hii ina maana kwamba, kwa Mungu hakuna chaajabu kuhusu VVU. Sisi wanatheolojia ni lazimatubadilishe hali hii ya VVU kwenda kwenyehuruma, kutokubagua, na kutokuhukumu ilikuondoa mateso yetu. Mungu yupo tayari kutu-saidia - Mungu anasaidia walio wake - lakiniwanatheolojia Wakristo wengi bado hawafikiriiVVU katika njia bora ya kuwatumikia watu.”

&Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! ni dhiki, au shida, au adha, aunjaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajiliyako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakinikatika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, walamalaika, wala wenye mamalaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenyeuwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.(Warumi 8: 35 - 39)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Upendo wa Kristo’

Page 15: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

13www.stratshope.org

Ushuhuda wa 2:

“Mimi nimekuwa mjane kwa miakatisa. Wakati mume wangu alipo-fariki nilipimwa VVU na kugundu-

liwa nimeambukizwa. Kwanza niliwaambiawatoto wangu - sio tu kuhusu hali yangu yakuwa na uambukizo wa VVU bali pia kuwamume wangu alifariki kwa VVU. Kijana wanguwa miaka tisa alilipokea vyema. Kwa kwelialikwisha kuhisi kuwa wazazi wake wotetulikuwa na VVU.

Niliwaeleza pia ndugu zangu lakinihawakukubali, kwa hiyo nikaamua kutangazahadharani nikianzia na kanisani. NilimwambiaMchungaji kwamba nilikuwa nataka nitangazehali yangu ya uambukizo wa VVU kwenyekusanyiko kanisani, lakini akaniomba nisifanyehivyo. Nilinyamaza kwa kitambo, lakini ilikuwavigumu mno. Napenda kushirikisha uzoefuwangu, na kama siwezi kufanya hivyo napatashida moyoni. Mwishowe niliamua kuwa nita-sema. Hivyo baada ya ibada Jumapili moja,wakati watu wanakaribishwa kujitambulisha aukusema walikokuwa wametembelea, nilisi-mama na kuliambia kusanyiko kuhusu haliyangu ya VVU. Nilisema ‘Napenda kuchukuanafasi hii kuwaambia kuwa nina uambukizo waVVU’. Baadaye Mchungaji wangu alinichukuapembeni na nilimwambia ilinipasa kusemaukweli ili niishi kwa matumaini. Nilitaka kuishi.Nilitaka niwasomeshe watoto wangu. Na njia

pekee ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuweka wazihali yangu ya maambukizi ya VVU.

Mabadiliko makubwa yametokea ndani yaKanisa langu toka nilipojitangaza hadharani.Watu zaidi walioambukizwa VVU wameji-tangaza, na Kanisa ina meza ya kushughulikiaVVU. Nazungumzia VVU kila ninapohubiri.Mnamo 1999, Handicap International ilitusaidiasana kwa kuwadhamini watu watatu wanawakena wanaume walio na VVU kwenda kwenyemakanisa mbalimbali na kutoa ushuhuda.Kanisa langu pia limenidhamini kuhudhuriamakongamano ya Kimataifa, kama ICASA2 hukoNairobi mwaka 2003, na pia walinisaidia katika kundi la TIPHA (Kujihusisha na WatuWanaoishi na VVU na UKIMWI).

Sasa mimi ni bibi na watoto wangu wotewameshaondoka nyumbani, lakini wanajivuniakuwa na mimi. Binti mmoja ambaye mumewake ni daktari wa hospitali ya Nandi Hill,alinikaribisha kuzungumza na wafanyakazi wahospitali juu ya kuishi kwa matumaini na VVU.Binti mwingine alinikaribisha kuzungumza katika shule yake ya sekondari.

Lakini bado nataka Kanisa langu lijihusishezaidi na mapambano dhidi ya UKIMWI, ilikwamba WAVIU waweze kukubaliwa na viongozi wao wa dini na waumini wenzao. Hii

Elsa AyugiOukoElsa Ayugi Ouko ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa WaalimuWenye Matumaini wa Kenya na Katibuwa umoja wa Wamama katika Kanisa la Anglikana la Kitale, Kenya.

2 Ni Kongamano la Kimataifa la Afrika kuhusu UKIMWI na Magonjwa ya Ngono.

Page 16: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org14

SAUTI ZENYE MATUMAINI

itawasaidia WAVIU kuendelea kuishi. Bilamabadiliko hayo, unyanyapaa na kubaguliwakwa WAVIU makanisani kunawafanya wengiwetu kufa kwa msongo wa mawazo nasononeko. Lakini kama watu wakiwa wazi ina-punguza kuenea kwa VVU ndani ya waumini.Kama mimi, kwa mfano - hakuna mwanaumeanayenitongoza kwa sababu wanajua kuwanina uambukizo wa VVU.

Sijawahi kujaribiwa kulala na mwanaumekutimiza haja yangu ya kimapenzi, kwa sababu

sioni uhitaji huo. Pindi mpenzi wako anapokufa,unajisikia kusongwa na mawazo hivyo hujisikiikufanya ngono na ni rahisi kuacha kufanya. Pianilitaka kutunza uthamani wangu wa Kikristo najina jema la familia yetu. Lakini huwezi kuishihivyo bila kikomo. Sasa ninaishi kwenye nyumbakubwa peke yangu, naona uhitaji wa mwenza,na hili ni tatizo kwangu, wanaume wa umrikama wangu au wakubwa zaidi hupendelea kuoamabinti wadogo sio mtu kama mimi mwenyemiaka 40 na zaidi. Nataka niongee na Mchungajiwangu kuhusu hili tatizo.”

&Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Nawote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuzamali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kilamtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani yahekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwafuraha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote.Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. (Matendo 2:43-47)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Waumini wanafanya mambo pamoja’

Page 17: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

15www.stratshope.org

Ushuhuda wa 3:

“Nimekuwa naishi na VVU tangumwaka 1993. Nilijitangaza hadharani mwaka 2001 na

kuanza dawa za kupunguza makali ya UKIMWIna kuongeza kinga za mwili (ARVs) mwaka2002. Taasisi yangu ya Mwanzo wa Tumaini,inafanya kazi na Misikiti na Makanisa katikakushawishi na kuelimisha juu ya VVU naUKIMWI. Kuna rafiki wengine wawili Waislamuambao wana uambukizo wa VVU kutoka msikitini kwangu ambao pia wanajihusisha naMwanzo wa Tumaini. Walijitangaza baada yamimi kufanya hivyo.

Niliamua kujitangaza baada ya kuona jinsiunyanyapaa na ubaguzi ulivyokuwa kwa wingimisikitini na makanisani. Nilijitangazamwenyewe redioni na kwenye runinga.Nilikuwa mtu wa kwanza wa Nigeria yakaskazini kufanya hivyo. Ndugu wengine wambali katika familia yangu walinikataa, lakinindugu zangu wote wa karibu walinisaidia.Walisema labda Mungu ana kusudi na mimi.Sijateseka sana kwa kubaguliwa. Ninaposema msikitini watu wanasema kunamagonjwa mengi sana, hivyo kwa ninikuwabagua wenye ugonjwa huu?

Taasisi ya Kimataifa ya ActionAid Nigeria imeni-pangia niwe na kipindi cha nusu saa kila wikiredioni kusaidia kupunguza unyanyapaa unao-tokana na VVU. Watu wanakuja kwenye kipindina kusema hali zao za maambukizi ya VVU,

kuna watu wawili au watatu wapya kila wiki.Hata neno ‘UKIMWI’ limejaa unyanyapaa ndiomaana hapa tunatumia neno la Kifaransa ‘SIDA’katika matangazo ya redio. Pia kuna manenoya kienyeji hapa, kanjumo (= kukonda),ambayo tumeamua kujizuia kuyatumia kwasababu yamejaa unyanyapaa. Pia runinga yaTaifa, NTA, ilikuwa inatumia picha ya fuvukatikati ya moyo kuonyesha unyanyapaa, lakinitulilipinga hilo kwani linaongeza hofu naunyanyapaa, na wameacha kufanya hivyo.

Mnamo Julai 2004, pamoja na Jamii ya Afya yaFamilia na Wahamasishaji wa Afya ya Uzazi,tuliandaa kongamano la siku tatu la viongozi32 wa dini - wakiwa karibu sawa kwa sawaWakristo na Waislamu. Mkutano huu ulionyeshajinsi ambavyo viongozi wa dini walivyo naelimu ndogo kuhusu VVU na UKIMWI. Kulikuwana Shekhe mmoja aliyesisitiza kuwa mwenyeVVU ni lazima amefanya uasherati. Mwisho wakongamano viongozi wote wa dini walisemawanahitaji habari zaidi na mafunzo ya ushauri-nasaha juu ya VVU na UKIMWI. Sasawachungaji wanatuma watu kwa Mwanzo waTumaini kwa ajili ya habari na ushauri wa VVU.

Mwanzo wa Tumaini wana mkutano wa kilamwezi wa kikundi cha wahudumu, unaohu-dhuriwa na watu wapatao 40 katika kilaJumamosi ya mwisho wa mwezi. Shughuli zetuni nyingi na tofauti tofauti - kutoa mrejeshowa kile ambacho wajumbe wamejifunza katika

Mamman MusaPumtaAlhaji Mamman Musa Pumta ni Muislam naMkurugenzi wa Mwanzo wa Tumaini,ambayo ni asasi ya mchanganyiko wa diniisiyo ya kiserikali (NGO) iliyopo Maiduguri,Jimbo la Borno nchini Nigeria. Piaanafanya kazi kama Afisa Mipango katikaWizara ya Serikali ya Ardhi na Usanifu.

Page 18: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org16

SAUTI ZENYE MATUMAINI

warsha sehemu nyingine; kuwahamasishawajumbe juu ya mambo mapya; kujadilimambo kama unyanyapaa na kubaguliwa;kushirikishana mawazo mapya; kuwatembeleawajumbe walio wagonjwa na wasiowezakuhudhuria mikutano; na kusambaza virutubisho chakula.

Kila wakati tunapokutana, Wakristo naWaislamu huketi pamoja na kuomba kwa ajiliya rehema za Mungu. Ushauri wa kiroho piahutolewa kupitia mawaidha, kwa kunukuukutoka kwenye Biblia Takatifu na KoraniTakatifu na kupitia huduma ya kutembeleamajumbani.

Nimejihusisha na ANERELA+ kwa muda mfupi tu,lakini ninafurahi kwamba ipo na inatanuka.Imeniimarisha kuamini kwangu kwamba viongoziwa dini wanaweza kuleta mabadiliko katikamtazamo wa jamii juu ya watu wanaoishi na VVUna UKIMWI, na hivyo kupunguza unyanyapaa,kubaguliwa na kukataliwa. Nimejifunza ujuzimpya kama jinsi ya kufanya mpango wa mkakatimahususi kupitia uchambuzi wa ‘SWOT’3, na jinsiya kuandika mchanganuo wa mradi. Pia nimeji-funza juu ya usawa wa kijinsia, ambacho ni kitumuhimu sana nchini Nigeria. Dini sio sababu yakuwaweka wanawake nyumbani. Na dini isitu-mike kuhalalisha vitendo vya ukeketaji ambavyovinawaweka wanawake katika hatari zaidi yakuambukizwa VVU.”

&Mwogope Allah popote utakapokuwa, na baada ya matendo mabaya fanya matendo mema ili yaweze kufuta yale mabaya, na kuwafanyia watu kwa wema.(Hadith 18)

Mtazamo kutoka Hadithi4: ‘Maisha ya maadili’

3Strength (Uwezo), Weaknesses (Madhaifu), Opportunities (Fursa) na Threats (Changamoto) - angalia kitabu cha 2 cha kitini cha Tumeitwa Kuhudumia:Fanikisha.

4Kitabu kitakatifu cha Kiislamu, chenye misemo ya Mtume Muhammad.

Page 19: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

17www.stratshope.org

Ushuhuda wa 4:

“Nimeambukizwa VVU, na pianimeathiriwa na VVU. Nimepotezawatoto wangu wa kwanza na wa

pili kwa sababu ya UKIMWI, na mke wangu pia.Bado namlea binti yangu wa miaka mitanoambaye pia ameambukizwa VVU. Mke wanguwa kwanza aliniacha kwa sababu tulikuwa namtoto mmoja tu ambapo tulitaka wengi, naminilikataa kufuata matakwa yake alipotakatwende kwa mganga wa kienyeji. Nilibaki pekeyangu kwa miaka mitatu, na mnamo mwaka1991 nilioa tena kanisani. Mimi na mke wangutuliishi vizuri kwa furaha. Alikuwa mwema sanakwangu.

Mnamo mwaka 1999 mke wangu akaanzakuumwa na ndipo tukampeleka hospitali mbalimbali lakini hakupata nafuu. Tukaendahospitali ya Jinja, ambako wote tulipima VVU,wote tukakutwa tumeambukizwa. Sikujua chakufanya. Nilifundishwa kuwapa ushauri-nasahawatu wanaoishi na VVU na UKIMWI na nilikuwanafanya hivyo kwa wengine. Lakini mafunzoyangu ya ushauri-nasaha yalinisaidiakukubaliana na hali yangu. Nilijua ukwelikuhusu VVU na UKIMWI, na kwamba hayahayawezi kubadilika. Lakini nilikuwa najiuliza‘Kanisa litanichukuliaje? Je nijiuzuru?’ Ndiponilipokwenda kumwona mwangalizi wangu,Mchungaji Samuel Mugote, ambaye alilipokeavizuri. Akasema, hapana, nisijiuzuru.Inanipasa kuendelea kumtumikia Mungu, na

labda Mungu ana mpango nami. Aliombapamoja nami kisha nikarudi nyumbani.

Nikamtunza mke wangu kwa mwaka mmoja,alikuwa anatembelewa na mhudumu wa afyanyumbani. Walinifundisha pia namna ya kum-fanyia huduma nyumbani. Baada ya mwakaalionekana kuwa anapata nafuu. Wakatinilipokaribishwa kuhudhuria mafunzo katikachuo cha Biblia Kampala, nilishauriana na mkewangu naye akanishawishi nihudhurie, hivyonikaenda. Lakini wiki mbili baadaye mimipasipo kujua, akaanza kuumwa. Baada yamwezi nilikuwa nafanya mtihani pale Chuocha Biblia, baada ya mtihani nikaitwa ofisinikwa mkurugenzi, ambako nilikuta wachungajiwengine wamekwisha kukusanyika, lakinihawakutaka kuzungumza nami. Mwishowemkurugenzi akaniambia kuwa mke wanguamefariki katika hospitali ya Jinja.

Baada ya kurudi nyumbani nikaanza kuumwa,na TASO5 wakaniambia nianze matibabu ya kutu-mia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI nakuongeza kinga za mwili, ambapo nilitaka kuanza ila sikuwa na pesa ya kutosha kununuadawa na kuchunguza chembechembe za CD4.Nilikutana na marafiki kadhaa wa kijijini kwetuna nikawaambia hali yangu ya VVU. Na pia nili-waeleza wazee wangu wa kanisa, nao wakanitiamoyo kuendelea kutumika kama mchungaji.Sikuwa nimewaambia watu wa kanisa langu,

Mchungaji DavidBalubenzeMchungaji David Balubenze ni Mchungajiwa kanisa la Kipentekoste katika Wilaya yaKamuli, Uganda.

5 TASO (The AIDS Support Organisation) ni Asasi (NGO) ya Uganda inayoendesha kliniki ya kushughulikia VVU na UKIMWI huko Jinja.

Page 20: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org18

SAUTI ZENYE MATUMAINI

kwani kama mpentekoste, hilo ni gumu sana.Naogopa watu watanilaumu kuwa nimefanyamambo mabaya na kusababisha kifo cha mkewangu.

Tayari katika kijiji nilichoenda hivi karibuni,watu walikuwa wanasema Wapentekoste niwadhambi inapohusishwa na ngono. Walisemahayo kwa sababu walijua mke wangu alikufa

kwa UKIMWI. Lakini nimeamua kwambanitaweka wazi hali yangu ya VVU kwa wauminiwangu na hata zaidi ya hapo. Na pia natakakusisitiza kuwa watu wote wanaotaka kuoanalazima wapewe ushauri-nasaha na wapime VVUkabla ya kuoana.”

&Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo za chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake,na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii. Nao watapigana nawe;lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe asema BWANA, ili nikuokoe. (Yeremia 1:18-19)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Mungu ana mpango na maisha yako’

Page 21: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

19www.stratshope.org

Ushuhuda wa 5:

“Niligundua nimeambukizwa VVUmiaka 16 iliyopita. Nina watotowatatu, wote hawajaambukizwa

VVU. Wawili wakubwa wanajua kuwa nime-ambukizwa VVU, lakini mdogo hajui bado.Mimi ni Mkristo niliyeokoka, na kila mtukanisani kwangu anajua nimeambukizwa VVU.

Wakati nilipogunduliwa nimeambukizwa VVUdaktari aliniambia kuwa nina miezi mitatu tuya kuishi. Pasipo kujua nilikimbia kutoka hospi-talini na kurudi nyumbani. Nilikuwa bikiranilipokuwa naolewa hivyo nilihisi nitakuwanimeambukizwa na mume wangu. Niliwekakaratasi ya majibu ya kipimo mbele ya puayake na kumwambia ‘angalia umeniua’. Alikuwa msaada mkubwa sana kwangu na aka-jitoa kwenda kupima VVU, lakini alikutwahajaambukizwa. Nadhani niliambukizwa kupitiasindano au wakati wa kuzaa au upasuaji.

Siku hizo watu waliokufa kwa sababu yaUKIMWI walikuwa wanafungwa kwenye mifukoya nailoni kwa mazishi. Sikutaka jambo hili linitokee mimi. Nilitaka nife haraka, bila mtuyeyote kujua hali yangu ya VVU. Niliacha kulachakula na kunywa dawa, ili kwamba nifemapema iwezekanavyo. Lakini baada ya wikimoja nilisikia sauti ikisema ‘Dharau taarifa yadaktari - unakwenda kuishi.’ Ilikuwa waziwazikama sauti ya binadamu kweli. Kuanzia hapo,nikaanza kula na kujijali tena.

Nilimwambia Mchungaji wangu na kiongozi wawanawake kanisani kwangu kuhusu hali yanguya VVU. Waliahidi kuniombea pia wakanisaidia,kama kuniendesha kwenda na kurudi kanisani.Pia waliniambia nisimwambie mtu mwingineyeyote kanisani. Lakini miaka saba iliyopitaniliamua kumwambia kila mtu. Hivyo siku mojabaada ya kusoma neno la kwenye Biblia la sikuile, niliwaambia kusanyiko lote kwambanimeambukizwa VVU. Mwanzoni watu hawaku-jua walipokeeje. Walilia na kunikumbatia, lakini baadaye walinitia moyo na kunisaidia.Hakuna mtu yeyote aliyenipa mgongo.

Kanisani kwangu mimi ni mwenyekiti waKamati ya Maendeleo na Umoja wa Wanawake,ni katekista na mwana kwaya. Mpaka sasa nimimi peke yangu kanisani kwetu ambaye nime-jitangaza waziwazi kuwa nimeambukizwa VVU. Nimekwisha kuzungumza na watu kuhusu kuishina VVU na UKIMWI katika maeneo mengi -hosipitalini, mashuleni, vikundi vya wachu-ngaji, vyama vya waliopima na kadhalika.Watu wananiambia ni lazima nitakuwa na aina‘takatifu’ ya VVU kwa sababu nimekuwa navirusi kwa muda mrefu sana na bado nina afyanjema na nina nguvu. Sijaanza kutumia dawabado.

Baadhi yetu tumeunda kikundi kinachochukuahatua pindi tunaposikia mchungaji aliye-mfukuza kanisani mtu ambaye ameambukizwaVVU kwa kuwahukumu wenye VVU - kwa mfano

Anisia KaranjaAnisia Karanja anaishi Nairobi, Kenya. Nimuumini wa Kanisa la Kimataifa la Kristo,na ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Kenyawa Viongozi wa Dini Wanaoishi auKuathiriwa Binafsi na VVU na UKIMWI(KENERELA+)

Page 22: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org20

SAUTI ZENYE MATUMAINI

kwa kutumia vifungu vya maneno kama ‘msha-hara wa dhambi ni mauti’. Tunakwenda nakumweleza mchungaji kwamba maneno yao namatendo yao yanawalazimisha watu kulikimbiakanisa.

Nchini Kenya ni watu wa kawaida tu mpakasasa waliojitokeza kuhusu hali zao za ma-ambukizi ya VVU. Ikiwa mchungaji atakiri kuwaameambukizwa VVU, atafukuzwa mara moja.Watu watamlaumu kuwa ndiye chanzo cha

kutoendelea kwa kanisa, na kumshambuliayeye moja kwa moja. Watasema manenokama, ‘inawezekana vipi wewe kutuombeaikiwa wewe mwenyewe ni mwenye dhambi?Wakristo wa kweli hawapati VVU. Huna imaniya kutosha ndio maana unaumwa.’

Mstari wa Biblia unaonifanya niendelee mbeleni Zaburi 118:17, unaosema: ‘Sitakufa balinitaishi, Nami nitayasimulia matendo yaBWANA.’”

&Basi Yesu aliwaambia tena, ‘Amini, amini, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wakondoo. Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi, lakini kondoohawakuwasikia. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingiana kutoka naye atapata malisho. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.’ (Yohana 10: 7-10)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Maisha katika utimilifu wake’

Page 23: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

21www.stratshope.org

Ushuhuda wa 6:

“Nilianza kujishughulisha na kazi zina-zohusu VVU na UKIMWI kwa kukaana ndugu yangu mkubwa na familia

yake wakati nasoma Lusaka. Mke wake ali-umwa na kufariki dunia, akiacha mtoto mdogowa miezi saba, ambaye pia baadaye aliugua nakufariki. Baadaye alipima na kukutwa ame-ambukizwa VVU. Ndugu zake wengi walikuwana mtazamo usio mzuri. Hata pamoja nakwamba hakuwaambia hali yake ya maambu-kizi ya VVU, walihisi na kukwepa kukutananaye. Nilimtunza pale nyumbani kwake, halafunyumbani kwangu, mpaka alipofariki mwakammoja na nusu baadaye.

Hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 1990,wakati uelewa na ufahamu wa jamii kuhusuVVU na UKIMWI ulikuwa bado ni wa chini sana.Watu walinihisi kuwa nimepata maambukizitoka kwa ndugu yangu aliyefariki, hivyowalinikwepa pia. Mwishowe nikaanza kuogopakwamba labda ni kweli nimeambukizwa VVU.Hatimaye mnamo mwaka 1997, nilienda kupi-ma VVU, majibu yakawa kuwa sina maambu-kizi! Baadaye niliondoka kwenda Sudani naSaudi Arabia kwa ajili ya masomo yangu, nilipima tena VVU zaidi ya mara moja, na kilawakati nilionekana sina maambukizi.

Niliporudi Zambia nilijishughulisha na shughulizinazohusu VVU, na muda sio mrefu nilianzakukaribishwa kwenye mikutano na majadiliano

mbalimbali. Nilikuwa mmoja miongoni mwawatu watatu kutoka Zambia waliohudhuriawarsha ya ANERELA+ kwa Viongozi wa DiniWanaoishi au Kuathiriwa Binafsi na VVU, ulio-fanyika Zimbabwe mwaka 2004. Jamii yaKiislamu nchini Zambia imeanza kuwa na jiti-hada zaidi kwenye shughuli zinazohusu VVU naUKIMWI. Kwa mfano, mwezi wa Oktoba 2004tuliitisha kongamamo la kitaifa lilioandaliwa naJumuiya ya Vijana wa Kiislamu wakishirikianana wadau wa Jumuiya ya Kimataifa ya VVU naUKIMWI, ikiwa na uwakilishi wa kimataifa katika wazo la Jihadi dhidi ya UKIMWI.

Mtazamo wa ANERELA+ juu ya viongozi wa dinini wa kipekee na wa muhimu sana kwa sababuviongozi wa dini ndio wahusika kutunza mamboya kiroho na maadili mema. Kwa sasa viongoziwa dini ndio wachangiaji wakuu wa unyanya-paa, kukataliwa na kubaguliwa kunakohusianana VVU. Inahuzunisha mtu aliye na maambukiziya VVU anapokwenda kwa viongozi wake wadini badala ya kupata msaada anakataliwa.Lakini kama viongozi wa dini wangekuwawameelimishwa vizuri na kufundishwa jinsi yakuwasaidia watu wanaoishi na VVU, wangejuajinsi ya kuwasaidia katika hali ya uelewa nabora zaidi.

Mpango wa ANERELA+ wa kuhusisha dini zotepamoja ni wa thamani sana. Hata hivyo kiladini ina mipango yake, lakini tunapoweka

Ali BandaShekhe Ali Banda ni Imam wa kituo chaKiislamu cha Kuomboka Lusaka, Zambia.Yeye pia ni mtawala na mwakilishi waBaraza la Ulimwengu la KiislamuZambia, na ni mjumbe wa bodi yaANERELA+.

Page 24: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org22

SAUTI ZENYE MATUMAINI

nguvu pamoja juu ya jambo fulani inakuwa nauzito zaidi. Katika nchi nyingi za Kiafrika watuwa imani tofauti wanaishi pamoja kama maji-rani kwenye jamii zao, na kama tungejaribukuweka vitu tofauti ingekuwa ni vigumu sanakushughulikia matatizo ambayo yanawakabiliwote.

Mkutano huu6 umefungua ukurasa mpya kwaANERELA+. Kwa njia ya kuongea na watu hapa,nimegundua kuwa tunakubaliana kimtazamojuu ya mambo kama unyanyapaa, aibu,

kukataliwa na kubaguliwa mambo ambayo nimuhimu sana kwa ANERELA+. Tusipokabilianana mambo haya, watu wataendelea kufamapema kwa UKIMWI. Kwa upande wanguimenisisimua kuona jinsi watu wanavyoongeajuu ya njia ya ki-Mungu ya kukabiliana na VVUna UKIMWI, na jinsi kila mtu anavyokubalianajuu ya uhitaji wa kuwapa viongozi wa dinihabari sahihi na kwa ufasaha. Viongozi wa diniwana hamu ya kujua zaidi kuhusu VVU naUKIMWI, na kukiwa na habari zaidi tutawezakupambana na janga hili kwa ufanisi zaidi.”

6 Kongamano la ufuatiliaji wa Kongamano lililofanyika Bangkok la Viongozi wa Dini Wanaoishi au Kuathiriwa Binafsi na VVU na UKIMWI, liliofanyikaMukono, Uganda, tarehe 1 - 7 Novemba, 2004, uliandaliwa na ANERELA+ na World Vision International.

&Haki haijalishi umetazama mashariki au magharibi. Mtu mwenye haki ni yuleanayeamini juu ya Siku ya Mwisho, juu ya malaika wa Kitabu na manabii; ambayejapo anaupenda sana, aweza kuutoa utajiri wake kwa nduguze, kwa yatima, kwamaskini sana, kwa wasafiri walio katika uhitaji na kwa ombaomba, na kwa ukombozi wa mateka; anayetimiza ibada na anayelipa zaka zake; mkweli katikaahadi zake na imara wakati wa majaribu na hatari na wakati wa vita. Hao ndiowaamini wa kweli; Hao ndio wamwabuduo Mungu. (Korani Takatifu sura ya 2, aya ya 177)

Mtazamo wa Korani: ‘Upendo kwa Mungu na Binadamu’

Page 25: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

23www.stratshope.org

Ushuhuda wa 7:

“Ninatoka katika familia ya kichungajina mimi ni Mkristo aliyeokoka.Nilipokuwa mdogo nilikuwa na aibu

sana na sikumfahamu mwanamke mpakanilipomuoa Sarah. Nilifanywa shemasi wakanisa la Uganda mwaka 1982. Nilioa mwaka1983 na nilibarikiwa kuwa mchungaji mwaka1984. Sarah alikuwa mhasibu na pia mwinjilisti.

Mwaka 1986 nikawa mhasibu wa dayosisi. Saraalikuwa na matatizo ya mfumo wa uzazi hivyoakafanyiwa upasuaji mwaka 1984, 1990, na1995. Mnamo miaka ya 1980 watu walikuwawanajitolea damu, na iliweza kutumika hospi-talini bila kupimwa VVU. Ilikuja kugundulikakuwa mmoja wa watu waliomtolea Sarah damualifariki kwa UKIMWI miezi mitatu baada yaupasuaji. Ilionekana kuwa Sarah alikuwaameambukizwa kwa njia hiyo. NilimshauriSarah apimwe VVU, lakini akakataa, na sikuwana ujasiri wa kumsisitiza, au hata mimimwenyewe kupima bila kumwambia yeye. Kwahiyo sikupima.

Siku ya Alhamisi Kuu, mwaka 2000, Sarahalianza kuumwa na akawa kitandani siku nzimaya Ijumaa Kuu mpaka Jumatatu ya Pasakaambapo alienda hosipitali. Alifariki wiki mojabaadaye.

Namshukuru Mungu kwa ajili ya mke wangumpendwa Sarah, ambaye nilikuwa na furaha

sana naye japo tulikuwa hatuna watoto.Mnamo mwezi wa Oktoba 2000, baada yakuongea na daktari, nilipima VVU na kukutwanina maambukizi. Siku mbili baadaye niliendakumuona Askofu wangu, ambaye alinipa polesana na kunitaka nianze matibabu harakainavyowezekana. Nikaenda hosipitali yaMildmay na nikaandikiwa dawa, ambazo badonatumia. Niliomba kwa muda wa saa nzimakwamba dawa zifanye kazi vizuri, na imekuwahivyo.

Mch Gideon Byamugisha alijua juu ya haliyangu na akanitembelea. Tulizungumza juu yakuishi na VVU ukiwa kama padre. Ilinisaidiakujikubali mwenyewe vile nilivyo na VVU. HataYesu alipigiliwa na misumari msalabani, amba-cho kilikuwa kifo cha muuaji. Mimi ni parokowa parokia na nawaombea wengine, nawanapona. Kwa hiyo na mimi pia najiombeamwenyewe kwa Mungu. Lakini hata sasa ninayomengi ya kushukuru. Gideon aliniambia nisikaepeke yangu kwa muda mrefu. Sikudhani kamanitaweza kuoa tena, lakini nimeoa, na Beatriceni mke mwema sana. Mungu na ambariki.

Ni ombi langu kuwa watu wanaoishi na VVU naUKIMWI wakubali hali zao, watafute matibabuna kuishi maisha yenye mafanikio, wakimtege-mea Mungu, ambaye anaweza na yu tayarikushughulika na matatizo yetu ili mradi tunamtumaini.”

PaulMuwanguziSentamuMchungaji Paul Muwanguzi Sentamu nimchungaji wa kanisa la Anglikana, parishiya Kampala, Uganda.

Page 26: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org24

SAUTI ZENYE MATUMAINI

&Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vileroho yako ifanikiwavyo (3 Yohana 2)

Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wakewakamuuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazaziwake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazaziwake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. (Yohana 9:1-3)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Afya katika mwili na roho’

Page 27: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

25www.stratshope.org

Ushuhuda wa 8:

“Mnamo mwaka 1993 nilirudi tokamasomoni nchini Nigeria na kukutakuwa mke wangu alikuwa

mgonjwa. Aligundulika kuwa na maambukizi yaVVU lakini pia alikuwa na tatizo la moyo.Nilikaa naye mpaka alipofariki mnamo mwaka1995, na baadaye nikajitenga peke yangu.Nilikuwa sijui la kufanya kwa sababu nchiniMalawi kujulikana kuwa wewe ni mtu mwenyeUKIMWI ni sababu ya aibu na fadhaa.

Mnamo mwezi wa Julai 1996 rafiki mmojaalinitia moyo kupima maambukizi ya VVU, nanikakutwa nimeambukizwa. Nilitunza habari hiipeke yangu, lakini nilifikiri kuwa ndio nakufana hakuna sababu ya kuendelea kamaMchungaji, hivyo niliwaambia viongozi wanguwa kanisa kuwa nataka kujiuzulu. Kwa kwelimimi ni Mkuregenzi Mkuu wa kanisa langu,hivyo watu ambao niliwaeleza walikuwa chiniyangu katika mfumo wa uongozi wa kanisa langu. Hata hivyo hilo halikufanya zoezi lakusema siri yangu kuwa rahisi. Nilichokuwanaogopa zaidi ni aibu, kwa sababu kwamtazamo wa jamii VVU na UKIMWI vina uhu-siano na kutokuwa mwaminifu katika ndoa.

Baadhi ya viongozi wa kanisa walinisihi nioetena na kuendelea na huduma. Nilipatamwanamke ambaye alikuwa tayari nimuoelakini nilisisitiza kuwa tupime VVU. Nilidhaniatakataa akikuta kuwa mimi nina maambukizi

ya VVU. Lakini wote tulikutwa tuna maambu-kizi na hata hivyo tulioana.

Mnamo mwaka 1999 nilipata mkanda wa jeshimkali sana na chembechembe zangu za CD4zilikuwa chini sana yaani 143, lakini niliende-lea kufanya kazi. Mnamo mwaka 2001 mmojawa viongozi wa kanisa alipendekeza nijiuzululakini baadaye aliondoa pendekezo lake.Mnamo Januari 2002 nilihudhuria kongamanonchini Zimbabwe lililojulikana kama ‘Kugeuzamagumu kuwa fursa’ lililokuwa limeandaliwana Mch Gideon Byamugisha. Walihudhuria viongozi wa dini kama 40. Kasisi KiongoziGideon alitushirikisha maono yake ya mtandaowa viongozi wa dini walioambukizwa aukuathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI. Mkutanohuu mwishowe ulipelekea kuundwa kwaANERELA+.

Mnamo Machi 2003 niliamua kusimama nakuwashirikisha viongozi wangu wa kanisa haliyangu ya kuwa na maambukizi ya VVU.Nilikuwa nimekwisha kuwaambia familia yanguna marafiki wa karibu. Baada ya kutangazakwa viongozi wangu wa dini kulikuwa naukimya wa ajabu - wote walishtuka sana.Niliweza kuwashawishi kuwa nilichokuwa nahitaji kutoka kwao ni msaada na kunielewa.

Nilianza dawa za virusi-geuzi (ARVs) mnamoMachi 2003, na miezi minane baadaye

Ephraim DisiMchungaji Ephraim Disi ni MkurugenziMkuu wa kanisa la kiinjili la Ndugukatika Kristo, Blantyre, Malawi.

Page 28: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org26

SAUTI ZENYE MATUMAINI

chembechembe zangu za CD4 zilikuwa zime-ongezeka mara mbili. Pia nikawa mshirikimzuri wa ANERELA+, na napenda kuwashukuruwadau wenzangu wote wa ANERELA+ kwamsaada wao. Nimejifunza mengi kupitiaANERELA+.

Sasa natambua kuwa kama kiongozi wa dinimwenye maambukizi ya VVU, nina kitu chaziada ninachopaswa kukitumia katika huduma

yangu. Kwanza kama kiongozi mkuu wa kanisa,watu wako tayari kunisikiliza. Fursa ya pili,watu wako huru kuzungumza waziwazi na mimikuhusu hofu zao, na kuhusisha kwa matumainikuhusu mimi. Pia marafiki zangu na wauminiwa kanisa langu wameona kupitia kwangukuwa maisha tele yanatafsiriwa na ubora wakena sio wingi wake. Ninaweza kuishi kila sikukatika ukamilifu na furaha pamoja na mapu-ngufu tunayoyakabili.”

&‘Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mamboyoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.Nayaweza mambo yote katika yeye anitaye nguvu.’ (Wafilipi 4: 12-13)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Nguvu kupitia imani’

Page 29: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

27www.stratshope.org

Ushuhuda wa 9:

“Kama mtawa wa kidini katika kanisala Kikatoliki, nimeguswa na kuathi-riwa binafsi na VVU na UKIMWI.

Nimempoteza mwana familia yangu kwasababu ya UKIMWI. Mbali na maumivu na majuto ya kumpoteza mpendwa wetu, badotunatakiwa kujitahidi kuendelea kuwatunzayatima na wajane walioachwa.

Katikati ya waumini wa dini yangu, wengi wetutunateseka kimya kimya kwa sababu kilammoja wetu ana habari ya kusononesha yakushirikishana kuhusu changamoto za VVU naUKIMWI. Popote ninapokwenda nakutana naukweli unaoumiza wa janga la VVU na UKIMWI.Kama sio wale wanaoishi na virusi kila siku,basi ni yatima na bibi au babu zao, ambaokatika uzee wao wanalazimika kuwahudumiawanafamilia walioambukizwa na watoto wao.

Sasa ninaelewa ukweli unaouma kuwa mtu yeyote ana hatari ya kuambukizwa VVU, pasipo

kujali uhusiano wa hadhi yake ya alikotoka,kiwango cha elimu yake, dini anayohusiananayo na taaluma yake. Inavuka mipaka yote.Hata hivyo, kama mtu binafsi, nimetambua yakwamba njia mojawapo ya kushughulika na hizichangamoto za VVU na UKIMWI ni kuzikubalichangamoto hizi na kuungana na wengine katika kuendeleza uelewa zaidi katika masualayanayozunguka janga hili, na kupambana naunyanyapaa, aibu, kukataliwa, kuhukumu, ujinga na mambo potofu yanayohusishwa naVVU na UKIMWI.

Hili linawezekana kama tutajifunza kukubali nakuwachukulia kaka na dada zetu wanaoishi naVVU na UKIMWI kwa uthamani na heshimawanayostahili kama binadamu. Hawahitajituwahurumie wala kuwasikitikia. Wanacho-hitaji na kutamani kutoka kwetu ni ukweli,upendo wa dhati toka moyoni na kuelewa. Njiamojawapo ya kupambana na VVU na UKIMWI niuwazi, hasa kwa watu ninao wathamini sana.”

LeonoraTorachMtawa Leonora Torach ni mwanachamawa shirika la masista wa Maria Mama waKanisa, jumuia ya Kikatoliki iliyoko katika dayosisi ya Lira, Uganda. Kwasasa anachukua shahada ya udhamili yaSaikolojia (Ushauri-nasaha) katika ChuoKikuu cha Makerere, Kampala

Page 30: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org28

SAUTI ZENYE MATUMAINI

&Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewamwiba katika mwili, mjumbe wa shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akani-ambia, ‘Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.’Basi nitajivunia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juuyangu. (2 Wakorintho 12: 7-10)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Kuteswa kwa ajili ya Kristo’

Page 31: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

29www.stratshope.org

Ushuhuda wa 10:

“Niligundulika nina uambukizo wa VVUmnamo mwezi wa Agusti 1987.Wakati huo nilikuwa bado mwana-

funzi wa Theolojia, katika Chuo Kikuu chaStellenbosch. Nililazimika kubadilibadili hospitali, na katika hospitali mpya niliyo-kwenda walijumuisha kipimo cha VVU katikavipimo vya kawaida vya damu. Nilipokwendakumuona daktari aliniambia kwa kawaida tukuwa nilikuwa na uambukizo wa VVU. Ulikuwani mshituko mkubwa sana kwangu, kwani siku-jua hata kama nilikuwa ninapimwa VVU.Daktari alihitimisha kuwa nitakuwa nime-ambukizwa na vimelea vya kugandisha damuambavyo nimekuwa ninachoma kwa sababunilikuwa na ugonjwa wa damu ujulikanao kamahaemophilia.

Wakati nagunduliwa kuwa na uambukizo waVVU nilikuwa nimeanza uhusiano na kutoka njena Liesel kwa miezi sita, ambaye nilikutananaye kanisani. Niliamua tusitishe uhusianonaye kwa sababu nilidhani kuwa nina mudamfupi tu wa kuishi. Nilifikiri kuwa isingekuwavyema kwa Liesel kuishi kwa kunyanyapaliwakwa sababu aliwahi kuolewa na mtu aliyekufakwa UKIMWI. Nilifikiri pia kuwa tusingewezakupata watoto kamwe, na ya kuwa Lieselmwenyewe angeweza kuambukizwa VVU.Lakini nilipomwambia Liesel haya yote, aka-pata hasira sana. Alisema alinipenda hatakabla sijajua kama nimeambukizwa VVU na

kwamba virusi visingeweza kubadilisha hilo.Hata hivyo, ilibadilisha mahusiano yetu, katikahilo mahusiano yetu yakazidi kuwa imara zaidikuliko ilivyokuwa mwanzo!

Miezi minane baadaye, Liesel na mimitukaoana. Ilikuwa ni siku ya kukumbuka kuza-liwa kwangu na pia Jumapili ya Ufufuko.Kwangu mimi hii ilikuwa ni ishara ya tumainiimara kwa kujua kwamba tunakumbuka kwamba Kristo alifufuka na akaleta tumainiulimwenguni. Ilinipa na mimi tumaini lakuweza kuishi maisha haya pamoja na Liesel.Tuliwaeleza watu wachache tu wa familiayangu kuhusu hali yangu ya uambukizo waVVU. Miezi tisa baada ya ndoa yetutukawaeleza wazazi wa Liesel kuhusu haliyangu ya uambukizo wa VVU lakini tuliwaombawaituze kama siri. Kwa miaka mitano wali-ubeba mzigo huo peke yao bila kuwaambiadada au kaka wa Liesel au ndugu wa karibu.

Mnamo mwezi Mei 1992 tuliamua kuwa nisemehadharani hali yangu ya uambukizo wa VVU.Tulikuwa tunaishi Windhoek, Namibia, ambakonilikuwa nafanya kazi kama mchungaji katikakanisa la hapo. Vyombo vya habari vilili-zungumzia kwa bidii jambo hilo, na wotewalikuwa wakinihurumia sana kwani nili-ambukizwa kupitia vimelea vya damunilivyokuwa napewa kama dawa. Vyombo vyahabari vilinichukulia kama nisiyekuwa na hatia,

ChristoGreylingMchungaji Christo Greyling ni mchun-gaji aliyebarikiwa wa Kanisa la DutchReformed la Afrika ya Kusini. LikoJohannesburg, anafanya kazi na WorldVision International kama Mshaurikuhusu VVU na UKIMWI na Taasisi zaUshirika wa Makanisa na Kiimani.

Page 32: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org30

SAUTI ZENYE MATUMAINI

lakini wale waliopata VVU kupitia ngonowanahukumiwa kuwa wamepata ‘kutokana namatendo yao’. Siku hizi sizungumzii jinsi nili-vyopata VVU kwa sababu inaonekana kama ninjia tu ya kuongeza kuhukumu na kubaguamambo ambayo bado yanaendelezwa kwa watuwaliopata maambukizo ya VVU kupitia ngonoau kujidunga madawa ya kulevya. Wotetumeanguka, kwa makosa na mapungufu yetu.Wote tu wahitaji wa neema ya Mungu.

Nilikuwa na maono ya kufanya kazi na vijana,kuwaambia kuhusu VVU na kuwaeleza kuwawatu wanaoishi na VVU ni wa kawaida, nasi piatunaweza kupeleka ujumbe wa matumaini.Hivyo tukarudi Afrika Kusini nilikofanya kazi naTaasisi ya Umoja wa Kikristo wa wanafunzikwenye mpango wa kuwafikia vijana, kwa kutu-mia mbinu ya uelimishaji-rika. Hata hivyo ika-dhihirika kwamba vijana walikuwa wana habarizaidi kuhusu VVU kuliko wazazi wao, kwa hiyokwa hakika tulihitaji kuifikia jamii yote. Halafunikajiunga na kampuni ya Bima ya Afrika Kusini,na miaka 8 iliyofuata Liesel na mimi tulielezahabari kuhusu VVU na UKIMWI na kushirikishauzoefu wetu wa kuishi na VVU makanisani,mashuleni, kwenye mikutano ya wanawake navikundi vingine nchi nzima.

Pole pole tumaini langu mwenyewe lilionge-zeka wakati wote huu. Mnamo Januari 1998rafiki yangu alinipa mche wa mti wa mzeituni,ambao ki-Biblia unawakilisha matumaini.Ulikuwa mche mdogo tu, na nikamwuliza kamahakuwa na mche mkubwa zaidi - mzeituniunachukua miaka mitatu au minne kuzaamatunda, nami sikutegemea kuishi mudamrefu hivyo. Lakini baada ya miaka mitatutukavuna matunda ya kwanza. TumehamiaJohannesburg na sasa tuna mizeituni sitamikubwa iliyopandwa kando kando ya barabaraya kuingia nyumbani - tumaini tele.

Hata kabla ya kuoana, tulikubaliana na ukwelikwamba tusingezaa watoto kwa sababu ya

hatari kubwa ya kuwaambukiza VVU tangukuzaliwa, na kulikuwa na hatari yakumwambukiza Liesel pia. Lakini mnamo Aprili2002, baada ya miaka 14 ya ndoa, na baada yamazungumzo mengi sana kuhusu iwapo tuzaewatoto au la, tuliamua kujaribu. Wakati huuwanasayansi ya afya walikwisha kupiga hatuakubwa. Kwa kunywa dawa za virusi-geuzi(ARVs) niliweza kupunguza wingi wa virusimwilini mwangu kiasi ambacho katika vipimovya madaktari virusi vilikuwa havionekani.Hadi kipindi hicho tulikuwa tunatumia kondomu ili kumkinga Liesel asiambukizwe nakuzuia mimba. Mara tulipoacha kutumia kondomu, chini ya mwezi mmoja, Liesel alipata uja uzito. Miezi tisa baadaye AnikaGreyling alizaliwa. Kwa hakika Anika ni zawadiinayotuonyesha jinsi tulivyoziona huruma zaMungu - huruma kwamba bado naishi, sayansiya afya imewezesha haya, na mtoto huyutumepewa kama silaha ya matumaini.

Miaka miwili baadaye, binti yetu wa pili Miaalizaliwa. Kweli Mungu anatenda miujiza hatawakati huu na miaka hii, na anafanya kwa njiazake za ajabu. Mimi na Liesel tunapoutazamauso mdogo wa Mia na kumshika Anika mikononimwetu, tunaona jinsi maisha yetu yalivyobadi-lika tangu tulipooana miaka 17 iliyopita. TenaLiesel wala hakudhani kuwa tutaiona siku yakumbukumbu ya kwanza ya harusi yetu. Na leohii, tuna watoto wawili wenye afya njema nahawana uambukizo wa VVU!

Kuna mithali ya ki-China inayosema: ‘Kamauna maono kwa mwaka mmoja, panda ngano;kama una maono ya miaka kumi, panda mti;kama una maono ya maisha mazima - zaawatoto!’ Sasa, na ashukuriwe Mungu kwa huruma zake, dawa za virusi-geuzi (ARVs) nakondomu, na kwa msaada wa familia yangu,marafiki na wafanyakazi wenzangu, nimepitiahatua zote tatu.”

&Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika KristoYesu. (Warumi 3: 23-24)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Neema ya Mungu’

Page 33: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

31www.stratshope.org

Ushuhuda wa 11:

“Japokuwa nina umri wa miaka 51 tu,wakati mwingine najihisi kama ninamiaka 90. Niliolewa nikapata mtoto

wa kiume, lakini mume wangu aliondokanyumbani mtoto alipokuwa na umri wa miezinane. Akarudi baada ya miaka mingi wakatimtoto yuko sekondari. Nilimkaribisha na kuendelea kuishi maisha ya ndoa. Alikuwaamepoteza kazi yake na hivyo tukaishi kwakutegemea mshahara wangu wa ualimu.

Mume wangu akawa mgonjwa na nikapende-keza akapimwe VVU, lakini alikataa na akawamkali sana. Siku moja niliporudi kutoka shuleni, nikakuta amefungasha begi lake naameondoka kwa mara nyingine tena, bilakuacha taarifa yeyote. Sijui alikokwenda.Nilienda kupima VVU na kukutwa nina uambu-kizo wa VVU. Ilikuwa ni anguko kubwa sana.Hapo nikabaki, mzazi peke yangu, sio mtotowangu tu aliyehitaji msaada wangu bali piawatoto wengine wanne wa dada yangualiyekuwa amefariki.

Nilipoanza kuugua, niliamua kuwaambia watoto wangu kuhusu hali yangu ya uambukizowa VVU. Niliwaita wote pamoja wakati wachakula cha jioni na kuwaambia kuwa ninauambukizo wa VVU, na walilipokea vizuri.Mtoto wangu wa kiume alisema kuwa alikuwatayari amekwisha kuhisi na akaniambia kuwanisihofu atanitunza.

Halafu nilienda shuleni na kumwambia mwalimu wangu mkuu na kumsihi asimwambiemtu yeyote kwa sababu nilikuwa naogopaunyanyapaa na kubaguliwa. Nilitaka niendeleekufanya kazi kama kawaida na kwa mudamrefu inavyowezekana. Alionekana kukubali,lakini siku iliyofuata shuleni wanafunzi wali-anza kuniangalia vibaya. Nilipowaomba wani-letee madaftari yao walikataa. Na hii ilikuwadhahiri kwamba mwalimu mkuu alikuwa ame-waambia waalimu na wao wakawaambia wana-funzi kuhusu hali yangu ya uambukizo wa VVU.Niligundua pia kuwa wenzangu walikuwawananikwepa, na wakati wazazi walipokujashuleni hawakuwa wanakutana nami. Na wanafunzi walinidhihaki kwa kuimba wimbounaohusu UKIMWI.

Hivyo nikakabidhi barua yangu ya kujiuzuru.Kwa miezi kadhaa sikuwa nafanya kazi nasikuwa napata mshahara au pesa ya kiinuamgongo, lakini mtoto wangu wa kiume alini-saidia. Mwishowe, baada ya miezi mingi yamahangaiko, mwajiri wangu alikubali kuwanitalipwa kiinua mgongo changu.

Nimepitia shida ya kubaguliwa ndani ya kanisalangu. Kwa mfano wakati mmoja, wakatinilipoenda kupokea sakramenti takatifu, Padrealiweka mkate mkononi mwangu badala yakwenye ulimi, kama alivyokuwa anafanya kwawatu wengine wote. Nilijisikia vibaya sana

JacintaMulatyaJacinta Mulatya ni mwalimu mstaafu washule ya msingi na kiongozi mlei wa Kikatoliki. Anaishi karibu na mji waKibwezi Kenya.

Page 34: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org32

SAUTI ZENYE MATUMAINI

lilipotokea hilo. Lakini Padre mwingine waparishi yetu kila wakati ananiwekea mkatekwenye ulimi. Pia waumini wengine wakanisani wamekuwa wa msaada wa ajabukwangu. Wamenichagua kuwa Mwenyekiti wakamati ya kanisa. Hivi karibuni wamenichaguatena, japokuwa niliwaambia kuwa ninashughuli nyingi na sikuwa mwenye afya njema.

Waumini kanisani wamekuwa wa msaadamkubwa kwa njia nyingi. Kwa mfano, kunaPadre mmoja aliyekuwa anakwepa kufanyakazi na mimi, japokuwa nilikuwa Mwenyekitiwa kamati ya kanisa. Lakini msaidizi wangualienda na kuzungumza naye, na mtazamowake kwangu umekuwa afadhali.

Pia nilianzisha kikundi cha kusaidiana kwamasuala ya VVU ambacho kinakutana mara

mbili kwa mwezi kanisani, japokuwawanachama wake wanatoka makanisa mbali-mbali. Kinaitwa ‘SAFUA’, neno lenye maana ya‘kaa hai kwa ajili yetu’. Kikundi kinawanachama zaidi ya 40 watu wazima ambaowana maambukizo ya VVU, zaidi ya wajane 50wazee wanao watunza yatima, na yatima zaidiya 90. Mikutano hii ni maarufu na inakuwa namahudhurio mazuri.

Sasa hakuna kubaguliwa kunakosababishwa naVVU wala unyanyapaa ndani ya kanisa langu,na makundi mengine ya kidini ndani ya eneoletu yanabadilika. Lakini kama si kwa msaadawa Mungu kupitia ANERELA+ na KENERELA+,nina mashaka kama ningekuwa hai sasa.”

&Bwana ndiye Mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majanimabichi hunilaza, Kando ya ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsiyangu na kuniongoza. Katika njia za haki kwa ajili ya Jina lake. (Zaburi 23: 1-3)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Bwana ndiye Mchungaji wangu’

Page 35: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

33www.stratshope.org

Ushuhuda wa 12:

“Mimi ni mchungaji msaidizi niliye-barikiwa katIka kanisa la KristoLililokombolewa la Mungu. Na

mimi pia ni daktari wa binadamu, na tangumwaka 1977 hadi 2000 nimekuwa nikitumikiajeshi la Nigeria.

Nimezaliwa ndani ya familia ya wa-Baptist nanimekuwa nikienda kanisani kila wakati.Baadaye nilienda chuo kikuu, ambako nikawaMkristo jina, niliweza kwenda kanisaniKrisimasi na Pasaka lakini si mara nyingine.Mnamo mwaka 1992 nilianza kusoma Bibliaukurasa hadi ukurasa. Ilikuwa ni ngumu sana,lakini nilivumilia na hatimaye nilimaliza.Nilijifunza mengi sana, lakini bado sikuwezakuanza kwenda kanisani mara kwa mara mpakamuuguzi mmoja wa hospitali ya Jeshialiponikaribisha, ndipo mwaka 1992 nilianzakuhudhuria kanisani tena.

Mwaka 1993 niligundua, kwa bahati mbaya tu,kuwa nilikuwa nina uambukizo wa VVU.Mgonjwa wa kike alihitaji kuongezewa damuna nilikuwa na kundi moja la damu na yeye,hivyo nikamchangia damu. Ilipimwa na kuo-nekana ina uambukizo wa VVU. Nilichukuliwakipimo tena kwa uthibitisho ambayo piailionekana kuwa na uambukizo wa VVU.Msaidizi wa maabara aliyekuwa anafanya kipimo alikuwa Mkristo na alinipa kitabu namkanda wa kaseti ulikokuwa na kichwa

Kusimamia Ahadi za Mungu. Kitabu hiki pamoja na yale ninayoyafahamu kuhusu VVUna UKIMWI kutokana na elimu yangu ya udaktari, vimenisaidia sana katika kushughu-likia hali yangu ya uambukizo wa VVU.

Nafahamu kuwa VVU kama vyenyewe haviui, nimagonjwa nyemelezi ndiyo yanayoua. Na pianilifahamu kuwa Mungu huutazama moyo, nasio utu wa nje. Hivyo nimesimamia neno laMungu katika kukubaliana na hali ya kuwa namaambukizi ya VVU. Watu wanaweza kudhanikuwa nitakuwa nimefanya kitu kibaya hukonyuma hata kuambukizwa VVU, lakini naaminikuwa Mungu hufurahi sana kwa mwenyedhambi mmoja atubuye kuliko mtu mwenyekujihesabia haki.

Mnamo mwaka 1998, kulipokuwa na mkutanomkubwa wa kanisa langu huko Nigeria,nilipokea unabii wa kupona na niliamua kupimatena. Sikuwa nimemwambia mtu yeyoteJeshini kuwa nina uambukizo wa VVU. Sikuwanimeiambia familia yangu pia - mke wangualikuwa London kwa matibabu na watoto wetuwalikuwa bado wadogo. Nilienda maabara nakumwomba Meja kuwa nilihitaji kupima.Alishangaa lakini alikubali kuchukua damuyangu na kuipima. Kwa wiki mbili zilizofuataalikuwa ananikwepa wakati wote. Ndipo akajaofisini kwangu amebeba maandiko mengiyanayohusiana na VVU na UKIMWI. Ndipo

PatMatemilolaDr Pat O. Matemilola ni Mratibu waTaifa wa Mtandao wa watu wanaoishina VVU na UKIMWI nchini Nigeria(NEPWHAN) Abuja, Nigeria.

Page 36: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org34

SAUTI ZENYE MATUMAINI

akaniambia kuwa nilikuwa nina uambukizo waVVU, jambo ambalo halikunishangaza, hivyonilikuwa mtulivu tu, lakini yeye alishangazwasana na hili. Niliendelea tu na kazi yanguJeshini.

Nilipoamua kujitangaza hadharani kuhusu haliyangu ya maambukizi ya VVU mnamo mwaka2000, ilinibidi kuwa wazi kwa watoto wangu,wazazi wangu na kanisa langu. (Wakati huomke wangu alikuwa ameshafariki, lakini siokwa UKIMWI). Watoto wangu walishtuka, lakinikwa haraka walilizoea. Wazazi wangu walini-uliza ‘Hiyo inamaanisha nini kwetu?’ Hivyonikawaeleza. Nilimwambia mchungaji wanguna alilichukulia katika hali ya utulivu. Lakiniwakati habari zinazonihusu zilipotoka kwenyemagazeti, watu wachache waumini wa kanisaniwalianza kunikwepa, hawakupeana mikononami, au kunikumbatia baada ya ibada. Mmojaalikwenda hata kwa mchungaji, lakini mchungaji alimwambia ‘kwa hiyo iweje?’ naakaendelea kunihusisha kwenye shughuli zakanisa. Sasa wale waliokuwa wananikwepawananichukulia kuwa mtu wa kawaida tena.

Watu wengine wachache kanisani kwanguwameniambia hali zao za kuwa na uambukizowa VVU, lakini bado hawajajitangaza hadha-rani.

Nilistaafu kazi Jeshini miaka minne iliyopita nanikawa Mratibu wa Taifa wa NEPWHAN.Nimekuwa mwenye afya njema, bila ugonjwawowote wa kutisha. Sijaanza matibabu yadawa za virusi-geuzi. Kazi zangu ni nyingi naza kuchosha mara kumi zaidi ya wakatinilipokuwa Jeshini lakini naweza kumudu.Mwaka jana chembechembe zangu za CD4 zilishuka hadi 240 lakini sasa zimepanda hadi696.

Nampa Mungu utukufu kwa sababu siku zoteyupo kwa ajili yetu na ni lazima tupokee kilaanachotupa cha kutusaidia katika maisha yetu.Kama watoto wa Mungu, naamini lazima tumrudie Mungu kwa ajili ya nguvu anayowezakutupa ili tuinuke juu ya majaribu yote. Nguvuya Mungu ndani yangu ni imara zaidi kulikonguvu ye yote duniani.”

&Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema: Watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya binadamu. (Mathayo 15: 7-9)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Unafiki’

Page 37: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

35www.stratshope.org

Ushuhuda wa 13:

“Nimekua katika kijiji kidogo nchiniKameruni. Mama yangu alikuwakiongozi wa kanisa na alinipeleka

kwenye mikutano mingi ya kanisa, hivyonilikua nikiwa muumini wa dini. Nilibatizwatarehe 1 Januari mwaka 1991, nikasoma sekondari na elimu ya juu kati ya mwaka 1987na 1995.

Ilikuwa mwaka 1995 nilipotoa maisha yangukwa Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokoziwangu. Siku mbili baadaye, nilikuwa nahu-dhuria ibada kanisani wakati mhubirialipokuwa anahubiri kutoka Matendo yaMitume 13:1-3. Nilijihisi kukamatwa na Rohowa Mungu ndipo nikayakabidhi maisha yanguhapo na kumtumikia Bwana wakati wote kamamhubiri wa Injili. Kwa miaka mitatu iliyofuatanilichukua masomo ya Seminari.

Wakati huo wote matamanio ya moyo wanguna maombi yangu kwa Mungu yalikuwa kwamba Bwana anichagulie mke ambayeatakuwa ni mshirika wangu mwema katikakueneza Injili. Katika mwaka wangu wa piliSeminari, kwa maombi nikampata marehemumke wangu. Nikamwomba tuoane, nayeakakubali. Wote tulishauriwa kabla ya kuoana,lakini mshauri akasahau kutaja umuhimu wakupima VVU kabla ya kuoana.

Kwa hiyo tukaendelea na maandalizi ya harusina tukaoana mnamo Januari 2000. Baada yahapo tukasoma pamoja seminari kwa mwakammoja zaidi na tukahitimu Juni mwaka 2001.Baadaye tuliitwa na kanisa na nikaanza kazikama mchungaji msaidizi.

Mwaka mmoja baadaye mke wangu alijifunguamtoto ambaye alifariki miezi minne baadaye.Sikuelewa kilichokuwa kinatokea kwa wakatiule, lakini hilo lilikuwa ni mwanga kabla yaradi. Mwaka uliofuata mke wangu aliangukawakati alipokuwa anachuma mboga shambani.Nilijulishwa na tukakimbia kumpeleka hospi-tali. Alipokuwa hospitalini alishauriwa naakakubali kupima VVU. Kipimo kilifanywa namajibu yakawa ana uambukizo wa VVU. Alipatanafuu na tukarudi nyumbani ila hakuniambiakama amepima VVU wala hali yake ya maa-mbukizi ya VVU.

Miezi kadhaa baadaye akapata kiharusi naakapelekwa hosipitali. Jioni moja nilipomte-mbelea hosipitalini, alianza kulia na kuniambiakuwa amepima na ana uambukizo wa VVU.Aliniomba nimsamehe kwa kutokuniambiakuwa alikuwa na uambukizo wa VVU. Haikuwarahisi kwangu kumsamehe, lakini nilihisi upendo mkuu wa Mungu kwetu katika Kristo.Halafu nikakumbuka kuwa kupitia Kristo,

‘Mark’‘Mark’7 ni mchungaji aliyebarikiwa naamefundishwa ushauri-nasaha wa Kikristojuu ya VVU na UKIMWI huko Kameruni.

5 Sio jina lake halisi.

Page 38: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org36

SAUTI ZENYE MATUMAINI

Mungu alinisamehe bila masharti nilipokuwasistahili. Baada ya kulia kwa muda nili-msamehe na kumhudumia hadi alipofarikimwaka 2003.

Na mimi nilipima VVU nikakutwa nina uambu-kizo. Tokea hapo maisha yangu yakawa tofautikuliko mwanzo. Kwa neema ya Mungu niliwezakutumika ndani ya lile kanisa kwa mwakammoja zaidi wa maombi. Wakati huo wote

nilitafuta kuyajua mapenzi ya Mungu nanikaamini kuwa Mungu alikuwa ananiandaakupitia maumivu haya katika kuhubiri uha-kikisho wake, neema na utoshelevu wake kwawanaoteseka, hasa kwa watu wanaoishi na VVUna UKIMWI. Baadaye nikaenda kwenye mafunzomengine ya zaidi kama mshauri-nasaha waKikristo na sasa nafanya kazi kama mchungaji,nikitoa huduma za kiroho na ushauri-nasahakwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI.

&Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikenimoyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, nakusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. (Wakolosai 3: 12-13)

Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza pia;Hakuna mtenda mema, la! hata mmoja. (Warumi 3: 10-12)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Msamaha’

Page 39: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

37www.stratshope.org

“Mimi ni mchungaji wa kwanza katikaKongo kujitangaza hadharani kuwanimeathirika na VVU na UKIMWI.

Ujumbe wangu ni mmoja, nao ni ujumbe usiowa kuhukumu, kwamba VVU sio laana kutokakwa Mungu, na kwamba watu wanaoishi naVVU wanahitaji msaada wa kitabia zaidi.

Miezi minne baada ya kuzaliwa kwa bintiyangu, ambaye mara kwa mara alikuwamgonjwa, daktari alimpima VVU. Miezi sitabaadaye akaniambia kuwa alikuwa na uambu-kizo wa VVU. Kwa hakika simlaumu daktarikwa kuchelewa hivyo kuniambia. Ilikuwa nivigumu sana kwake kwa sababu alijua kuwaina maana kwamba mke wangu, na labda namimi pia, tutaonekana kuwa na maambukizi.Sikuwa na ujasiri wa kumwambia mke wangu,lakini baada ya miezi 12 mingine nilimwambia.Wote tulipimwa VVU, na mke wangu akakutwaana uambukizo lakini mimi sikuwa na maambukizi.

Hatukumwambia mtu yeyote kwa sababu tuliogopa aibu ambayo ingetukuta kanisani.VVU ilikuwa inahusishwa na umalaya na tabiambaya, hivyo ilikuwa ni chanzo cha aibu. Kwaujumla ilitujeruhi sana. Kwa miaka saba tuliishi na ufahamu huo wa hali zetu za maambukizi ya VVU, pasipo kumwambia mtuyeyote. Tuliomba na kuomba kwamba kanisalisitunyanyapae wakati habari zitakapojulikana.

Ndipo mke wangu akafariki, na nikahisi kamaYesu ameniacha. Nilifikiri, kama ningejuakwamba hilo linaenda kunitokea nisingejaribukuwa mchungaji. Nilikuwa katika upinzanimkubwa na kanisa. Kwa kweli sikutakakushughulika na kanisa kwa lolote. Nilikuwanatenda kama mtu aliyekuwa amerukwa naakili. Watu wengine walidhani naomboleza kwasababu ya mke wangu, lakini hawakufahamukuwa alikufa kwa UKIMWI.

Mke wangu alifariki miaka mitatu iliyopita lakini binti yangu wa miaka 9, ambaye anauambukizo wa VVU, bado anaishi. Ni kamamoyo wangu. Tatizo langu kubwa ni jinsi yakumjulisha hali yake ya uambukizo wa VVU.Sijui la kufanya juu ya hili. Ningependa kujuajinsi watu wengine walivyolishughulikia tatizokama hili.

Nilipogundua kuwa mke wangu na binti yanguwameambukizwa VVU, sikuwa naogopa VVU auUKIMWI, ila tatizo ni kuona aibu kanisanikwangu. Wachungaji na wakristo wauminiwangesema nini? Je tulikuwa mfano gani sisikama familia? Nilifikiri Mungu anawezakuponya magonjwa na nikangojea uponyajiwake kwa mke wangu. Alipofariki nilijisikiakama Mungu ameniacha. Nilijiona kuaibikasana. Tunaishi katika ulimwengu ambapo VVUvinaangaliwa kama tatizo la watu wenye tabiambaya. Nilikuwa karibu nigombane na Yesu.

Ushuhuda wa 14:

Philippe NdembeMchungaji Philippe Ndembe ni mchungajiwa Kanisa la Baptist la Kristo lililoko Mtowa Kongo, Kinshasa katika Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo. Pia ni Mratibu waKanda wa ANERELA+ katika Afrika ya Kati.

Page 40: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

www.stratshope.org38

SAUTI ZENYE MATUMAINI

Nilikuwa nangojea kutengwa, lakini kanisalangu halikufanya hivyo.

Kanisa langu liliitikia kwa kuniacha nituliekwanza, na baadaye wakapendekeza kwambanimtembelee Kasisi Kiongozi GideonByamugisha nchini Uganda. Mwanzonisikukubaliana na hilo pendekezo. Nimepotezamke wangu kwa UKIMWI na mtoto wangu anaVVU na sasa kanisa linanishauri nimtembeleemchungaji mwenye VVU Uganda. Niliona kamalaana nyingine kutoka kwa Mungu. Nililia kamamtoto. Hatimaye nilisema ‘Sawa Yesu,nitafanya,’ lakini nilisema hivyo katika hasirasio kwamba nilishawishika kwamba hilililikuwa jambo ambalo Bwana alitaka nifanye,au nililotaka kufanya. Lakini hatimaye niliendakumtembelea Gideon mnamo Februari 2004.Mpaka wakati ule nilikwisha kupima mara tatuau nne na mara zote nilionekana sina ma-ambukizi ya VVU. Nilifika Uganda, na kingereza changu kibovu, Gideon alikuwaametoka lakini aliniachia ujumbe kuwanimkute kwenye nyumba ya wageniNamirembe, nami nikafanya hivyo.

Baada yakumtembelea Gideon mnamo Februari2004, Roho Mtakatifu alifanya kazi. Nilijisikiakuwa tayari kuanza kusema na watu wenginekuhusu VVU na UKIMWI. Kwa wakati ule sikuwanafanya kazi kwa nguvu kama mchungaji kwamuda wa miaka mitatu. Katibu Mkuu wangualikuwa tayari amependekeza kuwa nianzekutoa ushuhuda katika nchi nyingine sio Kongo.Lakini baada ya kumtembelea Gideon mweziwa Februari, nilifikiri - hapana, watu watagu-ndua tu kwa vyovyote kutoka kwenye mtandaoau barua pepe. Hivyo niliamua kuanzia Kongo.

Mnamo Aprili 2004, nilieleza ushuhuda wangukwenye mkutano wa Makasisi wa Kanisa laBaptist, ambako nilikuwa nalia wakati

ninawaambia. Mwishoni mmoja wao alianzakuimba wimbo mfulululizo8. Hiyo ilinipa ujasiriwa kueleza ushuhuda wangu kwenye ibadaJumapili, lakini nilihisi kama vile jani kavu linathamani sana mbele za Mungu kuliko nilivyo-fanya.

Ndipo nilipoandaa semina ya VVU kwa wachungaji ambao walikuja kwa wingi kutokamakanisa mbalimbali ya Kikristo ndani yaKongo. Nilipowaambia ushuhuda wangu wengiwalilia pamoja nami. Tangu wakati huonimezungumza na makundi mengine manne yaMakasisi waliokuja kwa mafunzo - jumla yaowote 120, na ushuhuda wangu sasa ni sehemuya mafunzo ya makasisi wote. Na waowalikuwa wanawaza na kusema juu ya VVU naUKIMWI kama watu wengine, lakini sasa wame-badilika. Watu wengi wako makini kusikilizahabari hizi mpya zinazohusu VVU na UKIMWI.

Bado sijajua maoni ya kanisa juu yangu mimi.Hakuna hata mmoja anayeniuliza maswali -labda hawana ujasiri. Labda ni kama Ayubu.Marafiki zake hawakusema neno kwa siku tatu,na walianza tu kuzungumza baada ya Ayubukuanza kusema. Lakini hali halisi katika nchiyetu itabadilika.

Tunaweza kufanya mengi kuleta mabadiliko.Angalia Marko Mtakatifu 2:1-12, uponyaji waaliyepooza. Yesu alipoona imani yao,alimwambia aliyepooza asimame na atembee.Tunaweza kufanya hivyo kwa watu walio namaambukizi ya VVU. Wale marafiki wanne wayule mtu aliyepooza wanaweza kutafsiriwakama sifa za kanisa: huruma, ushawishi, ujasirina kudhamiria. Uponyaji wa kwanza ni wa kiroho na tabia. Tunaweza kuponywa kwaimani katika Yesu. Na kama Yesu akituponya,kwa nini tujihukumu wenyewe?”

8 Usiogope, nakupenda, nitakuwa pamoja nawe, nakuahidi ahadi kuu, inayoendeleza imani yangu.

&Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunziwake, kumwuliza, ‘Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?’ Yesu akajibu akawaambia, ‘Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwiwanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. Naye heriawaye yote asiyechukizwa nami.’ (Mathayo 11: 2-6)

Mtazamo wa Kibiblia: ‘Imani katika Yesu’

Page 41: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

39www.stratshope.org

MisamiatiKIAMBATANISHO

Unyanyapaa: ni alama au doa la kuonyesha kutokuthamini au kudharau. Unyanyapaaunajionyesha katika kutokukubaliana, kuhukumu na kukataliwa na familia zao, majirani, waajiri, jamii ya waumini na sehemu nyingine zakijamii, kwa watu wenye uambukizo wa VVU na UKIMWI.

Aibu: ni hali ya kujisikia kutokuwa na thamani, kushushiwa uthamani wa ubinadamu, k.m. kwa sababu mtu amefanya jambo ambalo linahesabiwakuwa ni la maadili mabaya.

Kukataa: ni kukataa kukubaliana na jambo ambalo ni la ukweli k.m. kukataakuwepo kwa VVU na UKIMWI katika familia ya mtu au jamii ingawa kunauthibitisho wa wazi wa jambo hilo.

Kubaguliwa: ni kutokutendewa haki na mtu mwenye kushutumu au mwenye habaripotofu, k.m. kwa kuwatendea hivyo watu wa rangi au dini tofauti, auwatu wanaoishi na VVU au UKIMWI.

Kutokufanyiwa kitu: ni hali ya kutokufanyiwa kitu au kufanyiwa pole pole sana - watukukataa kuchukua hatua yeyote kwa ajili yako, k.m. kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi, hali ya hatari, au woga wa kutokufanikiwaau kutokukubalika na jamii.

Kutendewa vibaya: ni hali ya kufanya mambo kwa kuongozwa vibaya au bila kuwa na taarifasahihi, inayoweza kusababisha matokeo mabaya sana.

Page 42: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa
Page 43: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa
Page 44: Sauti Zenye Matumaini - stratshope.org · virusi-geuzi kwa ajili ya kuboresha kinga ya mwili ili kurefusha maisha VVU ni Virusi Vinavyosababisha UKIMWI ICASA ni Kongamano la Kimataifa

Kitini cha TUMEITWA KUHUDUMIA kinajumuisha matendo, vijitabu vyenye kuhusisha matendo na miongozo midogo kuhusu mambo yanayohusu VVU na UKIMWI, vilivyoandaliwa kwa matumizi ya viongozi wa kanisa, hasa kwa nchi zilizo Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Madhumuni ya mambo yaliyomo ni kuwawezesha wachungaji, mapadre, watawa wa kike na wa kiume, walei viongozi wa kanisa na waumini wao pamoja na jamii ili waweze:

qKutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ya janga la VVU na wito wa Kikristo wa kuitikia kwa huruma.

qKushinda unyanyapaa, ukimya, ubaguzi, kukataa, woga na kukataa kubadilika, hali ambazo zinazuia kanisa na jamii katika kukabiliana na mambo yanayohusu VVU na UKIMWI kwa ukamilifu zaidi.

qKuwaongoza waumini wao na jamii katika mchakato wa kujifunza na kubadilika kutakakopelekea kwenye matendo na mienendo ya kikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ili kupunguza kuenea kwa VVU na kupunguza athari za janga la VVU.

TUMEITWA KUHUDUMIA ni wazo la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini, ambao wanatayarisha na kutoa vitabu na video vinavyohamasisha mbinu madhubuti na michakato ya kijamii ya kuhudumia, kusaidia na kuzuia VVU na UKIMWI katika nchi zinazoendelea duniani, hasa zilizoko Afrika chini ya Jangwa la Sahara.

TUMEITWA KUHUDUMIA inatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, shirikisho la muungano wa makanisa, na taasisi nyingine za kidini, miundo ya kimataifa ya makanisa, wachapishaji, wasambazaji na washika dau wengine.

WAHARIRI

Kasisi Kiongozi Gideon Byamugisha ni mchungaji aliyebarikiwa katika Kanisa la Uganda na mtunzi wa vitabu vingi vinavyohusu masuala ya VVU na UKIMWI na kanisa. Pia yeye ni Mwenyekiti mwanzilishi wa ANERELA+.

Glen Williams ni mwandishi kuhusu afya na maendeleo kimataifa, na ni mhariri wa Mtiririko wa Maandiko ya Mikakati ya Kuleta Matumaini.

ISBN 978 1 905746 10 1

Kimehaririwa na Gideon Byamugisha na Glen Williams

Sauti Zenye MatumainiViongozi wa dini wanaoishi

au walioathiriwa binafsi na VVU na UKIMWI