20
MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJA (CUSTOMERS SERVICE CHARTER) Imeandaliwa na: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) S.L.P 120 CHALINZE Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.chaliwasa.go.tz 1

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

  • Upload
    others

  • View
    10

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE

MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJA (CUSTOMERS SERVICE CHARTER)

Imeandaliwa na:Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA)S.L.P 120CHALINZEBarua pepe: [email protected]: www.chaliwasa.go.tz

1

Page 2: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

Simu Na: 0753 250 636, 0752 801 178.

MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJAMAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE

YALIYOMO UKURASA

DIBAJI ………………………………………………………………………………………………………………………….. 3

TAFSIRI ………………………………………………………………………………………………………………………… 4

DIRA YA MAMLAKA ………….…………………………………………………………………………………………….. 5

DHAMIRA/ADHIMA ………………………………………………………………………………………………………… 5

MAADILI YA MAMLAKA YA CHALIWASA ………………………………………………………………………….. 5

MADHUMUNI YA MKATABA WA HUDUMA BORA KWA MTEJA ……………………………………………. 5

MAMBO YA JUMLA NA VIWANGO VYA UTOAJI HUDUMA ……………………………………………………. 6

1. UTARATIBU WA KUUNGANISHA MAJI KWA MTEJA ………………………………………………………… 7

2 USOMAJI WA TAKWIMU ZA MATUMIZI YA MAJI YA MTEJA ………………………………….….. 8 - 12

3. TAARIFA YA KATIZO LA MAJI ……………………………………………………………….……………. 12 - 13

4. HAKI NA WAJIBU MUHIMU WA MTEJA ……………………………………………………………….. 13 – 14

5. WAJIBU WA MAMLAKA KWA MTEJA ……………………………………………………………………… 14 -15

6. HAKI NA UWEZO WA KISHERIA WA MAMLAKA ……………………………………………………………. 15

2

Page 3: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

7. ULIPAJI WA FIDIA KWA WATEJA………………………………………………………………………………… 16

8. MAKOSA YA JINAI, YANAYOAINISHWA NA SHERIA YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRANAMBA 12 YA MWAKA 2009 …………………………………………………………………………………… 17

8. UFUATILIAJI, MALALAMIKO, MAULIZO NA MAOMBI YA MTEJA ………………..……………. 18 - 19

9. HUDUMA ZA SIMU ……………………………………………………………………………………………………. 19

DIBAJI

Mkataba wa Huduma bora kwa Mteja ni ahadi za kimaandishi kati ya Taasisina Wateja wake. Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Chalinze(CHALIWASA) imetambua umuhimu wa kutumia Mkataba wa Huduma borakwa Mteja kama Dhana ya kuleta mabadiliko chanya katika uwajibikaji wawatendaji wake kwa umma. Hatua hii ya Mamlaka kuanzisha mabadiliko yautendaji kupitia Mkataba wa Huduma Bora kwa Mteja una lengo la kuboreshahuduma kwa wateja wetu.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA)ilianzishwa rasmi tarehe 30 Novemba 2012 baada ya kutangazwa kwenyeGazeti la Serikali Na. 376.

Kwa kuzingatia umuhimu wa majukumu haya, Mamlaka imeandaa Mkatabahuu tarehe 12/08/2014 ambao unaainisha huduma inazotoa, viwango vyahuduma ambavyo tunaamini wateja wetu wana haki ya kupata, na kuelezeajinsi ya kupokea maoni au malalamiko na utatuzi wa matatizo paleyanapojitokeza na njia ya kuwasiliana na Mamlaka

Matarajio ya Mamlaka ni kutoa Huduma bora kwa wakati kulingana naviwango vilivyowekwa.Tunawashauri wateja na wadau wetu kwa ujumlakusoma na kuufahamu Mkataba huu na kuutumia ipasavyo. Tunaamini

3

Page 4: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

mkataba huu wa Huduma Bora kwa Mteja utaimarisha mahusiano mazurikatika utendaji na utoaji huduma kwa umma. Tunawakaribisha wateja naWadau wetu kutoa maoni mara kwa mara ili kuboresha huduma zetu.

…………….………………….Inj. Christer T. Mchomba

Mkurugenzi MtendajiCHALIWASA

…………………Tarehe

TAFSIRI

Tafsiri au vifupisho vya maneno vitakavyotumika kwenye Mkataba huu nikama ifuatavyo:-

CHALIWASA - Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chalinze, na ni Kifupisho katika lugha ya Kiingereza –

(Chalinze Water Supply and Sanitation Authority)

MAMLAKA - ina maana ya CHALIWASA.

EWURA - Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji;na ni kifupisho katika lugha ya Kiingereza – (Energyand Water Utilities Regulatory Authority)

ANKARA – Ina maana ya hati ya kudai malipo ya huduma yamaji kwa Mteja (Water bill)

4

Page 5: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE (CHALIWASA)

DIRA YA MAMLAKA (Vision)Kuwa Mamlaka bora na inayojitegemea katika utoaji wa huduma ya Majisafina Usafi wa Mazingira nchini Tanzania.

DHIMA YA MAMLAKA (Mission)Kutoa huduma ya majisafi ya kutosha na salama pamoja na kuondoamajitaka kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika vya ubora wa juu wa usafina Mazingira.

MAADILI YA CHALIWASA (Core Values)

Kufanya kazi kwa ushirikiano Kufanya kazi kwa ufanisi na kujituma Kufanya kazi kwa kuzingatia muda na mpango kazi Kuzingatia maadili ya kitaalam Kutoa huduma kwa uwazi Kutoa huduma kwa uadilifu na uaminifu Kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu Kuzingatia matumizi bora ya Rasilimali za Serikali Kujiheshimu na kuheshimiana

MADHUMUNI YA MKATABA WA HUDUMA BORA KWA MTEJA.

5

Page 6: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

Madhumuni ya Mkataba huu ni kukuza kiwango cha uelewa wa Wateja naWadau wetu kuhusu upatikanaji wa huduma zetu, ubora na viwango vyake.Vilevile Mkataba huu unalenga katika kuboresha utendaji kazi na unawekawazi utaratibu wa kupokea na kushughulikia maoni na malalamiko paleambapo huduma zinazotolewa hazikidhi matarajio ya wateja.

WATEJA WETU

i) Taasisiii) Viwanda iii) Wafanya Biasharaiv) Wateja wa Majumbaniv) Vioski (Mawakala)vi) Wawekezaji/Ujenzi

MAMBO YA JUMLA NA VIWANGO VYA UTOAJI HUDUMA

Mamlaka inakusudia kutoa huduma kwa viwango vya kitaifa na kimataifakwa muda wa haraka na kukidhi mahitaji ya watumiaji au wateja wake kwakuzingatia mambo ya msingi katika Maunganisho, ubora wa huduma namuda muafaka.

Aidha Mamlaka inakusudia kuwa Mamlaka yenye ufanisi wa kibiashara namtizamo wa huduma inayomjali mteja inayounga mkono maendeleo ya Taifalake na kufikia kiwango cha kuwa muhimili wa uzalishaji na usambazaji wahuduma ya majisafi, kukusanya/kuondoa na, kusafisha mazingira kwa ufanisina ushindani endelevu kwa namna inavyowezekana. Mamlaka inakusudiakutoa huduma ya maji kwa wastani wa Saa 24 kwa siku.

Mkataba huu unaweza kurekebishwa katika vipindi vya miaka mitatu (3)kulingana na mahitaji yatakayojitokeza, na pia kutokana na maoni ya wadaujuu ya kuboresha huduma ili kukidhi mahitaji ya wateja. Kwa sasa Ofisi yaCHALIWASA Makao makuu ipo Wami Darajani, umbali wa Kilomita 50 kutokaChalinze, kando ya Barabara ya Chalinze - Segera. Kadhalika, Ofisi ndogo yaHuduma kwa Mteja inapatikana mjini Chalinze eneo la Chahua, katika umbaliwa mita 500 kutoka Barabara ya Chalinze - Lukenge.

6

Page 7: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

1. UTARATIBU WA KUUNGANISHA MAJI KWA MTEJA

1.1 Kujaza fomu ya maombiMteja wa aina yeyote atakayetaka huduma ya maji atafanya hivyo kwakujaza fomu ya maombi na kulipia Tshs 5,000/= inayotolewa na Mamlaka.

Mteja hatakiwi kufanya mapatano ya kuunganishiwa huduma ya maji na mtuau mtumishi yeyote wa Mamlaka nje ya utaratibu wa ofisi.

1.2 Makadirio ya gharama za kuunganisha Maji kwa mteja

Kama mteja ameshajaza fomu ya kuomba huduma ya kuungiwa maji nakuwasilisha vielelezo vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na picha moja.a. Mteja atafanyiwa upimaji katika eneo lake na fundi wa mamlaka ndani ya

siku 2.b. Tathmini ya upimaji na gharama kuandaliwa baada ya siku 3.

1.3 Kulipia Gharama za Kuunganisha Majisafi

Baada ya kupewa makadirio ya gharama, mteja anatakiwa kulipa gharamaza kuunganisha maji ndani ya siku 30. Gharama zitabadilika/ongezekaiwapo mteja atalipia baada ya siku 30 kupita ili kufidia ongezeko la bei zabidhaa endapo litatokea.

a) CHALIWASA itaruhusu malipo ya maunganisho ya maji kwa fedhataslimu itakayolipwa kwa mkupuo mmoja tu au kwa malipo ya awamu.

7

Page 8: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

b) Maunganisho ya maji hayatafanyika kwa mkopo.c) Mteja ataunganishiwa maji ndani ya siku 14 baada ya kuzingatia

utaratibu wa malipo wa Mamlaka.d) Mteja hatakiwi kumwamini na kumpatia fundi au mtumishi yeyote wa

CHALIWASA fedha za malipo ya maunganisho ya maji akamlipie ofisini.Malipo yote yanatakiwa yafanyike kwenye ofisi za makao makuu Wami,ofisi ndogo ya Chahua na vituo vidogo vya Mamlaka vilivyopo Lugoba,Msata na Miono.

Kama mteja amelipa gharama zote zinazohitajika na kama ametimiza wajibukwa mujibu wa fomu ya maombi inavyotakiwa, muda ufuatao utazingatiwakatika kutoa huduma ya uunganishaji huduma ya maji kwa mteja:

a) Ndani ya siku 14 za kazi kama miundo mbinu iliyopo inawezakutumika.

b) Kama ndani ya siku 14 za kazi, ulazaji wa bomba na ujenziutashindikana, CHALIWASA inawajibika kutoa taarifa kwa mteja juu yakushindwa kwake kumaliza kazi ndani ya siku 5. Kama taarifahazikutolewa, mteja anayo haki ya kuwasilisha malalamiko yake yakucheleweshewa huduma kwa Mkurugenzi Mtendaji.

c) Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujengwa, au kamamfumo wa maji ni mkubwa na unahitaji kuongezwa muda kwa ajili yautekelezaji wa kazi husika Mamlaka itamtaarifu mteja kwa maandishijuu ya hitaji hilo.

d) Endapo Mamlaka itashindwa kumuunganishia mteja maji kwa mudaunaotakiwa, itawajibika kumtaarifu mteja ndani ya siku 5 kuhusianana hali hiyo, na mteja atafahamishwa ni lini ataunganishiwa hudumaya maji.

2. USOMAJI WA TAKWIMU ZA MATUMIZI YA MAJI YA MTEJA

2.1 Usomaji wa Mita/Dira za Wateja

a) Wateja wote wanaotumia mita/dira za maji, mita zao zitasomwa maramoja ndani ya mwezi mmoja na kwa wateja wakubwa zaidi ya maramoja inapoonekana uhutaji wa kufanya hivyo, kwa ajili ya kutayarishaAnkara. Kama mita haitasomwa katika mwezi mmoja na kama wakatiwa usomaji mita hiyo itakutwa/itabainika kuwa mbovu matumizi yamteja yatakadiriwa kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za maji.

8

Page 9: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

b) Mteja anahimizwa kutoa taarifa haraka kwenye ofisi za Mamlaka kwatatizo lolote linalohusiana na mita yake.

c) Usomaji wa mita wa ziada utafanyika kama mteja anahama kwenyesehemu iliyopo na mteja mwingine anaingia, au kusitisha huduma kwamuda kumaliza mkataba wa ukazi au uraia wa nchi, au kuuza eneo aukufunga kabisa kampuni ili baada ya kubadilisha mita, au kama mtejaatataka mita yake isomwe kwa ajili ya marekebisho ya Ankara aumalipo.

d) Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki aumatumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi yanyumbani kwenda matumizi mengine kama vile biashara, kiwanda,ujenzi, taasisi, n.k lazima watoe taarifa CHALIWASA angalau siku 30kabla ya mabadiliko hayo hayajafanyika katika ofisi za CHALINZE iliabadilishiwe gharama za matumizi anayostahili. Endapo hatatoataarifa, CHALIWASA italazimika kubadilisha gharama za matumizistahiki ya mteja bila taarifa na mabadiliko hayo yataonekana kwenyeAnkara ya maji ya mteja na mteja atalazimika kulipa deni husika yamaji.

e) Wamiliki wa nyumba/majengo lazima watoe taarifa ndani ya kipindi chasiku 30 kama wapangaji wao wanatarajia kuhama.

f) Kama mmiliki/wamiliki wa nyumba/jengo husika hawataitaarifuCHALIWASA kwa kipindi kilichoelezwa hapo juu, wao wenyewe auyeyote atakekutwa anatumia nyumba/jengo ambalo lina deni la majilililotelekezwa na mpangaji au mtu aliyekuwemo awali atalazimikakulipa deni la nyuma ambalo halikulipwa na mpangaji au mtualiyehama.

g) Kutotoa taarifa kama ilivyoelezwa hapo juu; na endapo mmiliki/wamilikiau yeyote aliyekuwa anatumia nyumba/jengo husika atashindwa kulipadeni la nyuma pale mpangaji anapoacha deni, CHALIWASA ina haki yakusitisha huduma ya maji mpaka deni linalodaiwa kwenyenyumba/jengo husika litakapolipwa kwa ukamilifu pamoja na gharamaza urejeshaji huduma. Iwapo halitalipwa CHALIWASA itamfikisha mtejaanayedaiwa Mahakamani.

2.2 Kuhoji Usahihi wa Mita za Matumizi ya Maji Kabla au Baada ya Malipo

a) Mteja ana haki ya kudai uchunguzi wa mita ya maji anapohisi kunatatizo linalohusiana na utendaji kazi wa mita au usomaji usio sahihi.

b) CHALIWASA ina wajibu wa kukubali ombi la mteja la kudai mitaichunguzwe. Mita itachunguzwa na kuthibitishwa mbele ya mteja kama

9

Page 10: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

iko sahihi au si sahihi. Endapo mita itakutwa sahihi bila tatizo lolote,mteja atalazimika kulipia gharama kulingana na tozo zilizowekwa naEWURA. Na endapo mita itathibitika ina tatizo la kiufundi, CHALIWASAitalazimika kufanya “service” ya mita au kubadilisha mita hiyo nakumfungia mteja mita nyingine mpya bila gharama yoyote.

c) Uchunguzi wa usahihi wa mita kwenye eneo la mteja utafanyika ndaniya siku 3 za kazi baada ya kupokea taarifa kwa mita za wateja wakawaida na siku 7 kwa mita kubwa

d) Gharama za uchunguzi wa mita zisizokuwa na matatizo zitakuwa kamazilivyoidhinishwa na EWURA.

e) Mteja ana wajibu wa kulinganisha usomaji wa mita ulioko kwenyeAnkara ya maji na ulioko kwenye mita yake kwa lengo la kujiridhishakama matumizi ya maji aliyotozwa kwa mwezi husika ni halali au sihalali au kama mita inasomwa au haisomwi. Na endapo mtejaatagundua matumizi si halali au mita yake haisomwi analazimika kutoataarifa haraka kwa Mkuu wa Kanda wa eneo anakoishi mteja au Mkuuwa Kitengo cha Huduma kwa Wateja au Meneja Biashara katika OfisiKuu ya CHALIWASA au ofisi ndogo Chalinze au vituo vidogo vyaHuduma vya Miono, Lugoba na Msata.

f) Kama mita haisomwi kwa muda mrefu mteja asifurahie kuletewaAnkara ya kiwango kidogo sana cha deni (service charge) akidhani nigharama halali za malipo ya maji (water charges) kumbe sivyo. Aidhakuna siku ukaguzi utafanyika na mita itakaposomwa kwa uhalaliitatozwa deni kubwa lililojilimbikiza kutokana na mita kutosomwa kwamuda mrefu na itamlazimu mteja kulipa deni lote maadamu majiyalikuwa yakitumika na CHALIWASA ina haki ya kutoza maji hayo bilakujali mteja alikuwa akipata Ankara ya deni dogo (service charge)ambayo haikujumuishwa kwenye tozo halisi la gharama ya matumiziya maji (water charges) yaliyokwisha kutumika bila kutozwa kwakipindi au vipindi husika.

2.3 Makadirio ya Matumizi ya Maji.CHALIWASA ina wajibu wa kufanya makadirio ya gharama za matumizi yamaji kwa mazingira ambayo itajiridhisha kwamba maji yalitumika bilakuhesabiwa kwa usahihi kwenye mita wakati mita ikiwa mbovu au kwamazingira ya kukwepa maji yasihesabiwe kupitia kwenye mita au kwa namnayoyote ambayo CHALIWASA itajiridhisha kuwepo haja ya kukadiria gharamaza matumizi ya maji kwa lengo la kufidia upotevu au wizi wa majiuliosababishwa na mteja.

10

Page 11: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

Kama italazimika kukadiria gharama za matumizi ya maji katika kipindifulani, msingi wa ukadiriaji utakaotumika kutoza deni la maji utakuwa niwastani wa matumizi sahihi ya maji kwa kipindi kisichopungua miezi mitatuya nyuma cha usomaji wa mita ya mteja.

2.4 Taratibu za Kudai na Kulipa Deni la MajiKama hakuna masharti mengine yaliyokubaliwa kabla kati ya Mamlaka namteja, masharti yafuatayo yatatumika:

a) CHALIWASA itatoa Ankara kila mwezi kwa wateja wote wanaotumiamita za maji na kila wiki kwa mawakala wote wa vioski.

b) Mteja/Wakala yeyote ana wajibu wa kulipa deni la maji linalodaiwakihalali na anatakiwa kulipa deni lote kila mwezi/wiki bila kulimbikiza

c) Kila mteja anawajibika kulipa deni lake lote la mwezi (current bill)ndani ya siku 14 kuanzia tarehe mosi ya mwezi unaofuata. Kamamalipo yatakuwa hayajafanyika baada ya hizo siku 14, huduma yamaji inaweza kusitishwa wakati wowote. Aidha huduma ya majiinaweza pia kusitishwa kabla ya hizo siku 14 kufika endapo itabainikamteja anadaiwa deni la kipindi cha nyuma (arrears) lililolimbikizwa

d) CHALIWASA inaweza kumtumia mteja ujumbe mfupi wa simu (SMS-billing) kumdai deni la maji au kama mteja hatapokea “SMS-billing”atalazimika kudai Ankara ya maji (water bill) kwa kufuatilia aukuwasiliana na ofisi za CHALIWASA kwa kutumia Ankara yoyote yazamani au kwa kutaja Akaunti namba yake ya maji (kamaanaikumbuka) katika ofisi zetu za malipo.

e) Mteja anaweza kulipa deni lake la maji kwa njia mbalimbali zifuatazo: Kwa wapokea fedha wa CHALIWASA (Cashiers) walioko dirishani

katika ofisi Kuu au ofisi ndogo ya Chalinze au Vituo vyaHuduma vilivyoko Lugoba, Msata na Miono au ofisi za Kandaambapo stakabadhi (receipt) itatolewa baada ya malipokufanyika

Kwa mitandao ya simu za mkononi au Benki zilizoingia mkatabana Mamlaka

f) Mteja atarekebisha kumbukumbu zake za simu na kuitaarifu Mamlakanamba sahihi za simu kwa ajili ya kupokea taarifa ya deni lake la majikwa ujumbe wa simu (SMS-billing) kila mwezi.

11

Page 12: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

g) Iwapo Ankara haikulipwa katika muda wa siku 30 tangu kutolewa kwaankara ya madai, itatozwa riba kiasi cha asilimia moja na nusu (1.5%)kwa mwezi endapo mteja atachelewa kulipa, na ikiwa mteja hatalipaAnkara katika muda wa siku 90 tangu kutolewa kwa Ankara yamadai ,itatozwa riba kiasi cha asilimia (2.5%).

h) CHALIWASA itadai deni la maji kwa mteja yeyote atayehusika auatayekutwa kwenye nyumba, kiwanja/kitalu (plot) au eneo ambapokuna mfumo wa maji bila kujali kwamba mteja aliyeko eneo hilo nimmiliki wa eneo husika au ni mpangaji. Aidha, mwenye nyumba,kiwanja/kitalu, eneo au mpangaji wa eneo husika anapotaka kuhamaau kutoka kwenye eneo hilo, atawajibika kulipa deni lote la maji kablaya kuhama au kutoka eneo hilo. Ikiwa atahama au atatoka kwenyeeneo hilo bila kulipa deni lote la maji linalodaiwa kwenye eneo husika,yeyote ambaye CHALIWASA itamkuta kahamia eneo ambalo deni lamaji halikulipwa atalazimika kulipa deni lote alilolikuta hapo ulipomfumo wa maji.

i) Endapo mteja atakuwa na mashaka na deni au gharama za majisafizilizotozwa kwenye Ankara yake atalazimika kufanya yafuatayo:

Kufika ofisi za CHALIWASA na kuonana na watumishi wa Kitengocha Mauzo na Huduma kwa Wateja ambao watachunguza uhalaliwa deni husika na kumpatia mteja majibu sahihi.

Kumwandikia barua ya malalamiko Mkurugenzi Mtendaji kwakuileta na kuikabidhi ofisi ya Masijala au kwa kuituma kupitiaanuani ya Posta iliyoko kwenye Mkataba huu wa Huduma kwaWateja, ambapo malalamiko yatafanyiwa uchunguzi na mtejaatajibiwa kwa maandishi.

2.5 Kukatiwa Huduma ya Maji.Kwa kuzingatia Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Namba 12 ya mwaka2009, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Chalinze inapewa haki nauwezo wa kusitisha huduma kwa mteja yeyote ambaye atakiuka wajibu wakimkataba wa kupatiwa huduma ya maji mpaka hapo atakapolipa deni lakelote pamoja na ada ya kurudishiwa huduma. Kwa hiyo:-

a) CHALIWASA itasitisha huduma kwa wateja wote wenye kukiukautaratibu uliowekwa.

12

Page 13: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

b) Kusitisha huduma kutafanyika siku 14 baada ya muda wa malipoulioelezwa kwenye Ankara za madai ambayo ni tarehe 15 ya mweziunaofuata.

c) Wateja wanaweza wasipewe taarifa nyingine ya ziada zaidi ya iliyokokwenye Ankara ya madai ambayo ni notisi iliyojitosheleza kabla yakusitishiwa huduma.

d) Kurudisha huduma kutafanyika mapema iwezekanavyo na siyo zaidi yasaa 48 ya kazi baada ya malipo ya madai ya matumizi na ada yakurudishiwa maji kufanyika.

e) Kusitishwa kwa huduma kutafanyika wakati wowote endapo mtejaatagundulika kuwa anatumia maji kinyume na sheria na kwa njia isivyohalali. Hatua hii itaenda sambamba na kuchukuliwa hatua za kisheria.

2.6 Maulizo ya Ankaraa) Kuhusu Ankara zinazohitaji uchunguzi, maulizo ya Ankara yaliyofanywa

na mteja kwa kufika mwenyewe sehemu ya huduma/kituo cha malipo,kwa maandishi au kwa simu, yatafanyiwa kazi na majibu au taarifaitatolewa katika muda wa siku 5 za kazi.

b) Mteja anaweza kuendelea kulipa deni la maji kwa kiwango ambachoanafikiri ni sahihi wakati uchunguzi wa tatizo la Ankara unaendeleakufanyika.

3. TAARIFA YA KATIZO LA MAJI

3.1 CHALIWASA itatumia njia muafaka za mawasilianokuwahabarisha wateja wake juu ya katizo la hudumalililopangwa.

Taarifa zitazingatia mambo yafuatayo:-

a) Muda ambao katizo limepangwa kutokea.b) Maeneo yatakayoathirikac) Sababu za katizo la huduma ya Majid) Matarajio ya Muda ambao huduma itarejeshwa.

3.2 Utaratibu wa Kutoa Taarifa ya Katizo la huduma ya Majisafi

a) Taarifa itatolewa kabla ya siku 3 ya katizo lililopangwa mfanolinalohusu usafishaji wa chemba zetu za maji.

b) Kwa wateja wakubwa, CHALIWASA na wateja watakubaliana juu yampango wa katizo. Kama haitawezekana, CHALIWASA itatuma taarifa

13

Page 14: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

kwa watumiaji wakubwa wa huduma ya Majisafi, kwa maandishi (baruahalisi), Simu au kupitia Barua pepe.

c) Kwa katizo la Maji ambalo halikupangwa na ambalo litaathiri sehemukubwa (ikiwemo kuzimika kwa gridi ya Taifa) CHALIWASA itaujulishaumma/wateja binafsi sababu za katizo. CHALIWASA itachagua njiamuafaka ya mawasiliano kuwajulisha wateja wake kuhusiana na katizololote la umeme ndani ya saa 24.

d) Kwa katizo la umeme lisilopangwa kwa mteja mmoja mmoja aumaeneo madogo, CHALIWASA itafanya bidii ya kurudisha maji ndani yasaa 24 kutegemeana na aina ya tatizo baada ya umeme kurudishwa..

e) Kwa tatizo ambalo haliwezi kurekebishwa ndani ya kipindi hicho kamavile kuharibika kwa kifaa kikubwa kutokana na matatizo ya kiufundi,wateja watajulishwa ndani ya kipindi kilichotajwa. Hata hivyo kwamatatizo madogo CHALIWASA itarudisha maji ndani ya saa 12.

f) Kama italazimika kupunguza matumizi ya maji kwa mgao maslahi yataifa yatalindwa kwa kutoa kipaumbele cha upatikanaji wa maji kwenyemaeneo muhimu na nyeti kama vile Ikulu, Ofisi za serikali, Mahospitalina Taasisi. Hivyo, kipaumbele cha kwanza kitabakia kuwa nikutowakatia maji wateja hao, isipokuwa kama hali ya upatikanaji wahuduma haitaruhusu kabisa.

4. HAKI NA WAJIBU MUHIMU WA MTEJA

4.1 Haki za Mteja

Mteja ana haki za:-a) Kujua usahihi wa vipimo vya matumizi ya majib) Kupata ankara zisizo na makosac) Kuhudumiwa kwa heshimad) Kupata huduma inayokidhi kiwangoe) Kupata huduma nzuri na kwa harakaf) Kuhudumiwa kwa usawag) Kutunziwa usiri wa habari zakeh) Kupata huduma yenye ubora stahikii) Kushirikishwa kwenye mambo yanayomhusuj) Kutoa maoni/malalamiko kuhusu hudumak) Kupata taarifa mbalimbali za maji.

4.2 Wajibu wa MtejaMteja atawajibika:-

14

Page 15: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

a) Kulipia Ankara ya maji kila mwezi bila kulimbikiza deni lolote.b) Kulinda mali za CHALIWASA kwenye maeneo yake.c) Kulinda mifumo ya CHALIWASA kutokana na uharibifu wowote ukiwemo

wa kiufundid) Kutoa taarifa kwa CHALIWASA mapema kabla ya kuhama kwenye

nyumba/jengoe) Kumwomba mmiliki wa eneo analotaka kuhamia kulipia madeni ya

eneo husika kabla ya yeye kuingia (CHALIWASA) haitaunga majikwenye eneo lenye deni kwa mteja mpya tofauti na aliyekuwepompaka deni lote lilipwe.

f) Kuruhusu ukaguzi wa mifumo yake ya ndani ya maji iwapo mamlakaitahitaji kufanya hivyo na kuchukua hatua muafaka za marekebishoyatakayohitajika

g) Kuhakikisha usalama wa mifumo yake ya Maji ndani pamoja na vifaavyote vya maji vilivyounganishwa kuanzia kwenye mita na kurudinyuma. Vilevile kutounganisha mota katika “service line” isipokuambele ya mita yake tu, mfano kutoa maji kutoka kwenye kisimakwenda kwenye matanki ya juu.

h) Kulinda na kutunza vyanzo vya Majii) Kulinda na kutoa taarifa ya hujuma ya miundombinu ya huduma ya

maji.j) Kutoa taarifa juu ya kuhama kwa mteja ambaye anaishi katika nyumba

ya kupanga ndani ya siku 30 kabla ya kuhama.

5. WAJIBU WA MAMLAKA KWA MTEJA

a) Kuwaomba wateja ushauri kuhusiana na huduma zinazotolewa naCHALIWASA.

b) Kuwajulisha wateja kuhusu viwango vya huduma zinazotolewa naMamlaka na wategemee nini kutoka CHALIWASA kama mtoa huduma.

c) Kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingirad) Kuwa waadilifu na wawazi katika kuwahudumia wateja.e) Kutoa habari kamili na sahihi kuhusiana na huduma zinazotolewa.f) Kufanya maboresho endelevu ya huduma kwa kukuza ubunifu na

kujifunza.g) Wajibu wa Mamlaka huishia kwenye mita na wajibu wa mteja huanzia

baada ya mitah) Kuwafidia wateja pale ambapo utandazaji wa maji umesababisha

uharibifu wa mali.

15

Page 16: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

i) Kuendeleza na kutunza miundombinu ya maji.j) Kulinda na kutunza vyanzo vya Majik) Kushauri Serikali katika masuala yanayohusu Sera na miongozo ya

ubora wa majil) Kupanga na kutekeleza miradi mipya ya majisafi na usafi wa mazingiram) Kuelimisha na kutoa taarifa za kiafya kuhusiana na masuala ya huduma

na utunzaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira.n) Kushirikiana na Serikali za Mitaa kuhusiana na upanuzi wa huduma ya

majisafi.o) Kukusanya ushuru kutoka kwa mteja kwa niaba ya mamlaka ya udhibiti

wa hudumap) Kupendekeza bei za huduma ya majisafi na usafi wa mazingira.q) Kufanya jambo lolote ambalo Bodi itaona inafaa kufanyika kwa nia ya

kuiwezesha mamlaka kutekeleza wajibu wake kisheriar) Kujitambulisha na kueleza nia ya uwepo wake kwa mteja

6. HAKI NA UWEZO WA KISHERIA WA MAMLAKA

Katika kutekeleza wajibu wake wa utoaji wa huduma za usambazaji wamajisafi nausafi wa mazingira, CHALIWASA ina mamlaka yafuatayo;-

a) Kuhifadhi, kupata kwa kununua, kujenga na kuendesha huduma yamajisafi na usafi wa mazingira.

b) Kupata njia kwa ajili ya kutandaza mabomba ya huduma ya majisafi nakuweka mabomba kwa ajili ya matumizi ya umma

c) Kufunga mita za maji kwa ajili ya kupima matumizi ya maji kwawatumiaji

d) Kutoza gharama kwa huduma inayotolewae) Kuingia makubaliano na mmiliki au mkazi wa eneo lenye maji na ardhi

kuhusu utunzaji na uhifadhi wa maji ambayo mamlaka inahitaji auinatumia.

f) Kudhibiti, kupunguza, kusitisha au kuahirisha usambazaji wa majig) Kutoa vifaa vya usambazaji wa maji kwa wateja wake.h) Kuingia kwa mteja yeyote na kufanya kazi inayohusiana na huduma ya

majisafi na Usafi wa Mazingira bila kuzuiwa kwa mbwa au mageti.i) Kutunga na kuidhinisha matumizi ya sheria ndogo ndogo (By-laws) kwa

ajili ya kutekeleza ufanisi wa sheria ya maji na usafi wa mazingira

16

Page 17: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

7. ULIPAJI WA FIDIA KWA MTEJA.

Ulipaji wa fidia utafanyika baada ya Mamlaka kuwa imefanya uchunguzi wakina kuhusiana na tatizo hilo kwa mteja.

a) Endapo itabainika Mamlaka imesitisha huduma ya maji (wrongdisconnection) kwa mteja kimakosa baada ya kuhisi hajalipia maji kwamuda mrefu isivyo sahihi. Utaratibu wa kudai fidia ni kwamba Mteja atalazimika kuulizia kuhususuala hilo kwa njia ya simu na kama hatapata utatuzi atawajibikakuandika kwa maandishi baada ya siku tano za kazi na kujibiwa ndaniya siku tatu za kazi. Na endapo hakutakuwa na suluhisho baada ya sikutano kupita mteja ataidai Mamlaka kiasi cha Tshs 1000 kwa kila sikuambayo itaongezeka akiwa hana huduma ya maji.

b) Pale ambapo mteja amechelewa kurudishiwa huduma ya majialiyokatiwa kwa kuwa na deni na yeye kufanikiwa kulipa deni loteambapo alitakiwa arudishiwe huduma ndani ya masaa 48.Utaratibu wa kudai fidia ni kwamba, Mteja atawajibika kuulizia kwa njiaya simu baada ya siku 3 kupita na endapo hakutakuwa na majibu yakuridhisha itampasa kuandika barua akielezea tatizo lake, na endapohatajibiwa lolote baada ya siku tano za kazi, mteja ataidai fidiamamlaka ya Tshs 1000 kwa kila siku kwa kukaa bila huduma ya maji.

c) Endapo Mteja ameshalipia maunganisho mapya ndani ya mudaalioelekezwa kufanya hivyo ambapo angetakiwa aunganishiwe ndaniya siku 14.Utaratibu wa kudai fidia ni kwamba, Mteja atalazimika kuulizia baadaya siku tano za kazi kupita kwa njia ya simu katika ofisi zetu na kamahata pewa majibu ya kuridhisha atatakiwa kuandika barua kuelezeatatizo lake baada ya siku tano za kazi kupita. Na endapo hatajibiwandani ya siku tano za kazi mteja ataidai mamlaka kiasi cha Tshs 1000kwa kila siku kwa kukaa bila huduma ya maji.

17

Page 18: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

8. MAKOSA YA JINAI YANAYOAINISHWA NA SHERIA YA MAJI NA USAFIWA MAZINGIRA NAMBA 12 YA MWAKA 2009

Kutokana na Sheria hii ya Maji kifungu namba 47, 48, 49, 50, 51, 52 na 53kila mwananchi anao wajibu wa kutii bila kushurutishwa kwa kuzingatia kuwaakitenda na kwenda kinyume ataadhibiwa kwa kanuni na adhabu zifuatazo:

a) Kuhusu kuingilia miundombinu ya majisafi kwa kuingiza au kuchukua majikutoka kwenye miundombinu bila idhini ni kosa, na adhabu yake ni kulipafaini ya Shilingi za Kitanzania isiyopungua Tshs 50,000/= hadi Tshs5,000,000/= au kifungo cha mwezi mmoja hadi miaka 5 jela au vyotekwa pamoja.

b) Kusababisha upotevu wa maji kwa makusudi au uzembe kutoka kwenyemiundombinu ya mamlaka ni kosa na adhabu yake ni faini isiyopunguaTshs 50,000/= au kuzidi Tshs 1,000,000/= au kifungo cha kati yamwezi mmoja au miezi 6 jela au vyote kwa pamoja.

c) Kusababisha kwenye mita ya maji uharibifu wa makusudi au uzembe nakusababisha mita kutofanya kazi yake ya kupima maji yanayopita kwausahihi na adhabu yake ni faini isiyopungua Tshs 500,000/= au kifungocha kati ya miezi 6 au mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja namita husika kubadilishwa kwa gharama ya mkosaji.

d) Kutumia huduma ya maji kinyume na malengo au maombi ya matumizi naadhabu yake ni faini isiyopungua Tshs 100,000/= na kifungo cha mwezimmoja bila kuathiri thamani ya maji yaliyotumika kimakosa.

e) Kuoga, kufua, kutupa uchafu, kuruhusu uchafu kuingia kwenye vyanzo aumiundombinu ya majisafi adhabu yake ni faini ya kiasi kisichozidi Tshs1,000,000/= au kifungo kisichozidi mwaka mmoja jela au vyote kwapamoja.

18

Page 19: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

f) Kumdhihaki, kumtishia, kumzuia au kumkwamisha mtumishi wa Mamlakakutekeleza majukumu yake halali yanayohusu utendaji wa mamlaka nikosa na adhabu yake ni faini isiyozidi Tshs 5,000,000/= na kifungokisichozidi miaka 3 jela au vyote kwa pamoja, pamoja na kulipa fidiakwa madhara yaliyotokea kwa mtumishi.

g) Kufanya tendo au jambo lolote lililo kinyume na sheria ya maji au ambalohalijafuatwa na sheria ni kosa na adhabu yake ni faini isiyopungua Tshs50,000/= au kifungo kisichozidi mwezi mmoja jela.

9. UFUATILIAJI, MALALAMIKO, MAULIZO, NA MAOMBI YA MTEJA

9.1 Malalamiko ya Mteja

a) Baada ya kupata lalamiko kwa simu kutoka kwa mteja, Mamlakaitafuatilia malalamiko hayo kupitia kumbukumbu za mteja na hatimayekwenda kutembelea eneo husika ili kujua ukweli wa lalamiko nakuweza kushuhulikiwa kwa wakati.

b) Malalamiko ya mteja yaliyowasilishwa kwa maandishi yatajibiwa kwamaandishi ndani ya siku 3 za kazi na tatizo litatafutiwa ufumbuzi ndaniya siku 7. Kama tatizo halitaweza kutatuliwa ndani ya siku hizo, mtejaatafahamishwa kwa njia ya simu na pia barua.

c) Utoaji wa fidia kwa mteja aliyekatiwa maji kwa makosa utafanyikabaada ya uthibitisho na vielelezo vya uhakiki kukamilika kulingana namazingira husika.

d) Pale ambapo huduma inayotolewa na CHALIWASA haitamridhishamteja, mteja anaweza kupeleka malalamiko yake EWURA baada yakujiridhisha kwamba CHALIWASA haiwezi kumsaidia.

9.2 Maulizo ya Mtejaa) Kama kazi ya uchunguzi inahitajika, maulizo yote kwa njia ya simu au

yaliyowasilishwa na mteja mwenyewe kwa kufika ofisini yatajibiwandani ya siku 3 za kazi.

b) Maulizo ya maandishi nayo yatajibiwa ndani ya siku 3 za kazi.c) Maulizo mengineyo yoyote yatatatuliwa ndani ya siku 7 za kazi.

9.3 Maombi ya MtejaMaombi yote ya mteja yaliyowasilishwa kwa maandishi (kwa mfanokusogeza mita, kubadili mita, kuhamisha bomba, kubadilisha mfumowa usambazaji), yatajibiwa na CHALIWASA kwa maandishi ndani ya

19

Page 20: MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA CHALINZE ... · d)Wamiliki wa nyumba/majengo wanaotarajia kubadilisha umiliki au matumizi ya nyumba/majengo yao kama vile kutoka matumizi

siku 3 baada ya kuyapokea. Majibu yatahusisha habari/taarifa kuhusugharama kwa mteja, wajibu wa mteja na muda wa kutekeleza maombihusika.

9.4 Bei na Tozo za Mbalimbali za Huduma ya Maji.

Jedwali Na. 9.4.1: Linaloonyesha bei za huduma ya maji kwa kila aina yamtejaS/N AINA YA MTEJA GHARAMA KWA “UNIT”1 Mteja wa nyumbani 1,200/=

2 Mteja wa biashara 1,540/=3 Mteja wa kioski 2,125/=4 Mteja wa kiwanda 1,555/=5 Mteja wa taasisi 1,220/=

Jedwali Na 9.4.2: Linaloonyesha tozo mbalimbali katika MamlakaNo. AINA YA HUDUMA GHARAMA1. Kurudishiwa huduma ya maji 21,000/=2. Kukagua mita 20,000/=3. Kuhamisha mita 30,000/=4. Fomu ya maombi ya maji 5,000/=5 Uharibifu wa mita 122,245/=6 Uharibifu/kugonga valvu, bomba, mita n.k. Gharama itategemea

tathmini

10. HUDUMA ZA SIMU

a) Huduma za simu za saa 24 zitatolewa kusaidia kutoa taarifa za hitilafuza mitambo na dharura.

b) CHALIWASA itatoa huduma kwa malalamiko, maombi na maulizo. c) Huduma hii itatolewa saa za kazi kwa simu namba 0753 250 636 na

0752 801 178.d) Mteja atatoa taarifa za kupasuka kwa mabomba, kukosekana kwa

Huduma, na matatizo mengine yenye kuhitaji uharaka (emergency)siku zote saba (7) za wiki kwa kutumia namba hizi za simu: 0753 250636 na 0752 801 178.

20