58
Mfululizo wa Masuala ya Kifikihi al-Qabdh’ Baina ‘l-Bid’ah wa ‘s-Sunnah Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna Kimeandikwa na: Sheikh Jafar Subhani Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page A

Je, Kufunga Mikono ni Bidaa au Sunna?

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Kufunga mikono kwenye Sala ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhekufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page E hebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.

Citation preview

Mfululizo wa Masuala ya Kifikihi

al-Qabdh’

Baina ‘l-Bid’ah wa ‘s-Sunnah

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna?

Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

Kimeandikwa na:Sheikh Jafar Subhani

Kimetarjumiwa na:Hemedi Lubumba Selemani

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page A

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 - 427 - 42 - 1

Kimeandikwa na:Sheikh Jafar Subhani

Kimetarjumiwa na:Hemedi Lubumba Selemani

P.O. Box 19701, Dar es Salaam.Tanzania.

Kimehaririwa na: Ustadh Abdallah Mohamed

Kupangwa katika Kompyuta na:Ukhti Pili Rajab

Toleo la kwanza: Julai 2007Nakala:1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

P.O. Box 19701 Dar es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2110640Fax: +255 22 2131036Email: [email protected]

Website: www.alitrah.org

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page B

YALIYOMO

Kufunga mikono kwenye Sala kati ya bidaa naSunna................................................................................2

Kufunga mikono ni bidaa iliyozushwa.............................4(a) Hadithi ya Abu Humeidi As-Saidiyu...............4(b) Hadithi ya Hammadi bin Isa.........................10

Dalili zinazosema kuwa kufunga mikono ndani ya sala nilazima........................................................................ 14

(a) Sura ya Kwanza ya Hadithi...........................18(b) Sura ya pili ya Hadithi..................................20(c) Sura ya Tatu ya Hadithi................................ 23

Hadithi ya Abdallah bin Mas’ud.....................................26Hadithi dhaifu zisizokuwa hoja......................................28Qubaysatu bin Hulbu......................................................29Sammaku Bin Harbu..................................................... 30

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page C

Hadithi ya Muhammad bin Abana Al-Answariy...........32Hadithi ya Aqabatu bin Sahbani.....................................33Hadithi ya Ghazuwani bin Jarir......................................35Hadithi mbili za kuvushwa za Ghadhifu na Shadadu....36Hadithi ya nafiu toka kwa Ibnu Umar...........................38Hadithi ya Ibnu Jarir Dhabiy...........................................39Hivi sasa haki imedhihirika............................................41Hadithi za Ahlul -Bayt................................................... 43

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page D

NENO LA MCHAPISHAJIKitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu chaKiarabu kwa jina la: "Al-Qabdh Baina ‘l-Bid’ah wa ‘s-Sunnah" Sisi tumekiita: "Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa auSunna? Kwenye Sala."

Kitabu hiki, "Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? KwenyeSala" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa naMwanachuoni wa Kiislamu, Jafar Subhany.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kilajambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompatamwanadamu katika sekta zote za maisha yake.

Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wame-hitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo yaibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwawafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongolisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafi-ana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambomachache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo.

Kufunga mikono kwenye Sala ni suala ambalo wanachuo wetuwamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhe-

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page E

hebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi yawanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya sualahili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitila-fu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kus-ababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hiiSheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina sualahili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachiamsomaji mwenyewe kutoa uamuzi.

Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wamaendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana naukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoekitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji waKiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na yakijamii.

Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani(Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjumakitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshirikikwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwakitabu hiki. Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page F

KUFUNGA MIKONO KWENYE SALA KATI YA BIDAANA SUNNA KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA.

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu mlezi wa ulimwen-gu. Rehma na Amani zimfikie mbora wa viumbe nahitimisho la mitume Wake, pia kizazi chake kitakatifu ambachondio kasha la elimu yake na hazina ya mafunzo yake. HakikaUislamu ni imani na sheria. Imani ni kuamini MwenyeziMungu, mitume Wake na Siku ya Mwisho. Na sheria ni huku-mu za Mwenyezi Mungu ambazo zina jukumu la kumpamwanadamu maisha bora na kumuhakikishia wema wa duniana akhera.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kilajambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompatamwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyoMwenyezi Mungu akasema:

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page i

“Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizienineema Yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe diniyenu.” ( 5:3 ).

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoniwa sheria wamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwaokuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jamboambalo limepelekea kutofautiana kuhusu masuala madodomadogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katikamtiririko wa masomo haya tumejaribu kuliweka sala hili juu yameza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganishamtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu. Kwani tofautiiliyopo si katika asili na misingi ya dini hata ipelekee kuwa nauadui na chuki bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zilizonasi-bishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilinganisha na mambomengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu.Na muongozo wetu katika njia hii ni kauli ya MwenyeziMungu:

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page ii

“Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyotewala msifarakiane. Na kumbukeni neema ya MwenyeziMungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziungan-isha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu.”(3:103)

Sheikh Jafar SubhaniTasisi ya Imam Sadiq (a.s.)Qum

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page iii

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 1

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna?Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

Hakika kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto ni

jambo mashuhuri lililohimizwa na wanafiqihi wa kisunni.

Wafuasi wa Hanafiy wamesema: “Hakika kufunga mikono niSunna na wala si wajibu, na lililo bora kwa mwanaume niaweke tumbo la kiganja chake cha kulia juu ya mgongo wakiganja chake cha kushoto chini ya kitovu chake, na kwamwanamke aweke mikono yake juu ya kifua chake.”

Wafuasi wa Shafiy wamesema: “Ni Sunna kwa mwanamumena mwanamke. Na lililo bora kwa mwanaume ni kuwekatumbo la kiganja chake cha kulia juu ya mgongo wa kiganjachake cha kushoto chini ya kifua na juu ya kitovu upande wakushoto.”

Wafuasi wa Hambal wamesema: “Hakika ni Sunna, na bora niaweke kiganja cha kulia juu ya mgongo wa kiganja chakushoto, aweke chini ya kitovu.”

Wafuasi wa Malik wamekwenda kinyume na hao, hivyo2

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 2

wakasema: “Ni Sunna kuachia mikono ndani ya Sala ya farad-hi.”

Na kuna kundi lililosema hivyo kabla yao, kati yao ni Abdullahbin Zubeiri, Saidi bin Al-Musayyabu, Saidi bin Jubairi, Atau,Ibnu Jariji, An-Nakhaiy, Hasani Al-Basriy, Ibnu Sirini na kundila wanafiqihi. Na ndio msimamo wa Alay-thu bin Saad,isipokuwa yeye kasema: “Isipokuwa atakaporefusha kisimamona akawa amechoka basi itambidi kufunga mikono.”

Na kauli iliyonukuliwa toka kwa Imam Al-Awzaiy ni hiyarikati ya kufunga mikono au kuachia. 1

Mufti wa madhehebu ya Malik huko Ad-Dayaru Al-Hijaziya,Muhammad Abidu ameona kuwa kuachia mikono na kufungani Sunna toka kwa Mtume na kuwa muumini anaporefushakisimamo ilihali kaachia mikono na akachoka basi anafungamikono. Akasema kuwa kuachia mikono ni asili na kufunga nitawi. 2

3

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

1 Muhammad Jawad Al-Mughuniyya: Al-Fiqihi ala Madh-habul-khamsa: 110 2 Angalia ujumbe mfupi kuhusu kuachia mikono wa Dr. Abdul-Hamidi bin Mubarak

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 3

Ama Shia Imamiyah mashuhuri kwao ni kuwa ni haramu nahubatilisha Sala, na ni wachache sana wamesema ni makuruhu,kama vile Al-Halbiy ndani ya Al-Kafiy3

Kufunga mikono ni bidaa iliyozushwa

Hakika kufunga mikono ni bidaa iliyozushwa iliyodhihiribaada ya kufariki Mtume mtukufu. Na tegemezi letu katikakuthibitisha hilo ni Hadithi mbili sahihi:

Moja kati ya hizo imepokewa kwa njia za Masunni, nanyingine imepokewa kwa njia ya Shia Imamiyah. Hadithi hizombili ni dalili yakinifu zinazothibitisha kuwa mwenendo waMtume na kizazi chake kitakasifu ulikuwa ni kuachia mikonondani ya Sala, na kuwa kufunga mikono ni bidaa iliyoanzishwabaada ya kifo cha Mtume.

a: Hadithi ya Abu Humeidi As-Saidiyu

Wanahadithi wengi zaidi ya mmoja wamepokea Hadithi yaAbu Humeidi As-Saidiyu, hapa tutaitaja kwa mujibu wa maele-zo ya Al-Bayhaqi. Amesema: Ametupa habari Abu Abdillah Al-

4

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

3 An-Najafiy: Jawahirul-Kalamu: 11/ 15- 16

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 4

Hafidhu: Akasema Abu Humeidi As-Saidiyu: “Mimi ni mjuzizaidi wa Sala ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Wakasema: “Kwa nini? Ilihali haukumfuata mara nyingi zaidiyetu wala hukutangulia kuwa nae kabla yetu?” Akasema:

“Ndio.” Wakasema: “Tuelezee.”

Akasema: “Mtume alipokuwa akisimama kuswali alikuwa aki-inua mikono yake mpaka iwe sawa na mabega yake, kisha ana-toa takbira mpaka kila kiungo kitulie sehemu yake huku akiwaamenyooka. Kisha anasoma, kisha anatoa takbira na kuinuamikono yake mpaka iwe sawa na mabega.

Kisha anarukuu na kuweka viganja vyake juu ya magoti yake,kisha ananyooka bila kunyanyua kichwa chake wala kukilaza.Kisha anainua kichwa chake na kusema: (Mwenyezi Munguamemsikia anaemuhimidi). Kisha anainua mikono yake mpakaiwe sawa na mabega yake mpaka kila kiungo kirudi sehemuyake akiwa amenyooka. Kisha anasema: Allahu Akbar.

Kisha anaporomoka ardhini anaweka mikono yake pembenimwake. Kisha anainua kichwa chake anakunja mguu wake wakushoto na kuukalia. Na anaposujudu hufungua vidole vya

5

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 5

miguu yake. Kisha anarudi kusujudu, kisha anainua kichwa nakusema: Allahu Akbar. Kisha anakunja mguu wake na kuukaliaakiwa amenyooka mpaka kila mfupa urudi au utulie sehemuyake.

Kisha anafanya hivyo hivyo katika rakaa nyingine. Kisha ana-posimama toka kwenye rakaa mbili hutoa takbira na kuinuamikono yake mpaka iwe sawa na mabega yake kama alivy-ofanya na kutoa takbira mwanzo wa Sala yake.

Kisha anafanya hivyo hivyo katika Sala yake yote mpakaanapofika katika sijida ya kutoa Salamu hapo hucheleweshamguu wake wa kushoto na kukaa mkao wa Tawaruku upandewake wa kushoto.”

Hapo wote wakasema: “Amesema kweli, hivyo ndivyoalivyokuwa akiswali Mtume wa Mwenyezi Mungu.”4

Na kinachoweka wazi usahihi wa kutegemea Hadithi hii nimambo yafuatayo:Kitendo cha maswahaba wakubwa kumsadikisha Abu

6

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

4Al-Bayhaqi: As-Sunan: 2/ 72, 73, 101, 102, . Abu Daud: As-Sunan:1/194,mlango wa kuanza Sala. Hadithi ya 730-736. Al-Tir’midhiy: As-Sunan: 2/98, mlango wa wasifu wa Sala. Musnad Ahmad: 5/ 424. Ibnu Khuzaymandani ya Sahih yake, mlango wa itidali ndani ya rukuu, namba 587

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 6

Humeidi5 kinaonyesha nguvu ya Hadithi, na kufaa kuitangulizakabla ya dalili nyingine.

Hakika yeye katoa wasifu wa Sala kuanzia faradhi zake hadiSunna zake wala hakutaja kufunga mikono, na wala maswaha-ba hawakumkosoa au kutaja kitu kinyume na alivyosema, ili-hali walikuwa na hamu ya kufanya hivyo kwa sababu mwanzohawakukubali kuwa yeye ni mjuzi wa Sala ya Mtume kulikowao. Lakini pamoja na hali hiyo wote walisema: Umesemakweli hivyo ndivyo alivyokuwa akiswali Mtume. Na iko mbalisana dhana ya kuwa wao wote walisahau ilihali walikuwamakumi na wako katika mazingira ya kukumbuka.

Asili katika kuweka mikono ni kunyoosha, kwa sababu ndiomaumbile, na Hadithi imeonyesha hilo.

Huwezi kudai kuwa Hadithi hii imekuja bila sharti lakini kunaHadithi nyingine zimekuja kuiwekea sharti. Haiwezekanihivyo kwa sababu katoa wasifu na kuorodhesha faradhi zote zaSala na Sunna zake na vyote vinavyokamilisha umbile la Sala,ilihali akiwa katika kuonyesha na kubainisha mafunzo, hivyokutotoa baadhi ya sifa ni kufanya khiyana. Na jambo hilo la

7

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

5. Miongoni mwao ni Abu Huraira, Sahl As-Saidiyu, Abu Usaydu As-Saidiyu, Abu Qatadatu Al-Harithu bin Rabiiyu na Muhammad bin Maslamati.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 7

khiyana liko mbali na yeye bali na wao.

Baadhi ya maswahaba waliokuwepo kati ya wale waliopokeaHadithi za kukunja mikono hawajapinga (Maelezo yake).Hivyo ikaonyesha kuwa kukunja mikono ni sheria iliyoishamuda wake, au kwa uchache inaruhusiwa kwa yule aliyere-fusha kisimamo ndani ya Sala yake, na si miongoni mwa Sunnaza Sala kama ilivyo kwa madhehebu ya Alaythu bin Saad naAl-Awzaiy na Malik.6

Ibnu Rushdi amesema: “Na sababu ya kutofautiana kwao nikuwa zimekuja riwaya thabiti zilizonukuu wasifu wa Sala yaMtume lakini haijanukuliwa kuwa alikuwa akiweka mkonowake wa kulia juu ya mkono wa kushoto.”7

Hapa limebakia swali moja nalo ni kuwa ni mashuhuri kuwawafuasi wa Malik hawafungi mikono na Imam wao alikataajambo hilo.

Akasema ndani ya Al-Mudawanati: “Malik amekataa kuweka

8

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

6 Dr. Abdul-Hamidi bin Mubarak: Ujumbe mfupi kuhusukuachia mikono: 117 Bidayatul-Muj’tahid

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 8

mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto ndani ya Sala naakasema: Silijui jambo hilo ndani ya faradhi, ilihali yeyemwenyewe ndani ya kitabu chake Al-Muwata amepokeaHadithi ya kukunja mikono, kwani amepokea toka kwa Sahlbin Saad kama alivyopokea kwa kuvushwa toka kwa Abdul-Karimu ibnu Abu Al-Makhariqu Al-Basriy kuwa alisema:“Miongoni mwa maneno ya unabii ni: Kama hauna haya tendalolote unalotaka, na kuweka mikono, mmoja juu ya mwinginendani ya Sala, kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wakushoto, na kuharakisha kufuturu na kuchelewesha kuladaku.”8

Nasema: Hakika kitabu Al-Muwata ni kitabu cha riwaya, hivyoImam anaweza kuipokea na wala asitoe fat’wa kufata riwayahiyo. Ndio maana utaona ndani ya Al-Mudawanat kuna fat’wazinazopingana na riwaya alizozipokea ndani ya Al-Muwatau.

Na atakayefuatilia fiqhi yake ataona kuwa kuna tofauti kubwakati ya riwaya zake zilizomo ndani ya Al-Muwatau na fat’wazake zilizoandikwa.

9

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

8 Al-Muwatau:1/158 mlango wa kuweka mkono juu ya mwingine ndani yaSala, Hadithi ya 46, 47

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 9

Dr. Abdul-Hamidi ndani ya ujumbe wake mfupi alioandikakuhusu kuachia mikono ameashiria sehemu hizo za tofauti. 9

Vyovyote vile ni kuwa kauli yake (Silijui jambo hilo ndani yafaradhi) ni dalili ya wazi kuwa matendo ya watu wa mji wakeni tofauti na kitendo hicho, kwani kauli (Silijui jambo hilondani ya faradhi) maana yake silijui jambo hilo kutoka kwenyematendo ya Maimam ambao ndio waliyokuja baada ya maswa-haba na wakachukua elimu toka kwa maswahaba.

Hii ndio Hadithi ambayo imesimama kubainisha namna ya Salaya Mtume, nayo imepokewa kwa njia ya Masunni, na tayariumeshajua hoja zake. Na sasa ni riwaya iliyopokewa na ShiaImamiyah.

b: Hadithi ya Hammadi bin Isa

Hammadi bin Isa amepokea toka kwa Imam Sadiqi (a.s.) kuwaalisema: “Ni jambo baya sana mtu kutimiza miaka sitini ausabini ilihali hajawahi kuswali hata Sala moja kwa ukamilifu.Hammadi akasema: Ukanifikia udhalili ndani ya nafsi yangu,nikasema: Niko chini yako, nifundishe Sala.”

10

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

9 Ujumbe mfupi kuhusu kuachia mikono: 6 - 7

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 10

Akasimama Abu Abdillah akiwa kaelekea kibla ilihali kany-ooka, akanyoosha mikono yake yote juu ya mapaja yake ilihalikabana vidole vyake na kasogeza nyayo zake mpaka kiwangocha uwazi wa vidole vitatu.

Akaelekeza kibla vidole vya miguu yake kwa unyenyekevu, nawala hakuvitoa kwenye kibla. Akasema: Allahu Akbar, kishaakasoma Al-Hamdu na Qul-huwa llahu ahadu. Kisha akasubirikidogo kwa kiwango cha kuvuta pumzi ilihali akiwa kasima-ma.

Kisha akasema: Allahu Akbar akiwa amesimama, kishaakarukuu na kujaza viganja vyake kwenye magotiyaliyoachana na akarudisha magoti yake nyuma mpaka mgon-go wake ukanyooka kiasi kwamba hata kama tone la maji aumafuta lingedondoka juu ya mgongo wake basi lingekaa.Akaendelea kunyoosha mgongo ilihali magoti yake kayarud-isha nyuma, akanyoosha mbele shingo yake huku kafumbamacho yake.

Kisha akamsabihi Mwenyezi Mungu akasema: AmetakasikaMola Wangu Mtukufu na kila sifa njema ni Zake. Kisha akasi-mama akiwa kanyooka na alipotulia akasema: MwenyeziMungu kamsikia aliyemuhimidi.

11

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 11

Kisha akatoa takbira ilihali kasimama. Akainua mikono yakemkabala na uso wake na kusujudu, akaweka mikono yake arid-hini kabla ya magoti yake na kusema mara tatu: AmetakasikaMola Wangu Mtukufu na kila sifa njema ni zake.

Wala hakuweka sehemu ya mwili wake juu ya sehemunyingine ya mwili wake. Akasujudu kutumia viungo nane:Bapa la uso, viganja viwili, macho ya magoti yake, vichwa vyavidole gumba vyake na pua. Hivi viungo saba ni lazima na puani Sunna, nayo ni kwa ajili ya kujidhalilisha.

Kisha akainua kichwa chake toka sijida, na alipokaa sawaakasema: Allahu akbar kisha akakaa kwa kulalia upande wakewa kushoto, akawa ameweka mgongo wa nyayo yake ya kuliajuu ya nyayo yake ya kushoto. Akasema: Namuomba Molawangu magh’fira na ninatubu kwake.

Kisha akatoa takbira ilihali kakaa. Akasujudu sijida ya pili,akasema kama alivyosema katika sijida ya kwanza. Wala haku-tumia sehemu ya mwili wake kuusaidia mwili wake katika siji-da yake na rukuu yake. Wala hakuweka dhiraa zake juu yaardhi.

Hivyo akaswali rakaa mbili kwa namna hii. Kisha akasema:

12

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 12

Ewe Hammadi, hivi ndivyo uswali wala usigeuke walausicheze kwa mikono yako na miguu yako wala usiteme matekushotoni mwako au kuliani au mbele yako.”10

Unaona kuwa riwaya hizi mbili zinabainisha namna ya Salawaliyofaradhishiwa watu, na ndani ya maelezo hayo hamnaishara yoyote inayogusia kufunga mikono kwa vigawanyovyake tofauti.

Laiti ingekuwa ni Sunna basi Imam asingeacha kubainisha kwasababu kwa kitendo chake anatujengea hali halisi ya Sala yaMtume kwa sababu kachukua toka kwa baba yake Imam Al-Baqir na yeye kachukua toka kwa baba zake toka kwa kiongoziwa waumini Imam Ali toka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hivyo kufunga mikono ndani ya Sala ni bidaa, kwa sababu nikupandikiza jambo ndani ya sheria ilihali lenyewe si katikasheria.

13

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

10. Al-huru Al-amiliy: Al-wasailu:4 mlango 1 mlango wa vitendovya sala. Hadithiu ya 1. Na angalia mlango wa 17 Hadithi ya 1,2.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 13

Dalili zinazosema kuwa kufunga mikonondani ya Sala ni lazima

Kisha hakika anayeruhusu kufunga mikono ana dalili, nasitutazichambua.

Hakika dalili zote zinazosihi kutolewa kuthibitisha kuwakufunga mikono ndani ya Sala ni Sunna hazizidi riwaya tatu:11

Hadithi ya Sahl bin Saad. Kaipokea Bukhari.

Hadithi ya Wailu bin Hajar kaipokea Muslim na kainukuu Al-Bayhaqiy kwa njia tatu.

3. Hadithi ya Abdallah bin Mas’ud kaipokea Al-Bayhaqiyndani ya Sunan yake na vitabu vingine.

Ufuatao ni uchambuzi wa kila Hadithi:

Hadithi ya Sahl bin Saad.Bukhari amepokea toka kwa Abu Hazimu toka kwa Sahl bin

14

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

11.Kuna dalili nyingine zisizo sahihi zinazozungumzia kufungamikono. Hayo ni kama inavyofahamika toka kwenye maneno ya Al-naswawiy ndani ya Shar’hu yake ya Sahih Muslim:4/358.Tutakuletea maneno yake.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 14

Saad amesema: Watu walikuwa wakiamrisha mtu awekemkono wa kulia juu ya dhiraa yake ya kushoto ndani ya Sala.Abu Hazimu akasema: Silijui jambo hili, labda kama hilolitanasibishwa na Mtume.12

Ismail13amesema: “Hilo litanasibishwa, hajasema atanasi-bisha.”

Riwaya imebeba jukumu la kubainisha namna ya kufungamikono, isipokuwa baada ya njia yake ya upokezi kukubalikatatizo linabakia kwenye hoja yake.

Wala riwaya haionyeshi Sunna ya kufunga mikono. Hilo nikwa vigezo viwili:Kwanza: Laiti kama Mtukufu Mtume angekuwa ndio muamr-ishaji wa kufunga mikono basi ni nini maana ya kauli “Watuwalikuwa wakiamrisha” Hivi haikuwa ni sahihi kusema

15

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

12. Ibnu Hajar: Fat’hul-Bari fi Shar’hi Sahih Bukhari: 2/224. mlan-go wa kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto. SahihMuslim: 2/13, mlango wa kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wakushoto. Al-Bayhaqi kaipokea ndani ya As-Sunanl-Kubra: 2/28,Hadithi ya 3, mlango wa kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wakushoto ndani ya Sala.13. Mlengwa ni Ismail bin Abu Awyasi, shekhe wa Bukhari. Hayo nikama alivyohakikisha Al-Humaidiyu. Angalia Fat’hul-Bari: 5/325

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 15

Mtume alikuwa akiamrisha?

Hivi huoni kuwa hii ni dalili kuwa hukumu ya kufunga mikonoilianza baada ya kufariki Mtukufu Mtume kiasi kwambamakhalifa na magavana wao walikuwa wakiwaamrisha watukufunga mikono kwa kudhania kuwa hali hiyo ndio iliyo karibusana na unyenyekevu? Na kwa ajili hiyo baada ya riwaya hiyoBukhari akaweka mlango maalum kwa jina la mlango waunyenyekevu.

Ibnu Hajar amesema: “Hekima ya muundo huu (kufungamikono) ni kuwa ni sifa ya muombaji dhalili, nalo ni jambolinalomzuwia mtu kuchezacheza na liko karibu sana naunyenyekevu, Bukhari alizingatia hekima hii hivyo baada yakeakaleta mlango wa unyenyekevu.

Kwa ibara nyingine ni kuwa: Kuamrisha kufunga mikono nidalili ya kuwa watu katika zama za Mtume na muda mfupibaada ya zama zake walikuwa wanaswali kwa kuachia mikono,kisha baadaye ikazushwa fikira hii na hivyo wakawaamrishawatu kufunga mikono.

Pili: Hakika mwishoni mwa njia ya upokezi kuna kitu kina-chounga mkono kuwa kufunga mikono ilikuwa ni kitendo chawaamrishaji wala si kitendo cha mwenyewe Mtukufu Mtume,

16

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 16

kwani amesema: Ismaili amesema: “Silijui jambo hili, labda kama hilo litanasi-bishwa kwa Mtume.” Hiyo ni kama tutasoma kwa tamko lakutomtaja mtendaji. Maana yake itakuwa yeye hajuwi kuwajambo hilo ni Sunna ndani ya Sala isipokuwa linanasibishwa tuna Mtume, hivyo riwaya aliyoipokea Sahl bin Saad itakuwaimevushwa (Yaani mlolongo mzima wa wapokezi hadi kum-fikia yeye haujatajwa).

Ibnu Hajar amesema: Na katika istilahi za fani ya Hadithi nikuwa mpokezi atakaposema; inanasibishwa, Maana yake nikuwa imevushwa toka kwa Mtume.14 (Yaani mlolongo mzimawa wapokezi hadi kumfikia yeye haujatajwa)

Haya yote ni iwapo tutasoma kwa tamko la kutomtaja mtenda-ji. Ama tukisoma kwa tamko la kumtaja mtendaji, maana yakeni kuwa Sahl ananasibisha hilo kwa Mtume.

Hivyo iwapo ikisihi kusoma kwa tamko la kumtaja mtendaji naHadithi ikawa si ya kuvushwa basi kauli: “Silijui jambo hili,labda kama….”Iinaonyesha udhaifu wa unasibishaji, na nikuwa alilisikia toka kwa mtu mwingine na hajamtaja jina.

Ibnu Hajar ndani ya Fat’hul-Bari amesema: Ad-Daniyu

17

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

14 Ibnu Hajari mwenyewe: hamishi namba 1

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 17

amezungumzia kuhusu kuvushwa kwa Hadithi hii akasema:Hii ina ila, kwa sababu ni dhana toka kwa Abu Hazimu, naimesemekana kuwa laiti ingekuwa imevushwa basi asingehita-jia kusema: “Silijui jambo hili”15.

Hadithi ya Wailu bin Hajar

Imepokewa kwa sura tofauti:

Sura ya kwanza ya hadithi:

Muslim amepokea toka kwa Wailu bin Hajar: Kuwa alimuonaMtume kainua mikono yake na kutoa takbira pindi alipoingiakwenye Sala, kisha akajifunika kwa nguo yake, kisha akawekamkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto. Alipotakakurukuu akatoa mikono yake ndani ya nguo kisha akaiinua nakutoa takbira kisha akarukuu…..16

Kutumia hoja ya Hadithi hii ni kutumia hoja ya kitendo na

18

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

15 Fat’hul-Bari: 4/12616 Muslim: Sahih:1/13 mlango wa 5 kitabu cha Sala, mlango wa kuwekamkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto. Na katika njia ya Hadithi yumoHamamu. Na kama anaekusudiwa ni Hamamu bin Yahya basi ni kuwa IbnuAmmari kamzungumzia kwa kusema: Yahya bin Al-Qatani alikuwa hamjaliHamamu. Umar bin Shaybatu amesema: Alitusimulia Affani akasema: Yahyabin Saidi alikuwa akimtia dosari Hamamu katika Hadithi zake nyingi. AbuHatimu akasema: Mwaminifu katika kuhifadhi. Angalia Huda Sariy:1/449.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 18

kitendo si hoja isipokuwa mpaka ijulikane kwa nini katendahivyo, na hilo ni jambo lisilojulikana. Kwa sababu dhahiri yaHadithi inaonyesha kuwa Mtume alikusanya pande za nguoyake akafunikia kifua chake na akaweka mkono wa kulia juuya mkono wa kushoto.

Je alifanya hivyo kwa kuwa ni jambo la Sunna au alifanyahivyo ili nguo yake isifunuke bali nguo igusane na mwili nakujikinga baridi kwa nguo hiyo?

Anuani ya kitendo haijulikani hivyo kitendo hakiwi hojampaka itakapojulikana kuwa alifanya hivyo kwa kuwa niSunna ndani ya Sala kufanya hivyo.

Na kuna uwezekano mwingine nao ni kuwa kitendo cha Mtumeilikuwa ni kuzuwia nguo isifunuke ndani ya Sala.

At-Tirmidhiy ametoa toka kwa Abu Huraira kuwa amesema:“Mtume alikataza kufunua nguo ndani ya Sala. Akasema:Kufunua ni mtu kuachia nguo bila kufumba pande za nguoyake mbele yake, hivyo iwapo akiifumba hatokuwa ameifunua,na imepokewa toka kwa Mtume kuwa ni karaha kufunua nguondani ya Sala.”17

Hakika Mtume aliswali pamoja na Muhajirina na Answari zaidi

19

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

17Sunanut -Tirmidhiy: 2/217 Hadithi ya 378.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 19

ya miaka kumi, hivyo laiti kama ingethibiti kufunga mikonotoka kwa Mtume basi suala hilo lingenukuliwa kwa wingi nakuenea, na wala asingepokea Wailu peke yake huku katikakunukuu kwake kuna uwezekano wa aina mbili.

Sura ya pili ya Hadithi: An-Nasai na Al-Bayhaqi wametoandani ya vitabu vyao kwa njia mbili tofauti toka kwa Wailu binHajar amesema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Munguanapokuwa kasimama ndani ya Sala hufunga mkono wake wakulia juu ya mkono wa kushoto.”18

Katika tamko la Al-Bayhaqi ni: “Anaposimama kwenye Salahufunga mkono wake wa kushoto kwa mkono wake wa kulia,na nilimuona Al-Qamah anafanya hivyo.”19

Kutumia Hadithii kama dalili kunategemea usahihi wa njia yaupokezi na kutimia kwa hoja.Ama upande wa njia ya upokezi ni kuwa japokuwa mashekhewawili (Bukhari na Muslim) wameinukuu kwa njia mbili tofau-

20

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

18 Sunanun-Nasaiy: 2/97 mlango wa kuweka mkono wa kulia juu yamkono wa kushoto ndani ya Sala.19 Sunan-Bayhaqiy: 1/28 mlango wa kuweka mkono wa kulia juu yamkono wa kushoto ndani ya Sala.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 20

ti lakini zote zimeshirikiana kwa kuwepo Abdallah ndani yanjia zote mbili.

Ndani ya Sunan An-Nasai: “Alitupa habari Abdullah”. Ndaniya Sunan Al-Bayhaqi: “Alitupa habari Abdullah bin Jafar” namkusudiwa ni Abdullahi bin Jafar bin Najihi Al-Saady.

Inatosha kuthibitisha udhaifu wake kwa aliyonukuu AbdallahIbnu Imam Ahmad toka kwa baba yake: “Wailu alipokuwa aki-fika kwenye Hadithi yake humtia dosari.” Sehemu nyingine akasema amenukuu toka kwa baba yake tokakwa mashekhe wake kuwa alisema: “Sikuwa naandika cho-chote katika Hadithi yake baada ya kunibainikia jambo lake.”

Ad-Dauriyu amesema toka kwa Ibnu Muini kuwa: Si chochote.

Abu Hatim amesema: Yazid ibnu Haruna aliuliza kuhusu yeye,akasema: “Msiulize kuhusu mambo.”Amr bin Ali amesema: “Ni dhaifu.”

Abu Hatimu amesema: Hadithi zake hukanushwa sana,anasimulia toka kwa waaminifu mambo yasiyokubalika. Mpaka akasema: An-Nasai amesema: ‘Hadithi zake huachwa.’Mara nyingine akasema: “Si mwaminifu.”20

21

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 21

Ama hoja ya Hadithi: Kwa sababu huenda Hadithi hii ni pichanyingine ya Hadithi ya kwanza, na tofauti ni kuwa Hadithi yakwanza ina nyongeza isiyokuwepo kwenye Hadithi hii, kwanikatika sura ya kwanza imesemwa kuwa alijifunika nguo yakekisha akaweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wakushoto.

Tayari imeshapita kuwa dhahiri ya Hadithi ni kuwa Mtumealikusanya pande za nguo zake akajifunikia kifua chake naakaweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto ilinguo yake isifunuke bali ibakie imegusana na mwili naajikingie mwili wake dhidi ya baridi.

Hivyo kwa kuwa anuani ya kitendo haijulikani Hadithi hiihaiwi hoja kwani haijulikani ni kwa nini alifanya hivyo.

Pamoja na hayo ni kuwa ndani ya Hadithi hii kuna ushahidiunaothibitisha kuwa kitendo cha kufunga mikono hakikuwakinajulikana kipindi cha mwanzo, kwa sababu ndani ya Hadithiimekuja kauli: “Nilimuona Al-Qamah akifanya hivyo.”

Hivyo laiti kufunga mikono ingekuwa ni jambo lililoenea katiya maswahaba na waliokuja baada ya maswahaba basi

22

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

20 Tahdhibul-Tahdhibu: 5/174, namba 298.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 22

kusingekuwepo na kigezo cha kunasibisha kitendo hiki kili-choenea kwa Al-Qamah mpokezi wa Hadithi toka kwa Wailu.

Na hii inaonyesha kuwa kufunga mkono ilikuwa ni jambolisiloenea na ndio maana Al-Qamah akalinukuu.

Sura ya tatu ya HadithiAn-Nasai ametoa kwa njia yake toka kwa Wailu bin Hajarkuwa alisema: Nikasema: Hapana….. Kwenye Sala ya Mtumewa Mwenyezi Mungu jinsi anavyoswali na nikamtazama.Akasimama akatoa takbira na akainua mikono yake mpakaikalingana na masikio yake, kisha akaweka mkono wake wakulia juu ya kiganja chake cha kushoto na fundo lake na muun-di. 21

Al-Bayhaqi naye ametoa ndani ya kitabu chake kwa tamko hilo

hilo.22

Kutumia riwaya hii kama hoja kunategemea usahihi wa njia yaupokezi na hoja yake.

23

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

21Sunanun-Nasaiy :2/97, mlango wa kuweka mkono wa kuliakwenye mkono wa kushoto ndani ya Sala.22 Al-Bayhaqi: 2/ 28, mlango wa kuweka mkono wa kulia juu yamkono wa kushoto ndani ya Sala.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 23

Ama kuhusu njia ya upokezi wa An-Nasai, ni kuwa njia hiyoimemjumuisha Aswimu bin Kulaybu Al-Kufiy. Ibnu Hajarametaja kuwa alimuuliza Ibnu Shahabu kuhusu dhehebu laKulaybu je alikuwa Mur’jia. Akasema: Sijui, lakini Shariku binAbdallah An-Nakhaiy amesema kuwa alikuwa Mur’jia.

Ibnu Al-Madainiy amesema: Hawi hoja akipokea peke yake.23

Ama njia ya Al-Bayhaqi yenyewe imemjumuisha Abdallah binRajau. Ibnu Hajar amenukuu toka kwa Ibnu Muini kuwa alise-ma: Alikuwa mwingi wa kukosea maneno, hana ubaya.

Amr bin Adiyu amesema: Ni mkweli, mwingi wa kuchanganyamaneno na kukosea, yeye si hoja, amefariki mwaka 219 au 220Hijiria. Na mkusudiwa hapa si Abdallah bin Rajau Al-Makiyuambaye hupokea toka kwa Imam Jafar Al-Sadiq (a.s.) nawengine.

Na hata kama tukijaalia mkusudiwa ni Abdallah bin Rajau Al-Makiyu bado hata yeye hajasalimika na dosari. Ibnu Hajaramenukuu toka kwa As-Sajiy kuwa alisema ana Hadithi zisi-zokubalika.

24

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

23 Tahdhibut-Tahdhibu:5/56 namba 89.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 24

Ahmad na Yahya wametofautiana kuhusu yeye. Ahmad amese-ma: Wamedai kuwa vitabu vyake vilitoweka hivyo akawaanaandika yale aliyoyahifadhi kichwani, na ana riwaya zisi-zokubalika, na wala sikusikia toka kwake isipokuwa Hadithimbili tu. Na maelezo kama haya kaeleza Al-Uqay’liyu tokakwa Ahmad.24

Ama hoja ya Hadithi ni kuwa hoja yake iko wazi kulikoHadithi mbili za mwanzo, na huenda vile vile ikawa Hadithi hiindio ile ile Hadithi ya mwanzo isipokuwa imenukuliwa kwanamna tofauti na hiyo tofauti inatoka kwa wapokezi.

Hivyo kwa kuwa huenda ikawa ndio ile ile Hadithi ya sura yakwanza basi umeshajua kuwa kitendo cha Mtume kinategeme-wa vigezo viwili (Ima kuzuwia nguo isifunuke au Sunna), nakwa ajili hiyo haiwi hoja.

Mpaka hapa umetimia uchambuzi kuhusu Hadithi mbili:

Ya kwanza: Hadithi ya Sahl As-Saidiyu.

Ya pili: Hadithi ya Wailu bin Hajar kwa sura tatu.Umeona upungufu wa hoja zake huku kukiwa na udhaifu kati-ka njia za upokezi wa Hadithi ya Wailu. Imebaki Hadithi ya

25

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

24 Tah’dhibut-Tah’dhibu: 5/211 namba 364

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 25

tatu wanayotumia kama dalili ya kufunga mikono kwenye Sala.

Hadithi ya Abdallah bin Mas’ud

An-Nasai ametoa toka kwa Al-Hujaju bin Abu Zainabu amese-ma: “Nilimsikia Abu Uthman akisimulia toka kwa Ibnu Mas’udalisema: Mtume aliniona nikiwa nimeweka mkono wa kushotojuu ya mkono wa kulia ndani ya Sala, basi akachukua mkonowangu wa kulia akauweka juu ya mkono wa kushoto.”25

Al-Bayhaqi naye kaitoa kwa tamko hili hili isipokuwa kwa njianyingine.

Kutumia Hadithi hii kama dalili kunategemea usahihi wa njiaya upokezi na hoja yake.

Ama kuhusu njia ya upokezi ni kuwa njia zote mbili zimemju-muisha Al-Hajaju bin Abu Zainabu As-Salmiy ambaye Ahmadbin Hambal amemzungumzia kwa kusema: Nahofia asiwe niyule mwenye Hadithi dhaifu.

Ibnu Muinu amesema: Hana ubaya.

26

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

25 Sunanun-Nasaiy: 2/97 mlango wa imamu atakapomuona mtukaweka mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 26

Hasani bin Shajau Al-Bal-khiy amesema toka kwa Ali bin Al-Madayniyu : Shekhe toka watu wa Wasitu ni dhaifu

An-Nasai amesema: Dhaifu.

Ibnu Ali amesema: Natarajia hana ubaya katika yale anayoy-apokea. Kisha akasema: Amesema Ad-Daruqutniy: “Ni dhaifuna wala si mwenye kuhifadhi.”26 Na mengine mengi.

Ama kuhusu hoja yake ni kuwa: Hebu angalia Abdallah binMas’ud alikuwa miongoni mwa watu waliotangulia kuingiandani ya Uislamu, alisilimu mwanzoni mwanzoni mwa utume,kwa ajili ya kumuamini kwake Mtume na Uislamu yakampatayaliyompata toka kwa Maquraishi. Hivi inawezekana mtukama huyu asijue namna ya kufunga mikono (ikiwa kama niSunna) hata aweke mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia.

27

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

26 Tah’dhibut-Tah’dhibu: 2/201 namba 372

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 27

Hadithi dhaifu zisizokuwa hoja

Hadithi tulizozitaja ndio tegemezi katika kutoa dalili yakuthibitisha kufunga mkono wa kulia juu ya mkono wakushoto. Tayari umeshajua hali zake na jinsi zisivyoweza kusi-mama kuthibitisha mada husika.

Kuna Hadithi nyingine na riwaya zilizopokewa ndani yavitabu, nazo kazikusanya Al-Bayhaqi ndani ya Sunan yake.Wala hakuna hata moja inayosihi kuwa dalili kutokana naudhaifu wa njia ya upokezi na hoja yake. Hivyo ili tukamilishevipengele vya uchambuzi tutazitoa hizo Hadithi na kuzicham-bua upande wa njia ya upokezi na hoja zake ili msomaji awezekujua sehemu zenye dosari.

1- Hadithi ya Hulbu

Tirmidhiy ametoa toka kwa Qutayba toka kwa Abul-ah’wasutoka kwa Sammaku bin Harbu toka kwa Qubaysatu bin Hulbutoka kwa baba yake amesema: “Mtume alikuwa akituswalishahivyo anachukua mkono wake wa kushoto kwa mkono wakewa kulia.”27

28

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

27 Sunanut-Tir-midhiy: 2/32, namba 252

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 28

Al-Bayhaqi ameipokea kwa tamko lingine, nalo ni: “NilimuonaMtume akiwa kaweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wakushoto ndani ya Sala.”28

Anajibiwa kuwa: Njia ya upokezi ni dhaifu kama ilivyo hojayake. Ama kuhusu njia ya upokezi angalia wasifu wa wapokeziwawili tu wa Hadithi hii:

Qubaysatu bin Hulbu

Ad-Dhahabi amesema: Al-Ajaliyu amesema: Ni mwaminifu,na Ibnu Hibana amemtaja katika orodha ya waaminifu.

Ibnu Al-Madainiyu amesema: “Hajulikani.” 29

Ibnu Hajar amesema: “Hajulikani, hakuna aliyepokea tokakwake isipokuwa Sammaku peke yake.”

An-Nasai amesema: “Hajulikani.” 30

29

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

28 Sunanul-Bayhaqiy: 2/2929 Mizanul-Itidali: 3/384 namba 686330 Tah’dhibut-Tah’dhibu: 8/350 namba 633

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 29

Sammaku Bin Harbu

Ad-Dhahabi amesema: Ni mkweli mno, mwema. IbnuMubarak amepokea toka kwa Sufiani kuwa ni dhaifu.

Jarir Ad-Dhabiyu amesema: “Nilikuja kwa Sammaku nika-muona akikojoa wima, hivyo nikarejea na wala sikumuuliza,nikasema: Ameharibikiwa akili.”

Ahmad bin Abu Mariam amepokea toka kwa Yahya: Sammakuni mwaminifu, Shaabatu alikuwa akimdhoofisha.

Ahmad amesema: “Sammaku ana Hadithi zenye dosari.”

Abu Hatimu amesema: “Ni mwaminifu, mkweli mno.”

Swaleh amesema: Amedhoofika.

An-Nasai amesema: “Akipokea peke yake hawi hoja, kwasababu alikuwa akisemezwa na anasema, na mengine zaidi yahayo miongoni mwa maneno ya kudhoofisha.”31

30

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

31 Mizanul-Itidali: 2/233 namba 3548.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 30

Ahmad amemzungumzia: “Ana Hadithi zenye dosari.”

Ibnu Abu Khaythamu amesema: “Nilimsikia Ibnu Muini aki-ulizwa kuhusu yeye, ni kitu gani kilichomtia dosari?”

Akasema: “Ameegemeza Hadithi ambazo hajaziegemezamwingine.”

Ibnu Ammara amesema: “Wanasema kuwa alikuwaakichanganya na wanatofautiana kuhusu Hadithi yake.”

At-Thauriyu alikuwa ikomdhoofisha katika baadhi ya dosari.

Yaqub bin Shayba amesema: “Nilimwambia Ibnu Al-Madainiyu: Vipi riwaya ya Sammaku toka kwa Akrimatu?Akasema: “Ina dosari”

Zakariya bin Ali amesema toka kwa Ibnu Mubarak: “Sammakuni dhaifu katika Hadithi.” Yaaqubu amesema: “Riwaya yakealiyohusika yeye peke yake toka kwa Akrima ina dosari.”32

Ama kuhusu hoja ya riwaya ni kuwa ndani ya riwaya hiyo hai-jatamkwa wazi kuwa ameweka mkono wake wa kulia juu yamkono wake wa kushoto katika hali ya kisomo tu, bali dhahiri

31

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

32 Tah’dhibut-Tah’dhibu: 8/350 namba 633

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 31

inayoonekana ni kuwa ameweka mkono wake wa kulia juu yamkono wake wa kushoto katika hali zake zote za Sala yake. Nahakuna aliyeshikamana na suala hilo.

2- Hadithi ya Muhammad bin Abana Al-Answariy

Al-Bayhaqi ametoa kwa njia yake toka kwa Muhammad binAbana Al-Answari toka kwa Aisha alisema: “Matatu ni kati yamambo ya unabii: Kuharakisha kufuturu, kuchelewesha dakuna kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto ndani yaSala.” 33

Aliyoyataja Bukhari ndani ya kitabu chake At-Tarikhul-Kabiruyanatosha kuonyesha udhaifu wa Hadithi hii. Baada yakunukuu Hadithi hii akasema: “Wala hatujui kusikia kwaMuhamad toka kwa Aisha.”

Katika nakala nyingine: “Wala haijulikani kusikia kwaMuhammad.” 34

Mtafiti wa kitabu At-Tarikhul-Kabiru cha Bukhari amenukuukuhusu kauli za baadhi ya wanazuoni wa fani ya elimu ya

32

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

33 Sunanul-Bayhaqiy: 2/2934 At-Tarikhul-Kabiru: 11/32 namba 47. Mizanul-Itidali: 3/454namba 7129.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 32

wapokezi kuhusu yeye, kisha akatoa matokeo kamili yafu-atayo:Hakika yeye ni Ansariyu mtu wa Madaniyu, kisha akawa mtuwa Al-Yamama, na yeye alivusha Hadithi toka kwa Aisha.35

3- Hadithi ya Aqabatu bin Sahbani

Al-Bayhaqi amepokea kwa njia yake toka kwa Hammadi binSal-matu toka kwa Asimu Al-Jahdariyu toka kwa Aqabatu binSahbani toka kwa Ali (a.s.) “Basi Swali kwa ajili ya Molawako, na uchinje”. Akasema: “Ni kuweka mkono wako wakulia juu ya mkono wako wa kushoto ndani ya Sala.”36

Anajibiwa kuhusu dalili hii kuwa: Kwanza: Asimu Al-Jahdariyu hajathibitishwa kuwa ni mwaminifu. Ad-Dhahabiamesema: Asimu bin Al-Ujaji Al-Jahdariyu Al-Basriyu ameso-ma kwa Yahya bin Yaamuru na Nasru bin Asimu. Salamu binAbu Al-Mundhiru na baadhi ya watu wamechukua toka kwakekisomo kilichokwenda kinyume chenye mambo yasiyo kubali-ka.37

33

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

35 At-Tarikhul-Kabiru: 11/3436 Sunanul-Bayhaqiy: 2/2937. Mizanul-Itidali: 2/354, namba 4057.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 33

Bukhari amemtaja ndani ya Historia yake akasema: Asimu Al-Jahdariyu anawekwa miongoni mwa watu wa Basra, toka kwaAqabatu bin Dhabiyanu na wala hajamthibitisha kuwa nimwaminifu38

Kisha kulingana na nukuu ya Al-Bayhaqi ni kuwa Hadithiinakomea kwa Aqabatu bin Sahbani. Al-Bayhaqi amesema: Naameipokea Bukhari ndani ya At-Tarikhu katika kutoa wasifuwa Aqabatu bin Dhabayani toka kwa Musa bin Ismaili tokakwa Hammadi bin Salmatu: Alimsikia Asimu Al-Jahdariyutoka kwa baba yake toka kwa kwa Aqabatu bin Dhabayani tokakwa Ali “Basi swali kwa ajili ya Mola na uchinje” akainuamkono wake wa kulia akauweka katikati ya muundi wake juuya kifua chake.

Kwa mujibu wa riwaya aliyoinukuu Al-Bayhaqi toka kwaBukhari ndani ya historia yake inatofautiana na ile aliyoipokeaAl-Bayhaqi yeye mwenyewe moja kwa moja, hiyo ni kwavigezo viwili:

Kwanza: Kwa riwaya ya Al-Bayhaqi njia ya upokezi waHadithi hiyo inakomea kwa Aqabatu bin Sahbani, na kwanukuu ya Bukhari inakomea kwa Aqabatu bin Dhabayani.Pili: Hakika kwa mujibu wa nukuu ya Al-Bayhaqi ni kuwa

34

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

38 At-Tarikhul-Kabiru: 6/486, namba 3061

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 34

Asimu Al-Jahdariyu amepokea toka kwa Aqabatu bin Sahbani,na kwa mujibu wa nukuu ya historia ya Bukhari ni kuwa Asimukanukuu toka kwa baba yake toka kwa Aqabatu bin Dhabayani.

Na bahati mbaya sana ni kuwa ndani ya vitabu vya fani yawapokezi hamna anuani ya Abu Aujaju. Hivyo Hadithi kamahii abadani haiwi hoja.

Hadithi ya Ghazuwani bin JarirAl-Bayhaqi amepokea toka kwa Ghazuwani bin Jarir toka kwababa yake amesema: Ali (a.s.) alikuwa akisimama kwenye Salana akatoa takbira huweka mkono wake wa kulia kwenye fundola mkono wake wa kushoto, hubakia katika chali hiyo mpakaanaporukuu, isipokuwa labda akune ngozi au aweke vizuringuo yake.39

Jarir mzazi wa Ghazawani hajulikani. Hiyo inatosha kud-hoofisha riwaya hii.

Ad-Dhahabi amesema: “Huyu Jariru Ad-Dhabiyu aliyepokeatoka kwa Ali na mwanae Ghazawani akapokea toka kwakehajulikani.”40

35

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

39 Sunanul-Bayhaqiy: 2/2940 Mizanul-Itidali: 1/397 namba 1474

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 35

Hadithi mbili za kuvushwa zaGhadhifu na Shadadu

Al-Bayhaqi amepokea akasema: “Tumepokea toka kwa Al-Harithu bin Ghadhifu Al-Kindi na Shadadu bin Shar’habilu Al-Ansari kuwa kila mmoja kati yao alimuona Mtume amefanyahivyo “Ameweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wakewa kushoto.”41

Haya ndio aliyoyapokea Al-Bayhaqi na Tirmidhi akaandikakwa namna ifuatayo: Ghatifu bin Al-Harithu.42

Kwa mujibu wa nukuu ya Al-Bayhaqi ni kuwa mpokezi ni Al-Harithu bin Ghadhifu Al-Kindi, ilihali kwa mujibu wa nukuuya Tirmidhiy mpokezi ni Ghadhifu bin Al-Harithu, hivyo babaakafananishwa na mtoto na hawajajulikana.

Kwa mujibu wa yale aliyonukuu Ibnu Hajar inaonekana kuwaalimdiriki Mtume akiwa mtoto. Ibnu Hajar amenukuu tokakwake akasema: “Nilikuwa mtoto nikipopoa mitende yaAnsari, wakanileta kwa Mtume, akapangusa kichwa changu na

36

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

41 Sunanul-Bayhaqiy: 2/2942 Sunanut Tirmidhiy: 2/32, Hadithi ya 252

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 36

kusema: ‘Kula zile zilizodondoka na wala usipopowe mitendeyao.”

Bali inaonekana toka kwa baadhi yao kuwa alikuwa miongonimwa waliokuja baada ya maswahaba na wala hajamdirikiMtume (s.a.w.w.).

Amesema: “Baadhi ya watu wamemtaja katika watu waliokujabaada ya maswahaba.”43

Hivyo kutokana na waliyoyataja tunapata muhtasari kuwaHadithi hii haiwi hoja, kwa sababu zifuatazo:

Kwanza: Ni Hadithi ya kuvushwa (Yaani mlolongo mzima wawapokezi haujatajwa), watu wa fani ya Hadithi hawana njiainayoelekea kwa hao wawili.

Pili: Alimdiriki Mtume akiwa bado mtoto, kwa ajili hiyo ndiomaana unaona wanamtambulisha kwa kusema: “Ana uswahi-ba” Yaani uswahiba mchache.

Tatu: Haijathibitika kuwa alikuwa ni swahaba, na kuna kundilimemuhesabu kuwa ni aliyekuja baada ya maswahaba.

37

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

43 Al-Isabatu: 3/186, namba 6912

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 37

Vyovyote vile ni kuwa hii ndio hali halisi ya Hadithi: Kwanzajina lake limechanganywa. Pili imechanganywa kati ya baba namtoto. Tatu kama ameishi na Mtume basi ni muda mchacheutotoni mwake. Nne haijathibitika kuwa aliishi na Mtume, balini miongoni mwa waliokuja baada ya Mtume. Haiwi hoja.

6- Hadithi ya nafiu toka kwa Ibnu Umar

Al-Bayhaqi ametoa kwa njia yake toka kwa Abdul-Majidi binAbdul-Azizi bin Abu Rawadu toka kwa baba yake toka kwaNafiu toka kwa Ibnu Umar kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisema:Sisi kundi la manabii tumeamrishwa mambo matatu:Kuharakisha kufuturu, kuchelewesha kula daku, na kuwekamkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto.

Hii ndio ile ile Hadithi aliyoipokea Muhammad bin Abana Al-Ansari toka kwa Aisha. Angalia namba mbili.

Al-Bayhaqi amesema: Abdul-Majid ameipokea peke yake, naanajulikana kwa jina la Talha bin Amr na yeye ni dhaifu.44

Ad-Dhahabi amemtambulisha kuwa ni mkweli mno na niMur’jiu kama baba yake.

38

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

44 Sunanul-Bayhaqiy: 2/29

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 38

Ibnu Muini amethibitisha uaminifu wake. Abu Daud amesema:Ni mwaminifu mwenye kulingania imani ya Ir’jai.

Ibnu Hibana amesema: “Anastahiki kuachwa, ana Hadithi zisi-zokubalika sana, hubadili habari na ananukuu toka kwawasimulizi mashuhuri riwaya zisizo kubalika.”

Abu Hatimu amesema: “Ni dhaifu, Hadithi yake huandikwa.”

Ad-Daru Qutniy amesema: “Hawi hoja na (wasimulizi) huwanaye makini. Ahmad bin Abu Mariam amesema toka kwa IbnuMuini kuwa: “Ni mkweli anapokea toka kwa watu madhaifu.”

Bukhari amesema: “Al-Humaidiyu alikuwa akimzungumzia,na pia akasema ndani ya Hadithi yake kuna baadhi ya tofauti,wala hazijulikani hata Hadithi tano sahihi toka kwake.”45

7-Hadithi ya Ibnu Jarir aDhabiy

Abu Daud ametoa toka kwa Jarir Dhabiyu toka kwa baba yakeamesema: “Nilimuona Ali (a.s.) ameshika mkono wake wakushoto kwa kutumia mkono wake wa kulia kwenye fundo lamkono juu ya kitovu.”

39

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

45Mizanul-Itidali: 2/648, namba 5183

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 39

Abu Daud amesema: “Imepokewa toka kwa Saidi bin Jubairu“Juu ya kitovu.” Abu Maj-lazu amesema: “Chini ya kitovu” naimepokewa toka kwa Abu Huraira kuwa ni dhaifu.46

Anajibiwa kuwa: Hakika Ibnu Jarir Dhabiyu ndio yule yuleGhazawani ibnu Jarir. Na tayari maneno yake kuhusu mzaziwake yameshatangulia, angalia namba nne. Na huenda Hadithihii ndio ile ile Hadithi iliyotangulia na wala si Hadithinyingine.

Ama Hadithi aliyopokea toka kwa Tausi amesema: Mtume waMwenyezi Mungu alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juuya mkono wake wa kushoto, kisha anaikaza kifuani kwake ili-hali akiwa ndani ya Sala47.

Yenyewe ni Hadithi ya kuvushwa kwa sababu Tausi ni mion-goni mwa watu waliokuja baada ya maswahaba.

Na kuna riwaya nyingine zimenasibishwa na Ibnu Zubeiri yakuwa alisema: Kuweka sawa nyayo mbili na kuweka mkono

40

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

46 Sunan Abu Daud: 1/201, mlango wa kuweka mono wa kulia juuya mkono wa kushoto ndani ya Sala, namba 757 na 759

47 Sunan Abu Daud: 1/201, mlango wa kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto ndani ya Sala, namba 757 na 759

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 40

juu ya mkono ni miongoni mwa Sunna.48

Kama alivyosema Abu Huraira: Alichukua kiganja akakiwekajuu ya kiganja ndani ya Sala chini ya kitovu.49

Maalum ni kuwa kauli ya sahaba si hoja iwapo haijatokana naMtume (s.a.w.w.).

Hivi sasa haki imedhihirika

Kutokana na uchambuzi wa mada hii yamebainika mamboyafuatayo:

Kwanza: Abu Humaidu As-Saidiyu ni kati ya walionukuu Salaya Mtume kwa vipengele vyake na wala hajataja chochotekuhusu kufunga mikono, na alinukuu namna ya Sala ya Mtumembele ya makumi ya maswahaba, na akapata usadikisho tokakwao.

Na wala kufunga mikono si jambo dogo mpaka mpokeziaghafilike nalo au maswahaba waliokuwepo waghafilike nalo.

41

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

48 Sunan Abu Daud: 1/200-221 namba 754 na 75849 Sunan Abu Daud: 1/200-221, namba 754 na 758.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 41

Hivyo laiti kama Sala ya Mtume ingekuwa ilikuwa na kitendocha kufunga mikono basi wangemkosoa na kumlaumu kwakuacha kukitaja.

Pili: Hadithi walizotoa kama dalili ya kuthibitisha kuwa kufun-ga mikono ndani ya Sala ni Sunna, Hadithi hizo nyingine hojayake ni dhaifu na nyingine njia ya upokezi wake ni dhaifu au nidhaifu vyote viwili.

Tatu: Laiti kufunga mikono ingekuwa ni Sunna basi Maimamwa Ahlul-Bayt wote wasingeipinga na kuihesabu kuwa nimwenendo wa Majusi, hiyo ni kama utakavyoona ndani yariwaya zao.

Nne: Jambo hili linazunguka kati ya bidaa na Sunna, na kwakanuni ya tahadhari ni kuacha kufunga mikono, kwa sababukutenda suala hilo huenda ikawa ni haramu na ni kutendabidaa. Kinyume na kuacha, kwani katika kuacha hutokua ume-fanya chochote bali utakuwa umeacha jambo la Sunna tu, nawala haijakatazwa kuacha Sunna.

Tano: Wanachostaajabisha wanazuoni wa fiq’hi wa Kisunni nikuwa wamegonga milango yote (Katika kutaka kujua ukweliwa jambo hili) isipokuwa mlango wa Ahlul-Bait!

42

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 42

Hadithi za Ahlul-BaytHakika Maimam wa Ahlul-Bayt walikuwa wakijizuia kufungamikono huku wakiona kuwa kitendo hicho ni kitendo chawaabudu moto wa Irani ya zamani mbele ya mfalme wao.

Muhammad bin Muslim amepokea toka kwa As-Sadiq au Al-Baqir (a.s.) amesema: “Nikamwambia: Vipi mtu anayewekamkono wake ndani ya Sala – na imeelezwa- mkono wa kuliajuu ya mkono wa kushoto?” Akasema: “Kufanya hivyo nikuwatukuza wafalme wa kifarisayo, (haifanywi ndani yaUislamu)50.

Zararatu amepokea toka kwa Abu Jafar (a.s.) kuwa alisema:“Ni wajibu juu yako kuielekea Sala yako na wala usitukuzewafalme wa kifarisayo, hakika hilo hufanywa na majusi.”51m

As-Suduq amepokea kwa njia yake toka kwa Ali (a.s.) kuwaalisema: “Ni wajibu juu yako kuielekea Sala yako na wala usi-tukuze wafalme wa kifarisayo, hakika hilo hufanywa namajusi.”

43

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

50. Al-Wassailu: 4 mlango wa 15 Hadithi ya 1 mlango wa vikatizaSala.51 Al-Wassailu: 4 mlango wa 15 Hadithi ya 2 na 3 na 7 mlango wavikatiza Sala.

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 43

As-Suduq amepokea kwa njia yake toka kwa Ali (a.s.) kuwaalisema: “Muislamu hakusanyi mikono yake ndani ya Salayake ilihali yeye kasimama mbele ya Allah Mtukufu akiji-fanananisha na watukuza wafalme - yaani majusi.”52

Na mwisho hebu tugeuze mtazamo wa msomaji kwa kuangaliamaneno yaliyotoka kwa Dr. Ali As-Salusi. Yeye baada yakunukuu mtazamo wa wanazuoni wa fiq’hi wa makundi yotemawili, aliwasifia wanaosema kuwa ni batili na haramu akase-ma: “Na hao waliona kuwa ni haramu na batili au haramu tu, haowanaonyesha chuki ya kimadhehebu na kupenda tofauti kwaajili ya kuwafarakisha Waisilamu.”53

Ni ipi dhambi ya Shia iwapo juhudi za kielimu na utafiti waKitabu na Sunnah umewaongoza kujua kuwa kufunga mikononi jambo lililozushwa baada ya Mtukufu Mtume, na watuwalikuwa wakiamrishwa kufanya hivyo zama za makhalifa.

44

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

52 Al-Wassailu: 4 mlango wa 15 Hadithi ya 2 na 3 na 7 mlan-go wa vikatiza Sala.

53 Fiqhi Shiatu Imamiyatu sehemu ya tofauti kati yake naMadhehebu manne:183

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 44

Atakayedai kuwa ni sehemu ya Sala kwa kuwa ni faradhi auSunna atakuwa amepandikiza ndani ya dini jambo lisilokuwe-mo. Je hivi malipo ya aliyetumia juhudi za kielimu ni kushutu-miwa kuwa ana chuki za kimadhehebu na kupendamfarakano?!

Na kama hilo ni sahihi, hivi inasihi kumnasibisha Imam Malikna sifa hiyo? Kwa sababu yeye alikuwa akichukia kufungamikono kwa namna yoyote ile. Hata tukijaalia kuwa ni sahihije, inasihi kumshutumu Imam wa Madina kuwa yeye alikuwaakipenda mfarakano?!

Naam, enyi viumbe kwa nini kutokunyoosha mikono na kui-funga hakuwi ni kuonyesha chuki ya kimadhehebu na kupendamfarakano kati ya Waisilamu?!

Imetafsiriwa na:Hemedi Lubumba Selemeni.

Simu: 0773-0171780715-0171780754-017178

45

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 45

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NAAL-ITRAH FOUNDATION:

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanzampaka kumi na sita

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Sala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

46

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 46

21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua kwa mujibu wa Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mtazamo wa Qur’an na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa

Mtazamo wa Qur’ani na Sunna43. Kupaka juu ya khofu

47

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 47

BACK COVER

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna?

Kufunga mikono katika Sala:Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kilajambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompatamwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyoMwenyezi Mungu akasema:

"Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neemaYangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (5:3).

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoniwa sheria wamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwaokuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jamboambalo limesababisha kutofautiana kuhusu masuala madodomadogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katikamtiririko wa masomo haya mwandishi amejaribu kuliweka salahili juu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia yakuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu.

48

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 48

Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hataisababishe kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo nikuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogoukilinganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati yamadhehebu za Kiislamu. Na mwongozo wetu katika njia hii nikauli ya Mwenyezi Mungu:

"Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyotewala msifarakiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Munguiliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyozenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu." (3:103)

Kimetolewa na kuchapishwa na:Al-Itrah Foundation P.O. Box 19701,Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Fax: +255 22 2131036Email: [email protected]

49

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

kufunga mikono.qxd 7/2/2011 10:40 AM Page 49