9
Somo la 11 kwa ajili ya Septemba 14, 2019

Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

  • Upload
    others

  • View
    2

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

Somo la 11 kwa ajili ya Septemba 14, 2019

Page 2: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

“Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.” (1 Wakorintho 15:19).

Kama wakristo, macho yetu yamewekwa nje ya mipaka ya maisha. Tunasubiri ujio wa pili wa Yesu na ufufuo wa wafu. Tunasubiri pia haki ya Mungu na ulimwengu ulio bora.

Tumaini hili linatuhamasisha kuliishi na kutenda itupasavyo.

Page 3: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

“BWANA hata lini wasio haki, hata lini wasio haki

watashangilia?” (Zaburi 94:3)

Pale watu watu wa Mungu wanapokuwa wamezungukwa na kandamizaji na udhalimu, wanamlilia Mungu wakisema: “Hata lini?”

Hata lini wangewekwa huru dhidi ya Wamisri? Hata lini wangewekwa huru dhidi ya Babeli? Hata lini wangewekwa huru dhidi ya Rumi? “Hata lini, kutohukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?” (Ufunuo 6:10).

Daima Mungu amekuwa akiingilia kati. Hata hivyo, bado wananyanyaswa na kufanyiwa udhalimu. Hata lini?

Bado tunasubiri haki ya Mungu na kuulilia wakati atakapokomesha uovu (Luka 18:1-8).

Page 4: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

“Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia

tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.” (Tito 2:12-13)

Yesu atakomesha umaskini na unyanyasaji. Kwahiyo, watu wengine hufikiria kuwa hakuna haja ya kupambana nao sasa.

Mungu ametutaka tuishi kwa haki katika ulimwengu huu. Kazi yetu ni kuwajali wenye uhitaji na kuwapatia mahitaji kulingana na uwezo wetu.

Kama tunaenda kuishi na Yesu milele, basi tuanze leo tuishi kama yeye alivyoishi, (Matendo 10:38).

Page 5: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

Kulingana na Mathayo 24-25, ni kwa namna gani tuishi wakati tunamsubiri Yesu arudi tena?

Msitishwe (Mathayo 24:6)

Msikwazane, kusalitiana wala kuchukia (aya. 10)

Kuwa na upendo wa kweli (aya. 12)

Kuvumili hata mwisho (aya. 13)

Kuhubiri injili (aya. 14)

Kuomba (aya. 20)

Kutowaamini makristo wa uongo na manabii wa uongo (aya. 23-24)

Kuwa na utambuzi (aya. 32-33)

Kuwa tayari daima (aya. 42-43; 25:13)

Kuwa waaminifu na tahadhari (aya. 45-46)

Kutowatendea wengine vibaya, wala kuandamana na wtendao uovu (v. 48-51)

Kujazwa mioyo yetu kwa Roho Mtakatifu (Mathayo 25:1-12)

Kufanya kazikwa bidii (aya. 14-30)

Kuwapa chakula wenye njaa na kuwakaribisha wageni (aya. 35)

Kuwavika walio uchi, kuwaona wagonjwa na walio kifungoni (aya. 36)

Page 6: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

Ufufuo wa Yesu ndiyo msingi wa tumaini letu (1Kor. 15:12-19). Kama Yesu asingelifufuka…

Ufufuo wa Yesu ndiyo uhakikisho aa ufufuo wetu. Mauti itaharibiwa kwa wema. Uovu unaosababisha dhuluma, umaskini na unyanyasaji utaharibiwa.

Hebu tuwasaidie wengine kwa kuwashirikisha tumaini la ufufuo.

Page 7: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

Bila tumaini la haki, bila tumaini la hukumu, bila tumaini la mambo kufanywa mema, matumaini yetu hakika yangelikuwa ulimwengu wa ujinga.

Kuna tumaini: “Mungu ataleta hukumuni kila kazi.” (Mhubiri 12:14)

Udhalimu katika ulimwengu huu hautasahauliwa. Siku moja, Yesu atayaweka mambo sawa. “Atamlipa kila mtu kwa kadri ya matendo yake.” (Mathayo 16:27)

Hii ni habari njema kwa wale wanaoumizwa na udhalimu leo.

Page 8: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

ULIMWENGU BORA UJAO

“Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” (Ufunuo 21:4)

Ulimwengu ulioahidiwa siyo kama tunaoishi leo. Hakutakuwa na kifo, machozi, kulia, umaskini, dhuluma, maumivu wala hofu.

Mungu atayafuta machozi yett na kutufariji. Atayaponya majeraha yaliyosababishwa na maumivu (Ufunuo 22:2).

Tunautarajia ulimwengu ulio bora kwa kutoa maneno ya wema, chakula kizuri, msaada wa matibabu, nguo au ushauri wa busara.

Hebu tuonyeshe upendo mzuri aliouonyesha Yesu alipokuwa akiishi duniani. Upendo huo huo atauonyesha atakapomfuta machozi kila mmoja wetu.

Page 9: Chidzidzo11 chaGunyana14, 2019 wedu mukuru noMuponesi, Jesu Kristu.” (Tito 2:12-13) Jesu uchagumisa urombo nekudzvinyirira. Nokudaro,vamwe vanhu vanogona kufunga kuti hazvina maturo

“Shikilia sana faraja, imani, tumaini ambavyo

Mungu amekupatia katika Neno Lake.

Usikatishwe tamaa kamwe… Inatupasa

‘kushikilia’ na kuishi kwa nuru yote tuliyoipokea

kutoka mbinguni. Kwanini?—Kwasababu Mungu

anatutaka tuupate ukweli wa umilele, na

kutenda kama mkono wake wa msaada kwa

kuwasilisha nuru kwa wale ambao hawajafikia

na habari yaupendo wake…

Ni lazima tuwe macho kwa ujio wa Bwana… kila

wakati ni lazima ufanyiwe kazi kwa uaminifu.” E.G.W. (Sons and Daughters of God, December 10)