19
ISSN 5618 - N0. 009 BEI: SH800/- KSH80/- USH1,200/- 21 SHAABAN 1436, JUMATATU, JUNI 8 - 14, 2015 www.islamicftz.org huwatoa watu gizani Usalafi usiwagawe Wanasunnah - Uk 9 SHEIKH AL-AMIN MAZRUI: Mwana mageuzi nguli katika Uislamu - Uk 7 Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, Tanzania Tell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected] Masheikh 7 wa uamsho watupwa selo ya adhabu UK. 3 Hijab, uarabu vyamnyima kitambulisho cha taifa NA MWANDISHI WETU M ke wa Sheikh mmoja mashuhuri wa kisunnah hapa jijini Dar es Salaam amenyimwa kitambul- isho cha uraia kwa kuhisiwa kuwa sio raia kwa sababu ya asili yake ya uara- bu. Mama huyo ambaye ni mtanzania halisi alinyimwa kitambulisho yeye na mtoto wake mmoja huku maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (NIDA) wakimwambia itabidi aanze mchakato upya. Mama huyo ambaye asili yake ni Tanga aliambiwa na afisa mmoja wa NIDA kuwa kita- INAENDELEA UK 5 Waislam wadai marekebisho MUSWADA WA HABARI

Imaan Newspaper issue 9

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Imaan Newspaper issue 9

Citation preview

ISSN 5618 - N0. 009 BEI: Sh800/- KSh80/- USh1,200/- 21 ShaaBaN 1436, JUmatatU, JUNI 8 - 14, 2015 www.islamicftz.org

huwatoa watu gizani

Usalafi usiwagawe Wanasunnah - Uk 9

Sheikh Al-Amin mAzrui: Mwana mageuzi nguli katika Uislamu - Uk 7

Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: [email protected]

Masheikh 7 wa uamsho watupwa selo ya adhabuUK. 3

Hijab, uarabu vyamnyima kitambulisho cha taifaNa MwaNdishi wetu

Mke wa Sheikh mmoja mashuhuri wa kisunnah hapa jijini Dar es Salaam amenyimwa kitambul-

isho cha uraia kwa kuhisiwa kuwa sio raia kwa sababu ya asili yake ya uara-bu.

Mama huyo ambaye ni mtanzania halisi alinyimwa kitambulisho yeye na mtoto wake mmoja huku maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (NIDA) wakimwambia itabidi aanze mchakato upya.

Mama huyo ambaye asili yake ni Tanga aliambiwa na afisa mmoja wa NIDA kuwa kita- INaENdElEa UK 5

Waislam wadai marekebishomuswada wa habari

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

2 Habari / tangazo

Na Khalid OMary

Vyombo vya habari vya Kiislam vimezidi kuongezeka baada ya kuzinduliwa kwa gazeti jipya la Iqra, (Hoja kwanza), Ijumaa iliy-

opita katika msikiti wa Mtambani, Kinon-doni jijini Dar es salaam.

Wakizungumza katika uzinduzi huo Imam wa msikiti wa Mtambani, Sheikh Suleiman Abdallah aliishukuru bodi ya Iqra Media kwa kufanya uzinduzi katika msikiti wake na kusema, kwa sasa Waislam wataen-delea kupata habari na elimu kupitia vyo-mbo vya Kiislam vinavyoongezeka kwa kasi.

“Tulikuwa na kilio katika suala la elimu, tunafurahi tumepiga hatua kubwa kwa kuzinduliwa kwa gazeti hili (Iqra). Tunatu-mai tutapata elimu kubwa”, alisema Sheikh Abdallah.

Naye, Mwenyekiti wa bodi ya Iqra Me-dia, Bilal Abdul-aziz amewataka Waislam

waweze kuviunga mkono vyombo vya Kiis-lam, kwani hakuna asiyekuwa Muislam atakaeweza kutoa msaada zaidi ya wao wenyewe.

Abul-aziz alisema: “Vyombo vya habari vya Kiislam vimekuwa na muamko mkubwa hasa baada ya kujitokeza kwa re-dio Imaan, tunahitaji ushirikiano kutoka kwa Waislam ili tuweze kufika mbali”.

Kwa upande wake, Sheikh Nurdin Kishk, mdau mwingine wa gazeti hilo, amewataka Waislam wasome fani ya habari, kwa saba-bu wengi wa wanaosoma fani hiyo si Wais-lam na ndiyo maana Uislam unachafuliwa na vyombo vya habari ulimwenguni.

Gazeti la Iqra linatolewa na Iqra Media, litakuwa likitoka kila Ijumaa kwa bei ya shilingi 800 likisheheni habari na makala za dini ya Kiislam na jamii kwa ujumla zina-zoandaliwa na masheikh mbalimbali pamo-ja na wanahabari wenye uzoefu.

gazeti jipya la kiislamu lazinduliwa

Yatima walelewe majumbani - Mkuu MuMNa MwaNdishi wetu

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waisla-mu Morogoro (MUM), Hajat Mwantumu Malale ametaka Waislamu waendelee na utarati-

bu wa zamani wa kulea yatima majumbani chini ya usimamizi wa ndugu wa karibu, jam-bo ambalo litawasaidia kutohisi uyatima wao.

Hajat Malale ametoa wito huo, hivi karibu-ni alipokuwa akizungumza katika konga-mano lililofanyika ukumbi wa DIT, jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na taasisi ya Wa-nawake wa Kiislamu inayojishughulisha na kusaidia kuboresha maisha ya watoto yatima wa majumbani (TAQWA).

Hajat Malale alikuwa ni mgeni rasmi kati-

ka kongamano hilo, ambapo alihimiza Wais-lamu kushiriki katika mpango wa kusaidia watoto yatima wa majumbani unaoendeshwa na taasisi hiyo.

Mpango wa kusaidia watoto wa mitaani walio majumbani ulianzishwa mwaka 2011, mwaka ambao taasisi hiyo pia ilianzishwa. Katika mpango huo, TAQWA ilipita majum-bani kuwasajili watoto na kuanza kuwasaidia kielimu na kiafya, wakiwa wanalelewa na jamaa zao.

Baada ya kuwasajili watoto hao, TAQWA inatafuta mdhamini ambaye atakuwa anatoa shilingi 55,000 kila mwezi kwa ajili ya kum-hudumia mtoto mpaka amalize elimu ya msingi, huku fedha hizo zikitumika kumlipia ada, kununulia sare za shule, chakula, vitabu

na vifaa vingine vya shule.Hajat Malale alisema: ”Unaweza

kuona kumchangia mtoto yatima 55,000 ni nyingi, lakini mbona mna-toa fedha nyingi kuchangia ’kitchen party’ na ’send off ’ na kununua nguo za gharama bila kukumbuka kuwa hiyo hela ukimpa yatima futari au kum-somesha ni amali yako itakayokuokoa kesho akhera”.

Naye Mkurugenzi wa TAQWA, Dr.Salha Mohammed, alisema uchun-guzi uliofanywa na taasisi yake un-aonesha kuwa, watoto yatima wa-naolelewa vituoni wanaathirika ki-saikolojia na kujiona kama wapo jela ya watoto, kwa sababu hawapati mapenzi ya mama, kwani mama mmo-ja anayeendesha kituo hicho hawezi kuhudumia na kuonesha mapenzi kwa

watoto wengi. Akizungumzia mafani-kio ya taasisi tangu TAQWA ianzishwe, Hajat Salha alisema, walianza na wad-hamini 11 mwaka 2011, lakini mpaka sasa wameongezeka hadi 68 wakihu-dumia watoto 108. Pia alisema, TAQWA inatarajia kuanzisha mpango wa kuwadhamini watoto yatima wal-ioko sekondari.

Kwa upande wake Ukhti Khadija Ally amesema, Quran na Sunnah za Mtume zimehimiza kulea yatima akinukuu Qur’an (93:9).

”Tukumbuke Mtume wetu Mu-hammad alikuwa yatima baada ya ku-fiwa na baba na mama yake katika umri mdogo, na hakuwahi kulelewa kwenye kituo, na ndio maana tuna-himiza watoto yatima tuwalee majum-bani mwetu”. Alisema Ukhti Khadija.

Ili kufanikisha toleo hilo maa-lum, tunakari-bisha ushiriki

wa watu binaf-si, taasisi, kam-puni, balozi na

misikiti mbalimbali kwa kutoa

makala na ma-tangazo.

TOLEO MAALUM:

Kwa mawasiliano zaidi, tupigie:0786 779 669, 0778 559 944

Email: [email protected]

Gazeti lako la Imaan, Ijumaa ya Juni 12, 2015 litachapisha toleo maalum la Mwezi Mtukufu wa Ramadhan litakalochambua

mafundisho na masuala mbali mbali kuhusiana na Ramadhan.

nyakatI za sWalaNa. mJI alFaJR dhUhUR aSR maGhaRIB ISha 1 DaR ES SaLaaM 11:16 6:22 9:44 12:15 1:25 2 zanzIBaR 11:15 6:22 9:45 12:16 1:26 3 tanGa 11:17 6:26 9:49 12:22 1:32 4 MOROGORO 11:27 6:40 9:52 12:22 1:32 5 MtWaRa 11:23 6:23 9:42 12:09 1:20 6 aRUSHa 11:22 6:35 10:00 12:34 1:44 7 DODOMa 11:27 6:35 9:58 12:29 1:39 8 MBEya 11:43 6:47 10:08 12:37 1:47 9 kIGOMa 11:50 6:59 10:22 12:55 2:05 10 MWanza 11:34 6:48 10:12 12:47 1:57 11 kaGERa 11:46 6:57 10:20 12:53 2:03 12 taBORa 11:39 6:48 10:11 12:43 1:53 13 SHInyanGa 11:36 6:47 10:11 12:45 1:55 14 SInGIDa 11:33 6:41 10:04 12:36 1:46 15 IRInGa 11:36 6:39 9:59 12:28 1:38

08 juNi - 14 juNi, 2015

Na bahati chuMe

Amiri wa Jukwaa la Vijana wa Kiis-lamu Mkoa wa Kilimanjaro, Ab-dalah Muhammed amewakum-busha Waislamu Mkoani Kili-

manjaro kujitokeza kwa wingi kujiandisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura pindi muda utakapo wadia.

Akizungumza na waandishi wa habari,

Muhammed alisema ili vijana wapate frusa ya kupiga kura na kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu wa madiwani, wabunge na rais ni lazima kujiandikisha katika daftari kama wapiga kura. Alisema Waislamu wame-kuwa wakipuuza jambo hilo na kwamba hiyo ni hatari kwani wanapoteza haki zao kama watanzania.

amiri wa Vijana K’njaro ahimiza kujiandikisha kupiga kura

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

3

Na MwaNdishi wetu

Uongozi wa gereza la Seg-erea umeamuru watuhu-miwa saba (7) wa ugaidi wa Jumuiya ya Uamsho

na Mihadhara ya Kiislam ya Zanzi-bar (JUMIKI) kutupwa katika ma-habusu maalum ya adhabu kwa kosa la kugoma kula.

Uamuzi wa kuwapeleka watuhu-miwa hao selo maalum ya adhabu ulichukuliwa na uongozi wa gereza hilo baada ya pande hizo mbili kushindwa kuafikiana katika mku-tano ulioandaliwa ili kupata suluhu ya mgomo wa kula, ambao masheikh hao waliuanza wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Ally Mbaruku, Katibu wa Kamati ya Maafa, Shura ya Maimamu (T), katika kikao hi-cho, maaafisa wa gereza hilo walijar-ibu kuwashawishi masheikh hao

kuacha mgomo wakiwahakikishia kuwa madai yao yanaendelea kushu-ghulikiwa, lakini masheikh hao wa-likataa.

Kwa mujibu wa Mbaruku, am-baye aliwatembelea masheikh hao huko gererani na kuonana na Sheikh Farid Hadi siku ya Ijumaa, alisema masheikh waliwaambia viongozi wa magereza kuwa, hawaoni dalili za madai yao kushughulikiwa na kwamba msimamo wao wa kuende-lea kugoma upo pale.

Hapo ndipo uongozi wa magere-za ulipoamua kuwapeleka selo ya adhabu, ambapo Sheikh Farid Hadi na Mselem Ally wamewataka Wais-lam kuzidisha dua kuwaombea masheikh hao.

Gazeti la Imaan lilipowatafuta mawakili wa masheikh hao, Abdal-lah Juma, Abdulfatah Ali na Abu-bakar Salum walithibitisha kusikia taarifa hizo kupitia njia ya ujumbe mfupi na kwamba wanatarajia kuli-fuatilia suala hilo na kulitolea ufa-

fanuzi wake baada ya kuonana na wateja wao siku ya Jumatatu ya Juni 8 katika mahaka-ma ya kisutu ambako kesi yao itata-jwa tena.

Naye, Mkuu wa Gereza la Segelea, Afande Kiyangi Abdallah, alipopigi-wa hakuwa tayari kutoa ushirikiano uliotarajiwa, akidai kuwa yeye si msemaji wa Jeshi hilo.

Akizungumzia sakata hilo katika mtazamo wa kisheria, wakili wa ku-jitegemea Juma Nassoro alisema,

kitendo cha masheikh hao kugoma kula na kunywa kisheria si makosa ambayo unaweza kuhojiwa mahaka-mani.

Wakili Juma Nassoro aliongeza kuwa, kitendo cha kususia kula na kunywa ni jitihada za masheikh hao kuonesha hisia zao kwa ulimwengu juu ya vitendo wanavyofanyiwa na kwamba ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe ili hatua ziweze kuchukuli-wa.

“Kugoma kula na kunywa si kosa kisheria, ni haki ya mtu kujieleza juu ya matatizo yanayowasumbua huko gerezani. Ni kama wanaonesha hisia zao kwa ulimwengu juu ya uonevu wanaofanyiwa ili hatua ziweze ku-chukuliwa” , Wakili Nassoro alise-ma.

Hata hivyo, wakili huyo alisema kwa taratibu na kanuni za uende-shaji za magereza, kugoma kula na kunywa inaweza kuwa ni kosa na kwamba adhabu yake huenda mtu akabadilishiwa gereza, lakini hawezi kushitakiwa mahakamani.

Masheikh wa uamsho walianza mgomo wa pili wa kususia kula na kunywa katikati ya wiki iliyopita wakishinikiza madai yao kwa seri-kali yapatiwe ufumbuzi mapema ili kuondokana na adha wanayoipata.

Masheikh hao wamekuwa waki-lalaamika kesi yao kupigwa danad-ana, ambapo mpaka sasa tayari masheikh wapatao 23 wameshakaa gerezani takriban mwaka mmoja bila ya kesi zao kupiga hatua ya maa-na.

Waislamu hao pia wanapinga kushtakiwa upande wa Tanzania bara, wakati makosa yao yalitendeka katika ardhi ya Zanzibar. Wanadai kesi hiyo irudishwe Zanzibar, kwani Zanzibar ni nchi ambayo ina ma-hakama, magereza kama ilivyo Bara.

Mbali na madai hayo, pia masheikh hao wanadai kutaka kukutana na wanasheria wakuu wa Tanzania bara na Zanzibar ili kusiki-lizwa kilio chao, hadi sasa madai hayajatimizwa. Pia masheikh hao wamelalamikia mateso wanayoyap-ata gerezani, ambapo wiki iliyopita walimwandikia Waziri Mkuu, Mi-zengo Pinda kumuomba awasaidie.

Baadhi ya viongozi na wafuasi wa Uamsho wakiwa mahakamani.

Habari

kitendo cha kususia kula na kunywa ni jitihada za masheikh hao kuonesha

hisia zao kwa ulimwengu juu ya vitendo wanavyofanyiwa na kwamba ni njia nzuri

ya kufikisha ujumbe ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Masheikh 7 wa uamsho watupwa selo ya adhabu

Khalid OMary Na seleMaNi MaGali

Waislam nchini wamei-taka serikali kuacha kubana uhuru wa ku-toa na kupokea habari

kwa kutunga sheria kali zinazokan-damiza uhuru huo, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Masheikh na wamiliki wa vyo-mbo vya habari vya Kiislam wameli-ambia gazeti hili kuwa, muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa 2015 ni kandamizi na unapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehma na

amani ziwe juu yake).Mwenyekiti wa taasisi ya The Is-

lamic Foundation inayomiliki vyo-mbo vya habari vya gazeti Imaan, radio na Tv Imaan, Aref Nahdi, amesema mswada huo unabana haki za msingi za raia za kutoa, kupokea na kusambaza taarifa pamoja na kuingilia sera za ndani za vyombo mbalimbali vya habari.

Nahdi alisema, vyombo vya habari vya Kiislam vitaathirika zaidi kwa sababu pamoja na kuzingatia sheria za nchi, vinatoa habari kwa misingi ya dini ya Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume Muham-mad (Rehma na amani ziwe juu yake), na si vinginevyo.

Nahdi alikuwa akirejea ibara ya

14(b)(iv) ya mswada huo inayotaka vyombo vya habari vya utangazaji (runinga na radio), kujiunga na kituo cha runinga cha taifa na kile cha radio kwa ajili ya taarifa ya habari kila siku ifikapo saa 2 usiku.

Nahdi alisema: “Vyombo vyetu sisi Waislam vinazingatia maadili maalum kwa mujibu maagizo ya Al-lah”. Akitoa mfano, alisema ni hara-mu na mwiko mkubwa kwa vyombo vya habari vya Kiislam kuonesha watu wamevaa hovyo, sherehe za ngoma, matangazo ya pombe na riba.

“Kwetu vitu hivyo ni haramu. Muswada huu utatuletea madhara na ni kinyume na dini yetu, na kama ukipita utatunyima haki yetu ya

msingi ya kikatiba ya kuabudu”, al-iongeza Nahdi.

Kwa upande wake, Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tan-zania, Sheikh Rajab Katimba alise-ma, serikali inataka kurudisha nyu-ma maendeleo na kuipeleka Tanza-nia miaka ya 70 na 80 ambako vyo-mbo pekee vya habari vilikuwa ni vya serikali, chama tawala na jumui-ya zake.

Sheikh Katimba alisema: “Vyo-mbo vya habari katika kipindi kama hiki ni lazima viachwe huru vifanye kazi yake na kwamba kuwadhibiti wanahabari ni kinyume na kanuni za kidemokrasia.”

Naye mchambuzi wa masuala ya siasa katika Shirika la Utangazaji la

Uingereza, (BBC) Sheikh Muham-mad Issa, amepinga muswada huo kwa sababu unafinya uhuru wa ku-jieleza kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano inavyoelekeza.

Mchambuzi huyo aliongeza kwa kusema, kupitishwa kwa muswada huo kutaleta mgongano mkubwa wa kisera miongoni mwa vyombo vya habari kutokana na ukweli kuwa kila chombo kina utaratibu wake wa uendeshaji.

Katika hatua nyingine Sheikh Issa ametoa wito kwa Serikali kuwa sikivu pale wadau wanapoibua hoja za kukosoa miswada ya sheria bada-la ya kupuuzia kwani hali hiyo in-aweza kupelekea uvunjifu wa ama-ni.

Waislam nao wadai marekebisho muswada wa habari

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

4

waislamu nchini wamehimizwa kuzidisha dua kutokana na matatizo yanayowasibu, kwani ku-muomba allah ni ibada kubwa na miongoni mwa sifa za mitume (amani iwe juu yao) na wema waliotangulia.

Nasaha hizo zimetolewa na sheikh abuu mussa

Waislamu wazidishe dua kwa yanayowasibu: sheikh Wangara

kUtOka mIsIKItInI

Na yusuFu ahMadi

Marehemu Bibi Titi Mohammed anatajwa kuwa miongoni mwa watu waliokorofishana vikali na Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa

kwanza wa Tanzania, kuhusiana na suala la Ju-muiya ya Waislamu ya Afrika Mashariki (EAMWS).

Inaelezwa kuwa katika miaka ya 1960 kuli-zuka mgogoro mkubwa miongoni mwa Wais-lamu na kuhusisha baadhi ya vyombo vya seri-kali. Mgogoro huo ulitokana na kampeni iliy-oanzishwa kipindi hicho ya kuivunja Jumuiya ya EAMWS. Bibi Titi yeye alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jumuiya hiyo. (Rejea: ‘Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes’ 1998 kilicho-andikwa na Mohammed Said).

Mgogoro huo unatajwa kuanza mara baada ya kijana mmoja aliyejulikana kama Adam Nasibu, mwalimu wa shule ya msingi na ali-yekuwa Katibu wa EAMWS kule Bukoba ku-tangaza maandamano kwenda kwenye ofisi ya chama cha TANU ya mkoa huo kumuunga mkono Mwalimu Nyerere na sera yake mpya ya Ujamaa iliyokuwemo kwenye Azimio la Arusha.

Inadaiwa kuwa, Nasibu alisema sera mpya ya Ujamaa ni sawa na mafundisho ya Qur’an Tukufu na kwenda mbali zaidi kwa kutoa miongozo kwa viongozi wa Kiislamu wa Bu-koba kufafanua Azimio la Arusha. Ni huyu ndiye aliyeongoza kampeni ya kuivunja EAMWS.

Katika kampeni hiyo, vyombo vya habari vya chama cha TANU na vile vya serikali, redio na magazeti, vilitumika kuishambulia EAMWS kwa kutumia baadhi ya Waislamu. Hoja kubwa iliyotumika kuishambulia EAMWS na kudai ifutwe ni uwepo wa Aga Khan kama mlezi wa jumuiya hiyo.

Inaaminika kuwa moja kati ya watu walio-shiriki katika kueneza propaganda hizo dhidi ya EAMWS ni rais wa awamu ya tatu, Ben-jamin Mkapa akitumia gazeti la Nationalist, ambapo aliandika chanya habari yoyote ya Adam Nasibu. Ikulu ilikuwa kimya wakati haya yakifanyika.

Kutokana na EAMWS kupitia misukosuko mingi inaelezwa kuwa Makamu wa Rais wa EAMWS hapa nchini, Bibi Titi Mohammed akishirikiana na Rais wake, Tewa Said Tewa, wakakusanya nguvu zao ili kuiokoa jumuiya hiyo.

Katika mzozo huo, marehemu Bibi Titi Mo-hammed alisimama thabiti kutetea uhai wa EAMWS. Katika kikao kimoja Bibi Titi alim-kosoa vikali mwalimu Nyerere kwa kile ali-chodai alikuwa anachangia kuiua jumuiya hiyo iliyokuwa muhimu kwa maendeleo ya Waisla-

mu Afrika Mashariki (rejea kitabu hicho hicho cha Mohammed Said).

Bibi Titi aliwahi kutoa maneno makali kati-ka mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU baada ya wanakamati wawili, Selemani Kitun-du na Rajab Diwani, kuomba imjadili Aga Khan na nafasi yake kama mlezi wa EAMWS.

Kitundu na Diwani walidai kuwa wana habari Aga Khan anataka kuitawala Tanganyi-ka kupitia Waislamu na EAMWS. Kwa ajili hii

basi wakapendekeza EAMWS ifungiwe. Ny-erere aliwaunga mkono, lakini Bibi Titi akasi-mama kishujaa dhidi yao.

Biti Titi aliwaambia Diwani, Kitundu na Nyerere hakuna kati yao aliyekuwa na haki ya kuifungia EAMWS, kwani taasisi hiyo ilikuwe-po kabla ya TANU ikitoa huduma kwa Waisla-mu, na kuongeza kuwa, kama walikuwepo watu ndani ya EAMWS walikuwa wanakwen-da kinyume na sheria basi wapelekwe mahaka-mani na sheria ichukue mkondo wake.

Inasemekana hasira zilipanda na kukawa na kutoleana maneno kati ya Bibi Titi na Ny-erere. Bibi Titi akamwambia Nyerere yeye ha-muogopi yeyote ila Allah. Haya ni kwa mujibu wa kitabu ‘Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes - 1998’ cha Mohammed Saidi.

Inadaiwa kuanzia hapo Mwalimu Nyerere akajenga chuki dhidi ya Bibi Titi Muhammed na mwaka 1965, yeye na Tewa Said Tewa waka-poteza viti vyao vya ubunge, hali ambayo in-aaminika Mwalimu Nyerere alihusika pa-kubwa.

Hali hiyo haikumkatisha tamaa marehemu Bibi Titi na mwenzake Tewa Said, kwani mwa-ka 1968, wakati njama za kuiua EAMWS zik-iendelea kushika kasi, walimfuata Mwalimu Nyerere ili kuonesha masikitiko yao ya namna radio ya Serikali na magazeti ya TANU yalivy-okuwa yakiishambulia jumuiya hiyo ya Kiisla-mu.

Wakati Bibi Titi na wenzake wakimtahad-harisha Nyerere kwa kuacha vyombo vya seri-kali kuchochea mgogoro ndani ya EAMWS, Nyerere aliwachukulia akina Bibi Titi kama maadui na kuwaambia uso kwa uso ‘Mmea-mua kunipiga vita, jiandaeni.’ (Rejea kitabu cha Historia ya Kuhuisha Uislamu Tanzania kili-choandikwa na Islamic Propagation Centre).

Vita dhidi ya EAMWS ilinoga zaidi baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Abeid Ama-ni Karume, kukiita chombo hicho kuwa ni cha kinyonyaji. Ikikabiliwa na mashambulizi kuto-ka kila upande, hatimaye mnamo mwaka 1968 EAMWS ilipigwa marufuku kwa amri ya Ny-erere na mali zake zote kukabidhiwa BAKWA-TA iliyoundwa na serikali, ambayo imekuwa ikidai siku zote kuwa haina dini. Tangu hapo BAKWATA imeendelea kuwapo na kuwa chanzo cha madhila na udhalili wa Waislamu Tanzania.

Katika kumuelezea Bibi Titi, katika makala yake aliyoiita, ‘Biti Titi Mohammed and The Historical Context of the Time in Tanzania’ ili-yotoka katika Awaaz Magazine toleo 3, juzuu ya 11; Joseph Lwannia alimsifu kuwa alikuwa Muislamu mwenye muono, kiongozi shupavu, mwenye muelekeo uliodhahiri na aliyejali mustakabali wa nchi yake, huku akiwa mfuasi wa demokrasia yenye ladha ya ubepari.

Mwandishi huyo anaendelea kuandika kuwa, tofauti za kiimani na kisiasa baina ya Mwalimu Nyerere aliyekuwa mfuasi mkubwa wa Ukatoliki na Ujamaa, na Bibi Titi mfuasi wa Uislamu zilileta mapambano makubwa katika chama cha TANU na hivyo kutishia kukigawa chama.

Bibi Titi kupotea katika ramani ya Tanza-nia:

Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa madai ya kupanga njama ya kutaka kuipindua serikali ya Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na wenzake sita, akiwemo Michael Kamaliza aliyekuwa Waziri wa Ulinzi.

Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwan-amke pekee na hatimaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Mwaka 1972 alipata msamaha wa rais Julius Nyerere. Baada ya kutolewa jela, Bibi Titi Mohammed aliishi maisha ya upweke. Mume wake al-imtelekeza wakati wa kesi, huku marafiki zake wengi wakimkimbia.

Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi alita-jwa kwenye makaratasi ya chama tawala kama ‘Shujaa wa kike aliyepigania uhuru wa Tangan-yika’. Na Novemba 5,

2000 Bibi Titi Mohammed alifariki katika hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannes-burg ambapo alikuwa akitibiwa.

tujiKuMbuSHe

bibi titi, nyerere walipokorofishana kwa ajili ya eaMWS

inaaminika kuwa moja kati ya watu walioshiriki katika kueneza propaganda hizo dhidi ya eamws ni rais wa awamu ya tatu, benjamin mkapa akitumia gazeti la nationalist, ambapo aliandika chanya

habari yoyote ya adam nasibu. ikulu ilikuwa kimya wakati haya yakifanyika.

Kishk aviasa vyombo vya habari vya KiislamVyombo vya habari vya Kiislam vimetakiwa kuwa nyenzo ya kwanza ya kuuendeleza na kuutangaza uislam na sio kuwa chanzo cha malumbano miongoni mwao.

hayo yalisemwa na sheikh Nurdin Kishk wakati akitoa khutba ya swala ya ijumaa katika msikiti wa mtambani uliopo Kinondoni jijini dar es salaam. sheikh Kishk alisema, endapo kama vyombo vya Kiislam vitatumika katika njia hiyo, basi uislam utasonga mbele. hata hivyo, badala ya kuutangaza uislam, vyombo hivyo vimekuwa viwanja vya kuushambulia

uislam. alisema, ulimwengu wa sasa unakua kwa kutegemea vyombo vya habari, kwani vinaweza kufanya uongo kuwa kweli na kweli kuwa uongo, na hata kama mtume angekuwepo angetumia njia ya vyombo vya habari kufikisha ujumbe wa mwenyezi mungu. sheikh Kishk aliongeza kuwa, kwa sasa vyombo vya habari ndio silaha muhimu ya kuen-deleza jambo lako na kama hutoitumia vizuri silaha hiyo utakuwa ni mwenye kupata hasara. (KHALID OMARY)

wangara katika khutba ya ibada ya swala ya ijumaa iliyoswaliwa msikiti wa mtoro, Kariakoo, jijini dar es salaam, na akabainisha tatizo kubwa lililopo katika umma wa waislam ni kutotenga muda kwa ajili ya kufanya maombi kwa allah.

sheikh wangara amewataka waislam kujilaz-imisha kuwa wanyenyekevu wanapoomba dua ili kuzitakasa ibada zao, kwani mja mwenye akili ni yule anayejitahadharisha na siku ya kukutana na mola wake (siku ya Qiyama) akinukuu aya za Qur’an : “Na ukipata faragha,fanya juhudi(94:7). Na mola wako mlezi ndio mshughulikie”(94:8).

akifafanua madhila yanayowakumba wais-lam, sheikh wangara amesema,kwa miaka 25 sasa waislam wamekuwa na madai kadha wa kadha kwa serikali, yakiwemo kupatiwa ma-hakama ya kadhi, lakini pia Tanzania kujiunga na shirikisho la nchi za Kiislam ulimwenguni bila mafanikio, hivyo kuwataka waislam kuutumia mwezi mtukufu wa ramadhan kumlilia allah ili awatatulie matatizo hayo. (YUSUPH AMIN)

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

5Habari / tangazo

“afya”is natural source of sweet drinking water from under-

ground stream which is blended

with essential minerals to sup-port and aid per-fect metabolism.

WATERCOM LIMITEDP.o. Box 20409, Plot N.4005, Kisarawe11 area

Temeke,Daresalaam, Tanzaniawww.watercomtz.com, E-mail:[email protected]

hijab, uarabu vyamnyima kitambulisho cha taifa

Na MwaNdishi wetu

Masheikh wa Jumuiya ya Uam-sho wanaotuhumiwa katika kesi ya ugaidi wanaendeleza da’awah ndani ya gereza la

Segerea, ambapo mmoja kati ya waliosil-imu Issa Kaiya Robert (22) ambaye kwa sasa ameachiwa huru amesimulia kuhusu harakati za masheikh hao.

Simulizi ya Robert inakuja takriban wiki mbili tu baada ya kijana mwingine, Nassor Emmanuel Malaja, kutoa ushuhu-da katika Kongamano lililofanyika msikiti wa Kichangani juu ya kazi nzuri ya da’awah ya masheikh hao.

Akizungumza na gazeti la Imaan, Issa amesema, anajisikia faraja kuingia katika nuru ya Uislam, kwani dini hiyo ni ya kwe-li.

Akifafanua da’awah inayofanywa na masheikh wa Uamsho, Issa amesema masheikh hao wamekuwa wakifanya juhudi kubwa ya kuwaingiza watu kwenye nuru ya Uislam kupitia tabia na mawaid-ha mema kila wapatapo nafasi, licha ya kunyimwa fursa na kubanwa na uongozi

wa gereza.Hata hivyo, kwa uwezo wa Allah

masheikh hao wamekuwa wakitumia muda mfupi kufikisha ujumbe wa dini ya Kiislamu na kupata kundi kubwa la watu wanaosilimu, ambapo kwa mujibu wa ki-jana Nassor aliyesilimu majuma kadhaa yaliyopita, mpaka sasa wameshasilimisha zaidi ya watu 15, wakiwemo watu wazima, vijana na watoto.

Hata hivyo, Nassor alisema, mara nyin-gi wanaosilimu wanachukiwa na wenzao. “Watu wengi wanaosilimu huitwa majina mabaya na kuhusishwa na tuhuma za ugaidi na vile vile kunyimwa fursa ya ku-fanya ibada ya swala”, alibainisha Nassor.

Akielezea sababu za kusilimu kwake, kijana Issa Robert amesema, ukarimu na ustaarabu uliooneshwa na masheikh kwa mwezi mmoja aliokuwa mahabusu ulipe-lekea kutaka kuifahamu dini hiyo kiunda-ni.

Alisema, baada ya kuvutiwa na tabia nzuri za masheikh hao aliwafuata na wakamlingania kwa njia ya kuoanisha vi-tabu vya Qur’an na Biblia, na hapo ndipo alipogundua ukweli.

uamsho waendeleza da’awah Segerea

mwingine aliyesilimishwa asimulia alikuwa Gift Robert, sasa ni Issa Robert

m b u l i s h o chaka na cha mwanawe vime-kwama na kwamba sasa ana-paswa kujaza fomu upya.

Mama huyo na mwanawe walipitia michakato yote mwaka 2013 pamoja na mumewe ikiwemo kujaza fomu, kuwasilisha vyeti vyake, kuwasilisha kitambulisho cha mpiga kura, kuchukuliwa alama za vidole, kupigwa picha na hata kurekebisha maelezo yaliyokuwapo katika fomu.

Akiongea na gazeti hili, mume wa mama huyo, am-baye yeye alishapata kitam-bulisho chake licha ya kuanza mchakato huo pamoja, ame-liambia gazeti la Imaan kuwa ameshutushwa na uamuzi huo wa NIDA.

“Walimwambia mke wan-gu uraia wako unatiliwa shaka kwa hiyo hutopewa kitambul-isho chako hadi uraia wako na wanao uhakikiwe na kujaza fomu upya”, Sheikh huyo alil-iambia Imaan. Kadhia hiyo pia imemkuta mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo ambaye yeye anafanana na wasomali na huvaa hijab.

N a y e m w a n a m k e mwingine wa kiislamu mwenye asili ya Kondoa alidai

alipokwenda kuchukua kita-mbulishao chake aliulizwa, mbona anaonekana kama msomali, swali ambalo lilim-shangaza kwani maelezo yake yote alishayatoa na walikuwa nayo. Mwanamke huyo alidai kwamba hawakuacha kum-hoji mpaka alipowaeleza kwamba yeye ni kutoka kabila la Wasi kutoka Kondoa ndipo wakampatia kitambulisho chake.

Wanawake wote hawa wawili walikuwa wameji-pamba kwa mavazi ya staha kamili ya hijabu ya kiislamu.

Hali hii ya Watanzania Waislamu wenye asili ya ki-arabu kutiliwa shaka uraia wao zinakuja wakati raia wen-gine wakihudumiwa pasina kutiliwa shaka jambo ambalo linaonesha kukosekana kwa usawa na ni hatari kwa usala-ma wa taifa.

“Kumbe watu wa kutiliwa shaka ni Waislamu tu, basi adui akikusudia ubaya kwa nchi yetu anachotakiwa ku-fanya ni kutojipamba kwa mavazi wala muonekano wa kiislamu”, Sheikh huyo alila-lamika.

Sheikh huyo aliongeza kwa kusema: “Maswali ambayo Waislamu tunajiuliza, hivi

Mtanzania ni nani? Ni yule mweusi tii kama mkaa? Kuna haja gani kumnyima mtu haki yake kwa mashaka tu?”

Dosari hizi za kutilia shaka watu kwa kuwa na ngozi nye-upe zimeripotiwa maeneo maeneo yote ya Tanzania am-bako zoezi hili limek-wishaendeshwa au linaende-lea kuendeshwa hususan mikoa ya Waislamu wengi ikiwemo Tanga, Zanzibar, Morogoro na Pwani na kupe-lekea baadhi ya watu kuhisi kuna hujuma na udini dhidi ya Waislamu. Huko Lindi na Mtwara hali ni hiyo hiyo kwani ni maeneo ya waislamu wengi.

Zoezi la kuandikisha watu kwa limekwishafanyika kati-ka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Mo-rogoro, Tanga na Visiwani Zanzibar ambapo watu zaidi ya mioni 6.1 wamek-wishaandikishwa hadi sasa.

INatoKa UK 1

Issa Kaiya Robert.

HutoleWa na KucHapiSHWathe islamic Foundation, p.o. box 6011 Morogoro, tanzania, e-mail: [email protected]

MHariri Mtendaji: 0715 559 944, MHariri: 0786 779 669, aFiSa MaSoKo: 0785 500 502toVuti: www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

taHariri / ucHaMbuzi6

Mwishoni mwa juma li-lilopita umma wa wais-lamu wa Tanzania uli-pata mgeni katika sekta

ya habari baada ya ujio wa gazeti jipya la Iqra hatua inayofanya idadi ya vyombo vya habari vya kiislamu kwa upande wa magazeti kufikia zai-di ya matano (5) ukijumuisha yale ya awali ambayo ni Annur,Al-hudaa,Kisiwa na Imaan.Hiyo ni hat-ua ya kupongezwa na ni faraja kwa umma wa kiislamu.

Kama inavyofahamika suala la upashaji habari ni moja kati ya nyen-zo muhimu katika kukabiliana na propaganda chafu halikadhalika ubunifu wa ajenda hasi zinazolenga kuuchafua uislamu ambazo zimeku-wepo tangu na tangu tokea enzi za manabii na mitume.

Ukilinganisha na vyombo visivyo vya kiislamu hali ya mambo haiko tofauti sana hata katika vyombo vya

habari vya kiislamu kwani misingi ya falsafa na maadili ya tasnia ya habari hivi leo imejikita katika mizizi ya itikadi na falsafa za magharibi am-bazo lengo lake ni kuangazia soko zaidi kuliko maslahi ya umma hali il-iyodumu tangia kuanzishwa tasnia ya uandishi wa habari (press) mna-mo karne ya 15 na mwanzoni mwa karne ya 16.

L a k i n i t u k i w a k a m a waislamu,tunapaswa kujenga mshikamano ili kufanikisha lengo la kuwepo kwetu hapa dunia kwani Al-lah Taala ametutaka kufanya hivyo,“ Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni

nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka”(Qur’an 3:103).

Hata hivyo tunaporejea historia ya kuanzishwa vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa utaona kulikuwa na malengo hasi,ingawa manufaa yake kwa sasa ni makubwa hususan kwa jamii ya waslamu kwani imera-hisisha ufanisi na utekelezaji wa mambo kadha wa kadha.

Kwa umoja wetu kama waislamu tunapaswa kutumia neema hizi za vyombo vya habari katika misingi ya dini iliyoainishwa ikiwemo,kuripoti jambo lililochunguzwa,kuripoti bila kutawaliwa na hisia binafsi,kuripoti bila kulazimisha mawazo na fikra binafsi,kuripoti bila kujali nani atas-oma au nani hatasoma kazi yako,kuripoti bila kujali nani atafu-rahi na nani atachukia na kuripoti pande zote mbili sawasawa (Balanc-ing). Kwa mfano inawezekana kwa

idadi ya vyombo vyote vya habari vilivyopo sasa kwa upande wa televisheni,radio na magazeti kuwa na nafasi kubwa ya kufanya mapin-duzi katika kupigania na kutetea haki za waislamu,lakini si hivyo tu bali pia kuielimisha na kuionya jamii juu ya hofu ya Allah subhanahu Wataala tofauti na ilivyo sasa kwa baadhi ya vyombo hivyo kuwa kiny-ume na malengo yaliyokusudiwa hivyo kukosa utofauti na vyombo vingine.

Pia ni vema wamiliki wa vyombo vya habari vya kiislamu pamoja na watendaji wake kwa ujumla kuweka kando itikadi za kimadhehebu ,kuepuka migongano na mifarakano katika mambo yasiyo na tija na dini yetu badala yake kuchukua fursa hiyo kuwa na kauli moja katika kuy-aendea mambo ya dini yetu na dunia kwa ujumla.

Tunashauri vyombo hivi vya

habari kuwa na umoja wenye nguvu kuanzia wamiliki wake, wahariri na wanahabari ili kuweza kujenga sauti moja inayofanana ya kuwapasha habari waislamu.

Chombo kama jukwaa la wahariri wa vyombo vya habari vya kiislamu, bodi ya wamiliki wa vyombo vya habari vya kiislamu vingeweza ku-undwa ili kuwaunganisha pamoja wadau katika sekta hii muhimu.

Tumalizizie kwa kusema,ili ku-wepo maana ya vyombo vingi vya habari vya kiislamu hapana budi kuwa kitu kimoja ili kufanikisha ajenda zetu.Katika kulifanikisha hilo ni jukumu letu kubuni wazo la uan-zishwaji wa jukwaa la wahariri kwa vyombo vya habari vya kiislamu ili kuweka mkazo katika nia ya pamoja ya kuujenga umma wa waislamu hu-susan katika wakati huu ambao jamii ya waislamu inakabiliwa na vita ya fikra na propaganda.

Vyombo vya habari viwe faraja kwa umma wa kiislamu

Ukweli kwamba kosa moja ambalo watanza-nia tutalifanya katika kipindi hiki linaweza

kutugharimu kwa miaka mitano au kumi ijayo unafanya zoezi lina-loendelea Dodoma la mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais wa CCM kuwa muhimu sana.

Watanzania tumeona na tu-naendelea kushuhudia wimbi kubwa la wanaowania nafasi ya kurithi mikoba ya Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Mu-ungano wa Tanzania wakiendelea kujitokeza katika viwanja vya Chimwaga kuchukua fomu za kuomba kupeperusha bendera ya CCM.

Mpaka Ijumaa iliyopita, wago-mbea 15 walishajitokeza kwenda Dodoma kuchukua fomu hizo, baadhi kwa mbwembwe na wen-gine kimya kimya.

Miongoni mwa waliokwisha kuchukua fomu ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Ghar-ib Bilal; Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira.

Wengine waliochukua fomu ni Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) huko Marekani, Amina Salum Ali na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, watoto wa marais wali-opita wa taifa la Tanzania; Charles Makongoro Nyerere na Balozi Ali Karume, mawaziri wawili wa zam-ani wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na Wiliam Ngeleja, mawaziri wakuu wastaafu, Fredrick Sumaye na Ed-ward Lowasa.

Makada wengine ambao wam-eonesha dhamira yao ya kutaka kuwatumikia watanzania ni Amos

Siyantemi, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Steven Wa-sira, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na Dk Ti-tus Kamani.

Kujitokeza kwa makada wengi kutaka kugombea nafasi hiyo ku-meibua mijadala mingi miongoni mwa jamii. Tukubaliane kuwa mwitikio mkubwa wa makada wa chama tawala kujitokeza katika mbio za kuwania urais kuna faida na hasara zake. Kuna uwezekano wa kupata kiongozi mbaya au mzuri.

Hasara na faida zimezalisha kambi mbili katika mjadala wa aidha wingi wa wagombea ni jam-bo zuri au baya.

Kuna wanaosema wagombea wengi hiyo ni ishara mbaya kwa mustakabali wa taifa kwa sababu katika mtifuano na mkanganyiko huo ni rahisi watu kuchanganyiki-

wa na kuishia kuchagua mtu am-baye atakatisha tamaa zaidi wa-nanchi ambao tayari wanaoneka-na wamekata tamaa na wame-poteza matumaini kutokana na changamoto za maisha.

Kundi hili linaamini kuwa in-awezekana hatua ya uchujaji itakuwa ngumu kiasi kwamba maamuzi magumu itabidi yafan-yike ili kukinusuru chama kisiga-wanyike.

Maamuzi magumu ni kama yale ya 2010 ambapo iliamriwa nafasi ya uspika ikamatwe na mwanamke. Maamuzi magumu ya namna hii sio muda wote yanaweza kuwa mazuri na yanawe-za kuacha wagombea wazuri.

Pia, ugumu wa kupata kiongozi mzuri unaweza kutokana na ghilba ya baadhi ya wagombea ambao tayari baadhi yao inasemekana wameanza kununua watu ili wa washangilie na kuonekana kuwa

wanapendwa na kukubalika. Wagombea wa aina hii, inase-

mekana, wameanza kununua hata wanahabari. Ingawa ushahidi sina, waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Lakini wapo pia watu wanaoo-na utitiri huu wa wagombea kama jambo zuri, na ni ishara njema kwa awamu ijayo.

Walio na matumaini kutokana na utitiri wa wagombea wa-naamini katika demokrasia, am-bapo wagombea wengi inamaani-sha una idadi kubwa ya watu am-bao utapata fursa ya kuwapima na kuchagua mgombea mzuri.

Katika orodha ya wana CCM waliojitokeza kuna maprofesa, madaktari, vijana, wazee, matajiri na masikini, wenye uzoefu na wachanga, wanadiplomasia na kadhalika.

Ni mgombea mwenye elimu, uzoefu na falsafa gani ataweza kuli-

vusha taifa ndio swali la msingi ambalo tukipata jawabu sahihi watanzania tutakuwa tumeula.

Ukiwaangalia wale wote ambao wamejitokeza na wale ambao wa-natajwa kutaka kujitokeza kujiun-ga na mbio hizo za kuelekea ikulu, unaweza kuhisi kabisa kuwa kuna watu wenye uwezo, ujasiri na nia ya dhati ya kutaka kuwapigania wananchi.

Kwa upande wangu nadhani kuwepo kwa utitiri wa makada ku-jitokeza kuchukua fomu ni hatua ya kupongezwa, kwani inaonesha namna chama tawala kilivyo na utajiri wa watu wanaojiamini kuwa wanaweza kuwavusha wa-tanzania.

Changamoto iliyopo ni kwa wa-nachama wa chama tawala ku-wasikiliza na kuwachuja vizuri vi-ongozi hawa na kisha kuchagua mtu ambaye anaweza kukabiliana na matatizo lukuki yanayoikabili nchi yetu kwa sasa, huku rushwa, ufisadi na kukosekana haki na uad-ilifu (hususan kwa wanajamii Waislam) ikiongoza orodha hiyo.

Kwa hiyo basi, hoja kamwe sio wimbi la wagombea wengi pale Chimwaga, lakini ni namna wana-nachi wanavyoweza kufaidika kutokana mwamko wa ki-demokrasia wa wingi wa wago-mbea hao waliojitokeza kwa kupa-ta kiongozi safi.

Nasaha zangu kwa viongozi wenye dhamana ya kuchuja wago-mbea, watumie uzalendo na busara katika kuteua mgombea mwenye sifa zisizo na shaka.

Nasaha hizi pia ziende kwa mu-ungano wa UKAWA na vyama vingine vya upinzani vinavyopanga kusimamisha mgombea urais mwaka huu. Kosa moja litaghar-imu maendeleo yetu miaka mi-tano

Kosa moja litagharimu maendeleo yetu miaka 5

kujitokeza kwa makada wengi kutaka kugombea nafasi hiyo kumeibua mijadala

mingi miongoni mwa jamii. tukubaliane kuwa mwitikio mkubwa wa makada wa chama tawala kujitokeza katika mbio

za kuwania urais kuna faida na hasara zake. kuna uwezekano wa kupata

kiongozi mbaya au mzuri.

SeleMani Magali

naSaHa za WiKi

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

7

Na yusuFu ahMadi

Sheikh Al –Amin ni baha-ri ya kina kirefu! Utazama...!Ukizuka utatoka na kitu kidogo

tu!”. Hayo ni maneno ya Marehe-mu AbdulKadir Said Al-Maamry alipoulizwa na Sayyid Ghalib At –Tameemi kuhusu maisha ya Sheikh Al –Amin Ali Mazrui.

Sayyid Ghalib At –Tameemi ambaye aliandika kitabu alichoki-ita, ‘Maisha ya Sheikh Al – Amin Ali Mazrui (1891 – 1947)’, anamu-elezea Sheikh Al – Amin kama mwanazuoni ambaye amekuwa kimbilio la utafiti wa wasomi wen-gi, wanasayansi na watafiti mbalimbali ulimwenguni kwa miaka mingi.

Umaarufu wa Sheikh Al – Amin unatokana na nafasi yake kama mwanamageuzi wa Kiisla-mu Afrika Mashariki aliyejitahidi kubadili mitazamo katika baadhi ya mambo yaliyoonekana kuwa hayastahili kufanywa na Waisla-mu na kuhimiza mambo muhimu ambayo Waislamu hawakuwa wakiyafanya.

Si ajabu basi kuwa, mwanawe, Prof Ali Mazrui, msomi maarufu duniani wa fani ya historia, anam-uelezea Sheikh Al Amin kama: ‘...mmoja kati ya wasomi wakubwa wa Afrika ya Mashariki aliyekuwa ulamaa, mwandishi, mhariri wa magazeti, hodari wa mashairi, mwanaharakati, aliyeanzisha har-akati za mageuzi na muelekeo mpya’.

sheIKh al-amIn nI nanI?

Sheikh Al-Amin Ali Maz-rui ambae alikuwa mtoto wa Sheikh Ali Bin Abdal-lah Mazrui alizaliwa

Januari 27, 1891 katika mji wa Mombasa nchini Kenya. Baba yake, Ali bin Abdallah Mazrui ali-fariki akiwa na miaka 4 tu.

Baada ya kifo cha baba yake, Sheikh Al – Amin alilelewa na mjomba wake, Sheikh Suleiman bin Ali bin Hamisi Mazrui. Inaelezwa kuwa wakati wa kukata roho, Sheikh Ali Mazrui alimkabi-dhi Sheikh Suleiman awe mlezi wa mwanae kwa kumwambia: “Na-kukabidhi mwanangu leo unirud-ishie mwenyewe kesho akhera”.

Maneno hayo ya Sheikh Ali Mazrui yananasibishwa na maneno ya Allah (52: 21): Na wal-io amini na dhuriya zao waka-wafuata kwa Imani tutawakutani-sha nao dhuriya zao, na wala hat-utawapunja hata kidogo katika vi-tendo vyao. Kila mtu lazima atap-ata alicho kichuma.

Sheikh Mazrui alijifunza dini ya Kiislamu chini ya mlezi wake, Sheikh Suleiman aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya enzi za Utawala wa Muingereza.

Katika safari yake ya kusaka elimu ya dini ya Kiislamu, Sheikh Al-Amin pia alifika visiwani Zan-zibar, ambapo alisoma kwa masheikh mashuhuri, wakiwemo Sheikh Sayyid Ahmad Bin Sumayt na Sheikh Abdalah Bakathir.

Pamoja na mambo mengine, Sheikh Al-Amin anasifika kwa uhodari katika utunzi wa mashairi,

jaji na msomi mahiri wa dini ya Kiislamu kuwahi kutokea katika ukanda wa Afrika mashariki.

Miongoni mwa maulamaa mashuhuri ambao Sheikh Al-Amin aliwafuatilia kiundani mafundisho yao ni Sheikh Ibn Taymiyya na Sheikh Muhammad Abdu.

UtUmIshI Wa sheIKh al-amIn

Mw a k a 1 9 1 0 , Sheikh A l -

Amin alianza kazi kama Katibu wa Ka-dhi wa Mombasa mpaka mwaka 1919 ambapo al iamua kuachana na cheo hi-cho na kuwa mwalimu wa somo la kiarabu katika shule ya kiarabu ya Mom-basa.

Lakini mwaka 1921 alirejea tena katika nafasi ya ukatibu wa Kadhi wa Mombasa mpaka mwa-ka 1932 alipofanikiwa kushika na-fasi ya Kadhi wa Mji wa Mombasa na mwaka 1937 akafanikiwa kuwa Kadhi Mkuu wa Kenya.

mageUzI KatIKa dInI

Katika utafiti wake bwa-na Randall L. Powels uliobeba kichwa cha habari,‘Sheikh Al-

Amin B. Ali Mazrui and Islamic modernism in East Africa, 1875-1947’ alioufanya kwa lengo la ku-tathmini mchango wa Sheikh Al-Amin katika maendeleo ya dini ya Kiislamu, anamtaja Sheikh huyo kama mtu muhimu hapa Afrika Mashariki aliyeleta mapinduzi makubwa katika dini hiyo.

Miongoni mwa mapinduzi makubwa aliyoyaleta Sheikh Al-Amin ni kuwahimiza Waislamu kufanya kazi zingine tofauti na za dini tu, akisisitiza kuwa dini ya Ki-islamu haijamkataza muumini kuacha kushiriki katika shughuli za dunia.

Moja ya harakati za Sheikh Al-amin ni kutaka mabadiliko katika Uislamu kuhusu walimu kujihusi-sha na uganga na kupiga ramli, waislamu kushiriki mambo ya

ngo-ma (beni) na pia uzushi kuhusu mambo ya sherehe za Maulid.(Kitabu cha Sheikh Al-amin-Kutizamia, uk 10)

Kwa maneno mengine, Sheikh Al-Amin ni muasisi wa harakati za kisunnah Afrika Mashariki ndiyo maana wanafunzi wake kama Sheikh Abdallah Saleh Farsy wa-likuja kuendeleza harakati hizo.

Lakini tofauti na masheikh wengi wa kisunnah leo, Sheikh Al-Amin hakujiona tofauti na waisla-mu wengine hata kama walikuwa wakiyafanya yale aliyokuwa akiya-pinga kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah. Kuhusiana na elimu ya kimagharibi (Western education), Sheikh Al-Amin aliwahimiza Waislamu kujifunza elimu ya say-ansi na teknolojia ya Magharibi ili waweze kupata maendeleo huku akisema kuwa, dini ya Kiislamu ni dini ya kisayansi na inayotumia tafakuri (Rationality).

Katika kuonesha kuwa ndani ya Uislamu kuna mambo ya kisay-ansi, Sheikh Al-Amin alitolea mfano wa nchi ya Misri iliyokuwa ya kiislamu ambapo Waislamu waliweza kufanya mapinduzi makubwa katika maendeleo ya

dunia kwenye nyanja za hesabu za aljebra, unajimu, kemia, tiba

(medicine), na falsafa (philos-ophy).

Katika kusisitiza juu ya suala hilo, Sheikh Al-

Amin aliwataka Wais-lamu kusoma vitabu vya nchi za Maghar-ibi kwa hoja kuwa maarifa yaliyomo humo baadhi yake yamechuku-liwa kutoka kati-ka mafundisho ya dini ya Kiisla-mu.

Na ili kuweza kufikia lengo hilo la watu kupata

elimu, Sheikh Al-Amin alihimiza

ujenzi wa shule za kisasa. Kadhalika, pia

alihimiza watu wa-jenge hospitali, makta-

ba, waunde silaha za kisasa na wafanye biashara. Katika kuleta mapinduzi za-

idi katika dini ya Kiislamu, Sheikh Al-Amin alipinga kwa jitihada zake zote mila potovu, yakiwemo matumizi ya madawa kutoka kwa waganga wa jadi kwa hoja kuwa suala hilo si sahihi katika ma-fundisho ya dini ya Kiislamu. Badala yake aliwataka Waumini wa dini ya Kiislamu kuhakikisha wana achana na mila potovu na kushikamana na mafundisho sa-hihi ya dini ya Kiislamu.

Kutokana na kuenea zaidi kwa mawazo ya nchi za Magharibi ka-tika pwani ya Afrika Mashariki na hivyo kuathiri mafundisho ya dini ya Kiislamu, Sheikh Al-Amin ali-wahimiza Waislamu kushikama-na na kuyapinga mawazo hatari ya nchi za Magharibi.

Pia Sheikh akishirikiana na mlezi wake, Sheikh Suleiman ali-pambana na wakoloni na vituko vyao mpaka wakoloni wakasalimu amri na wakawaheshimu. Baba yake naye alipambana na Sayyid Barghash mpaka akafungwa jela na mtawala huyo.

Kuanzisha vyombo vya habariKatika malengo yake ya kuua-

msha umma wa Kiislamu kuifa-hamu zaidi dini yao, mwaka 1930-1931, Sheikh Al-Amini alianzisha

gazeti lake la lugha ya kiswahili li-lilojulikana kama Sahifa na ku-fuatiwa na gazeti jingine lililoju-likana kama Al-Islah hapo mwaka 1932. Magazeti yote hayo mawili yalikuwa yakichapisha habari zili-zokuwa na lengo la kuufanya umma kupokea mawazo mapya ya kimaendeleo katika elimu huku yakisisitiza watu kufuata misingi sahihi ya Kiislamu.

Ukiachia mbali kutumia maga-zeti katika kuhakikisha Uislamu unaimarika katika mji wa Mom-basa, Sheikh Al-Amin alianzisha Jeshi la Upotovu (Going astray Army) dhidi ya ushawishi mbaya wa chini kwa chini uliokuwa uki-fanywa na jeshi la Uokovu (Salva-tion Army).

maandIshI na WanafUn-zI WaKe

Sheikh Al-Amin aliandika vitabu vingi vya dini ya Kiislamu katika lugha ya kiswahili na kiarabu,

ikiwemo kutafsiri Suratul Al-Baqara, Suratul Al- Imran na Su-ratul An-Nisaa. Pia alikuwa aki-andika makala katika jarida la Al-Manar la Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha nchini Misri.

Katika uhai wake, Sheikh Al-Amin alifundisha wanafunzi wen-gi, ambao baadhi yao walitoa mchango mkubwa katika maen-deleo ya dini ya Kiislamu. Baadhi ya wanafunzi wake wakubwa ni pamoja na Sheikh Muhammad Kassim na Sheikh Abdullah Saleh Al-farsy, ambao wote wamewahi kushika nafasi ya Kadhi Mkuu wa Kenya. Mwanafunzi wake mwingine mahiri ni Maalim Ghazali ambae nae alianzisha Ma-drasa ya Ghazali iliyokuja kuju-likana kama Shule ya msingi ya Mbaraki huko Kenya.

Sheikh Al-Amin atakumbukwa kwa utabiri wake aliouita ‘khatari nyeusi’ uliosema: “Jamaa wa bara watazitupa fagio na kuwa mabwa-na kwa sababu ya elimu na vitabu, na sisi tulio mabwana leo ndio tut-akaotupa vitabu tukaokota fagio”.

Sheikh Al-Amin pia alikuwa mtetezi mkubwa wa elimu ya wa-nawake, ambayo haikuwa iki-tolewa kwa kiasi kikubwa kwao na alizihimiza familia nyingi ku-wafunza elimu mabinti zao.

Sheikh Al-Amin alifariki dunia mwaka 1947 baada ya kuugua ki-fua kikuu kwa muda mrefu. Siku aliyokata roho, Sheikh Al-Amin alimuuliza mkewe, sasa ni saa ngapi? Akajibiwa ni alasiri. Akamwambia mkewe mkubwa, Bi Swafia bint Suleiman, amtawa-dhishe. Kisha, akainuliwa, akasali. Akatoa salamu kumaliza swala. Punde, Allah akachukua roho yake akiwa amezungukwa na wakeze wawili, wanawe na wanafunzi wake.

Allah amrehemu

SHeiKH al-aMin Mazruimwana mageuzi nguli katika Uislamu

ukiachia mbali kutumia magazeti katika kuhakikisha uislamu unaimarika

katika mji wa mombasa, sheikh al-amin alianzisha jeshi la upotovu (going

astray army) dhidi ya ushawishi mbaya wa chini kwa chini uliokuwa ukifanywa na

jeshi la uokovu (salvation army).

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

8

Na seleMaNi MaGali

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimejizolea umaarufu mkubwa katika ardhi ya

Tanzania kutokana na kazi yake ya kuhakikisha haki na usawa wa raia unaheshimiwa kwa kiwango cha hali ya juu.

Kituo hiki kimejipambanua kwa umma kama watetezi wa haki za kiraia katika nyanja za kisiasa, kiu-chumi, kijamii na kiutamaduni. Pia wamesimama kidete kutetea haki za makundi maalum huku wakitoa elimu ya uraia na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Hivi karibuni taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ilizindua taarifa yake juu ya hali ya haki za binadamu kwa kipindi cha mwaka 2014 ambayo il-ionesha hali ya haki za binadamu nchini bado ni tete na kwamba makundi mbalimbali kama ya wazee, wanawake, watoto na watu wenye ulemavu wameendelea kun-yanyasika katika nchi yao. Taarifa hiyo kwa umma iliibua hisia tofauti miongoni mwa jamii, huku Waisla-mu wakiikosoa vikali na kukosoa utendaji kazi wa kituo hicho am-bacho wanakituhumu kwa ubaguzi na kushindwa kutetea Waislamu.

Masheikh wamesema, kituo hi-cho kimekuwa kikipiga kimya ukiu-kaji wa haki za binadamu unapo-fanyika dhidi ya Waislamu, lakini kimekuwa mstari wa mbele kuse-mea makundi mengine ya kijamii.

Akizungumza na gazeti la Im-aan, Kaimu Katibu Mkuu wa Ju-muiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Rajabu Katimba alielezea

masikitiko yake juu ya tabia hiyo ya LHRC ya kuwatenga Waislamu.

Sheikh Katimba alisema, wa-naushahidi wa hujuma mbalimbali ambazo zilifanywa na Serikali dhidi ya Waislamu, lakini kituo hicho li-cha ya kuwa na taarifa walisita walau kutoa matamko ya kulaani, kama wanavyofanya katika ma-tukio mengine ya uvunjwaji wa haki za binadamu. Sheikh Katimba amesema, ukimya wa LHRC un-aweza kutafsirika kama mpango maalum unaolenga kukandamiza jamii ya Kiislamu.

Baadhi ya kadhia za uonevu na ukiukwaji mkubwa wa haki za bin-adamu zilizowakumba Waislamu, kwa mujibu wa Sheikh Katimba ni pamoja na Sheikh Issa Ponda kuho-jiwa wakati yupo kitandani na jera-ha bichi la risasi.

Tukio lingine ni la viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kikatili vilivyokiuka haki za bi-danamu. Matukio haya yote yalipita bila taasisi hiyo kukemea na kuwa-tetea masheikh hao.

Katimba alisema, baadhi ya masheikh wa JUMIKI wamewahi kuhojiwa wakiwa uchi, walipigwa kipigo cha mwizi, waliingiliwa kiny-ume cha maumbile, pamoja na

kushindiliwa jiti sehemu za siri.Sheikh Katimba ameongeza

kusema kuwa, hata ripoti ya hali ya haki za binadamu hapa nchini am-bayo imezinduliwa hivi karibuni ili-shindwa kuonyesha ukatili huo un-aofanywa na watekelezaji wa sheria, jambo linalojenga hofu miongoni mwa Waislamu juu ya uadilifu wa kituo hicho.

Katimba alisema, Sheikh anayedaiwa kufanyiwa udhalilishaji na jeshi la polisi ambaye pia ali-ithibitishia Mahakama ya Kisutu juu ya udhalilishwaji huo ni mtu mzima mwenye wake watatu na watoto wanane, na kuongeza kuwa, kitendo cha uzalilishaji alichofanyi-wa kilipaswa kukemewa kwa vikali, lakini kwa mshangao mkubwa hakuna mwanaharakati wa LHRC aliyeguswa na tukio hilo.

Naye, Amir wa Baraza la Vijana wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Shabaan Mapeyo ameitaka taasisi hiyo kujitathmini kupitia miaka 20 wanayoazimisha, ili wapime kama kweli malengo yao yamekamilika.

Mapeyo alikishutumu kituo hi-cho akisema, viongozi wake wame-kuwa wakitupilia mbali matatizo yanayoigusa jamii ya Kiislamu na hivyo basi wajitathmni kama wana-tenda haki na uadilifu katika jamii na kisha wajirekebishe.

Mapeyo alisema, kutokana na mfululizo wa matukio ya kiuonevu yanayotokea dhidi ya viongozi wa Kiislamu ni dhahiri kingekuwa ni kituo cha kupigania haki za raia wote, wangeingilia kati na kutoa matamko ya kulaani. “Hatujui kwa nini wanakuwa wazito kwa matukio yanayowagusa Waislamu”, alihoji Mapeyo na kuongeza: “Wakati kituo hicho kinasherehekea kutimi-za miaka 20 ya kupigania haki na usawa wa raia katika ardhi ya Tan-zania, Waislamu wamekuwa wak-isikitishwa na utendaji wao”.

Mapeyo alisema, kutopata taari-fa ya matukio hayo hakiwezi kuwa hoja ya kujifichia, kwani matukio mengi yamekuwa yakitagazwa ka-tika vyombo vya habari na kujadii-wa bungeni .

WanaChOsema KItUO Cha sheRIa

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtend-aji wa Kituo cha Sheria na haki za Binadamu Dr. Helen Kijo-Bisimba amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo, ambayo amesema, kwa muda mrefu wanahangaika namna ya ku-weza kuitatua.

Dr. Kijo-Bisimba alisema, Wais-lamu wamekuwa na mtazamo hasi juu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na wengi wao wame-

kuwa wakiamini kuwa kituo hakina msaada juu ya matukio yanayowa-gusa moja kwa moja Waislamu.

Akifafanua kwa nini taasisi yake imekuwa inashutumiwa juu ya utendaji kazi wake, Dr. Kijo-Bi-simba alisema, kwanza, jamii lazi-ma ifahamu kuwa taasisi yake hai-fanyi kazi kwa jicho la dini, bali ime-kuwa ikimulika haki ya raia yeyote yule bila kujali anatoka kundi gani.

“Ndugu yangu mwandishi, sisi kituo tunajitahidi sana kuhakikisha tunatoa huduma zetu kwa yeyote yule mwenye mahitaji, hoja ya kwamba tumekuwa kimya kwa masuala ya Waislamu kwetu haina mashiko, kwani tunahudumia jamii yote bila kujali dini wala kabila”, al-isema Kijo-Bisimba.

Dr. Bisimba ameendelea kusema kuwa, taasisi yake ilitumia rasilimali zake mwaka 1998 kuingilia sakata la Mwembechai, lakini suala lile lilii-sha bila mafanikio kutokana na Waislamu kushindwa kutoa ushiri-kiano wa kutosha.

Akizungumzia mafanikio am-bayo taasisi yake imeyapata kwa kipindi hicho cha miaka 20, Dr. Ki-jo-Bisimba alisema, wamefanikiwa kuinua uelewa miongoni mwa jamii, ambapo mpaka sasa Watan-zania wanaweza kuinuka na kudai haki zao wakiona zinapindishwa.

Masheikh Walalamikia ubaguzi Miaka 20 ya LHRC:

na SHeiKH taWaKKal juMa

KutoKa KatiKa Qur’an’ na SunnaH

Wiki iliyopita katika mfululizo wetu wa makala za ‘Kutoka katika Qur’an na

Sunnah tuliishilia pale Utubah al-ipolazimika kuuziba mdomo wa Mtume ili asiendelee aliposoma aya inayosema;

“Wakikengeuka, basi sema (ee Muhammad) Nakuhadharisheni swaa’iqah (mngurumo angamizi) mfano wa swaa’iqah ya kina ‘Aad na Thamuwd.” Utubah alimwam-bia Mtume: “Acha ewe Muham-mad, tafadhali usiendelee”.

Utubah aliporudi kwa watu wake aliwaambia: “Enyi watu wangu naomba mnitii kwa siku ya leo tu na mniasi katika siku ny-ingine zijazo. Naapa kwa hakika nimesikia kutoka kwa Muham-mad maneno ambayo sijawahi kusikia mfano wake katu.

Muacheni mtu huyu na mjitenge nae, nawaapia hatoacha analofanya, muachieni waarabu wengine, ikiwa atawashinda basi utukufu wake ni utukufu wenu, na cheo chake ni cheo chenu, yaani mtapata utukufu kwa utukufu wake na nguvu kwa nguvu zake, na ufalme wake utakuwa ufalme wenu.

Na kama hao waarabu wengine watamshinda, basi mtakuwa mmeepushwa shari zake kwa mikono ya watu wengine”.

Watu waliomtuma Utubah wa-kasema: “Hakika umeanza kumili (kuegemea) kwa Muhammad na jambo lako limekuajabisha na umeacha ibada za masanamu za watu wako”. Utubah akawaam-bia: “Maneno niliyosikia kutoka kwa Muhammad sio uchawi wala mashairi. Nimemsikia akisoma: ‘Wakikengeuka, basi sema (ee Mu-hammad) Nakuhadharisheni swaa’iqah (mungurumo angamizi) mfano wa swaa’iqah ya kina ‘Aad na Thamuwd’. Nikamsihi aache na nyinyi mnajua fika kuwa Muham-mad asemapo kitu huwa hasemi uongo, nikaogopa isije adhabu ikakuteremkieni”.

Mpenzi msomaji tunachojifun-za katika kisa hiki ni kuwa, Qur’an iko juu na itaendelea kuwa juu, na wenye Qur’an wako juu na wa-taendelea kuwa juu. Kama wako chini kuna mahali walikosea au hawajatimiza vigezo na masharti.

Ushindi hauteremki kutoka ka-tika ombwe wala hauji bila kutara-jiwa. Kushinda au kushindwa kupo na kunatawaliwa na kanuni na njia ambazo zimenukuliwa na Allah katika Qur’an ili waumini waweze kuzijua kwa yakini, elimu ya uhakika na kwa upeo mkubwa zaidi. Kanuni hizi hazibadiliki kwa kiasi kikubwa.

Allah anasema yafuatayo kuhu-su kanuni hizi: “Kabla yenu zimepita nyendo nyingi; basi tem-beeni katika ulimwengu muan-galie vipi ulikuwa mwisho wa wa-naokanusha” (3: 137).

Na pia, “Hii ni ada ya Allah iliy-okuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Allah” (33: 62). Na Anase-ma tena Allah aliyetukuka: “Huo ndio mwendo wa Allah uliok-wishapita zamani, wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Al-lah” (48: 23).

Kupotoka katika njia iliy-onyooka na kusahau ujumbe wetu ni moja kati ya sababu kubwa zi-nazotufanya Waislamu tushindwe.

Waislamu sasa hivi wameshindwa kutofautisha baina ya adui na rafiki na hawajui mikakati na nja-ma za adui dhidi yao na mikakati yao sahihi dhidi ya adui yao.

Hivyo, umma wa Kiislamu hautoweza kushinda dhidi ya adui yake hadi masharti fulani yat-imizwe. Kama kweli ikiwa Waisla-mu wanataka kushinda ni lazima wayafanyie kazi masharti hayo. Nyakati za ushindi ama kushindwa zinabadilishana mikono kutegem-ea kanuni hizo.

Allah anasema: “Kama yame-kupateni majeraha, basi na hao watu wengine yamewapata majer-aha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu ili Allah awapambanue wal-ioamini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi. Na Allah ha-wapendi madhalimu” (3: 140).

Imani ya kweli yenye nguvu ni sharti muhimu kwa Waislamu ku-washinda makafiri. Ikiwa Waisla-mu ni wakweli na waumini wa kiuhakika, basi wataweza ku-washinda maadui zao kila wakati

na lau kama Waislamu hawatawe-za kuwa juu ya adui yao, basi itakuwa Waislamu ndio wenye matatizo kiimani.

Waumini ndio walengwa wa kupata ushindi, kama Allah ana-vyomwambia Mtume wake: “Na wakitaka kukukhadaa basi Allah atakutosheleza. Kwani Yeye ndiye aliyekuunga mkono kwa nusura yake na kwa waumini. Na akazi-unga nyoyo zao. Na lau wewe un-gelitoa vyote viliomo duniani us-ingeliweza kuziunga nyoyo zao, la-kini Allah ndiye aliyewaungani-sha” (8: 62 – 63).

Wakati mwingine Allah anawa-tumia malaika ili wawasaidie wau-mini kama alivyosema: “Mola wako Mlezi alipowafunulia malai-ka: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walioamini. Nitatia woga katika nyoyo za wal-iokufuru” (8: 12).

Allah anasema tena: “Kisha Al-lah akateremsha utulivu wake juu ya mtume wake na juu ya wau-mini. Na Akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona, na akawaa-dhibu wale waliokufuru. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri” (9: 26).

Itaendelea

Mafunzo kutoka katika kisa cha utubah

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, juMatatu juni 8 - 14, 2015

9

Asalaam alaykum ndugu katika imani. Nimelaz-imika kuandika makala haya kutokana na hali

miongoni mwa wanasunnah Tan-zania ili kutekeleza mafundisho ya Qur’an: “Kumbusha huenda uku-mbusho ukafaa. Atakumbushika mwenye kumuogopa (Allah). Na atajitenga nao (ukumbusho) muovu” (87:9-11).

Tunashuhudia masheikh wa-kongwe wa kisunnah wanaku-furishwa na kuitwa majahili. Masheikh vijana wanawakosea adabu masheikh wenye umri mkubwa kinyume na adabu za kielimu na hadith ya Mtume (Re-hma na amani ziwe juu yake): “Si miongoni mwetu asiyewaonea huruma wadogo wetu na asiye-waheshimu wakubwa wetu” (Muslim).

Kibaya zaidi, wanasunnah Tanzania wametikisika kiasi kwamba ni vigumu kuwaleta pamoja kwa maslahi ya harakati za kisunnah, huku wapinzani wao wakiwapiga vita.

Hata tofauti za kimtazamo wa kielimu tu zinatosha kumtoa sheikh katika safu ya wanasunnah na kumuingiza katika upotevu, huku wakijua penye hitilafu miongoni mwa wanawazuoni, msimamo wa mmoja haulaz-imishwi kwa wengine.

Mambo haya yanayotokea sasa hivi katika safu za wanasunnah

Tanzania hayakuweko miaka michache nyuma, bali yamelipu-ka baada ya vita ya kwanza na ya pili ya Ghuba, ambapo wanasun-nah walianza kukufurishana.

Mtafaruku wa sasa miongoni mwa wanasunnah haukuwepo kabla ya harakati za kisalafi kushi-ka kasi, kwani wanasunnah wa mwanzo, kama Sheikh Al Amin Maftah, Sheikh Abdallah Saleh Farsy, Sheikh Jabir Yusuf Katura, na Sheikh Juma Poli hawakujita-mbulisha kama masalafi, bali An-swar Sunnah na wakatambuliwa hivyo.

Si kwamba masheikh hawa hawakuujua usalafi au waliupin-ga. Walifanya hivyo kwa kuwa ndilo lililokuwa jina mashuhuri wakati huo duniani, huku wakisi-mamia njia ya salafi kwa kauli na matendo yao kiasi alichowajaalia Allah Ta’ala. Wako waliotiwa mis-

ukosuko, wakafungwa magereza-ni, wakapigwa na hata kuathirika kiuchumi.

Hatimaye wanafunzi au wa-nafunzi wa wanafunzi wa masheikh wa kisunnah wakaenda kusoma nje na kukuta vuguvugu la ‘masalafi’. Waliporejea nchini, ikawa kama usalafi unaingia.

Vijana wakaja na ari kubwa ya kuufikisha usalafi walivyouelewa. Bahati mbaya ni kwamba ufik-ishaji umekuwa ni kwa mtindo wa ‘sisi’ na ‘wao’ na hivyo kuwa-gawa wanasunnah.

Kwa nini kubaguana?Usalafi si jina tu, bali ni manhaj

(njia) ya kuutekeleza Uislamu, ndiyo maana utasikia huyu hafua-ti ‘Manhaj Salafiyyah’ kwa maana hafuati mwenendo wa wema wal-iotangulia. Kama usalafi ni njia, kwa nini wanasunnah ambao wote wanajinasibu kufuata njia

hiyo wabaguane? Sababu kubwa ni baadhi ya

wanasunnah kuwaona wengine si masalafi wa kweli, hata kuthubu-tu kuwaita watu wa bid’a na kuwakufurisha (Mungu atue-pushe) kwa kuwa tu wanatofau-tiana nao mitazamo.

Ni wazi masalafi wa zama hizi kama zamani wanatofautiana ka-tika jinsi ya kuziendea dalili za kisharia. Masheikh wakubwa wa kisalafi duniani wanatofautiana, lakini hawakufurishani.

Uelewa wetu wa usalafi unaju-muisha masuala mengi ya msingi ambayo hayapewi kipaumbele na makundi ya kisalafi ya leo, ikiwemo msimamo kuhusu mas-uala ya kisasa ambayo watu wema waliotangulia (Salaf Swaalih) wenyewe hawakukumbana nayo.

Mambo hayo ni kama kupiga picha, uraia na kujinasibu kwa

utaifa, kusajili taasisi, kuanzisha na kujiunga na vyama vya kisiasa, kugombea nafasi za kisiasa na ku-piga kura, kuweka fedha benki, kusoma elimu za fani za kidunia na kadhalika.

Masuala haya yametolewa fa-taawa mbalimbali ambazo ni ‘ijti-haadi’ za wanawazuoni wa kisalafi wa leo, hata hivyo kamwe haziwe-zi kuwa ndio msimamo wa ‘Salaf Swaalih’ wa karne tatu njema kwa sababu wao hawakukumbana nayo. Kadhalika, hauwezi kuwa msimamo wa masalafi wote leo.

Jambo jingine lenye athari kubwa kwa Waislamu ni msima-mo wa baadhi ya masalafi kupiga vita Waislamu kusomea fani mbalimbali katika shule na vyuo vikuu kwa madai kuwa hiyo si elimu ya muhimu, kama msima-mo wa Boko Haram, Nigeria. Ma-tokeo yake, wanafunzi wa Kiisla-mu ikiwemo wanaosomea udak-tari wanaacha masomo na kuko-sesha umma wataalamu.

Hata hivyo, masalafi hao wa-naopinga kusomea udaktari, wa-napoumwa nao pia huenda kuti-biwa na madaktari makafiri kati-ka hospitali za makafiri kwa zana zilizotengenezwa na makafiri.

Ukiuliza kwa nini wanaenda, utaambiwa hiyo ni dharura. Kama kutibiwa katika hospitali zisizo za Kiislamu ni dharura kwa nini kusoma elimu ya udaktari pia isiwe dharu-

ncHa Ya KalaMuSHeiKH MuHaMMad iSSa

usalafi usiwagawe Wanasunnah

mtafaruku wa sasa miongoni mwa wanasunnah haukuwepo kabla ya

harakati za kisalafi kushika kasi, kwani wanasunnah wa mwanzo, kama sheikh al amin maftah, sheikh abdallah saleh

farsy, sheikh jabir yusuf katura, na sheikh juma poli hawakujitambulisha

kama masalafi, bali answar sunnah na wakatambuliwa hivyo. INaENdElEa UK 14

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

10 www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

11makala maalum

makala maalum

NA IDDI JENGO

Shukran za dhati anastahiki Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimuendee Mtume wake Muhammad. Katika makala

yetu ya leo tutajadili kwa pamoja dhana ya maandalizi ikiwa ni mada mahsusi tun-apokaribia kuingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Makala yetu itakuwa na dhamira kubwa mbili, moja kuelezea umuhimu wa maandalizi katika jambo lolote na pili kuangalia maandalilizi stahiki kwa ajili ya Ramadhani.

Kila binadamu anahitaji mafanikio ka-tika maisha na katika kila jambo lake, iwe kitaaluma, kisiasa, kiimani, kiuchumi au lolote lile. Kutafuta mafanikio imekuwa ndio kiu ya walimwengu mpaka baadhi ya watu wanatumia njia haramu.

Lakini kiujumla, maandalizi ndio kiini cha mafanikio ambayo mwanadamu ana-hitaji kuyapata., yawe ya binafsi au ya ki-jamii. Katika zama zetu mafanikio hupimwa kwa vipimo tofauti. Wapo wa-nao pima kwa kuangalia kiwango cha uta-jiri, idadi ya watoto, uzuri wa mke au mume, nyumba nzuri n.k.

Kimsingi mafanikio ndio kipimo cha utu wa mwanadamu anayejitambua. Hivyo basi, kwa kuwa msingi wa mafani-kio ni maandalizi, hebu tuone nini maana ya maandalizi na umuhimu wake.

Maandalizi ni matayarisho rasmi anay-oyafanya mtu au jumuiya fulani kabla ya kuliendea jambo ili kupata ufanisi. Kimsingi yapo maandalizi ya muda mrefu, na pili ni maandalizi ya muda mfupi.

Aina ya maandalizi hutegemea uzito na uelewa juu ya jambo linalokusudiwa ku-fanywa. Kukosa uelewa ni jambo la hatari sana ambalo hupelekea maandalizi duni.

Masiku machache yanayokuja umma wa Kiislam unaelekea katika ibada adhimu na nzito ya swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, tukio la kila mwaka la utekelezaji wa nguzo ya tatu ya Uislam, lilikuwapo tangu ilipofaradhish-wa swaumu na ambalo litaendelea ku-wapo mpaka mwisho wa ulimwengu huu.

Ramadhan ni katika kambi maalum za mafunzo zinazofunguliwa kila mwaka, ki-sha zinafungwa. Kutokana na Ramadhan, mwenye kutaka kupata faida hupata faida ndani yake na hula hasara mwenye kutaka kula hasara.

Ramadhan ni chuo maalum cha ma-funzo tulichowekewa na Mola wetu Mtukufu kwa ajili ya kupata mafunzo maalum kwa ulimwengu mzima.

Mafunzo hayo ni mafunzo ya kipindi cha siku ishirini na tisa au thelathini tu, haizidi na kila siku mlango mmoja un-afungwa. Kwa hivyo anayetaka kuwahi na awahi.

Kambi hii maalum ya mafunzo ni ras-mi kwa umma wa Kiislam na inatupasa kuukaribisha mwezi huu kwa shauku na moyo mkunjufu, kwani ndani yake mna kheri nyingi sana, na Allah husamehe madhambi kama tukiepuka yale makubwa.

Kutokana na manufaa mengi yaliyomo ndani ya mwezi huu, Mtume wetu mtuku-fu (Rehma na amani ziwe juu yake) alikuwa akiusubiri kwa hamu kubwa.

Huyu ni Mtume wa Allah (Rehma na amani zimshukie) aliyekwisha samehewa madhambi yake yaliyotangulia na yale yaliyofuatia. Mtume aliyekabidhiwa fun-guo zote za hazina za ardhini.

Dhana ya maandalizi kuelekea Ramadhan

Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) alikuwa mara unapoingia mwezi huu akiikaza barabara nguo yake ya chini (saruni) na nyakati za usiku akiwaamsha watu wake ili wajishughulishe na ibada na hii ni kwa sababu alikuwa akiujua vizuri utukufu wa Mola wake na alikuwa akiita-mbua vizuri zawadi aliyowatayarishia waja wake wanaoshindana katika kufanya mema ndani ya mwezi huu.

Imepokelewa kuwa maswahaba (Mun-gu awaridhie) walikuwa wakimuomba Mola wao kabla ya Ramadhan kwa miezi sita ili awawafikishe kuufikia mwezi huu, na baada ya kumalizika mwezi wa Ramad-han walikuwa wakiendelea kumuomba

Allah kwa muda wa miezi sita mingine ili azikubali amali zao njema walizofanya ndani yake na ili awaghufirie madhambi yao.

Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mwezi ambao ni hifadhi na kinga nzito ya kumuepusha mja na adhabu kali ya moto. Atakayefunga siku moja katika mwezi huo akitaraji kupata radhi za Allah Ta’ala na ikiwa hiyo itakuwa ndio siku ya mwisho ya maisha yake, basi ataingia peponi.

Swaumu ya mwezi wa Ramadhan ni miongoni mwa nguzo za Uislam na ndani yake kunapatikana usiku mtakatifu ambao ni bora kuliko miezi elfu moja.

Katika mwezi huu, milango ya pepo

huwa wazi, milango ya moto hufungwa na mashetani hufungwa minyororo.

Pamoja na kufahamu fadhila zote hizo zinazopatikana ndani ya mfungo wa Ram-adhani, moja ya jambo la hatari kwa zama zetu ni kuibuka mambo mabaya ambayo yanaelekea kuwa mazoea yanayopendwa na kupata wafuasi wa kutosha, hususan katika umma Kiislamu.

Hatari ya mambo hayo ni pale yana-poambatanishwa kama kianzio katika kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan. Yaani, badala ya watu kujiandaa kwa mam-bo mema ya kheri kama kuanza kujifunza kuhusu swaumu na masharti yake, kujizoe-sha kufunga swaumu za Sunnah, zikiwemo

za Jumatatu na Alhamisi na masiku meupe.Kutoa sadaka kwa masikini ili nao wap-

ate maandalizi mazuri ya mwezi huo wenye baraka, na mema mengine ambayo yanap-endeza kwa aliyetuumba; kinyume chake kumekuwa kuna wengi wenye majina ya Kiislam ambao huukaribisha mwezi huu mtukufu kwa kila aina ya maasi kwa jina la ‘vunja jungu’ kama ijulikanavyo katika mae-neo mengi Tanzania.

Jambo hilo sio tu halipo katika dini yetu hii safi na tukufu, bali pia ni jambo ambalo haliwezi kufanywa na Muislam mwenye imani na khofu ya Mola wake na ndio maa-na tukawaita hao wayafanyao hayo kuwa ni Waislam jina.

Katika siku za mwisho ya mwezi wa Shaaban, hususan mkesha wa kuamkia Ra-madhan, watu hao hukusanyana na kufan-ya sherehe kwa kusikiliza nyimbo na kuche-za muziki, kunywa pombe ambayo kama vile kisasi, na kujihusisha na uzinzi kwa kuwa wanaogopa kufanya hayo Ramad-han.

Wale wavuta sigara ambao kidogo wa-nachelea kuvuta katika mwezi wa Ramad-han nao zitavutwa kwa mfululizo, huku wala unga nao wakikomoa kokeini na her-oini bila kusahau wanaoenda pikniki ‘ku-tumbua maraha’.

Watu wanaofanya mambo hayo wan-amkebehi Mwenyezi Mungu na kumfanya

yeye Allah kuwa ni Mungu wa Ramadhan tu! Hawa wamemfanya Mwenyezi Mungu kuwa hana thamani katika miezi kumi na moja iliyobaki.

Kinyume na hao niliowataja hapo juu, wapo wengine ambao wanaukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa ku-nunua mikeka ya kuswalia pamoja na kan-zu na kofia, huku misikiti ikianza kusheheni hadi inakuwa kero badala ya furaha kwa wale wenye kudumisha swala za jamaa kwa miezi yote ya mwaka, kwani hata nafasi za mbele walizozoea kuzipata huwa ni adimu. Hizi ni tabia nzuri na zinapaswa kudumish-wa hata baada ya Ramadhan.

Kwa upande wa wakina dada ambao

walikuwa hawajui hata kuvaa hijabu, basi utawaona wanaanza kununua mitandio ya kujitanda huku soko la kanga nalo likikua. Wale wanaojitahidi zaidi hununua baibui.

Ndani ya baadhi ya nyumba za Waislam utaanza kusikia Qur’an zikisomwa kwenye redio na runinga na miziki ikipungua.

Hayo yote yanafanyika kama ‘heshima’ na ‘taadhima’ kwa mwezi huu. Ila wali-choghafilika ndugu zetu hawa, ni kuwa uelewa huo unamaanisha kuwa katika miezi iliyobaki hawapaswi kufanya hayo.

Ina maana kwamba, uwepo wa Mungu, uwezo wake, nguvu zake na amri zake hazi-na uzito wowote ila Ramadhan tu. Nayo ni dhana potofu. Mungu atuepushe nayo.

Ijulikane kuwa ni wajibu wa kila mwa-najamii linapoonekana jambo lolote ovu na baya kulizuia, kulikemea au kulikasiri-kia, ingawa hili la mwisho la ‘kukasirika tu’ ni katika udhaifu wa imani.

Alah Taala anasema:Na waumini wa-naume na waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika swalah, na hutoa zakaah, na humtii Mwenyezi Mun-gu na Mtume Wake. Hao Mwenyezi Mun-gu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mun-gu ni Mtukufu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima (9: 71).

Vile vile hadith kutoka kwa Mtume wetu mpenzi (Rehma na amani ziwe juu yake) iliyosimuliwa na Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhi za Allah zimshukie) am-baye amesema: Nilimsikia Mtume (Reh-ma na amani zimshukie) amesema:

“Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu basi akiondoe (akibadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni ud-haifu wa Imani” (Muslim).

[email protected] 0714 135 201

Ramadhan ni katika kambi

maalum za mafunzo

zinazo funguliwa

kila mwaka, kisha

zinafungwa. kutokana na

Ramadhan, mwenye kutaka

kupata faida hupata faida

ndani yake na hula hasaRa

mwenye kutaka kula

hasaRa.

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

12

Laana ya aLLah kwa kutokufanyika kazi ya da’awah

Kuonesha uzito wa wajibu wa kufanya kazi ya da’wah kwa Waislamu, Allah

ametahadharisha wasioifanya kazi hii kupata laana kama al-ivyosema katika Qur’an; “Hak-ika wale wafichao yale tuliyoya-teremsha katika ubainifu, baa-da ya kuyabainisha kwa watu katika kitabu, hao ndio waliola-aniwa na Allah na wamelaani-wa na kila chenye kulaani” (2:159).

Na maana ya laana ni ku-fukuzwa au kuwekwa mbali na rehma za Allah (Subhaanahuu wa taala). Matokeo ya kuwekwa mbali na rehma za Allah ni ku-dhihiri kwa maovu na uharibifu katika bara na baharini.

Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) akaweka wazi uzito wa kosa la kutokufanyika da’wah; “Yeyote afichaye elimu ambayo Allah hunufaisha watu kwao katika mambo ya dini, Al-lah atamfunga makongwa ya moto siku ya Qiyama” (Ibn Ma-jah).

Kuwa na Ilmu juu ya Uisla-mu kisha usiifikishe kwa wan-adamu ni sawa na kuificha elimu hiyo. Hivyo, mtu mwenye elimu anawajibika kuifikisha kwa watu kwa kufanya kazi ya da’wah.

Ni Waislamu wangapi wa-naishi na wanadamu wenzao nyumba moja, wanafanya kazi nao ofisi moja, wanauza nao soko moja kisha wasiwafikishie ujumbe wa Allah, lakini waka-wafikishia mambo waliyoyaona katika runinga zao, au waliyo-yasoma katika magazeti au kusikia katika radio zao yasiy-okuwa na manufaa nao? Ku-fanya hivyo ni sawa na kuificha elimu ya Allah kwa viumbe wake, ni khiyana ambayo Allah huilipa kwa kumlaani mtendaji (Allah atukinge na laana).

Nguzo za da’wah:Nguzo za da’wah ni tatu:

Ujumbe unaolinganiwa, Mlin-ganiaji (Daa’i) na wenye kulin-ganiwa. Kila moja kati ya nguzo hizi ina sifa zake, masharti yake na malengo yake.

Ili kufanya kazi ya da’wah ipasavyo yampasa mwenye ku-taka kuifanya kazi ya da’wah kuwa na elimu ya kutosha kuhusu kila nguzo ya da’wah.

Lengo la kazi ya da’wah ni kueneza mafundisho ya Uisla-mu kama yalivyofikishwa na Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ili dini

ya Allah iwe juu na dini za wale waliokufuru ziwe chini.

Kama ni kuwalingania Waislamu, lengo ni kusahihi-sha uelewa wao kuhusu mam-bo mbali mbali ya Uislamu, ikiwemo itikadi (aqidah), kupi-ga vita ushirikina na kupiga vita mambo ya uzushi (bid’a).

Mwana da’wah akifanya hivyo, ataonekana mgeni katika jamii ya leo, siyo tu kwa wasio Waislamu, bali hata kwa Wais-lamu wenzake. Mtume Mu-hammad (Rehma na amani ziwe juu yake) alisema; “Uisla-mu ulianza mgeni na utakuja kurejea mgeni kama ulivyoan-za. Basi hongera kwa wataka-okuwa wageni”.

Alipoulizwa “Ee Mtume wa Allah, hao wageni ni nani? Aka-jibu, “Ni wale watakaokuwa wanatengeneza pindi watu wa-napoharibu (dini) (Tirmidhy).

Lengo la da’wah limeelezwa katika Suurat An-Nahl (16:125): “ Na ita watu katika njia ya Mola wako”. Njia ya Al-lah ni Uislamu kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.

Kwa hiyo inampasa mwenye kutaka kufanya kazi ya da’wah ajiandae kwa elimu ili akifiki-sha basi iwe kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah, tena kwa ufahamu wa wema waliotan-gulia.

Akielezea zaidi aya tuliyoita-ja hapo juu, Sheikh Ibn Baaz (Allah amrehemu) anasema: “Njia ya Allah, Mwenye nguvu, Mtukufu, ni kujisalimisha kwake, ni njia iliyonyooka, ni dini ya Allah ambayo kwayo ali-watuma mitume.

Kwa hiyo hii ndiyo ambayo watu walinganiwe kuiendea, si madhehebu ya mtu fulani au fikra za yeyote …Njia ya Allah ni ile ambayo Qur’an na Sunnah sahihi za Mtume wa Allah zi-namuelekeza mtu.

Ni lazima kwa wafanyao kazi ya da’wah katika Uislamu kuwaita watu kwenye Uislamu kamili na siyo kuibua mita-faruku miongoni mwa Waisla-mu, wala wasiwe wafuatao mi-tazamo ya watu (madhehebu) kibubusa, wala kabila, wala sheikh, wala kiongozi.

Bali lengo lake liwe kuthibit-isha na kufafanua haki na kuwakinaisha watu kuhusu haki hiyo, hata kama kufanya hivyo kutapingana na mtazamo wa fulani na fulani” (Min Aqwaali Samaahat Shaykh Ab-dallah ibn Abdilaziz Fiy Da’wah, uk. 33-35).

Wiki iliyopita tulijifun-za kuwa, kutafuta elimu kuhusu mas-wala ya chakula na

lishe sio uzungu, bali ni katika ma-fundisho ya dini tukufu ya Kiisla-mu.

Wajibu wa kuitafuta elimu hiyo unakuwa mkubwa zaidi wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Mola akipenda.

Hivyo, Waislamu lazima wa-jipinde kuitafuta elimu ya mlo un-aofaa kwa futari na daku katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan ili tuweze kuzitekeleza aya zifuata-zo kwa ukamilifu: “Enyi mlioamini kuleni vizuri tulivyokuruzukuni, na Mumshukuru Mwenyezi Mun-gu, ikiwa mnamuabudu yeye peke yake” (Qur’an: 2:172).

Aya nyingine ni ile isemayo: “Na kuleni katika vile alivyokuruzuku-ni Mwenyezi Mungu vilivyo vizuri na halali na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye nyinyi mnamwa-mini (Qur’an: 5: 88).

Zaidi ya hayo, kujifundisha elimu ya mlo unaofaa wa futari na daku kutatuwezesha kufikia lengo la ujenzi na uimarishaji wa afya ya miili yetu kwa kupitia swaumu kama tulivyohimizwa na Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) katika hadith ifuatayo: “Fungeni mtapata siha (afya)”.

Ili mtu awe na nguvu na afya katika mwezi wa Ramadhan na baada ya hapo, lazima azingatie uchaguzi wa vyakula. Mtu ajitahidi kula chakula kutoka mafungu makuu yafuatayo: (a) mkate na nafaka (b) maziwa, nyama, sa-maki, kuku, maharage, (c) matun-da na (d) mboga za majani.

Mlo katika mwezi wa Ramad-han usitofautiane sana na milo ya nje ya Ramadhan. Mlo katika mwezi wa Ramadhan uwe wa hali ya kawaida, sio wa kifahari sana.

Vyakula vinaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili kwa kigezo cha muda wake wa ku-kaa tumboni. Kundi la kwanza ni vyakula vinavyo chukua muda mfupi, saa 3 mpaka 4 kusagwa. Mfano wa vyakula hivyo ni kama ndizi, viazi na vyakula vitamu (mfano: tende, matunda).

Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ametuhimiza sana tufuturu kwa kutumia tende. Kama umekosa tende, tumia maji. Baada ya kufu-turu, kula mlo wako, lakini uzinga-tie yanayoelezwa katika makala hizi. Tende ina sukari aina ya glu-cose kwa wingi ambayo hutumika kwa urahisi mwilini.

Kundi la pili la vyakula kwa kig-ezo cha muda wa kukaa tumboni

ni vyakula vinavyokaa tumboni kwa muda mrefu (kiasi cha saa 5 mpaka 8). Mfano wa vyakula hivi ni nafaka na mbegu – ngano, sha-hiri, mtama, mahindi, mchele na maharage.

Vyakula kama hivi viliwe kama daku au usiku sana kwa wale wa-naoshindwa kuamka na kula daku. Vyakula hivi vitawapa nguvu ya kuhimili mikiki mikiki ya swaumu mchana na pia wataweza kumudu majukumu mengine ya kazi za mchana.

Vyakula vya kukaanga, vyilivyotiwa viungo vin-gi na vyenye sukari na chumvi nyingi ni hatari

kwa afya, kwani husababisha kiun-gulia, gesi tumboni na uzito mkubwa. Mboga za majani na ma-tunda ni muhimu sana ili kupun-guza gesi tumboni, hasa kwa mfungaji.

Vilevile, ni muhimu sana kunywa maji safi na salama ya ku-tosha usiku wote wa Ramadhan ili kupunguza hatari ya mwili kukaa muda mrefu bila maji ya kutosha. Maji huondoa sumu kutoka katika mwili.

Hata hivyo, sio vizuri mtu kunywa chai au kahawa wakati wa kula mlo wa daku. Hii ni kwa saba-bu chai au kahawa hutengeneza mkojo mwingi, hivyo maji na madini yatapotea kwa njia ya mko-jo kunapo kucha.

Vilivile, milo yote wakati wa Ra-madhan isiwe na chumvi nyingi

kwa sababu mchana utakuwa na kiu sana na utapoteza maji kwa njia ya mkojo.

Ndizi ni nzuri kwa futari kama tulivyosema hapo juu, hata hivyo ndizi zinaweza kusababisha mlaji kukosa choo kikubwa. Ili kuepuka hilo, ni bora ndizi ziliwe na mboga za majani na matunda kama pa-pai.

Zaidi ya hayo hakuna haja ya kula sana wakati wa kufuturu, mlo wa usiku au mlo wa daku. Tabia ya kula sana ni kinyume cha ma-fundisho ya Qur’an na Sunna.

Qur’an inasema “......Na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri). La-kini msipite kiasi tu. Hakika yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao kiasi” (7:31).

Pia, ukila sana wakati wa Ram-adhan (na miezi mingine pia) mwili utashindwa kukitumia chakula kilichohifadhiwa. Mtu ak-iwa amefunga mwili wake unatu-mia chakula kilichohifadhiwa kama mafuta mwilini mwako. Mchana wa swaumu unakuwa na nguvu za kufanya kazi na unakuwa na afya imara.

Mafuta ya ziada yanapotumika wakati huu wa swaumu, mwili unanusurika na maradhi mengi ikiwemo moyo, presha, uzito mkubwa, kiharusi na kansa.

Na hapa ndipo tunapopata ya-kini ya ukweli wa maneno ya Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake): “Fungeni mtapata afya”.

mLo BoRa kwa mfunGaji Swaumu ya Ramadhan – 2

Pazi MwinyiMvuaafya yako

IlI mtu awe na nguvu na afya katIka mwezI wa

Ramadhan na baada ya hapo, lazIma azIngatIe uchaguzI wa vyakula. mtu ajItahIdI

kula chakula kutoka mafungu makuu yafuatayo:

(a) mkate na nafaka (b) mazIwa, nyama, samakI, kuku, mahaRage, (c) matunda na (d)

mboga za majanI.

MliNgaNiajiSHEiKH MuHaMMaD iSSa

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

13

Sh u k ra n i n a u t u k u f u n i wake Mfalme wa mbingu na

ardhi a l iye pekee , mw e ny e k u s t a h i k i kuabudiwa kwa haki. Sala na salam zimfikie Mtume aliye msifika, mjumbe wa Allah na re-hma kwa walimwengu wote. Kisha salam kwa wanaofuata muongozo.

Ndugu mpenzi mso-maji na mfuatiliaji wa safu hii juu ya uchumi na biashara katika mti-zamo wa Kiislamu kari-bu tena kwa mara ny-ingine katika mfululizo wa makala zetu.

Katika makala zetu za matoleo yaliyopita

tulidurusu aina mbalim-bali za ushirika, ikiwa ni namna ya kufanya bi-ashara na kuwezesha kujenga uchumi usio-jikita katika riba na w e n y e k u z i n g a t i a

Watu maarufu WasiokuWa Waislamu waseMavyo kuhusu uislaMu

maadili. Katika makala yetu hii ya leo, pia tutatizama namna nyingine ya kufanya biashara bila riba na kuzingatia maadili.

Napenda kusisitiza kuwa, moja ya kanuni ya msingi ya mfumo wa fedha wa Kiislamu

ni kuunganisha fedha na rasili-mali au bidhaa badala ya kufan-ya fedha yenyewe kuwa bidhaa.

Namna nyingine ya kufanya biashara katika utaratibu wa Kiislamu inaitwa ‘Ijarah’.

Ijarah ni mkataba wa kuko-disha rasilimali fulani kama vile gari au nyumba kwa malipo ya kodi, ambapo anaye kodisha hubakia kuwa mmiliki na anayekodi hunufaika kwa ma-tumizi ya rasilimali hiyo. Anaye-kodisha anatakiwa amiliki kwanza rasilimali hiyo kwa kui-nunua au kujenga au kwa nam-na nyingine inayokubalika kisharia kabla ya kukodisha.

Pia atawajibika kuihudumia kwa huduma zinazostahiki kwa nafasi yake kama mmiliki. Kwa upande mwingine, anayekodi anatakiwa kuitumia rasilimali

hiyo kwa matumizi yaliyoku-baliwa katika mkataba na kui-tunza.

Mkataba huu pia huweza kutumiwa na taasisi za kifedha katika kuwawezesha wateja wake ambao wanahitaji rasili-mali fulani katika biashara zao au matumizi mengine.

Taasisi ya fedha kama benki inaweza kununua rasilimali Fu-lani, kisha kuwakodisha wateja wake kwa kipindi maalum, na hivyo kunufaika na kodi am-bayo ni njia mbadala ya pato la benki lisilo tokana na riba.

Lakini taasisi za fedha nyingi kama benki ni kiungo baina ya wanaoweka akiba na wa-naowekeza. Hivyo basi, taasisi hizo zinatakiwa zisiwe mshirika wa kudumu au kujishughulisha katika miradi mingi ya kudumu ambayo itaifanya ishindwe ku-fanya kazi yake kuu.

Hivyo, kama ilivyo kwenye ushirika (Mushaarakah) am-bapo kunakuwa na ushirika wa kupungua mpaka benki inajitoa katika umiliki, kadhalika katika ‘Ijarah’ benki inaweza kuhami-sha umiliki baada ya mkataba kuisha. In sha Allah tutadurusu hilo katika makala ijayo.

[email protected] +255713 996 031

Dkt Idris Rashid, mkurugenzi wa benki ya Amana.

moja ya kanunI ya msIngI ya

mfumo wa fedha wa kIIslamu

nI kuunga nIsha

fedha na RasIlImalI au bIdhaa badala ya kufanya

fedha yenyewe

kuwa bIdhaa.

MIchAel h. hARt, mWansayansi Wa anga za juu (astro-physists) mmareka-ni, muasisi Wa mpan-go Wa vitabu katika mtandao (ebooks)

My choice of Muhammad to lead the list of the world’s most influential persons may surprise some readers

and may be questioned by others, but he was the only man in history who was supremely successful on both the reli-gious and secular level

Tafsiri: “uchaguzi wangu kumchagua muhammad kuongoza orodha ya watu muhimu zaidi duniani unaweza kuwashangaza baadhi ya wasomaji na kuhojiwa na wengine, lakini alikuwa mtu pekee katika historia aliyefanikiwa sana katika kiwango cha dini na dunia”. (Michael h. hart, “The 100:a Ranking of the Most influential Persons in history)

ijarah: mkataba wa kukodishana kwa malipo ya kodi

uchumi na biashara JaMaL iSSa

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

14

ra? Sasa inapo-tokea wanawazuoni wa kisalafi wa leo wakatofautiana, kwa nini baadhi wachukue misimamo ya kuwaku-furisha wengine kwa mambo yanay-ohitaji ‘ijtihaadi’ za wanawazuoni?

Tatizo kubwa ni kujitakasa nafsi zetu (Tazkiyatu-nnafsi) kunakopele-kea kuwaona wengine si masalafi wa kweli au hata si masalafi kabisa.

Tatizo jingine, ni kujikita katika kufukua mabaya ya wengine (Al jarh wat-ta’diyl) kiasi kwamba hakuna aliyesalimika sasa. Badala ya kujikita katika kuzitakasa nafsi zetu dhidi ya makosa yetu wenyewe twajikuta tukitakasa nafsi zetu na makundi yetu dhidi ya wengine.

Tatizo letu jingine, ni kuwa-chukulia Waislamu ambao bado ha-wajashika mwenendo wa kisalafi kama makafiri. Mtazamo huu un-azalisha kibri na kujiona (Al-ujub),

hususan kwa vijana wa kisalafi am-bao hawajakomaa kielimu, hali iliyo-sababisha kuwa mahiri katika kuko-soa makosa ya wengine na kutumia muda mwingi kuwatafuta wenye kukosea kuliko kutafuta elimu ya kujua yaliyo sahihi katika usalafi.

Utakuta kijana mbichi katika us-alafi akihifadhi majina ya masheikh‘wapotofu’ alioambiwa kuwa hawa hawako katika ‘manhaj ya salaf ’ na orodha ya masheikh wa kisalafi wanaokubalika. Huu ni msi-ba mkubwa. Tatizo jingine, ni utii wa moja kwa moja kwa masheikh wakubwa ambao hututolea fataawa. Yaani akisema sheikh ndiyo basi. Uislamu haufundishi utii wa moja kwa moja kwa binadamu mwingine

ila kwa mitume tu. Lakini leo in-aibuka misimamo mikali ya ta’subi si za kimadhehebu, bali kwa masheikh tuwapendao. Hata mtu apewe hoja yenye mashiko, hakiuki msimamo wa sheikh wake.

Kibaya zaidi usalafi huu wa sasa umeshachukua msimamo wa kitai-fa, huku baadhi wakifuata wanawa-zuoni wa Saudia, wengine wa Yemen nk. Tofauti za kisiasa za nchi za Kiis-lamu zimeingia hata kwenye misi-mamo ya kisalafi ya leo.

Jambo jingine, ni hili la masalafi wa leo kunyamaza kimya kuhusu watawala. Sheikh Ibn Taymiyyah ali-wakosoa sana watawala, kinyume na masalafi wa leo walioshupalia ku-kosoa masheikh wa kisunnah tu.

Imekuwa kama alama ya usalafi ni kunyamaza hadi baadhi ya wata-wala wanawaona masalafi kama masufi tu, wasiojishughulisha na dunia inayowazunguka.

Ndugu katika imani, tukumbuke kwamba, harakati za makundi ya kisalafi kama harakati nyingine za kibinadamu hazikosi upungufu na hata makosa. HiIi haifanyi usalafi uwe jambo baya. Kukosea ndio uka-milifu wa ubinadamu.

Makosa ya makundi ya kisalafi si makosa ya‘Manhaj Salafiyyah’, bali ni makosa ya binadamu wanaotu-mika kama nyenzo ya kufikisha manhaj hiyo. Ushahidi ni kuwepo mitazamo mbalimbali ya kisalafi; na bila shaka hakuna kundi lenye hati-

miliki ya usahihi mia kwa mia.Harakati za kisalafi zina mengi

mazuri si tu kwa Waislamu, bali wa-nadamu wote, lakini makosa hay-awezi kukosekana. Je haiwezekani kufifisha tofauti zetu na kuacha ku-shambuliana, ili tuelekeze nguvu zetu kwenye mambo ya msingi kwa maslahi ya Uislamu?

Kama masalafi hawatahisi cho-chote ndani ya mioyo juu ya madhila yanayowafika Waislamu ingawa ni watu wa bid’a, na badala yake kufu-rahia, ni taswira gani ya usalafi tuna-ijenga kwa Waislamu?

Masalafi wanao mchango mkubwa katika kusahihisha itikadi potofu, lakini ni vema tuelewe peke yetu hatuwezi kujitosheleza kwa kila kitu; na umma unahitaji kufikishi-wa. Tutawezaje kufikisha kwa watu ambao daima twawaona hawafai kutukaribia au sisi kuwakaribia?

swali: aliulizwa Sheikh Mu-hamad bin Ibrahim Alu Sheikh Allah amrehemu: Ni upi muda wa hedhi?

jawabu: Uchache wa hedhi ni usiku na mchana, na wingi wake ni siku kumi na tano. Lakini kauli yenye nguvu zaidi inaeleza kuwa hedhi haina muda maalum wa wingi wala uchache, kwani haku-na ushahidi wa wazi katika hilo. Na hili ndio chaguo la Sheikh Ta-qiyyud din (Allah amrehemu) [Fatawa warasailu Sheikh Muha-mad bin Ibrahim Alu Sheikh 2/97].

je kiwango cha chini na cha juu cha hedhi kinatambu-lika?

swali: Aliulizwa Sheikh Mu-hamad bin Swaleh Al-uthaymin (Allah amrehemu): Je kiwango cha chini na cha juu cha hedhi ki-natambulika kwa masiku?

jawabu: Kwa kauli sahihi, wingi wa hedhi au uchache haufa-hamiki kwa masiku. Allah anase-ma katika Qur’an: “Na wanaku-uliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wa-nawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wataharike” (2: 222). Allah hajaweka zuwio ukomo kwa siku maalum, i s i p o k u w a z u w i o u k o m o limewekwa kwa kutwaharika.

Na hapa ndipo tulipofahamu kuwa sababu ya hukumu ni kuwe-po au kutokuwepo kwa hedhi. Wakati wowote itakapopatikana hedhi, hukumu itathibiti, na wakati wowote atakapotwaharika hukumu itatoweka.

Ama suala la umri, kikomo na muda halina ushahidi, pamoja na kuwa kidharura ni jambo linalohi-tajia ufafanuzi. Na lau kama suala la umri kikomo au muda lingeth-ibiti kisharia, lingebainishwa kati-ka Qur’an na Sunnah za Mtume.

Na kwa kulizingatia hilo, damu yoyote atakayoithibitisha mwan-amke kuwa ni hedhi, basi hiyo ni hedhi, bila ya kuikadiria na muda maalum. Isipokuwa kama damu itaendelea kwa mwanamke na bila ya kukatika, au itakatika kwa muda mchache, kiasi cha siku au siku mbili katika mwezi, hapo ita-hesabika kama damu ya ujusi. (Fatawa na rasailu za sheikh ibn Uthaimin 4/271).

hedhi baada ya miaka 50

swali: Aliulizwa Sheikh Mu-hamad bin Ibrahim Alu Sheikh (Allah amrehemu): Ni ipi huku-mu ya hedhi baada ya miaka 50?

jawabu: Kauli sahihi ni kuwa hedhi haifungwi kwa miaka ham-sini. Isipokuwa muda wowote damu ikiendelea kutoka, kwa sifa na mpangilio wake, hiyo ni hedhi.

Ama hedhi ikipoteza mpangilio baada ya umri huo, haitozingati-wa kuwa ni hedhi, bali itazin-gatiwa kuwa ni damu ya ujusi.

Na neno la Bi Aisha (Allah amridhie): “Mwanamke atakapofikisha miaka hamsini hutoka kwenye ukomo wa hedhi” (Ahmad). Habari ya Bi Aisha inaa-shiria wingi wa ukomo wa he-dhi huwa ka-t i k a u m r i huu, au imeta-jwa kwa kuchun-g a m i s i n g i y a kisharia, kwani kia-sili masuala yanayo-husu aina mbalimbali za damu ni ya kimaumbile kama hakuna dalili inay-oitoa katika kundi la damu. (Fatawa na rasailu za Sheikh Muhamad bin Ibrahim 2/96).

ikipatikana damu kwa vig-ezo baada ya miaka 70

swali: Aliulizwa Sheikh Ab-dur Rahmani Assa’adiy (Allah amrehemu): Mwanamke ana-pofikisha umri wa miaka sabini na damu yake ikaendelea katika ka-waida yake, je ataketi?

jawabu: Mwanamke aliye-fikisha umri wa miaka 70 na damu haijasita na inaendelea kumtoka, mwanamke huyo atasimama kuendelea na ibada kwani sahihi ni kuwa, hedhi haina ukomo kwa mtu mwenye umri mdogo au umri mkubwa, na kihukumu hii ni

damu ya hedhi kwa nyanja zote.[ Al-maj-mua’tul kamilah limual-

lafaati Sheikh Ibn Sa’ad 7/98].

Mwanamke ana miaka hamsini na mbili, ndani ya kiasi cha siku tatu, humjia

damu kwa nguvu

swali : Al-iulizwa Sheikh

Abdul Aziz b in Baz: Kuna mwa-

namke ana umri wa miaka

52. Ndani ya siku tatu, hutokwa na

damu kwa nguvu, na siku zinazosalia ka-tika mwezi damu huto-

ka kwa wastani. Je damu hii inazingatiwa kuwa ni

damu ya hedhi, hasa ikizin-gatiwa yeye ana umri zaidi ya

miaka 50 na tukizingatia baadhi ya wakati damu humjia baada ya mwezi, miezi miwili, au miezi mi-tatu. Je ataswali faradhi wakati damu inamtoka? Na je ataswali swala za sunna na zile swala za usiku?

jawabu: Mwanamke kama huyu anatakiwa aizingatie damu hii iliyompata kuwa ni damu ya ujusi kwa umri wake na kukosa kwake mpangilio. Hali halisi inay-ofahamika kutoka kwa Bi Aisha, kuwa mwanamke akifikisha umri wa miaka 50, damu ya hedhi hu-katika na hukoma kupata mimba. Kupata damu bila ya mpangillio, na umri wake ni dalili ya kuwa

hiyo si hedhi na analazimika kuswali na damu hiyo itahesabika kama damu ya ujusi ambayo haimziwii kuswali wala kufunga, wala haimzuwii mume wake ku-muingilia. Kwa kauli sahihi zaidi za wanazuoni, analazimika kuta-wadha katika kila swala na atajihi-fadhi kwa pamba, au kwa namna nyingine, kama alivyosema Mtume kwa mwanamke mwenye damu ya ujusi: “Tawadha kwenye kila swala”. (Imepokewa na Bukhari) (Kitabu fataawad Da’awah cha sheikh Ibn Baz 2/72).

Mwanamke mmoja zaidi ya miaka 50 hupata hedhi kwa utaratibu uliozoeleka na mwingine hupata kwa utaratibu usiozoeleka

swali: Aliulizwa Sheikh Mu-hamad bin Swaleh Al-uthaimin (Allah amrehemu): Kuna mwan-amke ana miaka zaidi ya 50 na hupata hedhi kwa utaratibu ulio-zoeleka na kuna mwingine hupata hedhi kwa utaratibu usiozoeleka, isipokuwa huona rangi ya man-jano au hudhurungi?

jawabu: Mwanamke anaye-pata hedhi katika utaratibu ulio-zoeka, kwa kauli sahihi ya wana-zuoni, damu yake itakuwa ni damu ya hedhi kwa sababu haku-na umri kikomo katika suala la he-dhi. Na kwa hivyo, damu yake ita-chukuwa hukumu maarufu za damu ya hedhi, ataacha kuswali, kufunga, kukutana na mumewe na atalazimika kuoga na kulipa funga nk.

muda, uchache na winGi wa hedhi

fat-Wa kWa MwaNaMke wa kiislaMSHEiKH SHabani MuSSa

Kutoka kwa Kha’lid Al-ahmara alisema, “Aliulizwa Abdillahi ibn Hassan (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuhusu Abu Bakr na Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) akasema: “Allah awape amani na asimpe amani yule asiyewapa wawili hao amani” (sherh usuuli i’tiqaad ahlu s-sunnah, Mjalada wa 7 uk. 1381).

AlI (r.a) ANA-VYOWA-ZUNGUMZIA ABUBAKAR, UMAR NA Uth-MAAN (r.a):

INAtOKA UK 9

usalafi usiwagawe wanasunnah

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

15

kuelekea uchaguzi 2015 na yuSuFu aHMaDi

Wakati fulani, Tanzania ilitaka kujiunga na taasisi ya kiisla-

mu ya kimataifa ya OIC, jam-bo ambalo lilipelekea kam-peni kali ya kuzuia jambo hilo kutoka kwa makanisa. Hili ni suala la uhusiano wa kimatai-fa ambalo kama Waislamu tunapaswa kuwahoji wago-mbea mbalimbali wa nafasi za urais wanaojitokeza hivi sasa.

Katika nchi zilizoendelea, moja ya mambo muhimu ambayo wapiga kura wengi wanayaangalia wanapowap-ima wagombea waliojitokeza kuwania nafasi kubwa kama ya urais au uwaziri mkuu huwa ni sera zake kuelekea mataifa ya nje (Foreign poli-cies).

Wengi wa wapiga kura na wachambuzi humtathmini kwa kina mgombea na sera zake jinsi atakavyoshirikiana na mataifa ya nje, na pia atakavyokabil iana na changamoto mbali mbali zil-ioko nje ya taifa lao ili mradi tu wanaona zinaathiri maen-deleo yao.

Japo kila nchi huwa na sera zake maalum za nje zili-zoandikwa kama ilivyo hapa nchini kwetu, ila kwa baadhi ya nchi kubwa za wenzetu, mgombea nae huwa ananadi sera zake kuelekea mataifa ya kigeni.

Mfano, wakati Rais wa Marekani Barack Obama anawania nafasi hiyo kwa mara ya kwanza, moja ya sera zake kuelekea mataifa ya nje ilikuwa ni kurejesha uhu-siano ulioharibika baina ya taifa lake na ulimwengu wa Kiislam.

Jambo ambalo alilifanya muda mfupi mara baada ya kushika nafasi ya Urais kwa kwenda nchini Misri katika chuo kikuu cha Al-Azhar na kuhutubia mataifa ya ulim-wengu wa Kiislam, japo maneno ya hotuba hiyo na matendo ya nchi yake ni sawa na bure.

Hivyo ndivyo ilivyo desturi ya wagombea wa mataifa hayo, kwani bila kueleza kwa ufasaha sera zako kuelekea mataifa ya kigeni itakuwa vigumu sana kushinda nafasi kubwa kama ya Rais, kwani sera hizo zina nafasi yake ka-tika maendeleo.

Tuje hapa nchini kwetu, kwa sasa watanzania wa-naendelea kushuhudia mbwembwe, vituko na vim-

bwanga vya watangaza nia ya kugombea nafasi adhimu na kubwa katika Urais kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kila mtangaza nia ame-jaribu kusema kile ataka-chowafanyia watanzania en-dapo atapitishwa na chama chake na kisha kupigiwa kura katika uchaguzi mkuu wa hapo Octoba 25 mwaka huu na kushinda.

Yapo mengi ambayo yamesemwa na watangaza nia hao katika sera zao mbali mbali, lengo likiwa ni kuush-awishi umma wa Tanzania uwapigie kura .

Lakini kwa bahati mbaya au vinginevyo, takriban wa-tangaza nia hao hakuna hata mmoja aliewaelezea watan-

zania sera zake kuelekea mataifa ya kigeni.

Kama nilivyoeleza hapo juu, sera hizi kwa wenzetu ni muhimu sana, kwani zina-bainisha namna gani taifa lao litakavyo kuwa na muin-giliano na mataifa ya nje ka-tika nyanja mbali mbali.

Na kwa dunia ya sasa iliyo katika mfumo wa kibepari unaosimamiwa na nchi za Magharibi, huwezi ukazun-gumzia na kuandaa mikaka-ti ya jinsi ya kuzitatua changamoto za nchini kwa-ko bila kuwa na mikakati ya namna ya kushughulikia masuala mengine yalioko nje ya taifa lako.

Mfano, katika hawa wa-tangaza nia wetu, yupo mgo-mbea mmoja amesikika ak-

isema yeye ataendesha nchi katika misingi ya ujamaa, japo hautakuwa sawa na ule wa Mwalimu Nyerere.

Ila katika maelezo yake juu ya sera hiyo, mtangaza nia huyo hajawaambia wa-tanzania jinsi atakavyoweza kupambana na wanakide-dea wa ubepari katika sera zake kuelekea mataifa hayo ya magharibi.

Inafahamika wazi kwa dunia ya sasa kujitangaza wewe ni mjamaa hiyo tayari ni vita tosha, je, kajiandaa vipi dhidi ya hilo?

Mwingine anasema kuwa, atalifanya taifa hili liwe la viwanda na uchumi wa kati, ukiangalia mikakati atakayotumia inajionesha kabisa ni ya ndani ya nchi tu, pasina kuonesha mikakati ya nje.

Nae huyu ilibidi awaam-bie Watanzania, ni mikakati ipi ameandaa dhidi ya mataifa ya kigeni ili kuhak-ikisha anadhibiti ongezeko la bidhaa kutoka nchi za nje ambazo kwa kiasi kikubwa ndio zimechangia kuua vi-wanda anavyovililia yeye.

Leo, hii hata vijiti vya ku-chokonolea meno (Tooth-pick) katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu vinatoka nchini China wakati nchi yetu ina misitu y akutosha, je, sera zake ni zipi katika ku-kabiliana na hili janga.

Siku za hivi karibuni, tu-mekuwa tukimsikia Rais

Mstaafu wa Tanzania, Ben-jamin Mkapa akilalamika na kuwaasa viongozi wa Af-rika kuwa makini na mkata-ba wa ushirikianao wa kiu-chumi (EPA) ulioandaliwa na wazungu kuwa ni wak-inyonyaji kutokana na yaliy-omo ndani yake.

Hapa watanzania hawa-na budi kuwauliza watanga-za nia hao, mambo kama haya ya mikataba wanayajua vema, na kama ndio sera zao zinasema nini kuhusiana na mambo hayo kutoka kwa wenzetu wa huko ughaibuni ambao kwa kiasi kikubwa wana athari katika maen-deleo yetu.

Huyo alikuwa ni wa vi-wanda, mwingine yeye anasema ataendesha nchi kwa kutumia gesi tu ya Mt-wara, hapa alitakiwa awaambie watanzania ni sera gani kuelekea mataifa ya nje zitakazomsaidia kuk-abiliana na mashirika makubwa duniani ya kibi-ashara (Multinational cor-porations) ambayo nayo yamekuwa yakilalamikiwa kunyonya rasilimali za nchi m a s i k i n i , Ta n z a n i a ikiwemo.

Watanzania lazima waelewe kuwa kwa ulim-wengu wa sasa ulioko katika mfumo wa utandawazi hu-wezi ukampima mgombea wa nafasi kubwa ya Urais kwa kuangalia sera zake za ndani tu.

lakInI kwa bahatI mbaya

au vIngInevyo, takRIban

watangaza nIa hao hakuna

hata mmoja alIewaelezea

watanzanIa seRa zake kuelekea

mataIfa ya kIgenI.

watangaza nia watuambie na sera zao za nje

Stephen Wassira

Dkt John Magufuli

Dkt Mohammed Gharib Bilal

Frederick Sumaye

edward lowassa

Balozi Ali Karume

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

16 makaLa

na KHaLiD OMaRy

Vyombo vya habari hapa nchini vimekuwa na mchango mkubwa katika kuihudumia jamii kwa ku-

toa habari mbali mbali zinazoelimi-sha, kuburudisha na kuhabarisha, in-gawa kumekuwa na mbinu nyingi za kudhoofisha harakati zinazofanywa na vyombo hivyo.

Kwa hapa nchini, vipo vyombo mbali mbali vya habari vya kidini na visivyo vya kidini. Lengo langu ni ku-

vizungumzia hivi vya kidini, hu-susan vya Kiislamu, wamiliki na waendeshaji wake kwa ujumla.

Kabla sijaingia kwenye maudhui ya makala, hadi sasa, kuna vyombo vya habari vya Ki-islamu ikiwemo redio, magazeti na runinga visivyozidi 20, idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na vile vya Kikristo.

Katika utafiti wangu mdogo nilioufanya, hasa baada ya mi-jadala mikubwa ya sheria mbalimbali zinazoathiri fani ya habari hivi karibuni, baadhi ya wamiliki ama waendeshaji wa vyombo vya Kiislamu wal-ishindwa kunipa ushirikiano, jambo ambalo linaonesha ha-wafuatilii masuala ya siasa na ya kijamii.

Miswada na sheria hizi mbalimbali zinagusa wadau wa habari moja kwa moja, wak-iwemo wamiliki na waandishi, hivyo ilitegemewa viongozi hawa wa vyombo vyetu vya Kiis-

lamu wangekuwa na uelewa wa kuto-sha kuhusiana na sheria hizo.

Sheria ambazo zinaweza kuathiri vyombo vya habari zilizopitishwa hivi karibuni ni pamoja na ile ya makosa ya mtandao na ile ya takwimu.

Kadhalika, mswada mwingine ambao huenda ukajadiliwa na kupit-ishwa hivi karibuni ni ule wa huduma za vyombo va Habari.

Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari una mambo yanayowahu-su wamiliki wa vyombo vya habari, waandishi wa habari pamoja na wale wanaofanya kazi za uandishi kwa kuchangia kuandika makala kwenye magazeti.

Lakini katika muswada wote wa sheria hiyo mambo kadhaa yaliweza kuvuta na kugonga vichwa vya habari nchini.

Moja kati ya hayo ni kutoka kwenye

wanahabari wa kiislamu tufuatilie siasa za nchi

kipengele cha 14 (b)(iv) kina-choelekeza chombo chochote cha habari binafsi kujiunga na shirika la umma kwa ajili ya taarifa ya habari ya kila siku ya saa mbili usiku.

Ni kweli kuwa sio lazima uwe mwandishi au mtangazaji ndiyo uwe mmiliki au muende-shaji wa chombo chochote cha habari kiwe cha Kiislamu au kisicho kuwa cha Kiislamu, la-kini kwa kuwa unaendesha chombo cha habari nawe una-takiwa ufuatilie masuala ya ki-habari, ikiwemo sheria zinazo-athiri habari.

Miongoni mwa niliozun-gumza nao kwa ajili ya kupata mawazo yao juu ya muswada huo alikiri kuwa hafahamu chochote kuhusu muswada huo.

Haishangazi kuwa ukimu-ul iza mwanahabar i au mwendeshaji wa chombo cha habari cha Kiislamu kuhusu mambo yanayoendelea bun-geni ambayo yana athari kwa Uislamu asijue chochote, huku akisahau kuwa haya yanayo-tekelezwa leo ambayo tunay-alalamikia ni matokeo ya sera

zilizopangwa jana. I n a w e z e k a n a k a m a

kungekuwa na chombo kimoja kinachowaunganisha waende-shaji wa vyombo vya habari vya Kiislamu kusingekuwa na sin-tofahamu kama hii.

Hii ni kwa sababu dini ya Uislamu ina mafundisho yake ambayo hayaendani na mifu-mo ya uendeshaji wa vyombo visivyo vya Kiislamu kwa saba-bu mbali mbali.

Kwa mfano, vyombo vya Ki-islamu haviwezi kutoa picha inayoonesha maumbile ya mwanamke katika hali yoyote ila awe amejisitiri.

Moja ya mambo ambayo yanaonyesha kuwa baadhi wa-miliki ama waendeshaji wa vy-ombo vyetu vya Kiislamu ha-wapo makini katika kazi zao na kusahau kuwa hiyo ni taaluma nyeti kabisa hapa ulimweguni ni lile nililokutana nalo katika kituo kimoja cha redio.

Nilipotembelea chumba chao cha habari wakati waki-andaa taarifa ya habari ya mchana, nilikuta watangazaji na waandishi waliokuwepo wakinakili habari kutoka

kwenye magazeti mabalimbali ya kila siku na kuzigeuza katika mfumo utakaoweza kusomwa kama taarifa ya habari ya kwenye redio.

Hali ile ilinistaajabisha na kuniacha nikiwa nimepigwa na butwaa na kujiuliza maswali mengi huku nikikosa majibu.

Kwakweli jambo hilo linak-iuka misingi ya habari, haliku-paswa kutendwa na chombo hicho cha Kiislamu. Au ndio rasilimali fedha za kutuma waandishi kutafuta habari hamna? Kwa hali hii tutafika?

Waislamu wote tuliomo ka-tika fani hii ya habari, pamoja na wale ambao ni wachangiaji katika vyombo vyetu ni wajibu wetu kufuatilia matukio mbalimbali ya kisiasa na ki-jamii, kwani hii ndio kazi yetu ya msingi.

Na utafiti wetu uwe wa asili (original) sio wa kunakili utafiti wa waandishi wenzetu, tena kwa mambo ya nchini mwetu. Kuwa katika chombo cha Kiis-lam haimaanishi tuwe tunafua-tilia mambo ya Uislam pekee, kwani yapo mambo mengi ya-nayoizunguka jamii ambayo nayo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Waislamu ha-tuishi katika kisiwa. Matukio mbalimbali yanayotokea kati-ka nchi yanaathari kwa Uislam na Waislam.

Na ijulikane vilevile kuwa sio watu wa habari pekee wa-naotakiwa kufuatilia mambo yanayotokea duniani, bali pia ni haki na wajibu wa Waislam wote kwa ujumla, hususan ka-tika karne hii ambapo kila raia amekuwa mwanahabari.

Shukran kwa vifaa vya kisa-sa vya mawasiliano na katiba inayohakikishia raia haki za msingi, ikiwemo ya kujieleza.

Inasemwa njia pekee ya kumshambulia adui yako ni umjue kwanza.Sasa kama hatufuatilii mambo tutawezaje kumkabili adui yetu? Bila utafiti huna haki ya kusema.

Pichani juu ni uzinduzi wa gazeti jipya la Kiislamu (IQRA) uliofanyika wiki iliyopita katika msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam.

chini, mhariri wa redio Imaan, Kassim lyimo akiwa katika moja ya semina za mafunzo ya ndani kwa watendaji Imaan Media.

kuwa katIka chombo

cha kIIslam haImaanIshI

tuwe tunafuatIlIa

mambo ya uIslam pekee,

kwanI yapo mambo mengI

yanayo Izunguka

jamII ambayo nayo nI muhImu katIka

maIsha yetu ya kIla sIku

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

17makaLa ya kimataifa

Pindi kifo kikikar-ibia na wagonjwa mahututi wanap-opitia maumivu

yasiyovumilika, wajibu wa daktari unapaswa kubadi-lika kutoka kuponya hadi kuondoa maumivu, kwa kumsaidia kufa kama ana-vyotaka mgonjwa. Hili si suala la uhai dhidi ya kifo, bali ni kuamua jinsi ya kufa, na kimsingi si uamuzi wa daktari, ni uamuzi wa mgonjwa ” - Dkt. Marcia Angell.

Huyo ni daktari wa asasi iitwayo “Die with Dignity” ya huko Marekani ak-ielezea kampeni inayoen-delea duniani ya kutaka madaktari waruhusiwe ku-katisha uhai wa wagonjwa wao wanapoamua kutaka kufa kuepuka maumivu ya maradhi. Dkt. Angell al inukuliwa akisema: “Watu wanastahiki nafasi ya kuchagua mwishoni mwa uhai wao na madak-tari wanapaswa kuruhusi-wa kuwasaidia wagonjwa kupata huduma ya mwisho wa uhai waitakayo”.

Dkt. Angell anapigania kutungwa sheria ambazo zitajulikana kama ‘Death with Dignity laws’, yaani sheria za kufa kwa heshi-ma. Hi i maana yake m g o n j w a k u e n d e l e a kuteseka kwa maumivu hadi kifo ni kufa pasina h e s h i m a . I n a d a i w a kwamba, daktari kulazimi-ka kumpa mgonjwa ‘dawa’ ya kumuua ili kukatisha maumivu yake ni jambo gumu, kwa hiyo wagonjwa wawekewe njia ambazo wao wenyewe watajihudu-mia (self service) wanapoa-mua kufa, ili daktari asiji-hisi mkosaji kwa kumsaid-ia mgonjwa kujiua.

Harakati za ‘haki ya kufa’ zimepamba moto nchini Marekani, Afrika ya Kusini na Ulaya. Baadhi ya majimbo kama vile Origon, Washington na Vermont yalishapitisha sheria za ‘kufa kwa heshima’ na wag-onjwa wanaotaka kuamua namna ya kufa huhamia jimboni humo.

B t i t t a n y M a y n a r d mwenye umri wa miaka 29 aliamua kuhamia Origon na kujihudumia vidonge vya barbiturates alivy-opewa na daktari wake na akafa. Kabla ya kuzuka kampeni hizi, hilo lingeit-wa kosa la kumsaidia mtu kujiua. Lakini sasa si kosa tena, bali haki ya mgonjwa a m b a y o i n a p a s w a kulindwa.

Inadaiwa kwamba, mgonjwa kupewa ‘dawa’ za kujiua si kosa, kwa sababu ni uamuzi wake mwenyewe, na uamuzi wa mtu juu ya mwili wake ni jambo li-liloruhusiwa kikatiba.

Qur’an inakataza mtu kujiua pale Allah Ta’ala ali-posema “…Na

wala msiziue nafsi zenu, hakika Allah ni mwenye huruma kwenu” (4:29). Katika hadith ya Mtume (Rehma na amani ziwe juu

yake) kuhusu madhambi ya aina saba yenye kuangami-za akataja; “...na kuuwa nafsi ambayo Allah amei-haramisha ila kwa haki” (Bukhari Na. 2615, Muslim Na. 145).

Huko nyuma, madaka-tari walikuwa wapingaji wakubwa wa kusaidia wag-onjwa kujiua. Jumuiya ya madaktari nchini Marekani iliwahi kutoa tamko: “Dak-tari kumsaidia mgonjwa kujiua ni kinyume na waji-bu wake, ambao ni kum-saidia mgonjwa kupona”.

Lakini kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika huko Ulaya na Marekani kwa ku-wahoji madaktari 21,000, asilimia 58 kati yao waliun-ga mkono utoaji wa hudu-ma ya kuwasadia wagonjwa kujiua, kwa mujibu wa gazeti la The Atlantic la Marekani.

Majimbo zaidi nchini Marekani yanaelekea au

yako katika hatua mbali mbali za kutunga sheria ku-ruhusu wagonjwa kusaidi-wa kujiua. Wagonjwa wa baadhi ya magonjwa yanay-ochukua muda mrefu hadi mtu kufa kama vile kansa na ukimwi wanapigania haki ya kujiua.

Nchini Afrika ya Kusini, kampeni hii imekolea siku za hivi karibuni chini ya kauli mbiu ‘My Life, My Choice’, yaani ‘Uhai wangu, Chaguo langu’. Katika taari-fa yao kwa vyombo vya habari, ‘Die with Dignity SA’ wanasema: “Tunaamini kwamba, wananchi wa Af-rika ya Kusini wanaotaabi-ka kwa maumivu ya mwis-honi mwa uhai wao wa-nanyimwa haki yao kiny-ume cha sheria”.

Hata hivyo, Waziri wa Afya wa Afrika ya Kusini, Aaron Motsoaledi, anapin-ga madai ya sheria ya ku-ruhusu wagonjwa kusaidi-

wa kufa. Waziri alisema: ‘Madaktari si Mungu’, akiwa na maana haki ya kuamua mtu afe au asife ni ya Mun-gu pekee.

Akipinga suala hilo, Waziri huyo alisema, kutoa ruhusa kwa madaktari ku-wasaidia wagonjwa kujiua kutatoa mwanya wa familia kupanga njama za kuwaua wazazi au jamaa zao kwa kutaka kurithi mali zao au hata kulipwa pesa za bima za maisha walizokata.

Huu ni msiba mwingine baada ya ule wa ndoa za jin-sia moja kuhalalishwa na mataifa ya magharibi. Yote haya yanaashiria mwisho wa ustaarabu wa magharibi u m e k a r i b i a . Im a m u , mshairi maarufu, Ahmad Shawqiy (Allah amrehemu), alisema: “Hakika mataifa hubakia kuwepo kwa maadil i mema, iwapo maadili yao yakitoweka na wao pia watatoweka”.

madaktari wanapogeuka wauaji

Assala alaykum msomaji wa safu ya Tovuti za Kiislamu,ni jumatatu nyingine tunakutana

tena h ivyo hatuna budi kumshukuru Yule ambaye ali-yeumba mbingu na ardhi bila ya nguzo yoyote naye ni Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

muumba Hii leo tutataian-gazia tovuti kongwe ya Islam qa,com,ambayo ilianzishwa na Seikh Muhammad Al Munajjid mnamo mwaka 1997.Hii ni tovuti ambayo imejikusanyia wasomaji wengi ulimwenguni kote kutoka-na na kutumia lugha zaidi ya

kumi katika ufikishaji dini ya Mwenyezi Mungu.

Tovuti hii imejikita kwenye fatawa mbalimbali na kujibu maswali ambayo Waislamu wengi yamekuwa yakiwatatanisha.Kama jina la ytovuti lenyewe lilivyo Is-lam qa likimaanisha maswali na majibu juu ya Waislamu.

Katika utoaji wa huduma hiyo wameigawa tovuti kati-ka makundi tofauti tofauti ambayo yatakuwezesha ku-soma kile unacho kihitaji kwa urahisi na ufasaha zaidi,makundi hayo yanaeleza mada zilizopo

ndani yake. Miongoni mwa mada hizo ni historia ya Uislam, Malen-go makuu ya Imaan katika

kipengele hicho kinazun-gumzia madhumuni ya Im-aan l ak i n i p i a k i p o kipengele,namna ya kuishi na familia yako kwa kufua-ta misin gi ya Qur’an na Sunna za Mtume Muham-mad (Rehma na amani ziwe juu yake).

Vipengele vingine vina-vyopatikna ni kile kinacho wahusu wanawake wa kis-lamu na namna yao ya kui-shi, demokrasia na uislamu huku ikitoa rejea za namna masahaba walivyokuwa

wakiishi katika dhana hii ya demokrasia bila kusahau huwa

wanatoa ushauri juu ya jambo ambalo litakuwa linajutatiza.

Vilevile ukitembelea wavuti huu utaweza kusoma vitabu nmbalimbali vya dini ya Uislamu kuhusu dini lakini pia vipo vilivy-oandika Uislamu na maisha ya kidunia pamoja na masuala ya sayansi ambavyo vitaweza kuku-saidia katika kuongeza maarifa yako. Unaweza kutembelea kupi-tia www.Islam-qa. Hayo ndio machache ya tovuti hiyo niliyowe-za kukuandalia katika wiki hii,tukutane wiki ijayo panapo majaaliwa.

0683110006

toVuti za

na KHaLiD OMaRy

huko nyuma, madakataRI walIkuwa wapIngajI wakubwa

wa kusaIdIa wagonjwa

kujIua. jumuIya ya madaktaRI

nchInI maRekanI

IlIwahI kutoa tamko:

“daktaRI kumsaIdIa mgonjwa kujIua nI

kInyume na wajIbu wake,

ambao nI kumsaIdIa mgonjwa kupona”.

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

18

zaHRa EbRaHiMkona ya waToTo

Bi Sumaiya (Radhi za Al-lah ziwe juu yake) na fa-milia yake ni miongoni mwa watu wachache wa

kwanza kuukubali Uislamu. Yeye na familia yake walipitia mateso mengi mikononi mwa makafiri ambao walikuwa wakiwalazimisha kuacha Uislamu.

Licha ya umri wake, Sumaiya (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisi-mama kidete katika njia ya haki na alikuwa mvumilivu hata pale makafiri walipomkokota yeye na mumewe, Yasir, na mwanawe Am-

mar (Radhi za Allah ziwe juu yao) katika mchanga wa moto wa jang-wani na kuwapiga mawe.

Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) aliwaam-bia kuweni wavumilivu na aliwaa-hidi pepo.

Sumaiya (Radhi za Allah ziwe juu yake) alifariki kutokana na mateso, na hivyo basi kuwa mwan-

amke wa kwanza kufa shahidi tan-gu Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) alipoanza kuita watu katika dini ya haki, Uis-lamu.

Baada ya vifo vya wazazi wake wote wawili, Ammar (Radhi za Al-lah ziwe juu yake) alipendwa sana na Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake). Kila

Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) alipozun-gumza kuhusu familia ya Sumaiya (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa akiisifia.

zoezi: Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) ali-waahidi nini familia ya Yasir?

Ni nani mtoto wa Sumaiya (Ra-dhi za Allah ziwe juu yake)?Kwa nini makafiri waliwatesa Sumaiya na familia yake (Radhi za Allah ziwe juu yake)?Soma Surat Arrah’man na Surat Al-Waaqia’h (pamoja na maana) na elezea kuhusu pepo kwa maneno yako mwe-nyewe.

Sumaiya (Radhi za allah ziwe juu yake)

GET READY FOR ENGLISH PAPER:Choose the correct answer:1. Rachael and I …………… in the compound before the visitors arrived. (a) were playing (b) play (c) plays (d) were playing (e) were play2.If she ………….. We would see her beautiful dress. (a) Came (b) come (c) would come (d) will come (e) had come 3. They were …………………dancing in the class-room. (a) Saw (b) see (c) sea (d) seen (e) sewn4. Maryam …………………. Food for the family now . (a) cooks (b)cook (c) cooked (d) has cooked (e) cooking.5. Neither Nasser nor Khalid ………………………… brave enough to kill the lion. (a) am (b) can (c) are (d) were (e)was6. We shall ……………….. all children of God. (a) be (b) his (c) was (d) are (e) is 7. Grade seven pupils are looking forward to ………………….. for their national examinations. (a) sit (b) seat (c) sitting (d) seating (e) will sit8. Alot of maize ………………… in Iringa next year. (a) was produced (b) produce (c) will be produced (d) produces (e) produced.9.There …………………………. Be an East African tour in December 2015. (a) are (b) will (c) will be (d) will have (e) will be10. She …………… a pen before the teachers asked for it. (a) hidden (b) hide (c) hid (d) had hidden (e) has hidden11.He managed ……………………….. the snake by hands. (a) kill (b) killed (c) to kill (d) to killed (e) to kill-ing.12.I usually …………………….before I go to bed . (a) prays (b) praying (c) pray (d) are praying (e) are pray.13. Where ………………………. They gone ? (a) is (b) has (c) has (d) was (e) have 14. Tanzanians will be …………………… for presi-dency towards the end of the year. (a) Vote (b) voted (c) voting (d) votes (e) votting

15. A few weeks ago our school ……………….. by the minister of education. (a) was visited (b) visited (c) was visiting (d) visit-ing (d) had visited

seCTioN B: gRaMMaR:16. That is the place ………………………….. Bata shoes are made. (a) who (b) which (c) where (d) whose (e) whom17. Ali is one of …………………….. Pupils in his school. (a) Best (b) Better (c) Better than (d) the best (e) good18. Tanzania is ……………………….. the East African countries. ( a) Either (b) among (c) between (d) at (e) as 19. Boys …………………………… girls need to have some time to rest . (a) as well as (b) as well (c) also….. but (d) more than20.The place …………………….. we sat was very wet . (a) were (b) where (c) which (d) on (e) while.2 1 . A g o o d d r i v e r a l w a y s d r i v e s ……………………………… (a) careful (b) carefully (c) very care (d) care (e) cares22. Ramadhani is ………………….. than Juma. (a) Active (b) activier (c) more activist (d) more active (e) the most active 23 . T he y he lp us whene ver we ge t stuck,……………………………..? (a) Aren’t they (b) do they (c) don’t they (d) aren’t us (e) weren’t they.24. That car belongs to them. It is …………………………………….. (a) Theirs (b) theirs’ (c) they are (d) theres (e) there’s25.Anita is fond ……………………….. Playing in class. (a) for (b) of (c) about (d) with (e) to26. The teacher roared angrily,” ………………………. Were making noise?” (a) Why (b) which (c) when (d) who (e) whom27. Mwalimu Julius kambarage Nyerere was

…………………….. Honest man. (a) the (b) a (c) an (d) some (e) any.28. He is as ………………as a bee. (a) Dangerous (b) brave (c) coward (d) cunning (e) busy.

seCTioN C: CoMPosiTioN:Re- arranges these sentences to make a meaningful story. Use the letters A-J:29. who was also the first prime minister of Tangan-yika .30. This beautiful country was also under Mwalimu Julius Kambarage Nyerere as its first president.31. 1961 was the time for the British to let Tanganyi-ka, be independent.32. In 1984 he resigned and let Hon. Ali Hassan mwinyi be in power from 1985 to 1995.33. After being given full power, he managed to unite Tanganyika and Zanzibar in 1964.34. Hon.Ali Hassan Mwinyi passed the relay stick to Hon Benjamin William mkapa.35. From that union a beautiful country was born .36. Currently, Tanzania is a peaceful country shin-ing under the leadership of Hon. Jakaya Mrisho Kikwete.37. Handed over the country to the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere in 1962.38.Sir, Richard Turnbull, the last British governor in Tanganyika.

KagiMu MK. (SciEncE tEacHER) 0752 224 550

ansWers for get ready science digest as on may 25, 20151. a 11. c 21. b 31.c 41.a2. b 12. b 22. b 32. c 42.d3. c 13. a 23. b 33. b 43.c4. c 14. b 24. c 34. b 44.b5. c 15. b 25. b 35.b 45.b6. b 16. c 26. b 36.b 46.c7. b 17. d 27. b 37.c 47.c8. b 18. b 28. c 38.b 48.d9. c 19. c 29. a 39.a 49.c10. a 20. d 30. b 40.c 50.b

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

19watoto / tanGazo

masafa ya imaan FM

Kigoma

Moro

Arusha

Ruvuma

Dsm

Mtwara

Mwanza

Tabora

Mbeya

1 Daresalaam 104.5 Mhz2 Morogoro 96.3 Mhz3 Arusha 90.8 Mhz4 Mwanza 105.6 Mhz5 Kigoma 92.5 Mhz6 Tabora 101.6 Mhz

7 Mbeya 90.3 Mhz8 Dodoma 102 Mhz9 Ruvuma 94.2 Mhz10 Mtwara 90.9 Mhz11 Zanzibar 104.5 Mhz12 Pemba 104.5 Mhz

104.5 Mhz

104.5 Mhz

104.5 Mhz

104.5 Mhz

104.5 Mhz

104.5 Mhz

105.6 Mhz

101.6 Mhz

94.2 Mhz90.9 Mhz

92.5 Mhz

90.8 Mhz

Dodoma

102 Mhz

1 11:00 ….11:05 05 min Adhana ya Alfajir Sheikh: rec

2 11:05 ….11:30 25 min Dua Sheikh: rec

3 11:30 ….12:00 30 min Nyiradi za asubuhi Sheikh:i.Twaha rec

4 12:00 ….01:00 1 hr Nasaha za asubhi Sheikh: rec

5 01:00 ….01:20 20 min Dira ya habari/ live

6 01:20 ….04:00 3 hrs 40 min Majlis ya tv Imaan live

7 04:00 ….05:00 1 hr Tafsir ya Qur aan Sheikh Mselem Ally rec from Tv imaan

8 05:00 ….05:05 05 min Mukhtasar wa dira live

9 05:05 ….06:00 55 min Salaam za asubuhi live

10 06:00 ….06:45 45 min Ulimwengu wa Kiislaam Ust:Ally Ajran rec

11 06:45 …. 06:50 05 min Adhana ya Dhuhr Sheikh: rec

12 06:50 ….07:20 30 min Tarjuma Sheikh: rec

13 07:20 ….08:00 40 min Mimbar zetu Hasan Ninga live

14 08:00 ….09:00 1 hr Mawaidha Sheikh Nassor Bachu rec

15 09:00 ….09:20 20 min Dira ya habari/matangazo live

16 09:20 …09:45 25 min Tauhiid Sheikh Mohammed Nduli rec

17 09:45 ….09:50 05 min Adhana ya al-asr Sheikh: rec

18 09:50 ….10:20 30 min Tarjuma Sheikh: rec

19 10:20 ….11:00 40 min Kalima Sheikh rec

20 11:00 ….11:20 20 min Dira ya habari/ live

21 11:20 ….12:00 40 min Nasaha za washairi Kasim Lyimo live

22 12:00 ….12:30 30 min Adhkarul masaa Sheikh Mishari rec

23 12:30 ….12:35 05 min Adhana ya Magharib Sheikh: rec

24 12:35 ….01:00 25 min Qur aan Tukufu Sheikh: rec

25 01:00 ….01:45 45 min Nasaha marudio Sheikh rec

26 01:45 ….01:50 05 min Adhana ya Ishaa Sheikh: rec

27 01:50 ….02:20 30 min Qur aan Tukufu Sheikh: rec

28 02:20 ….03:00 40 min Mafundisho ya Qur aan Ust:Othmaan Thabit rec

29 03:00 ….03:20 20 min Dira ya habari/ live

30 03:20 ….04:20 1 hr Kipindi maalum rec/live

31 04:20 ….05:00 40 min Mawaidha Sheikh: rec

32 05:00 ….06:00 1 hr Familia Baba Kiruwasha rec

33 06:00 ….11:00 5 hrs Usiku wa Qur aan Sheikh: rec

Wakati WakatiMuda MudaKipindi KipindiS/No: TIME DURATION PROGRAM STATUS1 06:00 – 06:20 20MIN NYIRADI ZA ASUBUHI RECORDED

2 06:20 – 06:35 15MIN NASAHA ZA ASUBUHI RECORDED

3 06:35 – 06:45 10MIN KILMA KIZURI RECORDED

7 07:00 – 07:20 20MIN DIRA YA HABARI RECORDED

8 07:20 – 07:30 10MIN CHACHU YA DIRA LIVE

9 07:30 – 08:00 30MIN SUHUFA ZA MAGAZETI LIVE

10 08:00 –10:00 2HR MADA NYETI LIVE

11 10:00 – 11:00 1HR USALAMA BARABARANI MARUDIO

13 11:04 – 11:35 31MIN MAWAIDHA RECORDED

14 11:35 –12:00 25MIN BULUGHULMARAM RECORDED

18 12:14 –12:24 10MIN ENGLISH LECTURE RECORDED

20 12:26 – 12:56 30 MIN NAFASI YA MWANAMKE RECORDED

22 13:00 – 13:13 13MIN ENGLISH LECTURE RECORDED

25 14:00 – 14:45 45MIN KUTOKA SHULENI RECORDED

26 14:46 – 14:50 4MIN PROMO RECORDED

27 14:50 – 15:50 1 HR UISLAM NA TIBA MARUDIO

29 15:52 – 16:22 30MIN BUSATI LA KISWAHILI RECORDED

31 16:24 – 16:55 30MIN QUR'AN RECORDED

S/No: TIME DURATION PROGRAM STATUS35 17:11 – 17:33 30MIN SIMULIZI ZA BIBI ZAINAB RECORDED

37 17:45 – 18:00 15MIN ANNASHEED RECORDED

38 18:00 – 18:20 20MIN NYIRADI ZA JION RECORDED

39 18:20 – 18:40 20MIN DUA + ADHANA RECORDED

40 18:40 – 18:57 17MIN FAHAMU USIYO YAJUA RECORDED

42 19:00 – 19:30 30MIN MAWAIDHA RECORDED

44 19:31 – 20:04 33MIN MAWAIDHA RECORDED

47 20:10 – 20:32 22MIN ALINGANIWE RECORDED

50 20:40 - 21:10 30 MIN SUHUFA ZA MAGAZETI MARUDIO

51 21:10 - 23:10 2HRS MADA NYETI MARUDIO

52 23:15 - 23:30 15 MIN KABLA HUJALALA RECORDED

54 23:30 –06:00 6:30HRS USIKU WA QURAN LIVE

viPiNdi Radio iMaaN viPiNdi Tv iMaaN

www.islamicftz.org

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

20 wanahabari wa kiislamu tufuatilie siasa za nchi

Uk 16

21 Shaaban 1436, jumatatu juni 8 - 14, 2015

hutoleWa na kuchapishWa na the islamic foundation, p.o. box 6011 morogoro, tanzania e-mail: [email protected]

yuSuPH aMin

Ansaar Sunnah’, jina hili limekuwa likisikika kwa miongo kadhaa sasa kwa walio wengi,

lakini maana sahihi ya jina hili ni ipi? Answaaru Sunnah ni watetezi wa sunnah za Mtume (Rehma na amani ya Allah ziwe juu yake).

Sunnah ni kitendo, neno au jambo alilolifanya Mtume (Reh-ma na amani ziwe juu yake) au al-iloliona linafanywa kisha kulin-yamazia, ambapo mambo hayo yote Waislamu wanapaswa kuyafanya kwa kuzingatia usahihi wake.

Mtume Muhammad (Rehma na amani ziwe juu yake) amese-ma: ‘Hakika dini ni nyepesi, hatoi-tia uzito mtu dini ila itamshinda” (Bukhari). Kwa mujibu wa hadith hii, ni wazi kwamba masuala kad-ha wa kadha ya dini ya Kiislam kama vile kuziendea hukumu za sheria katika mambo ya kijamii hutegemea Qur’an na Sunnah (hadith).

Utaratibu wa kuzinusuru Sun-nah za Mtume ndio ulikuwa mwenendo wa waja wema walio-tangulia. Kwa mfano ukirejea kitabu kiitwacho kitabu Arrisala, Imam Shafii (Allah amrehemu) alikuwa akiitwa: ‘Naaswiru sun-nah wa Qaami’ul bida’i’’ yaani mtetezi wa sunnah za Mtume na mwenye kuvunjavunja bid’a.

Lakini hivi leo wako Waislam wanaolichukia jina ‘Answaaru Sunnah’. Neno ‘Ansaar’ ni wingi wa neno la kiarabu ‘Naaswiru’, yaani mwenye kunusuru.

Kwa hiyo, Waislam wanaojina-sibu na Imam Shafii (Mungu am-rehemu) wangepaswa kuwa ‘An-swaru Sunnah’, lakini kinyume chake wako wanaowapinga na hata kuwapa majina mabaya kama vile Wahabiya, watu wa bid’a na kadhalika.

Kwa hiyo, Ansaar Sunnah si dhehebu jipya kama wasiojua wa-navyoambiwa, kwa sababu kila imam katika maimam wanne wa Ahlusunnah wal Jamaa’a waliku-baliana katika kufuata sunnah ka-tika kuyaendea masuala yote ya dini ya Kiislam.

Kauli za maimam hao zinase-ma ‘inapothibiti hadith ya Mtume basi hayo ndiyo madhehebu yan-gu’ (Imamu Shafii) na pia wakase-ma ‘mnapoona kauli yangu imek-wenda kinyume na kauli ya Mtume wacheni kauli yangu, mfuate ya Mtume” (Imam Abu Hanifa).

Kwa muda mrefu baada ya karne tatu njema kupita, sunnah za Mtume hazikuwa zinaeleweka vilivyo, na si hivyo tu, bali watu hata hadith za uwongo walizifuata

wakihisi kuwa ni za kweli. Sababu hizo zilipelekea vijana

wa Kiislam waliosoma elimu ya dini na kuelimika kuona haja ya kuzinusuru sunnah za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake).

Katika eneo la Afrika Masha-riki, hususan nchi ya Kenya waliji-tokeza maimam kadhaa waliojita-hidi kuzihuisha sunnah za Mtume na pia kupambana na bida’a kama vile Imam Sheikh Ali Mazrui, am-bapo ushahidi wake upo katika kitabu chake kinachoitwa ‘Hidaa-yatul-atfaali’.

Pia, Sheikh Abdallah Saleh Al-farsy aliwahi kuandika vitabu mbalimbali vinavyopinga bid’a na kuibua ukweli, hali iliyopelekea kuibuka malumbano na mijadala baina ya Waislamu.

Ushabiki wa madhehebu na ujima ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kusababisha tofauti (Ikhtlafu) kwa umma wa Waislam ulimwenguni, japokuwa waanzili-shi wa madhehebu hayo hawakupitiwa na hali hii.

Pia, imeibainika kuwa, tofauti zinazojitokeza zinatokana na baa-dhi ya Waislam kuacha kutumia dalili za Qur’an na Sunnah katika kuyaendea mambo, badala yake kutumia fikra na utashi zaidi au kufuata kauli za masheikh pasina dalili.

Uelewa tofauti kuhusu sunnah baina ya Waislam na watu kujiin-giza katika utungaji wa hadith za uwongo ni baadhi ya changamoto zilizopelekea wanazuoni wa dini ya Kiislam Tanzania kuanzisha

jumuiya mbali mbali za Ansaar Sunnah.

Baada ya kuona haja ya kuun-ganisha jumuiya hizi za Ansaar Sunnah, ‘Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah’ (BASUTA) likaanzishwa mnamo mwezi Ago-sti 2007 katika mkutano uliofan-yika Kibaha mkoani Pwani, likiwa kama Baraza elekezi la wana Sun-nah wote nchini, kwa lengo la kuz-iunganisha jumuiya za kisunnah chini ya uongozi mmoja.

Sheikh Kombo Ali Fundi, am-baye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Madina, ni Amir wa baraza hilo nchini Tanzania.

Katika mahojiano yake na gazeti la Imaan amesema, watu wanaonusuru Sunnah za Mtume ni lazima wajisalimishe katika

kupokea sharia kwa kutanguliza Qur’an na Sunnah kuliko akili, na pia mapenzi yao yawe kwa ajili ya Allah, na kuchukia kwao kuwe ni kwa ajili ya Allah.

Aidha, Sheikh Kombo ame-bainisha baadhi ya sifa za watu wa Sunnah kuwa ni pamoja na kuy-aendea mambo ya dini katika hali ya uadilifu, kati kwa kati bila ya kupindukia mipaka, kuwa na subra katika kauli na da’awa, kuwa na pupa ya umoja na mshika-mano, kuwaita watu kwenye hilo na kupiga vita utengano.

Sifa nyingine ni kutokuwa na Imam mkuu ambaye watu wote watachukua maneno yake yote au kuiga vitendo vyake vyote ila Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake).

Kujiepusha na mizozo katika dini, kuwapa heshima wema wali-otangulia, na kuitakidi kuwa mwendo wao ni sahihi, kwani wao ni watu wa karne bora zilizosifiwa na Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake).

Kuhusiana na masuala ya itikadi, Sheikh Kombo amesema, watu wa Sunnah hawana budi kuafikiana katika mambo ya aqi-da na katika kumtegemea Allah pamoja na kufuata sababu za mai-sha na kujikita katika Ucha Mun-gu.

MaleNgo ya BasuTaMoja ya lengo kuu la Basuta ni

kuwakilisha wanasunnah wote wa Tanzania katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

Pia Basuta imejikita katika kuziunga mkono juhudi za wana-zuoni wa kisunnah na jumuiya shirika zinazofanya kazi ya ku-waongoza watu wa kada mbalim-bali kwa misingi ya Qur’an na Sunnah sahihi za Mtume Mu-hammad (Rehma na amani ya Al-lah ziwe juu yake).

ansaaR sunnah sI dhehebu jIpya kama wasIojua

wanavyo ambIwa, kwa sababu kIla Imam katIka

maImam wanne wa ahlusunnah

wal jamaa’a walIkubalIana katIka kufuata sunnah katIka

kuyaendea masuala yote

ya dInI ya kIIslam.

BaSutataasisi inayoongoza harakati za Sunnah