16
!"#2 JUNI 2015 BORESHA AFYA YAKO 5 MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA

g_SW_201506 (1)

Embed Size (px)

DESCRIPTION

tj biblia

Citation preview

  • !"#2 JUNI 2015

    BORESHA AFYA YAKO

    5MAMBOUNAYOWEZAKUFANYA

  • Je, ungependa kupata habari zaidi aukujifunza Biblia nyumbani kwako bila malipo?Tembelea www.jw.org/sw au utume ombi lakoukitumia mojawapo ya anwani zilizo hapa chini.JEHOVAHS WITNESSES: SOUTH AFRICA: Private Bag X2067,Krugersdorp, 1740. KENYA: International Bible Students Association,PO BOX 21290, 00505 Nairobi. Ili upate orodha kamili ya anwanizetu ulimwenguni pote, tazama www.jw.org/sw/mawasiliano.

    Gazeti hili haliuzwi. Ni sehemu ya kazi ya elimu ya Biblia ya ulimwenguni pote inayotegemezwa kwa michango yahiari. Isipokuwa iwe imeonyeshwa vingine, Maandiko yamenukuliwa kutoka katika Biblia TakatifuTafsiriya Ulimwengu Mpya.Awake! (ISSN 0005-237X) is published monthly by Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.;L. Weaver, Jr., President; G. F. Simonis, Secretary-Treasurer; 25 Columbia Heights, Brooklyn, NY 11201-2483,and printed by Watch Tower Bible and Tract Society of South Africa NPC, 1 Robert Broom Drive East, Rangeview,Krugersdorp, 1739. 2015 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania. Printed in South Africa.

    1 2 3 4 5H A B A R I K U U

    NJIA ZA KUBORESHAAFYA YAKO

    NANI anapenda kuwa mgonjwa? Hakuna anayependa,kwa kuwa ugonjwa ni kikwazo na ni chanzo cha ghara-ma. Unapokuwa mgonjwa, huhisi tu vibaya bali pia hue-nda ukashindwa kwenda kazini au shuleni, kutafutapesa, au kuitunza familia yako. Huenda hata ukahitajimtu fulani akutunze, na huenda ukahitaji kulipia ghara-ma za dawa na matibabu.

    Kuna msemo usemao Kinga ni bora kulikotiba. Baadhi ya magonjwa hayaepukiki. Hata hivyo,bado kuna mambo mengi unayoweza kufanya ili kupu-nguza au hata kuzuia kuanza kwa ugonjwa. Fikiria ma-mbo matano unayoweza kufanya ili kuwa na afya bora.

    !"#2

    KATIKA TOLEO HIL I2 HABARI KUU

    Njia za KuboreshaAfya Yako

    8 MSAADA KWA AJILI YA FAMILIAJinsi ya KuimarishaUwajibikaji Katika Ndoa

    10 TUNAYOJIFUNZA KUTOKANANA HISTORIAGalileo

    12 MAONI YA BIBLIAUzinzi

    14 Samaki Aina ya PonoMashine yaKutengeneza Mchanga

    16 KUUTAZAMA ULIMWENGUKumulika Mazingira

    Vol. 96, No. 6 / Monthly / SWAHILIKila Toleo Linalochapishwa: 51,788,000 Katika Lugha 103

  • 1 DUMISHA USAFIKULINGANA na Kliniki ya Mayo, njia mojabora zaidi ya kujikinga na ugonjwa na kue-puka kueneza ugonjwa ni kunawa mikono.Ni rahisi kupata homa au mafua kama uta-gusa pua au macho yako huku mikonoyako ikiwa na viini. Njia bora ya kujilindana maambukizi ni kunawa mikono yakokwa ukawaida. Kudumisha usafi kunawezapia kuepusha kuenea kwa magonjwa hata-ri kama vile, nimonia na magonjwa ya kuha-risha, ambayo kila mwaka husababisha vifovya watoto zaidi ya milioni mbili, walio chiniya umri wa miaka mitano. Hata kuenea kwaugonjwa hatari wa Ebola, kunaweza kupu-nguzwa kwa kuwa na kawaida ya kunawamikono.

    Kuna pindi ambazo ni muhimu kunawamikono ili kulinda afya yetu na ya wengine.Unapaswa kunawa mikono: Baada ya kutoka chooni. Baada ya kumbadilisha nepi mtoto au ku-

    msaidia kutumia choo. Kabla na baada ya kutibu jeraha au kidonda. Kabla na baada ya kumtembelea mgonjwa. Kabla ya kutayarisha, kuhudumia, au kula

    chakula. Baada ya kupiga chafya, kukohoa, au kupe-

    nga kamasi.

    Baada ya kumgusa mnyama au kinyesi chamnyama.

    Baada ya kutupa takataka.Usifikiri kwamba kunawa mikono yako ki-

    kamili ni jambo lisilo muhimu. Uchunguziumeonyesha kwamba asilimia kubwa yawale wanaotumia vyoo vya umma hawana-wi mikono yao vizuri au hawanawi kabisa.Unapaswa kunawa mikono yako jinsi gani? Lowesha mikono yako katika maji safi ya bo-

    mba na kisha utumie sabuni. Sugua mikono yako pamoja ili kupata povu,

    bila kusahau kusafisha kucha, vidole, pandezote za mkono, na katikati mwa vidole vyako.

    Endelea kusugua kwa sekunde 20 hivi. Safisha mikono yako katika maji safi yanayoti-

    ririka. Kausha mikono yako kwa kutumia kitambaa

    safi au karatasi ya kukaushia mikono.Ni rahisi kufanya mambo hayo, na ku-

    fanya hivyo kunaweza kuzuia ugonjwa nakuokoa uhai.

    Amkeni! Juni 2015 3

  • 2 TUMIA MAJI SAFIKATIKA nchi fulani si rahisi kupata majisafi ya kutosha kwa ajili ya matumizi yanyumbani. Hata hivyo, kutopatikana kwamaji safi kunaweza kuwa tatizo popote uli-mwenguni ikiwa chanzo kikuu cha maji safiya kunywa kitachafuliwa kutokana na mafu-riko, kimbunga, kuharibika kwa bomba, aujambo lingine lolote. Ikiwa chanzo cha majisi safi au hakijatunzwa vizuri, maji yanawe-za kusababisha magonjwa yanayotokanana vimelea, kama vile kipindupindu, ugo-njwa hatari wa kuharisha, homa ya matu-mbo, mchochota wa ini, na magonjwa me-ngine. Maji yasiyo salama ni moja yachanzo cha ugonjwa wa kuharisha kwa visavya watu bilioni 1.7 hivi kila mwaka.

    Mara nyingi mtu huambukizwa ugonjwawa kipindupindu baada ya kunywa maji aukula chakula kilicho na viini kutoka kwawatu walioambukizwa. Unaweza kuchukuahatua gani ili kujilinda hata baada ya kupa-twa na ugonjwa au maambukizo mengineyanayotokana na maji yasiyo salama? Hakikisha kwamba maji unayokunywa, kutia

    ndani maji unayotumia kusafisha meno, ku-gandisha barafu, kusafisha chakula na vyo-

    mbo, au kupikia, yanatoka kwenye chanzo sa-lama, kama vile bomba la umma, lenye majiyaliyowekwa dawa ili kuua viini au maji yachupa yanayotengenezwa na kampuni inayoa-minika.

    Ikiwa maji ya bomba unayotumia si safi, che-msha maji kabla ya kutumia au weka dawa yakuua viini.

    Unapotumia kemikali au dawa za kuua viinikatika maji, kama vile klorini au dawa za ku-safisha maji, fuata maelekezo ya watengene-zaji.

    Tumia mashine ya kuchujia maji iliyo bora iki-wa inapatikana na ikiwa unaweza kununua.

    Ikiwa hakuna dawa za kuua viini katika maji,tumia dawa ya kuondoa madoa, weka mato-ne mawili katika lita moja ya maji, changa-nya vizuri, na kisha acha maji yatulie kwa da-kika 30 kabla ya kuyatumia.

    Sikuzote hifadhi maji safi katika vyombo vi-livyo safi na ufunike ili kuzuia yasichafuliwekwa njia yoyote.

    Hakikisha kwamba vyombo vinavyotumiwakuchota maji kama vile kikombe ni safi.

    Mikono yako inapaswa kuwa safi unapotumiaau unapogusa vyombo vinavyotumiwa kutu-nza maji, na usitumbukize mikono yako au vi-dole katika maji ya kunywa.Kuna mambo mengi unayoweza

    kufanya ili kupunguza au kuzuiakuanza kwa ugonjwa

  • 3 KULA CHAKULA KINACHOFAAMTU anahitaji chakula chenye lishe bora iliawe na afya nzuri. Huenda ukahitaji ku-chunguza matumizi yako ya chumvi, vya-kula vyenye mafuta, sukari, na unapaswakujua kiasi cha chakula unachokula. Una-pokula tumia pia matunda, mboga, na uwena kawaida ya kula vyakula vya aina mbali-mbali. Soma maelezo yaliyo katika pakiti yabidhaa ili uweze kununua vyakula vya nafa-ka ambayo haijakobolewa kama vile mkate,nafaka yenyewe, tambi, au mchele. Vyaku-la hivi vina virutubisho na nyuzinyuzi kulikovyakula vinavyotokana na nafaka zilizoko-bolewa. Ili kupata protini, kula kiasi kidogocha nyama ya ngombe na kuku, na ikiwe-zekana jitahidi kula samaki mara kadhaakwa juma. Katika nchi fulani ni rahisi kupa-ta vyakula vyenye protini kutoka kwenyemboga.

    Ukiwa na zoea la kula vyakula vyenye su-kari nyingi na mafuta yaliyoganda, unawezakunenepa kupita kiasi. Ili kuepuka hilo, ku-nywa maji badala ya vinywaji vyenye suka-ri. Kula matunda zaidi badala ya vyakulavyenye sukari. Punguza kiasi cha vyakulavyenye mafuta unachotumia kama vile so-seji, nyama, siagi, keki, jibini, na biskuti. Nabadala ya kupika kwa kutumia mafuta yali-yoganda, lingekuwa jambo linalofaa kutu-mia mafuta yanayofaa mwili.

    Kutumia chumvi au sodiamu kupita kia-si unapokula, kunaweza kuongeza shiniki-zo la damu kwa kiwango kisichofaa kwamwili. Ikiwa una tatizo hilo, soma maelezoyaliyo katika pakiti ya chakula ili ujue jinsi

    ya kudhibiti matumizi yako ya sodiamu. Ba-dala ya kutumia chumvi, tumia vikolezo naviungo ili kufanya chakula chako kiwe na la-dha.Kiasi unachokula kina umuhimu sawa

    na chakula unachokula. Hivyo, usiendeleekula chakula ikiwa tayari umeshiba, hatakama unafurahia kula chakula hicho.

    Jambo lingine kuhusu lishe ni hatariya kula chakula kisichofaa. Chakula cho-chote kisipotayarishwa na kutunzwa vizurikinaweza kukuletea madhara. Kila mwaka,mtu 1 kati ya 6 nchini Marekani anauguakutokana na kula chakula kisichofaa. We-ngi wao hupona kwa muda mfupi, hata hi-vyo kuna wachache wanaokufa. Unawezakufanya nini ili kuepuka hatari hiyo? Kwa kuwa mboga hukuzwa katika udongo

    ambao huenda umewekwa mbolea, safishavizuri mboga kabla ya kupika.

    Safisha kwa maji moto yenye sabuni, mikonoyako, ubao unaotumia kukatia mboga, vyo-mbo, na kaunta za jikoni kabla ya kuanzakuandaa chakula.

    Ili kuepuka kuchafua chakula safi, epuka ku-kiweka katika sahani au chombo chochote ki-sichosafishwa kilichokuwa kimetumiwa kuwe-ka mayai mabichi, kuku, nyama, au samaki.

    Pika chakula vizuri na tunza mara moja kati-ka friji vyakula vyovyote vinavyoweza kuharibi-ka ikiwa unapanga kula baadaye.

    Tupa chakula chochote kinachoweza kuha-ribika kilichoachwa kwa zaidi ya saa mbiliau moja katika hali ya hewa inayozidi nyuzijoto 32.

    Amkeni! Juni 2015 5

  • Afya yako inaathiriwa na hali ambazo huwezi kuzuia kama vile,uchumi, upatikanaji wa huduma muhimu, na mambo mengi-ne. Pamoja na hayo, unapaswa kuhakikisha kwamba unafuatabaadhi ya mapendekezo yaliyotolewa katika makala iliyotangu-lia. Hilo linapatana na maneno haya ya mwanamume mwenyehekima aliyeishi nyakati za kale aliposema hivi: Mtu mwerevuni yule ambaye ameona msiba na kujificha.Methali 22:3.

    LINDA AFYAYAKO!

    4 FANYA MAZOEZIBILA kujali umri wako, unahitaji kufanyamazoezi kwa ukawaida ili uwe na afya nzu-ri. Watu wengi leo hawafanyi mazoezi ya ku-tosha. Kwa nini ni muhimu kufanya mazoe-zi? Kwa sababu kufanya mazoezi kunawezakukusaidia: Kulala vizuri. Kuweza kutembea kwa wepesi. Kuwa na mifupa na misuli yenye nguvu. Kudumisha au kuwa na uzito wa mwili unao-

    faa kiafya. Kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa ku-

    shuka moyo. Kupunguza hatari ya kufa mapema.

    Ikiwa haufanyimazoezi, huenda ukapa-twa na: Ugonjwa wa moyo. Ugonjwa wa kisukari aina ya 2. Kupatwa na shinikizo la damu. Mwili kuwa na kiwango cha juu cha

    kolesteroli. Kupatwa na kiharusi.

    Kwa kuwa mazoezi yanayofaa yanate-gemea umri na afya ya mtu, ni vizuri kuwa-siliana na daktari wako kabla ya kuanza ku-fanya mazoezi yoyote mapya. Kulingana namapendekezo mbalimbali, watoto na vija-na wanapaswa kutumia angalau dakika 60kila siku kufanya mazoezi rahisi na magu-mu. Watu wazima wanapaswa kutumia da-kika 150 za mazoezi rahisi au dakika 75 zamazoezi magumu kila juma.

    Fanya mazoezi utakayofurahia. Unawezakucheza mpira wa kikapu, tenisi, mpira wamiguu, kutembea haraka, kuendesha bai-skeli, kulima bustani, kukata kuni, kuoge-lea, kupiga kasia mtumbwi, kukimbia pole-pole, au mazoezi yoyote ya viungo. Utajuajekwamba mazoezi ni rahisi au ni magumu?Kwa ujumla mazoezi rahisi hukufanya utoejasho, lakini magumu ni yale ambayo una-poyafanya inakuwa vigumu kwako kuzungu-mza.

  • Wasomaji wa Maandiko Matakatifu wanafarijiwa na ahadiya kweli ya kwamba hivi karibuni, hakuna mkaaji atakayese-ma: Mimi ni mgonjwa. (Isaya 33:24) Kwa sasa, jitahidi kadi-ri uwezavyo kulinda afya yako na ya wapendwa wako. Kwa habari zaidi, soma kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? kilichochapishwa na Ma-shahidi wa Yehova, au tembelea Tovuti yetu ya www.jw.org /sw.

    5 LALA VYA KUTOSHAKIASI kinachohitajika cha usingizi kina-tofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.Watoto wengi wachanga hulala saa 16hadi 18 kwa siku, watoto kuanzia umri wamwaka mmoja hadi mitatu hulala saa 14na wale wenye umri wa miaka mitatu hadiminne hulala saa 11 au 12 hivi. Watotowalio na umri wa kutosha kwenda shulekwa ujumla wanahitaji kulala kwa saa 10,vijana kwa saa 9 au 10, na watu wazimakwa saa 7 hadi 8.

    Kulala vya kutosha hakupaswi kuonwakuwa ni uamuzi tu wa mtu. Kulingana nawataalamu, kulala vya kutosha ni muhimukwa ajili ya: Ukuzi na maendeleo ya watoto na vijana. Kujifunza na kukumbuka habari mpya. Kudumisha usawaziko unaofaa wa homoni zi-

    nazosaidia kumengenya chakula na uzito wamwili.

    Kudumisha moyo wenye afya nzuri. Kuzuia magonjwa.

    Kutolala vya kutosha kumetajwa kuwachanzo cha kunenepa kupita kiasi, kushu-

    ka moyo, ugonjwa wa moyo, kisukari nachanzo cha aksidenti mbaya. Bila shaka,mambo hayo yanatufanya tuwe na sababunzuri za kuhakikisha kwamba tunalala vyakutosha.

    Hivyo, ufanye nini ukigundua kwambahaulali vya kutosha? Lala na amka muda uleule kila siku. Jitahidi kufanya chumba chako cha kulala

    kiwe na utulivu, chenye giza, cha kustarehe-sha, na kisiwe na joto au baridi sana.

    Usitazame Televisheni au kutumia kifaa chakielektroniki unapokuwa kitandani.

    Jitahidi kadiri uwezavyo kufanya kitanda cha-ko kiwe chenye kustarehesha.

    Epuka kula vyakula vizito, kafeini, na kileokabla ya kulala.

    Ikiwa hata baada ya kufuata mapendekezohayo bado unakosa usingizi au una mago-njwa mengine yanayohusiana na usingizikama vile kulala au kusinzia kupita kiasimchana au kupumua kwa shida unapolala,huenda ikafaa zaidi kumwona daktari.

    Amkeni! Juni 2015 7

  • KIKWAZOSiku ulipofunga ndoa, uliwekanadhiri. Nadhiri hiyo ni uwajibi-kaji wa kudumu, yaani, kiapocha kuendelea kushikamana namwezi wako na kutatua matatizoyoyote yanayojitokeza.Hata hivyo, kwa miaka mingi,huenda mizozano imeharibuuhusiano wenu. Je, bado unahisiunahitaji kuwajibika kikamili kwamwezi wako?

    MAMBO UNAYOPASWA KUJUAUwajibikaji ni suluhisho, na sio tatizo. Leo watu wengihawapendi kuwajibika. Baadhi yao hufananisha uwajibika-ji na mzigo mzito. Badala ya kuwa na maoni kama hayo,ona uwajibikaji kuwa nanga inayoweza kuimarisha ndoayako. Megan, mwanamke aliyeolewa alisema hivi: Wakatiwa mzozano, jambo moja bora kuhusu uwajibikaji ni kujuakwamba wewe na mwenzi wako hamtaachana. Kuwana uhakika kwamba ndoa yako ni salama licha ya kwambamnakabili changamoto fulani, kunaweza kukupatia msingiwa kutatua matatizo yenu.Ona sanduku Uwajibikaji naUshikamanifu.Jambo la hakika: Ikiwa unakabili hali ngumu katika ndoayako, sasa ndio wakati wa kuimarisha uwajibikaji, wala sikuutilia shaka. Unaweza kufanya hivyo jinsi gani? Biblia inaruhusu wenzi wa ndoa kuachana ikiwa mwenzi mmoja amefanyauasherati. Ona makala Maoni ya BibliaUzinzi katika gazeti hili la Amkeni!

    MSA ADA KWA A J I L I YA FAM I L I A ND O A

    Jinsi yaKuimarishaUwajibikajiKatika Ndoa

    % Uwajibikaji ni kama nangainayoweza kuimarisha ndoa yako

    r Pata msaada zaidi kwa ajili ya familia kwenye www.jw.org /sw

  • Ikiwa wewe na mwenzi wako ni wa-shikamanifu, mnaweza kufurahiamuungano wenye kudumu. Mna-pofikiria miezi, miaka, na makumiya miaka inayokuja, mnajionamkiwa pamoja bado. Wazo la kwa-mba hamngekuwa mmeoana ha-liingii akilini hata kidogo, na mta-zamo huo hufanya ndoa yenu iwesalama. Mke mmoja anasema:Hata ninapomkasirikia [mumewangu] na kuudhiwa na jinsi ma-mbo yalivyo kati yetu, mimi siha-ngaiki eti ndoa yetu itavunjika. Ja-mbo linalonihangaisha ni jinsitutakavyorudia uhusiano tulioku-wa nao kabla ya mambo kuharibi-ka. Mimi huwa sina shaka hatakidogo kwamba tutatatua tatizohilo, ingawa wakati huo sijui jinsiya kufanya hivyo. Kutoka katikamakala ya gazeti la Mnara wa Mli-nzi la Septemba 15, 2003.

    UWAJIBIKAJI NA USHIKAMANIFU

    MAMBO UNAYOWEZA KUFANYAChunguza maoni yako. Ndoa ya maisha. Je, manenohayo hukufanya uhisi umefungwa au uko salama? Matati-zo yanapotokea, je, wewe huona kuachana kuwa suluhi-sho? Ili kuimarisha uwajibikaji, ni muhimu kuona kwambandoa ni muungano wa kudumu.Kanuni ya Biblia: Matha-yo 19:6.Chunguza historia yako.Maoni yako kuhusu uwajibikajihuenda yameathiriwa na mambo uliyoona kwa wazaziwako. Lea, mwanamke aliyeolewa alisema hivi: Wazaziwangu walitalikiana nilipokuwa mdogo. Nilikuwa na wasi-wasi kwamba hali hiyo ingenifanya niwe na maoni yasiyo-faa kuhusu uwajibikaji. Uwe na uhakika kwamba unawe-za kufanya mambo kwa njia tofauti kabisa katika ndoayako. Si lazima urudie makosa ya wazazi wako!Kanuni yaBiblia: Wagalatia 6:4, 5.Chunguza usemi wako. Unapokuwa katika hali ya ku-toelewana na mwenzi wako, jizuie kusema maneno amba-yo baadaye utajutia, kama vile Nitakuacha! au, Nitatafu-ta mwingine anayenithamini! Maneno kama hayohuathiri uwajibikaji, na badala ya kutatua tatizo yanakuwachanzo cha ugomvi wa maneno. Badala ya kutumia usemiwenye kuumiza, unaweza kusema hivi: Kwa kweli, sotetumeudhika. Tunaweza kufanya nini ili kutatua tatizo hili?Kanuni ya Biblia: Methali 12:18.Onyesha kwamba unaheshimu uwajibikaji. Weka pi-cha ya mwenzi wako katika meza ya ofisini mwako. Uwena maoni yanayofaa kuhusu ndoa yenu unapozungumzana wengine. Weka lengo la kumpigia simu mwenzi wakokila siku unapokuwa mbali naye. Daima tumia usemi sisi,na utumie maneno kama mimi na mke wangu au mimina mume wangu. Kwa kufanya hivyo, utakazia kwako nakwa wengine kwamba unawajibika kwa mwenzi wako.Iga mifano mizuri. Iga mifano ya wenzi wa ndoa wenyeumri mkubwa na ambao wametatua matatizo ya ndoa kwamafanikio. Waulize hivi: Uwajibikaji una umuhimu ganikatika ndoa yenu, na umewasaidia jinsi gani katika ndoa?Biblia inasema hivi: Chuma hunolewa kwa chuma. Ndivyomtu anavyounoa uso wa mwingine. (Methali 27:17) Ukiwana kanuni hiyo akilini, jitahidi ili unufaike kwa kufuataushauri wa wale waliofanikiwa katika ndoa.

    MAAND IKO MUH IMUKile ambacho Mungu ameungani-sha mtu yeyote asikitenganishe.Mathayo 19:6.

    Kwa maana kila mmoja ataubebamzigo wake mwenyewe.Wagalatia 6:5.

    Kuna mtu anayesema bila kufikirikama kwa upanga unaochoma, la-kini ulimi wa mwenye hekima hu-ponya.Methali 12:18.

    Amkeni! Juni 2015 9

  • KABLA ya kuwapo kwa Galileo, watu wengi waliaminikwamba jua, sayari, na nyota zilizunguka dunia.Imani hiyo ilikuwa miongoni mwamafundisho rasmi yaKanisa Katoliki.

    Akitumia darubini yake, Galileo alipata ushahidiunaopingana na mafundisho ya kisayansi yaliyokubali-wa na wengi. Kwa mfano, alipotazama madoa meusiyaliyoonekana katika uso wa jua yakihama, alitambuakwamba jua linazunguka katika mhimili. Utafiti kamahuo umemsaidia mwanadamu kuongeza ujuzi wakekuhusu ulimwengu kwa kiasi kikubwa, ijapokuwa uchu-nguzi huo ulikuwa chanzo cha ugomvi kati ya Galileo naKanisa Katoliki.

    SAYANSI NA DINIMiaka mingi mapema, mtaalamu wa nyota kutoka

    Poland, Nicolaus Copernicus, alianzisha nadharia yakwamba dunia inazunguka jua. Galileo alichunguza uta-fiti wa Copernicus kuhusu mwendo wa vitu vilivyo anga-ni na kukusanya ushahidi akitegemea nadharia hiyo.Mwanzoni, Galileo alisita kusema kuhusu utafiti wakekwa sababu ya kuhofu kwamba atadhihakiwa na ku-puuzwa.

    T U N AYO J I F U N Z A K U T O K A N A N A H I S T O R I A G A L I L E O

    GALILEOKati ya karne ya 14 na 16, wanasayansina wanafalsafa wa Ulaya walianza kuelewaulimwengu katika njia ambayo ilipingana namafundisho ya Kanisa Katoliki. Mtu mmojaaliyechunguza upya mbingu ni Galileo Galilei.

    TAARIFA FUPI) Galileo Galilei alizaliwa mwakawa 1564, katika Pisa, Italia, jijimaarufu kutokana na kuwa namnara unaoegama. Alifundishakatika Chuo Kikuu cha Padua nabaadaye akaishi na kufanya kazikatika jiji la Florence.

    ) Ingawa Galileo hakuvumbuadarubini, aliboresha sana uwezowake wa kukuza na hivyo kufanyaiwe yenye kufaa hata zaidi.

    ) Kwa sababu ya maoni yakekuhusu ulimwengu, Galileo aliitwamara mbili mbele ya Baraza laKikatoliki la Kuhukumu Wazushi,ambalo lilikuwa na jukumu lakutoa adhabu kali kwa waleambao waliacha kufuatamafundisho ya kanisa.

  • Akiwa ameshindwa kuzuia msisimuko wake kutokanana yale aliyoona kupitia darubini yake, Galileo alianzakusema kuhusu utafiti wake. Baadhi ya wanasayansiwaliona utafiti wake kuwa chanzo cha ubishi, na baadaya muda mfupi, makasisi walianza kutumia majukwaaya kanisa kumpinga Galileo.

    Katika mwaka wa 1616, Kadinali Bellarmine,mwanatheolojia maarufu wakati huo, alimweleza Ga-lileo kuhusu amri mpya iliyowekwa na Kanisa Katolikidhidi ya mawazo ya Copernicus. Alimsisitiza sana Gali-leo kukubaliana na amri hiyo, na kwa miaka mingi baa-daye, Galileo hakupinga waziwazi kwamba dunia inazu-nguka jua.

    Katika mwaka 1623, Papa Urban wa Nane, aliyeku-wa rafiki wa Galileo, alianza kutawala. Hivyo, katikamwaka wa 1624, Galileo alimwomba papa aondoeamri iliyowekwa mwaka 1616. Badala ya kufanya hivyo,Urban alimsihi Galileo kufafanua nadharia zinazopinga-na za Copernicus na Aristotle katika njia ambayo haita-pendelea yeyote kati ya hizo.

    Hivyo, Galileo akaandika kitabu chenye kichwa Dialo-gue on the Great World Systems. Ingawa papa alimwa-giza Galileo kutopendelea upande wowote, kitabu hi-cho kilipendelea mawazo ya Copernicus. Baada yamuda mfupi tu, maadui wa Galileo walianza kudai kwa-mba kitabu chake kinamdhihaki papa. Akiwa ameshita-kiwa kuwa mzushi wa kidini na kutishiwa kuteswa, Ga-lileo alilazimishwa kukataa mafundisho ya Corpenicus.Katika mwaka wa 1633, Baraza la Kikatoliki la Kuhuku-mu Wazushi, lilimhukumu kifungo cha kudumu chanyumbani, na kupiga marufuku vitabu vyake. Galileo ali-kufa akiwa nyumbani kwake katika mji wa Arcetri, kari-bu na Florence, Januari 8, 1642.

    Kwa mamia ya miaka, baadhi ya utafiti wa Galileouliendelea kuwa katika orodha ya vitabu ambavyo Wa-katoliki hawakuruhusiwa kusoma. Hata hivyo, katikamwaka wa 1979, kanisa hilo lilichunguza tena hatuailiyochukuliwa na Baraza la Kikatoliki la KuhukumuWazushi miaka 300 iliyopita. Mwishowe, katika mwakawa 1992, Papa John Paul wa Pili, alikubali kwamba Ka-nisa Katoliki lilimhukumu kimakosa Galileo.

    Papa John Paul wa Pili, alikubalikwamba Kanisa Katoliki lilimhukumukimakosa Galileo

    Page 10: Regional M. Vrubel Art Museum, Omsk/Bridgeman Images; page 11: Adoc-photos/Art Resource, NY

    Je, Baraza la Kikatoliki laKuhukumu WazushiLilimtesa Galileo?Baadhi ya wanahistoria wame-sema kwamba huenda Barazala Kikatoliki la Kuhukumu Wa-zushi lilimtesa kimwili Galileo.Nakala ya hukumu aliyopewainasema kwamba ili kujua niaya Galileo, ilikuwa lazima kufa-nya mahoji makali. Usemi huoambao hutumiwa katika mamboya kihukumu mara nyingi hu-maanisha kutesa, huendaukamaanisha maneno ya viti-sho au kutesa kimwili.Wataalamu husema kwambakuna hatua na viwango vya ma-teso. Huenda ikatia ndani ku-mwonyesha anayeteswa vifaa vi-navyotumiwa kutesa, kumfunga,au hata kumsababishia maumi-vu makali kwa kuendelea. Ainaya mahoji makali, aliyofanyiwaGalileo haijulikani mpaka leo.

    Amkeni! Juni 2015 11

  • MAON I YA B I B L I A U Z I N Z I

    U Z I N Z IIngawa uaminifu katika ndoa ni jambo linaloonwa kuwa muhimu,bado uzinzi unaendelea kuharibu familia nyingi.

    Uzinzi ni nini?WATU HUSEMA NINI? Baadhi ya watu hawaonikwamba ni kosa kufanya ngono nje yandoa, hasa kwa waume. Na wengine ha-waoni ndoa kuwa muungano wa kudumu.BIBLIA INASEMA NINI? Katika Biblia, kwa ka-waida uzinzi unatia ndani uhusiano wa ki-ngono kati ya mtu aliyefunga ndoa yaanimume au mke na mtu mwingine ambayesi mwenzi wake wa ndoa. (Ayubu 24:15;Methali 30:20) Uzinzi ni chukizo machonipa Mungu. Katika Israeli la kale adhabuya kosa hilo ilikuwa kifo. (Mambo ya Wala-wi 18:20, 22, 29) Yesu alifundisha kwa-mba wafuasi wake ni lazima wajiepushe nauzinzi.Mathayo 5:27, 28; Luka 18:18-20.

    KWA NINI JAMBO HILO NI MUHIMU? Wazinzi hu-vunja nadhiri waliyoweka kwa wenzi waosiku walipofunga ndoa. Hilo pia ni kumte-ndea Mungu dhambi. (Mwanzo 39:7-9) Uzi-nzi unaweza kuwatenganisha kikatili watotona wazazi. Zaidi ya hayo, Biblia huonya kwa-mba Mungu atawahukumu . . . wazinzi.Waebrania 13:4.

    Ndoa na iheshimiwe kati ya wote,na kitanda cha ndoa kiwe bilaunajisi.Waebrania 13:4.

    r Pata majibu ya maswali mengine ya Biblia kwenye www.jw.org/sw

  • Amkeni! Juni 2015 13

    Je, uzinzi unavunja ndoa?BIBLIA INASEMA NINI? Biblia inamruhusu mtualiyefunga ndoa kumtaliki mwenzi wake iki-wa tu mwenzi huyo amefanya uasherati.(Mathayo 19:9) Hilo humaanisha kwambabaada ya tendo la kukosa uaminifu katikandoa, mwenzi asiye na hatia ana haki yakuamua iwapo ataendelea kuishi na mwe-nzi asiye mwaminifu au kumpa talaka. Huuni uamuzi wa mtu binafsi.Wagalatia 6:5.

    Kwa upande mwingine, Mungu anaonandoa kuwa muungano wa kudumu. (1 Wa-korintho 7:39) Mungu huchukia talaka, mtu

    anapodai talaka kwa sababu ndogo-ndogo,kama vile kutoridhishwa na mwenzi wake.Kwa hiyo, uamuzi kuhusu talaka haupaswikuchukuliwa kwa urahisi.Malaki 2:16; Ma-thayo 19:3-6.

    Mimi ninawaambia ninyi kwambakila mtu anayemtaliki mke wake, isi-pokuwa kwa sababu ya uasherati,anamweka katika hali ya kuweza ku-fanya uzinzi.Mathayo 5:32.

    Je, uzinzi ni dhambi isiyosameheka?BIBLIA INASEMA NINI? Hapana. Biblia hu-sema kwamba Mungu huwaonyesha rehe-ma wale wote wanaotubu na kuacha dha-mbikutia ndani uzinzi. (Matendo 3:19;Wagalatia 5:19-21) Biblia inasimulia kuhu-su wanaume na wanawake ambao walia-cha kufanya uzinzi na baadaye wakawa rafi-ki za Mungu.1 Wakorintho 6:9-11.

    Rehema za Mungu zilionyeshwa katikakisa cha Mfalme Daudi wa Israeli la kale.Daudi alifanya uzinzi na mke wa mmoja wamaofisa wake wa jeshi. (2 Samweli 11:2-4)Biblia inaeleza wazi kwamba jambo amba-lo Daudi alikuwa amefanya likawa baya ma-choni pa Mungu. (2 Samweli 11:27) Baadaya kupewa karipio, Daudi alitubu na Mu-ngu akamsamehe. Hata hivyo, Daudi ange-teseka kwa sababu ya matokeo ya mate-ndo yake. (2 Samweli 12:13, 14) Mfalmemwenye hekima Sulemani baadaye aliandi-ka hivi: yeyote anayefanya uzinzi na mwa-namke amepungukiwa moyoni.Methali6:32.MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA Ikiwa umefanyauzinzi, unahitaji kuomba msamaha kwa

    Mungu na mwenzi wako. (Zaburi 51:1-5) Ji-funze kuchukia uzinzi kama Mungu. (Zaburi97:10) Azimia kuepuka kutazama ponogra-fia, kuwazia-wazia kuhusu ngono, kuchezeawengine kimahaba, au jambo lingine lolo-te linaloweza kufanya usitawishe upendowa kimahaba kwa mtu mwingine ambaye simwenzi wako wa ndoa.Mathayo 5:27, 28;Yakobo 1:14, 15.

    Ikiwa unaumia kwa sababu mwenzi wakoamefanya uzinzi, uwe na uhakika kwambaMungu anaelewa hisia zako. (Malaki 2:13,14) Sali akupe faraja nyororo na mwongozowake, naye mwenyewe atakutegemeza.(Zaburi 55:22) Ikiwa umeamua kumsame-he mwenzi wako na kuendeleza ndoa yenu,wote mnahitaji kujitahidi kujenga upyandoa yenu.Waefeso 4:32.

    Nabii Nathani alimwambia hivi Daudialiyetubu baada ya kufanya uzinzi:Yehova naye ameacha dhambiyako ipite.2 Samweli 12:13.

  • Mchanga hutoka wapi? Kuna vyanzovingi mbalimbali. Lakini huenda ukasha-ngazwa na moja ya chanzo kinachoelezwakatika makala hii. Ni samaki anayesaga tu-mbawe na kuwa mchanga lainisamakiaina ya pono!

    Pono (parrot fish) wanaishi katika majiya kitropiki ulimwenguni pote. Baada ya ku-meza kipande cha tumbawe, wanatafutachembechembe za chakula na kutemama-baki, ambayo ni mchanga. Ili kufanya kaziyake, samaki huyo anatumia taya za mido-mo yake imara na meno yake magumu.Baadhi jamii za samaki hao wanaweza kui-shi miaka 20 bila meno yake kupukutika.

    Katika maeneo yenye matumbawe yaliyo-kufa, samaki huyo hutafuna kwa urahisi nakutokeza mchanga kwa wingi kuliko cha-nzo kingine chochote cha asili. Watafiti fu-lani wanakadiria kwamba samaki huyo hu-zalisha mamia ya kilogramu za mchangakwa mwaka.

    Pono hufanya kazi nyingine muhimu.Anapokula matumbawe yaliyokufa, miani ili-yo kwenye tumbawe na majani, jambo hilohudumisha usafi wa tumbawe. Tumbawe nichakula muhimu kwa pono, na hii ndiyo sa-babu huyatunza matumbawe. Sehemuambazo hakuna pono na viumbe wenginewanaofanya hivyo, matumbawe huharibiwana miani na magugu-maji. Wengine hudaikwamba matumbawe yaliyopo sasa yasi-ngekuwa katika hali hiyo ikiwa kusingeku-wa na viumbe kama hao, kinaeleza kitabuReef Life.

    Kutokana na shughuli zote hizo za mcha-na, pono wanahitaji kupumzika vizuri waka-ti wa usiku, pindi hiyo pono hufanya jambolisilo la kawaida. Wakati wa usiku ni hatarikuwa katika matumbawe, kwa sababukuna viumbe wengi wanaowinda. Kwa ka-waida pono hulala mafichoni chini ya mwa-mba, lakini sehemu hiyo iliyofichika haiwe-zi kuwalinda wakati wote kutokana na papamwenye njaa.

    Ili kuwa salama zaidi, baadhi ya samakihao hujifunika wakati wa usiku. Wao hu-toa ute wenye utelezi ambao hufunika ka-bisa miili yao, na kuwa kama gauni jangavula usiku. Wanasayansi wa viumbe vya maji-ni wanaamini kwamba harufu mbaya inayo-toka kwenye ute huo huwalinda kutoka kwaviumbe wanaowawinda.

    Pono ni miongoni mwa samaki wanaovu-tia na wale wanaoonekana kwa urahisi kwe-nye matumbawe. Mara nyingi pono jike nadume huwa na rangi zinazongaa, ambazohubadilika kwa kadiri wanavyoendelea ku-kua. Lakini jambo zuri hata zaidi ni kwambapono hupatikana kwa wingi katika maeneoambayo hawavuliwi kupita kiasi. Hivyo, ni sa-maki wanaoonekana kwa urahisi.

    Unapomtazama kwa karibu pono na ku-msikiliza anapotafuna juu ya tumbawe, nibaadhi ya mambo ambayo watafiti wamiamba ya matumbawe hawawezi kusa-hau. Pia, pono wanapofanya kazi yao, hu-boresha mazingira kwa viumbe wenginekatika matumbawe na ili kufurahishawanadamu.

    SAMAKI AINA YA PONOMashine ya Kutengeneza Mchanga

  • Pono, samaki (anayejulikana na wana-sayansi kwa jina la Scaridae) ni jamii ku-bwa yenye aina mbalimbali 80 ambazohupatikana kwenye miamba ya matu-mbawe katika maeneo ya Kitropiki. Mdo-mo wa samaki huyo unafanana na mdo-mo wa kasuku. Pono ana urefu kati yasentimeta 50 hadi 100.

    UKWELI KUHUSU SAMAKIANAYEITWA PONO

    , Samaki aina ya pono/ Pono mweusi

    Amkeni! Juni 2015 15

  • g1

    5 0

    6-S

    W1

    50

    30

    2sPakua gazetihili na matoleoyaliyotanguliabila malipo

    Biblia inapatikanakwenye Intaneti katikalugha zaidi ya 100

    Tumia alama hiikufungua Tovutiyetu au utembeleewww.jw.org/sw

    no

    p

    K U U TA Z AMA U L I MWE NG U MA Z I N G I R A

    KUMULIKAMAZINGIRA

    Ingawa dunia hutoa hewa safi,chakula kizuri, na maji safi,wanadamu bado wanazidi kuharibuutendaji huo wa asili. Wanasayansiwanaendelea kujitahidi kutafutanjia za kutunza mazingira.

    JAMBO LA KUFIKIRIA: Kwa nini jitihada za wanadamuza kuzuia uharibifu wa mazingira haziwezikufanikiwa?Yeremia 10:23.

    Med

    iaBa

    kery

    AUSTRALIA Imekadiriwa kwambazaidi ya kilomita 500,000 za majiyasiyo na chumvi yako chini ya sa-kafu ya bahari ulimwenguni. Vin-cent mtaalamu wa elimu ya majiwa Chuo Kikuu cha Flinders, Ade-laide, anasema hivi: Kuna wakatiambapo usawa wa bahari ulikuwachini zaidi kuliko vile ilivyo sasahivi, hivyo ufuo uliokuwepo waka-ti huo umemezwa na maji. Wakatihuo, Mvua ingejaza maji mpakasehemu ya eneo ambalo kwasasa liko chini ya bahari. Wana-sayansi wanatumaini kwamba ku-hifadhiwa kwa sehemu hizo zachini ya bahari huenda kungesai-dia watu zaidi ya milioni 700ambao hawawezi kupata maji safina salama.

    JANGWA LA SAHARA Nusu ya idadi ya jamii ya wanyama wakubwa wa-liokuwa wakipatikana katika jangwa la Sahara wametoweka au ku-bakia kwa asilimia moja au chini zaidi ya idadi yao ya mwanzoni. Mi-sukosuko ya nchi na uwindaji wa wanyama ulioenea huchangiakupungua kwa wanyama hao. Ingawa jamii kubwa ya viumbe haiwalio katika jangwa hukosa misitu, watafiti husema kwamba kushi-ndwa kwa wanasayansi kuwatunza viumbe hai walio katika jangwahusababishwa na kukosa misaada ya kifedha. Matokeo ni kwa-mba, ni vigumu kwa wanaohifadhi mazingira kuwatunza viumbe wa-naoishi jangwani walio katika hatari ya kutoweka.

    ULIMWENGU Imekadiriwa kwamba kifo 1 kati ya 8 vilivyotokea mwaka2012 kilisababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa. Kulingana na Shi-rika la Afya Ulimwenguni, uchafuzi wa hali ya hewa ni tatizo kubwala mazingira ulimwenguni linalohatarisha afya.