68
1 Fataawa Za Wanachuoni [08] Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush ©

Fataawa Za Wanachuoni (8)

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Fataawa Za Wanachuoni (8)

Citation preview

1

����������������� ������������������

Fataawa Za Wanachuoni

[08]

Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

©

2

Dibaji:

Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili

kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji

elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya

Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.

Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu

zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe

nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila

Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa

jumla.

Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana

Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo

Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta

aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa

kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.

Jazaakumu Allaahu Khayra

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na

Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

3

Fataawa zilizomo ni hizi zifuatazo:

1. Muhammad al-´Ariyfiy Na Suurat-ut-Tufaahah 2. Wapumbavu Kama Hawa Wapuuzwe! 3. Kufanya Hijrah Kutoka Katika Mji Wa Kufuru 4. Kauli Ya Kufuru Ya Mu´tazilah Kwamba Mja Ndiye Mwenye

Kuumba Matendo Yake 5. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Uongozi Wa ´Uthmaan (Radhiya

Allaahu ´anhu) 6. Mwenye Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Kishasimamiwa Na Hoja

7. Kusoma Kiarabu Kwa Watu Wa Bid´ah

8. Masuala Ya Mtu Kupewa Udhuru Kwa Ujinga -1- 9. Je Mtu Anaweza Kuwa Salafiy Akawa Na Manhaj Ya Ikhwaaniy,

Tabliyghiy Au Suufiy? 10. Makafiri Ni Ndugu Zetu Kibinaadamu 11. Kwanini Salafiyyuun Mnafarakanisha Waislamu?

12. Ni Msiba Kuamini Kuwa Ibliys Alikuwa Muislamu

13. Kuwasalimia Watu Wanaolingania Katika Bid´ah

14. Aliyefanya Hijrah Kutoka Katika Mji Wa Kikafiri Hakatazwi Kurudi Kwa Dharurah Ya Kishari´ah

15. Leta Dalili Kuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah Alikhalifu Salaf

16. Je, Ni Kweli ´Allaamah al-Fawzaan Kawasifia Jamaa´at-ut-Tabliygh?

17. Ni Kina Nani Murji-ah Fuqahaa´? 18. Ni Muislamu Ila Hajui Kuwa Ni Lazima Mtu Kujiweka Mbali Na

Shirki 19. Jihaad Ya Panga Na Jihaad Ya Kupambana Na Watu Wa Bid´ah 20. Vipi Kumpiga Radd Mwenye Kuchukulia Sahali Kupigwa Radd

Watu Wa Bid´ah 21. Murji-ah Wanaamini Kuwa Matendo Ni Sharti Ya Kutimia Kwa

Imani 22. Wanaodai Kwamba Wanaweza Kujifunza Tawhiyd Kwa Dakika

Kadhaa Tu 23. Haya Ni Maneno Ya Suufiy Asiefahamu Tawhiyd 24. Masuala Ya Mtu Kupewa Udhuru Kwa Ujinga -2- 25. Mwenye Kuchukia Wanapotajwa Watu Wa Bid´ah Ni Katika Ahl-us-

Sunnah? 26. Kupakana Mafuta Katika Da´wah

4

27. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Kufuru Ya Yuusuf al-Qaradhwaawiy 28. Hukumu Ya Kuchelewesha Swalah 29. Kufumba Macho Wakati Wa Swalah 30. Kufunza Wanawake Pasina Pazia (Kizuizi) Kati Kati 31. Mchanganyiko Wa Wanawake Na Wanaume Katika Harusi 32. Kumpa Zakaah Mama, Baba, Dada, Kaka Na Ndugu 33. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Tawhiyd-ul-Haakimiyyah 34. Muislamu Kuweka Dishi Chaneli Za Kiislamu Tu Nyumbani Kwake 35. Hukumu Ya Kupunguza Ndevu Na Kuzipamba 36. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Kuendelea Kwa Masufi 37. Mwenye Ugonjwa Wa Kutokwatokwa Na Mkojo Kuwa Imamu

38. Jamaa´at-ut-Tabliygh Na al-Ikhwaan al-Muslimuun Ni Katika Makundi 72 Ya Motoni?

39. Haikuthibiti Kuwa Salaf Walikuwa Wakisema “Swadaqa Allaahu al-´Adhiym”

40. Kufunga Safari Kwa Ajili Ya Kufanya Itikaaf 41. Mwanamke Anaruhusiwa Kusoma Qur-aan Kwa Sauti Ndani Ya

Swalah? 42. Kumhijia Baba Ambae Alikuwa Anapuuza Swalah 43. Zakaah Ya Kondoo Na Mbuzi 44. Kukojoa Kwa Kusimama 45. Sehemu Kulikuwepo Kanisa Kujenga Msikiti 46. Kaapa Hatoenda Kisha Akaenda, Hukumu Yake 47. Hukumu Ya Kutoka Msikitini Baada Ya Kutolewa Adhaana 48. Kupunguza Ndevu Kwa Ajili Ya Kufanya Kazi Ya Udaktari 49. Mtu Mkubwa Akiingia Katika Uislamu Anatahiriwa? 50. Kutumia Dawa Yenye Alcohol 51. Kupandisha Miguu Wakati Wa Sujuud Ndani Ya Swalah 52. Ni Kina Nani Salafiyyuun? 53. Nimeingia Katika Uislamu Ila Nina Kaka Kafiri 54. Sijdah Ya Kusahau Ndani Ya Swalah 55. Inajuzu Kutoa Mimba Ya Zinaa Kabla Ya Siku Arubaini? 56. Mtu Akumbuka Katika Swalah Ya Subhi Kuwa Hakuswali Witr Jana

Usiku 57. Mwanamke Auliza "Je Nimeingiliwa Na Majini Usiku?” 58. Hukumu Ya Jina La "Abdul-Baaswitw" 59. Kufanya Kazi Kwenye Manyumba Ya Wazee Na Kuwahudumia

Pombe 60. Rakaa Nyongeza Aliyodiriki Mtu Na Imamu Haihesabiki 61. Je Malaika wanamuona Allaah (´Azza wa Jalla)? 62. Vitu Vyeupe Vinavyomtoka Mwanamke Mjamzito 63. Kumtolea Salaam Mwenye Kudhihirisha Maasi 64. Kusahau Kusema Rabbiy Ghufirliy Katika Swalah

5

65. Mwanamke Mjamzito Ana Ruqyah Maalumu? 66. Inajuzu Kwa Mwanamke Kuondosha Nywele Za Kwenye

Masharubu? 67. Sunnnah Ya Kunyanyua Mikono Wakati Wa Du´aa Ya Istisqaa 68. Hukumu Ya Kusoma Qur-aan Na Tajwiyd Kwa Watu Wa Bid´ah 69. Mwanamke Mjamzito Anataka Kujumuisha Swalah 70. Kuwapa Matumizi Wazazi Wawili Ni Wajibu? 71. Mama Kwenda Kumzuru Mwanawe Ambaye Haswali 72. Mzinifu Ni Lazima Tu Kupigwa Fimbo Au Kuuawa? 73. Kufanya Kazi Kwa Mtu Wa Bid´ah Ambaye Ni Ikhwaaniy 74. Hadiyth Kuhusu Kumpa Mgonjwa Swadaaqah

75. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Kutoongelea Tawhiyd Kwa Ajili Ya Kuchelea Matatizo

76. Hukumu Ya Kusema Kuwa Allaah Hachoki 77. Mwanamke Nimemnyonyesha Mwezi, Je Mimi Ni Mahram Wa

Watoto Wake? 78. Kapangusa Juu Ya Soksi Na Wakati Alipozivaa Alikuwa Hana

Wudhuu 79. Mjomba Wa Mume Ni Mahram? 80. Ambaye Yuko Nje Ya Swalah Anaweza Kumkosoa Anaeswali

Akisoma Vibaya Qur-aan? 81. Salafiyyah Ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah 82. Muislamu Aliyeingia Uislamu Jinsi Ya Kutangamana Wazazi Wake

Makafiri 83. Ni Ipi Da´wah Ya Salafiyyah?

Wanachuoni waliomo ni hawa wafuatao:

1. ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Ibn Baaz

2. Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

3. Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn

4. Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy

5. Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

6. Swaalih bin Sa´iyd as-Suhamiy

7. ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy

6

Bismillaahi Rahmaani Rahiym

1. Muhammad al-´Ariyfiy Na Suurat-ut-Tufaahah

Swali:

Kumejitokeza mnamo siku za nyuma Video ya Muhammad al-´Ariyfiy

akisema "Suurat-ut-Tuffaahah" ili kuchekesha watu. Halafu anasoma maneno

ya kuchekesha kama ambavyo inavyosomwa Qur-aan. Ipi hukumu ya hilo

katika Shari´ah?

´Allaamah ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy:

Tunamuomba Allaah afya na salama. Wamesema baadhi ya maulamaa,

atakaeleta Bid´ah Allaah Humtoa katika Sunnah kwa kiasi hicho hicho mpaka

atakapotubia. Kitendo hiki jambo dogo awezalo kusema mtu ni maskhara na

ukaragosi.

Na ni katika wapiga VISA ambao alikuwa Ibn ´Umar na wengineo katika

Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakimsikia

wanatoka Msikitini. Vipi lafudhi hii na Anashiyd inaweza kuitwa "Suurat-ut-

Tuffaahah" au kisomo cha "Suurat-ut-Tuffaahah"? Ambaye ataitakidi hivi

anakufuru. Ambaye kweli ataitakidi (ataamini) kuwa kuna Suurah inayoitwa

"Suurat-ut-Tuffaahah", mtu huyu kakufuru.

Ama mwenye kufanya kitendo hiki na haitakidi (haamini) huyu ni mkaragosi

na mfanyaji mzaha. Mtu huyu ahofiwa (hukumu yake ikawa nzito zaidi mbele

ya Allaah), kwa kuwa kitendo chake hiki ni katika kuzifanyia mzaha Aayah za

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=gwFpMbwqxQQ

7

2. Wapumbavu Kama Hawa Wapuuzwe!

Swali:

Baadhi ya vijana wanajiweka mbali na maulamaa na wanawasifu kuwa

hawajui mambo ya kisasa. Vipi unawanasihi nini watu hawa?

´Allaamah al-Fawzaan:

Watu hawa wapuuzwe. Watu hawa ni wapumbavu.

Mshairi anasena:

“Wakati mpumbavu anapotamka usimjibu, njia nzuri ya kumjibu ni kunyamaza.”

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=128570

Tarehe: 1423-09-18/2002-11-22

3. Kufanya Hijrah Kutoka Katika Mji Wa Kufuru

Swali:

Ikiwa mtawala katika mji wa Kiislamu anakubali ´Ibaadah ya makaburi na

anaitetea na anawaamrisha walinzi kuyalinda na anawaadhibu Madu´aat na

wanafunzi wanaokataza haya, ni wajibu kufanya Hijrah kutoka katika mji

huo?

8

´Allaamah al-Fawzaan:

Ndio ukiweza kutoka katika mji huu na kuhamia katika mji wa Tawhiyd

itakuwa wajibu kwako kufanya hivyo. Na ikiwa huwezi wewe utakuwa ni

mwenye udhuru mpaka hapo utakapoweza kuhama. Lakini ni lazima

ushikamane na Dini yako, ´Aqiydah yako na Da´wah kwa njia ya Allaah.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/2337

Tarehe: 1431-04-28/2010-04-12

4. Kauli Ya Kufuru Ya Mu´tazilah Kwamba Mja Ndiye Mwenye Kuumba

Matendo Yake

Swali:

Je Mu´tazilah wanakufuru kwa kusema kwao kuwa mja ndie mwenye

kuumba matendo yake mwenyewe? Na kwa nini maulamaa wasiwakufurishi

ikiwa shirki yao ni katika masuala kama haya?

´Allaamah al-Fawzaan:

Kwa kuwa wengi wao wanafuata kiupofu au hawakufahamu vizuri suala hili.

Wana utata. Tunawahukumu upotofu. Ama wakikusudia hili, watachukuliwa

kuwa ni makafiri. Lakini wengi wao hawakusudii, bali wanafuata kiupofu au

kiujinga. Mtu kama huyu ni mpotofu na akatazwe.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/2337

Tarehe: 1431-04-28/2010-04-12

9

5. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Uongozi Wa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu

´anhu)

Swali:

Yapi maoni yako kwa mwenye kuukashifu uongozi wa ´Uthmaan (Radhiya

Allaahu ´anhu) na anasema kuwa uongozi wa ´Aliy ni wakimaumbile baada

uongozi wa Abu Bakr na ´Umar?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Hawa ndo wale wanaosema kuwa uongozi wa ´Aliy ndo kuendelea kwa

maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi sasa Waislamu

walikubaliana uongozi wa ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu)

akambai´ usikivu na utiifu? Mwenye kumkashifu kawakosoa Muhaajiruun na

Answar.

Chanzo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (162 A)

Tarere: 1418-03-13/1997-07-18

6. Mwenye Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Kishasimamiwa Na Hoja

Swali:

Tumejua kuwa Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ndio inayomuingiza mtu katika

Uislamu na kwamba Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah hakuna anayeikataa. Na

ukasema kuwa dalili ya Tawhiyd iko wazi na Shirki haina dalili. Lakini

kumejitokeza katika mji wetu baadhi ya Madu´aat wanaosema kuwa

washirikina wenye kuabudu makaburi ni wenye kupewa udhuru kwa ajili ya

ujinga wao mpaka kwanza wasimamishiwe hoja. Lakini watu hawa wenye

10

kuabudu makaburi hawajui mtu ambaye anaweza kuwasimamishia hoja.

Badala yake wanamtuhumu kuwa ni "Wahabiy". Ipi hukumu kwa watu

hawa?

´Allaamah al-Fawzaan:

Hukumu ni kuwa hoja imekwishawasimamia. Wamesimamishiwa hoja kwa

kutumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na wao wanakiri

Risalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanadai kuwa

wanamfuata. Hoja imekwishawasimamia. Wanasoma Qur-aan. Wanahifadhi

Qur-aan. Hoja imekwishawasimamia.

و�� ��� � � وأو�� إ�� ھ�ا ا���آن ���ر

”Na nimefunuliwa Qur-aan hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo

mfikia.” (06:19)

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1821

Tarehe: 1431-04-07/2010-03-22

7. Kusoma Kiarabu Kwa Watu Wa Bid´ah

Swali:

Ipi hukumu ya kuhudhuria Duruus za Ahl-ul-Bid´ah?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

11

Ikiwa anahudhuria Duruus za watu wa Bid´ah kwa ajili ya kujadiliana nao na

kuwabainishia haki, jambo hili ni wajibu. Na kama anataka kusoma kwao

asisome kwao. Hata kama (anachokisomesha) si ´Aqiydah, kwa mfano

anasomesha sarufi na balaagha. Usiwasogelee. Wanaweza kukuweka sumu.

Hali kadhalika ukikaa nao huenda watu wakadanganyika. Wakafikiria kuwa

hakuna ubaya kuhudhuria katika Duruus za watu hawa.

Mwanafunzi:

Hata sarufi?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Hata sarufi. Allaah Ataleta mwengine (aliye bora).

Chanzo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (162 B)

Tarehe: 1418-03-13/1997-07-18

8. Masuala Ya Mtu Kupewa Udhuru Kwa Ujinga -1-

Swali:

Tunajua ya kwamba hapewi udhuru yeyote kwa ujinga katika Tawhiyd katika

masiku haya katika Waislamu ambao wamesimamishiwa hoja kwa kutumwa

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan inasomwa juu yao.

Vipi tutamradi anaesema, kwanini tusimpe udhuru yule mwenye Madu´aat

wanaomlingania kuwaabudu maiti na wanamwambia kitendo hiki ni katika

Uislamu?

´Allaamah al-Fawzaan:

12

Kuna Madu´aat wanaomlingania katika kuabudu maiti. Lakini kuna Madu´aat

wanaolingania katika Tawhiyd. Kwanini awatii hawa na awaache hao

wengine? Hoja imekwishamsimamia. Ingelikuwa kuna Madu´aat tu

wanaolingania katika Shirki, huenda angepewa udhuru. Lakini Madu´aat

wanaolingania katika Tawhiyd wako dhahiri na wameenea na vitabu na kazi.

Lakini wanasema Tawhiyd ni dini ya Mawahabiy. Hili ndio tatizo.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/2277

Tarere: 1431-04-21/2010-04-05

9. Je Mtu Anaweza Kuwa Salafiy Akawa Na Manhaj Ya Ikhwaaniy,

Tabliyghiy Au Suufiy?

Swali:

Je ni sahihi kuwa kunaweza kukusanyika ´Aqiydah ya Salafiyyah na Manhaj

ya Ikhwaaniy, Tabliyghiy au Suufiy kwa mtu mmoja?

´Allaamah al-Fawzaan:

Vitu viwili ambavyo ni kinyume haviwezi kuwa kitu kimoja katu. Vitu viwili

ambavyo ni kinyume haviwezi kuwa kimoja. Je, Tawhiyd na Shirki vyaweza

kuwa kitu kimoja? Haviwezi kuwa kitu kimoja. Vitu viwili ambavyo ni

kinyume haviwezi kuwa kitu kimoja katu. Na Bid´ah haiwezi kukusanyika na

Sunnah.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=128470

Tarere: 1423-09-21/2002-11-25

13

10. Makafiri Ni Ndugu Zetu Kibinaadamu

Swali:

Mwenye kusema makafiri ni ndugu zetu wa kibinaadamu na si katika dini, je

maneno yake haya ni sahihi?

´Allaamah al-Fawzaan:

Haitoshi kiubinaadamu. Wala mtu hasemi hivi kwa kutaka kuwapaka mafuta

au kupata hisia zao. Mtu hasemi hivi. Inatakiwa kusema wao ni maadui wetu

wala mtu hasemi ndugu zetu wa kibinaadamu. Bali mtu anatakiwa kusema ni

maadui wetu. Ikiwa ni maadui wetu katika dini, udugu wa kibinaadamu

utafidisha nini? Utafidisha nini? Firauni alikuwa pia binaadamu. Au sio? Je

alikuwa pia ndugu yetu? Haitakikani kusema hivi.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1875

Tarehe: 1431-04-14/2010-03-29

11. Kwanini Salafiyyuun Mnafarakanisha Waislamu?

Swali:

Mwenye kusema usiongelei Tawhiyd ili watu wasifarakane kwa kuwa

inafarakanisha na inatawanya Umoja. Ipi hukumu ya msemo kama huu?

14

´Allaamah al-Fawzaan:

Ndio inafarakanisha watu wapotofu na watu wa Shirki. Na wala

haifarakanishi watu wa Tawhiyd bali inawafanya kuwa wamoja. Watu wa

Tawhiyd na Waislamu inawafanya kuwa wamoja. Ama makafiri na

washirikina na walionao, Tawhiyd inawaweka mbali mbali na

kuwafarakanisha. Na sisi tunataka kuwafarakanisha. Tunataka kutofautisha

watu wapotofu, makafiri, washirikina. Hatutaki kuwachanga na Waislamu.

Hili ndo tulitakalo.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1875

Tarehe: 1431-04-14/2010-03-29

12. Ni Msiba Kuamini Kuwa Ibliys Alikuwa Muislamu

Swali:

Kuna wanaosema kuwa Ibliys hakukufuru kwa kuwa alisema:

رب

"Mola Wangu!" (15:36)

Na akasema tena:

!" #$%&

"Naapa kwa Utukufu Wako". (38:82)

Alikuwa ni mwenye kukubali Utukufu wa Allaah na Ubwana Wake.

15

´Allaamah al-Fawzaan:

Ndio, alikuwa ni mwenye kukubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hata Abuu

Jahl na Abuu Lahab walikuwa wakikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ilihali ni

makafiri na wataingia motoni, kwa kuwa walikataa Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

Ibliys alikata kutekeleza amri ya Mola Wake. Alimuasi Mola Wake na

akajivuna.

أ�, وا+*(%� و )ن �� ا�()&�'�

“Alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.” (02:34)

Haitoshi Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah mtu kusema tu "Mola Wangu", au kwa

kusema kwake "Naapa kwa Utukufu Wako". Halitoshi hili. Ikiwa kuna mtu

anaesema kuwa Ibliys alikuwa Muislamu, huu ni msiba.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1875

Tarere: 1431-04-14/2010-03-29

13. Kuwasalimia Watu Wanaolingania Katika Bid´ah

Swali:

Je, inajuzu kuwapa salaam wale wanaolingania katika Bid´ah?

´Allaamah al-Fawzaan:

Ikiwa Bid´ah zao ni za ukafiri, mtu asiwape Salaam. Ama Bid´ah zao zikiwa ni

duni ya ukafiri, ikiwa katika kuwahama kwao kutaleta athari mtu awahame.

16

Na ikiwa kuwahama kwao hakuna athari yoyote, mtu awape Salaam na

awakataze Bid´ah na awabainishie.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1821

Tarehe: 1431-04-07/2010-03-22

14. Aliyefanya Hijrah Kutoka Katika Mji Wa Kikafiri Hakatazwi Kurudi

Kwa Dharurah Ya Kishari´ah

Swali:

Je ni wajibu kwa mtu aliyefanya Hijrah kutoka katika mji wa kikafiri na

kwenda katika mji wa Kiislamu asirejee katika mji wake hata kama lau ni

kuhifadhi udugu, kazi au matibabu?

´Allaamah al-Fawzaan:

Ndio, aliefanya Hijrah asirejee katika mji wake wa kikafiri kwa ajili ya kuishi

baada ya Allaah Kumuokoa. Lakini anaweza kurejea wakati wa haja. Hakuna

ubaya kwa hilo. Maswahabah walifanya Hijrah kutoka Makkah na kwenda

Madiynah. Na walikuwa wakisafiri kwenda Makkah kwa haja kisha wakirejea

Madiynah. Walikuwa hawabaki Makkah.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1821

15. Leta Dalili Kuwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah Alikhalifu Salaf

17

Swali:

Wengi wanaokwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wanasema sisi, Ahl-us-

Sunnah, tumeegemea tu kwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na

wanachuoni wa Najdiy - Allaah Awarehemu wote. Wanasema kwamba wao

walikuja na mambo mapya yanayokwenda kinyume na Salaf. Unaweza

kunielekeza katika vitabu vinavyothibitisha anayosema Shaykh-ul-Islaam na

wanachuoni wa Najdiy, sawa ikiwa ni katika ´Aqiydah au mambo mengine.

´Allaamah al-Fawzaan:

Huyu anayesema walikwenda kinyume na Salaf alete dalili walipokhalifu

Salaf. Atupe jambo maalumu moja kwa moja. Ama kuwatuhumu tu bila ya

dalili halikubaliki. Huyu anafuata matamanio. Kama anasema kweli atupe

jambo maalumu analokwenda kinyume na Salaf. Atupe jambo maalumu

tuangalie. Lakini vipi ataweza kufanya jambo kama hili?

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1821

Tarehe: 1431-04-07/2010-03-22

16. Je, Ni Kweli ´Allaamah al-Fawzaan Kawasifia Jamaa´at-ut-Tabliygh?

Swali:

Je unaninasihi kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh khasa tunavyosikia kuwa

umesifia kikundi hiki siku zilizopita?

´Allaamah al-Fawzaan:

Anaesema kuwa mimi nimewasifia ni muongo. Mimi sikuwasifia. Mimi sisifii

ila Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wanalingania katika Tawhiyd, katika

´Aqiydah sahihi, wanawafunza watu elimu yenye manufaa. Watu hawa ndo

18

ambao tunawanasihi Waislamu kuwa pamoja nao. Ama watu wa Bid´ah na

watu wasiofahamu Tawhiyd na wala hawaiwekei uzito na wanafanya Bid´ah,

watu hawa tunatahadharisha watu dhidi yao vikali.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=128423

17. Ni Kina Nani Murji-ah Fuqahaa´?

Swali:

Yapi makusudio ya Murji-ah Fuqahaa´? Je ni katika Ahl-us-Sunnah?

´Allaamah al-Fawzaan:

Murji-ah Fuqahaa´ ni wanachuoni wa Kuufah, au baadhi yao na pakiwemo

Hanafiyyah. Hanafiyyah ni katika Ahl-us-Sunnah. Lakini katika masuala

haya1 wameenda kinyume na Ahl-us-Sunnah. La sivyo wanakiri Tawhiyd-ul-

Asmaa´ was-Swifaat, Qadar na kadhalika. ´Aqiydah yao ni ´Aqiydah ya Ahl-

us-Sunnah. Lakini katika suala hili wamekwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah,

hivyo wakaitwa "Murji-ah Fuqahaa´" au "Ahl-us-Sunnah Murji-ah". Kwa kuwa

Mu´tazilah na Jahmiyyah sio katika Ahl-us-Sunnah.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1821

1 Wanasema kwamba Imani ni ”Kauli na kuamini moyoni peke yake”; kisha wanasema ya kwamba ´amali ni sharti ya kutimia kwa Imani. Ama Ahl-us-Sunnah wanaamini ya kwamba Imani ni ”Kauli, kuamini moyoni na ´amali.” ´Amali inaingia katika neno Imani na si sharti ya kutimia kwa Imani. Wa Allaahu A´alam.

19

18. Ni Muislamu Ila Hajui Kuwa Ni Lazima Mtu Kujiweka Mbali Na Shirki

Swali:

Akitamka mtu kwa ulimi wake Laa ilaaha illa Allaah, akajinasibisha kwa

Uislamu na anaishi katika mji wa Kiislamu. Lakini hajui maana yake na wala

hajui kuwa ni lazima kujiweka mbali na kila kinachoabudiwa badala ya

Allaah, kwa kuwa hajui maana yake. Atachukuliwa kuwa ni Muislamu?

´Allaamah al-Fawzaan:

Ndio, atachukuliwa ni Muislamu. Atawekewa wazi maana yake na

kufafanuliwa maana yake mpaka aamini na aifanyie kazi.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1821

19. Jihaad Ya Panga Na Jihaad Ya Kupambana Na Watu Wa Bid´ah

Swali:

Ni zipi sharti za Jihaad kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Na je Waislamu leo

wanatimiza sharti hizo? Na je kuwapiga Radd watu wa Bid´ah ni katika

Jihaad?

´Allaamah al-Fawzaan:

Jihaad itakuwepo mpaka siku ya Qiyaamah. Jihaad katika njia ya Allaah ipo

mpaka siku ya Qiyaamah. Maadamu makafiri wapo Jihaad itaendelea

20

kuwepo. Na inakuwa Jihaad pamoja na kiongozi (mtawala) wa Waislamu.

Yeye ndie atakaeiamrisha. Na yeye ndie atayeandaa Jeshi na kikosi. Ni katika

mambo ya kiongozi wa Waislamu. Jihaad inakuwa pamoja na kiongozi wa

Waislamu sawa akiwa ni mwema au muovu mpaka siku ya Qiyaamah. Ili

kuinua Neno la Allaah (´Azza wa Jalla). Ni lazima makusudio iwe ni kuinua

Neno la Allaah (´Azza wa Jalla) liwe juu, kuunusuru Uislamu na Waislamu.

Na Jihaad inakuwa kwa silaha na inakuwa kwa ulimi, kuwapiga Radd watu

wa batili (wa Bid´ah) na kuponda shubuha zao katika vitabu, nyaraka,

vyombo vya habari na magazeti. Hii ni katika Jihaad katika njia ya Allaah.

Anasema Allaah (Ta´ala):

��4 ') أ'3) ا�-%� 1)ھ0 ا�(/)ر وا�.-)&

”Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki.” (09:73)

Makafiri wanapigwa Jihaad kwa silaha, na wanafiki wanapigwa Jihaad kwa

hoja na dalili.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=123843

20. Vipi Kumpiga Radd Mwenye Kuchukulia Sahali Kupigwa Radd Watu

Wa Bid´ah

Swali:

Ipi Radd kwa yule mwenye kuchukuliwa sahali kupigwa Radd watu wa

Bid´ah na anasema jambo hili linafanya elimu kupotea na hii sio njia ya Salaf?

´Allaamah al-Fawzaan:

21

Mwenye kusema maneno haya ni mjinga. Mwenye kwenda kinyume lazima

apigwe Radd na kubainisha kosa lake, kwa ajili aweze kurudi katika usawa na

kwa ajili wengine wasidanganyike kwa kosa lake. Na hii ni katika kupeana

nasaha. Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Dini ni kupeana nasaha." (Maswahabah tukasema): "Kwa nani?" Akasema

kwa Allaah, Kitabu chake, na Mtume wake, na kwa Viongozi wa Waislamu na

watu wa kawaida. [Muslim]

Ni katika nasaha kwa kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) kumpiga Radd mwenye kukosea katika haya na akawa na

uelewa wa kimakosa na akavifasiri kinyume na haki. Ni wajibu kumpiga

Radd na kubainisha kosa lake. Na hivyo inakuwa kwa kila ataekosea katika

jambo miongoni kwa mambo ya dini na ´Ibaadah, ni wajibu kubainisha. La

sivyo wangeliachwa watu kama hawa dini ingeliharibika.

Allaah (Jalla wa ´Alaa) kawaradi washirikina katika Qur-aan, Mayahudi,

Manaswara. Radd zipo ndani ya Qur-aan, (Allaah) Kawapiga Radd na wala

hakuwaacha. Kusema kwamba mwenye kwenda kinyume hapigwi Radd,

haya ni maneno ya mtu mjinga asiejua kitu.

Lakini mwenye kupiga Radd ni yule mwenye elimu. Enyi ndugu mwenye

kazi hii ya Radd ni wanachuoni, na si wajinga au walioanza kutafuta elimu.

Watu hawa wanakosea zaidi kuliko wanavyopatia. Na huenda kosa lao likawa

kubwa zaidi kuliko anaepigwa Radd, huenda akapiga Radd kwa ujinga. Kazi

hii isishike yeyote isipokuwa wanachuoni, wenye Baswiyrah na wenye

maarifa.

Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=123057

21. Murji-ah Wanaamini Kuwa Matendo Ni Sharti Ya Kutimia Kwa Imani

22

Swali:

Je matendo yote yanaingia katika Imani? Na unasemaje kwa mwenye kusema

matendo ni sharti ya kukamilika kwa Imani?

´Allaamah al-Fawzaan:

Hii ni kauli ya Murji-ah. Matendo ni katika Imani na si kwamba ni sharti tu,

bali ni katika imani. Matendo ni imani. Allaah kaita matendo kuwa ni "Imani".

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1820

22. Wanaodai Kwamba Wanaweza Kujifunza Tawhiyd Kwa Dakika

Kadhaa Tu

Swali:

Kuna baadhi ya watu wanaosema kuwa wanaweza kujifunza Tawhiyd kwa

wiki moja au siku moja tu...

´Allaamah al-Fawzaan:

Hapana, wanasema wanaweza kujifunza kwa dakika mbili tu. Baadhi yao

wanasema dakika mbili tu. Ina maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) kwa kulingania kwake watu miaka 13 katika Tawhiyd alijichokesha

bure. Ilikuwa yatosheleza dakika mbili tu. Makusudio yao ni kuachana na

Tawhiyd. Wanachukulia sahali masuala ya Tawhiyd. Hii ni katika mfumo

wao.

23

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1820

Tarehe: 1431-03-30/2010-03-15

23. Haya Ni Maneno Ya Suufiy Asiefahamu Tawhiyd

Swali:

Tumesikia wanaosema kuwa inatakikana kwa mtafutaji elimu (mwanafunzi)

anapotaka kujifunza elimu ya ´Aqiydah asome pia masuala ya kiroho, kwa

kuwa elimu ya ´Aqiydah inaufanya moyo kuwa mgumu. Je maneno haya ni

sahihi?

´Allaamah al-Fawzaan:

Haya maneno ni batili. Haya ni maneno ya Suufiy. Haya ni maneno ya Masufi.

Hawataki ´Aqiydah iwe safi. Hawataki ´Aqiydah iwe safi. Wanataka ´Aqiydah

ichanganyike na kitu kingine. Je Tawhiyd inaufanya moyo kuwa mgumu au

inaufanya moyo kuwa laini?

>�34� آ')" زاد"3� إ'.)�) و>�, ر�3� '*7 7�ن ا�.;�-7ن ا��'� إذا ذ � هللا و5�1 3�7�8� وإذا "54� إ�.)

”Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao hujaa khofu,

na wanapo somewa Aayah Zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola

Wao.” (08:02)

�@.A" هللا � �� Bهللا أ � �� �3�7�8 �@.A"ا7���ب ا��'� آ�-7ا و

”Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Allaah. Hakika

kwa kumkumbuka Allaah ndio nyoyo hutua!.” (13:28)

24

C� "4�� 7�1دھ� و3�7�8� إ�, ذ � هللا

”Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Allaah.” (39:23)

Tawhiyd inaufanya moyo kuwa laini. Ama mwenye kusema kuwa inaufanya

moyo kuwa mgumu, huyu hafahamu Tawhiyd wala haijui. Hawa ni Masufi

na ukhurafi wa Masufi. Anadhani kuwa (Tawhiyd) ndio inauathiri moyo na

kuufanya kuwa mgumu.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1820

Tarehe: 1431-03-30/2010-03-15

24. Masuala Ya Mtu Kupewa Udhuru Kwa Ujinga -2-

Swali:

Ambae anaabudu kaburi na kumchinjia aliemo ndani ya kaburi, je

anakufurishwa au ni lazima kwanza zitimie sharti na kusiwepo vikwazo?

´Allaamah al-Fawzaan:

Kama kishafikiwa na dalili, Da´wah na Qur-aan, hapewi udhuru:

� � و�� ��� وأو�� إ�� ھ�ا ا���آن ���ر

25

”Na nimefunuliwa Qur-aan hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo

mfikia.” (06:19)

Ambae imemfikia Qur-aan na anafahamu lugha yake ya kiarabu, huyu hoja

imekwishamsimamia. Huyu anakufurishwa kwa kitendo chake cha

ushirikisha na `Ibaadah kinyume na Allaah baada ya yeye kufikiwa na Qur-

aan inayokataza Shirki na inaamrisha ´Ibaadah kwa Allaah peke Yake

Asiyekuwa na mshirika. Atakuwa yeye ndo mpuuzi kwa kutozingatia kwake

Qur-aan na wala hakujifunza Qur-aan.

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1820

Tarehe: 1431-03-30/2010-03-15

25. Mwenye Kuchukia Wanapotajwa Watu Wa Bid´ah Ni Katika Ahl-us-

Sunnah?

Swali:

Je yule mwenye kuchukia na kumsema mtu ambae anatahadharisha watu

dhidi ya Ahl-ul-Bid´ah na makhurafi, je anakuwa mtu huyu katika Ahl-us-

Sunnah au hapana?

´Allaamah al-Fawzaan:

Hili ni jambo khatari kusaidia Bid´ah na akachukia Sunnah. Mtu kama huyu

yuko katika khatari kubwa. Lakini huenda ni mjinga au ana hasira au ana

ufanaa wa ki-Jaahiliyyah. Jambo hili likiisha, hurudi mtu huyu katika asli

yake. Ama akisema hivi naye akaona ni sawa tu, huyu yuko katika khatari

kubwa.

26

Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1820

Tarehe: 1431-03-30/2010-03-15

26. Kupakana Mafuta Katika Da´wah

Swali:

Katika mji wetu kuna Madu´aat wanaofanya Da´wah wanaona kuwa kuna

maslahi makubwa ya kukubaliana na Masufi kutoongelea kwa mfano

Kulingana sawa Juu ya ´Arsh, na kuwa ni Haramu kumuomba mtu mwengine

zaidi ya Allaah n,k katika mambo ya ´Ibaadah. Wanahoji kwa kusema Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikubaliana na Mayahudi. Je ni sahihi? Ipi

nasaha yako?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Hapana si sahihi. Kwa kuwa unachosema Allaah, ndio Kauli ya Allaah

Aliposema:

وا �7 "0ھ� &04ھ-7ن ود

”Wanatamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie.” (68:09)

Kupakana mafuta katika dini haijuzu. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) alipokubaliana na Mayahudi ilikuwa ni huyu asimvamii mwengine. Si

kwamba alikuwa radhi kwa dini yao, kamwe! Na Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) hawezi kuwa radhi kwa dini yao. Ulichosema wewe maana

yake ni wewe unakubaliana na walioemo ya batili. Makubaliano ya namna hii

27

ni kupakana mafuta. Na kupakana mafuta ni Haramu. Haijuzu kwa yeyote

kumpaka mafuta yeyote katika dini ya Allaah. Ni wajibu kubainisha haki kwa

hali yoyote.

Lakini watapoona kuna maslahi makubwa kwa mfano ya kutoanza Da´wah

moja kwa moja kwa kukataza, waanze kwa ufafanuzi sahihi. Kwa mfano

wakiongelea Kulingana sawa Juu ya ´Arsh, atafafanua maana ya "Istawaa" na

abainishe ukweli wake bila ya kusema kuna watu wengine wanaofasiri

(maana ya Istawaa) kadha. Ila hili ni baada ya watu kujifunza na kuijua haki

na wakawa na urahisi wa kuachana na batili na kushikama na haki.

Chanzo: Liqaa al-Baab al-Maftuuh (156 B)

Tarehe: 1418-01-23/1997-05-30

27. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Kufuru Ya Yuusuf al-Qaradhwaawiy

Yuusuf al-Qaradhwaawi:

“Enyi ndugu! Kabla ya kuacha sehemu hii, nataka kusema neno kuhusu

matukio ya uchaguzi wa Israaiyl. Waarabu walikuwa wameweka matumaini

yao yote kwa ushindi wa Barleen, hata hivyo Barleen imeshindwa. Na hili

tunaisifia Israaiyl. Twatamani nchi yetu ingekuwa kama nchi hii (Israaiyl).

Kwa ajili ya mjumuiko mdogo wa watu wenyewe ndo wanahukumu

(serikali). Hakuna asilimia 94% au asilimia 95% (ya uchaguzi) tofauti na

tunavyojua katika miji yetu, asilimia 99% kwa asilimia 100%. Mambo gani

haya?! Lau hata Allaah Mwenyewe Angehudhuria kwa watu asingelipata

kiasi chote hiki cha kura kutoka kwa watu... Huu ni uongo, udanganyifu na

hadaa. Tunaikaribisha Israaiyl kwa ilichofanya.”

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

28

Muulizaji anauliza, kuna mtu ameongelea kuhusu uchaguzi wa nchi moja na

akasema kuwa kuna mtu aliepata kura asilimia 99% kwa 100%. Kisha akasema

lau Allaah Mwenyewe angehudhuria kwa watu asingepata kiasi cha kura zote

hizi. A´udhubi Allaah. Ni wajibu kwa mtu huyu kutubia. Ni wajibu kwake

kutubia na kama hakutubia inatakiwa auawe, kwa kuwa kamfanya kiumbe ni

mjuzi (muweza) zaidi kuliko Muumba. Ni wajibu kwake kutubia kwa Allaah.

Akitubia Allaah Husamehe makosa ya mja Wake. La sivyo ni wajibu kwa

kiongozi wa nchi kumkata shingo lake (na panga).

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=OUx51eZx7As

28. Hukumu Ya Kuchelewesha Swalah

Swali:

Ipi hukumu ya mwenye kuchelewesha Swalah ya faradhi mpaka ukatoka

wakati wake, isitoshe ni kuwa kadumu kufanya hivi ?

Imaam Ibn Baaz:

Hili ni munkari Haramu kwake. Haijuzu kwake kufanya hivyo. Kwa kuwa ni

wajibu kwake kuswali Swalah kwa wakati wake. Hili ndo la wajibu, kama

Alivyosema Allaah (Ta´ala):

("787 � (�(* Eة )�5 >�, ا�.;�-4� Fإن ا�

”Hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu.”

(04:103)

29

Ina nyakati zake maalumu kwa waumini, yaani imefaradhishwa kwa nyakati

zake. Ni wajibu kwa muumini kuswali kwa wakati wake na asiicheleweshe

mpaka wakati wa mwisho, si kwa mwanaume wala mwanamke. Ni wajibu

kwa wote kuswali kwa wakati wake; aswali dhuhr kwa wakati wake, ´Aswr

kwa wakati wake, Maghrib kwa wakati wake, ´Ishaa kwa wakati wake na Fajr

kwa wakati wake. Haifai kwake kuchelewesha swalah ya fajr mpaka jua

likachomoza, haifai kwake kuchelewesha Maghrib mpaka ukaingia wakati wa

´Ishaa, hali kadhalika haifai kwake kuchelewesha Dhuhr mpaka ukaingia

wakati wa ´Aswr, hali kadhalika kuchelewesha ´Aswr mpaka jua likazama.

Hili halijuzu.

Ni juu ya mwenye kufanya hivi alete Tawbah kwa Allaah na arejee kwa

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na kuna baadhi ya wanachuoni

wamemkufurisha mwenye kufanya hivyo kwa kuwa kaacha kitu mpaka

kimetoka nje ya nyakati za Shari´ah. Asli ni kuwa jambo hili ni munkari

mkubwa ni wajibu mtu kuwa tahadhari kwalo. Na ajitahidi muumini

mwanaume na mwanamke kuswali Swalah kwa wakati wake.

Chanzo: http://www.ibnbaz.org.sa/

29. Kufumba Macho Wakati Wa Swalah

Swali:

Ipi hukumu ya kufumba macho ndani ya Swalah? Nafumba macho yangu

kwa kuwa nakhofia kuangalia huku na kule na kujishughulisha na mambo nje

ya Swalah?

Imaam Ibn Baaz:

30

Kufumba macho ndani ya Swalah ni jambo la makruhu. Na si Sunnah. Sunnah

ni kufumbua macho.

Chanzo: http://www.ibnbaz.org.sa/

30. Kufunza Wanawake Pasina Pazia (Kizuizi) Kati Kati

Swali:

Vipi kumpiga Radd mtu ambaye anawafunza wanawake, anawafanyia

mihadhara bila ya kizuizi baina yao (wanawake) na yeye?

Shaykh Dr. Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy:

Tunamwambia amche Allaah (Jalla wa ´Aala) katika nafsi yake. Hakika

wanawake ni fitina. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imethibiti

kwake kuwa kasema:

"Sijaacha katika Ummah wangu baada yangu mtihani ambao ni mkubwa

kuliko wanawake, na hakika mtihani wa Baniy Israaiyl wa kwanza ulikuwa ni

wa wanawake. Hivyo ogopeni moto na muogope wanawake".

Haya ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kukaa na

wanawake baina yako wewe na yeye, jambo hili halijuzu. Kukaa na

mwanamke baina yako wewe na yeye, jambo hili halijuzu. Na ikiwa

wanawake wamejumuika (ni wengi), hili huenda pia likapelekea mtu huyo

kuingia katika fitina. Kwa kule kuwaangalia katika nyuso zao na

kuwaangalia. Huenda moyo wa muongeaji huyu ukavutiwa na nyuso za

baadhi ya wanawake hawa, anawekwa mitihanini akatumbukia katika balaa.

[Mshairi anasema]:

31

"Sema mwanamke uliemo ndani ya khimari nyeusi, maendeleo yako ni vipi?"

Hata kama walikuwa wamejifunika nyuso zao, (wanawake hao) walimuweka

katika mitihani (mchaji Allaah huyu)...

Mtazamo huu ni balaa kubwa. Ni wajibu kwa mja kumcha Allaah

(Subhaanahu wa Ta´ala) katika nafsi yake na asiiweke nafsi yake katika fitina.

Ikiwa mwanamke kaamrishwa kutolegeza sauti yake asijekuteleza yule

mwenye maradhi katika moyo wake, vipi tusemeje kujidhihirisha? Bila shaka

fitina ya hili ni kubwa zaidi.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=bH5IsgHjaP0&feature=plcp

31. Mchanganyiko Wa Wanawake Na Wanaume Katika Harusi

Swali:

Kwetu Sudan na katika miji mingine ya kiarabu wakati wa harusi na sherehe

mbali mbali kuna ada ya mchanganyiko baina ya wanawake na wanaume, je

jambo hili ni sahihi au hapana?

Imaam Ibn Baaz:

Ama kusherehekea harusi kwa wanawake peke yao bila ya kuwa wala

kuonekana na wanaume, jambo hili halina ubaya. Hali kadhalika wakati wa

ndoa mume na mke kula au kunywa pamoja, hakuna ubaya kwa hilo. Ama

mchanganyiko wa wanaume na wanawake hili ni munkari halijuzu, hali

kadhalika kuchanganyike mume (bwana harusi) na wanawake hili ni munkari

halijuzu. Bali ni wajibu kukataza hilo wala haliruhusu. Kwa kuwa jambo hili

linapelekea katika fitina. Ni munkari na halijuzu.

32

Chanzo: http://www.ibnbaz.org.sa/

32. Kumpa Zakaah Mama, Baba, Dada, Kaka Na Ndugu

Swali:

Ipi hukumu ya kumpa Zakaah mama yangu, baba yangu, kaka yangu na dada

yangu?

Imaam Ibn Baaz:

Kuwapa Zakaah wazazi wawili, watoto haijuzu kwa makubaliano ya

wanachuoni. Bali wamepokea hili wengine kutoka kwa wanachuoni.

Ama kumpa kaka, dada, mjomba, mama mdogo au ndugu waliobaki wa

karibu hakuna ubaya ikiwa ni mafukara. Wakiwa ni katika watu wa fungu la

Zakaah.

Ama wazazi wawili utawapa mali ila si katika pesa za Zakaah. Hali kadhalika

watoto wako na mke wako, utawapa mali ila si katika pesa za Zakaah.

Zakaah haijuzu kuwapa wazazi wawili, mke wako wala watoto wako. Lakini

ndugu wengine ikiwa ni mafukara - kama kaka, mjomba, mama mdogo na

wengineo hakuna ubaya. Kwa sharti ikiwa ni mafukara.

Chanzo: http://www.ibnbaz.org.sa/

33. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Tawhiyd-ul-Haakimiyyah

33

Swali:

Unasemaje kwa mwenye kusema kuwa kuna aina ya tatu ya Tawhiyd iitwayo

Tawhiyd-ul-Haakimiyyah?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Tunasema mtu huyu kapotea na ni mjinga. Kwa kuwa Tawhiyd-ul-

Haakimiyyah ni Tawhiyd ya Allaah (´Azza wa Jalla). Mwenye kuhukumu ni

Allaah (´Azza wa Jalla). Ukisema Tawhiyd imegawanyika mafungu matatu,

kama walivyosema wanachuoni... Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, yaani Tawhiyd-

ul-Haakimiyyah inaingia katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Kwa kuwa

Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ina maana ni Allaah peke Yake ndo Mwenye

kuhukumu, vilevile ni Allaah (´Azza wa Jalla) ndiye Mwenye Kuumba na

kuendesha mambo yote. Kauli hii imezushwa na ni munkari. Na vipi

Tawhiyd-ul-Haakimiyyah itakuwa yenyewe? Kauli hii imezushwa na ni

munkari. Kama anamaanisha kuhukumu, mwenye kuhukumu ni Allaah peke

Yake nayo inaingia katika Tawhiyd-ul-Haakimiyyah. Kwa kuwa Mola ndiye

Mwenye Kuumba na Maalik Mwenye kuendesha mambo yote. Hii ni Bid´ah

na upotofu.

Chanzo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (150 A)

Tarehe: 1417-10-20/1997-02-27

34. Muislamu Kuweka Dishi Chaneli Za Kiislamu Tu Nyumbani Kwake

Swali:

Vipi kuuza dishi (paraboli) yenye kuonesha tu Chaneli za Kiislamu tu na za

dini? Ni Chaneli zipi ambazo unaninasihi kusikiliza?

34

Shaykh Dr. Swaalih as-Suhaymiy:

Nakunasihi kufunga mlango huu. Na utosheke na Kitabu cha Allaah na

Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa ukileta dishi

kila kitu kitapita humo. Hata Chaneli ni wachache sana ambao wamesalimika

na yanayopita humo, hata wale wanaodai ni Chaneli za Kiislamu, unakuta

faida ni ndogo sana Qur-aan au Sunnah tu, lakini mimi nakhofia siku mingoni

mwa siku ukaingia Chaneli fulani, siku nyingine ukaingia nyingine kusikiliza

taarifa ya habari siku baada ya siku mpaka mwisho wake ukaja kutumbukia

mitihanini. Funga mlango huu! Wafunze watoto wako - walee kwa elimu,

kumkumbuka Allaah (´Azza wa Jalla), Qur-aan na Sunnah. Wape badala yake

mambo mengine ambayo ni mubaha (yenye kuruhusu) mbali na Chaneli hizi.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=RkZjkfMcpT8

35. Hukumu Ya Kupunguza Ndevu Na Kuzipamba

Swali:

Ipi hukumu ya kuzifanya fupi ndevu (kupunguza) na kuzipamba2

Shaykh Dr. Swaalih as-Suhaymiy:

Haijuzu kufanya hivyo. Bali ni wajibu kuziacha zilivyo kama alivyokuwa

akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=iqmMgxRRm8M

2 Kwa kuchonga, kuweka misitari n,k

35

36. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Kuendelea Kwa Masufi

Swali:

Je Masufi wanamfuata ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz? Je, wana Manhaj3 yake?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Kamwe!

Muulizaji:

Kuna mtu alisema kuwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz alikuwa Suufiy.

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

"Watu wangelikuwa wanapata wanavyodai, wangedai hata wana haki ya

maisha ya watu na mali zao."

Tunawaambia walete dalili. Si kweli. Tunawaambia watu hawa kila mwenye

kuvaa "Suuf", mtu huyo anakuwa Suufiy. Isitoshe Usufi umeendelea. Kuna

watu katika Salaf waliokuwa na Taswawwuf4 bila shaka. Lakini si kama

Masufi wakali waliopo leo.

Leo Usufi umeendelea sana mpaka kufika kuamini Wahdat-ul-Wujuud5 -

A´udhubi Allaah. Mpaka kulikuwa mtu asemae, hakuna Allaah! Kila kitu ni

Allaah (´Azza wa Jalla). Mwengine akasema hakuna ndani ya joho langu

isipokuwa Allaah. Anasema Joho ndio Allaah! Na baadhi yao hushikwa

nawazimu na kusema:

3 Mfumo 4 Usufi 5 Kuamini kila unachoona, waweza kukishika, kukinusa, kukihisi, n,k basi ndio Allaah

36

"Hamisha hema langu motoni."

Hali kadhalika ndivyo alivyosimulia Shaykh-ul-Islaam nae ni mwaminifu.

Wengine wanasema:

"Subhaana Allaah. Subhaana Allaah. Mimi ndo Allaah."

Ndio, Usufi sio jambo sahali. Umeendelea sana.

Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (131 B)

Tarere: 1417-03-03/1996-07-18

37. Mwenye Ugonjwa Wa Kutokwatokwa Na Mkojo Kuwa Imamu

Swali:

Ipi hukumu ya mwenye kuwasalisha watu nae ana ugonjwa wa

kutokwatokwa na mkojo?

´Allaamah Ahmad an-Najmiy:

Mwenye ugonjwa huu haijuzu kwake kusalisha watu. Inajuzu kwake kuswali

peke yake, lakini kuwa Imamu kwa kusalisha watu haijuzu.

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=JWdW4_jFOSs

37

38. Jamaa´at-ut-Tabliygh Na al-Ikhwaan al-Muslimuun Ni Katika Makundi

72 Ya Motoni?

Swali:

Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila

moja tu." [Ahmad, Abu Dawuud, a-Tirmidhiy]

Je Jamaa´at-ut-Tabliygh na Shirki (ushirikina) na Bi´ah zao, na al-Ikhwaan al-

Muslimuun na makundi yao ya vyama (Tahazzub) na uasi wao kwa mtawala,

je ni katika makundi haya 72 yaliyopotea?

Imaam ´Abdul-´Aziyz bin Baaz:

Ni katika wao. Ataekwenda kinyume na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-

Jamaa´ah anaingia katika mapote haya 72. Maana ya naneo lake "Watu

wangu" ni wale wanaomuitikia Allaah na kumfuata. Ni makundi 73. Kundi

lililookoka ni lile linalomfuata na yale yale alokuja nayo. Katika hayo makundi

72 kuna ambayo ni makafiri, watu wa bid´ah na waasi.

Muulizaji:

Ina maana haya makundi mawili ni katika hayo makundi 72?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio. Ni katika hayo mapote 72 na Murji-ah na wengineo. Murji-ah na

Khawaarij. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa Khawaarij ni makafiri na

wakati huohuo ni katika mapote hayo 72.

Chanzo: http://binbaz.org.sa/mat/4094

38

39. Haikuthibiti Kuwa Salaf Walikuwa Wakisema “Swadaqa Allaahu al-

´Adhiym”

Swali:

Ipi hukumu ya kusema "Swadaqa Allaahu al-´Adhiym" baada ya kumaliza

kusoma Qur-aan?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hili walikuwa hawafanyi Salaf. Haikuthibiti kutoka kwa Salaf kuwa

walikuwa wakikhitimu kisomo kwa kusema "Swadaqa Allaahu al-´Adhiym"

si ndani ya Swalah wala nje ya Swalah. Pamoja na kuamini mja kuwa Allaah

(´Azza wa Jalla) ndiye Mkweli zaidi wa kusema.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2343

40. Kufunga Safari Kwa Ajili Ya Kufanya Itikaaf

Swali:

Mwenye kuweka nadhiri kuwa atafanya Itikaaf katika Msikiti wa Riyaadh

kwa mfano, je huchukuliwa hii ni katika kufunga safari kinyume na Misikiti

mitatu na upi wajibu wake?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

39

Ndio, asifunge safari ila katika Miskiti mitatu, akae Itikaaf katika Msikiti

ulioko karibu na yeye. Na Allaah Anajua zaidi.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2347

41. Mwanamke Anaruhusiwa Kusoma Qur-aan Kwa Sauti Ndani Ya

Swalah?

Swali:

Je mwanamke asome kwa sauti kama mwanaume katika Swalah za kusoma

kwa sauti akiswali peke yake au na wanawake wenzake tu?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio asome kwa sauti akiswali peke yake na mahala hapo hakuna

mwanaume ajinabi anaesikia sauti yake. Hali kadhalika kama anaswalisha

wanawake atasimama katikati yao na atasoma kwa sauti kwa sharti pasiwepo

wanaume ajinabi wanasikia sauti yake. Kwa kuwa sauti ya mwanamke ni

´Awrah hata kama ni Qur-aan.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2257

42. Kumhijia Baba Ambae Alikuwa Anapuuza Swalah

Swali:

40

Muulizaji kutoka Ireland, je inajuzu kumhijia baba yangu ambaye kafa na

alikuwa haswali?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Yategemea vipi alikuwa haswali. Ikiwa alikuwa anapinga uwajibu wa Swalah,

basi ni kafiri asimhijii. Na kama alikuwa hapingi anaswali wakati fulani na

wakati mwingine anaacha amhijie baba yake na amuombee kwa Allaah

msamaha na Amrehemu.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2254

43. Zakaah Ya Kondoo Na Mbuzi

Swali:

Mtu ambae anamiliki kondoo 20 na mbuzi 20 akizichanganya zinafika

Niswaab6, je atoe katika kondoo au katika mbuzi, kwa kuzingatia ya kwamba

katika mji wetu sisi mbuzi ndio bora zaidi?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Atoe kile ambacho ni bora zaidi.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2253

6 Kiwango cha chini ya kutoa Zakaah.

41

44. Kukojoa Kwa Kusimama

Swali:

Ipi hukumu ya kukojoa kwa kusimama? Na je alikujoa Mtume (��+و (�G, هللا >�4

kwa kusimama?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Wakati wa haja hakuna ubaya kukojoa kwa kusimama. Imethibiti kwa Mtume

�G) wakati alipokuwa sehemu iliokuwa juu akahofia akikaa, هللا >�4 و+��)

mikojo itamrukia mwilini, hivyo akakojoa kwa kusimama. Atapoona mtu

mikojo itampata akakojoa kwa kusimama, hakuna ubaya kwake.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2252

45. Sehemu Kulikuwepo Kanisa Kujenga Msikiti

Swali:

Katika mji wetu kuna kanisa ya zamani na imehamwa, je inajuzu kuigeuza

ikawa Msikiti baada ya kurejeshwa?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ikitengenezwa na kuwekwa sawa sehemu hii kujengwe Msikiti na hakuna

ubaya. Maadamu kanisa ilikuwa ni ya zamani na imeshahamwa,

kutengenezwe vizuri na kubaki ardhi tu na wafanye Msikiti kwa Waislamu.

42

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2250

46. Kaapa Hatoenda Kisha Akaenda, Hukumu Yake

Swali:

Kuna mtu kamwambia ndugu yake "Hapana Wallaahi sintoenda nawe",

akaenda, ipi hukumu ya hilo?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Huyu atatoa kafara ya Yamini7.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2247

47. Hukumu Ya Kutoka Msikitini Baada Ya Kutolewa Adhaana

Swali:

Kuna mtu alikuwa Msikitini akatoka kwa ajili ya haja (dharurah), je inajuzu?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

7 Kulisha masikini kumi, akishindwa mtu awavishe nguo, au kumuacha mtumwa huru wa Kiislamu, na mtu akishindwa yote hayo afunge siku tatu

43

Hakuna ubaya kwake. Makosa ni kwa yule ambae katoka baada ya kutolewa

adhaana Msikitini bila ya haja, huyu ndie ambaye anapata dhambi. Ama kwa

mwenye kutoka kwa haja hakuna juu yake kitu kamwe.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2246

48. Kupunguza Ndevu Kwa Ajili Ya Kufanya Kazi Ya Udaktari

Swali:

Nataka kufanya kazi katika Hospitali, na katika sheria zao ni kuwa ndevu

zako zisizidi kipimo fulani. Je inajuzu kwangu kuchukua (kukata) ndevu

zangu kwa kupata hii kazi?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hapana haijuzu kuchukua katika ndevu zako chochote, na Allaah Mwingi wa

Kuruzuku Atakupa riziki nyingine. Shikamana barabara na kamba ya Allaah

ambayo ni Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (´alayhis-Salaam).

Amini kuwa Allaah Hatokutupa hata ukiacha kazi hii ya Hospitali. Riziki

yako iko mikononi mwa Allaah na inateremka kutoka mbinguni haimwendei

yeyote ikiwa ni yako. Ziache ndevu zako kwa kumridhisha Allaah na

kumfuata Mtume (´alayahis-Salaam).

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2245

49. Mtu Mkubwa Akiingia Katika Uislamu Anatahiriwa?

44

Swali:

Ipi hukumu ya kutahiriwa kwa yule aliyeingia katika Uislamu umri mkubwa,

je ni wajibu au Mustahaba8?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ni wajibu kutokana na ukamilifu wa twahara na kuondoka kwa maudhi na

uchafu.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2243

50. Kutumia Dawa Yenye Alcohol

Swali:

Je inajuzu kutumia madawa ambayo yana kiasi fulani cha alcohol?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Muislamu ajiepushe nayo. Kwa kuwa alcohol inalewesha na ni Haramu. Na

imekuja katika Hadiyth kuwa:

"Hakika Allaah Hakufanya dawa zenu kwa yale Aliyowaharamishia."

Muislamu ajiepushe na dawa hizi zenye alcohol.

8 Imependekezwa

45

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2241

51. Kupandisha Miguu Wakati Wa Sujuud Ndani Ya Swalah

Swali:

Kuweka baadhi ya vidole vya miguu miwili katika Sujuud inakubalika au

hapana?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio inakubalika si kwa ukamili. Kamili ni kwa mwenye kuswali kuweka

vidole vyote vitano katika ardhi akiweza, hili ndo kamili. Ama kuweka baadhi

yavyo tu inakubalika, ama ikiwa hakuweka kidole hata kimoja katika ardhi -

yaani kwa mfano akipandisha miguu yake - Swalah yake ni batili.

Hali kadhalika akisujudu mbiombio na asiweze kuweka vidole vyake vizuri

katika ardhi, huyu Swalah yake ni batili haisihi. Kwa kauli ya Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Nimeamrishwa kusujudu kwa viungo visaba." Na miongoni mwavyo ni

vidole vya miguu.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2239

52. Ni Kina Nani Salafiyyuun?

46

Swali:

Tunasikia sana Salafiyyah na tunasikia pia wanaowaponda, ni kina nani

Salafiyyah?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Salafiyyah ni wafuasi wa Salaf-us-Swaalih9 katika Maswahabah wa Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maulamaa wa Sunnah katika karne

bora. Hawa ndio Salaf na wafuasi wao ni wale wanaopita katika athari zao

sawa katika elimu na matendo na Da´wah ya Jihaad. Na ni neno la haki na ni

neno Mustwalaha la Kishari´ah, hawalikatai Ahl-ul-´Ilm.

Na Allaah Amrehemu Imaam Ibn Taymiyyah kasema:

"Asipingwe yule atayejinasibisha na Salafiyyah, hakika Salafiyyah haiwi

ila ni haki."

Kwa wanachuoni (neno Salafiyyah) ni katika sifa nzuri yenye baraka. Lakini

asijiite nalo ila mtu wa Sunnah, watu wa Sunnah ndo wajiite Salafiyyuun.

Ama watu wa Bid´ah na upotofu hawana lolote kuhusiana na Salafiyyah, kwa

kiasi cha Bi´dah zao. Mtu Jahmiy ni Jahmiyyah, Mu´taziliy ni Mu´tazilah,

Ash´ariy ni Ash´aariyyah, Ikhwaaniy ni Ikhwaaniyyah, Tabliyghiy ni

Tabliyghiyyah, Suruuriy ni Suruuriyyah na namna hio katika mapote

yaliyoangamia sawa yalioko sasa na ya zamani.

Ama Salafiyyah ni wafuasi (wale wanaomfuata) Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) kikweli, kwa kuwa wao wanawafuata waliotangulia -

Maswahabah wema katika Muhaajiruun na Answaar na maimamu katika

karne bora. Na namna hii kila mwanachuoni anapita katika athari za watu

hawa.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2235

9 Wema waliotangulia

47

53. Nimeingia Katika Uislamu Ila Nina Kaka Kafiri

Swali:

Dada kutoka Ubeljiji, mimi ni Muislamu Alhamdulillaah na kaka yangu ni

kafiri. Je inazuju kwake kuwa kwangu? Na je inajuzu kujifunua mbele yake?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Tunampa pongezi kwa Uislamu na hio ni fadhili za Allaah Humpa Amtakae

na Allaah ni Mwingi wa fadhila. Na kaka yake huyu kafiri amlinganie kuingia

katika Uislamu na amtakie Uislamu, huenda akakubali kwa Da´wah yake, na

ikiwa atakataa shari ni kwake. Ama kujifunua kwake hakuna neno kwa kuwa

ni katika Mahaarim wake ila tu hana haki ya kumfungisha ndoa. Ajitahidi

kumfanyia Da´wah kuingia katika Uislamu, huenda Allaah (´Azza wa Jalla)

Akamfungua kifua chake na akawa mwenye kutapa ujira.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2234

54. Sijdah Ya Kusahau Ndani Ya Swalah

Swali:

Mtu aliechelewa anaingia na Imamu katika Swalah, akasujudu pamoja nae

Sijdah ya kusahau. Huyo aliyechelewa akasimama kutimiza Rakaa zilizompita

kisha akatoa Salaam. Baada ya Swalah akaambiwa kuwa anawajibika kupiga

Sijdah ya kusahau mwisho wa Swalah yake. Je hili ni sahihi?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

48

Ndio ni sahihi kwa kuwa Sijdah ya kusahau inakuwa mwisho wa Swalah.

Kwa kila mwenye kuswali.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2231

55. Inajuzu Kutoa Mimba Ya Zinaa Kabla Ya Siku Arubaini?

Swali:

Je inajuzu kutoa mimba kabla mtoto hajafikisha siku arubaini kwa hoja ya

kuwa ni mtoto wa zinaa?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Kutoa mimba haijuzu sawa ikiwa ni mtoto wa zinaa au mwengine. Lakini

ikitokea dharurah na haja kwa mwanamke kama maradhi na mfano wa hayo

akamtoa kabla hajapuliziwa pumzi katika arubaini ya kwanza, hakuna neno

kwake.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2230

56. Mtu Akumbuka Katika Swalah Ya Subhi Kuwa Hakuswali Witr Jana

Usiku

Swali:

Nikipitwa na Swalah ya Witr, je niswali subhi katika siku ya pili?

49

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Akilala mtu akapitwa na Swalah ya Witr na ikafika Swalah ya subhi kabla

hajaiswali, aiswali wakati wa Swalah ya dhuhaa (kama kuilipa Witr).

Anaweza kuswali Rakaa nne, sita au nane kadiri na awezavyo. Wala asiswali

Witr Rakaa moja, au tatu au tano, hapana! Hakuna Witr ya mchana.

Chnazo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2228

57. Mwanamke Auliza "Je Nimeingiliwa Na Majini Usiku?”

Swali:

Mwanamke mjamzito alipoamka kutoka usingizini akakuta majimaji chini ya

miguu yake yanayofanana na hina na huenda ikawa ni hina, je yawezekana

hili ikawa ni katika kitendo (yani kaingiliwa) na jini?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hapana haliwezekani hili na wala asiwe na fikra kama hizi. Yawezekana ni

kama alivyosema mwenyewe ni hina na mfano wa hayo. Majini Allaah

(Subhaanahu wa Ta´ala) Hakuyapa uwezo huo kwa Muislamu, khasa kwa

yule mwenye kushikamana na nyiradi za asubuhi na jioni. Ni juu ya huyu

mwanamke kusoma nyiradi za asubuhi na jioni.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2227

50

58. Hukumu Ya Jina La "Abdul-Baaswitw"

Swali:

Ipi hukumu ya kuitwa ´Abdul-Baaswitw?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hakuna ubaya.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2226

59. Kufanya Kazi Kwenye Manyumba Ya Wazee Na Kuwahudumia Pombe

Swali:

Dada kutoka Ufaransa anauliza. Mimi nafanya kazi katika nyumba ya wazee

Ufaransa, na wakati fulani tunalazimika kuwahudumia mvinyo (pombe)

wakaazi wa nyumba hii. Je inajuzu kwangu kufanya kazi hii kwa vile sikupata

kazi nyingine?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ikiwa ni Muislamu haijuzu kushiriki katika jambo hili kwani anasaidia na

kuendelea maasi. Atafuta kazi nyingine mbali na sehemu hii.

51

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2225

60. Rakaa Nyongeza Aliyodiriki Mtu Na Imamu Haihesabiki

Swali:

Mwenye kuwahi Rakaa tatu katika Swalah ya Rakaa nne pamoja na Imamu,

Imamu akasahau na akazidisha Rakaa ya tano. Je atachukuliwa kawahi kwa

Rakaa hii nyongeza10?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hili ni suala ya Khilaaf kwa wanachuoni. Kauli yenye nguvu ni kwamba

hakuwahi kwa kuwa hii ni Rakaa ya ziada na haihesabiki katika Swalah.

Haimtoshelezi.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2224

61. Je Malaika wanamuona Allaah (´Azza wa Jalla)?

Swali:

Je, Malaika wanamuona Allaah (´Azza wa Jalla)?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

10

Yaani hana haja tena ya kukamilisha Rakaa ya nne?

52

Allaah ndiye Anajua zaidi.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2223

62. Vitu Vyeupe Vinavyomtoka Mwanamke Mjamzito

Swali:

Dada kutoka Ufaransa anauliza. Mwanamke mjamzito anatokwa na kitu

cheupe, je ni wajibu kwake kutawadha kwa kila Swalah?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio, vikitoka atatawadha. Ikiwa kuteremka kwake kunakatika, vimtokapo

atajisafisha kisha atapahifadhi (kwa kuweka kitu kama kitamba n,k) kisha

atawadhe baada ya kuingia wakati halafu aswali.

Mwanafunzi:

Lakini si damu Shaykh, ni kitu cheupe?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hata kama, ni lazima ajisafishe vinapomtoka na apahifadhi ikiwa ni kitu

kinaendelea kumtoka kisha atawadhe baada ya kuingia kwa wakati halafu

aswali. Ama ikiwa anapojisafisha vinakwisha (havimtoki), si lazima

apahifadhi (kwa kitu) na wala si lazima kutawadha baada ya kuingia wakati,

bali atatawadha wakati wowote ikiwa vinakuja na kuisha.

53

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2222

63. Kumtolea Salaam Mwenye Kudhihirisha Maasi

Swali:

Ipi hukumu ya kumpa Salaam mwenye kudhihirisha maasi, je kitendo chake

(kumpa Salaam) ni maasi?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Jambo la kwanza ni kuwa kuanza kutoa Salaam ni Sunnah na si wajibu. Jambo

la pili ni kuwa inafaa kumtolea Salaam mtoto, mkubwa na kwa yule amjuae

na asiemjua.

Ama kwa mwenye kudhihirisha maasi na mtu wa Bid´ah, ni juu ya Muislamu

kuwasusa. Asimsalimie mwenye kudhihirisha maasi na mtu wa Bid´ah.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2221

64. Kusahau Kusema Rabbiy Ghufirliy Katika Swalah

Swali:

Ipi hukumu kwa mwenye kusahau kauli "Rabbiy Ghufirliy" baina ya Sijdah

mbili?

54

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Kaacha jambo la wajibu, ikiwa aliacha kwa kukusudia Swalah yake ni batili.

Na ikiwa aliacha kwa kusahau au alikuwa hajui, hakuna neno atasujudu

Sijdah ya kusahau. Na ni wajibu kwa mjinga kujifunza, akimbilie kujifunza.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2219

65. Mwanamke Mjamzito Ana Ruqyah Maalumu?

Swali:

Je, kuna Ruqyah maalumu kwa mwanamke mjamzito kwa ajili ya ujauzito?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ruqyah ni moja tu katika Qur-aan na Sunnah. Hakuna Dhikr au Aayah

maalumu kwa mwanamke mjamzito.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2218

66. Inajuzu Kwa Mwanamke Kuondosha Nywele Za Kwenye Masharubu?

Swali:

55

Muulizaji kutoka Ufaransa anasema. Je inajuzu kwa mwanamke kuondosha

nywele kwenye masharubu yake kwa vile anaonekana vibaya kwa mwenye

kumtazama?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hili ni jambo la nadra sana kutokea kwa wanawake. Anaweza kuzitoa hakuna

neno. Masharubu hakuna tofauti katika kuyatoa na mwanaume, hivyo kwa

mwanamke itakuwa aula zaidi. Lau nywele hizo zingekuwa sehemu ya

ndevu, anaweza pia kuzitoa hakuna neno. Kwa kuwa yeye hakukalifishwa

kuzirefusha nywele za ndevu.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2215

67. Sunnnah Ya Kunyanyua Mikono Wakati Wa Du´aa Ya Istisqaa

Swali:

Khatwiyb akinyanyua mikono yake kwa ajili ya Istisqaa11, je wanaomsikiliza

wanyanyue mikono yao au hapana?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio katika Sunnah ni wao kunyanyua mikono yao wakati khasa wa Istisqaa,

si katika Du´aa nyinginezo. Hakuna ubaya, bali ni Sunnah kunyanyua mikono

yao.

11

Du´aa (Swalah) ya kuomba mvua

56

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2213

68. Hukumu Ya Kusoma Qur-aan Na Tajwiyd Kwa Watu Wa Bid´ah

Swali:

Muulizaji kutoka UK anasema. Je inajuzu kwangu kusoma Tajwiyd katika

Msikiti wa watu wa Bid´ah, kwa kuzingatia ya kwamba kuna Msikiti wa

Salafiyyah lakini hakuna anaefunza Tajwiyd?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Maulamaa wametahadharisha kusoma kwa watu wa Bid´ah. Ni wajibu kwa

muulizaji kuwa tahadhari nao, kwa kuwa watamdanga wamuingize katika

mkumbo wao katika Bid´ah, akatumbukia katika yakumdhuru katika dini na

dunia yake. Ni juu ya muulizaji atafute mwalimu atakayemfunza Qur-aan na

Tajwiyd katika watu wa Sunnah ambao wamesalimika na Bid´ah, na asiingize

nafsi yake na watu kama hawa akaja kuwa mmoja katika wao. Tahadhari

kubwa kwa hilo.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2212

69. Mwanamke Mjamzito Anataka Kujumuisha Swalah

Swali:

Dada kutoka Holland anauliza. Ikiwa mwanamke ni mjamzito na anachoka na

wakati mwingine ana mabinti wawili, je anaweza kujumuisha Swalah?

57

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Asijumuishe Swalah ila yule mwenye maradhi mazito (kutokana na ujauzito

huo) na hawezi kuswali kila Swalah katika wakati wake. Ama mwenye hali

kama hii ni wajibu kwake kuomba msaada kwa Allaah na aswali kila Swalah

kwa wakati wake na wala asicheleweshe Swalah kutokana na umuhimu wa

Swalah na huenda ndo ikawa sababu ya kuondosha uzito huu wa mwili.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2211

70. Kuwapa Matumizi Wazazi Wawili Ni Wajibu?

Swali:

Je, watoto kuwapa matumizi wazazi wawili ni wajibu?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Matumizi kwa wazazi wakati kwa haja ni wajibu, bali ni faradhi kwake

kuwapa matumizi wazazi wake na awakabidhi mwenyewe.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2210

71. Mama Kwenda Kumzuru Mwanawe Ambaye Haswali

58

Swali:

Kuna mama kutoka Algeria anataka kusafiri kwenda kwa mtoto ambaye

anaishi Ufaranasa kwa ajili kufurahi na matibabu pia kwani afya yake si nzuri,

lakini mtoto wake haswali na anaishi na mwanamke wa Kifaransa kinyume na

ndoa ya Kishari´ah. Je inajuzu kwake kwenda na inajuzu kwake kupokea

zawadi ya mtoto wake na ambaye anaishi nae?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Mtu huyu hana kheri ila tu kama anataka (kwenda) kwa ajili ya kumnasihi na

kumpa adabu au kumhukumu kama mama ikiwa atakataa kurudi katika mji

wa Kiislamu wakamhukumu kinachomstahiki. Asifunge safari kwenda

kwake!

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2209

72. Mzinifu Ni Lazima Tu Kupigwa Fimbo Au Kuuawa?

Swali:

Akizini mtu katika mji ambapo hawasimamishi Huduud12, je Tawbah kwake

yamtosheleza au ni wajibu kujipeleka mwenyewe katika mji unaosimamisha

Huduud mpaka wamsimamishie Hadd?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ajisitiri kwa stara ya Allaah na afanye Tawbah yakweli na wala asiende katika

mji mwingine.

12 Adhabu

59

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2207

73. Kufanya Kazi Kwa Mtu Wa Bid´ah Ambaye Ni Ikhwaaniy

Swali:

Je inajuzu kufanya kazi kwa mtu ambaye anajulikana ni katika kundi la al-

Ikhwaan (al-Muslimuun) na kazi hii si wajibu?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Mtu wa Sunnah wa kihakika hawezi kudhurika na mtu wa Bid´ah ila awe na

tahadhari, kwa kuwa mtu wa Bid´ah hamu yake kubwa yeye ni kueneza

Bid´ah. Afadhali mtu wa Bid´a ambaye halinganii katika Bid´ah zake, anaweza

kufanya kazi kwake na watu wasimdhuru.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2205

74. Hadiyth Kuhusu Kumpa Mgonjwa Swadaaqah

Swali:

60

Upi usahihi wa Hadiyth "Watibuni wagonjwa wenu kwa kuwapa

Swadaaqah"? Na je imewekwa katika Shari´ah kwa yule mwenye mgonjwa

kumpa Swadaaqah kwa kufanyia kazi Hadiyth hii?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio hilo ni jambo limewekwa katika Shari´ah, lakini ni kadiri na hali yake na

si wajibu. Kumpa Swadaaqah ni jambo zuri kwani huenda ikawa ndio sababu

ya kupona kwa mgonjwa na anapata ujira kwa mwenye kutoa Swadaaqah.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2204

75. Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Kutoongelea Tawhiyd Kwa Ajili Ya

Kuchelea Matatizo

Swali:

Kuna mtu ambae analingania watu katika Uislamu sehemu ambapo kuna

watu wa Bid´ah. Kaanza kulingania watu katika fadhila za ´amali akaacha

Tawhid ili asije kupatwa na matatizo. Linajuzu hili?

Imaam Ibn ´Uthaymiyn:

Msingi wa Da´wah makusudio yake ni uongofu. Kama anaona anaweza

kuwaongoza kwa kutoanza kwanza kuwakataza baadhi ya makosa walionayo

katika Tawhiyd, wakati huo huo anaazimia kuuongelea Tawhiyd, badala yake

akawatuliza kwa kuwaongelea Swalah, Zakaah, Swawm, Hajj kisha baada ya

hapo ndio akaingia katika Tawhiyd, naona kuwa hakuna ubaya kwa hilo.

Ama ikiwa hataki kuongelea Tawhiyd moja kwa moja, anasema usiongelee

Tawhiyd kwa kuwa hili mwisho wake hupelekea katika shari na mfano wa

61

hayo, hili halijuzu. Lakini akifanya hili njia ili kufika katika kulingana katika

Tawhiyd, hakuna ubaya.

Chanzo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (167 B)

Tarehe: 1418-06-15/1997-10-17

76. Hukumu Ya Kusema Kuwa Allaah Hachoki

Swali:

Ipi hukumu ya kusema "Hakika Allaah Hachoki"?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Huu ni msemo wa Mayahudi "Hakika Allaah Alipomaliza kuumba mbingu na

ardhi alipumzika".

Akisema mtu "Hakika Allaah hochoki ili apumzike" hakuna ubaya.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2202

77. Mwanamke Nimemnyonyesha Mwezi, Je Mimi Ni Mahram Wa Watoto

Wake?

Swali:

62

Kuna mwanamke ambaye nilimnyonyesha karibu mwezi, je huchukuliwa ni

ndugu wa watoto wake na Mahram wao au hapana?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio huchukuliwa ni ndugu wa watoto wake na Mahram, hali kadhalika na

kwa mabanati zake na ndugu zake. Kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam):

"Ni Haramu kwa kunyonya, yale ambayo ni Haramu kwa nasabu."

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2201

78. Kapangusa Juu Ya Soksi Na Wakati Alipozivaa Alikuwa Hana Wudhuu

Swali:

Kavaa soksi hali ya kuwa alikuwa hana Wudhuu, kisha akatawadha na

kupangusa juu ya soksi. Ipi hukumu ya Swalah yake ya Dhuhr na ´Aswr

alizoswali kwa Wudhuu huo?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ni juu yake kulipa Swalah hizo. Katika masharti ya kupangusa juu ya soksi

azivae hali ya kuwa yuko na twahara. Alipe Swalah zake tena, aanze na

Dhuhr kisha ´Aswr.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2198

63

79. Mjomba Wa Mume Ni Mahram?

Swali:

Mjomba wa mume ni Mahram kwa mke?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hapana si Mahram wake, si kaka wa mume wala mjomba wa mume wala

Khaal13, wote hao si Mahaarim ni ajinabi. Ni wajibu kwake kjisitiri kwao.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2196

80. Ambaye Yuko Nje Ya Swalah Anaweza Kumkosoa Anaeswali Akisoma

Vibaya Qur-aan?

Swali:

Je mume anaweza kumsaidia mke wake ambae anaswali peke yake ikiwa

atakosea katika kisomo (cha Qur-aan)?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

13

Kaka wa mume

64

Ndio anaweza kufanya hivyo akamkumbusha. Kumkumbusha Imamu si

lazima mtu yule awepo ndani ya Swalah. Bali ataesikia kosa la msomaji katika

kisomo chake na akamsaidia, amefanya vizuri.

Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2195

81. Salafiyyah Ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah

Swali:

Je Salafiyyah ni kipote katika vipote? Na je vipi kujinasibisha mtu

analaumika? Na ni kina nani wanachuoni wao?

´Allaamah al-Fawzaan:

Salafiyyah ndiyo Firqah an-Naajiyah14, wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-

Jamaa'ah, sio kipote kama mapote tujuayo leo "Hizbiyyuun", ispokuwa ni

Jamaa'ah ilioko juu ya Sunnah na dini. Wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-

Jamaa´ah. Kasema Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam):

"Kutakuwepo kundi katika ummah wangu wenye kuidhihirisha haki bila

kujali lawama za wanaowalaumu wala kuwakhalifu"

Na akasema Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam):

"Na utagawanyika huu Ummah katika mapote 73, yote hayo yataingia Motoni

ila kundi moja tu" (Maswahaba) wakauliza: “Ni kina nani hao ewe Mtume wa

Allaah?”

14

Kundi lililookoka

65

Mtume akasema:

“Ni wale wataokuwemo kwa yale niliyomo leo na Maswahaba wangu.”

Salafiyyah ni kundi linalofuata madhehebu ya Salaf15, ambao wamo kwa yale

aliokuwemo Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) na Maswahabah wake.

Na sio kipote (Hizb) - katika mapote tujuayo leo, Bali ni Jamaa´ah ya tangu

zamani wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), itaendelea

kuwepo na hawatoacha kudhihirisha haki mpaka kifike Qiyaamah kama

alivyotueleza Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=-ceIh68uZ0g

82. Muislamu Aliyeingia Uislamu Jinsi Ya Kutangamana Wazazi Wake

Makafiri

Swali:

Mke wangu ni Muislamu kutoka Ufaransa, na watu wake wote ni makafiri. Je

inajuzu kwake kuwahama (kuwakata) na wala asiongee nao kabisa? Na vipi

atatangamana na wazazi wake kwa kuwa na wao pia ni makafiri?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Hapana, atangamane na wazazi wake kwa wema. Awazuru, awaongeleshe na

katika maongezi ayape kipaumbele maongezi ya kuwafanyia Da´wah wangie

katika Uislamu, na wakihitajia hata mali awape. Kama Alivyosema Allaah

(´Azza wa Jalla):

15 Maswahabah

66

4�) �$�و&) وا"% �%3.) &� ا�0(Gأ�)ب إ�� و �� H4%+ I

“Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anayeelekea

Kwangu.” (31:15)

Kuwatendea wema wazazi hata kama ni makafiri ni wajibu na imekatazwa

kuwakata.

Muulizaji:

Vipi kuwapa zawadi?

´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:

Ndio awape zawadi.

Chanzo: Maktabah Ya Fataawa Za Wanachuoni

83. Ni Ipi Da´wah Ya Salafiyyah?

“Na wale waliotangulia, wa kwanza - katika Muhaajiruun na Answaar, na

waliowafuata kwa wema, Allaah Ameridhika nao, na wao wameridhika Naye;

na Amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele.

Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (at-Tawbah 09:100)

Imaam Al-Albaaniy:

67

Hakika Aayah hii Tukufu ndio msingi ambao inatakiwa kwa kila Muislamu

kuufanyia kazi kwa kuifahamu Da´wah ambayo imepewa jina na baadhi ya

maulamaa wa zamani na wa sasa, kuita "Da´wah Ya Salafiyyah". Kuna ambao

wanaiita ni "Da´wah Answaar-us-Sunnah al-Muhammadiyyah". Na wengine

"Da´wat Ahl-il-Hadiyth". Na majina yote haya maana yake ni moja. Kwa

hivyo hakuna njia kwa Muislamu kama anataka kuwa katika Firqat-un-

Naajiyah ila kwa kufuata Kitabu na Sunnah na kwa yale waliokuwemo Salaf-

us-Swaalih. Hili jambo la tatu, ni wajibu awe imara kwa kujidhihirisha kwa

Waislamu wote (awalinganie) wawe wenye kuokoka siku ya Qiyaamah.

“Siku ambayo kwamba mali hayatofaa kitu wala watoto.” (26:8)

Hivyo baada ya kurejea katika yale wailokuwemo Salaf-us-Swaalih sawa

katika ufahamu wetu, fikra zetu na rai zetu - hii ndio sababu ya msingi

inayowafanya Waislamu kutofautiana katika madhehebu mengi na njia

nyingi. Ambaye anataka haki arejea katika Kitabu na Sunnah, analazimika

kurejea kwa yale waliokuwemo Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) na Taabi´iyn na waliowafuata baada yao.

“Allaah Ameridhika nao, na wao wameridhika Naye; na Amewaandalia

Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu

kukubwa.” (at-Tawbah 09:100).

Chanzo:

http://www.youtube.com/watch?v=Pf3M9yxpaNE&feature=youtu.be

68

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na

Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.