Upload
wanachuoni
View
297
Download
15
Embed Size (px)
DESCRIPTION
Fataawa Za Wanachuoni (6)
Citation preview
1
����������������� ������������������
Fataawa Za Wanachuoni
[06]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo ni hizi zifuatazo:
1. Kuna Dalili Inayokataza Mahari Yasiwe Makubwa?
2. Baba Hataki Kuwaozesha Mabinti Zake Kwa Kukhofia Riziki Zao
3. Biashara Ya Kompyuta
4. Kafunga Mwezi Mzima Wa Muharram, Kapatia?
5. Kuna Muda Maalumu Wa Mtu Kufanya Kijicho?
6. Je Siku Ya ´Aashuraa Kuna Chakula Maalumu?
7. Kuuza Katika Maeneo Ya Msikitini Kama Bustani La Msikitini N,k
8. Mwanaume Anaruhusiwa Kuvaa Pete?
9. Mtu Anataka Kulipa Deni Katika Pesa Za Zakaah
10. Imamu Kakumbuka Kuwa Nguo Yake Ina Madhiy1 Ndani Ya Swalah
11. Mtoto Kupitia Mbele Ya Mwenye Kuswali
12. Mwanamke Anatokwa Na Upepo Kwenye Tupu Ya Mbele, Hukumu Ya
Swalah Yake
13. Mwanamke Mgonjwa Anastanji2 Na Kujiosha Kwa Maji Ya Zamzam
14. Hukumu Ya Unyevu3 Umtokao Mwanamke
15. Hadiyth Ya Waislamu Kupeana Zawadi Ili Wapendana
16. Mfumo Wa Kusoma Kwa Dada Salafiy
17. Kafunga Sunnah Kisha Baadae Kaamua Kula
1 Ni maji meupe yanayonata yanayotoka katika sehemu za siri kwa sababu ya kuwaza tendo la ndoa au kutokana na matamanio yaliyozidi ya kimwili kwa kutazama, kushika, kushikwa n.k. Kawaida mtu hafahamu kwa uhakika kinachotoka. Inawatoka wanaume na wanawake, japokuwa kwa wanawake inakuwa ni nyingi zaidi. Wanazuoni wamekubaliana kuwa ni najisi. 2 Ni kuondosha chenye kutoka kwenye njia mbili sawa ye mbele au ya nyuma 3 Majimaji, Utoko umtokao mwanamke
4
18. Talaka Inatokana Na Alivyokusudia (Nia) Ya Mume
19. Dada Anataka Kubadilisha Rangi Ya Nywele Zake Nyeusi
20. Twawaaf Ya Kuaga Ni Wajibu Katika ´Umrah?
21. Kuswali Swalah Za Sunanh Kabla Ya Swalah Ya Ijuma
22. Ewe Kaka Wa Kiislamu, Mtume Wako Akuamrisha Kufuga Ndevu
23. Nasaha Kwa Wale Wenye Kueneza Uvumi, Kusema Uongo Na
Usengenyaji
24. Kipigo Cha Kutia Adabu Kinachoruhusu
25. Hukumu Ya Kubaki Macho Baada Ya Swalah Ya ´Ishaa
26. Du´aa Nzuri Wakati Mwanamke Anataka Kuzaa
27. Wazazi Wanataka Binti Aende Kusoma Masomo Ya Mchanganyiko
Holland
28. Imamu Na Muadhini Hawatakiwi Kuwa Ahl-ul-Bid´ah; Kama Suufiy,
Ash´ariy, Mu´taziliy, Jahmiy
29. Hukumu Ya Muislamu Kuwa Na Urafiki Na Makafiri
30. Kakasirika Sana Ramadhaan Akala, Nini Hukumu Yake?
31. Ufafanuzi Wa Mwanamke Kulipa Swawm Zilizompita Katika Mwezi
Wa Ramadhaan
32. Kijana Kila Anapotubia Anarudi Kufanya Dhambi Tena
33. Kaswali Maghrib Msikitini Kisha Akaswali Tena Nyumbani Na Ahli
Zake
34. Kaoa Mwanamke Wa Ahl-ul-Kitaab Ambae Hataki Kuingia Katika
Uislamu
35. Mgonjwa Mwenye Kutayamamu4 Na Sasa Kapatwa Na Janaba
36. Kwanini Ndoa Nyingi Za Ulaya Zina Matatizo Na Zinavunjika?
4 Kuweka twahawa (Wudhuu) kwa kutumia udongo msafi
5
37. Mume Na Mke Wanaishi Ufaransa, Mume Anasema Waswali Kama
Wasafiri
38. Nasaha Ya Shaykh al-Waswaabiy Kwa Wenye Kutaka Kuoana
39. Aina Mbalimbali Za Sigara Za Hukumu Zake
40. Hukumu Ya Kubadilisha Rangi Nywele Nyeusi
41. Baadhi Ya Sifa Zinazopasa Kuwa Na Mke Mtarajiwa
42. Nasaha Kwa Yule Aliemlaani Mke Wake
43. Inajuzu Kula Nyama Za Wakristo Na Mayahudi Wa Leo?
44. Je Mkaaji Eda Haruhusiwi Kutoka Nyumbani Kabisa?
45. Hukumu Ya Uchawi Katika Uislamu
46. Kubadilisha Nywele Kwa Kuweka Rangi Nyeusi
47. Swawm Za Ramadhaan Huwekwa Nia Mara Moja Au Kila Siku?
48. Je Salaf Waliwahi Kutofautiana Kunako ´Aqiydah?
49. Baadhi Ya Vitabu Bora Vilivyozungumzia Siyrah Ya Mtume (´alayhis-
Salaam)
50. Kitabu Cha Majina Ya Mtume (´alayhis-Salaam)
51. Kuwaweka Wazazi Katika Nyumba Ya Wazee
Wanachuoni waliomo ni hawa wafuatao:
1. Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
2. Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
3. Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
6
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1. Kuna Dalili Inayokataza Mahari Yasiwe Makubwa?
Swali:
Je, kuna dalili katika Sunnah inayokataza ukubwa wa mahari?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kakataza ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) mahari makubwa. Bora zaidi
mahari yawe madogo kwa kufuata Sunnah. Hakika ´Aaishah (Radhiya
Allaahu ´anha) anasema:
"Hakuzidisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mahari ya
mke wake wala mabanati zake zaidi ya Dirhamu tano.” [Hadiyth hii
imepokelewa na Muslim]
Na uongofu bora ni uongofu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam).
Atakaezidisha na akawa anaweza hilo hakuna ubaya. Kama alivyosema
Allaah:
“Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa
chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote.” (04:20)
Nukta muhimu:
”Na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali.” (04:20)
Ikiwa anaweza hakuna ubaya. Wala watu hawahukumiwi hukumu moja,
fulani alitoa kiwango fulani nawe toa kiwango fulani. Fulani anaweza kuwa
na uwezo, na huyu mwengine akawa hana uwezo.
7
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4750
2. Baba Hataki Kuwaozesha Mabinti Zake Kwa Kukhofia Riziki Zao
Swali:
Ipi hukumu ya baba ambaye hataki kuwaozesha mabinti zake kwa ajili ya
riziki zao?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Huchukuliwa kuwa ni dhalimu. Na Allaah Hawapendi madhalimu. Anasema
Allaah:
�ا� أ���� ��� � وا������� أ
”Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.” (76:31)
Riziki yao iko kwa Allaah. Akimuozesha binti yake riziki yake iko kwa Allaah.
Ajitahidi kumuozesha kwa mwanamume mwema ambaye atamsaidia katika
dini na dunia yake. Haijuzu kwake kumkatalia kwa kitu alichomhalalishia
Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4706
8
3. Biashara Ya Kompyuta
Swali:
Ipi hukumu ya uuzaji wa kompyuta?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Akijua kuwa mtu huyu ataitumia katika kufanya maasi, haijuzu kwako
kumsaidia katika maasi na uadui. Kutokana na kauli ya Allaah (´Azza wa
Jalla):
�� ا��� وا���وان �ا � و ���و
”Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (05:02)
Na ama akiwa hajui na akamdhania mtu huyo vizuri, In Shaa Allaah hakuna
neno.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4707
4. Kafunga Mwezi Mzima Wa Muharram, Kapatia?
Swali:
9
Atakaefunga mwezi wa Muharram wote au baadhi ya siku chache, je kitendo
chake hiki kapatia?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ndio ni sahihi. Muulizaji anasema kwa kuwa nimesikia katika Hadiyth:
"Swawm bora kwa Allaah baada ya Ramadhaan ni Swawm ya mwezi wa
Allaah Muharram. "Jibu ni ndio, Hadiyth hii ni sahihi.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4708
5. Kuna Muda Maalumu Wa Mtu Kufanya Kijicho?
Swali:
Je, kuna muda maalumu katika Kitabu na Sunnah ambao hutokea kijicho kwa
wale wenye vijicho?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Elimu ya jambo hili iko kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah Hufanya
Atakacho. Wewe ni juu yako kujitibu nafsi yako kwa kufanya Ruqyah ya
Kishari´ah na Allaah Hufanya Atakacho. Na haya ni kama maradhi mengine
yote. Ujitibu kwa yale aliyokuruhusu Allaah na lini maradhi yataisha, elimu
ya hili ni kwa Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4710
10
6. Je Siku Ya ´Aashuraa Kuna Chakula Maalumu?
Swali:
Je kuna chakula maalumu siku ya ´Aashuraa?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Wewe ndugu hakuna chakula maalumu siku ya ´Aashuraa. Hili huenda ikawa
ni katika matendo ya Mashia, kwa kuwa Mashia wana Ghuluu5 katika siku ya
´Aashuraa na wana Bid´ah nyingi.
Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawana chakula maalumu siku ya
´Aashuraa, isipokuwa wao hufunga siku ya Tasuua´ na siku ya ´Aashuraa. Na
ataefunga zaidi ya siku mbili Allaah Amjaze mtu huyo kheri, kama ilivyo
Fatwa ya Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Allaah Awarehemu)
kupendekezwa kufunga mwezi wa Muharram wote.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4711
7. Kuuza Katika Maeneo Ya Msikitini Kama Bustani La Msikitini N,k
5 Kuchupa mipaka
11
Swali:
Hukumu ya kuuza katika maeneo ya Msikitini?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Pale ambapo ni maeneo ya Msikitini haijuzu kuuza, kutokana na ujumla wa
Hadiyth (inayokataza kuuza Msikitini).
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4712
8. Mwanaume Anaruhusiwa Kuvaa Pete?
Swali:
Hukumu ya kuvaa pete kwa kijana?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hakuna tofauti kati ya kijana wala mzee, hukumu yao ni moja. Na pete
hakubainisha ni pete ipi, ikiwa ni ya dhahabu ni Haramu kwa wanaume.
Ikiwa ni ya fedha ni Sunnah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4713
12
9. Mtu Anataka Kulipa Deni Katika Pesa Za Zakaah
Swali:
Mtu ambaye mali yake imeeneza Niswaab6, na yeye ana madeni kwa baadhi
ya watu. Je, anaweza kulipa madeni hayo kwa kulipa Zakaah?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Fatwa za wanachuoni zinasema kuwa jambo hili halijuzu, kwa kuwa
anajihami mali yake kwa kutoa Zakaah. Lakini ampe fakiri Zakaah. Na fakiri
ikiwa ndio huyo aliyekuwa akimdai hakuna ubaya. Kwa sharti isiwe
alikubaliana naye kabla, mimi nakukopa na wewe utanirudishia. Hii ni
khiyana haijuzu.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4714
10. Imamu Kakumbuka Kuwa Nguo Yake Ina Madhiy7 Ndani Ya Swalah
Swali:
Akikumbuka Imamu kuwa katika nguo yake kuna Madhiy, atoke katika
Swalah au aitimize?
6 Kiwango cha chini cha kutolewa Zakaah 7 Ni maji meupe yanayonata yanayotoka katika sehemu za siri kwa sababu ya kuwaza tendo la ndoa au kutokana na matamanio yaliyozidi ya kimwili kwa kutazama, kushika, kushikwa n.k. Kawaida mtu hafahamu kwa uhakika kinachotoka. Inawatoka wanaume na wanawake, japokuwa kwa wanawake inakuwa ni nyingi zaidi. Wanazuoni wamekubaliana kuwa ni najisi.
13
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa Madhiy ni najisi. Akiweza kuvua nguo hii aivue na aendelee na
Swalah. Na akiwa hawezi atoke (ndani ya Swalah) na paingie nafasi yake mtu
mwengine.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=283
11. Mtoto Kupitia Mbele Ya Mwenye Kuswali
Swali:
Akipita mtoto mdogo wakiume au wakike mbele ya mwenye kuswali,
anaharibu Swalah?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni hapana, haiharibu. Lakini usimwache mtoto uhuru moja kwa moja, na
ikiwa atapita haaribu Swalah. Anaeharibu Swalah ni mwanamke aliye
baleghe8, lakini ambae hajabaleghe haaribu Swalah lakini inapungua kidogo.
Ikiwa Mtume alizuia mtoto wa kondoo asipite mbele yake mpaka tumbo lake
likagusa kwenye ukuta, itakuwa mtoto mdogo! Hali kadhalika kwa mtoto.
8 Shaykh Swaalih al-Fawzaan anasema kauli yenye nguvu kwa wanachuoni ni kwamba Swalah haiharibiki bali thawabu ndio hupungua, sawa awe mwenye kupitia ni mwanamke au mwengine yeyote. Wa Allaahu A´alaam.
14
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4854
12. Mwanamke Anatokwa Na Upepo Kwenye Tupu Ya Mbele, Hukumu Ya
Swalah Yake
Swali:
Mwanamke katawadha kisha anatokwa na upepo wakati wa kuswali
anapoenda kwenye Rukuu na Sujuud, akaamua kuswali hali ya kuwa amekaa
ili asitokwe na upepo.
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ikiwa Swalah ni ya faradhi kusimama ni nguzo (lazima). Na ikiwa ni Swalah
ya Naafilah9, akiswali hali ya kuwa amekaa hakuna ubaya.
Na kutokwa na upepo katika tupu ya mwanamke hakutengui Wudhuu.
Kutenguako Wudhuu ni kutokwa na upepo katika tupu ya nyuma.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4855
13. Mwanamke Mgonjwa Anastanji10 Na Kujiosha Kwa Maji Ya Zamzam
9 Swalah ya Sunnah 10 Ni kuondosha chenye kutoka kwenye njia mbili sawa ye mbele au ya nyuma
15
Swali:
Mwanamke ni mgonjwa, anajiosha kwa maji ya Zamzam bafuni na anastanji
nayo. Je, hili linajuzu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ikiwa anajitibu kwa hili hakuna ubaya. Kwa kuwa kustanji kunachukuliwa ni
dawa. Hakuna ubaya In Shaa Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4856
14. Hukumu Ya Unyevu11 Umtokao Mwanamke
Swali:
Anauliza kuhusu unyevunyevu umtokao mwanamke?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Fatwa za wanachuoni zinasema kuwa unatengua Wudhuu. Pia Fatwa ya al-
Lajnah ad-Daa´imah inasema hali kadhalika - Fatwa ya Shaykh Ibn Baaz.
Anatakiwa kustanji na aoshe sehemu ilipopatwa nguo yake na unyevu huo,
kisha atawadhe.
11 Majimaji, Utoko umtokao mwanamke
16
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4857
15. Hadiyth Ya Waislamu Kupeana Zawadi Ili Wapendana
Swali:
Hadiyth (ombeaneni Du´aa mtapendana), je makusudio yake ni watu kupeana
zawadi au ni uongofu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ni watu kupeana zawadi. Kumpa ndugu yako Muislamu zawadi, naye
akakurudishia zawadi. Zawadi inasababisha mapenzi, kama kutoleana Salaam
baina ya Waislamu pia yasababisha mapenzi baina yao.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4858
16. Mfumo Wa Kusoma Kwa Dada Salafiy
Swali:
17
Yuko na dada ambaye ni Salafiyyah na anataka kuanza kuhifadhi Qur-aan,
aanze na kuhifadhi Qur-aan au kuhifadhi ´Aqiydah?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Akiweza afanye yote mawili kuhifadhi Qur-aan na kuhifadhi ´Aqiydah. Qur-
aan kwa mfano ahifadhi Aayah 5-10 kwa siku na ´Aqiydah baadhi ya masuala.
Hali kadhalika Hadiyth, kila siku Hadiyth. ´Aqiydah, Qur-aan na Hadiyth.
Kila siku kwa mfano Hadiyth moja, kila siku kwa mfano Aayah 5, na kila siku
baadhi ya masuala kuhusiana na ´Aqiydah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4702
17. Kafunga Sunnah Kisha Baadae Kaamua Kula
Swali:
Kuna kunuia kufunga Swawm ya Naafil, akala wala hakutimiza Swawm yake.
Je huku ni kuharibu ´amali na kunaingia katika Kauli Yake Allaah:
�!��� �ا أ� و �#"
“Wala msiviharibu vitendo vyenu.” (47.33)
´Allaamah al-Waswaabiy:
18
Imekuja katika Hadiyth, anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Mwenye kufunga Swawm ya sunnah na msafiri wanakhiari, wakitaka
watafunga na wakitaka watakula."
Hakuna ubaya akila na lau angelitimiza Swawm yake ingelikuwa bora.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4701
18. Talaka Inatokana Na Alivyokusudia (Nia) Ya Mume
Swali:
Ipi hukumu mume kamwambia mke wake "Nikirudi kwenye ghala mimi si
mumewe tena", kisha akajirudi?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hili itatokana na nia yake. Je, makusudio yake ni talaka kwa hili? Hili
itatokana na nia yake. Ikiwa makusudio yake ni talaka atakuwa kamtaliki. Na
ikiwa hakukusudia talaka, itakuwa si talaka. Kasema Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam):
"Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa
kile alichokusudia."
(Akimwambia) wewe si mke wangu, wewe si mke wangu mwema, au
nimridhiae. Itatokana na anachokusudia (nia yake).
19
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4700
19. Dada Anataka Kubadilisha Rangi Ya Nywele Zake Nyeusi
Swali:
Dada anauliza kuhusu kubadilisha rangi ya nywele nyeusi kichwani?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ikiwa nywele za kichwani ni nyeusi hakuhitajiki kuzibadili. Tayari ziko
kwenye asili yake rangi nyeusi. Haifai kupoteza muda na mali katika mambo
yasiyokuwa na faida. Zinazobadilishwa ni nywele zenye rangi nyeupe (mvi),
kwa kuwa zimebadilika zilikuwa nyeusi. Mtu anabalidisha kwa rangi yoyote
isipkuwa nyeusi tu. Rangi nyeusi haijuzu mtu kujibadilisha kwayo. Kutokana
na Hadiyth inayokataza hilo.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4698
20. Twawaaf Ya Kuaga Ni Wajibu Katika ´Umrah?
Swali:
20
Twawaaf ya kuaga katika ´Umrah ni wajibu au ni Mustahab12?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ni Mustahab. Yaani katika Hajj ni wajibu na katika ´Umrah ni Mustahab.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4237
21. Kuswali Swalah Za Sunanh Kabla Ya Swalah Ya Ijuma
Swali:
Je, inajuzu kwa mtu kuswali kabla ya Swalah ya Ijumaa Nawaafil kadhaa, na
je ni sahihi kuwa masuala haya yana khilafu kwa wanachuoni, na ipi kauli
yenye nguvu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kasema hili Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika taaliki yake katika
Subul-us-Salaam na pamoja na maneno ya Swan-´aan pia katika Subul-us-
Salaam kuwa: "Hakuna ubaya kwa Muislamu kuswali kabla ya Swalah ya Ijumaa
katika Naafil (sunnah) au Swalah ya Dhuhaa apendacho." Na Ijumaa huwa haina
Sunnah za kabla, bali Sunnah zake ni baada. Kwa hiyo anaweza kuswali kabla
ya Ijumaa Swalah za Naafil, kadiri na Allaah Atavyomuwezesha. Hakuna
ubaya In Shaa Allaah.
12 Imependekezwa
21
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4238
22. Ewe Kaka Wa Kiislamu, Mtume Wako Akuamrisha Kufuga Ndevu
Swali:
Hukumu ya kunyoa ndevu au kutoa kitu humo?
´Allaamah al-Waaswabiy:
Kufuga ndevu ni wajibu. Na kuzinyoa au kutoa kitu humo ni Haramu. Kwa
kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Kuweni kinyume na washirikina; fugeni ndevu kwa wingi na punguzeni
masharubu." [Muttafaq, Ibn ´Umar]
Mtume (´alayhis-salaam) anakuamrisha kufuga ndevu. Wewe zifuge na wala
usitoe humo kitu. Na anakuamrisha kuacha masharubu, usiyafanye marefu
wala usiyatoe yote.
Na Allaah Anasema:
�اب أ��� أن �-�#�� ,01/ أو (-�#�� ,��+�ر ا��(� ()��'�ن � أ&%ه
“Basi nawatahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapatamsiba au
ikawapata adhabu chungu.” (24:63)
Usijiamini. Kumbuka yule mtu aliekuwa anakula kwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) kwa mkono wake wakushoto, akamwambia "Kula kwa
22
mkono wakulia!", akasema "Siwezi". Akamwambia "Hutoweza kamwe."
Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi. Hakika Mtume alimuamrisha kula kwa
mkono wakulia, akasema hapana siwezi. Akamuombea Du´aa kumwambia
"Hutoweza."
Wewe pia usijiamini. Akikuamrisha Allaah au Mtume Wake (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) basi tekeleza. Na akikukataza Allaah au Mtume Wake kwa
kitu, basi jitenge nacho.
�ا �1��, 30 �4���6�ل ,)�وه و&� إن و&� آ�4�� ا�% ;�(� ا��:�ب وا�:�ا هللا هللا
”Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho.
Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.” (59:07)
Chanzo: http://www.olamayemen.net
23. Nasaha Kwa Wale Wenye Kueneza Uvumi, Kusema Uongo Na
Usengenyaji
Swali:
Ipi nasaha zenu kwa mwenye kueneza uvumi, usengenyaji na uongo?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Nasaha kwetu na kwao ni kuwa tuchunge nafsi zetu ila kwa kheri tu. Na
tuchunge ndimi zetu daima na kila siku, uwe ulimi utasema kheri tu na
23
kutosema shari. Na walikuwa wakisema baadhi ya Salaf: "Sijaona kitu
kinachostahiki zaidi gereza kama ulimi." Ulimi ufungwe, kwa maana usisemi kitu
ila kwa mambo yanayofaa na kuruhusu. Mbali na hayo ni madhara matupu.
Nasaha kwetu na wengine ni kuhifadhi ulimi na kuacha dhambi hii kubwa;
usengenyaji, uvumi - ni kueneza ufisadi kati ya watu wawili au kundi kwa
kusema uongo, kutoa ushuhuda wa uongo, na maneno ya kijinga yasiyokuwa
na kheri, na filamu za uongo, yote haya hayajuzu kuwa na mtu mwenye
imani. Mtu awe na tahadhari kwayo na mtu ajishughulishe na mambo yenye
faida na yeye katika dunia yake, kaburi yake na Akhera yake kwa kuchunga
matendo ya ulimi.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2307
24. Kipigo Cha Kutia Adabu Kinachoruhusu
Swali:
Mwalimu anaweza kumpiga mwanafunzi kumuogopeshe ili arejee kufanya
jambo fulani au kuacha jambo fulani, je hili pia linangia katika tishio
(dhuluma)?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kipigo cha kumuweka (kumtia) adabu mwalimu mnasihiaji Mukhlisw kwa
mwanafunzi, kipigo cha kumuweka adabu kidogo halaumiwi kutokana na
maslahi kwake (mwanafunzi) na kumkinga na yatayomdhuru katika uhai
wake na Mustaqbal wake.
24
Pia kipigo cha baba kwa mtoto wake, na kwa mleaji - kama mtu mkubwa kwa
mdogo.
Hali kadhalika mume kwa mke wake katika baadhi ya hali kama ambavyo
Allaah Alivyotoa idhini hio. Hichi huitwa kipigo cha kuweka adabu na
kutengeneza. Ataekifanya hana makosa wala haingii katika kufanya dhuluma.
Lakini ikiwa atachupa mipaka katika kupiga, hapo atachukuliwa amefanya
dhuluma. Na ikiwa atapiga bila ya haki hata kama kitakuwa ni kipigo kidogo,
atachukuliwa ni dhalimu na siku ya Qiyaamah Allaah naye Atamlipiza.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2308
25. Hukumu Ya Kubaki Macho Baada Ya Swalah Ya ´Ishaa
Swali:
Je inajuzu kutoka kwenda kutembea na familia baada ya (Swalah ya) ´Ishaa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kuwa macho baada ya ´Ishaa hairuhusiwi ila kwa msafiri au mwenye
kuswali, au mtafutaji elimu (mwanafunzi), au kusaidia kidogo katika mambo
ya Waislamu. Kama kwa mwenye wilaya katika wilaya ya Waislamu sawa
iwe kwa jumla au hususan. Mbali na hayo kuwa macho inadhuru na huenda
ikawa sababu ya kukosa Swalah ya Jamaa´ah, bali hata Swalah kwa wakati
wake.
25
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2309
26. Du´aa Nzuri Wakati Mwanamke Anataka Kuzaa
Swali:
Dada kutoka Ubeljiji anauliza. Ni Du´aa ipi ambayo mwanamke anaweza
kuomba wakati wa kuzaa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Amuombe Allaah Amuweke wepesi. Na Du´aa iliyojumuisha mengi ni yeye
aseme:
"Allaahumma anta Rabbiy, Laa ilaaha illa Anta. Khalaqtaniy wa ana ´abduka, wa
anna ´alaa ahdika wa wa´adika mastatwa´atu. A´udhubika min-sharri maaswanaatu.
Abu-ulaka bi ne´ematika 'alayyah wa abu-u bidhambi, faghfirliy innahu laa yaghfiru
dhunuuba illa anta."
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2310
27. Wazazi Wanataka Binti Aende Kusoma Masomo Ya Mchanganyiko
Holland
26
Swali:
Dada kutoka Holland anauliza kuhusu masomo yake ambayo ni
mchanganyiko. Nidhamu kwao (Holland) hawezi mwanamke kuacha shule
ila mpaka aeneze miaka kumi na nane, na wazazi wake wanamuhimiza asome
kwa kuwa mji (serikali) itawakata pesa kiasi fulani ikiwa hatokamilisha
masomo yake mpaka aeneze miaka kumi na nane, afanye nini?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Tunawanasihi wazazi wake kuhama kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda
katika mji wa Kiislamu. Wajitahidi sana wazazi wake mpaka aweze kuhama
kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu. Isitoshe mji
wa Kiislamu achague mji ambao unatekeleza Shari´ah za Kiislamu na wala
kusewepo masomo ya mchanganyiko. Ama kusema ana udhuru, hana
udhuru:
"Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba."
Haifai kwake kwenda katika masomo ambayo ni mchanganyiko katika mji
huu na mji huo, na ufisadi huko unakuwa wazi kabisa. Ahifadhi heshima
yake, dini yake na karama yake na akae nyumbani kwake. Na anaweza
kusoma kwa njia zenye usalama In Shaa Allaah.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2312
28. Imamu Na Muadhini Hawatakiwi Kuwa Ahl-ul-Bid´ah; Kama Suufiy,
Ash´ariy, Mu´taziliy, Jahmiy
Swali:
27
Muulizaji kutoka UK. Hakuna katika Msikiti wetu muadhini, vipi
tutamchangua muadhini na kwa kitu gani tutaangalia kwa mwenye kufaa
kutoa adhaana?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kwa hakika ni kwamba ni lazima kwa waliohai kuwa na Msikiti, na ni lazima
kwa Msikiti kuwepo na Imamu na muadhini, ili watu wahifadhi wakati na
waswali Jamaa´ah.
Kwa Imamu anashurutishwa awe mtu mwenye ´Aqiydah sahihi na mjuzi. Na
muadhini anashurutishwa awe mtu mwenye ´Aqiydah sahihi, iliyo salama;
Asiwe Suufiy, Ash´ariy, Mu´taziliy, Jahmiy wala asiwe mwenye ´Aqiydah
(Itikadi) potofu.
Bali anatakiwa awe katika Manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na awe na
´Aqiydah yao katika mlango wa Majina na Sifa za Allaah na yanayofanana na
hayo katika mambo makubwa kuhusu ´Aqiydah na Tawhiyd. Awe ni mtu
anaehifadhi wakati (wa Swalah), mtu anajua Fiqh - katika twahara yake,
usomaji wake, Swalah yake kiasi ambacho akikwama Imamu muadhini
asimame nafasi yake na aswalishe Jamaa´ah.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2314
29. Hukumu Ya Muislamu Kuwa Na Urafiki Na Makafiri
Swali:
28
Ipi hukumu ya kufanya urafiki na makafiri na ipi sura ya kufanya nao urafiki?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ufanyaji urafiki na makafiri unalioharamishwa ni kukubaliana na dini yao, na
kupenda dini yao. Akimpenda Muislamu Mkristo kwa Ukristo wake na
Myahudi kwa Uyahudi wake, na mwenye kuabudu moto kwa hilo basi hapo
atakuwa kama wao13. Na urafiki kama huu umeharamishwa.
3�<, �!0 & ����&�0� و&� (1
”Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao.”
(05:51)
Ama urafiki wa kikazi tu; kununua na kuuza, na kubadilishana mambo yenye
manufaa, na khidma makafiri kwa Waislamu. Hakika si katika urafiki hata
ikiwa Muislamu atafanya kazi kwa kafiri ili apate mshahara wake. Hakuna
ubaya. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka mfanya kazi
siku ya kuhamia kwake kwenda Madiynah mtu ambaye alikuwa ni kafiri ili
amuoneshe njia ya kwenda Madiynah na akampa mshahara wake. Jambo hili
kuhusu urafiki linahitajia ufafanuzi.
Ataejenga nao urafiki na akawapenda kwa dini yao anakufuru. Kwa dalili ya
Aayah hii. Ama urafiki kwa maana kufanya nazo kazi katika jambo la maslahi
tu, hakuna ubaya na wala si katika jambo limelokatazwa.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2286
13 Kafiri
29
30. Kakasirika Sana Ramadhaan Akala, Nini Hukumu Yake?
Swali:
Kuna mtu alighadhibika mchana wa Ramadhaan ghadhabu (hasira) nyingi
akala, nini juu yake?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ni juu yake kulipa na ni juu yake kufanya tawbah. Kwa kuwa ghadhabu
haimfanyi mtu akala, lakini jambo kama hili ni nadra kupatikana kwa watu.
Kufanya jambo kama hili ni juu yake kutubia kwa Allaah na ni juu yake
kulipa siku moja kulipa siku hii.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2285
31. Ufafanuzi Wa Mwanamke Kulipa Swawm Zilizompita Katika Mwezi
Wa Ramadhaan
Swali:
Mume alikuwa karibu sana na mke wake mchana wa Ramadhaan akatokwa
na manii, nini juu yake?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ni juu yake kulipa. Kwa kuwa hakufikwa na hilo ila baada ya kufikiria sana.
Analazimika kulipa (siku hiyo) na hana juu yake kafara. Alipe siku moja.
30
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2284
32. Kijana Kila Anapotubia Anarudi Kufanya Dhambi Tena
Swali:
Mimi ni kijana nimefanya dhambi nikatubia, kisha nikatubia kwa Allaah
lakini nikarejea tena katika dhambi hii, ipi nasaha zako kwangu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Rejea uombe tena Tawbah yakweli na wala usikate tamaa kwa Rahmah za
Allaah. Lakini rejea uombe Tawbah yakweli na uwe mkweli kwa Allaah
(´Azza wa Jalla). Atakusamehe Allaah dhambi yako na Ataifanya kuwa mema.
Lakini kuwa mkweli katika Tawbah yako na Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2283
33. Kaswali Maghrib Msikitini Kisha Akaswali Tena Nyumbani Na Ahli
Zake
31
Swali:
Tuliswali Swalah ya Maghrib Jamaa´ah Msikitini kisha nikarejea nyumbani
wakaniomba ahli zangu niwaswalishe Jamaa´ah, ipi hukumu? Je huchukuliwa
kwangu hii kuwa ni Witr ilihali yajulikana kuwa hakuna Witr mbili katika
usiku mmoja?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ni sawa kwake kufanya hivyo, inajuzu. Kwa kuwa ni kwa ajili ya kuwafunza.
Muulizaji:
Je, huchukuliwa kwangu kuwa ni Witr?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hapana si Witr. Mchana hakuna Witr.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2281
34. Kaoa Mwanamke Wa Ahl-ul-Kitaab Ambae Hataki Kuingia Katika
Uislamu
Swali:
32
Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab14 kabla ya kuwa na msimamo, na
nimepewa Fatwa na baadhi ya wanafunzi kuwa na subira nae mpaka hapo
atapoingia katika Uislamu, na kumeshapita miaka mitatu na bado hajaingia
katika Uislamu na sina nae watoto, na kwa sasa niko na matatizo nae, ipi
nasaha zako?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Bila wasiwasi wowote Shari´ah inajuzisha kuoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab
hata kama hatosilimu. Inajuzu kwake hilo. Kwa dalili ya Qur-aan. Ama
kuhusiana na matatizo hilo ni jambo la kawaida hata baina ya mume na mke
ambao ni Waislamu, na baina ya hawa Ahl-ul-Kitaab. Ni juu yake kuangalia
ambavyo anaweza kupatana nae ikiwa bado anataka kubakia nae, na ikiwa
matatizo yao haikuwezekana, itakuwa ni kama Alivyosema Allaah atampa
Allaah kila mmoja wasaa wake.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2280
35. Mgonjwa Mwenye Kutayamamu15 Na Sasa Kapatwa Na Janaba
Swali:
Mgonjwa ambaye hatawadhi kwa ajili ya maradhi na akapatwa na janaba
akatayamamu kisha akaswali, na baada ya siku nne akapona. Je ni lazima
kwake kuoga kutokana na janaba ilihali tayari kisha tayamamu?
14
Mayahudi au manaswara
15 Kuweka twahawa (Wudhuu) kwa kutumia udongo msafi
33
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni ndio. Ni lazima aoge kwa janaba. Ama Swalah kishaziswali kwa
kutayamamu kwa kuwa alikuwa hawezi kutumia maji. Swalah kishaziswali
na hatozilipa. Na janaba anatakiwa kuoga baada ya kuwa sasa anaweza
kutumia maji.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=551
36. Kwanini Ndoa Nyingi Za Ulaya Zina Matatizo Na Zinavunjika?
Swali:
Muulizaji kutoka Amerika, katika miji ya kimagharibi kuna matatizo mengi
baina ya mume na mke, mfano wa hilo kuna mtu alimuhama mke wake kwa
sababu ya kutomtii?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Matatizo ya watu hayatotatulika isipokuwa kwa Uislamu. Watu
wakishikamana na Uislamu watapata suluhu ya matatizo yao. Hakuna suluhu
isipokuwa ni Uislamu. Kuhusiana na Waislamu tunawanasihi warejee kwa
wanachuoni katika kutatua masuala mbali mbali mpaka hapo matatizo yao
yatatatulika kwa idhini ya Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=556
34
37. Mume Na Mke Wanaishi Ufaransa, Mume Anasema Waswali Kama
Wasafiri
Swali:
Muulizaji kutoka Ufaransa anauliza, mume wake anachelewesha Swalah ya
´Ishaa mpaka katikati ya usiku, na anasema kwa kuwa sisi tunaishi katika mji
wa kikafiri na anamwambia "Usiswali Rawaatib16 kwa kuwa sisi nia yetu ni
safari"
´Allaamah al-Waswaabiy:
Wewe ni mkazi, vipi utasema nia yetu ni safari? Wewe ni mkazi hivyo
unatakiwa kuswali Rawaatib. Wewe unasema nia yetu ni safari, je wewe
unafupisha pia Swalah za Rakaa nne (kama msafiri)?! Huu ni mgongano!
Kuswali (Swalah) za faradhi Rakaa nne kisha msiswali Rawaatib, kisha
unasema nia yetu ni safari. Wewe ni mkazi unatakiwa kuswali Swalah kama
wakazi. Ninawanasihi kuhamia katika mji wa Kiislamu, na kutafuta elimu ya
Kishari´ah (ya dini), na kuwa na ufahamu katika dini. Hii dunia haitodumu
kwenu, wala nyinyi hamtodumu katika dunia hii. Kimbilieni katika kutafuta
elimu ili muweze kumuabudu Allaah kwa Baswiyrah (elimu).
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=554
16 Swalah za Sunnah
35
38. Nasaha Ya Shaykh al-Waswaabiy Kwa Wenye Kutaka Kuoana
Swali:
Vipi inakuwa ndoa ya Kishari´ah?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Inakuwa kwa kutimiza masharti yake na nguzo zake. Ndoa ya Kishari´ah ina
sharti zake na ina nguzo zake. Zikitimia sharti na nguzo zake hapo ndo
inakuwa ya Kishari´ah (inayokubalika kidini). Ninamnasihi yule ambaye
anataka kuoa ajifunze kwanza Ahkaam za ndoa ili asije kutumbukia katika
jambo ambalo linaenda kinyume na Shari´ah ilihali naye hajui. Anasema
Allaah:
��ن �4% إن 104� �� �ا أھ< ا���@6�,
“Basi waulizeni wenye ukumbusho (wanachuoni) kama nyinyi hamjui.”
(16:43)
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=558
39. Aina Mbalimbali Za Sigara Za Hukumu Zake
Swali:
Hukmu ya kuvuta aina mbalimbali za sigara?
36
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa yote haya ni katika maovu. Na kasema Allaah (´Azza wa Jalla)
katika kumsifu Mtume Wake Muhammad (´alayhis-Salaam):
ABC#(�ا ���� م و(+< ��� ا�"�#�ت و(+%
“Na anawahalalishia vizuri, na anawaharimishia viovu.” (07:157)
Na haya ni katika hayo.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=564
40. Hukumu Ya Kubadilisha Rangi Nywele Nyeusi
´Allaamah al-Waswaabiy:
Usibadili maumbile ya Allaah. Nywele nyeusi zinabaki asli yake nyeusi, kama
alivyoziumba Allaah. Zikibadilika, yaani zikiwa nyeupe huyu ndiye
anayebadili bila ya (rangi) nyeusi. (Kama anavyosema Mtume):
"Badilisheni, ila epukeni (kutumia rangi) nyeusi."
Na bora zaidi ni mtu kutumia hina.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=563
37
41. Baadhi Ya Sifa Zinazopasa Kuwa Na Mke Mtarajiwa
Swali:
Ipi nasaha zako kwa anayeoa kwa wale wasiyo katika jamii yake ambapo
anaishi, (mwanamke) kutoka magharibi kwa mfano?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ndugu yetu anatakiwa kuoa mwanamke Muislamu, mwema, mtiifu, mwenye
msimamo, atakaekusaidia katika mambo ya dini yako.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=567
42. Nasaha Kwa Yule Aliemlaani Mke Wake
Swali:
Ipi hukumu kwa yule anaemlaani mke wake?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
38
"Kumlaani Muislamu ni kama kumuua." [Muttafaq, kutoka kwa Thaabit bin
Dhwahaa]
Tunamwambia yule anaemlaani mke wake atubie kwa Allaah na ajitahidi
kumbembeleza hata ikibidi kumpa mali mpaka amsamehe (mke wake).
Hakika kumlaani Muislamu ni katika madhambi makubwa.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=566
43. Inajuzu Kula Nyama Za Wakristo Na Mayahudi Wa Leo?
Swali:
Je inajuzu kula michinjo ya Mayahudi na Manaswara katika zama zetu hizi?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni ndio, ikiwa watachinja katika njia za Kishari´ah. Iwe kuchinja na si
kutumia mashine, kunyonga, kuipiga kwa kitu na mfano wa hayo. Na itajiwe
jina la Allaah (kabla ya kuchinja) na si jina la Yesu.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=572
39
44. Je Mkaaji Eda Haruhusiwi Kutoka Nyumbani Kabisa?
Swali:
Je kwa mwenye kukaa Eda kwa kufa mume wake anaweza kutoka nje ya
nyumba na mmoja katika jamaa zake?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hakuna neno kukitokea haja (dharurah), kama kumzuru jirani yako, au katika
jamaa zako. Ila hutakiwi kubaki isipokuwa katika nyumba ya mume wako.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=570
45. Hukumu Ya Uchawi Katika Uislamu
Swali:
Mchawi akienda Msikitini na akasimama na mimi katika safu. Je, naweza
kukata safu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni ndio, kwa kuwa mchawi ni kafiri na swalah yake ni batili. Ikijulikana
kama kweli ni mchawi anajulikana kwa watu huyu ni kafiri, alinganiwe
kuingia katika Uislamu na aambiwe kuomba Tawbah kutokana na dhambi
40
yake hio. Anatakiwa kutubia kabla ya kujiunga na safu kwa kuwa hata
akiswali Swalah yake ni batili mpaka aingie upya katika Uislamu. Kama
Alivyosema Allaah:
�راG0 �0�ه ھ#�ء &�I, >� �ا &� �� وK�&0� إ�� &�
“Na tutayaendea yale waliyoyatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama
mavumbi yaliyo tawanyika.” (25:23)
Matendo yake atayafanya Allaah siku ya Qiyaamah mavumbi yaliyo
tawanyika - Swalah zake, Swawm zake, Swadaaqah, Hajj, ´Umrah na ´amali
zingine zote njema hatozikubali Allaah kwa kuwa ni kafiri. Kwanza
anatakiwa kukufuru Mashaytwaan na amuamini Allaah. Kama Alivyosema
Allaah:
�:, M� �&N)ت و�O�"�� %'!) ��, PQ�ا �& �; ��� K� �#�� ا�% R��6 م ��� وهللا�-'����%وة ا���:� ا TU�16ا
“Kwani Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anayemkataa
Shaytwaan na akamuamini Allaah bila ya shaka amekamata kishikio
madhubuti kisichovunjika. Na Allaah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.”
(2:256)
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=569
46. Kubadilisha Nywele Kwa Kuweka Rangi Nyeusi
41
Swali:
Inajuzu kwa mke wangu kubadilisha rangi ya nywele zake (kwa kuweka
rangi) nyeusi? Yaani nywele zake ni nyeupe, anauliza inajuzu kubadili kwa
kuweka rangi nyeusi?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kwamba haijuzu. Nywele ambazo ni nyeupe unazibadili kwa rangi
yoyote isipokuwa tu rangi nyeusi. Kama ilivyokuja katika Hadiyth:
"Zibadilisheni, na epukeni (rangi) nyeusi."
Na hili ni kwa wanamume na wanawake.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=574
47. Swawm Za Ramadhaan Huwekwa Nia Mara Moja Au Kila Siku?
Swali:
Swawm ya Ramadhaan mtu huweka nia mara moja au ni lazima kuweka upya
nia kila siku? Na je nia inakuwa na saa maalumu au inakuwa wakati wowote
wa usiku?
´Allaamah al-Waswaabiy:
42
Ni wajibu kuweka upya nia kila siku kutokana na kauli sahihi (yenye nguvu)
ya wanachuoni. Kwa kuwa kila siku moja huchukuliwa ni tendo la kivyake na
inahitajia nia yake.
Ama swali lako la pili, ni katika wakati wowote wa usiku unaweza kuweka
nia.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1718
48. Je Salaf Waliwahi Kutofautiana Kunako ´Aqiydah?
Swali:
Wanasema baadhi ya watu kwamba Salaf walitofautiana katika baadhi ya
masuala ya ´Aqiydah, kwa mfano "Je alimuona Mtume wa Allaah ( 3�� �� هللا V
�� Mola Wake Usiku wa Mi´iraaj?", na kuwa hili lilitokea zama za (و6
Maswahabah. Je, maneno haya ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hawakutofautiana katika masuala ya ´Aqiydah ewe ndugu. Masuala ya
´Aqiydah ni kuonekana Allaah Peponi. Ni kwamba waumini watamuona
Peponi. Ama duniani hakuna yeyote ataemuona. Hakuna yeyote ataemuona,
hata Mtume (´alayhis-Salaam) hakumuona, wala hakumuona Muusa (´alayhis-
Salaam) . Alisema:
P� K�ل رب أر�P أ��% إK T���ل �� �%ا
"Nionyeshe nikutazame." Allaah Akasema: "Hutoniona." (07:143)
43
Hili ni hapa duniani. Hawana tofauti katika ´Aqiydah. Hii ni tofauti je,
alimuona yeyote duniani au haikutokea. Hii sio tofauti katika ´Aqiydah.
Kuonekana Allaah Peponi hili wamekubaliana wote Ahl-us-Sunnah wal-
Jamaa´ah wala hawatofautiani.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2750
49. Baadhi Ya Vitabu Bora Vilivyozungumzia Siyrah Ya Mtume (´alayhis-
Salaam)
Swali:
Ni kitabu kipi bora kilichopokea sifa za Mtume ( ����3 و6 �� هللا V)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Vitabu vipo vingi ewe ndugu. Ni vitabu vya Siyrah. Vipo vingi, na miongoni
mwavyo ni "Zaad-il-Ma´aad" cha Ibnul Qayyim, "Siyrat-un-Nabiy (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam)" cha Ibnu Hishaam mukhtasari yake. Hadiyth
sahihi zilizopokelewa kuzungumzia Siyrah ya Mtume ( ����3 و6 �� هللا V).
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2749
44
50. Kitabu Cha Majina Ya Mtume (´alayhis-Salaam)
Swali:
Ni kitabu kipi ulichotaja ambacho kilicho na majina ya Mtume ( ��V 3�� هللا
�� ?(و6
´Allaamah al-Fawzaan:
“Jalaal-ul-Afhaam was-Swalaatu was-Salaam ´aala Khayri an-Naam” cha
Ibnul Qayyim.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2754
51. Kuwaweka Wazazi Katika Nyumba Ya Wazee
´Allaamah al-Fawzaan:
Kulinda udugu kunaleta athari duniani na Akhera. Na ikiwa kuulinda udugu
kunapelekea kuishi kwa muda mrefu, na kunapelekea ukunjufu wa ziriki,
hivyo wema kwa wazazi itakuwa aula zaidi kwa kuwa wao wako karibu zaidi
kuliko vyote.
Kuwatendea wema wazazi kunapelekea Allaah Anapanua maisha yako na
Anakurefushia umri wako. Na kutowatendea haki kunapelekea kuwa na umri
45
mfupi na ugumu wa kupata riziki. Kama ambavyo kuwatendea wema
tunapelekea katika urefu wa umri na riziki kuongezeka. Na jazaa (malipo) ni
sawa na alivyotenda mtu.
�ن و �WIون �إ &� 104� ���
”Wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda.” (36:54)
Unafikiria nini kwa ambacho kimezoeleka leo, kwa masikitiko makubwa
katika jamii za Kiislamu wakati wazazi wanapokuwa wazee wanatupwa
katika nyumba za Ihsaan, au nyumba za wazee kama wanavyoziita. Mtoto
ndie anaefanya hivyo anawaweka wazazi wake au mmoja wao katika nyumba
za wazee. Utafikiria kana kwamba si watoto wake, au utafikiria ya kwamba ni
wazazi wa watu hawa wanaofanya kazi katika nyumba za wazee. Yaa
Subhaana Allaah! Je, (anaefanya hivi) ni mtu kweli au ni mnyama?! Laa
hawlah wala Quwwata illa biLlaah. Huu ni katika ukosefu mkubwa wa
adabu. Hili halifanywi na yule ambaye kwenye moyo wake kuna khofu kwa
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Ungelijisikiaje lau mtoto wako angelikufanyia kitendo hiki?! Unapo zeeka na
kuwa mgonjwa wanakuchukua na kukuweka katika nyumba ya wazee.
Ungelijisikiaje? Ungeliwakasirikiaje? Na dhambi ipi ambayo mtoto wako
angeliibeba? Kwanini wewe unaomba haki yako na wewe hutimizi haki
ambayo iko juu yako?! Amche Allaah kila Muislamu.
Ukosefu wa adabu kwa wazazi umeenea sana katika zama hizi, nyoyo
zimekuwa ngumu na wandugu kufarakana. Tumejiwa na maadui wa
magharibi na makafiri; ambao hawana familia wala nyumba isipokuwa
nyumba zao ni kama nyumba za minyama. Nyumbani kwao wanaishi
wenyewe au na mbwa. Ama kukuta anaishi na wazazi wake, na watoto wake,
na ndugu zake, hapana! Hili halipo katika miji mingi ya kikafiri.
Jambo la kusikitisha ni kwamba baadhi ya Waislamu leo wanataka kuwaiga.
Wanataka kuwatupa wazazi wao au mmoja wao katika manyumba ya wazee
na ili wawe zao huru. Na kama ana aina fulani ya hisia huenda akaja siku ya
Idi kuwasalimia, kuwazuru tu. Au baada ya siku ndo anawapitia na
kuwasalimia. Na anachukulia kuwa hii ndo haki kubwa alionayo juu yao.
46
Ni juu ya Muislamu kutanabahi na kumcha Allaah; na ajue kuwa anachofanya
(anachotendea mwengine) naye atatendewa. Na atalipwa kwa kitendo chake,
na asitangulize katika haki za wazazi wawili chochote isipokuwa tu utiifu
(haki) za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ikiwa anataka ujira na anataka
thawabu asitangulize chochote katika matendo isipokuwa haki za wazazi,
isipokuwa tu haki za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Na kwa haya, namuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa Majina Yake Mazuri na
Sifa Zake kuu Awaongoze watoto na vizazi vya Waislamu. Na tunamuomba
Awarudishe Waislamu katika Uislamu wao kwa sura nzuri inayotakikana. Na
Awafanye Waislamu wawe ni wenye kupendana na Ayafanye manyumba yao
kuwa mazuri. Tunamuomba Allaah vile vile Awaepushe na kujifananisha na
makafiri na wanafiki, na wale ambao wamekata na kuvunja udugu wakawa
kama minyama au wakapotea zaidi. Wa laa hawla wa Quwwata illa biLlaah.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=e91nM8dW-10
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.