90
PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA AJILI YA KUPUNGUZA HATARI ZA KIFUA KIKUU NA VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA MAGEREZA NCHINI TANZANIA KIJITABU CHA MWONGOZO KWA WAELIMISHA RIKA JULAI 2017

Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

  • Upload
    others

  • View
    27

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA AJILI YA

KUPUNGUZA HATARI ZA KIFUA KIKUU NA

VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA MAGEREZA

NCHINI TANZANIA

KIJITABU CHA MWONGOZO

KWA WAELIMISHA RIKA

JULAI 2017

Page 2: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana
Page 3: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Kitabu hiki kimeweza kutolewa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa

Kupunguza UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa Ushirika

namba AID-OAA-A-14-00046. Yaliyomo ni wajibu wa programu ya AIDSFree na si lazima kuwa yanawakilisha mawazo ya shirika

la USAID, PEPFAR au Serikali ya Marekani.

PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA AJILI

YA KUPUNGUZA HATARI ZA KIFUA

KIKUU NA VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA

MAGEREZA NCHINI TANZANIA

KIJITABU CHA

MWONGOZO KWA

WAELIMISHA RIKA

JULAI 2017

Page 4: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

AIDSFree

Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI (AIDSFree) ni mkataba wa

miaka mitano unaofadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Ukimwi wa Rais wa Marekani

(PEPFAR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya

Mkataba wa Ushirika AID-OAA-A-14-00046. AIDSFree inatekelezwa na Taasisi ya Utafiti na

Mafunzo ya JSI na washirika Abt Associates Inc., Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation,

EnCompass LLC, IMA World Health, Umoja wa Kimataifa wa VVU / UKIMWI, Jhpiego

Corporation, na PATH. AIDSFree inasaidia na kuendeleza utekelezaji wa mikakati ya PEPFAR

kwa kujenda na kuendeleza uwezo wa kitaalam na kutoa ushauri wa kitaalam kwa USAID,

serikali za nchi husika na watekelezaji wa miradi ya UKIMWI katika ngazi ya wilaya, mkoa na

kitaifa.

Recommended Citation

Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI (AIDSFree). 2017. Elimu rika

kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi vya ukimwi katika magereza nchini

Tanzania: Kijitabu cha mwongozo kwa waelimisha Rika: Julai 2017. Arlington, VA: Programu

ya AIDSFree.

AIDSFree Tanzania Uniformed Services

JSI Research & Training Institute, Inc.

Plot No. 2 Mkwawa Road, Oyster Bay

P.O. Box 9263

Dar es Salaam, Tanzania

Page 5: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

SHUKRANI

Shukrani zetu za dhati kwanza ziwaendee watu wa Marekani kupitia Msaada wa Shirika la

USAID la Serikali ya Marekani kwa kufadhili utolewaji wa Kijitabu hiki

AIDSFree/JSI inatoa shukrani kwa Uongozi wa Magereza Tanzania, hasa Dkt. Juma Malewa,

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania kwa kuidhinisha na kupitisha utungaji na

uchapishaji wa Kijitabu hiki. Tunamshukuru Bwana Ali Abdalla Ali, Kamishna wa Chuo cha

Mafunzo Zanzibar aliyefunga rasmi mafunzo ya majaribio ya Kijitabu hiki.

Tunatambua ushiriki na mchango uliotolewa na waakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo

na Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali na maafisa 54 wa

magereza hususan Dkt. Wilson Rugamba, Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt. Richard

Mwankina (Mrakibu Mwandamizi wa Gereza la Ukonga ), Dkt. Juma A. Mwaibako (Mrakibu,

Gereza la Ruanda, Mbeya), Dkt. Hilda Mmari (Mrakibu Msaidizi wa Magereza – Makao

Makuu), Dkt. Abdilatif Mkingule (Inspekta, Ukonga Chuo), na Dkt. Dotto Pakacha (Inspekta,

Gereza la Segerea). Mapendekezo yao yamesaidia kukiboresha Kijitabu hiki.

Shukrani za pekee ziwaendee Dkt. Beati Mboya, Mkurugenzi Mkazi wa AIDSFree/Tanzania na

Dkt. Peter Maro, Mkurugenzi maswala ya kiufundi kwa uongozi wao katika hatua mbali mbali

zilizochangia kuwepo kwa chapisho hili. Tunatambua juhudi za Dkt. John Gulaka, Afisa wa

Uhusiano-Magereza wa AIDSFree/JSI katika hatua mbali mbali za mchakato wa kukiandaa

Kijitabu hiki. Kwa wataalam wetu Bwana Ignatio Chiyaka na Bi. Zuki Mihyo, Kijitabu hiki

hakingeweza kuwepo bila mchango wao kwenye kuandaa yote yaliomo na kujumuisha

maoni na mapendekezo ya wadau husika wakiwemo Uongozi wa Jeshi la Magereza Tanzania.

Msingi wa Kijitabu hiki umetokana na Kitabu cha PharmAccess cha Waelimishaji Rika kwa

Majeshi ya Polisi, Magereza na Uhamiaji cha Mwaka 2013.

Page 6: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

iv

Page 7: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

v

YALIYOMO

Vifupisho .......................................................................................................................................................... vii

Utangulizi ........................................................................................................................................................... 1

Jinsi ya kutumia kijitabu hiki ................................................................................................................................... 1

Namna ya kuanza ....................................................................................................................................................... 1

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU ............................................................................ 3

Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na UKIMWI .................................................................................................. 3

Somo 2: Viwango vya HATARI ya maambukizi ya VVU kwenye magereza ................................... 23

Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya maambukizi ya VVU ............................................................................ 23

Somo 3: Kifua kikuu na VVU: Matibabu, huduma na msaada ........................................................... 38

Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU ................................................................................................................. 38

Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU: matibabu, huduma, na msaada ................................................................ 50

Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ............................. 55

Somo 4: Kuvunja ukimya kuhusu kifua kikuu na VVU. ........................................................................ 58

Kipindi 4.1: Kutambua aina za shutuma katika magereza ......................................................................... 58

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu .......................................................... 67

Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya kuwa na VVU .......................................................................................... 67

Orodha ya maneno ....................................................................................................................................... 73

Mirejeo ............................................................................................................................................................. 77

Page 8: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

vi

Page 9: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

vii

VIFUPISHO

UKIMWI upungufu wa kinga mwilini

WAVIU watu waishio na virusi vya ukimwi

SOSPA toleo maalumu la sheria ya makosa ya

kujamiiana 1998

VVU virusi vya ukimwi

Page 10: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

viii

Page 11: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

1

UTANGULIZI

Malengo ya programu hii ni kusaidia kubadili tabia miongoni mwa wafungwa na wafanyakazi

wa magereza ili kupunguza hatari ya VVU na kifua kikuu kwa kuwaelimisha juu ya mambo

yanayochangia na kuhamasisha matumizi ya huduma za afya zipatikanazo. Waelimisha rika

kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza watatoa mafunzo ili kuhakikisha wenzao

wanapata elimu, manufaa na ujuzi wa namna ya kupambana na VVU na kifua kikuu mahali

popote iwe gerezani ama nje ya gereza. Kitabu hiki kimetungwa kwa ajili ya matumizi ya

waelimisha rika kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza na kimetengenezwa mahususi

kwa ajili ya kukidhi mazingira ya gerezani. Ingawa, masomo yanaweza kupangwa kwa namna

fulani ili kutumiwa pia na wanufaikaji wengine ikiwemo polisi.

Jinsi ya kutumia kijitabu hiki

Kitabu hiki kinawapa waelimisha rika shughuli na maelezo muhimu kwa ajili ya kutoa

mafunzo ya VVU na kifua kikuu kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza. Waelimisha rika

watatumia njia mbalimbali kuwashirikisha wenzao kwenye majadiliano, michezo, michezo ya

kuigiza, pamoja na maswali na majibu. Mafunzo haya yametengenezwa kwa ajili ya makundi

madogo madogo ya washiriki wasiozidi 20. Kila kundi linapaswa kukamilisha masomo yote

tano yaliyo kwenye ratiba. Ratiba ya mafunzo inaweza kupangwa kwa kuzingatia shughuli za

kila siku za magereza na uwepo wa wafanyakazi wa magereza kwa ajili ya kusimamia

nidhamu ya wafungwa.

Mwongozo huu una masomo matano. Kila somo lina utangulizi kwa ufupi sambamba na

maelezo ya kina na ya uhakika. Masomo yanahusisha mada zifuatazo:

1. Maelezo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI

2. Tabia hatarishi kwa maambukizi ya kifua kikuu na VVU gerezani

3. Matibabu ya kifua kikuu na VVU, huduma, na msaada

4. Kuvunja ukimya juu ya kifua kikuu na VVU

5. Kuishi kwa matumaini ukiwa na kifua kikuu au VVU

Namna ya kuanza

Kabla ya kufundisha chochote au kuongoza majadiliano ya kikundi, soma na pitia mwongozo

huu ili kutambua na kuelewa kwa kina mada na maelezo yaliyomo. Maandalizi haya

yatamsaidia mwelimisha rika kuongoza majadiliano kwa ufanisi na kujibu maswali yoyote

ambayo yanaweza kujitokeza.

Maelezo yaliyomo kwenye mwongozo huu yanakwenda sambamba na malengo ya serikali ya

Tanzania kuzuia maambukizi ya VVU na kifua kikuu pamoja na kuzuia maambukizi nyemelezi

miongoni mwa wafungwa na watu waishio na VVU, na hivyo kuboresha afya zao. Mwongozo

huu unatoa maelezo muhimu kwa wakati muafaka.

Page 12: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

2

Orodha ya maneno na maana zake imetolewa mwishoni mwa mwongozo huu kwa ajili ya

kuwasaidia waelimishaji kuyatumia wanapofafanua maneno magumu.

Page 13: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

3

SOMO 1: ELIMU YA MSINGI KUHUSU

KIFUA KIKUU NA VVU

Lengo

Kukuza kiwango cha elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU miongoni mwa wafungwa

na wafanyakazi wa magereza.

Madhumuni ya Mafunzo

Mwisho wa somo hili, washiriki watakuwa na uwezo wa:

Kueleza maana ya kifua kikuu, VVU na UKIMWI.

Kuelezea dalili na ishara za kifua kikuu, VVU, na UKIMWI.

Kueleza namna ambavyo kifua kikuu na VVU vinaweza kuenezwa uraiani na gerezani.

Kueleza namna ugonjwa unavyoendelea.

Kueleza mambo ya uhakika kuhusu kifua kikuu, VVU, na UKIMWI nchini Tanzania kwa

ujumla na hasa kwenye magereza.

Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na VVU gerezani.

Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na UKIMWI

Dakika 60

Kipindi 1.1: Mazoezi:

Kuelewa VVU na UKIMWI

VVU na UKIMWI ukweli/uongo

Ueneaji wa VVU na magonjwa ya ngono

Uhusiano kati ya VVU na jinsia

Mwisho wa kipindi washiriki watakuwa na uwezo wa:

Kueleza maana ya VVU na UKIMWI

Kutokomeza imani za upotoshaji kuhusu UKIMWI

Kueleza namna ambavyo VVU vinaenezwa

Kueleza hatua tano za dalili za UKIMWI.

Page 14: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

4

Zoezi 1.Kuelewa VVU na ukimwi

Dakika 20

Hatua 1: Utambulisho

Jitambulishe kwa jina na uzoefu wako wa shughuli za uwezeshaji wa kifua kikuu na VVU

(ukiwa nao). Eleza majukumu yako kama mwelimishaji rika. Wakaribishe washiriki kwenye

majadilianao yao ya kwanza juu ya kifua kikuu na VVU. Waombe wajitambulishe. Kwa

kifupi eleza mada kwa ajili ya majadiliano.

Tambua kwamba kipindi hiki kinaweza kuwa cha kibinafsi na chenye hisia kali. Ndani ya

kundi panaweza kuwepo na washiriki wenye VVU au wenye rafiki wa karibu au

wanafamilia wanaoishi na VVU au UKIMWI. Wakumbushe washiriki kwamba si vibaya

kuachana na swali na wahimize kutoa maelezo yale tu ambayo wanajisikia vizuri kuyatoa.

Kama hawajisikii vizuri kuzungumzia mambo haya kwenye kundi kubwa,wanaweza

kuzungumzia kwenye makundi madogo madogo ama wawili wawili au kutochangia

kabisa.

Hatua 2: Taratibu za mafunzo

Taja kanuni hizi muhimu

Usiri: Heshimu maelezo binafsi ya kila mshiriki. Jaribu kujizuia kutoa maelezo nje ya

kikundi lakini ikiwa utafanya hivyo, toa maelezo ya ujumla pasipo kutumia majina ya

washiriki.

Heshima: Mheshimu kila mtu kwenye kikundi. Hii inamaanisha kutowashambulia

wengine (kwa maneno au matendo) na kuwa muwazi na mwepesi wa kuhisi mitazamo ya

wengine. Kumbuka kutumia kauli ya “MIMI”. Inavutia zaidi kusema “vizuri kwa mimi

binafsi, ninahisi kwamba….” Badala ya kusema, “Hapana, umekosea, ukweli ni kwamba…”.

Uangalifu: Sikiliza wanachokizungumza wengine. Hutaishia kujifunza kitu fulani tu bali

utawafanya wengine wajisikie kuwa huru zaidi.

Uwazi: Washawishi wengine kuzungumzia uzoefu wao wenyewe, pasipo kuwazungumzia

wengine. Chukua tahadhari. Usiwe mwoga wa kuzungumza kwa uwazi bila ugomvi,

kutukana ama kuwa mtu asiyejali hisia za wenzake.

Hatua 3: Maswali na majibuvvu na UKIMWI ni nini?

Swali: VVU ni nini?

Jibu: VVU maana yake ni virusi visababishavyo upungufu wa kinga kwa binadamu. Virusi hivi

hushambulia mfumo wa kinga wa mwili ambao huulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Hatua 4: Utangulizi

VVU na UKIMWI nchini Tanzania kulingana na “Ripoti ya Kuzuia VVU na UKIMWI

2016”(AVERT 2017)

Page 15: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

5

Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU

Asilimia 4.7 ya watu wazima wana maambukizi ya

VVU

Maambukizi mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015

Vifo 36,000 vyenye uhusiano na UKIMWI

viliripotiwa mwaka 2015

Asilimia 53% ya watu wazima wenye VVU

wanapata tiba ya kupunguza makali

UKIMWI ni nini?

UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga mwilini. Kuambukizwa virusi vya ukimwi

hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa kinga. Jambo hili humfanya mtu aliye na VVU

kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa ambapo mtu asiye na maambukizi ya VVU huenda

asingepatwa au angepona kwa urahisi. VVU hushambulia na kuharibu chembechembe za

mfumo wa kinga zijulikanazo kama CD4 ambazo hupambana na maambukizi. Kupungua kwa

chembechembe za CD4 huufanya mwili kushindwa kupambana na maambukizi na baadhi ya

saratani. Pasipo matibabu, VVU vinaweza kuharibu taratibu mfumo wa kinga na hatimaye

kukua na kuwa ugonjwa unaoitwa UKIMWI.

Hatua baada ya dalili za awali

Waambie washiriki kwamba mtazungumzia hatua za ugonjwa zinazojitokeza baada ya

dalili za awali: maambukizi makali ya VVU, kukua na kuongezeka kwa VVU bila kuonesha

dalili, na UKIMWI.

Hatua 1: Dalili kali za VVU

Ndani ya wiki 1–4 baada ya maambukizi, virusi vimeanza kusambaa, na mtu anaweza

kukumbana na mlolongo wa dalili zijulikanazo kama dalili kali za VVU. Dalili katika hatua hii

zaweza kuwa pamoja na homa, kuumwa kichwa, maumivu ya miguu, kuwashwa kooni, kukua

kwa fundo limfu, uchovu, ukurutu mwilini, maumivu na kuuma kwa viungo , kuharisha,

kubadilika kwa tabia ya ulaji, na kichefu chefu. Hatua hii hujulikana kitaalamu kama “acute

retroviral syndrome” au “acute primary HIV infection,” na dalili hizi zinaweza kutokea kwa

kuwa mwili wako unakuwa ukipambana na virusi. Ni mwitikio wa asili wa mwili dhidi ya VVU.

Katika kipindi hiki kiwango kikubwa cha virusi huzalishwa. Katika hatua hii ya maambukizi

makali ya VVU, mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kueneza VVU kwa wapenzi ama

watumiaji wenza wa madawa ya kulevya kwa kutumia sindano kutokana na kuwepo kwa

kiwango kikubwa cha VVU kwenye mishipa yao ya damu. Kwa hiyo ni muhimu kuchukua

hatua za kupunguza hatari za kueneza virusi.

Page 16: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

6

Hatua 2VVU Kukua na kuishi mwilini bila kuonekana:

Baada ya hatua ya maambukizi makali ya VVU, ugonjwa huhamia kwenye hatua ijulikanayo

kama “kukua na kuishi kwa VVU mwilini bila kuonekana.” Kipindi cha virusi kutoonekana

maana yake ni kipindi ambapo virusi vinaishi na kukua ndani ya mwili wa mtu pasipo

kuonesha dalili zozote. Katika hatua ya ukuaji wa virusi pasipo kuonekana, watu wenye VVU

huwa hawaoni dalili zozote labda zile ndogo ndogo sana. Hatua hii mara nyingine huitwa

“dalili za maambukizi ya VVU” au “maambukizi sugu ya VVU.” Eleza kwamba katika hatua hii,

VVU bado vinazaliana na kuongezeka kwa kiwango kidogo sana, lakini bado vipo hai. Ikiwa

utakuwa kwenye matibabu ya kupunguza makali, unaweza kuishi kwenye hatua hii kwa

miongo kadhaa, kwa kuwa matibabu husaidia kuwepo kwa kiwango kidogo cha virusi.

Hatua 3: Ukimwi

Hatua ya mwisho ya maambukizi ya VVU hutokea pale ambapo mfumo wa kinga unakuwa

umeharibiwa vibaya na virusi na mtu huwa katika hatari kubwa zaidi au huwa hatarini

kupatwa na maambukizi mazito na hatari zaidi au magonjwa ya bacteria na ukungu

magonjwa ambayo vinginevyo angeweza kupambana nayo (“maambukizi nyemelezi”). Idadi

ya CD4 inaposhuka chini ya 200 kwa kiwango cha milimita za mchemraba za damu, yaani

(200 chembechembe/mm3), unahesabiwa kuwa sasa una UKIMWI. Kwa mtu mwenye mfumo

wa kinga imara, idadi ya CD4 huwa ni chembechembe 500–1,650 kwa milimita za

mchemraba. Vile vile utahesabiwa kuwa una UKIMWI ikiwa utapatwa na ugonjwa nyemelezi

mmoja ama zaidi, bila kujali idadi ya CD4 zako.

Dalili za UKIMWI

Kupungua uzito ghafla

Homa za mara kwa mara au kutokwa na jasho usiku

Uchovu wa kupindukia na usioelezeka

Kuendelea kuvimba kwa tezi za limfu kwenye kwapa, kinena, au shingo

Kuharisha kwa zaidi ya wiki moja (uharo usiosikia dawa)

Kuwashwa mdomoni, njia ya haja kubwa, na sehemu za siri

Kukohoa pasipo kukoma

Majibu yenye rangi nyekundu, kijivu, pinki, ama zambarau juu ya au chini ya ngozi au

ndani ya mdomo, pua au kope za macho.

Kupoteza kumbukumbu, unyonge, na maradhi mengine ya nyuroni.

Chembechembe za CD4 ni chembechembe za damu zinazofanya kazi kubwa ya kuulinda mwili

dhidi ya maambukizi. Virusi hutumia chembechembe hizi za CD4 (mara nyingi huitwa

chembechembe-T au chembechembe –T saidizi) kuzaliana zaidi na kuenea kote mwilini huku

zikiharibu chembechembe hizo za CD4. Baada ya hapo mwitikio wa kinga utaanza kupunguza

kiwango cha virusi mwilini hadi kufikia kiwango fulani thabiti mwilini mwako. Wakati huu

chembechembe mpya za CD4 zitaanza kuongezeka, lakini huenda zisifikie kiwango cha

chembechembe za CD4 zilizokwishaharibiwa.

Chembechembe za CD4 ni nini?

Page 17: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

7

Magonjwa makubwa makubwa

Tofauti ya VVU na UKIMWI ni ipi?

Mtu mwenye maambukizi ya VVU anaweza kuwa na afya njema kwa miaka kadhaa bila ya

kuwa na ishara au dalili za maambukizi mwilini. Mtu mwenye virusi bila ya dalili ni “mtu

anayeishi na VVU” au “mwenye maambukizi ya VVU”.UKIMWI ni hatua ya mwisho ya

maambukizi na si kila mwenye VVU hufikia hatua hii. Baada ya mtu kuambukizwa VVU kwa

kipindi fulani (mara nyingi kwa miaka mingi), dalili zinazosababishwa na virusi huanza

kujitokeza. Katika hatua hii, watu wenye VVU huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na

maambukizi nyemelezi. “UKIMWI” ni ufafanuzi wa kidaktari unaowalenga watu wenye VVU

wanaosumbuliwa na ambukizi moja au maambukizi kadhaa mahususi, ikiwemo kifua kikuu,

saratani kwa kiasi kidogo, macho, ngozi, na hali ya mfumo wa neva.

Zoezi 2. VVU zoezi la Kweli/Uongo

Dakika 20

Hatua 1: Zoezi

Eleza kwamba mtafanya zoezi la kutolea ufafanuzi upotoshaji kuhusu VVU na UKIMWI.

Waambie washiriki kwamba utasoma maelezo na kama wanaamini ya kwamba maelezo

ni ya“UKWELI” wasimame; na kama wanaamini kuwa maelezo ni ya “UONGO” wakae.

Hakikisha maelekezo yanaeleweka vizuri. Soma maelezo mara moja au mbili. Waruhusu

washiriki wajibu. Waombe waelezee kwa nini wanaamini ya kuwa maelezo ni ya

KWELI/UONGO na jadilianeni

Muongozo wa majibu:

MAELEZO KWELI/UONGO

1. Unaweza kuambukizwa VVU kwa

kung’atwa na mbu

UONGO: Imethibitishwa kwamba VVU haviwezi

kuenezwa kwa njia hii.

2. Kufanya mapenzi kinyume na

maumbile ni moja kati ya njia hatari

zaidi kwa ueneaji wa VVU.

KWELI: Kufanya mapenzi kinyume na maumbile

ni hatari zaidi katika ueneaji wa VVU kuliko namna

nyingine yoyote ya kujamiiana. Wakati wa

kujamiiana kwa njia hii, mboo inaweza kuchana

ngozi laini njia ya haja kubwa, jambo ambalo

litaviwezesha virusi kuingia kwenye mishipa ya

damu.

3. Watu wanaweza kuambukizwa VVU

ikiwa watafanya mapenzi mdomoni na

mtu mwenye maambukizi ya VVU

KWELI: VVU vipo kwenye shahawa za mtu

mwenye maambukizi. Hivyo, VVU vinaweza

kuenezwa ikiwa shahawa zitaingia mdomoni mwa

mtu. Hatari ya kuambukizwa VVU unapofanya

mapenzi mdomoni huongezeka ikiwa kuna

Page 18: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

8

MAELEZO KWELI/UONGO

vidonda mdomoni. Hatari yaweza kupunguzwa

kwa kuvaa kondomu na kuhakikisha hakuna

shahawa zinazoingia mdomoni mwa mwenza

wako.

Kibaiolojia inawezekana VVU kuenezwa kwa

kufanya mapenzi mdomoni na mwanamke

mwenye VVU, lakini jambo hili linadhaniwa kuwa

ni kwa kiasi kidogo. Kutumia kinga kama

kondomu au kiwambo cha meno wakati wa

kufanya mapenzi mdomoni kunaweza kuzuia

kueneza zaidi kwa VVU, magonjwa mengine ya

ngono, na homa ya ini. Kiwambo cha meno ni

kipande mraba chembamba cha mpira au silikoni

ambacho huwekwa juu ya meno wakati wa

kufanya mapenzi mdomoni.

4. Zinapotumiwa kwa usahihi, kondomu

zinaweza kuwakinga wanaume na

wanawake kutokana na maambukizi ya

VVU.

KWELI: Kondomu hutoa ulinzi dhidi ya VVU, magonjwa

mengine ya ngono, na mimba zisizotarajiwa.

Zikitumiwa mara kwa mara kwa usahihi, kondomu ni

moja kati ya njia bora zaidi za kujikinga na VVU.

5. Dawa maalumu zinaweza kutibu

maambukizi ya VVU.

UONGO: Hadi sasa, hakuna tiba wala chanjo kwa

maambukizi ya VVU. Ijapokuwa, kuna vidonge

vinavyoweza kupunguza uzalianaji wa virusi ndani ya

mwili wa mtu aishiye na VVU. Vile vile kuna dawa

zinazosaidia kukinga ama kutibu maambukizi

nyemelezi yaliyosababishwa na VVU.

6. VVU ni ugonjwa unaowaathiri

makahaba na wanaume wanaofanya

nao mapenzi peke yake.

UONGO: Mtu yeyote anaweza kuambukizwa

VVU.Hatari ya mtu kupata VVU haina uhusiano na

jinsi mtu alivyo, bali tabia aliyo nayo.

7. Ukiishi na mwenza mmoja tu, huwezi

kuambukizwa VVU.

UONGO: Watu walio waaminifu kwa wenza wao

bado wanaweza kuwa katika hatari ya kupata VVU

ikiwa wenzi wao wanashiriki kufanya mapenzi ama

kuchangia nyembe na watu wengine wenye

maambukizi.

8. Watu wenye magonjwa ya ngono

(maambukizi yaenezwayo kwa njia ya

kujamiiana) wapo katika hatari kubwa

ya kuambukizwa VVU kuliko wale wasio

na magonjwa ya ngono ikiwa watafanya

mapenzi na mtu mwenye maambukizi

KWELI: Magonjwa ya ngono sehemu za siri

huvipa VVU njia rahisi ya kupenya kwenye mishipa

ya damu.

Page 19: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

9

MAELEZO KWELI/UONGO

ya VVU.

9. Mtu anaweza kupona VVU kwa

kufanya mapenzi na bikira.

UONGO: Bikira hawana uwezo wowote wa kuwaponya

watu wenye maambukizi ya VVU. Hadi sasa bado

hakuna tiba kwa VVU.

10. Huwezi kupata VVU kwa sababu tu

unaishi kwenye nyumba moja na mtu

mwenye ugonjwa.

KWELI: Kuishi kwenye nyumba moja na mtu mwenye

VVU hakuwezi kuwaweka hatarini wale wanaoishi nae;

VVU havienezwi kwa migusano ya kawaida ndani ya

familia.

11. Wakati wote unaweza kutambua

kama mtu ana VVU kwa mwonekano

wake.

UONGO: Watu wengi wanaoambukizwa VVU

hawaoneshi dalili yoyote ya ugonjwa kwa miaka mingi.

Ingawa, virusi vinakuwepo mwilini mwao na vinaweza

kuenezwa kwa watu wengine.

12. VVU vinaweza kuenezwa kutoka kwa

mtu mmoja mwenye VVU kwenda kwa

mtu mwingine pale wanapochangia

sindano wanapotumia madawa ya

kulevya.

KWELI: Kuchangia sindano wakati wa utumiaji wa

madawa ya kulevya kunabeba hatari kubwa sana

ya ueneaji wa VVU. Damu yenye maambukizi

hupitishwa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja

kwenda kwa mtu mwingine kupitia sindano yenye

maambukizi au vifaa vingine vilivyotumika

kuandaa au kujidunga madawa.

Hatari kwa wanaume na wanawake

kuambukizwa VVU huongezeka pale

ambapo pana magonjwa ya ngono

mahali ambapo kiwango cha VVU kiko

juu.

KWELI: Magonjwa ya ngono kwa wanawake

hayatambuliwi kwa urahisi na mara nyingi huisha

pasipo kuchunguzwa. Magonjwa ya ngono

sehemu za siri huvipa VVU njia rahisi kuingia

kwenye mishipa ya damu. Unyanyapa kwa

wanawake pia ni kikwazo ambacho kinawavunja

moyo wanawake kutafuta matibabu ya

kutosheleza.

Zoezi 3: Jinsi VVU na magonjwa ya ngono yanavyoenezwa

Dakika 10

Hatua 1: Maswali na majibi—uenezwaji wa VVU

Swali: VVU vinaenezwaje?

Jibu: VVU haiambukizwi kwa urahisi kama surua au homa ya mafua. Kwa mfano, virusi kama

surua na homa ya mafua huenezwa kwa njia ya hewa kwenye maeneo yenye vizuizi palipo na

watu wenye maambukizi. VVU huishi kwenye majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa kama

vile damu, shahawa, majimaji kabla ya shahawa, uke, uteute kwenye njia ya haja kubwa, na

maziwa ya mama. VVU vinahitaji kuingia kwenye mwili wa mtu. Hivyo basi, VVU vinaweza

kuenezwa kwa njia zifuatazo:

Page 20: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

10

Majadiliano kuhusu mapenzi salama

hayatawezekana kwa kuwa

magereza ni mahali wanapokaa

wafungwa kulingana na jinsia zao

wenyewe. Kwa sababu hii hawawezi

kuzungumzia mapenzi salama kwa

watu wenye jinsia moja, lakini elimu

hii itawasaidia watakapomaliza

kutumikia vifungo vyao na kurudi

majumbani mwao au katika jamii.

Mapenzi salama katika magereza

Uwepo wa maambukizi yatokanayo na

ngono (kotokwa maji maji, vidonda, na

miwasho ) huongeza hatari ya kupata na

kueneza VVU. Hii ni kwa sababu watu wenye

VVU wenye maambukizi ya magonjwa ya

ngono wana kiwango kikubwa cha VVU

kwenye ute wa sehemu zao za siri na/au kwa

kuwa kuingia kwa virusi kumerahisihwa

kutokana na uwepo wa michubuko kwenye

mucosa

Jinsi magonjwa ya ngono huongeza hatari ya

kupata na kueneza VVU

Kufanya ngono na mtu mwenye maambukizi

Kuongezewa damu au mazao ya damu na mtu mwenye maambukizi ya VVU

Kuchangia matumizi ya sindano, mabomba ya sindano, na vitu vyenye ncha kali vilivyo na

bacteria na mtu mwenye maambukizi ya VVU

Kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, kuzaa ama

kunyonyesha.

Hatua 2: Eleza

Zungumzia magonjwa ya ngono

Hatua 3: Maswali na majibu

Swali: Jinsi gani VVU havienezwi?

Jibu:

Maji maji mengine mwilini kama, machozi,

mate, jasho, matapishi na mkojo

Migusano binafsi: busu kavu mdomoni

pasipo na vidonda, kukumbatiana,

kushikana mikono, kusalimiana kwa

kushikana mikono.

Mikusanyiko kijamii: wakati wa kazi, shuleni, kwenye sinema, mgahawani.

Hewa au maji: chafya, kukohoa, kuogelea bwawani/madimbwi

Vifaa: kalamu, vyoo, taulo, mashuka, sabuni, vifaa vya kulia chakula, mavazi.

Wadudu: kung’atwa na mbu ama wadudu wengine

Hatua 4: Maswali na majibu—upunguzaji wa ueneaji wa vvu

Swali: Ueneaji wa VVU unawezaje kupunguzwa?

Jibu: “Mpango mkakati wa UNAIDS 2016–2021” (ukurasa.58) eneo la matokeo 4, ili

kupunguza ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma na bidhaa, umezitaka serikali za

kitaifa kutoa kipaumbele kwenye upatikanaji wa huduma za kinga za VVU kwa makundi

maalumu, ikiwemo watu wanaotumia madawa ya kulevya na wakazi wenza, ili kupunguza

kwa haraka kwa kuwakinga na kusimamia haki za watu wote kupata huduma za kutosha

zenye ubora wa juu bila ubaguzi. Kupunguza hatari kwa vijana na makundi maalumu kupata

VVU na madhara yake kwenye maeneo yote yenye

maambukizi ni jambo muhimu katika kutokomeza

ugonjwa wa UKIMWI (2016).

Ikiwa wewe ni mfanyaji mapenzi, kuna mambo

kadhaa muhimu unayopaswa kuchukua ili

kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU.

Kutojamiiana ni njia mojawapo ya kuzuia kupata

Page 21: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

11

au kueneza VVU. Ikiwa huwezi kuacha kujamiiana, tumia kondomu (ya kiume ama kike)

wakati wote ufanyapo mapenzi kwenye uke, njia ya haja kubwa ama mdomoni. Inapotumiwa

wakati wote na kwa usahihi kondomu za kiume na kike njia bora zaidi katika kuzuia kuzuia

VVU. Shughuli mbalimbali za kimapenzi vile vile zinabeba viwango tofauti vya hatari ya VVU.

Ngono kinyume cha maumbile pasipo kutumia kondomu au ngono ya kulazimisha ni njia

hatari zaidi kwa ueneaji wa VVU kwa kuwa hupelekea kuchanika kwa kuta za uke na njia ya

haja kubwa:

Usichangie sindano, bomba za sindano na vifaa vingine vyenye ncha kali na mtu yeyote

ikiwa unatumia madawa ya kulevya.

Pata matibabu ya VVU ikiwa wewe ni mama mjamzito unayeishi na VVU ili kupunguza

hatari ya kumwambukiza mtoto wako wakati wa ujauzito, kuzaa na kunyonyesha.

Hakikisha kwamba mazao ya damu unayopokea yamefanyiwa uchunguzi wa VVU.

Vaa vifaa vya kujikinga (Kama glavu na miwani ya kuzuilia vumbi) na safisha mikono

baada ya kushika damu na maji maji mengine (hasa kwa wataalamu wa huduma za afya

au watoa huduma).

Tumia dawa za kurefusha maisha au kinga ili kujikinga na uwepo wa maambukizi (ikiwa

inapatikana) ikiwa upo katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.

Jitolee mwenyewe, katahiriwe hospitalini

Punguza idadi ya watu unaofanya nao mapenzi. Unapokuwa na idadi kubwa ya wapenzi

unajiongezea nafasi ya kupata mpenzi mwenye VVU au ugonjwa mwingine uenezwao

kwa njia ya ngono.

Hatua 5: Elezea

Elezea “mapenzi salama” kwenye magereza

Page 22: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

12

Zoezi 4: Uhusiano baina ya VVU na jinsi

Dakika 10

Hatua 1: Eleza

Kijamii jinsi imefafanuliwa, kwa kuzingatia zaidi majukumu ambayo wanaume na wanawake

huyafanya katika jamii.Jinsi inaweza kufanya jambo kubwa katika kupandikiza ufuasi. Kwa

pamoja jinsia na jinsi hutoa uzoefu wa kipekee kwa wanaume na wanawake waishio na VVU.

Kwa hiyo kuelewa desturi za jinsi na ukosefu wa usawa wa jinsi ni muhimu katika kupunguza

hatari ya VVU miongoni mwa wanaume na wanawake, wavulana na wasichana. Ijapokuwa

kuwa mambo yanayofanana baina ya vihatarishi vya VVU na tabia katika jinsi mbalimbali,

tofauti zipo na baadhi ya watu huambukizwa zaidi kuliko wengine.

Hatua 2: Maswali na majibu

Swali: Kuna mtu anayeweza kutupa mfano wa namna ambavyo majukumu ya kijinsi

yanavyoweza kuathiri uwezo wa mwanamke kutumia dawa.

Jibu: Wanawake wanaweza kukumbana na changamoto nyingi na vikwazo inapokuja suala la

afya zao wenyewe na ustawi wao. Wengi wanaishi kwenye mazingira ya uonevu,

wanakumbana na unyanyapaa na ubaguzi katika jamii, ukosefu wa amana za kiuchumi na

huduma za kiafya na mara kwa mara wao ndio watoa huduma wa kwanza katika familia.

Changamoto hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa uwezo wao wa kumwona daktari, kufuata

dawa, kunywa dawa, kupumzika na kushusha kiwango cha msongo wa mawazo.

Hatua 3: Hitimisho

Swali: Hivyo, nini kifanyike kuhusu jambo hili?

Jibu: Tukumbuke kwamba jinsia zetu, umri, hadhi katika jamii zetu, nakadhalika ni mambo

yanayobadilika ambayo yanaweza kumfanya kila mmoja wetu kuwa na kiwango tofauti cha

hatari, uzoefu na uwezo wa kupata huduma na fursa.

Kipindi 1.2 Ufahamu juu ya Kifua Kikuu

Dakika 110

Kipindi 1.2: Mazoezi

Utangulizi juu ya kifua kikuu na ugonjwa

Ueneaji wa kifua kikuu

Kifua kikuu kisichoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu

Jinsi ya kuchunguza kifua kikuu

Mambo ya uhakika na upotoshaji kuhusu kifua kikuu

Maambukizi ya kifua kikuu na changamoto za ugonjwa magerezani.

Page 23: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

13

Madhumuni ya kipindi

Mwisho wa kipindi hiki, washiriki wataweza:

Kuelezea aina mbili za kifua kikuu

Kuainisha kifua kikuu kulingana na sehemu ya mwili iliyoathiriwa

Kufuta dhana ya upotoshaji kuhusu kifua kikuu

Kuelezea namna ambavyo kifua kikuu kinaenezwa

Kuorodhesha viashiria na dalili za kifua kikuu

Kuelezea tofauti baina ya maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa kifua

kikuu.

Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na maambukizi ya VVU.

Zoezi 1. Utangulizi kuhusu maambukizi ya kifua kikuu na ugonjwa

Dakika 10

Hatua 1: Eleza—kifua kikuu na vvu

VVU na kifua kikuu ni muunganiko hatari mno. Kila ugonjwa huufanya ugonjwa mwingine

uenee haraka zaidi. VVU huufanya mfumo wa kinga wa mwili kuwa dhaifu na mtu mwenye

VVU halafu akaambukizwa kifua kikuu huwa katika nafasi kubwa kuugua ugonjwa wa kifua

kikuu kuliko yule mwenye kifua kikuu asiye na VVU.

Hatua 2: Elezakifua kikuu nchini tanzania

Shirika la afya ulimwenguni limeitaja Tanzania kama nchi yenye mzigo mkubwa wa kifua

kikuu (TB), na moja kati ya nchi zenye mzigo mzito wa kifua kikuu na VVU. Mnamo mwaka

2013, wagonjwa 64,000 wa kifua kikuu waliripotiwa na asilimia 83 (53,120) ya wagonjwa hawa

walikuwa wamepatiwa ushauri nasaha na kupimwa VVU. Katika kundi hili, asilimia 39 (20,717)

walikutwa wakiwa na maambukizi ya VVU. Mwezi Aprili 2016 kulikuwa na takribani wagonjwa

295 wa kifua kikuu mapafuni katika kila watu wazima 100,000 katika Tanzania (International

Organization for Migration in Tanzania 2016).

Serikali imeweka kipaumbele kutolewa kwa pamoja kwa huduma za kifua kikuu na VVU ili

kupunguza mzigo wa magonjwa haya. Kwa hiyo, watu waishio na VVU wanaotumia vidonge

vya kupunguza makali wana nafasi nzuri ya kupambana na maambukizi ya kifua kikuu. Utoaji

wa huduma hizi pamoja utahakikisha pia upatikanaji wa matibabu ya kifua kikuu na VVU kwa

kiwango kikubwa zaidi.

Hatua 3: Jadili

Kifupisho “TB” kinamaanisha nini?

Unadhani ni jambo gani husababisha kifua kikuu?

Page 24: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

14

Hatua 5: Elezavipi na kwa nini

Kifua kikuu kinasababishwa na bakiteria wanaoitwa Mycobacterium tuberculosis. Kwa kawaida

bakiteria hawa hushambulia mapafu, lakini bakiteria wa kifua kikuu wanaweza kushambulia

sehemu yoyote ya mwili ikiwemo figo, uti wa mgongo na ubongo. Si kila aliyeambukizwa na

bakiteria wa kifua kikuu huugua. Hivyo basi, kuna namna mbili zenye uhusiano na kifua

kikuu: maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu. Ikiwa

hautatibiwa vizuri, ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kuwa ugonjwa wa kifo. Wote wenye hali

fulani kiafya inayodhoofisha mfumo wa kinga vile vile huwa hatarini kupata kifua kikuu.

Maziringira yanayowafanya watu kuwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa haraka na ugonjwa

wa kifua kikuu ni pamoja na:

Maambukizi ya VVU

Matumizi mabaya ya madawa

Silikosisi/asbestosi: ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na kuvuta hewa iliyo na madini

ya silika ambayo ni sehemu ya mchanga, miamba na mawe yenye madini kama vile

kwazi. Baada ya muda, kuwepo katika mazingira yenye chembechembe za silika

husababisha makovu kwenye mapafu, ambayo yanaweza kuathiri uwezo wa mtu

kupumua.

Ugonjwa wa kisukari (aina ya 2): ugonjwa sugu wenye kiwango cha juu cha sukari

(glukosi) isivyo kawaida kwenye damu.

Ugonjwa mkali wa figo

Uzito mdogo wa mwili

Saratani

Matibabu kama vile corticosteroids au upandikizaji wa viungo.

Zoezi 2: Ueneaji wa kifua kikuu cha mapafu

Dakika 20

Hatua 1: Eleza: kifua kikuu cha mapafuni nchini Tanzania

Idadi ya waathirika wa kifua kikuu cha mapafuni katika Tanzania iliripotiwa kuwa watu 295

kati ya watu 100,000, kulingana na hotuba ya bajeti ya mwaka 2014/2015 ya waziri wa afya.

Kifua kikuu cha mapafuni ni moja kati ya maambukizi nyemelezi kwa wengi miongoni mwa

watu waishio na VVU. Karibu asilimia 39 ya wagonjwa wa kifua kikuu nchini Tanzania

wameambukizwa VVU (WHO 2012).

Hatua 2: Chemsha bongo

Wagawe washiriki katika makundi ya watu 3 au 4 na acha wajadili njia ambazo kifua kikuu

kinaenezwa kwa dakika 5. Yaombe makundi yawasilishe majibu yao.

Page 25: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

15

Kuvuta hewa yenye

matone madogo sana

ya erosoli ambayo

hutolewa pale mtu

mwenye PTB ambukizi

anapokohoa, piga

chafya, tema mate,

zungumza au kuimba.

Namna kifua kikuu cha

mapafu kinavyoweza

enezwa

Hatua 3: ElezaNamna kifua kikuu cha mapafu kinavyoweza

enezwa

Mtu anapovuta hewa iliyou na bakiteria wanaosababisha kifua

kikuu cha kwenye mapafu, bakiteria wanaweza kukaa kwenye

mapafu na kuanza kuzaliana. Kifua kikuu cha mapafu

kinaambukizwa, maana yake bacteria wanaweza kuenezwa kwa

watu wengine. Kifua kikuu kwenye sehemu nyingine za mwili,

kama vile, figo au uti wa mgongo hakiambukizi. Eleza zaidi

kwamba kuna aina mbili za kifua kikuu: (1) kifua kikuu ndani ya

mapafu, ambacho kinaambukiza, na (2) kifua kikuu nje ya

mapafu, ambacho hakiambukizi.

Hatua 4: Maswali na majibu: kwa nini kifua kikuu cha mapafu ni ambukizi

Swali: Kwa nini wanadhani kifua kikuu cha mapafu ni ambukizi?

Jibu: Kifua kikuu ndani ya mapafu kimo mapafuni. Kinaenea pale mtu mwenye kifua kikuu

ambukizi anapotoa hewa nje iliyo na bacteria wa kifua kikuu halafu mtu mwingine anawavuta

ndani bakiteria waliopo kwenye hewa hiyo. Mtu mwenye maabukizi ya kifua kikuu cha

mapafu hutoa bakiteria zaidi pale anapofanya vitendo kama kukohoa au kucheka. Kifua kikuu

nje ya mapafu hakiambukizwi kwa watu wengine kwani kipo katika sehemu nyingine za mwili

na sio kwenye mapafu. Watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu cha mapafu wana uwezekano

mkubwa wa kuueneza kwa watu wanaokuwa nao kwa karibu kila siku, ikiwemo wanafamilia,

rafiki, wafanya kazi wenzao na wafungwa.

Hatua 5: Fuatilia

Angalia kama washiriki wana maswali

Hatua 6: Fafanua zaidi

Kuna aina nyingine ya kifua kikuu inayoitwa bovine TB ambayo ipo zaidi Tanzania. Bovine TB,

au Kifua kikuu cha mifugo, kinaweza kuambukiza zaidi kwa wanyama, wakiwemo binadamu.

Bovine TB husababishwa na bacteria wajulikanao kitaalamu kama Mycobacterium bovis (M.

bovis) ambao ni sehemu ya aina ya wadudu wanaoambukiza kifua kikuu wajulikanao kama

Mycobacterium tuberculosis complex.

Hatua 7: Uliza

Mnadhani zipi ni dalili na viashiria vya kifua kikuu?

Pitia majibu yaliyoorodheshwa kwenye boksi.

Page 26: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

16

Viashiria na dalili za kifua kikuu

Kujisikia kuumwa au dhaifu

Kupungua uzito

Homa za jioni na kutoka jasho jingi usiku.

Kukohoa kwa zaidi ya wiki mbili

Maumivu ya kifua na kukohoa damu.

Zoezi 3: Maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana na ugonjwa wa kifua

kikuu

Dakika 10

Hatua 1: Eleza

Bakteria wa kifua kikuu wanaweza kuishi mwilini bila ya wewe kuugua. Hii hujulikana kama

maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana. Kwa watu wengi ambao wanawavuta bacteria wa

kifua kikuu na kuambukizwa, mwili huwa na uwezo wa kupambana na bacteria ili kuwazuia

wasikue. Watu wenye maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana:

Hawana dalili

Hawajisikii kuumwa

Hawawezi kueneza bacteria wa kifua kikuu kwa wengine

Mara nyingi huonekana kuwa na maambukizi ya kifua kikuu kwa kipimo cha kuchunguza

athari kwenye ngozi au kipimo cha damu.

Wengi huugua ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa hawatapatiwa matibabu kwa ajili ya

maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana.

Hatua 2: Taja

Watu wengi wenye maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana hawataugua ugonjwa wa kifua

kikuu. Kwa watu hawa, bacteria wa kifua kikuu hubaki mwilini bila kuwa na madhara kwa

kipindi chote cha maisha bila kusababisha ugonjwa. Lakini kwa watu wengine, hasa wale

wenye mifumo dhaifu ya kinga kutokana na maambukizi ya VVU, bakteria huweza kuleta

athari, kuzaliana, na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

Bakteria wa kifua kikuu huwa na athari ikiwa mfumo wa kinga hautakuwa na uwezo wa

kuwazuia kukua. Bakteria wa kifua kikuu wanapokuwa na athari (wanapoongezeka mwilini

mwako), hii huitwa ugonjwa wa kifua kikuu. Watu wenye ugonjwa wa kifua kikuu ni

wagonjwa. Wanaweza vili vile kueneza bacteria kwa watu wanaokuwa nao kila siku, hasa kwa

kifua kikuu cha kwenye mapafu. Baadhi ya watu hufikia kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu

mapema mara baada ya kuambukizwa (ndani ya wiki kadhaa) kabla hata ya mifumo yao ya

kinga kupambana na bakteria. Watu wengine wanaweza kuanza kuugua baada ya miaka

kadhaa pale ambapo mifumo yao ya kinga inapokuwa dhaifu kwa sababu nyingine.

Uwezekano wa kuugua ugonjwa wa kifua kikuu ni mkubwa kwa watu wenye VVU

ukilinganisha na wale ambao hawana maambukizi. Watu wenye mifumo dhaifu ya kinga,

Page 27: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

17

hasa wale wenye maambukizi ya VVU, wana hatari kubwa ya kupatwa na ugonjwa wa kifua

kikuu kuliko watu wenye mfumo wa kinga usio na maambukizi.

Zoezi 4: Tofauti kati ya kifua kikuu kisichoonekana na kifua kikuu cha

kwenye mapafu

Dakika10

Hatua 1: Maswali na majibu

Swali: Ni nini tofauti kati ya kifua kikuu kisichoonekana na kifua kikuu cha kwenye mapafu?

Jadili na pitia majibu yaliyopo kwenye jedwali hapa chini.

MTU MWENYE MAAMBUKIZI YA KIFUA KIKUU

KISICHOONEKANA

MTU MWENYE KIFUA KIKUU NDANI YA

MAPAFU

Hana dalili Dalili zaweza kuwa:

Kikohozi kibaya kinachochukua wiki 3

au zaidi

Maumivu kifuani

Kukohoa damu au makohozi

Udhaifu au uchovu

Kupoteza uzito

Kukosa hamu ya kula

Homa za baridi

Homa

Kutoka jasho usiku (kupita kiasi)

Hajisikii kuumwa Kwa kawaida hujisikia kuumwa

Hawezi kueneza bacteria wa kifua kikuu kwa

wengine

Anaweza kueneza kifua kikuu kwa

wengine

Kwa kawaida matokeo ya kipimo cha TB kwenye

ngozi ama damu huonesha kuwa ana

maambukizi ya TB

Kwa kawaida matokeo ya kipimo cha

ngozi ama damu huonesha kuwa ana

maambukizi ya kifua kikuu.

Kipimo cha x-ray ya kifua hakina shida na

makohozi hayana maambukizi.

Anaweza kuwa na kipimo cha x-ray ya

kifua kikionesha tatizo, au makohozi

yakaonesha maambukizi.

Anahitaji matibabu ili kuzuia kifua kikuu ndani

ya mapafu

Anahitaji matibabu kwa ajili ya kifua kikuu

ndani ya mapafu

Page 28: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

18

Zoezi 5: Uchunguzi wa kifua kikuu

Dakika 20

Hatua 1: Maswali na majibu

Swali: Nani anapaswa kupimwa kifua kikuu?

Jibu: Wale ambao wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa na bakiteria wa kifua

kikuu ikiwemo:

Watu wanaoishi kwa karibu na mtu mwenye ugonjwa wa kifua kikuu (kama, wanafamilia,

wafungwa)

Watu kutoka kwenye nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha kifua kikuu

Watu wanaoishi au kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi (kwa mfano: magerezani,

vituo vya kutolea matibabu ya kifua kikuu)

Watoa huduma za afya wanaowahudumia wagonjwa walio katika hatari zaidi ya ugonjwa

wa kifua kikuu.

Watoto wachanga, watoto, vijana walio pamoja na watu wa zima walio kwenye hatari

zaidi ya maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana au ugonjwa wa kifua kikuu.

Wenye VVU au wagonjwa wa UKIMWI.

Watu walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu

Wajawazito wenye VVU

Watu wenye maambukizi ya VVU

Watu waliopata maambukizi ya bakteria wa

kifua kikuu miaka miwili iliyopita

Watu ambao hawakupata matibabu ya kifua

kikuu vizuri hapo zamani

Watoto wachanga na watoto wadogo

Watu wanaojidunga madawa ya kulevya

Watu wanaoumwa magonjwa mengine

yanayodhoofisha mfumo wa kinga

Watu wenye umri mkubwa

Swali: Ni nani aliye katika hatari zaidi ya kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu?

Jibu: Eleza kwamba vipimo ya kifua kikuu kwa ujumla huwa havihitajiki kwa watu waliopo

kwenye hatari ndogo ya maambukizi ya bacteria wa kifua kikuu.

Hatua 2: Maswali na majibuUpimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu

Swali: Je mnafahamu jinsi ugonjwa wa kifua kikuu unavyopimwa?

Jibu: Elezea aina mbalimbali za vipimo kwa maambukizi ya kifua kikuu:

Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya ngozi (kipimo cha uchunguzi cha mantoux)

Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya damu

Makohozi (mchanganyiko wa mate na uteute uliokoholewa kutoka kwenye njia ya

upumuaji, hasa kama matokeo ya maambukizi au magonjwa mengine na mara nyingi

huchunguzwa kwa kutumia darubini ili kusaidia uchunguzi wa kitabibu.

Hatua 3: Eleza

Mtoa huduma za afya anapaswa kuchagua ni kipimo gani cha kifua kikuu anapaswa kutumia.

Vigezo katika kuchagua kipimo gani kitumike ni pamoja na sababu ya kufanya vipimo,

Page 29: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

19

uwepo wa vipimo, na gharama. Kwa ujumla, haishauriwi kumpima mtu kwa vipimo vyote

viwili yaani kipimo cha kifua kikuu kwenye ngozi na kile cha damu.

Zoezi 6: Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua kikuu cha kwenye mapafu

Dakika 15

Hatua 1: Eleza

Waambie washiriki kwamba utasoma maelezo na kama wanadhani maelezo ni UKWELI

wahamie upande wa kulia, na kama wanadhani ni UPOTOSHAJI wahamie kushoto. Kama

hawajui, wasihame. Hakikisha washiriki wameelewa maelekezo.Muulize mshiriki mmoja

ama wawili kutoa maelezo kwa nini wanadhani maelezo ni ukweli au uongo. Tumia

ufunguo wa majibu (chini) kwani una maelezo ya kina ambayo unaweza kuhitaji

kuwashirikisha washiriki ikibidi.

Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua kikuu cha kwenye mapafu

MAELEZO MAJIBU

Kifua kikuu cha kwenye mapafu hutokea

kwenye jamii masikini tu. UPOTOSHAJI Kifua kikuu cha kwenye mapafu

unaweza kumpata mtu yeyote. Ingawa, watu

fulani wapo katika hatari kubwa Zaidi ya

kupata kifua kikuu cha mapafu kushinda

wengine. Kama mtu anatambua vihatarishi,

inaweza kupunguza uwezekano wa mtu

kupata kifua kikuu cha mapafu.

Kwa kawaida matibabu ya kifua kikuu cha

kwenye mapafu huchukua miezi 6–8.

KWELI: Matibabu ya kifua kikuu cha kwenye

mapafu kwa kawaida huchukua miezi 6–8 na

yanaweza kufikia hadi miezi 12 kwa kesi

maalumu.

Hakuna tofauti kati ya ugonjwa wa kifua

kikuu cha mapafu na maambukizi ya kifua

kikuu.

UPOTOSHAJI: Mtu mwenye maambukizi ya

kifua kikuu haambukizi kwa kuwa wadudu

hawana athari ama hawaonekani. Mtu

hatambui kama ameambukizwa kwa kuwa

hakuna viashiria wala dalili zinazoonekana.

Mtu mwenye kifua kikuu cha mapafu

ameathirika kwa namna ya tofauti kabisa. Mtu

mwenye kifua kikuu cha mapafu anaweza

kuambukiza na ana viashiria na dalili.

Kama mtu anakohoa naweza kupata kifua

kikuu cha mapafu.

UPOTOSHAJI: Kifua kikuu cha mapafu

hakikoholeki kwa urahisi. Unalazimika kuwa

karibu kabisa na mtu mwenye kifua kikuu cha

mapafu kwa muda mrefu (kwa kawaida masaa

Page 30: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

20

MAELEZO MAJIBU

mengi au siku nyingi, kama vile gerezani).

Unapaswa kutambua dalili za ugonjwa ili

uweze kutafuta matibabu mapema

iwezekanavyo.

Kifua kikuu cha kwenye mapafu ni ugonjwa

unaoambukiza na unaweza kuenezwa kwa

njia ya hewa.

KWELI: Kifua kikuu cha kwenye mapafu ni

ugonjwa ambao unaenezwa kutoka kwa mtu

mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya

hewa wakati wa kukohoa, kupiga chafya,

kucheka, kuimba, kupiga makelele na hata

kuzungumza. Ikiwa mtu mwenye maambukizi

anakohoa ama kupiga chafya, vijidudu

husambaa hewani ambapo vinaweza kuvutwa

na wale waliopo katika eneo hilo.

Kama mgonjwa anakamilisha matibabu, kwa

kawaida huwa amepona.

KWELI: Kama hakuna usumbufu kwenye

matibabu na yamefuatwa kama ilivyoelekezwa

kwa kipindi husika, kwa kawaida unakuwa

umepona kifua kikuu cha mapafu.

Kumbuka: Kukamilisha matibabu maana yake

ni kumaliza kozi ya matibabu ya kifua kikuu

ndani ya mapafu na kufanyiwa uchunguzi wa

kifua kikuu na madaktari ili kuthibitisha

uponyaji.

Page 31: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

21

Zoezi 7: Kifua Kikuu Magerezani

Dakika 10

Hatua 1: Eleza

Kuzuia ueneaji wa kifua kikuu ni moja ya changamoto kubwa kwenye maeneo ya magereza

hasa pale kunapokuwa na msongomano wa watu.

Hatua 2: Jadili

Ni changamoto zipi zinazojitokeza wakati wa kukabiliana na maambukizi ya kifua kikuu

katika magereza?

Hatua 3: Eleza

Kuna changamoto nyingi: binafsi, kijamii na kiutamaduni, sera, na mazingira, ikiwemo

zifuatazo:

Upungufu wa mbinu za kuthibiti maambukizi na uwepo wa kiwango kidogo cha huduma

za afya kutokana na ufinyu wa rasilimali.

Wafungwa mara nyingi hutenganishwa kwenye vizimba ama sehemu ya wagonjwa bila ya

kufanyiwa vipimo vya kiafya (Wagonjwa wa kifua kikuu hutengwa).

Mlundikano, lishe hafifu, na ukosefu wa hewa ya kutosha.

Idadi ndogo ya wafanyakazi wa afya.

Upungufu wa rasilimali kuendesha uchunguzi wa kiafya na kununua madawa.

Kutofuata masharti ya matibabu miongoni mwa wakazi wenza.

Hatari kubwa miongoni mwa wafungwa kupata usugu wa kifua kikuu (kwa mfano,

wadudu wa TB kupata usugu kutoka kwenye dawa mbalimbali za TB) kutokana na

kutofuata masharti, ingawa utumiaji wa dawa chini ya uangalizi wa mtoa huduma ukiwa

umezingatiwa kila siku.

Zoezi 8: Uhusiano kati ya VVU na kifua kikuu

Dakika 15

Hatua 1: Mapitio

Waambie washiriki kuwa tumezungumzia VVU, kifua kikuu, na madhara ya VVU kwenye

mfumo wa kinga wa mwili wa binadamu.

Hatua 2: Jadili

Jinsi gani maambukizi ya VVU yanaweza kumwathiri mtu mwenye maambukizi ya kifua kikuu.

Pokea maoni machache.

Page 32: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU

22

Hatua 3: Eleza

VVU huongeza kasi ya maambukizi ya kifua kikuu kuwa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa

VVU hudhoofisha mfumo wa kinga. Ukiwa una maambukizi ya VVU una nafasi kubwa ya

kupata kifua kikuu kuliko mtu asiye na maambukizi ya VVU. Bakteria wa kifua kikuu wana

nafasi kubwa ya kuwa na madhara na kushambulia mapafu na sehemu nyingine za mwili.

Hatua 4: Maswali na majibu

Swali: Watu wafanyeje ikiwa wana VVU na kifua kikuu ndani ya mapafu?

Jibu: Wanalazimika kupata matibabu moja kwa moja pasipo kuchelewa ili kupunguza kuugua

zaidi. Kila mmoja anapaswa kutumia dawa zake kwa usahihi kabisa kama daktari au mtoa

huduma za afya alivyowaelekeza.

Hatua 5: Fafanua zaidi

Vidonge vya kifua kikuu ni vikali sana. Vinaweza kutibu kifua kikuu, hata kwa watu wenye

VVU kwa baadhi ya watu. Kumbuka, Vidonge vya kifua kikuu hufanya kazi vizuri pale tu

ambapo hutumiwa kulingana na maelekezo ya mtoa huduma za afya.

Page 33: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

23

SOMO 2: VIWANGO VYA HATARI YA

MAAMBUKIZI YA VVU KWENYE

MAGEREZA

Lengo

Kukuza elimu juu ya vihatarishi vya VVU katika maeneo ya magereza

Dhamira

Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

Kutambua na kuelezea viwango tofauti vya vihatarishi vinavyochochea hatari ya

maambukizi ya VVU katika magereza.

Kuainisha jinsia na kuchunguza namna gani desturi za kijinsia zinauhusiano na

maambukizi ya VVU.

Kueleza tofauti kati ya kuchukua tahadhari ya VVU na kukabiliana na hatari za VVU

Kutambua viwango vya hatari ya VVU kutokana na tabia mbalimbali za kimapenzi

Kutambua majukumu ya kijinsia yaliyopangwa na jamii kwa ajili ya wanaume na

wanawake.

Kulinganisha njia mbalimbali zilizopo za kujikinga na VVU

Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya maambukizi ya VVU

Masaa 2, dakika 15

Kipindi 2.1: Mazoezi

Utangulizi juu ya ngazi tatu za hatari za VVU

Jinsi na jinsia

Jinsi, jinsia na VVU: Kuchukua tahadhari na kukubaliana na hatari

Kiwango cha hatari

Igiza kama mwanaume, igiza kama mwanamke

Kufanya maamuzi kuhusu jambo linalofaa na lisilofaa

Page 34: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

24

Zoezi 1: Ngazi tatu za Viwango vya hatari vya VVU

Dakika 10

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi kubwa za kuandikia, ubao wa chaki

Hatua 1: ElezaViwango vya hatari

Wafahamishe washiriki kwamba kuna ngazi tatu za hatari za VVU:

Ngazi ya mtu binafsi

Ngazi ya familia

Ngazi ya jamii

Elezea zaidi kuhusu vihatarishi vya VVU:

Viwango vina uhusiano na mambo ambayo huwaweka watu kwenye hatari ya

maambukizi ya VVU.

Vihatarishi vya VVU katika viwango vya mtu binafsi, familia, na jamii na mifano ifuatayo

kwenye jedwali hapa chini:

NGAZI YA MTU BINAFSI NGAZI YA

FAMILIA NGAZI YA JAMII

Elimu (kwa mfano, Kutokuwa kabisa au

kuwepo na kiwango kidogo cha elimu)

Mtazamo (kwa mafano., dhana ya uwanaume

miongoni mwa wanaume ambayo inapelekea

tabia hatarishi, dhana ya uwanawake

miongoni mwa wanawake inayozuia

majadiliano kuhusu mapenzi salama)

Umri (kwa mfano, wakazi wenza vijana mara

nyingi huwa katika hatari kubwa kimwili,

kiakili, na ukatili wa kijinsia kutoka kwa

wakazi wenza wakubwa)

Matendo ya kimapenzi yasiyo salama

Kuchangia vitu vyenye ncha kali (kama,

nyembe)

Ukosefu wa elimu (kwa mfano, ukosefu wa

elimu kuhusu namna ambavyo VVU

huenezwa)

Matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na

pombe.

Mila za

kitamaduni na

imani

Miiko.

Mila za kijamii

(kwa mafano,

wajibu na

majukumu ya

wanaume na

wanawake)

Sera za serikali

Siasa/uimara wa

kisiasa

Rasilimali (kwa

mfano; ukosefu wa

vifaaa vya

kujifungulia kwa

wafungwa

wajawazito).

Page 35: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

25

Mazingira ya kizuizi na msongamano

ambayo mara nyingi hupelekea msongo,

wasiwasi, fadhaa, na unyanyasaji, ikiwemo

unyanyasaji wa kimapenzi.

Baadhi ya wafungwa wa kiume wanaweza

kukumbana na unyanyasaji wa kimapenzi

na kushiriki shughuli za mapenzi yasiyo

salama na wanaume wengine kwa

kubadilishana vitu ama huduma, kitu

kinachoongeza hatari kwao kuambukizwa

VVU.

Magonjwa ya ngono, kama herpes,

chlamydia, kaswende, au gono yapo

miongoni mwa wakazi wenza, huongeza

hatari yao kwa VVU.

(Serekali ya Muungano ya Tanzania 2010)

Mazingira hatarishi kwa VVU ndani ya

magereza Hatua 2: ElezaGerezani

Nchini Tanzania, tafiti zinaonesha uwepo wa

kiwango cha juu cha VVU (asilimia 6.7) ndani

ya magereza ukilinganisha na watu wazima

kwingineko (asilimia 5.1)(Das and Horton,

2016) kutokana na mazingira hatarishi

ambayo ni pamoja na: (tazama boksi la bluu).

Tanzania imetia sahihi na kuridhia hati zote

rasmi za haki za binadamu, sheria na sera za

kimataifa (umoja wa kimataifa) na kikanda

kuhusu uzuiaji wa VVU, zinazotoa idhini ya

kuwapima watu VVU kwa hiari, wakiwemo

wafungwa walio katika magereza.

Hatua 3

Kwa kina, jadili nini kifanyike ili kupunguza

mazingira haya hatarishi kwenye magereza.

Zoezi 2: Jinsi na Jinsia

Dakika 20

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi kubwa ya kuandikia na ubao

Maandalizi ya awali:

Andaa alama mbili moja iandikwe “jinsia” na nyingine iandikwe “jinsi” kwa ajili ya zoezi

hili.

Hatua 1: Eleza

Ingawa wafungwa hukaa kwenye vyumba vidogo kulingana na jinsia zao, ni muhimu

kwao kuwa na taarifa kuhusu usawa wa kijinsi, vurugu zenye misingi ya kijinsi, na ukatili

wa kijinsia. Elimu hiyo inaweza kuwasaidia wafungwa baada ya kutumikia vifungo vyao

kuendeleza mila sahihi za kijinsi na usawa wa kijinsi, ikiwa ni pamoja na kupambana na

ukatili wenye misingi ya kijinsi.

Hatua 2: Uliza na jadili maswali yafuatayo:

Jinsi maana yake ni nini?

Jinsi humaanisha sifa za kibaiolojia na kimaumbile za wanaume na wanawake ambazo

hazibadiliki isipokuwa kwa upasuaji. Mifano ya sifa za jinsia ni:

Page 36: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

26

Viungo vya mwili: uume, uke, matiti, korodani

Maumbile: mzunguko wa hedhi, uzalishaji manii

Muundo wa kijenetiki: kromosomu XX na XY.

1. Jinsia maana yake ni nini?

Jinsia humaanisha kazi, haki, majukumu, fursa, heshima, mipaka, matarajio na wajibu wa mtu

uliopangwa na jamii.

Sifa za jinsi ni:

Hutofautiana miongoni na ndani ya tamaduni

Hubadilika baada ya muda

Kazi na matarajio hupangwa kulingana na jinsia, umri, ukabila, dini, na sababu nyingine

za kitamaduni

Huwahusu wanaume, wavulana, wanawake, na wasichana; si wanawake pekee.

Hatua 3: Eleza

Baadhi ya mila za jinsi na ukosefu wa usawa wa kijinsi huwaweka wanaume, wavulana,

wanawake, na wasichana katika hatari mbalimbali za kupata maambukizi ya VVU:

Wanaume na wavulana wameathiriwa na matarajio ya jinsi ambayo yanaweza

kuhamasisha tabia za kujihatarisha, kupinga upatikanaji wa huduma za afya na kwa kiasi

kidogo kujipangia kazi zao kama wenza na wanafamilia. Kwa wasitani, kiwango cha

upimaji VVU na kupata matibabu ni mdogo miongoni mwa wanaume ukilinganisha na

wanawake. Kote mashariki na kusini mwa Afrika, kuna tofauti kubwa ya utumiaji na

unufaikaji wa huduma kati ya wanaume, wavulana, wanawake, na wasichana. Wanaume

na wavulana hupata huduma za afya kwa kiwango cha chini sana ukilinganisha na

wanawake na wasichana.

Asilimia 54 ya vifo vya watu wazima vyenye uhusiano na UKIMWI vilitokea miongoni mwa

wanaume mashariki na kusini mwa ukanda wa Afrika (makadirio ya UNAIDS 2016).

Huduma za afya haziwafikii wanaume wengi kusini mwa jangwa la Sahara, na hii

huchangia sana wanaume kuhitaji na kutumia kwa kiasi kidogo huduma za VVU katika

kanda hizi. Matarajio ya wanaume kuanza matibabu ni madogo sana, na mara nyingi

hutegemewa kuwa na kiwango cha chini cha CD4 wanapoanza na kukatiza matibabu na

kupoteza ufuatiliaji, hivyo kufikiwa kwa kiasi kidogo kupungua kwa virusi vya ukimwi (

Sonke Gender Justice and Men Engage, 2017).

Ukosefu wa usawa wa kijinsi na usiri wa ukatili wa wenza zinaweza kuwazuia wanawake

na wasichana, hasa wanawake vijana kujikinga wenyewe dhidi ya VVU. Nchini Tanzania,

wanawake wameathirika mno na VVU, Tanzania ina wanawake 690,000 wenye miaka 15

na zaidi waishio na VVU. Kulingana na Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria

Tanzania Mwaka 2011–12, (TACAIDS et al. 2011) maambukizi ya VVU kwa wanawake

yalikuwa asilimia 6.2, ukilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume. Wanawake wenye umri

wa miaka 23–24 walikuwa na uwezekano wa kuishi na VVU mara mbili zaidi ya wanaume

Page 37: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

27

wa umri huo. Wanawake huathiriwa mapema, kwa kuwa wana wapenzi wakubwa na

huolewa mapema. Lakini pia wanakumbana na wakati mgumu kujadiliana kuhusu

mapenzi salama kwa sababu ya ukosefu wa usawa wa kijinsi. Nchini Tanzania asilimia 35

ya wanawake inaaminika wamekumbana na ukatili wa siri kwa wapenzi. Utafiti kutoka

Tanzania unaonesha kuwa huku wanawake wakitegemewa kuwa watiifu kwa wapenzi

wao hata kama wapo kwenye mahusiano mabaya, wanaume wanashawishiwa kujihusisha

na mapenzi ya ziada yasiyosalama.

Hatua 3: Zoezi la jinsi na jinsia

Eleza kwamba sasa tutashiriki katika shuughuli ya pamoja ili kujifunza zaidi maneno jinsi

na jinsia.

Onesha alama mbili ambazo zimetengwa kwa umbali wa fiti kadhaa. Moja ina

neno“jinsia” lililoandikwa juu yake, na nyingine ina neno “jinsi.”

Soma sentensi moja moja na uwaombe washiriki kuhamia kwenye alama ambapo

wanadhani sentensi inaegemea yaani jinsia au jinsi. Baada ya kila mmoja kuhama,

endelea kwa kumwomba mtu mmoja aliyesimama upande mmoja wa chumba aeleze kwa

nini waliamua kusimama upande huo. Uliza ikiwa wengine wangependa kuchangia

sababu zao. Waulize kundi jingine kwa nini wameamua kusimama chini ya alama

waliyopo. Baada ya kufanya hivyo kwa muda soma sentensi inayofuata.

MAELEZO YA JINSIA AU JINSI MAJIBU

Wanawake huzaa watoto Jinsi

Wasichana ni wapole na wakimya Jinsia

Wavulana ni werevu na thabiti Jinsia

Wanawake hunyonyesha watoto Jinsi

Wanaume ni vichwa vya familia zao Jinsia

Wanaume huanzisha mapenzi kwa wenza wao Jinsia

Wanaume wana akili kuliko wanawake Jinsia

Zoezi 3: Jinsi, jinsia, na VVU: Kuchukua tahadhari, kukabiliana na hatari

Dakika 20

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi kubwa za kuandikia au ubao wa chaki

Page 38: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

28

Hatua 1. Utangulizi

Andika neno “hatari” kwenye karatasi ya ubaoni au kwenye ubao wa chaki. Andika

maelezo yao ya ufafanuzi kwenye karatasi ya ubaoni/ubao wa chaki. Fikieni muafaka

kuhusu maana ya neno hatari (tazama kisanduku)

Hatua 2: Uliza

Waombe washiriki watoe mifano ya mazingira ambayo wanaweza au mtu wanayemjua,

au watu wengine huchukua tahadhari au hukabiliana na hatari za VVU

Hatua 3: Maswali ya kujadiliana:

Kuhusiana na VVU, ni nani anayechukua tahadhari zaidi, mwanaume au mwanamke? Kwa

nini?

Kuhusiana na VVU, ni nani

anayekabiliana na hatari zaidi,

mwanaume au mwanamke? Kwa nini?

Nini faida na hasara za kuchukua

tahadhari na kukabiliana na hatari hizi kwa wanaume na wanawake?

Ni mambo gani mengine yanayoathiri tahadhari za VVU ambazo watu huchukua na

ambazo watu hukabiliana nazo?

Hatari hizi zinaweza kupunguzwa vipi?

Hatua 4: Eleza

Wanawake hukumbana na hatari zaidi za maambukizi ya VVU ukilinganisha na wanaume kwa

sababu ya mila za kijamii na kiutamaduni (jinsia) na sababu za kibaiolojia (jinsi) (tazama

sanduku chini):

MILA ZA KIJAMII NA KIUTAMADUNI

(JINSIA)

SABABU ZA KIBAIOLOJIA (JINSI)

Wanawake mara nyingi hawana nguvu na

maamuzi katika maisha yao ya kimapenzi.

Wanawake hawatarajiwi kujadili au

kuamua kuhusu mapenzi; jambo hili

huchukuliwa kama ni kazi ya mwanaume.

Wanawake wanaweza kuhisi kwamba

hawawezi kuuliza au kusisitiza kutumia

kondomu au njia yoyote ya kujikinga.

Wanawake wanaweza kujisikia, ingawa

hawawezi kukataa kufanya mapenzi hata

kama wanajua wanajiweka katika hatari

ya kupata mimba au kuambukizwa

magonjwa ya ngono au VVU.

Wanawake wana uwezekano mkubwa wa

kupata VVU kutokana na kitendo

chochote kimoja cha kufanya mapenzi

kwa sababu shahawa hubaki ndani ya uke

kwa muda mrefu baada ya kujamiiana, na

hivyo kuongeza uwezekano wa

kuambukizwa. Pia kuna virusi vingi

kwenye shahawa kuliko kwenye majimaji

ya ukeni. Kuta za uke ni laini sana na

zinaruhusu vitu kupenya, na kuruhusu

VVU kupenya, na ngozi laini ya ukeni ni

rahisi zaidi kupata michubuko au

kuchanika kuliko ngozi ya kawaida.

Maana ya hatari:

Hatari ni uwezekano au tishio la kupata

maambukizi (VVU, TB, n.k.), uharibifu, jeraha,

deni, upotevu, au matukio yoyote

yanayoweza kuzuiwa kwa kuchukua hatua

stahiki.

Page 39: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

29

MILA ZA KIJAMII NA KIUTAMADUNI

(JINSIA)

SABABU ZA KIBAIOLOJIA (JINSI)

Baadhi ya wanawake hujihusisha kwenye

mahusiano ya kimapenzi kupata, pesa,

simu, chakula, au namna nyingine za

hadhi na ulinzi.

Wanawake wanaweza kukumbana na

namna nyingi za mizozo kutokana na

unyonge wao katika jamii, na kuongeza

hatari za maambukizi ya VVU.

Wanawake ambao huwaambia wenza

wao kwamba wana ugonjwa wa

ngono/VVU wanaweza kukumbana na

ukatili wa kimwili, kiakili, au hisia au

kuachwa.

Wanawake wanaweza kudai matakwa ya

kimapenzi kwa wenza wao kuzuia,

kuzomewa, kuachwa, kupigwa, au

kuuawa.

Wanawake pia wanategemewa kuwa na

mahusiano ya kimapenzi na au kuolewa

na wazee, ambao wana uwezekano

mkubwa kuwa na VVU.

Wanaume wanahimizwa kufanya mapenzi

kadri iwezekanavyo, bila kufundishwa

jinsi ya kujilinda wenyewe, na hivyo

kuongeza hatari kwao kuambukizwa VVU.

Kiashiria kikuu cha uanaume na

mafanikio ni kuwa na wapenzi wengi wa

kike kadri iwezekanavyo. Kwa wanaume

waliooa na wale ambao hawajaoa,

wapenzi wengi ni jambo linalokubalika

kiutamaduni.

Wanaume wanaweza kudharauliwa na

kutaniwa kama hawataonesha kwamba

watachangamkia fursa zozote ama zote

za kimapenzi.

Ushindani husisitizwa kwa wanaume

kuonesha ni nani aliye mkuu na bora.

Kiashiria kingine cha uanaume ni kuwa na

uthubutu kwenye mapenzi, ikiwemo

Wanawake wapo katika hatari zaidi ya

kupata VVU wakati wa kujamiiana kuliko

wanaume kwani shahawa zinaweza

kusalia ndani ya uke kwa siku kadhaaa

baada ya kujamiiana, wakati wanaume

hujihatarisha na majimaji yenye

maambukizi ya VVU tu wakati wa

kujamiiana.

Wanaume ambao hawajatahiriwa wana

uwezekano mkubwa wa kuambukizwa

VVU ukilinganisha na wale waliotahiriwa.

Uume haupo kwenye hatari kubwa ya

kusababisha maambukizi kwa sababu

inakingwa na ngozi ngumu ukilinganisha

na uke ambao una sehemu kubwa

inayoweza kuruhusu maambukizi ya VVU

toka kwenye shahawa. Unapokuwa na

magonjwa ya ngono ambayo

hayajatibiwa kunaongeza uwezekano wa

mtu kupata VVU.

Page 40: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

30

MILA ZA KIJAMII NA KIUTAMADUNI

(JINSIA)

SABABU ZA KIBAIOLOJIA (JINSI)

kutotumia kondomu (matumizi ya

kondomu huchukuliwa kama ni ishara ya

udhuru na ni udhaifu).

Wanaume wengi wanaamini kuwa

kondomu hupunguza raha ya mapenzi au

ni kiashiria cha ukafiri na uzinzi.

Matumizi ya kondomu vile vile

yanakinzana na kile kinachoonekana

kama kiashiria muhimu cha uanaume—

kuwa na watoto wengi iwezekanavyo.

Zoezi 4: Viwango vya hatari mchezo wa kadi

Dakika 25

Vifaa vinavyohitajika:

Kadi zilizoandikwa “vielelezo” Andika yafuatayo kwenye kila kadi: Kuacha kabisa, kupiga

punyeto,mapenzi kwenye uke-bila kondomu, kumkumbatia mtu mwenye VVU, Kupiga busu,

mapenzi makavu-bila kondomu, Kuchua, Mwanaume aliyetahiriwa akijamiiana na

mwanamke, Kumnyonya mwanaume uume kwa kutumia kondomu, Kumnyonya mwanamke

ukeni bila kondomu, watoto wachanga kunyonya kwa mama mwenye maambukizi ya VVU,

Mapenzi kinyume na maumbile—bila kondomu

Kadi zilizoandikwa “kadi za hisa”: Andika viwango kwenye kadi za hisa kwa mfano. Hatari

kubwa zaidi, Hatari kidogo, Hatari kiasi, Hakuna hatari yenye uhusiano na ueneaji wa

VVU.

Hatua 1: Fahamisha

Wafahamishe washiriki kuwa wanakwenda kukamilisha zoezi linaloangazia tabia

zilizobeba hatari za kuambukiza VVU.

Weka kadi zenye tabia za kimapenzi kuelekea chini kwenye kitita (tazama orodha chini)

halafu waombe washiriki kuchukua kadi na kuiweka ukutani/sakafuni kwenye kipengele

sahihi, “Hatari kubwa” “Hatari kidogo” “Hatari kiasi” na “ Hakuna hatari” kuhusiana na

ueneaji wa VVU

Kuachana na mapenzi kabisa

Kupiga punyeto

Mapenzi ukeni-bila kondomu

Kumkumbatia mtu mwenye VVU

Kupiga busu

Page 41: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

31

Mapenzi makavu—bila kondomu

Kuchua

Mwanaume aliyetahiriwa akifanya mapenzi na mwanamke

Kumnyonya uume mwanaume kwa kutumia kondomu

Kumnyonya mwanamke ukeni bila kutumia kondomu

Watoto wachanga kunyonya kwa mama mwenye maambukizi ya VVU.

Mapenzi kinyume cha maumbile-bila kondomu.

Baada ya kadi zote kuwa ukutani/sakafuni, waombe washiriki wapitie mahali ambapo

kadi zimewekwa. Halafu waombe wajitolee kusema kama:

Hawakubaliani na mahali kadi zote zilipowekwa

Hawaelewi uwepo wa kadi zote mahali zilipo

Walipata wakati mgumu kuweka kadi zote.

Hatua 2: Jadili

Jadili uwepo wa baadhi ya kadi, hasa zile zenye utata kuhusu hatari, au kadi ambazo

zimewekwa dhahiri mahali pasipo sahihi. Anza kwa kuwauliza washiriki kwa nini

wanadhani kadi iliwekwa kwenye kipengele fulani. Pitia vipengele hapa chini kama huna

uhakika mahali ambapo tabia fulani inapaswa kuwapo.

Hatari za ueneaji wa VVU kutokana na shughuli za mapenzi

HAKUNA HATARI HATARI KIDOGO HATARI KIASI HATARI KUBWA

Kuachana na

mapenzi

Kupiga punyeto

Kumkumbatia mtu

mwenye VVU

Kupiga busu

Kuwaza tendo la

kimapenzi

Kuchua

Kufanya mapenzi

kwenye uke kwa

kondomu

Kumnyonya mboo

mwanaume

mwenye VVU-

kwa kutumia

kondomu

Kufanya mapenzi

mdomoni na

mwanamke

mwenye VVU

Kutumia

vidole/mikono/vit

u vilivyosafishwa

kabla ya

kuchangia

Watoto wachanga

kunyonya kutoka

kwa Mwanamke

mwenye VVU

Mapenzi kinyume

cha maumbile kwa

kutumia kondumu

na vilainishi

Mapenzi ukeni—

bila kondomu

Mapenzi kinyume

cha maumbile-

bila kondomu

Mapenzi

makavu-bila

kondomu

Page 42: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

32

Hatua 3: Uliza

Waombe washiriki watazame tabia zilizopo kwenye vipengele vya “Hatari kidogo” na

“Hakuna hatari”. Weka msisitizo kwenye dhana ya kwamba baadhi ya tabia za kimapenzi

zenye kufurahisha zina hatari kidogo au hazina hatari kabisa.

Hatua 4: Hitimisha

Hitimisha na sisitiza kwamba hatari hutegemea mazingira ya tabia au sababu zingine. Hizi

ni pamoja na mila za jinsio, ikiwa kama mwenza ameambukizwa au la, ikiwa kama mtu

ni/si mtoaji au mpokeaji wa tabia za kimapenzi, na ugumu wa kufahamu ikiwa kama

mwenza wa mtu ame/hajaambukizwa VVU.

Kiwango cha hatari kwa kiasi kikubwa kwa tabia hizi kitatofautiana kulingana na sababu

kadhaa. Hizi ni pamoja na mila na ukosefu wa usawa wa kijinsia, ikiwa kama mwenza ni/si

mwathirika wa VVU, ikiwa kama mtu ni/si mtoaji au mpokeaji wa tabia za kimapenzi, historia

ya kimapenzi na hali ya VVU kwa kila mwenza, na matumizi sahihi ya kondomu. Kwa mapenzi

ya mdomoni, uwepo wa vidonda, au fizi zinazotoa damu kunaweza kuongeza hatari ya

kuambukizwa VVU kwa mtoaji.

Zoezi 5: Igiza kama mwanaume, igiza kama mwanamke

Dakika 40

Vifaa vinavyohitajika:

Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki

Hatua 1: Uliza

Waulize washiriki kama wamewahi kuambiwa “kuigiza kama mwanaume” au “kuigiza

kama mwanamke.” Wape nafasi ya kuchangia baadhi ya uzoefu ambao mmoja wao

ameusema au kitu kinachofanana kwao. Kwa nini mtu kasema hili? Jambo hili linamfanya

mshiriki ajisikie vipi?

Hatua 2: Sema

Tutatazama kwa kina zaidi aya hizi mbili. Kwa kuzichunguza, tunaweza kuanza kuona namna

ambavyo jamii inatambua maana ya kuwa mwanaume au mwanamke.

Hatua 3: Chunguza “kama mwanaume”

Kwa herufi kubwa, chapa kwenye kipande cha karatasi ya ubaoni maneno, “Igiza kama

mwanaume.”

Waombe washiriki kuchangia mawazo yao kuhusu maana ya maneno haya. Andika

mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki

Page 43: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

33

“IGIZA KAMA MWANAUME”

Kuwa shupavu

Usilie

Wakoromee watu Usioneshe hisia

Walinde watu wengine (wanawake na

watoto)

Pambana na utakayokabiliana nayo

maishani , usionyeshe uwoga

Kuwa bosi

Ingiza kipato

Miliki wapenzi/wake zaidi ya mmoja

Safiri kutafuta ajira

Hatua 5: Jadili—“kama mwanaume”

Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya

matarajio ya kijamii?

Kunaweza kuwako na mipaka kwa mwanaume kutazamiwa kutenda namna hii? Kwa nini?

Ni hisia zipi wanaume hawapaswi kuzionesha?

Ni kwa namna gani “kujifanya mwanaume” kunaathiri mahusiano ya mwanaume na

mwenza na watoto wake?

Ni kwa namna gani mila za kijamii na matarajio ya “kuigiza kama mwanaume” yana

matokeo hasi kwenye afya ya uzazi na mapenzi kwa mwanaume?

Je inawezekana wanaume kutoa changamoto na kubadili majukumu yaliyopo kulingana

na jinsi?

Hatua 5: Chunguza “kama mwanamke”

Sasa kwa herufi kubwa, chapa kwenye kipande cha karatasi ya ubaoni maneno, “Igiza

kama mwanamke.”

Waombe washiriki kuchangia mawazo yao kuhusu maana ya maneno haya. Andika

mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki.

“IGIZA KAMA MWANAMKE”

Usioneshe hisia

Kuwa mwangalizi

Kuwa mrembo, ila usiwe mrembo sana

Kuwa nadhifu, ila usiwe nadhifu sana

Kuwa mkimya

Kuwa mke mwema

Kuwa mwaminifu

Kuwa mnyenyekevu

Hatua 6: Jadili

Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya

matarajio ya kijamii?

Kunaweza kuwako na mipaka kwa wanawake kutarajiwa kujimudu kwa namna hii? Kwa

nini?

Ni kwa namna gani “kuigiza kama mwanamke” kunaathiri mahusiano ya mwanamke na

mwenza na watoto wake?

Ni kwa jinsi gani mila za kijamiii na matarajio ya “kujifanya mwanamke” yana matokeo

hasi kwenye afya ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke?

Je wanawake wanaweza kuishi kinyume cha mambo haya?

Page 44: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

34

Je inawezekana wanawake kutoa changamoto na kubadilisha majukumu yaliyopo

kulingana na jinsia?

Hatua 7: Hitimisha

Hitimisha zoezi hili kwa kueleza kwa ufupi baadhi ya majadiliano na kuchangia mawazo

yoyote ya mwisho. Swali la mwisho laweza kuwa kama ifuatavyo:

Shughuli hii ni njia nzuri ya kuelewa maana ya mila za jinsi. Lakini kumbuka kuwa hizi mila za

jinsi zinaweza pia kuathiriwa na matabaka, utamaduni, kikundi fulani, na tofauti nyingine.

Ujumbe ambao wanaume wanaupata kutokana na “kuigiza kama mwanaume” ni pamoja

na:

• Kuwa shupavu na usilie

• Kuwa mwingizaji wa kipato

• Jisimamie na usirudi nyuma

• Fanya mapenzi unapohitaji

• Wanawake ni vitu fulani kuwa navyo—mali

Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi kufuatia “kuigiza kama mwanaume” zina

matokeo (madhara) yafuatayo kwenye mitazamo ya wanaume na uume:

Wanaume wanathaminiwa zaidi kuliko wanawake.

Wanaume wanaogopa kudhuriwa na kuonesha hisia zao.

Wanaume wanahitaji uthibitisho mara zote kwamba wao ni wanaume kweli.

Wanaume hutumia mapenzi kuthibitisha kuwa wao ni wanaume kweli.

Wanaume hutumia nguvu kuthibitisha kuwa wao ni wanaume kweli.

Ujumbe ambao wanawake wanapata kutokana na “kuigiza kama mwanamke” ni pamoja

na:

Kutoonesha hisia na kukaa kimya

Kuwa waangalizi na wajenzi wa nyumba

Jifanye mrembo, ila usiwe mrembo sana

Kuwa nadhifu, ila usiwe nadhifu sana

Fuata miongozo ya wanaume

Mtunze mmeo—mpe starehe ya mapenzi

Usilalamike

Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi kufuatia “kuigiza kama mwanamke” vile vile

yana matokeo (madhara) yafuatayo kwenye mitazamo ya wanawake na uke:

Mara nyingi wanawake hawajiamini

Wanawake huthaminiwa kwanza kama mama na si kama watu

Wanawake huwategemea wenza wao

Wanawake wana maamuzi kidogo kuliko wanaume kuhusu maisha yao kimapenzi

Wanawake wameathirika zaidi na VVU na UKIMWI na ukatili

Page 45: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

35

Mila za jinsia zisizo na manufaa huongeza hatari ya magonjwa ya ngono na VVU na

mimba zisizotarajiwa, na hutengeneza vikwazo vikubwa kwa maendeleo ya wanawake

kijamii, kiuchumi, na kisiasa.

Zoezi 6: Kufanya maamuzi kuhusu jambo linalofaa na lisilofaa

Dakika 30

Hatua 1: Eleza

Tutatazama mchakato wa kufanya maamuzi sahihi kwa kujitambua ili kujikinga na VVU.

Eleza kwamba watapewa orodha iliyo katika namna tofauti na wanapaswa kuonesha kwa

matamshi au kwenye karatasi kama hatua iliyochukuliwa ilikuwa “sahihi” au “si sahihi”

Hatua 2: Fafanua

Toa maana ya maneno haya: “kufaa” na “kutofaa.”

KUFAA KUTOFAA

“Kufaa inamaanisha kitendo au mwitikio

unaostahili, sahihi, au unaoendana na

mazingira ya uzuiaji VVU na mila za jinsia na

usawa kama ilivyojadiliwa katika shughuli

zilizotangulia.

Kutofaa inamaanisha kitendo au mwitikio

usiostahili, usio sahihi, na usioendana na

mazingira ya uzuiaji wa VVU na mila za jinsi

na usawa kama ilivyojadiliwa katika shughuli

zilizotangulia.

Hatua 3: Soma

Kariri hadithi ya kwanza (ukurasa unaofuata) halafu washiriki waseme wapi panafaa na

wapi hapafai na kwa nini.

Hatua 4: Jadili

Kufungua mjadala wa ukweli kuhusu mapenzi inaweza kuwa jambo gumu lakini ni

mhimu.

Watu wenye madaraka wasitumie vibaya nafasi zao kuwalazimisha wengine kutenda

kinyume na matakwa yao.

Watu wanapaswa kuheshimu haki za wengine kuchagua kama wanataka kufanya

mapenzi na kufanya mapenzi salama kwa kutumia kondomu za kike au kiume.

Ili mradi tabia za kimapenzi ni jambo la maridhiano pasipo kuumiza au kujeruhi, wengine

hawapaswi kuingilia.

Wapange washiriki wawili wawili halafu wape eneo la kujadili na kuamua kama linafaa au

halifai. Wape dakika 10 kufanya hivyo na elezea kwa kifupi kila eneo.

Page 46: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

36

Simulizi za Matukio

Tukio 1: Kumtembelea daktari

Afisa magereza ameambiwa na daktari kuwa ana kifua

kikuu, ambayo ni maambukizi nyemelezi ya kawaida

kwa wale waishio na VVU. Daktari akashauri kwamba

wote wawili afisa magaereza na mwenzi wake wapate

ushauri nasaha na kupima VVU. Afisa magereza

akamweleza mpenzi wake kuwa kikohozi chake

kisichoisha kinasababishwa na hali mbaya ya ubaridi

baada ya muda kitaisha.

Haifai: Afisa magereza ana wajibu wa kumfahamisha mwenza wake ukweli kuhusu mkutano

wake na daktari na kumpa nafasi mwenza wake kujilinda na kushughulika na uwezekano wa

kuwa mwathirika wa VVU.

Tukio 2 : Fadhaa za magonjwa ya ngono

Mfungwa ambaye hivi karibuni ameachiliwa kutoka gerezani amekutana na binti/kijana

mtaani na kuanza mahusiano naye kimapenzi. Siku moja wakati akioga, binti/kijana aliona

kidonda chekundu kwenye sehemu zake za siri. Anaona soni sana kuzungumza na mwenzi

wake lakini alimpeleka hospitali ili kupata vipimo na kumweleza dakitari kuhusu kidonda.

Haifai: Ni muhimu kabisa kumfahamisha mpenzi wako kuhusiana na ugonjwa wowote wa

ngono (VVU au vinginevyo) unaoutambua ili aweze kuchunguzwa. Hii si kwa ajili ya afya zao

tuu, lakini pia kwa ajili ya afya ya jamii nzima kwa sababu ugonjwa ukitibiwa mapema, ndivyo

unavyoweza kudhibitiwa mapema na kupunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine.

Tukio 3: Hakuna zawadi ya bure

Afisa magereza amekuwa akimchumbia msichana anayeuza machungwa na mayai sokoni.

Alinunua vitafunwa vyake kila mara alipomwona, pamoja na kumpa zawadi ndogo ndogo.

Alikuwa na usongo wa kufanya mapenzi nae. Jioni moja walipigana busu na alimtomasa

matiti yake. Mzuka ulimpanda sana lakini binti alisema hayuko tayari. Alimsukuma binti chini,

akamkandamiza mikono yake chini na akajilazimisha hadi akazama ndani yake.

Haifai: Afisa magereza huwenda alifikiri binti “alipaswa kumpa”mapenzi kwa kuchukua

chakula na zawadi lakini hakuwa na haki ya kumbaka. Ubakaji huongeza hatari ya

maambukizi ya VVU kwa kuwa wabakaji mara chache sana hutumia kondomu na kitendo cha

kutumia nguvu kufanya ubakaji hupelekea kuchanika kwa kuta za uke au njia ya haja kubwa.

Page 47: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU magerezani

37

Tukio 4: Matumizi mabaya ya cheo

Siku moja, mwalimu mkuu katika chuo cha mafunzo alimwomba mmoja wa wanafunzi wake

wa kike kubaki baada ya vipindi kwisha na kumwambia kwamba alitaka kujadiliana naye

kuhusu maendeleo yake kitaaluma. Baada ya vipindi msichana alibaki na mkuu wa chuo

alimsifia sana kuhusu uzuri wake. Kitendo hicho cha kumsifia kilimchukiza sana msichana,

lakini hakusema chochote kwa kuwa alikuwa mwalimu wake. Mwalimu alipoona kwamba

msichana hajafurahi, alimwambia awe makini sana, kwani matokeo ya maendeleo yake

kitaaluma yalikuwa mikononi mwake, na alimwomba msichana kwenda nyumbani kwake jioni

ile, kitu ambacho msichana alitii kwani aliogopeshwa kuwa hatafaulu mitihani yake.

Haifai: Mwalimu hakupaswa kutumia cheo chake au nafasi yake kumtisha msichana mdogo.

Ingawa msichana alikwenda nyumbani kwa mwalimu, ilikuwa ni kwa sababu ya vitisho

kwamba uhalali wa matokeo yake kitaaluma ungeharibiwa kama asingefuata alichoambiwa

na mwalimu kufanya.

Tukio 5: Tabia za kutowajibika

Afisa magereza alihamishwa kwenda gereza la wilaya ambapo alidhani angepaswa kwenda

bila ya mke wake na watoto ili kuepusha usumbufu kwao kuhusiana na mambo ya shule na

familia. Afisa alikaa peke yake katika makazi yake mapya. Siku moja, alipokuwa baa, alikutana

na mwanamke na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ulioendelea kwa kipindi fulani. Pamoja

na kuwa Afisa alikuwa ameoa na akijua kuwa mwanamke huyu alikuwa na mpenzi mwingine,

hakuona hili kama ni tatizo. Mwanamke alisisitiza kutumia kondomu, lakini Afisa hakuona

umuhimu wa kondomu, na baadaye baaada ya muda mwanamke aliacha kusisitizia.

Haifai: Pamoja na kwamba wote wawili walikuwa wawazi kuwa wana wapenzi wengi lakini

hawakuwajibika kwa kufanya mapenzi yasiyo salama, jambo ambalo haliwaweki wao tu katika

hatari lakini pia linawaweka wenzi wao wengine katika hatari ya maambukizi ya VVU, ambao

huenda hawafahamu kuwa wenzi wao walikuwa wakifanya mapenzi na watu wengine, na

mapenzi yasiyo salama.)

Tukio 6: Woga usiotakiwa

Mfungwa ajulikanaye kama Victor alihamishiwa kwenye chumba kimoja kidogo kutokana na

umri wake mdogo ukilinganisha na wengine ambao walionekana mabingwa na wenye

kupenda kutaniana. Victor alikuwa mpole na mwenye aibu na mara nyingi alipendelea kukaa

peke yake. Kwa tabia hiyo wenzake walimtania kwa kumwita mwanamke nakadhalika. Siku

moja wenzake walimzunguka, wakamsukuma, na kumvua suruali yake ili kuthibitisha kama

kweli alikuwa mwanaume au la. Mmoja wao alimshika kwa nguvu na kumtisha.

Haifai: Ingawa walikuwa ni wakazi wenza wa kiume, ukandamizaji na matendo mabaya

yanaweza kutokea kutokana na tofauti ya nguvu za mamlaka. Waelimisha rika wanapaswa

kujadiliana na wafungwa nini kinapaswa kufanyika kwenye tukio kama hili na taratibu

zinazopaswa kufuatwa katika kuripoti tukio kama hili.)

Page 48: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

38

SOMO 3: KIFUA KIKUU NA VVU:

MATIBABU, HUDUMA NA MSAADA

Lengo

Kupata maelezo ya msingi kuhusu kinga, matibabu, huduma, na msaada wa Kifua kikuu

na VVU.

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:

Kueleza umuhimu wa kujua hali yako ya kifua kikuu na VVU.

Kueleza maana ya upimaji VVU wa hiari na ule unaoasisiwa na mtoa huduma.

Kuelezea umuhimu wa huduma za upimaji VVU.

Kujadili dawa za kupunguza makali na mahali pa kupata huduma na msaada.

Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia kondomu za kike na kiume.

Kueleza kwa kifupi upatikanaji wa matibabu mengine kwa matatizo mtambuka ya kiafya

kama vile, magonjwa ya ngono, maambukizi kwenye njia ya uzazi, na maambukizi

nyemelezi.

Kueleza maana ya maneno kinga ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto na kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza mama mwenye VVU na mtoto.

Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU

Dakika 145

Kipindi 3.1: Mazoezi

Kuelezea maana ya maneno

Ufunguzi kuhusu upimaji wa VVU

Kweli/Uongo kuhusu upimaji VVU

Upimaji wa VVU kwa ujumla

Upimaji wa VVU gerezani

Matumizi ya kondomu za kike na kiume

Dhamira

Mwisho wa kipindi hiki washiriki wataweza:

Kufafanua upimaji wa hiari na ulioasisiwa na mtoa huduma

Page 49: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

39

Kueleza umuhimu wa kujua hali ya VVU

Kujadili umuhimu wa huduma za kupima VVU

Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia kondomu za kike na kiume

Zoezi 1: Kueleza maana ya maneno muhimu

Dakika 30

Shirika la afya duniani lilibadilisha maneno yao mwezi wa saba 2015 kutoka “ Ushauri nasaha

na upimaji wa VVU” kuwa “Huduma za upimaji wa VVU,” na nchi zinafuata inavyostahili

zinapokuwa zinahuisha miongozo yao. Maneno huduma za upimaji wa VVU yanatumika

kujumuisha huduma zote zinazopaswa kutolewa pamoja na upimaji wa VVU: ushauri nasaha

(maelezo ya ushauri nasaha kabla na baada ya kupima); zilizounganishwa na huduma stahiki

za kinga, matibabu na usimamizi na huduma zingine za kliniki na msaada; na kushirikiana na

huduma za maabara ili kusaidia uthibiti wa ubora na utolewaji wa majibu sahihi.

Hatua 1

Waambie washiriki kuwa watatumia dakika takribani 30 au chini yake wakitazama baadhi

ya maneno muhimu ambayo watakuwa wakiyatumia katika kipindi hiki na kwa muda

mrefu baada ya kozi.

Chaguo 1

Kwa kutumia karatasi ya ubaoni iliyoandaliwa yenye vifupisho vyote, ligawe kundi katika

timu mbili. Waambie washiriki kwamba watacheza mchezo wa vifupisho. Wafahamishe

kuwa vifupisho hivi vimeandikwa kwenye karatasi ya ubaoni ambayo mtaifungua mchezo

utapoanza. Taja kuwa kila kikundi kitachagua mwakilishi ambaye atachagua kifupisho

kimoja na kuwaambia wanakikundi maana yake. Atakapopatia kundi litapata alama 2

lakini akikosea kundi litapoteza alama 2. Waambie kuwa watapeana zamu mpaka

vifupisho vyote vitakapokwisha.

Chaguo 2

Waalike washiriki kukaa wawili wawili na kuchukua kipande cha karatasi. Wafahamishe

kwamba utatamka kifupisho ili wao waandike kwa kirefu kama pea. Kwa ufafanuzi zaidi

ziunganishe pea mbili ili ziweze kusahihishiana pale unapokuwa ukitoa majibu sahihi

kama yalivyotolewa kwenye kisanduku cha maneno kulia kwako

Hatua 2: Pongezi

Pongeza kundi zilizopata majibu kwa usahihi zaidi.

Page 50: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

40

Zoezi 2: Utangulizi kuhusu upimaji wa VVU

Dakika 20

Hatua 1: Eleza

Katika kipindi hiki tutatazama/zungumza mambo

kadhaa ya huduma za uchunguzi, uangalizi, matibabu,

na msaada, ikiwemo upimaji VVU wa hiari, upimaji

VVU ulioasisiwa na mtoa huduma na kuzuia

maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa

mtoto.

Hatua 2: Tamka

Shabaha mpya duniani 90–90–90 zinatoa wito

kwamba asilimia 90 ya watu waishio na VVU

kufanyiwa uchunguzi, asilimia 90 ya watu wenye VVU

waliofanyiwa vipimo kupatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, na asilimia 90

ya wale wanaotumia dawa za kupunguza makali wanalazimika kuwa na kiwango kidogo cha

virusi ifikapo 2020. Asilimia 90 ya kwanza (upimaji wa VVU), ni muhimu kwenye asilimia 90 ya

pili (kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa watu

waishio na VVU), na matokeo ya msingi ya asilimia 90 ya tatu (kupungua kwa virusi miongoni

mwa watu wanaotumia dawa za kupunguza makali virusi vya ukimwi), ambayo huboresha

matokeo ya wateja na kuzuia ueneaji wa VVU. Huku ikiwa ni jambo muhimu kupata watu

wengi zaidi kufanyiwa vipimo na kufanikiwa kuwafikisha kwenye huduma za matibabu na

uangalizi, ni muhimu kwamba kiwango cha ongezeko kisididimize ubora wa huduma.

Hatua 3: Zoezi la kikundi

Zoezi hili linazingatia faida na hasara kwa mtu kujua hali yake ya VVU.

Kabla ya kuanza zoezi, waulize washiriki kama wanafikiri ni lazima kujua hali zao za VVU.

Wapange washiriki katika makundi ya watu 4 ili waweze kujadili na kuorodhesha faida na

hasara za mtu kujua hali yake ya VVU.

Wape washiriki dakika 10 kufanya hivyo.

FAIDA MAELEZO

Ishi kwa muda mrefu Mpaka sasa dawa za kupunguza makali zimeweza kuimarisha afya

za watu waishio na VVU, na kwa kiasi kikubwa zimesaidia

kurefusha maisha kuanzia miaka 5–20. Inawezekana pia kuongeza

kipindi ambacho mfungwa mwenye maambukizi anaweza kuishi

kwa kubadili mfumo wa maisha na kupata matibabu ya

maambukizi nyemelezi. Kwa mfano, kujiepusha na hatari zaidi,

kupunguza unywaji wa pombe, na kula vizuri kunasaidia

Page 51: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

41

FAIDA MAELEZO

kurefusha maisha.

Kunamaliza wasiwasi

kuhusu hali yako

Kupima VVU kunaondoa wasiwasi kwamba umeambukizwa au la.

Wale wenye wasiwasi kuhusu tabia zao za zamani wanaweza

kupata nguvu mpya ya maisha kwa kutambua hali zao.

Kuanza kujikinga upya Kutambua kuwa hujaambukizwa VVU kunakupa wewe mwanzo

mpya ulio safi ambao kwao kunaweza kujengwa utamaduni wa

kufanya mapenzi salama. Kumbuka kwamba robo tatu ya watu

waliopima hawajaambukizwa.

Kuweka mipango ya

maisha yako yaliyobaki

Kwa wapenzi wachanga, kupima pamoja kabla ya kuoana

kunawawezesha kutambua ya kuwa wanaweza kupata watoto

ambao hawajaambukizwa ikiwa wataendelea kujikinga na

maambukizi. Wale watakaogundua kuwa wameambukizwa VVU

wanaweza sasa kupanga maisha yao yaliyobaki. Inaweza kuwa ni

miaka mingi ijayo kabla hawajaanza kuugua na hatimaye kufariki.

Wakati huo huo, wanaweza kuwakinga wenza wao na maambukizi

na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto. Wanaweza pia kupanga dhamana za hapo baadaye kwa

familia zao kwa kuandaa usia na kuweka mipango ya kifedha.

Hatua 4: Wahakikishie

Washukuru washiriki kwa ushiriki wao na eleza kuwa mara tutapoelewa ukweli kuhusu

VVU tutaweza kupunguza ueneaji wake na kuishi kwa muda mrefu, maisha yenye afya.

Pia tunaweza kujilinda na kuwalinda wengine kutokana na maambukizi ya VVU kwa kwa

kupunguza vihatarishi tunazokumbana nazo gerezanni na mara baada ya kutoka. Kama

mwelimisha rika, unaweza kuwahakikishia kuwa kama mwongozo wa kitaifa kuhusu VVU

utafuatwa na wafungwa na wafanyakazi wa magereza tunaweza kupunguza hatari nyingi za

maambukizi ya VVU magerezani na kusaidia upimaji wa VVU.

Zoezi 3: Kueleza maana ya ushauri nasaha na upimaji wa hiari na ushauri

nasaha na upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa huduma

Dakika 20

Hatua 1: Dadisi

Waulize washiriki wanafikiri nini tofauti kati ya upimaji VVU kwa hiari na ulioasisiwa na

mtoa huduma?

Page 52: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

42

Hatua 2: Elezea jedwali lifuatalo

USHAURI NASAHA NA UPIMAJI WA

HIARI

USHAURI NASAHA NA UPIMAJI WA VVU

ULIOASISIWA NA MTOA HUDUMA

Mtu huchagua kutafuta vipimo. Mtu anatafuta huduma za matibabu, halafu

upimaji unapendekezwa na kufanywa na daktari

kama sehemu ya mashauriano.

Huduma pasipokuweka jina au huduma

za siri zinaweza kutolewa.

Huduma zitolewazo ni za siri na hutunzwa

kwenye kumbukumbu za hospitali ili kuhakikisha

mwendelezo wa huduma.

Lengo la msingi limejikita katika kuzuia

ueneaji wa VVU kwa kutathimini hatari,

kupunguza hatari, na upimaji.

Lengo la msingi ni kuwatambua watu

walioambukizwa VVU na kuwaunganisha na

huduma za kinga, uangalizi na matibabu.

Maridhiano kwenye maandishi au alama

za vidole kwa wasiojua kuandika na

kusoma huhitajika.

Maridhiano ya mdomo huhitajika na yanapaswa

kutunzwa kwenye kumbukumbu za mgonjwa.

Mtumiaji wa kwanza wa matokeo ya

vipimo ni mteja, anayetumia taarifa

kufanya maamuzi binafsi ya maisha

yake.

Mtumiaji wa kwanza wa matokeo ya vipimo ni

mtoa huduma za afya kufanya uchunguzi sahihi

na kutoa matibabu sahihi.

Hatua 3: Faida za upimaji wa vvu ulioasisiwa na mtoa huduma

Waulize washiriki wanafikiri ni zipi faida za upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa huduma?

Elezea yafuatayo:

Huwasaidia wataalamu wa afya kuwatibu wateja wao kwa usahihi kwa kuwatambua wale

wanaohitaji matibabu/au program za uzima mapema.

Huwasaidia watoa huduma za afya kuboresha huduma za matibabu zitolewazo kwa

wateja wao na kupunguza ugonjwa na vifo.

Inasaidia kupunguza unyanyapaa katika jumuiya kama magerezani kwa kufanya upimaji

wa VVU kuwa ni jambo la kawaida.

Hatua 4: Sisitiza

Sisitiza kwamba bila kujali ni njia gani ya upimaji imetumika, kanuni tano za upimaji wa

VVU zinapaswa kufuatwa. Waulize washiriki “kanuni za upimaji wa VVU” ni nini. Washiriki

wanaweza kujibu au unaweza kueleza kanuni hizi tano kama ifuatavyo:

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

Ushauri Ushauri nasaha ni majadiliano baina ya mshauri wa VVU aliyepata mafunzo

Page 53: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

43

KANUNI ZA

UPIMAJI WA

VVU

MAELEZO

nasaha na mteja anayetafuta kupunguza kupata na kueneza VVU kupitia:

- Maelezo: Mteja hupokea maelezo kuhusu ueneaji na namna ya kujikinga na

VVU na maana ya matokeo ya vipimo vya VVU. Watu ambao hupima na

kuonekana hawana maambukizi ya VVU wanapaswa kupata maelezo ya

afya kwa kifupi juu ya matokeo ya vipimo vyao.

- Ushauri nasaha na kinga ya VVU: Wateja hupokea msaada ili kutambua

tabia hatarishi mahususi zinazopelekea kupata au kueneza VVU na kupiga

hatua ya kupunguza hatari hii.

Mpaka leo tafiti hazijaonesha kwamba kutoa ushauri nasaha kwa muda

mrefu kunahitajika au kunamanufaa zaidi. Isitoshe, utoaji ushauri nasaha kwa

muda mrefu baada ya vipimo kwa watu ambao hawakukutwa na maambukizi

unaweza kuelekezwa kwingine rasilimali zilizotengwa kwa ushauri nasaha

ambazo zinahitajika na wale wanaokutwa na VVU, wale ambao majibu yao

bado hayana hitimisho, na wale waliokutwa katika mahusiano ambayo

mmoja wao ana VVU na mwingine hana VVU

Kuridhia Mtoa vipimo amekupatia maelezo ya kina ili uweze kufanya maamuzi sahihi

kwa kujitambua kuhusu ikiwa kama unataka kupima au la, ikiwa ni pamoja na

uhuru wa kukataa kupima. Maelezo yanapaswa kugusia, vipimo vinahusisha

nini, majibu tarajiwa, na uwezekano wa matokeo yatokanayo. Upimaji wa

lazima haufai.

Usiri Kile unachokijadili na mshauri kitabaki kuwa siri yenu wawili. Mshauri

hataweza kumwambia mtu mwingine yeyote mlichokijadili au nini matokeo

ya vipimo vyako.

Usahihi Watu wote ambao vipimo vyao vinaonesha wana VVU wanapaswa kupimwa

tena ili kuthibitisha vipimo vyao kabla ya kuanzisha huduma na matibabu ya

VVU.

Mshikamano Kutoa huduma za upimaji VVU mahali ambapo hakuna upatikanaji wa

huduma, au uunganishwaji dhaifu kwenye huduma, ikiwepo dawa za

kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, una manufaa kidogo kwa wale wenye

VVU.

Page 54: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

44

Zoezi 4: Upimaji VVU: Zoezi Kweli/Uongo

Dakika 15

Hatua 1: Zoezi

Waelezee washiriki kuwa utataja orodha ya maelezo. Ungependa wao wasimame ikiwa

maelezo ni KWELI, au wakae ikiwa wanadhani maelezo ni UONGO. Waambie kuwa

utawauliza waeleze sababu za majibu yao.

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

Upimaji pasipo kutumia

jina maana yake unapewa

namba na hakuna anayejua

jina lako unapopimwa.

KWELI: Kutuliza hofu na kupunguza unyanyapaa baadhi ya

huduma za upimaji haziwahitaji wale walifanyiwa vipimo kutoa

majina yao. Sampuli ya damu zao hutambuliwa kwa kutumia

namba pekee. Huduma za upimaji wa VVU zinapaswa kuwa siri,

maana yake kile ambacho mtoa huduma na mteja wanajadili

hakitatolewa kwa mtu yeyote bila ya ridhaa ya mtu

anayepimwa. Usiri unapaswa kuheshimiwa, lakini usiruhusiwe

kutilia mkazo siri, unyanyapaa, au fedheha.

Mtu akigundulika kuwa na

VVU baada ya kufanya

vipimo ya lazima basi moja

kwa moja hufukuzwa kazi.

UONGO: Upimaji wa hiari unathaminiwa na watu wenye VVU

hawapaswi kufukuzwa kazi. Ingawa, baadhi ya waajiri huhitaji

wafanyakazi kupima kabla ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi.

Mtu anayekutwa na maambukizi ya VVU kwa kawaida

huruhusiwa kuendelea kufanya kazi lakini haruhusiwi kusafiri

nje ya nchi.

“Kipindi cha mficho” ni

kipindi ambacho kinga

dhidi ya VVU huenda

isionekane kwenye damu

ya mtu aliyeambukizwa.

KWELI: Huchukua hadi kati ya miezi mitatu hadi sita kwa kinga

ya VVU kuonekana kwenye damu. Ushauri siku zote kwa kila

anayepima VVU na kujikuta hana maambukizi ni kupima tena

baada ya “kipindi cha miezi mitatu” si sahihi. Marudio ya

upimaji yanahitajika kwa wale tu ambao matokeo ya vipimo

vyao yanaonesha hawajaambukizwa ambao wameripoti hivi

karibuni (miezi mitatu iliyopita) au uwepo katika hatari

enderevu. Kwa watu wengi ambao hawana maambukizi ya VVU

baada ya kupima, upimaji kwa mara nyingine kufanya uamuzi

wakati wa kipindi cha mficho si lazima na inaweza kupoteza

rasilimali.

Wale wanaokutwa bila

maambukizi ya VVU baada

ya kupima hawapaswi

kujizuia na tabia hatarishi

hapo baadaye

UONGO: Mtu anaweza kujiingiza katika mahusiano hatari ya

kimapenzi pasipo kuambukizwa. Lakini hii haimaanishi kuwa

hawataambukizwa kwenye shughuli zao za kufanya mapenzi

yasiyo salama zinazofuata

Page 55: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

45

MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)

Kila mmoja anapaswa

kupimwa.

KWELI: Upimaji wa VVU ni njia ya kujikinga, kupata matibabu,

uangalizi, na huduma zingine za msaada dhidi ya VVU. Uelewa

wa watu juu ya hali zao za VVU kupitia huduma za upimaji ni

muhimu kwenye mafanikio ya kupambana na VVU. Wigo wa

upimaji VVU miongoni mwa watoto ni mdogo. Mbinu

zinahitajika kuongeza uchunguzi wa mapema kwa watoto

wachanga na kuwaunganisha kwa wakati watoto wachanga

watakaogundulika kuwa na VVU kwenye matibabu na huduma.

Mbinu za ziada zinahitajika kuongeza utumiaji wa huduma za

upimaji VVU miongoni mwa wanaume, ikiwemo utolewaji wa

huduma za upimaji VVU katika maeneo ambayo yanafaa zaid

na kukubalika na wanaume, na kubadili njia za kuwahimiza

upimaji wa wenza wa wanaume katika maeneo ambapo kuna

uwepo mkubwa na kwa wapenzi na wenzi wa wanaume na

wanawake wenye VVU kwenye maeneo yote. Kuyafikia

makundi maalumu ya watu, kama vile wakazi wenza, ni jambo

la kupewa kipaumbele.

Kama mtu atagundulika

kuwa na VVU mtu huyu

anapaswa kuwaeleza wenzi

wake wote kuhusu majibu

ya vipimo.

KWELI: Ingawa kuweka wazi kwa wapenzi, wanafamilia wenye

msaada, na wafanyakazi wa afya, mara nyingi kuna manufaa,

hii inapaswa kufanywa na au kwa ridhaa ya mtu aliyepimwa.

Ushauri nasaha kwa wateja wenye VVU inapaswa kujadili

majibu yanayowezekana kuwekwa wazi, na hatari na manufaa

ya kuweka wazi, hasa miongoni mwa wanandoa na wapenzi.

Wape ushauri ili kusaidia kuweka wazi kwa pamoja. Wanandoa

na wenzi wanapaswa kupewa ushauri nasaha na upimaji wa

hiari pamoja na msaada wa kuweka wazi kwa pamoja. Mshauri

anapaswa kutazama hatari za vurugu za ndani za wapenzi na

kujadili hatua zinazowezekana ili kuhakikisha usalama wa

kimwili wa mteja hasa wanawake ambao wamegundulika kuwa

na VVU.

Mtu wa kwanza kwa

wanandoa kugundulika na

VVU ndiye aliyeleta virusi

kwenye familia.

UONGO: Wakati ambapo mtu anajua kuwa ana maambukizi ya

VVU hauna uhusiano na muda alioambukizwa. Baada ya

kipimo kuonesha uwepo wa VVU, unapaswa kuhimiza na

kuwapima wenzi, watoto, na wanafamilia wengine wa mteja.

Jambo hili linaweza kuwa mmoja mmoja, vipimo kwa wapenzi,

kupima kwa pamoja, au kumfahamisha mwenza kwa ridhaa.

Page 56: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

46

Zoezi 5: Upimaji wa VVU uraiani na magerezani

Dakika 30

Hatua 1: ElezaUpimaji wa VVU

Kupima VVU ni njia pekee na muhimu kujua kama una VVU. Ikiwa una VVU, ni jambo

muhimu kutambua ugonjwa. Jambo hili litakupa nafasi nzuri ya kupata matibabu na

huduma unazohitaji ili kuishi kwa afya. Unapokwenda kupima VVU, utakuwa na nafasi

kuzungumza na mtu aliyepata mafunzo, hivyo unaweza kuuliza swali lolote amabalo

unaweza kuwa nalo. Mtu anayekupima atakupatia maelezo jinsi ambavyo vipimo

vinafanyika na jinsi utavyopata majibu.

Kutegemeana na aina ya kipimo, utachukuliwa sampuli ndogo ya damu kutoka mkononi

mwako, au tone la damu kutoka kwenye kidole chako. Kuna baadhi ya vipimo hufanyika

kwa kutumia maji maji yanayopatikana kuzunguka fizi.

Kuna aina mbalimbali za vipimo vya VVU. Baadhi ya vipimo vya VVU huonesha uwepo wa

virusi halisi kwenye damu (kipimo cha antijeni) na vipimo vingine huonesha kinga za VVU

zinzofanya kazi ya kupambana na VVU. (kipimo cha kinga).

Ikiwa vipimo vitaonesha kuwa una VVU, inamaanisha una maambukizi ya VVU. Ikiwa

vipimo vitaonesha kuwa huna VVU, maana yake huna maambukizi ya VVU. Kwa baadhi ya

vipimo utahitaji kufanyiwa vipimo vya ufuatiliaji ikiwa majibu ya yataonesha kuwa una

maambukizi ya VVU.

Hatua 2: Maswali na majibu kipindi cha mficho

Swali: Kipindi cha mficho maana yake nini?

Jibu: Kipindi kuanzia ulipoambukizwa VVU mpaka pale ambapo mwili utatoa kinga ya

kutosha kwa VVU itakayoweza kuonekana kwa kutumia kipimo cha kinga ya VVU hujulikana

kama kipindi cha mficho. Watu wengi huweza kutengeneza kinga ya VVU ndani ya miezi

mitatu mara baada ya kupata maambukizi ya VVU. Lakini kipindi cha mficho kinaweza

kutofautiana kulingana na kipimo cha VVU kilichotumika. Kwa ujumla, mtu yeyote mwenye

matokeo hasi kupitia kipimo cha kinga ya VVU ndani ya miezi mitatu ya uwezekano wa kuwa

na VVU, anapaswa kupima tena baada ya miezi mitatu.

Hatua 3: Maswali na majibuupimaji wa VVU

Swali: Kipimo cha antijeni ni nini?

Jibu: Kipimo cha antijeni hugundua antijeni za VVU (sehemu ya virusi) kwenye damu. Kipimo

cha antijeni kinaweza kugundua maambukizi ya VVU kabla ya kinga ya kutosha ya VVU

haijatolewa ili kuweza kugunduliwa kwa kipimo cha kinga ya VVU.

Swali: Inachukua muda gani kupata majibu ya vipimo vya VVU?

Jibu: Matokeo ya haraka ya kipimo cha kinga ya VVU yanaweza kutolewa ndani ya dakika

15–30. Ingawa, inaweza kuchukua siku kadhaa au wiki kadhaa, kutegemeana na aina ya

Page 57: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

47

kipimo kilichotumika. Katika Tanzania matokeo chanya ya kipimo cha VVU ni lazima

yathibitishwe kwa kipimo cha uthibitishaji.

Swali: Watu waliopo nje ya gereza wanaweza kwenda kupima wapi?

Jibu: Watoa huduma za afya wanaweza kukufanyia vipimo vya VVU. Vipimo vya VVU vile vile

vinapatikana katika hospitali nyingi, kliniki za matibabu, vituo vya afya vya jamiii, vituo vya

ushauri nasaha na upimaji kwa hiari, na mashirika ya huduma za UKIMWI.

Hatua 4: Maswali na majibu—vipimo vya VVU gerezani

Swali: Ukiwa gerezani vipimo vya VVU hufanyika vipi?

Jibu: Vipimo vya VVU hutolewa katika vituo vya afya vya magereza ikiwemo huduma za

kliniki za ushauri nasaha na upimaji kwa hiari zinazotembea ambazo hutembelea maeneo ya

magereza. Ingawa, upimaji wa lazima kwa wafungwa ni kinyume cha maadili na hauna

ufanisi, upimaji unapaswa kuwa wa hiari ukiambatana na ushauri nasaha kabla na baada ya

kupima. Matokeo yanapaswa kutolewa kwa wafungwa na mfanyakazi wa afya ambaye

anapaswa kuhakikisha kutunza siri za kihospitali.

Hatua 5: Maswali na majibu—bada ya kugundua ugonjwa

Swali: Je unapaswa kufanya nini ikigundulika una VVU au hauna maambukizi ya VVU?

Page 58: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

48

UFANYE NINI IKIWA HUNA VVU

Kuachana kabisa na shuguli za

mapenzi ni njia bora zaidi kuzuia

kupata VVU. Kuepuka maambukizi

huja pale unapokuwa mwaminifu

kabisa kwa mpenzi mmoja, inayohitaji

wewe na mpenzi wako anagalau

kupima VVU kila mmoja, kwa

anagalau miezi mitatu tofauti; na

mkiamua kufanya mambo ya mapenzi

ya ndani ya(uke, mdomo, na njia ya

haja kubwa) kwamba mtumie kwa

usahihi kondomu ya kike au kiume.

UFANYE NINI IKIWA UNA VVU.

Kitu cha kwanza ambacho kliniki itakifanya ni

kupima kiwango cha CD4. Watachukua damu kutoka

kwako itakayopelekwa maambara ili kupima idadi ya

seli za CD4 kwenye ujazo wa mililita moja ya damu.

Hii itakusaidia kujua mfumo wako wa kinga una afya

kiasi gani. Inapendekezwa kuwa watu wenye VVU

wapime viwango vya CD4 zao kila baada ya miezi

sita. Pia unaweza kuhitaji kipimo cha kutaza wingi wa

virusi utapoanza kutumia ARVs na mara nyingine

baadaye kupima upunguaji wa virusi kwa kutumia

dawa za ARVs (ufanisi).Unapokuwa tayari na salama

kufanya hivyo, ni muhimu kuweka wazi kwa mwenzi

wako kuwa una VVU

Zoezi 6: Matumizi ya kondomu za kike na kiume

Kuzuia ueneaji wa VVU

Dakika 30

Hatua 1: Eleza

Eleza kwamba hii ni fursa kwa ajili yao kujifunza au kuchangia taarifa kuhusu jinsi ya

kutumia kondomu ya kiume na kike kwa ufasaha kama njia ya kujikinga na VVU.

Kuzungungumzia kuhusu kondomu kwenye maeneo ya gerezani inaweza kuwa ni jambo

gumu. Ingawa, ni muhimu kuweka wazi kuwa kondumu hazitagawiwa magerezani.

Hairuhusiwa na sheria za Tanzania. Kwa hiyo ni muhimu kupata taarifa hizi kuhusu kondomu

kwani zitawanufaisha mara baada ya kumaliza kifungo au kuachiliwa kutoka gerezani kwa

mfano, mahabusu.

Eleza kuwa kondomu hutoa kinga madhubuti dhidi ya VVU ikiwa itatumika kwa usahihi

na wakati wote. Ingawa kondomu zimezuiliwa gerezani, wafungwa wanaweza kutumia

kondomu mara baada ya kutoka gerezani.

Hatua 2: Uliza

Kwa kunyosha mikono wangapi wamewahi kutumia kondomu? Nani anaweza kueleza hatua

za namna ya kutumia kondomu ya kiume kuanzia mwanzo hadi mwisho?

Page 59: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

49

Hatua 3: Hatua jinsi ya kutumia kondomu ya kiume

Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kiume

Kata pakiti ya kondomu kwa kufuata alama pembeni mwa

pakiti. Unapofungua pakiti ya kondomu usitumie kucha wala

meno.

Iweke kondomu kwenye ncha ya uume halafu ikunjue kuelekea

chini ya urefu wa uboo kwa kuisukuma chini kwenye mzingo

wa duara wa kondomu.Valisha kondomu kwenye uboo ukiwa

bado umesimama. Minya chuchu ya kondomu katikati ya

kidole na kidole gumba cha mkono mmjoja (Ukiacha nafasi

nchani ili kukusanya shahawa au manii).

Baada ya kufanya mapenzi na kukojoa, shikilia mzingo wa

kondomu halafu toa uume nje kabla haujalala. Ifunge

kondomu katika kifundo kwenye manii au shahawa.

Itupe kondomu iliyotumika mahali salama. Kama vile kondomu

ya kike, kamwe usiidumbukize chooni kondomu ya kiume.

Inaweza kuziba choo chako na haiozi. Ifunike kwenye tishi

halafu itupe kwenye pipa la takataka au kwenye choo cha

shimo.

Hatua 4: Orodhesha

Jadili mambo magumu zaidi tunayokabiliana nayo wakati wa kutumia kondomu.

Waombe washiriki kupendekeza ni namna gani changamoto hizi zinaweza kutatuliwa.

Baadhi ya matatizo ya kawaida mara zote ni pamoja na:

Kujaribu kuiviringisha kondomu kuelekea chini wakati ikiwa “nje—ndani.”

Kondomu haikunjuki kuelekea kote chini.

Kondomu haijawekwa sawa kwenye kielelezo

Mtumiaji hana utulivu wakati akifungua pakiti au hutumia meno kuifungua.

Hewa kwenye chuchu haijatolewa

Kamwe usitumie mafuta ya mgando kama Vaseline® au mafuta ya taa kama kilainishi

wanapotumia kondomu.

Page 60: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

50

Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kike

Fungua pakiti ya kondomu. Chana moja ya mapengo mwishoni na

usitumie mkasi wala kisu. Kwani hutakiwi kuiharibu kondomu.

Shikilia sehemu ya juu ya kondomu na wakati huo huo sukumiza

sehemu ya ndani ya duara, huku sehemu ya wazi ikining’inia.

Utagundua kwamba kuna duara mbili kwenye kondomu ya kike,

tofauti na kondomu ya kiume. Duara ya nje, ambayo ipo wazi,

huenda nje ya kondomu. Duara ya ndani huenda ndani na husaidia

kushikilia kondomu juu wakati wa tendo la ndoa. Sukumiza

sehemu ya ndani, duara iliyofungwa.Mara baada ya duara

kuonekana ndefu na nyembamba, sasa ipo tayari kuingizwa ndani

ya uke.

Tafuta sehemu ya faragha na iingize sehemu ya ndani, sukumiza

duara ndani ya uke wako. Kama ni mara ya kwanza kuingiza kisodo

au kufanya mapenzi, itakuchukua muda kabla hujawa mzoefu wa

kuisokomeza hapo. Kiasi kidogo cha kilainishi kinaweza kusaidia

mambo kwenda shwari. Unaweza kutumia kidole cha kati

kuisukuma ila hakikisha haijageuzwa. Duara ya nje inapaswa kubaki

nje ya uke. Uko tayari kwenda! Ukiwa tayari, hakikisha

unamwongoza mpenzi wako kuingiza uume kwenye kondomu.

Hakikisha haingizi pembeni au kwa bahati mbaya kuikosa kabisa

kwa namna yoyote

Safisha. Ukishamaliza, geuza duara ya nje mara kadhaa ili kuifunga halafu ivute nje taratibu. Kama

ilivyo kwa kondomu ya kiume, kamwe usitupe kondomu ya kike kwenye choo cha maji. Inaweza

kuziba choo chako na haiozi. Ikunje kwenye tishu na uitupe kwenye pipa la takataka au choo cha

shimo.

Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU: matibabu, huduma, na msaada

Dakika 40

Kipindi 3.2: Mazoezi

Matibabu ya vvu na maambukizi nyemelezi

Matibabu ya mgonjwa mwenye maambukizi ya vvu

Page 61: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

51

Dhamira

Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:

Kueleza kwa kifupi uwepo wa matibabu kwa matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo,

magonjwa ya ngono, maambukizi ya njia ya uzazi, na maambukizi nyemelezi.

Zoezi 1: Matibabu ya VVU na maambukizi nyemelezi

Dakika 40

Hatua 1: Eleza

Waambie washiriki kwamba sasa watajadili matibabu ya maambukizi tuliyokwisha kujadili

kama VVU, kifua kikuu, magonjwa mengine ya ngono, na maambukizi ya njia ya uzazi.

Hatua 2: Maswali na majibu—maambukizi

Swali: Tunajikinga vipi na magonjwa ya ngono?

Chukua mawazo machache

Jibu: Njia bora ya kujikinga na magonjwa ya ngono ni kuzuia kuupata. Katika hatua hii ya

kwanza ya kujikinga, uwezekano wa kupata magonjwa ya ngono unaweza kupunguzwa kwa:

Usianze kufanya mapenzi mapema (kwa vijana wadogo)

Kupunguza idadi ya wapenzi

Kutumia kondomu kwa usahihi na wakati wote

Utambuzi wa haraka na kupata matibabu sahihi ya ugonjwa wa ngono

Swali: Maambukizi njia ya uzazi inamaanisha nini?

Jibu: Maambukizi kwenye njia ya uzazi ni maambukizi yaliyopo kwenye mkondo wa sehemu

za siri. Huwaathiri wanaume na wanawake. Baadhi ya magonjwa katika njia ya uzazi (kama

vile kaswende na gono) huambukizwa kwa njia ya kujamiiana lakini mengi yao

hayaambukizwi kwa njia hiyo (kama maambukizi ya fangasi). Njia bora ya kushughulikia

ugonjwa wa ngono ni kutafuta matibabu mara moja.

Hatua 3: Maswali na majibu—matibabu ya VVU

Swali: VVU hutibiwa vipi?

Unaweza usiwe na muda wa kupitia maswali yote yafuatayo. Pitia maelezo kwa ufupi

kuhusu dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI kwenye ukurasa ufuatao.

Jibu: Maambukizi ya VVU hutibiwa kwa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya

UKIMWI

Swali: Nini maana ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi?

Page 62: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

52

Jibu: Ni dawa zinazotumika kutibu mambukizi ya VVU. Watu wanaotumia dawa za

kupunguza makali hutumia muunganiko wa madawa (yaitwayo ARV regimen) kila siku. Kuna

muunganiko mbalimbali wa madawa. Dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI

zinapendekezwa kwa kila mtu mwenye maambukizi ya VVU. Dawa za kupunguza makali ya

ukimwi haziwezi kuponyesha kabisa VVU, bali huwasaidia watu kuishi kwa muda mrefu,

maisha yenye afya. Dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi pia hupunguza hatari ya

kueneza VVU kwa mtu mwingine. Nchini Tanzania, kwa watu wazima na vijana wadogo,

hatua ya mwanzo (ya kwanza) madawa ya ARV regimen ni miongoni mwa miunganiko

ifuatayo ya dawa tatu: (1) (tenofovir (TDF) + lamivudine (3TC) + efavirenz (EFV); (2)

zidovudine (AZT) + lamivudine (3TC) + lopinavir/ritonavir (LPV/r); or (3) abacavir (ABC) +

lamivudine (3TC) + nevirapine (NVP).

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI kwa kifupi

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya

UKIMWI ni utumiaji wa dawa za VVU

kutibu maambukizi ya VVU.

Inapendekezwa kwa kila aliyeambukizwa

na VVU, na husaidia watu wenye VVU

kuishi kwa muda mrefu, maisha yenye

afya.

Watu wenye VVU wanapaswa kuanza

kutumia dawa kulingana na mwongozo wa

kitaifa wa usimamizi wa VVU/UKIMWI. Kwa

watu wenye VVU wenye hali zifuatazo. Ni

muhimu sana kuanza matumizi ya mara

moja mwanamke akiwa na mimba

Magonjwa fulani yenye uhusiano na

maambukizi ya VVU kama vile utando

mdomoni, herpes simplex, mkanda wa

jeshi, dalili kiunoni, kansa ya mlango wa

kizazi, na kifua kikuu.

Toleo jipya la miongozo ya kimataifa

linapendekeza kutumia dawa mara baada

ya kugundulika na VVU (“Pima na Tibu”)

kwa kuanza matibabu mapema

yatapunguza hatari ya VVU na matatizo ya

kiafya yasiyo na uhusiano na VVU

miongoni mwa watu wenye VVU na

UKIMWI Na itapunguza wingi wa virusi

kwa kiwango kisichogundulika na hivyo

kupunguza hatari ya kuenea kwa VVU.

Ufanisi wa dawa hutegemea ufuasi mzuri

wa dawa—kutumia dawa kila siku kama

ulivyoelekezwa na mtoa huduma wa afya.

Kabla ya kuanza kutumia dawa, ni muhimu

kukabiliana na maswala yoyote

yatakayoathiri makali ya dawa.

Swali: Tiba ya virusi vya UKIMWI hufanya kazi vipi?

Jibu: VVU hushambulia na kuharibu seli za CD4 kwenye mfumo wa kinga ambazo

hupambana na maambukizi. Seli zikiwa chache, ni vigumu kwa mwili kupambana na

maambukizi na aina fulani za saratani. Dawa huzuia VVU kuongezeka (kuzaliana wenyewe),

kitu ambacho hupunguza kiwango cha VVU mwilini ingawa haiondoi VVU vyote mwilini.

Uwepo wa VVU wachache mwilini huupatia mfumo wa kinga nafasi ya kuponyesha na

kuzalisha seli za CD4 zaidi. Hata kama bado mna kiasi fulani cha VVU mwilini, mfumo wa

kinga una nguvu za kutosha kupambana na maambukizi na magonjwa yajulikanayo kama

maambukizi nyemelezi kama vile kifua kikuu, homa ya mapafu, na kansa ya mlango wa kizazi.

Maambukizi nyemelezi ni maambukizi ambayo hutokea mara kwa mara na huwa makubwa

Page 63: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

53

zaidi kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kinga, kama vile watu waishio na VVU. Kwa

kupunguza kiwango cha VVU mwilini, dawa za VVU zinaweza pia kupunguza hatari ya

kueneza VVU kwa mtu mwingine.

Swali: Ni wakati gani muafaka kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya

ukimwi?

Jibu: Watu wenye maambukizi ya VVU wanaostahili wanapaswa kuanza dawa mapema

iwezekanavyo. Watoa huduma za afya watashirikiana na wagonjwa ili kuona nani anastahili

kulingana na mwongozo wa kitaifa. Kwa watu wenye hali zifuatazo, ni muhimu sana kuanza

kutumia dawa mara moja: Ujauzito na magonjwa fulani yenye uhisiano na maambukizi ya

VVU kama utando mdomoni, mkanda wa jeshi, au kansa ya malango wa kizazi.

Kulingana na Mwongozo Wa Kitaifa Wa Kusimamia VVU Na UKIMWI Toleo 5 (Wizara ya Afya

na Maendeleo ya Jamii, Tanzania [MOHSW] 2015), dawa zinapaswa kuanzishwa kwa watu

wote wenye kifua kikuu na maambukizi ya uhusiano na VVU, bila kujali hatua za kliniki za

WHO au kiwango cha seli za CD4. Matibabu ya kifua kikuu yanapaswa kuanza kwanza,

yakifuatiwa na matibabu mapema iwezekanavyo, ndani ya wiki mbili za awali baada ya

kuanza matibabu ya kifua kikuu.Watu wenye VVU wasio na ishara wala dalili za uwepo wa

kifua kikuu wanastahili kupata dawa za kujikinga za isoniazid. Jitihada zote zinapaswa

kufanyika kupambana na maambukizi nyemelezi. Msisitizo unapaswa kuwekwa katika

utambuzi wa mapema, matibabu, na rufaa, pakiwa na ulazima.

Kumbuka: Mwongozo mpya unapendekeza kuanzisha dawa kwa wagonjwa wote mapema

mara maambukizi ya VVU yanapothibitishwa kuwepo. (“Pima na Tibu”). Serikali inaweza

kutengeneza miongozo mipya kulingana na kiwango cha utayari wao (usambazaji wa

madawa, uwezo wa maabara, rasilimali watu, fedha, nakadhalika).

Swali: Nini faida za kutumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi?

Jibu: Baadhi ya faida za dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:

Watu wenye VVU wanaotumia dawa wanaweza kuishi kwa muda mrefu ukilinganisha na

wale wasiotumia dawa.

Watu wanaotumia dawa wana magonjwa machache yenye uhusiano na VVU

ukilinganisha na wale wasiotumia dawa.

Kwa kuwa watu wanaotumia dawa kama ilivyoelekezwa wana afya bora, huenda hospitali

mara chache na huepuka gharama nyingine za kiafya.

Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia dawa wana muda zaidi kukamilisha malengo na

dira za maisha yao.

Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia dawa wanaweza kuzitunza familia zao vizuri

zaidi.

Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia dawa wanaweza kuishi kama kawaida.

Kwa kuwa watu wanaotumia dawa wana kiasi kidogo cha VVU ndani ya miili yao, wana

nafasi ndogo ya kueneza VVU kwa watu wengine.

Page 64: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

54

Hatua 4: Maswali na majibukuishi kwa kutumia dawa za kupunguza makali

Swali: Sababu kubwa ya dawa kuota usugu na matibabu kutofanya kazi ni nini?

Jibu: Ufuasi hafifu wa dawa huongeza hatari ya dawa kuota usugu na matibabu kutofanya

kazi. Kutumia dawa kila siku kama ilivyoelekezwa, ijulikanavyo kama “ufuasi,” ni muhimu sana

kwa dawa kuweza kufanya kazi. Baadhi ya watu huacha kutumia dawa kama ilivyoelekezwa

kwa kuwa hupatwa na madhara ya pembeni, au kwa kuwa wanajisikia kuwa na nguvu na

wenye afya na kudhani hawahitaji dawa tena. Baada ya muda, japo, bila ya dawa, VVU

huongezeka tena mwilini na watu huanza kuugua. Isitoshe, kuna uwezekano kwamba dawa

hizo hizo za kupunguza makali zisimsaidie tena huyu mtu mara atakapotaka kuanza

matibabu tena kwa kuwa VVU mwilini watakuwa wameshatengeneza usugu kwa dawa hizo.

Wanaweza wakaanza kutumia aina nyingine ya dawa, lakini inaweza kuwa ni vigumu sana

kuzipata na /au kukumbwa na madhara ya pembeni kuliko ulipokuwa ukitumia dawa za

mwanzo. Uenezaji wa kirusi kinachopelekea usugu wa dawa za VVU kwa njia ya mapenzi ni

jambo linalowezekana pia. Usugu ni sababu ya msingi kwa nini matibabu yanaweza yasifanye

kazi.

Swali: Ni kwa muda gani dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI humwezesha mtu

mwenye maambukizi kuishi?

Jibu: Watu wengi wanaotumia dawa kama ilivyoelekezwa huishi maisha ya kawaida na

huugua kwa vipindi sawa na watu wasio na maambukizi ya VVU.

Swali: Changamoto za dawa za kupunguza makali ya UKIMWI ni zipi?

Jibu: Uwezekano wa hatari za dawa ni pamoja na madhara ya pembeni (madhara yoyote ya

dawa, kemikali, au dawa nyingine ambazo ni za nyongeza kwa ajili ya madhara mahususi,

hasa madhara ambayo ni ya kudhuru au yenye maudhi) yanayosababishwa na dawa za

kupunguza makali au dawa nyingine ambazo mtu mwenye VVU anazitumia. Asili ya madhara

ya pembeni inategemeana na sehemu ya mwili ambako dawa imekusudiwa kutibu au namna

ambayo mwili unashughulika na dawa.

Dawa za kupunguza makali ni matibabu ya muda mrefu—mtu analazimika kutumia dawa

kila siku kama ilivyoelekezwa na mtoa huduma za afya. Ufuasi hafifu—kutotumia dawa

kila siku na kama ilivyoelekezwa—huongeza hatari ya dawa kuota usugu na matibabu

kutofanya kazi.

Dawa nyingi za kupunguza makali humezwa mara moja kwa siku, pamoja na au bila ya

chakula. Baadhi humezwa mara mbili kwa siku au zinapaswa kumezwa pamoja na

chakula.

Baadhi ya aina za dawa za kupunguza makali zinaweza kuwa na madhara ikiwa

zitamezwa pamoja na vidonge vingine au wakati wa mimba. Ni muhimu kuzungumza na

mtoa huduma za afya kuhusu dawa zingine unazotumia na mfahamishe kama una

mimba.

Page 65: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

55

Dawa za kupunguza makali zinaweza kusababisha matatizo mengine. Baadhi ya matatizo

yanaweza kutatuliwa baada ya wiki kadhaa za utumiaji, matatizo mengine yanahitaji

ushauri wa daktari au wataalamu wa afya.

Ikiwa dawa hazimezwi kila siku kama ilivyoelekezwa, dawa hazitafanya kazi vizuri na mtu

anaweza kuugua. Watu ambao dawa hazifanyi kazi kabisa wanalazimika kubadilisha na

kupata aina nyingine ya dawa, lakini machaguzi yao ya dawa hapo baadaye yatakuwa

yamepungua.

Ikiwa unapata matibabu kutibu matatizo mengine ya kiafya au kinzamimba (uzazi wa

mpango), ni muhimu kumfahamisha daktari wako. Baadhi ya dawa za kupunguza makali

(kama, efavirenz, nevirapine) huingiliana na baadhi ya madawa ya uzazi wa mpango.

Kutumia madawa ya kulevya (kama bangi, cocaine, ecstasy, na kadhalika) pia kunaweza

kusababisha dawa kuacha kufanya kazi vizuri.

Swali: Madhara ya pembeni ya kawaida ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI

ni yapi?

Jibu: Madhara ya pembeni ya dawa yanaweza kutofautiana kulingana na dawa na mtu

anayetumia dawa hizo. Watu wanaotumia aina moja ya dawa wanaweza kuwa na madhara ya

pembeni tofauti kabisa. Madhara ya pembeni ya kawaida ni pamoja na:

Maumivu ya kichwa, kizunguzungu cha mara kwa mara, ambayo huenda yasiwe

makubwa sana.

Kuvimba kwa mdomo na ulimi au kuharibiwa kwa ini, ambayo inaweza kutishia maisha

Ukurutu mwilini kote

Ganzi miguuni

Matatizo ya figo (hasa kwa matumizi ya tenofovir)

Ndoto za ajabu (hasa kwa matumizi ya efavirenz)

Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto

Dakika 30

Kipindi 3.1: Mazoezi

Utangulizi kuhusu kuzuia na kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:

Kueleza maana ya maneno kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto na kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza mama mwenye VVU na mtoto

Page 66: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

56

Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuzuia maambukizi kwenda kwa mtoto

Dakika 30

Hatua 1: Anza

Waulize washiriki wanaelewa nini kuhusu kuzuia na kukomesha maambukizi.

Hatua 2: Eleza

Eleza kuwa kuzuia inamaanisha kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa

mtoto na kukomesha inamaanisha kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama

kwenda kwa mtoto.

Hatua 3: Maswali na majibumaambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Swali: Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto maana yake ni nini?

Jibu: Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ya VVU hutoka kwa mama aliye na

VVU kwenda kwa mtoto wake wakati wa ujauzito, kuzaa, (hujulikana pia kama uchungu wa

uzazi na kujifungua), au wakati wa kunyonyesha (kwa njia ya maziwa ya mama). Maambukizi

ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto vile vile huitwa maambukizi ya perinatal ya

VVU. Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni njia ambayo mara nyingi watoto

wachanga huambukizwa VVU.

Swali: Unadhani maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanaweza

kukingwa?

Jibu: Ndiyo

Hatari za maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni ndogo pale ambapo

Wanawake wenye VVU wanapopata dawa

wakati wa ujauzito na kujifungua na katika

mazingira fulani, kuzaa kwa upasuaji

uliopangwa (mara nyingine hujulikana

kama C-section).

Watoto waliozaliwa na wanawake wenye

VVU hupokea dawa za VVU kwa kipindi

cha wiki sita baada ya kuzaliwa na

kunyonya maziwa ya mama kwa miezi sita

halafu anaachishwa

Hatua 4: Eleza

Wizara ya afya na ustawi wa jamii imeridhia njia bora kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto

wachanga na watoto wadogo ili kufikia lengo la kutokomeza maambukizi toka kwa mama

kwenda kwa mtoto. Mbinu ni pamoja na hizi zifuatazo:

Kinga za awali za maambukizi ya VVU kwa wanawake wenye umri wa kuzaa na wenza

wao.

Kuzuia mimba zisizotarajiwa kwa wanawake wenye VVU

Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa wanawake waathirika kwenda kwa watoto

wachanga

Page 67: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI

57

Kutoa matibabu, huduma, na msada kwa wanawake wenye maambukizi ya VVU, watoto

wao wachanga na familia zao.

Hatua 5: Maswali na majibu—wanaume na nafasi yao katika kuzuia maambukizi ya vvu

toka kwa mama kwenda kwa mtoto

Swali: kuna faida gani za kuwashirikisha wanaume kwenye kuzuia

maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto?

Jibu: Ushahidi unaonesha kwamba wanaume wanapounga

mkono huduma za afya kwa wanawake:

Utumiaji wa huduma za kuzuia na kupata matibabu ya VVU

kwa wanawake na watoto huongezeka.

Matokeo kiafya huboreka.

Kuna ongezeko na ufuasi wa matumizi ya dawa.

Kuna ongezeko la upimaji na matibabu miongoni mwa wanaume.

Unyanyapaa hupungua.

Hatua 6: Maswali na majibu—lengo

Swali: Nini lengo la kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini

Tanzania?

Jibu: Lengo ni kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa

matibabu kwa wajawazito wote wenye maambukizi ya VVU na watoto wao wenye VVU

wanaohudhuria afya ya mtoto na uzazi na huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa

mama kwenda kwa mtoto katika vituo vya afya gerezani. Hili linaweza kufikiwa kwa kutoa

huduma za upimaji wa VVU kwa wanawake wajawazito ikifuatiwa na kuwapa mbinu kwa

wanawake wenye VVU kuzuia maambukizi wima ya VVU kwa watoto wao wachanga.

Hatua 7: Fupisha

Kutokomeza maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini Tanzania

kunahitajika:Jitihada endelevu ili kuzuia maambukizi mapya miongoni mwa wanawake, na

kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake

waishio na VVUKuboresha upatikanaji wa huduma kabla ya kujifungua na wahudumu

wenye ujuzi wakati wa kuzaa kwa wanawake wote, bila kujali mali, hali, na makazi.

Uharakisha upanuzi wa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda

kwa mtoto zenye ubora wa juu kwenye huduma zote kabla ya uzazi na vituo vya

kujifungulia na kuimarisha uwepo wa huduma kwa kuzishirikisha jamii na vituo vya afya.

Ubora na mwendelezo wa huduma kwa wakati muafaka kwa mama na mtoto.

Ushirikishwaji wa wanaume kwenye jitihada za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa

mama kwenda kwa mtoto ni hatua muhimu ya kuweza kuwapima VVU wanaume.

Page 68: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

58

SOMO 4: KUVUNJA UKIMYA KUHUSU

KIFUA KIKUU NA VVU.

Lengo

Kukuza elimu na ujuzi wa mawasiliano kwa mfungwa ili aweze kuripoti shutuma zenye

uhusiano na kifua kikuu na VVU miongoni mwa wafungwa wenzake.

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa mafunzo, wafungwa na wafanyakazi wa magereza wataweza:

Kuelezea na kutambua aina za shutuma kwenye magereza.

Kuzungumzia shutuma za kimwili au kimapenzi kwa uwazi zaidi.

Kueleza maana na manufaa ya mawasiliano kwa wenza.

Kutambua njia za asili na zenye ufanisi za mawasiliano kwa mwenza miongoni mwa

wakazi wenza na wafanyakazi wa magereza.

Kuelezea njia za kutoa taarifa na kutafuta huduma miongoni mwa wakazi wenza.

Kutambua changamoto kuu na njia za kuzitatua.

Kipindi 4.1: Kutambua aina za shutuma katika magereza

Saa 2, Dakika 5.

Kipindi 4.1: Mazoezi

Aina za shutuma katika magereza

Kuzungumzia shutuma za kimwili na kimapenzi

Jinsi ya kuvunja mazoea ya ukimya

Zoezi 1: Aina za shutuma katika magereza

Dakika 20

Vifaa vinavyohitajika

Ubao wa chaki au karatasi za kuandikia ubaoni

Maandalizi ya awali

Ikiwezekana washirikishe baraza la magereza katika mjadala huu.

Page 69: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

59

Hatua 1: Fafanua

Wafahamishe washiriki kuwa wafungwa wanaweza kukumbana na uonevu wa kimwili au

kimapenzi na aina nyingine za vurugu na kuonewa na wafungwa wenzao na wafanyakazi wa

magereza na kushindwa kutoa taarifa ya uonevu kwa kuhofia ulipizaji kisasi.

Endelea kueleza kwamba wafungwa vile vile wanaweza kukumbana na mambo ya kutendewa

vibaya, kudhihakiwa, lugha zisizi na adabu, na uongo wa kupindukia kutoka kwa wafungwa

wenzao. Wafanya kazi wa magereza wanaweza kutumia kauli za vitisho kama njia ya

kuwaogopesha au kuwavunja moyo wafungwa wenzao ili kuwafanya watii kanuni na taratibu

za magereza

Hatua 2: Jadili

Eleza kwamba majadiliano haya yatatoa mwanga juu ya haya mambo hivyo wafungwa

pamoja na wafanyakazi wa magereza wanaweza kutatua mambo haya.

Matukio ya unyanyasaji kwa kiasi kikubwa husababishwa na sababu za kimazingira na mahali

kama vile umati mkubwa/msongamano, usimamizi hafifu, nguvu ya madaraka ambayo

inaweza kutengeneza fursa kwa aina mbalimbali za unyanyasaji. Madhara ya unyanyasaji wa

kimwili na kimapenzi yanaweza kuwa pamoja na majeraha, ugonjwa, kujiumiza mwenyewe,

msongo wa mawazo, na ugonjwa wa akili. Sababu hizi zinaweza kutatuliwa na kuzuiwa kwa

kuongeza usimamizi thabiti na kwa wafanyakazi wa magereza kuzungukia vizimba na

program za elimu rika na uhamasishaji. Usimamizi usio thabiti kutoka kwa maafisa wa

magereza huleta mianya kwa wafungwa kujiingiza kwenye vurugu na kuwatendea vibaya

wengine. Si rahisi kufuatilia shutuma za unyanyasaji au uonevu miongoni mwa wafungwa

wenye maelezo yasiyijitosheleza hasa kuhusu shutuma za unyanyasaji wa kimapenzi

miongoni mwa wafungwa wenzao. Hali hii imekuzwa na mazoea ya ukimya na ukosefu wa,

au upungufu wa, njia za ufuatiliaji na uwekaji kumbukumbu za shutuma hizo katika vizimba

vya magereza. Uwekaji wa kamera na vibonyezo hisishi kwenye vizimba kunaweza kusaidia

kufuatilia unyanyasaji na tabia za vurugu miongoni mwa wafungwa.

Hatua 3: Chemsha Bongo

Wapange washiriki wawili wawili kwa ajili ya chemsha bongo halafu waombe wajadili na

kuandika aina gani za unyanyasaji wa—kimwili, hisia na kimapenzi—ambao hutokea

katika magereza. Wape takiribani dakika 10.

Hatua 4: Maoni

Waombe washiriki kuchangia aina za unyanyasaji walizoziainisha.

Page 70: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

60

Hatua 5: Mapitio

Eleza maneno kwenye jedwali hapa chini:

NENO MAANA

Ukatili: Shirika la afya duniani (WHO) linaeleza ukatili kuwa ni “matumizi ya nguvu

za kimwili au madaraka kwa kukusudia, kutishwa au kwa uhalisia, dhidi ya

mtu mwenyewe, mtu mwingine, au dhidi ya kikundi au jumuiya ambayo

huenda yakasababisha au yakawa na uwezekano mkubwa sana wa

kusababisha majeraha, kifo, madhara ya kisaikolojia, maendeleo mabaya au

unyimaji” (Krug et al. 2002). maneno “Matumizi kwa kukusudia” ni ya

msingi mno ambayo yanatofautisha vurugu na madhara na majeraha ya

kutokukusudia.

Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani pamoja na kusimamia na kuwashawishi

watu wengine na matendo yao. Madaraka yanaweza kutumiwa kwa njia

chanya na hasi pia. Unyanyasaji unaweza kutokea iwapo madaraka

yatatumika kwa nia ya kudhulumu au kupata fadhila kutoka kwa mtu asiye

na nguvu kwa kubadilishana faida au ahadi. Ukosefu wa usawa wa

madaraka kati ya watu unaweza kufanywa kwa mabavu au kwa vitisho.

Miundo ya madaraka yaweza kuwa halisi au ya kutambua. Miundo ya

madaraka yaweza kuwa; kuwa na madaraka, uwezo wa kufanya maamuzi,

au umiliki wa chakula, pesa, au silaha.

Ridhaa: Maana yake ni kufanya uchaguzi sahihi wa kufanya jambo fulani kwa uhuru

na kwa hiari. Hakuna ridhaa pale ambapo makubaliano hufikiwa kwa njia

ya vitisho, nguvu, au njia nyingine za lazima, utekaji nyara, ulaghai,

udanganyifu, uwakilishi mbaya. Kutishia au kuzuilia au kuahidi kutoa

fadhila ili kupata ridhaa ya mtu ni matumizi mabaya ya madaraka. Matendo

yote ya ukatili na unyanyasaji wa kimapenzi hutokea bila ya ridhaa stahiki.

Hata kama mtu atasema ndiyo wakati wa moja ya matendo haya, si ridhaa

ikiwa alisema kwa kushinikizwa—yaani mkosaji alitumia nguvu fulani au

vishawishi ili kumshawishi mhanga kusema ndiyo.

Ukatili wa

kimwili:

Inamaanisha matumizi ya nguvu kwa kukusudia yenye nia ya kusababisha

kifo, ulemavu, majeraha, au madhara mengine. Matendo ya ukatili ni

pamoja na kukwaruza, kusukuma, kutupa, kukwida, kung’ata, kukaba,

kutikisa, kupiga kofi, kupiga ngumi, kuunguza, na matumizi ya silaha,

vizuizi, au ukubwa wa mwili wa mtu au nguvu dhidi ya mtu mwingine.

Ukatili wa

kimapenzi:

Inamaanisha matumizi ya nguvu kumlazimisha mtu kushiriki mapenzi

kinyume cha ridhaa yake, jaribio au kukamilisha kitendo bila ya ruhusa

yake au kuelewa, au mwingiliano wa ukatili wa kimapenzi. Vitendo vya

ukatili wa kimapenzi ni pamoja na, usumbufu wa kimapenzi, ubakaji, jaribio

Page 71: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

61

NENO MAANA

la ubakaji, ubakaji kwenye ndoa, unyonyaji, ukatili wa watoto

kimapenzi/uzinzi wa maharimu, vitendo vya kimapenzi (bila-kuingiliana

kimapenzi), ukahaba wa kulazimishwa, ukahaba kwa watoto, na biashara

za mapenzi. Unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili huambatana na tabia

hatarishi.Hatari ya ueneaji wa VVU huongezeka wakati wa ukatili wa

kimapenzi kwa kuwa nguvu nyingi hutumika, au kitendo cha kulazimisha

ambacho kinaweza kusababisha kuchanika kwa ngozi au ngozi

nyembamba na hivyo majimaji kuweza kupenya.

Hatua 6: Uliza

Waombe washiriki wataje baadhi ya njia za kuzungumzia ukatili wa kimapenzi kwa

ujumla.

Hatua 7: Tafakari

Jadili na washiriki kwa nini ni vigumu kuzungumzia ukatili kwenye mazingira ya magereza

na uandike kwenye karatasi ya kuandikia ubaoni au kwenye ubao wa chaki.

Mazoea ya kukaa kimya yaweza kuwa ni moja ya sababu zinazopelekea ugumu wa

kuzungumzia ukatili katika magereza.

Zoezi 2: Kuzungumzia ukatili wa kijinsia na kimwili: Kuvunja mazoea ya

ukimya

Dakika 45

Hatua 1: Eleza

Sema kwamba uongozi wa magereza nchini Tanzania umejipanga kuhakikisha uwepo wa

usalama kwa wafungwa. Ingawa, kama ilivyo kwenye magereza mengi ulimwenguni

(Dennehy na Nantel, 2006), Magereza ya Tanzania yanakumbana na changamoto nyingi za

uongozi mbaya, matumizi mabaya ya madaraka, na ukatili ambazo menejimenti ya magereza

inajaribu kuzishughulikia. Kama ilivyojadiliwa kwenye shughuli zilizotangulia, eleza kwamba,

wafungwa wanaweza kukumbana na ukatili wa kimapenzi, kimwili na namna nyinginezo za

ukatili ndani ya magereza kutoka kwenye mikono ya wafungwa wengine ama wafanyakazi wa

magereza wasio waaminifu.

Kwenye baadhi ya matukio wafungwa na wafanyakazi wanaamini ya kwamba kinachoendelea

nyuma ya ukuta wa gereza, hasa, ukatili wa kimapenzi, haupaswi kuwekwa wazi kwa umma.

Mitazamo kama hii hutambulika kama “Mazoea ya ukimya,” ambayo, isiposhughulikiwa,

inaweza kupelekea kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kimapenzi, kimwili, na ukatili

mwingine ndani ya magereza. Kutoshughulikia mazoea ya ukimya kunadumisha na

kuendeleza tabia za ukatili ambazo zinaongeza hatari ya kifua kikuu,, VVU, na magonjwa ya

Page 72: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

62

ngono, na hivyo kuwadhuru wafungwa na maofisa wa magereza (Dannehy na Nantel, 2006

uk. 177)

Hatua 2: Maswali na majibu—mazoea ya kukaa kimya

Swali: Mazoea ya kukaa kimya maana yake nini?”

Wape nafasi washiriki wakupe maoni yao wenyewe kabla hujawaelezea.

Jibu: ”Mazoea ya ukimya” (Martin 2002) maana yake ni hali ya wafungwa, wafanyakazi, au

uongozi kutokuwa tayari kuzungumzia kwa uwazi matukio ya uvunjifu wa sheria, ukiukaji wa

miiko, au yenye utata, kama vile ukatili wa kimapenzi. Mazoea ya ukimya yamejengwa katika

kanuni zisizozungumzika.

Wafungwa wengi hushabihia mazoea ya ukimya kwa sababu ya woga wa kulipiza kisasi na

kwamba wengine huenda wasiwalinde mara baada ya kuvunja ukimya. Wangeweza

kuhatarisha nidhamu kuliko kukiuka mazoea ya ukimya ndani ya gereza. Lakini ukimya huu si

sahihi kwani unawalinda wakosaji, hasa kwa kuwa lengo la magereza ni kuhakikisha usalama

na mazingira salama kwa watu kupitia usimamizi unaofaa na maofisa wanaowasimamia.

Uwepo wa tabia zinazokiuka maadili, matumizi mabaya ya madaraka, kufunika mambo

kunaweza kupelekea magereza kuwa mahali hatari kuishi na kufanya kazi kwa kuruhusu

makundi ya watu kutumia kanuni wanavyopenda wao pasipo kuwajibishwa. Jambo hili

hupelekea hasira, kuvunjika moyo, na mara nyingine huzuni na ugonjwa wa akili

Hatua 3: Eleza

Ili kushughulikia mazingira yasiyo salama yaliyosababishwa na ukatili wa kimapenzi na

namna nyingine za ukatili, mazoea ya ukimya yanapaswa kushughulikiwa kwa kuhakikisha

wafungwa wanaelewa tofauti kati ya kuaminiana, na kutii adhabu kwa ujumla. Kwa kutambua

kuwa, uaminifu ndani ya kikundi ni muhimu katika kuimarisha umoja, kukuza usalama, na

kujenga uaminifu, kutii dhamira za magereza za kuhakikisha usalama, ulinzi, na mazingira

wezeshi ni muhimu zaidi.

Hatua 4: Ufupisho

Fupisha kwa kusema kwamba ni muhimu kwa wafungwa kuvunja mazoea ya ukimya kwa

kuzungumzia ukatili gerezani, ikiwemo ukatili wa kimapenzi. Serikali ya Tanzania ina vyombo,

program na miradi kadhaa, ambayo inadhibiti unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili. Ikiwemo

“toleo maalumu la Sheria ya makosa ya kimapenzi ya mwaka1998 ambayo inaweka wazi aina

mbalimbali za makosa ya jinai yenye uhusiano wa ukatili wa kijinsi, ikiwemo ubakaji,

mashambulizi na maudhi kimapenzi, ukahaba, ukeketaji, na biashara ya mapenzi.

Hatua 5: Funga somo

Wape nakala (ikiwa zipo). Kama hakuna, soma nakala zifuatazo kwa washiriki:

Page 73: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

63

Toleo maalumu la Sheria ya makosa ya kimapenzi Tanzania (SOSPA)

Mnamo mwaka 1998 bunge la Tanzania lilipitisha Toleo Maalumu la Sheria ya Makosa ya

Kimapenzi (SOSPA)(Serikali ya Muungano wa Tanzania 1998) ili kulinda “heshima na uadilifu

wa wanawake na watoto,” iliyotambulisha makosa mapya kama vile maudhi kimapenzi,

unyanyasaji kimapenzi, na usafirishaji wa binadamu.

SOSPA Ni chombo kikuuu cha kitaifa kinachotoa idhini kupambana na ukatili wa kijinsi na

namna nyingine za unyanyasaji wa kimapenzi. Inatoa adhabu kali na haki ya kupata fidia kwa

wahanga wa ukatili.

SOSPA imerasimisha ubakaji kuwa ni kosa la jinai na inatoa adhabu kali kwa mbakaji.

SOSPA imeingizwa kwenye sheria za adhabu za Tanzania. Sheria za adhabu sura 16, Toleo

jipya, imeweka wazi yafuatayo:

Kifungu 130, sura 16, kinaeleza kuwa, ni kosa kwa mwanaume kumbaka msichana au

mwanamke. Mwanaume atakuwa ametenda kosa la ubakaji ikiwa atashirikiana mapenzi

na msichana au mwanamke ambaye si mke wake, au kuwa mkewe ambaye ameachana

naye; au bila ya ridhaa yake kufanya jambo hili wakati wa kufanya mapenzi; au kwa ridhaa

yake, pale ambapo ridhaa imepatikana kwa mabavu, vitisho, au kumweka katika hofu ya

kifo au majeraha

Mtu yeyote anayejaribu kubaka anatenda kosa la kujaribu kubaka na, isipokuwa kwa

mambo yaliyoainishwa kwenye kifungu kidogo cha 3, anastahili kifungo cha maisha

gerezani ikiwa kosa lake litathibitishwa, na kwa namna yoyote ile anastahili kifungo jela

kwa si chini ya miaka 30 pamoja na au bila ya adhabu ya viboko.

Mtu yeyote ambaye, anakusudia kusababisha maudhi kimapenzi kwa mtu yeyote kwa

kutamka neno lolote au sauti, kufanya ishara ya mwili, au kuonesha neno lolote au kitu

kwa nia kwamba neno hilo au sauti isikike, au ishara ya mwili au kitendo ionekane na mtu

mwingine, mtu huyu anatenda kosa la shambulizi kimapenzi. Ikithibitika, anastahili

adhabu ya kifungo gerezani kwa kipindi kisichozidi miaka mitano, faini isiyozidi shilingi

300, 000, au vyote viwili faini na kifungo.

Mtu yeyote ambaye, kwa kujifurahisha kimapenzi, anafanya kitendo chochote, kwa

kutumia sehemu zake za siri au kutumia vibaya sehemu nyingine yeyote ya mwili wa

binadamu au kitu chochote katika tundu lolote au sehemu ya mwili ya mtu mwingine

yeyote, iwe kitendo ambacho hakijumuishi ubakaji chini ya kifungu 130, ametenda kosa

kubwa la unyanyasaji wa kimapenzi.

Zoezi 3: Mazoezi ya jinsi ya kuvunja ukimya

Dakika 60

Vifaa vinavyohitajika

Ubao wa chaki au karatasi ya kuandikia ubaoni

Page 74: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

64

Maandalizi ya awali

Soma na elewa kipengele hiki.

Page 75: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

65

Hatua 1: Jadili

Fungua kwa kusema kwamba kwa namna nyingi gereza ni kama mji mdogo.

Katika mji huu wafungwa ndio raia. Na kama ilivyo katika mji wako na mji wangu, raia wa

gerezani wanapaswa kuwekwa mahali salama na pa uhakika. Hili hufanyika kwa kuwapa

makazi ambayo yanakidhi viwango vya afya ya jamii, huduma za afya kitabibu na kiakili

ambazo zinakidhi viwango vya kitaifa, vyakula ambavyo vina mahitaji ya msingi ya lishe, na

misaada mingine ili kusaidia urejeaji wenye mafanikio kwenye jamii zao.

Ingawa, kama ilivyo kwa miji midogo, magereza hayawezi kwa ufanisi huku kukiwa na

mazoea ya ukimya. Tunahitaji kuvunja mazoea ya ukimya kwa sababu inadidimiza lengo la

uwepo wa magereza: “Kutoa huduma rekebishi kwa kutengeneza maisha ya kirafiki na thabiti

na mazingira ya kazi kwa ajili ya wafungwa na wafanyakazi wasimamizi wa magereza.” (Smith

na Yarussi 2007)

Hatua 2: Eleza

Ukali wa aina yoyote ile, hasa ukatili wa kijinsia, ni aina kubwa zaidi ya ukiukwaji wa haki za

binadamu katika mazingira rekebishi. Ukatili wa kijinsia miongoni mwa wafungwa na au kati

ya wafanya kazi wa magereza pia ni jambo la kiusalama na ulinzi kwa:

Kuhatarisha usalama, ulinzi na afya za wafungwa na wafanya kazi

Kuongeza hatari ya kupata na kueneza VVU, magonjwa ya ngono, na maambukizi

yanayohusiana.

Kupunguza uaminifu na motisha miongoni mwa wafungwa na wafanyakazi gerezani.

Kupunguza heshima miongoni na baina ya wafungwa na wafanya kazi.

Kutishia usalama na ulinzi wa vituo vya magereza.

Kudhuru mahusiano ya kifamilia

Kujenga mtazamo hasi kwa umma juu ya magereza.

Kudumisha tabia za ukatili ndani na nje ya magereza.

Hatua 3: Maswali na majibu—wakati tunpovunja mazoea ya ukimya

Swali: Ni wakati gani tungeweza kusema mazoea ya ukimya yamevunjwa?

Chukua maoni machache

Jibu: ”Wafungwa huhakikishiwa usiri mara baada ya kuripoti matukio ya ukatili wa kimapenzi

kuwaepusha na maudhi au kisasi kutoka kwa wakosaji. Pasipo na kamera zinazotazama,

walalamikaji wanapaswa kuruhusiwa kuonesha ushahidi wa kimwili kuhusu kesi za

unyanyasaji wa kimwili na kimapenzi. Tekinolojia inaweza kusaidia kuvunja mazoea ya

ukimya kwa kuwa wafungwa na wafanyakazi wanajua kuwa kamera zinatazama matendo na

tabia zao.

Page 76: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU Magerezani

66

Hatua 4: Maelezo

Mfumo wa mawasiliano unaathiri sana namna ambavyo wafungwa wanavunja mazoea ya

ukimya. Kwa mfano wafungwa wa kiume na kike wanaweza kutofautiana tabia zao na mfumo

wa mawasiliano, hata kama hawajawahi kukumbana na ukatili katika mazingira ya magereza.

Ingawa, ni mhimu kwa wafungwa kujua kwamba endapowamewahi kunyanyaswa kimapenzi,

kushambuliwa, au kuudhiwa na wafungwa wenzao au wafanya kazi, wana haki ya kuripoti

kosa kwa usalama, kwa siri, na bila ya kutaja jina. Mfungwa anaweza kutoa taarifa zote au

kuminya kiwango cha taarifa anazozitoa kadri anavyoona yafaa. Ingawa, kadri taarifa nyingi

zinapotolewa, ndivyo itavyopelekea mfanyakazi wa magereza kuchukua hatua dhidi ya

mkosaji na kumweka mhanga na wafungwa wengine salama.

Hatua 5: Shauri

Mfungwa yeyote akikumbana na unyanyasaji wa kimapenzi, uonevu au kupigwa bila

sababu halali anatakiwa atoe taarifa kwa uongozi wa gereza mara moja.

Page 77: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

67

SOMO 5: KUISHI KWA MATUMAINI

UKIWA NA VVU NA KIFUA KIKUU

Lengo

Kuwajenga washiriki kiakili, kwa hisia, kiroho, na kimwili jinsi ya kukubaliana na kuishi na kifua

kikuu na VVU.

Dhamira za mafunzo

Mwisho wa somo hili washiriki wataweza:

Kusema umuhimu wa ufuasi mzuri na kuishi maisha yenye afya.

Kueleza madhara ya kifua kikuu na VVU, kimwili, kisaikolojia, kijamii, kitabia, na kiuchumi

miongoni mwa wafungwa na familia zao.

Kubainisha njia za kupunguza unyanyapaa, na ubaguzi dhidi ya watu wenye VVU.

Kueleza jinsi ya kuwasaidia watu waishio na VVU na magonjwa nyemelezi.

Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya kuwa na VVU

Dakika 60

Kipindi 5.1: Mazoezi

Utangulizi kuhusu kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na TB.

Kupunguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU

Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na TB

Dakika 30

Vifaa vinavyohitajika

Jadili maswali yaliyopo kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki

Vipeperushi vinavyoelezea kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU gerezani (ikiwezekana)

Maandalizi ya awali

Andika maswali ya kujadili (tazama hatua ya 3 chini) kwenye karatasi ya ubaoni au ubao

wa chaki

Hatua 1: Eleza

Kutambua ya kuwa una maambukizi ya VVU kutabadili maisha yako ghafla. Unaweza

kukumbana na wigo mpana wa hisia—wasiwasi, kupoteza, majonzi, huzuni, kukanwa, hasira,

Page 78: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

68

mashaka. Haijalishi ni kwa kiasi gani daktari na marafiki wanakuhakikishia, namna ambavyo

vidonge vina ufanisi mkubwa sasa na zitakavyokuwa hapo baadaye, udogo wa madhara

kimwili yatokanayo na kiwango kidogo cha maambukizi yaliyopo mwilini mwako kwa sasa,

au ni jinsi gani unapaswa kujiandaa kiakili na kimawazo, uhitaji wako wa msaada itakuwa

jambo bora. Maswala kisaikolijia yanayowakumba watu wengi wenye VVU hutofautiana.

Matumaini na matarajio ya maisha yako ya baadaye, mahusiano yako, na mwenendo wa

maisha yako yote yatahitaji mabadiliko fulani ili kukufanya uweze kukabiliana na hali ya kuwa

na VVU na kuishi maisha mazuri yenye afya.

Majadiliano haya yanalenga kujadili na kuibua mbinu na njia za namna ambavyo mtu

anaweza kukabiliana na hali ya kuthibitika kuwa na maambukizi ya Kifua Kikuuau VVU

gerezani mahali ambapo rasilimali zinaweza kuwa chache na kuna hatari ya ukatili,

unyanyapaa na ubaguzi.

Hatua 2: Jadili

Yapatie makundi ya watu wanne wanne maswali yafuatayo kwa ajili ya majadiliano:

Nini maana ya kuishi kwa matumaini ukiwa na Kifua Kikuu na VVU gerezani?

Mfungwa au mfanyakazi wa magereza anaweza kufanya nini ili kuishi kwa matumaini

akiwa na maambukizi?

Ni jinsi gani mafanyakazi wa magereza au mfungwa anaweza kumjali mtu aishie na VVU

gerezani?

Wafanye au wasifanye nini ili kuonesha kujali?

Hatua 3: Maelezo

Eleza kwa kifupi majibu kwa maswali haya pamoja na washiriki.

Gawa vipeperushi vifuatavyo (ikiwa vipo). Kama havipo, soma baadhi ya njia muhimu

kuonesha kuwajali watu wenye VVU magerezani.

Wafungwa waishio na VVU wanapaswa wajitahidi kuiweka miili yao kuwa na nguvu, kwa

kuhusisha yafuatayo:

Kula mlo uliokamilika au kuongeza kiwango, kila inapowezekana, ikiwemo vyakula vyenye

virutubisho ambavyo vina protini, vitamini, na wanga. Ukosefu wa virutubisho utachangia

sana kuharibiwa kwa mfumo wa kinga wa mwili. Mlo kamili huupatia mwili nguvu za

kuweza kupambana na magonjwa. Vyakula vya asili vinafaa zaini kuliko vile vya kwenye

makopo na vyakula vilivyosindikwa. Mboga mboga zina madini na vitamin mahususi kwa

ajili ya mwili kustawi .Chakula kinapaswa kusafishwa na kupikwa vizuri kabla ya kuliwa ili

kuulinda mwili kutokana na magonjwa yatokanayo na vyakula.

Kuwa mkakamavu kwa kufanya mazoezi na kupata muda wa kutosha kulala. Mazoezi ya

viungo yatapunguza msongo na uvunjikaji moyo na kuchangia kupata afya njema na

uvumilivu.

Kujiunga au kuunda vikundi saidizi na wafungwa wenzio ambao wana VVU

Page 79: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

69

Kuzungumza na wafungwa wengine kuhusu upimaji wa ugonjwa.

Kutafuta ushauri wa kidaktari pale mtu anapojisikia kuumwa, au kuwa na msongo, na

kufuata ushauri, ikiwemo kutafuta ushauri wa kidaktari, nasaha, na kijamii.

Ukiwa kwenye matumizi ya vidonge fuata maelekezo ya dawa uliyoandikiwa. Kuwa na

rafiki wa matibabu ambaye utakumbushana naye muda wa kunywa vidonge.

Usivute sigara na usitumie dawa bila ya maelekezo ya daktari.

Kuzungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako.

Kumwambia mtu fulani unayemwamini kwamba una VVU.

Njia za kuwahudumia watu waishio na VVU gerezani

Usijitenge na wafungwa wenzio au wafanyakazi wa magereza. Jenga urafiki. Ishi kama

ambavyo mmekuwa mkiishi kabla. Usibadilike kwa sababu tu unajua mtu fulani ana

maambukizi ya VVU.

Tambua hisia zao. Usiwafanye wafadhaike kutokana na hisia zao. Ni sawa kulia wanapolia

na kucheka wanapocheka. Ni jambo zuri kiafya kutoa hisia kuliko kuziweka moyoni.

Kuweka hisia mbaya moyoni husababisha msongo na msongo husababisha madhara

kwenye mfumo wa kinga.

Ikiwezekana waalike kwenye matembezi unapopata nafasi ya kufanya mazoezi. Kuwa

mwangalifu na nguvu za miili yao. Usiwaruhusu kufanya vitu ambavyo hawana nguvu za

kutosha kuvifanya.

Wasaidie kuweka mambo yao sawa. Watu wengi waishio na VVU hawapendi kufanya vitu

vigumu kama kuandika wosia au kuziambia familia zao kuhusu ugonjwa wao.

Washirikishe kwenye sikukuu za kidini au za asili au sherehe ikiwa inawezekana.

Jitolee kuwahudumia watu wenye VVU ili daktari wa magereza aweze kupumzika. Ikiwa ni

mfanya kazi wa magereza, wasaidie baadhi ya majukumu ili kurahisisha maisha.

Ni sawa kuzungumzia ugonjwa wao, lakini kuwa mwepesi wa kuhisi. Wafungwa wenzako

au wafanyakazi wa magereza wanaweza kuchagua siku ya kuzungumza. Itategemea na

namna ambavyo anajisikia siku hiyo.

Kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote, watu wenye VVU wana siku nzuri na mbaya.

Katika siku nzuri watendee kama ilivyo kawaida. Katika siku mbaya watendee kwa

kuwajali zaidi na huruma.

Kujali kunaweza kuoneshwa pasipo maneno. Huhitaji kuzungumza muda wote.

Wahimize kufanya maamuzi kwa muda mrefu iwezekanavyo kwa ajili yao. Mtu

anapoumwa, maamuzi mengi hutolewa kwao, hivyo basi waruhusu wafanye maamuzi

mengi iwezekanavyo.

Zingatia ahadi zako ikiwa utawaahidi watu waishio na VVU. Usiwaambie utawaona kesho

huku ukijua kuwa kesho hutaweza kuonana nao.

Kuwa tayari kuona watu waishio na VVU wakikasirika pasipo na sababu.

Hawajakukasirikia wewe. Wamekasirishwa na kile kinachoendelea kwao na kutokuwa na

uwezo wa kukishughulikia.

Usiwafanyie kile ambacho bado wana uwezo wa kukifanya.

Page 80: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

70

Jaribu kuwa na mtazamo chanya.

Kwa kujenga urafiki unaleta mwanga kwenye mazingira yenye giza nene.

Zoezi 2: Punguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU

Dakika 30

Vifaa vinavyohitajika

Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki

Maandalizi ya awali:

Andika maswali(tazama hatua 3 chini) kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki.

Hatua 1: Eleza

Uliza washiriki nini maana ya unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU.

Chukua maoni machache.

Hatua 2: Eleza

UNYANYAPAA UBAGUZI

Unyanyapaa maana yake ni tabia isiyopendeza au

isiyoya heshima ambayo mtu au kikundi kinakuwa

nayo ambayo hupelekea kushuka kwa hadhi ya

mtu au kikundi hicho katika macho ya jamii.

Unyanyapaa unaweza kuletwa na mwonekano

mwilini, kama vile, dalili za ugonjwa

zinazoonekana, au mtazamo hasi kwa kundi fulani

la watu au mtu

Ubaguzi unaweza kuelezewa kwa kujumuisha

mtazamo hasi au tabia fulani au vitendo. Mara

nyingi huelezewa kama ni utofauti unaojengwa

kuhusiana na mtu unaopelekea kutendewa bila

haki na bila kuthibitisha kwa misingi ya uhusika

wao, au kuchukuliwa kama wanahusika katika

kundi fulani. Kwa mfano unyanyapaa unaweza

kusababisha madhara na ubaguzi unaoelekezwa

kwa watu ambao kweli, au wanahisiwa tu kuwa na

VVU, na vikundi vya kijamii na watu wanaoishi

nao

Hatua 3: Zoezi

Wagawe washiriki kwenye makundi matano na wape kila kundi hadithi moja. Waeleze

washiriki kuwa watajadili maswali yafuatayo:

Kwa maoni yako, unadhani kwa nini katika hadithi hii watu wameonesha tabia hizo?

Unadhani nini kifanyike ili kupunguza unyanyapaa na ubaguzi?

Unadhani ni nani anaweza kuwasaidia watu wanaonyanyapaliwa au kubaguliwa?

Page 81: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

71

Hadithi 1

Siku moja afisa Mapendo aliporudi nyumbani kutoka

kwenye majukumu alikuta mke wake akilia. Baada ya

kumwuliza kwa nini analia, mkewe alisema ametoka

kliniki ya uzazi na ameambiwa kuwa ana VVU. Baada

ya kusikia haya, afisa Mapendo alighadhabika sana na

kuanza kumfokea mke wake, akisema kuwa amepata

maambukizi ya VVU kutoka kwa mwanaume

mwingine nje ya ndoa, na hivyo hastahili kuendelea

kuishi nae. Kwa hiyo, alimtolea vitu vyake ndani ya nyumba na kumfukuza nyumbani.

Hadithi 2

Jane ni muuguzi katika gereza mkoani mwanza.

Amefanya kazi pale kwa zaidi ya miaka 10. Anafanya

kazi kwa bidii anapotoa huduma kwa wagonjwa wake.

Mara zote anapogundua kuwa mgonjwa ana

maambukizi ya VVU, huhakikisha kuwa

anapomhudumia anavaa glavu na barakoa ili kuikinga

pua yake, hata kama mgonjwa hana vidonda

ambavyo vinaweza kusababisha maambukizi.Mara

nyingi mgonjwa anapogundua jambo hili huchukizwa.

Hadithi 3

Mariam ni mke wa mfungwa aliyefunguliwa gerezani

hivi karibuni. Ana shiriki katika vikundi vya ushirika

wa kukopa na kuweka katika mji wake. Anashirikiana

vizuri na wenzake kwenye shughuli zao za kila siku.

Miezi miwili iliyopita yeye na mmewe walikwenda

kliniki kupima VVU, na wote waligundulika kuwa na

maambukizi ya VVU. Tokea wakati huo wanachama

wenzake kwenye kikundi wamemtenga na

hawashirikiani naye tena kwenye shughuli zao za kikundi kwa kuhofia kuwa nao wangeweza

kuambukizwa VVU. Hali hii inamsikitisha Mariam na inatishia hali ya uchumi wa familia yake.

Hadithi 4

Salum ni mfungwa anayetumikia kifungo cha miaka mitano gerezani. Anaishi na VVU na

amekuwa akitumia vidonge vya ARV kwa miaka miwili. Kwa kipindi chote hicho amejitahidi

kuficha vidonge vyake ndani ya vitu vyake, lakini siku moja mfungwa mwenzake alivikuta na

alianza kumzungumzia na kufikia hatua ya kumtenga wakati wa chakula. Baada ya muda

Page 82: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu

72

Salum aligundua kuwa wenzake walikuwa wakijiweka kando na yeye, hivyo aliamua kueleza

hali halisi lakini waliendelea kumcheka na kumtenga.

Hadithi 5

Shida alifunguliwa kutoka gerezani. Alikuwa na furaha kubwa kurudi nyumbani kuungana

tena na familia, mke, na watoto wake. Alipokuwa gerezani Shida alipima VVU na aligundulika

kuwa navyo. Aliudhika sana kuhusu namna ambavyo atakwenda kumweleza mke wake kwa

kuwa hakutaka kuharibu siku yake ya furaha, hivyo aliendelea kuficha na usiku huo alifanya

mapenzi na mkewe bila ya kutumia kondomu.

Hatua 4: Eleza kwa kifupi

Toa fursa kwa kila kundi kujadili hadithi yao kwa kina.

Hatua 5: Jadili

Swali: Tunawezaje kupunguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU?

Jibu: Kuendeleza mbinu/njia zinazoshughulikia sababu kuu za unyanyapaa na makundi

maalumu ya waathirika, ikiwemo wafungwa. Zifuatazo ni baadhi ya njia tunazoweza kujaribu

na kupunguza unyanyapaa katika ngazi ya kisera na kijumuiya.

Kuzishirikisha jamii kuthibitisha kutoa msaada kwa watu waishio na VVU (kwa mfano.

biashara katika jamii, mashirika ya kijamii, mashule, na viongozi wa jumuiya).

Kukuza uongozi katika jamii kwa watu waishio na VVU.

Kukuza mbinu za kiafya kwa jamii kuhusu kinga na huduma ya Kifua Kikuu na VVU.

Kuendelea kutoa elimu kuhusu mambo yenye kuhusiana na Kifua Kikuu na VVU.

Page 83: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

73

ORODHA YA MANENO

CD4: Aina ya chembechembe –T ambazo huukinga mwili dhidi ya maambukizi na kuutunza

mfumo wa kinga. VVU hushambulia chembechembe za CD4 moja kwa moja, na kuhatarisha

mfumo wa kinga.

Daraja: Kikundi cha watu waliowekwa pamoja kulingana na viwango vyao vya mali na/au

kazi wanazofanya katika uchumi.

Dhuluma: Kujenga maoni thabiti mara nyingi maoni hasi kuhusu kitu fulani au mtu fulani

(kitengo cha kikundi cha watu) bila ya kuwa na elimu ya kutosha au uchunguzi wa mambo

kwa kina.

Haki za binadamu: Haki za binadamu ni za watu wote na hazitofautishwi. Kanuni ya

kiulimwengu ya haki za binadamu ndio msingi wa sheria za kimataifa za haki za binadamu

zilizotiliwa mkazo katika azimio la kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948, na

zimeelezewa katika mikutano, maazimio na maamuzi mbalimbali ya haki za binadamu za

kimataifa. Haki za binadamu zinarithiwa kwa wanadamu wote, bila kujali utaifa, makazi, jinsia,

taifa au asili ya kabila, dini, lugha, au hali nyingine.

Imani: Maoni thabiti na mara nyingi hutokana na misingi ya kidini na au kanuni za

kiutamaduni.

Jinsia: Kazi, haki, majukumu, fursa, mipaka, matarajio, stahili, na majukumu yanayotambuliwa

kijamii. Jinsi hutofautiana miongoni na ndani ya tamaduni na inaweza kubadilika baada ya

muda fulani.Majukumu ya jinsia huzingatia, jinsia, umri, kabila, dini, na sababu zingine za

kiutamaduni.

Jinsi: Sifa za kibaiolojia na kimaumbile za mwanaume na mwanamke ambazo hazibadiliki

bila ya kufanya upasuaji. Mfano wa viashiria vya jinsi: viungo: uume, uke, matiti, korodani;

maumbile: mzunguko wa hedhi, utengenezwaji wa shahawa; muundo wa kijenetiki:

kromosomu XX na XY.

Kujamiiana: Tabia zote za maisha ya watu kimapenzi, ikiwemo fikra, na hisia, shauku, tabia,

na sura.

Maambukizi yanayoenezwa kwa ngono: Kundi la maambukizi ambalo mara nyingi

huenezwa kwa njia ya mwingiliano wa mapenzi yasiyo salama na mtu mwenye maambukizi.

Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani pamoja na kusimamia na kuwashawishi watu

wengine na matendo yao. Madaraka yanaweza kutumiwa kwa njia chanya na hasi pia.

Makundi maalumu: Watu wanaotumia madawa, malaya, wasenge, watu wa jinsia mbili,

madereva wa masafa marefu, wachimbaji madini, wafungwa, na watoto wa mitaani ni

makundi maalumu. Makundi maalumu yana uwezo mdogo sana wa kupata huduma

zinazostahili, pia yana kiwango kikubwa cha hatari ya kupata na kueneza VVU, na viwango

Page 84: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

74

vikubwa vya kukumbwa na mauti na /au ugonjwa kwenye maeneo yenye magonjwa ya

mlipuko/kuambukiza ukilinganisha na makundi mengine katika jamii.

Mapenzi kinyume na maumbile: Mapenzi katika njia ya haja kubwa, bila kujali jinsi za

washiriki. Neno hili hutumiwa vibaya kwa kuchanganywa na ubakaji, ambayo hushindwa

kutofautisha mapenzi ya lazima bila ya ridhaa. Mapenzi kinyume na maumbile ni jinai pale tu

inapokuwa imelazimishwa.

Mapenzi salama: Hujulikana pia kama “mapenzi yenye kinga,” humaanisha kupunguza

hatari za maabmbukizi au mimba, mara nyingi kwa kufanya mapenzi kwa kutumia kondomu

ya kike au kiume au kwa kutafuta njia mbadala za ushirikiano wa mapenzi.

Mateso: Adhabu kali za kimwili au mateso kiakili yaliyofanywa chini ya mamlaka ya sheria.

Haijumuishi maumivu au mateso yanayotokana na, asili, au matukio ya vizuizi

kisheria.Ubakaji wa wafungwa umetambuliwa kama mfumo wa mateso na kitengo maalumu

cha umoja wa mataifa kinachoshughulikia mateso. Hii ni kesi bila kujali kitendo kimefanywa

na mfungwa au mfanyakazi wa magereza. Matendo mepesi ya unyanyasaji wa kijinsi

yanaweza kujumuisha, ukatili, unyama, au kuwatendea vibaya. Kamati ya umoja wa mataifa

inayoshughulikia mateso wakati wote imekuwa ikipambana na ukatili wa kijinsi dhidi ya

wafungwa na imetoa wito kwa serikali kuchukua hatua thabiti kushughulikia jambo hili.

Mila: Mfumo au mpangilio wa tabia unaokubalika na kuchukuliwa kuwa ni “jambo la

kawaida” katika jamii au ndani ya kikundi kwenye jamii.

Mitazamo: Maoni, mawazo na hisia za mtu kuhusu kitu au jambo fulani.

Sera: Mpango, au mfumo wa utendaji wa serikali, chama cha siasa, au biashara uliokusudiwa

kushawishi na kufikia maamuzi, matendo, na mambo mengine, kama vile sera za serikali

kwenye elimu, afya (ikiwemo VVU), au usawa wa jinsi, sera ya kampuni kuhusu ajira na

mafunzo au rasilimali watu/wafanyakazi.

Ridhaa: Mmakubaliano ya hiari bila ya matumizi ya nguvu. Hakuna ridha pale ambapo

mkosaji anatumia vibaya nafasi ya madaraka kumfanya mhanga “kukubali” kitendo cha

mapenzi. Hakuna ridhaa huru ikiwa kulihusisha, ulaghai, udanganyifu na ujanja. Sera zina

malengo ya jumla na malengo maalumu na taratibu zinazoweka mfumo au njia za utendaji

zilizochaguliwa miongoni mwa njia nyingine kwa kuzingatia mazingira fulani ili kutoa

mwongozo na kutambua maamuzi ya sasa na ya baadaye.

Sheria: Mifumo ya usimamizi, na mbinu za kurekebisha maovu zinaweza kutungwa na

chombo chenye mamlaka; sheria hujenga muundo wa siasa, uchumi na historia ya nchi kwa

ujumla kwa kufanya kazi kama msuluhishi wa mahusiano kati ya watu. Zinatungwa na

husimamiwa na katiba za nchi na zina mfumo au seti ya kanuni zilizotungwa na serikali za

miji, taifa, au nchi ambazo husimamiwa na taasisi za kijamii kuongoza mienendo. Sheria

zilizotungwa na serikali hutumika kutoa mwongozo wa namna ambavyo jamii zinapaswa

kuwa, kama vile, sheria zinazokataza kuendesha huku ukiwa umelewa, wizi, kuua, kutumia

madawa, au kumiliki bunduki.

Page 85: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

75

Ubaguzi: Huelezewa kuwa huenda ikajumuisha yote mawili mtazamo hasi au tabia fulani au

kitendo. Mara nyingi huelezewa kama tofauti inayotengenezwa kuhusu mtu inayosabaisha

mtu huyu kutendewa isivyofaa pasipo na haki kwa misingi ya uhusika wake ama kuhisiwa

kuhusika katika kundi fulani. Kwa mfano, unyanyapaa unaweza kusababisha madhara na

ubaguzi moja kwa moja kwa mtu ambaye kweli, au anahisiwa tu kuwa na maambukizi ya

VVU, na makundi katika jamii na watu wanaoshirikiana nao katika jamii.

Ubakaji: Kitendo chochote cha upenyezaji bila ya ridhaa kwenye uke, njia ya haja kubwa, au

mdomoni. Neno hili halibagui jinsi, wote mwanamke na mwanaume wanaweza kubakwa.

Uenevu: Kwa kawaida hutolewa kama asilimia, kama vile, uenevu wa VVU ni jamii yenye

maambukizi ya VVU katika kipindi fulani.

Ukatili: Shirika la afya duniani linaelezea ukatili kama ni “matumizi ya nguvu au madaraka

kwa makusudi, kutishia au kufanya kweli, dhidi ya mtu mwenyewe, mtu mwingine, au dhidi

ya kikundi au jamii ambapo kunaweza kupelekea uwezekano mkubwa wa majeraha, kifo,

madhara kisaikolojia, maendeleo mabaya, au unyimaji.” Neno” matumizi ya kukusudia” ni

kiungo muhimu ambacho kinatofautisha ukatili na majeraha au madhara ambayo

hayakukusudiwa.

Ukatili kimwili: Matumizi ya nguvu kwa kukusudia wenye nia ya kusababisha kifo, ulemavu,

mejeraha, au madhara mengine. Vitendo vya ukatili wa kimwili ni pamoja na kukwaruza,

kusukuma, kutupa, kukwida, kupiga, kukaba, kutikisa, kupiga kofi, kupiga ngumi, kuchoma,

na matumizi ya silaha, vizuizi, au kutumia ukubwa wa mwili wa mtu au nguvu dhidi ya

mwingine.

Ukatili wa kijinsia: Kudhuru kimwili, kimapenzi, au kisaikolojia kwa mwanaume au

mwanamke inayomlenga mtu kwa misingi ya jinsi yake. Ukosefu wa usawa wa kimamlaka

kati ya wanaume na wanawake unachangia kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia.Ukatili wa

kijinsia unalenga kudumisha ukosefu wa usawa wa kijinsia na/au kusisitiza wajibu wa kimila

wa jinsia kwa wanaume na wanawake.

Ukatili wa kimapenzi: Matumizi ya nguvu kumlazimisha mtu kushiriki tendo la kujamiiana

kinyume cha ridhaa yake, jaribio au kukamilisha kitendo bila ya ridhaa au uelewa wake, au

mwingiliano mbaya wa kimapenzi. Vitendo vya ukatili wa kimapenzi ni pamoja na usumbufu

kimapenzi, ubakaji, jaribio la ubakaji, ubakaji ndani ya ndoa, unyonyaji, unyanyasaji wa

watoto kimapenzi/ngono, vitendo vya mapenzi (bila upenyezaji) umalaya wa kulazimishwa,

umalaya kwa watoto, na biashara ya mapenzi.

Unyanyapaa: Mtazamo wa kijamii kuwa mtu au kikundi hakifai au ni cha hali ya chini.

Unyanyapaa unaweza kutokana na sifa za kimwili, kama vile, dalili za ugonjwa

zinazoonekana, au kutokana na mtazamo hasi unaoelekezwa kwenye kikundi fulani cha watu

au mtu.

Unyanyasaji: Matumizi ya kitu au kumtendea mtu isivyostahili, kwa kumdhuru, au kinyume

cha sheria.

Page 86: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

76

Unyanyasaji wa kijinsi: Aina yoyote ya mwingiliano wa kimapenzi isiyotakiwa kama vile,

kulazimisha busu, kulazimisha, ulawiti, umalaya, au upekuzi mbaya. Unyanyasaji wa kijinsia

huendekezwa na shauku ya kutumia mabavu, amri, na utawala-si mapenzi au tamaa. Mkosaji

anaweza kutumia nguvu au vitisho.

Usiri: Makubaliano au uwakilishi unaoweka wazi kwamba taarifa hazitatolewa. Kuwa na

uwezo wa kuzungumza kwa usiri ni muhimu kwa wahanga wengi wa unyanyasaji wa kijinsia,

na mara nyingi panakuwa hakuna usiri kwa waathirika.

Utamaduni: Imani, desturi, na mzoea ya jamii au kikundi ndani ya jamii (kama vile

utamaduni wa vijana) na tabia za jamii zilizopatwa.

Wakala wa mabadiliko: Tukio, shirika, vifaa, au, mara nyingi, mtu anayetenda kama

kichocheo cha mabadiliko.

Page 87: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

77

MIREJEO

AVERT. 2017. “HIV and AIDS in Tanzania.” http://www.avert.org/professionals/hiv-around-

world/sub-saharan-africa/tanzania.

Das, Pamela, and Richard Horton. 2016. “On Both Sides of the Prison Walls—Prisoners and

HIV.” The Lancet 388 (10049): 1032–33. doi:10.1016/S0140-6736(16)30892-3.

Dennehy, Kathleen M., and Kelly A. Nantel. 2006. “Improving Prison Safety: Breaking the

Code of Silence.” Washington University Journal of Law & Policy 22: 175–185.

http://openscholarship.wustl.edu/law_journal_law_policy/vol22/iss1/14.

International Organization for Migration (IOM). 2016. “Fighting Tuberculosis in Tanzania,”

April 15, 2016, Tanzania: Migration for the Benefit of All [website].

https://tanzania.iom.int/press-releases/fighting-tuberculosis-tanzania.

Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS). 2014a. The Gap Report.

http://www.unaids.org/sites/default/files/media_asset/UNAIDS_Gap_report_en.pdf

Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS). 2014b. On the Fast Track to End

AIDS: UNAIDS 2016–2021. Geneva, Switzerland: UNAIDS.

http://www.unaids.org/sites/default/files/media_asset/20151027_UNAIDS_PCB37_15_18_EN_rev1.

pdf.

Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS). 2016. Global AIDS Update 2016.

Geneva, Switzerland: UNAIDS. http://www.unaids.org/sites/default/files/media_asset/global-

AIDS-update-2016_en.pdf.

Krug, Etienne G., Linda L. Dahlberg, James A. Mercy, Anthony B. Zwi, and Rafael Lozano.

World Report on Violence and Health. Geneva, Switzerland: World Health Organization, 2002.

http://www.who.int/violence_injury_prevention/violence/world_report/en.

Martin, Keith L. “Cracking the Code of Silence.” Prisonerlife.com. July 6, 2002.

https://www.prearesourcecenter.org/sites/default/files/library/crackingthecodeofsilence7-6-

2002.pdf.

Mills Edward J., Nathan Ford, and Peter Mugyenyi. 2009. “Expanding HIV Care in Africa:

Making Men Matter.” The Lancet 374 (9686): 275–276. doi:10.1016/S0140-6736(09)61348-9.

Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights (OHCHR). 2005. Human

Rights and Prisons: A Compilation of International Human Rights Instruments Concerning the

Administration of Justice. Professional Training Series No. 11 Add.1.

https://www.un.org/ruleoflaw/files/training11Add1en.pdf.

Smith, Brenda V., and Jaime M. Yarussi. 2007. Breaking the Code of Silence: Correction

Officers' Handbook on Identifying and Addressing Sexual Misconduct. Washington, DC:

NIC/WCL Project on Addressing Prison Rape and National Institute of Corrections.

https://s3.amazonaws.com/static.nicic.gov/Library/022473.pdf.

Sonke Gender Justice Network and MenEngage. 2012. Addressing HIV and Sexual Violence in

Correctional Services Facilities: A Guide for Working with Members of the Correctional

Page 88: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

78

Department of Correctional Services. http://detentionjusticeforum.org.za/wp-

content/uploads/2013/09/Sonke-and-Just-Detention-International-Addressing-HIV-and-Sexual-

Violence-in-Correctional-Facilities-Guide-for-Correctional-Staff.pdf.

Sonke Gender Justice and MenEngage. 2017. “Men and HIV in the ESA Region.” Sonke

Gender Justice. Accessed January 25. http://www.genderjustice.org.za/publication/men-hiv-esa-

region/.

Page 89: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana

79

Page 90: Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na ... · Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU 5 Watu milioni 1.4 wanaishi naVVU Asilimia 4.7 ya watu wazima wana