24
ELIMU YA WATU WAZIMA Katika mada hii tunajifunza: 1. Maana ya Elimu ya Watu Wazima. 2. Sifa na mahitaji ya wanafunzi watu wazima. 3. Umuhimu wa EWW. 4. Mikakati ya utekelezaji wa EWW Tanzania. 5. Muundo wa uendeshaji wa EWW Tanzania. 6. KCM &KCK.

Elimu ya Watu Wazima(EWW)

  • Upload
    moevt

  • View
    15.703

  • Download
    98

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Bado kuna chaungamoto nyingi za Elimu ya Tanzania upande wa EWW bado idadi ya watu wazima wasiojua Kusoma Kuandika na Kuheasabu(KKK)

Citation preview

ELIMU YA WATU WAZIMA

• Katika mada hii tunajifunza:1. Maana ya Elimu ya Watu Wazima.

2. Sifa na mahitaji ya wanafunzi watu wazima.

3. Umuhimu wa EWW.

4. Mikakati ya utekelezaji wa EWW Tanzania.

5. Muundo wa uendeshaji wa EWW Tanzania.

6. KCM &KCK.

MAANA YA ELIMU YA WATU WAZIMA

• Ili kuelewa vizuri maana ya EWW inabidi kuelewa mambo yafuatayo:• Maana ya elimu• Mtu mzima ni nani?• Mwanafunzi mtu mzima ni nani?• Mapana ya elimu ya watu wazima.• Nani walengwa wa EWW.

MAANA YA ELIMU

• Ni tendo la kupata na kutumia misingi ya ujuzi, maarifa na muelekeo inayomuwezesha mtu kuishi ipasavyo katika jamii.

• Ni jumla ya mambo yote ya kuhusuyo ujuzi, stadi,maarifa na mwelekeo katika jamii.

• Elimu ni chombo cha ukombozi na ni chombo hutusaidia katika kutatua matatizo mbalimbali ili kuweza kupambambana na mazingira yetu vizuri.

MTU MZIMA NI NANI?

• Ni yule mwenye umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea kutokana na sifa zifuatazo:I. Kuweza kupiga kuraII. Kuoa/ kuolewaIII. Kugombea uongozi kuhukumiwa

kifungo cha ndani (magereza).

MWANAFUNZI MTU MZIMA NI NANI?

• Ni mtu anayejitambua, anaejitegemea na aliye na ujuzi na uzoefu mwingi wa mambo mbalimbali kutokana na kuishi kwake muda mrefu kwenye majukumu ya kifamilia na kijamii ambayo anayakubali na kuyakabili.

• Pia yuko tayari kujifunza kwa kwa bidii ili aweze kuyakabili vilivyo mazingira yake .

MAPANA YA ELIMU YA WATU WAZIMA

• EWW ni eneo pana sana ambalo ni pamoja ya kujifunza jambo lolote lenye shabaha ya kumwendeleza mwanadamu aweze kuyamudu mazingira yake.

• Mfano :• Elimu ya jadi,kisomo cha kujiendeleza,

masomo ya jioni, elimu kwa redio/ tv, masomo kwa njia ya posta n.k.

WALENGWA WA EWW

• Kwa ujumla ni watu wazima ambao hupata mafunzo ya elimu kwa mfumo usio wa kishule.

• Ki umri ni tangu anaestahili kuanza shule ya msingi na amevuka umri huo.

• Ki elimu ni tangu asiejua kusoma na kuandika hadi aliye na elimu ya juu (chuo kikuu).

• Kishughuri ni watuwote. Wakulima, wafanya biashara na wengineo.

MAANA YA EWW

• Kwa mtazamo wa kimataifa, EWW ni elimu yoyote inayotolewa kwa mtu aliye na umri wa miaka 18 na kuendelea.

• Nchini Tanzania maana hii inashindwa kuwa sahihi kutokana na utoaji wake, matakwa ya elimu hii katika jamii na mfumo mzima wa elimu wa nchi hii ambao ni 7:4:2:3+

Mwendelezo………..

• Hata hivyo maana ya EWW kwa kigezo cha umri ina utata kwani kuna wale wanaopitia mfumo wa eww wakiwa na umri chini ya miaka 18.

• Hivyo kushiriki katika darasa la EWW kunabadilika kutokana na mahitaji ya jamii.

• Mwanafalsafa J.K. Nyerere alitoa maana ya EWW kuwa ni “ Harakati za binadamu kujifunza kitu chochote kile ambacho kitamsaidia kuelewa mazingira anayoishi na jinsi atakavyoyakabiri.

Mwendelezo…………..

• Mawazo ya wataalamu wengine juu ya EWW.• Tunapozungumzia juu ya EWW tunaweza

tukamainisha aina yoyote ya mpango wa elimu wapatayo watu baada ya masomo yao ya shule.

• Tunaweza tukamaanisha aina ya Elimu itolewayo kwa watu waliokisha komaa tayari.

• (E.M. Hutchson-President Europian Bureau of Adul Education)

Mwendelezo……

• ….. EWW ni nguvu ambayo ikitumiwa vema huleta mabadiliko ya fikra katika jamii ya watu kwa muda mfupi iwezekanavyo.

• (Roy Prosser- Adult education Developing countries).

SIFA NA MAHITAJI YA MWANAFUNZI MTU MZIMA

1. Uzoefu wa mambo mbalimbali katika jamii kivitendo na kinadharia.

2. Kukomaa kwa akili.

3. Kukomaa kimaumbile.

4. Haiba nzuri na kujiheshimu.

5. Kuwa na busara na ushari mzuri kwa wengine.

6. Kuwa na majukumu mbalimbali ya kifamilia na ya kijamii.

Mwendelezo………

7.Kujitambua na kujiamini binafsi.

8. Uwezo wa kujiongoza mwenyewe na kujitegemea.

9. Kuheshimiwa na kutambuliwa na watu wengine.

10. Kutegemewa na familia, ndugu na jamaa zake pamoja na jamii nzima.

UMUHIMU WA EWW

• Humuwezesha mtu kutoka kwenye hali duni ya maisha ambayo watanzania wamekuwa wakiishi kwa karne nyingi zilizopita.

• Humwezesha mtu kujifunza jinsi ya kuinua hali ya maisha yake kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha mali zaidi, kuboresha afya yake na na kutengeneza thamani zake,kutengeneza zana zake na kufanya kazi mbalimbali.

Mwendelezo……..

• Kumfanya mtanzania aelewe sera ya chama tawala na ya vyama vingine vya siasa katika harakati za kuleta maendeleo ya watanzania.

• Kutoa elimu ya uongozi kwa viongozi wa Tanzania katika ngazi zote.

• Kufuta ujinga wa kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu.

• Husaidia kutoa ujuzi wa kazi mbalimbali na mwamko wa siasa; n.k.

Mwendelezo……..

• EWW husaidia kutoa ujuzi na maarifa ya aina mbalimbali kwa mfano kilimo, biashara, ufundi mbalimbali n.k.

• Kutoa elimu kwa shule za msingi na sekondari zenye mtaamo wa kumtayarisha mlengwa aweze kuishi vizuri vijijini na mjini kwa kuzingatia siasa na sheria za nchi yetu.

• Kusaidia kusawazisha pengo la elimu miongoni mwa watanzania.

Mwendelezo……..

• Husaidia kuanda wananchi kwa maendeleo yao na ya taifa lao kwa kukuza uchumi.

MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA EWW TANZANIA

• Tangu 1961 EWW imechukuliwa kuwa ni kati ya mambo ya kwanza kwa umuhimu katika maendeleo ya taifa letu.

• Mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka mitano (1964-1969) uliweka mkazo kwenye EWW.

• mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano(1969-1974) serikali ilichukua jukumu jipya ktk kuongoza na kutekeleza EWW.

Mwendelezo…….

• Kutangaza mwaka 1970 kuwa mwaka wa EWW kuliongeza nguvu zaidi.

• Tangu kipindi hiko hadi sasa kumekuwa na mikakati ifuatayo:

• Kuundwa kwa idara ya EWW.• Kuanzishwa kwa elimu ya wafanyakazi.• Kuanzisha kwa mabaraza ya wafanyakazi.• Kuteuliwa kwa wizara sita katika kampeni ya

kufuta ujinga.(Mafia, Ukerewe,kilimanjaro,Pare, masasi na dar es salaam).

Mwendelezo…….

• Kuanzishwa kwa kampeni mbalimbali nchini mfano:

• Mtu ni afya(1970).• Uchaguzi ni wako (1970).• Wakati wa furaha (1971).• Chakula ni uhai (1975).• Kufuta ujinga(1971-75). N.k.• Kuanzishwa kwa chama cha elimu ya watu

wazima Tanzania (CHEWATA).

Mwendelezo…….• Kuanzishwa kwa taasisi ya EWW (1975).• UPE kwa ajili ya kufuta ujinga.• Kuanzishwa kwa vyuo vya maendeleo ya wananchi 1975.• Mpango wa maendeleo wa 1964-1969 ulikuwa na lengo la

kuwaonesha Watanzania kuwa EWW ni haki ya kila mtu.• Agizo la WM(1973):Kuazishwa kwa Idara ya Wafanyakazi

– baada ya muda iliitwa Idara ya Elimu na ushirikishwaji wa Wafanyakazi 2.5.1974

• Kuanzishwa kwa vituo vya EWW katika kila mkoa.• Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT),n.k

MUUNDO WA UENDESHAJI WA EWW, TZ

Afisa Elimu Maarifa ya Nyumbani

Afisa Elimu Vielelezo EWW

Mwendelezo………

• Baada ya kutangazwa kuwa mwaka 1970 ni mwaka wa EWW nchini Tanzania;kulianza mipangilio mbalimbali ili kurahisisha utekelezaji