24
MWONGOZO KUHUSU MFUMO WA KODI NA UTARATIBU WA TOZO MBALIMBALI ZA MAZAO YA MISITU NCHINI TANZANIA CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU DISEMBA 2015

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

  • Upload
    others

  • View
    6

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 1

MWONGOZO KUHUSU MFUMO WA KODI NA UTARATIBU WA TOZO MBALIMBALI ZA

MAZAO YA MISITU NCHINI TANZANIA

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO

YA WADAU

DISEMBA 2015

Page 2: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya
Page 3: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 3

YALIYOMO

1.0 Utangulizi 4

Sehemu ya kwanza 5

Sheria mbalimbali za kodi za Mazao ya Misitu 5

1.0 Sheria ya Misitu No. 14 Mwaka 2002 5

1.1 Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 5

1.2 Sheria ya usajili wa Makampuni ya Mwaka 2002 5

1.3 Sheria ya Ushuru wa Forodha Afrika Mashariki 2002 6

1.4 Sheria ya Wakala wa Serikali ya Mwaka 1997 9

1.5 Mwongozo wa Uvunaji endelevu wa Mwaka 2007 10

1.6 Sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 10

Sehemu ya Pili 11

Kodi na tozo mbalimbali zitolewazo katika biashara ya mazao ya Misitu 11

Sehemu ya Tatu 14

Changamoto mbalimbali katika usimamizi wa tozo na kodi mbalimbali za mazao ya misitu nchini 14

Sehemu ya Nne 19

Mapendekezo katika mfumo wa kodi na tozo za mazao ya misitu nchini Tanzania 19

Hitimisho 21

Page 4: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

1.0 UTANGULIZI Tanzania ilijipatia uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo tarehe 9 mwezi Desemba Mwaka 1961. Mara baada ya uhuru, sheria na mifumo mbalimbali ya umiliki wa maliasili iliyokuwepo wakati wa ukoloni iliendelea kutumika. Pamoja na mabadiliko mbalimbali kufanywa katika sera na sheria, moja ya changamoto kubwa inaendelea kuikabili sekta ya maliasili ni usimamizi mbovu wa rasilimali kama vile, Madini, Misitu, Gesi, Mafuta na rasilimali nyingine.

Baada ya uhuru, Serikali iliweka njia mbalimbali za kusimamia uendeshaji wa rasilimali hizo na njia mojawapo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na taasisi mbalimbali zenye jukumu la kusimamia rasilimali hizo, mfano taasisi za kukusanya kodi, ushuru au tozo kutoka rasilimali mbalimbali nchini.

Kodi ni nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya taifa lolote duniani, imekuwa njia inayotumiwa na Tanzania katika kukusanya mapato kutoka vyanzo mbalimbali. Ili kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na mfumo mzuri wa kodi, sera huwekwa na Serikali za nchi husika na pia sheria mbalimbali hutungwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inajikusanya mapato ili kuboresha utoaji wa huduma muhimu za kijamii kwa wananchi wake. Nchini Tanzania kodi hutozwa katika njia mbalimbali, zipo kodi ambazo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 lakini pia zipo tozo zinazowekwa na sheria mbalimbali za kisekta.

Lakini ni vyema ikakumbukwa kuwa Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 sio sheria pekee inayohusiana na mambo ya kodi. Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki 2002, pia imekuwa ikitumika katika kutoza ushuru kwa usafirishaji wa mazao ya misitu nje ya nchi. Vilevile, Halmashauri mbalimbali za Wilaya nchini Tanzania pia hutoza kodi kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato katika wilaya husika.

Lengo kubwa la mwongozo huu ni kuchambua mfumo wa kodi na ongezeko la ukwepaji wa kodi katika biashara ya mazao ya misitu nchini. Mwongozo huu unachambua na kuziweka wazi sheria, kanuni na miongozo ya kodi na tozo mbalimbali za mazao ya Misitu. Vilevile unaainisha changamoto zinazowakabili wafanyabiashara, wadau na watendaji mbalimbali wa Serikali katika utekelezaji wa sheria husika.

Mwongozo huu ni matokeo ya kubaini mapungufu mbalimbali yaliyopo katika mfumo wa kodi na utaratibu wa tozo za mazao ya misitu nchini yaliyobainika kupitia Chama cha Wanasheria Watatezi wa Mazingira (LEAT) chini ya mradi wa Kampeni ya Mama Misitu unaofadhiliwa na Serikali ya Ufini.

4 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Page 5: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 5

SEHEMU YA KWANZA

1.0 SHERIA MBALIMBALI ZA KODI ZA MAZAO YA MISITU NCHINI TANZANIA

Mnamo Mwaka 1998 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliitangaza Sera ya Misitu Nchini, baadhi ya malengo makuu ya sera hiyo ni kuhakikisha kuwa madaraka ya usimamizi wa misitu yanapelekwa katika ngazi ya chini kabisa yaani kwa wananchi wenyewe. Vilevile, sera hii imejikita katika kuhakikisha kuwa misitu inatunzwa na kulindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

1.1 Sheria ya Misitu namba 14 ya Mwaka 2002 na Kanuni zake za Mwaka 2004 Kupitia tangazo la Serikali na.153 la Mwaka 2004:

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria hii kwa kuzingatia sera ya Taifa ya Misitu ya Mwaka 1998. Sheria hii kwa sehemu kubwa inaweka wajibu kwa mtu yeyote anayejihusisha na biashara ya mazao ya misitu kuhakikisha analipa kodi husika na kwa wakati. Kukiuka sheria hii ni kosa la jinai na pindi mtu anapobainika kutenda kosa chini ya sheria hii hatua mbalimbali za kisheria huchukuliwa mara moja dhidi yake.

Sehemu ya sita ya sheria hii yaani vifungu vya 49- 57 vinahusiana na vibali na leseni mbalimbali ambazo mfanyabiashara wa mazao ya misitu anapaswa kuwa nazo. Kwa namna moja au nyingine vifungu hivi vya sheria vina uhusiano wa moja kwa moja na kodi au tozo mbalimbali za mazao ya misitu.

Sehemu ya saba ya Sheria ya Misitu ya Mwaka 2002 inaelekeza utaratibu wa kusafirisha mazao ya Misitu. Kifungu cha 58 kinaelekeza kuwa ni marufuku kusafirisha mazao ya misitu nje ya nchi bila kuwa na kibali au leseni ya kusafirisha mazao husika. Ikumbukwe kuwa vifungu hivi vya sheria vinalenga kuhakikisha kuwa aina yoyote ya biashara ya mazao ya misitu nchini lazima iendeshwe kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa wa kodi na tozo husika.

1.2 Sheria ya kodi ya mapato ya Mwaka 2004, hii ni Sheria nyingine ambayo inaweka wajibu kwa mwananchi yoyote kulipa kodi ya mapato ambayo anayapata. Sheria hii pamoja na mambo mengine inaainisha maeneo matatu ambayo kodi hutozwa. Sheria hii inaelekeza kuwa kodi ya mapato itatozwa katika maeneo makuu matatu ambayo ni ajira, biashara na uwekezaji. Kwa kuhakikisha kuwa kila mtanzania anayejihusisha na biashara analipa kodi, kifungu cha 8 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya

Page 6: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

Mwaka 2004 kinamtaka kila mfanyabiashara kulipa kodi ya mapato. Hivyo ni vyema kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu kukumbuka kuwa ni wajibu wao kulipa kodi ya mapato kwa sababu biashara ya mazao ya misitu ni sawa na biashara nyingine yoyote.

Kutokana na ukweli huu, sheria hii ya kodi inamtaka kila mfanyabiashara wa mazao ya misitu kuhakikisha kuwa amesajiliwa na kutambuliwa na ahakikishe amepatiwa namba ya usajili ya mlipa kodi, (Taxpayer Identification Number) kama sharti la msingi ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kulizingatia. Mamlaka ya Mapato ya Tanzania ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa namba za utambulisho kwa mlipa kodi na hivyo kwa kuzingatia utaratibu huu ni kosa kwa mujibu wa sheria hii kufanya biashara yoyote ya mazao ya misitu bila kuwa na vibali maalumu au kutambulika kisheria kama mfanyabiashara halali wa mazao ya misitu nchini. Vilevile Sheria hii pia inayotoa misamaha mbalimbali ya kodi katika aina mbalimbali za biashara na mapato ya aina mbalimbali.

1.3 Mwongozo wa Uvunaji Endelevu wa Mazao ya Misitu wa Mwaka 2007Mwongozo huu unaelekeza namna ya upatikanaji wa leseni za uvunaji. Kipengere cha 3.3 cha mwongozo huu katika vipengere vidogo vya (a-c) vinaainisha aina tatu za leseni ambazo ni leseni za kusafirisha mazao nje ya nchi ambayo hutolewa na Makao Makuu Idara ya Misitu na Nyuki (kwa sasa jukumu hili lipo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania), leseni za uvunaji wa mazao ya misitu ambazo kwa mujibu wa mwongozo huu hutolewa na maafisa misitu katika Halmashauri za wilaya (Pia Halmashauri za Vijiji kwa sasa). Aina nyingine ya leseni inayotajwa na mwongozo huu ni Leseni za

6 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Page 7: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 7

uvunaji katika mashamba ya miti ya serikali ambazo hutolewa na meneja wa shamba husika. Ni vyema ikakumbukwa kuwa mbali na matakwa ya mwongozo huu, utaratibu huu wa kutoa leseni unalenga kuhakikisha kuwa kodi za mapato zinatolewa na kwamba kunakuwa na uvunaji endelevu wa mazao ya misitu. Wajibu huu upo kisheria na hivyo ni vyema mfanyabiashara wa mazao ya Misitu akauzingatia. Sheria inaweka utaratibu wa kuzingatia wakati wa kufanya biashara ya mazao ya misitu ndani ya nchi. Masharti ambayo yanapaswa kuzingatiwa na mfanyabiashara wa mazao ya misitu ndani ya nchi ni pampoja na:

a. Hati ya usajili wa kufanya biashara ya mazao ya misitu

b. Leseni ya biashara ya mazao ya Misitu kutoka wilaya husika

c. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Tax Payer Identification Number (TIN)

d. Wafanyabiashara binafsi wanapaswa kuwa na uthibitisho wa taarifa ya hesabu za fedha kwa ajili ya biashara hiyo ambayo imekaguliwa na kugongwa mhuri na mkaguzi wa mahesabu (Financial Audited Returns) za miaka iliyopita.

e. Stakabadhi halali za Serikali kwa malipo yaliyofanywa

Page 8: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

Sheria ya Misitu namba 14 ya Mwaka 2002 pia inaainisha waziwazi kuwa ni marufuku kufanya biashara ya mazao ya misitu nje ya nchi bila kuwa na vibali maalumu vya biashara husika. Kutokana na kifungu hiki masharti ya jumla yanayohusiana na kufanya biashara ya mazao ya Misitu nje yameianishwa ambapo mfanyabiashara anapaswa kuhakikisha yafuatayo:

a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number)

b. Hati ya usajili wa kampuni kutoka kwa Msajili wa Makampuni

c. Hati ya leseni ya biashara ya nje kutoka Wizara Viwanda na Biashara

d. Mkataba wa mauzo kutoka kwa mnunuzi utakaonyesha bei za mazao hayo kwa thamani ya dola za kimarekani au fedha zinazokubalika kimataifa, ujazo, uzito au idadi ya mazao

e. Hati ya usajili ya kufanya biashara ya mazao ya Misitu kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu

f. Hati ya usajili ya kusafirisha mazao ya misitu nje ya nchi kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu

g. Hati ya madaraja ya ubora wa mazao husika kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu

h. Uthibitisho wa kumiliki kiwanda cha misitu au mkataba kutoka kwa mwenye kiwanda kuwa mazao yatakayosafirishwa yatazalishwa katika kiwanda chake

i. Barua ya uthibitisho ya kuruhusiwa kusafirisha mazao ya misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu

j. Kibali (kama kinahitajika)kwa ajili ya kuruhusiwa kusafirisha mazao ambayo yameorodheshwa katika mkataba wa kimataifa wa kuzuia biashara ya mazao ya Misitu au mimea ambayo ipo hatarini kutoweka duniani (CITES). Kibali kinatolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

k. Hati ya ukaguzi wa ubora wa mazao ya misitu kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula (Phytosanitary Certificate)

l. Stakabadhi halali za Serikali kwa malipo yote yaliyofanyika

Masharti haya yana uhusiano wa moja kwa moja na kodi ambazo mfanyabiashara anapaswa kuzilipa. Masharti yaliyoainishwa hapo juu yanalenga kuhakikisha kuwa mfanyabiashara analipia kodi, ushuru au tozo mbalimbali zilizowekwa kisheria kama sharti la msingi la biashara halali ya mazao ya Misitu.

8 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Page 9: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 9

Vilevile ni vyema ikakumbukwa kuwa viwango vya kodi hutolewa kulingana na ukubwa na kipato cha kila mfanyabiasha husika kwa kuwa hakuna kiwango kimoja katika utoaji wa kodi. Hata hivyo viwango vilivyopo kisheria pia vinategemea kipato na ukubwa kwa biashara husika.

1.4 Sheria ya makampuni ya Mwaka 2002 inamtaka mfanyabiashara wa mazao ya Misitu anayetaka kufungua kampuni kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inafunguliwa na kusajiliwa kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kisheria. Usajili wa kampuni ni kielelezo cha uhalali wa uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kampuni. Hivyo pamoja na kuisajili kampuni, Mfanyabiashara wa mazao ya Misitu anapaswa kuonyesha nyaraka zote zinazohusiana na kodi na tozo mbalimbali ambazo anapaswa kuzifanya ili kuifanya biashara iwe halali.

Page 10: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

1.5 Sheria ya Usajili wa Makampuni: Hii ni Sheria ambayo inahusiana na utaratibu mzuri wa kutunza kumbukumbu za wafanyabiashara hasa kwa kutambua majina ya makampuni mbalimbali yanayoanzishwa nchini. Kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za majina na taarifa nyingine muhimu za makampuni ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na uthibiti wa uanzishwaji holela wa makampuni jambo ambalo linaweza kutoa mwanya kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu kukwepa kodi.

1.6 Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2002, hii ni Sheria inayohusiana na usafirishaji au uingizaji wa bidhaa mbalimbali nchini. Ni Sheria hii ambayo imekuwa ikitumiwa na Mamlaka ya Mapato Nchini kuhakikisha kodi zote stahiki na ushuru vimelipwa kabla ya kusafirisha au kuingiza bidhaa mbalimbali nchini ikiwemo mazao ya misitu.

1.7 Sheria inayoanzisha Wakala wa Serikali ya Mwaka 1997, hii ndio sheria iliyoanzisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS). Mamlaka ya ukusanyaji mapato, ushuru au tozo mbalimbali zinazotozwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni kutokana na Sheria hii. TFS imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli za usimamzi wa mazao ya misitu na nyuki katika Misitu yote ya Serikali na Misitu yote iliyopo katika ardhi ya kawaida (General Lands)

1.8 Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Na. 9 ya Mwaka 1982, Sheria hii inazipa mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka ushuru au tozo kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato kwenye mamlaka zake. Vifungu vya 13 na 14 vya Sheria hii vinazipa mamlaka za Serikali za mitaa kuweka kodi, tozo au ushuru kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya Halmashauri na pia viwango vinavyopaswa kulipwa. Moja ya bidhaa ambazo mamlaka hizi zinaweza kutoza kodi ni pamoja na mazao ya Misitu ikiwemo mbao. Ili kuweza kufikia azma hii mamlaka hizi zinaruhusiwa kisheria kupitia Sheria ndogo kuweka tozo hizo kuzitangaza kwa wananchi na kisha kuzitumia kama njia ya kukusanya mapato ndani ya halmashauri husika kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.

1.9 Sheria ya Uwekezaji ya Tanzania ya Mwaka 1997, hii ni Sheria inayosimamia uwekezaji nchini. Sheria hii inaanzisha Kituo cha Uwekekezaji nchini yaani (Tanzania Investment Centre) au kwa kifupi (TIC). Kwa mujibu wa sheria hii zipo motisha mbalimbali ambazo mwekezaji anaweza kuzipata kwa uwekezaji unaofanywa na mwekezaji wa nje au wa ndani. Moja ya sharti kubwa na la msingi ambalo ni mhimu kulielewa ni kwamba ili mwekezaji wa ndani aweze kupewa cheti cha motisha kinachotolewa na TIC inabidi angalau kima cha chini cha uwekezaji kiwe dola za kimarekani laki moja (100,000).

10 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Page 11: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 11

SEHEMU YA PILI

3.0 KODI NA TOZO MBALIMBALI ZITOLEWAZO KATIKA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU

Pamoja na kodi mbalimbali ambazo hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Misitu Namba 14 ya Mwaka 2002, zipo tozo mbalimbali ambazo hutozwa na vyombo vingine mfano Wakala wa Huduma za Misitu, Halmashauri za Wilaya na Vijiji ambavyo misitu husika hupatikana.

Kwa mfano kwa mwongozo uliotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu (Tanzania Forest Service) unaelekeza kuwa (mtu yeyote haruhusiwi kusafirisha mazao ya misitu kwa njia ya barabara na maji kati ya saa 12:00 jioni na saa 12:00 asubuhi na kwamba mtu akivunja kanuni hizo atafikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kupata adhabu ya kifungo kisichozidi miaka miwili au faini kati ya sh 30,000 na sh 1,000,000 au vyote viwili kwa pamoja”

Page 12: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

12 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Mwongozo wa uvunaji wa mazao ya Misitu wa Mwaka 2007 unamtaka mfanyabiashara wa mazao ya Misitu kulipa tozo mbalimbali zilizoanishwa kwenye mwongozo huu ni pamoja na:

a. Asilimia tano (5%) ya ushuru utakaoingia kwenye Mfuko Maalumu wa Misitu ambao fedha zake zitatumika

b. Maombi ya uvunaji

c. Leseni ya Biashara

d. Usajili wa unakovuna

e. Usajili wa sokoni

f. Ushuru wa mti unaovuna kwa mita za ujazo.

g. Ushuru wa mkaa kwa gunia kwa mfano ushuru huu unamtaka mtu yeyote anayejihusisha na usafirishaji wa mkaa kufanya hivyo kwa kupitia njia zilizoruhusiwa na afisa misitu, na pia mtu huyo atatakiwa alipe ushuru wa serikali kwa kila mfuko wa kilogramu (1kg) kwa sh 240 au kg 75 kwa sh 16,600 na mtu yeyote atakayesafirisha mkaa bila kutimiza masharti yaliyotajwa atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria.

Page 13: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 13

Kwa mujibu wa mwongozo wa uvunaji wa mwaka 2007 hairuhusiwi kusafirisha mkaa isipokuwa kwa mwenye leseni au kibali maalumu kutoka kwa Afisa Misitu wa wilaya au wakala, awe na hati ya kusafirisha mkaa na iwe imegongwa muhuri kila kituo cha ukaguzi wa mazao ya Misitu husika.

h. Tozo za mzabuni kwenye mageti

i. Tozo za viringo au mbao

j. Tozo kwa ajili ya usafirishaji ( Transit Pass)

k. Tozo kwa ajili ya kuni za miti pori kwa mita za ujazo

l. Malipo ya upandaji miti kwa kila gunia la mkaa

m. Tozo kwa biashara za mashine za kuranda mbao

Tozo hizi hutozwa na mamlaka mbalimbali zikiwemo Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Halmashauri za Wilaya kupitia Maafisa Misitu wake, Mamlaka za Vijiji na vyombo vingine vilivyowekwa kisheria. Tozo hizo zipo kwa mujibu wa Sheria na kanuni mbalimbali chini ya Sheria ya Misitu Namba 14 ya Mwaka 2002

Page 14: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

14 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

SEHEMU YA TATU

4.0 CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA USIMAMIZI WA TOZO NA KODI MBALIMBALI ZA MAZAO YA MISITU

Pamoja na Kuwepo Kwa Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayoelekeza kuhusu mfumo wa utozaji wa kodi na tozo mbalimbali kwa mazao ya Misitu husika, bado zipo kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa katika uendeshaji wa biashara ya mazao ya Misitu na usimamizi wake nchini. Changamoto hizi zinaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili ambazo ni tatizo la mfumo mzima wa usimamizi wa biashara ya mazao ya misitu na tatizo la uwepo wa kodi na tozo nyingi kwa wafanyabiashra. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na zifuatazo:

I. Uwepo kwa kodi na tozo nyingi ambazo zimekuwa mzigo kwa wafanyabiashara: Kwa mujibu wa mwongozo wa uvunaji endelevu wa mazao ya Misitu nchini wa Mwaka 2014, unamtaka mfanyabiashara wa mazao ya Misitu anapaswa kulipa tozo ya kusafirisha mazao ya Misitu yaani Transit Pass (TP) anaposafirisha mazao yake toka wilaya moja kwenda nyingine au nje ya mkoa.

Page 15: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

Utozaji huu humlazimu mfanyabiashara kulipa kodi mara mbili kwa mzigo uleule yaani anaposafirisha ndani ya mkoa na pale anapotaka kusafirisha nje ya mkoa. Hii ni changamoto nyingine kubwa kimfumo katika Usimamizi wa mfumo wa kodi na tozo mbalimbali katika mazao ya misitu nchini.

II. Uwepo wa tozo au ushuru tofauti kwa zao au hitaji moja linalofanana kwa wafanyabiashara wa Misitu kutoka eneo moja kwenda jingine.

Tatizo hili limesababisha uwepo wa tofauti katika utozaji wa kodi hizo na hivyo kuwafanya wafanyabiashara wengi kukwepa tozo hizo. Jedwali hili hapa chini linaonyesha baadhi ya tozo na jinsi zinavyotoutiana kutoka wilaya moja hadi nyingine.

Jedwali kuonyesha ulinganifu wa ushuru katika Mazao ya Mistu

AINA YA TOZO ANAYE-CHUKUA RUFIJI MKINGA MUHEZA

1.Maombi ya Uvunaji Kijijini Kijiji 100,000 100,000 50,000– 100,000

2. Leseni ya Biashara Halmashauri 100,000 200,000 101,000

3. Usajili unakovuna TFS usajili256,000fomu 50,000 265,000 306,000

4. Usajili wa sokoni TFS Usajili256,000Fomu 50,000 265,000 306,000

5. Kodi ya Mapato TRA 762,000 >100,000 318,000

6. Ushuru wa gogo Kijiji 2500 35,000 >20,000

7. Ushuru wa gunia la mkaa Serikali kuu 16,600 13,0008. ushuru wa mkaa kwa lori (kila kijiji na kiwango chake) kijiji Gunia 1000 20,000

– 50,000

8. Ushuru wa mzabuni kwenye mageti

Mzabuni wa Halmashauri ya Wilaya

1200 1000-1500 500

9. Ushuru wa kupanda miti toka kila unapata TP Halmashauri Mkaa 830 -

Mbao5,000Kuni 2000Mkaa 2000

10. Viringo/ Mbao Halmashauri 1000 1000 5,000

11. TP kwa kila gari TFS 6500 7500 15,000

12. Kuni za miti pori kwa mita ya ujazo TFS 5900 5900 5900

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 15

Page 16: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

16 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Ripoti za kitafiti kupitia Mradi wa Mama Misitu, 2014.Kutoka kwenye jedwali hapo juu ni dhahili kuwa mfumo wa utozaji wa tozo unakabiliwa na matatizo mengi kw sababu kati ya tozo zilizooainishwa hapo juu, kuna tozo nyingi ambazo mlipaji hapewi stakabadhi au risiti kwa malipo aliyoyafanya.

III. Changamoto nyingine ni kuwepo kwa vyombo mbalimbali vyenye mamlaka ya kutoza kodi au tozo mbalimbali za mazao ya Misitu: Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wataalamu wa LEAT kupitia mradi wa MAMA MISITU, ilibainika kuwa vipo vyombo mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitoza kodi au tozo au ushuru wa mazao ya Misitu. Wingi huu wa vyombo au mamlaka umesababisha mwingiliano wa majukumu na pia kuwafanya wadau au wafanyabiashara wa mazao ya misitu kutojua mahali sahihi pa kufanya malipo husika na nani hasa mwenye mamlaka ya kupokea malipo hayo.

Page 17: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 17

Katika utekelezaji wa mradi wa Mama Misitu, LEAT ilibaini kuwa vyombo au mamlaka zifuatazo zimekuwa zikitoza kodi au tozo mbalimbali za mazao ya Misitu.

• Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

• Wakala wa Misitu (TFS)

• Halmashauri za Wilaya

• Police (wanapokamata watu na mazao ya Misitu)

• Taasisi ya kudhibiti na kupambana na Rushwa (PCCB)

Page 18: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

18 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

• Halmashauri za Vijiji

• Kamati zinazopitisha maombi ya uvunaji.

• Vituo vya ukaguzi wa maliasili

Uwepo wa taasisi nyingi za ukusanyaji wa kodi na tozo katika biashara ya mazao ya misitu umesababisha zoezi la kukusanya kodi kuwa gumu na hivyo kusababisha baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kodi hasa kwa kukosekana stakabadhi sahihi kwa malipo halali ya Serikali.

IV. Tatizo lingine ni kuwepo kwa mirahaba midogo na usimamizi hafifu wa leseni: kutokana na mfumo mbovu wa utaoaji wa leseni na kuwepo kwa mirahaba midogo ya kodi. Inaweza kukumbukwa wazi kuwa mfumo wa sasa wa kodi umejenga kodi na tozo nyingi kwa wafanyabiashara wa mazao ya Misitu na hivyo kufanya mapato mengi kupotelea kwenye mikono ya watu wachache ambao malipo yanayofanywa huko imekuwa vigumu kuthibitisha uhalali wake.

V. Changamoto nyingine ni kuwepo kwa mfumo unaobadilikabadilika kila wakati wa utozaji wa mrahaba katika mazao ya Misitu: kwa mfano kutoka mwaka 1972 mpaka 2004, mrahaba katika mazao ya misitu umebadilishwa karibu mara kumi na tano na Mwaka 2007 pia mabadiliko mengine yalifanyika.

Pamoja na lengo zuri la mabadiliko haya bado changamoto kubwa imebaki katika mfumo mzima wa ukusanyaji wa mapato jambo ambalo limekuwa likiisababishia Serikali kupoteza mapato. Wakati mwingine mapitio ya mirahaba yamekuwa yakifanywa pasipo ushirikishwaji wa wadau na pasipo kuzingatia hali halisi ya soko la mazao husika.

VI. Vile vile kutokuwepo kwa motisha /vivutio /nafuu ya kodi katika uwekezaji kwenye sekta ya Misitu nchini hasa katika usafirishaji wa mazao ya Misitu nje ya nchi:

Miongoni mwa nchi zilizofanya vizuri ni China ambayo imerekebisha mfumo wake wa kodi kwa kuhakikisha kodi ya thamani inalipwa kabla ya kusafirisha mazao ya Misitu nje ya nchi. Kwa sasa Sheria ya Uwekezaji Na. 26 ya Mwaka 1997 inafafanua kuwa ili angalau mwekezaji wa ndani aweze kupata motisha wa kodi inabidi angalau kima cha chini cha uwekezaji wake uwe dola za Kimarekani laki moja (100,000). Bado kiwango hiki kiko juu ukilinganisha na uwezo halisi wa wawekezaji wa ndani.

Page 19: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 19

SEHEMU YA NNE

5.0 MAPENDEKEZO KATIKA KUBORESHA MFUMO WA KODI ZA MAZAO YA MISITU NCHINI

Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoainishwa hapo juu, ni vema mambo mbalimbali yakarekebishwa ili kujenga mfumo mzuri wa utozaji na usimamizi wa kodi mbalimbali za mazao ya misitu. Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ambayo ni mhimu kufanyiwa kazi:

Kwanza, kurekebisha mwongozo wa uvunaji: Kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na LEAT imebaini kuwa moja ya kasoro zilizopo kwa sasa kuhusu uvunaji na biashara nzima ya mazao ya misitu nchini ni kutokana na kutokuwepo kwa mfumo mzuri wa uainishaji wa malipo yote kisheria katika ngazi mbalimbali. Kwa mfano utaratibu wa otoaji wa Hati ya Usafirishali (Transit Pass) mara mbili yaani ndani ya mkoa na nje ya mkoa, utaoji mbovu wa leseni za uvuanji na kuwepo kwa mfumo mbovu wa tozo na kodi mbalimbali unatokana na mapungufu yaliyomo kwenye mwongozo huu. Vile vile mwongozo huu hauweki wazi kodi na tozo au ushuru ambao unapaswa kutolewa na mamlaka mbalimbali ambazo zinatoza tozo au ushuru huo kwa sasa. Ni ukweli usiopingika kuwa tatizo hili mbali na kulikosesha taifa mapato pia linachangia kukithiri kwa rushwa na hivyo kusababisha uharibifu wa misitu nchini.

Pamoja na kuwepo kwa miongozo ya uvunaji tafiti zinasema karibu hekta laki nne hupotea kila mwaka kutokana na uvunaji haramu wa mazao ya misitu. (FAO, 2010 na Naforma, 2015)

Pili, kodi na tozo za mazao ya Misitu zipunguzwe: kwa sasa mfanyabiashara anapaswa kulipa karibu kodi nane kwa mzigo mmoja. Ni vyema kukawa na utaratibu mzuri ambao utamtoza mfanyabiashara wa mazao ya misitu maramoja na jukumu la kugawa pesa hiyo kwa idara au mamlaka mbalimbali za kiserikali likabaki kwa serikali kuliko kuziachaia mamlaka na taasisi nyingi jukumu la kutoza ushuru au malipo mbalimbali ya mazao ya misitu. Pale ambapo inalazimika Serikali kuhamisha jukumu hilo kwa vyombo vya ngazi za chini ni vyema vikapewa utambulisho kisheria na pia kodi zote au ushuru ukawekewa stakabadhi stahiki kisheria ili kuondoa mwanya wa matumizi mabovu ya tozo, kodi au ushuru utokanao na mazao ya misitu nchini.

Page 20: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

Tatu, vyombo au mamlaka zenye jukumu la kukusanya kodi, tozo au ushuru wa mazao ya Misitu vipunguzwe/zipunguzwe: Hii itapunguza mianya ya rushwa na pia itarejesha imani kwa mlipa kodi. Kwa sasa baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali katika sekta ya misitu nchini hawaamini kama kile kinachotozwa kinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, mfano mzuri ni asilimia tano (5%) ya ushuru kwa ajili upandaji miti. Pamoja na malengo mazuri ya kuupa nguvu mfuko wa maendeleo ya misitu, inaonekana usimamizi wa fedha hizi bado unatia shaka. Katika kufanikisha azma hii ni vyema kuhakikisha kuwa hakuna mwingiliano katika utozaji na usimamizi wa mapato yatokanayo na mazao ya Misitu.

Nne, kuwepo kwa uwiano wa tozo na kodi zinazotozwa kwenye aina moja ya zao la misitu: hii itasaidia kuondoa tatizo la wafanyabiashara kulipa tozo tofauti kwa aina moja ya zao. Vilevile itasaidia kuhakikisha kuwa hakuna mfanyabiashara anayebebeshwa mzigo zaidi wa kodi au tozo. Lengo hili linaweza kufikiwa kwa kuwepo kwa mfumo wa huru wa utoaji wa taarifa kutoka wilaya zinazofanya vizuri katika usimamizi wa misitu yake. Likini Bunge au vyombo vingine husika vinaweza kuweka utaratibu utakao hakikisha kuwa kila mfanyabiashara analipa kodi ya namna moja kwa aina inayofanana ya zao la misitu.

Tano, sheria ziwe wazi kuhusu kile kinachopaswa kulipiwa kodi na kipi hakipaswi kulipiwa kodi: Hili linaweza kufikiwa kwa kuweka wazi na kuandaa machapisho ya kuwaelimisha wafanyabiashara wa mazao ya misitu. Inaweza kukumbukwa kuwa kwa sasa zipo tozo au ushuru ambao uhalali wake umekuwa wa kutiliwa shaka, hivyo ili kuweka mfumo wa uthibiti wa mapato ni vyema kukawa na mfumo wa kuwaelimisha wafanyabiashara na kutayarisha machapisho mbalimbali ili kuainisha tozo, kodi na ushuru unaotozwa na vyombo mbalimbali vya kiserikali.

Sita, Kuongeza ushiriki wa wadau katika utayarishaji wa sera na hata utungwaji wa Sheria za kodi: Hii ni nyenzo nyingine muhimu katika kujenga mfumo imara wa kodi na tozo mbalimbali za mazao ya Misitu. Wadau wanapaswa kushiriki katika hatua zote yaani uandaaji wa sera na pia katika kutunga sheria. Hii itasidia kuwafanya wananchi waone kuwa kodi ni wajibu wao na wanalipa kodi kwa manufaa yao na sio kwa manufaaa ya mtu mwingine yeyote yule isipokuwa wananchi wenyewe.

Saba, kupunguza vikwazo kiutendaji: Kwa mfano kuwepo na taratibu rahisi za utoaji wa vibali, mfumo rahisi wa kulipia kodi na tozo mbalimbali, utaratibu mzuri wa kufanya maombi hasa katika uvunaji kwenye ngazi ya kijiji na kupunguza mwingiliano

20 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Page 21: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

baina ya taasisi au vyombo mbalimbali vyenye mamlaka ya kufanya maamuzi. Ni vyema kuhakikisha kuwa mfumo wa kodi, tozo au ushuru wa mazao ya Misitu unakuwa wazi na rahisi kwa wahusika kama njia ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wa mazao ya Misitu wanafuata Sheria na kupunguza mianya ya rushwa na watu kukwepa Sheria makusudi.

5.0 HITIMISHOIli kujenga mfumo imara wa kodi na tozo za mazao ya misitu, ni vyema kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa. Mfumo huo imara unapaswa kujengwa kwa kuwa na taasisi imara zitakazohakikisha kuwa kodi sahihi zinalipwa ili kuondoa tatizo la wafanyabiashara kukwepa kodi. Ni vyema ikakumbukwa kuwa utaratibu mbovu wa kodi na tozo mbalimbali za mazao ya Misitu ni kikwazo kikubwa katika kuhakikisha kunakuwa na uvunaji endelevu wa mazao ya Misitu Nchini. Uharibifu wa Misitu sio tu unaathiri kizazi kilichopo bali hata vizazi vijavyo. Ni jukumu la kila mtanzania kulinda Misitu yetu lakini pia ni haki ya kila mtanzania kunufaika na rasilimali za nchi yake. Utawala bora wa rasilimali ni nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya taifa lolote lile duniani. Pamoja na mafanikio yaliyofikiwa ni vema kuziondoa changamoto zilizoainishwa kwenye mwongozo huu ili kuongeza kiwango cha mapato kwa Serikali na pia kuwajengea uwezo wa wafanyabiashara kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na kanuni mbalimbali zilizopo kisheria.

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 21

Page 22: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

22 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Page 23: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU | 23

Mama Misitu ni Kampeni ya mawasiliano inayolenga kuboresha utawala wa Misitu Tanzania, na kukuza matumizi endelevu ya mazao ya Misitu ili watu wa Tanzania wanufaike zaidi na rasilimali za Misitu. Kampeni ya Mama Misitu imebeba dhamira na maono ya kuhifadhi, kulinda na kuhamasisha matumizi endelevu ya Misitu. Kampeni ya Mama Misitu inatekelezwa na kikundi kazi cha misitu Tanzania na kuratibiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF).

Page 24: CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAUmamamisitu.com/wp-content/uploads/2016/10/Tax_Compliance-FIN… · a. Uthibitisho wa mlipa kodi yaani (Taxpayer Identification Number) b. Hati ya

24 | CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA WADAU

Uandaaji na uchapishaji wa mwongozo huu pamoja na Kampeni ya Mama Misitu vimefadhiliwa na Serikali ya Ufini.

Kampeni ya Mama Misitu, Namba 27 Mtaa wa Sangara - Mikocheni Dar es Salaam. | Tovuti: www.mamamisitu.com | Barua pepe: info@

mamamisitu.com | Simu: +255 758828398 | Facebook: www.facebook.com/mamamisitu | Twitter: www.twitter.com/mamamisitu