199
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tisa – Tarehe 12 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza asubuhi ya leo linaelekezwa kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na linaulizwa na Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto. Na. 68 Kukarabati Shule za Msingi na Sekondari - Lushoto MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Serikali imekuwa na utaratibu wa kukarabati shule zake za msingi na sekondari nchini:- Je, ni lini Serikali itazifanyia ukarabati Shule za Msingi Kwemashai, Bandi, Milungui, Kilole na Shule za Sekondari za Ntambwe, Ngulwi - Mazashai na Mdando?

BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA________

MAJADILIANO YA BUNGE_________

MKUTANO WA KUMI NA TANO

Kikao cha Tisa – Tarehe 12 Aprili, 2019

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Swali letu la kwanza asubuhi ya leolinaelekezwa kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na linaulizwa naMheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto.

Na. 68

Kukarabati Shule za Msingi na Sekondari - Lushoto

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:-

Serikali imekuwa na utaratibu wa kukarabati shulezake za msingi na sekondari nchini:-

Je, ni lini Serikali itazifanyia ukarabati Shule za MsingiKwemashai, Bandi, Milungui, Kilole na Shule za Sekondari zaNtambwe, Ngulwi - Mazashai na Mdando?

Page 2: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MWENYEKITI: Ahsante. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2018/2019, Serikali kupitia Program ya Lipa Kulingana naMatokeo (EPforR) imepeleka jumla ya shilingi milioni 467 kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili, matundu sita ya vyoo namadarasa mawili katika Shule ya Msingi Shukilai (Shule yaElimu Maalum) na ujenzi wa mabweni mawili Shule yaSekondari Magamba, ujenzi wa bweni moja na madarasamawili Shule ya Sekondari Umba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika mwaka waFedha 2018/2019, Serikali imetoa shilingi bilioni 29.9 kwa ajiliya ukamilishaji wa maboma 2,392 ya madarasa nchi nzimaambapo kati ya fedha hizo Halmashauri ya Wilaya ya Lushotoimepewa kiasi cha Sh.512,500,000 kwa ajili ya kukamilishamaboma 46 ya madarasa shule za sekondari. Serikaliitaendelea kukarabati na kujenga miundombinu ya elimukwa awamu kadri ya upatikanaji wa fedha.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Shekilindi.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali, nimpongeze Raiswangu Mungu azidi kumjaza hekima na maisha marefu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize maswalimawili ya nyongeza. Swali la kwanza, pamoja kwambatumepata fedha zote hizo kama nilivyosema nashukuru lakinibado sekondari nyingi katika Jimbo la Lushoto hazina hosteli

Page 3: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

na hii imepelekea watoto wengi kufeli na watoto wengi wakike kupata ujauzito. Je, Serikali ina mkakati gani sasa tenawa haraka kuhakikisha kwamba wanajenga hosteli katikasekondari ambazo hazina hosteli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wananchi waJimbo la Lushoto kwa nguvu zao wamejenga majengo yamaabara tena yote matatu lakini mpaka sasa majengo yalehayajamalizika. Je, Serikali haioni kuwa kuna umuhimu sasawa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusomaelimu kwa vitendo? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayomawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Mheshimiwa Waitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa Shekilindi maswalimawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nampongezaMheshimiwa Mbunge nimefika kwenye Jimbo lake la Lushoto,wananchi wa eneo lile na yeye mwenyewe wamefanya kazikubwa kuongeza miundombinu ya elimu lakini pia afya namaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanaomba kujua mpango wa Serikali kuongeza hosteli. Katikabajeti ambayo inaendelea kujadiliwa sasa kila mtu akipitiakwenye kitabu cha bajeti cha Mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utaona kuna maeneo mbalimbalifedha zimetengwa kwa kazi hiyo lakini iko miradi mingine yaelimu itakayoimarisha hosteli mbalimbali. Kwa hiyo, naombaMheshimiwa Mbunge avumilie mwaka huu wa fedhatumetenga fedha na kadri zitakavyopatikana tutawezakumaliza hiyo shida kwa watoto wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kuhusumaboma ya maabara, tumeanza kupeleka vifaa na

Page 4: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

kukamilisha maboma katika shule nyingi kadriitakavyowezekana. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbungetuwasiliane huenda shule au maeneo yake anayotajatutapeleka vifaa vya maabara lakini pia tutamalizia mabomaya maabara hizo. Lengo ni ili tupate wataalamu wa sayansiili tutakapoanza issue ya viwanda tuwe na wataalam wakutosha.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mbatia.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Kwa misingi ya elimu bora, sawa, shirikishikwa wote, elimu ya msingi inaanzia darasa la ngapi mpakala ngapi na elimu ya sekondari inaanzia darasa la ngapimpaka la ngapi?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu, Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa JamesMbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utaratibu tunaotumiatuna darasa la awali, darasa la kwanza mpaka la saba, formone mpaka form four na kidato cha tano na cha sitabaadaye elimu ya juu. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lubeleje.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba hivikaribuni Serikali imefanya ukarabati mkubwa wa shule zasekondari kongwe ikiwemo Shule ya sekondari ya Mpwapwalakini mimi nataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Wazirimnafanya ukarabati wa shule tu lakini nyumba za walimu

Page 5: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

zimechakaa kweli kweli. Je, mna mpango gani wakukarabati shule na nyumba ya walimu?

MWENYEKITI: Ahsante, mna mpango wa ukarabati wanyumba za walimu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa George MalimaLubeleje (Senator), kama lifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwambatunakarabati shule tu ukweli ni kwamba tumekarabati shulenyingi zaidi kuliko nyumba za walimu. Hata kwenye kitabucha bajeti tunachojadili sasa ambapo Mungu akipendatutahitimisha Jumatatu tarehe 15 akipitia kwenye majimbombalimbali ataona fedha zimetengwa kwa ajili ya ukarabatiwa nyumba za walimu. Uwezo wa Serikali siyo mkubwa sana,tunaomba Mheshimiwa Mbunge na wadau mbalimbalitushirikiane katika jambo hili kupunguza shida ya walimukatika nchi hii. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Catherine.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwa kuwa tumeona shule nyingi kongwezilizotoa viongozi mbalimbali zimekuwa zikikarabatiwa. KwaMkoa wangu wa Arusha, kuna Shule ya Arusha Sekondariambapo miundombinu yake ni mibovu na chakavu. Je,Serikali haioni umuhimu wa kutenga pesa kwa ajili yakukarabati shule hii kongwe ya Arusha Sekondari?

MWENYEKITI: Ahsante, shule kongwe ya ArushaSekondari.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la MheshimiwaCatherine Magige, msemaji mzuri sana wa Mkoa wa Arushana Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Page 6: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nia ya Serikali kukarabatishule zote kwa wakati mmoja kama ingewezekana lakini kwasababu ya ufinyu wa bajeti jambo hilo halijawezekana,tutakarabati kulingana na uwezo lakini pia kuna vigezombalimbali. Kwa hiyo, naomba nichukue hoja ya MheshimiwaMbunge, tufanye tathmini, tumeshamaliza awamu ya kwanzatupo kwenye mpango wa awamu ya pili, huenda kwenyeawamu ya tatu Shule ya Arusha Sekondari ikaingizwa kwenyempango huu wa Serikali wa kukarabati shule hizi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chegeni.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri sambamba na matatizo ya Lushoto,Wilaya ya Busega haikupata mgao wa fedha kwa ajili yaukamilishaji wa maboma. Je Mheshimiwa Naibu Waziri,unaweza ukatoa maelekezo katika mgao huu na Wilaya yaBusega tupate mgao huo?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri kwakifupi, pesa, pesa, pesa.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge waBusega swali lake la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natambua kazi nzuriambayo anaifanya katika Jimbo lake la Busega kuwasemeawananchi wake lakini sina hakika kwa sababu fedha zilezil isambazwa kwenye wilaya zote kwa maana yaHalmashauri inawezekana kwenye Jimbo hilo kuna bahatimbaya. Naomba tuwasiliane baada ya kipindi cha maswalina majibu tuone njia bora ya kumaliza shida hiyo. Ni nia yaSerikali kila Jimbo lipate mgao wa kupunguza shida yamaboma na kuchangia nguvu za wananchi ili wasilalamike.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea,swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa Zacharia Issaay,

Page 7: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Mbunge wa Mbulu Mjini na linaelekezwa ofisi hiyo hiyo yaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Na.69

Maboresho ya Mji wa Mbulu

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY atauliza:-

Serikali ina nia njema ya kuuweka Mji Mkongwe waMbulu kwenye mpango kabambe wa maboresho ya Miji naMajiji, Mikoa na Wilaya na kwenye Awamu ya Pili ya mpangohuo kwa ajili ya miundombinu ya masoko, barabara, vituovya mabasi na taa za barabarani:-

(a) Kwa kuwa Mji wa Mbulu ni mkongwe tokakuanzishwa kwake, je, ni lini sasa nia hiyo njema itatekelezwa?

(b) Je, mpango huo wa maboresho ya Mji utasaidiajemiundombinu ya barabara za mitaa ya Mji wa Mbulu ambazoni zaidi ya kilomita 40 za changarawe kwa kuwa ni kilomita1.8 za lami kwa sasa?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hiloMheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI MheshimiwaWaitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Zacharia Paul Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikalli kupitia Ofisiya Rais - TAMISEMI inatekeleza miradi ya uboreshaji MijiTanzania ambayo ni Urban Local Government StrengtheningProgramme (ULGSP) na Tanzania Strategic Cities Project(TSCP) na Dar es Salaam Metropolitan Development Project

Page 8: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

(DMDP) kwa fedha za mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.Mpaka sasa miradi hii inatekelezwa katika Majiji 6, Manispaa19 na Halmashaurui za Miji 6. Utekelezaji wa Programu yaKuzijengea Uwezo Mamlaka za Miji (Urban Local GovernmentStrengthening Programme-ULGSP) ulianza katika mwaka wafedha 2013/2014 na unatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha2019/2020. Wakati wa maandalizi ya programu hii, Mji waMbulu ulikuwa haujapata hadhi ya kuwa Halmashauri ya Mjina hivyo kukosa vigezo vya kujumuishwa kwenye programu.Serikali itatoa kipaumbele kwa Mji wa Mbulu kwenye awamunyingine za mradi huu.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Programu yaKuzijengea Uwezo Mamlaka za Miji inajumuisha ujenzi wamiundombinu ya msingi katika miji, kujenga uwezo waukusanyaji wa mapato ya ndani na kuwezesha uandaaji wamipango kabambe ya uendelezaji wa miji na kuboreshauwajibikaji na utawala bora. Hivyo Mji wa Mbulu ukijumuishwautanufaika na mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafahamu umuhimuwa kuboresha miundombinu ya barabara katika Mji waMbulu. Katika mwaka wa fedha 2018/2019 kupitia fedha zaMfuko wa Barabara, Serikali inajenga barabara yenye urefuwa kilomita 0.4 kwa kiwango cha lami nyepesi (doublesurface dressing) kwa gharama ya shilingi milioni 300 na kaziya ujenzi inaendelea.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Issaay.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili yanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, mpangounaotekelezwa sasa wa kilomita 0.4 ni ahadi ya MheshimiwaRais na kwa kuwa ahadi hii ya Mheshimiwa Rais ni kilomita 5katika Mji wa Mbulu, nini majibu ya Serikali kuelekea UchaguziMkuu wa mwaka 2020 kwa kuwa Rais atakuwa anataka

Page 9: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

ahadi hiyo iwe imetekelezwa na mimi nimeshatimiza wajibuwangu wa kuikumbusha Serikali mara kadhaa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, ni kweliMji wa Mbulu ni mji mpya ulioanzishwa lakini ni Halmashauriau Wilaya kongwe katika ya Wilaya kongwe Tanzania. Kwahivi sasa Mji wa Mbulu una kilomita 1.8 katika mitaa yake kwakiwango cha lami. Kwa kuwa hali ya barabara na madarajakatika kata kumi ukiacha kata zingine nane za vijijini ni mbaya;na kwa kuwa TARURA wanapewa fedha kidogo sana hivyokushindwa kutekeleza mahitaji yaliyoibuka, nini kauli ya Serikalikuwezesha miundombinu ya barabara katika Miji wa Mbulupamoja na ahadi hiyo ya Rais?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo,Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge Zakharia,Mbunge wa Mbulu Mji maswali mawili ya nyongeza kwapamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanauliza kuhusiana na ahadi ya Mheshimiwa Rais, naombanimhakikishie kwamba hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, kipenzicha Watanzania, namhakikishia kabla ya 2020 ahadi hiiitakuwa imekamilishwa ili Mheshimiwa Rais atakapoendakuomba kura kwa awamu nyingine kwa niaba ya Chamacha Mapinduzi, asipate vikwazo kwa wananchi wa Mji waMbulu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, anapenda kujuatuna mpango gani, nitoe maelekezo kwa TARURA Mkoa naWilaya yake ya Mbulu kama hali ya mji huu ni mbaya kiasihicho wafanye mchakato walete maandishi hapa tujuenamna ya kufanya ili tuweze kuboresha wakati tukisubirikutafuta fedha nyingi zaidi za kuboresha Mji wa Mbulu.Ahsante.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Katika majibu yake Mheshimiwa Naibu Waziriameeleza kwamba mipango ya kuendeleza barabara za mijini pamoja na Mpango wa DMDP. Katika Manispaa yaUbungo mpango wa DMDP, unatekelezwa kwa upande waJimbo la Ubungo peke yake lakini upande wa Jimbo laKibamba kwenye Kata sita za Kwembe, Msigani, Mbezi,Saranga, Goba mpango huu hautekelezwi kabisa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kupanua utekelezajiwa mpango wa DMDP ili kuzigusa kata sita za Jimbo laKibamba kwenye masuala ya miundombinu ya barabara?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo NaibuWaziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la MheshimiwaMnyika, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mkoa waDar es Salaam ikiwepo maeneo ambayo ametaja ya Ukongana maeneo mengine, tunatekeleza awamu ya kwanza yampango ya DMDP. Naomba niwahakikishie kwambaitakapokuja awamu ya pili Wabunge watashirikishwawaweze kuainisha maeneo yao ili tupanue wigo zaidi wakuendeleza Mji wetu wa Dar es Salaam.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Mji wa Mafingaulikuwa Mamlaka ya Mji Mdogo kwa miaka tisa na Julai 2015ikawa Halmashauri kamili ya mji. Je, Serikali inawezakuwahakikishia wana-Mafinga kwamba kwa kuwaHalmashauri ya Mji kamili na wao wameingia katika MpangoKabambe wa Maboresho ya Miji? Kwa sababu sasa hivi

Page 11: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Mafinga ni Halmashauri ya Mji kamili. Tunataka tukuhakikishiwa na sisi tunaingia katika awamu ya pili? Kwasababu ndiyo ukombozi wa barabara zetu?

MWENYEKITI: Ahsante, umeeleweka. Majibu kwa swalihilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI,Mheshimiwa Waitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la MheshimiwaCosato Chumi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongezaMheshimiwa Mbunge alikuwa na Mheshimiwa Raisamekubaliwa mambo yake yote manne leo amelala usingizimnono kabisa. Katika suala hili, kama nilivyojibu swali laMheshimiwa Zakharia, Mbunge wa Mbulu Mji, tutakapoanzakufanya mchakato miji mipya yote na huo mji wakoutaingizwa katika awamu hiyo.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali linalofuata, namba 70 linaulizwa na Mheshimiwa SaulHenry Amon, Mbunge wa Rungwe, linaelekezwa Ofisi ya Rais,TAMISEMI. Mheshimiwa Mwambalaswa, kwa niaba.

Na. 70

Barabara ya Kuunganisha Kata ya Kisondela – Rungwe

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. SAUL H.AMON) aliuliza:-

Hakuna barabara ya kuunganisha Daraja la Nyubatina Kata ya Kisondelea hadi Nzunyuke umbali wa zaidi yakilomita 30 kufika kijiji cha Nyubati:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabaraya kuunganisha Kijiji cha Nyubati na Kata ya Kisondelea?

Page 12: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

MWENYEKITI: Ahsante sana. Majibu ya swali hilo, NaibuWaziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saul HenryAmon, Mbunge wa Rungwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuwa wananchiwamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilometa 30 kwakuzunguka kutoka Nyubati hadi Nzunyuke kutokana nakukosekana kwa daraja. Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) umefanya usanifu na tathmini ya ujenzi wabarabara hiyo ambapo kiasi cha shilingi milioni 847.36kinahitajika ili kuitengeneza barabara hiyo kwa kiwango chachangarawe. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, TARURAimetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wabarabara ya Nyubati – Lutete yenye urefu wa kilometa 6inayounganisha Kijiji cha Nyubati na Kata ya Kisondelea.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwambalaswa.

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri sanaya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogoya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwamatatizo ya wananchi wa Rungwe kuhusu barabarayanafanana kabisa na matatizo ya wananchi wa Chunyahasa hasa kwa barabara inayotoka Chunya – Kiwanja -Ifumbo - Mjele, ambayo sasa hivi inaunganisha Mikoa miwiliya Songwe na Mbeya; na kwa kuwa Mamlaka ya Wakalawa Barabara (TARURA) toka imeanzishwa Chunya hakunabarabara hata moja ambayo wameikarabati. Je,Mheshimiwa Waziri anatoa maagizo kwa TARURA i l iwaikarabati barabara hiyo iweze kupitika?

Page 13: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, MheshimiwaNaibu Waziri kijana mchakapa kazi yupo tayari kuongozananame kwenda Chunya il i akaangalie kazi ambazowanafanya TARURA katika Halmshauri ya Chunya?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo,Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo,Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, swali la kwanza kwa barabara ambazoMheshimiwa Mbunge amezitaja na mipango iliyopo na kwasababu michakato hii inaanzia kwenye ngazi ya Halmashauri,inakuja kwenye Mkoa mpaka ngazi ya TAMISEMI, namwombaMheshimiwa Mbunge tuwasiliane baadaye tupate taarifasahihi ya eneo hili na tuweke mipango mahususi ambayoinaweza kutatua shida hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, MheshimiwaMbunge anauliza kama nipo tayari. Mimi nipo tayari sanawakati wowote. Tupande ratiba twende tuone eneo hili,turudi kufanya mipango ya kukamilisha na kuondoa kero zawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Zungu.

MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwanza naipongeza Serikali kwa mradi wakewa kuleta mpango wa DNDP kwenye Mkoa wa Dar esSalaam. Jimbo la Ilala tumepata Kilometa mbili tofauti namaeneo mengine wamepata zaidi ya Kilometa 40.

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuboreshabarabara za kata zote 10 za Jimbo la Ilala ili ziweze kuonekanaza kupitika kwa sababu ni katikati ya mji na zinasaidia

Page 14: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

kupunguza msongamano katikati ya mji kuelekea pembezonimwa mji? (Makofi)

MWENYEKITI: Naibu Waziri, majibu kwa swali hilo.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M.WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kuna miradi inaendeshwa katika Mji waDar es Salaam, UNDP na sasa kilichobaki, baada yakutengeneza barabara nzuri zaidi, ni vingumu zaidi barabaraza pembezoni zikawa nzuri. Sasa kwa sababu MheshimiwaMbunge tupo wote Ilala na tunampongeza Meneja waTARURA kwamba ni msikivu sana, tutawasiliana naye tuonemipango iliyopo na sisi tuishi kama Wabunge wa Dar esSalaam ili kuwezesha mipango ya kukamilisha barabara zetuna hasa wakati wa mafuriko watu wa Dar es Salaamwasiweze kupata shida zaidi.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mndolwa.

MHE. ZAINABU AMIR MNDOLWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niwezekuuliza swali dogo la nyongeza. Barabara itaokayo Korogwekupitia Kwa Mndolwa - Mkaalie - Tamota hadi kuunganishwana Kiwanda cha Chai Mponde ni takribani kilometa 40 lakinihaijajengwa kwa kiwango cha lami. Hii ni barabara muhimusana katika nchi kwa sababu mazao mengi kutoka Jimbo laBumbuli ambayo yanasafirishwa kwenda Dar es Salaamhupita pale, lakini wakati wa mvua barabara hii haipitikikabisa na kuna maporomoko ya mawe:-

Je, ni lini sasa Serikari itajenga hii kwa kiwango chalami? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Jibu la swali hilo, Naibu Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nampongeza kuendelea kuwasema

Page 15: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

wananchi wa Korogwe, lakini namwomba sana kwa sababutupo kwenye wakati wa bajeti hii aunge mkono bajeti yaTAMISEMI Jumatatu tutakapofika kwa majaliwa yaMwenyenzi Mungu tupate fedha hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilijibu swali hapanikasema, tuliunda timu ya wataalam, inapitia sasa namnaya ku-identify hizi barabara ili tuangalie ule Mfuko waTANROADS na TARURA. Nimesikia michango ya WaheshimiwaWabunge kwamba TARURA inafanya kazi nzuri sana. Shidahapa ni fedha. Tukipata chanzo realible cha fedha naformula ambayo ipo sawaswa na wadau mbalimbali nabajeti ikaungwa mkono. Nia ya Serikali ni kukamilishabarabara zote ikiwezekana kwa kiwango cha lami ikiwepohiyo ya Korogwe. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,tunaendelea. Swali linalofuata linaulizwa na MheshimiwaSuleiman Jumanne Zedi, Mbunge wa Bukene.

Na. 71

Barabara ya Tabora – Mambali – Itobo-Kagongwa

MHE. SELEMAN J. ZEDI atauliza:-

Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Tabora – Mambali –Itobo - Kagongwa yenye urefu wa Kilometa 149 utaanzakujengwa kwa kiwango cha lami? Kwani ni ahadi yaMheshimiwa Rais na pia imo kwenye Ilani ya Uchaguzi yaCCM 2015 - 2020.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi Uchukuzu na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Bukene,kama ifuatavyo:-

Page 16: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza kutekelezampango wa ujenzi wa barabara ya Tabora – Mambali – Itobo– Kagongwa yenye urefu Kilometa 149 kwa kuanzia na hatuaya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Serikali kupitiaWakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wameingiamkataba na Mhandisi Mshauri NIMETA Consult Ltd. kwa ajiliya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wabarabara ya Tabora – Mambali – Itobo – Kagongwa kwagharama ya shilingi milioni 789. Hadi sasa Mhandisi Mshauriamekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na kazi ya usanifuwa kina itakuwa imekamilika kufikia Juni, 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara baada ya kazi yaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina, gharama za ujenzipamoja na maandalizi ya nyaraka za zabuni kukamilika,Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi kwa kiwango chalami wa barabara hii. Aidha, wakati kazi ya usanifu ikiendelea,Wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)itaendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali kwabarabara hii ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Jumlaya shilingi 345 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya kazi hiyo. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Zedi.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naipongezea Serikali kwa kazi ambayo imefanywakwenye barabara hii. Kimsingi wakati naandika swali hili,kuliwa hakuna kazi yoyote ambayo imefanyika, lakini sasahivi nakubaliana kabisa na majibu ya Mheshimiwa NaibuWaziri kwamba Mshauri Mhandishi NIMETA Consultameshaanza kazi, nami mwenyewe ni shuhuda nimemwonaakifanya kazi hii ya usanifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba kwakuwa Serikali imesema kazi ya usanifu wa kina inaisha mweziJuni, 2019 na hii barabara ni ahadi ya Rais na pia ni jamboambalo lipo kwenye ilani:-

Page 17: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Je, Serikali inaweza ikatoa kauli hapa kwambabarabara hii kwa kuwa usanifu utakuwa umekamilika mweziJuni, sasa kwenye bajeti ijayo itatengewa fedha ili Mkandarasiwa kuanza kujenga aanze kazi kabla ya Awamu hii ya Tanohaijamaliza muda wake?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo,Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, MheshimiwaEng. Nditiye.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza tunapokea pongezi kwa moya wa dhati kabisa lakininapenda kumshukuru sana Mheshimiwa Selemani Zedi kwajinsi ambavyo anafuatilia sana kipande cha barabara hiiiliyotajwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mpango wa Serikali nania ya Serikali kuhakikisha kwamba barabara zote nchinikwanza zimepitika na pili zinaunganishwa kwa kiwango chalami. Nimhakikishie Mheshimiwa Zedi kwamba barabara yakekama tulivyoahidi kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi nakama ahadi ya Mheshimiwa Rais, tutaijenga kwa kiwangocha lami kabla ya mwaka 2020 kwisha.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Matiko halafuMheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kama ilivyo ahadi kwa Jimbo la Bukene,Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni zake na hataMheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne aliahidi kujengabarabara ya Tarime Mugumu ambayo ni kilometa 89 kwakiwango cha lami; na kwa kuwa hii barabara ikijengwaitakuza uchumi siyo tu wa Tarime au Mara, bali wa Taifa,maana yake watalii watakao toka Kenya wataweza kupitakwenye njia ile:-

Page 18: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Ni lini sasa hii ahadi ya Mheshimiwa Rais itatimilika kwakujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Tarime Mugumualmaarufu kama Nyabwaga Road?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hiloMheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mheshimiwa Eng. Nditiye.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kwamba Serikali iliahidi kujenga kipande cha kilometa44 kutoka Tarime mpaka Mugumu kwa kiwango cha lami.Naamini hata Mheshimiwa Mbunge anajua kwambaupembuzi yakinifu ulishafanyika, usanifu wa awaliulishafanyika na usanifu wa kina ulishafanyika. Sasa hivitunatafuta pesa kwa ajili ya kumpa Mkandarasi wa kujengakwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekitik, kwa hiyo, namshauriMheshimiwa Mbunge awe na subira kidogo, tutajenda hiyobarabara kwa sababu ya umuhimu wa utalii wa nchi yetukwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ritta Kabati.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa, naombanichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu, Dkt.John Magufuli kwa uzinduzi wa barabara ya kutokaMakambako mpaka Mufindi jana. Naomba niulize swali moja.Katika ujenzi wa barabara ya kutoka Dodoma - Mtera mpakaIringa, pale katika kona za Nyang’holo huwa kunakuwa namaporomoko makubwa sana ambayo huwa yanajitokezahasa wakati wa mvua:-

Je, Serikali inatusaidiaje? Maana kutakuja kutokeaajali kubwa sana, hata jana nimepita pale. Ahsante.

MWENYEKITI: Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kwa kifupi tu.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kwamba tayari ameshafika ofisini zaidi ya mara tatuakifuatilia kipande cha barabara hii ya kutoka Mtera - Iringahasa kwenye kona zile za Nyang’holo ambazo ni korofi kabisa.Tunakiri na bahati nzuri nimeshamwelekeza Meneja waTANROAD Mkoa kufuatilia eneo hilo ili tuanze tararibu zakulirekebisha kwa ajili ya usalama wa Watanzania. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mabula Stanslaus.

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipatia nafasi hii niulize swali dogo lanyongeza. Kwa kuwa mji wa Mwanza unaendelea kukua kilasiku na miundombinu ya barabara hasa barabara ya Kinyatainayotoka Mwanza Mjini kwenda Usagara hali yakekimsongamano siyo nzuri; na leo nauliza karibia mara ya nne:-

Ni lini sasa Wizara itakuwa tayari kuhakikisha barabarainayotoka Mwanza Mjini kupitia Igogo - Mkuyuni na Butimba- Nyegezi mpaka Buhongwa, inapanuliwa kwa njia nne sasana kuweza kuwa barabara inayofanana na maziringira halisiya mji wenyewe? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hiloMheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mheshimiwa Eng. Nditiye.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kabisa Jiji la Mwanza linapanuka kwa kasi sana na nimipango ya Serikali kuhakikisha kwamba Jiji hilo linaundiwaprogram maalum ya kupanua barabara zake kupunguzamsongamano. Namshauri Mheshimiwa Mbunge, baada yakikao hiki, baada ya kipindi cha Maswali na Majibu,tuambatane naye mpaka Wizarani akaone mipango yaSerikali kuhusu Jiji la Mwenza kurekebisha barabara zake.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Gashaza.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Kwakuwa Mhandisi Mshauri yupo site kwa ajili ya kufanyaupembuzi yakinifu na usanifu wa barabara ya Nyakahura -Lulenge – Mulugarama; na kwa kuwa barabara hii ni ya mudamrefu.

Ni lini sasa ujenzi wa barabara hii kwa kiwango chalami utaanza?

MWENYEKITI: Haya, kama utaweza kuli j ibu,Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana MheshimiwaGashaza, ni kwa muda mrefu sana amekuwa akifuatilia hiibarabara ambayo naomba niitamke kwa ladha yake;inaitwa Nyakahuura – Kumubuga, inapatia Murusangamba- Lulenge mpaka Murugarama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri anakiri kwambaMshauri Mwelekezi yupo pale kwa ajili ya kufanya upembuziyakinifu na baada ya kumaliza zoezi hilo atafanya usanifuwa awali kisha usanifu wa kina kupata michoro kwa ajilikutambua gharama za ujenzi. Hatua zinakwenda vizurimpaka sasa hivi. Namshauri Mheshimiwa Mbunge awe nasubira kidogo. Tukishapata nyaraka zote hizo husika, hiyobarabara itaanza kurekebishwa tena kwa kiwango cha lami.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea WaheshimiwaWabunge. Swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa LolesiaJeremiah Bukwimba, Mbunge wa Busanda, linaelekezwa kwaMheshimwia Waziri wa Maji.

Page 21: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Na. 72

Utelekelezaji Mradi wa Maji Katoro- Buseresere

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa mradi mkubwawa maji wa Katoro- Buseresere unaokusudia kutoa maji ZiwaVictoria?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, NaibuWaziri wa Maji Mheshimiwa Aweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji,naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia JeremiaBukwimba, Mbunge wa Jimbo la Busanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Tanoinaendelea kutekeleza miradi ya maji ambayo lengo lake nikufikisha huduma ya maji kwa asilimia 95 ya wakazi wa mijinina asilimia 85 ya wakazi wa vijijini hadi ifikapo mwaka 2020.Malengo hayo yanahusu pia maeneo ya Katoro naBuseresere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza maandaliziya utekelezaji wa mradi wa Majisafi kutoka Ziwa Victoriakwenda Miji ya Katoro na Buseresere ambapo hadi hivi sasamazungumzo ya awali kati ya Serikali kupitia Mamlaka yaMajisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) nawafadhili kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB)yamefanyika. EIB wameonesha nia ya kufanya mradi wa majikwa ajili ya miji hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, andiko ya mradi wa majikwa ajili ya miji ya Katoro na Buseresere limeshawasilishwaWizara ya Fedha na Mipango ili maombi yaweze kuwasilishwarasmi EIB. (Makofi)

Page 22: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bukwimba.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili yanyongeza. Kwanza naipongeza Serikali kwa hatua ambayoimechukua kuweza kuhakikisha kwamba kuna mradi wa majiwa kutoka Ziwa Victoria, Katoro, Buseresere. Wananchiwanahitaji kujua ni lini utekelezaji utaanza rasmi?

Swali la pili; kwa kuwa azma ya Serikali mpaka mwaka2020 ni kuhakikisha kwamba mijini asilimia 95 ya maji, asilimia85 vijijini, jambo ambalo nikiangalia hali halisi, kwa mfanokatika Mkoa wa Geita Jimbo la Busanda, naona hali iko chinisana. Napenda kujua sasa kwamba nini mkakati wa Serikalikuhakikisha kwamba tunapata maji kwa asilimia 85 katikaJimbo Busanda na asilimia 95 Mji wa Geita ambapo sisiwananchi wote ni Makao Makuu ya Mkoa wetu wa Geita?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Majibu kwa maswali hayo MheshimiwaNaibu Waziri wa Maji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote, nampongeza sana MheshimiwaLolesia kwa kazi nzuri sana ya kuwapigia wananchi wake.Kubwa, tunatambua kabisa maji hayana mbadala. Ndiyomaana sisi kama Wizara ya Maji tumefanya jitihada yakuwasilisha hili andiko kwa Wizara ya Fedha ili wawezekuwasilisha EIB. Wizara ya Maji itafanya ufatiliaji wa karibukatika kuhakikisha jambo hili linakamilika kwa wananchi wakeili mradi uweze kuanza kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha azma yaMheshimiwa Rais ya kumtua mwanamama ndoo kichwanina kutimiza Ilani ya Chama cha Mapinduzi asilimia 85 yaupatikanaji wa maji vijijini na asilimia 95 ya upatikanaji mijini,tumeshakamilisha miradi zaidi ya mitatu katika Jimbo lake.Moja, Nyakagongo, Luhuha pamoja na Mharamba katikakuhakikisha wananchi wale wanapata maji.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati uliokuwepo sasa hivini katika kuhakikisha tunakamilisha mradi wa zaidi ya shilingibilioni nne wa Nachankorongo ili mradi ule ukamilike kwawakati na umeshafikia zaidi ya asilimia 90 upo katika mudatu wa matazamio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa na la msingi kabisa,sasa hivi tunakamilisha mradi wa Lamugasa na tunajengamradi wa maji Nkome, Nzela ambao ni wa zaidi ya shilingibilioni 25 katika kuhakikisha tunatatua tatizo la maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishieMheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizara ya Maji katika miji 25katika mpango wa kutatua tatizo la maji, Mkoa wa Geitatumeuangalia kwa ukaribu zaidi na tunafanya jitihada kubwaya kutatua tatizo la maji. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kaboyoka.

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza.Kwa kuwa Bwawa la Yongoma, katika Mto wa Yongomalilikuwa-designed na Serikali ya Japan kupitia JICA tangu 2012;na kwa kuwa mwaka huu 2018/2019 liliwekwa kwenye bajetikwamba lijengwe, Serikali inatoa tamko gani kuhusu ujenziwa bwawa hili?

MWENYEKITI: Ahsante. Jibu kwa swali hilo, kwa kifupitu Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nimpongeze sana MheshimiwaKaboyoka. Kubwa ambalo nataka niseme ni utekelezaji wamiradi ya maji unategemeana na fedha. Nia ya Serikali badoipo pale pale, na sisi kama Wizara tunaendelea kuhakikishafedha hizi zinapatikana ili bwawa lile liweze kujengwa nawananchi waweze kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kuchauka.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona na kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza. Mji wa Liwale ni Mji unaokua kwa haraka sana nauna chanzo kimoja tu cha maji; na kutokana na mabadilikoya tabianchi, chanzo kile hakitoshelezi tena. Je, ule mradiwa kutafuta chanzo mbadala cha maji kwa Mji wa Liwale,umefikia wapi?

MWENYEKITI: Ahsante. Jibu kwa swali hilo MheshimiwaNaibu Waziri, Wizara ya Maji, mpango huo umefikia wapi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nimpongeze sana MheshimiwaMbunge, lakini na pili nimepata nafasi ya kufika katika Jimbolake la Liwale. Pamoja na jitihada kubwa za Serikalizinazofanyika lakini kiukweli, Liwale kuna changamoto. Sasasisi kama Wizara tulishawaagiza watu wetu wa rasilimali zamaji katika kuhakikisha wanafanya utafiti wa kina ili tuwezekupata chanzo cha uhakika, tuweze kubuni mradi mkubwaambao kwa ajili ya kutatua kabisa tatizo la maji Liwale.Nataka nimhakikishie sisi tutalifanya jambo hili kwa haraka iliwananchi wake wa Liwale waweze kupata maji ya uhakika.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Willy Qambalo.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Miradi ya maji katika Vijiji vya Matala, Kansay,Buger, Endonyawet na Getamock Wilayani Karatu chini yampango wa WSDP imejengwa chini ya kiwango na hivyohaifanyi kazi, karibu shilingi bilioni nne zimetumika nahaziwanufaishi wananchi. Tulimwomba Mheshimiwa Wazirimara nyingi aje Karatu ili aje atatue tatizo hilo…

MWENYEKITI: Uliza swali sasa.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba awaambie wananchi wa vijiji hivyo ni lini atakwendaili kutatua changamoto za miradi hiyo? Ahsante.

Page 25: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

MWENYEKITI: Ahsante. Jibu kwa swali hilo MheshimiwaNaibu Waziri, Wizara ya Maji, Mheshimiwa Aweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge,binafsi nilishapata taarifa za Karatu na nimefika, lakini kubwakuna miradi ambayo imefanyiwa ubadhirifu. Natakanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge sisi kama Viongozi waWizara tumesha-note na tumekubaliana tutakwenda katikamaeneo yale yote na wale walioshiriki katika ubadhirifu ule,lazima fedha watazitapika na hatua kubwa kali tutazichukua.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Makamba.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.Mradi wa bomba la Ziwa Victoria umeshafika katikaHalmashauri ya Mji wa Kahama, lakini usambazaji katika Katanyingi bado haujafanyika, Kata ya Mwenda kulima,Kagongwa, Iyenze, Isagee maji hayajafika. Je, Serikali inampango gani wa kusambaza maji ya Ziwa Victoria iliwananchi waweze kunufaika? Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo,Mheshimiwa Naibu Waziri, Wizara ya Maji, MheshimiwaAweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote kwanza tutambue jitahada kubwazilizofanywa na Serikali, tunatambua kabisa tulikuwa nachangamoto kubwa sana, katika Mji wa Kahama naShinyanga na Serikali ikaona haja sasa ya kuyatoa maji ZiwaVictoria kwa ajili ya kutatua matatizo haya ya maji, kikubwamaji yale yamekwishafika lakini imebaki changamoto tu yausambazaji. Hivyo, nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge,wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani, sisitumekwishawaita Wakurugenzi wote na tumekwishawaagizakatika mapato yao wanayoyakusanya watenge asilimiakatika kuhakikisha wanasambaza maji kwa wananchi iliwaweze kupata maji safi salama na yenye kuwatosheleza.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwamoto.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, naomba anijibu swali langu la nyongeza. MheshimiwaWaziri alifika katika Kata ya Ruaha Mbuyuni na akaona jinsimatatizo ya maji yanavyosumbua. Wananchi wamekuwawakipata kipindupindu kila mwaka na yeye aliahidi mambomakubwa. Sasa je, ni lini wananchi wa Ruaha Mbuyuniambao wanategemea kupata kituo cha afya watapata majipale?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hiloMheshimiwa Naibu Waziri, Wizara ya Maji, MheshimiwaAweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote nimpongeze Mbunge wa Kilolo,Mzee wangu, kwa kazi kubwa sana anayoifanya, lakinitulipata nafasi ya kufika Ruaha Mbuyuni. Changamotokubwa tuliyoiona kwa Wahandisi wetu walitengeneza tenkila maji lakini hawakuwa na chanzo cha maji. Kwa hiyotuliwaagiza watu wa rasilimali za maji wa bonde lile waendena wameshafanya tafiti kikubwa tunawaagiza watu waDDCA waende kuchimba kisima haraka katika kuhakikishamradi ule unafanya kazi kwa wakati.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bura.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza. Kwa kuwa ongezeko la watu na hasa Jiji laDodoma limekuwa kubwa baada ya Makao Makuu kuhamiaDodoma, je, Serikali ina mpango kabambe au mkakati ganiwa kuhakikisha kwamba maji ya Ziwa Victoria yaliyofikaTabora yanafika Dodoma kuwasaidia wananchi wa Dodomakutokana na upungufu wa maji?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri,majibu kwa swali hilo.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Bura kwaswali lake zuri sana, sisi kama Wizara ya Maji tunatambuakabisa sasa hivi kumekuwa na ongezeko kubwa sana katikaMkoa huu wa Dodoma, lakini jitihada kubwa ambazotulizozifanya sasa hivi, uzalishaji wetu zaidi ya lita milioni 55,lakini mahitaji lita kama milioni 44. Kwa hiyo, tuna maji kwakiasi kikubwa, kubwa ambalo tunaloliona hapa ni suala zimala usambazaji, lakini itakapobidi tutafanya kila jitihada katikakuhakikisha tunatatua tatizo la maji na wananchi waDodoma wasipate tatizo hilo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Selasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kutokana na shida kubwa ya maji hapa nchini,Bunge hili lilitengeneza, liliunda Wakala wa Maji, sasaningependa kujua, je, tayari, Serikali imeshatengeneza kanuniza huo Wakala na kama zitagawiwa kwa Wabunge?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu Mheshimiwa NaibuWaziri, Wizara ya Maji, Kanuni ziko tayari na lini zitagawiwa.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nilipongeze sana Bunge lako Tukufukutokana na jitihada kubwa walizofanya kupitisha Muswadawetu, pia kwa namna ya kipekee tumshukuru sanaMheshimiwa Rais. Baada ya Bunge kupitisha Muswada ule,Mheshimiwa Rais ameshasaini na imeshakuwa Sheria, sisikama Wizara ya Maji, tutazileta kwa haraka kanuni zile ilituanze utekelezaji kwa haraka sana. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Amar.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Napenda nimuulize Waziri, kwa kuwa kuna mradimkubwa wa maji kutoka Nyamtukuza katika Wilaya yaNyang’hwale, kupita Kakora, Kitongo, Ikangala, Kharumwa,Izunya hadi Bukwimba ambao umekuwa ukisuasua kwamuda mrefu, lakini Serikali ikiwa ikitoa pesa. Je, ni lini sasa

Page 28: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

mradi huu utakamilika na namwomba Mheshimiwa Waziribaada ya Bunge hili aende akauone mradi huo kwa niniunaendelea kusuasua?

MWENYEKITI: Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa NaibuWaziri, Wizara ya Maji, Mheshimiwa Aweso.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote kwanza nitumie nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Mbunge. Kubwa pamoja na mradihuo, lakini tumeshalipa zaidi ya bilioni moja na milioni miasaba certificate yake kwa Mkandarasi anayedai, ili mradiusikwame.

Kuhusu kusuasua kwa mradi, sisi kama Wizara ya Maji,Wahandisi ama Wakandarasi wababaishaji tutawawekapembeni, nataka nimhakikishie kabla ya Bunge tutakwendaNyang’hwale katika kuhakikisha tunaenda kuukagua mradiule na ikibidi kama Mkandarasi hana uwezo wa kutekelezamradi huo tutamwondoa mara moja. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge nimetumiamuda mrefu kwa swali hil i kwa sababu nafahamuchangamoto ya maji tuliyonayo nchini.

Waheshimiwa tunaendelea swali l inalofuatalinaulizwa na Mheshimiwa Hamidu Hassan Bobali, Mbungewa Mchinga, linaelekezwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Na. 73

Kupandisha Hadhi Chuo cha Kumbukumbu yaMwalimu Nyerere

MHE. KIZA H. MAYEYE (K.n.y. MHE. HAMIDU H. BOBALI)aliuliza:-

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni chamuda mrefu na pia kimetumika kuandaa viongozi wa nchiyetu na nchi jirani:-

Page 29: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

(a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhiChuo hicho kuwa Chuo Kikuu?

(b) Je, kwa nini Serikali haipeleki fedha za maendelokatika Chuo hicho kama zilivyopangwa?

MWENYEKITI: Ahsante. Kwa niaba, Mheshimiwa NaibuWaziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA - K.n.y. WAZIRIWA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Napendakujibu swali la Mheshimiwa Hamidu Hassan Bobali Mbungewa Mchinga, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Kumbukumbuya Mwalimu Nyerere ni Taasisi ya Elimu ya juu iliyoanzishwana Sheria Na.6 ya mwaka 2005. Chuo kinatekeleza majukumuyake makuu kuendesha mafunzo ya Kitaaluma katika faniya Sayansi ya Jamii katika ngazi za Cheti, Stashahada,Shahada ya Kwanza na umahiri. Aidha, Chuo kinaendeshamafunzo ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora, Mafunzo yaElimu ya kujiendeleza, kinafanya tafiti na kinatoa ushauri kwaumma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Serikali kwasasa si kupandisha hadhi Vyuo vilivyopo, bali ni kuboreshamazingira ya Vyuo Vikuu vilivyopo kwa kukarabati na kujengamiundombinu, kwa kuwa na vifaa vya kisasa na kuwa naWahadhiri wengi zaidi wenye Shahada ya Uzamivu. Hatuahizo zitawezesha kuongeza nafasi za Udahili na kuimarishaubora wa elimu itolewayo. Jitihada zinazofanyika katika Chuocha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni pamoja nazifuatazo:-

(i) Kupata wataalam zaidi katika fani zenyeuhaba ambapo Chuo kimepeleka wataalam 33 kwendakusoma Shahada za Uzamivu; na

Page 30: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

(ii) kuongeza miundombinu ya Chuo kama vileujenzi wa vyumba vya madarasa na kumbi za mihadharaambapo, ujenzi wa ukumbi wenye uwezo wa kuchukuawanafunzi 330 kwa wakati mmoja umekamilika nakuzinduliwa tarehe Mosi Aprili, 2019.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwaikipeleka fedha za maendeleo katika Chuo chaKumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kadri fedha hizozinavyopatikana, mfano mwaka 2017/2018, Serikali ilitoafedha zote zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maendeleokiasi cha shilingi Bilioni 1 nukta 89 ambazo zilitumikakukamilisha ujenzi wa hosteli ya wanafunzi, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiza Mayeye.

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.Kwanza, nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yakemazuri, lakini ningeomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.Swali la kwanza, Chuo hiki cha Mwalimu Nyerere kilijengwana Wazalendo wa nchi hii, tena kabla ya Uhuru na MwalimuNyerere alikipa jina ya Kivukoni lenye maana ya eneo lililopoChuo kilipo. Je, sasa Serikali haioni umuhimu wa kukipandishahadhi Chuo hiki kuwa Chuo Kikuu, ili tumuenzi Baba wa Taifa,ukizingatia kwamba Barani Afrika kuna nchi nyingi ambazowamezipa majina ya Waasisi kama Mandela South Africa,Kenyata Kenya lakini Nkurumah Ghana? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Chuo hiki,Mheshimiwa Waziri kuna bweni ambalo limejengwa tokamwaka 2013 kwa ajili ya wanafunzi hawa wa Shahada yaUzamivu, lakini mpaka sasa halijakamilika. Je, ni kwa ninihalijakamilika na ni lini litakamilika na nini kauli ya Serikali katikakukamilisha bweni hilo. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayoMheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa, kwa niaba.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA - K.n.y. WAZIRIWA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA): Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya MheshimiwaKiza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzalinaenda kwenye majibu ya swali langu la msingi, tumesemampango wa Serikali kwa sasa si kupandisha hadhi Vyuo.Vilevile tukubaliane kwamba ili kupandisha Chuo kuwa nalevel ya Chuo Kikuu, kuna vitu vingi inabidi kuzingatia, kwanzainabidi uunde Kikosi kazi cha Wataalam waende wapitieMitaala, aina ya Walimu kama wanatosha, eneo lenyeweHatimiliki ya eneo lao. Kwa hiyo kuna vitu vingi vya kuangalia,lakini kwa sababu tunazungumza kuna vitu vingi vya kufanya,tumesema tuboreshe hivi vilivyopo, itakapofika wakati, Serikaliikaona haja ya kufanya hivyo, tutafanya hivyo kwa kuzingatiataratibu na sheria za nchi ambazo zimewekwa kwa ajili yakazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, anasemakuna bweni ambalo halijakamilika, naomba hili tulichukuetulifanyie kazi, lakini kwa kweli kama kuna bweni lipo pale nakuna upungufu wa mabweni, tutafanyia kazi ili liwezekukamilika.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Halima Bulembo.

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii, wote tunatambua jambokubwa linalotuweka Watanzania pamoja ni kutokuwa naubaguzi, lakini mikopo ya wanafunzi wa Chuo Kikuu imekuwaikitolewa kwa ubaguzi. Mfano, mimi nimepata division onenasoma Feza, mwenzangu kapata division one anasomaMsalato, atakayepewa mkopo ni yule anayetoka Msalatokwa maana ya kwamba wa Feza ni wa kishua, wa Msalatoni maskini, huu ni ubaguzi wa hali juu, tunajua hustleszinazotumiwa na wazazi kuwapeleka watoto wao shule nzuritu na si kwamba wana pesa nyingi sana. Je, Wizaraitakubaliana na mimi umefika wakati sasa wa kubadilisha

Page 32: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

kigezo cha kupata mikopo na kigezo kikuu kiwe ni ufaulu wamwanafunzi badala ya kwamba huyu ana mahitaji zaidi yamwenzie? Nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu, nimekuona NaibuWaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI(K.n.y. NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA):Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la MheshimiwaHalima kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi vigezo vilivyowekwani hasa vinazingatia hali halisi ya uhitaji wa mwanafunzikwamba mwanafunzi mwingine hana uwezo. Kwa hiyo kamahana uwezo ndiyo atakayesaidiwa kwanza. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nnauye.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombautulivu.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.Pamoja na majibu mazuri ya msingi, kwenye swali la Kivukoni,mimi ni moja ya product ya Kivukoni. Kwa kuwa historia yaChuo hiki kilikuwa ni Chuo cha ku-train Viongozi na kutokanana changamoto tunazoziona katika utekelezaji wa majukumuyao hasa Viongozi kwenye Local Government, wilayani,Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa.

Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wakukirudishia chuo hiki kazi yake ya msingi ya kufundishaviongozi skills za namna ya kutekeleza majukumu yao kwenyemaeneo yao na nakubaliana na uamuzi wa Serikali wakutokukipandisha hadhi badala yake tukibadilishie sasamajukumu kitoke kwenye ku-train social sciences kiende

Page 33: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

kwenye ku-train viongozi wetu kwa sababu kwa kwelichangamoto ya utekelezaji wa majukumu yao kwenyemaeneo yao imekuwa ni kubwa sana?

MWENYEKITI: Ahsante, majibu kwa swali hilo kwa kifupitu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA - K.n.y. NAIBUWAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa niaba ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, naomba nimjibu Mheshimiwa NapeNnauye swali lake la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaamini kwamba Chuohiki kimeanzishwa kwa majukumu aliyoyataja MheshimiwaMbunge na yataendelea kufanyika hivyo, sasa kama kunaupungufu umeonekana, hilo ni jambo la kulichukua nakwenda kulifanyia kazi, lakini tunaamini kwamba kazi yamsingi iliyoanzishwa kwayo inaendelea kufanyika. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea WaheshimiwaWabunge, swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa SusanPeter Massele, Mbunge wa Viti Maalum na badolinaelekezwa kwa Wizara hiyo hiyo, kwa Mheshimiwa Waziriwa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Na. 74

Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Umma katika Mkoa wa Mwanza

MHE. SUSAN P. MASSELE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Chuo Kikuucha Umma au Vyuo Vikuu vya Umma vyenye hadhi ya juukatika Mkoa wa Mwanza?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo,Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa kwa niaba.

Page 34: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOANASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA - K.n.y NAIBUWAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naombakujibu swali la Mheshimiwa Susan Peter Massele, Mbunge waViti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimuwa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu katika kuandaarasilimali watu itakayochangia katika kufikia azma yaTanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Kwa sasa Serikali inatekeleza Mpango wa kuboresha VyuoVikuu na Taasisi za Elimu ya Juu zilizopo kwa kukarabati nakujenga miundombinu mipya pamoja na kuongeza vifaa vyakisasa vya kufundishia na kujifunzia ili kuongeza nafasi zaudahili na kuimarisha ubora wa elimu itolewayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa tuna idadi ya VyuoVikuu 11, Vyuo Vikuu vishiriki viwili na Taasisi za Elimu ya juu 32zinazotoa Elimu ya juu nchini. Mkoa wa Mwanza una matawiya Taasisi ya Elimu ya juu za Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi yaTeknolojia Dar es Salaam (DIT). Aidha, Mkoa una Tawi la Chuokikuu Huria cha Tanzania (OUT) mbali na Vyuo Vikuu vyaMtakatifu Augustino na Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Bugandoambavyo vinamilikiwa na taasisi binafsi. Vyuo Vikuu na Taasisiza Elimu ya Juu ni za Kitaifa ambapo hupokea wanafunzikutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali inaboreshamazingira vya Vyuo vilivyopo lakini kama itaona kunaumuhimu wa kuongeza Vyuo vingine itafanya hivyo katikamaeneo yatakayoonekana yanafaa. Wito wangu kwawananchi wa Mkoa wa Mwanza na maeneo mengine nikuendelea kutumia Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juuzilizopo katika Mkoa wa Mwanza. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Massele.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

MHE. SUSAN P. MASSELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza. Pamoja na majibu ya Serikali, ya Waziri,ambayo yanavunja moyo kabisa, kwa sababu hawajatoacommitment ni ni lini watamaliza huo ukarabati na ukizingatiaVyuo hivyo alivyovitaja viko kwenye hali mbaya sana naukizingatia pia Jiji la Mwanza, ni Jiji ambalo linakua kila siku.Vyuo vingine viko uchochoroni kabisa ambapo ni mazingiramabaya kwa wanafunzi na Wakufunzi katika kufanya kazi.Sasa katika majibu haya nina maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, mwaka janatuliona Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU)ikivichukulia hatua Vyuo Vikuu binafsi ambavyo havikuwa navigezo vya Vyuo Vikuu na kuviacha Vyuo Vikuu vya Ummaambavyo vilevile vilikuwa havina vigezo vya kuwa Vyuo Vikuukama alivyojibu kwenye swali la msingi. Je, Waziri haonikwamba zoezi hili lilikuwa linagandamiza Vyuo Vikuu vyabinafsi ambavyo vinatoa nafasi kubwa kwa wanafunziambao wamekosa nafasi kwenye Vyuo vya Umma na kupatanafasi?

MWENYEKITI: Sema tu straight.

MHE. SUSAN P. MASSELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, swalila pili, kwa kuwa Serikali ina ndoto ya Tanzania ya Viwandani lini sasa itajenga, Polytechnic College katika Mkoa waMwanza, ambapo itatoa ujuzi kwa ajili ya mahitaji ya viwandaukiachilia mbali Chuo cha … (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, inatosha. Mheshimiwa NaibuWaziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwaniaba.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA K.n.y. WAZIRI WAELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA): Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya MheshimiwaSusanne Maselle, kama ifuatavyo:-

Page 36: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwamba zoezi hililililofanyika lilikuwa la ugandamizi na ndiyo maana vyuoambavyo vilionekana vina matatizo havijalalamika, vimetiimasharti, vimeboresha vyuo vyao na wale ambaowamekamilisha wamekabidhiwa kuendelea kufanya kazi.Kwa hiyo, hii siyo kweli lakini na vyuo vya umma piavinazingatia utaratibu na ubora wa elimu kwa kadri yamiongozo iliyotolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, tumesemania ya Serikali si kuanzisha vyuo kila mkoa bali ni kuhakikishavyuo vilivyopo vinaendelea kuboreshwa kwa kuongezamiundombinu na wataalam waliobebea katika nyanja hizo.Vikiimarishwa vinatosha kutoa wataalam kwenye viwandana kubaki na kutumia utaalam wao nje ya nchi yetu.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa George MalimaLubeleje, Mbunge wa Mpwapwa linaelekezwa kwaMheshimiwa Waziri wa Nishati.

Na. 75

Kuvipatia Umeme vijiji vya Jimbo la Mpwapwa

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:-

Katika Jimbo la Mpwapwa Vijiji vya Mkanana,Nalamilo, Kiboriani, Igoji Kaskazini, Mbori, Tambi, Nana, Majani(Mwenzele), Mafuto, Kiegea, Kazania, Chimaligo, Mbugani,Chilembe, Mazaza, Mwanjili, (Makutupora) na Chibwegelehavina huduma ya umeme:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuvipatia hudumaya umeme vijiji hivyo?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu ya swali hilo, NaibuWaziri, Wizara ya Nishati, Mheshimiwa Mgalu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Page 37: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George MalimaLubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya vijiji 31 katika Wilayaya Mpwapwa vitapatiwa umeme kupitia Miradi ya UmemeVijijini inayoendelea. Kupitia Mradi wa REA III Mzunguko waKwanza unaoendelea jumla ya vijiji 14 vitapatiwa umeme.Hadi sasa Viji j i vya Mbori, Tambi, Mnase, Chuo chaMaendeleo ya Wananchi Mpwapwa, Kimangai na ChunyuSekondari vimepatiwa umeme kupitia Mradi wa KusambazaUmeme Vijijini (REA III) Mzunguko wa Kwanza unaoendeleakutekelezwa hivi sasa na mkandarasi Kampuni ya A2Z IfraEngineering Limited kutoka nchini India. Kazi za mradi katikaWilaya ya Mpwapwa zinahusisha ujenzi wa njia za umemewa msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 9.45, njiaza umeme wa msongo kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita68, ufungaji wa transfoma 34 za kVA 50 na 100, pamoja nakuunganisha umeme kwa wateja wa awali 1,148 na gharamaza mradi ni shilingi bilioni 2 na milioni 600.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vilivyosalia ikiwa nipamoja na Mkanana, Ngalamilo, Kiboriani, Nana, Majami,Mafuto, Kiegea, Kazania, Chimaligo, Mbugani, chihembe,Mazaza, Mwanjiri na Chibwegerea vitapatiwa umeme katikaMzunguko wa Pili wa Mradi wa REA III unaotarajiwa kuanzaJulai, 2019 na kukamilika Juni, 2021. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Lubeleje.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninamaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwaline inayopeleka umeme Wilaya ya Mpwapwa inahudumiapia Wilaya za Chamwino, Kongwa, Gairo na Mpwapwayenyewe na hivi karibuni line hiyo imeongezwa Tarafa yaMwitikila, Mpwayungu na Nagulo. Kwa hiyo, line hii imekuwaoverloaded na kusababisha kukatikakatika kwa umeme

Page 38: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

katika Mji wa Mpwapwa. Je, mko tayari kujenga line mpyaya umeme kuanzia Zuzu Main Station itakayopita KikomboStation, Kiegea mpaka Mbande ambako mtajengasubstation na pale ijengwe line moja kwa moja kuelekeaMpwapwa itakayojulikana kama Mpwapwa fider?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa vijijivya Mima, Sazima, Igoji Mbili, Isalaza, Chamanda na Iwondotayari vinapata huduma ya umeme lakini mkandarasi alirukaKijiji cha Igoji Moja na tatizo la sasa ni transfoma. Je, uko tayarikupeleka transfoma katika Kijiji cha Igoji Moja ili wananchiwa pale waweze kupata huduma ya umeme? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayomawili, Mheshimiwa Waziri Wizara ya Nishati, kwa kifupi tu.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanapenda nimpongeze sana Mheshimiwa Lubeleje kwakufuatilia masuala ya nishati kwa wananchi wa Mpwapwa,hongera sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na maswali mawiliya nyongeza ya Mheshimiwa Lubeleje la kwanza, ni kweliumeme unaokwenda Mpwapwa unatoka Zuzu ambapo niumbali wa kilomita 120 ni mbali sana. Mpango uliopo nikwamba sasa hivi Serikali kupitia TANESCO tumeanzautekelezaji wa kujenga line mpya ya kutoka Zuzu kupitaKikombo ambapo ni kilomita takribani 42 na kutoka Kikomompaka Msalato kilomita 45 lakini kwenda Mpwapwa tutatoasasa Kikombo kupita Kiegea kutoka Kiegea tunajengasubstation Mbande na pale Mbande kwenda mpakaMpwapwa itakuwa takribani kilomita 70. Kwa hiyo, wananchiwa Mpwapwa sasa wataanza kupata umeme kutokaMbande ambao utakuwa ni mkubwa kuweza kuwahudumiawananchi wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la pili, nikweli tumepeleka umeme kwenye vijiji takribani 32 Mpwapwalakini viko vijiji vya Mkanana, Mbande pamoja na maeneoaliyoyataja kama Igoji Moja au Igoji Kaskazini, nimpe taarifa

Page 39: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

Mheshimiwa Mbunge Igoji Kaskazini au Igoji Mojawakandarasi wameanza kazi tangu juzi na kufikia Jumapiliijayo watawasha umeme na watafunga transfoma nne zakilovoti 50 na kilomita zingine mbili wataweka na kufungatransfoma mbili za kilovoti 120 na wataunganisha wateja waawali 78 wa phase one na wateja 9 wa phase three. Kwahiyo, Igoji itakwenda kuwashwa umeme Jumapili ijayo.Nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea,swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa Sikudhani YassinChikambo, Mbunge wa Viti Maalum, linaelekezwa kwaMheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Na. 76

Kuwajengea Uwezo Wakulima na Wafugaji

MHE. DAIMU I. MPAKATE (K.n.y. MHE. SIKUDHANI Y.CHIKAMBO) aliuliza:-

Idadi ya watu nchini inazidi kuongezeka sambambana ongezeko la mahitaji ya ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwajengea uwezowakulima na wafugaji ili kuendeleza shughuli zao kwa tija nakuwaondolea adha wanazozipata?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, NaibuWaziri Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Ulega.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali laMheshimiwa Sikudhani Yassin Chikambo, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara yaMifugo na Uvuvi imeendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu

Page 40: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

ufugaji bora na uzalishaji wa malisho kupitia mashambadarasa ili kuwajengea uwezo wa kufuga kwa tija pamoja nakuendeleza malisho katika maeneo yaliyotengwa. Lengo lakutoa elimu hii ni kuhakikisha wafugaji wanaachana naufugaji wa kuhamahama na kutulia kwenye eneo moja lenyemalisho yaliyoboreshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya mashamba darasa265 yameanzishwa katika Halmashauri mbalimbali nchiniambapo wafugaji wanaweza kujifunza jinsi ya kuzalishambegu na malisho bora ya mifugo ili kuongeza upatikanajiwa uhakika wa mbegu na malisho ya mifugo. Aidha, katikamwaka wa 2018/2019, Serikali imeongeza hekta 2,500katika mashamba yake kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu zamalisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imepanga kutoamafunzo rejea kwa wafugaji na Maafisa Ugani nchi nzimajuu ya ufugaji bora unaozingatia ukubwa wa ardhi iliyopo.Mafunzo hayo tayari yameanza kutolewa katika Halmashauriya Simanjiro, Mkoani Manyara na Halmashauri ya Wilaya yaKaliua, Mkoani Tabora na kuendelea kutolewa kwa awamukatika Halmashauri zote nchini. Aidha, Serikali imeendeleana juhudi za kuwasaidia wafugaji kukabiliana na tatizo la majikwa ajili ya mifugo kwa kuchimba malambo 1,381 na visimavirefu 103 katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Mawaziri naneiliyoundwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania ili kutafuta suluhu ya migogoro ya matumizi yaardhi iliyoko nchini tunaamini itakuja na mapendekezochanya ambayo yatapelekea kuondoa migogoro na adhazinazowakabili wafugaji na wakulima nchini.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mpakate.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu mazuri kutoka kwa Naibu Waziri lakininina maswali mawili ya nyongeza.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwaSerikali imekiri kwamba itatoa mafunzo kwa wafugaji naMaafisa Ugani katika Halmashauri zetu, je, ni lini itatoamafunzo hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduruambayo wafugaji wanaongezeka kwa kasi kubwa sana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwaHalmashauri ya Wilaya ya Tunduru imetenga maeneo kwamaana ya vitalu vya wafugaji mbalimbali vinavyofikia 100;na kwa kuwa wakulima wengi wameshapewa maeneo hayolakini mpaka sasa hawajaenda. Nini kauli ya Serikali kuhusuhawa wafugaji ambao wameshindwa kwenda kwenyemaeneo yale ya wafugaji na kuendeleza migogoro nawakulima mbalimbali kwa mifugo yao kula mazao yawakulima? Ahsante? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayoNaibu Waziri Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Ulega.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Mpakate, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni linitutakwenda kupeleka mafunzo haya Wilayani Tunduru?Naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba timu yetuiliyoko Kaliua ikitoka huko itakwenda Tunduru na Halmashaurizingine katika nchi yetu kwa ajili ya kutoa elimu hii kwawafugaji na Maafisa Ugani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili analotaka kujuani namna gani na tunatoa kauli gani kwa wale waliopatavitalu. Kwanza nataka niwapongeze sana viongozi wote wakule Wilayani Tunduru kwa kazi kubwa waliyoifanya ya mfanoya kuandaa vitalu wao wenyewe Halmashauri na kuvigawakwa wafugaji kwa ajili ya kufanya kazi ya ufugaji iliyo na tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kauli ya Serikali ni kamaifuatvyo: Wafugaji wote waliopewa vitalu hivi na wakaachakuvitumia kwa wakati, tunawapa tahadhari kwamba

Page 42: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

watanyang’anywa na watapewa wafugaji wengine waliotayari kufanya kazi hii kwa ufanisi.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Shally Raymond.

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius KambarageNyerere Baba wa Taifa alisambaza mitamba bora katikamaeneo yote ambayo yanafanya zero grazing. Kwa kuwa nimuda mrefu sasa na cross breeding imeshafifisha mazao yaleni lini sasa Serikali itaweza kuboresha na kutawanya mitambabora, vifaranga bora vya kienyeji na vifaranga bora vyasamaki katika maeneo ya wafugaji kama Kilimanjaroambapo kuna wanawake wengi sana ambao niwafugaji?(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, NaibuWaziri, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Ulega.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa ShallyRaymond, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza swali ni zuri sana juuya Serikali kuhakikisha kwamba tunasambaza mitamba borakwa wafugaji hasa akina mama wa Mkoa wa Kilimanjaro naTaifa zima. Progamu hii Serikali tunayo kupitia mashamba yetuya mifugo yaliyosamba nchi nzima tunafanya kazi hii. Kwamfano tu ni kwamba hivi karibuni kupitia dirisha letu la sektabinafsi tumewawezesha Ushirika wa Wafugaji wa Ng’ombewa Maziwa Mkoani Tanga yaani TBCU, wamekopeshwa pesana Benki yetu ya Kilimo ili waweze kununua mitamba bora300 ambapo kufikia tarehe 30 ya mwezi huu mitamba ileitaenda kusambazwa kwa wafugaji wote wa Mkoa waTanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, tuko tayarikuhakikisha kwamba na wafugaji wengine kote nchiniwanapata fursa hii. Shime wafugaji wote wa ng’ombe wamaziwa, kuku hata wale wa samaki wajiunge katika vikundi

Page 43: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

ili waweze kutumia fursa hii inayopatikana kupitia dirisha letula ukopeshaji la Benki ya Kilimo.

MWENYEKITI: Ahnsate. Swali letu la mwisho kwa leolinaulizwa na Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbungewa Tunduma na linaelekezwa kwa Mheshimiwa Waziri waKilimo.

Na. 77

Serikali Kuunga Mkono Tamko la Kilimo Ndio Utiwa Mgongo

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaunga mkono tamko la Kilimo ndiyoUti wa Mgongo wa Taifa kwa vitendo?

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, NaibuWaziri wa Kilimo, Mheshimiwa Innocent Bashungwa.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. INNOCENT L.BASHUNGWA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa FrankGeorge Mwakajoka, Mbunge wa Jimbo la Tunduma, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu Serikaliinatambua na inaunga mkono tamko la Kilimo ni Uti waMgongo kwa Taifa. Umuhimu wa sekta ya kil imounajidhihirisha katika viashiria mbalimbali vya kiuchumi nakijamii kama vile mchango wa kilimo katika ajira, pato la Taifa,usalama wa chakula na malighafi za viwandani. Takribaniasilimia 65.5 ya wananchi wameajiriwa katika sekta ya kilimo,asilimia 28.7 ya pato la Taifa hutokana na sekta ya kilimo,mazao ya chakula huchangia kiasi cha asilimia 65 ya patola Taifa litokanalo na kilimo. Zao la mahindi huchangia zaidiya asilimia 20 ya pato la Taifa litokanalo na kilimo, mazao ya

Page 44: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

chakula na biashara yanachangia asilimia 70 ya kipato katikamaeneo ya vijijini. Aidha, sekta ya kilimo ni muhimu katikamikakati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini kwakuchangia takribani asilimia 65 ya malighafi za viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inayo mikakati namipango inayolenga kuimarisha sektya kilimo ili kuongeza tijana uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na kuwapatiawakulima masoko ya uhakika. Sera, mikakati na mipangoinayotekelezwa ni pamoja na Sera ya Taifa ya Kilimo yamwaka 2013, Programu ya Kuendeleza Sekta ya KilimoAwamu ya II (ASDP II) pamoja na sera, mikakati na mipangomingineyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya jitihada madhubutiya kutambua Kilimo ndiyo Uti wa Mgongo ni kuanzishwa kwaBenki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ambayoinatoa mikopo ya riba nafuu ya asilimia 8 tu. Aidha, Serikaliimeendelea kupunguza ada, tozo na kodi katika kilimo,kuimarisha huduma za utafiti ikiwa ni pamoja na kuanzishaTaasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na kuimarishaushirika ili uweze kuwezesha na kusimamia masoko ya mazaoya kimkakati.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuulizamaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la MKUKUTA na Ilaniya Chama cha Mapinduzi sekta ya kilimo ilikuwa ikue kwaasilimia 8 ndani ya miaka 10 lakini uhalisia kuanzia mwaka2011 na 2015 sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 3.4. Ndani yamiaka ya Awamu ya Tano katika miaka yake mitatu ya bajetisekta ya kilimo imekua kwa wastani wa asilimia 1.9. Uhalisiaunajionesha kwenye bajeti zake, bajeti ya mwaka 2016/2017…

MWENYEKITI: Uliza swali Mheshimiwa.

Page 45: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, mwaka 2016/2017 tulitenga shilingi bilioni 101katika sekta ya kilimo lakini fedha iliyotoka ilikuwa ni shilingibilioni 3 peke yake. Pia mwaka 2017/2018 tulitenga shilingibilioni 150 ikatoka shilingi bilioni 24. Swali, hii ndiyo tafsiri yaKilimo ni Uti wa Mgongo katika Taifa letu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wote tunajuakwamba Watanzania wengi wanaohitimu vyuo vikuu katikaTaifa hili ni 800,000 lakini watu ambao wanaajiriwa kwenyesekta rasmi karibu watu 20,000 tu ambapo 780,000wanakwenda kuajiriwa kwenye sekta ya kilimo. Hata hivyo,sekta ya kilimo kumekuwa na tatizo la uwekezaji, Serikali inampango gani wa kuhakikisha kwamba wahitimu hawawanapewa mikopo ili wajiajiri na wainue maisha yao pamojana kuchangia pato la Taifa? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo, kwakifupi Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Bashungwa.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. INNOCENT L.BASHUNGWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibumaswali mawili ya Mheshimiwa Mwakajoka, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza MheshimiwaMwakajoka anasema kwamba sekta ya kilimo imekua ikikuakwa asilimia ndogo kinyume na matarajio. Pamoja namipango mizuri ya Serikali katika kukuza sekta ya kilimo nchinilakini kuna mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaathiriproductivity ya kilimo nchini. Hata hivyo, Serikali inayomipango madhubuti kupitia Mpango wa Kilimo wa ASDP IIkama nilivyotaja kwenye majibu yangu ya msingi, kuhakikishatunatumia ardhi vizuri kwa kilimo, tunazingatia matumizimazuri ya utumiaji wa maji ili kwenda kwenye kilimo chaumwagiliaji yaani drip irrigation pamoja na mikakati mingineambayo tumeiweka ndani ya Serikali kupitia Mpango huuwa Maendeleo ya Kilimo wa ASDP II.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili la MheshimiwaMwakajoka ni kwamba tuna vijana wengi ambao

Page 46: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

wanahitimu kwenye vyuo vikuu lakini kuna changamoto yaajira; na wanaoenda kwenye kuajiriwa kwenye sekta ya kilimoni wachache, asilimia ni ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali katikahil i ni kuhakikisha tunaleta mageuzi ya kil imo nakufungamanisha kilimo na viwanda. Kama unavyojuaMheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge, Serikaliinaendelea kufanya jitihada hizi kuangalia kilimo kamanilivyosema kwenye majibu yangu ya msingi, asilimia 65 yamalighafi za viwandani zinategemea mazao yetu ya kilimo.Sasa mkakati wa Serikali ni kuongeza hizi asilimia ili tuwezekufungamanisha uchumi wa viwanda na kilimo.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge,muda wetu ndiyo huo mnauona wote.

Wageni wetu waliopo Bungeni asubuhi hii; wageniwaliopo jukwaa la Mheshimiwa Spika, wageni 30 waMheshimiwa Spika waliokuja kwa ajili ya Semina kuhusuMasuala ya Albino wakiongozwa na Ndugu Delivinus Mosha.Hebu msimame wageni wetu hao; karibuni sana ndugu zetu.Nitakuja kusema baadaye Waheshimiwa Wabunge, kunatangazo mahsusi kwa hilo. (Makofi)

Wageni wengine wa Mheshimiwa Spika ni viongozikutoka Benki ya CRDB ambao ni Dkt. Bennett Bankobeza,Mkuu wa Huduma za Serikali CRDB Makao Makuu; mwingineni Ndugu Suzan Shuma, Meneja Mwandamizi Serikali za MitaaCRDB Makao Makuu na watatu ni Ndugu Chabu Miswaro,Mkurugenzi wa Tawi la CRDB Dodoma. Huyu ni maarufu,mnamfahamu sana Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Tuna wageni 32 wa Mheshimiwa Naibu Spika,Mbunge, ambao ni wafanyakazi wa EFM Radio na ETV nawafanyakazi wa Benki ya NBC wakiongozwa na MheshimiwaMohammed Lukwili, Meneja Mkuu wa EFM na ETV pamojana Ndugu Jesca Mwanyika, Meneja Mawasiliano na Matukioya EFM na ETV na Ndugu Hellen Mzava, Meneja Rasilimaliwatukatika vituo hivyo.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Wageni wengine wawili wa Mheshimiwa Naibu Spikani kutoka National Bank of Commerce (NBC) ambao niMeneja Mawasiliano Sekta ya Umma NBC Bank NduguPascas Mhindi na Kaimu Mkurugenzi Wateja Binafsi NBC BankNdugu Gaudence Shawa. Karibuni sana wageni wetu.

Halafu tuna wageni wa Waheshimiwa Wabunge,wageni 13 wa Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe,Mbunge, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezoambao ni mmoja wa watunzi wa Wimbo wa Afrika MasharikiNdugu Joseph Mugango ambaye ameambatana na bintiyake Ndugu Johanitha John Mugango. Karibuni sana.Hongera sana kwa kazi nzuri uliyoifanya. (Makofi)

Wageni wengine 10 ni kutoka Kamati ya Maudhui yaMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiongozwa naMwenyekiti wa Kamati hiyo Ndugu Valarie Msoka.Mheshimiwa Msoka na timu yako karibuni sana. Waheshimiwawengi mnamfahamu Ndugu Valarie Msoka kwa mamboyake, mnayajua sana. Mliokuwa kwenye Bunge Maalum laKatiba mnamkumbuka sana. (Makofi)

Wengine ni Waheshimiwa saba wageni waMheshimiwa Cosato Chumi, ambao ni vijana wahitimu waVyuo Vikuu ambao wameamua kujiajiri na kujiinua kiuchumikwa kufuga kuku na nyuki kutoka Mafinga Mkoani Iringa,wakiongozwa na ndugu Loveness Hiluka. Mko wapi vijana?Hongereni sana, ninyi ni vijana wa mfano, tunapambana nahali zetu. (Makofi)

Wageni 12 wa Mheshimiwa Angelina Malembeka,ambao ni wanafamilia, Viongozi wa CCM Zanzibar nawanafunzi kutoka Zanzibar wakiongozwa na mume wakeNdugu Makame Ame Ussi. Karibuni sana ndugu zetu. TunayeAngelina pale anafanya kazi nzuri tu. (Makofi)

Tunao wageni 70 wa Mheshimiwa Daniel Mtuka,ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)wakiongozwa na Ndugu Meshack William Madole. Karibunisana.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Wageni 15 wa Mheshimiwa Ritta Kabati, ambao nikutoka Taasisi ya Jamii Tanzania wakiongozwa na Mwenyekitiwa Taasisi hiyo ndugu Richard Nnko. Karibuni sana wageniwetu. (Makofi)

Wengine ni wageni 17 wa Mheshimiwa BoniventuraKiswaga, ambao ni Katibu wa Jimbo Kata ya Kisesa pamojana wanafunzi wa UDOM wakiongozwa na Katibu wa MbungeNdugu Yambijonas Masuka, wako wapi karibuni wageni wetu.(Makofi)

Wageni waliopo Bungeni kwa ajili ya mafunzo tunayeNdugu Kondwani Nyirenda kutoka Mkoani Shinyanga,ambaye amekuja kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi zake.Karibu sana.

Tunao wageni watatu kutoka Taasisi ya SkyfreeInternational ya Arusha ambao ni Ndugu Samuel Malugu,Ndugu Mariam Ally na Ndugu Adilla Chigomelo. Pia tunaowanachuo 10 kutoka Chuo Kikuu cha UDOM wakiongozwana Ndugu Heri Daimon, karibuni. (Makofi)

Wengine ni wanafunzi 80 na walimu wawili kutokaShule ya Sekondari ya Miyuji iliyopo Jijini Dodoma ambaowamekuja kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi kwa leo.Karibuni sana kwa mafunzo. (Makofi)

Vile vile tunaye mgeni wa Mheshimiwa OmaryMgumba, Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, mgeni wake NduguCharles Mboma ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Kata yaMkambarani Morogoro, karibu sana.

Nilianza na hawa wageni wetu kwenye jukwaa laMheshimiwa Spika. Sasa ninalo tangazo kutoka kwa Katibuwa Bunge. Napenda niwatangazie Waheshimiwa Wabungewote kuwa Jumapili tarehe 14 Aprili, saa 5.00 asubunikutakuwa na Semina kwa Wabunge wote kuhusu Uelewa waMasuala ya Ualbino. Ndiyo maana hawa wenzetu wakohapa. Semina hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Msekwa naWabunge wote tunaombwa tuhudhurie. (Makofi)

Page 49: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Nilikuwa nimeruka wageni wengine sita waMheshimiwa George Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwaambao ni Viongozi wa CCM pamoja na wajasiriamali kutokaJijini Dodoma wakiongozwa na Diwani wa Mpwapwa,Mheshimiwa George Fuime. Karibuni sana ndugu zetu.(Makofi)

Nina tangazo lingine linatoka kwa Mheshimiwa ShallyJosepha Raymond, Mwenyekiti wa Jumuiya ya St. ThomasMoore hapa Bungeni anapenda kuwatangaziaWaheshimiwa Wabunge kwamba leo Ijumaa tarehe 12 Aprilikutakuwa na Ibada ya Njia ya Msalaba na Upatanisho kwaWakristo Wakatoliki mara baada ya kusitishwa shughuli zaBunge saa 7.00 mchana. Hii itakuwa katika Ukumbi waMsekwa ghorofa ya pili.

Aidha, Waheshimiwa Wabunge na wengine wotemnaopenda kushiriki Ibada hiyo mnakaribishwa sana.Wakristu wote, sio Wa-Roman Catholic tu na Wakristo wotemnakaribishwa.

Nadhani mimi hayo ndiyo matangazo niliyonayohapa.

Mheshimiwa Chief Whip wa Serikali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, ninaomba kutoa tangazo lifuatalo kwa niabaya Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabungewote, kufuatia uamuzi wa Serikali kuhamishia Makao Makuuya Serikali hapa Jijini Dodoma katika eneo la Mtumba,ninapenda kuwafahamisha kuwa Wabunge wote waJamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaalikwa sasa rasmikwenye sherehe za uzinduzi wa Mji Mkuu wa Serikali hapaDodoma Mtumba siku ya tarehe 13 Aprili, 2019 yaani keshosaa 2.30 asubuhi. Uzinduzi huo utafanywa na Mheshimiwa Dkt.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni utekelezaji wa Ilaniya Uchaguzi na ni tukio kubwa sana la kihstoria katika nchiyetu ya Tanzania. Hivyo, niwaombe sana WaheshimiwaWabunge wote kushiriki kwa ukamilifu katika tukio hilo siku yakesho katika eneo la Mtumba hapa Mjini Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Usafiri utatupa?

MBUNGE FULANI: Moja ya haki za Bunge.

MHE. ALLY K. MOHAMED: Utatupa usafiri?

MBUNGE FULANI: Utakuwepo?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, mnafahamumimi huwa sipendi mambo ya watu kuanza kuongea kwenyemicro-phone. Kanuni hazituruhusu. Ni lazima tuheshimu kanunizetu.

Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

MWENYEKITI: Hebu ngoja. Mheshimiwa Msigwa, hebuanza Mheshimiwa Msigwa, unataka Mwongozo?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nimesimama kwa Kanuni ya 68(7).

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku za hivi karibunikumezuka tabia ambayo inakiuka kabisa na haitambui kabisakwamba nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi, lakini mahali

Page 51: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

popote ambapo Mheshimiwa Rais anapita bendera zaChama cha Demokrasia na Maendeleo zinang’olewampaka kwenye Ofisi za Vyama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni Mafinga,bendera zimeng’olewa barabarani na zimewekwa zaChama cha Mapinduzi na ukija Iringa Mjini bendera za CCMzimewekwa mpaka kwenye nguzo (mistimu) kitu ambachokinakiuka kabisa na hakiakisi kwamba nchi hii ni ya Mfumowa Vyama Vingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili lichochea vuruguna chuki katikati ya Watanzania. Vile vile jambo hililinamdanganya Mheshimiwa Rais kwamba vyama vinginehavipo kwa kuweka bendera ya Chama cha Mapinduzi tu,kitu ambacho wasaidizi wake wanamdanganya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba utupemwongozo wako, nchi hii ni ya Mfumo wa Vyama nami nimwakilishi wa wananchi: Je, jambo hili linaruhusiwa kwambatukikuta bendera ya chama kingine tuing’oe? Ambapo nijambo linalochochea ghasia kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wakoili Taifa lipate kujua ni namna gani tupate kuendeleza amanina utulivu ambao kila siku inahubiriwa katika jengo hili.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mnyika.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya 51 ikisomwa pamojana Kanuni ya 37 ili kuweza kutoa hoja ya kuhusu haki za Bungekwa sababu tarehe 8 Aprili, 2019 hapa Bungeni kwa mujibuwa Kanuni ya 37, kuliwekwa Mezani Hati za Serikali na kati yahati hizo zilikuwa ni pamoja na ripoti za Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali. Siku hiyo Wabunge tuliombakupewe nakala za ripoti hizo kama ambavyo kimsingi Kanuniya 37 inataka hati zote zinazowekwa mezani Wabungetupewe nakala.

Page 52: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiti cha Spika kikajibu tukwamba, Kiti cha Spika kimepokea na Serikali itafanyautaratibu wa kutoa nakala kwa Wabunge, lakini mpakanaketi kwenye kiti hiki, nimeangalia kwenye pigeon holes nahapa Bungeni vilevile mpaka sasa ripoti za Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali nakala hizo 17 hazijatolewa kwa Wabunge.Jambo hili linaminya haki yetu kama Wabunge kuwezakupata taarifa za kuishauri na kuisimamia Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nipewefursa ya kuitoa hii hoja ili Bunge lijadili juu ya kunyimwa hakiya kupewa nyaraka muhimu za kuweza kuishauri nakuisimamia Serikali na kuiwajibisha Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hojakwamba jambo hili lijadiliwe na tukabidhiwe ripoti hizi siku yaleo muda huu tuweze kuzifanyia kazi kwenye mjadalaunaoendelea na kwenye kazi nyingine. Ahsante sana.(Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walisimama)

MWENYEKITI: Hebu kaeni Waheshimiwa Wabunge.

Waheshimiwa Wabunge, nimeombwa Mwongozo naMheshimiwa Msigwa kwa mujibu wa kanuni ya 68(7),nisingependa kurudia aliyoyasema, mimi naamini alitaka tukusikika, lakini tukio hilo kwa mujibu wa kanuni hiyo aliyoisema,halikutokea mapema hapa Bungeni. Kwa hiyo, naishia hapo,hakuna kitu cha kuniomba mwongozo kwa suala hilo.(Makofi)

Mheshimiwa Mnyika amesimama kwa mujibu waKanuni ya 51 ambayo inahusu haki za Bunge hili, ikisomwapamoja na Kanuni ya 38 ambayo ni uwasilishaji Mezani waHati na amelenga kwenye Report ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali kwamba tangu ziwasilishwe hapaMezani Waheshimiwa Wabunge hatujapata nafasi yakuzipata.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Nianze na moja, kama alivyosema Mheshimiwa NaibuSpika, Kanuni ya 38 ukiisoma vizuri unaanza na yale Magazetiya Serikali kwa sababu ni sheria za nchi; magazeti ya Serikaliyanayowasilishwa hapa, sheria ndogo zile kupitia gazeti laSerikali, lazima zipatiwe kwa Wabunge. Ninyi kama wawakilishiwa Wananchi myafahamu yale ambayo yametungwa kamasheria ndogo kwa maeneo yote ya Tanzania nayanayowahusu ninyi. Ndiyo dhana hiyo.

Kwa hati nyingine ambazo kisheria zinapaswaziwasilishwa hapa including Taarifa ya CAG, ukisoma tenakanuni, zina utaratibu wake. Hatua ya kwanza ya msingi nikuwasilishwa Mezani na mhusika, Waziri au MwanasheriaMkuu. Ziliwasilishwa.

Waheshimiwa Wabunge angalieni, hizi hapa. Hiindiyo fulfillment ya kwanza. Haiwezekani Serikali ikaja ikasematumewasilisha kitu hewa, hapana, ziko hapa. Ukishafanyahivyo, tumetekeleza jukumu hilo. Inafuata hatua ya pili, hizizitakapopatikana na Waheshimiwa Wabunge mjue hizi nigharama jamani, mimi nimeulizia na niseme WaheshimiwaWabunge, hatua yetu ya sasa kama ilivyowasilishwa hapamnajua inaenda kwenye Kamati husika. (Makofi/Kicheko)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Taarifa hiihaisomwi humu. Hatuwezi kubishana! Mwongozo wangu kwasuala hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 51 namuuliza MheshimiwaMnyika, anioneshe ni kifungu kipi cha Sheria ya Haki, Kingana Madaraka ya Bunge kinachosema kwamba hizizikiwasilishwa hapa ni lazima zigawiwe kwa Wabunge kwamujibu wa sheria yenyewe. Hatuwezi kwenda…

Mheshimiwa Zitto nakuomba ukae, ukionanimesimama nakuomba ukae. Aliyetoa hoja hii niMheshimiwa Mnyika ndiyo maana nimemuuliza yeye, anzana sheria sio kanuni, unapoenda na kifungu cha 51 ni haki zaBunge kwa mujibu wa Sheria ya Nchi. Hapana! Mimi

Page 54: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

nakuongoza kama Mwanasheria, mimi kazi yangu nikuwafundisha pia. (Makofi)

Haki zinazoongelewa ni zile ambazo zimetajwakwenye Sheria ya Haki na Kinga. Wewe umeomba hiyokwamba tusimamishe shughuli zetu kwa sababu mpaka ripotiya CAG ipatikane kwa Wabunge.

WABUNGE FULANI: Ndiyooooo.

MWENYEKITI: Hatuwezi kufanya shughuli za namnahiyo kwa mwongozo wangu ni kwamba…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Umeniuliza…

MWENYEKITI: Hapana Mheshimiwa, kaa chini. Uamuziwangu ni kwamba Serikali itawasilisha kwa Wabunge kupitiataratibu zetu hapa kwenye pegion holes kwa wakatimuafaka. (Makofi)

Katibu.

NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Ofisi ya

Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

(Majadiliano Yanaendelea)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunao wachangiaji wetu waleo, nianze na Mheshimiwa Mnyika, atafuatiwa naMheshimiwa Kiwelu na Mheshimiwa Munde ajiandae.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Leo asubuhi tulipoingia hapa, tulianza na dua,kwa hiyo tulianza na Mungu kwanza, sio kilimo kwanza auelimu kwanza, tulianza na Mungu kwanza na tulisali; “Ewe

Page 55: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mwenyezi Mungu Mtukufu, muumba mbingu na Dunia,umeweka katika Dunia Serikali za wanadamu na Mabungeya Mataifa ili haki yako itendeke. Twakuomba ibariki nchi yetuidumishe uhuru, umoja, haki na amani. Umjaalie Rais wetuhekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja nawanaomshauri wadumishe utawala bora.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaomba mchango wanguwa leo kwa kweli uongozwe na hii sala ambayo tumeisalileo. Kwa sababu tunachangia Ofisi ya Rais nitaomba bilakuvunja kanuni ya kujadili mwenendo wa Rais, nitaombaniguse maswali mbalimbali kuhusiana na Ofisi ya Rais, lakiniambalo naliomba sana Ofisi ya Rais, Utawala Bora naTAMISEMI, walitoleee kauli, hivi ilikuwa ni halali kwa Mkuu waMkoa wa Tabora kusema kwamba anakwenda kufanya niniMheshimiwa Selasini?

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Kumwomba Munguamshukuru Rais.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, yaanianamwomba Mungu amshukuru Rais, hii ni kufuru!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika, ongea na kiti.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niongee na kiti kwamba Ofisi ya Rais, Utawala Borana Ofisi ya Rais, TAMISEMI ituambie hivi ni halali kwa Wakuuwa Mikoa na viongozi wa Kiserikali kukufuru na kufanyadhihaka dhidi ya Mwenyezi Mungu? Wengine utasikiawanajiita Mungu wa Dar es Salaam na mambo mbalimbali.Serikali itoe kauli juu ya jambo hii ndani ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeelezwa hapa kwambaMheshimiwa Rais atakuja kesho kuzindua Makao Makuu,ujenzi wa Mji wa Serikali. Ningeomba sana sana Ofisi ya Raisimshauri Rais kama ambavyo anapata wasaa wa kuzungukakuzindua majengo pengine kupatikane wasaa wa siku mojawa Taifa letu na siku ya sala A National day of prayertuiombee nchi yetu. Pengine tutaponya majeraha ya Kibiti,

Page 56: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

majeraha ya watu kupigwa risasi kama Mheshimiwa TunduLissu, majeraha ya miili kuokotwa Coco beach na mambomengine ambayo kwa kweli, Mheshimiwa Selasini anasemakipindi cha Kwaresma yatatusaidia kutuweka pamoja kamaTaifa, kwani Taifa linalokwenda pamoja ni Taifa linalowezakwenda kwa kasi zaidi kuliko kasi tuliyonayo ya maendeleoya nchi yetu kwa sababu kasi yetu tunapewa takwimu zauongo Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaambiwa kwambauchumi wa nchi utakua kwa asilimia saba huku Shirika laFedha Duniani l inatoa taarifa kwamba hiyo asil imiainayosemwa na Serikali haiwezekani sanasana tukijitahidi niasilimia nne. Taifa la namna hii linahitaji uponyaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambaloningependa kulizungumza, tumeapa kulinda Katiba, naelewawenzetu tukisema kuhusu Katiba wanasema kipaumbele chamsingi cha wananchi ni maji, umeme na miradi mingine yamaendeleo, lakini tulipoapa na Mheshimiwa Rais aliapa chakwanza tuliapa juu ya katiba kwa sababu Katiba ndiyonyenzo ya kusimamia mambo yote na ndiyo nyenzo ya kuletamaendeleo ya nchi. Kwa hiyo, nasema Katiba ni jambo lapili muhimu sana kwa nchi yetu na kwa sababu Katiba nijambo la pili ningependa kuwakumbusha WaheshimiwaWabunge, Mheshimiwa Rais alipokuja kuhutubia Bungewakati anazindua Bunge aliahidi hapa Bungeni kwenyehotuba yake kwamba ataendeleza na kukamilisha mchakatowa Katiba mpya. (Makofi)

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,Taarifa.

MWENYEKITI: Hebu subiri tu Mheshimiwa Mnyika,Taarifa.

T A A R I F A

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nataka nimkumbushe mzungumzaji anayeongea kwamba

Page 57: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

siku Rais amekuja hapa kutoa maelekezo yake ya nchi yeyehakuwepo Bungeni, alijuaje hayo maneno? (Makofi)

MWENYEKITI: Endelea Mheshimiwa.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, niMbunge wa wapi ambaye hajui kwamba kila kinachojadiliwaBungeni kinawekwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge?Kwa hiyo analiaibisha Bunge tu. Naomba niendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Rais akiwa Chuo Kikuucha Dar es Salaam kwenye kongamano, kinyume na kauliyake ya Bungeni, Rais amesema eti hataki mchakato waKatiba mpya kuendelea kwa sababu kuna watu wanatakawapewe posho ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema Ofisi ya Raisikamkumbusha Rais. Wao walikaa kwenye Bunge Maalumwakapitisha Katiba inayopendekezwa kinyume na Katiba nawananchi kwa Sheria ya Kura ya Maoni na Sheria yaMabadliko ya Katiba, hatua inayofuata ni kura ya maoni dhidiya hizi rasimu mbili uamuzi wa wananchi kufanyika, jambohilo halihusu Wabunge kukaa kikao, jambo hilo halijusuWabunge kupewa posho.

Kwa hiyo kauli ya Rais ilikuwa inataka kupotosha tumjadala wa Katiba mpya ni muhimu katika majumuisho. Ofisiya Rais ikasema ni kwanini katika Bunge hili hakijatengwapesa kwa ajili ya kura ya maoni na kukamilisha mchakatowa Katiba mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusikubaliane kwa namnayoyote na kauli ya kwamba eti hakikuwa kipaumbele chenuwala kipaumbele cha Rais. Nimeisoma Ilani ya Uchaguzi yaCCM, Ilani ya Uchaguzi ya CCM imesema bayana, CCMitaendeleza na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya,tekelezeni Ilani yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitarudi kwenye hayamambo…

Page 58: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

T A A R I F A

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: MheshimiwaMwenyekiti, nataka nimtaarifu mzungumzaji anayezungumzakwamba Katiba inayopendekezwa tulishiriki wote Wabungetuliokuwepo Bunge lililopita na mchakato ule ulipofikia hatua,wenzetu wa upinzani hatukuwa nao mpaka hatua ya mwishowaliikataa. Leo hii wanakuja hapa kusema wanatakamchakato uendelee wa kupigia kura, Katiba ipi mpyainayopendekezwa wakati wao waliikataa na hawakushirikizoezi mpaka mwisho? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mnyika taarifa.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheriaya Kura ya Maoni inasema Katiba inapendekezwaikishapitishwa kwenye Bunge Maalum hatua inayofuata nikura ya maoni bila kujali nani alikuwepo na nani hakuwepo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuendelea.Nitaomba kupata ufafanuzi kutoka kwa Ofisi ya Rais, ripotiiliyopita ya CAG sio ya sasa, ripoti ya mwaka uliopita iliibuamadudu mengi kwenye sekta mbalimbali na Wizarambalimbali na kati ya mambo yaliyoibuliwa ni pamoja nasuala la 1.5 trillion ambayo baadaye ilipanda mpaka kuwa2.4 trillion. Katika ufafanuzi wa Serikali juu ya 1.5 trillion kunataarifa zilitolewa toka 1.5 mpaka 2.4 kwamba bilioni 976.96zilihamishwa kwenye Mafungu mbalimbali zikapelekwa kwamaana ya kibajeti reallocation zikapelekwa kwenye Fungula 20 la bajeti ambalo ni sehemu ya hotuba yetu ya leo Ofisiya Rais, Ikulu. Sasa mimi kama Mbunge naamini moja, Bungehalikupitisha uamuzi wa kufanya reallocation ya bilioni 976.96kupeleka Fungu namba 20 Ikulu. Pili… [Maneno Haya SiyoSehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika, hebu nisaidie Sheriaya Bajeti kuhusiana na reallocation inasemaje? Nisaidie?

Page 59: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu ya interests…

MWENYEKITI: Ni Bunge linafanya au mamlaka husikainafanya?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kwa interest ya time nijikite zaidi kwenye hoja yangu.

MWENYEKITI: Hapana.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,tukitaka kujadili hilo tuta…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,utalinda muda wangu?

MWENYEKITI: Naulinda! Mheshimiwa Mnyika naWaheshimiwa Wabunge, tusifanye generalization ambazohuwezi kuzi-defend hapa. Sisi wote hapa tumeshiriki, baadhiyetu tumeshiriki katika utungaji wa sheria hiyo.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Shut up!

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Nawaombeni Waheshimiwa Wabunge,kiwango ambacho kimetajwa na Sheria ya Bajeti kama kunaMbunge anataka ku-challenge hiyo, warrant ya reallocationinapowekwa na Serikali hapa wewe unapaswa sasa usemekwamba reallocation hiyo imezidi kiwango ambachokimewekwa na Bunge, ukomo, lakini hatuwezi hapa kujatunafanya generalization tu ili -m-get away na hiyo, hapanasi kweli! Waziri wa Fedha, jamani Wizara hiyo ni makini sana.Endelea. (Makofi)

Page 60: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ilituondoe utata kuhusu jambo hili la bilioni 976.96 kwa kuwaCAG anabanwa banwa kidogo kukagua Ikulu, Ofisi ya Raisikija kwenye majumuisho hapa itueleze hizi bilioni 976.96 Ikuluzilitumika kwa matumizi gani? Tupewe mchanganuo wakina…[Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, hatuwezi kusubiri kuja kujibu kuwaachiaWatanzania wanapotoshwa. Lazima watu wanaosemauongo ndani ya Bunge lako Tukufu wathibitishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakiomba kiti chakokimwelekeze Mheshimiwa Mnyika aweze kuthibitishakwamba CAG anabanwa banwa kukagua Fungu 20 la Ofisiya Rais, kwa sababu kinachofahamika kila Fungu lina ResidentAuditor kutoka Ofisi ya CAG including Fungu 20. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hiki kinachoelezwakisiwapotoshe Watanzania kule nje. Naomba iwekwe wazikwamba hakuna Fungu hata moja ambalo CAG anazuiwakulikagua na Fungu hili lilikaguliwa na CAG hakuja na hojahizi zinazoletwa kuwadanganya Watanzania humu ndani.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kiti chako kitendehaki kwenye jambo hil i i l i Watanzania wasiendeleekudanganywa na Mheshimiwa Rais wetu asiendeleekuchafuliwa bila sababu za msingi. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naamini ulilinda muda wangu, lakini mimi bado naombakatika majumuisho Ofisi ya Rais ilete mchanganuo hizi pesazimetumika kwenye kitu gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea. Hotuba hii ya…

MWENYEKITI: Una dakika mbili.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

MHE. JOHN J. MNYIKA… Utumishi wa Umma inahusumaslahi ya wafanyakazi wa umma…

KUHUSU UTARATIBU

MWENYEKITI: Kanuni namba ngapi?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, Kanuni ya 64(a).

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, Kanuni iliyovunjwa ni ya 64(a). Kanuni inasemahivi; Mbunge hatatoa ndani ya Bunge Taarifa ambazo hazinaukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la 1.5 tri l l ionlimeendelea kuongelewa humu ndani ya Bunge tenalimeongelewa kwa uongo. Kwa sababu nitahitajikakuthibitisha kuwa huo ni uongo, Ripoti ya PAC Mwenyekitiwake ambaye ni Mpinzani, Mheshimiwa mama Kaboyoka,Mbunge wa CHADEMA inasema hivi ukurasa wa 35;“Mheshimiwa Spika katika kuhitimisha suala la tofauti la 1.5trillion kati ya mapato ya Serikali na makusanyo kwa mwaka2016/2017, naomba kuweka kumbukumbu sahihi katikaBunge lako Tukufu kuwa tofauti hiyo haikuwepo baada yamarekebisho ya mahesabu kufanyika.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Bunge lakolimeendelea kutumika kama jukwaa la kuichafua Serikalikuwa imefanya matumizi ya 1.5 trillion na Bunge lako limekaakimya bila kuwakemea hawa. Watanzania wameendeleakupotoshwa na Bunge lako limekubali. Naomba likemewesuala hili na utoe maelekezo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlinga, umesimama kuhusuutaratibu, umetaja hiyo Kanuni ya 64(1)(a)…

Page 62: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, please. Howcan you get to (a) without reading 64? (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, naendelea, hatatoa ndaniya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli. Sasa Kanuni hii lazimauisome pamoja na Kanuni ya 63, Mbunge aliyekuwaanaongea hapa alikuwa ni Mheshimiwa Mnyika, kwa hiyo,ni Kanuni ya 63(2), inasema, Mbunge yeyote anapokuwaakisema Bungeni, hutachukuliwa unasema uongo kamaunafanya reference. Fasisli ya (3) inasema, Mbunge mwingineyeyote anaweza kusimama mahali pake na kutamka “kuhusuutaratibu’, tumemsikiliza Mheshimiwa Mbunge kafanya hivyona Mheshimiwa Mnyika kwa mujibu wa fasili ya (4), aliketi,lakini sasa huyu aliyesema wewe husemi ukweli anapaswaaseme kitu, atoe maelezo kwa kiwango ambachokinaliridhisha Bunge kwamba kuna uongo umesemwa.Ameenda mbali zaidi amesema Taarifa ya Kamati ya PACkuhusiana na amount hiyo, kwamba Kamati ya Kudumu yaBunge ya Hesabu za Serikali ilisema suala hilo si hoja tena,kwa hiyo, hiyo ni rekodi ya Bunge. (Makofi)

Kwa maana hiyo Mheshimiwa, kwa mujibu wa Kanunizetu, kwa sababu ya maamuzi ya Kamati ya Bunge ya PAC,kwa hayo iliyoyasema, wewe sasa ndiyo unatakiwa uthibitishekweli au si kweli. Kwa maana hiyo, nakupa options mbili tu,ya kwanza, ufute tu kauli yako kuhusiana na hayo maelezoyako, yale uliyosema ya bilioni ambazo zilikuwa summarizedzote, wewe umesema bilioni 900 lakini ukasema ni trilioni 2.4kwa maana kwamba 1.5 trillion kujumlisha na hizo bilioni ndiyounapata hiyo. Sasa maelezo ya 1.5 trillion yapo kwenye ripotiya PAC. Maana wewe umefanya majumuisho, sasanakupeleka ufute kauli yako au nikupe muda wa kujakuthibitisha Bungeni hapa, chagua mojawapo.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshmiwa Mwenyekiti,kwanza niweke rekodi sawa, nimesema…

Page 63: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

MWENYEKITI: Tunabishana tena?

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshmiwa Mwenyekiti,naomba niseme, naomba niweke rekodi sawa. Nimesema,nataka maelezo ya Serikali Bungeni juu ya shilingi bilioni 976.96zimetumika kwa matumizi gani? Nimesema jambo hili likooutstanding na hili ndilo linasababisha mjadala wa 1.5 trillionna 2.4 trillion kuendelea. Kwa hiyo, kama ni uthibitisho,nitakiwe kutoa uthibitisho kuhusu suala la shilingi bilioni 976.96za Vote 20 ya Ikulu. Nipewe nafasi ya kuzungumza kuhusuhilo. (Makofi) [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmiza Bunge]

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, huna hoja yoyote,unatupotezea muda wetu wa Bunge. Kwa sababu kamaissue yako ilikuwa ni 1.5 trillion kama ulivyoanza, usingekimbiliakutafuta 900 billion shillings. Ulifanya majumuisho ya 2.4 trillionna ndiyo maana Mheshimiwa Naibu Waziri akasimama.(Makofi)

Kwa hiyo, kama unataka tupitie Hansard ili tuonemtiririko wa argument yako. Mimi naagiza watu wa Hansardkabla ya sasa saba tupate Hansard hiyo halafu nitatoauamuzi wangu kuhusiana na hoja ya Mheshimiwa Mnyika.Ahsante. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshmiwa Mwenyekiti,naomba…

MWENYEKITI: Muda wako umekwisha, si nilikwambiadakika mbili.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshmiwa Mwenyekiti, mudawangu umekwisha wakati nimekuwa interrupted!

MWENYEKITI: Umekwisha!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshmiwa Mwenyekiti,naomba nimalizie muda wangu, nilikuwa nazungumzanikawa interrupted.

Page 64: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

MWENYEKITI: Sasa kama hutumii vizuri muda wako,umekwisha. Nimekulindia muda nikakwambia zilikuwazimebaki dakika mbili, umeongezewa nyingine mbili.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Heche, Heche, Heche, narudia Heche,please, please!

Haya tunaendelea na Mheshimiwa Kiwelu.

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa nafasi. Nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu kwa kunipa uhai na kuweza kusimama mbele yaBunge lako Tukufu kuchangia machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kupongezahotuba zetu zote mbili za Kambi ya Upinzani. Zimeelezamambo mengi mazuri na tunaishauri Serikali kuzingatia yaleyote yaliyoelezwa na kambi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa pole kwaWabunge wenzetu, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowepamoja na Mheshimiwa Esther Matiko ambao walikaagerezani kwa siku 104 kwa kunyimwa haki yao ya dhamana.Nimpongeze Jaji Rumanyika kwa kuweza kuona hilo na kutoahaki na hata leo wako nje kwa dhamana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumwambiaMwenyekiti wetu wa Chama, Mheshimiwa Freeman AikaelMbowe, tunakupongeza kwa uimara wako, pamoja na yoteambayo unafanyiwa umeendelea kuwa imara na wewendiwe Mwenyekiti wetu…

MBUNGE FULANI: Atabaki kuwa juu.

MHE. GRACE S. KIWELU: Najua wako ambaowanaumia kwa ajili ya wewe kuwa Mwenyekiti lakiniutaendelea kuwa juu. (Makofi/Kicheko)

Page 65: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia kuhusuTume huru ya Uchaguzi. Najua wengi watatushangaa ni kwanini tunazungumzia Tume hii lakini kitanda usichokilalia huwezikujua kunguni wake. Sisi tunayo maumivu tuliyoyapata kwasababu ya Tume hii ya Uchaguzi kutokuwa huru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi ambazo mfumowake ni wa kupata viongozi kwa mujibu wa sheria kwakupigiwa kura, viongozi wengi wameanza kudharauwapigakura wao na tumeona wakifanya maamuzi bila kujaliwanawaathiri vipi wapigakura wao. Tumefanya maamuzimengi bila kujali waliotupa dhamana ya kutuleta humu ndaniwanataka nini. Wanafanya haya kwa sababu wanajua Tumewameimiliki, si huru, wanafanya maamuzi bila kujali mawazoya wananchi wao ambao ndiyo wamewapa dhamana yakuwaleta humu. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. MAULID S. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MBUNGE FULANI: Kaa, jamani.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hii itakuwa nitaarifa ya mwisho.

MHE. MAULID S.A. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sawa.

MWENYEKITI: Tutumie muda wetu vizuri.

MBUNGE FULANI: Wewe poyoyo vipi?

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. MAULID S. A. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sishangai kwanza baadhi ya Wabunge wako nidhamu yaokuwa chini ni kwa sababu namna wengine wanavyopatikana

Page 66: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

ni aibu kuizungumza humu ndani. (Makofi) [Maneno HayaSiyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MBUNGE FULANI: Poyoyo.

MHE. MAULID S.A. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa yangu ni kwamba, Mheshimiwa Mbungeanazungumzia kwamba Tume ya Uchaguzi haiko huru, siyokweli. Nataka kumpa taarifa Tume ya Uchaguzi iko huru nawao hawana haki ya kupima uhuru wa Tume ya Uchaguzikwa sababu hata uchaguzi wenyewe siku hizi hawagombei.

MBUNGE FULANI: Wewe poyoyo.

MHE. MAULID S.A. MTULIA: Usipogombea huwezi kujua,Tume sasa hivi iko vizuri, inatenda haki, kila anayeshindaanatangazwa. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti…

MWENYEKITI: Ngoja kwanza msiende hivyo.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Kaeni kwanza, Waheshimiwa ninyi wawiliwote kaeni.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

Page 67: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

MHE. JOHN W. HECHE: Atuambie wamepatikanaje?

MWENYEKITI: Ngoja kwanza nitafika huko, please.Mheshimiwa Selasini na Mheshimiwa Esther Matiko kaeni chini.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,tumechoka.

MWENYEKITI: Aliyekuwa anapewa taarifa niMheshimiwa Kiwelu.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niendelee kwa sababu…

MHE. ESTHER N. MATIKO: Afute.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Kuhusu utaratibu, kaa tena MheshimiwaKiwelu.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, …

MWENYEKITI: Niambie Kanuni gani?

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kanuni ya 64(1)(g), Mbunge hatatumia lugha ya kuudhi auinayodhalilisha watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Mbunge waKinondoni akitoa mwongozo wake, alisema kwamba…

MWENYEKITI: Akitoa taarifa.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,akitoa taarifa alisema kwamba kuna baadhi ya Wabunge

Page 68: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

kupatikana kwao kunatia aibu. Sasa mimi napendaalithibitishie Bunge hao waliopatikana kwa njia ya aibuambayo haiwezi kusemekana ni watu gani na hiyo aibu ninini, vinginevyo afute kauli yake. (Makofi)

MWENYEKITI: Alikuwa anampa taarifa nani?

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,alikuwa anampa taarifa Mheshimiwa Kiwelu na kutoa taarifandani ya…

MWENYEKITI: Mheshimiwa ngoja tu, nawapelekapolepole tu, logically. Mheshimiwa Kiwelu, nilikuomba upokeetaarifa au unaikataa?

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naikataa lakini naomba utoe maelekezo kwake athibitishehiyo kauli yake aliyoisema. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleakufundishana Kanuni, yeye kasema…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, yeye katoamadai aliyoyasema kwa njia ya taarifa. Kama kuna Mbungesasa anasema kwamba amesema uongo, eleza kwakiwango ambacho utaliridhisha Bunge kwamba amesemauongo ili sasa burden ihamie kwake. Eleza maana yeyehajamtaja yeyote. Mtusaidie tu, maana umetumia Kanuni yakuhusu utaratibu siwezi kuiacha hivyo hivyo. MheshimiwaMatiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhusu utaratibu kama alivyokuwa amesema Mnadhimu. Hiiiko straight, mzungumzaji alisimama akitaka kutoa taarifa kwaMheshimiwa Grace Kiwelu kuhusiana na Tume huru lakinikatika kutaka kutoa taarifa yake akatumia lugha ya kuudhina kudhalilisha, wakati akitaka kutoa taarifa kuna baadhihuku waliongea akasema, kuna wengine upande huowanapatikana kwa kuuza

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,uliniambia nifafanue.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko, nilipenda weweuwe very specific.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda aliyetoa taarifa Mheshimiwa Mbunge waKinondoni, kwanza kabisa kwa Kanuni ya 64(1)(f) na (g), aidhaathibitishe kwa Bunge lako hili, ni Wabunge gani ambao wakoupande huu waliopata Ubunge kwa aibu. Maana yaketunajua Wabunge wanapatikana kwa kupigiwa kura, waweWabunge wa Viti Maalum au Wabunge wa Kuchaguliwa kwaMajimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa atuthibitishie kwambani Wabunge gani waliopatikana kwa aibu huku na ni aibugani hiyo waliyoifanya mpaka wakawa Wabunge? Kinyumecha hapo afute maneno yake. Hili Bunge lako siku hizilinatumika kudhalilisha akina mama, of which we wan’t agreeat all. (Makofi)

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Ahsante, umeeleweka.

MHE. MARGARET S. SITTA: Ataweza kuthibitisha hilo?

Page 70: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge wa Kinondoni…

MBUNGE FULANI: Umezoea.

MHE. MARGARET S. SITTA: Ni kweli.

MWENYEKITI: Unaweza ukafuta hayo maneno?(Makofi)

MHE. MARGARET S. SITTA: Afute hayo maneno bwana.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,afute bwana.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, ngoja natakatwende vizuri tu.

MHE. MARGARET S. SITTA: Afute hiyo bwana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sitta, umesimama kwaKanuni gani?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, Msigwa alisema hapa mpaka wabebe vidumuvya petroli.

MBUNGE FULANI: Kaa chini.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti,…

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, yeyeyule si alipatikana kwa aibu masanduku ya kura yalichukuliwayakahesabiwa kwake huyo.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

Page 71: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, msiongee,tulieni tu, hebu kaa tu Mheshimiwa Sitta. Mheshimiwa Mtulia.

MBUNGE FULANI: Huyu amezoea kudhalil ishawanawake.

MHE. MAULID SAID MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nafuta kauli japokuwa…

WABUNGE FULANI: Aaaaa.

MHE. MAULID S.A. MTULIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sikutaja wanawake, nafuta kauli yangu.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, ndiyo maananiliwapeleka kwa utaratibu.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Tusikilizane basi, Mheshimiwa nakusikiavizuri sana mpaka hapa, hebu tusikilizane. Ndiyo maananilitaka kusema kwa vile yeye amefuta kauli hiyo…

WABUNGE FULANI: Hajafuta.

MWENYEKITI: La pili niliwapeleka polepole kwautaratibu. Mimi sitaki kuendeleza mjadala huo kwa sababuhakuwa ametaja jina la mtu.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiwelu, endelea kuchangiatumelinda muda wako.

Page 72: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Mwenyekiti,niwaambie akina mama wa Kinondoni kwamba Mbungewao hana heshima kwa akina mama ambapo mama yakeamemzaa yeye na kuweza kuwa kiongozi leo. Wabungewanawake wa CHADEMA tumechaguliwa kamawalivyochaguliwa Wabunge wengine wa Viti Maalum kwakufuata taratibu na kanuni za chama chetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee, tumeshuhudiamabadiliko makubwa sana sasa hivi ya uteuzi waWakurugenzi wa Wilaya umeacha kufuata taaluma, taratibuna sheria zilizokuwa zinafanyika hapo awali lakini sasa hivikigezo namba moja ni kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi.Kibaya zaidi tunakwenda kwenye chaguzi za Serikali za Mitaaambazo tunajua Tume haina muundo mpaka chini,wanakwenda kuchukua watu kutoka TAMISEMI, sasa kwamuundo huu ambao Awamu ya Tano umeanza nao wakuchagua Wakurugenzi sifa zao wawe makada wa Chamacha Mapinduzi, tunawaambia mapema kwamba, kamawalivyosema wenzangu jana kwamba hatutakubalikudhulumiwa, wakatende haki kwa wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua haki hii haitatendekakwa sababu walishaonywa na Mkuu wa Nchi kuwawasipomtangaza mgombea anayetokana na chamatawala akatafute kazi nyingine na kauli hii haijawahi kufutwampaka leo. Kwa maana hiyo, Wakurugenzi, Maafisa Kataambao wako kwenye kata zetu zinazokwenda kufanyauchaguzi watakwenda kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunataka TAMISEMIituambie hawa Maafisa Kata walioletwa pamoja naWakurugenzi, wana haki kweli ya kuendelea kuwawasimamizi wa uchaguzi wakati wanakwenda kufuatamaelekezo ambayo walishapewa na Mkuu wa Nchi? Ndiyomaana tunaendelea kulalamika na kusema kwamba Tumehii si huru tunataka Tume huru itakayozingatia haki zawapigakura. (Makofi)

Page 73: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona uhuni uliofanyikakwenye chaguzi za marudio, watu wamepora maboksi nakwenda kujaza kura na kurudisha kwenye vituo wakisaidiwana Polisi. Pia tumeona kwenye vituo vya kupigia kura,mawakala tuko ndani tunaheshabu kura lakini Mapolisiwanabandika matokeo nje, wanaingia kuchukua maboksiya kura. Halafu mnatuambia hii ni Tume huru, kwa kweli Kambiya Upinzani na wapinzani wote bado tunaendelea kudaiTume huru ya Uchaguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala la ma-DC na Wakuu wa Mikoa. Mimi ninatoka Mkoa wa Kilimanjaro,sina tatizo na Mkuu wangu wa Mkoa, anafanya kazi zakevizuri, anatimiza wajibu wake kuleta maendeleo kwawananchi wake. Nina tatizo na Mkuu wa Wilaya ya Hai, DCSabaya. Huyu kabla ya uteuzi wake alikuwa Diwani Kata yaSambasha, Halmashauri ya Arusha DC, kwa Chama chaMapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, DC huyu ameletwa Wilayaya Hai, anasema anakuja kupambana na MheshimiwaMbowe. Namwambia hana ubavu wa kupambana naMheshimiwa Mbowe. Amekuwa akiingilia shughuli za vyamavya siasa, pia mmeona akiwa anawabughudhi wawekezaji.Tunajua Ma-DC na Wakuu wa Mikoa ni wanasiasa, lakinitunajua ziko sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili yakuwawesha kufanya kazi zao. (Makofi)

Mheshimiwa Sabaya amekuwa akikamata viongoziwetu wa chama kuzuia wasifanye vikao, tuna chaguzizinaendelea chini za chama, Mheshimiwa Sabaya hatakivikao vifanyike, lakini amekuwa akimsumbua Mwenyekiti waHalmashauri kwa kumbambikizia tuhuma za uongo.Nampongeza Mwenyekiti wa Halmashauri, ni mwanamke nayuko imara kweli kweli. Amekuwa akiwalazimisha Wenyevitiwetu wa Vijiji na Vitongoji kusaini barua za kujiuzulu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii siyo haki na siyo kazialiyotumwa kufanya Hai. Ametumwa akashirikiane nawananchi wa Hai kuleta maenendeleo na siyo vinginevyo.

Page 74: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Kama ni mwanasiasa, kwanza atekeleze kazi zake, akimalizandiyo akafanye siasa ya chama chake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala lakushuka kwa mapato kwa Halmashauri zetu. Halmashaurinyingi nchini zimeshindwa kukusanya mapato kutokana navyanzo vingi vikubwa vya mapato kuchukuliwa na SerikaliKuu. Hii imesababisha Halmashauri zetu kushindwa kuletamaendeleo na ile mipango waliyokuwa wamepangakushindwa kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naitaka Serikali, yalemapato ambayo waliyokuwa wanakusanya, ni wakatimuafaka sasa kurudisha kwenye Hamashauri zetu ili ziwezekujiendesha, kwa sababu kutakuwa hakuna maanakuanzisha Halmashauri ambazo zinashindwa kujiendesha.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mambo madogomadogo ambayo yalikuwa yanafanywa kutokana na hayomapato ya ndani ikiwemo ujenzi wa vyoo, kulipa bill za majina umeme, lakini yameshindwa kufanyika mpaka sasa.(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Kiwelu kwamchango wako. Mheshimiwa Munde. (Makofi)

MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa fursa hii nami niweze kuchangia. Nilikuwana mambo mengi ya kuchangia kuhusu Tabora, lakininimeona muda wangu kidogo nichukue kumjibu kaka yanguMheshimiwa Mnyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mnyikaamesema Mheshimiwa Rais kwa sababu ana nafasi yakufanya uzinduzi wa miradi, angechukua nafasi ile akafanyaSala ya Kitaifa kuiombea nchi hii. Mimi nadhani Mheshimiwa

Page 75: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Rais anafanya kazi kubwa na ndiyo maana kuna miradi mingiya kuzindua. Hiyo ni kazi, tena kubwa ya kuwaoneshaWatanzania ni nini Serikali yao inafanya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii ina dini; ina Wakristo,Waislam na dini tofauti tofauti. Kila siku tunasali kumwombaMwenyezi Mungu. Hapa leo ni Ijumaa, nikitoka hapa naendeMsikitini kusali, kumwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili yanguna familia na nchi yangu. Nadhani watu wote wanafanyahivyo.

Mheshimiwa Rais ameweza kuita viongozi wa dinimara kadhaa, anaongea nao kutaka maoni yao nakuwaomba waendelee kuiombea nchi yao. Mimi nadhaniMheshimiwa Mnyika labda ana stress. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mnyikaameongea kuhusu Katiba mpya. Ni hao walijiunga UKAWAmara ya kwanza kwa ajili ya kwenda kuipinga Katibailiyopendekezwa. Namshangaa leo anaidai Katiba hiyoambayo wao kwa mara ya kwanza waliungana kwendakupinga nchi nzima watu wasiiunge mkono Katibailiyopendekezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo namshangaa ndiyoniseme ndimi mbili, ndiyo niseme mna stress kwambahamtapata Ubunge tena, yaani nachanganyikiwa kwa kweli.Mliikataa Katiba, leo mnaitaka Katiba. Yote hiyo ni kui-frustrate Serikali ishindwe kufanya kazi yake, tukae na Katibatushindwe kuendeleza miradi iliyopo ili pesa yetu tuimaliziekwenye Katiba mje mseme kwamba Mheshimiwa Rais aliahidimaendeleo, ameshindwa kufanya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kusema tenaMheshimiwa Rais fanya kazi yako kama inavyostahili, achanana mambo ya Katiba, hukuwaahidi Watanzania Katiba,uliwaahidi maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongee tena kidogokwamba wamekuwa wanasema sana kwamba

Page 76: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Wakurugenzi, Ma-DC, ni wana CCM ni nani anaweza kufanyakazi na mtu ambaye hamwamini. Hata leo nikifungua duka,nitamweka ndugu yangu, nitamweka mtu ninayemwaminialiye karibu name. Ni nani anaweza kuwa Rais kati yao waoakachukua Mbunge wa CCM Munde akampa Ukuu waMkoa? Hatuwezi kufanya hivyo. Mheshimiwa Rais angaliawatu unaowaamini, uliowachuja, wakakuridhisha kufanyakazi na wewe kama vile wao ambavyo wanabebana,wanasaidiana wao kwa wao kwenye nafasi zao chungunzima ikiwepo Ubunge. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Wape dozi. (Kicheko)

MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niendelee na Bajeti Wizara. Naipongeza Wizara yaTAMISEMI kwa kazi nzuri wanayoifanya. TAMISEMI wamefanyakitu kizuri sana, wameboresha ukusanyaji wa mapato. Leo hiiukiwa popote, viongozi wa TAMISEMI wanaweza kuangaliaHalmashauri gani imekusanya shilingi ngapi, imetumia shilingingapi na imefanya nini? Hii ni hatua kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana kakayangu Mheshimiwa Jafo na Manaibu Waziri pamoja naMenejimenti nzima ya TAMISEMI. Vile vile naipongeza Wizaraya Utawala Bora, mzee wetu Mheshimiwa Mkuchika, mpenziwetu Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwatunakupongeza sana, mnafanya kazi kubwa mnotunawaona. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungumwendelee kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii system waliyoiweka ninzuri sana. Kwa kweli mimi nimefanya kazi Halmashauri,naomba ni-declare. Hakuna tena mtu atakayeweza kuibarevenue ya Halmashauri. Watu wataiba kwenye matumizihewa, kwenye ten percent, kuagiza vitu ambavyo siyo vyakweli. Kwenye revenue kwa kweli mmedhibiti na mtaachalegacy, hii kazi mmeifanya ni kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongee kuhusuvitambulisho. Wenzetu hawa wamekuwa wanaongea sana

Page 77: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

kuhusu vitambulisho vya 20,000 wakiviponda na kuvibeza.Kama nilivyosema, nimefanya kazi Halmashauri. Zamani akinaMama Lishe, Wamachinga walikuwa wanatozwa shilingi 500kwa siku. Anapewa risiti ya shilingi 500/=, kesho anapewa risitiya shilingi 500, analipia shilingi 500.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya wiki mbilianaenda kufurumuliwa, masufuria ya wali yanamwagwa,maharagwe yanamwagwa, mboga zao zinatupwa. LeoMheshimiwa Rais amewatambua kwenye Sekta Rasmi yaWamachinga kwa kuwapa vitambulisho wa shilingi 20,000.Nil idhani tutafurahi, tutaridhika wamama hawa,Wamachinga, vijana wetu hawatanyang’anywa tena vituvyao, watafanya kazi wakiwa na confidence zao nawameambiwa wasiguswe wafanye kazi popote. Mnaka nini?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zamani shilingi 500/=ukiizidisha mara siku 365 za mwaka walikuwa wanalipa shilingi182,000/=. Leo shilingi 20,000/= ukiigawa kwa siku 365,wanalipa shilingi 55/= kwa siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimetoka Tabora. Sisini maarufu sana wa kupika vitumbua. Mama anayepikavitumbua; kitumbua kimoja shilingi 500/=, akiuza vitumbua 40ana shilingi 20,000/=. Mwaka mmoja una wiki 52. Kila wikimama huyu aweke hela ya kitumbua kimoja tu 500, ndaniya wiki 40 amefikisha 20,000/=. Hivi mnataka nini jamani? Aummezoea kupinga tu? Mlipinga reli, mmepinga Stiegler’s,mnapinga ndege. Tumewazoea! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaambieSerikali, nimwambie Mheshimiwa Jafo, vitambulisho hiviviendelee, ni kitu kizuri sana, kinawatambua Wamachingawetu, Mama Lishe wetu, hawafukuzwi tena, hawamwagiwivitu vyao, lakini 20,000 ni reasonable price. Wale watu ilikuwavikishachukuliwa vile vitu vikamwagwa na Mgambo waowanawachukua wanawatumia kwenye maandamano.Safari hii mmewakosa. Safari hii mtoto wake ambaye yuko

Page 78: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

India, yuko Marekani, amlete aandamane. Wamachingatena hamwapati. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie harakaharaka. Niseme tu, ni lazima kila Mtanzania achangie patola Taifa. Tuache kujidanganya. Hamna nchi yoyote dunianiwatu hawalipi kodi; hamna nchi yoyote duniani watuwanafanya kazi bila kulipa ushuru; tusidanganyane. Hawawatu wenye sekta ambazo siyo rasmi, ndogo ndogo ndiowalio wengi. Kwani wanapita barabara zipi? Hospitaliwanatibiwa ipi? Kwa nini wasichangie pato la Taifa? Kwahiyo, tusitake kuivuga Serikali na kuitoa kwenye msimamowake thabiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kuhusu Jimbo laUlyankulu. Jimbo hili lina wakimbizi wengi sana. Wakimbizi haowamekubaliwa kupiga kura ya Mbunge na kura yaMheshimiwa Rais. Wakimbizi hawa wamekataliwa kuchaguaDiwani kwenye maeneo yao, hawachagui viongozi waSerikali za Mitaa, jambo linalotushangaza kabisa. Kwa sababuhuu ni uadui mkubwa. Huwezi kukaa na mtoto wa nduguyako ukambagua, hiki fanya, hiki usifanye. Kama walikuwahawatakiwi, wasingepewa uraia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu hawa wameshakuwaraia sasa, Watanzania, kwa nini mnawazuia wasichagueMadiwani? Kwa nini mnawazuia wasifanye uchaguzi waSerikali za Mitaa? Ukiangalia ni double standard. Kwa sababukwa yangu Mheshimiwa Kakoso kule kuna wakimbizi, lakiniwanachagua Madiwani, wanachagua Serikali za Mitaa,wanachagua Wabunge, wanachagua Rais. Sasa huku ninyimmetuwekea wachague Wabunge na Rais tu. Sasa kamaanamchagua Rais, anamchagua Mbunge, kwa niniunamkatilia asichague Diwani na umeshampa urai? Huyu niraia. Kwa hiyo, naomba mwatendee haki, wapate nafasi,wapate fursa nao wachague na wajichague. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeenda mbali zaidi,hawapati chochote cha Kiserikali wakati tumeshawapa urai.Juzi nilikuwa kule Kaliua, wamana hawo wanakataliwa

Page 79: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

kupata mikopo ya Halmashauri na wakati vikundi vyao nawakati tumeshawapa uraia: Je hii ni sahihi jamani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunatengezabomu ndani ya nchi yetu. Hawa tumekuwa kama tumewapauraia, lakini tunawabagua. Basi kama ni hivyo, tuwanyimeuraia, tuwanyang’anye. Kwa sababu tumeshawapa,naomba pia wakubaliwe kufanya kila kama wanavyofanyawengine. Kule kwa Mheshimiwa Kakoso, kwa kaka yanguMbogo kuna wakimbizi, lakini wanafanya kila tu. Kwa niniisiwepo na Ulyankulu hivyo hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Kambi za wakimbizizitafungwa? (Makofi)

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Munde.(Makofi)

Mheshimiwa Mwigulu.

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia.La kwanza, nitumie fursa hii kuwapa pole sana wananchiwangu wa Kata Tulya ambao wamepatwa na matatizo yashule ya msingi kuharibiwa na mvua pamoja na zahanati yao.Niwaambie wawe watulivu, nami nitapata fursa weekendkwenda kuungana nao katika shida hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pil i, nampongezaMheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayofanya yeye pamojana wasaidizi wake kwenye Wizara hizi ambazo leo hii tunamjadala mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, kwa sababu leo niweekend na nchi yetu itakuwa na jambo kubwa upande wamichezo, nawatakia kila la heri vijana wetu wa umri wa chiniya miaka 17 na wapeperushe vizuri bendera yetu ya Taifa.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Nawatakia kila heri pia club ya Simba ambao na wenyewewatakuwa wanapeperusha bendera ya nchi yetu kwaupande wa vilabu bingwa barani Afrika watakapopambanana wenzetu wa kule Kongo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuwanimeyasema hayo, niende moja kwa moja kwenye maombi.Jambo la kwanza ambalo ningependa kulileta mezani kwaMheshimiwa Waziri ni hili ambalo moja kwa moja linamuunganiko na dhahama iliyowapata ndugu zetu wa Kataya Tulya, kwamba kwa kuwa zahanati ile imeharibiwa na kwakuwa ndugu yetu Mheshimiwa Jafo amekuwa mstari wambele sana katika kusaidia upande wa Sekta ya Afya,naomba apatapo nafasi tena ya kutupatia vituo vya afya,basi Kata ya Tulya ambayo zahanati yake imeharibika katikaKijiji cha Doromoni, iweze kupewa kipaumbele. Sambambana hiyo, aikumbuke pia Kata ya Mtoa ambayo ni Kata yaMbugani ambako upatikanaji wa huduma za afya umekuwawa shida sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuwanimeyasema hayo, naomba niende kuweka ushauri kwenyemambo mawili makubwa. Jambo la kwanza, nimefuatiliamijadala tangu Waziri alipotoa hoja hii. Ni vizuri sananiwashauri Waheshimiwa Wabunge pamoja na Watanzania,kuna mambo ambayo tunatakiwa tuwe tunayabeba kwaumakini mkubwa sana, hasa katika kipindi hiki ambachoMheshimiwa Rais wetu ametangaza vita ya kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wakati wakubigania uhuru walikuwa na stahili zao za kupambana nawalikuwa na namna ambazo wanakumbana nazo. Sasa hiviambapo pana vita ya kiuchumi, hao watu tunaopambananao kwenye vita za kiuchumi ni watu wenye akili, ni watuwenye fedha, na ni watu watu wenye uwezo wa kijasusi. Kwamaana hiyo, kila jambo linapotokea kwenye nchi yetu nivyema sana tukawa tunalitafakari kwa uzito mkubwa badalaya kwenda kwenye uzito mwepesi kama sisi tunavyofanyamambo yanapotokea. (Makofi)

Page 81: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tumeshuhudiakatika nchi yetu yakitokea matukio ya kiuhalifu mengi mengihivi, ambayo kwa bahati nzuri sana Serikali iliyadhibiti yote;moja ya matukio mabaya ni kama yale ya Kibiti; matukiomengine kama yale ya utekwaji wa watoto kule Arusha;matukio mengine ni kama yale ya utekwaji watoto kuleNjombe; na mengine ya kiuhalifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matukio ya aina hii yoteyamedhibitiwa na Serikali kupitia vyombo vya dola hivi hivi.Ni jambo la ajabu sana linapotokea tukio mojawapo lakiuharifu, badala ya watu kuona kwamba nchi yetu imekuwana matukio ya kiuhalifu ambayo yanashughulikiwa na Serikali,kwa sababu za kisiasa na kutengeneza taswira chafu kwaSerikali, watu wanakimbilia kwenda kuhisi kwamba huendamatukio yanafanywa na vyombo vya dola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nilimsikiliza mchangiajimmoja, Mheshimiwa Mbunge wa kutoka Dar es Salaamakisema matukio ya aina hii kwa nini yasichukuliwe kwambayamefanywa na Serikali au kupitia vyombo vyake? Akatoleamfano tukio la kutekwa kwa Mo. Hata mwizi tu ambayeajaenda shule; mwizi wa mifugo aliyeko kijijini, hawezi kuibamfugo, akaenda kuchinjia ng’ombe wake wa wizi mlangonikwa nyumba yake. Sijui nimeongea Kiswahili cha Kikenya!Yaani mwizi hawezi kwenda kuiba ng’ombe, akamchukuango’ombe wa wizi akaenda kuchinjia nyumbani kwake amamlangoni kwake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ukianza kuwazakwamba vyombo vya dola vinaweza vikawa vimeshirikikwenye utekaji, halafu yule mtu akaokotwe, halafu vyombohivi vikampeleke pale; ni kitu ambacho ni kuwaza kwa harakaharaka na kwa kutafuta kuaminisha watu jambo ambalo silo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa watu wanaofikiria,unaweza ukaona na ni muunganiko mkubwa kwamba hawani watu wanaotengeneza chuki dhidi ya Serikali na mambo

Page 82: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

mengine yanaweza yakawa yanafanyika ya muundo huu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloniliona pia ni vyema nikalishauri, hiki ni chombo cha uongozi.Bunge ni chombo cha uongozi, ni chombo cha uamuzi, nichombo cha sera. Kwa kuwa ni chombo cha viongozi,tunapokuwa tunajadili hapa, ingefaa miaka kadhaaitakayokuja watu wakipitia Hansard zeweze kuwapa dirakwamba katika kipindi hiki Taifa lilikuwa linatekeleza mambogani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, sote tunajuakwamba tunatekeleza miradi mikubwa itakayoiwezesha nchikwenda uchumi wa kati. Kwa maana hiyo, kwa kilatunachokusanya kama Taifa na kwa kila Mtanzania siyoviongozi tu; kila mtanzania anatoa mchango wake katikakutekeleza masuala haya; ni vyema sisi tulio viongozitukaweka kipaumbele kuwaelezea Watanzania kwamba kilajambo linalotokea halitokei kwa bahati mbaya, bali linatokeakwa mpangilio kwamba tuna ajenda tunayoitekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, siyo halali kwaviongozi ambao wanajua kinachofanyika kuwa wa kwanzakulalamika kwamba hatuzioni fedha za matumizi mengineyo.Tunatekeleza miradi ambayo itafanya siku zijazo tupate fedhaza matumizi mengineyo nyingi kuliko za sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hilo tu, tunajenga vituovya afya ambavyo havikujengwa kwa muda mrefu; siyokwamba havijawahi kujengwa, vilishajengwa, lakini sasa hivipia kuna vituo vituo vinajengwa maeneo ambayo hajawahikuwa na kituo. Mfano kama Kinampanda pale hatukuwahikuwa na kituo lakini kimejengwa. Sasa tunapokuwatunatekeleza miradi ya aina hiyo tunatumia fedha hizo hizoambazo tunajibana Watanzania wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, inapotokeakwamba tunajibana ili tutekeleze miradi ya maendeleo,wengine wasitumie kama fursa ya kutengeneza chuki dhidi

Page 83: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

ya kundi mojawapo kwamba halijatendewa haki. Mifanoinayotolewa ya watumishi wa Umma; na wenyewe ni sehemuya mpango mkakati huu tunaotekeleza wa kuwezakuhakikisha kwamba tutakapokuwa tumeshatengenezamiradi itakayotengeneza fedha nyingi, tutawezakujipandishia mishahara tunavyotaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuwapandishiawatumishi wa umma…

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mwigulu.

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na MheshimiwaProfesa Jumanne Maghembe ajiandae.

MHE. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekjiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangiahoja ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora. Nitangulize kwakuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri hawa kwa kazi nzuriambayo wanaendelea kuifanya ya kumsaidia MheshimiwaRais pamoja na kulitumikia Taifa hili kwa juhudi kubwa na kwanidhamu kubwa. Naomba pia niwapongeze Manaibu Waziri,Mheshimiwa Mwita Waitara, Mheshimiwa Kandege naMheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa kwa kazi nzuriwanayoendelea kuifanya kuwasaidia Mawaziri na kumsaidiaRais katika kulitumikia Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na sekta ya afya;naomba kuchukua fursa hii kuishukuru sana Serikali ya Awamuya Tano na kuwashukuru sana Mawaziri kwa kutuwezesha sisiJimbo la Bagamoyo kuweza kupata vituo viwili vya afya. Vituohivi viwili vya afya kimoja kimejengwa Kata ya Kerege, kinginekimejengwa katika Kata ya Yombo. Vituo hivi vitachangiasana kutoa huduma nzuri ya afya kwa wananchi wetuakinababa na akinamama na watoto katika kata hizi na kwa

Page 84: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

maana hiyo pia kupunguza mzigo mkubwa ambaoulikuwepo katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambayoilikuwa inazidiwa kiasi cha kwamba inashindwa kutoahuduma nzuri. Tulitengewa pesa nyingi jumla ya shilingi milioni910 kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivi vya afya, lakini piatumetengewa pesa jumla ya shilingi milioni 400 kwa ajili yavifaa tiba kwa vituo hivi viwili. Nashukuru sana kwa kazi hiinzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba, hilijambo ni kubwa sana. Tunapozungumzia kuunganisha aukujumuisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchihapa ndipo ambapo kwa kweli mwananchi anawezaakaona ukuaji wa uchumi wa nchi yake na hili ndiyo jambokubwa la kumfanyia mwananchi wa Tanzania. Mwananchimfanyie mambo mawili; mpe elimu na mpe afya bora. Hivivitu viwili ndivyo vinatengeneza rasilimali kuu ya nchi yetuambayo ni mwananchi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania. Hakuna rasilimali zaidi ya rasilimali watu katika hiinchi yetu. Kwa hiyo niishukuru sana Serikali kwa jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kile cha afya katikaKata ya Kerege kimeshaanza kazi na kituo cha afya katikaKata ya Yombo kinatarajiwa kuanza kazi baada ya mudamfupi. Nimwombe Mheshimiwa Waziri, katika Kata yetu yaKerege ambapo kituo kimeanza kazi, lakini bado kinaupungufu. Upungufu ni katika theatre haijakamilika na vifaatiba bado havijakamilika, kwa maana hiyo hata upasuajibado inabidi tuendelee kuufanya kule katika hospitali yaWilaya ya Bagamoyo. Hivyo, tunaomba tusaidiwe iliupungufu huu uweze kuondoka, tuwe na jengo la OPD,theatre ikamilike ili wananchi wetu waweze kupata hudumaile ambayo inatarajiwa katika Kituo cha Afya cha Kerege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Yombochenyewe bado hakijakamilika kwa maana kinahitaji sasasamani na vifaa tiba ili kituo hiki kiweze kufanya kazi, lakinipia hakijapangiwa watumishi bado. Kwa hivyo, tumefanyakazi nzuri ya kujenga vituo hivi na nina imani kwamba, kwakazi nzuri ambayo tumeifanya na mwaka jana tulitangazwa

Page 85: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

kuwa ni Jimbo namna moja kwa ubora wa kituo cha afyatulichokijenga katika awamu ile. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziriatuunge mkono ili tukamilishe na hiki Kituo cha Afya chaYombo ili nacho kiweze kuanza kufanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maboresho hayayanapelekea wivu pia kwa sababu afya ni jambo muhimusana. Katika Jimbo langu la Bagamoyo, barabara hiiinayotoka Bagamoyo kwenda Msata njia nzima hii kuna zaidiya vijiji 20, Kijiji cha Makurunge, Kidomole, Fukayosi, Mwavi,Mkenge, Kiwangwa na vijiji kadhaa ndani ya Jimbo laChalinze vyote hivi havina huduma yoyote inayofanana nakituo cha afya. Kwa hivyo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisiya Rais, TAMISEMI kwa heshima na taadhima niombe katikabajeti hii inayokuja angalau tupate kituo kimoja cha afyakatika barabara hii ya Bagamoyo kwenda Msata ambachokiweze kuhudumia wananchi wengi katika vijiji vingi katikaeneo hili, pamoja na wasafiri kama ambavyo nakumbushwa.Barabara hii imeshaanza kuwa maarufu sana na inatumikana wananchi wengi wa Kanda ya Kaskazini. Kwa hiyo, nimuhimu sana tuwe na huduma nzuri ya afya katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kuhusuTARURA; Waheshimiwa Wabunge wamezungumza sana nahili jambo ni nyeti, ni muhimu sana Serikali ikaliangalia kwamapana yake. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo,barabara za TARURA zina jumla ya kilomita 332 lakini zikokatika hali ngumu sana. Mwaka huu wa fedha hakuna pesakabisa ambayo imetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleoya barabara za vijijini kwa maana hiyo hatuwezi kufunguabarabara, hatuwezi kuzitengeneza barabara katika hali nzurizaidi. Kipindi kama hili cha mvua barabara zimefungwakabisa, vijiji vimefungwa, huduma za jamii kama shule, afyana kadhalika zinakuwa mtihani kupatikana. Tumetoka safarindefu sana ya miaka mingi iliyopita wakati Wilaya zilikuwahazijaunganishwa kwa barabara za lami, mikoahaijaunganishwa na barabara za lami, lakini hivi sasa kwakazi kubwa ambayo zimefanywa na Serikali zilizopita naSerikali ya Awamu ya Tano mikoa yote inafikika kwa barabaraza lami na karibu Wilaya zote zinafikika pia. Sasa mkazo

Page 86: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

tuupeleke kwenye barabara za vijijini huku ambako wananchiwanaishi na huku ambapo wananchi wanafanya kazi nyingisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri Serikali yetuiangalie uwezekano hata wa kubadilisha mgao ule katikaMfuko wa Barabara ambao traditionally tulikuwa tunapelekaasilimia 70 ya TANROADS, asilimia 30 katika Halmashauri nakwa sasa TARURA ili angalau tuifanye 50 kwa 50 ili tuwezekufanyakazi nzuri zaidi ya barabara katika vijiji vyetu. Hukotutakuwa tumemkomboa mwananchi aweze kuzalishamazao na kufanya kazi zingine zitakazotuletea maendeleo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie eneo lampango wa kunusuru kaya maskini chini ya TASAF. Mpangohuu ni mkombozi sana kwa kaya maskini, ni mpango ambaounaleta tabasamu kwa kaya maskini, yaani hakuna jamboambalo limenifurahisha katika Jimbo langu kama palekukutana na mwananchi wa kaya maskini nayeanatabasamu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kwamchango wako.

MHE. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekjiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa ProfesaMaghembe atafuatiwa na Mheshimiwa Janeth Mbene naMheshimiwa Mussa Mbarouk ajiandae.

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi naminichangie katika Wizara hizi mbili ambazo zote kiongozi wakeni Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Napendanipongeze sana kwa kazi nzuri ambazo zinafanywa katika

Page 87: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Wizara zote hizi mbili. Pia ningependa niwashukuru sanaWaheshimiwa Suleiman Jafo, Mheshimiwa George Mkuchikana Waheshimiwa Manaibu Waziri wote kwa kazi nzuri ambayowameifanya katika kuendeleza Wizara hizi. Unaweza kusekachochote lakini Wizara hizi zinafanya kazi nzuri sana na ni vizurituzipongeze, tuzipe moyo ili waendelee kuwaletewaWatanzania maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa muda wenyewewa kuongea ni mchache nitapenda sana nizingatiemaendeleo kule kwenye Jimbo langu. Nikianza na sekta yaafya; napenda sana niipongeze tena Wizara hii ya TAMISEMIkwa kuvipangia ujenzi vituo hivi 95 katika bajeti hii ambayotunaijadili sasa. Hata hivyo, Mheshimiwa Suleiman Jafoatakumbuka kwamba nilimletea rasmi kabisa matatizoniliyonayo katika Wilaya ya Mwanga katika hospitali yetu yaWilaya ambayo awali i l ikuwa ni kituo cha afya nakupandishwa kuwa hospitali ya Wilaya, Mwanga ilipokuwaWilaya, kwamba tangu mwaka 1979 hadi leo hakuna kitukingine kilichofanywa juu ya kituo cha afya kubadilishwakuwa hospitali ya Wilaya. Hivi sasa majengo yamechakaa,theatre zimechakaa, vitendeakazi vimechakaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru MheshimiwaJafo kwa kutuma timu ambayo ilikwenda ikafanya tathminiya hospitali ile na kuona matatizo yaliyopo, lakini katikaorodha hi ya hospitali 95 siioni hospitali ya Wilaya ya Mwanga.Namwomba sana Mheshimiwa Waziri tafadhali ikiwezekanatwende sisi wawili tukaangalie pamoja ili uone shida kubwaambayo ipo. Hivi sasa theatre karibu inafungwa kwa sababuhakuna vitendeakazi, hakuna vifaa tiba, mortuary jengolimeanguka na majengo kwa ajili ya kuwapa uhifadhiwafanyakazi, nyumba za wafanyakazi hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sanaMheshimiwa Waziri atusaidie kama anavyosaidia kwenyeWilaya zingine ili hospitali hii iweze kutumika vizuri. Aidha,naendelea kushukuru na kupongeza sana katika hatuakubwa zilizofanywa za kujenga na kuboresha vituo vya afyana sisi katika Wilaya ya Mwanga awali tumepata shilingi bilioni

Page 88: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

1.4 kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kisangara na Kituo chaAfya cha Kigonigoni. Tunaendelea kushukuru na fedhaambazo zimepangwa katika bajeti hapa kwa ajili yakukamilisha Kituo cha Afya cha Kifaru. Hata hivyo, badowananchi wa Mwanga wamejenga vituo vingine viwiliambavyo ni karibu kumalizia kama hicho cha Kifaru, Kituocha Afya cha Mwaniko na cha Kileo ambapo tunawaombasana fedha zikipatikana basi tuwasaidie wananchikukamilisha. Wameshajenga, wamebakiza vitu vidogo sanaambavyo wangetupatia shilingi milioni 400 hivi, basi manenoyote yangekuwa tayari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha katika sekta hi yaafya, wananchi wa vijiji sita katika Wilaya ya Mwangawanaendelea kujenga zahanati na karibu zinakamilika.Zahanati hizi za Kituri, Mrigeni, Lembeni, Nyabinda,Lang’atabora na Vanywa ziko karibu kabisa kukamilika,wananchi wamejenga mpaka wamepaua lakiniwamechoka. Tunawaomba sana katika huu utaratibu wakumalizia maboma, ya kwao siyo maboma wameshapaua,basi watusaidie kukamilisha zahanati hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili kubwa ambalonataka niliongelee ni suala la elimu. Katika Wilaya yaMwanga na hasa katika elimu ya msingi nimesema hapamara nyingi shule zetu hazina Walimu kabisa. Kati ya shule117, shule 50 zina Walimu wawili, wawili peke yake na shulezingine 40 zina Walimu watatu, watatu, sasa utapiga hesabumwenyewe uone ni ngapi ambazo zina Walimu wanne.Hakuna shule ambayo ina zaidi ya hapo labda zile ambazoni za watoto wa mahitaji maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Mwangahatuhitaji Walimu wapya. Tunachoomba Serikali itupe niWalimu ambao watachukua nafasi za Walimu waliostaafu,wale ambao wamefariki au wale ambao wamehamishwana Serikali kwenda maeneo mengine kufanya kazi. Kwa hivyo,sioni sababu ya kuchukua mwaka na nusu kulishughulikiajambo hili. Watoto wanateketea, wanapotea, hawanaMwalimu wa kuwafundisha, Walimu wawili wakiingia kwenye

Page 89: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

madarasa saba, watoto wa madarasa matanowanabadilisha shule inakuwa soko. Kwa hivyo, tunawaombasana, hatuombi Walimu wapya, mishahara yao ipo kwasababu wale waliokuwepo walikuwa na mishahara nahakuna sababu yoyote ya kutotupa Ealimu kwa sababuEalimu wako barabarani hawana kazi. Kwahiyo nawaombatena…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Profesa kwa mchangowako mzuri.

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante na naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mbeneatafuatiwa na Mheshimiwa Mbarouk na ajiandaeMheshimiwa Mbatia

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotubaya Wizara hizi mbili muhimu sana. Nianze kwanza kwakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia siku njema, lakinivilevile nataka kuwapongeza sana Waheshimiwa Mawaziriwa Wizara hizi mbili, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu nawatendaji wote wa Wizara hizi muhimu sana kwa mustakabalina maendeleo ya nchi yetu. Hizi ni Wizara ambazo unawezaukasema ni pacha; moja inasimamia Utumishi na UtawalaBora, nyingine inasimamia utekelezaji wa miradi yamaendeleo katika ngazi ya halmashauri na miji yetu. Kwahali hiyo, kuna haja kubwa sana ya kuhakikisha kuwa kwanzazinawezeshwa kifedha, lakini vilevile kimfumo na pia kwawatumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeanza hivyo kwa sababutunapozungumzia utumishi na tunaposikia michango yote yaWabunge ikilalamikia watumishi na upungufu wake nafikiri

Page 90: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

kuna haja sasa ya kuchukua hatua ya makusudi ya kimkakatiya kujaza hizi nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna tatizo kubwa lawatumishi katika Wilaya zetu hasa kwenye sekta ya afya,kwenye sekta ya elimu, kwenye sekta ya maji yaani karibukila sehemu ina matatizo ya upungufu wa watumishi. Mimibinafsi katika wyangu nia upungufu mkubwa sana wa Walimukatika shule za msingi na shule za sekondari, lakini hasa hasakatika shule za sekondari ni Walimu wa sayansi. Tuna tatizokama alilolisema Mheshimiwa Maghembe kuwa sehemunyingine ni kujaza nafasi tu za watu ambao wameondokaaidha kwa kustaafu, au kwa kufa, au kwa kuhama. Sasa hilini jambo ambalo naamini halipaswi kuchukua mlolongomrefu kama vile ambavyo tunavyongojea vibali vya ajirampya labda nisahihishwe kuwa hivyo sivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nitakuwa mtovu washukurani kama sikutoa shukurani zangu kwa jinsi ambavyowilaya yetu imepatiwa fedha ya kumalizia hospitali ya wilayaambayo Awamu ya Nne tulipata fedha kwa ajili ya kuianzana sasa hivi tumepata bilioni moja na milioni mia tano kwaajili ya kuimalizia. Naamini fedha hii itatosha kumaliziahospitali, itajenga nyumba za Wauguzi na vilevile kumaliziamiundombinu yote iliyokuwa inahitajika, nawashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashukuru kwa kupatafedha ya vituo vya afya viwili vikubwa na tumeahidiwakingine cha tatu, lakini niombe tupate na cha nne kwasababu wilaya yangu mimi ina tatizo la miundombinumigumu; milima, mabonde na umbali kati ya kata mojakwenda nyingine. Hii kwa vyovyote vile inasababisha umbalikuwa mkubwa na bila kuwa na zahanati za kutosha hatavituo hivi vya afya vinaweza visisaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye zahanati;tulikuwa tumeweka kwenye bajeti yetu milioni 200 kwa ajiliya kukarabati maboma ya zahanati saba ambayoilishapitishwa kuwa zitakuwepo, lakini ghafla tukaja kuambiwatuziondoe katika bajeti yetu kwa sababu zinapelekwa Mbozi

Page 91: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

na Songwe. Hii imetuathiri sana kwa sababu haya mabomaya zahanati yameshafikia mahali pazuri kumaliziwa na hizifedha tulikuwa tumeshazitarajia kwa sababu zilikuwazimeshakubaliwa sasa kuja kuziondoa tu juu juu hivi zinatuathirisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema Wilayayangu miundombinu ni migumu, usipokuwa na zahanati hataya kuanzia tu kumtibu mwananchi kufikia vituo vya afya nitatizo hasa wakati wa mvua. Naomba sana Wizara yaTAMISEMI mliangalie hilo na mturudishie ile shilingi milioni 200ambayo mlikuwa mmeitoa wakati tayari tulikuwatumeshakubaliana kuwa itakuwepo katika ceiling zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kushukurukwa fedha iliyotolewa kwa Daraja la Mwalisi ambalolinaunganisha Wilaya yangu na Mgodi wa Kiwira. Hili darajalitatusaidia kwa sababu ilibidi kutoa makaa ya mawe nakuyapitishia Kyela na huko ilikuwa ni Wilaya nyingine of coursena ilikuwa inaleta gharama kubwa na usumbufu kutokanana umbali wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuzungumziasuala la TASAF. TASAF imekuwa msaada mkubwa sana kwanchi nzima na hata kwa Wilaya yangu. Nataka niombe vilevijiji 21 kati ya 71 ambavyo havijaingizwa katika mpango huubasi na vyenyewe viweze kuingizwa kwa sababu faida zakezimeonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kidogo nataka niongeleesuala zima la TAKUKURU au masuala mazima ya ufisadi aurushwa. Tunashukuru kuwa imeanzisha Mahakama ya Ufisadilakini kiwango cha watu wanaopelekwa pale cha bilionimoja ni kikubwa sana, mafisadi wengi sana wanaachwahapa chini hawawezi kufikia Mahakama hiyo kwa sababuhawajatuhumiwa kwa kiwango hicho kikubwa. Kiwango hikikingepunguzwa kidogo mafisadi au watuhumiwa wengi zaidiwangeweza kufikiwa na rushwa ikapungua lakini badorushwa ipo na inalalamikiwa sana, tusijidanganye. (Makofi)

Page 92: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo juhudi zinafanywalakini bado rushwa nyingi ni tena inafanywa waziwazi katikataasisi zilezile ambazo zimekuwa zikilalamikiwa siku zote Polisibarabarani, Mahakama na sehemu zinazotoa huduma zaafya na hata elimu. Naomba sana tusielegeze kamba rushwabado ipo, wanagundua misemo mipya, ohoo, sijui kula samakigizani, kuna maneno yanayotumika ambayo hayatufurahishikwa sababu rushwa inaondoa haki za kimsingi za watu wakawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nataka kuzungumziasuala la watumishi. Watendaji wakubwa katika taasisimbalimbali wanahitaji kupata mafunzo ya kutosha yauongozi. Tulikuwa na vyuo vyetu vilikuwa vinatoa elimu hiyolakini najua sasa hivi tuna Uongozi Institute, napenda sanakuona mpango mkakati wa jinsi gani ya kuwapelekawatendaji hawa kwenda kujifunza kwa sababu pamoja nakuwa ni viongozi wa taasisi mwenendo hauoneshi ileleadership ambayo inategemewa kwa viongozi wa ngazi hii.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine ambalolinaanza kuzoeleka la Watendaji Wakuu wanaopata nafasikuhamishwa kwenye taasisi aliyokuwa mwanzo kuanzakutengeneza himaya zao, wanaondoka na watu wao wotewaliokuwa nao kwenye taasisi moja wanawahamishiakwenye taasisi nyingine na kuleta sasa tabaka zawaliokuwepo na waliokuja, hii inaleta chuki na inavunja moyowale waliokuwepo. Mimi nafikiri suala hapa ni kujenga taasisiimara siyo kujenga Watendaji Wakuu wa taasisi imara. Kwahiyo, naomba hili pia liangaliwe la huu mtindo watu kuhamana ma-secretary wao na viti na meza za maofisini kama vilewanahama nchi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)

Page 93: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaMbarouk, Mheshimiwa Mbatia na Mheshimiwa Kiswagawatafuata.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Munguambaye ametuwezesha kuwa na afya njema na kuwezakukutana katika kikao chetu hiki cha Bunge na kuzungumziamambo mbalimbali ya nchi yetu. Pia nishukuru wapiga kurawangu wa Jimbo la Tanga bila kukusahau wewe kwa kunipanafasi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kuchangiaTAMISEMI, labda nami niwe miongoni mwa wale ambaotunashukuru kwa ule mpango wa kujenga vituo vya afya 300.Kwenye Jimbo langu la Tanga tumepata vituo vya Makorola,Mikanjuni na Ngamiani. Tumepata takribani shilingi bilionimoja na milioni mia nne. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile pia nisisahaukwamba tulikuwa mgogoro wa Hospali ya Wilaya ijengwesehemu gani. Baada ya kuwasiliana na Mheshimiwa Wazirihapo mambo yamewekwa sawa na sasa ujenzi unaendelea.Nishukuru kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije sasa kwenye suala laelimu hususani elimu bure. Elimu bure mimi niseme imepigiwadebe sana lakini wananchi na wazazi bado hawajaielewavizuri na hata badhi ya Wabunge nafikiri hawajaielewa vizurikwa saabu unaposema kitu bure ni ile free no charge sasawazazi kufuatia suala hilo wamekuwa wazito kuchangiamasuala ya umeme na maji, fedha ya mlinzi na hataakuchangia vifaa. Unapowahoji wanakwambia kwambatumeambiwa elimu bure na ndiyo maana watotowameongezeka sana katika shule zetu za msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niitake Serikali sasa, kwasababu watoto tumekuwa kama tunawaadhibu katikabaadhi ya shule maji yamekatwa kwa sababu kufuatia kauliya Mheshimiwa Rais ile anayosema maneno ni mawili ‘Kata’

Page 94: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

kwamba panapodaiwa maji na umeme kata. TANESCO naMamlaka za Maji sasa hivi hazitoi huduma zinafanya biasharamatokeo yake umeme na maji katika shule yamekatwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yaketunawaadhibu watoto. Wanafunzi hawa masikini ya Mungu,malaika wa Mungu hawana hata maji ya kunywa shuleniwanalazimika ama kubeba chupa za maji katika mabegi yaowanayoweka madaftari au kama wako shule basi pananyumba ya jirani karibu waende wakaombe maji ya kunywakatika nyumba za jirani. Naiona hii ni hatari kwa sababu katikabaadhi ya nyumba kuna watu wengine siyo wema, mathalaniwatoto wa kike tunaweza kuwahatarisha maisha yao kwakubakwa na kupata maradhi ya UKIMWI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Serikali isiongezefedha katika ule mpango wa kupeleka capitation na fedhaza matumizi katika shule tukaweza kulipia maji na umemekwenye shule zetu? Au kwa nini Serikali isisamahe kwenyeshule za msingi na sekondari lakini nifike mbali zaidi hatakwenye Misikiti na Makanisa kule ambako Mwenyezi Mungutunamwomba nchi iendelee kuwa amani tuweke hudumaya maji na umeme iwe bure? Kwa hiyo, naishauri Serikalilifanyiwe kazi suala hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa nini piatusiwape umeme wanafunzi wakaweza kutuumia katikakujifunza kwa sababu kuna mambo mengi. Sote tumepitiaelimu ya msingi panakuwa na umeme mnajifundisha mambomengi, sote tumeyaona haya. Kwa hiyo, naiomba Serikali hilowalifanyie kazi na tuliambiwa kwenye bajeti ya mwaka janakwenye Wizara ya Nishati na Madini kwamba kwenye huuumeme wa REA watahakikisha kuwa shule zote nchinizinawekwa umeme, naliomba suala hilo liharakishwe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nalotakakulizungumzia ni suala la dawa. Tumeona dawa zilitengewatakribani shilingi bilioni 531 lakini fedha iliyopokelewa ilikuwa

Page 95: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

ni shilingi milioni 81, pana tofauti ya takribani shilingi bilioni450. Kama ikiwa tunatenga fedha kubwa halafu fedhatunayopeleka ni kidogo hatuwasaidii wananchi wetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri hakuna haja yakuweka kasma kubwa halafu tunapelekea asilimia ndogo yafedha. Kama tumepanga shilingi milioni 5312 basi angalaukungepelekwa shil ingi milioni 400 hapo ingekuwatumewasaidia lakini katika shilingi bilioni 531 kupeleka shilingimilioni 81 tu tunawakwaza ama madaktari na watumishi wetuwa Idara ya Afya. Kwa hiyo, naiomba Serikali paleinapopanga bajeti ihakikishe fedha inapatikana nainapelekwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwenye Mfuko waMaji, Tanga tunayo miradi ya maji ya ile vijij i 10 kilaHalmashauri lakini kwa masikitiko makubwa niseme upandewa Kusini tulifanikiwa, maji yanatoka kuelekea upande waMarungu, Kirare, Tongoni na wananchi sasa hivi wanaombahuduma ya maji ipelekwe mpaka kwenye nyumba zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, katika mradi waKaskazini wa Mabokweni, Kibafuta, Mpirani na Chongoleanimpaka leo kuna kizungumkuti, maji hayatoki na wananchiwana shida ya maji na mimi mwenyewe nimefikanikashuhudia. Nitamwomba tu Mheshimiwa Waziri wa Majiau Naibu wake mara baada ya Bunge hili tutembelee ili tujuekikwazo kwa nini maji hayatoki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika mradi huohuowa maji, Kamati PAC ambayo nipo tumetembelea mradi wamaji ule wa Chalinze na maeneo mengine naona kuna hitilafukidogo kwa sababu fedha zilizoahidiwa katika mkopo ilikuwani takribani shilingi bilioni 158 mpaka sasa hivi zimetumikashilingi bilioni 93 lakini kuna shilingi bilioni 65 bado hazijatumika.Hata hivyo, kuna masharti ambayo katika miradi ile vifaavyote hadi bolt lazima itoke kwa yule mtu ambaye mmeingianaye mkataba kwamba awakopeshe.

Page 96: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, ule mradiunafadhiliwa na India sasa basi hata mipira, bolt, nati zakwenye mradi lazima zitoke India! Tunasema tunalindaviwanda vya ndani, tunalindaje viwanda vya ndani kwamiaktaba mibovu kiasi hiki? Ina maana watumishi sasabaadhi ya ma-expert ambao wapo hata Watanzaniawanashindwa kulipwa sawasawa na wale ma-expert waKihindi, naona hiyo ni dosari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nizungumzie utawalabora. Ukitazama Katiba, Ibara ya 146(1)(2)(c) kinaeleza hapakwamba, madhumuni ya kuwepo Serikali za Mitaa nikupeleka madaraka kwa wananchi na vyombo vya Serikaliza Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki nakuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli zautekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kotekwa ujumla. Ukienda kwenye kipengele (c) inasema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Thank you. Tunaendelea na MheshimiwaMbatia atafuatiwa na Mheshimiwa Kiswaga na MheshimiwaSeif Gulamali ajiandae.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipatia nafasi na mimi nitoe mawazoyangu kwenye hoja iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa leo ni SokoineDay, alikuwa kiongozi mashuhuri kwa Taifa letu, ni siku yakumkumbuka miaka 35. Mwenyezi Mungu amrehemu natutekeleze yale mema aliyofanya kwa Taifa la Tanzania.(Makofi)

Page 97: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraharaka nianze naTARURA. Nimpongeze Mtendaji Mkuu wa TARURA kwa kazinzuri kubwa anyoifanya kwa Taifa letu na TARURAHalmashauri ya Wilaya ya Moshi wanafanya kazi nzuri.Nachowakumbusha tu ni ahadi za Mheshimiwa Rais kwabarabara za Himo Mjini pamoja na barabara ya Kilema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Vunjo lina barabarazenye kilometa 389.3, TARURA walifanya kazi hii ya kupima,nawapongeza sana, wakishirikiana na Vunjo DevelopmentFoundation (VDF) na barabara hizi zitagharimu shilingi bilioni12.7, wananchi wameanza kuchanga wenyewe, Mbungenimenunua mashine, Serikali imeahidi kutoa shilingi milioni 200kwenye mradi huu kwenye barabara walizoweka kwenyekitabu, naipongeza Serikali. Hata hivyo, shilingi milioni 200 katiya shilingi bilioni 12.7, naomba waongeze fedha hizi.Waliotengewa shilingi milioni 200 ni barabara ya Chekereni -Kahe ambayo tunashukuru lakini ni kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni elimu msingi,nimeuliza swali asubuhi, naomba tu kujua na tulitendee Taifahaki, hapa tuna Sera ya Elimu na inafafanua vizuri maudhuiya Sera ya Elimu na elimu msingi ni ipi na elimu sekondari niipi. Je, Taifa hili leo hii linaongozwa na Sera ipi ya Elimukuandaa Taifa kwa miaka 30, 40 au 50 ijayo? Nitazungumziazaidi wakati wa bajeti ya elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongele kuhusu ikama yawatumishi. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kuna upungufuwa walimu 379, shule zingine zina walimu wawili, watatu nasekta ya afya pia ina matatizo makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tuko na wenzetuwenye albinism, niwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanyana mwaka huu ni wa kudumisha, kutetea na kulinda utu,heshima na mahitaji msingi ya watu wenye ulemavu.Nikiangalia bajeti iliyoletwa hapa bado walemavu wetuhatujaweza kuwaweka kwenye hali ya utu wao, heshima yaona mahitaji msingi yao ili na wao wajione ni binadamu. Sisiambao tunajiona tuna akili nzuri na tumekamilika tunawaita

Page 98: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

walemavu lakini kwa kiasi kikubwa ukiangalia sisi tunaowaitawalemavu ulemavu wetu wa fikra ni mkubwa kuliko ulemavuwao wa viungo vya nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimponge sana Dkt.Reginald Mengi na Taasisi yake ya kutetea na kukuza utu wawalemavu. Dkt. Mengi anafanya kazi nzuri sana na niiombeSerikali imuunge mkono. Tulikuwa na Mheshimiwa Makamuwa Rais tarehe 17 mwezi uliopita na Naibu Waziri, dada yanguMheshimiwa Stella Ikupa katika shughuli ya kuwajengea utuwalemavu, kwa hiyo wapewe nafasi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa kwenye mkutanowa Dkt. Martin Fatael Shao, Askofu Mstaafu naye amefanyautafiti kwenye sekta ya afya na watoto na imeonekana shulezetu haziko vizuri. Kwa kuwa nina ripoti yake hapa,nampongeza Askofu huyu kwa kazi nzuri anayofanya kwawalemavu, shule za msingi, elimu ya afya na kitabu hikinitakiweka Mezani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka haraka niingiekwenye utawala bora. Ndugu Isaac Newton anasema katikakila kanimkabala kuna kani iliyo mrejeo sawa na kinyume.Viongozi wowote wale hawaokotwi kwenye majalalaviongozi huandaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1995 weweulikuwepo Bungeni, alikuwepo Mheshimiwa Mzee Lubeleje,Mheshimiwa Ndassa na Mheshimiwa James Mbatia kati yaWabunge wote waliopo sasa, tulikuwa wanne. Wakati huotulivyokuwa Bungeni ukiwa Mwanasheria Mkuu viongoziwaliandaliwa kwa kupewa semina na kuelezwa jukumu lakwanza la Mbunge ni kwa Taifa lake; la pili kwa Jimbo lake laUchaguzi; la tatu kwa chama chake cha siasa; na la nnekwa dhamira yake binafsi.

Sasa hapa Bungeni leo hii watu wanachukuliamambo personal kana kwamba issues ni personal, sisitunapita tu, tuijenge nchi yetu, wanasema great minds discussideas, Taifa hili ni letu sote. (Makofi)

Page 99: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilibahatika kuongea naMheshimiwa Rais kwa mapana sana tu tukakubaliana Taifahili likiharibika au likienda mrama tunaangamia sisi sote,halichagui huyu ni wa chama gani, kwa hivyo, tuitazame nchiyetu. Let us think positive and big, let us think big yaani tufikirikwa mapana tu, nchi yetu miaka 50 itakuwa kwenye haligani. Kapteni Mstaafu Mheshimiwa Mkuchika unakumbukamwaka 1992, 1995 ukiwa DC wa Ilala wakati tunaanzishamfumo wa vyama vingi tulikuwa tunakuja ofisini kwako,tulikuwa tunaongea tuwe na Taifa gani baada ya miaka 25,miaka 30 ijayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimesema hayo?Nimesema hayo kwa sababu nimeisoma hotuba yaMheshimiwa Kapteni Mheshimiwa Mkuchika, ukiangaliaTaasisi ya Kupambana na Rushwa kazi walizonazo hapa nizaidi ya 10 au 15 kama sijakosea lakini ukiangalia bajeti yaoni ndogo kweli kuweza kuzama mpaka chini. Kauli mbiu yataasisi hii nilikuwa nao wiki iliyopita kwenye semina na dadayangu Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri paleTAKUKURU, tulitoa rai, huwezi ukasema unazuia, unapambanahalafu ndiyo unaelimisha, hapana. Nilitoa rai siku ile kwambatuanze na kuelimisha kwanza madhara ya rushwa.Tukishaelimisha ndiyo tutaenda sasa na hayo mengine yakuzuia na kupambana, tuelimishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tusiseme hapakwamba kesi ziko 476 na nyingine zinaongezeka tujengemazingira kesi zipungue zaidi kwa sababu ya watu kujuamadhara na kujielimisha zaidi badala ya kufikiri kwambazitaongezeka.tuwekeze kwenye kuondoa maovu zaidikwenye jamii badala ya kufikiria maovu yataongezekakwenye jamii. Hii ni namna ya jamii kujitambua na kwa moyowa dhati kabisa nimpongeze CP Diwani Athumani na timuyake kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuweza kupambanana rushwa katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali hii ukiangaliakwenye uongozi baada ya rushwa, unaona wamepewamajukumu nane ambako tungewekeza zaidi kwenye taasisi

Page 100: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

ukurasa ule wa 80, tulishakubaliana tangu mwaka 2002 naKomredi Mangula, Katibu Mkuu wa CCM, wakati huo tukokwenye TDC, nimpongeze sana Nsanzugwanko waanzilishiwa TDC (Tanzania center for Democracy) tulikubaliana Taifaliandae viongozi. Ukiangalia ma-RC, ma-DAS na ma-DEDwetu wanaibukaje, vetting yao ikoje katika utumishi wa ummawa Tanzania ili waweze kuwa ni endelevu katika kutekelezamajukumu yao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda kwa ma-DC naMa-RC wetu, tumpongeze Kapteni Mheshimiwa Mkuchikauliwahi kuzungumza hapa, wanaandaliwaje, wanapikwajeili waweze kutekeleza majukumu ipasavyo? Kwa hiyo,wasiibuke tu kila mtu na mambo yake, huyu anasema hili,yule anasema lile, kwa kweli tukiangalia kama wataendeleakufanya wanavyofanya tutakuwa hatulitendei Taifa letu haki.Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mheshimiwa Mwenyekiti, rasilimali kubwa kuliko zoteduniani leo hii ni rasilimali watu (umoja) na utawala bora is acollective approach inaanzia kwangu, kwako, kwa jamiinzima, kwa familia baadaye kwa Taifa. Mwalimu alikuwaanajua kwamba Taifa analipeleka wapi ndiyo wanafunzitukawa tunaimbishwa kama kasuku ahadi za mwana-TANU,unaambiwa binadamu wote ni ndugu zangu, unajua kuwahuyu ni ndugu yangu; unambiwa rushwa ni adui wa haki,sitapokea wala sitatoa rushwa, tulikuwa tunapata Taifaambalo linaendelea, ni shirikishi, la wote kwa kuwa nchi hii niyetu sote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kujitambua ni jambomuhimu sana na inatupasa sisi sote kwa pamoja kujuautawala bora ni wa pande mbili; anayeongoza naanayeongozwa, is a collective approach . Huweziukauchukulia utawala bora kwa yule tu anayeongoza.Ukikubali mawazo mbadala ukawa na utulivu; nimeona hatahapa Bungeni, unakuta Mbunge anaongea, mwingineamemwingilia, mwingine amefanya hivi. Hata MaandikoMatakatifu yanasema kujibu kabla ya kusikiliza ni upumbavuna aibu kwako ambaye hujataka kusikiliza. (Makofi)

Page 101: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Tusikilizane, tuvumiliane, tuwe na lugha ya staha. Taifahili ni letu sote. Tukiwa na mawazo mapana namna hiyo,ninaamini hapa tulipo leo hii tutatoka na Tanzania ya leo,nani mwenye kujua kesho?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji Taifa endelevukwa maslahi mapana ya mama Tanzania. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia, nakushukuru sanakwa mchango wako, ahsante sana. Ndiyo maana yauongozi. (Makofi)

Tunaendelea, Mheshimiwa Boniventura Kiswaga,Mheshimiwa Seif Gulamali na Mheshimiwa Ajali Akbar Rashidwajiandae. (Makofi)

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hotubahii. Moyo usio na shukrani hukausha mema mengi. Napendakuwapongeza Mawaziri; Mheshimiwa Jafo, MheshimiwaMkuchika na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja naWakuu wa Taasisi wanazoziongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa jambo hili kwanzanapongeza kwa sababu nimepata vituo viwili vya afya; nacha kwanza kiko hapa cha Kahangara kwenye mfano wahotuba hii. Bado nina vituo vya afya vitatu; Kituo cha Afyacha Kabila pamoja na Kituo cha Afya cha Kisesa naNyanguge. Vituo hivi ni muhimu sana, Serikali ione namna yakuweza kunisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Mheshimiwa Mbatiaanachangia hapa, ndiyo maana nimeanza na moyo usio na

Page 102: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

shukrani; Mheshimiwa Mbatia ameishukuru Serikali hii. Kamawapinzani wa nchi hii wangekuwa kama MheshimiwaMbatia, upinzani ungeweza kusaidia nchi. Kwa sababumichango aliyoitoa ni kwa maslahi ya Taifa hili. Munguakubariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii inaendeleakuboresha huduma. Kwenye hospitali, ninajua mnaendeleakujenga hospitali mpya, lakini hata hospitali yangu ya Magu,Mheshimiwa Jafo ni shahidi amefika mara mbili, inahitajiukarabati. Kwa sababu tumezungumza naye ninaaminijambo hili atalichukua kwa uzito wa pekee kwa sababu yeyeni shahidi amefika OPD, inaweza kuanguka wakati wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye barabara.Magu tuna kilometa za barabara 1,600. Kwenye bajeti hiitumepangiwa shilingi milioni 900, hazitoshi hata kidogo.Naiomba Serikali, kwa sababu TARURA inapokea asilimia 30na TANROADS inapokea asilimia 70, wangalie namna yakubadilisha sheria ili mradi TARURA ipate asilimia 50 naTANROADS ipate asilimia 50 ili barabara zetu za wilayani kuleziweze kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kumpongezasana Chief wa TARURA ni msikivu. Ukimpigia simu wakatiwowote anapokea, naye anazunguka kwenye barabarazote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna daraja pale Mahaha,Itubukiro kwako kule, tunaunganishwa na daraja, halipo. Ilikuunganisha mawasiliano ya kiuchumi ni vizuri waangalieTARURA namna yoyote ambayo wanaweza kutusaidiamadaraja ili tuweze kuunganisha hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna barabara ya Magu– Isolo, kuanzia Kabila – Isolo na Isawida kule kutokea Itilima,pale tunatenganishwa na daraja. Magu tumelima mpakakwenye mpaka wa Itilima na Itilima imelima mpaka kwenyempaka wa Magu; TARURA ninakuomba utupatie daraja natulikuja ofisini kwako na Mheshimiwa Njalu kuomba pale utupe

Page 103: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

daraja ili tuweze kuunganisha mawasiliano ya wilaya hizombili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Magu tumejenga mabomavijiji 21 ambayo yako tayari, zinahitajika fedha za kuwezakukamilisha na hili ni la ki-Ilani. Tulisema Ilani ya Chama chaMapinduzi kila kijiji kiwe na zahanati, wananchi wameitikia,wamejenga, wanahitaji kusaidiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara hii kamaambavyo inafanya kazi, iangalie namna ya kutoa fedha kwaajili ya maboma ya nchi hii ikiwemo Wilaya ya Magu ili tuwezekuwapa nguvu wananchi kwa kazi ambazo wamezifanya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mkanganyiko wawaraka. Waraka uliokuja unasisitiza nyaraka zilizopita, lakiniWakurugenzi wameshindwa kutafsiri waraka huu. Wamefutaper diem wamekwenda kusisitiza kwenye sitting pekee.Madiwani hawa ni viongozi, ndio wanaofanya kazi, ndioWenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata, ni vizuritukawaona. Kwa sababu hawa huwa tunachagua nao sikumoja, ni vizuri tukawapa maslahi yao ya kweli. Kuna Diwanianatoka kilometa 40, kuna Diwani anatoka kilometa 20; waowameangalia tu pale mwisho kwamba kama kunauwezekano wa kutolala wasilipwe per diem. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni Mbunge. Mbungena Diwani kila kunapokucha asubuhi watu wanajaa ukiwaJimboni au kwenye Kata yako. Ndiyo maana ikawekwa perdiem ili Diwani atoke kwenye familia yake aende akalaleMakao Makuu ili concentrate vikao vya Halmashauri. Kwahiyo, perdiem hii wanapaswa walipwe WaheshimiwaMadiwani hawa. Madiwani hawa hakuna shereheinayompita, hakuna kilio kinachompita na hakuna mgonjwaanayempita. Mimi nilikuwa Diwani na sasa ni Diwani kwamujibu wa sheria kwa sababu ya Ubunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana TAMISEMI,Mheshimiwa Kandege uko hapo. Kandege andika hili,

Page 104: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Kandege andika hili, mtafasiri waraka huu, ili Madiwaniwaweze kulipwa per diem yao. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kiswaga naonaumepandisha? Mwite tu Mheshimiwa Kandege.

MHE. MUNGE FULANI: Aongezwe dakika huyu.

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti,niongeze kwa mamlaka uliyokuwanayo.

MWENYEKITI: Tumia basi lugha ya Kibunge, mwiteWaziri Mheshimiwa Kandege.

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Kandege.Mheshimiwa Kandege. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Tena, rudia!

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Kandege,sikiliza hili na aandika ili mtafsiri waraka huu Madiwani wawezekulipwa perdiem. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sauti yangu ni ya msisitizo,nasisitiza tu, siyo kwamba, labda nafoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakwenda kwenye ServiceLevy. Hii Service Levy wakati inatungwa Sheria ya Serikali zaMitaa ilikuwa inalenga viwanda. Kwa mfano, kama kiwandacha Tanga Cement kimezalisha simenti na inauzwa hapaDodoma, Halmashauri ya Dodoma ina-claim madai yake yaService Levy Tanga. Leo Tanga Cement kama hapa Dodomaina tawi, inatozwa hapa, akinunua Dodoma hapa kupelekaMvumi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Kiswaga.

Page 105: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti,nilikuwa…

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti,basi naunga mkono hoja. Kumbe dakika 15 ni muhimu sana.

MWENYEKITI: Haya. Mheshimiwa Gulamali, halafuMheshimiwa Akbar na Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabuwajiandae.

MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi kuweza kuchangia Wizarahii ya TAMISEMI na Utawala Bora. Kwanza napenda kutumianafasi hii kuipongeza Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli kwa kazi kubwa ambazo inafanya, ama miradimikubwa ambayo inatekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona miradi kamaStieglers Gorge ambapo kwa ukamilishaji wa mradi huututapata Megawati kama 2,100 za umeme, tunaona ujenziwa Standard Gauge (SGR), ujenzi wa kisasa wa reli yetu,tunaona usambazaji wa umeme vijijini, vijiji vyote vitapataumeme, tunaona vituo vya afya na hospitali karibu 67zinajengwa nchi nzima. Miradi hii yote ikikamilika, ninaaminiTanzania itakuwa kati ya nchi 10 bora katika Bara la Afrikaout of 54 countries. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo zaSerikali katika kutekeleza miradi mikubwa, binafsi naungamkono na wananchi wa Jimbo la Manonga wanaungamkono harakati zote za Mheshimiwa Rais kupeleka nchi yetukatika uchumi wa kati. Sasa nianze kwa maombi yangu kamaWilaya na Jimbo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara yaTAMISEMI, kwanza nawashukuru kwa kunipatia fedha kwaajili ya Kituo cha Afya cha Simbo. Kituo kimekamilika, sasa

Page 106: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

kilichobaki ni vifaa tiba. Naiomba Wizara ya TAMISEMI ituleteevifaa tiba katika Kituo chetu cha Afya cha Simbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nawaomba Wizaraya TAMISEMI, Jimbo letu ni kubwa sana. Mwaka 2018 Agosti,alikuja Mheshimiwa Waziri Mkuu Jimboni, alituahidi kutupatiafedha shilingi milioni 400 kwa ajili ya Kituo cha Afya chaChoma cha Nkola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Chomabaada ya Hospitali ya Wilaya ya Igunga kinachofuatia ni Kituocha Afya cha Choma ambacho kinafanya operation ndogondogo. Karibu operation 150 wamekwishafanya, lakinichangamoto iliyoko pale hatuna jengo la akina mama nawatoto, hatuna jengo la kufulia nguo, hatuna mortuary,hatuna ward ya akina baba. Kwa hiyo, bado operation hiziwanapata changamoto sehemu ya kuwahifadhi wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri, nimeangalia kitabu chake sijaona bajeti ya fedhaambazo Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi katika ziara yake.Tunaomba fedha kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa Kituo chaAfya cha Choma cha Nkola ili kuweza kuhakikisha kwambatunasogeza huduma bora kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona bajeti hapa yaWizara ya Afya. Tumetenga fedha za ujenzi wa hospitali katikaWilaya mbalimbali nchini. Wilaya yetu ya Igunga MakaoMakuu ya Wilaya ni Igunga. Pale tuna hospitali ya wilaya.Hospitali yetu imechakaa sana, hatujapata fedha zamaboresho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaWaziri tuangalie katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, hatunaambulance. Nilinunua ambulance nikapeleka kwenye Kituochangu cha Afya cha Simbo. Sasa inachukuliwa ileambulance ya kijijini, kwenye Kituo cha Afya cha Simbo,inaletwa mjini. Kwa hiyo, ile adha ambayo nilikuwa nimeendakupunguza kwa wananchi inakosekana. Tunaombaambulance ya wilaya iletwe, ili iweze kuhudumia kwa sababu

Page 107: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

mahitaji ni makubwa na katika makao makuu ya wilaya watuni wengi sana wanahitaji kupata huduma hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena tupate fedhakwa ajili ya kuongeza matengenezo kwani hospitali ya wilayaimechakaa, haina uzio, hakuna maabara ya kisasa. Kwa hiyo,namwomba Mheshimiwa Waziri kwa sababu, mpo hapoWizara ya TAMISEMI, mtupatie fedha kwa ajili ya kuboreshahospitali yetu ya wilaya ili kuboresha na kusaidia kupatikanahuduma za afya katika Wilaya yetu ya Igunga, hasa MakaoMakuu ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kwenye shule zaSerikali za wasichana. Tumeona ujenzi wa shule za Serikali zawasichana zikijengwa maeneo mbalimbali katika nchi yetu.Tabora Mjini tunayo natambua iko Tabora Girls, nimeonaNzega pale imejengwa. Naomba sasa, katika Wilaya yetuya Igunga hatuna shule hata moja. Mimi binafsi katika Jimbolangu niko tayari na tuko tayari kutoa kiwanja kwa ajili yaujenzi wa shule, tukishirikiana na TAMISEMI, tutajenga pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba shule hizo zawasichana zijengwe katika Wilaya yetu ya Igunga paleChoma cha Nkola iweze kusaidia watoto wa kikewanaotembea umbali mrefu kutoka vijijini, kilometa nyingikuja shuleni. Kwa hiyo, tukijenga shule hii itasogeza huduma,lakini itawarahisishia watoto hawa wa kike kukaa shuleni nakusoma kwa utulivu, itasaidia kuongeza ufaulu wao katikamaisha yao ya kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiachilia mbali hilo, niiombeTAMISEMI, tuna upungufu wa ma-engineer. Engineer(mhandisi) wetu wa Wilaya tuliyenaye kwa masuala yamajengo inawezekana uwezo wake ni mdogo. NaombaTAMISEMI mtuletee engineer ambaye ataweza kutusaidiakuweza kusukuma hizi kazi za Kiserikali ambazo mmetuleteafedha ziweze kwenda kwa usahihi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia engineerwetu, tunanunua vifaa vingi sana mwisho wa siku vinabaki

Page 108: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

store, halafu inakuwa ni hasara katika maeneo yetu. Mfanoni Kituo cha Afya cha Simbo, tumenunua vifaa vingi haliambayo imesababisha hata fedha tuliyonayo tumeshindwakuwalipa wakandarasi wanaotudai. Naomba TAMISEMIituletee engineer ambaye ataweza kwenda na hesabuambazo zitaweza kukidhi mahitaji sambamba na maeneohusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia katikaupande wa TARURA. Upande wa TARURA fedha inayopatakatika Mkoa wa Tabora ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora nimkubwa kijiografia, ni mkoa wenye square metre karibu75,000, miundombinu yake ya barabara ni mikubwa sana,lakini fedha inazopata ni ndogo, hazilingani na mahitaji yamkoa wenyewe. Naomba TAMISEMI iangalie kutuongezeafedha katika upande wa TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna ujenzi mkubwa sanawa madaraja. Kwa mfano Mkoa wa Tabora kuunganisha naShinyanga. Kila sehemu kuna madaraja, kuna Mto mkubwawa Manonga. Kwa hiyo, ili uweze kuvuka upande wa piliinabidi kuwe na daraja. Kwa hiyo, mahitaji ya madaraja nimengi sana katika maeneo yetu, lakini fedha tunazoletewani ndogo, haziwezi kukidhi mahitaji ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba TAMISEMIituongezee fedha upande wa TARURA tuweze kujenga darajala Mto Manonga upande wa Mondo ili kurahisisha wananchiwetu kuweza kwenda Shinyanga kwa urahisi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia suala lautawala bora, kuna watumishi wengi sana wamekaa katikaHalmashauri ya Wilaya ya Igunga wanakaimu miaka mitatu,miaka minne, wakati tuna uwezo wa kuwapitishia hizo nafasiwakaweza kuzimiliki, wanalipwa fedha za kukaimu mudamrefu. Ni hasara kwa Serikali na Taifa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

Page 109: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Gulamali.Thank you. (Makofi)

MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Akbar halafuMheshimiwa Balozi Rajabu na Mheshimiwa Daniel Mtukawajiandae.

MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi nami nichangie katika Wizarahizi ambazo ni nyeti ambayo ni TAMISEMI pamoja na utawalabora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kutoa mchangowangu, katika Wizara hizi nyeti, nami niungane na Wabungewenzangu kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais j insianavyoweza kugawa maendeleo ya nchi hii bila kujaliWapinzani au ni Chama Tawala. Kwa kweli, namsifu sanaMheshimiwa Rais na ni kweli, tunaona juhudi zake jinsianavyofanya kazi kwelikweli. Kwa hiyo, nachukua nafasi hiikumpongeza sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hiikuwapongeza hawa watendaji Mawaziri ambao wapo katikaWizara zote hizi kwa maana ya TAMISEMI, lakini pamoja naUtawala Bora. Kwa kweli, wanafanya kazi pamoja nawasaidizi wao; nawapongeza ndugu yangu Mheshimiwa Jafona kaka yangu Mheshimiwa Mkuchika. Kwa hiyo, motomdundo waendelee kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizonichukue nafasi hii naomba kutoa mchango wangu kwenyeWizara hii ya TAMISEMI. Namwomba Mheshimiwa Jafo, kwakuwa tulikuwa wote kwenye ziara, nami nitoe mchangokwenye upande wa barabara. Kwa kweli, Halmashauri yaWilaya ya Newala ina barabara ambazo ni nyingi sana, lakinindiyo ambayo inalima karibu nusu ya korosho za Newala. Ila

Page 110: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

kutokana na mtandao, magari makubwa ambayo yanapitakatika barabara zile, nimwambie Mheshimiwa Waziri Jafo,kwa kweli, zile barabara ni mbovu nasi Wilaya ya Newala,TARURA haina gari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachukua nafasihii kumwomba Mheshimiwa Jafo tupate angalao gari mojakama walivyopata Halmashauri za wilaya nyingine. Maanayule bwana anashindwa kufanya kazi na kwa hiyo,tutashindwa kusomba korosho katika Halmashauri ya Wilayaya Newala. Kwa hiyo, nachukua nafasi hii kuomba kwamba,nasi tunahitaji gari moja kwa ajili ya TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, zile fedha ambazozinagawanywa za TARURA sisi tumepata shilingi bilioni 900.Kwa kweli hizi fedha ni ndogo sana, sijui ni kigezo ganiambacho kinatumika, lakini zile barabara zote zilizopo palewilayani ni mbovu na magari ambayo yanatumika kusombazile korosho ni mabovu. Kwa hiyo, vinginvyo zile barabarazikiwa mbovu tutashindwa kwenda mbele kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaJafo tuangalie kwamba kama zile barabara zitashindwa aukuongeza zile fedha, basi aangalie uwezekano yale maeneokorofi ambapo kuna milima, kwamba korosho zikishapakiwamagari yanashindwa kupanda, basi afanye utaratibu wakuangalia kwamba, basi anaweka japo kilometa moja mojaau mbili mbili za lami. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Mlima Miyuyukwenda Ndanda; ule mlima kwa kweli ni mlima mkubwa natulishamwandikia Mheshimiwa Waziri kuangalia uwezekanowa kuweza kupata angalau kilometa mbili za lami kutokaMiyuyu hadi kufikia Ndanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, barabara ya Mpaluhadi Mnyambe, wale watu wanalima sana korosho, lakinikutoka pale Mpalu kuna mlima ambao ni mkali sana. Magariyakienda pale yanashindwa kusomba korosho, Kwa kweli,hatuwezi kujenga barabara yote, lakini ile kilometa moja

Page 111: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

ambayo magari makubwa yanakwama tunaombaMheshimiwa Jafo na Mheshimiwa Kandege Ndugu yanguwaangalie uwezekano wa kuweka pale japo kilometa mojaya lami. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, paleinapoanzia chanzo cha maji Mitema pale Kitangali ambapoinakwenda barabara hadi kufika Mto Ngwele, ule mlima nimkali sana, tunaomba vilevile japo kilometa ya lami.Ikumbukwe kwamba uchumi wote wa korosho unaotokaNewala kwa kiasi kikubwa unatoka Kitangali. Kwa hiyo,tungeomba kwamba kilometa nne au tano, itaufanyauchumi huu ukue sana na wa kitaifa maana yake tutakuwatunapata mapato makubwa sana ya kitaifa. MheshimiwaKandege na Mheshimiwa Waziri Jafo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, nashukurukwamba tumepata milioni 200 kwa ajili ya Kituo cha AfyaMkwedu. Kuna kituo cha afya kipo Chihangu, kile Kituo chaAfya Chihangu ni cha muda mrefu sana, kipo tangu mwaka1969 na operesheni ndogo ndogo zinakwenda pale, lakinikwa kweli hatuna jengo la mama na mtoto.

Kwa hiyo, niwaombe sana Mheshimiwa Jafo naMheshimiwa Kandege wapeleke wataalam wakaangalieKituo cha Afya Chihangu kwa sababu wale akinamamawanajifungulia jikoni na kulala wanalala nje, kwa hiyoinakuwa ni ngumu sana wakati wa mvua wale akinamamakuwa na sehemu ya kujistiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile zile nyumba zawatumishi zote karibu zime-collapse tangu mwaka 1969ambapo kituo cha afya kile kilikuwa kimejengwa mpaka leokile kituo ni kibovu sana. Kama hiyo haitoshi, kile kituo chaafya kipo wazi kabisa, hakina fensi, maana yake hata kamawale watu ambao wanafanya utunzaji wa vile vifaa/rasilimalikwa mfano ile OPD ambayo ilikuwa imejengwa na Wajapanleo ulinzi wake unakuwa ni mgumu. Kwa hiyo, niwaombesanawaende wakakague ili tuweze kufanya matengenezo.(Makofi)

Page 112: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pil i; niungane naWaheshimiwa Madiwani wenzangu; kwa mfano Halmashauriya Wilaya ya Newala Vijijini ile ni kama Halmashauri mpya,haina mapato mengine. Baada ya kuwa hizi koroshozimeingia kwenye mtandao maana yake haina mapato,wale Madiwani wanakopwa mpaka vikao maana yake sasahivi mpaka sasa wanadai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe sanaMheshimiwa Jafo tuangalie namna gani, kama ambavyotumezungumza kwenye ziara ya Rais, namna gani hiziHalmashauri za Wilaya ambazo zinategemea kilimo hasakorosho na ushuru tulikuwa hatujapata, tutafanyaje ilikuwanusuru Madiwani hawa ambao wanadai malipo yao.Kwa hiyo, tuangalie namna nzuri ambayo tunawezatukawasaidia kwa kuwalipa posho hawa WaheshimiwaMadiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, tuwezekuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Halmashauri yaWilaya ya Newala ni pana sana kwa maana kwamba inaKata karibu 22 ambayo ina mtawanyiko wa wakulima wakorosho. Je, ni namna gani tutawasaidia japo pikipiki kamaitakuwa imeshindikana kuwapa mikopo ya magari, basituweze kuwanunulia japo pikipiki kama WaheshimiwaWabunge wenzangu walivyotoa mchango kwambatuangalie uwezekano wa hawa Waheshimiwa Madiwani ninamna gani tunaweza tukawawezesha kwa sababuwanatusaidia sana wakati wa kusimamia uchaguzi kwamaana ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hawa Madiwaniwanasafiri zaidi ya siku mbili kutoka Vijijini hadi kufika ilipoMakao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe sanaMheshimiwa Kandege na Mheshimiwa Waziri waangalienamna nzuri ambazo tunaweza tukawawezeshaWaheshimiwa Madiwani hawa na waangalie vilevile ninamna gani wanaweza wakawalipa posho kwa vile vikaoambavyo wameweza kuwakopa kwa muda mrefu. (Makofi)

Page 113: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.Tunaendelea, Mheshimiwa Balozi Adadi Rajab, atafuatiwana Mheshimiwa Mtuka.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kupata nafasi hii kuchangiakwenye Wizara hizi mbili ambazo ni muhimu sana; Wizara yaTAMISEMI na Wizara ya Utumishi na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nawasifu sanaMawaziri wote wawili kwa kazi nzuri ambazo wanazifanya.Namsifu sana Mheshimiwa Mkuchika na Naibu wakeMheshimiwa Mary kwa kweli tangu amehamishiwa kwenyewizara hiyo, wizara imetulia. Pia ningependa kuvisifu vyombovya ulinzi na usalama kwa sababu kazi ambazo wanazifanyasasa hivi za usalama sio siri kwamba uko vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongezakwa dhati kabisakazi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais na napongeza kabisakazi ambazo wanafanya Mawaziri wa TAMISEMI hasaMheshimiwa Jafo, Mheshimiwa Kandege na MheshimiwaMwita Waitara. Kwa kweli kazi ni nzuri na kwa kweli wanastahilisifa kubwa sana. Wamezunguka sana kwenye hii nchi nawamezunguka sana hasa kwenye Wilaya yetu; nakumbukaMawaziri wote hao ninaowataja wamefika Muheza nawameona kazi za Muheza ambazo wanazifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Muheza tumefaidika sanakwa sababu tumepewa kwanza bilioni 1.5 kwa ajili ya Hospitaliya Wilaya na kwenye mpango wa mwaka huu piatumeongezewa milioni 500 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi waHospitali ya Wilaya. Pia tulipewa karibu milioni 400 kwa ajiliya Kituo cha Afya cha Mkuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunajenga vituo vya afyakwenye kila Tarafa; kwenye Tarafa ya Amani, Misaraitunajenga kituo cha afya, Tarafa ya Bwembera tunajenga

Page 114: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

Potwe na Mhamba na kwenye Tarafa ya Ngomeni tunajengaUmba. Nakumbuka nilikuja ofisini na Mheshimiwa Wazirialiniahidi katika vituo vyote hivyo atajitahidi kadirianavyoweza kuhakikisha kwamba kituo kimoja ananipamilioni 400 kwa ajili ya jiografia ya Jimbo lenyewe kwa sababuya ukubwa wa Jimbo lile. Hata hivyo, nimeangalia kwenyekitabu bahati mbaya sijaona kituo chochote ambachokimepangiwa wakati huu, lakini namwomba MheshimiwaWaziri ajaribu kufikiria kutokana na ukubwa wa Jimbo laMuheza ambalo ni kubwa sana lenye kata karibu 37 na vijijikaribu 135.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maboma namadarasa, tunashukuru sana Muheza tumepata milioni 225kwa ajili ya kukamilisha maboma ya shule za sekondari natumeweza kuanza kazi hiyo karibu kwenye sekondari tisa. Kazihiyo inaendelea vizuri, isipokuwa tunalo tatizo kubwa sanaambalo ni la maabara, tuna maabara karibu shule zote zasekondari, karibu sekondari 21. Haya ni maboma ya maabaraambayo tulitegemea kabisa Serikali itusaidie kukamilishamaabara haya, hii imeleteleza tatizo linafanya hasawanafunzi wa sekondari katika Wilaya ya Muhezakutokusoma sana masomo ya sayansi. Kwa hiyo,tunawashukuru sana na tunaomba sana kwa msisitizomkubwa kwamba tuletewe fedha nyingine za maboma yamaabara ili tuweze kumaliza hili tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la upungufu wawatumishi pamoja na Walimu; suala hili ni kubwa sana nanitamwandikia barua Mheshimiwa Waziri kumpa takwimusahihi ambazo zinaonesha upungufu ulivyo mkubwa hasakwenye masomo ya sayansi na hisabati. Tuna upungufumkubwa na upungufu hasa wa Wauguzi pia na Madaktarikwenye zahanati na hiki kituo chetu cha afya ambachotunategemea kukifungua karibuni. Kwa hiyo, tunategemeakwamba upungufu huu utaweza kukamilika na kuwezakusaidiwa kuweza kupata Walimu hasa wa sayansi na hisabatikwenye sekondari.(Makofi)

Page 115: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna upungufu mkubwa piakwenye shule za msingi. Shule nyingi za msingi zina Walimukuanzia wawili, watatu, wanne; huwezi kutegemea Walimuwachache na shule ziweze kufanya vizuri. Matokeo yetu yamitihani ya shule za sekondari na msingi sio mazuri kutokanana kuwa na Walimu wachache. Kwa hiyo, nashukurukwamba tuweze kuangaliwa na kupewa Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala ambalo wenzanguwameliongelea la Madiwani, Madiwani tunawategemeasana kwenye hii miradi ambayo inaendelea sasa hivi.Wanafanya kazi kubwa sana Madiwani kwa sababu hasaForce Accountkwenye vituo vya afya na madarasawanajituma sana na wanakuwa ni wahamasishaji wakubwasana kwa wananchi wetu, ni vizuri suala lao la posholikaangaliwa ili waweze kuongezewa posho waweze kupataposho ambazo ni nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la TARURA, wenzanguwameolingelea kwa wingi sana lakini fedha ambazowanapewa TARURA kutokana na kazi yao kubwa ni ndogosana. Ni afadhali sasa hivi badala ya ile 70kwa30 basiikaongezeka kidogo. Sisi kwenye Kamati ya Baajetitunajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha kwambakwa kweli pendekezo hili linaweza kuchukuliwa kwa sababuTARURA kazi wanazofanya ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la miradi ya mikakati;miradi ya mikakati sisi Muheza tunategemea kujenga stendiya kisasa na tumeleta maombi yetu yote na tunaaminiyametelekezwa kwa ukamilifu kabisa, lakini tumeangalia piahapa sikuona Muheza ikipewa chochote. Nilikuwa nafikiriaWaheshimiwa Mawaziri wajaribu kwa kadiri ya uwezowaowaangalie kwamba wanaweza kutusaidia vipi,tunaamini kabisa kwamba tutakapopata fedha hizo zakujenga stendi mpya pale Muheza, basi tutaweza kujikimuna kuweza kujishughulikia na mambo yote ambayotunayaweza. (Makofi)

Page 116: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana na naunga hoja mkono. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Balozi Adadikwa mchango wako mzuri. Mheshimiwa Daniel Mtuka.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa fursa hii. Nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu kwa kutupa zawadi ya uhai tumekutana tena safarihii, hii ni bajeti ya nne; tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze jemedariwetu Mheshimiwa Dkt. Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya,kiongozi mahiri, wa kiwango na wa wakati huu. Nipongezewizara hizi mbili hasa zikiongozwa na Mawaziri mahiri;Mheshimiwa Kapt. (MST) George Mkuchika pamoja na kakayangu Mheshimiwa Jafo kwa kazi kubwa wanayoifanyapamoja na Naibu Mawaziri wao, Makatibu Wakuu, NaibuKatibu Wakuu na timu nzima katika idara zao katika wizarahizi mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niungane naMheshimiwa Mbatia leo ni tarehe 12 ni siku ambayotulimpoteza kiongozi mahiri kabisa, Waziri Mkuu wa zamaniMoringe Sokoine. Wote tunaungana naWatanzania wenzetukatika kukumbuka siku hii muhimu ambayo tulimpoteza shujaawetu, aliweka alama katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huu,niseme tu kwamba kwa kuanzia Wizara ya TAMISEMI wanayokazi kubwa kuwa na trilioni 6.2, asilimia 18 ya bajeti nzima; hilini fungu kubwa sana. Mnayo kazi kubwa ya kufanya lakininimpongeze Mheshimiwa Rais, timu ambayo ameiweka ninauhakika wanafanya kazi vizuri na fungu hili najua litapita.Niwaombe Wabunge wenzangu tuwapitishie bajeti hiiiliwaende wakafanye kazi. Naiona timu ni nzuri imehamasikawatafanya kazi kama ambavyo inatakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huo,niseme yafuatayo:-

Page 117: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe timu hii ya Wizarana sisi tunawaunga, washughulikie jambo la udhibiti wa uborahasa majengo na barabara, watusaidie sana. MheshimiwaKatibu Mkuu yeye niengineer Ndugu Nyamhanganamfahamu, adhibiti sana ubora wa majengo pamoja nabarabara. Hizi BOQ fedha hizi ni nyingi, ndipo tunapopigiwahapa kwenye utaalam; mimi nipo very much concernedhapa kwenye BOQ. Wahandisi wa Wilaya kwenyeHalmashauri zetu na Wakurugenzi wasimamie jambo hili.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie na mimi kamawenzangu ambavyo wamesema natoa shukrani zangunyingi/kubwa, wametutendea haki sisi Jimbo la ManyoniMashariki kama Wizara, kabisa. Nimepokea Jimbo hili likiwalimechoka sana katika miundombinu ya elimu na afya lakinihivi ninavyozungumza auheni ni kubwa sana. Tumepokeamilioni 900 katika vituo viwili vya afya, bilioni moja katikakuboresha huduma ya maji pale Manyoni Mjini, bilioni 2.2katika mradi wa vijiji 10 wa maji, milioni zaidi ya 600 katikamradi wa ujenzi wa madarasa hizi fedha za EP4R pamoja naEQUIP na mambo mengi ambayo siwezi kuyataja. Kwa kwelisasa Manyoni naona inakwenda kinyume na zamaniambavyo niliikuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninalo tatizo dogo lakini nikubwa la usimamizi wa fedha hizi, zinakuja nyingi lakiniusimamizi bado mimi nauona haupo vizuri. Wanisaidiealizungumza Mheshimiwa Nkamia jana, lakini mwingineamezungumza leo suala la kozi ya viongozi ni muhimu sanana ni msingi kabisa, tunavurugana sana kule. Mbungeanasema hivi na Mkurugenzi anasema hivi badala ya kwendakwa sauti moja kusimamia mambo haya na fedha hizi zaWatanzania tunabaki kuvurugana na fedha na mudavinapotea. Kozi hizi ni muhimu sana, Manyoni tuna shidakidogo ndio maana hata tunadaiwa benki; Madiwaniwanadai posho kwa sababu ya mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba MheshimiwaJafo na timu yake hebu waitazame Halmashauri ya Wilaya

Page 118: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

ya Manyoni watusaidie, ndiyo maana tupo hapa, hatuwezikukaa kimya wala kulindana tunataka Watanzania wapatehuduma sio kuzozana na kufukuzana na kukimbilia kwambahuyu ana cheo hiki au mimi ni mkubwa, haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri, Mbungeanaweza akaenda kufanya mikutano kule kwa wananchiakapokea malalamiko, yale malalamiko Mbunge yeye kaziyake ni kuyapekela sasa kwa wenzake; la Mkuu wa Wilayanalipeleka kwa Mkuu wa Wilaya na la Mkurugenzi nalipelekakwa Mkurugenzi. Sasa nikimpeleka asiseme mimi namtumakazi, ni katika utaratibu wa mgawanyo wa majukumu, miminapokea kila kitu. Lazima hawa watusaidie sisi, ndio wenyevyombo na watekelezaji, sisi ni wasimamizi; kozi hizi ni muhimujamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa ikama pia tunashida, upungufu wa watumishi idara ya afya na idara ya elimukwa kweli bado hali ni ngumu sana, watendaji ni wachachesana, watusaidie sana kwenye hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA fedha hii haitoshi,vijana wale wana moyo pamoja na kiongozi wao, wanamoyo sana. Mimi wamenifungulia vibarabara vitatu palewananchi wamefurahi sana, tumewaunganisha na vijanawana moyo wa kufanya kazi, lakini hawana fedha.Naungana na mimi na wenzangu waliotangulia angalau ileshare ya 70/30 iwe 60/40. Najua TANROAD wana barabarachache lakini zina gharama kubwa sawa lakini ile share ikiwa40/60 angalau tutapata fedha kule, ndio kwa wananchi kule.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kidogo kuhusuTAKUKURU, wawaongezee fedha, wawape nguvu, wanalindaheshima ya nchi hii.Hawa ndio ma-watchdog tunavyowaita.TAKUKURU bado ni chombo chenye heshima kubwa nanguvu, kama kuna watu wana matatizo wanashughulikiwa,lakini chombo chenyewe kama institution kinabaki bado kinanguvu, wawape hela wakafanye kazi. Naona vijana walewana mori wa kazi, lakini hawana mafuta hata ya kufanyia

Page 119: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

kazi, hawana magari na ofisi bado ni chache kwenye Wilayakule hebu tuwape nguvu walete heshima katika nchi hii.Mheshimiwa Rais tumsaidie analia sana, bado rushwa ipo,ndugu zangu naomba wanisikilizekwa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, niseme tukwamba naunga mkono hoja ya bajeti hizi mbilikwaasilimiamia moja. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mtuka, haondio wachangiaji wetu kwa mchana huu. Tuna matangazomawili; tangazo la kwanza linatoka Wizara ya Kilimo,mnakumbushwa Waheshimiwa Wabunge mnaotoka kwenyeWilaya zinazolima pamba ikiwemo Wilaya ya Bariadi, kikaocha saa nane mchana wa leo, wizarani pale mkabala naVETA, saa nane mchana huu.

Tangazo la pili ni marudio lile nililofanya asubuhi, sikuya Jumapili tarehe 14 Aprili, saa tano asubuhi kutakuwa nasemina kwa Wabunge wote katika Ukumbi wa Msekwakuhusu masuala ya ualbino. Semina hiyo itatolewa na Shirikala Under The Same Sun ambalo linaleta haki na ustawi wawatu wenye ulemavu hapa nchini na maeneo mengineduniani. Aidha, ujumbe wa shirika hilo upo hapa Bungeniwalitambulishwa asubuhi wakiongozwa na MkurugenziMtendaji Bwana BerthasiaLadslaus. Hayo ndiyo matangazo

Mwisho, tutakaoanza nao mchana huu niMheshimiwaKiza Mayeye, Mheshimiwa Joseph Haule (Profesa Jay) naMheshimiwa Vedastus Ngombale na wengine watafuatakwa mtiririko wa vyama vyetu humu Bungeni.

Sasa nasitisha shughuli za Bunge hadi saa kumi namoja Jioni leo.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge Lilirudia)

Page 120: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Kablahatujaendelea na wachangiaji niliowataja mchana, ninaorodha ya wageni wengine ambao wapo Bungeni. Tunaowageni 127 wa Mheshimiwa Antony Mavunde, Mbunge,Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira ambaoni Washereheshaji (MCs) kutoka mikoa yote Tanzaniawakiongozwa na Ndugu Obeid Sarungi. Karibuni sana MCs.(Makofi)

Tunao pia wageni wanne wa Mheshimiwa GoodluckMlinga, Mbunge, ambao ni Madaktari na Wauguzi waHospitali ya Wagala iliyopo Mvomero, Mkoani Morogoroambao ni Ndugu Eva Kisimbo, Ndugu Irene Kuhanga, NduguMathias Sui na Mdugu Slam Mganga. Karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, sasa tunaendelea nauchangiaji na tunaanza na Mheshimiwa Mayeye, atafuatiwana Mheshimiwa Joseph Haule na Mheshimiwa VedastoNgombale ajiandae.

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika hotubahii ya TAMISEMI na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimshukuru MwenyeziMungu ambaye amenipa afya nimeweza kusimama jioni hiiya leo. Kwa kipekee kabisa nimpongeze Fulbright Prof. IbrahimHaruna Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti wa Chama chaWananchi CUF. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia hotuba hizi zaWizara hizi mbili, natambua Serikali inapambana kuhakikishainaleta huduma bora kwa wananchi. Kwanza nianze na sualala TARURA. Barabara za vijijini ni muhimu sana katika maeneoyetu. Wote tunafahamu kwamba wakulima wote wako vijijinilakini barabara hizi ndizo ambazo zinaweza kuwasaidia kutoamazao mashambani na kuleta mijini kutafuta masoko lakinihali ya barabara hizi kiukweli ni changamoto kubwa. (Makofi)

Page 121: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi kubwaambayo TARURA wanaifanya, moja ya changamoto ambayoinawakabili ni suala zima la bajeti. Niiombe Serikali katikabajeti hii tunayokwenda nayo tuweze kuwasaidia TARURAwapate bajeti ya kutosha ili waweze kufanya kazi yao nakumaliza miradi hii ya barabara zetu huko vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la bajetitumeona TARURA wanapata asilimia 30 na TANROADSwanapata asilimia 70. Naelewa Serikali mmeunda KamatiMaalum kwa ajili ya suala hili na mimi nichangie na kuiombaSerikali kwamba at least sasa TARURA wabaki na 40 naTANROADS wapewe 60 kwa sababu ya barabara za viwangovya lami na madaraja kama ya Mfugale. Kwa hiyo,tuwasaidie watu wa TARURA, naamini wanafanya kazi nakama watapata bajeti ambayo inatosha watawezakutusaidia barabara zetu hizi kumalizika kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo hapo kwenye TARURAchangamoto nyingine ni vitendeakazi, watu hawa hawanamagari ya kuweza kutoka sehemu moja na kwenda site.Mfano Mkoa wangu wa Kigoma takribani wilaya zote, kuanziaKigoma DC, Buhigwe, Kasulu, watu wa TARURA hawanamagari na imekuwa ni usumbufu mkubwa katika utendajiwao wa kazi. Nikuombe sana Mheshimiwa Waziri muangalieni jinsi gani Kigoma wilaya zote tunaweza tukapata magarikwa watu hawa wa TARURA ili wafanye kazi kwa ufanisi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijielekeze katika suala laafya. Natambua Serikali mnajituma na mnafanya kazikuhakikisha mnaboresha vituo vya afya na kutuletea wauguzi.Niwashukuru kwamba Kigoma mwaka jana tuliomba,mmetuletea Kigoma nzima watumishi 402 lakini kiukweli badochangamoto ni kubwa. Maeneo mengi ukienda hospitali zaKigoma na hata maeneo mengine ya Tanzania bado hatunawauguzi wa kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka kufikia Novemba,2018 Kigoma tulikuwa na wafanyakazi 2,004, kiukweli bado

Page 122: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

idadi ya wafanyakazi ni ndogo ukizingatia Kigoma tuko zaidiya watu milioni mbili lakini ni mkoa ambao tuko mpakanitunahudumia mpaka wakimbizi kutoka Kongo na Burundi.Kwa hiyo, niiombe sana Serikali, pamoja na jitihada ambazomnafanya lakini mtuangalie kwa jicho la pili mtuongezeewauguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo hapo katika afya,Kigoma tuna Hospitali hii ya Mkoa ambayo inaitwa Maweni.Mpaka sasa hatuna vifaa kama CT Scan na x-ray machinesza kutosha hali inayosababisha usumbufu mkubwa sana kwawananchi watu wanakwenda kutibiwa pale wanahitajihuduma hii ya CT Scan wanapewa rufaa kwenda Mwanza(Bugando) au kwenda Muhimbili. Kulingana na hali ya maishailivyo, siyo watu wote wataweza kwenda Muhimbili auBugando kwa wakati. Sasa kama tunataka kuwasaidiawananchi ili tupunguze vifo, niombe sana Serikali muwezekutusaidia vifaa hivi vya CT Scan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado niko katika hospitaliya mkoa; hospitali hii kama nilivyosema inahudumia watuwengi sana lakini mpaka sasa hatuna ma-specialist wakutosha, tuna specialist mmoja wa akina mama na mmojawa watoto. Kuna magonjwa mengine kama haya ya kisukarihatuna ma-specialist. Niombe sana Serikali mtusaidie hospitalihii tuweze kupata ma-specialist wa kutosha, mtakuwammetusaidia watu wa Kigoma na maeneo mengine Tanzaniaambayo hakuna ma-specialist katika hospitali zao muwezekuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nigusie tena suala lamiundombinu hospitalini na kwenye shule zetu. Sote tunajuakwamba walimu, madaktari na wauguzi ni watu muhimu sanakatika maisha yetu, lakini watu hawa wamekuwa wakiishimaisha magumu kwa maana ya kwamba hata nyumba boraza kukaa hawana. Niombe sana Wizara muweze kuangaliasuala hilo, muwajengee nyumba wauguzi na walimu ili naowaweze kukaa katika mazingira bora. (Makofi)

Page 123: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala hili la moboma,kuna majengo ambayo wananchi wamejitoa, niseme tukwamba wananchi wanaunga mkono Serikali kwa kufanyavitu mbalimbali kama ujenzi wa zahanati, kujenga shule nahostels za wanafunzi lakini inafika muda na wao wanakwama.Niombe sana Serikali muwasaidie wananchi muwezekumalizia majengo haya ambayo yameishia kwenye lenta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano tu katika Mkoawangu wa Kigoma, Awamu ya Nne Rais aliyepita aliahidikujenga hospitali katika eneo la Nyarubanda na Mahembena wananchi waliitikia wakaanza kujenga lakini sasaimesimama na hakuna mwendelezo wowote. Niombe sanaSerikali muwasaidie watu hawa waweze kumalizia majengohaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala lavitambulisho. Niseme tu kwamba mimi ni mdau wamaendeleo na naunga mkono jitihada za Serikali katikaukusanyaji wa kodi lakini tuwe wakweli; pamoja na kwambaMheshimiwa Rais alisema hawa wajasiriamali wadogowakate vitambulisho lakini tuwaangalie hawa wajasiriamaliwadogo ni wa aina gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo katika Mkoa wangu waKigoma, mimi natokea Kijiji cha Mwandiga, baada ya Bungekuisha kuna akina mama nilikwenda kuwatembelea sokoni.Kuna mama ambaye anauza ndizi kwa sababu tu nyumbanikwake amepanda ndizi, anaona ndizi zimeiva anasemanipeleke sokoni nikapange chini ili wanangu waweze kupatadaftari na kupata mafuta ya taa. Sasa hawa ambaowanakwenda kutoa vitambulisho hivi unakwenda kumtozamama kama huyu Sh.20,000 anaitoa wapi wakati biasharaanayofanya haikutani mzunguko wake kupata Sh.20,000?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kiukwelimalalamiko ni mengi. Kama tunasema ni Serikali yawanyonge, wanyonge ndiyo hawa akina mama na vijana…

Page 124: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. Tunaendeleana Mheshimiwa Joseph Haule (Profesa Jay).

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangiakwenye bajeti ya Wizara hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, nijielekezekusoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibaraya 13(1) inasema: “Watu wote ni sawa mbele ya sheria, nawanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupatahaki sawa mbele ya sheria”. Vilevile Ibara ya 14, inasema:“Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutoka katika jamiihifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, najielekeza kwenye Wizaraya Utawala Bora. Wiki iliyopita nilisimama katika Bunge lakoTukufu nikizungumzia kwamba kuna upotevu wa watu kumikatika Jimbo la Mikumi maeneo ya Ruhembe, Kidodi pamojana Ruaha na niliongea hapa kwenye Bunge nikiaminikwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imohumu ndani. Pamoja na kuongea hapa Bungeni na kumfuataWaziri wa Maliasili na Utalii na kuwafuata wahusika wotempaka leo watu wamenyamaza kimya kana kwambahakuna kilichotokea katika Hifadhi za Mikumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimekuwa nikijiuliza,Serikali hii inajipambanua kwamba inajali utu, haki lakini piautawala bora, pamoja na hayo kila siku tunaimba kwambaTanzania ina amani lakini ni jambo la kushangaza sanaunapoona kwamba kuna watu kumi na tunaripoti kwenyeSerikali wamepotea katika mazingira ya kutatanisha tangutarehe 2 Aprili, leo ni tarehe 12, siku kumi hakuna mtu yeyote

Page 125: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

amezungumzia lolote katika Jamhuri ya Muungano waTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali hii imetusikitisha sana nabado majonzi yamekuwa makubwa sana katika Jimbo laMikumi maeneo Ruhembe na niseme kitu kimoja kwambahali hii inaendelea kuleta taharuki na imani ya wananchi kwaSerikali imekuwa ndogo na inazidi kushuka kila siku. Kwa kuwatunajua kwamba TANAPA na Polisi wana helikopta auhelikopta hizo zinakuwa kwa ajili ya intelijensia kuwakamatawapinzani tu na kushindwa kuelewa Watanzania wenginewasiokuwa na hatia wanaopotea katika Jamhuri yaMuungano wa Tanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku kumi ni nyingi watuwanapokuwa hawaonekani. Tukasema labda tupeleke kwaSerikali itatafuta namna ya kutupa majibu ya jambo kamahilo, inasikitisha sana kuona mpaka leo siku ya kumi watuwamekuwa na majonzi. Basi hatuombei labda wamekufatuseme lakini hatuombei hivyo, kama wamekufa basi mtupehata nguo zao ili tukazizike au tukaendelee na misiba katikaJimbo la Mikumi, labda huo ndiyo utawala bora mnaoujua.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana imeundwa Kamatiimekwenda kule, RCO pamoja na watu wa hifadhi, you can’tbe a judge of your own case, huwezi kuwapeleka watuambao tunahisi na wananchi wanalia kwamba watuwamepotea katika hifadhi yao, halafu bado wao wao ndiyowakaenda kuangalia na kufanya uchunguzi mpaka leohakuna majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo tunaombamliangalie kwa kina na tupate majibu ya Serikali hawa watukama wamekufa tujue, kama wamepotea tujue, tunatakiwatujue ripoti yao. Nina nia ya kuomba Bunge lako Tukufu liundeTume ambayo itakwenda kufanya uchunguzi katika maeneohayo ya Ruhembe ili tuweze kuwapa haki hawa wananchiambao ndugu zao wamepotea katika hifadhi. (Makofi)

Page 126: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonataka kuzungumzia ni kuhusu Tume ya Uchaguzi. Kila sikutumekuwa tukizungumza Tanzania ni kisiwa cha amani lakininaona watu wana nia ya kupoteza kisiwa cha amani chaTanzania. Labda niwashauri tu Wabunge wa CCM ambaomnashabikia sana kuhusu hii Tume ya Uchaguzi, muangaliesasa hivi katika TV za kimataifa, CNN, Al-Jazeera na sehemunyingine, jinsi ambavyo kumekuwa na unrest katika dunia kwasababu ya mambo kama haya. Watu wamefungwa mikono,watu wanashindwa kusema lakini Tume imekuwa haitendihaki kwa wapinzani wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Sudan mmeonakimemtokea nini Al-Bashir lakini ukiangalia Algeria naVenezuela kuna vitu kama hivyo na hapa Tanzania kamatutaendelea kucheka na hii Tume ya Uchaguzi ambayo sasamatokeo yamekuwa yakitangazwa vice versa, leo tuMahakama ya Mbeya imetoa hukumu kwamba katika Kataya Ndalambo ambapo alitangazwa mgombea wa CCMlakini wameona ni jinsi gani ambavyo Serikali ya CCMimekuwa ikiiba kura kila siku na sasa hivi wameonekanawameiba na mgombea wa CHADEMA ametangazwakushinda pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini watu wanasema Tumehii ni huru kwa sababu akina Profesa Jay walitangazwa;hamjui mbilinge tulizozifanya huko mpaka tukatangazwa.Tumefanya uchaguzi tarehe 25, tarehe 26 unaona magariyanakuja yanaondoka, tarehe 27 CCM wanabeba magariya matangazo wanataka kujitangaza kwa nguvu, nyomilinaongezeka pale na pale kweli asingetoka mtu. Napendakusema kwa Wanamikumi kwamba nitaendelea kusimamapamoja nanyi na niombe watu wote wapenda amani hapaTanzania wasimame pamoja kuhakikisha kwamba Tume hiiinabadilishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni mwanamuziki wa hiphop lakini pia napiga ngumi mbili, tatu, napenda boxing;kama wewe ni referee kama Tume ya Uchaguzi, basiusinifunge mikono mimi halafu ukamuacha jamaa anipige

Page 127: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

mangumi mengi mengi usoni, unanifunga kamba halafuunamwambia jamaa apige, haiwezekani. Ipo siku hizi kambazitakatika na nitawapiga manondo ya kutosha ndugu zangukwa sababu tunakwenda kushinda na tunaamini tutakwendakufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe tu watu woteambao wamepitia katika nyanja na matatizo mbalimbaliwaamini kwamba haya mambo ni ya kupita tu. Watu wanguwa upinzani tulizeni ball, mwaka huu ni wa uchaguzitunakwenda oya oya na mzuka kama kawaida maeneo yakatikati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,niende kwenye Wizara ya TAMISEMI kwa Mheshimiwa Jafo.Nashukuru sana ulifanya ziara Jimboni Mikumi lakini kiukwelikabisa ni kwamba katika Kituo cha Afya cha Mikumi baadaya ziara yako ndiyo mambo kidogo yameanza kwenda vizurina mimi kama Mbunge nimechangia mifuko 200 kuoneshakwamba nina-support kile kinachotokea kwa ajili ya Kituo chaAfya cha Mikumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya ni kwambawale wafanyakazi waliopewa kazi za ziada badohawajalipwa mpaka leo na wameniagiza nikwambiekwamba wameshaleta barua kwako wanasubiri uwasaidie.Wale ni walalahoi wa Mikumi wamefanya kazi pale wanatakauwasaidie wapate haki yao ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia wananchi waMalolo wanajenga Kituo cha Afya kwa nguvu zao wenyewena mimi kama Mbunge nimepeleka tena mifuko 200 ku-support juhudi hizo. Tunaomba Serikai nayo ituongezee helakidogo ili tuweze kukamilisha nia yao ya kuweza kuwa nakituo chao cha afya kama ambavyo sera inasema kila kataiwe na kituo cha afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Ulaya,nilishaongea muda mrefu kimechakaa, tunaomba Serikaliipeleke pesa kule. Pia Waziri wa Nishati alishafanya ziara pale,

Page 128: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

aliona kwamba hakuna umeme na alisema atatuleteaumeme, watu wanasubiri maeneo ya Mikumi, Ulaya paletuweze kupata umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwamba tuliombamagari, kwa sababu Mikumi pale kuna ajali nyingi sana Mitaaya Msimba, Ng’apa mpaka Ruaha Mbuyuni lakini sasa hivikinajengwa pale kituo cha dharura kwa ajili ya ajali nakwamba tutaletewa magari mawili kama ambavyo Mbungeniliomba. Kwa sababu tumegundua kwamba pale Mikumikuna matatizo mengi ya ajali mbugani na sehemu nyinginena tukasema kwamba tukipata magari ya wagonjwayatasaidia kukimbiza wale watu wanaopewa rufaa. Maanakutoka Mikumi mpaka Kilosa ni kilometa 78; Mikumi mpakaMorogoro kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni kilometa120; Mikumi mpaka Iringa ni zaidi ya kilometa 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe shukrani kwambatumeambiwa haya magari yapo, Wanamikumi wanayasubirikwa nguvu na kwa hamu kubwa ili tuweze kuwasaidiaWatanzania. Maana Mikumi pale inapita barabara kubwainayotoka Tanzania kwenda Zambia mpaka South Africa,tunaamini hata watu wa Nyanda za Juu wanaopata ajalimaeneo yale watapata nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye TARURA.Kwa kweli TARURA bajeti yao ni ndogo na ndiyo maanamwaka jana nilipiga kelele hapa nikisema Wilaya ya Kilosa nikubwa lakini imekuwa na bajeti ndogo sana, TARURA hawanahata gari. Nashukuru tumeletewa gari lakini bado TARURAuwezo wake ni mdogo. Kuna barabara kutoka RuahaMbuyuni - Malolo - Kibakwe; kuna barabara ya kutoka Dumila- Kilosa - Mikumi lakini pia kuna barabara nyingine ya kutokaUlaya – Madizini - Malolo, hizo zote ziko chini ya TARURA,tunaamini inaweza kutusaidia. Hii barabara ya Dumila – Kilosaiko chini ya TANROADS, naamini nao watatusikia wawezekutusaidia kwa sababu ni barabara muhimu sana kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kuongelea kuhusuupungufu wa watumishi na kwa Wizara ya Elimu katika Wilaya

Page 129: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

yetu ya Kilosa tumekuwa na upungufu mkubwa sana wawalimu. Mfano shule ya msingi ina wanafunzi wa awali wadarasa la kwanza hadi la saba 107,000 lakini walimu wako2,393 tu na tuna upungufu wa walimu 929. Pia tuna maboma39 tunaomba Serikali itusaidie; sekondari tuna madarasapungufu 129, majengo ya utawala 28, nyumba za walimu689 lakini pia tuna upungufu wa hostels 27. Wananchiwamefanya juhudi kubwa sana ya kujenga mabomatunaamini Serikali itatusaidia ili tuweze kuboresha elimu katikaWilaya yetu ya Kilosa ambayo ni wilaya kongwe sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nisemekwamba tuko pamoja na Kambi Rasmi ya Upinzani nanimheshimu sana Mheshimiwa Japhary Michael ambayeamewasilisha hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi yaUpinzani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Haule.Tunaendelea na Mheshimiwa Ngombale.

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi nami nisememachache katika Wizara hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na TAMISEMI na sualanzima la posho za Wenyeviti wa Vijiji na Vitongozi. Hawa niviongozi ambao wanachaguliwa kama ambavyo Madiwani,Wabunge na Rais wanavyochaguliwa, lakini hatujawekautaratibu wa kuangalia haki zao na hasa kuhakikishakwamba wanapata posho. Napendekeza kwamba kamaSerikali Kuu haina uwezo wa kuwawezesha viongozi hawakupata posho, basi itoe maelekezo maalum katikamakusanyo ya ndani ya vijiji husika, viongozi hawa walipwekutokana makusanyo hayo. Hiyo itawasaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni suala la vitambulishovya wajasiliamali, zoezi ili limeanza ghafla ghafla na limeletataharuki kubwa huko kwa wananchi na hasa pale Serikali

Page 130: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

inaposhindwa kubainisha ni yupi mjasiliamali ambayeanatakiwa apewe kitambulisho? Kumekuwa na sintofahamu,mama mwenye mafungu matatu ya mboga anatakiwa alipeshilingi 20,000/=, mama huyo huyo akiwa na mikungu mitanoya ndizi, anatakiwa alipe shilingi 20,000/= na sehemu nyinginekama kule kwangu mtu mmoja analazimishwa kulipia hatamara tatu kwa sababu ana biashara tatu tofauti. Hiyo nisintofahamu kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi,vitambulisho hivi vinaenda kubana kabisa mapato ya vijijina mapato ya Halmashauri. Halmashauri hizi zitastawi vipikama mapato yake kwa namna tofauti tofauti yanaendeleakuchukuliwa na Serikali Kuu? Naiomba Serikali hilowaliangalie, kwa sababu wananchi sasa wananituma,Mheshimiwa Mbunge, hebu tuulizie, hivi ile kodi ya kichwaimerudi? Maanda sasa kila tukizunguka ni vitambulisho,vitambulisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haipo familia ambayohahijihusishi na ujasiliamali sasa. Kila familia lazima ifanyeujasiliamali, vinginevyo maisha ni magumu. Sasa kamaunafanya ujasiliamali ni shilingi 20,000/=. Maisha kule nimagumu sana, naomba hilo liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusiana na ujenziwa zahanati kama sera inavyozungumza. Kwa bahati mbayakabisa, mimi katika Jimbo langu kuna Kata moja ainazahanati hata moja za Serikali. Ile kata inaitwa Kata yaNamayuni. Ile kata ina vijiji sita, kuna kijiji kimoja kinaitwa Kijijicha Naama, chenyewe wamejitahidi, wamejenga angalaukufikia boma. Naomba Wizara iwasaidie wale wananchiwapate ile zahanati iishe ili basi kata ile nzima iweze kupatahuduma kwa sababu wananchi wanatembea kilometa zaidiya 20 mpaka 50 kufuata huduma za matibabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, badokuna tatizo la miundombinu il iyokamilika kuendeleakutotumika. Katika Kata ya Mingumbi katika Kijiji chaLyomanga, Mfuko wa TASAF ulitoa fedha na kujenga zahanati

Page 131: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

toka mwaka 2009. Mpaka hivi tunavyozungumza, zahanatiile haijatumika na sasa inaelekea kubomoka. NaiombaSerikali ifuatilie hiyo zahanati na ione namna gani pesa zaSerikali zinapotea bila kuwa na sababu ili basi ikiwezekanawafanye marekibisho na wananchi wapate huduma yamatibabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la korosho.Nachukuwa fursa hii kuipongeza Serikali na hasa ile kauliiliyotolewa na Mheshimiwa Rais kuhusiana na kwambaitawalipa sasa wakulima wa korosho pamoja na walekangomba. Nikiri kabisa, sasa angalau tunaishi kwamatumaini, kwa sababu hali mwanzoni ilikuwa ni ngumu sana.Ingawa malipo yenyewe bado hayajafanyika, lakini tunayoimani kwamba siku moja tutalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hili niseme,Serikali iache tabia ya kuingilia michakato iliyopangwa kwamujibu wa sheria. Suala la korosho na utata uliotokeza ni kwasababu tu Bodi ya Mazao Mchanganyiko haina uzoefu wakusimamia zao la korosho. Katika namna ambayohatufahamu, ni kwa namna gani Bodi ya Korosho ambayoinatambulika kwa mujibu wa sheria ikawekwa pembeni nabadala yake ikachukuliwa Bodi ya Mazao Mchanganyikoambapo mzigo umewalemea mpaka sasa wanashindwakufanya malipo kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inajinasibu kwambaimetoa pesa, lakini bodi ile inashindwa kwa sababu hainauzoefu. Kwa hiyo, naomba hili liangaliwe sana. Kwa sababumaamuzi hayo yamepelekea hasara, athari za kisaikolojia,na kudumaza maendeleo, naitaka Serikali iwaombe radhiwakulima wa korosho kwa kitu kilichotokea. Kwa sababu kunawatu wamepoteza maisha, Serikali iwaombe radhi wakulimawa korosho kwa sababu lile lililofanyika, limefanywa kwamakusudi. Kwa hiyo, naomba hilo lifuatiliwe mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo napendaniseme ni suala zima la TARURA. TARURA wanafanya kazi vizurilakini bajeti yao haitoshi. Wanajitahidi, lakini bajeti yao

Page 132: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

haitoshi. Naitaka Serikali iongeze bajeti TARURA. Nami katikaJimbo langu, naomba TARURA ishughilikie barabara ya kutokaMbombwe – Anga - Nakindu mpaka Miangalaya; lakini piaishungulikie barabara ya kutoka Mkarango - Mitole na kutokaChumo mpaka Mkoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo,nikumbushe ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne.Hii nalizungumza kwa mara ya tatu nikiwa humu Bungeni. Raiswa Awamu ya Nne Mheshimiwa Kikwete akiwa katikaSherehe za Kumbukumbu za Vita ya Maji Maji pale Nandete,aliahidi kwamba atajenga barabara kutoka Nandete mpakaNyamwagi, ile ahadi mpaka sasa haijafanyiwa chochote.Naitaka Serikali ifuatilie utekelezaji wa ahadi ya MheshimiwaRais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni suala la ufuta.Jimbo la Kilwa Kaskazini na Kilwa ujumla, sisi ni wakulima wazuriwa ufuta. Mwaka 2018 kulitokea na tatizo kwamba ufutaambao hauna bodi ulilazimika kusimamiwa na Ofisi ya Mkoana siyo Halmashauri, matokeo yake yalipelekea mapato yaHalmashauri kupungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018 tulikwendaTAMISEMI, tulifuatilia sana. Tunaomba zao la ufuta lisimamiwena Halmashauri na siyo Mkoa kwa sababu zao hili halina bodina Halmashauri ina uwezo wa kufanya hivyo. Kwa kufanyahivyo, kung’ang’ania kusimamiwa na mkoa, mapato yaHalmashauri yanapungua. Tunaomba sana zao hil ilisimamiwe na Halmashauri na siyo vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nizungumzie kuhusuupandishwaji wa madaraja. Tunaomba Serikali ijitahidi sasakuona madaraja na mishahara ya watumishi inapandishwa.Watumishi hawa wanafanya kazi kwa kujitolea, wanafanyakazi kwa nguvu kubwa lakini wanakosa motisha kiasi kwambaufanisi wa kazi unapungua. Kwa hiyo, Walimu, Watumishi waAfya wote wale wapandishwe madaraja na mishaharaiongezeke. (Makofi)

Page 133: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine nizungumziekuhusiana na fedha za Mfuko wa Wanawake Vijana na WatuWenye Ulemavu. Hili limezungumzwa sana na Wajumbe waKamati yangu, lakini pia nami niongezee. Tumefanya ziarasehemu mbalimbali, Halmashauri ya Wilaya ya Kahamaimefanya vizuri sana na imefanya vizuri katika eneo hilo kwasababu imefanya maamuzi ya kuchukuwa hizi pesa badalaya kumpa mtu mmoja mmoja ikaandaa utaratibu ambaoutaenda kuwasaidia kundi hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iangalie ilemodel ya Halmashauri ya Kahama, ikiwezekana ifanyikesehemu nyingine. Kwa sababu sasa mianya imefungwa.Mwanya peke yake ambao kama hatutakuwa makini,Watendaji wa Halmashauri wanaweza kutumia kupiga sanapesa, ni katika pesa hizi za asilimia kumi. Kwa hiyo, tuwe makinisana, hizi pesa ikiwezekana tuzielekeze katika namnaambayo tunaweza kufuatilia na walengwa wakapatamahitaji yao stahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukukumbuke pia katikaeneo la walemavu bado walemavu wanashindwa kupatayale mahitaji yao kulingana na aina ya ulemavuwaliokuwanao. Tuangalie uwezekano wa kuwasaidiawalemavu wasioona wapate fimbo, walemavu viziwi wapateshimesikio, walemavu wa viongo wapate viungo bandia,wapate baiskeli na wale walemavu albino wapate mafutakwa ajili ya kujinusuru na adhari za miale ya mwanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukijielekeza huko tutakuwatumewasaidia sana, vinginevyo hii mikopo tunawezatukaipeleka na isiwe na marejesho. Ni heri tupeleke kwakuwasaidia Walemavu kwa ulemavu walionao…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Vedasto.

Page 134: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

MHE. VEDASTO E. NGOMBALE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa KitetoKoshuma, atafuatiwa na Mheshimiwa Mwantumu Dau,Mheshimiwa Desderius Mipata na Dkt. Christine Ishengomaajiandae. Mheshimiwa Kiteto Koshuma.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ili nami niendeleekutoa michango yangu katika Bunge lako Tukufu. Pianiendelee kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendeleakunijalia afya njema ili niweze kutoa michango yangu katikaBunge hili Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapoanza kuchangiakatika Wizara hii ya TAMISEMI na Utawala Bora, naombakuanza kwa kusema kuwa mwanazuoni mmoja ametafsiriviongozi wa kisiasa kuwa ni muhimu sana katika mamlaka zaSerikali na hufanya maamuzi sahihi yanayoweza kuletamanufaa zaidi katika ustawi wa Taifa na watu wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeamua kuanza kwakusema hivyo nikiamini kwamba sisi kama Wabunge waJamhuri ya Muungano wa Tanzania tukiwa kama viongoziwa kisiasa tunalo jukumu la kuhakikisha kuwa tunaishauriSerikali, tunaisimamia vyema ili kuhakikisha ustawi wa Taifaletu pamoja na wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongezaSerikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwasababu yeye ameonyesha mfano wa yale ambayonimeyatangulia kuongea, akiisimamia nchi yetu ya Tanzaniakuhakikisha kwamba Watanzania wanaongozwa vizuri katikasehemu ya Utawala Bora lakini pia Watanzania wanawezakupata ustawi na maendeleo katika nchi ya Tanzania.(Makofi)

Page 135: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niendekuchangia Wizara hii ya TAMISEMI nikianza na suala la ujenziwa vituo vya afya, pamoja na hospitali. Serikali imejitahidisana kujenga na kukarabati vituo vya afya na hospitali, hiyoyote ni katika kuhakikisha inaboresha huduma za afya katikamaeneo mbalimbali hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Mkoa wa Mwanzatumefaidika katika ukarabati na ujenzi wa vituo vya afyakama ambavyo imekuwa katika maeneo mbalimbali hapanchini, Mkoa wa Mwanza tumepata takribani shilingi bilioni10.3 ambayo imetusaidia kurekebisha vituo vya afya katikamaeneo mbalimbali Mkoani Mwanza vikiwemo Wilaya yaUkerewe, Wilaya ya Kwimba, Wilaya ya Magu, Wilaya yaMisungwi na Wilaya nyingine zote Mkoa wa Mwanzazimeweza kufaidika kwa kupata vituo vya afya na hospitaliza wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na juhudi hizo zaSerikali, zipo changamoto mbalimbali ambazo zinatokeakatika jamii yetu. Maeneo kama ya visiwani, badohawajaweza kupata huduma za afya kwa sababuwanatembea umbali mrefu na ukiangalia Mkoa wa Mwanzani Mkoa umezungukwa na visiwa vingi. Kwa maana hiyo,wananchi wanapata changamoto ya usafiri kuweza kufikiahuduma za afya kwa ukaribu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ukiangalia Wilaya yaUkerewe na Wilaya ya Ilemela, kuna Visiwa vya Irugwa Kisiwacha Bezi. Wananchi ambao wanahishi katika visiwa hivyoambavyo nimevitaja bado wanapata changamoto yakufikia huduma huduma za afya. Ombi langu kwa Serikali,naiomba Serikali katika bajeti yake hii waweze kutenga fedhakwa ajili ya kutengeneza kujenga vituo vya afya katikamaeneo hayo ya visiwani ili wananchi waweze kuzifikiahuduma za afya kwa ukaribu na hatimaye kuweza kuokoamaisha ya wananchi, hususani tukiwalenga kundi maalumambalo ni akina mama na watoto ili kuweza kupunguza vifovya akina mama na watoto.

Page 136: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mkoa wa Mwanza piatunayo Hospitali ya Ukerewe ya Wilaya ambayo ipo paleNansio. Hospitali hii ya Wilaya ya Ukerewe inawahudumiawananchi wengi sana kutoka maeneo ya visiwani kuleUkerewe. Sasa kuwapunguzia wananchi kutoka Ukerewekwenda kupata tiba au kwenda kupata huduma za kiafyaza kibigwa, ninaishauri Serikali kuweza kukarabati Hospitaliya Wilaya ya Ukerewe ambayo ipo pale Nansio. Hiiitawasaidia wananchi wanaotaka huduma maeneo yalekwani hawapati huduma za kibigwa za kiafya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo, naiombaSerikali iweze kutenga fedha katika kipindi hiki cha bajeti ilikuhakikisha kwamba hospitali hii ya Wilaya ya Ukereweambayo inahudumia wananchi wengi iweze kutoa hudumaza Kibigwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba kuchangiakatika suala la elimu. Pamoja na juhudi za Serikali kujengamadarasa na shule za mabweni katika maeneo mbalimbali,bado tunazo changamoto kwa watoto wetu wa kike ambaowanatembea mwendo mrefu kutoka sehemu moja kwendasehemu nyingine kupata elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtoto wa kikeanapotembea mwendo mrefu, njiani anakutana na vikwazombalimbali. Atakutana na madereva wa bodabodawatamshawishi kupanda usafiri ili aweze kufika haraka shuleni.Atakutana na watu tumezoea kuwaita mashunga dadys,wataweza kumrubuni mtoto wa kike na kukatisha masomoyake hatimaye aweze kupata ujauzito ama la aolewe akiwabado ni mdogo na hatimaye kukatisha ndoto zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na juhudi za Serikalikufanyika, lakini bado tunayo changamoto ambapo sehemumbalimbali ambazo ziko mbali na maeneo ya shule za msingi,zinazo-feed shule zetu za Kata za Serikali kwa wanafunzikutembea mwendo mrefu. Tunaishauri Serikali iweze kujengashule za mabweni katika shule zetu za kata ili iweze

Page 137: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

kuwasaidia watoto wa kike wasiweze kutembea mwendomrefu kwenda kupata elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Mkoawa Mwanza, sisi tunazo baadhi ya shule hapa ambazonitazitaja ili Serikali iweze kuzisaidia. Kwa sababu nimeonakatika ukurasa wa 124 katika kitabu hiki cha Wizara yaTAMISEMI wamesema kwamba watajenga shule za mabwenikwa kupitia EP4R. Kwa hiyo, naomba katika mpango huoshule hizi ikipendeza ziweze kuingia katika mpango huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shule ya Bwisiaambayo iko Wilayani Ukerewe, Shule ya Sekondari BujikuSakila ambayo ipo Kwimba, Shule ya Sekondari Kabilaambayo ipo Wilayani Magu na Shule ya SekondariNyamadoke ambayo ipo Buchosa. Sehemu hizi zote ambazonimejaribu kuziainisha, wanafunzi wanatembea zaidi yakilomita tano kwenda kutafuta elimu. Hivyo, naamini kabisakwa kufanya hivyo, wanafunzi wa kike wataweza kufaidikana hatimaye kufikia ndoto zao kama sisi wengine tulivyowezakuzifikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana kuongeleasuala la asilimia kumi ambalo linatakiwa kutenga naHalmashauri zetu kwa mujibu wa sheria ambayo tulipitishawenyewe hapa Bungeni kuhusiana na wanawake ambaowanapata asilimia nne, vijana ambao wanapata asilimia nnena asilimia mbili inatakiwa kutolewa kwa watu wenyeulemavu. Kwa bahati mbaya sana baadhi ya Halmashaurizetu hazitimizi sharti hili la kutenga hii asilimia kumi. Nafahamukabisa kwamba Halmashauri mbalimbali zinapatachangamoto ya mapato kuwa ni madogo lakini kwa sababuhiki kitu kimewekwa kisheria, ninaamini wanatakiwa kuzitengafedha hizi. Kwa bahati mbaya fedha hizi hazitengwi, matokeoyake, hata viongozi wakubwa wanapokuja kutembeleakatika Majimbo yetu, taarifa ambazo wanazopatiwa siyo zaukweli. Kwa mfano, wanaambiwa Halmashauri imetoa shilingimilioni 500, unajiuliza swali, hivi katika Halmashauri kwa mfanoya Jiji, hiyo ndiyo fedha pekee iliyopatikana? (Makofi)

Page 138: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Serikalikuhakikisha wanafuatilia Halmashauri ambazo hazitengifedha hizo za asilimia kumi ili waweze kuzitenga na kuwezakuwasaidia wananchi.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kwamchango wako mzuri.

MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana, naunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea. MheshimiwaMwantumu Dau na Mheshimiwa Mipata ajiandae.

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa ruhusa yako nami napenda kuongeleakatika taarifa hizi mbili za Wizara ya TAMISEMI na Serikali zaMitaa. Kwanza niweze kumpongeza Waziri wanguMheshimiwa Jafo pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuchika.

Vilevile niwapongeze na Manaibu wake wotealiokuwa nao jinsi wanavyoweza kufanya kazi. Pianampongeza mama yangu Mary Mwanjwela kwa kuteuliwakuwa Naibu wangu wa TAMISEMI na Serikali za Mitaa. (Makofi)

MWENYEKITI: Hebu jina likae, vizuri MheshimiwaMwantumu. Mheshimiwa Mwanjelwa.

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwanjelwanakupongeza sana, kuwa Naibu wangu wa Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niende moja kwa mojakwenye mchango wangu, kwanza nianze kuzungumzia sualala TARURA. TARURA ni chombo ambacho kinafanya kazi vizurina wanafanya kazi kwa juhudi kubwa, lakini kilaanayesimama hapa anaisifu TARURA. Katika kutembeleamiradi yetu, nimeiona TARURA kama kweli inafanya kazitulipokwenda Mtwara na nimeziona barabara zile za TARURAjinsi zinazofanya kazi.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokiona pale juu ya zilebarabara, kuna barabara zimejengwa 2017 tu, lakini tayarizimeshaanza mashimo. Katika kuangalia barabara zile, miminahisi yale malori yetu ambayo yanasimama katikabarabara, yanamwaga oil. Zikishamwaga oil, zile barabarazinavimba, zinafanya mashimo halafu utaziona zipo kwenyeuchakavu, kumbe zile barabara bado zingali mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuogelea katika sualahili napenda Serikali ifanye juu chini kutokana na zile barabaraza TARURA na yale malori jinsi yanavyomwaga ile oil wawezekuzifuatilia na kuzifanyia utaratibu kamili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niogelee katika sualala mradi wa TASAF. Kila ninaposimama nazungumzia mradiwa TASAF, nawapongeza sana kwa sababu wanafanya kazinzuri na kila siku nikisimama huwa nawaambia big up, maanawanafanya kazi kwa hali na mali, watu wetu ambaowaliokuwa wanyonge hivi sasa hivi wana wanajisikiakutokana na TASAF inavyofanya kazi. Wale watu wanapatapesa za TASAF, kisha wanafanya miradi yao na ile miradi yaoinaonekana; kuna wengine wana ufugaji wa mbuzi, kunawengine wanajenga nyumba zao, wanapata kustirika nawengine wanapeleka watoto wao shuleni. Kwa hiyo,naomba sana, TASAF isije ikaondolewa maana tayari nimkombozi wa wanyonge katika Tanzania yetu hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niogelee pia kwenye sualala uzazi salama; hivi sasa hili neno lazima tuliweke mbelekutokana na watoto wetu. Uzazi salama, watotowanapokuwa wamezaliwa na wazazi wao tayari wanakuwawanashughulikiwa na watoto wale kila mmoja anapata hakiyake kwa mama yake. Hata hivyo, kuna suala nimelionakwa macho yangu Dar es Salaam, kuna watoto ambaowanapelekeshwa na wazazi wao, wanakaa pembeni yabarabara na wanatumwa watoto wa miaka minne waje palekwenye barabara zile, gari zinapokuwa zimepaki, kujakuomba pesa. Hapa tayari wale watoto wameshakuwawanaanza kudhalilika, maana wazazi wamekaa pembeniwatoto wao ndio wanaotumikishwa. Kwa hiyo, naiomba

Page 140: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Serikali ifanye juhudi juu chini, juu ya kazi zao wanazozifanya,maana inaonekana limepungua sana suala li le laombaomba na kuwatumikisha watoto, lakini bado hili sualalinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niogelee katika sualala Bodi ya Mishahara ya Watumishi wa Umma. Bodi hiinimeangalia hapa vizuri tu katika taarifa ya MheshimiwaMkuchika kwamba kuna watumishi wa umma ambaowanafanyiwa utaratibu wa mishahara yao wapate kulipwamaslahi yao kiuhakika. Hata hivyo, bado watumishi wa ummawanasikitika hawapati mishahara yao kikamilifu na badowanasikitika hawajaongezewa mishahara. Mishahara yaobado haijaongezwa na bado inakawia kuingizwa il iwajikwamue kimaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mchango wangukwa hii leo nilikuwa nataka nijikite katika masuala hayo. Pianataka kumpongeza Rais wangu, Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Magufuli, kwa jitihada zake anazozichukua hivi sasakuzungukia mikoa yote na kesho tukijaaliwa tunaambiwayuko hapa Dodoma. Kwa hiyo, nampongeza sana pamojana Makamu wake, wanafanya kazi vizuri, waendelee kufanyakazi ili wazidi kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naomba kuungamkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa umeogeleavizuri. Tunaendelea na Mheshimiwa Mipata, atafuataMheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma na MheshimiwaBwanaussi ajiandae.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi. Pia nichukue nafasi hiikumshukuru Mwenyezi Mungu kutujaalia uzima. Vilevilenimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzurianazozifanya na kujitoa kwa moyo kutumikia Watanzania.Kazi anayoifanya tunaiona, tuko nyuma yake na kila mwenye

Page 141: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

macho anaona. Kwa hiyo tunamuunga mkono, hayuko pekeyake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza pia Mawaziriwote wawili mzee wangu Mheshimiwa Mkuchika naMheshimiwa Jafo, pamoja na Manaibu Waziri MheshimiwaKandege, Mheshimiwa Waitara na Mheshimiwa MwanjelwaMachuche. Wamekuwa wakitusaidia sana na siku zotewanatusikiliza na mara tunapofikishia hoja zetu wanatusaidiavizuri kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na miradi ya afya.Kazi nzuri sana imefanywa na Wizara hii ya TAMISEMI hasakatika eneo hili la afya, sisi kwetu tumefanikiwa kupata vituovya afya vitatu na sasa wanatuongezea kimoja lakini piatumepata Hospitali ya Wilaya tumepata hela za kutoshabilioni moja na milioni mia tano mwaka jana na mwaka huuwametuongezea milioni mia tano, jambo hili ni zuri sana.Kwangu mimi nimeweza kupata pia kituo cha afya chaWampembe ambacho Mheshimiwa Jafo aliwezakutembelea alipotushauri, tunamshukuru sana sana, kazi paleimefanyika vizuri na ushauri aliotupa tunaendelea nao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, nisemechangamoto moja, vituo hivi vinapokamilika kuna jambobado linabaki kuwa ni tatizo kwa akinamama wetu hata walewa vijiji vya jirani. Ningeshauri wazo hili liendelee kwenye vituovyote vinavyokamilika, tuwe tunaweza kujenga jengo lakuwafanya akinamama wajisubirie pale, maternity waitinghome, itatusaidia kufanya wale ambao wako mbali kidogowasogee na waweze kujisaidia vizuri zaidi na kupata hudumainayotakiwa. Vinginevyo habari ya kujifungulia nyumbaniitaendelea hata kama vituo vipo kwa sababu gharama zilewanashindwa kujimudu kwenda kukaa pale na kukaa kwandugu ni ngumu kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajenga vituo vya afyavingine Ninde, tunajenga kituo cha afya na wananchiwamejenga majengo mazuri, vyumba kumi wamekamilishalakini King’ombe tunajenga kituo cha afya, Kate pia

Page 142: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

wanajenga kituo cha afya, Kasu wanajenga kituo cha afya,tunaomba wanapopata nguvu tena waweze kutusaidiakwenye maeneo hayo. Hata hivyo, Kata ya Kala iko mbalisana na akipatikana mgonjwa kule anapata shida kufikakwenye kituo cha afya hasa akinamama na watoto, naombatupate gari ya wagonjwa ili isaidie katika kuhudumia katikaeneo hilo. Tumejenga zahanati nyingi zipatazo 10, zotezimefikia mtambaa panya, hatujapata uwezo wa kuwezakuezeka, lakini tunahamasisha wananchi ili tujenge. Naombamtusaidie ziko zahanati ya Kisambala, Kantawa, Kipande,Kalundi, Nkomachindo, Ifundwa, Tundu, Kilambo, Ntuchi naNchenje zimeezekwa, ni pesa kidogo tu zinatakiwa ilikuzikamilisha wananchi waanze kupata huduma. NaombaSerikali itusaidie na kama haiwezi kutusaidia itusaidie hatakuibana Halmashauri zaidi ili watusaidie katika zahanati hiziambazo karibu zinakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba vilevile nizungumziekuhusu Bima ya Afya. Bima ya Afya nzuri na inasaidia sanawananchi na mara nyingi watumishi wa taasisi mbalimbalina wa Serikali ndio wanaosaidiwa zaidi. Mpango wakuwezesha wananchi wote kwa ujumla Watanzania wapatehuduma ya Bima ya Afya umefikia wapi? Naomba nihimizeSerikali ione umuhimu wa kufanya hivyo. Sambamba na hiloniwaombe, nichukue nafasi hii kuwashukuru sana watumishiwa Bima ya Afya hasa waliojipanga kuhudumia Wabungeyupo Flora Mtabwa na Felister Mabula, hawa watu wakipatadharura wanachukua kwa haraka sana na wanatusaidia nawanajipanga vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niseme kuhusuhospitali ya Muhimbili, Muhimbili sasa hivi hudumazimejipanga vizuri, watu wanafanya kazi kama mchwa,ukipata dharura ndio unaweza ukajua kumbe sasa tunahospitali ya Taifa yenye kiwango na inahudumia vizuri sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Wagangahatuna, tunaomba Wauguzi kwetu kule Nkasi hatuna hasapembezoni. Mheshimiwa Kandege na Mheshimiwa Jafo

Page 143: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

watusikilize na Mheshimiwa Waziri anapajua, bahati nzuriumeshafika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kuhusuTARURA. TARURA kama wenzangu wanavyosema naungamkono tuwape asilimia 50 kwa 50, lakini sisi leo hii kutokanana TARURA hatuwezi kufikika kwenye vijiji kadhaa, Kijiji chaKisula siweze kufika kwa sababu barabara imekatika na mvuana hakuna fedha za dharura. Kwa hiyo TARURA haina hatauwezo wa kukabili dharura yoyote inayotokea mpakawaombe. Sasa jambo hili sio zuri sana, kwa hiyo naombasana Serikali itusaidie kuhakikisha kwamba TARURA wanapatapesa za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna daraja la Ninde, Katanzima haiwezi kufikika kwa sababu ina barabara moja, darajalimevunjika hakuna pesa na tumeshatuma maombi, lakinibado hatujapata pesa, sababu hawana pesa, kwa hiyotunaomba. TARURA pia hawana watumishi, watumishi wakewako kwa mkataba, naomba waajiriwe, kama ni kujaribiwawamejaribiwa muda wa kutosha ili watu waweze kujiamini.Sasa hivi wanafanya kazi kwa mikataba ya miezi mitanomitano au sita sita haiwezekani! Wapeni uwezo full mandatewaweze kufanya kazi vizuri itasaidia. Vilevile hawana magariya supervision hasa kule wilayani, lakini vilevile hata hukuhawana pesa za kutosha, naomba watusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendee katika eneo la maji.Kuna miradi ya maji ambayo inatekelezwa ya vijiji kumi hivivya Benki ya Dunia. Miradi mingi imefanya kazi bila utafitiwa kutosha, usanifu wake haukuwa mzuri, Kijiji cha Nkundikina mradi umegharimu zaidi ya bilioni mbili, lakini majihayatoki. Naomba Serikali ione utaratibu wa kuwezesha vijijikama hivi viweze kupata wataalam wa kutosha au kuonavikwazo gani vinafanya maji yasitoke katika gharama yotehii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Kisula vilevile majibado ingawaje wao wanaendelea na mradi. Miradi waMpasa, mradi wa Isale una zaidi ya bilioni tano katika Jimbo

Page 144: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

langu, lakini unaendelea vizuri, tumeshafanya kazi za kutosha,mkandarasi anaendelea vizuri, ila certificate tuliyoombabado haijarudi ili kazi iweze kuendelea vizuri zaidi. Kwa hiyo,naomba Serikali itupe hela ambayo tulishaomba il iMkandarasi aendelee na kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la umeme, kuna vijijivilirukwa katika awamu ya kwanza na ya pili, nikienda kulenaonekana kama kichekesho; Kijiji cha Katani, Kijiji chaMalongwe, Kijiji cha Nkana, Kijiji cha Sintali, Kijiji chaNkomachindo, ni vijiji ambavyo vinanitesa, nashindwa hatanamna gani niweze kwenda.

Naomba nitumie hadhara hii Mheshimiwa Waziri waNishati anisikie, vijiji hivi ni kero, nikienda jimboni, sina rahahasa kwa sababu wamezungukwa na vijiji vyote vyenyeumeme. Ingawaje bado kuna vijiji vingi kabisa ambavyohavina umeme, lakini hivi ndio zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kamanitapata muda ni kilimo, kilimo kikiboresha ndio halmashaurizinaweza kupata mapato ya kutosha. Kwa sasa hivi natoaushauri kwamba ruzuku iliyokuwa imewekwa kwenye kilimo,irudi kwa sababu ilikuwa inabeba watu wa chini zaidi. Ruzukuiliyoko sasa hivi inawabeba wakubwa wakubwa tu, wenyeuwezo wa kwenda kununua pembejeo madukani, lakini walewenzangu na mimi inakuwa ni ngumu sana kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia masoko ya mazao yawakulima, Mkoa wa Rukwa bila kuwa na masoko ya kutosha,wataalam mko wapi? Tutafutieni masoko ya wakulima kwasababu tunawahimiza wakulima walime, wanatupa sayansiza kuvuna vizuri zaid, sasa tukishavuna tunaweka vyakulavinaharibika na vinauzwa kwa bei ya chini, watu wanakufamoyo. Kwa hiyo naomba sana…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

Page 145: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana na naunga mkono hoja. Natambua sanakwamba Serikali ya Mitaa zinafanya kazi vizuri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Ili kumbukumbu zetuzikae vizuri jina la Mheshimiwa Naibu Waziri Mary MachucheMwanjelwa, yeye yupo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishiwa Umma na Utawala Bora na sio TAMISEMI.

Tunaendelea, Mheshimiwa Dkt. Ishengoma.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili niwezekuchangia machache kwenye Wizara hizi. Nianze kwakumpongeza Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu naWaheshimiwa Mawaziri hasa wa Wizara hizi pamoja naManaibu, nawapa hongeza sana kwa kazi nzuriwanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na mambo ya afya;kwa Mkoa wetu wa Morogoro kwa kweli na Tanzania nzimaafya imefanya vizuri sana, Nashukuru kuona kwenye bajetihii ya mwaka 2019/2020 tumeweza kutengewa fedha kwenyevituo vya afya Mkoani Morogoro ikiwepo Mvumi, ambayoimetengewa milioni 200 ambayo na mimi nimeshaichangiamatofali 2000. Pia napongeza kwa upande wa kituo chaafya cha Dumila ambao na wenyewe wametengewe milioni200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni kwa vituo vyaafya vingine ambavyo bado havijaweza kutengewa,kikiwepo kituo cha afya cha Mzinga, ambacho tayariwamejenga kwa nguvu za wananchi, lakini hakijakwisha,kikiwepo na Magadu pamoja na Mafisa na vituo vingineambavyo sikuvitaja kwenye Mkoa wetu wa Morogoro kwenyeHalmashauri zote za Mkoa wa Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natoa pongezi zangukwa Serikali kwa upande wa kutenga fedha za hospitali zaHalmashauri ya Wilaya. Tunashukuru sana kwa upande wa

Page 146: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Gairo, tumeweza kutengewa milioni 500, Kilombero milioni500, Mvomero milioni 500, pamoja na Morogoro Wilaya milioni500. Hii kwa kweli nashukuru kwa sababu Hospitali ya Mkoailikuwa inapata matatizo sana ya msongamano wawagonjwa hasa kwa upande wa wazazi ilikuwa ni kazi kweli,kwa sasa hivi naona tatizo hili litakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaona hela kwenyeupande wa hospitali ya Wilaya ya Manispaa ya Morogoroambayo inajengwa na inatumika, lakini haijatumikasawasawa kwa sababu bado haijakamilika. Kwa hiyo,naomba Serikali waweze kuangalia na waweze kunijibu kamakweli wamenitengea kwa sababu sijaona hela yoyote yahospitali ya Manispaa pale mjini. Naomba hospitali hii iwezekuangaliwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa watumishihasa kada ya afya pamoja na elimu kwa Mkoa wa Morogorobado tuna matatizo. Kwa upande wa wataalam wa afyana hasa ukikuta kwenye vituo vile ambavyo viko pembezonikwenye Wilaya za pembezoni kama Malinyi, Ulanga unakutakuwa kituo cha afya au zahanati inaweza ikawa na Mgangammoja ambaye hawezi. Halafu mimi mwenyewenimeshuhudia, unakuta hivi vituo vya afya vingine vinafungwasaa tisa. Jioni havifanyi kazi, usiku havifanyi kazi, hapo kwakweli sielewi. Naomba Wizara waliangalie kwa sababuugonjwa hauchagui ni saa ngapi unaumwa, saa yoyoteunaumwa, kwa hiyo naomba waliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa elimu,Walimu ni pungufu na hasa kwa upande wa Walimu wasayansi naomba watupatie hao Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo furaha sanakuipongeza Serikali kwenye miradi ya kimkakati kwa kweliManispaa ya Morogoro tunaringa na wananchi wanajivunana Mkoa wa Morogoro wote kwa sababu Manispaa ni kioo.Mpaka sasa hivi tuna soko ambalo tunajenga, soko zuri sanaambalo tumetengewa shilingi bilioni tati na milioni mia tanokwa bajeti hii. Kwa hiyo tunashukuru, pia tuna wale

Page 147: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

wanaopita pale Stendi, wote mnaiona kuwa Stendi yaMorogoro ni nzuri kwa hiyo tunaishukuru Serikali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya msingi bila malipo,Mkoa wa Morogoro kwa kweli Serikali inafanya vizuri chini yaMheshimiwa Rais, lazima niipongeze kwa sababu upande waelimu bila malipo, kwa upande wa shule za msingi tumewezakutengewa zaidi ya billioni sita na pia kwenye sekondari zaidiya bilioni sita. Tunaishukuru sana Serikali iendelee kufanyavizuri kama inavyofanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ninaloomba ni kwaupande wa hosteli, hospitali ambazo zitajengwa naombaziweze zijengwe kwenye shule za wasichana kwa sababuwatoto wa kike wanapata matatizo sana na wao wanayajuakwa mimba za utotoni na mambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kuwa kuna magarikama 40 ambayo yatanunuliwa na kutawanywa kwenyehalmashauri ambazo zina mazingira magumu. Kwa kwelikwenye Halmashauri ambazo zina mazingira magumunaomba kuomba kupatiwa gari moja kwa Halmashauri yaMalinyi, ambayo iko mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezeshaji wananchikiuchumi, asilimia nne kwa wanawake, asilimia nne kwa vijanana asilimia mbili kwa walemavu ni jambo zuri sana ambalolimeweza kufanywa na Serikali, lakini kuna wale ambaohawatimizi masharti. Naomba hayo masharti yaangaliwevizuri kusudi hao vijana waweze kurudisha kwa wakati na hizihela ziweze kuwasaidia. Kwa upande wa wanawakewanarudisha vizuri, lakini vikundi viko vingi, kwa hiyo naombaWizara wanisikilize, waweze kuangalia jinsi ya kuwasaidiahawa wanawake ili waweze kupata hela nyingi na zakutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TARURA, nikweli wanafanya vizuri lakini wanapata hela kidogo. Kwaupande wa Morogoro kwa barabara za vijijini naonahawajaweza kuendelea vizuri kwa sababu hela hazitoshi. Kwa

Page 148: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

hiyo, naomba waongezewa hela ili kusudi waweze kufanyavizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Manispaakuna barabara za pembezoni ambazo wanazisahau. Kwamfano kama barabara za Magadu na SUA kwa wasomi.Naomba na zenyewe waweze kuzitengeneza vizuri kadiriinavyowezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwa upande walishe. Tanzania yetu ina udumavu kwa watoto chini ya miakamitano ambapo 34% wamedumaa, kuna utapiamlo lakiniSerikali imeweza kuona kuwa ni jambo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Dkt.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja za Wizara zote mbili, ahsantesana na Mwenyezi Mungu awabariki. (Makofi)

MWENYEKITI: Ameen.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naMheshimiwa Bwanausi atafuatiwa na Mheshimiwa Prof. AnnaTibaijuka na Mheshimiwa Zuberi Kabwe ajiandae.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami nichangie kwenyehotuba ya Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa pamoja na Waziri wa Nchi anayeshughulikia mamboya Utumishi na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongezaMheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwaanayoifanya. Nimemshangaa sana ndugu ya MheshimiwaNgombale pale alipotamka kwamba anaitaka Serikaliiwaombe radhi wakulima wa korosho.

Page 149: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

Mimi nasema Serikali haiwezi kuomba radhi ilainapaswa kupongezwa kwa hatua il iyoichukua kwakuwanusuru wakulima wa korosho. Mheshimiwa Ngombaleyeye analima ufuta, nimeshangaa sana anaposema habariya korosho na Wilaya Masasi ambayo natoka mimi ndiyoWilaya ya pili kwa uzalishaji nchini baada ya Tandahimba.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nimpongezeMheshimiwa wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwajinsi alivyolishughulikia suala la korosho na kuwasamehe waleambao walinunua kinyume na utaratibu almaarufu kama‘kangomba’. Tunakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania tunashuhudiajinsi wananchi wanavyojitokeza kwa wingi, nimeona mkutanowa pale Mufindi, Iringa, Mtwara, Namtumbo, kwa kweliWatanzania wana imani kubwa na Rais wetu Dkt. JohnPombe Magufuli. Nadhani vyama vya upinzani mwakaniitabidi wajitafakari kuona kama kuna sababu ya kumwekamgombe Urais kwa sababu kwa hali ile navyoiona sidhanikama kutakuwa na mgombea yeyote atakayewezakushindana na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

WABUNGE FULANI: Aaaaaa.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimpongeze sana jirani yangu Waziri Jafo na wasaidizi wakendugu yangu Mheshimwa Kandege na Mheshimiwa Waitarakwa kazi kubwa mnayoifanya TAMISEMI, hongereni sana.Mheshimiwa Jafo namfahamu siku nyingi sana na wengitunamfahamu pale alipokuwa Plan International aliwahikuwa mfanyakazi bora lakini Bunge lililopita tulimchaguaMheshimiwa Jafo kutuwakilisha kwenye Bunge la SADC.Mheshimiwa Anne Makinda aliwahi kusimama hapaakasema anatuwakilisha vyema baada ya kupewa Kamatikule kwenye SADC, tunakupongeza sana. Kwa hiyo, hayaunayofanya TAMISEMI ni mtiririko wa utendaji kazi wakouliotukuka. (Makofi)

Page 150: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Waziri,Kapteni Mstaafu George Huruma Mkuchika na MheshimiwaDkt. Mwanjelwa, msaidizi wake katika Wizara hii.Tunapongeza tuna maana, Mheshimiwa George HurumaMkuchika, yeye ni kati ya wachache ambao wapomadarakani waliowahi kuteuliwa kwa nafasi mbalimbalikuanzia DC, RC hadi Waziri katika vipindi vyote vya Maraiswatano walioongoza nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Baba wa Taifaalimteua kuwa DC na Mheshimiwa Rais Mwinyi akamteuakuwa DC baadaye Mzee Mkapa akamteua kuwa RC.Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete na Mhehimiwa Dkt.Magufuli wote wammeteua Mzee huu kuwa Waziri katikaawamu zao. Kwa hiyo, kwa kweli tunampongeza kwautendaji wake mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye suala laTAMISEMI, hii ni Wizara ngumu sana. Bahati nzuri nimekuliaTAMISEMI, nimekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Diwanikwa miaka 10, Meya na sasa Mbunge, naifahamu TAMISEMIni ngumu sana. Kwa mfumo Mheshimiwa Jafo, Manaibu,Katibu Mkuu na watu wa TAMISEMI kwa ujumla sasahaitembei bali inakimbia kwa utendaji wenu wa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye afya elimu wengiwamezungumza sitaki kurudia sana lakini nikuombeMheshimiwa Jafo pamoja na juhudi ambazo zimeendeleakufanywa hasa katika Jimbo la Lulindi kama nilivyokuwanikieleza mara kwa mara kwamba sasa hivi kituokinachofanya kazi ni kimoja tu cha Nagani. NamshukuruMheshimiwa Rais nilipomuomba suala la gari amenikubaliana wananchi wa Lulindi wanashukuru sana kwa jinsi ambavyoamesikiliza kilio kile. Bado nikombe Mheshimiwa Jafo na NaibuKatibu Mkuu Afya na timu nzima ya Naibu Mawaziri, Munguakiwajalia mkapata fedha za kuongeza vituo vya afyatunahitaji kituo muhimu sana cha afya cha Mnavila kilichopompakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini naomba kituo hikikwa haraka sana? Tunalo tatizo kubwa sana la wananchiwetu kupoteza maisha na viungo kutokana na wimbi kubwala kuzaana kwa mamba katika Mto huu wa Ruvuma. Tatizolililopo ni kwamba hatuna kituo cha afya karibu, hivyo,kukitokea majanga ya namna hiyo wananchi wetuwanapata tatizo la kupoteza maisha ama kupata ulemavukwa sababu hakuna huduma ya haraka katika eneo hilo.Kutoka pale Mnavila kwenda kwenye kituo cha afya ni zaidiya kilomita 50. Kwa hiyo, nikuombe sana kwa huruma yakokwa kweli kituo hiki ni muhimu sana kipatikane ili tuwezekuwanusuru wananchi hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala hili hili la ujenziwa hospitali, nishukuru kwa kunipatia Hospitali ya Wilayaambayo inajengwa hivi sasa pamoja na kituo paleChingutwa. Nashauri kitengo kile kinachohusika na gharamaza majengo haya wawe waangalifu katika kutoa fedhaaidha shilingi milioni 400 au 500 kwa sababu kuna baadhi yamaeneo ambapo upatikanaji wa vifaa ni mgumu inapelekwashilingi milioni 400 lakini eneo ambalo halina tatizo inapelekwashilingi milioni 500. Kwa hiyo, nadhani hili ni suala tu lamarekebisho la kuangalia eneo ambalo lina changamotonyingi basi ndiyo lipelekewe fedha zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nishukuru kwa jinsiunavyoiongoza TARURA lakini bado Mheshimiwa Waziri…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana kwa mchango wako.

MHE. JEROME D. BWANAUSI: Ahsante sana na naungamkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka.

Page 152: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia.Naomba nianze kwa kuungana na walionitanguliakuwapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri wa TAMISEMI naUtumishi na Utawala Bora kwa kazi nzuri wanazofanya chiniya Ofisi ya Rais. Suala la utawala bora ni mtambuka na nyetina ndiyo maana labda Wizara hizi zipo chini ya Ofisi ya Rais,kwa hiyo, hapa tunazungumzia mustakabali wa Taifa letu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mantiki hiyo basi, nianzetu kwa kueleza kwamba mapema mwaka huu nilikuwa nachangamoto za kiafya nikaenda kutibiwa Marekani nikapatanafasi kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Katikamaongozi yetu, alinipongeza sana na alisema maeneoyafuatavyo, namnukuu, alisema: “You know Anna Tanzaniais unique”. Ina maana kwamba Tanzania ni nchi ya pekee.Akasema kwa sababu katika katika nchi za Afrika ni nchiambayo ina utamaduni na inaonyesha kwamba ina uwezowa kuwa na changamoto zake na ikazitatua yenyewe. Hayoni maneno ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Umoja waMataifa kwa Kiingereza anaitwa Secretary General of theUnited Nations, kuna wenzetu hapa walikuwa wanatakakukusikia Kiingereza chake. Tulipofika hapa katika dhananzima ya utawala bora, sina budi kuwapongeza majemedariwetu Waheshimiwa Mawaziri ambao wana dhamana yasekta hizi na Mheshimiwa Rais kwamba tulipofika si haba. Hiindiyo salamu ambayo naileta kutoka kwa marafiki zangu nawatu wengine ambao niko nao, juzi juzi nimetoka nchi zaNordic tulipofika si hapa. Ukiangalia Rais alipoanzia katikakuleta utawala bora tulianza na janga la madawa yakulevya…

MBUNGE FULANI: Aaaaa.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Kwa vyovyotemawazo yako juu ya mtu ni ya kwako lakini huwezi kusemamtu anayekuja kupambana na madawa ya kulevya atapata

Page 153: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

marafiki, hilo ni la kwanza na dunia inalitambua. Tukaingiakatika changamoto ya mikataba mibovu il iyokuwainatuumiza sana kwenye madini tukalikamilisha na mengineyanakuja. Kwa hiyo, katika dhana ya utawala bora, nafikiriaTaifa zima bila kuangalia itikadi ya mtu tunatakiwa tuwepamoja kuhakikisha kwamba tunaimarisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenyewe kwamaumbile yangu (by inclination) ni mtu ambaye napendasana hoja, ushindani na upinzani kama ikiwa lazima.Tunapozungumzia utawala bora lazima pia tuzungumzieupinzani bora maana hatuwezi kuwa na utawala bora kamahatuna upinzani bora, kwa sababu upinzani bora ndiyoutaleta utawala bora. Kwa hiyo, nataka kusema tunapokaahapa wakati mwingine tunasahau context ya tunachotakakufanya hapa.

T A A R I F A

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Profesa, kidogo tusikietaarifa, Mheshimiwa Mwakagenda.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, nataka kuumpa taarifa mzungumzajianayeongea ambaye ni Profesa Mbobevu katika nchi hii.Nataka kumpa taarifa kwamba alipokuwa anaongea nahuyo Kiongozi wa UN angemueleza kwamba upinzani boraunahitaji fairness. Kwa hiyo, nilifikiri kwamba angemsaidia nakumpa uwazi wa kinachofanyika katika Taifa letu.Mheshimiwa Profesa nataka nikukumbushe nawe ulikuwaWaziri wa awamu zil izopita na madawa hayo hayoyalikuwepo wakati wewe ukiwa Waziri. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Profesa, taarifa hiyo.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: MheshimiwaMwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Mwakagenda kwa hiyo

Page 154: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

perspective yake. Nimeshasema mimi ni mtu ambayenakaribisha mawazo mbadala ila naweza kumhakikishiamaongezi yangu na Katibu Mkuu yaligusa mambo yote hayona zaidi. Cha msingi ni kwamba Tanzania is unique, tulipofikani pazuri na tujipongeze na Rais wetu anakwenda vizuriMheshimiwa Mwakagenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ulinde dakikazangu alizozichukua Mheshimiwa Mwakagenda. BabaMtakatifu Francis katika kazi yake ya kujaribu ku-promoteutawala bora na uongozi wa kiroho alikuwa katika nchi zaUarabuni alifika Dubai, alitoa nasaha ambazo kwa ukosefumuda sitaweza kuzisoma hapa lakini naomba nikabidhinyaraka hii kama sehemu ya Hansard ya hotoba yangu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baba Mtakafitu anasema nilazima tujue changamoto zipo, tatizo siyo changamoto, tatizosiyo watu wanakusema, tatizo siyo kwamba watuwanakuonea, tatizo ni wewe una-respond namna gani? Kwahiyo, usikubali mtu yeyote aku-pull down, wewe weka hojamezani, nyaraka hii naikabidhi ili isaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ukiona kwenyemitandao Baba Mtakatifu anahakangaika na wenzetu waSouth Sudan. South Sudan watu hawaelewani, sasa BabaMtakatifu ameamua kuwapigia magoti, mtaona kwenyemitandao nadhani ina-trend, utawala bora pia unaamanishadhamira zetu, kama unataka utawala bora lazima uangaliepia dhamira zetu. Kwa mantiki hiyo basi na kwa sifa tulizonazotusizipoteze kwa kuokosa nation dialog. Ni kwa mantiki hiyobasi nataka kuchangia ifuatavyo:-

Mhehimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa utawala borautataka utawala wa sheria na haki. Utawala bora lazimautokane na sheria na haki, sheria peke yake bila haki haiwezikuleta utawala bora. Kwa mantiki hiyo, nataka kusemakwamba suala la haki Mheshimiwa Mkuchika na MheshimiwaDkt. Mary Mwanjelwa, naomba liangaliwe kwa umakini sana.

Page 155: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya MwendeshaMashtaka (DPP) ni lazima ijiangalie pia kwa sababu huwezikuwaweka watu gerezani bila kusikiliza kesi zao ukasema ninautawala bora. Hiyo naiweka kwa perspective niliyosemakwamba hapa tunachangia, hili ni Bunge la Jamhuri, tatizoletu hapa huwa ni ideologies zinatufanya tunashindwakwenda forward. Kama mtu unatuhumiwa una makosa nisawa lakini wachunguzi kama hawajawa na ushahidi, kusuditukae vizuri mbele ya Mataifa na majirani wanaotuangaliana humu ndani, naomba suala hilo tuliangalie na nalisemahili bila kuwa na usabiki wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Profesa, muda wakoumeisha.

WABUNGE FULANI: Aaaaaa.

MBUNGE FULANI: Mwongezee.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Dakika tano, badojamani, sijui kama nimeongea dakika tano. Kama nimemalizadakika zangu nitaweka…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tibaijuka, kwa sababuKanuni pia zinatambua watu fulani ambao wametoamchango mkubwa kwa nchi hii na kwa Bunge hili, kwa hiyo,nakuongezea dakika tano. (Makofi/Kicheko)

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa heshima hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali hiyo, naombaniende haraka na nitaweka hapa mchango wangu kamaulivyoandikwa, kwa sababu mimi ni Profesa nimeandikauingie wote kwenye Hansard. (Makofi)

Page 156: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ya muhimu yakusema, niende kwenye suala la kuwezesha watu wetu katikautawala bora, kuna suala la kuwalipa wakandarasi wa ndani.Wakandarasi wa ndani sasa hivi Mheshimiwa Mkuchika naMheshimiwa Dkt. Mwanjelwa nalileta kwenu ni suala lautawala bora kwa sababu wasipolipwa fedha hawawezikufanya kazi, hatuwezi kujijengea uwezo, tutabaki naWachina peke yao. Kwa sababu ya muda umekuwa mfupinimelifafanua katika hotuba yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba nikupe nyarakanyingine ambapo kuna kitu kinaitwa Ilani ya Usafi. Utawalabora pia ni mkono wa Serikali wa kushoto kujua wa kuliaunafanya nini. Sasa hivi kuna tabia mbaya, naomba nisemekwamba Maafisa Afya na Mazingira wanakwenda kwenyeshule binafsi na hapa na-declare interest kwa sababu ninashule, wanategemea uwape bahasha kama bahasha haipoimekula kwako, unakuta unaandikiwa Ilani Chafu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikukabidhi Ilanimoja hapa ambayo imeandikwa kwenye Shule yaWasichana ya Barbro ambayo huwa naisaidia, inasematuong’oe vyoo (WCs) kama hivi hapa Bungeni tuweke vyoovya kuchuchumaa. Hata hivyo, Bwana Afya hajui kwambakwa wanawake kuchuchumaa inaweza pia ikaeneza UTI,hapa ndipo tulipofika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalileta jambo hili hapa mtuatashangaa kuwa ni la kisekta, siyo la kisekta ni la kiutawalabora. Sheria ya Elimu ndiyo inatawala shule, watu wamazingira na watu wengine wale wakitaka kuingia kwenyeshule lazima waende na Mkaguzi wa Shule, vitu kama hivihavifanyiki vinatuletea matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijakaa hili lazimaniliseme ni muhumu sana, naomba sana MheshimiwaMkuchika na Mheshimiwa Dkt. Mwanjelwa na nadhani naMheshimiwa Rais pia atatusikia ni kuhusu suala la watumishiwalioachishwa kazi kwa sababu walidai kwambawamemaliza form four wakati hawakumaliza, naomba tena

Page 157: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Mheshimiwa Rais atumie huruma na hekima yake kuliangaliaupya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa nafasi yanguukiniuliza nasema kuna wengine walijaza form wakisemakwamba wana form four kwa sababu mabosi waowaliwaambia jaza form four. Tuje humu Bungeni, MheshimiwaLusinde leo sijui kama yupo au hayupo yeye huwa anapendakujiita darasa la saba lakini namjua ana-masters ni kwambahana cheti tu. Unaona ni persepective tu huwezi kusemaMheshimiwa Lusinde ni darasa la saba siyo darasa la sabahuyu, kwa elimu yake ana-masters na zaidi lakini kwa sababuya certification ndiyo tusema darasa la saba, sisi tumekwamakwenye certification tunashindwa kwenda mbele. Kwa hiyo,naomba niseme jamani, jamani suala hili ni muhimu sanakuangaliwa upya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya kutunza vyeti, siyokazi ya individual. Ni kazi ya NACTE, BRELA, Wizara ya Ardhina wengine. Sisi raia hatuna safe ambayo ni fireproof kwamfano. Kwa hiyo, cheti changu kikiungua nakwenda NACTEkuomba cheti changu. Sasa nina kesi za watu ambao niMaprofesa, wamesimamishwa kazi katika Vyuo Vikuu kwasababu walipoteza vyeti vya Form Four. This is not serious.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Profesa.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. Nitaleta kwa maandishi.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Zitto Kabwe atafuatiwa na MheshimiwaFreeman Mbowe.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namimi nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia Makadirioya Bajeti ya Wizara hizi ambazo ziko chini ya Ofisi Rais,TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora. Nianze na jambo la

Page 158: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Utawala Bora ambalo Mheshimiwa Prof. Tibaijuka ameligusiakidogo. Naomba nilipanue zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na utamadunihivi sasa, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka kukamata watu.Hatujui kama kesi hizo wanabambikiwa au ni kesi halali, lakinibaadaye tunaona kwamba watu wale wanakubaliana naOfisi ya DPP, wanalipa fedha kesi zinakwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nchi yetu ipateufafanuzi, kwa sababu namna ambavyo jambo hil ilinafanywa, kwanza inawezekana kuna uonevu mkubwasana kwamba kuna watu ambao wanabambikiwa kesi,wanapewa money laundering offences, wanawekwa ndaniili wakazungumze na DPP halafu waende Mahakamani wakiriwalipe faini ya kile kiwango ambacho wameshtakiwa nacho.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano dhahiri ni wa juzi,ambapo taarifa ambayo VODACOM wameitoa, kwa sababuVODACOM ni l isted Company; hawa watu wengineinawezekana negotiations zinafanyika na DPP zinaishia kimyakimya hatujui, lakini kwa VODACOM kwa sababu ni listedCompany waliweka taarifa yao ile public kwa sababu wakol isted kwenye Dar es Salaam Stock exchange naJohannesburg Stock exchange.

Mheshimiwa Mwenyekiti, VODACOM wanasema,VODACOM Tanzania has reached an agreement withDirector of Public Prosecutions (DPP) for five detainedemployees to be released. The agreement include paymentof five point two billion Tanzania Shillings by VODACOM toTanzania in order to settle charges initiated by DPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nipateuelewa. Nchi yetu haina sheria wala kanuni zinazowezeshapale ambapo mtu anakuwa ametuhumiwa kujadiliana naprosecuter ili ama kupunguza adhabu au kufuta adhabu aukulipa faini. Haya makubaliano ya DPP na watuhumiwayanaendeshwa kwa sheria ipi? (Makofi)

Page 159: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepewa revenue book,kila Mbunge amepewa. Ukitazama revenue books hizi, kunakila senti ambapo kila Idara ya Serikali inaingiza. NimeangaliaVote 35 - The National Prosecutions Services, kwa miakamitatu yote ya nyuma na hata mwaka huu, wanatarajiwakuingiza shilingi milioni 14 tu. Mwaka 2018 peke yake DPPwamefanya transactions za zaidi ya shilingi bilioni 23 kwa watuambao wanakamatwa na ku-settle kesi kati yao na DPPwanaenda Mahakamani kesi zinafutwa. Naomba kufahamu,kwa sheria ipi? Fedha zinakwenda wapi? Nani anazikaguahizo fedha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo ni jambo ambalotukilikalia kimya tunatengeneza a gangstar republic, kwambadola inaweza ikaenda ikamkata mtu, ikamzushia,ikamwambia ukitaka utoke, toa hela; watu wanatoa hela,wanatoka. Hatuwezi kuendesha nchi kama gangstars.Naomba tupate maelezo ya jambo hili, ni namna ganiambavyo linakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili…

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti,...

MBUNGE FULANI: Tulia wewe…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Stella Manyanya.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kwa mujibuwa kauni ya 64 1(a) na kuendelea, naomba kufuatia maelezoambayo Mheshimiwa Zitto anayazungumza, badala tu yakuyaweka kwa ujumla jumla na kwa sababu vyomboanavyovizungumzia ni vizito na vinavyoheshimika katika nchihii, ni vyema akatoa kwa vielelezo vikaja mbele ya kiti chakoili hata watakapokuja ku-respond wajue ni kitu ganianakizungumzia kwa uhakika. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zitto.

Page 160: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,jambo la pili ambalo nataka kulizungumzia ni TAKUKURU.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAKUKURU ndiyo Taasisiambayo tumeipa dhamana ya kupambana na Rushwa.Nimeona kwenye bajeti ya mwaka huu tunawaombea shilingibilioni 75, lakini taarifa ambazo ninazo za uhakika ni kwambakwa takribani miaka minane iliyopita TAKUKURU hesabu zakehazijawahi kukaguliwa na auditor yeyote yule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nifahamu kutokaOfisi ya Utawala Bora, ni kwa nini TAKUKURU, licha ya kwambasheria tuliyoitunga mwaka 2007 inataka wafunge mahesabuna wakaguliwe, kwa nini TAKUKURU hawakaguliwi na kilamwaka tunawatengea mabilioni ya fedha, tunawaaminikwamba wanapambana na rushwa, lakini wao wenyewefedha ambazo tunawapa hazikaguliwi na wala hili Bungehaliwezi kuziona? Ni kwa nini jambo hilo linaendeleakufanyika? Naomba Serikali iweze kutoa maelezo ya hilo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, utawala borapia na hili jambo ni la muhimu sana; kuna watu kwenye nchiambao ni lazima mhakikishe ya kwamba hawakugusiki namambo machafu au hata hisia. Nimesoma hotuba ya Ofisiya Rais hapa ukurasa wa 87 ambapo Bunge linajulishwa kuwakwa mujibu wa GN Na. 252 ya mwaka 2018, sasa Wakala waNdege za Serikali umehamishiwa Ofisi ya Rais kutoka Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unafahamu kwambamwaka 2017/2018 tulitenga fedha shilingi bilioni 509, mwakauliofuata shilingi bilioni 497 na mwaka huu zinaombwa shilingibilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege za ATCL. Sisi wotetunajua ATCL hawamiliki ndege zile. Ndege zile zinamilikiwana Wakala wa Ndege wa Serikali. ATCL inakodishiwa ndegezile. Halafu tumepitisha huko, tunategemea kwamba CAGatakwenda kukagua Wizara ya Ujenzi na kadhalika, ghaflatunaambiwa kwamba Wakala wa Ndege za Serikali hayuko

Page 161: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

tena Ujenzi, iko Ofisi ya Rais. Serikali inaenda kuficha nini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake mtu mwingineanafanya procurement, una mtu mwingine anamiliki ndege,una mtu mwingine anaziendesha zile ndege; Serikali inatakakuficha nini? Kwa nini mnafanya mambo bila kutumia maarifamnajaza jambo kama hili lenye ma-procurement ya helanyingi, chini ya Ofisi ya Rais? Likitokea doa hata kidogo,mmnamgusa Rais moja kwa moja. Nasi hatulaza damu,tutasema moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hivi vitu huwavinatenganishwa ili angalau Mkuu wa Nchi anakuwa juuaweze ku-deal na hawa wa chini. Mnalundika procurementyote, zenye utata hatujui zilitangazwa lini, negotiationszilikuwaje, ndege zinadondoka kila siku. Juzi hapa KQDreamliner yao imekwama, imetua Dar es Salaam. Ikiangukayetu hapa, twende tukamlaumu Rais? Hivi si ni vitu vyakawaida tu ambavyo wataalam mnapaswa kukaa namuepushe! Hata mwenyewe akitaka, mnamwambia mzeehatuwezi kufanya, tukifanya tutakuletea shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipate maelezo yaSerikali ni kwa nini maamuzi haya yamefanywa? Maamuzihaya mmefanya wakati Bunge linaendelea, maana yakeilikuwa Bunge linaendelea, ni Juni 2018, tayari tumeshapitishaBajeti inayokwenda kununua hizo ndege kwa ajili ya kwendaWizara ya Ujenzi, halafu pia mambo yote hayo yamepelekwaOfisi ya Rais na tunajua hapa kuna controversies za Vote 20ambazo naomba nipate maelezo haya ya Serikali... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. MheshimiwaFreeman Mbowe, atafuatiwa na Mheshimiwa Mlinga.

Page 162: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niungane na wenzangukuchangia katika hoja hii ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Utumishina Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanzia hapo ambapoamemalizia Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe, kuzungumziahoja ya utoaji haki katika Taifa na hilo suala amelizungumzavilevile Mheshimiwa Mama Tibaijuka. Nalizungumza kamamhanga ambaye nimekaa Magereza kwa siku 104 naMheshimiwa Matiko na fursa ile ya kuishi Magereza imetupanafasi kubwa sana ya kujua hali halisi ya nchi yetu. Imetupanafasi ya kujua hali halisi sisi Wabunge tunapotunga sheriatunafikiri sheria hizi hazituhusu, kwa hiyo, tunatunga sherianyingine ambazo ni ngumu na mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umekuwa ni utamaduni waSerikali kugeuza kesi za money laundering kama chanzo chamapato ya Serikali, yaani inaonekana kama kesi za moneylaundering ni mkakati mpya wa kukuza mapato ya Serikali.Watu wanakamatwa, uchunguzi unaendelea miezi sita aumwaka mzima, Magereza za Dar es Salaam zimejaamahabusu zaidi ya 5,000 ambao kesi zao zinaendeleahawapewi haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wamekaa ndanimiaka mitatu, wengine wamekaa miaka minne, kesi zaowengine hawazijui. Sasa tunalundika Magereza zetu kwawatu ambao kwa kweli walistahili kuwa nje kwa misingi yadhamana. Utamaduni huu unaharibu investment climate yanchi kwa sababu watu wanaokamatwa wanatoka kwenyeMakampuni na Mashirika makubwa ambayo yanatoamapato makubwa kwa Serikali yetu. Lazima Serikali iangalienamna ya ku-leverage haya mambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema kweli tukasimamiasheria na kukawa na haki katika Taifa, lakini upande wa pilitujue athari zake kwa uchumi wa nchi. Sasa tunakamata watuna watu wengine mnaowakamata, wanaoshtakiwa kwamakosa mbalimbali ya rushwa ni watu ambao wako katika

Page 163: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

miradi ambayo iko chini ya PPP. Leo Mkurugenzi na mke wakena viongozi wengine wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam wakomahabusu kwa kesi za money laundering na huyu mtu ni mbiawenu, mngeweza mkakaa nao kwenye Vikao vya Bodimkamaliza mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiendelea na utamadunihuu, ni nani atakuwa na confidence ya kuwekeza na Serikaliwakati Serikali yenyewe inawaweka ndani wabia wake?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema nilizungumze hilo.Waheshimiwa Wabunge, tunatunga sheria nyingine ambazozinawaumiza sana watu. Kuna watu kule wamekutwa namsokoto mmoja wa bangi, siungi mkono hoja ya bangi, lakiniwanafungwa miaka 30. Kuna watu wamekutwa na mirungikifurushi kimoja wanafungwa miaka 30. Ukienda Kenya,mirungi ni biashara halali. Hebu tujiangalie katika sehemu yadunia, tuko wapi katika kusimamia mambo haya il ikuhakikisha kwamba tunapotunga sheria, tusitunge kwaushabiki, tutambue kwamba zinawaumiza sana watu naBunge linalaaniwa sana katika Magereza zetu zote kwasababu halisimamii utoaji wa haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka hapo, nizungumzesuala la utawala la bora, yote haya nayazungumza katikamwamvuli wa utawala bora. Mheshimiwa Mkuchika weweni Waziri mzoefu sana, mnajua kwamba Vyama vya Siasavimeruhusiwa kufanya kazi katika nchi hii katika misingiambayo ni ya kweli kabisa. Jambo hili limezungumzwa nawengi, mimi kama Kiongozi wa Upinzani nilizungumzekulisisitiza. Ukiulizwa Serikalini, hivi mmezuia kazi za Vyama vyaSiasa, kwa sheria gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnaona sifa kutangazakwamba tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwamwaka huu; mnaona sifa kusema tutashinda uchaguzi wamwaka ujao, wakati mnazuia Vyama vya Siasa visifanye kazizake za Kikatiba. Hivi vyama ambavyo havina Wabunge,

Page 164: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

havina Madiwani, vitajitanua vipi? Vitaeleza vipi sera yakeviweze kushiriki uchaguzi wa mwaka ujao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maisha ya siasa ni maishayetu ya kila siku. Mnazuia Mikutano halafu mnakuwa proudkwamba tunawashinda Wapinzani. Mnaogopa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hofu hii, unaionahofu katika Taifa, watu wanaogopa. Leo nimekutana namsafara wa Mheshimiwa Rais, nimeogopa, nini kinaendeleanchi hii? Ni lazima Rais wetu alindwe, nakubali; na sipuuzikabisa umuhimu wa ulinzi wa msafara wa Rais, lakiniukiangalia uzito wa ulinzi wa ule unaona kwamba hata hawawanaomchunga Rais wanagundua kwamba kuna tatizomahali. Kwa hiyo, ulinzi unawekwa wa ziada sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, msururu wa magari karibu80, helikopta ziko angani. Sasa unajiuliza, ile nchi yetu yaamani na utulivu tumegeuka tena! Kile kisiwa chetu chaamani na utulivu kinakuwaje sasa? Tulizoea kuona viongoziwetu wakiwa huru, wakiwa wana-mix na watu wetu bila hofuyoyote, lakini kwa namna mambo yanavyokwenda sasa,tunaona kuna tatizo kubwa la msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaitaka Serikali naMheshimiwa Waziri atupe kauli, ruhusuni tukafanye kazi yasiasa. Msiwe marefarii na wakati huo huo mkawa wachezaji.Mnatufunga mikono halafu mnaringa hapa! Ruhusuni tufanyemikutano ya siasa, tukutane kwenye majukwaa ya wananchitukaone haki iko wapi? Hilo ni jambo moja ambaloningependa sana kulizungumza kwa sababu naona tuna-restrict sana democracy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo nizungumzieTume Huru ya Uchaguzi. Hoja ya Tume Huru ya Uchaguziimezungumzwa kwenye Bunge hili tangu mfumo wa VyamaVingi umerudi kwa mara ya pili mwaka 1992, hakuna mwakaunapita Tume Huru haizungumzwi. Mnaogopa Tume Huru yakazi gani? Tume Huru ndiyo inatupa misingi ya utawala bora,tunapata viongozi ambao wametokana na utashi wa

Page 165: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

wananchi, kila kiongozi anayeingia ndani ya Bunge hili ajioneyuko proud, akiwa wa CCM au wa Upinzani ajione yuko proudkwamba amechaguliwa katika uchaguzi ambao ulikuwahuru na haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnakwenda kwenyeuchaguzi na Tume yenu, Mheshimiwa Rais ambaye nayemdau; kuna conflict of interest hapa, anamchaguaMwenyekiti wa Tume, anachagua Makamishna,anawachagua Watendaji wake, anachagua Wakurugenziambao wanatokana na Chama cha Siasa, kitu ambachoSheria ya Utumishi wa Umma inakataza. Hatuheshimu tenasheria wala katiba yetu, tunalipeleka Taifa hili wapi? (Makofi)

Mheshimwia Mwenyekiti, sisi tunapendekeza verystrongly kwamba ni wakati muafaka sasa, kama tunatakaamani sustainable katika Taifa hili, tutafakari suala la kuwana Tume Huru ya Uchaguzi. Tusisubiri tuingie kwenyemachafuko kama Mataifa mengine, halafu tukajionakwamba tumeingia kwenye machafuko kwa sababuhatukujua tunafanya nini? Ningependa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbowe.Mheshimiwa Mlinga atafuatiwa na Mheshimiwa Esther Matikona Mheshimiwa Kingu ajiandae.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Naomba nianze nyuma niendembele. Naomba nianze na hilo la Tume ya Uchaguzi kwasababu limeongelewa sana.

Mheshimiwa Mewnyekiti, wewe ni Mwanasheria naKatiba ya mwaka 1977 na marekebisho yake yaliyofanywamara kwa mara, wewe ulihusika. Tume ya Uchaguziimeanzishwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 74 1(a). Katibaimeelezea Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anapatikanaje;japokuwa anachaguliwa na Rais, lakini (a) inasema,

Page 166: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

“Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu auMahakama ya Rufani, au mtu mwenye sifa ya kuwa Wakilina amekuwa na sifa na hizo kwa muda usiopungua miaka15.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kipengele (b) kimetaja“Makamu Mwenyekiti,” naye, hivyo hivyo atakuwa Jaji waMahakamu Kuu na sifa ambazo zinafanana. Wajumbewengine watachaguliwa kwa mujibu wa sheria ambazozimetungwa na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ibara ya 74(3) imetaja watuwafuatao ambao hawataweza kuwa Wajumbe wa Tume yaUchaguzi; imetaja Waziri au Naibu Waziri, Mbunge, Diwani,kiongozi yeyote wa chama cha siasa. Sasa hawawamewekwa kwa mujibu wa Katiba na wamewekwa na sifa.Hapa tumeona wapinzani wakiwasifia Majaji. Mfano, JajiRumanyika wamekuwa wakimsifia, sasa wangewekwa sifasawa na walizochaguliwa Wakurugenzi hawa sio wangesemamakada wa CCM au wanataka watumie mfumo ganikuwapata? Wangesema waje humu tuwapigie kura si badotungewachagua hao hao wa CCM maana yake Wabungewa CCM ni wengi.

MHE. ANTHONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, wanataka wajumbe wa namna ganiwachaguliwe kuwa…

MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa

MHE. ANTHONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa mzungumzaji anayeendeleakuzungumza. Tunavyosema Tume Huru ya Uchaguzi, tunamaana tume ambayo baada ya kuchaguliwa hataangekuwa ni Mheshimiwa Mbowe na Mheshimiwa Zitto ndioMakamishna au ndio Mwenyekiti na sijui nani wa tume kwamuundo uliopo hiyo tume haiwezi kuwa huru kwa sababu

Page 167: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

hiyo ina watumishi wengine wa kuazima kwenye TAMISEMIambao msingi wao wa uteuzi ni makada na ushahidi upo nahawawajibiki kwa tume, wanawajibika kwa wale waliowaajiriambao ni makada vilevile. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlinga unasemajekuhusiana na taarifa hiyo?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, siipokei hiyo taarifa kwa sababu namuheshimunitaendelea. Tume hiyo hiyo ambayo wanailaumuwanasema si huru, katika majimbo 262, mwaka 2015 CCMimechukua majimbo 188, CUF wamechukua majimbo 35,CHADEMA wamechukua majimbo 34, NCCR moja, ACT moja,Mheshimiwa Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa UKAWAamepata kura milioni sita, Mheshimiwa Magufuli amepatakura milioni nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tume hiyo hiyo ambayo siyohuru kuna Wabunge kama Mheshimiwa Halima Mdee ni maraya pili anaingia Bungeni, Mheshimiwa John Mnyika anaingiamara ya pili, Mheshimiwa Sugu anaingia mara ya pili,Mheshimiwa Zitto mara ya tatu tena kabadilisha na majimbobado kashinda, Mheshimiwa Mbowe mara ya pil i,Mheshimiwa Selasini mara…

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, sasa hiyo tume ya namna gani ambayo waowanaitaka, hao watu wangeingiaje

MWENYEKITI: Taarifa

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nataka nimpe taarifa poyoyo kwamba mimi kuingia marambili mara ya kwanza walikufa watu wawili…

Page 168: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sugu, hebu futa hilo nenouliloanza kutumia

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimefuta poyoyo. Mimi kushinda mara ya pili, mara ya kwanzakuna watu walizikwa, vita brother, matairi yamechomwa,watu wamelazwa, watu wamepigwa risasi, watu wamekaahospitali mwaka mzima, unaona wewe. Mara ya pili…

MWENYEKITI: Haya Mheshimiwa Mlinga taarifa hiyounasemaje?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza sishangai kuniita poyoyo kwa sababuumesikia mwenyekiti wake ametetea bangi kwa hiyo sio sualala kushangaa…

MHE. ALLY S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nirudi kwenye mada. Naomba nitoepongezi sana kwa Mheshimiwa…

MHE. ALLY S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nilindie muda wangu.

MHE. ALLY S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa

WABUNGE FULANI: Kaa chini wewe, kaa chini wewe.

MWENYEKITI: Ukiona nimenyamaza nimeikataa,endelea Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Nimeitwa poyoyo japokuwaimefutwa, lakini sishangai kwa sababu umesikia Mwenyekitiwake ametetea bangi kwa hiyo sishangai wafuasi wakekutetea mambo ya kijinga.

Page 169: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kuendelea.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mlinga naomba ukae. Sasanaku-address wewe Mheshimiwa Mlinga. Nakuomba sanaile kauli ya kumuhusisha kiongozi wa Kambi ya UpinzaniBungeni kwamba ameruhusu bangi, naomba uifute tu hiyo,uendelee kuchangia, futa kauli hiyo.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana nafuta hiyo kauli na naendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe pongezi kwaMheshimiwa Waziri…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Manaibu Waziri, KatibuMkuu na viongozi wote wa TAMISEMI…

MWENYEKITI: Nimekataa taarifa please.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa kweli Mheshimiwa Jafo ameitendea hakiWizara hii. Wizara hii ni kubwa sana na ina bajeti kubwa mnolakini ameitendea haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi waUlanga naomba nitoe shukrani kwa mwaka wa fedha uliopitatumepata shil ingi milioni 117 kwa aji l i ya kuboreshamiundombinu ya sekondari ya Celina Kombani tumepata

Page 170: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

milioni 400 kwa ajili ya uboreshaji wa kituo cha afya cha Lupilo,tumepata milioni 214 kwa ajili ya umaliziaji wa maboma,tumepata ujenzi wa shule na madarasa zaidi ya milioni 400.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepata pikipiki 19 na garimoja ya ukaguzi wa elimu, kwa kweli kazi inafanyika. Hatahivyo, nina jambo moja la uboreshaji wa kitengo cha ukaguzi.Wizara hii ni kubwa na bajeti yake ni kubwa ambayoinatolewa lakini bado kuna upungufu kwenye ufuatiliaji wamatumizi ya hizi pesa. Kuna kitengo cha financial trackingcha TAMISEMI, lakini hiko kitengo kinapata bajeti ndogo mno.

Mheshimiwa Mwenyekiti, CAG anakagua kwa mfanoUlanga, tunakaguliwa kila mwaka lakini CAG wanavyokaguawanafanya random sampling yaani kama miradi 10wanakagua miradi mitatu na wanatoa maksi kwa miradi yotekumi. Binafsi kitengo cha financial tracking kilivyokuja Ulangakilikuta madudu sio ya kurudi nyuma. Kwa mfano tulipangamatumizi ya milioni 75 kwa ajili ya posho ya mkurugenzi yasafari lakini mkurugenzi alitumia posho shilingi milioni 192 lakinifinancial tracking ndio waliogundua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wa Ulangawalichukua zaidi ya milioni 760 hawakuzipeleka benki nawalizitumia binafsi. Ilifika kipindi watumishi wanaokusanyapesa wanaziweka kwenye akaunti zao binafsi, lakini Kitengocha Financial Tracking ndio kilichogundua haya. Sasamambo ambayo yalifanyika Ulanga yana-reflect halmashaurinyingine yanavyofanyika. Kwa hiyo nashauri Kitengo chaFinancial Tracking cha TAMISEMI kiwezwe ili kiweze kufanyakazi yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwa Walimu.Nimekuwa msemaji sana wa Walimu. Walimu badowananyanyaswa mno, upandishaji wa madaraja umekuwawa shida, wanapata manyanyaso makubwa kutoka kwaMaafisa Utumishi kwani wamekuwa wazembe katikakufuatilia taarifa za Walimu kwa ajili ya kupandishwamadaraja. Matibabu yamekuwa shida, nilishuhudia kesi mojaMwalimu amesimamishwa kazi kwa kuambiwa mtoro kwa

Page 171: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

sababu aliandikiwa ED na kituo cha afya cha private, lakiniwanasema eti vituo vya afya vya private haviko kwenyestanding order mbona sisi Wabunge tunatibiwa Apollo, Apolloiko kwenye standing order. Kwa mfano Dar es Salaam kunaHospitali ya Hindu Mandal na Mwananyamala, sitojitendeahaki kama nitaenda Mwananyamala nitaacha kwendaHindu Mandal. Mbona NHIF wame-credit hivi vituo vyaprivate, kwa hiyo Walimu wote hawa wananyanyaswa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye posho zaMadiwani. Ukimuuliza Waziri swali hapa Bungeni atakwambiaMadiwani walipwe posho kulingana na uwezo wahalmashauri lakini kila kukicha TAMISEMI wanatoa waraka...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mlinga kwamchango wako.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, Mwongozo.

MWENYEKITI: Hapana nimeshakataa hayo,tunaendelea.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, Mwongozo kuna jambo limetokea hapa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kabla sijaanza kuchangia kwanza niweke rekodimaana naona Wabunge wa CCM wakisimama wanaanzakufanya reference kwa chaguzi ambazo zilifanyika 2015

Page 172: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

kurudi nyuma. Tuingize kwenye rekodi tu kwamba Maraiswaliotangulia hawakuwahi kutamka bayana kwambaWakurugenzi Watendaji ambao wameteuliwa na yeyewasipomtangaza mtu wa CCM watakuwa hawana kazi,hawajawahi kutamka bayana, lakini Rais Mheshimiwa Dkt.Magufuli ametamka bayana na amenukuliwa na vyombovyote. Kwa hiyo tukisimama hapa tukiongea inabidi wakaewakemee, vinginevyo wataingiza nchi kwenye machafuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niingize kwenye rekodikwamba Makatibu Mezani mnapunja sana muda waupinzani. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Kweli hiyoo, kweli hiyoo.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti waChama ameongea chini ya dakika saba na hajawainterrupted, sisi tulikuwa tunamrekodi hapa tunaomba muwefare kabisa maana yake wote tuna-deserve muda wakuongea hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie hoja hiiambayo ni muhimu sana kwenye mustakabali wa nchi yetu.Tumekuwa…

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NAUWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena kwamujibu wa…

MWENYEKITI: Ni kuhusu utaratibu.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,umemkatalia Chief Whip hapa..

MWENYEKITI: Kwa mujibu wa kanuni ganiMheshimiwa?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena nirudie kwa mujibuwa kanuni ya 64 kwamba Mbunge hatatoa maneno ya

Page 173: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

uwongo katika Bunge. Ninalotaka kusema ni kwambanamwomba mchangiaji aliyekuwa anakaa sasa hivi kwasababu anamzungumzia Mheshimiwa Rais ambayetunaamini kwamba anaamini katika uchaguzi na kwamaneno hayo aliyozungumza yaingie kwenye rekodi,ningeshauri yasiingie kwenye rekodi wakati yeye hajaletauthibitisho wa hayo maneno aliyozungumza Mheshimiwa Rais.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko, endeleakuchangia. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Tumekuwa tukishuhudia Mawaziriwanakuja wanaeleza wananchi kwamba uchumi wetuunakuwa kwa asilimia saba, yaani tumekuwa tukielezauchumi wa nchi unakuwa kinadharia zaidi kuliko kiuhalisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona kabisa taarifa yaShirika la Fedha Duniani imesema bayana kwamba uchumiwetu unakuwa kwa asilimia nne. Uchumi kukua tunaupimavipi, moja ya kigezo ni kuangalia pia na kiwango cha umaskinicha watu wetu wananchi. Ukiangalia kiwango cha wananchiwa Tanzania awamu hii…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko, wewe ni Mbungemzoefu sana ili ujenge hoja yako vizuri kuhusiana na ukuajiwa uchumi wa Tanzania kile kinachodaiwa na IMF ungelikuwanacho hapa, unasema hiki hapa nakiweka hapaunaendelea kuchangia.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba ulinde muda wangu ukitaka document…

MWENYEKITI: Narudia kama unayo just lay on thetable, unaendelea kuchangia

Page 174: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, I willlay it on the table right, I don’t have it now, but I will do that.

MWENYEKITI: Very good, ahsante.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ukuaji wa uchumi unapimwa pia kwa kuangalia umaskini wawananchi wetu. Ukiangalia Serikali ya Awamu ya Tanopamoja na kwamba sikatai lakini imejiegemeza sana kwenyemaendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu.Ukiangalia hata kwenye mpango hapa wameainishabayana kabisa kwamba ili kuweza kufikia uchumi wa katikichwa chao mojawapo watawekezwa kwenye maendeleoya watu. Maendeleo ya watu namaanisha elimu, afya, maji,kuhakikisha wanawawezesha wananchi wao kiuchumikupitia uwekezaji na vitu vingine lakini ukiangalia kiuhalisiaSerikali inafanya kwa kiwango kidogo sana katika kuhakikishakwamba inaweka maendeleo kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kwenye elimu,tumeshuhudia elimu yetu ambayo mmesema mnatoa elimubure…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Nimeshakataa taarifa Waheshimiwa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,tumeshuhudia kwamba tumeendelea kuona watoto wetuwanasoma kwa kurundikana wanafunzi 200 wenginewanasoma kwenye miti. Tumeendelea kuona Walimu wakiwawana-work load kubwa kinyume kabisa na uwiano wamwanafunzi kwa Mwalimu. Tumeendelea kushuhudia ajirahazitolewi kwa Walimu. Tumeona juzi wametangaza ajira4,000 tu lakini watanzania zaidi ya 91,300 wame-apply kwaajira 4,000 tu ambazo zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia, ningeombakuweka kwenye kumbukumbu, Mheshimiwa Waziri alivyoletataarifa hapa angetuambia upungufu wa Walimu ni kiasi gani,

Page 175: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

lakini ameonyesha tu kwamba Walimu waliopo mwaka janatumeajiri kiasi fulani, sasa hivi tunategemea kuajiri kiasi fulani.Tusipowekeza kwenye elimu, Taifa ambalo haliwekezi kwenyeelimu kamwe halitakaa liendelee. Haya mambotunayoyajenga sijui Stieglers Gorge, SGR, nimeenda juzi paleKinyerezi naambiwa hata wale wanaokuja kufanyamaintenance pale inabidi watoke nje kuja kufanyamaintenance ya vifaa vile vya Kinyerezi, ina maanavikiharibika mitambo mingine ibebwe ipelekwe nje hii yote nikazi, inabidi tuwekeze kwa watu wetu ili waweze kuja kuwawanahudumia hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia statistically kwaTarime tu mwaka jana nikiwa gerezani niliona watotowaliofaulu kwenda form one wengi wameachwa. Nilitarajiakuona Serikali ingewekeza kuhakikisha kwamba inamaliziamaboma yote ambayo yamejengwa na wananchi. Kwamfano Tarime wananchi walijitolea wakajenga maboma 40kwa shule za sekondari na tukaandika kuja wizarani ili tuwezekupata fedha, hatukuweza kupata fedha za kumaliziamaboma 40.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika halmashauri za Mkoawa Mara Tarime Mji na Bunda Mji ambapo mapato yetu nimadogo sana hatukuweza kupata hata senti tano yakumalizia maboma ili watoto wetu waweze kwendasekondari na waweze kusoma. Kwa hiyo utanona kwambakipaumbele cha Serikali ni kuwekeza kwenye vitu badala yakwenye maendeleo ya watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pia kwenye afyani the same hata kama tumejenga vituo mia tatu na kitu.Nashukuru Nkende nimepata kituo kimoja, lakini bado tatizohalimaliziki, tunahitaji kuenga vituo vya afya, tunahitajimahospitali yawe na dawa, vitendanishi na wataalam, waajiriMadaktari wa kutosha, tunahitaji kuona kwamba Mtanzaniamfanyabiashara, mkulima wanakuwa na afya bora kuwezakufanya maendeleo.

Page 176: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kusema tukwamba kwa Tarime Mji ile hospitali tunahudumia Rorya,Serengeti na wengine, lakini mnatupa fedha za basket fundkama vile ni watu wa Tarime Mji, watu 78,000. Tunaombamkiwa mnatoa fedha muweze ku-consider kwamba tunawork load kubwa. Vilevile Daktari wa Kinywa na Meno waTarime alifariki lakini mpaka sasa hivi hatujapatareplacement, wananchi wetu wanahangaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie vitambulishovya wajasiriamali, wamevizungumzia pamoja na kwambavimeathiri ushuru kwa maana ya kwa halmashauri zetumapato yanapungua, lakini nataka nijue zaidi. Hivivitambulisho tunaambiwa kwamba vimetengenezwa Ikulu,vimetengenezwa na Rais, nataka nijue vitambulisho hivivimetengenezwa kutoka fungu gani, maana yake sinakumbukumbu kama tulishawahi kupitisha fungu hapa kwaajili ya kwenda kutengeneza hivyo vitambulisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia je, hivi vitambulishovimefuata Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na.7 ya mwaka 2011na 2016? Je, walishindanisha tenda? Mzabuni ni nanialiyeshinda kutengeneza hivi maana yake mwisho wa sikuatakuja atapita CAG, halafu itakuja Audit quarries tujue.Mbaya zaidi hivi vitambulisho ambavyo wanasema laki sitawanaovitoa ni Ma-DC ambao sio Maafisa Masuuli. Kwa hiyo,hii inaacha maswali mengi sana na wananchi wanasemabadala ya Chama cha Mapinduzi kupeleka zile milioni 50kama walivyoahidi kwa kila kijiji, ila sasa wameenda tenakuwakata wale maskini elfu 20 kujaza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua, je, hivivitambulisho ni chaka ambalo linakusanya fedha kwa ajili yauchaguzi mkuu ujao au ni nini? Tunaomba watuondoe huowasiwasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Tarime ni Mji ambaounakua, tunahitaji taa za barabarani, hata Mheshimiwa Raisalivyopita alisema mji ule unakua. Kama ambavyowameweka Lamadi, tunaomba na Tarime nako waweze

Page 177: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

kutuwekea taa za barabarani. Uteuzi wa Wakurugenzitumeukemea hapa na tutaendelea kuukemea kwa mujibuwa sheria inatakiwa angalau Mkurugenzi anayeteuliwa aweametumikia kwenye utumishi wa umma angalau miakamitano, lakini tumeshuhudia wakurugenzi wanaoteuliwa nimakada. Mfano wa juzi tu wa somebody Mhagama, alikuwani Katibu wa CCM kateuliwa kuwa Mkurugenzi, wanaziuahalmashauri zetu kuleta watu ambao hawana, lazimatufanye succession plan kwenye halmashauri zetu. Wateuema-DC ambao ni makada wao lakini kwenye kada yaUkurugenzi, wazingatie sheria. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Matiko, mudawetu ndio huo.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mwongozo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu.

MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima na taadhima nitumie fursa hii kukushukuru wewebinafsi na Bunge lako tukufu kwa kunipa nafasi ya mimi kutoamchango katika ofisi ya Rais TAMISEMI na Utumishi na UtawalaBora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa mimi binafsinaomba ku-declare kwamba Mheshimiwa Freeman Mbowenamuheshimu sana kama kiongozi wa Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kwa sababu ni mtu makini nina imani. Hatahivyo, kuna vitu ambavyo kaka yangu Mheshimiwa Mboweamevizungumza naomba nivitolee ufafanuzi kidogo sanahasa katika suala zima la ulinzi wa Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ulinzi wa Rais,naomba nieleweke, kwa namna ambavyo Rais wetuamechukua maamuzi katika masuala mazima ya uchumi wanchi, usalama wa Rais wetu lazima utakuwa kwenye mashakamakubwa kwa sababu ya maamuzi Rais wetu aliyoyachukua.Wewe ni shahidi, Bunge lililopita Mheshimiwa Zitto Kabwe na

Page 178: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

timu yake walileta hoja hapa kuna watu walipiga fedhakatika masuala ya ESCROW, Mheshimiwa Rais Magufuliameingia madarakani, watuhumiwa wote waliokuwawamefanya ubadhirifu kwenye mambo ya ESCROW,amewakamata, sasa wako magerezani. Kwa kiwango chafedha zilizokuwa zimeliwa, Rais amekamata watu hawamnataka kuniambia hawa ma-Taikun hawana watuwanaoweza wakaleta insecurity kwa usalama wa Rais?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema Serikaliinatekeleza miradi ambayo Wazungu wanaipiga vita,Stiegler’s George, tunakwenda kuzalisha MW2400 za umeme,Wazungu wanapiga vita, Rais kwa ujasiri anatekeleza hilo.Hizi ni ahadi zilifanywa na Baba wa Taifa Hayati MwalimuJulius Kambarage Nyerere, jasiri na jemedari Rais wa Awamuya Tano anayetokana na Chama cha Mapinduzi ameingiamadarakani, hajaangalia Wazungu ameangalia maslahi yanchi, Stiegler’s George inajengwa, mnafikiri Wazunguwanafurahi? Mnafikiri usalama wa Rais utakuwa sawasawa?Leo tunavyozungumza Rais anajenga Standard Gauge,mnafikiri mataifa ya Ulaya wanapenda? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe taarifa, ulinziwa Rais tena uongezwe mara dufu kwa sababu usalama waRais wetu kwa mambo anayoyafanya kwa maslahi ya Taifahili hatuwezi kuacha usalama wa Rais ukawa katika stakekwa sababu tunaogopa kupiga makofi, Wazungu walikuwawanataka wavae vichupi wakapige picha kwenye Stiegler’sGeorge kule Ruvu, haiwezekani. Tunaomba Wabunge waChama cha Mapinduzi na sisi ndiyo majority, ndiyo sauti yanchi humu Bungeni, ulinzi wa Rais wetu ikiwezekanauongezwe hata mara kumi zaidi kwa sababu usalama wakehauko sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nalotakakulizungumza ni suala la utawala bora. Mwaka mmoja baadaya kuingia hapa Bungeni tuliona Taifa letu lilivyojaribiwa nahapa mimi nazungumza kwa sababu toka nimemalizakusoma chuo kikuu sijawahi kufanya kazi mahali popote zaidi

Page 179: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

ya kuitumikia Serikali hii. Tumeingia Bungeni hapa kunamambo mengine Serikali haiwezi kuya-disclose kwa sababuya siri za nchi, Mataifa ya Ulaya kwa kushirikiana na watundani ya nchi mmeona kilichokuwa kinatokea kule Rufiji, watuwameuawa Kibiti, ili Taifa kudhihirisha kwamba lina utawalabora, dola ya Tanzania imekwenda kudhibiti upumbavuuliokuwa unafanyika pale Kibiti na nchi imetulia. Natakaniseme katika suala la utawala bora hakuna mahali ambapotunaweza tukapigia kelele utawala bora, tunafanya vurugu,tuache Taifa letu liwe torn apart, never shall we allow this.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudi kwenye michango,moja ya vitu pia ambavyo tunaweza tukavizungumza katikautawala bora ni equal distribution of national cake.Nampongeza sana Mkurugenzi wa TARURA na timu yake naMheshimiwa Jafo na timu yake na Mzee wetu MheshimiwaMkuchika, toka nimeingia madarakani fedha zilizoletwa naSerikali ya Chama cha Mapinduzi kuwasaidia wapigakurawanyonge, walipa kodi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, tumeletewa fedha shilingi bilioni 1.3 na tumejengamadaraja; tumeletewa fedha za vituo vya afya Sepuka,Ihanja na sasa hivi tuna kituo cha afya kule Iyumbu, yote hayani mambo ya utawala bora. Zaidi ya hapo, hata kwa Jimbojirani la kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu ambayeamepata matatizo, hapa napozungumza Serikali ya CCM bilakujali hayupo na anaumwa, zimepelekwa fedha vijiji 19 watuwake wanachimbiwa maji. Leo mnataka kusema nini hapa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Mheshimiwa EstherMatiko anazungumza hapa, Serikali ya CCM hapanapozungumza imemjengea Kituo cha Afya cha Mkendekwa shilingi milioni 400. Hapa tunapozungumza Serikaliimemtengea shilingi bilioni 8 kumjengea soko la kisasa palekwake Tarime. Hapa tunapozungumza boma lake laHalmashauri amepelekewa shilingi bilioni 2 na shilingi milioni500 zimeshakwenda. Msije hapa kuwadanganyaWatanzania, msije hapa kuudanganya umma, sisitunachokisema Serikali ya Chama cha Mapinduzi, chini yaDkt. John Joseph Magufuli inafanya kazi. Nataka niwaambie,

Page 180: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

mimi kwenye Jimbo langu Rais alipata asilimia 73 ya kura yauchaguzi uliopita lakini kwa kazi hizi 2020, Rais anakwendakuchukua zaidi ya asilimia 95 ya kura. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba nitoe raikwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi…

KUHUSU UTARATIBU

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu subiri kidogo, Kanunigani?

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kanuni ya 64(1)(a). Sisi Wabunge ni taxpayer representatives,tuko hapa kuidhibiti Serikali namna ya kutumia fedha lakiniMbunge anayechangia sasa hivi anaharibu kwa kuonyeshakana kwamba Serikali inapoleta fedha ni fadhila kwawananchi. Kwa kusema hivyo tunali-lower Bunge, inaonekanakama Bunge tunapewa fadhila na Serikali. Hii ni kupotoshaumma na kuharibu utaratibu wa utendaji kazi wa Bunge.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba umwelekeze ajuekazi ya Bunge ni nini maana kuletewa fedha na Serikali nikama vile Serikali inatusaidia. Sisi Wabunge tumekuja hapakusimamia kodi ya wananchi na kodi hiyo ndiyo inaletamaendeleo. Sasa anaposifu tumeletewa, tumeletewa naWabunge wote hata nakotoka mimi kuna watu wanalipakodi, mimi fedha hizi sipewi bure. Sasa hebu tukuze kiwangocha Bunge, tunali-lower Bunge, tunatia aibu kwa watu,hatuonyeshi kama tumekuja kufanya kazi ya Bunge hapa.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, nadhani ulitakakuchangia tu lakini Mheshimiwa Kingu anatukumbusha sisikama Wabunge yale ambayo yanafanywa na Serikali kupitiabajeti hii bila kujali kama wewe unatoka upinzani au hautoki

Page 181: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

upinzani. Serikali inatenda haki kusukuma maendeleo kwawananchi wake wote na ndiyo hoja yake hiyo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, mnaona, nakataa sanataarifa hizi kwa sababu itapendeza zaidi kama tutatumia vizurimuda wetu kwa kujenga hoja kama anavyofanyaMheshimiwa sasa na kama alivyofanya Mheshimwa Mbowe.Huko ndiyo kujenga hoja. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Sisi mnatubana muda.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, wote hapatumeangalia muda.

MBUNGE FULANI: Na sisi tunarekodi hii hapa.

MWENYEKITI: That’s not official. (Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, please, hawa ni makinisana, nimeona hata mimi hapa.

WABUNGE FULANI: Hakuna, siyo kweli.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwakajoka liache hilolakini nawaomba sana sisi Wabunge tufahamu kwambatunajenga nyumba moja. Mheshimiwa Kingu endelea.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakuomba unilindie muda wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa nasema sinamaana kazi yangu hapa ni kuja kusifu tu lakini upotoshwajiunaofanywa juu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama chaMapinduzi, nikiwa kama Mbunge nayetokana na chama hikilazima tuje hapa Bungeni tuweze kufafanua ili dunia naWatanzania waweze kujua ni kweli chama chetu na Serikaliyetu inatekeleza au haitekelezi. Ndiyo maana nimetoamfano, Jimboni kwa kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissualiyepata matatizo, hayupo hapa Bungeni lakini Serikali yaChama cha Mapinduzi imepeleka miradi ya maji katika vijiji

Page 182: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

21 na hapa tunapozungumza miradi ya maji inaendeleakutekelezwa. Nimesema miongoni mwa mambo ambayoyanaweza yakaingia katika components za goodgovernance ni pamoja equal distribution of resources nanational cake na ndivyo Serikali ya Chama cha Mapindiziinavyofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka nimalize kwakusema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana, muda wako umekwisha.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja, kidumu Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kanuni ya 68, kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Tunaendelea.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu utaratibu, Kanuni ya 68(1), tafadhali.

MWENYEKITI: Kanuni ya 28?

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti,Kanuni ya 68(1) na Kanuni iliyovunjwa ni ya 62(1)(a). Kanuniinasema: “Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo kwenyeKanuni hizi, kila Mbunge anayejadili hoja, ataruhusiwa kusemahivyo kwa muda usiozidi dakika 15”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ilitolewa hoja wakatitunaanza Bunge kwamba dakika zile 15 tuchangie kwadakika 10. Sasa imekuwa trend ya watu wanaokaa hapo

Page 183: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

kupunja muda wa Wabunge wa Upinzani wanapochangia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki kitu kinaleta ubaguzi wahali ya juu na kutufanya sisi tu-feel kama second class. Kwasababu hapa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbowe wakatianazungumza ametumia dakika 6.47, this is very unfair. Hatakama wakitaka kuthibitisha wenyewe na mimi nimerekodihapa, unless mseme muda wetu ni tofauti na wa watuwengine wanaozungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tutendeane hakikama Wabunge tulioletwa na wananchi. Tunajisikia vibayasana mnavyotufanyia hapo, tafadhali sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuatautaratibu)

MWENYEKITI: Tutafika vizuri tu, nikuongoze tu kwenyeKanuni husika. Tuko kwenye Bunge la Bajeti, hoja yakotunahitimisha kama navyotaka kusema mimi sasa hivi lakinimlango wa kuingilia siyo ule uliotumia wewe. Mlangouliopaswa kutumia kufikia hapo hapo ni Kanuni ya 99(12), iliwote tufahamu namna ya kutumia kanuni hizi.

Waheshimiwa Wabunge, kuhusu suala la kuminyamuda, mimi nasema hivi, Makatibu hawa ni watumishi waBunge na hawategemewi kwamba watakuwa wanaminyamuda kwa sababu huyu ni Mbunge wa CCM, CHADEMA auCUF, hapana. Kwa hiyo, naomba sana WaheshimiwaWabunge, hiyo ni kauli nzito sana ya kubagua Wabunge,hakuna second class Mbunge humu, twende vizuri tu. Hapatunalinda muda wenu na ndiyo maana mimi huwa nasemanakulindia muda wako kama nimeku-interrupt.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naMheshimiwa Joseph Mkundi atafuatiwa na MheshimiwaDaimu Mpakate na Mheshimiwa Aron Njeza ajiandae.

Page 184: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa fursa hii ya kuchangia. Kwanzanimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii yauhai na kuweza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu lakininikushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwa sababu ni bajetiyangu ya kwanza nikiwa upande huu lakini hasa kwa sababuni bajeti ya kwanza tokea limetokea tukio baya sana lakuzama kwa kivuko cha MV Nyerere, nitumie nafasi hiikumwomba Mwenyezi Mungu ampumzishe roho zamarehemu wote 228 waliopoteza maisha kwenye ajali ile.Tatu, nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa RaisDkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa sana anayoifanyakuliongoza Taifa hili na kuwaletea maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze MheshimiwaWaziri Jafo na wasaidizi wake na Mheshimiwa Mkuchika nawasaidizi wake wote. Hakika wanafanya kazi kubwa sana,wanatendea haki Wizara zao na wanawatendea hakiwananchi wa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu utakuwakwenye maeneo mawili. La kwanza niombe tutambuekwamba tunaweza kwenda kasi sana kwa maendeleo katikanchi hii kama tutakuwa na Serikali za Mitaa zilizo imara.Kimsingi tunaposema uimara wa Serikali za Mitaa ni kwasababu huduma zote za kijamii ziko chini ya Serikali za Mitaa.Kwa hiyo, kama tutaimarisha Serikali za Mitaa, kasi yamaendeleo kama inavyokwenda sasa itakuwa nzuri naitawagusa zaidi wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa mpaka sasamambo yanaenda vizuri, naipongeza Serikali kwa kazi kubwasana wanayoifanya kwa mfano Ukerewe kwenye eneo laafya kazi kubwa sana imefanyika, vituo viwili vimepata pesa,vinakamilika. Nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri waTAMISEMI lakini nimpongeze zaidi Mheshimiwa Rais kwasababu baada ya matatizo yale alielekeza pesa zijenge Kituocha Afya cha Bwisya, kituo kinaelekea kukamilika na

Page 185: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

naipongeza sana Serikali kwa uamuzi huu. Tatizo kubwaambalo napenda Serikali itambue, ujenzi wa vituo hivi vyaafya iende sambamba na upatikanaji wa watumishi ili viwena tija, visikamilike halafu vikashindwa kutoa huduma ileiliyokuwa inatarajiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la elimu kazikubwa sana imefanyika kupitia elimu bila malipo, watotowengi sana wameweza kusajiliwa kwenye shule zetu zamsingi. Kusajiliwa kwa watoto wengi kumeenda sambambana upungufu wa miundombinu kama madarasa. Niipongezesana Serikali hivi karibuni imejitahidi kuleta pesa kwa ajili yakuboresha miundombinu na kwenye eneo letu la Ukerewekupitia Mfuko wa Jimbo lakini pamoja na wananchi,niwapongeze sana wananchi wa Visiwa vya Ukerewe,tumehamasishana tumejenga maboma zaidi ya 300 kwa ajiliya madarasa, niombe Serikali sasa itusaidie kuezekamadarasa haya. Kwa sababu wananchi wamejitoa sana naMbunge wao nimejitoa, nimepeleka mifuko zaidi ya 3,000kwenye shule zetu mbalimbali, basi Serikali itusaidie tuwezekuezeka maboma haya ili angalau watoto wetu wapatemadarasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri kwenye utekelezaji nimeona kuna wazeezaidi ya 700,000 wametambuliwa lakini katika wazee hao niasilimia 33 tu ya wazee hawa ndiyo waliopata vitambulishoili waweze kupata huduma ya afya. Kuna tatizo kubwa sanahuko chini, wazee wetu wananyanyasika sanawanapokwenda kupata huduma za afya. Niombe Wizara yaTAMISEMI iweke ukomo wa muda ili Halmashauri zetu ziwezekuwatambua wazee hawa na kupata vitambulisho ili wapatehuduma za afya kuliko kuendelea kunyanyasika kamaambavyo imekuwa inatokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende eneo la TARURA,wamesema Wabunge wengi sana, niwapongeze TARURAlakini nampongeza sana Mtendaji Mkuu wa TARURAamekuwa msikivu pamoja na changamoto mbalimbalianazokabiliana nazo. Kwa kazi kubwa wanazozifanya TARURA

Page 186: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

tukizingatia kwamba wana mtandao mkubwa sana wabarabara kilomita zaidi ya 100,000 ni nyingi sana lakini kwafedha wanazozipata tutaendelea kulalamika. Kwa hiyo,niombe katika bajeti tunayoendelea nayo Serikali iletependekezo tuweze kubadili fomula ya ugawaji wa pesa hiziili TARURA angalau waweze kupata asilima 40 au asilimia 50tuweze kuwapa uwezo washughulikie barabara zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipoanza kuzungumzanilisema juu ya umuhimu wa kuimarisha Serikali za Mitaa nahasa Halmashauri zetu kwa sababu ndipo sehemu ambapomiradi mingi inayowagusa wananchi inasimamiwa.Tunapoongelea Serikali za Mitaa hasa Halmashauritunaongelea Madiwani na watumishi. Kuna changamotokubwa katika suala zima la posho kwa ajili ya Madiwani wetu.Hili ni tatizo kubwa sana ambalo linaathiri utendaji waMadiwani wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni umetolewamwongozo juu ya posho za Madiwani katika vikao vyetu vyaHalmashauri. Madiwani hawa wanafanya kazi kubwa sanalakini wanapokwenda kuhudhuria vikao wanalipwa Sh.40,000ni fedha ndogo sana. Kwa hiyo, niombe TAMISEMI muangalieupya suala hili ili angalau kuweza kuwajengea kujiaminiMadiwani hawa ambao wanafanya kazi kubwa sana yakusimamia miradi yetu kule chini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la Wenyeviti waVijiji na Vitongoji, hawa ni watu muhimu sana lakini malipowanayopata; posho zao za kila mwezi lakini hata baada yakutoka kwenye nafasi zao wanazotumikia ni kitu ganiwanakipata? Nashauri TAMISEMI aingalie eneo hili pamojana kwamba inawezekana wakawa wengi sana Serikaliisiweze kuwalipa wote lakini tuangalie kama inawezekanabaada ya kipindi chao cha utumishi kuwe na package fulaniambayo wanaweza kuipata ili wawe na moyo wa kuendeleakufanya kazi na kusimamia maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano Ukerewe, Mwenyekitiwa Kitongoji analipwa Sh.3,000 kwa mwezi. Tafsiri yake ni nini?

Page 187: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Tafsiri yake ni kwamba kwa siku analipwa Sh.100 kwa ajili yakusimamia shughuli za maendeleo, inawavunja moyo. Kwahiyo, niombe Serikali iliangalie sana suala hili.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na MheshimiwaMpakate, muda wetu si rafiki.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia jioni ya leo. Kwanzanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uwezo wakusimama mbele ya Bunge lako Tukufu. Nitaenda moja kwamoja kwenye hoja ya msingi. Kwanza napenda kuungamkono kwa asilimia mia moja hoja zote mbili na nitaanziakwenye TAMISEMI kwa upande wa vituo vya afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali yetu kwakutupatia Jimbo letu la Tunduru Kusini vituo viwili vya afyaambavyo vimejengwa pale Mchoteka na kinginekimejengwa Rukasale. Nasikitika kwa kile kituo cha kwanzacha Rukasale kama Mheshimiwa Waziri alikuwa hana taarifa,bado hakijakamilika mpaka leo kutokana na matumizimabaya ya fedha yaliyotokana na usimamizi mbovu waWatendaji wetu. Hii imetokana na kwamba Halmashauri yaTunduru haina mhandisi ambaye angeweza kusimamia vizurikatika ujenzi wa zile zahanati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukurani hizo,Jimbo la Tunduru Kusini lina Kata 15 na katika Kata 15 tunavituo vya afya vitatu tu na tuna ahadi ya muda mrefu yaKituo cha Afya Narasi iliyotokana na Rais wa Awamu ya Nneambaye aliahidi kujenga kituo cha afya katika eneo lile.Nimeleta swali hili mara tatu katika Bunge lako Tukufu,

Page 188: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

nimeahidiwa kupewa pesa lakini hadi leo kile kituo badohakijajengwa na watu zaidi ya 30,000 wako katika Kata zilembili ambazo zinakitegemea sana na wapo mbali zaidi yakilometa 70 kutoka Mjini Tunduru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kuchangia katika hilo hilo, kulikuwa na ahadi vilevile ya Rais wa Awamu ya Nne ya kutoa gari kwa ajili ya Kituocha Afya Mchoteka. Jambo hili bado nalo ni tatizo naHalmashauri yetu ina gari chakavu, ukizingatia kwambaHamashauri ya Wilaya ya Tunduru ina eneo kubwa sana kulikohata Mkoa wa Mtwara kwa ujumla wake. Kwa hiyo, tunagari bovu la miaka ya 1980 mpaka leo hii, hatuna gari yoyoteambayo inaweza kusaidia wagonjwa wetu kutoka katikasehemu moja kwenda sehemu ya pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalonapenda kuzungumzia ni suala la elimu. Katika suala la elimutuishukuru Serikali kwa kutoa elimu ya msingi bila malipo, lakinikuna changamoto kubwa ambayo imejitokeza katikamaeneo yetu hasa katika Jimbo la Tunduru Kusini kwambawatoto wamekuwa wengi, madarasa yamekuwa kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii imesababisha watotowengi kusoma katika darasa moja zaidi ya 100 mpaka 200.Nikichukua mfano katika Shule ya Msingi Tuwe Macho inazaidi ya watoto 800; Shule ya Msingi Semeni ina zaidi yawatoto 900; Shule ya Msingi Mtina ina watoto zaidi ya 1,000,lakini madarasa yaliyokuwepo hayazidi saba au matano.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba katikamiundombinu ya shule za msingi iongezwe bajeti ili kuhakikishakwamba majengo yanajengwa ili watoto wale wawezekusoma katika mazingira mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kulizungumzia ni suala la watumishi. Kwa kweli tatizola watumishi limekuwa ni kubwa sana katika Halmashauri yaWilaya ya Tunduru. Tuna upungufu wa wafanyakazi katika

Page 189: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Sekta ya Afya zaidi ya asilimia 65. Katika Sekta ya Elimu zaidiya asilimia 50.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule nyingi za msingi katikajimbo langu zina walimu ambao hawazidi watano naminimum ni watatu; na shule hizo ziko kuanzia darasa lakwanza mpaka darasa la saba. Kwa kweli kwa walimu waleimekuwa ni mzigo mkubwa sana kufundisha madarasa sabawakiwa walimu watatu, wanne au watano. Naomba sanakwa kuwa tuko ndani ya bajeti tunaomba sana watumishiwa Sekta ya Elimu waongezwe ili kuhakikisha kwambawanaweza kufanya kazi vizuri kwa ajili ya watoto wetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, kunatatizo la walimu waliostaafu katika kipindi hiki ambachokikokotoo kipya kimetengenezwa. Walilipwa kwa hesabu ileya kikokotoo cha zamani. Wamekuja ofisini kwangu marambili mpaka mara tatu, wanasema itakuwaje? Tumelipwakwa kupunjwa na Rais amesema kikokotoo kitumike kile chazamani. Walimu hawa wanaulizia watapewa lini mapunjo yaoili waweze kujikimu katika maisha yao ya kustaafu kama ilivyosasa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kuzungumzia ni suala la Makatibu Tarafa.Naishukuru Serikali katika Jimbo kangu la Tunduru Kusini kunaTarafa tatu, mwaka 2018 tumepata watumishi wote, MaafisaTarafa watatu. Changamoto waliyokuwanayo, hawana ofisikabisa. Ofisi za Maafisa Tarafa hakuna kwenye Tarafa zetu.Halmashauri yote ina ofisi moja tu katika Tarafa saba. Kwahiyo, hawana ofisi, hawana nyumba za kuishi, tunabanananao humo humo kwenye maeneo yetu ambayo tunaishi.Tunaomba sana, mtengeneze angalau bajeti kwa kuwajalihao Maafisa Tarafa ili waweze kupata Ofisi na nyumba zakuishi waweze kufanya kazi vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tano ambalonapenda nizungumzie ni suala la TARURA. Kwa kweli TARURApamoja na kazi nzuri wanayoifanya, tatizo fedha inakuwa ni

Page 190: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

kidogo. Kwenye upande wa Jimbo langu la Tunduru Kusini,kuna barabara zina zaidi ya miaka 10 hazijawahikutengenezwa. Tulitegemea TARURA atakuwa ni mkombozikatika kutengenezea barabara zile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna barabara yaLukumbule – Imani – Kazamoyo, kuna barabara ya Mlingoti –Tuwemacho – Ligoma, kuna barabara ya Chemchemi –Namasakata – Liwanga mpaka Msechela, kuna barabaraya Namasakata – Amani – Msechela, kuna barabara yaNandembo – Mpanji mpaka Njenga, kuna barabara yaMchoteka – Masuguru – Malumba. Barabara hizi zina zaidiya miaka saba hazijafanyiwa kazi yoyote. TARURA kwa kwelikila unapoona hesabu yao, ukiangalia kwa sasa wamepewa1.3 billion na hizi barabara zina zaidi ya kilometa 455. Kwahela ile waliyopewa kwa matengenezo ya kawaida tu kwakweli haitaweza kukidhi haja ya kutengeneza barabara hizi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sanaTARURA waongezewe pesa il i waweze kufanyiamatengenezo barabara zetu ambazo zinatumika kwa ajili yamaendeleo ya wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalonapenda kulizungumza ni suala la mapato ya Halmashaurizetu. Hapa kuna shida, hasa kwenye mikoa ya kusini; mwakajana na mwaka juzi tulikuwa tunaenda vizuri, mapato yetumengi tunapata kutokana na ushuru wa korosho. Bahatimbaya mwaka huu biashara ilivyokwenda, hatukuwezakupata ushuru wa korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali, kwakutambua kwamba walikuwa na mipango na bajeti zao kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ambayo ilikuwepokwenye mahesabu, basi Serikali ifanye huruma kuwasaidiaangalau ruzuku Halmashauri zile ziweze kukidhi haja yakuweza kutekeleza ile miradi ambayo ilikuwa imepangwamwaka 2018/2019. (Makofi)

Page 191: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Oran Njeza.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa hii nafasi ili nami niwezekuchangia bajeti ya Wizara hizi muhimu, bajeti ya TAMISEMIna bajeti ya Utumishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwakuwapongeza Mawaziri wote wawili pamoja na team zotembili, kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana. Wanafanya kazinzuri na kwa ushahidi kabisa, kwenye Jimbo langu TAMISEMIwamefanya kazi nzuri sana katika eneo la TARURA, eneo laAfya na eneo la Elimu. Kwa kweli nawapongeza sana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda vilevilekumpongeza Mheshimiwa Rais naye kwa kazi nzuri iliyotukuka.Amefanya mageuzi makubwa ya nchi hii, amefanyamakubwa mno. Ushahidi ni mkubwa pamoja na miradi yakimkakati kwenye Jimbo langu, ni mambo mengi ambayoameyafanya na haijawahi kutokea toka enzi za ukoloni.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa suala la TARURA.TARURA chombo chenyewe ni kizuri sana, lakini kuna tatizokubwa kwamba TARURA haina pesa kabisa. Kwenye Jimbolangu nina mtandao wa barabara usiopungua 1,000. Bajetitumepewa shilingi bilioni 1.5 ambazo ni kilometa 35 kamasikosei. Kuna madaraja chungu nzima, hayapungui 200.Utamaliza miaka mingapi kukamilisha hiyo kazi? (Makofi)

Page 192: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri tungeenda kiuchumizaidi, tuangalie ni namna gani haya maeneo ambayo nimuhimu yapewe kipaumbele. Unapozungumzia MbeyaVijijini, unazungumzia kilimo cha nchi hii. Mazao yanatokakwenye mashamba, lakini hatuna barabara kabisa. Mazaohayawezi kutoka shambani kuja sokoni na vile vile hatuwezikupeleka pembejeo kwa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyozungumza hivi leo,barabara ya kuanzia Songwe Viwandani kwenda Jojohaipitiki kwa vile daraja lilikuwa limeshabomoka. Daraja hilomoja linahitaji zaidi ya shilingi milioni 250. Leo ni mwaka watatu wananchi wanasumbuka daraja halijajengwa. Pamojana maombi maalum, inavyoelekea, tatizo katika bajeti,tuangalie ni namna gani TARURA waongezewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna barabara nyingine yakuanzia Kawetere kwenda Ikukwa, barabara ya Irambo kujaIhango mpaka Nsonyanga, barabara za Mbonile mpakaNyarwerwa. Tuna barabara nyingi mno ambazo ni muhimuna za kiuchumi lakini hazimo kabisa hata kwenye mpangowa bajeti. Kama nilivyosema, kwa bajeti ya shilingi bilioni 1.5utafanya nini kwenye mtandao kilometa 1,000?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sana Serikali ijaribukuangalia ni namna gani itatunusuru kwenye barabara? Bilabarabara hakuna kilimo, bila barabara hakuna elimu, bilabarabara hakuna hata shughuli za afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalonapenda kuchangia kidogo katika Wizara hizi mbili ni sualala afya. Napenda kwanza kumpongeza Mheshimiwa Rais naWaziri Mheshimiwa Jafo, wamefanya kazi kubwa mno.Halmashauri ya Mbeya tulikuwa hatuna Hospitali ya Wilaya,tulikuwa hatuna vituo vya afya vya kutosha, lakiniwametupatia vituo vya afya vitatu; Kituo cha Afya chaIkukwa, Kituo cha Afya cha Ilembo na Kituo cha Afya chaSantiria. Vituo hivi vimebadilisha kabisa muundo na hudumaza afya katika Halmashauri yetu.

Page 193: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado tunahitaji mahitajimakubwa zaidi. Wananchi wamejenga zahanati, mabomahayapungui 70 ambayo yanahitaji msukumo na bajeti yaSerikali. Pia kuna vituo vya afya vilivyojengwa kwa nguvu zawananchi; kuna Kituo cha Afya cha Ifupa, wananchiwameshajenga, wametumia karibu shilingi milioni 200. Kwahiyo, tunaomba tu kama shilingi milioni 200 tuweze kumalizia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Kituo cha Afya chaIsuto, nacho kimefikia hatua nzuri, tuna Kituo cha Afya chaIhoho, Kituo cha Afya cha Maendeleo na Kata ya Tembela.Hivi viko katika hatua nzuri. Kama ikiwezekana, tunaiombatena TAMISEMI waangalie ni namna gani kwa upendeleokabisa hivi vituo vipate bajeti ya ku tosha ili tuwezekuvikamilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la elimu, naponapenda kupongeza tu kwa vile tumefanya vizuri, Serikali kwakweli imefanya jitihada na wananchi wenyewe naowamefanya jitihada kiasi cha Halmashauri yangu ya Mbeyakiufaulu tumefanya vizuri sana. Shule zimefanya vizuri nawananchi wameweza kufungua shule tatu ikiwemo moja yahigh school na shule moja ya wasichana ambayo ni ya bweni.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahitaji ni mengi. Sasaukiangalia tuna wanafunzi karibu 70,000, walimu tulionao ni1,035, angalia gap hiyo. Pamoja na jitihada za wazazi, badotunahitaji walimu ili waweze kuinua uchumi wa vijana wetu.Kuna shule ambayo ina mwalimu mmoja, inaitwa Ilindi. Hiishule ina wanafunzi karibu 300, mwalimu mmoja. Kimaajabuile shule imefaulisha watoto na ikapata nafasi nzuri. Kwamshangao wa kila mtu akauliza, itakuwaje shule ya mwalimummoja, madarasa saba ikafaulisha kuliko shule zenye walimuwengi? Tukagundua kumbe hata wazazi nao wanashirikikwenda darasani kufundisha watoto wao. (Makofi)

Page 194: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hali kama hii nafikirisiyo nzuri sana. Ili tuweze kushindana na wenzetu, inabidi elimuyetu nayo iwe nzuri, tufanye vizuri katika elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalonapenda nichangie kidogo, ni suala la uendelezaji wa mijina mipango miji. Kwa sisi ambao tunazunguka majiji, majijisasa hivi yamejaa na watu wengi ujenzi unakuja kwenye vijijivyetu ambavyo havijapimwa. Kwa hiyo, tunaongezasquatters zile ambazo tulizikuta. Sasa hivi squatters zinahamiakwenye Halmashauri ambazo zinaizunguka Jiji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Wizaraijaribu kuangalia iwe na mkakati wa kuhakikisha kuwa vijijivyote ambavyo vinazunguka majiji, vipimwe, viwe katikampangilio mzuri na yale maeneo ambayo yapo mijini kamamaeneo ya Tanganyika Parkers, haya yagawiwe kwawananchi. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Njeza.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Wageni.

Kuna wageni wanne wa Mheshimiwa GoodluckMlinga ambao ni Madaktari na Wauguzi wa Hospitali yaBwagala iliyopo Mvomero Mkoani Morogoro ambao niNdugu Eva Kisimbo, Ndugu Irene Kuhanga, Ndugu MathiasSuhi na Ndugu Slam Mganga.

Katibu wa Bunge anaomba niwatangazieWaheshimiwa Wabunge kuwa kesho tarehe 13 Aprili, 2019kutakuwa na usafiri wa mabasi hapa Bungeni kwa ajili yakuwapeleka Waheshimiwa Wabunge kwenye sherehe zauzinduzi wa Mji wa Serikali huko Mtumba. Mabasi yatakuwa

Page 195: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

katika maeneo ya Bunge na Waheshimiwa Wabunge wotewanaotaka kwenda; na tunaombwa wote twende, muwemmefika hapa Bungeni saa 12.00 asubuhi. (Makofi)

Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO:Mheshimiwa Mwwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa hii fupiniweze kuwataarifu rasmi Waheshimiwa Wabunge kwambaJumapili, tarehe 14 mwezi wa Nne mwaka huu, vijana wetuwa Serengeti Boys, Timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 17wanaingia Uwanja wa Taifa kupambana na wenzao kutokaTaifa la Nigeria. Ni mchezo mkubwa katika historia ya nchihii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nitumie nafasi hiikuwaomba sana Waheshimiwa Wabunge kwa sababu ni sikuya weekend, ingekuwa ni siku ya kazi ningeomba pengineKamati yangu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pengineniiombee kwa Spika, lakini kwa kweli kwa siku ya weekendnaomba tu Waheshimiwa Wabunge wote tuweze kufikauwanjani kuona kiwango cha soka ambacho Tanzaniatumefikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kamanitaweza pengine kupitia kwa Mheshimiwa Ngeleja, star wetuhapa wa michezo Bungeni, kupata majina ya WaheshimiwaWabunge wote ili niweze kuweka utaratibu mzuri waWaheshimiwa Wabunge kuacha magari mjini, nikawatafutiagari au basi la kuwapeleka uwanjani na vile vile kuwarudishaili kuepuka fujo ambazo zinaweza kuwapata maanamsongamano ni mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile naombaniwatangazie kwamba viingilio ni rafiki sana, ni shilingi 2,000kwa viti vya kawaida na shilingi 5,000/= viti vya VIP iliWatanzania wengi waweze kuingia na vile vile watoto wotewa shule ni bure. Watoto wa Shule za Msingi mradiwameongozwa na mwalimu wao, wataingia bure. Watoto

Page 196: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

wa Shule za Sekondari lazima waje na vitambulisho vyao vyashule ili waweze kuingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie kwambaWaheshimiwa Wabunge tuweze kufika kuwasindikiza watotowetu kwa kuwashangalia. Mgeni rasmi atakuwa ni WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaKassim Majaliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mwongozo wa Spika kuhusu hoja yatofauti ya shilingi trilioni 1.5 kati ya mapato ya Serikali namakusanyo na re-allocation ya shilingi bilioni 976.96iliyoibuliwa na Mheshimiwa John J. Mnyika, Mbunge.

Waheshimiwa Wabunge, leo asubuhi katikamajadiliano yetu ya Mkutano huu wa 15 unaoendelea wabajeti wakati wa kujadili hoja ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais(TAMISEMI) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi naUtawala Bora). Mheshimiwa Mnyika, Mbunge, alipata nafasiya kuchangia, katika mchango wake, pamoja na mambomengine, alizungumzia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali CAG, ya mwaka 2016/2017, kuhusu hojaya tofauti ya shilingi trilioni 1.5 kati ya mapato ya Serikali namakusanyo yake.

Katika mchango wake, alieleza ifuatavyo, nanukuu;“Ripoti ya mwaka uliopita iliibua suala la 1.5 trillion ambayobaadaye ilipanda mpaka kuwa 2.5 trillion. Katika ufafanuziwa Serikali juu ya trilioni 1.5, kuna taarifa zilitolewa toka trilioni1.5 mpaka tri l ioni 2.4, kwamba shil ingi bil ioni 976.96zilihamishwa kwenye mafungu mbalimbali zikapelekwa ku…kwa maana ya bajeti reallocation.” Mwisho wa kunukuu.

Aliendelea kueleza kuwa, yeye kama Mbungeanaamini kuwa, Bunge halikuridhia reallocation ya shilingibilioni 976.96 kupelekwa Fungu namba 20. Nilitoa ufafanuziwa hoja hiyo kwamba suala la reallocation huzingatiautaratibu uliowekwa na Sheria ya Bajeti, Mbunge anaweza

Page 197: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

kuhoji pale ambapo kiwango cha reallocation kimezidikiwango kilichowekwa kwa mujibu wa sheria.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya ufafanuzi huo,Mheshimiwa Mnyika aliibua hoja nyingine kutaka Serikalikutoa mchanganuo wa namna shilingi bilioni 976.96zilivyotumika. Alieleza, nanukuu; “Ili tuondoe utata kuhusujambo hili la shilingi bilioni 976.96, Ofisi ya Rais ikija kwenyemajumuisho hapa itueleze hizi shilingi bilioni 976.96, Ikuluzilitumika kwa matumizi yapi, tupewe mchanganuo wa kina.”

Waheshimiwa Wabunge, baada ya maelezo yaMheshimiwa Good luck Mlinga, Mbunge, alihoji uhalali waMheshimiwa Mbunge kuhoji suala la 1.5 trillion, wakati Kamatiya PAC ilikwishatoa taarifa na kueleza kwamba tofauti hiyoya 1.5 trill ion, haikuwepo baada ya marekebisho yamaheshabu kufanyika. Aliendelea kueleza kwamba sualahilo linaendelea kuzungumzwa ili kuichafua Serikali.

Waheshimiwa Wabunge, niliahidi kupitia Taarifa Rasmiya Bunge (Hansard) ya Kikao cha leo, nilifanya hivyo nanimejiridhisha kuwa Mheshimiwa Mnyika, Mbunge alikuwaanajadili suala ambalo Kamati ya PAC ilikwishalitoleaufafanuzi, ambapo katika Taarifa ya Shughuli za Kamati yaKudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa mwaka2018, katika ukurasa wa 35 ambapo ilibaini na kueleza kuwahapakuwepo na tofauti ya shilingi trilioni 1.5 kati ya mapatoya Serikali na makusanyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017,baada ya marekebisho ya hesabu kufanyika na nanukuu;“Mheshimiwa Spika, katika kuhitimisha suala la tofauti yashilingi trilioni 1.5 kati ya mapato ya Serikali na makusanyokwa mwaka wa fedha 2016/2017, naomba kuwekakumbukumbu sahihi katika Bunge lako tukufu kuwa tofautihiyo haikuwepo baada ya marekebisho ya hesabukufanyika.” Mwisho wa kunukuu.

Baada ya hapo Bunge liliazimia na kuthibitishakwamba hakuna tofauti ya shilingi trilioni 1.5 kati yamakusanyo na mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu kwa

Page 198: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

mwaka wa fedha 2016/2017, angalia ukurasa wa 73 wataarifa ya PAC.

Waheshimiwa Wabunge, wakati akianza kuchangiatena Mheshimiwa Mbunge Mnyika, aliongelea suala la 1.5trillion, ambazo zilipanda mpaka 2.4 trillion na kusema kuwabilioni 976.96 zilihamishwa kwa njia ya reallocation kwendaFungu namba 20.

Waheshimiwa Wabunge, unapoongelea suala latofauti ya shilingi trilioni 1.5 na trilioni 2.4 pamoja nareallocation ya shilingi bilioni 976.96, unakuwa unaongeleakitu kimoja. Jambo hili tayari Bunge lilikwishalitolea uamuzitarehe Mosi Februari, mwaka huu, wakati kiti kilipojibuMwongozo wa Mheshimiwa Jenista Joachim Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu), aliyehoji kuhusu uhalali wamchango wa Mheshimiwa Catherine Ruge, aliyedai kuwakwenye Taarifa ya CAG kuna reallocation ya shilingi bilioni997 na mchango wa Mheshimiwa Anatropia Theonest,aliyedai kwamba kiwango kilichopotea ni zaidi ya trilioni mbili.

Uamuzi uliotolewa na kiti ni kwamba, suala hilohaliruhusiwi, kwa kuwa, ufafanuzi ulishatolewa na CAG naKamati ya CAG kuhusu kutokuwepo tofauti hiyo ya shilingitrioni 1.5 kati ya mapato na makusanyo ya Serikali. Kiti kiliamuakuwa, mchango wa Mheshimiwa Ruge na MheshimiwaAnatropia Theonest, uondolewe kwenye Taarifa Rasmi yaBunge (Hansard).

Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 53(8) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, inakataza kujadilijambo ambalo lilikwishaamuriwa na Bunge katika mkutanouliopo au uliotangulia, nanukuu; “Mbunge yeyotehataruhusiwa kufufua jambo ambalo Bunge lilikwishakuliamua ama katika mkutano huo uliopo au ule uliotangulia,….isipokuwa kwa kufuata masharti ya Kanuni hizi...”

Vilevile Kanuni ya 64(1)(c), inazuia kujadili jambolililokwishaamuriwa na Bunge iwapo hakuna hoja mahususi

Page 199: BUNGE LA TANZANIA...wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo mawili, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

iliyotolewa na kanuni hiyo inasema; “Mbunge hatazungumziajambo lolote ambalo linasubiri uamuzi wa Mahakama aujambo lolote ambalo lilijadiliwa na kutolewa maamuzikwenye mkutano uliopo au uliotangulia na ambalohalikuletwa rasmi kwa njia ya hoja mahususi na vilevilehatapinga uamuzi wowote uliofanywa na Bunge, isipokuwatu kwa kutoa hoja mahususi inayopendekeza kuwa uamuzihuo uangaliwe upya;”

Waheshimiwa Wabunge, kutokana na uamuzi huo namasharti ya Kanuni hizo mbili nilizozitaja, naelekeza kwambasuala hilo lisiendelee kujadiliwa Bungeni na naelekezakwamba mchango wa Mheshimiwa John Mnyika, Mbungekuhusu hoja ya shilingi trilioni 1.5 na reallocation kuhusu sualahilo ifutwe kwenye Taarifa Rasmi za Bunge. Huo ndiyomwongozo wangu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, niwashukuruni sana kwa kazinzuri mliyoifanya kwa siku ya leo, kwa michango yenu nanimeshatoa matangazo. Tujitahidi kesho mapema saa kumina mbili, wale ambao, itapendeza kama tutachukua usafiriambao Bunge limetoa kwa sababu ya nafasi kuletunakokwenda itakuwa finyu kwa magari binafsi. Kwa hiyo,sina la ziada, kwa maana hiyo, naahirisha shughuli za Bungehadi siku ya Jumatatu, wiki ijayo saa tatu asubuhi.

(Saa 1.50 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumatatu,Tarehe 15 Aprili, 2019 Saa Tatu Asubuhi)