48
Maoni ya wageni Viungo Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya Sha'abaan 22, 1431. Soma Qur-aan Neno Kwa Neno Hukmu Za Tajwiyd Qur-aan Hadiyth Duaa - Adhkaar 'Aqiydah- Tawhiyd Fiqhi Ramadhaan-Swawm Swalah Zakaah Hajj Nasiha za Ijumaa Zingatio Makala Maswali-Majibu Visa Familia- Wanawake Mapishi Vitabu Flash Nyumbani Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 1 Tiba Kwa Njia ya Qur- aan na Sunnah 'Aqiydah-Tawhiyd (Na Fathi Al-Jundiy) Imefasiriwa na Ummu Ashraf Kutafuta tiba kwa njia ya Ruqyah na Qur-aan ni suala Yanayohusiana Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 4 Malipo ya fedha kwa ajili ya kufanya Ruqyah Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 3 - Tiba Enzi Za Ujahili Na Aina Mbili Za Ruqyah 'Aqiydah Yetu Hivi Leo Kufuru Na Aina Zake Kujitupa Kwa Mwenyezi Mungu (Ta’alluq Billah) Mfululizo Wa Mada Ya Majini (3) Mambo Yanayomtoa Tafuta Ndani Ya A lhidaaya Tafuta search_them e_fo 5290dc5ea9d29a

Tiba kwa ruqya

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Tiba kwa ruqya

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Sha'abaan 22, 1431.

Soma Qur-aan Neno

Kwa Neno Hukmu Za

Tajwiyd Qur-aan Hadiyth Duaa - Adhkaar 'Aqiydah-

Tawhiyd Fiqhi Ramadhaan-

Swawm Swalah Zakaah Hajj Nasiha za

Ijumaa Zingatio Makala Maswali-Majibu Visa Familia-

Wanawake Mapishi Vitabu Flash Mashairi

Sikiliza Quraan

Nyumbani

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 1 Tiba Kwa Njia ya Qur-aan na Sunnah

'Aqiydah-Tawhiyd

 

(Na Fathi Al-Jundiy)

Imefasiriwa na Ummu Ashraf

 

Kutafuta tiba kwa njia ya Ruqyah na Qur-aan ni suala zito linalohitaji ufafanuzi na mjadala wa wazi kutokana na ukweli kuwa yamezuka mambo mengi ya uzushi na ushirikina ambayo

Yanayohusiana Utaratibu Sahihi

Wa Kufanya Ruqyah - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 4 Malipo ya fedha kwa ajili ya kufanya Ruqyah

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 3 - Tiba Enzi Za Ujahili Na Aina Mbili Za Ruqyah

'Aqiydah Yetu Hivi Leo

Kufuru Na Aina Zake

Kujitupa Kwa Mwenyezi Mungu (Ta’alluq Billah)

Mfululizo Wa Mada Ya Majini (3)

Mambo Yanayomtoa Mtu Katika Uislam

Udhaifu Wa

Tafuta Ndani Ya Alhidaaya Tafuta search_theme_fo 5290dc5ea9d29a

Page 2: Tiba kwa ruqya

Mawaidha Du'a Na

Adhkaar English Lecture

Tazama Swahili Video Learn the

Arabic Language

User loginUsername: *

Password: *

Create new account

Request new password

Pokea Makala

Jaza anuani yako ya barua pepe (e-

mail) uweze kupokea

Makala zetu

Jiunge uanachama

Jitoe uanachama

hayana ushahidi wa Qur-aan, Sunna wala vielelezo kutoka kwa Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Mambo haya yamekuwa yakifanywa kwa jina la Ruqyah au ponyo la Qur-aan. Ingawaje Ruqyah hutafsiriwa kama “uganga,” au “uganga wa kitabu” lakini ainisho hili, kwa kiasi fulani, ni potofu na linabeba maana mbaya sana katika lugha ya Kiswahili.

Wakati neno uganga huhusishwa na mambo ya kishirikina (uchawi na mauzauza), Ruqyah maana yake ni usomaji wa Qur-aan na uombaji wa dua kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ili kupata msaada wake katika tiba ya ugonjwa na matatizo mengine na haihusiani kabisa na mambo ya uganga.

Ibn Hajr Al-Asqalanii kasema kuwa ainisho la Ruqyah linajumuisha ta’awwuth ambayo maana yake ni kuomba ulinzi. Kwa maneno yake kasema hivi:

“Hakuna khitilafu yoyote miongoni mwa wanazuoni kuhusiana na suala la kumuelekea MwenyeziMungu kumuomba msaada na ulinzi kwa hali yoyote itokeayo au inayotarajiwa kutokea. (Fath Al-Barii)

Imani… Alama Zake, Sababu Na Matibabu Yake - 1

Pepo 'Al-Jannah'

Feature

Kikokotoo (Calculator)

Log in

user_login_block

Tuma

Page 3: Tiba kwa ruqya

Suala la Ruqyah huendana na Aqida na Akhlaq za Kiislamu na ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la MwenyeziMungu kuwa Waislamu wamtegemee MwenyeziMungu tu katika mambo au matatizo yao yote.

Jambo la kusikitisha ni kwamba umezuka mtindo wa kufanya ‘tiba’ kwa Ruqyah kinyume na maana na lengo la Ruqyah. Hali hii imepelekea watu kupata “ajira isiyo rasmi” ya kufanya’uganga’ kwa maslahi binafsi huku wakijihami kwa kisingizio cha Ruqyah.

Sio siri hata kidogo kuwa kuna watu wamejipa uwezo wa “kuwatibu’ au’kuwaombea dua’ wengine ilihali hao wanaotibiwa au kuombewa dua hawana hata dalili moja ya imani juu ya MwenyeziMungu. Matokeo yake, “wateja” humtegemea zaidi “mganga” kuliko MwenyeziMungu.

‘Tiba’ kwa kisingizio cha Ruqyah sio tu imekuwa “kitega uchumi” bali pia kumekuwepo na ukiukaji wa maadili kwa baadhi ya wale wanaosemekana kuwa ni “wataalamu wa tiba ya Ruqyah”.

Kama ilivyokwishaelezwa kuwa Ruqyah sahihi huendana na Aqida na Akhlaq au maadili ya Kiislamu, lakini baadhi ya waganga magirini wamekuwa wakilitumia jambo hili kama

Cha ZakkahPiga Hesabu Za Zakaah Yako Unayotaka Kutoa Kwa Kutumia Kikokotoo (Calculator) Ya Kuhesabu Zakaah Yako

Zingatio La WikiDunia Si Chochote Si Lolote

Zingatio La Wiki

Wakati unayoyoma na hakuna awezaye kuuzuia usiende. Hakuna tofauti nyengine baina yetu na wale waliotangulia mbele ya haki ila ni wakati tu. Hakika wakati ndio unaomfanya mtu kuwa mtoto, kijana au kizee. Haukuwepo wakati na hii ni Neema Zake Muumba. Ni wakati huu ndio unaoufanya mchana ukaondoka kwa kuupisha usiku.

»

Login or register to post commentsEndelea

Page 4: Tiba kwa ruqya

mtego wa kunasia “akina dada na akina mama”.

Wateja hawa wa kike sio tu hutoa “ada” au “malipo” ya pesa kwa ajili ya ‘kufanyiwa Ruqyah’ bali wakati mwingine huwa wahanga wa maumbile yao.

Hushikwashikwa miili yao, hupapaswa maungo ya siri, huchojolewa nguo, hukogeshwa maji ya ‘dawa’ uchi’ au humwagiwa maji juu ya kanga ili igandamane na mwili mganga apate kukidhi matamanio yake, na wengine hufanyiwa kabisa uchafu wa zinaa!

Utafiti unaonesha kuwa wateja wengi wa “Matabibu hawa wa Ruqyah” huwa ni akina dada na akina mama, baadhi yao wakiwa ni wake za watu. Tamaa ya ngono kwa “tabibu wa Ruqyah”, mara nyingine huchochewa na “shida za akinadada” wanaotaka “kuombewa ili wapate waume!”

Kwa kweli kuna mambo ya ajabu sana ambayo japo yanafanyika chini ya mwamvuli wa Ruqyah lakini yanakiuka kabisa msingi, maana na lengo la Ruqyah!

Yawezekana makala hii ikawaudhi wahusika lakini lazima waukubali ukweli kuwa hii wanayofanya siyo Ruqyah iliyofundishwa na Mtume

Page 5: Tiba kwa ruqya

(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Hayo wanayoyanya wao ni kwa ajili ya matamanio ya nafsi zao na maslahi yao tu.

Kwa ajili hiyo, lazima wakubali kuwa, shughuli wanayofanya inawajengea ushirikiano wa karibu na shetani badala ya kuwakurubisha kwa MwenyeziMungu.

Lengo la Ruqyah sahihi ni kuwakurubisha waja kwa Mola wao. Na lengo la makala hii ni kuonesha tofauti kati ya Ruqyah inayoruhusiwa katika Uislamu na ‘Ruqyah feki’ inayofanywa na waganga magirini wanaohaha kuganga njaa zao.

Kwa minajili hiyo, makala hii, kwanza kabisa, inawahadharisha watu juu ya mambo ya uzushi yanayofanyika kwa jina la Ruqyah. Njia sahihi ya kuepukana na ghiliba zozote zile za ‘waganga’ ni kutafuta elimu sahihi ya Uislamu, kumuamini Allah na kumtegemea Yeye pekee.

                           

Moyo Wa Mwanaadamu

Moyo wa mwanadamu, kwa kawaida, hujaa mambo fulani na huwa hauruhusu kitu chochote kuingia mpaka kwanza kingine kilichomo ndani yake kitoke nje.

Page 6: Tiba kwa ruqya

Ibnul-Qayyim kasema “ili mahali paweze kuruhusu kitu fulani kukaa basi ni shurti kuondosha kitu kingine kilichopo hapo. Hii ndiyo kanuni ya kimaada na ndiyo kanuni ya imani na nafsi pia. (Taz. Al-Fawa’id)”

Mja muumini humjuwa ipasavyo Muumba wake, anajuwa kwa nini yeye ameumbwa na anajuwa mwisho wa safari yake

Pia mja anayemuamini Allah anajuwa kuwa wanadamu na majini hawana uwezo wa kuwadhuru wala kuwanufaisha viumbe. Na wala hawana mamlaka juu ya maisha ya uhai wao, mauti yao au kufufuka kwao bila ya idhini ya MwenyeziMungu.

Kwa hali hiyo, Muumini mwenye tauhiid huishi maisha ya utulivu kwani anajuwa fika kuwa hakuna mwenye uwezo juu yake isipokuwa MwenyeziMungu kama Anavyosema katika Qur-aan:

“Hakika waja wangu wewe hutakuwa na mamlaka juu yao isipokuwa wale wenye kukufuata katika hao wapotevu”. (15:42).

“Na kama MwenyeziMungu akikugusisha madhara basi hakuna yeyote awezaye kuyaondoa ila Yeye; na kama akikugusisha kheri, Yeye ndiye Muweza juu ya kila kitu”. (6:17).

Page 7: Tiba kwa ruqya

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimwambia Abdullah ibn Abbaas, “Ewe Kijana! Jichunge na MwenyeziMungu, Naye Atakuchunga. Chunga Haki Zake, Naye daima atakuwa pamoja nawe, ukilazimika kuomba basi muombe Yeye pekee; na ukihitaji msaada, Muombe msaada Allah pekee. Na kumbuka kuwa kama watu wote wakitaka kukunufaisha, hawataweza kukupa chochote isipokuwa kile tu alichokukadiria MwenyeziMungu na ikiwa wote wanataka kukudhuru basi hawataweza kukudhuru isipokuwa kile tu alichokupangia MwenyeziMungu. Kalamu zishasimamishwa na kuwekwa kando na wino wa (kuandikia) Kitabu (kadari) ushakauka”. (Ahmad na At-Tirmidhiy).

Kinyume cha hivyo, imani dhaifu katika kumpwekesha  Allah, ulegevu wa imani katika kumtegemea MwenyeziMungu na ukosefu wa elimu sahihi huufanya moyo uwe kichaka cha kufichia mambo ya kishetani, mambo ya udanganyifu na mambo ya kipuuzi.

Kuhusiana na hali hii ya hatari ya moyo, Ibnul Qayyim kaandika hivi: Mashetani, mara nyingi, huwachezea wale wenye uelekeo hafifu wa dini yao, na wale ambao nyoyo na ndimi zao zimekimbiwa na imani-hawa ni watu ambao hawamkumbuki

Page 8: Tiba kwa ruqya

MwenyeziMungu na hawana njia ya kuimarisha imani yao. Pale mashetani wanapokutana na mtu dhaifu, asiye na silaha, na mtupu, huweza kumuandama na kumshinda (Attib An-Nabawii).

Aidha Ibn Qayyim kasema: “Uchawi wa wachawi huwadhuru watu wenye nyoyo dhaifu na  watu waliogandamana na hadaa na tamaa za dunia...na wasioshughulika kusoma Qur-aan na nyiradi alizofundisha Mtume kila siku).

Wanazuoni wamesema: ‘wanaorogeka (wanaopatwa na uchawi) ni wale wanaoruhusu wenyewe kurogwa, kwani mara zote unakuta nyoyo zao zimekamatana na kushughulishwa na jambo hilo; na hivyo, nyoyo zao hizo hutetereshwa na jambo hili kulingana na kiwango ambacho zimeshikamana nalo, Allah ndiye Ajuwaye zaidi.”  (Al-Fawa’id).

Ufumbuzi wa tatizo hilo ni kuujaza moyo na kukijaza kichwa mambo ya  kumuabudia, kumfikiria na kumkumbuka Allah. Maisha yote ya mtu yatawaliwe na mambo haya. Kwa njiya hii imani hugeuka kuwa silaha kubwa ya kupambana na wale wanaotafuta uchawi na kiini macho ili kupata maslahi fulani.

Page 9: Tiba kwa ruqya

 

Uhalali Wa Kutafuta Tiba

Hapana shaka kuwa Uislamu ulikuja na nguvu ya kutibu moyo na kiwiliwili. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliitafuta tiba na pia aliwahimiza Maswahaba zake kufanya hivyo. Jabir kasimulia kuwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“kuna dawa kwa kila ugonjwa na dawa hiyo inapotumika kutibu ugonjwa, ugonjwa hutibika kwa idhini ya MwenyeziMungu Sunhaanahu wataala.” (Muslim).

Akisherehesha Hadith hii; Ibn Qayyim kaandika hivi: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliamrisha tiba kwa kutumia dawa inayowiyana na ugonjwa. Kila ugonjwa una dawa. Kupona ugonjwa shurti kuendane na dawa inayowiana na ugonjwa huo.

Hivyo dawa ikizidi mno kiasi, itasababisha ugonjwa mwingine. Kinyume chake, dawa ikitumika  chini ya kiasi kinachohitajika itashindwa kupambana na ugonjwa na kwa hali hiyo itaonekana kutofaa.

Hivyo basi, daktari asipogundua tiba halisi au iwapo tiba haihusiani na ugonjwa, suala la kupona huwa ni muhali. Zaidi ya

Page 10: Tiba kwa ruqya

hivyo ikiwa tiba inatolewa katika muda usiofaa, dawa haitasaidia kitu, au kama mwili haukubali dawa au mwili hauna nguvu kabisa ya kumudu dawa hiyo, au kuna kitu fulani kinachozuwia isifanye kazi, dawa haitasaidia. Lakini kinyume cha hivyo kama dawa inawiana na ugonjwa, tiba itafanya kazi kwa idhini ya Allah.” (Attib An-Nabawii).

Jambo la ajabu ni kwamba, kuna baadhi ya watu wanaopuuzia njia za kisasa za tiba na badala yake husingizia kukumbwa na majini, kurogwa au kutazamwa kwa jicho baya. Ujinga huu huweza hata kusababisha kifo kwa mgonjwa wakati watu wakipoteza muda kumtowa majini mgonjwa.

Hivyo, ni muhimu kwanza kugundua aina ya ugonjwa na kisha kujaribu kutafuta dawa sahihi inayoweza kutibu ugonjwa huo. Kwani kama mtu hana uhakika na aina ya ugonjwa, anawezaje kutoa tiba ya kufaa?

Baadhi ya watu wanaweza kuuliza je kutafuta tiba kunapingana na imani ya kumtegemea MwenyeziMungu (tawakkul). Kwa hakika Hadith chungutele za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ikiwemomoja iliyokwishatajwa hapo juu zinaunga mkono mtazamo huu kuwa kutafuta tiba ya dawa ni jambo

Page 11: Tiba kwa ruqya

linalokubalika kabisa, na limehimizwa katika Uislamu. Upo muafaka wa pamoja wa wanachuoni wa Kiislamu juu ya jambo hili.

 

Muungozo Wa Mtume Kuhusiana Na Kinga Na Tiba

Muongozo bora kabisa wa maisha yetu unapatikana kwa kuyasoma maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ambaye alituonesha namna ya kufanya mambo yetu katika mazingira yoyote yale.

MwenyeziMungu anamzungumzia Mtume hivi: “yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. (Na) kwa walioamini ni mpole na mwenye huruma.” (9:128).

Kwa hakika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katuongoza katika mema yote na kutuonya dhidi maovu yote. Muongozo wake unajumuisha na kinga dhidi ya aina zote za maradhi pamoja na njia za kupambana nayo pale yanapotokea.

Hapa tutaziangalia njia za kujikinga na maradhi alizofundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) pamoja na tiba mbalimbali za kutibu madhara ya kijicho na

Page 12: Tiba kwa ruqya

uchawi.

Kinga dhidi uovu kwa ujumla hupatikana kwa nguvu ya tauhiid (imani ya kumpwekesha MwenyeziMungu), kumsabihi kwa Majina na Sifa Zake tukufu, kufanya Ibada Zake kwa ikhilasi, kutii amri Zake, kumtegemea yeye tu,kumpenda na kumkumbuka mara kwa mara.

Hii ndiyo njiya ya kutafuta ulinzi wa jumla wa MwenyeziMungu. Aidha kuna maelezo kuhusu namna ya kutafuta ulinzi wake kwa njia mahususi, kama vile kuomba dua kabla ya kufanya tendo la ndoa ili kumkinga mtoto atakayezaliwa, kusoma Surati Baqara nyumbani, na kusoma Ayatu Kursiyu pamoja na sura tatu za mwisho za Qur-aan, Ikhilas (QulhuAllahuAhadu), Falaq (Qulaudhubirabilifalaq) na Surat n-Nasi (Qulaudhubirabinnas). Sura hizi hujulikana kama Al-Muawwithat

Hata hivyo, ni muhimu kubainisha kuwa kuna tofauti kubwa kati ya maneno yanayotamkwa kwa ikhilasi kutoka ndani kabisa ya moyo na

Page 13: Tiba kwa ruqya

maneno yanayotokea mdomoni tu.

Kinachohitajika hapa ni dhikri inayohusisha moyo na ulimi. Ibnul-Qayyim kailezea hali hii kama ni “aina ya mapambano”, akisema: “Mpiganaji huweza kumshinda aduwi yake iwapo silaha anayotumia ni madhubuti na ikiwa yeye mwenyewe ni mkakamavu (shupavu) katika kutumia silaha hiyo.

Endapo moja kati ya masharti haya mawili halitimizwi, basi silaha haitakuwa na maana. Na mambo yatakuwa mabaya zaidi kama masharti yote mawili hayatimizwi” (Attib An-Nabawii).

 

Inaendelea.../2

 

  

»

Login or register to post comments Email this page Chapisha

asalam alaikum warahmatullahSubmitted by aishaabdul on Wed, 11/18/2009 - 15:39.asalam alaikum warahmatullah ndugu zangu katika iman hasa kina mama tuwe waangalifu sana tusiwe tayari kudanganywa mtu

Page 14: Tiba kwa ruqya

unapakwa dawa eti mpaka sehem zako za siri alahu akbar

nimeyakinisha haya mambo toka kwa rafiki yangu kipenzi (jina nalihifadhi) alikwenda kwa mganga anaejiita sheikh hapa jijini kwetu huyu dada alikuwa akisumbuliwa na majini subhuhana llah

huyu anaejiita sheikh ndio alikuwa akimtibu kaisha zini nae mara mbili akisema ndio tiba mbadala ya kutoa jini jamani tena amezini nae ndani ya chumba wakiwa wamefunga mlango na mke wa sheikh yuko nje anachemsha dawa ama kweli siku zitapofichuka siri kuna makubwa na alipozini nae wala hajapata nafuu akarudi tena akamzini tena kuja kujua kama anadanganywa tayari kaisha zini mara mbilinilitamani nchi hii iwe ya kiislam niwe wa kwanza kumpiga mawe huyu bwana mpaka afe nimetamani nimtangaze wanawake wakae mbali nae lakini uwezo wangu ni mdogo inshaalah alah atamfedhehesha hapa duniani na kesho akhera.

»

Login or register to post comments

Rudi Juu

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Website hii imetengenezwa kuangaliwa vizuri zaidi katika resolution 1024 kwa 768 www.alhidaaya.com

Page 15: Tiba kwa ruqya

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Sha'abaan 22, 1431.

Soma Qur-aan Neno

Kwa Neno Hukmu Za

Tajwiyd Qur-aan Hadiyth Duaa - Adhkaar 'Aqiydah-

Tawhiyd Fiqhi Ramadhaan-

Swawm Swalah Zakaah Hajj Nasiha za

Ijumaa Zingatio Makala Maswali-Majibu Visa Familia-

Wanawake Mapishi Vitabu Flash Mashairi

Nyumbani

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi

'Aqiydah-Tawhiyd

 

(Na Fat-hi Al-Jundiy)

Imefasiriwa na Ummu Ashraf

 

 

Tiba Ya Jicho La Husda

Yanayohusiana Kujitupa Kwa

Mwenyezi Mungu (Ta’alluq Billah)

Kufuru Na Aina Zake

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 3 - Tiba Enzi Za Ujahili Na Aina Mbili Za Ruqyah

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 1 Tiba Kwa Njia ya Qur-aan na Sunnah

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 2

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 5

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 4 Malipo

Tafuta Ndani Ya Alhidaaya Tafuta search_theme_fo a0b9f5fb024b732

Page 16: Tiba kwa ruqya

Sikiliza Quraan Mawaidha Du'a Na

Adhkaar English Lecture

Tazama Swahili Video Learn the

Arabic Language

User loginUsername: *

Password: *

Create new account

Request new password

Pokea Makala

Jaza anuani yako ya barua pepe (e-

mail) uweze kupokea

Makala zetu

Jiunge uanachama

Jitoe uanachama

 

Uwezo wa kuwadhuru wengine kwa kuwatazama au kuonea kijicho ambao hujulikana kama “kijicho” kweli upo. Ibn Abbas kasimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)kasema: “madhara ya Kijicho (al-ayn) kweli yapo. Kwani kama kungelikuwa na jambo la kuitangulia kadari basi lingekuwa ni dhara la kijicho” (Muslim).

Ili kuzuwia madhara ya kijicho, mtu akiona mtu au jambo la kumpendeza machoni na akachelea atashidwa kuizuwia nafsi kulihusudu au kulionea kijicho, basi aseme “maa shaa-Allaah (akitakacho MwenyeziMungu kiwe ndicho huwa!) na kisha amuombe MwenyeziMungu amjaalie kheri mtu huyo aliyemtazama au akijaalie kheri kitu alichokitazama.

Tiba ya kijicho yaweza kufanyika bila kujali kama mtu aliyemtazama mwenziwe kwa kijicho kajulikana au hakujulikana. Ikiwa mtu aliyemuonea mwenziwe kijicho kajulikana basi ushahidi wa jinsi ya kufanya tiba unapatikana katika Hadith ifuatayo:

Abu Umamah ibn Sahl ibn Hunayf kasimulia hivi: “Baba yangu, Sahl ibn Hunayf, alifanya josho (ghusl) pale al-Kharrar.

ya fedha kwa ajili ya kufanya Ruqyah

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 4

Maana Ya 'Ibaadah

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 1

Feature

Log in

user_login_block

Tuma

Page 17: Tiba kwa ruqya

Akavua juba alilokuwa amelivaa huku Amir ibn Rabia akimtazama, na Sahl alikuwa na ngozi nyororo nyeupe.

Amir akasema: “Sijapata kuona  (ngozi) mfano wa hii ambayo nimeiona leo, haifanani hata na ngozi ya mwanamwali.” Papo hapo Sahl akawa mgonjwa na hali yake ikawa mbaya sana.

Mtu mmoja akaenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na kumwambia kuwa Sahl ni mgonjwa na asingeweza kujimudu kuja pale kwa Mtume. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)akaja pale alipokuwa Sahl. Sahl akamsimulia kilichotokea wakati alipokuwa na Amir.

 

Mtume wa Allaah akasema, “kwa nini mmoja wenu anamuua nduguye? Kwa nini (wewe Amir) hukusema ‘Tabarak-Allaah’ (MwenyeziMungu Akujaalie kheri)? Kijicho kipo kweli.”

Kisha Mtume akamwambia Amir, ‘tia udhu kwa ajili ya mwenzio’. Amir akatia udhu. Baada ya Amir kutia udhu, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)akanyunyiza maji ya udhu ya Amir kichwani na mwilini mwa Sahl. Halafu Sahl akaondoka pamoja na Mtume na hakuwa na ugonjwa tena”.

Kikokotoo (Calculator) Cha ZakkahPiga Hesabu Za Zakaah Yako Unayotaka Kutoa Kwa Kutumia Kikokotoo (Calculator) Ya Kuhesabu Zakaah Yako

Zingatio La WikiDunia Si Chochote Si Lolote

Zingatio La Wiki

Wakati unayoyoma na hakuna awezaye kuuzuia usiende. Hakuna tofauti nyengine baina yetu na wale

Page 18: Tiba kwa ruqya

(Ahmad).

 

Endapo mtu aliyemuonea kijicho mwenziwe hajulikani, basi tiba inaweza kufanywa kwa Ruqyahh, duwa zinazoswihi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) zikiambatana na unyenyekevu uliojaa ikhilasi kwa Allaah.

MwenyeziMungu daima huitikia maombi ya wenye shida.kama isemavyo Qur-aan, “Au yule anayemjibu anayedhikika amwombapo na kuondoa dhiki (yake)..?” (27:62).

 

Ibn Qayyim kasema: “miongoni mwa njia za kuomba ulinzi wa MwenyeziMungu na zile zinazojumuisha Ruqyah ni: usomaji wa mara kwa mara wa Surat al-Falaq, surati An-Nasi, surati Al-Fatiha na Ayatul Kursiyu.

 

Mtu pia asome dua za Mtume kama hizi:

*Kwa maneno haya thabiti ya Allaah, najikinga Kwake na shari aliyoiumba.

*Kwa maneno thabiti ya Allaah, naomba Ulinzi Kwake dhidi ya

waliotangulia mbele ya haki ila ni wakati tu. Hakika wakati ndio unaomfanya mtu kuwa mtoto, kijana au kizee. Haukuwepo wakati na hii ni Neema Zake Muumba. Ni wakati huu ndio unaoufanya mchana ukaondoka kwa kuupisha usiku.

»

Login or register to post commentsEndelea

Page 19: Tiba kwa ruqya

kila shetani, kila mnyama hatari na kila jicho baya.

*Kwa maneno thabiti ya Allaah ambayo si Muumini wala si muovu anayeweza kuyakhalifu, najikinga Kwake na shari ya alivyoviumba, akavipa uhai na akavizalisha.

*Allaah Anatutosheleza na ndiye Mlinzi bora kabisa. Allaah Ananitosha. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Kwake Yeye nategemeza imani yangu, Naye ndiye Mola wa Arshi kuu.

Watu ambao wamejitahidi kuomba dua hizi kwa hakika wamepata manufaa makubwa na kukidhiwa haja shida zao kubwa kubwa kwani duwa hizi zinazuwia na kuondosha madhara ya kijicho kutegemeana na imani ya mtu anayezisoma.

 

Kadri imani yake inavyokuwa na nguvu ndivyo utegemezi wake kwa MwenyeziMungu unavyokuwa mkubwa. Kwa hakika hii ndizo silaha (za kupambana na uovu)” (Attib An-Nabawii).

 

 

Tiba Ya Uchawi

Page 20: Tiba kwa ruqya

 

Huwa inasemwa kuwa Kinga ni bora kuliko Tiba. Kwa hiyo basi, mtu ajikinge na madhara ya uchawi kabla haujatokea. Pamoja na mambo mengine, kinga hii hupatikana kwa kumtii na kumuabudia Allaah pekee, kuamini Qudra na Qadari Yake, kuomba ulinzi Wake kwa kumdhukuru mara kwa mara na kusoma dua za Mtume katika nyakati zinazofaa.

 

Kula tende Ajwah ni njia nyingine ya kuzuia madhara ya uchawi kama ilivyobainishwa katika Hadith iliyosimuliwa na Sa’ad ambapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)kasema, “mtu akila tende Ajwah kila asubuhi, hatadhurika kwa sumu au uchawi kwa siku hiyo.” (Al-Bukhaariy na Muslim).

Ni muhimu kutambua kuwa wale wanaostahili kunufaika na Hadith hii ni wale tu wanaoamini kikwelikweli haya aliyoyasema mtume na wanaoamini kwa dhati kabisa kuwa kila alichosema ni ukweli, ama wathibishe ukweli wake au la. Na kuhusu tiba ya uchawi, mtu aliyerogwa aoneshe subira na airidhie kudra ya Allaah. Pia ni jambo la msingi kwake kujirudi kwa dhambi yoyote ambayo ameitenda na afanye

Page 21: Tiba kwa ruqya

toba ya kweli kwa dhambi hiyo.

Anapotafuta tiba, aepuke kabisa tiba za “kitekero” au”kisangoma”  zinazotolewa na waganga magirini. Kama ikibidi, basi anaweza kushirikiana na watu wachaMungu kumuomba msaada Allaah kwa utaratibu anaouridhia Allaah.

 

Inaendelea.../3

  

»

Login or register to post comments Email this page Chapisha

AssalamuSubmitted by Tabasam on Fri, 10/16/2009 - 03:43.Assalamu Aleikum,Nawashukuru kwa hii website...InshaAllah Allah awape baraka juu ya baraka ameen. nina swali..nini maana ya tende Ajwah?

»

Login or register to post comments

God bless you all this is aSubmitted by Lela on Mon, 11/17/2008 - 09:25.God bless you all this is a very educative website for muslim thank you and keep it up.

Page 22: Tiba kwa ruqya

»

Login or register to post comments

asalam alaykum warahmatulahiSubmitted by munira on Sat, 04/25/2009 - 22:41.asalam alaykum warahmatulahi wabarakatu,

it could be much better if your remember ALMIGHTY ALLAH and say MANSHAALAH MY ALLAH REWARD YOU IN THIS WORLD AND HEREAFTER . and may ALLAH SUBHANA WATA'A'LA PROTECT YOU FROM EVILS OF THIS WOLRD

WASALAM...

»

Login or register to post comments

Rudi Juu

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Website hii imetengenezwa kuangaliwa vizuri zaidi katika resolution 1024 kwa 768 www.alhidaaya.com

Page 23: Tiba kwa ruqya

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Sha'abaan 22, 1431.

Soma Qur-aan Neno

Kwa Neno Hukmu Za

Tajwiyd Qur-aan Hadiyth Duaa - Adhkaar 'Aqiydah-

Tawhiyd Fiqhi Ramadhaan-

Swawm Swalah Zakaah Hajj Nasiha za

Ijumaa Zingatio Makala Maswali-Majibu Visa Familia-

Wanawake Mapishi Vitabu Flash Mashairi

Sikiliza Quraan

Nyumbani

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 3 - Tiba Enzi Za Ujahili Na Aina Mbili Za Ruqyah

'Aqiydah-Tawhiyd

  

(Na Fat-hi Al-Jundiy)

Imefasiriwa na Ummu Ashraf

 

 

Yanayohusiana Utaratibu Sahihi

Wa Kufanya Ruqyah - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 4 Malipo ya fedha kwa ajili ya kufanya Ruqyah

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 1 Tiba Kwa Njia ya Qur-aan na Sunnah

'Aqiydah Yetu Hivi Leo

Kufuru Na Aina Zake

Mambo Yanayomtoa Mtu Katika Uislam

Mfululizo Wa Mada Ya Majini (3)

Kujitupa Kwa Mwenyezi Mungu (Ta’alluq Billah)

Pepo 'Al-Jannah'

Tafuta Ndani Ya Alhidaaya Tafuta search_theme_fo a0b9f5fb024b732

Page 24: Tiba kwa ruqya

Mawaidha Du'a Na

Adhkaar English Lecture

Tazama Swahili Video Learn the

Arabic Language

User loginUsername: *

Password: *

Create new account

Request new password

Pokea Makala

Jaza anuani yako ya barua pepe (e-

mail) uweze kupokea

Makala zetu

Jiunge uanachama

Jitoe uanachama

Tiba Enzi Za Ujahili

 

Yafahamika kuwa watu katika zama za ujahiliya walikuwa wakitamka maneno mengi ya uganga katika mazingira mbalimbali.

Jabir kasimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliharamisha uganga wa kienyeji. Ndipo familia ya Amr  ibn Hazm ikaja kwa Mtume wa Allaah na kusema: “Sisi tunayajua maneno  ambayo tunayatumia kuponeshea maumivu ya kung’atwa na n’nge, lakini wewe umeyakataza.”  Wakatamka maneno hayo ya tiba mbele yake, naye akasema, “sioni ubaya wowote wa jambo hili. Yeyote kati yenu anayeweza kumsaidia nduguye afanye hivyo.” (Muslim)

Auf ibn Malik Al-shja’ii naye kasimulia hivi: “Tulifanya tiba katika zama za ujahili na tukasema, “Ewe Mtume wa Allaah! Nini rai yako kuhusu jambo hili?” Akasema, ‘hebu nifahamisheni tiba yenu’ Na kisha akasema, ‘hapana ubaya katika tiba ambayo haihusishi shirki (ushirikina).” (Muslim).

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakuzikataa Aina za tiba zilizokwishakuwepo katika zama za ujahili wala

Misingi Minne Muhimu Katika Uislamu

Feature

Kikokotoo (Calculator) Cha Zakkah

Log in

user_login_block

Tuma

Page 25: Tiba kwa ruqya

hakuwaamuru Masahaba wake kuacha kuzitumia. Badala yake upo ushahidi wa kutosha wa Hadith unaoonesha kuwa aliwaruhusu Waislamu kuchambua aina mbalimbali  za tiba zilizokuwepo na kisha kuzikubali zile zisizohusisha mambo ya ushirikina au mambo yaliyoharamishwa ambayo yanaweza kusababisha jambo jingine la haramu.

 

 

Ruqyahh Na Du’aa

 

Ruqyah ni sawa tu na dua. Wakati ambapo  inapendelewa kutumia dua alizotufundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Wanazuoni wa Kiislamu wanakubaliana kuwa pia inajuzu kutumia dua ambazo hakutufundisha.

Sharti la kufanya hivyo ni kuwa dua hizo zisiwe na maneno ya haramu na wala zenyewe zisiwe dua za haramu au zinazokusudia jambo la haramu kama ilivyobainishwa na Hadith za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Anas kasimulia, “Mtu mmoja alikuja huku akihema na akaingia katika safu ya waumini na kusema, ‘Sifa njema ni za Allaah, Ahimidiwe na atukuzwe

Piga Hesabu Za Zakaah Yako Unayotaka Kutoa Kwa Kutumia Kikokotoo (Calculator) Ya Kuhesabu Zakaah Yako

Zingatio La WikiDunia Si Chochote Si Lolote

Zingatio La Wiki

Wakati unayoyoma na hakuna awezaye kuuzuia usiende. Hakuna tofauti nyengine baina yetu na wale waliotangulia mbele ya haki ila ni wakati tu. Hakika wakati ndio unaomfanya mtu kuwa mtoto, kijana au kizee. Haukuwepo wakati na hii ni Neema Zake Muumba. Ni wakati huu ndio unaoufanya mchana ukaondoka kwa kuupisha usiku.

»

Login or register to post commentsEndelea

Page 26: Tiba kwa ruqya

kwa wingi.’ Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipomaliza Swala akauliza, ‘ni nani miongoni mwenu aliyetamka maneno haya?’ Watu wakanyamaza kimya. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akauliza tena, ‘nani kati yenu aliyetamka maneno haya?’ Mtu huyo akasema, ‘hakuna ubaya’. Halafu akasema, ‘nilikuja huku nikiwa na tatizo la kupumua, kwa hiyo nikatamka maneno hayo.’ Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akajibu, ‘niliona Malaika kumi na wawili wakiangaliana kuwa nani kati yao ayachukue maneno hayo kuyapeleka kwa MwenyeziMungu.’ (Muslim)

Ule ukweli kuwa jamaa aliyetamka maneno hayo alinyamaza pale Mtume alipouliza swali mara ya kwanza, unaonesha kuwa alidhani kafanya kosa katika dua yake na akachelea kuwa huenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) asingeyaridhia yale aliyoyasema. Kwa hakika maneno haya ya mtu huyo yakaja kuwa mfano wa dua zinazokubalika ambazo zinampendeza Allaah Taala.

Ingawaje inajuzu kuomba dua za aina hii ambazo hazikutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), lakini kama ilivyoelezwa, zisiwe na maneno ya haramu, zisisababishe jambo

Page 27: Tiba kwa ruqya

la haramu, kama vile kuacha kabisa dua ambazo zimetoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Ni bora zaidi kufuatisha dua alizotufundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)]. Itazame Hadith hii ambayo inalibainisha jambo hili barabara.

Abu Hurayrah kasimulia kuwa Bedui mmoja aliingia msikitini wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipokuwa amekaa. Kisha Bedui huyo akaswali rakaa mbili za Sala na kusema, ‘Ewe MwenyeziMungu, Mrehemu Muhammad na Unirehemu mimi na Usimrehemu mwingine yeyote pamoja nasi’. Mtume (SalAllaahu alaihi wasalam ) akasema, “umelifinya jambo hilo (yaani umezifinya Rehema za Allaah) ambazo ni pana (nyingi) zaidi. (Ahmad na Abu Daawuud).

 

 

Aina Mbili Za Ruqyah

 

1. Ruqyah halali: Hii ni aina ya Ruqyah aliyoitumia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Ruqyah hii inajumuisha yafuatayo;  kuomba dua zinazojuzu na kupuliza mikono na kuiparazia (kuipitisha) katika

Page 28: Tiba kwa ruqya

sehemu ya mwili iliyodhurika kama ilivyobainishwa na aya za Qur-aan na Hadith Sahihi lakini pasina kutia nyongeza yoyote na bila kufanya jambo hilo kiajabu-ajabu (kiuganga-uganga).

2. Ruqyah haramu: Hii ni Ruqyah inayojumuisha maneno ya kishirikina, mauzauza (mayakayaka), au jambo lolote lilliloharamishwa katika Uislamu.

 

Ruqyah Halali

Ibn Hajar kasema, “Wanachuoni wa Kiislamu wanaafikiana kuwa Ruqyah ni halali maadam itimize masharti matatu:

Mosi, yatumike maneno ya MwenyeziMungu (yaani Qur-aan) ikiwa ni pamoja na Majina au Sifa Zake.

Pili, Ruqyah ifanywe kwa Kiarabu kinachoeleweka au hata kwa maneno ya lugha nyingine yanayoeleweka.

Tatu, wale wanaofanya Ruqyah lazima wawe waumini wenye yakini kuwa si ponyo   linayoponya bali Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndiye anayesababisha ponyo kuponya. (Taz. Fath Al-Barii).

Na kuhusu dua au maombi,

Page 29: Tiba kwa ruqya

nayo ni halali maadam tu yasikiuke au kupingana na mafundisho ya Uislamu wala yasipelekee katika shirki. Kama ni kufanya Ruqyah kwa dua ambazo hakufundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), basi pasiwe na maneno ya ajabu-ajabu, wala isifanyike kiuganga-uganga kama wafanyavyo wanamazingaombwe au waganga wa kienyeji.

 

 

Ruqyah ya maneno yasiyoeleweka, (maneno ya kupandisha mzuka) haifai kwani inaleta mambo ya bidaa na inaweza kuhalalisha kazi ya waganga  matapeli wa kienyeji. Kwa sababu hizi, kuelewa maana ya Ruqyah ni sharti la lazima katika kuitumia. Ikiwa ni hatua ya tahadhari, Ruqyah ya maneno yasiyoeleweka imeharamishwa.

Ibn Qudaamah kasema, “Imam Ahmad alifahamishwa na mtu mmoja kuhusu mtu mmoja aliyedai kupoza uchawi kwa kuweka maji kwenye chungu na kusema maneno yasiyoeleweka pamoja na mambo mengine. Ndipo Imam Ahmad, kwa kutoliridhia jambo hili, akamshika mkono mtu huyo na kusema, “mimi silijui jambo hili (la kipuuzi)” (Al-Kafii).

Page 30: Tiba kwa ruqya

Al-Bajii kasema, “Imam Malik aliona kuwa kutumia kifimbo cha chuma na chumvi wakati wa kufanya Ruqyah ni jambo la kuchukiza (makruhu) na kutumia vifundo na nyuzi ni jambo la kuchukiza zaidi.” (AlMuntaqa, Sharh Al-Muwatta).

Wanazuoni wengine wamekataa matumizi ya hirizi na visu na mambo mambo mengine kama vile kuuchanja chale mwili wa mgonjwa, hayo ni mambo yaliyoigwa kwa wachawi.

Muislamu lazima awe makini mno juu ya mambo haya na mara zote arejee katika Qur-aan na Sunnah pale anapokutana na jambo geni ili aone kama jambo hilo ni halali  kabla hajalifanya.

Mambo tata ambayo hayana ushahidi wa Qur-aan na Sunnah yakataliwe, la sivyo yanaweza kuwapelekea baadhi ya watu kuingia katika uchawi na uganga mbali ya kuwachanganya wale wasio na elimu ya kutosha.

Kuhusiana na uchawi MwenyeziMungu Anasema,

“Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani katika ufalme wa Suleiman; na Suleiman hakukufuru bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi  ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta katika (mji wa) Babil.

Page 31: Tiba kwa ruqya

Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yoyote mpaka wamwambie: “Hakika sisi ni mtihani basi msikufuru.” Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo walimfarakanisha mtu na mkewe. Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya MwenyeziMungu. Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa yakini wanajuwa kwamba aliyekhiyari haya hatakuwa na sehemu yoyote Akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wangelijua (2:102).

Kuhusiana na aya hii, Ibn Taymiyya anasema, “Wale (wanaofanya uchawi) wanajuwa fika kuwa hautakuwa na manufaa Akhera na kwamba wale wanaoufanya watakuwa miongoni mwa watakaopata hasara, lakini bado wanavutwa na maslahi yake katika dunia hii.” (Iqtidhaa’ Assirat Al-Mustaqiim).

Ar-Rabii  naye kasema, ‘nilimuuliza Imam Shafii kuhusu Ruqyah naye akasema, “Hakuna ubaya kufanya Ruqyah kwa kusoma Kitabu cha MwenyeziMungu na (kwa kutumia) aina zozote za dua anazozijua mtu...’ (Irshad As-Sarii).

Kwa hiyo mtu ajiepushe na utatanishi na badala yake aende kwenye msingi wa

Page 32: Tiba kwa ruqya

Ruqyah, ili kujua Ruqyah ni nini hasa. Kwamba Ruqyah ni njia ya kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa utaratibu sahihi wenye ikhilasi na Imani thabiti kwa Allaah.

 

Inaendelea .../4

 

Ruqyah Haramu

»

Login or register to post comments Email this page Chapisha

Rudi Juu

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Website hii imetengenezwa kuangaliwa vizuri zaidi katika resolution 1024 kwa 768 www.alhidaaya.com

Page 33: Tiba kwa ruqya

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Sha'abaan 22, 1431.

Soma Qur-aan Neno

Kwa Neno Hukmu Za

Tajwiyd Qur-aan Hadiyth Duaa - Adhkaar 'Aqiydah-

Tawhiyd Fiqhi Ramadhaan-

Swawm Swalah Zakaah Hajj Nasiha za

Ijumaa Zingatio Makala Maswali-Majibu Visa Familia-

Wanawake Mapishi Vitabu Flash Mashairi

Sikiliza Quraan

Nyumbani

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 4 Malipo ya fedha kwa ajili ya kufanya Ruqyah

'Aqiydah-Tawhiyd

 

(Na Fat-hi Al-Jundiy)

Imefasiriwa na Ummu Ashraf

 

 

Je Ni Halali Kutoza Au

Yanayohusiana Utaratibu Sahihi

Wa Kufanya Ruqyah - 3 - Tiba Enzi Za Ujahili Na Aina Mbili Za Ruqyah

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 1 Tiba Kwa Njia ya Qur-aan na Sunnah

Utaratibu Sahihi Wa Kufanya Ruqyah - 2 Tiba Ya Jicho la Husda Na Uchawi

Kujitupa Kwa Mwenyezi Mungu (Ta’alluq Billah)

'Aqiydah Yetu Hivi Leo

Kufuru Na Aina Zake

Mambo Yanayomtoa Mtu Katika Uislam

Mfululizo Wa Mada Ya Majini (3)

Mfululizo Wa Mada

Tafuta Ndani Ya Alhidaaya Tafuta search_theme_fo a0b9f5fb024b732

Page 34: Tiba kwa ruqya

Mawaidha Du'a Na

Adhkaar English Lecture

Tazama Swahili Video Learn the

Arabic Language

User loginUsername: *

Password: *

Create new account

Request new password

Pokea Makala

Jaza anuani yako ya barua pepe (e-

mail) uweze kupokea

Makala zetu

Jiunge uanachama

Jitoe uanachama

Kupokea Malipo Ya Ruqyah?

 

Qur-aan na Sunnah zinakemea isirafu ya fedha lakini ni watu wachache mno wanaozingatia makemeo hayo, hii yote ni kwa sasabu ya huba ye fedha waliyopandikizwa wanadamu.

Mbwa mwitu wawili wenye njaa waliotumwa kumwinda kondoo hawaleti madhara makubwa kulinganisha madhara yanayoipata dini kutokana na tamaa ya mali aliyonayo binadamu.” (Ahmad na At-Tirmidhiy).

Yahya ibn Muath kasema, “pesa ni kama nnge, kama hustahiki, basi usiichukue, kwani ikikutafuna,  kwa hakika sumu yake itakuua” Alipoulizwa ni kwa vipi mtu anastahiki, akajibu, ‘Ni kuichukua kwa kutumia njia halali na kuitumia katika njia sahihi.’ Pia akasema, ‘Mwanadamu atafikwa na misiba miwili akiwa na fedha katika sakaratimauti’. Alipoulizwa ni ipi misiba hiyo, akajibu, ‘Fedha zote zitachukuliwa kwake na ataulizwa kuhusu fedha zote hizo. (Mukhtasari Minhaj Al-Qasidiin) 

Wanazuoni wa Kiislamu wanakubali kuwa ni halali kuchukua fedha kwa kufanya Ruqyah. Hata hivyo, baadhi ya

Ya Majini (9)

Pepo 'Al-Jannah'

Feature

Kikokotoo (Calculator) Cha ZakkahPiga Hesabu Za

Log in

user_login_block

Tuma

Page 35: Tiba kwa ruqya

wanazuoni wanasema kuwa ni bora zaidi kutopokea malipo yoyote zaidi ya malipo ya MwenyeziMungu.

Hapa lazima tutofautishe kati ya mtu anayetoza fedha na mtu anayepewa fedha bila kuiomba. Umar ibnul-Khattab kasimulia hivi: “Mtume wa Allah alikuwa na kawaida ya kunipa kitu lakini mimi nikawa namwambia, “si ungempa mtu masikini na mwenye kuhitaji zaidi kuliko mimi?’ Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akaniambia, ‘kama unapewa kitu fulani bila kukiomba au bila ya kuwa na tamaa nacho, basi kichukue na kama hukupewa basi usikikimbilie (usikipupie)’. (Al-Bukhaariy).

Lakini haina maana kuwa mtu apokee malipo ya Ruqyah kutoka kwa watu ambao yeye anajuwa wako katika hali ngumu ila wanalazimika kutoa malipo ili kuepuka aibu. Katika mazingira haya ni kheri kuepuka kuchukua malipo hayo hasa hasa kama mtu anayefanya Ruqyah hana shida sana na malipo hayo.

Kuna ushahidi unaothibitisha kuwa malipo ya Ruqyah yatolewe iwapo mgonjwa amepona kabisa ugonjwa wake. Kwa maneno ya Abdul Barr  ‘...malipo ya kitu ambacho hakileti tija yoyote ni dhuluma

Zakaah Yako Unayotaka Kutoa Kwa Kutumia Kikokotoo (Calculator) Ya Kuhesabu Zakaah Yako

Zingatio La WikiDunia Si Chochote Si Lolote

Zingatio La Wiki

Wakati unayoyoma na hakuna awezaye kuuzuia usiende. Hakuna tofauti nyengine baina yetu na wale waliotangulia mbele ya haki ila ni wakati tu. Hakika wakati ndio unaomfanya mtu kuwa mtoto, kijana au kizee. Haukuwepo wakati na hii ni Neema Zake Muumba. Ni wakati huu ndio unaoufanya mchana ukaondoka kwa kuupisha usiku.

»

Login or register to post commentsEndelea

Page 36: Tiba kwa ruqya

na haramu” (At-Tamhiid).

Hii ni kinyume kabisa na vile wafanyavyo  ‘waganga’ wengi hivi leo ambao hutoza malipo ya kazi zao bila kutibu ugonjwa. Wengine wanazo kliniki na hospitali kabisa kupokea wagonjwa na kutoza malipo tofauti ya huduma kama vile malipo ya kufungua faili, kumuona daktari na malipo ya kusomewa Ruqyah!

Watu wamefanya hii ndio shughuli yao maalum wakiwahadaa watu wenye matatizo kuwa wao ni watu waliojaaliwa uwezo wa kutibu na kuponya. Kwa kuwa watu hawa hujipa haiba ya kuonekana kama ni watu wenye elimu kubwa ya dini, basi huweza kuwavuta watu wengi wenye matatizo.

 

 

Je Ruqyah Inaweza Kuwa Kazi Ya Kudumu?

 

Kwa kuangalia historia ya Mtume, historia ya Maswahaba na wanazuoni wachaMungu ambao wanafahamika kwa elimu yao ya dini, na kwa kazi waliyoifanya kwa jamii ya Waislamu, tutaona kuwa hakuna hata mmoja kati yao

Page 37: Tiba kwa ruqya

aliyejiajiri kutibu wagonjwa kwa njia ya Ruqyah.

Na wala hakuna yeyote miongoni mwao aliyekifanya kisomo cha Ruqyah kuwa ndiyo shughuli au kazi yake na kutambulika rasmi kwa kazi hiyo. Hakuna ubishi kuwa magonjwa yalikuwa mengi katika kila zama, lakini hakuna ushahidi  wowote kuwa Khalifa yeyote aliwahi kuteua “wasomaji wa Ruqyah” ili kuwasomea wagonjwa kama vile alivyoteua Mahakimu.

Kwa maana hiyo,  ni muhimu kwa mgonjwa  kujisomea mwenyewe na kama akipata mtu mwenye ilimu ambaye ni mwaminifu na mchaMungu, si vibaya kumuomba amfanyie Ruqyah huku na yeye mwenyewe akishiriki kiimani na si kubweteka tu ‘asomewe’ na kubakia na imani potofu kuwa kisomo ndicho kinachomsaidia badala ya MwenyeziMungu. 

Watu wanaofanyiwa Ruqyah bila ya wao wenyewe kuwa na imani wako katika hatari ya kuangukia katika shirki ya kuwategemea wale wanaowafanyia hiyo Ruqyah badala ya kumtegemea MwenyeziMungu.

Inafahamika kuwa matendo halali, wakati mwingine, huharamika iwapo yanafanywa kwa utaratibu unaopingana na

Page 38: Tiba kwa ruqya

mafundisho ya Sharia. Lau kungelikuwa na kheri katika kufanya kazi ya kudumu katika fani ya tiba ya Ruqyah basi basi sote tungeshindana kufanya kazi hiyo.

Tumalize makala hii kwa nukuu hii kutoka  kitabu kiitwacho, Sincere Devotion cha Mwandishi Saddiiq Hassan Khan;

Matendo yote na maombi yote ya kutibu ugonjwa yanajuzu kufanyika iwapo maneno yanayotumika yanatoka katika Qur-aan na Sunnah au kama maneno hayo yanatoka kwa wachaMungu wa jamii za nyuma za Waislamu ambayo yameepukana na shirki . Lakini kinyume chake mambo hayo huwa haramu na husababisha ushirikina.

Vipo vitabu vingi vinavyohusiana na Ruqyah lakini muumini anashauriwa kutafuta mambo sahihi katika vitabu hivi na kuachana na yale yanayopingana na mafundisho ya Uislamu. Haya ni pamoja na maandiko ya waganga wadanganyifu wanaoandika hirizi. Mambo haya hayafai kabisa.

“Kwa hakika MwenyeziMungu Anawatosha waja watiifu ikiwa hawategemei chochote isipokuwa Yeye na ambao hawatafuti njia nyingine kujitibu ila kwa dua alizofundisha

Page 39: Tiba kwa ruqya

Mtume (Salallahu alaihi wasalam) na tiba halali. Yeyote anayejiepusha na mambo ya shaka huitakasa dini na kuipamba heshima yake lakini yule anayejiingiza katika mambo ya shaka hujitumbukiza katika jambo la haramu. Kwa hiyo, shirki yaweza kufanywa bila kutambua, mtu achukue tahadhari mno ili kuiepuka”. 

 

-Mwisho-

 

  

»

Login or register to post comments Email this page Chapisha

Rudi Juu

Maoni ya wageni Viungo

Wasiliana Na Sisi Kuhusu Alhidaaya

Website hii imetengenezwa kuangaliwa vizuri zaidi katika resolution 1024 kwa 768 www.alhidaaya.com