259
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 18 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Migugo na Uvuvi, kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali tutaanza na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Mwantakaje Haji Juma, Mbunge wa Bububu sasa aulize swali lake.

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795577-18 MEI 2017.pdfuundwaji wa Kamati za kukabiliana na majanga katika ngazi ya Halmashauri

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 18 Mei, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati ifuatayo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI:

Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Kilimo, Migugo na Uvuvi, kwa Mwaka wa Fedha2017/2018.

NAIBU SPIKA: Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswalitutaanza na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa MwantakajeHaji Juma, Mbunge wa Bububu sasa aulize swali lake.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

Na. 229

Tatizo la Shule na Mabweni Kuungua Moto

MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA aliuliza:-

Kumekuwa na wimbi la mabweni na hata shulekuungua moto, hususan Tanzania Bara.

Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti hali hiyo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi Ofisi ya Rais TAMISEMI naomba kujibu swali la MheshimiwaMwantakaje Haji Juma, Mbunge wa Bububu, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kulikuwa na wimbila shule kuungua moto na mwaka 2016 pekee kuanzia mweziJanuari hadi Disemba nchi ilikuwa na janga kubwa lakuunguliwa na shule za sekondari 29, zikiwemo mbili zisizoza Serikali na shule za msingi mbili ikiwemo moja isiyo yaSerikali.

Matukio hayo yalitokea mfululizo na hata shulenyingine kukumbwa na tatizo hilo zaidi ya mara moja. Mbayazaidi, katika mwezi wa Agosti, 2016 kasi ya matukio ya shulekuungua moto iliongezeka ambapo kati ya tarehe Mosi hadi12 Agosti, 2016 jumla ya shule za sekondari za Serikali tanoziliungua. Tumeshukuru Mungu mwaka 2017 matukio hayaya moto hayajatokea tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa hakuna uhakikawa chanzo halisi cha matukio haya moto yanayojitokeza.Hata hivyo, inadhaniwa kuwa chanzo cha moto hususankatika shule kongwe ni hitilafu ya umeme iliyotokana nauchakavu wa miundombinu na hujuma kutoka kwa watuna vikundi visivyo na nia njema.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Mheshimiwa Naibu Spika, majanga ya moto katikashule zetu yanaweza kudhibitiwa ikiwa wote kwa pamojatutashirikiana kutambua na kudhibiti viashiria na vyanzoambavyo huleta majanga hayo. Serikali imetoa maelekezokwa Mikoa, Halmashauri na wadau wengine wa elimu ilikudhibiti majanga ya moto mashuleni ikiwa ni pamoja nauundwaji wa Kamati za kukabiliana na majanga katika ngaziya Halmashauri na katika ngazi za shule husika kwakushirikisha wadau muhimu wa elimu katika ngazimbalimbali.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwantakaje Juma, swalila nyongeza.

MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, je, ni vikundingapi zilizochukuliwa hatua mpaka sasa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya RaisTAMISEMI….

MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, samahani ni shule ngapi zilizochukuliwa hatua mpakasasa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanzanapenda kumshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababuameonesha concern kubwa ya suala zima la janga la motokatika maeneo yetu. Hili nimelisema katika jibu langu la msingitakribani shule 29.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala zima la chanzonani alisababisha imeonekana maeneo mbalimbali ni hitilafuya umeme, lakini bado hatujabaini hasa watu mahsusiambao wameshughulika katika suala la kuhujumumiundombinu hii na ndiyo maana tumeunda Kamati hizi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

shirikishi katika jamii zetu hasa katika ngazi za shule, lengo nikuzuia baadae watu watakapobainika basi tuwezekuwachukulia hatua katika maeneo hayo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Wilfred Lwakatare swali lanyongeza.

MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana. Ningependa kumuuliza MheshimiwaWaziri na kwa niaba ya Serikali, kwamba matukio ya motoambayo yanatokea katika shule, yamekuwa pia yakitokeakatika maeneo mbalimbali yakisababisha maafa makubwa.Lakini tatizo kubwa ambalo limeonekana kuchangia maafakuwa makubwa ni pale ambapo vikosi vyetu vya Zimamotovinapofika kwenye eneo la tukio na vikishafika pale magariyanaonekana yanakuja tu, labda kuja kutembea yanakuwahayana maji na wala hawana vifaa, matokeo yake wakatimwingine wamekuwa wakiambulia kipigo au matusi kutokakwa wananchi wenye hasira kali.

Je, Serikali inasemaje juu ya hili na wamejipangajekuliondoa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi majibu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaNaibu Spika, kunachangamoto nyingi ambazo panatokeamaendeleo na zenyewe zinajitokeza. Kwa mfano, mijiinapokua majengo yanapojengwa, kuna maeneo mengineyanakuwa hayajatoa provision za magari ya kisasa kuwezakufanya kazi ile ya zimamoto.

Kwa hiyo, sasa hivi tunashirikiana na Wizara zinginezinazohusika ili tuweke provison hizo ambazo zitawezeshawenzetu wa zimamoto waweze kufanya hivyo. Lakini pia hilojambo alilolisema lilishajitokeza maeneo mengi tumechukuahatua kuweza kuhakikisha kwamba, magari yanakuwa yakostandby na vitendea kazi vyote vinavyotakiwa kwa ajili yakwenda kuzima moto ili wasije wakafika kwanza halafu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

wakajikuta kwamba walikuwa na upungufu wa vitendeakazivinavyotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumelizingatia na hatatulivyopitisha kwenye bajeti tulilielezea jinsi ambavyotunakiunda upya kikosi kile kiweze kuwa na vitendeakazivinavyostahili kwa ajili ya kukabiliana na matukio ya ainahiyo aliyoyasema. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Wabunge kabla sijamuitaMbunge mwingine maswali ya nyongeza naomba sana yawemafupi kwa sababu Wabunge tuko wengi na kila mtuanaomba nafasi ya maswali. Kwa hiyo, uende moja kwamoja kwenye swali usianze kutoa hadithi ndefu wakatimwenye swali la msingi ameshamaliza. Mheshimiwa RuthMollel.

MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini shule za Serikalihawaweki provision ya kuwa na fire extinguisher ambayoinaweza ikatumika mara tu kama huduma ya kwanzawakati magari ya zimamoto yanaposubiriwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweliukiangalia kesi hizi za majanga ya moto na siyo shuleni pekeyake hata katika maeneo mbalimbali, ni kwa sababu katikakipindi kirefu tulikuwa tumejisahu kuweka fire extinguisher.Ndiyo maana sasa tumetoa maelekezo katika shule zetumbalimbali miongini mwa vitu ambavyo tunatakiwatuviweke viwe vya msingi ni suala la fire extinguisher. Hatahivyo, katika ujenzi wa mabweni yetu, zamani mabweniyalikuwa yakifunguka yanafungukia ndani, hata janga lamoto likitokea watoto wanavyogombania kufungua mlangokumbe ndiyo wanazidi kuufunga.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana katika sualala specification tukasema na mabweni yetu sasa hivi yotemilango inafungukia kwa nje ili kwamba inapotokea hatariya moto basi watoto wakiwa wanatoka mlangoni, iwe nirahisi sana kuweza katoka katika eneo lile pindi janga lamoto linapotokea.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni agizo letu na ninaombaniwasihi sana ni waagize Wakurugenzi wote katikaHalmashauri zetu kuhakikisha katika maeneo ya shule zetuzote zinakuwa na fire extinguisher as a back up strategy,endapo moto unapotokea, wakati unasubiria kupata magariya kuzima moto yaje, tuwe na mbinu mbadala wa kuwezakudhibiti moto mapema zaidi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwamoto.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi nami niulize swali.

Kwa kuwa ukiangalia shule nyingi zilizoungua, chanzokikuu huwa ni vibatari au mshumaa, hii ni kwa sababu yakukosekana kwa umeme; kwa kuwa Serikali imeshatoamaelekezo kwamba kila sehemu yenye taasisi kama shulena sehemu nyingine muhimu umeme upite, lakini mpaka leobaadhi ya sehemu wamekosa haki hiyo ya kupelekewaumeme. Je, Serikali inasemaje?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati naMadini.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaNaibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tu kwambashule zote katika Halmashauri zote kwa nchi nzimatumeshaanza sasa kuchukua stock taking kuona shule zamsingi na sekondari ambazo zimekamilika ili zipelekeweumeme kupitia mradi wa REA ambao umeshaanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuondoe wasiwasiMheshimiwa Mbunge na nimhakikishie kwamba Halmashauri

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

zote kwa kutumia nafasi hii, Wakurugenzi wote ambaohawajafanya hivyo niwaagize wafanye hivyo ili mradiutakapofika waweze kupitishiwa umeme haraka sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Amina Mollel swali fupi.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kuniona.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa Mikoa iliyoathirikana tukio hili la uchomaji wa shule za sekondari, waathirikawakubwa ni wanafunzi. Ningependa tu Waziri atufahamishekwamba ni hatua gani za haraka zinazochukuliwa na Serikalikatika kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaendelea namasomo badala ya kuziacha shule hizo kwa muda mrefupasipo kupewa msaada wowote na badala yake niwananchi ndiyo wanaojitolea na wasamaria wema.Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mkoawa Arusha ni miongoni mwa Mikoa ambayo ilipata janga lamoto. Tukumbuke kwamba janga hili liliikumba maeneombalimbali. Bahati nzuri unafahamu wewe ni mwenyeji waMkoa wa Mbeya, shule yetu ya Iyunga, Mbeya kulikuwa nasintofahamu kubwa sana, lakini ni nini tumekifanya katikamaeneo mbalimbali. Tulichokifanya kama Serikali si kwambaSerikali i l ikuwa inaangalia hivi na kuacha, hapana.Tumefanya harakati maeneo mbalimbali hasa kutumiaHalmashauri husika na ngazi Mikoa na Serikali Kuu. Ndiyomaana wanaofahamu kama mashahidi katika Mkoa waMbeya, shule ya Iyunga na mimi nilikuwepo site moto uleulivyokuwa umewaka pale, tumefanya kazi kubwa sana shuleyote ya Iyunga pale imebadilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, shule ya Mpwapwa kwaMzee wangu Mheshimiwa Lubeleje nimefika pale site hivi sasa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

bweni tunamaliza kulipaua. Pia maeneo mbalimbali harakatihizi zinaendelea, lakini tunaenda awamu kwa awamu,naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Amina Mollel kwambaKamati yetu ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha bahatinzuri wakati moto unawaka Monduli nilikuwepo pale.Nilienda na nilifanya tathmini hiyo, lengo kubwa ni kwambatutajitahidi kwa kadri iwezekanavyo sehemu yenyemapungufu yote tutashirikiana na jamii husika kuondoa tatizohili la watoto wetu ili wasikose maeneo ya kukaa.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleana Wizara ya Fedha na Mipango, Mheshimiwa KhamisMtumwa Ali, Mbunge wa Kiwengwa sasa aulize swali lake.

Na. 230

Ukaguzi wa Hesabu za Balozi Nje ya Nchi

MHE. KHAMIS MTUMWA ALI aliuliza:-

Taasisi za Muungano zinafanyiwa ukaguzi na Ofisi yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Je, ni mara ngapi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali imeshirikiana na Ofisi ya Mdhibiti naMkaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katikakukagua Taasisi za Ubalozi zilizoko nje ya nchi?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waFedha na Mipango napenda kujibu swali la MheshimiwaKhamis Mtumwa Ali, Mbunge wa Kiwengwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi waHesabu za Serikali imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambapomajukumu ya ofisi hii yameainishwa katika Ibara ya 143(2) yaKatiba hiyo, ambayo inamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi angalau mara moja

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

kila mwaka na kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu zaSerikali, Bunge na Mahakama. Aidha, majukumu hayo piayameanishwa katika kifungu cha 10 cha Sheria ya Ukaguziwa Umma ya mwaka 2008 na Kanuni zake za mwaka 2009.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukaguzi wa Baloziunafanyika chini ya Fungu 34, Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, kwakuwa na Ofisi zote za Ubalozi ni sehemu ya Fungu 34. Hivyobasi, ukaguzi wa Balozi kama ilivyo kwa taasisi nyingine zaMuungano unafanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mdhibiti na Mkaguzi waHesabu za Serikali wa Zanzibar majukumu yake yameanishwakwenye Ibara ya 112(3) ya Katiba ya Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar ya mwaka 1984. Kutokana na maelezo hayo Ofisiya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kilamoja ina mipaka yake ya kufanya ukaguzi. Jukumu la ukaguziwa taasisi za Muungano lipo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania haijawahi kumhusisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukaguziwa Balozi au ukaguzi wowote ule kama wa Umoja waMataifa kwa sababu hakuna ulazima wa kufanya hivyokikatiba na kisheria. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Khamis Mtumwa Ali swalila nyongeza.

MHE. KHAMIS MTUMWA ALI: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri,naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa taasisi hizi za Ubalozi ni taasisi za Muungano

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

je, haoni ipo haja sasa ya kushirikiana na Ofisi ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Zanzibar katikakukagua taasisi hizo?

Pili, kwa kuwa tuna mahusiano mazuri katika taasisihizi za Muungano, yeye Mheshimiwa Naibu Waziri amesemakwamba hajaona ulazima; je, haoni sasa imefika wakati wakushirikiana na kuonesha Muungano wetu huu unadumu nakuondosha kero ndogo ndogo ambazo zinatokezea kamahizi za kutokushirikishana? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha naMipango majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaNaibu Spika, nia ya Serikali yetu na lengo lake kwa Muunganoni kuudumisha Muungano wetu katika kila nyanja, kamaalivyosema Mheshimiwa Rais wetu katika sherehe zaMuungano za mwaka huu 2017 kwamba Serikali yetuinaupenda Muungano na tutaulinda kwa ngazi zote nanguvu zote, hiyo itabaki hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema mwanzojukumu hili la ukaguzi ni la Kikatiba na Kisheria. Ofisi zote zaMuungano hukaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali wa Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, lakini akiona inafaa Mkaguzi huyu anawezakumshirikisha Mkaguzi yule. Tuelewe tu kwamba kikatiba nakisheria siyo lazima, lakini kimahusiano anaweza akafanyahivyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, Ofisi ya Makamu waRais, Muungano na Mazingira.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuongezea katika majibu mazuri kabisayaliyotolewa na Naibu Waziri wa Fedha, kwamba pamojana mgawanyo wa majukumu ya kikatiba na kisheria kuhusumamlaka za ukaguzi maeneo na taasisi zinazopaswa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

kukaguliwa, napenda nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba Wakaguzi hawa na Wadhibiti Wakuu wa Serikalizote mbili wanashirikiana kwa karibu sana katikakubadilishana uzoefu, pia kujenga uwezo wa kitaasisi hasakwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa upande waZanzibar. Hilo ndilo ambalo tunalihimiza na tunalisisitizalamahusiano na ushirikiano wa taasisi za pande zote mbilihata katika masuala ambayo siyo ya Muungano.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ngwali swali la nyongeza.

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa kuwa fedha za Mfuko wa Jimbo hazijawahi kukaguliwaZanzibar na kwa kuwa hakuna utaratibu wowote kwasababu Hazina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezikukagua Hazina ya Zanzibar.

Je, fedha za Mfuko huu wa Jimbo zitakaguliwa linina kwa utaratibu gani? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais– TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, fedha ya Mfukowa Jimbo uko utaratibu kwamba hizi zinazoingia Bara nazile zinazoingia Zanzibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili waRais Zanzibar, hili kuna utaratibu wa wazi kule Ndugu yanguMheshimiwa Ngwali nadhani tukifanya consultation nawenzetu kutoka Baraza la Wawakilishi tutakuja kuona ni jinsigani wanafanya kule utaratibu mzima wa usimamizi wafedha katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaamini kwamba Barazala Wawakilishi litakuwa linafanya kazi yake kwa mujibu wautaratibu unaotakiwa, ili fedha hizi ziweze kutumiwa kamainavyokusudiwa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea.Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Mheshimiwa Ally Saleh Ally, Mbunge wa Malindi sasa aulizeswali lake.

Na. 231

Haja ya Serikali Kuwekeza katika Michezo Michache

MHE. ALLY SALEH ALLY aliuliza:-

Tanzania imesajili michezo kadhaa ambayo huingiakwenye medani ya Taifa kiushindani lakini kote huwa nimashamba yanayozaa visingizio.

(a) Je, Serikali haioni haja sasa ya kujipinda katikamichezo michache kiushindani Kimataifa?

(b) Je, kama kukiwa na uamuzi huo inaweza kuwamichezo ipi?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waHabari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Ally Saleh Ally, Mbunge wa Malindi, lenyesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imesajili michezombalimbali kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na taratibuzilizopo. Aidha, ili timu au mchezaji aweze kushiriki katikamashindano ya kimataifa kama vile michezo ya Olympic namichezo mingine, lazima awe amefikia viwangovilivyowekwa na mashirikisho ya kimataifa. Serikali inatoamwanya kuibua na kukuzwa kwa vipaji katika michezombalimbali bila upendeleo. Suala la kufanya vizuri katikamashindano linategemeana na viwango vya uelewa,mazoezi, mafunzo na uzoefu katika mchezo husika.

Aidha, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwaSerikali inatoa msaada wa hali na mali kufanikisha timu ama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

mchezaji aliyefikia viwango kushiriki michezo ya Kimataifaikiwa taarifa na taratibu zinazingatiwa tangu ngazi za awali.Kitendo cha kuchagua michezo kadhaa kinaweza kupelekeakupoteza vipaji ambavyo havijavumbuliwa na kukuzwakufikia kushiriki mashindano kitaifa na kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo Serikali itaendeleakuhamasisha michezo yote kupitia vyama vya michezo kwasababu kila mchezo unaweza kushiriki kiushindani. Hii inasaidiakutoa fursa kwa wanamichezo wenye vipaji tofauti kuwezakushiriki katika michezo ya kimataifa.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, maoni ya MheshimiwaMbunge ni mazuri kwa maana ya kujikita katika michezo ileambayo tunadhani itaweza kusaidia Taifa kufanya vizurikatika ushindani kimataifa, hili litawezekana kwa kusaidiatimu ama mchezaji aliyefuzu, kwani katika hali halisi huwezikuamua kuwa huu ndio mchezo unaoweza kufanya vizuribila kupata viwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, niseme kuwa kwasasa bado utaratibu huu hatujaanza kuutumia na kwa hiyosio rahisi kujua ni michezo gani kwani kila mchezounaandaliwa kwa kufuata taratibu na viwango husika namatokeo mazuri yanapatikana kwa kuibua na kukuza vipaji.Kwa kuchagua michezo kadhaa tutakatisha tamaa ukuajiwa vipaji katika michezo mingine. Lakini bado iko fursa kamawadau kufanya upembuzi wa kina na kuja na maoni juu yamichezo gani tuipatie kipaumbele kwa manufaa ya Taifa.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh Ally swali lanyongeza.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwamba katika halihalisi inavyoonesha kwamba Tanzania haijawahikuwakilishwa nje ya michezo ya kuogelea, mpira wa miguu,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

riadha, ngumi katika ile michezo ambayo huwa inatakaqualifications, lakini moja ya tatizo kubwa ni choice yamichezo yenyewe na pili ni ufadhili wa michezo yenyewe.Mimi siamini kwamba Serikali ndiyo isimamie kufadhili michezokwa sababu ina-priority nyingi.

Je, Waziri haoni kwamba wakati umefika sasa kujana mwongozo au sera ya namna ya corporate Tanzaniakuchangia katika michezo? Kwa mfano Uingereza Britishlottery ndiyo inayodhamini Olympic system nzima yaUingereza. (Makofi)

Swali la pili, ipo michezo ambayo kwa gharama zakena kwa uenezi wake ni rahisi sana kuenea, mchezo chessinvestment kubwa wanayotaka ni chess board ambayo in-cost labda dola sita au dola saba, baada ya hapo ni kuwa-train tu watoto au vijana.

Je, Serikali inaweza kushaurika kwamba huu ni mmojakati ya mchezo ambao unaweza kuwa kipaumbele katikaTaifa, kwa sababu hauna gharama na kwa sababu unawezaukaenea katika hali ya haraka katika nchi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, majibu.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanzanichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Ally SalehAlly kwa jinsi alivyo mdau mkubwa katika maendeleo yamichezo na amekuwa akichangia sana sana masuala yamichezo katika Bunge hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lake la kwamba kunamichezo ambayo haijawahi kuwakilishwa Kimataifa, nitoemfano tu kwamba kwa mchezo wa kuogelea nchi yetuimeshawahi kuwakilishwa, kuna vijana ambao walishawahikwenda Canada na wakaiwakilisha nchi yetu, tuliwapabendera na mmoja alishika namba nne, lakini pia hatariadha, walishawahi kuwakilisha nchi yetu kimataifa na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

mmojawapo ni Simbu na anamfahamu. Ndugu Simbuameshawahi kutuwakilisha Kimataifa na Serikali huwainatenga bajeti kwa ajili ya hawa, lakini hatua za awali huwazinafanywa na Tanzania Olympic Committee ambapoinawaandaa wale wachezaji na fedha zinatoka OlympicKimataifa na wanapofuzu sasa kushiriki mashindano yaleKimataifa ndipo Serikali inapowawezesha. Mwaka 2016/2017Serikali ilitenga fedha na wanariadha wetu waliwezakuiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olympic.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mwongozo waushiriki wa sekta binafsi tunakubaliana na hilo lakinitunakwenda hasa na sera kwa sababu, sera yetu inatutakakusimamia michezo sio tu kwa kuegemea kutambulikaKimataifa, tunasimamia michezo kwa madhuminimbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kuimarisha afya,afya ya Watanzania kwa ujumla, pia kudumisha amani,umoja, mshikamano na upendo, vilevile kuhakikishakwamba tunatambulika kimataifa kama anavyosema nakumjenga Mtanzania kuwa jasiri, kukabiliana na matatizombalimbali. Kwa hiyo, yako masuala ya msingi ambayoyanatupelekea Serikali kusimamia michezo.

Kwa upande wa mchezo anaoupendekeza wa chesskatika swali lake la pili, tunapenda sana kutoa wito kwawananchi wote kwa wananchi wote kwamba pale ambapokuna michezo wanayoiona ni mipya na inafaa kuingizwakatika sekta ya michezo na hasa katika shule za msingi nasekondari, ili wanafunzi wetu waweze kujifunza, tunahimizakwamba wananchi kama hao, Walimu ambao wanawezakufundisha michezo hiyo wajitokeze ili waweze kufundishakwa sababu, Azimio la Michezo la Umoja wa Mataifa lamwaka 1978 linahimiza wananchi wafanye ile michezowanayoiweza, michezo wanayoipenda, michezo ambayowana amani nayo. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Grace Kiwelu swali lanyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Timu yetu ya Serengeti imeendelea kufanyavizuri huko ilipo, ningependa kujua Serikali imetenga kiasi gani,kwa ajili ya kuisaidia timu yetu hii ili iweze kufanya vizuri nakurudi na kombe hapa nchini? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, majibu.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kwanzakwa kumpongeza sana Naibu Waziri kwa kujibu maswali vizurisana. Ninataka tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba timu hii ya Serengeti haijaibuka tu, tumeanza nayomiaka mitatu iliyopita, kwa kushindanisha vijana wa chiniya umri wa miaka kumi na tano, tukapata timu bora,tumeilea hiyo timu na kuhakikisha kwamba inashiriki kwenyemashindano ya kimataifa kabla ya hizi mechi 22 ambayohaijapata kutokea toka historia ya nchi hii, yote hii huu niuwezeshaji na uwekezaji wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka nisisitize kwambafigure kamili yaani ni kiasi gani tumetumia kama Serikalitutaiandaa tumpe Mheshimiwa Mbunge, lakini Serikaliimejitoa kwa hali na mali kuhakikisha kwamba timu hiiinatuletea ushindi katika mashindano haya. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zainab Katimba swali lanyongeza.

MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa fursa hii niulize swali la nyongeza.

Kwa niaba ya vijana wote wa Tanzania ambaowanaweza kuwa wanufaika wakubwa sana wa michezonaomba kuuliza swali la nyongeza lifuatalo:

Je, Serikali haioni umuhimu wa kwamba ni wakatimuafaka wa kuwa na shule maalum kwa ajili ya kukuza vipajikatika michezo kama sports academy? (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, majibu.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwakunipa nafasi. Ninampongeza kwa kuwatetea vijanakimichenzo, kama alisikiliza vizuri hotuba ya MheshimiwaWaziri wakati akiwasilisha bajeti yake ya mwaka 2017/2018ni kwamba tumedhamiria. Serikali sasa hivi imekwishatengashule takribani 55 ambazo ziko katika Mikoa yote ya Tanzania,hizi ndizo ambazo tutazichukulia kama ndizo academy zetu.Vilevile michezo ya UMISETA, michezo ya UMITASHUMTA itasaidiasana kuibua vipaji, hata hivyo tunashirikiana sana na Wizaraya Elimu kuhakikisha kwamba michezo inafundishwa katikangazi zote za elimu tangu awali, sekondari na vyuoni.Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maria Kangoye swali lanyongeza.

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza nakwa niaba ya vijana wa Kitanzania ningependa kujua ni liniSerikali itarudisha programu ya michezo katika shule zetu zasekondari na msingi? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais– TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kamaalivyozungumza Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza katikasuala zima la shule hizi, juzi tumezindua michezo ya UMISETAhapa rasmi, bahati nzuri Kitaifa tumezindulia hapa Dodoma,tuna shule zipatazo 55.

Hata hivyo, tumetoa maelekezo maalum kwa Ofisiza Mikoa yote sasa programu ya michezo sasa imeishaanzakurudi mashuleni na tumetoa maelekezo kwamba MaafisaMichezo wote waweze kuwezeshwa katika Mikoa yote na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

katika Halmashauri zote ili kuhakikisha kwamba tunaibuavipaji katika michezo ya watoto wa shule za msingi na watotowa shule za sekondari.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbungenaomba nikuhakikishie kwamba Serikali imeshalichukua sualahili na sasa liko katika utekelezaji. Tunawashukuru sanawenzetu wa CocaCola ambao mwaka huu wanafadhilimichezo hii ya UMISETA hapa Tanzania, nayo imeishaanzavizuri na tunashukuru sana kwa kweli. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fredy swali fupi.

MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa fursa niweze kuuliza swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wewe ni miongoni mwawatu ambao ni washabiki na wapenzi wa ngoma za asili,pamoja na kwamba wewe ni mpenzi wa ngoma za asili,hata huku Dodoma kuna ngoma za asili zinaitwa Chigogo.

Je, Serikali imejipangaje kuwezesha wale woteambao wanaanzisha ngoma za asili katika mashindanohayo? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Mawaziri sioni mtuanayetaka kusimama, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, majibu.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Swalilake liko nje ya michezo, lakini liko ndani ya Wizara yetu ningoma za asili.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendeleakuhamasisha wananchi wote waendelee kuenzi ngoma za

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

asili, hata vyombo vya habari tunavihamasisha ili viwezekupiga ngoma za asili katika vipindi vyake kwa zile asilimia60 za local content ambazo zimepewa. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, majibu.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongezeMheshimiwa Naibu Waziri kwa kujibu vizuri hilo swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hiikukupongeza wewe binafsi kwa ubunifu, ujasiri na uthubutukuanzisha mashindano ya ngoma zetu za utamaduni katikaUkanda wa Kusini.

Mheshimiwa Naibu Spika, lilivyoanza hili WaheshimiwaWabunge ilikuwa kwa Wilaya mbili tu, Wilaya ya Rungwe naKyela sasa imepanuliwa zaidi kuhusisha Mkoa mzima na Mikoaya jirani. Ninatoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge wotekatika maeneo yenu tusisubiri Serikali ianzishe hayo, hebutufuate mfano alioutoa Naibu Spika, wote tuanzishe hayomashindano. Sisi kama Serikali tutasaidia kuboresha hizongoma zetu za utamaduni. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,Mheshimiwa Susan Anselm Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum,sasa aulize swali lake.

Na. 232

Sera ya Elimu ya Mwaka 2014

MHE. SUSAN A. J. LYIMO aliuliza:-

Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inaeleza wazi kuhusumitaala na utaratibu wa masomo katika elimu ya msingi(kidato cha kwanza - nne) na inasema watoto wa kidato

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

cha kwanza – pili watasoma masomo yote ya sayansi nawanapoingia kidato cha tatu watachagua masomowayatakayo kutokana na uwezo wao.

(a) Je, Waziri alipata wapi mamlaka ya kutangazakuwa vijana wote wa elimu ya msingi hada kidato cha nnekusoma masomo yote ya sayansi?

(b) Je, kuna utafiti gani uliofanyika na matokeokuonesha haja ya vijana wote kusoma sayansi yaani kemiana fizikia?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali laMheshimiwa Susan Anselm Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya Pili kipengelecha 4(1) na 5(f) cha Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 iliyofanyiwamarekebisho mwaka 1995 inampa Mamlaka Waziri mwenyedhamana ya Elimu kutangaza jambo lolote lenye maslahikwa Taifa kutokana na hali halisi iliyopo kwa wakati huo.Kwa sasa kuna haja kubwa ya kuhamasisha ongezeko lawanasayansi kulingana na hali halisi ya mahitaji. Kwa mfano,kuna upunfufu wa walimu wa sayansi na hisabati 24,716,upungufu wa walimu 355 wa masomo ya ufundi katika shuleza sekondari za ufundi na mafundi sanifu wa maabara washule takribani 10,000. Moja ya jukumu kuu la Waziri nikuhamasisha wanafunzi katika elimu ikiwa ni pamoja nakuchukua masomo ya sayansi.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katikasehemu (a) taarifa mbalimbali zikiwemo za kimazingira halisi(evidence based) zinathibitisha juu ya upungufu wa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

wataalam wa sayansi, mfano kwa upande wa afya, ilikupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifunguainatakiwa kina mama hao wahudumiwe na matabibuwenye ujuzi lakini hawapo wa kutosha, Wizara imekuwaikihamasisha wanafunzi kuchukua masomo ya Sayansi ilikupunguza tatizo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojiahaijatoa waraka wowote unaowataka wanafunzi wotekusoma masomo ya sayansi, badala yake imejikita katikakuimarisha miundombinu ya maabara, vifaa vya kufundishiana kujifunzia na kupeleka walimu wa sayansi shuleni.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Lyimo swali lanyongeza.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikitishwa sana namajibu ya Wizara. Suala kwamba tuna wataalam wachachewa sayansi, sikubaliani nalo kwa sababu hivi karibuni tuMheshimiwa Rais alikuwa ameishatoa kibali madaktari wetu500 kwenda kufanya kazi nchini Kenya. Vilevile tunatumbuakwamba kuna manesi wengi wako mitaani hawajaajiriwakwa sababu ya kukosa vibali.

Mheshimiwa Naib Spika, kwa hiyo, swali langu lamsingi ninataka kuuliza ni kwamba ni kweli kwambaMheshimiwa Waziri alitoa tamko na mimi nashukuru kwambaumesema waraka bado haujatoa na ninajua kwambagovernment moves with papers. Kwa kuwa masomo yasayansi najua ni muhimu sana na kwa kuwa kwa bajeti yamwaka huu ukiangalia tuna upungufu wa maabara nyingisana, vilevile ili kumfanya mtoto asome sayansi inabidi kuwena madarasa mazuri. Kwa mwaka huu tuna upungufu wamadarasa 158,000 na Serikali imesema inaweza ikajengamadarasa 2,000, hii ina maana itachukua miaka 79 kuwezakukamilisha hayo madarasa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Mheshimiwa Naibu Spika, kama lengo la Serikali nikufanya watoto wetu wasome sayansi, nini mpango mkakatiwa Serikali kuhakikisha kwamba wanajenga mazingiramazuri na sio tu kutoa matamko wanafunzi wasome sayansi?

Swali la pili, kwa kuwa tunatambua kwamba nchi hiihaihitaji tu wanasayansi bali pia inahitaji wengine, kwamfano mameneja wanahitajika watu waliosoma, lawyerskama Mheshimiwa Naibu Spika na wengine, ni kwa nini sasaSerikali isihamasishe pia wanafunzi wasome masomomengine kwa bidii?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi, na Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba nijibumaswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Waziri Kivuli wa Wizarayetu Mheshimiwa Susan Lyimo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ieleweke bajeti zoteza Wizara zinapitishwa na Bunge lako Tukufu na Bunge hililinao uwezo mkubwa sana wa kusema jambo hili lipewekipaumbele au jambo hili lisubiri kidogo, kama ambavyotumeona kwenye Wizara ya Maji wote kwa pamojatumesema iongezewe fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imekuwa ikijitahidisana kuhakikisha inatafuta wafadhili kila kona ya duniakuhakikisha kwamba tunapunguza tatizo hilo. Mfano nimadarasa ambayo yamejengwa mwaka huu zaidi yamadarasa 2,000, vyoo tulivyojenga na hali hiyo itaendeleakufanyika hivyo. Pamoja na kwamba kwa upande wakoMheshinimwa Waziri Kivuli unaona hakuna upungufu wawanasayansi, nataka nikuhakikishie kutokana na mikakatiya Serikali ya kutaka uchumi uwe uchumi wa viwanda,uchumi wa viwanda unaendeshwa na sekta tofauti tofauti,kwenye kiwanda utahitaji watu wa afya, kwenye kiwandautahitaji watu wa ujuzi wa ufundi, kwenye kiwanda utahitajimambo mengi, lakini hali kadhalika kwenye sehemu zetu za

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

kuhudumia afya zinahitaji wataalam wa aina hiyo. Kwa hiyo,ukiangalia kwa mapana yake huwezi ku-plan kwa kuangalialeo unaangalia kwa mapana, sisi tunaona iko haja kubwasana ya wanafunzi wetu kuchukua masomo ya sayansi kwawingi zaidi ili kukidhi maeneo ambayo bado yana upungufu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni pamoja nahiyo ya kusema kwamba tunatamka tamka, niseme tukwamba suala siyo kutamka, unapohamasisha lughaunayotumia ni yoyote inayowezeshwa kutoa hamasa kwawale vijana na wakafanya maamuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani swali la pili lanyongeza yako naomba limenitoka kidogo, kama unawezaukarudia.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri naombauzime microphone yako ili aweze kuzungumza. MheshimiwaSusan Lyimo.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Naomba labda awe pia anaandika wakati mtuanauliza ili isimletee shida. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili niliulizakwamba kwa sababu nchi hii nadhani pia ameshalijibuamechanganya kwamba kwa sababu tunahitaji wataalamumbalimbali ni kwa nini pia Serikali isihamasishe masomomengine, kwa sababu hatuhitaji tu wanasayansi tunahitajivariety ya watu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi mbali ya hayo niliyomjibuninayo ya kumuongezea na nilikuwa nataka nijue kama nawewe bado unakumbuka swali lako vizuri. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la wanafunzi katikamaeneo mengine Wizara yetu haijajikita kwenye sayansi pekeyake. Kwa mfano sasa hivi tunaendelea kuona namna

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

ambavyo tunaweza hata tukaingiza somo la kuwezeshawanafunzi katika masuala ya moyo (mindset). Unakuta mtuanao uwezo wa kufanya jambo lakini kwa sababu tu kimoyohajawa tayari anashindwa hata kusoma. Kwa hiyo, kunamasomo mengi pamoja na hilo, lakini haya ya sayansitumeyapa kipaumbele kutokana na uhaba wake mkubwa.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anne Kilango Malecelaswali la nyongeza.

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, napata taabu kidogomaana yake na mimi ni mwalimu, iwapo Serikali tutaachakwenda kwenye specialization na tukafanya watoto wotewakasoma sayansi. Mimi nina wasiwasi kwamba tutapatawanasayansi wabovu zaidi.

Je, Serikali haioni kwamba specialization ni importantkuliko ambavyo sasa tunakwenda kumfanya kila mtotoasome sayansi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, specialization inaanza na msingina niseme tu kwamba tunawahitaji wataalam wa ainatofauti tofauti. Kuna hao specialization ambao wanakuwawamekuwa vertical yaani anajikita katika eneo moja piatunawahitaji wale ambao wanakua kimapana (wideknowledgeable people) ambao wanaweza wakaoanishaupande huu na upande huu. Kwa hiyo, katika ku-specializekupo lakini lazima kuwe na msingi ni wa eneo gani ambalohuyu mtu atafanya specialization. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joshua Nassari swali lanyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kuniona.

Swali langu lilitaka kufanana kidogo na Mama AnneKilango na nikichukulia mwenyewe kuwa mfano, lakini kwasababu Mheshimiwa Naibu Waziri amekwishajibu labdanilisogeze mbele kidogo kwamba kama kweli lengo letu nikuongeza idadi ya wanasayansi kwenye nchi hii na hususanwalimu wa masomo ya sayansi kwenye shule zetu, ni kwanini basi ile Programu ya Serikali ya Awamu ya Nne, Serikaliya Chama hiki cha Mapinduzi ambayo ilianzisha programmaalum kwa ajili ya watoto, Chuo Kikuu cha Dodoma kwaajili ya kutengeneza walimu wengi wa sayansi kwenye nchihii, ni kwa nini basi watoto wale walifukuzwa mwaka janatena kwa polisi na mbwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa ElimuSayansi na Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TAKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, wanafunzi wale hawakufukuzwakwa sababu wako kwenye vyuo kumi ambavyowanaendelea na masomo yao na bado Serikali inaendeleakuwalipia. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pudenciana Kikwembe.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaNaibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu li l ikuwalinafanana kabisa na swali la Mheshimiwa Anne Kilango,amekwishauliza sidhani kama naweza kuendelea kuuliza.Ahsante.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa RichardMbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Elimu imerithi Vyuovya Maendeleo ya Wananchi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamiikutoka Wizaraya Afya. Je, kwa Chuo cha Maendeleo yaWananchi cha Msaginya kilichoko Jimbo la Nsimbo, Mkoawa Katavi, kuna mkandarasi miaka miwili amesimama kazianaidai Serikali. Je, Serikali ina mpango gani wa kumlipa ilikukamilisha ukarabati wa majengo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, kama Mkandarasi anadai, kimsingikama ambavyo mnafahamu vyuo hivi vimeletwa kwenyeWizara yetu katika kipindi cha mwaka huu wa fedhaunaoishia. Tunachofanya ni kwanza kuvitembelea na kuwezakuviangalia viko katika hali gani, kama kuna Mkandarasialikuwa anafanya kazi eneo hilo na hakulipwa, Wizara tunaowajibu wa kumlipa lakini baada ya kufanya uhakiki na kujuakwamba kazi aliyoifanya inafanana na uhalisia na awezekulipwa kwa kadri ya kazi yake.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tunaendelea na Wizaraya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Mheshimiwa Othman Omar Haji, Mbunge wa Gando sasaaulize swali lake.

Na. 233

Mkataba wa Ushirikiano baina ya Tanzania naCuba katika Sekta ya Afya

MHE. OTHMAN OMAR HAJI aliuliza:-

Moja kati ya maeneo yaliyomo kwenye mkataba waushirikiano baina ya Tanzania na Cuba (1986) ni pamoja nakuimarisha sekta ya afya.

Je, ni kwa kiasi gani Tanzania imefaidika na utekelezajiwa mkataba huo katika sekta ya afya?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, naombakujibu swali la Mheshimiwa Othman Omar Haji, Mbunge waJimbo la Gando, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana na Serikali yaCuba katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sektaya afya tangu 1986, ambapo mkataba ulisainiwa kati yaSerikali hizi mbili. Kupitia mkataba huo, Serikali ya Tanzaniaimekuwa ikipokea Madaktari Bingwa kutoka Cuba ambaowamekuwa wakifanyakazi katika hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Hospitali ya Tumbi naHospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Madaktari hawawamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za Kibingwa kwawananchi na kuwajengea uwezo madaktari wanaofanyanao kazi katika hospitali hizo. Aidha, kwa kushirikiana nakampuni ya Labiofarm ya Cuba, Serikali imeweza kujengakiwanda cha kutengeneza viuadudu vya kibaiolojia yaanibiolarvicides kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezaomalaria. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniailigharamia ujenzi wa kiwanda hicho na Serikali ya Cuba ilitoamsaada wa wataalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, matarajio yetu ni kuwa,wataalamu hao watawajengea uwezo Watanzania iliwaweze kutengeneza bidhaa hizo bila kutegemea wataalamkutoka nje ya nchi kwa siku zijazo. Viuadudu hivyo vimeanzakutengenezwa kuanzia mwezi Disemba 2016, na kwa sasauhamasishaji wa Halmashauri mbalimbali nchini kununuabidhaa hizo umeanza. Endapo viuadudu hivyo vitatumiwavizuri vitasaidia kupunguza mbu waenezao malaria na hivyokupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria nchini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Othman swali la nyongeza.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MHE. OTHMAN OMAR HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,nina maswala mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, pamoja na kuhamasishwaHalmashauri mbalimbali kununua dawa hizizinazotengenezwa na kiwanda hiki, Wizara ya Afya ni mtejamkuu ambaye alitegemewa kununua dawa hii inayozalishwana kiwanda hicho, lakini wameshindwa kutokana na kukosapesa, jambo ambalo limepelekea kiwanda kutafuta watejakutoka nchi za nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, namuomba Naibu Waziriatueleze hapa imekuwaje Wizara kutokutenga pesa kwa ajiliya kuwanusuru Watanzania ambao wanasumbuliwa naugonjwa huu wa malaria hapa nchini?

Swali la pili,kwa sababu teknolojia hii ya kuzalishaviuadudu vya kuulia viluilui vya mbu ni mpya hapa Tanzaniana Bara zima la Afrika, Mheshimiwa Naibu Waziri anawezakutueleza ni maeneo gani katika Jamhuri yetu ya Tanzaniawamewahi kuchukua angalau sampuli ya kiwanda kile nakuweza kuifanyia majaribio ili kuweza kujua ubora wa dawahizo? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa AfyaMaendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba arudie swali la pili walikuwa wanapiga makofi,sikumsikia vizuri.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Othman Haji naombaurudie swali lako la pili.

MHE. OTHMAN OMAR HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika,nimemuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba kwa sababuteknolojia hii ya kuzalisha viuadudu vya kuulia viluilui vya mbuwanaoeneza malaria ni mpya hapa Tanzania na Bara zimala la Afrika.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Je, Wizara imewahi angalau kwenda kuchukuasampuli kule kiwandani na kuweza kuifanyia majaribio nakuweza kujua ubora wa hii dawa? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Nitaanza na swali la pili kwamba je, Wizara imewahikwenda kuchukua sample kwenye kiwanda kile na kuzifanyiautafiti?

Kwanza naomba nimhakikishie kwamba teknolojiaya biolarvicides kuingia hapa nchini na kukubalika kutumikakuna mchakato mrefu wa kisayansi ambao umefuatwa.

Kwa hivyo, katika hatua hii ambapo inazalishwa kwawingi wala hakuna haja ya kufanya utafiti wa majaribio, kwasababu pale mwanzoni wakati ugunduzi wa teknolojiaunafanyika zilifanyika tafiti ambazo kisayansi zinajulikanakama clinical tries za kubaini efficacy ya biolarvicide ambayoinatumika lakini pia kubaini kama kuna any emergency yaresistance yaani usugu dhidi ya biolarvicide yenyewe ambayoinatumika na hatimaye ikafikiwa kuthibitishwa kwamba niteknolojia ambayo ni effective.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano walipoanzakufanya tafiti hizi miaka hiyo ya zamani walitumia bacteriaambaye anajulikana kama bacillus sphaericus katika hatuaza awali mpaka wakafikia mwisho wakakamilisha uchunguzina ikaonekana kwamba bacillus sphaericus ana-developresistance kiurahisi sana, wakahama wakaweka bacillusthuringiensis vara israelensis ambayo ni second generation.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kumuweka huyubacillus wa aina ya pili yaani kwa kifupi BTI ikaonekanakwamba yeye ni effective zaidi kuliko yule wa kwanza. Kwahivyo, ikaonekana kwamba sasa tutumie generaly BTI kwaajili ya biolarvicide. Kwa hivyo ni teknolojia ambayo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

imethibitishwa na haina shaka, na sisi Tanzania tunapaswakujivuna kwa kuwa tuna kiwanda hicho hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza kiwandakile kitazalisha full capacity yake biolarvicides lita milioni sita.Malengo hasa ya kuanzisha kiwanda kile sio kwa ajili yaTanzania peke yake, ni kwa ajili ya Tanzania na nchi nyingineza Afrika na dunia ambazo zitakuja kununua biolarvicidehapa nchini. Kwa mfano mpaka sasa tayari tuna nchi zaSerbia, tuna nchi ya Cuba, yenyewe tuna nchi za Sweden,tuna nchi ya Niger ambazo zimenunua biolarvicide kutokaTanzania, kwa sababu kuanzia hiyo mwezi Desemba, 2016mpaka sasa tumezalisha lita milioni mbili na tumeuza kwenyehizo nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hapa TanzaniaHalmashauri takribani tano zimeonesha nia ya kununua,Halmashauri mbili zimekwisha nunua japokua kwa kiasikidogo na zimekwishatumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niwapongezeHalmashauri ya Wilaya ya Mbogwe na Halmashauri ya Wilayaya Geita ambao wao walikuwa ni wa kwanza kwaHalmashauri za hapa nchini kununua biolarvicide. Kwa hiyoswali lake la msingi linasema kwamba Wizara ya Afyatungepaswa tununue si sahihi kwa sababu malengo ni sisikuwezesha kiwanda kile kuwepo na baada ya hapoHalmashauri ziweke kwenye bajeti zao wao wenyewewaweze kununua pale kadri ambavyo wanahitaji. Ndiyomaana tunaendelea na uhamasishaji wa Halmashauri zotenchini kununua biolarvicide kwa ajili ya control ya malaria.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, baada yamajibu hayo bado mna maswali. Mheshimiwa Antony Komuswali la nyongeza.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana.

Kwa kuwa ugonjwa wa malaria ni ugonjwa ambao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

unaongoza kwa kuua katika nchi hii na ninaamini kwambaWizara imetenga fedha kwa ajili ya kupambana na malaria.Ni kwa nini Waziri asione kuna umuhimu wa fedha zoteambazo zimetengwa kwa ajili ya kupambana na malariazikapelekwa kwenda kununua dawa za viuadudu Kibaha ilikupambana na malaria ikizingatiwa hicho kiwanda sasahivi kimesimama kuzalisha kwa sababu ya kukosa soko labidhaa zake?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,kwamba kwa nini tusichukue fedha zote tukapeleka kwa ajiliya kununua biolarvicide pale Kibaha kwa ajili ya Halmashaurizetu nchini. Hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu udhibiti wamalaria siyo kuua larva peke yake tunamu-attack adui mbukatika hatua nyingi tofauti tofauti, lakini pia tunamu-attackkile kijidudu chenyewe ambacho kinaambukiza malaria yaaniplasmodium falciparum katika hatua nyingi tofauti. Kwahivyo, mikakati ni mingi ambayo inamlenga adui mmojakwamba yule vector ambaye ni mbu either wa aina yaanopheles ama tunamu-attack plasmodium mwenyeweakiishaingia kwenye damu ndiyo control inakuwa hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo hatuwezikutumia njia moja kumu-attack adui kwamba tunaua tumazalia yaani larvae halafu tunasema basi ndiyo tumemaliza,hapana! Lazima kuwe kuna tiba. Kwa hiyo, ndiyo maanatuna mkakati wa kusambaza ALU (Artemether naLumefantrine combination) nchi nzima na tunagawa bure ilituue plasmodium falciparum ambaye yumo kwenye damu.Ndiyo maana tuna mkakati wa wajawazito, tunatumia SP(Sulfadoxine Pyrimethamine) kwa ajili ya kumuua mdudu mbuambaye anawa-attack akina mama wajawazito.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana tuna net kwaajili ya kuzuia mbu ambao wanapenda kuishi ndani yanyumba na wanauma saa sita usiku kuambukiza malaria.Sasa tuna mikakati mingi, tunatumia IRS – Indoor Residual

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Spraying kwa ajili ya kumu-attack mbu ambaye anapendakubaki ndani ya nyumba, mchana hatoki nje anabaki ndaniili asiwepo. Kuna mikakati ya kumuua mbu kama atakuwanje kwenye mzingira. Sasa hii ya kwenye mazingira ndiyotunaona teknolojia hii mpya ya biolarvicides itatusaidia.Vinginevyo tungetumia DDT. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Khalifa Mohamed, swali lanyongeza.

MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na ushirikiano mzuriwa ndugu zetu hawa wa Cuba katika mambo ya tibaTanzania, kwa kule Zanzibar ndugu zetu hawa walikuwa naprogramu maalum ya kuwafunza vijana wetu Udaktari nakwa kweli tayari sasa hivi intake mbili zimeshatoka, mojamadaktari wanaendelea na kazi zao na wengine wakokatika internship sasa hivi. Kwa kweli inaonekana kwambawana mafanikio makubwa.

Je, kwa hapa Tanzania Bara programu hiiimeanzishwa au imeshafikiriwa kuanzishwa kwa kuwatumiahawa ndugu zetu wa Cuba? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwanza Cuba ni marafiki wa kihistoria wa Tanzania.Comradeship iliyotengenezwa na Fidel Castro na MwalimuJulius Kambarage Nyerere ni ya muda mrefu na imezaamatunda mengi katika nchi zote mbili, zaidi sisi tukiwawafaidika kuliko wenzetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ushirikiano huo,Watanzania wengi, hususan kwenye fani hii ya afyawamepelekwa Cuba kwa ajili ya masomo na wamesoma

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

masomo ya ubingwa lakini pia katika nyakatimbalimbali hata wanajeshi wetu ambao wanahusika namambo ya tiba na uokoaji pia wamepelekwa Cuba kwaajili ya kusoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1986 ikaonekanakwamba isitoshe tu kuwa na exchange ya Watanzaniakwenda kufundishwa kule Cuba mambo ya afya, ikaonekanakwamba tusaini mkataba mwingine ili waje hapa hapawatujengee uwezo. Kwa hivyo, harakati za kujenga uwezozimekuwa zikifanyika kila mahali ambako madaktari waCuba wamekuwepo, pia wamekuwa wakifundisha katikavyuo vyetu hapa nchini, hivyo hata kwa Tanzania Bara tunao.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi ninavyozungumzahapa, tuna Madaktari Bingwa kumi na moja wanaotokeaCuba ambao wapo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya na Hospitali ya Rufaaya Mkoa wa Ruvuma. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Swali la mwisho, Mheshimiwa StanslausNyongo.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kuniona. Natambua Mheshimiwa Dkt.Kigwangalla wewe ni mtaalam na unafahamu kabisakwamba katika prevention za malaria kuna primaryprevention na kuna secondary prevention, nashukuruumeelezea vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa NaibuWaziri kiwanda cha viuadudu kama tutaweza kufanikiwa,dawa ikasambaa vya kutosha tuka-control wale vectorkwenye hiyo level ya wale wadudu kutafuna larva, huonikwamba tutakuwa tume-eradicate kabisa malaria na niwajibu wa kila Hamashauri kununua zile dawa ili kusudi kilekiwanda kifufuke na tuweze kuzuia malaria? Ahsante sana.

NAIBU SIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,majibu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Anachokisema ni sahihi kabisa, tukitumia hiiteknolojia ya biolarvicides effectively tunaweza tuka-controlmalaria na hatimae kuidhibiti kabisa katika muda mfupi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaweza tukawa tupoconstrained kibajeti na nadhani mkakati wetu kama nchisiyo kwa Wizara ya Afya kununua na kusambaza nchi nzimakwasababu majukumu yetu sisi kwakweli ni prevention, lakinipia tiba na mambo mengine na tuna support kwa kupitiapesa tunazozipata kutoka kwa wabia wa PMI pamoja naGlobal Fund.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana hili suala labiolarvicides tunawahamasisha Halmashauri zote nchini kwakutumia mapato yao ya ndani washiriki kwa kutenga pesakwa ajili ya kununua hizi biolarvicides na kuzisambaza nakuzitumia kwenye maeneo yao. Sisi kama Wizara ya Afyatumekwishakutengeneza mwongozo wa namna ya waokutumia teknolojia hii ku-control hawa bio larvae kwakutumia biolarvicides katika maeneo yao. Kwa hivyo, sisi kaziyetu ni hiyo tu, kutoa mwongozo na tumekwishatoa. SasaHalamshauri zote including Halmashauri ya Maswa mnunue.Wenzenu wa Kondoa wameshaweka order, wenzenu waSongwe, Namtumbo, Mbogwe na Geita pia wamewekaorder.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hivyo Halmashaurinyingine na ninyi mhamasishe kwa kutumia mapato yenu yandani muweze kununua biolarvicides kwa ajili ya control yamalaria. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumefikamwisho wa kipindi chetu cha maswali na majibu. Ninayomatangazo machache hapa.

Tangazo la kwanza linahusu wageni, tunae mgeni waMheshimiwa Abdallah Bulembo ambaye aliwahi kuwaMbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ambalo sasa hivi ni

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

Wilaya ya Butiama na huyu ni Balozi Paulo Ndobo, karibusana Mheshimiwa Balozi. (Makofi)

Tunao pia wageni mbalimbali wa WaheshimiwaWabunge pamoja na wanafunzi waliokuja Bungeni kwa ajiliya mafunzo. Karibuni sana wageni wetu na wanafunzi,tunaamini mnaweza kujifunza kutoka hapa Bungeni mambokadhaa na namna tunavyofanya kazi.

Waheshimiwa Wabunge, tangazo lingine linatokakwa Kepteni wa volleyball kwa wanaume Mheshimiwa CecilMwambe anawatangazia kwamba wachezaji wa volleyballkwa upande wa wanawake na wanaume wajiandikishe leokwa ajili ya kuanza mipango ya mazoezi.

Waheshimiwa Wabunge, na hili nisisitize Wabungewengi hapa mlisimama kwenye swali la michezo na wenginehata hamfanyi mazoezi popote lakini mlisimama kutakakuuliza swali kwenye michezo. Sasa niwakumbushe tu,mlishasisitizwa hapa na Mheshimiwa Spika kwamba mfanyemazoezi, kwa hiyo nawakumbusha. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, lingine na la mwisho nikuhusu maswali ya nyongeza. Kanuni zetu zinataka Wazirianapoulizwa swali ajibu swali kikamilifu, lakini Wabungetunatakiwa kumpa fursa hiyo ya kujibu maswali kikamilifukwa kukuuliza maswali yanayotokana na swali la msingi.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, mnakipa Kiti wakati mgumukumzuia Waziri kujibu swali kwanza kwa sababu kipindi hichowapiga kura wenu wanakuwa wanaangalia. Kwa hiyo, kunamawili either Kiti kikuzuie wewe unayeuliza swali na kisemehilo swali halitokani na swali la msingi, kwa hiyo, achaguliwemtu mwingine au kikusikilize halafu kimzuie Waziri kujibu hiloswali.

Sasa kwa sababu Kanuni zetu zinataka maswaliyajibiwe kikamilifu basi Waheshimiwa Wabunge tutoe fursahiyo kwa Serikali kutoa majibu kikamilifu kwa kuuliza maswali

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

ya nyongeza yanayotokana na maswali ya msingi. Ukitokanje ya swali la msingi unaipungukia Kanuni yetu kwa sababusasa huwezi kupewa majibu yanayotosheleza kwa kuwaWaziri atakuwa hajajipanga kujibu swali la namna hiyo kwasiku hiyo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nimewakumbusha ikitokeasiku Mbunge ameambiwa swali lako haliendani na swali lamsingi asijisikie vibaya ama Waziri akazuiwa kujibu hilo swalikwa sababu halitokani na swali la msingi basi MheshimiwaMbunge asijisikie vibaya.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayotunaendelea na ratiba yetu. Katibu.

MHE. MARWA R. CHACHA: Hoja ya kuahirisha shughuliza Bunge.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika,mwongozo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa anayetaka kuahirishashughuli za Bunge. (Kicheko)

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwa mujibu wa Kanuni ya 47(1), (2) na kuendeleanaomba nisisome, nisome ya kwanza; baada ya muda wamaswali kuisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwashughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye orodha yashughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharurana muhimu kwa umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilimuandikia Spika waBunge kuhusu tatizo la tembo Serengeti. Sasa hivi Wilayayangu ina njaa kweli, wananchi wamelima mazao,yanakaribia kuvunwa, lakini mazao hayo yanashambuliwana tembo kwa wingi makundi mengi kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kila ninapomwambia Waziriwa Maliasili na Utalii hawana msaada wowote katika Wilaya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

yangu ya Serengeti, hata kutupa tu lita moja ya mafutahakuna! Tunasumbuka sisi Halmashauri kwa mapato ya ndanitunayoyapata kwenye minada, kwenye masoko.

Sasa ninaomba kutoa hoja kwamba shughuli zaBunge ziahirishwe kwa dakika kumi ili tujadili suala hili hapaili tuweze kupata muafaka wa jambo hili la tembo ndani yaWilaya ya Serengeti. Wananchi wangu wana njaa, wanamatatizo makubwa, lakini Wizara hii huyu Waziri hawasikilizikabisa. Naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika,naafiki.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hoja haitolewikwa namna hiyo ya kutumia Kanuni ya 47. Kwa hiyo,Mheshimiwa naomba ukae, Waheshimiwa Wabungehalafu… sawa, naomba tufuate utaratibu tuliouweka kwenyeKanuni. (Kicheko)

Mheshimiwa Cecil Mwambe.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika,naombwa Mwongozo wako kwa kutumia Kanuni ya 68,sitaisoma. Ninafahamu kwamba Tanzania ni Jamhuriiliyoundwa kwa kuunganisha Zanzibar pamoja na TanzaniaBara, Tanganyika wakati huo, lakini kuna mikoa zaidi ya 35ndiyo inayofanya kuitwa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kupataMwongozo wako ili Waziri wa Fedha atueleze ni kwa niniunapoleta mzigo kutoka nchi za nje kupitia border yaNamanga kuleta Dar es Salaam haulipi kodi ya ziada, lakiniunapoleta mzigo kutokea Zanzibar kuleta Dar es Salaamambapo ni Mkoa wa Tanzania unatakiwa kulipa kiasi chaziada? Hii inatuletea mkanganyiko mkubwa sanaWatanzania. Tunaomba ufafanuzi wako. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaNaibu Spika, niliomba Mwongozo.

NAIBU SPIKA: Waheshimimiwa Wabunge,nimeombwa Mwongozo na Mheshimiwa Cecil Mwambe,kwa mujibu wa Kanuni 68(7) akitoa maelezo ambayo wotetumemsikia kuhusu kudaiwa kodi kwa vitu vinavyotokaZanzibar kuingia Dar es Salaam ama kuingia Tanzana Bara.Ametoa maelezo yake kwamba nchi yetu kama ambavyoina majirani wengi, vitu vikitoka nchi hizo vinafananishwakana kwamba vinatoka nje ya Tanzania na kwa hivyovinavyotoka Zanzibar na sisi tuna Muungano ni kana kwambana vyenyewe vinatoka nje ya Tanzania. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, niwakumbushe tena, sualahilo halijatokea hapa Bungeni. Kwa hiyo, Kiti hakitoiMwongozo wowote kuhusu jambo hilo na ushauri tu kwaMheshimiwa Cecil Mwambe hili jambo lilishaulizwa maranyingi sana hapa ndani na kama majibu yanayotolewa naSerikali hayaridhishi basi ufuate utaratibu mwingine ambaoutakupa wewe fursa ya kuweza kulifanya hili jambo kwa utashiunaopaswa pia kwa kufuata Kanuni zetu. Kwa hiyo, Kitihakina Mwongozo juu ya jambo hil i l i l i loombwa naMheshimiwa Cecil Mwambe.

Mheshimiwa Marwa Chacha ametoa hoja yakuahirisha Bunge na ametumia Kanuni ya 47. WaheshimiwaWabunge tusikilizane kuna wengine mnazungumza ndiyomaana wakati wa kutumia hizi Kanuni tunarudia makosayale yale kila wakati. Hoja ya Kuahirisha Bunge iko Kanuni ya69.

Waheshimiwa Wabunge, Hoja ya Kuahirisha Bungeiko Kanuni ya 69. Kanuni ya 47 inazungumzia kuahirishashughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura na MheshimiwaChacha Marwa ametoa hoja yake akisema kwamba kunajambo ambalo kwake yeye anasema ni la dharura, tembowameingia katika Jimbo lake na Serengeti tunafahamu wotekwamba kuna mbuga yetu inayoitwa Serengeti, kwa hiyoJimbo lake liko karibu sana na eneo hili na tembo hawa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

wanakula mazao ya wananchi. Kwa hiyo, kwa maelezoaliyoyatoa anasema kuna njaa Serengeti kwa sababu tembowanakula ama wamekula mazao ya wananchi kwa hiyowamesababisha njaa. Kwa hivyo, nilimsihi asitoe hoja kwanzakwa kuwa Kanuni zetu zinataka mimi kwanza nimpe fursaya kutoa hoja ikiwa nimeridhika kama hilo jambo ni ladharura ama hapana.

Waheshimiwa Wabunge, jambo hili la tembo kuwamaeneo mbalimbali ambayo wapo wananchi lipo nasi sikuzote kwa sababu tembo wapo na wananchi wapo. Kwahiyo, Wizara huwa inajibu mara nyingi hapa ndani kuoneshanamna ambavyo kila mahali linapotokea tatizo inabidilikashughulikiwe wakati huo. Hapa juzi tu tumesikia kunatembo walikuwa Chuo cha Dodoma na wataalam watoamaelezo kwamba pengine yale yalikuwa ni mapitio yatembo kwa hiyo tembo wamekumbuka njia yao.

Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 47 huwainapaswa kusomwa na Kanuni ya 48, kwa sababu 47 ndiyoinayoruhusu kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo ladharura lakini 48 inasema masharti ya jumla kuhusu jambola dharura. Sasa jambo la dharura ili sisi tuweze kuahirishashughuli zingine tujadili jambo hilo ni lile ambalo haliwezikufanyiwa kazi kwa namna iliyo ya kawaida. Sasa hili latembo kuingia Serengeti lina uwezo wa kushughulikiwa kwataratibu zilizopo. Kwa hivyo, hatutaahirisha Bunge kwa ajiliya kujadili hoja ya Mheshimiwa Chacha Marwa.

Baada ya kusema hayo, nimetaarifiwa kwamba kunaMheshimiwa mwingine alisimama kwa ajili ya Mwongozo,huo utakuwa ni Mwongozo wa mwisho halafu tutaendelea.Mheshimiwa Kikwembe.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo wakokwa ruhusa yako kwa sababu Serikali iko hapa isikie kwaniaba ya wananchi wote wa Tanzania.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni tumesikia sualala kuhusu ugonjwa wa Ebola na huu ugonjwa umethibitikakuwepo nchi ya Congo, nchi ya Congo na ukanda wa kwetuLake Tanganyika na Jimbo la Kavuu kumekuwa namaingiliano wa watu ya kila siku. Naiomba Serikali iangalieni namna gani itatoa udhibiti na kuelimisha wananchiwanaoingia ukanda ule ili kudhibiti ugonjwa huu, kwasababu ni hatari sana kuliko UKIMWI.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Mwongozowetu wa mwisho umetoka kwa Mheshimiwa Dkt.Pudenciana Kikwembe akitoa maelezo ambayo wotetumemsikia, hayahitaji Mwongozo wowote wa Kiti. Kwa hiyo,kama yeye alivyoomba kwamba Serikali imsikie, basiimekwisha kumsikia na nadhani Mheshimiwa Waziriatalifanyia kazi hilo jambo. Kwa hiyo, Kiti kwenye jambo hilihakina Mwongozo wowote.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayotunaendelea na ratiba iliyo mbele yetu. Katibu.

NDG. CHARLES MLOKA - KATIBU MEZANI

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na

Uwekezaji

(Majadiliano yanaendelea)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleana majadiliano ya hoja ya Mheshimiwa Waziri wa ViwandaBiashara na Uwekezaji. Ninayo majina hapa ya WaheshimiwaWabunge kutoka Vyama mbalimbali kwa uwiano wao, kwahiyo tutaanza na orodha kama ifuatavyo:-

Waheshimiwa Wabunge, tutaanza na Mheshimiwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

Venance Mwamoto atafuatiwa na Dkt. Shukuru Kawambwa,Mheshimiwa Martha Umbulla ajiandae.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa NaibuSpika, nami kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kupata nafasi hii ili niweze kuchangia leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nianze kwakupongeza Wizara hii kwa jinsi ambavyo kwa kweliwameandika vizuri, kama tungelipata muda mrefu wakuweza kusoma hiki kitabu, nafikiri michango yetuingepungua kwa sababu kimeandikwa vizuri sana namaeneo yote yameguswa, na ukisoma unaona kweli Serikaliimedhamilia kutuingiza kwenye uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo leo kazi yangukubwa hasa ni kushauri, lakini kabla sijaanza kushauri pianiipongeze Serikali jana nilitoa taarifa hapa kwa Waziri waKilimo kwamba kuna paka ameingia kule Ilula, amejeruhizaidi ya watu saba na alikuwa anajeruhi sehemu ambazoanazijua yeye, jana timu imetumwa na kazi imefanyika, kwahiyo, naipongeza hii Serikali kweli hapa kazi tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema miminitaenda kwenye ushauri, ukiangalia dhana nzima ya Serikaliyetu tumejikita kwenye uchumi wa viwanda, walioteuliwawataalamu kwenda kwenye Wizara ile wote ni makini, lakinikitu ambacho ninaomba ni kimoja nitatoa mfano, Wahehemimi natoka Iringa, Mhehe na Mgogo, Mhehe akiongeaKihehe, Mgogo anaelewa na Mgogo akiongea Kigogo,Mhehe anamuelewa, tatizo linakuwa Mhehe anapotakakuongea Kigogo na Mgogo anataka kuongea Kihehewanapotea njia. Maana yangu ni nini, mwanasiasa ninyiwataalam wa Wizara hii ongeeni kitaalam, msianze kwendakwenye siasa mkiongea kitaalam sisi wanasiasa tutajuamnachozungumza na sisi wanasiasa hatuwezi kuingiliakwenye utaalam wenu tutaongea kisiasa mtatuelewa, lakinitatizo linakuja pamoja na mipango mizuri tukiingiza siasamtataka kuwa wanasiasa, mkiashaingiza siasa mipango yotemizuri itaaribika.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Kwa hiyo, naomba mjikite Mheshimiwa Mwijagenakufahamu vizuri, ulipokuwa unasoma Tosamagangaulikuwa unaitwa kijiko cha jikoni hakiogopi moto, sasa huomoto wako kweli upeleke. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajenga viwanda,mwanzo ni ujenzi wa viwanda, unapojenga viwanda kunavitu ambavyo unatakiwa uwe navyo ni pamoja namalighafi. Watu wa Mchuchuma ndugu yangu paleamezungumza sana tunajenga viwanda tumejitayarisha?Sasa ilikuwa ni wakati muafaka kuhakikisha chuma chetukile tunakiandaa ili tuweze kukitumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni wakati sasa wa kutumiamalighafi nitatoa mfano mzuri, tupo kwenye ujenzi waMakao Makuu ambapo kiasi kikubwa cha mbao zinatokaWilaya ya Kilolo, mimi naomba Mheshimiwa Rais najuaanasikiliza na anafuatilia, asilimia 75 zinatoka Kilolo naMufindi, lakini miundombinu ya Wilaya ya Kilolo barabarasiyo rafiki?

Sasa Wizara ya Viwanda naomba utoe ushauri kwaWizara ya Miundombinu wahakikishe ile barabara inawezakutengenezwa ili iwe rahisi kusafirisha mbao ambayo nimalighafi ya kujenga viwanda na itasaidia kupunguzagharama. Bila kufanya hivyo utakuwa hujatutendea haki.Mimi ninaomba tu Mheshimiwa Rais huko aliko anasikia siyombaya akiamua kuahirisha sikukuu moja zile fedha zikaendazikajenga barabara ya kutoka Iringa mpaka Kilolo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine ambaloningependa kulisemea ni Ilula Wilaya ya Kilolo tumejengaKiwanda cha Nyanya, lakini kiwanda cha nyanya kile nyanyatunalima sehemu oevu ambayo maji yanatuama ili tuwezekupata mazao vizuri, leo hii imekuja tafsiri mbaya sanawanasema kwamba wananchi wasilime kwenye vyanzo vyamaji. Sasa tafsiri ya vyanzo vya maji Mheshimiwa JanuaryMakamba upo mimi nakuomba Jumapili nipo tayari hatakukuchangia hata mafuta uende, tatizo ni kubwa, sivyo vileambavyo unafikiria.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Naibu Spika, watu sasa hiviwananyanyasika tunaita kilimo cha vinyungu, MheshimiwaChumi amepiga kelele, Waheshimiwa wa Wilaya ya Mufundiwamepiga kelele na mimi napiga kelele, tusaidie kwa sababutukilima nyanya ndizo ambazo tutapeleka kwenye kiwanda.Sasa hatujatengeneza miundombinu mizuri ya kuwawezeshawatu wa Kilolo na sehemu nyingine waweze kuzalisha iliwapeleke kwenye kiwanda sasa hatujatengenezamiundombinu mizuri ya kuwawezesha watu wa Kilolo nasehemu nyingine waweze kuzalisha ili wapeleke kwenyekiwanda, bila kufanya hivyo uchumi utatoka wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mwijageshirikiana Mheshimiwa January Makamba nami namuombaikiwezekana kama haiwezekani toa kauli waachekuwasumbua wananchi tuweke mipango kwanza. Shirikianana watu wa kil imo watengeneze miundombinu yaumwagiliaji lakini leo unavyosema chanzo cha maji Wilayaya Kilolo au Mkoa wa Iringa ambao unasifika nchi hii kwakutunza vyanzo vya maji, sasa leo unavyokwendakuwabugudhi ni sawa sawa ukiwa na kuku anayetaga mayaiya dhahabu ukimsumbua utakosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba utusaidie katikahilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine ambaloningependa kulizungumza Mheshimiwa ni mpango wa SIDO.Kwa kuwa tunakwenda kwenye viwanda, tujikite sasakuhakikisha kwamba kila Wilaya angalau tunawatayarishawatu kwa kuwa na SIDO, kama usipowatayarisha watuambao wanakwenda kwenye utekelezaji wa viwandausitegemee kama tutapata chochote, lakini Mheshimiwaninakusifu, ukiangalia na ukitaka kujua kazi nzuri ya Wizarayako ukienda ukurasa wa 107 kwenye malengo mambo yotemazuri yamezungumzwa humo kwa hiyo tujikite pake tusomena wengine wanabeza hapa wanasema viwanda havipo.Nenda kwenye ukurasa wa 167 utaona orodha ya viwanda,ukishaona orodha ya viwanda ambavyo viko kila mkoanenda kwenye Mkoa wako kaulize.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu ambachokinatusumbua Mheshimiwa Waziri ni tafsiri ya viwanda,unaposema viwanda una maana gani, ndipo hapo ambapokuna kuwa na ukakasi kidogo. Pia Mheshimiwa WaziriMwijage, hivi viwanda ambavyo tunanaza kuna vingiineambayo wanaweza kuanzisha Watanzania, leo hii ukiendapale kuna Wachina wanauza juice, wanauza ice creamwewe kama Waziri unasemaje, maana yake ni viwandawatakuambiwa ni viwanda vile. Kwa hiyo, utusaidieMheshimiwa Mwijage vile viwanda ambavyo vinawezakuanzishwa na Watanzania basi vianzishwe na Watanzaniawenyewe bila kujali mambo yanakwenda vipi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambaloningependa kulizungumza ni suala la kilimo, Mheshimiwa Rais,anatuletea trekta nimesikia zaidi 2000 shirikiana naMheshimiwa Waziri wa Ulinzi kuna trekta zile ambazozilitolewa mwanzo lakini leo hii wananchi wanaanzakunyang’anywa tena, hii haipendezi, tuweke tu mkakati mzurikwamba wananchi wanazitumia zile trekta ili tuende kwenyekilimo.

Kiwanda cha ngozi mmezungumza vizuri, kwambaleo hii wafugaji nyama haina thamani, ngozi hazina thamani,ngozi ilikuwa inauzwa shilingi 4000 leo hii kwa kilo ngozi nishilingi 2000 hazina thamani tena, sasa tusipoelekeza nguvuyetu kwenye viwanda kama hivyo matokeo yaketutaendeleza ugomvi wa wakulima na wafugaji wakatisuluhu unazo wewe Mheshimiwa Mwijage.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nizungumzie habari yamigogoro ya wakulima na wafugaji, mtu ambaye anawezaakatusaidia ni Waziri wa Viwanda kwenye jambo hili,ukishirikiana na Waziri husika, tukatenga maeneo haya ni yaviwanda, haya ni ya kilimo, haya ni ya mifugo ugomvihautakuwepo na kutoa thamani kwenye mazao yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Nyuzi, kwamfano Kiwanda cha Pamba huwezi kujenga Iringa na ndiyomaana nilisema siasa, unaweza ukafanya siasa kikajengwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

Iringa, leo hii pale sisi Ilula mmetujengea kiwanda cha nyanyalakini bado tunahitaji kiwanda kwa ajili ya vitunguu, tunahitajikiwanda kwa ajili ya juice na mambo mengine ili wananchiwale wapate ajira, lakini ukisema tu viwanda vijengwe halafuhavina muungozo itakuwa ni shida. Pia kuna athari zaviwanda kwa sababu kuna mambo ya hali ya hewa lazimakuzingatia, kwa sababu unaweza kukuta baadae tumefikamwisho hali ya hewa, mazingira yanachafuka na watuwanaanza kupata athari mbaya, sasa hilo pia uzingatie.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ambaloningependa kuzungumza ni kwamba tuangalie kwambakiwanda hiki kinajegwa wapi na hiki kinajengwa wapi ilituende sambamba na ukuaji wa uchumi kwa kutumiaviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Dkt. ShukuruKawambwa atafuatiwa na Mheshimiwa Martha Umbulla,Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu ajiandae.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaNaibu Spika nikushukuru kunipa fursa hii ya kuchangia katikahoja iliyokuwa mbele yetu, na nitangulie kwa kuunga mkonohoja. Naomba kuchukua fursa hii kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri ya bajeti pamoja nautekelezaji mzuri wa Ilani wa Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuchukua fursahii kuipongeza Serikali kwa utekelezaji wa mkakati wa ujenziwa viwanda ili Tanzania iweze kufikia hadhi ya nchi ya uchumiwa kati ifikapo mwaka 2025. Hili ni jambo jema sana nijambo lenye tija kwa uchumi wa nchi yetu Tanzania lakini niukombozi kwa mamilioni ya vijana wa Tanzania wa kike nawakiume.

Mheshimiwa Naibu Spika, shida kubwa ya vijana wetu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

wa kike na wa kiume wanaoingia kwenye soko la ajira sasahivi ni ukosefu wa kazi, ujenzi wa viwanda maana yakeviwanda vingi maana yake ni ajira nyingi. Tutawapa hadhivijana wa Kitanzania watajisikia binadamu, watajisikia kuwana heshima na wataweza kuchangia maendeleo ya nchi yaokwa kiasi kikubwa iwezekanavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri katika Jimbolangu la Bagamoyo Serikali imetenga ardhi, jumla ya hekta9,080 ama kwa kipimo cha ekari 22,700 hili ni kwa ajili yaujenzi wa viwanda katika kata ya Zinga na kata ya Kiromojumla ya vijiji vitano vitahusika na mradi huu. Tathminiimefanywa mwaka 2008 jumla ya wafidiwa 2,180 na kwakipindi hicho thamani ya fidia ilikuwa shilingi bilioni 60, mpakahivi sasa Serikali imelipa bilioni 26.4 kwa wafidiwa 1,155. Kwahiyo, kuna wafidiwa 1,025 ambao bado hawajapata fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika na Mheshimiwa Wazirimwaka 2008 mpaka leo mwaka 2017 ni jumla ya miaka kumisasa. Mheshimiwa Waziri ungekuwa kule kijijini ujifanye weweni mzee kijijini kule Kagera mwaka 2008 shamba lako nanyumba limezuiliwa na Serikali ili liweze kufanywa mradi waEPZ na ukazuiliwa kufanya maendelezo katika nyumba ile,ukazuiliwa kufanya maendelezo katika shamba lako, usubirifidia kwa miaka kumi, fidia usiione. Mheshimiwa Waziri saahizi baada ya miaka kumi hali ya nyumba yako ikoje, hali yashamba lako ikoje, hali ya maisha yako kwa ujumla na familiayako ingekuwa namna gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo ndiyo madhira yawananchi wa Bagamoyo ambao tangu mwaka 2008wamezuiliwa maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa viwanda,wako katika hali mbaya sana. Mimi kama Mbunge nashindwakupita hawanielewi, hakuna jambo ambalo nawezanikawaambia wakanisikiliza. Sasa hivi Mheshimiwa Waziri unafursa kubwa hii ya azma nzuri ya Serikali ya Awamu ya Tanoya kujenga viwanda, viwanda havijengwi hewani vinajegwaardhini lazima ardhi hii iweze kulipiwa hivi sasa baada yamiaka kumi ili wananchi nao wajisikie nao wako katika nchiyao huru na wanaweza wakaendeleza maisha yao.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziriutakapokuja kujumuisha hoja yako unipe, ama utupe majibumazuri na ya uhakika kwamba ni lini wananchi hawa waZinga, Kondo, Pande na Kiromo watalipwa fidia zao kwasababu Mheshimiwa Waziri kwa madhira haya, wewe ni rafikiyangu na mimi nilishawahi kuwa kwenye Serikali nitaona aibusana lakini nitakuwa sina namna nyingine bali kutangazaazma yangu ya kushikilia shilingi kama sitapata majibu yauhakika, kwamba lini wananchi hawa watalipwa fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziriamesema pia katika hotuba yake kwamba fidia hiziinategemewa zitalipwa na mwekezaji mwenyewe jambozuri, lakini Mheshimiwa Waziri niulize, kwa nini Serikaliimebadilisha utaratibu, utaratibu ambao tumejiwekeakwamba fidia za ardhi ya wananchi wetu tulikuwa tunazilipasisi wenyewe kama Serikali, mwaka 2012/2013 kwa ajili yamradi wa EPZ, tulitenga shilingi bilioni 50 lakini zilitoka bilioni10.9, mwaka 2013/2014 tulitenga bilioni tisa zikatoka bilionitatu, mwaka 2014/2015 tulitenga shilingi bilioni saba,zikatoka bilioni saba zote na huo ndiyo ulikuwa utaratibuwakati wote tunaposema kwamba mwekezaji alipie fidiaya ardhi maana yake tunapunguza vivutio kwa wawekezajihao na mitaji inatafutwa dunia nzima, unapopata mtu anamtaji basi huyo ni wa kumshikilia na kimojawapo ni kigezohiki ambacho Serikali inaweza ikalipia fidia zake kamatulivyokuwa tunafanya lakini pia nimuambie Mheshiwa Wazirihata kama mwekezaji atalipa fidia katika eneo hili eneo laEPZ ni hekta 9,080 na mwekezaji yule amesema ata develophekta 3000 peke yake, hizi hekta 6000 zingine nani atalipia?miaka 10 baadae nani atalipia?

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi haowataendelea kuteseka, wananchi hawa wataendeleakuchukia Serikali yao, wananchi hao watashindwakujiendeleza katika maisha yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa MheshimiwaWaziri atakapofanya majumuisho atueleze vizuri kwa ninitumefanya mabadiliko haya na uhakika upi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

utakaotuwezesha wananchi hawa waweze kulipwa fidia zaokikamilifu na mapema.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa pia kuelezeakwamba mradi huu wa Special Economic Zone Bagamoyounajumuisha pia ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Bandarimpya ya Bagamoyo, bandari yenye uwezo mkubwa zaidikushinda bandari yoyote katika mwambao wa AfrikaMashariki na kusema kweli ni mwambao wa Afrika nzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2002 ndiyo kwamara ya kwanza mwezi Septemba tulisaini MoU ya ujenzi wabandari, na mwaka 2013 Machi, Rais Xi Jinping wa Serikaliya China na aliyekuwa Rais wa Tanzania, walishuhudia kutiwasaini kwa framework agreement ya ujenzi wa bandari hii,mwezi Machi 2013 mpaka leo ni mwaka wa tano sasa na nimradi ambao umeshuhudiwa kuwekewa saini na Rais XiJinping, tena wakati ule ana wiki chache tu baada yakuteuliwa kuwa Rais wa Taifa kubwa lile, huo ni mradimuhimu sana kwa nchi ya China. China ni rafiki zetu, Chinawamekubali kutusaidia, pesa ni ya kwao na tumesainiframework agreement Machi 2013 lakini mpaka sasa hivimiaka Mitano ni muda mrefu hatupaswi kukaa muda huowakati mtaji tumeushikilia, mtaji huu kila mmoja ndani yaBara la Afrika na nje ya Afrika wanautafuta.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipindi hiki tunaongea naChina Merchant Port kipindi hiki hawa wa China MerchantPort wamekamilisha maongezi na Serikali ya Sri Lanka sasahivi wanaendesha Colombo International Container Terminalwamekamilisha maongozi na Togo, wanaendesha Lome PortContainer Terminal, wamekamilisha maongezi na Nigeriawanaendesha Tincan Port Island Container Terminal nawamekamilisha miradi kadhaa mingine ambayo kwa ukosefuwa muda sitaweza kuisema, kipindi hiki tangu 2012 mpakaleo tunajadiliana nao mpaka lini?

Mheshimiwa Waziri nakuomba utakapokuja hapauweze kusema kwamba ni lini bandari hii itajengwa, linitutakamilisha maongezi na China Merchant Port?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili la bandari nalopia lina mgogoro wa fidia, wananchi 687 walipunjwa fidiazao, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo alithibitisha hivyo naMthamini Mkuu wa Serikali ameshafanyia tathimini tayari.Mheshimiwa Waziri ndani ya bajeti yako hakuna pesa zakuwalipa hawa wananchi, naomba utakapotoa majumuishoutuambie hawa wananchi 687 waliopunjwa fidia yaowatalipwa lini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala kubwa zaidi,katika kipindi hiki cha maandalizi Serikali iliwaahidi wananchihawa jumla ya kaya 2000, kwamba itawahamishia mahalipengine na shule yao ya msingi ya Pande itajengwa huko,zahanati yao waliyojenga kwa nguvu zao wananchi nanguvu za wahisani itahamishiwa kule, Ofisi ya Serikali ya Kijijiitahamishiwa kule, nyumba zao za ibada, makanisa namisikiti itajengwa kule ili wawe na makazi mapya. Nyumbawatajenga wenyewe lakini miundombinu hii ya jamiiitajengwa kule, hili jambo halijatokea mpaka hivi sasa, nawananchi hawa wanaishi kwa wasiwasi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, aliyekuwa Katibu Mkuu waWizara yako ya Viwanda ambaye wakati ule alikuwa DGwa EPZA anakumbuka safari zangu nyingi ambazo nilikuwanimeenda kule EPZA kufuatilia jambo la makazi mapya.

Mheshimiwa Waziri utakapofanya majumuishotafadhali chonde chonde uwaambie wananchi waBagamoyo hao wanaopisha bandari lini watapata makaziyao mapya ili waondoke pale na nchi yetu iweze kujengabandari mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaNaibu Spika, nashukuru sana kwa muda ulionipa na naungamkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa MarthaUmbula atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu,Mheshimiwa Hussein Bashe ajiandae.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Naibu Spika,na mimi nakushukuru kupata fursa hii niweze kuchangia hojaya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi pia niungane naWabunge wenzangu kumpongeza sana Mheshimiwa Wazirikwa kazi kubwa anayoifanyia nchi yetu katika sekta yaviwanda. Kama kweli kila mtu amesoma vizuri kitabu hiki,na mimi ni mara chache sana nasoma vitabu vya Wizara,lakini katika wizara hii nadhani kwa sababu nilikuwa najuakwamba nitachangia nimesoma vizuri sana; kusema kwelinia njema ya Serikali yetu baada ya kusoma kitabu hiki yakuhakikisha kwamba inatuvusha kwenda uchumi wa kati nauchumi wa viwanda, nina hakika tutafikiwa hasa kwatakwimu ambazo zimesheheni katika kitabu hiki cha Waziri.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze mchango wangunikianza na sekta ya viwanda, katika nchi yetu. Sekta yaViwanda ni ya kimkakati, kwa nini nasema ni ya kimkakati?Si tu inaenda kupeleka nchi yetu katika uchumi wa kati lakiniinakwenda kutatua changamoto nyingi ambazo nchi yetuna wananchi wetu wamekuwa wakipigia kelele sana,nikianza na migogoro ya wakulima na wafugaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na wafugaji. Kamatutazingatia maelekezo ya nia ya Serikali yetu katikakutupeleka kwenye viwanda, nina hakika wafugaji wetuwanakwenda kuachana na matatizo ya kuhangaikakugombania ardhi, kunyanganyana ardhi na wakulima kwasababu azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba inaendakujenga viwanda vya nyama, ngozi, pamoja na maziwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Kama tutapata viwanda hivi na mazao yote yanayotokanana mifugo nina hakika kwamba wakulima wetuwanakwenda kupunguza mifugo yao maradufu na matatizoya kuhamahama na mifugo kuhakikisha kwamba nchi yetusasa inafuga kwa namna ambayo wana uwezo wa kupatakunufaika kwa mifugo yao na nina hakika migogoro hiyoitapungua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwa wakulima.Wakulima wetu wamekuwa na matatizo makubwa yakukosa masoko. Hamasa kubwa ya mkulima nikumuhakikishia soko. Kama viwanda vyetu vitakwendakuchukua malighafi ya kilimo nina hakika kwamba wakulimawetu watahamasika vilivyo, watalima kwa bidii, tena kwaubora unaotakiwa ili malighafi ambazo zitatumika katikaviwanda vyetu hivi vitokane na mazao ya kilimo. Kwa hiyo,nina hakika kwamba hata umasikini wa kipato ambao badoumekidhiri baina ya watanzania, umasikini pamoja naMKUKUTA I, II, III uliokuwepo bado umebaki palepale.Tutakapogusa sekta inayowaajiri watu wengi ambayo nikilimo na ufugaji nina hakika umaskini utapungua maradufukatika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nirudi kwenye pointyangu ya kusema kwamba viwanda ni mkakati maalum wakuvusha nchi yetu kuondokana na matatizo mbalimbali.Tutakuwa na biashara ya uhakika, tutakuwa tumepunguzaumasikini kwa jinsi nilivyoeleza, kwa sababu sekta inayogusawatu wengi ni ya kilimo na ufugaji. Tutakuwa tumehamasishapia vijana kujiunga na kil imo kwa hivyo tutakuwatumeongeza ajira kwa wananchi wetu, lakini pia tutakuwatumepunguza migogoro ya wakulima na wafugaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kidogo kuhusubiashara ya utalii. Katika biashara ya utalii nchi yetu badohaijanufaika kadri ambavyo inalingana na maliasil ituliyonayo, rasilimali tulizonazo katika sekta hii. Tunayo maporimazuri sana katika nchi yetu ambayo hayapo kule duniani,tunao wanyamapori wazuri ambao hawapo katika nchi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

mbalimbali, lakini nchi yetu bado haijanufaika kwa jinsiambavyo tuna maliasili hiyo niliyotaja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais wetu kwanamna ambavyo amekuwa mbunifu ameona kamatutakuwa na maliasili ya aina hii, tuwe na mapori mazuri,wanyama wazuri, lakini kama watalii hawaji kwetu kujakuangalia maeneo haya, bado hatutakuwa tumenufaika.Kwa hiyo, amekuwa mbunifu, na biashara ni ubunifu naviwanda ni mbunifu. Amenunua ndege ambazo atahakikishawatalii wetu watakuja Tanzania, watakuja kutembeleamapori niliyoyataja kwa ajili ya kuona wanyama wetu nahivyo uchumi wetu utakwenda kasi na kuhakikisha kwambatunanufaika na sekta hiyo ya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya Kambi ya UpinzaniBungeni ukurasa wa 23 imebeza ununuzi wa ndege. Kubezasikatai kwa sababu ni kazi yao, lakini wabeze kwa takwimu.Mimi nimeeleza kwamba huo ni mkakati kwa sababu hataBiblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosamaarifa. Hayo ni maarifa ya kuhakikisha kwamba tunawaletawatalii nchini mwetu ili tunufaike na sekta yetu ya utalii.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niweze kutoa ushaurikwa Serikali. Tozo katika sekta hii bado ni tatizo. Wataliiwakisikia kwamba Tanzania wanatoza VAT kwenye hudumaza utali i, bado kuna hatari ya kupunguza manufaatutakayopata kwa sababu atakwenda katika nchi nyinginena sisi tutabaki kulalamika. Ninaomba Serikali yangu kamasi tatizo kubwa iondoe tozo la VAT kwenye huduma za utaliiili tuweze kunufaika maradufu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kuhusu Benkiya Rasilimali (TIB). Benki hii iko Dar es Salaam, biashara nimikopo, tunaomba Benki ya Biashara ifungue matawi yakekatika mikoa mbalimbali ili wananchi wetu waweze kukopa,wakulima waweze kukopa ili waweze kupata mitaji yakutosha kuweza kuendesha biashara zao. Ninaiomba Serikaliyangu iweze kufikiria jambo hilo. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie sasa Mkoawangu wa Manyara. Mkoa wetu wa Manyara uko pembezonina mkoa huu uchumi wake uko chini, lakini cha kushangazani kwamba tunayo mazao mengi ambayo mengine piahayapo popote pale Tanzania. Kwa mfano zao la pareto,linalimwa kwa uchache sana kule kusini lakini mazao mengiya pareto yanaozeana kwenye godown kwa sababu hakunasoko.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaiomba Serikali iwezekuangalia uwezekano wa kuanzisha kiwanda kule Bashnetambako tunalima sana zao la pareto. Pareto ni zao zuri sana,dawa ya mbu ambayo ni very effective kuliko dawa zote,inaitwa expel inatengenezwa kutokana na pareto. Kwahivyo, tunaiomba Serikali iweze kutujengea kiwanda katikaMkoa wetu wa Manyara hususan Bashnet. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tunalima vitunguusaumu. Vitunguu saumu ni zao ambalo kwa kweli uborawake sina haja ya kueleza, lakini wakulima wanalima kwakutumia zana duni, wakulima hawanufaiki kwa sababu,masoko bado yako chini. Ninaiomba Serikali yangu katikaharakati hii ya kuanzisha viwanda hasa kujenga mkoa wetuwa Manyara ambao upo pembezoni na uchumi wake ukochini lakini una rasilimali nyingi iweze kutujengea kiwandakule Mbulu ambako tunalima zao la vitunguu saumu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, inashangaza kidogo,maeneo ambayo yana mifugo mingi kanda ya kaskazinimkoa wangu wa Manyara, Wilaya ya Mbulu inaongoza kuwana mifugo mingi, Wilaya ya Kiteto, Simanjiro na Hanang, lakinicha kushangaza kiwanda cha nyama kipo Arusha.Tunaiomba Serikali na sisi Manyara iweze kutujengea kiwandacha nyama Mkoa wa Arusha ili wananchi wetu wafugajiwaweze kunufaika kutokana na mazao yao ya mifugo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kwa msisitizokabisa mikoa ya pembezoni kama Manyara ni mikoa ambayoinalimwa mazao mengi kama mahindi, maharage na mazao

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

mengine ndiyo maana bodi nyingi za mazao yameanzishwa,bodi ya korosho, bodi ya katani, lakini sisi hatuna bodi huko.Lakini tunaomba recognition ya Serikali kuona kwambamkoa wetu unazalisha mazao mengi ya biashara, tunaombaviwanda vielekezwe kule ili na sisi tuweze kunufaika na sektahii ya viwanda na biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kueleza hayanaomba kuunga mkono hoja, na nashukuru kwa kunisikiliza.(Makofi)

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi kwa mara ya pili kujadilibajeti hii ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilishatoa pole kwa waleambao walifiwa kwenye maafa mbalimbali hivyo naombaniende moja kwa moja kwenye hoja hii ya Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda ni lazima kwaustawi wa wananchi wa nchi yoyote. Ninasema hivi kwasababu viwanda na kilimo kwa pamoja ndivyo vinavyosaidiakwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleoyake, huo ndio ukweli. Kwa hiyo, kama nchi haisisitiziviwanda na kilimo hakitaendelea kwa sababu kilimo kwakiasi kikubwa kinasaidiana sana na viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kuipongezaSerikali na siipongezi tu kwa maneno na kwa vitendo kwasababu sekta hii imekuwa kwa asilimia 7.8 ukilinganisha naukuaji wake mwaka uliopita wa asilimia 6.5, na imekuwaikikuwa hivi wakati zamani ukuaji wa viwanda ulikuwa chini.Ukuaji huu umetokana na sera nzuri ambayo kuna wenginewalisema imekaa muda mrefu, Sera ya Maendeleo(Sustainable Industrial Development) ya mwaka 1996 mpaka2020. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uzuri wa sera ni kukaa mudawa kutosha ili muda wa utekelezaji uwe unatosheleza. Kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

hivyo, ninaomba niipongeze wizara hii kwa kuendeleakutekeleza sera hii ambayo kwa kiasi kikubwa inatakaviwanda visambae nchi nzima na vifike hata kulepembezoni ili maendeleo ya nchi yawe na uwiano mzuri. Kwahivyo, ni sera nzuri ninaomba tuendelee kuitekeleza, namwaka 2020 utakapofika tutaifanyia kazi changamoto ilituboreshe sera nyingine itakayofuata.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kutokana na sera hii SIDOimekuwa na program inayoitwa MUVI ambapo imetaka kilamkoa uwe na viwanda ambavyo una malighafi yake na iliuwiano wa maendeleo kwenye mikoa yetu iweze kufanana.Hii programu karibu itakwisha. Ninaomba Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji ijiandae baada ya MUVIkutakuwa na nini? Kwa sababu mwenendo na mwelekeowa MUVI ni mzuri sana. Unapokuwa na specialization kwakila mkoa unawezesha kuwe na biashara kutoka mkoa hadimkoa, na ndiyo baishara ya ndani itakavyokuwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nataka nitoe mfanokwa Wilaya yangu ya Hanang ambapo il ipangiwakutengeneza kuwa na viwanda vidogo vya ngozi kwasababu sisi ni wafugaji na mazao mengine yanayotokanana mifugo na Singida imepewa specialization ya mafuta yaalizeti kwa sababu inalima alizeti. Kwa hiyo, watu wa Singidawatakuja kununua bidhaa za ngozi kwetu na sisi tunanunuamafuta kule. Tukiwa na utaratibu wa namna hii nchi nzimatutaendelea na maendeleo yatakuwa na uwiano mzuri,hakutakuwa na mahali ambapo patabaki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba MUVI ifuatiliweili muda wake utakapokwisha tuwe na programu nyinginenzuri, na tumeifanya program; mimi nasema hivyo kwasababu nilikuwa Wizara ya Viwanda; ili muda wake usiishe,huu si mradi ni programu na programu haina mwisho wake.Kwa hivyo ndugu zangu ninaomba sana tufanye hivyo ilituongeze ajira kwa watu wetu, ili tuongeze mauzo ya nje.Nilipokuwa Wizara ya Viwanda tulikazana, kuna miaka miwilitulipita mauzo ya kwenda Kenya kuliko ununuzi wa bidhaakutoka Kenya, inawezekana.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mtajitahidi kutekelezasera hii ya sustainable Industrial Development tutafika pazurina hata tutaipita hii Kenya kwa sababu sisi tuna resourcesau maliasili nyingi kuliko hiyo Kenya ambayo inatupita kwaviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili viwanda vilete manufaanchini lazima tuwe na uwiano mzuri. Kwa sasa hivi kwa mujibuwa hiki kitabu cha Mheshimiwa Waziri viwanda vidogo sanani asilimi 85, viwanda vidogo asilimia 14, viwanda vya katiasilimia 0.35, viwanda vikubwa asilimia 0.5 uwiano huuu simzuri. Tunataka tuwe na uwiano mzuri wa viwanda vidogokuwa vingi kama asilimi 65; vya kati vifuate na vikubwa hatavikiwa asilimia 5 haitakuwa mbaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, uwiano huu utatusaidiasana kuona kwamba malighafi zinatumika vya kutosha,itatufanya tuone kwamba mazao ya kilimo yanapatamasoko kwa sababu viwanda ndio soko la uhakika la mazaoya kilimo. Vilevile itaajiri wananchi wengi. Hata hivyo ajiraimeongezeka. Mwaka 2016 viwanda viliajiri watu 146,892ukilinganisha na mwaka jana ambapo 139,000 waliajiriwa,kwa hivyo, trend ni kukua lakini ajira hii haitoshi na ndiomaana nasisitiza umuhimu wa uwiano wa viwanda.

Ninaomba niongelee kidogo Kurasini Logistic Center,sijui mtakuwa mmefika wapi jamani. Tulianzisha LogisticCenter ya Kurasini ili tuweze kuagiza vitu kwa bulk purchasesna wafanyabiashara wa Kongo, Rwanda waje pale iliKariakoo iwe Hong Kong ya Afrika, hilo ni moja. Hata hivyokuna watu wanaogopa kwamba tutakuwa tunaagiza vitukutoka China. Kutokana na Logistic Center tutajua mahitajiya watu na nchi ambazo zinazunguka Tanzania na viwandavitaanzishwa kwa haraka sana.

Kwa hiyo naomba sana Logistic Center ianze. Vilevilenataka tuongeze mauzo kwenda nje…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Nagu muda wakoumemalizika.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru lakini ninaomba Liganga ni kiwanda mamatukisisitize kianzishwe. Ninaunga mkono na ninampongezasana Mheshimiwa Waziri wetu anafanya kazi nzuri. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Hussein Basheatafuatiwa na Mheshimiwa Maria Kangoye, MheshimiwaCatherine Magige ajiandae.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie fursa hiikumpongeza kwa dhati kabisa Mheshimiwa Rais kwa ku-revive dream ya kuwa na industries katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1967 Mwalimu Nyererealiasisi dhana ya kuwa na viwanda, na focus ikawa importsubstitution industries, viwanda ambavyo baadaye vilikujakufa. Kwenye bajeti ya mwaka jana nilimuahidi kaka yanguMwijage, kwamba tutakutana na nilionesha mashaka yangujuu ya utekelezaji wa dhamira ya yeye kufikia yale ambayoalikuwa ametarajia, na leo tunayaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, vision ya Rais ni kujengauchumi wa viwanda ambao utalijenga Taifa hili kujitegemea,hii ndiyo vision ya Rais. Kwenye battle field, Chief of Staff naGenerals wanachora vita kwenye meza, wanaoendakupiganisha vita hii ni makamanda. Tuna tatizo kubwa laku-link vision ya Rais na mikakati yetu ya kuweza kufikiamalengo aliyokuwa nayo Mheshimiwa Rais ya kuwa naviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nitoe mifanomichache, kwa taarifa ya BOT ya mwezi Aprili, manufacturingindustry imeshuka kutoka 1.4 million US Dollar mpaka 817million US Dollar, maana yake tumepoteza dola milioni 500.Re-Export ime-drop kwa dola milioni 80, fish and fish productsime-drop kwa dola milioni 20, lakini on the other hand credits

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

kwenye agro sector zime-drop mpaka kufika negative 9.2,transport and communication zime-drop by negative 21.6,building by negative 3, hotel and restaurant ime-drop by 7%.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, export of traditional crops,bidhaa pekee iliyo-grow ni korosho na not because of volume,because of price. Tobacco imeshuka kutoka mwaka 2015,three hundred and forty three million US Dollar mpaka milioni281 mwaka 2017 Machi. Cotton imeshuka kwa dola milioni10, kahawa imeshuka kwa dola milioni tisa, karafuu imeshukakwa dola milioni 13. Sisal ime-grow only for one million USDollar. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, capital goods, capitalequipments. Capital goods zimeshuka mpaka negative 16.7,transport imeshuka kwa 23.9, building 19.3, machinery 11.3,what is the problem? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, problem ni un-predictabilityya sera zetu za kodi. Nitatoa mfano wa Sheria ya Uwekezaji,kifungu namba 19. Sheria hii tumeibadilisha mwaka 2009 kwakufuta utaratibu wa deemed capital goods, ikashushainvestiment. Tukaibadilisha mwaka 2010;tukaibadilishamwaka 2012; tunafuta na kurudisha, tukaibadilisha 2014 natumeibadilisha mwaka 2015. This is the same country sheriaile ile, leo unweka incentive kesho unafuta. MheshimiwaMwijage hata ahubiri kwa Injili na Qurani, we will never gothrough. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nichukue mfano,success ya industrialization ni private sector na MheshimiwaRais amesema. Nimechukua kitabu cha miaka mitano champango, hakuna hata page moja inayoongelea namna ganiprivate sector itakuwa included kwenye growth of economyof this country. The problem is a Ministry of Finance that is ourbiggest problem. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikupe mfanomwingine, ninayo Ripoti ya World Bank iliyoifanya Tanzania

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Micro Reform for Agri-Business. Ili uanzishe kiwanda kidogocha kuzalisha maziwa unatakiwa uwe na documentszifuatazo, upate Incorporation Business Licence kutoka BRELA,Premise Registration, Equipment and Truck Registration,Product Testing and Registration, Staff Health Certificate, OnGoing Inspection, Import Permit/Export Permit, WeighMeasures; ili uzipate hizi zinatakiwa zipite BRELA, TFDA, TBS,Diary Board, OSHA, Ministry of Labour, Weigh and Measure,NEMC, all of these! Nani anakuja kuwekeza hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu, DeputyManaging Director of International Monitory Fund alikuwepoTanzania, amesifia sana uchumi wetu kwa kipindi cha miaka20, lakini amesema mambo matatu na naomba ninukuu:-

“(i) It is essential to increase investiment in an effectiveway to address key bottlenecks in the economy and createmore jobs.”

Mheshimiwa Naibu Spika, our area to create jobs niku-link industrialization na agriculture, tusipofanya namna hiyohatuwezi ku-create kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe mfano waWamachinga, na nimeongea na Mheshimiwa Waziri waTAMISEMI ameahidi kuipitia hii Sheria ya Fedha ya Serikali zaMitaa. Leo tuna Sheria ya Fedha tuliyoifanyia mabadilikomwaka 2012 ambayo inamtaka mfanyabiashara alipe servicelevy ya 0.3 percent. Wewe ukiwa unauza coca cola, doubletaxation angalia hii. Cocacola Kwanza atalipa service levykutokana na turn over na muuzaji wa Nzega anatakiwa alipe0.3 on the same product ambayo mmei-tax from the producermnakuja kum-tax from the agent na mnakuja kum-tax retailseller. How can we grow business like this? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kaka yangu MheshimiwaMwijage, utazunguka all over the world. Nataka niwapemfano kuhusu leather industry, waliongea WaheshimiwaWabunge hapa. Kuzalisha one square feet ya ngozi Tanzaniani senti 14 dola, Ethiopia ni senti 8, India ni senti 7, Pakistan ni

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

senti 8, how can we compete? Na why, kwa sababu, sisitumeweka export duty ukizalisha ngozi Tanzania kui-exportunalipia kodi, uki-import chemicals kwa ajili ya ku-processngozi unalipa 25% tax, unalipa 18% VAT, how can we grow?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima kabisa natakaniiombe Serikali na Mheshimiwa Waziri wa Fedha, there is nowhere in the World una-tax inputs. Kodi zote lazima ziwekwekwenye output, una-tax vipi inputs! Unaongeza cost ofproduction, nani atawekeza? BOT imefanya mabadilikokwenye mfumo wake wa interest, nani ataenda kukopa?There is no way! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana ripoti ya BOTinaonesha lending imeendelea kushuka kwa sababu hakunasehemu ya kwenda kufanya biashara. Sasa hivi wanachingatunakusanya kodi za Halmashauri vibaya mno, hawakui hawawatu, mkulima kodi, mmachinga kodi akianza kufanyabiashara yake, mwekezaji kodi. Nataka niishauriSerikali, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda toa direction duniaijue.

Mheshimiwa Naibu Spika, umefanyika Mkutano waIFC juzi, one week ago, kujadili emerging economies and whereto put money kwenye private sector, Tanzania inakuwadiscussed ni area ambayo ni unpredictable. Leo mna sheriahii kesho akija Waziri huyu anabadilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, there is no way kama Wizaraya Fedha haitaelewa kwamba kodi ni secondary, numberone is creation of wealth and creation of job. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kiisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Bashe, mudawako umemalizika.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Waheshimiwa Wabunge tunaendelea, MheshimiwaMaria Kangoye atafuatiwa na Mheshimiwa Catherine Magigena Mheshimiwa Gimbi Masaba ajiandae.

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mungu kwakunipatia afya na kuniwezesha kusimama ndani ya Bungelako Tukufu. Pia, niipongeze Serikali yangu ya Awamu ya Tanokwa kazi nzuri inayofanya. Niipongeze pia Wizara hii yaViwanda Biashara na Uwekezaji kwa kazi nzuri na jitihadazake katika kuijenga Tanzania ya Viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwakuanzisha programu ya kuwapa vijana 1,000 elimu yautengenezaji wa bidhaa za ngozi kutoka katika Chuo chaDIT Mkoani Mwanza na tayari 90 wamehitimu wiki iliyopitana wengine wanaendelea kujiunga na kozi hiyo. Pamoja napongezi hizo bado ipo haja ya wanafunzi hawa kutafutiwaviwanda ambapo wataweza kufanya internship.

Mheshimiwa Naibu Spika, niiombe Serikali yangu, kipokiwanda ambacho kilikuwa chini ya Mwanza Tanneries chakutengeneza bidhaa za ngozi ambacho kilibinafsishwa namwekezaji yule hajulikani hata alipo, lakini hata mashinezilizomo mle ndani zimeshatolewa. Nipende kuiomba Serikaliyangu sikivu iweze kukirejesha kile kiwanda kwa Serikali, iliwanafunzi waweze kupata sehemu ya kufanyia practicals,na vile vile lakini waweze kupata sehemu ya kufanyiainternship na kuajiriwa kama ikiwezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya uwekezaji nchini sirafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje, hivyo ipo haja yaSerikali kutengeneza mazingira mazuri. Mimi binafsi na-declareinterest kwamba ni mmiliki wa kiwanda cha mavazi na tauloza kike. Ninapoongea hapa ninaongea kutokana na kileninachokifahamu, ni ukweli kwamba hatutaweza kuijengaTanzania ya viwanda kama hatutakaa na kupitia hizi kodina tozo mbalimbali ambazo ni nyingi na zimekuwa zikiathiriuwekezaji ndani ya nchi hii. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Mheshimiwa Naibu Spika, tozo hizi na kodizimesababisha bidhaa zetu kuwa za gharama kuliko hatazile zinazotoka nje. Haiwezekani leo mfanyabisahara ambayeananunua pamba kutoka kwa wakulima inafika hatua ana-prefer kuuza nje ya nchi kwa sababu hatalipa VAT. Pambahiyo hiyo ikienda nje inatengenezwa nguo, nguo zinaingiandani bila kulipa VAT, sasa inakuwaje kwamba, viwandavyetu viuziwe kwa wafanyabiashara wale watalipa VAT nasisi pia huku ndani tuuze na tulipe VAT? Ina maana hatutawezaku-compete na masoko ya nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano mzuri tunauonakwamba hata mbolea inayotoka Kenya leo hii ni ya bei ndogoikifika nchini kuliko ile mbolea ambayo tunazalisha hapa.Kwa namna hii hatutaweza kutengeneza Tanzania yaviwanda. Suala hili liangaliwe kwa umakini kwa sababu sasalimeanza kuhamasisha wawekezaji wa ndani ya Tanzaniakwenda kuwekeza katika nchi za jirani kwa sababu wanajuawakiwekeza kule wataleta bidhaa zao nchini na hawatalipaVAT. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sina mashaka na kazi nzurianayofanya Mheshimiwa Waziri na wasaidizi wake wote,lakini kama tunavyofahamu kwamba Wizara hii nimtambuka na inahitaji cooperation kutoka katika Wizarambalimbali kama ya Afya, Kilimo, Fedha, Nishati nanyinginezo. Hata hivyo bado inahitaji ushirikiano kutokaTaasisi mbalimbali za Kiserikali kama TFDA, EPZA, TIC, NDC,SIDO, NEMC na nyinginezo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo langu hapa ni urasimumrefu. Kumekuwa na urasimu mrefu sana katika uwekezajiwa Tanzania ambao umekatisha tamaa viwanda vingi. Kwamfano, mwekezaji wa kiwanda cha dawa atahitaji kwendaTFDA, NEMC, atahitaji kupitia kwa Msajili wa Kampuni,ataenda TRA na kote anakokwenda kunakuwa na mudamrefu wa kusubiria matokeo ambayo anataka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kuishauri Serikalikuliangalia hilo kwa ukaribu kwa sababu imesababisha sisi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

kupoteza wawekezaji wazuri na wameenda kuwekeza katikanchi nyingine. Kwa mfano kiwanda cha Omnicane ambachokilitaka kujengwa hapa Tanzania, lakini kutokana na urasimuhuu na changamoto hizi nilizotaja hapo awali kimeendakuwekeza Mauritius ambapo leo kimeajiri wafanyakazi 1,472lakini kinazalisha umeme kutokana na makapi ya miwagigawatts 717 ambayo ina-produce katika communityinayowazunguka, lakini pia, kwa siku kina-produce sukari tani8,500. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa tulicheza karatambovu kwa kweli, kwa sababu sisi ndio tungekuwatunanufaika na haya. Tuki-compare kwa haraka harakaviwanda vyetu vikubwa ambavyo ni Kilombero na Mtibwakwa mwaka vinazalisha sukari tani 80,000 ambayo niproduction ya siku tatu ya Kiwanda cha Omnicane. Chakushangaza zaidi pamoja na ukosefu wa sukari ya kutoshandani ya nchi yetu na experience hiyo ambayo nimeitoakutokana na kiwanda cha Omnicane bado tunaendeleakuweka mazingira magumu kwa viwanda ambavyovinataka kuanzishwa hapa vya sukari. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano mzuri ni kule Tarime.Tarime kuna mwekezaji ambaye yupo tayari kufunguakiwanda cha sukari, lakini kumetokea vita iliyoanzishwa naMbunge wa Tarime Vijijini ili kukwamisha kiwanda hikikujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda hicho kikijengwakitanufaisha wananchi wa Tarafa za Ingwe na Inchageambavyo ni…

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika,Taarifa!

MHE. MARIA N. KANGOYE: …ambavyo ni vijiji vinnevya Biswalu, Mrito Matongo na Kijiji cha Wegita…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maria Kangoye, kunaTaarifa. Mheshimiwa Esther Matiko!

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

T A A R I F A

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu spika,ningependa nimpe Mheshimiwa Maria Kangoye taarifakwamba kwa sababu Mbunge wa Tarime Vijijini hayupo, nakwa sababu najua sakata lote kuhusiana na uwekezajikwenye shamba la miwa kule Biswalu, ningependa tu nimpetaarifa kwamba Mbunge wa Tarime Vijijini hapingi uwekezaji,bali anataka process zifuatwe ili tuepushe yale ambayoyanatokea Nyamongo watu wanakufa, wanapokwa ardhibila kufuata process za ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimpehiyo Taarifa kwamba Mbunge, Madiwani na Halmashauri yaTarime Vijijini haipingi uwekezaji. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maria Kangoye, unaipokeahiyo taarifa?

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa hiyo siipokei kwa sababu hata wiki iliyopita wananchiwa vijiji hivyo vinne vya Biswalu, Mrito, Matongo na Wegitakijiji wanakotokea wanangu mimi Bhoke na Ryoba walikujahapa Dodoma na mabasi mawili, wamekuja kuandamanana kuja kuonana na Waziri wa TAMISEMI. Na mimi nimekaanao, nimepata taarifa hiyo, hata taarifa ya habari ilioneshahivyo.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa!

MHE. MARIA N. KANGOYE: Kwa hiyo, sipokei taarifahiyo. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa!

NAIBU SPIKA: Ameshapewa taarifa kuhusu jambo hilo,Mheshimiwa Kangoye endelea.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,ni muhimu sana, huyu anapotosha watu hapa, si kweli.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kwanza usiwachemicrophone, unatakiwa usimame uonwe au umuandikieSpika. Ukiwasha wewe akiwasha na yule, akiwasha mwinginetutaweza kuwasil iana humu ndani? Naomba ukae,Mheshimiwa Kangoye malizia.

MHE. MARIA N. KANGOYE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Ni matumaini yangu kwamba, muda wanguutalindwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda hikikitakapojengwa pale kitanufaisha tarafa za Ingwe naInchage katika vijiji hivyo vinne ambavyo ni Biswalu, Mrito,Matongo na Wegita, kijiji ambacho wanangu wanatokeaBhoke na Ryoba. Pamoja na hayo yote kiwanda hikikikijengwa kitatoa ajira kwa wananchi 15,000 lakinikitapunguza changamoto ya ukosefu wa sukari ndani ya nchihii. Vilevile pia kitaongeza maendeleo katika vijiji hivyo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kuiomba Serikaliyangu kuwa makini na suala hili iweze kuingilia kati nakusimamia, ili kiwanda hiki kiweze kuanzishwa kule Tarime.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo yotenaomba niunge mkono hoja asilimia mia moja. (Makofi)

NAIBU SPIA: Ahsante sana, Mheshimiwa CatherineMagige atafuatiwa na Mhshimiwa Gimbi Masaba naMheshimiwa Japhary Michael ajiandae.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Kwanza kabisa naomba sana niipongeze Serikaliyangu ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais John PombeMagufuli kwa kuendelea kutimiza Ilani yetu ya Chama chaMapinduzi kuwa tunajenga Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa nikiongea kilasiku hapa kuhusu Kiwanda cha General Tyre cha Arushanimeona kimetengewa pesa ili kianze, lakini ninachoombaje, tumejipangaje kuhusu viwanda vingine vinavyotengenezamatairi hasa vya nje? Je, Kiwanda cha General Tyretumejipangaje ili kifanye biashara vizuri? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nilikuwa naombareli ya Tanga – Arusha mpaka Moshi. Reli hii itasaidia sanakatika usafirishaji wa matairi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Arusha kuna viwanda vingitu, kuna Kiwanda cha Lodhia Plastic. Kiwanda hiki kimeajiriWatanzania 700; ni kiwanda cha mabomba na ma-sim tank.Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokuja tulitembelea kiwanda hiki,ni kiwanda chenye ubora wa hali ya juu na aliagiza baadhiya ofisi zetu za Serikali zitumie kiwanda hiki, lakini ma-engineerwa Serikali wamekuwa wakikwamisha kiwanda hiki.Wamekuwa wakiagiza mabomba nje ya Arusha, wamekuwawakiagiza mabomba Dar es Salaam ambapo kwanza nigharama kubwa sana, wamekuwa wakiagiza wakandarasiwanunue mabomba kwenye viwanda fulani, sijui kuna nini(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hizo figisu figisu hizo nahisikuna rushwa. Tumekuwa tunakwamisha Watanzania ambaowanajitokeza kuendeleza viwanda vyao kutimiza kauli yaRais wetu Tanzania yenye viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sanaMheshimiwa Waziri aangalie hili, Mheshimiwa Waziri Mkuualishatoa amri sijui kama kuna amri nyingine zaidi ya WaziriMkuu. Tujue hawa ma-engineer wa Serikali ni kitu gani hasawanapata mpaka wanatoa amri kwa makandarasi iliwaende wakachukue mabomba kutoka kwenye viwanda

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

vya nje ya Arusha, kwa sababu kwanza ni gharama.Tunasema tunabana matumizi matumizi gani tunabanakama ni hivi? Tunahujumu na tunamhujumu Rais wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Arusha tuna Kiwanda chaGypsum kinaitwa Saint Gabain Lodhia Gypsum. Kiwanda hikikinatumia makaa ya mawe wanatoa Kiwira, mpaka wafikeArusha wanatumia dola 120 mpaka 130. Kiwanda hikikimekuwa kinatozwa pesa nyingi tofauti na viwanda vingine.Wamekuwa wananunua makaa ya mawe dola 65 mpaka70; huku viwanda vingine vimekuwa vinatoa dola 35.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninamwomba Waziriaangalie sana, tunazidi kukwamisha jitihada za Rais wetuza kuwainua Watanzania. Pia kiwanda hiki kimeajiriWatanzania 450. Hiki cha plastic tayari Watanzania 250wameshapunguzwa kwa ajil i ya hawa watu ambaowanatuhujumu. Ninaomba sana kwa kweli MheshimiwaWaziri mimi nitashika shilingi nisipopata jibu la kiwanda hikicha plastic, nisipopata jibu kiwanda hiki ambacho kinatumiaMakaa ya Mawe ya Kiwira. Naomba Mheshimiwa Waziri ujena majibu yanayoeleweka ama sivyo sitakuelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri Mkuu alikujatulitembelea Kiwanda kimoja cha Hans Paul. Yule niMtanzania ana kiwanda, anachukua magari Anaya-designyanakuwa magari ya kubebea taka. Magari yake anauzashilingi milioni 200 mpaka 220. Mheshimiwa Waziri Mkuumwenyewe aliona alishaanga sana hakutegemea kamawatanzania wanaweza wakawa na ujuzi kama huo. Nimagari mazuri na yana ubora wa hali ya juu. Ningeshauribaadhi ya Halmashauri zetu zitembelee zione kuliko uangizemagari kwa bei zaidi ya shilingi milioni 500 huku tunawezatukapata magari yenye ubora wa juu hapa hapa nchini kwashilingi milioni 220. Naomba sana tulinde viwanda vya ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Arusha tulikuwa na kiwandakikubwa sana cha dawa kimefungwa mpaka leo nakimefungwa na Tanzania tuna uhaba wa dawa. Kwa ninikisifunguliwe hata kisaidie hata Kanda ya Kaskazini yote?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Naomba sana Mheshimiwa Waziri uje kunijibu na hili kiwandacha dawa cha Arusha kimefungwa mpaka leo. Naomba sanakiwanda hiki kifunguliwe Serikali ijipange ifungue kiwandahiki. Tunayosema Tanzania yenye viwanda haitakuwa yenyeviwanda bila kutekeleza haya ninayokuambia Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua kuna watu ambaowalipewa viwanda vilivyokuwa vya Serikali, lakini viwandavile wameng’oa mashine, viwanda vingi tu havitumiki tena.Tunaomba viwanda hivi mkiweza mvirudishe Serikalini ilivifanye kazi, Watanzania waweze kupata ajira tuwezekutumia na sisi bidhaa zetu. Watu wengi walipwa viwandalakini wamefanya ma-godown.

Mheshimiwa Naibu Spika, Arusha tunajua ni mkoaambao unaongoza sana kwa mifugo, ni Mkoa ambao unawafugaji wengi sana. Tunaomba na sisi mtuwekee angalukiwanda cha ngozi ili tuweze kutumia mifugo yetu naitufaidishe tuweze kutengeza viatu. Ngozi inatengeza vituvingi sana tunaombasana mtuangalie Arusha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na malalamikomakubwa sana kwa wafanyabiashara, wanakata tamaawanashindwa kuendelea, tunakwamisha jitihada zaWatanzania. Kuna process ndefu sana katika kupata vibalicha kuanzisha biashara. Wanapitia sehemu nyingi sanampaka wanakata tamaa. Tunaomba sana MheshimiwaWaziri wasaidie Watanzania wengi, hiki ni kilio cha watuwengi sana. Tunakuomba Mheshimiwa Waziri narudia tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba sana mimi leokweli nitashika shilingi Mheshimiwa Waziri asiponijibu kuhusuKiwanda cha Plastiki cha Lodhia. Vilevile nilikuwa naombawashirikiane na Waziri wa Maji hata idara zetu za maji mfanokama AUWSA watumie watu ambao wako kwenye mikoayao maana viwanda ni vizuri, kuna hujuma hapa; na hawama-engineer wa Manispaa wa mikoa yetu nilitaka nifahamuwenyewe wana nguvu gani kuliko Mheshimiwa Waziri Mkuu?Kama Mheshimiwa Waziri Mkuu anatoa amri hawaitekeleziwanatuma mabomba wakachukue mabomba Dar es

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Salaam inawezekana kweli? Wanapatanini? Kwanzagharama ni kubwa; tunasema Serikali yetu tunabanamatumizi naomba tusimuangushe Mheshimiwa Rais ana nianzuri na Watanzania ana nia nzuri na nchi yetu, ana nia nzurina chama chake ambacho ndiyo anatekeleza Ilani yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, sina mengi, naunga mkonohoja, lakini Mheshimiwa Waziri nitashika shilingi leo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa GimbiMasaba atafuatiwa na Mheshimiwa Raphael JapharyMichael, Mheshimiwa Ahmed Juma Ngwali ajiandae.

MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia Wizaraya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Awali ya yote napenda nimshukuru Mwenyezi Mungukwa kunipa afya njema kwa siku ya leo ili niweze kutekelezamajukumu yangu kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu.Vilevile nishukuru Mwenyenzi Mungu; amsaidie mwenyekitiwangu wa Kanda ya Ziwa Serengeti Mheshimiwa Hecheaweze kupata nafuu ili aweze kuja kutekeleza majukumuyake. Nimeona jinsi ambavyo ameanza kunyemelewa nakashfa na kwa jinsi ambavyo namfahamu mimi siyo muuminiwa kupinga maendeleo. Nafahamu hilo yeye ni Mwenyekitina mimi ni Makamu wake kwa hiyo tunafanya kazi ofisi moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayonaomba tu nizungumze kwamba tunapozungumza Tanzaniaya viwanda naamini kabisa hakuna Mtanzania anayepingaTanzania ya viwanda. Hata hivyo ninachokiona ni kwambahatuendani na kauli ya Tanzania ya viwanda. Ninasema hayakwa sababu katika taarifa ya Waziri amezungumza mambomengi sana na mimi kama Mbunge ninayetoka katika Mkoawa Simiyu tunapozungumza viwanda maana yake tunagusamalighafi za maeneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Simiyu tunalimakila kitu, lakini cha kushangaza sijaona mahali popote

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

ambapo Mkoa wa Simiyu unazungumziwa kuhusu kupatakiwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi niliuliza swali ambalolinahusiana na viwanda ambavyo vilikuwepo kwa mudamrefu, viwanda ginnery na nilivitaja kama viwanda vitano,Nasa Ginnery, Ngasamo Ginnery, Maswa na Malampaka,viwanda vyote hivi vimekufa na nikahoji Serikali inampangogani kuvifufua viwanda ambavyo vimekufa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri alisemamkakati wa Serikali na jukumu alilopewa ni kuhakikishaviwanda vyote vilivyokufa vinafanya kazi. Sasa ninatakakujua kauli ya Serikali, hivyo viwanda ni lini vitaanzakufanyakazi ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu waanzekunufanikana na viwanda hivyo vya kuchambua pamba?

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumzia viwandalazima tulipe kipaumbele zao la pamba. Mkoa wa Simiyuzao la pamba limekufa, wakulima hawalimi tena zao lapamba kutokana na kwamba soko hili la pamba halipo.Wananchi wanatumia gharama kubwa kuandaa mashambaya pamba kama vile palizi pamoja na vitu vingine lakini chaajabu wanakwenda kuuza kilo ya pamba shilingi 1,000;jambo ambalo siyo zuri hata kidogo kwa Watanzania waMkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninachotaka kuombakama kweli Serikali inadhamira ya dhati na kwa kutambuaMkoa wa Simiyu kwamba ni wa wakulima wakubwa sana,ninaomba ipewe kipaumbele kikubwa sana ili kuhakikishakwamba tunapata viwanda vya kila aina.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumza wakulimana wafugaji, Mkoa wa Simiyu tuna wakulima na wafugaji.Lakini pamoja na malighafi zote hizi hakuna kinachofanyikakule Mkoa wa Simiyu. Sisi ni wafugaji lakini cha kushangazahakuna hata kiwanda cha kusindika nyama, hakuna.Wafugaji anapakia ng’ombe kwenye malori kupeleka Dares Salaam. Mmewahi kuona wapi sisi binadamu tunakwenda

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Jiji la Dar es Salaam kutalii ng’ombe nao wanakwendakuangalia jiji la Dar es Salaam? Ni aibu kwa Taifa hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Serikali isitengenezeviwanda ili wananchi hawa waweze kunufaika? Miminiombe sana, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda niko kwenyekamati yako. Kilio changu kikubwa sijawahi kuchangianikizungumza suala la kimataifa. Mara nyingi nazungumziaMkoa wa Simiyu na Wabunge wenzangu wanaotoka Mkoawa Simiyu kila siku tunapiga kelele kuhusiana na suala yaMkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunalima choroko, tunalimazao la alzeti, tunafuga, bado ndani ya mifugo tunazalishambolea, kwa nini sasa tusiwe hata na kiwanda chakutengeneza biogas inatokana na vinyesi vya ng’ombe? Kwanini kila kitu hakuna? Halafu tunakuja tunasema Tanzania yaviwanda! Sipingani na kauli ya Tanzania viwanda lakinimatendo yetu hayaendani na Tanzania ya viwanda. Miminiombe sana kwamba tuangalie ni namna gani tunawezakuusaidia mkoa huu wa Simiyu ili tuweze kuendena na kasiya Tanzania ya viwanda ambayo mnaizungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri waViwanda wewe unatoka Mkoa wa Kagera. Mkoa wa Kageraunazalisha ndizi, lakini cha kushangaza sisi unatudanganyaunatuambia una viwanda una nini, kwako hakuna hatakiwanda cha kuchakata ndizi, hakipo. Naomba uoneshemfano sasa wewe vinginevyo utaingia kwenye mkumbo waMawaziri hewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika tumekuwa na changamotokatika historia ya Tanzania. Historia ya Tanzania tumeshuhudiakwamba Serikali imekuwa ikiyakopesha mabenki kutokaBenki Kuu kwenda kwenye benki ndogo ndogo wamekuwawakiwakopesha. Wakikopesha fedha zile benki wananchiwetu wananufaika kukopa hususan akina mama ntilie.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni kwa mara yakwanza Serikali ya Awamu ya Tano kunyang’anya fedha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

kwenye mabenki na kuzirudisha Benki Kuu; jambo ambalolimesababisha sana kuyumba kwa uchumi. Lakini hizi fedhazingekuwa kwenye mabenki ya kawaida mama zetuwangeweza kukopa, lakini sasa hivi wamefungia kule benkitumebaki tunalia; mama analia, baba analia kila mtu analia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Wabunge form onetuliambiwa kwamba ukiwa Mbunge unakuwa na fedhanyingi sana. Lakini sasa hivi tunalia hata kuliko mwananchiwa kawaida. Jambo ambalo ni aibu kwa Taifa hili. Hatahivyo naamini kabisa kwamba Wabunge tuna hali mbayalakini tunashindwa kulia kwa sababu ya utu uzima wetu,kwamba unawezaje kulia wakati na mtoto kule analia; kwahiyo inabidi mama unyamaze kimpya uendelee kuumiapolepole. Lakini mimi ninachokiamini kabisa ni kwambabaada ya miaka kadhaa tutajikuta tumepata maradhiambayo yametokana na stress zilizosababishwa na ugumuwa maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachoomba kusema sasani kwamba Mheshimiwa Waziri wa Viwanda atakapokujakuhitimisha hapa nitahitaji kufahamu suala la viwanda vyaginnery vilivyokufa, ni lini vile viwanda vitafufuliwa, la pilli,nini tamko la Serikali itakapofika msimu wa kuuza pambawananchi wauze kwa shilingi ngapi ili tuweze kuendana nakasi ya Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayoninakushukuru sana Mungu akubariki.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Masaba.Nilikuwa nimesikia mahali kwamba Simiyu ndio inatoa mfanomzuri wa viwanda ama sijasikia sawasawa. Nimesikia Simiyumna kiwanda sijui cha chaki, maziwa hebu tusaidie ni kwenuhuko tunatakiwa kuja kujifunza au?

MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante Kiwanda ambacho Mheshimiwa Waziri wa Viwandaanajifunia nacho ni kwamba kilianzishwa na kikundi cha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

vijana kwa ajili ya kutengeneza chaki na Halmashauri ikaingiaikachukua hicho kiwanda. Kwa hiyo, ndicho tunachojivunianacho. Lakini sisi tunadai viwanda vinavyotokana na pembeza ng’ombe tunaka tutengeneze hata vifungo.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa sawa, mimi niliyekuulizanimekuelewa. Mheshimiwa Nyongo nilikuwa nimemuulizaswali kwa hiyo alikuwa ananijibu mimi sasa hiyo taarifa labdakama unanipa mimi. (Makofi)

Waheshimiwa tunaendelea, Mheshimiwa RaphaelJaphary Michael atafuatiwa na Mheshimiwa Ahmed JumaNgwali, Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni ajiandae.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia kwenyeWizara ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba ya KambiRasmi ya Upinzani kuna hoja ambayo imekuwa-raisedkwamba inawezekana ndoto yetu ya kufikia Tanzania yaviwanda ina mashaka makubwa. Lakini imeonekana kamavile ni uchokozi ambao upande mwingine haukuutaka.Lengo la Kambi ya Upinzani kuonyesha wasiwasi wetu kwadhana hii kufikiwa, ni vizuri Serikali ikalichukulia hili kamachangamoto na isiwe ni sababu ya kuanza kuletamalumbano yasiyo ya lazima.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1967 Tanzaniailishaanza hatua hizo za kujijenga katika dhana mzima yaIndustrial Revolution na bahati mbaya tulienda na dhana hiyotukiwa na mtu ambaye ni dedicated ambaye alikuwa Raiswetu wa Kwanza wa nchi hii. Hata hivyo mwaka 1996 dhanaile tuliiua wenyewe. Na bahati nzuri mwaka 1996 kwa lengohilo la ubinafsishaji tulikuwa na dhamira kwamba tunawezatuka-develop zaidi kama tutakuwa tume-adopt vizuri dhanaya ubinafshaji ambayo bahati mbaya hatukuweza kuifanyiakazi vizuri. Sasa wasiwasi wetu ni kwamba kama Sustainable

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

Industrial Development Policy ya tangu mwaka 1996 mpakaleo haijaweza kufanya kazi vizuri, nini miujiza ya kuifanya kwamiaka mitano? Ndio wasiwasi wetu. Sasa nafiki ni vizuritungeichukua kama changomoto muhimu sana Serikaliilituweze kuifanyiakazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa kipindi hichovikwazo vilivyokuwa vinakabili sekta ya viwanda ndiyoambavyo viko sasa, tangu 1996. Wachambuzi waliokuwawanatunga hii Sera ya Sustainable Industrial DevelopmentPolicy waliona kwamba tuna vikwazo vya unfavorable legaland regulatory framework ambazo zilikuwa ni kikwazokimojawapo, limited access of SMEs to finance, cha pili; chatatu kilikuwa infective and poor coordinated institutionalsupport framework; vitu ambavyo mpaka leotunavizungumza kwamba ni tatizo katika nchi hii.

Sasa lazima tuone kwamba tuna mahali ambapopanatukwamisha na kwa pamoja tufikiri namna ganitunatoka hapa kwenda mbele ili tufikie hiyo ndoto yaTanzania ya viwanda. Kwa hiyo ni vizuri mkaichukua kwauzito wake hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la pili ambalolinafanya tuone mashaka ya viwanda ni soko letu la ndani.Tuna soko la ndani la kiwango gani. Nini uwezo wa watuwetu kununua katika soko letu la ndani, purchasing poweryetu. Ukizingatia kwamba viwanda anavyovihubiriMheshimiwa Waziri ni viwanda vidogo sana vyenye kuajirimtu mmoja mpaka watu watano; viwanda vidogovinavyofuatia vyenye kuajiri watu watano mpaka watu 49na viwanda vya kati vyenye kuajiri watu 49 mpaka 99.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda hivi vinatengemeasana soko la ndani, soko ambalo hatuna kwa sababu Serikaliya Awamu ya Tano imechukua fedha zote ambazo zilikuwaza Serikali ikaziamishia Benki Kuu na ni sawa tu na hadithi ileya mtu aliyechukua rupia akaifukia chini ya ardhi. Haiwezekaniuchukue fedha zile ambazo zilikuwa kwenye mzungukouzipeleke benki ukiamini ndio uwekezaji.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Kwa hiyo, matokeo yake tumepunguza sanamzunguko wa fedha katika uchumi wetu, tumepungusauwezo wa uwekezaji katika uchumi wetu na kwa misingi hiyopurchasing power ya watu imepungua, sasa kwa hawa watuwanaozalisha wanakwenda kumuuzia nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio leo tunaambiwakwamba kuna hata soko la kuuzia bidhaa za kiwanda chabidhaa za kupambana na malaria zimekosa soko kwasababu hatuna soko la ndani. Sasa tunafikiaje haya malengo?Hili ndilo suala la msingi la kujadili kwa pamoja ili tuonetunavyoweza kufikia lengo la kuwa na Tanzania ya viwanda.Kwa hiyo ni vizuri tukayachukua haya masuala kwa uzitowake.

Mheshimiwa Naibu Spika, wafanyabiashara wa ndanikama wengi walivyosema hawana mazingira rafiki yakibiashara, kuna vitu vingi vya kuwakwaza, ni lazimatuviangalie, tuwapende wafanyabiashara wa ndani.Wafanyabiashara wa ndani tunawaumiza, tunaonekanakama hatuna haja nao, tunaonekana kuvutia zaidiwafanyabiashara wa nje ambao hata wenyewe hatunavivutio vya kutosha vya kuwavutia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni vizuri tuone namnagani tunajiweka vizuri katika maeneo hayo ili tufikie katikadhana ya Tanzania ya Viwanda. Kila mtu anaona uthubutuwa kufikia hiyo dhamira ya kuwa na Tanzania ya Viwandailiyoonyeshwa na Serikali hii, lakini lazima sasa tuone tunafikajekatika hatua hiyo kwa pamoja wote kama Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la Mkoawa Kilimanjaro. Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa na viwandazaidi ya 15, leo hakuna kiwanda kinachofanya kazi ukiondoaKiwanda cha Bonite peke yake. Sasa nataka MheshimiwaWaziri aniambie ni lini atahakikisha Kiwanda cha Madawaya Mimea kinafanya kazi? Kiwanda kile kimewekeza fedhaza Watanzania nyingi mno za mikopo lakini kiwanda kilehakuna siku kimefanya kazi na Watanzania wanadaiwamadeni kutokana na fedha ambazo Serikali hii ilikopa lakini

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

kiwanda kimekuwa pale ni white elephant haifanyi kaziyoyote mpaka leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nil ikuwa naombaMheshimiwa Waziri aniasaidie ni lini kiwanda kile kitafanyakazi? Ni lini Kiwanda cha Machine Tools kitafanya kazi?Kiwanda ambacho katika zama za Mwalimu Nyererekilikuwa ni kiwanda mama kama vilivyokuwa viwanda vyachuma vya Tanga. Kama ninavyozungumzia Liganga naMchuchuma, lakini leo kiwanda kile hakifanyi kazi, na nikiwanda ambacho kilikuwa ni cha tatu katika Afrika, lakinileo hakifanyi kazi; na mnaimba Tanzania ya viwanda,mnafikiaje hilo lengo la kufika Tanzania ya viwanda kamakiwanda mama hamuwezi kukifanya kikafanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nilikuwa najiulizakiwanda cha magunia Mheshimiwa Waziri umeorodheshakwenye hotuba yako Kilimanjaro viwanda vimebinafsishwahavifanyi kazi. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais ameoneshadhamira kwamba anataka Tanzania ya viwanda, kunakigugumizi gani cha kuwanyang’anya wale watu viwandaambao hawavifanyii kazi? Nini kigugumizi cha Serikali? Kwanini hapo mnakosa uthubutu wa kufanya maamuzimagumu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama watu wamechukuaviwanda tangu mwaka 1996 mpaka leo hawavifanyii kazi,ni kwa nini mnapata vigugumizi ya kuchukua vile viwanda?Kiwanda cha Magunia kil ichokuwa kikiajiri watu waKilimanjaro leo hakifanyi kazi, kimekuwa godown la kuwekeabidhaa, kwanini tunawalea hawa watu na nyie mnaona nijambo la kawaida. Bahati mbaya kuliko vitu vyote Serikaliyenu haifanyi kazi kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wa Moshitumegundua kwamba hamtaki kufufua vile viwanda.Tumeanzisha mipango yetu ya kujiendeleza wenyewe,tumetaka kujenga stendi ya kisasa pale ya kushindana nasoko letu lakini mpaka leo Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMIhataki kutupa kibali, kwa nini? Kwa sababu ni eneo la

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

upinzani ama sababu ni nini? Tumeomba kwamba Moshi iweJiji ina sifa zote, lakini leo tunanyimwa kwa nini? Sasamtakuzaje huu uchumi na mnafikaje Tanzania ya viwanda?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilikuwa nafikiri nivizuri kama kuna lengo la kufikia Tanzania ya viwanda tuonetunafikaje huko, lakini kuanza kuhujumiana kwa sababu zakisiasa ni jambo la ajabu sana. Kama hamtaki huu mfumowa vyama vingi vya siasa futeni ili wengine tukafanye biasharazetu zingine kwa sababu hatuwezi kuja hapa kuwawakilishawananchi, tujenge mawazo ambayo ni constructive halafumyakatae unnecessary bila sababu yoyote ya kimsingi, kwanini?

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa natamani sananione mlivyo-link katika suala la kufikia Tanzania ya viwanda,namna gani mnamsaidia Mheshimiwa Rais. MheshimiwaBashe amewaambia na Mheshimiwa Zitto amewaambia;namna gani mnamsaidia Rais ili ndoto yake itimie. Otherwisemtazungumza kama ilivyozungumzwa tangu mwaka 1967,mtazungumza kama ilivyozungumzwa tangu 1996 mpakaleo na mtazungumza mpaka miaka mingine 40 ijayo mbelehamuwezi kufikia Tanzania ya viwanda. Hatutaki kwambamfike hapo, hii nchi ya kwetu wote, tunataka tu-achievelengo la kuwa na Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lazima na nyiemheshimu mawazo ya watu wengine muone kwambawanaweza wakafanya. Lengo la viongozi ni kuwa wabunifu,ziacheni Halmashauri Madiwani wabuni mipango yao namuwape support Madiwani. Acheni kule chiniwafanyabiashara wafanye biashara zao vizuri, waacheniwamachinga wa-develop ili dhana ya SME ifanyike. Sasamsipoyafanya haya mnaifikiaje Tanzania ya viwanda?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimependakuyaonesha haya kwamba Kilimanjaro tuna shida. Kiwandacha Ngozi leo kinazalisha kidogo; Ofisi ya Makamu wa Rais,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Mazingira itusaidie kuhakikisha kwamba kile kiwandakinatumia teknolojia ya kisasa; watu pale wanaumia kwaharufu ya kile kiwanda. Sasa hatutaki kifungwe kwa sababuhatuna viwanda, lakini tunataka kilazimishwe kuzalishwa kateknolojia ya kisasa ili kulinda afya za watu wa Moshi maanakuna watu pale wanapata maradhi, mtawalipa na nini namtawafidia kwa kitu gani kwa roho za? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilikuwa naombasana ichukuliwe kwamba lengo letu ni jema na ni la msingikwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunakuwa na Tanzania yaViwanda kweli. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana muda wako umeishaMheshimiwa Japhary. Mheshimiwa Ahmed Juma Ngwaliatafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni naMheshimiwa Seif Gulamali ajiandae.

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza mimi nioneshe masikitiko yangu makubwa kwaWizara ya Viwanda. Kimsingi niseme tu kwamba Kamati yaBunge ambayo inasimamia viwanda na biashara ni Kamatiambayo inatakiwa imshauri Rais kuhusu mambo ya viwandalakini kamati hiyo haijawahi kwenda hata gerezani kukaguaviwanda wala haijawahi kwenda Kenya, China wala India;sasa sijui inamshauri vipi Mheshimiwa Waziri na viwandavyake. Kwa hiyo, mimi nioneshe tu masikitiko yangu kwambajambo hili si sahihi kwa kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hasa nil itakakuzungumzia maeneo kama mawili ama matatu na hasanataka kuongelea Tanzania and China Logistic Centre yaKurasini. Mara ya kwanza mradi huu ulizungumzwa katika ileChina-Africa Corporation mwaka 2009 kule Cairo. Mradi huumwaka 2012 ulianza kuingia katika Bunge na kuwashawishiWabunge. Katibu Mkuu wa Viwanda sasa Dkt. Meru alikuwawakati huo mimi nikiwa kama Mjumbe wa Kamati yaViwanda na Biashara alikuwa haondoki katika Kamati kamavile yeye ni Mjumbe wa Kamati na kuishawishi Kamati ikubalihuu mradi wa Kurasini.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

Mheshimiwa Naibu Spika, tulianza kutathmini ilethamani ya wale watu ambao wanatakiwa kulipwa fidia,uthamini ule. Uthamini wakati huo ukawa shilingi bilioni 60,tukashawishiwa kwamba lazima tufanye uthamini harakaharaka il i muda usije ukaongezeka huyu mwekezajiakakimbia. Hata hivyo tukakaa kwa miaka mitatu baadaye,tulipokuja kulipa shilingi bilioni 60 tukaambiwa fedhazimeongezeka shilingi bilioni 40 tena. Kwahivyo, tumelipashilingi bilioni 101 badala ya shilingi bilioni 60; lakini baadaetukaambiwa mradi huo haupo, mradi huo umekwenda wapiooh yule mbia kaondoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kuna shilingi bilioni hizozote zimelipwa wala huo mradi wenyewe haupo natukashawishiwa kuambiwa kwamba mradi huu utaingizaajira za moja kwa moja milioni 25 na ajira indirect zaitakuwalaki moja. Kwa hiyo, sisi tukaingia katika malumbanomakubwa na Serikali kwenye jambo hili kutaka EPZA wapewepesa ili huu mradi uweze kwenda. Mheshimiwa Mwijagemradi uko wapi? Mradi huna. Ukisoma huu mpango wamwaka mmoja huoni hasa kipi ni kipi na Serikali ya Chinawakati ule ilisema kwamba itatoa shilingi bilioni 600 tukilipashilingi bilioni 60, jambo ambalo mmetudanganya, hakunakitu kinachoendelea baada ya miaka minne. (Makofi)

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mwijage nataka ujibu hasa,usije ukatuambia maneno ya ajabu ajabu, uje ujibu hasa kwanini mradi huo haupo na fidia imetolewa na fedhazimeongezeka na lini mradi huu utaanza na upo katikampango wa mwaka mmoja, sidhani kama katika mpangohuu tunaweza kuona jambo hilo, hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nazungumzia MiniTiger Plan ambao mimi nina interest kwa sababu mradi uleikiwa utasimama basi na Zanzibar itafunguka kiuchumi. Kwahiyo, huu ni mradi kila siku nilikuwa ninauombea dua, ulikujanao mwaka 2002. Ule mradi ukasema kwamba una awamumbili; awamu ya kwanza ni kulipa fidia hekta 2500 lakinitufanye kwa ujumla, mpaka sasa kumelipwa shilingi bilioni26.6; zinahitajika kulipwa shilingi bilioni 51.1 lakini mradi haupo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

na baadhi ya watu 1700 wamelipwa fidia na wenginehawajalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nataka kujua kwambahuu mradi upo? Ukitizama kitabu chenu cha Mpango waMaendeleo ya mwaka mmoja utakuta kwamba hata huyomwekezaji hayupo. Wakati ule tulikuwa tukiambiwa Omanna China wapo watakuja, na lakini Mheshimiwa Rais piamwenyewe kasema kwamba hiyo sio priority yake. Palepalikuwa pana mradi wa bandari na viwanda lakini humundani mnasema kwamba mtajenga barabara katika eneohilo la Bagamoyo, reli, umeme na maji. Ni reli ganiitakayokwenda kule kwa mwaka mmoja? Jamani tuwerealistic katika mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo, MheshimiwaMwijage utujibu, na huu mradi upo? Isije ikawa kamatulivyofanyiwa Kurasini, watu walikuwa wana deal yaowakalipwa fidia na baada ya kulipwa fidia mradi ukapoteana huku mnataka muwalipe watu fidia halafu mradi upoteekama ambavyo mmetufanyia huku. Safari hii tunazaa nawewe Mheshimiwa Mwijage. (Makofi) [Maneno Haya SioSehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna fedha za CBE shilingimilioni 400 ambazo…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ngwali kwa ajili ya kuwekakumbukumbu vizuri hebu ondoa hayo maneno yako yautazaa na Mheshimiwa Waziri.

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nimeondoa hayo hayana tatizo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, milioni 400 CBE zimetafunwana Mkurugenzi wa Fedha pamoja na Mkuu wa Chuo. Jambohilo alilisema Mheshimiwa Waitara mwaka wa jana hapa,lakini hakuna ripoti yoyote. Badala ya kwenda kufanya ukaguziDar es Salaam ambapo ndiko zilikoliwa ninyi mkaendamkafanya ukaguzi Dodoma na Mwanza, inawezekanaje?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Fedha zimeliwa kwa wengine mnakwenda kufanya ukaguzikwa wengine… (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara taarifa.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nimpe taarifa Mheshimiwa anayechangia kwambajambo hilo lil ikuja Bungeni bajeti il iyopita 2016/2017;Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Katibu Mkuuwanalijua. Katibu Mkuu aliandika barua ya terehe 19 Mei,2016 kuomba ukaguzi akataja vyuo vinne Dar es Salaam CBEambayo kuna shilingi milioni 400 anasema na utumishi mbayawa madaraka, Mwanza, Dodoma na Mbeya. Taarifa zilizoponi kwamba ukaguzi umefanyika Mwanza na Dodoma pekeyake na Dar es Salaam taarifa haipo. Kwa hiyo, hiyo ni taarifakamili iliyopo na makablasha yapo hapa na MheshimiwaWaziri anayo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Ngwali nakupa taarifahiyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ngwali unaipokea taarifahiyo?

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nimeipokea taarifa hiyo kwa upendo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, twende sasa katikamisamaha ya kodi. Nakubaliana na alichosema jana nduguyangu Mheshimiwa Serukamba kuhusu misamaha ya kodi nakodi ambazo zinasumbua hasa upande wa TanzaniaInvestment Centre. Lakini ukija sasa kwenye maeneo yauwekezaji SEZ misamaha ya kodi ambayo ipo haina haja yakuongezwa tena, ni mingi sana. Naomba nisome baadhiya misamaha ya kodi ambayo inawavutia wawekezaji katikaeneo la uwekezaji la SEZ. Msamaha wa malipo ya kodi yaushuru kwa mashine, vifaa, magari ya mizigo, vifaa vya ujenzina bidhaa nyingine yoyote ya mtaji mkubwa itakayotumikakwa madhumuni ya maendeleo ya miundombinu ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

uwekezaji katika maeneo maalum ya SEZ, huo ni msamahawa kwanza. Lakini msamaha wa pili ni msamaha juu yamalipo ya kodi kwenye kampuni katika kipindi cha miakakumi, msamaha wa tatu ni msamaha juu ya malipo ya kodiya zuio la kodi, gawio na riba kwa miaka kumi, msamahajuu ya malipo ya kodi ya malipo kwa miaka kumi, msamahawa ushuru wa forodha, kodi ya ongezeko la thamani na kodinyingine; msamaha wa malipo ya ushuru wa stamp kwenyevyombo vyote vinavyofanya hivyo na mambo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upendeleo yauhamiaji hadi wa watu watano katika kipindi cha mwanzocha uwekezaji na baadae wakizingatia mashartiwataongezwa; msamaha wa malipo ya VAT. Kwa hiyo, kunamisamaha katika SEZ ambayo ni mingi sana EPZA, hakunahaja ya kuongeza misamaha kwenye eneo hilo. Tuangaliezaidi kwenye TIC tujue ni namna gani tunafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la tatu ni kuhusu PVoC;tunazungumza ile Pre-shipment Verification of Conformity.Eneo hili ilipitishwa programu ya kuzuia bidhaa bandiakuingia ndani ya nchi, tukapitisha hiyo na TBS ikapitisha. Lakinijambo la ajabu toka mwaka 2012 bidhaa bandia zimezagaakatika Tanzania, TBS, FCC na FDA wapo. Sasa namna ganibidhaa zinazagaa? TBS aidha hawafanyi kazi yao vizuri kwasababu kwanza kuna tatizo, tatizo lililopo ni kwamba TBSwanazuia sub-standard lakini hawana uwezo wa kuzuia fakekwa sababu substandard na fake ni vitu tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kikiwa chini ya kiwangona kitu fake vinatofautiana kabisa, kwamba ikiwa chini yakiwango maana yake ni kwamba kile kitu sio halisia lakinihalisia, unaweza kitu original kimetengenezwa na Kampuniya Sony akakitengeneza mtu katika eneo vile vile kuliko kilelakini hicho kikawa ni fake na si sub-standard.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo bidhaa bandiaMheshimiwa Mwijage kila kona ya Tanzania inatusumbua.Mkiulizwa kila siku mnasema mnawafanyakazi kidogo nakuna vituo vingi, maana kuna vituo 38 au 48 lakini mnadhibiti

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

vipi bidhaa fake? Hiyo ndio issue yetu tunataka. TBSwamekwenda mbali Tanzania mpaka tunaingiza mafutamachafu, TBS wanakwenda kukagua wanaruhusu mafutamachafu yanaingia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi leo nilikuwana hayo lakini nimwambie tu Mheshimiwa Mwijage…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ngwali.Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni atafuatiwa naMheshimiwa Seif Gulamali na Mheshimiwa Subira Mgaluajiandae. (Kicheko)

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa NaibuSpika, na mimi nashukuru sana kupata nafasi hii ili niwezekuchangia Hotuba ya Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji. Nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na timuyake wameandaa hotuba nzuri sana ambayo nadhaniimetupa changamoto ya kuijadili hapa ndani. Vilevileningependa nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, yeye anajina lake ambalo kule mtaani katika vile viunga vya viwandatunamuita mzee wa sound, halafu anasema kwamba yeyemke wake anamwita ni handsome boy. Kazi yake ni nzurisana Mheshimiwa handsome boy, Mheshimiwa Waziri waViwanda na Biashara. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ningependakuzungumzia masuala makuu matatu. La kwanza, kuna hajakubwa sana sasa ya kujaribu kuoanisha vizuri sana kazianayofanya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na kazi ambayoMheshimiwa Waziri wa Fedha anaifanya, kwa sababu palendipo tunapoanzia kutofautiana. Mheshimiwa Waziri waViwanda anafanya kazi kubwa sana ya kupiga debe nakuhakikisha hii philosophy ya uchumi wa viwanda inaanzakwa kasi sana hapa nchini, lakini bado kuna hiccup kubwasana upande wa Wizara ya Fedha; kwa sababu huyu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

ataweza tu kuwa na philosophy ya uchumi wa viwandakama na mambo yote yanayohusu mambo ya kodi na vivutiokwa wawekezaji yanakwenda samabamba. Vinginevyoitakuwa ni wimbo ambao utaendelea kuimbwa nahatutapata majibu ya haraka haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda nimuombeMheshimiwa Waziri atoe tafsiri zaidi anaposema viwanda,kwa sababu tumekuwa tukichangia hapa tunasema mimikwangu hakuna kiwanda, viwanda vimesimama sijuimagunia na kadhalika. Tafsiri ya kiwanda kutoka kwaindustrial economist ni kitu chochote ambacho kinaweza ku-transform bidhaa moja kwenda kuwa bidhaa nyingineinayoweza kutumika. Kama ni mbao kuwa kitu au meza nakadhalika, kama ni kuchanganya dawa basi iweze kutumikakama dawa na kadhalika, from chemicals to drugs.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo katika hali yakawaida bado tunapata ukakasi kwamba ni namna ganitunazungumzia dhima nzima ya uchumi wa viwanda.Ukiangalia Serikali inajaribu kuweka miundombinu namazingira ya kumfanya mfanyabiashara au biashara iwezekufanyika hapa nchini.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu kwa miakamitano iliyopita, Tanzania tumeweza ku-export nje, Indiabidhaa zenye thamani ya dola bilioni 1.12, Kenya dola milioni793, South Africa dola milioni 698, China dola milioni 620,Japan dola milioni 370. Lakini tumeweza ku-import, SaudiArabia peke yake ni bidhaa za zaidi ya shilingi bilioni 5.6, Chinashilingi bilioni 2.23, India shilingi bilioni 1.24, Uarabuni shilingimilioni 789 na South Africa shilingi milioni 567. Kwa hiyo,ukiangalia Tanzania tumeweza ku-export lakini tumeingizazaidi na hii ndiyo changamoto ambayo inaanzia pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia katika suranzima, maeneo ya msingi lazima tuangalie namna ya kuwezakuongeza uwekezaji utakaoondoa ukiritimba wote nakuongeza ajira na tija kwa Watanzania, bila kufanya hivyotutaimba wimbo huu hatutafanikiwa kuufikia. Hii nasema kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

sababu kumekuwa na tatizo kubwa sana sasa hivi hasa lawawekezaji. Wenzangu wamesema, nisingependa kurudiakwamba nchi yetu lazima tuweke utaratibu utakaowezakuwa rafiki kwa wawekezaji kuwekeza hapa nchini. Mtuhawezi kuwekeza hapa nchini kama kuna uncertainties naunpredictable tax regimes, haiwezekani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimininachoomba sana katika hili tumsaidie Mheshimiwa Waziriwa Viwanda, si la kwake peke yake; na Bunge hili tuna jukumula kuishauri Serikali yetu, kwamba ni namna gani masualahaya yanaweza kuoanishwa na kuhuishwa kwa ajili yakuchochea uwekezaji hapa nchini. Sisi si kisiwa, Tanzania tunavivutio vingi sana, tuna maeneo mengi sana ya kuwekezalakini sisi na wenzetu tuna-compete hivyo lazima tuwekemazingira ambayo yatajenga assurance kwa mwekezajianapokuja hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tutambue uwepo naushiriki kamilifu wa sekta binafsi, hili ni suala la msingi sana.Najua tumekuwa na kasumba kwanza kutokutaka kuipendaprivate sector, lakini Waheshimiwa Wabunge, bila kuipendaprivate sector na kuipa nafasi ya ushiriki vizuri hatutawezakutoka hapa tulipo. Acha Serikali iwekeze pale ambapopanatakiwa huduma itolewe na pengine pasipo faida, lakinimaeneo ambayo yanahitaji kupata faida tuwekeze zaidi kwahawa wawekezaji binafsi na tuingie utaratibu wa PPP, huuutasaidia kuipunguzia Serikali mzigo wa kutumia fedha zakekatika kuwekeza na matokeo yake tuisaidie private sectoriweze kuwekeza zaidi, Serikali inachotakiwa pale ni kuvunakodi. Mimi naomba sana hili tuweze kuliangalia.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tuangaliemustakabali mzima kwamba Watanzania tunatoka hapatulipo namna gani, uwekezaji huu unakuwa na tija gani kwaMtanzania, lazima tupate tija ya uwekezaji huu katikahuduma za afya, elimu na kadhalika. Hata hivyo tatizo lililoposasa hivi ni mitaji, liquidity sasa hivi kwenye economyimekuwa so tight, lending rates zimekuwa kubwa, watuwanashindwa kukopa fedha na kuwekeza. Njia pekee ni ku-

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

attract mitaji kutoka nje ili kusaidia kuwekeza hapa nchinilakini tutafanya vile kama wawekezaji hawa tutawawekeamazingira mazuri ya wao kuwekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa na hadithi yaMchuchuma na Liganga miaka nenda-rudi. MheshimiwaWaziri, hebu tusaidie, pale ambapo unadhani kabisakwamba inakushinda naomba Bunge hili likusaidie ili utusaidietutoke hapa tulipo tuache kuimba nyimbo na ngonjera zakila wakati. Ukiangalia ufanyaji biashara hapa Tanzania kilakukicha unakuwa ghali zaidi. Kwenye sekta ya utalii pekeyake kuna kodi zaidi ya 36, hivi kweli mtu atawekeza kwakodi hizi 36? Haiwezekani! Mimi sitaki kuzisoma, ni nyingi sana.Kitu ambacho ninaomba sana Serikali yetu ijaribu kuwa sikivu,na hasa Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lililopita niliwahikusema Mheshimiwa Waziri wa Fedha atusaidie na kusaidiamaana yake ni kwamba ajaribu kuwa kiungo na simtenganishi wa masuala ya uchumi katika nchi. Nina imanikabisa kwamba Watanzania kama tutafuata msingi mzuriwa uwekezaji, tutasonga mbele. Dhima na dhana aliyonayoMheshimiwa Waziri wa Viwanda ni nzuri, tunamsikia kilamahali anazunguka, hata ukikutana naye ukamwambiaMheshimiwa nataka kiwanda, anakwambia ntakupakiwanda, anakupa hata matumaini hata kama hana, hiyoinatosha Mheshimiwa Waziri, unatupa matumaini. Hata hivyoninaomba utuambie hapa vizuri zaidi tafsiri ya viwanda ilituweze kuelewa kwa sababu unapotuambia viwandatunawaza viwanda vikubwa tu. Kuna viwanda vidogo, vyakati na vikubwa, lakini kunakuwa na linkage ambayoinakuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tunasifika kwakuwa na uchumi unaokuwa pamoja na sera nzuri au tulivuza uchumi. Hizi lazima ziwe translated katika mahitaji yaWatanzania. Level ya umaskini Tanzania bado ipo katikakiwango cha juu na ndiyo maana hata Mheshimiwa Raisanasema sitaki kuona wananchi masikini wanateseka, he isfor the poors, lakini sisi tunafanya nini kusaidia kauli mbiu hii.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mheshimiwa Rais amejitahidi sana na kwa muda mfupitunaweza kuona kwamba nchi sasa inaanza kusonga mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeanzisha na miradiambayo ni mikubwa yenye kusimika uchumi wa nchi, kwasababu bila kuwa na logistics and division systems huweziukapanua nchi yako. Lakini sisi kama Tanzania, leo ujenzi wareli ni mardi mkubwa sana, unahitaji gharama kubwa sanalakini pindi utakapokwisha utakuwa ni uti wa mgongo wauchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuunga mkonohotuba hii, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Seif Gulamaliatafuatiwa na Mheshimiwa Subira Mgalu na MheshimiwaJaneth Mbene ajiandae.

MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kupata nafasi siku ya leo kuwezakuchangia kwenye Wizara hii ya Viwanda, Biashara naUwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi leo, kwanzaninamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Waziri kwa jitihadambalimbali zinazofanyika katika kuhakikisha kwambaTanzania ya viwanda inafikiwa. Pia ninashukuru kwa sababudhana hii inapozidi kuzungumzwa sana, mwisho wa sikuinatafsirika na watu wanaamini na wanaingia katikauwekezaji wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa sababu hiyoMheshimiwa Waziri mimi nijielekeze, najua unajua nikisimamakuzungumzia kiwanda siwezi nikazungumza mambomengine nikakiacha kile kilichopo pale kwangu Manonga,Manonga Ginnery. Mheshimiwa Waziri toka nimekuwaMbunge na siku yangu ya kwanza kuzungumza ndani yaBunge, nimezungumzia suala la Kiwanda cha Pamba ndaniya Wilaya yetu ya Igunga. Kiwanda hiki ni cha zamani sana,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

toka enzi za mkoloni mpaka juzijuzi kikabinafsishwa akapewaRajan, Rajan amekiendesha mpaka na yeye akakishindwaakakiacha, amefikia hatua amefariki, amemuachia mtotowake, mtoto wake yuko Uingereza mara sehemu mbalimbali.Tumezungumza tukakwambia wapo Igembensabowanakitaka hiki kiwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda hiki asilimia 80anamiliki Rajan, asil imia 20 anamiliki Igembensabo.Igembensabo anataka kukinunua hiki kiwanda, amewekamezani shilingi milioni 500 lakini Rajan amekinunua shilingimilioni 700 anataka kukiuza shilingi 1,500,000,000, kiwandakimesimama anataka kukiuza kama vile kinafanya kazi,kinaingiza faida na huyu ni mbia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, lakinitulikuomba uwakutanishe hawa watu wakae chini, waowako tayari. Umetuahidi mara nyingi hawa watuutawakutanisha wakae chini wazungumze Igembensaboyuko tayari, hata wao wako tayari, issue yako kama Waziri nikuwaita hawa ofisini kwako. Juzi juzi hapa katika majibuumesema umefanya jitihada mbalimbali, umetuambiakwamba huyu mtoto wa Rajan yuko Uingereza anakujabaada ya miezi sijui sita au saba, anachelwa. Hivi Serikali hiiya Dkt. John Pombe Magufuli ikitaka kumuita huyu kijanaitashindikana kweli? Yaani akakae Uingereza na kiwandachetu huku, kama hataki kukiendeleza si akiachie wapewewatu wengine waweze kuki-run? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi siamini kwambaSerikali hii imeshindwa kumuita, haiwezekani na siamini.Inawezekana, labda Mheshimiwa kwa sababu weweunasema unapiga-sound inawezekana na mimi kijana wakounanipiga sound, nielewe kwamba hiyo ndiyo sehemu yakupigana sound, lakini mimi siamini kwamba wewe zile soundunazosema unapiga unamaanisha kwamba unanipigasound kweli. Nikuombe Mheshimiwa Waziri, hebu muite huyukijana ikiwezekana, kama inashindikana si mkitaifishe sasa,mmeshamuita amekataa. Inawezekana hamjamtafuta nawao wako tayari kuja. Mheshimiwa Waziri tunakuomba, na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

Mbunge mmoja wa Simiyu amesema eti zao la pambalimekufa, si kweli, halijafa, uzalishaji wake umepungua na sikufa. Maana yake ukisema kufa maana yake watu hawalimikabisa, haiwezekani, kulima tunalima ila si katika kiwangoambacho Serikali ama nchi inataka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kweli uzalishaji wa pambaumepungua si tu katika eneo letu la Wilaya ya Igunga amaSimiyu, katika nchi yetu ya Tanzania uzalishaji wa pambaumepungua; na Serikali haijawekeza vya kutosha na kamahivyo viwanda, ginneries zipo nyingi zimetajwa, na mojawapo ya ginneries kongwe hii ya Manonga ni ginnerykongwe. Katika Mkoa wa Tabora ukizungumza Manongahakuna ambaye hajui, hakuna Rais ambaye hajui ginnery hii,lakini sijaona Serikali ama Waziri ukiwekeza katika kuhakikishakwamba kiwanda hiki kinafanya kazi. Waweke chini hawawatu wafanye mazungumzo, watauziana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wetu waTabora uangalie hizi fursa. Sisi tunalima sana maembe Mkoawa Tabora, tuna nyuki, tumbaku, ngozi nyingi sana, hasa kwasababu tuna ng’ombe wengi. Hivi Mheshimiwa katikamakabrasha haya hauhamasishi katika uwekezaji hukukwetu? Maana kila siku ninasikia tulikuja mpaka airportwawekezaji wameondoka tena, hivi wawekezaji wa kuishiaairport kweli? Hawa walikuwa wawekezaji au wasanii?

Mheshimiwa Naibu Spika, nikuombe MheshimiwaWaziri, hebu sukuma hili jambo ili kila mkoa uwe na fursamaana ukizungumza viwanda hapa vingi viko pwani na sisihuko kwetu Bara tunahitaji viwanda hivi vije, maanaviwanda vikiwepo vitapunguza msongamano wa vijanakuwepo Dar es Salaam. Ndiyo hii unasikia kila siku Dar esSalaam vijana wanavuta bangi, wanavuta dawa za kulevya,hizi vurugu zote zipo Dar es Salaam huko na miji minginehuku kwetu haipo katika kiwango hicho. Hebu tuletee hiviviwanda huko vijana wasikimbie vijijini ama wasikimbiewilayani wakakimbilia mikoa ya pwani huko. Hii itasaidiasana kwa sababu leo hii wanabaki bibi zetu kule nyumbanikwetu wanaonekana vikongwe hawa ama wachawi. Hebu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

muache kuleta hii dhana, leteni hivyo viwanda ili kupunguza,vijana wawepo wawasaidie wazazi wao, waendelezemaisha na itasaidia kuokoa maisha yetu katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hata hili suala la ngozilimekuwa linazungumzwa sana. Ni kweli tunataka tuwe naviwanda vya ngozi ndani ya nchi yetu, sasa ngozi imekuwanyingi kiasi kwamba wanunuzi hawapo. Tumeweka kodi ku-discourage ku-export ngozi yetu nje ya nchi, lakini sasa hawaambao tulionao viwanda vyetu havitoshelezi kununua ngozi,mwisho wa siku ngozi zinabaki kwenye machinjio, watuwananunua wanaacha katika maeneo yao. Hebutupunguze kodi ama tuwa-encourage hawa watu ili kamatumeshindwa kununua ngozi yote badala ya kuharibika wai-export tupate hizo dola ambazo zinatoka nje ya nchi ziinginendani ya nchi yetu. Mheshimiwa Waziri nafikiri hilo utakuwaumelisikia na utawasaidia hawa wafanyabiashara wa ngozi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine mimi ninalotakakulizungumzia ni hii issue ya One Stop Center. Leo tunaonamtu anapokuwa na kiwanda chake wanakuja watu waOSHA, NEMC, madubwasha yako mengi. Kwa nini isiwekwamba mtu yeyote anayetaka kuanzisha kiwanda aendesehemu moja, kama ni TRA alipie madubwasha yote, yeyepale apewe karatasi au sticker moja ambayo ndani yakeyumo OSHA, NEMC, TRA na watu wote ili akija mtu wa NEMCiwe ni kujiridhisha tu. Sasa mtu ana kiwanda anaki-run, sikumbili anakuja OSHA anampiga faini anamwambia fungakiwanda, mtu amewekeza kwa gharama kubwa halafuanaambiwa funga kiwanda. Hebu tuwe sehemu ya ku-encourage viwanda vyetu na tuwe sehemu ya kuwasahihishawenye viwanda ili waweze kuendelea kufanya hii kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi viwanda vinasaidiakutoa ajira kwa vijana wetu na hii inasaidia kupunguza tatizola vijana mitaani. Unapo-discourage watu wa viwandaunasababisha hawa vijana warudi mtaani wanageukamajambazi, wanageuka vibaka na hatimaye hawa hawawanageuka kuwa watu ambao si watu wema katika jamii.Tuombe Serikali iwasaidie wenye viwanda hata kama wana

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

matatizo ninyi muwe sehemu ya kutatua matatizo yao namsiwe sehemu ya kuzuia kufanya miradi au kazi zao. NiombeWizara, nafikiri mtakuwa mmelisikia hilo; naomba sanamuwasaidie wafanyabiashara, maana yake tafsiri yamfanyabiashara sijaelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninachojua,mfanyabiashara ni Mtanzania yeyote ambaye anaanzakutafuta kipato chake, mkulima ni mfanyabiashara. Kunamkulima gani ambaye anazalisha chakula halafu asikiuze?Huyo si mfanyabiashara. Mkulima ni mfanyabiashara kwasababu anazalisha, anauza. Mwalimu anafundisha, ama sisiWabunge hapa, wengine tuna hoteli, tuna guest houses,tunafanya biashara, maana biashara ikiharibika mpakakwenye hoteli zetu biashara zinaharibika huko. Humu ndaniya Bunge katika asilimia 100, asilimia 99 ni wafanyabiashara,tunatofautiana biashara gani tunafanya. Unaweza ukawaWaziri ukawa mfanyabiashara. (Makofi)

Suala lingine kabla sijafika mwisho, nafikiri mudawangu utakuwa si rafiki; kuna mtu alichangia jana hapaakasema Rais wa Kenya amepata chakula kutoka Mexicona chakula kile kinagawiwa kwa bei ya kutoka shilingi 3,000ya Tanzania kwa maana ya Kenyan shilings 150 kupunguzakwa shilingi 90 ya Kenya sawa na 1,800 ya Tanzania. Hivi kwasaa 24 inawezekanaje Rais akatoa tangazo halafu beiikashuka kwa kiwango hicho, inawezekana kweli au tunaletapropaganda ndani ya Bunge hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba hatakule alikosema kwamba ametoa chakula kile, Mexico,kwanza tutambue, Kenya sasa hivi kuna Uchaguzi Mkuu,Uchaguzi Mkuu ni pressure kwa Rais aliyepo hata kwawapinzani. Kwa hiyo kinachofanyika ndani ya nchi ya Kenyani siasa, tunachozungumza leo Balozi wa Mexicoamekanusha amesema kile chakula hakijatoka Mexico, kwahiyo tusidanganyane. Mtu analeta taarifa za kutoka hukoanasema kwamba eti Kenya wameshusha bei ya chakula,chakula kingi kiasi kwamba…, tuzungume ukweli paleambapo panastahili ukweli… (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, muda wako umekwishaMheshimiwa Gulamali.

MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Subira Mgaluatafuatiwa na Mheshimiwa Janet Mbene na MheshimiwaStanslaus Mabula ajiandae.

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi ya kuchangia katikaWizara hii muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kabisakumpongeza Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu naMheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, viongozi hawawameutendea haki Mkoa wa Pwani. Kwa nyakati mbalimbaliwamefika kutufanyia shughuli mbalimbali za uwekaji wa jiwela msingi, ufunguzi na hata ukaguzi wa viwanda mbalimbalivinavyoendelea kujengwa katika Mkoa wetu wa Pwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndoto ya Mheshimiwa Raisambayo imeelezewa kinagaubaga kwenye Ilani ya Chamacha Mapinduzi kwangu mimi naiona ina mwelekeo mzuri wakutimia. Kwa nini nasema hivyo, ukiangalia hotuba yaMheshimiwa Waziri na ninampongeza sana kwa kazi nzurikama nilivyotangulia kusema, katika ukurasa wa 16, tofautina hotuba ya mwaka jana ameeleza kinagaubaga miradiya viwanda tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingiemadarakani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ukurasa huo wa 16mpaka 29 katika moja ya aya kwenye hotuba yake, ameelezaviwanda vikubwa 393 vyenye jumla ya mtaji wa dola zaKimarekani milioni 2000, kama shilingi trilioni 5,000 naameeleza; ukisoma hotuba yake na ukisoma viambatanisho

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

vyake, majedwali kuanzia 7(b), 7(c) na 7(d) utaona kabisa niaina gani ya kiwanda, mwekezaji, ajira ngapi zitatekelezekana ni investment ya kiasi gani. Kwa hiyo, mimi nadhani kwamaelezo yale inatosha kabisa kutoa dira kwamba sera hii yauchumi wa viwanda inawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, naombanimpongeze Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani, Wakuu waWilaya pamoja na Wakurugenzi kwa kuandaa mazingirawezeshi ya viwanda vyetu. Hapa naomba nisemee viwandavya chuma vilivyopo Kibaha, cha Kilua, Kibaha Mjini naMkuranga na ninaomba pia nijielekeze kwenye viwanda vyausindikaji matunda vilivyopo Mboga ambacho kinakaribiakukamilika, Bagamoyo pamoja na Mapinga.

Vilevile naomba nijielekeze, na nipongeze nawekakumbukumbu kwenye Hansard na mimi mwenyewe binafsibaadhi nilivitembelea, Kiwanda vya Vigae kilichopoMkuranga ambacho ni kikubwa sana, kinatarajia kutoa ajira4,500. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo,ninaomba nijielekeze kwenye eneo letu la viwanda la TAMCOna nimeona nia ya Serikali ni njema, na ukiangalia hata bajetiya maendeleo ya Wizara hii imeongezeka. Mwaka wa janatulilalamika hapa zilitengwa shilingi bilioni 40, lakini Serikaliimeonesha dhamira, imetenga shilingi bilioni 82, ni zaidi yamara mbili ya pesa ambazo imetengwa mwaka wa jana.Ndani ya pesa hizi zimetengwa kwa ajili ya eneo la viwandala TAMCO, Kibaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuombe MheshimiwaWaziri na Serikali kwa ujumla, eneo lile kama ambavyolimeelezwa na Kamati yenyewe, kama ambavyo Serikaliimeeleza namna gani eneo lilivyopangwa, upembuzi yakinifuumekamilika, ramani yake imekamilika, tunatarajia viwandavya nguo, kuunganisha magari, dawa za binadamu pamojana viwanda vya aina mbalimbali. Pia ninaiona dhamira yaSerikali, hasa kwa kutumia mifuko ya hifadhi ya jamii kujengaviwanda. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Mheshimiwa Naibu Spika, tulizoea mifuko hii kujenganyumba mbalimbali ambazo tunaziona sasa hazina soko,lakini dhamira ya kutumia mifuko hii, tumeona ni namna ganimifuko hii inavyoshirikiana ikajenga kiwanda kikubwa chasukari Mkulazi, naunga mkono. Vile vile tumeona namna ganimifuko hii inayoshirikiana na MSD, TIRDO, Tanzania InvestmentBank kujenga viwanda vinavyotumia mazao ya pamba. Kwahiyo, unaiona dhamira ya Serikali kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo,naomba niulize; Wilaya yetu ya Rufiji ina maeneo ambayotuliyatenga kupitia RUBADA na kuna maeneo yalikuwayanatolewa na tulikuwa tunatarajia kujenga viwanda vyasukari, Mheshimiwa Waziri sijaona mahali popote alipotajajuu ya ujenzi wa viwanda hivi katika Wilaya yetu ya Rufiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hilo, pia Wilayaya Kisarawe tulipima eneo (Kisarawe Industrial Park), lipotayari na tulijitahidi kama Halmashauri na Serikali Wilayanimpaka miundombinu, lakini pia sijaona litajwe popote. Lileeneo lipo sehemu nzuri, limepitiwa na reli ya kati, limepitiwana reli ya TAZARA, lipo karibu na viwanja vya ndege Dar esSalaam na pia lipo karibu na bandari. Kwa hiyo, unaonamkoa wetu umekaa kama mkoa wa kimkakati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba Serikali,mwekezaji yeyote atahitaji athibitishiwe usalama wake, lakinipia anahitaji vivutio mbalimbali. Nina imani baada yamkutano wa Mheshimiwa Rais na Baraza la Biashara pamojana sekta binafsi, nina imani majadiliano yatakayoendeleandani ya Bunge hasa itakapofika wakati wa Finance Bill,vikwazo mbalimbali vya kisheria, vya kodi na vya vivutionadhani vitapatiwa tiba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeeleza kwenyemchango wangu kwamba wawekezaji wetu hasa wa Mkoawa Pwani wanahitaji ulinzi wa mali zao. Naiomba Serikali,pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendelea, lakinikuimarisha ulinzi wa maeneo yetu. Naamini wawekezajipamoja na nia waliyoonesha, lakini kwa matukio

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

yanayoendelea pamoja na kazi nzuri ya Serikali, yanawezakabisa kufifisha jitihada hizo za uwekezaji katika maeneohaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo yote hayayanakwenda sambamba na namwomba MheshimiwaWaziri, kama ambavyo ameonesha kushirikiana na Waziri waWizara ya Maji, basi Wizara ya Kilimo na Mifugo, Wizara yaFedha, Wizara ya Sheria na Katiba, Wizara ya Miundombinuna Wizara nyingine za kimkakati zijitahidi kufanya kazi kwapamoja na Wizara ya Nishati na Madini ili kuonesha yalemambo yanayotegemeana na viwanda ili yaweze kufanyikakama inavyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani sisi kamaWabunge, binafsi mimi ninayetokea Mkoa wa Pwani, naaminiwajibu wangu ni kuhamasisha wananchi wa maeneo hayakutumia fursa ya viwanda vizuri. Viwanda vyetu vitahitajirasilimali, niwaombe vijana, wanawake na wananchi waPwani kutumia fursa ya viwanda vizuri. Tulime kilimoambacho kitaleta tija, tujitoe kufanya kazi katika hivyoviwanda ili ajira inavyosemekana, nimepiga mahesabu, ajirakatika viwanda vyote vinavyotarajiwa Mkoa wa Pwani nikama 10,000 zile za moja kwa moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, siyo ajira chache.Fursa hii isije ikaonekana kwamba viwanda vinajengwa lakiniajira nyingi zinakwenda nje; sitarajii kwamba iwe za Pwanitu peke yake, lakini wote ni Watanzania, tuzitumie fursa hizolakini wenyewe pia wa Mkoa wa Pwani tuzitumie fursa hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine nimalizie kwakuomba Wizara ya Viwanda na Biashara ulipaji wa fidia.Mheshimiwa Mbunge wa Bagamoyo amezungumza leo nahili jambo kwa kweli katika maeneo yale; na maeneo hayaya kimkakati kwa uwekezaji yanasaidia mno, ni maeneomaalum. Tulitembelea eneo maalum la Benjamin Mkapa(Special Economic Zone), tumeona viwanda vya nguo vilivyopale, tumeona ubora wa bidhaa wanazozitengeneza,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

tumeona namna gani hata viwanda vile vilivyopo paleBenjamin Mkapa (Special Economic Zone) havijaweza kukidhisoko. Zaidi ya asilimia 30 bado halijakidhi soko la nje. Kwahiyo, nina imani Serikali ikilipa fidia katika maeneo yoteyaliyotengwa nchi nzima na kwa wakati na wawekezajiwakapatikana, uwezo wa kuzalisha bidhaa na kuzisafirishanje ya nchi upo na masoko yapo.

Mheshimiwa naibu Spika, nimalizie kwa kuungamkono hoja. Nashukuru sana kwa kazi nzuri inayoendeleakufanywa na naendelea kuamini Sera ya Viwanda, Uchumiwa Viwanda itawezekana. Naendelea kuamini changamotozilizopo zinaweza zikatatuliwa mezani; na naendelea kuaminiMheshimiwa Rais ana nia njema na ipo siku tutashuhudiamapinduzi makubwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wakoumekwisha. Mheshimiwa Janet Mbene atafuatiwa naMheshimiwa Stanslaus Mabula, Mheshimiwa Moshi Kakosoajiandae.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Nianzekwanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa fursaya kuiona siku hii ya leo, lakini vile vile naomba nimshukurusana Mheshimiwa Mwijage, Waziri wa Viwanda, kwa kweliametutendea haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii hotuba kwa mtu ambayeanataka kuisoma na kuielewa, kwa kweli hakupaswa hatakuwa na maswali humu ndani. Nampongeza sana kwa kuwahotuba hii imesheheni kila aina ya taarifa. Kuna takwimu,kuna maelezo, kuna mchanganuo; sasa sijui mtu unalalamikakuwa dhana ya viwanda huioni, unataka uione vipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuipongeza sanaSerikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, safari hii huu mkakati

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

jamani utafanyika. Kwa vielelezo hivi vilivyomo humu ndanini wazi kabisa viwanda vitakuja kufanyika. Mifano,tumeshaiona, viwanda vipya vimeshajitokeza vingi sana;someni haya majedwali jamani! Kama hamtaki kusoma hiil iterature yote kubwa, nendeni huku nyuma kwenyemajedwali, yameainishwa kiwanda kipi, wapi, ukubwa gani,kwa faida ipi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niipongeze sanaSerikali yangu, nimpongeze Mheshimiwa Waziri na watendajiwote walioko chini yake. Kwanza tunaambiwa kabisa katikamaendeleo yoyote ya uchumi duniani, nchi lazima iwe napolitical commitment. Commitment tumeiona kwa kupitiaRais wetu na Marais wengine wote waliopita. Commitmentya kuwa na viwanda nchi hii imekuwepo na sasa hivi ndiyoimetiliwa mkazo zaidi kwa kuweka kabisa mkakati wa kuwasasa hivi tunaelekea kwenye maendeleo ya viwanda pekeyake.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa suala linalofuata nitaasisi. Tunaambiwa kabisa ili nchi iendelee au ionekanaekuwa inaendelea inapaswa kuwa na taasisi muhimu. Taasisihizo zinahusiana na masuala ya hatimiliki. Sisi chini ya Wizarahii tuna Taasisi ya Property Rights, tuna Taasisi zinazosimamiaubora wa mazao au bidhaa, tuna taasisi zinazosimamiamiundombinu ya viwanda vidogo na vikubwa, tuna taasisizinazoshughulikia usuluhishi wa migogoro kwenye biashara,tuna taasisi ambazo zinakwenda kujenga ufanisi wa viwandakuanzia vidogo kabisa hadi vile vikubwa; tuna sheriaambayo inasimamia, tuna mkakati wa kimaendeleo waviwanda wa tangu 1996 mpaka sasa hivi ambao umerejewana sasa hivi umeboreshwa. Sasa zaidi ya hapo tunawezajekusema kuwa hatuna mwelekeo wa viwanda? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukitoka hapo tunakujakwenye masuala mazima ya utekelezaji wa huo mkakatimzima wa viwanda nchini mwetu. Tunaona jinsi ambavyokwa sasa hivi kwa mtazamo huu wa Serikali ya Awamu yaTano kuwa sasa hivi viwanda hivi vinakwenda kuwajumuishawananchi wengi zaidi. Kama zamani ilikuwa inaonekana

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

viwanda viko sehemu chache tu za nchi, sasa hivi viwandavinakwenda mpaka vijijini kwetu, vinakwenda mpakakwenye Wilaya zetu, vinakwenda kwenye Halmashauri zetu,maeneo ya mikoa na wilaya ambayo yako tayari kwa ajiliya viwanda yameainishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri zetu wotewana ufahamu na uelewa kuwa wanahitaji kuwa naviwanda; tuna program zilizokuwepo chini ya Wizara hiizilizokuwa zikisema kila Wilaya iainishe zao moja ambalowanaliona hilo ndiyo litakuwa linafaa kwa aji l i yakuendelezwa hadi kufukia level ya kiwanda; na hayoyamefanyika. Tuna Taasisi muhimu za kusimamia kama SIDO;kila mtu aliyesimama hapa amezungmzia SIDO, ni kwasababuameuona umuhimu wake. Sana sana tutakachowezakusema kwenye Serikali ni kuwa SIDO iwezeshwe zaidi kwamaana ya mitaji, kwa maana ya wafanyakazi, kwa maanaya program za kwenda kusambaza katika kila eneo kamaambavyo sera inasema.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutazungumzia BRELA.BRELA zamani ilikuwa inasajili majina ya Makampuni kwamaana ya wakubwa. Sasa hivi hata akinamama zangu kulekijijini wanaweza kusajili majina ya Kampuni zao au shughulizao wanazozifanya. Hii imerahisishwa kiasi kwamba hatahawana haja ya kutembea kwenda Dar es Salaam aukwenye Kanda yoyote, hata kwa kutumia mitandao tu yasimu, Mabenki ambayo yameunganishwa. Sasa jamaniunalalamika kuwa eti sijui urasimu; urasimu umepunguzwakwa kiasi kikubwa. Ni sisi sasa kama viongozi katikaHalmashauri zetu kuhamasisha wananchi kuwaelewesha jinsigani ya kutumia nyenzo hizi ambazo Serikali imeziweka.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuzungumzia sualala Stakabadhi ya Mazao Ghalani. Jamani, naniatakayeendelea kubisha sasa kuwa huo siyo mfumo ambaoumewasaidia sana wakulima kupata bei bora kwa ajili yamazao yao? Tuombe sasa mfumo huu wa stakabadhiuenezwe Tanzania nzima maana yake ulikuwa kwenye mazaomachache, lakini vile vile haukuwa kila mahali. Wale

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo na wengi waowakiwa ni wanawake wangependa sana na wao sasakujumuishwa katika mfumo huu na kwa hali hiyo hayamaghala na huu usimamizi upelekwe mpaka kwenye Wilayazetu ili sasa wananchi wetu waache kurubuniwa na madalaliwa mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuzungumzia sera.Jana kuna mtu alikuwa anakashifu Sera ya Viwanda ya 1996ambayo inaisha mwaka 2020. Mambo mawili makuuambayo sera hii il ikuwa imelenga; kwanza ilikuwa nikusambaza viwanda nchi nzima. Jamani, sera ikiwa inasemakitu kama hicho, ina ubaya gani? Inazungumzia inclusivenessya viwanda nchi nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera hii vile vile ilikuwainazungumzia kueneza viwanda kwenye maeneo yapembezoni. Mimi natoka kwenye eneo la pembezoni; Ileje niWilaya ya pembezoni na kwa muda mrefu sana tumekaakwa kweli hatuna maendeleo makubwa sana zaidi ya kuwani wakulima wazuri, tunazalisha vitu vizuri. Sasa hivi naonaMkoa wa Songwe na wenyewe uko katika maeneo ya kujakuwekezwa kwenye viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ktika Wilaya yangu, tayariSIDO wameshakuja kupata eneo na wako tayari kujakuanzisha viwanda; Wilaya yangu sasa hivi inakwendakubadilika, siyo ile Ileje ambayo mlikuwa mmezoea kuisikia.Wengine hata mlikuwa hamjui Ileje iko wapi? Sasa hivimnaijua Ileje iko wapi. Ileje inaenda kupata barabara ya lamikubwa itakayofungua uchumi ule kwa kiasi kikubwa sana.Ileje kwa uzalishaji wake, sasa hivi inaenda kupatamiundombinu ya Kituo cha Forodha mpakani na Malawi.Haya yote ni maendeleo. Tunaenda kupata Chuo chaUhamiaji cha Kikanda, yote haya ni maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachosema mimi, kilimochetu sasa hivi kinaenda kufanya usindikaji wa hali ya juu.Nasema barabara ile itakapoanza tu, Ileje itakuwa kama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

mzinga wa nyuki, shughuli zitavyoanza pale. Sasa hivi tu tayarituna watu wengi sana wako tayari kuja Ileje, wanaviziabarabara ikifunguliwa tu! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziriwa Viwanda, anisikilize. Afanye kazi kwa karibu sana naWaziri wa Maji ambaye namshukuru Mungu safari hiiametuwekea fedha ya kutosha kuboresha miundombinu yamaji Ileje. Mheshimiwa Mwijage, Ileje tunalima sana mazaomengi; nafaka, mazao ya biashara kama pareto, tunalimasoya, alizeti, mihogo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbene muda wakoumemalizika.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba viwanda Ileje nimeshaongea na Mheshimiwa Wazirimara nyingi, maeneo yapo tunamkaribisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi,najua hii hoja naweza nikaizungumza kutwa nzima. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Haya, ahsante sana. MheshimiwaStanslaus Mabula atafuatiwa na Mheshimiwa Moshi Kakosona Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika ajiandae.

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangiakwenye Wizara hii muhimu kabisa katika ustawi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze tu kamaWaheshimiwa Wabunge wengine, ambavyowamempongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba yake nzuriambayo kwa kweli inaonesha matumaini ya hili sualatunalolizungumza juu ya Serikali ya viwanda inawezekana.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nampongezaMheshimiwa Rais kwa namna ya kipekee kwa kutambuaumuhimu wa kuwa na viwanda ambavyo ndiyo unawezakuwa msingi wa wakulima wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na ufahamu huutulionao wote, lakini pamoja na hii ambayo ndiyo kauli mbiuya Mheshimiwa Rais kwa sasa, bado tunayo kila sababu yakuhakikisha vyuo vyetu vya VETA na mitaala tuliyonayoinatambua umuhimu wa Serikali hii au Taifa hili kuwa naviwanda ili viweze kuchukua sehemu kubwa sana ya vijanakama ajira lakini ya uzalishaji mali na mazao ambayoyatakuwa yanatumika zaidi kwa wananchi hawa wanyongelakini na kuuza nje ya nchi kama ambavyo tunatarajiakupata kipato kikubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunatambua, nami leonitajikita sana kwenye viwanda ambavyo, pamoja nautaratibu huu tunaoufikiria sasa wa kuwa na viwanda vipyaau ujenzi wa viwanda vipya katika maeneo mbalimbali yanchi hii lakini nataka nimkumbushe Mheshimiwa Wazirikwamba tunayo kila sababu viwanda hivi tunavyovijengakwa sasa ni lazima tuwe na kipaumbele na viwandatunavyovihitaji kwa ajili ya maslahi ya Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu muda wamiaka mitano ni mchache sana; tukisema miaka hii mitanotunaondoka na viwanda 100, 200, 3,000 au mia ngapi, badotutakuwa tunajidanganya, tutakuwa na ma-carpenter wengi,hatutakuwa na SIDO nyingi halafu tunahisi tuna viwandavikubwa ambavyo vinaweza vikasaidia Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunaona mfano;tunapozungumzia uhaba wa sukari nchi hii, tunazungumziamoja kwa moja uzalishaji hafifu wa viwanda vyetutulivyonavyo hapa nchini. Pamoja na uhafifu huo, tunayomifano; Kenya, Uganda na nchi nyingine zinazotuzunguka,nataka tufikirie kuwa na viwanda vyenye vipaumbele.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na uchache huu,leo Mheshimiwa Waziri anaweza akajinadi na ana kila sababuya kujisifu; hata bei ya sukari tunayolalamika sisi iko chini,huwezi kulinganisha na nchi za majirani zetu kama Ugandana Kenya. Sasa maana yangu ni nini? Unapokuwa naviwanda vya sukari vyenye kuweza kuzalisha zaidi,Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo tulikuwa tunazungumzanaye pale, wamekamata sukari ya Kilombero inaingizwaKenya kule kwa magendo; na sababu ni moja tu;inawezekana uhaba huu tulionao bado sukari yetuinavushwa nje. Sasa maana yangu ni nini? Nataka tuwe naviwanda vyenye vipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tukiwa na viwandayenye vipaumbele kwa miaka hii mitano, tutajikuta tunafanyakitu ambacho kitakuwa kinaonekana kwa Watanzania kulikokubaki na historia ya ujenzi wa viwanda lukuki ambavyohavina vipaumbele kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine; nimesemambali ya kuwa na viwanda vya kipaumbele, lazima sasatuangalie, tunapiga hatua 100 mbele kufikiria viwanda vipya,tuna mawazo gani juu ya viwanda tulivyokuwanavyo tokazamani na leo tulivibinafsisha na haviwezi kufanya kazi yakesawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pale Mwanza tunavyoviwanda vya Tanneries, tunacho kiwanda cha MWATEX lakinitunavyo Viwanda vya Samaki. Kiwanda cha MWATEXambacho toka mwaka 1995 kilibinafsishwa, wafanyakazizaidi ya 1,720 ambao waliachishwa kazi na mpaka leohawajalipwa, lakini kiwanda kile pamoja na mambo yakemengi, hivi tunavyozungumza, uwezo wa kiwanda hikikuzalisha hata asilimia 30 ya yale yaliyokuwa yanazalishwamiaka karibia 12 iliyopita, hakijafikia malengo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha MWATEX kilammoja anafahamu, kila mmoja anajua umuhimu waviwanda hivi; ni wakati gani tuko tayari kurudi kwenyeviwanda hivi na tushughulike navyo viweze kuzalisha kama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

zamani? Mbali ya ajira kubwa ya zaidi ya watu 2,000, lakinivilikuwa na uwezo wa kuzalisha na tutasafirisha nje kwenyenchi za majirani na kwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tumeongeleaKiwanda cha Tanneries. Kiwanda cha Tannerieskimebinafsishwa. Kiwanda hiki sasa Mheshimiwa Jenistapamoja na Wizara yake wameanzisha mafunzo muhimukutoka nchi nzima vijana wanapelekwa pale zaidi ya 1,000.Hawa vijana wakimaliza kujifunza pale wanakwendakufanya kazi wapi? Kiwanda hiki tangu kibinafsishwehakijawahi kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba na hiki nachenyewe tukiangalie. Hawa vijana wanaotoka DIT kwenyemafunzo ya utengenezaji wa mikanda, viatu na mikoba,kiwanda hiki ikiwezekana kama siyo kurudishwa; naMheshimiwa Rais aliahidi, tuangalie uwezekano wa kurudishakiwanda hiki kije; vijana wanaotoka kujifunza hawa badalaya kwenda mtaani, watakuwa wanazalisha mali zilizokuwana ubora. Wafanye kazi kwenye kiwanda hiki, wazalishe malizenye ubora, tuuze ndani na nje ya nchi kwenye majeshi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, ni viwanda vyasamaki. Tuna viwanda saba vya samaki. Hii ni lazimaMheshimiwa Waziri akubali kuungana na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili waweze kuona. Miaka minne iliyopitakiwanda kimoja peke yake kilikuwa kinakata shift nne,watumishi zaidi ya 1,400, kikiwa kinakata tani 280 za samakikwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo kiwanda kimojakinaitwa Vicfish kimeshafungwa; na hivi vilivyopo kimoja kinauwezo wa kuzalisha tani sita mpaka 12 kwa siku,kimepunguza wafanyakazi kutoka 1,400 mpaka 300 mpaka150. Tafsiri yake ni nini? Tunaongeza Machinga, tunaongezawafanyabiashara ndogondogo, ajira hakuna na kumbetunaweza kushirikiana tukatengeneza ajira nyingi zaidi kama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

viwanda hivi vinaweza vikaboreshwa upya. Kazi inayofanyikani nzuri, lakini lazima tunapokwenda mbele tukumbuke natulikotoka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia mpango wasasa, viwanda tutakavyovijenga Mwanza, vinategemeakuzalisha ajira 1,004. Hawa tunaozungumza viwandavilivyokufa, zaidi ya ajira 2,900 zimepotea. Tafsiri yake,tunahitaji viwanda hivi viangaliwe upya na ushirikiano katiya Wizara mbili au tatu ni lazima uwe wa karibu ili kujengamsingi wa viwanda tunavyozungumza viweze kufikiamalengo yake tunayoyatarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri waViwanda lazima akubali kushirikiana. Watumishi hawaambao miaka 12 hawapo, leo wapo mtaani, wenginewameshakuwa wazee, tunahitaji kujua ni lini watalipwamafao yao ambayo hawajawahi kuyapata miaka 12?Tukifanya hivyo itatusaidia, tutakwenda mbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naungamkono hoja. Mungu akubariki sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Moshi Kakosoatafuatiwa na wachangiaji ambao watachangia kwadakika tano, tano. Mheshimiwa Jadi Kadika halafuMheshimiwa Frank Mwakajoka.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Nami nianze kwakuipongeza Serikali kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya.Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa dhamira ya dhati yakuleta viwanda nchi nzima. Sera ya Viwanda ni sera nzurisana ambayo kimsingi, yeyote atakayeipinga ni yule ambayehajui umuhimu wa viwanda katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sera hii imeoanishamazingira mazuri kwamba kila mkoa ni lazima kuwe naviwanda ambayo vitawasaidia wananchi wetu kuwezakukuza uchumi ndani ya maeneo yao. Nzuri zaidi ni pale

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

ambapo sera hii inaonesha maeneo ambayo yalisahaulikahasa pembezoni, yapewe kipaumbele ili yaweze kunufaikana mpango wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niishauri tu Serikalikwamba, katika sera ambayo imewekwa, Sera ya Viwandani vyema wakaangalia mazingira ili tupeleke viwanda mahaliambapo uhitaji wa viwanda unafanana na mazingirayenyewe. Leo hii unapopeleka kiwanda cha kusindika ngozikwenye maeneo ambayo hayana hata mifugo, hujawasaidiawananchi pale, hasa wale ambao wanatoka kwenyemaeneo ya ufugaji. Ni vyema vile viwanda ambavyovitakuwa vinahusiana na Sekta ya Mifugo, tukawapelekeakwenye maeneo husika ya uzalishaji ili viweze kutoa ajirakwenye maeneo ambayo wananchi wenyewe wanahusikana kulengwa moja kwa moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tulikuwa tunaombakuangalia mazingira ya kuboresha Sekta ya Viwanda hasaviwanda vidogo vidogo. Kwenye maeneo haya ni vemaSerikali sasa wakawa na mipango thabiti itakayokuwainaunganisha nchi nzima na kwa kuwashirikisha Wakuu waMikoa ili waweze kutenga maeneo ambayo yatakuwa rafikikuwasaidia wananchi ambao kimsingi tukiboresha kwenyeSekta ya Viwanda vidogo vidogo, tumewasaidia wananchiwalio wengi. Huko ndiko ambako ajira zinatengenezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri, lazima aje na mpango mkakati wa kuwashirikishaWakuu wa Mikoa ili kuhakikisha maeneo ya viwanda vidogovidogo yanapewa kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali itusaidiemikoa ya pembezoni; kule tunazalisha. Mkoa wanguulishatenga maeneo ya uwekezaji. Nafikiri kila kitu kipo sawa,lakini tunaomba sasa ielekeze suala zima la kuwekeza kwenyemazao yanayozalishwa na wananchi hasa kwenye Sekta yaKilimo. Tukielekeza huko, tutawasaidia sana wananchiambao ni wengi. Mazao ya mafuta yanayozalishwa,tukiweka mipango mikakati mizuri, kwamba yale mazao ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

mbegu za mafuta ambayo yanazalishwa, tukajengaviwanda vidogo vidogo huko, tutakuwa tumewasaidia sanawananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo mazao ya chakula.Mkoani kwangu tunazalisha chakula kingi na tunauza mazaoambayo bado hayajasindikwa. Naiomba Serikali, paleambapo tunafikiria mikoa ya pembezoni; Mkoa wa Katavi,Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Kigoma ni vema sasa tukawana viwanda ambavyo vitafanya kazi ya kuwasaidiawananchi kwenye maeneo hayo na eneo hilo likawa naukuzaji wa kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bado tuna mazao yabiashara; tuna zao la tumbaku kwenye Mikoa hiyo ya Tabora,Kigoma na Katavi. Hatujakuwa na kiwanda maalumambacho kitasaidia kukuza zao hili. Ni vema sasa Serikaliikaja na mpango ambao utasaidia maeneo hayo ili kupatakiwanda ambacho kitasaidia kukuza uchumi ndani yamaeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna maeneo mazuri yakivutio cha uwekezaji. Lipo zao la miwa, kama Mkoa waKigoma wangepewa fursa, wana mabonde mazuri. Mfano,bonde la Mto Malagarasi; katika Mkoa wa Katavi, Rukwavile vile; tunahitaji tupate Kiwanda cha Sukari kwenyemaeneo haya ili tuweze kupunguza bei ya sukari kwenyemaeneo ya pembezoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado naiomba Serikaliiandae mazingira ya kujenga Kiwanda cha Saruji kwenyemaeneo haya; ni maeneo ambayo bei za saruji ni kubwakweli kwa sababu viwanda vingi vimeelekezwa Mkoa waDar es Salaam, Mkoa wa Pwani lakini maeneo ya pembezonihakuna. Naiomba Serikali iweze kutengeneza mazingiramazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho nizungumziedhamira ya Serikali. Serikali imeonesha wawekezaji wengikwa kushirikisha Mifuko ya Maendeleo ya Jamii; NSSF, PPF, PSPF

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

na mengine, mashirika ambayo tukiweka ubia yana nafasiya kuweza kusaidia kukuza uchumi. Ni dhamira nzuri ambayoSerikali imeweka; ni vizuri sasa tukawa na uwiano kwenyemaeneo yote yasiwe yanaelekezwa kwenye maeneo maalumtu hasa Kanda ya Mashariki. Naomba Serikali iangaliemazingira haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nizungumzie eneoambalo watu wengi wamekuja wanafananisha bei zachakula nchini Kenya na bei za kwetu hapa. Niwaambiewananchi tu kwamba, zipo propaganda ambazozinaenezwa. Tukiangalia uhalisia, bado bei ya sukari kwa nchiyetu ipo chini kuliko bei ya sukari kwenye maeneo ya nchiambazo ni jirani zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya leo hii bei ya sukarini Sh.3,195/=, Uganda ni Sh.3,550/= mpaka Sh.4,000/=, Burundini Sh.3,700/= mpaka Sh.4,000/=. Tanzania bei ya sukari ipokati ya Sh.2,700/= mpaka Sh.3,000/=. Bado maeneo mengineyote yanayotuzunguka yanahitaji kutoka kwetu kupatabidhaa muhimu kama hiyo. Ni vema sasa watu wakaachakutumia propaganda ambazo kimsingi wenzetu sasa hiviwanazitumia kwa masuala ya kisiasa. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Kakoso.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge watakaotajwawanachangia kwa dakika tano, tano. Mheshimiwa MgeniJadi Kadika na Mheshimiwa Frank Mwakajoka. Kama mudawetu utakuwa bado upo, Mheshimiwa Yosepher Kombaatachangia.

MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

na kuweza kusimama na kuchangia hotuba ya Wizara yaViwanda, Biashara na Uwekezaji. Pia nakushukuru wewe kwakunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Tano,imejipanga katika uchumi wa viwanda; na ina nia nzuri tuya kutoa ajira kwa Watanzania. Nchi yetu kama mtajengaviwanda vingi kama utitiri, lakini ikiwa havina usimamizi nawataalam waliobobea kiuweledi mkubwa, basi viwandahivi vitakufa kama vilivyokufa vilivyokuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nataka nichangie ujenziwa Viwanda vya Minofu ya Samaki katika Ukanda wa Pwani.Nchi yetu inayo maeneo makubwa ya bahari, lakini hakunakiwanda hata kimoja. Viwanda vyote vinaelekezwa kwenyeUkanda wa Ziwa. Kwa hiyo, naishauri Serikali ijenge viwandakwenye eneo la bahari kama vile Dar es Salaam, Tanga, Lindi,Mtwara, Pemba na Unguja. Ujenzi huu utatoa ajira nautainua maisha ya wavuvi na kupunguza umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nakuja kwenyeViwanda vya Mabati. Viwanda hivi vinazalisha mabati chiniya kiwango katika baadhi ya viwanda, yakiwemo mabatiambayo yanaingia kutu haraka, mabati mengineyanachakaa haraka na pia yanavuja siku za mvua. Pia beiya mabati hayo iko juu, kulingana na bei ya saruji ambayokwa sasa imeshuka. Kwa hiyo, Serikali ina mkakati gani wakusimamia ubora wa viwango vya mabati na pamoja nakudhibiti bei? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bidhaa fekizimezungumzwa na wenzangu wengi hapa, lakini naminataka nizungumzie kuhusu bidhaa feki. Kuna bidhaa fekinyingi zinazoingizwa katika nchi yetu. Maziwa ya watoto yanamadhara makubwa juu ya kutumia maziwa haya. Nyaya zaumeme zinaunguza majumba yetu, zinapelekea maafa.Matairi kupasuka kwa muda mfupi tu na kusababisha ajalinyingi barabarani. Vipodozi vinaharibu ngozi za akinamamana wengi wanapata kansa. Je, Serikali inatuambiaje kuhususuala hili. (Makofi/Kicheko)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli wanawakewengi tuko ambao huwa tunatumia vipodozi natunaharibika ngozi na wengi wanapata kansa, wenginewanakufa, uzuri wao umepotea. Kwa hiyo, hili sualalinatakiwa lishughulikiwe kwa nguvu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nazungumzia kuhusuviwanda. Vimo viwanda vingi tu, SIDO, lakini hata vikiwekwaviwanda vikubwa kwa kuwaboreshea wakulima mazaoyao, itakuwa ni bora zaidi. Nashauri kila kiwanda kiwekwekila mkoa ili wazalishaji waweze kutumia viwanda hivi kwakuyaokoa mazao yao; kama vile mananasi,maembe,machungwa, mazao kama nyanya na mazao menginemengi tu yanaharibika.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hivyo,naona muda wangu umekwisha, naunga mkono hoja yaKambi ya Upinzani. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mgeni, naonaumeshangiliwa sana na Mheshimiwa Waziri hapa. Nadhaniameandika yote uliyokuwa unayasema. Vipodozivinavyotokana na maganda ya korosho, jana tumeambiwa.(Kicheko)

Mheshimiwa Frank Mwakajoka.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa NaibuSpika, awali ya yote, nianze kwa kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwakuwasilisha hotuba nzuri ambayo imetoa ushauri wa kutoshana tumemshauri sana Mheshimiwa Mwijage kwamba ajitahidisana kutumia hotuba hii ili aweze kutekeleza malengo yaSerikali ya Viwanda katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ambacho natakakukizungumza hapa, kwanza nianze kabisa na mazingira

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

mabaya kabisa ambayo yako katika nchi yetu kwa ajili yakuendeleza biashara katika nchi hii. Wote tunafahamu nawote tunajua kwamba katika nchi yetu kumetokea na wimbikubwa sana la wafanyabiashara kufunga biashara zaoyakiwemo maduka, mahoteli, lakini pia na wanaoendeleakuuza biashara zao hizo, wanafunga na hawafanyi tenabiashara kutokana na mazingira magumu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa tunauliza sanandani ya Bunge kwamba Serikali ina mpango gani wakuhakikisha kwamba inanusuru tatizo hili ambalo linajitokezala wafanyabiashara kufunga biashara zao? Sababu kubwani nini? Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanalalamikakwamba mazingira ni mabaya, Serikali inawabana tofautina jinsi inavyotakiwa. Wajibu wa Serikali siku zote nikuhakikisha kwamba inatengeneza mazingira mazuri yawafanyabiashara kuendelea kufanya biashara zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa inatoamajibu ndani ya Bunge inasema kwamba kuna watuwanafunga, lakini kuna watu wengine wanafungua. Hayomajibu hayawaridhishi kabisa Watanzania. Hivi ni kweli Serikaliinataka kwenda kwenye Serikali ya Viwanda, inaona biasharazinafungwa na inasema kwamba wacha zifungwe, nyinginezitafunguliwa. Kwa hiyo, tafsiri ni kwamba biashara nyinginezifungwe na nyingine zifunguliwe! Naona tunafanya biasharaya sifuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri sana Serikali hiiikagundua na ikashughulikia matatizo ya wafanyabishara.Lazima tuzungumze hapa ndani ya Bunge hili, kwambamazingira ya kuanzisha viwanda katika nchi hii, kamawafanyabiashara wa ndani wanashindwa kufanya biasharana biashara zao zinafungwa, ni mwendawazimu ganimfanyabishara kutoka nje anaweza kuja kuwekeza nakufanya biashara katika nchi hii? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni lazima kwanzatuangalie mazingira mazuri ya kuhakikisha kwambawafanyabiashara wetu ndani ya nchi hii wanafanya biashara

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

vizuri na biashara zao zinaendelea, ndipo watu kutoka njewatakuja kufanya biashara ndani ya nchi hii. Kama hatuwezikuangalia matatizo ya wafanyabiashara wetu ndani ya nchi,halafu tukafikiria kwamba kuna wawekezaji watatoka njewaje kuweka biashara zao hapa, hili jambo tulisahau,halitaweza kutekelezeka hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukubaliane kabisakwamba nchi hii kumekuwa na matamko mengi sana yavitisho. Juzi nilikuwa nasikiliza Taarifa ya Habari, wanasemakwamba hata wakulima sasa hivi wanaopata mazao mengini lazima waanze kulipa kodi. Nashangaa sana, yaaniwanataka kutuambia kwamba wakulima hawa hawalipikodi. Hakuna Mtanzania yeyote katika nchi hii ambaye halipikodi. Tunalipa kodi katika njia tofauti tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakulima hawa wanalimamazao haya kwa kutumia fedha zao na Serikali haiwasaidiihata kidogo. Tumeendelea kuzungumza kuhusiana napembejeo za kilimo hapa, zinafika kidogo; lakini leo Serikaliinafikiria kwamba ni lazima iwakamue wakulima hawa, etihawalipi kodi. Hilo siyo jambo la kawaida. Ni kwamba kodizinakusanywa katika maeneo mbalimbali, siyo lazimaukachukue kodi kwenye yale mazao, lakini kodizinakusanywa. Yule mkulima akishalima anakwenda kuuza,analipa kodi. Bado pia yule mkulima anakwenda mbele zaidi,anakwenda kununua mizigo ambayo tayari imeshalipiwakodi, anakuwa ameshachangia Taifa lake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba sana,ni lazima Serikali iwe inafika mahali, inapotaka kuanzishajambo fulani lazima ifikirie. Tunajiuliza sana kwambamahusiano kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizaraya Fedha, kuna mahusiano gani hapa? Maana tunaona sanakwamba Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja nawatendaji wake wa Serikali wamejipanga sana kuhakikishakwamba nchi inakuwa ya viwanda; lakini Wizara ya Fedhainakwamisha kutokana na sera na mipango mbalimbaliambayo inafika mahali inakuwa inapingana na dhana nzimaya kuanzisha viwanda katika nchi hii. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Kwa hiyo, ni lazima Wizara ya Viwanda na Wizaranyingine zinazofuatia na Wizara ya Fedha lazima wakaepamoja kupanga na kukaa, kuangalia ni namna ganiwanaweza wakapunguza kero ambazo zinasababishaviwanda visianzishwe katika nchi hii. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Muda wako umekwishaMheshimiwa.

Waheshimiwa Wabunge tumefika mwisho wauchangiaji kwa kipindi chetu cha asubuhi. Mchanatutamalizia wachangiaji wachache waliobaki. MheshimiwaMusa Bakari Mbarouk, kwa dakika tano; MheshimiwaYosepher Komba, kwa dakika tano, Mheshimiwa JoyceSokombi, kwa dakika tano; Mheshimiwa Devotha Minja; kwadakika tano; na Mheshimiwa Dunstan Kitandula kwa dakikakumi.

Waheshimiwa Wabunge, ninayo matangazo mawili,Mheshimiwa Waitara aliacha kitabu cha Hisabati cha Kidatocha Pili, ambacho ni cha maswali na majibu ya mitihaniiliyopita. Anaomba aliyekichukua, tafadhali amrudishie.Maswali na Majibu, Hisabati, Mitihani ya Kidato cha Pili.Anaomba arudishiwe kitabu chake.

Waheshimiwa Wabunge tangazo lingine linatokakwa Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini,anawakumbusha Waheshimiwa Wabunge, kwamba leo saa8.00 mpaka saa 10.00 lile tangazo la jana kwamba leoWakandarasi wa REA, awamu ya tatu wanakuja.

Kwa hiyo, wanaomba mwende eneo linaloitwaTreasury Square. Muda ni saa 8.00 mpaka saa 10.00mkashuhudie namna ambavyo Wakandarasi wa mikoa yenuwanakabidhiwa mikataba. Kwa hiyo, maswali kwaMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, nadhani baada ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

leo watu watakuwa hawasimami wengi humu maanawatapata majibu kule pengine. Kwa hiyo, mnakumbushwahivyo, mnaombwa kuhudhuria.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nasitisha shughuli za Bunge mpaka saa 11.00 jioni leo.

(Saa 7.00 Mchana Bunge Lilisitishwa Mpaka Saa 11.00 Jioni)

(Saa 10. 00 Jioni Bunge Lilirudia)

NAIBU SPIKA: Tukae.

Waheshimiwa Wabunge, kuna wachangiajiwachache kabla mtoa hoja hajaja kuhitimisha. Tutaanza naMheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk atafuatiwa naMheshimiwa Yosepher Komba na Mheshimiwa Joyce Sokombi,ajiandae, dakika tano tano, Makatibu.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kuniona. Nami nichukue fursa hii, kuchangiakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tupo katika enzi ya viwandana uchumi wa kati, lakini kiukweli kabisa ni kwambayanahitajika maandalizi thabiti. Sasa ni maeneo mengiambayo tumekusudia kuyafanyia kazi. Jambo la kwanzakabisa ili tuwe na viwanda vya uhakika, ni lazima vilevilepia tuwe na umeme wa uhakika. Sasa ni mara nyingitumekuwa na tatizo la umeme. Mheshimiwa Waziriatakapokuja naomba atuthibitishie, ni kweli tutakuwa naumeme wa uhakika? Kwa sababu viwanda bila umemeinakuwa ni kama kazi bure. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine Tanzania sisi ni watatu wa idadi kubwa ya mifugo; kama sikosei, baada yaEthiopia na Botswana ni sisi tunaofuatia Tanzania. Ukiangaliawenzetu wa Botswana, ng’ombe anapoingia katika kiwandacha kuchakata nyama, hakuna kinachotoka. Ngozi inashughuli yake, nyama ina shughuli yake, pembe ina shughuli

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

yake na kwato zina shughuli yake. Sisi Watanzania pamojana mifugo tuliyokuwa nayo, bado hatujaweza kuitumiamifugo vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali, tutafutewawekezaji wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kusindikanyama. Vilevile pia wenzetu wa Ethiopia, kwa mwaka 2016,wamepata takriban Dola 186,000 kutokana na ngozi pekeyake. Wanatarajia mwaka 2017 kupata vilevile Dola zaKimarekani kuongeza idadi ya Dola 90,000,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mantiki hiyo, mpaka2017 ikimalizika watapata zaidi ya Dola 276,000,000. SisiWatanzania badala ya kuitumia mifugo vizuri, imekuwatunazalisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati mwingine iliwahikutokea hapa kwamba Maafisa wa Wanyamapori,wakagombana na wafugaji, ng’ombe wakapigwa risasi,wafugaji wale wakadhalilishwa, hadi kupelekea baadhi yaMawaziri kujiuzulu katika Serikali ya awamu iliyopita. Kwa hiyo,naishauri Serikali tutumie mifugo vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo Watanzania tumekuwatunashindwa na baadhi ya nchi ambazo zimekuwa na vitaya wenyewe kwa wenyewe. Tukumbuke Ethiopia waliwahikuwa na vita na Djibout, lakini baada ya kumaliza vita,wamekaa wamepanga mambo mazuri namna hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hilo halitoshi,ng’ombe pia wanazalisha maziwa, lakini Watanzaniatumeshindwa kuyasindika. Matokeo yake tunaagiza maziwaya kopo kutoka nje. Tunaagiza Nido, Lactogen, Nan; hali yakuwa maziwa ya ng’ombe yangepakiwa vizuri, yangewezakuwasaidia wananchi wetu. Kwa hiyo, naishauri Serikaliitafute wawekezaji wa uhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine kwenye sualazima la viwanda; tuna matunda. Kwa mfano, katika Mkoawetu wa Tanga, Lushoto ni wazalishaji wa matunda na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

mboga mboga za aina nyingi. Muheza kuna kilimo kikubwacha machungwa, lakini pia unakuta tunaagiza juice za Cerieskutoka South Africa na Saud Arabia ambayo ni nchi ikojangwani. Inakuwaje sisi ambao tunazalisha machungwa bynature lakini tunashindwa kuyachakata tunaagiza juicekutoka nje? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali tutafutewawekezaji wa uhakika. Tusizungumze suala la viwandakisiasa; tuwe na dhamira ya dhati na ya kweli. Viwanda hivyovitakapojengwa wananchi wetu watapata ajira lakini vilevileSerikali pia itapata mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, l ingine nil i lotakakuzungumza, moja ya matatizo yanayofanya wawekezajiwasije Tanzania, ni mifumo mibovu ya kodi, umeme usiokuwawa uhakika, lakini vilevile pia kuna kitu kinaitwa urasimu.Mtu akitaka kuwekeza kiwanda Tanzania, atahangaishwa,itafika miaka miwili. Wenzetu Uganda ndani ya masaa 48ukitaka kuwekeza unapata kila aina ya msaada unaotakana Serikali inakwambia, kama unataka kuongezewa mtajipia iko tayari, lakini Tanzania hilo hatulifanyi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naishauri Serikaliihakikishe kwanza inaweka miundombinu rafiki, mifumomizuri ya kodi, lakini tuondoe urasimu. Vilevile pia natakakuiambia Serikali…

(Hapa kengelee ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.Mheshimiwa Yosepher Komba atafuatiwa na MheshimiwaJoyce Sokombi na Mheshimiwa Devotha Minja ajiandae.Dakika tano, tano.

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Napenda ku-declare interest angalau haiko kwenyehela lakini mimi nimetokea Tanga na mnajua historia ya Mkoawa Tanga katika suala la viwanda. Mnajua Tanga miaka ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

1980 ni kati ya Mkoa ambao ulikuwa maarufu sana kwaviwanda kwa Tanzania hii. Tunavyoongea sasa hivi, viwandavingi vimefungwa, vilivyobinafsishwa, vimekufa, watuwameiba vifaa, viwanda Tanga hakuna tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanga tumejaliwa kuwa nabandari, viwanja vya ndege na reli ambayo mpaka sasa hivihatujajua Serikali lini itaamua kutujengea kwa kiwango chastandard gauge.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi pia natokea Muheza,Wilaya ambayo ni maarufu sana kwa kilimo cha matundahasa machungwa. Wilaya ambayo ina hali zote za hewatunazozijua; kuna hali ya baridi na joto, kiasi kwambatunaweza kulima mazao yanayotokana na baridi na mazaoyanayotokana na joto.

Mheshimia Naibu Spika, nakumbuka MheshimiwaWaziri wa Viwanda niliwahi kumgusia suala la Muhezanikaomba kwamba atafute mwekezaji kwa aji l i yamachungwa yetu yanayozalishwa Muheza. Wakulimawamekuwa wakipata hasara sana ya machungwayanayozalishwa pale, yamekuwa yakioza. Wamekuwa kamawana uwezo zaidi kutegemea soko la Kenya lakini Tanzaniahakuna kiwanda karibu; Tanzania, Muheza hakuna kiwandawakulima wanapata shida sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri tunajualengo la Tanzania ya viwanda ni jema, lakini kamatusipokuwa makini hatuwezi kufikia huko. Kamahamkujiandaa, tafuteni namna nyingine ya kuliweka sawa.Kwa nini nasema hivyo? Waziri wa Viwanda yeye kama yeyehawezi kufikia lengo la viwanda kama Wizara nyinginehazijaonesha ushirikiano kwako. Yeye kama yeye hawezikufikia kwenye viwanda, kama Wizara ya Fedha haijaamuakuona kama suala la viwanda ni muhimu. Pia hawezi kufikialengo kama Wizara ya Ardhi na Wizara ya Usalama namambo mengine hazijamsaidia. Kwa hiyo, inatakiwa sualala viwanda liwe ni la nchi, siyo Wizara. Kwa kufanya hivyo,tutakuwa na miundombinu mizuri kwa ajili ya uwekezaji.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee viwanda nawanawake. Sensa ya viwanda inaonesha asilimia 99.15 niviwanda vidogo sana na viwanda vidogo. Kwa harakaharaka ukiangalia katika sensa hii, utaona viwanda vidogosana ni kati ya mtu mmoja mpaka wanne; viwanda vidogoni kati ya mtu mmoja mpaka 50. Ukiangalia kwa undani zaidiutakuta hivi viwanda vidogo vingi vinamilikiwa nawanawake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, sijaona popotekwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri ambapo ameoneshanamna ambavyo atamsaidia mwanamke aingie kwenyeuchumi wa viwanda akiwa anajiaamini. Tunajua hali yakipato cha wanawake wengi wa nchi hii ni cha chini. Wizarahaijaandaa utaratibu wowote kumwezesha mwanamkeambaye kwa asilimia kubwa ndio amewekeza kwenye hiviviwanda vidogo aweze kujikwamua. Kwa hiyo, tunaviwanda vingi vya mtu mmoja mpaka watano, tutafika lini?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kitu kinginetunapoongelea Tanzania ya viwanda, lazima tukubali natuamue tunataka viwanda vya aina gani? Hatuwezi kuwana viwanda nchi nzima kwa mara moja. Lazima tutengemaeneo, lazima tuwe na point ya kuanzia. Tanzania tunatakaviwanda ndiyo, tunataka viwanda vya aina gani? Tunatakaviwanda vya kutumia malighafi gani? Tutakapokuwatumefanya hayo maamuzi, itakuwa ni rahisi. Hatuwezikujenga viwanda nchi nzima, lazima tuamue baada yamiaka 10 miaka 15 tunataka katika viwanda Tanzaniaijulikane katika kitu gani? Ziko nchi ambazo zinajulikana kwaajili ya kuzalisha products za maziwa peke yake. Tanzaniatunataka tujulikane kwenye nini katika viwanda? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niongee suala la VETA.Tunajua inatakiwa kuwe na elimu na ujuzi wa kutosha ilituingie kwenye viwanda tukiwa tunajiamini. Kumekuwa natatizo kubwa sana katika Vyuo vyetu vya VETA, siyo tu udahililakini pia vifaa na mashine zinazotengenezwa VETA zina beighali kuliko sehemu nyingine yoyote. Sasa kwa namna hii

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

hamwezi ku-encourage viwanda wakati watengenezajiwetu wa ndani wanapitia mazingira magumu katika kuandahizo zana za kufikia kwenye viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naiomba Serikaliisaidie wale wataalam wa VETA ambao wanatengenezamashine ambazo zinaweza zikatumika kwenye nchi yetu,wapunguzieni kodi ambazo ni mzigo kwa wafanyabiasharawengi...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wakoumemalizika. Mheshimiwa Joyce Sokombi, atafuatiwa naMheshimiwa Devotha Minja, na Mheshimiwa DunstanKitandula ajiandae.

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kupata nafasi hii. Pia namshukuru MwenyeziMungu kwa kunipa uzima na afya njema. Kabla ya yote,napenda tu pia kumpa pole Mwenyekiti wangu wa Kanda,Mbunge wa Tarime Vijijini, Mheshimiwa John Heche kwakuumwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine pia napendanisemee kitu kidogo, imesemewa hoja yake iliyotolewa hapaasubuhi; ni mbaya sana kumsema mtu ambaye anaumwa,yuko hoi kitandani. Ni vizuri mkamwacha akapona ndiyo ajeaambiwe hayo maneno anayoambiwa ili ayajibu yeyemwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niseme tu kwambaMheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, MheshimiwaMbunge hajakataa kiwanda kisijengwe Tarime, isipokuwautaratibu ufuatwe unavyotakiwa na mwendemkawashirikishe wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu kuishauri Serikalikwamba Wizara ya Viwanda na Biashara ni vizuri ikaungana

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

ikawa pamoja na Wizara ya Kilimo, kwa sababu bila kuwana Wizara ya Kilimo, viwanda haviwezi kufanya kazi zozotekwa sababu wanaendesha viwanda kwa kutoa malighafiwapi? Maana malighafi inatoka kwa wakulima. Kwa maanahiyo basi, ni vizuri hizi Wizara zikaungana ili yale mazaoyanayopatikana kutoka kwa wakulima yaende yakafanyekazi katika viwanda. Maana huwezi kusema mnafanya kazikatika viwanda kwa kutegemea mazao ya wakulima halafuWizara yenyewe inajitegemea yenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano, viwanda vyamafuta; huwezi kuchenjua mafuta bila kutoka kwenye vitukama karanga, mbegu za pamba, ufuta au alizeti. Kwa hiyo,basi ni vizuri hizi Wizara mbili zikaungana. Kwa mfano, katikaMkoa wa Mara tulikuwa na viwanda vingi sana, karibuviwanda kumi na kitu, lakini sasa hivi ni viwanda vitatu tuvinavyofanya kazi; na ni viwanda vya watu binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshauri Waziri waViwanda na Biashara kwa nini asivifufue vile viwanda vyaMkoa wa Mara? Kwa mfano, kile Kiwanda cha MUTEX, kilekiwanda kilikuwa kinasaidia kutoa ajira nyingi sana kwawakazi wa Mkoa wa Mara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimshauri tuMheshimiwa Waziri na Mkoa wa Mara una sifa kuu kubwamoja ambapo ametokea Baba wa Taifa. Ili kumuenzi Babawa Taifa ni vizuri ikaonekana kwamba kuna kitu ambachokinaleta manufaa kwa wananchi wake katika Mkoa waMara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumuulizaMheshimiwa Waziri, ni lini atavifufua vile viwanda vya Mkoawa Mara? Maana tulikuwa na Kiwanda cha Mara Oilambacho sasa hivi hakifanyi kazi; kuna Mugango Ginnery,tuna Jarif Ginnery, ORAM Ginnery; hivi vingine vilikuwa vyawatu binafsi na Buramba Ginnery, vyote hivi havifanyi kazi.

Pia tulikuwa na viwanda vya samaki; na hivi viwandavya samaki, sasa hivi kinachofanya kazi ni kiwanda kimoja

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

tu ambacho ni cha Musoma Fish. Sasa Mheshimiwa Wazirihaoni umuhimu kwamba wale wavuvi wanapovua samaki,kwa nini wasiwe wanapeleka kwenye kiwanda kuchenjuaminofu ya samaki ambayo inasafirishwa kupelekwa nje iliwasilete usumbufu wowote, wawe wanachambulia palepale Mkoani Mara?

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine kikubwa, nilazima iwepo mikakati ya Wizara hizi mbili ili izingatie namnaya kumsaidia mkulima pamoja na kuweza kuwasaidia vijanawetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Sokombi,muda wako umekwisha. Mheshimiwa Devotha Minja,atafuatiwa na Mheshimiwa Dunstan Kitandula naMheshimiwa Olenasha ajiandae.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangiaWizara hii muhimu kwa maisha na maendeleo yaWatanzania. Vision ya viwanda, Mwalimu Nyerere aliwahikuiona na ilikuwa implemented kuanzia miaka 1967, ambapomikoa mbalimbali ilionesha kwa vitendo kwa kuwa naviwanda na vilikuwa vikifanya kazi. Mkoa wa Morogoro nimiongoni mwa Mikoa ambayo ilinufaika na vision hiyo kwakuwa na viwanda zaidi ya 20.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasatunavyozungumza viwanda vilivyokuwa vimewekeza katikaMkoa wa Morogoro kwa miaka hiyo ya 1960 viliwezeshawananchi wa Mkoa wa Morogoro kupata fursa za kupataajira. Ilikuwa siyo rahisi kwa Mkoa wa Morogoro kupata housegirl; ilikuwa siyo rahisi kwa Mkoa wa Morogoro kupita kukutawatu wanacheza bao; ilikuwa siyo rahisi kwa Mkoa waMorogoro kupita kukuta Wamachinga; ilikuwa siyo rahisi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

kupita Mkoa wa Morogoro ukakuta watu wamekaa vijiweni,kwa sababu kulikuwa na viwanda na viwanda vile vilikuwavikitoa ajira kwa wananchi walio wengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo sasa, namwombaMheshimiwa Waziri, nimejaribu kupitia sana katika taarifayake hii, iko wapi mikakati ya kufufua viwanda vya Mkoawa Morogoro vilivyokufa? Ubinafsishaji wa viwanda badalaya kuongeza efficiency, ubinafsishaji wa viwanda umekuwani wa kunufaisha watu wachache ambao wamechukuaviwanda kama collateral kwenda kukopa katika mabenki,kunufaika wenyewe na wananchi kukosa ajira. Kwa hiyo,naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujumuisha,atuambie uko wapi mkakati halisi wa kuvirudisha viwandavya Mkoa wa Morogoro? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wa Morogorohivi sasa kuna viwanda, kwa mfano, Kiwanda cha Canvasambacho kil ikuwa kikinua hata pamba kutoka kwawananchi wa Wilaya ya Kilosa, lakini hivi sasa wameachakulima pamba kwa sababu kiwanda kimekufa. Kipo kiwandacha Asante Moproco cha Mafuta; kiwanda hiki wananchiwalikuwa wanalima alizeti kwa sababu walikuwa na uhakikawa sehemu ya kuuza. Hivi sasa wananchi hawalimi alizetikwa kuwa hakuna kiwanda. Kipo kiwanda cha Komoa, kipokiwanda cha CERAMIC, Morogoro Leather Shoe, UNNAT chaMatunda ambacho kil ikuwa kikinunua matunda yawananchi wa Mkoa Morogoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri atupe mkakati wa kufufua viwanda hivi. Siyo hivyo tu,atuambie Serikali ina mpango gani wa kuwachukulia hatuawawekezaji hawa ambao kwa makusudi waliviua viwandahivi? Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha watu hawaambao wengine kwenye viwanda vile wameuza vipuri, hivisasa yamebaki kuwa magodauni na wengine wanachungambuzi. Je, ni sahihi kwa watu hawa kutumia collateral kupatafaida lakini wanaviua viwanda badala ya kunufaisha?Atuambie, Mheshimiwa Rais alipita Morogoro akasemaatalishughulikia, tunataka kuona kwa vitendo kwamba

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

hawa wamiliki wa viwanda ambao wameziweka ajira zawananchi wa Mkoa wa Morogoro mfukoni, wanachukuliwahatua gani kama kweli mna nia ya kuleta viwanda kwa nchihii?

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la nyumba.Wakati wa ubinafsishaji zipo nyumba ambazo zilikuwazinamilikiwa na viwanda vile na zilikuwa ni nyumba za Serikali.Zile nyumba hivi sasa zinamilikiwa na watu ambao ndiowaliobinafsishiwa viwanda, lakini hivi sasa wafanyakazi waSerikali hawana nyumba, hawana pa kuishi. Wale watuwamepeana nyumba zile kinyemela, hawalipi pango nahawalipi kodi. Maofisa wanakosa mahali pa kuishi lakini watuwaliobinafsishiwa wanang’anga’nia kuishi kwenye nyumbahizi. Hii siyo sahihi kabisa. Tunamwomba Mheshimiwa Waziriamulike, aangalie ili hatua mahususi ziweze kuchukuliwa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia biashara yamwendokasi; mabasi ya Dar es Salaam, tuna mengi yakujiuliza. Biashara hii imekuwa kama ni ya watu wachache.Serikali imeamua kuleta mabasi ya mwendokasi kwa lengola kusaidia kupunguza msongamano, lakini kuna wazawa,kuna Watanzania ambao walikuwa wakifanya biashara zadaladala ambao nao walikuwa na uwezo wa kupata fursaya kuwekeza katika mwendokasi...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa, muda wakoumekwisha. Mheshimiwa Dunstan Kitandula, atafuatiwa naMheshimiwa William Olenasha na Mheshimiwa MwiguluNchemba ajiandae.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii nami nichangiekwenye hotuba hii ya Wizara ya Viwanda. Namshukuru sanaMungu kwa kunipa fursa hii ya kuweza kuzungumza katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Bunge lako Tukufu. Nianze kwa kusema naiunga mkono hojailiyoko mbele yetu, nikiwa na reservation kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpongeze nduguyangu Mheshimiwa Mwijage kwa kazi kubwa anayoifanyaya kuleta hamasa kwa Watanzania kuona umuhimu wakumiliki viwanda. Amefanya kazi kubwa ya kuwahamasishaWatanzania kubadili mitazamo ya uwekezaji ili wajielekezekwenye kumiliki viwanda; viwe viwanda vidogo, viwandavya kati, lakini vile vile viwanda vikubwa. Hongera sana,ameitendea haki taalum yake ya Masoko. Naomba sasa hililisiwe jukumu lake peke yake, Wizara ilichukue hili kwa ujumlawake. Ongezeni nguvu katika kuhamasisha Watanzaniawabadilishe mitazamo katika umiliki wa viwanda katika nchiyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya,nataka nieleze masikitiko yangu; pamoja na nia nzuri yakuanzisha viwanda, lakini yapo mambo yanakwamisha sanaukuzaji wa viwanda katika nchi yetu. Ukifuatilia mijadala nasisi tunaopitia pitia tafiti zinazofanyika katika nchi hii, mojakubwa ni lack of coordination. Kuna maeneo tunakwendahatua moja mbele, tunarudi hatua mbili nyuma; na nitatoamfano.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nataka nizungumzieSekta ya Maziwa. Utafiti wa wenzetu wa ESRF unaoneshakwamba mwaka 2010 tulikuwa tunaingiza maziwa kutokanje takriban lita milioni 40 zenye thamani ya dola milioni 20.Ilipofika mwaka 2014 uingizaji wa maziwa ukaongezekakutoka lita milioni 40 ukapanda mpaka lita milioni 70 zenyethamani ya dola milioni 40. Unaweza kuona ni jinsi ganitunapoteza fedha kwa kuingiza maziwa kutoka nje. Wakatitukiingiza maziwa kwa kiasi hicho, sisi tunazalisha takribanlita bilioni mbili, lakini zinazosindikwa hazifiki lita 150,000.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia 62 ya maziwatunayoingiza yanatoka Kenya, asilimia 32 yanatoka SouthAfrica, asilimia nne Uganda. Hata haya yanayopitia South

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Africa, kuna walakini mkubwa. Tunaambiwa ni uchochorowa kukwepa kodi. Nitayasema baadaye haya. Masikitikoyangu ni yapi? Kiwanda cha Tanga Fresh ambacho ndiyokinazalisha kwa wingi sasa, kinazalisha lita 50,000 kwa siku.Ni kiwanda ambacho tulitakiwa kukilinda kwa nguvu zetuzote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda hiki miaka minneiliyopita, walitaka kuongeza uzalishaji kutoka lita 50,000kwenda lita 120,000 na tulikuwa tumepata grant ya kuwezakufanya jukumu hilo. Wenzetu wa Bodi ya Ushindaniwakawapiga faini ya shilingi bilioni nne wakisema walinunuaassets kinyume na utaratibu. Assets zilizonunuliwa zilikuwa zakiwanda kilichokufa, kwa hiyo, hoja ya kuua ushindani haipo.Tumeminyana, faini ile imepungua mpaka sasa hivi badoimeng’ang’aniwa shilingi milioni 400. Hiki ni kiwandaambacho kingeongeza uzalishaji katika nchi yetu. Fedha ileimepotea! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanga Fresh wameamuakukopa sasa. Wanataka kutumia assets zao, majengo yaowaende wakakope. TRA wanakuja wanazuia wanasemahawawezi kutumia majengo yale kukopa kwa sababualiyewauzia hakulipa kodi stahiki. Vitu vya ajabu sana! Yaanialiyekwepa kodi yupo, anajulikana; anaendelea kufanyabiashara kwenye nchi hii, TRA, hawaendi kumbana,wanaenda kumbana Tanga Fresh ambaye hahusiki. Mamboya ovyo sana! Tunashindwa kukuza viwanda vyetu kwamambo ya ovyo kiasi hiki! Leo hii ninapozungumza, vituo 28vya kukusanya maziwa kule Morogoro vimefungwa,wananchi hawana sehemu ya kuuzia maziwa yao kwasababu hayawezi kupokelewa Tanga Fresh. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanga Fresh wananunuamaziwa Mkoa mzima wa Tanga; Tanga Fresh wananunuamaziwa kutoka kwa wakulima Mkoa wa Pwani; Tanga Freshwananunua maziwa kutoka Morogoro. Hivininavyozungumza, Tanga Fresh wameombwa na wakulimakutoka Mbeya wanunue maziwa yao, wanashindwa! Maziwayanamwagwa. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaingiza maziwa yamabilioni haya kutoka Kenya, halafu tunakuja hapatunasema tunataka kuendeleza viwanda, hii haiwezi kuwasawa. Napiga kelele kwa Mheshimiwa Waziri wa Viwandakwa sababu sera ya ukuzaji wa viwanda iko kwake, lakininajua mchawi wetu hapa ni Wizara ya Fedha. Najua jitihadaalizofanya ndugu yangu Mheshimiwa Mwijage ili jambo hililiishe, lakini barua ile aliyoandika mpaka leo imekaliwa paleWizara ya Fedha hakuna kinachoendelea. Tutaendeleanamna hii namna gani? Lazima tubadilike. Naiomba Serikaliyangu jambo hili lishughulikieni, tuondoleeni aibu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kichekesho kingine,tulipitisha hapa Sheria ya VAT kwenye bidhaa za maziwa,tuliingizwa mkenge na wenzetu Kenya lakini Kenya wananchiwalipopiga kelele, wenzetu wakafuta kodi i le, sisitumeendelea nayo. Wabunge tukisimama tukisema hapa,tunaonekana vituko. Tuliyasema hapa kwenye Sekta ya Utaliihatukusikilizwa, Sekta ya Maziwa nayo imeingiliwa, hebutuwe smart; tunapokubaliana na hawa wenzetu, tukionawamekiuka makubaliano, mara moja na sisi tugeuke.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu korosho; nilikuwaMakamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, kipindikilichopita, tuliahidiwa viwanda sita vya Korosho, leo hiihavipo. Ndugu yangu Mheshimiwa Mwijage, taarifa za Bodiya Korosho wanatuambia mwaka huu, tani zilizouzwakorosho ghafi, tani 260,000 tusiendelee kuangalia jambo hili,tutumie Mfuko ule wa Export Levy kujenga viwanda. Nendenimkafanye utafiti tujue, kama tunataka korosho yetuibanguliwe hapa, angalau nusu ya tani hizi, tunahitajiviwanda vingapi, tutengeneze Mfuko wa Mikopo kutokanana Export Processing Levy tuitangaze, watu waje wakopefedha zile tujenge viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza natoa shukurani zangu kwako kwa kunipatia fursahii ya kuchangia katika hotuba ya Wizara hii ambayo nimiongoni mwa Wizara muhimu katika Taifa letu.

Pili, natoa pongezi kubwa kwa Mheshimiwa Waziri,pamoja na watendaji wake wote kwa matayarisho yakitaalam ya hotuba ya Wizara hii. Nawaomba wazidikushirikiana ili kufanikisha malengo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotubahii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Sekta binafsi ni sektamuhimu katika nchi yetu. Sekta hii inawagusa wananchi wakipato tofauti wenye azma ya kujiendeleza kiuchumi. Sektahii inakabiliwa na matatizo kadhaa, kama vile upatikanajiwa maeneo ya uwekezaji ambayo huwa yanawakatishatamaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikaliiwaondolee urasimu huu ili kuwawekea mazingira rafiki iliiwe kama ni vivutio kwa sekta hii. Aidha, Serikali iwapunguzietozo ambazo hazina ulazima. Tozo nyingi huwa zinaidaiwakwa sekta binafsi mapema kabla ya mwekezaji binafsihajaanza kazi. Ni vyema tozo (tax) zidaiwe baada yauwekezaji kuimarika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ujenzi wa viwandanchini; naipongeza Serikali yetu kwa azma nzuri ya kujengaviwanda, ujenzi wa viwanda utaongeza tija katika nchi nakuongeza nafasi za uajiri. Ujenzi wa viwanda unahitajimatayarisho mengi kabla ya kuanza. Kwa mfano, huwezikujenga kiwanda mahali ambapo hakuna umeme, maji namiundombinu ya barabara. Naiomba Serikali kuchukuajuhudi za makusudi kuimarisha miundombinu hii ambayoitawashawishi wawekezaji wa nje na ndani kuwekeza katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Sekta ya Viwanda. Aidha, naomba Serikali ipunguze baadhiya kodi kwa wawekezaji wakubwa wa nje na ndani ili piaiwe ni kivutio kwa wawekezaji wa aina hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu matayarisho yarasilimali watu; Serikali ina azma nzuri ya kufikia na kukuzauchumi kwa kupitia Sekta ya Viwanda. Sekta ya Viwanda niya kitaalam ambayo inahitaji weledi wa kupanga nakuendesha sekta hii. Naishauri Serikali kuchukua juhudi zamakusudi kuanza kuwatayarisha Watanzania kwa kuwapatiamafunzo ya kila ngazi ili kujiweka tayari kuendesha sekta hii.Aidha, ni vyema kuwafundisha na kuwapa kipaumbelewazawa na kuepuka kabisa kutumia wataalam kutoka njeya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkonohoja.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba niishauri Serikali mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali yaAwamu ya Tano imepania kuwa na Tanzania ya viwanda,naiomba Serikali ianzishe au itafute wawekezaji kwa ajili yaMkoa wa Njombe. Njombe ni katika mikoa inayozalisha kwawingi chakula kama vile mahindi, ngano, alizeti na matunda.Hivyo, naiomba Serikali itafute wawekezaji kwa ajili yakiwanda cha kusindika matunda, unga wa mahindi na ungawa ngano Mkoani Njombe. Pia naiomba Serikali ianzishe auitafute wawekezaji kwa ajili ya viwanda vya karatasi, lami,kiwi na toothpicks.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwa kuwa Mkoa waNjombe unazalisha viazi kwa wingi, naiomba Serikali itafutewawekezaji kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kutengenezabidhaa zinazotokana na viazi kama crisps, katika Mkoa waNjombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwawafanyabiashara wananyanyasika sana na TRA kutokana na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

kuwa na tozo nyingi, naiomba Serikali iangalie namna yakuwasaidia wafanyabiashara wasikatishwe tamaa kwakukimbizwa na tozo nyingi na hasa kwa wafanyabiasharawadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wafanyabiashara wadogowadogo (wajasiliamali) wa Njombe watafutiwe eneo rafikikwa ajili ya kufanyia biashara zao. Napendekeza eneo hiloliandaliwe maeneo ya stendi mpya iliyopo Mji Mwema.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaNaibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotubaya bajeti nzuri na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwautekelezaji wa mkakati wa ujenzi wa viwanda ili Tanzaniaifikie hadhi ya nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Ni jambola tija sana kwa uchumi wa nchi yetu na ukombozi kwa sualala ukosefu wa ajira kwa vijana na wananchi wetu. Serikaliimezuia eneo la SEZ Bagamoyo jumla hekta 9,080. Mwaka2008. Serikali ilitathmini eneo lenye ukubwa wa hekta 5,742katika Vijiji vitano vya Zinga, Kondo, Pande, Mlingotini naKiromo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wafidiwa walioainishwa ni2,180 na fidia ya wakati huo ilikuwa ni shilingi bilioni 60. Mpakahii leo hekta 2,399 zimetwaliwa, wafidiwa 1,155 wamelipwajumla ya shilingi bilioni 26.4. Wananchi 1,025 hawajalipwampaka leo; miaka 10 sasa tangu mwaka 2008! Wananchihawa wanadai jumla ya shilingi bilioni 51 (pamoja na interest).

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi hawawamesubiri miaka 10 kulipwa fidia na wamepata madhilamengi. Mheshimiwa Waziri atakapofanya majumuishoatuambie, lini wananchi hawa watalipwa fidia zao? Kwavile mwekezaji ameainisha eneo atakalotumia kuwa hekta3,000 tu: Je, hekta zilizobaki zitalipwa na nani? Lini? Kwa bajetiipi? Mtindo huu wa kumtaka mwekezaji alipe fidia ya ardhi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

inapunguza vivutio vya uwekezaji katika nchi yetu, Serikaliirudishe utaratibu wa Serikali kulipa fidia ili kushawishiwawekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa bandariBagamoyo ni sehemu ya SEZ ya Bagamoyo. Ila katika mradikuna wananchi 687 ambao wamepunjwa fidia zao. Sasawameshahakikiwa na Mthamini Mkuu wa Serikali. Serikaliiwalipe fidia zao halali wananchi hawa. Mbona katika bajetihii ya 2017/2018 haina kasma kwa ajili ya malipo ya fidia hii?Mheshimiwa Waziri awape jibu sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu wa ujenzi wabandari Bagamoyo utahamisha kaya zinazofikia 2,000.Wananchi hawa waliahidiwa makazi mapya katika shambala Kidogoni - Bagamoyo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwandani shahidi wa jambo hili, yeye alilisimamia alipokuwa DG,EPZA. Nyaraka mbalimbali za EPZA zinaonesha mpango naahadi hiyo. Kwa vile Mwekezaji yuko tayari kulipa fidia,naiomba Serikali ifanye maongezi na mwekezaji afidieshamba la Kidogoni ili wananchi wahame eneo la bandariharaka.

Mheshimiwa Waziri atakapofanya majumuishoatueleze ni lini wananchi wanaopisha mradi wa bandariwatapewa eneo la makazi yao mapya? Kuhusu mradi waujenzi wa bandari ya Bagamoyo, Serikali yetu imesainimikataba ifuatayo: MoU Septemba, 2012; FrameworkAgreement, Machi 2013; na Implementation Agreement,Desemba, 2013. Kutia saini Fremework Agreementkulishuhudiwa na Rais Mstaafu Mheshimiwa Kikwete na Raiswa China Mheshimiwa Xi Jingping.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni mwaka wa tano.Kwa vile CMPort Holding na mbia wako Oman wana mtajina uzoefu; na kwa vile CMPort watalipa fidia ya ardhi,naiomba Serikali yangu Tukufu Iharakishe majadiliano naMwekezaji huyo ili ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uanzemapema. Tangu tumeanza majadiliano mwaka 2012,CMPort wamekamilisha mikataba ifuatavyo:-

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

(i) Sri Lanka, tayari wanaendesha ColomboInternational Container Terminal (CICT).

(ii) Nigeria, tayari CMPort inaendesha Tin-CanIsland Container Teminal.

(iii) Togo, tayari, CMPort inaendesha Lome PortContainer Terminal.

(iv) Djibouti, tayari CMPort inaendesha bandari yaDjibouti na Container Terminal.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi zinatuacha nyuma!Mheshimiwa Waziri akija kufanya majumuisho atuambie nilini Serikali itakamilisha Mikataba na CMPort Holding? Ni liniujenzi wa Bandari, Bagamoyo utaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba majibu na msimamo wa Wizara katika yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Wizara itasaidiaupatikanaji wa Kiwanda cha Matunda Wilaya ya Muheza;kwa kuwa wafanyabiashara na wakulima wa Wilaya Muhezahawanufaiki na zao la matunda hasa machungwa? KatikaWilaya ya Tanga Mjini Kata ya Kiomoni, kuna Kampuni inaitwaNEEL KHANT Lime Limited Tanga, kinachomilikiwa na BwanaRashidi Liemba.

Kiwanda hiki kimekuwa na madhara makubwa kwawakazi wanaozunguka eneo hilo hasa wanafunzi wa Shuleya Msingi na Sekondari Kiomoni. Wizara inafahamuchangamoto hiyo? Iko tayari kushirikiana na NEMC kufuatiliausalama wa raia wa eneo hilo?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini Tanga SpecialEconomic Zone (SEZ) imetengewa fedha kidogo; shilingi bilioni2.7 katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wamwaka 2016/2017 - 2020/2021 wakati Tanga ni Mkoa wa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

Viwanda? Katika historia ya nchi, Tanga ndiyo mkoa wakwanza ndani ya nchi hii kuwa na viwanda vingi miaka ya1980.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwanamke na viwanda.Sensa ya Viwanda inaonesha asilimia 99.5 ni viwanda vidogosana na viwanda vidogo. Kwa takwimu hizi, ni wazi viwandavingi vidogo vinamilikiwa na wanawake. Je, Wizaraimejipangaje kuhamasisha wanawake kujiunga katika Sektahii ya Viwanda?

Je, Serikali kupitia Wizara ina mkakati gani wakuhakikisha kuwa viwanda vinakuwa gender sensitive katikaproduct na ajira?

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza kabisa naunga mkono hoja. Changamototuliyonayo kubwa inayokabili viwanda nchini ni pamoja naukosefu wa mitaji na teknolojia ya uzalishaji kupitwa nawakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto nyinginekubwa ni kutokuwa na uhakika wa umeme na maji ambayoinafanya viwanda vyetu kutoimarika, hivyo nashauri kuwa iliviwanda viimarike nchini, Serikali ihakikishe umeme na majivimepatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa namwenendo usioridhisha kutoa fedha za miradi ya maendeleo,hivyo kuchelewesha utekelezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali iangalienamna bora ya kuiwezesha Benki ya Rasilimali Tanzania(Tanzania Investment Bank) ili ifungue matawi mikoani hasaMkoa wa Kagera, hatua ambavyo itasaidia mikopokuwafikia Watanzania walio wengi. Kuna changamoto yakukosekana kwa soko kwa baadhi ya bidhaazinazotengenezwa nchini kwa sababu ya kukosa uboraunaotokana na gharama za uzalishaji kuwa juu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Ongezeko laThamani (VAT), hususan kwa wawekezaji wa viwanda vyamadawa ya kilimo na mifugo kutozwa kodi ya ongezeko lathamani (VAT), unapunguza ushindani wa bidhaa zinazoingianchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali iboresheKiwanda cha Kagera Sugar ili kiweze kutoa sukari kwa wingiili kukidhi mahitaji ya Watanzania hasa waliopo Mkoa waKagera.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Kagera Sugarkipo Mkoani Kagera, lakini wananchi hawanufaiki nakiwanda hicho kwa sababu sukari inakuwa ni ya bei ya juusana. Hivyo, naiomba Serikali iweze kutusaidia wananchi waKagera kupata sukari kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeongeza ugumukatika hatua ya kuanzisha biashara kwa kuongeza tozo zausajili. Jambo hili linaathiri juhudi za kuongeza ajira kwavijana. Pia inafanya wajasiriamali wasifanye shughuli rasmiza kuingiza mapato ya Serikali na kupunguza ajira zitokanazona biashara rasmi.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika,nchi yetu imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati ambaounategemea uimarishaji wa viwanda. Tanzania tulikuwa naviwanda vingi miaka ya nyuma lakini tulifika mahali tukauzaau kuvibinafsisha vingine, tena kwa bei ndogo sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali kurudinyuma katika kipindi kile cha uuzaji wa viwanda, kuangaliamikataba ile yote ili kubaini ni vipi tunaweza kurejeshaviwanda mikononi mwa Serikali. Ujenzi wa viwanda ni ghalisana na ni bora na rahisi kufufua vile vya zamani kulikokuweka viwanda vipya.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda maana yake niajira kwa vijana wetu. Serikali hii ina mipango mizuri kwenye

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

makaratasi, lakini kwa kweli kiuhalisia bado kabisa viwandahavionekani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali kuanzishaviwanda vile ambavyo malighafi yake inaweza kupatikananchini. Tunayo mazao ya mashambani, tunayo mifugo mingisana na pia tunayo madini mengi. Viwanda pia vilengekatika kukuza uzalishaji wa mazao hayo ya hapo juu. Nijambo la kuhuzunisha, kwani mazao yanalimwa hapa nchinilakini yanasindikwa nje. Mfano, nchi yetu inazalisha koroshonyingi lakini inabanguliwa nje. Huku ni kukosesha Watanzaniaajira na pia kupoteza mapato ya Serikali.

MHE. LEONIDAS T. GAMA: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda nitumie nafasi hii kuipongeza sana Serikali yaAwamu ya Tano chini ya Kamanda wake Mahiri Dkt. JohnPombe Magufuli, kwa kazi nzuri na ya wazi ya kupeleka nchiyetu katika uchumi wa viwanda. Juhudi za wazi zinajionesha,kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa uongozi wake,viwanda vimeanza kuchipuka, SIDO imekua sana nawananchi wamekuwa wakijitokeza kuanzisha viwandakatika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Serikalikwa kazi nzuri inayofanyika. Mheshimiwa Waziri, pamoja najuhudi zote hizi zinazofanyika, bado Mkoa wa Ruvuma, Serikalina Wizara yake, haijatoa msukumo wa kuingiza Mkoa waRuvuma katika viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujua Serikali inampango gani wa kuingiza viwanda Mkoani Ruvuma? KipoKiwanda cha Tumbaku ambacho mwezi Januari, 2016Mheshimiwa Waziri Mkuu, alikitembelea na kujioneamwenyewe hali ya kiwanda hicho na alitoa maelekezo yanamna ya kufufua kiwanda hicho. Je, ni mipango gani yaWizara ya kufufua kiwanda hicho?

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Songeahawana kiwanda chochote na hivyo kukosa ajira namanufaa yatokanayo na uwezo wa viwanda. Tegemeo letu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

kubwa ni pale ambapo Serikali ilionesha dhamira yakuanzisha viwanda kwa kutenga eneo la EPZA pale SongeaMjini, lakini ni masikitiko makubwa kwamba hadi sasa eneola EPZA l imepimwa na watu wamehamishwa, lakinihawajalipwa fedha zao za fidia kutokana na ardhi na malizao katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi hawa hadi sasa,hawana mahali pa kwenda, umaskini umewapata, maanahakuna ardhi ya kilimo, hawana makazi wala hawanamaendeleo wanayoweza kuyafanya kutokana na kushindwakupata maeneo ya kufanyia shughuli za maendeleo. Piawanazuiwa kuendeleza maeneo waliyokuwa wakiishi nakutakiwa kupisha shughuli za EPZA.

Mheshimiwa Naibu Spika, inatukatisha tamaa sanakwa namna tunavyoona wale wananchi wakipata shidakatika eneo ambalo walikubali kulitoa kwa dhamira nzuriya shughuli za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, tunawapatia liniwananchi hawa fidia zao wanazozidai? Ni imani yangu kuwakuwalipa fidia wananchi hawa kutafuatia juhudi za kazi zaSerikali kuanza kulitangaza eneo hili la Songea Mjini kwawawekezaji waanze kuwekeza viwanda katika Mkoa waRuvuma.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kupata nafasi hii. Nianze kumpongeza MheshimiwaWaziri, Mwijage, kwa hotuba nzuri ya bajeti yenye kuletamatumaini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee namshukuru sanaMheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwakuweka mbele mapinduzi ya viwanda. Juhudi hizi tumeanzakuona matunda chanya na Tanzania ya viwanda sasainaonekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Kisiwa chaMafia wamehamasika katika kilimo cha miwa na kwa kiasi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

kikubwa wamefanikiwa kupata mazao mengi, lakini tatizolimekuwa ni kutokuwepo na kiwanda cha kuchakata miwaili kupunguza ukubwa wa mzigo na kujirahisishia usafirishajiwa mazao. Namwomba tu Mheshimiwa Waziri kupitia Shirikala SIDO, aangalie uwezekano wa Mtaalam kuja na kiwandarahisi kusaidia wakulima wa miwa wa Mafia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kisiwa cha Mafia pia nimaarufu kwa ulimaji wa zao la nazi. Kwa kuwa zao la nazilinatoa mafuta na tui kwa matumizi ya mwanadamu,nichukue fursa hii kumwomba Mheshimiwa Waziri aangalieuwezekano wa kutupatia kiwanda kitakachochakatamazao yatokanayo na nazi ili kusaidia kukuza kipato chamwananchi wa Mafia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais mwakaanazindua Bunge hili la Kumi na Moja alionesha masikitikoyake ya kukosekana kiwanda cha kusindika samaki kwaukanda mzima wa Pwani kuanzia Mkoa wa Tanga mpakaMsimbati Mtwara. Namwomba Mheshimiwa Waziri aliangaliekwa ukaribu suala hili la kiwanda cha kusindika samaki.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nijadili suala Kitaifa laviwanda. Niiombe tu Serikali yangu kwenye kuelekeaviwanda, mkazo uwekwe kwenye kuweka mazingira wezeshiili sekta binafsi badala ya Serikali kujenga viwanda vyakeyenyewe. Serikali haifanyi biashara, Serikali isubiri kutoza kodina kupata fursa ya kutoa ajira kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine, naombaSerikali ianzishe vyuo aina ya VETA katika makambi yetu yaJeshi la Kujenga Taifa. Aina ya viwanda inayokuja sasa, lazimatuandae vijana wetu kwenye kada za kuendesha mashine(Machines Operators). Hii itasaidia kwao kupata ajira kwenyeviwanda hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuoanishauanzishaji wa viwanda na kilimo chetu. Sisi mazao yetu mengiya matunda yanaoza mashambani kwa kukosa kiwanda chakusindika matunda.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na ukweli kwambatuna kiwanda cha Azam pale Mkuranga, lakini kiasi kikubwawanaagiza matunda concentrate kutoka nje ya nchi. Hiiinatokana na ukweli kwamba matunda yetu hayalimwikitaalam na kupelekea shamba moja kutoa matunda yenyeladha tofauti na kushindwa kutengenezwa juice. Kilimo chakisasa ndiyo namna pekee ya kuoanisha ladha ya mazaohaya ya matunda ili yaweze kutumika kutengeneza juice.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naungamkono hoja.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Naibu Spika,nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara naUwekezaji kwa kazi nzuri, kadhalika na Watendaji wa Wizarahii. Suala la Makaa ya Mawe, Mchuchuma na chuma chaLiganga, Ludewa ni la muda mrefu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hotuba yaMheshimiwa Waziri, hakuna maelezo yanayojitoshelezakuhusu utekelezaji wa mradi. Kila kipindi cha bajeti, maelezoni hayo hayo ya Kamati ya Watalaam kupitia mapendekezoya mwekezaji. Serikali ieleze Bunge lako Tukufu tatizo lauwekezaji Mchuchuma na Liganga. Tunajenga reli tunahitajichuma! Tutaagiza chuma kutoka nje ya nchi wakati Mungukatujaalia chuma Liganga!

Mheshimiwa Naibu Spika, CAMARTEC ni kiwandakinachotengeneza zana za kilimo. Hata hivyo, vifaa vyaCAMARTEC havipatikani kwa wingi kwa wakulima;wangeweza kufanya kazi kubwa na kwa wepesi zaidi kwakutumia vifaa vya CAMARTEC; vifaa vya kupandia, kupalilia,kuvunia na kuchakata mazao. Kwa kuwa viwanda vingi vyahapa nchini vinategemea malighafi ya mazao ya hapanchini, naomba Serikali kuhakikisha kuwa vifaa vinavyowezakumrahisishia mkulima kazi, viuzwe kwa wingi na kwa beinafuu kwa wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania tunatamanikuwa na viwanda vingi kila Wilaya au kila Mkoa, lakini je,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

tumejiandaa vipi kuhusu malighafi, barabara, umeme,mifugo bora, mazao bora na yanayolimwa mwaka mzimana kadhalika? Maandalizi yanahitajika sana kwa wananchikulima mazao bora yanayolimwa mwaka mzima, ufugaji wakisasa na umeme usio na shaka kwa wenye viwanda nakadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiamini Serikali ya Awamuya Tano, hivyo ni kukumbushana mambo muhimu kwamaandalizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, waliouziwa viwanda nakuvigeuza maghala na vingine havitumiki kabisa: Je, Serikaliinasema nini juu ya viwanda hivyo? Naomba maelezo yaKiwanda cha Maziwa Utegi, Rorya kilichobinafsishwa nakilikuwa na mali nyingi na mpaka sasa hakifanyi kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tuna mifugo yakutosha na tungeweza kuuza bidhaa/mazao ya mifugo nakuingiza fedha nyingi nchini. Tatizo letu ni viwanda vya mazaoya mifugo. Hatuna viwanda vya nyama, ngozi, maziwa nakadhalika. Serikali ina mpango gani wa kuanzisha viwandavya kusindika nyama, maziwa na ngozi? Viwanda vilivyopovya watu binafsi havikidhi mahitaji ikilinganishwa na mifugoiliyopo. Naamini tukitumia vizuri Sekta ya Mifugo kelele/ugomvi kwa wakulima na wafugaji ungekwisha kwa amanina kwa urahisi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mifuko ya Hifadhi ya Jamiiinafanya kazi nzuri kwa maendeleo ya Taifa hili. Mifuko hiyoimejenga majengo makubwa mazuri katika miji yetu; na kwasababu mifuko hiyo, inatarajia kujenga viwanda katikamaeneo mbalimbali. Kwa taarifa zisizo rasmi, Mfuko wa PSPFhaupo vizuri sana kifedha: Je, utakuwa na uwezo wauwekezaji kama Hotuba ya Mheshimiwa Waziri inavyojielezaukurasa wa 170?

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kiti chako,napenda kuchangia Wizara hii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara hii inahusisha piauwekezaji ambao kwa kiasi kikubwa uwekezaji badohaujapewa kipaumbele. Kwa kiasi kikubwa hotuba ya WaziriMheshimiwa Mwijage imejikita katika kuzungumzia viwandaambavyo kwa kiasi kikubwa ni mbwembwe kuliko uhalisia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Taasisi zote za Umma zenyemitaji ya umma ilitakiwa tuelezwe, kwa kuwa taasisi hizi,mfano Mifuko ya Hifadhi yote inajikita katika uwekezaji. Kwakiasi kikubwa uwekezaji huu hauna tija. Nilitegemea hotubaya Mheshimiwa Waziri ieleze juu ya uwekezaji butuunaofanywa na Mifuko ya Hifadhi za Jamii pamoja na Taasisiza Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, ununuzi wa viwanja bei niza juu, hifadhi za Jamii kama LAPF wamenunua KiwanjaMwanza Square metre moja kwa Sh.255,000/= kitu ambachosiyo kweli. Kuna harufu ya matumizi mabaya ya Ofisi. Mtwarawamenunua kiwanja eneo la Rahaleo Square metre moja niSh.155,000/= eneo ambalo mimi nalijua. Niliwaambia haya,wakasema valuer ameruhusu. Valuers wanacheza deal nawahusika. Tunataka uwekezaji wenye tija kama Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo Kikuu cha Dar esSalaam kimeingia mkataba wa miaka 50 na mwekezajikutoka Botswana. Huu mkataba unampa mamlaka yakukusanya kila anachokipata na kuipa Serikali asilimia 10%tu. Hali hii haikubaliki. Kibaya zaidi, anajenga vibanda naanakusanya billions of money. Hivi baada ya miaka 50vibanda vile vitakuwa na thamani kweli?

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri apitie uwekezaji unaofanywa na Taasisi za Umma siokuwaza viwanda vya watu ambao yawezekana wasijekabisa kujenga. Hivi vilivyopo vifanyiwe uhakiki wa kina.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumuuliza Waziri,Mheshimiwa Mwijage, Kiwanda cha Mbolea Mtwara kinatatizo gani? Kwa nini hakijengwi wakati mwekezaji yupotayari? Kwa nini hawawezeshwi kujenga kiwanda hicho?Kwa nini hawampi rasilimali anazotaka ili ajenge kiwandaMtwara? Kila kitu kipo mpaka kwenye eneo, kigugumizi chanini au Mheshimiwa Waziri hataki maendeleo ya Mtwara?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mtwara Mjini kulikuwa naViwanda vingi vya Korosho, vyote sasa hivi havipo. Baya zaidikilikuwepo kiwanda cha OLAM, mwekezaji aliwekeza MtwaraMjini na kiwanda hiki kilikuwa kinaajiri wananchi wengi sana,lakini Serikali ilimwekea mazingira mabaya ya kodi; huyumwekezaji, amehamisha kiwanda na kukipeleka Msumbiji.Kwani kuna nini wawekezaji wa Mtwara hamwatakiwawekeze Mtwara? Au Wizara inataka Mheshimiwa Rais ajetena Mtwara atamke aliyotamka tarehe 4 Machi, 2017?Naomba wawekezaji wenye nia ya kuwekeza Mtwarawapewe mazingira rafiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu third party katikaajira, UCC Dangote Mtwara; kuna usumbufu mkubwakiwanda cha Dangote kwa kuwa kuna mtu kati anaitwaUCC ndio anayesimamia na kuajiri watu, baadaye anampamahindi na mahindi anampeleka Dangote. Hawa watuwakati wanapokonya haki za waajiriwa kiwandani,wananyanyasika sana, wafanyakazi hawana utaratibu,wanadhulumiwa haki zao wakidai mwajiri anasemahawamhusu na anamwambia UCC wafanyakazi kadhaahawatakiwi na wanafukuzwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuuliza, Serikaliilitoa waraka mwaka 2014 wa kuzuia mtu kati kutoa ajira yamawakala, umefikia wapi?

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika,pongezi sana kwa Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, kwa juhudi zake nzuri za kufufua na kujengaviwanda katika nchi yetu ya Tanzania. Tumeona jitihadakubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano. Nakubaliana kabisa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

kuwa nchi ya Tanzania ni tajiri sana, ina kila kitu, lakini tatizokubwa ilikuwa ni maamuzi magumu tu. Sasa tumepata Raismwenye maamuzi magumu na sahihi. Serikali haijengiviwanda, lakini Serikali inasaidia katika kutoa miongozo yakujenga viwanda na kuvutia wawekezaji kuja kuwekezaTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Mufindi Kusini tunaviwanda vingi sana kwa mfano, Kiwanda cha Chai (UniliverTea Company Limited), Mufindi Paper Mill Limited (MPM);Mufindi Tea Company Limited. (MTL), Kiwanda cha Pareto,Kiwanda cha Mbao (Sao Hill); pia kuna viwanda vidogovidogo vingi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri kwa Serikali,naomba Serikali ijenge miundombinu ya barabara, umemena maji ili kuwezesha wawekezaji kufanikisha uzalishaji wabidhaa bila matatizo. Viwanda vinashindwa kusafirishabidhaa kwa sababu ya babaraba mbovu. Barabara hiyo niMafinga hadi Mgogolo, Nyololo hadi Mtwango. Kuna tatizokubwa la stendi ya reli pale Mgololo ili bidhaa ziwezekusafirishwa kwa njia ya treni.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono. Ahsante.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika,Ukerewe ni moja kati ya maeneo ambayo yana rasilimali zakutosha kwa ajili ya malighafi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na uzalishajimkubwa wa samaki na matunda (mananasi, machungwana maembe), Wizara ielekeza wawekezaji kwa ajili yaviwanda vya kuchakata samaki na matunda katika eneohili ili kuokoa matunda mengi kuharibika kwa kukosa soko.Jambo hili litasaidia pia kukuza uchumi wa wananchi hasavijana na akinamama kwenye visiwa hivi vya Ukerewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kutokana na uzalishajimkubwa wa samaki katika Visiwa vya Ukerewe, litakuwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

jambo lenye maslahi kwa Taifa iwapo vitajengwa viwandavya kuchakata samaki kwenye maeneo haya badala yakuwasafirisha kuwapeleka katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuchangia kwenye sekta ya viwanda kamaifuatavyo:-

(i) Serikali itafute wawekezaji wa kufufuaviwanda vil ivyotaifishwa na Serikali na kuwakabidhiwawekezaji wazawa ambao wameshindwa kuviendeleza.

(ii) Serikali itafute wawekezaji kwenye viwandavidogo vya matunda, viungo (nyanya - tomato sauce),viwanda vya juisi za machungwa, maembe, nanasi (simplemachines) kwenye maeneo yanayozalisha matunda yanyanya na pilipili.

(iii) Viwanda vinahitaji umeme wa kutosha nawenye uhakika na wa gharama nafuu. Haiingii akilini kuwana umeme wa gharama kubwa wakati tunazalisha kwa gesiya Mtwara.

(iv) Kuimarisha sekta ya kil imo kutasaidiaupatikanaji wa rasilimali/malighafi za viwanda. Hivyo basikilimo endelevu ni cha kumwagilia na matumizi bora yapembejeo. Agriculture - Raw materials - Industrial goods/product.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu biashara napendakuchangia yafuatayo:-

(i) Biashara zinafungwa nchini kwa sababu yamazingira ya kufanya biashara kutokuwa rafiki. Serikaliinawabana sana wafanyabiashara kwa kuweka kodi nyingisana za uingizaji wa bidhaa toka nje. Hii ni hatari kwauchumi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

(ii) Mfanyabiashara mpya na hasa wale wadogowanawekewa makadirio makubwa ya kodi TRA hata kablahajaanza kuzalisha. Serikali iruhusu waanze biashara kwanzakisha itoze kodi tena inayokubalika.

(iii) Leseni za biashara ndogo hazitolewi mpakamfanyabiashara akalipe kodi TRA apewe tax clearance ndipoakakate leseni ya biashara Halmashauri. TRA hawako efficient/available hasa vijijini kama Wilaya ya Kakonko, hawapompaka mfanyabiashara aende Kibondo, Mtambo wa TINhaupo Kakonko wala Kibondo mpaka Kigoma sawa nakm.300. Hivyo wafanyabiashara wanashindwa kwendaKigoma (300km) il i kupata TIN number. Nashauriwafanyabiashara hawa wakate leseni za biashara zaHalmashauri ili nazo zipate fedha wakati TRA ikiweka utaratibuwa kutoa TIN vijijini.

(iv) Machinga kuuza bidhaa zao holela hasamaeneo ya Kariakoo soko la wafanyabiashara wakubwa.Hii ni kwa sababu wao hawalipi kodi hivyo huchukua bidhaaza wafanyabiashara dukani na kuziuza bila ushuru wowote.Hivyo wenye maduka Kariakoo hawalipi kodi kwani bidhaazao zinauzwa nje na machinga, kwa sababu zina bei ndogona wenye maduka kutotumia EFD machines.

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa wawekezaji,nashauri wapewe masharti nafuu ili wahamasike kujakuwekeza nchini. Mazingira rafiki na ya kuvutiayatawakaribisha wengi, invite more coming on board.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika,viwanda na elimu. Kulingana na umuhimu wa kuwa naviwanda nchini kwetu, ni lazima kutoa elimu kwa wananchijuu ya umuhimu wa kuanzisha viwanda na faidazitakazopatikana baada ya kuwa na viwanda nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuboresha kilimo. Kulinganana utaratibu wa viwanda ni vyema wananchi wakabadili

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

utaratibu wa kilimo cha mazao na badala yake walime aukuanzisha kilimo chenye tija kwa ajili ya kuhudumia viwandavitakavyokuwa vinazunguka maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda na ajira kwa vijana. Ilisuala la viwanda lifanikiwe ni vyema elimu ikatolewa zaidikwa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa ambao watanufaikana viwanda badala ya kuchukuwa vijana wa nje ya nchiyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzisha elimu ya viwandamashuleni. Kulingana na umuhimu wa suala la kuanzishaviwanda ni vyema kama wanafunzi katika masomo wakawana elimu au mada juu ya kuanzisha na kuendeleza viwandanchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuwawezesha wakulima.Kwa kuwa viwanda vingi na kwa asil imia kubwavinategemea kilimo na ili suala hili la viwanda lifanikiwe nivema wanawake wakulima wawezeshwe kuanzishaviwanda hata kama ni vidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda na mazao yabiashara. Ni vema Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa namkakati wa kudumu na endelevu kwa kuwa na viwandabora vya kuandaa mazao ya biashara ili kilimo kiwezekuwakomboa wakulima wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzisha vyuo vya VETAMkoa wa Rukwa. Vyuo hivi vitasaidia vijana kupata ujuziutakaosaidia kuendesha viwanda vitakavyoanzishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, masoko ni tatizo kubwakwa wakulima hasa wa Mkoa wa Rukwa mpakawanaelekea kukata tamaa kutokana na changamoto hii.Naomba Serikali ishughulikie suala hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Serikali ifufueviwanda vilivyokufa vya nguo, nyama, maji na kilimo(pembejeo).

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.

MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kutoa pongezi za dhati kwa Wizara hii na kwaviongozi wake wote. Natambua Wizara hii ni kiungo muhimukati ya wafanyabiashara na Serikali. Bila Wizara hii kufanyakazi kwa umakini na uweledi, basi ndoto ya Serikali yetu yakuwa na viwanda itakuwa ndoto isiyotimia. Kwa sababukumekuwa na kila aina ya matamko na sheria za ovyoovyoza kuua biashara ndani ya nchi hii hasa kutoka katikamamlaka zilizopo kama EWURA, TBS, NEMC, SUMATRA nazinginezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, ili mtu apateleseni ya NEMC ya Petrol Station, kwanza lazima apateconsultant ambaye amepitishwa na NEMC na baada yahapo asajili mradi, consultant pekee analipwa shilingi millionisaba (Sh.7,000,000/=) na kusajili mradi napo fedha. Ukimalizaconsultant, ili watu wa NEMC waje kukagua ripoti yaconsultant nao unalipa gharama zao za kuja site.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo wakiridhikakukupa leseni, unalipa shilingi milioni kumi (Sh.10,000,000/=)na baada ya hapo utaendelea kulipa ada ya kila mwakashilingi laki tatu (Sh.300,000/=). Utakuta inagharimu zaidi yashilingi milioni ishirini na tano kupata Leseni ya NEMC kwakituo kimoja na bila kujali kipo kijijini au mjini. Je, kwa faidaya Sh.90 kwa lita kuna biashara hapo, bado gharama zakodi, upungufu wa mafuta, mishahara na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii nimetoa mfano kwakituo cha mafuta lakini ndiyo hivyo hivyo kwa hoteli auviwanda ukitaka kupata leseni ya NEMC. Kwa mfano huumdogo, Wizara hii inachukua hatua gani kuhakikishamamlaka zilizopo zinafanya kazi zake kwa ufanisi na siyokuwa wakusanya faini na watoza kodi au Wizara hii ni jinatu? Kwa nini chochote kinachofanywa na mamlaka kuhusubiashara ndani ya nchi hii kisihusishe Wizara kwanza kablaya sheria na kanuni zao?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba majibu.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa NaibuSpika, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri na Viwandana Biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wa viwanda nabiashara katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Zipochangamoto nyingi katika kutekeleza sekta zilizopo chini yaWizara husika hasa changamoto ya urasimu usiokuwa walazima kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda nchini.Wawekezaji ni lulu inayosakwa na mataifa mbalimbaliduniani ni lazima kuwa makini. Nashauri Wizara ya Viwandana Biashara kuhakikisha kwamba Tanzania Investment Centre(TIC) inatoa huduma zote zinazotakiwa kwa mwekezajikatika sehemu moja hasa suala la vibali na uhakiki ufanyikeunder one roof.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Viwanda naBiashara ni Wizara mtambuka inayopashwa kufanya kazizake kwa kushirikiana na wadau na Wizara zingine kamavile Wizara ya Fedha kupitia sekta za mabenki, bima na TRA.Benki zinapofanya kazi zake vizuri na kuwa na riba rafikikatika uwekezaji mitaji katika sekta ya viwanda na kodimbalimbali zinazotozwa zikiwa rafiki zitasaidia katika sektazilizoko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa viwanda nchinikunategemea kwa kiwango kikubwa upatikanaji wamalighafi kama vile chuma na umeme wa uhakika. Kwakuwa nchi yetu imejaliwa kuwa na utajiri mkubwa kwauwepo wa kiwango kikubwa madini ya chuma na makaaya mawe na kwa kuwa makaa ya mawe yanapatikanaMchuchuma na Chuma cha Liganga, katika zoezi zima lauzalishaji chuma, makaa ya mawe hutumika nakinachozalishwa huwa ni chuma pamoja na umeme.

Nashauri Wizara kupitia Shirika la Maendeleo Nchini(NDC) lifanye kila linalowezakana kuhakikisha kwambauzalishaji wa chuma Mchuchuma na Liganga unakamilika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

kwa sababu upatikanaji wa chuma na umeme nafuuutarahisisha uwekezaji katika viwanda nchini. Pia uwepo wausafiri madhubuti wa reli na barabara na huduma borakatika bandari zetu hasa bandari ya Dar es Salaam kwanihili ni lango kuu la shughuli za kiuchumi katika ukanda waAfrika Mashariki, Kati na Kusini kutasaidia ukuaji wa sekta yaviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Viwanda naBiashara inao mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta yaviwanda vya nguo katika Ukanda wa Ziwa ambako zao lapamba linazalishwa kwa wingi. Je, Serikali ina mpango ganiwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya nguo na ukamuajiwa mafuta, kwani uongezaji thamani wa mazao yetu utaletatija kwa wakulima wetu na kuboresha maisha yao nakuchangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja yaMheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

MHE HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwakazi kubwa anayofanya katika Wizara hii muhimu lakinianaifanya peke yake bila hata kuwa na Naibu Waziri wakumsaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuoneshamalalamiko yangu juu ya kukosekana kwa soko la uhakikala zao la ufuta. Namwomba Mheshimiwa Waziri aliangaliesuala hili ili tupate soko la uhakika la zao la ufuta, wakulimawaweze kupata fedha stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu suala lakuwezesha wakulima wa chumvi kupata uwezeshaji wakupata mkopo wa mashine ya kusindika chumvi ili kuinunakipato chao. Naomba Mheshimiwa Waziri awezekuwaunganisha wakulima hao wa chumvi na SIDO ili SIDOiwapatie mashine hizo hata kwa mkopo ili tuweze kufunguakiwanda cha kusindika chumvi hivyo wakulima hao wawezekujiongezea kipato zaidi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutambua miakamichache iliyopita kulikuwa na taarifa ya uwepo wa Kiwandacha Simenti pale Mchinga. Taarifa za kiwanda hichozilikuwepo tangu wakati Jimbo la Mchinga linaongozwa naMheshimiwa Mudhihir Mohamed Mudhihir lakini hadi sasahatuna taarifa zozote kutoka katika mamlaka husika.Tunaomba kujulishwa kiwanda hiki kimefikia wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusuhatua ya viwanda vya LNG. Tunasikia kuwa kuna watuwanataka kuhujumu jambo hili, je, taarifa hizi ni kweli au la?

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu viwandavya korosho ambavyo vimebinafsishwa lakini watuwaliovichukua wanavigeuza kuwa ni maghala tu badalaya kuvitumia kwa ajili ya kuongeza thamani ya korosho kwakuzibangua. Mheshimiwa Waziri tunaomba wale wotewaliochukua viwanda vyetu vya mtama, Nachingwea,Newala na kadhalika wanyang’anywe na viwanda hivyowapewe watu ambao watavitumia kwa lengolililokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa NaibuSpika, awali ya yote namshukuru Mungu kwa kunipa uhai nanguvu za kuendelea kuwatumikia wananchi wangu waJimbo la Kyerwa. Pia namshukuru Mungu kupata nafasi yakuchangia katika Wizara hii muhimu kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee napendakumpongeza Mheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa JohnPombe Magufuli kwa moyo wake wa dhati wa kusimamiaahadi ya kufanya Tanzania kuwa ya viwanda ili kuinua uchumiwa viwanda. Nchi zilizoendelea kiuchumi ziliwekeza sanakatika uchumi wa viwanda maana hapo ndipo penyemafanikio makubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimpongezeMheshimiwa Waziri Mwijage, Katibu Mkuu na Watendaji

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

wengine kwa kusimamia kikamilifu sera ya Tanzania yaviwanda, kweli kasi inayoendelea inaonekana. Nawashauriwasikatishwe tamaa na kelele za wasioitakia mema nchi yetu.

MheshimiwaMwenyekiti, ili kuinua uchumi wa nchiyetu haraka na kuwanufaisha Watanzania wengi, nashauriWizara kuwekeza sana katika viwanda ambavyo malighafizake zinapatikana hapa nchini mfano malighafizinazotokana na mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Pia nchiyetu imejaliwa kuwa na madini mengi sana tuombe Serikalikuwavutia wawekezaji kuwekeza viwanda ambavyotutatumia madini yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe mfano Kyerwatumejaliwa madini ya tini ambayo yanapatikana maeneomengi ya Wilaya. Madini haya yamekuwa yakinufaisha nchimajirani zetu kwa njia ya magendo. Niombe Wizarakuwavutia wawekezaji kuwekeza Kyerwa kwa sababumahitaji ya mabati ni mengi na hii itainua uchumi wa nchiyetu na kuwapa ajira wananchi wangu wa Jimbo la Kyerwana Tanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, sera na mkakati wa Serikaliyetu ni kuwawezesha wananchi kwa kuwawekea mazingirarafiki wakulima wetu ili wanapolima wawe na uhakika nasoko la bidhaa zao. Wananchi wetu wanajitahidi sana kulimalakini hakuna soko la uhakika. Jimbo langu la Kyerwa likompakani, Serikali imekuwa ikikosa mapato kwa sababu yabiashara ya magendo ya kupeleka bidhaa nchi jirani kwasababu wananchi hawana sehemu ya kuuza bidhaa zao. Ilikuepuka kuikosesha Serikali mapato na kuwaondoleawananchi usumbufu na wale wanaopoteza maisha MtoKagera kwa biashara ya magendo, naiomba sana Serikalikufufua masoko ya Kimataifa yaliyojengwa Murongo naNkwenda ambayo yametelekezwa bila kukamilika na mpakasasa hatujui nini kinaendelea na nani msimamizi wa masokohaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, masoko haya yakikamilikawananchi wetu watakuwa na soko la uhakika kitu ambacho

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

kitainua kipato chao na uchumi wa nchi yetu utaongezekana tutaepusha biashara ya magendo na madharawanayoyapata. Naomba Mheshimiwa Waziri anapohitimishaawaambie Wanakyerwa nini hatma ya haya masoko.

Mheshimiwa Naibu Spika, niiombe na kuishauri Serikaliyangu tunayowavutia wawekezaji kuwekeza ufugaji naviwanda vya nyama, mfano Mkoa wa Kagera tuna mifugomingi niwaombe Wizara kuwakaribisha wawekezajiwawekeze Kyerwa kiwanda cha nyama na maziwa tunaong‘ombe wengi, mbuzi na mifugo mingine ili kuwainuawananchi wetu kimapato na uchumi wa Taifa letuutaongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili Watanzania waendeleekuwa sawa lazima tuwavutie wawekezaji maeneo yote iliisionekane maeneo fulani ndiyo tumewekeza nguvu halafumaeneo mengine yameachwa. Nasema hili kwa sababuinaonesha mfano Mkoa kama Kagera umesahaulikakiuwekezaji wakati kuna fursa nyingi na ndiyo wazalishajiwakubwa wa ndizi, uvuvi, madini, ufugaji na kadhalika.Mkoa wa Kagera tumejaliwa kila kitu na tunaweza kulimana kuvuna zaidi ya mara mbili kwa mwaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuwekezakwenye viwanda vikubwa ambavyo vinaajiri sehemu ndogoya Watanzania lakini pia tuweke kipaumbele katika kuwekamazingira wezeshi kwa viwanda vinavyoajiri watu wengikama viwanda vitakavyotumia malighafi zinazopatikanandani mfano kahawa, alizeti, pamba, korosho na kadhalika.Kwa kufanya hivyo tutainua kipato cha wananchi wetu nauchumi wa Taifa na tutapata baraka maana hapawataguswa Watanzania wengi na watanufaika sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,narudia kumpongeza Mheshimiwa Waziri hakika kazianaiweza sana tumuunge mkono Watanzania kwa umojawetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kutoa mchango wangu kwenye Wizara hii hasakwenye eneo la uwezeshaji na uwekezaji. Katika Jimbo laMlalo, Halmashauri ya Lushoto, wakulima wadogowameanzisha kilimo cha mazao ya mchaichai ambacho kinatija kubwa kwa sababu ni malighafi ya bidhaa mbalimbali.Tatizo kubwa ni udhaifu mkubwa wa Idara ya Biashara yaHalmashauri kuziona fursa za kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa soko pekeetunalolitegemea ni Kisiwani Pemba ambalo ni soko la katina siyo soko la moja kwa moja kwa mlaji. Tunaomba kwadhati, Wizara hii iwatafutie wananchi wa Mlalo masoko yamoja kwa moja ya bidhaa ghafi ya mchaichai ili wawezekukuza uchumi na kipato chao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mdau wa ndaniwananchi wa Mlalo wamethubutu kukopa mtambo wakusaga na kukamua majani ya mchaichai kuepuka adha yakusafirisha majani ghafi kwenda Pemba ambako kwa sasandiko soko la kati lilipo. Kupitia kampuni ya kukopeshamitambo ya EFICA mdau ameweza kukopa mtambo na sasawananchi wamepata hamasa kubwa ya kuchangamkiafursa hii adhimu tatizo pekee sasa ni soko la moja kwa moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Kusindika Chaicha Mponde kule Bumbuli bado ni changamoto. Wawekezajiteule wa Mfuko wa Hifadhi wa LAPF bado hawajaonyeshadhamira ya dhati ya haraka ya kufanikisha zoezi hili. Katazaidi ya 15 zinategemea chai kama zao kuu la kiuchumi, tozoza Halmashauri zinapatikana kupitia chai, tunaiomba Serikaliilione hili kwa jicho la huruma sana kuwasaidia wananchiwa Bumbuli.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha AFRITEX Tangakinachotengeneza nguo pale Tanga mjini kimefungwa kwasababu ya kodi. Tafadhali naomba tufuatilie ili kuona tatizohili ambalo limefanya ajira zaidi watu 2,000 za moja kwamoja ziwe hatarini.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda cha RHINOCEMENT kimeshusha uzalishaji baada ya kukosa malighafi zakutosha za makaa ya mawe kutoka Liganga na Mchuchuma.Napendekeza sana wapewe mrahaba kama waliopewawawekezaji wa Dangote ile waweze kupata malighafi yakutosha. Kiwanda kina uwezo wa kuzalisha saruji tani 20,000kwa mwezi lakini upatikanaji wa malighafi ni chini ya tani1,000 kwa mwezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na nia njema yaSerikali ya kuelekea uchumi wa kati unaotokana na uchumiwa viwanda, bado hatupaswi hata kidogo kupuuzamatatizo ya viwanda vilivyopo. Kiwanda cha Sabuni chaFoma, TIP Soap Industries vyote vimekufa, Tanga kunani?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kwa jitihadazake za vitendo kuhakikisha nchi yetu inakuwa ya viwanda.Napongeza kazi nzuri inayofanywa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji ya kufufua na kujenga viwanda, hukuakihamasisha wawekezaji kuingia nchini na kufanyika kwabiashara ya kiushindani kwa maendeleo ya wananchi wetu.Natoa pongezi za dhati kwa Wizara hii kwa jinsi wanavyojitoakwa maslahi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Rukwa niwakulima bora na wazalishaji kwa ziada kubwa nakuchangia chakula kwa Taifa letu. Mkoa wa Rukwa tunaviwanda vidogo vinavyoendeshwa na sekta binafsi na tangu2015 hadi sasa tuna viwanda 137 vyenye ajira ya 411 (mpya).

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wamekuwawanapata mfumuko wa bei ya unga pamoja na kuwa namahindi ya kutosha. Hivi sasa bei ya unga Mkoa wa Rukwasokoni kilo moja ni Sh.1500, kilo tano ni Sh.8,000/= na kilo 25ni Sh.37,000/=. Naomba Serikali kuwawekea mazingira borahawa wenye viwanda hivi vidogo kuzalisha kwa wingi nakupelekea kuteremsha bei ya unga. Pia mahindi yaliyomo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

ndani ya maghala ya Taifa ya miaka iliyopita yatolewe nakuuziwa wenye viwanda vya unga (sembe) kuliko kuharibika.Tunaomba wawekezaji waelekezwe Rukwa tupate ajira kwavijana wetu na kuteremsha mfumuko wa bei ndani ya sokokwa maisha ya wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wetu wengiwanakimbilia kufanya biashara mbalimbali ila hawanauelewa wa uendelevu wa biashara zao. Tatizo ni upungufuwa rasilimali watu katika maeneo yetu, Maafisa Biasharakuwa wahusika na leseni za biashara badala ya kuwainuawafanyabiashara kuwa na biashara zenye tija. NaombaSerikali kutoa ajira kwani tunao vijana waliohitimu kwenyevyuo vyetu vya CBE ili tupate wataalam wa kukidhi mahitaji,tupate wafanyabiashara watakaoendana na ushindani wakiulimwengu na wa ndani ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa ushaurikwamba kwa kuwa tunakwenda kwenye nchi ya viwanda,ni vema maeneo kama Rukwa tuhakikishe tunawaimarishiaChuo cha VETA na kuboresha Kituo cha SIDO.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Waziri waViwanda kutuangalia sisi wa mikoa ya pembezoni kwabidhaa kadhaa kuwa na bei za juu mfano sukari kilo moja niSh.2,200/=, sementi mfuko ni Sh.14,000/=. Kutokana namaeneo ya ujenzi wa viwanda yapo, tunaombakuelekezewa wawekezaji wa kujenga viwanda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. LATHIFAH H. CHANDE: Mheshimiwa Naibu Spika,ni mwaka wa pili sasa tangu Serikali ya Awamu ya Tanoijinasibu kuwa hii ni Tanzania ya viwanda. Kwanza kabisa,napenda kuzungumzia juu ya rasilimali tulizonazo. Gesi asiliailigundulika kwa mara ya kwanza katika visiwa vya SongoSongo, Mkoani Lindi mwaka 1974. Ikagunduliwa Mtwara Vijijini(Mnazi Bay mwaka 1982 na Ntorya mwaka 2012), MkurangaMkoa wa Pwani mwaka 2007 na Lindi, Kiliwani mwaka 2008.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

Mheshimiwa Naibu Spika, kiasi cha gesi asil iiliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa futiza ujazo trilioni nane. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopitakumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji mafuta na gesi asiliauliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari na kiasicha gesi asilia iliyogunduliwa katika kina kirefu cha maji nitakribani futi za ujazo trilioni 33.7. Jumla ya gesi asiliiliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafika takribani futi zaujazo trilioni 41.7. Rasilimali hii ya gesi asilia inaweza kutumikakatika maeneo mbalimbali yakiwemo kuzalisha umeme,malighafi ya kuzalisha mbolea na kemikali, nishativiwandani, majumbani na kwenye taasisi mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa Mkoa wa Lindihauna hata kiwanda kimoja cha kuzalisha mbolea zaviwandani licha ya gesi kuwepo mkoani hapo. Ni wakatisasa wa Serikali kutafuta na kuelekeza wawekezaji wakuzalisha mbolea katika Mkoa wa Lindi ukizingatia ukamilikajiwa barabara ya Masasi-Ruvuma kupitia Tunduru utafanyausafirishaji uwe rahisi wa mbolea hiyo hasa ukizingatia Mikoaya Nyanda za Juu Kusini ndiyo watumiaji wakubwa wambolea hiyo ya viwandani. Ujenzi huu wa viwanda utasaidiavijana wa Lindi ambao zaidi ya asilimia arobaini (40%)hawana ajira, jambo ambalo litapunguza kama si kuondoakabisa tatizo la ajira kwa vijana Mkoani Lindi na Kanda yaKusini kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuzungumziajuu ya usindikaji na kuongeza thamani mazao. Mkoa wa Lindiunazalisha kwa wingi mazao kama korosho, ufuta, muhogo,mbaazi na mengine mengi. Kwa sasa duniani kote faida yakilimo chochote kiko kwenye usindikaji na uongezaji thamaniya zao husika. Mkulima wa Lindi na Mtwara bado hajanufaikana anachokizalisha kwa kuwa mteja wake mkuu ni mlanguziambaye ananunua kwa mkulima na kuuza kwenye masokona makampuni makubwa kwa bei itakayompa faida.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoani Lindi kulikuwa naviwanda vya korosho ambavyo vilikuwa na mashine zakubangua korosho lakini sasa viwanda hivi havifanyi kazi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

Matokeo yake korosho zinauzwa bila kuongezwa thamanina kupelekea kupunguza kipato. Naiomba Serikali ijikitekatika kufufua viwanda hivi Mkoani Lindi na pia katikakujenga viwanda vingine hata kwa kushirikisha private sectorsili kuweza kumnufaisha mkulima, kutoa ajira kwa vijana,kudhibiti walanguzi na hatimaye kuongeza pato la Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulikuwa na viwanda vyanguo hapa nchini, vipo wapi sasa? Mitumba leo inapigwamarufuku huku Serikali haijaleta njia mbadala wa kuleta nguoza bei nafuu kuweza kukidhi mahitaji ya majority.Makubaliano ya East African Common Market ni kwambamitumba marufuku ikifika 2019. Wenzetu Rwanda wameanzakuwapa mafunzo akinamama kutengeneza nguo zagharama nafuu kwa kutumia materials zinazopatikana kwawingi. Imebaki miaka miwili tu tutapiga marufuku mitumbaya Ulaya badala yake tutanunua za bei rahisi kutoka Rwandana China. Sisi tutanufaika na nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kiwanda Morogorokinaitwa Mazava ambacho kinazalisha sport wear lakinibidhaa zote zinapelekwa Ulaya na Marekani wakati Tanzaniahakuna product yoyote sokoni. Tunahitaji kuwa na viwandavya nguo vitakavyoweza kuzalisha, kujiendesha pia wakatihuo huo nguo ziweze kuuzwa kwa bei nafuu. Tukiwa naviwanda vyetu vitakavyozalisha kwa wingi itasaidia kushushagharama za uzalishaji na bei ya kuuza itakuwa rahisi namwananchi wa kawaida ataweza kumudu.

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu Kenya wana kitukinaitwa Vision 2030. Kwenye manufacturing wana-targetkutoka kwenye kumiliki soko kwa 7% hadi kufikia 15% ambayoni zaidi ya mara mbili. Kwa maana hiyo viwandawalivyonavyo sasa wataviongeza mara mbili. Kipaumbelekimoja cha Wizara ya Viwanda na Biashara Kenya nikutengeneza skilled technical human resources.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya vituvinavyoangusha watu wetu hapa hawana uwezo wakushindana kimataifa, skill level iko chini. Kwa hiyo, hata

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

tukijenga viwanda bila kuwa na programu maalum yakunyanyua skill za watu wetu, bado effect kwenye uchumiwa viwanda itakuwa ndogo maana kazi zitakujakuchukuliwa na watu wa mataifa ya jirani ambaowameandaliwa Kenya na Rwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kushauri Serikaliijikite katika kujenga viwanda na vilevile kutayarisha vijanakwa kutengeneza skilled technical human resources iliwaweze kupata ajira katika hivi viwanda. Vilevile Serikaliiboreshe miundombinu ili kuwezesha movement ya bidhaazinazotengenezwa, maana kuongelea Tanzania ya Viwandabila kuwa na uhakika wa miundombinu ya barabara ni sawana kuongelea mwili wa binadamu bila damu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana, nami nichangie kidogo kwenye Wizarahii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Jimboni kwanguMikumi kuna kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambachokinafanya kazi nzuri sana ya uzalishaji wa sukari, lakinikumekuwa na malalamiko ya muda mrefu sana kutoka kwawafanyakazi zaidi ya 3,000 waliofukuzwa kazi bila kulipwamafao yao mwanzoni mwa mwaka 2000.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa sanaMheshimiwa Waziri atakapokuja kujumuisha afafanue ni linihawa wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi KilomberoSugar Company kabla haijabinafsishwa kwa Illovo watalipwamafao yao? Pia kumekuwa na malalamiko kutoka kwawakulima wa nje (outgrowers) ambao wamekuwawakilalamika kuhusu kupunjwa sana kwenye mzani ambaounamilikiwa na wenye kiwanda. Je ni lini Serikali itawaagizawenye kiwanda cha Illovo kuweka mzani utakaokuwa wauwazi ili kuwafanya wakulima kupata haki yao ya kujuamazao yao yanayoingizwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia wakulima wa miwa waBonde la Ruhembe wamekuwa na malalamiko ya muda

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

mrefu ya kipimo cha Sucrose (utamu) ambayo wamekuwawakipunjwa kwa kuambiwa utamu wa miwa yao ni mdogosana hivyo kulipwa fedha kidogo sana pia. Wakulima wabonde la Ruhembe wamekuwa wakiomba sana kwambapamoja na kulipwa sucrose pia walipwe na molasses nabuggers ambazo zinatumiwa na watu wa kiwanda cha Illovokutengeneza mashudu, mbolea, spirit na hata umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakulima wa Bonde laRuhembe wanalia sana bila matumaini kwa nini wanalipwautamu (sucrose) peke yake wakati mazao yao yanatoa piaproducts zingine ambazo wenye kiwanda cha Illovowanazitumia na kuuza bila kuwalipa tofauti na nchi za jiranikama Kenya na Malawi ambako wakulima wanalipwa piafedha za bugger na molasses na kuwasaidia sana kufaidikazaidi na kilimo hicho cha miwa na kuwaongezea zaidi uchumiwao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana MheshimiwaWaziri, atakapokuja ku-wind up atuambie ni kwa nini Serikalihaiwaagizi wamiliki wa viwanda kwanza kuwalipawakulima wa miwa bei nzuri za Bugger na molasses?Sambamba na hilo kwa nini bado bei ya tani ya miwa kutokakwa wakulima wa nje bado inasuasua?

Mheshimiwa Naibu Spika, tuliambiwa kuwa pale Kijijicha Mufilisi kingejengwa kiwanda kingine kidogo cha Sukariifikapo mwaka huu wa 2017, lakini mpaka sasa hakuna daliliyoyote ya kujengwa kwa kiwanda hicho cha sukari paleMufilisi ambacho kingesaidia sana kuleta ajira na piakurahisisha usafirishaji wa miwa kutoka Kata za Mikumi naKisanga. Je mpango huo wa kiwanda cha sukari cha Mufilisikimefikia wapi na ni lini kitakamilika na kuanza kazi? Au ndiyoyale yale ya kwenye utaratibu bila kutekelezeka?

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa kwenyeJimbo la Mikumi Kata za Malolo, Masanga, Mhenda,Mabuerebuere, Kilangali na Tindiga kuna mazao ya ainambalimbali tena kwa wingi sana, nadhani sasa Serikali iliiweze kufikia malengo yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

ya viwanda basi ingeangalia sana umuhimu wa kujengaviwanda vidogo vidogo kwenye Jimbo la Mikumi, ambayopia vingeenda sambamba na kuhakikisha umeme unafikakwenye kata hizi za Jimbo la Mikumi na Wilaya ya Kilosa kwaujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika kurekebishamiundombinu ya barabara, naamini kabisa kil imokinacholimwa Jimboni Mikumi kitasaidia sana kufanikishakutoa ajira kwa wananchi wengi zaidi; pia kufikia malengoya Serikali hii ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,lakini vile vile kufanikisha kuufanya Mkoa wa Morogoro kuwaghala la Taifa. Tumebakiwa na ardhi nzuri, kubwa na yenyerutuba na Wanamorogoro wapo tayari kulima kwa bidii; chamsingi ni kuwawekea viwanda ili wapate uhakika wamasoko ya mazao yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Naibu Spika,ubadhirifu wa shamba zaidi ya heka 1000 kwa ajili yauwekezaji katika Kata ya Kakese, Manispaa ya MpandaMkoani Katavi. Shamba hili la kulima mpunga lipo katikaKata ya Kakese, Kijiji cha Mbungani na linamilikiwa na CharlesDofu na Lucas Busanda. Lilimilikiwa 1985, mwaka 1987walianza kilimo cha biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la kuchukua eneo hiliilikuwa ni kwa ajili ya uwekezaji ambapo awali lilikuwa lawananchi. Wawekezaji hawa wanachukua mikopo benki nakuilipa kwa kuwachangisha wananchi, wanajipatia fedhakwa kupitia kundi kubwa la zaidi ya wananchi 5000.

Mheshimiwa Naibu Spika, je ni kwa nini Serikaliimemuacha mwekezaji huyu fake kuendelea kuwalaghaiwananchi na kujipatia mikopo mikubwa ikiwepo NBC nawanaposhindwa kulipa mkopo wanataka wananchi walipemkopo huo?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wanalipishwagharama kubwa wanapokodi mashamba. Kwa hekawanakodishwa kwa zaidi ya Sh.500,000/= kwa sababu nieneo lenye udongo mzuri. Wananchi wanapiga keleleshamba lirudi kwa wananchi na Serikali ya Kijiji ili walime kwabei ya chini na hivyo wajikwamue kiuchumi. Wananchi hawawanatishia kuchoma moto shamba hili ambalo lina zaidi yawakazi 8000. Hatua ya dharura inahitajika kuchukuliwa ilikuvunja Mkataba wa kujipatia maeneo kupitia kuwalaghaiwananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wanatakakuandamana mpaka kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu na Wazirihusika; kuna hali ya tafrani katika eneo hili. Ili kunusuru vuruguzisitokee naomba Serikali itatue huu mgogoro mkubwakatika Kata hii ya Kakese. Serikali imekuwa ikitatua kero nyingikatika nchi hii kwa maslahi ya Taifa na amani; miminimewazuia wananchi kuja Dodoma kwa maandamanonikiamini kwamba Serikali italifanyia kazi tatizo hili kwaharaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi walifunguliwakesi na hawa wamiliki wakatumia rushwa kuhonga polisi.Wananchi wakapigwa ili kuondoka ilihali lilipatikana kutokakwa wananchi. Je hamuoni kwamba Serikali inaibiwa kupitiawawekezaji hawa wahuni kwa umma? Tunahitaji majibukuhusu shamba hili; lirudi kwa wananchi, hali ni mbaya, nimwizi huyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile niipongeze hatuaya Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kutoa mwelekeo wa bajetimbadala kwa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hii ya CCM hainamapenzi mema na wananchi wake katika kuwasaidia vijanakupata ajira kupitia viwanda vidogo vidogo. Tuna wimbikubwa la vijana waliokosa kazi vijijini kwa takwimu hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Uanzishwaji wa Mradi waViwanda Vidogo Vidogo Vijijini 2016/2017. Serikali imeanzisha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

viwanda vipya 161 vidogo viji j ini Tanzania nzima nakufanikiwa kuajiri vijana 1,098. Ajira hizi ni chache ukizingatiavijana wengi wako vijijini na hawana elimu. Tulitegemeavijana hawa wangewekewa mkakati wa kuwapatia ajirana si kuwadidimiza kiuchumi vijana wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuboresha mazingira yauwekezaji ni jukumu la Serikali ili kuhakikisha sheria kanuni nautendaji wa sekta ya umma unakuwa rafiki kwa wawekezajii l i kutoa ajira, kuwalipa vijana kwa wakati, kuachaunyanyasaji kwa vijana wanaofanya kazi migodini katikaTanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mgodi wa Isulamilomo(Nsimbo Katavi), kuna mwekezaji mchimbaji yuko pale nahana leseni; amepora eneo kubwa na vijana wamebakihawana maeneo. Huyu bwana (Mbogo) Simon Mdandilaanazua tafrani na uvunjifu wa amani kwa kuwanyima fursavijana kupitia kujiajiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, vijana zaidi ya 450wanashindwa kuchimba katika maeneo yao kwa rushwailiyofanywa na huyu bwana Mbogo. Je Serikali ina mkakatigani wa kuhakikisha inawazuia wawekezaji wa aina hiiwanaotumia rushwa kuhodhi maeneo katika eneo lauchimbaji na huku vijana wakihangaika kupata ajira?Uwekezaji huu wa aina hii wenye lengo la kuwatesawananchi pamoja na hali ngumu waliyo nayo usimamiweipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ubadhirifu wa Kiwanda chaKukoboa na Kusaga. Mashine hii ilinunuliwa na Halmashauriikayeyuka, ilikuwa na thamani ya milioni mia moja lakini leohii wananchi wakihoji hawapati majibu ya wizi huu wa wazikabisa. Je Serikali hii kwa kuendelea kuwalea weziwanaokula fedha za viwanda vya uwekezaji katika Manispaaya Mpanda kwa kutochukua hatua yoyote hamuoni kwambamnapoteza fursa za vijana kwa kuwalea wabadhirifu hawabila kuwachukulia hatua?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Mheshimiwa Naibu Spika, uchumi wa viwandauendane sambamba na ukuaji wa sekta ya nishati naumeme. Je ni mkakati gani wa haraka wa kuuhakikishiauchumi wa viwanda upatikanaji wa umeme unaoendasambamba na mazingira ya uwekezaji sawia nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya CCM badohaijajipanga pia kujiendeleza kiuchumi kupitia viwanda.Bajeti yenye asilimia 0.36 ya pato hili, je, Wizara hii imejipangakweli kuwasaidia wananchi au utani?

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS:Mheshimiwa Naibu Spika,namshukuru Allah Subhanahu Wataala kwa neema ya uhaina afya njema. Nikushukuru wewe pia kwa nafasi hii muhimusana kwangu ili nitoe mchango wangu ingawa kwa ufupikatika Wizara hii muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze na bidhaabandia. Pamoja na kwamba Serikali kupitia (TBS) imewekaprogram ya kudhibiti bidhaa bandia kutoka nje ya nchi lakinikinyume chake bidhaa bandia zinazagaa kila sehemu yanchi yetu, wakati mamlaka ya udhibiti (TBS) wapo na jambohili wanalijua na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa.Jambo hili la bidhaa bandia linaweza kuleta madharamakubwa katika nchi na kwa wananchi wenyewe kwaujumla. Pamoja na kuzorotesha bidhaa za ndani ya nchi lakinipia wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu juu ya jambohili ni kwamba, kwa sababu (TBS) wanashughulikia bidhaabandia, na kwa kuwa (TBS) hawana uwezo wa kushughulikiabidhaa bandia na kwa kuwa (TBS) hawana uwezo wakushughulikia na bidhaa fake na kwa sababu (TFDA) pamojana mambo mengine inajishughulisha na dawa zilizokuwachini ya kiwango na kwa sababu (FCC) inashughulika nabidhaa fake, kwa mantiki hiyo ni bora taasisi hizi kufanya kazikwa pamoja ili kuleta ufanisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la ngozi.Tanzania tuna ng’ombe million 21.3; mbuzi millioni 1.5; na

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

tunao kondoo millioni 6.4. Pamoja na kuwa na mifugo mingikiasi hiki jambo la ajabu Tanzania tunasafirisha ngozi ghafikatika kiwango ambacho hakiendani na rasilimali tuliyonayoukilinganisha na Kenya ambayo inasafirisha ngozi ghafi nyingikuliko Tanzania. Pia Sekta ya ngozi haitengenezi ajira walahaiongezi pato la Taifa kwa hiyo inachangia pato kidogosana la Taifa. Pamoja na juhudi za Serikali za mara kwa maraza kuongeza kodi mpaka kufikia asilimia 90 ili kuzuiausafirishaji wa ngozi ghafi nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, mpango huuhaujasaidia kwa sababu bado ngozi zinasafirishwa kwamagendo hivyo kukosesha mapato ya Serikali kutokana nakodi iliyowekwa. Pia hata ngozi ingebaki ndani ya nchizingeoza kwa sababu hakuna viwanda vya ku-process ngoziwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali iwekemkakati wa makusudi wa kuokoa sekta hii ya ngozi. Kama sihivyo basi wingi wa mifugo tulionao hautasaidia vemauchumi wa nchi yetu. Tutabaki na changamoto zile zile zasiku zote kati ya wakulima na wafugaji kugombania malisho.Naomba tuwe makini kuhusu hili.

MHE. ELIAS J. KWANDIKWA: Mheshimiwa Naibu Spika,nianze kwa kuunga mkono hoja. Bidhaa zinazoingizwa bilakukidhi viwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kushauri kuwavifaa vinavyokamatwa kutoka nchi za nje kama mabatiambayo tatizo lake ni Specfication, yaani geji isiyokuwa sahihibadala ya kuviharibu vitiwe chapa ya bei kulingana na haliyake halisi ili vitumike kwa shughuli nyingine kama kujengeamabanda ya mifugo kuwekea fensi pia ujenzi wa nyumbaza muda mfupi. Kuviharibu ni kupunguza level ya uchumi navina impact kwenye GDP kwani kuna fedha zimetumika tokakwa wazawa (domestic).

Mheshimiwa Naibu Spika, bei za bidhaa kuwa juu(bidhaa za viwanda vyetu). Wizara hii ishirikiane na Wizara

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

ya Fedha kulinda bei ya bidhaa inayotengenezwa ndani;kuweka VAT kwenye bidhaa inayoanza kuzalishwa nchini nakupandisha bidhaa hiyo kwa walaji wa ndani kwa kuwainamvutia mzalishaji kuuza nje ya nchi kwa ajili ya zero ratedconcept ya export zote. Pia kupoteza ushindani kwa bidhaainayozalishwa au kuingizwa kutoka nje hususani nje kwenyeupatikanaji wa material ya bei rahisi, technology ya hali yajuu na sera zao juu ya exports zao. Nashauri VAT itazamwevizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya pembejeo.Nashauri Wizara iweke mkazo sana kwenye viwandavitakavyozalisha pembejeo, yaani mbolea, madawapamoja na vifaa vya kilimo. Pia maduka ya vifaa vya kilimoyawekwe maeneo ya wakulima sambamba na mafunzo kwawananchi ili wajue au wapate elimu ya umuhimu wa kutumiavifaa vya kisasa kuwawezesha kuwa na kilimo chenye Tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho naunga mkonohoja kwa asilimia mia moja.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri yakutekeleza adhma ya Serikali ya viwanda. Ombi, Mkoa waKagera tunasahaulika kwenye vipaumbele vya flagshipprojects hususan uanzishwaji wa viwanda vinavyoendanana comperative advantage za mkoa husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba MheshimiwaWaziri, wakati ana-wind up atueleze Wanakagera ni liniSerikali itasukuma uwekezaji wa kiwanda cha kusindika nyamaili kusaidia kutunza uchumi wa mkoa kwa kuwa unaongozakwa wingi na ufugaji ng’ombe nchini. Kufanya hivi kutasaidiakutatua migogoro ya wakulima na wafugajiinayosababishwa na ng‘ombe wengi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara itusaidie vijana waKagera hususani Wilaya ya Karagwe waweze kuwafikiria naSIDO‘s SME guarantee scheme.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru MheshimiwaWaziri kwa kunisikiliza.

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa NaibuSpika, nianze kuunga hoja mkono. Tanzania ni nchi yenyerasilimali nyingi ambapo kama zitatumiwa vizuri katikaviwanda vyetu zitaleta manufaa makubwa sana katikaTanzania yetu. Hata hivyo, changamoto kubwa inayovikabiliviwanda nchini ni ukosefu wa mitaji, teknolojia, umeme,malighafi zisizokuwa za uhakika pamoja na ukosefu wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na changamotonil iozitaja hapo juu bado hakuna vivutio vizuri kwawawekezaji kutoka nchi za nje na mlolongo wa kodi nyingiambazo zinawavunja moyo wawekezaji wa ndani na nje.Ningeshauri Serikali kwa changamoto ambazo nimezitajahapo hasa za ukosefu wa umeme, teknolojia na maji ni vemasasa Wizara ya Viwanda ikakaa pamoja na kuwa namikakati ya pamoja na Wizara ya Nishati, Kilimo na Maji ilikuunganisha nguvu kwa pamoja na kuwa na mkakatimmoja kwa kuwa Wizara nil izozitaja hapo juu zinamahusiano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mlolongo wa kodini vema sasa Serikali ikawa na chombo kimoja ambachokitakuwa na mamlaka ya kutoza kodi ambacho kitasimamiautozaji wa kodi zote kwa wawekezaji. Mkoa wa Singida nimkoa unaosifika kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nabiashara. Mazao ya biashara ni alizeti, vitunguu, pamba,ufuta, karanga na choroko. Mazao ya chakula ni mahindi,mtama, viazi vitamu na uwele, lakini bado hakuna viwandavya kutosha. Pia Singida ni wafugaji wa ng’ombe, mbuzi nakondoo. Mazao yote niliyotaja hapo juu yangeweza kuwamalighafi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika viwanda mbalimbaliambavyo vingeanzishwa Mkoa wa Singida. Mkoa wa Singidani maarufu kwa ukulima wa alizeti, alizeti inayozalishwaSingida ni maarufu Afrika Mashariki na Kati. Singida ina jumla

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

ya viwanda 126 vya alizeti, kikubwa kimoja, vitatu vya katina vidogo vidogo 122. Hivi vidogo vidogo vinategemeamitaji kutoka SIDO.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningeishauri Serikali yangukuona uwezekano wa kuwaongezea uwezo SIDO, ili wawezekuwakopesha viwanda vidogo vidogo mitaji ya kutosha.Kwa sasa SIDO inakopesha shilingi milioni sita. Iwapoitaongezewa uwezo angalu kuwakopesha wajasiriamali waviwanda vidogo vodogo milioni ishirini itakuwa ni jambojema sana. Kwani wajasiriamali wadogo wadogo hawanauwezo wa kwenda kukopa kwenye benki na taasisimbalimbali za fedha kwa kuwa wanatoza riba kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambaloningeomba Wizara hii kuuangalia Mkoa wa Singida kwa jichola pekee kwa sababu kila Wilaya/Halmashauri tayari kunamaeneo kwa ajili ya kuanzisha viwanda, kinachokosekanani mitaji, hivyo iwapo Serikali itapata mitaji itasaidia sanakuweka miundombinu ya viwanda kwa kuwa malighafi siza kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Waziriwa Viwanda Mheshimiwa Mwaijage kwa kazi nzurianayoifanya katika kuleta mageuzi katika viwanda yeyepamoja na timu yake, nawatia moyo waendelee kukaza butikazi ni nzuri na yenye tija.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,natoa pongezi kwa hotuba nzuri yenye kusheheni mambomazuri na taarifa kwa umma. MUVI, imefanya wilaya namikoa saba tu hivyo basi ni muhimu kuongeza wilaya nyinginena hasa Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Mpanda katikaHalmashauri ya Nsimbo.

Mheshimiwa Naibu Spika, NEDF. Mfuko huu badohaujasaidia wajasiriamali kwa kuwa bajeti ni ndogo hivyoSerikali itoe kipaumbele kwa kuongeza mtaji ili wananchiwakope.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

Mheshimiwa Naibu Spika, Maafisa Biashara katikaHalmashauri. Bado hatujaona jinsi Maafisa Biashara katikaHalmashauri wanavyotumika kuendeleza kazi za Wizarakatika Halmashauri zetu, hivyo basi Sekretarieti ya Mkoa inafaakupewa majukumu ya kuendeleza masuala ya viwandakatika mkoa.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaaliaafya njema na kuweza kuchangia bajeti ya Wizara hii.Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja hatua ya KambiRasmi ya Upinzani. Tanga ulikuwa ni mji wa viwanda nabiashara pamoja na kilimo cha zao la mkonge (palikuwepomashamba 72).

Mheshimiwa Naibu Spika, Viwanda vya Zamani.Tanga ina bandari na reli ambavyo viliweza kusafirishabidhaa zinazozalishwa viwandani, wakati ule katika miakaya 1970 -1990 ambapo pia ajira zilipatikana kwa wingi.Viwanda vingi vimelenga kwa ama kubinafsishwa nakupewa (kuuziwa) watu wasio na uwezo wa kuendesha ainaza viwanda hivyo. Mfano Tanga, Steel Rolling Mill (chuma)kimekufa, hali ya kuwa chuma bado kinahitajika na kina sokokubwa katika ujenzi wa madaraja, nyumba, mabodi yamagari na bidhaa nyingine za chuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha KambaNgomeni Tanga kilikuwa kikizalisha kamba zitokanazo na zaola katani ambazo kwa sasa, mkonge umepata soko kubwakatika Soko la Dunia na kwamba bidhaa zitokanazo nakatani zinahitajika sana kwa matumizi mbalimbali. Zana/bidhaa za mkonge zina soko na mahitaji yake ni ndani nanje ya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni mategemeo yangu kuwakutokana na soko kuwa kubwa Serikali itawekeza upya aukutafuta wawekezaji makini na wenye uwezo wa kuendeshaviwanda vya korona na viwanda vya kamba kwa lengo lakutoa ajira kwa Watanzania, lakini pia kuiwezesha Serikalikupata kodi na kuongeza mapato ya nchi yetu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanga kulikuwa na viwandavya sabuni kama Foma, Mbuni, Gardenia, mafuta ya nazi(nocolin) na kadhalika. Viwanda vyote nilivyovitaja vimekufakatika zoezi la ubinafsishaji mbovu lakini pia ukosekanaji waumeme wa uhakika; vile vile kodi kubwa zilizopo. Hivyonadhani kwa sababu nilizozitaja nimeeleweka. Ushauriwangu; viwanda vyote vilivyokufa au vilivyoshindwakuendeshwa na wawekezaji wanavyovimiliki, vifufuliwe kwakupewa wawekezaji wapya lakini pia Serikali ihakikishekunapatikana yafuatayo:-

(i) Umeme wa uhakika na bei nafuu;

(ii) Mfumo wa kodi uwe rafiki kwa wawekezaji(VAT/CUSTOMs DUTY);

(iii) Vivutio vya kibiashara (Tax Holiday et cetera);na

(iv) Sheria ziwe rafiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, Viwanda Vipya vya Nyamana Ngozi. Tanzania ni nchi ya tatu Afrika kwa kuwa na mifugomingi lakini nchi yetu haipati/haifaidiki na mifugo hiyoukilinganisha na nchi kama Ethiopia na Botswana. Vile vilemifugo (ng‘ombe) hutoa maziwa ambayo pia tunashindwakuyasindika na kusimamia na hatimaye tunaagiza nyama zakopo (beaf tin) na maziwa ya kopo ya Lactogen, NIDO, NAN,Kerrygold, kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ethiopia imepata USDmilioni 186 (2016) kwa mazao ya ngozi na inatarajia kuongezaUS $ milioni 90 (2017) na kufikia USD 276 (2017). Je Tanzaniainapata USD ngapi kwa 2015 – 2020? Zaidi ni migogoro yawakulima na wafugaji, Maafisa Wanyamapori kuwapiga risasing’ombe na wafugaji na kashfa ile na kusababisha Mawazirikujiuzulu.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili (scandal) yaWizara ya Maliasili na Utalii ilisababisha baadhi ya Mawaziri

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

kujiuzulu. Ushauri wangu, (Serikali itafute wawekezajiwakubwa kuboresha sekta ya mifugo ili viwanda vya nyamana ngozi vijengwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya kusindikamboga/matunda. Tanzania imejaaliwa na Mwenyezi Mungukatika mikoa na kanda aina mbalimbali za matunda namboga mboga. Pia Tanzania inayo mito na maziwa yenyemaji ya kutosha na kama tukifanya Irrigation scheme for fruitsand vegetables tunaweza kupata mapato kwa wananchi(kujiajiri wenyewe). Serikali za mitaa zitapata mapato naSerikali kuu pia itapata mapato kutokana na kodi baada yakulifanyia kazi kikamilifu eneo hili la kilimo cha matunda namboga mboga.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mazao ya Matunda naMboga Mboga Katika Mkoa wa Tanga. Mkoa wa Tanga unazowilaya nane (8) na kati ya hizi zipo ambazo ni wazalishajiwakubwa wa mazao husika na wilaya hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muheza ni Wilayainayozalisha matunda aina ya machungwa, machenza,madalanzi, malimao, mashuza, mafenesi na mapera,ambayo ikiwa Serikali itatafuta wawekezaji wa viwanda vyakusindika matunda ajira na mapato yatapatikana. Lushoto,ni wazalishaji wakubwa wa aina zote za mbogamboga namatunda (nyanya, vitunguu maji/saumu, cabages, spinaches,matango pamoja na pilipili hoho. Aina zote hizi zina sokokubwa katika Soko la Dunia (Europe na America) Serikali iletewawekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda bila umeme nisawa na gari bila mafuta. Umeme ndio Enquire kuu zaviwanda, bila ya umeme wa uhakika, wataalam waliobobeana wenye weledi na uzalendo hata tujenge viwanda vingikama utitiri baada ya muda vyote vitakufa tena. Ushauri,Serikali inahitajika kuhakikisha kwamba umeme wa uhakikaunapatikana, mifumo ya kodi iwe rafiki na tuondoe urasimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasilisha.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia Wizara hii muhimu ya Viwanda, Biasharana Uwekezaji. Nimefuatilia sana taarifa ya Mheshimiwa Waziriwa Viwanda, Biashara na Uwekezaji lakini katika hotuba yakehakuzungumza mkakati wa kufufua viwanda vilivyokufa.

Mheshimiwa Naibu Spika, wazo la Tanzania yaViwanda lilikuwepo na Mwalimu Nyerere miaka 1967 alikuwana vision hiyo na ali-implement wakati ule kwa kuhakikishaviwanda vingi vinaanzishwa katika mikoa mbalimbaliukiwemo mkoa wa Morogoro. Mkoa wa Morogoro pekeeulikuwa na viwanda zaidi ya 40, lakini hivi sasa viwanda vingivimekufa vikiwemo viwanda vya Canvas, Komoa, AsanteMoprocco, Ceramic Tanzania, Leather Shoe, Unnats nakadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa aje na majibu, upi mkakati wa Serikaliwa kufufua viwanda vya Mkoa wa Morogoro ambavyovilikuwa vikitoa ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro?

Mheshimiwa Naibu Spika, ubinafsishaji wa viwandaulikuwa na lengo la kuongeza ufanisi wa uzalishaji na si kuuaviwanda. Sasa kwa nini uwekezaji umetumika kuongeza tijakwa mwekezaji na kuua ajira? Wawekezaji kwa masikitikomakubwa wametumia viwanda hivi kama Collateralkuchukua mikopo mikubwa katika mabenki badala yakuendeleza kwenye biashara za malori, mabasi na kuuaviwanda hii sio sawa. Tunataka kuona Serikali inachukuahatua mahsusi kwa wawekezaji hao kwa makusudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nyumba za Serikalizilizonunuliwa na wawekezaji hata baada ya kuua viwandakwa nini wawekezaji hawa wasirudishe nyumba hizozikatumika kwa wafanyakazi wa Serikali? Hawalipi kodihawalipi pango, huku wameua viwanda; ni kwa nini Serikaliisichukue nyumba hizi zikatumika kwa maofisa wa Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, biashara ya Mwendo KasiJiji la Dar es Salaam, ni kama imekuwa monopolized na watu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

wachache. Kabla ya mwendo kasi wapo wamiliki wa mabasiya daladala ambao walikuwa wakifanya biashara tena kwamkopo na wengine wakijifunga mkanda kuuza nyumba, malina kuingia kwenye biashara ya daladala. Serikali imekuja nampango wa mabasi yaendayo kasi; kwa nini wasiwape fursawafanyabiashara wa daladala nao kama wana uwezowawekeze katika mabasi hayo?

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa mabasi ya mwendokasi ambayo yalikuwa yanatoa huduma kwenye njia pekeesasa hivi yanafanya biashara kwenye njia ambazo si maalum;wa mfano Mbezi Louis, Muhimbili; hali hii inawawekapembezoni wafanyabiashara wanyonge wa daladalaambao nao wangeweza kupata fursa hizo kama wazawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tafsiri ya viwanda sasaitekelezwe kwa vitendo ambapo tunatarajia kuona Serikaliinafanya kazi kwa pamoja na Wizara nyingine mtambukakama vile Wizara ya Kilimo na Mifugo, Nishati na Madinipamoja naWizara ya Maji na Umwagiliaji. Hakuna viwandabila uhakika wa umeme na malighafi.

MHE. HAMAD SALIM MAALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba nianze mchango wangu kwa kumshukuruAllah kwa kunijaalia afya njema na kuweza kutoa mchangowangu katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.Nchi yetu ni nchi ya kilimo ambapo wakulima huzalishamatunda kama maembe, machungwa, mananasi namengineyo. Kwa vile tumekusudia kujenga Tanzania yaViwanda kwa nini basi mazao kama hayo ambayonimeyataja hapo juu ambayo huzalishwa kwa msimutunashindwa kuyatengenezea viwanda na kuyasindika kwamatumizi ya baadaye?

Mheshimiwa Naibu Spika, matunda hayo kamayangesarifiwa nina imani kwamba nchi yetu ingeweza kuuzanje ya nchi na kupata fedha za kigeni na hivyo kupelekeakuongeza uchumi wetu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kweli tunatakaTanzania ya Viwanda ni vema tukaangalia kwa kina ninikilisababisha viwanda vyetu vingi vimekufa, tena vileambavyo malighafi zake zinapatikana ndani ya nchi yetu.Kama tatizo ni wataalam basi kabla ya kuanzisha ufufuajiwa viwanda hivyo, basi vijana wapewe taalumainayolingana na viwanda hivyo; lakini lakini tatizo ni uongozimbovu basi ni vema kukawa na usimamizi wa hali ya juu auwa mara kwa mara ili kugundua hizo kasoro zinazopelekeaviwanda kufa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania yetu ya leotunazalisha mpira kwa wingi lakini General Tyre imekufa natunaagiza mipira kutoka nje ya nchi. Pia tunazalisha ngozikwa wingi lakini tunashindwa kuzalisha viatu, mabegi na hatamikanda, vitu vyote hivi tunaagiza kutoka nje ya nchi. Hivikweli kwa msingi huo tuna lengo thabiti la kuwa na Tanzaniaya Viwanda?

Mheshimiwa Naibu Spika, masikitiko yangu makubwani kushindwa hata kuanzisha viwanda vidogo vidogoambavyo vingeweza kusaidia kutoa ajira ndogo ndogo kwavijana wetu. Leo Tanzania ni nchi ya tatu katika Afrika kwaufugaji lakini tunaagiza maziwa kutoka nje. Pia maembeyanazalishwa kwa wingi Zanzibar lakini yanasafirishwa katikanchi za kiarabu tena huuziwa hapa nchini kwa fedha zetuza Tanzania. Hili linalikosesha mapato mengi Taifa letu.

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa NaibuSpika, Kiwanda cha Korosho Masasi kina mwekezajialiyepaswa kukifufua, lakini kimegeuzwa ghala la korosho;tafadhali tunaomba majibu juu ya hoja hii. MheshimiwaWaziri mfumo uliopo sasa hauwezi kuwafanya wajasiriamaliwenye viwanda vidogo vya ubanguaji kupata malighafi,wasiliana na Mheshimiwa Waziri wa Kilimo ili kuchocheaukuaji wa viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kusini kuna malighafi ya juisi(mabibo na maembe mengi) mpango wa Serikali ni upikatika uwekezaji?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja. Ahsante sana.

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI: MheshimiwaNaibu Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwajuhudi zake za kuiendeleza nchi katika sera ya Viwandailiyowekwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufulikwa kutekeleza kwa vitendo, kwa kweli viwanda ni kitumuhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Nakupongeza sanaMheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuomba sanaSerikali yangu ya CCM kujaribu kulimaliza tatizo la Ligangana Mchuchuma kwa kuwalipa fidia wale wananchi waLudewa na kuendeleza yale machimbo na kumtafutamwekezaji mwenye uwezo kwani ni muda mrefu sasa tokatuseme kuna mwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ni upatikanajiwa vibali vya uwekezaji wa haraka kwani TIC kuna urasimusana na hivyo kupeleka wawekezaji kuondoka na kufanyauwekezaji kwenda na mwendo wa kusuasua, hivyotutachelewa kufikia malengo ambayo tumejiwekea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa haya machache,naunga mkono hoja.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza kabisa nimpongeze Waziri wa Viwanda naBiashara pamoja na timu yake yote kwa ujumla kwa hotubayake nzuri inayoonesha matumaini makubwa na zana nzimaya Tanzania ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama inavyofahamika kuwaWilaya ya Lushoto ni ya Wakulima wa matunda nambogamboga, na ndiyo biashara inayoipatia Halmashaurimapato makubwa. Pamoja na hayo asilimia kubwa yamatunda yale na mbogamboga vinaoza kwa kukosa soko.Kwa hiyo, niombe pamoja na kuishauri Serikali yangu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

iwakumbuke wakulima wa Lushoto kwa kuwawekeakiwanda angalau hata kimoja tu ili mazao ya wakulimayasiharibike.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama inavyofahamikaTanga ni Mkoa wa Viwanda lakini viwanda vilivyokuwa Mkoawa Tanga vyote vimekufa, mfano kiwanda cha nondo,kiwanda cha sabuni, kiwanda cha nguo, kiwanda chakatani, kiwanda cha Mkumbara, kiwanda cha mbolea,kiwanda cha chai cha Mponde kimefungwa mpaka leo.Wakulima wa chai wanapata tabu hawajui hatma yakiwanda kile na maisha yao yamekuwa ya tabu mno naukizingatia kiwanda kile hakina tatizo lolote.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara ya mwisho Wazirialisema kiwanda cha chai Mponde ameshakikabidhi kwenyeMfuko wa Jamii (LAPF), lakini mpaka sasa Mfuko huu wa Jamiihaujaonekana na wala hawajaonesha nia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba MheshimiwaWaziri, uwafuatilie watu hao then utupe majibu ya kuaminikawawekezaji hawa watakwenda kufungua kiwanda kile.Pamoja na majibu hayo utakayoyatoa pia tungeombaukayatoe wewe mwenyewe kwa wakulima wale kwaniimefika hatua hawatuamini kabisa sisi viongozi wao. Msemakweli ni mpenzi wa Mungu kiwanda kile mpaka sasa kinamiaka minne sasa hakuna muafaka, leo tusipopata majibuya kuridhisha tutashika shilingi juu ya hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja. Mwisho kabisa nimwombe MheshimiwaWaziri, aikumbuke Tanga na aikumbuke Wilaya ya Lushoto.

MHE. ABDALLAH HAJI ALI: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu muumba wamambo yote. Pili, nakushukuru wewe binafsi kwa ujasiri wakowa kuliongoza Bunge kwa umahiri mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchangia katikaWizara hii angalau kwa uchache kati ya mengi ya Wizara hii

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

ya Biashara na Viwanda. Viwanda ni kichocheo chamaendeleo katika kila Taifa duniani, viwanda ni mkomboziwa wananchi kupitia ajira na kuimarisha biashara na ustawiwa hali za wananchi kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, uwepo na uimarishaji waviwanda katika nchi na duniani kote unapitia hali au hatuambalimbali, uamuzi wa nchi yetu kuja na mkakati wa kujengaviwanda ni wa busara sana ila kabla ya kufikia huko kwanzakuna hizi hali mbalimbali mpaka kufikia uchumi wa viwanda,lazima zitekelezwe ili manufaa tunayoyafikiria yawezekupatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vinahitajiwataalam na injinia mbalimbali ili waweze kuviendesha kwauzalishaji, hivyo naishauri Serikali kujipanga na wataalamwazawa na wazalendo kwa kuwasomesha vijana wakutosha ili viwanda tuviendeleze viwe na wafanyakaziwazawa na wataalam wazawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ambalo naishauriSerikali ikubali kutenga fedha kiasi cha kutosha ili kutoa nguvukubwa juu ya kupata elimu kwa wataalam watarajiwa,ambao watafanya kazi katika viwanda hivyo. Lakini jambola kusikitisha ni bajeti ndogo itengewayo Wizara ya Elimu ilikusimamia mafunzo na elimu ya kuzalisha wataalam, hivyotumekuwa hatufikii lengo kutokana na bajeti ndogoitolewayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uchumi tunaouendeani wazi kwamba tunahitaji mafundi mchundo wa kutosha ilikukidhi haja ya viwanda vyetu vinginevyo kama Serikalihaikutilia mkazo jambo la elimu tutakuwa siku zote wa kuajiriwataalam toka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, India ni nchi inayoendeleakama Tanzania lakini sitaki kusema kwamba tuko sawa naIndia lakini India imelipa uzito mkubwa suala la elimu kiasikwamba India wanatenga zaidi ya asilimia 10 ya bajeti yanchi yao kwa upande wa elimu, sisi Tanzania bado tuko

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

nyuma si zaidi ya asilimia 4.5, hivyo India imefanikiwa kuzalishawasomi na wataalam wengi sana wametosha India nawanauza wataalam duniani kote. Mfano, katika kampunikubwa kama Microsoft ya Bill Gates takwimu zinaonesha zaidiya wafanyakazi mabingwa asilimia 10 ni kutoka India. PiaMadaktari Bingwa wengi walioko Marekani na duniani koteni Wahindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, siri ya mafanikio hayo nimkakati wa makusudi wa kuwekeza katika elimu. Kwa halihii ni lazima na sisi tusiwe nyuma kwa kuiweka elimu kuwa nikitu cha chini, huwezi kuendelea katika nyanja yoyote dunianibila elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri tena Serikali itiliemaanani juu ya elimu katika nyanja zote hasa katika sualazima la utafiti, jambo ambalo halionekani kupewa nafasikubwa wakati inafahamika wazi kwamba bila utafiti huwezikuleta ufanisi wowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali itakuwa tayarikuiwezesha elimu na sisi tutazalisha wataalam wengi kwaajili ya viwanda vyetu na ziada tunaweza kuuza nje,vinginevyo kama hatukuwa makini kwa uwekezaji juu yaelimu baada ya kuzalisha wataalam tutakuwa tukizalishawatumishi tu.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,Napenda kuunga mkono hoja mapendekezo ya hotuba yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, aseme ni lini ataenda Jimbola Mlimba katika Kata ya Namwawala, Kata ya Mofu, Vijijivya Idandu na Miyomboni ili kuweka utaratibu wa ujenzi nakilimo cha miwa ya sukari na wananchi waweze kunufaikaili kuwaondolea tabu wanazoendelea na kupata miakamingi sasa bila kuwa na uongozi wa Serikali za Vijiji kwa kuwani eneo la uwekezaji wa kiwanda cha sukari.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Jimbo la Mlimbani eneo la kilimo kikubwa cha mpunga, lakini Serikalihaijaweka mkakati na uendelezaji wa wakulima kuongezathamani ya mazao yao kwa kuwawezesha kuwepo kwaviwanda vya uchakataji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika,kuhusu MPM - Kiwanda cha Karatasi Mgololo. Mara kadhaanimeongea na Mheshimiwa Waziri kuhusu kiwanda hiki nahata nimefikia kumwandikia, kuomba ridhaa ya kuuona nakuupitia mkataba wa ubinafsishaji wa kiwanda hichoambacho awali kilijulikana kwa jina la SPM.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapoenda uchumi waviwanda jambo ambalo Serikali ilisisitiza ni kuhakikisha kuwawote waliopewa viwanda kuhakikisha vinazalisha katikauwepo na malengo yaliyokusudiwa. Hata hivyo, MPMwanazalisha katika stage fulani kisha wanasafirisha materialkwenda kufanya finishing Kenya, kisha karatasi zinarejeshwakuja kuuzwa hapa nchini, hapa kuna double loss.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, hawazalishi endproduct kwa maana ya karatasi, tunapoteza sehemu ya ajirakwa sehemu ya finishing kwenda kufanyiwa Kenya, lakini piatunapoteza mapato maana tungeweza kupata fedha zandani na kigeni kwa kuuza ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya masualaya East Africa Community kuhusu rules of origin, MPMinatuletea karatasi kutoka Kenya na ushuru unaolipiwa is only10% na siyo 25% maana sote tupo ndani ya EAC.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri, kiwanda hikikinauziwa magogo nusu ya bei 14,300/= kwa cubic meter,inapewa magogo hayo na Serikali (Sao Hill Forest). Je, kinasababu gani ya kutozalisha finished product kwa maana yakaratasi? Kusimamia na kuhakikisha kuwa ile machine Na.1inafanya kazi italeta tija na kuipa Serikali heshima kuwa ina

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

maanisha ilichosema kuwa, itahakikisha wote waliopewaviwanda wanatenda kadri ya malengo yaliyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, One Stop Centre ,Uanzishwaji biashara za kati na za chini ni suala lenye malengomarefu kiasi kwamba inasababisha biashara nyingi kutokuwarasmi. Ushauri, tuwe na one stop centre, mfano wa TIC kilaMkoa, kuliko ilivyo sasa mara BRELA, mara TIN, mara OSHA.Tuki-centralize katika level ya mkoa itarahisisha suala zimala kuanzishwa biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya masuala ambayoukizungumza na Jumuiya ya Kibalozi (Diplomatic Community)ni suala la Double Taxation na Protection of Investments,wanasema mahusiano katika dunia ya sasa ni kuhusukuimarisha fursa za kibiashara (Trade Opportunities) na ilikuzifaidi fursa hizo ni lazima pawepo mazingira bora yakufanyia biashara na uwekezaji. Mazingira hayo mojawaponi hili la double taxation na protection of investments.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nchi nyingi mfanoOman, Kuwait na za South East Asia, kama Korea, Japan nahata China ziko tayari kushawishi watu wao kuja kuwekezahapa nchini, lakini ukakasi upo kwenye assurance yaohususani katika masuala hayo ya double taxation naprotection of investments.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu ni kwambatupunguze woga, tupo na mashaka mno, kila jambo tunahisitutaibiwa au kudhulumiwa, naamini tunao wataalamambao watatufanya tufikie ile tunaita win win agreement.Hivyo ili yafanikiwe ni lazima Wizara ishirikiane na Wizara yaMambo ya Nje na Wizara ya Fedha, ambao focus yao nikukusanya tu pasipo kuangalia kuwa bila ushiriki wao katikasuala zima la double taxation , itakuwa haileti ti jailiyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Maafisa Biashara.Katika mchango wangu bajeti iliyopita niligusia suala hili,kuwa tunapoenda uchumi wa viwanda na reflection yake

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

kiuwekezaji kama lilivyo jina la Wizara, Muundo wa Kada hiikuendelea kufichwa ndani ya Idara ya Fedha katikaHalmashauri zetu sio sahihi. Ikiwa Nyuki tu ni Kitengo kwanini hii isifanywe Idara au angalau Kitengo?

Mheshimiwa Naibu Spika, Maafisa Biashara wamebakikufanya kazi ya kukagua leseni, wapo vijana ni wasomi wazurilakini wako under utilization, kwa sababu hata Wakurugenziwanajikuta wanawapangia kazi ambazo sio za utaalamwao. Ni wakati sasa kada hii, ninyi Wizara muongee naUtumishi na TAMISEMI muweze kuipa nguvu kimuundo iliwatumike ipasavyo hasa katika suala zima la biashara nauwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mafinga Mjini na Uchumiwa Mazao ya Misitu (Mbao). Mji wa Mafinga ni kitovu chashughuli za kiuchumi na uzalishaji katika Wilaya ya Mufindina Mkoa wa Iringa. Hata hivyo watu hawa hawajapata fursaya kupata huduma mbalimbali na changamotowanazokutana nazo hasa katika sekta ya mbao, uzalishajiwa nguzo na milunda. Ombi langu, naomba waje hapaDodoma kutokana na Waziri na Watendaji ili msikie maonina ushauri wao kwa namna gani mnaweza kuwasaidiakushiriki ipasavyo katika suala zima la kuelekea uchumi waviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu SIDO, inafanya kazivizuri lakini SIDO wamejikita level ya Mkoani tu, Mafinga inafursa yingi, tungependa SIDO ishirikiane na Halmashauri yaMji wa Mafinga katika suala zima la kuwepo ama kutengaIndustrial clusters kama walivyofanya Mkoa wa Mbeya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Industrial Cluster’s, jambohili lilijitokeza mwaka 2016/2017, hata hivyo nikifanya tathminini Halmashauri chache zimelitekeleza. Nashauri, kwakushirikiana na TAMISEMI, Halmashauri zipewe maelekezomaalum kutenga maeneo hayo na ikibidi wapewe deadlinemaana hatuwezi kuwa na viwanda pasipo kutenga hizoIndustrial Cluster’s.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa jitihada kubwa anazofanya kwakushirikiana na viongozi mbalimbali wa Wizara yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kuchangia hotubahii nikiamini kabisa nchi yoyote duniani ambayo ina viwandaimara vinavyozalisha, uchumi wa nchi yake utakuwa imara.Nchi yetu ina fursa pengine kuliko nchi zilizo jirani nasi je,tutapataje fedha za kigeni bila kuuza nje? Tuna maeneomengi ambayo yana fursa ya mali lakini tatizo ni usimamiziambao siyo mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo maeneo ya nchi yetumiaka ya nyuma yalikuwa na viwanda, mfano Mkoa waTanga lakini viwanda vimekufa, japo nimeona jitihada zakuvirejesha hali hiyo kwa kuona ujenzi wa viwanda vyasementi katika mkoa wetu. Tanga tuna reli inayoanzia Tangakupitia Moshi, Arusha baadaye Musoma, tukijenga viwandavingi Tanga na uwepo wa reli ya Tanga tutarejea mafanikiomakubwa kwenye fikra ya nchi ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya nchi yetu kuelekeakuwa nchi ya viwanda, bado kuna tatizo la wawekezaji wetukukosa mazingira au ushirikiano kutoka baadhi ya taasisi zilizochini ya Wizara, hili litazamwe sana. Mfano yupo mwekezajiambaye anataka kujenga kiwanda cha mabati, Wilaya yaMkuranga ameshindwa kuanza uzalishaji kutokana naBaraza la Mazingira (NEMC) kutompa kibali, hili lifuatiliwe kwakaribu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lingine juu ya ugawajiwa fursa hizi katika maeneo ya nchi yetu, baadhi ya mikoaya nchi yetu ina viwanda vingi kuliko mikoa mingine na sikwa sababu tu maeneo haya yana fursa zaidi kuliko mikoamingine bali kuna tatizo la kutotoa fursa sawa. Nashaurisana tena sana tutoe fursa sawa kwa kila eneo muhimu, fursaipatikane eneo hilo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano, Wilaya ya Kilindi nieneo lenye shughuli kubwa za kilimo, pamoja na shughuli zamifugo. Naomba sana nasi tupewe fursa katika maeneohayo. Mfano tunaweza kupewa kiwanda cha uchakataji wasiagi kwa sababu tuna mifugo mingi, aidha tunawezakupatiwa kiwanda cha ngozi kwa sababu tunayo mifugo yakutosha. Naomba Mheshimiwa Waziri achukue ushauri huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naishauri Serikali kuangaliakilimo na elimu kuwa kipaumbele cha kwanza ili viwandavyetu viweze kupata malighafi kutoka kwa wakulima wetuili kukuza uchumi wa kaya. Nishauri Serikali kupitia sera zakeza viwanda kuzihuisha ili ziendane na wakati wa sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nashauri Serikali itungesheria na adhabu kali zinazotokana na uharibifu wamazingira, hasa utiririshaji maji ya viwandani ambayoyamekuwa kero kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri Serikali kurejeshaviwanda vyote vilivyobinafsishwa kutumika kinyume namkataba wa awali. Mfano, Kiwanda cha Korosho Kibahakimegeuzwa mahali pa kutunzia bidhaa, hivyo matumiziyaliyoainishwa wakati wa mkataba kukiukwa. NaishauriSerikali kupunguza urasimu katika kusajili biashara nakupelekea wawekezaji kushindwa kuwekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu viwanda nawanawake, naishauri Serikali kuwaangalia kwa jicho lahuruma wasaidiwe ili kuweza kupata mikopo ya kuanzishaviwanda vidogo vidogo. Mfano, viwanda vya vyakula vyakuku na mashine za kutotolea vifaranga il i wawezekujikwamua kiuchumi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

MHE. CECIL D. MWAMBE: May your Table be pleasedto read my contribution in English as it is research based, itshould also be read with Intoxicating Liquour Act. of 1968/1966 and 1981.

Justification for cashew value addition in Tanzania.Cashew Apple Processing: In Tanzania, cashew apples areunder utilized. In most cashew-growing areas, small quantitiesof cashew apples are consumed as fruits, though they are notsold in markets as there is no demand for them. A few cashewapples are locally used in production of alcoholic and nonalcoholic beverage, but the majority of cashew apples areleft to not in the field. Some farmers in Brazil plant cashewprimarily for its fruits and the nut is a secondary product whichis thrown away, yet they realize a very good profit.

It should be noted that Cashew apple have vitaminC, five times than that in citrus fruits, have high carotene andhence they have good health benefits.

The estimated amount of cashew apple produced inTanzania is over 1,300,000 tons in major cashew growing areasbased on current National cashew production levels.Assuming that only 10% of it (Approximately 130,000 tons) isutilized for production of juice at extraction rate of 70% about91.000 tons (approximately 91 million liters) of cashew applejuice will be produced. If each liter is sold at a farm-gate priceof $o.5,about $45.5 million will be realized in a season.

Equally, if 90% of the remaining cashew apples(Approximately 1,100,000 tons) is used to produce cashew gin(Nipa), farmer could earn even more money than the amountobtained in juice above.

It should be noted that Farmers are alreadyknowledgeable in the production of cashew gin, but theyare not aware if there is a law that allows them to distill alcoholas long as they have a valid distilling license from relevantauthority. As a result, they produce gin (Nipa) in hiding andonce they are caught by Police they face prosecution. This

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

calls the need to create awareness to our farmers. Nipa iscalled illegal illicit alcohol simply because the producers donot have a licensed to do so. The law is clear that gin (Nipa)can be produced but the producer must have a valid license.

The institute has done a research on cashew applesprocessing into juice, Jam and Wine. They are in the final stageof commercializing the value addition to juice and wine.Equally the institute has also undertaken research on cashewbutter production. They are also in the final stage of studyingshelf life of the cashew butter. Broken cashew kernel are soldat Tshs 6,000/kg. Once the 1kg of broken kernels is processedinto butter it will produce three jars (each 330 mls) and will besold at Tsh 6,000 per jar making a total of Tshs18,000.

It should be noted that Cashew kernel is cholesterolfree or zero cholesterol therefore it is good for health. Thesehealth benefits are the main reason why cashews are quiteexpensive worldwide. Cashew farmers can double theirincome if they will add value to cashew kernels, cashew shellsand cashew apples.

Convincing farmers to produce Gin (Nipa) for valueaddition into Ethanol and Methanol will give them moreincome. The reason for further processing is due to the factthat Nipa has about 2% methyl alcohol which is not good forhealth. It makes people blind but it is mainly used in hospitals(popularly) known as methylate spirit). This means addingvalue to Nipa will make our people more health and equallyfarmers will tend to sell to get more money.

Naliendele Research Institute is in the process ofinstalling a small scale cashew distilling plants to be specificFractional Distillation Equipment to separate Nipa into methylalcohol and ethyl alcohol. The objective is to undertakeeconomic analysis to find out how much more farmer cangain if they sale their Nipa to authorize agent. It is estimatedthat at moment the Nipa is sold at about Tshs 500 per Fantabottle which is approximately 330 mls. This means Nipa willbe sold at about Tshs 1500 per litre. On the other hand, 100

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

mls of the methylated sprit (methl alcohol 70% v/v) is soldbetween Tshs 1,000-2000 in pharmacies.

Naliendele Research want to establish how much canbe obtained from the Nipa if it is fractionally distilled. Datafrom this study will show how much more farmer can get fromcashew apples which are sometimes thrown away or underutilize. It is no doubt that they will earn more than selling theNipa at Tshs 1,500 per litre. Another advantage of addingvalue to cashew apples in creation of employment in theentire cashew value chain.

Reviving Cashew Processing is Possible; Cashewprocessors in Tanzania complains that they cannot competewith foreign buyers in buying raw cashewnuts in the warehousebecause they hardly get raw cashewnuts when bidding. Onthe other hand, they also complain that they do not makeprofit due to high prices. One of the reason why they do notmake profit is due to the fact that they depend on only oneproduct when processing and these are the cashew kernel.The cashew shells are not value added. They can produceCashewnut Shell Liguid(CNSL) and shell cakes to be used asfuel.

The CNSL also can produce several products as follows:-

• Brake linings• Lubricant is high temperature areas• Cosmetics• Insecticides to fumigated buildings• Ceiling boards for high moisture conditions

Cashewnut produce the following:-

• Kernels (20-25% by weight of raw cashewnuts• Cashew shells (70-80% by weight)• Cashew shell produce CNSL –(20-25%) of

weight of raw cashewnuts• Cashew shell cake for fuels (50-60%) by weight

of raw cashewnuts

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

It is important for the local processors to be given ahigh priority in buying cashewnuts in the auction thoughwarehouse receipt system. Arrangement can be done tomake sure the local processors do not need go to the auction.They need to be allocate 20-25% of the amount thecashewnuts which was given the highest price during auction.

When a foreign buyer bid and get a certain amountof cashewanuts, 20-25% will be allocated for local processorsto buy at the same market price. In this way, farmer willcontinue getting higher prices while the local processors willhave an access to the raw cashewnuts until they satisfied.

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika,nampongeza Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais naMheshimiwa Waziri Mkuu kwa jinsi ambavyo wameendeleakutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara hii,hakika naiunga mkono Tanzania mpya ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Wazirimwenye dhamana na kwa weledi mkubwa, juhudi na jinsianavyojituma kupitia Wizara hii, hakika ni Wazirimchapakazi. Pia niipongeze sana timu ya Wizara kwa jinsiya utendaji wao na kuwapatia Watanzania tumaini laviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanda cha General Tyre,naomba ufafanuzi wa kina wa kiwanda cha General Tyrekwani maelezo yanayotolewa ama maelekezo ambayoyamekuwa yakitolewa ndani ya Bunge hili na maelezo yahotuba ya leo yanakinzana. Maelezo kuhusu Kiwanda chaGeneral Tyre kwenye Hotuba za bajeti kwa miaka 2015/2016na 2016/2017 ni tofauti (kila mwaka yanaletwa maelezomengine mapya. Naomba ufafanuzi wa kina, maelezo ganini sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa mtoahoja anifafanulie wakati anahitimisha hoja yake.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa William Tate Olenasha,dakika tano, atafuatiwa na Mheshimiwa Mwigulu Nchemba,dakika 10.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Naibu Spika, nianze mapema kabisa kuanzakuiunga mkono hoja iliyopo mezani ili nisije nikasahau. Vilevilenitumie nafasi hii kutoa pongezi sana kwa Mheshimiwa Waziripamoja na timu yake kwa hotuba nzuri, lakini vile vile kwajitihada kubwa ambayo ameonesha katika kutupeleka katikanchi ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, yeyote yule anayebezajitihada za Mheshimiwa Waziri na Timu yake, najua atafanyahadharani lakini nina hakika kimoyo moyo anampongeza.Kwa sababu haiwezekani kwamba ndani ya kipindi chamwaka mmoja na nusu tu tayari tunashuhudia uanzishwajiwa viwanda zaidi ya 300. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya WaheshimiwaWabunge wakati wanachangia, wameibua masualayanayogusa kilimo ambayo ningependa kuyatolea ufafanuzikwa muda mfupi nilionao. Baadhi ya Waheshimiwa Wabungewameongelea kuhusiana na biashara ya chakula na bidhaazinazotokana na kilimo katika ukanda wetu wa AfrikaMashariki, wakiashiria kwamba wangetaka na sisi tufuatekinachofanyika kwenye nchi nyingine kuagiza chakula kutokanje.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuwafahamishaWaheshimiwa Wabunge kwamba pamoja na changamotoya chakula tuliyopata katika mwaka uliopita, lakiniukifananisha na picha tuliyonayo katika ukanda wetu waAfrika Mashiriki, nchi yetu imeendelea kuwa na hali nzuri yachakula kuliko nchi yoyote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukichukua baadhi tu yabidhaa za chakula tutaona picha kuhusiana na hali halisi yabei kwa sasa. Tukichukua zao la mahindi, bei ya wastani

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Uganda tunavyozungumza leo ni Sh. 96,000/=, wakati Kenyani Sh.114,000/=; Rwanda ni Sh.88,000/=, Juba au Sudani yaKusini ni Sh.135,000/=, Burundi ni Sh.152,000/= wakati kwetubei ya wastani kwa leo ni Sh.95,000/=. Kwa hiyo, unawezaukaona tumekaaje katika mizania ya kikanda ikija suala labei ya mahindi. Hata zile nchi nyingine ambazo zinaelekeazina bei nzuri kama Rwanda ni kwa sababu wao wameagizakutoka Brazil. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tukiangalia zao lamchele au basi chakula cha mchele, tunaona kwamba beiya wastani Uganda kwa leo ni Sh.203,000/=, Kenya niSh.267,000/=, Rwanda ni Sh. 204,000/= lakini Burundi niSh.236,000/= na kwetu bei ya wastani wa mchele kwa leo niSh.174,000/=. Unaweza ukaona kwamba bado sisi tukiangaliakikanda tuko katika hali nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile imezungumzwasana kuhusu sukari. Ukiangalia bei ya sukari katika Nchi zaAfrika Mashariki, utagundua kwamba nchi yetu bado tukokatika hali nzuri ukifananisha na nchi za jirani. Bei ya wastaniBurundi kwa leo ni kati ya Sh.3,700/= mpaka Sh.4,000/=;Uganda kati ya Sh.3,500 mpaka Sh.4,000/=; Kenya ni kati yaSh.3,500/= mpaka Sh.5,000/=. Kwa hiyo, ukiangalia sisiTanzania tuko katika hali nzuri bei ya sukari ni kati ya Sh.2,500/= mpaka Sh.3,000/=.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo asubuhi nilipata wasaawa kuongea na Ma-DC wa Wilaya za mpakani za Kakongo,Misenyi, Ngorongoro, Rombo na Tarime, kujaribu kuangaliahali ya chakula na kimsingi wote wanasema kwamba sisikama nchi bado tuna hali nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungewaliokuwa wanataka na sisi tuagize chakula kutoka nje,wangeshauriwa vizuri zaidi kuhusiana na athari ambazo nchiyetu ingeweza kupata kwa kufanya kama hivyo. KimsingiKenya na Rwanda wao wameagiza chakula kutoka nje kwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

sababu wao wana changamoto kubwa ya chakula, hali yaoya chakula siyo nzuri; wakati sisi mwaka uliopita tulikuwa naziada ya tani milioni tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tathmini ambayotumeifanya karibu mikoa yote inatuonesha kwamba mwakahuu inaelekea kwamba tutapata chakula kingi zaidi. Sisihatuna haja ya kuagiza. Kenya wameagiza chakula kutokaMexico kwa sababu hali yao ni mbaya, lakini kawaida waowanategemea Tanzania na Uganda katika kupata chakula.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wakoumekwisha.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa MwiguluNchemba, atafuatiwa na Mheshimiwa Sospeter Muhongo.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa fursa nami nichangie hojailiyoko mezani. Kimsingi hoja hii ni ajenda ya Serikali ya Awamuya Tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie WaheshimiwaWabunge, tunapojadili hoja hii, tunapaswa kuwaWatanzania il i tuunge mkono jitihada anazofanyaMheshimiwa Rais, kiu ambayo Watanzania wamekuwa nayokwa siku nyingi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mjadala huutunaojadili, ukiangalia haraka haraka, unaweza tu ukaingaliahotuba ya Mheshimiwa Waziri, lakini ukaacha kuangaliauamuzi wa makusudi ambao Serikali imeufanya kwa nia

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

njema ya kutekeleza Sera yake ya Tanzania ya Viwanda. Nibahati mbaya sana Watanzania tulio wengi huwatunapenda matokeo ya haraka haraka kama ya kamari vile,kwamba unacheza halafu unapata matokeo; kamaumepatia, umepatia; kama umekosea, umekosea.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo tunalolizungumzialeo, siyo jambo linaloota kama uyoga, ni jambo ambalolinahitaji utengenezaji wa vitu vingi sana ndiyo matokeo yakeuweze kuyaona. Kwa mfano, leo hii tunavyoongea, tangumuda mwingi sana Serikali iliondoka kwenye sera ya kujengaviwanda, lakini leo tunapoongea kwenye Awamu ya Tano,Serikali imeweka mkono wake kwenye kujenga viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni hatua kubwa na niutekelezaji wa vitendo wa dira ya Mheshimiwa Rais aliyoitoawakati wa Kampeni, wakati wa kuzindua Bunge, lakini piana kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wengine mnasema Wazirianahamasisha, anahamasisha, lakini Serikali ilisema itajengaviwanda; mimi niwakumbushe, Serikali imetafuta dirishaambalo itaweka mkono wake wa kujengea viwanda. Hivileo tunavyoongea, Taasisi ama Mashirika ambayo yako chiniya Serikali kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, kwa Dira yaMheshimiwa Rais, yamebadili mwelekeo ambao yalikuwayakifanya kwa muda mrefu ambao haijafanyiwa tathminina ikaingia kwenye utekelezaji wa ujenzi wa viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyoongea, PPFwalishaingia mkataba na Magereza wa kufufua kiwanda chaviatu kule Karanga na mwelekeo na maelekezo tuliyoyapatana ambayo tumekubaliana kama Wizara, wateja wa kwanzatutakuwa watumishi wenyewe wanaopatikana kwenyevyombo vyetu vilivyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndanina tutakwenda na kwenye Taasisi nyingine ambazowanahitaji viatu hivyo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, kwa tathmini yaharaka ni kwamba soko la bidhaa hizo zitakuwepo na hivyoitawezesha kiwanda kuwa endelevu. Maana yake lilikuweposwali lingine kwamba ni namna gani mtahakikisha kwambaviwanda mnavyovijenga havitakufa? Kwa hiyo, moja ya sifa,utakuwepo upatikanaji wa soko.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, tumeongelea hikialichotoka kukielezea Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusumambo ya sukari. Ni kweli sukari bei yake imepandaukilinganisha na miaka kadhaa iliyopita. Hata hivyo, Tanzaniasiyo kisiwa; panapokuwepo na bei za juu sana kwenye nchizinazotuzunguka, ni kanuni za kiuchumi kwamba lazima nasisi tutaathirika na bei zitapanda. Ukiangalia kwa mfano,Uganda kwa bei ya Kitanzania sukari inakaribia Sh.5,000/=,ukienda Kenya inacheza kwenye Sh.4,300/= hadi Sh.5,000/=.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo, kamatuna sukari kwetu huku na wao bei yao iko juu namna hiyo,ni lazima itaathiri bei kwa sababu watu watatorosha. Hatuaza muda mfupi na za muda mrefu tunazochukua, kwanzatunakataza utoroshaji wa sukari na nimeelekeza taasisi zilizochini ya Wizara ya Mambo ya Ndani kuchukua hatua kwawale wote watakaofanya zoezi la kutorosha sukari nakusababisha upungufu na kusababisha madhara ya bei katikanchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haijaishia kuchukuahatua za mpito hizo za kuzuia za kuweka doria, MheshimiwaRais ameelekeza na dira hiyo inafuatwa na Wizarazinazohusika ikiwepo kinara Wizara ya Viwanda na Biashara,Wizara ya Kazi, Wizara ya Mambo ya Ndani; hivitunavyoongea, ndani ya wiki chache utekelezaji kwa maanaya kupata mtengenezaji wa kiwanda katika Gereza la Mbigiliutakuwa umekamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua za awali sasa hivi zautengenezaji wa mradi huo zilishatekelezwa na kiwandahicho kitaweza kuzalisha sukari kati ya tani 30,000 mpaka50,000.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maelekezo yaMheshimiwa Rais, haijaishia hapo; kutakuwepo na mradimkubwa wa Mkulazi ambao tuliuweka kwenye Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano, kwenye Hotuba ya MheshimiwaRais na kwenye Hotuba ya Waziri wa Fedha na kwenyeHotuba ya Waziri mwenye dhamana ya Viwanda, katikavipindi vyote ambavyo amekuwa akisemea.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili unaona kwambalitaenda kutuondolea kabisa upungufu uliokuwa unajitokezakatika eneo hilo na liko katika hatua za mwisho za kwendakwenye utekelezaji. Maandalizi ya eneo katika utekelezaji huouko katika hatua za juu kama ambavyo atabainishaMheshimiwa Waziri mwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mazingira ambayoni tathmini ya jumla ya ajenda ya viwanda, wenginewalikuwa wanasema kwamba mwekezaji atawekezajewakati vivutio tumeviondoa?

Waheshimiwa Wabunge, siyo siku nyingi sana kwenyemijadala yetu, ukichukua Hansard za Bunge lililopita, mijadalayetu ilikuwa inajikita kwamba vivutio tunavyovitoa siyovyenyewe. Kwa kuwa tulikuwa tunasema vivutiotunavyovitoa siyo vyenyewe, sababu tulizokuwa tunatoa nikwamba baadhi ya nchi bado zinatuzidi kwenye wawekezajiilikuwa ni aina ya vivutio. Sasa Mheshimiwa Rais amelengakwenye vivutio vyenyewe ambavyo vinatumika Kimataifa,vinavyoondoa vikwazo kwenye uwekezaji na kuleta sifa halisiya mwekezaji kuweza kuvutiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya vitu ambavyovinavutia kwa kiwango kikubwa na Serikali imechukua hatuakubwa, Mawaziri wenye Sekta watasema kwa kirefu,mojawapo ni kasi kubwa inayofanyika kwenye umeme.Mojawapo ni kasi kubwa inayofanyika kwenye barabara;mojawapo ni kasi kubwa ya ujenzi inayofanyika kwenye relina nyingine ni vita kubwa inayopiganwa ambayoMheshimiwa Rais ameiishi kwenye maneno na kwenye vitendoya mambo ya rushwa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye nchinyingine utasifia kwamba wamefanikisha mradi kwa haraka,lakini utakuta wametumia vibaya fedha za walipa kodi wanchi zao. Sisi tunaenda katika utaratibu ambao tunapatamradi ukiwa umejumlishwa na matumizi bora ya fedha zawalipa kodi. Kwa mwekezaji yeyote asiye mbabaishaji,atapenda sifa hizo kwamba pana umeme, panaamani, pana muunganiko wa kusafirisha bidhaa, lakini piapana matumizi bora ya fedha za walipa kodi katika nchihusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi vyote lazima vitaongezaufanisi, vivutio vingine ambavyo tulikuwa tunavisema vyarejareja vinatumiwa zaidi na wawekezaji wababaishaji, lakinikatika nchi zao ambako na nchi ambako tunatumia kamamifano walikowekeza vivutio vikubwa ambavyo ni standardkatika uwekezaji, huwa ni vya aina hiyo na ndivyo ambavyomwekezaji asiye mbabaishaji angependa avikute katika Taifahusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo,nampongeza Mheshimiwa Rais kwa dira yake hii na kwenyehistoria za nchi yetu Marais hukumbukwa watakapokuwawameshaweka alama. Kwa hiyo, hizi kelele nyingi, miezimitatu tu baada ya kumaliza awamu zake mbili, watakuwawakiona mwekezaji mbabaishaji amepewa fursa,wanasema enzi za Mheshimiwa Magufuli hili lisingetokea.Watakuwa wakiona rushwa imetokea mahali wanasema enziya Magufuli hili lisingetokea hili, watakuwa wakiona viwandavinaanza kufa, ama ndege zilizokuwa tano zinaanza kurudikuwa nne, watasema enzi ya Magufuli hili lisingetokea. Sasakwa sababu Tanzania itaendelea kuwa chini ya CCM, tunahakika haya anayoyafanya Mheshimiwa Magufuliyanatengeneza viwanja kwa ajili ya nchi yetu kuweza ku-take off.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe Watanzaniawote wafunge mikanda, tuiandae nchi yetu, kwa dira yaMheshimiwa Rais ili tuweze kuiona Tanzania ya viwanda nahiyo ndiyo itakayotengeneza ajira nyingi na sisi tutakuwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

wauzaji wa bidhaa na sio waagizaji wa bidhaa kamaambavyo kwa kipindi kirefu tumeishi katika mazingira hayo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja yapacha wangu na huku nikimshukuru kwa kuwekeza kwenyeGereza la Karanga ambako ukiondoa viatu vyako na vyaMheshimiwa Waziri Mkuu, basi humu Bungeni mimi ndionimependeza zaidi viatu vilivyotoka Gereza la Karanga,vimetengenezwa hapa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naungamkono hoja.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa ProfesaSospeter Mwijarubi Muhongo, dakika kumi.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge,huwezi ukatenganisha viwanda na umeme. Umeme, tunasiku mbili; wiki ijayo, Alhamisi na Ijumaa, tunzeni maswali yenuyote, hebu leo tushughulikie viwanda tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa uagizaji wamakaa ya mawe kutoka nje. Kama unalipenda Taifa lako, nilazima utapiga marufuku makaa ya mawe na gypsum yaanijasi isitoke nje. Twende kwa takwimu; ni kwamba tulikuwana mtaalam mmoja tu, bahati mbaya amefariki Dkt.Semkiwa, alifanya Ph.D yake University ya Colon Ujerumani,Profesa wake alikuwa wa kutoka Australia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ilikuwa wakati huo miakaya 1990 wamepiga mahesabu kwamba tuna mashapodeposit ya bilioni tano ya ‘B’, ya baba. Miaka mitatu nyumaalivyoendelea na utafiti akasema, tunaweza tukafika bilionikumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa unayesema turuhusumakaa kutoka nje, nawe tupatie takwimu za kuonesha

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

kwamba hatuna makaa ya kutosha, lakini bila takwimu,msimamo wa Serikali ni kwamba bado tutazuia makaayasitoke nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa hivi, Ngakawalikuwa wanayumbayumba, wanazalisha tani 80,000 kwasiku; Magamba wanazalisha tani 1,000 kwa siku; Kabuloambayo ni ya STAMICO wameanza tarehe 30 mwezi wa Nnesasa hivi wana tani 500. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge,kama kuna mtu ana kiwanda cha saruji anakudanganyakwamba makaa hayapo, mwambie aje Wizarani kwanguaende Ngaka, aende Magamba, aende Kabulo, makaa yamawe tunayo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu wa Lindi naMtwara wamelalamika kwamba hakuna viwanda huko.Sehemu pekee kwenye Taifa hili kwa miaka kumi au ishiriniinayokuja ambayo itaendelea kwa kasi, nasi wote tutahamiahuko, ni Lindi na Mtwara. Mikoa mingine itabaki ni Mikoa yakizamani; ya pamba, korosho, na dhahabu, mikoa yakizamani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Lindi hakuna uwekezajimkubwa ambao umeshafanyika wa kihistoria kama ambaoutafanyika Lindi wa LNG; ni bilioni, bilioni, bilioni tena ya ‘B’;bilioni 30 ambayo ilikuwa inazidiwa na reli ya TAZAMAikafuata bomba hili, inalofuata ni pale Likong’o Lindi.Utasemaje kwamba Lindi imesahaulika ina uwekezaji wabilioni 30. Haiwezekani!

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua viwandavikubwa vikubwa, hivyo vidogo namwachia MheshimiwaMwijage ndio anaviweza mwenyewe. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Kiwanda cha Mboleakitajengwa Lindi tena mmoja nadhani sikuwepo, alitoa kaulimpaka Balozi wa Ujerumani amenipigia simu jana anasikitikasana, sijui alipata wapi taarifa.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaeleze, tunaviwanda viwil i vitajengwa; cha mbolea cha Kilwakitajengwa na Kampuni ya Ferrostaal. Hizi ni kampuni zaKimataifa na kile cha Mtwara kitajengwa na kampuni yaHelium nayo ni ya Ujerumani. Hayo ni makampuni yaKimataifa, eeh! Sikiliza sasa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, hii ya KilwaFerrostaal Balozi huyu aliyemaliza muda wake kablahajaondoka tunataka kwenda kuzindua groundbreakingceremony. Siyo kuweka nini; ile tunaenda kabla ya tarehe 1Julai, uwekezaji wake ni bilioni 1.92. Bilioni ‘B’! Utasemajekwamba Lindi na Mtwara imesahaulika? Itazalisha mboleaUrea tani 2,200 kwa siku; Ammonium tani 3,850 kwa siku yaUrea. Utasemaje Mbeya wamesahaulika? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu wa Mtwara,nitamwachia ndugu yangu Mheshimiwa Mwijage aongee yacement ya Dangote, lakini kuna kiwanda kingine cha mboleacha Helium, haya ni makampuni makubwa! Nenda u-searchu-google mwenyewe utayaona. Ni uwekezaji wa bilioni ya‘B’ siyo milioni 1.26 na itazalisha tani 3,700 kwa siku. UtasemajeLindi na Mtwara imesahaulika? Lindi na Mtwara ndiyo Mikoamipya kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, umeme nimesema tuonanewiki ijayo. Nakuja suala la Liganga. Bado nina dakika tano!Niongeze speed eeh!

Mheshimiwa Naibu Spika, mwanzoni wakatitunafanya utafiti, hatukujua namna ya kutenganisha iron,titanium na vanadium. Ph.D alifanya Profesa Mahinda, miminilikuwa bado mwanafunzi Dar es Salaam Chuo Kikuu,tulikuwa tunapigania chuma tu, lakini dunia sasa imebadilika,hii chuma haina thamani kubwa kuliko titanium na vanadium.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa huyu mwekezaji kazimoja kubwa anayoifanya ni ya kutenganisha iron fromtitanium, from vanadium. Hiyo inataka muda, inataka vivutio;na hivi vivutio vinataka sheria zije humu zibadilishwe. Huwezi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

ukaweka vivutio kwa ajili ya Liganga na Mchuchuma pekeyake, kwa hiyo, inamaanisha tupitie vivutio vyote; hatavivutio vilivyopo vya TIC uwekezaji wa umeme unahesabikasio strategic.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndugu zangutukubali kwamba hatujachelewa na hii itafanyiwa kazi.Kingine ambacho ni muhimu ilikuwa ni mchuchuma, yaanikwenye makaa ya mawe. Wenyewe wakati wanatengenezamradi, tulikuwa na matatizo ya umeme wakataka wauzesenti 13 kwa unit moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mahesabu yaoyote ya kuchimba chuma na makaa kuzalisha umeme,yalijikita kwenye senti 13. Kwa kuwa tuna umeme mwingi,huo sasa hivi tunauita umeme wa bei mbaya. Kwa hiyo,inabidi waje kwenye model ya senti saba au nane kwa unit.Hiyo model nayo inataka muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, msisemekwamba vitu havifanyiki. Ameshafanya experiments kubwasana za kujaribu kutenganisha iron, titanium, vanadium,lazima aje na model wa senti saba mpaka nane wa kuzalishaumeme wa Liganga. Kwa hiyo, Waheshimiwa ni kwambakazi zinafanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaoneshe,wenyewe tunataka kuzalisha tani milioni moja; vile viletunabadilisha mawazo. Mawazo yalikuwa kuzalisha chumakusafirisha nje ya nchi, lakini sisi ni kama wachezaji, ni kamatunachezea njugu. Wapo wasafirishaji wakubwa. Kwa hiyo,lazima tubadili concept hiyo. Kwa mfano, Australia mwaka2016 chuma iliyozalishwa duniani, ilikuwa tani bilioni 3.4.Imewatosha?

MBUNGE FULANI: Inatosha!

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Haya ahsante. Jamanihili la Liganga Mchuchuma, mwache, ni mambo ya kitaalam,linaenda vizuri. Ahsanteni. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Profesa Muhongo, ulikuwaunataja hapo hizo bilioni. Ni dola au ni hela za Kitanzania?Zote tu ulizotaja hayo mabilioni ni hela za Tanzania ama nidola?

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa NaibuSpika, nilishawahi kuwaeleza, miradi yangu yote huku ni dola.(Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge,leo naona tumepewa changamoto. Ameanza na sisi Waziriwa Afya asubuhi ametupa misamiati mikali hapa,tumemalizia na Waziri wa Nishati na Madini. Nadhani inabiditukatafute google iko wapi. (Kicheko)

Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara naUwekezaji, mtoa hoja.

WAZIRI WA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kutujalia wote nguvu na afya njemaili kuweza kujadili hii bajeti yetu kwa siku mbili. Hii ndiyo bajetiinayobeba Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wenye dhimaya kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.Nawashukuru sana Wabunge wote mlivyojadili bajeti hii,napenda niseme mmeitendea haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya kipekeenamshukuru Mheshimiwa Stanslaus Nyongo, Mbunge waMaswa; yeye na Kamati yake kwa jinsi walivyoichambuabajeti yangu na kwa jinsi walivyosimamia Wizara yangu,mpaka kutupelekea kuandika hii bajeti ambayo kilaanayeisikia, anaomba nakala halisi pamoja na kwamba ikokwenye mtandao.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, naomba nimshukurukipekee Waziri kivuli wangu, Mheshimwa Antony Komu kwahotuba yake ya kufikirisha ambayo inakufanya ufikirie miakamingi mbele, uende maili nyingi. Waziri Kivuli nakushukuru.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Mheshimiwa Naibu Spika, mbali na ushauri mzuri,uliotolewa na Kamati na Waheshimiwa Wabunge kwaujumla, Wizara na taasisi zilizoko chini yake imepokeapongezi nyingi kwa kuweza kutekeleza masuala ambayowananchi wamekuwa wakiyatarajia. Hakika pongezi hizozinatupa hali ya moyo ya kujibidiisha zaidi katika kubuni,kupanga na kuboresha mbinu za utendaji ili Taifa naWatanzania kwa ujumla wanufaike zaidi na matunda ya fursazilizomo. Nami nawaahidi kuwa tutaendelea kujibidiisha nawala hatutawaangusha.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge kwa michango yenu. Waliochangiakwa kuongea moja kwa moja ni Waheshimiwa Wabunge44; waliochangia kwa njia ya maandishi ni WaheshimiwaWabunge 48; waliochangia Wizara hii kwa kina katika bajetiza Mawaziri wenzangu waliotangulia ni WaheshimiwaWabunge 10, ujumla wake watu 101 wameiunda upya Wizarayangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nijitahidi kujaribu kuwekasawa kwa mujibu baadhi ya hoja, lakini ni kweli wataalamwangu wote wako hapa, wamejiandaa watatengenezamajibu ya kina; na kama nilivyosema, mtazamo wetu katikakujenga uchumi wa viwanda mmeujenga upya. Kwamaneno rahisi, mmeuimarisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na swali la kwanza,the misconception, what is not, mawasiliano ya kati na ndaniya Serikali siyo mazuri; the misconception, siyo kweli.Mawasiliano ndani ya Serikali ya Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli, ni mazuri. Sina muda wakuzungumza zaidi, nitawapa vielelezo. Serikali hufanya kazikwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni Taarifa ya Wizara yanguambayo nimemwandikia Waziri wa Fedha baada ya yeyekunitaka kwa maandishi kwamba ni vivutio gani unavitakaili wawekezaji wako waweze kuwekeza unavyotaka, iko

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

hapa. Akaenda zaidi, ni kodi gani ziongezwe au zishushwe ilimambo yaende vizuri? Ndiyo hayo! Kwa hiyo, mawasilianoni mazuri na Serikali inafanya kwa makaratasi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, watu wasipatewasiwasi kwamba nchi hii inaingia vitani, hapana! Tunafanyakazi vizuri na nakumbuka, bahati mbaya simu zangunimezifungia, mawasiliano ya mwisho alinipigia akiwaMarekani kwamba hakikisha andiko hili linapelekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimempa maelekezo KatibuMkuu wangu anayeshughulikia biashara na uwekezaji,anayeshiriki kwenye chombo cha Kitaifa kinachopitia bajetikabla ya kwenda kwa Mheshimiwa Waziri kwamba yaleniliyoyapendekeza mimi msiongeze wala kupunguzachochote. Kama mnakataa, andika mmekataa, kusudi sikuya siku waje waone tunavyoshirikiana. Serikali hii ni moja.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kifupi, nimeelezeahivyo, lakini nitatoa mifano mingine zaidi. Tunawasiliana!

Waheshimiwa Wabunge, zimekuwepo hoja nammesema ukweli kwamba kasi ya kujenga uchumi waviwanda inakwenda taratibu. Napenda nikiri na nitambuemchango wenu, lakini nyie sio wa kwanza. Kuna wakati mimina Mheshimiwa Waziri Mkuu tulikuwa hatuangaliani machoni;nikawauliza Wasaidizi wake, vipi? Wanasema, haoniviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mama Samiakuna wakati aliniiita nyumbani kwake, akasema Mwijagenataka viwanda vya madawa! Bahati nzuri MheshimiwaUmmy amekwenda kutafuta viwanda hivyo, hayupo hapa.Tajiri huyo ndio alikuwa hataki kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nitambuemchango wa Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi, MheshimiwaKijazi, nikamwambia mzee nifanyaje? Akasema kamahawakuelewi andika! Nikaandika kitabu hiki kinaitwa strategy

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

for fast tracking in industrialization in Tanzania. Yotemliyoyasema yako humu. Wakakipeleka kwa tajiri. Tajirinamba moja; wewe unalinda duka tu, tajiri ni mmoja tu!(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nil i juaje kwambaMheshimiwa Rais ameona kitabu hiki? Tulipowaitawawekezaji, Mheshimiwa Rais alitamka kwamba wakati wakuwekeza ni sasa na atakayetaka vivutio, aje aniambie.Nikajua ugonjwa umepata dawa. Nimewasiliana, Serikaliinawasiliana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo ni vielelezo viwilikwamba the Government is coordinated; na kitabu hiki siyochangu tena, kimeshapelekwa kwenye Kamati ya Wabungewote na kinakwenda kwenye Baraza la Mawaziri. Kwa hiyo,Serikali inawasiliana. Naweza kutoa ushuhuda, MheshimiwaMpina alizungumza nini, tulibishana nini kuhusu hii; na vilevikwazo vyote na gear zote za kwenda kasi, zimezungumzwahumu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushirikiano wa Sekta Binafsina Serikali. Viongozi wa Sekta Binafsi wako pale; TanzaniaPrivate Sector Foundation, CEO wao Dkt. Simbeye yuko pale.Jana mliona uwanja wote ulijaa suti za bei mbaya! Hao niwawekezaji hao! Walikuwepo hata wale akinamama waVICOBA, wote ni wawekezaji. Tungekuwa na mahusianomabaya wasingekuja. Kwa hiyo, mawasiliano yetu ni mazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi huu tukiwa Bungeni,mimi na Mheshimiwa Mpango tuliitisha mkutano wawawekezaji wote, mliona; uwanja wa ndege wa Dodomaulionekana mdogo, ulijaa ndege! Wawekezaji wa Madiniwalikuwepo; wa umeme walikuwepo, tukakutana,tukajadiliana; na tukawekeana maazimio. Tumekubalianakila miezi mitatu tuitishe mkutano mkubwa. Sekta Binafsi naSerikali tunafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, ngazi ya Kitaifa, Baraza laBiashara la Taifa ambalo Mwenyekiti wake ni Mheshimiwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

Rais, tumekutana juzi. Wale mnaotumia mitandao, ndiyo ileclip ya Millard Ayo inayozungumza, ikichukua yale manenomatatu aliyoyasema Mheshimiwa Rais, wakati wa kuwekezani sasa. Atakayekukwamisha njoo uniambie. Ukitaka vivutio,nitakupa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama Mheshimiwa Raisanasema ukitaka vivutio nitakupa, wewe unaogopa ninikumfuata? Si anaonekana! Amekwambia ukitaka vivutioatakupa. Nenda kamwambie sasa akupe, si yupo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namba tatu ni viwandavilivyobinafsishwa. Mheshimiwa Devotha, wewe bado ni rafikiyangu. Usidhani urafiki wangu ulikufa kwa sababu ulifanyahivyo, hapana, bado ni rafiki yangu. Tatizo la Morogoro halipotena. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, mnitendee haki.Msome kitabu changu, kina majibu ya kila kitu. Moro Canvaskaribu mambo yake yatakwisha. Kutoa kiwanda kwenyeownership moja kwenda ownership nyingine kuna mamboya kimikataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikwambie nimetumianguvu zangu zote na muda wangu wote, mimi nina maslahi.Nimekwambia Mheshimiwa Devotha urafiki wangu na wewehautakufa. Nilikasirika kipindi, sasa hasira zimekwisha, eeh!Kuna wakati alibadilisha mwelekeo wetu na miminikakasirika, sasa nimetulia. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, MOPROCOinaanza mwezi wa Sita. Matatizo ya MOPROCO yamekwishana nimeshaeleza kwenye kitabu changu kwamba pamojana ku-crush mbegu ita-crush hata mashudu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, MOPROCOinaanza, haina tatizo na Moro Canvas inaanza. Hivi vingineviwanda vya Ceramic, siyo tatizo, tutavishughulikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye viwandavil ivyobinafsishwa, nimeandika kwenye mambonitakayoyafanya kwamba mfumo wa sasa wa kushughulikia

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

viwanda vil ivyobinafsishwa utabadilishwa. Lazimatumhusishe Mkuu wa Mkoa, tuhusishe Wizara ya Kisekta,tumhusishe kikamilifu Attorney General na lazima tuihusisheWizara yangu kama anavyosema bosi wangu wa zamani,jeshi la mtu mmoja. Kwa hiyo, viwanda vilivyobinafsishwandiyo hatma yake.

Mheshimiwa Japhary rafiki yangu, Mheshimiwa Raisamekuja juzi anasema viwanda vya Moshi vifanye kazi. KamaMheshimiwa Rais anasema, mimi nitapingaje? Juzi mtummoja amenipigia simu, anataka Kiwanda cha Viberiti. Kwanini Kiwanda cha Viberiti kilikufa? Mlikuwa mnaagiza viberitikutoka Pakistan vya bei rahisi wakati vya hapa mnaviacha.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumza Waziri waMambo ya Ndani, atanisaidia kuhakikisha smuggled itemshaziingii nchini. Mheshimiwa Mwigulu nami itabidi niendelindo. Ni hilo naweza kuwaeleza kwenye viwandavilivyobinafsishwa. Azma ya Serikali ndiyo hiyo, tunaongezanguvu, kazi ya Treasury Registrer, Wizara za Kisekta, twendepamoja. Mama, viwanda vya Korosho ni chapterinajisimamia yenyewe; tutazalisha na ile kitu ambayo ukiionaunasema astaghfiru Allah. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namba nne; mazingira yakufanya biashara. Mazingira ya kufanya biashara naombanilizungumze hili na Waheshimiwa Wabunge tusikilizane,unajua mtu akitusikiliza, lakini hiki ni kikao cha wakubwa,ndiyo maana hata mitandao mingine hairuhusiwi kusikiliza.Kwa hiyo, wakubwa mnaponyukana huko chumbani,mnanyukana mtu wa nje asisikie.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu akitusikiliza atadhaniTanzania hapafai kuwekeza, hapana! Ni kwa sababutunakopataka siyo hapa. Kwa hiyo, muumini mkubwa wamazingira mazuri ya kuwekeza ni mimi namba moja. Nikipatamuda nitawasimulia. Niliwahi kupoteza kazi yangu nzuri kwasababu ya mazingira mabovu ya uwekezaji.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma report ya dunia yamwaka 2017, wepesi wa kufanya shughuli, Tanzania tunanafasi ya 132, tulipoanza tulikuwa 139 katika nchi 190. Mzaziyeyote akipeleka mwanaye shule, hawezi kufurahi kwambamwanawe awe wa 132; lakini siyo sababu ya kupiga keleleau ya kulalamika kana kwamba kuna mtu kafa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwaambie sababumoja inayofanya Tanzania kuwa ni sehemu ambayo siyo nzuriya kuwekeza. Wale wanaotupima, wanaangalia wepesi wawatu kulipa kodi na ule mfumo wa kodi. Sasa watu wengiwanaojadili wanaangalia upande ule unaolipisha kodi,wanaangalia madhaifu ya TRA, lakini hawaangalii wepesiwa mtu kulipa kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi nyingine zilizoendeleaambazo ziko better ranked, namba moja, namba kumi, mtuanadai risiti, anasema lazima unipe risiti, unioneshe kodi.Hapa, unamwambia andika kwamba hii bidhaa ya shilingimilioni moja, niandikie laki moja halafu, basi, basi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wepesi wa kulipakodi ni kigezo. Kwa hiyo kama ningekuwa mhubiri kamaambavyo mdogo wangu Bashe anaamini ningewaambiatujitazame, tuwe wepesi wa kulipa kodi na tuwaambiewapiga kura na ndugu zetu tuwe walipa kodi wazuri kusudiwawekezaji waje. Mwekezaji makini hawezi kuwekeza katikanchi ambako mmoja analipa kodi, mwingine halipi kodi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, rafiki yangu paleMnyampala anasema, mbona makampuni yamekufa?Mbona biashara inakufa? Mbona maduka yanafungwa?Inaitwa paradigm shift. Kama ulizoea kuleta bidhaa yakohulipi kodi, sasa utaratibu ni kulipa kodi, uta-collapse. Kamaulikuwa unalipa chumba Kariakoo kwa kodi ambayo nikubwa kuliko London, haiwezekani chumba Kariakoo kikazidiLondon, huo unaitwa uchumi bandia. Sasa ni uchumi halisi.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, haowataondoka. Sasa tutahesabu shilingi kwa ya pili, tutajengauchumi imara na mfanyabiashara atakayelipa kodi atawezakustawi. Huo ni upande wa pili wa sisi walipa kodi. Upandemwingine ambao walio wengi na mimi nikiwa Mbungetunausemea ni upungufu wa TRA. Nawaahidi, mimi ni sehemuya Serikali, tutaishughulikia. TRA ina upungufu, tutaiboresha.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma taarifa ya Wizarayangu aliyosimamia Profesa Mkenda, wepesi wa kufanyashughuli Tanzania, walipotu-rank Wazungu na sisi tukaji-rank;unajua mtu akikwambia wewe ni handsome boy, kajiangaliekwenye kioo, kweli wewe ni handsome au anakudanganya?(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Wazunguwalipotufanyia ranking, nasi tukajifanyia ranking wenyewe.Tukatengeneza zoezi la wepesi wa kufanya biashara. Katikakitabu hiki alichokiongoza Profesa Mkenda, kimehusishaWatendaji wa Wizara zote za Serikali, wote wamehusishwa.Kwa hiyo, NEMC kama anakosea, tunasema anakosea; TBSana makosa, ana makosa; TFDA, ana makosa, ana makosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kitabu hiki shangazi,kodi 25 za Kagera zimeandikwa. Rafiki yangu Gimbi anasemaumefanya nini nyumbani? Nimepigana kodi 25 zitoke, ngojaaje Tizeba kesho. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma kitabu hiki kinaelezakwamba kila Waziri aliyepewa mamlaka, yale mamboambayo kutokana na regulations anaweza kuyabadilisha,ayabadilishe. Ndivyo inavyosema. Kwa hiyo, kero zotetutaziondoa moja baada ya nyingine. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge,kwa hiyo, nashukuru mmepaza sauti. Mlitupa jukwaa kamalilivyo, tumeshughulikia. Tuliyoyaona ndiyo hayo, fast trackingof industrialization lakini vikwazo viko hapa, tumemaliza.Kilichobaki ni utekelezaji.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya point tatu hizikatika 25 nitakazozisema, Waheshimiwa Wabunge kwa pointtatu nawaomba mjiandae kwa heshima na taadhima nabashasha na nderemo kunipitishia Bajeti yangu niendekuitekeleza. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Viwanda. Hapana,kwanza niwaeleze viwanda ni nini? Halafu nije niwaelezeSera ya Viwanda. Mheshimiwa Nape na WaheshimiwaWabunge wengine wametaka kujua tafsiri ya viwanda.Shughuli yoyote, viwanda vina tafsiri mbili; i le tafsiriinayohusisha mambo ya construction, uzalishaji wa gesikwamba ni viwanda, mimi si itumiii. Naitumia ile yamanufacturing, ya kuongeza thamani ya kuchukua maweseyakatoa mafuta, mbegu za alizeti kutoa mafuta, cottonkutoa suti nzuri kama niliyovaa leo hii. Hivyo ndiyo viwandaunavyovihesabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ngoja niwaeleze,kiwanda kidogo sana ni kiwanda kinachoajiri mtu mmojampaka wanne; na kiwe na thamani isiyozidi shilingi milionitano. Kiwanda kidogo sana! Watu wanakwenda zaidi,wanasema ukiwa na vyerehani vinne ni kiwanda kidogo.Najua kuna Mbunge mmoja hapa alianza na vyerehani vinne,leo ana vyerehani 30.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Katani, amekuwa mkweli. Amesimamaakawaambia, Mwijage alinielekeza nimekwenda, nimeonanimetekeleza. Waheshimiwa Wabunge, tuambizane. Kamakuna kasungura, umwambie na mwenzako.

Mheshimiwa Naibu Spika, huyo ninayemsemaMheshimiwa Mbunge, alianza na vyerehani vinne, leo anavyerehani 30 na cherehani kimoja ni shilingi milioni tatu, ninetymillion, anaajiri watu wa kutosha. Kiwanda kidogo kinaajiriwatu watano mpaka 49 na kina thamani ya milioni tanompaka 200. Hivyo ndivyo sisi Wabunge tunavimudu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha kati kinaajiriwatu 50 mpaka 99. Shilingi milioni 200 mpaka shililngi milioni800 na hivi Wabunge tunavimudu. Ndiyo vile viwanda vyaakina Mheshimiwa Captain Rweikiza vya kutengenezanyanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kwenye viwandavikubwa, vinaajiri watu 100 na vinatumia shilingi milioni 800na kuendelea, ndiyo viwanda vya akina Mheshimiwa Salum,vya Jambo, ndiyo viwanda vya akina La Cairo, vimo humu.Kwa hiyo, hivyo ndivyo viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niwaeleze Sera yaviwanda ambayo nilizungumza mimi na Mheshimiwa MamaLulida, shangazi yangu. Ni shangazi yangu kweli, tumetokambali shangazi Lulida na wengine waliochangia. Sasaniwaeleze, sifa ya Sera kama walivyosema Wabunge nanimshukuru mtangulizi wangu Mheshimiwa Mama Mary Nagu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera yoyote ina sifa mojakubwa, lazima iishi muda mrefu, lakini na nyie mmechangia,kwamba sera mbona zinabadilika? Kumbe mlisahau,mnataka sera inayoishi muda mrefu, sasa ya 1996 mpaka2020 huu ni muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uzuri wa sera hii kuliko yote,inazungumza mambo mawili ambayo mmeyasema.Inasema viwanda visambae Tanzania yote. Nani hatakiviwanda visambae Tanzania yote? Kama imepitwa nawakati, kwa hiyo, tuibadilishe viwanda vikae sehemu moja?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia inasema kwambamikoa ya pembezoni ipewe vivutio; kwamba pamoja navivutio kwa wawekezaji wote, lakini mikoa ya pembezoniipewe more incentives. Kuna ubaya gani? Huwezi kwendakuwekeza Kigoma bila kupewa incentives za ziada! Ni mbalisana! Uipiganie ndugu yangu Wamugabwa. (Kicheko/Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndiyo hiyo Seraya Viwanda ya Mwaka 1996 mpaka 2020. Kutokana na Serahii, tumetengeneza mkakati wa integrated au fungamanishola maendeleo ya viwanda, kutokana na Sera hiitumetengeneza vision ya 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka wakati huomimi nilikuwa officer, Mwenyekiti wangu wa Bodi ProfesaMwandosya akiwa yeye anashiriki kwenye timu iliyotengenezavision ya 2025, tumetoka mbali. Nilikuwa nabeba mkoba,sera hii inatengenezwa. Sasa ni mimi, Mr. mimi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, msambao wa viwanda.Viwanda vina namna mbili. Sera inasema viwandavisambae; wawekezaji wanapokuja, Serikali au Waziri uwezowangu wa ushawishi kiwanda kiende wapi ni mdogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wawekezaji wanaokuja siyombumbumbu, wawekezaji wanaijua Tanzania kulikotunavyoijua sisi. Akija Mjerumani anajua madini yako wapi.Labda wamwondoe Profesa Muhongo mtaalam wamiamba, lakini mwingine anakuja anakuonesha dhahabuziko hapa. Ndiyo maana kila mara wanakuja wanajidaikwenda kuangalia makaburi ya babu zao. Wanaangalia yakemambo waliyoyaweka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, viwanda viko vyanamna mbili, FDI, nina influence kidogo ya kueleza ziendewapi. Kuna LGI (Local Grown Industries), ndipo tunapokwendakwamba unaanza na kiwanda kidogo sana, unakileakinakwenda kuwa kiwanda kidogo, kinakuwa kiwanda chakati na kiwanda kikubwa. Mdogo wangu MheshimiwaKitandula, ni mdogo wangu kabisa, tumefanya kazi wote,nimemlea, nimemfundisha kazi, tumefanya kazi wote. Polesana na Tanga Fresh.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Kitandulaangeniambia kwamba barua yake iliyokwenda Hazinahawakushughulikia ningeshakwenda mimi. Naombaanikumbushe nitakwenda Hazina huyo aliyekata aniandikiemimi, I am a Minister, kwa nini alinyamaza? Mimi nilisemamtu huyu hana hatia afunguliwe, yeye akakaa na baruaakanyamaza. Angeniambia ningemwambia Mzee Mpango,huyu ni mtu wa Mungu anaelewa. Unajua MheshimiwaMpango watu hawamwelewi, unamtegea wakati anatokakusali unamwambia shida yako, atakusainia tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, viwanda vidogosana, vidogo na vikubwa ndivyo viwanda tutakavyokwendanavyo ila watu wanavidharau kwa neno la viwanda vidogo.Waheshimiwa kiwanda cha shilingi milioni 200 kinazaa sana.Angekuwepo Mheshimiwa Katani angewaelezamchanganuo na namshukuru sana Mheshimiwa Katani hatausiku nimemuota. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Katani,amenikumbusha Profesa Aba Mpesha, Baba Mchungaji wakutoka Michigan University aliyenifundisha biashara ndogona viwanda vidogo, aliyefanya utafiti wa korosho, watu wakorosho, wanasiasa wa Mtwara ndiyo waliomwekeamtimanyongo. Kama mnamtaka naweza nikampigia simuakatoka Michigan akaja, lakini kama mmejirekebisha.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwaeleze,wawekezaji wanakuja kule kwenye Mikoa na Halmashaurimnawawekea mtimanyongo kama ile kesi yangu ya Tabora.Mwekezaji ametoka China yupo uwanja wa ndege watuwakapiga figisu, wakamwambia umekuja Tanzania hupaswikwenda Tabora, Tabora siyo Tanzania, yule Mchinaakashangaa akarudi kwao. Inabidi niwaambie kusudimwelewe tunayoyapata. Nichukue nafasi hii kumwombeakijana wangu Mheshimiwa Heche apone vizuri aje afanyekazi, tunafanana sura lakini ana pilikapilika nyingi. (Makofi/Kicheko)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwaambie suala laHeche limekwisha, wale wawekezaji watakuja, mkitakataratibu nitasimamia mimi wawekeze Tarime. Yaleyamekwisha na nikitoka hapa nakwenda Dar es Salaamnikazungumze naye, mwambie afanye kazi moja mamboyamekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba niwaelezeWabunge kuwapata wawekezaji ni shida, msiwaseme nenobaya na Tanzania si nchi peke yake ya kuwekeza. Miminapoteza wawekezaji wanakwenda Zimbabwe,Mozambique, Ethiopia, Rwanda na baya zaidi wanakwendakuzalisha Rwanda kusudi sisi tugeuke soko, msiniumize.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaeleza FDI na LGI,LGI ndiyo inaweza kusambaa nchi zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwongozo wa Tawala zaMikoa, tutafanya nini? Nimewaahidi kwenye hotuba yangutunamalizia mwongozo, Wakuu wa Mikoa tutawapamwongozo. Hii imetokana na nini? Baadhi ya Wabungewananilaumu kwamba mimi napendelea mikoa fulani namingine naiacha, tarehe 28 nakwenda Tanga. NiwaelezeWabunge wa Tabora, Mheshimiwa Mwanry ameshafanyabooking kwamba nikapige kongamano kule. MjiandaeWaheshimiwa wa Tabora, tupige kongamano nanimemweleza Mheshimiwa Maige rafiki zake wa Genevaawaambie na wenyewe waje watuletee viwanda twendeTabora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naletamwongozo kwa sababu imekuwepo kutolingana kati yamkoa na mkoa. Ukifungua Facebook ni Simiyu, WhatsApp niSimiyu, sasa tunataka kuwaambia Wakuu wa Mikoa wotewaingie kwenye Facebook na Instragram na mitandao yote.

WABUNGE FULANI: Eeeeeee. (Makofi/Kicheko)

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Ndiyo, wawekezaji wanatafutwa, kwa hiyo, nitatoa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

mwongozo wa kuweza kutekeleza hilo. Kwa hiyo, mwitikiowa mikoa haulingani lakini haya ni maelekezo ya MheshimiwaWaziri Mkuu, tutaandika mwongozo, nitauweka dibaji mimi,ataweka dibaji Mheshimiwa Simbachawene na Mkuu yeyoteataweka dibaji twende mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, kasi ya ujenzi wa viwanda,nimeilezea fast tracking. Jukumu la ujenzi wa viwandalinatafsiriwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda seti kubwana ujenzi wa viwanda vya subset. Sekta binafsi ndiyo itajengaviwanda, Serikali inaweka mazingira wezeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaeleza katika kipindiambacho Mheshimiwa Rais yupo madarakani, viwanda vyasekta binafsi kwa address humu yaani mpaka wenye viwandanimewawekea simu zao, wamejenga viwanda kwa mtajiwa shilingi trilioni tano, una mashaka wapigie simu, lakininimeweka picha na beacon za mahali walipo unawezakwenda ku-trace. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini napenda niwaambiemimi siyo saizi ya kuzalisha viwanda vya shilingi trilioni tanokwa mwaka mmoja, I want more, ndiyo maana nikaleta fasttracking, ndiyo maana nikazungumzia kuweka mazingirabora ya biashara. Kwa hiyo, nashukuru na nyie hamridhiki siosaizi yetu tunapaswa kukimbia. Hatupaswi kuwa soko la watuwengine, tunapaswa kuzalisha tuwauzie watu wengine.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ulinzi wa viwanda.Niwashukuru Waheshimiwa wote waliozungumzia kuhusuulinzi wa viwanda. Sitaki kurudi nyuma, nimeshampongezaKivuli changu, unajua ukiona Kivuli kina mashaka hata namtu mwenyewe ana mashaka, sasa Kivuli changu ni kizurisiwezi kusema zaidi, lakini Nunua Tanzania inaendelea.Mwaka jana ilipigiwa sana kampeni na Mheshimiwa Makamuwa Rais alipozindua 620GS1 lakini tulipokwenda kutoa awardza Brand 50 mshindi akawa Alaska Rice, huyo mama AlaskaRice ni mke wa Mheshimiwa Bashungwa, Mbunge mwenzetu,anatengeneza branded product zinapendwa Dar es Salaam

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

Supermarket zote. Hata pilipili, watu wanaokwenda kununuawanasema nataka ile pilipil i ya Alaska, branded naMheshimiwa Mbunge. Jamani Wabunge muwemnaambizana tunaishi vipi siyo tunakuona unaendeshamtambo mkubwa hutuambii, tuambizane. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ulinzi wa viwandatunauzungumzia. Ulinzi wa viwanda upo chini ya TBS, FairCompetition na upo chini ya Polisi. Niwahakikishie taasisizilizopo chini yangu zitafanya kazi sasa kuliko wakati wowote.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimehakikishiwa nisemeninachopewa na mimi nimekwenda kuwaambia wakubwa,bidhaa feki inapita, nimezungumza wakaniambia semaunachotaka nimewaambia, kwa hiyo, tutafanya kazi.Niwaeleze wawekezaji wengi kwa mfano kwenye sukariwalikuwa wanakataa kwa sababu ya sukari inayokuwasmuggled in, kwa sababu ya mchele ulikuwa smuggled in,sasa watu wana confidence baada ya ku-control. Hata hivyo,namwomba Mheshimiwa Mwigulu tu-control zaidi bado,bado, bado. Kwa hiyo, vitu vya feki na qualitytutalizungumzia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie fungamanishola viwanda na sekta nyingine. Waheshimiwa Wabunge kunafungamanisho kuliko maelezo. Ukisoma mkakati wa pambampaka mavazi ni fungamanisho. Ndiyo maana Waziri waMambo ya Ndani, Mheshimiwa Mwigulu huwa ananiitapacha. Ni kwamba mimi ndiye niliyebuni mradi wa viatu waKaranga lakini mwenye dhamana ni Waziri wa Mambo yaNdani. Nilijua tukitengeneza viatu Magereza vitasambazwakatika majeshi yote na yule mzalishaji anapata soko lakuanzia, kuna fungamanisho hapo. Soma mkakati wapamba mpaka mavazi kuna fungamanisho, soma mkakatiwa alizeti kuna fungamanisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa maziwa, somaRipoti ya SAGCOT inazungumzia mradi wa maziwa. Nikiri kwamasikitiko kwamba hatufanyi vizuri kwenye maziwa, lakini

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

mambo ya Tanga Fresh tutayashughulikia na viwanda vinginevianze. Niwaeleze jambo moja, ASAS ana kiwanda chenyeuwezo wa kuchakata lita 50,000 kwa siku lakini maziwaanayopata ni lita 12,500. Kwa hiyo, kuna haja ya kuwezakuwasaidia watu wa Nyanda za Juu Kusini kuweza kuzalishamaziwa zaidi na chini ya hapo atakuja aeleze Waziri waKilimo ndiyo tunakuja na mpango wa SAGCOT wa kuletaIFAD kutoka Ulaya kusudi waende kule. Sitaki kusoma hotubaya mwenzangu ngoja aje aseme mwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya kipaumbele,nitafika baba ikibidi nitaomba muda. Ipo hoja ameulizaMheshimiwa Mbunge, jina lake nimelisahau kidogo ila ame-declare interest kwamba yeye ni mwana Tanga na mimiTanga nakwenda tarehe 28, kwa hiyo, huenda tutakutanahuko. Nakwenda kupiga, mnaita sound, kuhamasishaviwanda, anasema tuwe na kipaumbele. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Saruji chaSimba, kimeongeza uwezo kwa tani 750,000, ndiyoalichokizungumza Mwenyekiti wa Kamati yangu kwamba ilenafuu waliopaswa kupewa haijatoka. Mwenyekiti wa Kamatina wewe ni sehemu ya Serikali waambie watu wa Tangawalete karatasi zao tutakwenda Hazina wanieleze mimi kwanini hawatoi. Kama mtu amewekeza na tani zinaonekanakwa nini msimpe? Halafu unajua watu sijui kwa nini,mkikwama huko mje kwangu, mimi ndiyo Waziri mwenyedhamana nitawapeleka huko mnakoshindwa kufika.Wanasema huwezi kwenda kwa Baba mpaka upite kwaMwana, Mwana ni mimi. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ukisoma mkakatiwa fungamanisho la viwanda, Mheshimiwa Mbungealiyesema hatuna kipaumbele, kwenye mkakati wafungamanisho la viwanda imeelezwa na hicho kiwandakingine cha Tanga kitazalisha tani milioni saba, kitawaajiriwatu milioni nane na 60% ya saruji itauzwa nje ya nchi, sisitutabaki na 40%. Kinawekwa jiwe la msingi, kwa sababu sinamamlaka ya kutamka kinawekwa jiwe la msingi mwaka huu,kitapata vivutio.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwaaliyesema kwamba hatuna vipaumbele asome mkakati wafungamanisho la viwanda liko kwenye website yangu.Tutaweka kwenye viwanda vya sukari, Mkulazi tani 2000,Mbigiri 30,000, tutapanua Kagera Sugar na Kilombero. Juzimbele ya Mheshimiwa Rais nimemueleza Mheshimiwa Zumakwamba aisaidie Ilovo iongeze Kilombero One na KilomberoTwo waache kutonunua miwa ya wananchi, kwa hiyotumeyazungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika hilo kunapamba, mafuta ya kula ya alizeti, ngozi na bidhaa za ngozina matunda. Kwa matunda ndiyo tunazungumza naKiwanda cha Matunda cha Sayona. Nimewasikia Nduguzangu wa Tanga, tunazungumzia Kiwanda cha Eveline lakinitunazungumzia Kiwanda cha Matunda cha Handeni, kwahiyo, tunaendelea na imeainishwa. Tunazungumzia maziwa,tunaweza kuwa hatujatekeleza kama alivyosemaMheshimiwa Kitandula lakini ndiyo dhamira yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunazungumziwa viwandavya nyama, watu wa Manyara mwambie yule mwana mamaaliyekuwa na matatizo ya kiwanda chake cha nyama,matatizo yake yameainishwa kwenye Ripoti ya ProfesaMkenda. Wale waliokuwa wanamkwamisha, sitakikuwasema wasijisikie vibaya wakashindwa kula, dawa yaoimeshapatikana aje tumpeleke wampe nyaraka zake.Unamkwamisha mtu na kikaratasi asitengeneze kiwanda chanyama, ng’ombe wanakwenda Kenya wanarudi,ningependa tuwe wawazi tuambizane. Hicho ni kiwanda chaChobo Investment kipo Mwanza, anachinja ng’ombe 600 kwasiku, kijana amejaribu. Matatizo yako yote watayasema keshokwenye Wizara inayohusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu viwanda vyachakula na katika hili niwaeleze, nimekuwa nikisema hapaBungeni, nikiwaambia Waheshimiwa Wabunge hakunasababu ya kutoa mahindi Katavi kuyapeleka Dar es Salaam,msage mahindi kule, mfanye packaging vizuri, muwekekwenye maroli mpeleke sokoni. Ndiyo maana nachukua fursa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

hii kumpongeza Mheshimiwa Aeshi ametengeneza kiwandakikubwa sana cha kusaga nafaka na zitakuja sokoni.Waheshimiwa tuambizane, kama umewekeza mwambiemwenzako wewe umepata wapi namna, tuelezane. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa na rafiki yangummoja Kenya nilipotaka kuingia kwenye siasa nikamuagaaliniuliza Mwijage utaziweza siasa. Nikamwambia nitaziweza,I can talk. Akaniambia politics is not about talking.Akaniambia ninyi Watanzania mna tatizo moja. Akaniulizaadui yenu ni nani? Nikamwambia umaskini. Akaniambiambona mnaogopa utajiri? Ukikutana na mwanasiasa waTanzania ukimwambia wewe tajiri anasema mimi maskinibwana, hapana! Mheshimiwa Aeshi amejenga kiwanda chamfano cha kutengeneza nafaka, tunataka hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wanasema sembenzuri inalimwa Ileje. Mheshimiwa Mbunge wa Ileje, jasiria, SIDOwanakuja weka kiwanda Ileje, mjini tunataka watuwaondoke warudi shamba, zile by-product, mmetoa mfanomzuri wa pumba zibaki kule. Akinamama wapepetemahindi, wafanye packing, wakaangalie watoto wakimalizapumba wawape mifugo, nazungumzia mifugo ng’ombesizungumzii astaghfiru Allah. Unajua kuna wengine pumbawanamlisha astaghfiru Allah, hapana. Wamlishe ng’ombeakamuliwe maziwa, akikamuliwa maziwa mama auze namtoto anywe. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, maamuzi yaSerikali ni kwamba ziliko rasilimali ndiko vitajengwa viwanda.Ndiyo maana Mheshimiwa wa Simiyu, maamuzi yamefanyikakiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na pamba nimeandikakwenye ripoti kitajengwa Simiyu kitatumia pamba tani milioni50 na kitatuokoa na aibu ya kuagiza vifaa pamba toka nje.Tuna aibu nyingi na tutazimaliza. Tunaagiza hata drip ile yakumwekea mgonjwa kutoka Uganda, hizo aibu zotetunazifuta. Soma ripoti hiyo, mimi aibu zote nimezianikakusudi mnione halafu mnipange vizuri.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

Mheshimiwa Naibu Spika, nayasema yote haya iliWaheshimiwa Wabunge wasiwe na tatizo la kuangaliavifungu ila wakubaliane tupitishe moja kwa moja. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ni petrolchemicals. Petrol chemicals ni vile viwanda vya MheshimiwaMuhongo. Kiwanda cha Ferrostaal Mheshimiwa Muhongoamekwenda zaidi mpaka ametaja tarehe ya kwenda Kilwana mimi nimeshapata mwaliko kutoka Ujerumani, Profesanitakuwa karibu na wewe. Unajua watu siku hiziwananichanganya na mimi wananiita Profesa, kwa hiyo,tutakuwa wote. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kiwandaFerrostaal karibu kitaanza na kiwanda cha Helium kitaanza,kwa hiyo ni petrol chemicals zimeandikwa. Nawaelezavipaumbele mvijue kwa sababu uwekezaji katika kiwandacha mbolea utatuwezesha kuzalisha mbolea tani 2,600,000katika viwanda viwili wakati mahitaji ya mbolea Tanzaniamnatumia tani 400,000. Kwa hiyo, is a break throughtutatumia mbolea zaidi, tutapata tija na viwanda vitafufuka.Ni kwa uwekezaji wa namna hiyo kuongeza tija ginnerieszitafufuka, akina Manonga watafufuka pamba ikizalishwakwa wingi na tukawa na viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya uwekezaji,Kurasini Logistic Centre. Kama nilivyoeleza kwenye ripotiyangu inatengenezwa. Mheshimiwa Ngwali, Kurasini LogisticCentre haiwezi kufika mwezi Julai. Nichukue fursa hiikuwaeleza watendaji ninaofanya kazi nao, mimi huwanasema wazi, nimeshamwambia Waziri Mkuu kwambaperformance ya EPZ si nzuri kwenye Kurasini Logistic Centre.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaandikia memoMakatibu Wakuu wangu kwamba I am not happy na speedya EPZ on Kurasini, nimeshamwambia Mheshimiwa WaziriMkuu baada ya hapo ni kwenda kwa tajiri. Naitaka KurasiniLogistic Centre ianze, namna nilivyokaangwa hapa na rafikiyangu Mheshimiwa Ngwali siwezi kukubali mimi ni mtumzima. Kurasini Logistic Centre tutakuwa na nafasi nzuri kabla

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

ya Bunge kuwaambia ni kitu gani kinafanyika, ikibidi kuitishaBodi nitaitisha Bodi. Naitaka Kurasini Logistic Centre, mimi nimtu wa Temeke nani asiyejua bwana, Mbunge wangu yupohapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bagamoyo SpecialEconomic Zone, bandari ipo na itachimbwa na mwekezaji.Nimeulizwa kwa nini tumetaka private sector ilipe fidia? Mimiwazo hili nimelipeleka kwa wakubwa nikajenga hojawakanikubalia. Wewe mtu umemthamini mwaka 2008unamlipa kidogo kidogo huwezi kuona, tena Kamati yangundiyo iliniambia kwamba Mwijage itakuhitaji miaka 30kumaliza, basi nikawaomba wakubwa tutafute private sectorwameingia lakini malipo yote tutayasimamia sisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze nimepata baruasasa hivi, kuna mwekezaji nguli kutoka China ananifuatahapa anataka nimpe eneo la kuweka Special Economic Zone.Nimeshawaeleza watu wote tunaofanya kazi pamoja, watuwa EPZA, Makatibu Wakuu mnahusika, huyo Mchina hataasiponiona mimi mpelekeni Bagamoyo, mpelekeni Kibaha,ninazo hekari 5,000 Kibaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze watu wa Pwani,Mheshimiwa Subira Mgalu na Wabunge wote sijawahi kuonaukarimu kama wa Pwani. Mkuu wa Mkoa anachosemandicho anachosema Diwani. Unajua ngoja niseme niokokena nitakayemsema msimchukulie hatua yoyote. Watu waMorogoro waliniangusha na nimemwambia Mzee Mbena.Nimemleta mwekezaji toka Singapore amefika paleMadiwani wanatokea huku wanakwenda huku, tumepotezaviwanda vitano kutoka Mauritius juzi vyenye kuweza kuajiriwatu 7,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, niliwaambia nina kiwanjaMorogoro, wakienda Morogoro wanatokea hapa wanaingiahapa, mara umeme mara nini. Umeme hauwahusu, umememniambie mimi, mimi Mzee Muhongo naongea naye wakatiwowote, substation ni shilingi bilioni tatu, mbele ya kuingizawawekezaji watano wanaozalisha ajira 7,000 ni kitu gani?

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

Mheshimiwa Devota nisaidie hilo, acha longolongo namambo ya master plan tunataka eneo lile. Kwa hiyo,Bagamoyo itatekezwa na watu watalipwa haki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, TAMCO Kibaha,tunaendelea kutekeleza. Maeneo ya mikoani, Kigoma naSongea kwenye bajeti nimewaweka. Kwenye bajeti inayokujanaomba mnitendee haki msome vitabu vyangu. MheshimiwaSpecial Economic Zone, nimesaini kwa mkono wangu SpecialEconomic Zone nane za sekta binafsi, kwa hiyo, Serikaliinapenda sekta binafsi. Nitambue nafasi ya WaheshimiwaWabunge walioniahidi kunipa maeneo, Mheshimiwa Bashetaratibu, kama sikuwekeza leo na kesho ipo, wewe niombenibaki kwenye nafasi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuwezesha SME, SIDO, TBSna TanTrade wamekuwa wakiwezesha SME. Ninachotakakuwaambia hatutalegeza viwango hasa kwa walewatengenezaji wa chakula, TFDA atashirikiana na TBShatutalegeza viwango. Ila katika maelekezo ya Serikali zaMikoa mnapotenga maeneo wale akinamama, watuwamehoji nimesema nini kwa akinamama, akinamamamuwajengee mabanda ambayo TBS atawapa mafunzo. TBSatakupa mafunzo na certificate na gharama za certificateatalipa yeye mpaka utakapokuwa mjasiriamali mwenyenguvu. Nimetoa maagizo na mamlaka inaniruhusu kufanyahivyo, akinamama niwapende zaidi ya hapo niwapendenamna gani? (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuongeza hisa kwenyemakampuni. Jambo ambalo nimekuwa na ushawishi naloni Urafiki. Mwekezaji wa Urafiki amekubali kupunguza hisazake alikuwa na hisa 51. Majadiliano yanaendelea,wanafanya valuation na tumeshapata wawekezaji waTanzania. Kwa hiyo, hicho ndicho naweza kusema kuhusuUrafiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu TANALEC, sinamamlaka nayo ila mimi nawashawishi TANALEC waendekwenye Dar es Salaam Stock Exchange. Hata hivyo, katika

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

kulinda uchumi wa viwanda Mheshimiwa Muhongoalishasema na kwenye tenda zake amesema transformer nacables zote zote kwenye REA Awamu ya Tatu zitanunuliwaTanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge,orodha ya viwanda ni kubwa, kuna kiwanda kimejengwaTanzania cha kutengeneza waya, kina uwezo wakutengeneza kilometa 100 za waya kwa masaa nane kikoMwenge. Viko vitatu kimoja kiko Nigeria, kingine kikoMwenge na kingine kiko South Africa, ni kijana mdogoukimwona hutaamini.

Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya makaa yamawe. Mheshimiwa Profesa Muhongo amezungumza lakinimojawapo ya faida ya kutumia makaa ya mawe ya Tanzaniayamechangamsha uchumi. Pale wanapopita wenye malori,mama ntil ie anapika lakini spea na mechanicwanatengeneza Watanzania. Naomba mtuelewe,tumefanya hivyo kwa nia nje lakini hali hiyo imefanya wenyemigodi waone kwamba kuna soko wamefungua migodiyao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie korosho.Maelezo aliyozungumza comrade Mwambe, unajua ukiwacomrade hata ukijipaka matope mtu akikuangalia tumichango yako ni ya ki-comrade tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, michango yakeMheshimiwa comrade na mchango wa Profesa Masawe waNaliendele tutaufanyia kazi na tutamuunganisha na COSTECHkusudi zile bidhaa zinazotokana na korosho tuweze kuzitumia.Suala ni research na Profesa Masawe amefanya research,kuna bidhaa nyingi, brake lining na kile kinywaji ambachowewe ukikiangalia unasema astaghfur Allah lakini kinaingizapesa. Kwa hiyo, vyote hivyo tutavishughulikia na naombatuendelee kufanya kazi wote. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kipekee kunafaida kwa kuchambua korosho hapa ndani

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

tunaposhughulikia viwanda vilivyobinafsishwa. Kamaalivyosema Mheshimiwa Kitandula zile export levy, mabilioniyale, tutakaa tuwaulize wenye dhamana kama tunawezakuchukua viwanda vya kuanzia kusudi msimu unaokujatuweze kuanza na baadhi ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la CBE. MheshimiwaMwita ameleta suala la CBE akalipitisha kwa MheshimiwaNgwali akaona haitoshi akalipitisha kwa MheshimiwaMwambe akaona haitoshi, ikanipa shida. Nikaenda kutafutaRipoti ya CAG.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya MheshimiwaWaitara ni kwamba waliokwenda kukagua CAG hakukaguaDar es Salaam. Nakala niliyo nayo iliyowekwa lakiri na CAGanasema yeye CAG alikagua Dar es Salaam, lakini kwamamlaka ya kiutawala, Waziri nikishapata ripoti, siruhusiwikufanya lolote kwa watendaji napitia kwenye Bodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waitara najuayeye amesoma sayansi mambo ya utawala hayajui. Ukiingiliamoja kwa moja watendaji bila kupitia kwenye Bodi akiendamahakamani anakushinda. Kwa hiyo, mimi nimepata ripotiyangu nitaiandikia Bodi na itachukua action isipochukuaaction ndio mimi kwa mamlaka niliyonayo au kwa mamlakaya uteuzi naweza kuchukua hatua. Nimhakikishie I have thereport anaweza kuisoma, nimemshikil ia kwa sababuimeandikwa siri na yeye siyo mmoja wa siri, sisi ndiyo watuwa siri, kwa hiyo mambo ndiyo hayo CBE Dar es Salaamilikaguliwa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la TangaFresh…

MHE. CECIL D. MWAMBE: Umeshalizungumza.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Nimeshalizungumza, ahsante sana kama mmeridhika.Ahsante sana Mheshimiwa Mwambe.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo,naomba nihitimishe kwa kuwashukuru kwa namna yakipekee Waheshimiwa Wabunge na kupitia kwenuWatanzania wote ambao tunawawakilisha kwa ushirikianomnaotupa katika kuendeleza sekta yetu na hususan ujenziwa uchumi wa viwanda. Wizara daima itaendelea kuwasikivu, kupokea mchango wa mawazo na ushaurikatika kuboresha utendaji wa Wizara na sekta kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe kuendelea naushirikiano huo katika kuhakikisha kuwa rasil imalitunazozipata zinatumika kwa umakini mkubwa ili mipangona mikakati ya sekta iweze kuleta matokeo chanya katikakufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Ni dhahiri kuwaushiriki wa sekta binafsi na uthubutu wao ni nyenzo muhimukatika kuleta mageuzi na matokeo yenye ushindaniutakaotokana na juhudi za uendeshaji na uanzishwaji waviwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo, biasharandogo pamoja na uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni jukumu letu tukiwa ndiyowawakilishi wa wananchi wetu kuwajengea ufahamuwa mipango, sera, mikakati mbalimbali ya kisektaili kuwaongoza ipasavyo katika ujenzi wa Tanzania yaviwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hojaimeungwa mkono japokuwa nilitaraji kwa makofi yale Bungezima lingekuwa limesimama. Tutaendelea na taratibuzinazofuata, Katibu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

NDG. CHARLES MLOKA- KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 44 - Viwanda

Kif.1001- Administration and HR Management….......................Sh.11,838,840,000/=

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kifungu hikindicho chenye mshahara wa Waziri na nina orodha ndefukabisa hapa ya watu wanaotaka kushika shilingi. Tutaanzana Mheshimiwa Deo Sanga, huyu anatoka CCM.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali lakinimasikitiko yangu ni kwamba, yale niliyochangia jana yaanihapa nilipo hata machozi yanataka kutoka, kweli kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kauli ya Serikali kwafidia niliyosema jana ya wananchi wa Makambako ambaowameteseka kwa muda mrefu zaidi ya miaka 16hawajalipwa fidia yao. Kama nilivyosema kwamba kwenyebajeti ya mwaka 2016/2017, waliwekwa kulipwa hizi fedhaambazo muda unakwisha Juni ambayo ni kesho kutwa tu.Kwenye bajeti hii ambayo tunaipitisha leo hapa ya mwaka2017/2018 hawajawekwa. Kwa hiyo, naomba kauli ya Serikalini namna gani watalipwa fidia kama nilivyosema?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nilisema jana piatunaomba tupate kauli ya Liganga na Mchuchuma ni kitugani kimekwamisha kwa mwekezaji huyu ambaye tayari yukopale na fedha za kulipa fidia zipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pasipo kupata kauli yaSerikali naomba mniunge mkono nashika shilingi. Naombakauli ya Serikali, Waziri wa Fedha yuko hapa, nimesema…

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umekwisha.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Kanuni zetukuhusu mshahara wa Waziri, Kanuni ya 101(3) ili tusipate tabukipindi hiki nitawasomea kwa haraka inasema hivi:-

“Mbunge atakayeamua kutumia kifungu chenyemshahara wa Waziri, ataruhusiwa tu iwapo ataomba ufafanuziwa suala mahususi la sera na hatazungumzia zaidi ya jambomoja”. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, kwenyemshahara wa Waziri kwanza ni jambo moja lakini pia liwe lasera. Sasa Mheshimiwa Sanga hapa amezungumzia mambomawili la kwanza halikuwa la sera, kwa hiyo MheshimiwaWaziri endelea na suala la pili.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti…

MWENYEKITI: Mheshimiwa mtoa hoja, MheshimiwaWaziri wa Nishati na Madini alikuwa amesimama.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: It’sokay.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa NaibuSpika, nadhani Mheshimiwa Sanga hakuwepo labda wakatinilikuwa naelezea suala la Liganga. Jamani kwanza hapakuna suala la teknolojia ilivyobadilika. Mara ya kwanza sisiWatanzania tulitaka chuma kwa ajili ya kupeleka nje ya nchi,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

tukawa tunang’ang’ania iron. Sasa ukichukua madini yaleni kwamba kuna iron ndani yake kuna titanium halafu kunavanadium, hivi vitu vitatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i le model wakati sisitunaanza tulikuwa hatujui kwamba vanadium na titaniumitakuwa na faida kubwa sana duniani. Titanium sasa hiviukienda kwenye mambo ya ndege ndiyo ipo, vanadiumvilevile ndiyo inatengeneza hata dawa za blood pressurehata mambo ya moyo. Hii titanium yenyewe ni nyepesi lakinini ngumu kuzidi hata chuma. Kwa hiyo, huyu mwekezajimuda mwingi aliouchukua ni namna ya kuja kutenganisha,hizi ni melting point yaani atenganishe titanium, vanadiumna iron, hilo ni la kwanza linachukua muda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, lilikuwa ni kwamba,kwa sababu miradi iliungaishwa pamoja na makaa ya maweyeye akawa na model kwamba atatumia yale makaa yamawe kwa ajili ya smelting, vilevile atauza umeme. Kwa hiyo,kwenye mahesabu yake ilikuwa atengeneze fedha kutokanana umeme aje kuweka kwenye mgodi. Sasa ndiyo maanatukamwambia, wakati huo hesabu zake alizozileta zilikuwaUS sent 13 kwa unit lakini duniani tunajua umeme wa makaaya mawe ni kati ya senti sita mpaka nane, kwa hiyo, inabidiarudi kwenye hiyo model.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyingine alikuwa anatakakuzalisha megawati 600, 300 atumie na 300 aweke kwenyegrid. Kwa hiyo, tunachokisema inabidi vilevile tu-revisit, turudievile vivutio tulivyompatia lakini vile vivutio tulivyompatia nilazima tuje hapa Bungeni tubadilishe sheria.

MWENYEKITI: Ahsante sana Profesa. Mheshimiwa DeoSanga.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamojana maelezo ya Mheshimiwa Waziri bado nakusudia kushikashilingi kwa sababu katika maelezo yake hajaeleza sasanamna ambavyo wale walivyokuwa tayari kulipa fidia nafidia nazo wamesimamisha kwa sababu ya kufanya utafiti

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

huo ambao ameelezea Waziri? Kwa sababu wale wananchiwalikuwa tayari wanasubiri kulipwa fidia ambayo mwekezajialikuwa tayari kuilipa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naendelea kushikashilingi naomba wenzangu mniunge mkono.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sanga hoja iliyoko hapaMezani sasa hivi ni ile ya Mchuchuma na Liganga kwa sababuhiyo ya fidia haikuwa ya kisera. Sasa kama unashika shilingiutoe maelezo sekunde thelathini kuhusu hoja ya Liganga naMchuchuma kwamba ndiyo unashika shilingi baada yamaelezo ya Profesa. Hiyo hoja nyingine haipo mezani sasahivi.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, unajuani lugha tu jambo ni lile lile. Ni namna gani Mchuchumaitaanza, naomba kauli ya Serikali hapa ndiyo maananimeomba wenzangu mniunge mkono, naendelea kushikashilingi.

MBUNGE FULANI: Toa hoja.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoahoja.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hojahaijaungwa mkono.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,imeungwa mkono.

MWENYEKITI: Inaungwa mkono na idadi ya Wabungekadhaa, sasa hapa mlisimama sijui mko wangapi, naonandiyo mnaanza kuota kidogo. Kama mnataka kuungamkono hoja mnasimama wote, kwa sababu huwezi kuwaunasimama mmoja, mwingine na mwingine. Sawa, hojaimeungwa mkono, naomba wale ambao hawahitajikuchangia wakae ili tuone akina nani wataweza kuchangia.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

Mheshimiwa Deo Ngalawa, Mheshimiwa StanslausNyongo, Mheshimiwa Mary Nagu, Mheshimiwa ProfesaMuhongo na Naibu Waziri wa Fedha. Tunaanza naMheshimiwa Deo Ngalawa.

MHE. DEO F. NGALAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nikushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia hoja hiina naunga mkono hoja iliyoletwa na Mheshimiwa DeoSanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makaa ya mawe yaMchuchuma na chuma cha Liganga ni mkataba ambaotayari ulishaingiwa kati ya Serikali ikiwasilishwa na NDCpamoja na mbia. Mheshimiwa Waziri amejaribu kuzungumziasuala la utenganifu wa madini ya titanium na vanadium.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umekwisha,Mheshimiwa Stanslaus Nyongo.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Nami naungana na Mheshimiwa MzeeSanga hapa ni kwamba, sisi tulifuatil ia hil i suala,tulichoambiwa ni kwamba, Government Notice haijatoka,mwekezaji yupo na ana pesa za kutosha ili aweze kuendeleana uwekezaji. Sasa leo tunasikia tena kumbe kuna masualaya ku-separate kati ya chuma na madini mengine. Tunaombacommitment ya Serikali, lini watatoa hiyo Government Noticeili huu mradi uweze kufanya kazi? Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Sanga kwa sababumwekezaji ambaye yupo tumemchagua kutokana na uwezowake wa kutenganisha titanium na vanadium kutoka kwenyeiron na ana uwezo huo jamani, ila sasa yale mambo yaincentive yamalizike na iron ianze kutengenezwa. Hatuwezi

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

kuwa nchi ya viwanda bila kuwa na chuma na chuma hikijamani duniani hakipo, kipo karibu na mkaa. Naombatusipoteze muda na sisi tutarudisha hiyo shilingi kamacommitment ya Serikali itatoka ya kutoa Notice. Nashukurusana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi hii. Naomba tunimwombe Mheshimiwa Deo Sanga, kutokana na maelezoya kitaalam aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri wa Nishati naMadini, aachie shilingi. Nimwambie ni azma ya Serikali yetukuhakikisha kwamba uchumi wa viwanda unakamilika naunasimama ndani ya nchi yetu. Pamoja na mambo yakitaalam aliyoyasema Mheshimiwa Waziri wa Nishati naMadini, lakini katika masuala ya kodi Serikali inaendeleakufanya analysis kwa umakini wa hali ya juu kuhakikisha sualahili linakaa vizuri kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano mmoja tu katikaSheria ya VAT, mwekezaji tunayemsema kwa sasa alitakaaruhusiwe kukusanya na kutumia Kodi ya Ongezeko laThamani kwa miaka 15, kisheria hili suala halipo. Ndiyomaana tunasema tupate muda Serikali, tunaendeleakulifanyia kazi, masuala ya kisayansi, masuala ya kisheria zakodi na Serikali yetu ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha sualahili linafika mwisho mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirejee tu kumuomba nduguyangu, mtani wangu Mheshimiwa Deo Sanga aiachie shilingiya Mheshimiwa Waziri tutakapoyakamilisha masuala hayatutaendelea kama nilivyosema mwanzo dhamira ya Serikaliyetu ni njema kabisa. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa ProfesaMuhongo.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, bado narudi pale pale. Huwezi ukabadili kitu

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

kimoja ukawa na model uliyokuwanayo kwa miaka 10 nilazima uibadili, ukibadili kimoja lazima uende na kingine. Kwamfano, bei ya chuma duniani ilikuwa chini Dola 50 kwa tani,juzi ndiyo imepanda imefika karibu 80. Hata kwenye uraniummnaona tumesimamisha leseni kwa sababu bei ya uraniumiko chini, yule anayewekeza hatapata faida na Serikalihaitapata faida, ndiyo maana ya kufanya hivi vitu na modelssiyo kwamba wameshindwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine na Mheshimiwamwenyewe anajua ni kwamba, mwanzoni mawazo yetuyalikuwa kusafirisha chuma nje, sasa tumeamua tutatumiakwa sababu huyu mtu hawezi kupambana na productionya China ambayo ni 1.38 billion tones per annum, ana-produce Mchina. Wachina hii chuma yote unayoiona, chumaimekuwa nyingi China ndiyo wanaileta huku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni lazima tubadilimodels kwamba chuma ya Liganga sasa ni yetu sisi kuitumiandani ya nchi badala ya kufikiria kuisafirisha. Sasa hizo modelsni lazima twende kwenye vile vivutio na vingine kubadilishwani lazima tuje tena Bungeni hapa. Kwa hiyo, commitment yaSerikali ni kwamba tutakamilisha vivutio na tutawaleteaWabunge wapitishe kusudi mradi uanze. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Deo Sanga.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kutokana na majibu ya Serikali yanayoridhisha ambayoyanaonekana yana nia njema na Liganga na Mchuchuma,nami nitakuwa jirani kufuatilia. Kwa maelezo haya, basinarudisha shilingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Deo.Anayefuata ni Mheshimiwa Subira Mgalu.

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya hoja ya

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

Mheshimiwa Waziri, lakini naomba nipate maelezo ya kinaya namna ya kufungamanisha sekta hii ya viwanda na sektanyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye maelezo yakeamejitahidi kutoa mifano, lakini hata katika hotuba yakesijaona kwa kina maelezo ya ufungamanishaji wa sekta hiiya viwanda na sekta kama vile maji, barabara namiundombinu mingine na nikizingatia vipo viwanda katikamaeneo mbalimbali vimefunguliwa, lakini vina changamotokubwa ya miundombinu ya barabara, maji pamoja naumeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombaMheshimiwa Waziri ajaribu kutueleza kwa kina na kamasitaridhika na maelezo yake nitatoa shilingi. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa mtoa hoja.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu hoja ya Mheshimiwa Subira Mgalu,Mbunge kutoka Mkoa wa Pwani, ambao punde hapanimewapongeza kwamba ni watu wazuri sana kwenyekuhamasisha ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa uchumi waviwanda, niliwahi kuwaona Waandishi wa Habari wanasemaMheshimiwa Magufuli apanga bajeti ya viwanda ya shilingitrilioni 29. Maana yake ni nini? Katika ujenzi wa uchumi waviwanda kuna kitu kinaitwa viwanda, lakini kunamiundombinu wezeshi na miundombinu saidizi. Miundombinuwezeshi, unapozalisha bidhaa katika kiwanda kuna cost ofproduction, unapohamisha bidhaa ama malighafi kutokasehemu moja kwenda sehemu nyingine kuna gharama zilezinaitwa transaction cost. Ili uweze kupata nguvu yakiushindani sokoni lazima production cost iwe ndogo natransaction cost iwe ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fungamanisho la uchumi waviwanda ndiyo maana Mheshimiwa Rais anapigana

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

kutengeneza standard gauge rail kusudi mawese ya Kigomayakija kuchakatwa Dar-es-Salaam yaje kwa gharama ndogokuliko kuchukua CPO kutoka Malaysia. Ndiyo maanatunasema barabara zinazokwenda kwenye malighafi, kwamfano kiwanda changu cha Mkuranga kinachotengenezavigae square meter 80,000 kwa siku, barabara zotezinazokwenda kwenye vyanzo vya madini yale zotezitatengenezwa na Wizara ya Ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tunazungumzakwamba, iwepo miundombinu wezeshi ya ICT kuwezeshamawasiliano kufanyika. Ndilo hilo fungamanisho, i lanililizungumza kwa haraka, unajua unapokuwa pale na ninyiWabunge mmetulia, nakuwa na wasiwasi. MheshimiwaMbunge wala usiende mbali sana fungamanisho lipo,miundombinu wezeshi na miundombinu saidizi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Subira Mgalu.

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na maelezo yake naendelea na hoja yangu ya kutoashilingi ili Mheshimiwa Waziri abaini ukubwa wa tatizo hili.Mimi najielekeza kwenye vile viwanda ambavyo vimeshaanzauzalishaji. Amekitaja kiwanda chetu cha tiles cha Mkuranga,naomba nimtaarifu kiwanda kile kimetumia zaidi ya shilingibilioni 110 lakini kiwanda kimeanza kazi kinatumia malighafimaeneo yale ya Mkuranga, Mkamba, Kimanzichana,Kisarawe lakini barabara haipitiki mpaka sasa imetitia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Wazirianaposema ni kweli hiyo mikakati ipo lakini, je, viwandavilivyoanza kazi, anafahamu kwa mfano, Kiwanda chaSayona kilichopo katika Kijiji cha Mboga kinatarajia kuanzakazi hakina maji na yeye mwenyewe amekitembeleaamekiona? Sasa kwa jitihada za namna hiyo zinafifisha moyowa wawekezaji wetu. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba WaheshimiwaWabunge waniunge mkono ilia one ukubwa wa tatizo katikamaeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha.

WABUNGE FULANI: Toa hoja.

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti,natoa hoja ili ijadiliwe na Bunge, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya, hoja imeungwa mkono. Waleambao hawatataka kuchangia wakae ili tuone nanianataka kuchangia hoja hii. Mheshimiwa Kitandula,Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mheshimiwa ZaynabuVulu, Mheshimiwa Ngonyani, Mheshimiwa Naibu Waziri waMaji, Mheshimiwa Waziri wa Maji na Mheshimiwa Waziri waNishati na Madini. Tutaanza na Mheshimiwa DunstanKitandula.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kumuunga mkono Mheshimiwa Subirakatika hoja yake ya fungamanisho ambayo kwa kweli jambola namna hii ndiyo maana nilisema tunapiga hatua mojambele tunarudi hatua mbili nyuma na nikatoa mfano kwenyesekta ya maziwa. Kwa miaka mitano Tanga Fresh wanaombakibali waweze kupanua kiwanda chao lakini tu kwa sababukuna watu ndani ya Wizara ya Fedha, hususan TRA, wanazuiabila sababu za msingi, hivi hii nia ya viwanda kwelitutakwenda kwa mpango huu? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zaynabu Vullu.

MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Niseme kwamba, pamoja na nia njema yakutuletea viwanda ambavyo vitatusaidia kupata bidhaakwa bei nafuu lakini pia vimesaidia kutoa ajira, hofuiliyokuwepo ya mtoa hoja ni kwamba miundombinuiliyokuwepo ni hatarishi kwa maana ya kwamba zile raw

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

materials zinaweza zisifike kwa wakati kwenye viwanda nauzalishaji usiwepo, Serikali ikapata hasara, dhamira yaawamu ya viwanda ikawa haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali ituambiebarabara ambazo zinachukua malighafi, mfano Kiwandacha Tiles ambacho kiko Mkiu, Mkuranga, malighafi zinatokaWilaya ya Mkuranga na Wilaya ya Kisarawe lakini barabarani mbovu. (Makofi)

MWENYEKITI: Umeshaeleweka Mheshimiwa ZaynabuVulu, ahsante. Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa fursa hii na nimpongeze mtoa hojakwa kuikumbusha Serikali juu ya miundombinu mibovu iliyopokule Mkuranga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kumwombaarudishe shilingi kwa Mheshimiwa Waziri kwa sababu kwanzayeye kama mjukuu wangu, pamoja na Mheshimiwa Ulegana Mheshimiwa Zaynab Matitu Vullu, wanapaswawaipongeze Serikali kwa kufanya jitihada za kupelekaviwanda vingi sana Mkoani Pwani katika Awamu hii ya Tano.Hakuna mkoa umepata viwanda vingi vipya katika Awamuya Nne na hii ya Tano kama Mkoa wa Pwani. Kwa hivyo,hata ule uwezo wetu kama Serikali wa kujenga miundombinukwa haraka kadri ambavyo viwanda vinaingia kwa wingi,umekuwa mdogo kwa sababu, viwanda ni vingi mno Pwanina vitaendelea kuwa vingi kwa sababu ni karibu na bandari,ni karibu na jiji kubwa la kibiashara katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, niwaombe sanawaipe Serikali muda, wampe Waziri muda afike kwenyemaeneo yale aangalie changamoto za kutatua kwa harakana ndiyo hizo aanze nazo kuliko kutoa shilingi na kumkatishatamaa. Nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ngonyani.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, niko hapakumwomba Mheshimiwa aliyeshika shilingi aiachie kwasababu, Mheshimiwa Mama yangu pale Mheshimiwa Mgalualishauliza maswali siku za nyuma, tulishayajibu na majibutuliyoyasema yalionesha commitment ya Serikali inaendawapi. Labda tu mengine ambayo wakati ule sikusema,niyaongezee leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vitu ambavyotumeelekezwa na Serikali, sisi Wizara ya Miundombinu nikuhakikisha kwamba tuna-facilitate uanzishaji wa viwandanchi nzima. Kwa hiyo, katika priority kwa zile fedhawanazotugawia kitu cha kwanza tunachoangalia nikuondoa madeni, kama ambavyo mara nyingi naongeleawakati najibu maswali mbalimbali, tunaondoa yale madeniambayo yanamaliza hela zetu kuwalipa watu wakatiwamekaa idle, ni kwa sababu tu wamecheleweshewakulipwa. Kwa hiyo, priority namba moja ni hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, priority namba mbili nimaeneo ya viwanda.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa. MheshimiwaNaibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kupata nafasi hii.Moja kwa moja nianze kumwomba mtoa hoja aondoeshilingi kwa sababu zifuatazo…

WABUNGE FULANI: Arejeshe.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Arejeshe,arejeshe. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba arejeshe shilingikwa sababu zifuatazo. Amezungumzia Kiwanda cha Sayonaambacho kinajengwa pale Chalinze, kwanza hakijaanza kazilakini pili ni kwamba pale Chalinze tumefanya miradi mitatu,

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

mmoja ndiyo bado haujakamilika, jumla ya hiyo miradimitatu ambayo inatoa maji kutoka Mto Wami inakaribiashilingi bilioni 168. Mwaka huu wa fedha Serikali ilitenga shilingibilioni 915, mpaka sasa hivi tumeshaingia mikataba ya shilingibilioni 710 kwa ajili ya kuleta huduma ya maji, tukiwatunatambua kwamba kiwanda bila maji hakiwezi kufanyakazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tatu, tayaritumeshaongea na Sayona ambaye ndiyo mwekezaji paleChalinze, tumefikia makubaliano. Jana nimetoa taarifa kwaMheshimiwa Mbunge wa Jimbo hilo kwamba tunamaliziataratibu, mashine zimenunuliwa, kinachopitiwa nawataalam ni masuala ya specification tufunge ili Sayonaapate maji kazi ianze kufanyika. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa ProfesaSospeter Muhongo.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, hili siyo tatizo la Wizara hii, ni lazima Watanzaniatukubali tuna udhaifu wa mipango ya maendeleo. Mtuanaamua kwenda sehemu, cha kwanza akishapata ardhitu anaanza kujenga kiwanda lakini haangalii maji na umemeyako wapi. Kwa hiyo, kusema kweli kumlaumu Waziri waViwanda unamwonea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano hicho kiwandacha Mkuranga, sisi wenyewe tumefanya kazi mchana na usikukuwapatia gesi na Mheshimiwa Ulega anajua. Kila sikutukionana nao gesi lakini kabla ya kuweka kiwandahawakuweza kutuona sisi. Vilevile Dangote wameweka palekiwanda hawakutuona kutuambia kwamba wanahitaji gesi,tukafanya kazi mchana na usiku. Kwa hiyo, tukubali kwamba,mtindo wetu sio mzuri, mtu akipata ardhi anaanza kujenganyumba, hajui kwamba ana umeme au maji. Hata hivyo,kwa mambo ya umeme mimi nadhani nisitoe hotuba yangu,tusubiri mpaka Alhamisi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Subira Mgalu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa na nashukuru nimesikia majibuya Mawaziri mbalimbali. Nimalizie aliposema MheshimiwaMuhongo, namheshimu sana, lakini naamini kibali cha ujenziwa viwanda kinatolewa na Wizara husika na Wizarainapotoa kibali inakuwa imejiridhisha na si suala la mjenziwa kiwanda kung’amua kwamba sehemu anayojengakiwanda kuna maji, umeme na kadhalika. Hata hivyo,nimeridhika na majibu ya Mawaziri wengine, nimeonacommitment zao, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri waViwanda kwa kazi yake nzuri. Nataka tu ajue ukubwa watatizo kwamba ujenzi wa viwanda uendane na kufanya kazikwa vizuri kwa kila sekta ili mapato yapatikane. Ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Unarudisha shilingi?

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nimerudisha shilingi yake ili aje tena Pwani. Ahsante.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa RashidShangazi.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nakusudia kushika shilingi kama majibu ya Wazirihayatakuwa yanaridhisha katika eneo ambalo nataka nili-address.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na tatizo la nchihii kila wakati tunalipigia debe viwanda vipya lakini vile vyazamani hatuvilei. Kwa hiyo, inaonekana Wizara hii inapigasound kwa ajili ya viwanda vipya lakini vile vya zamanihawavilei, hawaangalii vina shida gani mwisho wa sikuviwanda vingi sana vinafungwa. Sasa hivi kila mkoaunaozunguka viwanda vimefungwa. Sasa tutakuwa kilamwaka tunahubiri vipya na huku vya zamani vinafungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itoe tamkonini wanafanya kuhakikisha kwamba viwanda vilivyopo

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

vinaendelea kulindwa na kutoa huduma kama ambavyotunakusudia? Kama sitaridhika na majibu nakusudia kutoashilingi kwenye mshahara wa Waziri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa ViwandaBiashara na Uwekezaji.

WAZIRI WA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo ya majukumu yangu nikulea viwanda. Imeandikwa hivyo kwenye bajeti yangu yamwaka huu tunaomalizia na nimerudia kuwaelezea kwambamimi nitalea viwanda na nimekuwa nikivilea acha hivi vipyamjomba mimi siachi chungu cha zamani kukimbilia chungukipya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie katika speechyangu nimeelezea nilivyohamasisha brand 50 za bidhaa zaTanzania. Ninapokuja kuhamasisha brand ya Tanzania inamaana natambua kwamba hawa watu wanafanya kazi navigezo ninavyopitia kuja kuitambua kwamba hii ni brandnaangalia anajiri watu wangapi, anahifadhi vipi mazingira,analipa kodi kiasi gani na vitu kama hivyo, hiyo ni mojawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ninazo taasisi zangu yaTBS na yangu TIRDO wanakwenda viwandani si kamamapolisi, wanakwenda viwandani ili kwenda kuwafundishawazalishe bidhaa zenye ubora zinazokidhi masoko yaTanzania na masoko ya nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, navilea viwanda kwanamna hiyo na nina imani viwanda vyangu vinaendelea vizurina ndiyo maana Tanzania mnaweza kuona bidhaa yaTanzania. Zaidi ya hapo mwaka jana na nitarudia na mwakahuu, niliitisha maonyesho ya viwanda vya Tanzania tu navilishiriki na yalifanyika maonesho pale Sabasaba na mwakahuu mwezi Novemba, nitaviitisha tena chini ya Kauli Mbiu yaTanzania sasa tunajenga viwanda.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rashid Shangazi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,inawezekana labda mimi na Mheshimiwa Waziri tunaishiTanzania tofauti, yeye ana ya kwake na mimi nina ya kwangu.Kwa sababu anaposema analea viwanda viko wapiViwanda vya KIBO MATCH, MOPROCO, Sungura Tex, Kili Tex,Mbeya Tex, Tabora Spinning, hapa tunazungumzia viwandavyote nchini ambavyo vilikuwepo tangu enzi za Mwalimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza leoTanzania viwanda tunasahau kwamba wakati wa MwalimuNyerere viwanda hivi vilikuwa vimetapakaa mikoa yotehapa nchini. Sasa Mheshimiwa Waziri anaposema analeaviwanda ni viwanda vipi anavyovilea na hivi ninavyovitajavyote vimegeuka kuwa ma-godown?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe hoja naWabunge wenzangu waniunge mkono tuweze kulijadilijambo hili tusiwe tuna nadi viwanda vipya wakati vyazamani vinakufa. Waheshimiwa Wabunge, naomba mniungemkono. (Makofi)

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono. Wale ambaohawachangii wakae ili tuanze kuandika wachangiaji.Mheshimiwa Shahari Mngwali, Mheshimiwa Japhary,Mheshimiwa Emanuel Mwakasaka, Mheshimiwa Dkt. ChristineIshengoma, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha, NaibuWaziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi. Tunaanza na Mheshimiwa Shahari.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nami niunge mkono hoja ya baba mkwewangu Mheshimiwa Shangazi kwamba, we are serious lakiniwe have to be more serious. Kwa sababu haya mamboambayo tunaambiwa tu tutafanya, tutatekeleza lakini bilakuwa na mwonekano wa wazi kwamba kweli vinatekelezwana hapa maelezo kwamba hivi viwanda vil ivyokufavinafavywaje, maelezo yanatolewa kiujumla ambayo hatahivyo yalishatolewa miaka mingi iliyopita wimbo ni ule ule.(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wa sasa wanasematujiongeze ili tukijadili tujadili. Failure ya ile integrated bajetiniliyoisema mwaka jana ndiyo hii hapa sasa. Ile hoja yamwanzo ni hiyo kwamba kila mtu kipande chake halafutunalazimisha kuungana haviungani. Viwanda vyoteambavyo vimekufa huyo mlezi hatumwoni anavilea vipi nawale watoto waliokufa sijui kama watafufuka hatuelewi.Naomba itoke kauli yenye kuthibitika. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Japhary Michael.

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami naunga mkono Mheshimiwa Mbunge Shangazi kuhusumkakati thabiti wa Serikali wa kuhakikisha kwamba viwandahivi ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa kama havifanyi kazivinafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri wakatiMheshimiwa Rais anajinadi pale Moshi alisema apewe siku37 tangu atakapochaguliwa viwanda vile vyote vya Moshivitakuwa vimeshafufuka. Mwaka mmoja na nusu sasa hatakiwanda kimoja hakijafufuka na kimojawapo kikiwakiwanda cha vibiriti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokiomba nakumuunga mkono Mheshimiwa Shangazi ni kupatacommitment ya Serikali kwamba ni lini sasa hivyo viwandavitachukuliwa kwa hawa ambao wameshindwakuviendesha, virudi katika mikono ya watu sahihi wakuviendesha. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Emanuel Mwakasaka.

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Naomba niunge mkono hoja naMheshimiwa Shangazi. Mheshimiwa Mwijageanapozungumza suala la ulezi wa viwanda najiuliza uleziupi? Juzi juzi tu hapa nilipouliza swali linalohusiana naKiwanda cha Nyuzi Tabora, akajibu kwamba kila mtuatabeba mzigo wake sijui kama amesahau. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashindwa kuelewa naviwanda hivi vinakufa. Juzi juzi aliinuka msemaji mmojahapa akasema kwamba kile kiwanda bado ni godown. Vikowapi viwanda vya kusindika nyama kama cha Shinyangana vinginevyo. Mimi huu ulezi anaouzungumzia MheshimiwaMwijage sioni kama upo. Namuunga mkono MheshimiwaShangazi kwa hoja yake ya kushikilia shilingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Ishengoma.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Nami namuunga mkonoMheshimiwa Shangazi kwa sababu licha ya kuanzishaviwanda vipya lakini viwanda vya zamani ni vizuri vifufuke.Kwa mfano Mkoa wa Morogoro ulikuwa ni mkoa waviwanda lakini kama tulivyochangia jana viwanda vingivimekufa. Kwa mfano, Kiwanda cha Ngozi, Kiwanda chaViatu, Kiwanda cha Ceramic (cha vyombo), vingi vimekufa.Kwa hiyo, namuunga mkono Mheshimiwa Shangazi tuanzisheviwanda vipya lakini na vile vya zamani viweze kufufuka nakufanya kazi. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Niendelee kurejea azma yaSerikali yetu ni kuchochea uchumi wa viwanda. Hiyo lazimaikae hiyo na hatuwezi kuchochea uchumi wa viwanda bilakulea viwanda vilivyokuwepo na bila kuangalia vilevilivyokuwepo kwa nini vilikufa ili tuje na mkakati sasa wakuhakikisha viwanda hivyo vinapofufuka kama alivyosemadada yangu Mheshimiwa Riziki kwamba tutakapovifufuavisife tena, hiyo ndiyo dhamira ya Serikali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kulitekeleza hili Msajiliwa Hazina alifanya tathmini, uhakiki na research ili sasa ajekuieleza Serikali ni kwa nini viwanda hivi viliishia njiani. Baadaya kujua ni matatizo gani tulikumbana nayo tuje na mpangona mkakati mzuri wa kuhuisha viwanda vyetu na kuwezakuwa na viwanda endelevu na kuhakikisha kwamba kama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

alivyosema Mheshimiwa Rais wetu Tanzania ya Magufuli niya viwanda na tuna uhakika ndani ya miaka mitano viwandavyetu vyote vitakuwa vimeuhishwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa WilliamOlenasha.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Mwenyekiti, namsihi sana Mheshimiwa Shangaziaachie shilingi ya Mheshimiwa Waziri, asimpunguzie kasiandelee kwenda kufanya kazi ambayo ameifanya kwa uzurisana kwa sababu zifuatazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali inajaribukuhimiza uchumi wa viwanda siyo tu kwamba tunahimizaujenzi wa viwanda vipya lakini vilevile kuangalia vilivyopolakini ikiwezekana kurudi nyuma na hata kuangalia vilevilivyokufa kama kuna haja au uwezekano wa kuvifufua.Katika kufanya hivyo ni vizuri kuangalia mambo kadhaa, kunaviwanda vingine vimekufa ambavyo ukijaribu kuvifufuainawezekana ukatumia fedha nyingi zaidi na jitihada kulikoukianzisha kipya. Vilevile kuna vingine technologyimekuwa obsolete huwezi kusema tu nirudi kwenyeteknolojia ya zamani kwa sababu mambo sasayamebadilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimfahamishe tuMheshimiwa Shangazi kwamba kuna jitihada kubwa zaSerikali kufufua baadhi ya viwanda, nitavitaja tu baadhi kwamfano Kiwanda cha Triple S (Shinyanga), Kiwanda chaGeneral Tyre (Arusha), Kiwanda cha Nyama (Mbeya), Kiwandacha Chai (Bumbuli) na viwanda vingine. Kwa hiyo, jitihadazipo lakini lazima tuangalie mazingira ya kila kiwanda kablaya kusema tu tunafufua. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Shangazi arudisheshilingi na kwamba Mheshimiwa Waziri amepokea concernya kufufua viwanda nikielewa kwamba hicho ndichoalichomanisha. Kwenye swali lake alikuwa anaongelea kuleana akataja viwanda vilivyokufa, Waziri halei makaburi yaviwanda ambavyo vimekufa ila analea viwanda ambavyovipo na ulezi wake anaoufanya utaona katika sera alizotoaWaziri wa Fedha akishirikiana na Waziri wa Viwandawanafanya control ya damping ya bidhaa kutoka maeneomengine ambapo huwa zinachangia kuua viwanda vyandani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile mmeona vitabuambavyo ametuonesha ambapo wengine tumeshavisomaambavyo ameelezea mikakati ambayo italea vile viwandavya ndani. Pia mmeona jitihada kama Naibu Waziri wa Kilimokama ambavyo ameelezea viwanda ambavyovimefufuliwa. Kufufua kama alivyoelezea Naibu Waziri waKilimo si tu jambo la kwenda kufufua kama unainua uziokwa sababu lazima uangalie kitu gani kil ichokuwakinafanyika, ni kitu gani kilichosababisha kifeli na je,mabadiliko ya teknolojia yanaendana na kufufua vyumavilivyokuwepo, lakini mpango nzima unakuwa wa kuwa naviwanda vinavyoendana na raw material ambazo zipo naambazo zitaweza kupata soko na ushindani wa bidhaazinazotoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombeMheshimiwa Shangazi aridhie mpango mkakati wa Serikalikwa ujumla wake ambao Wizara inayoongoza kutoampango wa viwanda imeshatoa, Wizara ya Fedha imeshatoalakini na Wizara zingine za Kisekta tunaendelea kushirikianana Wizara ya Viwanda kama ambavyo mnaonatunawekeza kwenye Kiwanda cha Viatu kule Moshi pamojana Kiwanda cha Sukari Mbigili ambavyo miaka iliyopitavilishakufa. Kwa hiyo, hizo ndiyo jitihada ambazo Wizarainafanya na ndiyo dira ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa kwenyeSerikali ya viwanda.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rashid Shangazi.

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na maelezo mengi lakini bado hayajajibu yaleambayo nilikuwa nakusudia. Teknolojia inapobadilika siyokwamba inakuja kuondoa uhitaji wa kitu, hapotunachozungumzia, kwa mfano zamani tulikuwa na kiwandakama Zana za Kilimo Mbeya, je, sasa hivi hatuhitaji majembe,mabeleshi na mikokoteni, ni vitu ambavyo bado vinahitajika.Kwa hiyo, kama teknolojia imebadilika ni kuviboresha tu lakinisiyo kwamba uhitaji haupo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi nimwonee tu hurumanimrudishie shilingi yake lakini bado eneo hili linahitajiusimamizi makini ili yale malengo ya Mwalimu Nyererealiyoyapanga kutawanya rasilimali za Taifa nchi nzimayaweze kuendana na Taifa letu. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge kwamamlaka niliyonayo chini ya Kanuni ya 104, naongeza nususaa. Mheshimiwa Antony Komu.

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami naomba maelezo ya Serikali kuhusiana na marufukualiyotoa Waziri Mkuu kwenye vifungashio vya pombe ainaya viroba na kama maelezo hayatakuwa ya kuridhisha basinitatoa shilingi ya Waziri na nitaomba Bunge liniunge mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ieleweke wazikabisa kwamba na mimi ni mmoja wa watu ambao siungimkono matumizi ya ile pombe ambayo il ikuwainafungashwa kwenye viroba. Ninachosema ni kwambabaada ya marufuku hii Serikali ilitoa maelekezo kwambawale wenye stock ya pombe ile katika vifungashio hivyovilivyopigwa marufuku ifanyiwe stock taking na Polisiwalifanya hivyo, TRA na TFDA walikwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo, Serikaliilisema itatoa maelekezo ili vikafanyiwe repacking lakini leoni zaidi ya miezi miwili tokea jambo hilo lifanyike na kama

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

jana nilivyosema limewagharimu watu sana kwa sababuwana ma-godown wanayalipia, wanapaswa kufanyamarejesho katika benki, wako wengine wenye mtaji unaozidishil ingi milioni 300 na kadhalika. Kwa hiyo, naombacommitment ya Serikali au maelezo ya Serikali juu ya jambohili ambalo kwa kweli liko kila mahali katika nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa unyenyekevu kujibuhoja ya Waziri Kivuli wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.Masikitiko yangu ni kwamba tulikuwa hatujawasiliana mimina yeye lakini wazalishaji wote ambao wote kimsingi,ningejua ningekuja na barua wanakubaliana na maamuziya Serikali ya kuzuia vifungasho vya namna hiyo, wote kwabarua na ninazo na bahati mbaya hiyo sikuijuawameshapewa maelekezo ya hatua za kufanya. Mojawapoya hatua za kufanya ni ku-pack bidhaa hiyo kwenye chupamaalum ambazo zitaondoa vishawishi na ile easy portability.Tumewasiliana na Megatrade ya Arusha na TBL namna yaku- handle bidhaa hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii na ndiyocommitment ya Serikali, yeyote ambaye bidhaa yake itakuwailizuiliwa, iko kwenye ma-godown mikoani aende Ofisi yaMheshimiwa Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira aonanena Katibu Mkuu, Profesa Kamuzora ili ampe maekelezonamna ya kutoa bidhaa kutoka point moja kwenda pointya pili na kuhakikishia zile bidhaa zinakuwa handled katikahali ambayo haitakwenda mtaani. Kama alivyosema yeyekwamba vitoke kwenye makatarasi ziwekwe kwenye chupaya lita moja, lita tano hata lita kumi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Antony Komu.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,maelezo ya Waziri yanaridhisha sana kwa hicho kipande chakwamba wakamwone Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu ya Rais.Hata hivyo, kuna jambo moja tu ambalo kwa sababu yamuda ukimruhusu tena akaji-commit basi nitamaliza hiibiashara hapa hapa. Hizo gharama za kurudisha kwenyekiwanda ni nani atazishughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba huruma yako.(Makofi)

MWENYEKITI: Huruma hiyo umeipata maadamhujatoa shilingi. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nijibu hoja ya MheshimiwaWaziri Kivuli, hawa ni wadau wetu tunaelewana na ndiyomaana nikasema waende wakamwone Katibu Mkuu, ProfesaKamuzora watapewa logistic zote. Ngoja niseme zaidi,tumetoa maamuzi, kutoa bidhaa kutoka godown mojakwenda nyingine italindwa na ulinzi wa Polisi. Tuko serious najambo hilo kuhakikisha kwamba hakuna kiroba kitaingiamtaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tuko seriouswaende wapewe maelekezo, hatuwezi kumwaga mtamakwenye kuku wengi. Maelekezo ndiyo hayo, kuna ulinzi mkalikutoa bidhaa kutoka kwenye godown moja kuipelekakiwandani. Pia tutasimamia vile viwanda vinavyokwendakutoa kwenye makatarasi kuweka kwenye chupa. Hiyodhamira ya Serikali kuhusu viroba bado iko pale pale.Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwambalitatekelezwa na katika hili nitaomba msaada waketusaidiane kusudi tusirudi nyuma twende mbele.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anthony Komu kikanunihapo tena tutakuwa tumetoka nje. Mheshimiwa Waziri,nadhani swali la Mheshimiwa Komu ilikuwa ni kuhusugharama za kubadilisha kutoka kwenye kale kamfukokuelekea kwenye chupa, nani hapo anahusika? (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Waziri sihusiki na mamboya kiutendaji, nazungumza ninachokiamini na msema ukwelini mpenzi wa Mungu. Ndiyo maana nikasema Katibu Mkuuanayeshughulikia anajua yote hayo na hawa wajasiriamalimnaowasema wanawasiliana na Katibu Mkuu huyo.Nimemsema TBL na Mheshimiwa rafiki yangu tukitoka hapanikakuoneshe barua, nimemsema Megatrade, tumefikiahatua mpaka ya kuwapa model ya ku-bottle na kuwapanamna ya kuweza kuweka alama za siri za ku-protect hiyovitu, hiki kitu ni sensitive, watu wamekufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba uliache kati yangumimi na yeye ndiyo kivuli changu nitashughulikia. Gharamawatazibeba wenye mzigo ule. (Kicheko)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleana Mheshimiwa Ahmed Ngwali.

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika mchango wangu nilizungumzia zaidi suala la TBS kuhusubidhaa bandia na nikasema kwamba TBS tunatekelezaprogramu ya PVoC ambayo tuliianzisha mwaka 2012 sasa nimiaka sita haionekani athari yake na tukayapa makampuniSGS wakati ule na Intertek wapo pamoja na Bureau Veritas.Sasa toka tuanze hiyo programu ya kuzuia bidhaa bandiakutoka nje zisiingie Tanzania bidhaa bandia ndiyo zimeingiakabisa. Kwa hiyo, niseme kwamba kama hoja yangu hiihaikupatiwa majibu sahihi ya Serikali basi nina kusudio lakutoa shilingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachokisema bidhaabandia ambazo ni substandard zipo kila eneo na MheshimiwaWaziri anajua na mnasema kwamba mmeshindwa kuzuiabidhaa bandia kuingia kwa sababu kuna vituo bandia vyabahari kama vituo 36 pamoja na mipakani. Sasa Serikali inampango gani wa kuzuia bidhaa bandia zisiingie nchini?(Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu rafiki yanguMheshimiwa Ngwali kuhusu bidhaa bandia na bidhaazisizokidhi viwango. Niwaombe tena Waheshimiwa Wabungemchukue muda mkisome kile kitabu changu ambacho watuwengine wamekiita kitabu cha rejea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bidhaa bandia zinaingiaTanzania mojawapo ya njia zinazoingiza bidhaa hiyo ni hizinjia za panya, yako majahazi yanaingiza bidhaa hapa, watuwangu waliopo bandarini hawawezi kuziona, nitazizuiaje?Ndiyo maana aliyesimama kuchangia ni Waziri wa Mamboya Ndani na nimemwomba atanisaidia lakini nitamwambiaMheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Rais ili ikibidi tupewenyambizi atakayekuja na mashua na bidhaa bandiatumzamishe, niseme nini zaidi ya hapo? (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, magendo inaingiza bidhaahumu nchini, inaua viwanda na inawaumiza na wananchi.Wanaofanya magendo Watanzania mnawajua, bidhaazinazoshuka Tanga, Kilwa na Kunduchi mnajua zinatokawapi. Mzee Ngwali kwa nini unanipa shida kwa tatizoambalo unalijua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanaoingiza bidhaa kwamagendo ndiyo ambao wanatupa shida. Wale wanaopitiabandarini nimesema jana kwamba waliopo chini yanguwahakikishe bidhaa haipiti. Mheshimiwa Ngwali ikibiditutakwenda wote ukakague hizo PVoC unazozisema Chinana Hongkong, siwezi kushindwa nauli ya kwenda mimi nawewe. Nakuhakikishia zikiingia humu ndani kupitia bandarinimtu anaondoka, lakini za magendo ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba unipe dakika moja,ngoja niwaambie tulikosa wawekezaji wa sukari kwa sababusukari ilikuwa inashuka magendo hapa nchini. Tulikosawawekezaji kwenye kilimo cha mpunga/mchele na hata

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

Kilombero Plantation alitaka kuondoka nchini kwa sababuya kuleta mchele wa Pakistani wenye miaka 30 kwenye ma-godown kwa njia za magendo, tunadhibiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza na rafikiyangu hapa amesema atanisaidia lakini nitakwenda na kwaMheshimiwa Waziri Mkuu na kwa Mheshimiwa Rais,atakayeingiza atapambana na Jeshi la Wananchi. Tukizuiamagendo bidhaa bandia na feki haziingii. MheshimiwaNgwali usiende mbali wewe ni rafiki yangu na kila mtuanakujua hapa. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ngwali pamoja na ahadiya kwenda nchini China bado umesimama? (Kicheko)

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,jambo hili sio la leo, ni jambo la zamani sana na Wazirianataka kutumia polisi, polisi hao ambao wamepewadhamana kwa muda mrefu na wameshindwa kutekelezakazi hiyo. Siyo tu bandari bubu lakini pia mipakani bidhaabandia zinapita. Pia TBS wana wafanyakazi wachache kukidhikupambana na tatizo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nauliza ni mkakati ganiwa Serikali ambao upo sasa kwa sababu Bureau Veritas naSGS wameshindwa kazi na bado mnaendelea wala hakunaripoti yoyote. Nataka commitment ya Serikali ni mkakati ganimlionao kuzuia tatizo hili?

WABUNGE FULANI: Toa hoja.

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kutoa shilingi hoja hii ijadiliwe.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hojaimeungwa mkono, wale wanaochangia ndiyo wabakiwamesimama sasa.

Mheshimiwa Halima Mohammed, MheshimiwaSalome Makamba, Mheshimiwa Mwamoto, Mheshimiwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

Allan Kiula, Naibu Waziri wa Mazingira, Naibu Waziri waTAMISEMI, Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchina Mheshimiwa Cosato Chumi. Tunaanza na MheshimiwaHalima Mohamed.

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Naunga mkono hoja yaMheshimiwa Ngwali azuie shilingi. Nasema hivyo kwa sababunina mfano hai, kuna miswaki ukiutia mdomoni mara mojatu unakatika, nafikiri mtaniunga mkono WaheshimiwaWabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Waziri hapa alizuia simufeki lakini bado chaja zipo feki madukani, tunafanyajeMheshimiwa Waziri? Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa SalomeMakamba.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nami niunge mkono hoja ya MheshimiwaNgwali. Mheshimiwa Waziri suala la vitu feki wala sio lakujadili, linajulikana na lipo wazi. Mheshimiwa Waziri mlitokakutuambia humu Bungeni kwamba Usalama wa Taifa wakokila sehemu lakini leo Usalama wa Taifa wako kwenyemikutano ya hadhara inayoandaliwa na CHADEMA tu,kwenye vitu feki wewe unasema umeshindwa na unakirihapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda dukani leounaulizwa unataka feki au original? Kweli hilo nalo linahitajitutafute jeshi kutoka nje kuja kutusaidia? Mheshimiwa Wazirimtueleze ni nini dhamira ya Serikali kusitisha suala la bidhaafeki Tanzania. Mmesema habari ya simu feki, mmewaumizawananchi, simu zimechukuliwa lakini wananchi walilipa kodina wananunua vocha na wanaingiza pato la nchi hii kupitiasimu hizo feki. Mheshimiwa Waziri tunaomba atupe majibuyanayoeleweka, Watanzania wanaumia sana. (Makofi)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa VenanceMwamoto.

MHE. VENANCE M. MWAMOTO: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimwombe Mheshimiwa Ngwali rafikiyangu arejeshe shilingi kwa sababu amesema njia za panyaambazo sio rasmi. Kwa hiyo, ningeomba MheshimiwaMwigulu aongozane na Mheshimiwa huyu amwoneshe hizonjia za panya ili tuwakamate hao watu kwa sababuwatakuwa wanazuia Serikali ya Awamu hii kufanya mambomazuri ambayo wamekusudia. Mheshimiwa Ngwali achiahiyo shilingi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Allan Kiula.

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kidogo jambohili na nimwombe Mheshimiwa Ngwali amrudishie Wazirishilingi ili aweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosemamchangiaji aliyepita ni kwamba amesema bidhaa bandia,sasa bidhaa bandia sote tunajua kwamba tuna porousborder. Sisi mipaka yetu ina njia za panya nyingi sana ambazobidhaa feki ambazo zinaingia pale. Sasa bidhaa feki hazinauhusiano na kazi ya Bureau Veritas kwa sababu Bureau Veritasna kampuni nyingine ambazo tumezikasimu kazi hiyozinakagua na zinakuja bidhaa sahihi. Sasa hizi zinazoingiakwa njia ya panya ndiyo zinaleta matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine sisi kamaWatanzania lazima tukatae kununua bidhaa feki. Kamatunanunua bidhaa feki wale ambao wanaingiza bidhaa fekiwanaendelea kuingiza, lakini pia tutoe taarifa. Tunaonabidhaa feki hatutoi taarifa, mamlaka zinazohusikazitachukuaje hatua? Kwa hiyo, namwomba MheshimiwaNgwali arudishe shilingi lakini pia Wizara husika ijipange ilikuweka mikakati zaidi kwa kushirikiana na Wizara nyinginekama Wizara ya Mambo ya Ndani kuweza kuzuia suala labidhaa feki.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

MWENYEKITI: Ahsante sana. Naibu Waziri wa Uchukuzi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namuombaMheshimiwa Ngwali arudishe shilingi kwa sababu anafahamukwamba hivi sasa tumeshaunda timu ambayo ndani yakekuna Wakuu wa Mikoa wote ambao wapo katikamwambao wa bahari na karibuni tutaenda kuunda timuinayohusisha maziwa yote makuu. Hii ni kuhakikisha kwambatunazuia operation za bandari bubu. Huo mkakati tayari upona tutahakikisha tunausimamia kwa ukamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja lililotulazimisha tufanyemabadiliko makubwa katika bandari kwa maana yaMamlaka ya Bandari ni hilo. Kwa hiyo, tumeshaanzakuchukua hatua, tumesafisha uchafu kwenye bandari natumeweka watu sasa ambao tunaenda nao sambambakatika kuhakikisha kwamba masuala ya bandari bubuhatimaye yanakwisha.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Naibu Waziri waMazingira.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nimkumbushe tuMheshimiwa Ngwali ambaye yeye alikuwa mjumbe wanguwa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakati uletuliyoyafanya sasa hivi amesahau. Makampuni yote dhaifuwakati ule yaliyokuwa yakishughulika na PVoC tulimwambiaWaziri wa Viwanda na Biashara wa kipindi kile yoteyaliondolewa na anajua kabisa kwamba Serikali ilichukuahatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile anajua hatuatulizozichukua katika Kamati hiyo kwamba tuliiambia Serikaliiongeze watumishi TBS na Serikali i l ikubali ikaongezawatumishi zaidi ya 200 na yeye anajua. Leo anasema Serikali

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

haichukui hatua, Mheshimiwa Ahmed anayakumbuka hayana anajua kabisa kwamba Serikali inachukua hatua katikasuala hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kuthibitisha nikwamba mapambano ya kuingia kwa bidhaa bandia nchinitumepambana nayo kwa kiwango kikubwa enzi hii ya Serikaliya Awamu ya Tano. Isipokuwa kinachokosekana hapa nitakwimu za kuthibitisha kwamba tumepunguza kiasi gani.Wafanyabiashara tulipokutana nao katika kikao cha pamojamajuzi ambao tuliwaita hapa, waliitwa na MheshimiwaWaziri wa Viwanda na Biashara wote walithibitisha kwambahali sasa inaendelea vizuri kwa kupungua kwa watu hawaambao wanaingiza bidhaa bandia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile suala la elimu,tumeimarisha sasa hivi kuhakikisha kwamba meli zotezinazotua kwenye bandari zil izoruhusiwa na bandarizisizoruhusiwa zinaonekana na tunazifanyia ukaguzi. Kwahiyo, Watanzania wanatakiwa watu-support,wanapokumbana na bidhaa bandia watueleze zipo wapi.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Naibu Waziri wa TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwaheshima tuliyopata Watanzania kutoka kwa Serengeti Boys,nataka niwape taarifa tumeshinda mechi hiyo. Kwa hilo tulinamfanya Mheshimiwa Ngwali ambaye ni mchezaji mzurisana akarudisha shilingi kwa furaha aliyonayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kwambabahati nzuri watu mbalimbali wamechangia lakinicommitment ya Serikali hasa ukiangalia hii Awamu ya Tanojinsi gani tumefanya, Mheshimiwa Mpina ameelezea sualazima la ajira kwamba kuongeza kikosi kazi kuweza kufanyakazi hiyo. Kubwa zaidi ambalo napenda kulizungumza,katika ajenda hii sasa ukiangalia mentality ya Watanzaniaimebadilika katika suala zima la uzalendo.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababutunajipambanua katika uchumi wa viwanda, nisemekwamba Mheshimiwa Rais ametuelekeza sana katika sualazima la uzalendo na hili tulivae sisi Watanzania wote kwambakwa sababu tunajenga viwanda na tuna kila sababu yakuhakikisha kwamba tunapata bidhaa bora suala la elimulazima liwe jukumu la kila mmoja wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Ngwali kwa sababu Serikali imejenga One StopBorder Post na inaweka nguvu kubwa sana katika suala zimala ulinzi, inaajiri watu na Serikali imejizatiti kabisa kuhakikishakwamba uchumi wa Tanzania unapanda, hili jambo tulivaewote na tumuachie Mheshimiwa Waziri mwenye dhamanashilingi yake, lengo kubwa nchi yetu iweze kwenda mbele.Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, nimweleze Mheshimiwa Ngwali kwamba shilingianakotaka kuichukulia sio mahali pake. Zoezi la uingiaji wabidhaa feki linasimamiwa na vyombo vya ulinzi na usalama.Nami nimwambie tu wale wanaoingiza bidhaa feki walahatuwaombi kuacha kufanya hivyo lakini tunawaambiakwamba tutapambana nao kwa nguvu zote na kuhakikishakwamba tunatokomeza utaratibu huo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema NaibuWaziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, ni vile tu hatujaorodheshatakwimu, lakini utaweza kuona katika maeneo mengi sanatumeweza kufuta kwa kiwango kikubwa uingizwaji wabidhaa feki. Kama ambavyo tulipata orodha bidhaa fekizilizokuwa zinakuja zilikuwa katika nyanja nyingi sana na zotehizo tumepambana nazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa commitment ya Serikalini kwamba tutapambana kuhakikisha kwamba tunadhibiti,lakini pia tunachukua hatua kwa wale ambao wataweza

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

kupenya na tukagundua kwamba walishapenya. Kwanamna hiyo, wenzetu wa viwanda wataweza kuinua zaidiviwanda vya bidhaa halali ambazo zinazalishwa kwetu nazina viwango ambavyo ni makini kwa matumizi yaWatanzania wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, MheshimiwaNgwali arudishe shilingi lakini na wao ni viongozi wenzetutusaidiane kupeana taarifa na kutoa elimu kwa wananchiwetu. Kila mtu akikataa bidhaa feki na yenyewe hiyo ni hatuakubwa ya wale ambao wameingiza bidhaa feki kutokurudiatena kuingiza bidhaa feki.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ngwali.

MHE. AHMED JUMA NGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwa sababu bidhaa feki zinaweza kuleta athari kwa wewemwenyewe, Mheshimiwa Mwigulu, Mwanasheria Mkuukutokana na kununua bidhaa feki bila kujitambua, naombajambo hili tuliamue kwa kura, nazuia shilingi yangu. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa hapo Mheshimiwa Ngwali siyokwamba majibu unayajua tayari? Haya, nitahoji kuhusu hojaya Mheshimiwa Ngwali.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

MWENYEKITI: Hoja ya Mheshimiwa Ngwaliimekataliwa, kwa hiyo, shilingi ya Mheshimiwa Waziri ipopalepale. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea, MheshimiwaDkt. Shukuru Kawambwa.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekiti, katika mchango wangu nilimhoji MheshimiwaWaziri, kwamba wananchi ambao wanapisha Mradi wa SEZBagamoyo wamesubiri kwa miaka kumi kuweza kupata fidiakwa ajili ya mali zao katika eneo hilo. Ni utaratibu wetu wa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

kisheria na kisera kwamba pale ambapo Serikali inalazimikakutwaa eneo la wananchi kwa ajili ya mradi wa maendeleo,basi wananchi hao walipwe fidia zao halali kufuatana nathamani ya soko na kwa wakati. Hata hivyo, katika maeneomengi nchini mwetu Tanzania ulipaji huu wa fidia umesuasuasana, mifano ni mingi katika mikoa mingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kupata maelezoya Mheshimiwa Waziri, ni mkakati gani ambao upo wakuhakikisha kwamba mateso ambayo wananchiwanayapata kwa kusubiri miaka mingi hadi kupata hakiambayo imetajwa kisheria na kisera yanaondolewa nawananchi hawa wa Bagamoyo kwenye Mradi wa SEZ wawezekupata fidia zao?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu hoja ya kaka yangu,Mheshimiwa Dkt. Shukuru, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali kutwaayale maeneo kwa ajili ya viwanda ilikuwa nzuri na bado ninzuri. Kama anavyojua yeye, kwa sababu kiti nilichokikaliamimi leo alikuwepo yeye jana, haya maeneo yamechukuliwamiaka ya 2008 na 2010, Serikali imekuwa na utaratibu wakuwalipa watu fidia na pale inapokuwa imechelewainawalipa riba lakini kama alivyosema, ni kweli watuwanaumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza kwenye maelezoyangu baada ya kuona kwamba watu wanaendelea kuumiakwa Bagamoyo Serikali mwezi Desemba ilikubali kwambasekta binafsi iingie ilipe fidia dhamira ikiwa bado ni ileile yakujenga viwanda. Maslahi ya mwananchi yatasimamiwa naSerikali, mwananchi anaishika Serikali, Serikali inatafuta watuwa kusaidiana naye kulipa fidia.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maeneo mengine yanchi kwenye bajeti yangu humu nimeeleza kinagaubaganamna gani Songea, Kigoma tutaweza kufanya hivyo.Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, katika vitu ambavyovitanipa faraja ni kuona mradi wa Bagamoyo watuwanalipwa fidia. Nimesema, wale wabia wawili wa Omanna China wameshaleta proposal na imeshakubaliwa,wataalam wetu wameshaijibu inakwenda kwenye kikao chaMakatibu Wakuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimezungumzakwamba mwekezaji mwingine wa kwenye industrial parkamekuja na tumeshakubaliana na Katibu Mkuu, Dkt. Meru,kwamba akija huyu mtu kile kipande kingine kinachobakicha Bagamoyo agawiwe. Kwa hiyo, nia yetu ni njema, nikujenga viwanda. Nawasihi wananchi tengeni maeneo,kuna sisi, wanetu na wajukuu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwanaona ameridhika na maelezo.

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa maelezo haya ya Mheshimiwa Waziri nakuhisi nia yake thabiti ya kutatua mgogoro huu, basinaridhika naomba tu Serikali ijitahidi kutekeleza hili vizuri.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Mheshimiwa JacquelineMsongozi.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awamu ya Tano yaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kabisakukuza uchumi wa viwanda. Katika mpango huo wa Serikaliwa kukuza viwanda, nafikiri kwamba Serikali na EPZwangekwenda sambamba kwa maana ya kulipa fidiakwenye maeneo ya wananchi ambayo wamechukua nawanashindwa kulipa fedha ambazo wananchi wanatakiwa

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

wapate fidia. Kwenye eneo hili mimi nataka nipate maelezoya kina ambayo kimsingi kama sitaridhika nayo nipo tayarikuondoa shilingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, kunaeneo ambalo liko pale Songea Mjini katika Kata yaMwengemshindo EPZ toka mwaka 2008 mpaka leo wananchiwana kilio kikubwa, hawajalipwa pesa zao takribani shilingibilioni 2.5 ilikuwa shilingi bilioni nne wakalipa nusu na nusubado haijalipwa, wananchi hawaelewi nini wafanye mpakasasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba maelezo ya kina,ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, sekunde thelathini.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe maelezoMheshimiwa Mbunge kwamba kwenye kitabu changu baadaya kuzungumza na Mheshimiwa Gama, Mbunge wa Songeana kwa kufuatilia wakati natengeneza bajeti, nimepangapesa ya kumalizia hiyo sehemu iliyobaki. Kwa hiyo, tufanyesala tukusanye mapato, watu walipwe, mambo yawemazuri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jacqueline Msongozi,naomba ukae.

Waheshimiwa Wabunge, muda wetu ulipofikia Kanuniyetu ya 104, inataka tuingie kwenye kupitisha Mafungu yotekwa pamoja, Katibu.

Fungu 44 – Viwanda

Kif. 1001 – Administration and HR Management .....................Sh.11,838,840,000/=

Kif. 1002 – Finance and Accounts ................. Sh.363,889,000/=Kif. 1003 – Policy and Planning ....................Sh.1,043,882,000/=

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

Kif. 1004 – Government Communication Unit.......................Sh.81,701,000/=

Kif. 1005 – Internal Audit Unit .........................Sh.200,381,000/=Kif. 1006 – Legal Services Unit...........................Sh.96,218,000/=Kif. 1007 – Manangement

Information System .......................Sh.259,686,000/=Kif. 1008 – Procurement Mgnt Unit ................Sh.181,304,000/=Kif. 2001 – Industry ......................................Sh.5,078,406,000/=Kif. 2002 – Small and Medium

Enterprises Division ....................Sh.5,028,186,000/=Kif. 3001 – Commerce ...................................................Sh.0/=Kif. 4002 – Commodity Market Development................Sh.0/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 60 – Biashara na Uwekezaji

Kif. 3001 – Commerce Division ......................Sh.991,528,000/=Kif. 3002 – Investment Division .....................Sh.1,603,730,000/=Kif. 4002 – Commodity Market

Development Division ..............Sh.15,256,981,750/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 44 – Viwanda

Kif. 1003 – Policy and Planning................. Sh. 71,460,377,000/=Kif. 2001 – Industry.......................................Sh.2,380,000,000/=Kif. 2002 – Small and Medium

Enterprises Division........................................Sh. 0/=Kif. 4002 – Commodity Market Development...............Sh. 0/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

Fungu 60 – Biashara na Uwekezaji

Kif. 4002 – Commodity Market Development Division................Sh.6,350,000,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NDG. ASIA MINJA – KATIBU MEZANI: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kutoa taarifa kwamba Kamati yaMatumizi imekamilisha kazi yake.

MWENYEKITI: Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Tukae. Mtoa hoja taarifa.

T A A R I F A

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lako likikaa kama Kamatiya Matumizi limekamilisha kazi zake. Naomba Taarifa yaKamati ya Matumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaNaibu Spika, naafiki.

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono, sasanitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na

Uwekezaji yalipitishwa na Bunge)

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika,mwongozo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bobali, naomba ukae.

Waheshimiwa Wabunge, nichukue fursa hii kwanzakumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara naUwekezaji kwa Bunge kupitisha bajeti yake na wataalamwake wako hapa, tuwatakie kila la kheri katika utekelezajiwa yale mliyoyaahidi mwaka huu maana mwakanitutakutana tena hapa na vitabu vitakuwa vitatu vyakuvitazama. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, yapo matangazo mawilikabla sijamruhusu Mheshimiwa Bobali. Tangazo la Kwanzalinahusu kikao cha Wabunge wa CCM ambacho kitaanzamara baada ya kumaliza kikao hiki. Waheshimiwa Wabungewote wa CCM wanatakiwa kuelekea White House natangazo linatoka kwa Katibu wa Wabunge wa CCM,Mheshimiwa Jasson Rweikiza.

Waheshimiwa Wabunge, tangazo lingine ni kwambaleo kulikuwa na mechi kati ya Serengeti Boys na Angola naSerengeti Boys imeshida goli mbili na Angola wamepata golimoja. Kwa hiyo, vijana wetu wanafanya vizuri, tuendeleekuwa pamoja nao kwa hali na mali ili waweze kufika mbalizaidi kama ambavyo tumefurahi leo. (Makofi)

MWONGOZO WA SPIKA

NAIBU SPIKA: Nitaruhusu Mwongozo mmoja kutokakwa Mheshimiwa Bobali.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika,nikushukuru kwa kunipa fursa hii kuomba Mwongozo wakonikitumia Kanuni ya 68(7) pamoja na Kanuni ya 101 ya Kanunizetu za Kudumu.

Mheshimiwa Naibu Spika, muda mfupi uliopitatulikuwa tunapitisha bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

na Uwekezaji lakini tumepitisha mafungu kwa mfumo wakupitisha kwa pamoja (guillotine). Mfumo huu umekuwaukitumika katika Wizara nyingi kama siyo zote zilizopita,jambo ambalo linatunyima fursa Wabunge kuitendea hakihotuba hii. Mimi binafsi nimeipitia, hotuba hii ni nzuri na inamambo mazuri lakini kuna mambo tulihitaji tupate ufafanuzikwa kupitia kifungu kwa kifungu badala ya kupitisha vyotekwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa itakavyokupendeza,naomba Mwongozo wako, kwa nini tusiwe tunachukua amawawili kutoka kwenye upande wa Ruling Party na hukummoja katika mshahara wa Waziri ili tuweze ku-balance,tupate watu watatu tuache kujadili bajeti za mambomengine kwamba mtu anakuja na sera yake na jambo lake,tujadili hotuba na vifungu vilivyopo kwenye hotuba yaMheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMwongozo wako kwa Kanuni hizo ambazo nimezisoma.Nakushukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nimeombwaMwongozo kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7) na MheshimiwaBobali. Maelezo ya Mheshimiwa Bobali wote tumeyasikia,yanahusu utaratibu wetu wa kupitisha Mafungu kwa pamojakwa mujibu wa Kanuni ya 104. Mheshimiwa Bobali anaonautaratibu huu unawafanya Waheshimiwa Wabungewashindwe kupitia mafungu mengine baada ya kuwa mudawote unaishia kwenye mshahara wa Waziri.

Waheshimiwa Wabunge, hizi Kanuni zetu uzuri wakezinazungumza kuhusu kila jambo. Ni sisi wenyewe ndiyotunaoamua namna tunavyotaka kufanya. Mwongozo huuuliwahi kuombwa na Mheshimiwa Dkt. Sware Semesi namaelezo yaliyotoka wakati huo ndiyo yatakayotoka sasa.

Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 101, Kanuni ya 103na Kanuni ya 104, ukizisoma hizi kwa pamoja, hasa Kanuni

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

ya 103 ndiyo inayozungumzia kuhusu kushika shilingi. Sasa,Bunge limeamua kuwa na utaratibu huo, si Bunge kamataasisi, kwa maana ya Wabunge wameamua kuwa nautaratibu huo ama niseme tumeamua kuwa na utaratibuhuo, kila mtu anataka kushika shilingi na kila mtu anatakakuchangia hoja ya mtu anayetaka kushika shilingi.

Kwa hiyo, kama tunataka kuyapitia Mafungu yote,tuache kushika shilingi ambayo haishikiki kwa sababu kunaMbunge anasimama tu hapa anataka kushika shilingi lakinihata jirani yake pale hajazungumza naye kwamba anatakakushika shilingi ili amuunge mkono. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, huu utaratibutumejitengenezea wenyewe na kwa kuwa tumetengenezawenyewe na hizi Kanuni ni za kwetu wenyewe basi matumiziyake sisi tuangalie tunataka kuangalia ipi, kama mshaharawa Waziri ndiyo ambao tunaupenda sana basi ni Kanuni ya103 ndiyo inayotufanya tukae muda wote tukijadili kifungukimoja. Kama tunaona tunataka kuangalia mafungumengine, matumizi ya kifungu cha 103 tuyapunguze.

Kwa hiyo, ni sisi wenyewe kwa kweli tunaoamuanamna ya kufanya na nadhani Bunge hili limeamua huopengine ndiyo utaratibu, lakini bajeti ya mwaka jana si kilabajeti ilikuwa inapita kwa utaratibu huu, ilikuwa inapitiwavifungu lakini safari hii tumeamua kutumia Kanuni yetu ya103 nayo ipo humu. Kwa hiyo, huwezi kuwazuia watuwanaotaka kushika shilingi kwa sababu na yenyewe niKanuni.

Waheshimiwa Wabunge, lakini sasa wapo Wabungewanaotoa hoja kana kwamba tunaweza kwenda zaidi yahuo muda wa nusu saa ambao Mwenyekiti amepewamamlaka akiwa kwenye Kamati ya Matumizi kama mudauliosalia haukutosha anaongeza nusu saa. Kanuni yetu ya104, haitoi fursa hiyo ya kuongeza muda zaidi ya nusu saa.Kwa hiyo, ndiyo utaratibu ambao tumejiwekea.

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Bobali ametoahapo na pendekezo kwamba kwa nini uwiano usiende hivi.Sasa uwiano ni namba, kwa hiyo ni sisi wenyewe Wabungetuambizane, mtu anaposimama kushika shilingi kamahaishikiki msiunge mkono kaeni ili hoja yake ife tuendelee nahoja nyingine. Tukisimama maana yake ni sisi wenyeweambao tunaamua kutumia muda wetu kwenye Kanuni ya103 badala ya Kanuni nyingine. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho, tarehe 19, Mei,saa tatu asubuhi.

(Saa 2.18 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Ijumaa,Tarehe 19 Mei, 2017, Saa Tatu Asubuhi)