100
1 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA THELATHINI NA TANO – TAREHE 26 JULAI, 2005 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa Mwaka 2001 – 2003, (The Annual Report and Accounts of the Tanzania Investment Centre for the Year 2001 - 2003). Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji) kwa Mwaka wa Fedha 2005/2006 MHE. IDDI M. SIMBA - (k.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI): Maoni ya Kamati ya Fedha na Uchumi Kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji) kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006. MHE. HAMADI RASHID MOHAMED - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji) kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni yake Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006. Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

  • Upload
    others

  • View
    9

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

1

BUNGE LA TANZANIA _______________

MAJADILIANO YA BUNGE _______________

MKUTANO WA ISHIRINI

KIKAO CHA THELATHINI NA TANO – TAREHE 26 JULAI, 2005

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI:

Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa Mwaka 2001 – 2003, (The Annual Report and Accounts of the Tanzania Investment Centre for theYear 2001 - 2003).

Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji) kwa Mwaka wa Fedha 2005/2006

MHE. IDDI M. SIMBA - (k.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI):

Maoni ya Kamati ya Fedha na Uchumi Kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji) kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006.

MHE. HAMADI RASHID MOHAMED - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI

Maoni ya Kambi ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji) kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na Maoni yake Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2005/2006.

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

2

MASWALI NA MAJIBU

Na. 333

Ushuru wa Soko kwa Wafanyabiashara Ndogondogo MHE. DR. HAJI MWITA HAJI - (k.n.y. MHE. RUTH B. MSAFIRI) aliuliza:-

Kwa kuwa, wafanyabiashara ndogondogo hutozwa ushuru wa soko kila siku, na kwa kuwa, tozo hilo huwa mzigo kwa mfanyabiashara ndogondogo kwa kuwa wakati mwingine hudaiwa tozo hilo hata kabla ya kuuza bidhaa zake jambo ambalo huzua ugomvi sokoni na wakati mwingine mfanyabiashara huyo hipigwa, hunyang’anywa bidhaa zake na wakati mwingine bidhaa zake humwagwa kitu ambacho ni kero kubwa.

(a) Je, ni lini Serikali itafuta utaratibu wa wafanyabiashara ndogondogo kutozwa ushuru huo wa kila siku?

(b) Je, Serikali itakubaliana nami kwamba, sasa ni wakati muafaka kuanzisha leseni

ya nguvu kazi inayoweza kutumika kati ya siku 30 hadi 90 ili mfanyabiashara ndogondogo aweze kubakia na kipato cha kujikumu?

(c) Je, ni lini Serikali italeta marekebisho ya sheria hiyo Bungeni?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI

ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Ruth Msafiri, Mbunge wa Muleba Kaskazini, ninaomba kutoa maelezo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa katika mwaka wa fedha wa 2003/2004 Serikali

ilifuta baadhi ya vilivyokuwa vyanzo vya mapato vya Serikali za Mitaa ambavyo ukusanyaji wake ulionekana kuwa ni kero kwa wananchi na pengine haukuwa na tija. Katika jedwali lililoambatanishwa na Muswada wa Sheria ambao hatimaye Bunge lilitoa maamuzi ya kukubalina na azma ya Serikali ya kufuta kodi za aina hiyo, kuna maelezo kwamba Halmashauri zinaruhusiwa kuendelea kutoza kodi mbalimbali ukiwemo pia Ushuru wa Masoko au ukodishaji wa mali kama ifuatavyo:-

(a) Kutoza Kodi kwenye Nyumba za Halmashauri. (b) Kutoza Kodi kwenye meza na vibanda vya masoko yaliyotajwa chini ya Sheria ya

Masoko Sura ya 106. (c) Magulio (d) Minada

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

3

(a) Sheria ilizuia Kuwatoza ushuru wakulima wanaouza mazao yao kwa utaratibu wa

kuja kutoka mashambani kwao na kuondoka mara baada ya kuuza mazao yao. (b) Vilevile, sheria iliwazuia kutoza ushuru wa Halmashauri kwenye magulio ya

Serikali za Vijiji.

(c) Ilizuia kuwatoza ushuru wachuuzi wadogowadogo wanaouza vyakula vilivyopikwa kama vile maandazi, samaki wa kukaanga na vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo mengine kilichokatazwa ni kuwatoza ushuru

wananchi wanaouza bidhaa zao mahali ambako Halmashauri haikuweka miundombinu ya aina yoyote. Lakini, pale ambapo kuna huduma zinazotolewa na Halmashauri, mfano jengo au choo, au maji au umeme, ni lazima watumiaji wa eneo hilo walipe ushuru kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na uwekaji wa eneo hilo kuwa katika hali ya kutumika.

Hata hivyo ikumbukwe kwamba, uamuzi huu, haukuruhusu kuvunja sheria za

matumizi ya Ardhi au Maendeleo ya Miji, kwa maana kwamba sasa biashara inaweza kufanyika mahali popote kiholela bila kuruhusiwa. Wafanyabiashara ndogondogo watakaoendesha shughuli zao kwenye maeneo ambayo hayakutengwa kwa madhumuni hayo ni dhahiri Mamlaka za Serikali za Mitaa za maeneo husika zitawaondoa. Vilevile kama biashara itaendeshwa kwenye maeneo yanayohatarisha Afya ya Jamii nazo zitaondolewa kwa mujibu wa Sheria zinazohusika.

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo, sasa ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Ruth

Msafiri, Mbunge wa Muleba Kaskazini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha kuelezea hapo mwanzo, Wafanyabiashara

wadogowadogo wa kila siku ambao kwa uhakika sio wakulima bali ni watu wa kati baina kwa mkulima na mlaji na kila siku wako kwenye maeneo yaliyowekewa huduma za Halmashauri, wanatakiwa kulipa ushuru wa kutumia maeneo hayo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, hali ya badaye ya kutungwa kwa Sheria ya kuongoza shughuli za

wafanyabiashara ndogondogo na hususani sekta isiyo rasmi itajulikana baada ya kukamilika kwa mpango ulioanzishwa wa kutambua sekta hiyo chini ya utaratibu ujulikanao kama Mkakati ya Kurasmisha Raslimali na Biashara Tanzania yaani MKURABITA.

Mheshimiwa Spika, ningependa kutoa wito kwa wafanyabiashara ndogondogo

kufuata matakwa ya Sheria na pia kuwa na ushirikiano wa kutosha na viongozi wa Serikali za Mitaa katika maeneo wanakoishi. Ushirikiano huo utasaidia kuondokana na tabia ya kukimbizana hovyohovyo au kumwagiwa au kunyang’anywa bidhaa zao wanaokuwa wako tayari kuziuza. Hali ya msuguano wa aina hii kwa wakati mwingine inatokea endapo kuna upande mmoja unapoamua kujichukulia sheria mkononi mwake.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

4

MHE. DR. HAJI MWITA HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa

nafasi kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa suala lililokuwepo hapa ni suala la biashara ndogondogo na ambapo kwa

kweli katika maeneo hasa kama Kariakoo, Shule ya Uhuru na Barabara ya Msimbazi shughuli kama hizi zimekuwa ni nyingi sana na hutendwa sana nyakati za usiku. Hii ina maana kwamba hata hizo nafasi ambazo zimetengwa hazitoshi.

Mheshimiwa Spika, Je, Mheshimiwa Waziri anatuambia nini kuhusu vijana hasa wale wa maduka ya mikononi na wauza biashara ya usiku usiku katika sehemu hizi za kariakoo na Buguruni pamoja na Shule ya Uhuru? Ahsante sana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI

ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dr. Haji Mwita, ambalo ningependa kulieleza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, wakati tunazingatia haki za wafanyabiashara ndogondogo

kufanya biashara zao vilevile tusisahau kwamba jumuiya/ jamii nayo vilevile ina haki zake. Wakati mfanyabiashara huyu anataka kutandika biashara kwenye eneo ambalo ni la wapita kwa miguu ajue kwamba vilevile anawanyima haki wananchi wenye haki ya kutumia eneo hilo. Kwa hiyo, hapo ni lazima sheria zilizowekwa zifuatwe.

Na. 334

Tatizo la Walimu Nchini

MHE. AGGREY D. J. MWANRI aliuliza:-

Kwa kuwa, juhudi kubwa zimeonekana katika mpango wa Elimu ya Msingi MMEM na Sekondari MMES, na kwa kuwa, katika hatua za awali za mipango hiyo limejitokeza tatizo kubwa la walimu.

(a) Je, kwa nini Serikali isikubali kuwaajiri kwa mkataba walimu waliostaafu na wale walioondolewa kazini kwa kupunguzwa ili kuondoa tatizo hilo hasa katika Jimbo la Siha?

(b) Kama utaratibu wa Mkataba upo, Je, kwa nini kumekuwa na urasimu mkubwa

katika kupata mkataba huo na hivyo kukwamisha walimu husika na nchi kuendelea kubaki katika tatizo hilo?

NAIBU WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO

(k.n.y. WAZIRI WA ELIMU NA UTAMADUNI) alijibu:-

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

5

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Utamaduni napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aggrey Joshua Mwanri, Mbunge wa Siha, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Walimu walioacha kazi kwa kustaafu au kupunguzwa kazini kwa

mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma Kifungu 17 (3) toleo la mwaka 2003, hawaruhusiwi kuajiriwa tena katika Utumishi wa Umma isipokuwa kwa idhini ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu hivi sasa imo katika zoezi la kubaini walimu

wanaostaafu hivi karibuni ambao watapenda kuajiriwa kwa mkataba kwa lengo la kuafikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili kuangalia uwezekano wa kumwomba Katibu Mkuu Kiongozi atoe idhini ya Walimu hao kuajiriwa kwa mkataba katika kipindi hiki cha utekelezaji wa MMES 2004 – 2009 ambapo wanafunzi wa Sekondari wataendelea kuongezeka kutoka 525,000 mwaka huu hadi 2,000,000 ifikapo mwaka 2010. Kwa maoni yangu ushauri wa Mheshimiwa Mbunge unafaa sana inafaa wahusika wote Serikalini tuufanyie kazi upesi sana.

MHE. AGGREY D. J. MWANRI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana ninashukuru kwa kunipa swali la nyongeza na ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri ambayo ameyatoa kwa niaba ya Serikali. Kwa kuwa, anazungumzia habari ya kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi na kwa kuwa tunakiri sisi wote hapa kwamba kuna hilo tatizo kubwa la walimu katika nchi yetu na tunao mapango wa MMEM na mpango wa MMES ambao tunakiri kabisa kwamba kuna tatizo la walimu.

Je, ni kwa nini sasa Serikali isishauri haraka haraka kwamba Katibu Mkuu Kiongozi

huyu afanye uamuzi wa kuwachukua hao walimu ili waweze kufanya hivyo? Katika Jimbo langu la Siha kuna Shule nyingi ambazo hazina walimu na wako

walimu wastaafu ambao wamepitisha maombi yao kupitia kwangu. Je, wakati tunasubiri huo mpango wa Katibu Mkuu Kiongozi, Jimbo la Siha linaweza likapatiwa kibali maaluma ili walimu hao waweze kusaidia katika hizo shule?

NAIBU WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO (K.n.y WAZIRI WA ELIMU NA UTAMADUNI): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali miwili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwanri, Mbunge wa Siha kama ifuatavyo.

Hili suala la kutoa ushauri wa haraka haraka ndicho tulichokuwa tumejibu katika jibu

letu la swali la msingi kwamba tumeshaanza kuwasiliana na Katibu Mkuu Kiongozi tuone umuhimu wa kuwachukua hawa walimu ambao wanakaribia kustaafu hivi karibuni. Lakini msisitizo ambao tunauweka Serikali ni kuandaa walimu wapya ndiyo maana tumegeuza baadhi ya Vyuo vya Ualimu viwe Vyuo Vikuu shirikishi ili kupata walimu watakaoweza kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi.

Hili suala la kuchukua walimu waliostaafu ni mpango tu wa muda lakini msingi

mkubwa au msisitizo mkubwa tunauweka na kuwaandaa walimu wapya.

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

6

Kuhusu Siha, ningependa nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tatizo hili la upungufu wa walimu halipo Siha tu, lipo kila mahali hata kule katika Jimbo la Mchinga kuna Shule mbili za Melola na Mchinga ambazo bado hazina walimu kwa hiyo ningependa nitumie nafasi hii kumwomba Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wengine wote wavute subira wakati Wizara inafuata taratibu za kuzungumza na Katibu Mkuu Kiongozi kuweza kupata Walimu hao. (Makofi)

Na. 335

Kompyuta kwa Shule za Msingi na Sekondari

MHE. THOMAS NGAWAIYA – (k.n.y. MHE. DR. WILLBROD P. SLAA)

aliuliza:- Kwa kuwa, katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya

Mwaka 1999/2000 imeonyesha udhaifu mkubwa katika ununuzi wa Kompyuta zenye thamani ya shilingi 311,065,658/- kwa ajili ya shule za Msingi na za Sekondari, na kwa kuwa, iliagizwa kuandaa vyumba kwa ajili ya vifaa hivyo na fedha nyingi zimetumika kwa kazi hiyo lakini baadaye kompyuta hizo hazikupelekwa kwenye shule hizo.

(a) Kwa kuwa, kuna taarifa kuwa Kompyuta hizo ziliagizwa zikiwa mbovu na utaratibu wa kawaida wa tenda haukutumika, Je, ni shule ngapi za Sekondari ziligawiwa kompyuta hizo kwa majina na ni kampuni gani kwa jina iliyopewa jukumu kuagiza na kuleta nchini kompyuta hizo, zilikuwa ngapi, zilinunuliwa kutoka nchi gani na ni kampuni gani ilituuzia vifaa hivyo?

(b) Kwa kuwa, Serikali imepata hasara kubwa kutokana na ununuzi wa kompyuta

hizo pamoja na gharama kubwa za kuandaa vyumba kwa ajili hiyo ambavyo vimebaki tupu. Je, wahusika kwa maana ya kampuni iliyohusika kuingiza kompyuta hizo na viongozi wa Wizara husika ambao hawakusimamia vizuri wala kudhibiti kanuni na taratibu w za manunuzi wa mali ya Serikali wanachukuliwa hatua gani?

(c) Je, Serikali ina mpango gani sasa madhubuti wa kuzipatia shule za Sekondari

kompyuta zinazofaa na za kisasa ili wanafunzi wetu katika shule hizo wanufaike na matunda ya karne hii ya Sayansi na Teknolojia?

NAIBU WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO

(k.n.y. WAZIRI WA ELIMU NA UTAMADUNI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Utamaduni

naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Willbrod Slaa, Mbunge wa Karatu, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

7

(a) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iligawa Kompyuta 638 kwa Vyuo na Shule za Sekondari 128. Majina ya Vyuo na Shule hizo yameambatanishwa. Kampuni iitwayo IT-GENSBRUG ndiyo iliyoiuzia Serikali na kuziingiza nchini kompyuta 815.

(b)Mheshimiwa Spika, Kampuni iliyouza Kompyuta hizo na maafisa waliohusika na

ununuzi wa kompyuta hizo hawajachukuliwa hatua yoyote kwa sababu suala hili liko mikononi mwa PCB na Serikali inasubiri taarifa rasmi ya chombo hicho ili iweze kuchukua hatua zinastahili kutokana na ukweli utakaojitokeza katika taarifa hiyo.

(c) Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika hotuba ya Bajeti ya Wizara yangu,

Serikali imechukua hatua madhubuti ya kuanza kufundisha somo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yaani TEHAMA katika Vyuo vya Ualimu vyote kuanzia mwaka huu wa fedha. Somo hilo litakuwa la lazima kwa kila Mwalimu Tarajali na aidha mafundi wataandaliwa kwa ajili ya utunzaji mzuri wa kompyuta na Maabara za Kompyuta zitakazokuwepo katika kila Chuo cha Ualimu. Baada ya mafanikio ya hatua hii muhimu ndipo itafuata hatua ya mradi wa kuanzisha somo hilo kwa uhakika katika shule za Msingi na Sekondari tukiwa na uhakika wa Walimu, Mafundi, Vifaa na Umeme kwa ajili ya kompyuta.

MHE. THOMAS NGAWAIYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru na pia ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini pamoja na majibu hayo ningeuliza maswali madogo mawili.

(a) Kwa kuwa, kompyuta nyingi zinatengenezeka, yaani unaweza kusema ni mbovu

lakini zinatengenezeka. Je ni hatua gani Serikali imechukua kuhakikisha kwamba hizo Kompyuta kweli ni mbovu au zinahitaji labda baadhi ya vifaa tu?

(b) Kwa kuwa, kompyuta ni chombo muhimu kinachotumika mashuleni na dunia

nzima na kwa kuwa shule zetu nyingi hazina umeme, Wizara ina mpango gani kwa kuhakikisha at least kunapatikana umeme mashuleni na umeme unaofaa?

NAIBU WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO (K.n.y. WAZIRI WA ELIMU NA UTAMADUNI): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali miwili ya Mheshimiwa Thomas Ngawaiya, Mbunge wa Moshi Vijijini, kama ifuatavyo:-

(a) Ni kweli kwamba kompyuta zinatengeneza kama vifaa vingene vyovyote vya

electronics, lakini kwa sababu suala hili linalohusu kompyuta hizi sasa hivi linashughulikiwa na PCB kujaribu kugundua huo ubovu unaodaiwa na namna zilivyoingizwa. Tukianza tena kuzichezea kompyuta hizo hizo kuna uwezekano wa kuharibu hayo yanayotafutwa na wenzetu wa PCB ndiyo maana hatukuamua kuchukua hatua za kuzifanyia marekebisho katika kipindi hiki.

(b) Suala la umeme, pamoja na kwamba tunafahamu umeme wa TANESCO unaweza

ukachelewa kuzifikia shule nyingi utaratibu unafanywa na Wizara ya Elimu na Utamaduni kuangalia uwezekano wa kufikisha umeme hata wa solar walau katika kile

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

8

chumba tu au maabara ya kompyuta ili kompyuta hizo ziweze kufanya kazi mara tutakapokuwa tumeshaandaa walimu watarajali, mafundi na maabara.

Na. 336

Wafanyakazi wa Kiraia Katika JWTZ

MHE. KHAMIS AWESU ABOUD – (k.n.y. MHE. RAMADHANI NYONJE PANDU) aliuliza:-

Kwa kuwa, katika ajira ndani ya JWTZ huajiriwa pia wafanyakazi wa Kiraia (wahudumu) ambao wengi wao huwa wanawake, lakini mara nyingi wafanyakazi hao wanapofariki huwa mikataba yao haifuatwi, na warithi wao wanapofuatilia stahili za marehemu wanasumbuliwa sana hadi wanakata tamaa na kuacha kabisa kufuatilia na kusamehe madai hayo bila kutaka.

(a) Je, ni nini haki za mfanyakazi wa aina hiyo ndani ya JWTZ anapofariki

zinazostahili kulipwa kwa warithi wake, au familia yake wanatakiwa kukaa muda gani baada ya taratibu za vielelezo vyote vya marehemu kukamilika ili kwenda kuchukua haki, mafao na stahili zao na kuepuka usumbufu?

(b) Je, usumbufu unaofanywa na Maofisa husika, Serikali haioni kuwa huo ni

mpango maalumu wenye lengo la makusudi la kutaka kuwaibia, kuwanyang’anya na kuwadhulumu warithi wa marehemu kwa maana ya kuwa aliyekufa na lake halipo?

(c) Je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa kabisa kero hizo kwa jamaa wa

marehemu hasa wanaosafiri kutoka Mikoani kwenda Makao Makuu ya Jeshi hilo – Dar es Salaam ambao wanapata hasara kutokana na gharama kubwa za kufuatilia stahili hizo bila mafanikio?

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI (k.n.y. WAZIRI WA ULINZI

NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kabla

ya kujibu swali la Mheshimiwa Ramadhani Nyonje Pandu, Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, napenda kutoa maelezo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, watumishi raia wanaofanya kazi jeshini wanatawaliwa na sheria

zilezile zinazowatawala watumishi raia wengine wote Serikalini, yaani watumishi wa Umma walioko katika Wizara na Taasisi nyingine za Serikali. Watumishi hao wamegawanyika katika makundi miwili yaani walioko kwenye masharti ya kudumu (Pensionable) na wale wasio kwenye masharti ya kudumua yaani Operational Service.

Mheshimiwa Spika, watumishi walioko kwenye masharti ya kudumu yaani

Pensionable wanatawaliwa na Sheria Na. 2 ya mwaka 1999 na wale wa Operational Service wanatawaliwa na Sheria Na. 28 ya mwaka 1997.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

9

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na JKT

sasa napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pandu, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:

(a) Malipo ya Mirathi yaani Death Gratuity yanamhusu mtumishi aliyefariki ambaye

alikuwa katika Mashariti ya Kudumu. Malipo haya hutolewa kwa wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki. Wategemezi hao

wanaweza kuwa na watoto, mjane au wazazi ambao walikuwa wakimtegemea marehemu kwa kiasi kikubwa katika kuendesha maisha yao. Ili madai yaweze kulipwa hati zifuatazo pale zinapohusika lazima ziwasilishwe katika Mfuko:-

(i) Hati ya usimamizi wa Mirathi ikionyesha Mahakama ambayo malipo ya Mirathi

yatalipwa. (ii) Cheti halisi cha Kifo yaani Original copy. (iii) Picha mbili passport size za msimamizi wa mirathi. (iv) Cheti/vyeti vya kuzaliwa watoto wenye umri usiozidi miaka 18 kwa wale

wasiosoma na wale wenye umri zaidi ya miaka 18 ambao bado wako masomoni. (v) Picha za watoto – 3 kila mmoja. (vi) Cheti cha ndoa na kiapo cha Mjane. (vii) Picha za Mjane – 3. (viii) Hati ya kiapo cha mlezi wa watoto. (ix) Hati ya uthibitisho wa wategemezi wengine zaidi ya Mke/mume na watoto

ambao walikuwa wakimtegemea marehemu kwa asilimia 100. (x) Muhtasari wa kikao cha wanafamilia cha uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi.Baada

ya kutimiza masharti yaliyotajwa hapo juu malipo yafuatayo hufanywa kwa wategemezi wa mtumishi aliyefariki.

(i) Malipo ya mirathi ambayo yatalipwa mara moja kupitia Mahakama ambapo

Mirathi ilifunguliwa. (ii) Malipo ya wategemezi ya kila mwezi hadi atakapofikia miaka 21 kwa kila

mtegemezi. (iii)Malipo ya Mirathi yatalipwa baada ya kukamilisha taratibu zote za mirathi kupitia

Mahakamani.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

10

Mheshimiwa Spika, Sheria Na. 28 ya mwaka 1997 ilianzisha Mfuko wa Hifadhi ya

Jamii ili kutoa huduma kwa watumishi wa Serikali ambao wako katika masharti ya Operational Service, pamoja na waajiriwa binafsi na walioajiriwa katika Sekta binafsi.Mfuko huu wa Hifadhi ya Jamii hutoa mafao ya aina zifuatazo:-

(i) Pensheni itokanayo na kustaafu; (ii) Pensheni ya ulemavu; (iii) Msaada wa mazishi; (iv) Mafao ya uzazi; (v) Mafao ya kuumia kazini; na (vi) Bima ya afya. (b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haina taarifa kuhusu usumbufu uliokithiri

unaofanywa na Maofisa pale Wizarani na kama wapo naomba Mheshimiwa Mbunge anipatie taarifa kamili ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao kwani siyo sera ya Serikali wala nia ya Serikali kuwatesa wananchi wake.

(c) Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia maafisa wake waandamizi itaendelea kuwaelimisha watumishi wake ili waweze kuzielewa vema sheria hizi na hivyo kuweza kuwa makini zaidi katika kuwaelekeza wafiwa kuhusu taratibu zote za kulipwa mafao ya marehemu kwa kuzingatia kwamba mafao hutolewa kwa warithi kupitia Mahakama walikofungulia mirathi.

MHE. KHAMIS AWESU ABOUD: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupata

nafasi hii ili niulize maswali miwili ya nyongeza kama ifuatavyo. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba niulize hivi:-

Kwa kuwa, hawa wafanyakazi wanafanya kazi private katika maeneo ya Jeshi na

ndiyo maana wakapata usumbufu kama huu uliotokea. Kwa nini Serikali sasa haiwaajiri kama wanajeshi kamili ili kuondoa huu usumbufu? Kwa kuwa, matatizo haya yametokea muda mrefu sana kutokulipwa mafao ya warithi wa marehemu sasa kwa maelezo ya Naibu Waziri kuna Vielelezo mbalimbali wanavyotakiwa wapeleke huko Serikalini ili waweze kulipwa hayo mafao yao. Sasa Serikali ina mpango gani wa kuwafahamisha hao warithi wa marehemu wafuate hizo taratibu na wapate mafao yao kwa wakati unaofaa. Ahsante.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI (k.n.y. WAZIRI WA ULINZI

NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khamis Awesu, Mbunge wa Mkanyageni Pemba, kama ifuatavyo:-

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

11

Mheshimiwa Spika, katika majeshi yote kuna baadhi ya kazi ambazo wanaajiri raia

na kuna kazi ambazo raia wanaajiriwa kule na kujiunga na jeshi ni hiari ya mtu si kwamba kila mtu akiishaajiriwa kwa kazi fulani ndani ya Jeshi basi moja kwa moja alazimishwe awe mwanajeshi. Huo utaratibu haupo na kwa hiyo hatuwezi kusema kila raia ambaye anafanya kazi jeshini moja kwa moja tumtie katika Jeshi, hapana kama kuna vijana wataka kuingia katika jeshi na sifa wanazo za kuingia katika Jeshi wanaweza wakapokelewa lakini si lazima kila raia ndani ya Jeshi alazimishwe kuwa Mwanajeshi.

Mheshimiwa Spika, sasa kuhusu hili la muda mrefu, dhana kwamba watumishi raia

ndani ya Jeshi pale ambapo wanapofiwa au wanapofariki mafao yao yanachukua muda mrefu si dhana sahihi. Kama yule Mhusika ametekeleza haya masharti ambayo nimeyasema hizi nyaraka ambazo nimezitaja. Jambo kubwa ambalo Mheshimiwa Mbunge nataka uelewe na raia na wananchi kwa ujumla ni kwamba malipo ya mafao yanaendana na nyaraka mbalimbali, sasa baadhi ya Watanzania wengi utunzaji wa nyaraka hizi na Kumbukumbu hizi hawafuati. Sasa tujenge utamaduni mpya wa kutunza hizi nyaraka kama vyeti vya watoto, vyeti vya vifo na nyaraka zote zinazohitajika. Kwa kweli tukitunza hizi nyaraka na zikipelekwa kunakohusika kwa wakati, malipo yatalipwa kwa wakati.

MHE. MZEE NGWALI ZUBEIR: Nashukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuuliza

swali au maswali madogo miwili ya nyongeza. SPIKA: Hapana swali moja tu. MHE. MZEE NGWALI ZUBEIR : Mheshimiwa Spika, namwuliza kama hivi

ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kuwa urasimu unaosababisha kwa

uchelewashaji wa kulipwa na suala hili kwa kweli lipo na linaendelea. Je, Serikali haioni ipo haja wakati ambapo Mtumishi yupo hai aweke mrithi wake maalumu ambaye atashughulikia wakati ambapo kifo kinatokea?

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI – (k.n.y. WAZIRI WA

ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zubeir Ngwali Mzee, Mbunge wa Nungwi kama ifuatavyo.Kuhusu mfanyakazi kabla hajafariki kuteua mrithi wake ili kupunguza mlolongo, huo utaratibu upo. Unapojaza zile fomu za ajira, zile fomu binafsi za ajira kuna, kipengele pale ambacho kinasema endapo kunatokea jambo lisilotegemewa unataka nani wawe warithi wako, unajaza pale. Kwa hiyo, hili si tatizo. Tatizo ni kwamba huyo sasa ambaye ameteuliwa kufuata hizo taratibu kwanza tu kwenda mahakamani kwenda kuapishwa kwamba ateuliwe kuwa ndiye mshika mirathi kuna baadhi ya maeneo mwaka mzima kupata zile hati za kushika mirathi inachukua mwaka mzima.

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

12

Sasa kupeleka vyeti vingine, picha, vyeti vya ndoa, mwingine anapeleka cheti cha kifo nakala kumbe inatakiwa original kwa hiyo haya mambo haya Watanzania tukishayaelewa vizuri kwa kweli itasaidia sana kupunguza hili tatizo.

Na. 337

Kituo cha Polisi Longido

MHE. DR. MASUMBUKO R. M. LAMWAI (k.n.y. MHE. LAIZER M. LEKULE) aliuliza:-

Kwa kuwa, Kituo cha Polisi Longido kilijengwa na Wakoloni mwaka 1939 na kimebaki na majengo hayo hayo hata baada ya kuongezwa kwa askari lakini nyumba hazijaongezwa au kuboreshwa zile zilizopo.

(a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga nyumba zaidi kwenye kituo hicho

ambacho kinahudumia eneo kubwa la mpakani? (b)Kwa kuwa Kituo hicho kiko mbali na Makao Makuu ya Wilaya, Je, kwa nini

Serikali isiwapatie gari jipya ili kuwawezesha askari kuzungukia jimbo lote kuliko kila mara kutoa taarifa Wilayani kuomba gari wakati wa matukio hatari?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Michael Laizer,

Mbunge wa Longido, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa nyumba za kituo cha Polisi Longido

zilijengwa na wakoloni na hazifanyiwa ukarabati kwa hiyo ni chakavu. Hali hii ndivyo ilivyo katika Vituo vingi vya Polisi katika maeneo mengi hapa nchini. Serikali tayari inao mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba za Polisi pote nchini, na kujenga zingine mpya. Mpango huu umeanza kutekelezwa kwa awamu. Kwa hiyo, nyumba za Longido nazo zitafikiwa kwa wakati muafaka.

Aidha, kwa sasa Kituo cha Longido kina nyumba tatu za askari zenye uwezo wa

kuishi familia tisa (9) ambazo zinatosheleza idadi ya askari waliopo kwa hivi sasa. Jambo muhimu pale Longido ni kuzifanyia ukarabati nyumba hizo mara fedha zikipatikana.

(b) Mheshimiwa Spika, kituo cha Polisi Longido kipo umbali wa kilometa 25 kutoka kituo cha mpakani cha Namanga. Gari iliyopo Namanga ina jukumu la kufanya doria katika maeneo ya Namanga, Longido na Oldonyo Sambu.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

13

Tunaamini kwa sasa gari hilo linatosheleza mahitaji ya ulinzi na usalama wa eneo la Longido kwa kuwa hali ya uhalifu katika eneo hilo iko chini sana. Mathalani, kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2004 na Januari hadi Juni, 2005 matukio makubwa ya uhalifu yaliyoripotiwa katika Kituo cha Polisi Longido yalikuwa matatu tu. MHE. AGGREY D. J. MWANRI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa Kituo hicho cha Longido kina- save pia Jimbo la Siha ambalo liko mpakani na karibu sana na Jimbo la Longido; na kwa kuwa kumekuwa kuna matukio makubwa ya wizi hasa wa mifugo. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana na mimi sasa kwamba wakati umefika wa kutoa gari kwa ajili ya Kituo Sanya juu ambacho kina save pia katika Jimbo hilo la Longido? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kama tulivyoeleza wakati ule wa hotuba yetu ya Bajeti kwamba kwa sasa hivi uwezo uliopo wa Serikali ni kupeleka magari katika Vituo vikubwa vya Wilaya kwa ma-OCD na kwa ma-OCID wale wapelelezi hizo ofisi mbili. Vituo vya nje ya Makao Makuu ya Wilaya kama kile cha Siha uwezo wa kupeleka gari sasa hivi haupo. Lakini hayo magari ambayo tunapeleka sasa hivi kwa sababu pale Wilaya ya Hai mtakuwa na magari mawili, moja la OCD na OCID sasa wanapata uwezo kwa kweli na kuhudumia sasa mpaka Siha kwa karibu zaidi. Hata hilo la Longido kwa sababu umesema mko karibu karibu na shughuli za Polisi hazina mipaka. Kwa hiyo, hilo gari la Namanga na Longido vilevile litafika mpaka Siha kwa sababu kazi za Polisi hazina mpaka.

Na.338

Matengenezo ya Barabara ya Mbande – Kongwa MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Kwa kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa kuifanyia matengenezo makubwa (kwa mpango wa HIPC) barabara ya Mbande-Kongwa-Chunyu hadi Mpwapwa; na kwa kuwa mpango huo umetekelezwa kwa matengenezo ya barabara ya kutoka Mbande hadi Kongwa. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuiweka katika Mpango wa HIPC barabara ya kutoka Kongwa - Nghambi – Chunyu- Hadi Mpwapwa ili ifanyiwe matengenezo makubwa kuliko hali ilivyo sasa ya matengenezo madogo madogo ambayo yanaigharimu Serikali fedha nyingi?

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

14

(b) Je, Serikali inafahamu kwamba barabara hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wa Wilaya ya Mpwapwa kwa sababu ndiyo barabara kuu ya Wilaya hiyo? NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa George Malima Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, lenye sehemu (a) na (b) naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, barabara ya Mbande-Kongwa-Chunyu -Mpwapwa kama ilivyotajwa na Mheshimiwa Mbunge inajumuisha barabara tatu zinazohudumiwa na Wizara ya Ujenzi kwa kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoani Dodoma. Sehemu ya barabara ya Mbande – Kongwa yenye urefu wa kilometa 16 iko katika barabara ya Mbande – Kongwa- Suguta, na sehemu Kongwa Junction - Ng’ambi yenye urefu wa kilometa 5.9 iko katika barabara ya Manchali – Ng’ambai - Kongwa Junction - Hogoro Junction na sehemu ya Ng’ambi - Chunyu – Mpwapwa yenye urefu wa kilometa 31.6 iko katika barabara ya Ng’ambi – Mpwapwa - Lupeta – Pandambili. Baada ya maelezo hayo mafupi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George M. Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuzifanyia matengenezo makubwa barabara za Mbande - Kongwa, Kongwa Junction – Ng’ambi – Chunyu hadi Mpwapwa. Kupitia Mpango wa HIPC sehemu ya barabara ya Mbande hadi Kongwa yenye urefu wa kilometa 16 imefanyiwa matengenezo makubwa. Sehemu ya barabara ya Kongwa Junction – Ng’ambi - Chunyu – Mpwapwa yenye urefu wa kilometa 37.7 imejumuishwa katika mpango wa matengenezo ya barabara ya mwaka 2005/2006 kwa kufanyia matengenezo ya muda maalum (periodic maintenance) sehemu ya Ng’ambi - Chunyu - Mpwapwa yenye jumla ya urefu wa kilometa 8 na sehemu iliyobaki itafanyiwa matengenezo ya kawaida. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii kwa maendeleo ya uchumi wa Wilaya ya Mpwapwa ndiyo maana inaendelea kuipa kipaumbele katika matengenezo ili iweze kupitika wakati wote. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali itaendelea kuzifanyia matengenezo barabara zote nchini ikiwa ni pamoja na barabara za Jimbo la Mpwapwa kadri ya uwezo wake utakavyoruhusu. Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Mbunge George Lubeleje, kwa ufuatiliaji wake wa makini kuhusu barabara za Wilaya ya Mpwapwa kwa ujumla.

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

15

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwanza, napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jinsi anavyojitahidi kujibu maswali yetu na kufuatilia utekelezaji wa matengenezo ya barabara. (a) Kwa kuwa Serikali imekubali kutengeneza barabara ya Kata ya Matomondo, Isovu- Mima- Iyoma na Mkanana. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana nami kwamba iwapo barabara hizo zitatengenezwa mapema zitasaidia maendeleo katika vijiji hivyo? (b)Kwa kuwa barabara ya Mbande- Mpwapwa inapitisha magari zaidi ya 50 kwa siku kwa ajili ya kusomba mazao kutoka Ikaranga, Jipusamu pale Msagari. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana nami kwamba barabara hii ikishatengenezwa basi haitagharimu Serikali fedha nyingi badala ya kutengeneza kila siku matengenezo madogo madogo? Ahsante. NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba barabara ya Matomondo inatengenezwa kwa fedha za Road Fund na yenyewe inatengenezwa wakati wote fedha zinapopatikana kwa kiwango kinachopaswa. Nakubaliana kabisa kwamba barabara hiyo ikitengenezwa kwa uhakika inaweza kuhudumia Wilaya hii kwa makini kabisa. Mheshimiwa Spika, barabara ya Mbande-Mpwapwa ni barabara ya Mkoa. Barabara hii tungependa kuitengeneza kwa kiwango kikubwa sana. Lakini Mheshimiwa Mbunge ni shahidi kwamba Bajeti yetu iliyopita imeonyesha jinsi gani tumegawanya sungura mdogo kwa nchi nzima. Kwa hiyo, wananchi wa Mpwapwa wastahimili tu kwamba tutatengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe kwa kile kiasi ambacho sisi fedha zinaturuhusu.

Na. 339

Kuunganisha Makao Makuu ya Mkoa kwa Barabara MHE. LUCAS L. SELELII aliuliza:- Kwa kuwa ni lengo la Serikali kuunganisha Makao Makuu ya Mikoa kwa barabara za lami:- Je, kuna mpango gani wa kuunganisha Mji wa Tabora na Makao Makuu ya Kigoma, Shinyanga, Mbeya na Rukwa? NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

16

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Lucas Selelii, Mbunge wa Nzega, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nia ya Serikali ni kujenga kwa kiwango cha lami mtandao wote wa Barabara Kuu nchini na wakati huo huo kuhakikisha barabara zote za Mikoa na zile muhimu za Wilaya na Miji zinakarabatiwa na kufanyiwa matengenezo yanayotosheleza ili ziweze kupitika vizuri katika majira yote ya mwaka. Lengo kuu ni kuunganisha na kuboresha huduma za mawasiliano kati ya nchi jirani, Mikoa, Wilaya na Miji. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami unakwenda sambamba na mkakati wa Kitaifa wa kufuta umaskini katika nchi yetu ifikapo mwaka 2025. Aidha, Ujenzi wa barabara zetu kwa kiwango cha lami utatekelezwa kwa awamu, kulingana na upatikanaji wa fedha. Mipango iliyopo ya kuunganisha Mji wa Tabora na Makao Makuu ya Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Mbeya na Rukwa kwa barabara za lami ni kama ifuatavyo:- (i) Tabora – Kigoma: Barabara ya Itigi-Tabora, Ipole ilishafanyiwa usanifu na kukamilika mwaka 1997, ikiwa ni sehemu ya mradi wa Itigi Tabora-Ipole-Kaliua-Malagarasi-Uvinza-Kigoma. Katika mwaka wa fedha 2002/2003, utekelezaji wa mradi huu ulianza sehemu ya uvinza – Malagarasi Kilomita 54. Aidha, katika mwaka wa fedha 2004/2005, Serikali iliweka katika bajeti yake fedha za kufanyia usanifu wa kina wa ujenzi kwa kiwango cha lami, sehemu iliyobakia ya Kigoma- Uvinza na Tabora- Kaliua (ii) Tabora – Mbeya: Barabara ya Mbeya –Chunya – Makongorosi kilomita 115 imekwishafanyiwa usanifu wa kina kwa lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami. Hatua itakayofuata ni ile ya kumpata Mkandarasi na kwa wakati huu makabrasha ya zabuni yanapitiwa. Aidha, ujenzi wa barabara hii umepangwa kuanza ndani ya mwaka wa fedha wa 2005/2006. Ujenzi wa barabara hii unagharamiwa moja kwa moja na fedha zetu za ndani. (iii) Tabora – Shinyanga: Mpango wa kuijenga barabara ya Nzega – Tabora kilomita 105 kwa kiwango cha lami utaanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa fedha 2008/2009. Aidha, barabara kati ya Nzega – Manonga mpakani mwa Mkoa wa Shinyanga yenye urefu wa kilometa 30 inajengwa kwa kiwango cha lami hivi sasa. Ujenzi huu umepangwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka 2005. Fedha kwa ajili ya kugharamia ujenzi huu zimetolewa na Jumuiya ya Ulaya. (iv) Tabora – Rukwa: Barabara ya Tabora – Ipole kilomita 90 imepangwa kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia mwaka wa fedha wa 2008/2009. Barabara kati ya Ipole - Mpanda kupitia Inyonga imo pia katika mpango ambao unalenga kuhakikisha ifikapo mwaka 2011 barabara zote kuu nchini zitakuwa zimejengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, barabara ya Tunduma - Sumbawanga – Mpanda kilomita 462, inafanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

17

lami. Zoezi hili limekamilika kati ya Tunduma – Sumbawanga kilomita 230 kwa fedha toka Benki ya Dunia. MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, nakushukura sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, inaelekea eneo hilo la Kanda ya Magharibi au Western Corridor litapata barabara za lami ifikapo mwaka 2010. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kwamba ni aibu kubwa kwa eneo hilo ambalo lina uzalishaji wa kutosha, lina watu wa kutosha na lina madini ya kutosha kucheleweshwa hadi wakati huo kama fedha zimepatikana isingewezekana katika mwaka wa fedha ujao 2006/2007 na kwa sababu usanifu upo tayari barabara hizo zikajengwa ili kujenga uchumi wa kijiografia? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba sehemu hiyo ambayo nimeizungumzia hapa itapata barabara polepole hadi mwaka 2011. Lakini hii ni kutokana na kutokuwa na uwezo wetu sisi wenyewe wa kuweka fedha mara moja. Kama fedha zingepatikana hata mwakani uwezo wa Western Corridor kupata barabara kabla ya mwaka 2009 upo ila tatizo ni uwezo wa kifedha Serikali lazima ipange na kupanga ni kuchagua. MHE. ELIACHIM J. SIMPASA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Upembuzi yakinifu unachukua muda mrefu sana. Kuna barabara hii ya kutoka Arusha kwenda Iringa upembuzi yakinifu umefanyika kwa miaka mingi. Kuna barabara hii ya kutoka Tunduma kwenda Sumbawanga walisema mwaka 2002/2003 kwamba upembuzi yakinifu umefanywa. Sasa watafanya upembuzi yakinifu mara ngapi ili barabara hizi zianze kutengenezwa si kupanga ni kuchagua, wachague jamani wanafanya kazi ya namna gani? (Kicheko) NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara una matatizo kidogo, unafanya upembuzi yakinifu leo na ukakosa fedha za kujengea barabara na baada ya miaka mitatu kama hujajenga barabara hiyo maana yake utarudi tena kufanya upembuzi yakinifu ama siyo utajenga barabara ya zamani na siyo katika mkondo mpya. Tofauti sana kwa mfano barabara ya kutoka Morogoro kuja Dodoma hii haifanywi tena upembuzi yakinifu. Hii ni barabara ambayo ipo na tunataka kuikamilisha kwa kiwango cha lami mpya. Hivyo, wanaotengeneza barabara hiyo unawapa uwezo wa ku-design kwa kupanua kidogo barabara hiyo lakini siyo kufanya usanifu upya. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndiyo maana mnaona mara nyingi tunarudia rudia upembuzi yakinifu na usanifu siyo kwamba tunapenda, lakini kwa sababu watoaji fedha wanaweza wakatoa fedha kwa sababu ya upembuzi yakinifu, lakini baadaye watakupa fedha kwa sababu ya usanifu. Upembuzi yakinifu ni kuangalia kama barabara katika mwelekeo huo ina faida kupita hapa ama hapana. Upembuzi sanifu ni ku-design barabara yenyewe hatua kwa hatua na hizo ni hatua muhimu kabisa kwa barabara kutengenezwa. MHE. RHODA L. KAHATANO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika swali la msingi ilikuwa ni kuunganisha Mikoa na Wilaya kwa barabara za lami na katika Mkoa wa Kagera tuna

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

18

tatizo kama hilo la kuunganisha barabara ya Ngara-Karagwe-Bukoba-Biharamulo-Muleba na Bukoba. Mheshimiwa Spika, Serikali inaiangaliaje sehemu hiyo ambayo sasa hivi ina matatizo ya majambazi na ni kwamba unapotaka kutoka Bukoba kwenda Karagwe-Ngara lazima uende na askari na unapotaka kwenda Biharamulo lazima uende na askari wa kukulinda kwa sababu majambazi yamezidi kutoka nchi za jirani. Lakini tunaamini kwamba kama kutakuwa na barabara ya lami na usafiri utakuwa ni rahisi labda. Je, ni lini Serikali inapanga kujenga barabara za lami Ngara, Karagwe na Biharamulo kuungana na ofisi ya Mkoa Kagera? NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara nzuri na barabara mbaya hazizuii ujambazi. Majambazi wale ambao wapo pale wamepatiwa dawa kidogo baada ya Serikali kugundua kwamba pana misitu pale mikubwa na wao wanajificha humo ndani. Kwa hiyo, wanatoa escort ya kwenda huko na barabara ikiwa nzuri zaidi ya lami ujambazi utakuwa wa aina yake ya kisasa kwa sababu watakuwa na usafiri bora, wanaweza kwenda kasi na pengine kuongezeka zaidi kulikoni ilivyo sasa. Lakini hiyo haizuii sisi kutengeneza barabara bora pale ambapo uwezo utatuwezesha tutatengeneza barabara ya lami kutoka Ngara-Karagwe-Biharamulo hadi Bukoba.

Na. 340

Makandarasi wasio na Sifa HE. DR. THADEUS M. LUOGA aliuliza:- Kwa kuwa barabara na madaraja hapa nchini huharibika haraka haraka baada ya matengenezo kutokana na Bodi ya Zabuni ya Barabara kutoa kazi kwa Wakandarasi wasio na sifa, kama vile kutokuwa na vifaa, uzoefu na hata wakati mwingine kutokuwa na Wataalam muhimu:- Je, linapotokea jambo kama hilo hatua gani zinachukuliwa kwa Bodi yenyewe na pia kwa Mkandarasi? NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Thadeus Luoga, Mbunge wa Mbinga Magharibi, ninaomba nitoe maelezo mafupi kama yafuatayo:- Mheshimiwa Spikia, Bodi ya Zabuni ya Barabara hutoa kazi kufuatana na Sheria Na.3 ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001 (Public Procurement Act No.3 of 2001) ambayo inataka Mkandarasi anayepewa kazi awe na sifa zinazotakiwa kwa ajili ya kazi iliyotangazwa ikiwa ni pamoja na kusajiliwa katika daraja linalotakiwa katika Bodi ya Makandarasi. Aidha, kwa upande mwingine Bodi ya Makandarasi imeweka mikakati maalum kuhakikisha kwamba Makandarasi wote waliosajiliwa wanaendelea kuwa na

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

19

sifa zinazohitajika katika madaraja waliyosajiliwa wakati wote. Mikakati hii ni pamoja na kutoa mafunzo kwa makandarasi na kukusanya Annual Return Forms’ kila mwaka, zinazoiwezesha Bodi kuwa na kumbukumbu za vifaa, Wataalam na uwezo alionao mkandarasi katika mwaka huo. Pia Bodi kupitia Kitengo chake cha Udhibiti (enforcement) hufanya ukaguzi katika kila Mkoa ili kukagua kama makandarasi wana sifa zinazotakiwa katika madaraja waliyosajiliwa na kama waendesha shughuli zao kwa mujibu wa Sheria Na. 17 ya mwaka 1997 (Contractors Registration Act and its B-Laws). Baada ya ufafanuzi huo, sasa ninaomba kujibu swali la msingi la Mheshimiwa Dr. Thadeus Luoga, Mbunge wa Mbinga Magharibi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, endapo Bodi ya Usajili wa Makandarasi itagundua kwamba mkandarasi hana tena sifa zilizomfanya asajiliwe katika daraja lake au ikipokea malalamiko kutoka kwa mteja juu ya utendaji kazi mbaya wa mkandarasi ama ikigunduliwa kuwa mkandarasi ameikodisha ama ameiazimisha Kampuni yake kwa mtu mwingine ili aifanyie kazi ya ukandarasi Mkandarasi anayehusika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Contractors Registration Act ya mwaka 1997 na By-Laws zake za mwaka 1999. Katika kutimiza jukumu hilo, katika mwaka 2004/2005 jumla ya Makandarasi 351 wamefutiwa usajili wao kwa sababu mbalimbali zikiwemo utendaji mbovu wa kazi za miradi ya ujenzi hususan barabara na madaraja. Hii inafanya jumla ya makandarasi waliofutiwa usajili na Bodi toka mwaka 1999 kufikia 1,666. Aidha, kama nilivyoeleza hapo awali, Bodi za Zabuni zinateua Makandarasi na Washauri kulingana na Sheria Na. 3 ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001 (Public Procurement Act No.3 of 2001). MHE. DR. THADEUS M. LUOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri yanayoleta matumaini ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Ningeomba kupata ufafanuzi kwa yafuatayo:- Kwanza naipongeza Serikali kwa kuchukua hatua nzuri kwa wale wanaokosea kutekeleza wajibu wao kinyume na mkataba.Hao Makandarasi wababaishaji mara zote wanaajiri wafanyakazi kule wanakofanya kazi na wanapomaliza kazi zao hawawalipi wale wafanyakazi, wanawatafuta lakini hawapatikani na madeni mengi ya hao Makandarasi kutokana na wale waliowapa kazi bado wanadai. Je, Serikali itawasaidia vipi hao wafanyakazi? NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Makandarasi popote pale ambapo watafanya kazi ya Ukandarasi wanatakiwa wengi katika wafanyakazi waajiri wananchi wa hapo na mkataba kati ya mwananchi anayeajiriwa na mkandarasi ni mkataba wa kazi baina ya mtu anayeajiri na mwajiriwa hahusiani kabisa na mkataba wa Mkandarasi na Wizara ya Ujenzi. Kwa hiyo, ushauri wangu kwa wananchi wote ambao wametapeliwa na Wakandarasi wawapeleke Mahakamani. (Makofi) MHE NJELU E. M. KASAKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na maelezo mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ninataka kujua kuna Mkandarasi anayeitwa KONOIKE akijenga barabara, baadhi ya barabara zake baadaye zinaweka matuta matuta nadhani hujikusanya kusanya na kufanya matuta matuta na hizo unaweza kuziona hata pale Dar es Salaam. Je, hii inatokana na udhaifu wa usimamizi kwa upande

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

20

wa Wizara ama ni ubovu wa Mkandarasi mwenyewe na kwa ajili hiyo je, bado anazo sifa za kupewa Kandarasi? NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, mara nyingi sana wakandarasi wanapotengeneza barabara wanakuwepo na watu ambao wanasimamia kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi wanaitwa consultant. Utengenezaji wa barabara nao una mkataba kwamba atakabidhi barabara hiyo baada ya mwaka. Katika kipindi hicho cha mwaka bado anatakuwa na retention money katika Wizara ya Ujenzi hatalipwa hicho kiwango fulani na bado atatakiwa akarabati barabara hiyo pale ambapo itaharibika na consultant bado atafuatilia barabara hiyo na kumwambia hapa pabovu. Lakini baada ya mwaka matengenezo yanarudishwa Wizarani. Mheshimiwa Spika, pale inapotokea matuta matuta hasa mara nyingi ni kwamba barabara hiyo inaanza kutumiwa na magari mazito zaidi kuliko ilivyotengenezwa kwa uzito wake. Kwa hiyo, mara nyingi lami inaharibika na inakandamizwa zaidi kwa mizigo mikubwa sana na hizi barabara nyingi ziko hasa Mijini na hiyo ni kwa sababu hatuwezi ku-control malori yale makubwa kupita kwenye barabara duni. Lakini pale ambapo ndiyo kwenye highway ni ubovu wa ardhi yenyewe. Mheshimiwa Spika, kwa mfano Kitonga magari yalikuwa yanakwenda polepole sana na yanaharibu barabara kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba imebidi tutengeneze barabara pale kwa utaalam wa kutumia sementi na wenzetu wa Japan wanaujua zaidi hivyo wakaja na wametusaidia tumetengeneza. Hii ni kwa sababu magari yanapopanda milimani yanakandamiza lami sana na yanatokea matatu. Pale yanapotokea matuta ni udhaifu huo mkubwa sana. Vilevile katika nchi za tropical jua linaharibu sana lami. (Makofi)

Na. 341

Kampuni ya Simu Tanzania MHE. MUSSA A. LUPATU (k.n.y. MHE. HENRY D. SHEKIFFU) aliuliza:- Kwa kuwa Kampuni ya Simu - TTCL ni Kampuni Mama ya CELTEL; na kwamba, Serikali inamiliki asilimia 65 na wawekezaji wa nje (MSI) wanamiliki asilimia 35 :- (a) Je, Muundo wa Bodi ya Wakurugenzi wa CELTEL na wajumbe wake wanateuliwa na nani? (b) Je, mtaji wa CELTEL ulitolewa na nani na kwa asilimia ngapi? (c) Je, tangu mtandao wa CELTEL uanzishwe, hesabu zake zimeshakaguliwa na zinapaswa kuwasilishwa Bungeni kama ilivyo kwa Kampuni husika (TTCL)?

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

21

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Henry D. Shekiffu, Mbunge wa Lushoto, lenye sehemu (a), (b) na (c) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, hapo awali uteuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa CELTEL ulifanyika kwa mujibu wa Mkataba wa Uendeshaji wa TTCL, Bodi inaundwa na wajumbe kutoka upande wa CELTEL International na wale wa upande wa Serikali ya Tanzania. Muundo wa Bodi ya Wakurugenzi ya CELTEL na wajumbe wake wanateuliewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL) iliyoundwa na Wenye hisa. Mtaji wa CELTEL ni sehemu ya fedha za Kampuni ya TTCL (Consolidated Accounts) zilizolipwa kwa kiwango cha uwiano wa asilimia 65:35 za wenye hisa.

Aidha, baadaye Serikali ilianzisha mazungunzo ya CELTEL International Limited yenye lengo la kutenganisha shughuli za TTCL na zile za CELTEL Tanzania Limited kwa madhumuni ya kuweka sawa mazingira ya utoaji huduma za simu hasa za mkononi kwa misingi ya ushindani na biashara ya soko huria. Mazungumzo hayo hivi sasa yamekamilika na kuhusu uongozi na muundo itakuwa kama ifuatavyo: Kwa upande wa TTCL, Mkataba wa uendeshaji na Bodi utakuwa chini ya Serikali ambapo Bodi itakuwa na wajumbe watano, wajumbe wanne kati ya hao watateuliwa na Serikali akiwemo Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya TTCL. Mjumbe mmoja atateuliwa na CELTEL International Ltd. Kwa upande wa CELTEL Tanzania Limited, Mkataba wa uendeshaji wa Bodi ya CELTEL (T) Limited utakuwa chini ya CELTEL International Limited. Bodi itakuwa na wajumbe saba, kati ya hao wajumbe wawili watateuliwa na Serikali ambapo mjumbe mmoja kati ya hao atakuwa Msajili wa Hazina. Wajumbe watano akiwemo Mwenyekiti watateuliwa na CELTEL International Limited. Hakuna mjumbe atakayekuwa kwenye Bodi zote mbili. Mheshimiwa Spika, tangu mtandao wa CELTEL uanzishwe, hesabu zake za mwaka 2001, 2002, 2003, na 2004 zimekwishakaguliwa na Kampuni ya Ernest and Young na kupata hati safi. Aidha, kwa kuwa CELTEL ni Kampuni tanzu ya TTCL mahesabu yake yanakuwa ndani ya mahesabu ya Kampuni ya TTCL. Mahesabu ya jumla ya TTCL (TTCL’s Consolidated Accounts) ambayo yamejumuisha yale ya CELTEL.

Na. 342

Mradi wa Umwagiliaji – Wilayani Kondoa

MHE. KHALID S. SURU aliuliza:-

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

22

Kwa kuwa kuna mradi wa mpya wa Umwagiliaji Maji Mashambani unaojengwa kwenye Kata ya Kisese Wilayani Kondoa, ambao ulianza rasmi mwaka 2003/2004 kwa kazi mbalimbali za kujenga kitegeo cha maji (intake), ujenzi wa tanki na kupima maeneo ya shughuli za kilimo hicho:- (a) Je, ni Vijiji vingapi vinatarajiwa kufaidika na mradi huo, vitajwe kwa majina na idadi ya watu wao kwa kila Kijiji? (b) Je, kazi za mradi zimefikia kiwango gani cha asilimia kwa mujibu wa malengo ya kazi yenyewe na je, tupo kwenye muda uliokusudiwa, tumechelewa au tupo mbele ya ratiba? (c) Je, mradi huo unatarajiwa kukamilika lini ili wananchi walengwa waanze kufaidika? NAIBU WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO(k.n.y. WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Chakula, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khalid S. Suru, Mbunge wa Kondoa Kaskazini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Jumla ya vijiji vinne vinatarajiwa kufaidika na mradi wa umwagiliaji maji mashambani wa Kisese. Vijiji hivyo ni Mapinduzi, chenye watu 819, Kisese Disa, chenye watu 2,487, Kisese Sauna, chenye watu 2, 227 na Kisese Madisa, chenye watu 1,992.

(b) Ujenzi wa Mradi wa Umwagiliaji Maji mashambani wa Kisese ulianza

mwaka wa 2003/2004 na ulipangwa kukamilika katika mwaka wa 2005/2006. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 2.5 ambapo jumla ya shilingi milioni 24 zimetumika. Fedha hizo zilitolewa na Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Kilimo wa Wilaya ya Kondoa. Ili kukamilisha ujenzi wa sehemu iliyobaki jumla ya shilingi milioni 95 zimetengwa katika bajeti ya Wizara ya Kilimo na Chakula ya mwaka wa 2005/2006. Ujenzi wa mradi huo bado upo ndani ya muda uliokusudiwa kwa sababu ilipangwa ukamilishwe ndani ya miezi 36 na hadi sasa ni miezi 24 imepita tangu ujenzi uanze.

(c) Mradi unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi wa Julai, 2006 kama ilivyopangwa.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda wa maswali imekwisha. Kwa hiyo, tunaendelea na shughuli nyingine.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

23

Kwanza matangazo mawili ya vikao. Kamati ya Fedha na Uchumi Mwenyekiti wake anaomba wajumbe wa Kamati hiyo wakutane leo saa 6.00 mchana chumba Na. 231. Mheshimiwa Chief Whip wa Upinzani anawatangazia wajumbe wote wa Kambi hiyo kwamba saa 7.00 mchana kutakuwa na kikao cha mwisho kama Kambi ya Upinzani. Kwa hiyo, anawaomba wote wahudhurie. (Makofi) Basi baada ya hapo Waheshimiwa Wabunge sasa hivi wahudumu wanagawa kadi za mwaliko. Tumeona ni vizuri tuzigawe humu ndani kwa sababu tunataka kila mtu apate taarifa kwamba siku ya kesho kutwa tarehe 28 Julai, ndiyo ya mwisho kabisa ya vikao vya Bajeti. Kwa hiyo Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni ameandaa tafrija ya kuhitimisha kikao hiki pamoja na kuhitimisha maisha ya miaka mitano ya Bunge hili. Tungependa wote tuwepo, kwa sababu Alhamisi ndiyo kikao cha mwisho cha kazi kesho yake tunamsikiliza Mheshimiwa Rais tu na yeye akituaga. Kwa hiyo Mheshimiwa Rais atatuhutubia wakati wa asubuhi yaani hatutakuwa na maswali ni asubuhi ili baada ya hapo Waheshimiwa Wabunge waweze kupanga mipango yao ya safari. (Makofi) Mwisho wa matangazo Katibu tuendelee na Order paper.

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2005/2006 Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, baada ya taarifa iliyowasilishwa asubuhi hii hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi iliyochambua makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji kwa mwaka 2005/2006, naomba kutoa hoja kwamba, sasa Bunge lako Tukufu likubali kujadili na hatimaye kupitisha makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji pamoja na Asasi zake kwa mwaka wa fedha wa 2005/2006.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii awali ya yote kuishukuru kwa dhati kabisa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi chini ya kiongozi wake shupavu na mchapakazi Mheshimiwa Njelu Kasaka, Mbunge wa Lupa, kwa mchango mkubwa ilioutoa wakati ikijadili kwa kina na umakini na hatimaye kuyapitisha makadirio haya. Aidha, napenda kukupongeza wewe binafsi na Waheshimiwa Wabunge wote kwa uvumilivu na umakini wenu wakati wa kazi hii ngumu ya kupitia, kujadili na kupitisha makadirio ya bajeti za wizara mbalimbali tangu kuanza kwa Bunge hili la Bajeti tarehe 8 Juni, 2005.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu nyingi kwa Wakurugenzi, Viongozi wa Asasi na wafanyakazi wote wa Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Dr. Enos S. Bukuku na Naibu Katibu Mkuu wake,

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

24

Ndugu Omar Bendera, kwa ushirikiano wao uliowezesha kufanikisha maandalizi ya makadirio haya na kutekeleza kwa kiwango cha juu na kwa mafanikio, malengo tuliyojiwekea katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita wa 2004/2005. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji na kwa niaba yangu mwenyewe kutoa rambirambi zetu kwako wewe Mheshimiwa Spika, kwa Waheshimiwa Wabunge wote, kwa familia, jamaa na marafiki kwa misiba ya wabunge waliotutoka. Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi. (Amin)

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji katika mwaka wa

fedha 2004/2005 iliendelea kuishauri Serikali katika masuala yanayohusu usimamizi wa uchumi pamoja na maendeleo ya kijamii. Katika kipindi hicho, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji ilielekeza nguvu zake katika majukumu ya kipaumbele yafuatayo:-

• Kuboresha na kuendeleza mazingira ya sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta maendeleo na kuimarisha uchumi wa soko;

• Kutoa taarifa na takwimu zilizochambuliwa zinazohusu masuala ya

maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili zitumike katika kutoa maamuzi sahihi ya kisera;

• Kuwapatia watumishi vitendea kazi na mafunzo ili kuinua uwezo wao katika kuchambua na kuandaa sera pamoja na kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya kiuchumi na kijamii;

• Kuimarisha mtandao wa taarifa za kiuchumi na kijamii na kuongeza

upatikanaji na ubora wa taarifa kwenye Tovuti ya Taifa ; • Kuimarisha na kutunza miundombinu ya Ofisi pamoja na vitendea kazi; • Kutathmini na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya

kiuchumi na kijamii; • Kuratibu urekebishaji na ubinafsishaji wa mashirika ya umma na utendaji

wa mashirika yaliyobinafsishwa; • Kuratibu uwekezaji rasilimali na maendeleo ya sekta binafsi;

• Kujenga na kuendeleza uwezo kwa wadau mbalimbali wa maendeleo

katika taaluma za takwimu na mipango ya maendeleo; na • Kuendeleza ushirikiano wa kikanda na kimataifa. Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo kuhusu majukumu ya Ofisi ya Rais,

Mipango na Ubinafsishaji pamoja na asasi zake kwa mwaka 2004/2005 naomba sasa

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

25

kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa malengo ya Ofisi kwa mwaka wa fedha 2004/2005 kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji ikishirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliendelea kuboresha ukusanyaji, uchambuzi na utoaji wa takwimu mbalimbali katika muda uliohitajika. Ufanisi katika kazi hii uliiwezesha Serikali kupanga mipango madhubuti na kutoa maamuzi sahihi juu ya maendeleo ya nchi. Maeneo yaliyohusishwa ni pamoja na takwimu za Pato la Taifa; takwimu za kilimo; tafiti kuhusu janga la ukimwi na hali ya afya ya mama na mtoto; takwimu za ajira na mapato; takwimu za uzalishaji viwandani; takwimu za bei za rejereja kwa ajili ya fahirisi ya bei za bidhaa zitumiwazo na mlaji wa mwisho na mfumuko wa bei; na tafiti za hoteli na utalii. Takwimu zilizokusanywa na kuchambuliwa zilitumika katika uandaaji wa taarifa ya Hali ya Uchumi katika Mwaka 2004 na Sera za Jumla za Uchumi na Maendeleo ya Jamii katika Kipindi cha Mwaka 2005/2006 – 2007/2008.

Mheshimiwa Spika, zoezi la sensa hukusanya takwimu nyingi zaidi ambazo ni

muhimu katika kuandaa mipango ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi zikiwemo sekta rasmi na isiyo rasmi, hali ya ulemavu, hali ya makazi, hali ya ndoa na takwimu zinazopima hali ya umaskini. Katika utayarishaji wa sera mbalimbali hapa nchini takwimu zilizotajwa hapo juu hutumika katika ngazi zote zikijumuisha taifa, mkoa na wilaya. Kwa mfano, Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Kuondoa Umaskini katika Mkakati wa Kuondoa Umaskini (Poverty Reduction Strategy (PRS) na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA), takwimu za sensa zinatumika kujua hali ya umaskini ilivyo. Pia katika Millennium Development Goals (MDGs) takwimu za sensa hutumika kuoanisha hali halisi ya idadi ya watu na maendeleo yao.

Mheshimiwa Spika, katika kila wilaya, takwimu hizi za sensa zimetolewa kisekta, zikijumuisha takwimu za elimu ambazo hutumika katika sera na mipango ya sekta ya elimu, takwimu za afya, ambazo ni pamoja na vifo vya watoto, akina mama na uzazi hutumika katika sekta ya afya. Pia zipo takwimu za kiumri na kijinsia katika kila wilaya ambazo hutumika katika sekta zote zikihusisha umri wa kwenda shule, umri wa kuanza kazi na umri wa kuoa na kuolewa. Katika kuboresha matumizi sahihi ya takwimu zilizotajwa hapa juu, mafunzo yaliendeshwa kwa maafisa mipango wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, miji na manispaa, juu ya uoanishaji wa masuala ya idadi ya watu katika sera na mipango ya wilaya.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, kazi ya uchambuzi wa Takwimu za

Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 iliendelea. Baadhi ya taarifa zilizochapishwa katika mwaka 2004/2005 ni pamoja na: “Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia” (Age and Sex Distribution Report - Volume II) kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili na “Mchanganuo wa Hali ya Kijamii na Kiuchumi katika Wilaya zote 129 nchini” (District Profiles -Volume IV) kwa lugha ya Kiingereza. Taarifa ambazo zinaendelea kuchapishwa ni pamoja na mchanganuo wa takwimu katika ngazi ya kijiji zitakazojumuisha mgawanyo wa kijiji/mtaa, kiumri, kijinsia, watoto yatima (orphanhood), kaya ambazo

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

26

wakuu wa kaya ni watoto walio na umri chini ya miaka kumi na nane (child-headed households); mchanganuo wa hali ya kiuchumi na kijamii katika ngazi ya mkoa na taifa; na makadirio ya idadi ya watu katika ngazi ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2025 (Population Projections at National Level 2003 - 2025). Taarifa zilizo tayari zimesambazwa kwa wadau mbalimbali, wakiwemo Waheshimiwa Wabunge na kuwekwa kwenye Tovuti ya Taifa na pia kuwekwa kwenye Tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Mheshimiwa Spika, ili kuhamasisha utumiaji wa takwimu hizo, mafunzo ya namna ya kuzitumia yaliendelea kutolewa kwa watendaji katika ngazi za wilaya, mkoa na taifa. Mafunzo maalumu yaliyohusu utumiaji wa kompyuta yalitolewa Desemba 2004 kwa Maafisa Mipango wa Mikoa na Wilaya na Maafisa Takwimu wa Mikoa yote. Mafunzo haya yalipewa msukumo mpya kwa kuwapa na kuwafundisha Maafisa Mipango jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa ya kutayarisha majedwali watakayoyahitaji kutoka kwenye takwimu zao za mkoa. Vilevile, walipewa teknolojia mpya kwa ajili ya kufanya makisio ya idadi ya watu katika kata na vijiji (Super Cross and People Softwares).

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji iliendelea kuratibu Uwekezaji wa ndani na nje katika fursa mbalimbali kwa kutumia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Katika mwaka 2004, Kituo kilisajili jumla ya miradi 454 yenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 1.26. Kati ya miradi hiyo, 269 ilikuwa mipya na 185 ya kupanua na kufanyia ukarabati. Miradi 208 ilikuwa ya wawekezaji wa ndani, 119 wawekezaji wa nje na 127 ilikuwa ya ubia. Katika kuendeleza huduma hiyo kituo kilihudumia masuala ya ajira za wageni 1,809, vibali vya uhamiaji 1,790, masuala ya kodi 2,398, uanzishaji makampuni 183, leseni za biashara 269 na maombi ya ardhi 151. Ili kuvutia wawekezaji kutoka nje, Kituo kilifanya semina za uhamasishaji uwekezaji katika nchi za Uingereza, Afrika Kusini, Italia, China, India, Japan Vietnam, Uholanzi, Msumbiji, Korea Kusini na Nchi za Falme za Kiarabu (UAE). Baadhi ya semina hizi zilifanywa kwa kushirikiana na Taasisi ya Ulaya – Centre for Development Enterprises (CDE) na ProInvest. Madhumuni ya semina hizi ni kuendelea kuitangaza Tanzania na kunadi fursa za uwekezaji nchini pamoja na kukaribisha wawekezaji. Nachukua fursa hii kuwashukuru Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kushiriki na kuongoza baadhi ya semina hizi. Kituo pia kwa kushirikiana na UNIDO na TCCIA kiliendesha semina za kuhamasisha uwekezaji katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mtwara, Mwanza na Kilimanjaro. Lengo la semina hizo lilikuwa ni kuelimisha jamii ya Kitanzania kuhusu sera na Sheria ya Uwekezaji, madhumuni na faida zake ili waweze kuanzisha miradi yao wenyewe.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji kupitia TIC ilikamilisha zoezi la kuainisha ardhi inayofaa kuwekeza na kuweka kumbumkumbu kwenye kompyuta (Land Bank) kwa ajili ya wawekezaji. Jumla ya wawekezaji 13 wa kigeni walipata hatimiliki za ardhi (Derivative Titles) kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo, viwanda na mahoteli. Sheria ya Ardhi ya mwaka 2003 [Land (Amendment) Act, 2003] imepitishwa na kanuni za kuongoza utekelezaji wake zinatayarishwa.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

27

Mheshimiwa Spika, TIC iliendelea na matayarisho ya zoezi la kufungua ofisi za kanda ambapo uanzishwaji wa ofisi hizo hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji kifungu Na. 11(2). Uanzishwaji wa ofisi hizi unafanywa pia kulingana na utayari wa mikoa husika kwenye kanda kuzingatia Bajeti ya TIC. Katika mwaka 2004/2005, Ofisi ya Kituo cha Kanda ya kaskazini ilifunguliwa mjini Moshi ambayo inahudumia mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyokuwa katika kipindi kilichotangulia, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji kupitia PSRC iliendelea kuweka mkazo katika juhudi za urekebishaji na ubinafsishaji wa mashirika ya huduma na miundombinu na mashirika yaliyosalia ya kibiashara.

Mashirika makubwa yaliyoshughulikiwa na ambayo yapo katika hatua

mbalimbali za ubinafsishaji ni pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC), Marine Services Company, vitengo vingine vya kibiashara vya Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) mbali na kitengo cha makontena, Kampuni ya Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Bima la Taifa (NIC), National Microfinance Bank (NMB) na viwanda vya kubangua korosho.

Mashirika kama vile TRC yatakodishwa na siyo kuuzwa. Kwa upande wa TANESCO changamoto kubwa ni kuongeza ufanisi wa shirika na kulirekebisha kwa madhumuni ya kutenganisha katika muundo wa shirika, shughuli za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme (ring-fencing generation, transmission and distribution for efficiency considerations). Kwa kuzingatia ngazi ya maendeleo ya nchi yetu, pamoja na ukweli kwamba ni karibu asilimia 10 tu ya wananchi wanaopata huduma ya umeme, kwa muda mrefu ujao, ujenzi wa miundombinu muhimu ya umeme utatekelezwa na Serikali. Hata hivyo, Serikali inakaribisha sekta binafsi katika kuendeleza na kuongeza kiwango cha uzalishaji umeme kwa kuzingatia hoja za ubora, ufanisi na unafuu.

Mheshimiwa Spika, taratibu za kuandaa mipango ya utekelezaji zitakazotumika kuendesha mamlaka za udhibiti ambazo ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA); Tume ya Ushindani wa Haki (Fair Competition Commission (FCC); na Mahakama ya Ushindani wa Haki (Fair Competition Tribunal (FCT) ziliandaliwa na kukamilika.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji iliendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kutumia njia mbalimbali, zikiwemo kukarabati jengo lake kwa awamu, kununua vitendea kazi kama kompyuta, mashine za kurudufia na samani.

Aidha, wafanyakazi walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje

ya nchi. Ofisi pia iliajiri wachumi na watakwimu wapya ili kukabili upungufu wa wafanyakazi katika idara na taasisi zake. Vilevile, ukarabati wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu uliendelea kwa awamu.

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

28

Mheshimiwa Spika, Tovuti ya Taifa na zile za asasi ziliendelea kuboreshwa kwa

kuongeza upatikanaji wa taarifa nyingi zaidi na kwa wakati. Tovuti zimesaidia kwa kiasi kikubwa kusambaza taarifa na takwimu muhimu kwa wadau mbalimbali kwa haraka na usahihi, kama vile hotuba za viongozi wa kitaifa, nyaraka za sera mbalimbali za taifa na za kisekta, taarifa za kitafiti, taarifa za kibajeti, miongozo ya mipango na Bajeti, hali ya uchumi wa nchi, matokeo ya mitihani pamoja na matokeo ya chaguzi.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji imeshiriki katika kuendeleza ushirikiano wa kikanda na kimataifa kwa manufaa ya Taifa, ikiwa ni pamoja na:-

• Kukamilisha maandalizi ya matumizi ya itifaki ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki ambao ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 1 Januari, 2005. Aidha, sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipitishwa na kuridhiwa na Bunge mwezi Oktoba, 2004;

• Kutayarisha programu za kutekelezwa chini ya Mpango wa Ushirikiano

Mpya ili Kuleta Maendeleo Barani Afrika (NEPAD) ikijumuisha ujenzi wa barabara za kanda tano za Afrika Mashariki na Daraja la Umoja kati ya Msumbiji na Tanzania chini ya Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor). Aidha,Tanzania ilijiunga na utaratibu chini ya NEPAD unaotoa fursa kwa nchi kujitathmini zenyewe na kutathminiwa na jopo la watu mashuhuri (African Peer Review Mechanism (APRM) ili kuimarisha utawala bora wa kiuchumi, kiutendaji na kisiasa barani Afrika;

• Ofisi ilishiriki kikamilifu katika vikao mbalimbali vya Kimataifa kuhusu

ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na vikao vya nchi za Afrika Mashariki (EAC), SADC, Ushirikiano wa Nchi za Maziwa Makuu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Kimataifa la Biashara (WTO).

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutekeleza Programu ya Uimarishaji na

Uboreshaji wa Mazingira Bora ya Biashara Tanzania (BEST Programme) ambayo inalenga katika kuondoa vikwazo vya kibiashara hapa nchini, hasa kwa kufanya marekebisho ya sheria na kanuni zinazoongoza biashara kwa lengo la kuvutia na kuendeleza uwekezaji katika fursa mbalimbali zilizobainishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Programu ya BEST imeanza kushughulikia uboreshaji wa usuluhishi wa migogoro ya kibiashara na ubadilishaji wa mtizamo wa utamaduni wa sekta ya umma kuhusu sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, kazi zinazotekelezwa na programu ya BEST ni pamoja na:

kuleta msukumo wa pekee na thabiti wa kuendeleza sekta binafsi katika kuchangia na kukuza uchumi na Mkakati wa Kupunguza Umaskini kwa kuweka mazingira bora ya kibiashara nchini hususan, uboreshaji wa sheria, kanuni na kuimarisha vyombo na taasisi

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

29

mbalimbali zikiwemo TIC na BRELA. Katika programu hii maboresho ya sheria na kanuni yanaendelea katika sheria za leseni za biashara, sheria za kazi, sheria na kanuni za utekelezaji wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, sheria za bodi za mazao, maboresho katika taratibu na mbinu mbadala za usuluhishaji wa migogoro ya kibiashara, na usuluhishaji wa migogoro ya kibiashara, uaandaji wa mikakati ya kuboresha utamaduni na mtazamo wa sekta binafsi kuhusu sekta ya umma, ili kukuza ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza uchumi.

Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji inaendelea na uaandaji wa Mkakati wa

Maendeleo ya Sekta Binafsi. Wataalamu waelekezi(consultants) tayari wamewasilisha taarifa ya awali ambayo inafanyiwa kazi. Kukamilika kwa mkakati huu kutaongeza kasi ya maendeleo ya sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, Baraza la Taifa la Biashara liliendelea kuwakutanisha viongozi wa juu wa Serikali na wafanyabishara toka ndani na nje ya nchi, chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa. Mikutano miwili ya Baraza (TNBC) na miwili ya wawekezaji toka nje (International Investors’ Round Table (IIRT), ilifanyika katika mwaka 2004/2005. Madhumuni ya mikutano hiyo ni kuishauri Serikali kuhusu mazingira bora ya uwekezaji nchini. Serikali imekuwa ikipokea ushauri unaotokana na mikutano hiyo na hivyo kuondoa baadhi ya kero zinazoathiri biashara, uwekezaji, uwekaji amana na huduma.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji imeendelea kuboresha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – Dodoma pamoja na Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika, ili viweze kutoa wataalam wa mipango na takwimu. Vyuo hivyo vimeendelea kupanuliwa kwa kuongeza na kukarabati miundombinu yake, kuajiri wakufunzi zaidi na kuvipatia vitendea kazi ili kukidhi mahitaji ya wakati uliopo na ujao.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, Chuo cha Mipango ya Maendeleo

Vijijini - Dodoma kimetoa mafunzo ya Cheti katika Mipango ya Maendeleo Vijijini, Stashahada ya Juu katika Mipango ya Mazingira, Stashahada ya Uzamili katika Mipango ya Mikoa na Stashahada ya Uzamili katika Mipango ya Mazingira. Jumla ya wanafunzi 64 walihudhuria mafunzo ya Cheti, 301 mafunzo ya Stashahada ya Juu na 53 mafunzo ya Stashahada ya Uzamili. Aidha, mafunzo ya muda mfupi yalitolewa kwa walengwa mbalimbali, wakiwemo maafisa watendaji wa kata 514 na wa vijiji 8,124.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, Chuo pia kiliendelea kuandaa mitaala inayolenga kutoa umahiri katika mafunzo ya Shahada ya Kwanza katika fani za Mipango ya Maendeleo ya Mikoa; Mipango na Usimamizi wa Mazingira na Mipango ya Idadi ya Watu na Maendeleo kwa wahitimu wake kuweza kukidhi mahitaji ya soko katika fani ya mipango. Ili kukidhi ongezeko la wanafunzi, Chuo kiliendelea na awamu nyingine ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.

Mheshimiwa Spika, mafunzo ya kawaida ya cheti na stashahada yaliendelea kutolewa na Chuo cha Takwimu ili kuboresha taaluma ya ukusanyaji na utunzaji wa

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

30

takwimu. Katika mwaka 2004/2005, Chuo kilikuwa na jumla ya wanafunzi 72 ikijumuisha wanafunzi kutoka Botswana (2), Afrika ya Kusini (4), Uganda (4), Tanzania Bara (48) na Tanzania - Zanzibar (14).

Kati ya wanafunzi hao 40 walikuwa wa cheti na 32 wa stashahada. Wanafunzi 24

wa Tanzania Bara ni waajiriwa wa Serikali za mitaa (TAMISEMI) waliofadhiliwa na Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji katika Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Kukusanya na Kuchambua Takwimu za Kiutawala chini ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini nchini.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika kiliendesha mafunzo ya muda mfupi ya namna ya kutunza takwimu kwa kutumia kompyuta (Database Management) kwa waajiriwa 260 wa TAMISEMI. Mafunzo ya muda mfupi ya kimataifa yaliendeshwa mara mbili na kunufaisha washiriki 45 kutoka nchi 21.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Tanzania imeanza kutekeleza mapendekezo ya

Tume ya Kimataifa kuhusu Masuala ya Kijamii katika Utandawazi (The World Commission on the Social Dimension of Globalization) kwa kuunda Kamati ya Kitaifa ya Utandawazi inayounganisha sekta mbalimbali za Serikali, asasi na taasisi za elimu ya juu na zile za utafiti chini ya uenyekiti wa Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji. Kamati hii imeweza kuchambua mapendekezo ya Tume na kuandaa mpango wa utekelezaji wa muda wa kati na muda mrefu. Mpango huu unaendelea kujadiliwa na Serikali pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Aidha, Kamati imetafsiri muhtasari wa Taarifa ya Tume kwa lugha ya Kiswahili ili iweze kueleweka vizuri kwa walio wengi.

Mheshimiwa Spika, katika kuandaa bajeti ya mwaka 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji imezingatia azma ya Serikali ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na Mpango wa Muda wa Kati. Aidha, matayarisho ya Bajeti yamezingatia maelekezo yaliyomo kwenye Mwongozo wa Mpango na Bajeti wa mwaka 2005/06 – 2007/08.

Mheshimiwa Spika, Idara na Asasi za Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji zinashirikiana katika kutekeleza majukumu yake, kama yalivyobainishwa katika Mpango Mkakati. Katika mwaka wa fedha 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji pamoja na Asasi zake itaendelea na majukumu yake kwa kushirikiana na wizara, asasi na taasisi zingine kukamilisha kazi nzuri ya Serikali ya Awamu ya Tatu na kuanza kazi katika Awamu ya Nne ya uongozi wa nchi yetu. Kazi zilizopangwa kufanyika katika kipindi hiki ni pamoja na zifuatazo:

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2005/2006 Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuongeza vitendea kazi na samani. Ofisi pia itaendelea kuboresha utendaji kazi wa maafisa wake kwa kuwapeleka kuhudhuria mafunzo ndani na nje ya nchi.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

31

Mheshimiwa Spika, Ofisi itaendelea na awamu ya tatu ya ukarabati wa jengo ili kupunguza uhaba wa ofisi. Ofisi pia itanunua vifaa vya ulinzi kwa ajili ya kuimarisha usalama na kumalizia uwekaji wa vifaa vya kuzimia moto. Aidha, ukarabati wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa awamu utaendelea ambapo utahusu ukarabati wa jengo kubwa sehemu ya ghorofa ya kwanza pamoja na ununuzi wa samani mpya ambazo zitawekwa kwenye ofisi zilizofanyiwa ukarabati.

Mheshimiwa Spika, kama inavyoeleweka, UKIMWI ni janga la kitaifa, janga ambalo ni tishio linaloteketeza nguvukazi ya Taifa. Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itaungana na wizara na taasisi nyingine katika kupunguza au kutokomeza kabisa maambukizi mapya ya UKIMWI katika sehemu za kazi. Kwa hivi sasa utafiti wa kutathmini hali ya UKIMWI katika Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji na Asasi zake umeshaanza. Lengo la utafiti huu ni kujua hali halisi ya UKIMWI katika Ofisi ili kubuni mpango mkakati utakaosaidia kupunguza maambukizo mapya na kuwasaidia wale wote watakaokubali kupima afya zao kwa hiari na kugundulika kuwa na virusi vya UKIMWI.

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyosisitizwa mara nyingi, Mpango wa Maendeleo wa Muda wa Kati na MKUKUTA vinalenga katika kutoa kipaumbele kwenye suala zima la kukuza uchumi kama nyenzo muhimu ya kupunguza umaskini na kuleta maendeleo ya kijamii, hivyo kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji kama msimamizi na mshauri wa masuala ya kiuchumi, inalo jukumu kubwa la kusimamia utekelezaji wa mpango na mkakati huu. Katika mwaka 2005/2006 Ofisi itaratibu utayarishaji na usambazaji wa muundo wa kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Muda wa Kati sambamba na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA).

Kazi ya kutengeneza zana za uchambuzi wa uchumi jumla kwa madhumuni ya kuimarisha na kujenga uwezo wa kubainisha mwelekeo wa mwenendo wa uchumi itaendelea, lengo likiwa ni kuboresha utayarishaji wa sera za uchumi jumla na mfumo wa matumizi ya rasilimali za Serikali. Aidha, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itatumia wataalam na asasi zake kufanya utafiti katika baadhi ya sekta za uzalishaji na miundombinu ili kubaini fursa zilizopo za kukuza uzalishaji mali na huduma na kuandaa mkakati wa kuendeleza utumiaji wa fursa hizo. Utafiti huo utafanyika kwa awamu kwa kuhusisha sekta kadhaa kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kufanya tafiti na ukusanyaji wa takwimu mbali mbali za kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha mwaka 2005/2006, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itakamilisha ukusanyaji, uandaaji na usambazaji wa takwimu na taarifa zitokanazo na Utafiti wa Shughuli za Kiuchumi (Business Survey) na Utafiti wa Afya ya Mama na Mtoto (Demographic and Health Survey). Aidha, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, itaendelea na maandalizi ya tafiti za Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi (Integrated Labour Force Survey) na Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (Household Budget Survey). Katika kipindi cha mwaka 2005/2006, Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi utakuwa katika hatua za ukamilishaji wa

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

32

dodoso kwa kushirikisha wadau mbali mbali, utayarishaji wa sampuli, ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za miezi sita ya awali kati ya miezi 12 zinazohusu hali ya ajira, shughuli za watoto, sekta isiyo rasmi na matumizi ya muda (time use) kwa wanakaya wa jinsia na rika zote. Kwa upande wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, utafiti utakuwa katika hatua ya ukamilishaji wa dodoso kwa kushirikiana na wadau pamoja na kulifanyia majaribio.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2005/2006, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea na kazi ya kuchambua takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002. Kazi zitakazofanywa kwa kushirikiana na mikoa, Serikali za mitaa na vijiji katika kipindi hicho ni pamoja na kuchanganua, kuchapisha na kusambaza takwimu za sensa katika ngazi za wilaya 129 awamu ya kwanza (The Village Statistics Report Phase 1); mikoa 26 (26 Regional Profiles); na ngazi ya taifa (Analytical Report). Aidha, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itachapisha na kusambaza Makadirio ya Idadi ya Watu kwa kipindi cha 2003-2025 katika ngazi ya taifa. Ofisi hiyo pia itaendelea na programu za kuendeleza taaluma ya uoanishaji wa masuala ya idadi ya watu katika sera na mipango ya kisekta na wilaya.

Mheshimiwa Spika, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA)

imekuwa chombo muhimu katika harakati za kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na utoaji huduma mbalimbali. Teknolojia hii ni nyenzo na kichocheo katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Malengo ya Milenia. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, itaandaa Mkakati wa Ofisi wa kutekeleza sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, Ofisi pia inatarajia kuboresha Tovuti ya Taifa kwa kuifanya

iwe “database-driven”. Lengo ni kurahisisha na kuifanya iwe rahisi kusomwa na watumiaji wengi zaidi. Tovuti za jinsi hiyo (database-driven websites) huweza kuhifadhi taarifa nyingi zaidi na zinazoweza kufikiwa na mtumiaji kwa urahisi. Aidha, maktaba ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itaboreshwa kwa kununua machapisho na vitabu vipya vya taaluma mbalimbali na vinavyokidhi matarajio ya watumiaji wake. Maktaba ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji hutumiwa na wizara, asasi na taasisi mbalimbali kama maktaba rejea. Ofisi pia itaendelea kuweka mfumo wa kutoa huduma za maktaba kwa njia ya mtandao wa kompyuta wa ndani (Local Area Network).

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na

Ubinafsishaji, kupitia kitengo chake cha “Better Regulation Unit” itaendelea na kazi zake za uratibu wa mradi wa Uimarishaji na Uboreshaji wa Mazingira Bora ya Biashara (BEST). Kazi zitakazofanyika katika kipindi hicho ni pamoja na kuendelea kutoa msukumo wa pekee na thabiti wa kuendeleza sekta binafsi kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini, hususan uboreshaji wa sera, sheria, taratibu, utawala bora na kuimarisha vyombo na taasisi zikiwamo TIC na BRELA, marekebisho ya sheria za leseni za biashara, sheria za kazi, masuala ya sheria za ardhi na Mahakama ya Biashara.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

33

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha 2005/2006, Serikali itaendelea kuhimiza wawekezaji wa ndani kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati vya kusindika mazao ili kuongeza thamani ya mauzo ya nje na kuchangia katika kupanua nafasi za ajira. Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuendeleza sekta binafsi kwa kuendelea na utekelezaji wa programu ya Uimarishaji na Uboreshaji wa Mazingira Bora ya Biashara pamoja na kuitangaza Tanzania ili kuvutia wawekezaji pamoja na kuainisha maeneo yenye kero kwa wawekezaji na kutoa ufumbuzi wa kudumu. Aidha, Kituo cha Uwekezaji Tanzania kitafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi kujenga rajamu ya Tanzania (Branding Tanzania) kuifanya Tanzania ijulikane duniani kote kama eneo bora la uwekezaji katika Bara la Afrika. Pamoja na juhudi hizo kituo kitaendelea kutangaza fursa za uwekezaji nje, ikiwa ni pamoja na Arabuni, Asia, Marekani, Afrika na Ulaya.

Mheshimiwa Spika, vilevile Serikali itaendelea kuratibu na kutangaza miradi ya

Watanzania ambayo ipo katika ngazi mbalimbali za kutafuta wabia, mitaji na teknolojia. Aidha, Kituo kimeandaa mkakati wa kuwahamasisha na kuwasaidia wawekezaji wadogo na wa kati ili waweze kubuni na kuandaa miradi inayouzika (Bankable and Feasible Projects). Hii ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali, kuwakutanisha na wawekezaji toka nje kwa nia ya kuingia ubia, kuwaunganisha na benki (Microfinance Bank) kwa lengo la kupata mikopo ya riba nafuu. Katika jitihada za kusogeza huduma za Kituo karibu na wanachi wengi na kuboresha ufanisi, Kituo cha Uwekezaji Tanzania kinategemea kufungua ofisi nyingine ya kanda jijini Mwanza katika mwaka wa fedha 2005/2006, ambayo itahudumia mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora na Kigoma. Pia kituo kitaendelea na semina za uhamasishaji uwekezaji mikoani kwa kushirikiana na mikoa itakayokuwa tayari kuandaa semina hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kukiwezesha Kituo kutekeleza majukumu yake kwa

ufanisi, Serikali itaendelea kujenga uwezo wa Kituo, ili kiweze kuwahudumia wawekezaji kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika kuendeleza uchumi, hivyo itaendeleza mijadala na sekta binafsi katika mikutano kupitia Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na wawekezaji toka ndani na nje ya nchi. Baraza litaanzisha mijadala ya maendeleo (Smart Partnership Dialogues) kwa kuanza na baadhi ya mikoa, ikishirikisha Serikali za mitaa, sekta binafsi, mashirika yasiyokuwa ya Serikali (NGOs), wanawake, vijana, waandishi wa habari, na kadhyalika. Maeneo yatakayojadiliwa ni utawala bora, vita dhidi ya rushwa, ununuzi wa bidhaa na huduma (procurement) na uwezeshaji (empowerment).

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji ikishirikiana na PSRC itaendelea kushughulikia kwa makini urekebishaji na ubinafsishaji wa mashirika ya huduma, miundombinu na mashirika yaliyosalia ya kibiashara. Mashirika yaliyo katika hatua mbali mbali za ubinafsishaji ni pamoja na Shirika la Reli Tanzania (TRC), vitengo vilivyosalia vya kibiashara vya Mamlaka ya Bandari (THA) ukiondoa kitengo cha makontena, Shirika la Bima la Taifa (NIC), Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Shirika la Posta

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

34

Tanzania (TPC) na Marine Services Company inayotoa huduma ya usafiri katika maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa.

Kama nilivyosema hapo awali, kampuni ya TANESCO itarekebishwa kwa madhumuni ya kutenganisha katika muundo wa shirika, shughuli za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme (ring-fencing generation, transmission and distribution for efficiency considerations). Ofisi pia itaendelea kushughulikia majukumu ya uundwaji wa mamlaka za udhibiti kwa mashirika ya huduma na miundombinu.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itaendelea kusimamia na kuboresha taaluma za takwimu na mipango ya maendelo kwa kuimarisha Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – Dodoma. Kama inavyojulikana, wahitimu wa vyuo hivyo wanaajiriwa nchi nzima kuwiana na mahitaji ya maeneo husika.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/206, Chuo cha Takwimu cha

Mashariki mwa Afrika kitaendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, kufanya tafiti na kutoa ushauri kwa Wizara na Idara mbalimbali za Serikali na wadau wengine. Aidha, Chuo kitaendelea kuboreshwa kwa kuajiri walimu zaidi wenye ujuzi na watumishi wenye taaluma zinazohitajika kukiendesha, na kuimarisha mazingira ya Chuo na kuhamasisha mafunzo kwa walio kazini. Chuo pia kitakamilisha uchimbaji wa kisima cha maji ili kutatua tatizo sugu la ukosefu wa maji. Chuo kitashirikiana na Kikosi cha Ulinzi wa Anga, Manispaa ya Kinondoni na Wizara ya Ujenzi kutafuta ufumbuzi wa tatizo la barabara.

Mheshimiwa Spika, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya wataalamu wa mipango ya maendeleo vijijini, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – Dodoma kitapanua na kuboresha huduma zake, ikiwa ni pamoja na kujenga jengo la maktaba lenye uwezo wa kuhudumia watumiaji 600 kwa wakati mmoja na jengo la taaluma litakalokuwa na vyumba vya madarasa, mihadhara, semina na studio.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itaendeleza ushirikano wa kikanda na kimataifa kwa manufaa ya Taifa. Baadhi ya mambo yatakayozingatiwa ni pamoja na: • Kutathmini na kubaini fursa za kuendeleza biashara ya nje pamoja na kufuatilia

maazimio ya taasisi na programu za kimataifa kama WTO, AGOA, EU/ACP, Canadian Initiative, Japanese Initiative, n.k.;

• Kuchambua na kubainisha fursa za kuchochea maendeleo ya kiuchumi kutokana na ushirikiano wa kimataifa na kikanda;

• Kutathmini mwenendo wa uchumi duniani na kubaini ulinganifu wake na maendeleo ya uchumi wa taifa;

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

35

• Kuratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mpango wa Ushirikiano Mpya ili kuleta Maendeleo Barani Afrika (NEPAD); na

• Kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea kwa shabaha ya kuongeza kasi ya kuleta maendeleo katika nchi hizo kwa kutumia uzoefu uliopo kati ya nchi na nchi (TCDC).

Mheshimiwa Spika, katika azma ya kuleta msukumo mpya wa kuongeza kasi ya

ukuaji wa Pato la Taifa, kupunguza umaskini nchini, na kuongeza ajira na mauzo nje, Serikali imekamilisha mkakati mpya wa kuharakisha maendeleo ya Tanzania kwa kuzingatia uzoefu wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia.

Mheshimiwa Spika, Mkakati huu unalenga kujenga mazingira mazuri ya kuvutia kwa wingi uwekezaji kutoka nje na ndani ya Tanzania kwa kuanzisha maeneo maalum ya uwekezaji (Special Economic Zones). Katika maeneo hayo maalum, Serikali itajenga miuondombinu ya msingi ili kuwapunguzia wawekezaji gharama za kuanzisha miradi na itaweka mfumo wa uendeshaji wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji kwa ufanisi na kutatua haraka matatizo ya utekelezaji. Aidha, Serikali itaboresha mazingira ya kisheria na kutangaza kwa nguvu zaidi fursa za maeneo maalum ya uwekezaji na fursa nyingine.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2005/2006, Serikali

itasambaza ripoti ya utandawazi kwa wadau wengi, zikiwemo taasisi za elimu ya juu na utafiti, na asasi nyingine ili waweze kupata uelewa wa changamoto zilizo mbele yetu. Ili kubaini kiasi cha rasilimali kinachohitajika katika mpango ulioandaliwa wa utekelezaji, uchambuzi zaidi utafanywa ili kujua maeneo yanayohitaji rasilimali za ziada nje ya mfumo wa matumizi ya Serikali (MTEF).

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi za Utafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) na ile ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (ERB) itafanya tafiti mbalimbali zitakazotuwezesha kubaini vikwazo na fursa tulizo nazo katika ulingo wa utandawazi. Serikali pia kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), itafanya kongamano la utandawazi katika ngazi ya taifa na mijadala na wadau, zikiwemo asasi za kimataifa na pia kuanzisha mfumo wa uratibu na usimamizi wa masuala ya utandawazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo ya utekelezaji wa malengo ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji katika kipindi cha mwaka 2004/2005 pamoja na kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2005/2006, napenda kuchukua nafasi hii kwa dhati kabisa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Rais Benjamini William Mkapa, kwa mafanikio makubwa iliyopata katika kutengemaza uchumi. Pamoja na kwamba kwa watu wengine itaonekana ni kero kuyasikia mara kwa mara, bado hatuna budi kuyasema wazi wazi pale tunapopata nafasi, ili kukumbushana tulikotoka, tulipo na kule tunakotaka kwenda, lengo likiwa ni kuepuka kurudi kule tulikotoka. Sambamba na Serikali ya Awamu ya Tatu, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mimi binafsi na wafanyakazi wote wa Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji na asasi zilizo chini yake, kwa kutuwezesha kufanya kazi nzuri ya kusimamia uchumi.

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

36

Baadhi ya mafanikio ya wazi kabisa ya kujivunia ya Serikali ya Awamu ya Tatu ni pamoja na: • Kuimarika kwa ukuaji wa uchumi kulikotokana na hatua za kisera na kimkakati

zilizochukuliwa na Serikali katika jitihada zake za kuboresha uchumi na ustawi wa jamii;

• Kuongezeka kwa ukuaji wa Pato la Taifa toka asilimia 3.6 mwaka 1995 hadi 6.7 mwaka 2004;

• Kupungua kwa kasi ya upandaji bei kutokana na sera thabiti za kudhibiti

ongezeko la ujazi wa fedha na karadha; kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya Serikali; mkakati na mfumo wa kudhibiti matumizi ya Serikali; juhudi za wananchi katika kuongeza uzalishaji kwenye baadhi ya mazao ya chakula; na upatikanaji na usambazaji mzuri wa bidhaa muhimu za matumizi ya kawaida;

• Kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya ndani toka wastani wa shilingi bilioni

25 kwa mwezi mwaka 1995/1996 hadi wastani wa shilingi bilioni 145 kwa mwezi kwa mwaka 2004/2005;

• Kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje kwa kuweka mazingira mazuri na bora ya kibiashara;

• Utulivu wa kisiasa, utawala bora na utengemavu wa uchumi vilivyoijengea

heshima Tanzania na kuifanya ikopesheke na hatimaye kufutiwa madeni; • Kuwa na akiba ya fedha za kigeni zinazoweza kukidhi mahitaji ya manunuzi toka

nje ya miezi miwili mwaka 1995 hadi miezi minane mwaka 2004;

• Kuimarika kwa ushirikiano wa nchi yetu na nchi nyingine duniani katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa;

• Kuboreka kwa huduma muhimu kwa wananchi;

• Kuiondolea Serikali mzigo wa kutoa ruzuku kwa mashirika ya kibiashara;

• Kuingiza nchini Teknolojia ya kisasa kutokana na ongezeko la kasi ya uwekezaji wa ndani na nje; na

• Kuongeza ajira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja.

Mheshimiwa Spika, Mafanikio yote haya yamewezekana chini ya uongozi thabiti wa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Benjamin William Mkapa. Kwa hakika, katika kipindi chake cha utawala wa miaka kumi, Rais Mkapa amepandisha chati ya Tanzania na ameiletea nchi yetu sifa kemkem.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

37

Katika kipindi cha hivi karibuni, ameiletea heshima na sifa nchi yetu kwa ushiriki wake katika “Tume ya Utandawazi”, “Tume ya Afrika”, Mkutano wa AU, Sirte, Libya, na Mkutano wa G8 huko Gleneagles, Scotland. Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa. Juhudi zake za toka awali za kuitayarisha na kufanikiwa kuiingiza Tanzania katika msamaha wa madeni wa HIPC, na baadaye tena katika msamaha wa madeni wa G8/Gleneagles ni mambo yanayostahili kupongezwa kwa dhati na sisi sote.

Mhesshimiwa Spika, mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Awamu ya Tatu yanatakiwa kuenziwa na kulindwa ili tuweze kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kufanya kazi kwa bidii na kutumia kwa makini na kwa uadilifu fursa na rasilimali tulizonazo ili kulinda mafanikio hayo. Ni matumaini yangu kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi za kujiletea maendeleo. Yote yanawezekana kama kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake.

Mheshimwa Spika, ili kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana, na ili kuepusha uwezekano wa kufumua au kubomoa mafanikio na misingi iliyojengeka wakati wa Awamu ya Tatu, ya kuimarisha, kukuza na kutengemaza uchumi, inashauriwa Serikali ya Awamu ya Nne ijikite kuyapa kipaumbele yafuatayo:-

(i) Kuendeleza utengamavu wa uchumi na kulinda sera, mifumo na taasisi muhimu katika uendeshaji uchumi (ring fencing sound macro-policy stances and key and strategic institutions in the management of the economy);

(ii) Kuendeleza rasilimaliwatu;

(iii) Kuendeleza mikakati ya kukuza sekta binafsi, uwekezaji na mauzo

nje;

(iv) Kujenga na kuendeleza miundombinu;

(v) Kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na uwekezaji;

(vi) Kuendeleza na kuboresha huduma za jamii;

(vii) Kuendeleza sayasi na teknolojia;

(viii) Kujenga uwezo wa ushindani kikanda na kimataifa na kuweka

mifumo thabiti ya udhibiti;

(ix) Kulinda, kuendeleza na kudumisha amani na utulivu; na (x) Kuendeleza na kudumisha utawala bora.

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

38

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, katika kipindi cha mwaka 2005/2006 mkazo utaelekezwa zaidi katika kutekeleza malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini, lengo likiwa ni kukamilisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2000 kwa mafanikio na kuanza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2005.

Kama ilivyo ada, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji itaendelea kutekeleza

jukumu lake la msingi la kuishauri Serikali pamoja na Taasisi zingine za kiuchumi katika masuala yahusuyo usimamizi wa Uchumi na Maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa ujumla. Malengo ya muda wa kati ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji ni kuhimiza usawa na ukuaji endelevu wa uchumi na kuboresha ustawi wa jamii wa watanzania.

Katika kutimiza wajibu wake Ofisi itaongozwa na Mpango Mkakati ambao

umebainisha wazi Dira, Dhamira, Maadili, Malengo pamoja na Mikakati. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naomba sasa Bunge lako likubali na

kuidhinisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi 33,592,629,700 (bilioni thelathini na tatu, milioni mia tano tisini na mbili, mia sita ishirini na tisa elfu na mia) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji pamoja na Asasi zilizo chini yake kwa mwaka 2005/06 kwa mchanganuo ufuatao: • Bajeti ya Maendeleo ni shilingi 21,012,311,200 (bilioni ishirini na moja, milioni

kumi na mbili, mia tatu kumi na moja elfu na mia mbili) ambazo kati ya hizo shilingi 5,600,000,000 (bilioni tano na milioni mia sita) ni fedha za ndani na shilingi 15,412,311,200 (bilioni kumi na tano, milioni mia nne kumi na mbili, mia tatu kumi na moja elfu na mia mbili) ni fedha za nje.

• Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ni shilingi 12,580,318,500 (bilioni kumi na mbili,

milioni mia tano themanini, mia tatu kumi na nane elfu na mia tano). Kati ya fedha hizo, shilingi 2,650,172,000 (bilioni mbili, milioni mia sita hamsini na mia moja sabini na mbili elfu) ni kwa ajili ya mishahara na shilingi 9,930,146,500 (bilioni tisa, milioni mia tisa thelathini, mia moja arobaini na sita elfu na mia tano) ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi) WAZIRI WA ARDHI, MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika,

naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MHE. IDDI M. SIMBA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI): Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (1) ya Kanuni za

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

39

Bunge, Toleo la 2004, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, maoni ya Kamati ya Fedha na Uchumi, kwa mwaka wa fedha 2004/2005, pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2005/2006. Kabla sijafanya hivyo, napenda kutumia fursa hii, kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Wajumbe wote wa Kamati yetu, kutoa pole na salamu za rambirambi kwa Chama Cha Mapinduzi, familia, ndugu na jamaa wote, kwa misiba yote iliyotupata kwa kipindi kizima cha Bunge hili, Mwenyezi Mungu, azilaze mahali pema peponi roho za marahemu hawa. Amina. Mheshimiwa Spika, naomba pia kuchukua nafasi hii, kukipongeza Chama Cha Mapinduzi, kwa kukamilisha mchakato wa kumpata Mgombea wa Kiti cha Urais, uliofanyika tarehe 4 Mei, 2005, Chimwaga hapa Dodoma. Katika mchakato ule, nadhani nitaeleweka nikipendekeza Bunge lako liwapongeze wale wajasiri wote 11, mimi nikiwa mmoja wao waliothubutu kugombea nafasi hiyo, mpaka akapatikana mshindi. Huyo ndiye mshindi ambaye, kwa vigezo vyote tunavyovijua, Mungu akipenda, atakuwa Rais wetu baada ya uchaguzi. (Makofi) Nampongeza sana Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa ushindi wake wa kusisimua. Nampongeza pia Mheshimiwa Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, kuwa Mgombea Mwenza na mwisho nampongeza Mheshimiwa Amani Abeid Karume, kwa kuteuliwa kwake kuwa Mgombea wa Kiti cha Urais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mheshimiwa Spika, naomba kwa namna ya pekee, nichukue fursa hii, kuwasalimu Wananchi wa Ilala - Dar es Salaam. Nawashukuru sana kwa kunichagua kwa vipindi viwili kuwawakilisha hapa Bungeni, katika Manispaa ya Ilala na katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa baraka zao, niliwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri na kwa miaka saba nilikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi. Baada ya miaka 10 ya utumishi huu na nikizingatia mazingira mazuri yaliyopo, nimeona vema nisigombee tena nafasi hii ya Ubunge na pengine huu ndiyo wakati mwafaka wa kutoa tamko hili. (Makofi) Kwa ngazi zote za utawala, Jimbo la Ilala ni salama sana kwa Chama cha Mapinduzi, ninaamini hakutakuwa na maajabu huko Ilala. Chama cha Mapinduzi kitashinda tu kama ambavyo tumekwisha shinda katika nafasi zote za Serikali za Mitaa katika jimbo hilo. Sijajitoa kabisa katika shughuli za kisiasa. Nitaendelea kukitumikia Chama changu na Serikali zake, kwa namna yoyote itakoyofaa katika siku zijazo na huu pia si ujumbe wa ajabu ni tamko la kawaida. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tarehe 16 Juni, 2005, Kamati yangu ilikutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, Mheshimiwa Dr. Abdallah Omar Kigoda, pamoja na Katibu wake Mkuu, Dr. Enos Bukuku na Maafisa Waandamizi kutoka Idara mbalimbali za Wizara yake, ambapo Kamati yangu ilipata fursa ya kupitia, kuchambua na kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2004/2005 na Taarifa ya Shabaha na Malengo ya Ofisi hiyo, kama ilivyo kwenye Makadirio ya Matumizi kwa mwaka 2005/2006.

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

40

Mheshimiwa Spika, Kamati inampongeza Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu na Wasaidizi wao wote, kwa kazi za kuridhisha walizofanya kwa kipindi chote cha mwaka 2004 na cha matayarisho ya Bajeti ya mwaka huu. Pamoja na kujadili taarifa hizo, Kamati ilipata fursa ya kuzifahamu Idara mbalimbali za Wizara, Mashirika na Asasi mbalimbali, pamoja na majukumu yake ya kusimamia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, pamoja na Sera na Mikakati ya kupambana na umaskini (Poverty Reduction Strategy) na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji ilitekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika taarifa ya Kamati kwenye ukurasa wa tano mpaka wa sita. Katika kufanikisha majukumu hayo, katika mwaka wa fedha wa 2004/2005, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, ilitengewa jumla ya shilingi bilioni 10.5 kwa Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, takriban shilingi 2,010,000,000 zilikuwa kwa ajili ya mishahara na takriban shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya matumizi mengineyo. Hadi mwisho wa robo ya tatu ya mwaka, yaani mwisho wa Machi, 2005, Hesabu zinaonesha kuwa, kiasi cha takriban shilingi bilioni 1.5, sawa na asilimia 74.2 ya makiso ya mwaka 2004/2005, zilikuwa zimeshatumika kulipia mishahara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, pamoja na Asasi zake na shilingi 4,354,000,000, sawa na asilimia 51.1 ya makisio ya mwaka, zilikuwa zimetumika kwa matumizi mengineyo. Aidha, katika mwaka wa fedha wa 2004/2005, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, ilitengewa kiasi cha shilingi 600,000,000 fedha za ndani na takriban shilingi bilioni 14 fedha za nje, kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo. Hadi kufikia mwisho wa Machi, 2005, fedha za ndani zilizotumika ni shilingi 122,090,690, sawa na asilimia 20.3 ya makisio ya mwaka na shilingi 4,098,308,154, sawa na asilimia 29 ya makisio ya mwaka ya fedha za nje. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, Kamati ilitoa maagizo matano kwa utekelezaji, maagizo haya yameorodheshwa katika ukurasa wa nane mpaka wa tisa katika taarifa ya Kamati. Maagizo haya utekelezaji wake umefanyika kwa viwango tofauti na Serikali inaendelea na jitihada za kufanikisha utekelezaji kamili kama ilivyoagizwa na Kamati. Mheshimiwa Spika, katika kuandaa Bajeti ya mwaka 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, imezingatia azma ya Serikali ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, MKUKUTA na Mpango wa Kati. Aidha, katika kutekeleza Mpango wa Bajeti, Wizara italenga katika jitihada za Serikali za kukuza uchumi jumla, sambamba na mwelekeo wa utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Wizara imebainisha kuendeleza biashara ya nje, pamoja na kujenga mazingira ya uwekezaji rasilimali nchini, kushirikiana na nchi za nje, pamoja na kufuatilia Maazimio ya Taasisi na Programu za Kimataifa kama vile WTO, European Union na ACP.

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

41

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendeleza kuratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Mpango Mpya wa Ushirikiano ili kuleta maendeleo Barani Afrika (NEPAD), hususan kuanza utekelezaji wa Mpango wa African Review Machanism (APRM) na kushiriki Mikutano ya Kimataifa ya Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD III). Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ambayo Wizara inatarajia kuimarisha ni pamoja na shughuli zinazofanywa na Idara za Uwekezaji Mitaji ya Umma, Mikakati ya Kukuza Uchumi, Idara ya Uchumi Jumla na Idara ya Huduma za Jamii na Rasilimali watu, kwa kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Programu za MKUKUTA kwa kipindi cha 2005/2006 - 2007/2008 na Tanzania Mini-Tiger Plan 2020. Mheshimiwa Spika, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kitaendelea kuimarishwa kwa kufanya upanuzi na uboreshaji wa miundombinu ili kiweze kutekeleza majukumu yake ya kimsingi ya kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, kufanya tafiti mbalimbali na kutoa ushauri na uelekezi kwa wadau wote wa maendeleo hasa katika ngazi za vitongoji, vijiji na Wilaya. Aidha, Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika, kitaendelea kutoa mafunzo ya taaluma ya takwimu kwa lengo la kuboresha ukusanyaji, uchambuzi na kuzisambaza kwa matumizi mbalimbali. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2005/2006, Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC), itaendelea kushughulikia ubinafsishaji wa Mashirika ya huduma, miundombinu na Mashirika yaliyosalia ya biashara. Mashirika yaliyo katika hatua mbalimbali za ubinafsishaji ni pamoja na Shirika la Reli, Vitengo vilivyosalia vya kibiashara vya Mamlaka ya Bandari, Kampuni ya Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Bima, Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Shirika la Posta Tanzania, NMB na Marine Services Company, inayotoa huduma ya safari katika Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Tume pia itaendelea kushughulikia majukumu ya uundwaji wa Mamlaka za Udhibiti kwa Mashirika ya huduma na miundombinu. Mheshimiwa Spika, maendeleo ya Wananchi walio wengi msingi wake mkubwa ni kilimo na viwanda vidogo vidogo, pamoja na viwanda vikubwa. Aidha, sekta hizi mbili ndizo zinazotegemewa kwa kiwango kikubwa katika kuchangia na kukuza Pato la Taifa. Haiyumkini kwamba, sekta hizi ziwe bado hazijaendelezwa kwa kiwango cha kuzifanya kuwa Mhimili Mkuu wa kujenga uchumi ulio imara. Kwa mfano, hivi sasa Sekta ya Viwanda inachangia kwa asilimia 8.3 katika Pato la Taifa na Sekta ya Kilimo inayobeba asilimia 80 ya Watanzania inachangia kwa asilimia 48 ya Pato la Taifa. Ni maoni ya Kamati yetu kuwa, Serikali itekeleze kwa vitendo azma yake ya kuanzisha Benki ya Kuendeleza Kilimo (Agricultural Development Bank) na pia kuendeleza Viwanda, iundwe pia Benki ya aina hiyo (Industrial Development Bank). Aidha, Kamati inaona ni vema kuweka utaratibu wa kutoa mikopo midogo na mikubwa kwa wakulima na kusimamia uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo, sambamba na kuendeleza sekta nyingine kama vile uvuvi, ufugaji, madini, pamoja na kuimarisha miundombinu vijijini. Kadhalika, uzoefu wa nchi nyingi Duniani, umeonesha kuwa sekta hizi mbili, hutegemeana katika uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa ndani na nje ya nchi. Hivyo basi,

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

42

Kamati inaendelea kuishauri Serikali kuharakisha zoezi la mchakato wa uanzishaji wa Benki ya Maendeleo (Tanzania Development Bank). Mheshimiwa Spika, sekta nyingine ambayo ni kiungo kikubwa katika kuendeleza kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi yetu ni miundombinu, hususan barabara. Kamati inaipongeza kwa dhati Serikali, kwa hatua kubwa zilizofikiwa katika ujenzi wa barabara zetu hapa nchini. Pamoja na mafanikio haya mazuri, Kamati inashauri Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kuendeleza mawazo na mipango mipya na kuishauri Serikali jinsi ya kuunganisha barabara kuu kati ya Mikoa ya Kaskazini ya Kati mpaka Kusini na Mashariki ya Kati na mpaka Magharibi, pamoja na barabara za pembezoni mwa nchi. Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwa mafanikio mazuri yaliyopatikana kufuatia zoezi la ubinafsishaji wa yaliyokuwa Mashirika ya Umma. Aidha, Mheshimiwa Waziri, ameipa taarifa Kamati yangu kuwa, katika mwaka wa 2005/2006, Serikali inakusudia kukamilisha zoezi la Urekebishaji na Ubinafsishaji wa Mashirika ya huduma na miundombinu kama vile TRC, THA, TANESCO, NIC, NMB, TAZARA na Mashirika mengine ya kibiashara. Mheshimiwa Spika, uzoefu wa hata nchi zilizoendelea, unaonesha kuwa mashirika nyeti kwa uchumi wa nchi kama haya, huwa hayauzwi moja kwa moja. Kamati inashauri Serikali ifanye maamuzi ya ukodishaji kwa Mashirika haya ili pale wawekezaji wanaposhindwa kuyaendeleza, basi Serikali ifanye maamuzi ya kutoa fursa ya kuyaendeleza kwa wawekezaji wengine. Aidha, uwekezaji au ukodishaji huo ushirikishe wawekezaji wa ndani na wa nje, mfano wa DAWASA ni jibu. Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha kutekeleza kazi za Wizara na Asasi zilizo chini yake, Mheshimiwa Waziri, anaomba fedha kama alivyoeleza yeye mwenyewe katika hotuba yake. Kamati inaliomba Bunge lako Tukufu, liidhinishe maombi hayo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba niungane na wenzangu wengi hapa Bungeni, kumpongeza Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa, kwa mema yote aliyowafanyia Watanzania katika kipindi chake chote cha utawala. Kwa vigezo vyote, Tanzania ya leo kimaendeleo siyo ile tuliyokuwa nayo miaka 10 iliyopita. Kupitia kwako, Mheshimiwa Spika, mimi na Wananchi wa Ilala, tunaomba Mheshimiwa Rais, Mawaziri wake na Serikali yote anayoiongoza, pamoja na Watumishi wa Serikali, wapokee salamu zetu za kheri. (Makofi) Mheshimiwa Spika, napenda nichukue nafasi hii, niwapongeze kwa dhati kabisa, Wajumbe wote wa Kamati yetu kwa michango, maoni na kwa kufanya kazi zote za Kamati bila kuchoka. Pia nawashukuru Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati nyingine, ambao kila tulipokuwa na jambo nyeti katika Kamti yetu, walituunga mkono na wakaja kushiriki pamoja nasi. (Makofi)

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

43

Mheshimiwa Spika, naomba niwatambue wajumbe hao kwa majina yao mbele ya Bunge lako Tukufu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Njelu E. M. Kasaka, Mwenyekiti wetu, Mheshimiwa Lephy B. Gembe, Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Raphael N. Mlolwa, Mheshimiwa Elisa D. Mollel, Mimi mwenyewe Iddi M. Simba, Mheshimiwa Kilontsi M. M. Mporogomyi, Mheshimiwa Abdullatif H.ussein Esmail, Mheshimiwa Profesa Simon M. Mbilinyi, Mheshimiwa Edson M. Halinga, Mheshimiwa Mwanamkuu Makame Kombo, Mheshimiwa Mossy Suleiman Mussa, Mheshimiwa Stanley H. Kolimba, Mheshimiwa Suleiman A. Sadiq, Mheshimiwa Dr. Raphael M. Chegeni, Mheshimiwa Dr. Hassy H.B. Kitine, Mheshimiwa Dr. Talala B. Mbise, Mheshimiwa Lediana M. Mng’ong’o, Mheshimiwa Omar Juma Omar, Mheshimiwa Felix C. Mrema, Mheshimiwa Hasnain M. Murji, Mheshimiwa John L. Mwakipesile, Mheshimiwa Venance M. Mwamoto, Mheshimiwa Chrisant M. Mzindakaya, Mheshimiwa Esther K. Nyawazwa, Mheshimiwa Issa Mohamed Salim, Mheshimiwa Rostam Aziz na Katibu wetu mchapa kazi, Ndugu James J. Warburg. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napenda nikushukuru wewe binafsi, kwa kutoa miongozo na maelekezo mbalimbali kwa Kamati yetu ambayo wakati wote, yamefanikisha kazi za Kamati. Aidha, napenda pia kumshukuru na kumpongeza Katibu wetu wa Bunge, Bwana Damian S. L. Foka na Sekretarieti ya Kamati, kwa kuipa Kamati uwezo na nyenzo zote katika kufanikisha kazi za Kamati yetu. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, napenda kutamka kuwa, naunga mkono hoja na pia naomba kuwasilisha. (Makofi) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge wafuatao, wamejiandikisha kuchangia hoja hii: Mheshimiwa Balozi Getrude Mongella, Mheshimiwa Maria Watondoha, Mheshimiwa Dr. Chrisant M. Mzindakaya na Mheshimiwa Thomas Ngawaiya, ndiyo watakuwa wanne wa mwanzo, wapo wengine lakini hawa ndiyo watakuwa wanne wa mwanzo. Sasa namwita Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, atoe maoni ya Kambi hiyo. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI KWA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 43(5)(b)(c), toleo la 2004, naomba kwa ruhusa yako, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, kuwasilisha maoni yetu kuhusu Bajeti ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji kwa mwaka 2005/2006. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza Waziri, wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, Mheshimiwa Dr. Abdallah Kigoda, pamoja na Katibu Mkuu, ambaye ni shemeji yangu, kwa jinsi alivyoahidi kuweka mwelekeo wa uchumi wetu kwa kipindi alichotumikia Taifa letu akiwa Waziri katika Wizara hii. Tunampongeza, japokuwa bado tuna mapungufu na tumekuwa tukijitahidi kuyaweka bayana katika hotuba zetu tulizozitoa hapa Bungeni.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

44

Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi kwa Waziri na timu yake, naomba kugusia kwa ufupi, utendaji na ufanisi wa baadhi ya idara zilizo chini ya Wizara yake. Mheshimiwa Spika, katika Kitengo cha Takwimu, kwa kipindi cha miaka kumi, kumekuwa na mafanikio ya wastani katika ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu. Tunaomba kuipongeza Wizara kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa takwimu. Pamoja na umahiri wa ukusanyaji takwimu, lakini kwa maoni ya Kambi ya Upinzani, tunaona kwamba, bado takwimu zinazokusanywa ama wakati mwingine zinagongana na kutotoa taarifa inayohitajika. Kwa mfano, kwa mujibu wa Jedwali Namba 87(e), Taarifa ya Hali ya Uchumi, inaelezea idadi ya vitanda katika hospitali zote nchini katika mwaka 2004, lakini haielezei mahitaji ya vitanda katika Hospitali za Rufaa nchini, bali imetoa idadi ya vitanda vilivyopo tu 3,965. Hivyo hivyo kwa Hospitali za Mikoa 5,243 na Wilaya 8,889. Zimetajwa hospitali nyingine 12,506 hatujui ni zipi maana hakuna uchambuzi wake. Vituo vya Afya 8,035 na zahanati 10,445 na jumla ikatolewa 49,074. (Makofi) Mheshimiwa Spika, takwimu hazisemi kuna upungufu wa kiasi gani kwa kila ngazi niliyoitaja. Haya ni mapungufu makubwa katika kutaka kuzitumia takwimu katika kutathmini mpango wa muda mfupi, wa kati na wa muda mrefu. Aidha, takwimu hazituelezei kuwa katika zahanati 5,576 za Serikali, je, Serikali ilikuwa na mpango gani wa kujenga zahanati na ngapi ilipanga kuzijenga na pengo litajazwa na nani ni Mashirika ya Dini, watu binafsi na kadhalika? Taarifa hizi zingeweza kusaidia kujua eneo la kuongeza nguvu zetu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kasoro nyingine ya kutisha ni kukosekana kwa baadhi ya takwimu. Kwa mfano, Jedwali Namba 87 linaloelezea idadi ya Wataalam wa Afya, baadhi ya kada, takwimu zake hazioneshi na mimi naamini takwimu hizi zipo Wizara ya Afya, ila haieleweki ni vipi Kitengo cha Takwimu kilishindwa kuzipata hasa za miaka ya 2000, 2001, 2002, 2003 na 2004 wakati teknolojia imeongezeka sana sasa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, mbali na baadhi ya takwimu kukosekana, hata hizo zilizopo hazielezi ni wataalam wangapi kwa kila kada wanahitajika na upungufu ni kiasi gani, kwa hiyo, hatuwezi kujipima kisayansi hatua tuliyofikia. (Makofi) Mheshimiwa Spika, hii ni mifano michache tu niliyoitoa, ninaamini iko mingine mingi ya aina hii. Ninafikiri Waziri atatusaidia maelezo. Kama Ofisi ya Takwimu ya Taifa takwimu zake ziko hivi; je, huko Wilayani ngazi ya Kata hali ikoje? Waswahili wa Kipemba wanasema, ikiwa kilemba kimeroa, mkuti ukoje? (Makofi) Mheshimiwa Spika, mkuti ni ile shuka tunayovaa chini au seruni wanaita watu. Sasa kama kilemba juu kimeroa, basi mkuti uko na hali mbaya sana chini. (Makofi/Kicheko) Mheshimiwa Spika, kutokana na mapungufu haya, ni wazi kuwa, ipo kasoro kubwa juu ya takwimu hizi za mafanikio yetu, ama zimepunguzwa au kuongezwa. Lakini kutokana na umaskini wa kipato kuendelea kuongezeka, ni dhahiri kuwa, takwimu zetu hazielezei hali halisi ilivyo katika maeneo tunayozungumzia. (Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

45

Mheshimiwa Spika, kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kupanga mipango itakayowaondoa Watanzania katika dimbwi la umaskini wa kipato. Kambi ya Upinzani, inaipongeza Serikali kwa kuandaa programu nyingi kiasi cha kwamba tunapata wasiwasi kwamba, Wananchi wetu wana uwezo wa kuzielewa programu zetu kama MKUKUTA, MKURABITA na kadhalika. Upo uwezo wa kuratibu, kutathmini mipango yenyewe hasa katika ngazi ya Wilaya, Kata na Tarafa, tukitilia maanani kuwa hata fedha zipatazo shilingi milioni 400 zilipelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya mikopo kwa vijana. Ni Halmashauri nne tu ndizo zilizorejesha mikopo hiyo. Kiwango cha elimu cha watu wote, ambao kutokana na takwimu za Wizara ya Elimu ni kwamba, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari kidato cha kwanza bado ni chini ya theluthi moja ya wanafunzi wote wanaofanya mitihani ya darasa ya saba Mikoa ya Tanzania Bara, wastani wa asilimia 20 tu. Mheshimiwa Spika, jana Waziri wa Elimu, alisema ni wastani wa asilimia 10, nalo hili ni tatizo la takwimu. Hivyo, katika vijana 7,083,063 ni vijana 401,598 tu ndiyo walioko katika Secondary Schools na kati ya hao 31,001 tu ndiyo walioko katika kidato cha tano na sita na kati ya hao 26,475 ndiyo walioko katika Vyuo vya Elimu ya Juu. Ukiwa na wastani wa watoto 6,000,000 tu kwa mwaka wa saba wa masomo, ambao hawapati Elimu ya Sekondari, hili ni kundi kubwa la nguvu kazi. Hivyo, katika mipango yetu, tulihitaji kupanga Martial Plan ya kuondokana na dosari hii. Mheshimiwa Spika, leo wafanyakazi wa mahotelini asilimia kubwa wanatoka Kenya. Hivyo, Kambi ya Upinzani ikipata ridhaa ya Wananchi, itaandaa mipango yote ya matumizi kuelekeza nguvu zake kwenye elimu kama ifuatavyo: - (i) Kwa kumaliza tatizo la vijana kutoingia kidato cha kwanza na cha tano; (ii) Kusomesha walimu wa kutosha na katika kipindi cha mpito tutaajiri walimu kutoka nje ya nchi hasa India; (iii) Kila kanda kuwa na bohari yenye vitabu na vifaa vya kufundishia vya kutosha; (iv) Kupunguza muda wa kujenga shule na vyuo kwa kutumia prefabricated badala ya kujenga kwa miezi kumi na mbili, miezi miwili shule iwe tayari; (v) Kuhakikisha walimu hawakopwi na wanalipwa vizuri; na (vi) Kuhakikisha kuwa mwalimu anafundisha vipindi vinavyoweza kutoa tija, maana unaweza kuambiwa shule kuna walimu wawili, lakini ndiyo wanafundisha shule nzima. Kwa hiyo, huoni tija yoyote inayopatikana kwa sababu mwalimu mmoja ana vipindi vingi anavyofundisha. (Makofi)

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

46

Mheshimiwa Spika, tumeshuhudia Serikali kwa kipindi cha miaka takriban kumi, ikichukua hatua mbalimbali za kuinua uchumi katika kutekeleza ilani zake za uchaguzi zilizopita, ikiwa ni pamoja na ubinafsishaji wa mashirika mbalimbali yaliyokuwa yakimilikiwa na Serikali kwa asilimia kubwa. Naomba nikumbushe niliyoyanukuu kutoka kwenye Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa 2000, kuhusu ubinafsishaji na jinsi ambavyo ingelinda maslahi ya Watanzania. Mheshimiwa Spika, ilani ilisema yafuatayo: - (i) Mashirika ambayo ni ya msingi na nyeti, yaani Bandari, Reli, Posta, Simu, Mabenki ya Umma na Nishati kwa maendeleo ya Taifa, yataendelea kumilikiwa na dola; (Makofi) (ii) Sera ya Kurekebisha Mashirika ya Umma itakwenda sambamba na hatua za kulinda wafanyakazi wa mashirika yatakayohusika na CCM itahakikisha kuwa, ajira ya wafanyakazi inalindwa kwa kadri inavyowezekana na fidia za haki kwa wafanyakazi watakaoachishwa kazi zinatolewa; na (iii) Wafanyakazi wanaoachishwa kazi wanasaidiwa nao waingie katika Sekta ya Wananchi wanaojiajiri. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inauliza; je, misingi hii ya Ilani ya CCM imeheshimiwa na Serikali ya CCM? (Makofi) Sote ni mashahidi wa wafanyakazi wetu waliotumikia Taifa hili kwa maagizo na miongozo ya Serikali yao, wanavyosumbuka na kutaabishwa katika kudai haki zao zilizotokana na ahadi za Serikali. Wapo waliokufa bila kupata haki zao, wapo ambao mpaka sasa wako mahakamani na wapo wanaokuja kila mara hapa Bungeni, kuwafuata Waheshimiwa Wabunge wakihitaji msaada wao ili Serikali iwape haki zao baada ya mashirika yao kubinafsishwa, japokuwa mali zilizokuwa zikimilikiwa na mashirika hayo ni kubwa kuliko bei ya kuuzwa mashirika hayo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya IMF ni kwamba, Serikali haijanufaika na zoezi hili la ubinafsishaji, kwa maana ya faida kutokana na mauzo ya Mashirika ya Umma. Fedha ambazo zimepatikana ni kidogo mno ikilinganishwa na madeni na hili limethibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Hazina, Bwana Kijja, alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa magazeti ya Kampuni ya Business Times Limited, kuwa mpaka sasa matarajio yaliyotakiwa kutokana na zoezi zima bado hayajafikiwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ardhi ni rasilimali muhimu katika maisha ya mwanadamu na bila ya ardhi hakuna uhai kwa mwanadamu. Pamoja na ukweli huo, kuhusu rasilimali hii nyeti ya ardhi, mahusiano baina ya makundi mbalimbali yatumiayo rasilimali hii yamekuwa ya shari. Mathalan, maeneo kama Kilosa, Hanang’ na Ngorongoro ni kati ya maeneo ambayo yamekuwa na migogoro mingi ya ardhi, ambayo imekuwa ikisababisha kuibuka kwa mapigano makali. Ubinafsishaji wa mashamba ya NAFCO Wilayani Hanang’, umewaacha Wananchi kuzidi kuwa maskini siku hadi siku. Kambi ya

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

47

Upinzani inamwomba Waziri vile vile atoe tathmini ni Watanzania wa rika lipi wanaonufaika na Serikali imenufaika vipi na ubinafsishaji huu wa mashamba ya NAFCO na yale yaliyokuwa mashamba ya mifugo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ili kuondoa migogoro ya ardhi, Kambi ya Upinzani, ikipata ridhaa ya Watanzania, itahakikisha kunakuwa na utenganisho wa mipaka kati ya ardhi inayomilikiwa Kitaifa na ile inayomilikiwa na vijiji na kwamba, Serikali iwe na mamlaka na ardhi ya Taifa tu. Umiliki wa ardhi kimila unapewa hadhi sawa na umiliki wa ardhi wa hati. Zinawekwa taratibu za kutosha kulinda ardhi za vijiji zisipokonywe na watu wa nje ya vijiji vinavyohusika kwa njia za udanyanyifu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu mfumo wa mipango ya usimamizi wa uchumi, Kambi ya Upinzani kila mwaka imekuwa ikiishauri Serikali ibainishe maeneo yanayofanya uchumi wetu kuwa ghali. Majibu ya Serikali yamekuwa kwamba, nishati ndiyo eneo moja linalofanya uchumi wetu kuwa ghali. Nakubaliana kabisa na maelezo haya, lakini hivi sasa viwanda vyetu vilivyoko kwenye Sekta ya Ujenzi vinatumia gesi ya Songo Songo, mfano, viwanda vya saruji, mabati na kadhalika. Mheshimiwa Spika, pamoja na viwanda hivyo kutumia gesi ya Songo Songo katika kupata umeme wake, bado hatujaona tofauti ya bei ya bidhaa wanazozalisha. Kwa mfano, mfuko mmoja wa saruji miezi mitatu iliyopita ulikuwa Sh.7,600/=, leo ni Sh.9,000/= na kila mwuzaji ana bei yake. Bei hii ni ya mjini, vijijini ambako ndiko kwenye Watanzania waliozama katika dimbwi la umaskini, bei ya mfuko mmoja wa saruji kwa mfano, Kagera ni Sh.15,000/=, Pemba ni Sh.9,000/=. Bei ya sukari, unga na bidhaa nyingine hazisemeki. Je, uchumi utakuwa rahisi kuweza kupenya kwenye masoko ya wenzetu? Mtanzania hasa aliyeko kijijini ataondokana na umaskini uliokithiri wakati hata pamba yake, karafuu zake, haipati bei muafaka? (Makofi) Mheshimiwa Spika, ninamwomba Mheshimiwa Waziri, atuelezee hatua za uhakika wanazochukua za kupunguza ughali wa uchumi wetu ambao unaongezeka kila panapokucha. (Makofi) Mheshimiwa Spika, jambo lingine linalosababisha ughali wa uchumi wetu ni ukosefu wa uratibu (coordination), kati ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji na Wizara nyingine. Mfano, ukiangalia bajeti yetu, kila Wizara, Idara au Asasi, ina fungu la UKIMWI, lakini ukiuliza ni nani anayeratibu, anayehakiki na kutathmini mafanikio au matatizo ya kila Wizara juu ya UKIMWI huwezi kupata majibu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, siyo kweli kwamba, kila Wizara au Asasi, wapo wataalam wa masuala ya UKIMWI. Kambi ya Upinzani, inaamini kuwa hatuwezi kupunguza ughali wa uchumi wetu na mzigo wa madeni bila ya kuwa na proper coordination ya uwekezaji na utumiaji wa rasilimali zetu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu tathmini ya mikopo na misaada, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, naomba kuipongeza Serikali kwa kushirikisha wadau wote katika matayarisho ya bajeti yake, pamoja na kwamba, muda na namna wanavyoshirikishwa

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

48

wadau hao, bado kuna haja ya kuboreshwa hasa katika maandalizi ya awali ya mipango na bajeti ya kila mwaka. (Makofi) Aidha, ninaipongeza Serikali kwa jitihada za kutoa taarifa juu ya mapato na matumizi ya Serikali, yanayotokana na mapato ya ndani na ile ya misaada na mikopo. Inawezekana baadhi yetu hatupati muda wa kushiriki katika vikao hivyo au kusoma taarifa zinazotolewa ndani ya Bunge, Kamati za Bunge na hata katika tovuti za Serikali. Hivyo, siyo sahihi kusema kwamba, Wabunge wako wa Bunge hili Tukufu , hawawatumikii kwa uadilifu Watanzania au kwamba hakuna taarifa za mapato na matumizi ya Serikali. Kilichopo na kinachotakiwa kuwepo ni uboreshaji wa mapato kwa kuziba mianya ya misamaha holela ya kodi, ukusanyaji bora wa mapato, kuziba mianya ya rushwa na matumizi ya mapato hayo yasiwe ya isirafu. Mheshimiwa Spika, kwa kiwango kikubwa Bunge lako Tukufu limeweza kusimamia kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa sana. Kwa mfano, Bunge lako Tukufu kuanzia mwaka 1999 hadi 2004/2005, fedha zilizoainishwa kwa ajili ya maendeleo kwa Wizara na Idara za Serikali na Mikoa zinakaribia kuwa Shilingi trilioni 3.6. Kambi ya Upinzani jambo ambalo linaitaka Serikali ifanye na kama ilivyoahidi huko nyuma ni: - (i) Ifanye tathmini ya kujua ni kiasi gani cha fedha za misaada na mikopo zimekwenda kwenye utawala wetu ambao ni mkubwa sana, utawala wa waliotupa misaada (Technical Assistants) na ni kiasi gani kinakwenda kwenye miradi na ni kiasi gani kinakwenda kwenye semina na warsha tunazozifanya kila siku. (Makofi) (ii) Kuweza kujua namna bora ya kutumia misaada na mikopo hiyo ili tuweze kujua tathmini halisi kulingana na fedha iliyotumika (value for money). (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu uwekezaji, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani napenda kuipongeza Serikali na hasa Rais wetu tunayemuaga kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuitangaza Tanzania kama sehemu nzuri ya uwekezaji. Kazi hii haikuwa rahisi, kwani wakati huu kila nchi inatangaza vivutio mbalimbali kwa ajili ya wawekezaji katika nchi zao. (Makofi) Mheshimiwa Spika, katika hatua hii ya kuwashawishi wawekezaji, Watanzania walio wengi, walijenga matumaini kuwa uwekezaji utawaongezea ajira katika muda mfupi sana, lakini ni kweli yapo mafanikio ambayo yatachukua muda mrefu kuonekana moja kwa moja, kwani kuna mambo mengine ni lazima yatekelezwe ili matunda hayo yapatikane kwa Mtanzania wa kawaida. Mheshimiwa Spika, kwa mfano, ili uweze kupata mapato yanayotokana na madini ni lazima uwe na mambo yafuatayo: - (i) Uwe na wanataaluma waliobobea katika fani ya uchimbaji wa madini (Experts of Various Fields in Mining);

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

49

(ii) Uwe na watu wenye ujuzi (Skilled People); (iii) Uwe na uwezo wa kuzalisha angalau asilimia 60 ya mitambo na vifaa vinavyohitajika katika uchimbaji; (iv) Uwe na vyombo vya fedha vyenye uwezo wa kutoa mikopo ya muda mrefu kwa wawekezaji wa miradi hiyo; (v) Uwe na uwezo wa utaalamu wa kufuatilia masoko, thamani ya bidhaa inayozalishwa; na (vi) Ikiwezekana uwe na uwezo wa kuongeza thamani ya bidhaa yenyewe kwa kuwa na viwanda vinavyotoa bidhaa hiyo ndani ya nchi. Mheshimiwa Spika, ikiwa una mambo sita hayo niliyotaja hapo juu, unaweza ukasamehe kodi, kwani utapata kodi kwa njia nyingine. Kwa sababu yote hayo hapo juu hayapo, ni dhahiri mapato yanayotokana na madini, itachukua muda mrefu kuonekana kusaidia kukua kwa uchumi wetu na kuongeza ajira. Matokeo ya kasoro hii, tumetunga sheria inayoipa Mamlaka TIC, kumshauri Waziri wa Fedha, awasamehe kodi wawekezaji hao ambao watatimiza masharti ya sheria ya uwekezaji. Mheshimiwa Spika, kutokana na uwezo mdogo wa TIC wa kutathmini, kuhakiki maombi ya wawekezaji, kituo kimekuwa kikitumika kama sehemu ya kupata msamaha wa kodi kinyume na matarajio ya Watanzania. Hivyo, ili tuweze kupata matunda ya uwekezaji, ipo haja ya kufanya ukaguzi wa kina juu ya uwekezaji (Management Auditing). (Makofi) Mheshimiwa Spika, kama hatujawa na sera ya kuhakikisha kuwa, Watanzania wenyewe wanawezeshwa kumiliki angalau asilimia 40 ya miradi inayowekezwa nchini, asilimia 60 ya uajiri, ni dhahiri tunapalilia umaskini. Tofauti ya walionacho na wasionacho itapanuka siku hadi siku, hivyo tutahatarisha usalama wa nchi yetu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mambo mengi niliyasema wakati nilipowasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kwenye Hotuba ya Bajeti, naamini ujumbe umefika. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hii ni hotuba yangu ya mwisho, naomba nichukue nafasi hii, nimpongeze Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa, kwa hotuba yake aliyoitoa Zanzibar wakati akizindua Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa ya kusimamia mustakabali wa kisiasa nchini kwetu kwamba, ikilazimika atatumia vyombo vya dola kuhakikisha kuwa, uchaguzi unakuwa huru, haki na salama. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ni matumaini yetu kwamba, atatekeleza kauli yake kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinatimiza wajibu wao wa

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

50

kulinda raia na mali zao na wao hawatajiingiza katika masuala ya kisiasa kwa kushabikia upande wowote. (Makofi) Aidha, kama Amiri Jeshi Mkuu, namwomba ahakikishe kuwa, yale Majimbo kama la Wawi, Mkanyageni na kadhalika, yenye vikosi aina sita vya ulinzi katika Jimbo la watu 15,000, yaani Jeshi la Wananchi, Polisi, JKU, KMKM, JVZ na Zimamoto, vinabaki kambini na kuliacha Jeshi la Polisi lifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na sheria nyingine za nchi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Rais wetu amefanya kazi kubwa, anahitaji apumzike akiwa na matumaini ya kwamba, Watanzania wataondokana na dimbwi la umaskini. Hivyo, naomba kurudia kauli yangu kwamba, ni wajibu wetu sote, kushirikiana na Rais wetu katika kuhakikisha kuwa, tunakuwa na uchaguzi ulio huru, haki na salama. Mungu ibariki Tanzania. (Makofi) Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na kuunga mkono hoja. (Makofi) MHE. BALOZI GETRUDE I. MONGELLA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami nichangie Hotuba ya Waziri wa Mipango na Ubinafsishaji. Kwanza kabisa, ningependa kusema kwamba, ni mara ya kwanza, kusimama katika kipindi hiki cha Bunge hili la Bajeti kwa sababu siku za nyuma nimekuwa na shughuli nyingi za kifamilia na pia za Kitaifa na za Kimataifa, kwa hiyo, sikuwepo kwa muda mrefu na ninashukuru nimerudi Bungeni salama. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nami ningependa kusema kwa masikitiko makubwa kwamba, tumempoteza mwenzetu, Marehemu Mheshimiwa Margareth Bwana, ambaye kwa kweli alikuwa si yupo tu, kuna kuwepo kuwepo ndani ya Bunge, lakini kuna kuwa na uwakilishi na unaonekana kwa kazi. Kwa hiyo, mwenzetu tumempoteza, ambaye alikuwa yupo kweli, ameshika nafasi katika Bunge hili na ni masikitiko makubwa kwamba, hatunaye tena. Mwenyezi Mungu, aweke roho yake mahali pema peponi na wale wengine wote waliotutangulia mbele ya haki. Amin. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ningependa kwa sababu tumefika kipindi cha mwisho cha kumaliza contract, tunayo contract ya miaka mitano mitano na sasa tarehe 29 kipenga kitalia ili tujipange upya katika kutafuta nafasi za Ubunge, ningependa niyaseme machache ya jumla. Moja, nami naungana na wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Rais na Askari wake wa Miavuli, ambao wamefanya kazi katika mazingira magumu. Kuongoza nchi maskini siyo kazi rahisi kama watu wengi wanavyofikiri, ni kujitoa mhanga, ni kufanya kazi kwa uvumilivu na kwa umakini kabisa. Kwa hiyo, naomba niwapongeze Mheshimiwa Rais, pamoja na Askari wake wa Miavuli, Mawaziri wote na Manaibu Waziri, kwa kazi nzuri ambayo wameifanya. (Makofi)

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

51

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, kazi ambazo zimetuonesha mafanikio zinatupatia matumaini makubwa ya kurudisha Chama cha Mapinduzi katika uongozi wa nchi hii. Ukiangalia kitabu cha takwimu kipindi kilichopita ni kwamba, Wana-CCM 257 walichaguliwa kuingia katika Bunge hili, Wanachama wa CUF 22 waliingia katika Bunge hili, Wanachama watano wa CHADEMA waliingia katika Bunge hili, Wanachama watano wa UDP waliingia pia na Wanachama wawili wa NCCR-Mageuzi waliingia katika Bunge hili. Mheshimiwa Spika, kwa takwimu hizo, inaonesha itakuwa ni maajabu kwa takwimu kama za Chama cha NCCR-Mageuzi, watu wawili kuja kushika nafasi ya kuongoza Taifa hili na wengine wote ambao wako chini ya asilimia hata kumi ya Bunge hili kuja kugeuza mara moja. Isipokuwa ninachotaka kukisema kwa Wapinzani, napenda niseme wamekuwa makini, wamefanya kazi yao vizuri kama wa upande wa Upinzani ambapo ndiyo kazi inayopaswa kufanywa ndani ya Bunge. Sisi wa Chama cha Mapinduzi tunaheshimu Upinzani, kwa sababu ndicho Chama ambacho kiliamua ya kwamba, tuwe na Siasa ya Vyama Vingi. Ukielewa hivyo ni lazima pia ukubali kazi nzuri inayofanywa na Upinzani, kwa sababu unasaidia CCM yenye Wabunge wengi hapa kukaa macho na makini katika kuendeleza shughuli za nchi hii. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kama ukiangalia aliyemaliza kuzungumza sasa hivi, Mheshimiwa Hamad Rashid Mohammed, ni kijana aliyelelewa vizuri na Chama cha Mapinduzi na tulipoanza vyama vingi, akaamua kwa hiari yake kama tulivyotegemea ndani ya Katiba, akaenda kwenye Upinzani. Bado anaendelea na mwenendo ule ule wa CCM, wa kuchambua kwa makini na kuweka bayana yale ambayo anafikiri yazingatiwe na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi) Kwa hiyo, napenda wenzangu wa Upinzani, niwapongeze na wengi ni marafiki zangu wa kutoka Kojani, wa kutoka visiwa vya maji ya chumvi na wengine kutoka Bara, naomba niwapongeze na tunafikiria kwamba, Chama cha Mapinduzi, tutaendelea kushika hatamu na kushirikiana nanyi na muendelee kuchambua kwa makini. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ningependa niseme machache juu ya Wabunge walivyokuwa makini katika kipindi hiki. Haya yote yasingewezekana kama Wabunge tusingeshiriki na hasa ukizingatia kwamba, ukiwa na chama kimoja ambacho ndiyo kina nguvu zaidi, kuna hatari ya kuzembea. Lakini Wabunge wa Bunge hili hata wale wa Chama cha Mapinduzi, ambao ndiyo wanashika hatamu hawakuzembea hata kidogo katika kuchambua mambo haya na ninawatakia wenzangu wa Chama cha Mapinduzi kila la kheri. Wale wote wenye nia mbaya na ninyi, Mungu awaadhibu pale pale kwa sababu hatuendi kwenye siasa za chuki, tunaenda kwenye siasa za ushindani na Mungu anasikia dua zangu na wale watakaothubutu kuvuruga Ukerewe watakipata cha moto. (Kicheko/Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, napenda niseme haya yafuatayo juu yangu binafsi: Ninawashukuru zaidi kwa sababu Bunge hili limenienzi, likanipa nafasi ya kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika na baada ya hapo, Wabunge wenzangu wa Afrika wakanipa nafasi ya kuwa Rais wa Bunge la Afrika, nafasi ambayo nisingeipata kama ninyi Wabunge wenzangu, msingekuwa na imani na mimi. (Makofi)

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

52

Mheshimiwa Spika, kutokana na hayo, dunia nzima imeona kazi ambayo ninaifanya ndani ya nchi yangu na nje ya nchi na nimepata tuzo mbalimbali katika kipindi hiki. Kila ninapozipokea tuzo hizi, ninasema katika hotuba zangu kwamba, ninazipokea kwa niaba ya Watanzania wote na hasa wale ambao waliniona ninafaa kuifanya kazi hiyo. Nimeshapokea tuzo mbalimbali, moja ni ya Martin Luther King kutoka Marekani. Tuzo hiyo inamuenzi Muasisi wa Haki za Binadamu kati ya watu mashuhuri waliokuwa wanagombea haki za binadamu Marekani, Martin Luther King. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tuzo nyingine nimeipata ambayo ni ya kujenga uelewano kati ya binadamu, ambayo nilipewa na Chuo Kikuu cha Marekani cha Atlanta Georgia na nyingine nimeipata kutokana na Wanawake wa Nigeria ambayo wamenipa juzi, Utumishi Bora wa Mwanamke wa Afrika. Nimepata pia Doctorate (Ph.D.) kutoka katika Chuo cha Korea, kwa kazi nzuri ambayo wanafikiria nimechangia katika maendeleo ya dunia hii. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ziko nyingine nyingi, lakini ningependa tu niseme kwamba, bila ninyi kuninyanyua, bila ninyi kunienzi, mimi si chochote. Naomba niwashukuru, nitakapoenda kwenye jimbo langu, nitawaeleza haya haya ya kwamba, mlipoweka ndiyo kwangu, mlikuwa na maana ya kuwapa fursa Waheshimiwa Wabunge wenzangu, pia kunienzi nawashukuru sana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ningependa kusema kuhusu nchi yetu ambayo inatokana na mipango. Nia yetu ni nini, kupanga ili tupate kazi au tupate Watumishi wa Wizara au tuwe Wabunge kwa sababu ya kuwa Wabunge, nia ya mipango yote duniani...

(Hapa kengele ililia kuashilia kumalizika muda wa mzungumzaji) MHE. BALOZI GETRUDE I. MONGELLA: Ahaa! Hiyo mmenionea, ni dakika ngapi? (Kicheko) Mheshimiwa Spika, baada ya hayo, ningependa kusema nia kubwa ni kuwawezesha Watanzania na Mtanzania mmoja ndiyo kilio cha Watanzania. Ukiangalia katika takwimu zetu, Watanzania wamegawanyika katika makundi makubwa na hasa kundi kubwa katika takwimu ni vijana. Bahati nzuri tu juzi nimerudi kutawazwa Ukamanda wa Vijana wa Mkoa wa Mwanza, ni wimbi kubwa la vijana ambao tunawahitaji sisi sote. Kwa hiyo, tutakapokuwa tumerudi hapa Bungeni, kazi yetu kubwa nadhani ni kuliangalia hili kundi la vijana ambao ndiyo daraja la maendeleo ya Taifa letu. (Makofi)

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

53

Lakini tutawaendelezaje? Ukiangalia nchi ambazo zimepiga hatua kama hiyo nchi ya Korea nilikopata Doctorate, miaka 40 iliyopita maendeleo yao yalikuwa ni sawa sawa na Zambia kwa wakati huo. Lakini kwa nini wao wamepiga hatua na sasa hivi wameingia katika kundi la Mataifa ambayo sasa yanaanza kutoa misaada katika Tanzania, wameshatoa msaada wa kuongezea kujenga Vyuo vya VETA vinne katika nchi hii, watu ambao walikuwa sawa sawa Zambia miaka 40 iliyopita na sasa wamegeuka kuwa ni donors. (Makofi) Sababu moja kubwa ni elimu, wana vyuo, hakuna chuo chenye wanafunzi chini ya 20,000, ambavyo ni sawa sawa na wanafunzi tulionao hapa Tanzania. Kwa hiyo, msukumo kwa miaka mingi wamewekeza sana katika elimu. Natumaini ya kwamba, mipango yetu inayokuja tutajifunza hilo, Korea imeonesha hivyo, India imeonesha hivyo, Japan imeonesha hivyo, Malaysia imeonesha hivyo katika nchi za dunia ya tatu, ambao walijikwamua na hasa Japan ilipomaliza vita, kazi kubwa ilikuwa ni kujenga elimu. Natumaini ya kwamba, hilo tutalifanya tutakaporudi katika kipindi kijacho ili angalau tuwe na msingi bora wa kuwaelimisha Wananchi wetu, tumeanza na safari haijakamilika. Mheshimiwa Spika, mapengo yaliyooneshwa na Kambi ya Upinzani, katika hotuba hii ya Bajeti, nasema yale ni sawa sawa na tunachofanya kila siku. Kila kukicha hatujaacha kuoga na kujitazama kwenye kioo. Kwa hiyo, tuyapokee, pamoja na mawazo ya Wabunge wengine, tutayaweka katika mkakati wa kuyatekeleza ili tuweze kuboresha hii safari yetu ya kujenga nchi ambayo ni nchi yenye nguvu kiuchumi, nchi ambayo haina umaskini. Katika suala la umaskini, tutahitaji mikakati ya hali ya juu zaidi ili kuondokana na umaskini. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ningependa nigusie jinsi ya kuwaimarisha Watanzania katika kuwekeza katika uchumi wa nchi yao. Sisi Ukerewe tulikuwa na hoteli ilijengwa na cha Chama cha TANU akapewa Mzungu mmoja, akatudanganya, akatutapeli eti majamvi yale ndiyo akayafanya kuwa ceiling board. Juzi ametokea kijana mvuvi, amepewa fursa ameibadilisha ile hoteli imekuwa ni ya kisasa na watu wanaanza kusema kumbe tukiwaamini watu wetu, tunaweza tukafanya, huo ni mfano mdogo tu. (Makofi) Mji wa Mwanza sasa hivi unaanza kujengwa na wavuvi, wafugaji, ukiuliza lile ghorofa la nani watakwambia la mvuvi mmoja, wanakutajia na jina. Ukiuliza utaambiwa kuna baba mmoja kule Maswa ana ng’ombe wengi ndiyo ameijenga hii hoteli. Ni lazima turudi pale ambapo tunamuwezesha Mtanzania, aweze kuifanya kazi hii. Haya siyo maajabu, Nigeria wanafanya hivyo, Ghana wanafanya hivyo. Kwa hiyo, ili tuweze kushika uchumi wa nchi hii, ni lazima tuwawezeshe wale ambao ni watu wa hapa, wenye uchungu na nchi hii na walio na haki na nchi, kwa uwazi wazi bila kuona aibu. Sisi Wilayani Ukerewe, tutaendelea kuwawezesha vijana wetu wavuvi wakipata visenti vyao hata sekondari za binafsi wajenge ili watoto wetu waweze kusoma. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ningesema kuna fursa nyingi ambazo Watanzania tunaweza kuzifanya katika mipango, kuwawezesha Wananchi wetu kujikwamua kimaisha na niwatakie kila la kheri na nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

54

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii. (Makofi) MHE. MARIA D. WATONDOHA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami nichangie katika Mjadala huu wa leo wa Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji. Awali ya yote, niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu, kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Mheshimiwa Margareth Bwana, mpendwa wetu, ambaye ametangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu, ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin. Mheshimiwa Spika, hii ni mara yangu ya pili kuchangia na ningependa kuanza kuwapongeza Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji, Mheshimiwa Waziri mwenyewe, Katibu Mkuu wake na timu yake nzima ya Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa maelezo yake binafsi na ya Kamati, kazi kubwa ya Wizara hii ni uratibu. Tukiwa na mipango ya uhakika inayolenga Wananchi, Taifa letu litasonga mbele sana. Mambo mengi mema yametekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Mwenye macho wala haambiwi ona. (Makofi) Sasa kutuambia kwamba, tutaajiri walimu kutoka India ndiyo mafanikio, sioni kama itaweza kutusaidia. Ambacho ningeitaka Serikali sasa ifanye ni kuongeza juhudi zake katika kupata walimu wengi na wa uhakika. Mpango wetu wa MMEM ni mzuri na umetusaidia kufanikiwa kupata madarasa mazuri tu Vijijini, ambapo tulikuwa hatuna madarasa. Kila Mtanzania anafahamu sasa kwamba, sura za shule zetu za msingi zimebadilika. Mpango unaofuatia sasa ni wa MMES, tungeitaka Serikali ihakikishe iwe na utaratibu mzuri na wa makini. Zile fedha zinazotolewa kweli ziende zikafanye kazi iliyopangiwa. Kwa sababu fedha za Serikali zina kipindi chake, ikishafika tarehe 30 Juni, mwaka wa fedha ule umepita fedha zile kama hazikutumika zinarudishwa. Kwa msingi huo, nilikuwa nataka kuishauri Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji, pamoja na kuratibu iwe na uhakika kwamba, ina mpango wa ufuatiliaji wa utekelezaji katika ngazi zote. Tunao utaratibu wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri zetu na Serikali ya Mkoa. Lakini kazi ya mipango ni ya kitaalam na sijui kama tuna Maafisa Mipango ambao ni graduates katika Halmashauri zetu, maana pale tunapokosa Maafisa Mipango thabiti, Halmashauri nyingine zinakosa mipango sahihi ya utekelezaji. Hata tunapokosa Maafisa Mipango thabiti wa kuratibu kule Mkoani, tunaweza tusipate mipango mizuri. Kwa hiyo, ningeshauri kwamba, Wizara hii iratibu na ifuatilie mafanikio ya mipango, maana tukiacha tu mipango inakwenda halafu hakuna ufuatiliaji, uwezekano wa mambo kukwama ni mkubwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, katika mipango hii, natarajia wataalam watoe ufafanuzi na ushauri kwa viongozi wetu wa kisiasa. Kwa mfano, sasa hivi tuna mpango wa kujenga shule za sekondari katika kila Kata. Sisi Mkoa wa Lindi, jumla ya wakazi wote ni 800,000, hiyo ni pamoja na watoto na watu wazima. Kuna Kata zina kijiji kimoja au viwili, kweli ni mpango mzuri kuwa na shule ya sekondari katika kila Kata, lakini je,

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

55

tumeangalia wakazi waliopo, ama sivyo tutajenga shule ya sekondari itakuwa na wanafunzi wawili, Serikali itapeleka walimu wakati shule zilizopo zina upungufu? Kwa hiyo, nilikuwa nashauri pamoja na kwamba, hiyo ni sera yetu na utaratibu wetu, Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji, isadie kuratibu na kutoa ushauri unaofaa kwenye Mikoa na Halmashauri ili tusijenge white elephants, kwa nguvu za Wananchi halafu hazitumiki. Ningeshauri vile vile kwamba, mipango mizuri ya Serikali ambayo inaanzishwa na Wakuu wa Mikoa wale wanapohama, basi iendelezwe na wengine wanaofuatia. Tusije tukawa na kwamba huyu ametekeleza ametoka basi ya kwake hayatekelezwi yanaachwa inaanza mingine, kwa hiyo, mnaendelea kuwa na mipango ya ubunifu kila baada ya miaka mitano. Tungekuwa na mikakati mizuri ya vision 2025 na iwe endelevu katika kila Mkoa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo ningependa kushauri ni suala la Mikoa ambayo iko nyuma. Nasema iko nyuma si kwamba, Mikoa hii haina rasilimali au haina watu, lakini kutokana na historia, Mkoa wa Lindi umebaki nyuma si kwa sababu watu wake hawataki maendeleo ni kwa sababu Mkoa ule ulikuwa mstari wa mbele katika mapambano ya Uhuru wa Afrika. Tulikuwa na makambi pale, tulikuwa na wapiganaji kule, kwa hiyo, tulikuwa restricted area, watu walikuwa wanakuja wachache sana. Sasa ndiyo, Afrika nzima iko huru, kule kumefunguliwa vizuri sana. Lakini tunakosa miundombinu muhimu, kwa sababu tunakosa miundombinu muhimu, hatuna hata wawekezaji. Narudia tena kilio cha Songo Songo Gas, imekwenda Dar es Salaam ni sawa sawa kuchukua ndizi Dodoma kupeleka Bukoba. Sisi kule tumebaki hatuna umeme. Ni kweli tutapata umeme wa Mnazi Bay, Mungu akijalia huo umeme upatikane. Lakini tunakosa wawekezaji, nina hakika Mikoa mingine inaendelea kwa sababu wanapata wawekezaji. Barabara yetu tunatumaini itakamilika, maana angalau sasa unaweza kwenda kwa muda wa saa kumi ukafika Lindi kwa usalama, barabara yetu ikikamilika tutaweza kufungua. Lakini tusipokuwa na umeme wa uhakika, tusipokuwa na bandari nzuri, wawekezaji hawatafika. Kwa hiyo, nilikuwa naomba na kutoa ushauri kwa Serikali kwamba, Mikoa ambayo iko nyuma basi iangaliwe na wahakikishe kwamba, wanapelekewa miundombinu kuliko kuiacha na inaendelea kusuasua. Ukiangalia kwa ukubwa, Mkoa wa Lindi kwa mujibu wa takwimu hizi, nafikiri ni wa tano. Wa kwanza kwa ukubwa kieneo ni Mkoa wa Tabora, nafikiri Mkoa wa Lindi unakuja kama wa tano hivi. Lakini pamoja na ukubwa wetu, zaidi ya nusu ya Mbuga ya Selous iko Mkoa wa Lindi. Bado hatujaona matunda. (Makofi) Mheshimiwa Spika, eneo la tatu ambalo ningependa kutoa ushauri ni suala la ubinafsishaji. Naipongeza kazi nzuri ambayo inafanywa na Wizara hii katika kuratibu. L akini sisi pale Nachingwea tuna kiwanda cha Ilulu kilikuwa cha kukamua mafuta ya ufuta. Kile kiwanda ni sleeping giant, tunaambiwa kilibinafsishwa, Lindi ni wazalishaji wakubwa wa ufuta, lakini ufuta wetu wote tunauza kwa bei ya chini, pamoja na maelezo ya Serikali kwamba, tuongeze thamani ya mazao kwa kusindika, sisi hatuna kiwanda. Kiwanda kile kilikuwepo, kimefungwa, kilinunuliwa sijui na nani, mpaka leo. Sasa hebu mtuambie mpango wa Serikali ni nini? Mkimwuzia mtu mnaratibu vipi kufuatilia

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

56

kwamba, hiki kiwanda kilichonunuliwa kweli kinafanya kazi badala ya kubaki magofu ambayo kwa kweli hayatusaidii. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tunavyo viwanda vya korosho vile vile tunaambiwa kile cha Lindi nacho kimebinafsishwa, lakini hatujaona nguvu yoyote inayoonesha, maana tukiwa na viwanda angalau tunakuwa na uhakika kwamba, vijana wetu nao wanaweza kupata ajira. Kwa hiyo, ushauri wangu kwa Serikali katika suala la viwanda, tuhimize viwanda vidogo vidogo. Bei za mashine mbalimbali kwa mfano, za kukamulia ufuta ni shilingi milioni tatu. Inawezekana zimepanda kutokana na kodi, tunaomba basi Serikali iangalie namna ya kupunguza kodi ili kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana, kutumia kwa kufungua viwanda vidogo vidogo na tuweze kuzalisha mafuta badala ya kutegemea Korie tu itoke Dar es Salaam kwenda mpaka Lindi. Wangeweza kuzalisha mafuta kwa kutumia ufuta tulionao katika Mkoa ule. Mheshimiwa Spika, la nne, ambalo ningependa kutoa ushauri kwa Wizara hii katika mipango yao ni suala la hifadhi ya chakula. Katika Mkoa wa Lindi, mwaka huu tumekuwa na mvua nzuri, lakini sehemu kubwa kule kwetu walikuwepo panya. Sasa wengine hapa watasema mbona hamkula, panya wale waliokuwepo hawaliwi. Panya wanaoliwa ni wale wakubwa, panya buku, panya waliokuwepo ni wale wadogo wadogo ambao walikuwa wanakula miche. Mjue kabisa hilo, maana mtaanza Mama Watondoha, analalamikia panya, mbona hamkula, wale hawaliwi. Wale ni panya waharibifu na kwa kweli wamesababisha madhara makubwa, mahindi hayakupatikana kwa wingi katika eneo kubwa la Mkoa. Lakini ufuta upo, korosho tunatumaini zitakuwepo. Kwa hiyo, naiomba Serikali iwe na mipango ya uhakika, wakati ukifika, kama kweli tutakuwa na upungufu mkubwa chakula, kiwepo na kuhakikishe kwamba, tunahitaji chakula na chakula kinapatikana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, eneo la tano, ni suala la kuondoa umaskini. Mikakati ya MKUKUTA na MKURABITA, inawapa matumaini Wananchi wengi sana. Mimi nilikuwa na ushauri ufuatao katika suala hili: Tungeandaa vijarida kwa lugha nzuri, nyepesi, ili vifike mpaka Vijijini, Wananchi wafahamu Mkakati wa MKUKUTA, yule aliye Milola, yule aliye Nanjilinji, yule aliye Nangaru, yule aliye Kilolambwani, unamsaidiaje. Maana katika mikakati hii kuna mambo mengi na kama Wizara ya Mipango ndiyo mratibu, basi waangalie wanaratibu vipi. Tukiwa na mikakati ambayo haiwafikii Wananchi moja kwa moja, ni tatizo. Afrika ya Kusini, wameendelea sana, lakini wameendelea kwa sababu nchi ile imefunguliwa, kuna barabara ambazo zinakupeleka katika kila kona ya nchi ile. Sisi tuna maeneo mazuri yanayozalisha lakini barabara hazifiki bado. Kwa mujibu wa takwimu hizi, tuna rural roads zote ni unpaved kwa mujibu wa takwimu hizi. Kilomita 20,000 na kilomita 27,500 zote ni unpaved. Tunapokuwa na unpaved road, ndiyo hizo tunapeleka fedha kila mwaka kutokana na road fund zitengenezwe, mvua ikija zinaoshwa, kwa hiyo, mnabaki pale pale alifu kwa kijiti, mnarudia mnasema barabara hazijatengenezwa mnapeleka hela tena. Kwa hiyo, hatupanui. Tuwe na mipango sasa ya kuhakikisha kwamba, barabara hizi zinatengenezwa ili ziweze kupitika wakati wote, maana wakulima hawa tutahimiza walime, kama hatuwezi kuwafikia tukatoa mazao yao, hatuwezi kufanikiwa. (Makofi)

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

57

Juzi nilikuwa katika Kijiji cha Kiwawa, lori lilikwenda kule likashindwa kuchukua ufuta ingawa uko mwingi, lakini wameshindwa kununua. Lori la tani saba lilibeba ufuta wa tani moja tu kwa sababu barabara mbaya. Wale Wananchi wamelima sasa wapeleke wapi mazao yao, hawana haki ya kuuziwa mazao yao, lakini barabara ile ingetengenezwa tungekuwa na uhakika kwamba, Wananchi wale mazao yao yanauzwa na maendeleo yanawafikia wananchi vijijini. Sasa tuhakikishe kwamba, tuna mipango mizuri ambayo inawafikia. Lingine katika MKUKUTA huu ni suala la uanzishwaji wa Ushirika mdogo mdogo Vijijini. Upo utaratibu ulioanzishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais unaoitwa Village Community Banks (VICOBA), sisi Mkoa wa Lindi tumeshafanya mafunzo ya vikundi mara mbili, nataka kuwaambia wanawake wa Lindi, VIKOBA vinakuja tena, tumepata fedha. Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi) MHE. DR. CHRISANT M. MZINDAKAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii, ili niweze kuchangia kuhusu hoja ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji. Awali kabisa, ningependa kusema kwamba, naunga mkono hoja hii. Vile vile ningependa kutumia nafasi hii, kumpongeza Mheshimiwa Waziri na wataalam wake, kwa kazi nzuri ambayo wameifanya katika kipindi hiki kigumu cha kujenga uchumi wa nchi na Taasisi zake, kwa kweli zimeonesha mfano mzuri. PSRC wamefanya kazi nzuri, TIC wamefanya kazi nzuri, wote hawa tunawapongeza. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka kusema mambo ya msingi matatu. La kwanza, bado naendelea kusema, kilimo japo tumekipa heshima ya kukiita ni uti wa mgongo, lakini nchi hii bado inalishwa na wakulima wadogo sana, lugha ya ovyo tuseme peasants, wala hatujafikia kiwango cha small holders. Mkulima mdogo wa kisasa, hatujafika hapo. Wakati wa Siasa ni Kilimo ya Iringa, tulikubaliana na kuweka lengo la kufikia angalau kwa wastani wa gunia 15 za mazao kama mahindi kwa eka mpaka sasa hatujafika kiwango hicho cha mavuno kwa mkulima. Kwa sababu gani? Mkulima yuko peke yake, hata mabwana shamba wa Vijijini hawako na wakulima wako peke yao. Extension service katika nchi hii hakuna. Kwa hiyo, kilimo hakiwezi kusonga mbele na mfano upo kwa sababu kwa takwimu zilizotolewa na Waziri mwenyewe kwenye kitabu cha The Economy Survey mwaka 2004, mazao yote humu yameshuka hakuna zao ambalo limeongezeka, ukiona pamba takwimu zinaonesha pamba haikuongezeka. Lakini uzuri wameonesha takwimu hizi zinasaidia tangu mwaka 1977/78 mpaka mwaka 2004. Sasa ukiona kwa mfano, angalia uzalishaji wa sukari ndiyo umeongezeka lakini mazao mengine kama korosho, pamba, kahawa, yote yameshuka kwa sababu wakulima wanafanya wenyewe na pembejeo hazipatikani kwa wakati unaotakiwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nasema haya kwa sababu najua tunakaribia tarehe 30 ndiyo tunafanya uchaguzi, namtakia Mheshimiwa Waziri, kila la kheri, akafanye vizuri kwenye jimbo lake. Lakini maneno haya ninayosema, nayasemea kwa Serikali ya Awamu ya Nne kwa sababu ndiyo itaendeleza Bajeti hii. Nina hakika Serikali

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

58

itakayokuwa madarakani ni ya CCM kwa hiyo, haya tunayosema Wabunge naomba Mungu akitujalia wale watakaochaguliwa na kuingia kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, wazingatie haya tunayosema. (Makofi) Rais wetu ni mwaminifu sana, amesema mwenyewe kwamba, katika sekta ambayo hajaridhika sana ni kilimo na ni kweli kilimo hatujafanya vizuri kwa miaka kumi iliyopita. Hata marafiki zangu wengine Mawaziri, waliopewa kazi hii sitaki kumtaja mtu, Waziri mmoja alipochaguliwa nilikunywa champaigne lakini matokeo yamekuwa tofauti, hamna kitu. Sasa ni tatizo kubwa. Kama Mkoa wa Rukwa, ndiyo unatoa ziada lakini wakubwa wa Wizara hawajapata kufika wala hawajui tunachofanya, ni tatizo. Tumekubaliana wakulima wapewe ruzuku ya mbolea, takwimu zinazosomwa humu Bungeni na zilizo kijijini kule mikoani tofauti ni kubwa mno. Mkoa wa Rukwa kwa mwaka mzima wa 2004, mahitaji yetu ya mbolea yalikuwa tani 36,000, tulipata tani 800 tu, sasa hebu linganisha hesabu hiyo ni utani. Lakini Rais anasema hakuna kitu ambacho amekuwa akikilalamikia kama kilimo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Rais wetu alipokuja mara ya pili alizungumzia habari ya processing industry. Leo niliona nije na sample, viwanda vya Tanzania vinavyotengeneza bidhaa za matunda hakuna, wanaagiza unga kutoka nje ya nchi, wanakuja kuchanganya ile poda kupata juice. Lakini nchi kama Uarabuni, ambayo hakuna miti ya matunda, wanatuletea tuna-import juice ya matunda halisi kutoka Uarabuni. Ukiingia Dar es Salaam ukienda mpaka Morogoro machungwa yanaoza, lakini viwanda vinavyotengeneza juice Tanzania vinaingizwa chemicals za kuchanganya na maji ili kupata juice! Sasa hii ni fedheha, ni aibu ya waziwazi. Wakulima wa matunda Lushoto, wamebakia wale wale na kiwango ni kile kile na matunda yanatoka South Africa. Kwa hiyo, nilitaka niseme mambo haya bado si mazuri. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nitatoa mfano mzuri, ukichukua Kenya na Uganda kwa pamoja, Tanzania ndiyo nchi yenye makundi mengi ya nyuki na mwaka 2003 nchi ilipata shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya nyuki, mwaka huu tumeshuka tumepata shilingi 0.15 bilioni. Kwa hiyo, ungefuga nyuki tu Tanzania, ungepata fedha za kutosha kuendesha nchi hii. Lakini haya mambo tunayaweka pembeni kama hayana maana. Mheshimiwa Spika, tulishasema vile vile viwanda vinavyojengwa, lazima Serikali ielekeze aina gani ya viwanda. Leo Tanzania bado tunalima kwa jembe la mkono na Tanzania ndiyo nchi ambayo siasa ni kilimo, lakini haina viwanda vya kutengeneza zana za kilimo. Plough tunaagiza nje, hata jembe la mkono tunaagiza nje. Tulipopata Uhuru, Wazungu walisema, ninyi hamtengenezi hata sindano mtapata Uhuru. Rais wa kwanza akasema tupeni Uhuru tutatengeneza. Sasa nasema majembe ya mkono haya tunaagiza kutoka nje, tunawezaje kuendeleza kilimo wakati viwanda vinavyojengwa hatuweki umuhimu wa kutengeneza zana za mkulima? Kwa hiyo, hilo nalo nimeona niliseme. (Makofi) Mheshimiwa Spika, halafu jambo lingine ambalo ningependa kulisema hapa ni kuwa, Serikali iwe na msimamo wa uhakika kwa sababu inatuchanganya. Waziri alipokuwa akizungumza pale alisema kwamba, Mashirika muhimu kama TRC, yanaweza

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

59

kukodishwa, lakini siyo kubinafsishwa. Lakini hotuba hii ambayo nimeisoma na imegawiwa na itawekwa kwenye kumbukumbu, yale aliyosoma kwenye notes zake yanasema, TRC haitabinafsishwa, lakini hiki kitabu ambacho Watanzania wengi na wengine wataweka kumbukumbu kimesema, TRC itabinafsishwa. Sasa nilitaka tupate maelezo kwa sababu sisi washauri wa Serikali bado tunang’ang’ania kusema TRC isibinafsishwe, ikodishwe management. Tunasema vile vile Tanzania Harbours Authority isibinafsishwe, ikodishwe. Ile bandari inatosha kuendesha nchi, ile ni dhahabu ya Tanzania. (Makofi) Kuna nchi ambazo tunazijua wanaishi kwa kuendesha Serikali zao kwa kutumia Bandari tu na sisi tungeweza kufanya hivyo hivyo. Mimi nataka niipongeze Serikali kwamba mpaka sasa ujenzi na infrastructure ya Bandari inaridhisha. Tukifanya zaidi ya pale tunaweza vizuri zaidi. Kwa hiyo, naomba hiyo tusiibinafsishe, badala yake tukodishe, maana ni mali zetu hizi! (Makofi) Mheshimiwa Spika, nataka niipongeze Serikali kwamba uchumi ni mzuri na kusamehewa kwa madeni yetu nchi itaweza ikaokoa Shilingi Dola milioni tano kwa

mwezi. Naomba anisahihishe maana sitaki kuweka kumbukumbu vibaya, yeye anajua zaidi. Mimi nafikiri kwa hesabu nilizofanya mimi inawezekana tukawa

tunapata Dola milioni tano kwa mwezi ambazo tulikuwa tunalipa madeni. Mimi naishauri Serikali fedha hizi zisaidie sana kujenga miundombinu na miundombinu

ya kwanza iwe ni barabara. Kwa sababu maendeleo ya Tanzania ni barabara tu hakuna kitu kingine. Usafirishaji wa mazao ya mkulima yatategemea barabara. Leo

Rukwa tuna zaidi ya tani 31,000 za mahindi hayajatoka pale kwa sababu ya gharama ya kuyaondoa mahindi pale. (Makofi)

Pili, elimu na afya vipewe kipaumbele. Haya ndiyo ningeshauri Serikali iyatazame. Lakini vile vile naiomba Serikali yetu kama nilivyosema matumaini CCM kuongoza tena, ninaomba mishahara ya wafanyakazi wa Serikali itazamwe tena upya. Watanzania tuna vijana wetu wengi wamesoma. Wakitoka hapa wakienda kwingine wanalipwa mishahara mizuri zaidi na wanaanza kuondoka kwa sababu mishahara sio mizuri. Naamini kwamba kwa mapato ya Tanzania leo, uwezekano wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi upo. (Makofi) Kuna kasoro ambayo naisema wazi wazi na Waziri atakubaliana na mimi, gharama ya kuendesha Serikali Tanzania ni kubwa sana. Tunaweza tukapunguza gharama za kuendesha Serikali. Mifano ni mingi. Leo magari yaliyouzwa Serikalini hayajapata kutokea katika awamu zote. Serikali hii ina magari mengi mno. Hata watu ambao wasingeweza kuwa na gari wamepewa magari na hayafanyi kazi yanazurura tu. (Makofi) Wale Makatibu Kata, Watendaji wa Kata, hawana pikipiki lakini magari yote yamelundikwa Dar es Salaam kwa Watawala. Hii sio sawa. Yanaongeza gharama bure, tena magari yenyewe ni VX magari makubwa makubwa. Hakuna mtu anayeendesha Suzuki. Yaani Serikali yetu imeshakuwa tajiri kiasi cha kuwa na magari ya gharama mno

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

60

kuyaendesha. Mimi nasema sio sawa. Lazima jambo hili turudie, tutazame upya. Gharama ni kubwa sana ya kuiendesha Serikali. (Makofi) Vile vile Mheshimiwa Rais alipoingia niliona amenuna, lakini maskini ya Mungu baadaye ameona atafanyaje. Nitatoa mfano. Ukiingia katika nyumba ukakuta inahitaji matengenezo usiihamie, itengeneze kwanza ndiyo uingie, kwa sababu ukiingia utaizoea, utaona kama vile ilivyo ni sawa. Leo Mikutano inayofanyika Tanzania inatisha. Watu hawafanyi kazi, kila siku Semina Arusha, Semina Morogoro, Mikutano! Maofisa wote wameachia Makarani kuendesha Ofisi kwa sababu wakubwa wote kila siku wako kwenye Semina. Kinachobadilika ni mahala pa kwenda kufanyia. Zote hizi ni fedha. Rais alinunia, alifoka, lakini wanaomsaidia wakaona ni sawa tu. Mimi nataka niseme kwamba nikijaliwa kurudi Bungeni nitafanya study juu ya Semina, zinaigharimu Serikali Shilingi ngapi na Mikutano yote hii. Kwa sababu hatuwezi kuendelea na mambo haya. Hata fedha zinazokuja kusaidia watu wa UKIMWI nyingi zinatumika kwa Semina kuliko kushughulikia wagonjwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Ninaunga mkono hoja hii, lakini narudia tena kutia mkazo kwamba uchumi wa nchi yetu ni kilimo na kilimo hatujafanya vizuri bado. (Makofi) Naunga mkono hoja hii. Ahsante sana. (Makofi) MHE. THOMAS NGAWAIYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia Sekta hii ya Mipango. Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nichukue nafasi hii kumsifu Waziri Kigoda kwa kazi yake na Mipango anayoifanya. Lakini zaidi ni katika mipango ambayo mimi mwenyewe nimeona ninafanikiwa binafsi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Sekta ya Mipango ni muhimu sana, ni sawa sawa na damu kwenye mwili. Sawa sawa na mishipa ya damu kwenye mwili. Kama huna mipango mizuri huwezi kuendesha nchi na mipango huanzia nyumbani kwenye familia. Kwa hiyo, unaanza kwenye familia unakuja kwenye Kijiji, Mkoa, unakuja Taifani. Bila kupanga huwezi kufanya chochote. Bila kupanga namna ya kutengeneza barabara huwezi kutengeneza hiyo barabara. Bila kupanga namna ya kujenga nyumba, huwezi kujenga hiyo nyumba. Kwa hiyo, bila kupanga vile vile namna ya maendeleo ya Taifa hili huwezi kufanya maendeleo. Kwa hiyo, sekta hii ni sekta muhimu sana ambayo kwa kweli katika nchi hii kama ikifa Sekta ya Mipango maana yake na nchi itakuwa imekufa. Kwa hiyo, ni Sekta ambayo kwa kweli nimeona ni muhimu niisemee kidogo. Mheshimiwa Spika, mimi kama binadamu wa kawaida, Mbunge nawakilisha Jimbo la Moshi Vijijini na mimi nilikuja na mipango yangu. Mipango ya kwanza

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

61

nilipanga kuomba Wizara kuhusu mipango yake ya kubinafsisha shamba la TPC ambako kulikuwa na Shilingi milioni 186 ambazo zilipunjwa Halmashauri ya Wilaya Moshi Vijijini, lakini kwa ushirikiano na Waziri aliliona hilo na akakiri na zile fedha milioni 186 zikalipwa Moshi Vijijini. Nashukuru sana. (Makofi) Hiyo ni Mipango. Lakini vile vile nilipanga kuikumbusha Serikali kwamba kuna mipango yake ya lami iliyoko Kibosho ambayo imekaa muda mrefu, inahitaji kutumika na Serikali ilikubaliana na mimi. Hii leo nina barua mfukoni inayosema kwamba Waziri wa Ujenzi atatengeneza barabara Kilometa saba ili ile lami itumike. Naipongeza Serikali kwa hilo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, sambamba na yote hayo katika kuwakilisha Jimbo langu na katika mipango yenyewe, vile vile nilipanga kudai hela za KNCU ambazo walipunjwa mwaka 1988 Shilingi milioni 560 na Serikali imeamua kulipa hizo fedha milioni 560. Kwa kweli mimi nimeamini sasa kwamba kama unajenga hoja vizuri ndani ya Bunge, utafanikiwa. (Makofi) Mimi nafikiri matatizo ya watu wengine ni kwamba hawajengi hoja vizuri. Lakini mimi nimejenga hoja nzito nzito namna hiyo na yote nimefanikiwa. Sasa hivi Moshi Vijijini asilimia 80 kuna umeme. Hebu fikiria, kuna umeme asilimia 80 hiyo ni mipango, lakini ni katika hoja ninazojenga hapa. (Kicheko) Tumepanga kuweka maji Moshi Vijijini, tayari Serikali imepanga na kusaini Shilingi milioni 92 kwa ajili ya kuweka maji Kilimanjaro yote pamoja na Moshi Vijijini. Kwa hiyo, mimi nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali kwa hayo. (Makofi) Nitakuwa sina fadhila wakati leo ni hotuba yangu ya mwisho kama sitaipongeza Serikali kwa yale niliyokuwa nimeiomba Serikali na kunitekelezea. Kwa niaba ya wananchi, mimi nakuja siyo kama Chama, nakuja kama mwakilishi wa wananchi wale. Ukishachaguliwa unakuwa ni Mbunge wa kuwakilisha wananchi. Sasa wale wananchi walichonituma, nimefanikiwa na leo nimeamua kulisema hapa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, moja ambalo nilitaka niendelee kusema ni kuhusu mipango yetu ya kitaifa. Mimi kama nilivyo katika kilimo nimeingia hapa, nimekuwa katika Kamati ya Kilimo na Msemaji Mkuu wa Kilimo mpaka sasa hivi. Hilo nimelisemea. Nataka niseme tofauti na Wabunge wenzangu kuhusu Wizara ya Kilimo. Naipongeza Wizara ya Kilimo, ilichofanya isingeweza kufanya zaidi. Mabadiliko haya kwa miaka 40 hayakubadilika, lakini sasa hivi tungekuwa tunaomba chakula cha njaa. Leo hii taarifa ambayo ninayo kama Mwanakamati ni kwamba, kuna hundred plus three ya chakula nchini mwaka huu. (Makofi) Kwa hiyo, ina maana kwamba kwa miaka mingi tumekuwa tukiomba chakula cha njaa. Ina maana mwaka huu kwa bidii ya Wizara imebadilika. Tumekuwa hatuwezi kuomba chakula cha njaa na tuna nyongeza ya kuuza nje ya nchi. Sasa hilo tunaipongeza Wizara. Hatuwezi kusema kwamba Wizara imefanikiwa hundred percent, hilo sijasema.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

62

Au sijasema 50 percent lakini angalau tumeona yale yaliyokuwa yanatusibu ya njaa hakuna. Sasa leo kwa nini tumlaumu Waziri? Hatuwezi kumlaumu Waziri wala Wizara. Wizara imefanya kazi yake, tunasema waongeze bidii. (Makofi) Mheshimiwa Spika, hii ni kwa Waziri wa Mipango, naomba anisikilize vizuri. Kama hatuwezi kupanga namna ya kusaidia sekta binafsi ili waweze kufanya kazi hizo za kilimo, hatuwezi kwenda. Tutasema MKUKUTA, MKURUBITA sijui TASAF lakini hatuwezi kwenda kama hatupangi namna hiyo. Tumekwishakubaliana kwamba Serikali haifanyi biashara. Sasa akina Ngawaiya kama watu binafsi ndiyo watakaofanya biashara. Lakini unawa-empower namna gani hawa watu binafsi? Mheshimiwa Spika, nchi nyingine zina mipango yake na katika mipango yake wanatupangia na sisi Watanzania na naomba Waziri akubaliane na hili kwa sababu utakuta sasa hivi tuna mpango wa kuondoa umaskini, mpango wa kuondoa umaskini ifikapo mwaka 2025. Lakini nilivyoangalia Mkataba wa Cotonou Agreement uliofanyika Benin nilikuta ni maelekezo ya huo Mkutano uliofanyika Benin wa Cotonou Agrement siyo mipango yetu Watanzania. Lakini na sisi tunasema ndiyo mipango yetu Watanzania. Sasa nasema ya kwetu sisi iko vipi? Au tunachukua shinikizo hilo la watu wa nje? Tunasema tutaondoa umaskini ifikapo mwaka 2025, lakini nimesoma Mkataba wa Mkutano unaoitwa Cotonou Agrement umefanyika Benin, unaelezea wazi wazi namna unavyotaka tuondoe umaskini ifikapo mwaka 2025. Sasa hiyo ni mipango yetu au ni mipango ya Millennium goal ya hiyo Cotonou Agreement uliofanyika Benin?

Mheshimiwa Spika, nilitaka sisi tuwe na mipango yetu. Wale wanatupangia

mipango, vile vile wanasema wafanya biashara nendeni mkawekeze Tanzania, wafanya biashara wanakuja kutoka Amerika, kutoka Uingereza, kutoka Afrika Kusini wanakuja kuwekeza Tanzania. Lakini nataka niseme tu katika uchunguzi wangu, wale wafanyabiashara hawana hela zao. Wao wana write up tu wanaiambia Serikali yao, Serikali yao inawaambia okay nyinyi ni wataalam tutawakopesha hizi hela mtalipa interest ya only three percent or two percent. Nendeni mkachukue hayo mashamba huko Tanzania na wanakuja kwa ajili hiyo, wakiwa wanapewa hela na Serikali zao.

Hiyo ndiyo mipango ya Serikali zao, nenda kachukue kiwanda Tanzania,

kachukue kiwanda cha Bia, chukua fedha hizi. Ni Serikali yao inawapa. Ni mipango ya Serikali yao. Nenda kalime shamba fulani, nenda kule Tchibo kule Kibosho kuna Tchibo Estate shamba kubwa kabisa. Lilikuwa limelala kwa miaka yote 40 ilikuwa hakuna kitu walikuwa wanaishi paka tu na wanyama wa porini mle. Lakini lile shamba sasa hivi ni zuri sana.

Mheshimiwa Spika, lakini ninachotaka kusema hapa, wafanyakazi wa kule

shambani ni Watanzania. Ni nini kilichoongezeka hapo? Ni nini kilichotunyima sisi mipango yetu kama Watanzania kutoweka vizuri lile shamba mpaka leo tungoje mtu anaitwa Mzungu aje tu kusimamia pale? (Makofi)

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

63

Shamba liwe zuri, lakini wanaolima kule wanaopanda mbegu za kahawa ni Watanzania, ni za hapo Lyamungo. Mbegu zenyewe za kahawa ni zetu. Maji ni ya kwetu sisi wenyewe. Ni kwa nini tunangoja watupangie wao halafu waje watusimamie kwenye kazi hizo? Mimi ningeshauri tujipangie na sisi. Tupange ya kwetu kama Watanzania tuwe na mipango yetu na kuisimamia na hiyo mipango kama hatuwezi kuwa na mipango ya namna ya kupata fedha ni ngumu kwa sababu Wizara inafanya kazi ya kupanga. Mipango ni mingi na ukiiangalia ile mipango ukisoma kwenye vitabu hivi kwenye madroo yetu yamejaa hapa ni mizuri. Lakini nani akafanye bila fedha? Utaenda pale, mimi Ngawaiya nataka kulima ekari 100 yaani utasema kwa mdomo lima ikalimika bila pesa. Hawezi kufanya bila pesa! Nchi hii inafanyaje mipango yake ya kuhakikisha kwamba mipango tunayopanga inaendana na fedha tuliyokuwa nayo angalau kidogo kidogo! Niliwahi kusema kwamba ukinipa Morogoro peke yake Shilingi bilioni 20 ambazo tunaokota hapa zaidi ya bilioni 140 kwa miaka mitatu, Morogoro peke yake inaweza kulisha Tanzania mwaka mzima na Mashishanga Mkuu wa Mkoa pale alikubaliana na mimi wakati akitoa hotuba Kamati ya Kilimo tulipokwenda pale. Lakini kwa nini haifanyiki? Ni kwa sababu hatuna mipango ya kuwezesha Sekta binafsi. Tuwe na mipango ya kuwezesha Sekta binafsi. Tuache mambo ya kizamani, tusioneane wivu. Kama Ngawaiya anaweza kulima unashindwa nini kumpa hata Shilingi bilioni mbili, tatu akalime na ukamsimamia kwa mipango yako? Wananchi watakula! Unasema sasa Ngawaiya bwana chukua Shilingi bilioni tatu! Kama atafanya kwa maelekezo; why? Mheshimiwa Spika, nchi nyingine wenye mabenki yale yanayokopesha, kunakuwa na wataalam wa kilimo na wale wataalam wanamwangalia huyu anayekuja kukopa yukoje. Ana uwezo? Anayo plan sawasawa? Wanafuatilia mwanzo mpaka mwisho na mpaka wakati wa kuvuna na wanahakikisha mazao yake yameuzwa na hela zinapatikana na utajiri unakua katika nchi. Kwa hiyo, mimi nimesimama hapa kwanza niishukuru Serikali hii kwa bidii wanayoifanya. Kwa kweli siwezi kuacha kushukuru. Siyo suala la kuingia CCM. Mimi nimekuja hapa Bungeni kama Mbunge na sio kama jambo lingine lolote. Kwani CCM siyo Chama? Vyote ni Vyama lakini ukishakuja hapa hushughulika na Chama unashughulika namna ya kuwatetea wale waliokutuma kule kwako. (Makofi) Kwa hiyo, yale mliyonitendea ndugu zangu Viongozi wa Serikali hii, nashukuru sana na naomba Waziri wa Kilimo aendelee kwani anaendelea vizuri. Mwaka huu tumeanza kidogo kidogo hatutaomba tena chakula. Lakini tufanye speed zaidi tutegemee mipango yako Mheshimiwa Waziri upange vizuri ili tuweze kuendelea vizuri. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. (Makofi)

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

64

MHE. PHILIP A. MAGANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii na mimi nichangie kidogo hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji. Awali ya yote, nichukue nafasi hii kumpongeza tena Waziri, Ndugu Abdallah Kigoda kwa hotuba nzuri, fupi lakini ambayo imegusa maeneo yote. Nichukue nafasi hii kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dr. Enos Bukuku ambaye kwa ujasiri wake na utaalam wake uki-combine na ule utaalam wa Dr. Kigoda bila shaka ndiyo umezaa hotuba hii ambayo iko mbele yetu. Nawapongeza sana. (Makofi) Nina maeneo matatu nitakayochangia. La kwanza kabisa, nichukue nafasi hii kuipongeza Wizara kwa maamuzi ambayo imeyafanya ya kufungua Ofisi za Kanda za TIC. Nadhani hii ni busara sana kwa sababu sasa wale ambao walikuwa wawekezaji potential huko Vijijini mahali ambako barabara zenyewe siyo nzuri sana. Walikuwa wanapata taabu sana ya kusafiri kuja Dar es Salaam kufuata huduma ya TIC. Kwa utaratibu huu ambao umewekwa sasa na ambao ni matumaini yangu kwamba utaenea katika Kandai zilizobaki, ni utaratibun mzuri ambao unahakikisha kwamba Ofisi hii sasa ipo karibu na walengwa. Naomba Waziri atakayekuja katika sekta hii aendeleze mazuri haya ambayo yameanzishwa na viongozi niliowataja. Ya pili nitaongelea kwa ufupi tu, juu ya mashirika ya huduma na miundombinu, public utilities. Kama Waziri alivyozungumzia katika paragraph ya 15 kwamba ubinafsishaji wa Mashirika haya hautakwenda kama ilivyofanyika katika yale Mashirika ya biashara. Uamuzi huu ni mzuri kwa sababu Mashirika haya public unitilities mara nyingi hutarajii kwamba ni Mashirika ambayo yanafanya kazi yake kibiashara, kwa maana ya kujiendeleza yenyewe. Sehemu kubwa ya Mashirika haya ni kutoa huduma kwa sekta nyingine. Mimi nadhani fundisho tulilopata la ubinafsishaji wa DAWASA ni tosha kuifanya Serikali ifikiri upya jinsi gani waweze kuendesha kama wanataka kubinafsisha yale mashirika yaliyobaki. Iwe kwa kukodisha, unamkodisha mtu kwa mkataba maalum, kama akishindwa kuendeleza mkataba unamfukuza. Aidha, kama kuna uwezekano wa kurudia sehemu fulani fulani kibiashara, basi mimi nashauri kwamba ubinafsishaji huo ufanywe kwa mtindo wa Serikali yenyewe kuwa ndani pamoja na hiyo private sector kama wanavyoita wataalam PPP yaani Private Public Partinership. Nadhani utaratibu kama huu utawezesha kutoa ka-element ka ruzuku katika maeneo yale ambayo yanahitaji ruzuku kwa kutumia ule mtaji wa Serikali. Mheshimiwa Spika, katika area hii, kama alivyosema Ndugu Mzindakaya kuwa Bandari ni lulu ya Tanzania, lazima tuichunge sana kuhakikisha kwamba tunapata huduma za kutosheleza pale na kuvutia wawekezaji wengine na wafanyabiashara kutoka nchi jirani kutumia services za bandari yetu ya Dar es Salaam hasa. Lakini tunapotazama huduma za Bandari tusitazame huduma za Bandari peke yake, kuna huduma nyingine za muhimu pale ambazo zinaendana na shughuli za Bandari. Kwa mfano, reli na barabara.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

65

Napenda kuzungumzia barabara. Barabara yetu ni nzuri na inazidi kuboreka siku hata siku. Nampongeza Waziri mhusika kwa kazi nzuri anayoifanya katika sekta hii. Lakini naomba vile vile atazame upya utendaji wa shughuli za barabara hususan weigh bridges. Juzi nilipotoka hapa kwenda Dar es Salaam, nilikuta kasheshe pale Kibaha kwenye weigh bridge, kuna mlolongo mrefu wa magari yanangoja kupata huduma ya weigh bridge. Mtu yeyote kutoka nchi jirani ambaye anataka kusafirisha mazao yake kupitisha Bandari ya Dar es Salaam akiona vile atafikiri mara mbili. Ndiyo nakubali kwamba ni lazima tulinde barabara zetu. Lakini magari haya yote yanayokuja pale yameshapimwa kule Bandarini. Kwa nini yapimwe mara ya pili maili 25 tu kutoka Bandarini? Tulikuwa tunachukua mizigo mingine? Kwa nini usitafutwe uwezekano kwamba baada ya mizigo kupimwa pale Bandarini, gari husika liwekewe seal. Kwa hiyo, ikifika sehemu kama Kibaha, wale road inspectors wangalie tu kwamba ile iko au haiko, kama haiko apeleke kwenye weigh bridge, kama ipo unamwambia wewe pita. Nadhani hii ingesaidia sana kupunguza congestion ya traffic katika barabara yetu. Tatizo la tatu ninalotaka kuzungumzia ni juu ya Mtwara Development Corridor, kama ikihitimishwa kwa kweli itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa watu wa Kusini. Lakini niwaambie ndugu zangu wa Mikoa ya Kusini kwamba kuwepo corridor peke yake hakuhakikishi kuwa tutapata maendeleo. Ni lazima sisi wenyewe tuhakikishe kwamba tunaweka mipango iliyo wazi ya kutumia services ambazo zitatolewa na hiyo corridor. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tutakuwa na barabara pale, kutakuwa na reli, bandari nzuri, kutakuwa na umeme kutoka Mnazi Bay, lakini kama hatuna mipango ya kutumia services hizi sisi tutabaki kuwa watazamaji tu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kupitia hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, ninaomba kutoa rai kwa ndugu zangu ambao corridor inapitia wajipange vizuri. Kuna huduma nyingi ambazo zinaweza kufanywa na wao wenyewe bila kutegemea Serikali zile zifanye. Kwa mfano, sisi katika Wilaya ya Ruangwa sekta kubwa ambayo inatuwezesha kuishi ni ya kilimo. Kilimo chetu ni cha jembe la mkono. Lakini hata hivyo tumeweka mipango ambayo tunadhani itatusaidia kupanua kilimo hicho kwa kutumia nguvu kazi ya vijana. Tumeanzisha utaratibu wa mashamba katika kila Kijiji mashamba ya vijana. Mashamba hayo siyo ya Ushirika. Kila mtu ana shamba lake, lakini kila kijana anapewa shamba lililopimwa na anapata huduma ya Serikali kwa maana ya kupewa pembejeo na ushauri, ni jinsi gani afanye katika kilimo chake. Katika mpango kama huu, kama tukiupanua kwa Vijiji vyote katika Mikoa yote ya Mtwara na Lindi na Ruvuma utahakikisha kwamba vijana wetu wanakuwa engaged kwenye production process na vile vile huduma ambayo itapatikana na service za Mtwara development corridor tutazitumia kwa faida ya wananchi wa sehemu hizo.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

66

Mheshimiwa Spika, napenda kuzungumzia kidogo tu juu ya huduma kwa wachimbaji madini wadogo wadogo. Sisi katika Wilaya ya Ruangwa tuna machimbo ya wachimbaji wadogo. Mheshimiwa Kigoda amewahi kutembelea mashimo hayo, lakini tangu alitoka katika Wizara ile, wananchi wale ambao wanafanya hizo shughuli za migodi hiyo wanalalamika kwamba hawapati huduma kutoka Wizara husika. Walilalamika sana alipowatembelea juzi hawana services kama za Hospitali, Shule na kadhalika. Viongozi hawatembelei pale. Kwa hiyo, vijana hawa wanabaki hawana mtu wa kuwasaidia katika shughuli zao za uchimbaji na katika mahitaji yao mengine. Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ruangwa ina madini mengi na juzi nimeshangaa nimekuta ndugu zangu Wasukuma wamejaa pale tele katika Kijiji kimoja kumbe wamegundua reef gold. Sijui kama Serikali inayo habari hiyo! Kama hawana, naomba waje niwapeleke pale wakatazame ile deposit na utajua jinsi gani ya kuwasaidia wale wachimbaji wadogo bila kuwanyang’anya kwa kuwaleta wawekezaji wakubwa. Hivyo, naomba sana Serikali iwasaidie vijana hawa ili waendeleze uchumi wa Wilaya yetu. (Makofi) Kabla sijamaliza mchango wangu napenda kuchukua nafasi hii kwa sababu ndiyo nafasi yangu ya mwisho kuzungumza katika uhai wa Bunge hili, niwashukuru wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa support ambayo wamenipa wakati wote ambao nimekuwa Mbunge wao na kwa kweli kupitia kwao tumeweza kujenga Wilaya mpya ambayo ni ya kujivunia. (Makofi) Hata Mheshimiwa Rais amewahi kuitaja Wilaya ya Ruangwa katika hotuba zake si mara moja kwamba Wilaya ya Ruangwa imefanya vitu vyake bila kutegemea Serikali na ni mfano wa kuigwa. (Makofi) Lakini hiyo imewezekana tu kwa sababu ya ushirikiano tuliokuwa nao, yaani wananchi wenyewe na Mbunge pamoja na Madiwani ambao wanawahudumia wananchi wale. Napenda kusema kwamba nitakuwa mkosefu wa fadhila nisipowashukuru wananchi hawa wa Ruangwa kwa kunipa fursa hii ya kuchangia mchakato wa maendeleo ya Wilaya yetu. Ni matumaini yangu kwamba imani hiyo na wao watairudisha wakati muafaka ili tuendelee na kazi tuliyoianza kufanya katika Wilaya ya Ruangwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba nichukue nafasi hii kumpongeza tena Waziri na timu yake kwa hotuba nzuri. Naunga mkono hotuba hii mia kwa mia. Ahsante sana. (Makofi) MHE. RAYNALD A. MROPE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kutoa mchango wangu kwa hotuba safi sana iliyotolewa na Mheshimiwa Kigoda, ambayo inaelezea mambo gani Wizara yake itafanya na hasa tutegemee nini katika kipindi kijacho. Nawashukuru sana Waziri, Katibu Mkuu pamoja na Watumishi wa Wizara hii hasa kwa kuhusika kwao kwa namna moja au nyingine kukuza uchumi katika nchi yetu. Hili ni jambo kubwa walilolifanya. Haiwezekani tukawa

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

67

leo tunasherekea ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.7 na kadhalika bila kuona kwamba hapo tulipofikia tumewawezesha na hao wenzetu tuliokuwa tumewapa kazi hiyo. Kwa hiyo, tunawashukuru sana. Mheshimiwa Spika, katika mchango wangu, nilitaka kujikita zaidi katika maendeleo ya Mikoa ya Kusini hususani, Lindi na Mtwara katika Mtwara Development Corridor. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nataka kuishukuru sana Serikali kwamba imeanza kujitahidi sana katika kutengeneza miundombinu itakayotuwezesha nasi wa Kusini kuweza kupita mpaka kufika Dar es Salaam kupeleka bidhaa zetu na kadhalika kama wanavyofanya katika Mikoa mingine. Dalili hizi zinaonekana kiuwazi. Kama ukisafiri katika barabara hiyo na sasa inaleta matumaini makubwa, nami naishukuru sana Serikali kwa hatua hiyo. (Makofi) Mwenzangu aliyemaliza kuzungumza sasa hivi amezungumzia kidogo juu ya suala hili la Mtwara Corridor na mimi nataka kuongezea tu kwamba naiomba Wizara ya Mipango itusaidie sana watu wa Kusini katika kuhakikisha tunaibua mipango mizuri ambayo itatunufaisha kutokana na miundombinu tuliyoitengeneza. Mimi nasema haitoshi kuwaambia wananchi waibue mipango hiyo, lakini nasema Serikali iwawezeshe wananchi hao wa Kusini kuweza kuibua na hasa ionyeshe dhamira ya kitu gani kifanyike ili maendeleo yawepo katika Mikoa hii ya Kusini. Mimi nataka kutoa mfano, katika Mikoa hii kwa upande wa kilimo. Kuna mito mingi mikubwa, kuna Mto Rufiji, kuna Mto Ruvuma, kuna mito kama Matandu, Lukuledi, Mbwemkulu na kadhalika. Maeneo haya yote ni maeneo makubwa ambayo yanaweza kutumika kwa umwagiliaji, lakini Mheshimiwa Waziri usidhani mtu mmoja mmoja anaweza akachukua maji hayo ili yaweze kumnufaisha. Inatakiwa hasa mpango wa Taifa, yaani kuwe na Irrigation Master Plan ya kuhakikisha maji haya yanatumika vizuri, ndio hapo wakulima wadogo wadogo wataweza kunufaika. Lakini tusije tukajidangaya kwamba wao wenyewe waibue hizo fursa na wapate manufaa kutokana na maji yale. Kwa hiyo, naiomba Wizara hii ihakikishe kwamba wanatengeneza hizo Master Plan na pia mimi nilifarijika sana niliposikia kwamba Mikoa ya Kusini itakuwepo katika mpango ule wa SEZ yaani Special Economic Zone Plan.

Ningeomba tuingie moja kwa moja kwenye suala hili la kilimo na hasa suala la umwagiliaji, wenzetu wa kilimo, mipango iko wapi ya kuhakikisha kwamba maji haya yanatumika vizuri? Haya ndio niliyokuwa nategemea kutoka kwa wenzetu wakiongozwa na Wizara ya Mipango. Mipango itutafute wawekezaji mbalimbali watakaoibua fursa hizi maeneo yale. Kuna suala la kuibua fursa kuu ya utalii.

Hivi sasa tuna fukwe nyingi, ukitoka Kilwa mpaka Lindi, Mtwara, ni maeneo

yenye fukwe safi sana na fukwe mojawapo ya pale Mchinga, Mchinga watu wengine hawaielewi sawa sawa lakini fukwe ya Mchinga ni safi mno, lakini haitumiki sasa hivi.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

68

Iko wapi mipango ya kuwawezesha watalii wafike? Watalii wana mahitaji maalum, wanahitaji hoteli zilizo safi, wanahitaji chakula cha uhakika na ndio utaona wanakuja mara kwa mara. (Makofi)

Sasa ningeomba kwa upande wa Serikali watusaidie katika kuhakikisha kwamba

tunapata wawekezaji katika maeneo haya kwa ujenzi wa mahoteli. Sisi Mtwara Corridor tutahakikisha tunalima sana ili tuhakikishe kwamba watalii watakaokuja hapa watapata chakula bila wasiwasi. Lakini haya yote ni lazima kuwe na mpango maalum na mpango huo nafikiri wakati wake ndio huu katika hii Bajeti ili Mheshimiwa Waziri aweze kutusaidia kuweza kufanya mambo haya.

Kwa upande wa nishati, Mtwara Corridor ina bahati kubwa ya kuwa na gesi

nyingi hiyo ya Songo Songo na sasa Mnazi Bay. Unaweza kusema Kusini yote imebarikiwa kupata vyanzo vya umeme ambavyo vinaweza kutosheleza Tanzania na kuuza nje ya Tanzania. Sasa ningeomba katika kuendeleza hizo fursa, Wizara ya Mipango iwe na utaratibu wa kuhakikisha kwamba hatutumii gesi tu peke yake, lakini tutumie ile gesi kuanzisha viwanda, viwanda vya mbolea na kadhalika.

Suala la Kilwamko limeishia wapi? Maana katika mpango wa awali ilikuwa

kwamba gesi itengenezwe mbolea pale Kilwa na kuendelea. Tunaomba gesi hii pamoja na ya Mnazi Bay, tuwe na mipangoya kutengeneza mbolea pamoja na utengenezaji wa vyombo na vifaa mbalimbali vya plastic. Kwa kuwa gesi ile ina uwezo huo na kwamba hivi sasa tuichimbue ili tuwe na viwanda hivyo vidogo vidogo kwa ajili ya kutengeneza vyombo vya plastic.

Wizara ya Mipango, sijui kama mnatuelewa wakati mwingine tunaposema katika

upande wa Mtwara Corridor tuanzishe Secretariat ili iweze kuendeleza mipango mbalimbali katika Mtwara Corridor. Mimi sielewi kwa nini mpaka sasa hivi tunang’ang’ania kuiweka Mtwara Development Corridor upande wa NDC. Hakuna chochote inachotusaidia! Waziri anzisha Secretariat ya Mtwara Development Corridor. Ukianzisha hii ndio itakayowezesha kuangalia na kufanya studies mbalimbali za eneo hili na kuona nani atawekeza na wakati huo huo nini kitafanyika kwa maendeleo ya watu wa kusini. (Makofi)

Mimi naomba sana mfikirie suala hili la Secretariat na hata hivyo Mtwara

Development Corridor ipo tu katika Wizara ambayo kwa kweli sio yake, ingefaa hii Secretariat na mambo mengine yawe katika Wizara yako ya Mipango na Ubinafsishaji. Tunaamini ikiwepo hapo ndio itatekeleza majukumu yake. Hebu irudisheni Mtwara Development Corridor mahali pake ambapo ni Wizara yako na ujenge Secretariat ambayo Makao Makuu yake itakuwa Mtwara. (Makofi)

Mwisho, kwa kuwa nami ni hotuba yangu ya mwisho katika Bunge hili, kwanza

nataka kuwashukuru sana sana Wapigakura wangu wa Jimbo la Masasi kwa kunipa nafasi niingie Bungeni. Labda niwaelezeni tu wenzangu kwamba kwa kweli walinipa nafasi hiyo kwa kishindo kwa sababu mimi nilipata kura 54,000 na aliyenifuata ambaye

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

69

alikuwa ni wa CUF alipata kura 4,000. Sasa naomba mwaka huu kishindo hicho kiwe mara mbili zaidi, tuonyeshe kwamba lile ni eneo la CCM tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nikushuru sana kwa jinsi ulivyoliongoza Bunge hili

na kwa experience niliyopata hii ya miaka mitano. Mimi sina wasiwasi, nasema wewe unafaa, kuendelea, utuombee sisi turudi, tukirudi tutakurudisha na wewe. Hivyo hivyo nataka kuwaombea mafanikio mema wenzangu Wabunge wote. Wenzetu wengi wamekimbia huko kwenda Majimboni kufukuza ngedere, kwa hiyo, naamini tutarudi ili liwe Bunge safi zaidi la kuendeleza mafaniko makubwa haya ya awamu ya tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba sana kuunga mkono hoja.

Ahsante. (Makofi) MHE. STEPHEN M. KAZI: Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana kwa

kunipa nafasi na mimi nitoe maoni yangu kuhusiana na Wizara yetu ya Mipango. Kwanza kabisa ningeomba kupitia nafasi hii niwape pole Wana-Mwanza kutokana na mioto ya mfululizo miwili ambayo imejitokeza na imeleta maafa makubwa . Wa kwanza ulihusiana na nyumba ya mtumishi na Afisa wetu wa ardhi na hivi juzi kumejitokeza moto katika bweni la wasichana wa Shule ya St. Joseph Seminary. Matukio yote haya kwa kweli lazima nikiri kwamba hata mimi yamenigusa sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawapa pole Wana-Mwanza na niihimize Serikali,

baada ya kuzungumzia Wizara yetu ya Serikali za Mitaa na pia Wizara hii ya Mipango kuhusiana na utaratibu mzima wa kuboresha huduma kwa wananchi kwamba bajeti tuliyoipitia katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani, basi waharakishe kununua magari ya Zimamoto ili yapelekwe katika Vituo namna hiyo yaweze kusaidia jamii matukio yanapojitokeza. Niliweza tu kuhudhuria na kwenda kuwapa pole wale wa moto wa kwanza kwa Afisa wetu wa ardhi, lakini sasa kwa hili la juzi sijaweza kupata nafasi.

Mheshimiwa Spika, mimi nianze na kumshukuru sana Waziri wa Mipango, Ofisi

ya Rais kuhusiana na hotuba yake, hotuba ambayo kwa kweli mimi imeniridhisha na imenipa picha kwamba anajali na ana nia ya kuleta maendeleo kwenye nchi yetu. Wizara ya Mipango lazima tuelewe ndio jicho la uchumi, ndio jicho tunapaswa sasa lituelekeze pa kwenda itupatie utaratibu na liweze kutupa mwelekeo mzuri kwa kuweka malengo mazuri ili utekelezaji uweze kufuatwa. Shukrani hizi pia ningeomba zimfikie Katibu Mkuu wa Wizara kwa kushirikiana na Waziri kwa kuweza kutupatia hotuba hii Watendaji wote wa Wizara na wengine wahusika katika Wizara, kwa kweli hotuba hii mimi imenipatia mwanga mzuri na imeelezwa kwa kifupi ni yale tumekaa tukiyaandaa hapa katika kipindi kizima hiki cha mwaka baada ya kuangalia uzoefu wa mwaka jana 2004. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi labda ningependa nianze na kusema kwamba Wizara ya

Mipango pamoja na uwezo wote ambao inauweka katika kuweka mipango na malengo, Idara yake ya takwimu ndio moyo wa shughuli zake na ningeomba ielewe hii Idara ikomazwe iweze kuwa na vituo mpaka kwenye Mikoa labda waweke Kanda mbalimbali ambako takwimu zinakusanywa ambako Idara ya Takwimu ina Vituo ili kwamba

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

70

takwimu ziweze kuwa sahihi na zikiwa sahihi zitatusaidia sana kuweka malengo yetu sawa sawa.

Lakini pia lazima nishukuru kwa kweli kutokana na matokeo ya sensa ya mwaka 2002. Mimi hiyo inaniongoza kwa mambo mengi sana, hata kwenye Jimbo langu naitumia, inanipa picha na mchanganuo wa ndani kabisa kuhusiana na wingi wa watu, maeneo, jinsia na inakwenda mpaka ndani hata kuweka mategemeo ya watu ambao wanaelekea kwenda Shule. Ukifafanua kwa undani na kuisoma kwa undani hiyo report ya sensa inakupa picha nzuri sana. Kwa hiyo, ningeomba wakae wanaisahihisha wasiiache ikadumaa, wawe wanai-update ili tuweze kuitumia wakati wote na iweze kutusaidia katika mambo yetu ya pamoja.

Kitu kimoja ambacho kwa kweli naiomba Wizara, niseme wazi kwamba sasa tuko

katika hali hii ya kutafuta njia ya kuendelea. Tunapenda tuendelee, tunapenda tuwe na uwezo, tunapenda Watanzania wawe na uwezo wa kifedha, wajenge nyumba nzuri, tuweke mabarabara sawa sawa, tuwe na Hospitali za kututosha kabisa na za ngazi ambayo inastahili. Wazo hili ambalo Wizara imeanza kulitumia, la kwanza angalau kuangalia uzoefu wa wenzetu wengine ambao wanaendelea.

Kwa mfano ukichukua mifano ya Asia, nchi kama Uchina, Indonesia na wengine

wa aina hiyo kwa kweli sasa imeanza kunipa mwanga mzuri zaidi kwamba Wizara inatafuta mahali ambapo tukianzia hatuwezi tukakosea. Tumekuwa na Semina nyingi katika kipindi hiki cha Bunge hili na Semina hizi zimetusaidia sana kuona Wizara inaelekea wapi. Sasa ningeomba kwenye hili, niombe kwa dhati kabisa kwamba mwelekeo huu wa Wizara na msimamo wa Wizara wa kuangalia maeneo ambayo angalau tunafanana nayo maeneo ambayo wanaona kwamba tukijifunza kutoka kwao tunaweza angalau kunukuu kitu tusitoke kapa kama tukiweza kujilinganisha na watu walioendelea sana.

Mpango wa Min Tiger kwa mfano, taratibu za Economic Special Zones ambazo

tunaanza kuzianzisha sasa, pia tukiongeza mipango ya EPZ mimi ningeomba Wizara isimamie haya kwa karibu iyawekee malengo izidi kuweka uzoefu sasa kwa wananchi wetu. Mimi naona misingi itatusaidia kwa sababu tuna matatizo mengi tunaangalia sehemu mbalimbali na nia yetu ni kutaka kujua tufanye nini ili tuweze kuendelea.

Lakini kimoja ambacho ningeomba niisisitizie sana Wizara ni kuhusiana na suala

la utaalam na elimu. Hili ningeomba kwa kiwango kikubwa Wizara ijaribu sana kukubaliana na Wizara ya Elimu kuweka malengo makubwa na mazuri ili tuweze kupata watu wenye elimu za kutosha. Kama nia yetu ni kufanya shughuli za maendeleo za ngazi ya juu kama hizi, itakuwa sio rahisi kuendesha Vituo kwa mfano vya Economic Special Zones. Kama hatuna elimu, wataalam mbalimbali wa ngazi hizo tujaribu sisi wenyewe tuweze kufanya. Sio kukodisha watu wa nje.

Hii ndio moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakiturudisha nyuma. Mnaleta mtu

kutoka nje ndio anakuwa yeye ndio mwenye maamuzi makubwa, sasa huwezi ukajua ndani ya kichwa chake yeye hasa anataka tuendelee au anataka kutuweka mahali tuzidi kuhangaika na kupiga mark time.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

71

Lakini tukiwa na Wazalendo, wananchi wenye uwezo huo, wachumi wa ngazi

hiyo, ma-engineer wa ngazi hiyo, madaktari wa ngazi hizo, sayansi na teknolojia ambayo kwa kiwango cha kuridhisha kabisa kwamba tunafika tunasema hapa kweli inatosha. Haya mimi ningeomba Wizara iyachukue yawe ndio moja ya mzigo mkubwa wa kuyawekea utaratibu tuweze kufika hapo ili tuweze kufanya kazi zetu, mipango yetu na pia nia yetu.

Kwa kweli umaskini ni mbaya tu, hatuutaki na mimi siutaki umaskini, kabisa

siutaki na sifurahi kumwona mwenzangu maskini. Mimi ningependa kabisa kwa pamoja tutoke kwenye umaskini tuweze kujihesabu sasa tunaanza kwenda mbele na tuna kipato ambacho kinaweza kikatusaidia.

Mheshimiwa Spika, mimi ningeomba sasa hapa niiombe Wizara ijaribu kuona

kama itatusaidia watu wa Mwanza. Suala la utalii, nashukuru sana pamoja na juhudi ambazo zimefanyika, tumeweza kufanya mambo vizuri ya uvuvi, migodi, tunachimba dhahabu na sasa mipango mizuri inazidi kwenda mbele kufufua vizuri zao letu la pamba. Juhudi naziona ziko wazi.

Sasa kwa hali ilivyo Mwanza, sasa kuna potential kubwa ya utalii. Kwanza

ukiangalia Mwanza, ukilinganisha na mbuga za wanyama, kutoka Arusha kuja Ngorongoro ni Kilometa karibu 500 ni mbali sana. Unaanza Arusha asubuhi utafika kwenye mbuga mchana au jioni ukienda polepole, nashukuru sasa wamepata barabara itawaidia. Lakini Mwanza kuingia Serengeti ni muda wa saa moja na nusu karibu mawili tu. Mwanza vivutio kama vya ziwa na Visiwa vipo pale,sasa nilikuwa naomba Wizara kwa uwezo wake na utaratibu wake mzima pamoja na mipango Central Corridor tuone kwamba tutasisimua namna gani utalii katika eneo lile la ukanda wa ziwa.

Mheshimiwa Spika, kikubwa ambacho moja ya vitu ambavyo ni pingamizi ni utaratibu na hali ya mahoteli katika eneo hilo, bado inahitaji kuwekewa utaratibu mzima kuboresha zaidi usafiri na pia Kiwanja cha Ndege cha Mwanza. Wizara iweke katika mipango yake ielekeze hili sasa ili sisi Mwanza tuanze na kufaidika na hili kwa sababu tunayo hiyo natural resource iko pale na tunaweza tukaitumia tu kama tutaanza kuiangalia kibiashara, kimaendeleo.

Mheshimiwa Spika, kama uchumi wa nchi unavyoeleza na mipango ya nchi

inavyoeleza tutakuwa na nafasi kubwa ya kuwaendeleza Wana-Mwanza na kuwaondoa katika umaskini kutumia hii potential ya utalii. Nafasi ni kubwa na uwezekano ni mkubwa mradi tu mipango iwekwe sawa sawa na ianze kujitokeza katika eneo letu na sisi tuanze kuitumia.

Mheshimiwa Spika, mwisho ningeomba na mimi nichukue nafasi hii kutoa

shukrani zangu za dhati kwa Wapigakura wa Mwanza. Lazima niwashukuru sana. Nakumbuka nilivyoanza na ndio dalili inavyojionyesha leo nasikia kwenye gazeti

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

72

wameandika kwamba tuko kumi na moja, sasa sijui kama wanakuja kwa ajili yangu au wanakuja kwa wenyewe wale wanaoingilia eneo hilo!

Lakini kikubwa ni kwamba kwa kweli Wapigakura wa Mwanza wamenisaidia

sana, wamenipa mapenzi makubwa na shughuli nyingi, tumefanya nao kazi kwa karibu. Mimi nina imani na nimekwishawaambia kwamba nitarudi tena kugombea, wamenipa ridhaa.

Kwa hiyo, uhakika wa kwenda huko ninao. Sasa wameshanikubalia niende

nikafanye haya mambo nina imani wataniunga mkono, hayo mambo ya magazeti yasitutie wasiwasi sana. Watanisaidia na tutafanya nao kazi ya karibu, kwa sababu wana macho wanaona tumefanya nini na wana masikio, wana uwezo wa kujieleza, inaeleweka vizuri kabisa. Hii inanipa imani kubwa na ninakuwa na mategemeo makubwa kwamba mambo yangu nitakwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia naomba nikushukuru sana wewe mwenyewe, umenisaidia

sana katika Bunge hili, umenipa nafasi ya kuuliza maswali, umeongeza Bunge vizuri, unanipa nafasi za kuchangia kama hizi, kwa kweli nakutakia kheri sana. Kama alivyosema Mheshimiwa Mrope, kwamba tukirudi, wewe tutakurudisha utakuwa pamoja na sisi bila wasiwasi.

Naibu Spika, lazima nimshukuru sana, amefanya kazi kubwa, Katibu wake na

Watumishi wote wa Bunge. Kwa kweli wametusaidia sana katika kuendesha shughuli zetu za Bunge na nina imani kwamba Mungu atatusaidia, tutakuwa pamoja nao. (Makofi)

Mwisho kabisa na kwa dhati kabisa ni Wabunge wenzangu. Lazima na mimi

niwatakie kheri sana wote kwa kweli. Kama ingekuwa ni kuamua tu, mimi ningeamua Wabunge wote warudi kwa sababu wameleta mchango mkubwa sana katika Bunge la kipindi hiki.

Hata wewe mwenyewe unakiri, hata Serikali inakiri kwamba Wabunge

wameisaidia sana katika kufanya kazi zake na mabadiliko haya yanayojitokeza ni msimamo wa Wabunge na namna walivyochangia katika shughuli zao mbalimbali na walivyoleta hoja zao kutoka kwenye Majimbo, wameleta hoja za kweli, hawakuleta maneno ya kutaka kuleta vurugu katika Serikali. Wameleta kabisa waliyoyaona kule na yanapoangaliwa yanakutwa kweli kwamba yanahitaji kufanyiwa kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hilo, nashukuru sana. Naunga mkono hoja.

Ahsanteni sana. (Makofi)

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

73

SPIKA: Mpaka hapo Waheshimiwa Wabunge tunafikia mwisho wa kipindi cha

asubuhi. Katika wale ambao walikuwa hawajachangia zaidi ya mara mbili huko tulikotoka wamebaki wawili. Watapata nafasi kipindi cha mchana, Mheshimiwa Kitine na Mheshimiwa Kimiti.

Baada ya maelezo hayo, sasa nasitisha shughuli za Bunge hadi saa kumi na moja

jioni.

(Saa 6.54 mchana Bunge lilifungwa mpaka saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia) MHE. DR. HASSY H. B. KITINE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia kidogo. Mheshimiwa Spika, ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba yake nzuri na kwa sababu hiyo ninaunga mkono hotuba yake moja kwa moja. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nichukue tena nafasi hii ya kuwashukuru wananchi wa Makete kwa kunichagua kwa muda wa miaka hii mitano na niwaambie tena kwamba ninarudi tena kwenda kupambana na hao wanaokuja. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji ndiyo inafanya kazi ya kujumuisha mipango yote ya ukuaji wa uchumi wa nchi na katika mipango hiyo makabrasha mengi sana tunayasoma yanayotoka Wizara ya Mipango na kwa kweli nadhani ni vizuri tukampongeza tena Mheshimiwa Waziri na Wataalamu wake wote kwa kazi nzuri wanayoifanya. Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu ukuaji wa uchumi. Ukuaji wa uchumi hauna budi kuzingatia baadhi ya mambo muhimu katika kukua kwa uchumi huo na nitataja kidogo mambo matatu au manne. Mheshimiwa Spika, la kwanza ni kwamba ukuaji wa uchumi ni lazima kwa hali yoyote uambatane na ongezeko la watu yaani Watanzania. Kwa bahati mbaya ongezeko la watu katika nchi zote zinazoendelea kwa kawaida na kwa wastani inakuwa kama asilimia kati ya 2.8 na 3. Ongezeko hili kwa kukua kwa uchumi kwa kiasi cha 6% au 6.7% kama tuna matengemeo ya kwamba inataraji haitoshi ni lazima Mipango hii iendane na Mipango ya Family Planning kiswahili chake sijui maana yake nini. Mipango ya Family Planning ili kusudi watu wetu wanapokuwa, vijana wetu wanavyooa waanze kadri muda unavyokwenda kuwa na tofauti ya tabia ya ukubwa wa familia zao.

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

74

Kwa mfano huko tunakokwenda vijana wetu wawe wanakuwa na watoto wasiozidi watatu kwa kila familia na hiyo inasaidia kuweza kujua kuwa na impact ya ukuaji wa uchumi kwa namna ambayo kwa kweli unakuwa uchumi na kuweza kubadili hali ya maisha Watanzania. Kwa sababu sasa hivi mipango ya familia mimi nadhani kuna namna, it is demanding kuna namna ambayo pengine tungeweza kutumia resource zaidi kuweza kufanya Family Planning, vijana waanze kuwa na tabia au familia zinakuwa ndogo zaidi kuliko zilivyokuwa huko nyuma. Mheshimiwa Spika, sasa hii sijui kama tunafanya na ningependa Mheshimiwa Waziri wakati ana summarize aweze kujaribu kueleza kama ni kweli Family Planning inafanyika au haifanyiki kwa sababu naona kwa casual observation naona kama watu wetu tunazaana tu. Tunazaana tu, hakuna mipango yaani hakuna trend yoyote inayoonyesha kwamba familia zinapungua kwa kufanya hivyo, hivyo ndivyo hali ya uchumi inaweza kuwa nzuri zaidi. Najua kuna tatizo la UKIMWI kwa maana hiyo, unaweza kusema linasaidia kukua kwa uchumi lakini hili ni tatizo ambalo siyo la makusudi, it is not a planning problem. Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni muhimu sana kuwa na ufahamu kamili wa hali ya ajira ya vijana wetu na siyo vijana tu, bali watu wote ambao wanaweza kuajiriwa mpaka miaka 60 sasa hivi kwa sababu Bunge hili limeongeza umri huo. Family Planning, employment na unemployment figures lazima Serikali iwe makini kama vile inavyokuwa makini katika kutengeneza takwimu za ukuaji wa uchumi wenyewe. Sasa sina uhakika kama ufahamu huu sasa kwa sababu hizi takwimu za unemployment hizi nchi nyingine wakubwa nchi zao wanajua kabisa nchi kama Ujerumani unemployment labda ni 8% , Uingereza ni 6% au 7%, Waamerika 4% na Wajapani 5%. Wao wanakuwa wanajua infact namna ya kuweza kujua hizi takwimu kama zinakuwa ni takwimu za uhakika. Mheshimiwa Spika, sasa sisi mimi sina uhakika wengine huwa wanasema asilimia ya kutokuwa na ajira ni kama 40% hata ikiwa asilimia 20 hata ikiwa 10% hii ni kubwa sana kwa maana ya kukua uchumi ili kusudi uwe na trickle down effect yaani wananchi waone kwamba wao maisha yao yanabadilika kwa sababu hali zao zinabadilika, lakini haiwezekani kama Serikali hatujui hizi tarakimu za ajira, kama hatujui vizuri tarakimu za upangaji wa familia na kama hatujui vizuri namna ya kuhakikisha watu ambao wanakuwa ndani ya nchi au bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zinaweza kuwatosheleza na kuweza kubadilisha maisha yao yaweze kuonekana kama yanabadilika. Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ni juu ya Foreign Reserves. Mheshimiwa Waziri amezungumza juu ya Foreign Reserves yaani pesa ambazo zinaweza kutumika kuweza kuingiza mazao yaani ku-import mazao kutoka nje sasa hivi ni kama miezi 7 au 8 tunaweza kuingiza mazao kutoka nje muda wa miezi 7 au 8 bila kuongeza hii Foreign Reserve nyingine.

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

75

Mheshimiwa Spika, sasa ningependa kusema hivi Foreign Reserve zinatakiwa ziwe zinatokana na productivity, ziwe zinatokana na uzalishaji wa bidhaa (goods and services) ndani ya uchumi wetu. Lakini hizi mimi nadhani na nafahamu sina haja ya kuji-excuse, nafahamu kama hizi hazitokani na uzalishaji most of it hazitokani na uzalishaji, zinatokana na sources ambazo ni external au wafadhili wanatusaidia hizi pesa kwa namna moja au nyingine ili kuweza kuongeza reserves hizo. Kwa hiyo, kwa kweli tuna kazi kubwa sana kuweza kuongeza hizi pesa ili ziwe zinatokana na uzalishaji wa mazao ndani uchumi wetu. Mheshimiwa Spika, jambo la tano ni juu ya maendeleo vijijini. Maendeleo vijijini mimi nadhani there is a lot, that is demanding kwamba maendeleo ndani ya vijiji kwa kweli bado na hii ndiyo effect yenyewe, nasema trickle down effect lazima ionekane na ionekane kadri Serikali inavyosema uchumi unakua. Lazima ukuaji wa uchumi uambatane na mabadiliko ya wananchi katika maisha yao na huko vijijini, najua ni kazi kubwa kufanya maisha ya vijijini yaweze kubadilika ili kusudi wananchi au vijana wapunguze kwenda mijini kwenda kujaa katika miji na kuweza kuharibu mipango yote ya ukuaji wa uchumi. Mheshimiwa Spika, sababu kubwa ya vijana kwenda mijini kwa mfano Dar es Salaam nadhani kwa mwaka mmoja vijana wanaingia katika mji wa Dar es Salaam kati ya 7,000,000 na 1,000,000,000. Sasa hii hata kama kuna mipango kama mnataka mipango ya huduma katika Jiji la Dar es Salaam ni vigumu sana kuweza kuweka mipango ambayo itaweza kuridhisha hawa watu wote wanaoingia Dar es Salaam kwa mwaka mzima na hii ni hivyo hivyo katika miji mingine mikubwa mikubwa. Vile vile hii inatokana na ukweli kwamba Vijijini hakuna maendeleo. Kama umeme ungekuwepo, kama maji yangekuwepo ya kutosha vijijini, kama hospitali zingekuwapo za kutosha vijijini, kama shule zingekuwa za kutosha vijijini wananchi wanaokuja hasa vijana wanaoingia mijini wangepungua sana kwa sababu hizi huduma wanazozikimbilia mijini zingekuwa ziko vijijini. Najua ni matatizo na siyo rahisi kuweza kufanya haya mambo moja kwa moja lakini Serikali ni vizuri katika mipango yake kuweza kujua kwamba ni vizuri kuwa na mipango ambayo itafanya vijana wapungue kwenda mijini. (Makofi) Mheshimiwa Spika, jambo la sita ambalo ni muhimu kulisema katika ukuaji wa uchumi ni juu ya inayoitwa miundombinu yaani infrastructure. Waziri alizungumza juu ya infrastructure, pengine ni vizuri tukasema hivi, hizi infrastructure ziko aina mbili kubwa wanaita Economic and Social Infrastructure. Hii Economic ndiyo barabara na yale mawasiliano ya mambo ya simu na mengine yote ambayo ni physical yaani yanaonekana, halafu Social Infrastructure ambayo mara nyingi inakuwa ni Afya, Elimu, Maji na hata Utalii. Mheshimiwa Spika, lakini ningependa kusema muundombinu wa Railway. Reli ni tricky sana juu ya namna vipi Reli tunaweza kusaidia katika nchi inaweza kuongeza hali yake ya uchumi kwa kuboresha Reli.

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

76

Mheshimiwa Spika, ni matumaini yangu Serikali inajua hili kwamba ni tricky sana. Reli huwezi kubinafsisha, huwezi kubinafsisha hizi utility zinazoitwa utility huwezi kubinafsisha kwa sababu au kuwafanya watu waje kuwekeza kwa sababu ni aghali sana. Watu kuwekeza katika infrastructure ya Reli kwa sababu ni aghali sana na inachukua muda mrefu sana kuwa na return. Kwa hiyo, wakati wote itakuwa watu wanakuja wanafanya mchezo wanapata hizo pesa halafu wanakwenda zao. Kwa hiyo, Serikali lazima iwe na umakini mkubwa katika kujaribu kuona namna gani Reli inaweza kubinafsishwa. Pengine hizi nyingine ni rahisi ukilinganisha na miundombinu mingine ni rahisi kwa kulinganisha na Reli. Mheshimiwa Spika, mwisho ningependa tu nizungumze juu ya competitiveness yaani ushindani katika sekta binafsi. Mheshimiwa Spika, ushindani ni moja ya njia kubwa na muhimu zinazofanya uchumi uweze kuendelea na kukua, ushindani inasemekana kila siku Private Sector ndiyo engine ya economic growth na kwamba ndiyo maana Serikali haijiingizi katika hii shughuli za binafsi. Lakini ziko dalili ambazo si nzuri ambazo kuna baadhi ya sectors au sub-sectors kuna tendency ya kuwa na monopoly. Mheshimiwa Spika, kwa mfano katika sekta ya viwanda, hasa kiwanda nitatoa mfano wa Kiwanda cha Sigara yaani TCC. Lakini taarifa zangu nilizonazo ni kwamba hiki kiwanda wanajaribu sana kuzuia viwanda vingine visiweze kuanzishwa ndani ya nchi kwa sababu vikiingizwa na vikianza viwanda vingine basi faida za TCC zitapungua na zikipungua faida zao, madhumuni ya kuwekeza kwao yatakuwa yameharibika. Mheshimiwa Spika, nadhani ni kosa kubwa kama Serikali haiwezi kusaidia kuongeza competitiveness na mashindano siyo ndani ya kiwanda hiki cha Sigara tu, hata katika viwanda vingine vyote. Mheshimiwa Spika, unaweza kuwa na monopoly pale ukiritimba wa aina fulani, lakini siyo katika sekta muhimu, sasa kwa mfano najua kwamba wako wazawa fulani wanataka kuanzisha kutengeneza sigara lakini wanapata matatizo makubwa sana, wanapata matatizo ya vizuizi huku na huku sana, unasema sasa hiki kiwanda TCC kime-monopolize toka nchi imekuwa hata kabla ya Uhuru. Mheshimiwa Spika, sasa wanataka kuendelea na ukiritimba huo watatoa lini nafasi na ku-influence Serikali watatoa lini nafasi ya kuleta ushindani katika sekta hii ili tuweze kuona wananchi waweze kuvuta sigara za aina mbalimbali ingawa sigara nazo zina matatizo yake lakini najua kwamba kwa mfano, wako wazawa wanaanzisha kiwanda pale Dar es Salaam wanaanzisha kiwanda kikubwa tu lakini kinapata matatizo kweli kweli kinapata mikwara mikubwa kabisa na hiki ni kiwanda cha waswahili kama sisi wenyewe. Mheshimiwa Spika, nakushuku na ninasema naunga tena hoja mkono. (Makofi)

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

77

MHE. PAUL P. KIMITI: Mheshimiwa Spika, na mimi napenda nikushukuru kwa kunipa nafasi nichangie hoja hii muhimu ambayo tunadhani ndiyo msingi wa maisha ya Watanzania na sisi wote tuliopo hapa. Mheshimiwa Spika, kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza kabisa kwa dhati Mheshimiwa Waziri Dr. Abdallah Kigoda, kwa kazi nzuri anayoifanya katika Wizara hii akisaidiwa na Katibu wake Mkuu Ndugu yangu Dr. Bukuku na watumishi wote wa Wizara. Kwa kweli wamejitahidi kutufikisha hapa tulipo. Mheshimiwa Spika, mimi nawapongeza sana kwa kazi nzuri waliyoifanya.(Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini pia naomba nitumie nafasi hii kumpongeza tena kwa ziada Mheshimiwa Dr. Abdallah Kigoda, kwa kule kuthubutu kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi. Nampongeza kwa sababu tuko wengi tulikuwa na hamu ya kujaribu lakini tulipoona pana uzito kwa sababu kwenye majimbo yetu kwenyewe tunatoana jasho, tukasema hivi kwenye urais si ndiyo tutatoana jasho zaidi. Lakini Dr. Abdallah Kigoda, hakujali akasema nina haki. Mimi nakupongeza kwa hatua yote uliyofikia, inshallah katika Jimbo lako tunategemea utakuwa ni mfano na chachu kwa maendeleo ya wananchi wote. (Makofi) Mheshimiwa Spika, niitumie nafasi hii kupongeza Kamati yetu ya Kudumu ya Bunge iliyopotia hoja hii, yupo Mheshimiwa Iddi M. Simba, aliitoa kwa ufasaha. Mengi waliyozungumza tunaungana nayo. Pia nimpongeze Msemaji wa Kambi ya Upinzani Ndugu yangu Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, alijitahidi sana na pia aliunga mkono hoja hii. Mimi nasema nampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya hii ya uchambuzi. Mheshimiwa Spika, sasa nina matatu ya kuzungumza, mengine nitaungana na Mheshimiwa Dr. Hassy Kitine, kwa sababu ni mambo ya msingi na kwa sababu mimi mwenyewe kama Mwenyekiti wa Kamati ya Chama chetu cha Wabunge ambao tunashughulikia idadi ya watu na maendeleo. Mimi nadhani nitafanya makosa kama sitazungumzia kidogo kuhusiana na kukua kwa uchumi na ongezeko la idadi ya watu katika nchi yetu. Lakini pia niishukuru Wizara kwa kuandaa Taarifa ya Uchumi ya mwaka 2004. Hii Taarifa kweli tukiitumia vizuri itakuwa ndiyo kabisa njia ya kutusaidia katika Kampeni zetu za uchaguzi katika mwaka huu. Jitihada ambayo Serikali ya Rais Benjamin Mkapa imefanya kwa kipindi cha miaka yote hiyo. Mimi nadhani ni vizuri tukaisoma vizuri na kama kuna masahihisho yoyote tutamwomba Mheshimiwa Waziri atusaidie kutuletea masahihisho ili tusije tukatoa takwimu nyingine ambazo labda zina kasoro katika taarifa zake hizo. Mheshimiwa Spika, sasa baada ya kusema hayo tujue shabaha ya mipango yetu ya Serikali mahali popote ni kuboresha maisha ya wananchi wetu. Hiyo ndiyo shabaha yake ya kwanza. Maana yake ni mipango inayohusu watu si inayohusu vitu vingine.

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

78

Kwa kuwa idadi ya watu hubadilika mara kwa mara ni lazima tukubaliane pia kwamba mahitaji yao pia yatabadilika. Lakini kwa sababu ongezeko linaongezeka haraka iwezekanavyo na mahitaji yao muhimu yataendelea kuongezeka. Nikichukua mfano wa mahitaji ya chakula, mavazi, maji, afya, elimu yote yataongezeka na hii ni gharama kubwa sana kwa Serikali. Huwezi kuondoa umaskini kama uchumi hauendani sambamba na ongezeko la watu, wataalam mahali popote na wengi wako hapa wanatuambia ya kwamba kama watu wanaongezeka kwa 1% basi uchumi wako lazima ukue kwa 3%. Usipoenda sambamba hivyo hutafanikiwa katika malengo yako. Mheshimiwa Spika, tukichukua mfano wa nchi yetu ya Tanzania uchumi unaongezeka kwa 6% maana yake idadi ya watu ilitakiwa isiongezeke zaidi 2% kama tunaelewana. Kama tunaongezeka kwa 2% basi itakuwa ni 2 mara 3 maana yake uchumi ukue kwa 6% lakini kwa ajili tunaongezeka kwa 3% maana yake uchumi lazima tujitahidi ufikie 9% ndiyo angalau uweze kusema ya kwamba unaweza kuhakikisha kwamba watu wako wataishi vizuri. Mheshimiwa Spika, sasa kwa miaka yote hii wote mnafahamu hatujawahi kufikia zaidi ya 7%, nadhani tunaishia 6.7, wakati mmoja tulifikia 6.7 kukua kwa uchumi ambao ilikuwa ni jitihada kubwa sana. Sasa nini unatakiwa ufanye? Kuna option 2 tu, la kwanza ni kujitahidi ili uchumi wako ukue kwa 9% au uhakikishe ya kwamba idadi ya watu katika eneo lako inakwenda chini ya 2% mawili yote hayo. Aidha, ukubali jitihada za kila namna uhakikishe hamuongezeki zaidi ya 2% kwa mwaka na kama huwezi basi jitahidi uchumi uongezeke kwa 9%. Mheshimiwa Spika, wenzetu katika nchi nyingine zilizoendelea msione wameendelea, wamejaribu kudhibiti sana ongezeko kubwa la watu. China walifikia mahali fulani wakaanza kutoa sheria kwamba mtu mmoja, familia moja na mtoto mmoja, ukitaka wa pili ni mpaka upate kibali. Sisi hatukutaka tufikie hapo kinachotakiwa ni elimu ya watu wetu waone uzito wa uzito wa kuendelea kuongeza uzito wa familia zikiwa kubwa namna ya kuzitunza na mahitaji yao yatakuwa ni makubwa. Yanakuwa ni mzigo kwa familia, hiyo ni kazi mojawapo. Hivyo elimu ni lazima itatumika. Lakini pia lazima tuiombe Wizara ielekeze nguvu zake zote katika mikoa yenye matatizo makubwa, mikoa kama Kigoma, Rukwa ambao ongezeko lake la watu ni zaidi ya 4% hivi kweli Wizara hailitambui hilo? Na kama inalitambua inafanya nini kusaidia mikoa hiyo? Tunafanya hivyo kwa sababu takwimu tulizonazo Mkoa wa Rukwa ni kati ya Mikoa michache ambayo idadi ya watoto wanaokufa kabla ya kutimiza umri wa miaka ni kubwa sana. Lakini miradi yote haiko Rukwa, miradi iko katika Mikoa mingine, hivi takwimu hizo zinasaidia nini kwa mikoa ambayo inakuwa na matatizo kama hayo? Tunataka takwimu sasa zifanye kazi ambayo inakusudiwa, tuangalie takwimu tuwaelekeze wahisani watoe misaada katika maeneo yote yanayohusika, ni vizuri hilo likapewa umuhimu wake.

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

79

Mheshimiwa Spika, pia tungeshauri kuangalia sera ya idadi ya watu sasa ipewe kipaumbele maana inaonekana sasa imechukua miaka mingi sijui kigugumizi kiko wapi hatuwezi kuendesha nchi bila kuwa na sera inayojulikana juu ya idadi ya watu. Mwanzoni mwa mwaka 1992 tulipoanza tulikuwa na kigugumizi kwa ajili ya kisiasa lakini tukaendelea kuongeza kigugumizi kingine bila kuangalia tunafanya nini na kuweka mikakati ya utekelezaji wa Sera. Hatutafika mahali popote kwa sababu tutaendelea kuzungumzia juu ya umaskini wa watu wetu kwa sababu tumeshindwa kuoanisha uchumi na ongezeko la watu. Hivyo ningeshauri kuhusiana na sera mambo miwili ya kwamba mikakati ya utekelezaji wa sera iandaliwe lakini la pili Tume ambayo itashughulikia au Kamati maalum ya idadi ya watu na maendeleo basi iundwe haraka iwezekanavyo ili isaidiane na Wizara katika kuhakikisha mambo haya sasa yanatekelezwa kama inavyotakiwa. Mheshimiwa Spika, tuna imani mpango wetu wa MKUKUTA utasaidia sana kupunguza kasi ya umaskini katika maeneo yetu lakini umaskini utapungua tu kama walengwa watasaidiwa kupata nafasi ya kupewa elimu ya kutosha ili wajue namna ya kupanga mipango yao. Tuna matatizo katika vijiji vyetu kila mtu katika kijiji anaweza kuona ya kwamba kipaumbele katika maeneo yake ni kipi. Ukichukua mfano ukimuuliza mtu mmoja ambaye anauliza juu ya kipaumbele cha kilimo wengine watasema tupatiwe pembejeo, wengine watasema hapana kipaumbele ni masoko, wengine watasema hapana kipaumbele ni barabara. Sasa wananchi wetu ni lazima tukae nao ili kuwaeleza na waelewe umuhimu wa barabara ili waweze kusafirisha mazao yao katika maeneo mbalimbali. Mheshimiwa Spika, lingine ni muhimu katika kipindi hiki kuna suala zima halizungumziwi sana ni suala la ujasiriamali linakuwa ni kama somo jipya lakini ni somo ambalo litasaidia hasa vijana wetu kuanzia mashuleni mpaka vikundi vya akinamama na vijana ambao wanafanyabiashara ili wajue namna ya kuendesha shughuli zao za biashara kabla hata ya kupata mikopo. Unaweza kutoa mikopo lakini kama hukupata elimu inayotakiwa mikopo ile inatumika vibaya na wakati mwingine inakuwa ni hasara na mzigo kwa wanaohusika. Mheshimiwa Spika, tunaweza kuwalaumu bure lakini wakati mwingine tunafanya makosa kama hatujawaandaa vya kutosha na kuwapa kila aina ya elimu ili wajue namna ya kutumia mikopo yao. Tulidhani Wizara isaidie ili kuhakikisha hili linatelezwa. Mheshimiwa Spika, lingine ni suala la Sera ya Uwezeshaji. Tungeomba nalo liangaliwe kwa sababu tuna imani kabisa ili kuwezesha watu hasa wakulima lazima tuwe na uhakika ya kwamba uwezeshaji unaandaliwa, unakwenda sambamba na kuangalia uwezekano wa kuanzisha Benki ambazo zitasaidia kwa mfano wakulima tunaiita Benki ya kilimo ambayo inaweza kusaidia. Nashukuru Kamati ya Kudumua imetoa mapendekezo ya kwamba uwezekano wa kuwa na Benki ya Kilimo na Benki ya Viwanda uangaliwe ili uoanishwe katika mipango ya kufufua uchumi.

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

80

Mheshimiwa Spika, mengi nimeweka katika maandishi ambayo nimekwisha mpelekea Mheshimiwa Waziri lakini nilitaka kwa kutoa pongezi kwa wachache. Kwanza nataka nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Balozi Getrude I. Mongella, kwa kupata Shahada ya Heshima ya Udaktari ambayo ameipata. Bahati mbaya sisi wengine tulikuwa hatuna habari kwa sababu alikuwa na msiba ndiyo maana hatukuwa na taarifa lakini nataka kweli nimpongeze anastahili kupata heshima hiyo. Lakini pia alipata heshima ya Tuzo la Martin Luther. Martin Luther ni mpigania haki. Yule mtu alikuwa anaheshimika duniani kote na unapopata tuzo na heshima yake basi wewe wameku-recognise katika dunia hii. Mheshimiwa Balozi Getrude Mongella, unatujengea heshima sana katika Tanzania. Tunakutakia kila la kheri na tuna imani kabisa katika Jimbo lako wananchi wa Ukerewe wataona umuhimu wa mtu kama wewe kuendelea kuwaongoza katika maeneo yao. (Makofi) Mheshimiwa Spika, mwisho nataka nitumie nafasi hii nikupongeze wewe, maana ndiyo nafasi yetu ya lala salama. Umekuwa kiongozi wetu kwa muda mrefu, mimi nimekuwa na bahati wakati uko Makao Makuu ya Chama kama Katibu Mkuu, mimi nilikuwa Katibu Msaidizi wako, tulifanya na wewe kazi, ukapata nafasi ya kwenda Chuo Kikuu, ukarudi ukapata nafasi za uongozi mbalimbali lakini ambalo nalikumbuka ulipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Aliyekurithi na kuchukua nafasi yako ni mimi. Nafuata nyayo zako, sijui nitaomba Uspika na mimi siku moja. (Kicheko/ Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini kweli kwa moyo wa dhati nataka niseme umeongoza Bunge hili kwa hekima ya hali ya juu sana. Hekima na busara ndiyo zimetufikisha hapa tulipo, angekuwapo mtu mwingine tungekuwa tumetwangana makofi humu ndani, lakini hekima yako uliyoiomba kwa Mwenyezi Mungu imekufikisha hapa ulipo. Sisi tuna imani kabisa mtu yoyote anapoongoza kwa kutumia hekima atafanikiwa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kitu kimoja tu wote mnakumbuka, Mfalme Suleiman alipoambiwa na Mwenyezi Mungu ya kwamba unataka nikupe zawadi gani. Utajiri hata ukitaka urudi katika ujana nitakupa, akasema Mwenyezi Mungu sina lolote la kukuomba ni hekima na busara ili niongoze watu wangu vizuri. Mheshimiwa Spika, hiyo hiyo hekima ndiyo ilimsaidia wakati alipopata tatizo moja kubwa sana. Akinamama wawili walipokwenda wote wanasema mtoto huyu ni wetu. Mfalme Suleiman akasema kama wote mnang’ang’ania ya kwamba mtoto ni wenu basi tumpasue katikati wewe uchukue kipande kimoja na mwingine achukue kingine. Mheshimiwa Spika, yule mwenye mtoto ambaye ni mtoto halali akasema hapana kama mwenzangu anang’ng’ania mpe mtoto mimi nikose. Mfalme Suleiman akaona kumbe mwenye mtoto ni yule aliyekataa, akamrudishia mtoto ikaonekana hekima imefanya kazi yake. (Makofi) Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii. Ahsante sana.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

81

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. PROF. SIMON M. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, hongera na pongezi

tele kwa kazi nzuri ya Wizara na Hotuba murua. Pongezi hizi ni za Mheshimiwa Waziri na Watendaji wake wote wakiongozwa na Katibu Mkuu Dr. Enos Bukuku.

Mheshimiwa Spika, kabla ya yote naunga mkono hoja. Mchango wangu ni wa

kutaka kupata maelezo zaidi. Zamani wanauchumi wote wa Serikali walikuwa wanaongozwa na kusimamiwa na Wizara hii. Je, hali hii bado ipo?

Mheshimiwa Spika, napenda kuzungumzia kuhusu suala la ubinafsishaji. Kuna

Makampuni kadhaa yaliyonunua Makampuni ya Serikali na kuyabomoa au kubadili matumizi yake na kufanya mambo mengine. Kama ALAT wameng’oa baadhi ya mashine na kuendeleza uzalishaji Kenya na kutufanya sisi Tanzania soko tu. Kwa nini asinyang’anywe?

Mfumo wa mishahara ya Serikali hairidhishi hasa kwa watumishi wake. Fungu linalotengwa kwa mishahara ni dogo na lile linalotengwa kwa marupurupu ni kubwa mara tatu hata nne. Tuna viraka vya mishahara hasa ikiwa Wahisani wanalipa mfano TRA, PSRC, LART na kadhalika iweze kuzalisha tofauti hizo, hatuwezi kuiacha kazi hiyo kwa Utumishi kuu peke yao, hawana uwezo.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na ninaunga mkono hoja. MHE. MUTTAMWEGA B. MGAYWA: Mheshimiwa Spika, punguzo la kodi

au kuondolewa kodi zote kwa viwanda vya Vijijini ili visaidie ajira Vijijini na kupunguza mfumuko wa watu Mijini, unafuu huu uwe angalau kwa miaka mitano.

Mheshimiwa Spika, ubinafsishaji wa viwanda au mali ya umma, upendeleo uwe

ni kwa wazawa kwanza. Mheshimiwa Spika, MKUKUTA/MINI-TIGER, katika kukuza uchumi wa Taifa

na wananchi ni muhimu kuwawezesha wananchi na kwa kuwa eneo lote la madini katika Jimbo la Mwibara wamepewa wageni na kwa vile sasa wanamwibara wanao uwezo wa kuchimba kwa kutumia vifaa vya kisasa: Je, Serikali itakuwa tayari kuwarudishia wananchi ardhi yenye madini ili wachimbe kwa ustawi wa Taifa?

Mheshimiwa Ndugu yangu Doctor, nakutakia ushindi Jimboni. MHE. PAUL P. KIMITI: Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hii kutoa

shukrani zangu na pongezi kubwa kwa Mheshimiwa Waziri Abdallah Omar Kigoda na Katibu Mkuu wake Dr. E. Bukuku wakisaidiwa na Wakuu wa Idara na Watumishi wao kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuandaa mipango yetu vizuri. Naunga mkono hoja hii.

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

82

Mheshimiwa Spika, nashukuru pia kwa kupewa taarifa ya Hali ya Uchumi (2004). Huu ni msahafu utakaosaidia katika kampeni zetu huko kwenye Majimbo. Kama kuna masahihisho yoyote ni vizuri tukapelekewa masahihisho.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kupitia Wizara hii kwa kuanzisha kozi ya

shahada katika fani ya idadi ya watu. Hili naliunga mkono kwa sababu, mipango yetu ni ya watu na hivyo ongezeko la watu na kukua kwa uchumi ni budi yaende sambamba. Kukua kwa uchumi kwa asilimia 6.2 wakati watu wanaongezeka kwa asilimia takribani tatu, hatuwezi kuondoa umaskini katika hali hiyo. Labda tuongeze kasi ya kukua uchumi kwa asilimia tisa au watu wetu wasiongezeke kwa kasi ya zaidi ya asilimia mbili.

Mheshimiwa Spika, suala la ongezeko la watu hasa Vijijini tegemeo lao ni kilimo.

Hivyo, suala la uwezeshaji wao na mipango yao ni budi iende sambamba na kuona uwezekano wa kuanzisha Benki ya Kilimo.

Mheshimiwa Spika, takwimu zetu lazima zitumike kuelekeza Wahisani ili waende

sehemu zenye matatizo na siyo kuwaachia Wahisani wawe wanaamua wapi waende sisi tuwaelekeze.

Mheshimiwa Spika, sera ya idadi ya watu inaendeleaje kukamilishwa ili mkakati

wa utekelezaji uzingatie hali halisi? Nashauri Tume au Kamisheni iandaliwe haraka ili iwe na jukumu la kusimamia sera yenyewe.

Mpango wa MKUKUTA utasaidia sana kupunguza umaskini nchini.

Kinachotakiwa ni elimu kwa watu wetu ili wajue namna ya kupanga mipango yao. Mheshimiwa Spika, suala la somo la ujasiriamali kwa watu wetu ni muhimu

likapewa umuhimu wa kwanza kwa vijana na wanawake ili liwasaidie kujua namna ya kuendesha biashara zao kwa maadili ya juu kabisa.

Mheshimiwa Spika, sera ya uwezeshaji sasa iandaliwe mkakati wa utekelezaji ili

iende sambamba na mipango yetu shirikishi. Huu umeweza kuwa mwanzo wa kupambana na umaskini.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii. MHE. SEMINDU K. PAWA: Mheshimiwa Spika, natoa shukrani nyingi sana

kwa Mheshimiwa Waziri wa Mipango Comrade Dr. Abdallah Omar Kigoda kwa kazi nzuri ndani ya Wizara hii, kwa kweli ameimudu. Hii inatokana na ushirikiano na mshikamano wake yeye, Katibu Mkuu wake, Makamishna na Watendaji wote hapo Makao Makuu, hongera sana. Naomba watumishi na mimi tuungane kumwombea arudi Bungeni bila ya nongwa zozote.

Mheshimiwa Spika, napenda kuzungumzia kuhusu zao la matunda. Nchi hii ina

matunda mengi sana hasa Lushoto, Morogoro au baadhi ya maeneo ya Pwani na Muheza. Serikali ina mpango gani kuleta wawekezaji kujenga viwanda vya concentrates maeneo

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

83

ya Tandai, Matombo, Muheza, Mkuyuni, Kinole, Lushoto? Naomba majibu ya kunipa moyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uwekezaji na ubinafsishaji, naomba sana niipongeze

PSRC na TIC kwa kazi nzuri. Lakini kuna tatizo la urasimu TIC kwa wawekezaji eneo la kilimo. Jinsi gani Hotel ya Kilimanjaro inapendeza, ni siri ya mwekezaji huyo lakini isibadilishwe jina iwe Kilimanjaro Hotel.

Mheshimiwa Spika, pili, Hotel ya Royal Palm ilikuwa Sheraton sasa hivi inaitwa

jina lingine, baadaye itaitwa Pawa Palm, Msekwa Palm, Malecela Palm; mtindo huu siyo mzuri. Naomba maelezo. Hivi hakuna siri yoyote ya fedha za kificho?

Mheshimiwa Spika, bei ya mazao, watu binafsi wanawanyonya wakulima mfano

pamba, ufuta na kahawa. Hivi sasa wananchi wamekata tamaa. Mheshimiwa Spika, nina maombi yafuatayo:- (1) Kuomba Waziri Abdallah Kigoda arudishwe na wananchi wake hapa Bungeni,

bado tunamuhitaji sisi Wabunge; (2) Kuomba kuweka vipaumbele vya matakwa yetu kwa kuhoji Mikoa RCC ili

miradi ipate vipaumbele vya Mikoa hiyo; (3) Mradi wa mifugo ndani ya ranchi zinazobinafsishwa zisibadilishwe matumizi;

na (4) Mheshimiwa Spika, Makamishna watembelee miradi mikubwa nchini. MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mipango iwe pekee, isichanganye mambo ya

ubinafsishaji. Kuna mpango gani wa kuwawezesha wakulima kuondokana na jembe la mkono?

Ni muda gani uliowekwa? Ni mkakati gani uliotayarishwa?

Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kilimo kinamwondolea umaskini mwananchi?

Mheshimiwa Spika, hawa wawekezaji wanaokuja kuuza karanga, soda,

wafukuzwe mara moja. Nawatakia kila la kheri na baraka kwa mwaka 2005/2006. MHE. OMAR MJAKA ALI: Mheshimiwa Spika, kwanza ninaitumia nafasi hii

kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji, Katibu Mkuu, Maafisa na Watendaji wote wa Wizara hii kwa hotuba yao hii nzuri yenye upeo na mwelekeo wa hali ya juu ya maendeleo ya nchi yetu kuanzia ilipotoka, ilipo hivi sasa pamoja na siku zinazokuja.

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

84

Mheshimiwa Spika, ninaiunga mkono hotuba hii asilimia mia kwa mia na

ninamtakia kila la kheri Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na Watendaji wote Wakuu wa Wizara hii kuendelea kuisimamia Wizara hii kwa mafanikio makubwa zaidi kama yalivyopangwa katika mipango ya Wizara na Serikali, pamoja na sera na mikakati yote.

Mheshimiwa Spika, bila ya kuwa na mipango mizuri na endelevu, huwezi kufikia yale malengo ambayo umepangia. Kwa hiyo, ninaiomba Wizara yetu hii isimamie mipango yote ambayo imepangwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu hii ya Tanzania na kwa wananchi wote kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, hotuba ya Mheshimiwa Waziri ni mzuri sana. Ninaiomba

isimamiwe vizuri ili kuleta mafanikio yaliyotarajiwa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi yetu na kwa wananchi wote kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri katika ukurasa wa

18 unaelezea kuwa, katika kuandaa Bajeti ya mwaka 2005/2006, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji imezingatia azma ya Serikali ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025. Ninaipongeza sana Wizara hii kwa kuandaa Bajeti yao hii ambayo azma yake ni kutekeleza Dira yetu ya Taifa ya mwaka 2025. Ninaomba kusimamia ipasavyo mpango huu ili kuleta mafanikio yaliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa 25 tunaelezwa kuwa, katika kipindi cha

mwaka 2005/2006, Serikali itaendelea kuhimiza wawekezaji wa ndani kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati vya kusindika mazao ili kuongeza thamani ya mazao ya nje na kuchangia katika kupanua nafasi za ajira.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli ninaitumia nafasi hii hapa kuipongeza sana

Wizara na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuelezea juu ya yale ambayo yatahimizwa kwa wawekezaji wa ndani katika kipindi hicho cha mwaka 2005/2006.

Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha uhimizwaji huu kwa wawekezaji wa

ndani, ni vizuri ukalenga zaidi katika maeneo ya Vijijini ambako huko ndiko kwenye wakulima wengi, mazao mengi na ya aina mbalimbali na hata vijana wengi ambao hawana ajira nyingine ya msingi zaidi ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kunaweza kukaelezwa kuwa Vijijini hakuna umeme,

lakini kutokana kuongezeka kwa Teknolojia ya Nishati Duniani na hata hapa nchini petu Tanzania tuhimize Vijijini kujengwa viwanda hivi vidogo ambavyo wawekezaji wetu wa ndani wanaweza kutumia hata umeme wa solar.

Mheshimiwa Spika, kama Vijijini kutapelekwa viwanda hivi vidogo vitawezesha wakulima wetu na mazao yao hayaathiriki kwani yataweza kusindikwa na baadaye kutafutiwa soko la ndani na nje yakiwa katika hali mzuri na ambayo itayanusuru kuharibika.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

85

Ppia tuwawezesha wakulima wetu walioko katika Vijiji mbalimbali hapa nchini kwa kupelekwa kwa watalaam wa sekta mbalimbali za uzalishaji katika Vijiji hivyo. Pia, wananchi na wakulima wetu wadogo wadogo walioko Vijijini, wawezeshwe kwa kupatiwa misaada ya fedha na vifaa mbalimbali ili waweze kuzalisha mazao mbalimbali ambayo yataweza kutumika katika kuyasindika mazao hayo ili kuyafikia yale malengo yote yaliyopangwa ya kuwaletea maendeleo wananchi na nchi yetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika mchango wangu huu wa maandishi

ninaoandika leo hii, ninaiomba sana Wizara hii na Serikali yetu kuzipongeza nchi na Viongozi wa nchi za G.8 kwa heshima kubwa waliyompa Mheshimiwa Rais wetu Benjamin William Mkapa kwa kumwalika katika Mkutano wao uliofanyika huko Scotland Uingereza mwanzoni mwa mwezi huu wa Julai, 2005.

Mheshimiwa Spika, vilevile ni vizuri kwa nchi yetu kuitumia fursa hiyo ya

Mheshimiwa Rais wetu kualikwa katika Mkutano huo wa G.8 kujenga uhusiano mzuri sana na nchi hizi za G.8 na pia tuitumie fursa hiyo kujenga uchumi wa nchi yetu pamoja na ulinzi kwa kiwango cha kuwa Taifa kubwa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kiulinzi (Kijeshi) katika eneo zima hili la Bara letu la Afrika na duniani kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyaandika haya katika mchango wangu huu,

ninarudia kuiunga mkono hotuba hii kwa asilimia mia kwa mia. MHE. MUSA A. LUPATU: Mheshimiwa Spika, ninampongeza sana

Mheshimiwa Dr. Abdallah O. Kigoda - Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji pamoja na wataalam wote wa Wizara yake kwa kazi nzuri ya kuongoza Wizara na ushauri mzuri wa kuimarisha uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Spika, katika mchango wangu huu wa maandishi naomba kuweka

bayana masuala ya muda mrefu katika Wilaya yetu ya Korogwe ambayo bado hayajapata ufumbuzi kamili wa Serikali, nayo ni masuala ya mkonge.

Mheshimiwa Spika, liko tatizo la wafanyakazi wa mashamba ya mkonge wa iliyokuwa Mamlaka ya Mkonge la kutolipwa mafao yao hadi leo. Katika Wilaya nzima, tuna zaidi ya mashamba 15. Pia, yako matatizo ya wafanyakazi wa Katani Limited kutolipwa mishahara na mafao kama ilivyoelekeza Serikali. Yako matatizo hayo hayo kwa mashamba yaliyokuwa ya Chavda na hatimaye kuchukuliwa na CRDB na baadhi kama Kwashemshi.

Mheshimiwa Spika, pili, maeneo yaliyomegwa toka Mamlaka ya Mkonge

ambayo yalipewa Vijiji vinavyozunguka mashamba hayo, hadi leo wananchi hawajakabidhiwa mashamba hayo hasa yale yaliyochukuliwa na Katani Limited. Tatizo la tatu ni utata uliopo hadi leo kuhusu hatua ya Katani Limited na mashamba yao. Naomba Serikali ifanye juhudi kutunza matatizo haya ambayo ni kero kubwa kwa wananchi.

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

86

Mheshimiwa Spika, mwisho ni tatizo la mashamba ya chai ya wamiliki binafsi ya Balangui/Dindira na Ambangulu ambayo yanadaiwa malimbikizo ya mishahara na wafanyakzi kwa zaidi ya miaka mitano. Mbaya zaidi wamiliki wa mashamba haya wanauziana na kubadilisha umiliki bila usimamizi wa Serikali, hivyo kuwaacha wafanyakazi bila mwelekeo na utatuzi wa madai yao ya mishahara. Mfano mashamba haya yameuzwa zaidi ya mara tatu katika kipindi kifupi, lakini wafanyakazi hawaelewi hatma yao mara shamba linapouzwa. Ninaomba Serikali itatue tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naunga mkono hoja. MHE. MOHAMED H. MISSANGA: Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri

Dr. Abdallah Omar Kigoda na Katibu Mkuu wake na Watendaji wote kwa ujumla. Mheshimiwa Spika, napongeza kazi ya ubinafsishaji iliyofanyika ingawa zoezi

hili lilianza na matatizo makubwa, lakini sasa Wizara inachukua hatua nzuri za kurekebisha kasoro hizo kwa mfano:-

(1) Kutojali ushauri wa Watendaji, wataalam wetu na badala yake kupendelea

external consultants; (2) Kupuuza suala kuwalipa wafanyakazi waliopunguzwa kazi katika Taasisi

mbalimbali mpaka wafanyakazi hao walipogoma na kuzusha malumbano; (3) Kuifanya Mikataba kuwa ya siri na Mikataba yenyewe kuwa na walakini

example TTCL – ATCL nakadhalika; na (4) Kubinafsisha Mashirika kadhaa kwa Makaburu jambo ambalo ni hatari kwa

usalama wa Taifa. Mheshimiwa Spika, Mashirika ya Bima na TANESCO nayo inafaa yabinafsishwe

kwani utendaji kazi wake unasuasua. Bima sasa wamekuwa wababaishaji, wateja hawalipwi inavyofaa na hawalipwi kwa wakati muafaka, inachukua miaka kadhaa kumlipa mteja. Hata malipo yenyewe ni ya utapeli, wamefilisika na hivyo hawana uwezo. Bima wabinafsishwe haraka sana, TANESCO pia wabinafsishwe haraka.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara itafute Wawekezaji Singida hasa Hotel

karibu na Ziwa Kindai. Manispaa ya Singida inakua kwa haraka sana hasa baada ya barabara ya Dodoma Singida – Mwanza kumalizika na vilevile barabara ya Singida – Babati hadi Arusha ikimalizika, hivyo ipo haja kubwa kuwa na Hotel kubwa ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. MHE. ISSA MOHAMMED SULEIMAN: Mheshimiwa Spika, naomba na

mimi nichangie hoja hii ambayo ina umuhimu mkubwa sana, sio tu kwa maendeleo ya Taifa letu, bali pia kwa kutoa heshima ya Taifa hili duniani.

Mchango wangu upo kwenye kijitabu kinachoitwa Tanzania in Figures 2004.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

87

Kwenye ukurasa wa tatu wa kijitabu hicho, kuna maelezo yanayoonyesha wazi

kwamba Zanzibar imekuwa huru Desemba, 1963 na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar imeundwa baada ya Mapinduzi ya Tarehe 12 Januari, 1964.

Nakubaliana na Taarifa hiyo. Katika maandishi ya uhakika ya kuweka kumbukumbu kama hizi na hata kwenye Katiba zetu zinatumia maneo Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Kwenye ukurasa wa tano wa kitabu hiki ninachokinakili, kilipoelezea Area

kimetaja Major Island Tanzania Mainland ni Ukerewe na Mafia. Kitabu kikaendelea – Major Island Zanzibar, Unguja na Pemba. Maelezo hayo sio sahihi.

Mheshimiwa Spika, usahihi ni kwamba Major Islands Tanzania Zanzibar ni Tumbatu, Uzi, Kisiwa Panza.

Angalia pia maelezo yake ya Ukurasa wa tatu ndani ya kitabu hiki, uliposema: “The two Sovereign Republics formed the United Republic of Tanzania on 26th April, 1984.”

Moja kati ya Jamhuri hizo ni Jamhuri ya Visiwa vya Zanzibar, naomba masahihisho.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa hoja hii ya Waziri aliyoiwasilisha Bungeni leo naiunga mkono.

Mheshimiwa Spika, angalia misingi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MHE. LEONARD N. DEREFA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri kwa asilimia mia moja. Ninao ushauri na maombi yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Nyama cha Old Shinyanga, kwa muda wa zaidi ya miaka 10 nikiwepo hapa Bungeni nilikuwa nikifuatilia ubinafsishaji wa kiwanda hiki, lakini hadi leo kiwanda hiki kimeshindikana pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu kuagiza kuwa kiwanda hicho kipewe wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga na kadhalika ili wao washiriki kutafuta mwekezaji atakayeshirikiana na mwekezaji yeyote. Mheshimiwa Spika, naomba sana wakati Mheshimiwa anahitimisha bajeti nipate maelezo ya kutosha ni kitu gani hasa kimekwamisha ubinafsishaji wa kiwanda hiki pamoja na kuwa Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Tabora kuna mifugo zaidi ya milioni 10? Hii ingeliboresha soko kwa mifugo na kuwapa wananchi wa Shinyanga Mjini. Pia, nitapenda kujua kwa nini mwekezaji wa Kiwanda cha kukoboa mpunga cha NMC hajapewa kiwanda hicho pamoja na kwamba ameshalipa fedha ya awali.

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

88

Kuhusu ubinafsishaji wa TRC, nashauri pamoja na kwamba Serikali inataka kubinafisisha Shirika hili, ni vyema likaendelea kupewa fedha za kufanya ukarabati wa njia mabehewa na engines. Maana hali ya reli na mabehewa hamna maji, umeme kwenye mabehewa na kadhalika. Suala la mabehewa kuishia Dodoma badala ya Dar es Salaam imeathiri sana usafirishaji mizigo kutoka Mikoani kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kwenda Mikoani. Naomba kabisa suala hili TRC iendelee kuboreshwa maana ndiyo Blood Stream ya uchumi wa Mikoa ya Ziwa. Nawatakia utekelezaji mwema wa mipango yote, naomba tusaidiane haraka kwa hili. MHE. AGGREY D. J. MWANRI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo langu la Siha, naomba kuchukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Spika Dr. Abdallah Kigoda kwa hotuba yake nzuri ambayo imekuwa na uchambuzi wa kina iliyotolewa asubuhi hii. Hongera sana Mheshimiwa Waziri. Kipekee, naomba kuchukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Dr. Abdallah Kigoda kwa ziara ambayo aliifanya mapema mwaka huu katika Jimbo langu la Siha. Kwa muda wa siku tatu mfululizo Mheshimiwa Dr. Kigoda alikaa Jimboni kwetu na kufanya mazungumzo ya kina na wananchi hususani wale MASKOTA wa West Kilimanjaro. Mheshimiwa Spika, katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri aliifuta rasmi dhana na msamiati USKOTA. Tunashukuru sana kwa jitihada zake. Aidha, naomba nichukue fursa hii kukumbushia ombi maalum lililotolewa na wananchi kwa Mheshimiwa Kigoda la kupatiwa Shamba la NAFCO la Journey’s End. Eneo hilo ambalo Mheshimiwa Waziri alipata fursa ya kulitembelea ni muhimu kwa ajili ya kuwapatia makazi ya kudumu hasa kwa wale wananchi waishio eneo la Mji Mdogo wa Ngare - Nairobi ambalo linakua kwa kasi kubwa kiidadi ya watu na hata katika upanukaji wa Mji huo mdogo. Mheshimiwa Spika, Mji huu unakuwa haraka na hivyo unahitaji huduma muhumu kama Shule za Msingi na Sekondari, Benki, Posta, Hospitali, Zahanati, Vituo vya Polisi na kadhalika. Ni matumaini yetu kuwa Waziri ataendelea kulipa msukumo wa hali ya juu ili eneo hilo liweze kutumika kwa makusudi niliyoyaeleza na hivyo kuondokana na migogoro isiyokuwa ya lazima. Mheshimiwa Spika, wananchi wa Siha hawana tatizo na suala au sera ya ubinafsishaji, ila hofu yao ni kwamba kama sera hiyo basi, tutakuwa tunazalisha mgogoro ambao utawafanya wawekezaji washindwe kuwekeza kwa amani na utulivu. Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba, eneo hili litolewe kwa wananchi ili kuepusha shari. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kukubali kulifanyia kazi tatizo hili na ni imani yangu kuwa hatimaye Serikali itatukubalia ombi letu. Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

89

MHE. KHAMIS AWESU ABOUD: Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu, Maafisa mbalimbali pamoja na wafanyakazi wote wa Waziri hii. Wizari hii ni muhimu sana, hivyo Serikali isimamie vizuri matatizo yanayojitokeza kama ifuatavyo:-

Yapo Mashirika yaliyobinafsishwa lakini yanaendeshwa kwa hasara jambo ambalo linaleta usumbufu na kero kwa Serikali yetu. Je, kwa kuwa Wizara inajua tatizo hili, itachukua hatua gani ili matatizo hayo yasitokee tena? Wananchi walio wengi hawajafahamu vizuri maana ya kubinafsisha viwanda na kadhalika.

Kumejitokeza matatizo ya wafanyakazi wale ambao walikuwa wafanyakazi kabla

Mashirika hayajabinafsishwa walikuwa wakifanya kazi katika Taasisi mbalimbali, kwa vile wale waliochukua Mashirika wanakuwa na uamuzi wao wenyewe wa kuendelea na wafanyakazi wa zamani au wanaweza wakaajiri wafanyakazi wengine; sasa wale waliokuwa wafanyakazi na hawakupata nafasi ya ajira mpya, Serikali iwe makini kuwalipa mafao yao.

Wapo wafanyakazi ambao wameshastaafu na hawajalipwa mafao yao. Wizara hii isimamie kupatikana kwa mafao hayo. Lakini inachukuwa muda mrefu kupata mafao yao, hivyo ninaomba Serikali isimamie matatizo hayo.

Ninaomba wanaopewa Mashirika kwa njia ya kubinafsishwa, ni bora Serikali ibadilishe mfumo. Baada ya kubinafsisha sasa wakodishwe kwa masharti maalum.

Mheshimiwa Spika, wapo wataalam ambao wanachimba madini kama vile dhahabu, lakini asilimia ya mapato tunayoyapata hapa nchini ni ndogo sana ukilinganisha na nchi nyingine. Mfano Botswana wao wanachimba madini ya almasi na wanaochimba ni wataalam wanaotoka nchi nyingi lakini mgao wa mapato ni asilimia 50 ya nchi yao na asilimia 50 ya wale wanaochimba madini. Sasa kwa nini Serikali yetu inapata asilimia ndogo? Ninaomba Serikali isimamie niliyoshauri na baadaye mawazo haya iyafanyie kazi. Mwisho naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia. Ahsante sana. MHE. AZIZA SLEYUM ALI: Mheshimiwa Spika nachukua nafasi hii kukushukuru kwa kutoa nafasi ya kuchangia kwa maandishi. Mheshimiwa Spika, nampongeza Rais Mkapa kwa kutuletea utaratibu wa ubinafsishaji. Hii ni mojawapo ya mkakati wa kuendeleza nchi yeu na kumpa jukumu la kusimamia Wizara hii Mheshimiwa Abdallah Kigoda.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchunguza katika masuala yafuatayo:-

Kuhusu bidhaa ambazo zinatofautiana kwa bei katika Mikoa, tatizo kubwa hudai ni usafiri, lakini usafiri huu ni kwa vifaa tu vya ujenzi si kwa vinywaji? Kwa nini bei ya beer hulingana bei kwa nchi nzima na usafiri upo? Pia kama kwa vifaa vya ujenzi na hata sigara, kwa nini kwa vifaa vya ujenzi hasa cement mtumiaji wa mwisho ndie huumia sana

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

90

katika manunuzi hayo? Kulingana na hilo, ni wazi kuwa Mkukuta haumsaidii mwananchi wa hali ya chini au ununuzi wa mwisho. Naomba ufafanuzi wa kina kwa hili.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Hoteli ya Kitalii ya Mikumi Lodge kufungwa kwa muda mrefu na kuacha ikiharibika kwa muda wote huu, kwa kuwa suala la mwekezaji huyo kuwa Mahakamani, hamwoni sasa kuna haja ya kufikia maamuzi ya mwisho ili hoteli hiyo ifanye kazi na isiharibike kwa kiwango kikubwa? Hata hivi sasa imeshaharibika kwa kukaa bila ya kufanya kazi. Je, Serikali haioni hapo pana haja ya kukaa na kuzungumzia hoteli hii ijulikane hatima yake. Pia, nawapongeza kwa mafanikio makubwa ya Wizara ambayo mmeyafanya kwa umahiri mkubwa zaidi. Naunga mkono hoja.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, tunashukuru sana kwa mchango wote tulioupata kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge. Tumepokea mchango kwa maandishi na vile vile tumepokea mchango wa kauli kupitia hapa Bungeni. (Makofi) Mheshimiwa Spika, naomba nianze kuwatambua wale waliochangia kwa maandishi Mheshimiwa Semindu K. Pawa, Mheshimiwa Leonard Derefa, Mheshimiwa Aziza Sleyum Ali, Mheshimiwa Lucas Selelii, Mheshimiwa Issa Mohammed Suleiman, Mheshimiwa Profesa Simon Mbilinyi, Mheshimiwa Musa Lupatu, Mheshimiwa Omar Mjaka Ali, Mheshimiwa Paul Kimiti, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Mheshimiwa Khamis Awesu Aboud, Mheshimiwa Muttamwega Mgaywa na Mheshimiwa Mohamed Missanga. (Makofi) Mheshimiwa Spika, niwatambue waliochangia kwa kauli Mheshimiwa Iddi Simba, Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Mheshimiwa Balozi Getrude Mongella, Mheshimiwa Maria Watondoha, Mheshimiwa Dr. Chrisant Mzindakaya, Mheshimiwa Thomas Ngawaiya, Mheshimiwa Philip Magani, Mheshimiwa Raynald Mrope, Mheshimiwa Stephen Kazi, Mheshimiwa Dr. Hassy Kitine na mwisho Mheshimiwa Paul Kimiti. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tunakubaliana kabisa na hoja alizozitoa Mheshimiwa Iddi Simba, Serikali inakubali kwamba upo umuhimu wa kuanzisha Benki ya Maendeleo ili kusaidia na kuendeleza Viwanda na Kilimo. Kwa sababu sote tunafahamu kwamba tutakapoendeleza kilimo ni pamoja na viwanda na hasa viwanda vya usindikaji, kasi ya kupanda kwa uchumi wa nchi itakuwa ni kubwa sana.Nafikiri hili ni eneo pia aliloligusia Mheshimiwa Dr. Chrisant Mzindakaya. Kwa hiyo, hoja hii kwa kweli Serikali inaichukua na ninaelewa sasa hivi kwamba Serikali inafanya utaratibu wa kuanzisha hiyo Benki ya Maendeleo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, vile vile tunakubaliana na Mheshimiwa Idd Simba, kwamba hakuna nchi inayoweza kupiga maendeleo bila ya kuwa na miundombinu bora na miundombinu bora hiyo ni pamoja na barabara, mawasiliano na nishati. Nadhani hili ni eneo ambalo sasa hivi Serikali inalifanyia kazi na hata kwenye mikutano ya Kimataifa

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

91

sasa hivi hata yale mabenki yanayofadhili nchi zinazoendelea sasa wameanza kuona kwamba kama wanataka kuzisaidia nchi hizo kwa kiwango cha juu ni lazima msukumo uwekwe katika uboreshaji wa miundombinu. Tanzania tutaendelea kulipigia kelele hili kwa niaba ya nchi za Afrika ili hata misaada tutakayopata iendeleze miundombinu hasa barabara. Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, amezungumzia suala la takwimu na mimi nakubali kwamba takwimu ni muhimu. Lakini sasa hivi msukumo unaotolewa wa kuboresha Ofisi ya Takwimu ya Taifa, nina hakika kwamba tutaongeza uwezo wa kujiimarisha wa uzalishaji bora wa takwimu. Suala la takwimu ni muhimu kama nilivyosema katika hotuba yangu katika kuweka mipango sahihi na kuelewa mwelekeo wa uchumi tunaelekea wapi. Mheshimiwa Spika, vile vile napenda kumhakikishia Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kweli lengo lake ni kuona kwamba katika kipindi kijacho maendeleo yanakua kwa kasi kubwa zaidi. Kwa hiyo, programu tulizozipanga kwa mfano MKUKUTA, MKURABITA tuna hakika utekelezaji wake utafuatilia hadi ngazi za chini. Mheshimiwa Spika, hoja ya kuwa Serikali haijaweka kipaumbele katika elimu si sahihi tunao ushahidi wa MMEM, tunao ushahidi wa MMES. Lakini vile vile hata dhana zima ya kufuta ada za shule na kuendeleza Vyuo Vikuu ni viashirio vya kutosha kuonyesha juhudi za Serikali katika kuendeleza suala la elimu. Kwa vile CCM itaongoza tena miaka mitano ijayo kauli ya Waziri Kivuli Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, itakuwa haina nguvu baada ya kipindi hicho cha miaka mitano, tunamhakikishia kabisa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kimsingi Serikali imelipa mafao yote ya kisheria kwa wafanyakazi waliokuwa kwenye viwanda vilivyobinafsishwa. Eneo lililobakia ni pale malipo yatokanayo na mikataba ya hiari na malipo ya pensheni. Pensheni ambayo haikukabidhiwa kwenye vyombo husika au Taasisi husika wakati zilipohitajika zifanyike hivyo na ndiyo maana Serikali sasa hivi inapanga bajeti ya pensheni katika bajeti yake kupunguza tatizo hilo. Nina hakika jinsi tunavyoendelea tatizo hili litakuwa limepungua. Mheshimiwa Spika, vile vile labda Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, afanye utafiti wake vizuri katika ubinafsishaji wa Mashirika ya Mashamba ya NAFCO kule Hanang, mashamba mawili makubwa yamegaiwa moja kwa moja kwa wananchi. Kwa hiyo, siyo kwamba mashamba yote yamebinafsishwa. Mheshimiwa Spika, hali ya uchumi bado tunaendelea nayo kwa muda katika kipindi hiki cha kurekebisha uchumi. Aidha, pembejeo nyingi na malighafi nyingi tunazotumia mara nyingine tunaziagiza kutoka nje. Kwa mfano, mafuta na kadhalika na hiyo huchangia katika kuongezeka kwa gharama za uzalishaji. Lakini sasa hivi tunaelewa kwamba bei ya mafuta imepanda kwa kiwango kikubwa sana mpaka kufikia zaidi ya dola 50 kwa pipa na wakati miaka minne, mitano iliyopita ilikuwa ni dola 25 kwa pipa. Tuna hakika matumizi mapana ya gesi ya

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

92

Songosongo na ya Mnazi Bay itapunguza gharama za ughali wa uchumi wetu na kwa sababu tumeanza mwaka jana mwishoni jinsi tutakavyozidi kupanua matumizi ya gesi hiyo kwa vyovyote vile gharama zitapungua. Mheshimiwa Spika, TIC inafanya kazi kwa tija na ufanisi na TIC katika sheria zake haina mahali popote ambapo inaruhusiwa kutoa misamaha ya kodi. Sasa dhana ya kusema kwamba TIC inatoa misamaha ya kodi si dhana sahihi. Lakini vile vile napenda kumhakikishia Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, kwamba mwaka 2004 Kituo chetu cha Tanzania Investment Centre kimekuwa Kituo cha kwanza bora Barani Afrika kwa kazi nzuri iliyofanyika. (Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini itabidi tuongeze juhudi kwa sababu mkakati wa sasa ni kuongeza uwekezaji kama tunavyosema siku zote investment drive lazima iwe kubwa na ndiyo maana Serikali ya CCM safari hii imekuja na mkakati wa kuendeleza uchumi haraka (Tanzania Mini Tiger Plan) na tukasisitiza uanzishwaji wa maeneo maalum ya uwekezaji kwa maana ya Special Economic Zones na Export Processing Zones tunadhani kwamba haya yatakuwa ni maeneo ambayo yataongeza kasi ya kukuza uchumi wetu. Mheshimiwa Balozi Getrude Mongella nakubaliana naye kuwa uchumi jumla utiririke kwa wananchi hivi sasa. Hili ndilo alilolizungumza pia Mheshimiwa Paul Kimiti na alilolizungumzia pia Mheshimiwa Dr. Hassy Kitine. Tunapoendelea na suala zima la urekebishaji wa uchumi wetu changamoto kubwa tunayoipata ni kwamba ni jinsi gani mafanikio ya uchumi jumla yanawafikia wananchi Vijijini. Kwa maana ya macro inafikaje kwenye micro level. Mimi nadhani mkakati wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi wa kupunguza umaskini usio wa kipato kupitia elimu, afya, maji ni mwanzo mzuri. Lakini sera ya uwezeshaji MKURABITA, sera ya kuendeleza viwanda vidogo na vya kati, sera ya mikopo, msukumo mkubwa hasa kwa kwenye kilimo na uboreshaji wa miundombinu itasaidia sana kukuza ajira na kuongeza mapato na hivyo kupunguza umaskini wa kipato. Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Balozi Getrude Mongella, vile vile nakubaliana na Mheshimiwa Maria Watondoha, kuwa ipo haja ya kuendeleza elimu nchini ili tupate nguvu kazi yenye ujuzi. Tunahitaji walimu wengi tupambane na changamoto ya mafanikio, MMEM na MMES imeshajionyesha kwamba ni mafanikio. Pamoja na dhana kwamba itakuwa siyo vizuri kujenga Shule za Sekondari katika kila Kata. Lakini ningemshauri Mheshimiwa Maria Watondoha, tujitahidi kuhamasisha wananchi kila itakapowezekana, ikiwezekana tujenge Shule za Sekondari katika kila Kata ya nchi hii tutakuwa tumemaliza tatizo moja, tutabakia na tatizo lingine. Lakini ujenzi wa Shule za Sekondari ni muhimu sana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Maria Watondoha kwamba dhana ya Lindi kuwa Mkoa wa nyuma itakwisha baada ya muda si mrefu kuanzia sasa. Serikali imekuwa ikipeleka rasilimali nyingi sana katika Mikoa ya Kusini hasa katika uboreshaji wa miundombinu. Hivi sasa barabara zinajengwa na hivi sasa tunaendelea na mradi wa Mtwara Corridor. Lakini vile vile hata Mradi wa gesi ya Mnazi Bay utaleta mafanikio makubwa sana katika Mikoa ya Kusini.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

93

Mheshimiwa Spika, lakini ni vyema tuchukue tahadhari aliyoitoa Mheshimiwa Philip Magani, kwamba pamoja na kuibua rasilimali hizi ili zitoe huduma za kukuza uchumi wa maeneo haya kama huduma hizi tusipozitumia kikamilifu basi jitihada zote hizi zitakuwa cosmetic, kama alivyosema Mheshimiwa Philip Magani, itakuwa tunaziangalia tu fursa hizi na wanaofaidika na huduma hizo ni maeneo mengine na siyo maeneo yale ya Mikoa ya Kusini. Fursa zinapoibuliwa zitumike vizuri na uelewa wa wananchi vijijini wa mpango wa MKUKUTA na MKURABITA ni muhimu sana katika kuendeleza jitihada hizo. Mheshimiwa Dr. Chrisant Mzindakaya, napenda kumhakikishia yeye na Watanzania wote kuwa Mashirika yetu yote ya miundombinu kama vile TRC na Bandari hayatauzwa, Mashirika haya yatakodishwa. Hili kwa kweli tunalisisitiza tutayakodisha tu, hakuna Mashirika ambayo yatauzwa na ndiyo maana nimesisitiza kwamba ubinafsishaji wa sasa wa miundombinu hii kama alivyosema Mheshimiwa Dr. Hassy Kitine, inabidi tuufanye kwa makini sana. Kwa sababu uzoefu umetuonyesha katika nchi mbalimbali zilizobinafsisha reli kwa kuiuza zimejikuta zina matatizo mengi sana pamoja na nchi zingine zilizoendelea hata Uingereza walibinafsisha reli kwa kuiuza na walipata matatizo makubwa sana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, napenda kuwahakikisha wananchi wote kwamba Mashirika haya yatakodishwa na wala hayatauzwa. Nikubaliane na yeye Mheshimiwa Dr. Chrisant Mzindakaya, ametoa takwimu sahihi kwamba ile akiba tunayoipata kwa mwezi kutokana na msamaha ule wa madeni ni kweli ni shilingi bilioni 5 kwa maana ni dola milioni 5. Namhakikishia kwamba Serikali itazielekeza fedha hizo kwenye uboreshaji wa miundombinu pamoja na kuendeleza huduma za jamii. (Makofi) Mheshimiwa Spika, suala la mishahara ya Serikali kwamba inaweza kupanda nadhani hili litawezekana tukiongeza jitihada za kukuza uchumi wetu. Mimi nafikiri ni vizuri tuwahamasishe wananchi kwamba tunapozungumzia matumizi, tuwe tumekwishajiandaa na jinsi ya kuongeza mapato yetu ili kukidhi matakwa na haja mbalimbali katika uchumi wetu. Mheshimiwa Thomas Ngawaiya, leo ameisifu mipango ya Serikali ya CCM tunakushukuru sana. Ameisifu mipango ya CCM mpaka akasema yeye anapoingia hapa Bungeni hawakilishi Chama, yeye anawakilisha wale anaowawakilisha. Inatia faraja sana kwamba mipango yake mingi imekamilika. Nimhakikishie kwamba mipango yetu hivi sasa ni yetu wenyewe si mipango ambayo iunatekelezwa kutoka nje. Kwa sababu kama mipango inayotekelezwa kutoka nje ingekuwa vigumu sana sisi kuendelea na utaratibu wa cash budget. Lakini mipango tunaipanga sisi wenyewe na nimhakikishie vile vigezo vinavyowekwa ni vya Kimataifa tu kuna 2025, kuna 2020, sasa hata Cotounou Agreement kama utaona kwamba tumeonyesha 2025 kukuza uchumi wa nchi zinazoendelea kwa kweli ile ni International Standard ya kutuweka mahali pazuri. (Makofi)

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

94

Mheshimiwa Spika, vile vile lazima tukubali kwamba mara nyingine tunashindwa kutekeleza uendeshaji wa shughuli zetu za kiuchumi kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi, management bora na nidhamu ya kazi na hii ni changamoto kubwa sana kwetu. Mheshimiwa Philip Magani, amesisitiza hoja aliyoitoa Mheshimiwa Dr. Chrisant Mzindakaya, kwamba Mashirika ya miundombinu yasiuzwe. Narudia Mashirika hayo hayatauzwa yatakodishwa. Tutaendelea kufungua ofisi za Kanda kwa TIC na tutawashauri Wizara ya Nishati na Madini kuwatembelea wachimbaji wadogo Ruangwa ili Wizara hiyo ione itawasaidiaje. Lakini la msingi hao watasaidiwa vizuri kama watakuwa organized. Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Raynald Mrope, kuwa Serikali itafanya kila jitihada za kuhakikisha kuwa mipango inayoelekezwa Mikoa ya Kusini itakuwa na lengo la kuibua fursa zilizopo ili kukuza maendeleo ya eneo hilo na ushauri wake kuhusu kuanzisha Secretariet ya Mtwara Corridor iwe chini ya Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji, ushauri huo tutaupeleka mbele. (Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini vile vile katika kuhamasisha ukuaji wa uchumi katika Mikoa ya Kusini nafikiri atakumbuka kwamba kulikuwa na Semina ya Uwekezaji iliyofanyika Mtwara Agosti, 2004 ambapo wawekezaji wengi walikutanika kule kuelezea fursa zilizopo katika kuwekeza katika eneo la Mikoa hiyo ya Kusini. Mheshimiwa Spika, lakini vile vile wakati wa kuchangia hoja hapa Mheshimiwa Maria Watondoha, alizungumzia adha ya usafiri wanayoipata wakulima wa ufuta wa Kijiji cha Kiwawa huko Milola. Tatizo la barabara Milola hadi Kiwawa limekuwa likifuatiliwa vizuri sana na Mbunge wa huko Mheshimiwa Mudhihir Mudhihir na taarifa tulizozipata ni kwamba ufumbuzi umepatikana na barabara ile imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 96.79 kwa ajili ya tatizo la barabara la Milola hadi Kiwawa. Mimi nafikiri tatizo hilo litamalizika sasa. (Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini nikubaliane na Mheshimiwa Maria Watondoha, kwamba sasa hivi tunapotengeneza barabara zetu za Wilayani kwa utaratibu wa TANROADS haileti maana sana kusambaza fedha kidogo katika maeneo makubwa ni vizuri ukatumia utaratibu wa kawia ufike ili barabara zile tunazozikarabati tuhakikishe haturudii tena kuzikarabati. Lakini vile vile upo umuhimu wa kuanza kufungua barabara za Makao Makuu ya Kata kwenda Vijijini. Kwa hiyo, ushauri alioutoa ni ushauri mzuri tu. Mheshimiwa Spika,Mheshimiwa Dr. Hassy Kitine, ni kweli sisi Tanzania tuna changamoto kubwa sana ingawa tunasema uchumi wetu unakua kwa asilimia 6.7 bado tunahitajika kufanya kazi kubwa sana.Uchumi wetu sasa hivi unatakiwa ukue kati ya asilimia 8 hadi 10 ili ukuaji wetu wa uchumi ulingane na ukuaji wetu wa idadi ya watu. Sasa Mipango ya Familia (Family Planning) inafanyika kuna Nyota ya Kijani, kuna matumizi ya vidonge vya uzazi na sasa hivi kuna matumizi ya kondomu, zote hizo ni njia mojawapo ambazo watu wanatumia katika kuhakikisha kwamba tunadhibiti uzazi holela.

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

95

Mheshimiwa Spika, lakini suala hili vile vile pia linagusa mambo ya kijamii na vile vile ni la kisiasa. India walipoleta utaratibu wa kudhibiti watu kuzaliwa ilileta vurugu kubwa sana na sasa hivi habari tunazozifahamu ni kwamba population structure ya Wachina, Wachina wengi bado wamekuwa ni vijana, wengi ni vijana sasa, lakini vile vile watoto hao hao waliozaliwa na Wachina wamefika wakati ambapo wamejiingiza katika matatizo mengi sana ya uadilifu kwa sababu ya kudekezwa sana. Sasa hizo ni sociological study ambazo zinafanyika ambazo na sisi vile vile inabidi tuzizingatie. Mheshimiwa Spika, nakubaliana kwamba ukosefu wa ajira kwa takwimu za mwaka 2002 Tanzania ilikuwa ni asilimia 13, lakini inawezekana kabisa asilimia hii ikaendelea hasa Mijini na nakubali kwamba Foreign Exchange Reserves zetu ni lazima zitokane na uzalishaji mali nchini badala ya kutegemea mikopo kutoka nje na maendeleo vijijini ni muhimu kwa sababu tunaelewa kwamba maendeleo hayo yatapunguza watu wengi kwenda Mijini kutoka Vijijini. Wenzetu wa China tatizo wanalolipata sasa ni kuwaondoa watu kutoka Vijijini kwenda Mijini na sisi tunapata tatizo la kuwaondoa watu Mijini kwenda Vijijini sasa hizo ni gymnastics za uchumi ambazo zinaendana na mazingira ya kiuchumi yalivyo katika maeneo mbalimbali. Mheshimiwa Spika, nakubaliana kuna miundombinu ya aina tatu. Kuna miundombinu migumu, kuna miundombinu laini, lakini vile vile kuna miundombinu ya kitaasisi ambayo tunatakiwa tuiendeleze ili tuweze kukuza uchumi wetu. (Makofi) Mheshimwia Dr. Hassy Kitine, kama alivyosema reli haitauzwa itakodishwa, ninakubaliana kwamba ni lazima viwanda vyetu vijifunze taratibu za ushindani kwa sababu tunajua uchumi hodhi ule wa monopoly kwa kweli unaharibu rasilimali. Sasa hii habari ya sigara tunaifahamu na nadhani iko katika mfumo wa Serikali na linafuatiliwa hilo kuona kwamba kila kiwanda kinapata mazingira mazuri ya ushindani ili watu washindane kwa kuzalisha kwa tija na ufanisi badala ya ule ushindani wa kukatana makoo. Mheshimiwa Paul Kimiti, amezungumzia taarifa ya uchumi ni nzuri kwamba uchumi wetu lazima ukue kulingana na idadi ya watu kitu ambacho nimeishakizungumzia. Lakini vile vile amezungumzia masuala ya tofauti za uwekezaji wa mitaji katika maeneo mbalimbali ya Mikoa yetu iendane na ifuatiliwe kutokana na takwimu tunazoziandaa nadhani hilo ni la msingi sana. Sera ya idadi ya watu ipewe umuhimu, nakubali, ujasirimali ni muhimu kuwa na elimu na sera ya uwezeshaji yote hayo ni muhimu na kama tunavyojua Waheshimiwa Wabunge mambo yote hayo yamefuatiliwa vizuri sana na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kama hayajaanzishwa ni mambo ambayo tunatarajia kuyaendeleza katika kipindi kinachofuata. Mheshimiwa Musa Lupatu, aliulizia kuhusu tatizo la mafao ya wafanyakazi katika mashamba ya Mkonge. Mafao hayo yalilipwa mwaka 1997 lakini yalitokea malalamiko ya kupunjwa kwa mafao hayo. Serikali kupitia PSRC inalifuatilia suala hilo kubaini ukweli. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Katani Limited. Sasa hivi Katani Limited wamesharudisha mashamba nane Serikalini na pamoja

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

96

na kurudisha mashamba hayo nane Serikalini, sasa hivi Katani Limited wataingia ubia na wakulima wadogo wadogo wa katani kumiliki mashine za kusindika katani katika mashamba hayo. (Makofi) Mheshimiwa Profesa Simon Mbilinyi amezungumzia kama wachumi wote bado wanasimamiwa na Wizara ya Mipango na Ubinafsishaji ni kweli wachumi wote wako chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji na Mheshimiwa Aziza Sleyum Ali ameulizia kuhusu hoteli ya Mikumi, bado ina mgogoro wa kisheria tutakapomaliza hapo utaratibu wa ubinafsishaji utaendelea. Pia Mheshimiwa Issa Mohammed Suleiman, tumepokea masahihisho uliyotuletea katika kitabu kile, figure za ukurasa wa tano, tumeona kwamba siyo sahihi kuhusu maelezo ya visiwa vya Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Leonard Derefa, Serikali sasa inaendelea na jitihada za kupata wawekezaji kwa kiwanda cha nyama. Kulikuwa na tatizo la je, ubinafsishaji ule uhusishe pia eneo la kuwekea mifugo, sasa hili tumeshalimaliza ni kwamba ubinafsishaji wa kiwanda kile vile vile uhusishe ile holding ground ya mifugo. Kwa hiyo, kiwanda hicho sasa Serikali inahimiza kwa dhati kabisa wafanyabiashara wa Mkoa wa Shinyanga pia wakijitokeza tuweze kufanya taratibu ya wao kuweza kukimiliki na kuendesha kiwanda hicho kwa faida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimejaribu kwa uwezo tuliokuwa nao wa kujibu baadhi ya hoja nyingi ambazo zimetolewa na Waheshimiwa Wabunge. Tumeshaandaa majibu kwa ufasaha na kwa kina zaidi na kama kawaida ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji tutafanya utaratibu wa kutoa nakala za majibu hayo ili kila Mheshimiwa Mbunge aweze kuwa na nakala hiyo. Mwisho, napenda kuchukua fursa hii na mimi kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa ushirikiano mzuri tuliokuwa nao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Tumeshirikiana vizuri na nina hakika kwamba ushauri wenu ndio umefanya hata uchumi wetu ukakua kufikia hapa tulipo. Kwa sababu bila ya mchango wenu Serikali ingekosa input ambayo ni muhimu sana katika kuendeleza maendeleo yetu kwa ujumla na uchumi wetu wa nchi kwa ujumla wake. Mheshimiwa Spika, kama walivyosema wenzangu nami nachukua fursa hii kukushukuru na kukupongeza sana kwa jinsi ulivyotuongoza ndani ya Bunge hili. Umefanya kazi kubwa sana, tumekuwa tukikutegemea kwa ushauri na kwa kweli session nyingi za Bunge ziliendelea vizuri chini ya usimamizi wako. Tunakuombea kila la kheri baada ya kufunga Bunge hili kwa njia moja au nyingine tuonane mahali pengine tena. Kama sio hapa Bungeni sehemu nyingine. Lakini tunakuombea kila la kheri. Nichukue fursa hii adimu kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo la Handeni kwa imani yao kubwa waliyonipa.Wamenipa imani kubwa, wamenilea mpaka nilipofikia na wao na mimi tumeleta maendeleo ya kuonekana katika Wilaya yetu ya Handeni. Kwa hiyo, nawashukuru sana na nitakuwa tayari tena kuwatumikia kama kawaida yangu kwa ufanisi mkubwa sana. Waheshimiwa Wabunge wote waliopo hapa kwa uwezo wa Mwenyezi

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

97

Mungu nawaombeni tukutane tena katika Bunge lijalo. Tumeishi kwa mazoea mazuri, kwa mahusiano mazuri, tumejenga undugu wakati wa kuleta maendeleo ya nchi yetu, nafikiri hili ni zuri zaidi. Kwa hiyo, Mungu atatusaidia tutarudi tena. (Makofi) Mheshimiwa Spika, shukrani zangu za mwisho kwa familia yangu. Natoa shukrani zangu kwa Rasul, Omar, Jabir na kwa Amina. Naomba Waheshimiwa Wabunge tupitishe hoja hii mtupatie fedha tukasimamie MKUKUTA na MKURABITA chini ya Serikali ya Awamu ya Nne. (Makofi) Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hatua hiyo ya mjadala sasa imekamilika. Katibu hatua inayofuata.

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 66 - Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji Kifungu 1001 - Administration and General ... ... ... ... ... ... 7,711,075,800/= MHE. LEONARD N. DEREFA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka tu nipate clarification. Kwanza napenda nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kusema kwamba lile tatizo la Kiwanda ambacho kilianza kujengwa mwaka 1976 sasa Serikali italimaliza.Lakini wakati nachangia kwa maandishi nilimwomba vile vile anieleze pale Shinyanga Mjini kuna Kiwanda cha National Milling Corporation ambacho kilibinafsishwa na mnunuzi akalipa fedha. Lakini nafikiri leo karibu miaka miwili na nusu kiwanda hicho hakijakabidhiwa. Kwa hiyo, napenda nipate maelezo kwa nini kiwanda hakijakabidhiwa pamoja na kwamba mnunuzi ameshalipa fedha? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa maelezo ya swali la Mheshimiwa Leonard Derefa, kama ifuatavyo. Tatizo la mwekezaji huyo aliyenunua Bohari hilo la National Milling Corporation kwa Kampuni ya Best Link tunalifahamu na tumekwisha kulitathmini sisi na PSRC nadhani haitachukua muda mrefu kwa kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha kwamba yule ambaye yumo katika godown lile anaondoka ili tumwachie huyo mwekezaji aliyetoa hizo fedha.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

98

MHE. MUTTAMWEGA B. MGAYWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishukuru kwa kunipa nafasi hii kuweza kupata ufafanuzi wa mambo mawili kutoka kwa Mheshimiwa Waziri. Kwanza naomba nimpongeze kwamba anajitahidi. Pili, ni kwamba nilikuwa nimemwomba Mheshimiwa Waziri anisaidie mambo mawili. Mojawapo ni kwamba wageni tunawapa tax holiday ambayo ni karibu miaka mitano, nikaomba kwamba na sisi ambao tunataka ku-invest vijijini. Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kutoa tax holiday kwa ajili ya investment ya vijijini ili vijana wasiondoke vijijini kwenda mijini kutafuta kazi. Halafu lingine ilikuwa ni kuhusu investment ya madini ambayo niliwahi kuiongea mara nyingi sana kwamba katika eneo letu la Jimbo la Mwibara eneo lote sasa hivi liko chini ya wazungu na wanaotakiwa wachimbe ni wazungu peke yao. Nilikuwa nimeiomba Wizara, nimewahi kwenda mpaka Wizarani nikawaomba kwamba hivi sasa Watanzania wanaoishi Mwibara wanao uwezo wa kupata vifaa kama walivyonavyo Geita na Nyamongo, hawakunisikia. Nikawaambia kwamba haya yatatupa matatizo makubwa sana. Kwa mfano juzi kumetokea mauaji Nyamongo, wananchi wameuawa kwa sababu walikuwa wanakwenda kuiba mafuta ya taa. Inafikia wananchi wanaozunguka migodi wanakwenda kutafuta mafuta ya taa, wanauliwa na hii yote inatokana na umaskini ambao tunaowatakia. Sasa nikasema kwamba wananchi wa jimbo langu hawatakiwi kuwa vibarua wa mzungu ndani ya migodi hiyo, wanatakiwa wao wenyewe ndio wachimbe na uwezo wa kuchimba tunao kama walivyo Geita na tukaiomba Wizara kwamba tuko tayari kutoa asilimia 20 badala ya asilimia 3 ambayo inatolewa na hao wazungu. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri utoe kauli yako kwamba je, uko tayari kugawa upya eneo la jimbo la Mwibara lenye madini ili Watanzania wanaoishi pale waweze kuchimba na kuipatia nchi yetu kodi kama mnavyotaka. Ahsante. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumjibu Mheshimiwa Muttamwega Mgaywa, Mbunge wa Mwibara, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, dhana ya tax holiday ilikwishamalizika. Tulifuta utaratibu wa tax holidays. Kwa hiyo, hakuna mwekezaji yoyote anayepata tax holiday hivi sasa. Tumelizungumza mara nyingi sana hapa Bungeni kwamba sasa hilo limekwishafutwa. Lakini la pili, kwanza nasikitika sana kama wananchi wako wameuawa kwa sababu ya kwenda kuiba mafuta ya taa. Naomba uwashauri wasifanye hivyo kwa sababu inawapa matatizo ambayo sio lazima. Lakini vile vile kama kweli wananchi wa Mwibara wana uwezo sasa wa kufungua migodi na sidhani kama eneo lote la Mwibara sasa hivi limechukuliwa na hao wazungu na kama hivyo ndivyo, mimi nafikiri ni vizuri Mheshimiwa Mbunge, mimi, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini tukakaa pamoja tukaona tutalifanyia utaratibu gani suala hilo. (Makofi) MHE. MUTTAMWEGA B. MGAYWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kuuawa watu ni jambo zito, naomba Mheshimiwa Waziri utoe kauli yako kama unadhani

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

99

ni sahihi hawa Watanzania waliouawa na wageni kwa sababu ya madini katika hili eneo la Nyamongo. Sio eneo langu na nisingependa niliongelee sana lakini kwa sababu ni Watanzania wenzangu ninaongea hivyo. Mheshimiwa Spika, ila ninachosema ni kwamba nimewahi kufika katika Wizara, nilichojibiwa ni kwamba eneo wameshapewa wazungu na ninachoweza mimi kama nitawaambia wananchi wasiondoke basi hakuna tatizo wao watapita chini, sisi tutabaki juu halafu tukirudi chini wao watakuja juu. Nilijibiwa hiyo kauli na Wizara kwamba wao hawana shida wana uwezo watachimba chini. Sasa hiyo ni kauli ya jeuri kwa Watanzania. Ndiyo maana nasema hili suala sio masihara nataka Hansard irekodi kwamba hata kama namaliza kipindi changu cha Ubunge sikuridhika na ardhi ya wananchi wale kumilikishwa wageni bila hiari yao. Hili moja. Pili, ninaomba utoe hiyo kauli kwamba je, nikija Wizarani tutakaa na kupata muafaka huo unaosema au ni ile porojo ya kumaliza Bunge ili niwaambie wananchi ukweli halisi kwamba twendeni tukachukue vibali tuchimbe maadamu uwezo tunao. (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bungeni si mahali pa kutoa porojo na kauli za Serikali si porojo. Nimesimamia Wizara ya Nishati na Madini kwa muda wa miaka miwili, nimekushauri wewe pamoja na mimi na Waziri wa Nishati na Madini tukae tuangalie hali hiyo ili tuipatie ufumbuzi. Sasa hiyo sio porojo.(Makofi) Lakini la pili, nikuhakikishie sifurahii wala sipendi kusikia Watanzania wanapoteza maisha yao kutoka kwa wawekezaji wowote wale awe wa nje au wa ndani kwa sababu huo sio msingi wa kuendesha nchi. Lakini ninachosema ni kwamba kwa sababu uliyoitoa kwamba wamekwenda kuiba mafuta ya taa. Nimesema uwashauri utaratibu huo sio mzuri, hicho ndicho nilichosema. (Makofi)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kifungu 1002 - Finance and Accounts... ... ... ... ... ... ... ... ... ...294,731,200/= Kifungu 1003 - Policy Information Development ... ... ... ... ...626,134,600/= Kifungu 2001 - Macro-Economy... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...551,793,900/= Kifungu 2002 - External Sector ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 525,492,500/= Kifungu 3001 - Social Services and Human Resource Development ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 525,150,200/= Kifungu 5001 - Public Investment Planning... ... ... ... ... ... ... ...541,412,200/= Kifungu 5002 - Growth Strategies... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 1,804,528,100/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MIPANGO YA MAENDELEO

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE ...parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1466055636-HS...1 BUNGE LA TANZANIA _____ MAJADILIANO YA BUNGE _____ MKUTANO WA ISHIRINI KIKAO CHA

100

Fungu 66 - Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji

Kifungu 1001 - Administration and General ... ... ... ... ... ... 9,791,637,000/= Kifungu 1003 - Policy Information Development .. ... ... ... 1,155,000,000/= Kifungu 2001 - Macro-Economy... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 57,300,000/= Kifungu 2002 - External Sector ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 4,160,000,000/= Kifungu 3001 - Social Services and Human Resource Development... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... 276,727,600/= Kifungu 5001 - Public Investment Planning ... ... ... ... ... ... ... ..95,000,000/= Kifungu 5002 - Growth Strategies ... ... ... ... ... ... ... ... ... ... ...5,476,646,600/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa kwamba baada ya Bunge lako Tukufu kukaa kama Kamati ya Matumizi na kupitia kifungu kwa kifungu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2005/2006 kwa ajili ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji na limeyapitisha bila ya mabadiliko yoyote. Naomba kutoa hoja kwamba Makadirio hayo sasa yakubaliwe. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi) WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naafiki. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji

yalipitishwa na Bunge)

(Saa 12.13 jioni Bunge liliahirishwa mpaka siku ya Jumatano Tarehe 27 Julai, 2005 saa tatu asubuhi)