´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    1/32

    www.alhidaaya.com

    ’Aqiydah Ya Maimaam Wa

    Hadiyth 

     اعتقد ئة الحث

    اسعي

     

    بكر

     

    م بي

    Imaam Abu Bakr Ismaa`iyliy

    (277-371)

    Mfasiri:

    Abu Bakr al-Khatwiyb al-Atrush

    Imepitiwa Na:

    Abu ‘Abdillaah Muhammad Baawazir

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    2/32

    www.alhidaaya.com

    YALIYOMO

    Msingi Wa Itikadi Ya Ahlul-Hadiyth ..............................................................................4

    Kauli Kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake ...............................................................4

    Baadhi Ya Vipimo Hususan Vya Ubwana Wake ..........................................................5

    Kuthibitisha Asmaauhu Al-Husnaa (Majina Mazuri) Ya Allaah Na Swifaatuhul

    `Ulaa (Sifa Zake Kuu) .........................................................................................................5

    Kuthibitisha Sifa Ya Mikono ............................................................................................5

    Kauli Yao Kuhusu Sifa Ya Uso Wake, Kusikia Kwake, Kuona, Elimu, Uwezo Na

    Maneno Yake ........................................................................................................................6

    Kuthibitisha Mashiy-ah (Matakwa) Ya Allaah ..............................................................9Elimu Ya Allaah..................................................................................................................10

    Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah........................................................................................10

    Matendo Ya Waja Yameumbwa Na Allaah ..................................................................10

    Kheri Na Shari Inatoka Kwa Allaah ..............................................................................13

    Kushuka (Kwa Allaah) Katika As-Samaa' Ad-Dunyaa (Mbingu Ya Dunia).........13

     Waumini Kumuona Mola Wao Aakhirah .....................................................................14

    Ukweli Wa Iymaan ............................................................................................................15

    Kauli Yao Kuhusu Yule Mwenye Kufanya Madhambi Makubwa .........................15

    Hukmu Ya Mwenye Kuacha Swalah Kwa Makusudi................................................16

    Kauli Za Wanachuoni Kuhusu Tofauti Kati Ya Uislamu Na Iymaan .....................17

    Shafaa’ah (maombezi), Hawdh (Kisima cha Mtume), Ma’aad (Qiyaamah) NaHesabu..................................................................................................................................19

    Kutoa Ushuhuda Mmoja Katika Watu Wa Tawhiyd Kwa Pepo Au Moto.............19

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    3/32

    www.alhidaaya.com

    Adhabu Ya kaburi..............................................................................................................20

    Maswali Ya Munkar Na Nakiyr ......................................................................................22

    Kuacha Ugomvi Na Majadiliano Katika Dini..............................................................22

    Ukhalifa (Uongozi) Wa Al-Khulafaa' Ar-Raashiduwn ...............................................23

    Ubora Baina Ya Maswahaba ............................................................................................23

    Kauli Yao Juu Ya wale wanaowachukia Maswahaba.................................................24

    Swalah Ya Ijumaa Nyuma Ya Kila Imaam Muislamu, Sawa Wakiwa Wema Au

     Waovu...................................................................................................................................27

     Jihaad Pamoja Na Viongozi Hata Kama Waovu..........................................................28

    Nchi Ya Kiislamu ...............................................................................................................28

    Matendo Ya Waja Hayawajibishi Kuingia Peponi, Bali Ni Kutokana Na Fadhila

    Za Allaah..............................................................................................................................28

    Allaah Ndiye Ar-Razzaaq (Mwenye Kuruzuku Daima)............................................29

    Allaah Ndiye Kaumba Mashayatwiyn Na Wasiwasi Wao ........................................30

    Uchawi Na wachawi ..........................................................................................................30

    Kujitenga Na Bid’ah ..........................................................................................................30

    Kujifunza Elimu.................................................................................................................31

    Kujizuia [Kuwaongelea Vibaya] Maswahaba .............................................................31

    Kushikamana Na Jamaa’ah ..............................................................................................31

    Uwajibu Wa Kushikamana Na Madh-hab Ya Ahlul-Hadiyth, Firqatun-Naajiyah 

    (Kipote Kitakachookoka) .................................................................................................31

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    4/32

    www.alhidaaya.com

    Ibn Qudaamah kasema: Ametujulisha ash-Shariyf Abul-´Abbaas Mas´uud bin

    ´Abdil-Waaahid bin Matwar al-Haashimiy kasilimulia na kusema: Haafidh Abul-

    ´Alaa Sa´iyd bin Yasaar al-Harawiy katusimulia: Abul-Hasan ´Aliy bin

    Muhammad al-Jurjaaniy katusimulia: Abul-Qaasim Hamzah bin Yuusuf as-

    Sahmiy katusimulia: Abu Bakr Ahmad bin Ibraahiym Ismaa´iyliy kasema: 

    Msingi Wa Itikadi Ya Ahlul-Hadiyth

     Jua – Allaah Atubariki sisi na ninyi ya kwamba Madhehebu ya Ahlul-

    Hadiyth, Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah imejengwa chini ya msingi wa

    kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake na kukubali yale

    yaliyokuja katika kitabu cha Allaah (Ta´ala), na yale yaliothibiti katika

    riwaya sahihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa

    sallam).

    Hakuna kuyafanyia ta-awiyl yale yaliosimuliwa kutoka Kwake na wala hakuna

    nafasi ya kuyakataa. Yote haya kwa kuwa wameamrishwa kufuata Kitabu

    na Sunnah. Wanaamini kuwa yote yana uongofu na wanashuhudia kwamba

    Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) anaongoza katika Njia

    iliyonyooka wakati huohuo wanachukua tahadhari kwenda kinyume naye

    kutokana na fitnah na adhabu iumizayo isije kuwapata. 

    Kauli Kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake 

    Na wanaitakidi kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anaombwa kwaMajina Yake mazuri ambayo Kajiita Kwayo Mwenyewe, na Sifa Zake ambazo

    Kajisifia nazo Mwenyewe na kwa Majina na Sifa ambazo Mtume Wake (Swalla

    Allaahu ´alayhi wa aalihi wa sallam) kamsifu au kumueleza Kwazo. Alimuumba

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    5/32

    www.alhidaaya.com

    Aadam (´Alayhis Salaam) kwa Mkono Wake. Mikono Yake ni mikunjufu

    na Huitumia Apendavyo, bila Kayf (kutaka kujua vipi au ikoje). Hakika Allaah

    (Ta’ala) istawaa  juu ya ’Arshi Yake na Hakueleza istiwaa  (Kuwa Kwake juu ya

    ’Arsh) Yake ni vipi na kukoje!

    Baadhi Ya Vipimo Hususan Vya Ubwana Wake 

    Yeye ndiye Mmiliki wa uumbaji Wake. Hakuumba kwa sababu Anafanya lolote

    Atakalo na Anahukumu kama Apendavyo. Haulizwi kwa

    Alifanyalo, lakini viumbe wao wataulizwa kwa yale waliyoyatenda.

    Kuthibitisha Asmaauhu Al-Husnaa (Majina Mazuri) Ya Allaah Na Swifaatuhul

    `Ulaa (Sifa Zake Kuu)

    Yeye huitwa (huombwa) kwa Majina Yake, na Yeye husifiwa kwa Sifa Zake

    Alizojisifia nazo Mwenyewe na alizosifiwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu

    ´alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna kitu chochote katika ardhi wala mbingunikisichowezekana Kwake. Hasifiki kwa kasoro au mapungufu, hakika Allaah

    (Ta’ala) yuko mbali na hayo.

    Kuthibitisha Sifa Ya Mikono

    Alipomuumba Aadam (‘Alayhis Salaam) Alimuumba kwa mikono Yake. Mikono

    Yake ni mikunjufu na Anaitumia Atakavyo, bila ya kuwa na haja ya kuitakidi 

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    6/32

    www.alhidaaya.com

    ikoje mikono Yake, kwa kuwa Kitabu cha Allaah (Ta’ala) hakikuzungumzia ni

    namna gani ilivyo.

    Wala isiitakidike (kwa mtu) ya kwamba Ana viungo, urefu, upana, unene,

    wembamba au mfano wa sifa kama hizo ambazo ni mfano wa sifa za viumbe

    Wake. Na Yeye (Tabaaraka wa Ta’ala) hakuna kitu mfano Wake, umetukukawajihi wa Bwana wetu, Subhaanahu wa Ta’ala.

    Hawaamini kama Mu`tazilah wasemavyo kuwa Majina ya Allaah (‘Azza wa Jalla)

    yameumbwa, kama pia wanavyoamini Khawaarij na makundi mengine katika

    makundi ya watu wa matamanio (Ahlul-Bid’ah).

    Kauli Yao Kuhusu Sifa Ya Uso Wake, Kusikia Kwake, Kuona,

    Elimu, Uwezo Na Maneno Yake 

    Wao wanathibitisha Uso Wake, Kusikia Kwake, Kuona, Elimu, Uwezo, Nguvu,

    Maneno, lakini si kwa njia ya watu wapotofu kama Mu`tazilah na wengine

    wanavyosema, isipokuwa ni kama Yeye (Ta’ala) Alivyosema:

    ِّربك ذو الجالل واإلكرام  ويبقى وجه 

    “Na Utabakia Uso wa Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu” [Ar-Rahmaan

    55: 27].

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    7/32

    www.alhidaaya.com

    Na Anasema:

    َنزله بعلمه  

    “Ameyateremsha kwa kujua Kwake” [An-Nisaa 4: 166].

    Na Anasema:

     من علمه إال بما شا ِشي ِ ٍ ِّ

     وال يحيطون ب

    “Wala wao hawajui chochote katika vilio katika (elimu) ujuzi Wake, ila kwa

    Atakalo Mwenyewe.” [Al-Baqarah 2: 255].

    Vilevile Anasema:

    كلم الطيب والعمل الصالح يرفعه والذين يمكرون السيئات له ِ َّ ِ ِِّ َِّّ ُ َ ُ ُ

    َّ

    من كان يريد العزة فلله العزة جميعا إليه يصعد ال ِ ِ َّ ِ ِ َّ

    ُولئك هو يبور  عذاب شديد ومكر 

    “Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Allaah. Kwake Yeye

    hupanda neno zuri, na ’amali njema Yeye Huitukuza. Na wanaopanga vitimbi

    vya maovu watapata adhabu kali. Na vitimbi vya haovitaondokea patupu.”

    [Faatwir 35: 10].

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    8/32

    www.alhidaaya.com

    Pia kasema:

    َشد منهم قوة َن الله الذي خلقهم هو  َولم يروا ُ ْ ُ

    ِ َّ َّ 

     

    “Kwani wao hawakuona kwamba Allaah Aliyewaumba ni Mwenye nguvu

    kushinda wao? [Fusswilat 41: 15] 

    Pia kasema:

    المتين

     

    القوة

     

    ذو

     

    الرزاق

     

    هو

     

    الله

     

    ََّّإن َّ َّ

     

    “Hakika Allaah ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.”  [Adh-

    Dhaariyat 51: 58].

    Yeye (Subhaanahu wa Ta’ala) Ana Elimu, Nguvu, Usikivu, Uoni, na Maneno,

    kama Yeye (Subhaanahu wa Ta’ala) Anavyosema:

     ولتصنع على عيني

    “Ili ulelewe machoni Mwangu.” [Twaahaa 20: 39].

    بَعيننا ووحينا  واصنع الفلك 

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    9/32

    www.alhidaaya.com

    “Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu.” [Huwd

    11: 37].

    كالم

     يسمع

     حتى

     جره

    َ

    ف

     استجارك

     المشركين

     من

     حد

    َ

     ِّوان

     

    “Na ikiwa mmojawapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi

    apate kusikia maneno ya Allaah.” [At-Tawbah 9: 06].

    َّوكلم الله موسى تكليما  

    “Na Allaah Alizungumza na Muwsaa kwa maneno.” [An-Nisaa 4: 164].

    َن يقول له كن فيكون َراد شيئا  َمره إذا  َّإنما   

    “Hakika amri Yake Anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.” [Yaasiyn

    36: 82].

    Kuthibitisha Mashiy-ah (Matakwa) Ya Allaah

    Wanasema kama wasemavyo Waislamu wote:

    "Kile Apendacho Alllaah hutokea, na kila Asichopenda hakitokei.”

    Kama Alivyosema Allaah (Ta’ala):

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    10/32

    10 

    www.alhidaaya.com

     الله رب العالمين َن يشا َُّّوما تشاؤون إال   

    “Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Mola wa walimwengu wote.” 

    [At-Takwiyr 81: 29].

    Elimu Ya Allaah

    Wanasema kwamba hakuna njia kwa mtu yeyote ya kuweza kuzidi Elimu ya

    Allaah, na wala hakuna tendo la mtu au matakwa yawezayo kushinda Matakwa

    ya Allaah, wala kubadilisha Elimu ya Allaah, kwa kuwa Yeye ni Mwenye ujuzi[elimu] na hatumbukii kwenye ujinga wala kusahau. Yeye ni mwenye Uwezo na

    ambao hakuna awezaye kuushinda.

    Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah

    Wanasema kwamba Qur-aan ni Maneno ya Allaah nahayakuumbwa. Hayakuumbwa jinsi msomaji atavyoyasoma na kuyatamka, na

    yamehifadhiwa kwenye vifua, yakisomwa kwa ndimi, yameandikwa kwenye

    msahafu. Yule atayesema kuwa utamshi wa Qur-aan umeumbwa na akikusudia

    Qur-aan, atakuwa amesema kwamba Qur-aan imeumbwa.

    Matendo Ya Waja Yameumbwa Na Allaah

    Wanasema kwamba hakuna Muumba halisi isipokuwa Allaah (‘Azza wa Jalla).

    Mafanikio ya waja wote yameumbwa na Allaah. Allaah Humuongoza Amtakaye

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    11/32

    11 

    www.alhidaaya.com

    na Humpoteza Amtakaye. Hahojiwi kwa yule ambaye Allaah (‘Azza wa Jalla)

    kampoteza, kama Asemavyo Allaah (Ta’ala):

    جمعين

    َ

     لهداكم  قل فلله الحجة البالغة فلو شا ِ  

    “Sema: Basi Allaah ndiye Mwenye hoja yakukata. Na kama Angelipenda Aangeli

    kuhidini nyote.” [Al-An’aam 6: 149].

    Pia Kasema:

    بدَكم تعودون  كما 

    “Kama Alivyokuumbeni mwanzo ndivyo mtavyorudi” [Al-A´araaf 7: 29].

    Pia Kasema:

    َّفريقا هدى وفريقا حق عليهم الضاللة  

    “Hali ya kuwa kundi moja Amelihidi, na kundi jingine limethibitikiwa na

    upotofu.” [Al-A’araaf 07 : 30 ].

    Pia Kasema:

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    12/32

    12 

    www.alhidaaya.com

    ولقد ذرأنا لجهنم كثيرا من الجن واإلنسِّ

    َّ  

    “Na Tumeiumbia Jahannam majini wengi na watu.” [Al-A´aaraf 7: 179].

    Pia Kasema:

    ها

    َ

    ربن نَ َنفسكم إال في كتاب من قبل  َصاب من مصيبة في األرض وال في  ما ِّ

    ِ ِ

    ِ

    ِ ٍ  

    “Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwishaandikwa

    katika Kitabu kabla Hatujauumba.” [Al-Hadiyd 57: 22].

    ”Nabra-ahaa” maana yake ni kuumba bila ya utata wowote katika lugha.

    Anasema kuhusu watu wa Peponi:

    الله

     

    هدانا

     

    ن

    َ

     

    لوال

     

    لنهتدي

     

    كنا

     

    وما

     

    ذا هـل

     

    هدانا

     

    الذي

     

    ه ِ ِ َِّ لل

     

    الحمد

     

    “AlhamduliLlaah! Kuhimidiwa ni kwa Allaah, ambaye Ametuhidi kufikia haya.

    Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingelikuwa Allaah Hakutuhidi.”  [Al-

    A’araaf 7 : 43].

    Pia Kasema:

     الله لهدى الناس جميعا  َّلو يشا

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    13/32

    13 

    www.alhidaaya.com

    “Allaah Angelitaka bila ya shaka Angeliwaongoa watu wote”  [Ar-Ra`d 13: 31].

    Pia Kasema:

    مختلفين

     

    يزالون

     

    وال

     

    واحدة

     

    مة

    ُ

     

    الناس

     

    لجعل

     

    ربك

     

    شا

     

    َّولو

    ُّ  

    “Na Angelitaka Mola wako Angewafanya watu wote wakawa ummah mmoja.

    Lakini hawaachi kukhitalifiana” [Huwd 11: 118].

    Pia Kasema:

    ربك

     رحم

     من

     ُّإال َّ َّ

     

    “Isipokuwa wale ambao Mola wako Amewarehemu” [Huwd 11: 119].

    Kheri Na Shari Inatoka Kwa Allaah

    Wanasema kwamba kheri na shari, mazuri na mabaya ni kutokana na matakwaya Allaah (‘Azza wa Jalla). Ameyaacha yatokee na kuyakadiria tangu mwanzo

    (kwa hekima Yake), na hayamiliki madhara wala natija – isipokuwa Apendavyo

    Allaah. Wao ni mafukara mbele ya Allaah (‘Azza wa Jalla) Ambaye kamwe hawi

    na haja yao.

    Kushuka (Kwa Allaah) Katika As-Samaa' Ad-Dunyaa (Mbingu Ya Dunia)

    Yeye (‘Azza wa Jalla) Hushuka katika mbingu ya dunia kutokana na mapokezi

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    14/32

    14 

    www.alhidaaya.com

    sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa

    sallam) – bila ya itikadi ya Kayf  (kuuliza Anashukaje).

     Waumini Kumuona Mola Wao Aakhirah 

    Wanasema waja wamchao Allaah watamuona Allaah (‘Azza wa Jalla) Siku ya

    Qiyaamah, si Duniani. Na wale ambao Allaah Amewavika katika mavazi Yake

    Atakuja kuwajaalia hilo siku ya Qiyaamah, kama Alivyosema Allaah:

    وجوه يومئذ ناضرةإلى ربها ناظرة  َ َ َ

    ِّ

    َّ  

    “Zipo nyuso siku hiyo zitakazong’ara, Zinamwangalia Mola wao.” [Al-Qiyaamah

    75: 22-23].

    Yeye (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema kuhusu Makafiri:

    لمحجوبون

     يومئذ

     ربهم

     عن

     إنهم

     َّكال َّ َّ

     

    “Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa (kumuona Allaah).” [Al-

    Mutwaffifiyn 83: 15].

    Ingekuwa Waumini na makafiri wote wasingelimuona (Allaah), wangezuiliwakumuona. Na hili bila ya itikadi ya kumpigia mithali ya mwili Allaah na bila ya

    kumfanyia mipaka. Bali watamuona Allaah (’Azza wa Jall) kwa macho yao kwa

    njia Atakayo, bila ya Kayf (kuuliza namna ipi ).

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    15/32

    15 

    www.alhidaaya.com

    Ukweli Wa Iymaan

    Wanasema kuwa Iymaan ni kauli na matendo na maarifa. Inaongezeka kwa utiifu

    na inapungua kwa maasi. Yule anayetii sana Iymaan yake inazidi kuliko yule

    mwenye utiifu mdogo.

    Kauli Yao Kuhusu Yule Mwenye Kufanya Madhambi Makubwa

    Wanasema ikiwa mmoja katika watu wa Tawhiyd ambaye anaswali kuelekea

    Qiblah cha Waislamu akifanya dhambi, au madhambi; makubwa, au madogo

    pamoja na kuwa ana itikadi ya Tawhiyd kwa Allaah huku akikubali yale ambayo

    Allaah kamuwajibishia juu yake, hahukumiwi kuwa kafiri kwa sababu ya

    kufanya hayo [madhambi]. Wanamtarajia [mtu huyo] msamaha. Anasema

    (Subhaanahu wa Ta’ala):

     ويغفر ما دون ذلك لمن يشا

    ”Na Husamehe mengine yasiyokuwa hayo (Shirk) kwa amtakaye.” [An-Nisaa 4:

    48].

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    16/32

    16 

    www.alhidaaya.com

    Hukmu Ya Mwenye Kuacha Swalah Kwa Makusudi 

    Wametofautiana juu ya mtu ambaye kaacha swalah za faradhi kwa makusudi na

    bila ya dharurah mpaka muda wake ukatoweka. Baadhi yao wamewakufurisha

    kutokana na riwaya zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi

    wa sallam):

    ك الصال الک و العب  

    “Baina ya mja na baina ya Kufru [ukafiri] ni [mtu] kuacha Swalah” [Swahiyh at-

    Targhiyb Wat-Tarhiyb, Hadiyth 563. Kutoka kwa Ibn Maajah].

    na:

     كك الصالة ف م

    “Yeyote mwenye kuacha Swalah basi amekufuru” [Swahiyh at-Targhiyb Wat-Tarhiyb, Hadiyth 575].

    na:

    أت منه ذمة ا ك الصالة ف م  

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    17/32

    17 

    www.alhidaaya.com

    “Yeyote yule mwenye kuacha Swalah, sina ulinzi wa Allaah kutoka kwake” 

    [Swahiyh at-Targhiyb Wat-Tarhiyb, Hadiyth 569 kutoka kwenye ukusanyaji wa

    atw-Twabaraaniy].

    Na kundi lingine wamelifasiri (kinyume kwa kukataa) hili…. wanasema ni

    mpaka akatae uwajibu wake. Kama alivyosema Yuwsuf (‘Alayhis-Salaam):

    ََّّي تركت ملة قوم ال يؤمنون بالله  إن

    “Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomuamini Allaah” [Yuwsuf 12: 37]. 

    Hivyo wameacha [kuamini] ndio Kufru.

    Kauli Za Wanachuoni Kuhusu Tofauti Kati Ya Uislamu Na Iymaan 

    Baadhi yao wanasema kuwa Iymaan ni kauli na matendo, na Uislamu ni kufanyayale matendo ambayo mtu kawajibishiwa kuyafanya. Hivyo kukasemwa kwamba

    Waumini na Waislamu ni maneno mamoja yenye maana tofauti; kukitajwa [neno]

    moja hakukusudiwi lingine. Lakini ikiwa kutatajwa [neno] moja, huingia yote

    mawili. Anasema Allaah (Ta’ala):

     ومن يبتغ غير اإلسالم دينا فلن يقبل منه

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    18/32

    18 

    www.alhidaaya.com

    “Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitokubaliwa kwake.” [Al-´Imraan 3:

    85].

    Hivyo mtu akichagua Iymaan nyingine [dini kinyume na Uislamu], hatokubaliwa.

    Na Akasema tena Allaah (Ta’ala):

    فما وجدنا فيها غير بيت من المسلمينفما وجدنا فيها غير بيت من المسلمين ٍ ِ ِ ِِّ

     

     

    “Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu...” [Adh-

    Dhaariyaat 51: 36-7].

    Wengine wakasema kuwa Uislamu na Iymaan ni [neno] moja. Kama Alivyosema

    Allaah (‘Azza wa Jalla):

    فَخرجنا من كان فيها من المؤمنينفما وجدنا فيها غير بيت من المسلمين ٍ ِ ِ  

     

    “Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walioamini. Lakini hatukupata humo ila

    nyumba moja tu yenye Waislamu!” [Adh-Dhaariyaat 51: 36-37]. 

    Akasema tena:

    َسلمنا ولما يدخل اإليمان في قلوبكم قالت األعراب منا قل لم تؤمنوا ولكن قولوا  َ ُ َ

    َّ

    َّ  

    “Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni:

    Tumesilimu. Kwani Iymaan haijaingia katika nyoyo zenu.” [Al-Hujuraat 49: 14]. 

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    19/32

    19 

    www.alhidaaya.com

    Na Akasema tena:

    َن هداكم لإليمان َسلموا قل ال تمنوا علي إسالمكم بل الله يمن عليكم  َن  ُّيمنون عليك  ُّ َ

    ُ

    ُ

    َّ

    ُ َ َ

    َّ  

    “Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu.

    Bali Allaah ndiye aliyekufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Iymaan” [Al-

    Hujuraat 49: 17]. 

    Na hizi ni dalili za wale wanaosema kuwa yote ni mamoja.

    Shafaa’ah (maombezi), Hawdh (Kisima cha Mtume), Ma’aad (Qiyaamah) Na

    Hesabu

    Wanasema Allaah Atawatoa Motoni watu wa Tawhiyd (Ahlul-Tawhiyd) baada ya

    uombezi wa waombezi. Na kwamba Shafaa’ah (maombezi) ni kweli. Hawdh ni

    kweli. Qiyaamah ni kweli na Hesabu ni kweli.

    Kutoa Ushuhuda Mmoja Katika Watu Wa Tawhiyd Kwa Pepo Au Moto

    Hawamthibitishii yeyote katika watu wa Tawhiyd kwamba ni katika watu wa

    Peponi au Motoni, kwa sababu elimu hiyo imefichikana kwao na hawajui ni

    katika hali ipi mtu kafa kwayo; Iymaan au Kufr? Lakini wanasema ikiwa mtu

    amekufa katika Uislamu bila ya kuwa na madhambi makubwa, hawaa na

    matendo machafu basi [huyo] ni katika watu Peponi. Kutokana na kauli Yake

    (Subhaanahu wa Ta’ala):

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    20/32

    20 

    www.alhidaaya.com

    إن الذين منوا وعملوا الصالحات ِ َّ  

    “Hakika walioamini na wakatenda mema,...” [Al-Bayyinah 98: 7-8].

    Wala (Allaah) Hajasema wakafanya madhambi.

    َّجزاؤهم عند ربهم جنات عدن ِّ  * ُولئك هم خير البرية  

    “.... hao ndio bora wa viumbe” “Malipo yao kwa Mola wao ni Bustani za daima

    (Peponi).” [Al-Bayyinah 98: 7-8]. 

    Pia yule ambaye Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kamshuhudia Pepo

    ambayo yamepokewa katika Hadiyth sahihi, nao (Ahlul-Hadiyth) humshuhudia

    [mtu huyo] kwa kumfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)

    na kuthibitisha maneno yake. 

    Adhabu Ya kaburi

    Wanasema kuwa adhabu ya kaburi ni kweli. Allaah Atamuadhibu yule

    anayestahiki kuadhibiwa Akitaka, na Humsamehe Akitaka. Allaah (Ta’ala)

    Anasema:

    العذاب

     

    شد

    َ

     

    فرعون

     

    دخلوا ل

    َ

     

    الساعة

     

    تقوم

     

    ويوم

     

    وعشيا

     

    غدوا

     

    عليها

     

    يعرضون

     

    النار

    َّ

    َ َ ََّ

    َّ  

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    21/32

    21 

    www.alhidaaya.com

    “Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itakapofika Saa ya Qiyaamah

    patasemwa: ”Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa.” [Ghaafir

    40: 46]. 

    Hivyo imethibitishwa ya kuwa maadamu masiku yangali ya maisha haya ya

    dunia - mchana na usiku - Allaah Atawaadhibu usiku na mchana mpaka siku

    Qiyaamah kitapokuja watapewa adhabu kali bila ya kupunguziwa kutokana na

    waliyoyafanya duniani. Allaah Anasema:

    َعرض عن ذكري فإن له معيشة ضنكا ومن  ُ َ

    َّ  

    “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenyedhiki,” [Twaahaa 20: 124]. 

    Maana yake ni kabla ya kuisha maisha ya duniani, kutokana na kauli Yake

    (Subhaanahu wa Ta’ala):

    عمى

    َ

     ونحشره يوم القيامة 

    “... na Siku ya Qiyaamah tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Twaahaa 20: 124]. 

    Yaani (maana yake) kwamba maisha ya dhiki huja kabla ya siku ya Qiyaamah.

    Kutokana na uzoefu wetu wetu Mayahudi, Wakristo na Washirikina wana maisha

    ya raha na ustawi. Ni juu yetu kujua ya kwamba dhiki hii haina chochote

    kuhusiana na hali ya riziki kwa kuwa (twajua sote kwamba) washirikina wako

    katika hali nzuri kuhusiana na riziki hapa duniani. Kikusudiwacho ni maisha

    baada ya kifo na kabla ya Qiyaamah.

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    22/32

    22 

    www.alhidaaya.com

    Maswali Ya Munkar Na Nakiyr

    Wanaamini pia maswali ya Munkar na Nakiyr kutokana na habari zilizothibiti

    sahihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kauli

    ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

    يثبت الله الذين منوا بالقول الثابت في الحياة الدنيا وفي اآلخرة ويضل الله الظالمين ويفعل الله ما يشا ُ َ ُ ُ َ

    ِ ِ ِ ِ

    ُّ

    ِ ِ

    ُّ

    ِّ  

    “Allaah Huwathibitisha imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha

    ya dunia na katika Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotea hao wenye

    kudhulumu. Na Allaah hufanya Apendavyo.” [Ibraahiym 14 : 27]. 

    Na kufuata haya kwa tafsiri iliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu

    ‘alayhi wa sallam).

    Kuacha Ugomvi Na Majadiliano Katika Dini

    Wanaonelea kuacha ugomvi na mabishano juu ya masuala ya Qur-aan na

    mengineyo, kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

    َّما يجادل في يات الله إال الذين كفروا ِ َّ ِ ِ ِ 

    “Hawazibishii Ishara za Allaah ila ambao wamekufuru.” [Ghaafir 40: 04]. 

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    23/32

    23 

    www.alhidaaya.com

    Yaani wanayajadili (watu kwa wengine) na kuyasemea uongo, na Allaah Anajua

    zaidi.

    Ukhalifa (Uongozi) Wa Al-Khulafaa' Ar-Raashiduwn 

    Wanathibitisha ukhalifa wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) baada ya Mtume

    wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwa sababu Maswahaba

    walimteuwa; halafu ukhalifa wa 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) baada ya Abu

    Bakr kumteua kama Khaliyfah; halafu ukhalifa wa 'Uthmaan (Radhiya Allaahu

    ‘anhu) baada ya makubaliano ya mashauri ya Waislamu yaliyofanyika kwa

    utaratibu wa ’Umar. Halafu ukhalifa wa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu

    ‘anhu) chini ya msingi wa ba`iyah na ahadi iliyotolewa na wale ambaowalioshuhudia vita vya Badr, kama ‘Ammaar bin Yaasir, na Sahl bin Hunayf, na

    Maswahaba wengine waliyowafuata katika hilo kutokana na haki na fadhila

    zilizotajwa (za ‘Aliy).

    Ubora Baina Ya Maswahaba

    Wanasema Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) ndio watu bora kutokana na

    Kauli Yake Allaah:

    لقد رضي الله عن المؤمنين إذ يبايعونك تحت الشجرةُ َ ُ

    َّ  

    “Kwa hakika Allaah Amewapa radhi Waumini walipofungamana nawe chini ya

    mti.” [Al-Fath 48: 18]. 

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    24/32

    24 

    www.alhidaaya.com

    Pia Kasema:

    ورضوا عنه الذين اتبعوهم بإحسان رضي الله عنهم  ُ َ ُ َ

    َّ

    َّ

    والسابقون األولون من المهاجرين واألنصار وَّ

    َّ  

     

    “Na wale waliotangulia, wa kwanza, katika Muhaajiruwn na Answaar, na

    waliowafuata kwa wema, Allaah Ameridhika nao, na wao wameridhika naye;...”

    [At-Tawbah 9: 100]. 

    Yule ambaye Kathibitisha Allaah radhi Zake juu yake, hatokuja kupatwa baada ya

    hilo na kitu kitachosababisha kupatwa na hasira za Allaah (‘Azza wa Jalla). Wale

    wanaowachukia na kuwaponda hawapewi uzito wowote na huchukuliwa si

    lolote wala chochote.

    Kauli Yao Juu Ya wale wanaowachukia Maswahaba

    Yule mwenye kuchukia kutokana na nafasi zao kwa Allaah, hakuna hofu kubwa

    kwa kitu kama hofu kubwa iliyoko (ahofiwayo) juu yake. Kutokana na kauli Yake

    Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

     بينهم تراهم ركعا سجدا يبتغون فضال من الله ورضوان  على الكفار رحما َشدا َّه  َّ َّ ْ َ ْ ُ ُ

    َّ

    َّ

    َّمحمد رسول الله والذين مع ِ َّ َّ

    َّ ُّ

    شطَه فآزره فاستغلظ  َخرج  كزرع  َثر السجود ذلك مثلهم في التوراة ومثلهم في اإلنجيل  سيماهم في وجوههم من ُ َ ْ ُ

    ِ

    ِ ِ ِ

    َّ

    وَجر  فاستوى على سوقه يعجب الزراع ليغيظ بهم الكفار وعد الله الذين منوا وعملوا الصالحات منهم مغفرة 

    َ

    ِ ِ ِ ِ ِ َّ َّ

    َ ُ َ َ

    ُّ

     عظيما

     

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    25/32

    25 

    www.alhidaaya.com

    “Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya

    makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama nakusujudu

    wakitafuta fadhila na radhi za Allaah. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari

    ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Tawraat. Na mfano wao katika Injiyl ni

    kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene,

    ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili

    kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Allaah Amewaahidi walioamini nawakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.“ [Al-Fat-h 48: 29]. 

    Hivyo Kasema ya kwamba Kawafanya (Maswahaba) kuwa wakali mbele ya

    Makafiri.

    Wanasema kuhusu ukhalifa wao ni sahihi, kutokana na kauli Yake Allaah

    (Subhaanahu wa Ta’ala):

    وعد الله الذين منوا منكم وعملوا الصالحات ِ ِ ِ َ

     

    “Allaah Amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema,...”

    [An-Nuwr 24: 55]. 

    Kwa kauli Yake ”miongoni mwenu” ni dalili ya kwamba ni wale ambao

    walikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kunako dini

    yake. Akaendelea kusema:

    َّليستخلفنهم في األرض كما استخلف الذين من قبلهم وليمكنن لهم دينهم الذي ارتضى لهم وليبدلنهم من بع ِ ِ ِ ِ َُّ َ

    ْ ُ ُ ْ ُ

    َّ

    َ َ َ

    َ

    ِّ

    شيئا

     

    بي

     

    يشركون

     

    ال

     

    يعبدونني

     

    منا

    َ

     

    خوفهم

     

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    26/32

    26 

    www.alhidaaya.com

    “...Atawafanya Makhalifa (Waongozi) katika ardhi kama alivyowafanya

    makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini Atawasimamishia Dini yao

    Aliyowapendelea, na Atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe

    wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote.” [An-Nuwr 24: 55]. 

    Allaah kaipa Dini uimara kupitia nguvu za Abu Bakr, 'Umar na `Uthmaan; Allaah

    Kawapa ahadi ya usalama, walipigana vita na kushinda wao na hawakushindwa,

    na walitisha maadui zao na hawakuwahi kutishwa na maadui zao.

    Allaah pia Kasema kwa wale waliobaki nyuma na Mtume katika vita ya kwamba

    Atawapambanua katika kupigana kwa kauli Yake:

    َبدا ولن تقاتلوا معي عدوا إنكم رضيت فإن رجعك الله إلى طآئفة منهم فاستأذنوك للخروج فقل لن تخرجوا معي  ْ َ َ

    ِ ِ َّ ِ

    ْ ُ ُ

    َّ

    ُ

    ِّ

    َّ

    َول مرة فاقعدوا مع الخالفين َّ

    َّ

     بالقعود 

    “Basi Allaah Akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na

    wakakutaka idhini ya kutoka - sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala

    hamtopigana na adui pamoja nami. Nyinyi mliridhia kukaa nyuma mara yakwanza, basi kaeni pamoja na hao watakaobakia nyuma.” [At-Tawbah 9: 83]. 

    Hivyo waliokuwa hai wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)

    walimuomba ruhusa ya kwenda nje kwenye vita dhidi ya adui, lakini (Mtume)

    hakuwapa ruhusa. Ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alipoteremsha (aayah)

    zifuatazo:

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    27/32

    27 

    www.alhidaaya.com

    َن يبدلوا كالم الله قل لن تتبعونا كذلك َّسيقول المخلفون إذا انطلقتم إلى مغانم لتأخذوها ذرونا نتبعكم يريدون  ِ َّ ِ َ ُ َ

    َّ

    ِّ

    ُ ُ

    َّقال الله من قبل فسيقولون بل تحسدوننا بل كانوا ال يفقهون إال قليال  

    “Waliobaki nyuma watasema: Mtakapokwenda kuchukua ngawira, tuacheni

    tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Allaah. Sema: Hamtotufuata kabisa.Allaah Alikwishasema kama hivi zamani. Hapo watasema: Bali nyinyi

    mnatuhusudu. Sio, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo.” [Al-Fat-h 48: 15]. 

    Wale watu waliokuwa hai zama za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa

    sallam) ndio wanaokumbushwa (wanaohusishwa na) Ayaah hizi kwa sababu ya

    kutomtii. Baadhi yao walikuwa bado hai wakati wa Abu Bakr, ’Umar na

    `Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhum), na kutii kwao wangelipwa ujira, na kuacha

    kutii kwao ni adhabu kali. Huu ni unadi wetu kuhusu ukhalifa wao (Allaah

    Awawie radhi wote) Na Allaah Asijaalie katika nyoyo zetu chuki dhidi ya mmoja

    katika wao; kama moja ya ukhalifa wao ni imara, hivyo umethibiti ukhalifa wa

    mmoja wao basi umekwenda kwa mpangilio ukhalifa wa wote wanne.

    Swalah Ya Ijumaa Nyuma Ya Kila Imaam Muislamu, Sawa Wakiwa Wema Au

     Waovu 

    Wanaonelea kuswali - Swalah ya Ijumaa na nyinginezo - nyuma ya kila Imaam

    Muislamu, sawa akiwa ni mchaji Allaah au muovu. Hakika Allaah (Subhaanahu

    wa Ta’ala) Kaamrisha kuswali Swalah ya Jumu’ah kama wajibu kamili, pamoja na

    elimu Yake Allaah (Ta’ala) Anajua baadhi ya viongozi ambao wataojitokeza

    watakuja kuwa mafajiri na mafasiqi. Hata hivyo hakutenga wakati na kuacha

    wakati mwengine, wala hakuamrisha (utoaji wa) adhaana siku ya Ijumaa pekee

    bila siku zingine.

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    28/32

    28 

    www.alhidaaya.com

     Jihaad Pamoja Na Viongozi Hata Kama Waovu

    Wanaonelea kuwa kwa Jihaad dhidi ya Makafiri pamoja na Viongozi hata kama

    watakuwa waovu, na wanaonelea kuwaombea du’aa kwa wema na kurudi

    kwenye uongofu. Na hawaonelei (kujuzu) kufanya Khuruuj (uasi) dhidi yao(Viongozi) kwa kuwasimamishia panga wala mapigano kwa sababu ya

    fitnah. Wanaonelea kujuzu kupigana pamoja na kiongozi muadilifu dhidi ya

    makundi maovu ikiwa masharti ya hilo yatatimia.

    Nchi Ya Kiislamu 

    Wanaonelea ya kwamba nchi ya Kiislamu si nchi ya kikafiri kama waonavyo

    Mu`tazilah, maadamu tu wanaadhini (wazi) kwa ajili ya Swalah na utawala uko

    wazi [wa Uislamu] na watu wake wanaweza kuitekeleza (Swalah hiyo) kwa

    amani.

    Matendo Ya Waja Hayawajibishi Kuingia Peponi, Bali Ni Kutokana Na Fadhila

    Za Allaah 

    Wanaonelea ya kwamba mtu hawajibiki kuingia Peponi kutokana na matendo

    yake - bila kujali hata akifanya matendo gani - ila ni kwa fadhila na rahma za

    Allaah ambazo Huzihusisha kwa Amtakaye. Hata kama Allaah Asingelitoa

    fadhila Zake, hakuna yeyote angeliweza kumwambia lolote. Kama Alivyosema

    Allaah:

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    29/32

    29 

    www.alhidaaya.com

    َبدا ولكن الله يزكي من يشا َحد  ولوال فضل الله عليكم ورحمته ما زكا منكم من 

    ُ

    َ َ َ ُ

    ٍ ِ

    ِّ

     

    “Na lau kuwa si fadhila ya Allaah na rahma Yake juu yenu, asingelitakasika

    miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Allaah Humtakasa Amtakaye.” [An-

    Nuwr 24: 21]. 

    Pia Kasema:

    ولوال فضل الله عليكم ورحمته التبعتم الشيطان إال قليال ْ ْ

     

    “Na lau kuwa si fadhila ya Allaah juu yenu na rahma Yake mngelimfuatashaytwaan ila wachache wenu tu.” [An-Nuwr 4: 83]. 

    Pia Kasema:

    ُّيختص برحمته من يشا  

     

    “Na Allaah Humkusudia kumpa rahma Yake Ampendaye.” [Al-Baqarah 2: 105]. 

    Allaah Ndiye Ar-Razzaaq (Mwenye Kuruzuku Daima)

    Na hakika Allaah (Ta’ala) Humpa riziki, nguvu na chakula kila kiumbe hai katika

    maisha yake. Naye Allaah ndiye Huvilisha viumbe waliosalia (wanyama n.k). Na

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    30/32

    30 

    www.alhidaaya.com

    ni Yeye ndiye Huruzuku katika (kutoa) Halali au Haramu. Hali kadhalika ni Yeye

    ndiye Huruzuku mazuri na yanayotumika katika kupata hayo.

    Allaah Ndiye Kaumba Mashayatwiyn Na Wasiwasi Wao

    Wanaamini kwamba Allaah (Ta’ala) ndiye kaumba shayaatwiyn wawatiao

    wasiwasi watoto wa Aadam, kuwashawishi, kuwadanganya na kwamba

    shaytwaan humuathiri binaadamu.

    Uchawi Na wachawi

    Kwamba katika dunia kuna wachawi na uchawi; na kwamba kuutumia uchawi ni

    Kufr (ukafiri) na kuamini kwamba ndio unaoleta faida na madhara bila idhini ya

    Allaah (‘Azza wa Jalla).

    Kujitenga Na Bid’ah

    Wanaonelea kujitenga mbali na Bid ‘ah, pamoja na madhambi, kiburi, majivuno,

    ulaghai, hila, rushwa na dhulma. Na wanaonelea (mtu) kuacha kabisa kuleta

    madhara kwa watu na kuacha ghiybah (usengenyaji), isipokuwa kwa yule

    anayeifanya na kuilingania Bid’ah hadharani, kumuongelea mtu huyo si

    usengenyaji kwao.

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    31/32

    31 

    www.alhidaaya.com

    Kujifunza Elimu

    Wanaonelea kwamba elimu ni lazima ichukuliwe (ya dini) na itafutwe kutoka

    kwa watu wake. Na ichukuliwe mkazo sana katika kujifunza Qur-aan na sayansi

    yake na tafsiri yake. Na kusikiliza Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa

    sallam), kuzikusanya zote na kuzifahamu kwa yale yaliyomo; na kutafuta Aathaar

    za Maswahaba.

    Kujizuia [Kuwaongelea Vibaya] Maswahaba

    Wanajiepusha kuwaongelea vibaya Maswahaba na kuwaeleza kiubaya

    wao. Wanamkabidhi Allaah (‘Azza wa Jalla) kwa yale yaliyotokea baina yao.

    Kushikamana Na Jamaa’ah

    (Wananasihi watu wote) Kushikamana na Jamaa’ah. Wanakula, kunywa na kuvaa

    kati kwa kati. Wanashaji`ishana kufanya kheri, kuamrisha mema na kukatazamaovu. Na kujiepusha na wajinga mpaka watapojua na kubainishiwa haki.

    Halafu baada ya kubainishiwa haki wakaikataa, hapo udhuru utakuwa

    umetoweka baina yao (waliyoikataa) na wao.

    Uwajibu Wa Kushikamana Na Madh-hab Ya Ahlul-Hadiyth, Firqatun-Naajiyah 

    (Kipote Kitakachookoka)

  • 8/18/2019 ´Aqiydah Ya Maimamu Wa Hadiyth - Imaam Abu Bakr Ismaa´iyliy

    32/32

    32 

    www.alhidaaya.com

    Huu ndio msingi wa Dini na Madh-hab, (hii ndo) itikadi ya Maimaam wa

    Hadiyth ambao hawakuathiriwa na Bid’ah na wala hawakutumbukia katika

    mambo ya fitnah. Wao si walaini katika masuala ambayo ni makruhu (yenye

    kuchukiza) katika Dini, na wala hawatofautiani katika hili.

    Na jua ya kwamba Allaah (Ta’ala) Kawajibisha katika kitabu Chake mapenzi na

    msamaha Wake kwa wale wataomfuata Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam) na Akawajaalia kuwa ni kikundi kitakachookoka (Firqatun-Naajiyah)  na

    kikundi kimfuatacho (Yeye). Kasema (Allaah) kumwambia anayedai kumpenda

    Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

    تم تحبون الله فاتبعوني يحببكم الله ويغفر لكم ذنوبكم ُ ُ َ

    َّ

    ُّ

     قل إن كن

    “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah

    Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu.” [Al-`Imraan 03 : 31]

    Allaah Atujaalie sisi na nyinyi elimu na kuwa na taqwa (uchaji Allaah) kutokana

    na shub-hah na upotofu kwa neema na rahma Zake.