4
- %ffi MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI Toleo Nam. ZMA/MZN 0110412020 Tarehe 28lO4l2O2O Kwa Wamiliki wa Meli, lGmpuni za Meli,Kampuni za Ukaguzi za Meli,Mawakala wa Meli, Wakaguzi wa Meli KICHWA CHA HABARI: MWONGOZO WA HATUA ZA KUSAIDIA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MARADHI YA MAFUA MAKALI (CORONA VIRUS DISEASE 2019) KATIKA SHUGHUTT ZA MELI 1.0 Madhumuni Toleo hili linakusudia kuwajuilisha wadau wote husika kuhusiana na hali ya maradhi ya mafua makali (COVID-19) na hatua za dharura zinazochukuliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini kukabiliana na matatizo yatakayosababishwa na maradhi hayo katika shughuli za uendeshaji meli. 2.0 Chimbuko Mnamo Januari 31, 2020 Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Usafiri Baharini (IMO) , kwa Toleo Nam. 4202, lilitoa taarifa na mwongozo wa hatua za kufuatwa katika kupunguza madhara ya maradhi ya mafua makali (COVID - 19) kwa mabaharia, abiria na watu wengine kwenye meli. Taarifa na mwongozo huo zilijikita kwenye mapendekezo ya Shirika la Afya Dunia (WHO) yaliyotolewa tarehe 30 Januari 2020, wakati lilipotangaza mripuko wa maradhi ya mafua makali kuwa ni dharura ya a$ra ya umma ya wasi wasi wa kimabaifa (PHEIC). Toleo la IMO lilifuatiwa na marekebisho kadhaa yaliyotolewa na IMO yenyewe na baadhi ya mashirika mengine ya tasnia ya meli ili kuhakikisha kwamba tasnia ya meli ina hatua zinazofaa za kupunguza matatizo yatakayosababishwa na maradhi ya mafua makali kwa shughuli za meli. Marekebisho hayo yalilenga katika masuala tofauti,

 · Created Date: 4/30/2020 11:38:51 AM

  • Upload
    others

  • View
    7

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1:  · Created Date: 4/30/2020 11:38:51 AM

-

%ffiMAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI

Toleo Nam. ZMA/MZN 0110412020 Tarehe 28lO4l2O2O

Kwa Wamiliki wa Meli, lGmpuni za Meli,Kampuni za Ukaguzi za Meli,Mawakala wa Meli,Wakaguzi wa Meli

KICHWA CHA HABARI: MWONGOZO WA HATUA ZA KUSAIDIA KUKABILIANANA ATHARI ZA MARADHI YA MAFUA MAKALI (CORONA VIRUS DISEASE

2019) KATIKA SHUGHUTT ZA MELI

1.0 Madhumuni

Toleo hili linakusudia kuwajuilisha wadau wote husika kuhusiana na hali ya maradhi yamafua makali (COVID-19) na hatua za dharura zinazochukuliwa na Mamlaka ya UsafiriBaharini kukabiliana na matatizo yatakayosababishwa na maradhi hayo katika shughuliza uendeshaji meli.

2.0 Chimbuko

Mnamo Januari 31, 2020 Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Usafiri Baharini(IMO) , kwa Toleo Nam. 4202, lilitoa taarifa na mwongozo wa hatua za kufuatwa katikakupunguza madhara ya maradhi ya mafua makali (COVID - 19) kwa mabaharia, abiriana watu wengine kwenye meli. Taarifa na mwongozo huo zilijikita kwenyemapendekezo ya Shirika la Afya Dunia (WHO) yaliyotolewa tarehe 30 Januari 2020,wakati lilipotangaza mripuko wa maradhi ya mafua makali kuwa ni dharura ya a$ra yaumma ya wasi wasi wa kimabaifa (PHEIC).

Toleo la IMO lilifuatiwa na marekebisho kadhaa yaliyotolewa na IMO yenyewe nabaadhi ya mashirika mengine ya tasnia ya meli ili kuhakikisha kwamba tasnia ya meliina hatua zinazofaa za kupunguza matatizo yatakayosababishwa na maradhi ya mafuamakali kwa shughuli za meli. Marekebisho hayo yalilenga katika masuala tofauti,

Page 2:  · Created Date: 4/30/2020 11:38:51 AM

yakiwemo ushauri juu ya utekelezaji na usimamizi wa mashafti ya lazima ya IMO,mwitikio wa kukabiliana na maradhi ya mafua makali na kuueneza kwa jumuiya ya meli,mazingatio ya kiuendeshaji kwa kusimamia/kukabiliana na miripuko ya maradhi melini,na mwongozo kwa waendesha meli katika kinga ya afya ya mabaharia.

Kutokana na mripuko wa maradhi ya mafua makali, ueneaji wake wa kasi dunianlpamoja na usumbufu unaotokana na vizuizi vya kusafiri na kukaa ndani ambavyovinaweza kuathiri shughuli za meli, Mamlaka ya Usafiri Baharini imetayarisha hatua zamuda kuhusiana na utekelezji na usimamizi wa masharti ya lazima ya IMO kwa sababuya matukio yasiyoweza kuepukika.

3.0 Hatua za Muda

3.1 Ukaguzi wa lazima (Mandatory surveys and audits)

Mamlaka itaongeza muda wa kufanya ukaguzi wa lazima wa meli chini ya mikatabambali mbali ya IMO (mandatory surveys and audits under SOLAS, MARPOL, LOADLINE,ISM, ISPS, etc) mpaka tarehe 30 Juni,2020 kwa utaratibu ufuatao:

(a) Wamiliki wa Meli ambao meli zao ziko chini ya Kampuni za Ukaguzi (ROs)wawasilishe maombi yao kwa maandishi kwa kampuni za ukaguzi wanazofanyal<azi nazo kwa ajili ya maombi yao kuidhinishwa;

(b)Wamiliki wa Meli ambao meli zao haziko chini ya Kampuni za Ukaguzi (ROs)wawasilishe maombi yao kwa maandishi kwa Mamlaka;

(c) Kampuni za Ukaguzi (ROs) ziwasilishe maombi ya wamiliki wa meli kwa Mamlakaiwapo tu wakaguzi wao hawawezi kuihudumia/kuikagua meli kutokana na vizuizivilivyowekwa na mamlaka za bandari kufuatia kwa mripuko wa maradhi yamafua makali (COVID-19);

(d) Kampuni za Ukaguzi au Wakaguzi zitayarishe na kuwasilisha kwa wamiliki wameli hatua za muda kwa kuzingatia taratibu na matakwa yao ili zifuatwe nawamiliki wa meli katika kuhakikisha usalama wa meli ndani ya kipindi hiki.

(e) Wamiliki wa meli wawasilishe kwa Mamlaka kwa kupitia Kampuni zao za tJkaguziau wao wenyewe (kwa wasio na Kampuni) kielelezo cha kujikagua (SelfInspection Checklist) ili kuthibitisha wamejikagua wenyewe kwa kuhakikisha halisalama ya meli zao.

Page 3:  · Created Date: 4/30/2020 11:38:51 AM

3.2 Kuongeza Muda wa Meli Kwenda Chelezoni (Dry Docking Extension)

Mamlaka itaongeza muda wa kwenda chelezoni au kufanya huduma za lazima kwa meliza Tanzania Zanzibar mpaka tarehe 30 June, 2020 kwa taratibu zifuatazo-

(a) Wamlliki wa Meli ambao meli zao ziko chini ya Kampuni za Ukaguzi (ROs)wawasilishe maombi yao kwa maandishi kwa kampuni za ukaguzi wanazofanyakazi nazo kwa uthibitisho wa maombi yao;

(b)Wamiliki wa Meli ambao meli zao haziko chini ya Kampuni za Ukaguzl (ROs)wawasilishe maombi yao kwa maandishi kwa Mamlaka.

(a) Kampuni za Ukaguzi (ROs) ziwasilishe maombi ya wamiliki wa meli kwa Mamlakazikiwa na barua zao za uthibitisho wiki mbili kabla ya tarehe ya ukaguzikumalizika;

(b) Maombi yaambatane na barua ya kampuni ya chelezo ya kukataa kuipokea melihiyo kwa sababu ya mripuko wa maradhi ya mafua makali (COVID -19 ), baruaya uthibitisho ya Kampuni ya Ukaguzi kwa wamiliki wa meli wanaotumia Kampuniza Ukaguzi au wakaguzi binafsi na ripoti ya ukaguzi wa meli chini ya maji(undenrvater survey report).

Hatua hizi zitasita kutumika pale itakapotangazwa rasmi na WHO kwamba maradhi yamafua makali (COVID -19) yamemalizika na madhara yake hayapo, lakini zinawezakurekebishwa na muda kuongezwa iwapo hali itaendelea.

l

Hatua hizi hazitatumika kwa wamiliki wa meli na mameneja ambao hawatapatamatatizo kwenye matayarisho ya huduma za ukaguzi, kupeleka chelezoni na huduma zalazima kwa meli zao kwa kipindi hiki,

3.3 Hati za Kieletroniki (Electronic Ceftificates)

Meli yoyote inayolngia katika hatua za muda zilizoelezwa, itapewa hati ya elekroniki naKampuni ya Ukaguzi, Mkaguzi au Mamlaka, itakayotumika hadi tarehe 30 Juni, 2020.

Mara utakapomalizika muda uliotajwa hapo juu na hali ikaruhusu kwa kaguzi za lazimakufanywa kufuatana na miongozo ya. ukaguzi ya IMO , hati zote za kielektronikizilizotolewa chini ya hatua hizi za muda zitabadilishwa na hati za kawaida ili kuendeleana mzunguko uliopo wa uthibitisho wa meli.

Page 4:  · Created Date: 4/30/2020 11:38:51 AM

4. Hatua zinazotakiwa

Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa meli na mameneja wa kampuni za melikwamba bado wana jukumu la-

(a) Kuweka viwango vya usalama, mazingira ya bahari na wafanyakazi katikameli zao kulingana na masharti yanayotumika kwa kipindi chote chakuongezwa muda;

(b) Kutoa taarifa mara moja kwa Mamlaka juu ya tatizo la kiufundi, upungufu nakutofuata masharti yatakayotokea wakati wa kipindi hiki;

(c) Kuhakikisha miongozo ya kiuendeshaji ya kusimamia matukio ya maradhi yamafua makali (COVID -19) melini na muongozo wa kinga ya afya yamabaharia inafuatwa kwa ukamilifu.

Aidha, wamiliki wa meli watachukua hatua zifuatazo kuhakikisha abiria namabaharia wanapata kinga dhidi ya maradhi ya mafua makali:-

(a) Wawapatie mabaharia wote barakoa na "gloves" zenye ubora unaofaa;(b) Waweke vipima joto kwa mabaharia na abiria wanaotumia meli zao;(c) Waweke vitakasa mikono (sanitizers) zenye ubora katika sehemu mbali mbali

za meli;(d) Meli zipuliziwe dawa zenye ubora kila baada ya muda na kwa meli za abiria

muda mfupi kabla ya abirla kupanda melini.

Toleo hili linaweza kurekebishwa au kufutwa wakati wowote ndani ya kipindi hiki kwakuzingatia mabadiliko au ushauri wowote utakaotolewa na Mamlaka husika kuhusiana na

maradhi ya mafua makali (COVID-19).

Toleo hili linaanza kufanyakazi tarehe 01 Mei, 2020

Maulizo yoyote kuhusiana na mah ya toleo hili yatumwe kwa:

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Usafiri BahariniS.L.P:401

Zanzibar

Simu: +255 242236795Tovuti: www.zma.go,UBaruapepe: . [email protected]

BO

MKU MKUUMAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI

*tl4F1tffi:rrPl.*Y:+:rffi