Transcript
Page 1: A tour to johannesburg south africa

A TOUR TO JOHANNESBURG SOUTH AFRICA.Ilikuwa kama ndoto yangu siku moja kuja kujivunia juu ya kile ninachokifahamu kuhusu mpira wa miguu na ulimwengu wa soka kwani sio siri mpira upo kwenye damu yangu tangu nazaliwa,nilianza kupenda mpira wa miguu ningali nikiwa mdogo sana kiumri kiasi cha kwenda kutazama mechi za timu za mtaani zikicheza mbali na mazingira ya nyumban kwetu na ilifikia kipind mpaka nikaenda mlandizi kutazama mpira tena bila kuaga kwa wazazi wangu na kwa bahati nzuri hawakuwah kufahamu na haikuishia hapo kwani mpira niliupenda sana kiasi cha kuucheza kwa nafasi toafuti kiwanjani! Kuna kipindi nilikuwa nikipendelea kucheza nafasi ya mlinda mlango “goal keeper” lakin kuna kipindi nilipoanza kupata tamaa ya kuucheza huu mpira kwa hali ya umakini zaidi,hapo ndipo nilipoamua kucheza nafasi ya ulinzi kwa kucheza namba tano au “central defender” na kwa kpdi chote hicho nilicheza kwa mafanikio kiasi cha kushiriki mashindano mbalimbali makubwa yakiwemo sober na ligi kadhaa za mtaani kwetu ikiwemo kugombania kreti la soda au mnyama kuku kama sehemu ya kujipongeza na kwa mara kadhaa timu yangu ilikuwa ikifanya vyema kwenye mashindano mbalimbali tuliokuwa tukipata kushiriki na timu yangu ya kwanza kuchezea ilikuwa ikiitwa savannah f.c nay a pili kuchezea ilikuwa ikiitwa Kosovo au msewe kids. Baada ya muda mwing kupita na masomo kuanza kunibana,taratibu nikaanza na kuachana kucheza soka na kuingiwa na mapenz makubwa na soka la ulaya na hasa club ilionivutia kwa kipindi hiko ilikuwa “Manchester united” nakumbuka kipindi hiko ndo man united ilikuwa ikifanya vizuri kwenye miaka ya 1999 mpaka 2000 hasa pale walipochukua vikombe vitatu muhimu katika msimu mmoja na tangu hapo mapenzi yangu ya kutazama na kuufuatilia mpira au soka la ulaya au nje ya nchi kwa ujumla yakshamiri kupita kiasi mpaka leo hii.

Ilipofika mwaka 2011 siku moja nikiwa nyumban natazama televishen,ndipo nikakutana na kipindi kinaitwa “Guinness Football Challenge” ambapo niliona vijana toka nchi mbali mbali wakichuana kuonyesha ujuzi katika soka hasa katika vipengele vya “Football Skills” na “Knowledge of the game of Football” nilisisimka sana kuona kile kipind japokuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza na sikuwa nikifahamu ratiba ya kile kipindi lakin nikafanya juhud kuataka kujua ni muda gani na siku gani huwa kinaruka hewani katika ile televishen ndipo nikapata kujua siku na saa ambayo kile kipindi kinaruka hewani,nikapata shauku kubwa ya kutak kujua kiundani ni namna gani ukitaka kuwa mshiriki au kushiriki kwa kuwa niliamin kilichokuwa kikifanyika ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wangu na ukizingatia mapenzi makubwa niliokuwa nayo katika mchezo wa mpira wa miguu na ndipo nikapata msukumo kutoka ndani ya moyo wangu ukiniambia kuwa nenda kashirik na utapata nafasi. Tarehe ikatangazwa na nikaamua kuwa nitamchukua kijana wangu mmoja namuaminia sana anaitwa abuu kwa jina la utani “banju” ni moja kati ya vijana wenye uwzo na utulivu sana ndani na nje ya uwanja na hiyo ndo sababu kubwa ya mimi kumchagua na kutaka awe team mate wangu lakin hali haikuwa hivyo kwani tulishindwa kwenda kushiriki kwa mwaka huo wa 2011 na hatimaye kuamua kwenda kushiriki mashindano hayo yatakapofanyika mwaka ujao ambao ni mwaka 2012 kwa kuwa bado matumaini nilikuwa nayo na kijana abuu akiwa bado na ari ile ile.

Page 2: A tour to johannesburg south africa

Recommended