26
Mafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda hawakupata faida” (Waebrania 13:9). Mstari ambao ndio kinchwa cha mafundisho haya ni onyo dhidi ya mafundisho ya uongo. Hii ilikuwa onyo ambayo ilipewe wakristo wa Waebrania. Hii ni onyo ambayo pia leo inahitajika kwa wakristo wote kama tu wale wakristo wa miaka iliyopita. Mmoja anaweza kuuliza je, ni kwa nini lilikuwa jambo la muhimu kuwaonya wakristo wasichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni? Ukweli ni kwamba silaha kubwa ambayo shetani anatumia kuharibu maisha ya nafsi ni kuhakikisha kwamba anaeneza mafundisho ya uongo. Yeye shetani tangu mwanzo alikuwa mwuaji na mwongo. Yeye anazunguka-zunguka kama simba ambaye anatufuta mtu wa kumtafuna. Yeye kila wakati huwa anawahimiza watu kuendelea katika tamaduni zao na katika mafundisho ya uongo. Yeye huwahimiza watu kutolea miungu sadaka, kuwa waasi, watu wenye ghadhabu, kuabudu sanamu, kuteseka kwa ajili ya uongo, kuwaweka mateka, kutoa sadaka za watoto wao na kuendelea na vita miongoni mwao, yote haya ni kazi ya shetani.

Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

  • Upload
    dothien

  • View
    390

  • Download
    16

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Mafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni."Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya ki-geni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda hawakupata faida” (Waebrania 13:9). Mstari ambao ndio kinchwa cha mafundisho haya ni onyo dhidi ya ma-fundisho ya uongo. Hii ilikuwa onyo ambayo ilipewe wakristo wa Wae-brania. Hii ni onyo ambayo pia leo inahitajika kwa wakristo wote kama tu wale wakristo wa miaka iliyopita. Mmoja anaweza kuuliza je, ni kwa nini lilikuwa jambo la muhimu kuwaonya wakristo wasichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni? Ukweli ni kwamba silaha kubwa ambayo shetani anatumia kuharibu maisha ya nafsi ni kuhakikisha kwamba anaeneza mafundisho ya uongo. Yeye shetani tangu mwanzo alikuwa mwuaji na mwongo. Yeye anazun-guka-zunguka kama simba ambaye anatufuta mtu wa kumtafuna. Yeye kila wakati huwa anawahimiza watu kuendelea katika tamaduni zao na katika mafundisho ya uongo. Yeye huwahimiza watu kutolea miungu sadaka, kuwa waasi, watu wenye ghadhabu, kuabudu sanamu, kuteseka kwa ajili ya uongo, kuwaweka mateka, kutoa sadaka za watoto wao na kuendelea na vita miongoni mwao, yote haya ni kazi ya shetani. Kazi yake shetani ni kuharibu. Yeye kila wakati hufanya kazi ya kuleta ma-fundisho ya uongo katika kanisa, ili watu wa Mungu waiache imani ya kweli. Yeye akiona kwamba hawezi kuzuia mafundisho mazuri kuende-lea, yeye hujaribu kuyachanganya mafundisho mazuri na yale ya uongo. Hii ndio sababu yeye anaitwa mwaribifu.Kanisa la kristo limepewa silaha moja na Roho Matakatifu ya kumpinga shetani na kumshinda, silaha hiyo ni Neno la Mungu. Neno la Mungu ndio silaha ya pekee ambayo shetani anapaswa kupigwa nayo. Ni wakati neno la Mungu linafafanuliwa vyema na kubadilisha mioyo ndipo shetani atakaposhindwa katika mipango yake yote. Ni neo la Mungu am-balo Yesu Kristo alitumia wakati shetani alimjaribu katika jangwa. Kila wakati alipojaribiwa, alijibu kwa kusema, “imeandikwa.” Ni neno la Mungu ambalo watumishi wote wa Mungu wanapaswa kutumia ikiwa watapata ushindi dhidi ya shetani. Biblia ndio silaha ya kanisa ikiwa itahubiriwa na kufafanuliwa kwa uaminifu.

Page 2: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Ninakusihi msomaji wangu utilie manani mstari ambao ndio kinchwa cha mafundisho haya. Ninasema hivi kwa sababu tunaishi katika nyakati ambazo wengi hawapendi mafundisho ya kweli na hawana msimamo wowote wa kidini. Leo ikiwa utakuwa mtu wa kutilia maneno ma-fundisho ya kweli ya Biblia na kukemea wale ambao wanafundisha ma-fundisho ya uongo, wengi watasema kwamba wewe ni mtu ambaye hu-pendi kutumia akili yako. Hutapendwa na wengi, bali wengi watakuchukia sana. Lakini hata wakati unachukiwa kukumbuka maandiko lazima yatimie. Kwa hivyo ninataka tutazame mafundisho ya mstari huu wa Waebrania 13:9.I. Kwanza, kuna onyo: “msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni” II. Pili, kunahimizo: “..maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao walikwenda navyo hawakupata faida.” III. Tatu, kuna ukweli juu ya vitu ambayo havina faida: “..wala si kwa vyakula ambavyo wao walikwenda navyo hawakupata faida.” Kuna mafundisho muhimu sana katika kila sehemu ya mstari huu.1.Kwanza, kuna onyo: “msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni.” Maana ya maneno haya, “msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni,” ni kwamba tusichukuliwa na kila aina ya mafundisho ya uongo kama vile mashua ambayo haina chombo cha kuielekeza. Mafundisho ya uongo itaendelea kuwepo katika ulimwengu na kujidhirisha kwa njia tofauti tofauti, lakini lengo likiwa moja tu, la kuwaelekeza watu kinyume na mapenzi ya mungu. Hata leo kuna wal-imu wengi wa uongo katika makanisa mengi hapa ulimwenguni. Lakini hata kama wapo katika makanisa, hatufai kuogopa, bali tunafaa kuwa wangalifu sana. Hii ndio onyo ambayo mwandishi wa kitabu cha Wae-brania anatuonya nayo. Mwandishi wa kitabu cha Waebrania alinukuu tu yale ambayo Bwana Yesu Kristo alikuwa amefundisha katika mahubiri yake akiwa mlimani. Bwana Yesu kristo alituonya kwamba, “Jihadhirini na manabii wa uongo, watu wanao wajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani, ni mbwa mwitu wakali” (Mathayo 7:15). Paulo katika ujumbe

Page 3: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

wake wa mwisho kwa wachungaji wa Efeso alisema, “..tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao” (Matendo ya Mitume 20:30). Katika waraka wa pili wa Wakorintho tunasoma haya, “lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawa-haribu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo” (2 wakoritho 11:3). Katika kitabu cha Wagalatia tunasoma kwamba, “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi Yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia njili ya namna nyingine...Enyi wagalatia msiyo na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya ma-cho yenu ya kuwa amesulubiwa...Je, mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?...Basi sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo many-onge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka....Katika ungwana huo Kristo ali-tuandika nuru; kwa kuwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa” (Wagalatia 1:6; 3:1, 3; 4:9, 10, 11; 5:1).Katika kitabu cha waefeso tunasoma, “..ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu” (Waefeso 4:14). Katika kitabu cha wakolosai tunasoma, “Angalieni mtu asi-wafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Wakolosai 2:8). Katika kitabu cha Timotheo tunasoma pia, “basi Roho anena wazi wazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani” (1Timotheo 4:1). Katika kitabu cha Petro tunasoma, “lakini kuliondokea manabi wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia” (2 Petro 2:1). Yohana naye aliandika akisema, “wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetoka na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” (1 Yohana 4:1). Yuda aliandika akisema,

Page 4: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

“Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sis sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo” (Yuda 1:3- 4). Maneno haya yote yaliandikwa kwa ajili yetu tuweze kupata kufundishwa. Je, tunapaswa kusema nini kuhusu mistari hii yote? Mistari hii inatuonyesha kwamba hata katika kanisa la kwanza, kulikuwamo na matatizo ya mafundisho, yaani hapo zamani kuwekuwepo na walaimu wa uongo. Ni jukumu la kila mchungaji kuwaonya washirika wake kuhusu mafundisho ya uongo. Ikiwa mchungaji hatawaonya watu wake, basi yeye atakuwa anakosea sana katika majukumu yake ya uchungaji. Hii ndio sababu Paulo anasema, “uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata” (1Timotheo 4:6).Tunahitaji mafundisho ambayo inawaonya wengi juu ya walimu wa uongo. Tangu zamani walimu wa uongo wamekuwepo na hata leo wako wengi sana. Wao wanaendelea na:--Kuongezea mambo yao juu ya ukweli na wengine wakiondoa katika ukweli yale ambayo ni kweli.--Kuficha ukweli na wengine kufanya ukweli uonekane kuwa sio uk-weli.--Kuwa waganga na kutoamini ukweli. --Kufuata tu dini na mafundisho ya shetani.--Kuabudu miungu.Katika mambo haya yote, wao wanaendela na kupinga na kuharibu ujumbe wa injili. Wachungaji wengi wanaendelea na kutoa mafundisho ya uongo kuhusu mambo muhimu ya Biblia kama, Kifo cha Yesu Kristo, Uunga wa Kristo, Biblia ni neno la pekee la Mungu, ukweli kuhusu miu-jiza, hukumu ya wale ambao wanamkataa Kristo, kuhusu kanisa; affisi za kanisa, meza ya Bwana, ubatizo, toba, heshima kwa Maria na maombi kwa wale ambao wamekufa. Mambo haya yote wengi wanaihu-biri kwa uongo. Wao wanatumia kila fursa katika maandishi yao, katika

Page 5: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

mahubiri yao, katika magazeti na katika makanisa mwao, kuona kwamba wanaeneza uongo kwa watu wote. Unapotazama nchi nzima utapata kwamba nchi yote imejawa na walimu wengi wa uongo na ma-fundisho yao yako kila mahali. Kukata ukweli huu, ni kuwa mpumbavu. Ukweli ni kwamba tuko katika siku mbaya sana na za hatari. Kwa sababu ya ukweli huu, mwandishi wa Waebrania anatuonya, “Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya ki-geni.” Mafundisho ya uongo ni hatari sana, Unapoangalia walimu wengi wa uongo, utaona kwamba ni watu ambao wako na bidii sana na kwa sababu ya bidii hii, wengi wanawaza kwamba wao ni walimu wa kweli. Wengi wa walimu hawa ni watu ambao wamesoma sana na wanajua kuzungumza sana na watu. Wengi wanapendwa sana kwa sababu ya elimu yao na mazungumzo yao. Wengi wao pia ni watu ambao wanapenda kufanya mambo zuri juu ya wale ambao wanaonekan kuwa watu ambo ni maskini au wagonjwa au wako katika hali ya mahitaji. Wengi wao wanatosheka na msemo wa kwamba hakuna mtu ambaye hafanyi makosa. Wengi wa walimu hawa wa uongo mafundisho yao huwa wanaichanganya na ukweli kidogo ili kuwapotosha wasikilizaji wao. Wengi wanapowasikia, wao husema kweli huyu mtu ni mwalimu wa kweli kwa sababu katika maneno yake kuna ukweli. Lakini wanakosa kujua kwamba ukweli huo unapeanwa husu au kidogo lakini maneno ya uongo ndio huwa yanakuwa mengi sana. Kile pia wasikilizaji wao huwa hawajui ni kwamba biblia inafundisha kwamba shetani huwa anajigeuza kuwa kama malaika wa nuru (2 wakorintho 11:14). Kuna hali ya unyonge katika wakristo wengi, kwa sababu mara kwa mara walimu wengi wa uongo wanaposema hadithi kwa njia ambyo ni ya kuwapen-deze na wawe wanazungumza maneno ambayo inaguza mioyo yao na kuwafanya wafurahi, wao mara mingi huwa wanamwamini mtu huyu. Ikiwa mtu anampinga, basi wataona kwamba kweli huyu mtu anakatiliwa kwa sababu ya ukweli. Haya mambo yote yapo nasi leo kila mahali. Hili si jambo la kukataliwa na mtu yeyote, kwa sababu ya walimu hawa na uongo, ni lazima kila wakati tupaze sauti kwa kuwaonya wengi kwamba, “msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni.”

Page 6: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Swali ni je, tunawezaje kujilinda kutokana na mafundisho ya uongo? Jibu ni, silaha ambayo tuko nayo ni neno la Mungu. Ikiwa kila siku tuta-soma Biblia, katika maombi yetu tutaomba kulingana na mafundisho ya Biblia, na kujifundisha Biblia kila siku na kuitii, basi ndipo tutaweza ku-jilinda kutokana na mafundisho ya uongo. Ni lazima kila wakati tutafute kusikia kutoka kwa Mungu ambaye ndiye Baba wetu. Ni lazima tusome Biblia kwa njia ya uangalifu sana (Yohana 5:39). Ikiwa tunataka silaha ambayo itatuwezesha kumshinda shetani, basi ni lazima tutumie upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu. Lakini pia ndipo tuweze kulitumia vyema neno la Mungu, ni lazima tulisome kila siku na tuombe kila wakati kwamba Mungu ataendelea kutufundisha neno lake. Wengi huwa wanaanguka kwa sababu ya kupuuza neon la Mungu. Katika nyakati kama za leo wakati watu wengi wanashughulika na mambo mengi, ni wachache sana ambao wanasoma Biblia zao jinsi inawapaswa kuisoma. Ni jambo la huzuni kwamba vitabu vingine vinasomwa sana kuliko jinis Biblia inavyosomwa ambayo iko na nguvu za kuleta wokovu. Kama kungekuwa na wengi ambao walikuwa wanaisoma na kuimini Biblia kwa ukweli, basi madhehebu mengine mengi hayageleta uharibifu mkubwa katika kanisa ambao tunaona sasa. Kanisa ambalo linasoma Biblia na kuitii ni kanisa lenye nguvu sana na kanisa ambalo limelindwa sana na Mungu. Biblia ni kitabu kimojaBwana Yesus Kristo na mitume wake kila mara walinukuu sana Agano la Kale, kutuonyesha umuhimu wa Agano hilo. Agano la kale liko na nguvu kama tu Agano Jipya. Wao walinukuu Agano hili na walilifa-hamu kuwa ni neon la Mungu. Miujiza ambayo ilifanyika katika Agano la kale, inadhihirika kuwa ya ukweli na kwamba hakuna mtu yeytoe am-baye anaweza kukosa kuiamini. Maandiko ya Musa katika kitabu cha Mwanzo had Kumbukumbu la Torati, ni mambao amabyo yanatajwa kama ya kistoria na kwa hivyo ni ya ukweli. Katika Agano hilo la kale, tunasoma kuhusu kifo cha yesus Kristo kama sadaka kwa ajili ya watu wake. Jambo hilo tunalisoma katika Biblia yote hadi kitabu cha Ufunuo. Pia katika Biblia tunasoma kuhusu muujiza mkuu ambao ni kufufka kwa Kristo Yesu. Kufufuka huko kunadhibitishwa na ushahidi mwingi sana ambao yeyote ambaye anaukata, kweli yeye hatawahi kuamini lolote.

Page 7: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Unaposma mambo haya yote utaoan kwamba ni vigumu sana kukosa kuamini. Ni jambo la hatari sana kukosa kuamini. Ikiwa hatutatilia maanani Biblia, tutabaki tukiwa wale ambao hatuamini.Unaposoma Agano Jipya, utaona kwamba hakuna mahali ambapo kumetajwa kutolewa kwa sadaka za Agano la Kale ambazo wengi leo wanaendelea kuhubiri kama njia ya wokovu. Katika agano hili hatusomi lolote kuhusu ubatizo kama njia ya ubatizo. Unaposma utaona kwamba meza ya Bwana ni jambo la muhimu sana lakini si njia ya wokovu. Una-posoma hutaona mahali popote ambapo kazi ya wachungaji ni kutoa sadaka za wanyama au meza bwana kuitwa sadaka au kwamba ni kazi ya kasisi kuwasamehe watu dhambi zao. Pia unaposoma Agano hilo hutaona mahali ambapo tunanaambiwa tuakishe misuma au tuleta maua katika kanisa. Hakuna mahali ambapo tunaanmbiwa tubebe bendera au tuombe tukiangalia mahali fulani au tuchome ubani au tumwombe maria mama wa Yesu au malaika au mitume. Haya ni mambo ambayo hutapata katika biblia. Ikiwa hatutaki kuchukuliwa na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni, basi ni lazima tukumbuke maneno ya Bwana Yesu katika Biblia. Ni lazima tuisome Biblia kwa uangalifu sana. Kutojua au kupu-uza Biblia ndio mwanzo wa mafundisho ya uongo. Kujua na kutii Biblia indio mwanzo silaha kali dhidi ya mafundisho ya uongo. II. Pili, kunahimizo: “..maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao walikwenda navyo hawakupata faida.”Kuna maneno mawili katika mstari huu ambayo tunafaa kuelewa vizuri; “vyakula” na “neema.” Kufahamu umuhimu wa “vyakula,” lazima tukumbuke kwanza sheria ya Wayahudi ambayo ilihusu vyakula. Ukisoma kitabu cha Walawi, utapata kwamba kulikuwa na baadhi ya wanyama na ndege ambao walikubalika kuliwa na wengine walikuwa wamekataliwa. Kuna vyakula ambavyo vilihesabika kuwa safi na vingine chafu. Ulaji wa wanyama fulani am-bao walikuwa wamekataliwa, ulimfanya yule ambaye alikuwa umekula mnyama huyu kuwa mchafu mbele za Mungu. Kwa sababu hiyo, watu hawakula wanyama hawa ambao walikuwa wamekataliwa. Swali ni je, sheria hii iliendelea hata baada ya Kristo kurudi mbinguni au ujumbe wa

Page 8: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

injili unafanya sheria hii iwe au haipo tena? Je, Wayahudi ambao wa-likuwa hawajaamini walihitajika kutii sheria hizi? Je, Wayahudi ambao walikuwa wamemwamini Kristo walihitajika kutii sheria hii kabla ya Kristo kufa msalabani na kabla ya pazia la hekalu kupasuka katika vipanda viwili? Je, sheria hii kuhusu vyakula iliondolewa kabisa au la? Je, wale ambao wamemwamini Kristo dhamira zao zitawasumbua kwa sababu ya kula vyakula fulani?Maswali kama haya, ndio msingi wa mafundisho mengi ya uongo. Kwa kawaida wengi wanayazingatia sana na kumaliza muda wao mwingi wakiyazungmzia. Paulo aliyazungumzia mambo haya katika vitabu vi-tatu vya biblia ambavyo yeye mwenyewe aliviandika. Alisema, “lakini chakula hakitudhuhurishi mbele za Mungu....Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa....Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji” (1 Wakorintho 8:8; Warumi 14:17; Wakolosai 2:16). Hali ya mwanadamu kushikama na mambo haya inadhirisha wazi uovu wa mwanadamu. Leo wengi wanahusisha wokovu na kula au kunywa kwa vyakula au vinywaji fulani. Yaani wanasema kwamba ikiwa mtu anakula nguruwe, basi mtu huyu hajaokoka na yeye anaenda jahanum. Huu ni uongo kwani hatuingia mbinguni kwa kula vyakula fulani au kunywa vinywaji Fulani, baali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hivyo wakati mwandishi wa Waebrania anazungulza kuhusu vyakula, anazungumzia kuhusus sheria za vyakula au sheria ambazo zimetungwa na wanadmu au kuhusu sheria za Mungu ambazo zimetimika katika In-jili ya kristo Yesus. Hili jambo la vyakula lilifahamika vyema zaidi katika nyakati za mitume kwa sababu wao walikuwa watu wa kutoka Is-raeli.Kwa upande mwingine anapozungumza kuhusu neema, anazungumzia kuhusu Injili ya Yesus Kristo. Kulingana na ujumbe wa injili ya Kristo Yesu, neema ndio inafafanua ujumbe wa injili kwa wote, neema ndio chanzo, neema ndio inatekeleza na ni neema ambayo inafanya mwanadamu aokolewe. Tunahesabiwa wenye haki kwa neema. Tunaitwa kuwa wana wa Mungu kwa neema. Tunasamehewa dhambi zetu kwa neema. Tumaini ambalo tuko nalo, limetufikia kwa neema. Tunaamini ujumbe wa injili kwa neema. Tunachaguliwa kuokoka kwa neema. Kwa sababu ya haya yote,

Page 9: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Paulo anaandika katika Warumi akisema kwamba, tunahesabiwa haki kwa neema (Warumi 3:24). Pia anamwambia Tito kwamba, neema ya Mungu ambayo inaleta wokovu imefunuliwa kwa wanadamu wote (Tito 2:11; Wagalatia 1:15; Waefeso 1:7; 2 Wathesalonike 2:16; Matendo ya Mitume 18:27; Warumi 1;15; Waefeso 2:5; Warumi 6:15).Mwandishi wa Waebrania anatfautisha mambo haya mawili; vyakula na neema, kuonyesha kwamba haya mambo mwili yako kinyume. Sheria ya vyakula na neema ni mambo mawili tofautu kabisa. Neema inatuonye-sha upendo mkuu wa Mungu ndani ya Kristo Yesu. Anaendela kuonye-sha kwamba wokovu na maisha ya wokovu ni kwa neema na si kwa she-ria ya vyakula fulani fulani. Maisha ya ukristo inejengwa kwa neema ya Mungu na si kwa kuzingatia vyakula fulani au sheria ambazo zime-tungwa na wanadamu fulani. Kuna wale ambao wanataka kumjua Kristo. Wao wanatamani kujengwa kiroho sana kwa sababu wanajua kwamba wao bado wako na dhambi ndani mwao na kwamba wamepungukiwa na kufahamu katika mambo ya Mungu. Wao wanaona na kuhisis uzito wa dhambi katika mioyo yao na wanajua kwamba ni Mungu pekee ambaye anaweza kuwasaidia katika Kristo Yesu. Imani yao ni dhaifu na tumaini lao ni hafifu na faraja yao ni kodogo. Wao wako na kiu cha kujua mengi zaidi, na kwa hivyo hawapumzika kila wakati wanatafutua ukweli. Je, wakristo hawa watapata wapi faraja na tumani la kweli na uhakika wa kweli? Wakiwa katika hali hii, adui wa nafsi zao huja na kuwaonyesha njia ya uongo. Yeye anawaonyesha kwamba injili ya kweli haitoshi, wao wanahitaji kuongezea vitu fulani fulani ili waweze kupata faraja na uhakika katika maisha yao ya kiroho. Yeye anawaonyesha kwamba ikiwa watafuata njia ambayo anawaonyesha, ni wazi kwamba wao watapata faraja na nguvu na tumani la kuingia mbinguni.Kwa mfano, utasikia wengi wakiwaambia, njoo katika kanisa letu. “Ji-unge na kanisa letu kwa sababu hilo ndilo kanisa ambalo linahubiri uk-weli na hatukosei popote. Njoo kwetu na Mungu atajibu maombi yako yote na utapata baraka nyingi sana katika maisha yako. Kuja na maisha yako hayatakuwa jnsi yalivyo sasa. Mchungaji wetu ni mtu ambaye ameitwa na kupakwa mafuta na Mungu, yeye akikuombea, wewe hutakuwa wa kawaida tena. Kuja leo kanisani mwetu na upokea baraka

Page 10: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

zote za Mungu na upate pumzisho kutoka kwa taabu za dunia hii. Wengine wanawaambia, “kuja kwetu, wachana na makanisa ambayo yanakufunga na hayakuptie nafasi ya kuwa huru ndani ya Kristo. Wachana na makanisa ambayo kila wakati wanahubiri tu wokovu na hawakuambii jinsi unapaswa kupata pesa na kufurahia maisha ya hapa ulimwenguni. Mungu hakukuumba uwe maskini au uwe mgonjwa, Mungu anataka akupatie kila kitu unataka, lakini uko katika kanisa mbaya.” Ukweli ni kwamba, haya mambo yote huwa yanasemwa na wale ambao hawana haja ya kuwaona watu wakiokoka na kufuata njia ya ukweli. Leo unapotazama katika makanisa mengi, utaona kwamba wengi wameumizwa katika nafis zao. Walimu wa uongo huziteka nyara zile nafsi ambazo hazina msimamo wa kiroho na kuziongoza katika shida mingi za kiroho kwa mingi nyingi sana. Je, Biblia inasema nini kuhusu jambo hili? Katika kila jambo lazima tuhakikishe kwamba tunafahamu kile Biblia inasema kwa sababu Biblia ni neno la Mungu na d Mungu ndiye huwa anatuongoza katika kila jambo. Paulo anaandika akisema kwamba, wokovu au kukua katika wokovu huja kwa neema na si kwa kula vyakula na kunywa vinywaji fu-lani fulani. Anasema, “mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kun-yenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamma za mwili” (Wakosai 2:23). Lakini mambo haya, hayana nguvu za kuleta wokovu au uponyaji wa nafsi. Huwa yanamwacha yule ambaye anayaamini kuwa mtu mwenye shida zaidi.Ufahamu wa kazi ya neema ya Mungu, kusudi la neema hiyo, na jinsi in-avyowokoa mwenye dhambi kupitia kwa kazi ya kristo Yesu; Kuelewa vyema mafundisho ya neema ya Mungu, na upendo wa Mungu katika Kristo na kuhesabiwa haki kupitia kwa imani na kazi ambayo Kristo anaendela kufanya akiwa Kuhani Mkuu, mambo ambayo yanamfanya mtu aokoke na aendelee katika wokovu maishani mwake mwote. Hivi ndivyo wote amabo wamewamini Kristo na kuendelea kumwamini wamepata nafasi ya kuingia ufalme wa Mungu na kupata amani ya milele. Hii ndiyo tabibu ya kweli ya nafis ambayo inataka kuwa amani na tumaini na imani ya kweli. Hii inaweza kuonekana kuwa ni jambo

Page 11: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

rahisi sana, lakini ukweli ni kwamba mambo na sheria za wanadamu haziwezi kamwe kuleta amani na tumaini na imani ya ukweli kwa nafis ambayo imo katika dhambi. Sababu kwa nini wengi wanaischukia njia hii, ni kwa sababu ya kiburi na majivuno.Leo pia tunapaswa kutumia njia hiyo hiyo ambayo ilitumika na wengi ambo sasa wako mbinguni na wengi ambao bado wako katika ulimwengu huu. Hii ndio njia ya kweli. Pia leo kuna wakristo ambao wamechukuliwa na mafundisho ya namna nyingine nyingeni na ya ki-geni kwa sabau wanatafuta ukweli katika mikono ya walimu wa uongo. Sisi ambao ni wahubiri wa neno la Mungu wa kweli, tuenedelee kwa bidii sana na bila kukoma kuwaeleza wote kila mahali kwamba, ni kwa neema pekee yake ambapo mtu anahesabiawa mwenye haki, na ni kwa neema pekee mtu anaendelea na maisha ya wokovu, wala si kwa sheria za vyakula na vinywaji fulani fulani. Tupaze sauti zetu na tuhubiri neema ya Mungu kwa wote kupitia kwa imani ndani ya kristo Yesu. Tangu siku za mitume, wakuwepo wengi ambao wamedai kuwa wako na dawa za kuponya nafis za wanadamu kutoka katika dhambi kwa nguvu zao. Hata katika makanisa yetu leo, kuna wale ambao katika mioyo yao, wamerudi nyuma katika imani kwa sababu hawapendezwi na kuabudu Mungu kwa ukweli na wamerudia sheria za wanadamu na mitindo ya wanadamu. Wao wanapenda kusikia kwamba ni kujitahidi kwa mwanadamu ambako kunamwigiza mbinguni. Wao wamefurahish-swa na kusikia kwamba katika meza ya Bwana, mkate ni mwili halisi wa Kristo na kikombe ni damu halisi ya Kristo Yesu. Wamepuuza neema na kupenda tamaduni za wanadamu. Wao huhudhuria makanisa kwa sababu ya siku ya mazishi yao waombewe, au miili yao iweze kuzikwa mashambani mwao au watoto wao wabatizwe hata kama wao hawa-jokoka na kila siku wawe wanamwendea kasisi awasamehe dhambi zao. Mambo haya yote ni bure na ni mambo ya giza na wale ambao wanayafanya, ni watu wa giza na wanaenda gizani wasipotubu. Wao wamesahau neema ya Mungu na wejitolea katika sheria za vyakula na tamaduni za wanadamu.Wale ambao tumeokoka, tujichunguze ili kwamba tuhakikishe kama ukristo wetu msingi wake ni neema ya Mungu katika Kristo Yesu. Tuhakikishe kwamba tunafahamu vyema mafundisho ya neema ya

Page 12: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Mungu. Hakuna jambo ambalo litatuhimiza katika siku za magonjwa, siku za majaribia makali, wakati tunakufa na wakati wa uchungu, isipokuwa neema ya Mungu kwetu ndani ya Kristo. Ni neema ya Kristo Yesu pekee katika mioyo yetu na ikiwa msingi wa ukristo wetu, ndio itatuletea amani katika maisha yetu na katika mioyo yetu. Ikiwa tutazin-gatia mafundisho ya wanadamu na tamaduni zao, basi tujue kwamba tuko katika hatari kubwa sana ya kuingia jahanum. Dini za uongo, zi-naweza kuonekana kuwa ni za kweli kwa sababu ya wale ambao wanaongoza ni watu wenye hekima na masoma ya juu sana na kwamba wanatenda miujiza mingi sana, lakini ukweli ni kwamba ni dini za uongo kwa sababu msingi wake ni tamaduni na hekima ya mwadamu. Lakini ikiwa dini zetu msingi wake ni neema ya Kristo katika kila kitu, basi tutaendelea kujengwa kiroho na kuhimizwa na tutakua zaidi ndani ya Kristo.III. Tatu, kuna ukweli juu ya vitu ambayo havina faida: “..wala si kwa vyakula ambavyo wao walikwenda navyo hawakupata faida.” Maneno haya ni kwa wale wote ambao wamegeukia sheria za vyakula na za wadamu na kuyaacha mafundisho ya neema. Katika mioyo ya watu hawa hakuna furaha na dini yao haiwaletei furaha yoyote au faida yoyote. Sheria za mwanadamu na mambo ambayo ameyaongeza juu ya injili ya Bwana Kristo hayajamletea mwanadamu faidia yoyote ya kiroho hata kama wengi wanayapenda na kuyafundisha kwa bidii. Hawana amani katika mioyo yao; hakuna utakatifu ambao huwa yanam-wongoza mwanadamu ndani; pia hayamfanyi mwanadamu akue katika neema na pia huwa yanamfanya mwanadamu asiwe mwenye faida yey-ote kwa kanisa na hata kwa walimwengu. Ukweli ni kwamba sheria za vyakula na tamaduni za wanadamu hazimfaidi mwanadamu.Katika historia, kumekuwepo na dini, madhehebu na watu ambao waliji-tolea sana katika dini zao na walionekana na wengi kuwa watu ambao walimpenda Mungu sana. Wale ambao walikuwa karibu walijua kwamba kweli madhehebu hayo au watu hawa, walikuwa watu ambao walimcha Mungu sana. Lakini unaposoma kwa karibu sana kuhusu mad-hehebu haya na watu hawa, utaona kwamba hawa ni watu ambao hawakuwa na amani katika mioyo yao. Unaposoma utaona kwamba hawa watu hawakusaidia chohcote katika ulimwengu katika mambo ya

Page 13: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

kiroho.Hakuna nafsi ambazo walisaidia kuingia katika ufalme wa mbin-guni. Sababu ya kutofaulu kwao ni, wao walisisitiza sana tamaduni za wanadamu na sheria za vyakula badala ya kuhubiri neema ya Mungu ambayo inawafikia wanadamu katika Kristo Yesu. Wao walizingatia sana sheria badala ya neema ya Mungu.Ni jambo la kusikitisha kwamba kuna wengi ambao wameacha makanisa ambayo inafundisha neno la Mungu la kweli na kuwaongoza wengi kwa Kristo na wameenda katika makanisa ambayo inazingatia sheria za wanadamu and mitindo ya kitamaduni kwa sababu mioyo yao inataka mambo kama hayo. Kwa kufanya hivi, wao wamegeuka kutoka kwa neema na wamegeukia sheria na tamaduni za wanadamu. Kwa sababu ya tabia hii, wao sasa hawana uzuri wowote ambao sasa wanaleta kwa kanisa la Kristo. Wao sasa ni wapinga Kristo. Ukweli ni kwamba sheria za vyakula hazifaidi mtu yeyote hata wale ambao wanadai kuzifuata. Dini ambayo inazingatia tamaduni za wanadamu na sheria zao, huwa haimletei mtu yeyote faidi kiroho. Ni ujumbe wa Injili ya Yesus Kristo ambayo huwa inaleta uzima katika nafsi ya mtu na wale ambao wanakataa ujumbe huu, basi wanapoteza maisha yao na kujitayarisha wenyewe kwa ajili ya jahanum. Sasa nataka tutatazama nguvu za ujumbe wa injili ya neema ambayo in-abadilisha maisha ya wengi. Wale ambao wamefaidika kutokana na ujumbe ni wale ambao hawakuongeza chochote juu ya ujumbe huo wala kuondoa chochote juu ya ujumbe huo. Wao hawakuzingatai tamaduni za wanadamu wala sheria za vyakula.Ni kwa neema Martin Luther alifanya kazi ambayo alipewa na Mungu katika ulimwengu huu. Alifaulu kwa sababu aliendelea kuwaeleza wote kwamba tunahesabiwa haki kwa imani pekee ndani ya kristo, wala si kwa kuzingatia sheria. Huu ndio ukweli ambao ulimwezesha kuleta nuru katika bara la Uropa na kuondoa wengi katika minyororo ya kikatoliki.Ni kwa neema na si kwa sheria ya vyakula wengi waliuliwa kwa sababu ya kuenena injili ya Kristo. Wao walifahamu vyema kabisa neema ni nini na walifundisha kwa wazi kabisa kwamba Yesu Kristo ndiye Kuhani Mkuu na kwamba wokovu unapatikana kwa neema pekee. Wao waliheshimu neema ya Mungu na Mungu naye aliwatunikia heshima.

Page 14: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

Ni kwa neema pekee na si kwa sheria ya vyakula wengi wamejitoa kabisa kuhubiri injili ya Kristo iletayo nuru. Wengi wa hawa watu haja-soma sana na hawakuheshimiwa na mtu, lakini hata hivyo walifundisha na kuhubiri injili ya neema.Ni kwa neema watumishi wengi wa Mungu wamewafaidi wengi kiroho kwa miaka mingi sasa. Wamefanya hivi kwa kutegemea na kufundisha tu neema ya Mungu kila wakati. Kwa kufanya hivi Mungu aliwatunukia heshima. Wao walijitoa kutangaza neema ya Mungu na neema hiyo ili-wafanya wawasaidie wengi kiroho.Unaposoma kuhusu historia ya dini ya ukristo utaona kwamba wale am-bao wameutingisha ulimwengu na kuacha vizazi vingi vikiamini Mungu; wale ambao wameamsha dhamara za wengi na kuwaonyesha wengi njia ya wokovu na kuijenga jamii ya Mungu, si wale ambao wamezingatia sheria za wanadamu na sheria za vyakula, bali ni wale ambao wameihu-biri neema ya Mungu. Ni vizuri ikiwa tutazingatia ukweli, kwa sababu ni ukweli ambao utatusaidia kujua kwamba ukristo wa ukweli hautokani na sheria za wanadamu au sheria za vyakula. Tuzingatie sana ukweli kutoka katika histori na sasa, na tutaona kwamba dini ambayo inazingatia sheria za vyakula haimfaidi yeyote hata yule ambaye anaifuata na kuihimiza. Ni dini ya neema ambayo inaleta amani ya kweli moyoni, maisha ya utakatifu na kuwa mtu mwenye kuwasaidia wengi kiroho.Ninapomalizia, ninataka tuone tunajifunza nini sisi leo kutokana na fundisho haya kwa sababu hata leo tunaishi katika siku ambazo kuna waongo wengi sana. Kwa hivyo maneno ambayo ninataka kusema hapa yanapaswa kuzingatiwa sana na kila mmoja wetu.1. Kwanza, Tusishangae jinsis walimu wa uongo wanavyoendela kuwa wengi na kuonekana kwamba wanafaulu katika uongo wao. Jambo hili limekuwepo tangu siku za mitume, manabii wa uongo wakuwepo siku zote. Kristo Yesu na mitume wake, walitabiri kwamba walimu wa uongo watakuwepo wengi kabla ya mwisho wa dunia kufika. Hii imekusudiwa na Mungu kufanya imani yetu ndani ya Kristo kuwa dhabiti na kuona kwamba ni nani ambaye kweli imani yake ni ya kweli. Kama hawa wal-imu hawangekuwepo katika ulimwengu huu, basi ni wazi kwamba, Bib-lia ingekuwa inasema uongo. Lakini tukumbuke Biblia ni neno la Mungu, na kile Mungu amesema katika neno la Mungu, sharti kitimie.

Page 15: Web viewMafundisho ya namna nyingine, nyingine na ya kigeni. "Msichukuliwa na mafundisho ya namna nyingine, nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa

2. Pili, tuko na waajibu wa kupinga mafundisho ya uongo na kukata kuchukuliwa na mafundisho ya kila aina na ya kigeni. Tusilale kwa sababu kila mtu ambaye ako karibu nasi, tajiri au maskini, mtoto au mtu mzima, wote wanachukuliwa na mafundisho haya ya uongo. Tuwe dhibiti katika imani ya kweli.Tupinge mafundisho ya uongo na tuendelee kushikilia imani ya kweli. Tusiogope kuwaeleza wengi kuhusu imani yetu ndani ya Kristo na kuwa imara katika imani hiyo. Shetani ni mwizi na ikiwa tutaogopa kuzungumza na kukosa kumpinga na mafundisho yake, tutakuwa tu-namweshimu na kumkosea Mungu heshima ambaye anastahili Yeye pe-kee. 3. Tatu, tuendelea kuzingatia kanuni za Biblia za kanisa na tuwa-fundishe watoto wetu na wengine kanuni hizo. Tusiwasikilize wale am-bao wangependa tuziache kanisa zetu ambazo zinahuibiri ukweli wakati ambapo kunamatatizo. Tujaribu kuona kwamba tunaendeleza msingi bora wa mafundisho bora katika makanisa yetu. Hata wakati kuna shida, tuendelee kuona kwamba tunatatua shida hizo kwa njia ya Biblia.4. Nne, tuhakikishe kwamba tunaeldelea katika wokovu. Tuhakikishe kwamba sisi wenyewe tumeokoka. Wakati hatari ipo hii ya walimu wa uongo, ni wakati wa kujichunguza kila mmoja wetu awone kama kweli yeye ameokoka au la. Si vyema kutosheka kwamba kwa sababu wewe si wa dini fulani na kwamba wewe unajua Biblia, basi ni wazi kwamba wewe ni mtoto wa Mungu na unaenda mbinguni. Tusisahau jambo hili kamwe. Tusipumzike hadi tumejua kwamba kweli tumeoshwa dhamira zetu na damu ya Yesus Kristo. Na kwamba pia, Roho Mtakatifu anashuhudia katika mioyo yetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu. Huu ndio ukweli na hii ndio dini ya kweli. Huu ndio ukweli ambao ni wa milele. Hii ni kuwa na neema ndani ya moyo wako na si tu hekima ya wanadamu ambayo haimsaidii mtu yeyote.