70
MAKALA YA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA Julai, 2015 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

  • Upload
    others

  • View
    50

  • Download
    2

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

MAKALA YA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

Julai, 2015

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Page 2: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

MAKALA YA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

Julai, 2015

PICHA:Juu Kushoto: Hifadhi ya Mazingira Asilia–Uluguru

Juu Kulia: Makao Makuu ya TFS Chini Kushoto: Ufugaji nyuki-Babati

Chini Kulia: Shamba la miti ya Mikaratusi

Page 3: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

ii

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Mr. Juma S. Mgoo (Mtendaji Mkuu)

Makala ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania imeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kutoa taarifa za mafanikio ya Wakala tangu kuanzishwa kwake. Makala hii imeandaliwa kwa mujibu wa maelekezo ya Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inayozitaka Wakala zote za Serikali kuandaa Makala za utendaji wake tangu kuanzishwa kwake. Lengo la Makala hii kwa mujibu wa hadidu za rejea ni pamoja na:

Kuainisha kwa kina taarifa za kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), ikiwa ni pamoja na lengo kuu la kuanzishwa kwake, Dira, Dhima, maadili makuu, Majukumu makuu; pamoja na taarifa/kumbukumbu mbalimbali za Wakala;

Kuelezea changamoto mbalimbali pamoja na wazo, sababu za ndani au za nje zilizopelekea kuanzishwa kwa Wakala;

Kuanisha Changamoto mbalimbali za ndani na nje ambazo Wakala umekabiliana au unakabiliana nazo tangu kuanzishwa kwake;

Kufanya tathimini ya Wakala kwa kuelezea hali ya utendaji kabla na baada ya kuwa Wakala, kwa lengo la kuainisha na kuzielezea tofauti za kiutendaji zilizokuwepo;

Kutoa taarifa za rasilimaliwatu, mapato na matumizi na mwenendo wake.

Wakala wa Huduma za Misitu umekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, aidha kumekuwepo na changamoto kadhaa ambazo Wakala umekabiliana nazo tangua utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa kwanza 2010/11-2013/14 (Kwasasa Wakala unatekeleza Mpango Mkakati wa pili 2014/15 -2018/19).

Ninayo furaha kuwasilisha Makala hii inayoainisha mafanikio ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu (2010/11-2013/14) tangu kuanzishwa kwake.

Juma S. Mgoo

DIBAJI

Page 4: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

iii

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

MUHTSARI

Makala hii inaelezea kuhusu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ambao ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011. Kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002.

Makala inaainisha Dira, Dhima, Maadili makuu pamoja na Majukumu Makuu ya Wakala. Makala hii inaainisha kwa kina utendaji kazi wa Wakala tangu kuanzishwa kwake, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto mbalimbali ulizokabiliana nazo. Aidha, makala inafanya tathimini ya kina ya kuonesha utekelezaji wa majukumu kabla na baada ya kuanzishwa kwake. Pamoja na mambo mengine Makala hii inaainisha changamoto zilizokuwepo kabla ya kuanzishwa kwa Wakala (Idara ya Misitu na Nyuki), ikiwa ni Changamoto za ndani ya Idara ya Misitu na Nyuki na zile za nje ya Idara.

Uwepo wa Wakala unazingatia agizo la kuanzishwa kwake kwa mujibu wa Hati ya mwaka 2010 ambayo imebainisha kwa kina kuhusu utawala, muundo na majukumu ya msingi katika utendaji wa shughuli za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Aidha, hati imebainisha majukumu ya Bodi ya Ushauri ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kumshauri Waziri wa Maliasili na

Utalii (WMU) kuhusu utendaji na ufanisi wa Wakala. Hati pia imeainisha orodha ya misitu yote ya hifadhi inayopaswa kusimamiwa na Wakala.

Katika Makala hii Muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umeelezewa. Muundo huo unajumuisha Mtendaji Mkuu, Wakurugenzi watatu, Meneja wawili wa Vitengo vya Sheria na ugavi, Mhasibu Mkuu na Mkaguzi Mkuu wa ndani. Wakala pia una Mameneja wa Kanda saba (7) na wa Mashamba ya miti 18. Vile vile Wakala umeboresha utendaji wake kupitia wilaya; ambapo Mameneja wa wilaya 118 wameteuliwa na kupatiwa nyenzo za kazi. Kanda hizo za Wakala ni; Mashariki, Kaskazini, Kati, Kusini, Nyanda za juu Kusini, Ziwa na Magharibi.

Makala inaelezea kuhusu mifumo mbalimbali ya kimenejimenti iliyowekwa na Wakala kwa malengo ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji, kuboresha utoaji huduma kwa wadau na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za Wakala. Mifumo hii ni pamoja na Mwongozo wa Utendaji Kazi, Hati ya Kuanzisha Wakala, Mpango Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma kwa Mteja pamoja na Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko. Aidha, mifumo mingine iliyoelezewa katika makal hii ni Mfumo wa usimamizi na uhakiki wa fedha (Integrated Financial Management System (IFMS)), Human Capital Information Management System, Masjala na Uhasibu.

Page 5: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

iv

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Makala inaelezea utendaji Kazi wa Wakala kwa kuzingatia Sheria ya Wakala za Serikali, Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)” Sheria ya Misitu Sur 323 ya mwaka 2002, Sheria ya Ufugaji Nyuki Sura 224 ya mwaka 2002 na Programu za Taifa za Misitu na Nyuki za mwaka 2001 ambazo ziliandaliwa kama vyombo vya kutekeleza Sera za Taifa ya Misitu na ya Nyuki. Makala pia inatoa maelezo ya kuhusu utekelezaji wa shuguli zake kwa kupitia: Mpango Mkakati (Strategic plan 2010/2014); Mipango ya Biashara ya kila mwaka (Business Plans); Mfumo wa wazi wa kupima utendaji kazi (OPRAS); Uperembaji na Tathmini (Monitoring and Evaluation) pamoja na huduma Mkataba wa Huduma kwa Mteja, Mfumo wa Malalamiko; na Mfumo wa Usimamizi na uhakiki wa fedha (IFMS). Makala imeainisha muhtasari wa masuala makuu yaliyofanikiwa chini ya Wakala katika kipindi cha miaka mitatu yakilinganishwa na yale yaliyotekelezwa na Idara ya Misitu na Nyuki katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya kukabidhi majukumu kwa Wakala.

Ufanisi wa Makusanyo ya maduhuli kwa miaka mitatu (2011/12-2013/14) chini ya Wakala umeongezeka, ambapo makusanyo halisi yalikuwa TAS 199,771,416,440 ambayo ni asilimia 101(101%) ya matarajio (maoteo) ya makusanyo ya TAS 197,467,522,456. Mwenendo wa ukusanyaji wa maduhuli unaonesha kuwa ukasanyaji ulikuwa unaongezeka mwaka hadi mwaka. Wakala unakusanya wastani wa TAS 66 bilioni kwa mwaka tangu kuanzishwa kwake ukilinganisha na kiwango cha juu cha makusanyo ya TASTAS billioni 28 kwa Mwaka kilichowahi kukusanywa na Idara kwa muda wote wa utendaji. Aidha, Mapato ya TRA yaliyokusanywa na Wakala kutokana na mauzo ya miti ya kupandwa kutoka kwa wateja wake yalifi kia jumla ya TAS 108,740,000,000. Kwa sasa ukusanyaji mapato wa Wakala ni zaidi ya asilimia 100 ya maoteo. Kwa mfano

Mwaka 2014/15 Wakala umekusanya kiasi cha TZS 85,475,560,582 ambacho ni sawa na asilimia 105 ya maoteo ya shilingi 81,228,595,000 yaliyokadiriwa.

Vilevile Wakala umewezesha sekta ndogo ya ufugaji nyuki katika uzalishaji wa mazao ya nyuki, ambapo tani 1,605 za nta zilizalishwa zikiwa na thamani ya TAS. 10,644,056,759, na tani 728 za asali zenye thamani ta Tsh. 2,753,284,771 zilizalishwa na kuwezesha sekta ndogo ya ufugaji nyuki iliweza kuchangia katika pato la taifa na kupunguza umaskini.

Katika kuboresha usimamizi na uendelezaji misitu, Wakala umeweza kuongeza kasi ya upandaji miti katika mashamba ya miti kila mwaka ili kukidhi mahitaji ya mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na kwa kushirikisha wadau mbalimbali kama wananchi/ jamii na taasisi kama shule katika kupanda miti na kuimarisha uhifadhi. Katika kipindi cha 2011/12 hadi 2013/14 jumla ya miti 21,000,000 ilipandwa na jamii, wananchi na taasisi mbalimbali. Uendelezaji wa mashamba ya miti ya Wakala umekuwa hekta 39,776 (2010/11 – 2014/15) ambapo upanuzi ni hekta 15,080.5 na upandaji wa kurudishia maeneo yaliyovunwa hekta 24,695.5. Upandaji huo ni sawa na wastani wa hekta 7,955 kwa mwaka.

Page 6: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

v

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

DIBAJI ................................................................................................................................ iiMUHTSARI ...................................................................................................................... iiiORODHA YA JEDWALI .................................................................................................... vii 1. UTANGULIZI .......................................................................................................... 1 1.1 Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania .......... 1 1.2 Dira ............................................................................................................ 1 1.3 Dhima ........................................................................................................ 1 1.4 Maadili makuu ........................................................................................... 1 1.5 Majukumu Makuu ..................................................................................... 2 1.6 Madhumuni ya Makala .............................................................................. 2

2. CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KABLA YA KUANZISHWA KWA WAKALA ..3 2.1 Changamoto za Ndani ya Idara .................................................................. 3 2.2 Changamoto za Nje ya Idara ..................................................................... 3

3. TATHMINI YA UTENDAJI KAZI KABLA NA BAADA YA KUWA WAKALA .... 4 3.1 Hali ya Utendaji kabla ya kuanzishwa Wakala .......................................... 4 3.2 Hali ya Utendaji baada kuanzishwa kwa Wakala ...................................... 8 3.2.1 Makao Makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ..8 3.2.2 Kanda za Wakala na Mashamba ya miti .................................... 10 3.3 Mifumo ya Utendaji ya Wakala Baada ya Kuanzishwa ...................... 11 3.3.1 Mwongozo wa Utendaji Kazi (Framework document) .............. 11 3.3.2 Hati ya Kuanzisha Wakala (Establishment Order) ..................... 12 3.3.3 Mpango Mkakati (Strategic plan) .............................................. 12 3.3.4 Mpango wa Biashara wa mwaka (Business Plan) ..................... 12 3.3.5 Mfumo wa wazi wa kupima utendaji kazi (OPRAS) .................. 12 3.3.6 Uperembaji na Tathmini (Monitoring and Evaluation) ............... 12 3.3.7 Mkataba wa Huduma kwa Mteja .............................................. 12 3.3.8 Mfumo wa Malalamiko ............................................................. 13 3.3.9 Mfumo wa Usimamizi na uhakiki wa fedha (IFMS) ................... 13 3.3.10 Mfumo wa Uhasibu ................................................................. 13 3.3.11 Human Capital Information Management System ................... 13 3.3.12 Masjala ya Wazi na Siri ............................................................. 14 3.4 Sheria zingine ambazo Wakala unazitumia kufanikisha utendaji ............ 14 3.4.1 Sheria ya Mazingira ya 2004 ..................................................... 14 3.4.2 Sheria ya Manunuzi ya Umma 2011 ......................................... 14

YALIYOMO

Page 7: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

vi

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

3.4.3 Sheria ya Fedha 2001 ................................................................ 14 3.4.4 Sheria ya Ardhi 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji 1999 .............. 18 3.4.5 Matumizi ya TEHAMA .............................................................. 18 3.5 Tathmini ya kazi za Wakala baada ya kuanzishwa ....................... 18

4. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TANGU KUANZISHWA WAKALA .. 19

5. MUHTASARI WA MCHANGUNUO WA UTENDAJI KABLA NA BAADA YA KUANZISHWA WAKALA ................................................................ 34

6. RASILIMALI FEDHA ............................................................................... 36

6.1 Mapato kabla ya kuanzishwa Wakala .......................................... 36 6.2 Mapato baada ya kuanzishwa Wakala ......................................... 38

7. RASILIMALI WATU ............................................................................. 39 8. MAPATO NA MATUMIZI YA WAKALA ............................................. 43 8.1 Vyanzo vya mapato ya Wakala kulingana na kasma /vifungu ...... 44 8.2 Mwenendo wa matumizi kabla ya Wakala .................................. 45 8.3 Mwenendo wa matumizi baada ya kuanzishwa Wakala ............. 46

9. UTOAJI WA TAARIFA ZA FEDHA ...................................................... 48 10. MIPANGO YA WAKALA ...................................................................... 48 10.1 Mipango Mkakati ya Wakala ....................................................... 48 10.2 Mpango wa Kibiashara ................................................................ 49 10.3 Utekelezaji wa Mipango .............................................................. 50 10.4 Uwasilishaji wa Mipango na Taarifa ............................................ 50

11. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA ..................................................... 51 11.1 Changamoto za utekelezaji majukumu ya Wakala ...................... 52 11.2 Changamoto zilizo nje ya Uwezo wa Wakala ............................. 52 11.2.1 Kucheleshwa kuhuishwa kwa Muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu .................................................................................. 52 11.2.2 Kuchelewa kwa kuhuishwa kwa Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002 ............................................................................ 52 11.2.3 Kuchelewa kukamilisha manunuzi .......................................... 52

12. MIPANGO YA BAADAYE YA WAKALA .............................................. 52

13. MIKAKATI ENDELEVU YA KUJITEGEMEA ........................................ 53

14. MASUALA MAKUU YA BAADAYE NA YA KIPAUMBELE KWA WAKALA ................................................................................................. 60

Page 8: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

vii

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ORODHA YA JEDWALI

Jedwali Na.1: Mafanikio/Shughuli za Idara Kabla ya kuanzishwa Wakala ................................ 6

Jedwali Na 2: Majengo na vitendea kazi vya FBD/TFS katika Makao Makuu na vituo vya nje..10

Jedwali Na. 3: Mashamba ya miti chini ya usimamizi wa Wakala kwa hadi mwaka 2014 ... 22

Jedwali Na. 4: Ujazo uliovunwa (cm) kutoka mashamba ya miti 2011/12-2013/14 .............. 22

Jedwali Na. 5a: Upandaji miti kitaifa kwa kipindi cha miaka 2011/12 - 2013/14 ...................... 23

Jedwali Na. 5b: Baadhi ya Mazao yatokanayo na misitu yaliyovunwa katika miaka mitatu ..... 25

Jedwali Na. 6: Eneo na Hali ya hifadhi za nyuki zilizopendekezwa ......................................... 26

Jedwali Na. 7: Idadi ya manzuki na mizinga inayosimamiwa na TFS ..................................... 27

Jedwali Na.8: Misitu ya Hifadhi iliyokuwa na wavamizi ....................................................... 24

Jedwali Na. 9: Makusanyo kutokana na Ukaguzi maalumu ................................................... 30

Jedwali 10: Watumishi wa TFS waliohudhuria mafunzo (2011/12 -2013/14) ......................... 31

Jedwali Na.11: Watumishi wapya kwa Kada walioajiriwa na Wakala ..................................... 31

Jedwali Na.12: Idadi ya vituo vya Wakala vilivyotembelewa kwa ajili ya Uperembaji kwa ........ Kanda 7 kati ya 2012/13 na 2013/14 .............................................................. 33

Jedwali Na. 13: Muhtasari wa Mchanganuo wa Utendaji wa Wakala .................................... 34

Jedwali Na.14: Bajeti ya Matumizi ya kawaida inajumuisha Idara na taasisi zake kwa ........... miaka minne (2007/08 - 2010/11) .................................................................. 37

Jedwali Na.15: Makadirio ya fedha za Miradi ya maendeleo kipindi cha 2007/08 - 2010/11 . 38

Jedwali Na 16: Rasilimali watu walioazimwa kutoka Idara ya Misitu .................................... 40

Jedwali Na.17: Mahitaji halisi ya Rasilimali ya Wakala .......................................................... 42

Jedwali Na18: Mwenendo wa mapato na Maoteo 2011/2012 hadi 2013/2015 .................... 43

Jedwali Na 19: Mgawanyo wa mapato ya Wakala (TFS) ........................................................ 44

Jedwali Na.20: Vyanzo vya Mapato ya Wakala (2011/2012 hadi 2013/2014) ......................... 44

Jedwali Na. 21: Takwimu za mazao ya nyuki (Asali na Nta) yanayosafi rishwa nje ya Nchi ...... 45

Jedwali Na 22: Muhtasari wa matumizi ya Wakala kwa malengo kipindi cha 2011/2012 hadi

2013/2014 ..................................................................................................... 46

Jedwali Na 23: Fursa za kukuza utalii ikolojia katika hifadhi asilia ........................................... 56

Page 9: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

viii

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

AIDSAcquired Immuno-Defi ciency Syndrome

BP Business Plan

BTCBelgium Technical Cooperation

BTIBeekeeping Training Institute

CAGController and Audit General

CM Cubic metre

EAMCEFEastern Arc Mountains Conservation Endowment Fund

FAOFood and Agricultural Organization

FBDForest and Beekeeping Division

FITIForest Industries Training Institute

FSU Forest Surveillance Unit

FTI Forest Training Institute

GEFGlobal Environmental Facility

GNGovernment Notice Number

Ha Hectare

HIVHuman Immuno-defi ciency Virus

LMDALogging and Miscellaneous Deposit Account

MNRPManagement of Natural Resources Programme

NAFOBEDANational Forest and Beekeeping Database

NAFORMA National Forest Resources Monitoring and Assessment

NBRs National Bee Reserves

NFPNational Forest Programme

NORADNorwegian Agency for Development Cooperation

OC Operational Cost

OPRASOpen Performance Review and appraisal System

PFMParticipatory Forest management

PO-PSMPresident Offi ce Public Service Management

PPP Public Private Partnership

RM Running metres

SAPStrategic Analysis and Planning

SPI Strategic Plan I

SPII Strategic Plan II

TaFF Tanzania Forest Fund

TAFORITanzania Forest Research Institute

TFCMPTanzania Forest Conservation and Management Project

TFSTanzania Forest Services Agency

TP Transit Pass

TRATanzania Revenue Authority

TAS Tanzania Shillings

UNDPUnited Nations Development Programme

USD United States Dollar

VAT Value Added Tax

VBRs Village Bee Reserves

VLFRsVillage Land Forest Reserves

VNRCsVillage Natural Resource Committees

WMUWaziri wa Maliasili na Utalii

VIFUPISHO (ACRONYMS AND ABBREVIATIONS)

Page 10: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

1

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

1. UTANGULIZI

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) Agency)) ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la tarehe 30/7/2010 na kuzinduliwa rasmi tarehe 18/7/2011. Kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002.

Aidha, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania uliundwa kwa kuzingatia Programu ya Serikali ya Maboresho katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2000 (Public Service Reforms Programme (PSRP 2000)). Programu hii ililenga kuimarisha Idara na Wakala (Ministerial Departments & Agencies (MDAs)) katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora na madhubuti katika utumishi wa umma, ambapo Wakala zinakuwa na uwezo, motisha na mbinu za mabadiliko yenye kuleta ufanisi na tija kiutendaji.

1.1 Lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Huduma za Misitu TanzaniaKwa kuzingatia programu tajwa, Wakala wa Huduma za Misitu umeundwa kwa madhumuni ya kuhakikisha: Uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki; kuongeza ubora na thamani ya kifedha katika kutoa huduma kwa umma; na kuendelea kukuza na kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa umma. Katika muktadha huu, masuala ya uendelezaji sera na sheria, pamoja na kanuni na taratibu zake yanashughuliwa na Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii. Hata hivyo majukumu ya Wakala yameongezeka licha ya kutoshughulikia sera na sheria. Wakala umepanua wigo kibiashara na kuongeza maeneo ya uzalishaji miti na mazao ya nyuki ili kukidhi mahitaji halisi, shughuli za uwekezaji, kuboresha njia mbadala za mapato na uboreshaji wa hifadhi za misitu na nyuki kwa ujumla.

1.2 Dira

“Kuwa kielelezo bora katika usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki.”

1.3 Dhima “Kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali za kitaifa za misitu na nyuki ili kuchangia mahitaji ya kijamii, kiuchumi, ki-ikolojia na kiutamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho”.

1.4 Maadili makuu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unaongozwa na maadili makuu kama yanavyoainishwa hapa chini:

a. Uadilifu

b. Usiri/Kutunza siri

c. Kutoa huduma bora kwa wateja

d. Ubunifu na kuleta mabadiliko

e. Ufanisi na ufasaha

f. Kuzingatia weledi

Page 11: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

2

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

g. Uwazi na uwajibikaji

h. Kufanya kazi kwa ushirikiano

1.5 Majukumu Makuu Majukumu makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu ni pamoja na:

a. Kuanzisha na kusimamia Misitu ya hifadhi na Hifadhi za Nyuki za Serikali kuu;

b. Kuanzisha na kusimamia mashamba ya miti (Picha Na.1) na manzuki za Serikali kuu;

c. Kusimamia rasilimali za misitu na nyuki katika ardhi ya jumla (General Land);

d. Kusimamia utekelezaji wa Sheria za Misitu na Ufugaji Nyuki katika maeneo yaliyo chini ya Wakala;

e. Kukusanya Maduhuli yatokanayo na mazao ya misitu;

f. Kutoa huduma za ugani katika maeneo ya Wakala;

g. Kufanya biashara ya mazao na huduma za Misitu na Ufugaji Nyuki;

h. Uperembaji na tathimini kuhusu utekelezaji wa kazi za Wakala.

1.6 Madhumuni ya MakalaMadhumuni ya makala hii ni kuainisha kwa kina utendaji kazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania tangu kuanzishwa kwake, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto mbalimbali ulizokabiliana nazo. Aidha, makala inafanya tathimini ya kina ya kuonesha utekelezaji wa majukumu kabla na baada ya kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania

Tathimini ya rasilimali za misitu; Kulia: Uandaaji miche ya miti kitaluni

Picha Na.6:

Page 12: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

3

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

2. CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KABLA YA KUANZISHWA KWA WAKALA

Sehemu hii inaainisha changamoto mbalimabli zilizokuwepo kabla ya kuanzishwa kwa Wakala (Idara ya Misitu na Nyuki). Idara ilikabiliwa na changamoto nyingi ambazo ziliifanya ishindwe kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa ufanisi. Changamoto hizo zilikuwa ni za ndani ya Idara yenyewe na za nje ya Idara, kama zinavyoainishwa hapa chini:

2.1 Changamoto za Ndani ya Idara(a) Kasi kubwa ya ukataji miti katika misitu ya hifadhi na misitu katika ardhi ya

jumla

Mfumo wa usimamizi wa misitu ya hifadhi ulikuwa dhaifu na hivyo kushindwa kuthibiti uvunaji haramu kwa kutumia sheria. Hali hii ilitokana na: Uwezo mdogo wa idara katika upande wa watumishi na kifedha, taratibu ndefu na zenye urasimu za kukata leseni ambazo wakati mwingine zilipelekea kuwepo na mazingira ya rushwa.

(b) Mfumo wa Kiutendaji wa Idara usio wa kibiashara

Mfumo huu haukutoa nafasi ya kuwepo kwa mazingira ya ufanisi wa kibiashara, utekelezaji na utoaji wa huduma bora kwa mteja. Mfumo haukuzingatia huduma kwa mteja na ulikuwa na majukumu mengi yanayokinzana kwa hiyo haukuweza kuleta ufanisi. Aidha kulikuwa na uwezo mdogo wa kutoa motisha kwa watumishi kulikopelekea kupungua kwa morali ya kazi kwa watumishi.

(c) Makusanyo madogo ya maduhuli

Mapungufu katika utawala bora katika sekta ya misitu, hususani katika usimamizi wa ukusanyaji maduhuli, na kukosekana kwa uwajibikaji na usimamizi mahiri katika utendaji kazi kulikwamisha mafanikio katika ukusanyaji wa maduhuli. Mrahaba na ushuru wa leseni uliokusanywa na serikali ulitokana na bei zilizopangwa kiutawala na hivyo hazikuzingatia thamani yake kiuchumi wala nguvu ya soko.

(d) Uhaba wa takwimu sahihi

Idara ya Misitu na Nyuki haikuwa na mfumo madhubuti wa Usimamizi wa Takwimu ambao ungeweza kuleta ufanisi na ufasaha katika hatua za mipango na utoaji wa maamuzi muhimu.

(e) Ushiriki mdogo wa jamii katika usimamizi wa rasilimali za misitu na nyuki

Licha ya Sera za Taifa za Misitu na Nyuki kutamka wazi kuwa jukumu la kusimamia misitu ni la wananchi wote, dhana ya ushirikishwaji ilikuwa ngeni kwa wananchi na watumishi kwa ujumla.

2.2 Changamoto za Nje ya Idara(a) Kutofautiana kwa mamlaka katika usimamizi wa misitu

Mfumo wa usimamizi wa misitu katika ngazi ya mkoa na wilaya haukuendana na

Page 13: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

4

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ule wa Idara ya Misitu na Nyuki (Serikali Kuu, Serikali za Mitaa/Halmashauri na Vijiji), hivyo kusababisha migongano ya kiutendaji na usimamizi hafi fu wa misitu kwa kushindwa kutekelezwa kwa sheria katika uhifadhi (Rejea Mchoro Na.1).

(b) Matakwa ya Wahisani yaliyokinzana na Muundo wa utendaji wa Idara

Miradi mingi iliyokuwa inapata fedha kutoka kwa wahisani ilikuwa imetengeneza mifumo yake ya usimamizi ambayo haikuendana na vipaumbele vya Idara ya Misitu na Nyuki. Miradi hiyo ilikuwa ikifanya kazi zake nje ya mifumo ya Idara ya Misitu na Nyuki. Hali hii ilikwamisha kuunganishwa kwa kazi katika miradi ya maendeleo iliyokuwa inafadhiliwa na wahisani katika mifumo ya serikali kuu na serikali za mitaa na hivyo kuifanya miradi hiyo isiweze kuwa endelevu.

(c) Kushindwa kutekeleza Makubaliano ya Kimataifa ipasavyo

Idara ilishindwa kutekeleza ipasavyo majukumu ya makubaliano ya kimataifa kutokana na ukosefu wa fedha za kutekeleza maazimio ya mikataba ambayo Tanzania imeridhia, kama vile mikataba ya mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa bioanuwai, kukabiliana na jangwa na kadhalika.

3. TATHMINI YA UTENDAJI KAZI KABLA NA BAADA YA KUWA WAKALA

Sehemu hii inaainisha tofauti ambayo imepatikana baada ya kuanzishwa kwa Wakala katika utendaji, aidha inaelezea mabadiliko ya majukumu, upatikanaji wa rasilimali fedha, hali ya miundombinu na vitendea kazi kabla na baada ya kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

3.1 Hali ya Utendaji kabla ya kuanzishwa WakalaKabla ya kuanzishwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Idara ya Misitu na Nyuki (FBD) ilikuwa inatekeleza majukumu ya Programu ya Misitu ya Taifa. Hivyo majukumu ya idara kama yalivyoanishwa chini ya Programu ya Misitu ya Taifa yalikuwa kama ifuatayo: Kuendeleza na kusimamia Sera na Sheria za Misitu na Ufugaji Nyuki; Uperembaji na tathmini ya utekelezaji wa sera; Maendeleo ya rasilimali watu; Usimamizi wa vyuo vya misitu na ufugaji nyuki; Usimamizi wa misitu ya hifadhi yakiwemo mashamba ya miti; Uongoaji wa maeneo yaliyoharibika nje ya misitu ya hifadhi; Uratibu na utoaji wa huduma za ugani; Usimamizi wa rasilimali ya misitu na nyuki katika ardhi ya jumla; Utungaji na usimamizi wa Sera, Sheria na Kanuni; pamoja na Uratibu wa mafunzo na utafi ti. Aidha, Wizara ilikuwa inaandaa Mipango Mkakati (Strategic Plans) ambayo ilibainisha mikakati ya utekelezaji kwa ajili ya kutekelezwa na Idara zake. Vilevile, Mipango Kazi iliandaliwa kila mwaka ili kutekeleza mikakati iliyoainishwa. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara iliongozwa na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki (Director of Forestry and Beekeeping) akisaidiwa na Wakurugenzi Wasaidizi (Assistant Directors) wanne. Huduma za uhasibu, sheria na manunuzi zilikuwa zinafanywa chini ya Vitengo vya Wizara.

Page 14: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

5

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Mchoro Na.1: Mamlaka ya usimamizi wa Misitu kabla ya Wakala

Page 15: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

6

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Aidha, Idara ilikuwa na kanda saba za Uenezi na vikosi vya Doria za misitu (Forest Surveillance Unit - FSU) ambazo zilikuwa zinafanya kazi za misitu kwa kushirikiana na serikali za mitaa chini ya Mkurugenzi Msaidizi wa Misitu (Matumizi ya Misitu na Ughani). Vilevile, Idara ilikuwa inatekeleza Miradi iliyokuwa inapata fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali. Kwa kupitia fedha za wahisani wa maendeleo Idara iliweza kutekeleza shughuli nyingi za maendeleo. Aidha, Idara ilikuwa inapewa fedha kidogo za retention na Wizara ya Maliasili na Utalii. Vilevile shughuli/miradi ilishindwa kuwa endelevu kwa kuwa ilikuwa tegemezi kwa asilimia 100%, hivyo kukoma mara baada ya ufadhili kufi kia kikomo. Jedwali Na.1 linaonesha mafanikio/shughuli za Idara kwa miaka mitatu (Julai 2007/08 – 2009/10) kabla ya Wakala.

Jedwali Na.1: Mafanikio/Shughuli za Idara Kabla ya kuanzishwa Wakala

SHUGHULI ZILIZOFANYIKA VYANZO VYA FEDHA/UFADHILI

Hali ya misitu ya asili iliboreka kama vile uoto wa asili,

kuongezeka maji na kupungua kwa uvunaji haramu

na uvamizi (encroachment). Hali hii ilitokana na

ushirikishwaji wa wananchi katika usimamizi shirikishi

wa misitu (PFM). Takribani hekari milioni 4 za misitu

ambazo ni asilimia 12.8 ya misitu yote iliwekwa chini

ya Usimamizi Shirikishi (PFM); Aidha Maeneo ya

misitu ya Mikoko nayo yaliongezeka

Miradi ya Usimamizi Shirkishi (PFM)

chini ya uhisani wa Denmark, Finland,

World Bank/IDA Credit kupitia Mradi wa

TFCMP, Serikali ya Norway (NORAD)

kupitia Mradi wa Management of Natural

Resources Programme (MNRP)

Uendekezaji wa mashamba 16 ya miti ulikuwa hekta

6,376 (2005/06- 2009/10) ambapo ni wastani wa hekta

1275.2 kwa mwaka

Idara ya Misitu na Nyuki - Fedha za

Logging Miscellaneous Development

Account (LMDA)

Upimaji wa misitu ulifanyika katika wilaya 11 ambazo

zina rasilimali kubwa ya misitu kama msingi wa

kuandaa mipango ya usimamizi. Wilaya hizo ni Kilwa,

Nachingwea, Liwale, Tunduru, Rufi ji, Mkuranga/

Kisarawe, Kilombero, Mvomero/Morogoro, Ulanga,

Handeni/Kilindi na Mpanda;

SAP- Strategic Analysis and Planning -

SIDA

Mradi wa Uboreshaji Ufugaji Nyuki (Beekeeping

Improvement Project) ulianzishwa katika wilaya 30.

Chini ya Mradi huu vikundi vya wafugaji nyuki 135

vilianzishwa vikijumuisha watu 2,270 kutoka vijiji 75

katika wilaya 25.

Serikali ya Ubelgiji kupitia Belgium

Technical Cooperation (BTC)

Kuongezeka kwa maduhuli na hivyo kuongezeka kwa

fedha za retention scheme. Mwaka 2007/08 takribani

TAS 23 bilioni za maduhuli zilikusanywa na mwaka

2008/2009 TAS15.5 bilioni maduhuli zilikusanywa.

Retention scheme, World Bank/IDA

Credit kupitia Mradi wa TFCMP

Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) ulianzishwa kama

chanzo cha fedha kwa ajili ya shughuli za sekta.

World Bank/IDA Credit kupitia Mradi wa

TFCMP

Vigezo vya ukusanyaji wa maduhuli na utaratibu wa

kuimarisha uuzaji wa magogo na mfumo wa kuuza nje

ya nchi mazao ya misitu ulitayarishwa. Mfumo wa

usafi rishaji mkaa na kuni ulitayarishwa pia

World Bank/IDA Credit kupitia Mradi wa

TFCMP

Page 16: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

7

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

SHUGHULI ZILIZOFANYIKA VYANZO VYA FEDHA/UFADHILI

Mfuko wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki

(Eastern Arc Mountains Conservation Endowment

Fund (EAMCEF) ulianzishwa kama njia endelevu ya

kupata fedha kwa ajili ya uhifadhi wa Misitu ya Milima

ya Tao la Mashariki

GEF/UNDP na World Bank kupitia

Mradi wa TFCMP

Kuanzishwa kwa Kikosi cha Doria (Forest Surveillance

Unit (FSU) katika kanda nane kuhakikisha utii wa

sheria (law compliance)

World Bank/IDA Credit kupitia Mradi wa TFCMP

Mwongozo wa Uvunaji Endelevu ulitayarishwa na

Kamati za wilaya za kusimamia uvunaji zilianzishwa;

World Bank/IDA Credit kupitia Mradi wa TFCMP

Eneo la mikoko liliongezeka kwa kiasi cha asilimia 16

(16%) kutoka hekta 15,500 ha hadi hekta 133,480;

Norway (NORAD) kupitia Mradi

wa Management of Natural Resources

Programme (MNRP)

Mwongozo wa kupima ubora wa mazao ya nyuki

uliandaliwa na sampuli 43 za asali zilikusanywa kwa ajili

ya kupimwa kemikali

Retention scheme chini ya FBD

Mapitio ya Mitaala ya Chuo cha Ufugaji Nyuki na

Chuo cha Misitu yalifanyika

Mradi wa Finland - NFP- ISP

Jumla ya watumishi 344 (19.1%) walihudhuria kozi za

muda mrefu za misitu na ufugaji nyuki pamoja na kozi

zingine. Kozi kama vile MSc -28, Diploma and Cheti -

314; na watumishi 45 walihudhuria kozi fupi

Retention scheme FBD na World Bank/

IDA Credit kupitia Mradi wa TFCMP

Jengo la Makao Makuu ya TFS (Tanzania Forest

Services - Mpingo House) lilikamilika na kuhamiwa na

watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii

World Bank/IDA Credit kupitia Mradi wa

TFCMP

Majengo matatu ya Chuo cha FTI na BTI yalikarabatiwa . Vifaa vya ofi si vilinunuliwa na huduma ya mtandao iliwekwa katika vyuo vya FTI, BTI na FITI

Finland kupitia mradi wa Vyuo NFP- ISP

Mradi wa National Forest Resource Monitoring and Assessment (NAFORMA) ulianzishwa kwa ajili ya kupata taarifa za kitaifa katika rasilimali ya misitu ambazo zitatumika kama msingi wa kuandaa kanzidata za taifa;

Retention scheme na Finland na FAO na

World Bank Credit kupitia Mradi wa -

TFCMP

Hifadhi Asilia tatu zilianzishwa; Nilo, Kilombero na Uluguru kama sehemu ya kuboresha uhifadhi wa bionuwai ya misitu, Hifadhi za Asili 4 ziliingizwa kwenye mchakato wa kupandishwa hadhi (Magamba, Chome, Mkingu na Uzungwa scarp)

GEF/ na Germany kupitia UNDP,

Retention scheme na World Bank Credit

kupitia Mradi wa - TFCMP

Kanzidata ya Taifa ya Misitu na Nyuki (NAFOBEDA) ilienezwa katika wilaya 67 na iko katika Tovuti ya Wizara

Miradi ya Danida, Finland na World

Bank/ (IDACredit kupitia TFCMP

Mafanikio ya shughuli za Idara ya Misitu na Nyuki kwa misaada ya wahisani wa maendeleo pamoja na mkopo kutoka World Bank kupitia TFCMP vimekuwa msingi bora wa mchakato wa kuanzishwa na kuingia kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Page 17: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

8

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

3.2 Hali ya Utendaji baada kuanzishwa kwa WakalaMchakato wa kuanzisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umewezeshwa na Mradi wa Usimamizi na Uhifadhi wa Misitu Tanzania (Tanzania Forest Conservation Management Project(TFCMP)) kupitia mkopo wa Benki ya Dunia (IDA Credit). Utekelezaji wa mradi ulikuwa chini ya uangalizi wa Kamati ya Uendeshaji ya Programu ya Taifa ya Misitu (NFP Steering Committee). Hata hivyo utekelezaji wa shughuli za mradi ulijumuishwa na shughuli za Idara ya Misitu na Nyuki. Mratibu wa TFCMP pamoja na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki na watumishi wa Idara ya Misitu na Nyuki waliwajibika katika utekelezaji wa Mradi. Mchakato wa kuanzisha Wakala huu ulichukua muda mrefu na ulitumia sehemu ya budget ya mradi wa TFCMP ya kiasi cha takribani dola za Kimarekani (USD) milioni 37.0.

3.2.1 Makao Makuu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Makao Makuu ya Wakala yako katika Jiji la Dar es Salaam–katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakala umepewa nafasi katika ghorofa ya Tatu ya jengo la Mpingo (Picha Na.2) lililopo 40 Barabara ya Nyerere, 15472 Dar es Salaam. Aidha, kuna majengo ambayo yanatumiwa na Mradi wa NAFORMA na Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) katika eneo la Ivory Room.

Picha Na.2: Jengo la Mpingo-Yalipo Makao Makuu ya TFS

Kulingana na muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Mchoro Na.2) upo mgawanyiko katika maeneo makuu matatu: Makao Makuu, Kanda na Mashamba ya miti. Makao makuu inaundwa na menejimenti inayojumuisha Mtendaji Mkuu, Wakurugenzi watatu, Meneja wawili wa Vitengo vya Sheria na ugavi, Mhasibu Mkuu na Mkaguzi Mkuu wa ndani. Menejimenti ya Wakala na baadhi ya watumishi wengine wako katika jengo la Mpingo gorofa ya tatu. Wakala pia una Meneja wa Kanda saba (7) na Mashamba ya miti 18. Vile vile Wakala umeboresha utendaji wake kupitia wilaya; ambapo Meneja wa wilaya 118 wameteuliwa na kupatiwa nyenzo za kazi. Tofauti na Kanda saba za awali za Uenezi na vikosi vya Doria za misitu chini ya Idara; Muundo unaojumuisha Kanda saba za Wakala umeboresha tija katika utendaji kwa kuimarisha uhifadhi na usimamizi wa misitu, ukusanyaji wa mapato, uenezi, na ulinzi wa misitu.

Page 18: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

9

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Mchoro Na. 2: Muundo wa Wakala (TFS)

Page 19: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

10

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

3.2.2 Kanda za Wakala na Mashamba ya mitiWakala una Meneja wa Kanda saba (7). Kanda hizo ni Mashariki, Kaskazini, Kati, Kusini, Nyanda za juu Kusini, Ziwa na Magharibi. Vile vile Wakala umeimarisha utendaji katika ngazi ya Wilaya kwa kuteua na kusambaza Meneja wa Wilaya 118. Aidha katika ofi si 6 za kanda, Wakala unatumia majengo yaliyokuwa ya FBD ambayo yamefanyiwa ukarabati ili yaweze kutumika. Katika kanda ya Kusini, Wakala umekodi nyumba mjini Masasi. Aidha, wapo Meneja wa mashamba ya miti 18 ambayo ni: Buhindi, Kawetire, Kiwira, Korogwe, Longuza, Mbizi, Meru, Mtibwa, Kilimanjaro Kaskazini, Kilimanjaro Magharibi, Ruvu Kaskazini, Rondo, Rubare, Rubya, Sao Hill, Shume Ukaguru na Wini-Ifi nga. Meneja wa mashamba ya miti 15 wanatumia majengo yaliyokuwa chini ya FBD. Meneja wa Mashamba mapya wanatumia majengo yaliyopangishwa kwa Wakala au ofi si za zamani za idara ya misitu zilizotolewa na Halmashauri za Wilaya husika. Kila Meneja wa Kanda na wa shamba wana vitendea kazi kama magari, pikipiki, mitambo, kompyuta za vipakatalishi na mezani pamoja na vifaa vingine muhimu vya ofi si kwa ajili ya kufanyia kazi za Wakala.

Pamoja na vitendea kazi kuwa vichakavu, kila Meneja ana bajeti ambayo iko kwenye mpango kazi wa kibiashara ukianisha shughuli za Wakala katika ngazi hiyo mfano, ukarabati wa majengo, barabara na ununuzi wa vitendea kazi; kama vile magari, pikipiki na matumizi mengine. Jedwali Na. 2 linaonesha majengo na vitendea kazi vya FBD na TFS katika Makao Makuu na vituo vya nje.

Jedwali Na 2: Majengo na vitendea kazi vya FBD na TFS katika Makao Makuu na

vituo vya nje.

Vifaa Idadi vitendea kazi vilivyorithiwa kotoka FBD

Idadi Vilivyonunuliwa na Wakala

Jumla ya Vitendea Kazi vilivyopo

Mitambo mikubwa

i) Bulldozer 5 5

ii) Motor grader 4 1 5

iii) Wheel loader 3 1 4

iv) Stone crusher 1 1

v) Tractors and Trailers 16 4 20

Other working facilities

vi) Generators 10 1 11

vii) Water pumps 2 2

i) Computers 42 105 147

ii) Fax machines 3 3

iii) Photocopier 11 11

i) Telephones 16 (stations) 16

ii) Radio communication Systems 3 (stations) 3

iii) E-Mail/Internet systems 6 1 7

Transport Equipment

i) Lorries 26 32 58

Page 20: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

11

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ii) Light vehicles (4WD/SW) 109 30 139

iii) Motor cycles 383 339 722

iv) Bicycles 122 122 244

v) Passanger Service Bus 1 3 4

vi) Boat

Buildings &Structures

i) Offi ce buildings 63 7 70

ii) Residential buildings 580 580

iii) Workshops & Garages 23 23

iv) Dispensaries 09 09

v) Social Hall/ Facilities 12 12

vi) Stores 7 7

Majengo na vitendea kazi yaliyokuwa ya FBD yote yamechukuliwa na Wakala (TFS) na kwa sasa ni mali ya TFS. Hali ya majengo yote yanayotumika ni nzuri kwa vile yanafanyiwa ukarabati mara kwa mara. Aidha, Wakala una mpango wa kujenga majengo ya vitega uchumi katika miji ya Mbeya, Kibaha na Dar es Salaam. Hii ni pamoja na kukaratiba majengo ambayo yalikuwa chini ya FBD ambayo kwa sasa hayatumiki ili kuweza kutumika kama vitega uchumi vya Wakala. Majengo hayo yapo miji ya Morogoro, Moshi, Tanga na Shinyanga.

3.3 Mifumo ya Utendaji ya Wakala Baada ya KuanzishwaWakala wa Huduma za Misitu Tanzania umeweka mifumo mbalimbali ya kimenejimenti kwa malengo ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji, kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za Wakala. Kwa sehemu kubwa Mifumo hii inaratibiwa na Kurugenzi ya Huduma na Uendeshaji Shughuli katika Wakala. Mifumo hii ni pamoja na Mwongozo wa Utendaji Kazi, Hati ya Kuanzisha Wakala, Mpango Mkakati, Mpango wa Biashara wa Mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma kwa Mteja na Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko. Aidha mifumo mingine inayotumiwa na Wakala kutekeleza majukumu yake ni Mfumo wa usimamizi na uhakiki wa fedha (Integrated Financial Management System (IFMS)), Human Capital Information Management System, Masjala na Uhasibu.

3.3.1 Mwongozo wa Utendaji Kazi (Framework document)Mwongozo wa Utendaji Kazi unaelezea kwa kina namna ambavyo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unaendesha majukumu yake kwa kuzingatia Sheria ya Wakala za Serikali, Na. 30 ya mwaka 1997, Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002, Sheria ya Ufugaji Nyuki Na. 15 ya mwaka 2002 na Programu ya Taifa ya Misitu na Nyuki ya mwaka 2001 ambayo iliandaliwa kama chombo cha kutekeleza Sera ya Taifa ya Misitu na Nyuki.

Page 21: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

12

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

3.3.2 Hati ya Kuanzisha Wakala (Establishment Order)Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali, Na. 30 ya mwaka 1997 iliyorekebishwa mwaka 2009 (Cap. 245). Uwepo wa Wakala unazingatia agizo la kuanzishwa kwake kwa mujibu wa Hati ya mwaka 2010 ambayo imebainisha kwa kina kuhusu utawala, muundo na majukumu ya msingi katika utendaji wa shughuli za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Aidha, hati imebainisha majukumu ya Bodi ya Ushauri ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kumshauri Waziri wa Maliasili na Utalii (WMU) kuhusu utendaji na ufanisi wa Wakala. Hati pia imeainisha orodha ya misitu yote ya hifadhi inayopaswa kusimamiwa na Wakala.

3.3.3 Mpango Mkakati (Strategic plan)Ili kufi kia malengo na kuleta mabadiliko chanya katika utendaji kazi, Wakala umeandaa na kutekeleza Mpango Mkakati wa awali wa Miaka mitatu (3) kati ya 2010/11–2013/14; na hatimaye Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) kati ya 2014/15-2018/19 unaotekelezwa sasa. Mpango Mkakati wa miaka mitano utafanyiwa mapitio ya katikati ya kipindi cha mpango. Mpango Mkakati umeainisha dira, dhima, maadili makuu, malengo na matokeo yanayotarajiwa, mikakati ya utekelezaji malengo hayo kulingana na bajeti/matumizi.

3.3.4 Mpango wa Biashara wa mwaka (Business Plan)Mpango wa Biashara (Picha Na. 18) huandaliwa kila mwaka kutokana na Mpango Mkakati husika. Mpango huo unaainisha kwa kina shughuli zitakazotekelezwa na Wakala katika mwaka wa fedha husika.

3.3.5 Mfumo wa wazi wa kupima utendaji kazi (OPRAS)OPRAS ni mfumo wa kutekeleza malengo ya menejimenti katika Utumishi wa Umma na kujenga uhusiano mzuri wa utendaji kazi kati ya viongozi na wanaoongozwa. Wakala unazingatia matumizi ya OPRAS kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka 2004 ikiwa ni hatua muhimu katika kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa Umma. Nia ya kupima utendaji kazi ni kuwezesha Wakala kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa watumishi na kuwa na usimamizi mzuri wa Rasilimali watu.

3.3.6 Uperembaji na Tathmini (Monitoring and Evaluation) Uperembaji na Tathmini ni mfumo wa kubaini tija na ufanisi katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wakala kwa kupima matokeo kulingana na Mpango kazi na bajeti. Mfumo huu unaongozwa na mpango maalumu ulioundwa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Wakala. Kupitia mfumo huu watumishi wameongeza ufanisi na tija katika utendaji.

3.3.7 Mkataba wa Huduma kwa Mteja Ili kuboresha huduma kwa wananchi, Wakala wa Huduma za Misitu umeandaa Mkataba wa

Page 22: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

13

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Huduma kwa Mteja kwa malengo ya kupata ufanisi katika kazi zake. Matumizi ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja yanaonesha kuwa Wakala umefanikiwa kwa kujenga utamaduni mzuri wa uwajibikaji hivyo kuongeza tija na kutumia rasilimali fedha kwa uangalifu mkubwa. Baada ya kutekeleza mfumo huu wateja wameridhika na huduma zinazotolewa na Wakala, hivyo kupunguza malalamiko yaliyokuwa yanajitokeza. Malalamiko yamekuwa machache kutokana na bidii katika kazi. Aidha wafanyakazi wamekuwa wepesi kukubali mfumo huu mpya.

3.3.8 Mfumo wa Malalamiko Utaratibu wa kushughulikia Malalamiko katika Wakala ni moja ya juhudi za kuongeza uwajibikaji na kuimarisha taratibu za kuwasikiliza wateja. Mfumo huu unawezesha Wakala kushughulikia malalamiko ya wateja kwa ufanisi kwa kuwa unaharakisha ushughulikiwaji wa malalamiko, ni wa wazi, unasisitiza kutunza siri na ni rahisi kutumika.

3.3.9 Mfumo wa Usimamizi na uhakiki wa fedha (IFMS)Mfumo huu (Integrated Financial Management System-IFMS) ulianzishwa rasmi na Wakala mwaka 2012/13 ili kuboresha utoaji wa huduma kwa watumishi na wadau wa Wakala wa ndani na nje. Kupitia mfumo huu ufanisi wa utendaji kazi umeboreshwa kwa: kutunza mahesabu ya Wakala kwa urahisi, utoaji wa taarifa za mapato na matumizi kwa wakati, kurahisisha malipo kwa wakati na kurahisisha usahihi wa vitabu vya hesabu na benki. Wakala unakusudia kuboresha mafunzo kwa watumishi wa kitengo cha uhasibu ili kuwa na tija katika uendeshaji wa mfumo huu. Vile vile Wakala unakusudia kusambaza mfumo huu katika vituo vyake vya Kanda na mashamba ya miti ili kuwepo na muunganiko wa mfumo kuanzia Makao Makuu ya Wakala hadi vituo vyake.

3.3.10 Mfumo wa UhasibuUhasibu ni mojawapo ya mifumo muhimu iliyosimikwa na Wakala. Kupitia mfumo wa uhasibu huduma imetolewa kwa wadau wa ndani na nje kwa uwazi na uwajibikaji katika: kushughulikia malipo kwa wakati, kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mapato na matumizi ya Wakala kwa njia ya ushirikishwaji na uwazi kwa Mtendaji Mkuu ambaye huwasilisha katika Bodi ya Ushauri ya Wizara na hatimaye kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Kupitia mfumo huu ofi si ya Makao Makuu ya Wakala na ofi si za Kanda na Mashamba ya miti zinaunganishwa katika uandaaji wa mahitaji ya fedha za kazi na matumizi, taarifa za mapato na uwekaji fedha kupitia benki. Mfumo huu umetenda kazi kwa ufanisi zaidi kupitia kuwepo kwa programu ya Uhasibu yaani Integrated Financial Management System.

3.3.11 Human Capital Information Management System Huu ni mfumo unaoendeshwa kitaifa chini ya Ofi si ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma. Wakala umeingiza mfumo huu katika mifumo yake ya kawaida ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi. Kupitia mfumo huu Wakala umeweza kupanga na

Page 23: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

14

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

kusimamia orodha za watumishi za mishahara, kufanya marekebisho yanayohusiana na mishahara kwa wakati na kwa ufanisi, kuondoa kwa wakati watumishi waliofi kia ukomo wa ajira, kuingiza watumishi wapya katika orodha ya malipo na kurahisisha malipo ya mishahara ya watumishi kwa wakati ikiwa ni pamoja na taarifa za malimbikizo. Aidha kupitia mfumo huu Wakala ambaye ni mwajiri ameunganishwa vema na ofi si ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma kwenye masuala ya stahiki za watumishi.

3.3.12 Masjala ya Wazi na SiriMfumo wa Masjala unahusika na utoaji wa huduma kwa watumishi na wadau wa ndani na nje. Kupitia mfumo huu Wakala umeweza kuboresha huduma kwa kupitia: utendaji kazi wa uwazi lakini wenye kuzingatia usiri wa taarifa za watumishi, uwajibikaji katika kuhakikisha kuwa kumbukumbu za watumishi wa Wakala zinatunzwa vizuri kuanzia wanapoajiriwa hadi kustaafu, kufuatilia majalada ya ndani na nje (PSPF, NSSF, Hazina nk). Mfumo huu umeboresha utoaji wa huduma kwa wakati na kuboresha ufanisi wa watumishi ambao hutumia muda mfupi kufuatilia masuala ya ajira zao na stahiki zao.

3.4 Sheria zingine ambazo Wakala unazitumia kufanikisha utendajiKatika kutekeleza majukumu yake, Wakala (TFS) unatekeleza Sheria mbalimbali kama: Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004, Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011, Sheria ya Fedha Na. 14 ya mwaka 2001, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, pamoja na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999.

3.4.1 Sheria ya Mazingira ya 2004Sheria hii inaweka misingi ya usimamizi endelevu wa mazingira kwa ajili ya kuhifadhi na kudhibiti uharibifu. Aidha, Sheria inaelekeza utekelezaji wa tathmini ya athari ya mazingira kabla ya kufanya uwekezaji katika misitu chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira.

3.4.2 Sheria ya Manunuzi ya Umma 2011Katika kuhakikisha kuwepo kwa mfumo wenye ufanisi na uwazi katika manunuzi na usimamizi wa manunuzi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unatekeleza Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 (Public Procurement Act, 2011). Sheria hii inabainisha misingi bora na miongozo inayowezesha Wakala kupata huduma kama vifaa (magari, mitambo) na huduma za ujenzi wa miundombinu mbalimbali kulingana na thamani halisi ya fedha.

3.4.3 Sheria ya Fedha 2001Sheria hii (Finance Act 2001) inaweka misingi ya kudhibiti Kodi na mapato ya Serikali kwa nia ya kuongeza makusanyo (mapato ya Serikali). Wakala wa Huduma za Misitu umekuwa mstari wa mbele katika makusanyo ya Serikali hususan Kodi ya ongezeko la

Page 24: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

15

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Wakala umehusika kutekeleza majukumu ya kiutendaji yaliyokuwa yanafanywa na Idara ya Misitu na Nyuki katika maeneo ya hifadhi kwa; Kubaini na kuimarisha mipaka; Kuondoa wavamizi; Kuandaa mipango ya uvunaji; Kuimarisha doria katika misitu ya hifadhi; Kushirikisha sekta binafsi na jamii katika uhifadhi na matumizi; Kuweka na kutekeleza mipango ya kudhibiti moto (Picha Na. 3); Kuimarisha vituo vya ukaguzi; pamoja na Kuimarisha ulinzi wa misitu kwa kuajiri kada ya walinzi wa misitu (forest guard) pamoja na kuimarisha usimamizi shirikishi wa misitu nchini.

Katika Kuboresha usimamizi na uendelezaji mashamba ya miti ya kupandwa Wakala umehusika katika: Kuongeza kasi ya upandaji miti na kupanua mashamba ya miti (Picha Na. 4); Kuongeza ubora wa mazao ya misitu; Kuanzisha mpango wa uvunaji na ugawaji wa malighafi ; Kuhamasisha wadau katika matumizi ya teknolojia ya kisasa; Kuhakikisha mashamba ya miti yanapata cheti cha ubora; Kutumia mbegu bora na viini tete; pamoja na Kushirikisha wadau wengine katika kuongeza maeneo ya mashamba ya miti.

Uzinduzi wa shamba jipya la miti-Mbizi, Sumbawanga

b) Kuboresha usimamizi na uendelezaji mashamba

Bango lenye ujumbe wa uhifadhi wa misitu ya asili;

(a) Uhifadhi na udhibiti

Kudhibiti moto katika hifadhi (shamba la miti Sao Hill)

Upogoaji katika shamba la miti Meru;

Picha Na.4:

Picha Na.3:

Page 25: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

16

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

(c) Kuboresha ukusanyaji maduhuli

Ili kuboresha ukusanyaji wa maduhuli Wakala umeweka Mifumo/Miundombinu imara ya ukusanyaji na matumizi ya fedha (Picha Na.5); Kupanga na kudhibiti tozo kulingana na nguvu ya soko; Kuwapatia motisha na vitendea kazi watumishi wanaokusanya maduhuli; Kuweka mfumo wa kugawanya gharama; pamoja na Kubainisha vyanzo vipya vya mapato.

Picha Na.5:

Juu:

Kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu na nyuki Nangurukuru, Kilwa

Chini:

Kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu Nyangao, Lindi Vijijini

Page 26: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

17

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Wakala umeongeza huduma na uzalishaji wa

mazao ya nyuki; Kuanzisha na kuendeleza

mashamba (manzuki) na hifadhi za nyuki;

Kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya

kisasa katika viwanda vilivyojikita katika

masuala ya ufugaji nyuki; Kudumisha na

kuendeleza ubora wa mazao ya nyuki;

Kuhamasisha matumizi ya vifaa sahihi vya

ufugaji nyuki (Picha Na. 6); Kuanzisha

na kuendeleza mashamba ya uzalishaji wa

mazao ya nyuki; Kuandaa na kutekeleza

mpango wa udhibiti wa kemikali katika

asali; Kuandaa na kutekeleza mfumo

wa ufuatiliaji wa mazao ya nyuki; Kutoa

mafunzo ya: uzalishaji wa malkia ili

kuongeza makundi ya nyuki, uchakataji,

ufungashaji na taarifa za masoko; pamoja

na Kuwezesha utafi ti na upatikanaji wa

taarifa ya shughuli za ufugaji nyuki.

(d) Kuendeleza ufugaji nyuki

Picha Na.6:

Juu:

Watumishi wakishiriki kuhamasisha matumizi ya vifaa bora vya nyuki;

Katikati:

Kituo cha ufugaji cha kikundi, Singida;

Chini:

Uwekaji mizinga kwa njia salama na rahisi

(e) Kujenga uwezo wa Kitaasisi

Wakala umewapatia watumishi mafunzo; Usimamizi wa fedha kwa mfumo wa kibiashara; Kuandaa mipango ya biashara kila mwaka; Kuimarisha na kuboresha miundo mbinu katika maeneo ya misitu; Kutumia mfumo wa OPRAS wa kupima utendaji kazi; Kuajiri watumishi kulingana na mahitaji; pamoja na Kuboresha maslahi ya watumishi.

Kwa kuzingatia mikakati iliyowekwa hapo juu, Wakala umeimarisha usimamizi wa rasilimali za misitu na nyuki, umepanga watumishi wake wa kada mbalimbali ili kufi kia malengo yake katika Kanda na baadhi ya wilaya ambazo zina rasilimali kubwa za misitu na nyuki. Wakala unazingatia sifa, jinsi na uhitaji. Aidha, Wakala unatoa mafunzo kwa watumishi wake ili kuboresha utendaji wao na kutoa motisha kadri unavyowezekana.

Page 27: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

18

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

thamani (Value Added Tax - VAT).

3.4.4 Sheria ya Ardhi 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji 1999Sheria hizi zinaweka misingi kwa Vijiji kumiliki na kusimamia rasilimali za misitu katika ardhi ya Kijiji na kuzitumia katika misingi endelevu kwa kutengeneza na kusimamia Sheria ndogo kupitia Kamati za Maliasili (Village Natural Resources Committees – VNRCs)) na mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (Participatory Forest Management – PFM).

3.4.5 Matumizi ya TEHAMA Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hususan kompyuta yanakua kwa kasi kubwa duniani. Shughuli nyingi za uendeshaji wa ofi si, kama vile kuchapa taarifa mbalimbali, mawasiliano na hata kuhifadhi nyaraka na taarifa zinafanywa kwa kutumia TEHAMA. Hali hii imefanya TEHAMA kuwa sehemu muhimu ya uendeshaji wa ofi si za Serikali. Mojawapo ya mikakati ya Serikali kupitia Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika Awamu ya pili ya Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma, ni kuimarisha matumizi ya mtandao wa kompyuta unaojulikana kama Serikali-Mtandao kwa sekta zote za Serikali. Awamu hii ya pili, imelenga kuboresha utoaji huduma kwa wananchi kwa kuzingatia utendaji unaojali matokeo na uwajibikaji.

Wakala wa Huduma za misitu Tanzania umesimika mifumo ya TEHAMA kama sehemu ya utekelezaji wa azma hiyo ya serikali ambayo inahimiza waajiri na watumishi wa umma kufuata maelekezo na utaratibu bora katika matumizi mbalimbali ya TEHAMA na vifaa vinavyohusiana na teknolojia hiyo ikiwemo matumizi ya barua pepe, vitunza kumbukumbu na huduma za mtandao.

Baadhi ya Mifumo iliyosimikwa na kuanza kufanya kazi katika utekelezaji wa majukumu ya Wakala ni pamoja na Mfumo wa ufuatiliaji miti inayokatwa (Log track), Mfumo wa Kudhibiti moto msituni (Fire Monitoring system), Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya rasilimali misitu (NAFORMA). Aidha, Wakala unatumia Tovuti (www.tfs.tz) inayotoa taarifa mbalimbali za misitu na nyuki kwa jamii na Mitandao ya kijamii (Facebook) inayoruhusu mazungumzo na jamiii inayotaka kufahamu taarifa za misitu na nyuki.

3.5 Tathmini ya kazi za Wakala baada ya kuanzishwaBaada ya kuanzishwa Wakala majukumu ya awali yaliyokuwa chini ya Idara ya Misitu na Nyuki na ambayo yalipaswa kutekelezwa na Wakala yaliongozeka kutokana na kuimarishwa kwa rasilimali fedha na vitendea kazi. Ili kutimiza majukumu yake Wakala uliandaa Mpango Mkakati (kwa kipindi cha miaka 5) na Mpango wa Kibiashara unaoandaliwa kila mwaka. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, kwa sasa upo katika Mpango Mkakati wa Pili ((Strategic Plan II (SPII)). Mpango Mkakati wa Wakala huainisha mikakati mbalimbali ya kutekeleza majukumu yake. Katika kipindi cha Mpango Mkakati wa kwanza mikakati ya Wakala wa Huduma za Misitu ilikuwa;

Page 28: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

19

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Picha Na.7:

Juu: Viongozi wa Timu ya NAFORMA wakiwa kazini

Chini Kushoto: Makala ya NAFORMA

Chini Kulia: Mtaalam wa NAFORMA akifanya tathmini ya miti

4. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TANGU KUANZISHWA WAKALA

Sehemu hii inaainisha mafanikio ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wakala kwa mwaka 2011/12 - 2013/14. Aidha, mwaka 2010/11 kilikuwa kipindi cha mpito cha Wakala ambacho kilitumika kujipanga kuhusu namna ya kufanikisha majukumu yake.

i) Jumla ya watumishi 2,031 kutoka TFS, mikoa na wilaya na wanavijiji 1,484 wamehamasishwa kuhusu kuchukua tahadhari na kupimwa HIV/AIDS kupitia warsha na semina. Matokeo ya uhamasishaji na uelimishwaji umewezesha watumishi zaidi kujua hali zao na idadi ya waliopima kwa hiari iliongezeka kutoka 53 hadi 277. Watumishi 31wanaoishi na UKIMWI walisaidiwa chakula.

ii) Kufanya Tathmini na Uperembaji wa Rasilimali za Misitu (National Forest Resource Monitoring and Assessment (NAFORMA); (Picha Na. 7), ambayo ilianzishwa ili kupata taarifa sahihi na za uhakika kuhusu hali halisi, ukubwa, na matumizi ya rasilimali ya misitu ambayo ni muhimu kwa ajili ya kutoa maamuzi na kuandaa sera na programu za kutekeleza usimamizi endelevu wa misitu. Taarifa ya NAFORMA inapatikana katika tovuti ya Wakala (www.tfs.go.tz).

Page 29: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

20

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

iii) Wakala unasimamia mashamba ya miti 18 (Kati ya hayo mashamba 3 yameanzishwa na Wakala ndani ya kipindi cha miaka mitatu). Mashamba haya (18) yana jumla ya eneo la hekta 205,522. Aidha kati ya eneo hili ha 91,662 zimepandwa miti (Jedwali Na. 3). Uoteshaji wa miti umefanyika katika hekta 14,255 za maeneo ya mashamba ya miti (Picha Na. 8) na jumla ya hekta 7,947 zimepandwa katika maeneo mapya (extension) katika mashamba 15;

iv) Miti iliyosimama (Standing wood stock) ina meta za ujazo wa 11,808,599 ikiwa ni sawa na ongezeko la meta 528,704 kwa mwaka. Uvunaji wa meta za ujazo 2,960,833 (Jedwali Na.4) umefanyika katika miaka mitatu ya Mpango Mkakati wa kwanza.

Picha Na.8: Bustani ya miche shamba la miti West Kilimanjaro.

Page 30: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

21

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Picha Na.9:

Upandaji miti kitaifa

Kushoto : Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal (Kisarawe).

Kulia : Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (Singida) Wakipanda miti siku ya maadhimisho ya upandaji miti kitaifa

Picha Na.10: Kushoto: Uwekaji wa maboya ya mpaka -msitu wa hifadhi Geita; Kulia: Kibao cha alama ya msitu wa hifadhi Kitulang’alo

Page 31: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

22

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na. 3: Mashamba ya miti chini ya usimamizi wa Wakala kwa hadi mwaka 2014

S/N JINA LA SHAMBA MAHALIENEO LA SHAMBA (Ha)

ENEO LA UPANUZI (Ha)

JUMLA YA ENEO (Ha)

UJAZO WA MITI (m3)

1 Sao Hill Mufi ndi 52,070 36,003 88,073 8,341,371

2 Shume Lushoto 4,227 140 4,367 510,792

3 Longuza Muheza 1,904 200 2,104 242,450

4 West Kilimanjaro Hai 4,149 337 4,486 377,601

5 North Kilimanjaro Rombo 6,177 200 6,377 563,941

6 Ukaguru Kilosa 976 941 1,917 60,189

7 Kiwira Rungwe 2,784 45 2,829 334,290

8 Kawetire Mbeya 2,131 517 2,648 137,439

9 Rondo Lindi 864 1,541 2,405 13,869

10 Rubya Ukerewe 1,771 181 1,952 243,930

11 Buhindi Sengerema 3,810 7,569 11,379 261,095

12 Meru Arumeru 6,110 0 6,110 548,954

13 Rubare Bukoba 1,227 1,920 3,147 23,275

14 Mtibwa Mvomero 1,86 7 75 1,942 149,274

15 Wino-Ifi nga1 Songea 1,380 10,000 11,380 130

16 Mbizi2 Sumbawanga 158 11,442 11,600 0

17 Korogwe2 Handeni 0 10,805 10,805 0

18 North Ruvu2 Kibaha/Bagamoyo 56 32,000 0

  Total   91,662 81,916 205,522 11,808,600

Chanzo: Taarifa ya utekelezaji ya Mashamba ya miti ya TFS kwa mwaka 2013/14

1 Mashamba ya miti mapya

2 Misitu ya hifadhi iliyobadilishwa kuwa mashamba ya miti

Jedwali Na. 4: Ujazo uliovunwa (cm) kutoka mashamba ya miti 2011/12-2013/14

JINA LA SHAMBA 2011/2012 2012/13 2013/14 Total

Sao Hill 824,000 807,000 850,000 2,481,000

Shume 22,236 21,453 22,211 65,900

West Kilimanjaro 24,700 18,000 1,750 44,450

North Kilimanjaro 20,000 20,000 20,000 60,000

Buhindi 22,770 22,770 24,270 69,810

Rubare 800 0 0 800

Longuza 14,481 15,412 15,000 44,893

Rubya 4,895 6,473 6,900 18,268

Kiwira 5,000 144 2,000 7,144

Kawetire 8,940 1,500 10,425 20,865

Mtibwa 23,955 25,508 15,689 65,152

Matogoro 2,421 1,000   3,421

Rondo 0 13,630 10,500 24,130

Meru 10,000 24,000 21,000 55,000

Total 984,198 976,890 999,745 2,960,833

Chanzo: Taarifa ya utekelezaji ya Mashamba ya miti ya TFS kwa mwaka 2011/12- 2013/14

Page 32: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

23

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

v) Uimarishaji wa mipaka umefanyika katika misitu ya asili ya hifadhi 102 iliyotengwa kwa ajili ya uzalishaji (production forests) kwa kufanya soroveya ya pili (resurvey) kwa mipaka yenye urefu wa kilomita 9,975; kuweka maboya 1,600 na kuweka vibao vya alama 3,300 (sign boards); kuchimba mashimo ya mwelekeo 162 (directional trenches) na kupanda miti kwenye mpaka wa urefu wa kilomita 110. Aidha, upandaji wa miche 253,600 (sawa na hekta 210) ya aina tofauti ya miti katika maeneo ya misitu yaliyoharibika (degraded forests) ulifanyika (Picha Na.9).

vi) Katika kuboresha usimamizi na uendelezaji misitu Wakala umeongeza kasi ya upandaji miti katika maeneo mapya kila mwaka ili kukidhi mahitaji ya mazao ya miti kwa kushirikisha wadau mbalimbali kama wananchi/ jamii na taasisi kama shule katika kupanda miti na kuimarisha uhifadhi. Katika kipindi cha 2011/12 hadi 2013/14 jumla ya miti 21,000,000 ilipandwa. Jedwali Namba 5a linaonesha idadi ya miti iliyopandwa katika maeneo ya jamii na taasisi kupitia uwezeshaji wa Wakala katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Wakala

Grafu Na. 1: Mazao makuu ya Misitu yaliyovunwa 2011/12-13/14

Jedwali Na. 5a: Upandaji miti kitaifa kwa kipindi cha miaka 2011/12 - 2013/14

Mwaka Idadi ya miti iliyopandwa

2011/12 7,000,000

2012/13 7,000,000

2013/14 7,000,000

Jumla 21,000,000

Page 33: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

24

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

viii) Urekebishaji wa ramani 23 za misitu ya hifadhi ya asili kwa ajili ya uzalishaji, pamoja na Mipango ya kina ya usimamizi kwa misitu 9 ilitayarishwa katika jumla ya hekta 273,274.

ix) Wakala uliweza kusimamia Mipango ya uvunaji (sample harvesting plan) ya wilaya chini ya kanda zake 7, ambapo katika kipindi cha miaka mitatu mazao mbalimbali ya misitu yalivunwa (Jedwali Na. 5b na Grafu Na. 1). Aidha, mwaka 2011/12 kuni na nguzo vilivunwa kwa wingi; mwaka 2012/13 Mkaa na mbao; na mwaka 2013/14 mazao ya misitu ya Mkaa, nguzo na mbao yalivunwa kwa wingi. Mkaa na nguzo vikionyesha kuwa ni mazao ya misitu yanayotegemewa zaidi katika matumizi.

Picha Na. 11: Mazao ya nyuki kutokana na mafunzo; Katikati: Mizinga ya TFS ya kugawanywa kwa wadau; Kulia: Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo ya ufugaji nyuki

Picha Na.12: Kushoto: Mafunzo ya utundikaji mizinga kwa kikundi cha ufugaji Haysali, Mbulu; Kulia: Mizinga iliyogawanywa na TFS kwa kikundi cha Nguvukazi, Biharamulo

vii) Wakala uliweza kuimarisha mipaka katika misitu ya hifadhi ya asili (protection forests) kwa kufanya soroveya ya kuhakiki mipaka ya misitu ya hifadhi ya kilomita 3,262.78; Usimikaji wa maboya 227 na kuweka vibao vya alama 425 (Picha Na.10); kuchimba mashimo ya mwelekeo 511 na kupanda miti kwenye mipaka wa kilomita 17. Aidha, uzalishaji wa ramani 40 za misitu ya hifadhi na ramani 3 za hifadhi za nyuki zinazopendekezwa ulifanyika.

Page 34: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

25

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na. 5b: Baadhi ya Mazao yatokanayo na misitu yaliyovunwa katika miaka mitatu

ZAO/MWAKA 2011/12 2012/13 2013/14 TOTAL

Magogo (CBM) 14,140.0 29,100.3 21,378.0 64,618.3

Kuni (CBM) 701,264.0 54,359.9 86,163.6 841,787.5

Mkaa (Magunia) 265,966.0 641,703.2 1,000,837.1 1,908,506.3

Nguzo (RM) pamoja na nguzo za mikoko

552,300.0 235,739.4 706,550.9 1,494,590.3

Mbao (CBM) 97,834.2 409,866.6 485,015.2 992,716.0

Chanzo: Taarifa za Kanda za TFS

x) Wakala umeandaa Mpango Mkakati wa pili (SP II) ambao pamoja na mambo mengine unaainisha mikakati ya kuondokana na upungufu wa timbao ifi kapo mwaka 2030. Takribani hekta 185,000 zitapandwa kila mwaka kwa kushirikisha wadau wote. Utayarishaji wa Mipango ya Usimamizi katika mashamba ya miti umekamilika kwa asilimia 100. Mipango inaonesha ujazo unaelekea kuwa endelevu kwa Wakala; Jumla ya hekta 69,613 za hifadhi za nyuki zinazopendekezwa ambazo zitajumuisha za Taifa ((NBRs-(37,166ha)) na za Vijiji (VBRs)- 32,447 ha)) zipo katika hatua mbalimabli kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na.6.

Picha Na. 13: Nyumba ya kulea malkia wa nyuki Kituo cha Kibaha, DSM

Page 35: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

26

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na. 6: Eneo na Hali ya hifadhi za nyuki zilizopendekezwa

Mahali Eneo (ha) Hadhi

Kanda ya Kati (Jongolo-1000ha, Wambura sendeko-1700ha, Wairo- 447ha and Mialo 500 ha Kondoa.

3,647 Eneo limepimwa na kukubaliwa na Serikali ya Kijiji.

Msemembo and Aghondi -Manyoni) 1,700  Eneo limetambuliwa linasubiri maamuzi ya kijiji

Kanda ya Magharibi: Buha - Kibondo 2,524 Eneo limetambuliwa na kupimwa

Kanda ya ziwa: (Sengerema, Maswa, Bukombe, Misenyi, Bunda, Nyangwale, Biharamulo)

29,980 Eneo limetambuliwa

Kanda ya Kusini: (Enje-Nachingwea and Lilindindo - Namtumbo)

4,000Eneo limetambuliwa , ramani imechorwa na mpango wa usimamizi umeandaliwa Usimamizi wa pamoja utafanyika kati ya Wakala na Kijiji

Kanda ya Kaskazini: Kangata (1439ha), Kwenyunga Magiri (138 ha) - Handeni

1,578 Hifadhi ipo katika hatua za mwisho za kutangazwa

Sambu Kilindi 567 Eneo limetambuliwa na kuidhinishwa na kijiji

Kanda ya Kusini Nyanda za juu: Kipembwawe in Chunya and Ndarambo

23,150Eneo limepimwa, ramani imechorwa na hifadhi ipo katika hatua za mwisho za ktangazwa

Shinji and Ndarambo - Momba District 2,000 Eneo limetambuliwa

Kanda ya Mashariki: Lukenge – Kibaha; Leshata and lsitu - Kilosa)

467 Eneo limetambuliwa na kufanyiwa soroveya

Msingisi, Lungo and Mlumbilo villages - Gairo and Mvomero

Jumla Kuu ya Maeneo yote 69,613

Chanzo: Taarifa ya utekelezaji za mwaka za TFS 2011/12-2013/14

xi) Katika kipindi cha Mpango Mkakati (SPI), manzuki 21 zenye mizinga 3,870 zilisimamiwa, aidha Wakala ulitoa mafunzo kwa vikundi 921 (Washiriki 7,320) vya wafugaji nyuki, katika vijiji 242 kutoka wilaya 30.Vilevile Wakala uligawa bure mizinga 14,076 (Picha Na. 11 & 12).

xii) Tangu kuanzishwa kwa TFS wilaya 29 na mashamba ya miti 7 zimeanzisha manzuki

Picha Na 14: Kushoto: Mbao zilizokamatwa; Kulia: Uondoaji wa wavamizi -msitu wa hifadhi wa Nyahua Mbuga

Page 36: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

27

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

36 na kutundika mizinga 4,184 katika misitu ya hifadhi na mashamba ya miti kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 7.

Jedwali Na. 7: Idadi ya manzuki na mizinga inayosimamiwa na TFS

Mahali Idadi ya Manzuki Idadi ya mizinga

Kanda ya Kaskazini 15 508

Kanda ya Kusini 10 1,500

Kanda ya Mashariki 1 42

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

3 1,400

Mashamba ya miti 7 724

JUMLA 36 4,184

Chanzo: Taarifa ya Utekelezaji ya miaka mitatu 2011/12-2013/14

xiii) Wakala ulitoa mafunzo ya kulea malkia wa nyuki kwa watumishi 58, aidha Kituo cha kulelea malkia wa nyuki kimeanzishwa katika Kanda ya Mashariki (Picha Na 13). Katika Mpango Mkakati wa pili Wakala unakusudia kuwa na vituo vya kulea malkia katika kanda zote. Lengo likiwa ni kuhakikisha kuna upatikanaji mkubwa wa makundi ya nyuki. Mafunzo ya ubora wa asali, masoko na ufungashaji wa mazao ya nyuki na ujasiliamali, kanuni za ufugaji nyuki ziliendeshwa kwa wafugaji nyuki na wafanya biashara 241kutoka wilaya 25. Aidha, upimaji wa sampuli 172 za ubora wa asali ulifanyika na kugundua kuwa asali yetu inakidhi viwango vya masoko la kitaifa na kimataifa.

xiv) Katika kipindi cha miaka 3 Wakala uliweza kufanya doria katika misitu ya hifadhi, hifadhi za nyuki, manzuki, misitu katika ardhi ya jumla na maeneo ya masoko. Jumla ya siku za doria 300,139 zilitumika. Kutokana na doria hizi uvunaji haramu wa mazao ya misitu umepungua kwa asilimia zaidi ya 50%. Baadhi ya mazao ya misitu yaliyokamatwa na kutaifi shwa ni mbao 295,508 (Picha Na.14-Kushto), magunia ya mkaa 97,451, milango 1,380, magogo 13,983 na nguzo 148,397. Vilevile TFS

Picha Na. 15: Ukarabati wa nyumba za watumishi Chuo cha FTI, Olmotonyi- Arusha

Page 37: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

28

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ilitoa mchango wa fedha na nguvu kazi katika operesheni maalum ya kupambana na ujangili, uvunaji haramu, na wavamizi wa misitu ya hifadhi. Kupitia operesheni hii jumla ya vipande vya mbao 15,143 magunia ya mkaa 678, magogo 135 na misumeno 60 ilikamatwa. Aidha, Kikosi kazi kilichokuwa kimeundwa na serikali na kuwezeshwa na TFS kushughulikia masuala ya uvunaji haramu na biashara katika mpaka kati ya Msumbiji na Tanzania kilifanikiwa kukamata mbao 32,085 na wahalifu 14 .

xv) Wakala uliweza kuwaondoa wavamizi katika misitu ya hifadhi takribani 52 (Jedwali Na. 8) na (Picha Na. 14–Kulia) kwa kufanya siku za doria 99,335 wahalifu 1,328 walikamatwa, mali zao zilikamatwa pamoja na kulipishwa faini na kesi 60 ziko mahakamani.

Jedwali Na.8: Misitu ya Hifadhi iliyokuwa na wavamizi

S/N Msitu wa Hifadhi Mahali/Wilaya

1 Nyahua Mbuga na Goweko Sikonge - Tabora

2 Uyui-Kigwa – Rubuga na Urumwa Uyui - Tabora

3 Igombe River, North Ugala and MpandalineKaliua/Urambo -

Tabora

4 MkweniKahama -

Shinyanga

5 Inyonga West and Mlele Hills Mlele - Katavi

6 North-East Mpanda, Uruwa Mpanda - Katavi

7 Ilombelo Nzega - Tabora

8 Kising’alugalo Iringa - Iringa

9 Mbeya Range Mbeya - Mbeya

10 Kipembawe Chunya - Mbeya

12 MangalisaMpwapwa -

Dodoma

13 CheneneMpwapwa -

Dodoma

14North Mamiwa-Kisara and South Mawiwa – Kisara,

Palaulanga, Ukwiva, Mamboya na MilindoKilosa - Morogoro

15 Biharamulo and Nyantakala Biharamulo -

Kagera

17 Minziro NR Misenyi - Kagera

18 Ruvu South & North Kibaha - Pwani

19 Amani NR, Kwani, Tongwe, Muheza - Tanga

20 Magamba NR Lushoto Tanga

21 Mkingu NRMvomero -

Morogoro

22 Chome NRSame -

Kilimanjaro

23 Bombo East and Bombo West, Nilo NR, Bubamavumbi Korogwe- Tanga

Page 38: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

29

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

24 Kilindi Kilindi - Tanga

25 Korogwe Fuel wood, Kwasumba and Jungu Handeni - Tanga

26 Mkuti, Makere North, Makere South and MwalyeMorogoro -

Morogoro

27 Geita Geita - Geita

28 SayangaKondoa -

Dodoma

29 NikongaKahama -

Shinyanga

30 Rau Moshi -

Kilimanjaro

31 Hifadhi ya Mikoko ukanda wa kaskaziniTanga rural -

Tanga

32 Hifadhi ya Mikoko ukanda wa kati Rufi ji delta

33 Kazimzumbwi Kisarawe

34 Mselezi Ulanga

35 Nandembo na Mhuwesi Tunduru

36 Kipiki Namtumbo

xvi) Katika kutoa elimu ya uhifadhi na kudhibiti moto jumla ya vijiji 1,772 vilivyo karibu na, misitu ya hifadhi vilihamasishwa. Vipindi vya redio 266, vipindi vya runinga 55, maonesho ya video 44, vipeperushi 99, nakala 400 za utendaji bora na nakala 22,886 ya vijitabu vya ugani zilitayarishwa na kusambazwa.

xvii) Uongoaji wa hekta 10,951.5 za maeneo yaliyoharibika kwa kupanda miti 208,500 na kutoa misaada kwa jamii kama: viriba kilo 12,515 na mbegu za miti kilo 2,004 ili kupanda jumla ya miti 13,412,704 katika maeneo yaliyoharibika, vijishamba, mashamba binafsi, vijiji na kuzunguka shule.

xviii) Hekta 52.42 za shamba la kamba Mafi a na hekta 562 za mashamba ya chumvi katika wilaya za Mkuranga, Rufi ji delta, Kilwa, Lindi na Mtwara zimetenga na kupimwa. Aidha, Kilomita 268.9 za njia za utalii (nature trails) zimejengwa; kilomita 69.3 za njia za gari (drive routes), kilomita 64 za njia ya utalii (nature trails), maeneo 10 ya kupumzika (resting points/picnic site) na maeneo 21 ya kuweka kambi (campsites); zimeimarishwa.Takribani hekta 135,000 zimetambuliwa na mchakato wa kuziweka katika usimamizi shirikishi unaendelea.

xix) Miongozo ya usimamizi shirikishi imetayarishwa pamoja na Mwongozo wa mfumo wa kugawana faida na majukumu umetayarishwa na kukubaliwa na wadau. Mikataba 19 ya usimamizi wa pamoja wa misitu ya hifadhi ya taifa na sheria ndogo katika vijiji vinavyozunguka misitu ya hifadhi iliandaliwa, aidha mikataba 57 ya usimamizi wa msitu kwa ajili ya kurasimisha shughuli za usimamizi wa pamoja ilikubaliwa. Vilevile Vijiji 163 vimefundishwa na kuwezeshwa juu ya shughuli za kipato mbadala. Hadi kufi kia 2014 jumla ya hekta 7.7 zimewekwa katika usimamizi shirikishi na jamii, ikiwa ni ongezeko la hekta milioni 3.6 ya eneo chini ya usimamizi shirikishi ukilinganisha na eneo la awali la hekta 4.1 milioni za mwaka 2006.

Page 39: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

30

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

xx) Katika kutekeleza Mpango Kazi wa Nishati timbao jumla ya vituo 101 vya kukusanyia na kuuzia mkaa kandokando ya barabara za Dar es salaam – Morogoro – Segera pamoja na wilaya za Songea, Namtumbo, Mbinga, Handeni, Korogwe, Biharamulo, Kigoma, Shinyanga, Kilosa, Rufi ji, Gairo, Mvomero na Masasi vimeanzishwa. Aidha washiriki 30 kutoka kijiji cha Mbangamawe wilaya ya Songea walifundishwa njia za kuzalisha mkaa bora. Vilevile Wanawake 120 kutoka vijiji 6 vya wilaya za Mbozi, Chunya na Momba walifundishwa jinsi ya kutengeneza na kutumia jiko banifu. Wakala utaendelea kuongeza na kudhibiti vituo vya kuuzia mkaa.

xxi) Ukaguzi maalumu wa maduhuli ulifanyika na jumla ya TAS 7.62 bilioni ziliokolewa kama inavyooneshwa katika Jedwali Na.9. Aidha kaguzi hizi zimeweza kuongeza utii wa sheria bila shuruti.

Jedwali Na. 9: Makusanyo kutokana na Ukaguzi maalumu

Mwaka Idadi ya Kaguzi Maduhuli yaliyookolewa (Billion TZS)

2011/12 2 1.4

2012/13 6 3.95

2013/14 3 2.27

Jumla 11 7.62

Chanzo: Taarifa za utekelezaji za mwaka za TFS 2011/12-2013/14

xxii) Jumla ya wilaya 85 kati ya wilaya lengwa 80 ziliwezeshwa kuandaa mipango ya uvunaji, kufanya mikutano ya kamati za uvunaji na kudhibiti uvunaji.

xxiii) Jumla ya wakaguzi wa maduhuli 82 kati ya 200 wa Wizara ya Maliasili na Utalii na halmashauri za wilaya walishiriki kwenye warsha ya mafunzo ili kuboresha uwezo wa kukusanya maduhuli kwa kutumia vitabu vya kukusanyia maduhuli, utaratibu wa kupiga faini na matumizi ya kanuni za misitu; Vituo vya ukaguzi 35 viliwezeshwa kukagua, kuhakiki uhalali, kupitisha vibali vya kusafi risha (TP) mazao ya misitu na vituo vipya 25 vya ukaguzi vimeanzishwa ili kuimarisha utii wa sheria.

xxiv) Mapitio ya mirahaba na ada za mazao ya misitu na huduma yalifanyika na kuidhinishwa na Waziri mwenye dhamana.

xxv) Wakala umeweza kusaidia vyuo vya Misitu (FITI/FTI) na Nyuki (BTI) kununua vitabu, kukarabati nyumba za watumishi (Picha Na 15), madarasa uwanja wa michezo na mabweni ya wanafunzi;

xxvi) Ili kuinua kiwango cha ufanisi wa kazi Wakala umetoa mafunzo kwa watumishi 57 kwa mafunzo ya muda mrefu na watumishi 132 - mafunzo ya muda mfupi (Jedwali 10). Aidha watumishi wengi wamepatiwa mafunzo mbalimbali ikilinganishwa na kipindi cha Idara.

Page 40: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

31

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali 10: Watumishi wa TFS waliohudhuria mafunzo (2011/12 -2013/14)

Mwaka Watumishi wa waliohudhuria kozi ndefu

Watumishi wa waliohudhuria kozi fupi

Malengo Mafanikio Malengo Mafanikio

2011/2012 47 39 151 11

2012/2013 67 76 120 25

2013/2014 61 57 100 68

Jumla 371 132

Chanzo: Taarifa za utekelezaji za mwaka za TFS 2011/12-2013/14xxvii) Mwaka 2013/14 Wakala umeajiri watumishi wapya 354 kama Jedwali Na. 11

linavyoonyesha

Jedwali Na.11: Watumishi wapya kwa Kada walioajiriwa na Wakala

S/N Category 2013/14

Afi sa Misitu 41

Afi sa Nyuki 10

Msaidizi Misitu 244

Msaidizi Nyuki II 16

Katibu Muhtasi III 12

6 Afi sa Rasilimali watu 01

7 Msaidizi Masjala II 13

8 Dereva II 03

9 Mlinzi 02

Picha Na. 16: Ofi si ya Hifadhi asilia Uluguru, Morogoro

Page 41: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

32

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

10 Msaidizi wa Ofi si 06

11 Fundi Sanifu (Mechanical Technician) 03

12 Mhudumu Kituo cha afya (Medical Attendant) 02

13 Mgavi Msaidizi II 01

Jumla 354

Chanzo: Taarifa za utekelezaji za mwaka za TFS 2012/13-2013/14

xxviii) Wakala umeweza kulipa watumishi wake stahiki zao, marupurupu na motisha, kununua huduma na kulipia huduma za ofi si kwa kanda 7, mashamba 18 na Makao makuu.

xxix) Wakala umefanya maboresho ya makazi ya watumishi, ofi si (Picha Na. 16) pamoja na miundo mbinu kama: kuratibu ujenzi ofi si 1 na nyumba za wakuu wa safu 12, na kukarabati nyumba 5 kwa kutumia fedha za UNDP na Serikali ya Ujerumani. Vilevile Wakala umegharimia ujenzi wa majengo 7 katika mashamba ya miti Mtibwa (2), Rubare (1), Wino-Ifi nga (1), Ukaguru (2), Rondo (1). Ukarabati wa nyumba za watumishi 287 na majengo ya ofi si, pia nyumba 2 za nyuki zilijengwa katika Mradi wa Buha beekeeping project - Kibondo. Wakala umeweza kujenga barabara mpya za msituni zenye urefu wa kilomita 161, na kukarabati kilomita 7,672, Madaraja 53 na mnara 1 wa kufanyia doria za moto.

xxx) Wakala umeweza kuandaa Mfumo wa uperembaji na tathmini na tayari unatumika. Aidha Wakala uliandaa Warsha ya mafunzo kwa watumishi 60 kuelimisha mpango wa uperembaji na tathmini. Jumla ya kanda 7 na mashamba 15 yalifanyiwa uperembaji. Jumla ya vituo 73 kati ya vituo 97 (75.2%) vilitembelewa na kufanyiwa ukaguzi (Jedwali Na.12). Vilevile ukaguzi wa ndani ulifanyika kama sehemu ya uperembaji kwenye mashamba 13 na kanda 5. Ukaguzi nje (external auditing) wa mahesabu kwa mwaka 2011/12 na 2012/13 ulifanyika na matokeo yalikuwa mazuri (“satisfactorily unqualifi ed audit report”).

xxxi) Mkakati wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana Rushwa ulitekelezwa ambapo warsha 7 za kuelimisha zilifanyika na kuhudhuriwa na watumishi 841 katika ngazi tofauti. Kwa sasa Mkakati wa kupambana na Rushwa wa Wakala (Picha Na.17) umeandaliwa na utekelezaji wake unatarajiwa kuleta mabadiliko yenye ufanisi kwa Wakala.

xxxii) Huduma kwa Mteja inatekelezwa na inatarajiwa kuwa madhubuti ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji na hivyo kuongeza ufanisi kazini. Wakala umeandaa andiko la Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Picha Na.18) unaotarajiwa kuongeza tija katika utoaji wa huduma.

Page 42: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

33

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Picha Na.17: Mkakati wa Kupambana na Picha Na.18: Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Rushwa

Jedwali Na.12: Idadi ya vituo vya Wakala vilivyotembelewa kwa ajili ya Uperembaji kwa Kanda 7 kati ya 2012/13 na 2013/14

S/N Kanda Idadi ya Vituo Idadi ya maeneo yaliyotembelewa

1 Kaskazini 18 11

2 Mashariki 15 9

3 Magharibi 9 7

4 Kati 18 16

5 Kusini 17 14

6 Ziwa 12 10

7 Nyanda za Juu Kusini 8 6

Jumla 97 73

xxxiii) Wakala umeweza kuboresha maswala ya jinsi: asilimia 40 ya Wakuu wa Vitengo/ Meneja Waandamizi wa TFS Makao Makuu ni wanawake, asilimia 57 ya wasaidizi wa Meneja katika kanda za TFS ni wanawake, aidha wanawake 2 ni Meneja wa mashamba ya miti na mmoja ni Meneja wa Hifadhi Asilia.

Page 43: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

34

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

5. MUHTASARI WA MCHANGUNUO WA UTENDAJI KABLA NA BAADA YA KUANZISHWA WAKALA

Mchanganuo ufuatao (Jedwali Na. 13) ni muhtasari wa masuala makuu yaliyofanikiwa chini ya Wakala katika kipindi cha miaka mitatu yakilinganishwa na yale yaliyotekelezwa na Idara ya Misitu na Nyuki katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya kukabidhi majukumu kwa Wakala (TFS)

Jedwali Na. 13: Muhtasari wa Mchanganuo wa Utendaji wa Wakala

Na. Suala Kabla ya Wakala

(Idara ya Misitu na Nyuki)

Baada ya Uanzishwaji wa Wakala (TFS)

1 Ukusanyaji wa Mapato/Maduhuli

Mapato kwa miaka Mitatu (2007/8-2009/2010) yalikuwa ni jumla ya Takribani TAS Bilioni 87, ikiwa ni wastani wa billioni 29 kwa Mwaka.

Mapato kwa miaka Mitatu (2011/12-2013/2014) yalikuwa ni jumla ya Takribani TAS Bilion 199.7, ikiwa ni wastani billion wa 67 kwa Mwaka.

Mapato makubwa yalitokana na mrahaba, ambao ulichangia asilimia zaidi ya 92 ya mapato yote

Mapato makubwa yalitokana na mrahaba ambao ulichangia asilimia zaidi ya 66 ya mapato yote

2 Uhifadhi Mipango ya usimamizi wa misitu asili yenye eneo la hekta 1,338,800 ya uzalishaji na uhifadhi iliandaliwa, kati ya eneo hili misitu 8 ilikuwa ni misitu lindimaji yenye viumbe ndwele na bioanuwai ya hali ya juu ikiwemo misitu ya hifadhi ya Amani, Kilombero, Nilo, Uluguru, Magamba, Uzungwa, Mkingu na Chome

Wakala ulisimamia ha 4,164,463 za misitu asili. Aidha, mipango ya kina ya usimamizi wa misitu ya asili yenye eneo la hekta 181,669 ya uzalishaji na uhifadhi iliandaliwa, Aidha Wakala uliendelea kutoa kipaumbele kwa misitu asilia 11 yenye bioanuwai nyingi na viumbe ndwele na adimu yaani: Amani, Kilombero, Nilo, Uluguru, Magamba, Uzungwa, Mkingu, Chome, Mt. Rungwe, Rondo na Minziro

Mipango ya usimamizi wa Mashamba ya miti ya kupandwa yenye jumla ya eneo la hekta 150,000 ilitayarishwa kwa kipindi cha 2008/2009

Mipango ya usimamizi wa Mashamba ya miti ya kupandwa yenye jumla ya eneo la ha 205,522 ilitayarishwa kwa kipindi cha 2012/2013 (likiwa ni ongezeko la ha. 55,522).

Idara ilikuwa haina takwimu za rasilimali za misitu zinazotoa taarifa sahihi na za uhakika kuhusu hali halisi, ukubwa, na matumizi ya rasilimali za misitu ambazo zingesaidia katika kuandaa sera na programu za kutekeleza

usimamizi endelevu wa misitu

Uendelezaji wa mashamba ya miti ulikuwa hekta 6,376 (2005/06 – 2009/10)ambapo ni wastani wa hekta 1275.2 kwa mwaka

Wakala umefanya Tathmini ya Rasilimali za Misitu (National Forest Resource Monitoring and Assessment (NAFORMA) inayotoa taarifa sahihi na za uhakika kuhusu hali halisi, ukubwa, na matumizi ya rasilimali ya misitu ambayo ni muhimu kwa ajili ya kutoa maamuzi na kuandaa sera na programu za kutekeleza usimamizi endelevu wa misitu.

Uendelezaji wa mashamba ya miti umekuwa hekta 39,776 (2010/11 – 2014/15) ambapo upanuzi ni hekta 15,080.5 na upandaji wa kurudishia maeneo yaliyovunwa hekta 24,695.5. Upandaji huo ni sawa na wastani wa hekta 7,955 kwa mwaka.

Page 44: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

35

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Misitu mingi ya hifadhi haikufyekewa na kuhakikiwa mipaka hivyo ilivamiwa na kupoteza hadhi kutokana na migogoro ya uvamizi na kukosekana kwa mipaka

Mipaka iliimarishwa na kupandishwa hadhi kwa asilimia 25 ya maeneo ya hifadhi. Takriban kilomita 9,975 za mipaka katika misitu ya asili ya hifadhi kwa ajili ya uzalishaji; Pamoja na urefu km 3,263 za mipaka ya misitu ya hifadhi asilia (Asilia/lindi maji) iliimarishwa.

Idara ilikuwa na vituo 4 vyenye jumla ya manzuki 21

Wakala umeendeleza vituo 4 na kuanzisha manzuki 57 na kutundika mizinga 8,054 katika misitu ya hifadhi na mashamba ya miti

3 Vitendea Kazi/Mazingira ya Kazi

Idara ilikuwa na vitendea kazi/majengo na miundo mbinu chakavu iliyohitaji ukarabati katika ngazi mbalimbali (ukarabati mkubwa/ukarabati mdogo)

Wakala umefanya maboresho ya makazi ya watumishi pamoja na miundo mbinu; kama kujenga ofi si 1 na nyumba za wakuu wa safu 12, na kukarabati nyumba 5 kwa kutumia fedha za UNDP na Serikali ya Ujerumani. Vilevile Wakala umefanya Ujenzi wa majengo 7 katika mashamba ya miti Mtibwa (2), Rubare (1), Wino-Ifi nga (1), Ukaguru (2), Rondo (1). Ukarabati wa nyumba za watumishi 287 na majengo ya ofi si, pia Nyumba 2 za nyuki zilijengwa katika Mradi wa ufugaji nyuki-Kibondo. Wakala umeweza kujenga barabara mpya za msituni zenye urefu wa kilimita 161, na kukarabati kilomita 7,672 , Madaraja 53, mnara (1) wa kufanyia doria za moto.

4 Wafanyakazi Idara ilikuwa na Wafanyakazi wachache, wengi wao wakiwa wanatimiza muda wa kustaafu; na mafunzo hayakujumuisha watumishi wengi.

Wakala umeajiri na kupanga watumishi wa kada mbalimbali katika Kanda na baadhi ya wilaya ambazo zina rasilimali kubwa za misitu na nyuki. Wakala unazingatia sifa, jinsi na uhitaji. Aidha, Wakala umetoa mafunzo kwa idadi kubwa ya watumishi wake ili kuboresha utendaji wao na kutoa motisha kadri inavyowezekana.

5 Mipango (SP/BP)

Idara ilitekeleza Mipango Mkakati kama sehemu ya Mpango Mkakati wa Wizara. Aidha, Idara haikuwa na Mipango ya Kibiashara.

Wakala umeanda Mipango Mkakati wa kwanza na wa pili, na unaandaa na kutekeleza Mipango ya Kibiashara ya kila mwaka

6 Bajeti na Matumizi

Idara ilikuwa na bajeti ya TAS bilioni 24.8. Bajeti ya matumizi ya kawaida (OC) pamoja na taasisi zake ilikuwa na wastani wa TAS 11.5 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2007/8-2010/11 na bajeti ya matumizi ya maendeleo ilikuwa na wastani wa TAS 13.3 bilioni) kwa kipindi cha 2007/08-2010/11

Bajeti ya Wakala ilikuwa ni wastani wa TAS 119.2 bilioni na matumizi ya TAS 100.3 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2011/12 – 2013/14

Page 45: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

36

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

7 Uwekezaji endelevu

Idara haikuwa na njozi/ndoto ya uwekezaji na mikakati thabiti ya uendelevu kulingana na mazingira ya kibiashara ambayo hayakuwepo wakati wa Idara

Vitega uchumiWakala umeweka njozi ya kuendeleza ofi si zake zilizo katika miji mashuhuri na majiji ili kugeuza kuwa majengo ya kisasa ya uwekezaji. Ofi si hizo za Wakala ni zile zilizopo katika majiji ya Mbeya, Tanga na miji ya Morogoro na Moshi. Mkakati uliopo ni kujenga majengo ya kisasa yenye hadhi na kukodisha sehemu za majengo hayo kwa wawekezaji wa kibiashara. Sera ya Uwekezaji : Wakala upo katika mchakato wa kuandaa sera ya uwekezaji (investment policy) ili kuwa na uwekezaji wa aina mbalimbali

Makao Makuu Mapya ya Wakala: Wakala upo katika mchakato wa kujenga ofi si mpya ya kisasa itakayokuwa na vitega uchumi. Vilevile Wakala upo katika mchakato wa kuomba kuwa Mamlaka (Authority)

8 Utegemezi Idara ilikuwa inapata ruzuku Kutoka Serikalini kulipia matumizi ya Kawaida pamoja na mishahara. Aidha bajeti za maendeleo zilitolewa na Wahisani kwa takribani asilimia 100.

Wakala unapata Malipo ya Mishahara ya Wafanyakazi wake kutoka Serikalini (Vote 69); Hata hivyo mishahara hiyo inatokana na fungu la mchango kutoka katika makusanyo ya Wakala kwenda Hazina. Hivyo Wakala unajitegemea kwa asilimia 100 ya matumizi yake ya kawaida

9 Mchango wa Wakala kwa Serikali

Serikali ilikuwa inatoa ruzuku kulipia matumizi ya Kawaida pamoja na mishahara

Wakala ulichangia TAS 108.7 bilioni kwenda serikalini katika kipindi cha miaka mitatu (2011/12 - 2013/14) kwa mgawanyo ufuatao:

Hazini (81.5 bilion); VAT (15.7 bilion), TaFF (9.2 bilion) & CESS (2.2 bilion).

6. RASILIMALI FEDHA

6.1 Mapato kabla ya kuanzishwa Wakala

Idara ya Misitu na Nyuki ilikuwa inapata mapato kutokana na vyanzo vifuatavyo;

a) Makusanyo ya maduhuli kutokana na rasilimali za misitu na nyuki (mashamba ya miti na misitu ya asili)

b) Fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kulipa mishahara

c) Fedha za miradi kutoka kwa Washiriki katika maendeleo

d) Mikopo na Misaada.

Page 46: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

37

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Idara ya Misitu na Nyuki ilikuwa na madaraka kupitia sheria ya Misitu Na. 14 ya 2002 ya kukusanya ada na mrahaba wa mazao na huduma za misitu kutoka misitu ya hifadhi ya taifa na misitu iliyopo kwenye ardhi ya jumla (Kifungu II na Kifungu X cha sheria ya misitu ya 2002). Ingawaje, ada na mrahaba kutoka misitu ya hifadhi ya serikali za mitaa na misitu ya vijiji inakusanywa na serikali za mitaa na serikali za vijiji. Aidha, serikali za mitaa zina madaraka kupitia sheria ya fedha ya mwaka 1982 kukusanya ushuru wa asilimia 5 ya mapato (CESS) yanayotokana na mazao ya misitu yanayovunwa ndani ya wilaya husika.

Ada na mrahaba hulipwa wakati mazao kama magogo, nguzo, fi to, kuni, mkaa, mbegu, miche nk. vinapovunwa kutoka katika misitu (iliyohifadhiwa na ya ardhi ya jumla) kwa leseni kwa mujibu wa (Kifungu VI cha sheria ya misitu 2002). Maduhuli yanayokusanywa kutoka misitu ya hifadhi ya taifa na misitu kwenye ardhi ya jumla yanapelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii na hatimaye kupelekwa Wizara ya Fedha (Hazina) kwa ajili ya matumizi ya kitaifa. Wizara ya Maliasili na Utalii ilikuwa ni mojawapo ya Wizara zilizokuwa katika Retention Scheme na hivyo ilikuwa inarudishiwa asilimia 70% ya mapato yote kwa ajili ya matumizi ya Wizara.

i) Tathmini kwa ujumla inaonesha kuwa maduhuli yaliyokusanywa na Idara ya Misitu na Nyuki yaliongezeka kutoka TAS 4.5 bilioni katika mwaka 2003/04 hadi TAS 21.8 bilioni katika mwaka 2007/08 (ikiwa ni kiwango cha juu kilichokusanywa).

ii) Wastani wa makusanyo kwa mwaka ulikuwa ni takribani ya TAS 17.5 bilioni ambayo ni asilimia 43 ya makusanyo tarajiwa ambayo yangekusanywa. Makusanyo makubwa yalitokana na mrahaba ambao ulichangia asilimia zaidi ya 92 (92%) ya makusanyo yote. Tafsiri ya matokeo ni kwamba kulikuwa na takribani asilimia 57 ya maduhuli ambayo yalikuwa hayakusanywi na inawezeka yalipotea kutokana na uwezo mdogo wa Idara, hivyo kusababisha mianya ya rushwa, nyaraka za kugushi na uvunaji haramu wa mazao ya misitu.

iii) Bajeti ya matumizi ya kawaida (OC) pamoja na taasisi zake ilikuwa na wastani wa TAS 11.5 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2007/8-2010/11 (Jedwali Na.14) na bajeti ya matumizi ya maendeleo ilikuwa na wastani wa TAS 13.5 bilioni. Jedwali Na. 15 linaonyesha maoteo (makadirio) ya fedha za Idara toka ndani na nje yakionyesha tofauti kubwa ya utegemezi toka nje ya Wizara ikilinganishwa na mapato halisi ya kuendesha Idara.

Jedwali Na.14: Bajeti ya Matumizi ya kawaida inajumuisha Idara na taasisi zake kwa miaka minne (2007/08 - 2010/11)

2007/2008 2008/2009 2009/2010 2010/211

Mishahara Mishahara 5,108,766,000 Mishahara 6,967,516,600 Mishahara 7,778,66200

Mengineyo 5,243,129,000 Mengineyo 4,278,440,000 Mengineyo 7,785,999,000 Mengineyo 8,641,118,900

Jumla 5,243,129,000 Jumla 9,387,206,000 Jumla 14,753,515,600 Jumla 16,419,781,100

Page 47: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

38

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na.15: Makadirio ya fedha za Miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne (2007/08 - 2010/11)

Makadirio ya fedha 2007/2008

Makadirio ya fedha 2008/2009 Makadirio ya fedha 2009/2010

Makadirio ya fedha 2010/2011

Fedha za ndani

Fedha za nje Fedha za ndani

Fedha za nje Fedha za ndani

Fedha za nje Fedha za ndani Fedha za nje

481,300,000 5,657,594,000 19,492,540 11,062,575,000 19,208,800 12,380,005,800 5,472,964,600 17,916,800,000

6,138,894,000 11,082,067,540 12,399,214,600 23,389,764,600

6.2 Mapato baada ya kuanzishwa Wakala

Baada ya kuundwa kwa TFS mali zote zilizokuwa zinamilikiwa na Idara ya Misitu na Nyuki zilimilikishwa kwa TFS hizi ni pamoja na: magari/mitambo, majengo yaliyopo Makao Makuu na vituo vya nje, samani pamoja na vifaa mbalimbali vya ofi si. Aidha Regista ya mali iliandaliwa ikiwa na takwimu zote zinazohitajika kwa ajili ya mchakato wa uhaulishaji. Aidha mali hizi zilikabidhiwa zikiwa ni chakavu. Vilevile Kwa mujibu wa Tangazo la uanzishwaji wa Wakala (Establishment Order), Wakala umepewa dhamana ya kusimamia misitu yote ya hifadhi ya taifa pamoja na kusimamia misitu iliyopo kwenye ardhi ya jumla.

Mahitaji ya rasilimali ya Wakala yanapatikana kutokana na ukusanyaji wa maduhuli ya mauzo ya mazao na huduma za misitu na nyuki. Wakala ni taasisi yenye mamlaka nusu (Semi autonomous) hivyo ina mamlaka ya kukusanya maduhuli na kutumia kulingana na Mpango wa Kibiashara (Business Plan). Wakala unatarajiwa kukidhi mahitaji yake kifedha kutokana na vyanzo vyake mbalimbali kama ifuatavyo;

a) Makusanyo ya maduhuli kutokana na rasilimali za misitu na nyuki (mashamba ya miti na misitu ya asili)

b) Fedha za miradi kutoka kwa Washiriki katika maendeleo.

Makusanyo ya maduhuli kwa miaka mitatu (2011/12-2013/14) yalikuwa TAS 199,771,416,440 ambayo ni asilimia 101(101%) ya matarajio (maoteo) ya makusanyo ya TAS 197,467,522,456. Mwenendo wa ukusanyaji wa maduhuli unaonesha kuwa ukasanyaji ulikuwa unaongezeka mwaka hadi mwaka (Jedwali 14). Mwaka 2010/11 Wakala ulikuwa kwenye hatua za awali za utekelezaji. Mafanikio haya ya ukusanyaji wa maduhuli yamechangiwa na hatua zilizofanywa za kuinua makusanyo kama zifuatazo:

i) Usimamizi madhubuti wa uvunaji kutoka mashamba ya miti ya kupandwa;

ii) Usimamizi madhubuti na hatua za kuimarisha usimamizi wa sheria katika misitu ya asili kwa ajili ya kupunguza uvujaji wa maduhuli kama vile: kuwa na mipango ya uvunaji; kuwezesha timu za doria; kufanya doria za mara kwa mara; kutoa vitendea kazi (magari, nyaraka za ukusanyaji), kuimarisha vituo vya ukaguzi; kuongeza uwezo wa wakusanyaji maduhuli.

iii) Kuimarisha udhibiti wa ndani kupitia uperembaji na kufanyia kazi taarifa za

Page 48: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

39

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ukaguzi wa ndani na maelekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG);

iv) Mauzo ya miti ya misaji kwa njia ya mnada na mikataba binafsi;

v) Kuajiri watumishi wengi wa Wakala na kuwapanga kwenye Kanda, Mashamba ya miti na wilayani kumeongeza uwezo wa kutekeleza Mpango wa Kibiashara na kupunguza mianya ya upotevu wa maduhuli. Mkazo ulikuwa kuimarisha doria na ukaguzi katika usafi rishaji na maeneo ya masoko;

vi) Mapitio ya Gazeti la Serikali Na. 432 la mwaka 2011 ya mirahaba na ada ya mazao ya misitu na huduma ilionyesha ongezeko kwa kiasi cha takribani asilimia 20 kulingana na utafi ti uliofanyika mwaka 2011. Utafi ti ulipendekeza kuwa mapitio ya mrahaba na ada za mazao ya misitu na huduma ufanyike kila baada ya mwaka au miaka miwili.

vii) Idadi ya vizuia vya ukaguzi wa mazao ya misitu imeongezeka na kuimarishwa. Jumla ya vizuia 49 vipya vimeanzishwa.

viii) Utoaji wa elimu ya uelewa juu ya taratibu za kisheria za uvunaji na biashara ya mazao ya misitu imeongezeka miongoni mwa wasimamizi wa sheria na wafanya biashara. Mikutano 300 imefanyika katika kutoa elimu.

ix) Kamati za uvunaji za wilaya zimeimarishwa na kupewa uwezo zaidi wa kuchambua na kutoa maamuzi.

x) Dhana ya uboreshaji huduma kwa mteja (services excellency) imeboreshwa kwa kutoa elimu zaidi kwa watumishi na wafanya biashara.

xi) Ushirikiano wa kiutendaji katika ukusanyaji mapato na Halmashauri za wilaya umeimarishwa.

xii) Mfumo wa kudhibiti uvunaji na usafi rishaji unaanza kutekelezwa (Log tracking system)

Kutokana na mwenendo wa ukusanyaji maduhuli wa miaka mitatu tumejifunza kuwa kuna fursa za Wakala kuweka mikakati endelevu ya mapato. Mikakati hii inajumuisha upanuzi wa mashamba ya miti; kuimarisha mifumo iliyopo na kuendeleza mifumo mipya ya kupunguza mianya ya upotevu wa maduhuli kama vile mfumo madhubuti wa kufuatilia maduhuli (tracking system); kuanzisha vyanzo vipya vya maduhuli kama kuuza hewa ukaa na malipo ya huduma za mifumo ikolojia (ecosystem services) na kuwekeza katika majengo ya Wakala.

7. RASILIMALI WATU

i) Wakala wa huduma za Misitu unatekeleza shughuli zake kwa kuajiri kada za wataalam mbalimbali ikiwemo kada za taaluma na vibarua. Lakini mara tu ulipoanzishwa kabla taratibu za ajira hazijakamilika Wakala uliazima watumishi kutoka Idara ya Misitu na Nyuki ambapo jumla ya watumishi 1,712 waliazimwa, kati yao 363 sawa na asilimia 21 ni wanawake na 1,349 sawa na asilimia 79 ni wanaume.

Page 49: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

40

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ii) Watumishi 1,483 walikuwa ni wataalam wa misitu na nyuki, 57 walikuwa wanasheria, maafi sa ugavi na maafi sa utumishi, na watumishi 172 wakiwa wa kada saidizi mbalimabli (Jedwali Na 16).

Jedwali Na 16: Rasilimali watu walioazimwa kutoka Idara ya Misitu

Kada ya rasilimali watu NambaWafanyakazi wa Misitu(i) Maafi sa Misitu Wakuu (I&II)

(ii) Maafi sa Misitu Waandamizi

(iii) Maafi sa Misitu (I&II)

(iv) Wasaidizi Misitu Wakuu

(v) Wasaidizi Misitu waandamizi

(vi) Wasaidizi Misitu (I&II)

(vii) Wasaidizi Misitu (Shughuli za utendaji)

1411921038817223206727

Maafi sa Nyuki(i) Msaidizi Nyuki

(ii) Msaidizi Nyuki Mkuu

(iii) Msaidizi nyuki (1)

(iv) Msaidizi Nyuki II

(v) Msaidizi Nyuki Mwandamizi

(vi) Afi sa Nyuki II

(vii) Afi sa Nyuki I

(viii) Afi sa Nyuki Mwandamizi

(ix) Afi sa Nyuki Mkuu(I & II)

7242912036243

Maafi sa wasaidizi 228(i) Maafi sa Rasilimali watu 1

(ii) Wanasheria II 1

(iii) Mchumi Mkuu 1

(iv) Afi sa Ugavi msaidizi 2(v) Afi sa ugavi daraja la II 4(vi) Afi sa ugavi Msaidizi daraja la II 2(vii) Afi sa ugavi Mwandamizi 3(viii) Mkaguzi wa ndani Mwandamizi 1(ix) Mhasibu msaidizi 9(x) Mhasibu daraja la II 5(xi) Mhasibu Msaidizi daraja la II 4(xii) Mhasibu daraja la 1 5

(xiii) Dereva Mitambo daraja la II 6

(xiv) Mwendesha Mitambo Msaidizi 1(xv) Dereva Daraja la II 39

Page 50: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

41

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

(xvi) Dereva daraja la I 10(xvii) Dereva Mwandamizi 5(xviii) Tabibu mwandamizi 9(xix) Tabibu msaidizi 6(xx) Muuguzi Msaidizi 1(xxi) Tabibu daraja la II 2(xxii) Tabibu Daraja la I 1(xxiii) Tabibu Mkuu 1(xxiv) Assistant Technician 1(xxv) Fundi Sanifu Msaidizi 2(xxvi) Fundi Sanifu II 7(xxvii) Fundi sanifu I 9(xxviii) Fundi sanifu Mwandamizi 3(xxix) Fundi sanifu mkuu 1(xxx) Mlinzi II 12(xxxi) Mlinzi Mwandamizi 2(xxxii) Mlinzi Mkuu 20(xxxiii) Mapokezi II 19(xxxiv) Msaidizi Ofi si Mkuu 1(xxxv) Msaidizi Kumbukumbu I 3(xxxvi) Msaidizi kumbukumbu

..........Mwandamizi2

(xxxvii) Msaidizi kumbukumbu Mkuu II 1(xxxviii) Mtunza kumbukumbu Mkuu I 1(xxxix) Katibu Mahsusi II 17(xl) Katibu Muhtasi I 3

iii) Kwa sasa Wakala una watumishi 1,823, wakiwemo maafi sa nyuki, maafi sa Misitu, mafundi mchundo na kada nyingine saidizi kama maafi sa rasilimali watu, wanasheria, wachumi, Afi sa Habari,na wengineo. Wengi wa watumishi wa Wakala wanapatikana kwenye Mashamba na ofi si za kanda ambapo idadi kubwa ni Wasaidizi misitu na vibarua (kama inavyoonesha kwenye jedwali). Idadi ya Watumishi 1,712 ambayo Wakala iliazima toka Idara ya Misitu na nyuki inaonesha kuwa na tofauti ndogo kwa watumishi wa sasa (1,823); hii ni kwa sababu watumishi wengi walioazimwa wamestaafu au kufariki. Hata hivyo kuna upungufu wa watumishi ukizingatia kuwa Menejimenti ya misitu kitaalam unamtaka mtu kusimamia eneo lisilozidi hekta 5,000 lakini kwa sasa uwiano ni 1:20,000 hii inafanya upungufu wa wafanyakazi 2,077. Mahitaji halisi ya watumishi wa Wakala yameoneshwa katika Jedwali Na. 17

iv) Ili kuboresha utendaji Wakala unafanya uchambuzi wa kina utakaopelekea kuandaa Mpango wa mafunzo ya kuendeleza rasilimali watu. Aidha ufuatiliaji wa muundo wa Utumishi unaendelea kufanyika ili utumike kuongeza motisha kwa wafanyakazi.

Page 51: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

42

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na.17: Mahitaji halisi ya Rasilimali ya Wakala

Kada ya rasilimali watu Waliopo Mahitajii) Mtendaji Mkuu 1 0ii) Wakurugenzi 3 0iii) Wakuu wa Vitengo 4 0iv) Meneja Wa Kanda 7 0

Wafanyakazi wa Misitui) Maafi sa Misitu Wakuu (I&II)

ii) Maafi sa Misitu Waandamizi

iii) Maafi sa Misitu (I&II)

iv) Wasaidizi Misitu Wakuu

v) Wasaidizi Misitu waandamizi

vi) Wasaidizi Misitu (I&II)

vii) Wasaidizi Misitu (Shughuli za utendaji)

1498425016215324392675

2875125119648270160868675

Maafi sa Nyukii) Maafi sa Nyuki Wakuu

ii) Maafi sa Nyuki waandamizi

iii) Maafi sa Nyuki

iv) Wasaidizi Nyuki Wakuu

v) Wasaidizi Nyuki Waandamizi

vi) Wasaidizi wa Nyuki (I &II)

vii) Wasaidizi wa Nyuki (Shughuli za utendaji)

12755251933238

7274657207393830238

Maafi sa wasaidizi 198 298i) Maafi sa Rasilimali watu 5 11

ii) Wanasheria II 2 3

iii) Mwanasheria Mkuu 1 1iv) Mchumi Mkuu 1 2v) Mtunza kumbukumbu Msaidizi 19 21vi) Wasaidizi waofi si 12 18vii) Katibu Muhtasi/Wahudumu 22 25viii) Mafundi 17 22ix) Madereva 38 47x) Waendesha mashamba 6 9xi) Walinzi 23 26xii) Wahasibu 41 60xiii) Maafi sa ugavi 9 28xiv) Wakaguzi wa Ndani 2 6xv) Wataalam wa Tiba 17 20

Page 52: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

43

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

8. MAPATO NA MATUMIZI YA WAKALA

Wakala unakusanya wastani wa TAS 66 bilioni kwa mwaka tangu kuanzishwa kwake. Kwa sasa ukusanyaji mapato ni asilimia 100 au zaidi kidogo ukilinganisha na maoteo. Kwa mfano ukusanyaji wa mapato baada ya kuanzishwa kwa Wakala kwa kipindi cha miaka mitatu (2011/2012 hadi 2013/2014) ulikuwa ni asilimia 101 (101%). Katika kipindi cha miaka mitatu maoteo ya ukusanyaji mapato yalikuwa ni TAS 197,467,522,456, wakati kiasi halisi kilichokusanywa kilikuwa ni TAS 199,771,416,440 (Jedwali Na 18).

Jedwali Na18: Mwenendo wa mapato na Maoteo 2011/2012 hadi 2013/2015

Mwaka Maoteo (TAS) Ukusanyaji Halisi (TAS)

2011/12 54,156,888,816 63,752,485,873

2012/13 75,137,556,879 62,959,638,116

2013/14 68,173,076,760 73,059,292,451

2014/15 74,435,881,000 85,475,760,582

2015/16 80,299,745,000

Mafanikio ya ukusanyaji wa maduhuli yamewezesha Wakala kusimamia na kuendeleza shughuli zake kama zilivyoainishwa kwenye Mipango ya Kibiashara na Wakala umeweza kukidhi matakwa ya kupeleka fedha Hazina. Aidha, Wakala unakusanya maduhuli kwa Serikali za Mitaa kama CESS (5%) ya mrahaba wa mazao ya misitu), kukusanya Kodi ya Mapato (VAT) ya asilimia 18 ya mirahaba ya mazao ya misitu kutoka mashamba ya misitu inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Wakala unakusanya maduhuli ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) kulingana na Sheria ya Misitu Cap. 323; na makusanyo ya asilimia 3 ya mrahaba ya mazao ya misitu, asilimia 2 ya ada na asilimia 100 ya makusanyo ya mauzo ya mazao yaliyotaifi shwa na faini. Mapato yaliyopelekwa na Wakala katika mamlaka husika kama vile Hazina, Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Halmashauri za Wilaya (CESS) na TRA (VAT) ni kama inavyooneshwa katika (Jedwali Na.19). Mapato ya TRA yalitokana na mauzo ya miti ya kupandwa kutoka kwa wateja wa Wakala. Jumla ya fedha TAS 108,740,000,000 zilipelekwa kwa mamlaka husika.

Page 53: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

44

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na 19: Mgawanyo wa mapato ya Wakala (TFS)

Mwaka Hazina (TAS Bill) TaFF(TAS Bill) CESS(TZS Bill) VAT(TAS Bill) JUMLA (TAS Bill)

2011/12 31, 007 3,340 660 4,120 39,190

2012/13 20, 450 3,190 870 4,970 29,490

2013/14 30, 000 2,690 700 6,680 40,070

Total 81,530 9,220 2,220 15,770 108,740

8.1 Vyanzo vya mapato ya Wakala kulingana na kasma /vifungu

Vyanzo vya mapato vya Wakala vimeongezeka na kuimarishwa. Vyanzo hivyo ni pamoja na mauzo ya miti ya kupandwa kutoka katika mashamba ya Wakala, ushuru wa miti ya asili inayovunwa kwenye maeneo yaliyotengwa kwa uvunaji, ushuru wa mkaa, ushuru wa mirunda (poles), ushuru wa mitambo ya mawasiliano inayowekwa kwenye misitu, ushuru wa uchimbaji madini ndani ya hifadhi, ushuru wa hati za usajili kwa wafanya biashara, ushuru wa hati za kusafi rishia mazao ya misitu, faini zitokanazo na makosa mbalimbali, mauzo ya mazao ya misitu yaliyotaifi shwa, mauzo ya vifaa vya stoo visivyotumika, ushuru wa biashara ya asali na mauzo ya asali, ushuru wa utalii ikolojia ndani ya hifadhi, ushuru wa utafi ti ndani ya hifadhi za misitu, ushuru wa kambi za utalii, na ushuru wa mazao ya misitu yanayosafi rishwa nje ya nchi. Jedwali Na.20 linaelezea mwenendo wa mapato na vyanzo vyake.

Jedwali Na.20: Vyanzo vya Mapato ya Wakala (2011/2012 hadi 2013/2014)

MWENENDO WA MAPATO NA VYANZO VYAKE (TSH)Namba ya

Kifungu

Chanzo cha mapato

(zao/huduma)2011/2012 2012/2013 2013/2014 TOTAL

110620

Ushuru wa hati za

kusafi rishia mazao ya

misitu

313,324,005 621,284,814 522,553,924 1,457,162,743

140112Ushuru wa mitambo ya

mawasiliano 0 18,885,000 14,000,000 32,885,000

140354 Mrahaba 45,719,098,965 39,648,773,868 46,853,491,332 132,221,364,165

140313Ushuru wa hati za

usajili811,004,567 1,525,584,438 5,496,468,022 7,833,057,027

140,340Faini zitokanazo na

makosa mbalimbali95,905,585 1,221,899,993 747,786,616 2,065,592,194

140347ushuru wa uchimbaji

madini ndani ya hifadhi0 11,748,000

2,108,000

11,748,000

140,261Ushuru wa biashara ya

asali na nta6,907,200 7,180,060 21,162,616 35,249,876

140357 Mauzo ya mazao ya

misitu yaliyotaifi shwa,  21,888,954 374,894,437 396,783,391

140365Mauzo ya vifaa vya stoo

visivyotumika0 4,355,750 58,000 4,413,750

140345 Ushuru wa mazao ya

misitu yanayosafi rishwa  320,209,965 3,130,674 323,340,639

Page 54: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

45

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

140344 Ushuru wa kuingia hifadhi asilia   21,375,690 4,164,800 25,540,490

140346Ushuru wa kupiga kambi ndani ya hifadhi asilia

  101,493,765 3,130,674 104,624,439

140370 Ushuru wa pesa ya serikali iliyookolewa     100,000 100,000

140283 Ushuru wa mauzo ya vitabu vya zabuni   1,250,000 3,700,000 4,950,000

140343 Ushuru wa utafi ti ndani

ya hifadhi    39,807,460 39,807,460

140368 Ushuru wa mapato yasiyo na kasma 2,292,399,589 602,847,082 3,648,215,679 6,543,462,350

  Nyaraka zisizowasilishwa   3,205,539,771   3,205,539,771

 Upcountry Collection

Accounts untransfered  704,122,500   704,122,500

 JUMLA NDOGO ya

mapato ya TFS49,238,639,911 48,038,439,649 57,734,772,234 155,009,743,795

  LMDA 11,174,962,860 11,732,889,363 12,636,282,939 35,544,135,162

 Mfuko wa Misitu

Tanzania (TaFF)3,338,883,101 3,188,309,104 2,690,345,278 9,217,537,483

  JUMLA NDOGO 14,513,845,962 14,921,198,467 15,326,628,216 44,761,672,645

  JUMLA KUU 63,752,485,873 62,959,638,116 73,061,400,451 199,771,416,440

Vilevile Wakala uliwezesha sekta ndogo ya ufugaji nyuki katika kuzalisha mazao ya nyuki, ambapo tani 1,605 za nta zilizalishwa zikiwa na thamani ya Tsh. 10,644,056,759, na tani 728 za asali zenye thamani ta Tsh. 2,753,284,771 zilizalishwa (Jedwali Na. 21). Hivyo sekta ndogo ya ufugaji nyuki iliweza kuchangia katika pato la taifa na kupunguza umaskini.

Jedwali Na. 21: Takwimu za mazao ya nyuki (Asali na Nta) yanayosafi rishwa nje ya Nchi

  Nta Asali

Mwaka Tani Th amani (Tsh) Th amani (USD)

Tani Th amani (Tsh) Th amani (USD)

2010/2011 534 3,898,239,826 2,598,826 343 1,034,000,369 646,250

2011/2012 418 3,908,518,470 2,473,461 209 967,351,780 644,253

2012/2013 241 2,050,210,503 1,520,560 93 670,754,700 406,518

2013/14 412 787,087,960 4,657,284 83 81,177,922 109,350

Total 1,605 10,644,056,759 11,250,131 728 2,753,284,771 1,806,371

Chanzo: Taarifa za mwaka za utekelezaji za TFS

8.2 Mwenendo wa matumizi kabla ya Wakala

Kabla ya kuanzishwa Wakala (TFS), bajeti ya Idara ya Misitu ilikuwa ni ndogo kuweza kutekeleza mipango kazi ya Idara. Kiasi cha fedha kilichokuwa kikitolewa kwa mwaka katika kutekeleza majukumu ya Idara ilikuwa ni wastani wa shilingi wa bilioni nne (4 bilioni) kwa mwaka.

Page 55: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

46

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

8.3 Mwenendo wa matumizi baada ya kuanzishwa Wakala

Mojawapo ya majukumu ya Mtendaji Mkuu ni kusimamia ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za Wakala kulingana na Mipango Mkakati na Mipango ya Kibiashara ya Wakala iliyoidhinishwa. Vilevile Katibu Mkuu wa Wizara anawajibika kutoa maelekezo na ushauri kwa Mtendaji Mkuu juu ya uendeshaji wa kazi za Wakala ikiwemo mapato na matumizi ya fedha za Wakala. Katibu Mkuu hufanya mapitio ya malengo ya Wakala na kuyaridhia kama yanawiana na utekelezaji wa mpango mkakati, mipango ya kibiashara, mipango kazi na bajeti. Kwa kipindi cha miaka mitatu Wakala umeweza kutengeneza Mipango Mkakati (Strategic Plans), Mipango ya Kibiashara (Business Plans) ya kila mwaka pamoja na Mipango Kazi.

Mwenendo wa matumizi unafafanuliwa vizuri kwenye Mipango ya Kibiashara na Mipango Kazi ya Wakala. Tangu Wakala uzinduliwe umeshaandaa Mipango Mkakati miwili (Julai 2010– Juni 2013 na 2014/2015–2018/2019) (Rejea Mipango Mkakati). Bajeti ya utekelezaji wa kazi imeongezeka. Kwa wastani kwa mwaka, kiasi cha shilingi bilioni 30 zimekuwa zikitumika kutekeleza kazi za Wakala. Jedwali (Na 22) linaonesha mwenendo wa matumizi ya Wakala katika utekelezaji wa kazi zake kwa kipindi cha miaka mitatu (2011/2012-2013/2014). Fedha zote za matumizi ya Wakala, zimetokana na makusanyo ya ndani ya Wakala. Bajeti ya Wakala ni ya kujitegemea, na hakuna mhisani aliyechangia bajeti hiyo. Bajeti kwa kipindi hicho cha miaka mitatu ilikuwa ni shilingi (TAS) 119,171,737,372, na matumizi halisi yalikuwa ni shilingi (TAS) 100,308,344,935 sawa na asilimia 84.17 (84%). Hata hivyo, iwapo Wakala ungepata vitendea kazi na nguvu kazi kwa wakati, mafanikio yangekuwa zaidi ya asilimia 84.

Jedwali Na 22: Muhtasari wa matumizi ya Wakala kwa kila lengo la kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 hadi 2013/2014

Objective / Target 2011/2012 2012/2013 2013/2014 Total

OBJECTIVE A: HIV/AIDS infections reduced and supportive services to people living with HIV/AIDS improved;

 

Target 01: Supportive services

established and operating by June

2013

24,150,000 153,894,500 191,981,500 370,026,000

TOTAL OBJECTIVE A 24,150,000 153,894,500 191,981,500 370,026,000

OBJECTIVE B: Sustainable supply of quality forest and bee products enhanced

TARGET 01: 1.36 million ha of

production forest reserves (natural

and plantation) managed based on

management plans by June 2013;

15,093,704,104 7,812,884,592 7,185,342,462 30,091,931,158

Target 02: 50,000 ha of new

forest plantations and 26,083 ha

of bee reserves gazetted by June

2013.

60,705,500 589,896,612 9,679,633,798 10,330,235,910

Target 03: Beekeeping

Improvement Programme

implemented in 30 districts and

4 demonstration centres by June

2013.

568,416,042 587,515,619 375,300,714 1,531,232,375

Page 56: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

47

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Target 04: Compliance to

regulations, operations and

quality standards of forest and bee

products and services attained at

50% by June 2013.

183,104,096 2,690,438,076 5,552,341,699 8,425,883,871

TOTAL OBJECTIVE B 15,905,929,742 11,680,734,899 22,792,618,673 50,379,283,314

OBJECTIVE C: Stable ecosystem and biological diversity maintained

Target 01: 1.8 million ha of

protection forests assessed and

managed by June 2013. 1,553,618,261 3,266,072,540 2,774,074,956 7,593,765,757

Target 02: Area under PFM

increased from 4.1 million to 4.5

million ha by June 2013. 54,945,500 413,978,355 161,509,342 630,433,197

Target 03: Wood fuel Action Plan

implemented by June 2013.  51,965,200 59,129,500 111,094,700

TOTAL OBJECTIVE C 1,608,563,761 3,732,016,095 2,994,713,798 8,335,293,654

OBJECTIVE D: Institutional capacity to deliver services strengthened

Target 01: Revenue accrued from

Forest and beekeeping resources

increased from TZS. 33 to TZS.

35 billion by June 2013.

1,681,145,770 1,048,645,134 807,602,608 3,537,393,512

Target 02: TFS Human resource

capacity developed by June 2013 101,894,523 1,182,287,888 1,342,764,737 2,626,947,148

Target 03: Level of provision of

requisite working facilities and

utilities, statutory rights and

administrative operations attained

60% by 2013.

1,735,302,853 10,803,218,495 16,120,217,521 28,658,738,869

Target 04: Physical infrastructure

and service provision maintained

and increased by 30% by June

2013.

1,138,661,569 1,738,936,533 2,877,598,102

Target 05: Monitoring and

evaluation system developed and

implemented by June 2013. 364,346,535 1,048,834,810 1,788,485,491 3,201,666,836

TOTAL OBJECTIVE D 3,882,689,681 15,221,647,896 21,798,006,890

40,902,344,467

OBJECTIVE E: Good governance and gender balance enhanced.

Target 01: Good governance and

National Anticorruption Strategy

Action Plan implemented by

2013.

84,050,000 113,522,880 123,824,620 321,397,500

TOTAL OBJECTIVE E 84,050,000 113,522,880 123,824,620 321,397,500

GRAND TOTAL 21,505,383,184 30,901,816,270 47,901,145,481 100,308,344,935

Page 57: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

48

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

9. UTOAJI WA TAARIFA ZA FEDHA

Mtendaji Mkuu ambaye ni Afi sa Masuhuli wa Wakala, ndiye mwenye jukumu la kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Wakala. Bodi ya Ushauri ya Wizara hupitia, kushauri na kuidhinisha Mpango Mkakati na Mipango ya Kibiashara ya Wakala pamoja na taarifa za ukusanyaji wa mapato na utekelezaji kazi. Taarifa ya mapato na matumizi ya fedha hutolewa kwa mujibu wa kanuni/taratibu za fedha za Wakala (the Agency’s Financial Regulations and Accounting Manual) pamoja na Sheria ya Fedha (the Financial Act No. 6 of 2001 and its Regulations). Aidha, Mtendaji Mkuu anawajibika kusimamia na kutunza taarifa zote za kihasibu za Wakala kama zinavyoelekezwa na Wizara ya Fedha, pamoja na usimamizi wa rasilimali zote za Wakala ikiwemo rasilimali watu kwa mujibu wa miongozo kutoka Ofi si ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma (President’s Offi ce – Public Service Management (PO-PSM), pamoja na mapendekezo yaliyokubaliwa na Serikali kutoka Kamati za Bunge za Ukaguzi (the Public Accounts and other Parliamentary Committees). Bodi ya Ushauri kwa upande mwingine inahusika kupokea, kushauri na/au kupitisha taarifa ya mwaka ya fedha (Annual Financial Statements) na hatimaye Mtendaji Mkuu huiwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kupitia Katibu Mkuu. Vile vile Bodi imekuwa ikiwajibika kutoa ushauri kuhusu vipaumbele katika malengo ya kiutendaji ya mwaka wa fedha.

Aidha Mtendaji Mkuu huwasilisha taarifa za fedha kwa wakaguzi wa ndani wa Wizara kulingana na mwongozo wa usimamizi wa fedha za Wakala, na Wizara ya fedha (in accordance with the standards set by the Ministry of Finance, and TFS Accounting Manual). Mkaguzi wa Ndani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, anayo haki ya kupitia utendaji wa Wakala na kutoa ushauri huru kwa Katibu Mkuu. Hata hivyo Wakala una Mkaguzi wa ndani kulingana na Muundo wake wa kiutendaji ambaye hufanya ukaguzi na kuhakiki mapato ya Wakala na kumshauri Mtendaji Mkuu. Vilevile Wakala hufanyiwa ukaguzi wa nje (external audit), kila mwaka wa fedha. Katika kipindi cha 2011/12 na 2012/13 Wakala ulipata Hati safi ya usimamizi wa fedha. Aidha Wakala umekwisha andaa taarifa ya fedha kwa mwaka 2013/14 tayari kwa ukaguzi.

10. MIPANGO YA WAKALA

Mipango ya Wakala (TFS) inaratibiwa na Kurugenzi ya Mipango na Matumizi ya Rasilimali chini ya Mtendaji Mkuu. Mipango hii huandaliwa kwa njia ya ushirikishwaji kuanzia ngazi za chini katika vituo vya Kanda na Mashamba ya miti ya Wakala; kisha kuwasilishwa katika kikao cha pamoja chenye uwakilishi wa vituo na vitengo vyote vya Wakala na kuandaa kwa pamoja mpango mkubwa wa Wakala. Tofauti na Idara iliyokuwa ikitekeleza mipango mkakati iliyoandaliwa na Wizara; Wakala inaandaa mipango yake ambayo inaainisha mgawanyiko wa majukumu ya utendaji inayogusa vituo vyote. Mipango ya Wakala inayoandaliwa ili kufi kia dira na malengo ya Wakala ni; Mpango Mkakati ya miaka mitano, Mipango ya Kibiashara (Mipango kazi) ya kila mwaka na bajeti za Wakala. Mipango ya Kibiashara huainisha pia mipango ya ukusanyaji mapato, maoteo ya mapato na vyanzo vya mapato.

10.1 Mipango Mkakati ya Wakala

Wakala wa Huduma za Misitu umeshaandaa mipango mkakati miwili (2010/11 – 2013/14) na (2014/15-2018/2019) (Picha Na 19). Mpango Mkakati umeainisha Dira, Dhima,

Page 58: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

49

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Maadili Makuu, Malengo, Matokeo yanayotarajiwa, Mikakati ya utekelezaji wa malengo, Bajeti kwa kila lengo; na vigezo vya upimaji wa mafanikio kwa kila lengo; mpango kazi wa uperembaji na tathimini; tathimini ya masuala yenye kuathiri uwezo wa kiutendaji wa Wakala; pamoja na mtazamo wa kiona mbali kuhusu mazingira yanayoweza kuingilia ufanisi na utendaji wa Wakala.

Picha Na 19: Mpango Mkakati wa Kwanza na wa Pili wa Wakala

10.2 Mpango wa Kibiashara

Mpango wa Kibiashara (Picha Na 20) unaandaliwa kila mwaka ndani ya Mpango Mkakati husika. Mpango huo unaainisha kwa kina shughuli zote zinazopaswa kutekelezwa na Wakala wa Huduma za Misitu katika mwaka wa fedha husika. Mpango wa Kibiashara unazingatia yafuatayo:

(i) Dira, Dhima na Maadili makuu ya Wakala;

(ii) Mikakati ya usimamizi, zana za Wakala, wadau wakuu na matarajio yao kwa Wakala;

(iii) Malengo tarajiwa na mikakati ya kiutendaji kwa kila lengo kwa mwaka;

(iv) Bajeti, na maoteo ya mapato na matumizi;

(v) Kalenda ya kazi;

(vi) Tathimini ya maswala yaliyo nje ya uwezo wa Wakala ambayo yanaweza kuathiri utendaji wa Wakala katika kufi kia malengo, pamoja na mtazamo wa kiona mbali kuhusu mazingira yanayoweza kuingilia ufanisi na utendaji wa Wakala (assumptions); pamoja na

(vii) Mazingira ya utendaji na changamoto zake katika kufi kia matumizi yenye thamani sahihi ya fedha na ubora wa huduma na mazao ya miti/misitu na nyuki yenye viwango bora.

Page 59: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

50

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Picha Na. 20: Mipango ya Kibiashara ya Wakala ya 2012, 2013 na 2014

10.3 Utekelezaji wa Mipango

Utekelezaji wa mipango ya Wakala unafanyika mara baada ya Bodi kuidhinisha Mpango na hatimaye Bunge kupitia bajeti ya Wizara iliyojumuisha ya Wakala pia. Bajeti ya Wakala huzingatia kiwango cha makusanyo ya mapato. Taarifa za utekelezaji zinaandaliwa kwa vipindi vya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka kwa kila kituo, Kitengo au Sehemu kisha Wakala huandaa taarifa moja ya utekelezaji kwa kipindi husika. Mtendaji Mkuu amekasimiwa madaraka ya kufanya rejea ya kazi na bajeti (budget reallocation) kulingana na hitaji na umuhimu wa kazi itakayoleta ufanisi kwa Wakala. Mfano, vikao vya dharura vya Bodi ya Ushauri au hitaji la kufanya ziara katika vituo vya Wakala kutatua changamoto iliyojitokeza na/ au kushughulikia dharura iliyosababishwa na mioto au mafuriko.

10.4 Uwasilishaji wa Mipango na Taarifa

Mpango Mkakati na Mipango ya Kibiashara (Business plans) ya Mwaka zimekuwa zikiwasilishwa na Mtendaji Mkuu kwenye Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupata ridhaa ya Bodi ya matumizi ya bajeti iliyowasilishwa. Hali kadhalika taarifa za utendaji za kipindi cha Robo mwaka, nusu mwaka na mwaka zimewasilishwa kwa Bodi kwa ajili kuonyesha maendeleo ya utendaji na kupata ushauri wa kiutendaji na idhini ya kusambaza taarifa kwa wadau. Aidha, Mtendaji Mkuu amefanya (pale ilipobidi) mapitio ya Mpango Kazi wa Mwaka ndani ya mwaka wa utekelezaji kwa kuzingatia ushauri wa Bodi na/ au changamoto mbalimbali za kiutekelezaji, ikiwemo kukidhi mabadiliko mbalimbali ya Kisera na vipaumbele vya matumizi ya rasilimali. Kupitishwa kwa Mipango hii (Mpango Mkakati na Mpango Kazi) kumeiwezesha Wakala kufanya kazi kwa uhuru zaidi bila ya kuingiliwa na Wizara. Bodi ya Ushauri, kwa upande mwingine imeiwakilisha vyema Wakala kwa kuwasilisha taarifa za ushauri kwa Waziri wa Maliasili na Utalii zilizolenga katika kuibua masuala muhimu yenye changamoto za utendaji; na kutoa ushauri wa namna ya kutatua ili kuboresha ufanisi wa utendaji wa Wakala na kufi kia malengo tarajiwa. Vile vile, Bodi ilifanya tathmini ya Wakala (kama sehemu ya jukumu lake) baada ya kipindi cha miaka mitatu (2010/11 -2013/14) ya utendaji wa Wakala kupitia Mpango Mkakati wa awamu ya kwanza. Taarifa ya Tathmini iliwasilishwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Hitimisho la utekelezaji wa Mpango Mkakati wa awamu ya kwanza liliambatana na uandaaji wa taarifa ya utendaji ya miaka mitatu iliyoainisha mafanikio na changamoto dhidi ya malengo. Taarifa ya miaka mitatu iliwasilishwa kwenye

Page 60: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

51

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Bodi, kwa Mh. Waziri kupitia kwa Katibu Mkuu na watumishi (watekelezaji wa malengo) katika vituo vya Wakala. Aidha taarifa ya fedha za kila mwaka huwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kwa ukaguzi.

11. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA

Katika kipindi cha kuwepo kwa Wakala tangu kuanzishwa kwake kumekuwepo na changamoto mbalimbali, baadhi ya changamoto zimekuwa ndani ya uwezo wa Wakala na zingine zipo nje ya Wakala kuweza kukabiliana nazo. Changamoto mbalimbali na mikakati ya kukabiliana nazo ni kama zilivyoainishwa chini:

11.1 Changamoto za utekelezaji majukumu ya Wakala

Katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji, Wakala umekabiliwa na changamoto mbalimbali. Aidha, katika kipindi hiki Wakala umeweza kupanga mikakati mbalimbali ya kupambana na baadhi ya changamoto hizi, hususan zilizo ndani ya uwezo wa Wakala. Baadhi ya changamoto ni kama zifuatavyo:

i) Uvamizi wa maeneo ya misitu unaotokana na ongezeko la shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ufugaji, makazi, ukataji miti kwa ajili ya biashara na matumizi ya nyumbani na uchimbaji wa madini;

ii) Matukio ya Moto katika misitu kila mwaka. Moto umeendelea kuwa changamoto kubwa. Takwimu zinaonesha kuwa, takriban asilimia 10 -14 ya eneo la nchi linaathirika na mioto ambayo ni kama hekta milioni 11 kila mwaka. Matukio ya moto yanapungua kwenye maeneo ya Magharibi ya nchi lakini yanaongezeka Kusini mwa nchi;

iii) Sekta ya misitu kutokuwa kipaumbele katika mipango ya maendeleo taifa;

iv) Utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo kikuu cha nishati ambapo zaidi ya asilimia 90 ya nishati inatokana na miti na idadi kubwa ya watanzania kutegemea nishati ya kuni na mkaa;

v) Misitu kuwa chanzo rahisi cha kujipatia kipato kama vile kutengeneza mkaa, kupasua mbao, kukata nguzo na kadhalika;

vi) Uhaba wa watumishi walioajiriwa na Wakala ukilinganisha na eneo la misitu wanalolisimamia. Kitaalam, mtalaam mmoja anatakiwa kusimamia takriban eneo la hekta 5,000 za misitu hata hivyo mtaalam mmoja kwa sasa anawajibika kusimamia takriban zaidi ya hekta 20,000. Pamoja na uhaba wa wataalam, serikali haijaajiri watalaam wa misitu na nyuki kwa muda wa miaka mitatu (tangu 2010 hadi sasa);

vii) Kutokuwepo kwa uratibu wa matumizi bora ya ardhi baina ya sekta mbalimbali, kumechangia uvamizi na uharibifu wa misitu nchini.

viii) Mahitaji makubwa ya mazao ya misitu ndani na nje ya nchi, kumechochea uvunaji holela na vitendo vya upokeaji na utoaji rushwa katika mfumo mzima wa biashara ya mazao ya misitu.

Page 61: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

52

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

11.2 Changamoto zilizo nje ya Uwezo wa Wakala

Baadhi ya changamoto zinazoikabili Wakala zimo nje ya uwezo wa Wakala kukabiliana nazo kimikakati, changamoto hizi kama zinavyoainishwa hapa chini ni pamoja na Kuchelewa kwa muundo wa Kiutumishi wa Wakala (Scheme of Services), Kuchelewa kwa mapitio na uhuishwaji wa sheria ya misitu ya mwaka 2012 ili ikidhi mahitaji ya Wakala kimuundo na kiutendaji na kuchelewa kwa upatikanaji wa vifaa kulingana na Kanuni za Manunuzi.

11.2.1 Kucheleshwa kuhuishwa kwa Muundo wa Wakala wa Huduma za Misitu

Wakala unahitaji muundo maalum wa kiutumishi (Scheme of Service) kwa ajili ya kuleta ufanisi na tija katika shughuli zake za kiutendaji. Muundo huo ni muhimu katika kuboresha maslahi ya watumishi wa Wakala. Muundo umekwisha andaliwa, na kuwasilishwa Ofi si ya Rais, Menejiment ya Utumishi ila haujapata idhini. Mchakato wa kuridhia muundo ikiwa ni pamoja na ajira husika umechukua muda mrefu. Kuchelewa kuhuishwa kwa Muundo huo kumeathiri ujazaji wa nafasi zinazopatikana kwa ushindani. Changamoto hii iliathiri pia mchakato wa kuanzisha Wakala hii ambao ulichukua takriban miaka kumi.

11.2.2 Kuchelewa kwa kuhuishwa kwa Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002

Wakala unahitaji muundo maalum wa kiutendaji kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake za kila siku kwa mujibu wa Tangazo la uanzishwaji wa Wakala (Establishment Order). Sheria ya Misitu ya Mwaka 2002 inahitaji kufanyiwa marekebisho ya baadhi ya tafsiri na maelekezo ili kumpa Mtendaji Mkuu wa Wakala mamlaka ya kitafsiri na kiutekelezaji kwa mujibu wa hati ya uanzishwaji (Establishment Order). Mfano, Mtendaji Mkuu wa Wakala hatajwi na Sheria ya Misitu katika usimamizi (enforcement) wa sheria ya misitu, hii inamnyima mamlaka ya kisheria na kuleta migongano ya tafsiri mbalimbali za kiutekelezaji.

11.2.3 Kuchelewa kukamilisha manunuzi

Utekelezaji wa sheria na kanuni za manunuzi ya Umma zenye mlolongo mrefu husababisha ucheleweshaji wa upatikanaji wa vifaa, magari, mitambo, majengo na shughuli mbalimbali zinazohusu ushauri wa kitalaamu (consultancy services).

12. MIPANGO YA BAADAYE YA WAKALA

Wakala wa Huduma za Misitu unatarajia kuwa kitovu cha uhifadhi uliotukuka na upatikanaji endelevu wa mazao na huduma za misitu na nyuki Tanzania kwa kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki kwa ajili ya kuchangia mahitaji ya kijamii, kiuchumi, ki-ikolojia na kiutamaduni kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Ili kufi kia lengo hili kuu Wakala unakusudia kuendelea kuandaa mipango mkakati ya awamu za miaka mitano ambayo itafanyiwa tathmini za nusu kipindi na mwisho wa awamu na kuboresha mazingira ya utendaji kulingana na maoni/ushauri wa tathmini. Malengo ya Mpango Mkakati yatatekelezwa kupitia Mipango ya Kibiashara (mipango kazi) ya kila mwaka kwa kuzingatia yafuatayo:

i) Kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao ya miti kwa kuanzisha mashamba mapya na kuongeza kasi ya upandaji miti katika maeneo mapya kila mwaka ili kukidhi mahitaji ya mazao ya miti; kushirikisha wadau wengine kama taasisi zinazojitegemea katika kuongeza mashamba ya miti; na Kuhamasisha wadau katika matumizi ya teknolojia ya kisasa;

Page 62: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

53

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

ii) Kuongeza pato la Wakala kwa kuandaa mpango wa uwekezaji ifi kapo 2015/16 ambao utajumuisha ukuzaji na uboreshaji wa utalii ikolojia kwa kutunza na kuboresha bio-anuai na mifumo ikolojia iliyo imara na vivutio vilivyopo; na kujenga majengo ya kupangisha kama vitega uchumi;

iii) Kuendelea kuimarisha uwezo wa kitaasisi wa kutoa huduma zilizo bora kwa kuongeza usimamizi wa fedha kibiashara (commercial style accrual accounting), Kuajiri watumishi kulingana na mahitaji na kuwapatia watumishi mafunzo, kuboresha maslahi, vitendea kazi na kuimarisha utawala bora na usawa wa jinsia.

iv) Kuboresha ukusanyaji maduhuli kwa: mifumo ya ukusanyaji na matumizi ya fedha itaanzishwa na kuimarishwa, kama vile kadi nadhifu (smart card); integrated fi nancial management system), kupanga na kudhibiti tozo kulingana na nguvu ya soko; Kuwapatia motisha na vitendea kazi watumishi wanaokusanya maduhuli; kuingia mikataba na wadau kusaidia katika ukusanyaji mapato; na Kubainisha vyanzo vipya vya mapato;

v) Kuboresha huduma kwa waishio na virusi vya ukimwi (HIV/AIDS) na kuhakikisha maambukizi ya virusi yanapunguzwa;

vi) Wakala unatarajia kuanza mchakato wa kuwa mamlaka ifi kapo 2016/17 na juhudi zimeanza kwa kuandaa andiko la kusudio (concept note) litakalowasilishwa ngazi mbalimbali kabla ya andiko kamili;

vii) Wakala unakusudia kujenga Ofi si mpya na wakati wa mchakato wa ujenzi Wakala unatarajia kutafuta eneo la kupanga katika kipindi cha 2015/16. Hii itaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa Wakala na ufanisi katika utoaji wa huduma; pamoja na;

viii) Kuongeza huduma na uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa: Kuanzisha na kuendeleza mashamba (manzuki) na hifadhi za nyuki, kuzalisha malkia wa nyuki ili kuboresha upatikanaji wa makundi ya nyuki na ujenzi wa vituo vya kulea malkia; Kuimarisha viwanda, Kuhamasisha matumizi ya vifaa sahihi vya ufugaji nyuki na Kuanzisha na kuendeleza mashamba darasa kwa ajili ya kuelimisha jamii.

ix) Kukuza ushirikishwaji wa wadau wa hifadhi na usimamizi wa misitu ikiwa ni pamoja na kupunguza tofauti za mamlaka mbalimbali zinazokinzana na uhifadhi.

13. MIKAKATI ENDELEVU YA KUJITEGEMEA

Wakala umejipanga kimkakati kuhakikisha inajitegemea na kupunguza utegemezi kwa Serikali Kuu. Miongoni mwa mikakati hiyo ni;

(a) Kupanua na/au kuanzisha mashamba ya miti ya kupandwa mapya

Mashamba ya miti yaliyopo yatapanuliwa kwa hekta zipatazo 63,583.56 Ha. Mashamba hayo ni: Saohill (33,933 Ha), Kilimanjaro Magharibi (188 Ha), Buhindi (6,787 Ha), Ukaguru (1,181 Ha), Rubare (2,223 Ha), Kawetire (1,577.1 Ha) na Kilimanjaro Kaskazini-Rongai (1,387.2 Ha).

Page 63: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

54

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Pia kuanzisha/kuendeleza mashamba mapya manne (4) ya miti yenye jumla ya hekta 52,805 kwa ajili ya uzalishaji wa miti ya magogo (mbao) na nishati (kuni na mkaa). Mashamba hayo mapya ni:

i) Wino-ifi nga (10,000 Ha)

ii) Mbizi (12,000 Ha)

iii) Korogwe (10,805 Ha)

iv) North Ruvu (20,000 Ha)

Vilevile Wakala unakusudia kuyabadilisha maeneo yaliyoharibika na kuwa mashamba ya miti kuanzia mwaka wa fedha ujao wa 2015/2016. Maeneo hayo ni msitu wa nishati wa Morogoro (Morogoro/Mvomero)((Ha. 12,950), Msitu wa hifadhi wa Liwilikitesa (Mbinga) (Ha. 375), Msitu wa Hifadhi Ziwani (Mtwara Vijijini) (Ha 689) na msitu wa hifadhi wa Masasi hills (Masasi) (Ha 233).

(b) Uzalishaji wa miti bora

Wakala pia umejizatiti katika uzalishaji wa mazao bora ya miti kwenye mashamba mapya yenye mchanganyiko wa miti laini, miti migumu, miti ya mianzi na miti inayotoa malighafi ya tetefya (plywood) kwa muda mfupi. Uzalishaji wa miti inayokua kwa muda mfupi utapanua wigo wa upatikanaji wa malighafi na kuziba pengo la utegemezi wa mbao za miti inayochukua muda mrefu, hali inayoongeza gharama kubwa za uzalishaji. Aidha wawekezaji wameshajitokeza tayari hivyo Wakala utatumia fursa hiyo muhimu. Wakala pia umeanzisha shamba la mianzi la majaribio lenye hekta 6 katika msitu wa Ruvu Kaskazini. Wakala umekuwa ukiagiza mbegu bora za pine kutoka Zimbabwe kupitia Wakala wa mbegu za miti kwa mashamba yake 16. Ukuaji wa miche ya mbegu kutoka Zimbabwe umekuwa ni mara dufu ukilinganisha na miche ya Tanzania. Vilevile Wakala kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafi ti wa Misitu (TAFORI), umeanzisha mpango wa kupanda miti ya mikaratusi kwa kutumia vinasaba vilivyoboreshwa (genetic improvement). Jumla ya mashamba 3 yamefanyiwa majaribio ya upandaji miti ya vinasaba vilivyoboreshwa. Wakala unaweka mkazo katika kuhudumia mashamba yake yote ya miti (kwa kufuata vizuri ratiba ya upogoaji matawi na upunguzaji miti) ili kupata mazao yaliyo bora na kukidhi viwango bora vya kimataifa katika uzalishaji wa miti ya magogo.

(c) Uanzishaji/uendelezaji wa manzuki

Wakala umeanzisha manzuki/mashamba, hifadhi za nyuki na vituo vya uzalishaji malkia wa nyuki kwa ajili ya kuongeza mapato ya wakala na kuisaidia jamii katika kujiongezea kipato na kupunguza umaskini. Jumla ya hekta 69,613 ambazo aidha zimetambuliwa, kupimwa, kuchorewa ramani na/au kupitishwa na mamlaka husika za vijiji na Wilaya zitaendelezwa na kusajiliwa kisheria na kusimamiwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa zaidi ya asilimia 50 hivyo kuongeza pato la mwananchi na Taifa kwa ujumla. Wakala unatarajia kuwa na manzuki katika mashamba ya miti yote 18.

Page 64: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

55

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Wakala umeanzisha vituo vitatu vya kuzalishia malkia wa nyuki. Mafunzo zaidi yatatolewa kwa watumishi na juhudi za kuzalisha malkia wa nyuki zitaendelezwa ili kukuza uwezo wa mazao yatokanayo na nyuki

(d) Uendelezaji na uboreshaji wa misitu ya asili

Wakala utaendelea kutoa kipaumbele katika uhifadhi wa misitu ya asili ipatayo 445 ikiwa ni pamoja na misitu ya mazingira ya asilia (nature reserves) ambayo ipo katika hadhi ya juu ya uhifadhi. Pia Wakala utaboresha uongoaji wa maeneo ya hifadhi yaliyoharibika ili kupandisha hadhi ya uhifadhi ya misitu hiyo.

(e) Mikakati ya Uwekezaji

Sera ya uwekezaji (Investment Policy) ya Wakala inaandaliwa ili kuweza kupanua wigo wa uwekezaji kwa kushirikiana na mashirika ya ndani na nje ya nchi katika kujenga uwezo wa Wakala kutekeleza kazi zake kuepuka utegemezi. Lengo la Sera hii ni kuhakikisha kunakuwepo na uwekezaji utakaoleta matokeo ya vipindi vya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Sera ya uwekezaji inatarajia kukamilika mwaka huu wa fedha 2014/2015. Sera ya uwekezaji ya Wakala itatoa fursa ya kuandaliwa kwa Mpango wa uwekezaji mwaka 2015/16 ambao tayari umeainisha maeneo tarajiwa kama ifuatavyo:

(f ) Utalii ikolojia wa Hifadhi asili (nature reserves)

Hifadhi asilia 11 zilizo chini ya wakala zimeendelea kuimarishwa ili kukuza utalii ikolojia na kuongeza mapato ya Wakala na jamii inayozunguka hifadhi hizo. Hifadhi hizi zinazo rasilimali nyingi za vivutio kama vile mimea na wanyama zaidi ya makabila 200; na viumbe (wanyama na mimea) ndwele na adimu duniani. Wapo wanyama ndwele wapatao 159 na walio hatarini kutoweka ni 21; wakati mimea ndwele ni 36. Jedwali Na 23 linaonesha fursa zilizopo za kukuza utalii ikolojia katika hifadhi asilia (nature reserves).

Page 65: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

56

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Jedwali Na 23: Fursa za kukuza utalii ikolojia katika hifadhi asilia

NaHifadhi asilia

Eneo la Uwekezaji

FursaMaboresho yanayohitajika

1 Amani

Utalii

ikolojia

-Uwepo wa bioanuwai na

viumbe adimu na ndwele

- Hosteli

-Maeneo ya kambi za

kupumzikia

-Maeneo ya picnic

-View points

-Huduma za malazi na

chakula

-Ukarabati na uboreshwaji

wa hosteli

-Ukarabati wa kituo cha

habari (information centre)

2 Nilo

Utalii

ikolojia

-Uwepo wa bioanuwai na

viumbe adimu na ndwele

-Maeneo ya kambi za

kupumzikia

-Maeneo ya picnic

-View points

-Maporomoko ya maji

-Hosteli

-Kuongeza waongoza

watalii

3 Uluguru

-Utalii

ikolojia

-Hiking

-Maporomoko ya maji

-Vinyonga wenye pembe 2

-Mimea adimu takribani

135

-Ndege na vipepeo wa aina

mbalimbali

-Huduma za malazi na

chakula

-Ujenzi wa kituo cha habari

(information centre

- Kuajiri waongoza watalii

4 Chome

-Utalii

ikolojia

-Utalii wa

kupanda

mlima

-Uwepo wa bioanuwai za

mimea na wanyama (ndege

adimu)

-Maeneo ya kambi

-Chemichemi za maji

- View points

- Kuajiri waongoza watalii

-Uboreshaji wa kituo cha

habari (information centre

5 Magamba

-Utalii

ikolojia

-Hiking

- Uwepo wa bioanuwai za

mimea na wanyama (ndege

wa kuvutia na mimea aina

mbalimbali

- Chemichemi za maji

-Uboreshaji wa barabara za

utalii,

-view points

-Information centre

i) Utalii Rufi ji Delta

Eneo hili lina kivutio kizuri cha mazalia ya samaki (kamba), utalii wa boti na uwepo wa visiwa 11 vyenye mandhari ya kuvutia. Wakala utaendeleza

Page 66: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

57

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

Picha Na. 21: Mti aina ya Mvule uliopo katika Msitu wa Hifadhi wa Rau, Moshi-Kilimanjaro

utalii ikolojia wa misitu ya mikoko kwa kuimarisha miundombinu ya Rufi ji –Delta ili kuongeza mapato ya Wakala na jamii inayozunguka Rufi ji Delta.

ii) Utalii katika Mlima Hanang –Mkoa wa Manyara

Mlima Hanang ni mojawapo ya maeneo mazuri ya kukuza utalii ikilojia kupitia vivutio vilivyopo. Upo utalii wa kupanda mlima; maeneo mazuri ya kuona maeneo mbalimbali (view points) kama mji wa Hanang, Kondoa na Babati. Zipo njia za asili na vyanzo vya maji. Wakala unakusudia kuendeleza utalii ikolojia ili kuboresha mapato na ajira kwa wananchi wa eneo hilo.

iii) Eneo la mapumziko Msitu wa Rau (Recretional area)

Msitu wa hifadhi wa Rau uliopo karibu na mji wa Moshi unayo mandhari nzuri na sifa ya utalii wa kiikolojia. Wakala umeweka mpango maalumu wa kukuza utalii katika msitu huu, hivyo kuongeza mapato ya Wakala. Upekee wa Msitu huu unachangiwa na kuwepo kwa mti aina ya mvule wenye umri zaidi ya miaka 180, urefu wa mita 51 na kipenyo cha mita tatu (Picha Na. 21). Mti huu umekuwa kivutio kikubwa kwa watalii, watafi ti, wanafunzi ndani na nje ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Page 67: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

58

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

iv) Eneo la utalii ikolojia msitu wa Kimboza

Wakala unakusudia kuendeleza vivutio vilivyopo katika msitu wa hifadhi wa Kimboza uliopo wilaya ya Morogoro vijijini. Vivutio vilivyopo katika msitu huu ni pamoja na vipepeo wa aina mbalimbali, bwawa la asili na pango lenye historia ya kiutamaduni wa eneo hilo. Wakala utaboresha utalii wa kiiokolojia katika eneo hilo ili kuongeza mapato yake.

v) Msitu wa hifadhi Vikindu

Vikindu ni msitu wa hifadhi katika Wilaya Mkuranga wenye ukubwa wa hekta 1,599 ambao uko katika mazingira mazuri ya kuendelezwa kiutalii. Hifadhi hii ina kituo cha habari (information centre), njia za miguu za kitalii na za gari (nature trails & drive routes) na eneo la kupiga kambi (camping sites) ambalo limeshafanyiwa soroveya. Wakala umeweka mkakati wa kuboresha eneo hili ili kukuza mapato yake. Mkakati uliopo ni kujenga maeneo ya kambi yakupumzikia na kutengeneza eneo la kufugia wanyama (zoo) kwa ajili ya utalii.

Katika kuimarisha usimamizi wa msitu wa Vikindu Wakala umeingia makubaliano ya miaka mitano (5) (20014/15-2018/2019) na Chama cha Maskauti Tanzania (Tanzania Scout Association) ili kuweza kuwashirikisha vijana na jamii kwa ujumla kutekeleza dhana ya usimamizi shirikishi pamoja na kuweka kambi za mafunzo ya ukakamavu kwa vijana ndani ya hifadhi. Miongoni mwa mafunzo hayo kwa vijana ni elimu ya ujasiriamali. Uwepo wa vijana hawa utasaidia pia ulinzi wa msitu huu.

vi) Eneo la Msitu wa Kinyerezi

Msitu wa Kinyerezi unamilikiwa na Wakala. Msitu huu una ukubwa wa hekari nne (4 Ha). Eneo hili la msitu lina miti mchanganyiko (asili na ya kupandwa), na lina mandhari nzuri ambayo inaweza kuwa ni fursa nzuri kwa Wakala katika kuliendeleza na hivyo kuiongezea mapato Wakala. Wakala inayo njozi ya kuendeleza eneo hilo kuwa “Forest Park” na kuanzisha na kuboresha miundo mbinu hivyo kugeuka kuwa kitega uchumi muhimu

Picha Na. 22: Ofi si ya habari ya Vikindu (Information centre)

Page 68: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

59

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

kwa Wakala.

vii) Ujenzi wa majengo ya vitega uchumi

Wakala umeweka njozi ya kuendeleza ofi si zake zilizo katika miji mashuhuri na majiji ili kugeuzwa kuwa majengo ya kisasa ya uwekezaji. Ofi si hizo zipo katika majiji ya Mbeya, Tanga na miji ya Morogoro na Moshi. Mpango uliopo ni kujenga majengo ya kisasa yenye hadhi na kukodisha sehemu za majengo hayo kwa wawekezaji wa kibiashara.

viii) Kodi za Minara ya simu na majengo

Wakala utafanya tathmini ya minara ya simu/mawasiliano na majengo yaliyo ndani ya misitu ya hifadhi inayomilikiwa na Wakala ili kubaini idadi ya minara na kodi inayohitajika kulipwa kwa mwaka dhidi ya ile inayolipwa sasa. Hii ni kwa sababu ipo kodi isiyotozwa na Wakala badala yake inakwenda serikali za mitaa na kuisababishia Wakala kukosa mapato mengi.

Vilevile ada inayolipwa na Snow view Hotel Kilimanjaro itapitiwa upya kwani ni ndogo na haiendani na wakati hivyo kupunguza pato la Wakala.

ix) Msitu wa kupandwa wa kuni –Mbeya (Mbeya Fuel wood plantation)

Kitega uchumi tarajiwa kitakuza uchumi kwa Wakala nai kwa wakazi wa jiji la Mbeya.

Picha Na. 23: Bango linaloelekeza Msitu wa Kinyerezi

Page 69: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

60

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WA TANZANIA

x) Treasury Bond

Wakala utafanya utafi ti kufahamu sheria, kanuni na taratibu za Wakala wa serikali kumiliki Treasury Bond. Iwapo Wakala unaruhusiwa umiliki utaratibu utafanyika wa kujua benki inayotoa ongezeko kubwa ili kupata faida kubwa kwa kipindi kifupi.

14. MASUALA MAKUU YA BAADAYE NA YA KIPAUMBELE KWA WAKALA

Wakala una ndoto (vision) mbalimbali zinazolenga katika azma yake ya uhifadhi uliotukuka, ndoto hizi ni pamoja na kukusudia kuwa Mamlaka, Kuwa na vitega uchumi mbalimbali, kujenga makao makuu mapya ya kisasa.

a) Kuwa mamlaka

Wakala upo katika mchakato wa kuomba kuwa Mamlaka (Authority)

b) Wakala Kuwa na vitega uchumi

Wakala upo katika mchakato wa kuandaa sera ya uwekezaji (investment policy) ili kuwa na uwekezaji wa aina mbalimbali

c) Makao Makuu Mapya ya Wakala

Wakala upo katika mchakato wa kuhama kutoka katika jengo lake la Mpingo na kuwa na makao makuu mapya eneo lingine, hii ni pamoja na kujenga ofi si mpya ya kisasa itakayokuwa na vitega uchumi vingine ndani yake.

Wakala inakusudia kuomba kibali toka kwa

Waziri wa Maliasili na Utalii ili kubadilisha

matumizi ya awali ya eneo la hekta 67.3 ili

litumiwe kuwa eneo la uwekezaji kwa ajili ya

biashara. Eneo la awali lilikuwa hekta 315.7

ambapo lilipunguzwa na kuwa makazi

ya wananchi na taasisi za Serikali. Eneo

tarajiwa litatumiwa kujenga jengo la kitega

uchumi kama mradi maalum kwa njia ya

ubia. Mradi huu wa ujenzi utahusisha Public

Private Partnership (PPP) kama wadau

ambao watakuwa katika ubia na Wakala.

Eneo la kitega uchumi linatarajiwa kuwa na

ukumbi wa mikutano, majengo ya maduka

(shopping centre /super market, bustani ya

kupumzikia, na nyumba za kupanga. Picha Na 24: Eneo dogo la kijani la msitu -Mbeya lenye mpaka chini linalokusudiwa kuwa kitega uchumi

Page 70: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - TFS...Mkakati, Mpango wa Biashara wa kila mwaka, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), Uperembaji na Tathmini, Mkataba wa Huduma

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA

S.L.P 40832 Dar es Salaam

Simu +255 22 2864249

Fax +255 22 2864255

Barua pepe: [email protected]