9
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box 3001, Morogoro, Tanzania Tel.: +255 23 260 4 649 Uzalishaji bora wa mpunga Matumizi sahihi ya mbolea na mbinu nyingine za kilimo nchini Tanzania

Uzalishaji bora wa mpungaafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/.../74...flipchart.pdf · 1 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo P. O. Box 3001, Morogoro, Tanzania

  • Upload
    others

  • View
    21

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

1

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,Idara ya Sayansi ya UdongoP. O. Box 3001, Morogoro, Tanzania Tel.: +255 23 260 4 649

Uzalishaji bora wa mpunga

Matumizi sahihi ya mbolea na mbinu nyingine za kilimo nchini Tanzania

2

Andaa mashamba mapema kabla msimu wa kupanda haujaanza ili kupanda kwa wakati unaotakiwa.

Unaweza kufyeka, kung’oa visiki au kulima.

Baada ya kulima, shamba linawekwa maji ili liloane vizuri na kisha udongo unachanganywa vizuri na maji ili kutengeneza tope. Hii ni kuchavanga (puddling). Hii inarahisisha kupandikiza miche na kuhifadhi maji.

Kuandaa shamba

3

Tumia mbegu zilizoboreshwa ili kupata mazao mengi na bora.

Nafasi ya kupanda mpunga ni 15 sm kwa 15 smau 20 sm kwa 20 sm. Kwenye mpangilio wa mistari miwili miwili (double rows), nafasi kati ya mistari miwili ni 10 sm, nafasi kati ya mmea na mmea katika kila mstari ni 20 sm, na nafasi kati ya mistari miwili na mistari miwili mingine (double rows) ni 40 sm.

Mpunga unaweza kupandwa kwa kupandikiza au kupanda mbegu kwenye mashimo.

Kupanda

4

Kabla ya kuweka mbolea tengeneza majaruba ili kuhakikisha maji hayaingii na kutoka kiholela.

Mbolea ya kupandia huwekwa kwa kusia katika jaruba kabla ya kuchavanga.

Aina ya mbolea zakupandia

Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa hektari

Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa ekari

DAP 3 1Minjingu fosfati 2 1½

Minjingu Mazao 4½ 2

Kuweka mbolea

5

Palilia wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda ili kuondoa magugu.

Palilia kwa kung’oa kwa mkono, kwa mashine au kwa kutumua viua magugu (herbicides) kama inavyoshauriwa.

Magugu hunyonya virutubisho ardhini na yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa.

Tumia Urea, Calcium Ammonium Nitrate (CAN) au Sulphate of Ammonia (SA) kama mbolea za kukuzia.

Mbolea inayotumika mara kwa mara ni Urea. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa kila shina.

Kupalilia

6

Fosfati (Phosphorus): Kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa membamba. Kwenye mimea ya nafaka inayopacha kama mpunga, upachaji unapungua.

Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau.

Potashi (Potassium): Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea na kudumaa.

Upungufu ukiwa mkubwa sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis). Majani yanakuwa na michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated).

 

Naitrojeni (Nitrogen): Mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa mazao kidogo. Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka kuwa njano.

Dalili ya upungufu wa virutubisho

7

Rice blast (ukungu), Brown leaf spot na Sheath rot kwa kawaida hushambulia mpunga.

Rice yellow mottle (kimnyanga), White flies (funza weupe) na Rice stalk borer ni wadudu wanaoshambulia mpunga.

Tumia dawa na njia zinginezo ilikuzuia magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea.

Magonjwa na wadudu

8

Vuna kwa kukata bua pamoja na suke.

Kausha juani kwa siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mpunga ukauke vizuri ili usioze ukiwekwa ghalani.

Rundika pahali pakavu k.m. kwenye tuta la jaruba halafu pigapiga (thresh) ili kutenganisha masuke na mpunga.

Pepeta ili kuondoa mapepe.

Hifadhi kwa kuweka kwenye gunia na magunia kupangwa ghalani juu ya mbao yasiguse sakafu.

Vuna mpunga wakati asilimia themanini (80%) ya rangi kwenye masuke imebadilika na kuwa dhahabu.

Kuvuna na kuhifadhi

9

Kufanya kazi kwa pamoja na wadau/wabia kutayarisha taarifa zinazohusu mbinu husishi za afya ya udongo