24
Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini Mwongozo kwa ajili ya Asasi za Kiraia • Kutoendana na baina ya sera ya madini 2009 na muswada mpya • Kukosekana kwa kifungu cha msingi cha leseni ya wachimbaji wadogo HAYA NI MAPUNGUFU TULIYOYAONA KWENYE MUSWADA

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

  • Upload
    others

  • View
    18

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Mwongozo kwa ajili ya Asasi za Kiraia

• Kutoendana na baina ya sera ya madini 2009 na muswada mpya

• Kukosekana kwa kifungu cha msingi cha leseni ya wachimbaji wadogo

HAYA NI MAPUNGUFU

TULIYOYAONA KWENYE

MUSWADA

Page 2: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi
Page 3: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

i

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Mwongozo kwa ajili ya Asasi za KiraiaPolicy Forum

Page 4: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

ii

Policy Forum

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini: Mwongozo kwa ajili ya Asasi za Kiraia

Page 5: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

iii

Yanayohusiana na mwongozo huu

Mwongozo huu umetolewa na Policy Forum katika jitihada zake za kurekodi yale yaliyojiri waliposhirikiana na wabunge katika kuchangia sheria mpya ya madini Tanzania, na kuboresha uwezo wa asasi za kiraia na vyombo vya habari katika kusimamia utendaji wa serikali kwenye sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini). Programu hii ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Revenue Watch.

Hivyo basi, kusudi la mwongozo huu ni kuimarisha mikakati ya asasi za kiraia ya ushawishi wa bunge, ikiwa pamoja na zile ambazo zinataka kufanya ushawishi, kampeni, na kutumia vyombo vya habari katika kushawishi utungaji wa sheria kwenye sekta ya uziduaji. Pia mwongozo huu unawalenga wale ambao watapenda kujifunza uzoefu wa asasi za kiraia Tanzania zilizoshiriki katika michakato ya kutunga sheria mpya ya madini ya mwaka 2010. Mfumo uliotumika kueleza ni namna ya kisa mkasa, lakini wenye mambo ya kujifunza ikiwa pamoja na maoni kwa ajili ya mazoezi ya vikundi wakati wa kujifunza.

Policy Forum (PF) ni mtandao wa asasi za kiraia zaidi ya 100 zinazolenga kuimarisha ushiriki wa asasi hizo katika michakato ya sera Tanzania. Lengo kuu likiwa ni kuzifanya sera ziwanufaishe Watanzania hususan maskini, na kuwa na michakato ya sera iliyowazi zaidi, ya kidemokrasia, shirikishi na inayowajibika.

Shukrani

Maandishi: Semkae Kilonzo na Alex Ruchyahinduru wa Policy ForumWaandishi wanapenda kuwashukuru wanachama wa Policy Forum: Agenda Participation 2000, Legal and Human Rights Centre na HakiMadini kwa mchango wao muhimu. Shukrani hizi pia ziwaendee wafuatao: Matteo Pelligrini, Silas O’lang na Alina Meyer wa RWIMichoro: Nathan MpangalaUsanifu: Identity Promotion Limited

ISBN: 978-9987-708-04-8 ©Policy Forum 2011 Maswali na maoni yanakaribishwa na yapelekwe: Policy ForumS.L.P 38486, Dar es SalaamSimu/Nukushi: +255 22 2772611/2701433Anuani ya barua pepe: [email protected]: www.policyforum.or.tz

Page 6: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

iv

YaliyomoPolicy Forum.......................................................................................... 2

Ushawishi wa Bunge katika Tasnia ya Uziduaji: Mwongozo kwa ajili ya Asasi za Kiraia....................................................... 2

Yanayohusiana na mwongozo huu............................................................ 3

Shukrani............................................................................................... 6 Uwasilishaji wa mwongozo wa ushawishi bungeni......................................... 6

Habari Gazetini...................................................................................... 7

Maudhui............................................................................................... 8 Njia ya haraka....................................................................................... 9

Uhitaji wa majibu ya haraka.................................................................... 9

Uhamasishaji kupitia vyombo vya habari Kuuboresha Muswada.................... 1

Udhaifu wa Muswada.............................................................................. 12

Mafanikio.............................................................................................. 13

Sababu za mafanikio.............................................................................. 13

Kuandaa mkakati wa ushawishi bungeni: misingi muhimu Ifahamu mada husika 15

Umoja ni muhimu................................................................................... 16

Fikiria kutumia vyombo vya habari Kulishawishi bunge Usiishie hapo............. 21

Marejeo ya ushawishi katika uchimbaji madini................................................ 23

Faharasa............................................................................................... 24

Page 7: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

1

Uwasilishaji wa mwongozo wa ushawishi wa bunge

Kama zilivyo nchi nyingine nyingi za kiafrika, Tanzania ni nchi yenye utajiri wa maliasili, ikijaliwa kuwa na madini mengi kama almasi, dhahabu, kobalti, shaba, nikeli, chuma aina ya platinamu, fedha na madini ya kipekee Tanzanite. Pamoja na kuwa na utajiri huu, madini hayajaweza kutoa mchango wa kutosha katika kuboresha maisha ya maskini, hususan wanaoishi vijijini yaliko madini, tangu sekta iwe huria mapema miaka ya 1990.

Hali hii ikiambatana na usiri katika mikataba ya madini na mapato, imepelekea Watanzania wengi kuamini kuwa mazingira yaliyopo sasa ya sekta ya madini yanatoa mwanya wa mgawanyo usio sawa kwa kuyapa faida ya uchimbaji makampuni ya kimataifa.

Miaka ya 2000 tulishuhudia shinikizo la umma na bunge likiongezeka ambapo hatimaye ililazimu Serikali kuunda Tume iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani, (maarufu kama ‘Tume ya Bomani’), ili kupitia upya mikataba ya kibiashara ya madini na kutoa mapendekezo ambayo yangewezesha nchi kuleta maelewano na wawekezaji yenye faida katika sekta ya madini. Ripoti ya Tume ya Bomani ilipelekea serikali ya Tanzania kuahidi kufanya mabadiliko katika sera na sheria ya madini. Mnamo mwaka 2009 sera ya madini ilikamilika na sheria mpya ya madini ilitungwa na kupitishwa mwaka 2010.Ili kukabiliana na tatizo la uwazi katika mapato kutoka kwenye madini, Tanzania ilijiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) mwaka 20091 na ripoti ya kwanza ya EITI ilizinduliwa Februari 2011.

Mbali na mchakato wa Bomani unavyoelekeza katika hatua hizi muhimu, pia ilipelekea kuibuka kwa wabunge machachari ambao wanaendelea kushinikiza uwazi na mageuzi katika sekta hii. Msimamo huu mpya wa wabunge sasa unaendana na uhamasishaji wa asasi za kiraia. Vikundi vya kidini kama vile Baraza Kuu la Wailslamu Tanzania (BAKWATA), Baraza la Maaskofu Wakatoliki (TEC) na Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), vimepelekea jumuiya za wachimbaji madini kudai haki katika madini. Muungano wa kampeni Tanzania wa chapisha unacholipa (Publish What You Pay Campaign -PWYP), pia ulianzishwa Juni 2009. Mtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi na wabunge katika jitihada za kuwaweka pamoja wanaharakati katika sekta ya madini Tanzania.Maendeleo yote haya yalifanyika pale ambapo umma unazidi kuamka juu ya umuhimu wa kuiwajibisha serikali na wawakilishi wao katika usimamizi wa fedha za umma.

Mwongozo huu unaongelea juu ya yaliyojiri wakati asasi za Kitanzania zikijihusisha katika kutunga Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na umeandaliwa ili kutoa baadhi ya mapendekezo ya msingi kwa wale wanaopenda kufanya ushawishi wa bunge katika masuala ya tasnia ya uziduaji nchini mwao. Umejikita katika uzoefu wa asasi za kiraia zinazofanya kazi Tanzania, lakini tunadhani kuna mapendekezo ya kutosha yanayoweza kuendana na muktadha wenu na kuwavutia kufikiria namna ya kufanya.

Tuna matumaini kuwa habari tunayoifafanua katika mwongozo huu itawapa hamasa ya kuchukua hatua, iwe mnahusika na ushawishi wa bunge katika sekta ya uziduaji au mnafanya kazi katika maeneo mengine yanayolenga katika kujihusisha na wabunge na utungaji sheria kama vile michakato ya bajeti, afya, elimu na mazingira. Tunajaribu kuyaeleza masuala haya katika njia rahisi na kutoa mwongozo na vidokezo kuhusu jinsi ya kuandaa mkakati wa ushawishi wa bunge ili kushawishi marekebisho ya sheria.Matumaini yetu ni kwamba utatumia mwongozo huu kuchukua baadhi ya vidokezo ili kufanikisha kazi ya ushawishi wa bunge unaolenga kupambana na matatizo yanayokwamisha maendeleo ya nchi yako.

1 http://eiti.org/Tanzania. Mpango huu unaweka kiwango cha kimataifa kwa ajili ya uwazi katika mafuta, gesi asilia na madini. Ni jitihada ya kuyafanya maliasili yanufaishe wote; ni muungano wa serikali, makampuni na asasi za kiraia; ni kiwango cha kuyafanya makampuni kuchapisha wanacholipa na kwa serikali kuweka wazi inachopata. Jifunze zaidi: http://eiti.org/

Page 8: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

2

Habari Gazetini

MuhtasariMkakati wa uhamasishaji ulio makini kwa kikundi maalum unaweza kutoa mchango wenye kuleta ushawishi. Kuvileta pamoja vikundi ambavyo tayari vina uelewa, utaalamu na mafunzo katika suala maalum la ushawishi, ni njia nzuri ya kushughulikia michakato ya sera na utungaji sheria.

Ushiriki wa Policy Forum katika mchakato wa kutunga sheria ya madini ya mwaka 2010 ni mfano halisi ya kwamba umoja si lazima uwe na idadi kubwa ya asasi. Ukihusisha watu sahihi na kutumia njia sahihi kuwasilisha ujumbe wako wa msingi, kwa hakika unaweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

MaudhuiKatika kujibu lawama kwamba kulikuwa na hitilafu katika mafanikio ya kifedha ya sekta ya uziduaji Tanzania na faida isiyoeleweka kwa maisha ya Mtanzania, serikali ilianza kupitia upya sera ya madini mwaka 2008. Ilianza kufanya mijadala iliyowahusisha wadau wakubwa iliyolenga kuleta utaratibu wa tofauti ambao ungeleta manufaa zaidi kwa Watanzania na nchi.

Hata hivyo, dhamira ya kubadili sera na sheria ya madini ilipotea, na mabadiliko yaliyotarajiwa kuwasilishwa bungeni Februari 2009 hayakufanyika. Rasimu ziliwasilishwa kwa wadau wachache tu Desemba 2009 na Januari 2010.

Pia haikuwa wazi ni lini rasimu ya muswada ingewasilishwa kwa watu wengi. Mchakato huu haukuwa wazi na asasi za kiraia ziliona kuwa zimebaguliwa na kuondolewa katika mchakato.

Dar es Salaam — Jana asasi za kiraia ziliungana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, katika kukosoa Muswada wa Madini wa 2010 kuwa una dosari, akisema kuwa hauhamasishi kwa uwazi katika tasnia hiyo...

Katika tamko lao, Policy Forum walisema Muswada unaainisha taarifa nyingi ikiwa pamoja na vitabu vya ukaguzi vya makampuni ya madini na malipo yao kwa serikali.

“…Kwa kuwa Tanzania ni nchi inayokaribia kujiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji (EITI), sheria hii ingepaswa kuingiza kipengele maalum kuhusu suala hili”…

Taasisi hii, mwamvuli wa asasi za kiraia inayofuatilia sera za serikali, ilisema nchi iliweka wazi kwamba imedhamiria kuwa na uwazi katika sekta ya madini ilipoomba kujiunga na EITI, na hivyo sheria mpya ya madini inapaswa kuonesha dhamira hiyo.

Policy Forum ilikuwa mojawapo ya wadau waliowasilisha uchambuzi wa kina wa Muswada wa Madini 2010 kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika mkutano wa hadhara uliofanyika juma lililopita Dodoma.

“Kwa ufupi, na kutokana na uchambuzi wetu, muswada mpya hauendi mbali katika kukidhi mapendekezo ya Tume ya Bomani ya Mapitio ya Sekta ya Madini ambayo ilipitia upya sekta ya madini miaka miwili iliyopita,” Policy Forum walidai. 19/04/2010.

DAILYNEWS

Page 9: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

3

Hatua za haraka

Mnamo Aprili 13, 2010 Kamati ya Nishati na Madini ilithibitisha kwa RWI kwamba Waziri wa Nishati na Madini angewasilisha muswada chini ya Hati ya Dharura Aprili 16 na kufuatiwa na mkutano wa hadhara uliopangwa siku inayofuata.

Kwa kuzingatia shinikizo la asasi za kiraia kupitia vyombo vya habari, la kuipitia upya ratiba ya kipindi kifupi, mkutano ulipangwa upya hadi Aprili 18 ili kutoa muda zaidi kwa ajili ya maandalizi na ushiriki. Hata hivyo muswada haukuweza kupatikana kwa umma. Kwa ugumu uliogubika muswada huu hati ya dharua ingesababisha ugumu zaidi kwa umma.

Mbali na wito kutoka kwenye asasi za kiraia wa kutumia utaratibu wa kawaida, Waziri aliomba hati ya dharura na kushinikiza marejeo na kuupitisha mchakato ndani ya siku 10.

Uhitaji wa majibu ya haraka

Policy Forum iliamua kuandaa kikundi cha asasi zilizo mstari wa mbele zinazoshiriki programu ya uwezeshaji ya RWI ikiwa pamoja na Kamati ya Ushirikiano wa Kidini.

Pamoja na kuwepo muda mfinyu, kikundi kilijiunda haraka na kuja na mkakati wa mwingiliano wenye nyanja mbili:

Wadau

• Policy Forum, mtandao wenye zaidi ya asasi 100 zinazolenga kuimarisha ushiriki wa asasi za kiraia katika michakato ya sera Tanzania.

• Wabunge, ikiwa pamoja na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini

• Kamati ya Ushirikiano wa Kidini, moja ya vikundi vinavyoaminika na kusikika zaidi katika uchimbaji madini Tanzania

• Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

• HakiMadini• ForDIA• Wachimbaji wakubwa na wadodo• Taasisi ya Revenue Watch (RWI)

inayofanyakazi kuboresha uwezo wa bunge

Hati ya Dharura

Japo inaruhusiwa kisheria kwa Waziri kuwasilisha muswada chini ya hati ya dharura kwa ridhaa ya Rais, utaratibu huu unazidi kulaumiwa kuwa unazuia fursa ya kujadiliwa na umma. Kwa utaratibu wa kawaida, muswada unasomwa kwa mara ya kwanza bila kujadiliwa, ili kutoa fursa kwa kamati husika ya kupata maoni ya wananchi na kuuchambua muswada kabla ya kujadiliwa katika kikao kinachofuata (kusoma mara ya pili). Hati ya dharura inalazimisha mchakato huu ufanywe katika kikao kimoja tu.

Page 10: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

4

Uhamasishaji kupitia vyombo vya habari

Mchakato wa kuandaa tamko kwa vyombo vya habari Aprili 13/14 ulianza kwa ushirikiano wa asasi za kiraia wakati wa warsha ya Januari 2010 PF/RWI. Agenda Participation 2000, mwanachama wa PF na mshiriki katika warsha, iliandaa na kurusha matangazo 40 katika runinga ikiomba umma kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kawaida wa kujadili na kupitisha muswada. Matangazo ya runinga ya kuwataka wabunge kuwa ngangari wakati wa kuujadili muswada pia yalirushwa. Huu ulikuwa ujumbe mzito na mzuri kwa wabunge. Namba mbili za mkononi za kupiga moja kwa moja zilifunguliwa ili kukusanya maoni kutoka kwa wananchi. Maoni ya wananchi yalikusanywa kwa siku mbili na kupelekwa bungeni wakati wa mkutano wa hadhara.

Kunako Aprili 13, Policy Forum, na asasi zingine za kiraia, zilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu muswada.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kiliandaa mkutano na waandishi wa habari Aprili 14, kikiainisha dosari katika mchakato wa muswada, ikiwa pamoja na utata wa kutumia hati ya dharura. Tukio hili lilifuatiwa na mjadala kwenye runinga katika kipindi maarufu cha “PAMBANUA” (yaani “chambua”). Wasemaji watatu kati ya wanne walitoka programu ya uwezeshaji ya RWI. Watendaji wa wizara walioalikwa kwenye mdahalo hawakujitokeza.

Kuuboresha Muswada

Kazi hii, kwa kushirikiana kwa karibu na bunge, ilikuwa na changamoto kwa kuwa nakala ya muswada ilipokelewa Aprili 15, (kutoka Kamati ya Nishati na Madini) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara. Wachambuzi wa kisheria wa RWI walifanya haraka kuipitia rasimu na kuandaa maoni ya kitaalamu. Chambuzi tatu za ziada zilifanywa na Agenda Participation 2000, LHRC na HakiMadini. Kazi ngumu ya uchambuzi wa RWI ilishirikishwa kwa asasi zaidi ya 20 zilizokusanyika Dodoma1 na kuwasilishwa kwa Kamati ya Nishati na Madini. Chambuzi nne zililinganishwa na kupata msimamo mmoja katika kikao cha Dodoma, na kuwasilishwa wakati wa mkutano

2Makao Makuu ya Tanzania, linakokutana Bunge

Ratiba ya Mchakato

Februari 2009

• Mabadilio ya kisheria katika sheria mpya

Desemba 2009/ Januari 2010

• Kuwasilishwa kwa rasimu kwa “kundi la wadau wachache”.

Aprili 2010

• Aprili 13: Uthibitisho kwamba muswada utawasilishwa chini ya hati ya dharura

• Aprili 15: Muswada kutolewa kwa umma

• Aprili 16: Kutolewa kwa hati ya dharura

• Kubadili mkutano wa hadhara kutoka Apriili 17 hadi Aprili 18

Ratiba ya Mikakati

Januari 2010

• Warsha ya PF/RWI

Machi 8, Aprili 10, 2010

• Matangazo 40 katika runinga na Agenda Participation 2000

• Namba ya kupiga wananchi

Aprili 13, 2010

• Taarifa kwa vyombo vya habari na PF na asasi

• Mkutano na wandishi wa habari na LHRC na kipindi kwenye runinga

Aprili 15, 2010

• Kupokelewa Muswada na kufanyiwa kazi na RWI

Page 11: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

5

Kamati ya Nishati na Madini iliwaalika wananchi Aprili 17 ili kukutana Aprili 18. Mkutano huu ulifanyika bungeni kama ulivyopangwa.

Wakati wa mchakato huu RWI pia iliwezesha ushirikishwaji wa taarifa na mjadala kati ya asasi za kiraia na kamati, ikisaidia katika kuweka misingi mizuri ya wadau hawa muhimu. Asasi za kiraia ziliibuka kuwa kundi la wadau waliojipanga vizuri. Waliwasilisha tamko la pamoja kwenye kamati ambalo liliwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiMadini, Amani Mustapha.

Udhaifu wa Muswada

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. William Ngeleja, aliwasilisha dondoo muhimu sita za muswada (angalia kushoto).

Tamko la pamoja la asasi za kiraia liliainisha udhaifu ufuatao:• Kukosekana maelezo ya wachimbaji

Dondoo muhimu za Sheria ya Madini

1. Ushiriki wa Serikali na umma katika miradi ya uchimbaji madini ambapo serikali inakuwa na hisa katika miradi ya madini

2. Leseni Maalum ya Uchimbaji na Mikataba ya Uendelezaji Madini na kipindi na namna ya utengamano/uthibiti wa mabadiliko katika utozaji kodi.

3. Udhibiti katika kutoa vibali vya uchimbaji madini ya urani

4. Ugatuzi wa mamlaka za leseni (ofisi za kanda za madini)

5. Kuanzishwa Bodi ya Ushauri ya Madini

6. Mabadiliko ya viwango vya mrabaha na kanuni ya ukokotoaji kwa madini yote.

wadogo na uchimbaji wa vito vya thamani

• Kukosekana muunganiko kati ya sera ya 2009 na Muswada mpya

• Kuondolewa kwa kifungu cha Leseni ya Awali (na kufanya iwe marufuku kwa wenyeji kutafuta na kutafiti madini)

• Leseni ya uchimbaji inayotolewa itakuwa na muda uliokadiriwa wa madini au muda atakaoomba mwombaji

• Kuondolewa kwa vipimo vya ufanisi na kukosekana kwa kufungiwa kwa ambaye hakidhi vigezo

• Vifungu vya siri dhidi ya utekelezaji wa mpango wa uwazi katika tasnia ya uziduaji (EITI)

• Madaraka makubwa ya Waziri katika kujua ajenda za maendeleo ya sekta ya madini ambayo yana maslahi ya kitaifa

Page 12: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

6

Mafanikio

Udhaifu ulioanishwa hapo juu ulifanyiwa marekebisho kwenye rasimu mpya ya muswada. Asasi za kiraia pia zilitoa mapendekezo kadhaa ambayo yaliingizwa kwenye rasimu mpya ya muswada. Haya yalijumuisha: makubaliano ya msingi ya uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Madini (Mfuko wa Utajiri wa Nchi) wa kuelezea hali ya asili ya madini kuwa ni rasilimali inayoisha, wabunge (kama Mhe. Zitto Kabwe) waliunga mkono kwa nguvu zote mfuko huu na kuwepo kwa sheria maalum kuhusu Mpango wa Kimataifa wa Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji (EITI). Aidha, sheria iliyorekebishwa itatamka kwamba leseni ya awali itakuwa na muda wa miaka mitano, inayoweza kuombwa tena baada ya

miaka mitano. Nafasi ya wachimbaji wadogo katika sheria imewekwa vizuri.

Sababu za mafanikio

Ukweli kwamba asasi za kiraia zilijiandaa tangu Januari 2010 na kuungwa mkono na jitihada za uwezeshaji za Policy Forum na RWI ulipelekea kuwepo kwa vikundi mbalimbali vikiwa na uelewa, utaalamu na mafunzo katika suala husika la ushawishi. Asasi hizi pia ziliweza kuhamasishwa katika hatua muhimu wakati wa mchakato. Kupatikana kwa mafunzo ya kitaalamu kutoka RWI kuliwezesha kufanya tathmini makini ya rasimu ya muswada katika kipindi kifupi sana (siku 2).

Msaada wa vyombo vya habari ulisaidia kupeleka ujumbe kwa watu wengi, na hususan vipindi vya redio na runinga, vilisaidia kuleta mwamko. Kufanya kazi kwa pamoja na wabunge kulikuwa na mafanikio sana, na uungwaji mkono na baraza la mawaziri ulirahisisha mapendekezo kukubaliwa na kuingizwa kwenye muswada mpya.

Mfuko wa Maendeleo ya Madini

Ukiwa na lengo la kusaidia mkakati wa uwekezaji wa umma katika maeneo kama miundombinu, ili kuwainua wachimbaji wadogo, pamoja na mambo mengine, kuwaendeleza kielimu na kiujuzi.

• Kutoendana na baina ya sera ya madini 2009 na muswada mpya

• Kukosekana kwa kifungu cha msingi cha leseni ya wachimbaji wadogo

HAYA NI MAPUNGUFU

TULIYOYAONA KWENYE

MUSWADA

Page 13: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

7

Kuandaa mkakati wa ushawishi bungeni: misingi muhimu

Kutokana na uzoefu wetu katika kurekebisha muswada wa madini 2010, tunaweza kuorodhesha sababu nne ambazo ni muhimu katika kampeni ya ushawishi wenye mafanikio:

Ifahamu mada husika

Unakuwa unaguswa sana na tatizo linalohusu maendeleo au haki, na unakuwa unapenda kujihusisha katika kulishughulikia lakini unahisi kuwa huna ujuzi wa kukabiliana na masuala magumu. Unafanyaje? Matatizo mengi ya kimaendeleo na kijamii kwa asili yake ni magumu, lakini kwa uzoefu wetu yanaweza kutatuliwa. Mathalani, masuala ya fedha ya tasnia ya uziduaji, yanaweza kuonekana kama ya kitaalamu sana kuyakabili kwa kikundi cha kawaida cha ushawishi, lakini kama ilivyo kwa jambo lolote, tunaweza kujifunza.

Hata hivyo, ieleweke kuwa hakuna kukwepa ulazima wa kuelewa misingi na kutafuta mafunzo ya kitaalamu yanayoweza kukusaidia kujenga ufahamu wako juu ya masuala magumu kama yanayohusiana na usimamizi wa sekta ya uziduaji. Uelewa na kuwa na taarifa kutajenga msingi wa uhakika wa uchambuzi wa kazi yako na kutumiwa katika ushawishi. Uchambuzi dhaifu unafanya vikundi vya ushawawishi kupuuzwa kirahisi kwamba hawafai na serikali au makampuni ya kimataifa.

Lakini je, unapataje uwezo huu? Kuna taasisi nyingi za kimataifa na kikanda zinazoweza kusaidia (baadhi zimeorodheshwa kwenye kipengele cha marejeo ya ushawishi ukurasa wa 13). Policy Forum ilianza kwa kushirikiana na Taasisi ya Revenue Watch (RWI) kwa malengo ya:

• Kuwapatia wanachama wetu, wawakilishi wengine wa asasi za kiraia wenye uhitaji, vyombo vya habari na wabunge, uelewa wa awali, masomo, na mafunzo, ili waweze kuisimamia serikali kwa ufanisi katika sekta ya uziduaji.

• Kutoa mifano ya mafanikio kwa asasi za kiraia, wataalamu wa vyombo vya habari, na wabunge, katika kubadili utajiri wa maliasili kuwa mafaniko ya kiuchumi.

Kazi za kujenga uwezo zilizofanyika:

1. Kuleta mwamko na kujenga uwezo kuhusu Utawala wa Tasnia ya Uziduaji.

2. Kutoa utaalamu na Mifano ya Mafanikio wakati wa kupitia upya sheria mpya ya madini.

3. Kuongeza uelewa wa wabunge kuhusu matumizi ya gesi asilia, mapato na usimamizi wake Tanzania, na uwezekanao wa kuzalisha mafuta.

4. Kazi mtambuko

• Ushiriki wa wafanyakazi wateule wa bunge na asasi teule kwenda kwenye mafunzo ya RWI ya majira ya kiangazi kuhusu tasnia ya uziduaji

• Ruzuku ndogo kwa ajili ya kazi za kukusanya ushahidi

• Kuibua hoja ya tasnia ya uziduaji wakati wa kampeni za uchaguzi

• Mikutano ya kimataifa ya miradi kama hiyo kwa ajili kuelimishana

Page 14: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

8

• Kujenga ushirikiano kati ya wabunge na asasi za kiraia, na wadau wengine kama RWI, wanaoshughulika na uziduaji.

• Kujenga ubadilishanaji uzoefu kati ya asasi za kiraia, wataalamu wa vyombo vya habari na wabunge toka Tanzania na wale wa nchi zingine ili kuwepo na mtiririko wa habari na mawazo kuhusu kuboresha utawala unaowajibika katika sekta ya uziduaji.

• Kuzisaidia asasi za kiraia kufanya uchunguzi na kukusanya taarifa za kusaidia mijadala yao bungeni.

Ni uelewa kutoka katika kazi hizi za kujengewa uwezo ambao ulitusaidia kushiriki katika mchakato wa kutunga sheria wakati wa kuupitisha muswada.

Umoja ni muhimu

Kuwa na umoja wenye ufanisi ni muhimu, uwe mkubwa au mdogo. Ndani ya kikundi, wajumbe wanasaidiana katika ujuzi na uzoefu, na kuongeza uwanja mpana wa uelewa. Kila mjumbe pia anakuwa na mahusiano na watu au taasisi nje ya kikundi, ambayo yanaweza kutumiwa ili kupata mafunzo zaidi na kuimarisha umoja.

Katika kikundi chetu tulikuwa na mwanasheria ambaye ni mtoto wa mchimba madini, na ambaye ana uhusiano wa vikundi vya wachimbaji wadogo akiwa na uelewa mzuri kuhusu jumuiya za watu wa ngazi ya chini. Pia tulikuwa na watu wenye ujuzi katika mawasiliano, serikali za mitaa, uzoefu wa masuala ya kupunguza umaskini, uozefu katika makampuni ya kimataifa na haki za binadamu.

Inakubalika kimataifa kuwa ili umoja ufanikiwe hapana budi kuwepo na lengo moja. Kwa upande wetu lengo letu lisingekuwa wazi zaidi ya hapo kuelekea kazi hii: sheria mpya ya madini yenye kuongeza manufaa kwa Watanzania ya uziduaji maliasili ya mafuta, gesi asilia na madini. Ingawa ni vema kwamba vikundi vya umoja vinapaswa kuwa na muundo wa uongozi unaoeleweka ili kuondoa kuwepo kwa migogoro, kwa lengo la muswada husika, umoja wetu tayari ulikuwa umejengeka chini ya mpango wa mafunzo.

Page 15: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

9

Fikiria kutumia vyombo vya habari

Asasi za kiraia haziwezi kukwepa kazi ya vyombo vya habari kama zinataka kusikilizwa na watoa maamuzi kama wabunge na watunga sera, kuongeza mwamko wa umma katika suala husika na kuondoa hodhi iliyonayo serikali na sekta binafsi kama vyanzo vyake vya habari.

Katika uingiliaji kati huu, ingawa umma kwa ujumla haukupendezwa na namna mfumo wa utawala wa madini ulivyopangwa, katika kile ulichodhani unayapendelea makampuni ya uchimbaji madini, haukujua mchakato wa kutunga sheria mpya ya madini. Kazi yetu na vyombo vya habari mara hii ilisaidia kujenga mwamko wa umma siyo katika mchakato tu, bali maudhui ya muswada wenyewe na kuweka hali ya kisiasa kuishinikiza serikali na wabunge kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya watu.

Pale maafisa wa serikali na wabunge wanapolala na kuamkia habari, huku watoa maoni na malalamiko ya wananchi yakiwa na ujumbe uleule mmoja wa tatizo la muswada, watataka kujibu kwa kufanya maamuzi ambayo wanahisi yatalinda hadhi yao mbele ya macho ya umma.

Kulishawishi bunge

Ili kuweza kuboresha sera, utungaji sheria na usimamizi mkali dhidi ya serikali katika masuala yanayohusiana na tasnia ya uziduaji, asasi za kiraia hazina budi kujenga mahusiano na wabunge. Hata hivyo, angalizo ni kwamba japo kazi ya asasi za kiraia na wabunge zinaingiliana, kuna nyakati ambazo ukinzani unatokea. Nyakati hizi ni za kawaida na mara nyingi hutokea kutegemeana na suala husika.

Mfano kwa Tanzania, Policy Forum ilipinga (na bado inapinga) uanzishwaji wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDCF) mwaka 2008, njia nyingine ya kufadhili maendeleo yanayoibuliwa na wananchi (kutokana na mapato ya ndani), ambao unasimamiwa na wabunge katika ngazi ya jimbo. Policy Forum ilidhani haukuwa ndani ya mamlaka ya wabunge (ambao kazi zao ni kusimamia serikali na kutunga sheria) kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuwa hili litavuka mipaka kati ya majukumu ya serikali na ya bunge, na kwahiyo bunge liliunga mkono kinyume na kuwepo kwake. Matokeo yake, wabunge hawakufurahia asasi za kiraia na wengine waliapa kutofanya kazi na Policy Forum siku zijazo. Hata hivyo, muswada wa CDCF uliwasilishwa na kupitishwa na bunge mwaka 2009.

Misingi ya kuhusisha vyombo vya habari

• Jizoeze jinsi magazeti, na vituo vya redio na runinga vinavyotoa taarifa kuhusu tasnia ya uziduaji. Hii itakupa mwongozo wa wandishi gani watapendelea kutoa ripoti ya habari yako.

• Andaa orodha ya mawasiliano na vyombo vya habari (majina, namba za simu, anuani za barua pepe, nk). Tumia orodha hiyo kuwatumia wandishi habari ambazo zitawavutia.

• Chagua wasemaji. Baadhi ya vikundi vya ushawishi hupendelea kuwa na msemaji mmoja anayelijua somo husika na yuko huru kuongea na vyombo vya habari, na ambaye ni mtulivu katika hali tete.

Page 16: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

10

Kwa kuwepo hali hii, Policy Forum ilishughulika na ushawishi wa muswada wa madini wa mwaka 2010 kwa makini kwa kuogopa uhusiano wa ugomvi iliyokuwa nao na wabunge. Woga huu ukawa hauna msingi kwasababu mbili. Kwanza, wabunge tayari walikuwa wamepitisha muswada wa CDCF na kwahiyo hawakuona mfuko uko hatarini. Pili, madini yalikuwa suala nyeti miongoni mwa wapiga kura muda huo na 2010 ulikuwa mwaka wa uchaguzi mkuu. Hivyo basi wabunge walitaka kuwa upande sahihi wa hoja na kuendana na maoni ya wananchi.

Je, sasa unaanzaje ushawishi unaolenga wabunge? La kwanza usiwaendee mmoja mmoja kiholela kwa kuwa haina tija na utapoteza muda wako adhimu. Chunguza wabunge machachari katika bunge kwa hoja yako. Unaweza ukawa umesoma au umesikia wabunge waliongelea vizuri kuhusu suala unalolipigania au rafiki anayejua mambo ya bunge angeweza kukupa mwongozo mzuri. Ukipata kikundi makini cha wabunge unaweza kupanga siku ya kuonana na wasaidizi wao au ofisi ya bunge huku ukihakikisha kuwa unatuma mapema hoja yako ili kuokoa muda.

Katika mfano wetu, tulimpata mbunge mmoja machachari na kupanga kuonana naye kabla ya mkutano wa hadhara. Alitupa vidokezo muhimu ikiwa pamoja na namna ya kupangilia taarifa. Jambo moja ambalo pia lilikuwa na tija katika kikao hiki ni kwamba kuna matokeo mazuri ya kutenga muda wa kulielewa suala husika kwa pande zote mbili. Wabunge hutumia muda mwingi kusikiliza hoja zinazokinzana kuhusu jambo fulani, hivyo basi vikundi vya ushawishi viwe tayari kujibu maswali ya kiushawishi.

Hivi ni vidokezo vya kutiliwa maanani kabla ya mkutano na mbunge au wananchi:

• Vijitabu vilivyoandikwa viwe kwa ufupi! Kijitabu cha kurasa mbili (angalia mfano ukurasa wa 16) ni kile ambacho mbunge anaweza kutenga muda kusoma. Sambamba na hilo, uwasilishaji wako wa maneno uwe wa dakika 10 au chini ya hapo.

• Lenga hoja. Wabunge husikiliza sera, sheria, na ripoti nyingi katika muhula wao. Kwahiyo maelezo kama “kutokana na sera ya madini,” huwaacha wakistaajabu kama unaongelea sera ya madini ya 1998 au 2009.

• Iwe rahisi na lugha inayoeleweka, bila vifupisho na lugha ya kitaalamu. Si wabunge wote wanaojua misamiati “MDAs” (Mineral Development Agreements) na “PSAs” (Production Sharing Agreements).

• Uchaguzi wa mtu wa kuwasilisha wakati wa mkutano wa hadhara unaweza kufanikisha au kuharibu uwasilishaji. Anaweza kuwa mtu anayelijua somo au aliyezoeana na wabunge. Kwa upande wetu tulichagua mjumbe ambaye ni mtoto wa mchimbaji madini mdogo, aliyekuliwa migodini na mwanasheria. Huu ulikuwa muunganiko mzuri kwa kuwa tulikuwa tunaingiza kwenye rasimu ukiendana na eneo alikokulia mwasilishaji. Wachimbaji wadogo ni jukwaa muhimu kwa wabunge hasa wanaowakilisha jamii za wachimbaji. Katika kila uwasilishaji, hoja inayolingana hapa ni kuzungumzia majimbo. Je, ujumbe wako mkuu unawanufaisha vipi watu katika nchi yako? Kwa maneno mengine, msaidie mbunge awakilishe maslahi ya wananchi.

Page 17: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Mfano wa kijitabu cha kwanza kwa wabunge

Page 18: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

12

Usiishie hapa!

Baada ya kutoa mchango wako na kuingizwa kwenye sheria, je, ni wakati wa kusherehekea na kisha kuchagua vita nyingine? Hivyo sivyo. Hivi ni vitu vingine vya kufikiria wakati na baada ya ushawishi:

• Fuatilia ahidi zilizotolewa! Wakati wa kusikiliza wananchi, kwa kuwa maafisa wa serikali hujibu maswali au maoni kuhusu muswada, huwa wanatoa ahadi (zinazorekodiwa kama kumbukumbu rasmi za bunge - hansard). Wakati wa mkutano na wananchi, tuliuliza kwanini rasimu ya muswada haiongelei Mpango wa Kimataifa wa Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji (EITI). Serikali ilijibu kuwa ni sheria tofauti itakayotungwa mbeleni. Baada tu ya sheria ya madini kukubaliwa, tulianza kampeni ya ushawishi kuhamasisha uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika sekta ya madini. Hii ilihusisha kuzinduliwa vipindi kwenye runinga na redio wakati wa kampeni za 2010.

• Imarisha uhusiano ulioujenga wakati wa ushawishi. Usiwapigie tu simu wabunge unapohitaji msaada wao. Kama unataka kuendelea na ushawishi wa bunge bila shaka utahitaji msaada wao siku za mbele kwa jambo lingine.

• Anza kufikiria jinsi ya kuandika habari ya ushawishi (uingiliaji kati) wako. Kimsingi kuandika kunapaswa kuwa sehemu ya ushawishi (unapotekeleza). Hata hivyo, kama ni kitu ulichokiacha wakati wa utekelezaji, jikite katika safari ya kuandika mara tu baada ya kumaliza ushawishi.

Page 19: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

13

Marejeo ya ushawishi katika uchimbaji madini

Asasi zinazofanya kazi katika ushawishi wa tasnia ya uziduaji

The Revenue Watch Institute ni taasisi ya kisera isiyokuwa ya kiserikali na ni taasisi inayotoa ruzuku kwa ajili ya kudumisha usimamizi bora, uwazi na uwajibikaji wa rasilimali za mafuta, gesi na madini kwa manufaa ya umma. Kwa njia ya kujenga uwezo, misaada ya kiufundi, utafiti na ushawishi ili kuisaidia nchi kutambua faida ya maendeleo ya maliasili yao. Visit: http://www.revenuewatch.org

Publish What You Pay (PWYP) ni mtandao wa kimataifa wa mashirika ya kiraia yaliyoungana kwa ajili ya mapato ya mafuta, gesi na madini kwa msingi wa maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida katika utajiri wa rasilimali za nchi zao. PWYP hufanya kampeni na uchemuzi wa sera zinazoshirikisha watu katika kuleta uwazi wa taarifa juu ya mapato ya sekta ya madini na mikataba. Tembelea: http://www.publishwhatyoupay.org

AfrikaPolicy Forum ni asasi huru yenye dhamira ya kuhusisha wananchi, asasi zisizo za kiserikali, na sekta zote zingine za jamii katika michakato ya uundwaji wa sera. Dhamira hii pia inahusisha kuwezesha hatua zote za michakato ya uundwaji wa sera zinaelimisha wananchi, zinakuza uwezo wao wa kujihusisha na zinaendeshwa kwa njia inayotoa nafasi ya uwajibikaji. Kwa maelezo zaidi tembelea: http://www.policyforum-tz.org

Africa Institute for Energy Governance (AFIEGO) ilisajiliwa na serikali ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Florida ya Jamhuri ya Uganda mwaka 2004 chini ya Sheria ya Usajili wa asasi isiyokuwa ya kiserikali. AFIEGO inafanya shughuli tofauti-tofauti ili kuona Serikali ya Uganda inatumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi wake na inajishughulisha na kuboresha usalama wa nishati na maendeleo endelevu kwa njia ya utafiti wa sera na ushawishi. Tembelea http://www.afiego-ug.org

Norwegian Church Aid (NCA) inapambana pamoja na watu na mashirika mengi duniani ili kuondoa umaskini na kukosekana kwa haki. NCA hutoa msaada wa dharura katika maafa na kazi kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu katika jamii. tembelea, http://www.kirkensnodhjelp.no/en/

PWYP Ghana kwa muda mrefu imekuwa ikichangia sana katika utekelezaji wa tasnia ya uziduaji nchini Ghana, PWYP-Ghana imekuwa ikitoa wito wa sheria za kitaifa kuhusu uwazi katika sekta za madini, wakiamini hii itarahisisha upatikanaji wa mikataba, pamoja na taarifa juu ya sekta za madini. Tembelea, http://pwyp-ghana.org

The Integrated Social Development Centre (ISODEC) (ISODEC) ni asasi isiyo ya kiserikali yenye nia ya kuendeleza haki za binadamu (hasa haki za kijamii na kiuchumi) na haki za kijamii kwa watu wote, hasa wale wanaobaguliwa, dhulumiwa na kukosa uwezo. Visit: http://www.isodec.org.gh

The National Advocacy Coalition on Extractives (NACE) (NACE) awali ilianza kama Diamond Area Community Development Fund (DACDF), lengo la umoja huo ulikuwa kufuatilia na kuhakikisha ufanisi wa kuendesha shughuli za fedha na ulianzishwa katika jamii almasi. Visit: http://www.nacesl.org/

The Parliamentary Centre Tangu kuanzishwa kwake (kwa mara ya pili) mwaka 1992, Bunge la Ghana limekuwa likifanya kazi kwa bidii ili kuboresha uwezo wake wa kuchangia katika utawala bora wa Ghana.

Page 20: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

14

Kamati maalum juu ya Kupunguza Umaskini sasa imeundwa Ghana yenye mamlaka ya kuzingatia na kutoa taarifa kwa Bunge kwa kuzingatia maudhui, na utoshelevu au vinginevyo wa GPRS. Tembelea: http://www.parlcent.ca/africa/ghana_desc_e.php

Tax Justice Network-Africa (TJN-A) ni mpango wa Afrika yote ulioanzishwa mwaka 2007 na mwanachama wa Mtandao wa Haki ya Kodi ya kimataifa. TJN inakusudia kuendeleza mifumo ya kijamii ya kodi, demokrasia na maendeleo katika Afrika, kutetea sheria za kodi kwa maskini na uimarishaji wa sheria za kodi na kukuza rasilimali za ndani. Tembea: http://www.taxjusticeafrica.net/

Tanzania Publish What You Pay ni mwakilishi wa mashirika ya kiraia ya Kusini mwa Afrika ambayo ni wanachama wa Publish What You Pay (PWYP) wa umoja wa kimataifa, ambao wanafanya kampeni kwa ajili ya usimamizi wa uwazi na uwajibikaji wa mapato ya mafuta, gesi na madini. tembelea: http://www.publishwhatyoupay.org/category/countries/tanzania

HakiMadini ni asasi ya kijamii na isiyokuwa ya kiserikali ilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2001 chini ya sheria ya jamii.Ilianza shughuli katika miaka ya 1990 kama kundi la wanaharakati kwa wachimba-madini wadogo.Tembelea, http://hakimadini.org/about-us/

Page 21: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

15

Page 22: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

Ushawishi Bungeni katika Tasnia ya Madini

16

Page 23: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi
Page 24: Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madiniswahili.policyforum-tz.org/files/AdvocacyManualSwahili.pdfMtandao wa Policy Forum, muungano wa asasi za kiraia zaidi ya 100, pia umefanya kazi

270 Kiko Avenue (Off Old Bagamoyo Rd), Mikocheni B,S.L.P 38486, Dar es Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2772611, Nukushi: +255 22 2701433, Simu ya kiganjani: +255 782 317434Barua pepe:[email protected], Tovuti:www.policyforum.or.tz

ISBN: 978-9987-708-04-8