27
Ukatili wa kijinsia na athari zake TAMWA

Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

  • Upload
    others

  • View
    22

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

Ukatili wa kijinsia na athari zake

TAMWA

Page 2: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

Kitabu hiki kimetolewa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)

kwa ufadhili wa DANIDA

TAMWA© 2017

S. L. P 8981, Sinza Mori, Dar es Salaam, Tanzania,Simu: +255 22 2772681, Nukushi: +255 22 2772681,

B. Pepe: [email protected],

: www.tamwa.org : TAMWA

: tamwaofficialpage : TAMWA_

: TAMWA TV

Yaliyomo

Nukuu ya Mkurugenzi wa TAMWA ....... 1

Utangulizi ............................................. 2

Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao

ya kijamii .............................................. 4

Ukatili wa kijinsia mitaani ...................... 6

Wanawake hustahili msaada kutoka kwa waume zao ........................................... 8

Ubakaji ................................................. 10

Vishawishi na ulaghai ............................ 12

Utumikishwaji wa watoto ..................... 14

Haki ya kuwa kiongozi .......................... 16

Kutelekeza familia ................................. 18

Kutelekeza familia nyakati za neema ...... 20

i ii

Page 3: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

1

Nukuu ya Mkurugenzi wa TAMWA

“Ukatili wa kijinsia ni uhalifu kama uhalifu mwingine. Ni lazima jamii iamke na kukataa kwa nguvu aina zote za ukatili wa kijinsia. Pia hakuna zawadi bora kwa mtoto kuliko elimu ... mzawadie sasa”.

Edda SangaMkurugenzi Mtendaji - TAMWA

Haki ya urithi ........................................ 22

Ukeketaji ............................................... 24

Huduma bora na uzazi salama ................ 26

Kipigo kwa mwanamke (1) ..................... 28

Kipigo kwa mwanamke (2) ..................... 30

Mjamzito ana haki ya kupumzika ............ 32

Haki ya elimu kwa mtoto ....................... 34

Ndoa katika umri mdogo ...................... 36

Upotoshaji wa kaulimbiu ........................ 38

Urithi wa mali na wajane ....................... 40

Elimu kuhusu masuala ya kijinsia ............. 42

Mimba katika umri mdogo ..................... 44

Ukatili haujali tabaka .............................. 46

iii

Page 4: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

2 3

Utangulizi

Msomaji,

Kitabu hiki kitakuwezesha kutambua maana na umuhimu wa kukomesha ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto. Pia kinatoa mifano ya aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia kama vile ubakaji, kutelekeza watoto, mimba za utotoni, vipigo na haki za watoto kupata elimu.

Ni mategemeo yetu kuwa, msomaji atajifunza vya kutosha, atatafakari na kisha kuchukua hatua stahiki dhidi ya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii yake.

Ukatili wa kijinsia ni nini?Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na kutishiwa maisha, kunyimwa uhuru, iwe hadharani au kwa kificho. Kupinga ukatili wa kijinsia ni wajibu!

Page 5: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

4 5

Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii

Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao haujajulikana vema kwa watu wengi. Ukatili huu huwakuta zaidi vijana wanaotumia vyombo vya habari vinavyohusisha mawasiliano ya kimtandao.

Ukatili wa kijinsia kwa njia ya mitandao unapotekelezwa husababisha athari nyingi hasa za kisaikolojia. Mtu anayetendewa ukatili huu huwa na hofu, wasiwasi, hukosa amani na furaha na pia husononeka na kukosa kujiamini. Mara nyingine muathirika anaweza hata kujidhuru.

Tumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya maendeleo na sio kuendeleza ukatili wa kijinsia.

Page 6: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

6 7

Ukatili wa kijinsia mitaani

Uchokozi kwa wanawake na wasichana mitaani ni ukatili wa kijinsia.

Mara nyingi wanawake na wasichana hudhalilishwa, huogopeshwa na hivyo hukosa kujiamini wawapo mitaani.

Kumbuka ...

Kila mtu ana haki ya kuwa huru mahali popote bila ya kubugudhiwa.

Kemea udhalilishaji wa wanawake na watoto mitaani.

Kunyamazia ukatili ni ukatili zaidi.

Mwanangu akizingua mtie bonge la bao

Oyaaa warembo hebu subirini hapo

Mhhh!!Naogopa

Huyu wangu tu

Page 7: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

8 9

Wanawake hustahili msaada kutoka kwa waume zao

Wanawake wengi hujikuta wanakabiliwa na majukumu mengi ya kifamilia bila usaidizi kutoka kwa waume zao.

Mwanamke asipopata ushirikiano wa mmewe katika majukumu ya nyumbani, huchoka, huwa na hasira, husongwa na mawazo na hukosa nafasi ya kushiriki katika masuala ya kijamii.

Ni wajibu kwa kila mwanaume kumsaidia mke wake majukumu ya nyumbani.

Page 8: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

10 11

Ubakaji

Ubakaji ni udhalilishaji wa kingono na pia ni ukatili wa kijinsia.

Mtu aliyebakwa hupata maumivu makali, huwa na msongo wa mawazo, hukosa kujiamini, huwa na hofu, huweza kupata maambukizi, na hujiona hafai katika jamii.

Piga vita ubakaji kwa kuwafichua wote wanaofanya vitendo hivi katika jamii.

Utafiti uliofanywa na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) unaonyesha kuwa kwa mwaka 2015 pekee jumla ya wanawake 5,902 walibakwa. Pia takwimu za jeshi la polisi zinaonyesha watoto 2,571 wa kike na wa kiume walibakwa na kulawitiwa katika kipindi cha miezi saba kuanzia January hadi July 2016.

Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha kamba matukio ya ubakaji, wakiwemo watoto yameongezeka kutoka 6,985 mwaka 2016 hadi 7,460 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 6.8.

Page 9: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

12 13

Vishawishi na ulaghai

Vishawishi na ulaghai kwa watoto wa kike ni ukatili wa kijinsia.

Umbali wa kwenda shuleni kwa wanafunzi ni tatizo kubwa, hasa kwa watoto wa kike.

Baadhi ya watoto hujikuta katika ushawishi na ulaghai hali inayosababisha kukata tamaa na kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata mimba na kuolewa katika umri mdogo.

Jamii inawajibu wa kutafakari na kuchukua hatua hasa kuongeza ulinzi kwa watoto.

Wazazi wana wajibu wa kufuatilia mienendo ya watoto wao.

Page 10: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

14 15

Utumikishwaji wa watoto

Utumikishaji wa watoto ni ukatili wa kijinsia.

Utumikishwaji wa watoto huwakosesha watoto haki zao za msingi, pia huwaathiri kisaikolojia na kimwili.

Kila mmoja wetu anawajibu wa kuzuia na kupinga utumikishaji wa watoto katika jamii yake.

Wape watoto haki zao zote!

Page 11: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

16 17

Haki ya kuwa kiongozi

Uongozi ni haki ya kila mtu bila kujali jinsia.

Maamuzi shirikishi yanayozingatia jinsia zote huleta amani, usawa na maendeleo kwa wote katika jamii.

Hakikisha wanawake wanashirikishwa katika kufanya maamuzi katika nyanja zote.

Page 12: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

18 19

Kutelekeza familia

Kutelekeza familia ni ukatili wa kijinsia.

Tabia hii husababisha chuki, maradhi na watoto kukosa haki zao za msingi.

Jukumu la malezi ya watoto ni la wazazi wote.

Page 13: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

20 21

Kutelekeza familia nyakati za neema

Wakati wa mavuno baadhi ya wanaume hutumia vibaya mali bila ya kutimiza mahitaji ya familia zao. Huu ni ukatili wa kijinsia kiuchumi.

Wanandoa washirikiane katika kupanga matumizi ya rasilimali za familia na mahitaji ya watoto yapewe kipaumbele katika mipango hiyo.

Page 14: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

22 23

Haki ya Urithi

Kugawana mali za marehemu bila ya ridhaa ya mjane ni ukatili wa kijinsia.

Kugawana mali za marehemu na kutelekeza familia yake husababisha familia kuwa na hali ngumu ya maisha. Vitendo kama hivi husababisha wajane kukata tamaa, kusononeka kuwa na chuki na hata visasi.

Hakikisha haki za wajane zinalindwa na kuheshimiwa.

Page 15: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

24 25

Ukeketaji

Ukeketaji ni kitendo cha kuondoa au kukata sehemu ya uke.

Ukeketaji husababisha maumivu makali ya kidonda, kutokwa na damu nyingi, kuzimia, maumivu ya kisaikolojia, kuziba kwa njia ya mkojo, kuchanika vibaya wakati wa kujifungua, kuchelewa kujifungua na kupata maambukizi ya magonjwa kama VVU, fistula, homa ya manjano na hata kifo.

Saidia kuelimisha jamii kuhusu athari za ukeketaji zinazotokana na mila na desturi hatarishi.

Utafiti uliofanywa na TDHS 2015/16 unaonyesha kuwa mwanamke mmoja kati ya 10 amekeketwa.

Page 16: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

26 27

Huduma bora na uzazi salama

Mazingira rafiki ya huduma za uzazi ni haki ya kila mwanamke.

Umbali mrefu kufikia huduma za afya husababisha wajawazito kujifungulia njiani, kukosa huduma bora na salama za uzazi na vifo vya mama wajawazito.

Shiriki katika vikao vya jamii kuhamasisha ujenzi wa zahanati.

Takwimu za serikali ya Tanzania za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa wajawazito 556 kati ya 100,000 hufariki kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali.

Theluthi 2 ya wanawake nchini Tanzania waliripotiwa kukutana na vikwazo mbalimbali katika kupata huduma za afya.

Page 17: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

28 29

Kipigo kwa mwanamke (1)

Kumpiga mwanamke ni unyanyasaji na udhalilishaji.

Kipigo husababisha chuki, woga, visasi na uhusiano mbaya ndani ya familia.

Mwanaume wa kweli hawezi kumpiga mwanamke. Mwanamke jasiri hutoa taarifa kuhusu vipigo.

Utafiti uliofanywa na TDHS unaonyesha kuwa kila wanawake 10 wanawake 3 wamewahi kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Na kwamba wanawake wa 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Page 18: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

30 31

Kipigo kwa mwanamke (2)

Kumpiga mwanamke ni ukatili wa kijinsia.

Kipigo huondoa upendo, furaha, ushirikiano mzuri katika familia, pia husababisha chuki, visasi kwa watoto na athari za kisaikolojia katika familia.

Mazungumzo na majadiliano ni njia bora ya kutatua migogoro.

Asilimia 58 ya wanawake na 40 ya wanaume wanakuibali kwamba ni sahihi mume kumpiga mke wake kwa sababu mbalimbali (TDHs 2015/2016).

Page 19: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

32 33

Mjamzito ana haki ya kupumzika

Kumpa majukumu mengi mjamzito ni ukatili wa kijinsia.

Kazi ngumu kwa mjamzito huweza kusababisha kuharibika kwa mimba na matatizo mengine ya kiafya.

Mjamzito apunguziwe majukumu na apewa muda wa kutosha kupumzika.

Page 20: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

34 35

Haki ya elimu kwa mtoto

Elimu ni haki ya mtoto wa kike na wa kiume.

Kumyima elimu mtoto wa kike ni ukatili wa kijinsia.

Hali ya mtoto wa kike kukosa elimu huchagiza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ongezeko la unyanyasaji kwa watoto kike.

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inaeleza kwamba ni jukumu la mzazi, mlezi au mtu yeyote anayeishi na mtoto kumpa haki ya elimu na kujifunza.

Mpe mtoto wa kike elimu umkomboe na vitendo vya ukatili wa kijinsia. Hakuna zawadi bora kwa mtoto kuliko elimu ... mzawadie sasa!

Page 21: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

36 37

Ndoa katika umri mdogo

Ndoa za utotoni ni ukatili wa kijinsia.

Pia ndoa za utotoni ni ubakaji.

Athari za ndoa katika umri mdogo ni pamoja na kukosa elimu, matatizo wakati wa kujifungua, kuelemewa na majukumu, kukosa haki ya maamuzi, mimba za utotoni na hata tatizo la fistula.

Usiruhusu mtoto wa kike kupoteza afya yake, fursa ya kupata elimu na kufurahia utoto wake kwa kumuingiza katika ndoa akiwa na umri mdogo.

Page 22: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

38 39

Upotoshaji wa kaulimbiu

Mapokeo mabaya ya kauli mbiu yanaweza kutumika kuhalalisha vitendo viovu vya ukatili wa kijinsia.

Tabia hii husababisha ukatili wa kijinsia kuonekana ni jambo linalokubalika katika jamii.

Kemea tafsiri mbaya na zinazochochea ukatili wa kijinsia.

Page 23: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

40 41

Urithi wa mali na wajane

Desturi ya kurithi mali za marehemu na wajane ni ukatili wa kijinsia.

Ukatili huu unaweza kusababisha umasikini katika familia husika. Hali kadhalika wajane hukata tamaa ya maisha, hujenga chuki, visasi, msongo wa mawazo na matatizo ya kisaikolojia.

Tambua, mali za marehemu ni haki ya familia yake.

Page 24: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

42 43

Elimu kuhusu masuala ya kijinsia

Jamii nyingi hazijapati elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.

Viongozi wa jamii na Waragabishi wana wajibu mkubwa wa kuielimisha jamii kuhusu sababu aina na athari za ukatili wa kijinsia. Wanufaika wa elimu hii wanao mchango mkubwa katika kubadilisha mitazamo na matendo ya wanajamii wengine. Kwa ushirikiano huo tunaweza kubadilisha mitazamo ya wanajamii kuhusu usawa wa kijinsia.

Saidia kuwaelimisha ndugu, jamaa na marafiki kuhusu madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia.

Page 25: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

44 45

Mimba katika umri mdogo

Mimba za utotoni ni kikwazo cha maendeleo kwa mtoto wa kike.

Mara nyingi athari za mimba za utotoni huathiri kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

Utafiti uliofanywa na TDHS unaonyesha tatizo la mimba za utotoni nchini limeongezeka kutoka asilimia 23% mwaka 2010 hadi kufikia 27% mwaka 2016/17.

Hali hii hukutokana na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19.

Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni.

Page 26: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

46 47

Ukatili haujali tabaka

Je. wanawake na wasichana kutoka katika familia zenye hali nzuri ya kiuchumi pia huathiriwa na ukatili wa kijinsia?

Watu wengi hudhani kuwa wanawake na wasichana kutoka katika familia zenye ukwasi hawana matatizo na wana uhuru sana. La hasha!

Kwa uzoefu wa TAMWA, kundi hili pia linakutana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ukatili unaotokea nyumbani, kazini, mitandaoni na hata barabarani au mitaani.

Tushiriki kupinga ukatili wa kijinsia kwani hauchagui tabaka la mtu.

Page 27: Ukatili wa kijinsia na athari zakekwa vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19. Hakikisha unamsaidia mtoto wa kike kuepuka mimba za utotoni. 46 47 Ukatili haujali tabaka Je. wanawake

48

S. L. P 8981, Sinza Mori, Dar es Salaam, Tanzania,Simu: +255 22 2772681, Nukushi: +255 22 2772681,

B. Pepe: [email protected], Tovuti: www.tamwa.org