3
UCHUMI WA KANDA YA ZIWA MIKONONI MWA WACHENJUAJI DHAHABU KWA NJIA YA MFYONZO Kwa asili wakazi wa kanda ya ziwa ni wafugaji na wavuvi.Baada ya ujio wa Wajerumani na baadae Waingereza, wakazi wa Kanda ya ziwa walianza shughuli ya uchimbaji madini katika migodi ya Wajerumani na Waingereza. Baada ya kufahamu ujuzi wa kuchimba na kuchenjua dhahabu, wakazi wa kanda ya ziwa wamebobea katika shughuli hiyo hadi hii leo.Shughuli hizo za Madini kwa kanda ya ziwa zimeendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi. Mwishoni mwa miaka ya tisini, uwekezaji katika migodi mikubwa ulianza nchini.Baada ya kuanza kwa uwekezaji huo,maeneo mengi ya wachimbaji wadogo wadogo yalichukuliwa.Inasadikiwa zaidi ya wachimbaji 150,000 waliondoka maeneo ya Lusu Nzega baada ya kuanza kwa Mgodi wa Resolute.Aidha maeneo ya namba tisa na bulyanhulu halikadhalika kiasi kama hicho cha wachimbaji wadogo waliondoka baada ya eneo kuchukuliwa na mgodi wa Kahama Mining kipindi hicho. Taarifa ya ILO inakadiria barani Africa kuna zaidi ya Wachimbaji wadogo wa Madini ya metali wafikiao

Uchumi Wa Kanda Ya Ziwa Mikononi Mwa Wachenjuaji Dhahabu Kwa Njia Ya Mfyonzo

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Wataalamu tushiriki kuanzisha VAT Leaching ili ziwe sehemu ya mafunzo kwa wananchi kama ilivyo katika kilimo-shamba darasa.

Citation preview

UCHUMI WA KANDA YA ZIWA MIKONONI MWA WACHENJUAJI DHAHABU KWA NJIA YA MFYONZOKwa asili wakazi wa kanda ya ziwa ni wafugaji na wavuvi.Baada ya ujio wa Wajerumani na baadae Waingereza, wakazi wa Kanda ya ziwa walianza shughuli ya uchimbaji madini katika migodi ya Wajerumani na Waingereza.Baada ya kufahamu ujuzi wa kuchimba na kuchenjua dhahabu, wakazi wa kanda ya ziwa wamebobea katika shughuli hiyo hadi hii leo.Shughuli hizo za Madini kwa kanda ya ziwa zimeendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi.Mwishoni mwa miaka ya tisini, uwekezaji katika migodi mikubwa ulianza nchini.Baada ya kuanza kwa uwekezaji huo,maeneo mengi ya wachimbaji wadogo wadogo yalichukuliwa.Inasadikiwa zaidi ya wachimbaji 150,000 waliondoka maeneo ya Lusu Nzega baada ya kuanza kwa Mgodi wa Resolute.Aidha maeneo ya namba tisa na bulyanhulu halikadhalika kiasi kama hicho cha wachimbaji wadogo waliondoka baada ya eneo kuchukuliwa na mgodi wa Kahama Mining kipindi hicho.Taarifa ya ILO inakadiria barani Africa kuna zaidi ya Wachimbaji wadogo wa Madini ya metali wafikiao zaidi ya milioni moja na nusu.

Maeneo mengine ya Buhemba na Nyangoto Mkoni Mara yalikumbwa na kadhia hiyo.Baada ya hali hii kujitokeza, wakazi wa kanda ya ziwa hasa vijana waliamua kupata ajira katika migodi mikubwa na watu wazima kuhamia katika shughuli za Uvuvi.Hivyo basi shughuli za wachimbaji wadogo kanda ya ziwa wanaokadiriwa kufikia 600,000 waliacha shughuli hiyo kutokana na sababu tajwa.Mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 shughuli za wachimabji wa dogo zilipungua sana na shughuli ya Uvuvi ikashamiri sana kanda ya ziwa.Kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea shughuli za uvuvi zikapambamoto na biashara ya samaki ikatawala kanda ya ziwa.Baada ya kushamiri sana makampuni ya nje yalianza kununua samaki na pia viwanda vya ndani vya kusindika samaki vikafunguliwa jijini Mwanza.Ni katika kipindi hiki tutakumbuka ilianza pia biashara ya mapanki ya samaki.Mpaka sasa biashara ya samaki inaendelea na samaki kwa wakazi wa kanda ya ziwa imekuwa ni bidhaa ya ghali sana baada ya wenye viwanda kuleta vifaa vya kisasa vya kuvulia na hivyo wavuvi wadogo kukosa samaki.Miaka ya 2009 na kuendelea mzunguko wa shughuli za uchimaji Madini kwa wachimbaji wadogo ulianza kurejea baada ya shughuli za uvuvi kwa wakazi kuwa mgumu kutokana na wenye viwanda kuwa na vifaa vya kisasa ama kukodi mitumbwi na nyavu kwaajili ya kupata samaki za viwandani tu.Wavuvi waliamua kurejea kwenye shughuli za uchimbaji wa Madini ya metali hususni dhahabu. Aidha katika kipindi hiki ilijitokeza tekinolojia mpya ya uchenjuaji wa dhahabu iitwayo VAT LEACHING TECHNOLOGY kwa kiingereza na Kiswahili twaweza ita TEKINOLOJIA YA MFYONZO WA DHAHABU ..Uchejuaji dhahabu kwa njia ya mfyonzo (tafasiri ya mwandishi).Tekinolojia hii iliingia nchini kwa kuanzia kanda ya Ziwa ikitokea Zimbabwe.Baadhi ya wazimbabwe waliokuja kufanyakazi katika migodi mikubwa waliona fursa ya tekinolojia hii kufanywa na wachimbaji wadogo na kati.Waanzilishi wa awali kwa maelezo ya wakazi hao ni BARAKA AND CHACHA COMPANY LTD.Tekinolojia ya uchejuaji dhahabu kwa mfyonzo ni shughuli yenye uhakika na inaoshikilia uchumi wa kanda ya ziwa.Itaendelea wiki ijayo kwa kuelezea nini hasa uchejuaji dhahabu kwa njia ya mfyonzo.