Upload
lenhi
View
431
Download
9
Embed Size (px)
Citation preview
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
UCHAGUZI WA RAIS WA ZANZIBAR, WAJUMBE WA BARAZA LA
WAWAKILISHI NA MADIWANI 2015
Kimetolewa na:
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
Septemba 2015
1
MAELEKEZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
SALAMU ZA MKURUGENZI
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itaendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 siku ya
Jumapili tarehe 25 Oktoba 2015. Uchaguzi huo utatoa fursa kwa Wazanzibari kumchagua
Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani. Kwa kuwa kazi hiyo
huambatana na mambo mengi sana yanayopaswa kutekelezwa kwa uhakika na kila
atakayekabidhiwa majukumu katika uchaguzi mkuu huo, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
imeandaa maelekezo yatakayotumiwa kama mwongozo wa kazi hiyo kwa Wasimamizi wa
vituo vya kupigia kura watakaoteuliwa kwa kazi hii.
Madhumuni ya Maelekezo haya ni kuwaongoza Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura ili
waweze kutekeleza vizuri majukumu yao katika vituo watakavyopangiwa kufanya kazi.
Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wanashauriwa wayasome maelekezo haya kwa
makini pamoja na Sheria ya Uchaguzi Nambari 11 ya 1984 na Kanuni za Uchaguzi, 2015.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakuwa karibu sana Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura
ili kuufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR
ZANZIBAR
2
1. UTEUZI WA WASIMAMIZI VITUO VYA KUPIGIA KURA
Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, watateuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi kwa
mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Nam. 11 ya 1984, kifungu cha 63(b) na (c).
Taratibu zifuatazo zitazingatiwa katika uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura
na Wasaidizi wao:
i. Kutangaza nafasi ili wenye sifa zinazostahili waombe.
ii. Kuwafanyia usaili waombaji wote wenye sifa.
iii. Kutangaza majina ya waombaji walioteuliwa.
iv. Kutoa nafasi kwa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi kutoa pingamizi kama
wanazo katika muda usiozidi siku nne.
v. Kufanya uteuzi rasmi, na watakaoteuliwa wajaze fomu za mkataba wa ajira. Idadi
ya walioteuliwa ilingane na mahitaji.
2. MAJUKUMU YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wanateuliwa kwa lengo la kusimamia shughuli
mbalimbali za upigaji kura katika vituo ambavyo wanavisimamia kwa kazi hiyo. Kwa hivyo
ili kulitekeleza jukumu hilo kwa usahihi wanawajibika kufanya mambo yafuatayo katika
kazi zao:-
i. Kuhakikisha katika vituo wamepatiwa vifaa vyote vinavyohusika na upigishaji wa
kura;
ii. Kuhakikisha hali ya amani na utulivu katika kituo;
iii. Kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji wa kura katika kituo linaendeshwa kwa kufuata
Sheria za uchaguzi, Kanuni na Sheria nyengine zinazohusiana na uchaguzi.
iv. Kuhakikisha kuwa wapiga kura walioandikishwa katika kituo anachosimamia
wanaopatiwa nafasi ya kupiga kura;
v. Kuhakikisha kwamba kura zilizopigwa katika kituo anachokisimamia zinahesabiwa
kwa njia ya uadilifu na utaratibu sahihi;
vi. Kuhakikisha kuwa anabandika fomu ya matokeo ya kituo baada ya kukamilika kazi
ya kuhesabu kura;
3
vii. Kuhakikisha kuwa anawasilisha mara moja kwa Msimamizi wa Uchaguzi fomu ya
matokeo ya kura ya kituo alichokisimamia;
viii. Kuhakikisha kuwa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji na kuhesabu kura
anaorodhesha vifaa vyote vilivyobakia katika kituo na kuikabidihi orodha kwa
Msimamizi wa Uchaguzi kwa uthibitisho; na
ix. Atafanya kazi yoyote inayohusiana na shughuli za uchaguzi kama atakavyopangiwa
na Msimamizi wa Uchaguzi.
3. WATENDAJI WA UCHAGUZI NDANI YA VITUO VYA KUPIGIA KURA
Kwa ajili ya kurahihisha kazi za upigishaji kura kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na
watendaji wafuatao:-
i. Msimamizi wa Kituo (Presiding Officer - PO);
ii. Msimamizi Msaidizi wa Kituo Namba 1 (Polling Assistant 1 – PA1);
iii. Msimamizi Msaidizi wa Kituo Namba 2 (Polling Assistant 2 – PA2).
iv. Mwongozaji wa wapiga kura (Direction Clerk – DC)
4. MSIMAMIZI WA KITUO (PO)
Atakuwa na kazi ya kusimamia shughuli zote za uchaguzi ndani ya kituo. Atakuwa ni
dhamana wa masuala yote yatakayojitokeza na yanayohitajia kutekelezwa ndadi ya kituo
cha kupigia kura. Pamoja na majukumu hayo, Msimamizi wa Kituo atahakikisha kuwa
majina ya wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura la kituo anachokisimamia
yameorodheshwa. Atawajibika kuchunguza kwa uangalifu maelezo (taarifa za mpiga
kura) kwenye shahada yake kujiandikisha ya kujiandikisha.
Kabla ya kutoa maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi, Msimamizi wa Kituo, anawajibika
kukikagua KIDOLE CHA SHAHADA cha mkono wa kushoto cha mpiga kura ili kupata
uthibitisho kuwa mpiga kura huyo anapiga kura yake mara ya kwanza. Pia atamtaka
mpiga kura huyo kuonyesha mikono yake ili kuwathibithishia mawakala na waangalizi
waliopo kama mpiga kura huyo hajapiga kura. Iwapo alama ya wino itaonesha katika
4
vidole au katika sehemu nyengine ya mpiga kura huyo, Msimamizi wa Kituo atamtaka
kueleza sababu ya wino huo. Iwapo hakuridhika atampeleka kwa mpiga kura kwa
Msimamizi wa eneo la kupigia kura ambaye ataishughulikia hali hiyo.
Baada ya Msimamizi wa kituo kuridhika na taarifa za mpiga kura katika Daftari la Kudumu
la kituo anachokisimamia, atasoma kwa sauti kubwa kiasi cha kuwa mawakala walioomo
katika kituo waweze kusikia jina la mpiga kura huyo na ataweka alama ya √ (vyema au
tiki) kwenye picha ya mpiga kura ndani ya Daftari la Wapiga Kura kuashiria kuwa mpiga
kura huyo tayari amepiga kura.
5. MSIMAMIZI MSAIDIZI WA KITUO NAM. 1 (PA 1)
Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nam. 1 atakuwa na jukumu la kutoa karatasi za kura kwa
wapiga kura waliothibitishwa na Msimamizi wa Kituo. Baada ya mpiga kura kuelekezwa
kwake atafanya mambo yafuatayo:-
i. Atakata kutoka katika kitabu karatasi ya kupigia kura;
ii. Atamuelekeza mpiga kura namna ya kukunja karatasi ya kura yaani, kwanza kwa
mapana, kisha nusu na nusu tena;
iii. Atagonga muhuri wa kituo cha kupigia kura juu ya pande zote mbili za karatasi ya
kura iliyokunjwa kwa namna ambayo muhuri utaweza kuonekana.
iv. Atampa mpiga kura karatasi ya kura na kumwelekeza:-
• Kwenda kwenye Kituturi cha kupigia kura na kuweka alama ya “√” ndani ya
chumba kilichowekwa chini ya picha ya mgombea anayemtaka;
• Baada ya kuweka alama, aikunje karatasi ya kupigia kura na kuitumbukiza
kwenye sanduku la kura ambalo mfuniko wake una rangi inayofanana na rangi
ya karatasi ya kura aliyonayo mkononi.
Endapo Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nambari 1 anahisi kuwa mpiga kura huyo anahitaji
kusaidiwa katika kupiga kura, atawasiliana na Msimamizi wa Kituo kabla ya kumpa
karatasi ya kupigia kura.
5
6. MSIMAMIZI MSAIDIZI WA KITUO NAM. 2 (PA 2)
Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nam. 2 atakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa kila mpiga
kura anayemaliza kupiga kura amewekwa alama ya wino usiofutika katika kidole KIDOLE
CHA SHAHADA cha mkono wa kushoto cha mpiga kura. Msaidizi Msimamizi kabla ya
kumpaka wino mpiga kura atahakikisha kuwa mpiga kura huyo anafuta kidole
kinachohitajika kuwekwa wino usiofutika ili kuondoa kitu kitakachozuia wino kufika katika
sehemu za kidole zinazokusudiwa.
7. MWONGOZAJI WA WAPIGA KURA (DC)
Katika kila eneo la kupigia kura kutakuwa na waongozaji wa wapiga kura kulingana na
idadi ya vituo vya kupigia kura vilivyopo katika eneo husika. Kazi ya waongoza wapiga
kura katika eneo la kupigia kura ni kuwaelekeza wapiga kura katika vyumba ambavyo
wanastahiki kupiga kura na kujipanga katika mistari kulingana na wingi wa wapiga kura
watakaokuwepo vituoni.
Vile vile, atawajibika kuwasaidia wapiga kura ambao ni walemavu, akinamama
wajawazito, wagonjwa, wazee, ili waweze kupewa kipaumbele cha kupiga kura mapema
kama ambavyo atakuwa ameelekezwa na Tume ya Uchaguzi. Atashirikiana pia na
watendaji wa kituo na mlinzi wa kituo katika kufanikisha shughuli za upigaji kura katika
kituo alichopangiwa. Kwa kila kituo cha kupigia kura katika eneo la kupigia kura kutakuwa
na mwongozaji mistari mmoja.
8. MSIMAMIZI WA ENEO LA KUPIGIA KURA
Katika kila eneo la kupigia kura (Polling Centre) Msimamizi wa Uchaguzi atateua mtu
mmoja kuwa Msimamizi wa eneo la kupigia kura. Msimamizi wa eneo la kupigia kura,
atakuwa na kazi ya kuwasaidia Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura vilivyomo katika
eneo kuyapatia ufumbuzi wa haraka matatizo yote ambayo yanatokea katika vituo vya
kupigia kura vya eneo analolisimamia. Msimamizi Msaidizi eneo atakuwa ni kiungo kati ya
Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura vya eneo analolisimamia na Msimamizi wa
6
Uchaguzi wa Jimbo.
Katika utendaji wake wa kazi atakuwa akimpatia Msimamizi wa Jimbo taarifa zote
kuhusiana na kazi ya upigishaji kura katika eneo analolisimamia ikiwemo namna
alivyosaidiana na Msimamizi/Wasimamizi wa Vituo kusawazisha matatizo/ upungufu wa
vifaa katika vituo anavyovisimamia, hali ya upigaji wa kura, mahudhurio ya wapiga kura,
usalama na utulivu wa eneo la kupigia kura kwa ujumla wake.
9. VIFAA VYA KITUO CHA KUPIGIA KURA
Kila Msimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura atakabidhiwa vifaa ili aweze kutekeleza
majukumu yake ya kupigisha kura katika kituo cha kupigia kura kwa ufanisi. Msimamizi
wa Kituo ni lazima ahakikishe kuwa anayaelewa na kuyazingatia maelekezo yote
atakayopewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo juu ya matumizi ya vifaa hivyo katika
kituo cha kupigia kura. Hivyo, ni jukumu lake pia kuhakikisha kuwa anapatiwa vifaa vya
kutosha vinavyohitajika katika kituo cha kupigia kura. Msimamizi wa kituo atakabidhiwa
vifaa hivyo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo kwa maandishi. Vifaa hivyo ni
vifuatavyo:-
Vifaa vinavyohitajika kutumiwa na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura ni:-
Nam. Vifaa Matumizi
1. Masanduku ya kupigia kura
Masanduku yenye mifuniko
myeupe
Hutumika kwa kupigia kura kwa
uchaguzi wa Rais
Masanduku yenye mifuniko myeusi Hutumika kwa kupigia kura kwa
uchaguzi wa Diwani
Masanduku yenye mifuniko ya
buluu
Hutumika kwa kupigia kura kwa
uchaguzi wa Mwakilishi
2. Vitabu vya Karatasi za kura
7
Nam. Vifaa Matumizi
Vitabu vya Karatasi za Kura
ambavyo karatasi zake kwa nyuma
zitakuwa na mistari myeupe na
waridi.
Hutumika kumpigia kura Mgombea
Urais.
Vitabu vya Karatasi za Kura
ambavyo karatasi zake kwa nyuma
zitakuwa na mistari myeupe na
buluu.
Hutumika kumpigia kura Mgombea
Uwakilishi.
Vitabu vya Karatasi za Kura
ambavyo karatasi zake kwa nyuma
zitakuwa na mistari myeupe na
myeusi.
Hutumika kumpigia kura Mgombea
Udiwani.
3. Muhuri wa Kituo Hutumika kugonga nyuma ya karatasi
ya kura kabla kukabidhiwa mpiga kura.
Pia hutumika katika nyaraka nyengine
zinazotumika kituoni.
4. Wino usiofutika Hutumika kumpaka mpiga kura kwenye
kidole cha shahada cha mkono wa
kushoto baada ya kumaliza kupiga kura.
5. Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura wa kituo cha kupigia kura
Hutumika kuthibitisha wapiga kura
wanaostahiki kupiga kura katika kituo
anachokisimamia kwa kulinganisha na
taarifa za mpiga kura zilizomo katika
shahada yake ya kupigia kura.
6. Kibati cha wino wa muhuri Hutumika kwa ajili ya muhuri wa kituo
7. Bahasha za Kituo Hutumika kuhifadhia vifaa na nyaraka
mbalimbali zinazotumika katika kituo
cha kupigia kura
8
Nam. Vifaa Matumizi
8.
Vifungio vya plastiki vya kufungia masanduku
Vifungio vya Rangi Nyeupe Kufungia sanduku la Kura la Urais
Vifungio vya Rangi ya Buluu Kufungia sanduku la Kura la Uwakilishi
Vifungio vya Rangi Nyeusi Kufungia sanduku la Kura la Udiwani
Vifungio vya Rangi Nyekundu Kufungia sanduku la vifaa vya Kura
ANGALIZO
Vifungio vya plastiki vya kufungia masanduku ya kupigia kura (seals)
hutumika kufungia masanduku ya kura kabla ya kuanza kazi ya kupiga kura
na baada ya kukamilika kazi ya kuhesabu kura kituoni.
10. Utepe wa gundi (Cellotape) Hutumika kwa kubandikia au kufungia
vitu mbalimbali kituoni
11. Karatasi za kukaushia
(Tissues)
Hutumika kwa ajili ya kusafishia mikono
ya wapiga kura au kaushia wino.
12. Mkasi Hutumika kwa kukatia vifungio vya
masanduku (seals)
13. Karatasi za kuandikia Hutumika kwa kuandikia kumbukumbu
za matukio yanayojitokeza katika kituo
cha kupigia kura.
14. Kalamu Hutumika kwa kiandikia taarifa
mbalimbali za kituo cha kupigia kura.
Vile vile hutumika kwa kupigia kura
15.a Bango la Kituo cha Kupigia
Kura
Hutumika kutambulisha kituo cha
kupigia kura na linatakiwa libandikwe
nje ya kituo kabla ya kituo kufunguliwa
15.b Bango la Kituo cha Kuhesabia
Kura
Hutumika kutambulisha kituo cha
kuhesabia kura na linatakiwa libandikwe
nje ya kituo kabla ya kuanza kuhesabu
kura
9
Nam. Vifaa Matumizi
16. Mistari (Rulers) Hutumika kwa matumizi mbalimbali ya
kituo ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa
usahihi majina ya wapiga kura katika
Daftari la Kudumu la wapiga kura la
kituo.
Pia hutumika kwa kuchania karatasi za
kura.
17. Karatasi za kura za mfano kwa
wagombea Urais, Uwakilishi na
Udiwani
Hutumika kuwatambulisha wagombea
kwa kuonyesha majina yao, picha na
nembo za vyama vyao.
18. Taa na Betri zake Hutumika katika kituo cha kupigia na
kuhesabia kura inapotokezea haja ya
matumizi yake.
19. “Tactile Ballot Papers
Template”
Rais, Mwakilishi na Diwani
Hutumika kuwawezesha wapiga kura
wasioona kupiga kura bila ya kusaidiwa.
20. Vituturi (Polling Booths) Hutumika kwa ajili ya kuandaa sehemu
ya faragha ili kumwezesha wapiga kura
kupiga kura zao kwa siri kituoni
21. Kitabu cha Fomu mbalimbali za Kituo cha kupigia kura ambacho
ndani yake mna fomu zifuatazo:-
i. Kumbukumbu ya mahudhurio ya
Msimamizi na Wasaidizi
Wasimamizi wa kituo cha kupigia
kura Nam. PS 2
Hutumika kwa ajili ya kuchukua taarifa
za Msimamizi na Wasaidizi Wasimamizi
wa kituo cha kupigia kura wanapowasili
kituoni na wanapoondoka kituoni baada
ya kuhesabiwa kwa kura
ii. Shahada ya kufungua kituo cha
kupigia kura Nam. PS 3
Hutumika kuthibitisha muda ambao
kituo cha kupigia kura kimefunguliwa
10
Nam. Vifaa Matumizi
iii. Shahada ya kufunga kituo Nam. PS
8
Hutumika kwa uthibitisho wa kufunga
kituo cha kuhesabia kura
iv. Kumbukumbu ya Vifungio vya
masanduku na mihuri ya kituo
iliyopokelewa Nam. PS 4
Hutumika kuthibitisha idadi ya vifungio
vya masanduku ya kura vilivyopokelewa
katika kituo cha kupigia kura
v. Kumbukumbu ya vifungio
vilivyotumika (Vilivyowekwa na
kuondolewa katika sanduku la kura
la):-
o Urais Fomu Nam. PS 5A
o Uwakilishi Fomu Nam. PS 5B
o Udiwani Fomu Nam. PS 5C
Ni kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya
vifuniko vinavyotumika kwa ajili
kufunga na kufungua masanduku ya
wagombea Urais, Uwakilishi na Udiwani
katika kituo cha kupigia kura
vi. Hesabu ya Karatasi za Kura vituoni
kwa:-
o Urais Nam. PS 7A
o Uwakilishi Nam. PS 7B
o Udiwani Nam. PS 7C
Ni kwa ajili ya kuwekea kumbukumbu
ya hesabu ya karatasi za kura
zilizopokelewa na zilizotumika katika
kituo cha kupigia kura kwa Urais,
Uwakilishi na Udiwani
vii. Taarifa ya Kura za kila mgombea
baada ya hesabu ya kituo kwa:-
o Urais Fomu Nam. PS 12A
o Uwakilishi Fomu Nam. PS 22B
o Udiwani Fomu Nam. PS 32C
Hutumika kuchukulia matokeo ya kura
za wagombea ya kituo kimoja kimoja
katika jimbo kwa wagombea wa Urais,
Uwakilishi na Udiwani
viii. Orodha ya Wapiga Kura
waliosaidiwa kupiga kura Fomu
Nam. PS 6
Hutumika kuweka kumbukumbu ya
watu waliosaidiwa kupiga kura na watu
waliofuatana nao
ix. Shahada ya kufungua kituo cha
kuhesabia kura Fomu Nam. PS 9
Hutumiwa kuwekea kumbukumbu kwa
Uthibitisho wa kufungua kituo cha
kuhesabia kura
11
Nam. Vifaa Matumizi
x. Shahada ya kufunga kituo cha
kuhesabia kura Fomu Nam. PS 10
Hutumiwa kuwekea kumbukumbu kwa
Uthibitisho wa kufunga kituo cha
kuhesabia kura
23. Bahasha mbali mbali za kituo cha kupigia kura
i. Bahasha Nam. 2A, 2B na 2C Hutumika kuhifadhia vishina vya vitabu
vya Karatasi za kura zilizotumika.
- 2A kwa Uchaguzi wa Rais
- 2B kwa uchaguzi wa Mwakilishi
- 2C kwa Uchaguzi wa Diwani
ii. Bahasha Nam. 3A, 3B na 3C Hutumika kuhifadhia vishina vya
Karatasi za kura ambazo hazikutumika
pamoja na zilizoharibika.
- 3A kwa Uchaguzi wa Rais
- 3B kwa uchaguzi wa Mwakilishi
- 3C kwa Uchaguzi wa Diwani
iii. Bahasha Nam. 4 Hutumika kuhifadhia Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura, shahada za Watumishi
wa Uchaguzi na shahada maalum
iv. Bahasha Nam. 5A, 5B na 5C Hutumika kuhifadhia kura zenye
mgogoro kama zitakuwepo.
- 5A kwa Uchaguzi wa Rais
- 5B kwa uchaguzi wa Mwakilishi
- 5C kwa Uchaguzi wa Diwani
v. Bahasha Nam. 6A, 6B na 6C Hutumika kuhifadhia kura zilizokataliwa
kama zitakuwepo.
- 6A kwa Uchaguzi wa Rais
- 6B kwa uchaguzi wa Mwakilishi
- 6C kwa Uchaguzi wa Diwani
12
Nam. Vifaa Matumizi
vi. Bahasha Nam. 7A, 7B na 7C Hutumika kuhifadhia Kura halali za
wagombea.
- 7A kwa Uchaguzi wa Rais
- 7B kwa Uchaguzi wa Mwakilishi
- 7C kwa Uchaguzi wa Diwani
Angalizo:
Vifaa vifuatavyo vitatakiwa viorodheshwe baada ya kukamilika kwa kazi ya kuhesabu kura
na akabidhiwe Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo. Hivyo ni vyema kukawa na umakini wa
hali ya juu katika utunzwaji wake. Vifaa hivyo ni vifuatavyo:-
i. Masanduku ya Kura;
ii. Karatasi za Kura;
iii. Fomu za malalamiko;
iv. Fomu za matokeo ya Uchaguzi;
v. Mihuri ya Kituo;
vi. Uniform za watendaji (Vikoti);
vii. Taa;
viii. Kitabu cha fomu mbalimbali
10. MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA SIKU YA KUPIGA KURA
Siku ya kupiga kura, kituo cha kupigia kura huwa na kazi nyingi ambazo zinahitajia
kufanywa mapema sana na kwa wakati ili kuuwezesha upigaji kura katika kituo kufanyika
kwa ufanisi. Hivyo, kabla ya siku ya kupiga kura, Msimamizi wa Kituo anawajibika
kutekeleza mambo muhimu yafuatayo:-
i. Kuhakikisha kwamba amekabidhiwa vifaa vyote vya kupigia kura vinavyohitajika kwa
kituo alichopangiwa kusimamia upigishaji wa kura na kuvihakiki kama inavyojionesha
Fomu maalum iliyowekwa katika kitabu cha Fomu mbalimbali.
ii. Kuhakikisha kuwa amepatiwa kitabu cha fomu mbalimbali za kituo cha kupigia kura.
13
iii. Kuhakikisha kuwa amezipanga vizuri fomu zote zinazohitajia kujazwa na wahusika
(mawakala) kabla ya kuanza kwa kazi ya upigaji wa kura.
iv. Kuhakikisha kuwa anavitunza vifaa vyote alivyokabidhiwa katika sehemu salama hadi
siku ya upigaji wa kura.
v. Kuhakikisha kuwa amepatiwa majina ya mawakala watakaokuwemo katika kituo cha
wapiga kura kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
vi. Kuhakikisha kuwa kuna utaratibu utakaomwezesha kila Msimamizi Msaidizi wa Kituo
chake kufika kituoni na kuondoka kwa wakati baada ya kukamilika kwa kazi ya
kuhesabu kura.
Baada ya kuwa amepanga vizuri utaratibu mzima wa shughuli ya upigaji kura katika kituo,
Msimamizi wa kituo kabla ya kuanza upigishaji wa kura atampatia kila wakala ambaye
atakuwa kituoni Fomu Nam. PS 03 ili ajaze kuonyesha kuridhika au kutoridhika kwake na
maandalizi ya kituo cha kupigia kura. Wakala atatakiwa kutoa sababu iwapo hataridhika
na maandalizi ya kituo. Msimamizi wa kituo atapaswa kuonyesha jinsi alivyoyashughulikia
malalamiko hayo kama yapo.
Angalizo:
Kwa kuwa nafasi iliyopo katika fomu hii ni ndogo mno kutoa maelezo mengi, tumia nafasi
iliyowekwa katika kitabu cha fomu mbalimbali kujaza sababu za kutoridhika kwa wakala
na matayarisho ya kituo. Katika karatasi hiyo ya ziada ataandika jina lake, chama chake
na kuweka saini yake.
11. DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la kituo lenye
orodha ya wapiga kura wote wanaostahiki kupiga kura katika kituo hicho. Ni Daftari la
kudumu la wapiga kura lililotayarishwa na Tume pekee ndilo linalopaswa kutumika kwa
shughuli za upigishaji wa kura kituoni. Mawakala wa upigaji kura wameruhusika kuingia
na Daftari la wapiga kura katika kituo cha kupigia kura.
14
12. UPANGAJI WA KITUO CHA KUPIGIA KURA
Vituo vya kupigia kura hupangwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushauriana na
Msimamizi wa Uchaguzi. Katika kupanga kituo cha kupigia kura Msimamizi wa Kituo
anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:-
i. Kupanga meza ya Msimamizi wa Kituo kumwezesha kuangalia majina ya wapiga
kura katika Daftari la wapiga kura wakati wanapofika kituoni bila ya matatizo.
ii. Kupanga meza ya Msimamizi Msaidizi wa Kituo Nambari 1 ambaye atakuwa na
jukumu la kutoa na kupiga muhuri karatasi za kura.
iii. Kupanga meza ya Msimamizi Msaidizi wa kituo Nambari 2 ambaye atakuwa na kazi
ya kupaka wino usiofutika kwa wapiga kura wanapomaliza kutumbukiza kura
katika masanduku ya kupigia kura.
iv. Kupanga sehemu ya faragha ambayo itatumika kuweka kituturi kwa ajili ya kupiga
kura.
v. Kuandaa sehemu nzuri ya wazi ndani ya kituo kwa ajili ya kuweka sanduku la kura
na
vi. Kupanga sehemu maalum kwa ajili ya Mawakala/ Wagombea na Waangalizi wa
upigaji kura.
15
Mchoro wa Kituo cha Kupigia Kura
ANGALIZO
Kumbuka kuwa mtu yeyote ambaye ameandikishwa kuwa mpiga kura katika Daftari la
Kudumu la wapiga kura, atakuwa na haki ya kupiga kura katika kituo alichopangiwa na
Tume kupiga kura yake. Aidha, mtu yeyote ambaye jina lake halimo katika Daftari la
Wapiga kura la kituo hata kama anayo shahada ya kupigia kura hataruhusiwa kupiga kura
katika kituo atakachoomba kupiga kura.
13. UTHIBITISHO WA MPIGA KURA
Kila anayefika kituoni kwa ajili ya kupiga kura, atalazimika kuonesha shahada yake ya
kupigia kura kwa Msimamizi wa Kituo. Msimamizi wa Kituo baada ya kuthibitisha kuwa
16
taarifa za mpiga kura huyo zimo katika Daftari la wapiga kura na hajapiga kura,
atamruhusu mtu huyo kuendelea na taratibu za kupiga kura.
14. USAMBAZAJI ZA KARATASI ZA KURA
Tume itakabidhi karatasi zote za kura kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ambaye
kwa kusaidiana na Msimamizi wa Jimbo watazigawa kwa Wasimamizi wa Vituo Vya
Kupigia Kura katika majimbo yao. Wakati wa kupokea karatasi za kura za kituo, Msimamizi
wa Kituo atalazimika kujaza Fomu Nam. PS 7A kwa karatasi za kura za wagombea Urais,
Fomu Nam. PS 7B kwa karatasi za kura za wagombea Uwakilishi na Fomu Nam. PS 7C
kwa karatasi za kura za wagombea Udiwani. Anatakiwa kunukuu kwa usahihi nambari za
karatasi za kura katika kila hatua kama inavyoonyeshwa katika fomu hizo.
Wakati upigaji kura unaendelea, Msimamizi wa Kituo atakuwa akitoa kitabu cha karatasi
za kura kimoja baada ya chengine kulingana na mahitaji ya Msaidizi Msimamizi wa Kituo
Nambari 1 ambaye ndiye dhamana wa kutoa karatasi hizo kwa wapiga kura. Msimamizi
Msaidizi wa Kituo Nambari 1 akishatoa karatasi ya mwisho ya kura kutoka kwenye kitabu
alichopewa, atamkabidhi Msimamizi wa Kituo vishina vya kitabu kilichokwishatumika ili
akabidhiwe kitabu chengine cha karatasi za kura.Utaratibu huo utaendelea mpaka
kumalizika kwa kazi ya upigishaji wa kura.
15. KUFUNGUA KITUO CHA KUPIGIA KURA
Kituo cha kupigia kura ni msingi wa kazi ya uchaguzi. Ili kazi ya kupiga kura ifanyike kwa
ufanisi mkubwa ni vyema kukawa na maandalizi mazuri. Hivyo, kabla ya kufungua kituo
cha kupigia kura, Msimamizi wa Kituo atafanya mambo yafuatayo:-
i. Atahakikisha usalama wa kituo.
ii. Atatoa maelezo kwa mawakala na wapiga kura waliokuwepo kuhusu utaratibu
mzima wa upigaji wa kura kituoni.
iii. Atajaza fomu zote zinazohusiana na kufungua kituo.
iv. Atawaonyesha Mawakala na watu waliopo kituoni masanduku ya kura
17
yaliyoondolewa mifuniko kuthibitisha kuwa ndani ya masanduku ya kura hamna
kitu (matupu).
v. Atalifunga sanduku la kura katika sehemu zake zote kwa kutumia vifungio vya
plastiki, isipokuwa ataacha wazi sehemu ya kuingizia kura.
vi. Ataanza upigishaji kura Saa moja kamili asubuhi.
vii. Ataifunga sehemu ya kuingizia kura kwa kifungio cha plastiki mara baada ya mtu
wa mwisho kumaliza kupiga kura yake.
Michoro iliyoainishwa chini inaonyesha hatua muhimu za kuzingatiwa wakati wa kufunga
sanduku la kura
Mchoro juu ya Ufungaji wa Sanduku la Kura
18
ANGALIZO
Tahadhari LAZIMA ichukuliwe kuhakikisha kuwa vifungio vinatumika kwa uangalifu kwa
kuwa kila kituo cha kupigia kura hupewa idadi inayotosha ya vifungio kwa kazi hiyo na
ziada huwa ni kidogo sana. Sehemu ya kuingizia kura ibaki imefungwa wakati wote hata
kama vifungio vyengine vimetolewa wakati wa kuhesabu kura.
16. WATU WANAORUHUSIWA KUINGIA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA
Watu wanaoruhusiwa kuwemo katika kituo cha kupigia kura ni hawa wafuatao:-
i. Msimamizi wa Kituo.
ii. Msimamizi Msaidizi wa kituo.
iii. Mawakala wa upigaji kura.
iv. Wagombea.
v. Wapiga kura.
19
vi. Mtu anayemsaidia mpiga kura anayehitajia msaada ndani ya kituo.
vii. Mwangalizi wa Uchaguzi aliyeruhusiwa na Tume kwa maandishi.
viii. Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
ix. Mkurugenzi wa Uchaguzi.
x. Askari Polisi na askari wa aina nyengine ikibidi kwa ajili ya kuweka usalama
katika kituo cha upigaji wa kura.
17. KUPANGA MISTARI YA WAPIGA KURA
Wapiga kura watahitajika kujipanga kwa mistari wanapoingia kituoni kupiga kura.
Kutakuwa na mistari miwili ya wapiga kura kwa kuzingatia jinsia, kwa wanawake na
wanaume. Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura itambidi ahakikishe kuwa wapiga kura
wanaingia ndani ya kituo cha kupigia kura kwa zamu ili kusitokee mivutano isiyo ya lazima
wakati wa upigaji kura. Mwongozaji wa wapiga kura (DC) ahakikishe kuwa wapiga kura
waliojipanga katika misitari wamejipanga kulingana na vituo vyao vya kupigia kura.
Wasiohusika na kituo anachokisimamia achukue juhudi ya kuwaelekeza vituo sahihi
wanavyostahiki kupiga kura zao.
Msimamizi wa kituo kwa upande wake ahakikishe kuwa anaandaa utaratibu
utakaowawezesha wapiga kura wenye mahitaji maalum (wazee, watu wenye ulemavu,
wagonjwa, wajawazito, na wenye watoto wachanga) wanapiga kura bila ya kulazimika
kujipanga katika misitari iliyopo ili kuwaondolea usumbufu kutokana na hali zao. Tume
ya Uchaguzi imewapatia watu wenye ulemavu vitambulisho maalum kwa ajili ya
kuwasaidia kufika katika vituo vya kupigia kura bila ya kupanga mstari. Kitambulisho hicho
kinalazimika kubakia katika kituo cha kupiga kura mara baada ya Mpiga kura kumaliza
kupiga kura yake. Mtu ambaye anamsaidia mpiga kura naye anaruhusiwa kupiga kura
yake wakati huo huo ikiwa anastahiki kupiga kura katika kituo hicho.
20
18. SIRI YA KURA
Sehemu ya kupigia kura lazima iwekwe kwa namna ambayo hapana mtu awezaye kuona
ndani wakati mpiga kura akiweka alama kwenye karatasi ya kupigia kura. Watu
watakaokuwemo ndani ya kituo wanakatazwa na Sheria kumshawishi mpiga kura juu ya
namna ya kupiga kura yake.
Mpiga kura asiulizwe vipi anavyotaka kupiga kura au vipi amepiga kura. Mpiga kura
anatakiwa aikunje karatasi ya kura kama alivyoelekezwa na Msaidizi Msimamizi wa Kituo
Nambari 1 kiasi cha kuwa mtu yeyote asiione alama iliyotiwa katika karatasi ya kura
wakati atakapotoka sehemu ya kupigia kura.
ANGALIZO
Msimamizi wa Kituo lazima avikague mara kwa mara vituturi vya kupigia kura ili
kuhakikisha kuwa kalamu ya kuwekea alama katika karatasi ya kura ipo mahali
inapotakiwa.
19. WAPIGA KURA WANAOHITAJI MSAADA
Mpiga kura ambaye ameondokewa na uwezo wa kuona au sababu nyengine ya
kimaumbile au asiyejua kusoma na kuandika anaweza kumuomba Msimamizi wa Kituo,
ruhusa ya kusaidiwa kupiga kura na mtu aliyefuatana naye. Mtu huyo anaweza kuwa
baba, mama, kaka, ndugu, dada, mume, mke, mtoto ambaye amefikia umri wa miaka 18
au mtu ambaye ana haki ya kupiga kura kama mpiga kura katika uchaguzi.
Msimamizi wa Kituo, atamruhusu mpiga kura huyo baada ya kuridhika kuwa ombi la
mpiga kura huyo lina uzito. Mtu anayemsaidia mpiga kura, analazimika kuweka alama
katika karatasi ya kupigia kura kulingana na matakwa ya mpiga kura.
Inapotokea mpiga kura hana jamaa, Msimamizi wa Kituo, atamtaka mpiga kura huyo
kuteua mtu wa kumsaidia ambaye anamuamini na ataandika taarifa za mpiga kura na
21
msaidizi wake kwa kujaza majina yao kwenye Fomu Nam. PS 6 iliyomo katika kitabu cha
fomu mbalimbali za kituo cha kupigia kura na ataruhusu mpiga kura huyo kusaidiwa.
20. WINO USIOFUTIKA
Msimamizi wa Uchaguzi atakipatia kila kituo cha kupigia kura chupa moja ya wino
usiofutika. Kiasi hicho cha wino uliomo kwenye chupa moja kinatosha kuhudumia wapiga
kura 400. Msimamizi wa kituo atatakiwa kuwa mwangalifu katika matumizi ya wino huo
wakati mpiga kura anapopakwa kidoleni kuashiria kuwa amemaliza kupiga kura. Hadhari
lazima ichukuliwe kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinachoweza kuzuia wino kuingia na
kuganda katika sehemu zinazohusika. Msaidizi Msimamizi wa Kituo atamtia wino mpiga
kura kwa kukichovya kidole cha shahada cha mkono wa kushoto.
ANGALIZO
Mtu yeyote aliyemsaidia mpiga kura atatakiwa kutiwa wino kidole cha kati cha mkono wa
kushoto ili kuthibitisha kwamba ameshamsaidia mpiga kura. Mtu mmoja anaruhusiwa
kumsaidia mpiga kura mmoja tu.
21. YANAYOKATAZWA SIKU YA UPIGAJI WA KURA
Zoezi la kupiga kura kufanikiwa kwake kunategemea hali ya utulivu kutoka kwa jamii.
Kuhakikisha utulivu unapatikana katika maeneo ya vituo vya kupigia. Wapiga kura
wanakatazwa na Kanuni kufanya mambo yafuatayo wakati wa kupiga kura:-
i. Kupiga kampeni.
ii. Kufanya au kusababisha vurugu.
iii. Kutoa maneno ya uchochezi.
iv. Kubeba silaha ya aina yoyote kwa siri au dhahiri katika maeneo ya kupigia kura.
v. Kuvaa nguo yoyote yenye rangi inayoashiria alama au rangi za chama cha siasa.
vi. Kukaa kituoni bila ya kazi maalum baada ya kumaliza kupiga kura yake.
22
22. KUAHIRISHA UPIGAJI KURA
Upigaji kura katika kituo unaweza kuahirishwa iwapo umeingiliwa na ghasia au kutokea
kwa maafa ya kimaumbile. Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura, anaweza kuahirisha
upigaji kura kwa muda kituoni mpaka hali ya utulivu itakaporejea. Msimamizi wa kituo
atalazimika kumjulisha Msimamizi wa Jimbo haraka juu ya uamuzi huo kwa ajili ya kupata
maelekezo juu ya hatua nyengine madhubuti za kuchukuliwa kukabiliana na hali
iliyotokezea kituoni.
Endapo sababu zilizopelekea kuahirishwa zimechukuwa muda mrefu, Msimamizi wa Kituo
ataahirisha upigaji kura mpaka siku inayofuata na haraka atatoa taarifa hiyo kwa
Msimamizi wa Jimbo. Sababu za uahirishaji lazima ziandikwe kwenye Daftari la
kumbukumbu la kituo cha kupigia kura.
23. MAWASILIANO
Mawasiliano kati ya watendaji wa kituo cha kupigia kura, Msimamizi wa Jimbo na
Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya yana umuhimu mkubwa sana. Kwa hivyo ni vyema
Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya kupatiwa taarifa mara kwa mara kutoka kwa
Msimamizi wa Jimbo. Vile vile Msimamizi wa Jimbo atahitajika kupatiwa taarifa za mara
kwa mara kutoka kwa Msimamizi wa Kituo kupitia kwa Msimamizi wa Eneo la kupigia
kura. Msimamizi wa Eneo la kupigia kura atakuwa akipatiwa taarifa na Msimamizi wa
Kituo cha kupigia kura kila linapotokezea tatizo linalohitajia ufumbuzi kituoni. Msimamizi
wa Kituo kwa upande wake atawasilisha taarifa juu ya tatizo hilo kwa Msimamizi wa Jimbo
ambaye pia atawasilisha taarifa hiyo kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya.
24. KUFUNGA UPIGAJI WA KURA
Kituo cha kupigia kura kitafungwa saa 10.00 za jioni. Hata hivyo, kabla ya muda halisi
wa kufunga kituo, Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura itampasa amwamuru Askari Polisi
au Msimamizi Msaidizi wa Kituo, kusimama nyuma ya mtu wa mwisho katika msitari wa
wapiga kura ifikapo saa 10.00 jioni. Upigaji kura kituoni utaendelea mpaka mpiga kura
23
wa mwisho kutoka kwenye msitari atakapopiga kura yake.
25. UTARATIBU WA KUFUNGA KITUO
Baada ya mpiga kura wa mwisho kupiga kura yake katika kituo, Msimamizi wa Kituo,
atamtaka kila wakala aliyekuwepo katika kituo cha kupigia kura kuweka maelezo katika
Fomu Nam. PS 8 akionyesha kuridhika au kutoridhika na mwenendo wa upigaji wa kura,
iwapo hakuridhika, aelezee sababu za kutoridhika kwake. Msimamizi wa Kituo anatakiwa
kukiri kupokea malalamiko hayo kwa kuweka jina lake na saini yake na wakati wa kupokea
malalamiko hayo. Kukataa kwa wakala kujaza fomu hizo hakutamzuia Msimamizi wa kituo
kuendelea na majukumu mengine.
Baada ya mawakala kukamilisha kujaza Fomu Nam. PS 8, Msimamizi wa kituo atawajibika
kutoa maelezo juu ya mambo mengine ambayo yanafanyika kituoni kabla ya kuhesabiwa
kwa kura. Baada ya taarifa hiyo atafanya mambo yafuatayo:-
i. Ataufunga upenyo wa juu wa sanduku la kura uliokuwa ukitumika kwa kupenyezea
karatasi za kura kwa kutumia vifungio vya sanduku la kura ili mtu yoyote asiweze
kutumbukiza karatasi nyengine ya kura ama kitu chochote kile.
ii. Atamaliza kuandika hesabu ya karatasi za kura kwa kutumia Fomu Nam. 7A, 7B
na 7C alizopatiwa kwa uchaguzi wa Rais, Wawakilishi na Madiwani ambazo zimo
ndani ya kitabu cha fomu mbalimbali za kituo. Ni muhimu sana kujaza hesabu hizi
sawa sawa bila ya kufanya makosa.
iii. Ataviweka vishina vya karatasi za kura zilizotumika ndani ya bahasha zinazohusika
(ambazo ni 2A kwa karatasi za kura za Urais, 2B kwa karatasi za kura za Uwakilishi
na 2C kwa karatasi za kura za Udiwani). Endapo itatokezea kuwa kuna kitabu cha
karatasi za kura ambacho hakikumalizika chote, itabidi avitenganishe vishina vya
karatasi zilizotumika kutoka kwenye kitabu hicho na kuviweka pamoja na vile
vinavyotokana na vitabu vilivyomalizika vyote na kuviweka ndani ya bahasha
kulingana na uchaguzi na baadae kuzifunga.
iv. Ataziweka pamoja karatasi za kura ambazo hazikutumika na zile zilizoharibika na
sehemu ya karatasi zilizokuwa hazikutumika ndani ya bahasha zinazohusika
24
(bahasha 3A kwa karatasi za kura za Urais, bahasha 3B kwa karatasi za kura za
Uwakilishi na bahasha 3C kwa karatasi za kura za Udiwani.
v. Ataweka ndani ya bahasha Namba 4, Daftari la Kudumu la wapiga kura.
vi. Kwa kila bahasha ya kituo aandike nambari ya sanduku la kura husika. Bahasha
zinazohusika ni kama zifuatazo:-
• Bahasha Nam. 2A, 2B na 2C – Vishina vya Karatasi za Kura zilizotumika
• Bahasha Nam. 3A, 3B na3C – Karatasi za kura ambazo hazikutumika
• Bahasha Nam. 5A, 5B na 5C – Kura zenye mgogoro
• Bahasha Nam. 6A, 6B na 6C – Kura zilizokataliwa
• Bahasha Nam. 7A, 7B na 7C – Kura halali
vii. Avikusanye vifaa vyengine vyote vilivyokuwa vikitumika katika kituo na aviweke
ndani ya bahasha ya kituo (isifungwe) mpaka baada ya kuhesabu kura. Taa na
kichupa cha wino visiwekwe ndani ya bahasha. Bahasha ya kituo isiwekwe ndani
ya sanduku la kura.
ANGALIZO
Msimamizi wa kituo anawajibika kufanya shughuli zote hizo kwa kushuhudiwa na
mawakala wa upigaji kura ama wagombea. Kutokuwepo kwa watu hao hakuzuii shughuli
hiyo kufanyika kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu. Aidha, ahakikishe kuwa fomu za
matokeo na kura zenye mgogoro haziingizi ndani ya sanduku la kura.
26. KUHESABU KURA
Kura kwa kawaida zinahesabiwa katika vituo vya kupigia kura. Hivyo, mara baada ya
kukamilika kwa kazi ya upigaji kura na kituo hicho kufungwa rasmi kwa kazi hiyo, kituo
hicho kinabadilika na kuwa kituo cha kuhesabia kura. Msimamizi wa Kituo, atawatangazia
watu wanaoruhusiwa kuwemo ndani ya kituo juu ya mabadiliko ya kituo (kutoka Kituo
cha Kupigia Kura na kuwa Kituo cha Kuhesabia Kura); na kuwaeleza utaratibu
utakaotumika katika kuhesabu kura.
25
27. WANAORUHUSIWA KUWEMO WAKATI WA KUHESABU KURA
Watu wanaoruhusiwa kuwemo katika kituo cha kuhesabu kura ni hawa wafuatao:-
i. Msimamizi wa kituo
ii. Msimamizi Msaidizi wa kituo
iii. Wakala wa kupiga kura au kuhesabu kura
iv. Mgombea
v. Mjumbe wa Tume
vi. Msimamizi wa Uchaguzi
vii. Afisa wa Uchaguzi
viii. Mwangalizi aliyeruhusiwa na Tume kwa maandishi na
ix. Afisa wa Polisi au mtu mwengine mwenye dhamana ya ulinzi katika sehemu
ambayo kura zinahesabiwa
28. MAMBO YA KUZINGATIWA WAKATI WA KUHESABU KURA
Msimamizi wa Kituo na wasaidizi wake ndio watakaohesabu kura mbele ya watu wote
walioruhusiwa kisheria kuwepo kituoni wakati wa kuhesabu kura. Katika kuifanya kazi
hiyo, Msimamizi wa Kituo anawajibika na mambo yafuatayo:-
i. Kuhakikisha kuwa baada ya kazi ya upigishaji kura kukamilika na kufungwa kituo
wanafanya maandalizi kwa ajili ya kuhesabu kura.
ii. Kuhakikisha kuwa kabla ya kuhesabu kura wagombea au mawakala wa kuhesabu
wa kura wanaeleza kuridhika au kutoridhika na maandalizi ya kituo cha kuhesabu
kura kwa kujaza maelezo yao katika Fomu Nam. PS 9. Msimamizi wa kituo
ataelezea kwa maandishi malamiko yaliyotolewa na jinsi alivyoyashughulikia.
29. UTARATIBU WA KUHESABU KURA
Kazi ya kuhesabu kura itafanywa kwa mpangilio ufuatao:-
i. Atakata vifungio vya masanduku ya kura akianzia na sanduku la kura la wagombea
Urais, baadae zitafuata kura za wagombea Uwakilishi na hatimaye kura za
26
wagombea Udiwani.
ii. Atamimina kura zote juu ya meza ama katika sehemu maalum iliyoandaliwa kwa
ajili ya kazi ya kuhesabu kura.
iii. Atahesabu kura moja baada ya nyengine kwa sauti ili kujua idadi ya kura zilizomo
katika sanduku la kupigia kura.
iv. Atandaka katika buku la kumbukumbu (Note book) idadi ya kura zote zilizopatikana
katika kila sanduku la kura.
v. Atahakikisha kuwa idadi ya kura katika sanduku la kura inalingana na idadi ya watu
wote waliopiga kura kituoni hapo.
vi. Baada ya idadi ya kura zote katika sanduku kujulikana, Msimamizi wa kituo
atakunjua kura moja baada ya nyengine kwa kuonyesha upande wenye picha za
wagombea na atatangaza kwa sauti kubwa
• Mgombea aliyepigiwa kura au
• Karatasi ya kura haina alama yoyote au
• Kura imeharibika
Alama inayokubalika katika chumba kinachokuwa chini ya picha ya mgombea ni
alama ya “√”. Endapo mpiga kura atashindwa kuweka alama katika chumba
kilichopo chini ya picha ya mgombea lakini ameweka alama hiyo katika picha ya
mgombea au katika alama ya chama chake, alama hiyo itakubaliwa na ni kura
halali.
vii. Atazipanga kura kwa mafungu tofauti kwa kila mgombea na upande wa picha za
wagombea uelekezwe juu. Kura zitakazokataliwa na zile zenye mgogoro zipangwe
sehemu tofauti.
viii. Baada ya kukamilisha hatua hiyo, Msimamizi wa kituo atahesabu kwa sauti kubwa
hesabu ya kura kwa kila fungu na baadae ataandika idadi ya kura zilizopatikana
kwa kila fungu.
ix. Atalinganisha idadi ya kura alizopata kwa kila mgombea, kura zilizokataliwa na
kura zenye mgogoro na idadi ya kura zilizopatikana katika sanduku la kura
zilizopigwa katika kituo.
27
x. Baada ya kumaliza kuhesabu kura, Msimamizi wa kituo atazifunga kura hizo na
kuziweka kwenye bahasha tofauti kama ifuatavyo:-
• Kura zenye mgogoro- Bahasha Nam. 5A – Urais, 5B- Uwakilishi na 5C-
Udiwani.
• Kura zilizokataliwa- Bahasha Nam. 6A – Urais, 6B –Uwakilishi na 6C –
Udiwani.
• Kura halali –Bahasha Nam. 7A – Urais, 7B – Uwakilishi na 7C – Udiwani.
xi. Msimamizi wa kituo baada ya hatua zote hizo atajaza matokeo ya Uchaguzi wa
Rais, Uwakilishi na Udiwani katika kituo chake kwa kujaza Fomu Nam. 12A kwa
Urais, Fomu Namba 22A kwa Uwakilishi na Fomu Namba 32A kwa Udiwani ambazo
zinauwezo wa kutoa kopi.
xii. Baada ya kuhesabu kura mawakala wajaze Fomu Nam. PS 10 kuthibitisha kwamba
wanaridhika au hawakuridhika na namna kura zilivyohesabiwa na iwapo wana
malalamiko yoyote.
xiii. Mawakala ama wagombea katika kituo cha kuhesabia kura ambao wameshuhudia
kazi za kuhesabu kura wataandikwa majina katika fomu hizo na watatia saini katika
fomu ya matokeo ya kituo kuthibitisha kuwa wameshuhudia matokeo ya
wagombea katika kura zilizohesabiwa kituoni.
xiv. Msimamizi wa Kituo atapeleka ukurasa wa kwanza wa fomu ya matokeo kwa kila
uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo wakati wa majumuisho ya jimbo.
xv. Atabandika nakala moja ya fomu ya matokeo nje ya kituo cha kuhesabia kura na
nakala nyengine za matokeo atawakabidhi mawakala walioshuhudia kazi ya
kuhesabu kura kituoni.
xvi. Msimamizi wa Kituo ataziweka bahasha za kura halali na kura zilizokataliwa kwenye
masanduku ya kupigia kura kulingana na uchaguzi husika. Bahasha ya kituo cha
kupigia kura na fomu zote za matokeo zisiwekwe ndani ya sanduku.
28
ANGALIZO
1. Vifungio vinavyokatwa ni vya pembeni tu. Kifungio kilichozuia sehemu ya kuingizia
kura visikatwe.
2. Wakati wa kuhesabu kura, karatasi za kura zitakazoonekana katika sanduku
lisilohusika zitahesabiwa katika sanduku linalohusika.
3. Kuhesabu kura upya kutafanyika endapo mgombea au wakala wa mgombea wa
kuhesabu kura ataomba kura zihesabiwe tena. Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi
ombi la kwanza lazima kura zihesabiwe. Ombi la pili lazima kura zihesabiwe na ombi
la tatu, Msimamizi wa kituo anaweza kukataa endapo matokeo ya hesabu ya ombi la
kwanza na la pili ni yale yale.
4. Wakala wa kuhesabu kura haruhusiwi kuhesabu kura wala kushika karatasi za kura
wakati wa zoezi la kuhesabu kura.
30. KURA AMBAZO HAZITAHESABIWA KUWA NI KURA HALALI
Uamuzi wa kura halali na isiyo halali
Wakati wa kuhesabu kura, uamuzi wa mwisho juu ya uhalali wa kura itakayohesabiwa ni
wa Msimamizi wa Kituo. Kwa hiyo, iwapo Msimamizi wa Kituo ataridhika kuwa kura
imeharibika ataikataa na haitahesabiwa na ataandika nyuma ya karatasi hiyo ya kura
maneno yanayosomeka ”IMEKATALIWA”. Iwapo uamuzi huo wa Msimamizi wa Kituo
utapingwa na wakala, Msimamizi wa Kituo ataandika nyuma ya karatasi hiyo maneno
yanayosomeka ”UAMUZI UMEPINGWA NA”......... (Ataandika jina na chama cha
anaepinga). Kura ambayo imepingwa itachukuliwa kuwa ni kura yenye mgogoro.
Kura zilizoharibika
Kura itahesabiwa kuwa imeharibika iwapo:-
• Haina muhuri wa Kituo.
• Ina alama ya maandishi yanayoweza kumtambulisha mtu aliyepiga kura hiyo na.
• Aliyopigiwa zaidi ya mgombea mmoja.
29
31. KURA ZENYE MGOGORO
Kura zenye mgogoro zitaamuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi wakati wa kujumlisha kura.
Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kufanya uamuzi wa kura zenye mgogoro atajaza
matokeo husika kwenye fomu ya majumuisho ya jimbo Namba. 12B kwa Urais, Namba
22B kwa Uwakilishi na Namba 32B kwa Udiwani.
32. MAKABIDHIANO YA VIFAA
Baada ya kumaliza shughuli zote za kuhesabu kura kama zilivyoainishwa katika maelekezo
haya, Msimamizi wa Kituo atawajibika kufanya yafuatayo:-
i. Atamkabidhi Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo masanduku yote ya kura, bahasha
pamoja na vifaa vyote alivyokabidhiwa.
ii. Baada ya makabidhiano hayo ahakikishe kuwa amepewa uthibitisho kuwa vitu vyote
ni sawa na salama na kazi ya Msimamizi wa Kituo itakuwa imemalizika.
33. TAHADHARI KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo
wanatahadharishwa wasitumie vibaya nafasi wanazokabidhiwa. Ni makosa kutumia nafasi
hizo kwa lengo la kumtia adabu mpiga kura asipige kura. Wasimamizi wa Vituo vya
kupigia kura na Wasaidizi wao pia wanatahadharishwa kujiepusha na mambo yafuatayo:-
i. Kutoa au kutumia karatasi za kura kinyume na maelekezo.
ii. Kufanya makosa ya kuwapa karatasi za kura watu wasiostahiki.
iii. Kujaribu kufungua masanduku ya kura au bahasha zilizofungwa.
iv. Kuacha kupiga muhuri wa Kituo katika karatasi ya kura kwa makusudi au kwa
uzembe.
v. Kuficha karatasi za kura ili wananchi wenye haki wasiweze kupiga kura zao
kutokana na hila hiyo.
30
34. MAKOSA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA
Ifahamike kuwa ni makosa kufanya jambo lolote ambalo litaingilia, litatatiza au litaleta
ucheleweshaji wa mwenendo wa upigaji kura.
Makosa hayo ni:-
i. Kutaka kupiga kura kabla ya kituo hakijafunguliwa au baada ya kufungwa.
ii. Kupiga kura au kukusudia kupiga kura ikiwa mtu hana haki ya kufanya hivyo.
iii. Kupiga kura au kukusudia kupiga kura zaidi ya mara moja.
iv. Kupiga kura kwa jina la mtu mwengine.
v. Kutia ndani ya sanduku la kura kitu chengine chochote zaidi ya kura.
vi. Kubandua katika eneo la kituo cha kupigia kura karatasi yoyote ya matangazo
halali kuhusu upigaji kura.
vii. Kuingiza au kuharibu karatasi ya kura au shahada ya matokeo au fomu yoyote
inayohusiana na kupiga kura.
viii. Kuchapisha au kuwa na au kumpa mtu yeyote karatasi ya kura bila ya kuwa na
mamlaka ya kisheria.
ix. Kuwa na sanduku la kura bila ya kuwa na mamlaka hayo.
x. Kuzuia au kuingilia kazi za Msaidizi Msimamizi wa kituo.
xi. Kumlazimisha mpiga kura kupiga kura.
xii. Kumzuia au kumkinga mpiga kura kupiga kura yake katika hali ya faragha.
xiii. Kutoa taarifa juu ya namna alivyopiga kura.
xiv. Kuonesha jinsi alivyopiga kura yake.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imewateuwa nyinyi kutokana na maombi mengi
yaliyowasilishwa kwetu. Tunawaomba mfanye kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
Ahsanteni
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR INAWATAKIA KAZI NJEMA
31
MIFANO YA KURA ZINAZOKUBALIKA NA ZISIZOKUBALIKA
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
///
Chama Chama Chama
Alama iliyowekwa kwenye picha ya mgombea kinyume na maelekezo
(uso wa mgombea): nia ya mpiga kura inaeleweka
Picha ya Mgombea
Picha ya mgombea
Picha ya Mgombea
Chama Chama √ Chama
Alama ya √ (vyema) imewekwa katika alama ya chama (logo) nia ya mpiga kura
inaeleweka, kura hiyo itahesabiwa.
32
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
√
Chama Chama Chama
Ni alama sahihi inayoruhusiwa moja kwa moja na sheria.
MFANO WA KURA ZISIZOKUBALIKA
Kuweka alama √ (vyema) katika chumba kinachokubalika na alama ya X katika sura au
picha ya mgombea. Kura hii haikubaliki kwa sababu nia ya mpiga kura haiko wazi.
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
X
√
CHAMA CHAMA CHAMA
33
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Chama Chama Chama
√
Alama ya √ (Vyema) imewekwa nje ya eneo lote la kupigia kura
(iko nje chumba kinachopendekezwa); haitahesabiwa
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
√
√
√
Chama Chama Chama
Alama za VYEMA (√) ziko kama ilivyoelekezwa chini ya picha za wagombea wote, kura
hiyo haikubaliki kwani mpiga kura hakumpigia mgombea moja kama anavyotakiwa na
Sheria.
34
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Picha ya Mgombea
Chama Chama Chama
Karatasi ya kura ambayo haikupigwa muhuri wa kituo sehemu ya nyuma kama
inavyoelekezwa na Sheria, karatasi hiyo haifunguliwi na haihesabiwi.