39
1 [SURA ya 1 T.L. 2002] Sheria ya Utafsiri wa Sheria ___ SURA YA KWANZA _______ SHERIA YA UTAFSIRI WA SHERIA [SHERIA KUU] MPANGILIO WA VIFUNGU Kifungu Jina SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI 1. Jina la sheria na tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria 2. Matumizi 3. Jamhuri kufungwa na Sheria SEHEMU YA PILI MASHARTI YA JUMLA YA TAFSIRI 4. Ufafanuzi utumikao katika sheria. 5. Matumizi. 6. Sheria hunena daima 7. Sehemu ya matamshi na miundo ya fasihi. 8. Jinsia na tarakimu. 9. Rejeo ya neno Waziri katika sheria. 10. Marejeo kwa tarakimu, kujumuishwa. 11. Tafsiri ya rejeo ndani ya kifungu, n.k. 12. Rejeo kwenye sheria kama ilivyorekebishwa. 13. Tafsiri ya neno “au”. SEHEMU YA TATU KUANZA KUTUMIKA NA KUTAJWA KWA SHERIA 14. Tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria. 15. Muda wa kuanza kutumika kwa sheria. 16. Kuanza kutumika kwa sheria palipo na kifungu cha masharti ya kutolewa kwa taarifa ya kuanza kutumika. 17. Tafsiri ya uwezo wa kupanga tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria. 18. Ushahidi wa tarehe ya kusainiwa. 19. Utekelezaji wa uwezo kabla ya kuanza kutumika. 20. Kutajwa kwa sheria. 21. Marejeo ya sheria kwa siku ya kuanza kutumika.

Sheria ya Utafsiri wa Sheria

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

1

[SURA ya 1 T.L. 2002] Sheria ya Utafsiri wa Sheria

___

SURA YA KWANZA

_______

SHERIA YA UTAFSIRI WA SHERIA

[SHERIA KUU]

MPANGILIO WA VIFUNGU

Kifungu Jina

SEHEMU YA KWANZA

MASHARTI YA UTANGULIZI

1. Jina la sheria na tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria

2. Matumizi

3. Jamhuri kufungwa na Sheria

SEHEMU YA PILI

MASHARTI YA JUMLA YA TAFSIRI

4. Ufafanuzi utumikao katika sheria.

5. Matumizi.

6. Sheria hunena daima

7. Sehemu ya matamshi na miundo ya fasihi.

8. Jinsia na tarakimu.

9. Rejeo ya neno Waziri katika sheria.

10. Marejeo kwa tarakimu, kujumuishwa.

11. Tafsiri ya rejeo ndani ya kifungu, n.k.

12. Rejeo kwenye sheria kama ilivyorekebishwa.

13. Tafsiri ya neno “au”.

SEHEMU YA TATU

KUANZA KUTUMIKA NA KUTAJWA KWA SHERIA

14. Tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria.

15. Muda wa kuanza kutumika kwa sheria.

16. Kuanza kutumika kwa sheria palipo na kifungu cha masharti ya kutolewa

kwa taarifa ya kuanza kutumika.

17. Tafsiri ya uwezo wa kupanga tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria.

18. Ushahidi wa tarehe ya kusainiwa.

19. Utekelezaji wa uwezo kabla ya kuanza kutumika.

20. Kutajwa kwa sheria.

21. Marejeo ya sheria kwa siku ya kuanza kutumika.

Page 2: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

2

SEHEMU YA NNE

MASHARTI YA UTUNGAJI NA UTUMIKAJI WA SHERIA.

22. Sheria kuwa sheria za umma.

23. Vifungu kujitosheleza kama sheria kamili.

24. Sheria yaweza kurekebishwa au kufutwa katika kikao hicho hicho.

25. Utangulizi na Majedwali.

26. Vichwa, maelezo ya pembeni, rejeo chini ya ukurasa na marekebisho ya

makosa.

SEHEMU YA TANO

MAREKEBISHO NA KUFUTWA KWA SHERIA

27. Fasiri ya sheria inayorekebisha sheria nyingine pamoja na marekebisho

yake.

28. Kufutwa kwa sheria kama ilivyorekebishwa.

29. Kufuta kwa kufuta.

30. Kufuta na kubadilisha.

31. Athari ya masharti mbadala.

32. Vifungu vya jumla vinavyobakizwa baada ya kufutwa.

33. Athari ya kufutwa kwa sheria kwenye sheria ndogo.

34. Athari ya kumalizika kwa muda wa kutumika kwa sheria.

SEHEMU YA SITA

MASHARTI YANAYOHUSU SHERIA NDOGO

35. Rais anaweza kutunga sheria ndogo.

36. Masharti ya jumla kuhusu uwezo wa kutunga sheria ndogo.

37. Utangazaji na kuanza kutumika kwa sheria ndogo.

38. Kuwasilisha wa Kanuni Bungeni na kukataliwa.

39. Tafsiri ya sheria ndogo.

40. Kutajwa kwa sheria ndogo.

41. Marejeo ya sheria kujumuisha sheria ndogo.

42. Matendo chini ya sheria ndogo kuchukuliwa kama yamefanyika chini ya

sheria.

43. Ada na tozo.

SEHEMU YA SABA

UWEZO NA WAJIBU WA KISHERIA

44. Muda wa utekelezaji wa uwezo au wajibu kwa mujibu wa sheria.

45. Rejeo kwa mshika ofisi itajumuisha warithi.

46. Tafsiri ya maneno ya kuwezesha.

47. Uwezo wa kutoa leseni, n.k.., ni wa hiari.

48. Uwezo wa kuteua unajumuisha uwezo wa kusimamisha au kufukuza n.k.

49. Uteuzi kwa jina au ofisi n.k., na uteuzi wa Mwenyekiti, n.k. Bodi, n.k...,.

Page 3: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

3

50. Uwezo wa walio wengi, akidi, n.k.

51. Utekelezaji wa uwezo unaweza kusahihishwa.

52. Athari ya uteuzi wakati afisa anayestaafu akiwa likizo.

53. “Inaweza/Anaweza”, itakuwa na maana ya hiari, “ata/ita”, itakuwa na

maana ya lazima.

54. Uwezo wa Bodi, n.k. hautaathirika kwa nafasi iliyowazi au mapungufu

mengine.

55. Utekelezaji wa mamlaka fulani kwa anayekaimu.

56. Rejeo kwa eneo kwa kutumia mipaka.

57. Tafsiri ya uwezo wa kukasimu.

58. Ni nani ataweka lakiri ya kampuni.

59. Haki za Serikali.

SEHEMU YA NANE

MASHARTI KUHUSU MUDA NA UMBALI

60. Kukokotoa muda..

61. Kuhesabu miezi.

62. Masharti pale muda haujapangwa.

63. Tafsiri ya uwezo wa kuongeza muda.

64. Kwenda kinyume na fomu.

65. Vipimo vya umbali.

SEHEMU YA TISA

TARATIBU NA ADHABU

66. Mashauri ya wadhifa wa kiofisi hayakomi baada ya kifo.

67. Kanuni za Mahakama.

68. Kutolewa kwa adhabu, si kizuizi cha kesi ya madai.

69. Upatikanaji wa faini na adhabu.

70. Kutia hatiani maradufu.

71. Matumizi ya sheria za adhabu kwa makampuni.

72. Masharti ya makosa chini ya sheria mbili au zaidi.

73. Marekebisho ya adhabu.

74. Maagizo ya adhabu ya juu, ya chini, ya siku, na za pamoja.

75. Vifungu vinavyohusu kujaribu.

76. Utoaji wa mali au vitu vilivyotwaliwa.

77. Uwajibikaji wa mwajiri au mkuu.

78. Ushahidi wa agizo, kibali au ridhaa ya mtumishi wa umma.

79. Utekelezaji wa mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka wakati hayupo.

80. Tamko la adhabu mwishoni mwa kifungu.

81. Makosa yanayoendelea.

Page 4: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

4

SEHEMU YA KUMI

MASHARTI MBALIMBALI

82. Uwasilishaji wa nyaraka kwa njia ya posta.

83. Uwasilishaji wa nyaraka kwa ujumla.

84. Lugha ya sheria za Tanzania.

85. [Kufutwa kwa Sheria Na. 30 ya mwaka 1972.]

JEDWALI

(Kifungu cha 4 )

Page 5: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

5

[SURA ya 1 T.L. 2002] Sheria ya Utafsiri wa Sheria

______________________________________________________________________

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SURA YA KWANZA

______

SHERIA YA UTAFSIRI WA SHERIA

Sheria ya majumuisho ya kanuni za msingi zinazohusu maana,ufafanuzi na

matumizi ya sheria zilizotungwa, na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

[............................]

Sheria Na.

4 ya1996 na

17 ya 1996

SEHEMU YA KWANZA

MASHARTI YA UTANGULIZI

Jina la sheria na

tarehe ya kuanza

kutumika kwa

sheria

1.-(1) sheria hii inaitwa Sheria ya Utafsiri wa Sheria.

(2) Sheria hii itaanza kutumika tarehe ambapo Toleo la 2002 la

Sheria zilizofanyiwa marekebisho zitakapoanza kutumika. (3) Katika kifungu hiki “Toleo la 2002 la Sheria zilizofanyiwa

marekebisho” ina maana ya Sheria za Tanzania zilizofanyiwa

marekebisho na kuchapishwa. Matumizi 2.-(1) Sheria hii itatumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar,

kwa minajili ya sheria zitumikazo sehemu zote za Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania. (2) Vifungu vya Sheria hii vitatumika katika, na kuhusiana na

Sheria yoyote iliyotungwa, nyaraka za umma, hata kama sheria na

nyaraka hizo zimetungwa, kupitishwa au kutolewa kabla au baada ya

kuanza kutumika kwa Sheria hii, isipokuwa kama Sheria na nyaraka

hizo:– (a) Zitakuwa na vifungu vinavyoelekeza vinginevyo, na

kuhusiana na sheria, dhamira na malengo yake au maudhui,

muktadha au mazingira ya sheria hiyo hayaruhusu, au sheria

yenyewe imetoa ufafanuzi; (b) zinahusu sheria ndogo, kama madhumuni na malengo ya

sheria kuu ambayo chini yake sheria ndogo zimetungwa,

haziruhusu matumizi ya ufafanuzi huo; au

Page 6: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

6

(c) Zinahusu sheria ndogo, kama madhumuni na malengo ya

sheria kuu ambayo sheria ndogo zimetungwa, hayapatani na

matumizi ya ufafanuzi huo. (3) Vifungu vya Sheria hii vitatumika katika Sheria hii kama

vitumikavyo katika sheria iliyotungwa baada ya kuanza kutumika kwa

Sheria hii. (4) Katika vifungu 13, 15, 19, 20, 22, 23, 24, 33, 36(6), 43, 46, au

62 marejeo katika sheria yoyote au sheria ndogo iliyopitishwa au

kutungwa baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii yatatafsiriwa ili

yasiwe na maana ya kugusa sheria yoyote ambayo inaendelea kutumika

au ambayo inarekebisha moja kwa moja sheria nyingine, lakini

haibatilishi au kufuta sheria iliyopo. Jamhuri

kufungwa na

sheria

3. Jamhuri kufungwa na sheria.

SEHEMU YA PILI

MASHARTI YA JUMLA YA TAFSIRI Ufafanuzi

utumikao katika

sheria,

Sura ya 16.

4. Katika Sheria hii na katika sheria zingine:–

"shiriki kutenda jinai" kwa maana ya maneno yenye asili hii au misemo

inayoshabihiana itakuwa na maana kama ilivyoainishwa katika

sheria ya Kanuni za Adhabu; "tendo" ikitumiwa kuainisha kosa la jinai au kosa la madai itajumuisha

kushindwa kutenda wajibu na itahusu msururu wa vitendo vya

kushindwa kutekeleza wajibu; "Sheria" itumikapo kuhusiana na sheria yoyote, itakuwa na maana ya

sheria za zamani, amri au sheria zilizotungwa na Bunge la

Jamhuri au Baraza la Wakilishi la Zanzibar au Baraza lolote lenye

mamlaka ya kutunga sheria Tanzania au kuhusiana na Zanzibar,

sheria, amri au sheria za zamani zilizoridhiwa na au kwa niaba ya

Rais au mamlaka yoyote ya kutunga sheria, lakini haitahusu sheria

ya Jumuiya; "afisa tawala" maana yake ni afisa tawala wa ngazi yoyote; "wakili" maana yake ni mtu yeyote anayeruhusiwa kuendesha shughuli

za uwakili katika Mahakama Kuu au Mahakama za chini yake,

kwa mujibu wa sheria inayohusu uratibu wa shughuli za

mawakili; "hati ya kiapo" kuhusiana na watu wanaoruhusiwa kushuhudia viapo au

kupokea ushuhuda badala ya kiapo, itahusu vile vile tamko la

dhati, uthibitisho au azimio; "rekebisha au batilisha" maana yake ni kubadilisha, kufuta au kurekebisha

sehemu yote au sehemu tu, au kuongeza au kupunguza au kufanya

aina yoyote ya marekebisho kwenye sheria au sehemu yake; "sheria ya mapokeo" maana yake ni Sheria yoyote ya India au Sheria ya

Page 7: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

7

Uingereza, ikijumuisha Amri za Baraza la Kifalme ambayo katika

wakati huu inatumika Tanzania; "sheria ndogo" maana yake ni sheria ndogo iliyotungwa kwa mujibu wa

sheria kuu; "mwezi" maana yake ni kipindi kuanzia siku ya kwanza ya mwezi hadi

siku ya mwisho ya mwezi husika; "mwaka" maana yake ni kipindi kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa

Januari hadi siku ya thelathini na moja ya mwezi wa Desemba ya

mwaka husika; "sura", "sehemu", "kifungu" na "Nyongeza" maana yake ni sura, sehemu,

kifungu na Nyongeza ya sheria husika na “kifungu kidogo” maana

yake ni kifungu kidogo cha kifungu ambamo neno hilo

limetumika; "Katibu Mkuu Kiongozi" maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuwa Katibu

Mkuu kwenye Ofisi ya Rais; "hakimu" maana yake ni hakimu mkazi, hakimu wa wilaya, hakimu wa

mahakama ya mwanzo na maelezo mengine yoyote kuhusu

hakimu yaliyotolewa chini ya Sheria ya Mahakama za Mahakimu; "sarafu" maana yake ni kipande cha chuma cha aina yoyote, kiwe chuma

cha thamani au kisicho cha thamani na ambacho kwa wakati

husika, kinatumika kama fedha halali ya Jamhuri ya Muungano; "mwanzo wa kutumika" itumikapo kuhusiana na sheria maana yake ni

wakati ambapo sheria husika itaanza kutumika; "sheria zisizoandikwa" maana yake ni sheria zisizoandikwa za Uingereza; "Jumuiya ya Madola" maana yake ni mfungamano wa nchi za Madola na

nchi tegemezi ndani ya Jumuiya; na “mwanachama wa Jumuiya”

au “nchi ya Jumuiya in maana ya Jamhuri ya Muungano na nchi

zilizoorodheshwa katika Nyongeza ya Sheria hii; "Jumuiya" maana yake ni Jumiya ya Afrika ya Mashariki iliyoundwa

chini ya Mkataba wa Jumuiya;

Sura ya 2

"Mfuko Mkuu wa Hazina" maana yake ni Mfuko Mkuu wa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

"Katiba" maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya

Mwaka 1977 iliyotungwa na Bunge Maalumu la Jamhuri ya

Muungano; "vunja" itumikapo kuhusiana na matakwa au wajibu kisheria au ruhusa

au idhini, hakimiliki, leseni au mamlaka kwa mujibu wa sheria

itajumuisha vile vile kushindwa kutii masharti au maelekezo ya

sheria; "mahakama" maana yake ni mahakama yoyote yenye mamlaka katika

Jamhuri ya Muungano;

Sura ya 141 "Mhakama ya Rufaa" maana yake ni mahakama inyosikiliza rufaa zote

zikatwazo kwa mujibu wa Sehemu ya Pili ya Sheria ya Mamlaka

ya Mahakama ya Rufaa; "Wakala wa Mfalme" maana yake ni watu kwa wakati huu wanafanya

kazi kama Wakala wa Mfalme kwa Serikali na Utawala wa kigeni

Page 8: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

8

au yeyote wa namna hiyo;

Sura ya 358

"Sheria ya Kimila" maana yake ni kanuni au mfungamano wa kanuni

ambazo zinaainisha haki na wajibu, na ambazo zinatokana na

mazoea, kurithiwa au kutungwa, na zinakubaliwa na Jamii ya

Kiafrika nchini Tanzania na zenye nguvu ya kisheria, ikijumuisha

matangazo ya kanuni mpya au marekebisho yake yanayotungwa

chini ya kifungu cha 12 cha sheria ya Usimamiaji wa Haki na

Matumizi ya Sheria, na marejeo kwa, “Sheria za Jadi” au Sheria

za Jadi na Mila zitakuwa na tafsiri sawa; "ufafanuzi" maana yake ni ufafanuzi uliotolewa kwa mujibu wa sheria

ukitoa maana kwa neno au msemo; "Naibu Waziri" maana yake ni Naibu wa Waziri aliyeteuliwa kwa mujibu

wa Ibara ya 55 ya Katiba; "Wilaya" maana yake ni sehemu yoyote ya Jamhuri iliyotangazwa au

kubainishwa hivyo kwa mujibu wa Ibara ya 2 (2) ya Katiba; "hakimu wa wilaya" inajumuisha hakimu mkazi; "Hati" inajumuisha chapisho la aina yoyote, waraka wa maandishi ya aina

yoyote, yaliyoandikwa au kuelezwa kwenye kitu chochote kwa

herufi, tarakimu alama kwa namna moja zaidi ya hizo zilizotajwa,

kwa madhumuni ya kutumiwa kwa lengo la kuweka kumbukumbu

ndani au juu yake; "Mamlaka ya Afrika ya Mashariki" maana yake ni Mamlaka ya Afrika ya

Mashariki iliyoundwa chini ya Mkataba husika; "sheria iliyotungwa" maana yake ni sheria iliyotungwa au sehemu ya

sheria husika; "shamba", ikitumika kuhusiana na ardhi, itajumuisha vile vile haki ya

kisheria au maslahi, maslahi ya haki, haki ya njia katika ardhi,

hakimiliki, dai, dai la kumiliki hadi deni lilipwe, au zuio juu ya

miliki ya ardhi; "mwaka wa fedha" maana yake ni kipindi cha miezi 12 kinachoishia

tarehe 30 Juni; "Afisa Mambo ya Nje" maana yake ni afisa aliyeteuliwa au anayekaimu

nafasi ya Afisa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano; "shughuli/kazi" itajumuisha mamlaka, kazi, wajibu, uwezo wa kisheria

na mamlaka ya kisheria; "Gazeti" au "Gazeti la Serikali" maana yake ni Gazeti linalopigwa chapa

na kutangazwa na Mpiga Chapa wa Serikali ya Jamhuri kwa amri

ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na inajumuisha nyongeza

zake na toleo Maalum la Gazeti hilo; "Taarifa ya Kawaida" maana yake ni tangazo lisilohusiana na utungwaji

wa sheria lililochapishwa katika Gazeti au kwa idhini ya Rais au

Waziri; "Serikali" maana yake ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano; "Mkemia Mkuu wa Serikali" inajumuisha msaidizi wake au mkemia

yeyote aliyeajiriwa na Serikali; "Tangazo la Serikali" maana yake ni sheria ndogo iliyotungwa na Rais,

Page 9: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

9

Waziri au afisa wa serikali au mamlaka yoyote yenye uwezo

kutunga sheria ndogo kwa mujibu wa sheria husika; "Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali" maana yake ni Mpiga Chapa wa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano na mpiga chapa yeyote

aliyeidhinishwa kuchapa sheria na nyaraka zingine za Serikali; "Kamisheni" maana yake ni Kamisheni ya Afrika ya Mashariki

iliyoundwa kwa Maagizo ya Mfalme ya Kuanzishwa kwa

Kamisheni ya Afrika ya Mashariki, kati ya miaka ya 1947 na 1961

na rejeo katika sheria yoyote kuhusu Kamisheni yatafafanuliwa

kama ifuatavyo:– (a) kwa kipindi ambacho Sheria ya Mkataba wa Uendelezaji wa

Huduma za Pamoja katika Afrika ya Mashariki ilikuwa

ikitumika, kipindi hicho kitafafanuliwa kama Mfumo wa

Huduma za Pamoja; (b) kwa kipindi baada ya kufutwa kwa Sheria iliyounda

Kamisheni, kitafafanuliwa kama kipindi cha Jumuiya; "Mahakama Kuu" maana yake ni Mahakama Kuu ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania au Mahakama Kuu ya Zanzibar; "Sheria za Kifalme" maana yake ni Sheria zilizotungwa na Bunge la

Ufalme wa Uingereza;

"mtu binafsi" maana yake ni mtu mmoja;

"Jaji" maana yake ni Jaji wa Mahakama Kuu na inajumuisha vile vile

Naibu Jaji;

"mlinzi wa amani" maana yake ni mtu mwenye mamlaka ya kutunza

amani;

"ardhi" inajumuisha majengo na aina nyingine ya majengo, na

iliyofunikwa na maji, milki yoyote, maslahi, haki ya kutumia njia

na haki ya vilivyomo juu au chini ya ardhi husika; "Afisa Sheria" maana yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na afisa

mwingine mzoefu kwenye taaluma ya sheria katika Ofisi ya

Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia ngazi ya Wakili wa

Serikali Mkuu Mwandamizi au Mwandishi wa Sheria Mkuu

Mwandamizi; "mamlaka ya serikali za mtaa" maana yake ni–

Sura ya 287

(a) baraza la kijiji, kitongoji, mji, wilaya au mamlaka yoyote ya

serikali ya mtaa iliyoundwa chini ya sheria ya Serikali za

Mtaa na Mamlaka ya Wilaya; au

Suraya .288

(b) katika sehemu za mji, ni baraza la mtaa, mji, manispaa au

baraza la Jiji liloundwa chini ya Sheria ya Serikali za Mtaa

(Mjini);

Sura ya 11

"hakimu" maana yake ni hakimu mkazi, hakimu wa wilaya hakimu wa

mahakama ya mwanzo na mwingine yeyote aliyeteuliwa kama

hakimu kwa mujibu wa Sheria ya Mahakimu;

Sura ya 29

"ndoa" maana yake ni ndoa iliyofungwa na inayotambuliwa kwa mujibu

wa Sheria ya Ndoa, na neno “mume”, “mke” au “mwanandoa”

litafafanuliwa kutokana na neno la msingi la aliyeoa au kuolewa;

Page 10: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

10

"Waziri" ina maana kama ilivyofafanuliwa katika kifungu cha 9 cha

sheria hii na vile vile itajumuisha Makamu wa Rais, Waziri Mkuu;

na Waziri maana yake ni waziri mwenye dhamana ya kusimamia

shughuli husika na itajumuisha Naibu Waziri kwa wakati huu

anayetekeleza kazi za Waziri au kama hakuna waziri wa

kusimamia jambo husika, maana yake ni Rais; "mtoto" maana yake ni mtu ambaye hajafikia umri wa miaka kumi na

minane, na neno “mtoto” na mtoto mchanga” yatafafanuliwa kwa

maana hiyo; "mwezi" maana yake ni mwezi katika mwaka, isipokuwa kama neno la

sayari limeongezwa ikimaanisha mwezi wa sayari; hivyo, mwezi

ukitajwa kuanza au kuhesabiwa katika tarehe isiyokuwa ya

kwanza ya mwezi husika, basi mwezi utatimia katika siku ya pili

ya tarehe ya mwezi unaofuata, hata kama kipindi husika

kinajumuisha siku nyingi au pungufu ya siku thelathini; "mwenyeji " maana yake ni mtu yeyote mwenye asili ya Kiafrika; "kiapo" na "hati ya kiapo", anayetakiwa au anayeruhusiwa kuthibitisha

bila ya kula kiapo, inajumuisha tamko la dhati na azimio, na

“kuapa”, itajumuisha “tamka kwa dhati” na “azimia”; "Sheria ya zamani" inajumuisha sheria ya ina yoyote, tangazo la kisheria

au sheria iliyotungwa au kutolewa kabla ya Amri ya Kifalme

kuhusu Tanganyika ya mwaka 1920, na iliyoidhinishwa na Amri

hiyo ya Baraza la Kifalme, na sheria ndogo zilizotungwa na

kuidhinishwa kutumika chini ya Amri hiyo ya Kifalme, na

(isipokuwa ufafanuzi wa neno “Sheria” na “Bunge” katika

kifungu hiki) itajumuisha Sheria ya Bunge na sheria ndogo

zilizotungwa chini ya sheria husika; "Bunge":- (a) katika Sheria za zamani, au katika nyaraka za serikali

zilizotolewa au kutangazwa kabla ya tarehe tisa, Desemba,

1961, ina maana ya Bunge la Uingereza na “Bunge la

Mfalme” ina maana kama hiyo; (b) katika sheria za Bunge la Tanganyika au za Bunge la

Jamhuri ya Muungano, au nyaraka za Serikali iliyotungwa

au kutolewa baada ya siku ya nane, ya Desemba, 1961, au

sheria ya Bunge Maalum la Tanganyika itakuwa na maana

ya Bunge le Jamhuri ya Muungano (na matumizi ya neno

“Sheria ya Bunge” yatajumuisha sheria iliyotungwa na

Bunge Maalum la Tanganyika); "tekeleza" itumikapo kuhusiana na kazi au shughuli, itajumuisha vile vile

kutumia uwezo uliotolewa kisheria, kutekeleza wajibu au

mamlaka ya kisheria; "Katibu Mkuu" maana yake ni mtu aliyeteuliwa na Rais kushika wadhifa

wa Katibu Mkuu; “mtu" maana yake ni neno au msemo utumikao kuelezea mtu binafsi au

kampuni, shirika au mamlaka iliyoundwa kisheria, au isiyopewa

Page 11: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

11

hadhi ya nafsi;

Sura ya 322

"afisa polisi" maana yake ni askari yeyote wa Jeshi la Polisi mwenye cheo

cha konstebo au zaidi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Jeshi

la Polisi na Majeshi ya Nyongeza; "uwezo" inajumuisha hadhi, mamlaka au hiari ya kuamua; "iliyoagizwa au ainishwa" ina maana ya– (a) iliyoainishwa na au chini ya sharia husika ambapo neno hilo

limetumika; (b) kwa pale litumikapo kurejelea kwenye kitu chochote

kilichoainishwa kwenye sheria nyingine ukiacha sheria

ambamo neno hilo limetumika, itajumuisha kitu chochote

kilichoainishwa ndani ya sheria ndogo iliyotungwa kwa

mujibu wa sheria husika; "Rais" maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, na inajumuisha mtu

yeyote mwenye mamlaka ya kutekeleza majukumu ya Rais kwa

mujibu wa kifungu cha 137 cha Katiba; "Tangazo" maana yake ni tangazo la Rais lililochapishwa katika Gazeti la

Serikali; "Chapisho" maana yake ni:- (a) maandiko au machapisho ya aina zote; (b) kumbukumbu ya aina yoyote, kinasa sauti, waya, maandishi

ya matundu, filamu ya senema, au vivuli, kumbukumbu

zitokanazo na uvumbuzi wowote, zitokanazo kwa njia ya

elektronik au umeme, zilizorudufuliwa au kuainishwa na

kupelekwa kwa njia hizo; (c) kitu cha aina yoyote kinachofanana na vile vilivyoelezwa

katika kifungu kidogo cha (b) cha ufafanuzi huu au hata

kama haviwiani, vikiwa katika hali ya kuweza kuonekana

aidha kwa jinsi vilivyo, maumbile yake au kwa namna

yoyote vinaweza kutoa au kurudufu au kunakilisha au

kuwasilisha maneno au mawazo; na (d) kila nakala na rudufisho la chapisho lolote lililoainishwa

katika vifungu vidogo vya (a), (b) au (c);

Sura ya 212

"shirika la umma" maana yake ni kampuni iliyoundwa kwa sheria ya

kipekee na si chini ya Sheria ya Makampuni, na inajumuisha

shirika dogo la kipekee lililoundwa kwa utaratibu usio chini ya

Sheria ya Makampuni;

Sura ya 35

"siku ya mapumziko" maana yake ni siku ambayo imetangazwa kuwa

siku ya mapumziko chini ya Sheria ya Siku za Mapumziko;

"mtumishi wa umma" au "idara ya umma" inajumuisha kila afisa au idara

iliyopewa mamlaka ya kushughulikia mambo ya umma, aidha

chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Rais au

vinginevyo, na inajumuisha afisa au idara chini ya Mamlaka ya

Serikali ya Mtaa, Jumuiya au Shirika la Umma; "sehemu ya wazi au umma" inajumuisha:- (a) mtaa, barabara, gati au bustani ya umma;

Page 12: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

12

(b) jengo, mahala au chombo kitumikacho kwa usafiri wa umma

au ambacho kila mtu anayo haki au anaruhusiwa kukitumia

au kuwemo aidha bila ya masharti au kwa masharti au kwa

kulipa ada au kiingilio; (c) jengo au mahala au chombo kitumikacho kwa umma kwa

ajili ya shughuli za mikutano ya kidini au mkusanyiko wa

watu au kama mahakama; "mhuri wa umma" maana yake ni mhuri wa Jamhuri ya Muungano; "Mkoa" maana yake ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano iliyotangazwa

au inayofahamika kutolewa Tamko na Rais chini ya Ibara ndogo

(2) ya Ibara ya 2 ya Katiba kuwa ni mkoa; "Mkuu wa Mkoa " maana yake ni mtu aliyeteuliwa na Rais kuwa mkuu

wa mkoa, na “Mkuu wa Mkoa” ni mkuu wa mkoa husika; "kanuni" maana yake ni kanuni zilizotungwa chini ya sheria ambamo

neno hilo limetumika; "futa au batilisha" inajumuisha kutengua, kubadili, kusawazisha au

kufuta; "Jamhuri" maana yake ni Jamhuri ya Tanganyika na inajumuisha Jamhuri

ya Muungano;

Sura ya 11 "hakimu mkazi" maana yake ni hakimu mkazi wa daraja lolote

aliyeteuliwa hivyo chini ya Sheria ya Mahakama ya Mahakimu; "afisa mapato" maana yake ni afisa aliyeteuliwa na Katibu Mkuu wa

Hazina kufanya shughuli za kukusanya mapato ya Jamhuri ya

Muungano; "taratibu" maana yake ni, taratibu zilizotungwa chini ya sheria husika

ambamo neno hilo limetumika; "taratibu za mahakama" itumikapo kuhusiana na mahakama, maana yake

ni taratibu zilizotungwa na mamlaka yenye uwezo wa kutunga

kanuni, kutoa maagizo ya kuratibu utendaji na taratibu za

uendeshaji wa shughuli za mahakama; "uza au kuuza" inajumuisha kubadilishana bidhaa, kutoa kwa ajili ya

kuuza na kutandaza bidhaa hadharani kwa ajili ya kuuza; "wasilisha " pale sheria inaporuhusu au kuhitaji hati yoyote kuwasilishwa

kwa mtu yeyote, ikiwa msemo wa “kuwasilisha”, au msemo wa

“toa” au “peleka” au msemo mwingine wowote ukitumika basi

isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo, kuwasilisha

kutakamilika kwa kuandika anuani sahihi na kuituma kwa posta,

baada ya kulipa tozo husika, barua yenye hati na isipokuwa kama

kinyume chake kimedhibitishwa, uwasilishaji utachukuliwa kama

umeshawasilishwa katika muda wa kawaida wa huduma za posta; "saini" ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kisarufi chake na asili ya

msemo wa neno hili, itajumuisha jina au alama, kwa mtu

asiyeweza kuandika; "siku za vikao" likitumika kuhusiana na Bunge, maana yake ni siku

ambapo Bunge limekaa; "tamko la kisheria", kama likitolewa:-

Page 13: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

13

Sura ya 34

(a) nchini Tanzania, maana yake ni tamko lililofanywa chini ya

Sheria ya Viapo na Matamko ya Kisheria;

(b) katika nchi nyingine ya Jumuiya ya Madola, maana yake ni

tamko chini ya kiapo kilichotolewa mbele ya mlinzi wa

amani, mthibitishaji rasmi au mtu mwingine yeyote

mwenye mamlaka ya kutoa au tamko kupokea viapo kwa

mujibu wa sheria yoyote inayotumika katika nchi hiyo; (c) katika nchi nyingine yoyote, maana yake tamko chini ya

kiapo kilichotolewa mbele ya Afisa wa Mambo ya Nchi za

Nje mwenye mamlaka ya chini ya sheria yoyote kuhusu

kupokea viapo au mtu mwingine yeyote aliyeteuliwa na

kukasimiwa madaraka hayo na Waziri wa Mambo ya nje

kwa mujibu wa Tangazo lililochapishwa katika Gazeti la

Serikali; "sheria ndogo" maana yake ni amri, tamko la kisheria, kanuni, kanuni za

mahakama, tangazo, sheria ndogo za miji, kijiji au chama au hati

ya kisheria iliyotolewa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Sheria

husika; "tia hatiani/papohapo" maana yake ni kutolewa kwa hukumu na

mahakama yenye mamlaka ya kutoa hukumu papo hapo; "apa/apisha" kwa mtu anayeruhusiwa kwa mujibu wa sheria kutoa tamko

la dhati au uthibitisho badala ya kiapo, itajumuisha kutoa tamko la

dhati kutoa uthibitisho wa dhati; "maji ya taifa" maana yake ni maji ya bahari, mto au ziwa yaliyopo ndani

ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano; "himaya" maana yake ni Tanganyika;

Sura ya 323

"Mkataba" maana yake ni Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya

Mashariki ulioainishwa katika Nyongeza ya Sheria ya

(Kutekeleza) Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ya

mwaka 1967 ambayo ilifutwa chini ya Sheria ya Mkataba wa

Usuluhishi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki; "chini" itumikapo kuhusiana na sheria au kifungu chochote cha sheria,

itajumuisha “ya”, “kwa mujibu wa” “kufuatana na” na “kutokana

na”; "Siku ya Muungano" maana yake ni tarehe 26 Aprili, 1964;

"Falme Zilizoungana" maana yake ni Uingereza na Ireland ya Kaskazini;

"Jamhuri ya Muungano" maana yake– (a) kwa kipindi baada ya terehe 11 Desemba, 1964 ni Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania; (b) kwa kipindi kilichoanzia Siku ya Muungano na kuishia

tarehe 11 Desemba, 1964 ni Jamhuri ya Muungano wa

Tanganyika na Zanzibar;

"Makamu wa Rais" maana yake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya

Muungano;

"wosia" inajumuisha sehemu ya wosia, kiambatanisho cha wosia au

Page 14: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

14

kiambatanisho cha wosia kinachotangua sehemu ya wosia;

"maneno" yanajumuisha tarakimu na alama; "maandiko/maandishi", na maelezo yanayotaja maandiko au maandishi

yatajuisha vilevile picha, lithographia, kuandika au kuchora na

jiwe na aina zozote za kuonyesha maandiko au kurudufu maneno

kwa namna ya kuonekana; "sheria za Bunge" maana yake ni Sheria zote zilizotungwa na Bunge

ambazo kwa wakati husika zinatumika pamoja na sheria ndogo

zote zinazotumika zikiwepo na Sheria za Jumuiya pamoja na

sheria zote zilizoazimwa; "mwaka" maana yake ni kipindi cha miezi kumi na miwili.

Matumizi 5. Fasili au kanuni za ufafanuzi zilizomo katika sheria yoyote

zitatumika kufafanua vipengele vya sheria ambamo vipo au kanuni za

ufafanuzi zilizopo katika sheria hiyo, pamoja na vipengele vingine vya

sheria hiyo. Sheria hunena

daima 6. Sheria ya Bunge itachukuliwa kama inanena wakati wote na

litokeapo jambo au kitu kimeelezwa katika wakati wa sasa, ifahamike

kuwa inajumuisha nyakati zote, ili kila sehemu yoyote ya sheria husika

ipewe maana yake halisi kulingana na maudhui na malengo ya sheria

husika. Sehemu ya

matamshi na

miundo ya fasihi

7. Mahali ambapo neno au fungu la maneno vimefafanuliwa

katika sheria, sehemu zingine za msemo au vifungu vya maneno vitakuwa

na maana sawia. Jinsia na

tarakimu 8. Katika sheria yoyote:-

(a) maneno yanayoonyesha jinsia ya kiume yatajumuisha

vilevile jinsia ya kike;

(b) maneno yanayoonyesha jinsia ya kike yatajumuisha vilevile

jinsia ya kiume;

(c) maneno ya umoja yatajumuisha vilevile uwingi na maneno

ya uwingi yatajumuisha umoja; Rejeo ya neno

Waziri katika

sheria

9. Anapotajwa Waziri katika sheria tafsiri yake itakuwa ni moja

ya zifuatazo–

(a) anapotajwa Waziri ndani ya sheria, ifafanuliwe kuwa ndiye

waziri mwenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria

hiyo, au kama ni katika vifungu vya sheria ambamo au kwa

mujibu wa vifungu hivyo neno hilo limetumika, itakuwa na

maana kwamba mwenye dhamana wakati huo ni Rais; (b) iwapo ni kwenye sheria ndogo, neno waziri mwenye

dhamana ya kusimamia utekelezaji wa Sheria au vifungu vya

sheria, itakuwa na maana mwenye dhamana wakati huo ni

Rais; na

Page 15: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

15

(c) itajumuisha Kaimu Waziri badala ya Waziri husika kama

ilivyoelekezwa katika kifungu (a) au (b). Marejeo kwa

tarakimu

kujumuishwa

10. Rejeo kwenye sheria kwa kutumia namba au herufi au kwa

namba na herufi kwa pamoja, au kwa sehemu mbili au zaidi ya sheria

husika, itatafsiriwa kama inajumuisha sehemu iliyoelezwa kwa kutumia

rejeo iliyofafanuliwa awali na ile iliyorejewa mwishoni.

Tafsiri ya rejeo

ndani ya kifungu,

n.k.

11.-(1) Endapo katika sheria, rejeo imefanywa kwenye sura,

sehemu, nyongeza, kiambatanisho au fomu bila ya maelezo mengine ya

kuonyesha rejeo imefanywa kwenye sura, sehemu, kifungu nyongeza,

kiambatanisho au fomu ya au kwa mujibu wa sheria nyingine, basi rejeo

hiyo itatafsiriwa kana kwamba inahusiana na sheria husika ambamo rejeo

limefanywa. (2) Endapo katika kifungu cha sheria, rejeolimefanywa kwenye

kifungu kidogo, aya, aya ndogo, au kipengele chini ya hivyo, na bila ya

maelezo mengine ya kuonyesha kama rejeo la kifungu kidogo, aya, aya

ndogo au kipengele kidogo chini ya hivyo imefanywa kwa mujibu wa

sehemu nyingine au kifungu kingine, basi rejeo hilo litakuwa kwa mujibu

wa na itatafsiriwa kana kwamba ni rejeo kwa kifungu kidogo, aya, aya

ndogo au sehemu ya kifungu ambamo rejeo hilo limefanyika. (3) Endapo katika nyongeza ya sheria, rejeo imefanywa kwenye

kipengele, aya, au sehemu nyingine bila ya maelezo ya kuonyesha kwa

mahsusi, kipengele, kipengele kidogo, aya au sehemu nyingine mahsusi,

basi rejeo hilo litakuwa kwa mujibu wa na litatafsiriwa kana kwamba ni

rejeo kwenye kipengele, kipengele kidogo, aya, au sehemu nyingine ya

nyongeza ambayo rejeo hilo limefanyika. (4) Masharti ya vifungu (1), (2), na (3) yatatumika baada ya

kuzingatia mabadiliko ya lazima kuhusiana na ufafanuzi wa maudhui ya

sheria ndogo husika. Rejeo kwenye

sheria kama

ilivyorekebishwa

12.-(1) Rejeo katika sheria kwenye sheria nyingine, litachukuliwa

kujumuisha rejeo kwenye sharia hiyo kama ilivyorekebishwa.

(2) Rejeo katika sheria kwenye kifungu cha sheria, litatafsiriwa kama

rejeo kwenye kifungu husika kama kitakavyorekebishwa. (3) Rejeo katika sheria kwenye Sheria ya Kifalme, au kwenye kifungu

cha Sheria ya Kifalme, litatafsiriwa kujumuisha rejeo kwenye sheria hiyo

ya Kifalme au kifungu kama kitakavyorekebishwa. Tafsiri ya neno

"au" kitofauti 13. Kuhusiana na sheria iliyotungwa au kupitishwa baada ya

kuanza kutumika kwa Sheria hii, lakini kwa kuzingatia kifungu cha 2 (4),

"au", "ingine" na "vinginevyo" yatatafsiriwa kuelezea tofauti na sio

lazima kuonyesha usawa au uwiano, isipokuwa kama neno "a kufanana"

au maneno mengine yenye maana hiyo yameongezwa.

Page 16: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

16

SEHEMU YA TATU

KUANZA KUTUMIKA NA KUTAJWA KWA SHERIA Tarehe ya kuanza

kutumika kwa

sheria

14. Kila sheria itaanza kutumika katika tarehe ya kuchapishwa

kwake katika Gazeti la Serikali, isipokuwa kama imeelekezwa

vinginevyo au kama imeelekezwa katika sheria husika au katika sheria

nyingine kwamba sheria hiyo itaanza kutumika katika tarehe nyingine. Muda wa kuanza

kutumika kwa

sheria

15. Ikielekezwa kwamba sheria itaanza kutumika siku Fulani, basi

sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia alfajiri ya siku hiyo.

Kuanza kutumika

kwa sheria palipo

na kifungu cha

masharti ya

kutolewa taarifa

ya kuanza

kutumika

16. Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 14, kwa pale ambapo

sheria imeelekeza au kifungu cha sheria hiyo kimeelekeza kuwa sheria

itaanza kutumika katika tarehe itakayoteuliwa kwenye tangazo, kifungu

hicho na kile kinachotoa jina la sheria, vitaanza kutumika tarehe Sheria

inaposainiwa na Rais, isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo.

Tafsiri ya uwezo

wa kupanga siku

ya kuanza

kutumika kwa

sheria

17. Uwezo wa kutangaza siku ya kuanza kutumika kwa sheria

haujumuishi uwezo wa kuainisha au kutangaza-

(a) siku ya nyuma kabla ya tarehe ambapo tangazo hilo

linachapishwa katika Gazeti la Serikali; au (b) siku tofauti kwa vifungu tofauti vya sheria hiyo, isipokuwa

kama kuna vifungu dhahiri vinavyoruhusu kufanya hivyo. Ushahidi wa

tarehe ya

kusainiwa

18. Pale ambapo inaonekana tarehe katika nakala ya Sheria

iliyochapishwa, au inayodaiwa kuchapishwa na Mchapa Mkuu wa

Serikali, ikionyeesha kuwa ndiyo tarehe ambapo Rais aliridhia na kusaini

Sheria hiyo au sehemu yake, tarehe hiyo inayoonekana ndiyo

itakayochukuliwa kama ushahidi kuwa siku hiyo ndiyo ambamo Rais

aliweka saini yake katika Sheria hiyo, na mahakama zitaridhia hivyo. Utekelezaji wa

uwezo kabla ya

kuanza kutumika

19.-(1) Endapo kifungu cha sheria hakianzi kutumika baada ya

kutungwa kwa sheria husika na kifungu hicho kama kingeanza kutumika

kingeweza kutoa mamlaka ya– (a) kutolewa hati/agizo la kisheria au kiutawala;

(b) kutoa notisi au hati ya aina nyingine;

(c) kuteua mtu kushika madaraka fulani;

(d) kuanzisha mamlaka inayoundwa na watu fulani, mamlaka

ambayo ni ya kisheria au siyo ya kisheria, au

(e) kufanya jambo lolote kwa mujibu wa sheria hiyo; Basi, uwezo huo wa kisheria, bila ya kujali kwamba kifungu hicho

hakijaanza kutumika, lakini kwa kuzingatia masharti ya vifungu vya (3)

na (4), uwezo huo waweza kutumika wakati wowote baada ya kutungwa

kwa sheria hiyo kwa jinsi ikatavyoonekana ni lazima au ni muhimu kwa

lengo la kuwezesha sheria hiyo au vifungu vyake kuanza kutumika, au

Page 17: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

17

vifungu vyake kutumika mara baada vifungu hivyo kuanza kutumika. -(2) Kwa pale ambapo– (a) kifungu cha sheria hakianzi kutumika baada ya kutungwa

kwa sheria na kifungu hicho kingerekebisha Sheria kama

kingeanza kutumika; (b) kifungu cha ile sheria nyingine kingeweza, kama kifungu

kilichotajwa awali kingeanza kutumika kutoa uwezo wa– (i) kutoa amri au hati yenye nguvu kisheria au

kiutawala;

(ii) kutoa notisi au hati ya aina nyingine;

(iii) kuteua mtu kushika wadhfa au madaraka ya ofisi

fulani;

(iv) kuunda chombo maalumu chenye au kisichokuwa

na taaswira ya kampuni; au

(v) kufanya jambo lolote kwa madhumuni ya ile sheria

nyingine, basi, uwezo huo, bila ya kujali kuwa kifungu kilichotajwa awali

hakijaanza kutumika, lakini kwa kuzingatia matakwa ya vifungu vya (3)

na (4) vyaweza kutumika wakati wowote baada ya kupitishwa kwa sheria

ambamo kifungu kilichotajwa awali kimo, na kwa jinsi ilivyo lazima au

muhimu kwa lengo la kuwezesha ile sheria nyingine iweze kutumika au

vipengele vya sheria ile, mnamo au baada ya kifungu kilichotajwa awali

kuanza kutumika. -(3) Kwa pale ambapo uwezo wa kutoa hati au amri zenye nguvu

kisheria au kiutawala upo, au uwezo wa kutoa notisi au hati nyingine,

uwezo huo waweza kutumiwa kama ilivyoelekezwa katika kifungu

kidogo cha (1) au cha (2), na hati hiyo, au notisi yaweza kuwa na

nguvu/kuanza kutumika:- (a) katika siku ambayo sharti lililorejewa katika kifungu kidogo

cha (1) au, kama itakavyokuwa, sharti lililotajwa mwanzo

katika kifungu kidogo cha (2) kinaanza kutumika; au (b) katika siku ambayo kingeanza kutumika, iwapo muda ule

ambapo hati ilipotolewa, au notisi au waraka , kifungu

kilichotajwa au kilichotajwa awali kitakuwa kimeanza

kutumika, kutegemea na kitakachotokea mwishoni. -(4) Pale uwezo wa kuteua mtu katika ofisi fulani, au kuunda

taasisi unatekelezwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) au cha (2),

mtu aliyeteuliwa kushika wadhifa huo anaweza kutekeleza majukumu ya

ofisi hiyo, au vyovyote itakavyokuwa, taasisi iliyoundwa inaweza

kukutana na kutekeleza kazi, wajibu na uwezo, lakini tu kwa kuzingatia

madhumuni yaliyorejewa katika kifungu kidogo cha (1) au cha (2)

kutegemeana na kifungu kidogo kitakachotumika; na kwa madhumuni ya

kifungu chochote kinachohusu muda, kitachukuliwa kutokuanza mpaka

kifungu husika kilichorejewa katika kifungu cha (1) au cha (2) kwa

vyovyote itakavyokuwa, kuanza kutumika. (5) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (4) cha

Page 18: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

18

kifungu cha (2), kifungu hiki kitatumika katika sheria zilizopitishwa

baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii. Kutajwa kwa

Sheria 20.-(1) Pale sheria imerejewa, itakuwa inatosheleza kwa

madhumuni yote kutaja au kurejea sheria hiyo kwa:- (a) jina fupi au mtajo (kama upo) kwa jinsi ambavyo sheria hiyo

imetajwa; (b) kama ni sheria, mwaka ilipopitishwa na namba yake kati ya

sheria nyingine za mwaka huo; (c) kama ni sheria, namba ya Sura ya sheria hiyo katika Juzuu za

sheria zilizorekebishwa. (2) Kifungu cha sheria kinaweza kutajwa kwa rejeo la sehemu,

kifungu, kanuni, taratibu, ibara au mgawanyo wowote wa sheria ambapo

kifungu hicho kinapatikana. (3) Mtajo wa sheria yoyote utafanywa kutegemeana na nakala ya

chapisho la sheria, au chapisho linalodhaniwa kuwa limechapwa na

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali. Marejeo ya sheria

kwa siku ya

kuanza kutumika

21. Rejeo la sheria kuhusu siku ya kuanza kutumika itakuwa,

pale, baadhi ya vifungu vinaanza kutumika katika tarehe tofauti, itakuwa

siku ile ambayo kifungu husika cha sheria hiyo kinaanza kutumika.

SEHEMU YA NNE

MASHARTI YA UTUNGWAJI WA SHERIA NA UTUMIKAJI WA SHERIA Sheria kuwa

sheria ya Umma 22. Kila sheria itahesabiwa kuwa iko wazi na inafahamika kwa

umma wote, isipokuwa kama kutakuwa na maelezo ya kuonyesha

vinginevyo, na mahakama zote zitatilia maanani kuwa sheria zote

zinafahamika kwa umma. Vifungu

kujitosheleza

kama sheria

kamili

23. Kila kifungu cha sheria kitakuwa na maana na uwezo timilifu

kama sheria bila ya kuwa na haja ya / ulazima wa maelezo ya utangulizi /

dibaji. Kifungu

kinaweza

kurukwa au

kufutwa katika

Kikao hicho

hicho

24. Sheria inaweza kurekebishwa au kufutwa katika kikao hicho

hicho cha Bunge kama kile kilichopitisha sheria hiyo.

Utangulizi na

Majedwali 25.-(1) Utangulizi katika sheria, ni sehemu ya sheria husika, na

unapaswa kutafasiriwa kama sheria yenyewe, kwa madhumuni ya

kusaidia kutoa ufafanuzi na madhumuni ya sheria hiyo. (2) Kiambatanisho au Jedwali au orodha katika sheria pamoja na

maelezo mafupi vitakuwa ni sehemu ya sheria hiyo. Vichwa, maelezo 26.-(1) Vichwa vya habari ya sehemu, mgawanyo na sehemu ya

Page 19: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

19

ya pembeni, na

marejeo chini ya

ukurasa na

marekebisho

makosa ya Na 17

ya 1996 Jedwali.

mgawanyo vitahesabika kama sehemu ya sheria hiyo.

(2) Maelezo ya pembeni au rejeo za chini ya kurasa katika sheria,

na bila ya kuathiri kifungu cha (1), kichwa cha sehemu ya sheria, kanuni,

taratibu sheria-ndogo au ibara ya sheria havitahesabika, kama sehemu ya

sheria. (3) Ikiwa kutakuwa na kosa lolote la maandishi au uchapishaji wa

Muswada wa Sheria au Sheria yenyewe kwenye Gazeti la Serikali,

Mwandishi Mkuu wa Sheria au afisa yeyote wa Ofisi ya Mwanasheria

Mkuu wa Serikali aliyepewa madaraka kwa maandishi kwa niaba hiyo na

Mwandishi Mkuu wa Sheria anaweza kwa amri iliyochapishwa katika

gazeti la Serikali kutoa maelekezo ya kusahihisha makosa hayo na kila

agizo litasomeka pamoja na Muswada au Sheria inayohusiana nayo na

Mswada huo au Sheria, kuanzia tarehe ya kuchapishwa itaanza kutumika

kama ilivyosahihishwa.

SEHEMU YA TANO

MAREKEBISHO NA KUFUTWA KWA SHERIA Fasiri ya sheria

inayorekebisha

Sheria pamoja na

marekebisho

yake

27. Pale ambapo sheria inarekebisha sheria nyingine,

marekebisho ya Sheria hiyo, kama yatakuwa yamebeba maudhui ya

Sheria inayorekebishwa bila ya kuwa na madhumuni mengine,

itafafanuliwa na kufasiriwa kama sehemu ya Sheria iliyorekebishwa. Kufutwa kwa

Sheria kama

ilivyorekebishwa

28. Pale ambapo Sheria iliyorekebishwa kwa Sheria nyingine

imefutwa, kufutwa kwa Sheria hiyo kutahusu pia kufutwa kwa vipengele

vyote vya ile Sheria ya mwanzo ambayo ilirekebishwa. Kufuta kwa

kufuta 29. Pale ambapo Sheria inafuta Sheria inayorekebisha, kufuta

huko hakutahuisha sheria yoyote ambayo ilikuwa imefutwa, isipokuwa

kama yameongezwa maneno ya kuhuisha sheria hiyo. Kufuta na

Kubadilisha 30. Pale ambapo Sheria inarekebisha Sheria nyingine na kuweka

vifungu vingine mbadala, Sheria iliyorekebishwa itabakia hai na

itaendelea kutumika hadi hapo vifungu vilivyowekwa mbadala

vitakapoanza kutumika. Amri ya masharti

mbadala 31. Pale ambapo Sheria inarekebisha na inatunga sheria nyingine

pamoja na au bila ya mabadiliko, katika sheria yoyote iliyotungwa:- (a) wilaya zote au mgawanyo wa maeneo mengine;

(b) halmashauri zote, mashirika, bodi, mabaraza, kamisheni,

bodi za wadhamini au mamlaka zingine zilizoundwa na

chaguzi zote na uteuzi wowote uliofanywa; na

(c) ofisi zote zilizoanzishwa na uteuzi wowote wa maafisa

uliofanywa;

(d) sheria ndogo zote, hati, vyeti na nyaraka zilizotolewa; na

(e) matendo mengine yote, mambo na vitu,

Page 20: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

20

ambavyo wakati sheria inayofuta inaanza kutumika yalikuwepo, au

yalikuwa na nguvu kisheria, kwa mujibu wa vifungu vya sheria hiyo,

yataendelea kuwa halali kama kwa mujibu wa vifungu hivyo

yanaruhusiwa kuendelea, au yamehuishwa, yamefanywa au kutendwa na

yamechimbuka au kuhalalishwa au kutendwa kwa mujibu wa sheria hiyo. Vifungu vya

jumla

vinavyobakizwa

baada ya kufutwa

32.-(1) Pale ambapo Sheria inafuta au kurekebisha Sheria

nyingine, sheria iliyofutwa, isipokuwa kama kuna madhumuni tofauti-

(a) haitahuisha jambo lolote ambalo halikutumika au

halikuwepo wakati ufutwaji unaanza kutumika; (b) hautaathiri matumizi yaliyopita ya sheria iliyofutwa au kitu

chochote kilichofanywa kwa usahihi kuhamishwa chini ya

sheria hiyo; (c) haitaathiri haki yoyote, maslahi, hatimiliki, uwezo,

upendeleo uliotolewa, uliopatikana, uliojitokeza,

ulioanzishwa au uliotekelezwa au hadhi yoyote au uwezo

kabla ya ufutwaji; (d) haitaathiri wajibu wowote, shuruti, kuwiwa au wajibu wa

kuthibitisha uliotwikwa, uliotolewa au ulioingiwa; (e) haitaathiri utwaaji adhabu au utwaaji ulioingiwa au wajibu

wa kuingiwa kutokana na kosa lililotendwa dhidi ya sheria

hiyo; (f) haitaathiri uchunguzi wowote, mwenendo wa kisheria au

nafuu kuhusiana na haki yoyote, maslahi, hakimiliki, uwezo,

hadhi, wajibu, shuruti au wajibu wa kuthibitisha, adhabu au

kutwaliwa kwa mali; na uchunguzi wowote, mwenendo wa kisheria au unafuu unaweza

kuanzishwa, kuendelezwa au kutekelezwa na adhabu yoyote hiyo au

utwaaji unaweza kutwikwa na kutekelezwa kama vile sheria inayofutwa

hayapitishwa au kutolewa. (2) Kuwepo kwa vifungu vinavyobakizwa dhahiri kuhusiana na

kufutwa kulikofanyika hakutachukuliwa kuathiri matumizi ya kifungu

hiki kuhusiana na athari ya kufutwa kulikofanyika. Athari ya

kufutwa kwa

sheria kwenye

sheria ndogo

33.-(1) Pale ambapo sheria:-

(a) inafuta au kurekebisha sheria nyingine na kuweka vifungu

mbadala au ;

(b) inafuta na kutunga sheria nyingine bila ya au pamoja na

marekebisho, Sheria ndogo zote zilizotungwa chini ya Sheria inayofutwa na ambazo

zilikuwa zinatumika kabla ya kuanza kutumika kwa sheria inayofuta

sheria nyingine, kama zinzenda sambamba na Sheria inayofuta Sheria

nyingine, zitaendelea kutumika na kuwa na nguvu kisheria kana kwamba

sheria ndogo hizo zimetungwa chini ya Sheria inayofuta sheria nyingine.. (2) Sheria ndogo inayoendelea kutumika chini ya kifungu kidogo

cha (1), inaweza kurekebishwa au kufutwa kama vile imetungwa chini ya

Page 21: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

21

Sheria inayofuta sheria nyingine. Athari ya

kumalizika kwa

muda wa

kutumika kwa

sheria

34. Mara baada ya muda wa kutumika kwa Sheria utakapoisha, au

kutumika kwa Sheria kutakapofikia tamati, kifungu cha 33 kitatumika

kama vile Sheria iliyotungwa itakuwa imefutwa .

SEHEMU YA SITA

MASHARTI YANAYOHUSU SHERIA NDOGO Rais anaweza

kutunga Sheria

Ndogo

35. Iwapo sheria yoyote inaruhusu au imeweka masharti ya

kutungwa kwa sheria ndogo na haielekezi ni nani mwenye mamlaka ya

kutunga sheria ndogo hizo, basi ndogo hizo zinaweza kutungwa na Rais. Masharti ya

jumla kuhusu

uwezo wa

kutunga Sheria

Ndogo

36.-(1) Sheria ndogo haitakuwa kinyume na masharti ya Sheria

Kuu ambayo imetoa mamlaka ya kutungwa kwa, Sheria Ndogo hiyo, au

sheria nyingine, na Sheria Ndogo itakuwa batili kwa kiasi ilivyokuwa

kinyume na matakwa ya Sheria Kuu.

(2) Pale Sheria Ndogo inaelekea kutungwa kwa kutekeleza

mamlaka fulani au mamlaka nyingine, itachukuliwa kuwa imetungwa

kwa kutekeleza mamlaka zote ambazo zimepelekea kutungwa kwa Sheria

hiyo . (3) Itachukuliwa kwamba panapokuwa hakuna ushahidi

vinginevyo, masharti yote na hatua za mwanzo muhimu ya kutungwa kwa

Sheria Ndogo zitakuwa zimefuatwa na kufanywa. (4) Pale Sheria inatoa uwezo wa kutunga Sheria Ndogo,

itachukuliwa kwamba imejumuisha mamlaka ya kutekeleza kwa utaratibu

kwa namna hiyo na kwa mujibu wa masharti (kama yatakuwepo) ya

kurekebisha au kufuta Sheria Ndogo yoyote; na kama mtu aliyepewa

mamlaka hayo atakuwa amebadilishwa kabisa au kupewa mtu mwingine,

uwezo uliotolewa chini ya kifungu kidogo hiki, juu ya mtu wa mwanzo

unaweza ukafanywa na mtu aliyebadilishwa juu ya mambo yote au vitu

ambavyo viko chini ya mamlaka yake kama vile ni mtu wa mwanzo (5) Pale ambapo Sheria inampa uwezo mtu wa kutunga Sheria

Ndogo kwa madhumuni ya jumla na pia kwa madhumuni yoyote maalum

yanayohusiana na maudhui hayo, kutajwa kwa madhumuni maalum

hakutaathiri ujumla wa mamlaka au uwezo wa kutunga Sheria kwa

madhumuni ya jumla yaliyoainishwa. (6) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (4) cha Kifungu cha 2,

Sheria Ndogo inaweza kuweka masharti kwamba kukiukwa kwa sheria

ndogo ni kosa linaloweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini kuhusiana na

kosa hilo kwa kiwango kisichozidi shilingi laki sita. (7) Uwezo wa kutunga Sheria Ndogo unaweza ukafanywa– (a) ama kuhusiana na jambo lolote ambalo uwezo huo

umetolewa, au kuhusiana na mambo yote ambayo

yametolewa maelezo maalum, au kuhusiana na jambo

maalum au mambo yaliyoainishwa; na

Page 22: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

22

(b) kwa ajili ya kuweka, kwa ajili ya mambo ambayo

yanatekelezeka – (i) sharti sawa kwa mambo yote yanayohusu uwezo

unaotekelezwa au kifungu tofauti kwa mambo

tofauti au aina au mambo au masharti tofauti kwa

jambo linalofanana au aina mbalimbali ya mambo

kwa madhumuni tofauti ya sheria; au (ii) sharti jingine lolote ama bila masharti au kwa sharti

lolote maalum. (8) Sheria Ndogo inaweza kutungwa– (a) kwa ajili ya kutumika– (i) muda wote au muda maalum; (ii) wakati wote au katika sehemu maalumu ya; (b) kwa ajili ya kuhitaji jambo lolote litakalokuwa limeathiriwa

na sheria kuwa–

(i) kwa mujibu wa viwango maalum au matakwa

maalum; (ii) iliyoidhinishwa na au kwa kuridhika kwa mtu

maalum au chombo au aina ya watu maalum au

chombo; (c) kwa ajili ya kumpa mamlaka ya ridhaa kwa mtu maalum au

chombo au aina maalum ya watu au chombo; na (d) kwa ajili ya kutoa katika jambo maalum au aina ya mambo

kwa ajili ya kutoa watu au vitu au aina ya watu au vitu

kutoka kwenye masharti ya sheria ndogo ama kwa masharti

maalum ama vyote au kwa kiwango maalum kilichoelezwa. (9) Kwenye vifungu vidogo vya (7) na (8), neno “Maalum” maana

yake maalum kwenye Sheria Ndogo. Utangazaji na

kuanza kutumika

kwa Sheria

Ndogo

37.-(1) Pale Sheria inapotoa mamlaka ya kutunga Sheria Ndogo,

Sheria Ndogo zote zilizotungwa chini ya mamlaka hiyo isipokuwa kama

nia iliyokinyume inajitokeza – (a) inatangazwa kwenye Gazeti la Serikali; (b) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2) na kifungu cha 39,,

itaanza kutumika siku ya kutangazwa, au pale siku nyingine

maalum itakapotamkwa au kutolewa katika Sheria Ndogo

kwenye siku hiyo. (2) Sheria Ndogo haitatamka kuanza kutumika katika siku kabla

ya siku ya kutangazwa, pale inapotokea iwapo Sheria Ndogo imeanza

kutumika:- (a) haki ya mtu yeyote (ambaye si Serikali au taasisi ya serikali)

iliyopo mara kabla ya siku ya utangazaji itaathiriwa kwa

namna ambayo itamuathiri mtu huyo; au (b) wajibu utatwikwa kwa mtu yeyote (ambaye si serikali wala

Serkali au taasisi ya serikali) kuhusiana na kitu chochote

kilichofanywa au kutofanywa kabla ya siku ya utangazaji,

Page 23: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

23

na iwapo sharti lolote limefanywa kinyume na kifungu kidogo hiki, sharti

hilo litakuwa batili. (3) Mamlaka ya kupanga siku ambayo Sheria Ndogo itaanza

kutumika haitajumisha mamlaka ya kupanga siku tofauti kwa masharti

tofauti ya Sheria hiyo, labda kama sharti la wazi limefanywa kwa ajili

hiyo . Kuwasilisha

Kanuni Bungeni

na kukataliwa

38.-(1) Kanuni au sheria ndogo zote zitawasilishwa Bungeni ndani

ya kipindi cha siku sita za kukaa kwa Bunge kufuatia utangazaji

utakaofuata wa kanuni katika Gazeti la Serikali. (2) Bila ya kuathiri kifungu chochote kinachoelekeza vinginevyo

katika sheria, iwapo Bunge litapitisha Azimio la kukataa kanuni yoyote

ambayo taarifa ya azimio hilo litatolewa ndani ya siku 14 ya kukaa kwa

bunge baada kanuni hizo zimekwishawasilishwa bungeni au kama

kanuni zozote hazijawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa kifungu kidogo

cha (1), kanuni hizo zitakoma kutumika , lakini bila ya kuathiri uhalali au

kuhalalisha chochote kilichotendwa au kilichoachwa kutendwa katika

wakati huo. (3) Kifungu kidogo cha (2) kitatumika bila ya kujali

kwambakipindi cha siku 14 kichotajwa katika kifungu kidogo hicho au

sehemu ya kipindi hicho hakitatokea katika au wakati wa kikao hicho

hicho cha Bunge kile ambacho kanuni zimewasilishwa Bungeni

kinahusika . (4) Bila ya kujali sharti lolote katika Sheria yoyote iliyo kinyume,

kama Bunge katika kipindi chochote litapitisha azimio la kubadilisha

kanuni yoyote au kuweka kanuni mbadala au sehemu ya kanuni ambayo

imekataliwa na Bunge chini ya kifungu kidogo cha (2), katika kupitisha

azimio lolote– (a) linalorekebisha Kanuni au sehemu ya kanuni, kanuni

iliyobadilishwa baada ya kuisha kwa siku saba, kutoka siku

ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali ya taarifa iliyotolewa

katika kifungu kidogo cha (5), itaanza kutumika kama

ilivyorekebishwa. (b) kuweka kanuni mbadala au sehemu ya kanuni, kanuni

iliyobadilishwa baada ya kuisha kwa siku saba, kutoka siku

ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali ya taarifa iliyotolewa

katika kifungu kidogo cha (5), itaanza kutumika kama

ilivyorekebishwa. (5) Baada ya kupitishwa kwa Azimio kwa mujibu wa kifungu

kidogo cha (2) cha kifungu cha (4), Taarifa ya Azimio hilo itachapishwa

kwenye Gazeti la Serikali ndani ya muda wa siku 21 baada ya kupitishwa

kwa Azimio hilo. (6) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha

kifungu cha 34, pale ambapo– (a) kanuni hazikubaliki chini ya kifungu hiki; na

Page 24: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

24

(b) kanuni hizo zilizorekebishwa au kufuta kanuni ambazo

zilikuwa zinatumika mara kabla ya kanuni zilizotajwa kwa

mara ya kwanza hazijaanza kutumika,

kukataliwa kwa kanuni hizo kutahuisha kanuni za awali kwenye ile siku

na siku ya kukataliwa. (7) Iwapo Sheria ambayo inatoa uwezo au inaelekeza

kutengeneza kwa kanuni na mtu yeyote isipokuwa Rais,na inataka

kanuni hizo kukubalika au kuthibitishwa na Rais au mtu mwingine

yeyote au taasisi kabla kanuni hizo hazijatakuwa na nguvu za kisheria,

kifungu kidogo cha (1) hakitatumika kwenye kanuni hizo isipokuwa

kama zitakubalika au kuthibitiswa kama inavyotakiwa. (8) Katika kifungu hiki, neno “kanuni” linajumuisha kanuni na

Sheria Ndogo. Tafsiri ya sheria

ndogo 39.-(1) Maneno na misamiati inayotumiwa katika Sheria Ndogo

itakuwa na maana sawa na Sheria iliyotungwa chini ya Sheria Ndogo. (2) Rejeo katika Sheria Ndogo kwa neno “Sheria” litafafanuliwa

kumaanisha rejeo kwenye Sheria ambayo, Sheria Ndogo imetungwa.

Kutajwa kwa

sheria ndogo

40. Sheria Ndogo itatajwa kwa kurejea kwenye jina fupi kama

litakuwepo, au kwa kurejea kwenye namba ya Tangazo inayotolewa

kwenye Gazeti la Serikali. Marejeo ya

sheria

kujumuisha

sheria ndogo

41.-(1) Rejeo kwenye Sheria liltafchukuliwa kujumuisha rejeo

kwenye Sheria Ndogo yeyote iliyotungwa kwa mujibu wa Sheria

mama/kuu husika.

(2) Rejeo kwenye Sheria kwa Sheria ya mapokezi litafafanuliwa

vilevile kuhusu rejeo kwenye Sheria Ndogo iliyotungwa chini ya Sheria

mama. Matendo chini ya

sheria ndogo

kuchukuliwa

kama

yamefanyika

chini ya Sheria

42. Rejeo chini ya Sheria Ndogo kwenye sheria inayotumika

litatafsiriwa kujumuisha rejeo kwenye Sheria Ndogo iliyotungwa chini ya

Sheria mama.

Ada na tozo 43.-(1) Sheria Ndogo inaweza kuweka masharti ya kutozwa kwa

ada na tozo zinazohusiana na jambo lolote kwa kutilia maanani masharti

yaliyo wekwa katika Sheria Ndogo au katika Sheria ambayo, Sheria

Ndogo imetungwa. (2) Pale kifungu kimewekwa na Sheria Ndogo kinachohusu ada au

tozo, Sheria Ndogo husika yaweza kuweka mojawapo au baadhi ya

masharti yafuatayo– (a) ada maalumu au tozo;

(b) kuweka kiwango cha juu au cha chini cha ada au tozo ya aina

Page 25: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

25

nyingine;

(c) kiwango cha juu na cha chini cha ada au tozo;

(d) ada au tozo kulingana na thamani ya kitu;

(e) kulipwa kwa ada au tozo kwa pamoja au kwa chini ya

masharti maalumu au mazingira yaliyoainishwa; na

(f) kupunguziwa, kusamehewa au kurejeshewa, kiasi chote au

sehemu ya ada au tozo. (3) Iwapo patakuwa na punguzo, msamaha au kurejeshewa, kwa

ada yeyote au sehemu ya ada au tozo ilivyotozwa na Sheria Ndogo,

punguzo hilo au msamaha au rejesho vyaweza kuchukuliwa kutumika au

kutumika kwa ujumla au kwa masharti maalum– (a) kuhusiana na mambo fulani au shughuli fulani au mambo au

aina ya mambo au shughuli;

(b) kuhusiana na nyaraka fulani au aina ya nyaraka;

(c) pale tukio linapotokea au wakati tukio linapoacha kutokea;

(d) kuhusiana na watu wa aina fulani au tabaka la watu fulani;

au

(e) kuhusiana na mchanganyiko wa mambo, shughuli, nyaraka,

matukio au watu, na yaweza kuelezewa kutumika au

kutumika kwa masharti yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo

au kwa uamuzi wa mtu yeyote aliyeainishwa katika Sheria

Ndogo. (4) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 2

cha kifungu hiki kitatumika kwenye Sheria Ndogo zilizotungwa chini ya

mamlaka iliyopewa ya kutunga Sheria baada ya kuanza kutumika kwa

Sheria hii.

SEHEMU YA SABA

UWEZO NA WAJIBU WA KISHERIA Muda wa

utekelezaji

uwezo au wajibu

kwa mujibu wa

sheria

44. Pale ambapo Sheria imetoa mamlaka au kuweka wajibu,

mamlaka hayo ya waweza kutekelezwa na wajibu huo kutekelezwa mara

kwa mara wakati tukio litahitaji.

Rejeo kwa

mshika ofisi

itajumuisha

warithi

45. Pale Sheria itatoa mamlaka au kutoa wajibu kwa afisa

aliyeshika madaraka ya ofisi ya umma, mamlaka hayo yanaweza

kutekelezwa na wajibu utafanywa na mtu ambaye kwa wakati uliopo

atakuwa ameshika nafasi hiyo kihalali, anakaimu au kutekeleza

majukumu ya ofisi. Tafsiri ya

maneno ya

kuwezesha.

46.-(1) Pale ambapo sheria imetoa mamlaka kwa mtu kufanya au

kupelekea kufanyika kwa kitu chochote au jambo, uwezo huo

utachukuliwa kuwa umetolewa kwa watu, ili kumwezesha mhusika

kufanya jambo au kusimamia kisheria utekelezwaji wa kitu au jambo. (2) Bila ya kuathiri ujumla wa matakwa ya kifungu kidogo cha

Page 26: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

26

(1), pale sheria inatoa uwezo– (a) wa kutoa ,kuzuia ,kudhibiti au kusimamia jambo lolote,

uwezo huo utajumuisha uwezo wa kufanya hivyo sawa kwa

kutoa leseni au kusajili au kutoa vibali na uwezo wa kuzuia

vitendo kwa njia ya makatazo, kudhibiti au kusimamia kitu

hicho kunaweza kuepukwa; (b) kutoa leseni, kusajili,kupangisha, kutoa hakimiliki,

kibali,mamlaka, kuithibitisha au kutoa msamaha, uwezo huo

unajumuisha uwezo wa kutoa masharti kulingana na, leseni,

usajili,kupangisha, kumiliki, kibali,mamlaka, idhini au

msamaha vinaweza kutolewa; (c) kuithibitisha mtu yoyote, jambo au kitu, na uwezo huo

utajumuisha uwezo wa kufuta idhini iliyotolewa; (d) kutoa maelekezo, na uwezo huo utajumuisha uwezo wa

kutoa maelekezo sawa kwa aina ya makatazo. (3) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 2,

kifungu hiki kitatumika kwenye Sheria zilizotungwa au kupitishwa baada

ya kuanza kutumika kwa Sheria hii. Uwezo wa kutoa

leseni, nk., kwa

kwa hiari

47.-(1) Pale ambapo sheria inapotoa uwezo kwa mtu kutoa leseni

au kuhuisha,kutoa au kuisajiri tena leseni yeyote, kusajili,kupangisha,

kutoa hakimiliki,mamlaka, kuthibitisha, kutoa kibali, au msamaha, mtu

huyo aliyepewa uwezo huo anaweza kutumia mamlaka yake ,kutoa,

kuhisha leseni,au kukataa kutoa, usajili tena leseni

hiyo,kusajiri,kupangisha, kumiliki, mamlaka, kuidhinisha, kumpakibali

au kusamehe. (2) Hakuna katika Kifungu hiki kitakachoathiri haki iliyotolewa

na sheria nyingine yeyote kwa mtu yeyote kukata rufaa dhidi ya kukataa

kutoa,kumpa, kuhuishiwa leseni yeyote, kusajiliwa,kupangisha, kumiliki,

kuidhinishiwa au kupewa msamaha. Uwezo wa kuteua

unajumuisha

uwezo wa

kusimamisha, au

kuondoa

madarakani nk.

48.-(1) Pale ambapo Sheria inapotoa mamlaka au inapotoa wajibu

kwa mtu yeyote kuteua afisa au nafasi,ikijumuisha uteuzi wa kukaimu

nafasi, mtu aliyepewa mamlaka hayo atakuwa pia na uwezo wa–

(a) kumuondoa, kumsimamisha mtu aliyeteuliwa kwenye ofisi

au nafasi hiyo, na kumteua tena au kumrejesha kwenye

nafasi hiyo,mtu yeyote aliyeteuliwa kutekeleza uwezo au

wajibu huo; (b) pale mtu aliyeteuliwa kushika madaraka ya ofisi au nafasi,

atasimamishwa au atashindwa, au anaelekea kushindwa kwa

sababu yoyote kutekeleza kazi za ofisi hiyo au nafasi

aliyoteuliwa, atateua mtu mwingine kukaimu nafasi hiyo

kwa muda kwa niaba ya yule aliyeteuliwa, aliyesimamishwa

kwa muda wote ambao mtu huyo amesimamishwa au hawezi

kutekeleza wajibu wake, lakini mtu huyo atateuliwa kukaimu

Page 27: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

27

kama tu anastahili nakuwa na sifa za kuteuliwa kwenye ofisi

au nafasi hiyo; na (c) kuainisha muda ambao mtu yeyote aliyeteuliwa kutekeleza

mamlaka au wajibu atashika madaraka ya nafasi

aliyoteuliwa. (2) Kwa mujibu wa aya ya (b) ya kifungu kidogo cha (1)

“sababu” linajumuisha– (a) ugonjwa;

(b) kutokuwepo kwa muda, ndani ya Jamhuri ya Muungano; na

(c) mgongano wa kimaslahi. (3) Uhalali wa jambo lolote lililotendwa au kufanywa na mtu

yeyote kwa madai ya kuteuliwa chini ya ibara ya (c) ya kifungu kidogo

cha (1) haitahojiwa kwa madai kuwa uteuzi wake haukukamilika au

ulikoma. (4) Pale ambapo Sheria imetoa mamlaka au imetoa wajibu kwa

mtu yoyote kufanya uteuzi kwenye ofisi au nafasi na uwezo huo au

wajibu huo waweza kutekelezwa tu baada ya uteuzi au mapendekezo ya

majina, au kama uteuzi huo shurti uridhiwe, au uthibitishwe au ukubaliwe

na watu wengine, basi uwezo uliotolewa kwa mujibu wa aya ya (a) hadi

(c) za kifungu kidogo cha (1) utatumiwa kwa kuzingatia uteuzi au

mapendekezo au kwa kuzingatia uthibitisho, kuungwa mkono au ridhaa. (5) Hakuna jambo lolote katika kifungu hiki litaathiri muda wa

kushika madaraka ya ofisi au wadhifa wa mtu yoyote, kwa mujibu wa

masharti ya Sheria yeyote ya Bunge. Uteuzi kwa jina

au ofisi, nk. Na

uteuzi wa

Mwenyekiti wa

Bodi,

49.-(1) Pale ambapo Sheria inatoa mamlaka au kutoa wajibu kwa

mtu kuteua au kutaja mtu na kumpa madaraka ya–

(a) kufanya kazi yeyote;

(b) kuwa mjumbe wa Bodi, baraza la nyumba, kamisheni,

kamati au baraza au kitu kingine kilichoundwa kwa namna

hiyo; au

(c) kuwa au kufanya jambo lolote, mtu huyo aweza kuteua kwa kumtaja mtu kwa jina lake au kwa kuteua

mtu aliyeshika kwa masharti ya uteuzi wa ofisi yake; na uteuzi wowote

wa afisa anayeshikilia ofisi hiyo kutatafsiriwa kama uteuzi wa mtu huyo

mara kwa mara atakayeshikilia nafasi hiyo,tatakayekaimu, au

atakayekuwa akitekeleza kihalali kazi za ofisi hiyo. (2) Pale kwa au chini ya Sheria yoyote imetoa mamlaka kwa mtu

yoyote au mamlaka kuteua wajumbe wa bodi, kamisheni, kamati au

chombo chochote kinachofanana nayo, mtu huyo au, mamlaka

hiyo,inaweza isipokuwa kama itaenda kinyume na dhamira

itakayojitokeza itateua au kuweka kanuni, za uteuzi wa Mwenyekiti au

Makamu Mwenyekiti na katibu wa bodi, kamisheni, kamati au chombo

kingine kinachofanana na aina hiyo. Uwezo wa walio

wengi, akidi nk. 50.-(1) Pale ambapo Sheria inapotoa mamlaka au majukumu kwa

Page 28: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

28

bodi au idadi ya watu ambao hawapungui watatu,kazi hiyo inaweza

ikafanywa na wengi kati ya watu hao. (2) Pale ambapo Sheria imeunda bodi, kamisheni, kamati au

baraza au aina yeyote ya chombo kinachofanana na hivyo na yenye

wajumbe 3 au zaidi (katika kifungu hiki ikijulikana kama “ushirika”)– (a) katika mkutano wa jumuiya, idadi ya wajumbe iko sawa na– (i) angalau nusu ya idadi ya wajumbe iliyotolewa na

sheria yeyote ya bunge, kama namba hiyo imetajwa

maalum;na

(ii) kama namba ya wajumbe imeainishwa katika

sheria haikutaja idadi kamili, lakini ipo katika

kiwango cha juu au chini, angalau nusu ya idadi ni

wanachama wapo katika ofisi kama idadi hiyo iko

katika kiwango, kinachofikia akidi; na (b) tendo au jambo lolote liliofanywa na idadi kubwa ya

wajumbe waliohudhuria kwenye mkutano, kama wajumbe

waliopo wanafikia akidi, kuchukuliwa kuwa imeamuliwa na

ushirika. Utekelezaji wa

uwezo unaweza

kusahihishwa

51. Pale ambapo Sheria inatoa uwezo au jukumu kwa mtu

kufanya jambo au kitu cha kiutawala au cha madaraka au kufanya uteuzi

wowote, uwezo au jukumu linaweza kufanywa au kutekelezwa mara

kwa mara kama itakavyoonekana inafaa, kusahihisha makosa yoyote au

kuacha jambo ambalo lilitakiwa kufanywa huko nyuma au kutekelezwaji

wa uwezo au jukumu, bila ya kujali kuwa uwezo au jukumu hilo haliwezi

kutekelezeka kwa ujumla au kufanyika mara kwa mara. Athari ya uteuzi

wakati afisa

anayestaafu

yuko likizo

52. Wakati afisa anayeshikilia madaraka katika ofisi yeyote

iliyoundwa chini ya Sheria yeyote yuko kwenye likizo akisubiri kuachia

madaraka kwenye ofisi yake, itakuwa halali kisheria kwa mtu mwingine

kuteuliwa rasmi kushika wadhifa wa ofisi hiyo. "Inaweza au

anaweza” ina

maana ya hiari

na neno “ata” au

“ita” lina maana

ya lazima

53.-(1)Pale katika Sheria, litumikapo neno “inaweza” au

“anaweza” litatumika kutoa uwezo, neno hilo litatafiriwa kumaanisha

kuwa uwezo uliotolewa unaweza kutekelezeka au kutokutekelezeka kwa

kuamuwa.

(2) Katika Sheria litumikapo neno “ata” au “ita” litatumika

kutwisha jukumu, na neno hilo litatafsiriwa kumaanisha majukumu

yaliotwishwa sharti yafanyike. Uwezo wa bodi

n.k

havitaathiriwa

kwa nafasi

iliyowazi au

mapungufu

mengine

54. Pale ambapo bodi, baraza la nyumba, tume, kamati au baraza

au chombo kingine kinachofanana na hicho ,yaweza ikawa shirika au

kampuni ,litaanzishwa chini ya Sheria, mamlaka ya chombo hicho

havitaathiriwa na–

(a) kuwepo kwa nafasi yoyote ya wazi ya mwanachama wa

Page 29: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

29

bodi;

(b) mapungufu yoyote yatakayojitokeza katika uteuzi au sifa ya

mtu yeyote aliyetarajiwa kuwa mjumbe wa bodi au kukaimu

nafasi ya mjumbe;

(c) kasoro ndogo itakayotokea katika kuitisha au kuendesha

mikutano ya bodi, au

(d) kuwepo au kushiriki katika mikutano kwa mtu ambaye

hastahili kuwepo au kushiriki katika mkutano. Utekelezaji wa

mamlaka Fulani

kwa anayekasimu

55. Pale ambapo Sheria ianelekeza kuwa utendaji wa kazi yoyote

na mtu utategemea na maoni, imani au ufahamu wa mtu huyo juu ya kitu

chochote na kazi hiyo alivyokasimiwa chini ya sheria yoyote, kazi hiyo

inaweza kutekelezwa na muwakilishi kwa kuzingatia maoni, imani, au

ufahamu wa mtu anayekasimu kuhusiana na jambo hilo. Rejeo kwenye

eneo kwa

kutumia mipaka

56.-(1) Pale Sheria inaporejea au kutaja sehemu yoyote ya

Jamhuri ya Muungano kwa tamko maalum, itatumika kumaanisha, kwa

jinsi hiyo, sehemu hiyo kama itakavyotajwa ambayo mara kwa mara

imefafanuliwa, mpaka wake umewekwa au kuainishwa, isipokuwa kama

imeelekezwa vinginevyo. (2) Pale ambapo eneo limetengwa kwa, kurejea kwenye eneo

lolote ambalo limebadilishwa, marejeo katika sheria yeyote juu ya eneo

liliyobadilishwa kutoka kwenye eneo la zamani, yatafafanuliwa kama

rejeo la eneo lililotengwa.

Tafsiri ya Uwezo

wa kukasimu

57.-(1) Pale Sheria inatoa uwezo kwa mtu kukasimu utekelezaji

wowote wa mamlaka au majukumu ya wajibu wowote aliopewa au

kuwekwa juu yake chini ya sheria– (a) uwakilishi huo hautamzuia mtu aliyekasimiwa, kutekeleza na

kufanya katika muda wowote mamlaka au majukumu yake

aliyokasimiwa; (b) uwakilishi huo unawaweza kufanywa kwa kuzingatia

masharti yoyote, sifa, ukomo au vigezo maalumu ambavyo

mtu aliyeteuliwa anaweza kuainisha; (c) iwapo uwakilishi unaweza kufanywa tu kwakuthibitiswa na

uteuzi huo na marekebisho yoyote ya kukasimu, yanaweza

yakafanywa kwa kuzingatia masharti,sifa , ukomo au sababu

maalumu ambazo mtu aliyethibitishwa ataziainisha; (d) uwakilishi huo unaweza ukafanywa kwa mtu aliyeainishwa

au watu lililoainishwa katika daraja, au yaweza ikafanywa

kwa mtu aliyeshikilia madaraka au watu walioshikilia

madaraka kwa wakati huo wanakuwa kwenye ofisi au aina

za ofisi; (e) uwakilishi huo unaweza kurekebishwa au kufutwa kwa hati

iliyoandikwa na kusainiwa na mtu aliyekasimiwa madaraka;

Page 30: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

30

(f) ikiwa mamlaka aliyopewa mtu kwa ambapo uwezo wa

kuteua mwakilishi umetolewa kwa mtu kwa kuzingatia

masharti yaliyoanzisha ofisi, kukasimu huko

hakutachukuliwa kuwa na madhara kwa sababu tu za

kubadilishwa, mtu anayeshikilia ofisi kihalali, anayekaimu

au kutekeleza kazi za ofisi hiyo. (2) Kukasimu madaraka kutachukuliwa kujumuisha uwakilishi

unaoambatana au uanohusiana na majukumu, na kukasimu kwa

uwakilishi huoutachukuliwa kujumuisha uwakilishi unaoambatana au

kuhusiana na uwezo huo. (3) Pale chini ya Sheria, kitendo au jambo laweza au linatakiwa

kufanywa kwa kurejea kwenye au kuhusiana na mtu, na mtu huyo kwa

mujibu wa sheria amepewa uwezo wa kukasimu kazi iliyopewa au

kuwekwa kwake kuhusiana na au matokeo yanayotokana na kufanya kwa

kitendo hicho au jambo hilo, kwa kurejea kwenye kitendo au kuhusiana

na mtu ambaye amekasimiwa jukumu hilo. Ni nani ataweka

lakiri ya kampuni

au shirika

58. Pale ambapo Sheria inaruhusu bodi au kamati kufanya kitu

chochote, jambo lolote, au kitu itachukuliwa kumaanisha kwambakitendo

hiko,jambo hilo au kitu hicho kinaweza au kufanywa na bodi au kamati

kama itatokea.

Haki za Serikali 59. Hakuna Sheria kwa namna yoyote itakayoibana au kuathiri

haki za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa kama Sheria hiyo

imetamka, au kama itaonekana ni muhimu kwamba Serikali ya Jamhuri

kubanwa na sheria hiyo.

SEHEMU YA NANE

MASHARTI KUHUSU, MUDA NA UMBALI Kukokotoa Muda 60.-(1) Katika kukokotoa wakati kwa mujibu wa Sheria ya

Bunge– (a) pale ambapo muda umeelezwa kwa, juu ya au katika siku

iliyoainishwa, siku hiyo itajumuishwa katika kipindi hicho; (b) pale kipindi kimeelezwa kuwa kinakokotolewa tokea, au

baada , siku maalumu, siku hiyo haitajumuishwa katika

kipindi hicho; (c) pale ambapo jambo fulani linatakiwa kufanywa ndani ya

muda kabla ya siku iliyoainishwa, muda huo

hautajumuisha kwenye siku iliyotajwa; (d) pale ambapo muda umeelezwa kukoma mnamo,juu au

ndani ya siku iliyotajwa, au kuendelea hadi siku iliyotajwa,

siku hiyo itajumuishwa katika kipindi hicho; (e) pale ambapo muda wa kutendwa jambo fulani unakoma,

Page 31: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

31

au unaangukia katika siku ambayo imetolewa katika

orodha, jambo hilo laweza kufanywa katika siku inayofuata

ambayo haijaondolewa katika orodha; (f) pale ambapo kuna rejeo ya idadi ya siku kamili, au

“angalau” au “isiyopungua”au “isiyozidi”, idadi ya siku

yaliyotajwa, siku hizo zitahesabiwa kwa kuondoa siku

ambazo zimo ndani ya matukio yaliyotajwa; (g) pale ambapo kuna rejeo kwenye idadi ya siku ambazo

hazikutajwa au “angalau siku”, au “isiyopungua siku” idadi

ya siku katika matukio mawili, katika kuhesabu idadi ya

siku inatakiwa kuondoa siku ambayo tukio la kwanza

linatokea na kuondoa siku ambapo tukio la pili linatokea

zitaondolewa katika orodha; (h) Pale ambapo kitendo au mwenendo umeelekezwa moja

kwa moja au unaruhusu kufanyika au kufanywa katika siku

fulani, au kwenye hiyo siku au kabla ya siku fulani, basi

kama siku hiyo imeondolewa katika orodha, tendo hilo au

mwenendo huo vitafanywa au vitahesabika kuwa

vimefanywa katika siku muafaka iwapo vitafanyika

aukuchukuliwa kufanyika siku ya pili ambayo sio siku

ambayo imeondolewa kwenye orodha. (2) Kwa minajili ya kifungu hiki, “siku zilizoachwa nje ya

orodha” ina maana siku za Jumamosi, Jumapili au siku yoyote ya likizo

au ile sehemu inayohusiana na siku ambayo tukio, tendo, kitu, hatua au

mwenendo kuchukuliwa.

Kuhesabu miezi 61.-(1) Katika Sheria, neno “mwezi” lina maana ya mwezi wa

kalenda, ikimaanisha, mwezi unaohesabiwa kwa kufuata kalenda. (2) Kama kipindi cha mwezi mmoja kilichoainishwa katika

Sheria ya Bunge kinaanza katika siku isiyokuwa siku ya kwanza kati ya

miezi 12 ya kalenda, siku hiyo itahesabiwa kuanzia siku ambapo inaanza

hadi siku kama hiyo ya mwezi unaofuata, baada ya kutoa moja, au kama

hakuna tarehe iliyo sawa, itakuwa siku ya mwisho ya mwezi huo. Kwa mfano: mwezi unaoanzia tarehe 15 Januari utashia tarehe 14

Februari na mwezi unaoanzia tarehe 30, 31 Januari utaishia tarehe 28

Februari (au 29 Februari katika mwaka mrefu). (3) Kama kipindi kilichotajwa katika Sheria ya Bunge ni miezi 2,

3 au mwezi mrefu, kitaanza kuhesabiwa kuanzia tarehe kipindi hicho

kinatakiwa kuanza hadi namba inayowiana, ukiondoa moja ,katika ya pili,

ya tatu au miezi mingine inayofuata baada ya hapo, au kama hakuna

tarehe zinazofanana, siku ya mwisho ya mwezi huo unaofuata. Kwa mfano: kipindi cha miezi 6 kinachoanza tarehe 15 Agosti,

kinaishia tarehe 14 Februari na kipindi cha miezi 6 kinachoanzia tarehe

30 au 31 Agosti kinaishia tarehe 28 Februari (au tarehe 29 Februari katika

mwaka mrefu).

Page 32: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

32

Masharti

palemuda

haujapangwa

62. Pale ambapo muda kamili haukutajwa au kuruhusu kufanya

tendo au kitu, kitendo hicho au jambo hilo laweza kufanywa kwa haraka

iwezekanavyo, na kwa nyakati mbalimbali, kadri matukio yatakavyo

jitokeza. Tafsiri uwezo

kuongeza muda 63.-(1) Pale ambapo Sheria ya Bunge imeweka muda maalumu au

imeruhusu jambo fulani kutendwa au kufanya mwenendo wowote na

kimahakama imepewa uwezo au mamalaka nyingine kuongeza muda,

uwezo huo waweza kufanywa na mahakama au mamlaka nyingine

ingawaje kuongeza muda hakukufanywa mpaka baada ya kuisha kwa

muda uliowekwa au kuruhusiwa. (2) Kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) kifungu hiki yatumika

kuhusiana na Sheria za Bunge ziliotungwa au kupitishwa baada ya kuanza

kutumika kwa Sheria hii. Mkengeuko wa

matumizi ya

fomu, taratibu

64. Isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo, fomu

zilizoainishwa, kukengeuka huko hakutaathiri msingi na hakutahesabiwa

kupotosha, kupunguza nguvu au uzito wa taarifa zake. Vipimo vya

umbali 65. Katika kupima umbali kwa ajili ya madhumuni ya Sheria

yeyote ya Bunge, umbali utapimwa kwa mstari ulionyooka katika mlalo

ulio sawa.

SEHEMU YA TISA

TARATIBU NA ADHABU Mashauri ya

wadhifa wa

kiofisi hayakomi

baada ya kifo.

66. Mashauri ya madai au jinai dhidi ya mtu yeyote kwa misingi

ya wadhfa wake hayatasimamishwa au kukoma kutokana na kifo,

kujiuzulu, kutokuwepo au kuondolewa madarakani kwa mtu huyo, bali

yaweza kuendelezwa na au dhidi ya mtu mwingine yeyote,kama

itakavyowezekana, na mtu ambaye, atakuwa ameshikilia madaraka ya

ofisi hiyo. Kanuni za

mahakama 67.-(1) Katika Sheria ya Bunge, maneno “kanuni za mahakama”

kuhusiana na mahakama, yana maana ya kanuni zilizotungwa na

mamlaka yenye uwezo kwa wakati uliopo, wa kutunga kanuni au amri za

kusimamia utendaji na mwenendo katika mahakama husika. (2) Uwezo wa mamlaka uliotajwa katika kifungu kidogo cha (1)

unajumuisha uwezo wa kutunga kanuni za mahakama kwa ajili ya sheria

yoyote inayoelekeza au kuruhusu jambo lolote lifanywe na au kwa

mujibu wa kanuni za mahakama. kutolewa kwa

adhabu si kizuizi

cha kesi ya

madai

68. Kutolewa kwa adhabu au faini na au kwa mujibu wa

mamlaka ya Sheria yeyote, kama hakuna masharti yaelekezavyo

vinginevyo, hakutatoa ahueni ya wajibu kwa mtu kushtakiwa kwa

Page 33: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

33

madhumuni ya kumwajibisha mtu huyo kutoa fidia kwa mtu yeyote

aliyejeruiwa Upatikanaji wa

faini na adhabu

Sura ya .20

69. Pale ambapo faini au adhabu za aina nyingine zimetozwa

chini ya Sheria, na hakuna taratibu zilizowekwa na Sheria za namna ya

upatikanaji wa faini au adhabu, itachukuliwa kwamba faini au adhabu

hizo zinaweza kutozwa au kupatikana kwa dharura, chini ya vifungu vya

Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kwa mashauri ya dharura kwa njia

ya muhtasari au chini ya sheria nyingine yoyote ambayo itakuwa

inatumika kwa ajili hiyo. Kutia hatiani

mara dufu 70. Pale ambapo tendo limetamka kosa mara mbili au zaidi iwe ni

kwa mujibu wa Sheria moja au vinginevyo, mkosaji atashtakiwa kwa

kosa lolote au makosa yote lakini hataadhibiwa mara mbili kwa kosa la

aina moja. Matumizi ya

Sheria ya Kanuni

za Adhabu kwa

Makampuni.

71.-(1) Sheria yoyote inayo ainisha makosa ambayo adhabu zake

baada ya kutiwa hatiani, au kwa kutiwa hatiani kwa muhtasari, itahusisha

pia kampuni, mashirika, taasisi na watu binafsi. (2) Pale ambapo Sheria kukamatwa kwa mali kwa ajili ya kufidia

mwathirika wa kosa,au adhabu inatolewa kwa kwa mtu aliyeudhiwa,

faini, tozo au fidia hiyo italipwa kwa shirika, kampuni au taasisi

iliyodhurika kama taasisi hiyo itakuwa ni sehemu ya waasirika wa kosa

husika. (3) Isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo, pale ambapo

adhabu imeainishwa katika Sheria dhidi ya kosa ambalo adhabu yake

haijumuishi kulipwa kwa faini, mahakama ambayo inasikiliza kesi hiyo

inaweza , kwa mkosaji ambaye ni shirika, kampuni au taasisi kutoza

faini– (a) pale ambapo adhabu ni kifungo kisichozidi miezi sita, faini

itozwe ya Shilingi Milioni Mbili; (b) pale ambapo adhabu ni kifungo kisichozidi miezi sita lakini

kisochozidi mwaka mmoja itatolewa, faini itozwe ya Shilingi

Milioni Tatu; (c) pale ambapo adhabu ni kifungo kinachozidi mwaka mmoja

lakini hakizidi miaka miwili itatolewa, itozwe faini ya

Shilingi Milioni Tano; (d) pale ambapo adhabu ni kifungo kinachozidi miaka mitatu

itatolewa, itozwe faini ya Shilingi Milioni Kumi.

Masharti ya

makosa chini ya

sheria mbili au

zaidi

72. Pale ambapo tendo la aina moja limeainishwa kama kosa chini ya

Sheria mbili au zaidi, mkosaji isipokuwa kama dhamira itajitokeza,

litashitakiwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa Sheria yoyote mojawapo,

lakini hataadhibiwa zaidi ya mara moja kwa kosa linalofanana.

Page 34: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

34

Marekebisho ya

adhabu 73. Pale ambapo tendo limepelekea kosa,na adhabu kwa kosa hilo

imerekebishwa kati ya muda ambao kosa hilo limetendeka na baada ya

kutiwa hatiani, mshtakiwa isipokuwa kama marekebisho ya adhabu

yameelekeza dhamira yake vinginevyo,, ataadhibiwa kwa kutumia

adhabu iliyokuwa ikitumika wakati wa kutendeka kwa kosa hilo. Maagizo ya

adhabu ya juu ,

ya chini, ya kila

siku na ya

pamoja

74.-(1) Pale ambapo Sheria ya Bunge imeainisha adhabu kwa

kosa, ile adhabu iliyoainishwa ndiyo itakayokuwa ya juu kwa kosa hilo.

(2) Pale ambapo Sheria imeainisha adhabu zaidi ya moja kwa kosa

moja, matumizi ya neno “na” katikati ya adhabu hizo mbili, itamaanisha

adhabu hizo zaweza kutozwa moja pekee au zitozwe zote mbili kwa

pamoja. (3) Pale ambapo Sheria imeainisha kiwango cha juu cha adhabu

na cha adhabu ya chini kwa kosa moja, kosa hilo laweza kutolewa

adhabu isiyopungua kiwango cha chini cha adhabu na isiyozidi kiwango

cha juu. (4) Pale ambapo Sheria imeainisha kiwango cha chini cha adhabu

kwa kosa, kosa hilo litatolewa adhabu isiyo chini ya kiwango cha chini

cha adhabu. (5) Pale ambapo Sheria imeainisha adhabu inayotolewa au

kutozwa kila siku kwa kosa llilotamkwa, elekezo hilo lina maana

kwamba, adhabu isiyopungua adhabu iliyotamkwa kwa kila sikuinaweza,

ikatolewa na nyongeza ya adhabu nyingine kwa kosa hilo, na itatozwa

kwa kila siku au sehemu ya siku ambapo kosa hilo litaendelea kutendwa. Vifungu

vinavyohusu

kujaribu

75. Kifungu katika Sheria kinachopelekea kosa, isipokuwa kama

dhamira itajitokeza litachukuliwa kama jaribio la kutaka kutenda kosa

litakuwa ni kosa chini ya kifungu hicho, linalostahili adhabu kana

kwamba kosa lenyewe limetendwa. Utoaji wa mali

au vitu

vilivyotwaliwa

76.-(1) Pale ambapo chini ya Sheria yoyote inaelekeza

kukamatwa kwa mnyama au kitu chochote kwa amri ya mahakama au

mamlaka yoyote, itaweza isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo au kama

itaelezwa na sheria kuchukuliwa na mtu yeyote ,kuchukuliwa na Serikali

ya Jamhuri ya Muungano, na mapato yote yatakayopatikana, kama

yataamuliwa na mamlaka husika kuuzwa, gharama zitalipwa na

kuhesabiwa kama sehemu ya mapato ya umma, isipokuwa kama vifungu

vingine vitaelekeza vinginevyo. (2) Hakuna kitu chochote katika kifungu hiki kitakachoathiri

kifungu chochote katika Sheria yoyote ya Bunge ambayo kwayo, sehemu

ya faini au mali iliyotwaliwa, au mwenendo wa mali yoyote iliyotwaliwa,

vimeelekezwa vitwaliwe na mtu yeyote au vitolewe na mtu au mamlaka

yoyote kwa mtu yeyote . Uwajibikaji wa

mwajiri au mkuu 77. Pale kosa lolote chini ya Sheria limetendwa na mtu kama

Page 35: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

35

wakala au mtumishi , isipokuwa kama dhamira nyingine imeelezwa, na

wakala huyo au mwajiriwa, pamoja na mwajiri au mkuu wa sehemu hiyo

watakuwa wametenda kosa na endapo watapatikana na hatia wanaweza

kushtakiwa na kuadhibiwa sawia, isipokuwa kama ataithibitishia

mahakama kwamba hakujua chochote kuhusu uhalifu huo, na kwa

kutumia busara ya kawaida, asingeweza kufahamu kutendeka kwa kosa

hilo. Ushahidi wa

agizo , kibali au

ridhaa ya

mtumishi wa

umma

78. Wakati wowote ambapo amri au agizo la kiutawala, idhini au

kibali cha afisa wa serikali kinahitajiwa kabla ya kuanza kuendesha kesi

au mashauri, hati yoyote inayoonyesha kuwa amri, agizo au ridhaa

imetolewa, itachukuliwa kama ushahidi wa kutosha katika kesi au

mashauri, bila ya kuhitaji ushahidi mwingine kuthibitisha kwamba saini

iliyoko kwenye hati hiyo, ni ya afisa wa serikali mhusika. Utekelezaji wa

mamlaka ya

Mkurugenzi wa

Mashtaka (DPP)

wakati hayupo

79. Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka yanaweza

kutekelezwa na Afisa wa Sheria aliyeteuliwa na Mwanasheria Mkuu wa

Serikali kwa madhumuni hayo, iwapo Mkurugenzi wa Mashtaka.

atakuwa hayupo Makao Makuu ya Ofisi yake, au atakuwa hawezi

kutekeleza majukumu yake kutokana na ugonjwa au kwa sababu nyingine

yoyote , Tamko la adhabu

mwishoni mwa

kifungu

80.-(1) Pale ambapo katika Sheria, adhabu–

(a) imeainishwa bila ya masharti yoyote kutajwa mwishoni mwa

kifungu, (b) imeainishwa mwishoni mwa kifungu kidogo cha Sheria,

lakini sio chini ya kifungu;au (c) imeainishwa mwishoni mwa kifungu cha Sheria na kuelezwa

kuwa kitatumika kwenye na kifungu kidogo katika kifungu

hicho, basi, isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo, kuainishwa huko

kunamaanisha kwamba ukiukwaji wa kifungu au kifungu kidogo, au

kama itakavyohusu, kifungu chochote kidogo, ni kosa ambalo

linaadhibiwa kwa adhabu isiyopungua ile iliyotajwa. Makosa

yanayoendelea 81.-(1) Pale ambapo–

(a) kwa mujibu au chini ya Sheria, kitendo au kitu inatakiwa au

imeelekezwa kifanywe ndani ya muda fulani au kabla ya

wakati fulani; na (b) kushindwa kutenda kitendo hicho au kitu hicho ndani ya

muda au kabla ya wakati ilioelezwa katika aya(a) litakuwa ni

kosa; na (c) kitendo hicho au jambo hilo litafanyika ndani ya muda

uliotajwa au katika wakati uliotajwa kama ilivyoelezwa aya

(a), vifungu vifuatavyo vitahusika– (i) jukumu la kutenda kitendo au jambo hilo

litaendelea, bila ya kujali kwamba kipindi

Page 36: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

36

kilichopangwa kimepita au muda uliowekwa

umepita, hadi hapo kitendo hicho au jambo hilo

litakuwa limetendwa; (ii) pale ambapo mtu ametiwa hatiani kwa kosa

ambalo, kwa mujibu aya (i) limetokana na

kushindwa kutenda kitendo au jambo baada ya

kuisha kwa kipindi kilichowekwa au baada ya

muda uliopangwa,kama utakuwepo , mtu huyo

atakuwa ametenda makosa tofauti, na kosa jingine

yanayofuata kwa kila siku baada ya siku ya

kuhukumiwa, kwa kosa hilo au jambo hilo kwa kila

siku inayoendelea; na (iii) isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo, adhabu

itozwayo kwa kila kosa pekee na makosa mengine

yanayofuata itakuwa ni kiasi kilicho sawa na

Shilingi Elfu Thelathini. (2) Pale ambapo– (a) kwa mujibu wa au chini ya Sheria, tendo au kitu kinatakiwa

au kimeelekezwa kifanywe lakini hakuna kipindi au muda

uliowekwa wa kufanya kitendo au kitu hicho; na (b) kushindwa kufanya kitendo hicho au kitu hicho ni kosa; na (c) mtu anatiwa hatiani kwa kosa la kushindwa kufanya kitendo

hicho au kufanya jambo hilo, mtu huyo atakuwa ametenda kosa la kipekee na kosa jingine linalofuata

kwa kila siku baada ya siku ya kutiwa hatiani,na iwapo atashindwa

kutenda kitendo hicho au kufanya jambo hilo kunaendelea na, isipokuwa

kama imeelekezwa vinginevyo, adhabu itozwayo kwa kila kosa ambalo ni

tofauti na makosa mengine yanayofuata atatozwa kiasi cha Shilingi Elfu

Thelathini. (3) Mashtaka dhidi ya mtu mmoja kwa makosa mbalimbali chini

ya aya ya (ii) cha kifungu kidogo cha (1) au kifungu kidogo cha (2)

yaweza kuunganishwa katika taarifa moja au mashtaka kama makosa

husika yanahusiana na kushindwa kufanya kitendo kinachofanana au kitu. (4) Kama mtu atatiwa hatiani kwa kosa zaidi ya mojawapo ya

chini ya aya (ii) cha kifungu cha (1) au zaidi ya makosa chini ya kifungu

kidogo cha (2), mahakama yaweza kutoa adhabu moja kwa makosa yote

ambayo mtuhumiwa ametiwa hatiani chini ya kifungu kidogo husika,

lakini adhabu yake haitazidi kiwango cha juu cha adhabu inayoweza

kutozwa kama adhabu hiyo ingetozwa otfauti kwa kila kosa.

SEHEMU YA KUMI

MASHARTI YA JUMLA Uwasilishaji wa

Nyaraka kwa njia 82.-(1) Pale ambapo Sheria ya Bunge inaruhusu au kutaka kuwa

Page 37: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

37

ya posta hati iwasilishwe kwa njia ya posta, iwapo neno “wasilisha” au maneno

mengine kama vile, “patia”, “kupata”, au “peleka” au maneno mengine ya

yanayofanana, au tafsiri itakayotumika ,kuwasilisha kutachukuliwa kuwa

kuwasilisha kwa utimilifu kwa kuandika anuani sahihi na kuposti kwa

(kulipa gharama stahiki) hati ya kupeleka barua kwa kutumia anuani ya

mwisho ya anayepelekewa, na isipokuwa kama itathibitiswa vinginevyo,

itahesabiwa kwamba kutaathiri muda ambao barua hiyo ingewasilishwa

kwa njia ya kawaida ya posta. (2) Pale ambapo Sheria inaruhusu au inaelekeza kuwa hati ya

kuwasilishwa iwasilishwe kwa njia ya rejesta ya posta, hata kama neno la

“wasilisha” au maneno mengine kama “patia”, “peleka” au “wasilisha” au

maneno mengine ya msemo kama huo yametumika, basi kama hati hiyo

inasomeka na inakubalika kwa kuwasilishwa kama barua iliyothibitishwa,

kuwasilishwa kwa hati hiyo kwaweza kufanywa ama kwa rejesta ya

posta, au kwa njia ya barua iliyothibitishwa. (3) Vifungu vidogo vya (1) na (2) vitahusika, isipokuwa kama

dhamira nyingine inaonekana na kifungu kidogo cha (2) hakitahusika pale

ambapo Sheria imeelekeza kutolewa kwa uthibitisho au stakabadhi

iliyosainiwa na mtu ambaye hati hiyo imepelekwa kupitia anuani yake na

hiyo itaashiria kuwa hati hiyo imewasilishwa kwa mhusika. Uwasilishaji wa

Nyaraka kwa

ujumla

83. Pale ambapo Sheria inaruhusu au kuelekeza kuwa hati

iwasilishwe, hata kama neno “wasilisha”, “patia”,”peleka” au “wasilisha”

au neno lingine kama hilo au msemo wa aina hiyo umetumika lakini bila

ya kuelekeza kuwa uwasilishwaji ufanywe kwa namna gani, basi hati

hiyo itakuwa imewasilishwa kikamilifu kwa mhusika:– (a) kwa kupeleka hati hiyo kwa mtu huyo binafsi; au

(b) kwa njia ya posta kulingana na maelekezo ya kifungu kidogo

cha (1) cha kifungu cha 82; au

(c) kwa kuacha hati kwa mhusika kwenye makazi yake ya

kawaida au yale ya mwisho yaliyokuwa yanafahamika, au

kama ni mkuu wa biashara makao makuu ya biashara zake,

au

(d) kama mhusika ni kampuni au shirika au taasisi au chama, au

jumuiya ya watu (bila ya kujali kama imeandikishwa kama

kampuniau la), kwa kuwasilisha, au kuiacha nyaraka au

kuiposti kama barua kwa anuani ya kampuni, shirika, taasisi

au chama kwenye makao makuu ya biashara au ofisi kuu

zilizomo ndani ya Jamhuri ya Muungano. Lugha ya sheria

za Tanzania 84.-(1) Lugha za Sheria za Tanzania zitakuwa ni Kiswahi au

Kiingereza au lugha zote mbili. (2) Pale ambapo Sheria yoyote imetafsiriwa kutoka lugha moja

kwenda lugha nyingine na kuchapishwa kwa lugha zote mbili, na iwapo

itatokea mgongano au kutakuwa na mashaka ya maana ya maneno au

maelezo, lugha ambayo imetumika wakati wa kupitisha Sheria hiyo na

Page 38: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

38

Bunge, ndiyo itakayokuwa ya kipaumbele (3) Pale ambapo Sheria imeandikwa kwa lugha zote mbili na

ukatokea mgongano au mashaka kuhusiana na maana ya neno lolote au

maelezo, tafsiri ya Kiingereza ndiyo itakayotumika. Kufutwa kwa

Sheria ya Bunge

Na 30 ya mwaka

1972

85. [Inafuta Sheria ya Kanuni za Ufafanuzi wa Sheria na Vifungu

vya Ujumla]

___

NYONGEZA

______

(Kifungu cha 4)

NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA

Antigua and Bermuda Namibia

Australia Nauru

The Bahamas New Zealand

Bangladesh Nigeria

Barbados Papua New Guinea

Belize Visiwa vya Ushelisheli

Botswana Sierra Leone

Brunei Darusalaam Singapura

Canada Visiwa vya Solomoni

Maurishas Afrika ya Kusini

Cyprus Shiri Lanka

Dominica St. Kitts and Nevis

The Gambia St. Lucia

Ghana St. Vincent and the Grenadines

Grenada Swaziland

Pakistan Tanzania

Guiyana Tonga

India Trinidad na Tobago

Jamaika Tuvalu

Kenya Uganda

Kiribati Ufalme wa Uingereza [United Kingdom]

Lesotho Vanuatu

Malawi Samoa ya Magharibi [Western Somoa]

Malaysia Zambia

Maldives Zimbabwe

Malta Rwanda

Msumbiji

Page 39: Sheria ya Utafsiri wa Sheria

39

_________________