15
©NHK WORLD-JAPAN 6 Tembelea NHK WORLD-JAPAN S o m o l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam すみません。 Sumimase n. Samahani. はるさんハウスはどこですか。 Haru-san-Ha usu wa do ko de su ka. Nyumba ya Haru-san iko wapi? かい Kaito はるさんハウス? Haru-san-Ha usu? Nyumba ya Haru-san? あれ? ぼくたちのうちだよね。 Are? Bo kutachi no uchi da yo ne. Oh? Ndiko tunakoishi. ミーヤー Mi Ya すぐ近 ちか くです。 Su gu chi kaku de su. Ni jirani. いっ しょ に行 きましょう。 Issho ni ikimasho o. Tunaweza kwenda pamoja. かい Kaito こっちだよ。 Kocchi da yo. Ni huku. タム Tam はい。ありがとうございます。 Ha i. Ari gatoo gozaima su. Sawa. Asante sana. Msamiati すみません samahani sumimase n どこ wapi do ko ぼくたち sisi bo kutachi うち nyumbani uchi すぐ近 ちか く jirani sana su gu chi kaku いっ しょ に pamoja issho ni く kwenda iku こっち huku kocchi はい sawa ha i Mazungumzo ya leo Haru-san-Hausu wa doko desu ka Nyumba ya Haru-san iko wapi?

S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

  • Upload
    others

  • View
    3

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN6 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Somo la

1 はるさんハウスはどこですか

タムTam

: すみません。Sumimase⎤n.

Samahani.

はるさんハウスはどこですか。Haru-san-Ha⎤usu wa do⎤ko de⎤su ka.

Nyumba ya Haru-san iko wapi?

海かい

斗と

Kaito: はるさんハウス?

Haru-san-Ha⎤usu?Nyumba ya Haru-san?

あれ? ぼくたちのうちだよね。Are? Bo⎤kutachi no uchi⎤ da yo ne.

Oh? Ndiko tunakoishi.

ミーヤーMi Ya

: すぐ近ちか

くです。Su⎤gu chi⎤kaku de⎤su.

Ni jirani.

一いっ

緒しょ

に行い

きましょう。Issho ni ikimasho⎤o.

Tunaweza kwenda pamoja.

海かい

斗と

Kaito: こっちだよ。

Kocchi⎤ da yo.Ni huku.

タムTam

: はい。ありがとうございます。Ha⎤i. Ari⎤gatoo gozaima⎤su.

Sawa. Asante sana.

Msamiati

すみません samahanisumimase⎤n

どこ wapido⎤ko

ぼくたち sisi bo⎤kutachi

うち nyumbaniuchi

すぐ近ち か

く jirani sanasu⎤gu chi⎤kaku

一い っ

緒し ょ

に pamojaissho ni

行い

く kwendaiku

こっち hukukocchi⎤

はい sawaha⎤i

Mazungumzo ya leo

Haru-san-Hausu wa doko desu kaNyumba ya Haru-san iko wapi?

Page 2: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 7https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Usemi wa Msingi

はるさんハウスはどこですか。Haru-san-Ha⎤usu wa do⎤ko de⎤su ka.

Nyumba ya Haru-san iko wapi?Ili kuulizia mahali, taja “[sehemu] wa doko desu ka.” “Wa” ni kiunganishi cha mada ambacho hufuata baada ya nomino. Huandikwa “は (ha)” kwa herufi ya Hiragana lakini hutamkwa “wa.” Kwa kuongeza “desu ka” baada ya kiulizi “doko” au "wapi" na kupandisha kiimbo chako itafanya iwe swali.

Tumia!

すみません。トイレはどこですか。Sumimase⎤n. To⎤ire wa do⎤ko de⎤su ka.

あそこです。Asoko de⎤su.

Samahani. Choo kiko wapi? Ni pale.

Jaribu!

すみません。~はどこですか。Sumimase⎤n. ~wa do⎤ko de⎤su ka.

Samahani. ~ -ko wapi?

① 駅え き

e⎤ki kituo

② コンビニkonbini

duka la saa 24

Usemi wa ziadaありがとうございます。Ari⎤gatoo gozaima⎤su.Asante sana.

Usemi huo unaelezea shukrani. Kama unamshukuru mtu aliye na uhusiano wa karibu na wewe, kama rafiki au mtu wa familia, unaweza kusema tu “arigatoo.”

Can-do! Kuulizia mahali

Page 3: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN8 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Majibu ① すみません。駅えき

はどこですか。 Sumimase⎤n. E⎤ki wa do⎤ko de⎤su ka.② すみません。コンビニはどこですか。 Sumimase⎤n. Konbini wa do⎤ko de⎤su ka.

Silabi nyingi za Kijapani zimeundwa kwa konsonanti moja na irabu moja.

Lafudhi ya Kijapani inatokana na toni, si sauti za nguvu au sauti dhaifu. Kila neno lina sehemu ya msisitizo; baadhi ya maneno yana toni isiyo na msisitizo, wakati baadhi ya maneno yana sehemu ambazo toni hushuka, ambapo sehemu hizo huoneshwa kwa alama ⎤.

かka

konsonanti irabu k a

Sauti za Kijapani

Mvua ilinyesha.

mvua pipi

Pipi imedondoka.

Page 4: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 9https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Somo la

2 タムです。学が く

生せ い

です

ミーヤーMi Ya

: ただいま。Tadaima.

Nimerudi.

海かい

斗と

Kaito: はるさん、新

あたら

しい住じゅう

人にん

が着つ

きましたよ。Ha⎤ru-san, atarashi⎤i juunin ga tsukima⎤shita yo.

Haru-san, mkazi mpya amewasili.

はるHaru

: はーい。Haa⎤i.

Sawa.

ようこそいらっしゃいました。Yo⎤okoso irasshaima⎤shita.

Karibu.

タムTam

: え、ロボット?E, ro⎤botto?

Oh, ni roboti?

海かい

斗と

Kaito: そう。大

おお

家や

のはるさんです。So⎤o. O⎤oya no Ha⎤ru-san de⎤su.

Ndiyo. Yeye ni mwenyenyumba wetu, Haru-san.

タムTam

: はじめまして。Hajimema⎤shite.

Habari.

タムです。学がく

生せい

です。Ta⎤mu de⎤su. Gakusee de⎤su.

Mimi ni Tam. Ni mwanafunzi.

よろしくお願ねが

いします。Yoroshiku onegai-shima⎤su.

Tafadhali tuendelee kuwa na ushirikiano mwema.

Msamiati

新あたら

しい mpya atarashi⎤i

住じゅう

人に ん

 mkazijuunin

着つ

く wasilitsu⎤ku

ロボット robotiro⎤botto

大おお

家や

 mwenyenyumbao⎤oya

学が く

生せ い

 mwanafunzigakusee

Mazungumzo ya leo

Tamu desu. Gakusee desuMimi ni Tam. Ni mwanafunzi.

Page 5: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN10 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Usemi wa Msingi

タムです。学が く

生せ い

です。Ta⎤mu de⎤su. Gakusee de⎤su.Mimi ni Tam. Ni mwanafunzi.

Katika “[jina/kazi] desu,” “desu” huja baada ya nomino ili kukamilisha sentensi. Kwenye “A wa B desu” ama “A ni B,” A ni mada au kiima na B inaelezea juu ya kiima. Katika usemi wa msingi, sehemu ya “A wa,” ambayo ni “watashi wa” yaani “Mimi ni” haijajumuishwa.

Tumia!

はじめまして。アンナです。学がく

生せい

です。Hajimema⎤shite. A⎤nna de⎤su. Gakusee de⎤su.

はじめまして。鈴すず

木き

です。Hajimema⎤shite. Suzuki de⎤su.

Habari. Mimi ni Anna. Ni mwanafunzi.Nafurahi kukufahamu. Mimi ni Suzuki.

Jaribu!

はじめまして。【jina】です。【kazi】です。Hajimema⎤shite. 【jina】 de⎤su. 【kazi】 de⎤su.

Habari. Mimi ni [jina]. Ni [kazi ufanyayo].

① トーマスTo⎤omasu

Thomas

会か い

社し ゃ

員い ん

kaisha⎤inmwajiriwa wa kampuni

② エリンE⎤rin

Erin

教きょう

師し

kyo⎤oshimwalimu

Usemi wa ziadaよろしくお願

ね が

いします。Yoroshiku onegai-shima⎤su.Tuendelee kuwa na ushirikiano mwema.

Unautumia usemi huu kwa mtu utakayekuwa unashirikiana naye. Mara nyingi unatumika kujitambulisha. Iwapo mtu unayezungumza naye ni rafiki au ni mdogo kwako, unaweza kufupisha na kusema tu “yoroshiku.”

Can-do! Kujitambulisha jina na kazi ufanyayo

Page 6: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 11https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Kijapani kina aina tatu za herufi -- Kanji, Hiragana na Katakana. Kwa mfano, kuandika kwa Kijapani usemi “Watashi wa Tam desu” au “Mimi ni Tam” itakuwa:

私はタムです

“私” ni Kanji, “は” na “です” ni Hiragana, na “タム” ni Katakana.

Katakana hutumika kuandika majina na maneno kutoka lugha zingine. Hiragana hutumika kwa vitu vingine. Herufi za kifonetiki za Katakana na Hiragana zimeundwa kutoka Kanji. Kanji ni idiogramu na hutumika kuandika masuala muhimu.

Majibu ① はじめまして。トーマスです。会かい

社しゃ

員いん

です。 Hajimema⎤shite. To⎤omasu de⎤su. Kaisha⎤in de⎤su.② はじめまして。エリンです。教

きょう

師し

です。 Hajimema⎤shite. E⎤rin de⎤su. Kyo⎤oshi de⎤su.

Katakana: a Hiragana: a Kanji: yama (mlima)

Mabango yaliyoandikwa kwa Kijapani

Herufi za Kijapani

Page 7: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN12 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Somo la

3 ベトナムから来き

ました

海かい

斗と

Kaito: タムさん、たくさん食

べてね。Ta⎤mu-san, takusan ta⎤bete ne.

Furahia mlo, Tam-san.

タムTam

: はい。Ha⎤i.

Asante, nitafurahia.

タムです。ベトナムから来き

ました。Ta⎤mu de⎤su. Betonamu kara kima⎤shita.

Mimi ni Tam. Ninatokea Vietnamu.

ミーヤーMi Ya

: ミーヤーです。中ちゅう

国ごく

からです。Mi⎤iyaa de⎤su. Chu⎤ugoku kara⎤ de⎤su.

Mimi ni Mi Ya. Ninatokea China.

写しゃ

真しん

家か

です。Shashinka de⎤su.

Ni mpigapicha.

海かい

斗と

Kaito: ぼくは海

かい

斗と

。学がく

生せい

です。Bo⎤ku wa Ka⎤ito. Gakusee de⎤su.

Mimi ni Kaito. Ni mwanafunzi.

はるHaru

: わたくし、大おお

家や

のはるです。Watakushi, o⎤oya no Ha⎤ru de⎤su.

Mimi ni mwenyenyumba, Haru.

ミーヤーMi Ya

: はるさんは何なん

でも知し

っています。Ha⎤ru-san wa nan de mo shitte ima⎤su.

Haru-san anafahamu kila kitu.

タムTam

: そうですか。よろしくお願ねが

いします。So⎤o de⎤su ka. Yoroshiku onegai-shima⎤su.

Oh kumbe. Tuendelee kuwa na ushirikiano mwema.

Msamiati

たくさん kingitakusan

食た

べる kulatabe⎤ru

来く

る kujaku⎤ru

写し ゃ

真し ん

家か

 mpigapichashashinka

ぼく mimi (mwanamume)bo⎤ku

知し

っている fahamu shitte iru

Mazungumzo ya leo

Betonamu kara kimashitaNinatokea Vietnamu.

Page 8: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 13https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Usemi wa Msingi

ベトナムから来き

ました。Betonamu kara kima⎤shita.

Ninatokea Vietnamu.Ili kusema unakotokea, taja “[sehemu] kara kimashita.” “Kara” ni kiunganishi kinachoonesha mwanzo au sehemu yako ya asili unayotokea. “Kimashita” ni wakati uliopita wa kitenzi “kuru” yaani “kuja.” Unaweza kubadili kitenzi hicho kwa kuweka “desu” na kusema “Betonamu kara desu” yaani “Ninatokea Vietnamu.”

Tumia!

どちらからですか。Do⎤chira kara⎤ de⎤su ka.

アメリカから来き

ました。Amerika kara kima⎤shita.

Unatokea wapi?Ninatokea Marekani.

Jaribu!

~から来き

ました。~kara kima⎤shita.

Ninatokea ~.

① タイTa⎤i

Thailand

② ブラジルBurajiru

Brazili

Usemi wa ziadaそうですか。So⎤o de⎤su ka.Kumbe.

Huo ni mwitikio wa kuonesha kuwa unaelewa kile ambacho mtu unayezungumza naye amekiongea. Hakikisha haupandishi kiimbo chako mwishoni mwa sentensi hiyo.

Can-do! Kutaja unakotokea

Page 9: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN14 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Ushauri wa Haru-san

Majibu ① タイから来き

ました。 Ta⎤i kara kima⎤shita.② ブラジルから来

ました。 Burajiru kara kima⎤shita.

Kuinama ni desturi nchini Japani wakati wa kusalimiana. Uhusiano wako na mtu unayesalimiana naye utaamua jinsi utakavyoinama zaidi. Kama ni mkubwa kwako, utainama zaidi.

Kama mtu huyo ni rika lako au mdogo kwako, kuinamisha kichwa tu itatosha.

Kusalimiana kwa kupeana mikono au kukumbatiana si kawaida sana nchini Japani.

©AFLO ©The Japan Foundation

Jinsi ya kusalimia watu nchini Japani

Page 10: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 15https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Somo la

4 大だ い

学が く

で日に

本ほ ん

語ご

を勉べ ん

強きょう

します

タムTam

: これ、どこですか。Kore, do⎤ko de⎤su ka.

Huku ni wapi?

ミーヤーMi Ya

: 沖おき

縄なわ

です。Okinawa de⎤su.

Ni Okinawa.

タムTam

: へえ。Hee.

Wow!

ミーヤーMi Ya

: これは京きょう

都と

です。Kore wa Kyo⎤oto de⎤su.

Huku ni Kyoto.

京きょう

都と

はとてもきれいですよ。Kyo⎤oto wa totemo ki⎤ree de⎤su yo.

Kyoto ni kuzuri sana.

タムTam

: そうですね。So⎤o de⎤su ne.

Hakika.

ミーヤーMi Ya

: タムさんは日に

本ほん

で何なに

をしますか。Ta⎤mu-san wa Niho⎤n de na⎤ni o shima⎤su ka.

Tam-san, utafanya nini nchini Japani?

タムTam

: 大だい

学がく

で日に

本ほん

語ご

を勉べん

強きょう

します。Daigaku de Nihongo o benkyoo-shima⎤su.

Nitasoma Kijapani katika chuo kikuu.

ミーヤーMi Ya

: いいですね。I⎤i de⎤su ne.

Hivyo ni vizuri.

タムTam

: はい、楽たの

しみです。Ha⎤i, tanoshi⎤mi de⎤su.

Ndiyo, ninatazamia hilo.

Msamiati

大だ い

学が く

 chuo kikuudaigaku

日に

本ほん

語ご

 lugha ya KijapaniNihongo

勉べ ん

強きょう

する jifunza / somabenkyoo-suru

Daigaku de Nihongo o benkyoo-shimasu Nitasoma Kijapani katika chuo kikuu.

Mazungumzo ya leo

Page 11: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN16 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Usemi wa Msingi

大だ い

学が く

で日に

本ほ ん

語ご

を勉べ ん

強きょう

します。Daigaku de Nihongo o benkyoo-shima⎤su.

Nitasoma Kijapani katika chuo kikuu.Ili kuelezea utakachofanya, tumia kitenzi cha umbo la MASU (chenye kuishia na neno “masu”) kama vile “benkyoo-shimasu” yaani “nitasoma.” Umbo hilo hutumika unapozungumza kiungwana. “De” ni kiunganishi kinachoashiria mahali na “o” ni kiunganishi kinachoelezea shamirisho. Kitenzi huja mwishoni mwa sentensi.

Tumia!

日に

本ほん

で何なに

をしますか。Niho⎤n de na⎤ni o shima⎤su ka.

買か

い物もの

をします。Kaimono o shima⎤su.

Utafanya nini nchini Japani?Nitafanya manunuzi.

Jaribu!

【shamirisho】を~ます。【shamirisho】o~ma⎤su.

Nita- [shamirisho].

① 天て ん

ぷらtenpura

tempura

食た

べます(食た

べる)tabema⎤su (tabe⎤ru)

kula

② 歌か

舞ぶ

伎き

kabuki Kabuki

見み

ます(見み

る)mima⎤su (mi⎤ru)

tazama

Usemi wa ziada楽た の

しみです。Tanoshi⎤mi desu.Ninatazamia hilo.

Huu ni usemi unaoelezea kitu unachokitarajia kwa furaha.

Can-do! Kusema unachotarajia kufanya

Page 12: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 17https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Mwongozo wa safari wa Mi Ya

Okinawa

Nikko, Mkoa wa Tochigi

HokkaidoKyoto

©Niseko Village

©Nikko Toshogu Shrine

©OCVB

©Ninnaji-Temple

Unaweza kufurahia mandhari ya misimu minne tofauti kote nchini Japani. Kwa mfano, msimu wa machipuo ni msimu wa kuchanua kwa maua ya micheri. Kyoto iliyotajwa kwenye somo hili ni sehemu maarufu kwa maua hayo. Katika msimu wa joto, watu wengi hufurahia kupanda milima na kwenda kwenye fukwe. Katika msimu wa pukutizi, kubadilika kwa rangi ya majani kunapendeza sana. Na msimu wa baridi pia unavutia kwa sababu ya theluji. Unaweza kufurahia kuteleza kwenye theluji na michezo mingine ya baridi.

Majibu ① 天てん

ぷらを食た

べます。 Tenpura o tabema⎤su.② 歌

舞ぶ

伎き

を見み

ます。 Kabuki o mima⎤su.

Uzuri wa sehemu mbalimbali nchini Japani

Page 13: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN18 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Somo la

5 ラジオで勉べ ん

強きょう

しました

はるHaru

: タムさん、今き ょ う

日から学がっ

校こう

ですね。Ta⎤mu-san, kyo⎤o kara gakkoo de⎤su ne.

Tam-san, chuo chenu kinafunguliwa leo, sivyo?

タムTam

: はい。Ha⎤i.

Ndiyo.

はるHaru

: あらまあ! どうしたんですか。A⎤ra ma⎤a! Do⎤o shitan de⎤su ka.

Oh! Una tatizo gani?

タムTam

: 日に

本ほん

語ご

が心しん

配ぱい

です。Nihongo ga shinpai de⎤su.

Nina mashaka na Kijapani changu.

はるHaru

: タムさんは日に

本ほん

語ご

、お上じょうず

手ですよ。Ta⎤mu-san wa Nihongo, ojoozu⎤ de⎤su yo.

Tam-san, unazungumza Kijapani kizuri.

タムTam

: いいえ、まだまだです。Iie, ma⎤da ma⎤da de⎤su.

Hapana, si kizuri vya kutosha.

はるHaru

: ベトナムで勉べん

強きょう

したんでしょう?Betonamu de benkyoo-shita⎤n deshoo?

Umejifunza nchini Vietnamu, si ndiyo?

タムTam

: はい、ラジオで勉べん

強きょう

しました。Ha⎤i, ra⎤jio de benkyoo-shima⎤shita.

Ndiyo, nimejifunza kwa kusikiliza redio.

はるHaru

: それなら、大だい

丈じょう

夫ぶ

ですよ。Sore na⎤ra, daijo⎤obu de⎤su yo.

Basi, utakuwa sawa.

Msamiati

今き ょ う

日 leokyo⎤o

はい ndiyoha⎤i

心し ん

配ぱ い

(な) mashakashinpai (na)

上じょう

手ず

(な) -enye ujuzijoozu⎤ (na)

ラジオ rediora⎤jio

大だ い

丈じょう

夫ぶ

(な) sawadaijo⎤obu (na)

Mazungumzo ya leo

Rajio de benkyoo-shimashitaNimejifunza kwa kusikiliza redio.

Page 14: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN 19https://www.nhk.or.jp/lesson/sw/

Usemi wa Msingi

ラジオで勉べ ん

強きょう

しました。Ra⎤jio de benkyoo-shima⎤shita.

Nimejifunza kwa kusikiliza redio.Ili kuelezea kitu ulichokifanya wakati uliopita, badili mwisho wa kitenzi cha umbo la MASU kutoka “masu” kuwa “mashita.” Kiunganishi “de” katika maneno “rajio de” kinaonesha njia iliyotumika au kivipi. Kiima “watashi wa” yaani “Mimi ni-” na shamirisho “Nihongo o” yaani “Kijapani” vimeachwa kwa sababu vinajulikana katika muktadha huo.

Tumia!

あ、日に

本ほん

語ご

! どうやって勉べん

強きょう

しましたか。A, Nihongo! Do⎤oyatte benkyoo-shima⎤shita ka.

インターネットで勉べん

強きょう

しました。Intaane⎤tto de benkyoo-shima⎤shita.

Oh, lugha ya Kijapani! Umejifunzaje?Nimejifunza kupitia Intaneti.

Jaribu!

~で勉べん

強きょう

しました。~de benkyoo-shima⎤shita.

Nimejifunza kupitia ~.

① アニメanime

katuni za anime

② 学が っ

校こ う

gakkoo shule

Usemi wa ziadaいいえ、まだまだです。Iie, ma⎤da ma⎤da de⎤su.Hapana, si kizuri vya kutosha.

Ni usemi wa kinyenyekevu unaoweza kuutumia pale mtu anapokusifia. “Iie” inamaanisha “hapana” na “mada mada desu” inamaanisha “hakitoshi.”

Can-do! Kusema jinsi ulivyojifunza Kijapani

Page 15: S om la はるさんハウスはどこですか - NHK · 6 NHK ORD-JAPAN Tembele NHK JAPAN S o m l a 1 はるさんハウスはどこですか タム Tam :すみません。 Sumimase⎤n

©NHK WORLD-JAPAN20 Tembelea NHK WORLD-JAPAN

Ushauri wa Haru-san

Majibu ① アニメで勉べん

強きょう

しました。 Anime de benkyoo-shima⎤shita.② 学

がっ

校こう

で勉べん

強きょう

しました。 Gakkoo de benkyoo-shima⎤shita.

Endapo mtu anakusifia, akisema “Kijapani chako ni kizuri,” utamjibu vipi?

1) Asante sana. 2) Hapana, si kizuri vya kutosha. 3) Ndiyo, nimejifunza katika chuo kikuu.

Wajapani wengi wangejibu kwa namna ya unyenyekevu na kusema si kizuri vya kutosha kama namba 2) “Iie, mada mada desu.” Kijapani kina semi nyingine nyingi za unyenyekevu. Kwa mfano, hata wakati mtu ameandaa meza iliyojaa vyakula kwa ajili ya mgeni, namna ya kawaida ya kukaribisha inaweza kuwa “Hatuna kitu isipokuwa hiki.”

Semi za unyenyekevu