17
Toleo NO. 044 Januari – Machi 2014 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937 MVIWATA yapata wawakilishi wawili ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Ushirikiano wa MVIWATA na NFRA Dhana ya Utandawazi: Dunia ni Kijiji au Pori la Utanda-wizi? Rasimu ya katiba mpya: Je! imezingatia maslahi ya mkulima mdogo? Yaliyomo Uk. 11 Uk. 13 Uk. 9

Rasimu ya katiba mpya

Embed Size (px)

Citation preview

Toleo NO. 044 Januari – Machi 2014 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

MVIWATA yapata wawakilishi wawili ndani ya Bunge Maalumu la Katiba

Ushirikiano wa MVIWATA na NFRA Dhana ya Utandawazi: Dunia ni Kijiji au Pori la Utanda-wizi?

Rasimu ya katiba mpya:Je! imezingatia maslahi ya

mkulima mdogo?

Yaliyomo Uk. 11 Uk. 13Uk. 9

1Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014b

Je! Rasimu ya Katiba Mpya imezingatia maslahi ya

mkulima mdogo?

Na Al-amani Mutarubukwa

Wakati safari ya Watanzania kuelekea kupata Katiba mpya imeiva na maandalizi ya kukamilisha mchakato huo yakipamba moto, wakulima wadogo nchini bado wanadadisi na wana shauku ya kujua nini nafasi yao katika katiba hiyo inayoandikwa.

safi na salama, haki ya elimu na kujifunza, haki ya mtoto, haki na wajibu wa vijana, haki za watu wenye ulemavu, haki za makundi madogo katika jamii na haki za wanawake na wazee.

“ K a t i k a mfululizo wa m a k u n d i mbal imbal i na haki zao, sijaona k i f u n g u kinachotaja kundi la wakulima na haki zao...hata nikajiuliza labda haki za wakulima zimetajwa kwenye haki za makundi madogo madogo.”

Hata hivyo, Bw.Kibamba alihoji iweje haki za wakulima na wafugaji ambao ndiyo kundi kubwa la watu nchini waingizwe kwenye kundi la

makundi madogo madogo tena kwa ufinyu mkubwa.

“La hasha! wakulima siyo kundi la watu wadogo wadogo,”

alisisitiza.Akinukuu miaka ya

1960-1970 na sasa Bw. Kibamba a l i s e m a “ n y a r a k a nyingi za nchi za miaka hiyo zilikuwa zikiwatambua

sana wakulima wakifuatiwa na

wafanyakazi lakini kwa sasa wakulima

hawatambuliwi na ukiangalia hata ilani za

vyama vya kisiasa husikii zikitaja wakulima na hata kama zingetaja basi zingesema nchi hii ni nchi ya wafanyabiashara na wawekezaji.”

MADA MAALUM

Endelea Uk wa 2

Awali Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa rasimu ya kwanza katikati ya mwaka

2013 na kuigawa kwa wananchi ambao nao waliichambua na kubaini mapungufu yaliyomo kwa kadri walivyoona kisha, kupitia majukwaa mbalimbali, waliwasilisha mapendekezo yao.

Nalo shirika la Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), kama chombo kikuu cha kuwajengea sauti ya pamoja wakulima wadogo nchini liliwaalika wakulima nchini kujadili mustakabali na kujua nafasi yao ndani ya rasimu hiyo.

Hata hivyo wataalamu wenye uzoefu mwingi hasa kwenye michakato ya uundwaji katiba mpya barani Afrika wanainyoshea tume kidole kwa kuwa rasimu iliyotolewa imemsahau mkulima mdogo, kwani haki na stahiki za kundi hilo hazikutajwa bayana.

Akiwaongoza wakulima hao, katika uchambuzi wa rasimu ya Katiba Bw. Deus Kibamba, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini, alibainisha maeneo muhimu ya rasimu ambayo yanataja haki mbalimbali za raia wa Tanzania kiujumla.

Alisema kwenye rasmu ya Katiba kuanzia ibara ya 22-47 imeorodhesha haki za watu kimakundi ikiwemo haki ya wafanyakazi na waajiri, haki ya kumiliki mali, haki ya uraia, haki ya mtuhumiwa na mfungwa, haki ya watu walio chini ya ulinzi.

Haki nyingine ni haki ya mazingira

Rasimu

Toleo NO. 044 Januari – Machi 2014 Bei Shs. 500/=ISSN 0856-5937

MharIrI MkuuStephen Ruvuga

WaharIrIJacueline Massawe na Al-amani Mutarubukwa

BODI Ya WakuruGENZI Ya MVIWaTa Mwenyekiti – Habibu SimbamkutiMakamu Mwenyekiti – Veronica SophuMweka Hazina – Esther Mallya

WaJuMBEJoseph KilowokoPrisca JohnAmina KazibureProjestus IshekanyoroHaji Ussi HajiPaul Joseph

Katibu - Stephen Ruvuga- (Mkurugenzi Mtendaji)

LINaTOLEWa Na kuSaMBaZWa Na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA)

S.L.P 3220 Morogoro, TanzaniaSimu: 023 261 41 84Faksi: 023 261 41 84Barua pepe: [email protected], [email protected]: www.mviwata.org

uSaNIFu Na uChaPIShaJIPENplus Ltd – 022 2182059

Picha ya Jalada: Wanachama wa MVIWATA waliochaguliwa kuwa kwenye Bunge maalumu la katiba.

TahaririKatiba mpya iwape

watanzania uhuru na ulinzi wa kumiliki rasilimali (ardhi)

Katika Tanzania ya leo na miaka mingi ijayo, hakuna jambo lolote muhimu kwa wanajamii kuliko

ardhi na rasilimali zake. Rasilimali hizo ni chanzo cha uhai, kielelezo cha utamaduni, utambulisho wa utu, tegemeo la kuishi maisha ya kujitegemea na ishara ya heshima.

Tanzania ni moja kati ya nchi za Afrika zilizopata uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1960 ikiwa na matumaini mapya ya kutumia rasilimali zake katika kujiletea maendeleo na hakika maendeleo halisia ya jamii ya Tanzania bado yanategemea zaidi ardhi na raslimali zake. Lakini leo baada ya miaka 50 ya uhuru huo, matumaini hayo yamepotea. Kiwango cha umasikini kwa wananchi kimeongezeka, huku wananchi wachache wakimiliki uchumi na kufaidi rasilimali za taifa wakati wengi wakihangaikia mlo wa kila siku. Ardhi ambayo ndiyo rasilimali pekee kwa masikini wengi inaanza nayo kuwaponyoka, ikielekezwa kwa wawekezaji, kwa kuamini kwamba wao ndiyo watakoleta mapinduzi ya kilimo Tanzania.

Baada ya serikali kuhimiza uwekezaji hasa wa kutoka nje, kumekuwa na ongezeko la uporaji wa ardhi ya vijiji ambao umesababisha migogoro mingi. Hali ni hiyo hiyo katika uchimbaji madini ambapo wazalishaji wadogo wamefukuzwa ili kupisha wawekezaji na hivyo kuwanyang’anya njia yao pekee ya maisha yao na kuwafukarisha.

Ndiyo maana, licha ya kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete

kwa kuanzisha mchakato wa uandishi wa Katiba mpya pamoja na uteuzi wa wanachama wawili wa MVIWATA kwenye Bunge Maalum la Katiba, tunaomba andiko hilo litoe majibu ya kisheria juu ya mustakabali wa rasilimali hizi.

Kama asasi pamoja na wanachama wetu tumeshiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni juu ya Katiba mpya na kisha tukapata fursa ya kupitia Rasimu ya Katiba kama Baraza la Katiba.

Kufuatia mwenendo wa mjadala wa awali wa Bunge maalumu la Katiba, tuna mashaka kuwa huenda mvutano wa kuhusu idadi ya serikali zinazopendekezwa ukagubika hata vipengere nyeti vya Katiba kama haki na ulinzi wa rasilimali ardhi ambavyo ni muhimili wa wazalishaji wadogo. Tunatambua kuwa uwepo na ongezeko la migogoro ya ardhi baina wazalishaji wadogo unatokana na ulinzi na usimamizi hafifu wa rasilimali kisheria, kwa hiyo tunatoa rai suala la ardhi ni muhimu sana kuingizwa kwenye katiba mpya na litamke bayana uhuru na watanzania kumiliki na kutumia rasilimali za nchi yao.

Ardhi inapaswa kuwekwa kwenye katiba kama mojawapo ya haki za binadamu ikiunganishwa na haki zingine za kumiliki mali, haki ya kuishi na haki zinginezo.

Tunapoendelea na mjadala au mchakato wa kuunda Katiba mpya, ardhi na ulinzi wa rasilimali unapaswa kuangaliwa upya ili kuleta ustawi wa kweli wa taifa na watu wake wote tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaonufaika na rasilimali za nchi ni wachache, aghalabu wawekezaji kutoka nje.

3Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 20142

MADA MAALUM MADA MAALUM

Endelea Uk wa 3

Inatoka uk. wa 2Inatoka uk. wa 1

Akitoa mfano alisema, haki za mfanyakazi na waajiriwa zimeorodheshwa kwa mapana ikiwemo; Kufanya kazi bila ubaguzi wowote, kupata ujira na malipo halali kulingana na kiasi na sifa za kazi anayofanya.

Kwa upande wa haki za mtuhumiwa na mfungwa, alisema, wamepewa haki ya kuwasiliana na mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa na pia kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake.

Akianisha haki za makundi madogo madogo katika jamii alisema “moja ya haki za kundi hili ni pamoja na kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi hayo huitumia kama eneo la kuishi na kupata riziki ya chakula”.

Bw. Kibamba alihoji kama mfanyakazi analipwa ujira na malipo kulingana na kiasi cha sifa na kazi anayofanya kwa nini basi mkulima naye asiuze mazao yake kwenye soko lenye u h a k i k a na kupata ujira wake k u l i n g a n a na gharama a l i z o t u m i a wakati wa uzalishaji.

Mbali na hilo alisema pia kwenye sura ya pili ibara ya kumi na moja kipengele cha (v-vii) kimegusia baadhi ya mambo yanayowahusu wazalishaji wadogo wakiwemo wakulima, wafugaji na wavuvi kama vile kuwapatia ardhi pamoja na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.

Pia kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao

yao bila kusahau kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizani ya bei na mazao na pembejeo.

Hofu ya Bw. Kibamba ni juu ya utekelezwaji wa mambo haya kwani

yameorodheshwa kama malengo makuu na hayapo katika

kipengele cha utekelezaji wa

malengo.

Mbali na w a k u l i m a kuonyesha mas ik i t i ko yao ya kusahaulika

k w e n y e rasimu ya

katiba na hasa katika masuala

ya umiliki wa ardhi kwa kigezo cha kuwa

ni masuala ya nchi husika, lakini hawakuacha kumuuliza Bw. Kibamba maswali ikiwemo kutaka kufahamu kama katiba haitokamilika kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 itakuwaje na kama kutakuwa na muda mwingine wa kukusanya maoni ii kutunga katiba ya Tanganyika kama katiba mpya itaruhusu serikali tatu, swali hilo lililoulizwa na Ndugu Nyasa mkulima toka Masasi.Akijibu swali hilo Bw.Kibamba alisema pendekezo la jukwaa la

katiba ni kutaka kusukwa upya kwa Tume ya Uchaguzi ili kuandaa utaratibu utakaotumika mwaka 2015 wakati wa uchaguzi jinsi katiba itakavyokuwa imeeleza.

Na kuhusiana na katiba ya Tanganyika kama mfumo wa seriaklai tatu utapita, alijibu kuwa yatatumika maoni yaliyokusanywa mwanzo halikadhalika aliongeza pia kuna uwezekano wa Zanzibar nao kufanyia marekebisho katiba yao kulingana na katiba ya muungano itakavyokuwa.

Naye Bi. Nelly Muhando mkulima kutoka Morogoro alihitaji kufahamu kama fedha za vigogo zilizohifadhiwa nje ya nchi zitarudishwa Tanzania, kwa nguvu ya katiba mpya, ili ziweze kufanya kazi nyingine kwa kuwa huenda zimechotwa nchini kibadhirifu.

Bw. Kibamba alimjibu Bi. Mhando kwa kumwambia kuwa inatakiwa zirudishwe nchini mara moja japo rasimu ya katiba haijaelekeza zirudi kwa utaratibu gani, hata hivyo aliwasihi wakulima kutafakari pamoja njia ya kuhakikisha fedha hizo zinarudi mikononi mwa Watanzania.Akijibu swali la Bw.Nasoro Rusonje mkulima toka Tanga aliyeuliza wakuu wa mikoa na wilaya watawajibika

kwa nani kama nafasi ya Waziri Mkuu imeondolewa kwenye rasimu ya katiba, Bw. Kibamba alijibu jambo hii ni moja ya mapungufu ya rasimu ya katiba mpya.

Naye Christina Nathani mkulima toka Manyara alipenda kufahamu imekuwaje kipindi cha kuanzia mwaka 2005 nchi haikuwa na madeni lakini kwa kipindi cha miaka saba na nusu hadi leo nchi imekuwa na madeni makubwa ambapo wananchi hawaelewi msingi wa madeni hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo wa Jukwaa la Katiba alijibu madeni haya yanatokana na kukopa fedha kwa wahisani kwa ajili kufanya baadhi ya shughuli nchini na wakati mwingine mikopo hiyo inakuwa na riba kubwa lakini kipindi cha nyuma si kwamba nchi haikuwa na madeni bali ilipata msamaha wa madeni yake.

Hata hivyo Bw. Kibamba hakuacha kubainisha baadhi ya mambo mazuri katika rasimu hii ya katiba na kusema endapo rasimu hii itapita basi hii itakuwa Katiba ya kwanza shirikishi.Katiba hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itayopatikana kwa kupendekezwa na Bunge Maaalum la Katiba “itakuwa imetungwa na sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kura za maoni.”Hali kadhalika, mtaalamu huyu

aliisifu rasimu kwa kuwa imeongeza tunu za kitaifa kutoka nne hadi saba ambazo ni Utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya taifa, pia kuwepo kwa idadi sawa ya wabunge wa kuchaguliwa bungeni nusu kwa nusu kijinsia.

“Pia idadi ya wabunge itapungua kutoka 360 waliopo sasa toka Tanzania bara na visiwani na kubaki 75 wakiwemo watano wa kuteuliwa wenye ulemavu na pia mawaziri watakaoteuliwa hatavuka 15 tofauti na walipo sasa 60,” alisema.

Mchakato wenyeweAwali, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na Jaji Mstaafu Joseph Warioba ilikamilisha hatua ya mwanzo ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba wanayoitaka. Na baada ya kukamilisha hatua hiyo, Tume ilitoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba na kisha kuanzisha mchakato wa mabaraza ya Katiba.

Mchakato wa mabaraza ya Katiba ulizipa asasi, taasisi na makundi mbalimbali fursa ya kuketi kama mabaraza ya katiba ambao walijadili rasimu ya kwanza na kutoa mapendekezo yao kwa Tume, kisha tume ikayachambua na kuunda rasimu ya pili ya Katiba iliyotoa Desemba,2013.Hatua nyingine ni uteuzi wa wajumbe wa Wajumbe wa Bunge

la Katiba unaofanywa na Rais, ambapo wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali ya kiraia na vyama walijumuika na wabunge na wawakilishi kwa kazi maalum ya kujadili Rasimu ya Pili ili kuzaa Rasimu ya mwisho.

Rasimu hiyo itakayopitishwa na Bunge Maalum ndiyo itakayopigiwa kura ya maoni, na endapo itakubaliwa na wananchi, Tanzania itakuwa imeandika historia kwa kuwa na Katiba Mpya.Ushiriki wa MVIWATA katika mchakato wa katiba mpya ulikuwa kama ifuatavyo:

a) Kuisoma na kuangalia mapungufu katika katiba ya sasa ya nchi

b) Kukusanya maoni ya wanachama kupitia kikao cha pamoja cha wanachama

c) Kurasimisha maoni katika mkutano mkuu wa wanachama

d) Kuwasilisha maoni rasmi ya MVIWATA kwa Tume ya Marekebisho ya Katiba

e) Kusoma na kuweka maoni katika rasimu ya kwanza ya katiba mpya

f) Kukutana kama baraza la katiba baada ya kupata kibali cha Tume ya Marekebisho ya Katiba. Wakati huo huo kuna wanachama binafsi ambao waliomba na kupitishwa kuwa katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya

g) Kuwasilisha maoni kwa Tume ya Marekebisho ya Katiba juu ya rasimu mpya

h) Kuomba kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba: majina 9 yaliwasilishwa, mawili yaliteuliwa na Mh. Rais. Kulikuwa na taasisi zaidi ya 200 na majina takriban 4000.

i) Kukutana na wawakilishi wa wazalishaji katika Bungela Katiba na kuandaa ibara zinazohusu ardhi kwa ajili ya kutumia kama nyenzo ya ushawasihi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Ndugu Deus Kibamba. Rasimu ya Katiba haijazitaja haki za mkulima mdogo kama ilivyofanya kwa makundi mengine.

Mkulima akichangia maoni juu ya rasimu ya Katiba kwenye Mkutano Mkuu wa 18 wa MVIWATA hivi karibuni

5Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 20144

KATIBA KATIBA

Endelea Uk wa 5

Na Jacueline Massawe

Kufuatia kibali kilichotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuruhusu Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), kuunda Baraza la Katiba la kitaasisi, ilitekeleza jukumu hilo kupitia Mkutano wake Mkuu wa tarehe 23-26 Julai 2013 mijini Morogoro na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 2000.

MVIWATA yaketi kama Baraza kujadili na kutoa maoni juu ya

Rasimu ya Katiba Mpya

Aidha, Baraza liiliketi tena tarehe 26-27 Agosti 2013 kwa ajili ya kujumuisha maoni

yote na kujadili maoni yoyote mapya katika rasimu ya Katiba, jumla ya washiriki 53 kutoka mikoa ya bara na visiwani, wanawake wakiwa 26 na wanaume 27 walishiriki katika Baraza hili.

Kisha shirika, kama asasi nyingine za wanachama, liliwasilisha Mapendekezo ya Uchambuzi kuhusiana na Rasimu ya Katiba kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyokua imeelekezwa.

Akizungumza kwenye baraza hilo, Mkurugenzi wa MVIWATA Bw. Stephen Ruvuga ameishauri Serikali kuwa makini na mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya akisema ni vyema ikaangalia ni jinsi gani itaainisha masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya wakulima wadogo nchini.

Aliyasema hayo mjini Morogoro tarehe 26/9/2013 wakati asasi hiyo ilipokuwa ikijumuisha mapendekezo ya Rasimu ya Katiba Mpya.

Bw. Ruvuga alisema, mchakato unaoendelea wa uundwaji wa Katiba mpya unaibua maswali makuu mawili kwa wakulima wadogo nchini ikiwemo, suala la kupoteza umiliki wao wa rasilimali ardhi ambayo ni muhimu katika maisha yao, hali kadhalika kuwepo kwa michakato inayowasukuma kando wakulima wadogo na wazalishaji kutoka kwenye maeneo yao ya uzalishaji ili kuwapisha wawekezaji.

“Wakulima tumetoa maoni mengi sana ambayo ni maisha yetu ya kila siku lakini hayaonekani katika Rasimu ya Kwanza ya Katiba na hakuna mwingine anayeweza kututetea kama siyo sisi wenyewe wakulima. Kama katiba hii haitutambui basi

ina mwelekeo kuwa hatuna thamani katika nchi yetu ila mazao yetu ndiyo yenye thamani,” alisema Bw. Ruvuga.

Akifafanua hayo alisema, Katiba iliyopo sasa ina mapungufu kwani mifumo ya umiliki wa ardhi hasa kwa wakulima wadogo haiko bayana wakati kwa uhalisia kumekuwa na usumbufu mkubwa hata kumkatisha tamaa mkulima mdogo kufuatilia hati-miliki ya ardhi yake kinyume na mwekezaji anapohitaji kumiliki ardhi huwa haichukui muda mrefu kupata hatimiliki hiyo.

Mapungufu mengine ni mamlaka ya usimamizi wa ardhi kuwa katika mipaka finyu na kushindwa kutekeleza makujukumu yake kwa uhuru zaidi.

Pia nchi inaendelea kushuhudia uwekezaji wa ardhi unaokiuka haki na utu wa wakulima wadogo hata kuchangia kuporwa ardhi yao kwa utumiaji wa nguvu ya ziada hata kusababisha vifo miongoni mwao.

Kuhusu haki za msingi ambazo wakulima wadogo wanapaswa kuzipata na kusisitiza ni vyema kama zitaainishwa kwenye Katiba ijayo Bw. Ruvuga alisema ni pamoja na haki ya kutumia rasilimali asilia na hasa ardhi pasipo kubugudhiwa.

“Wakulima kupata huduma za msingi zinazoendana na shughuli zao ikiwemo mikopo, masoko, pembejeo na huduma za ugani kama sehemu ya wajibu wa Serikali kwa umma.

Haki nyingine ni pamoja na kupata huduma za kijamii ikiwemo huduma ya afya, elimu na hasa kwa watoto wa wakulima pamoja na haki za kawaida za ulinzi wa binadamu.”

Kwa upande wake Bw. Thomas Laiser, Afisa Sera na Utetezi MVIWATA, alisema pamoja na kupata nafasi kama shirika na wanachama wake ambao ni wakulima wadogo toka Tanzania bara na Zanzibar kukaa kama baraza la Katiba ili kuweza kuijadili rasimu, wamegundua kuwa Rasimu ina mapungufu kwani imekwepa k u z u n g u m z i a masuala ya umiliki wa ardhi.

“ R a s i m u i m e s e m a suala la umiliki wa ardhi litabaki kuwa la nchi washirika kama k u t a k u b a l i k a kuwa na Serikali tatu, hofu yetu ni kuwa kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano haijazungumzia suala hilo je, nchi washirika watawezaje kubainisha umiliki wa rasilimali ardhi katika Katiba zao kama Katiba mama

haijalizungumzia,” alihoji Bw. Laiser.

Kwa upande wake Bi. Ester Mallya mkulima mdogo toka Kilimanjaro alisema, rasimu ya katiba haijabainisha mkulima mdogo ni yupi, hivyo tafsiri ya jumla kwa mkulima wa kati na mkubwa husababisha wakulima wadogo wanaofanya asilimia 80 ya watanzania kupoteza fursa hata za mikopo na pembejeo za kilimo kuishia kwa wakulima wakubwa.

Naye Bw. Piter Iyambi, mkulima mdogo toka Manyara alisema rasimu

hii haijazungumzia kabisa haki za wakulima

na hata maoni wa l i yochang i a

wakati Tume i k i k u s a n y a maoni hayapo katika rasimu hiyo ya katiba jambo l i na lowat i a hofu kuwa

katiba ijayo h a i t o k u w a

shirikishi kama Serikali inavyosema.

Bi. Hawa Kihwele, mkulima mdogo kutoka Mbeya, kwa upande wake alisema rasimu hiyo haijabainisha ukomo wa deni la serikali kwa kuwa deni hilo limeendelea kuwa kubwa na mwisho

Afisa Ushawishi na Utetezi, Bw Thomas Laiser akiongoza mjadala na wajumbe wa Baraza la Katiba la MVIWATA hivi karibuni

Wajumbe wa Baraza la Katiba la MVIWATA wakijadili Rasimu ya Katiba ili kubaini mapungufu na kuyatolea mapendekezo

wa siku wanaolipa madeni hayo ni wananchi kupitia kodi mbalimbali.

“Ilikuwa busara kama Rasimu ya Katiba Mpya ingetamka bayana kiwango cha mwisho deni la taifa.... na isitoshe fedha zenyewe hazijatufanisha na mwisho wa siku wakulima tusionufaika na rasilimali yoyote nchini ikiwemo ardhi tunayoitumia ndiyo tunaoumia na madeni hayo,” alibainisha Bi. Kihwele.

Naye ndugu Habibu Simbamkuti, Mwenyekiti wa MVIWATA, alisema wakati umefika wakulima nao wapate haki ya kikatiba ya kupata malipo ya mafao ya uzeeni kama wanavyolipwa wafanyakazi wastaafu wa serikalini.

“Wakulima tunachangia pato la taifa maradufu na kukatwa kodi za mazao yetu, ajabu ni kwamba Serikali imetusahau katika suala la mafao. Hii ni dhahiri kuwa mkulima hathaminiwi tofauti na kinavyothaminiwa anachokizalisha tena kwa jembe la mkono na kuuza kwa bei isiyokidhi gharama za uzalishaji,” alimalizia Bw. Simbamkuti.

Baada ya uchambuzi wa Rasimu hiyo ya Kwanza ya Katiba, Baraza hilo lilifanya majumuisho na kupanga kuwasilisha mapendekezo yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Akizungumzia hatua ambazo shirika litachukua kama mapendekezo hayo hayataingizwa katika rasimu ya katiba Bw. Thomas Laiser Afisa Sera na Utetezi alisema, “Haya ni mapambano ya kupaza sauti, bado tuna nafasi ya kupiga kura ya Ndiyo au kuikataa rasimu ya katiba kama itakuwa haijabeba ujumbe wetu na hasa kwa kuwatetea wakulima wadogo.”

Mbali na hatua hiyo aliwashauri viongozi wa kisiasa kutokuingilia mchakato huo wa katiba kwa maslahi yao binafsi ama maslahi ya vyama vyao kwa kuwa Katiba mpya inapaswa kubeba maoni ya watanzania kulingana na makundi yao na siyo maoni ya wanasiasa.

Inatoka uk. wa 4

7Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 20146

KATIBA KATIBA

Endelea Uk wa 8Endelea Uk wa 7

Sura Ya kWaNZaSEhEMu Ya kWaNZaIbara ya 2; Eneo la Jamhuri litaje ardhi badala ianishapo “eneo” kama ilivyobainisha bahari.

Ibara ya 5; Tunu za Taifa; Mbali na tunu zilizotajwa, “historia” ya taifa iongezewe iwe ni tunu mojawapo ya taifa

SEhEMu Ya PILIIbara ya 6; Mamlaka ya nchi Kipengele (b) mwisho wa

sentesi liongezwe neno “wote bila ubaguzi”.

Kipengele (c) idokeze masuala ya msingi ambayo serikali itawajibika kwayo badala ya kutumika lugha ya jumla kwenye rasimu.

Ibara ya 7; Watu na Serikali Ibara ndogo ya pili ya ibara

hii kipengele cha (a) isomeke “haki za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa” na neno utu libaki katika kipengele (g)

Kipengele (d) kinachozungumzia ardhi, kibainishe mgawanyo wa ardhi Mf ardhi ya kilimo (ikibainisha pia ardhi kwa wakulima wadogo na kwa kilimo cha biashara),ardhi ya hifadhi, na ardhi ya jumla.

Kipengele (e) kisomeke: maendeleo ya uchumi wa Taifa yanapangwa “kwa njia shirikishi” na kukuzwa kwa ulinganifu “vijijini na mijini” na kwa pamoja na kwa namna ambayo inawanufaisha wananchi wote “bila ubaguzi”.

Mapendekezo ya Mtandao wa Vikundi Vya Wakulima Tanzania (MVIWATA)

Katika Rasimu Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Kufuatia Mikutano Ya Mabaraza Ya Katiba Ya Tarehe 25 Julai 2013, Tarehe 26 – 27 Agosti

2013 Morogoro

Katika ibara hii ya saba, ibara ndogo ya 2 kiongezwe kipengele (l) na kisomeke “Raslimali na maliasili za nchi zinalindwa”

Baada ya ibara ya 7, na kwa kuzingatia umuhimu wa raslimali ardhi; wajumbe wa baraza la katiba la MVIWATA wamependekeza suala la ardhi liwe na ibara yake pekee ambayo itajikita kuzingatia masuala yafuatayo;

1) Mifumo ya umiliki na matumizi ya ardhi ya jamii za makundi mbalimbali itambuliwe na ilindwe kwa mujibu wa sheria dhidi ya uhamishwaji na uingiliwaji wa kijinai au wa aina nyingine yoyote bila ushirikiano wao.

2) Mfumo wa umiliki usimamizi na matumizi ya ardhi utazingatia misingi ya haki, usawa, uwazi, uhifadhi wa ardhi na matumizi endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae

3) Katiba iweke masharti

ya kuweka taratibu z i t a k a z o w e z e s h a mwananchi mzawa kuwa na uhakika na ulinzi wa kuendelea kumiliki na kutumia ardhi yake bila hofu ya kupoteza ardhi.

Sura Ya PILIIbara ya 11, ibara ndogo ya (1)

kuhusiana na Malengo makuu, liongezewe neno “rasilimali za taifa” kama mojawapo ya masuala yanahitaji ulinzi wa katiba ili isomeke; Kulinda ……….,, rasiliamali za taifa

Ibara ndogo ya 3, (a) (i) kisiasa;… “ubaguzi utokanao na itikadi ya kisiasa” ijumuishwe kati ya masuala ambayo serikali itahakikisha inayakabili kupambana na dhulma katika kutekeleza malengo ya Taifa kisiasa.

Ibara ndogo ya 3 (b) (ii) kijamii …“ubaguzi utokanao na itikadi ya kisiasa” ijumuishwe kati ya masuala ambayo serikali itahakikisha inayakabili kupambana na dhuluma katika kutekeleza malengo ya Taifa kijamii.

Ibara ndogo ya 3 (b) (iv) kijamii; maneno “msaada na…” yaondolewe na kifungu hicho kisomeke “kuhakikisha kuwa hifadhi ya jamii inatolewa kwa watu wasiojiweza, wazee, wagonjwa, watoto na watu wenye ulemavu.”

Ibara ndogo ya 3 (c) (i) kiuchumi; neno “kuwaletea…” liondolewe na kifungu hicho kisomeke “kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora kwa kuondoa umaskini”.

Ibara ndogo ya 3 (c) (iii) neno “…uwakilishi wa…” liondolewe, na badala yake kifungu hicho kisomeke “kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya wakulima, wafugaji na wavuvi”

Ibara hiyo ndogo ya 3 (c) (v) ibadilishwe namna inavyosomeka na isomeke “kuweka mazingira bora na kuhakikisha upatikanaji wa nyenzo kwa ajili ya kukuza kilimo,ufugaji na uvuvi”

Chini ya kipengele hicho cha 3 (c) (v) kiongezeke kipengele cha 3 (c) (vi) na kisomeke kama ifuatavyo; “kuhakikisha kuwa kila mkulima na kila mfugaji anakuwa na umiliki wa ardhi unaotambuliwa na kwamba kunakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi unaohakikisha makundi hayo yanaishi bila migogoro”.

Sura Ya TaTuSEhEMu Ya kWaNZaIbara ya 13 ibara ndogo ya (1)

(b) yaongezwe maneno “…wote bila ubaguzi” ili kifungu hicho kisomeke “yanatoa wajibu kwa kiongozi kuwatumikia wananchi wote bila ubaguzi”

Ibara ya 15.(1) ifanyiwe marekebisho na kifungu hicho kisomeke “Zawadi au Kitu chochote kitakachotolewa kwa mtumishi wa umma, kiongozi au mwenza wake wa ndoa, au watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane katika shughuli za umma ni zawadi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na itawasilishwa kwa katibu mkuu kiongozi kupitia kwa katibu mkuu wa wizara au taasisi ya umma inayohusika”.

Ibara ya 15 (2) (a) iondolewe kutoka ibara hii na kuhamishiwa Ibara ya 20 inayozungumzia miiko ya uongozi wa umma na iingizwe katika ibara ndogo ya (2) (a) chini ya kipengele (iii) na chenyewe kiwe (iv).

Ibara ya 20 ibara ndogo ya (3) kipengele (c) kiisomeke kama ifuatavyo; “….atasimamishwa kazi au uongozi mpaka tuhuma anazokabiliwa nazo zitakapothibitishwa na kuamuliwa kwa mujibu wa sheria au taratibu nyingine zinazowahusu viongozi wa umma”.

Sura Ya NNESEhEMu Ya kWaNZaIbara ya 30 (1) (a) isomeke

“kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa sahihi na kuzambaza taarifa hizo.”

Ibara ya 36 ibara ndogo ya (2) inatakiwa igawanyike katika vipengele vidogo viwili ili kujitosheleza kimaudhui na isomeke ifuatavyo;

a) bila kuathiri ibara ndogo ya (1) itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake

b) bila kuathiri ibara ndogo ya (2) mali itakayo taifishwa itatolewa malipo kulingana na thamani halisi ya mali hiyo.

Baada ya ibara ya 35, inapendekezwa kuwepo kwa ibara ya (36) kama ifuatavyo;

Ibara ya 36; Haki za Mkulima Mdogo Kila mkulima ana haki ya

1) kumiliki na kuitumia ardhi.

2) kuuza mazao yatokanayo na shughuli zake za kilimo bila vikwazo wala kubughudhiwa ndani na nje ya nchi kwa bei anayoona inafaa

3) kupata kwa wakati pembejeo zenye ubora na katika bei ambayo mkulima anaimudu

4) Kupata huduma bora za ugani kwa wakati

5) Kushiriki katika kufanya maamuzi, utungaji sera na sheria zinazohusu wakulima.

6) Kupata na kuhakikishiwa hifadhi ya jamii uzeeni

7) Kuhakikishiwa huduma za msingi na za kijamii hususani elimu kwa watoto wa wakulima, usalama, afya na miundo mbinu na nishati

8) Kupata mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa riba nafuu.

9) Kupata taarifa ya fedha na maendeleo ya mipango na miradi ya kilimo inayotekelezwa katika maeneo wanapoishi.

SEHEMU YA PILIIbara ya 52, ibara ndogo ya (1)

(a) “…uhuru wa mtu binafsi bila kukiuka sheria ya nchi”

Ibara ya 52, ibara ndogo ya (2) neno “nafuu” lililotumika katika kifungu cha maneno ya ibara hiyo ndogo libadilishwe na badala yake neno “haki” litumike.

Sura Ya TISaBuNGE La JaMuhurI Ya MuuNGaNOIbara ya 107 (2) (h); Pamoja na

maelezo yaliyotolewa katika kipengele hiki, ni vema raslimali na maliasili hizo zikaanishwa katika katiba.

Ibara ya 110 ibara ndogo ya (3) ifanyiwe marekebisho na kusomeka ifuatavyo, “Wakati wa kuandaa muswada wa sheria kuhusu jambo lolote la Muungano, Serikali ya Jamuhuri

Inatoka uk. wa 6

9Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 20148

Bi. Catherine Sibuti, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba

KATIBA KATIBA

Inatoka uk. wa 7

ya Muungano itahakikisha kwamba inawashirikisha makundi ya wananchi wenye maslahi kuhusiana na sheria inayotungwa kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswaada huo.

Ibara ya 111 (1) iwe kipengele kinachobainisha nafasi na jukumu la wananchi katika kufanya mabadiliko yoyote ya katiba badala ya jukumu hilo kuwa la wabunge pekee.

Ibara ya 115 (2) kifanyiwe marekebisho kwani kina utatanishi (wa kueleweka mantiki yake) na kinaonekana kulinyang’anya bunge mamlaka yake ya kuiwajibisha serikali.

Ibara ya 116 (4) inayopendekeza uteuzi mbunge iwapo aliyepo amepoteza sifa ya kuwa mbunge ifanyiwe marekebisho ili badala ya uteuzi kufanywa kujaza nafasi hiyo ufanyike uchaguzi.

Ibara ya 117 (1) (a) inayozungumzia Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge, inapendekezwa kiongezwe kipindi cha ukomo wa madaraka, hivyo isomeke “… mtu yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo, ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na tano wakati wa kugombea na asiyezidi miaka 65.

Ibara ya 117 (2) (c) isomeke Ikiwa mtu huyo am-

etiwa hatiani na ma-hakama yoyote ile ka-tika Jamhuri ya Muun-gano wa Tanzania kwa makosa ya kuhujumu uchumi, ufisadi, rush-wa, mauaji, ubakaji, madawa ya kulevya, kutumia madaraka yake vibaya au ma-kosa mengine yoyote yanayoambatana na kukosa uaminifu.

Ibara ya 121 iboreshwe kwa maneno.

• Mishahara, posho na stahili nyingine za wabunge zitawekwa wazi kwa umma.

Ibara ya 122 1) d) isomeke atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa miezi 9 mfululizo kutokana ugonjwa. • Kiongezwe kifungu

kipya g) atakutwa na hatia ya kosa la jinai kama ilivyobainishwa katika ibara ya 117 (2) (c)

• Ibara ya 127 (2) liongezwe

maneno…Taarifa itawekwa wazi kwa wananchi katika njia itakayoamuliwa na sheria.

Sura Ya kuMI Na MBILIuChaGuZI kaTIka VYOMBO VYa uWakILIShI Na VYa SIaSaIbara ya 180 (4) maneno “…

kila mpiga kura yaondolewe na mahala pake isomeke “…kila mgombea”.

Ibara ya 181 (2) isomeke Tume huru ya uchaguzi itaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine saba ambao watapendekezwa na Tume ya Uteuzi na kujadiliwa na Bunge kabla ya uteuzi wa mwisho utakaofanywa na Rais.

(4) (e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kw kosa lolote la jinai ikiwemo makosa ya kuhujumu uchumi, ufisadi, rushwa, mauaji, ubakaji, madawa ya kulevya, kutumia madaraka yake vibaya au makosa mengine yoyote yanayoambatana na kukosa uaminifu.

5) (e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai ikiwemo kwa makosa ya kuhujumu uchumi, ufisadi, rushwa, mauaji, ubakaji,

madawa ya kulevya, kutumia madaraka yake vibaya au makosa mengine yoyote yanayoambatana na kukosa uaminifu.

(6) (c); kifungu kifutwe Ibara ya 182 (1) iongezwe

kipengele (h) na isomeke “wawakilishi wawili kutoka vyama vya kiraia”

Ibara ya 182 (4) kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3) Kamati ya Uteuzi mara baada ya kuchambua majina ya watu walioomba kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi itapeleka Bungeni majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kuyajadili na kuyapitisha kabla ya kuwasiisha kwa Rais kwa uteuzi.

Ibara ya 183 (2) (e) isomeke kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai ikiwemo makosa ya kuhujumu uchumi, ufisadi, rushwa, mauaji, ubakaji, madawa ya kulevya, kutumia madaraka yake vibaya au makosa mengine yoyote yanayoambatana na kukosa uaminifu.

Ibara ya 183 (4) iongezwe (e) Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Ibara 188 (4) iongezwe (e) awe hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai ikiwemo makosa ya kuhujumu uchumi, ufisadi, rushwa, mauaji, ubakaji, madawa ya kulevya, kutumia madaraka yake vibaya au makosa mengine yoyote yanayoambatana na kukosa uaminifuIbara ya 189 (2) (l) badala ya

kusomeka “kuomba msaada” isomeke “kutaka taarifa”

Endelea Uk wa 10 Endelea Uk wa 10

MVIWATA yapata wawakilishi wawili ndani ya Bunge Maalum

la KatibaNa Al-amani Mutarubukwa

Baada ya kimya kirefu pamoja na shauku ya Watanzania kutaka kufahamu ni nani

wangeteuliwa kuwa ndani ya Bunge maalumu kuijadili Rasimu ya pili ya Katiba, hatimaye Rais amevunja ukimya huo na kuanika hadharani majina 201 kati ya maelfu ya majina yaliyomfikia mezani kwake yakipendekezwa kuteuliwa.

Katika orodha ya majina hayo iliyotangazwa tarehe 7/2/2014 wanachama wawili wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) wameuliwa na Mh Rais kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba.

Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya taasisi 732 toka Tanzania Bara na visiwani ziliwasilisha jumla ya majina 3,754 katika kuitikia wito wa Rais wa kupendekeza majina, lakini katika ya majina hayo ni majina 201 tu ndiyo yaliyoteuliwa.

Kwa upande wa vyama vya wakulima, vyama 157 vilivyopeleka

Bi.Verenica Sophu, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba

majina na kati ya hivyo na majina 20 pekee ndiyo yameteuliwa ambapo kati ya hayo yapo majina mawili ya wakulima kutoka MVIWATA.Akizungumzia nafasi hizo mbili kwa shirika, Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA, Bw. Stephen Ruvuga alisema ni jambo la heshima sana kwa shirika kupata wawakilishi wawili kati ya tisa waliokuwa wamependekezwa na kufafanua kuwa, “Kati ya majina 2,762 yaliyopendekezwa ambayo yanatoka katika Taasisi 554 Tanzania bara ni majina 201 tu ndiyo yaliyopita na kati ya hayo, huku washiriki wawili wanatoka MVIWATA.”

Jambo la kujivunia ni kuwa katika mchakato huo kulikuwa na majina mengi yaliyopendekezwa na taasisi mbalimbali ambapo yapo mashirika ambayo hayakujapata uwakilishi huo hata kwa nafasi moja, alisema na akaongeza; “Kwa shirika kupata wawakilishi wawili ni jambo la zuri na hii inatoa nafasi ya kupenyeza maoni yetu kama taasisi ya wakulima wadogo

kwenye Bunge la Katiba.”Akidokeza mapungufu ya moja kwa moja yaliyomo ndani ya Rasimu ya Katiba, Bw. Ruvuga alisema kuwa Rasimu hii inawatazama wakulima kama kundi dogo, kitu ambacho siyo sahihi na kuwa ilifaa ifahamike kuwa wakulima ni kundi kubwa nchini na hivyo wapewe uwakilishi mkubwa katika bunge hilo la Katiba.

Wanachama hao wa MVIWATA walioteuliwa na Rais kujumuika na wenzao 18 kutoka asasi zingine watakaowakilisha mawazo ya wakulima wote nchini ni Bi.Verenica Sophu wa Mbarali, Mbeya na Bi. Catherine Sibuti toka Tarime, Mara.

Akizungumza na Pambazuko baada ya uteuzi huo, Bi. Sophu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa MVIWATA alisema kuwa, mbali na kupokea kwa mshtuko uteuzi huo , matarajio yake makubwa ni kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kuwawakilisha wakulima wadogo nchini kwa kupeleka maoni yao na si vinginevyo.

“Nilishtushwa na uteuzi huo, nakumshukuru sana Mwenyezi Mungu. Kwangu hii ni mwanya wa kupeleka ya wakulima wadogo wenzangu ili Katiba hiyo mpya itutambue kama kundi kuu lenye haki zake nchini.”

Kwa upande wake Bi. Catherine Sibuti toka Tarime ,Mara, ambaye pia ni promota (mkulima mwezeshaji wa masuala ya ardhi) , anasema anaamini kuwa jukumu alilonalo ni kubwa la kuwakilisha kundi kubwa la wakulima nchini na hasa kero zinazowakabili kila kukicha ikianza na ile ya rasimu ya pili ya katiba

11Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201410

Endelea Uk wa 12

Ushirikiano wa MVIWATA na NFRA: Wakulima wauza

tani 4,500 zenye thamani ya Sh2.3bilioni

Na Al-amani Mutarubukwa

Mpango wa ununuzi wa mazao uliofanywa kwa makubaliano kati ya

Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) na MVIWATA umetajwa kuwa na matokeo bora kwa wakulima katika msimu uliopita.

Katika msimu huo pekee, kupitia masoko ya Mkata, Igagala na Matai, wakulima wameiuzia NFRA jumla ya tani 4,500 za mahindi.

Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa Timu ya Uwezeshaji Kiuchumi ya MVIWATA Bwana Nickson Elly kwenye kikao cha kutathimini hali

ya ununuaji mazao katika masoko yaliyojengwa na MVIWATA kutoka kwa wanavikundi katika maeneo mbali mbali.

“Moja ya fanikio kuu ni kuwa bei ya mazao katika maeneo mengi ambapo NFRA ilinunua mahindi imepanda kutoka Sh430 hadi kufikia Sh500 kwa kilo, ikiwa ni pamoja na wakulima kutumia miundo mbinu ya masoko ambayo ipo vijijini,” alisema Bw.Elly.

Kwa mujibu wa Bw. Nicodemus Masawa, Mchumi kutoka NFRA alitaja kuwa kwa mwaka 2013 NFRA wameweza kunua mazao mengi kuliko miaka yote. Lengo lilikuwa kununua tani 200,000 lakini wameweza kununua tani 218,000 hivyo kuzidi lengo lililowekwa.

Alitaja kuwa kwa mwaka huu NFRA imeweza kununua mazao kutumia njia tatu ambazo ni kwa kufungua vituo vya kununulia mazao, 64% ya mazao yalipatikana kwa njia hii,

Soko la nafaka Mkata. Mpango wa ununuzi mazao kati ya MVIWATA na Wakala wa Chakula wa Taifa umeleta tija kwenye masoko ya shirika kwa msimu uliopita

Watumishi wa NFRA na MVIWATA wakiwa katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya MVIWATA, Morogoro

KATIBA KUTOKA MITANDAONI

kuwatambua wakulima kama kundi dogo nchini jambo ambalo si la kweli.“Kumekuwa na dhana mbaya inayozidi kujengeka miongoni mwa taasisi mbalimbali kuwa wakulima ni kundi lisilo na thamani na halina nguvu ya kufanya maamuzi yake lenyewe hivyo basi dhana hii kupelekea wakulima kutokupata haki zao wanazostahili bila kuangalia

Sura Ya kuMI Na NNEIbara ya 206 ibaki pasipokuwa

na vipengele kwa maana ya fedha zote kuwemo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ili kuzuia ubadhirifu.

Ibara ya 209 (1) inayotoa mwanya wa serikali kufanya matumizi pasipo kupata kibali cha Bunge kifanyiwe marekebisho ambayo yatazuia aina yoyote ya matumizi kufanyika pasipo kupata idhini ya Bunge.

Ibara ya 212 (Deni la Taifa): inahitaji kuongezwa ibara mpya itakayoelekeza ukomo wa deni la taifa

Ibara ya 213 (2) (b) kipengele hicho kirekebishwe ili taarifa zinazotolewa bungeni zisiishie bungeni bali zitolewe kwa wananchi wote.

Ibara ya 215 (a) bidhaa za kutozwa ushuru kwa ajili ya mapato ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ziwekwe wazi kwa kutajwa kwenye katiba.

Chini ya kipengele (d) kiongezwe kipengele (e) kitaelezea gawio kutoka Benki Kuu kama chanzo cha mapato ya serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Sura Ya kuMI Na TaNOuLINZI Na uSaLaMa kaTIka JaMuhurI Ya MuuNGaNOIbara ya 219 (2) irekebishwe na

kusomeka ifuatavyo; “…ikiwa ni pamoja na anga na bahari kuu, ardhi, watu wake, mali zao, haki, uhuru na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje”.

Ibara ya 220 (4); iwekewe nyongeza katika maelezo yake ya awali na kusomeka, “ kikundi cha watu au mtu hataruhusiwa kuanzisha taasisi, kampuni, jumuia au shirika linalohusiana na ulinzi na usalama…”

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa upepelezi wa Makosa ya Jinai, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Shirika la kupamabana na rushwa (kwa sasa Takukuru), Mkuu wa Jeshi la Magereza …na manaibu wao Waajiriwe kwa utaratibu ufuatao;a) Nafasi zitangazwe kwa

uwazib) Waombaji watume

Inatoka uk. wa 9

Inatoka uk. wa 8

MVIWATA yapata wawakilishi...

kama wao pia hukuza pato la nchi hii kwa kile wanachozalisha.”“Haki zetu nyingi za kimsingi hatuzipati na hatuthaminiwi labda kipindi cha chaguzi za serikali. Ardhi yetu inagawiwa kwa wawekezaji na sisi kutupwa kando, hii ndiyo sababu migogoro ya ardhi imekuwa ikigharimu maisha ya wenzetu kila kukicha....lakini pia, suala la sisi kukosa pembejeo za kilimo, kutokuwa na masoko ya uhakika wa kile tunachozalisha ni mambo

nyeti yanayopaswa kutamkwa na Katiba mpya,” alielezea Bi. Sibuti.

Wajumbe hao wawili wa MVIWATA tayari wameungana na wabunge wenzao wa bunge hilo maalumu la katiba mjini Dodoma, ambalo litadumu kwa hata miezi mitatu endapo italazimu kuongezwa muda ili kukamilisha kazi iliyopo mbele yao ya kuwapatia rasimu ya mwisho watanzania ambayo wataipigia kura ya maoni kuikubali au kuikataa.

maombi yao kwa Tume ya utumishi, Tume ya utumishi wa Mahakama, Tume ya utumishi wa Polisi, Tume ya utumishi wa Magereza i.e. tume ambazo hazipo zinapendekezwa kuuundwa kwa mujibu wa sheria

c) Majina yachambuliwe na tume za utumishi ili kuchuja . Waombaji wachache waliochujwa wafanyiwe usaili wa wazi

d) Yachaguliwe majina matatu kwa nafasi kwa ajili ya uteuzi ambapo majina hayo yatapekwa kuthibitishwa na Bunge kabla ya kupelekwa kwa rais kwa ajili ya uteuzi.

kutumia jina Tanganyika badala ya Tanzania Bara

Katika rasimu hii ya katiba ambayo inapendekeza uwepo wa Serikali tatu, yaani serikali za nchi washirika ambazo ni Tanzania Bara na Zanzibar, ni mapendekezo yetu kuwa pale pote ambapo jina “Tanzania Bara” limetumika liondolewe na badala yake jina “Tanganyika” litumike. Hii ni kwa kuzingatia historia kwani nchi mbili zilizoungana tarehe 26 Aprili 1964 zilikuwa ni nchi mbili huru ambazo ni Tanganyika na Zanzibar.

Mapendekezo ya Mtandao...

13Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201412

Kununua kwa kutumia mawakala, 29% ya mazao yalinunuliwa kwa kutumia njia hii na Kununua kwa njia ya vikundi, ambapo 7.8% ya mazao yalinunuliwa kwa njia hii.

Aliyataja maeneo ya ununuzi wa mazao kuwa yalikuwa Sumbawanga, Makambako, Songea, Morogoro, Njombe, Songea na Arusha.“Lengo kubwa lilikuwa kunua mazao kutoka kwa vikundi vya wakulima, na NFRA ilipenda kuweka mkataba na vikundi ili kuwa na uhakika wa kupata mazao lakini pia ili vikundi kuwa na uhakika wa kuuza mazao yao,” alisema.

Hata hivyo, licha ya zoezi kuwa na mafanikio kwa maeneo ununuzi huu ulipoendeshwa, wajumbe wa taasisi hizi mbili walibainisha changamoto zilizolikumba zoezi hili kuwa ni pamoja na vikundi kushindwa kuuza mazao yao katika maeneo mbali mbali kutokana na vikundi hivyo kutokuwa na uhakika kuwa NFRA watanunua mazao na hivyo kushindwa kujipanga vizuri.Changamoto nyingine ni kutokana

na ukweli kuwa kulikuwa na kipindi kifupi cha ununuaji hivyo baadhi ya wakulima kupitwa na zoezi hilo wakidhani lingechukua muda mrefu.

“Pia kulikuwa na baadhi ya vikundi vilivyotumika kibiashara kwa kununua mazao ya wakulima wengine, yaani, vikundi viliingia mkataba kwa kuonyesha mazao kidogo na baadaye kununua kwa wakulima na kuja kuuzia NFRA. Kwa kuendelea na hali hii vikundi vilileta mazao zaidi wakati tayari NFRA tulikuwa tumefunga ununuzi,” alisema Ndugu Masawa.

Changamoto nyingine ni ile ya NFRA kuchelewa kulipa madeni ya baadhi ya wakulima kutokana na kuchelewa kwa pesa kutoka serikalini.

Naye Meneja wa Kanda ya Kipawa, Bw. Emmanuel Msuya, ambaye kanda yake inahusika kununua mazao katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga aliwasilisha changamoto kuu katika ununuzi wa mazao ni kiwango cha ubora, hasa ukaukaji. Bw.Msuya aliongeza kuwa elimu kwa wakulima bado

Vijana wa soko la Mkata wakishona magunia ya mahindi yaliyonunuliwa na Wakala wa Chakula wa Taifa tayari kwa kusafirisha

ni ndogo hasa kwenye suala la ubora kwani mahindi yaliyokuwa yanauzwa mengine yalikuwa machafu na mengine madogo sana.

Akielezea baadhi ya changamoto za mfumo huu ambazo MVIWATA imeziona , Bw.Elly alisema baadhi ya maeneo yanakosa vianikio vya kutosha (maturubai) na hivyo kuchelewesha zoezi la ununuaji wa mazao.

Pia suala la kununua mazao ya wakulima kwa mkopo na kutolipa kwa wakati ni moja ya changamoto kuu kwani hali hiyo inawakwamisha wakulima kukidhi mahitaji yao ya msingi kwa wakati.

Nyingine ni wakulima kukosa elimu ya kutosha juu ya ubora wa mazao na hivyo kupima mazao zaidi ya mara moja, Kwa baadhi ya maeneo wabebaji kutoka mbali hivyo kuleta mgongano wa maslahi kwa nguvu kazi iliyo katika maeneo husika, alisema afisa huyo.

Katika hatua nyingine, ushirikiano huo umejipanga kuwa na vikao vya pamoja mara kwa mara ili kutathimini na wakulima jinsi ya kuboresha ununuzi wa mazao kutoka kwa vikundi.

Kikao hicho kitajumuisha maafisa wa NFRA , MVIWATA na viongozi watatu wa vikundi vilivyoshiriki kuuza mazao mwaka 2013 kutoa mikoa ya Njombe, Songea, Iringa, Katavi, Arusha, Kigoma, Sumbawanga, Rukwa, Singida, Tanga, Morogoro. “Kikao hiki kitatuwezesha kuwa na mfumo wa kumbukumbu (database) ya vikundi amabavyo vitatambuliwa na NFRA kimkataba katika ununuzi huu wa mazao,” aliongeza Bw.Masawa.

Alisema mfumo huo utawezesha vikundi hivyo kuviunganisha na Wakala wa mbegu au pembejeo na wakulima wa vikundi hivyo kufanya malipo baada ya kuuza mazao yao kwa NFRA.

Inatoka uk. wa 11 Dhana ya Utandawazi: Dunia ni Kijiji au Pori la Utanda-wizi?

Na Al-amani Mutarubukwa

Wakati uliberali mamboleo unapatiwa sura mpya ya kuwa Utandawazi, mazao

na maliasili za Tanzania zinanunuliwa kwa bei ya hasara wakati bidhaa zitokazo nchi za kibeberu zikipandishwa bei na kuuzwa kwa bei wanayoitaka wao bila kupangiwa.

Kwa mujibu wa Bw.Sabatho Nyamsenda, ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, neno “Utandawazi” ambalo linahubiriwa na watawala, wafanyabiashara wakubwa na wasomi waliobobea kwa nyakati hizi ni dhana ya ufyonzaji iliyokuja katika sura ya kificho.

Ndugu Sabatho alikuwa akizungumza katika warsha ya Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) iliyofanyika tarehe 23 Julai 2013 mjini Morogoro wakati akiwasilisha mada ya utandawazi na athari zake kwa wazalishaji wadogo.

Alisema kuwa kati ya nguzo muhimu za utandawazi ni maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo yamerahisisha ueneaji wa habari katika kila kona ya dunia, lakini pia imekuwa rahisi kusafiri katika sehemu mbalimbali za dunia.

“Na urahisi huo haukomei katika usafiri na mawasiliano tu pia umetamalaki katika biashara inayoendeshwa na kuhodhiwa na makampuni makubwa, ambapo vikwazo vya uhamishaji wa mitaji faida vimeondolewa katika nchi nyingi duniani.”

Aliongeza kuwa dhana inayotumika kuyaeleza yote hayo ni dhana ya kijiji, na katika nchi maskini kama Tanzania neno kijiji lina maaana ya pekee sana na wanapolitaja hujenga dhana yenye taswira mbili.“Upande wa kwanza wa taswira mbaya na isiyofurahisha ni umaskini

uliokithiri unaoambatana na ukosekanaji wa huduma za msingi kama vile elimu, afya, maji na usafiri.

Upande wa pili hutoa taswira inayofurahisha na kujenga matumaini juu ya jamii ya binadamu na huonekana kama mfumo wa maisha wanayoishi watu wa kijiji ambapo huishi kwa pamoja, hushirikiana na kusaidiana katika shida na raha na k u s a b a b i s h a pengo kati ya walio nacho na wasio nacho katika vijiji ni dogo sana na ninadra sana kumkuta mtu anaishi kwa kuwanyonya w e n z a k e , ” anasema Ndg.Sabatho.

Aidha watu wa kijijini ni wachapa kazi na kila mtu huishi kwa jasho lake na dhana ya kujitegemea utaikuta kijijini kwa kuona wanakijiji wanachimba visima, barabara na wana mifumo yao wenyewe ya ulinzi katika jamii yao hata asiye nacho huthaminiwa na wenzake kama alivyo mtu mwingine yeyote duniani.

“Je! hayo utayakuta katika kijiji cha utandawazi?,” anahoji msomi huyo na kuendelea kusema.

“Kwa mifano hii miwili inaonyesha hali ya maisha katika kona mbalimbali za kijiji cha utandawazi ya kuwa mishahara ya watendaji wakuu wa kampuni kumi wanalipwa

mishahara minono kupita wote nchini Marekani, jumla

ya mishahara ya watendaji hao kwa

2012 ni dola za marekani bilioni 4.7 (sawa na trilioni 7.5 za kitanzania).”

“ M s h a h a r a wa watu kumi

pekee ulikuwa sawa na nusu ya

bajeti ya Tanzania kwa mwaka wa fedha

wa 2012/2013, ambayo nayo haikutekelezwa kikamilifu kutokana na kukosekana kwa fedha,” alisema mhadhiri huyo kijana.

Aliongeza mfano mwingine ni maisha ya anasa wanayoishi matajiri katika nchi zilizoendelea ilihali wanyonge wa nchi maskini wakitaabika na hata kupoteza maisha kwa kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii.

“Neno anasa maana yake ni utumiaji wa fedha katika kununua vitu vya starehe na visivyo vya lazima ambavyo mtu akivikosa hawezi kupoteza maisha.”

Kwa maana hiyo, vitu kama vipodozi, manukato, sigara, pombe na hata magari ya kutembelea ni vitu vya anasa na huwezi kulinganisha vitu na mahitaji kama dawa na vifaa vya matibabu,vitabu vya shuleni, chakula, maji, malazi yenye hadhi ya binadamu ambvyo binadamu akivikosa anaisha

Endelea Uk wa 14

Bw.Sabatho Nyamsenda, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada ya Utandawazi na athari zake kwenye Mkutano Mkuu wa 18 wa MVIWATA

KUTOKA MITANDAONI MAKALA

15Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201414

katika mateso na hata kufa, alisema.

Ndugu Sabatho aliendelea kuufafanulia mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya wanachama 2000 wa MVIWATA kuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, Nchi zote za ulimwengu wa tatu (nchi zinazoendelea) zilihitaji fedha za nyongeza kiasi cha dola bilioni 6 (Sawa na shilingi trilioni 9.6) ili kutoa elimu ya msingi kwa watoto wote, ilihali jumla ya fedha zilizotumika kununua vipodozi nchini Marekani ni dola bilioni 8 (Sawa na shilingi trilioni 12.8).Halikadhalika Nchi zinazoendelea zilihitaji nyongeza ya dola bilioni 9 (Sawa na shilingi trilioni 14.4) ili kutoa huduma ya afya ya uzazi kwa akina mama na dola bilioni 13 (Sawa na shilingi trilioni 20.8) kutoa huduma ya afya ya msingi na lishe.

“Nchi hizo maskini zilishindwa kupata fedha hizo na hivyo wanyonge kuendelea kutaabika wakati huko ulaya na Marekani mambo yalikuwa tofauti ambapo walitumia dola bilioni 11 (Sawa na shilingi trilioni 17.6) kula barafu (ice cream), dola bilioni 12 (Sawa na shilingi trilioni 19.2) kununulia manukato (Perfumes) na dola bilioni 17 (Sawa na shilingi trilioni 27.2) kununulia vyakula vya mbwa na paka.

Ameongeza kuwa jumla ya fedha zote za nyongeza kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwa nchi maskini kama yalivyotajwa katika ufafanuzi ni bilioni 40 (Sawa na shilingi trilioni 64) kiasi ambacho si kidogo ukilinganisha na dola bilioni 50 (shilingi trilioni 80) zilizotumiwa na watu wa Ulaya na Marekani kuvuta sigara au dola bilioni 105 (shilingi trilioni 168) zilizotumika kunua pombe hicho ndicho kijiji cha utandawazi kilicho na kona tofauti tofauti.

Ndugu Sabatho, anaendelea kusema kuwa wapo waishio katika kona ya matajiri penye maisha ya anasa na kuna kona ya maskini walalao njaa na wanaokufa kwa kukosa huduma na mahitaji ya msingi, ilihali wenye

nguvu ya pesa wana nguvu ya kijeshi na aghalabu huvamia kona za wanyonge na kuwachinja watawala wasiowataka kisha kupandikiza vibaraka na kupora rasilimali zenu.

Ameongeza kuwa “Wenye nguvu ya pesa ndiyo wenye teknolojia ya mawasiliano na habari na ni wao ndiyo wanaamua ni habari ipi irushwe katika kijiji, labda mgeweza kuvumilia kama maisha ya anasa wanayoishi wanakijiji wenzenu wa huko Ulaya na Marekani yangekuwa ni zao la jasho lao au rasilimali zao, lakini sivyo kuna uhusiano wa umaskini uliokithiri wa nchi za ulimwengu wa tatu na anasa za nchi tajiri.”Aidha mfumo unawafanya ninyi watu wa ulimwengu wa tatu kuwa maskini ndiyo huo huo unaowafanya wenzenu wa ulimwengu wa kwanza wawe na matajiri kwa lugha nyepesi ninyi lazima mfukarishwe ili wao wawe matajiri, mfumo huo ni katili na wa kinyonyaji unaitwa ubepari tangu karne ya 15 ulipoanza, ubepari umekua ukijibadili sura lakini damu yake imebaki ile ile ya uporaji wa rasilimali na unyonyaji wa jasho la wanyonge.

Amebainisha kuwa kati ya karne ya 15 na 19 ubepari ulijitokeza katika sura ya biashara ya utumwa na uporaji wa rasilimali uharamia Waafrika zaidi ya milioni 40 waligeuzwa bidhaa za kuuzwa na kununuliwa sokoni, walipakiwa katika meli kama dagaa na kupelekwa katika nchi za Amerika kwa ajili ya kuzalisha mashambani na migodini wakati malipo yao yalikua ni viboko na kuchinjwa mithili ya mbuzi na ndicho kilichowapa utajiri na maendeleo ulaya na Marekani ni biashara ya utumwa.

Amesema kati ya karne ya 19 na 20 ubepari ulichukua sura mpya ya ukoloni ambapo mataifa makubwa ya ulaya yaligawana bara la Afrika ili kuendelea kupora rasilimali zake bila kuingiliana. Karne ya 20 katikati miaka ya 1960 hadi karne ya 20 mwishoni miaka ya 1980 ubepari ulichukua sura mpya ya ukoloni mamboleo ambapo pamoja na kuziacha nchi za kiafrika zijitawale

mabeberu waliendelea kuzinyonya kupitia mfumo wa biashara ya kimataifa pamoja na kupandikiza watawala vibaraka.

Amesema kuwa juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa kutaifisha njia kuu za uzalishaji mali hazikufua dafu kwani ni nchi za kibeberu ndizo hupanga bei ya rasilimali na malighafi kutoka katika nchi maskini, mazao na rasilimali zenu zikanunuliwa kwa bei ya kutupa huku bidhaa zitokazo viwandani kwao zikipandishwa bei kila kukicha.

“Kuanzia mwishoni mwa karne ya 20 miaka ya 1980 hadi sasa ubepari umechukua sura mpya ya uliberali mamboleo ambalo jina jingine ni Utandawazi, hii ndiyo sura katili pengine kuliko hata biashara ya utumwa au ukoloni ambapo mabeberu wameongeza kasi ya uporaji kupitia uwekezaji na ubinafsishaji, viongozi wa nchi wanaokataa kusalimisha rasilimali zao hunyongwa au kuchinjwa na kila rasilimali ya mnyonge hata iliyo ndogo huporwa” Alisema Ndiugu Sabatho.

Akifafanua baadhi ya maswali kutoka kwa wakulima yanayohusina na sheria ya kumiliki ardhi na ufafanuzi mbalimbali unaohusiana na mkulima mdogo, wao wapo kwa ajili yao na jambo kubwa ni kuhakikisha wanashirikiana vizuri na mtandao wao wa MVIWATA vizuri katika kuwasilisha mahitaji yao na hatimae mtandao huo utawasiliana nao na kupanga namna gani ya kuwasaidia hatimae wakulima kuwa na sauti moja ya kitaifa na ulinzi wa rasilimali zao kama ardhi na mzao kwakupanga bei wao wenyewe.

Ameongeza kuwa utandawazi siyo kitu kipya bali ni mvinyo wa zamani katika chupa jipya au Joka lililo jivua gamba na kujivalisha gwanda ili kuficha sura yake halisi lakini damu yake, meno yake, mifupa yake inasumu kali, sumu tuionayo katika uporaji wa waziwazi wa rasilimali ubidhaishaji wa huduma za msingi

Inatoka uk. wa 13

KUTOKA MITANDAONI

Endelea Uk wa 20

Bunge launda kamati kuchunguza migogoro ya wakulima na wafugaji

Dodoma.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, ameunda Kamati Teule ya Bunge itakayochunguza na

kuchambua migororo ya ardhi nchini. Kamati hiyo itafanya uchambuzi wa sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo, maji na uwekezaji, kwa lengo la kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi.

Hatua hiyo imefikiwa na Spika Makinda, siku chache baada ya Bunge kuridhia kuundwa kwa kamati hiyo.Uamuzi huu, unafuatia malalamiko ya wabunge bungeni, kuhusu migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, ambayo kwa muda mrefu haijapatiwa ufumbuzi na kusababisha madhara ikiwamo mauaji.

Kwa mujibu wa Spika Makinda baada ya kamati hiyo kufanya kazi hiyo, itapeleka mapendekezo yake bungeni ili yatekelezwe na serikali kupunguza au kuondoa migogoro ya muda mrefu kati ya wakulima, wafugaji, wawekezaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Alizitaja hadidu rejea za kamati hiyo kuwa ni kuchambua sera mbalimbali zinazohusiana na matumizi ya ardhi

ili kubainisha kasoro zilizomo na kuchunguza mikakati ya utekelezaji wa sera hizo iliyowekwa na serikali.

Hadidu rejea ya pili, ni kufanya mapitio ya taarifa nyingine za kamati na tume zilizoundwa huko nyuma kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji.

Ya tatu, ni kuchambua mikakati yote ya serikali ya kusuluhisha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Hadidu rejea ya nne, ni kuchambua mikakati ya kulinda vyanzo vya maji pamoja na uharibifu wa mazingira.Ya tano, kutoa mapendekezo yatakayoondoa migogoro iliyopo na kudumisha uhusiano mzuri na utangamano kati ya wakulima na wafugaji.Hadidu rejea ya sita ni kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua za kiuajibikaji pale kasoro za utekelezaji wa kisera zimetokana na udhaifu wa kiuongozi na utendaji.Ya saba, ni mambo mengine yoyote, ambayo kamati itayaona yanafaa.

“…Kama mlivyoona hadidu za rejea na ukubwa wa tatizo lenyewe la migogoro ya ardhi, kati ya wakulima, wafugaji, hifadhi, wawekezaji na watumiaji wengine wa ardhi, na kama

Bi.Zawadi Chande , mkulima wa Mgongola, Mvomero akiongea mbele ya Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza vyanzo vya migogoro ya ardhi ilipotembelea maeneo hayo.

nilivyosema wakati wa kuhitimisha mjadala wa hoja iliyowasilishwa kwamba kamati teule itakwenda kuangalia kwa ukubwa wake suala zima la migogoro kati ya wakulima, wafugaji na mambo yanayohusu mambo ya hifadhi na vitu kama hivyo,” alisema Spika Makinda.

Alisema kazi ya kamati hiyo itakuwa kubwa na kwamba itahitaji umakini wa hali ya juu na muda wa kutosha katika kufikia mapendekezo yatakayowasilishwa Bungeni.

Hata hivyo, alisema kutokana na uharaka wa jambo lenyewe, itabidi kamati ifanye kazi hiyo kwa kuzingatia kwamba, kuchelewa kutoa taarifa yake kunaweza kukuza tatizo.

Alisema pamoja na kazi ya kamati kuwa kubwa, kanuni ya Bunge ya 121 (1) toleo la Aprili 2013, inaweka masharti kwamba, wajumbe wa kamati teule wasizidi watano.

Aliwataja wabunge aliowateua kuunda kamati na kufanya kazi hiyo kuwa ni Profesa Peter Msola (Kilolo-CCM), Jenista Mhagama (Peramiho-CCM), Magdalena Sakaya (Viti Maalumu-CUF), Joseph Selasini (Rombo-Chadema) na Christopher Ole Sendeka (Simanjiro-CCM).

Alisema katika uteuzi alioufanya, amezingatia mambo muhimu, ikiwamo uwakilishi wa vyama vilivyopo Bungeni, uelewa wa tatizo na migogoro iliyopo inayoikabili nchi, uzoefu katika masuala ya ufugaji na jinsia.

Makinda alisema wakati wabunge walipojadili hoja ya kuahirisha shughuli ya Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura linalohusu maelezo ya serikali kuhusu mgogoro kati ya wakulima na wafugaji, hifadhi, uwekezaji, waliipa kazi Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kufanya kazi mbili kuu.

KUTOKA MITANDAONI

17Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201416

KUTOKA MITANDAONI

Na Geofrey Mwakafilwa

Morogoro/kiteto. Mtandao wa Vikundi Vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), umeendela kuwa karibu na vikundi vya wanaoishi na virusi vya ukumwi (WAVIU) kama moja ya wanachama wake katika kuhakikisha wanakuwa na shughuli za kiuchumi ili kuweza kijiendeleza kimaisha.

Katika kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani inayofanyika kila Disemba mosi, MVIWATA wilaya ya Mvomero iliandaa hafla iliyowajumuisha watu wa kada mbalimbali kujikumbusha mambo muhimu juu ya janga hilo linaloitikisa dunia.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Kigugu, tarafa ya Turiani, wilayani Mvomero na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 310 wakiwemo wanawake 200 na wanaume 110 yakibeba ujumbe usemao “Tanzania bila maambukizo mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi Inawezekana.”

Kwa mujibu wa Bw. Abdalla Iddi, ambaye ni mhamasishaji wa shughuli za shirika katika maeneo hayo alisema, MVIWATA kama mdau wa maendeleo ni sehemu ya jukumu lake kuwatambua na kuwaunganisha WAVIU katika vikundi na kuwawezesha kupata elimu mbalimbali ikiwemo kuwashauri namna ya kufanya shughuli za kiuchumi pamoja na kuondoa unyanyapaa na kujinyanyapaa wenyewe.

Kupitia elimu hiyo jinsi ya kufanya shughuli za kiuchumi, MVIWATA kwa mwaka jana iliweza kuhamasisha WAVIU wapatao 75 na kuwawezesha kuanzisha shughuli za kiuchumi kupitia zao la viazi vitamu katika vikundi vinne ambavyo ni Tawa, Konde, Kigugu na shule ya msingi Kigugu zote kutoka wilaya za Morogoro vijijini na Mvomero.

Kutokana na zoezi hilo kupokelewa kwa hamasa na walengwa Bw. Iddi alisema, shirika lina matarajio makubwa ya kuwawezesha WAVIU wengi kujiunga katika vikundi na hatimaye kufikia malengo yao.

“Kwa kuwa WAVIU wengi wameona ipo faida kujiendeleza kiuchumi kupitia viazi lishe, hivyo basi ni matarajio yetu kwa msimu ujao ambao ni kuanzia mwezi wa nne hadi wa tano kuwa na hekari za viazi lishe 60 ambazo watapanda kwenye mashamba yao kupitia vikundi husika,” alisema Bw. Iddi.

Pia kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Antony Mtaka, ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, aliongelea hali ya maambukizi ya ukimwi wilayani Mvomero na kusema mbali na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kuzuia maambukizi ya ukimwi ikiwemo utoaji wa elimu, bado hali ni mbaya na hasa kwa upande wa wanawake.

Halikadhalika, Mh. Mtaka aliishukuru MVIWATA kwa kugawa mbegu za viazi lishe kwa waathirika na kutokana na hilo aliahidi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero itatoa mashine

moja ya kusindika kwa kikundi cha Mapambano cha Kigugu.

Kwenye risala yao kwa mgeni rasmi, WAVIU hao walikumbushana kuwa ni vyema wakaikubali hali hiyo na kujikubali wenyewe bila kusahau kuwa uwazi juu ya hali zao mbele ya jamii ni muhimu ili kuzuia maambukizi kwa watu wengine.

Maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi duniani kwa Wilaya ya Mvomero yalitanguliwa na siku moja ya upimaji wa afya kwa washiriki katika Kituo cha Afya cha Chazi na shule ya msingi Kigugu na hivyo kufanya idadi ya waliopima kwa siku hizo mbili kufikia 800 wanawake wakiwa 503 na wanaume 297.

Maadhimisho mengine wilayani kiteto.

Nako huko Mkoani Manyara, wilaya ya Kiteto katika kijiji cha Engasiro, MVIWATA kwa ushirikiano na wanachama wake wa vikundi vya watu waishio na virusi vya Ukimwi waliadhimisha siku hiyo wakiwa na ujumbe kwa jamii husika kuwa wao pia wanathamani na mchango mkubwa katika jamii na hivyo

MVIWATA yaendelea na juhudi za kuwawezesha WAVIU kiuchumi

Baadhi ya washiriki wa maadhimisho Siku ya UKIMWI duniani wakifanya usajiri, wilayani Kiteto

KUTOKA MITANDAONI

Changamoto za umiliki wa Ardhi kwa Wanawake zabainishwa

Na Jacueline Massawe

Shirika la Oxfam limebainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake

nchini katika umiliki wa ardhi hali inayowafanya wazidi kuonekana kuwa bado hawana haki ya kumiliki ardhi pamoja ilihali wao ni wazalishaji wakuu.

Changamoto hizo zilibainishwa na Bw. Marc Wegerif, Mratibu wa Kampeni za Haki za Kiuchumi kutoka Oxfam ,alipokuwa akiendesha warsha iliyojumuisha wakulima na wafugaji toka nchi ya Kenya, Uganda na Tanzania wakiwemo pia wanachama wa MVIWATA.

Warsha hiyo iliyozungumzia juu ya Mapambano ya kudai maliasili katika Muktadha wa “Uporaji wa Ardhi” ilifanyika wakati wa tamasha la kumi na moja la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Kwa mujibu wa Bw. Wegerif, changamoto hizo zinazowakabili wanawake zinachangiwa na wimbi kubwa la wawekezaji wanaokuja Afrika kwa ajili ya kuwekeza katika ardhi kwa madhumuni ya kupata nishati mbadala pamoja na kulima

mazao ya chakula na kufanya shughuli nyingine ikiwemo za utalii, madini, viwanda, misitu na ufugaji.

Akibainisha changamoto hizo Bw. Wegerif alisema, wanawake wanazalisha asilimia 60-80 ya chakula katika bara la Afrika, lakini bado wanakumbwa na vikwazo lukuki katika kumiliki ardhi tofauti na wanaume.

Kutokana na utafiti uliofanywa inasadikiwa kuwa wanawake hawa wanamiliki asilimia moja ya ardhi ya kusajiliwa wakati huo huo wanapata asilimia 10 ya mikopo kwa wakulima wadogo jambo linalorudisha nyuma maendeleo yao kutokana na ukweli kuwa mikopo hiyo ni kidogo mno kwa shughuli za ujariamali.

Lakini mbali na kuwa wanapokea asilimia 7 ya huduma za ugani kitendo ambacho kinamuongezea mzigo wa ziada wakati wa uzalishaji na ikizingatiwa kuwa mwanamke ndiye mzalishaji mkuu anayegemewa kuanzia ngazi ya kaya hadi ya kitaifa bado pia wana sauti ndogo katika maamuzi ya nchi na hata wakiongea mawazo yao hayathaminiwi.

Changamoto nyingine ni pamoja na

kuwa wanawake wana haki hafifu linapokuja suala la fidia, wanawake hupata fidia kidogo sana au kukosa kabisa na fidia yote huenda kwa mume na mwisho mwanamke hubaki akitangatanga pasipokujua mstakabali wa maisha yake.

Hali kadhalika hata wakati mwekezaji anakuja wanawake hawahusishwi katika kufanya maamuzi mbali na hilo hawapati kazi za kufanya katika maeneo ya wawekezaji hao kwani asilimia kubwa ya vibarua ni wanaume hata kama wanawake wakipata kazi basi zinakuwa kazi za vibarua zenye malipo madogo sana tofauti na angekuwa na ardhi yake apangilie jinsi ya kuitumia ili kupata kipato.

Mbali na changamoto hizo alizozibainisha Bw. Wegerif, wakulima hao na wafugaji walipata nafasi ya kuelezea changamoto nyingine wanazokumbana nazo katika kumiliki ardhi.

Kwa upande wake Bi. Sekelaga Sandube mwanachama wa Mviwata kutoka kijiji cha Kapunga wilaya ya mbalali Mbeya alisema kwa miaka saba sasa wananyanyasika katika kijiji chao baada ya mwekezaji kuvunja kaya 18 ili kujenga kiwanja chake cha ndege.

“Mbali na kubomoa kaya hizo wanaume walikimbia familia zao na hivyo kina mama na watoto huishi chini ya miti wakinyeshewa na mvua kwani hata mazao waliyokuwa wamehifadhi ndani ya nyumba zao yalizolewa pamoja na kifusi wakati nyumba hizo zikibomolewa,” alisema Bi.Sandube kwa masikitiko.

Naye Bi. Antonia Edward, mwanachama wa Mviwata kutoka kijiji cha Namabengwa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, alisema viongozi wengi wa Serikali kwa sasa wameingiwa tamaa ya kumiliki ardhi

Maadhimiisho ya miaka 20 ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) jijini Dar es Salaam Endelea Uk wa 20Endelea Uk wa 20

KUTOKA MITANDAONI

19Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201418

Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mkindo, Ndugu Moses Temi akiwapa maelekezo wahitimu wa mafunzo ya Mashamba darasa wilayani Mvomero hivi karibuni

Afisa Ushawishi na Utetezi, Bw.Thomas Laiser akiongea kwenye kongamano la Mtandao wa Jinsia lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wawezeshaji kutoka shirika la TAMADI Bw.Rishikanta wa tatu kushoto na mkalimani wake wakifafanua jambo kwa washiriki wa semina iliyohusu Utali Vijijini.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa kuhitimisha mradi wa Chungu cha Dhahabu, Manyara.

Benjamin Nkomolla, Afisa asasi za fedha wa MVIWATA akiwapa mafunzo viongozi wa moja ya SACCOS-Ludewa.

Mratibu wa MVIWATA Manyara, Bw Martin Pius akiwasilisha mada ya Uongozi kwa viongozi wapya Ngazi ya Kati Morogoro.

KAMERA YA MVIWaTa MITANDAONI

Promota wa MVIWATA, wilayani Kiteto, Bw. Apollo Chamwela akiwasilisha kazi ya kikundi kwenye semina ya Shirikisho la Vyama vya Wakulima Afrika Mashariki lililofanyika Bujumbura, Burundi.

Viongozi wa MVIWATA na wajumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja siku ya uzinduzi wa mradi wa FACT mjini Arusha.

Wajumbe wa Bodi za MVIWATA na TFCG wakiwa kwenye mjadala na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi kuhusu shughuli za DADPS.

Vikundi vya wakulima na watumishi wa Diocese ya Karagwe wakiwa kwenye picha ya pamoja walipotembelea Ofisi za MVIWATA Morogoro ili kubadilishana uzoefu.

Wahitimu wa mafunzo ya mashamba darasa kutoka Chuo cha Kilimo Mkindo, Mvomero wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Wanawake viongozi wa MVIWATA walionyakua Tunzo ya Uongozi Bora kwenye shindano la uhitimishaji wa mradi wa Chungu cha Dhahabu, mkoani Manyara.

KAMERA KAMERA

21Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201420

Inatoka uk. wa 17

Inatoka uk. wa 14

Inatoka uk. wa 16

washiriki walikubaliana kuwa Katiba iandikwe kuwa ni marufuku kuuza ardhi yoyote katika nchi pia itamke kuwa mali ya kifamilia mwanaume hana mamlaka ya kuuza bila idhini ya mwenzi wake (mkewe).

“Mikataba yote ya wawekezaji ipitiwe upya na umiliki wake uwe wa muda mfupi na ulioshirikishi na wazi kwa wanakijiji wa eneo husika. Ardhi yote ambayo haitumiki kwa sasa irudishwe kwa wananchi ili waweze kuimiliki kwa ajili ya uzalishaji na hasa wanawake,” alisema Bi.Matemu.

Hali kadhalika katiba itaje wazi kuwa kila mtu ana haki ya kumiliki ardhi na maliasili zilizopo chini pasipokuangalia jinsia na kuwa Serikali ya kijiji ihakikishe inatoa hatimiliki za kimila ili kuwezesha kila mwanakijiji kuwa na hatimiliki ya ardhi anayoitumia.

Pia katiba itamke kuwa wakati wa uandikaji wa mikataba ya uwekezaji wanawake washirikishwe kwa asilimia 75 na viongozi wasihusike tena kunadi ardhi ya Tanzania.

Laiser, Afisa Sera na utetezi Mviwata alisema tabu na manyanyaso yote yanayowakumba kina mama na raia wengine katika kumiliki ardhi ikiwemo migogoro mbalimbali yanatokana na serikali kushindwa kuwa wakala mzuri kwa wananchi wake pamoja na maliasili zinazowazunguka na badala yake wamevaa jukumu la kuwa mawakala wa wawekezaji.

Akiendesha mjadala wa nini kifanyike kwenye katiba mpya kupitia rasimu inayojadaliwa sasa ili kumwezesha mwanamke kuwa na umiliki katika ardhi, Bi. Zenais Matemu, Afisa ushawishi na haki za ardhi kwa wanawake ,aliwaambia washiriki wa warsha hiyo ni vyema wakawa imara katika kutetea haki zao kwenye ardhi.

Alisema mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi kama mojawapo ya rasilimali kwani inampatia nafasi ya kuendelea kiuchumi pamoja na kuendeleza familia yake kupitia uzalishaji wa chakula na mazao mengine anayolima kwa ajili ya kuuza.Na hivyo basi kwa kauli moja

kimabavu na hivyo kuwafanya wanawake baada ya kufikiri upatikanaji wa soko la mazao yake na kuilisha famila yake kama zamani anabaki akiwaza jinsi ya kupata fedha ya kumlipa mwekezaji ili walau alime chakula cha familia tu.

“Tumekuwa tukilima katika ardhi yetu ya kijiji kwa muda mrefu lakini baadhi ya viongozi kutoka kijiji jirani cha mabwegere walimega ardhi yetu na hivyo kutufanya kupoteza maeneo ya kulima na kilichopo kwa sasa tunakodi ardhi kwa wawekezaji kwa kila heka tunalipa 70,000,” alisema Bi. Edward.

Aliongeza kuwa mbali na kulipia gharama hiyo ya kukodi shamba lakini pia baada ya kuvuna wanapaswa kumlipa mwekezaji huyo gunia moja la zao husika na kama itatokea mvua haikunyesha mbali na kupoteza 70,000 ya kukodi shamba bali pia mwekezaji humpangia mkulima idadi ya madebe anayopaswa kumlipa. Kwa upande wake Bw. Thomasi

KUTOKA MITANDAONI

Wakulima Mviwata wapatiwa elimu ya vifungashio

Na Jacueline Massawe

Wanachama wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA)

toka Mikoa kumi ya Tanzania bara na visiwani wamepatiwa elimu kuhusiana na vifungashio vya bidhaa wanazouza kama njia mojawapo ya kuwawezesha kuuza bidhaa zenye ubora na zinazokubalika sokoni.

Bw. Nickson Elly Afisa Masoko toka Mviwata alisema shirika limeona kuna haja ya kuwapatia elimu hiyo ya vifungashio wanachama wake baada ya kuona baadhi yao wamekuwa wakikosa masoko bora na endelevu na hivyo kushindwa kufikia malengo yao.

“Wapo wakulima ambao ni

wazalishaji wazuri sana lakini wamekuwa wakikosa masoko hata katika mikoa yao kutokana na bidhaa zao kutokufungashwa na kukosa lebo na hivyo kuwafanya kukosa soko lenye ushindani,” alisema Bw. Elly.

Elimu hiyo ilitolewa na Bi. Joan Steven Afisa kutoka shirika la maendeleo la viwanda vidogovidogo (SIDO) anayehusika na uendelezaji teknolojia ya chakula. Bi Steven aliwaambia wakulima kuwa ufungashaji unasaida bidhaa kudumu kwa muda mrefu kwa ajili ya matumizi ya baadae na kuleta mvuto kwa mtumiaji au mteja.

Akitaja faida zitokanazo na ufungashaji wa bidhaa Bi. Steven alisema, kifungashio kinatoa taarifa

za msingi ikiwemo kuonyesha aina ya bidhaa, imetoka wapi, tarehe iliyofungashwa, tarehe inayoharibika, jina la mfungashaji ama kikundi husika, anwani, barua pepe ama namba za simu.

Faida nyingine ni pamoja na kuzuia vijidudu kutoingia kwenye bidhaa, kumrahisishia muuzaji ubebaji na pia husaidia kuhifadhi bidhaa kwa muda mrefu.

Mbali na faida hizo Bi. Steven aliwaambia wakulima hao kuwa ili bidhaa yoyote itangazike na kuaminiwa na walaji inapaswa kuwa na nembo ya Shirika la Ubora wa Viwango Tanzania (TBS).

“Nembo ya ubora ya shirika la viwango inapaswa kuwepo katika kila bidhaa kwani inazingatia vitu vingi tangu bidhaa inapoanza kutengenezwa, anayetengeneza bidhaa hiyo, sehemu ilipotengenezwa, jinsi ilivyofungashwa pamoja na mawasiliano”.

Aliongeza pia nembo ya ubora inamhakikishia mlaji usalama wa afya na hali kadhalika bidhaa kupata soko la ndani na nje ya nchi.

Bi. Steven aliwasisitiza wakulima hao kuzingatia kanuni na uzalishaji bora wa bidhaa ikiwemo usafi na usalama kuanzia sehemu ya eneo la kuzalishia bidhaa, vifaa vya kufungashia pamoja na hali ya afya ya mzalishaji, kupata leseni ya kuzalisha bidhaa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) pamoja na usajili wa sehemu bidhaa inapozalishiwa. Pia kuhakikisha bidhaa inakuwa na namba zinazotambulisha bidhaa ni ya nchi gani au Mkoa upi, nani mtengenezaji, bei ya bidhaa husika pamoja na aina ya bidhaa.

Endelea Uk wa 23Wanachama wa MVIWATA kwenye maonyesho ya Nanenane, Morogoro. Elimu ya kufungasha mazao yanaongeza thamani bidhaa za wakulima

na uvamizi wa kijeshi kwa Nchi zinazosita kusalimisha rasilimali zake kama ilivyotokea Iraq mwaka 2003 na Libya mwaka 2011.

Amehitimisha kwa kusema kuwa uporaji, uonezi na ukatili huo hauwezi kutokea katika kijiji na hasa baina ya wanakijiji wenyewe, mambo ambayo mkubwa kumtafuna mdogo, mwenye nguvu kumwonea mnyonge hutokea porini baina ya wanyama sio binadamu utandawazi ni unyama kama baadhi ya wana harakati mfano Profesa Chachage aliuita ni mfumo wa Utanda-wizi. Alihitimisha kwa kuwataka wakulima washikane kwa kuwa na umoja maana mkombozi wa mkulima ni mkulima mwenyewe!

wanapaswa kuthaminiwa na kusikilizwa.

Mbali na ujumbe huo, baadhi ya WAVIU hao walishukuru shirika la MVIWATA kwa jitihada wanazofanya na zaidi kuwa nao karibu kupitia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi.Pia waliomba shirika na hasa kupitia watendaji wake katika maeneo hayo wasiache kuwasisitiza WAVIU kujiunga na MVIWATA ili kuweza kupata mbinu mbalimbali za kuboresha hali zao za kiuchumi na hatua za kimaendeleo na kuachana na dhana iliyoenea maeneo mengine kuwa “WAVIU hawawezi.”Hata hivyo watu hao wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) ambao ni wanachama wa MVIWATA hawakuacha kuiomba serikali

MVIWATA yaendelea... kupeleka huduma za upimaji mara kwa mara maeneo ya vijijini ili watu waweze kupima na kuzitambua afya zao.“Imekuwa vigumu sana sisi kufikiwa na huduma hii ya upimaji wa hiari mara kwa mara labda mpaka mtu aende hospitali tena kwa umbali mrefu au hadi wakati wa ujauzito, lakini kama serikali ingekuwa inatoa huduma hii mara kwa mara nadhani ingetuwezesha kutambua afya zetu na kuweza kuishi kwa kufuata kanuni bora za kiafya,” alishauri mmoja wa WAVIU hao.

MVIWATA imedhamiria kuendelea kufanya kazi pamoja na WAVIU kupitia shughuli zake za kiuchumi ikiwemo kujenga uelewa wa wakulima juu ya VVU/UKIMWI kama sehemu ya moja ya shughuli za masuala mtambuka kama ilivyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa shirika.

Dunia ni Kijiji...

Changamoto za umiliki...

KUTOKA MITANDAONI

23Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201422

Endelea Uk wa 23

Wakulima Wilayani Mvomero wawatembelea wadau kuzitambua fursaNa Jacueline Massawe

Wakulima toka wilaya ya Mvomero tarafa ya Turiani wamefanya

Ziara ya siku mbili Mjini Morogoro ili kuweza kutambua fursa zinazowazunguka kama njia mojawapo ya kujiendeleza katika sekta ya kilimo.

Ziara hiyo ni zao la mafunzo ya siku sita yaliyoendeshwa wilayani Mvomero na Bw. Abdalla Iddi Mkulima mwezeshaji wa MVIWATA yaliyokuwa na lengo la kuamsha uwelewa wa wakulima ili kuweza kutambua fursa zinazowazunguka.

Mbali na kutaja lengo kuu la ziara hiyo ambayo ni kujenga mahusiano na mawasiliano na wadau na kuweza kutambua fursa zilizopo na namna ya kuzitumia, Bw. Iddi alitaja pia maeneo makuu matano ambayo walimbelea ikiwa ni pamoja na MVIWATA Makao Makuu, Ofisi ya MVIWATA Mkoa, Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Taasisi ya Kifedha (CRDB ), na Makampuni ya wakala wa Pembejeo.

Akizungumzia matunda ya ziara

yao, mmoja wa wakulima hao Bi. Rose Lazaro toka kijiji cha Kigungu kata ya Songaji alisema, wamepata mapokezi mazuri toka MVIWATA Makao Makuu pamoja na kuelezewa fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia ikiwemo kuwatumia wataalamu waliopo Ofisini hapo muda wote ikiwemo rasilimali nyingine za shirika pamoja na kupata ushauri wa masula mbalimbali yanayowatatiza.

Aidha, kwa upande wa Ofisi ya MVIWATA Mkoa, waliweza kubaini shughuli zifanywazo ikiwemo jinsi wakulima wadogo wanavyoweza kufaidika na mfuko wa mkopo wa Mkoa baada ya SACCOS zao kuwa mwanachama katika chombo hicho cha MOMFISECO (Morogoro and Mvomero District Financial and Enterprises Cooperative) baada ya kukidhi vigezo na hivyo kuendeleza shughuli zao za kilimo.

Na kwa upande wa fursa zilizopo katika Taasisi ya kifedha ya CRDB, ambako wakulima hao walitembelea, Bw. Charles Danieli mkulima toka kijiji cha Lukengo kata ya Mtibwa alifafanua ni pamoja na elimu kwa wazalishaji wadogo juu ya matumizi ya fedha na umuhimu wa mikopo.

Mmoja wa wakulima wa Mvomero akitambulisha wengine alioambatana nao katika ziara ya kutambua fursa mbele ya Mkurugenzi wa MVIWATA

Kupitia Meneja mahusiano mwandamizi wa CRDB Bw. Boniface Shija aliwaambia taasisi hiyo ipo tayari kwenda katika maeneo yao kutoa elimu ya ujasiriamali pamoja na kutoa mikopo ili kuwawezesha kiutimiza malengo yao.

Kwa upande wa Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Mvomero wakulima hao walikutana na wakuu wa vitengo mbalimbali kama vile kitengo cha masuala ya pembejeo, mfuko wa pembejeo na kitengo cha mambo ya umwagiliaji.

wakuu hao wa vitengo waliweza kuwabainishia fursa zilizopo katika ofisi ya Halmashauri na hasa kuhusu mfuko wa pembejeo na hasa kwenye masuala ya udhamini wa pembejeo na hasa matrekta na namna ya upatikanaji wake.

Akisifia juhudi walizofanya wakulima hao Mkurugenzi wa Shirika la MVIWATA, Bw. Stephen Ruvuga, alisema wengi wa wakulima nchini wamekuwa na dhana potofu kuwa kamwe hawawezi kufanya shughuli za kilimo kwa kutumia fedha zao za mfukoni bila kutegemea misaada na kusubiri wengine wafanye kwa niaba yao.

“ Lakini hii imekuwa tofauti kwenu kukubali kutumia gharama zenu wenyewe ili kufikia malengo yenu, kwa hilo nawapongeza sana.”

Aliongeza kuwa uamuzi waliouchukua wakulima hao wa Mvomero wa kujigharamia kwa siku tatu mjini Morogoro ni mfano bora wa kuigwa na wakulima wengine nchini kama watakuwa na nia ya kupiga hatua kwa kutekeleza maamuzi yao kivitendo.

“Inawapasa kuungana na kuwa na sauti moja katika kutetea maslahi yenu kiuchumi na kijamii wengi badala ya kulalamika kuwa sisi

vifungashio...Inatoka uk. wa 21

Inatoka uk. wa 22

Wakizungumzia umuhimu wa elimu hiyo wakulima walikiri kuwa imekuwa msaada mkubwa sana kwao kwani wamekuwa wakiuza bidhaa zao kiholela bila kuwa na vifungashio na hivyo kukosa soko lenye uhakika tofauti na wakulima wenzao ambao wamekuwa wakitumia vifungashio.

“ Mwanzoni nilikuwa nafungasha bidhaa zangu za asali kirejareja kwenye madumu yenye ujazo tofauti kuanzia lita moja hadi lita tano na wakati mwingine namwekea mteja hata kwenye dumu la lita 20 kutokana na hitaji lake na nikawa najipa moyo kuwa nafaidika lakini elimu ya leo imenifungua ufahamu na kujua naweza kupata soko hata nje ya nchi kama nikiwa na lebo yenye mawasiliano yangu kamili na hivyo kufanya biashara yangu kuwa endelevu,” alisema Bi. Anasitanzia Robert toka Shinyanga.

Mwajuma Mwiyoha toka Dodoma anasema, pamoja na kufungasha bidhaa zake lakini anakiri kuwa hajafikia kiwango cha ubora unaotakiwa kama walivyofundishwa na aliahidi kwenda kutumia vikao vya serikali za vijiji kuwapa wakulima wenzake kwenye Mtandao elimu hiyo ili kulifikia soko la uhakika.

Kwa upande wake Ameli Ngilangwa toka Iringa Njombe anasema hajawi fungusha bidhaa zake hata siku moja na amekuwa akiwaona wakulima wenzake toka mikoa ya jirani wanaofungasha bidhaa kama wanapoteza muda.

“Kwa kweli siku zote nilikuwa

wakulima tunadharaulika kila mahali na hivyo basi hatuna haki kama yalivyo makundi mengine acha tuendelee kugandamizwa,” alisema Bw. Ruvuga.

Mbali na kuikemea dhana hiyo potofu, aliwahimiza wakulima hao kuendelea kutumia rasilimali watu ambao ni wataalamu walio ajiriwa na shirika katika shughuli zao za kila siku za kilimo ikiwemo kupata taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo kwani hilo ndio jukumu lao kuwahudumia wakulima katika mitandao yote ya ngazi za kati na MVIWATA Taifa.

Akielezea hofu yake kuhusiana na sekta ya kilimo alisema, kwa sasa nchi imepoteza muelekeo haijulikani kilimo kinaenda wapi na hii ni kutokana na fikra potofu kuwa kilimo cha mkono hakifai kwa sasa na wakulima wadogo hawawezi kuendeleza kilimo na hivyo serikali kuamua kuleta wawekezaji.

Bw. Ruvuga alisema kauli hii imekuwa ni moja kati ya kichocheo kikubwa cha migogoro ya ardhi nchini baina ya wakulima na wawekezaji kwa madai kuwa kupitia kilimo hicho cha mkono mkulima mdogo hawezi kuzalisha kibiashara na kusahau kuwa tangu enzi za ukoloni wakulima wadogo ndio wamekuwa wazalishaji wakuu nchini.

Akihitimisha ziara hiyo ya siku mbili Bw. Ruvuga aliwaasa wakulima hao kutumia vizuri ushauri waliopewa maeneo yote waliyozungukia pamoja na kuwaambia kuwa hatua waliyoianza ya kutafuta fursa isiishie hapo na kamwe wasikubali kukatishwa tamaa na kauli za watu mbalimbali kikubwa ni kuwaonyesha kuwa wanaweza kwa sauti yao ya pamoja kwani kukubali kudharaulika ndio mwanzo wa kukatisha ndoto zao za mafanikio katika sekta ya kilimo.

nikiwaona wakulima wenzangu wanaofungasha bidhaa zao kama hawana kazi ya kufanya zaidi ya kupoteza muda wao, lakini elimu niliyoipata sitoitumia peke yangu kwani nimeona ina faida kubwa kwa wakulima wenzangu katika mtandao na hivyo nimeamua kuchukua mfano wa bidhaa iliyofungashwa ili kuwaonyesha mfano na mapema tuanze kufungasha bidhaa zetu”.Mkulima mwingine Bi. Oliva Mwenda kutoka Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro alisema wakulima wengi wamekuwa wakifungasha bidhaa kiholela holela na pindi soko linapokosekana wanabaki kujuta na kulaumu kumbe kosa si la mlaji bali ni la muuzaji.

“ Tumekuwa tukifungasha bidhaa zetu katika hali zisizovutia ikiwemo kuweka juisi, karanga, asali na bidhaa nyingine kwenye machupa ya uhai yaliyokwisha tumika hali inayochangia hata mlaji kuona kuwa bidhaa hizo zimetengenzwa katika hali ya uchafu na hivyo kukosa soko la uhakika na endelevu lakini elimu hii tuliyopatiwa kupitia Mviwata itatusaidia wakulima wadogo kuendelea kujitangaza kwa kutumia vifungashio vyenye lebo na alama ya shirika la viwango hali iatakayopelekea bidhaa zetu kutambulika hata nchi jirani na kuzidi kukua kiuchumi”.

Kwa upande wake Bi. Marcelina Charles kutoka Morogoro aliwaasa wakulima hao kuitumia elimu waliyopewa vizuri na kwa vitendo kwani kwenda kinyume na makusudi ya elimu hiyo ni kuchezea rasilimali za shirika.

Akihitimisha mafunzo hayo Bw. Nickson Elly aliwasisistiza wakulima wanaporudi mikoani mwao ni vyema wakatembelea mashirika ya SIDO ili waweze kujifunza zaidi na kufanikisha lengo ambalo Mviwata limekusudia wakati wa utolewaji wa elimu hii halikadhalika kuwapa wenzao elimu hii.

Wakulima Mvomero...

KUTOKA MITANDAONI KUTOKA MITANDAONI

25Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201424

Upotevu mazao baada ya mavuno unadhoofisha kipato cha mkulima

Na Jacueline Massawe

arusha/kilimanjaro. Wakulima wa Kilimanjaro na Arusha wamebainisha

sababu mbalimbali zinazopelekea kuwepo na upotevu wa chakula baada ya mavuno hali inayosababisha kutokuwa na uhakika na usalama wa chakula na kutokuwa na kipato kizuri chenye faida kulingana na gharama za uzalishaji.

Wakulima hao kutoka wilaya tatu ambazo ni Simanjiro, Hai na Monduli, waliyasema hayo walipokuwa wakifanya mashauriano na wataalamu kutoka MVIWATA (maafisa ugani) ambao wanasimamia mradi wa SAUTI YA MKULIMA unaotekelezwa kwa ubia kati ya MVIWATA na shirika la TRIAS kwa ufadhili wa Jumuia ya Ulaya.

Akizitaja sababu kuu nne zinazopelekea wakulima wengi kupoteza sehemu ya mavuno yao, Bw. Eliud Akyoo, Afisa ugani

wa MVIWATA kutoka wilaya ya Monduli alisema, upotevu wa kwanza unafanyika wakati wa uvunaji wa mazao hayo hadi yanapofikishwa nyumbani na kutenganishwa mazao na makapi. Upotevu wa pili unatokea wakati wa kuhifadhi kulingana na vifaa vinavyotumika kuhifadhia hata kuchangia mazao hayo kuliwa na wadudu na pia mahali mazao hayo yanapotunzwa kwani mengine hunyeshewa na mvua na kuharibika.

Wakati wa uuzaji ni sababu ya tatu na hasa mnunuzi anapomlazimisha muuzaji ampimie mazao hayo kwa kipimo kisicho halali pamoja na bei anayoitaka yeye.

Na sababu ya nne matumizi na uuzaji holela wa mazao hayo kwa ajili ya kufanya shughuli zisizo na umuhimu kama vile sherehe za kimila na unywaji wa pombe.

Wakulima hao walisema sababu kubwa inayochangia upotevu wa mazao na kutokuwa na

uhakika na usalama wa chakula baada ya kuvuna mazao yao ya mpunga, mahindi na maharage ni kukosekana kwa soko la uhakika la mazao yao hali inayochangia kuamua kuyauza mazao hayo shambani tena kwa bei ya hasara kupitia madalali.

Kuvuna mazao kabla ya wakati kwani mazao yanakuwa hayajakomaa na hivyo kutokuwa na ujazo mzuri unaoshauriwa kitaalamu na pia kuchelewa kuvuna kwa wakati muafaka na hivyo kupelekea mazao hayo kukaa shambani kwa muda mrefu na hatimaye kuliwa na wadudu pamoja na wanyama.

Kwa upande wake, Bw. Deonard Laiser, Afisa Ugani toka wilaya ya Simanjiro, alisema sababu nyingine ni kutokana nakukosekana nguvu kazi ya kutosha wakati wa uvunaji kwa kuwa wakulima wengi wamekuwa wakitumia wanafamilia kuvuna na sio kutafuta vibarua.

Sababu nyingine ni kukosekana kwa vifaa bora vya kuhifadhia mazao hayo kwani wengi wao huhifadhi kwenye mifuko duni ya viloba, juu ya dari ama pembeni ya jiko pasipo kuweka dawa mazao hayo hali inayochangia mazao hayo kushambuliwa na wadudu waharibifu wa mazao.

Alisema hali hiyo ya kutokuwa na mbinu za kitaalamu za kuhifadhi mazao inatokana na ukosefu wa elimu kwani kiutaalamu wanapaswa kuhifadhi katika pipa au kwa kutumia stakabadhi ghalani ambapo mazao hayo yanaweza kukaa hata kwa miaka 15.

Bw. Laiser aliongeza sababu nyingine iliyotajwa na wakulima hao kuwa ni wakati wa usafirishaji kwani mazao mengi yamekuwa

Mtumishi wa MVIWATA Bw.Godfrey Kabuka akiwa kwenye mafunzo ya mradi wa Sauti ya Mkulima jijini Arusha hivi karibuni Endelea Uk wa 27

MVIWATA yashirikiana na TAMADI kufufua mradi wa Utalii vijijini

Na: Al-amani Mutarubukwa

Kwa kushirikiana na shirika la kifaransa linalojukana kama TAMADI, Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) imeibua upya mradi wa Utalii vijijini ambao unalenga kuwaongezea kipato wakulima wanao wapokea wageni au watalii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, kwenye kikao cha wadau hapa Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Ndugu Stephen Ruvuga alisema mpango huu ni fursa ya kuwakutanisha wageni kutoka mataifa mbalimbali na wakulima na kujifunza tamaduni za kitanzania.

“Ni fursa ya kubadilishana uzoefu wa mila na desturi kutoka nchi mbalimbali, na kutembelea maeneo yetu na kufanya yale tunayoyafanya sisi kila siku katika jamii zetu,” alisema.

Aliongeza kuwa mbali na mradi huu kukuza mahusiano bora baina ya Tanzania na mataifa mengine, lakini pia wageni hao watapata nafasi ya kuangalia vivutio asilia vinavyowazunguka wazawa hao ikiwemo aina za mifugo ya majumbani pamoja na shughuli wanazofanya kila siku.

Pia utunzaji wa mazingira, pamoja na bunifu/sanaa wanazotengeneza wenyeji kwenye maeneo yao ya asili, kazi ambazo ni utambulisho wa makabila au jamii fulani hapa nchini kama vile nyumba za tembe mkoani Dodoma, vyakula mahsusi kwa jamii flani na hata swala la mavazi.

Kwa upande wake kiongozi wa mradi huu wa TAMADI kutoka nchini Ufaransa, Bi. Veronique Dave alisema, mradi huu wamekuwa wakiutekeleza katika nchi nyingine za kiafrika kama vile

Mali, Madagaska, India na nchi za Magharibi mwa jangwa la sahara (western sahara).

Alifafanua kuwa katika maeneo yote hayo, huwa wanatumia usafiri wa ndani wa kawaida au kijamii wa nchi husika (mfano, daladala na bodaboda) na pia hulala kwenye nyumba za wazawa na wakati huo huo wazawa hutakiwa kuendelea kuishi maisha yao halisia ya kila siku kwa kupitia tamaduni zao na mazingira husika bila kuigiza au kuwafurahisha wageni.

Na hivyo basi alisema na kwa Tanzania mradi utatekelezwa kwa jinsi hiyo hiyo bila kuharibu wala kuathiri tamaduni za jamii itakayo wapokea wageni hao ambao hutoka nchi mbalimbali kutoka bara la Ulaya, Amerika na kwingineko.

Kwa upande wa malipo kiongozi wa msafara, mkalimani, jamii au familia zitakazowapokea wageni hao, mashirika pamoja na waratibu wa Taifa husika hulipwa kiasi cha fedha kulingana na mgawanyiko wa huduma zao.

Hata hivyo Bi. Dave alihusia ni vyema kama mradi huu wa utalii vijijini ukachukuliwa kama chanzo cha ziada cha kuziniingizia mapato familia, shirika na wadau wengine katika maeneo husika, japokuwa msistizo ni kuona faida inayopatikana inatumika katika kuendeleza shughuli za kimaendeleo katika jamii.

Kupitia mradi huu baadhi ya wakulima kutoka maeneo husika ambao ni wanachama wa MVIWATA wameweza kupatiwa mafunzo mbalimbali na hasa jinsi ya uendeshaji wa shughuli hiyo ya utalii vijijini.

Aina za mafunzo hayo ni pamoja na maandalizi ya aina ya vyakula ambavyo ni asilia kulingana na jamii

ya eneo husika, malazi, huduma ya kwanza, elimu kuhusiana na utambuzi wa mimea au miti ya aina mbalimbali elimu iliyotolewa na watu wa misitu.

Halikadhalika jinsi ya kuweza kustahimili na kuhudumia idadi kubwa ya watalii kwa makundi yao ikiwa ni pamoja na kufahamu tabia na tamaduni zao na jinsi gani zinavyoweza kuingiliana na za kwetu.

Mmoja kati ya wakulima toka familia pokezi za wageni hao alisema mradi huu utasaidia kuchangia kipato katika familia zao kuliko kipindi cha nyuma walipokuwa wakitegemea chanzo kimoja cha mapato.

“Mradi huu umekuja wakati mzuri sana, sisi kama wakulima tumekuwa tukitegemea kilimo kwa muda mrefu kama chanzo kikuu cha mapato kuendesha maisha yetu, lakini kupitia mradi huu tumeambiwa jamii zitakazokaa na wageni hawa zitakuwa zikipata kiasi fulani cha fedha kutoka kwenye mradi huo,” alisema Bw. Joseph Kwakega.

Naye Bw. Haji Husi Haji kutoka Zanzibar alisema mradi huu ni wa kipekee kwani mbali na shughuli nyingine lakini unawaleta pamoja watu toka mataifa mbalimbali kwa lengo la kujifunza baina yao maisha yao ya kila siku.

Tangu uzinduzi wa mradi huu mnamo mwezi Februari mwaka huu, wageni kutoka ughaibuni wamekuwa wakitembelea si tu kwenye mbuga za wanyama, bali pia wanazunguka na kuishi kwenye vijiji vya wakulima wa miji ya Morogoro (Tchenzima), Dodoma (Chamkoroma), Babati (Majengo na Kashi), Moshi (Shiri -mgungani na Shiri-njoro), Lushoto (Kwekanga) na huko Zanzibar walifika kijiji cha Mpapa.

KUTOKA MITANDAONIKUTOKA MITANDAONI

27Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201426

UTALII VIJIJINI

Mgeni akipata huduma ya tiba ya asili kijijini Kwekanga.

Kijana akiuza vikapu kijijini kwekanga. Kazi za mikono ni moja ya vivutio vya kitalii

Watumishi wa TAMADI na MVIWATA wakifurahia vyakula vya asili na wenyeji kwenye moja ya vijiji vya mradi.

Ukamuaji wa juisi ya miwa kwa teknolojia ya kienyeji kijijini Kwalei, Tanga

Paa lililoezekwa kwa mifuniko ya pipa. Ubunifu kama huu huvutia watalii.

Watumishi wa TAMADI wakiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wao MVIWATA walipotembelea mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.

KIMATAIFA

AU yautangaza mwaka 2014 kuwa mwaka wa Kilimo na usalama wa

chakula barani AfrikaNa Al-amani Mutarubukwa

Addis Ababa. Umoja wa Afrika umeazimia kuwa mwaka 2014 uwe ni mwaka wa kuhakikisha shughuli za kilimo zinaboreka ili kuimarisha hali ya usalama wa chakula barani Afrika.

Azma hiyo limefanywa na nchi za Kiafrika kwenye mkutano wao wa 22 uliofanywa tangu Januari 21 hadi 31, 2014 huko Adis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Kufuatia uamuzi huo, Shirika la Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (FAO) limeisifia hatua hiyo kwa kusema kuwa hilo ni azimio muhimu sana kuwahi kufanywa na viongozi wa kiafrika kwa minajili ya kuondoa njaa barani Afrika ifikapo mwaka 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO Bw. Jose Graziano da Silva ameahidi kuwa Umoja wa Mataifa upo tayari katika kuhakikisha maono hayo yanafikiwa kwa kutoa msaada wa hali na mali.“Hili ni azimio muhimu sana katika historia ya viongozi wa Afrika katika kutaka kuondosha njaa na inaonyesha kujiamini kwao kufanya kazi nasi, na ni wazi kuwa tukifanya kazi kwa pamoja tutaweza kuondosha shaa duniani kote.”

“Bara la Afrika limeshuhudia ukuaji wa uchumi usiowiana, lakini pia ni bara pekee ambalo jumla ya watu wenye njaa imeongezeka tangu mwaka 1990,” alisema na kuongeza kuwa, “ changamoto kuu ni jinsi viongozi hao watakavyobadili maono hayo kuwa vitendo katika

kupambana na vyanzo mbalimbali vya njaa barani humo.”

“Uwekezaji kwenye kilimo, uwezeshaji jamii za watu maskini, ulinzi wa haki ya kupata ardhi na vyanzo vya maji pamoja na kuwaangalia wakulima wadogo na vijana itakuwa ni jambo la msingi kufikia azima hiyo,” aliongeza Bw. Da Silva.Lengo la kuondoa njaa ifikapo mwaka 2025 lilipendekkezwa kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa usalama wa chakula barani Afrika ulioandaliwa na Umoja wa Afrika nchini Brazil ukiongozwa na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva mwaka 2013.

Serikali, mashirika ya kimataifa, asasi zisizo za kiserikali na taasisi binafsi walikubaliana na lengo hilo kama njia ya kuhamasisha mipango mathubuti ya kujenga yale waliokubaliana kwenye mpango wa kuendeleza kilimo barani Afrika (CAADP).

Pia Bw. Graziano da Silva alissisitiza kwa tume ya uongozi ya Umoja wa Afrika pamoja na Mwenyekiti wake Bi Nkosazana Dlamini Zuma kuupeleka mchakato huu mbele kama njia ya kuudhihirishia ulimwengu kuwa mpango huu unamilikiwa na waAfrika wenyewe.

Kwa mujibu wa FAO, takribani nchi 11 za kiafrika zimeshafikia malengo ya kwanza ya milenia (MDG) kwa kupunguza watu wenye shida ya njaa kati ya mwaka 1990 na 2014. Nchi hizo ni Algeria, Angola, Benin, Cameroon, Djibouti, Ghana, Malawi, Niger, Nigeria, Sao Tomé na Príncipe na Togo.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akisalimiana na Rais za zamani wa Malawi Dkt. Bingu wa Muthalika baada tu ya ufunguzi wa Mkutano wa Umoja wa nchi za Kiafrika mjini Addis Ababa. Endelea Uk wa 28

29Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 2014Pambazuko Na. 44 Toleo la Januari – Machi 201428

“Huu ni ushahidi tosha ya kuwa nchi hizi zinapiga hatua katika muelekeo sahihi.”

Nchi tatu kati hizo, Djibouti, Ghana, Sao Tome na Principe - tayari wamevuka lengo la Mkutano wa Chakula wa Dunia wa mwaka 1996 la kuounguza kwa nusu idadi hiyo.

Lengo hili jipya lililotangazwa mwaka huu linaenda sambamba na changamoto ya kuondoa njaa kabisa barani humu iliyowahi kutangazwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon mwaka 2012.

Muongo mmoja uliopita, viongozi wa kiafrika waliweka azima kama hiyo ya pamoja ya kutaka kuinua sekta ya kilimo. Kupitia Azimio la Maputo Julai 2003 kwenye mkutano kama huo, viongozi wa nchi za kiafrika waliahidi kutenga angalau asilimia 10 ya bajeti za nchi zao kwenye sekta ya kilimo huku sekta hiyo ikitegemewa kukua kwa asilimia 6.

Lakini swali kuu ni kuwa Je, viongozi hawa na wafadhili wameweza kutekeleza ahadi yao kwa kukifanya kilimo kama njia kuu ya kuondoa umasikini ?

Kwa tafiti za Shirika la Kampeni na Ushawishi wa masuala ya Kilimo (ONE), zilizofanyika kwenye nchi 19 na wafadhiri 8 kwa kutazama kiasi na ubora wa uwekezaji katika kilimo kwa miaka kumi iliyopita, umeonyesha nafuu kiasi.

Nafuu hiyo inajitokeza kwenye muitikio na utashi wa kisiasa, uwekezaji wa ndani, misaada na mipango mkakati vikiunganishwa hatua kiasi za kukuza kilimo na kupunguza umaskini zimefikiwa.

Hata hivyo shirika hilo linasema Azimio la Maputo la serikali kutenga kiasi cha kutosha kwa ajili ya kilimo halijafuatwa kwa kiasi kikubwa, wahisani wametoa nusu tu ya ahadi zao na huku mipango mingi ya kilimo ya serikali barani humo ikipewa asimilia 50 tu ya fedha yote.

Mpaka hapo azima hii itakapotekelezwa kwa vitendo, ndipo suala la kuondoa umaskini na njaa barani Afrika kwa kutumia kilimo litawezekana.

Jipatie nakala ya Jarida la Pambazuko katika ofisi za MVIWaTa ngazi za kati zifuatazo

MratibuMVIWATA MorogoroS.L.P 3220 MorogoroMahali: Uwanja wa Maonyesho NaneNane mkabala na ofisi za TASOSimu/Faksi: 023 261 41 84 Barua Pepe: [email protected]

MratibuMVIWATA RukwaS.L.P 468 SumbawangaMahali: JENGO LA MAENDELEO (Caritas na Maendeleo)- KATANDALAFaksi: 025-2802558, Barua pepe: [email protected]

Mratibu MVIWATA MbeyaS.L.P 3015 MbeyaMahali: Jengo la Bima na CRDB Bank (Ghorofa ya mwisho) Simu: 255-025-250 3062, Faksi: (255) - 025- 250 3062Barua pepe: [email protected]

MratibuMVIWATA ChunyaS.L.P 171 ChunyaMahali: Jengo la Halmashauri, chumba No.3Simu: +255 787 089133, +255 768 089 133Barua pepe: [email protected]

Mratibu MVIWATA IringaS.L.P 918 NjombeMahali: Jengo la Njoroma, Njombe mjiniSimu: 0782 241 224, Barua pepe: [email protected]

Mratibu MVIWATA Kilimanjaro S.L.P 7389 Moshi Mahali: Mbuyuni sokoni- ghorofa ya GOLDEN GROWN LODGESimu: 255-27-275 1639, Barua pepe: [email protected]

Mratibu MVIWATA KageraS.L.P 713 KageraMahali: Mtaa wa Zamzam Bukoba mjiniSimu: 255-28-2220046, Faksi: 028 2220046Barua pepe: [email protected]

MratibuMVIWATA DodomaS.L.P 3293 DodomaMahali:Area C Dodoma eneo la INADES Formation Tz,mkabala na msikiti wa Area CSimu:255-26-2350013, Faksi: +255 26 2350744Barua pepe: [email protected]

Mratibu MVIWATA Monduli (MVIWAMO) S.L.P 47 Monduli Mahali: Barabara ya Boma-Moringe Sekondari, Monduli MjiniSimu: 255-27-253 8029, +255 27 253 8337 Faksi: +255 27 253 8338Barua pepe: [email protected]

Mratibu MVIWATA ManyaraS. L. P. 446,Babati ManyaraSIMU: +255 27 253 0385Baruapepe: [email protected]

MratibuMVIWATA TaboraMahali: Ofisi ya Maji jingo la Lake TanganyikaS.L.P 7004 TaboraSimu: +255 755 252969/+255 754 532855/+255 787 532855Barua pepe: [email protected]

MratibuMVIWATA ZanzibarS.L.P 149 ZanzibarMahali: Mwana kwereke- mkabala na shule ya sekondari M’kwereke A Simu:+255 777 485 936, +255 717 058 331 Barua pepe: [email protected]

MratibuMVIWATA RuvumaS.L.P 696 Songea ManispaaMahali: Jengo la TTCL ghorofa ya 2Simu: +255-25-2600626, 0756 096 291 Barua pepe: [email protected]

MratibuMVIWATA MkurangaS.L.P 56 MkurangaMahali: Karibu na stendi ya KimanzichanaSimu: 0786 158 646 Barua pepe: [email protected]

Mwenyekiti MVIWATA KigomaS.L.P 1144 KigomaMahali: Ndani ya ofisi ya KIKANGONET, Lumumba road jengo la NHC chumba 205Simu: 0713 565 252, 0762 565 252 Barua pepe: [email protected]

Mwenyekiti:MVIWATA ShinyangaMahali: Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Shinyanga (Kizumbi)Simu: 0763 74 0 675 Faksi: +255 28 2762609Barua pepe: [email protected]

MAWAKALA

AU yautangaza mwaka...

KUTOKA MITANDAONI

yakipotea njiani na hii ni kutokana na wakulima kuona wanaingia gharama kubwa kukodisha usafiri mara mbili au tatu na hivyo kuamua kusombelea mazao yote kwa safari moja na hatimaye kupotea kwa wingi njiani na ukizingatia jiografia ya mashamba yao yapo mbali na makazi wanayoishi pamoja na barabara kuwa mbaya.

Akielezea hatua inayofuata baada ya nyenzo hii ya mashauriano kufanikiwa, Bw. Felix Urio, Afisa Ugani kutoka wilaya ya Hai alisema wanategemea kuandaa andiko ambalo litakuwa linaelezea kero na changamoto wanazokumbana nazo wakulima na kuweza kuwafikia wadau mbalimbali nchini ili kuweza kutafutiwa suluhisho.

Pia andiko hilo litahusisha sera zote zinazotakiwa kufanyiwa marekebesho ili kufanikiwa kumuondelea mkulima tatizo hili la upotevu wa mazao yake na kupelekea kukosa ziada na hasa kwa kuwaruhusu kuuza mazao yao nje ya nchi kama kuna soko zuri na la uhakika kuliko kuendelea kuyauza kwa bei ya hasara yakiwa shambani.

Pia uboresha mfumo wa skabadhi ghalani ili wakulima waweze kuondokana na utunzaji holela wa mazao na hasa kwa kutumia nyenzo duni zisizofaa unaopelekea upotevu mkubwa na hasa kwa kuliwa na wadudu pia uboreshaji wa miuondo mbinu vijijini ikiwemo barabara.

Mbali na hayo Bw. Urio alishauri pia ni vyema kama maafisa ugani wa serikali wakawa karibu na wakulima kuanzia kipindi cha kuandaa mashamba hadi kipindi cha kuvuna ili kuwawezesha kufuata kanuni bora za uzalishaji na hatimaye kufanikiwa kuwa na uhakika wa mavuno yao.

Sauti ya Mkulima kama jina la mradi lilivyo limetokana na kauli mbiu ya MVIWATA isemayo Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima Mwenyewe, lengo ni kuona kuwa mkulima anaweza kujitetea mwenyewe kwa kupaza sauti akiwa kwenye kikundi au kupitia Mtandao wake. Huu ni mradi unaotekelezwa katika nchi tatu yaani Kenya, Uganda na Tanzania alisema Bw. Godfrey Kabuka, ambaye ni afisa msimamizi wa mradi huu wa Sauti ya Mkulima kwa upande wa MVIWATA.

Inatoka uk. wa 31

Inatoka uk. wa 24

Upotevu mazao...

IJUE MVIWATA Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania- MVIWaTa

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) ni chombo cha kuunganisha wakulima wadogo ili kuwa na sauti moja katika utetezi wa maslahi yao ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa.

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1993 na wakulima wadogo. Kauli mbiu ya MVIWATA ni ‘Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima Mwenyewe’.

Falsafa, utume na dira ya MVIWATAFalsafa ya MVIWATA inajengwa katika ya misingi ya ushawishi na utetezi wa maendeleo ya wakulima wadogo katika nyanja za kiuchumi na kijamii; kuwezesha mawasiliano na kujifunza kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wakulima.

utume wetu:Kuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbali mbali ili kujenga mtandao wa kitaifa wenye nguvu ya kuwezesha ushiriki na uwakilishi wa kweli wa maslahi ya wakulima wadogo katika ngazi zote za maamuzi.

Dira yetu:MVIWATA ni kuwa chombo imara chenye nguvu za ushiriki na uwakilishi wa mawazo ya mkulima katika mchakato wa maamuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kuwa na uwezo wa kutekeleza na kufuatilia michakato na shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maslahi ya wakulima wadogo.

Malengo ya MVIWATA1. Kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wakulima wadogo ili kujenga kwa pamoja mbinu na mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maslahi

ya wakulima wadogo, kiuchumi na kijamii.2. Kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu juu ya kilimo na shughuli mbalimbali za wakulima ili kuboresha maisha na kuinua hali yao kiuchumi na kijamii.3. Kuwakilisha wakulima wadogo katika mashauriano na serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu au yanayoathiri ufanisi na maslahi ya

wakulima wadogo wa Tanzania.

Maeneo makuu ya mpango mkakati1. Ushawishi na Utetezi: Kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kutetea maslahi yao.2. Uwezo wa kiuchumi: kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kiuchumi kupitia njia za akiba na mikopo, kuunganisha wakulima na

masoko na elimu ya ujasiliamali 3. Kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima kwa lengo la kujipanga na kujitetea.4. Masuala mtambuka: Kujenga uelewa wa wakulima juu ya Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Tabia ya nchi. 5. Ujenzi wa kitaaasisi kwa lengo la kuimarisha shirika

MuundoMuundo wa MVIWATA una ngazi tatu ambazo ni Ngazi ya Taifa, Ngazi ya Kati na Ngazi ya Msingi. Ngazi ya Kati inaundwa na mitandao ya kimkoa na kiwilaya wakati Ngazi ya Msingi inaundwa na mitandao ya Kata na Vijiji.

Shughuli kuu1. Kujenga uwezo wa wakulima wadogo kwa kupitia mafunzo shirikishi juu ya mbinu za ushawishi na utetezi, mbinu za kuimarisha uchumi wa

wakulima wadogo na uendelevu wa rasilimali kwa njia za warsha, mafunzo, mikutano na ziara za mafunzo.2. Kuhamasisha wakulima wadogo kujiunga katika vikundi vya kijamii na kiuchumi, mitandao ya msingi (kata na vijiji) na mitandao ya kati

(mikoa na wilaya). Mpaka sasa MVIWATA imeanzisha mitandao ya kimkoa katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga kwa Tanzania Bara. MVIWATA pia imeanzisha mitandao ya kiwilaya katika Wilaya za Monduli (Arusha) na Chunya (Mbeya). Tanzania Visiwani, MVIWATA Zanzibar imeanzishwa na kusajiliwa (Usajili namba 401). Mkakati unaendelea wa kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha mitandao mipya.

3. Kukusanya, kuweka katika kumbukumbu na kusambaza habari zinazohusu ujuzi na uzoefu wa wakulima, sera za kitaifa na kimataifa kwa kupitia jarida la Pambazuko Sauti ya Wakulima, vipindi vya radio, vipeperushi, vijitabu na machapisho mengine.

4. Kuhamasisha na kuwezesha wakulima kubuni na kuendesha miradi shirikishi ya kiuchumi na uzalishaji kwa lengo la kuboresha uchumi wa wakulima wadogo kama vile vyama vya mazao, vyama vya kuweka na kukopa na masoko ya mazao.

5. Kuandaa mikutano na warsha kuhusiana na mada zinazowagusa au kuathiri maslahi ya wakulima wadogo.

Uanachama na jinsi ya kujiunga na shirikaMVIWATA ina wanachama wa aina tatu (3).

aina ya kwanza ni Wanachama wa kawaida ambao wamegawanyika katika makundi mawili; a) Kikundi cha wakulima wadogo au b) Mkulima mdogo binafsi aliye mwanachama katika Kikundi au Mtandao. Mkulima atakuwa mwanachama wa kawaida wa MVIWATA mara tu Kikundi

au Mtandao wake utakapokubaliwa kuwa mwanachama. Atapewa kadi ya uanachama na kikundi au mtandao utapewa cheti cha utambulisho.

aina ya pili ni Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo. Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo vinavyojishughulisha na utetezi na ushawishi wa maslahi ya wakulima wadogo vilivyosajiliwa chini ya sheria yoyote ya Tanzania katika Ngazi za Wilaya, Mkoa au Taifa vinaweza kuomba kuwa mwanachama wa MVIWATA iwapo vinakubaliana kwa dhati na malengo na madhumuni ya Shirika.

aina ya tatu ni Wanachama WashirikiNi mtu yeyote, taasisi au kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono malengo na madhumuni ya Shirika. Mwanachama mshiriki anatamkwa na Mkutano Mkuu wa MVIWATA.

Kila mwanachama, isipokuwa mwanachama mshiriki atalipa kiingilio na ada ya kila mwaka. Maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kujiunga na ada yanapatikana kutoka kwa kiongozi au ofisi ya MVIWATA.

Kwa mawasiliano zaidiOfisi Kuu ya MVIWATAMkurugenzi MtendajiMVIWATA S.L.P 3220 MorogoroSimu: 023 261 41 84Faksi: 023 261 41 84Barua pepe: [email protected]: www.mviwata.org