4
Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu? Tangu mwaka 2012, Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) umekuwa ukitekeleza dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika wilaya 3 wamekuwa wakitekeleza utaratibu huo. Vijiji vimefanikiwa kuanzisha misitu ya hifadhi ya vijiji yenye ukubwa wa hekta 94,847 zikiwemo hekta 10,933 zilizotengwa kwa ajili ya uzalishaji Mkaa endelevu na vijiji vimefanikiwa kupata zaidi ya shilingi bilioni 0.5 fedha za Kitanzania. Makala hii inaelezea vipengele muhimu vinavyounda utaratibu wa Uzalishaji Mkaa Endelevu yenye nia ya kuchangia uendelevu wake. Vile vile makala hii inaainisha maeneo muhimu ya kufanyia tafiti ili kuboresha na kuendeleza mfumo huu katika maeneo mengine zaidi. Tunamaanisha nini tukisema “Endelevu”? Umoja wa Kimataifa (UN) unatafsiri Usimamizi Endelevu wa Misitu kama dhana yenye mabadiliko inayolenga kuimarisha na kuboresha thamani zote za kiuchumi, kijamii na kimazingira zitokanazo na misitu kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kwa kuzingatia tafsiri ya UN, Mfumo wa uzalishaji mkaa endelevu unalenga kuimarisha na kuendeleza kazi za kimazingira, kiuchumi na kijamii za misitu aina ya miombo (Matajiwazi). Nini maana ya Msitu wa miombo (Matajiwazi)? Miombo inajumuisha misitu iliyoko Afrika ya Kati, Kusini na Mashariki yenye tabia ya kupukutisha majani kila mwaka na kutawaliwa na miti aina ya Msani, Myombo na Mtondoro. Uoto wa asili hutofautiana kuanzia ukuaji wa nyasi nyingi mpaka miti midogo na nyasi zilizoota mbalimbali. Maeneo yenye miombo yanakadiriwa kuwa na aina 8,500 ya mimea, na zaidi ya asilimia 54 ya mimea hiyo iko katika hatari ya kutoweka. Miti aina ya miombo inakadiriwa kusambaa katika eneo la kilomita za mraba milioni 2.7 zinazopata mvua zaidi ya milimita 700 (>700 mm) kwa mwaka, kwenye jiolojia za kizamani na kwenye udongo wenye rutuba duni. Moto ni mojawapo ya sifa kuu ya misitu aina ya miombo, hii ni kutokana na utafiti wa Campbell na wenzake wa mwaka 1996.. Kwa upande mwingine, matokeo ya awali ya utafiti uliyofanywa kwa ufadhili wa Mradi yanapendekeza kwamba uchungaji wa mifugo wa wastani katika eneo lililovunwa huongeza uchipuaji wa miti kwa sababu mifugo hupunguza nyasi zinazosababisha moto wa mara kwa mara kwenye msitu. Mfumo wa Uzalishaji Mkaa Endelevu unaotekelezwa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa umebuniwa ili kutekelezwa kwenye misitu aina ya miombo hata hivyo mfumo huu hauwezi kufaa kutekelezwa kwenye misitu aina nyingine. Ili kutekeleza utaratibu wa uzalishaji mkaa endelevu katika eneo husika ni muhimu kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mfumo ikolojia wa msitu unaotakiwa kuvunwa. Pia inawezekana kabisa kutengeneza mifumo mingine kama hii inayoweza kutekelezwa kwenye aina nyingine ya misitu nchini. Kwa mfano, huko Kenya, utafiti unaonyesha kwamba uzalishaji wa mkaa endelevu unaweza kutekelezwa kwenye misitu aina ya migunga. Uendelevu wa Kiikolojia Mkaa Endelevu na Misitu aina ya Miombo Mfumo wa uzalishaji mkaa endelevu unaotekelezwa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania umebuniwa kwa ajili ya usimamizi wa misitu aina ya Miombo. Misitu aina ya miombo ina mfumo ikolojia wenye uwezo wa kuhimili usumbufu unaotokana na moto. Miti aina ya miombo huwa na uwezo wa kuchipua kutoka kwenye mizizi,maoteo na kutoka kwenye visiki na kwenye matawi. Kwa kiwango kidogo, uchipuaji pia hutokea kutokana na miche ya miti iliyopo kwenye ardhi na mbegu. Misitu aina ya miombo inajulikana kwa uwezo wake wa kuvumilia usumbufu ikiwemo ukataji wa miti. Endapo visiki, mizizi, miche na mbegu zitaachwa misitu aina ya miombo ina uwezo mkubwa wa kujirudia katika hali yake. Shughuli za usimamizi zinaweza kurekebishwa ili kuimarisha hatua za uchipuaji. Kwa mfano, baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba uchipuaji unafanyika vizuri zaidi kwenye miti iliyokatwa juu kidogo toka kwenye shina au urefu wa wastani. Kwa kuzingatia matokeo ya utafiti uliofanywa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya mkaa, mzalishaji mkaa endelevu anatakiwa kukata mti kwenye urefu wa zaidi ya sentimita 50 na kuvuna miti yenye kipenyo cha zaidi ya sentimita 15. Uchipuaji pia unafanikiwa zaidi kama uvunaji utafanyika mapema kabla ya mvua kuanza. Ni muhimu sana kulinda machipukizi na miche dhidi ya uharibifu wa moto katika kipindi cha miaka 2 baada ya eneo kukatwa miti.

Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu? · 2018-07-30 · dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika

  • Upload
    others

  • View
    1

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu? · 2018-07-30 · dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika

Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu?Tangu mwaka 2012, Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) umekuwa ukitekeleza dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika wilaya 3 wamekuwa wakitekeleza utaratibu huo. Vijiji vimefanikiwa kuanzisha misitu ya hifadhi ya vijiji yenye ukubwa wa hekta 94,847 zikiwemo hekta 10,933 zilizotengwa kwa ajili ya uzalishaji Mkaa endelevu na vijiji vimefanikiwa kupata zaidi ya shilingi bilioni 0.5 fedha za Kitanzania. Makala hii inaelezea vipengele muhimu vinavyounda utaratibu wa Uzalishaji Mkaa Endelevu yenye nia ya kuchangia uendelevu wake. Vile vile makala hii inaainisha maeneo muhimu ya kufanyia tafiti ili kuboresha na kuendeleza mfumo huu katika maeneo mengine zaidi.

Tunamaanisha nini tukisema “Endelevu”?

Umoja wa Kimataifa (UN) unatafsiri Usimamizi Endelevu wa Misitu kama dhana yenye mabadiliko inayolenga kuimarisha na kuboresha thamani zote za kiuchumi, kijamii na kimazingira zitokanazo na misitu kwa faida

ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kwa kuzingatia tafsiri ya UN, Mfumo wa uzalishaji mkaa endelevu unalenga kuimarisha na kuendeleza kazi za kimazingira, kiuchumi na kijamii za misitu aina ya miombo (Matajiwazi).

Nini maana ya Msitu wa miombo (Matajiwazi)?

Miombo inajumuisha misitu iliyoko Afrika ya Kati, Kusini na Mashariki yenye tabia ya kupukutisha majani kila mwaka na kutawaliwa na miti aina ya Msani, Myombo na Mtondoro. Uoto wa asili hutofautiana kuanzia ukuaji wa nyasi nyingi mpaka miti midogo na nyasi zilizoota mbalimbali.

Maeneo yenye miombo yanakadiriwa kuwa na aina 8,500 ya mimea, na zaidi ya asilimia 54 ya mimea hiyo iko katika hatari ya kutoweka. Miti aina ya miombo inakadiriwa kusambaa katika eneo la kilomita za mraba milioni 2.7 zinazopata mvua zaidi ya milimita 700 (>700 mm) kwa mwaka, kwenye jiolojia za kizamani na kwenye udongo wenye rutuba duni. Moto ni mojawapo ya sifa kuu ya misitu aina ya miombo, hii ni kutokana na utafiti wa Campbell na wenzake wa mwaka 1996..

Kwa upande mwingine, matokeo ya awali ya utafiti uliyofanywa kwa ufadhili wa Mradi yanapendekeza kwamba uchungaji wa mifugo wa wastani katika eneo lililovunwa huongeza uchipuaji wa miti kwa sababu mifugo hupunguza nyasi zinazosababisha moto wa mara kwa mara kwenye msitu. Mfumo wa Uzalishaji Mkaa Endelevu unaotekelezwa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa umebuniwa ili kutekelezwa kwenye misitu aina ya miombo hata hivyo mfumo huu hauwezi kufaa kutekelezwa kwenye misitu aina nyingine. Ili kutekeleza utaratibu wa uzalishaji mkaa endelevu katika eneo husika ni muhimu kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mfumo ikolojia wa msitu unaotakiwa kuvunwa. Pia inawezekana kabisa kutengeneza mifumo mingine kama hii inayoweza kutekelezwa kwenye aina nyingine ya misitu nchini. Kwa mfano, huko Kenya, utafiti unaonyesha kwamba uzalishaji wa mkaa endelevu unaweza kutekelezwa kwenye misitu aina ya migunga.

Uendelevu wa KiikolojiaMkaa Endelevu na Misitu aina ya Miombo

Mfumo wa uzalishaji mkaa endelevu unaotekelezwa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania umebuniwa kwa ajili ya usimamizi wa misitu aina ya Miombo. Misitu aina ya miombo ina mfumo ikolojia wenye uwezo wa kuhimili usumbufu unaotokana na moto. Miti aina ya miombo huwa na uwezo wa kuchipua kutoka kwenye mizizi,maoteo na kutoka kwenye visiki na kwenye matawi.

Kwa kiwango kidogo, uchipuaji pia hutokea kutokana na miche ya miti iliyopo kwenye ardhi na mbegu. Misitu aina ya miombo inajulikana kwa uwezo wake wa kuvumilia usumbufu ikiwemo ukataji wa miti. Endapo visiki, mizizi, miche na mbegu zitaachwa misitu aina ya miombo ina uwezo mkubwa wa kujirudia katika hali yake. Shughuli za usimamizi zinaweza kurekebishwa ili kuimarisha hatua za uchipuaji. Kwa mfano, baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba uchipuaji unafanyika vizuri zaidi kwenye miti iliyokatwa juu kidogo toka kwenye shina au urefu wa wastani. Kwa kuzingatia matokeo ya utafiti uliofanywa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya mkaa, mzalishaji mkaa endelevu anatakiwa kukata mti kwenye urefu wa zaidi ya sentimita 50 na kuvuna miti yenye kipenyo cha zaidi ya sentimita 15. Uchipuaji pia unafanikiwa zaidi kama uvunaji utafanyika mapema kabla ya mvua kuanza.

Ni muhimu sana kulinda machipukizi na miche dhidi ya uharibifu wa moto katika kipindi cha miaka 2 baada ya eneo kukatwa miti.

Page 2: Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu? · 2018-07-30 · dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika

Wakati wa kufanya maamuzi kuhusu mzunguko mzuri wa uvunaji, kunahitaji uamuzi utakaotathimini maana halisi ya uendelevu/ au je inahusu kurejesha msitu wa awali au kupata wastani wa juu wa ongezeko la msitu kwa mwaka au kulifanya eneo kujirudi katika hali yake ya awali kabla halijavunwa. Kuna njia nyingi za kuangalia jambo hilo na hatimaye mmiliki wa msitu kupima faida na hasara za njia mbalimbali na kufanya maamuzi yanayofaa. Katika nchi za Afrika Magharibi na Mexico, muda wa mzunguko wa miaka 9-15 hutumika katika usimamizi wa msitu kwa ajili ya uzalishaji mkaa endelevu.

Wakati huo huo, baadhi ya maeneo nchini Zambia, mzunguko wa miaka 20-30 ndo imekuwa ikitumika. Kwa upande wa Tanzania, Mradi umechagua mfumo unaoruhusu mzunguko wa miaka 24 kipindi ambacho ni kirefu zaidi cha kupata wastani wa kiwango cha juu cha ukuaji kwa mwaka. Huu ni mfumo usiopenda mabadiliko na umeanzishwa ili kupunguza hatari ya miti kuchipua polepole zaidi kwenye vijiji vya mradi

Eneo la uvunaji wa mkaa endelevu la miaka 3 katika Kijiji cha Ulaya Mbuyuni, Wilaya ya Kilosa likionyesha kiwango cha uchipuaji.

kuliko kwenye misitu ya miombo ambapo takwimu za uchipuaji zimetolewa. Tafiti za muda mrefu zinatakiwa ili kufanya tathmini ya uendelevu wa muda wa mzunguko unaotumiwa na mifumo mbalimbali. Kwa mfano, utafiti unaonyesha kwamba miti aina ya miombo ina uwezo wa kukua kwa wastani wa mita 2.5 katika kipindi cha miaka 6 ya mwanzo. Mathalani miti imekatwa kwa kimo cha zaidi ya mita 0.5, hii inamanisha kwamba ndani ya miaka sita, eneo lililovunwa litakuwa na miti yenye urefu wa mita 3 ambacho ni kiwango cha chini cha urefu wa miti kinachotafsiriwa kisheria kama msitu nchini Tanzania.

Tafsiri rasmi ya Msitu nchini Tanzania

Msitu maana yake ni eneo la ardhi lenye ukubwa angalau wa hekta 0.5 na kiwango cha chini cha msitu kufunga/kufunika kwa asilimia 10 au eneo lenye miti aina mbalimbali iliyopandwa au ya asili ambayo ina uwezo wa kufikia zaidi ya asilimia10 ya msitu uliofunga kwa juu, na miti ambayo ina uwezo au kufikia kiwango cha chini cha urefu wa mita 3 ya ukomavu wa msitu ( URT, 2017). Taarifa ya Takwimu ya Hali ya Hewa ya Ukaa iliyowasilishwa UNFCCC.

Japokuwa eneo lililovunwa linaweza kuchukuliwa kama msitu baada ya miaka 6 bado mashina yaliyo mengi yanakuwa madogo kwa ajili ya uzalishaji mkaa kwa kuzingatia kiwango cha chini cha mti unaotakiwa kuvunwa wenye kipenyo cha sentimita 15. Njia nyingine inayoweza kutumika ni kukata miti kipindi ambacho kunakuwa na ongezeko.

Je ni kiwango gani cha Miombo kipo Tanzania?

Mfumo wa uzalishaji mkaa endelevu umebuniwa ili kutekelezwa kwenye misitu aina ya miombo (matajiwazi). Misitu aina ya miombo (matajiwazi) inapatikana maeneo ya kati, kusini na magharibi mwa Tanzania. Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani mita za ujazo 462,548 za miombo kwenye maeneo ya mvua nyingi, maeneo makavu na yenye msimu wa mvua. Hii ni kutokana na taarifa ya tathmini ya eneo la miombo ya mwaka 1984. Tathmini za misitu za hivi karibuni zimeshindwa kutofautisha misitu aina ya miombo na aina zingine za misitu. Kwa mfano, Taarifa ya NAFORMA ya mwaka 2015 inaonyesha kuwepo kwa kilomita za mraba 447,000 za misitu ikijumuisha miombo na aina nyingine ya misitu kama migunga. Taarifa sahihi kuhusu kiwango cha misitu aina ya miombo kwenye ardhi za vijiji zinahitajika ili kufahamu fursa zilizopo za kupeleka utaratibu huu katika maeneo mengine. Kwa upande wa umiliki wa misitu, asilimia 45.7 ya misitu ya miombo iko kwenye ardhi za vijiji. Hata hivyo mchanganuo huo haujaweza kutenganisha miombo na aina nyingine ya misitu. Tafiti zaidi kwa kutumia takwimu za NAFORMA zinaweza kutumika kufanya tathimini au makadirio ya eneo la misitu, mgawanyiko na aina ya umiliki wa misitu ya matajiwazi iliyobaki nchini Tanzania. Misitu aina ya miombo (matajiwazi) iliyoko katika mikoa ya Tabora, Singida na Kigoma inaathirika zaidi na ukataji wa miti.

Mzunguko wa uvunaji umebuniwa kuonyesha Uwezo wa Kuchipua kwa Misitu aina ya Miombo.

Ramani ya misitu aina ya miombo barani Afrika, kutokana na taarifa ya White, 1983.

Page 3: Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu? · 2018-07-30 · dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika

Uvunaji unaweza kufanyika pale ambapo ongezeko la kiwango cha miti ni kidogo na/au ni kabla ya muda wa kuvunwa.

Mmoja ya uchaguzi ni kuvuna katika kiwango ambacho ongezeko la miti kwa mwaka linafikia katikamwaka wa 18

Mchoro 3: Mpango wa maeneo ya uvunaji katika Eneo dogo la Uvunaji wa mkaa.

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! ! ! ! ! !

! ! ! !

85030

84449 84451 84453 84455 84458 84460 84462 84464

85295 85298 85300 85302 85304 85307 85309

83333 83335 83338 83340

83609 83611 83613 83615 83618 83620

83889 83891 83893 83895 83898 83900 83902

84169 84171 84173 84175 84178 84180 84182

85578 85580 85582 85584 85587 85589

85858 85860 85862 85864 85867

86138 86140 86142 86144 86147

86420 86422 86424

86700 86702 86704

86982 86984

84448 84450 84452 84454 84456 84457 84459 84461 84463 84465 84466

85296 85297 85299 85301 85303 85305 85306 85308 85310

84731 84733 84735 84738 84740 84742 84744 84747 84749 84751

85013 85015 85018 85020 85022 85024 85027 85029 85031

83327 83328 83332 83334 83336 83337 83339

83607 83608 83610 83612 83614 83616 83617 83619

83887 83888 83890 83892 83894 83896 83897 83899 83901

84167 84168 84170 84172 84174 84176 84177 84179 84181 84183

85577 85579 85581 85583 85585 85586 85588

85859 85861 85863 85865 85866 85868

86139 86141 86143 86145 86146

86419 86421 86423 86425 86426

86701 86703 86705 86706

86983 86985

84730 84732 84734 84736 84737 84739 84741 84743 84745 84746 84748 84750

85014 85016 85017 85019 85021 85023 85025 85026 85028

264800.000000

264800.000000

265000.000000

265000.000000

265200.000000

265200.000000

265400.000000

265400.000000

265600.000000

265600.000000

265800.000000

265800.000000

266000.000000

266000.0000009167

700.0

0000

0

9167

700.0

0000

0

9167

800.0

0000

0

9167

800.0

0000

0

9167

900.0

0000

0

9167

900.0

0000

0

9168

000.0

0000

0

9168

000.0

0000

0

9168

100.0

0000

0

9168

100.0

0000

0

9168

200.0

0000

0

9168

200.0

0000

0

9168

300.0

0000

0

9168

300.0

0000

0

9168

400.0

0000

0

9168

400.0

0000

0

9168

500.0

0000

0

9168

500.0

0000

0

9168

600.0

0000

0

9168

600.0

0000

0

A total of 8 plots per yearqualify for sustainable charcoal

harvesting out of 188 coups from this FMU

This is equivalent to 1.9 hectaresper year out of 47 hectares

which is dedicated for sustainablecharcoal harvesiting in a period

of 24 year's cycle

MAP SHOWING SUSTAINABLE CHARCOAL HARVESTING COUPS - MSIMBA VILLAGE (KILOSA)

Legend! South West Corner of a Coup

River

FMU Buffer/No harvesting

MSIMBA VILLAGE MAP

A Buffer of 60m of a River

A coup for Harvesting Sustainable Charcoal 1st 12 year's Cycle

A Coup for Harvesting Sustainable Charcoal 2nd year's Cycle

±0 0.150.075 km

May, 2016

Mfumo unaotumika na mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) unapendekeza kiwango cha juu cha asilimia 20 cha eneo ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Kijiji kutengwa kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa endelevu. Asilimia 80 inayobaki inatengwa kwa ajili ya uhifadhi na uvunaji wa mbao kwa kuchagua. Kwa kutenga kiasi cha asilimia 20 tu cha eneo la Hifadhi ya Msitu wa Kijiji kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa endelevu, unaongeza uwezo wa msitu kuhimili hatari ya kutoweza kuoteana/kuchipua, na/au kukabiliana na usumbufu mwingine unaojitokeza ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Kijiji. Kwa Mfano, kama uchipuaji wa visiki haukutokea kama ilivyo tarajiwa au sehemu ya Eneo Dogo la Usimamizi (EDU) limeathiriwa na moto au uvunaji holela, kijiji kinaweza kikapitia upya mpango wao wa uvunaji ili kujumuisha maeneo mapya na hivyo kufikia malengo yake. Kwa njia hii, mradi umejumuisha mpango mkakati wa kuangalia hatari ndani ya utaratibu huu. Pamoja na hayo, kanda za uhifadhi ndani ya Hifadhi ya msitu wa Kijiji unatoa mwanya wa kuhifadhi na kulinda huduma za mfumo ikolojia katika maeneo yote ndani ya msitu. Hata hivyo, utafiti zaidi unahitajika ili kujua kiwango cha uwiano baina ya maeneo ya uzalishaji na maeneo ya uhifadhi yakiwa chini ya hali tofauti ili kuwa na uwelewa mzuri na bora zaidi wa hatari zilizopo.

Mpango wa uvunaji kwa kila EDU unajumuisha mfumo

wa uangalizi mithili ya mchezo wa draft ‘checker board’ ambao unaonyesha kanda za uvunaji. Kila kanda ya uvunaji ndani ya EDU ina ukubwa wa mita 50 kwa 50. Mfumo huu wa ‘checker board’ umeundwa kutengeneza muonekanao wa uoto wa misitu katika hatua mbalimbali za uchipuaji. Kila mwaka 1/24 ya kanda ya uvunaji inaweza kuvunwa. Eneo hili dogo la uvunaji linasaidia msitu kuhimili uwezekano wa athari za mmomonyoko wa udongo, uharibifu wa makazi ya wanyama, na kupungua kwa usambazaji wa mbegu katika maeneo yaliyovunywa. Mfumo huu wa mradi wa TTCS unataka kwamba eneo lililovunwa linapaswa kuachwa na kuchipua kwa angalau miaka 10 kabla eneo lililoko pembezoni mwake kuvunywa. Kiwango kinacho paswa kuvunywa kinakokotelewa kulingana na tathmini ya miti iliyopo. Kiwango limbikizi cha uvunaji kutoka katika eneo la uvunaji kwa kila mwaka kinakupa kiwango kiwango cha miti kinachotakiwa kuvunwa kwa mwaka kwa kijiji. Mipaka ya maeneo yote ya uvunaji inatengwa na kamati ya maliasili ya kijiji. Wazalishaji wa mkaa wanapaswa kuvuna katika maeneo yaliyotengwa tu. Jambo la msingi ni kwamba maeneo mengine yote yanapaswa kulindwa vyema ili kuruhusu uchipuaji na uoteaji wa miti vizuri. Hii inamaanisha kutoruhusu moto kwa angalau miaka 2 ya mwanzo baada ya kuvunywa, ulishaji wa mifugo ndani ya maeneo hayo unasimamiwa na kilimo kutofanyika katika maeneo hayo.

Mfumo wa ‘checker board’ wa uvunaji unaonekana kirahisi katika picha hii ya setilaiti ya kijiji cha Ulaya Mbuyuni.

Hata hivyo, kwa kurudia mzunguko wa uvunaji hauwezi kupelekea ongezeko la msitu. Kwa upande wa uzalishaji mkaa endelevu, siyo lazima miti ifikie kipenyo cha juu kabisa, hii ni tofauti na uvunaji wa miti kwa ajili ya mbao, ambapo mzunguko wa muda mrefu unahitajika ili kufikia kiwango cha juu cha ukomavu kinachotakiwa kuvunwa.

Japokuwa Mradi umeamua kutumia mzunguko wa miaka 24, miradi mingine inaweza kufanyia majaribio na kufuatilia matokeo ya mizunguko mifupi au mirefu ya uzalishaji mkaa endelevu.

Kuendeleza Uendelevu katika mgawanyo wa maeneo ya uvunaji

Mchoro 1: Kiwango cha ongezeko cha miti kwa mwaka (mg ha-1yr-1) Chanzo: Frost, 1996

Njia nyingine ingekuwa kudhamiria kurudi kwenye miti ambayo haijavunwa. Hii inaweza kuchukua miaka 50 na zaidi.

Mchoro 2: Kiwango cha misitu kinaongezeka kutokana na uwepo wa miti na umri wa maoteo pamoja na machipukizi ya miti katika maeneo ya miombo. Chanzo: Frost 1996

Page 4: Nini kinafanya Mkaa Endelevu kuwa Endelevu? · 2018-07-30 · dhana ya uzalishaji mkaa endelevu kwenye misitu ya hifadhi ya vijiji. Mpaka kufikia mwaka 2017, jumla ya vijiji 22 katika

Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la USWISIwww.sdc.admin.ch

Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tan-zania (TFCG) [email protected] www.tfcg.org

Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA)

[email protected] www.mjumita.org

Shirika la Kuendeleza Nishati Asilia Tanzania (TaTEDO)[email protected]

www.tatedo.org

Kuhusu Watekelezaji wa Mradi

Mikakati mingine iliyotengenezwa kuongeza uendelevuMradi wa TTCS unahimiza wananchi kuwa na mipango mingi ya kuongeza uendelevu wa mazingira katika utaratibu huu ili kupunguza athari za kimazingira zinazoweza kujitokeza. Mipango hii ni pamoja na;

- Hakuna kuvuna mti au miti yenye kipenyo cha sentimita 15 au chini ya hapo na angalau miti 3 yenye kipenyo zaidi ya sentimita 15 inapaswa kuachwa katika kila eneo la mita 50 kwa 50.

- Kuweka kikomo katika kiwango cha chini cha nafasi ya kuachwa kati ya vyanzo vya maji na maeneo ya kuvunwa.

- Kutoruhusu uvunaji katika miteremko yenye kiwango kisichozidi asilimia 30.

- Mfumo huu unalinda aina ya miti yenye thamani kubwa kisoko kwa ajili ya mbao kama vile Mvule, Mninga na Mpingo. Miti mingine yenye thamani ya kibioanuwai kama vile yenye makazi ya wanyama wadogo kama ndege na wanyama wengine hairuhusiwi kuvunwa.

Jukumu la Uvunaji wa Mkaa kwa Njia endelevu katika kupunguza ukataji wa mitiIli kuwa na uendelevu, msingi mkuu wa mfumo huu umejikita katika kupunguza ukataji wa miti kwa kutoa motisha kwa jamii ili waendeleze na kutokata miti/misitu yao. Mradi umepunguza ukataji wa miti ukilinganisha na maeneo mengine ndani ya wilaya, na ukilinganisha na kiwango cha ukataji wa miti miaka ya nyuma. Kwa mfano, vijiji kumi vya Wilaya ya Kilosa ambavyo vilijiunga na kutekeleza mradi kati ya mwaka 2013-2015 vimepunguza kiwango chao cha upotevu wa misitu kutoka asilimia 2.37 kwa mwaka 2010-2014 hadi kufikia asilimia 1.91 kwa mwaka 2014-2015, na kufikia chini ya asilimia 0.78 ndani ya Hifadhi za Misitu ya vijiji. Kupungua huku kwa kiwango cha ukataji wa miti katika vijiji vya mradi kinatofautiana na ongezeko la ujumla la ukataji wa miti katika maeneo mengine ya Wilaya ya Kilosa kutoka asilimia 1.93 kwa mwaka 2014 hadi asilimia 2.64 mwaka 2016

Ufanisi wa NishatiMradi unaendeleza matanuri ya kichuguu udongo kutokana na uwezo wa matanuri haya kuongeza ufanisi wa mchakato wa ukabonishaji ukilinganisha na matanuri ya kienyeji.

Uendelevu wa Kiuchumi na KijamiiMfumo huu umetengenezwa uwe endelevu kiuchumi, jamii hutoza ushuru kwa kila gunia la mkaa linalozalishwa kijijini. Vijiji vinavyoshiriki kutekeleza mradi huu kwa pamoja vimepata jumla ya bilioni 0.3 ya fedha ya Kitanzania kama ushuru wa mkaa. Maamuzi ya namna ya kutumia mapato hayo katika ngazi ya kijiji hufanywa kwenye mkutano mkuu wa Kijiji. Kiwango cha mapato hutengwa kwa ajili ya kulipia gharama za usimamizi wa msitu wa kijiji pamoja na kusimamia utaratibu wa uzalishaji mkaa endelevu. Gharama hizo zinajumuisha doria, kununua vifaa kwa ajili ya wajumbe wa doria na kamati ya maliasili ya kijiji. Kiwango cha mapato kinachobaki, huwekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya kijiji. Mpaka sasa jamii zimefanikiwa kutumia mapato yatokanayo na mkaa endelevu kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kulipia bima ya afya kwa wananchi wote katika vijiji husika, ujenzi wa madarasa na nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa afya na walimu.

Misitu aina ya miombo ina mchango mkubwa wa kuboresha maisha ya jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu. Misitu hiyo hutoa aina nyingi za vyakula kwa ajili ya watu ikiwemo matunda, uyoga, asali, mboga za majani na mizizi. Pia Misitu ya miombo hutoa vifaa vya kujengea,dawa, zana za kilimo, vyombo na thamani za nyumbani. Kuilinda jamii ili iendelee kupata rasilimali hizi ni muhimu kwa uendelevu wa mfumo wa uzalishaji wa mkaa endelevu. Haki za jamii kuvuna rasilimali zilizoko

msituni zimeainishwa kwenye Mipango ya usimamizi wa Hifadhi za Misitu ya vijiji.

Nyingi ya thamani hizi za ziada ni maalumu kwenye misitu aina ya miombo tu, na haiwezi kutekelezwa kwenye misitu isiyokuwa na miti aina ya miombo. Tafiti kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania zimeonyesha kwamba usimamizi wa jamii wa rasilimali za misitu na uhakika wa upatikanaji wa rasilimali hizo unaimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Utawala bora, uwajibikaji na usawa wa kijinsia ni mambo muhimu sana katika uendelevu wa kijamii ya mfumo huu.

TAFITI ZAIDI

Mradi kwa kushirikiana na Taasisi za kitaaluma nchini Tanzania ikiwemo Chuo Kikuu Cha Sokoine (SUA) wanafanya tafiti kwenye baadhi ya maswali ikiwemo kufanya ufuatiliaji wa uchipuaji na upotevu wa misitu, pia kuangalia matokeo ya moto na mifugo kwenye eneo la usimamizi wa misitu. Mradi unakaribisha ushirikiano na taasisi mbalimbali za utafiti na wako tayari kupokea mbinu zenye ushahidi wa kuboresha na kuendeleza muundo huu katika maeneo mengine.

Ili kujua zaidi kuhusu Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania, tafadhali tembelea tovuti yetu; http//www.tfcg.org/sustainablecharcoal.html