Upload
others
View
17
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
RIPOTI KAMILIFU YA UCHUMI WA KENYA Kufika Juni 2010/Toleo la 2
Toleo Fupi
Kutegemea ‘injini’ Moja: hali ya uchumi wa Kenya unaoyumbayumba
Na Kiangazio maalum cha Bandari ya Mombasa
Kitengo cha Kupunguza Umaskini na Kusimamia masuala ya Kiuchumi- Eneo la Afrika
UTANGULIZI ili ni toleo la pili la Ripoti Kamilifu ya Uchumi wa Kenya. Kuzinduliwa kwa ripoti hii pia kunaadhimisha miaka 50 ya kuwepo kwa Benki ya Dunia nchini Kenya. Kwa miaka hiyo 50
iliyopita, tumewahi kujenga ushirikiano mwingi na umma, serikali, taasisi za elimu, sekta ya kibinafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kimaendeleo na washika dau wengine. Ripoti hizi za kiuchumi zimetayarishwa kwa ushirikiano wa karibu sana na washika dau nchini Kenya na zinawakilisha mfumo mpya wa kushirikishana kimawazo na washirika wetu wenyeji. Shukran zetu za dhati ziendee Benki Kuu ya Kenya, Ofisi ya Naibu wa Waziri Mkuu na Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango na Maendeleo, Halmashauri ya Bandari nchini Kenya, Idara ya Kitaifa ya Takwimu nchini Kenya na Taasisi ya Uchanganuzi wa Utafiti kuhusu Sera za Umma nchini Kenya, ambao wamechangia katika ripoti hii na kutoa mwongozo katika utayarishaji wake. Ripoti hii, kama iliyoitangulia, inatoa habari timilifu za mielekeo ya hivi majuzi ya kiuchumi na pia kulenga kwa njia mahsusi masuala katika nyanja fulani teule. Ripoti hizi zinanuia kusaidia wote wanaotaka kuimarisha usimamizi wa kiuchumi nchini Kenya.Zinalenga kusaidia katika kuwafahamisha na kuchochea maarifa na mjadala kuhusu masuala ya sera muhimu, na ili kutoa mchango katika kuifanya nchi ya Kenya itumie uwezo wake wa kujiendeleza kikamilifu. Toleo hili la Ripoti Kamilifu ya Kiuchumi lina hoja tatu muhimu. Kwanza, uchumi wa Kenya unaendelea kuimarika. Baada ya miaka miwili ya kuzorota kwa uchumi, tunatazamia ukuaji wa uchumi kwa asilimia 4.0 katika mwaka wa 2010, ikiwa na maana kuwa Wakenya wataanza tena kuona hali zao za maisha zikiimarika. Pili, Kenya imekuwa ‘ikiendeshwa kwa injini moja’‐ ambayo ndiyo maudhui ya ripoti hii. Soko la humu nchini ndilo tegemeo kubwa kwa uchumi wa Kenya, ilhali soko la uuzaji bidhaa nje likiwa jambo lisilotegemewa na hata la kuudhi kibiashara. Zaidi ya mwongo mmoja uliopita, hali hii ya kutolingana nguvu baina ya masoko haya mawili hata imezidi kudhihirika zaidi, kama ilivyoonyeshwa katika hali za kiuchumi za sekta mbali mbali nchini Kenya‐ sekta tofauti za kutoa huduma nchini sasa zimeipita sekta ya viwanda, ambayo ilituamia na kukwamia katika asilimia 11. Kwa taifa la Kenya kufikia na kudumisha hali za juu za ukuaji wa kiuchumi, itahitaji kuzindua upya biashara ya kuuza bidhaa nje. Tatu, sababu moja kuu ya uchumi wa Kenya kukosa usawia katika sekta mbali mbali na kutolingana ni ukosefu wa miundo msingi nchini. Katika ripoti hii, tunaangazia dhima na hali ya utendakazi ya Bandari ya Mombasa, ambayo ni rasilmali muhimu sana katika miundo msingi ya Afrika Mashariki.Licha ya kuboreshwa hapa na pale, bandari hii bado haitekelezi majukumu yake ipasavyo. Mabadiliko yaliyofanywa hayajaweza kuenda sambamba na kasi ya mataifa mengine ya Afrika na bandari imebakia kuwa na msongamano mkubwa, hali inayoelezea kwa nini imepoteza biashara nyingi muhimu kama bandari ya kupitishia shehena zinazoingia kwa meli .Katika miaka kadha ijayo, shinikizo katika bandari hiyo itazidi kuongezeka. Chumi za mataifa ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kukua kwa asilimia 5. Tukifikiria wazo la uchimbaji mafuta nchini Uganda na uhusiano wa dhati zaidi wa Sudan Kusini na eneo hili, bandari ya Mombasa ina fursa kuu ya kuwa kituo muhimu zaidi cha kibiashara katika kanda hii.Hii ni nafasi ambayo Kenya haipaswi kuikosa.
Johannes Zutt Mkurugenzi wa Benki ya Dunia,
Nchini Kenya
MUHTASARI enya imeingia katika mwongo mpya ikiwa na msukumo mpya wa maendeleo yenye nguvu na ya kudumu. Kama sehemu muhimu ya kufufuka kwa uchumi barani Afrika baada ya mgogoro wa
kiuchumi ulimwenguni na kama kiongozi katika utoaji wa huduma katika kanda hii, Kenya ina matumaini makubwa ya kujiimarisha kiuchumi katika mwongo huu mpya. Baada ya miaka miwili ya kuzorota kiuchumi, Benki ya Dunia inatazamia ukuaji wa asilimia 4.0 katika mwaka wa 2010, kumaanisha kuwa Wakenya watashuhudia tena hali zao za kimaisha zikiimarika. Ili kufikia na kudumisha hali ya juu ya ukuaji wa kiuchumi nchini, Kenya haina budi ila kujaribu kusawazisha hali zake za kiuchumi, kukwepa hali ngumu za soko la humu nchini na kukabiliana na athari za baadaye za migogoro ya kiuchumi kutoka nje. Maudhui ya Ripoti hii Kamilifu ya pili ya Kiuchumi nchini Kenya, “Utegemeaji wa kipengele kimoja/Kundeshwa kwa ‘injini’ moja, inaonyesha kutolingana kwa miundo ya hali za kisasa za kiuchumi nchini Kenya‐ yaani ‘injini’ iliyo na nguvu ni soko la humu nchini na ‘injini’ iliyo dhaifu ni soko la kuuza bidhaa nje.Ili kuanzisha ‘injini’ ya soko la nje, Kenya itahitaji kukabiliana na masuala kadhaa, hasa upungufu wa miundo msingi. Bandari ya Mombasa, kwa mfano, ndio rasilmali muhimu na yenye nguvu ya miundo msingi nchini Kenya. Kama sehemu mahsusi ya ripoti hii inayopigia darubini bandari ya Mombasa inavyohitimisha, bandari inahitaji mabadiliko makubwa na kuinuliwa kufikia kiwango cha kimataifa na kuweza kukabiliana na mahitaji yanayokua na kuongezeka ya Mwungano wa Afrika Mashariki.
KUFUFUKA KWA UCHUMI WA KENYA
‐ 1 ‐
chumi wa Kenya unaelekea na kuendelea kufufuka — pole pole lakini kwa uhakika. Katika mwaka wa 2010,
Benki ya Dunia inatazamia kuwa ukuaji wa uchumi wa Kenya utafikia asilimia 4.0, ambayo inawakilisha uimarikaji dhabiti baada ya Kenya kupata pigo mara nne mtawalia kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita. Iwapo uchumi utaendelea kipiga hatua, Kenya inaweza kuinuka kwa asilimia 5 katika mwaka wa 2011, na kuirejesha nchi hii katika hali ya ukuaji iliyokuwa ikishuhudiwa baina ya mwaka 2004‐2007. Maendeleo ya kiuchumi ya hivi majuzi yamekuwa ni ya kutia moyo na kuleta matumaini kuwa Kenya itaanza mwongo mpya kwa mwelekeo wa kuimarika kiuchumi. Mwishoni mwa mwaka wa 2009, ukuaji wa uchumi wa Kenya uliongeza kasi yake na msukumo huo wa uimarikaji ukaendelea na kuingia mwaka wa 2010. Mvua kubwa imesaidia katika ufufuaji wa sekta ya kilimo‐ iliyokuwa tayari imesongeshwa hatua na athari za pamoja za ukuaji wa asilimia 7.5 katika mwaka wa 2008 na 2009. Uzalishaji wa kutegemewa wa kawi tangu mwaka wa 2010
ulisaidia kidogo katika kuinua sekta ya utengenezaji bidhaa (viwanda). Utoaji wa huduma unaendelea kuimarika huku mabadiliko katika Teknohama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) yakiendelea kwa mwendo kama wa mwaka uliopita.Idadi ya waliomiliki simu wanaweza kuwa ilipita hata milioni 20, kumaanisha kitakwimu kuwa kila mtu mzima nchini Kenya sasa ana simu. Kenya, sambamba na mataifa mengi barani Afrika, ilijikuta katika mgogoro wa kiuchumi wakati bado inajivunia hali yake ya biashara ndogo ndogo zilizo imara na hatimaye ikaweza kukabiliana barabara na hali ya kuporomoka kwa uchumi wa ulimwengu. Hali imara ya kifedha, mageuzi katika sekta ya benki na hali ya mkurupuko wa kifedha iliyokuwa inapungua iliiruhusu serikali kukabiliana na mgogoro huo kimbele kwa kupunguza riba za mikopo na kuandaa mpango wa kusisimua uchumi (kusaidia maslahi ya kijamii na kuimarisha uwekezaji katika miundo msingi). Nguzo nyingi za uchumi wa kitaifa nchini Kenya kwa jumla ziliimarika licha ya mgogoro huu. Mkurupuko wa kifedha ulipungua tena na kuenda chini ya asilimia
‐ 2 ‐
tano kufikia mwisho wa 2009, na kuwezesha Kenya kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wateja wa humu nchini. Mikopo ambayo hailipiki ilipungua katika mwaka wa 2009 kuliko ilivyokuwa katika mwaka wa 2007. Changamoto inayoikabili Kenya leo si kutafuta rasilmali‐ ila ni kutekeleza mfumo bainifu wa matumizi yake ya fedha za umma. Huku hali ya kifedha nchini Kenya ikibakia kuwa imara, utekelezaji wa hatua za kusisimua uchumi umejikokota. Mapato ya kitaifa ya humu nchini yamebakia kuwa mojawapo ya yale yaliyo katika viwango vya juu zaidi barani Afrika. Upungufu katika bajeti kwa mwongo mmoja uliopita umekuwa chini na bado kukiwa na imariko la kiuchumi kwa kiwango fulani. Kenya imeweza kupunguza viwango vya deni lake kutoka asilimia 60 ya Jumla ya Mapato ya Kitaifa‐GDP (mwaka wa 2000) hadi asilimia 40 (mwaka 2008) licha ya kuwa haikupata ruzuku au msamaha wa deni ulioweza kutegemewa. Hali hii imara ya kifedha iliruhusu serikali kuanzisha mradi wa kusisimua uchumi kwa gharama ya Sh22 bilioni, sawa na asilimia moja ya Jumla ya Mapato ya Kitaifa‐GDP ambayo iliongezea upungufu wa fedha uliotazamiwa na kufikia asilimia 6.6. Hata hivyo, miezi tisa baadaye katika mwaka huo wa kifedha serikali imefanikiwa kutumia asilimia 57 tu ya fedha hizo kusisimua uchumi, jambo ambalo, likichanganyika na hali ya mazoea ya serikali ya udhaifu wa kutekeleza bajeti za maendeleo, inaweza kuwa ni kutumia kiasi cha chini mno cha fedha katika mradi muhimu zaidi wa uwekezaji wa umma nchini Kenya. Kutokana na hilo, upungufu huu wa kifedha kwa jumla katika mwaka 2009/2010 unaweza hata ukazidi asilimia 5.
Tukiendelea zaidi, Kenya inaweza kuwa sambamba na viwango vya ukuaji wa kiuchumi barani Afrika iwapo itaepukana na mapigo ya athari mbaya za humu nchini na iweze kuthibiti misukumo na athari za baadaye za migogoro kutoka nje. Bara la Afrika na Asia Mashiriki zimeimarika kwa haraka zaidi kutokana na mgogoro wa uchumi wa dunia wa mwaka wa 2009. Kufikia mwaka wa 2011, viwango vya ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika vinatazamiwa tena vipite asilimia 5, ambayo ni karibu kiwango ilichokuwa kabla ya mgogoro huu. Kenya ina uwezo wa kukua, sambamba na kadiri Afrika ikuavyo, licha ya kuwa ukuaji wa pato‐la‐kila‐mtu unaweza kuwa chini (tazama mchoro 1). Ili haya kutokea, Serikali ya Kenya itahitaji kukwepa mapigo yenye athari mbaya kiuchumi, kwa mfano kwa kusimamia na kufanikisha mfumo wa kura ya maoni kuhusu katiba mwaka huu na janga lolote la ukame litakalokuja. Migogoro kutoka nje pia inaweza kuathiri vibaya matazamio na matumaini ya ukuaji wa uchumi wa Kenya. Kukatizwa kwa safari za ndege za kibiashara kuelekea Ulaya mapema mwaka wa 2010, kulikosababishwa na mlipuko wa Volcano ya Iceland uliochafua hewa kwa jivu lake, uliathiri kwa muda mfupi mauzo ya nje ya kilimo cha bustani maua, mboga na matunda kutoka Kenya. Mgogoro wa sasa katika maeneo inakotumiwa sarafu ya Euro, ulioletwa na hali ya deni sugu la Ugiriki, umepelekea kuimarika kwa shilingi ya Kenya. Baada ya muda fulani sarafu dhaifu ya Euro inaweza kusababisha kupungua kwa mauzo ya nje ya maua, mboga na matunda katika soko la Ulaya na pia kupungua kwa watalii wanaotembelea Kenya kutoka sehemu hiyo.Kenya inaweza kukabiliana na athari za uwezekano wa migogoro hii ya kutoka nje kwa kutafuta masoko mbadala kwa mazao yake ya kilimo na pia watalii wake.
Jedwali1: Uchumi wa Kenya unafufuka‐ pole pole lakini kwa uhakika
‐2
‐1
0
1
2
3
4
5
6
7
8
2007 2008 2009 2010 2011
Asi
lim
ia
GDP Kenya GDP SSA Percapita Kenya Percapita SSA
Asili: Idara ya Kitaifa ya Takwimu nchini Kenya (KNBS), Makadirio ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia. GDP Kenya = Jumla ya Mapato ya Kitaifa‐Kenya, GDP SSA = Jumla ya Mapato ya Kitaifa SSA, Percapita Kenya = Pato‐la‐kadiri‐la‐kila‐mtu Kenya, Percapita SSA‐ Pato‐la‐kadiri‐la‐kila‐mtu nchini‐SSA KUTEGEMEA ‘INJINI’ MOJA
‐ 3 ‐
yenzo za kusukuma uchumi wa Kenya bado zinayumba yumba. Hata kama nchi hii itaepukana na mgogoro
mwingine katika miaka ijayo, itakuwa vigumu kwa Kenya kuufikia viwango vya juu vya ukuaji kwa muda mrefu kutokana na hali yake ya sasa ya kiuchumi inayoyumbayumba. ‘Injini’ yenye nguvu inayoendesha uchumi wa Kenya ni soko la humu nchini, ambalo huchangia asilimia 75 ya Jumla ya Mapato ya Kitaifa‐(GDP). Nayo mauzo ya bidhaa nje ya nchi hii yanaweza kufananishwa na ‘injini’ yake dhaifu ambayo imekuwa ikizorota kwa umuhimu wake kila kuchao. Kenya ni baadhi ya mataifa machache yanayoendelea duniani ambayo yameshuhudia soko lake kuuza bidhaa nje likinywea badala ya kukua kwa miongo mitano iliyopita. Mauzo ya bidhaa za Kenya nje kama sehemu ya Jumla ya Mapato ya Kitaifa – GDP yamepungua kutoka asilimia 40 mnamo 1960 hadi asilimia 26 2009. Huku mataifa yenye chumi chipukizi yakiwa yamewekeza katika uzalishaji wa bidhaa za
kuuzwa nje, Kenya imeshuhudia mauzo ya nje iliyoyazoea tangu zamani ya kilimo, hasa kahawa na majani chai, yakidorora kutokana na usimamizi usiofaa wa taasisi zinazohusika na mauzo. Wakati huo huo, Kenya imejijengea biashara yenye nguvu ya kuuza nje mazao ya kilimo cha bustani yaani (maua na mboga) na pia imeshuhudia uimarikaji wa utoaji huduma nje, hasa utalii na usafiri wa ndege, na pia sekta chipukizi ya kutafuta wataalamu wa kandarasi fulani ( kama vile vituo vya ushauri). Hata hivyo, nyanja hizi mpya za ukuaji hazikutosha kukumbana na mwelekeo ya kuporomoka kwa soko la mauzo ya bidhaa nje kama asilimia fulani ya Jumla ya Mapato ya Kitaifa. Kutokana na ongezeko la haraka la uagizaji wa bidhaa za kimsingi kama vile (mafuta, mabaki ya makaa ya kutengeneza saruji na hata mahindi) ili kusaidia uchumi wa nyumbani, na hivyo kukwamiza soko la kuuza bidhaa nje, upungufu katika biashara ya humu nchini umekuwa ukiongezeka katika miaka iliyopita. Upungufu huu katika mfuko wa serikali wa matumizi ya dharura umekuwa ukifidiwa na kuongezea ufadhili wa mtaji zaidi na washika dau, hadi ukafikia kiwango cha kustaajabisha cha asilimia 9.5 ya Jumla ya Mapato ya Kitaifa – GDP kufikia mwaka wa 2009. Hii ilikuwa hatua kuu na ya kutia moyo ikikumbukwa kuwa mgogoro wa kiuchumi duniani na msaada wa kigeni uliopatikana kufadhilia miradi (FDI), ulikuwa ni haba nchini Kenya. Nyongeza hizi zilichangia katika kuendesha uwekezaji wa ujenzi na utoaji wa huduma, zilisaidia kuondoa Kenya katika hali ya deni mbaya na kuimarisha viwango vya kubadilishana sarafu. Hali za kiuchumi zinazosababisha kutoimarika kwa sekta ya kuuza bidhaa nje zinaweza kudhihirika pia katika sekta mbali mbali nchini Kenya. Sekta zinazozalisha bidhaa za kuuzwa humu nchini (zisizouzika nje) imekuwa ikinawiri sana, hasa sekta imara ya utoaji wa huduma. Sekta zinazozalisha bidhaa za kuuzwa nje (zinazouzika ng’ambo), zimekuwa kwa upande mwingine zikizorota sana, licha ya kuwa baadhi ya vijisekta na hata kampuni
dhabiti hazikutingizwa na hilo k.m. wazalishaji katika sekta ya kilimo cha bustani. Sekta ambayo imekuwa ikidorora zaidi katika mwongo mmoja uliopita ni ile ya viwanda yaani utengenezaji wa bidhaa/usanidi. Katika mataifa yenye chumi zinazoinukia, kuwepo kwa sekta imara ya viwanda kunahusishwa na kunawiri kwa mauzo ya bidhaa nje. Katika mwaka wa 2000, sekta ya viwanda ilikuwa ya pili katika uchumi wa Kenya baada ya sekta ya kilimo. Kufikia mwaka wa 2009, utengenezaji bidhaa ikaporomoka chini na kushika nafasi ya nne. Katika mwongo huo mzima sekta ya viwanda (utengenezaji) wa bidhaa iliimarika katika uchumi na kubakia kutoa mchango wake wa asilimia 11. Katika kipindi hicho, huduma ziliongezeka na sekta mbili za uchukuzi na mawasiliano zikachukua nafasi iliyoshikiliwa na utengezaji bidhaa na zikawa sekta ya pili kuu muhimu nchini Kenya, na mnamo 2007 biashara za jumla na reja reja nazo zikaishinda sekta ya viwanda kwa asilimia yake katika Jumla ya Mapato ya Kitaifa (GDP), tazama mchoro: 2.
‐ 4 ‐
Mchoro wa 2: Sekta za huduma zaipita ile ya viwanda
Mapato ya GDP ya kila sekta (as ilimia)
S oko la jumla na la rejareja, lajirekebis ha
Uchukuz i na Mawas iliano
V iwanda
9
10
11
12
13
14
15
2000 2001 2002 2003 2004 2005 2006 2007 2008 2009
%ya
Map
ato
yaG
DP
S ekta ya viw anda yapitw a na ile ya Uchukuz i na Maw as iliano
Utengenez aji bidhaa w apitw a na s oko la jumla na reja reja
Asili: Idara ya Kitaifa ya Takwimu nchini Kenya (KNBS), Makadirio ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia, TZ: Sekta zote zilionyesha viwango sawa vya GDP Ili kuboresha na kuimarisha ukuaji wa uchumi wenye mtazamo mpana, muundo wa uzalishaji bidhaa unahitaji kuelekezwa upya katika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma zinazouzika. Lengo hili linaweza kufikiwa kupitia utoaji motisha ili kupanua na kuimarisha viwango vya kuuza huduma nje,
kuanzisha upya mauzo ya nje ya bidhaa zilizotengenezewa hapa nchini, na kupunguza taratibu viwango vya soko la humu nchini na nafasi ya serikali katika matakwa ya kijumla.
KUZINDUA ‘INJINI’ YA SOKO LA NJE ‐ KUTUMIA BANDARI YA MOMBASA
li Kenya ianzishe upya ‘injini’ yake ya soko la nje, serikali itahitaji itekeleze na miradi kadhaa ya uwekezaji na kuanzisha
sera, ikiwa ni pamoja na zile zitakazonyoosha utendakazi na kupanua uwezo wa Bandari ya Mombasa, ambayo ni lango kuu la kuagizia bidhaa za mafuta na mali ghafi kuingia nchini Kenya. Kenya inahitaji kukabili na kusuluhisha masuala kadha yanayohusiana kwa njia moja au nyingine katika juhudi zake za kunyoosha utendakazi wa bandari hii, (kuboresha idara ya forodha na taratibu za ukaguzi, zinazoitwa ‘muundo‐ msingi‐mwororo’) na kupanua uwezo wake wa kukabiliana vilivyo na ongezeko la shehena linalozidi kukua kila kuchao.Bandari inayoendeshwa ipasavyo, yaani iliyo na uwezo wa kukabiliana na viwango vinavyokua vya mahitaji ya kanda hii ya kuuza na kuagiza bidhaa kutoka ng’ambo, yahitaji kuwa ni kipengele muhimu sana katika mikakati ya Kenya ya kujiimarisha kiuchumi. Itakapodhihirika kwa wawekezaji wa nyumbani na wa kigeni kuwa nia ya serikali ni kustawisha shughuli katika Bandari ya Mombasa, wana uwezekano zaidi wa kuwekeza kwa muda wa wastani katika sekta kama vile ya viwanda. Bandari ya Mombasa hata inaweza kuwa kipande cha kipekee cha muundo msingi muhimu zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki na ina uwezo wa kuwa kitovu cha uchukuzi kilicho thaminiwa zaidi katika kanda hii. Tayari bandari hii ndilo tegemeo kuu kwa uagizaji kutoka nje wa mali ghafi nyingi na bidhaa za mafuta zinazozohitajika katika Afrika Mashariki. Katika miaka ijayo, chumi za Afrika Mashariki zinatarajiwa kukua kwa asilimia 5, hatua ambayo itaongeza uagizaji wa bidhaa kupitia bandari za Afrika Mashariki. Baada ya kipindi kifupi, uchimbaji mafuta nchini Uganda
‐ 5 ‐
unatarajiwa kusababisha uagiziaji wa bidhaa nyingi na hatimaye uuzaji nje wa mafuta na bidhaa za petroli, vyote hivi vitapitia katika bandari ya Mombasa. Kuongezeka kwa harakati za kiuchumi nchini Sudan Kusini kunaweza kusababisha mahitaji mengi zaidi katika uwezo wa bandari ya Mombasa kukabiliana na viwango vya juu vya uagizaji wa mali ghafi ya kukidhi uchumi unaoinukia. Fauka ya hayo, bandari hii inao uwezo ambao haujatumika kikamilifu wa kuwa kama njia ya kupitishia bidhaa mpya zilizotengenezewa Kenya na kuuzwa nje kwa kuwa zaidi ya thuluthi tatu za makasha/kontena ambazo huleta bidhaa bandarini hurejea bila shehena yoyote. Bandari hii pia inaweza kuhudumu kama kitovu cha kupitishia shehena ziletwazo kwa meli kwa nia ya kuuzwa katika soko la Afrika Kusini na Mashariki. Bandari ya Mombasa inafanya kazi kwa uwezo wake wote ila si kwa ushwari na unyoofu unaohitajika, na gharama inayotokana na hilo huathiri uchumi, na hatimaye kuathiri sekta ya viwanda na shughuli zinginezo zinazohusiana na uagizaji bidhaa kutoka ng’ambo. Hali hii huwa hasa inaweza kuwa mbaya zaidi tukiangazia uchukuzi wa makasha, kwa kuwa ukosefu wa mageuzi fanikishi na uwekezaji mpya vitasababisha ongezeko la visa vya kuchelewesha meli, malipo ya kulimbikiza bidhaa bandarini na gharama za juu kwa wateja. Zaidi ya hayo, matumizi ya teknolojia mpya ili kuharakisha taratibu za kutoa shehena na kuleta uwazi zaidi katika shughuli za bandarini unapaswa kuwa hasa ndiyo njia ya haraka na suluhisho mwafaka la kuimarisha utendaji bora. Marekebisho katika bandari yanawezekana: bandari nyingi barani Afrika na kwingineko zimedhihirisha kuwa uboreshaji unaweza kufanyika tena kwa haraka. Nchini Nigeria kwa mfano, utekelezaji wa mtindo wa ‘Bandari Kabaila’ mwaka 2006, umechangia katika kuleta ongezeko la kiajabu la uwekezaji wa sekta ya kibinafsi na kuraharakisha unyooshaji wa utendakazi bora bandarini. Mtindo huu unahusu ushirikiana wa sekta mbili; ya umma
na ile ya kibinafsi hivi kwamba ile sekta umma (Serikali) inarekebisha kanuni na kuzidhibiti huku sekta ya kibinafsi wakiwekeza na kuendesha bandari. Ghana kwa upande mwingine nao waliufumbatia mtindo huu wa Kabaila‐wa Bandari” mnamo 2007 kama sehemu ya walichokiia ‘Ghana Gateway’ yaani ‘Lango la Ghana’ ili kuhudumia majirani zake ambao wamezingirwa na nchi kavu na pia kukidhi mahitaji yao wenyewe ya kiuchumi. Matokeo yamekuwa ya kutia moyo sana na bandari ya Accra imekuwa ikitoa hudumu ambayo ina ushindani mkubwa na hata inaweza kukaribia viwango vya kimataifa. Jordan nayo imeongeza kiwango cha uwezo wake wa kubeba shehena kupitia mfumo wa kudhibiti lori za bei ya chini katika mwaka 2005 hatua ambayo iliwezesha kuwepo kwa ongezeko la 25% ya shehena zaidi inayotolewa na kuingia katika bandari ya Aqaba kwa kutumia idadi sawa ya kubeba mzigo. Serikali ya Kenya inahitaji kuchukua hatua sasa ili izuie bandari ya Mombasa isiwe kikwazo kwa ukuaji wa kiuchumi. Serikali ya Kenya imeshindwa kukabiliana na changamoto kadha zinazohusishwa na ukosefu wa utendakazi bora na usimamizi wa bandari licha ya mipango kuwa imeandaliwa hapo zamani. Serikali inaweza kuboresha utendakazi katika bandari hii baada ya muda mfupi iwapo ingetekeleza marekebisho kadha na uwekezaji sasa. Baina ya hatua muhimu zaidi zinazofaa ni:
Kwa miezi 3 hadi 6 ijayo • Kutambuliwe asasi itakayoongoza bandari na iwe na mamlaka ya kufanya marekebisho.
• Kuteuliwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bandari nchini (KPA) kwa kipindi cha miaka 3 kutegemea tathmini ya utendakazi wake.
• Kuamua itapitia wapi barabara kuu ya kuunga jiji la Mombasa na kuanza kutekeleza mipango huku ikioanishwa na ya barabara ya kutoka bandarini
‐ 6 ‐
• Kuanzisha mfumo wa kutoa motisha ili kuwezesha kuwepo na shughuli kamili za bandarini kwa saa 24 kutoka kwa wadau wengi.
• Kutekeleza mfumo uliojikita katika jamii iishiyo karibu na bandari ambao utasukumwa na teknolojia mpya ya kisasa.
• Kuruhusu ubinafsishaji kikandarasi kwa vituo vya 11‐ 14 bandarini kupitia kwa njia ya wazi na iliyoshindaniwa vilivyo.
Katika miezi 6 hadi 12 ijayo
• Kufafanua ratiba ya udhibiti kanuni za bandari usimamizi, uwekezaji kwa kufanya bandari iwe na mfumo wa ‘Bandari Kabaila’ na kubainisha jukumu la Halmashauri ya Bandari nchini (KPA).
• Kufafanuliwe majukumu na wajibu wa washikadau wa kibinafsi na wa umma bandarini.
• Kufanyia marekebisho utoshaji ushuru wa forodha na kuunyosha na kuifanya iwe shughuli ya wazi.
• Kuimarisha uwezo wa kiutekelezi wa Wizara ya Uchukuzi.
Kwa muhtasari, Kenya imeandaa mipangilio katika miaka michache iliyopita ambayo itasisimua uchumi na itayarishe nchi kwa kukua upya. Hata hivyo, Kenya imekuwa ikitegemea ‘injini’ moja, ambayo ni soko la humu nchini, huku ikikumbana na upungufu mkubwa na sugu wa fedha za matumizi ya dharura. Kwa mipango ya usoni ya uimarikaji wa kiuchumi wa kuanzia asilimia kumi kwenda juu, Kenya itahitaji imakinikie zaidi soko lake la nje, pamoja na sekta ya viwanda vya kutengeneza bidhaa. Uwekezaji utaanza kuingia katika viwanda, kama ulivyoingia katika sekta za mawasiliano na utoaji wa huduma, iwapo ustawi wa kisiasa utaendelea kwa muda fulani na mazingira ya sera yabakie kuwa ya kuridhisha. La muhimu na kutia motisha hapa ni kuwa bandari ya Mombasa imeshuhudia kuimarika katika uwezo wake na ubora wa utendakazi kwa jumla.
Bandari ya Mombasa
‐ 7 ‐
KIANGAZIO MAALUM – BANDARI YA MOMBASA ehemu hii ya kiangazio maalum inapigia darubini na kuichambua bandari ya Mombasa. Bandari hii ina umuhimu mkubwa hata nje ya mipaka ya Kenya. Kama bandari kubwa zaidi
Afrika Mashariki, ndiyo lango kuu la bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na zinazouzwa nje sio tu kwa Kenya bali pia kwa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Sudan Kusini na Ethiopia Kusini. Utekelezaji duni wa shughuli na ukosefu wa rasilmali umekuwa hatari kuu kwa ukuaji wa Kenya na mataifa jirani. Ni tatizo ambalo huenda likawa mbaya zaidi ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa sasa. Ripoti inaeleza msururu wa hatua za kufuatiliza ambazo serikali inafaa kuchukua na kueleza kuwa ikiwa uwekezaji hautafanywa haraka na mageuzi bandarini kutekelezwa, bandari hii haitaweza kumudu ongezeko linalotarajiwa la bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, na kwa kiasi kidogo, zile zinazouzwa nje, ifikapo mwaka 2011 na baadaye. 1. Umuhimu wa Bandari
Bidhaa zinazoingizwa katika bandari ya Mombasa kutoka nje zimekuwa zikiongezeka kila mwaka tangu 2005, isipokuwa mwaka 2008. Uagizaji wa bidhaa maji maji (sehemu kuu ikiwa bidhaa za mafuta) umekuwa ukiongezeka kwa kiwango cha kadiri cha asilimia 9.7 kila mwaka, mizigo iliyo kwenye makasha kwa asilimia 11.5 na bidhaa kavu (hasa mahindi, mabaki ya makaa na ngano) katika asilimia 23 (Tazama jedwali klifuatalo).
andari ya Mombasa ndiyo kubwa zaidi Afrika Mashariki na ni kiingilio kikuu cha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje
hadi Kenya na mataifa jirani (Tazama mchoro14). Bidhaa zinazopitia bandari hiyo kutoka nje zina umuhimu mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa Kenya, na jirani zake. Bidhaa majimaji, hasa petroli, mafuta na vilainishi, ndizo bidhaa kubwa zaidi kwa uzito zinayoagizwa kutoka nje. Bila hizi, uchumi wa Kenya (na mataifa mengi ya EAC), ambao hutegemea uagizaji kutimiza mahitaji yake ya bidhaa za mafuta na petroli, hauwezi kukua. Bidhaa nne zinazofuata kwa uzito, mahindi, ngano, chuma (iron) na chuma ngumu (steel) zina umuhimu mkubwa katika kutimiza mahitaji ya vyakula ya taifa na kusaidia sekta yake ya ujenzi inayokua kwa haraka.
Uzito wa bidhaa zilizoagizwa zikiwa ndani ya makasha umeongezeka kwa asilimia 55 tangu 2005. Kiwango cha ukuaji wa mizigo iliyowekwa ndani ya makasha kilipunguza kasi mwaka 2008, sawa na uchumi wa Kenya. Uagizaji wa bidhaa majimaji na bidhaa kavu uliongezeka mwaka 2009 kutokana na mahitaji zaidi ya kawi yaliyosababishwa na ukame. Mafuta kutoka nje yanaendelea kuhitajika kusaidia uzalishaji wa stima kutoka kwa maji ambao umekuwa ukipungua, huku mahindi yaliyoagizwa kujaza pengo lililosababishwa na ukame yakichangia ongezeko la bidhaa kavu zilizoagizwa.
Mchoro 14: Mombasa – Kiingilio kikuu
cha Afrika Mashariki
Licha ya ongezeko kubwa la bidhaa zinazoagizwa, bidhaa kwa jumla zinazoshughulikiwa Mombasa bado ziko chini kuambatana na viwango vya kimataifa. Mwaka 2008, Mombasa ilihudumia Vipimo Sawa na Futi Ishirini 616,000 (TEU ambacho ni kipimo kilichokubaliwa kupima shughuli bandarini) vya bidhaa. Hii ni mara dufu, idadi ya mizigo iliyoshughulikiwa katika bandari Dar Asili: Halmashauri ya Bandari za Kenya
‐ 8 ‐
es Salaam, lakini chini ya robo ya Durban na asilimia 2‐2.5 pekee ya mizigo ambayo hushughulikiwa katika bandari zenye shughuli nyingi zaidi duniani, Singapore na Hong Kong (Tazama mchoro 15).
Jedwali: Bidhaa muhimu zilizoagizwa kutoka
nje mnamo 2009 Bidhaa ‘000’ DWT
Petroli, mafuta na vilainishi 5,671
Mahindi 1,561
Mabaki ya Makaa 1,135
Ngano 1,074
Chuma 780
Plastiki 402
Mchele 387
Sukari 281
Kemikali na dawa za kuua wadudu 218
Magari na malori 296
Karatasi na bidhaa za karatasi 296
‐ 9 ‐
Asili: Jarida la kudarisi takwimu za kila mwaka la Halmashauri ya Bandari ya Kenya 2009
Mchoro 15: Singapore hushughulikia bidhaa mara 50
zaidi ya Mombasa (katika maelfu ya TEU) TEU
Uwezo wa bandari kwa tani za (TE Us)
0
5
10
15
20
25
30
S ingapore Hong Kong Rotterdam Durban Lagos Mombas a Dar esS alaam
Mam
ilion
i ya uz
ani k
wa
TEUs
ASILI: Shirika la makasha la Kimataifa Mtandaoni (www.ci‐online.co.uk) 20‐05‐2010 Mwaka 2009 bidhaa zilizoagizwa zilijumuisha asilimia 87 ya jumla ya uzito wa bidhaa zote zilizoshughulikiwa katika bandari hiyo. Mombasa ndiyo njia kuu ya kuingizia mafuta na bidhaa ghafi za kutumiwa viwandani nchini Kenya. Kati ya bidhaa zote zilizoagiziwa
Mombasa, asilimia 72 zilikuwa zikielekezwa katika soko la Kenya na zilizosalia zikiwa safarini kwenda katika mataifa jirani. Tangu 2005, uzito wa bidhaa zilizo safarini umeongezeka kwa asilimia 38 kutoka 3,202 hadi 4,412 kwa maelfu ya tani za kishehena yaani (‘000’DWT). Uganda ndiyo iliyokuwa soko kuu la bidhaa zinazopitia ikiwa na asilimia 80, huku sehemu ya mashariki ya DRC ikiwa ya pili kwa ukubwa(tazama mchoro 16). Bandari ya Mombasa pia ni kipima hali cha ukosefu wa usawa wa Kenya: bidhaa zinazouzwa nje ni asilimia 13 pekee ya bidhaa zote zinazoshughulikiwa katika bandari hiyo. Bidhaa za mboga na matunda, ambazo zina umuhimu mkubwa katika uchumi wa Kenya, husafirishwa kwa ndege na bidhaa nyingi zinazoundwa katika viwanda vya Kenya husafirishwa hadi mataifa jirani kupitia barabara. Bidhaa nyingi za kuuzwa nje zinazopitia Mombasa hutoka Kenya, ambazo ni asilimia 85 ya jumla ya bidhaa zote. Uganda ndiyo ya pili kwa ukubwa wa uuzaji bidhaa nje kupitia Mombasa ikiwa na asilimia 12. Bidhaa nyingi huwa zimewekwa ndani ya makasha, ingawa kati ya makasha 300,000 yaliyoagizwa kutoka nje ya nchini mwaka 2009, ni makasha 96,000 au thuluthi moja pekee yaliyotolewa nje ya nchi yakiwa yamejaa, huku yale mengine ambayo ni thuluthi mbili yakitoka bila chochote1.
Mchoro 16: Bidhaa nyingi zinazopitia Mombasa huelekea Kenya au Uganda
Asili: Jarida la kudarisi takwimu za kila mwaka la Halmashauri ya Bandari za Kenya 2009
1 Asili: Jarida la kudarisi takwimu za kila mwaka la Halmashauri ya Bandari za Kenya 2009
Kiasi cha mizigo inayopitia bandari hiyo ikiwa ndani ya meli kuelekea maeneo mengine imekuwa ikipungua katika miaka ya hivi karibuni. Sasa,bidhaa hizi hujumuisha sehemu ndogo tu ya shughuli bandarini (chini ya asilimia 1 ya bidhaa zote kwa jumla zilizoshughulikiwa mwaka 2009). Halmashauri ya Bandari za Kenya (KPA) kwa sasa inakataa mizigo iliyo ndani ya meli ambayo inapitia bandarini kutokana na changamoto za nafasi na uwezo, na kupunguza uwezo na nafasi ya Mombasa kama bandari iliyo kitovu cha eneo hili. Kupunguzwa kwa vikwazo vya kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni katika mataifa ya EAC kumeongeza umuhimu wa miundomsingi katika kufanikisha ushindani wa viwanda vya humu nchini. Miundo msingi ya barabara na bandari ni nguzo kuu ya ufungamano wa eneo hili. Kama kiunganishi muhimu katika utekelezaji shughuli na njia kuu ya uagizaji wa mali ghafi ya kutumiwa katika viwanda nchini Kenya na jirani zake, utendakazi bora wa bandari ya Mombasa una uwezo mkubwa wa kuimarisha ushindani wa biashara za Kenya na gharama kwa jumla ya bidhaa zinazotayarishiwa katika Mwungano wa Afrika Mashariki‐EAC.
Kati ya karibu makasha/kontena 300,000 zilizoagizwa kama zimejaa mnamo 2009, ni 96,000 pekee ambazo ni zilipelekwa nje kama zimejaa bidhaa, na theluthi mbili zilizobakia ziliuzwa nje zikiwa tupu.
‐ 10 ‐
2. Uendeshaji Shughuli kwa kutumia uwezo wote na bila utenda kazi bora
‐ 11 ‐
andari ya Mombasa imezidisha uwezo wake kama ilivyojengwa, ilihali inatarajiwa kuendelea
kushughulikia bidhaa zinaoagizwa na zinazouzwa nje ya nchi zinazoendelea kuongezeka. Tayari inatekeleza shughuli zake kwa kutumia uwezo wake wote kwa mizigo ya kawaida na ile iliyowekwa kwenye makasha na itaendelea kushuhudia upungufu wa uwezo wake wa kutenda kazi ikiwa masuala ya uwezo wake na utenda kazi wake bora hayataangaziwa. Kuhusu uwezo wake, makasha yanayoagizwa kupitia bandari hiyo yamekuwa yakiongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka tangu 20052, licha ya ukuaji mdogo wa kiuchumi (GDP) miaka 2007‐2008. Huku ukuaji katika mataifa ya Afrika Mashariki ukitarajiwa kufikia asilimia 5 kila mwaka na kuongezeka katika miaka mitano itakayofuata, mtindo huu unaonekana kuendelea. Na miradi mikubwa ya uhandisi katika eneo hili pia itaongeza mzigo katika bandari hiyo. Kampuni ya Tullow Oil, kwa mfano ilikadiria haja ya kuagiza makasha 200,000 ya bidhaa kila mwaka kuanzia mwaka 2011 ili kuiwezesha kutumia vyema mafuta yaliyopatikana nchini Uganda, — likiwa ni ongezeko la asilimia 5 katika uzito wa bidhaa zinazoagizwa zikiwa ndani ya makasha. Katika viwango vya utenda kazi, masuala kadha kuu yanafaa kuangaziwa kuhusu bidhaa zinazoagizwa na zinazouzwa nje ya nchi na ambayo yanahusiana na muda mrefu unaotumiwa kupitishia bidhaa katika bandari hiyo, na utenda kazi duni unaosababishwa na usimamizi wa uwekaji wa mizigo katika malori na upakuaji wa bidhaa, ukusanyaji wa ushuru, ukaguzi na kadhalika. Uwezo wa kuhudumia mizigo iliyo kwenye makasha una uhaba mkubwa. Huku ukuaji wa msimu katika nusu ya pili ya mwaka 2010 na ukuaji zaidi aktika mwaka 2011 ukitarajiwa, bandari ya Mombasa inakabiliwa na katika muda huu tatizokubwa la uwezo. Athari za hivi karibuni zinakuwa ongezeko la kucheleweshwa
2 TEUs‐ Vipimo vya urefu wa futi ishirini
kwa meli, msongamano bandarini, utozaji ada, na ushughulikiaji wa mizigo michache katika bandari (kukiwa na msongamano) na kupelekea kuchelewa zaidi na kuwagharimu waagizaji pesa zaidi. Wanauza bidhaa nje nao pia watakabiliwa na ongezeko la gharama kutokana na uwezekano wa ucheleweshaji bandarini, na kuwavunja moyo wateja ambao wana uamuzi wa kibinafsi wa kufanya katika ratiba zenye muda maalumu wa uwasilishaji bidhaa. Kwa jumla, masuala kuhusu uwezo katika bandari ya Mombasa yanaweza kuwa breki katika ukuaji wa uchumi katika eneo hili. Tukiangazia mbele, uuzaji bidhaa nje, hasa kutoka kwa mataifa yaliyogundua mafuta hivi majuzi huenda ukawa shughuli kuu katika bandari hiyo katika muda wa wastani. Viwango vya juu zaidi vya ukuaji katika bandari za Afrika katika miaka michache iliyopita vimeshuhudiwa katika mataifa yanayotoa mafuta kama vile Nigeria na Cameroon. Kugunduliwa kwa mafuta hivi majuzi nchini Uganda, bila shaka kutakuwa ana athari kubwa katika idadi ya mali ghafi na bidhaa zilizotayarishwa viwandani zinazouzwa nje kupitia Mombasa. Hazina za mafuta nchini Uganda zinakadiriwa kufikia mapipa 800 milioni. Hata kukiwa na uwezo wa kusafisha mafuta nchini Uganda, ili kutimiza mahitaji ya eneo hili ya kati mafuta na bidhaa za mafuta ambayo ni kati ya mapipa 150,000 hadi 200,000 kila siku kutahitaji baadhi yauzwe nje.Kadhalika, kugunduliwa kwa mafuta katika eneo la Albertine mashariki mwa DRC kunatarajiwa wakati wowote. Mombasa, bila shaka ni bandari iliyo katika nafasi bora ya kutumiwa kwa kuwa ndiyo njia fupi zaidi, lakini itahitaji uwekezaji mkubwa kuimarisha uwezo wake wa kuhifadhi mizigo. Mwisho kabisa, kura ya maoni mwaka 2011 huenda ikapelekea kujitenga kwa Sudan kusini kutoka kwa kaskazini, hatua ambayo itatilia umuhimu mkubwa katika njia za kusini za kusafirisha bidhaa, kama vile Mombasa, huku Sudan Kusini ikitafuta njia za kufikia bahari kupitia Njia Kuu ya Kaskazini.
‐ 12 ‐
Serikali ya Kenya inafaa kushughulikia masuala mengi yanayohusu kuongeza uwezo wa bandari wa nafasi na miundo msingi na kuimarisha usimamizi wa shughuli za bandari. Kwa upana, masuala yanayoathiri utenda kazi wa bandari ni: a) uwezo wa bandari kuhudumia meli katika liko (au mahali pa meli kutia nanga); b) uwezo wa uga (kuweka bidhaa kabla ya kuchukuliwa); na c) Kupitisha mizigo bandarini: a) Utenda kazi bora likoni
Mambo mawili makuu yanayoathiri utenda kazi bora katika liko ni – muda ambao meli huwekwa ikisubiri kuingia bandarini, na punde baada ya kutia nanga, kasi ya kupakua na kupakia mizigo katika meli. Mashirika ya meli mara nyingi yanaonekana kutuma meli zisizo na haja kuu na zisizo na gharama kuu katika bandari ya Mombasa kutokana na kutotabirika kwake, na muda wa kukaa bandarini jambo linalotishia ratiba za meli ambazo huwa na umuhimu mkubwa katika bishara hizo. Mwaka 2009, muda wa kadiri wa meli kukaa bandarini Mombasa ulikuwa siku 2.3 na muda wa kadiri wa meli yenye makasha ulikuwa siku 3.1. Uwiano kati ya muda wa kukaa bandarini na muda meli inaotumia ikiwa imetia nanga ambao huitwa kwa Kiingereza ‘waiting gratio’ unafikia kiwango cha kadiri cha asilimia 74 kwa meli zenye makasha katika bandari ya Mombasa. Meli zilizojaa makasha bila shaka hazitakubali zaidi ya asilimia 10 ya uwiano huo. Zikikubali, zitatoza ada kubwa au kuongeza gharama kwa watakaofikiwa na mizigo. Asilimia kubwa ya uwiano huu huwafukuza wahudumu wa mashirika ya meli kutoka bandari fulani. Lakini zaidi ya hayo, sehemu ya tatizo hili ni idadi ndogo sana ya bidhaa zinazopitia Mombasa. Hii imepelekea kuhudumu kwa meli chache za kubeba makasha na meli nyingine katika bandari ya Mombasa ikilinganishwa na meli kubwa za kubeba makasha na meli za mafuta ambazo hufika katika bandari kuu duniani. Utenda kazi bora katika bandari ya Mombasa, ufungamano bora wa eneo katika eneo la Njia Kuu ya Kaskazini na ongezeko la
uwezo wake kwa meli zinazopitia bandarini ni miongoni mwa mambo makuu ambayo yatavutia na kuongeza mizigo inayohudumiwa bandarini. Ili Kenya ifaidike kutokana na kupunguzwa kwa gharama zinazoshuhudiwa katika usafirishaji wa bidhaa duniani bandari hiyo itafaa kustawishwa na itekeleze kazi zake vyema zaidi. Tafadhali rejelea Kiambatisho cha 12 kwa nakala ya Kingereza, kinaeleza kwa kina uhusiano duni wa Mombasa na njia kuu za kibiashara duniani ( Annex 12: Kenya’s Poor Connectivity with Global Trade Routes). Mabadiliko katika utenda kazi wa bandari yana gharama kuu kwa kampuni za usafiri wa meli kwa kuwa hufanya vigumu kazi yao ya kupanga safari za meli. Katika miaka ya hivi majuzi, KPA imewekeza katika kustawisha mfumo wake wa kushughulikia makasha bandarini, lakini mifumo mingi yake imepitwa na wakati na huwa haitunzwi vyema. Kituo cha mwisho kinachofanikisha meli‐kwa‐ufuo, chenye vifaa vya kutosha, na chenye uwezo wa kisasa wa kuhudumia makasha kinafanikisha muda wa chini wa safari 40 kwa kila saa katika meli, lengo la kawaida likiwa 60 na zaidi. Licha ya kukumbatiwa kwa ufanya kazi masaa 24 bandarini, KPA iliandikisha kwa kadiri safari 14 kwa kila saa mwaka 2009, kukiwa na tofauti kubwa kuambatana na upatikanaji wa wafanyakazi na hali ya vifaa na mitambo. b) Uwezo wa ua
Msongamano bandarini huja na matatizo yake. Ingawa KPA inaweza kudai kuwa imefanikiwa katika kupunguza msongamano bandarini, — kwa kadiri muda wa meli kukaa bandarini ni siku 5.73, kuambatana na pale mizigo inapoelekea – hii hailingani vyema na viwango vya kimataifa ambavyo ni kati ya siku 1‐3. Mombasa imekuwa ikikabiliana na msongamano kwa muda kutokana na ukosefu wa nafasi bandarini ya kuwkea makasha na bidhaa nyingine. Hali inazindishwa na uzembe katika mifumo ya upitishaji bidhaa katika afisi za forodha ambayo inamaanisha kuwa uwezo
3 KPA, Utafiti wa Muda unaotumiwa na kasha katika Bandari ya Mombasa, Machi 2010.
wa bandari huwa hautumiwi vyema. Suluhisho la uagizaji bidhaa kwa Kenya lilikuwa ni kuhamisha huduma ya kupitisha mizigo kwa depo za wahudumu wa kibinafsi, ambazo hujulikana kama ‘Container Freight Services’ (CFS) yaani ‐Huduma za Kusheheni Makasha‐ ndani na karibu na mji wa Mombasa, ambapo makasha huwekwa baada ya kupitishwa katika bandari. Takwimu za KPA kuhusu muda ambao bidhaa hukaa bandarini huwa hazionyeshi idadi kubwa ya mizigo ambayo hipitia kwa CFS. Kumekuwa na usafirishaji wa bidhaa nyingi zinazoelekea katika soko la Kenya kutoka kwa usimamizi wa KPA hadi kwa CFS tangu 2007 (kutoka zaidi tu ya 8 milioni hadi karibu 12 milioni DWT – tazama mchoro 17). KPA inataja muda wa siku 11.3 mwaka 2007 hadi 5.9 katika robo ya pili ya 2009, ingawa takwimu hizo hazionyeshi hali halisi ya utekelezaji shughuli kwa bidhaa kutoka nyumbani. Mizigo kutoka nyumbani hupita haraka kutoka kwa usimamizi wa KPA (kwa kadiri siku 3.74) hadi kwa CFSs ambapo hutumia siku 115. Mizigo iliyo safarini (ambayo huwa haipitii CFSs), hutumia muda mrefu katika bandari ikikaguliwa. KPA hukadiria muda unaotumiwa na mizigo iliyo aktika bandari kuwa siku 7.5 kwa kadiri. Ili Kenya inufaike kutokana na kupunguzwa kwa gharama ya usafirishaji bidhaa duniani, bandari itahitaji kustawishwa na kutekeleza shughuli zake vyema zaidi.
‐ 13 ‐
c) Kupitisha mizigo bandarini
Shughuli za kupitisha mizigo bandari zimeendelea kuwa za mwendo wa kinyonga na hukabiliwa sana na ufisadi. Ukosefu wa habari kuhusu mizigo uliopo ni kikwazo kikuu katika utenda kazi wa mfumo wote. Kuanzisha kwa Mfumo wa Bandari wenye msingi wa Kijamii (PCBS) ambao ungeweza kuongeza pakubwa utenda kazi na kupunguza ufisadi umekuwa ukitekelezwa kwa zaidi ya mwaka 1.5 kwa sasa, kukiwa hakuna takwimu zozote
4 KPA, Utafiti wa Muda unaotumiwa na kasha katika Bandari ya Mombasa, Machi 2010. 5 Udadisi wa Benki ya Dunia wa 2010 kufuatia mahojiano na wahudumu wa CFS na sekta ya kibinafsi.
zilizotayarishwa. Matumizi ya mifumo ya kisasa ya forodha na mifumo ya tekonolojia (IT) iliyofungamanishwa katika shughuli za bandari yanafaa kuwa lengo kuu kwa Kenya, hasa shughuli zenye uwazi na uwajibikaji zaidi ambazo zingesaidia kupunguza visa vya ufisadi. Mfumo wa PSBC unaofanya kazi unaweza kusaidia sana katika jukumu la Kenya la kutoa shughuli yenye usalama siku zijazo. Mchro 17: Muda unaotumiwa na mizigo hupungua
huku wa CFSs ukiongezeka
Asili: Halmashauri ya Kuratibu Usafirishaji wa Mizigo iliyo safarini katika Njia Kuu ya Kaskazini, 2009, Volume of goods = Kiasi cha bidhaa Kijisanduku cha 1: Mfumo wa Bandari wenye msingi wa
Kijamii (PCBS) ni gani?
PCBS ni mfumo wa IT wenye lengo la kulainisha shguhuli za utawala bandarini. Mfumo huu huwaruhusu washika dau wanaoendesha shughuli bandarini kubadilishana habari na kutekeleza shughuli za kibiashara kwa njia iliyounganishwa, salama na yenye muundo mahsusi. Huhakikisha kuwa pande zote husika hupokea habari sahihi na kwa wakati ufaao katika kila shughuli ya kibiashara, na kuhakikisha kwamba shughuli inafanya kwa njia inayofaa. Kuwa na PCBS huongeza sana kasi na uwazi bandarini. Pia, hutumia vyema miundo msingi na kusaidia kusimamia utenda kazi bora wa shughuli bandarini kwa jumla. Asili: Wafanyakazi wa Benki ya Dunia 2010
‐ 14 ‐
Halmashauri ya Mapato ya Kenya (KRA) inakabiliwa na changamoto mbili katika upitishaji wa mizigo: kuanzisha mfumo utakaofanya kazi vyema wa kusimamia hatari, kwa kuwa kwa sasa makasha yanayoagizwa hupitia shughuli inayochukua muda mwingi ya ukaguzi, na kuimarisha utenda kazi na uwazi katika shughuli zake. Upitishaji wa mizigo huhusisha shughuli za serikali zilizochangamana za mipango pamoja na miundo msingi ya uchukuzi. Tangu 2005, na kuanzishwa kwa mfumo wa Halmashauri ya Ushuru nchini Kenya ‐KRA wa kiteknolijia huitwao SIMBA IT, shughuli ya kutekeleza upitishaji wa meli kupitia mtandao inayofanywa na kampuni za meli na utangazaji wa forodha unaofanywa na idara za upitishaji bidhaa (C&F), kwa pamoja kumeimarisha kasi ya udadisi wa mapato. Hata hivyo, mfumo wa SIMBA huwa hauarifu idara nyingine za kusimamia mipaka, kwa mfano kuwa mizigo imepitishwa na huwa haiwasiliani moja kwa moja kuhusu hali ya mizigo inayosubiri kupitishwa. Kwa hivyo, wenye mizigo huwa hawana uwezo wa kujua ni wapi mifumo ina udhaifu katika mfumo wote wa upitishaji mizigo. Kuimarika kwa biashara ya eneo kunaweza kushuhudiwa ikiwa mifumo ya kupitisha mizigo katika idara za forodha na ukaguzi wa bidhaa zote za EAC unafanyika Mombasa. Chini ya Muungano wa forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, ukusanyaji wa mapato katika bandari ya kiingilio, kwa mfano Mombasa (labda kupitia uangalizi wa pamoja), unaweza kuimarisha utendaji shughuli na upitishaji mizigo na kusaidia kutatua suala la bidhaa zinazofaa kupitishwa kutupwa Kenya. Ikiwa shughuli zote za upitisaji bidhaa zitaanzishwa, kwa mfano ukaguzi kufanyika, hii inaweza kupunguza muda unaotumiwa na bidhaamizigo inayopitishiwa bandarini.
Gharama za kuingiza na kupitia bandari ya Mombasa zina athari kubwa katika gharama ya kuendesha biashara katika Kenya na EAC.Ukosefu wa mfumo unaofanya kazi na uliofungamanishwa wa reli na barabara una maana kuwa bandari ya Mombasa haina uwezo wa kushughulikia makasha na bidhaa nyingine.Kuunganisha huduma za bandari na Njia Kuu ya Kaskazini kuna umuhimu mkubwa katika kufanikisha biashara na ufungamano. Ongezeko la bidhaa za kuagizwa, limeweka mzigo katika uchukuzi wa barabara na kuleta haja ya kuwa na mfumo wa kasi wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya uchukuzi. Upigaji hatua katika nyanja hii umekuwa duni. Kushindwa kwa mfumo wa gari moshi kumepelekea kuwepo kwa safari nyingi za malori makubwa na kuzidisha tatizo la msongamano na uegeshaji na kuharibu barabara. Uchukuzi wa reli awali ulijumuisha asilimia 80 ya bidhaa zilizopitia Mombasa mapema miaka ya 1970. Leo, ni asilimia 5 pekee ya mizigo ambayo hupitia reli, upungufu ambao umesababishwa na ukosefu wa uwekezaji endelevu wa serikali katika uchukuzi wa gari moshi na hivi karibuni zaidi, ukosefu wa uwekezaji unaofanywa na Rift Valley Railways, kampuni iliyopewa jukumu la kusimamia njia ya reli ya Mombasa hadi Nairobi. Kwa sasa, hakuna njia mbadala ya mbali na utumizi wa malori makubwa kupitia mji ambao unaendelea kukumbwa na msongamano. Matumizi ya mifumo ya kisasa ya forodha, mifumo ya habari na mifumo ya teknolojia iliyofungamanishwa katika shughuli za bandari yanafaa kuwa lengo kuu la Kenya.
Mchoro 18: Huchukua siku 19 kwa kasha kupitia bandari na kwa kutumia barabara kufika Nairobi, Kenya.
Asili: Halmashauri ya kusimamia Usafirishaji wa shehena kupitia njia kuu ya Kaskazini, 2009, Uchambuzi wa Benki ya Dunia wa KPA wa mwaka 2010
Mchoro 19: Huchukua siku 22 kwa kasha kupitia bandari na kwa kutumia barabara kufika Kampala, Uganda.
Asili: Halmashauri ya kusimamia Usafirishaji wa shehena kupitia njia kuu ya Kaskazini, 2009, Uchambuzi wa Benki ya Dunia wa KPA wa mwaka 2010
Mchoro 20: Huchukua siku 24 kwa kasha kupitia bandari na kwa kutumia barabara kufika Kigali, Rwanda
Asili: Halmashauri ya kusimamia Usafirishaji wa shehena kupitia njia kuu ya Kaskazini, 2009, Uchambuzi wa Benki ya Dunia wa KPA wa mwaka 2010
‐ 15 ‐
Kuanguka kwa mfumo wa reli nchini kumesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya malori makubwa ya mizigo kuanza safari mpya kuingia na kutoka bandarini.
‐ 16 ‐
Utenda kazi duni wa bandari ya Mombasa una athari kubwa katika muda wa usafirishaji wa mizigo iliyoagizwa kufika Kenya na jirani zake katika EAC. Michoro 18, 19 na 20 inaonyesha mchango wa bandari ya Mombasa katika muda unaochukuliwa kusafirisha bidhaa hadi Nairobi, Kampala na Kigali mtawalia kutoka wakati zinapofika bandarini. Kwa bidhaa zinazoelekea Kenya, uwiano wa muda unaotumiwa katika majumba ya KPA, pamoja na maghala ya hukadiriwa kuwa asilimia 90 ya muda unaochukuliwa kusafirisha bidhaa kuanzia kufika kwake na meli hadi Nairobi. Gharama zinazohusishwa na bandari kwa bidhaa za gharama za chini kama vile mali ghafi za viwanda au nafaka, ambayo hujumuisha sehemu kubwa na mizigo inayoingi abandarini, inaweza kuwa zaidi ya asilimia 15 ya thamani yake sokoni. Na gharama hii kwa biashara na watumizi wa bidhaa huzidishwa na kutotabirika kwa muda wa uwasilishaji kutokana na kutoautiana kwa utenda kazi bandarini. Ada za malori makubwa katika eneo hili pia huwa juu sana. Ni ghali kusafirisha kasha kutoka Mombasa hadi Kampala kuliko ilivyo kusafirisha kasha lilo hilo kutoka Japan hadi Mombasa kwa kutumia meli. Fauka ya hayo, KRA huwa na mfumo wa utoaji leseni mara mbili kwa malori ambao hutaka wale wanaoidhinishwa kubeba tu bidhaa zinazopitia
nchini, wasirejee katika taifa lao asili na mizigo yakuagizwa, maana yake ni kwamba sharti warudi makasha yakiwa matupu. Hii huongeza zaidi gharama ya uendeshaji shughuli katika mataifa nje ya mipaka ya Kenya. Kusambaratika kwa mfumo wa reli kumepeleea idadi kubwa ya safari za malori makubwa ndani na katika maeneo yaliyo karibu na bandari. Ni ghali zaidi kusafirisha kasha kutoka Mombasa hadi Kampala kuliko ilivyo kusafirisha kasha lilo hilo kutoka Japan hadi Mombasa kwa kutumia meli
Kijisanduku 2: Bandari Kabaila ni gani?
Mfumo ulio maarufu sana duniani wa kusimamia bandari ni ule wa bandari kabaila, ambao sekta ya umma, katika hali ya Mombasa Halmashauri ya Bandari za Kenya, hujiondoa kutoka shughuli za mbele za kushughulikia mizigo, na kuwapatia wawekezaji wa kibinafsi jukumu hilo.Halmashauri ya bandari huangazia mambo mengine makuu ya ustawishaji wa bandari kama vile usimamizi wa nyumba, uelekezi na mipango. Mfumo huu hutumiwa sana Ulaya, Amerika na Asia. Ni mbinu inayokumbatiwa mfumo ambao pia unakumbatiwa Afrika, lakini haujaanza kutumiwa sana.Kwa ufasaha, katika hali nyingi, hatua ya kwanza katika kuelekea njia hii huwa ni kujiondoa kwa halmashauri ya bandari kama msimamizi wa shughuli za mizigo katika vituo vya mwisho na kukubali kampuni ya kibinafsi ichukue usukani na usimamizi.Shughuli hii ya kukabidhi jukumu la usimamizi imelenga kutumia utaalamu unaotolewa na wasimamizi wa vituo vya mwisho wa kimataifa. Serikali ya Kenya iliahidi kubadilisha bandari ya Mombasa kuwa bandari kabaila kufikia mwaka 2002, lakini hakujakuwa na hatua zozote zilizopigwa katika utekelezaji wa wazo hili mbali na uamuzi wa sasa wa kuendelea kukabidhi usimamizi bandari 11‐14. Jedwali 2 linaeleza baadhi ya matokeo ya kupendeza yaliyopatikana nchini Nigeria na Ghana, mataifa ambayo yamekumbatia muundo wa bandari kabaila.
3. Siku za Usoni za Bandari ya Mombasa – Ajenda ya Utekelezaji erikali ya Kenya inafaa kuchukua hatua sasa na kutekeleza mageuzi ya usimamizi ambayo yanahitajika sana na kutekeleza ahadi yake ya kugeuza bandari ya Mombasa kuwa bandari kabaila. Ni muhimu kwamba mageuzi yatekelezwe kabla au sambamba na uwekezaji mkubwa
katika miundo msingi. Muundo uliochangamana wa bandari, ambapo idara mbalimbali za serikali huhusika moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, umekuwa changamoto kuu katika masuala kuu ya usimamizi wa bandari. Katika Bandari ya Mombasa, ni kikwazo kikuu katika utayarishaji wa mfumo shirikishi wa upanuzi wa bandari na mageuzi. Katika miaka ya hivi majuzi, badnari kadha za Afrika zimeanza mageuzi ya bandari. Nigeria imeongoza katika mageuzi Afrika ikiwa na alama 80 (kati ya 100) ikwia ni ishara ya kuimarika katika sheria, ubadilishaji wa muundo wa usimamizi, ufuatilizi wa sera na kuhusishwa kwa sekta ya kibinafsi. Kenya kwa upande mwingine ina alama 40, ikiwa ya tatu kutoka taifa linalovuta mkia Afrika.6 Jedwali 2: Mageuzi ya bandari yanawezekana: mifano kutoka Afrika na Mashariki ya Kati.Vitendo vya mageuzi Matokeo Nigeria
Kukumbatiwa kwa mfumo wa bandari kabaila mwaka 2006
‐Mfumo wa sera unaoangazia Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Kibinafsi ‐Uwekezaji wa kibinafsi unaopangiwa Dola za Kiamerika $ 500m (asilimia 55 ya jumla ya uwekezaji wa sekta ya kibinafsi katika bandari za SSA ) ‐ Halmashauri ya Bandari ya Nigeria sasa inajisimamia kifedha ‐ Wahudumu wa kibinafsi watailipa serikali ada za matumizi/ukodishaji za jumla ya Dola za Kiamerika $ 5 ‐ Kupunguzwa kwa msongamano kuliwezesha uchumi wa Nigeria kuokoa Dola za Kiamerika $310 milioni miezi michache tu baada ya halmashauri kujiondoa kwenye usimamizi ‐ Kuimarika kwa muda unaotumiwa na meli na mizigo ‐ kuimarika kwa ushughulikiaji wa mizigo
Ghana
Kukumbatiwa kwa mfumo wa bandari kabaila mwaka 2007
‐ Ustawishaji uliofanywa kwa kutilia maanani mahitaji ya kitaifa nay a mataifa jirani chini ya mradi wa ‘Lango kuu la Ghana.’ ‐ Ongezeko la mizigo ya kitaifa na ile inayopitia nchini ‐ Upigaji hatua katika kutoa huduma zenye ushindani kuambatana na viwango vya kimataifa
Aqaba, Jordan
Ukabidhi wa usimamizi wa vituo vya mwisho na kuanzishwa kwa mfumo wa kielektoronini wa Kudhibiti Malori Makubwa mwaka 2005 ili kuratibu malori yanapingia na kutoka bandarini.
‐ mfumo ulitekelezwa katika muda wa miezi 3. ‐ gharama za uchumi kuingia bara zilishuka kwa asilimia 25. ‐ asilimia 25 ya mizigo zaidi huweza kusafirishwa na idadi ile ile ya malori.
Asili: Makadirio ya wafanya kazi wa benki ya Dunia
6 ‘Kipimo cha mageuzi ya Bandari’ kitolewa katika mkutano wa kuichunguza miundo misingi ya kitaifa barani Afrika, Benki ya Dunia, 2009. Tangu takwimu hizi kukusanywa kuna uwezekano kuwa Kenya imepoteza alama zake kwa sababu kumekuwa na mageuzi muhimu nchini Senegal, Angola na Benin, mataifa yote yaliyokuwa yameorodheshwa nchini Kenya.
‐ 17 ‐
‐ 18 ‐
Matokeo ya mageuzi Afrika na katika maeneo mengine yanafaa kuwa zaidi ya ishara za manufaa ya kuridhisha. Mwaka 2006, Nigeria ilikumbatia mfumo unaopendelewa kimataifa wa bandari kabaila. Ghana ilikumbatia mfumo huo mwaka 2007, huku mageuzi ya bandari yakiwa yamepewa kipaumbele katika ajenda ya sertikali inapojitayarisha kuanzisha lango lisilo na vizuizi la mizigo kwa mataifa mengine. ‘Orodha ya Mageuzi ya Bandari’ imetolewa katika Udadisi wa Miundo Misingi ya Mataifa ya Afrika, Benki ya Dunia, 2009. Tangu kukusanywa kwa takwimu hizo, kunauwezekano kwamba Kenya imepoteza nafasi zaidi kwa kuwa kumekuwa na mageuzi makuu nchini Senegal, Angola na benin, mataifa ambayo yaliorodheshwa nyuma ya Kenya. Mnamo 2004, mradi wa ustawishaji uchumi uliigharimu Jordan mabilioni ya dola uliangazia kuiamrisha bandari yake ya pekee Aqaba. Sekta ya usafirishaji mizigo ilikuwa inafanya kazi duni sana kutokana na mfumo wa zamani wa taifa hilo wa kusimamia safari barabarani ambao ulidhibitiwa sana, kugawanywa na uliokosa vishawishi. Mfumo wa elektroniki wa udhibiti wa malori ulibadilisha hali kabisa, na ulitekelezwa katika muda wa miezi 3. Kwa pamoja, ulileta mhudumu wa kibinafsi, kwanza kupitia kandarasi ya usimamizi ya miaka miwili ba baadaye mkataba wa kukabidhiwa usimamizi kabisa, na kuiamrisha utenda kazi wa bandari bila ya kuwa na uwekezaji wowote mpya kwenye miundo msingi. Matokeo ya mageuzi haya yameorodheshwa kwenye Jedwali 2. Serikali pia inahitaji kuwa na lengo wazi katika bandari ya Mombasa. Ingawa bandari hii ina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha ushindani wa biashara za Kenya, na kufanikisha ufungamano wa eneo la Afrika Mashariki, huwa haitajwi sana katika ruwaza ya maendeleo ya serikali ya mwaka 2030. Ingawa malengo ya kufanya mageuzi katika bandari huenda yakawa tofauti na huhusisha haja ya kupanua na kustawisha uwezo wa kushughulikia makasha, kuzalisha mapato na kupunguza matumizi ya fedha za umma pamoja na kusisimua ukuaji wa uchumi wa
uchumi wa usambazaji ulioelekezewa macho katika bandari iliyo kitovu cha eneo, serikali inafaa kuwa wazi zaidi kuhusu lengo lake hasa. Kenya haitimizi mahitaji.Katika muda ambao serikali imetumia kuutengeneza upya mpango mkuu wa bandari ya Mombasa, Dubai Wrld imejenga kituo cha mwisho kipya Doraleh katika eneo mpya kabisa nchini Djibouti. Kituo hicho cha Djibouti kina uwezo wa TEU 1.2 milioni kila mwaka na kwa sasa ndicho kikubwa zaidi na cha kisasa Afrika Mashariki. Katika muda huo, Nigeria ilikabidhi usimamizi wa bandari kadha kwa wasimamizi wa kibinafsi. Mpango Mkuu wa Bandari wa KPA wa mwaka 2004 ulitengenezwa upya 2009. Mpango huo Mkuu haukuangazia vyema uhusiano kati ya miundo msingi na usimamizi uliohitajika ili kuibadili Mombasa kuwa bandari ya hadhi ya dunia. Na haukuangazia mabadiliko mengi ya kitaasisi, usimamizi na kisheria ambayo yanahitajika. Ilipendekeza miradi kadha ya kipindi kifupi, inayofaa kukamilishwa mwaka 2013, na miradi ya kipndi kirefu ya hadi miaka 2015 na 2030. Mapendekezo ya kipindi kifupi yalikuwa pamoja na kukabidhi usimamizi wa bandari 11‐14 kwa wahudumu wa kibinafsi ili kuongeza uwezo wa kushughulikia makasha zaidi na ujenzi wa kituo cha pili cha mwisho chenye uwezo wa TEU 700,000 kila mwaka (kinachofaa kusimamiwa na sekta ya kibinafsi) na kuzolewa taka kwenye mlangobahari ili kuwezesha kuhudumiwa kwa meli kubwa. Mipango ya kipindi kirefu ya ustawishaji ilijumuisha ujenzi wa barabara unganishi ya Mombasa ya kuunganisha njia kuu ya kaskazini na eneo la pwani kusini na Tanzania kaskazini. Mfumo wa vishawishi ukiunganishwa na uimarishaji katika usimamizi unafaa kutekelezwa sasa ili kuiwezesha bandari ya Mombasa iende sambamba na mahitaji kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo kipya. Kenya na eneo hili kwa jumla haiwezi kungoja kwa miaka 2‐3 ili kituo kipya cha kushughulikia makasha kikamilishwe bila kuathirika kiuchumi. Uwezo wa bandari unaweza
‐ 19 ‐
kuongezeka sana katika kipindi kifupi kwa kutoa mfumo wa vishawishi na kuwatia moyo wadau katika bandari kwa mfano huduma za benki na idara zote za serikali, zianzishe utoaji huduma maasaa 24 kila siku. Kadhalika, utekelezaji wa PCBS unafaa kuharakishwa. Vile vile, mfumo wa kudhibiti malori, sawa na ule unaotekelezwa nchini Jordanunaweza kuimarisha ushughulikiaji wa mizigo na kuongeza uwezo. Utekelezaji wa mifumo kama hiyo ya IT itakayotumia programu za kompyuta unafaa kupimwa kwa miezi na wala si miaka kama hali ilivyo Mombasa. Serikali ya Kenya inakabiliwa na shughuli ghali sana, inayochukua muda mwingi na inayosumbua sana ikiwa mabadiliko hayatafanywa katika taasisi na usimamizi kwa sasa, sambamba na mipango ya upanuzi na ukabidhi wa usimamizi wa bandari 11‐14. Juhudi za awali zilizofeli za kuhusisha kikamilifu sekta ya kibinafsi katika shughuli za bandari na uwekezaji ni ushahidi tosha wa haya. Mageuzi katika KPA hayatafanikiwa kabisa ikiwa hakutakuwa na mageuzi yatakayotekelezwa pamoja aktika shughuli za forodha na idara nyingine za serikali bandarini ili kulainisha shughuli zake. Mabadiliko katika majukumu ya baadhi ya idara, huenda yakahitaji marekebisho katika sheria ambazo zilibuni idara hizo. Hakuwezi kuwa na mpango mahsusi wa bandari hadi majukumu ya umma na sekta ya kibinafsi yaelezwe bayana na kukosa kufanya hivi kunaweza kuathiri vibaya ukabidhi wa usimamizi wa bandari 11‐ 14. Hakuwezi kuwa na mpango mahsusi wa bandari hadi majukumu ya umma na sekta ya kibinafsi yaelezwe bayana na kukosa kufanya hivi kunaweza kuathiri vibaya ukabidhi wa usimamizi wa bandari 11‐ 14. Kusongesha mpaka kati ya serikali na wahudumu wa kibinafsi huhitaji matayarisho ya mikakati, kufafanuliwa upya kwa mamlaka na majukumu, na mabadiliko ya kisheria kabla ya kuandaliwa kwa shughuli ya utoaji tenda. Kukosa kufaulu wka mpango wa ukabidhi wa usimamizi kunaweza kuweka kufanya vigumu mapendekezo ya uwekezaji wa sekta ya kibinafsi bandarini siku za usoni pamoja na kuzidisha matatizo yaliyoko sasa.
Uwazi kuhusu jukumu la siku za usoni la KPA unahitajika. Ahadi ya serikali kwamba itabadilisha bandari kuwa bandari kabaila ni kidokezo kuwa KPA itajiondoa kutoka shughuli za mbele na msururu mwingine wa ukabidhi wa usimamizi wa vituo vya mwisho vinavyosimamiwa na KPA kwa sasa utafanyika. KPA ambayo hudhibitiwa na serikali, kwa sasa humiliki miundo msingi mingi bandarini na hutekeleza shughuli nyingi bandarini. Mabadiliko katika jukumu la KPA kutoka kwa mtoaji huduma bandarini na kuwa kabaila na mdhibiti yatakuwa shughuli ngumu ya kubadilisha usimamizi. Yatahitaji ujuzi mpya, uwezo wa taasisi, na shughuli zikiwemo udhibiti wa haki na ushindani unaofaa, kutayarisha na kujadiliana kuhusu kandarasi na wahudumu wa kibinafsi wa huduma za bandari, uchunguzi wa utenda kazi na kuhakikisha kufuatwa kwa viwango vilivyowekwa. Uamuzi kuhusu barabara ya pembeni ya Mombasa unahitajika sasa. Mji wa Mombasa unakabiliwa na mkingamano na njia ya kuelekea uwanja wa ndege wa Mombasa itazibwa ikiwa kazi haitaanza barabara mpya ya pembeni na ya kuunganisha haitaanza mara moja. Ikiwa ujenzi wa barabara hiyo ya pembeni hautaharakishwa na kuoanishwa na uongezaji wa uwezo unaopangwa katika bandari (kupitia ukabidhi wa usimamizi na upanuzi), msongamano utakuwa tatizo kubwa kuliko ilivyo sasa, na uwekezaji mpya hautafanikiwa. Vile vile serikali inafaa kuangazia barabara mpya ya kufiki bandarini na kuiunganisha na barabara ya pembeni la sivyo uwezo wote mpya wa bandari utaendelea kupitishwa katikati wa jiji, eneo ambalo tayari linakabiliwa na msongamano. Jambo la kusikitisha ni kwamba, wastawishaji aktika sekta ya kibinafsi ambao kwa sasa wanataka kuishirikisha serikali katika masuala haya yenye umuhimu mkubwa hujipata wakilazimika kushauriana na KPA, Wizara ya uchukuzi na Wizara ya Barabara. Hii hufanya mipango ya mikakati ya vipindi virefu kuwa ngumu kukiwa hakuna msimamo wa pamoja kuhusu jinsi miradi binafsi huhusiana na mingine. Mipango ya kustawisha bandari ya
‐ 20 ‐
Mombasa sharti iangazie mbali na kuiamrisha miundo msingi ya sasa ya bandari na kuendeleza juhudi zilizoratibiwa kwa pamoja za kuimarisha mifumo ya babara na reli ambayo huunganisha bandari na Njia Kuu la Kaskazini na masoko katika mataifa jirani. KPA sharti iwe bila uingiliaji wa kisiasa na mameneja wakurugenzi wawe wakiteuliwa kwa kandarasi utenda kazi katika usimamizi za miaka 3 kupitia njia ya wazi na ushindani. Katika kipindi cha miaka KPA tangu kubuniwa kwa KPA, imekwua na mameneja wakurugenzi 14. Katika kipindi sawa na hicho, Halmashauri ya ya Bandari ya Tanzania imekuwa na 3. Ukosefu wa uthabiti katika uongozi wa KPA si hauwezi kupelekea mipango bora na mageuzi. Kwa uhalisia, serikali inafaa kuendesha shughuli ya kimataifa ya kumtafuta na kumteua mtu aliyehitimu. Maslahi finyu ya wachache yamezuia uwekezaji na mageuzi katika bandari ya Mombasa kwa miaka mingi.Changamoto nyingi zilizoorodheshwa kwenye ripoti hii pamoja na mageuzi yanayohitajika, vyote vinajulikana vyema. Kilicho kipya ni kukithiri kwa tatizo. Uwekezaji wa sekta ya kibinafsi ambao ungepelekea kubuniwa kwa nafasi mpya za kazi kwa wakazi, utenda kazi bora wa bandari na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hili, umezuiwa na maslahi finyu ya wachache wanaolenga kuendeleza hali ilivyo kwa sasa ili waendelee kunufaika.Mfano ni mipango ya kujenga kituo kipya cha kusimamia mbolea bandarini, ambacho kingepelekea kusuka kwa gharama ya mbolea katika eneo hili, haijaendelea kutokana na uingiliaji na kukataa kwa maafisa.Wengi wa wastawishaji na wafadhili juondoka bila kufanya lolote. Na ingawa miungano ya wafanya kazi na wafanya kazi wake huenda ina haki ya kuogopa kuachishwa kazi kwa baadhi, hatua hii inafaa kutazamwa katika uktadha wa wa mipango ya serikali ya kupanua bandari na hali nyanjani kwa sasa. Kwa mfano, licha ya hofu kuelezwa, kukabidhiwa wka usimamizi wa bandari katika sehemu nyingine duniani umepelekea ongezeko la jumla la nafasi za kazi na faida aktika bandari na viwanda husika.Changamoto
nyingi zilizoorodheshwa kwenye ripoti hii pamoja na mageuzi yanayohitajika, vyote vinajulikana vyema. Kilicho kipya ni kukithiri kwa tatizo. Nia nzuri ya kisiasa, na uwazi katika mamlaka ya kutekeleza mageuzi inahitajika. Ingawa Wiizara ya Uchukuzi ndiyo idara inayoongoza katika bandari ya Mombasa, haijaweka uwezo mkuu wa uendeshaji shughuli ili kufanikisha mageuzi bandarini na katika usimamizi.Aidha huwa haiwakilishi maslahi ya wote wanaohusika katika shughuli za bandari. Uendehaji shughuli, usimamizni na upanuzi wa bandari ya Mombasa utahitaji msimamo wa serikali usiogawanyika na taasisi yenye nguvu ya kuratibu na kutekeleza mageuzi yanayohitajika. Mukhtasari wa mageuzi makuu ambayo serikali inafaa kutekeleza ili kuimarisha utekelezaji shughuli bandarini unatolewa hapa chini: Kijisanduku 3: Mukhtasari wa mapendekezo makuu ya
mageuzi bandarini
Katika miezi 3 hadi 6 ijayo • Tambua taasisi ya kuratibu na ambayo itakuwa na mamlaka ya kutekeleza mageuzi. • Teua meneja mkurugenzi wa KPA kwa kandarasi ya utenda kazi ya miaka 3. • Amua kuhusu njia ya pembeni ya Mombasa na anza utekelezaji pamoja na barabara ya kuiunganisha na bandari. • Anzisha mfumo wa vishawishi kuwezesha uendeshaji shughuli wa masaa 24 bandarini miongoni mwa wadau mbalimbali • Tekeleza Mfumo wa Habari na Teknolojia (IT) Bandarini wenye Msingi katika Jamii. • Idhinisha ukabidhi wa usimamizi wa bandari 11‐14 kupitia shughuli zenye ushindani na kwa uwazi.
Katika miezi 6 hadi 12 ijayo • Eleza bayana ratiba ya utekelezaji wa bandari kabaila pamoja na jukumu la KPA. • Eleza bayana jukumu na mamlaka ya washika dau wa umma na kibinafsi bandarini. • Tekeleza mageuzi katika ukusanyaji wa forodha, na kuufanya uwe bora zaidi na ulio na uwazi. • Tia nguvu uwezo wa Wizara ya Uchukuzi wa kuendesha shughuli zake bandarini.