32
Draft 03 MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MWENGE MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA MAENDELEO YA KANISA 2013-2017

MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

  • Upload
    vankhue

  • View
    959

  • Download
    25

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

i

MWENGE

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO

MWENGE

MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA

MAENDELEO YA KANISA 2013-2017

Page 2: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

ii

YALIYOMO

1. UTANGULIZI ....................................................................................................................... 1

1.1 Lengo kuu .................................................................................................................... 1

1.2 Historia kwa ufupi ....................................................................................................... 1

1.3 Malengo ya mkakati .................................................................................................... 2

Rasilimali za Kiroho ........................................................................................................... 4

1.3.2 Rasilimali Watu ................................................................................................... 5

1.3.3 Rasilimali Fedha .................................................................................................. 6

1.3.4 Rasilimali Miongozo ............................................................................................ 6

1.3.5 Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu ................................................. 7

1.3.6 Miradi mikuu ya ujenzi ........................................................................................ 7

2. DHIMA, DIRA, NA KAULI MBIU ................................................................................ 8

2.1 Dhima (Mission) ......................................................................................................... 8

2.2 Dira (Vision) ............................................................................................................... 8

2.3 Kauli mbiu (Mission Statement) ................................................................................. 8

3. MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KUANZIA 2013-2017 .......................... 8

3.1 Mfumo wa uongozi ..................................................................................................... 8

3.2 Idadi ya washiriki na Makisio ya ukuaji wa kanisa kuanzia 2005-2020 ..................... 9

3.3 Mambo muhimu (Key issues) ................................................................................... 10

3.4 Mikakati ya kukabili changamoto zilizoainishwa ..................................................... 11

4. MAENEO YA UTEKELEZAJI KIMKAKATI .............................................................. 11

4.1 Uwakili ........................................................................................................................... 11

4.2 Huduma za Kanisa ......................................................................................................... 12

4.3 Elimu .............................................................................................................................. 12

4.4 Vijana ............................................................................................................................. 12

4.5 Shule ya Sabato .............................................................................................................. 12

4.6 Huduma za watoto .......................................................................................................... 13

4.7 Afya ................................................................................................................................ 13

4.8 Kwaya za Kanisa na vikundi vya uimbaji ................................................................. 13

4.9 Ofisi ya Karani wa Kanisa ............................................................................................ 13

4.10 Mawasiliano ................................................................................................................. 14

4.11 MIUNDO MBINU (Majengo ya kanisa, vyoo, viwanja).......................................... 14

4.11.1 Hali ilivyo sasa ................................................................................................... 14

Page 3: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

iii

4.11.2 Maboresho ya Miundombinu (Majengo, Viwanja) ........................................... 14

4.11.3 Uboreshaji wa mandhari ya eneo na Jengo la Kanisa (Mwenge) ..................... 14

................................................................................................................................... 15

4.11.3.1 Faida na Hasara za mapendekezo ya upanuzi wajengo la kanisa la sasa.... 15

4.11.4 Ujenzi wa Jengo la matumizi anuai ................................................................... 16

4.11.5 Majengo Kanisa Makundini ............................................................................... 16

4.11.6 Ukarabati wa nyumba ya mchungaji .................................................................... 17

4.11.7 Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi makao mapya ya ETC ................................... 17

5. MIKAKATI YA KUPATA FEDHA KWAAJILI YA MIRADI YA MAJENGO .......... 17

5.1. Kuanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa ................................................. 17

5.2 Kikosi kazi cha watu 100-200 .................................................................................. 18

5.3 Washiriki wote wa kanisa kuhusishwa...................................................................... 18

5.4 Changizo kutoka watu wa nje ya kanisa kwa njia ya harambee ............................... 18

6. RAMANI YA UTEKELEZAJI ........................................................................................ 19

6.1 Ramani yaa kila mwaka ya utekelezaji wa mpango mkakati ......................................... 19

6.2 Ramani ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa mwaka 2013 ................................. 21

7. BAJETI YA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI ..................................................... 23

8. VIELELEZO NA VIAMBATANISHI ........................................................................... 26

8.1 Ramani ya upanuzi wa Kanisa (Sehemu za office .................................................... 26

8.2 Picha au mtazamo wa kisanifu katika picha za pande tatu (3D Views photos) ........ 28

Page 4: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

1

1. UTANGULIZI

Mpango ni mfumo wa kimaandishi unaoonesha kazi zinazotakiwa kufanywa na hatua

mbalimbali za kufikia malengo yaliyowekwa kwa muda maalumu. Mpango mkakati husaidia

ufanisi katika utekelezaji na kuweka mpangilio mzuri wa matumizi ya rasilimali. Pia husaidia

kuratibu kazi zote ili kufikia malengo kwa kuweka vipaumbele. Ni muhimu sana kuwa na

mpango mkakati kwa kuwa utatupatia mwelekeo wa ni wapi tunataka kwenda na tutafika

kwa namna gani. Shughuli mbalimbali na maeneo ya kimkakati huwekwa bayana, hii

inasaidia kufahamu nyenzo na raslimali zinazohitajika na namna ya kuzipata. Ugawaji wa

majukumu na dhamana miongoni mwa viongozi au washiriki ni moja ya faida za kuwa na

mpango kazi. Mipango mkakati huwezesha kufanya tathmini kuona kama malengo na

mipango tuliyojiwekea imefanikiwa au haikufanikiwa kama ilivyopangwa.

Kanisa la Mwenge limekuwa na mipango ya muda mfupi mfupi hususani kila mwaka, hali

ambayo haiwezi kutoa dira endelevu kwa kanisa. Hivyo mpango huu ni hatua muhimu katika

kulipatia kanisa dira ya kuliongoza katika mipango mbalimbali bila kujali mabadiliko ya

uongozi yanayofanyika kila mwaka. Hii italiwezesha kanisa kuwa na mipango endelevu

itakayokuwa ikitekelezwa na kila uongozi unapoingia madarakani wakati wa uhai wa

mpango husika.

1.1 Lengo kuu

Lengo kuu la mpango mkakati huu ni kuliongoza katika uendeshaji wa majukumu yake

makubwa ambayo ni: malezi ya washiriki kiroho, uinjilisti, uwakili na majengo kwa kuweka

malengo mahususi na namna ya kufikia malengo hayo ifikapo mwaka 2017.

1.2 Historia kwa ufupi

Kanisa la Waadventista wa Sabato Mwenge ni miongoni mwa makanisa mengi ya

waadventista wa Sabato Tanzania ambalo liko katika eneo la Mwenge, kando kidogo mwa

barabara mpya ya Bagamoyo, likipapakana na zahanati ya Mwenge kijijini wilaya ya

Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Kanisa lilianza mwaka 1967 likiwa ni tawi la Shule ya Sabato Lugalo Sergeant Mess. Tawi

liliendelea hadi mwaka 1980 lilipopewa hadhi ya kuwa Kundi la Shule ya Sabato. Kutokana na

matatizo yaliyojitokeza ya kutokuwa na uhuru wa kuingia eneo la jeshi kufanya ibada, mwaka 1981

likawa ni kundi la Kanisa la Magomeni na kuendelea kukua hadi Juni mwaka 1985

lilipotengwa rasmi kwa kupewa hadhi ya kuwa Kanisa kamili na hivyo kutambuliwa rasmi

kuwa miongoni mwa makanisa mahalia ya Waadventista wa Sabato ulimwenguni. Kanisa

liliendelea kukua kwa kuanzisha makundi ambayo nayo yalitengwa kuwa makanisa.

Makanisa ambayo ni zao la Mwenge ni pamoja na Ushindi, Bagamoyo, Lugalo, Tegeta,

Mbezi Beach, Mbezi juu, Kerege na Bunju. Kwa sasa Kanisa lina makundi 7 ambayo ni:

Bumafa, Chivilikiti, Mabwepande, Zinga, Amani, Kimele na Vikawe; pia kuna tawi moja la

shule ya Sabato katika shule ya sekondari ya Lord Barden. Hadi kutengwa kuwa Kanisa,

Kanisa halikuwa na nyumba ya kuabudia, hivyo juhudi zilifanyika za kutafuta kiwanja na

Page 5: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

2

hatimaye kiwanja kilipatikana eneo la Mwenge na ujenzi kuanza rasmi mwaka 1989; jengo la

Kanisa kwa wakati huo lilisanifiwa kuwa na uwezo wa kuchukua waumini 900 wakiwa

wamekaa, ujenzi uliendelea hadi mwaka 2000 ulipokamilika.

Baada ya shughuli za ujenzi kukamilika, utaratibu wa kuliweka wakfu ulifanyika. Tarehe 22-

12-2002 jengo la kanisa liliwekwa wakfu rasmi; huduma hiyo ilifanywa na Mchungaji Dr.

Herry Mhando.

Idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka licha ya washiriki wengine

kuhamia makanisa mengine, idadi ya washiriki hadi kufikia Juni mwaka 2012 ilikuwa ni

2,330.

1.3 Malengo ya mkakati Kwa kipindi cha kuanzia 2013 – 2017 kanisa linaazimia kuwa na maeneo makuu ya

kimkakati yafuatayo:

A: Rasilimali za kiroho

Lengo #1: Kuongeza washiriki kwa 100% ifikapo 2017

Lengo #2: Makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 (Zinga,

Mabwepande, Kimele, na Bumafa)

Lengo #3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo

mwaka 2017 au baadaya 2017

Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo

2017

Lengo #5: Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana

kuhusiana na mtindo na mwenendo wa maisha ya ki-adventista

katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na

maburudisho.

B: Rasilimali watu

Lengo #1: Kuelimisha Wainjilisti Walei 15 wanaoweza kutumwa kama

wainjilisti ifikapo mwaka 2017.

Lengo #2: Kusomesha wanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo

mwaka 2017

Lengo #3: Kuhakikisha kuwa asilimia tisini (90%) ya wahubiri

wawe na elimu ya homilia ifikapo mwaka 2017

C: Rasilimali fedha

Lengo #1: Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango

inaongezeka mara tatu zaidi ya miaka ya nyuma ifikapo 2017

Lengo #2: Kuwezesha asilimia sabini (70% ) ya washiriki wasio na ajira na wale wenye

kupenda kujianjiri na kuanzisha biashara wawe na elimu ya ujasiriamali ya

ujasiliamali ifikapo 2017.

Page 6: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

3

D: Rasilimali miongozo

Lengo: Kuhakikisha kuwa 100% ya washiriki wanafundishwa na kuelewa misingi 28 ya

kanisa; waumini na viongozi wawe wamefundishwa kufuata sera na taratibu za

kanisa, na washiriki wawe ameelimishwa kuhusu utumiaji wa maandishi ya Roho

ya unabii ifikapo 2017.

E: Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu

Lengo: Kuhakikisha vitabu 20,000 vinanunuliwa na kusambazwa.

F: Miradi mikuu ya ujenzi

Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa

majengo ya ibada makundini.

Lengo #2: Kukarabati nyumba ya mchungaji

Lengo #3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao mapya ya ETC.

Lengo #4: Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii

Kwa kila eneo la kimkakati malengo mahsusi yameainishwa katika jedwali hapa chini.

Page 7: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

4

Rasilimali za Kiroho

MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA

Lengo 1: Kuongeza washiriki kwa 100%

ifikapo 2017

Washiriki wa makundini wote

wamejumlishwa

Semina za uinjilisti kwa washiriki –kanisani na makundini

mara moja kila robo

Unijilisti kwa njia ya machapisho ikihusisha masomo kwa njia

ya sauti ya unabii, vitabu, vijizuu na magazeti.

Mikutano ya injili ya hadhara mitatu kwa mwaka, mmoja

ukifanyika kupitia radio ya Morning Star 105.3 FM.

Uinjilisti kupitia shule ya sabato: o Vikosi vya shule ya sabato

o Sabato za wageni

o Kuanzisha matawi ya kujifunza biblia kwa kaya zilizo karibu na

kuhusisha wasio washiriki pia.

Elimu ya dini shuleni-vipindi vya dini (uinjilisti na malezi)

o kufikia kila shule iliyopo katika eneo letu la kiutawala

kuimarisha utaandaaji {kila idara/ chama knsn kuweka mkakati wa kuongoa roho}

- Mzee wa kanisa

-Mkuu wa

huduma za kanisa

-Mkurugenzi

VOP

-Mkurugenzi wa

S/Sabato

-Kiongozi wa

uchapishaji

-Mkurugenzi wa

Elimu

-Kiongozi wa

Champlensia

-Sabato ya kwanza ya

kila mwezi

-Mwezi Aprili/Juni

na Septemba/Okt.

-Sabato ya 2 ya

robo

-kila Sabato

-Mei/Oktoba

Lengo 2: Kutenga makundi yaliyopo sasa

kuwa makanisa ifikapo 2017

(Zinga - 2013, Mabwepande -

2014, Kimele- 2015 , Bumafa-

2016, na Vikawe – 2017)

kuwaandaa washirki wa makundini kujitegemea kiroho,

kiuchumi na kijamii.

-Kiongozi wa

Kundi/mzee wa

kanisa

-Sabato ya

kwanza ya kila

mwezi.

Lengo 3:

Kuimarisha na kuyawezesha

makundi kujitegemea

ifikapo mwaka 2017 au baada

ya hapo.

Kuyajengea uwezo wa wa kuimarika, makundi mapya yaanzishwe

pale tu inapobidi. Hii itatupati fursa ya kuyahudumia vyema

makundi yaliyopo sasa kwa kuyawezesha kuwa na nyumba za

ibada zilizokamilika na zenye kuleta utukufu kwa Mungu.

Wazee wa

kanisa/Mchungaji

Mara moja kila

robo

Page 8: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

5

Lengo 4: Kuwa na 60% ya washiriki

wanaosoma Biblia na Lesoni

ifikapo 2017

kuwatembelea washiriki nyumbani. kila mshiriki atembelewe

angalau mara moja kwa mwaka.

kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa lesoni kwa njia

tofauti,,,mpesa kwa fue

[[kila idara/chama itengeneze mkakati itakavyohusika na

mpango]]

Wazee wa kanisa

/mashemasi/... /…

/SS, utandaaji/

huduma

Kila sabato

kupitia vipindi

vya mchana

Lengo 5: Kuhakikisha kuwa 70% ya

washiriki wana ufahamu mpana

kuhusiana na mtindo na

mwenendo wa maisha ya ki-

adventista katika nyanja za afya,

elimu, vyakula na vinywaji, na,

maburudisho.

Semina, mafundisho, na mahubiri

- semina mara moja kwa mwezi muda wa mchana

Wazee wa kanisa

/Mchungaji/

Kila sabato

kupitia vipindi

vya mchana

1.3.2 Rasilimali Watu

MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA

Lengo 1:

Kuelimisha wainjilisti walei 15

wanaoweza kutumwa kama

wainjilisti ifikapo 2017.

Kuimarisha mfuko wa uinjilisti hasa kwenye eneo linalohusu

udhamini wa mafunzo ya uinjilisti.

Mchungaji wa

Mtaa

N/A

Lengo 2:

Kusomesha mwanafunzi wawili

elimu ya uchungaji ifikapo 17.

Kutenga sehemu kidogo kutoka katika bajeti ya kanisa

Kutumia washiriki wa kanisa kuchangisha pesa

Mchungaji wa

Mtaa

Mratibu wa

mpango

atakayechaguliwa

na uongozi wa

kanisa

N/A

Lengo 3:

90% ya wahubiri wawe na elimu

ya homilia ifikapo 2017

Semina ifanyike mara moja kwa mwaka

Mchungaji wa

Mtaa

Mara moja au

mbili kwa mwaka

Page 9: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

6

1.3.3 Rasilimali Fedha

MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA

Lengo 1

Kuhakikisha idadi ya washiriki

wanaorudisha zaka na wanaotoa

kwa mpango inaongezeka kwa

asilimia hamsini (50%) ya

washiriki.

Mafundisho/mahubiri/Semina za zaka na sadaka kila mwezi (wiki

ya mwisho)

Kiongozi/Katibu

wa Uwakili na

Maendeleo

kanisani

Mchungaji

Wazee wa

kanisa

Mara moja kila

mwezi. Wiki ya

mwisho ya kila

mwezi

Lengo 2

Kuwezesha 70% ya washiriki

wasio na ajira wawe na elimu ya

ujasiliamali na wale wanaopenda

kuanzisha na kuendeleza biashara

wawe na elimu ya ujasiriamali.

Washiriki wa ndani watumike kufundisha mara moja kwa kila robo

na utaratibu maalumu uwekwe kuratibu semina hizo.

ATAP wahusishwe katika kufanikisha azima hii

Kiongozi/Katibu

wa Uwakili na

Maendeleo

kanisani

Kiongozi wa

ATAP

Mara mbili kwa

kila mwaka

1.3.4 Rasilimali Miongozo

MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA

Lengo: 1

Kuhakikisha kuwa 100% ya

washiriki wanafundishwa na

kuelewa masomo muhimu

yafuatayo :

misingi 28 ya kanisa

kufuata sera na taratibu za

kanisa

utumiaji wa vitabu vya Roho

ya Unabii.

Mahubiri/mafundisho na semina zifanyike mara mbili kwa robo

Washiriki waelezwe kuhususiana na vitabu bora na vya uhakika

ambavyo havikuchakachuliwa.

Mchungaji

Wazee wa

kanisa

Kiongozi wa

Roho ya unabii

Kila sabato

kupitia vipindi

vya mchana na

pia kupitia

mahubiri ya

ibada kuu.

Page 10: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

7

1.3.5 Mradi wa kusambaza kitabu cha Pambano Kuu

MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA

Lengo: 1

Kuhakikisha vitabu 20,000

vitanunuliwa na kusambazwa.

Uhamasishaji na kila mshiriki ahakikishe amechangia angalau

vitabu 5 kila mwaka kwa miaka mitano hadi 2017.

Mkurugenzi wa

Uchapishaji

kanisani

Mara moja kila

robo ya mwaka.

1.3.6 Miradi mikuu ya ujenzi

MPANGO MKAKATI MHUSIKA MUDA

Lengo: 1

Kufanya ukarabati mkubwa wa

jengo la kanisa na kukamilisha

ujenzi wa majengo ya ibada

makundini.

Kukusanya michango kutoka kwa washiriki au familia hadi 200

watakao kuwa tayari kuchangia shilingi 1,000, 000 kila mmoja kwa

mwaka.

Kwa kutumia michango kutoka kwa washiriki wote

Changizo kutoka kwa watu mbalimbali ndani na nje ya kanisa

Kiongozi /

kamati ya

majengo

Mzee wa

kanisa

Kamati ya

uwakili-

(Maendeleo)

Endelevu hadi

lengo lifikiwe

kwa kuanzia na

mwaka 2013

Lengo: 2

Kukarabati nyumba ya mchungaji

Kutumia sehemu ya bajeti ya kanisa kadri itakavyoamuliwa na

baraza la kanisa na, au mashauri ya kanisa kulingana na mgawanyo

wa mtaa

Michango ya washiriki

Kamati ya

majengo

Mzee wa

kanisa

Wakati wowote

itakapohitajika

Lengo: 3

Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi

makao makuu mapya ya ETC.

Kutumia sehemu ya bajeti ya kanisa kadri itakavyoamuliwa na

baraza la kanisa na au mashauri ya kanisa

Michango ya washiriki

Kamati ya majengo

Mzee wa kanisa

Wakati wowote

itakapohitajika

Lengo: 4

Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa

Jamii

Kukusanya michango kutoka kwa washiriki au familia hadi 200

watakao kuwa tayari kuchangia shilingi 1,000, 000 kila mmoja kwa

mwaka.

Ramani ya jengo na michoro yote iwe tayari ifikapo Septemba

2013 (Architectural drawing, Structural drawing, Plumbing

drawings, Electrical drawings)

Kiongozi /

kamati ya

majengo

kanisa la

Mwenge

Mzee wa

kanisa

Endelevu hadi

lengo lifikiwe

Page 11: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

8

2. DHIMA, DIRA, NA KAULI MBIU

2.1 Dhima (Mission)

Dhima yetu ni kutekeleza agizo kuu la utume wa Yesu la Mathayo 28:19,20 na kushuhudia

ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 kwa watu wa mataifa yote ili wampokee Yesu

kuwa Bwana na mwokozi wao na waweze kujiunga na kanisa la Mungu la masalio

kuhudumia jamii na kujiweka tayari kwa marejeo yake mara ya pili.

2.2 Dira (Vision)

Kuwa kanisa la mfano nchini Tanzania na duniani lenye kumpenda Mungu na kushuhudia

upendo wake kwa ajili ya wokovu wa kila mmoja kabla ya marejeo yake mara ya pili

kuwachukuwa wateule wake mbinguni (Mathayo 22:37-39).

2.3 Kauli mbiu (Mission Statement)

Kutangaza injili ya milele kwa watu wote katika muktadha wa ujumbe wa malaika wa tatu

wa Ufunuo 14:6-12.

3. MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO KUANZIA 2013-2017

3.1 Mfumo wa uongozi

Kanisa la Mwenge linaongozwa na Mchungaji anayesaidiana kwa karibu na wazee wa

kanisa ambao wanawajibika kwa baraza la kanisa katika kuongoza shughuli za kila siku za

kanisa. Kikao kikubwa cha maamuzi ya mwisho ni mashauri ya kanisa ambayo ndiyo kikao

kikubwa chenye kufanya maamuzi muhimu kwa ajili ya kanisa. Muundo wa uongozi uko

kama ulivyoonyeshwa kwenye mchoro hapa chini.

Page 12: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

9

3.2 Idadi ya washiriki na Makisio ya ukuaji wa kanisa kuanzia 2005-2020

Kwa mujibu wa taarifa ya mwezi June 2012 kanisa la Mwenge lina washiriki wapatao

…………… Katika kipindi cha miaka mktano iliyopita idadi ya washiriki ilikuwa kama

ifuatavyo:

Mwaka Idadi ya washiriki

2007

2008

2009

2010

2011

June 2012

Kwa kuzingatia ukuaji wa kanisa kwa ongezeko la watani wa washiriki ………….. kwa

mwaka. Matarajio ya ongezeko la washiriki ifikapo mwaka 2020 ni washiriki wapatao

………

Hii inaleta changamoto ya miundo mbinu hasa jengo la ibada kukabiliana na ongezeko hili.

Baraza la Mashauri ya Kanisa

Baraza la Kanisa

Wazee wa Kanisa

Maofisa wasimamizi

(Karani mkuu, Mhazini, Shemasi mkuu

Maofisa watendaji

(Wakuu wa Idara za Kanisa)

Mchungaji

Page 13: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

10

3.3 Mambo muhimu (Key issues)

Ili kujiweka katika mazingira ya kujitambu na kuweka malengo na mbinu za kusonga mbele ,

mambo muhimu yameainishwa hapa chini kuonyesha uwezo wetu, udhaifu na fursa tulizo

nazo. Hii itatuwezesha kupanga na kutekeleza maeneo ya vipaumbele.

Uwezo tulionao

Washiriki

Kanisa lina idadi kubwa ya washiriki wa jinsi zote za na rika zote

Kanisa lina washiriki wengi wenye taaluma na ujuzi mbalimbali

Kanisa lina washiriki wenye uchumi mzuri kwa maana ni waajiriwa na

wafanya biashara

Kanisa lina washiriki wenye mwitikio wa kujitoa kufanya kazi ya Mungu

na kuchangia maendeleo ya kanisa katika nyanja mbalimbali

Mali za kanisa

Kanisa lina mali kadha ikiwemo viti, meza, vyombo vya meza ya Bwana, na

vyombo vya mawasiliano. Pia lina Majengo ya kanisa japo yanahitaji

kukarabatiwa na viwanja vya kanisa

Uzoefu (kuanzia mwaka 1981)

Kanisa linauzoefu wa muda mrefu wa kuanzia mwaka 1981, hii ni takribani miaka 31

Tuko mjini kijiografia

Kanisa liko sehemu nzuri kijiografia na linafikika kwa urahisi kutoka pande zote za

jiji la Dar es Salaam.

Udhaifu na changamoto

Kanisa halina mipango endelevu

Utunzaji hafifu wa kumbukumbu mbalimbali za kanisa

Mawasiliano hafifu kunasababisha muingiliano wa majukumu

Mahudhurio hafifu sana katika vipindi vya mchana

Udhaifu katika utunzaji wa wakati kwenye ibada

Udhaifu katika makabidhiano ya kazi mwisho wa mwaka,

Udhaifu katika kutayarisha na kuwasilisha taarifa kwa wakati hasa za kila robo

Mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi kwa mujibu wa taratibu zilizoainishwa na

kanuni ya kanisa.

Kushindwa kufahamu washiriki walipo, wanapoishi na uwezo wao kiuchumi

Kufuatilia michango mbalimbali itolewayo na washiriki hususani ahadi

Mahudhurio hafifu ya washiriki katika vikao vya mashauri ya kanisa

Page 14: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

11

Fursa zilizopo

Kuweka miradi ya kanisa kwenye maeneo tuliyonayo

Kuweza kutumia rasilimali watu tulionao na rasilimali walizo nazo washiriki

Tunao marafiki wetu wengi wanaoweza kutuchangia na kutusaidia

Changamoto

Kukusanya rasilimali fedha kutoka ndani na nje ya kanisa (zaka, sadaka, na

michango mingine)

Kuwafikia washiriki wote na kuwetambelea

Urasimu uliopo - tukitaka kufanya mambo yetu kwa wakati tunahitaji kupitia

utaratibu wa kirasimu kiuongozi

Mfumo wa uchaguzi – inaonekana kuwa washiriki wanachaguliwa katika nafasi

mbalimbali za uongozi ni walewale karibu kila mwaka.

3.4 Mikakati ya kukabili changamoto zilizoainishwa

Ili kukabiliana na changamoto zilizoainishwa, mambo yafuatayo yanapendekezwa:

Kutumia madarasa ya shule ya sabato kuwafikia washiriki kwa njia ya kutembeleana

Kuboresha mfumo wa uwekaji kumbukumbu wa kanisa (Database)

Kuboresha mikakati ya ukusanyaji wa fesha za kanisa hasa katika maeneo ya majengo

na uinjilisti.

Semina zitolewe kuhusiana na uchaguzi wa maofisa wa kanisa

Tuweke sehemu ya kutunza vitu na tuwaelemishe watu jinsi ya kutunza kumbukumbu

Kutoa mafunzo ya utawala kwa maofisa wa kanisa

Ili kuongeza na kuhamasisha utoaji wa zaka, sadaka na michango mingine, tangazo

kuhusiu utoaji liwekwe kwenye jalida la matangazo (Bulletin) muda wote wa mwaka

Washiriki watembelewe kuhimizwa kutoa zaka na sadaka na kufundishwa somo la

uaminifu.

Washiriki wote kuanzia kwa wachungaji, wazee wa kanisa na maofisa wote

kuhimizwa kuzingatia uwakili wa muda katika utendaji.

4. MAENEO YA UTEKELEZAJI KIMKAKATI

Kanisa litatekeleza mpango wa maendeleao unaohusisha idara zake zote za kanisa, na pia

kuweka kipaumbele maeneo maalumu ya kimkakati.

4.1 Uwakili

Uwakili ni eneo muhimu sana kwa ukuaji wa kanisa kiroho na kiuchumi kwa kuwa

unahusisha kila kitu katika maisha ya mkristo. Baadhi ya mambo muhimu katika uwakili

ambayo kanisa linapaswa kuboresha na kuongeza juhudi ni pamoja na:

Uwakili wa wakati

Kuwahi katika ibada za siku ya Sabato

Kufuata muda katika ratiba za siku ya ibada

Uwakili wa mali za bwana

Page 15: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

12

Majengo ya kanisa, viti, mazingira

Zaka na sadaka

Uwakili wa uwezo alionao mtu/mshiriki mmoja mmoja.

4.2 Huduma za Kanisa

Hudama za kanisa zinahusisha mipango inayolenga ukuaji wa kanisa kiroho na kuunganisha

baadhi ya idara katika majukumu na utendaji, hii ni pamoja na kupanga:

Mipango ya uinjilisti hususani mikutano ya hadhara

Semina za malezi ya kanisa (kiroho)

Uelimishaji kuhusiana na mambo mbalimbli ya uhai wa washiriki na kanisa kwa

ujumla.

4.3 Elimu

Katika kukabiliana na changamoto za elimu kwa watoto na vijana wetu, kanisa halina budi

kuwa na mipango madhubuti kwa ajili ya kuanzisha shule za awali hadi za sekondary. Hivyo

basi, kanisa azimia kuweka mipango ya elimu kama ifuatavyo:

Kuanzisha shule ya chekechea

Kuanzisha mfuko wa maendeleo ya elimu

Kutoa huduma za elimu ya dini mashuleni

4.4 Vijana

Vijana ni nguzo kubwa ya kanisa katika nyanja zote, hivyo wanapaswa kuandaliwa

kulitumikia na kuliwezesha kanisa kupitia raslimali watu na fedha. Kwa hiyo, kanisa

linakusudia kuwaimarisha vijana katika maeneo yafuatayo

i. Kutoa mafunzo ya ujasiriamali

ii. Kuongeza mafundisho ya kiimani ili kutengeza/kuandaa kanisa la kesho

iii. Kuhamasisha vijana wengi zaidi washiriki kwenye vyama na shughuli zinazowahusu

iv. Kuimarisha vyama vya vijana

v. Kutumia vyama vya vijana kuwapa mafundisho ya ujuzi ili kukabiliana na

changamoto za maisha

4.5 Shule ya Sabato

Shule ya Sabato ni moyo na uhai wa kanisa. Kanisa linakusudia kuendelea kuboresha shule

ya sabato kama ifuatavyo:

i. Kuimarisha vikosi vya madarasa ya shule sabato

ii. Kutembeleana na kufanya uinjilisti kule mitaani kwetu na uhamasishaji wa kusoma

lesoni na biblia

iii. Ualikaji wa wageni-liwe jambo la kudumu

Page 16: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

13

4.6 Huduma za watoto

Huduma za watoto ni jambo muhimu kwa kanisa na kwa jamii nzima. Huduma kwa watoto

zinalenga kukuza imani ya watoto wakiwa hawajazaliwa hadi wafikishapo umri wa miaka 14

wakiongozwa na kukua katika maadili ya Kikristo na kutambua mfumo wa kanisa. Hivyo,

kanisa litaendelea kuwapa umuhimu unaostahili watoto kwa kuwapa huduma za kiroho na

kijamii ili wakue ndani ya kanisa wakiwa na madili yanayofaa wakionyesha mfano mzuri

wakiwa watoto wakristo wa adventista. Hii ni kwa kuwa watoto wana upeo mwepesi wa

kushika mafundisho ya injili na wana uwezo wa kuyaweka katika vitendo maishani mwao.

4.7 Afya

Kanisa lina amini katika wajibu wa kumfanya Kristo ajulikane ulimwenguni ni pamoja na

wajibu wa kiroho wa kutunza utu wa binadamu kwa kuhakikisha usalama wa afya yake

kimwili, kiakili na na kiroho. Kanisa linakusudia kuendelea kutoa huduma za elimu ya afya

kwa uana wake wote kwa nia ya kuzuia magonjwa na kutoa elimu ya afya itakayowawezesha

washiriki kuwa na afya njema katika maisha yao hasa kuhusiana na vyakula, vinyaji na

maburudisho.

4.8 Kwaya za Kanisa na vikundi vya uimbaji

Huduma ya kwaya au nyimbo ni muhimu katika ibada kwa kuongoa roho kupitia ujumbe wa

injili unaoimbwa katika nyimbo. Kanisa litadumisha huduma za kwaya na uimbaji kupitia

vikundi vilivyojiambatanisha na huduma za uimbaji ili kuhakikisha kuwa nyimbo, na aina ya

muziki wa dini unaimbwa na kupigwa kanisani unafuata misingi ya kiadventista. Kwa

kuzingatia mafunuo na mafundisho kuhusu muziki, kanisa litasimamia weledi katika muziki

wa kidini unaoimbwa na kwaya na vikundi vyote kanisani, na kuhakikisha kuwa uimbaji na

upigaji wa ala za muziki usiofaa au usioendana na Biblia unaachwa mara moja, mfano

midundo ya ngoma na mchanganyiko wa manyanga kwenye nyimbo unaachwa mara moja.

Mkazo utawekwa katika kufundisha elimu ya muziki kwa waimbaji wote pamoja na

mafunzo ya vinanda ili waimbaji waimbe nyimbo zilizochezwa kwa weledi mkubwa kwa

kinanda pasipo kutumia midundo kuongoza muziki, bali muziki uongoze nyimbo.

4.9 Ofisi ya Karani wa Kanisa

Hii ni ofisi muhimu sana katika uendeshaji wa shughuli za kanisa na utunzaji wa

kumbukumbu.. Ofisi hii inatakiwa iwezeshwe kwa kupatiwa vifaa vya kisasa vya kufanyia

kazi. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo ofisi hi itawezeshwa kwa kupatiwa nyenzo

zifuatazo:

1. Kompyuta mpya

2. Printer yenye kasi (high speed printer)

3. Machine ya kudurufia (photocopier machine)

Page 17: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

14

4.10 Mawasiliano

Mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa walengwa. Ili kuwepo

mawasiliano mazuri kanisani, hatuna budi kujizatiti kuwa na vifaa bora nyenye kiwango cha

juu cha ufanisi. Hivyo, kanisa linakusudia kuboresha mfumo wa mawasiliano kanisani kwa

kununua vifaa vya kisasa vya mawasialino vifuatayo:

i. Mfumo mzima wa vipaza sauti na nyenzo zake (Complete PA system and

accessories)

ii. Kununua kinanda kikubwa kwa ajili ya ibada (Church Piano/Organ)

iii. Kununua LCD screen 4 za dijitali

iv. Kununua vifaa vya ukalimani (Translation equipments)

4.11 MIUNDO MBINU (Majengo ya kanisa, vyoo, viwanja)

Kanisa linakusudia kuweka msisitizo mkubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya kanisa

hasa majengo, viwanja na huduma msingi kwa kanisa na makundi yake yote, ili kuweka

mazingira mazuri ya ibada na utendaji mzuri wa kazi ya Mungu.

4.11.1 Hali ilivyo sasa

Kwa sasa jengo la kanisa linachakaa na kuhitaji kufanyiwa ukarabati na marekebisha

makubwa ya sakafu, kuondoa paa la Asbestos, kurekebisha madirisha na kuangalia

uwezekano wa kuweka vipoza hewa (air conditioning) kwa ajili ya kukabiliana na hali ya joto

la Dar es salaam. Pia kiwanja cha kanisa hakijafanyiwa landscaping na kupanga vizuri

maeneo kwa ajili ya kuegesha magari.

Kanisa lina choo cha kisasa ambacho kipo katika hali nzuri na kinahudumiwa vizuri kwa

usafi muda wote wa wiki. Kanisa pia lina kisima cha ubatizo ambacho hakiko katika hali

nzuri kiafya. Hii inaleta changamoto ya kufanya maboresho katika kisima hiki.

4.11.2 Maboresho ya Miundombinu (Majengo, Viwanja)

Kwa kuzingatia mahitaji ya baadaye ya kanisa, na hali ya sasa ya uchakavu wa kanisa; ni

njozi yetu kuwa na mpango mkakati wa kuwezesha kanisa kuwa na nyumba nzuri ya ibada.

Njozi hii ni pamoja na kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la ibada la sasa kwa kuliongeza

(kulipanua) au kwa kwenda juu (vertical extension) au kwa kulipanua kiusambamba

(horizontal extension). Hii itaendana na uandaaji wa eneo la kanisa kwa ajili ya kutengeza

mandhari ya eneo la kanisa na maegesho ya magari (landscaping and car parking lots).

Kwa upande wa makundi, ni kusudi letu kukamilisha ujenzi wa nyumba za ibada katika

makundio yote na kuweka vifaa muhimu kwa ajili ya ibada.

4.11.3 Uboreshaji wa mandhari ya eneo na Jengo la Kanisa (Mwenge)

Kanisa lina azimia kuweka jitihada ya kuboresha mazingira ya eneo la kanisa. Maboresho

hayo yatahusisha mabadiliko makubwa kwenye jengo la kanisa na mandhari yote ya eneo la

kanisa. Kanisa linakusudia kufanya ukarabati mkubwa na maboresho kwenye jengo la sasa

Page 18: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

15

ili kukidhi ongezeko la washiriki, na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kinda na mafundi

mitambo. Katika kutekeleza nia hii, yafuatayo yapaswa yatekelezwe:

Kufanya upanuzi na maboresho ya eneo la kanisa utakaohusisha mambo

yafuatayo:

o Kuongeza nafasi kwa ajili ya office ya karani, mchungaji, mashemasi,

wazee, na wahazini kwa kuongeza kwa mita tatu sehemu ya jengo la

kanisa zilipo ofisi za sasa;

o Kujenga ndani kisima cha ubatizo;

o Kupanua kanisa ili kuongeza nafasi kwa ajili ya kuwezesha kuchukua watu

wengi zaidi. upanuzi waweza kufanyika kwa kwenda juu (vertical

extension) au kwa upanda upande (horizontal extension). Faida na hasara

za kila kila chaguzi zimeainishwa katika kipengele 4.12.3.1 na 4.12.3.2

o Kuboresha sakafu kwa kuweka sakafu mpya ya kisasa na yenye kudumu

muda mrefu;

o Kurekebisha paa la kanisa na kuondoa asbestos;

o Kutengeneza mandhari ya eneo la kanisa (landscaping);

o Kujenga mfumo wa kutolea maji ya mvua;

o Kuweka vipoza hewa kwenye ofisi zote za kanisa.

Kufanya matengenezo ya uzio kwa kupaka rangi na kuweka bango elekezi la

mawasiliano;

Kutengeneza au kuboresha barabara ya kuingilia kanisani kwa kuweka moram na

kushindilia;

Kuweka uzio katika nyumba ya mchungaji.

Kuweka uzio katika nyumba ya mlinzi

(a) Sehemu ya kanisa ilivyo kwa sasa (b) Kisima cha ubatizo kinavyoonekana kwa

sasa

4.11.3.1 Faida na Hasara za mapendekezo ya upanuzi wajengo la kanisa la sasa

Upanuzi kwenda juu (Vertical extension)

Faida zake

Matumizi mazuri ya nafasi ya juu (good use of sky space) na eneo la kanisa

halitapungua

Jengo la kanisa litakuwa na mwonekano mzuri (aesthetics)

Page 19: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

16

Changamoto zake

Zinahitaji fedha nyingi kwa wakati mmoja ili kutekeleza

Kanisa halitakuwa likitumika kwa ibada wakati wa ujenzi, hii itasababisha kanisa

kuingia gharama kukodisha mahema ili kufanyia ibada nje wakati ujenzi ukiendelea

kwa kipindi chote.

Ujenzi lazima ufanyike wote kwa mara moja

Upanuzi kwenda upende upande (Horizontal l extension)

Faida zake

Ibada wakati wa ujenzi zitaendelea ndani ya kanisa

Haihitaji uwekezaji mkubwa sana na ujenzi unaweza kufanywa kwa awamu

Changamoto zake

Nafasi ya eneo la kanisa itapunguka

Mwonekana wa kanisa hautakuwa mzuri (aesthetics)

4.11.4 Ujenzi wa Jengo la matumizi anuai

Ujenzi wa jengo kubwa la kisasa kwa matumizi mbalimbali ya kanisa ikiwa ni pamoja na

sehemu ya ibada kwa watoto unapaswa kutekelezwa ili kukabiliana na baadhi ya changamoto

zilizoanishwa hapo juu. Kwa mfano, jengo hilo litakapokamilika litakuwa limepatia

ufumbuzi tatizo la ufinyu wa ofisi za idara za uangalizi (Ofisi ya wazee, karani wa kanisa,

mhazini) na store kwa ajili ya utunzaji wa vifaa vya kanisa. Hivyo, basi michoro na mipango

ambayo ilikwishaanza miaka ya nyuma inapaswa iendelezwe. Gharama isiwe ni kikwazo cha

kutokuanza kwa mradi huu. Kwa kuwa tayari kanisa lilishaingia gharama kubwa kusanifu

michoro ya jengo husika, inapendekezwa kwamba michoro ya usanifu ujenzi wa jengo

upitishwe rasmi na kanisa ili taratibu zingine za kutafuta vibali vya ujenzi kutoka mamlaka za

manispaa ziweze kuendelea.

Ni vyema mradi huu usikwamishwe kwa sababu za matumizi ya jengo kwani matumizi

yanaweza kubadilishwa pasipo kukwamisha mradi husika.

4.11.5 Majengo Kanisa Makundini

Ni kusudi la Kanisa kuhakikisha kuwa ujwnzi wa majengo ya ibada makundini unakamilika

kwa ukamilifu ili ibada zifanyike katika nzuri na yenye utukufu. Hivyo, majengo ya kanisa

katika makundi yaliyoainishwa katika vipengle hapa chini yatakamilishwa kwa kuwekewa

sakafu, madirisha na viti ili yafae kwa ibada. Gharama za kukamisha ujenzi wa majengo haya

zimeainishwa katika jedwali la gharama za utekelezaji mpango mkakati.

Page 20: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

17

Bumafa

Chivilikiti

Mabwepande

Zinga

Amani

Kimele

Mnyambe

Mpekeso

4.11.6 Ukarabati wa nyumba ya mchungaji

Kulingana na sera za kanisa, mtaa unapaswa kumjengea na ama kukarabati nyumba ya

mchungaji. Hivyo, Kanisa la Mwenge litachangia sehemu yake kwenye ukarabati wa

nyumba ya mchungaji pale itakapohitajika kulingana na mgawanyo wa uchangiaji katika

mtaa wa Mwenge.

4.11.7 Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi makao mapya ya ETC

Kanisa litachukua jukumu la kuchangia sehemu yake kwenye mchango wa mtaa pale

gharama halisi za ujenzi huo zitakapokuwa zimeainishwa na kugawanywa kwenye makanisa

ya mtaa wa. Mchungaji wa mtaa anapaswa kuulizia gharama hizi kutoka ofisi ya Konferensi.

5. MIKAKATI YA KUPATA FEDHA KWAAJILI YA MIRADI YA MAJENGO

Ili kutekeleza mipango yote iliyoainishwa katika mpango huu, kiasi kikubwa cha fedha

kinahitajika. Fedha hizi zinapaswa kutafutwa kutoka vyanzo mbalimbali, wahusika wakuu

wakiwa ni washiriki wenyewe. Pia kunahitajika mikakati mahususi kuhakikisha yote

yaliyopangwa na kukubaliwa na washiriki yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Mapendekezo ya kupata fedha ni yafuatayo:

1. Kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kanisa utakao

hamasishwa na idara ya uwakili kwa kushirikiana na idara ya majengo

2. Kuwa na kikosi kazi cha washiriki wachache watakaoongoza changizo za

ujenzi.

3. Kuwashirikisha washiriki wote katika kuchangia shughuli za maendeleo ya

kanisa.

4. Kuendesha harambee za kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi

5.1. Kuanzisha mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa

Inapendekezwa kuanzishwa kwa mfuko maalum wa maendeleo ya kanisa. Mfuko huu

utakuwa maalumu kwa ajili ya miradi mikubwa ya ujenzi wa makanisa na jengo la huduma

kwa matumizi anuai. Washiriki wataombwa kuchangia katika mfuko huu kila wiki kwa kadri

wanavyobarikiwa, na pia kuwe na changizo maalumu kwa ajili hiyo.

Page 21: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

18

5.2 Kikosi kazi cha watu 100-200

Ili kuwezesha kazi ya ujenzi wa jengo la matumizi mbalimbali unafanyika, kuwe na kikosi

ongozi cha watu au familia 100 hadi 200 zitakazoombwa kuchangia kila mtu/familia kuanzia

kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa mwaka; lengo ni kukusanya kiasi cha Shilingi 100,000,000

hadi 200,000,000 kwa mwaka kinachohitajika kwa kuanzia ili kutekeleza miradi mikubwa ya

ujenzi ambayo itatekelezwa kwa kufuata kipaumbele kwa kuanzia na: 1. Maboresho na

upanuzi wa jengo la kanisa, na 2. ujenzi wa jengo la matumizi mbalimbali.

5.3 Washiriki wote wa kanisa kuhusishwa

Kwa kuwa ushiriki wa washiriki wote ni muhimu kwa kila kazi ya kanisa, washiriki wote

watakuwa sehemu ya kuchangia kwa kutumia njia mbalimbali zifuatazo:

○ Fomu za kuchangisha watu mbalimbali kwa kila mshiriki (wasio washiriki wa

mwenge, na pia kwa watu wengine wa madhehebu mengine na kwa marafiki)

kwa kuomba vibali vya kitaifa na kanisa.

○ Uchangiaji kwa njia ya simu i.e. tuma neno Mwenge kwenda 15555 kwa

kutumia mitandao ya simu iliyopo kama vodacom, airtel n.k.

○ Uuzaji wa bidhaa za kanisa kwa bei ya juu kidogo kwa washiriki na watu

wengine i.e Tshirts, Kalenda n.k.

○ Washiriki wa mwenge wa zamani kuhusishwa (ndani na nje ya nchi).

○ Kuweka Magoli kwa kila mshiriki/familia

○ Kila mshiriki apeleke kadi maalumu zilizochapwa majina kwa watu watano

wa karibu (wasiwe washiriki wa mwenge na au wawe ni marafiki,

wafanyakazi wenzetu katika sehemu za kazi n.k)

○ Kutoa matangazo ya changizo kupitia Morning Star radio

5.4 Changizo kutoka watu wa nje ya kanisa kwa njia ya harambee

Kanisa halijatumia ipasavyo fursa ya kufanya harambee za uchangiaji zenye kuwahusisha

watu wasio washiriki wa kanisa la waadventista wasabato katika kuchangia shughuli za

maendeleo. Hivyo, inapendekezwa kwamba njia hii itumike pia kama sehemu ya mkakati wa

kukusanya pesa. Harambee iliyotayarishwa vizuri kwa kuwaalika watu wenye nafasi kubwa

serikalini na katika taasisi za umma na watu binafsi ifanyike, hii itakuwa katika mfumo

ufuatao:

Ifanyike nje ya eneo la kanisa

Iwe ni katika mfumo wa chakula cha jioni (dinner)

Michoro ya kanisa na model zake iwe tayari wakati wa harambee

Kamati maalumu iundwe kuandaa harambee hii ili kuangalia sehemu ya kufanyia harambee,

watu wa kualikwa, utaratibu utakaotumika unaozingatia misingi ya kanisa n.k

Page 22: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

19

6. RAMANI YA UTEKELEZAJI

6.1 Ramani ya kila mwaka ya utekelezaji wa mpango mkakati

2013 2014 2015 2016 2017 IDARA HUSIKA

A: RASILIMALI ZA KIROHO

Lengo 1: Kuongeza washiriki kwa 100% ifikapo 2017 20% 20% 20% 20% 20% Wazee wa Kanisa

Mchungaji

Huduma

Shule ya Sabato

Lengo 2: Kutenga makundi yaliyopo sasa kuwa makanisa ifikapo 2017 Zinga M'Pande Kimele Bumafa Vikawe

Lengo 3: Kuimarisha na kuyawezesha makundi kujitegemea ifikapo mwaka 2017 au baada ya

hapo. Zinga M'Pande Kimele Bumafa Vikawe

Lengo 4:

i). Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia na Lesoni ifikapo 2017 10% 15% 15%

15%

15%

Wazee wa Kanisa

Huduma

Shule ya Sabato

ii). Kuhakikisha kuwa 70% ya washiriki wana ufahamu mpana kuhusiana na mtindo na mwenendo wa

maisha ya ki-adventista katika nyanja za afya, elimu, vyakula na vinywaji, na, maburudisho.

10% 15% 15% 15% 15% Afya na Kiasi

Elimu

Uwakili

B: RASILIMALI WATU

Lengo 1: Kuelimisha wainjilisti walei 15 wanaoweza kutumwa kama wainjilisti ifikapo 2017. 3 3 3 3 3 Wazee wa Kanisa

Mchungaji

Huduma

Lengo 2: Kusomesha mwanafunzi wawili elimu ya uchungaji ifikapo 17 Hezron Mgwenya & Nathaniel

Wazee wa Kanisa

Mchungaji

Huduma

Lengo 3: 90% ya wahubiri wawe na elimu ya homilia ifikapo 2017 15% 15% 20% 20% 20% Mchungaji

Page 23: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

20

2013 2014 2015 2016 2017 IDARA HUSIKA

C: RASILIMALI FEDHA

Lengo 1: Kuhakikisha idadi ya washiriki wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango

inaongezeka kwa asilimia hamsini (50%) ya washiriki.

10% 10% 10% 10% 10% Mchungaji

Wazee wa Kanisa

Uwakili

Lengo 2: Kuwezesha 70% ya washiriki wasio na ajira wawe na elimu ya ujasiliamali na

wale wanaopenda kuanzisha na kuendeleza biashara wawe na elimu ya ujasiriamali.

10% 15% 15% 15% 15% ATAP

Uwakili

Huduma za wanawake

D: RASILIMALI MIONGOZO

Lengo1: Kuhakikisha kuwa 100% ya washiriki wanafundishwa na kuelewa masomo

muhimu yafuatayo :

20% 20% 20% 20% 20%

Mchungaji

Wazee wa Kanisa

Roho ya Unabii

Idara ya huduma · misingi 28 ya kanisa

· kufuata sera na taratibu za kanisa

· utumiaji wa vitabu vya Roho ya Unabii.

E: MRADI WA KUSAMBAZA KITABU CHA PAMBANO KUU

Lengo 1: Kuhakikisha vitabu 20,000 vitanunuliwa na kusambazwa 4000 4000 4000 4000 4000 Wazee wa Kanisa

Roho ya Unabii

F: MIRADI MIKUU YA UJENZI

Lengo 1: Kufanya ukarabati mkubwa wa jengo la kanisa na kukamilisha ujenzi wa

majengo ya ibada makundini.

Mwenge

kukusanya

200,000,000

na kuanza

upanuzi wa

ofisi za kanisa

Kuendelea

kukusanya

fedha za

ujenzi

Kuanza

upanuzi na

maboresho

ya kanisa

Kuendelea

na ujenzi

Kukamilish

a maboresho

na upanuzi

wote

Wazee wa Kanisa

Majengo

Uwakili

Lengo 2: Kukarabati nyumba ya mchungaji Kwa kadri ya mahitaji kwa mwaka husika Wazee wa Kanisa

Majengo

Lengo 3: Ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi makao makuu mapya ya ETC. Kadri ya bajeti itakayoletwa na conference kwa kuzingatia mgawanyo

wa uchangiaji kimtaa

Wazee wa Kanisa

Mchungaji

Lengo 4: Ujenzi wa Jengo la Ustawi wa Jamii

Kuandaa na

kukamilisha

michoro yote

ya usanifu

Page 24: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

21

6.2 Ramani ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi kwa mwaka 2013

F: MIRADI MIKUU YA

UJENZI JANUARI FEBRUARI MACHI APRILI MEI JUNI

Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 W1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4

Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa na

upanuzi wa jengo la kanisa na

kukamilisha ujenzi wa majengo ya

kuabudia makundini

Kutengeneza 3D model ya kanisa

litakapokamilika (3D Physical Model)

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya familia 100-200, na michango ya

washiriki

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya kuchangisha kutumia kadi kutoka

kwa watu wa nje ya kanisa.

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa

njia ya "majengo day" ndani ya kanisa

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa

njia ya "majengo day" ndani ya kanisa na nje

ya kanisa.

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa

njia SMS namba maalum.

Ukusanyaji wa fedha za kutekeleza mradi

Kuanza ujenzi wa upanuzi wa ofisi za kanisa

Lengo #2 : Kukarabati nyumba ya

mchungaji

Pale itakapohitajika

Lengo # 3: Ujenzi wa nyumba ya

mkurugenzi makao makuu mapya ya

ETC

Pale itakapohitajika

Lengo # 4: Ujenzi wa Jengo la ustawi wa

jamii

i). Kupitia upya michoro iliyopo kuona kama

inakidhi haja za sasa na wakati ujao ili

kufanya marekebisho pale inapobidi.

ii). Kuandaa michoro mipya (kama kutakuwa na mabadiliko)

iii). Kuandaa michoro ya kihandisi

(structural engineering drawings).

iv). Kuandaa michoro ya mfumo wa maji

v). Kuandaa michoro ya mfumo wa umeme

Page 25: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

22

F: MIRADI MIKUU YA

UJENZI

JULAI AGOSTI SEPTEMBA OCTOBA NOVEMBA DESEMBA

Wk

1

Wk2 Wk3 Wk4 Wk

1

Wk

2

Wk

3

Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4 Wk1 Wk2 Wk3 Wk4

Lengo #1: Kufanya ukarabati mkubwa na

upanuzi wa jengo la kanisa na

kukamilisha ujenzi wa majengo ya

kuabudia makundini

Kutengeneza 3D model ya kanisa

litakapokamilika

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa

njia ya familia 100-200, na michango ya

washiriki

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa

njia ya kuchangisha kutumia kadi kutoka kwa watu wa nje ya kanisa

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa njia ya "majengo day" ndani ya kanisa na nje

ya kanisa

Kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa

njia SMS namba maalum

Ukusanyaji wa fedha za kutekeleza mradi

Kuanza ujenzi wa upanuzi wa ofisi za kanisa

Lengo #2 : Kukarabati nyumba ya

mchungaji

Pale itakapohitajika

Lengo # 3: Ujenzi wa nyumba ya

mkurugenzi makao makuu mapya ya

ETC

Pale itakapohitajika

Lengo # 4: Ujenzi wa Jengo la ustawi wa

jamii

i). Kupitia upya michoro iliyopo kuona kama inakidhi haja za sasa na wakati ujao ili

kufanya marekebisho pale inapobidi.

ii). Kuandaa michoro mipya (kama kutakuwa na mabadiliko)

iii). Kuandaa michoro ya kihandisi

(structural engineering drawings).

iv). Kuandaa michoro ya mfumo wa maji

v). Kuandaa michoro ya mfumo wa umeme

Page 26: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

23

7. BAJETI YA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI

7.1 MAJENGO YA IBADA MAKUNDINI

KUNDI LA BUMAFA

Maelezo SHS.

1. Kuweka sakafu

2. Kupiga lipu (plaster) ndani na nje ya jengo

3. Kuweka grill kwenye madirisha

4. Kuweka milango

5. Kujenga choo

Jumla ya gharama inayohitajika 11,403,700.00

KUNDI LA CHIVILIKITI

1. Kuweka lipu ndani na nje

2. Kuweka madirisha

3. Kuweka milango

Jumla ya gharama inayohitajika 5,170,000.00

KUNDI LA MABWEPANDE

1. Kupiga lipu na kuziba nyufa

2. Kuweka umeme

3. Kufanya marekebisho ya mimbari

Jumla ya gharama inayohitajika 1,300,000.00

KUNDI LA ZINGA

Kufuatilia fidia kwa kuwa sehemu ya Kanisa iko

katika hifadhi ya barabara. Hivyo kwa sasa hakuna

shughuli za ujenzi zinazohitajika

Jumla ya gharama inayohitajika 0.00

KUNDI LA AMANI

1. Kuweka sakafu

2. Kuweka lipu ya ndani na nje

3. Kufanya ukarafati wa choo kwa kuziba nyufa

4. Kubadilisha mlango mmoja wa choo

5. Kuweka milango

Jumla ya gharama inayohitajika 4,361,500.00

Page 27: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

24

KUNDI LA KIMELE

1 Kuweka lipu ndani na nje ya jengo

2 Kweka milango (frame na milango)

3 Kuweka madirisha

4 Kuta za ndani za kutenganisha

5 Kukarabati nyufa kwenye choo

Jumla ya gharama inayohitajika 7,290,000.00

KANISA LA MNYAMBE

1

Ujenzi wa kanisa lenye uwezo wa kuchukua

waumini 200 waliokaa vitini

Jumla ya gharama inayohitajika 29,524,375.00

JUMLA KUU KWA MAKUNDI YOTE 59,049,575.00

NB: Mchanganuo wa gharama kwa kila kipengele utatolewa na idara ya majengo

(Sehemu hii ni kwa ajili ya kuweka bajeti nzima ya kutekeleza mpango huu)

Page 28: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

25

7.2 GHARAMA ZA MABORESHO YA MAZINGIRA YA KANISA LA MWENGE

Page 29: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

26

8. VIELELEZO NA VIAMBATANISHI

8.1 Ramani ya upanuzi wa Kanisa (Sehemu za office)

Picha 1: Sehemu ya chini (Ground floor) ikionyesha offisi ofisi za kanisa na kisima cha ubatizo

Page 30: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

27

Picha 2: Sehemu ya juu (First floor) ikionyesha ofisi za mbalimbali za kanisa

Page 31: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

28

8.2 Picha au mtazamo wa kisanifu katika picha za pande tatu (3D Views photos)

Picha 3: Mwonekano wa Kanisa upande wa kuingilia kwenye ofisi mpya

Picha 4: Mwonekano wa Kanisa upande wa mbele

Page 32: MWENGE KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO … robo2 2017/MPANGO MKAKATI SD… · Lengo #4: Kuwa na 60% ya washiriki wanaosoma Biblia, Lesoni ifikapo ... Lengo: Kuhakikisha kuwa 100%

Draft 03

29

Picha 5: Mwonekano wa Kanisa upande wa kushoto

Picha 6: Mwonekano wa Kanisa kwa ndani