26
Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu Toleo la Lugha Nyepesi

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

Toleo la Lugha Nyepesi

Page 2: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

Kimetolewa na:Kituo cha Habari kuhusu UlemavuSLP 75576 Dar es SalaamSimu: +255 22 2400227, + 255 732 991 485Barua pepe: [email protected]: www.icd-tanzania.org

Comprehensive Community Based Rehabilitation Tanzania (CCBRT)SLP 23310Dar es Salaam.Simu: + 255 22 260 1543Nukushi: + 255 22 260 1544 Barua pepe: [email protected]: www.ccbrt.or.tz

Tafsiri:Byekwaso na Wenzake

Katuni:Marco Tibasima

Usanifu:Kaganzi RutachwamagyoMarco Tibasima

Uhariri:Kituo cha Habari kuhusu UlemavuComprehensive Community Based Rehabilitation - Tanzania (CCBRT)

Hakimiliki:ICD, mwaka 2010CCBRT, mwaka 2010

Shukrani kwa wote walioshiriki katika kufanikisha utayarishaji wa chapisho hili.

Page 3: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

i

YaliyomoUtangulizi ..........................................................................................................................................................................iiIbara ya 1 - Madhumuni .............................................................................................................................................1Ibara ya 2 - Fasili .............................................................................................................................................................1Ibara ya 3 - Kanuni za jumla ......................................................................................................................................2Ibara ya 4 - Wajibu wa jumla .....................................................................................................................................2Ibara ya 5 - Usawa na kutobagua ............................................................................................................................3Ibara ya 6 - Wanawake wenye ulemavu .................................................................................................................4Ibara ya 7 - Watoto wenye ulemavu ........................................................................................................................4Ibara ya 8 - Kukuza ufahamu .....................................................................................................................................5Ibara ya 9 - Ufikikaji na upatikanaji .............................................................................................................................5Ibara ya 10 - Haki ya kuishi ..........................................................................................................................................6Ibara ya 11 - Hali ya hatari na dharura kutokana na majanga ........................................................................7Ibara ya 12 - Usawa wa kutambuliwa kama mtu mbele ya sheria ................................................................7Ibara ya 13 - Kuzifikia mamlaka za kisheria ...........................................................................................................8Ibara ya 14 - Kujiamulia na usalama .........................................................................................................................8Ibara ya 15 - Kutofanyiwa mateso, ukatili au kudhalilishwa ............................................................................9Ibara ya 16 - Kutonyonywa, kutofanyiwa vurugu au kunyanyaswa ..............................................................9Ibara ya 17 - Kuheshimu tofauti ..................................................................................................................................10Ibara ya 18 - Uhuru wa kutembea na kuwa na uraia .........................................................................................10Ibara ya 19 - Kuishi kwa kujiamulia na kujumuishwa kwenye jamii ..............................................................11Ibara ya 20 - Matembezi binafsi ................................................................................................................................11Ibara ya 21 - Uhuru wa kujieleza, kutoa maoni na kupata habari .................................................................12Ibara ya 22 - Kuheshimu faragha ..............................................................................................................................12Ibara ya 23 - Kuheshimu maisha ya kifamilia na familia ...................................................................................13Ibara ya 24 - Elimu ..........................................................................................................................................................13Ibara ya 25 - Afya ............................................................................................................................................................14Ibara ya 26 - Marekebisho na utengamao .............................................................................................................15Ibara ya 27 - Kazi na ajira ..............................................................................................................................................16Ibara ya 28 - Kiwango stahiki cha kuishi na hifadhi ya jamii ............................................................................17Ibara ya 29 - Ushiriki katika masuala ya kisiasa na kijamii .................................................................................17Ibara ya 30 - Ushiriki katika masuala ya kiutamaduni, burudani, mapumziko na michezo ...................18Ibara ya 31 - Ukusanyaji wa taarifa na takwimu ....................................................................................................19Ibara ya 32 hadi 50 - Majukumu ya serikali ............................................................................................................20

Page 4: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

ii

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Utangulizi

Mkataba wa Watu wenye Ulemavu una maana gani?

Haya ni maafikiano ya kimataifa yenye kufafanua na kuzibana nchi mbalimbali kuzitekeleza haki za watu wenye ulemavu. Yaani kuzilinda na kuhakikikisha kuwa wahusika wanazifuatilia kikamilifu na kwa usawa ikiwa ni pamoja na hiari ya msingi. Kuheshimu utu wa kuzaliwa nao ndicho kiini cha Mkataba wenyewe.

* Kwa mujibu wa Mkataba huu, nchi humaanisha taifa au jumuiya za kikanda zilizouridhia.

Kwa nini mkataba huu unahitajika?

Licha ya kuwepo kwa mikataba mingi ya haki za binadamu, bado watu wenye ulemavu wameendelea kuteseka kwa kubaguliwa. Daima haki zao haziheshimiwi kama ilivyo kwa watu wengine. Hivyo mkataba huu:

* Unafafanua kabisa na kuhusisha kanuni zilizopo za haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu;

* Unatoa mamlaka kwa misingi ya maafikiano ya kimataifa kwa nchi husika kuandaa sheria na sera zinazoendana nao;

* Unatoa mfumo wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mkataba wenyewe ikiwa ni pamoja na uandaaji wa taarifa za vipindi vya utekelezaji;

* Unatambua hali tete inayowakabili wanawake na watoto wenye ulemavu.

Ni nani wanaoweza kusaini na kuridhia mkataba huu?

* Nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa taratibu zake za ndani.

* Jumuiya za kikanda kwa kuzingatia mamlaka zilizokasimiwa kwake na nchi zinazoiunda jumuiya yenyewe.

Je, Tanzania nayo imechukua hatua gani hadi sasa?

* Tanzania imesaini na kuuridhia mkataba huu. Hivi sasa inaendelea na mchakato wa kutunga sheria ya watu wenye ulemavu ili iwe ndiyo zana ya kutekelezea mkataba wenyewe.

Na hiyo itifaki ya hiari maana yake nini?

Itifaki hii ni chombo cha kusimamia utekelezaji wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu ngazi ya kimataifa. Kamati maalum itakuwa ikipokea taarifa za kila nchi iliyouridhia na hata kutoka kwa wadau binafsi na jumuiya za kikanda. Hatua zitafuatia kulingana na ukweli uliomo kwenye taarifa husika.

Page 5: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

1

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Kutokana na mambo yote yaliyoorodheshwa hapa, nchi ambazo ni sehemu ya maafikiano haya zimekubaliana kama ifuatavyo:

Ibara ya 1 - Madhumuni

Maafikiano haya yameandaliwa ili kuhakikisha kwamba:

Watu wenye ulemavu ni pamoja na watu wenye vilema vya kudumu (mathalani: viungo, akili n.k) na wale ambao kwa sababu mbalimbali hawajumuishwi katika jamii (mfano kutokana na vizuizi vya kimtazamo, lugha, mazingira na sheria).

Ibara ya 2 - Fasili

“Mawasiliano” neno linalomaanisha njia mbalimbali watu watumiazo katika kuwasiliana (matha-lani lugha ya kuongea, lugha ya alama, matini, Breli, kugusa, maandishi yaliyokuzwa, machapisho, kusikia, lugha nyepesi na kuwepo kwa wasomaji kwa ajili ya wasioona.

“Lugha” humaanisha aina zote za lugha (mathalani maongezi, ishara na lugha nyingine zisizo za kimatamshi).

“Ubaguzi” kwa misingi ya ulemavu, humaanisha mtu kuweza kutengwa kufungiwa nje au kuzuiwa kufanya mambo kutokana na ulemavu alionao. Ubaguzi wa aina hii unaweza kuwa katika nyanja zote za maisha.

“Marekebisho stahili” humaanisha kuwa mtu anaweza kuhitaji mabadiliko fulani fulani yafanyike ili kumuwezesha kuzipata haki zake (mathalani mabadiliko mahali anapoishi au kufanyia kazi)ili mradi yasihitaji gharama kubwa au ni magumu kutekelezeka.

Page 6: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

2

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

“Usanifu unaozingatia mahitaji ya wote” humaanisha kwamba, vitu hutengenezwa, mipango huandaliwa na maeneo husanifiwa kwa ajili ya matumizi ya watu wote. Wakati mwingine mtu fulani mwenye aina maalum ya ulemavu anaweza kuhitaji kutengenezewa kifaa maalum ili aweze kuzipata haki zake.

Ibara ya 3 - Kanuni za Jumla

Maafikiano haya yanajikita kwenye kanuni hizi:-

* Utu

* Uwezo wa kuchagua

* Kujitegemea

* Kutobagua

* Kushiriki

* Ujumuishaji

* Kuheshimu tofauti (uanuwai)

* Kukubali kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu ya binadamu

* Usawa wa fursa

* Ufikikaji na upatikanaji

* Usawa wa wanawake na wanaume

* Kuheshimu watoto

Ibara ya 4 - Wajibu wa Jumla

1. Nchi zilizoyakubali Maafikiano haya, zinaahidi kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinawa- gusa watu wote bila kubagua kwa msingi wa ulemavu. Katika kutimiza ahadi hii, nchi hizi :

a) Zitatunga sheria, sera, na kuanzisha mazoea mapya katika nchi zao ili yafanane na yale yaliyo kwenye Maafikiano hayo.

Page 7: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

3

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

b) Zitarekebisha au kufuta sheria za zamani na desturi zinazowabagua watu wenye ulemavu.c) Zitahakikisha kwamba haki za watu wenye ulemavu zinajumuishwa katika sera na mipango yote.d) Zitajizuia kufanya kitu chochote kinachoenda kinyume na maafikiano haya na pia kuhakikisha kwamba hata watu wengine wanayaheshimu.e) Zitachukua hatua ya kuwazuia watu binafsi, mashirika au makampuni kubagua kwa kigezo cha ulemavu.f ) Zitatengeneza na kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa, huduma, vifaa na nyenzo za gharama nafuu ambavyo watu wote wenye ulemavu kote duniani wanaweza kuvitumia.g) Zitabuni na kuendeleza teknolojia mpya katika nyanja zote za maisha ambazo zina-faa kwa watu wenye ulemavu.h) Zitatoa taarifa kuhusu aina zote za misaada ikiwa ni pamoja na teknolojia katika hali ambayo watu wote wenye ulemavu wataielewa.i) Zitaendeleza mafunzo juu ya haki ndani ya makubaliano haya kwa ajili ya wale wanaojishughulisha na watu wenye ulemavu.j) Zitatafsiri kivitendo sheria na kanuni zinazohusiana na uchumi, jamii na haki zakitamaduni kwa kadri inavyowezekana kulingana na rasilimali zilizopo. Ikibidi, zitashirikiana na nchi nyingine katika kuzitekeleza haki hizi. Haki nyingine zote lazima zitekelezwe mara moja.k) Zitazungumza na kuwahusisha watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na watoto wenye ulemavu kwa kupitia asasi zinazowawakilisha wakati wa kuandaa sheria na kanuni za maafikiano haya.l) Hazitabadilisha sheria au kanuni yoyote ambayo ni nzuri kwa ajili ya haki za watu wenye ulemavu. Nchi haipashwi kuyatumia maafikiano haya kama kisingizio cha kutotekeleza haki ambazo tayari zipo.m) Zitatumia maafikino haya katika nchi nzima.

Ibara ya 5 - Usawa na kutobagua

1. Watu wote wenye ulemavu wako sawa mbele ya sheria na wanalindwa na sheria bila ubaguzi wowote.2. Ubaguzi kwa kigezo cha ulemavu hautaruhusiwa na watu wenye ulemavu watalindwa dhidi ya ubaguzi wa aina hiyo.3. Kama mtu mwenye ulemavu atahitaji mabadiliko yafanyike kwenye mazingira yake ili aweze kuzifaidi haki zake, basi mabadiliko hayo yafanyike.

Page 8: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

4

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

4. Iwapo watu wenye ulemavu wanahitaji hatua mahususi zichukuliwe ili waweze kuwa sawa na wengine, huduma za aina hii hazitachukuliwa kuwa ni kutowatendea haki wengine.

Ibara ya 6 - Wanawake wenye ulemavu

1. Wanawake na wasichana wenye ulemavu hukabiliwa na aina nyingi za ubaguzi. Nchi zitahakikisha kuwa wasichana na wanawake watapata kikamilifu na kwa usawa uhuru na haki za binadamu.2. Nchi zitachukua hatua ili kusaidia ukuaji na uwezeshaji wa wanawake wenye ulemavu kuweza kutumia na kufaidi haki zao.

Ibara ya 7 - Watoto wenye ulemavu

1. Watoto wenye ulemnavu wana haki sawa na watoto wengine.2. Kitu chochote kinacho muhusu mtoto mwenye ulemavu, lazima kifanyike kwa manufaa ya mtoto mwenyewe.3. Watoto wenye ulemavu wana haki ya kutoa maoni yao na yakasikilizwa. Watoto wenye ulemavu wanapashwa kusaidiwa ipasavyo ili watoe maoni yao kwa kuzingatia umri wao.

Page 9: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

5

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 8 - Kukuza ufahamu

1. Nchi:a) Zitazisaidia familia na watu wote ndani ya jamii katika kupata ufahamu zaidi juu yamasuala yanayohusu watu wenye ulemavu. Zitahakikisha kwamba haki na utu wa watu wenye ulemavu zinaheshimika.b) Zitapigana dhidi ya imani potofu na chuki kuhusu watu wenye ulemavu kwa vile imani hizi ndilo chimbuko la ubaguzi dhidi ya kundi hili.c) Zitamsaidia kila mtu kufahamu ni mambo yapi watu wenye ulemavu wanaweza kuyafanya na jinsi wanavyoweza kusaidia maendeleo ya nchi.

2. Kadhalika nchi:a) Zitamfanya kila mmoja awe na ufahamu kuhusu haki za watu wenye ulemavu kwa:

i. Kuonyesha kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na mtu mwingine yeyote;ii. Kufuatilia suala la ulemavu ndani ya jamii na kubainisha mkanganyiko utakaojitokeza;iii. Kuonyesha stadi za watu wenye ulemavu na jinsi zinavyoweza kutumika.

b) Kuhakikisha kuwa shule zinafundisha juu ya haki za watu wenye ulemavu.c) Kuhimiza vyombo vya habari kama vile radio, televisheni, magazeti na majarida kuonyesha taswira ya watu wenye ulemavu inayoendeleza haki za wahusika.d) Kuendeleza programu za mafunzo ya kuwafanya watu wawe na ufahamu juu ya haki za watu wenye ulemavu.

Ibara ya 9 - Ufikikaji na Upatikanaji

1. Nchi zitaondoa vizuizi vinavyowakabili watu wenye ulemavu. Kwa njia hiyo, watu wenye ulemavu wanaweza kuishi kwa kujitegemea na kwa namna wapendavyo. Nchi zitaondoa vizuizi kwenye:

a) Majengo, barabara, usafiri, vitu vya ndani na nje, (mfano shuleni; majumbani, mahospitalini, vituo vya afya na sehemu za kazi).b) Habari, mawasiliano na huduma nyinginezo (mathalani huduma za kielektroni na zile za dharura).

Page 10: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

6

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

2. Kadhalika nchi:a) Zitaweka viwango vya ufikikaji wa maeneo ya umma na huduma.b) Zitahakikisha kwamba shughuli za makampuni kwa ajili ya umma zinafikika.c) Kuwapatia watu mafunzo kuhusu mahi- taji ya watu wenye ulemavu pale suala la ufikikaji linapohusika.d) Kuwa na alama za Breli na taarifa zinazosomeka kiurahisi kwenye majengo ya umma.e) Kutoa msaada ili watu wenye ulemavu wamudu kuyafikia majengo yanayohudumia umma (mathalani wasomaji, wakalimani wa lugha ya alama, wasindikizaji).f ) Kutoa aina nyinginezo za misaada inayohitajiwa na watu wenye ulemavu katika kupata habari.g) Kutoa teknolojia mpya kwa watu wenye ulemavu.h) Kuendeleza teknolojia mpya inayoboresha upatikanaji wa habari na mawasiliano kwa watu wenye ulemavu.

Ibara ya 10 - Haki ya kuishi

Watu wote wenye ulemavu wana haki ya kuishi. Nchi zita-chukua hatua ili kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wananufaika na haki hii.

Page 11: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

7

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 11 - Hali ya Hatari na Dharura kutokana na majanga

Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanalindwa wakati wa vita, majanga ya asili au dharura nyinginezo.

Ibara ya 12 - Usawa wa kutambuliwa kama mtu mbele ya sheria

Watu wenye ulemavu:

* Wana haki ya kutambu liwa kama watu mbele ya sheria.

* Wana uwezo sawa na watu wengine juu ya masuala ya kisheria yanayohusu maisha yao.

* Wana haki ya kupata msaada wanaouhitaji katika kufanya maamuzi juu ya masuala ya kisheria.Pale wanapohitaji kusaidiwa kuhusu masuala ya kisheria na kifedha: a) Watalindwa dhidi ya dhuluma. b) Haki zao na chaguo lao vitalindwa.

Page 12: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

8

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

c) Wasaidizi hawatawalazimisha kufanya maamuzi haraka haraka.d) Msaada utolewe pale tu unapohitajika na kwa kiasi kile tu kinachohitajika.e) Mahakama zitarekebisha aina ya msaada wa kisheria utolewao.

5. Nchi zitahakikisha kwamba, watu wenye ulemavu:a) Wana haki ya kumiliki au kupata malib) Wana haki ya kusimamia fedha zao au masuala mengine ya kifedha.c) Wana fursa sawa na watu wangine za kupata mikopo ya mabenki, dhamana na miamana.d) Hawawezi kunyang’anywa mali zao kiholela.

Ibara ya 13 - Kuzifikia Mamlaka za Kisheria

1. Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaifikia mifumo ya kisheria nchini mwao kama ilivyo kwa watu wengine. Kanuni zozote za jinsi ya kuendesha mambo (kimahakama) sharti ziwekwe katika hali ambayo watu wenye ulemavu wanaweza kuhusishwa katika hatua

zote za michakato ya kisheria (mathalani kuwa mashahidi).2. Watumishi katika mfumo wa sheria (mfano maafisa wa polisi na magereza) sharti wapewe mafunzo ya jinsi ya kuboresha ufikiaji wa watu wenye ulemavu.

Ibara ya 14 - Kujiamulia na Usalama

Nchi: a) Zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa ya kujiamu lia na kuwa salama. b) Zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawapokonywi haki hii kwa vile tu wana ulemavu au katika hali yeyote isiyo halali.

2. Nchi zitahakikisha kuwa iwapo mtu atapokonywa haki yake, sheria itamlinda. Kadhalika

Page 13: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

9

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

zitahakikisha kuwa kila inapohitajika, mabadiliko yanafanywa kwenye mazingira ya mtu mmoja mmoja ili kumuwezesha kuzipata haki zake sambamba na zile za kimataifa.

Ibara 15 - Kutofanyiwa mateso, ukatili au kudhalil-ishwa

1. Hakuna mtu atakayeteswa, kutendewa au kuadhibiwa katika hali ya kikatili au kiudhalilishaji. Hakuna mtu atakayelazimishwa kushiriki katika majaribio ya kisayansi au kitabibu.2. Nchi zinakubaliana kutunga sheria na kuchukua hatua nyingine ili kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanalindwa dhidi ya mateso kama ilivyo kwa watu wengine.

Ibara ya 16 - Kutonyonywa kutofanyiwa vurugu au kunyanyaswa

Nchi:1. Zitapitisha sheria na kuchukua hatua nyinginezo ili kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawanyonywi au kudhalilishwa wakiwa nyumbani au nje ya nyumbani.2. Zitachukua hatua ya kuzuia udhalilishaji wa watu wenye ulemavu kwa kuwapa misaada na taarifa sahihi wao wenyewe na familia zao.3. Zitahakikisha kuwa sehemu na programu zinazowa- hudumia watu wenye

ulemavu zinakaguliwa kila mara ili kudhibiti ukatili na manyanyaso.

Page 14: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

10

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

4. Zitawasaidia watu wenye ulemavu kupata ahueni na kuwachangamanisha kwenye jamii baada ya kuathiriwa na vitendo vya kikatili na manyanyaso.

Ibara 17 - Kuheshimuutofauti

Watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine ya kuheshimiwa kama walivyo kimaumbile na kiakili.

Ibara 18 - Uhuru wa kutambuliwa na kuwa na uraia

1. Watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine ya kutembea ndani na nje ya nchi, kuchagua mahali pa kuishi na kuwa na utaifa. Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu:

a) Wana haki ya kupata na kubadilisha uraia. Hakuna atakayewapokonya utaifa wao bila ya sababu au kwa sababu ya ulemavu.b) Hawawezi kupokonywa hati zao za kusafiria au vitambulisho vya uraia bila sababu au kwa kuwa na ulemavu ama kwa kuruhisiwa kwenda nchi nyingine.c) Wanaruhusiwa kuondoka nchini mwao au nchi nyingine yoyoted) Hawazuiliwi kuingia tena nchini mwao bila sababu au kutokana na ulemavu.

2. Watoto wenye ulemavu watasajiliwa mara baada ya kuzaliwa. Watakuwa na haki ya kupewa jina, uraia na kwa kadri inavyowezekana kuwajua na kulelewa na wazazi wao.

Page 15: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

11

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 19 - Kuishi kwa kujiamulia na kujumuishwa kwenye jamii

Watu wenye ulemavu wana haki sawa na mwingine yeyote ya kuishi ndani ya jamii kwa kujumuishwa na kushiriki kikamilifu.Nchi zitahakikisha kwamba watu wenye ulemavu:

a) Wanapata fursa sawa na watu wengine ya kujiamulia ni nani wanai-shi naye na mahali gani wanaishi. Hawatashur-utishwa kuishi kwenye makazi au kwenye mipangilio mingine yamakazi wasiyoitaka.b) Wanakuwa na wigo mpana wa kuchagua eneo na jinsi ya kuishi ndani ya jamii, ikiwa ni pamoja na kuwa`na wasaidizi binafsi wa kuwasaidia kujumuika kwenye jamii na kuwalinda wasitengwe.c) Wanaweza kutumia huduma zilizopo ndani ya jamii ambazo pale inapobidi zirekebishwe ili kukidhi mahitaji binafsi.

Ibara 20 - Matembezi binafsi

Nchi zitahakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanaweza kuvinjari wao wenyewe kwa kadri inavyowezekana ikiwa ni pamoja na:

a) Kutembeatembea katika hali na muda waliojichagulia na kwa gharama wanayoimudu.b) Kuwasaidia kupata nyenzo na teknolojia za kujimudu kutembea na kuwahakikisha unafuu wa gharama.c) Kutoa mafunzo ya jinsi ya kujimudu kutembea wao wenyewe na watumishi wanaojishughulisha nao.d) Kuwahimiza wale wanaozalisha nyenzo na teknolojia za kujimudu kutembea kuweka maanani hali zote za miondoko (nyendo).

Page 16: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

12

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 21 - Uhuru wa kujieleza, kutoa maoni na kupata habari

Nchi zitahakikisha uheshimikaji wa haki ya watu wenye ulemavu ya kuongea mawazo yao kwa njia ya Breli, lugha ya alama au aina nyingine ya mawasiliano watakayoichagua.

Nchi zitahakikisha uheshimikaji wa haki ya kupokea na kutoa habari sawa na wengine. Hii ni pamoja na:

a) Kuwapa habari zinazoulenga umma kwa namna ambayo wataielewa bila kuwaingizia gharama za ziada (mfano maandishi ya nukta nundu).b) Kuzirahisisha njia za mawasiliano wazitumiazo.c) Kuhimiza wafanya biashara na mashirika binafsi yanayohudumia umma kuzifanya huduma zao kufikiwa kwa urahisi zaidi.d) Kuhimiza vyombo vya habari kuwawezesha kuzipata habari.e) Kuitambua na kuieneza lugha ya alama.

Ibara ya 22 - Kuheshimu faragha

1. Bila kujali wanapoishi watu wenye ulemavu, hakuna mtu mwenye mamlaka kuingilia maisha yao binafsi, kuwaingilia majumbani, kufungua barua, kusumbua familia zao, kuwaharibia sifa bila sababu za msingi. Watu wenye ulemavu wana haki ya kulindwa na sheria dhidi ya mashambulio ya aina hiyo.2. Taarifa kuwahusu watu wenye ulemavu, afya zao na marekebisho vinabakia kuwa ni siri inayolindwa kama ilivyo kwa

watu wengine.

Page 17: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

13

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara 23 - Kuheshimu maisha ya kifamilia na familia

1. Nchi zitakataza ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu pale mahusiano ya kindoa na kifamilia yanapohusika na kuhakikisha kuwa:

a) Wanatendewa haki sawa na watu wengine ya kuoa na kuwa na familia.b) Wanatendewa haki ya kuzaa watoto, kuamua idadi ya watoto wa kuwazaa na lini wazaliwe sawa na watu wengine. Wanapaswa kupata taarifa ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango, kadhalika kusaidiwa kuzielewa taarifa hizi. Kadhalika wana haki sawa na mtu mwingine yeyote ya kuhifadhi kizazi chao.

2. Watu wenye ulemavu wana haki na wajibu kuhusu matunzo na kuasili watoto kwa kutilia maanani umuhimu wa suala la maslahi ya mtoto. Nchi zitawapa watu wenye ulemavu kila aina ya msaada katika malezi ya watoto wao.3. Watoto wenye ulemavu wana haki ya maisha ya kifamilia sawa na mtoto mwingine yeyote. Ili kuzuia manyanyaso, nchi zitatoa taarifa, huduma na kuwasaidia watoto wenye ulemavu na famila zao.4. Watoto wenye ulemavu hawaondolewi kwa wazazi wao bila ridhaa yao ila kama ni kwa ajili ya maslahi yao. Pia katika kufanya hivyo, sheria izingatiwe. Mtoto hawezi kutengwa na mzazi wake kutokana na ulemavu wa mzazi au wake yeye mwenyewe.5. Iwapo ndugu au jamaa wa karibu hawawezi kumtunza mtoto mwenye ulemavu, nchi

zitamtafuta jamaa mwingine au mwanajamii atakayemtunza.

Ibara 24 - Elimu

1. Watu wote wana haki ya kupata elimu. Nchi zitahakikisha kwamba mfumo mzima wa elimu unajumuisha watu wenye ulemavu; na kwamba mfumo wa uelimishaji unaelekeza:a) Kuendeleza uwezo wa kila mwanadamu, utu wake na kujithamini ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu, uhuru na tofauti.

Page 18: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

14

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

b) Kuendeleza haiba na vipawa vya watu wenye ulemavu hadi kufikia ukomo wa kila mmoja wao.c) Kumwezesha mtu mwenye ulemavu kushiriki kwenye jamii huru.

2. Ili kuyafanikisha haya, nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu:a) Hawatengwi kielimu kutokana na ulemavu wala kunyimwa fursa ya elimu ya bure ngazi za msingi na sekondari kutokana na ulemavu.b) Wanachagua aina ya elimu inayowajumuisha na kupatikana kwenye jamii waishimo.c) Wanafanyiwa marekebisho ya kuridhisha kwenye mazingira jenzi ili kuhakikisha kuwa wananufaika na elimu kwa kadri inavyowezekana.d) Wanapata msaada wanaouhitaji ili kunufaika kielimu.e) Wanatimiziwa mahitaji binafsi.

3. Nchi zitawezesha watu wenye ulemavu kujifunza elimu ya jamii na stadi za maisha wanazozihitaji ili kwenda shule na kuchangamana kwenye jamii. Nchi zitafanya hivyo kwa:

a) Kuwaaandaa wanafunzi kujifunza stadi za kimawasiliano (mfano Breli) ujongeaji na kwamba watapata usaidizi kutoka kwa wengine ikiwa ni pamoja na wanarika.b) Kufundisha lugha ya alama.c) Kuhakikisha kuwa watoto wenye ulemavu hususani wasioona, viziwi na viziwi wasioona wanafundishwa kwa njia sadifu za kimawasiliano ili waweze kunufaishwa na elimu kadri iwezekanavyo.

4. Ili kuhakikisha kuwa haki hizi zinatafsiriwa kivitendo, nchi zitawaajiri walimu wenye ulemavu, walimu wataalam wa Breli na lugha ya alama. Kadhalika yatatolewa mafunzo kwa walimu na watumishi katika ngazi mbalimbali za elimu kuhusu jinsi ya kutoa elimu bora kwa watu wenye ulemavu.5. Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wana fursa sawa ya kupata mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya Chuo Kikuu na ujifunzaji katika maisha yote sawa na watu wengine na zitafanya marekebisho yanayohitajika katika kulifanikisha hili.

Ibara ya 25 - Afya

Watu wote wenye ulemavu wana haki sawa ya huduma bora za afya bila kubaguliwa kwa misingi ya ulemavu.Nchi zitahakikisha kuwa huduma za afya na marekebesho zinapati-kana ikiwa ni pamoja na :

a) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma za kiafya za aina mbalimbali, zenye viwango vya ubora na bila/au kwa gharama nafuu.

Page 19: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

15

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

b) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kupata huduma wanazozihitaji kutokana na aina ya ulemavu wao na kukingwa dhidi ya ongezeko la kiwango cha ulemavu au athari zake.c) Huduma za afya zinapatikana ndani ya jamii.d) Kuhakikisha kuwa kwa njia ya mafunzo ya kutosha, watumishi wa afya wanatoa uangalizi wenye ubora ule ule kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kupata ridhaa yao.e) Kuacha ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu katika masuala ya bima za afya na za maisha.f ) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawatobaguliwa na kunyimwa matunzo ya kiafya au huduma za afya, chakula vinywaji kutokana na ulemavu wao.

Ibara ya 26 - Marekebisho na Utengamao

1. Nchi zitachukua hatua (mathalani kwa kukuza hali ya kusaidiana miongoni mwa wanarika) ili kuwawezesha watu mwenye ulemavu kufikia na kuendeleza hali ya kujitegemea kwa kadri iwezekanavyo, na kujumuika katika masuala yote ya maisha. Ili kufikia lengo hili, nchi zitaandaa, kuimarisha na kupanua huduma za marekebisho na utengamao katika nyanja zote za maisha ili:

a) Zianzie katika hatua za awali kadri itavyowezekana kulingana na mahitaji na uwezo wa mhusika binafsi; b) Kusaidia ushiriki na ujumuishwaji wa wahusika katika jamii kwa hiari na kwa`kadri inavyowezekana, kadhalika kupatikana kwenye maeneo yaliyo karibu na jamii waishimo.

2. Nchi zitaendeleza mafunzo kwa ajili ya wataalamu na watumishi wanaofanyakazi katika fani za marekebesho na utengamao.3. Nchi zitapanua matumizi ya vifaa saidizi na nyenzo nyinginezo kama zinavyohusiana na marekebesho na utengamanisho.

Page 20: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

16

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 27 - Kazi na Ajira

1. Watu wenye ulemavu wana haki ya kufanya kazi sawa na watu wengine; wana haki ya kupata riziki kutokana na kazi walizojiamulia kuzifanya katika mazingira yaliyo wazi na yanayofikiwa na watu wote. Nchi zitatunga sheria na kuchukua hatua nyingi zinazofaa ili:

a) Kuondoa ubaguzi kwa misingi ya ulemavu katika maeneo yote ya ajira ikiwa ni pamoja na katika hali ya kutafuta kazi, kuajiriwa kuendelea na ajira, kupandishwa cheo kazini na kufanya kazi katika mazingira salama kiafya;b) Kulinda ajira za watu wenye ulemavu kuhusu usawa katika malipo ya ujira kwa kazi ile ile, usawa wa fursa, usalama kazini na uwezo wa kutoa malalamiko;c) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kujiunga pamoja na kuingia kwenye vyama vya wafanyakazi sawa na mtu mwingine yeyote;d) Kuweka uwezekano wa watu wenye ulemavu kupata huduma za ushauri wa mafunzo kazini.e) Kupanua fursa za kazi, kuandishwa vyeo na kuwasaidia watu wenye ulemavu kutafuta kazi na kudumu kazini;f ) Kuendeleza ajira binafsi, fursa za biashara, ushirika na kuanzisha biashara;g) Kuajiri watu wenye ulemavu serikalini;h) Kuhimiza na kuwasaidia waajiri kuajiri watu wenye ulemavu;i) Kuwarahisishia watu wenye ulemavu kumudu kazi na mazingira yake kwa kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika kwa ajili yao;j) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata uzoefu wa kazi katika soko la ajira;k) Kukuza programu zinazowasaidia watu wenye ulemavu kurudi kazini na kudumu na ajira zao.

2. Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawafanywi watumwa/watwana. Nchi zitawalinda dhidi ya ajira za kushurutishwa sawa na wanavyolindwa watu wengine.

Page 21: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

17

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 28 - Kiwango stahiki cha kuishi na hifadhi ya jamii

1. Watu wenye ulemavu wana haki ya kuwa na viwango stahiki vya maisha wao wenyewe na familia zao. Hii ni pamoja na kupata chakula cha kutosha, mavazi, malazi na kuendelea kuboresha hali yao ya kuishi.2. Watu wenye ulemavu wana haki ya kupata huduma za hifadhi ya jamii toka serikalini bila kubaguliwa kwa kigezo cha ulemavu. Nchi zitailinda haki hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu:

a) Wanaweza kupata huduma, vifaa na msaada wanaouhitaji;b) Wanapata msaada wa kifedha na programu za kuwasaidia kuondokana na umaskini. Hii ni muhimu hasa kwa wanawake, wasichana na wazee wenye ulemavu;c) Wananufaika na progamu za serikali za nyumba na makazi;d) Wanaweza kupata pensheni;

Hali kadhalika familia za watu wenye ulemavu zinazokabiliwa na umaskini nazo pia zitapata msaada toka serikalini ili kuziweze-sha kulipia matumizi yanayohusiana na ulemavu wa wanafamilia.

Ibara ya 29 - Ushiriki katika masuala ya kisiasa na kijamii

Watu wenye ulemavu wana haki katika masuala ya kisiasa sawa na watu wengine. Nchi:

a) Zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza

kushiriki kikamilifu katika

Page 22: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

18

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

masuala ya kisiasa na kijamii; mathalani kuwa na haki ya kupiga kura na kuchaguliwa. Katika kuyatekeleza matakwa haya, itahakikishwa kuwa:

i. Mchakato wa upigaji kura ni rahisi na unafikika;ii. Watu wenye ulemavu wanaweza kupiga kura kwa siri na kuchaguliwa kushika madaraka;iii. Inapobidi, watu wenye ulemavu wanaweza kupiga kura kwa msaada wa watu waliojichagulia wao wenyewe.

b) Kuwahimiza watu wenye ulemavu kujihusisha na mambo ya kiserikali na ya umma ikiwa ni pamoja na:

i) Kujishirikisha na asasi za kiraia na vyama vyenye mtazamo wa kisiasa;ii) Kuunda na kuwa wanachama wa vyama vinavyowakilisha watu wenye ulemavu ngazi za msingi, kitaifa, kikanda na kimataifa.

Ibara ya 30 - Ushiriki katika masuala ya kitamaduni, burudani, mapumziko na michezo

1. Watu wenye ulemavu wanayo haki ya kushiriki katika masuala ya kitamaduni. Nchi zitachukua hatua kadhaa ili kuhakikisha kuwa:

a) Wanapata machapisho, maandiko na sanaa katika hali ambayo watayaelewa;b) Wanaweza kupata programu za televisheni,filamu, maonyesho/ tamthilia na shughuli nyinginezo za kitamaduni katika hali watakayoelewa, (mathalani madokezo na lugha ya alama katika vipindi vya televisheni);c) Watu wenye ulemavu wanaweza kuyafikia maeneo ya kitamaduni kama vile maktaba, makumbusho, nyumba za maonyesho na maeneo mengine muhimu.

2. Nchi zitawezesha watu wenye ulemavu kuendeleza na kutumia vipawa vyao vya kiubunifu, kisanii n.k. kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla.3. Nchi zitahakikisha kuwa sheria zinazolinda nyaraka, maandiko na ubunifu mwingine dhidi ya tabia ya kugushi na kunakilisha, hazitumiki kuwabagua watu wenye ulemavu.

Page 23: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

19

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

4. Watu wenye ulemavu wana haki sawa na mtu mwingine ya kuwa na utamaduni na lugha yao vinavyotambuliwa (mathalani lugha ya alama na utamaduni wa viziwi).5. Watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine ya kushiriki kwenye burudani, mapumziko na michezo. Nchi zitachukua hatua ili:

a) Kuwahimiza kushiriki michezo na watu wasio na ulemavu katika ngazi mbalimbali;b) Kuhakikisha kuwa wanapewa fursa za kuandaa na kushiriki kwenye shughuli za michezo na kupata mafunzo yale yale na misaada kama wavipatavyo watu wengine;c) Kuhakikisha kuwa wanaweza kuyafikia maeneo ya michezo na burudani sawa na watu wengine wanavyoweza;d) Kuhakikisha kuwa wanaweza kushiriki kwenye michezo na riadha shuleni kama ilivyo kuwa watoto wengine,e) Kuhakikisha kuwa wanaweza kupata huduma za kuwasaidia kuaandaa shughuli za michezo na burudani.

Ibara ya 31 - Ukusanyaji wa taarifa na takwimu

1. Nchi zitakusanya na kuchambua taarifa kuhusu watu wenye ulemavu kwa ajili ya kutekeleza maafikiano haya. Katika kukusanya na kutumia taarifa hizi, watazingatia:

a) Kuheshimu haki ya watu ya faragha. Taarifa zitatolewa pale tu wahusika watakaporid-hia.b) Kuheshimu haki za bin-adamu na maadili kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.

2. Taarifa zilizoku- sanywa, zitawekwa kwenye makundi yanayofaa kiasi kwamba nchi zinaweza kujifunza vizuri zaidi jinsi ya kuteleza kivitendo maafikiano haya.3. Nchi zinalo jukumu la kutoa taarifa hizi na kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanaweza kuzisoma na kuzielewa.

Page 24: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

20

Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Toleo la Lugha Nyepesi)

Ibara ya 32 hadi 50 Majukumu ya serikali

Ibara hizi zinafafanua jinsi mtu mmoja mmoja na serikali zitakavyofanya kazi pamoja ili kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanazipata haki zao zote.Mawazo makuu ni:

* Nchi lazima zishirikiane katika kutekeleza maafikiano haya.

* Watu wenye ulemavu na vyama vyao sharti wajumuishwe kwenye shughuli hii.

* Kamati chini ya Umoja wa Mataifa itaundwa ili kuhakikisha kuwa Nchi zinatimiza ahadi zao mintarafu maafikiano haya.

* Nchi zitaaandaa taarifa za mara kwa mara kwa ajili ya Kamati (chini ya Umoja wa Mataifa) zikielezea jinsi zinavyotekeleza Maafikiano haya kivitendo.

* Kamati (chini ya Umoja wa Mataifa) itatoa taarifa za mara kwa mara kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa na makundi mengineyo ikiwa ni pamoja na kutoa maoni jinsi Maafikiano haya yanavyotekelezwa ipasavyo.

* Nchi zilizotia saini Maafikiano haya zina wajibu wa kuyatekeleza kivitendo. Hata hivyo, kila nchi moja moja inaweza kuamua kuvikataa baadhi ya vipengele isivyoridhika navyo ndani ya Maafikiano haya.

* Maafikiano haya yanapaswa kupatikana katika namna ambayo watu wenye ulemavu watayasoma na kuyaelewa.

Kumbuka - Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliyapitia Maafikiano haya mnamo Desemba 2006. Nchi nyingi sasa zimekwisha yasaini na kuyaridhia. Kwa maana hiyo, Maafikiano haya sasa ni sheria ya Kimataifa.

Page 25: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu
Page 26: Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

Kituo cha Habari kuhusu UlemavuSLP 75576 Dar es Salaam.Simu: +255 22 2400227/ + 255 732 991 485Barua pepe: [email protected]: www.icd-tanzania.org

CCBRTSLP 23310

Dar es Salaam.Simu: + 255 22 260 1543

Nukushi: + 255 22 260 1544 Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.ccbrt.or.tz